Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

1. Neno la hekima 2.

1. Neno la hekima 2. Neno la maarifa 3. Kupambanua roho 4. Imani 5. Karama za kuponya 6. Matendo ya miujiza 7. Unabii 8. Kunena kwa lugha 9. Tafsiri za lugha Hizi “karama za Roho” naweza kuzitafsiri kuwa ni “karama za udhihirisho” (Manifestational gifts). Maana yake zenyewe zinatenda kazi ya kudhihirisha utendaji wa Roho Mtakatifu ndani ya waamini ambao wamekirimiwa huduma na utumishi wa kiroho katika mwili wa Kristo. Orodha ya “ofisi za huduma” zilizotajwa katika Waefeso 4:11: ni kama ifuatayo: 1. Mitume 2. Manabii 3. Wainjilisti 4. Wachungaji 5. Waalimu Hizi zinaitwa “ofisi za huduma” ambazo nimeziita “karama za uwezesho” kwa sababu zinafanya kazi ya kuwakamilisha watakatifu ili kazi ya huduma itendeke. Ni karama za kuwezesha waamini kupata uzoefu wa kutumika katika kuujenga mwili wa Kristo. Orodha ya “karama za neema” zilizotajwa katika Warumi 12 ni kama ifuatavyo: 1. Uhamasishaji 2. Utoaji 8

3. Uongozi 4. Rehema 5. Unabii 6. Huduma 7. Ualimu Hizi ni “karama za neema” ambazo zinaitwa “karama za utumishi” (Serving Gifts). Mungu Baba huwagawia waamini karama za neema ili wapate kutumikiana wenyewe kwa wenyewe mara baada ya kukamilishwa na zile “karama za uwezo” ambazo ni “ofisi za huduma”. 3. Tofauti Kati Ya Vipaji Vya Asili Na Karama Za Kiroho Kwanza kabisa ni muhimu kutambua mapema ya kwamba “vipaji vya asili” si “karama za kiroho”. Kwa kifupi ni kwamba, “kipaji cha asili” chimbuko lake ni kibaiolojia (natural and biological); na “karama za Roho” asili yake ni ya kiroho na ya kiungu (spiritual and supernatural). Jambo muhimu la pili ni kwamba, kila binadamu (mwamini na asiye mwamini) huzaliwa na vipaji vya asili lakini kimojawapo kati ya vingine ndicho hujitokeza zaidi na mhusika akajulikana kupitia kipaji hicho cha asili. Lakini si kila binadamu anayezaliwa kibaiolojia huzaliwa akiwa na “karama za kiroho”. Tumejifunza ya kwamba “karama za kiroho” ni kwa ajili ya “waamini peke yao”, na kwa ajili ya matumizi ya kiroho peke yake. Kwa hiyo, kipaji cha asili mtu huzaliwa nacho kwa mara ya kwanza, lakini “karama za kiroho” hupokelewa na mtu akiisha kuzaliwa mara ya pili kiroho. Jambo muhimu la tatu ni kwamba, “vipaji vya asili” huwanufaisha zaidi wenye kuzaliwa navyo ikiwa ni pamoja na kuwaneemesha kwa maslahi ya kibinafsi. Lakini “karama za 9

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
“Baridi Fusion”: Asili Joto, Myeyungano Nyuklia, Tesla, Free Nishati = Pseudo-Sayansi ? (muhtasari katika Kiswahili) / Cold Fusion, Tesla, Free Energy = Pseudo Science?
100%
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook