Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

2. Ngazi Ya Uzalishaji

2. Ngazi Ya Uzalishaji Neno la pili katika ngazi za utendaji wa vipaji lilikuwa ni “mkaongezeke”. Neno hili ndilo linatuleta katika ngazi ya pili ya “uzalishaji”. Katika ngazi hii, mtoto ameondoka katika ngazi ya utoto wa kuwa tegemezi anaanza kuyatendea kazi mawazo yake mapya ambayo tayari amekwisha kuyajaribu na kupata mwelekeo wa ni nini anatakiwa kuwekeza nguvu zake zote katika uzalishaji wa kile ambacho ni kipaji chake cha asili. Katika ngazi ya uzalishaji, muhusika anatarajiwa kuwa amefikia umri wa miaka 25 na ataendelea katika nguvu za kuzalisha mpaka miaka 45. Hii inaitwa ngazi ya uzalishaji kwa sababu ndio wakati kwa mwenye kipaji anapokuwa amewekeza nguvu zake katika vipaumbele vya mambo ambayo alikwisha kuyajaribu yakaonesha mafanikio, au yakadhihirisha uwezo alio nao wa kufikia viwango vyake vya ubora. Na ndio wakati ambapo kipaji chake kinaanza kumpatia mhusika matunda au malipo stahiki. Ndio wakati wa kufanya mikataba ya malipo au kuendesha huduma za kujitegemea na kutengeneza ajira kwa wengine. 3. Ngazi Ya Usimamizi Usimamizi ni ngazi ya tatu katika kukuza na kutendea kazi vipaji vya asili. Usimamizi unaotamkwa hapa ni uzoefu unaofikia hekima na busara ya kuanza kuweka akiba na kutunza mali na fedha zilizokwisha kupatikana kutokana na uzalishaji mzito uliotangulia katika ile hatua ya pili. Umri wenyewe ambao ni kuanzia miaka 45 hadi kufikia miaka 55 ndipo akili za wenye vipaji hupata msukumo wa kutunza kile kinachozalishwa kupitia vipaji na taaluma zao huku wakihisi nguvu za mwili zinaanza kupungua. 44

Aidha, hii ndiyo hatua ambayo wenye vipaji wenye hekima wanapoanza kupunguza majukumu na kukaimisha au kunaibisha kwa wale wanaotarajia kuwarithisha majukumu ya kiuchumi na kiuongozi. Na ndio wakati huu ambapo kizazi kipya cha umri wa miaka 25 kinapojaribiwa katika kubeba baadhi ya majukumu ili kunoa vipaji vyao vya asili katika uzalishaji na uongozi pia. Mwasisi aliyekuwa ndiye Mtendaji Mkuu wa kampuni au taasisi ya huduma hupunguza majukumu na kuyagawa kwa walioko chini yake ambao anawaandaa kushika hatamu badala yake. Lile neno “kutiisha” katika Biblia kwa kiingereza linaitwa “replenish” likimaanisha kujaza tena, au kuziba utupu uliokuwepo mahali. Katika usimamizi wa vipaji, kutiisha ni kuongeza nguvu mahali ambapo nguvu zilianza kupungua katika uzalishaji. Ni kuongeza nguvu katika usimamizi wa vilivyokwisha kuzalishwa ili vidumu na kuendelea kusaidia kizazi kinachoinukia. 4. Ngazi Ya Urithishaji Urithishaji ndio hatua ya nne na ya mwisho katika kukuza na kutendea kazi vipaji vya asili. Nitaelezea kwa kina kipengele hiki katika Sura ya Nne kwa sababu kinawahusu zaidi warithishaji kuliko warithishwaji. Hata hivyo, kwa muktadha wa hatua za ukuaji na utendaji wa vipaji vya asili, hatua hii ndiyo ya juu na mwisho kwa wote wenye umri kuanzia miaka 55-65. Hiki ndicho kizazi kinachotakiwa kustaafu na kukabidhi majukumu ya uzalishaji na uongozi kwa kizazi kipya. Lakini ni muhimu kutambua kuwa kukabidhi sio kususa au kukimbia majukumu ghafla, eti kwa sababu ya uzee. Kukabidhi 45

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
100%
Finding The Pleasure Free Ebook
GOLDINI