Views
4 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

ni: “mwanandoa

ni: “mwanandoa anapojamiiana na mtu/watu wengine nje ya mwanandoa mwenziwe”. Kwa mujibu wa maandiko ya Biblia, tendo la ndoa linatakiwa kufanywa na mwanamume na mwanamke ambao wameamua kufunga ndoa ili kuishi pamoja kwa maisha yao yote mpaka kifo. Mtu ambaye hajafunga ndoa halali haruhusiwi kujamiiana mpaka atakapofikia umri na muda wa kufunga ndoa rasmi. Mojawapo ya amri kumi maarufu katika Biblia ni pamoja na “usizini” (Kut. 20:14). Zinaa ni miongoni mwa tabia sugu zenye kuharibu utendaji wa vipaji vya wanadamu na ndiyo maana imekatazwa kimaadili. Madhara Ya Tabia Sugu Ya Zinaa Kimaadili Mojawapo ya athari za tabia sugu ya zinaa ni “kupungukiwa na akili”: “Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.” (Hosea 4:11) Biblia inaposema zinaa inaondoa “fahamu za wanadamu”, maana yake inalenga uharibifu wa kitabia wenye kuathiri utendaji wa vipaji vya asili. Mtu akiisha kujiingiza katika vitendo vya zinaa, tayari fahamu zake au fikira zake zinaathirika na kupoteza mwelekeo wa kimaadili na hivyo kudhoofisha utendaji bora wa vipaji vyake. Maandiko mengine yamerejea kusisitiza ya kwamba mwenye kufanya zinaa tayari ana matatizo ya kiakili: “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” (Mit. 6:32) Hapa tunasoma habari kuhusu zinaa inavyozuzua akili za mtu mpaka anajiingiza kwenye mazingira ya kuhatarisha uhai wake lakini hata hajali. Kumbuka wakati huo maandiko haya 70

yalipoandikwa, hukumu ya zinaa ilikuwa ni mtu “kupigwa mawe mpaka kufa” (Law. 20:10). Kwa hiyo, mtu akiisha kuonja zinaa humponza kiasi cha kujitoa mhanga kupigwa mawe hadi kufa kama atafumaniwa. Kufuatia athari mbaya za kimaadili zinazotokana na tabia sugu ya zinaa, maandiko yametoa mwongozo wa kila mtu kujiepusha nayo kwa kadiri iwezekanavyo kama ilivyoandikwa hapa chini: “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda juu ya mwili wake mwenyewe.” (1 Kor. 6:18) Vichocheo Vya Zinaa Pamoja na makatazo ya vitendo vya zinaa bado kumekuwepo mmomonyoko wa kimaadili wenye kusababisha kukithiri kwa vitendo hivyo katika jamii. Baadhi ya vichocheo vya zinaa ni pamoja na: • Tamaa za ujanani • Mila na desturi zisizoheshimu ndoa ya mke na mume mmoja • Ngoma na miziki inayohamasisha vitendo vya ngono • Picha za ngono katika magazeti, luninga, video na tovuti • Mavazi yasiyo ya staha • Ulevi na madawa ya kulevya • Umaskini Athari Za Nyingine Za Tabia Sugu Ya Zinaa • Zinaa huleta unajisi unaomtenga mtu na Mungu kiroho • Zinaa huathiri utu kwa kuvunja hadhi ya mtu binafsi • Zinaa hivunjia taasisi ya ndoa heshima yake mbele za jamii • Zinaa husababisha kuzaliwa watoto nje ya ndoa na kukosa malezi bora 71

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
100 %
“Baridi Fusion”: Asili Joto, Myeyungano Nyuklia, Tesla, Free Nishati = Pseudo-Sayansi ? (muhtasari katika Kiswahili) / Cold Fusion, Tesla, Free Energy = Pseudo Science?
Valentine_s_Day_Anthology_2015
Please click here to view the postcard. - City of Longwood
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
100 Jahre