08.06.2013 Views

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Hapa tena, kitu ambacho Yesu anajali ni kwamba wanafunzi Wake wawe tayari kwa

ajili ya kurudi Kwake. Hicho ndicho kilisababisha yote aliyosema kabla ya hapa na baada

ya hapa, katika mafundisho Yake. Maonyo Yake mwengi kwamba wawe tayari na

wakeshe si kwamba ni kwa kuwa kurudi Kwake kutakuwa kwa kushtukiza, bali ni ishara

ya jinsi ambavyo itakuwa vigumu kwa sababu ya upinzani wa wakati wenyewe,

kuendelea kuwa macho na kuwa tayari. Basi, wale wanaotarajia Unyakuo kabla ya Dhiki,

wakati wowote, wanaodhani kwamba wako tayari kuliko Wakristo wengine, wanaweza

wasiwe tayari kwa uhalisi kabisa, kwa kile kinachokuja. Kama hawatazamii dhiki yoyote

na wajikute katikati ya mateso ya dunia nzima, wakati wa utawala wa mpingakristo,

jaribu la kuanguka linaweza kuwazidi nguvu. Afadhali kuwa tayari kwa kile

kinachofundishwa na Maandiko kwamba kitatokea.

Halafu tena – kama ungemwuliza Petro, Yakobo au Yohana kwamba walitazamia

kumwona lini Yesu akirudi, wangekwambia kuhusu ishara hizo zote ambzo Yesu

aliwaambia zingetokea, kabla ya kurudi Kwake. Wasingetazamia kumwona kabla ya

kipindi cha dhiki, au kutokea kwa mpingakristo.

Mwivi Usiku

Ona kwamba hata mfano wa Yesu wa “mwivi usiku” uko katika mantiki ya Yeye

kudhihirisha ishara nyingi ambazo zingewasaidia wanafunzi Wake wasinaswe ghafula

kwa kurudi Kwake. Basi, mfano huo hauwezi kutumiwa kisahihi kuonyesha kwamba

hakuna mtu anayeweza kuwa na wazo lolote kuhusu Yesu anarudi lini.

Paulo na Petro walitumia mfano wa Yesu wa “mwivi usiku” walipokuwa wanaandika

kuhusu “siku ya Bwana” (ona 1Wathes. 5:2-4; 2Petro 3:10). Waliamini huo mfano

ulikuwa na maana kwa habari ya Yesu kurudi kwa ghadhabu wakati wa au mwisho wa

Dhiki ya miaka saba. Ila, Paulo aliwaambia hivi wasomaji wake: “Bali ninyi, ndugu,

hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi” (1Wathes. 5:4). Yeye alitafsiri kwa

usahihi mfano wa Yesu, akitambua kwamba wale walio macho na makini kuona zile

ishara, na wenye kumfuata Yesu kwa utiifu, hawakuwa gizani mpaka kuja kwa Kristo

kuwapate kwa ghafula. Kwa watu namna hiyo, Yesu asingekuja kama mwivi usiku. Ni

wale walio gizani tu ndiyo wangeshtushwa – na ndivyo Yesu alivyofundisha. (Ona vile

vile matumizi ya Yesu ya maneno “mwivi usiku” katika Ufunuo 3:3 na 16:15. Hapo

anatumia maneno hayo kusema juu ya kuja Kwake kwenye vita ya Har-magedoni.)

Kuanzia hapa na kuendelea katika Mafundisho Yake ya pale Mlima wa Mizeituni,

Yesu alirudia kuwaonya wanafunzi Wake kuwa tayari kwa ajili ya kurudi Kwake. Hapo

hapo akawaambia pia jinsi ya kuwa tayari, aliposema mifano kuhusu mtumwa asiyekuwa

mwaminifu, kuhusu wanawali kumi, na kuhusu talanta, na baadaye akatabiri hukumu ya

kondoo na mbuzi (yote inafaa kusomwa). Katika hiyo mifano yote, aliwaonya kwamba

jehanamu ilikuwa inawasubiri wale wote wasiokuwa tayari kwa ajili ya kurudi Kwake

(ona Mathayo 24:50, 51; 25:30, 41-46). Njia ya kuwa tayari ni kupatikana ukifanya

mapenzi ya Mungu, wakati Yesu atakaporudi. 10

10 Ni dhahiri kwamba uwezekano wa wanafunzi wa Yesu kutokuwa tayari wakati wa kurudi Kwake

ulikuwepo, maana aliwaonya sana kuhusu hilo. Kama aliwaambia kwamba adhabu ni hukumu ya milele

kwa kutokuwa tayari kwa sababu ya dhambi, basi ilikuwa inawezekana kwao kupoteza wokovu kwa

sababu ya dhambi. Hili linapaswa kutupa angalizo juu ya umuhimu wa utakatifu, na tutambue kwamba ni

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!