Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Aidha, inasadikiwa pia

Aidha, inasadikiwa pia ya kuwa vitendo vya uchawi vinavyoongoza Tanzania ni pamoja na juju, utoaji wa kafara kwa mizimu kwa ajili ya bahati za kupata vyeo, utajiri na umaarufu katika michezo na muziki. Sasa basi, katika mazingira kama haya, tunaweza kuona jinsi ushirikina na uchawi vinavyodhoofisha vipaji vya asili kwa sababu ya wahusika kutegemea ndumba badala ya kutambua na kunoa vipaji vijiendeshe vyenyewe. 3. Mifumo Butu Ya Elimu Mifumo butu ya elimu ni “mitaala ya elimu isiyolenga kunoa vipaji vya wanafunzi.” Pamoja na kwamba elimu inayotolewa kweli inawapatia wanafunzi maarifa ya kawaida ya kujua kusoma na kuandika pamoja na ujuzi katika masomo mengineyo; changamoto kubwa ni pale ambapo wahitimu wengi hawana uwezo wa kujitegemea kiuchumi pasipo fursa ya ajira. Wakati kipaji kinamjengea mtoto uwezo wa kubuni na ustadi wa kazi atakayoimiliki mwenyewe; elimu bado ni butu kwa kuwa haimwezeshi mtoto kutambua na kunoa kipaji chake ambacho akihitimu kitamwezesha kujitegemea moja kwa moja. Elimu ya sasa inamfanya mwanafunzi akihitimu awazie kutafuta ajira peke yake, badala ya kubuni na kusimamia kazi yake mwenyewe. Ndiyo maana changamoto ya ukosefu wa ajira itaendelea kuwepo kwa muda mrefu kwa sababu uzalishaji wa wahitimu hauendani na fursa za ajira zilizopo katika jamii. Ufumbuzi kamili wa tatizo la ukosefu wa ajira ni lazima uanzie kwenye mitaala ya elimu ambayo italenga kuibua na kunoa vipaji vya watoto ili wanapohitimu wanakuwa na ujuzi kubuni kazi zao wenyewe na kujitegemea kiuchumi badala ya kutegemea ajira. 52

Athari Za Utandawazi Dhidi Ya Vipaji Vya Asili Tafsiri Ya Utandawazi “Mfumo wa uhusiano wa kimataifa katika nyanja mbali mbali kama vile biashara, uchumi au siasa uliowezeshwa na maendeleo ya teknolojia ya habari yanayofanya mataifa kuwasiliana kwa urahisi.” (Kamusi Ya Kiswahili Sanifu). Nguvu Za Mitandao Ya Kijamii Miaka ya hivi karibu, mitandao ya kijamii imekuwa na ushawishi mkubwa kiulimwengu kwa kiasi ambacho kasi yake ni tishio kwa maadili ya kizazi kipya. Katika mwaka 2017 kiwango cha ushawishi wa mitandao ya kijamii kimepanda kwa viwango vifuatavyo: • Facebook hivi sasa ina watumiaji zaidi ya milioni 900 • 50% ya ulimwengu mzima iko chini ya umri wa miaka 50 • 96% ya umri kuanzia miaka 18-35 wako ni watumiaji wa mitandao ya kijamii • Kama facebook ingekuwa ni nchi, ingeshika nafasi ya tatu kwa ukubwa ulimwenguni • Mtumiaji wa kawaida wa facebook ana marafiki 130 • Youtube ni ya pili kwa mtandao mkubwa ulimwenguni • Twitter nayo immeshafikia watumiani milioni 500 • Kama Twitter ingelikuwa ni nchi ingekuwa ya 12 kwa ukubwa duniani. Kuna watu 750 wanao-twiti kila nukta. • Kuna wenye kurasa (blogs) zaidi ya milioni 200 • Kuna kurasa mpya mlioni 3 zinazofunguliwa kwenye internet kila mwezi • Kuna picha milioni 5 zinazorushwa kwenye instagram kila siku • Watu zaidi ya bilioni 6.9 wamekwisha kutazama Youtube channel 53