11.07.2015 Views

Mwili Mmoja - Norges Kristne Råd

Mwili Mmoja - Norges Kristne Råd

Mwili Mmoja - Norges Kristne Råd

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Afrika Kusini Angola Botswana Denmark Finland Iceland Lesotho Malawi Msumbiji Namibia Norway Swaziland Sweden Tanzania Zambia ZimbabweUSHIRIKIANO WA MAKANISA YA NORDIC – FOCCISA<strong>Mwili</strong><strong>Mmoja</strong>kitabu cha 2Ukimwi na Jamii Inayoabudu


<strong>Mwili</strong> <strong>Mmoja</strong>KITABU CHA 2Ukimwi na Jamii inayoabuduMafunzo ya Biblia, Liturjià na Hadithi Binafsi Kutoka Kusini na KaskaziniUSHIRIKIANO WA MAKANISA YA NORDIC – FOCCISAUTANGULIZI 1


UTANGULIZIKuabudu Katika Namna Tofautidenmark Hali Halisidenmark Yubile ya Maono kwa Kanisazambia Kuvunja Ukimya na Fedhehanorway Unyanyapaa na Utunorway Mahali Salama kwa Mazungumzonorway Biblia Kitabu Kitakatifuzambia Kujifunza BibliaKANISAzambia Kanisa Lenye HurumaMSUMBIJI Kuwakumbatia Waliosahauliwadenmark Kutengeneza Jumuia Mpya Zenye Tumaininorway Kuwa <strong>Mwili</strong> <strong>Mmoja</strong>norway Mwanamke Aliyekuwa Apigwe Mawedenmark Pumziko Lenye Tumainiujinsia wa binadamuzambia Ubaba, Jinsia na Yesuzambia Ujinsia – Kipawa na Wajibunorway Nani Anayediriki Kurusha Jiwe la Kwanzadenmark Maana, Kifo na UpotevuSURA ZA MUNGUdenmark Imanizambia Matendo ya Uponyaji ya Yesudenmark Sura Nne za Munguzambia Mungu Anayesamehezambia Mungu wa Uumbajinorway Mwanamke Mlemavuzambia Hakuna Hukumunorway Utaratibu wa Ibada Kwa Vituodenmark Juu ya Ukaribudenmark Mungu anayetugusadenmark Kuwasha Mishumaadenmark Sala Siku ya UKIMWI Duniani3561012141618212224262930333436404344464849505254586062642 UTANGULIZI


Kuabudu KatikaNamna TofautiNA JAPHET NDLOVU, BARAZA LA MAKANISA LA ZAMBIAJAN BJARNE SØDAL, JUMUIA YA KIKRISTO YA NORWAYBIRTHE JUEL CHRISTENSEN, DANCHURCHAID – DENMARKELIAS MASSICAME, JUMUIA YA KIKRISTO YA MSUMBIJITangu mwanzo Wakristo wengi wamechukulia kuabudu kamatendo muhimu la utambulisho wao. Wanathiolojia wengi waKikristo wamemfasili binadamu kama homo adoran: yaani kiumbeambaye asili yake ni kuabudu. Hii ina maana kwambakumwabudu Mungu ndiyo kiini cha kuwa mwanadamu. Ni katikaibada zetu – roho za maisha yetu katika jumuia – tunapowezakuwasiliana na kumleta Mungu katika maisha binafsi.Kama sehemu muhimu katika mradi wa pamoja juu yamtazamo wa kithiolojia kuhusu VVU na Ukimwi wa Jumuiaza Kikristo Kusini mwa Afrika na Nchi za Ulaya za Nordic –FOCCISA – tumekuwa tukishughulikia masuala ya Liturjia nakujifunza Biblia. Katika Biblia na kupitia mafunzo ya Biblia nakwa kutengeneza majaribio kiliturujia, tumegundua vyanzo namsukumo mpya. Hii inaonyesha uhitaji wa njia sahihi ambaokwa pamoja unaleta neno la Mungu katika maisha yetu, katikamtazamo wa VVU na Ukimwi na katika uhalisi wa changamotona mahitaji ambayo ugonjwa umeleta.Liturjia ya kanisa imejengeka katika uzoefu wa jumuia fulani.Kwa ujumla jumuia hizi zinaonyesha