14.02.2018 Views

vipaji_pages1-100

hugggugu

hugggugu

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Nafsi - Vipaji Vya Asili - Kutoka 31:2-6

Karama Za Kiroho-1 Kor. 12, Efe. 4:11, Rum. 12:6-8

SURA YA KWANZA

CHIMBUKO LA VIPAJI VYA ASILI NA

KARAMA ZA KIROHO

1. Jinsi Binadamu Alivyoumbwa Kwa Ajabu Na Kutisha

Binadamu kwa asili ameumbwa kwa jinsi ya ajabu na

kutisha kweli kweli. Haya si maneno yangu binafsi, bali ni maandiko

ya mtunga Zaburi katika Biblia ambaye ndiye wa kwaza kufanya

ugunduzi huu na kuandika kama ifuatavyo:

“Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu

na kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, na nafsi yangu yajua sana.”

(Zab. 139:14)

Vipaji Vya Asili Na Karama Za Kiroho Katika Maumbile Ya

Binadamu

Mwili - Milango 5 Ya Fahamu

Roho

1

Maandiko matakatifu yanayosimulia historia ya kuumbwa

kwa binadamu kulivyokuwa kwa jinsi ya ajabu kama tunavyosoma

hapa chini:

“Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa

sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na

wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho

juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano

wa Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba”

(Mwa. 1:26-27)

Hapa tunajifunza ya kwamba, binadamu aliumbwa akiwa

tofauti kabisa na viumbe hai vingine vyote, kuanzia malaika,

wanyama na vitu vingine vyote. Kisha tunajifunza binadamu

ameumbwa kwa mfano na sura ya Mungu mwenyewe. Hii ndiyo

ajabu na ya kutisha.

Mfano wa Mungu na sura ya Mungu! Hapa haina maana

ya kwamba Mungu aliumba Mungu mwingine mwenye kufanana

naye. Mungu ni mmoja haumbwi wala kuumbika. Maandiko

yanachomaanisha hapa ni kuwa Mungu katika uumbaji wake wa

kiungu; aliamua kumuumba “kiumbe mtu” katika mfumo wenye

kufanana naye kwa hekima na tabia ili aweze kumwakilisha Mungu

katika utawala juu ya nchi na viumbe vyote vilivyomo.

Maana Ya Mfano Wa Mungu Katika Binadamu

Tumesoma maandiko yakisema, “... kwa mfano wa Mungu

alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba.” Ni nini

maana hasa ya mfano wa Mungu na sura ya Mungu?

Jina la kwanza la Mungu lililotumika katika Mwanzo wakati

aliposema maneno haya, ni jina la Kiebrania la Elohim. Jina hili

liko katika wingi wenye kumaanisha Mungu mmoja mwenye nafsi

zaidi ya moja. Ni Mungu mmoja kwa sababu imeandikwa “Mungu

akasema….” Lakini Mungu ana nafsi zaidi ya moja kwa kuwa

maandiko yanasema “na tumfanye mtu kwa mfano wetu na sura

yetu ...”.

2

Haya maneno ya “mfano wetu” na “sura yetu” ndiyo yenye

kuashiria Mungu mmoja lakini aliyejitambulisha katika nafsi zaidi ya

moja. Kwa mukhtadha huu, Mungu aliamua kumuumba binadamu

kwa mfano wake ambao ni “nafsi tatu” kama tunavyoshuhudia

katika maandiko yafuatayo:

“BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,

akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi.” (Mwa. 2:7)

Maandiko tuliyosoma hapo juu yanadhihirisha mfumo

wa utatu wa binadamu kimaumbile. Mavumbi ya ardhi ndiyo

yalitengeneza mwili na “pumzi ya uhai” ni sehemu ya roho kutoka

kwa Mungu mwenyewe aliyoipulizia ndani ya mwili; na kisha

tunaona mtu anakuwa “nafsi hai”.

Aidha, kila sehemu ya binadamu kuanzia mwili, nafsi na

roho inavyo vitu vinavyoifanya kuwa sehemu kamili kiutendaji.

Mathalan, mwili wa binadamu una kitu kinaitwa “milango ya

maarifa” ambayo ni kuona, kusikia, kuonja, kugusa na kunusa.

Milango hii hutenda kazi kupitia mfumo wa ubongo ambao ndiyo

kama injini ya mwili.

Nafsi ya mtu inavyo vitu vitatu ambavyo ni akili, hisia na

utashi. Na roho nayo inavyo vitatu ambavyo ni “dhamiri”, “ushirika”

na “utambuzi” ambavyo ndivyo Mungu huwasiliana na kuhusiana

na binadamu katika roho.

Uhai wa binadamu huonekana kupitia mwili. Nafsi ya

binadamu ambayo ndiyo yenye akili na hisia na utashi ndiyo

huufanya mwili kufanya mambo yenye kuonekana na wengine,

kuazia kusema na kutenda kwake.

Ukiutazama mchoro hapo juu utakuta jinsi ambavyo mduara

mkubwa wa nje unawakilisha mwili. Mduara wa pili unawakilisha

nafsi, na ule mduara mdogo wa katikati unawakilisha roho ya

binadamu.

3

Kwa mantiki hii, wakati ambapo “nafsi” ya mtu hujidhihirisha

kupitia mwili; hali kadhalika na roho ya binadamu, ambayo ndiyo

kiungo cha mawasiliano kati ya Mungu kiroho, utendaji wake

unadhihirika kupitia nafsi.

2. Tafsiri Ya Misamiati Ya Vipaji Na Karama

Kipaji

Kwa mujibu wa maandiko katika Biblia, kuna ushahidi

wa kuwepo kwa vipaji vya asili ambavyo kusudi lake ni kufanya

mambo ya kiufundi na kitaaluma lakini pasipo kupitia kwanza

kwenye mafunzo na mfumo rasmi wa kielimu.

Kipaji ni neno la Kiswahili ambalo Kamusi ya Kiswahili Sanifu

imelitafsiri kuwa ni “kipawa”. Na neno “kipawa” limetafsiriwa

kuwa ni “uwezo mtu aliozaliwa nao” ambao humwezesha kufanya

jambo fulani vizuri.

Hata hivyo, neno “kipaji” limetafsiriwa kwa lugha nyingine

za kibiblia ambazo ni Kiebrania na kiyunani. Neno la Kiebrania

lililotumika kutafsiri “kipaji” ni chokmah na limetajwa mara 149

katika toleo la Kingereza la KJV.

Tafsiri ya neno chokmah ni “hekima”. Katika Biblia kipaji

cha asili kimetafsiriwa kwa neno “hekima” ambalo kwa lugha ya

kiebrania limetumika neno chokmah na limetajwa mara 149 katika

KJV. Maana ya neno chokmah ni: “fundi” wa silaha za kijeshi

wakati wa vita; au “mbunifu” na mwerevu wa mitambo na vifaa

vya ufundi; au stadi wa kazi za mikono.

Kwa hiyo msamiati wa kibiblia wa neno kipaji ni hekima.

Tunaweza kupata matumizi ya neno chokmah katika maandiko

matakatifu yafuatayo:

4

“Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa

Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; nami nimemjaza roho ya

Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya

kila aina, ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa

fedha, na wa shaba, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora

miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.” (Kut. 31:2-5)

“... ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa

fedha, na wa shaba, Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja

naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani;

nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima,

ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza” (Kut. 31:4-6)

Katika maandiko haya kila mahali neno “hekima” kwa

kiebrania ni chokmah likimaanisha vipaji mbali mbali kwa ajili

ya ubunifu, ufundi na ustadi wa vifaa vya ujenzi na vyombo vya

kutumia kwenye hema ya Mungu kukutana na wana wa Israeli.

Tukiyachunguza maandiko ya Agano Jipya kwa lugha ya

Kiyunani tunakutana na msamiati wa neno “Sophia” pia likiwa

limetafsiriwa kuwa ni hekima ambalo linamaanisha vipaji vya asili.

Neno sophia ambalo kwa Kiswahili ni hekima maana yake

ni “uwezo mpana wa kujifunza na kushughulikia mambo mapya

(full of intelligence); uwezo wa kutendea kazi maarifa na ufundi wa

mambo mtambuka.” Neno sophia limetajwa mara 51 katika toleo

la KJV kwenye Agano Jipya.

Tunaweza kupata matumizi ya neno sophia kwenye

maandiko matakatifu ya Agano Jipya ambayo ni haya yafuatayo:

“Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima,

na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.” (Luk. 2:40)

“Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo,

akimpendeza Mungu na wanadamu.” (Luk. 2:52)

5

Neno hekima ambalo limetajwa kwa Yesu ni sophia

likimaanisha vipaji vya asili. Yesu aliishi kwa muda wa miaka

30 kabla ya kuanza huduma za kiroho ambapo alianza kutumia

uwezo wa Roho Mtakatifu.

Yesu Kristo tangu utoto hadi ujana wake alikuwa amejaa

vipaji vya asili, ikiwemo kazi za ufundi seremala ambayo ilikuwa ni

kazi ya Yusufu baba yake mlezi.

Katika kitabu hiki, msamiati wa neno “kipaji cha asili” ndio

utatumika ambao kwa mujibu wa Biblia ni hekima.

Kipaji cha asili kinaitwa hivyo kwa sababu ya uwezo

maalum wa asili unaomwezesha mtu kufanya jambo kwa viwango

vya juu vya uzuri, ufundi na ubora pasipo kupitia mafunzo rasmi

ya kitaaluma.

Uwezo huu maalum wa asili ndio humfanya mtu kuonekana

wa tofauti na watu wengine katika utendaji wa jambo fulani.

Uwezo huu wa asili ambao ni wa kuzaliwa nao, ndio humfanya

muhusika kujulikana au kuwa mtu maarufu katika jambo lile

ambalo amekirimiwa kulijua na kulifanya kwa viwango vya ubora

katika jamii.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika na wataalamu, kuna vipaji

vya asili kama saba ambavyo vimeorodheshwa kama ifuatavyo: 1.

Ubunifu, 2. Uhusiano, 3. Lugha, 4. Hesabu, 5. Michezo, 6. Muziki,

na 7. Picha.

Japokuwa sio kila mtu huzaliwa na vipaji vyote saba,

uchunguzi uliofanywa umebaini ya kwamba kila binadamu

angalau huzaliwa na aina mojawapo ya kipaji kati ya vipaji hivi, na

kama akipewa fursa ya kubaini na kuendeleza kipaji hicho, kuna

uwezekano kwa kila mtu kuishi maisha bora kutokana na kipaji

chake cha asili.

6

Karama

Kamusi ya Kiswahili Sanifu imetafsiri neno “karama” kuwa

ni “kipawa anachokuwa nacho mtu kwa sababu ya kumwabudu

sana Mungu, aghalabu humpa uwezo wa kuomba haja kwa

Mwenyezi Mungu na kukubaliwa mara moja; ridhaa ya kupokelewa

haja iombwayo”

Kwa mujibu wa kamusi za Biblia, kabla ya kuchambua

maana ya karama za kiroho, hatuna budi tupate kufahamu ya kuwa

Biblia haitoi tafsiri na msamiati huu wa “karama za kiroho” lakini

imetoa maelezo ya kina kuhusu asili yake na jinsi zinavyotenda

kazi. Msamiati wa neno “karama” ndio umetafsiriwa kwa kiyunani

kama “charismata” likiwa na maana ya “karama za neema” na

likilenga “karama” au uwezo maalum kutoka kwa Mungu ambao

hutolewa kwa waamini kupitia Roho Mtakatifu.

Pia kuna tofauti kati ya “karama za kiroho” au “karama za

Roho Mtakatifu na “kipawa cha Roho Mtakatifu”. Kuna aina nyingi

za karama za kiroho, lakini Roho Mtakatifu ni mmoja tu. Kipawa

cha Roho Mtakatifu hupokelewa baada ya mtu kumpokea Yesu

Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wake na kuzaliwa upya kiroho.

(Mdo. 2:38).

Aidha, kuna mgawanyiko maalum wa “karama za kiroho”

ambao ni “karama za Roho”, “ofisi za huduma”, na “karama

za neema”. Wakati ambapo “karama za Roho” ni utendaji wa

Roho Mtakatifu ndani ya mwamini kama ilivyoandikwa katika

1 Wakorintho 12; pia ziko “ofisi za huduma” ambazo ni vipawa

vya kiroho vya utendaji huduma tofauti kama zilivyotajwa katika

Waefeso 4:11. Na pia kuna “karama za Neema” ambazo ni

utendaji wa Mungu kwa ajili ya waamini kama ulivyoanishwa

kwenye Warumi 12.

Orodha ya “karama za Roho” zilizotajwa katika 1 Wakorintho

12: ni kama ifuatayo:

7

1. Neno la hekima

2. Neno la maarifa

3. Kupambanua roho

4. Imani

5. Karama za kuponya

6. Matendo ya miujiza

7. Unabii

8. Kunena kwa lugha

9. Tafsiri za lugha

Hizi “karama za Roho” naweza kuzitafsiri kuwa ni “karama

za udhihirisho” (Manifestational gifts). Maana yake zenyewe

zinatenda kazi ya kudhihirisha utendaji wa Roho Mtakatifu ndani

ya waamini ambao wamekirimiwa huduma na utumishi wa kiroho

katika mwili wa Kristo.

Orodha ya “ofisi za huduma” zilizotajwa katika Waefeso

4:11: ni kama ifuatayo:

1. Mitume

2. Manabii

3. Wainjilisti

4. Wachungaji

5. Waalimu

Hizi zinaitwa “ofisi za huduma” ambazo nimeziita “karama

za uwezesho” kwa sababu zinafanya kazi ya kuwakamilisha

watakatifu ili kazi ya huduma itendeke. Ni karama za kuwezesha

waamini kupata uzoefu wa kutumika katika kuujenga mwili wa

Kristo.

Orodha ya “karama za neema” zilizotajwa katika Warumi

12 ni kama ifuatavyo:

1. Uhamasishaji

2. Utoaji

8

3. Uongozi

4. Rehema

5. Unabii

6. Huduma

7. Ualimu

Hizi ni “karama za neema” ambazo zinaitwa “karama za

utumishi” (Serving Gifts). Mungu Baba huwagawia waamini

karama za neema ili wapate kutumikiana wenyewe kwa wenyewe

mara baada ya kukamilishwa na zile “karama za uwezo” ambazo

ni “ofisi za huduma”.

3. Tofauti Kati Ya Vipaji Vya Asili Na Karama Za Kiroho

Kwanza kabisa ni muhimu kutambua mapema ya kwamba

“vipaji vya asili” si “karama za kiroho”. Kwa kifupi ni kwamba, “kipaji

cha asili” chimbuko lake ni kibaiolojia (natural and biological); na

“karama za Roho” asili yake ni ya kiroho na ya kiungu (spiritual

and supernatural).

Jambo muhimu la pili ni kwamba, kila binadamu (mwamini

na asiye mwamini) huzaliwa na vipaji vya asili lakini kimojawapo

kati ya vingine ndicho hujitokeza zaidi na mhusika akajulikana

kupitia kipaji hicho cha asili.

Lakini si kila binadamu anayezaliwa kibaiolojia huzaliwa

akiwa na “karama za kiroho”. Tumejifunza ya kwamba “karama za

kiroho” ni kwa ajili ya “waamini peke yao”, na kwa ajili ya matumizi

ya kiroho peke yake. Kwa hiyo, kipaji cha asili mtu huzaliwa nacho

kwa mara ya kwanza, lakini “karama za kiroho” hupokelewa na

mtu akiisha kuzaliwa mara ya pili kiroho.

Jambo muhimu la tatu ni kwamba, “vipaji vya asili”

huwanufaisha zaidi wenye kuzaliwa navyo ikiwa ni pamoja na

kuwaneemesha kwa maslahi ya kibinafsi. Lakini “karama za

9

kiroho” kusudi lake ni “kuwahudumia na kuwanufaisha wengine”

ambao Mungu anapenda kuwasaidia kupitia uwezo wake wa

kiungu (supernatural means).

Jambo muhimu la nne, ni kwamba vipaji vya asili vinahitaji

kuendelezwa kwa mafunzo na mazoezi; wakati ambapo “karama

za kiroho” zenyewe hutenda kazi kulingana na kiwango cha ukuaji

wa kiroho wa mwamini na uhusiano wa karibu wa kiroho kati yake

na Mungu.

Vipaji Vya Asili Hukaa Katika Nafsi Ya Mtu

Katika uchambuzi wa utendaji wa vipaji vya asili na karama

za kiroho, tutaona ya kwamba, vipaji vya asili chimbuko lake ni

katika nafsi ya binadamu, na chimbuko la “karama za kiroho”

chimbuko lake ni katika roho ya binadamu.

Hebu tupitie kwa ufupi kuhusu “vipaji vya asili” jinsi

vinavyotenda kazi kutokea kwenye nafsi. Ndani ya nafsi ndimo

mna vitu vikuu vitatu ambavyo ni akili, hisia na utashi. Kila “kipaji

cha asili” kwa asili yake lazima “kitumie akili” ambayo ni sehemu

ya nafsi, lazima “kiguse hisia” ambayo sehemu ya nafsi, na lazima

kitokane na “utashi wa mtu’ ambao pia ni sehemu ya nafsi.

• Ni rahisi kwako kuliko mengine na wengine

• Hutumii nguvu nyingi kupita kawaida

• Inaeleweka kwa urahisi

• Unaona ni kawaida na unashangaa kwanini wengine hawawezi

• Unafanya kwa ubora zaidi

• Unafanya kwa furaha na shauku ya moyo

Karama Za Kiroho Makao Yake Ni Katika Roho Ya Mtu

Utendaji wa “karama za kiroho”, tofuati na “vipaji vya

asili”, wenyewe chimbuko lake ni katika roho ya binadamu.

Kama tulivyojifunza kwamba roho ya binadamu inatokana na vitu

10

vitatu ambavyo ni dhamiri, ushirika na utambuzi. Kwa kuwa asili

ya karama za kiroho ni “hali ya kiungu” (supernatural source) na

hutenda kazi kutokea ndani ya roho yake.

Kwa mujibu wa maandiko matakatifu, tunajifunza ya kuwa

Roho Mtakatifu ndiye mdhibiti mkuu wa karama na vipawa vya

huduma za kiroho. Hatua ya kwanza kazi ya Roho Mtakatifu ni

kumzaa mtu mara ya pili (Yoh. 3:3), na tunafundishwa hali hii ya

kuzaliwa mara ya pili hufanyika ndani ya roho ya mtu (Yoh. 3:6).

Baada ya Roho Mtakatifu kumzaa upya mtu katika roho

yake, hatua ya pili ni kujaa ndani ya mtu na kufanya makao ya

kudumu ndani roho ya binadamu. Na humo ndimo utendaji wa

karama za Roho pamoja na vipawa vya huduma za kiroho hutokea

na kudhihirika katika nafsi ya mtu.

11

SURA YA PILI

UCHAMBUZI WA VIPAJI VYA ASILI

Utangulizi

Kwa kuwa kipaji ni kitu cha asili ya kuzaliwa nacho, kila

binadamu katika mfumo wa ubongo amesukwa kufikiri na kutenda

kulingana na nguvu za fikra zilizowekwa ndani yake. Kwa hiyo

katika kuchambua vipaji tunakwenda kupitia na kujifunza kuhusu

uwezo wa asili alionao mwenye kipaji cha asili.

Kimsingi, kipaji cha asili ndicho kinachomtofautisha mtu

na watu wengine na ndio utambulisho wake kwa wengine katika

jamii. Na hii inatokana na taarifa kutoka katika maandiko ya Bibilia

pamoja na tafiti za kisayansi ambazo zinathibitisha ukweli huu.

Ziko nadharia nyingi zinazofundisha habari ya vipaji vya

asili, lakini katika sura hii, tunakwenda kufanya uchambuzi wa aina

saba tu za vipaji vya asili ambavyo vimo ndani ya kila binadamu

ukiwemo na wewe msomaji wa kitabu hiki.

Katika kufanya uchambuzi kuhusu nguvu na uwezo alionao

mwenye kipaji husika, pia tutachambua viashira vya ufanisi kwa

kila kipaji. Viashiria vya ufanisi ni maeneo maalum ambayo kila

kipaji huonesha upekee na umaalum wa ubora kupitia mwenye

kipaji husika.

Mwisho kabisa, uchambuzi wa vipaji vya asili utabainisha

aina mbali mbali za fursa za kitaaluma ambazo mwenye kipaji

anaweza kuzimudu kwa viwango vya ubora wake. Vipaji vya asili

viko saba kama vilivyoorodheshwa hapa:

12

1. Kipaji cha Ubunifu wa mawazo

2. Kipaji cha Mahusiano

3. Kipaji cha Lugha

4. Kipaji cha Hesabu

5. Kipaji cha Michezo

6. Kipaji cha Muziki

7. Kipaji cha Picha

Kumbuka ya kwamba kila binadamu anapozaliwa viashiria

vya mambo saba haya ya vipaji vya asili huwa vimo ndani yake.

Lakini kuna kipaji kimojawapo ambacho hujitokeza na kuonekana

zaidi kuliko vingine na hicho ndicho hutafsiriwa kuwa kipaji cha

mhusika.

Kwa hiyo, tunakwenda kupitia kwanza nguvu za kimaumbile

za kila kipaji, pili, tunachambua viashiria vya ufanisi wa kila kipaji,

na tatu, tunaorodhesha aina ya fursa za kitaaluma zinazoambatana

na vipaji vya asili kwa wahusika.

13

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA

UBUNIFU

14

Kipaji cha ubunifu kwa lugha ya Kiingereza ni Intrapersonal

Intelligence ambacho kimebeba uwezo maalum wa kubuni

mambo mapya.

Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Ubunifu

Mwenye kipaji hiki ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa

katika kufikiri, kupata na kukusanya mawazo pamoja.

Kimaumbile katika mfumo wake wa ubongo seli za

fahamu zimesukwa katika hali ya fikra zenye kina, kukusanya

mawazo pamoja, kufanya maamuzi yenye mwelekeo, uwezo wa

kuchambua katika hali ya uhuru wa hiari.

Mwenye kipaji cha ubunifu pia anao uwezo mkubwa wa

kujitathmini na kujifahamu kibinafsi kuanzia mawazo, hisia na

utambuzi wa ndani.

Kana kwamba hii haitoshi, mwenye kipaji cha ubunifu

ana uwezo mkubwa wa kuiongoza tabia binafsi, kujua nguvu na

udhaifu binafsi, kubuni fikira mpya, kupanga shughuli na kutatua

matatizo.

Viashiria Vya Ufanisi Wa Kipaji Cha Ubunifu

Kila mwenye kipaji cha ubunifu atajulikana na kutambulika

kwenye maeneo yake ya ufanisi unatokana na nguvu za kipaji

chake. Baadhi ya maeneo ya ufanisi wa kipaji cha ubunifu ni

pamoja na:

• Utambuzi wa viwango vya hisia binafsi

• Uwezo wa kujitawala na kufanyia kazi mawazo na hisia binafsi

• Njia nyepesi za kueleza mawazo binafsi

• Hamasa ya kubaini na kutekeleza malengo

• Ufanisi wa kazi uwapo huru mwenyewe na peke yako

15

• Udadisi wa kujua maana ya maisha

• Uwezo wa kujitawala kibinafsi wakati wa kujifunza

• Kutamani sana kupata uzoefu wa ndani ya nafsi

• Uwezeshaji na uhamasishaji wengine

• Kufurahia kufikiri mikakati, kuandika makala na kupenda

mikakati ya kujitathimini binafsi

• Kujua ukomo wa mipaka ya uwezo wako

• Uwezo wa kuchambua, kubaini na kutathmini mambo/

mazingira

Fursa Za Kitaaluma

Kipaji cha ubunifu kina fursa nyingi za kitaaluma iwapo

mwenye kipaji hiki atajaliwa kujitambua mapema na kukinoa kwa

ajili ya matumizi yenye tija. Baadhi ya fursa ambazo mwenye kipaji

cha ubunifu anaweza kuzimudu kwa ufanisi mkubwa ni pamoja na

kuwa:

• Jaji

• Mshauri

• Wakili

• Mkufunzi

• Mwanasheria

• Mtaalamu wa matibabu

• Mwanandishi wa riwaya

• Muuguzi wa magonjwa ya akili

• Mwana falsafa

• Mtaalamu wa hisabati

• Kiongozi

16

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA

UHUSIANO

17

Kipaji cha uhusiano kwa lugha ya Kiingereza ni Interpersonal

Intelligence ambacho kimebeba uwezo maalum wa kutengeneza

na kudumisha mahusiano.

Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Uhusiano

Kimauimbile, mtu mwenye kipaji cha uhusiano, katika

mfumo wa ubongo wake anazo seli za neva zenye kumwezesha

kutengeneza mawasiliano na wengine. Anao uwezo mkubwa wa

mwingiliano wa kijamii, usikivu, ushirikishaji, kujenga mahusiano,

utoaji na uwezo wa kuelewa na kufanya kazi vizuri na watu.

Mtu mwenye kipaji cha uhusiano ni mwepesi na mwenye

ukaribu wa kuchukuliana na watu na ushiriki wa kihisia wa mambo

wanayopitia. Hii ni pamoja na uwezo wa kutawala, kusuluhisha,

kuhamasisha, kuongoza, kuelekeza na kushauri wengine.

Viashiria Vya Ufanisi Wa Kipaji Cha Uhusiano

Mwenye kipaji cha uhusiano hutambulika kwa viashiria vya

uhusiano ambavyo ni pamoja na:

• Nguvu za kuongoza

• Ufanisi katika kujenga mtandao na wengine

• Uwezo wa kujadiliana, kujenga hoja za utetezi na mzuri katika

usuluhishi

• Uwezo wa kuongea na kupangilia mambo

• Kufurahia kuwa mlezi wa vipaji vya wengine

• Uwezo wa kutanguliza wengine

• Uwezo wa kuhisi na kutambua hisia, hulka, tabia na matarajio

ya wengine

• Uwezo wa kushawishi wengine

• Ufanisi katika kufanya kazi na kundi, juhudi za pamoja katika

kikundi na utendaji wa pamoja

• Uwezo wa kuunganisha watu wakawa wamoja

• Uwezo wa kujenga mahusiano ya kijamii ya kudumu

18

Fursa Za Kitaaluma

Kipaji cha uhusiano kina fursa nyingi za kitaaluma ambazo

mhusika anaweza kuonesha ufanisi wa kitaaluma. Baadhi ya fursa

za kitaaluma ni pamoja na hizi zifuatazo:

• Mwanasiasa

• Kiongozi wa dini

• Muuzaji

• Mkufunzi

• Mshauri

• Mtaalamu wa sayansi ya jamii

• Msemaji/Mtalaamu wa lugha

• Mtaalamu wa kijamii

• Mtaalamu wa saiklojia

• Afisa mahusiano

• Mkurugenzi wa rasilimali watu

• Meneja

• Mhamasishaji

19

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA

LUGHA

20

Kipaji cha lugha kwa lugha ya Kiingereza ni Linguistic

Thinking ambacho kimebeba uwezo maalum wa umahili katika

lugha.

Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Lugha

Kimauimbile mtu mwenye kipaji cha lugha, katika mfumo

wa ubongo wake anazo seli za neva zinazojenga umahili wa lugha

na umakini wa maana za maneno, sauti, mahadhi pamoja na

matumizi tofauti ya lugha mbali mbali.

Uwezo wa kufikiri kwa njia ya maneno na kutumia maneno

kwa ufasaha katika kuongea na kuandika.

Pia mwenye kipaji cha lugha huwa ni mwepesi wa kujifunza

mifumo na miundo ya lugha na matumizi yake.

Viashiria Vya Ufanisi Wa Kipaji Cha Lugha

• Huhitaji kujieleza kibinafsi kwa kuandika au kutumia maneno

mengi

• Hupenda kulumbana, kuhoji, kuburudisha na kuelekeza

• Hupenda kuandika, kucheza na maneno, kusoma na kusimulia

visa na hadithi

• Huwa na kiwango kizuri cha elimu ya jumla

• Huuliza maswali mengi

• Hupenda kuongoza/kushiriki katika mijadala

• Hupendelea mbao za kuandikia, vifaa vya kutunza maneno, na

vifaa vya kunakili maneno

• Utamkaji vizuri wa maneno

• Kujifunza lugha kwa urahisi

• Huwa na kumbukumbu nzuri ya majina, tarehe, na majina ya

maeneo

21

Fursa Za Kitaaluma

• Mhariri

• Mwandishi wa hotuba

• Mtunga mashairi

• Mwandishi wa riwaya

• Mwanasiasa

• Mtunza hakimiliki

• Msemaji/Mtaalamu wa lugha

• Mwandishi wa michezo ya kuigiza

• Mwanasheria/Wakili

• Mwandishi wa habari

• Mkufunzi

22

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA

HESABU

23

Kipaji cha hesabu kwa lugha ya Kiingereza ni Logic/

Mathematical Thinking ambacho kimebeba uwezo maalum wa

kuchanganua matatizo ya kinadharia kwa kutumia mahesabu.

Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Hesabu

Kimauimbile, mtu mwenye kipaji cha hesabu, katika mfumo

wa ubongo wake anazo seli za neva zinazojenga uwezo wa kufikiri

na kuchambua mambo kisayansi; uwezo wa kuelewa kanuni na

mifumo na michanganuo ya kimahesabu.

Viashiria Vya Kipaji Cha Hesabu

• Uwezo wa nidhamu ya ndani katika kufikiri

• Uwezo wa kuhesabu na kuthibisha majibu ya hesabu

• Uwezo wa kufikiria sana mambo

• Shauku ya kujua nini kinafuata mbeleni

• Kupenda kutafakari mambo kimahesabu

• Kupenda kubuni nadharia zinazoonesha jinsi kufanya mambo

• Hupenda kuthibitisha usahihi wa kitu kabla ya kukitumia

• Kuonesha uwezo wa kutambua na kutatua matatizo

Fursa Za Kitaaluma

• Mwanasayansi

• Daktari wa tiba

• Mwanahisabati

• Meneja wa mradi

• Mhasibu

• Mkutubi wa chuo kikuu

• Mhandisi

• Mtafiti

• Mtaalamu wa programu za kompyuta

• Mtaalamu wa tiba ya mifuba

• Mtaalamu wa benki

• Mwanasheria

• Mpelelezi

• Mwindaji wanyama

• Mfanyabiashara/mjasiriamali

24

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA

MICHEZO

25

Kipaji cha michezo kwa lugha ya Kiingereza ni Kinesthetic

Thinking ambacho kimebeba uwezo maalum wa ufundi wa

kutumia viungo vya mwili na miondoko; na uwezo kumudu vitu au

mambo yanayokuzunguka.

Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Michezo

Kimauimbile, mtu mwenye kipaji cha michezo, katika

mfumo wa ubongo wake anazo seli za neva ufundi wa miondoko,

kugeuza maungo ya mwili, na mizunguko hususani kucheza mpira

wa miguu, riadha, kubiringika juu ya kiti bila kuumia, kujigeuza

mwili pasipo maumivu;

Hali kadhalika mwenye kipaji cha michezo ana ufundi wa

asili wa kutumia viungo vya mwili na miondoko; na uwezo wa

kumudu vitu au mambo yanayokuzunguka; Wenye vipaji vya

michezo ni watu walioumbwa kujifunza na kufikia viwango vya

ubora wa vipaji kwa njia ya michezo.

Viashiria Vya Ufanisi Wa Kipaji Cha Michezo

• Uwezo mzuri wa kujikusanya kimwili

• Mwepesi kuwahi muda na kufanya kwa wakati

• Hukabiliana na matatizo kwa nguvu za mwili

• Kupenda kunyoosha viungo vya mwili na mazoezi

• Kupenda michezo ya kuigiza

• Kupenda kucheza ngoma/muziki

• Hufikiri wakati wa miondoko

• Hupenda kuchonga vinyago na burudani

• Kubuni vitu vipya vya kimichezo

Fursa Za Kitaaluma

• Mwigizaji

• Mwanariadha

• Mcheza mziki

26

• Mvumbuzi

• Sonara

• Mchongaji

• Mwanasanaa

• Dreva wa mashindano ya magari

• Mtaalamu wa tiba maungo

27

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA

MUZIKI

28

Kipaji cha muziki kwa lugha ya Kiingereza ni Musical

Thinking ambacho kimebeba uwezo maalum wa kutumia sehemu

ya ubongo iitwayo sular ambayo imejaa fikira za muziki na hutumia

utambuzi wa ndani wa kufahamu mambo yasiyo dhahiri.

Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Muziki

Kimauimbile, mtu mwenye kipaji cha muziki, katika mfumo

wa ubongo wake anazo seli za neva zenye uwezo wa kuimba

au kupiga vyombo vya muziki, uwezo wa kutambua mahadhi na

kupambanua mambo yasiyo dhahiri kupitia muziki. Pia mwenye

kipaji cha muziki ana uwezo wa kuwasoma watu kwa kusikiliza

sauti zao na lugha kupitia maungo ya mwili, na sio kwa kusikiliza

maneno peke yake.

Viashiria Vya Ufanisi Wa Kipaji Cha Muziki

• Utambuzi wa ndani wa kuhisi wakati mambo ni mazuri au

mabaya

• Hafanyi mambo mpaka amejisikia yuko sahihi

• Hawezi kujieleza lakini ana hisia za kutambua ni nani wa

kuaminiwa na ambaye sio

• Yuko makini na hisia kali na mazingira na kujisikia au kutojisikia

raha katika maeneo fulani

• Hutafuta kusikiliza sauti, huvutiwa na muziki, na hupenda

kutunga nyimbo/muziki

• Uwezo wa kuimba vizuri kwa vina na mjuzi wa kupiga vyombo

• Kutunza muda katika kuimba

• Uwezo wa kusikiliza na kukosoa muziki

• Ukusanyaji wa nyimbo, ala na muziki

• Hupenda kuchezesha miguu, vidole au kalamu anapofanya

kazi au kusikiliza jambo

29

Fursa Za Kitaaluma

• Mwongozaji

• Mtunga ala

• Mtunzi wa nyimbo

• Mhandisi wa muziki

• Mtaalamu wa kinanda

• Msimamizi wa disko

• Mwalimu wa Muziki

• Mtaalamu wa nyimbo za ala

• Mchezaji wa jukwaani

• Mchezaji muziki

• Mwanamuziki

Mwimbaji

• Mhadisi wa uzalishaji muziki

• Msemaji wa shughuli au mshehereshaji (MC)

30

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA

PICHA

31

Kipaji cha picha kwa lugha ya Kiingereza ni Visual/Spatial

Thinking ambacho kimebeba uwezo maalum kupokea kutoka

ulimwengu wa picha/maumbo na kuyachora, hadi kutoa kitu halisi

kwa mfano wa picha kutoka akilini.

Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Picha

Kimauimbile, mtu mwenye kipaji cha picha katika mfumo

wa ubongo wake anazo seli za neva za kutazama rangi, mwanga,

umbo na vina vya vitu; ikiwa ni pamoja na kufumba macho na

kutafakari, kuona mambo ambayo hayaonekani kwa macho ya

asili; uwezo wa kukitoa kitu kwenye nafsi ya ndani (non-conscious)

hadi kwenye akili (consciousness).

Viashiria Vya Ufanisi Wa Kipaji Cha Picha

• Hufikiri katika mfumo wa picha na kutafsiri michoro/picha kwa

urahisi

• Uwezo wa kupokea mawazo kwa njia ya maumbo na kuyachora

mawazo hayo katika mfumo wa picha

• Uwezo wa kukumbuka sura lakini husahau majina

• Huweza kuvusha mawazo huku akiendelea kusikiliza

Fursa Za Kitaaluma

• Mchongaji

• Mwanamazingira

• Kiongozi

• Mtendaji mkuu

• Mbunifu wa michoro

• Mhandisi

• Mwandishi wa Sheria

• Nahodha

• Mtaalamu wa video

• Mpiga picha

32

• Mpaka rangi

• Mwendeshaji

• Mtaalamu wa mikakati ya vita

• Msanifu wa majengo

• Rubani

33

Njia Za Kutambua Kipaji Chako

Utangulizi

Kujitathmini na kutambua una kipaji gani cha asili si kazi

nyepesi. Si tukio la mara moja bali ni mchakato. Na mchakato

wenyewe unategemea mambo mengi kuanzia umri wako,

mazingira unamoishi na kukulia kimalezi; aina ya watu walio karibu

na wewe mfano wazazi au walezi na jamaa wa karibu; kama ni

mwanafunzi ni aina gani ya shule, chuo na masomo unayochukua.

Yote haya ni mazingira ambayo yana mchango mkubwa kwako

katika kufanikisha au kutokufanisha zoezi la kujitathmini na

kutambua kipaji chako.

Hata hivyo, kwa kuwa kipaji cha asili ni hali ya kuzaliwa

nayo, uchunguzi unaonesha kwamba mpaka mtu anapofikia umri

wa miaka 14 tayari anaweza kujitathmini na kubaini kipaji chake.

Kama mtu hakupatwa majanga ya kuathiri afya yake, uwezo wa

vipaji ndani yake huendelea kuwemo ndani kama atadhamiria

kujitathmini kwa kutafuta kujua anaweza nini ili kujipanga kupata

elimu itakayomsaidia kunoa kipaji chake.

Uwezo wa kuzaliwa nao hauwezi kuathiriwa na upungufu

wa elimu au uzoefu, japokuwa elimu na uzoefu vinaweza kutumika

kuboresha uwezo wa kipaji cha asili alichonacho mtu.

Kila mtu amezaliwa na uwezo pekee na maalum ambao

humfanya kuwa tofauti na wengine katika jamii. Yafuatayo ni

baadhi ya mambo machache ya kukusaidia kutambua una vipaji

au kipaji gani:

1. Kitu Gani Kilicho Kushughulisha Sana Utotoni?

Kama wewe ni mtu mzima tayari, hasa kuanzia miaka 30

na kuendelea, hebu tumia muda kama dakika mbili kujikumbusha

enzi zako za furaha kuanzia shule ya msingi. Ni jambo gani

34

ambapo ushiriki wako ulikuwa unapata furaha sana kiasi kwamba

unapokumbuka unasisimka mpaka leo. Na jambo gani hasa

lililochukulia muda mwingi na hata kukufanya ukorofishane na

wazazi au walimu au watoto wenzako wakati kumbe hilo ndilo

ulilokuwa ukilifurahia sana?

Pengine ulikuwa unahamasika kushiriki mashindano

katika michezo kama mpira wa miguu au riadha. Marafiki zako

walikufurahia sana ukiwa katika timu yao wakitarajia watashinda

kwa sababu yako. Na wewe uliifurahia sana hali hiyo. Pengine

ulikuwa unapendelea sana kuimba kwaya au mashairi au ngoma,

na hata kuwa kiongozi wa kwaya au kutunga na kufundisha

nyimbo au mashairi. Pengine ulikuwa unapenda sana michezo ya

kuigiza na kila mara ulikuwa nyota katika michezo uliyoshiriki.

Hapa ni muhimu kutofautisha kupenda kitu kwa sababu kina

umaarufu, na kuwa na uwezo wa kufanya kitu hicho kwa viwango

vya ubora bila kutumia nguvu nyingi kama wengine. Maana watu

wengi wanapenda mambo ambayo wanaona yamewafanya

wengine kuwa maarufu na wao wanatafuta umaarufu kwa kuiga

lakini hawana uwezo wa kufanya mambo hayo kwa viwango vya

ubora. Kumbuka “kupenda sana” ni tofauti na “kuweza sana.”

Kwa hiyo, katika kutafakari enzi zako za utotoni, hebu

fuatilia ni jambo gani ambalo limeendelea kushika nafsi yako

mpaka wakati huu wa ukubwani.

Bado unapenda kushiriki mashindano ingawa hivi sasa

ushindani wako umeuelekeza labda kwenye biashara mpya, bado

unaweza kuwa unapendelea kufanya mambo magumu magumu,

na miradi ya kimkakati japokuwa sasa unaifanyia kwenye

makampuni ya ushauri.

Mpaka hivi sasa, vipaji vya asili hujidhihirisha kupitia

mambo tunayopenda sana na tunajikuta tuna uwezo nayo kuliko

mengine.

