Views
8 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Kwa muktadha wa maneno

Kwa muktadha wa maneno nocham na metanoia, yote yanatoa maana ya mtu kujutia hali yake ya dhambi, kuamua kubadili nia na mtazamo wake kuhusu dhambi zake, na kugeuka nyuma kisha kurejea katika uhusiano wa kiroho na Mungu. Watu wengi huchanganya maana ya maneno “toba” na “ungamo” wakidhani ni kitu kile kile. Ukweli ni kwamba “kutubu” ni tofauti na “kuungama” tu. Kuungama ni “kukubali na kukiri ukweli wa makosa yaliyofanywa.” Lakini “kutubu” ni “kujutia na kubadili nia” kwa “kuachana na mwenendo wa dhambi na kumgeukia Mungu” ili kuishi maisha tofauti na yaliyopita. Agizo La Toba Mungu amekwisha kutoa agizo maalum kwa watu wote ambao ni waathirika wa tabia sugu zilizotajwa katika sura hii wapate kutubu kwake kama ilivyoandikwa: “Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu. Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.” (Mdo. 17:30-31) Maandiko haya yaliandikwa kwa ajili ya kuwataka watu wote waliokuwa ni waathirika na imani za uchawi na ushirikina pamoja na tabia sugu wabadili nia zao na kumrudia Mungu Muumbaji wao na kujiweka salama wasiagukie kwenye maangamizi yaliyokuwa yakiwakabili. Mchakato wa kufanya matengenezo dhidi ya madhara ya changamoto zenye kuathiri vipaji na karama unatakiwa kuanza na toba kwa mujibu wa maandiko tuliyosoma. Uzuri wa maandiko haya ni kwamba Mungu yuko tayari kuachilia makosa yaliyokwisha kufanyika kwa kujifanya kama hayajui kwa sababu yalifanyika kutokana na kutokujua. 76

Faida Za Toba Kutoka Katika Mitego Ya Ibilisi Shetani ndiye chimbuko kuu la changamoto zote za nje na za ndani ambazo zinadhoofisha utendaji wa vipaji vya wanadamu. Kufanya toba ya kweli ndio mlango wa kutoka katika mtego wa Ibilisi ambao aliutumia kuwanasa wengi katika vifungo vya dhambi na tabia sugu: “akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli; wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Ibilisi, ambao hao wametegwa naye, hata kuyafanya mapenzi yake.” (2 Tim. 2:25-26) Maandiko haya yanataja habari za “kupata tena fahamu” ambazo hapo awali ziliharibiwa na tabia sugu za ulevi na zinaa. Pili, tunasoma habari za “kutoka katika mtego wa Ibilisi” ambao ni vishawishi au vitisho vyenye kuwafanya waathirika kuzama katika maisha ya imani za uchawi na ushirikina. Katika kufanya toba ya kweli tunasoma kuna kufumbuliwa macho ya kiroho na kutambua kuwa uko gizani na kuamua kuigeukia nuru: “uwafumbue macho yao, na kuwageuza waiache giza na kuigeukia nuru, waziache na nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu; kisha wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu mimi.” (Mdo. 26:18) Maandiko haya yanataja pia habari za “kuziacha nguvu za shetani” ambazo zinasababishwa na imani za uchawi na ushirika pamoja na vifungo vya tabia sugu zlizokwisha kutajwa katika sura hii. 77

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 100 ...
Andy! Oxidation paintings by Mambo - Paetau, Kristofer
Valentine_s_Day_Anthology_2015
Chapter 78
TPCC Annual Report 2008.indd - HeidelbergCement
Tanzania Breweries Limited Annual Report and ... - SABMiller
BE-100-6_Quran_and_World_Peace
TOP 100