Views
9 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Kipaji cha uhusiano kwa

Kipaji cha uhusiano kwa lugha ya Kiingereza ni Interpersonal Intelligence ambacho kimebeba uwezo maalum wa kutengeneza na kudumisha mahusiano. Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Uhusiano Kimauimbile, mtu mwenye kipaji cha uhusiano, katika mfumo wa ubongo wake anazo seli za neva zenye kumwezesha kutengeneza mawasiliano na wengine. Anao uwezo mkubwa wa mwingiliano wa kijamii, usikivu, ushirikishaji, kujenga mahusiano, utoaji na uwezo wa kuelewa na kufanya kazi vizuri na watu. Mtu mwenye kipaji cha uhusiano ni mwepesi na mwenye ukaribu wa kuchukuliana na watu na ushiriki wa kihisia wa mambo wanayopitia. Hii ni pamoja na uwezo wa kutawala, kusuluhisha, kuhamasisha, kuongoza, kuelekeza na kushauri wengine. Viashiria Vya Ufanisi Wa Kipaji Cha Uhusiano Mwenye kipaji cha uhusiano hutambulika kwa viashiria vya uhusiano ambavyo ni pamoja na: • Nguvu za kuongoza • Ufanisi katika kujenga mtandao na wengine • Uwezo wa kujadiliana, kujenga hoja za utetezi na mzuri katika usuluhishi • Uwezo wa kuongea na kupangilia mambo • Kufurahia kuwa mlezi wa vipaji vya wengine • Uwezo wa kutanguliza wengine • Uwezo wa kuhisi na kutambua hisia, hulka, tabia na matarajio ya wengine • Uwezo wa kushawishi wengine • Ufanisi katika kufanya kazi na kundi, juhudi za pamoja katika kikundi na utendaji wa pamoja • Uwezo wa kuunganisha watu wakawa wamoja • Uwezo wa kujenga mahusiano ya kijamii ya kudumu 18

Fursa Za Kitaaluma Kipaji cha uhusiano kina fursa nyingi za kitaaluma ambazo mhusika anaweza kuonesha ufanisi wa kitaaluma. Baadhi ya fursa za kitaaluma ni pamoja na hizi zifuatazo: • Mwanasiasa • Kiongozi wa dini • Muuzaji • Mkufunzi • Mshauri • Mtaalamu wa sayansi ya jamii • Msemaji/Mtalaamu wa lugha • Mtaalamu wa kijamii • Mtaalamu wa saiklojia • Afisa mahusiano • Mkurugenzi wa rasilimali watu • Meneja • Mhamasishaji 19

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
100%
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
GOLDINI
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet