Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Mwenye kipaji cha asili

Mwenye kipaji cha asili katika uongozi uwe wa kisiasa au kikanisa, hatumii nguvu kubwa kujinadi wala hatumii hila na ujanja wa kujitangaza kwa vyeo akidhani vyeo ndio umaarufu. Mwenye kipaji hujikuta akiwa maarufu kutokana na ushawishi alionao wa kusikilizwa na kufuatwa na wengi kwa sababu ya mvuto wa kipaji uliomo ndani yake. 2. Wivu Wa Kuharibu Mafanikio Ya Wengine Kuna kundi jingine la watu wenye wivu wa kutokufurahia mafanikio ya watu wengine. Kundi hili hujiona kwa kuwa lenyewe bado halijafanikiwa, basi hakuna haki kwa wengine kufanikiwa, na kama wakifanikiwa basi mafanikio yao kwa mtazamo wao wanayahesabu si halali. Katika msukumo wa wivu, watu hawa hujikuta wakitumia kila njia za kuzuia, kukwamisha, na hata kuharibu mafanikio ya watu wengine, na wanatafsiri kuwa hivyo ndivyo vipaji vyao vya asili! Hakuna vipaji vya kupambana na kuweka vikwazo vya kuharibu mafanikio ya wengine. Mwenye kipaji cha asili, hasumbuliwi na wivu dhidi ya mafanikio ya wengine. Badala yake hufurahia na kusifia mafanikio ya wengine na hata kujifunza mbinu za kufanikiwa kama wao ikiwa atapewa fursa hiyo. Mwenye kipaji anaweza kutumia kipaji chake kufanikisha mambo ya wengine ili mradi tu apate uzoefu kabla ya kuanza kufanya mambo yake mwenyewe. 3. Wizi Wa Mawazo Ya Wengine Kundi jingine la kujihadhari nalo ni lile la wenye tamaa ya kuiba mawazo ya wengine kwa kudhani watakuwa maarufu kama wenye maono waliyodokoa bila ridhaa ya wahusika. Kundi hili linajulkana kama “copy cats”. 40

Tamaa hii inafanana kidogo na ile ya kutafuta umaarufu kwa sababu ya utajiri wa haraka haraka. Ila tamaa ya jinsi hii hujikita katika kutafuta kupeleleza na kudokoa au kuiba mawazo ya wale wanaoonekana kufanikiwa ili na wao wafanikiwe kama wale wenye maono halisi. Kwa kiasi fulani wanaweza kufanikiwa ila hawafikii viwango vya ubora wa maono yale waliyoiba kwa wengine. Kuiba mawazo ya wengine sio kipaji cha asili. Huu ni wizi wa kawaida hata kama hakuna ushahidi wa kukamatwa kwa wenye tabia hizi. Ngazi Za Ukuaji Na Utendaji Wa Vipaji Vya Asili Utangulizi Baada ya kuchambua aina za vipaji vya asili na jinsi vinavyotenda kazi, sasa tunakuja kwenye ngazi au hatua za kutenda kazi kuanzia umri mdogo mpaka uzeeni. Tumejifunza katika sura ya kwanza ya kuwa vipaji vya asili ni vipaji vya kuzaliwa navyo kibaiolojia na kisaikolojia. Hii ikimaanisha ya kwamba vipaji huanza tangu mtu anapotungwa mimba katika tumbo la mama yake. Jambo jingine la kujikumbusha ni kwamba kila binadamu huumbwa na kipaji cha asili ambacho ndicho humtofautisha na binadamu wengine katika jamii. Hivyo ndivyo Mungu alivyomkusudia kila binadamu atakayezaliwa na kuishi duniani. Tunasoma ngazi za ukuaji wa kipaji cha mtu katika maandiko yafuatayo: “Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha; mkatawale...” (Mwa.1:28) 41