35

Mara nyingi msukumo wa kupenda au kuchagua kufanya

mambo fulani ambayo unayamudu vizuri kuliko wengine hutokana

na nguvu za vipaji vya asili vilivyomo katika nafsi zetu.

2. Jambo Gani Unalipenda Sana?

Swali hili ni kwa kila mtu. Jambo gani unalipenda sana.

Tafadhali zingatia, kupenda kunakotajwa hapa ni mvuto wa hisia

za ndani za kutamani kufanya jambo fulani hata kama hutapata

malipo yoyote. Tena wakati mwingine wewe ndio uko tayari kulipia

gharama za kufanya jambo unalolipenda sana badala ya wewe

kulipwa.

Haya tuseme leo ni jumamosi ambapo si siku ya kazi. Una

muda ambao ni huru wa kufanya jambo unalolipenda. Pengine

ni kupiga gitaa au kinanda au kuandika riwaya au jambo jingine

lolote (lakini isiwe kutazama tv na tamthilia).

Hili jambo ambalo umeamua kulifanya, kila mara

unapolifanya, linakuvuta kweli kweli. Akili zote, mwili na hisia na

utambuzi wa ndani vinajikuta vikilifanya kwa ukamilifu na kwa

kunogewa hasa. Unazama katika kufanya jambo hilo mpaka

unasahau ni saa ngapi, na hata unasahu muda wa kula.

Haya, fikiria kazi unayoifanya katika siku za kawaida za

kazi, kama ungeifanya katika msukumo na mvuto na mzamo

kama ulivyozama kwenye jambo hili la Jumamosi huru, ufanisi

wako ungelikuwaje kazini?

Nakwambia watu wengi wanafanya kazi kwa sababu ya

malipo ya mshahara lakini sio kwamba wanafanya kwa msukumo

wa vipaji vya asili. Ndiyo maana kufanya kazi ambazo haziendani

na vipaji vya asili hakuleti ufanisi mkubwa na maendeleo yake ni

duni.

36

Lakini kama mtu akifanya kazi ambayo inaendana na kipaji

chake, hataangalia saa ya kumaliza kazi bali anavutwa kufanikisha

kazi ile ifikie viwango vya ubora stahiki na hiyo ndiyo inayomfanya

ajitume kufanya vema kuliko wengine.

Pasipo kujali mazingira uliyomo hivi sasa, na mambo

unayoyafanya kwa sababu ya desturi tu, hebu tafakari ni jambo

gani ambalo una msukumo wa ndani unaokushuhudia kuwa

ukilifanya utalimudu vizuri bila kutumia nguvu nyingi na utafanya

kwa viwango vya ubora tofauti na wengine?

Inawezekana jambo hilo ni tofauti kabisa na shughuli

unayoifanya hivi sasa ambayo pengine ndiyo inayokupatia riziki.

Au pengine bado ni mwanafunzi lakini masomo unayochukua

hayaendani na jambo lile unalolitamani sana kulifanya na ukipewa

fursa utalimudu vizuri kuliko hata masomo unayochukua hivi sasa.

Kama unahusika katika eneo hili, ujue kwamba unakabiliwa

na changamoto ya mgongano wa kimaslahi kati ya kipaji cha asili

na mambo unayoyafanya hivi sasa yanayokupatia riziki au msaada

wa kimaisha. Unahitaji hekima ya Mungu katika kuyaweka kwenye

mizania sawa.

Ushauri wangu hapa ni kwamba wakati wa muda wako wa

ziada ambapo hauko kazini au masomoni, wakati umekamilisha

majukumu yako ya kila siku kwa mujibu wa mkataba, tumia

muda wa ziada katika kufanyia mazoezi hilo jambo ambalo una

msukumo nalo.

Kama ni mwanafunzi omba ushauri kwa wazazi/walezi na

walimu kuhusu msukumo uliomo ndani yako na jinsi unavyofikiria

kama ungepewa fursa ya kufanya jambo hilo ungetimiza ndoto

yako kuhusu hatma yako.

Kama ni mfanyakazi uliyeajiriwa au mjasiliamali

unayejitegemea, hakikisha unajipanga vizuri kuhusu jinsi

37

utakavyolianza jambo hilo pasipo kuingiliana na mambo yako

yanayokuwezesha kupata riziki au msaada wa mahitaji yako ya

sasa. Tafuta ushauri na pengine anza taratibu kwa muda wa ziada.

Inategemea ni jambo gani na kama linawezekana kwa

muda wa ziada. Lakini ujue kwamba kama jambo hilo linakunyima

usingizi na linakukereketa kila mara, huenda kipaji chako cha asili

kimebebwa kwenye jambo hilo.

3. Wengine Wanasemaje Juu Yako?

Njia nyingine ya kutambua una kipaji gani cha asili ni maoni

ya wengine walio karibu na wewe. Ni muhimu kusikiliza kwa makini

vile wengine walio karibu na wewe wanavyokutafsiri vile ulivyo.

Kwa kuwa kipaji cha asili kazi yake ni kuhudumia wengine

katika jambo lile ulilopewa uwezo kulifanya kwa viwango vya

ubora kuliko wengine, lazima wahusika watasema habari zako

kuhusu uwezo wako.

Hebu tafakari ni jambo gani ambalo watu huja kwako

kutafuta msaada wako, au kukuomba utoe huduma kwao kwa

jambo hilo.

Maoni ya wengi kuhusu jambo unalolimudu vizuri ni

sehemu ya ushahidi kwamba una kipaji cha asili katika jambo

hilo. Na hasa ikiwa watu wako tayari kukulipa kwa ajili ya jambo

hilo. Sio kwamba wanakupenda wewe bali wanapenda kipaji

chako. Wanakihitaji katika kuboresha mambo yao ambayo wewe

ni mmoja wa waboreshaji wao.

4. Jambo Gani Unaliweza Kwa Urahisi?

Kimsingi hakuna jambo jepesi hata kama ni dogo. Lakini

kwa muktadha wa mada hii, kati ya mambo ambayo ni magumu

kwa wengine, huenda kuna jambo ambalo kwako ni jepesi kwako

38

na halikupi shida wala kukuhenyesha kama wengine.

Mara nyingi mambo ambayo ni rahisi sasa kwako, sio

kwamba ni rahisi bali wewe umejaliwa uwezo maalum wa

kuyamudu ndiyo maana yanakuwa mepesi kwako. Katika hayo

mepesi, ambayo yanawatoa jasho wengine, huenda ndipo kipaji

chako cha asili kilipolalia.

Matumizi Mabaya Ya Vipaji Vya Asili

Katika harakati za kutafuta na kufanya mambo kwa

muktadha wa vipaji vya asili, yako mambo ambayo hayatakiwi

kutafsiriwa kuwa ni vipaji vya asili. Japokuwa wahusika wanaweza

kulazimisha na kushinikiza ya kwamba wanatumia vipaji vya asili

kufanya mambo hayo, ukweli unabakia kwamba vipaji vya asili

vinatambuliwa kwa nguvu na viashiria vyake vya ufanisi. Baadhi

ya mambo ambayo si vipaji vya asili ni haya yafuatayo:

1. Tamaa Ya Umaarufu Wa Kutajirika Haraka

Kuna watu wenye tamaa ya kutafuta utajiri wa haraka na

huwa tayari kuupata kwa haraka pasipo kufuata taratibu halali za

kuupata utajiri huo. Kundi hili hutafuta “umaarufu” kama njia ya

mkato ya kujipatia utajiri wa haraka.

Wako tayari kuwania fursa za umaarufu kama uongozi wa

kisiasa au huduma za kikanisa kwa sababu tu huko ndiko kuna

majukwaa ya kuwafikia watu wengi.

Misukumo ya jinsi hii haiwezi kutafsiriwa kuwa ni “vipaji vya

asili” kwa sababu wahusika pamoja na kutumia nguvu kubwa za

kujinadi ili wapate kukubalika, bado hushindwa kuonesha viwango

vya utendaji bora katika nafasi walizozivamia tu kwa tamaa zao

wenyewe.

39

Mwenye kipaji cha asili katika uongozi uwe wa kisiasa au

kikanisa, hatumii nguvu kubwa kujinadi wala hatumii hila na ujanja

wa kujitangaza kwa vyeo akidhani vyeo ndio umaarufu. Mwenye

kipaji hujikuta akiwa maarufu kutokana na ushawishi alionao wa

kusikilizwa na kufuatwa na wengi kwa sababu ya mvuto wa kipaji

uliomo ndani yake.

2. Wivu Wa Kuharibu Mafanikio Ya Wengine

Kuna kundi jingine la watu wenye wivu wa kutokufurahia

mafanikio ya watu wengine. Kundi hili hujiona kwa kuwa lenyewe

bado halijafanikiwa, basi hakuna haki kwa wengine kufanikiwa,

na kama wakifanikiwa basi mafanikio yao kwa mtazamo wao

wanayahesabu si halali.

Katika msukumo wa wivu, watu hawa hujikuta wakitumia

kila njia za kuzuia, kukwamisha, na hata kuharibu mafanikio

ya watu wengine, na wanatafsiri kuwa hivyo ndivyo vipaji vyao

vya asili! Hakuna vipaji vya kupambana na kuweka vikwazo vya

kuharibu mafanikio ya wengine.

Mwenye kipaji cha asili, hasumbuliwi na wivu dhidi ya

mafanikio ya wengine. Badala yake hufurahia na kusifia mafanikio

ya wengine na hata kujifunza mbinu za kufanikiwa kama wao ikiwa

atapewa fursa hiyo. Mwenye kipaji anaweza kutumia kipaji chake

kufanikisha mambo ya wengine ili mradi tu apate uzoefu kabla ya

kuanza kufanya mambo yake mwenyewe.

3. Wizi Wa Mawazo Ya Wengine

Kundi jingine la kujihadhari nalo ni lile la wenye tamaa ya

kuiba mawazo ya wengine kwa kudhani watakuwa maarufu kama

wenye maono waliyodokoa bila ridhaa ya wahusika. Kundi hili

linajulkana kama “copy cats”.

40

Tamaa hii inafanana kidogo na ile ya kutafuta umaarufu

kwa sababu ya utajiri wa haraka haraka. Ila tamaa ya jinsi hii

hujikita katika kutafuta kupeleleza na kudokoa au kuiba mawazo

ya wale wanaoonekana kufanikiwa ili na wao wafanikiwe kama

wale wenye maono halisi.

Kwa kiasi fulani wanaweza kufanikiwa ila hawafikii viwango

vya ubora wa maono yale waliyoiba kwa wengine. Kuiba mawazo

ya wengine sio kipaji cha asili. Huu ni wizi wa kawaida hata kama

hakuna ushahidi wa kukamatwa kwa wenye tabia hizi.

Ngazi Za Ukuaji Na Utendaji Wa Vipaji Vya Asili

Utangulizi

Baada ya kuchambua aina za vipaji vya asili na jinsi

vinavyotenda kazi, sasa tunakuja kwenye ngazi au hatua za

kutenda kazi kuanzia umri mdogo mpaka uzeeni.

Tumejifunza katika sura ya kwanza ya kuwa vipaji vya

asili ni vipaji vya kuzaliwa navyo kibaiolojia na kisaikolojia. Hii

ikimaanisha ya kwamba vipaji huanza tangu mtu anapotungwa

mimba katika tumbo la mama yake.

Jambo jingine la kujikumbusha ni kwamba kila binadamu

huumbwa na kipaji cha asili ambacho ndicho humtofautisha

na binadamu wengine katika jamii. Hivyo ndivyo Mungu

alivyomkusudia kila binadamu atakayezaliwa na kuishi duniani.

Tunasoma ngazi za ukuaji wa kipaji cha mtu katika maandiko

yafuatayo:

“Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni,

mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha; mkatawale...” (Mwa.1:28)

41

Katika maandiko haya tunakuta maneno muhimu yafuatayo:

“zaeni”, “mkaongezeke”, “mkaijaze nchi”na “kuitiisha”. Katika

maneno haya tunapata kuziona ngazi za utendaji wa vipaji ndani

ya mtu katika mtiririko wa ngazi ya “ubunifu”, ngazi ya “uzalishaji”,

ngazi ya “usimamizi” na ngazi ya “urithishaji”:

1. Ngazi Ya Ubunifu

Wengi hulitafsiri neno hili kwa maana moja tu “wana ndoa

kuzaa watoto”! Lakini neno hili “zaeni” lina maana kubwa zaidi

“kuzaa watoto”. Neno “zaeni” linabeba maana nzito ya “ubunifu

wa mawazo mapya”. Kuzaa kunaanzia katika wazo kwanza. Ngazi

ya kuzaa ni ngazi ya ubunifu wa mawazo ambayo wengi huyaita

“maono mapya”.

Wanandoa wanapoanza maisha, hatua yao ya kwanza ni

ya “ubunifu wa mawazo mapya” ya jinsi wanavyotaka kuendesha

maisha yao ya ndoa, kila mwanandoa akitimiza wajibu wake katika

sehemu yake. Kuzaa watoto huanza katika ngazi ya ubunifu wa

kuona umuhimu wa kuwa na watoto na jinsi ya kuwalea mpaka

watakapokuwa watu wazima kama wao.

Hatua ya kwanza ambapo kipaji ndani ya mtu kinapoanza

kutenda kazi katika ubongo wake. Umri unaokadiriwa kwa kipaji

kuanza ubunifu katika ngazi ya mawazo ni miaka 12-25.

Muda huu ndipo mtoto anapokuwa katika mabadiliko

makubwa ya kibaiolojia na kisaikolojia. Ndipo wakati anapokuwa

na mawazo ya ubishi mwingi na kuhoji mambo mengi na wakati

mwingine hata kujiamulia mambo kulingana na anavyowaza akilini

mwake.

Huu ndio wakati wa mafunzo ya kunoa vipaji unapotakiwa.

Wakati anapokuwa shuleni ndio wakati ambapo waalimu na

waangalizi wanatakiwa kumsoma mtoto ana kipaji gani. Na

sio kumsoma tu bali kuanza kumwandaa kisaikolojia mtoto

42

ajitambue na kujiandaa kwa ajili ya kutumikia kipaji chake wakati

atakapohitimu masomo yake.

Hapa ndipo mifumo yetu ya elimu katika nchi za kiafrika

ilipodhoofishwa na wakoloni waliotawala mataifa ya kiafrika. Kwa

ujanja walituandalia mifumo ya elimu kwa nia ya kutufanya vibarua

katika mashamba na miradi yao, na sio kwa ajili ya kuwaandaa

watoto wa kiafrika wagundue na kunoa vipaji vyao ili wakihitimu

waweze kujitegemea kupitia vipaji vyao vya asili.

Kwa bahati mbaya, mpaka hivi sasa bado mifumo ya “elimu

tegemezi” inaendelea kutumika; na ndiyo chimbuko la “dhana ya

kuajiriwa”. Badala ya mhitimu kuwa na mtazamo wa “kujitegemea”

kwa yeye kubuni kazi zake za ustadi na kutoa huduma za kulipwa

kulingana na thamani ya viwango vya ubora; yeye anataka “nafasi

ya kuajiriwa”.

Naomba ieleweke kwamba si makosa wala si dhambi

kuajiriwa. Mantiki hapa ni kwamba nafasi za ajira katika serikali

na taasisi za umma ambazo ni haki ya kila mhitimu ni chache

kuliko idadi ya wahitimu. Na hata sekta binafsi ina vigezo vyake

vya kuajiri ikiwa ni pamoja na malipo ya chini ili kutengeneza faida

kubwa. Hii ndiyo changamoto ya kutegemea ajira peke yake.

Kama nilivyokwisha kusema tangu awali, kila mtoto

ambaye ni binadamu kamili, mwenye afya njema na akili timamu,

anacho kipaji cha asili ndani yake cha kumwezesha kuishi maisha

ya kujitegemea pindi atakapokuwa mtu mzima.

Lakini basi, katika ngazi hii ya ubunifu, ndipo mtoto

anapotumia uwezo wake wa kufikiri kuelekea aina ya kipaji chake

alichoumbiwa tangu tumboni mwa mama yake.

43

2. Ngazi Ya Uzalishaji

Neno la pili katika ngazi za utendaji wa vipaji lilikuwa ni

“mkaongezeke”. Neno hili ndilo linatuleta katika ngazi ya pili ya

“uzalishaji”. Katika ngazi hii, mtoto ameondoka katika ngazi ya

utoto wa kuwa tegemezi anaanza kuyatendea kazi mawazo yake

mapya ambayo tayari amekwisha kuyajaribu na kupata mwelekeo

wa ni nini anatakiwa kuwekeza nguvu zake zote katika uzalishaji

wa kile ambacho ni kipaji chake cha asili.

Katika ngazi ya uzalishaji, muhusika anatarajiwa kuwa

amefikia umri wa miaka 25 na ataendelea katika nguvu za kuzalisha

mpaka miaka 45.

Hii inaitwa ngazi ya uzalishaji kwa sababu ndio wakati

kwa mwenye kipaji anapokuwa amewekeza nguvu zake katika

vipaumbele vya mambo ambayo alikwisha kuyajaribu yakaonesha

mafanikio, au yakadhihirisha uwezo alio nao wa kufikia viwango

vyake vya ubora. Na ndio wakati ambapo kipaji chake kinaanza

kumpatia mhusika matunda au malipo stahiki. Ndio wakati wa

kufanya mikataba ya malipo au kuendesha huduma za kujitegemea

na kutengeneza ajira kwa wengine.

3. Ngazi Ya Usimamizi

Usimamizi ni ngazi ya tatu katika kukuza na kutendea kazi

vipaji vya asili. Usimamizi unaotamkwa hapa ni uzoefu unaofikia

hekima na busara ya kuanza kuweka akiba na kutunza mali na

fedha zilizokwisha kupatikana kutokana na uzalishaji mzito

uliotangulia katika ile hatua ya pili.

Umri wenyewe ambao ni kuanzia miaka 45 hadi kufikia

miaka 55 ndipo akili za wenye vipaji hupata msukumo wa kutunza

kile kinachozalishwa kupitia vipaji na taaluma zao huku wakihisi

nguvu za mwili zinaanza kupungua.

44

Aidha, hii ndiyo hatua ambayo wenye vipaji wenye hekima

wanapoanza kupunguza majukumu na kukaimisha au kunaibisha

kwa wale wanaotarajia kuwarithisha majukumu ya kiuchumi na

kiuongozi.

Na ndio wakati huu ambapo kizazi kipya cha umri wa miaka

25 kinapojaribiwa katika kubeba baadhi ya majukumu ili kunoa

vipaji vyao vya asili katika uzalishaji na uongozi pia.

Mwasisi aliyekuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa kampuni

au taasisi ya huduma hupunguza majukumu na kuyagawa kwa

walioko chini yake ambao anawaandaa kushika hatamu badala

yake.

Lile neno “kutiisha” katika Biblia kwa kiingereza linaitwa

“replenish” likimaanisha kujaza tena, au kuziba utupu uliokuwepo

mahali. Katika usimamizi wa vipaji, kutiisha ni kuongeza nguvu

mahali ambapo nguvu zilianza kupungua katika uzalishaji. Ni

kuongeza nguvu katika usimamizi wa vilivyokwisha kuzalishwa ili

vidumu na kuendelea kusaidia kizazi kinachoinukia.

4. Ngazi Ya Urithishaji

Urithishaji ndio hatua ya nne na ya mwisho katika kukuza

na kutendea kazi vipaji vya asili. Nitaelezea kwa kina kipengele

hiki katika Sura ya Nne kwa sababu kinawahusu zaidi warithishaji

kuliko warithishwaji.

Hata hivyo, kwa muktadha wa hatua za ukuaji na utendaji

wa vipaji vya asili, hatua hii ndiyo ya juu na mwisho kwa wote

wenye umri kuanzia miaka 55-65. Hiki ndicho kizazi kinachotakiwa

kustaafu na kukabidhi majukumu ya uzalishaji na uongozi kwa

kizazi kipya.

Lakini ni muhimu kutambua kuwa kukabidhi sio kususa au

kukimbia majukumu ghafla, eti kwa sababu ya uzee. Kukabidhi

45

lazima kuwe ni mchakato wa taratibu na wenye kukabidhi

wanabaki kutoa ushauri elekezi kwa waliowarithisha.

46

SURA TA TATU

CHANGAMOTO ZINAZOATHIRI VIPAJI

VYA ASILI

Utangulizi

Baada ya kujifunza utajiri mkubwa uliomo katika vipaji

vya asili na michakato ya kuvikuza, maswali makubwa yanakuja

akilini na kuhoji kama kweli kila binadamu huzaliwa na kipaji cha

kumwinua na kumfanikisha kwa viwango vya ubora wa hali ya

juu, je, kwanini sasa hatuvioni vipaji hivi vikifanya kazi kwa kila

mtu katika jamii? Kwanini ni watu wachache sana ambao ndio

wanatokea kuwa maarufu kupitia vipaji vya asili?

Katika kusaidia kupatikana kwa majibu ya maswali haya

na mengine yenye kufanana na haya, ndiyo maana sura hii

imeandaliwa ili kufanya uchambuzi makini kuhusu changamoto

zenye kuathiri vipaji vya asili, tukianza na kipengele cha vikwazo

vya maendeleo ya vipaji na karama.

Changamoto maana yake ni mambo yanayojitokeza

kinyume na maendeleo ya mtu. Hata hivyo, changamoto ni

sehemu ya maisha ya kila mtu na ndiyo maana maisha hutafsiriwa

kuwa ni “mapambano” dhidi ya “changamoto”.

Sasa tunapokuja katika suala la vipaji, napo zipo changamoto

ambazo kusudi lake kama sio kuharibu kabisa, basi ni kudhoofisha

utendaji wa vipaji ndani ya wahusika. Kwa hiyo ndiyo maana ni

vema kuzifahamu, na kisha kupata mbinu za kupambana nazo

kikamilifu. Changamoto zenyewe zimegawanyika katika sehemu

kuu mbili.

47

Sehemu ya kwanza ni “changamoto za nje” kwa maana

ya mambo hasi yanayomzunguka kila mtu ili kudhoofisha kipaji

chake. Pili, ni “changamoto za ndani” ambazo ni mambo hasi

ya ndani yanayomwathiri kila mtu binafsi kitabia. Hebu tuanze

kuchambua baadhi ya hizo changamoto za nje.

Changamoto Za Nje

Katika ulimwengu tunamoishi tumezungukwa na mambo hasi

mengi yaliyoko kinyume nasi ambayo ni lazima tupambane

nayo ikiwa kweli tunataka kuendeleza vipaji vyetu kama Mungu

alivyotukusudia. Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na:

1. Marafiki Wabaya

Binadamu ameumbwa na hulka ya ushirika na binadamu

wengine. Katika hulka hizo, kuna binadamu wanakuwa na ushirika

wa karibu zaidi kuliko binadamu wengine. Na ndipo msamiati wa

neno urafiki unapoanzia. Katika harakati za kutambua na kukuza

vipaji mbali mbali lazima kuwepo kwa ushirikiano na watu wengine

hususan wenye vipaji vinavyoshabihiana. Ni katika harakati za

kutafuta kukuza na kutumia kukuza vipaji ndipo mtu hujenga

ukaribu na watu wapya ambao huwa marafiki.

Tafsiri Ya Marafiki Wabaya

Tafsiri ya msamiati wa neno rafiki maana yake ni “mtu

anayependana na kuaminiana na mwingine; sahibu, mwandani,

bui, somo, na mbasi.” Maneno muhimu ya tafsiri ya urafiki ni

“kupendana” na “kuaminiana.”

Lakini kwa muktadha wa kipengele hiki, ni muhimu

kufahamu kuna “marafiki wema” na “marafiki wabaya.” Kuwa na

marafiki wabaya maana yake ni “kupendana na kuaminiana na

marafiki wabaya”

48

Aina Za Marafiki Wabaya

Kwa mujibu wa maandiko matakatifu, “marafiki wabaya”

wamegawanyika katika makundi mbali mbali ambayo ni kama

haya yafuatayo:

“Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki;

wala hakusimama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani

pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na

sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti

uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, uzaao matunda yake kwa

majira yake, wala jani lake halikauki; na kila alitendalo litafanikiwa.

Sivyo walivyo wasio haki; hao ni kama makapi yapeperushwayo

na upepo. Kwa hiyo, wasio haki hawatasimama hukumuni, wala

wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. Kwa kuwa BWANA

anaijua njia ya wenye haki, bali njia ya wasio haki itapotea.” (Zab.

1:3-6)

Katika maandiko haya tunasoma kuhusu “shauri la wasio

haki”, “njia ya wakosaji” na “baraza la wenye mizaha”. Kupitia

maneno haya ndipo tunayapata makundi ya aina tatu ya “marafiki

wabaya”.

Kundi la kwanza la marafiki wabaya ni “wasio haki” ambao

tafsiri yake ni “watu waovu au wahalifu”. Na maana ya “kutokwenda

katika shauri la wasio haki” maana yake ni kutokupokea na

kutendea kazi “ushauri wa waovu au wahalifu.”

Kundi la pili la “marafiki wabaya” ni “wakosaji” ambao

tafsiri yake ni watu “watenda dhambi” au “wasio na maadili ya

kimungu”. Makatazo ya “kutokusimama katika njia ya wakosaji”

tafsiri yake ni “kujitenga na vitendo vya dhambi za hao “watenda

dhambi”.

Kundi la tatu la “marafiki wabaya” ni la watu “wenye

mizaha” ambao maana yake ni “watu wenye maneno ya dhihaka,

49

kejeli, na dharau, dhidi ya itikadi za watu wengine”. Maandiko

yanamkataza mchaji Mungu kutojumuika na makundi ya watu

wenye “kudhihaki” na “kukejeli” itikadi za wengine.

Athari Za Marafiki Wabaya

Muktadha wa “marafiki wabaya” unalenga watu wenye

tabia mbaya wanapokuwa na ushawishi wa kuvutia kwa “watu

wema” hata wakajenga urafiki baina yao. Biblia ndiyo imeandika

habari za kutahadharisha “watu wema” kujihadhari katika kujenga

ushirika wa kirafiki na watu wabaya ambao huathiri vibaya tabia

njema:

“Msidanganyike; mazungumuzo mabaya huharibu tabia

njema.” (1 Kor. 15:33)

“Do not be deceived: [a] Bad company corrupts good

morals.”

Maandiko haya hapo juu yanashuhudia jinsi ambavyo

marafiki wabaya wanavyoweza kuathiri tabia njema za wachaji

Mungu.

Marafiki wabaya sio tu hauthiri tabia njema za watu wema,

lakini pia huathiri utendaji wa vipaji vya asili vya watu wema.

Pale mtu mwenye kutaka kunoa kipaji chake anaposhirikiana na

marafiki wabaya, urafiki huo husababisha kukwamisha juhudi za

kutumia kipaji chake kwa viwango vyake vya ubora, maana hata

yeye huharibika.

Kutokana na kuwa na marafiki wabaya, kuna vipaji vingi

vimeathiriwa kwa sababu ya wahusika nao kuharibika kitabia.

2. Imani za uchawi na ushirikina

Uchawi na ushirikina ni changamoto inayoongoza katika

kudhoofisha utendaji bora wa vipaji vya asili. Tafsiri ya ‘uchawi’

50

maana yake ni ufundi wa kutumia dawa au vitabu maalum vya

uganga ili kuleta madhara kwa viumbe; na maana nyingine ni

‘vifaa vinavyotumika katika shughuli za kurogea’.

Utafiti uliofanyika umeonesha dhahiri ya kwamba imani za

uchawi na ushirikina ni kikwazo kikubwa sana kwa maendeleo ya

vipaji vya asili. Pamoja na kwamba Biblia imekataza watu kushiriki

katika vitendo vya uchawi na ushirikina, lakini bado vitendo

hivyo vimekuwa vikiongoza katika kuvuta watu wengi wakidhani

wanakwenda kupata nguvu za kunoa vipaji kumbe wanajikuta

wanapokea nguvu za kukwamisha na kuharibu vipaji vyao. Ndiyo

maana maandiko matakatifu yalikataza na kupiga marufuku

ushiriki wa vitendo vya uchawi na ushirikina kama ilivyoandikwa

hapa chini:

“Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti

yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu

atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye

pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu

atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya

hayo BWANA, Mungu wako, anawafukuza mbele yako”(Kumb.

18:10-12)

Ni miaka miwili iliyopita tangu Tanzania ilipotangazwa

kushika nafasi ya kwanza kwa umahiri wa kuamini katika uchawi

kimataifa. Mojawapo ya taasisi zilizoitangaza Tanzania kwamba

imekithiri kwa mambo ya uchawi ni Pew Research lenye makao

yake Washington DC nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa zake inasadikiwa kwamba miongoni

mwa nchi 19 za kusini mwa Jangwa la Sahara zilizofanyiwa

utafiti, Tanzania iliongoza kwa kuwa na idadi ya watanzania 93%

wanaoamini katika uchawi na ushirikina.

51

Aidha, inasadikiwa pia ya kuwa vitendo vya uchawi

vinavyoongoza Tanzania ni pamoja na juju, utoaji wa kafara kwa

mizimu kwa ajili ya bahati za kupata vyeo, utajiri na umaarufu

katika michezo na muziki.

Sasa basi, katika mazingira kama haya, tunaweza kuona

jinsi ushirikina na uchawi vinavyodhoofisha vipaji vya asili kwa

sababu ya wahusika kutegemea ndumba badala ya kutambua na

kunoa vipaji vijiendeshe vyenyewe.

3. Mifumo Butu Ya Elimu

Mifumo butu ya elimu ni “mitaala ya elimu isiyolenga kunoa

vipaji vya wanafunzi.” Pamoja na kwamba elimu inayotolewa

kweli inawapatia wanafunzi maarifa ya kawaida ya kujua kusoma

na kuandika pamoja na ujuzi katika masomo mengineyo;

changamoto kubwa ni pale ambapo wahitimu wengi hawana

uwezo wa kujitegemea kiuchumi pasipo fursa ya ajira.

Wakati kipaji kinamjengea mtoto uwezo wa kubuni na

ustadi wa kazi atakayoimiliki mwenyewe; elimu bado ni butu

kwa kuwa haimwezeshi mtoto kutambua na kunoa kipaji chake

ambacho akihitimu kitamwezesha kujitegemea moja kwa moja.

Elimu ya sasa inamfanya mwanafunzi akihitimu awazie

kutafuta ajira peke yake, badala ya kubuni na kusimamia kazi

yake mwenyewe. Ndiyo maana changamoto ya ukosefu wa ajira

itaendelea kuwepo kwa muda mrefu kwa sababu uzalishaji wa

wahitimu hauendani na fursa za ajira zilizopo katika jamii.

Ufumbuzi kamili wa tatizo la ukosefu wa ajira ni lazima

uanzie kwenye mitaala ya elimu ambayo italenga kuibua na kunoa

vipaji vya watoto ili wanapohitimu wanakuwa na ujuzi kubuni kazi

zao wenyewe na kujitegemea kiuchumi badala ya kutegemea

ajira.

52

Athari Za Utandawazi Dhidi Ya Vipaji Vya Asili

Tafsiri Ya Utandawazi

“Mfumo wa uhusiano wa kimataifa katika nyanja mbali mbali

kama vile biashara, uchumi au siasa uliowezeshwa na maendeleo

ya teknolojia ya habari yanayofanya mataifa kuwasiliana kwa

urahisi.” (Kamusi Ya Kiswahili Sanifu).

Nguvu Za Mitandao Ya Kijamii

Miaka ya hivi karibu, mitandao ya kijamii imekuwa na

ushawishi mkubwa kiulimwengu kwa kiasi ambacho kasi yake ni

tishio kwa maadili ya kizazi kipya. Katika mwaka 2017 kiwango

cha ushawishi wa mitandao ya kijamii kimepanda kwa viwango

vifuatavyo:

• Facebook hivi sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 900

• 50% ya ulimwengu mzima iko chini ya umri wa miaka 50

• 96% ya umri kuanzia miaka 18-35 wako ni watumiaji wa

mitandao ya kijamii

• Kama facebook ingekuwa ni nchi, ingeshika nafasi ya tatu kwa

ukubwa ulimwenguni

• Mtumiaji wa kawaida wa facebook ana marafiki 130

• Youtube ni ya pili kwa mtandao mkubwa ulimwenguni

• Twitter nayo immeshafikia watumiani milioni 500

• Kama Twitter ingelikuwa ni nchi ingekuwa ya 12 kwa ukubwa

duniani. Kuna watu 750 wanao-twiti kila nukta.

• Kuna wenye kurasa (blogs) zaidi ya milioni 200

• Kuna kurasa mpya mlioni 3 zinazofunguliwa kwenye internet

kila mwezi

• Kuna picha milioni 5 zinazorushwa kwenye instagram kila siku

• Watu zaidi ya bilioni 6.9 wamekwisha kutazama Youtube

channel

53

Matokeo Chanya Ya Matumizi Ya Mitandao Ya Kijamii

Kama ilivyo kawaida ya vuguvugu jipya linaloibuka katika

jamii linakuwa na matokeo ya aina zote mbili. Kuna matokeo

chanya na pia kuna matokeo hasi. Hebu tuangalie matokeo

chanya ya matumizi ya mitandao ya kijamii:

• Husaidia kujenga mitandao ya kibiashara na huduma za

kijamii. Matangazo ya biashara kupitia redio, televisheni na

magazeti yana gharama kubwa. Lakini kupitia mitandao ya

kijamii matangazo yanawafikia wateja wengi kwa gharama

nafuu sana na wakati mwingine bure.

• Mitandao ya kijamii imetoa fursa kwa wenye vipaji na taaluma

mbali mbali kuwasiliana na kupeana taarifa na wateja wao

kuliko ilivyokuwa huko nyuma.

• Mitandao ya kijamii imeondoa vikwavyo vya mawasiliano ya

moja kwa moja. Wanafunzi wanawasiliana na wataalamu na

kubadilisha taarifa muhimu.

• Mitandao ya kijamii imeunganisha watu kimawasiliano na

kuwezeshana katika kutimiza malengo kuanzia ngazi ya

kifamilia, kitaifa na kimataifa (dunia nzima imekuwa kijiji

kimoja).

• Kuna soko pana zaidi. Unaweza kuuza bidhaa nyingi zaidi na

kupata faida, na hata kutengeneza ajira.

• Walaji nao hunufaika. Ushindani hufanya bidhaa kuwa na bei

za chini, na upatikanaji haraka wa bidhaa mpya.

Matokeo Hasi Ya Matumizi Ya Mitandao Ya Kijamii

• Inashika Nafsi Kama Ulevi Sugu.

• Kutumia muda mwingi zaidi kwenye mitandao ya kijamii na

kushindwa kufanya mambo mengine yenye tija.

• Inadhoofisha Mahusiano Ya Ana Kwa Ana

• Inadhoofisha motisha wa kuhusiana na watu moja kwa moja,

na hasa kwa vijana na wanafunzi.

• Wanakuwa tegemezi kwenye teknolojia na internet zaidi kuliko

54

kujifunza kwa akili ili kupata ujuzi wa maisha ya kila siku.

• Jumbe Za Vitisho Na Udhalilishaji (Cyberbullying)

• Shirika moja lijulikanalo kama Enough is Enough, lilifanya utafiti

na kugundua kwamba 95% vijana wanaotumia mitandao ya

kijamii wameshuhudia mawasiliano ya vitisho na udhalilisha na

33% yao ni waathirika wa mawasliano hayo

• Watoto Huathirika Vibaya Zaidi Na Mitandao Ya Kijamii

Wasipodhibitiwa

• Hii ni kwa sababu kwenye mitandao hii zinarushwa picha

mbaya za ugomvi na picha za uchi ambazo huwaathiri

kisaikolojia watoto na vijana. Baadaye husababisha watoto na

vijana kujihusisha na vitendo vya uhalifu na ngono haramu.

• Kichocheo Cha Mkengeuko Wa Maadili Mema

• Maambukizi ya mkengeuko wa maadili ya kimaani na

kiutamaduni kwa sababu ya mwingiliano wa walioharibika

kitabia, waliojaa tamaa ya kupata faida kubwa bila kujali

maadili mema katika nchi husika.

Changamoto Za Ndani

Katika utangulizi wa sehemu hii tumepata tafsiri kuhusu

changamoto za ndani kuwa ni mambo hasi ya ndani yanayomwathiri

kila mtu binafsi kitabia. Katika uchambuzi wa changamoto za

ndani tunakwenda kutumia msamiati mpya ambao unaitwa “tabia

sugu”. Msamiati huu unalenga kuchambua tabia sugu zenye

kuathiri utendaji wa vipaji ndani ya mhusika.

Tafsiri Ya Misamiati Ya Tabia Sugu

Sasa tumefikia kipengele ambacho hasa ndio kikwazo

sugu chenye kuathiri vipaji vya asili katika jamii. Labda nianze na

uchambuzi wa misamiati. Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili

Sanifu, neno “tabia” limetafsiriwa kuwa ni: “mazoea yatokanayo

na kurudiarudia hali, mwenendo au matendo”

55

Kamusi ya Kiswahili Sanifu imelitafsiri neno “sugu”

kuwa ni “hali isiyoweza kuondolewa kwa urahisi”. Usemi “tabia

sugu” haumo katika kamusi kama msamiati; isipokuwa mimi

nimeyaunganisha maneno mawili, “tabia” na “sugu” na kupata

usemi maalum wa “tabia sugu”.

Kwa hiyo kama ukiunganisha tafsiri za maneno “tabia” na

“sugu” unapata maana ya usemi wetu wa “tabia sugu”ambao tafsiri

yake ni: “mazoea yatokanayo na kurudiarudia hali, mwenendo au

matendo isiyoweza kuondolewa kwa urahisi”.

Maeneo Ya Uharibifu Wa Tabia Sugu

Uharibifu Wa Kitabia

Sehemu ya kwanza ya madhara ya tabia sugu ni uharibifu

wa kitabia unaolenga kuharibu “utu”, “ubinadamu” na “uungwana”

katika maisha ya mwathirika. Pengine ni vizuri tukaangalia

misamiati ya maneno haya ya “utu”, “ubinadamu” na “uungwana”

ili tujue maana zake:

Neno “utu” limetafsiriwa kuwa ni: “hali ya kuwa na tabia

zinazolingana na hadhi ya mtu”. Neno “ubindamu” limetafsiriwa

kuwa ni: “hali ya utambuzi wa jinsi ya kutekeleza wajibu juu ya

maisha katika jamii”. Neno “uungwana” limetafsiriwa kuwa ni:

“mtu mwenye adabu na tabia zinazokubalika katika jamii”.

Baada ya kupata tafsiri ya misamiati hapo juu tunaweza

kuona kwamba madhara mabaya ya “tabia sugu” kwa mhusika

ni: kumharibia (utu); ambao ni hadhi yake kama mtu; kumharibia

(ubinadamu wake) ambao ni hali ya utambuzi wa kutekeleza

wajibu wake kwa jamii; kumharibia (uungwana) ambao ni

adabu na kumfanya kutokukubalika kitabia katika jamii. Haya

ndiyo madhara ya “tabia sugu” ambayo kimsingi, ndiyo yenye

kukwamisha utendaji wa vipaji ndani ya walio navyo, na kukwama

kufikia viwango vya mafanikio kulinganana vipaji vyao.

56

Hata hivyo, ashukuriwe Mungu kupitia Bwana Yesu Kristo

ambaye kwa neema yake ametoa ufumbuzi wa kupambana na

kukomesha madhara ya tabia sugu, ikiwa masharti na kanuni

zitazingatiwa:

“Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani,

ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa TABIA YA UUNGU

mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (1

Pet. 1:4)

Mungu ameahidi, kupitia Yesu Kristo, waathirika wa tabia

sugu, wanaweza kubadilika, na kunusurika na uharibifu wa dunia

hii unaosababishwa na tamaa na kwa kubadilika kitabia na kuwa

wachaji Mungu na raia wema katika jamii.

Uharibifu Wa Kiafya

Kudhoofisha mishipa inayosafirisha damu moyoni, uharibu

wa mfumo wa neva, ambao huanzia katika kudhoofisha uwezo

wa kufikiri na hatimaye kuishia kuwa zezeta; saratani ya damu;

shinikizo la damu na maradhi ya moyo; maradhi ya mtoto wa

jicho; saratani ya mlango wa kizazi; saratani ya figo; saratani ya

kongosho; saratani ya tumbo; maradhi ya uasherati na zinaa na

VVU/UKIMWI.