uzoefu tofauti na hali zakimaisha – vijana na wazee, matajiri na masikini, wenye afyana wagonjwa, wanaume na wanawake, wenye VVU na wasio naVVU, familia na waseja, watu wanaoteseka kwa kukosa amanina walio na amani, wale wenye furaha na wale wenye huzuni.Liturjia ya kanisa inaonyesha ibada ya jumuia yote, kwa hiyokuabudu lazima kuwe ni kwa kubadilika ili kuweza kugusachangamoto mbalimbali zinazowakabili wanadamu. Ni lazimapia kuwe na majumuisho: ili kwamba kwa kuongea kuhusu aukumwelezea Mungu, ni lazima tuelewe umuhimu wa kukwepaunyanyapaa au hali za kutengana na lugha tunazotumia. Tumejaribukuchunguza kanuni hizi katika liturjia na mafundishoyetu ya Biblia, ili kufanya zikubalike kadiri inavyowezekana.Tumefanya maamuzi yakini kutengeneza kitabu chenyeshuhuda binafsi kutoka kwa watu waishio na VVU na Ukimwi,kutoka Kaskazini na Kusini mwa dunia. Shuhuda hizi zinaamshamaswali muhimu juu ya kutambua, au kuelewa upya, imaniUTANGULIZI 3


utanguliziya Ukristo. Matumaini yetu ni kwamba kitabu chote kitatoasehemu ya jibu – angalau uradhi wa kuanzisha kwa pamojaLiturjia na mafunzo ya biblia, kama sehemu ya changamotoambayo makanisa yanapitia dunia nzima, katika nyakati hiziza Ukimwi.Ushirikiano Kati ya Kusini na KaskaziniMradi huu ulitengenezwa na Jumuia tano za nchi za Nordicna nchi kumi na moja za Kusini mwa Afrika chini yakivuli cha ushirikiano wa Kikanisa (NORDIC-FOCCISA),ulipewa msukumo na makanisa nchini Zambia, Msumbiji,Norway na Denmark ikiwa na lengo la kukuza mtazamowa kithiolojia katika masuala yaliyosababishwa na maambukiziya VVU.Katika kitabu hiki, utajua njia za kutumia nyakati za Ukimwi,Liturjia, mafunzo ya biblia, ibada au hali zozote. Njia hizini pamoja na shuhuda binafsi, mafundisho ya biblia, liturjia,mashairi na fikra mbalimbali. Hizi zimeandikwa au kuandaliwana watu waishio na VVU au Ukimwi au wanaohusiananao kwa karibu na ambao wanatambua kuwa rasilimali zilizopohazilingani na mahitaji ya makundi yao au makanisakwa wakati huu.Kitabu hiki kimelengwa kwa watu katika jumuia za chini(mitaa), katika kaskazini na kusini pia, walio na majukumuya kufundisha, kuhubiri, kuabudu na kazi nyingine za mikusanyikoya waumini. Uhitaji ni mkubwa, katika utoaji waelimu ya Biblia na liturjia kwa ajili ya matumizi katika wakatiwa VVU na Ukimwi. Hata hivyo, desturi zetu kiliturjia ziko tofautisana, na hatujifanyi kuwa makusanyo yaliyomo katikakitabu hiki yanatosha sana kuelezea mahitaji yote yaliyopo.Badala yake mradi huu unaonyesha uzoefu wa Kikristo uliotofauti kiasili kuhusiana na VVU na Ukimwi.Dhamira TatuMalengo, kama ilivyo katika kitabu cha kwanza katika mtiririkohuu, yapo katika dhamira tatu kama zilivyoainishwa na uzoefuwa VVU.1) Kujumuisha Kanisa2) Kujamiiana3) Mfano ( au sura ya) wa MunguTulichokifanya ni kuleta pamoja viini vya dhamira yetu kwakutumia vipengele vya Biblia, na kujiuliza namna Liturjia auelimu ya Biblia inavyoweza kuwa katika mtazamo wetu – kamailivyoonyeshwa katika kitabu cha kwanza – juu ya kujamiiana,kanisa na mfano au sura ya Mungu. Kwa hiyo, maandiko,yanatofautiana kutokana na hali halisi ya eneo yalipoandikwa.Hatuonyeshi kuwa hizi ni njia pekee ambazo maandiko yaBiblia yanaweza kutumika. Hii itatofautiana kutokana na halina mazingira ya wale wanaoyatumia. Malengo yamekuwa nikuwa makusanyo haya ya maandiko yaonyeshe umoja kadiriya namna tulivyoitwa: Hali ya kuwa katika namna tofauti yamwili mmoja wa Kristo tunaouita Kanisa.Unaweza kutumia maandiko haya kadiri unavyotaka. Unakaribishwakuchagua, kuchukua au kubandika katika namnaunavyoona inafaa katika desturi na mazingira yako.Tunatumaini kuwa maandiko haya yatahamasisha na kukuzamitazamo zaidi, itakayosababisha kuanzisha kwa liturjia mpyana elimu ya Biblia katika masuala yanayohusu VVU na Ukimwi.Zaidi ya yote ni matumaini yetu kuwa utaratibu tulioutumiakatika kutoa maandishi haya, utapanda mbegu ndogo ambazozinaweza kusababisha kuanzishwa kwa mikusanyiko ya pamojamakanisani, kidunia, kitaifa pamoja na kimitaa au kifamilia.Kokote tunakotoka, vyovyote tulivyo, iwe tuna VVU au hatuna,tunategemeana ili kuwa kama tulivyo kwa namna Mungualivyodhamiria tuwe – <strong>Mwili</strong> <strong>Mmoja</strong> katika Kristo.4 UTANGULIZI


Hali Halisi- Nina VVUNinaogopa....Ninajiogopa mimi mwenyewe, ninauogopa ugonjwa nilionao.-Kwani itatokea lini, itatokea lini?Kifo cha taratibu, au labda cha haraka na bila maumivu?Watu...Wale wasionionyesha upendoWale wasionipa ulinzi ninaohitaji.Tatizo la kifedha...Ambapo hakuna msaada unaoweza kuonekanaHufanya maumivu kuwa makali zaidi.Wote wananitazama na kutikisa vichwa vyao...“Hata hivyo unaenda kufa”“Hatujui mbele hali itakuwaje”“Una bima ya maisha?”“Sithubutu kukupenda, Je kama ukifa na kuniacha!”“Je ukiniambukiza?”Ninataka kujiua...Nitafunga kamba kuzunguka shingo yanguNitajirushaNitameza vidonge,lakini labda kesho,katika makutano ya barabaraau ndege ya kijeshi kuangukia katika sebule yanguHapana....Nimetahadharishwa.Tahadhari ambayo watu wachache tu hupata.Je inanifanya mimi kuwa wa pekee?Kitu cha pekee?Inanifanya niogope- lakini pia mwenye furaha.Imenifundisha kupenda maishaNa kuyathaminiBadala ya kuishi tu.Sasa nahitaji kuishiNahitaji kuujua upendo.Nahitaji kujua usalama.Niamini....Nifanye msikivuSikiliza sauti yangu ya ndani.Sauti.Hufanya ninyenyue kichwa changu juuNa kutabasamu juu ya hatima yangu.Inanifanya niishi kwa matumainiNa kuniambia ni vyema,maisha yangu yatakuwa mafupi kuliko ya wengineLakini labda mazuri zaidi?Ninatumaini....DORTHE, AISHIE NA VVU, DENMARKUTANGULIZI 5


