Views
9 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

Kuparaganyika kwa

Kuparaganyika kwa familia nyingi kumezalisha changamoto kubwa nyingine ya ongezeko la kizazi kinachoitwa kwa jina maarufu kama “watoto wa mitaani”. Hawa ni watoto ambao baadhi yao hawana wazazi au walezi na wamekosa malezi ya kifamilia na ndio maana wameishia mitaani. Hiki nacho ni kizazi ambacho badala ya kurithishwa msingi wa kimaendeleo wanaishia kurithi umaskini na maisha ya uhalifu. Si lengo la kitabu hiki kuzungumuzia matatizo ya kifamilia, ila haya yanatajwa kama viashiria vya familia kushindwa kutimiza wajibu wake wa kurithisha kizazi kipya. Wito makini wa ujumbe wa kitabu hiki kwa kila familia yenye mtoto au watoto, wawe wa kuwazaa au kuwalea, ni kurejea katika utamaduni wa kijamii wa kurithisha majukumu na rasilimali kwa watoto pindi wanapofikia umri wa kujitegemea na kuwa watu wazima. Urithishaji Wa Ngazi Ya Kitaasisi Uritishaji wa kitaasisi ni urithishaji wa mali na madaraka ya kusimamia taasisi husika. Taasisi hapa tunajumuisha makampuni binafsi, vikundi vya uzalishaji, na vikundi vinginevyo ambavyo madhumuni yake ni uzalishaji na wanahisa kugawana mapato kwa mujibu wa makubaliano ya kisheria. Katika ngazi hii ya urithishaji wa kitaasisi, viongozi waasisi ndio wenye wajibu wa kurithisha madaraka ya usimamizi wa taasisi. Japokuwa jambo la kurithisha uongozi litaelezwa kwa kina katika vipengele vinavyofuata, hapa ni muhimu kuzingatia mapema ya kuwa kila mwasisi na mtendaji mkuu wa kampuni ya kifamilia au kijamii atie akilini mwake kuwa ni muhimu kumwandaa mrithi wake wakati bado ana nguvu. Mwasisi asisubiri wakati amezeeka ndipo akabidhi majukumu. Kurithisha majukumu ya uongozi na utawala katika mambo ya uzalishaji sio kama kurithisha mali za marehemu. Unahitaji muda wa kutosha wa kuachilia baadhi ya majukumu 88

kwa watoto au warithi ambao wanapata uzoefu wakati mwasisi bado yuko hai. Urithishaji Kwa Kizazi Cha Kitaifa Ngazi ya urithishaji kwa kizazi cha kitaifa ni hatua ya juu kabisa katika jamii. Hapa tunazungumuzia ngazi ya kitaifa. Taifa kama Tanzania ambalo mna makabila zaidi ya 120 yanayounganishwa na utaifa wenye sifa ya uraia mmoja. Tanzania kama taifa, linayo jamii ya watu waliozaliwa kwa wakati mmoja wa historia, ambao kwa lugha nyingine huitwa rika moja. Hawa ndio huitwa kizazi cha kitaifa. Lakini tunapo itathmini Tanzania kijamii tunakuta kuna mgawanyiko wa sehemu mbili za vizazi vya kitaifa; kuna kizazi cha watoto, na pili, kuna kizazi cha watu wazima. Kizazi cha watoto kinatambuliwa kwa umri kuanzia mwaka mmoja (1) mpaka miaka kumi na saba (17). Watu wote katika umri huu hawaruhusiwi kufanya maamuzi huru kama watu wazima. Wahusika wanahesabiwa kuwa chini ya uangalizi wa kifamilia na malezi ya kitaifa. Ishara iliyo wazi zaidi ni kuwa hawaruhusiwi kupiga kura kwenye uchaguzi wa uongozi wa kitaifa. Kizazi cha watu wazima ni kuanzia umri wa miaka kumi na nane (18) mpaka sitini (60). Hiki ndicho kizazi chenye idhini ya kufanya maamuzi na kuwajibika kisheria. Wahusika wanaruhusiwa kupiga kura na kuwania madaraka ya uongozi katika ngazi mbali mbali za utumishi wa umma kitaifa. Katika ngazi ya kizazi cha kitaifa, wenye wajibu wa kurithisha ni wazee ambao wamefikia umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria. Hiki ndicho kigezo muhimu cha Urithishaji wa kizazi. Wazee wanapostaafu huwaachia majukumu ya uzalishaji na usimamizi vijana ambao wamechukua nafasi zao. 89

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
100%
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook
GOLDINI