Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

• Zinaa huharibu akili

• Zinaa huharibu akili na uwezo wa kufikiri mambo ya maana • Zinaa husababisha umaskini kwa matumizi ya anasa zisizo na udhibiti • Zinaa husababisha uhasama/chuki/uadui mpaka mauaji • Zinaa husababisha migogoro na kusambaratisha familia • Zinaa hueneza maambukizo ya maradhi ya zinaa na VVU Tabia Sugu Ya Chuki Na Hasira Tabia ya chuki na hasira imetokea kuwa miongoni mwa tabia sugu ambazo zinaathiri vipaji vya asili kwa sababu waathirika wengi ni vijana, tena ambao ndio nguvu kazi ya taifa. Kimaumbile kila binadamu ana “hisia hasi” za chuki na hasira. Lakini hisia hizi zinatakiwa kudhibitiwa ili kudumisha mahusiano mema ya kifamilia na kijamii. Pale ambapo mtu anashindwa kudhibiti chuki na hasira matokeo yake atajikuta amesababisha madhara yenye kuathiri utendaji wa vipaji vya asili, kwa yeye mwenyewe na kwa jamii inayomzunguka pia. Tafsiri Ya Misamiati Ya Chuki Na Hasira. Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu, neno “chuki” limetafsiriwa kuwa ni: “ tabia ya kutopenda watu au hali ya kuwa na roho mbaya, au kinyongo.” Neno hasira limetafsiriwa kuwa ni: “ ghadhabu au hamaki au fundo.” Hapa nitoe angalizo ya kwamba, hii “tabia sugu ya chuki na hasira”, inatofautiana na ile “tabia sugu ya kulalamika na kuhukumu” ambayo tayari tumejifunza habari zake. Mtu mmoja anaweza kuwa na tabia sugu zote mbili, lakini sio lazima aliye na tabia moja kati ya hizi awe na tabia ya pili. Kuna watu wameathiriwa na “tabia sugu ya chuki na hasira” lakini hawana hulka ya “tabia sugu ya kulalamika na kuhukumu” wengine hadharani. Waathirika wa “chuki na hasira” wanaweza kuchukua hatua kali za kulipa visasi pasipo kupiga kelele hata kidogo. 72

Wakati huo huo, watu wenye “tabia sugu ya kulalamika na kuhukumu wengine” huwa ni chanzo kikuu cha kuwachochea watu walioathiriwa na “tabia sugu ya chuki na hasira” ambao huhamaki na kutafuta kulipiza visasi dhidi ya mahasimu wao. Vyanzo Vya Hasira Na Chuki Hisia hasi za chuki na hasira zina vyanzo viwili tofauti. Kuna vyanzo vya nje ambavyo ni maumivu ya nafsi yatokanayo na kunenewa au kutendewa mabaya; au uchungu wa kukosa huduma na haki stahili kutoka kwenye mamlaka husika. Chanzo cha pili ambacho ni kutoka ndani kinajumuisha hisia ya ndani ambayo ni ama aibu ya moyoni itokanayo na kushindwa au kutokufanikiwa katika jambo mbele za watu, au kusutwa na dhamiri kwa sababu ya makosa au dhambi zilizofanywa na hazijasuluhishwa bado. “BWANA akamwambiaKaini, kwanini una ghadhabu? Kwanini uso wako umekunjamana?Kama ukitenda vema hutapata kibali?Usipotenda vema dhambi iko inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.” (Mwa. 4:6-7) Athari Za Hasira Na Hamaki Pamoja na kwamba mwenye hasira na chuki anaweza kujihesabia haki kutokana na sababu anazoziona kuwa ni halali kwake; pasipo kujitambua kumbe anajisababishia athari yeye mwenyewe ambazo baadhi yake ni kama hizi zifuatazo: Kudhoofisha Kazi Za Kimaendeleo Mwenye chuki na hasira hujikuta hajali muda na kuchelewa kufika kwenye shughuli za kimaendeleo na kazini kwa sababu ameshuka moyo wa kufanya kazi. Wengine hujiingiza kwenye vitendo vya ulevi, kula kupita kiasi, kuwa tegemezi kwa wengine, 73

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
“Baridi Fusion”: Asili Joto, Myeyungano Nyuklia, Tesla, Free Nishati = Pseudo-Sayansi ? (muhtasari katika Kiswahili) / Cold Fusion, Tesla, Free Energy = Pseudo Science?
100%
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook