Views
3 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

SURA YA PILI UCHAMBUZI

SURA YA PILI UCHAMBUZI WA VIPAJI VYA ASILI Utangulizi Kwa kuwa kipaji ni kitu cha asili ya kuzaliwa nacho, kila binadamu katika mfumo wa ubongo amesukwa kufikiri na kutenda kulingana na nguvu za fikra zilizowekwa ndani yake. Kwa hiyo katika kuchambua vipaji tunakwenda kupitia na kujifunza kuhusu uwezo wa asili alionao mwenye kipaji cha asili. Kimsingi, kipaji cha asili ndicho kinachomtofautisha mtu na watu wengine na ndio utambulisho wake kwa wengine katika jamii. Na hii inatokana na taarifa kutoka katika maandiko ya Bibilia pamoja na tafiti za kisayansi ambazo zinathibitisha ukweli huu. Ziko nadharia nyingi zinazofundisha habari ya vipaji vya asili, lakini katika sura hii, tunakwenda kufanya uchambuzi wa aina saba tu za vipaji vya asili ambavyo vimo ndani ya kila binadamu ukiwemo na wewe msomaji wa kitabu hiki. Katika kufanya uchambuzi kuhusu nguvu na uwezo alionao mwenye kipaji husika, pia tutachambua viashira vya ufanisi kwa kila kipaji. Viashiria vya ufanisi ni maeneo maalum ambayo kila kipaji huonesha upekee na umaalum wa ubora kupitia mwenye kipaji husika. Mwisho kabisa, uchambuzi wa vipaji vya asili utabainisha aina mbali mbali za fursa za kitaaluma ambazo mwenye kipaji anaweza kuzimudu kwa viwango vya ubora wake. Vipaji vya asili viko saba kama vilivyoorodheshwa hapa: 12

1. Kipaji cha Ubunifu wa mawazo 2. Kipaji cha Mahusiano 3. Kipaji cha Lugha 4. Kipaji cha Hesabu 5. Kipaji cha Michezo 6. Kipaji cha Muziki 7. Kipaji cha Picha Kumbuka ya kwamba kila binadamu anapozaliwa viashiria vya mambo saba haya ya vipaji vya asili huwa vimo ndani yake. Lakini kuna kipaji kimojawapo ambacho hujitokeza na kuonekana zaidi kuliko vingine na hicho ndicho hutafsiriwa kuwa kipaji cha mhusika. Kwa hiyo, tunakwenda kupitia kwanza nguvu za kimaumbile za kila kipaji, pili, tunachambua viashiria vya ufanisi wa kila kipaji, na tatu, tunaorodhesha aina ya fursa za kitaaluma zinazoambatana na vipaji vya asili kwa wahusika. 13

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
100%
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
GOLDINI