Views
3 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

lazima kuwe ni mchakato

lazima kuwe ni mchakato wa taratibu na wenye kukabidhi wanabaki kutoa ushauri elekezi kwa waliowarithisha. 46

SURA TA TATU CHANGAMOTO ZINAZOATHIRI VIPAJI VYA ASILI Utangulizi Baada ya kujifunza utajiri mkubwa uliomo katika vipaji vya asili na michakato ya kuvikuza, maswali makubwa yanakuja akilini na kuhoji kama kweli kila binadamu huzaliwa na kipaji cha kumwinua na kumfanikisha kwa viwango vya ubora wa hali ya juu, je, kwanini sasa hatuvioni vipaji hivi vikifanya kazi kwa kila mtu katika jamii? Kwanini ni watu wachache sana ambao ndio wanatokea kuwa maarufu kupitia vipaji vya asili? Katika kusaidia kupatikana kwa majibu ya maswali haya na mengine yenye kufanana na haya, ndiyo maana sura hii imeandaliwa ili kufanya uchambuzi makini kuhusu changamoto zenye kuathiri vipaji vya asili, tukianza na kipengele cha vikwazo vya maendeleo ya vipaji na karama. Changamoto maana yake ni mambo yanayojitokeza kinyume na maendeleo ya mtu. Hata hivyo, changamoto ni sehemu ya maisha ya kila mtu na ndiyo maana maisha hutafsiriwa kuwa ni “mapambano” dhidi ya “changamoto”. Sasa tunapokuja katika suala la vipaji, napo zipo changamoto ambazo kusudi lake kama sio kuharibu kabisa, basi ni kudhoofisha utendaji wa vipaji ndani ya wahusika. Kwa hiyo ndiyo maana ni vema kuzifahamu, na kisha kupata mbinu za kupambana nazo kikamilifu. Changamoto zenyewe zimegawanyika katika sehemu kuu mbili. 47