Views
8 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Sehemu ya kwanza ni

Sehemu ya kwanza ni “changamoto za nje” kwa maana ya mambo hasi yanayomzunguka kila mtu ili kudhoofisha kipaji chake. Pili, ni “changamoto za ndani” ambazo ni mambo hasi ya ndani yanayomwathiri kila mtu binafsi kitabia. Hebu tuanze kuchambua baadhi ya hizo changamoto za nje. Changamoto Za Nje Katika ulimwengu tunamoishi tumezungukwa na mambo hasi mengi yaliyoko kinyume nasi ambayo ni lazima tupambane nayo ikiwa kweli tunataka kuendeleza vipaji vyetu kama Mungu alivyotukusudia. Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na: 1. Marafiki Wabaya Binadamu ameumbwa na hulka ya ushirika na binadamu wengine. Katika hulka hizo, kuna binadamu wanakuwa na ushirika wa karibu zaidi kuliko binadamu wengine. Na ndipo msamiati wa neno urafiki unapoanzia. Katika harakati za kutambua na kukuza vipaji mbali mbali lazima kuwepo kwa ushirikiano na watu wengine hususan wenye vipaji vinavyoshabihiana. Ni katika harakati za kutafuta kukuza na kutumia kukuza vipaji ndipo mtu hujenga ukaribu na watu wapya ambao huwa marafiki. Tafsiri Ya Marafiki Wabaya Tafsiri ya msamiati wa neno rafiki maana yake ni “mtu anayependana na kuaminiana na mwingine; sahibu, mwandani, bui, somo, na mbasi.” Maneno muhimu ya tafsiri ya urafiki ni “kupendana” na “kuaminiana.” Lakini kwa muktadha wa kipengele hiki, ni muhimu kufahamu kuna “marafiki wema” na “marafiki wabaya.” Kuwa na marafiki wabaya maana yake ni “kupendana na kuaminiana na marafiki wabaya” 48

Aina Za Marafiki Wabaya Kwa mujibu wa maandiko matakatifu, “marafiki wabaya” wamegawanyika katika makundi mbali mbali ambayo ni kama haya yafuatayo: “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; wala hakusimama katika njia ya wakosaji; wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, uzaao matunda yake kwa majira yake, wala jani lake halikauki; na kila alitendalo litafanikiwa. Sivyo walivyo wasio haki; hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwa hiyo, wasio haki hawatasimama hukumuni, wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, bali njia ya wasio haki itapotea.” (Zab. 1:3-6) Katika maandiko haya tunasoma kuhusu “shauri la wasio haki”, “njia ya wakosaji” na “baraza la wenye mizaha”. Kupitia maneno haya ndipo tunayapata makundi ya aina tatu ya “marafiki wabaya”. Kundi la kwanza la marafiki wabaya ni “wasio haki” ambao tafsiri yake ni “watu waovu au wahalifu”. Na maana ya “kutokwenda katika shauri la wasio haki” maana yake ni kutokupokea na kutendea kazi “ushauri wa waovu au wahalifu.” Kundi la pili la “marafiki wabaya” ni “wakosaji” ambao tafsiri yake ni watu “watenda dhambi” au “wasio na maadili ya kimungu”. Makatazo ya “kutokusimama katika njia ya wakosaji” tafsiri yake ni “kujitenga na vitendo vya dhambi za hao “watenda dhambi”. Kundi la tatu la “marafiki wabaya” ni la watu “wenye mizaha” ambao maana yake ni “watu wenye maneno ya dhihaka, 49

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
Valentine_s_Day_Anthology_2015
100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 ...
Andy! Oxidation paintings by Mambo - Paetau, Kristofer
Chapter 78
TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
Tanzania Breweries Limited Annual Report and ... - SABMiller
BE-100-6_Quran_and_World_Peace
TOP 100