Uharibifu Wa Kifamilia

Uharibifu wa kifamilia utokanao na tabia sugu ni pamoja

na: Migororo sugu katika ndoa; ugumba na utasa (utoaji mimba/

madawa ya kuzuia mimba); wanandoa kutelekezana/kuvunjika

kwa ndoa; malezi mabovu kwa watoto; ongezeko la watoto wa

mitaani.

57

Uharibifu Wa Kiuchumi

Uharibifu wa kiuchumi utokanao na tabia sugu ni pamoja

na: Ufukara katika familia; udhaifu katika ubunifu wa mipango

endelevu ya kiuchumi; rasilimali asilia kuwanufaisha wageni badala

ya wenyeji; uharibifu wa mazingira; wenyeji kuwa watumwa wa

wageni katika nchi yao wenyewe.

Aina 5 Za Tabia Sugu Zenye Kuharibu Vipaji

1. Tabia Ya Kunung’unika Na Kuhukumu

Kunung’unika ni hali ya “kusema kwa sauti ya chini, aghalabu

peke yako; kusema kwa kulalamika kwa sababu yakutokuridhika

na jambo.”

Kuhukumu ni hali ya “kuhesabia wengine makosa pasipo

ushahidi” “kusema makosa ya wengine pasipo ridhaa yao na kwa

nia ya kuwadhalilisha”.

Mtu mlalamishi na mgung’unikaji na mwenye kuhukumu

wengine huwa ni mwathirika wa mtazamo hasi dhidi ya wengine.

Ni mtu aliyejawa na mawazo mabaya ya kutafuta makosa ili apate

kukosoa na kuhukumu kwa nia ya kuona wahusika wanapatwa na

mabaya kama adhabu ya makosa yao.

Je, Unapenda kukosoa na kutoa lawama dhidi ya wengine?

Unasukumwa kutafuta makosa katika kila jambo au kwa kila mtu?

Huwa unaona ugumu au uzito wa kuona jambo jema pasipo kuona

makosa? Unajiona huru kukosoa na kulaumu wengine hadharani

pasipo kujali hisia zao wala heshima zao? Kama majibu ya maswali

haya kwako ni “ndiyo” maana yake wewe ni mwathirika wa fikra

na mtazamo hasi wa kulaumu na kuhukumu wengine.

58

Angalizo

Si kila kukosoa ni mtazamo hasi. Wala kuona makosa

na kuyasema kwa nia ya kusahihisha sio vibaya. Muktadha

wa kipengele hiki ni kwa wale walioathiriwa na “tabia sugu ya

kulalamika na kuhukumu wengine”.

Mtu ambaye hajaathiriwa na tabia sugu ya kulalamika

na kuhukumu wengine anapoona makosa huchukua hatua za

kumwendea mkosaji na kumwelimisha kwa nia njema na lugha

ya upole, tena baada ya kumsikiliza kwanza na kupata uhakika

kutoka kwa muhusika.

Lakini mwathirika wa tabia sugu ya kulalamika na kuhukumu

wengine, hata kama analalamikia mambo ya kweli, huwa hatumii

njia ya kuelimisha bali lugha ya kudhalilisha hadharani kwa kuanika

makosa ya wengine. Tatizo huwa sio “kuona makosa” bali “njia ya

kushughukilia makosa yenyewe”

Mtu ambaye ni mwathirika wa “tabia sugu ya kulalamika

na kuhukumu wengine” anaweza hata kujitetea ya kwamba ana

mzigo wa kuwasaidia wale anaowakosoa wajirekebishe; lakini

lugha inayotumika katika kukosoa ni ya kuudhi, kuumiza hisia,

kudhalilisha, na kuwavunjia heshima wengine hadharani, wale

anaodai kuwakosoa.

Dalili Kuu Za Tabia Ya Kulalamika Na Kuhukumu Wengine

Ulalamishi

Mlalamishi ni mtu mwenye hulka ya kutokuridhika

na mambo ya wengine. Hata pale mambo yakifanyika vizuri

walalamishi hawana shukrani wala pongezi kwa wengine. Lakini

likitokea dosari au udhaifu wao wataukomalia huo utafikiri hakuna

jambo jema kwa wale wanaolalamikiwa.

59

“Ndugu msinung’unukiane, msije mkahukumiwa. Angalieni,

mwamuzi amesimama mlangoni.” (Yak. 5:9)

“Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala

mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama,

wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi

kilichopotoka’ ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga

katika ulimwengu.” (Flp. 2:14-15)

Tabia ya kuhukumu wengine

Mwenye lawama za hukumu ni mtu aliyeathiriwa na

mtazamo hasi wa kuhukumu wengine kwa dhana pasipo ushahidi

kamili. Mwepesi wa kulaumu bila hata kusikia upande wa pili

unasemaje kuhusu jambo husika. Hujiamini sana kwamba ana

ujuzi wa kugundua makosa ya wengine lakini yeye mwenyewe

haoni makosa yake mwenyewe.

“Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona

huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.” (Yak. 2:13)

Usengenyaji

Msengenyaji ni yule mwenye kufunua mambo binafsi ya siri

za wengine kwa nia ya kuwadhalilisha na kuwavunjia heshima zao

mbele za wengine. Msengenyaji hujifanya kuwa na taarifa nyeti za

mambo ya watu lakini mwenyewe hayuko tayari kujulikana kama

ndiye chanzo cha taarifa hizo.

“Tena pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizungukazunguka

nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni

wachongezi na wadadisi wakinena maneno yasiyowapasa.”

(1 Tim. 5:13)

60

Udhalilishaji

Mdhalilishaji ni mtu anayezua mambo ya uongo kwa nia ya

kuharibu heshima na hadhi za wengine hadharani. Mdhalilishaji

huzalisha kashfa ili kuharibu maisha ya wengine.

“Basi wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na

husuda na masingizio yote.” (1 Pet. 2:1)

Madhara Ya Kulalamika Na Kuhukumu Wengine

Hudhoofisha Ubunifu Wa Kipaji

Mwathirika wa mtazamo hasi wa kulalamika na kuhukumu

hukiathiri kipaji chake cha asili kwa kudhoofisha uwezo wake wa

asili wa kubuni mambo mapya. Kumbuka ya kwamba utendaji wa

kipaji unategemea nguvu za ubunifu wa mambo mapya. Na nguvu

za ubunifu hutokana na mawazo chanya.

Kimaumbile “mawazo hasi” hayawezi kutenda kazi kwa

wakati mmoja na “mawazo chanya”. Kila kimoja kinafanya kazi

kwa wakati wake kinapokuwa kimepewa nafasi ya kwanza. Kwa

hiyo, “mawazo hasi” huamsha “hisia hasi” ambazo huwa kikwazo

cha utendaji wa mawazo chanya. Wakati mwathirika wa mtazamo

hasi hutumia mawazo hasi na kughubikwa na hisia hasi; hali hiyo

huzuia upande wa pili wa mawazo chanya na hisia chanya kufanya

kazi kwa wakati mmoja.

Changamoto iliyopo hapa ni kwamba, muda wote ambapo

mawazo hasi, na hisia hasi vinatenda kazi ndani ya mwathirika,

kipaji chake kinakuwa kimefungiwa ule uwezo wake wa kutenda

kazi yenye tija kwa muhusika. Kwa hiyo, muda mwingi unaopotea

kwenye kulalamika na kuhukumu wengine, mambo yake

mwenyewe husimama au kukwama.

61

Huharibu Mahusiano Na Wengine

Mara nyingi, mwathirika wa “tabia sugu ya kulalamika na

kuhukumu wengine” huwa hana marafiki wengi. Na hata akiwapata

hawadumu pamoja naye kwa muda mrefu. Hata wale wachache

anaobaki nao hugombana nao mara kwa mara. Tena baadhi ya

hao marafiki wachache nao pia huwa ni waathirika wa tabia sugu

hiyo hiyo ya kulalamika na kuhukumu wengine kama yeye.

Katika mazingira ya kuwa na marafiki wachache, au

kukimbiwa na marafiki, hali hii husababisha vipaji vya mwathirika

kutokuwafikia na kuwahudumia walengwa wa vipaji vyake. Maana

mwathirika wa “tabia sugu ya kulalamika na kuhukumu wengine”

anaweza kuwa na kipaji kizuri sana lakini kimeathiriwa na hulka

yake. Kila anapokitumia kinakuwa kama chakula kitamu lakini

chenye pilipili kupita kiasi. Kila anayekula lazima pua zitalowa kwa

mafua na macho kutoka machozi mengi.

Kwenda Kinyume Na Makatazo Ya Yesu Kristo

Yesu Kristo mwenyewe pamoja na kwamba alikuwa

mkali katika kukosoa mitazamo hasi ya jamii ya Mafarisayo

na Masadukayo; bado alipiga marufuku kwa wanafunzi wake

kuendekeza tabia ya kulalamika na kuhukumu wengine:

“Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi

hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.” (Luk. 6:37)

Makatazo ya Yesu kuhusu tabia ya kulaumu na kuhukumu

kunadhirisha matokeo ya tabia hiyo kuwa inaambatana na

malipizo yake. Unapomlaumu na kumhukumu mtu mwingine na

kumsababishia maumivu pamoja na madhara, maana yake wewe

pia tarajia kupatwa na lawama na hukumu zitakazokusababishia

maumivu na madhara kama ulivyowafanyia wengine. Hii ni kanuni

ya kiroho na inafanya kazi chini ya udhibiti wa Mungu mwenyewe.

62

Kana kwamba hii haikutosha, Yesu alitoa sababu ya msingi

ya kutokulaumu na kuhukumu wengine kwa sababu mwenye

kufanya hivyo kwa wengine pengine ana makosa kama wao au

zaidi ya hao anaowakosoa.

“Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa

hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile

mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Basi mbona wakitazama

kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani

ya jicho lako mwenyewe huiangalii. Au utamwambiaje nduguyo,

niache nitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani

ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe itoe kwanza ile boriti

katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile

kibanzi katika jicho la ndugu yako.” (Mat. 7:1-5)

Katika maandiko haya, Yesu anaonesha udhaifu wa tabia

ya kuhukumu wengine pasipo kujitathmini binafsi kama hatuna

makosa yale yale au yenye kufanana na ya wale tunaowahukumu.

Aidha, Yesu anatafsiri kuwa ni unafiki mtupu kuwa na tabia ya

kulalamika na kulaumu wengine wakati mhusika naye ana

madhambi yake mwenyewe.

Na kisha Yesu akaagiza kwamba badala ya kutumia

nguvu kubwa kutuhumu na kuhukumu wengine, tumia fursa hiyo

kujichunguza na kujirekebisha kwanza kisha ndipo utakuwa na

uzoefu wa kukosoa wengine.

Tena kuna mahali pengine ambapo Yesu alitoa mwongozo

pale ambapo kunatokea kutokuelewana au kukoseana ambapo

hatua stahiki ni kukutana wahusika peke yao na kujaribu

kusuluhishana. Na pale inaposhindikana basi kesi hiyo iwasilishwe

kwenye ngazi ya juu, hatua kwa hatua mpaka muafaka upatikane.

63

Tabia Sugu Ya Uvivu

Uvivu ni hali ya “kutokutaka kufanya kazi” au hali ya

“ulegevu katika kazi”, au “utepetevu” na “ulegevu”. Tabia sugu ya

uvivu ni mojawapo ya changamoto zinazokiandama kizazi kipya.

Kuna ushahidi wa kutosha kwamba vijana wengi hawapendi

kufanya kazi za nguvu au wakifanya basi hufanya kwa ulegevu.

Kwa mujibu wa Biblia tunajifunza ya kwamba mtu mvivu mikono

yake hukataa kufanya kazi:

“Matakwa ya mtu mvivu humfisha kwa maana mikono yake

hukataa kufanya kazi.” (Mit. 21:25).

Kwa kifupi, mtu mvivu hukataa kufanya kazi (Mit.12:27);

hataki kulima wakati wa baridi (Mit. 20:4); hupenda sana uzingizi

(Mit. 6:9); huwa na njaa (Mit.19:15); kazi yake ni kuomba omba

misaada (Mit.20:4).

Kwa dalili hizi, kazi ya kunoa kipaji nayo ni ngumu kwa

mwathirika wa tabia sugu ya uvivu. Mojawapo ya sifa ya utendaji

wa kipaji ni kufanya kazi kwa ustadi na viwango vya ubora.

Mwathirika wa uvivu sio kwamba hawezi bali pia hataki kutoka

jasho. Anataka mafanikio ya haraka bila jasho.

Madhara Ya Tabia Sugu Ya Uvivu

Umaskini Wa Kipato

Madhara makubwa yampatayo mwathirika wa tabia sugu

ya uvivu ni umaskini wa kipato. Tumekwisha kuthibitisha ukweli

huu kupitia maandiko matakatifu na baadhi yake ni haya yafuatayo:

“Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; bali

mkono wake aliye na bidii hutajirisha.” (Mit. 10:4)

64

Maandiko yametuhakikishia kwamba uvivu husababisha

umaskini. Mtu asipofanya kazi kwa makusudi hatapata mapato

na hivyo kuishia kuwa maskini.

Kuwa mzigo kwa wengine

Mwathirika wa tabia sugu ya uvivu kwa kuwa hana kipato,

lakini bado ana mahitaji ya lazima ya kula, kunywa, kuvaa, malazi

na mengine, haya yote huwatwika watu wengine wabebe mzigo

huo.

“Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa

mavuno ataomba, hana kitu.” (Mit. 20:4)

Kwa sababu shida za mvivu haziishi, leo ana shida hii

kesho ana shida ile na asiposaidiwa atalaumu na kulalamika

kana kwamba ni haki yake kusaidiwa wakati si mlemavu. Hii

husababisha kero kwa wale walio karibu naye.

Kupoteza Fursa Matumizi Ya Vipaji

Mwathirika wa tabia ya uvivu hushindwa kutumia kipaji

chake kila anapopewa fursa ya kuzalisha. Yesu alitoa mfano wa

talanta ambapo tajiri aliwapa watumwa wake talanta za kuzalisha.

Mmoja kati yao aliyepewa talanta moja kwa sababu ya uvivu wake

alishindwa kuzalisha lakini akaja na visingizio kama ifuatavyo:

“… Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana,

nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda,

wakusanya usipotawanya; basi nikaogopa, nikaenda nikaificha

talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. Bwana wake

akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua

ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; basi,

ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija

ningalipata iliyo yangu na faida yake. Basi, mnyang’anyeni talanta

hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye

kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile

65

alicho nacho atanyang’anywa.” (Mat. 25:24-29)

Katika maandiko haya tunasoma maneno haya “… Wewe

mtumwa mbaya na mlegevu.” Unaona? Anatajwa moja kwa

moja ya kuwa kilichomfanya akashindwa kutumia kipaji chake ni

ulegevu wake mwenyewe na madhara yake ni kunyang’anywa

hata hicho alichokuwa nacho.

Tabia Sugu Ya Ulevi Na Madawa Ya Kulevya

Miaka 3,000 iliyopita kabla ya elimu ya sayansi kuwepo,

manabii walitoa maonyo kuhusu matumizi ya pombe wakisema

athari zake ni pamoja na kuharibu fahamu za wanadamu:

“Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.”

(Hos. 4:11)

Maandiko haya yanathibitisha kwamba pombe ina athari

kubwa kwa kipaji cha binadamu kwa kuwa inadhoofisha uwezo

wa kufikiri. Kwa mantiki hii divai mpya inajumuisha kila kitu

kinacholewesha ikiwemo uvutaji wa bangi; matumizi ya dawa za

kulevya unaojumuisha unga wa kubugia, kunusa, au uchomaji

sindano.

Maandiko matakatifu, kama jina lake lilivyo, yameandika

waziwazi ya kwamba ndani ya pombe mna sumu inayoharibu

tabia ya mtu na kumwondolea ubinadamu wake na kufanya awe

kama hayawani:

“Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali

mjazwe Roho.” (Efe.5:18)

Neno “ufisadi” katika maandiko haya linamaanisha “uchafu

uliokithiri”. Huu si uchafu wa mwili bali vitendo haramu visivyo vya

kimaadili. Ndiyo maana nimeorodhesha ulevi kuwa ni “tabia sugu”

inayoharibu utendaji wa vipaji ndani ya binadamu.

66

Madhara Ya Pombe Mwilini

Madhara ya kwanza ya pombe ni kuathiri mfumo wa

ubongo ambao ndio asili ya nguvu ya vipaji vya asili. Baadhi ya

athari za pombe katika ubongo ni kama zifuatazo:

• Mishipa ya ubongo kupanuka kupita kawaida.

• Ukosefu wa baadhi ya vitamin katika ubongo (mlevi hali mlo

kamili)

• Ukosefu wa vitamin B unaweza kusababisha matatizo ya akili

katika ubongo

• Kubadilika kitabia, kudhoofika kwa uwezo wa kufikiri, kupoteza

kumbukumbu

Athari kubwa zaidi za pombe katika ubongo ni eneo la

mfumo wa neva. Wakati kisingizio cha matumizi ya pombe huwa

ni kama kitulizo katika mfumo wa neva, badala yale pombe

hutumika katika kuzikandamiza seli za neva katika ubongo kwa

kuzifanya butu na kuuharibu uwezo wake wa kufanya kazi, hali

ambayo hupelekea kusinzia, kuzimia na hata kifo.

Madhara mengine ya pombe kwenye mfumo wa neva ni

pamoja na haya yafuatayo:

• Kudhoofisha uwezo wa kuona

• Kubadilisha utambuzi wa muda na mahali

• Kupoteza uwezo wa kusikia vizuri

• Kupatwa na uzito katika kuitikia mambo

• Kupoteza hisia ya harufu na ladha

Kana kwamba hii haitoshi, madhara ya pombe hayaishii

kuathiri ubongo na mfumo wa neva peke yake. Pombe huathiri

kiungo kingine muhimu cha mwili ambacho ni moyo. Baadhi ya

maeneo ambayo moyo huathiriwa na pombe ni pamoja na haya

yafuatayo:

67

• Moyo huathirika kwa ukosefu wa baadhi ya vitamini.

• Mapigo ya moyo hudhoofika

• Kupanuka kwa moyo

• Ongezeko la shinikizo la damu

• Huzuia uzalishaji wa seli nyekundu na nyeupe za damu

• Hatari za ugonjwa wa moyo na kiharusi

Viungo vingine ambavyo huathiriwa na pombe ni ini ambapo

seli za ini huharibika na kudhoofisha utendaji wa ini (Cirrhosis).

Imebainika ya kwamba theluthi mbili za wagonjwa wa Cirrhosis

Uingereza husababishwa na pombe.

Pombe pi huathiri tumbo kwa kusababisha maumivu na

vidonda vya tumbo pamoja na matatizo katika mfumo wa usagaji

chakula. Madhara mengine ya pombe ni dhidi ya ngozi ambapo

mishipa ya damu hupanuka na ngozi kujaa damu nyingi, na pia

pombe husababisha mwili kuwa na joto kubwa na rangi ya ngozi

hubadilika.

