Views
6 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Kamusi ya Kiswahili

Kamusi ya Kiswahili Sanifu imelitafsiri neno “sugu” kuwa ni “hali isiyoweza kuondolewa kwa urahisi”. Usemi “tabia sugu” haumo katika kamusi kama msamiati; isipokuwa mimi nimeyaunganisha maneno mawili, “tabia” na “sugu” na kupata usemi maalum wa “tabia sugu”. Kwa hiyo kama ukiunganisha tafsiri za maneno “tabia” na “sugu” unapata maana ya usemi wetu wa “tabia sugu”ambao tafsiri yake ni: “mazoea yatokanayo na kurudiarudia hali, mwenendo au matendo isiyoweza kuondolewa kwa urahisi”. Maeneo Ya Uharibifu Wa Tabia Sugu Uharibifu Wa Kitabia Sehemu ya kwanza ya madhara ya tabia sugu ni uharibifu wa kitabia unaolenga kuharibu “utu”, “ubinadamu” na “uungwana” katika maisha ya mwathirika. Pengine ni vizuri tukaangalia misamiati ya maneno haya ya “utu”, “ubinadamu” na “uungwana” ili tujue maana zake: Neno “utu” limetafsiriwa kuwa ni: “hali ya kuwa na tabia zinazolingana na hadhi ya mtu”. Neno “ubindamu” limetafsiriwa kuwa ni: “hali ya utambuzi wa jinsi ya kutekeleza wajibu juu ya maisha katika jamii”. Neno “uungwana” limetafsiriwa kuwa ni: “mtu mwenye adabu na tabia zinazokubalika katika jamii”. Baada ya kupata tafsiri ya misamiati hapo juu tunaweza kuona kwamba madhara mabaya ya “tabia sugu” kwa mhusika ni: kumharibia (utu); ambao ni hadhi yake kama mtu; kumharibia (ubinadamu wake) ambao ni hali ya utambuzi wa kutekeleza wajibu wake kwa jamii; kumharibia (uungwana) ambao ni adabu na kumfanya kutokukubalika kitabia katika jamii. Haya ndiyo madhara ya “tabia sugu” ambayo kimsingi, ndiyo yenye kukwamisha utendaji wa vipaji ndani ya walio navyo, na kukwama kufikia viwango vya mafanikio kulinganana vipaji vyao. 56

Hata hivyo, ashukuriwe Mungu kupitia Bwana Yesu Kristo ambaye kwa neema yake ametoa ufumbuzi wa kupambana na kukomesha madhara ya tabia sugu, ikiwa masharti na kanuni zitazingatiwa: “Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa TABIA YA UUNGU mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (1 Pet. 1:4) Mungu ameahidi, kupitia Yesu Kristo, waathirika wa tabia sugu, wanaweza kubadilika, na kunusurika na uharibifu wa dunia hii unaosababishwa na tamaa na kwa kubadilika kitabia na kuwa wachaji Mungu na raia wema katika jamii. Uharibifu Wa Kiafya Kudhoofisha mishipa inayosafirisha damu moyoni, uharibu wa mfumo wa neva, ambao huanzia katika kudhoofisha uwezo wa kufikiri na hatimaye kuishia kuwa zezeta; saratani ya damu; shinikizo la damu na maradhi ya moyo; maradhi ya mtoto wa jicho; saratani ya mlango wa kizazi; saratani ya figo; saratani ya kongosho; saratani ya tumbo; maradhi ya uasherati na zinaa na VVU/UKIMWI. Uharibifu Wa Kifamilia Uharibifu wa kifamilia utokanao na tabia sugu ni pamoja na: Migororo sugu katika ndoa; ugumba na utasa (utoaji mimba/ madawa ya kuzuia mimba); wanandoa kutelekezana/kuvunjika kwa ndoa; malezi mabovu kwa watoto; ongezeko la watoto wa mitaani. 57

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
100%
100€
Das Weihnachtsevangelium
Professional Photography Heber City
View the Annual report PDF (4.67Mb) - SABMiller
Download N.S.E Announcement - Nairobi Stock Exchange
Financial Statements 2011 - Investing In Africa