Views
4 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Kuzaliwa Upya Faida ya

Kuzaliwa Upya Faida ya pili ya kufanya toba ya kweli ni muujiza wa mabadiliko ya ndani ya kiroho ambayo hufanywa na Mungu mwenyewe kwa kumtumia Roho wake Mtakatifu: “si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu” (Tit. 3:5) Itakumbukwa ya kwamba maana ya tabia sugu ni “mazoea yatokanayo na kurudiarudia hali isiyoweza kuondolewa kwa urahisi”. Katika hatua ya kufanya toba, pasipo kutumia nguvu za kibinadamu za kujibadilisha kitabia, kuna rehema za Mungu zinazomshukia mwenye kutubu na kuihuisha roho yake kupata nguvu za mabadiliko ya kiroho. Mabadiliko haya ndiyo yanajulikana kuwa ni “kuzaliwa kwa pili” na “kufanywa upya” na Roho Mtakatifu. 2. Kupokea Nguvu Za Kiungu Za Kudhibiti Tabia Sugu Baada ya kufanya toba ya kweli na kupata mabadiliko ya ndani ya kiroho; hatua inayofuata ni kupokea nguvu za kiungu za kudhibiti tabia sugu ambazo ni “mazoea yatokanayo na kurudiarudia hali isiyoweza kuondolewa kwa urahisi” Maandiko yafuatayo yanatuthibitishia uhakika wa kudhibiti tabia sugu kama ifuatavyo: “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa, nayo yatufundisha kutaa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa.” (Tit. 2:11) Maandiko hayo hapo juu yanatujulisha jinsi ambavyo Mungu amekwisha kutoa neema ya kuwaokoa wanadamu wote, kama wakiamua kutubu kwa dhati na kumrudia yeye. Na neema 78

hii inafanya kazi ya kutufundisha jinsi ya kukataa ubaya na tamaa za kidunia ambazo zinadhoofisha utendaji wa vipaji na karama ndani yetu. Katika maandiko mengine tunajulishwa kukirimiwa ahadi kubwa za thamani za kutuwezesha kupokea tabia za uungu ambazo huweza kudhibiti tabia sugu: “Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washiriki wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.” ( 2 Pet. 1:4) 3. Kuutafuta Kwanza Ufalme Wa Mungu Na Haki Yake Changamoto kubwa ya binadamu hapa duniani ni kutafuta maisha kwa kila njia, ziwe halali au haramu. Kipaumbele chake ni kufanikiwa katika kujipatia na kujilimbikizia mali nyingi. Hata hivyo, mambo ni tofauti kwa mtu aliyekwisha kumrudia Mungu kwa njia ya toba. Baada ya kuchukua hatua za kiroho zilizotangulia, kinachofuata ni kupanga upya vipaumbele vya maisha: “Msisumbuke, basi, mkisema, tule nini? Au Tunywe nini? Au tuvae nini? Kwa maana hayo yote mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hao yote. Bali utafute kwanza ufalme wake na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” (Mat.6:32-33) Maandiko haya yametafsiriwa kinyume na maana yake kwa nadharia zinazokataza watu kufanya kazi eti badala yake wategemee sala peke yake kwa kuwa Mungu anajua mahitaji yao. Dhana ya kutokufanya kazi na kutegemea kuishi kwa miujiza peke yake sio muktadha wa maandiko haya. Kile Yesu alichomaanisha hapa ni wanafunzi wake kubadili mtazamo kuhusu maisha na kuweka upya vipaumbele kwa kigezo cha kutanguliza ufalme wa Mungu. Yesu hakukataza kufanya kazi, alitoa mwongozo wa kufanikiwa kupitia vipaumbele na Mungu 79