Views
8 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

jinsi hii, ni hali

jinsi hii, ni hali ambayo iko nje ya uwezo na uamuzi wa mhusika, na hivyo analazimika kuishi kwa kutegemea fadhila za binadamu ambao si walemavu katika jamii. Majanga Ya Kimazingira: Majanga ya kimazingira ni kama vile mafuriko, matetemeko au vita vya kiraia. Haya ni matukio ambayo huharibu rasilimali za watu na kupoteza muda wa jamii kufanya kazi za uzalishaji mpaka mazingira yarejee katika hali inayoruhusu uzalishaji. Katika mazingira kama haya waathirika hujikuta hawana rasilimali wala kipato cha kuwawezesha kukidhi mahitaji yao, isipokuwa nao wanaishi kwa fadhila za binadamu wengine ambao hawajakumbwa na majanga ya kimazingira. Uvivu Na Anasa: Tafsiri ya uvivu ni “hali ya kutotaka kufanya kazi; hali ya ulegevu katika kazi; utepetevu na ulegevu.” Ikiwa mtu mzima, ambaye si mlemavu, si mgonjwa, si mzee kikongwe; halafu mtu mwenyewe anaishi kwenye mazingira yenye fursa za uzalishaji mali (ardhi yenye rutuba, maji ya kutosha, ustawi wa mimea na malisho ya mifugo), halafu mtu huyo katikati ya mazingira hayo bado hana shughuli maalum inayompatia kipato; basi tena, huyo mtu sifa yake ni moja tu, ni mvivu. Kutokufanya kazi; au kuwa mlegevu katika kazi, husababisha ukosefu wa kipato na matokeo yake ni umasikini wa kipato na rasilimali. Huu ndio umaskini ambao Bill Gates alisema, “mtu akifa katika umaskini wa jinsi hii ni makosa ya mhusika’. Tafsiri ya anasa ni “mambo au hali ya starehe na raha nyingi; au kitu chenye thamani kubwa ambacho sio muhimu.” Unaona? Haya ni maisha ambayo watu wanatumia rasilimali zao kwa mambo yasiyo na tija iwe ni katika familia au katika jamii. 94

Uvivu hupelekea ukosefu wa kipato wakati anasa ni matumizi yasiyo na muhimu na kupita kiasi. Jambo lenye kushangaza na kusikitisha ni pale ambapo mtu asiye na kipato cha uhakika na akapata msaada wa kumwezesha kujikwamua katika umaskini, lakini anaamua kuutumia msaada ule kwenye anasa za ulevi, ulaji na kununua vitu vya thamani kubwa kuliko mahitaji yake ya muhimu. Matumizi ya anasa matokeo yake ni umaskini. Umaskini ambao haukupaswa kuwepo kabisa, lakini unamkumba mtu kwa sababu sio kwamba hakupata bali alipata akatumia vibaya, kwa anasa. Kumbuka kwamba matumizi ya anasa ni kuzalisha umaskini. Huu ndio umaskini ambao Bill Gates alisema, “mtu akifa katika umaskini wa jinsi hii ni makosa ya mhusika”. Umaskini wa namna hii unaweza kuzuilika kwa utashi na sio kwa misaada. Tunaweza kuukataa umaskini huu usiendelee kuanzia katika ngazi ya familia, ngazi ya kitaasisi na ngazi ya kitaifa. Hitaji Kuu La Viongozi Wa Kizazi Kipya Ni lazima tukubali kwamba hivi sasa, kwa sababu ya mmomonyoko wa maadili ya kimani; hata sifa na kanuni za kuwapata viongozi wenye uwezo stahili navyo vimechakachuliwa kabisa. Tumejikuta tuko katika mazingira ya kuwa na “bora viongozi” badala ya “viongozi bora”. Kwa mtindo huu kamwe hatuwezi kutarajia kwamba “uongozi wa kizazi kinachoinukia” utakuwa bora iwapo hatukuamua kwa makusudi kurejea katika kuweka “viongozi bora” ili wawe mwongozo kwa kikazi kinachoinukia. Kama ambavyo, kitaifa tuko kwenye mchakato wa mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kimifumo; bila shaka suala la uongozi nalo ni lazima lipewe kipaumbele ndani ya katiba, angalau kwa kuweka sifa na vigezo makini vyenye kuliwezesha 95

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
100%
Finding The Pleasure Free Ebook
GOLDINI
100-ideeënboek
100% Digital