Eneo la mwisho lakini lenye athari kubwa zitokanazo na

pombe ni katika mfumo wa uzazi. Pombe husababisha kudhoofika

kwa mfumo wa uzazi katika maeneo yafuatayo:

• Kudhoofika kwa nguvu za kiume

• Kwa wanawake katika ujauzito kizazi huathirika

• Kuzaliwa kwa watoto njiti

• kudhoofisha uwezo wa akili wa mtoto

• Mtoto kurithi tabia ya ulevi

• Viungo vya uzazi kudhoofika na kusababisha ugumba

• Kwa wanawake hatari ya kupata saratani ya matiti

Athari Za Kiuchumi

Pombe haikomei katika kuathiri afya bali husababisha hata athari

za kiuchumi. Kwa mujibu wa maandiko ya Biblia tunaonywa

kuhusu ulafi na ulevi kama ifuatavyo:

68

“Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo; miongoni mwa

walao nyama kwa pupa; kwa maana mlevi na mlafi huingia

umaskini, na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.” (Mit. 23:20-

21)

Baadhi ya athari za kiuchumi zitokanazo na pombe ni kama

hizi zifuatavyo:

• Kudhoofika kwa viwango vya ubunifu wa mipango endelevu

ya kiuchumi

• Kudhoofika kwa uwezo wa kufanya kazi

• Utoro makazini

• Kupoteza ajira

• Kufilisika kibiashara/kimiradi

• Kukumbwa na umaskini wa kujitakia kibinafsi, familia na jamii

kwa jumla

Athari Za Kijamii

• Kudhoofisha uwajibikaji wa mtu kama mwanandoa au kama

mzazi

• Kusababisha ugomvi katika familia

• Kukaa nje ya familia kwa muda mrefu

• Kutelekeza familia na kuwasababishia wasiwasi, mashaka na

msongo wa mawazo

• Kuchochea vitendo vya zinaa ambavyo hueneza maambukizo

ya VVU

• Malezi duni kwa watoto

Tabia Sugu Ya Zinaa

Msamiati wa neno “zinaa” unajumuisha matumizi ya

maneno mawili maarufu kama “uasherati” na “Uzinzi”. Tafsiri

rasmi ya neno uasherati maana yake ni “tendo la kujamiiana

linalofanywa na mtu/watu ambao hawajaoa wala kuolewa kwa

mujibu wa sheria”. Na tafsiri rasmi ya neno uzinzi maana yake

69

ni: “mwanandoa anapojamiiana na mtu/watu wengine nje ya

mwanandoa mwenziwe”.

Kwa mujibu wa maandiko ya Biblia, tendo la ndoa linatakiwa

kufanywa na mwanamume na mwanamke ambao wameamua

kufunga ndoa ili kuishi pamoja kwa maisha yao yote mpaka kifo.

Mtu ambaye hajafunga ndoa halali haruhusiwi kujamiiana mpaka

atakapofikia umri na muda wa kufunga ndoa rasmi.

Mojawapo ya amri kumi maarufu katika Biblia ni pamoja

na “usizini” (Kut. 20:14). Zinaa ni miongoni mwa tabia sugu zenye

kuharibu utendaji wa vipaji vya wanadamu na ndiyo maana

imekatazwa kimaadili.

Madhara Ya Tabia Sugu Ya Zinaa Kimaadili

Mojawapo ya athari za tabia sugu ya zinaa ni “kupungukiwa na

akili”:

“Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.”

(Hosea 4:11)

Biblia inaposema zinaa inaondoa “fahamu za wanadamu”,

maana yake inalenga uharibifu wa kitabia wenye kuathiri utendaji

wa vipaji vya asili. Mtu akiisha kujiingiza katika vitendo vya

zinaa, tayari fahamu zake au fikira zake zinaathirika na kupoteza

mwelekeo wa kimaadili na hivyo kudhoofisha utendaji bora wa

vipaji vyake. Maandiko mengine yamerejea kusisitiza ya kwamba

mwenye kufanya zinaa tayari ana matatizo ya kiakili:

“Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo

litakalomwangamiza nafsi yake.” (Mit. 6:32)

Hapa tunasoma habari kuhusu zinaa inavyozuzua akili za

mtu mpaka anajiingiza kwenye mazingira ya kuhatarisha uhai

wake lakini hata hajali. Kumbuka wakati huo maandiko haya

70

yalipoandikwa, hukumu ya zinaa ilikuwa ni mtu “kupigwa mawe

mpaka kufa” (Law. 20:10). Kwa hiyo, mtu akiisha kuonja zinaa

humponza kiasi cha kujitoa mhanga kupigwa mawe hadi kufa

kama atafumaniwa.

Kufuatia athari mbaya za kimaadili zinazotokana na

tabia sugu ya zinaa, maandiko yametoa mwongozo wa kila mtu

kujiepusha nayo kwa kadiri iwezekanavyo kama ilivyoandikwa

hapa chini:

“Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje

ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda juu ya mwili wake

mwenyewe.” (1 Kor. 6:18)

Vichocheo Vya Zinaa

Pamoja na makatazo ya vitendo vya zinaa bado

kumekuwepo mmomonyoko wa kimaadili wenye kusababisha

kukithiri kwa vitendo hivyo katika jamii. Baadhi ya vichocheo vya

zinaa ni pamoja na:

• Tamaa za ujanani

• Mila na desturi zisizoheshimu ndoa ya mke na mume mmoja

• Ngoma na miziki inayohamasisha vitendo vya ngono

• Picha za ngono katika magazeti, luninga, video na tovuti

• Mavazi yasiyo ya staha

• Ulevi na madawa ya kulevya

• Umaskini

Athari Za Nyingine Za Tabia Sugu Ya Zinaa

• Zinaa huleta unajisi unaomtenga mtu na Mungu kiroho

• Zinaa huathiri utu kwa kuvunja hadhi ya mtu binafsi

• Zinaa hivunjia taasisi ya ndoa heshima yake mbele za jamii

• Zinaa husababisha kuzaliwa watoto nje ya ndoa na kukosa

malezi bora

71

• Zinaa huharibu akili na uwezo wa kufikiri mambo ya maana

• Zinaa husababisha umaskini kwa matumizi ya anasa zisizo na

udhibiti

• Zinaa husababisha uhasama/chuki/uadui mpaka mauaji

• Zinaa husababisha migogoro na kusambaratisha familia

• Zinaa hueneza maambukizo ya maradhi ya zinaa na VVU

Tabia Sugu Ya Chuki Na Hasira

Tabia ya chuki na hasira imetokea kuwa miongoni mwa

tabia sugu ambazo zinaathiri vipaji vya asili kwa sababu waathirika

wengi ni vijana, tena ambao ndio nguvu kazi ya taifa. Kimaumbile

kila binadamu ana “hisia hasi” za chuki na hasira. Lakini hisia

hizi zinatakiwa kudhibitiwa ili kudumisha mahusiano mema ya

kifamilia na kijamii. Pale ambapo mtu anashindwa kudhibiti chuki

na hasira matokeo yake atajikuta amesababisha madhara yenye

kuathiri utendaji wa vipaji vya asili, kwa yeye mwenyewe na kwa

jamii inayomzunguka pia.

Tafsiri Ya Misamiati Ya Chuki Na Hasira.

Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, neno “chuki”

limetafsiriwa kuwa ni: “ tabia ya kutopenda watu au hali ya kuwa

na roho mbaya, au kinyongo.” Neno hasira limetafsiriwa kuwa ni:

“ ghadhabu au hamaki au fundo.”

Hapa nitoe angalizo ya kwamba, hii “tabia sugu ya chuki

na hasira”, inatofautiana na ile “tabia sugu ya kulalamika na

kuhukumu” ambayo tayari tumejifunza habari zake. Mtu mmoja

anaweza kuwa na tabia sugu zote mbili, lakini sio lazima aliye na

tabia moja kati ya hizi awe na tabia ya pili.

Kuna watu wameathiriwa na “tabia sugu ya chuki na hasira”

lakini hawana hulka ya “tabia sugu ya kulalamika na kuhukumu”

wengine hadharani. Waathirika wa “chuki na hasira” wanaweza

kuchukua hatua kali za kulipa visasi pasipo kupiga kelele hata

kidogo.

72

Wakati huo huo, watu wenye “tabia sugu ya kulalamika

na kuhukumu wengine” huwa ni chanzo kikuu cha kuwachochea

watu walioathiriwa na “tabia sugu ya chuki na hasira” ambao

huhamaki na kutafuta kulipiza visasi dhidi ya mahasimu wao.

Vyanzo Vya Hasira Na Chuki

Hisia hasi za chuki na hasira zina vyanzo viwili tofauti.

Kuna vyanzo vya nje ambavyo ni maumivu ya nafsi yatokanayo

na kunenewa au kutendewa mabaya; au uchungu wa kukosa

huduma na haki stahili kutoka kwenye mamlaka husika.

Chanzo cha pili ambacho ni kutoka ndani kinajumuisha hisia

ya ndani ambayo ni ama aibu ya moyoni itokanayo na kushindwa

au kutokufanikiwa katika jambo mbele za watu, au kusutwa

na dhamiri kwa sababu ya makosa au dhambi zilizofanywa na

hazijasuluhishwa bado.

“BWANA akamwambiaKaini, kwanini una ghadhabu?

Kwanini uso wako umekunjamana?Kama ukitenda vema hutapata

kibali?Usipotenda vema dhambi iko inakuotea mlangoni, nayo

inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.” (Mwa. 4:6-7)

Athari Za Hasira Na Hamaki

Pamoja na kwamba mwenye hasira na chuki anaweza

kujihesabia haki kutokana na sababu anazoziona kuwa ni halali

kwake; pasipo kujitambua kumbe anajisababishia athari yeye

mwenyewe ambazo baadhi yake ni kama hizi zifuatazo:

Kudhoofisha Kazi Za Kimaendeleo

Mwenye chuki na hasira hujikuta hajali muda na kuchelewa

kufika kwenye shughuli za kimaendeleo na kazini kwa sababu

ameshuka moyo wa kufanya kazi. Wengine hujiingiza kwenye

vitendo vya ulevi, kula kupita kiasi, kuwa tegemezi kwa wengine,

73

na ulemavu wa kihisia.

Madhara Ya Kiafya

• Hasira hupandisha mwendo wa moyo kutoka kiasi cha 80

mpaka 180 hata zaidi kwa dakika

• Shinikizo la damu nalo kupanda kutoka 120 kwa 80 kwenda

220 kwa 130 au zaidi

• Kasi ya kupumua huongezeka ili kuingiza hewa safi mwilini

• Mlipuko wa nguvu husababisha kushuka kwa sukari kiasi mtu

huweza hata kutetemeka

• Mwili hutoa kemikali za kugandisha damu kana kwamba kuna

ajali imetokea mwilini hali ambayo mgando wa damu huenda

moyoni au katika ubongo

• Mwenye hasira hukabiliwa na hatari ya mlipuko wa moyo au

ugonjwa wa kiharusi

• Hasira sugu husababisha mfadhaiko na msongo wa mambo

ambavyo hupelekea vidonda vya tumbo

• Hasira sugu hudhoofisha mfumo wa kinga na kusababisha

pumu, maradhi ya ngozi, ugonjwa wa baridi yabisi.

Mchakato Wa Kudhibiti Changamoto Zenye Kudhoofisha

Vipaji

Baada ya kuzipitia baadhi ya changamoto zilizoanishwa

katika sura hii, sasa ni wakati muafaka wa kutafuta kujua mbinu za

kupambana na kuudhibiti huu udhoofishaji wa vipaji. Tumezipitia

changamoto za nje ambazo ni marafiki wabaya, imani za uchawi

na ushirikina, mifumo butu ya elimu, na athari za utandawazi

kupitia mitando ya kijamii. Pili, tumepitia changamoto za ndani

kupitia “tabia sugu zenye kuathiri utendaji wa vipaji kutokea ndani

ya wahusika.

Suala zima la kudhibiti changamoto hizi haliwezi kuwa

tukio la mara moja tu. Lazima liwe katika mfumo wa kimchakato.

Madhara yaliyopo hayakujitokeza siku moja bali yalichukua muda

74

mrefu. Hali kadhalika na mchakato wa kuyadhibiti kunahitaji

muda ili tuweze kuona matokeo. Hakuna njia ya mkato katika

kurekebisha mambo yaliyojisokota kwa muda mrefu.

Zifuatazo ni ngazi makini za kufanya matengenezo ya

madhara yaliyokwisha kufanyika na mbinu za kujikinga ili athari

zisiendelee kujitokeza tena huko mbeleni:

1. Kumrudia Mungu Muumbaji Wetu

Tumejifunza habari za vipaji na karama kwamba ni vitu

vinavyotoka kwa Mungu aliyemwumba binadamu kwa mfano

wake na sura yake. Aidha tumejifunza pia ya kwamba, Mungu

ndiye anayejua kusudi la kuwepo kwako na pia ndiye mwenye

kujua mwanzo na mwisho wa kila binadamu hapa duniani.

Kwa hiyo, tunapotafuta kufanya matengenezo ya kitabia na

kunoa vipaji vilivyomo ndani yetu, lazima kwanza tumrudie Mungu

na kujenga uhusiano wa kiroho pamoja naye. Uzuri ni kwamba

sio sisi tunayemrudia Mungu kwa juhudi zetu wenyewe, bali yeye

mwenyewe alikwisha kututafuta na kutuonesha njia ya kumrudia

bila gharama yoyote. Katika kumrudia Mungu tunaanza na hatua

ya kwanza inayojulikana kama toba.

Tafsiri Ya Toba

Biblia imeandika kuhusu toba ikitumia maneno ya

Kiebrania na Kiyunani. Kwa Kiebrania neno lililotumika kuhusu

toba ni nocham. Maana yake ni kuugulia, kuomboleza, kujuta

na kuacha kutenda dhambi na kugeuka na kurejea kwa Mungu.

Kwa Kiyunani neno lililotumika kuhusu toba ni metanoia. Maana

yake ni kubadilia nia na kuachana na kusudi la kuendeleza jambo,

kugeuka nyuma na kurudi ulikotoka.

75

Kwa muktadha wa maneno nocham na metanoia, yote

yanatoa maana ya mtu kujutia hali yake ya dhambi, kuamua

kubadili nia na mtazamo wake kuhusu dhambi zake, na kugeuka

nyuma kisha kurejea katika uhusiano wa kiroho na Mungu.

Watu wengi huchanganya maana ya maneno “toba” na

“ungamo” wakidhani ni kitu kile kile. Ukweli ni kwamba “kutubu” ni

tofauti na “kuungama” tu. Kuungama ni “kukubali na kukiri ukweli

wa makosa yaliyofanywa.” Lakini “kutubu” ni “kujutia na kubadili

nia” kwa “kuachana na mwenendo wa dhambi na kumgeukia

Mungu” ili kuishi maisha tofauti na yaliyopita.

Agizo La Toba

Mungu amekwisha kutoa agizo maalum kwa watu wote

ambao ni waathirika wa tabia sugu zilizotajwa katika sura hii

wapate kutubu kwake kama ilivyoandikwa:

“Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni;

bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu. Kwa

maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki,

kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa

mambo haya kwa kumfufua katika wafu.” (Mdo. 17:30-31)

Maandiko haya yaliandikwa kwa ajili ya kuwataka watu wote

waliokuwa ni waathirika na imani za uchawi na ushirikina pamoja

na tabia sugu wabadili nia zao na kumrudia Mungu Muumbaji wao

na kujiweka salama wasiagukie kwenye maangamizi yaliyokuwa

yakiwakabili.

Mchakato wa kufanya matengenezo dhidi ya madhara ya

changamoto zenye kuathiri vipaji na karama unatakiwa kuanza na

toba kwa mujibu wa maandiko tuliyosoma. Uzuri wa maandiko

haya ni kwamba Mungu yuko tayari kuachilia makosa yaliyokwisha

kufanyika kwa kujifanya kama hayajui kwa sababu yalifanyika

kutokana na kutokujua.

76

Faida Za Toba

Kutoka Katika Mitego Ya Ibilisi

Shetani ndiye chimbuko kuu la changamoto zote za nje na

za ndani ambazo zinadhoofisha utendaji wa vipaji vya wanadamu.

Kufanya toba ya kweli ndio mlango wa kutoka katika mtego wa

Ibilisi ambao aliutumia kuwanasa wengi katika vifungo vya dhambi

na tabia sugu:

“akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama

ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli; wapate

tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao

wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.” (2 Tim. 2:25-26)

Maandiko haya yanataja habari za “kupata tena fahamu”

ambazo hapo awali ziliharibiwa na tabia sugu za ulevi na zinaa.

Pili, tunasoma habari za “kutoka katika mtego wa Ibilisi” ambao ni

vishawishi au vitisho vyenye kuwafanya waathirika kuzama katika

maisha ya imani za uchawi na ushirikina.

Katika kufanya toba ya kweli tunasoma kuna kufumbuliwa

macho ya kiroho na kutambua kuwa uko gizani na kuamua

kuigeukia nuru:

“uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na

kuigeukia nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea

Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni

mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.” (Mdo. 26:18)

Maandiko haya yanataja pia habari za “kuziacha nguvu za

shetani” ambazo zinasababishwa na imani za uchawi na ushirika

pamoja na vifungo vya tabia sugu zlizokwisha kutajwa katika sura

hii.

77

Kuzaliwa Upya

Faida ya pili ya kufanya toba ya kweli ni muujiza wa

mabadiliko ya ndani ya kiroho ambayo hufanywa na Mungu

mwenyewe kwa kumtumia Roho wake Mtakatifu:

“si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali

kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa

upya na Roho Mtakatifu” (Tit. 3:5)

Itakumbukwa ya kwamba maana ya tabia sugu ni

“mazoea yatokanayo na kurudiarudia hali isiyoweza kuondolewa

kwa urahisi”. Katika hatua ya kufanya toba, pasipo kutumia

nguvu za kibinadamu za kujibadilisha kitabia, kuna rehema za

Mungu zinazomshukia mwenye kutubu na kuihuisha roho yake

kupata nguvu za mabadiliko ya kiroho. Mabadiliko haya ndiyo

yanajulikana kuwa ni “kuzaliwa kwa pili” na “kufanywa upya” na

Roho Mtakatifu.

2. Kupokea Nguvu Za Kiungu Za Kudhibiti Tabia Sugu

Baada ya kufanya toba ya kweli na kupata mabadiliko ya

ndani ya kiroho; hatua inayofuata ni kupokea nguvu za kiungu

za kudhibiti tabia sugu ambazo ni “mazoea yatokanayo na

kurudiarudia hali isiyoweza kuondolewa kwa urahisi” Maandiko

yafuatayo yanatuthibitishia uhakika wa kudhibiti tabia sugu kama

ifuatavyo:

“Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote

imefunuliwa, nayo yatufundisha kutaa ubaya na tamaa za kidunia;

tupate kuishi kwa kiasi, haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa

sasa.” (Tit. 2:11)

Maandiko hayo hapo juu yanatujulisha jinsi ambavyo

Mungu amekwisha kutoa neema ya kuwaokoa wanadamu wote,

kama wakiamua kutubu kwa dhati na kumrudia yeye. Na neema

78

hii inafanya kazi ya kutufundisha jinsi ya kukataa ubaya na tamaa

za kidunia ambazo zinadhoofisha utendaji wa vipaji na karama

ndani yetu. Katika maandiko mengine tunajulishwa kukirimiwa

ahadi kubwa za thamani za kutuwezesha kupokea tabia za uungu

ambazo huweza kudhibiti tabia sugu:

“Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani,

ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washiriki wa tabia ya Uungu,

mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.” (

2 Pet. 1:4)

3. Kuutafuta Kwanza Ufalme Wa Mungu Na Haki Yake

Changamoto kubwa ya binadamu hapa duniani ni kutafuta

maisha kwa kila njia, ziwe halali au haramu. Kipaumbele chake ni

kufanikiwa katika kujipatia na kujilimbikizia mali nyingi. Hata hivyo,

mambo ni tofauti kwa mtu aliyekwisha kumrudia Mungu kwa

njia ya toba. Baada ya kuchukua hatua za kiroho zilizotangulia,

kinachofuata ni kupanga upya vipaumbele vya maisha:

“Msisumbuke, basi, mkisema, tule nini? Au Tunywe nini?

Au tuvae nini? Kwa maana hayo yote mataifa huyatafuta; kwa

sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hao

yote. Bali utafute kwanza ufalme wake na haki yake; na hayo yote

mtazidishiwa.” (Mat.6:32-33)

Maandiko haya yametafsiriwa kinyume na maana yake

kwa nadharia zinazokataza watu kufanya kazi eti badala yake

wategemee sala peke yake kwa kuwa Mungu anajua mahitaji yao.

Dhana ya kutokufanya kazi na kutegemea kuishi kwa miujiza peke

yake sio muktadha wa maandiko haya.

Kile Yesu alichomaanisha hapa ni wanafunzi wake kubadili

mtazamo kuhusu maisha na kuweka upya vipaumbele kwa kigezo

cha kutanguliza ufalme wa Mungu. Yesu hakukataza kufanya kazi,

alitoa mwongozo wa kufanikiwa kupitia vipaumbele na Mungu

79

akiwa ndiye kipaumbele cha kwanza.

Wakati watu wasiomcha Mungu wanaabudu mali za duniani

hii lakini hawana ushirika na Mungu aliyewaumba; wanafunzi

wa Yesu waliagizwa kumtafuta na kumtanguliza Mungu kwanza

katika kutafuta kwao ili kufanikiwa kwao chimbuko lake liwe ni

Mungu badala ya shetani.

Kutafuta kwanza ufalme wa Mungu ni kumtafuta Mungu

akufunulie na kukudhihirishia kusudi lake katika maisha yako.

Na atafanya hivyo kwa kuanza kuibua vipaji vyako, na karama za

Roho ili utendaji wako utokane na nguvu alizowekeza ndani yako.

Kuweza kufanikisha zoezi hili unahitaji mshauri wa kiroho

mwenye uzoefu na maisha ya ukuzaji vipaji kwa mujibu wa maadili

ya kibibilia.

Lakini, hatua hizi tatu ukizipa uzito unaostahili, tayari

utakuwa umefanikiwa kupata ujuzi na uwezo wa kupambana na

changamoto zenye kudhoofisha vipaji na kuzishinda. Inaweza

kuonekana ni ngumu lakini sio kwamba haiwezekani kabisa.

Ni uamuzi wako binafsi kama unataka mabadiliko chanya ya

kutambua na kuchochea vipaji vyako.

80

SURA YA NNE

Utangulizi

WAJIBU KWA KIZAZI CHA SASA

KURITHISHA KIZAZI KIPYA

Kitabu hiki hakitakuwa na msaada kwa msomaji kama

hakutakuwepo na uchambuzi makini unaohusu wajibu kwa kizazi

cha sasa, kizazi cha wazee, kutambua wajibu mkuu wa kurithisha

majukumu ya kijamii, kiuchumi na kiuongozi kwa kizazi kipya.

Kizazi kilichopo hivi sasa kimefikia mahali kilipo hivi sasa

kwa sababu kizazi cha zamani, kilichotangulia kiliacha misingi

ambayo kiliirithisha kwa kizazi kinachomaliza muda wake sasa.

Kwa bahati mbaya, nadharia ya uritishaji imeanza

kupoteza umuhimu wake kwa jamii kiasi kwamba kizazi kipya

hakina matumaini wala mwelekeo wa kule kinakojiandaa

kuelekea. Muktadha wa kitabu hiki ni kukihimiza kizazi cha sasa

kinachomaliza muda wake kutimiza wajibu wake wa kurithisha

kizazi kipya majukumu ya msingi kwa mustakabari wa taifa.

Makundi muhimu yenye wajibu wa kusimamia mchakato

wa urithishaji kwa kizazi kipya unaanzia na “wazazi” au “walezi”

katika ngazi ya familia. Ngazi ya familia ndio kitovu cha malezi

kuanzia mtoto anapozaliwa, kukua hadi anapofikia umri wa

kujitegemea kama mtu mzima.

Kundi la pili ambalo linahusika katika wajibu wa kurithisha

kizazi kipya ni kanisa. Natumia msamiati kanisa kwa maana ya

taasisi inayosimamia kueneza na kurithisha maadili ya kiimani

kwa wafuasi wake. Wakati familia ni mlezi mkuu wa maisha ya

81

mtoto kijamii, kanisa ni mlezi mkuu kimaadili. Kundi la tatu lenye

wajibu mkuu katika kurithisha kizazi kipya ni serikali na vyombo

vyake vya dola na taasisi zake za umma.

Katika sura hii tunakwenda kupitia mtiririko wa kihistoria

kuhusu nadharia ya urithishaji, sababu za msingi wa urithishaji,

hatua za urithishaji, vitu muhimu vya kurithisha na visivyofaa

kurithishwa kizazi kipya. Tutapitia pia ukweli kuhusu ukomo wa

umri wa kuishi wa kizazi kilichopo pamoja na ukomo wa nadharia

za uchumi na uongozi. Kisha tutahitimisha na uchambuzi kuhusu

hitaji kuu la viongozi wa kizazi kipya pamoja na mchakato wa

kuandaa uongozi wa kizazi kipya.

Historia Ya Nadharia Ya Urithishaji

Nadharia ya urithishaji yaweza kuonekana kama kitu kipya

kwa baadhi ya watu katika jamii. Kihistoria, nadharia ya urithishaji

chimbuko lake ni taasisi ya ndoa ambayo ni “muungano wa

mwanamume na mwanamke walioamua kuishi pamoja maisha

yao yote“. Baada ya mwanamume na mwanamke kuoana na

kuzaa watoto, wahusika hupanda daraja na kuitwa baba na mama

au wazazi. Ni katika ngazi hii tunapata jina familia.

Katika ngazi ya familia maisha na shughuli za uzalishaji

na utunzaji wa familia yakiwemo malezi ya watoto hufanyika na

kustawi katika jamii. Kilele cha malezi ya wazazi kwa watoto, ni

pale ambapo watoto wamekuwa watu wazima na kufikia daraja

la kuanzisha taasisi mpya za ndoa na kuanza kuishi maisha yao

wenyewe.

Kama ni binti huagwa na wazazi kwa zawadi na hatarajiwi

kurejea kwao na kuwa sehemu ya familia ile tena. Na kwa upande

wa mtoto wa kiume, huwezeshwa katika kuandaa mahali pake

maalum, nyumba au chumba atakapoishi na mkewe; kulipiwa

mahari, na kufanyiwa sherehe ya arusi.

82

Kuanzia wakati huo, bwana arusi hutambuliwa kuwa mtu

mzima anayestahili kuendesha maisha mapya ya taasisi ya ndoa

yake, na anatarajiwa kuacha kabisa kuwa tegemezi kwa wazazi

kama alivyokuwa kijana asiye na ndoa.

Kwa baadhi ya makabila au mataifa mengine, nadharia ya

urithishaji, huanza kutekelezwa na wazazi katika hatua ya kuozesha

au kufungisha ndoa za watoto wao. Lakini kwa makabila mengine

hatua ya urithishaji hufanyika wakati baba wa familia amefariki

dunia. Baada ya kuhitimisha msiba wake, ndipo wanafamilia

wakisaidiana na ukoo hutekeleza nadharia ya kurithisha mali za

marehemu kwa mjane na watoto wote pasipo kujali wana ndoa au

hawana ndoa.

Sababu Za Msingi Wa Urithishaji

Ukomo Wa Umri Wa Kuishi

Biblia imetabiri ukomo wa umri wa kuishi ni miaka 70 mpaka

80. Dalili za kizazi kinachomaliza muda wake kimekadiriwa watu

kuanzia miaka 50 na kuendelea. Ukomo wa umri wa kutumikia

serikali na taasisi za umma ni miaka 60.

Kwa hiyo, watu wote wenye umri wa kuanzia miaka 50 na

kuendelea, popote walipo, kwa mambo yoyote wanayofanya,

mojawapo ya mipango muhimu kwetu ni kujiandaa kuachia

majukumu tuliyo nayo na kuyarithisha kwa kizazi kinachoinukia

hivi sasa.

Umri wa kizazi kinachotakiwa kurithishwa ni kuanzia miaka

18 mpaka 49. Kipindi cha kurithisha kinahitaji maandalizi yasiyozidi

miaka 10 kwa watu waliofikisha miaka 50.

Kwa hiyo tunalazimika kurithisha kwa sababu ya ukomo

wa umri wa kuishi ambao hatuna udhibiti nao. Kwa bahati

mbaya baadhi yetu tunaogopa kurithisha mapema kwa hofu

83

ya kupinduliwa au kupoteza umaarufu tuliojijengea katika jamii.

Lakini tusipotumia muda muafaka tutamaliza vibaya na kuacha

migogoro ya kifamilia na kijamii nyuma yetu.

Wana-rika wenzangu, tusiposhituka na kuanza maandalizi

ya urithishaji wa uchumi na uongozi hivi sasa, muda hautungoji.

Miaka 10 iliyoko mbele yetu inakimbia mbio za kasi, kufumba na

kufumbua tutajikuta iko mbele yetu.

Uzalishaji na usimamizi ni mambo yanayotegemea nguvu

na akili. Kwa kadiri umri unavyoongezeka ndivyo na nguvu za

uzalishaji na akili za kufanya maamuzi hubadilka. Kwa lugha

nyingine kasi ya kufanya mambo hupungua na uzito katika kufanya

maamuzi nao huongezeka.

Kwenye suala la uchumi ambapo ulimwengu unabadilika

kila kukicha, mambo mapya yanazaliwa na elimu inaongezeka

kwa kasi, wakati jamii ya wazee bado iko katika enzi zao. Bahati

mbaya kasi na hamu ya kujifunza mambo mapya kwa wazee

huzidi kupungua. Hizi ndizo dalili zinazoashiria kwamba, wakati

wa kurithisha wengine wenye uwezo na nguvu umekaribia.

Kuendeleza Jina

Maendeleo ya kiuchumi na kijamii hufanywa na watu, kila

mtu mmoja mmoja, na kwa ushirikiano wa kimakundi. Mojawapo

ya hamasa za kimaisha, ni mtu kutoa mchango wa kimaendeleo

ambao utakumbukwa baada ya kuondoka kwake duniani. Hii

ndiyo inaitwa “kuacha jina”. Kuna mambo ambayo baadhi ya

wazee waliotutangulia walifanya enzi za ujana wao, na sisi

tumeyakuta, tumeyarithi, na tunawakumbuka kwa ajili ya mambo

hayo. Wenyewe wamekufa, lakini mambo yao bado yako hai,

na hivyo majina yao yanaendelea kutajwa japokuwa wenyewe

hawapo tena.

84

Kuendeleza Kizazi

Sababu nyingine muhimu sana ni kukiwezesha kiuchumi

na kiuongozi kizazi kipya cha watoto waliozaliwa na kulelewa

katika mazingira ya kifamilia, kitaasisi na kitaifa. Sababu ya

kwanza ya kurithisha tulisema ni kigezo cha ukomo wa muda

wa kuishi. Sababu hii ndiyo inapaswa kuchochea moyo wa

kizazi kinachomaliza muda wake kufanya maandalizi mapema ya

kukabidhi majukumu ya kiuchumi na kuiongozi kwa kizazi kipya.

Katika ngazi ya familia, ni fahari ya wazazi pale ambapo

watoto wao waliowazaa wanapofikia umri wa kutaka kujitegemea

kimaisha.

Vijana wa kiume wanapofikia umri wa kuoa huhimizwa na

wazazi na kufundishwa, na hata kusaidiwa jinsi ya kujenga misingi

ya kujitegemea kama kuwa na shughuli maalum ya uzalisha wa

kujipatia kipato binafsi, kujenga nyumba, kuwa na samani za

ndani n.k.

Kwa upande wa vijana wa kike, wanapofikia umri wa

kuolewa huandaliwa rasmi jinsi ya kuishi katika ndoa na kutunza

familia zao mpya baada ya kuolewa.

Kuendeleza Maono Ya Kitaasisi

Changamoto katika urithishaji ziko kwenye ngazi ya

kitaasisi na kitaifa. Katika ngazi ya kitaasisi, kuna jamii ya watu

waitwao “waasisi”. Hawa ni waanzilishi wa mawazo ya awali

ya kuanzishwa kwa taasisi husika na kwa njia hiyo wamekuwa

viongozi wake tangu ngazi ya uchanga mpaka hapo ambapo

taasisi hizo zimekomaa kiutendaji. Ninaposema taasisi nina

maana ya vyama vya hiari, au madhehebu ya dini, au vikundi vya

kijamii ambavyo vimesajiliwa kwa mujibu wa sheria.

85

Katika ngazi ya kitaasisi, (tofuati na serikali na taasisi za

kiserikali, ambazo utumishi wake una ukomo kwa mujibu wa sheria)

baadhi ya taasisi binafsi hazina utamaduni wa kisheria wa ukomo

wa utumishi. Katika ngazi hii, mara nyingi wale waitwao “waasisi”

kwa maana ya walioanzisha taasisi au huduma hizo huwa wazito

sana kuachia madaraka ya uongozi kwa vijana wao. Kuacha

utumishi katika ngazi ya kitaasisi hushinikizwa na maaradhi, au

kifo; au shinikizo la uasi ndani ya taasisi ambao matokeo yake

husababisha mifarakano na matengano ya kitaasisi.

Kuendeleza Kizazi Cha Kijaamii Kitaifa

Katika ngazi hii, urithishaji unategemea mfumo wa utawala

na uzoefu katika zoezi ya kuachia madaraka. Kwa upande wa

Tanzania, kisiasa tuna sifa njema katika Bara la Afrika kwa kuwa

na utamaduni wa watawala wa kitaifa kuachia madaraka mara

baada ya kufikia ukomo wa muda wao.

Hata hivyo, changamoto iliyopo katika ngazi hii, ni pale

ambapo wale wanaomaliza muda wao wa utumishi wa umma

kupewa mikataba maalum na kuendelea kutumika. Utetezi

unaotumika katika kulinda utaratibu huu ni kuwepo kwa baadhi

ya nafasi za utumishi ambazo bado hazina watu wenye ujuzi na

uzoefu; na hivyo wastaafu husika wakaonekana bado wanahitajika

kutumika katika ngazi husika.

Pamoja na utetezi huu, pia kumekuwepo na upande

mwingine wenye malalamiko dhidi ya utaratibu huu kwamba

unawanyima haki wengine waliostahili kushika nafasi za wastaafu

kwa mujibu wa sheria.

86

Ngazi Muhimu Za Urithishaji

Urithishaji Wa Ngazi Ya Kifamilia

Katika ngazi hii, ni wazazi ndio hurithisha watoto mali

walizochuma katika familia. Kama tulivyokwisha kupitia kihistoria

kuhusu urithishaji katika ngazi ya familia, hapa ni muhimu

tuzingatie kwamba jamii ya kizazi chetu kwa sehemu kubwa

imepoteza utamaduni wa kurithisha majukumu na raslimali kwa

kizazi kinachoinukia.

Ushahidi ni kuongezeka kwa migogoro na kesi za mirathi

zilizojaa mahakamani siku hizi. Badala ya walezi kifamilia

kusimamia mchakato wa urithishaji kwa watoto wa marehemu

au wale wanaostahili kurithishwa, wao ndio wanateka mali hizo

na kuzitapanya kwa sababu za kibinafsi na watoto wanaanza

kuhangaika.

Kupotea kwa utamaduni wa kurithisha pia kumechangiwa

kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya kimaendeleo na kijamii

ambapo familia zimetawanyika mijini na vijijini. Lakini pia ukosefu

wa wazazi kuandika wosia mapema kuhusu mgawanyo wa mali

kwa familia.

Jambo linalosikitisha zaidi katika udhaifu wa kutokurithisha

ni pale ambapo wazazi huishia kuzaa watoto lakini hawana

mpango maalum wa kutunza urithi kwa ajili ya watoto. Badala

yake wazazi wanafanya kazi ya kuchuma na kutafuta bila kuweka

akiba kwa ajili ya watoto.

Kuna ongezeko la kuparaganyika kwa familia kunakotokana

na mmomonyoko wa maadili katika jamii. Hii imezalisha familia za

aina tofauti ambazo watoto wanaozaliwa au kulelewa ndani yake

wanakosa mwelekeo wa kimaadili na hivyo kupotoka kitabia.

87

Kuparaganyika kwa familia nyingi kumezalisha changamoto

kubwa nyingine ya ongezeko la kizazi kinachoitwa kwa jina maarufu

kama “watoto wa mitaani”. Hawa ni watoto ambao baadhi yao

hawana wazazi au walezi na wamekosa malezi ya kifamilia na ndio

maana wameishia mitaani. Hiki nacho ni kizazi ambacho badala

ya kurithishwa msingi wa kimaendeleo wanaishia kurithi umaskini

na maisha ya uhalifu.

Si lengo la kitabu hiki kuzungumuzia matatizo ya kifamilia,

ila haya yanatajwa kama viashiria vya familia kushindwa kutimiza

wajibu wake wa kurithisha kizazi kipya. Wito makini wa ujumbe

wa kitabu hiki kwa kila familia yenye mtoto au watoto, wawe wa

kuwazaa au kuwalea, ni kurejea katika utamaduni wa kijamii wa

kurithisha majukumu na rasilimali kwa watoto pindi wanapofikia

umri wa kujitegemea na kuwa watu wazima.

Urithishaji Wa Ngazi Ya Kitaasisi

Uritishaji wa kitaasisi ni urithishaji wa mali na madaraka ya

kusimamia taasisi husika. Taasisi hapa tunajumuisha makampuni

binafsi, vikundi vya uzalishaji, na vikundi vinginevyo ambavyo

madhumuni yake ni uzalishaji na wanahisa kugawana mapato

kwa mujibu wa makubaliano ya kisheria.

Katika ngazi hii ya urithishaji wa kitaasisi, viongozi waasisi

ndio wenye wajibu wa kurithisha madaraka ya usimamizi wa

taasisi. Japokuwa jambo la kurithisha uongozi litaelezwa kwa

kina katika vipengele vinavyofuata, hapa ni muhimu kuzingatia

mapema ya kuwa kila mwasisi na mtendaji mkuu wa kampuni ya

kifamilia au kijamii atie akilini mwake kuwa ni muhimu kumwandaa

mrithi wake wakati bado ana nguvu.

Mwasisi asisubiri wakati amezeeka ndipo akabidhi

majukumu. Kurithisha majukumu ya uongozi na utawala katika

mambo ya uzalishaji sio kama kurithisha mali za marehemu.

Unahitaji muda wa kutosha wa kuachilia baadhi ya majukumu

88

kwa watoto au warithi ambao wanapata uzoefu wakati mwasisi

bado yuko hai.

Urithishaji Kwa Kizazi Cha Kitaifa

Ngazi ya urithishaji kwa kizazi cha kitaifa ni hatua ya

juu kabisa katika jamii. Hapa tunazungumuzia ngazi ya kitaifa.

Taifa kama Tanzania ambalo mna makabila zaidi ya 120

yanayounganishwa na utaifa wenye sifa ya uraia mmoja.

Tanzania kama taifa, linayo jamii ya watu waliozaliwa kwa

wakati mmoja wa historia, ambao kwa lugha nyingine huitwa rika

moja. Hawa ndio huitwa kizazi cha kitaifa. Lakini tunapo itathmini

Tanzania kijamii tunakuta kuna mgawanyiko wa sehemu mbili za

vizazi vya kitaifa; kuna kizazi cha watoto, na pili, kuna kizazi cha

watu wazima.

Kizazi cha watoto kinatambuliwa kwa umri kuanzia mwaka

mmoja (1) mpaka miaka kumi na saba (17). Watu wote katika umri

huu hawaruhusiwi kufanya maamuzi huru kama watu wazima.

Wahusika wanahesabiwa kuwa chini ya uangalizi wa kifamilia

na malezi ya kitaifa. Ishara iliyo wazi zaidi ni kuwa hawaruhusiwi

kupiga kura kwenye uchaguzi wa uongozi wa kitaifa.

Kizazi cha watu wazima ni kuanzia umri wa miaka kumi

na nane (18) mpaka sitini (60). Hiki ndicho kizazi chenye idhini ya

kufanya maamuzi na kuwajibika kisheria. Wahusika wanaruhusiwa

kupiga kura na kuwania madaraka ya uongozi katika ngazi mbali

mbali za utumishi wa umma kitaifa.

Katika ngazi ya kizazi cha kitaifa, wenye wajibu wa

kurithisha ni wazee ambao wamefikia umri wa kustaafu kwa

mujibu wa sheria. Hiki ndicho kigezo muhimu cha Urithishaji wa

kizazi. Wazee wanapostaafu huwaachia majukumu ya uzalishaji

na usimamizi vijana ambao wamechukua nafasi zao.

89

Vitu Muhimu Vya Kurithisha

Elimu Na Ujuzi

Zamani za wahenga wetu, urithi ulihusu mali zilizoachwa

na marehemu tu. Na hii ndiyo asili ya neno Urithi. Mali au vitu

vinavyoachwa na marehemu na kupewa mtu fulani wa ukoo

husika. Lakini siku hizi mambo yamekwisha kubadilika. Urithi wa

kwanza na wa kudumu ni elimu na ujuzi.

