08.06.2013 Views

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

Mchungaji Afanyaye Watu Kuwa Wanafunzi Sura Ya Ishirini Na Tisa ...

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

linatufanya tuseme kwamba wamenyakuliwa, hawajauawa – ni waaminio

waliokombolewa kutoka katika dhiki ile kuu.

Ni sahihi kudhani kwamba Unyakuo utatokea wakati fulani mara tu baada ya matukio

hayo ya mbinguni yanayotajwa katika Ufunuo 6:12 na 13, kwa sababu yanafanana na

yale aliyosema Yesu katika Mathayo 24:29-31. Ila, hatuna ishara iliyo dhahiri kuhusu

wakati wa kutokea hayo mambo yanayotajwa katika Ufunuo 6:12 na 13, katika kipindi

cha dhiki ya miaka saba. Kama matukio yanayotajwa katika Ufunuo 6:1-13 yanafuatana,

na kama Unyakuo unatokea mara tu baada ya 6:13, hilo linatuongoza kuamini kwamba

Unyakuo hautatokea mpaka baada ya kufunuliwa kwa mpingakristo (ona 6:1, 2), na vita

ya dunia nzima (ona 6:3-4), njaa (ona 6:5, 6), kufa kwa robo ya watu wa duniani kwa

vita, njaa, magonjwa na wanyama wakali (ona Ufunuo 6:7-8), na wafia dini wengi

kupatikana (ona Ufunuo 6:9-11). Hakika matukio hayo yote yanayotajwa yanaweza

kutokea kabla ya kumalizika kipindi cha Dhiki cha miaka saba, lakini pia yanaweza kuwa

ndiyo yatakayotokea katika kipindi chote cha miaka saba cha dhiki, na Unyakuo kuwa

mwisho kabisa.

Wazo la Unyakuo kutokea kabla ya mwisho wa miaka saba ya dhiki linaongezewa

uzito na kweli kwamba Kitabu cha Ufunuo kinaeleza juu ya makundi mawili ya hukumu

saba, baada ya Ufunuo sura ya 8, kama ifuatavyo: “hukumu za baragumu” na “hukumu

za vitasa”. Hizi za vitasa zinasemekana ndiyo mwisho wa ghadhabu ya Mungu (ona

15:1). Lakini, kabla ya hukumu hizo za vitasa kuanza, Yohana anawaona “wale wenye

kushinda, watokao kwa yule mnyama na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake,

wamesimama kandokando ya hiyo bahari ya kioo” (15:2). Hawa watakatifu washindi

yawezekana walinyakuliwa. Lakini tena, yawezekana walifia imani yao. Maandiko

hayaelezi. Tena, hatujui kama mambo ya 15:2 yana uhusiano wowote na maelezo ya

mambo yanayotajwa hapo.

Kweli nyingine inayopatikana katika Ufunuo, yenye kuweza kuongezea uzito kwenye

wazo la Unyakuo kutokea kabla ya mwisho wa miaka saba, ni hili: Wakati wa “hukumu

ya baragumu” ya tano katika Ufunuo 9:1-12, tunaambiwa kwamba nzige wenye kuuma

wataruhusiwa kuwadhuru wale tu “wasiokuwa na muhuri ya Mungu kwenye vipaji vya

nyuso zao” (9:4). Watu pekee tunaoambiwa watakuwa na muhuri ni Waisraeli mia na

arobaini na nne elfu (144,000) tu (ona Ufunuo 7:3-8). Basi inaonekana kwamba waamini

wengine wote itabidi wanyakuliwe kabla ya baragumu hiyo ya tano ya hukumu;

vinginevyo, hawataepuka nguvu za hao nzige waumao. Tena, kwa sababu nzige hao

watawaumiza watu kwa miezi mitano (9:5, 10), inadhaniwa kwamba ni lazima Unyakuo

utokee miezi mitano kabla ya kumalizika kwa miaka ile saba ya Dhiki.

Kuna jinsi ya kufafanua hoja hizo. Pengine kuna wengine waliotiwa muhuru ambao

hawatajwi katika kitabu cha Ufunuo. Vyovyote vile, kama hili linathibitisha kwamba

Unyakuo utatokea kabla ya hukumu yabaragumu ya tano, pia linaonyesha kwamba kuna

kundi moja la waamini ambao hawatanyakuliwa kabla ya kuachiwa kwa hao nzige

waumao – wale Waisraeli mia na arobaini na nne elfu (144,000) waliotiwa muhuri. Ila,

watakuwa na alama ya kuwalinda wasipatikane na ghadhabu ya Mungu, itakayokuwa

inatolewa kwa njia ya nzige hao waumao.

Tuhitimishe. Cha kusema ni kwamba bila shaka Unyakuo utatokea karibu na mwisho

au mwishoni kabisa mwa ile miaka saba ya Dhiki. Waamini wasihofu kuhusu ghadhabu

ya Mungu, lakini pia wawe tayari kwa ajili ya mateso makali na hata kufa kwa ajili ya

imani yao.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!