Views
8 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA UBUNIFU 14

Kipaji cha ubunifu kwa lugha ya Kiingereza ni Intrapersonal Intelligence ambacho kimebeba uwezo maalum wa kubuni mambo mapya. Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Ubunifu Mwenye kipaji hiki ni mtu ambaye ana uwezo mkubwa katika kufikiri, kupata na kukusanya mawazo pamoja. Kimaumbile katika mfumo wake wa ubongo seli za fahamu zimesukwa katika hali ya fikra zenye kina, kukusanya mawazo pamoja, kufanya maamuzi yenye mwelekeo, uwezo wa kuchambua katika hali ya uhuru wa hiari. Mwenye kipaji cha ubunifu pia anao uwezo mkubwa wa kujitathmini na kujifahamu kibinafsi kuanzia mawazo, hisia na utambuzi wa ndani. Kana kwamba hii haitoshi, mwenye kipaji cha ubunifu ana uwezo mkubwa wa kuiongoza tabia binafsi, kujua nguvu na udhaifu binafsi, kubuni fikira mpya, kupanga shughuli na kutatua matatizo. Viashiria Vya Ufanisi Wa Kipaji Cha Ubunifu Kila mwenye kipaji cha ubunifu atajulikana na kutambulika kwenye maeneo yake ya ufanisi unatokana na nguvu za kipaji chake. Baadhi ya maeneo ya ufanisi wa kipaji cha ubunifu ni pamoja na: • Utambuzi wa viwango vya hisia binafsi • Uwezo wa kujitawala na kufanyia kazi mawazo na hisia binafsi • Njia nyepesi za kueleza mawazo binafsi • Hamasa ya kubaini na kutekeleza malengo • Ufanisi wa kazi uwapo huru mwenyewe na peke yako 15

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
100%
Finding The Pleasure Free Ebook
GOLDINI
100% Digital
100-ideeënboek