Kama tulivyokwisha kusoma sehemu uliyotangulia ya kuwa

wajibu wa kurithisha elimu na ujuzi unaanzia katika ngazi ya familia,

halafu unakuja kwenye taasisi na kisha ngazi ya kitaifa. Isitoshe,

ni haki ya kibinadamu kwa kila mtu kupata elimu ili kujiendeleza

kiujuzi.

Kwa kuwa kitabu hiki kinahusu vipaji vya asili, huko mbeleni

nitaweka bayana ni aina gani ya elimu na ujuzi vinavyotakiwa

kurithishwa kama njia ya kuinua na kunoa vipaji.

Rasilimali

Msamiati wa neno rasilimali umetafsiriwa kuwa ni “jumla

ya mali aliyonayo mtu au nchi.” Kama nilivyotangulia kudokeza

hapa juu kwamba, rasilimali ndio urithi unaofahamika tangu enzi

za wahenga na hata sasa bado umeendelea kuwepo.

Hapa inabidi tuzingatie kwamba rasilimali ni mali

iliyozalishwa na kumilikiwa na familia. Ni wajibu wa kila familia

kufanya kazi kwa bidii, kuchuma mali na kuzimiliki kifamilia.

Tufahamu kwamba kiasi cha rasilimali ilichonacho familia ndicho

kinachoweza kurithishwa kwa watoto wanapokuwa watu wazima.

Ngazi ya pili ya kurithisha rasilimali ni ngazi ya kitaifa.

Hapa nikiwa na maana ya serikali ya nchi kuhakikisha kila raia

anatengenezewa mazingira ya kumwezesha kuzalisha na kumiliki

90

asilimali kwa njia halali na kwa mujibu wa sheria.

Aidha, ni kuhakikisha rasilimali za asili katika nchi zinalindwa

kwa matumizi ya sasa na vizazi vijavyo; na Kipaumbele katika

matumizi ya rasilimali za asili kiwe ni kuwawezesha raia kuwa na

haki ya umiliki wake kisheria.

Uongozi

Tumekwisha kujifunza kwamba uongozi ni mojawapo ya

sehemu ya vipaji vya asili. Kimsingi, kipaji hakiwezi kurithishwa

toka mtu kwenda mtu mwingine. Muktadha wa “uongozi wa

kurithisha” ni ile nafasi au madaraka ya usimamizi na utawala, iwe

ni katika taasisi na makampuni binafsi, au katika serikali na taasisi

zake za umma.

Kwa mantiki hii, uongozi nao ni kitu maalum ambacho

kinatakiwa kurithishwa. Japokuwa si kila mtu anaweza kurithishwa

uongozi, lakini uongozi kama nadharia na mfumo lazima urithishwe

ili kuweza kusimamia masuala ya uchumi na huduma za kijamii

kwa raia wa nchi husika.

Njia za urithishaji wa uongozi hazianzi na kugawa vyeo vya

utawala bila kuzingatia uwezo wa kuongoza. Njia za kurithisha

uongozi lazima ziwe na vigezo vilivyo wazi na makini tena kwa

mujibu wa sheria na taratibu rasmi, ili warithishwe watu wenye

uwezo wa kuongoza. Kama nilivyotangulia kudokeza kabla, ni

kwamba nitachambua kwa kina suala la urithithishaji wa uongozi

huko mbeleni katika sura hii.

Vitu Visivyofaa Kurithishwa Kizazi Kipya

Ujinga

Kuna usemi uliozoeleka usemao: “Kama unaona elimu

ni ghali, basi jaribu ujinga”. Kizazi cha utawala kilichopo hivi

91

sasa kinaweza kuona kwamba kuwekeza katika “elimu na ujuzi”

ni gharama kubwa, na kutafuta unafuu na urahisi ili kukwepa

kugharimia viwango bora vya elimu na ujuzi. Kumbe katika

kushusha “viwango vya ubora” tayari tumechagua kurithisha

“viwango duni vya elimu” kwa kizazi kinachoinukia ambacho

hakitaweza kumudu ushindani wa kimataifa katika uzalishaji.

Sio siri hivi sasa kuona kwamba watoto na vijana wetu

wamesongwa katika mazingira magumu ya kimfumo wa huduma

za elimu kwa sababu mbali mbali. Baadhi ya sababu za watoto na

vijana wetu kukosa kupata elimu bora ni pamoja na: i) uhaba wa

nafasi za kuendelea na elimu ya juu katika mfumo wa elimu yetu.

ii) udhaifu wa mitaala isiyokidhi viwango vya ubora wa elimu ya

kimataifa. iii) Vitendo vya uchakachuaji wa mitihani kunakotokana

na kukithiri kwa rushwa katika taasisi zinazosimamia mitihani. iv)

Walimu kukosa motisha katika utoaji wa elimu kwa wanafunzi.

Kwa kadiri ambavyo idadi kubwa ya watoto na vijana

wengine wanavyoishia katika viwango vya chini vya elimu;

hiyo ndiyo dalili iliyo waziwazi kwamba kizazi chetu tuliopo hivi

sasa tumeamua kurithisha ujinga kwa kizazi kijacho. Kimsingi,

tumekuwa tukifanya zoezi la kurithisha ujinga na kizazi kinachokuja

kitatukumbuka kwa urithi wa ujinga tuliokiachia.

Mabadiliko yoyote ya kimfumo hayaji kwa miujiza. Yanakuja

kwa utashi na uamuzi wa nguvu. Lazima tuutumie utashi wetu

na kufanya uamuzi wa kukataa kuendelea kurithisha ujinga kwa

watoto na vijana wetu. Uwezo na nguvu tunazo, kinachokosekana

ni nia ya dhati. Lazima tukatae kurithisha ujinga kwa watoto na

vijana wetu.

Umaskini

Kuna mtu mmoja maarufu sana anayeongoza kwa utajiri

hapa duniani anaitwa Bill Gates. Miaka ya hivi karibuni alitoa kauli

ambayo imezua mjadala mpaka hivi sasa, lakini ina ushawishi

92

mkubwa kiasi ambacho hakuna ambaye amefaulu kuipinga na

akashinda. Alisema hivi:“kama umezaliwa katika familia masikini

sio kosa lako; lakini ukifa maskini hilo ni kosa lako mwenyewe”.

Kwa kauli hii ni rahisi sana Bill Gates kutafsiriwa kuwa

amejikinai kwa kuwahukumu watu wanaokufa maskini kwamba

hayo ni makosa yao. Lakini baada ya kuutafakari kwa makini

usemi wake nilipata kumwelewa kwa sehemu kile alichokuwa

amemaanisha.

Bila shaka alikuwa anatoa ujumbe kwamba mtu

anapozaliwa katika familia ambayo ni maskini sio kosa lake kwa

sababu sio yeye aliyechangia wala kufanya maamuzi ya kimaisha

hata kusababisha umaskini alioukuta. Kwa maneno mengine mtu

hajichagulii azaliwe katika familia ya namna gani, bali hujikuta

amezaliwa katika familia husika.

Lakini iwapo muhusika aliyezaliwa katika familia maskini

anapokuwa mtu mzima ana uhuru wa kufanya maamuzi ya mwisho

kuhusu maisha yake. Na hii ni pamoja na kutafuta fursa nyingi

zilizopo mbele yake na kuanza kuzitumia kwa uzalishaji, kwa nia

ya kubadili maisha yake ya umaskini wa kuzaliwa na kuitwa jina

tofauti katika jamii.

Neno Umaskini limetafsiriwa na Kamusi ya Kiswahili Sanifu

kuwa ni “hali ya kukosa mali; ufukara, uhitaji, na ukata”. Najua

kwamba kuna nadharia na dhana nyingi kwa habari ya umaskini,

hususan huu wa kipato. Aidha kumekuwepo na itikadi zenye

kutetea umaskini kama janga linalowapata watu pasipo wenyewe

kutaka au kuusababisha. Kwa utafiti wangu naweza kutafsiri

sababu za umaskini katika sehemu zifuatazo:

Ulemavu:

Ulemavu wa viungo vya mwili au akili ambao mlemavu

hawezi kufanya shughuli halali ya kujipatia kipato. Ulemavu wa

93

jinsi hii, ni hali ambayo iko nje ya uwezo na uamuzi wa mhusika,

na hivyo analazimika kuishi kwa kutegemea fadhila za binadamu

ambao si walemavu katika jamii.

Majanga Ya Kimazingira:

Majanga ya kimazingira ni kama vile mafuriko, matetemeko

au vita vya kiraia. Haya ni matukio ambayo huharibu rasilimali za

watu na kupoteza muda wa jamii kufanya kazi za uzalishaji mpaka

mazingira yarejee katika hali inayoruhusu uzalishaji.

Katika mazingira kama haya waathirika hujikuta hawana rasilimali

wala kipato cha kuwawezesha kukidhi mahitaji yao, isipokuwa nao

wanaishi kwa fadhila za binadamu wengine ambao hawajakumbwa

na majanga ya kimazingira.

Uvivu Na Anasa:

Tafsiri ya uvivu ni “hali ya kutotaka kufanya kazi; hali ya

ulegevu katika kazi; utepetevu na ulegevu.” Ikiwa mtu mzima,

ambaye si mlemavu, si mgonjwa, si mzee kikongwe; halafu mtu

mwenyewe anaishi kwenye mazingira yenye fursa za uzalishaji

mali (ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha, ustawi wa mimea na

malisho ya mifugo), halafu mtu huyo katikati ya mazingira hayo

bado hana shughuli maalum inayompatia kipato; basi tena, huyo

mtu sifa yake ni moja tu, ni mvivu.

Kutokufanya kazi; au kuwa mlegevu katika kazi,

husababisha ukosefu wa kipato na matokeo yake ni umasikini wa

kipato na rasilimali. Huu ndio umaskini ambao Bill Gates alisema,

“mtu akifa katika umaskini wa jinsi hii ni makosa ya mhusika’.

Tafsiri ya anasa ni “mambo au hali ya starehe na raha

nyingi; au kitu chenye thamani kubwa ambacho sio muhimu.”

Unaona? Haya ni maisha ambayo watu wanatumia rasilimali zao

kwa mambo yasiyo na tija iwe ni katika familia au katika jamii.

94

Uvivu hupelekea ukosefu wa kipato wakati anasa ni matumizi

yasiyo na muhimu na kupita kiasi. Jambo lenye kushangaza na

kusikitisha ni pale ambapo mtu asiye na kipato cha uhakika na

akapata msaada wa kumwezesha kujikwamua katika umaskini,

lakini anaamua kuutumia msaada ule kwenye anasa za ulevi,

ulaji na kununua vitu vya thamani kubwa kuliko mahitaji yake ya

muhimu.

Matumizi ya anasa matokeo yake ni umaskini. Umaskini

ambao haukupaswa kuwepo kabisa, lakini unamkumba mtu

kwa sababu sio kwamba hakupata bali alipata akatumia vibaya,

kwa anasa. Kumbuka kwamba matumizi ya anasa ni kuzalisha

umaskini.

Huu ndio umaskini ambao Bill Gates alisema, “mtu akifa

katika umaskini wa jinsi hii ni makosa ya mhusika”. Umaskini wa

namna hii unaweza kuzuilika kwa utashi na sio kwa misaada.

Tunaweza kuukataa umaskini huu usiendelee kuanzia katika ngazi

ya familia, ngazi ya kitaasisi na ngazi ya kitaifa.

Hitaji Kuu La Viongozi Wa Kizazi Kipya

Ni lazima tukubali kwamba hivi sasa, kwa sababu ya

mmomonyoko wa maadili ya kimani; hata sifa na kanuni za

kuwapata viongozi wenye uwezo stahili navyo vimechakachuliwa

kabisa. Tumejikuta tuko katika mazingira ya kuwa na “bora

viongozi” badala ya “viongozi bora”. Kwa mtindo huu kamwe

hatuwezi kutarajia kwamba “uongozi wa kizazi kinachoinukia”

utakuwa bora iwapo hatukuamua kwa makusudi kurejea

katika kuweka “viongozi bora” ili wawe mwongozo kwa kikazi

kinachoinukia.

Kama ambavyo, kitaifa tuko kwenye mchakato wa

mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kimifumo; bila shaka suala

la uongozi nalo ni lazima lipewe kipaumbele ndani ya katiba,

angalau kwa kuweka sifa na vigezo makini vyenye kuliwezesha

95

taifa kuwapata viongozi bora. Sisi ambao ni kizazi kinachomaliza

muda wake ni lazima tufumbe macho na kuacha kuangalia aina

ya viongozi waliopo sasa hivi kuwa ndio kigezo cha viongozi wa

kizazi kinachoinukia. Tuamue kukinusuru kizazi kipya kwa kuweka

vigezo vya kuwapata viongozi bora, hususan, viongozi wenye

vipaji vya uongozi na kuwanoa mapema ili wapate uzoefu wa

kuongoza kizazi chao kinachoinukia.

Kwa uzoefu wangu binafsi, pamoja na tafiti mbali mbali

zilizofanyika kwa habari ya “aina ya viongozi bora”, kuna ushahidi

kamili kwamba suala la “uongozi bora” linatakiwa kuzingatia

mambo makuu matatu yafuatayo:

1. Kipaji

2. Uzoefu

3. Uadilifu

Kipaji kinawakilisha uwezo wa kuongoza kwa ushawishi

wa nguvu za hoja na hekima ya kufanya maamuzi yenye kuleta

ufumbuzi badala ya kusababisha matatizo makubwa zaidi. Kipaji

cha uongozi kinahitaji mazoezi maalum ili kipate kunolewa kwa njia

mbali mbali ambapo ndipo kigezo cha “uzoefu” kinachukua nafasi

yake. Kimsingi kipaji cha uongozi hujidhihirisha chenyewe ndani

ya mtu na wala hakuhitajiki kazi za “kupiga ramli za kindumba ili

kukitambua”.

Kipaji cha uongozi kikidhihirika ndani ya wahusika, lazima

jamii iwe na mfumo wa kuwawezesha kufanya mazoezi ya

kuongoza ili kigezo cha uzoefu nacho kichukue mkondo wake.

Suala la uadilifu ni matunda ya maadili ya kiimani ambayo ndiyo

mazingira wahusika wamefundwa na kukulia tangu ngazi ya

familia, na imani kwa Mungu na huu ndio msingi wa kuwafanya

kukamilisha sifa za kiuongozi.

Tunapotaka kurithisha maono kwa kizazi kipya, tukija

kwenye suala la uongozi, kipaji, uzoefu na uadilifu ni vitu

96

vinavyotakiwa kuwa mwongozo kwa wanoaji na warithishaji

maono kwa kizazi kipya.

Kwa kuwa shina la uongozi mbovu linatokana na

mmomonyoko wa maadili ya kiimani katika jamii; bila shaka hapa

ndipo mahali pa kuanzia kufanya maandalizi ya viongozi bora.

Kuweka mkazo wa maadili ya kiimani, maadili ya kitaaluma na

maadili ya uongozi.

Malezi ya kimaadili ya kiimani huanzia nyumbani katika

familia. Ni wakati muafaka kwa kanisa kuandaa mipango

ya mafunzo ya kimaadili kwa wazazi ili yawasaidie kuwalea

watoto wao kimaadili. Bila shaka, wazazi wenyewe nao lazima

wanatambua kwamba wajibu wa kulea watoto kimaadili unaanzia

kwao kama wazazi katika kuyashika maadili yenyewe ili wawe

mfano kwa watoto wao.

Wakati huo huo, juhudi zielekezwe katika kuandaa

mitaala ya maadili kwa wanafunzi mashuleni na vyuoni ambapo

watoto watafundishwa somo la maadili, huku kanisa likisimamia

majukumu ya maadili ya kiimani.

Ili tuweze kuona matokeo mazuri lazima tuanze na watoto

na vijana wa kizazi kipya ambao muda si mrefu watakuwa

wanakabiliwa na changamoto za uongozi wa kizazi kinachomaliza

muda wake duniani. Katika vizazi vilivyopita, kila taifa ambalo

liliweka kipaumbele kwa malezi ya kimaadili, limetoa viongozi

bora ambao wameweka rekodi ya uongozi katika historia na

wanakumbukwa mpaka hivi leo.

Mchakato Wa Kuandaa Uongozi Wa Kizazi Kipya

Kama nilivyotangulia kusema hapa juu kuwa suala la

uongozi linahusiana na kipaji, hapa nataka kusisitiza kwamba,

lazima kuwepo kwa mchakato mahsusi wa kuvibaini vipaji vya

uongozi.

97

Kuvibaini Vipawa Vya Uongozi

Ziko nadharia za aina nyingi katika kushughulikia maandalizi

ya viongozi. Nadharia moja inadai kwamba uongozi ni kipawa na

hivyo hakuhitajiki mafunzo ya kitaaluma ya kuandaa kiongozi.

Nadharia ya pili inadai kwamba, uongozi ni taaluma ya kawaida

ambayo kila mtu anatakiwa kupitia mafunzo ili apate ujuzi wa

kuongoza kwa mujibu wa taaluma yenyewe.

Binafsi nimekwisha kuonesha msimamo kwamba, uongozi

ni kipawa. Lakini ili kuweza kubaini kipawa cha uongozi lazima

uwepo mkakati mahususi wenye kutafuta na kugundua kila

mwenye nacho. Kama nilivyokwisha kusema hapo awali, malezi

ya kimaadili kwa vijana wa kizazi kipya lazima yaende sambamba

na kuvibaini vipawa vya uongozi kwa ajili ya kuvitambua na

kutengenezea mazingira ya kutumika kwa wakati muafaka.

Mafunzo Ya Kunoa Vipawa Vya Uongozi

Baada ya kuvibaini vipawa vya uongozi, hatua inayofuata ni

kuandaa mafunzo maalum ya kuvinoa kwa ajili ya matumizi yenye

ufanisi unaozingatia viwango vya ubora. Kuvitambua vipawa

na kuanza kuvitumia bila mafunzo ni kusababisha vituko katika

uongozi. Kipawa kinahitaji kunolewa ili kuweza kuleta matokeo

yanayotarajiwa.

Ile nadharia kwamba kila mtu anaweza kujifunza taaluma

ya uongozi na akaweza kuongoza hata kama hana kipawa, bado

ina upungufu. Tunao viongozi wengine waliopata mafunzo ya

uongozi na wakapewa uongozi lakina wamekuwa si wabunifu,

wala hawana ushawishi kwa wale wanaowaongoza. Lakini

mwenye kipawa cha uongozi akipata mafunzo; ni sawa na upanga

kunolewa ili kuboresha makali yake wakati wa kutumika.

98

Majaribio Ya Uongozi

Baada ya kuvinoa vipawa kimafunzo, ndipo unafika sasa

wakati muafaka wa kuvifanyia majaribio ya uongozi. Kuvifanyia

vipawa majaribio ya uongozi ni pamoja na kuwapa fursa wenye

vipawa kushika nafasi za uongozi kuanzia ngazi za chini na huku

wakitathminiwa jinsi wanavyodhihirisha uwezo na sifa zao kabla

hawajaanza kuonja madaraka makubwa na ya juu katika ngazi za

uongozi.

Mbinu mbali mbali za kufanya majaribio ya uongozi ni

pamoja na kuunda vyama na jumuiya mbali mbali zitakazotoa

fursa za uongozi ili wale wanaojaribiwa wapewe uongozi na kisha

wakionekana wameiva waanze kupewa nafasi zile za kiutendaji

zisizotakiwa kufanya majaribio.

99

Vyanzo Vya Rejea Vilivyotumika

1. Biblia Takatifu

2. BlueBibleLetter.or

3. King James Version Bible

4. Amplified Bible (AMP)

5. Kamusi ya Kiswahili Sanifu

6. https://www.wikipedia.org/

7. The Gift in You (7 Pillars of Thinking designed to discover your

Gift) Dr. Caroline Leaf

8. drleaf.com/blog/perfectly-you-online-program-introduction

9. The Seven Pillars of Thinking with the Copeland’s and Dr.

Caroline Leaf

10. www.biblestudytools.com/kjv

WAPO Mission International Makao Makuu

Mbezi Beach, Barabara Ya Bagamoyo, Jogoo, Dar-es-Salaam

Tovuti: www.wapo.or.tz

S.L.P. 6178 Dar-es-Salaam, Tanzania

100

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!