Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Katika ngazi ya

Katika ngazi ya kitaasisi, (tofuati na serikali na taasisi za kiserikali, ambazo utumishi wake una ukomo kwa mujibu wa sheria) baadhi ya taasisi binafsi hazina utamaduni wa kisheria wa ukomo wa utumishi. Katika ngazi hii, mara nyingi wale waitwao “waasisi” kwa maana ya walioanzisha taasisi au huduma hizo huwa wazito sana kuachia madaraka ya uongozi kwa vijana wao. Kuacha utumishi katika ngazi ya kitaasisi hushinikizwa na maaradhi, au kifo; au shinikizo la uasi ndani ya taasisi ambao matokeo yake husababisha mifarakano na matengano ya kitaasisi. Kuendeleza Kizazi Cha Kijaamii Kitaifa Katika ngazi hii, urithishaji unategemea mfumo wa utawala na uzoefu katika zoezi ya kuachia madaraka. Kwa upande wa Tanzania, kisiasa tuna sifa njema katika Bara la Afrika kwa kuwa na utamaduni wa watawala wa kitaifa kuachia madaraka mara baada ya kufikia ukomo wa muda wao. Hata hivyo, changamoto iliyopo katika ngazi hii, ni pale ambapo wale wanaomaliza muda wao wa utumishi wa umma kupewa mikataba maalum na kuendelea kutumika. Utetezi unaotumika katika kulinda utaratibu huu ni kuwepo kwa baadhi ya nafasi za utumishi ambazo bado hazina watu wenye ujuzi na uzoefu; na hivyo wastaafu husika wakaonekana bado wanahitajika kutumika katika ngazi husika. Pamoja na utetezi huu, pia kumekuwepo na upande mwingine wenye malalamiko dhidi ya utaratibu huu kwamba unawanyima haki wengine waliostahili kushika nafasi za wastaafu kwa mujibu wa sheria. 86

Ngazi Muhimu Za Urithishaji Urithishaji Wa Ngazi Ya Kifamilia Katika ngazi hii, ni wazazi ndio hurithisha watoto mali walizochuma katika familia. Kama tulivyokwisha kupitia kihistoria kuhusu urithishaji katika ngazi ya familia, hapa ni muhimu tuzingatie kwamba jamii ya kizazi chetu kwa sehemu kubwa imepoteza utamaduni wa kurithisha majukumu na raslimali kwa kizazi kinachoinukia. Ushahidi ni kuongezeka kwa migogoro na kesi za mirathi zilizojaa mahakamani siku hizi. Badala ya walezi kifamilia kusimamia mchakato wa urithishaji kwa watoto wa marehemu au wale wanaostahili kurithishwa, wao ndio wanateka mali hizo na kuzitapanya kwa sababu za kibinafsi na watoto wanaanza kuhangaika. Kupotea kwa utamaduni wa kurithisha pia kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya kimaendeleo na kijamii ambapo familia zimetawanyika mijini na vijijini. Lakini pia ukosefu wa wazazi kuandika wosia mapema kuhusu mgawanyo wa mali kwa familia. Jambo linalosikitisha zaidi katika udhaifu wa kutokurithisha ni pale ambapo wazazi huishia kuzaa watoto lakini hawana mpango maalum wa kutunza urithi kwa ajili ya watoto. Badala yake wazazi wanafanya kazi ya kuchuma na kutafuta bila kuweka akiba kwa ajili ya watoto. Kuna ongezeko la kuparaganyika kwa familia kunakotokana na mmomonyoko wa maadili katika jamii. Hii imezalisha familia za aina tofauti ambazo watoto wanaozaliwa au kulelewa ndani yake wanakosa mwelekeo wa kimaadili na hivyo kupotoka kitabia. 87

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
100%
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
GOLDINI