Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Huharibu Mahusiano Na

Huharibu Mahusiano Na Wengine Mara nyingi, mwathirika wa “tabia sugu ya kulalamika na kuhukumu wengine” huwa hana marafiki wengi. Na hata akiwapata hawadumu pamoja naye kwa muda mrefu. Hata wale wachache anaobaki nao hugombana nao mara kwa mara. Tena baadhi ya hao marafiki wachache nao pia huwa ni waathirika wa tabia sugu hiyo hiyo ya kulalamika na kuhukumu wengine kama yeye. Katika mazingira ya kuwa na marafiki wachache, au kukimbiwa na marafiki, hali hii husababisha vipaji vya mwathirika kutokuwafikia na kuwahudumia walengwa wa vipaji vyake. Maana mwathirika wa “tabia sugu ya kulalamika na kuhukumu wengine” anaweza kuwa na kipaji kizuri sana lakini kimeathiriwa na hulka yake. Kila anapokitumia kinakuwa kama chakula kitamu lakini chenye pilipili kupita kiasi. Kila anayekula lazima pua zitalowa kwa mafua na macho kutoka machozi mengi. Kwenda Kinyume Na Makatazo Ya Yesu Kristo Yesu Kristo mwenyewe pamoja na kwamba alikuwa mkali katika kukosoa mitazamo hasi ya jamii ya Mafarisayo na Masadukayo; bado alipiga marufuku kwa wanafunzi wake kuendekeza tabia ya kulalamika na kuhukumu wengine: “Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa.” (Luk. 6:37) Makatazo ya Yesu kuhusu tabia ya kulaumu na kuhukumu kunadhirisha matokeo ya tabia hiyo kuwa inaambatana na malipizo yake. Unapomlaumu na kumhukumu mtu mwingine na kumsababishia maumivu pamoja na madhara, maana yake wewe pia tarajia kupatwa na lawama na hukumu zitakazokusababishia maumivu na madhara kama ulivyowafanyia wengine. Hii ni kanuni ya kiroho na inafanya kazi chini ya udhibiti wa Mungu mwenyewe. 62

Kana kwamba hii haikutosha, Yesu alitoa sababu ya msingi ya kutokulaumu na kuhukumu wengine kwa sababu mwenye kufanya hivyo kwa wengine pengine ana makosa kama wao au zaidi ya hao anaowakosoa. “Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Basi mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii. Au utamwambiaje nduguyo, niache nitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.” (Mat. 7:1-5) Katika maandiko haya, Yesu anaonesha udhaifu wa tabia ya kuhukumu wengine pasipo kujitathmini binafsi kama hatuna makosa yale yale au yenye kufanana na ya wale tunaowahukumu. Aidha, Yesu anatafsiri kuwa ni unafiki mtupu kuwa na tabia ya kulalamika na kulaumu wengine wakati mhusika naye ana madhambi yake mwenyewe. Na kisha Yesu akaagiza kwamba badala ya kutumia nguvu kubwa kutuhumu na kuhukumu wengine, tumia fursa hiyo kujichunguza na kujirekebisha kwanza kisha ndipo utakuwa na uzoefu wa kukosoa wengine. Tena kuna mahali pengine ambapo Yesu alitoa mwongozo pale ambapo kunatokea kutokuelewana au kukoseana ambapo hatua stahiki ni kukutana wahusika peke yao na kujaribu kusuluhishana. Na pale inaposhindikana basi kesi hiyo iwasilishwe kwenye ngazi ya juu, hatua kwa hatua mpaka muafaka upatikane. 63

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
100%
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook
GOLDINI
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet