Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

na ulemavu wa kihisia.

na ulemavu wa kihisia. Madhara Ya Kiafya • Hasira hupandisha mwendo wa moyo kutoka kiasi cha 80 mpaka 180 hata zaidi kwa dakika • Shinikizo la damu nalo kupanda kutoka 120 kwa 80 kwenda 220 kwa 130 au zaidi • Kasi ya kupumua huongezeka ili kuingiza hewa safi mwilini • Mlipuko wa nguvu husababisha kushuka kwa sukari kiasi mtu huweza hata kutetemeka • Mwili hutoa kemikali za kugandisha damu kana kwamba kuna ajali imetokea mwilini hali ambayo mgando wa damu huenda moyoni au katika ubongo • Mwenye hasira hukabiliwa na hatari ya mlipuko wa moyo au ugonjwa wa kiharusi • Hasira sugu husababisha mfadhaiko na msongo wa mambo ambavyo hupelekea vidonda vya tumbo • Hasira sugu hudhoofisha mfumo wa kinga na kusababisha pumu, maradhi ya ngozi, ugonjwa wa baridi yabisi. Mchakato Wa Kudhibiti Changamoto Zenye Kudhoofisha Vipaji Baada ya kuzipitia baadhi ya changamoto zilizoanishwa katika sura hii, sasa ni wakati muafaka wa kutafuta kujua mbinu za kupambana na kuudhibiti huu udhoofishaji wa vipaji. Tumezipitia changamoto za nje ambazo ni marafiki wabaya, imani za uchawi na ushirikina, mifumo butu ya elimu, na athari za utandawazi kupitia mitando ya kijamii. Pili, tumepitia changamoto za ndani kupitia “tabia sugu zenye kuathiri utendaji wa vipaji kutokea ndani ya wahusika. Suala zima la kudhibiti changamoto hizi haliwezi kuwa tukio la mara moja tu. Lazima liwe katika mfumo wa kimchakato. Madhara yaliyopo hayakujitokeza siku moja bali yalichukua muda 74

mrefu. Hali kadhalika na mchakato wa kuyadhibiti kunahitaji muda ili tuweze kuona matokeo. Hakuna njia ya mkato katika kurekebisha mambo yaliyojisokota kwa muda mrefu. Zifuatazo ni ngazi makini za kufanya matengenezo ya madhara yaliyokwisha kufanyika na mbinu za kujikinga ili athari zisiendelee kujitokeza tena huko mbeleni: 1. Kumrudia Mungu Muumbaji Wetu Tumejifunza habari za vipaji na karama kwamba ni vitu vinavyotoka kwa Mungu aliyemwumba binadamu kwa mfano wake na sura yake. Aidha tumejifunza pia ya kwamba, Mungu ndiye anayejua kusudi la kuwepo kwako na pia ndiye mwenye kujua mwanzo na mwisho wa kila binadamu hapa duniani. Kwa hiyo, tunapotafuta kufanya matengenezo ya kitabia na kunoa vipaji vilivyomo ndani yetu, lazima kwanza tumrudie Mungu na kujenga uhusiano wa kiroho pamoja naye. Uzuri ni kwamba sio sisi tunayemrudia Mungu kwa juhudi zetu wenyewe, bali yeye mwenyewe alikwisha kututafuta na kutuonesha njia ya kumrudia bila gharama yoyote. Katika kumrudia Mungu tunaanza na hatua ya kwanza inayojulikana kama toba. Tafsiri Ya Toba Biblia imeandika kuhusu toba ikitumia maneno ya Kiebrania na Kiyunani. Kwa Kiebrania neno lililotumika kuhusu toba ni nocham. Maana yake ni kuugulia, kuomboleza, kujuta na kuacha kutenda dhambi na kugeuka na kurejea kwa Mungu. Kwa Kiyunani neno lililotumika kuhusu toba ni metanoia. Maana yake ni kubadilia nia na kuachana na kusudi la kuendeleza jambo, kugeuka nyuma na kurudi ulikotoka. 75

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
100%
“Baridi Fusion”: Asili Joto, Myeyungano Nyuklia, Tesla, Free Nishati = Pseudo-Sayansi ? (muhtasari katika Kiswahili) / Cold Fusion, Tesla, Free Energy = Pseudo Science?
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook