Views
6 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

sasa kinaweza kuona

sasa kinaweza kuona kwamba kuwekeza katika “elimu na ujuzi” ni gharama kubwa, na kutafuta unafuu na urahisi ili kukwepa kugharimia viwango bora vya elimu na ujuzi. Kumbe katika kushusha “viwango vya ubora” tayari tumechagua kurithisha “viwango duni vya elimu” kwa kizazi kinachoinukia ambacho hakitaweza kumudu ushindani wa kimataifa katika uzalishaji. Sio siri hivi sasa kuona kwamba watoto na vijana wetu wamesongwa katika mazingira magumu ya kimfumo wa huduma za elimu kwa sababu mbali mbali. Baadhi ya sababu za watoto na vijana wetu kukosa kupata elimu bora ni pamoja na: i) uhaba wa nafasi za kuendelea na elimu ya juu katika mfumo wa elimu yetu. ii) udhaifu wa mitaala isiyokidhi viwango vya ubora wa elimu ya kimataifa. iii) Vitendo vya uchakachuaji wa mitihani kunakotokana na kukithiri kwa rushwa katika taasisi zinazosimamia mitihani. iv) Walimu kukosa motisha katika utoaji wa elimu kwa wanafunzi. Kwa kadiri ambavyo idadi kubwa ya watoto na vijana wengine wanavyoishia katika viwango vya chini vya elimu; hiyo ndiyo dalili iliyo waziwazi kwamba kizazi chetu tuliopo hivi sasa tumeamua kurithisha ujinga kwa kizazi kijacho. Kimsingi, tumekuwa tukifanya zoezi la kurithisha ujinga na kizazi kinachokuja kitatukumbuka kwa urithi wa ujinga tuliokiachia. Mabadiliko yoyote ya kimfumo hayaji kwa miujiza. Yanakuja kwa utashi na uamuzi wa nguvu. Lazima tuutumie utashi wetu na kufanya uamuzi wa kukataa kuendelea kurithisha ujinga kwa watoto na vijana wetu. Uwezo na nguvu tunazo, kinachokosekana ni nia ya dhati. Lazima tukatae kurithisha ujinga kwa watoto na vijana wetu. Umaskini Kuna mtu mmoja maarufu sana anayeongoza kwa utajiri hapa duniani anaitwa Bill Gates. Miaka ya hivi karibuni alitoa kauli ambayo imezua mjadala mpaka hivi sasa, lakini ina ushawishi 92

mkubwa kiasi ambacho hakuna ambaye amefaulu kuipinga na akashinda. Alisema hivi:“kama umezaliwa katika familia masikini sio kosa lako; lakini ukifa maskini hilo ni kosa lako mwenyewe”. Kwa kauli hii ni rahisi sana Bill Gates kutafsiriwa kuwa amejikinai kwa kuwahukumu watu wanaokufa maskini kwamba hayo ni makosa yao. Lakini baada ya kuutafakari kwa makini usemi wake nilipata kumwelewa kwa sehemu kile alichokuwa amemaanisha. Bila shaka alikuwa anatoa ujumbe kwamba mtu anapozaliwa katika familia ambayo ni maskini sio kosa lake kwa sababu sio yeye aliyechangia wala kufanya maamuzi ya kimaisha hata kusababisha umaskini alioukuta. Kwa maneno mengine mtu hajichagulii azaliwe katika familia ya namna gani, bali hujikuta amezaliwa katika familia husika. Lakini iwapo muhusika aliyezaliwa katika familia maskini anapokuwa mtu mzima ana uhuru wa kufanya maamuzi ya mwisho kuhusu maisha yake. Na hii ni pamoja na kutafuta fursa nyingi zilizopo mbele yake na kuanza kuzitumia kwa uzalishaji, kwa nia ya kubadili maisha yake ya umaskini wa kuzaliwa na kuitwa jina tofauti katika jamii. Neno Umaskini limetafsiriwa na Kamusi ya Kiswahili Sanifu kuwa ni “hali ya kukosa mali; ufukara, uhitaji, na ukata”. Najua kwamba kuna nadharia na dhana nyingi kwa habari ya umaskini, hususan huu wa kipato. Aidha kumekuwepo na itikadi zenye kutetea umaskini kama janga linalowapata watu pasipo wenyewe kutaka au kuusababisha. Kwa utafiti wangu naweza kutafsiri sababu za umaskini katika sehemu zifuatazo: Ulemavu: Ulemavu wa viungo vya mwili au akili ambao mlemavu hawezi kufanya shughuli halali ya kujipatia kipato. Ulemavu wa 93

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
100%
100€
Das Weihnachtsevangelium
Professional Photography Heber City
View the Annual report PDF (4.67Mb) - SABMiller
Download N.S.E Announcement - Nairobi Stock Exchange
Financial Statements 2011 - Investing In Africa