Views
8 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA

UCHAMBUZI WA KIPAJI CHA LUGHA 20

Kipaji cha lugha kwa lugha ya Kiingereza ni Linguistic Thinking ambacho kimebeba uwezo maalum wa umahili katika lugha. Nguvu Za Asili Za Kipaji Cha Lugha Kimauimbile mtu mwenye kipaji cha lugha, katika mfumo wa ubongo wake anazo seli za neva zinazojenga umahili wa lugha na umakini wa maana za maneno, sauti, mahadhi pamoja na matumizi tofauti ya lugha mbali mbali. Uwezo wa kufikiri kwa njia ya maneno na kutumia maneno kwa ufasaha katika kuongea na kuandika. Pia mwenye kipaji cha lugha huwa ni mwepesi wa kujifunza mifumo na miundo ya lugha na matumizi yake. Viashiria Vya Ufanisi Wa Kipaji Cha Lugha • Huhitaji kujieleza kibinafsi kwa kuandika au kutumia maneno mengi • Hupenda kulumbana, kuhoji, kuburudisha na kuelekeza • Hupenda kuandika, kucheza na maneno, kusoma na kusimulia visa na hadithi • Huwa na kiwango kizuri cha elimu ya jumla • Huuliza maswali mengi • Hupenda kuongoza/kushiriki katika mijadala • Hupendelea mbao za kuandikia, vifaa vya kutunza maneno, na vifaa vya kunakili maneno • Utamkaji vizuri wa maneno • Kujifunza lugha kwa urahisi • Huwa na kumbukumbu nzuri ya majina, tarehe, na majina ya maeneo 21