08.06.2013 Views

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe (Mathayo 24:32-

35).

Yesu hakutaka wanafunzi Wake wanaswe bila kufahamu – na hilo ndilo jambo la

msingi katika Mafundisho ya pale Mlima wa Mizeituni. Wangejua kwamba “yuko

malangoni” baada ya kuona “mambo hayo yote” – dhiki duniani kote, kurudi nyuma kwa

watu, kutokea kwa manabii na makristo wa uongo, tangazo la mpingakristo kwamba ni

Mungu, na kutiwa giza jua na mwezi pamoja na kuanguka kwa nyota, wakati karibu na

kurudi Kwake.

Ila, baada tu ya kuwaambia kuhusu ishara zitakazotangulia kuja Kwake kwa miaka

michache, au miezi au siku, aliwaambia sasa wakati hasa wa kurudi Kwake ungebakia

kuwa siri.

Walakini kwa habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika

walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake (Mathayo 24:36).

Mara nyingi andiko hili linatajwa kinyume cha mantiki yake! Kwa kawaida linatajwa

ili kuunga mkono dhana kwamba hatuna habari Yesu atarudi lini, kwa sababu anaweza

kurudi wakati wowote na kunyakua kanisa. Lakini katika mantiki yake, Yesu

hakumaanisha hicho. Alikuwa ndiyo kamaliza kuhakikisha kwamba wanafunzi Wake

wangekuwa tayari kwa ajili ya kurudi Kwake kwa kuwaambia ishara nyingi ambazo

zingetokea muda mfupi tu kabla ya kurudi Kwake. Sasa anachowaambia ni kwamba, siku

hasa na saa havitafunuliwa kwao. Tena, Yesu hasemi juu ya kuja Kwake mara ya kwanza

kabla ya kipindi cha Dhiki ya miaka saba kuanza, wakati ambapo kanisa lingenyakuliwa,

bali kuhusu kurudi Kwake wakati wa mwisho au karibia mwisho wa Dhiki. Hilo halina

matatizo ukitazama mantiki vizuri.

Je, Kurudi Kwake Hakujulikani Kabisa?

Hoja ambayo mara nyingi hutumika dhidi ya Unyakuo kutokea karibu au wakati wa

mwisho wa Dhiki ni kwamba kurudi kwa namna hiyo kusingekuwa kitu kisichojulikana

kama Yesu alivyodaiwa kusema, kwa sababu kurudi kwa namna hiyo kungetazamiwa

kwa matukio ya Dhiki. Lazima kuwe na Unyakuo kabla ya dhiki, la sivyo waamini

wasingehitaji kuwa tayari na kukaa macho kama Maandiko yasemavyo wanapaswa

kuwa, maana watajua ni miaka saba au zaidi kabla ya Yesu kurudi.

Ila, hoja hii inapingwa na ukweli kwamba lengo kuu la Mafundisho ya Yesu pale

Mlima wa Mizeituni lilikuwa ni kuhakikisha kwamba wanafunzi Wake wawe tayari kwa

ajili ya kurudi Kwake wakati au karibu na mwisho wa Dhiki, naye aliwafunulia ishara

nyingi tu ambazo zingetangulia kuja Kwake. Mbona Mafundisho ya Mlimani yamejaa

mashauri mengi sana kwamba watu wawe tayari na kuwa macho, ingawa Yesu alijua

kwamba kurudi Kwake kuko mbele miaka mingi sana baada ya kusema maneno hayo?

Bila shaka ni kwa sababu Yesu aliamini kwamba Wakristo wanahitaji kuwa tayari na

kuwa macho hata ingawa kurudi Kwake bado kuko miaka mingi mbele. Mitume ambao

hayo yote yatafanyika katika kizazi kimoja, au pengine kwamba taifa la Wakristo (au Wayahudi basi)

lisingepita mpaka mambo hayo yote yatimie.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!