Views
8 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

kejeli, na dharau, dhidi

kejeli, na dharau, dhidi ya itikadi za watu wengine”. Maandiko yanamkataza mchaji Mungu kutojumuika na makundi ya watu wenye “kudhihaki” na “kukejeli” itikadi za wengine. Athari Za Marafiki Wabaya Muktadha wa “marafiki wabaya” unalenga watu wenye tabia mbaya wanapokuwa na ushawishi wa kuvutia kwa “watu wema” hata wakajenga urafiki baina yao. Biblia ndiyo imeandika habari za kutahadharisha “watu wema” kujihadhari katika kujenga ushirika wa kirafiki na watu wabaya ambao huathiri vibaya tabia njema: “Msidanganyike; mazungumuzo mabaya huharibu tabia njema.” (1 Kor. 15:33) “Do not be deceived: [a] Bad company corrupts good morals.” Maandiko haya hapo juu yanashuhudia jinsi ambavyo marafiki wabaya wanavyoweza kuathiri tabia njema za wachaji Mungu. Marafiki wabaya sio tu hauthiri tabia njema za watu wema, lakini pia huathiri utendaji wa vipaji vya asili vya watu wema. Pale mtu mwenye kutaka kunoa kipaji chake anaposhirikiana na marafiki wabaya, urafiki huo husababisha kukwamisha juhudi za kutumia kipaji chake kwa viwango vyake vya ubora, maana hata yeye huharibika. Kutokana na kuwa na marafiki wabaya, kuna vipaji vingi vimeathiriwa kwa sababu ya wahusika nao kuharibika kitabia. 2. Imani za uchawi na ushirikina Uchawi na ushirikina ni changamoto inayoongoza katika kudhoofisha utendaji bora wa vipaji vya asili. Tafsiri ya ‘uchawi’ 50

maana yake ni ufundi wa kutumia dawa au vitabu maalum vya uganga ili kuleta madhara kwa viumbe; na maana nyingine ni ‘vifaa vinavyotumika katika shughuli za kurogea’. Utafiti uliofanyika umeonesha dhahiri ya kwamba imani za uchawi na ushirikina ni kikwazo kikubwa sana kwa maendeleo ya vipaji vya asili. Pamoja na kwamba Biblia imekataza watu kushiriki katika vitendo vya uchawi na ushirikina, lakini bado vitendo hivyo vimekuwa vikiongoza katika kuvuta watu wengi wakidhani wanakwenda kupata nguvu za kunoa vipaji kumbe wanajikuta wanapokea nguvu za kukwamisha na kuharibu vipaji vyao. Ndiyo maana maandiko matakatifu yalikataza na kupiga marufuku ushiriki wa vitendo vya uchawi na ushirikina kama ilivyoandikwa hapa chini: “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA, Mungu wako, anawafukuza mbele yako”(Kumb. 18:10-12) Ni miaka miwili iliyopita tangu Tanzania ilipotangazwa kushika nafasi ya kwanza kwa umahiri wa kuamini katika uchawi kimataifa. Mojawapo ya taasisi zilizoitangaza Tanzania kwamba imekithiri kwa mambo ya uchawi ni Pew Research lenye makao yake Washington DC nchini Marekani. Kwa mujibu wa taarifa zake inasadikiwa kwamba miongoni mwa nchi 19 za kusini mwa Jangwa la Sahara zilizofanyiwa utafiti, Tanzania iliongoza kwa kuwa na idadi ya watanzania 93% wanaoamini katika uchawi na ushirikina. 51

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
100%
SACCOS_Traing_Guide
Finding The Pleasure Free Ebook
GOLDINI
100-ideeënboek
100% Digital
ÉNERGIE 100