Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

ya kupinduliwa au

ya kupinduliwa au kupoteza umaarufu tuliojijengea katika jamii. Lakini tusipotumia muda muafaka tutamaliza vibaya na kuacha migogoro ya kifamilia na kijamii nyuma yetu. Wana-rika wenzangu, tusiposhituka na kuanza maandalizi ya urithishaji wa uchumi na uongozi hivi sasa, muda hautungoji. Miaka 10 iliyoko mbele yetu inakimbia mbio za kasi, kufumba na kufumbua tutajikuta iko mbele yetu. Uzalishaji na usimamizi ni mambo yanayotegemea nguvu na akili. Kwa kadiri umri unavyoongezeka ndivyo na nguvu za uzalishaji na akili za kufanya maamuzi hubadilka. Kwa lugha nyingine kasi ya kufanya mambo hupungua na uzito katika kufanya maamuzi nao huongezeka. Kwenye suala la uchumi ambapo ulimwengu unabadilika kila kukicha, mambo mapya yanazaliwa na elimu inaongezeka kwa kasi, wakati jamii ya wazee bado iko katika enzi zao. Bahati mbaya kasi na hamu ya kujifunza mambo mapya kwa wazee huzidi kupungua. Hizi ndizo dalili zinazoashiria kwamba, wakati wa kurithisha wengine wenye uwezo na nguvu umekaribia. Kuendeleza Jina Maendeleo ya kiuchumi na kijamii hufanywa na watu, kila mtu mmoja mmoja, na kwa ushirikiano wa kimakundi. Mojawapo ya hamasa za kimaisha, ni mtu kutoa mchango wa kimaendeleo ambao utakumbukwa baada ya kuondoka kwake duniani. Hii ndiyo inaitwa “kuacha jina”. Kuna mambo ambayo baadhi ya wazee waliotutangulia walifanya enzi za ujana wao, na sisi tumeyakuta, tumeyarithi, na tunawakumbuka kwa ajili ya mambo hayo. Wenyewe wamekufa, lakini mambo yao bado yako hai, na hivyo majina yao yanaendelea kutajwa japokuwa wenyewe hawapo tena. 84

Kuendeleza Kizazi Sababu nyingine muhimu sana ni kukiwezesha kiuchumi na kiuongozi kizazi kipya cha watoto waliozaliwa na kulelewa katika mazingira ya kifamilia, kitaasisi na kitaifa. Sababu ya kwanza ya kurithisha tulisema ni kigezo cha ukomo wa muda wa kuishi. Sababu hii ndiyo inapaswa kuchochea moyo wa kizazi kinachomaliza muda wake kufanya maandalizi mapema ya kukabidhi majukumu ya kiuchumi na kuiongozi kwa kizazi kipya. Katika ngazi ya familia, ni fahari ya wazazi pale ambapo watoto wao waliowazaa wanapofikia umri wa kutaka kujitegemea kimaisha. Vijana wa kiume wanapofikia umri wa kuoa huhimizwa na wazazi na kufundishwa, na hata kusaidiwa jinsi ya kujenga misingi ya kujitegemea kama kuwa na shughuli maalum ya uzalisha wa kujipatia kipato binafsi, kujenga nyumba, kuwa na samani za ndani n.k. Kwa upande wa vijana wa kike, wanapofikia umri wa kuolewa huandaliwa rasmi jinsi ya kuishi katika ndoa na kutunza familia zao mpya baada ya kuolewa. Kuendeleza Maono Ya Kitaasisi Changamoto katika urithishaji ziko kwenye ngazi ya kitaasisi na kitaifa. Katika ngazi ya kitaasisi, kuna jamii ya watu waitwao “waasisi”. Hawa ni waanzilishi wa mawazo ya awali ya kuanzishwa kwa taasisi husika na kwa njia hiyo wamekuwa viongozi wake tangu ngazi ya uchanga mpaka hapo ambapo taasisi hizo zimekomaa kiutendaji. Ninaposema taasisi nina maana ya vyama vya hiari, au madhehebu ya dini, au vikundi vya kijamii ambavyo vimesajiliwa kwa mujibu wa sheria. 85

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
“Baridi Fusion”: Asili Joto, Myeyungano Nyuklia, Tesla, Free Nishati = Pseudo-Sayansi ? (muhtasari katika Kiswahili) / Cold Fusion, Tesla, Free Energy = Pseudo Science?
100%
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook