Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Mara nyingi msukumo wa

Mara nyingi msukumo wa kupenda au kuchagua kufanya mambo fulani ambayo unayamudu vizuri kuliko wengine hutokana na nguvu za vipaji vya asili vilivyomo katika nafsi zetu. 2. Jambo Gani Unalipenda Sana? Swali hili ni kwa kila mtu. Jambo gani unalipenda sana. Tafadhali zingatia, kupenda kunakotajwa hapa ni mvuto wa hisia za ndani za kutamani kufanya jambo fulani hata kama hutapata malipo yoyote. Tena wakati mwingine wewe ndio uko tayari kulipia gharama za kufanya jambo unalolipenda sana badala ya wewe kulipwa. Haya tuseme leo ni jumamosi ambapo si siku ya kazi. Una muda ambao ni huru wa kufanya jambo unalolipenda. Pengine ni kupiga gitaa au kinanda au kuandika riwaya au jambo jingine lolote (lakini isiwe kutazama tv na tamthilia). Hili jambo ambalo umeamua kulifanya, kila mara unapolifanya, linakuvuta kweli kweli. Akili zote, mwili na hisia na utambuzi wa ndani vinajikuta vikilifanya kwa ukamilifu na kwa kunogewa hasa. Unazama katika kufanya jambo hilo mpaka unasahau ni saa ngapi, na hata unasahu muda wa kula. Haya, fikiria kazi unayoifanya katika siku za kawaida za kazi, kama ungeifanya katika msukumo na mvuto na mzamo kama ulivyozama kwenye jambo hili la Jumamosi huru, ufanisi wako ungelikuwaje kazini? Nakwambia watu wengi wanafanya kazi kwa sababu ya malipo ya mshahara lakini sio kwamba wanafanya kwa msukumo wa vipaji vya asili. Ndiyo maana kufanya kazi ambazo haziendani na vipaji vya asili hakuleti ufanisi mkubwa na maendeleo yake ni duni. 36

Lakini kama mtu akifanya kazi ambayo inaendana na kipaji chake, hataangalia saa ya kumaliza kazi bali anavutwa kufanikisha kazi ile ifikie viwango vya ubora stahiki na hiyo ndiyo inayomfanya ajitume kufanya vema kuliko wengine. Pasipo kujali mazingira uliyomo hivi sasa, na mambo unayoyafanya kwa sababu ya desturi tu, hebu tafakari ni jambo gani ambalo una msukumo wa ndani unaokushuhudia kuwa ukilifanya utalimudu vizuri bila kutumia nguvu nyingi na utafanya kwa viwango vya ubora tofauti na wengine? Inawezekana jambo hilo ni tofauti kabisa na shughuli unayoifanya hivi sasa ambayo pengine ndiyo inayokupatia riziki. Au pengine bado ni mwanafunzi lakini masomo unayochukua hayaendani na jambo lile unalolitamani sana kulifanya na ukipewa fursa utalimudu vizuri kuliko hata masomo unayochukua hivi sasa. Kama unahusika katika eneo hili, ujue kwamba unakabiliwa na changamoto ya mgongano wa kimaslahi kati ya kipaji cha asili na mambo unayoyafanya hivi sasa yanayokupatia riziki au msaada wa kimaisha. Unahitaji hekima ya Mungu katika kuyaweka kwenye mizania sawa. Ushauri wangu hapa ni kwamba wakati wa muda wako wa ziada ambapo hauko kazini au masomoni, wakati umekamilisha majukumu yako ya kila siku kwa mujibu wa mkataba, tumia muda wa ziada katika kufanyia mazoezi hilo jambo ambalo una msukumo nalo. Kama ni mwanafunzi omba ushauri kwa wazazi/walezi na walimu kuhusu msukumo uliomo ndani yako na jinsi unavyofikiria kama ungepewa fursa ya kufanya jambo hilo ungetimiza ndoto yako kuhusu hatma yako. Kama ni mfanyakazi uliyeajiriwa au mjasiliamali unayejitegemea, hakikisha unajipanga vizuri kuhusu jinsi 37

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
100%
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
GOLDINI