Views
10 months ago

vipaji_pages1-100

hugggugu

taifa kuwapata viongozi

taifa kuwapata viongozi bora. Sisi ambao ni kizazi kinachomaliza muda wake ni lazima tufumbe macho na kuacha kuangalia aina ya viongozi waliopo sasa hivi kuwa ndio kigezo cha viongozi wa kizazi kinachoinukia. Tuamue kukinusuru kizazi kipya kwa kuweka vigezo vya kuwapata viongozi bora, hususan, viongozi wenye vipaji vya uongozi na kuwanoa mapema ili wapate uzoefu wa kuongoza kizazi chao kinachoinukia. Kwa uzoefu wangu binafsi, pamoja na tafiti mbali mbali zilizofanyika kwa habari ya “aina ya viongozi bora”, kuna ushahidi kamili kwamba suala la “uongozi bora” linatakiwa kuzingatia mambo makuu matatu yafuatayo: 1. Kipaji 2. Uzoefu 3. Uadilifu Kipaji kinawakilisha uwezo wa kuongoza kwa ushawishi wa nguvu za hoja na hekima ya kufanya maamuzi yenye kuleta ufumbuzi badala ya kusababisha matatizo makubwa zaidi. Kipaji cha uongozi kinahitaji mazoezi maalum ili kipate kunolewa kwa njia mbali mbali ambapo ndipo kigezo cha “uzoefu” kinachukua nafasi yake. Kimsingi kipaji cha uongozi hujidhihirisha chenyewe ndani ya mtu na wala hakuhitajiki kazi za “kupiga ramli za kindumba ili kukitambua”. Kipaji cha uongozi kikidhihirika ndani ya wahusika, lazima jamii iwe na mfumo wa kuwawezesha kufanya mazoezi ya kuongoza ili kigezo cha uzoefu nacho kichukue mkondo wake. Suala la uadilifu ni matunda ya maadili ya kiimani ambayo ndiyo mazingira wahusika wamefundwa na kukulia tangu ngazi ya familia, na imani kwa Mungu na huu ndio msingi wa kuwafanya kukamilisha sifa za kiuongozi. Tunapotaka kurithisha maono kwa kizazi kipya, tukija kwenye suala la uongozi, kipaji, uzoefu na uadilifu ni vitu 96

vinavyotakiwa kuwa mwongozo kwa wanoaji na warithishaji maono kwa kizazi kipya. Kwa kuwa shina la uongozi mbovu linatokana na mmomonyoko wa maadili ya kiimani katika jamii; bila shaka hapa ndipo mahali pa kuanzia kufanya maandalizi ya viongozi bora. Kuweka mkazo wa maadili ya kiimani, maadili ya kitaaluma na maadili ya uongozi. Malezi ya kimaadili ya kiimani huanzia nyumbani katika familia. Ni wakati muafaka kwa kanisa kuandaa mipango ya mafunzo ya kimaadili kwa wazazi ili yawasaidie kuwalea watoto wao kimaadili. Bila shaka, wazazi wenyewe nao lazima wanatambua kwamba wajibu wa kulea watoto kimaadili unaanzia kwao kama wazazi katika kuyashika maadili yenyewe ili wawe mfano kwa watoto wao. Wakati huo huo, juhudi zielekezwe katika kuandaa mitaala ya maadili kwa wanafunzi mashuleni na vyuoni ambapo watoto watafundishwa somo la maadili, huku kanisa likisimamia majukumu ya maadili ya kiimani. Ili tuweze kuona matokeo mazuri lazima tuanze na watoto na vijana wa kizazi kipya ambao muda si mrefu watakuwa wanakabiliwa na changamoto za uongozi wa kizazi kinachomaliza muda wake duniani. Katika vizazi vilivyopita, kila taifa ambalo liliweka kipaumbele kwa malezi ya kimaadili, limetoa viongozi bora ambao wameweka rekodi ya uongozi katika historia na wanakumbukwa mpaka hivi leo. Mchakato Wa Kuandaa Uongozi Wa Kizazi Kipya Kama nilivyotangulia kusema hapa juu kuwa suala la uongozi linahusiana na kipaji, hapa nataka kusisitiza kwamba, lazima kuwepo kwa mchakato mahsusi wa kuvibaini vipaji vya uongozi. 97

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
SACCOS_Traing_Guide
constitution of kenya review commision ckrc ... - ConstitutionNet
100%
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet
verbatim report of constituency public hearings ... - ConstitutionNet
Finding The Pleasure Free Ebook
constitution of kenya review commission ckrc ... - ConstitutionNet
GOLDINI