Ushuhuda Kutoka Kwa MhangaWa Siku NyingiYubile yaNA PREBEN BAKBO SLOTHUkiwa kijana unatakiwa kuangalia mbele, kutengeneza mipango,kuwa na maono na kuota ndoto. Kuangalia mateso na kifocha awali kwa kawaida hatuvioanishi na ujana. Lakini kuwa naVVU katika umri wa miaka 24 hubadilisha mtazamo wako. Kwakuongeza, katika maongezi yetu, daktari aliniambia nina kamamiaka mitano iliyosalia ya kuishi. Wakati ujao ukawa ni tishio,kupanga kukawa hakuna maana, maono ikawa ni ukwepaji,ndoto – kufikirika na matumaini ya uongo.Kuadhiriwa na mtu ambaye hakujali kukuambia ukweli, ilikuwani pigo langu kubwa kuwaamini watu wengine. Nitawezajekuwaamini wengine, wakati imani yangu imesalitiwa kabisakiasi cha kunipa virusi hatari? Nitaurudishaje ujasiri wangu katikamaamuzi yangu mwenyewe? Nitaweza tena kujitegemeana kujisimamia maisha yangu mwenyewe? Maswali haya yalisababishakujidharau na hisia ya kutojijali na iliwavunja mioyowatu wengine.Wakati huo wafuasi wengine wa mrengo wa kulia wa kanisawalikuwa wakihubiri kuwa VVU na Ukimwi ni adhabukutoka kwa Mungu juu ya maisha ya dhambi. Nikiwa nimepoozatayari na mshtuko wa kuhukumiwa kifo, haikuwa rahisikutoyaweka mahubiri yao moyoni, kupokea hukumu hiiya Mungu mimi binafsi, kujitwika mabegani mwangu na kujaribukukubali namna hii ya hukumu takatifu ya ajabu. Nandivyo ilivyokuwa mimi, na alama ya kifo ya VVU juu yangu,iliyobandikwa na hasira ya Mungu, katika hali ya mgogoro(wa ugonjwa) unaoandamwa na aibu na kujihukumu, nilionahaiwezekani kutaka msaada kutoka kwa mtu mwingine. Sikudhubutukumwendea yeyote kumshirikisha taabu zangu,kwa sababu nilikwisha ridhia kuwa kila mtu hatonijali, kamavile Mungu alivyokwisha fanya.Huwezi kumdanganya Mungu, lakini watu unaweza kujaribu.Matokeo yalikuwa ni kuishi miaka miwili na siri yangu moyoni.Miaka miwili ya mateso kisaikolojia, kiroho na kimhemuko. Miakamiwili ya kudanyanya, visingizio na kunyamaza. Miaka miwiliiliyonichukua mbali, mbali sana na marafiki na familia yangu,kwenye baridi na giza la upweke. Nililikimbia kanisa ambamonilikuwa mshirika, kwa kuwa nilipambana na kutengwa.6 UTANGULIZI


utanguliziMaono Kwa KanisaDenmarkMfano Mpya wa MunguIlikuwa ni baada ya miaka miwili ya kwanza nilipothubutu kutafutamsaada, kujihatarisha kwa kuwa wazi kuhusu hali yangukiafya, kujua kama VVU ni adhabu kutoka kwa Mungu na kufikiriamimi kama mfano wa Mungu. Mungu aliongea nami pia,kwa kutumia picha zilizoniambia kwa uwazi kuwa ninawezakutoka kanisani, lakini Mungu hataniruhusu niondoke. Nilipatanyumba ya kiroho katika kusanyiko dogo mjini Copenhagen.Hapa nilipewa hamasa, walinielewa, walinikubali na kunijali.Nilikutana na watu wengine wenye Ukimwi, hali iliyoanzishamchakato wa uponyaji ambao haujamalizika mpaka leo, miakakumi na tano. Nilijua kuwa hakuna kitu, hata VVU na ukimwi,kinachoweza kunitenganisha na Upendo wa Mungu (Warumi8:38). Katika mazingira ya kushirikishwa na kupendwa hisia yahukumu na aibu haraka ilitoweka.Mahubiri kuhusu upendo wa Mungu usio na masharti naushirika unaojali uliumba sura mpya ya Mungu kwa ajili yangu.Sura ambayo niliweza kujiona na kupata nguvu. Taratibu imaniyangu kwa watu wengine na kwangu ilianza kujengeka.Mchakato kufikia kujiheshimu na ujasiri ndani yangu na kwawengine ulichukua miaka mingi na ulifanikishwa kwa uvumilivu,upendo na uelewa wa watu wote ndani na nje ya kanisa, nauzoefu wa hali inayojirudia ya kutojisikia kuachwa na MunguUzima Huuliza MaanaMaswali mengine mengi na matatizo yameacha makovu katikamiaka kumi na nane iliyopita. Woga wa kujisikia mdhaifu, wogawa maumivu, woga wa kifo, hali ya kujisikia kukata tamaa nakutokuwa wa maana baada ya kupoteza marafiki wengi nakuachwa, kutoamini maisha ya mbele nk. Wakati mwingineimekuwa ni vigumu kuwa na malengo hata ya muda mfupi,bila kutaja kuwa na maana katika maisha katikati ya maumivu,hasara na mateso. Ni katika miaka minne tu iliyopita nimetambuakuwa kama maisha na kifo yana maana, basi matesolazima yana maana pia. Bila kuamini katika maana, au uhiariwa kutafuta maana, ningelikwisha kata tamaa, ningeona kilakitu hakina maana na kumegeka kiroho na kiakili. Kwa hakikani uzima pekee ndio huuliza maana na ni lazima nijibu. Nijibukwa kutafuta na kupata maana, maana katika hatua tofauti katikamaisha ziletazo majibu.Kuzungumza na Mungu, maombi na kumtafakari, katika kuangaliamaisha yangu ndani ya injili na kitabu cha Zaburi, kukutanikana kuzungumza katika kanisa na kukutanika na wenginewalio na ukimwi imekuwa ni vyombo vya Mungu katika mchakatohuu wa uponyaji.Jumuia ya kanisa na kukutana na wakristo wengine imekuwani msaada usio na kifani. Wamesaidia kujenga daraja kutokamauti hadi uzima, kutoka katika kuvunjika hadi kutovunjika nakutoka kujichukia hadi upendo.Kanisa lina UkimwiMpambano wangu na kanisa na ujumbe wake, mara baada yakuambukizwa, ilikuwa ni kusikia ujumbe wa kuhukumiwa. Lakini“ kuhukumu ni kuficha upendo wa Mungu”, kama mchungajiCarina Wøhlk alivyosema wakati fulani katika siku yaukimwi duniani. Ni kwa nini kanisa, au angalau sehemu yake,ni msemaji wa hukumu? Ninaona mifano mingi ndani ya Bibliakuwa umbo halisi la tabia ya Mungu juu ya wanyonge, walio katikahatari na waliotengwa ni kuwaingiza kundini, kuwapendana kuwajali. Na kama ulivyomtendea mmoja wa wanafamiliayangu, umenitendea mimi – kwa mema au mabaya.Kwa Paulo kulinganisha kanisa kama mwili katika akili, wakatimwingine huwa ninaona kama baadhi ya wanathiolojia na watafsiriwa maandiko ni meno, nami ni sehemu ya ute ambaomwili unataka kuutoa! Lakini wakati sehemu moja ya mwiliina Ukimwi, mwili wote huumia, na kwa hiyo kanisa lote linaukimwi. Kanisa ni lazima lionyeshe huruma kwa kujali, kamalinataka kuishi kufuatana na mtazamo wa Paulo. Kama halitakikufanya hivyo, basi lijiite kitu kingine, kwa sababu limekuwachanzo cha kuvunja moyo, kukatisha tamaa na mateso.UTANGULIZI 7


Kukosa MakaziNimekuwa nikiwa na kanisa, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Denmark,kama nyumba yangu ya pili. Kwa namna ile ile nilivyoifahamunyumba yangu mwenyewe, nilizoea maisha ya kanisani,ibada na lugha zake na nilijisikia kuwa nyumbani. Lakini nilipogunduakatika moja ya nyumba zangu siwezi kusema maumivuna mateso yanayohusiana na kuishi na VVU, ghafla nilijisikiakutokuwa nyumbani katika nyumba yangu mwenyewe.Wakati mwingine maumivu na mateso yamekuwa ni makalikiasi kwamba nimelazimika kuzungumza na mtu yeyote, nawakati imani ya ujasiri wangu inapokutana na ukimya na chukimbaya iliyofichika, najisikia kukosa makazi katika nyumbayangu mwenyewe. Ningejigawa. Kama ningeweza kujigawa ilikupata sehemu ya mwili wangu yenye afya, inayofanya vizuri,inayoheshimika, basi ingekuwa ni maumivu kidogo kuiachanyumba na kubakia kama ulivyo na ukiwa na maumivu – lakiniusiye na makazi.Kusikia wanafamilia yangu na washirika wa kanisa wakisemawamejisikia kudhalilika kwa sababu yangu iliniongezea hali hiiya kujisikia kutokuwa na makazi.Kanisa linapowakataa watu wenye VVU kwa namna hii, wanatakiwawawe na imani kubwa au uzoefu mkubwa wa dinivinginevyo wanaweza kumwacha kumwamini Mungu. Lakinisi matokeo yanayojulikana kwa kanisa.Kuwa Mtu Mkamilifundani ya Nyumba ya MunguMungu aliumba watu wakamilifu. Roho, nafsi na mwili. Nakwa hiyo ndani ya nyumba ya Mungu mtu mkamilifu lazimaaangaliwe na pia kumjali. Kwa asili, hii inajumuisha ushauri wakichungaji, uongozi wa kiroho, maombi nk. – lakini kwa mtumwenye magonjwa yanayonyanyapaliwa kama VVU na Ukimwi,haitoshi kujua tu kuwa unaweza kwenda kanisani na matatizoyako ya kiroho.Kanisa ni lazima litoe taarifa za jumla na zisizo na mwishokuwa watu wenye VVU wanakaribishwa. VVU, Ukimwi, kujamiiana,unyanyapaa nk, ni lazima kila wakati kuwa kwenyeajenda za kanisa – siyo tu kuihusianisha na Siku ya UkimwiDuniani.Kwa bahati ninaona makanisa katika sehemu nyingine za duniaambayo yanaishi nje ya maono yao ya Ufalme wa Mungu,katika ibada zao na jumuia zao. Lakini kukiwa na watu millioniarobaini duniani wenye VVU hili ni hitaji la muhimu. Katika halihii kanisa lazima lijitoe katika fikra zilizozoeleka na kupooza,kunyanyasa na thiolojia ya matengano na mila iliyozoeleka.Kama tawi la mwaka wa sherehe wa Agano la Kale – japo hililinaweza kuwa halijawekwa katika vitendo – kanisa linawezakutangaza mwaka wa sherehe, wakati wa sherehe na mahalipa sherehe.Itaweza kuleta furaha na uhuru kutoka katika kujihukumu naaibu – kwa kuonyesha kujali na kukubali watu walio na VVU.Sherehe itahusisha maombi kwa ajili ya msamaha kwa miakamingi ya kuzembea kufanya hivi. Kutakuwa sherehe kwa ajiliya jamuia ambayo kila mtu huchukuliwa kwa usawa: ambapobusara, uzoefu na hekima ya watu wenye VVU inathaminiwana kutumiwa. Sherehe kwa ajili ya watu ambao wamewekwahuru kutokana na mateso yaliyowafanya kupooza. Sherehekwa sababu tunaweza kuanza kuishi maisha yenye ubora.Sherehe kwa kuiona heshima ya watu wenye VVU ikikua nauwezo wao ukionekana kwa faida ya kila mtu.UjasiriWapi kanisa litapata ujasiri wa kufanya haya yote? Nadhaniinatubidi tuanze kuchunguza hisia zetu – na si hizia zetu zamapenzi tu. Pia maumivu, huzuni, simanzi na hasira vinawezakuwa hali ya mabadiliko ya hali ya akili inayoweza kutuunganishana watu wengine na jamii zinazotuzunguka. Ni lazimatuchunguze mahitaji ya watu wenye VVU, tusikilize maoni yaona tutafute njia na namna ya kuyatatua.Lazima tuombe kwa ajili ya ushujaa, kumtumaini Mungu nasisi wenyewe pia, kwa ajili ya imani ambayo roho wa Munguatatupa ili kufanya maono ya sherehe ya kumbukumbu itimie:chumba chenye wingi wa matarajio maishani na uhuruna matumaini, pamoja na kuta zenye upendo, kujali, heshimana imani.Kama kazi yote ya kanisa inaweza kwa moyo wa uwazi nakuaminiana, kama Kaka Roger wa Taizé alivyosema, basi watuwenye VVU hawataogopa kuliendea kanisa.8 UTANGULIZI


utanguliziTumainiTuna tumaini la mbingu mpya na nchi mpya, ambamo amani inaishi, ambapo pumzi ya Mungu ndiyo uzima na hutengeneza upindewa mvua wenye rangi na maumbo tofauti. Tuna tumaini la mbingu na nchi mpya, ambamo upendo unaishi, ambamo roho yaYesu Kristo itoayo uzima hukaa ndani ya watu na kati ya watu, ambamo mateso yameteswa, kifo kimekufa na kaburi li wazi kamalilivyokuwa asubuhi ya Pasaka. Tuna tumaini la mbingu mpya na nchi mpya, ambamo furaha inaishi, ambamo Roho Mtakatifu waMungu anaendelea kuumba upya ibada kwa wanadamu na tumaini lisilozuilika la maisha bila mipaka.Amen.<strong>Mwili</strong> wa UlimwenguLazima nitubu kwa sababu nadhani mara nyingi kanisa ni hodari kujiweka katika upande ambao unaegemeamawazo ya umma – na kwa kufanya hivyo linapuuza wajibu wa asili lililokuwa nao kama taasisi na nguvukwa ajili ya mema. Wajibu wa kanisa ulikuwa ni kuwaendea watu na kuonyesha kuwa inawezekana kufikiritofauti. Kwamba kulikuwa na njia mbadala namna ya kuwaangalia watu, na mtazamo wa uhai.Wewe ni Mkristo hasa, uliye na imani ya kutosha na ninajisikia mshirika halali wa kanisa, kama unaishi naukimwi kama ambavyo unaweza kuwa na kansa au kifua kikuu au ugonjwa mwingine wowote. Ninawezakuelewa kuwa baadhi ya watu wanajisikia kuwa kanisa haliwakaribishi – na hilo linanitia huzuni, kwa sababukanisa limepuuza wajibu wake na kukwepa jukumu lake la asili la kuwa mahali pa kukutanika wanyongena waliokataliwa na jamii.Kama kanisa linatakiwa kuwa la watu wote, lazima limjumuishe kila mmoja, hata wale wanaoishi na VVU– na wanaweza kupatikana katika makundi yote ya jamii. Hakuna anayekwepa. Kanisa la pamoja linawezakukusanya kila mtu katika mbawa zake. Hii ni changamoto kubwa kwa kanisa wakati huu, kuonyesha kwamapana namna linavyoweza kuwafikia wengi. Kuonyesha kuwa siyo mahali pa kukutana kwa wanaojulikanana wanathiolojia. Kwamba ni mahali ambapo watu wanaweza kuja na kupata faraja, nguvu na ongezekowanalohitaji kuwawezesha kukua kiakili, kiroho na kimwili. Hii inajumuisha si kwa wagonjwa tu, bali piakwa walio karibu nao.Tatizo la Ukimwi ni la kila mahali kwa watu wote. Hitaji hili la kibinadamu ndilo kanisa linatakiwa kulitimizana hakuna shaka kwamba hamasa ipo kutokana na amri ya Yesu kuhusu upendo. Kuna nafasi kwa ajiliyetu sote ndani ya maneno hayo na haitakiwi kuhukumiana sisi kwa sisi.USHUHUDA WA JESPER, ALIYEKUFA KWA UKIMWI, DENMARKUTANGULIZI 9


zambiaKupima na Kuishi kwa MatumainiKuvunja Ukimya na FedhehaNA JOY LUBINGA, MRATIBU WA DUARA ZA MATUMAINISiyo rahisi kukabiliana na ukweli kuwa karibuni au baadayenitakufa kwa sababu nimeathirika kwa ugonjwa usio na tiba.Japokuwa siku moja nilikuwa na ujasiri na kwenda kupima nanikaonekana nimeathiriwa na VVU.Mimi ni mjane wa miaka 52 ninayeishi na VVU. Nilipima mwaka2003. Nina watoto watano – wote wa kike- wana umri kati ya miaka3 hadi 13, na ninamwangalia mpwa wangu ambaye wazaziwake walikufa kwa Ukimwi.Mume wangu alichunguzwa na kuonekana ana kifua kikuumwaka 1998. Baadaye alionekana kuwa na homa ya uti wamgongo inayosababishwa na fangasi, na madaktari waliniambiaalikuwa na Ukimwi na angekufa wakati wowote au kuwa kichaa.Habari hii ilinifanya nitetemeke sana kwa sababu nilihisi kuwaninaweza kuwa na VVU. Siku moja nilipokuwa nimerudi nyumbanikutoka kazini, ninakumbuka watoto wangu walivyoniambiakuwa baba yao alikuwa hajaamka kutoka kitandani. Niliingiana kumuuliza jinsi alivyokuwa akijisikia. Aliangalia pembeni.Huu ulikuwa mwanzo wa ugonjwa wa muda mrefu, alikwendakila mara hospitali mpaka alipokufa tarehe 5 September 1998.baada ya kuambiwa alikuwa na kifua kikuu, alipoteza tumaini naalitumia dawa za kifua kikuu kwa muda mfupi. Ninahisi kuwa hiindiyo sababu iliyofanya afe mapema.Tangu hapo maisha yangu yaliendelea kama kawaida. Niliishina watoto wangu, na kuwasaidia kwa mahitaji ya msingi ambayowaliyahitaji kwa ajili ya shule. Haikuwa rahisi. Lakini nilijitahidikwa kiasi fulani. Wazo la kupima halikunijia kwa sababu sikuwana dalili za ugonjwa wowote.Kupima na Kuonekana NimeathirikaMwaka 2003 kitu fulani kilinitokea nikiwa ofisini mwangukilichonisumbua kwa kuwa sikukubaliana nacho. Hii ilikuwa nimwanzo wa maumivu yasiyoisha ya kichwa, kukosa hamu yakula na kupoteza uzito. Si kuwa na furaha na nilipoteza uzitoghafla. Nilionekana mbaya kwa sababu nilipata vipele miguunina usoni. Sikuweza kuvaa nguo fupi. Mpaka pale afya yanguilipoanza kuzorota ndipo nilipokumbuka madaktari waliniambiamume wangu alikuwa na Ukimwi. Hili lilinifanya niendekupima VVU.Kuonekana nimeathirika halikuwa jambo la kushtusha kwangu.Lakini lilikuwa ni pigo kubwa kwangu kukabiliana na ukwelikwamba sasa nilikuwa ninaishi na VVU. Kitu cha kwanzanilichofikiria ilikuwa ni kifo, na ukweli kuwa ningeweza kuachawatoto wangu wakiwa yatima. Wazo hili daima limeniletea huzunina mtu wa kwanza kumshirikisha habari hizi alikuwa nibinti yangu mkubwa. Tulilia pamoja na alinipa maneno mengiya matumaini na kunitia moyo.Baada ya hapo nilifanya vipimo vyote vya muhimu. Mwanzonikiwango changu cha chembechembe nyeupe za damu (CD4)kilikuwa 314 ambacho hakikuwa kibaya kutokana na muundowa Zambia. Lakini kwa sababu ya wasiwasi mwingi, zilishukana kuwa 119 katika muda mfupi – ndani ya mwezi mmoja hivi.Nilishauriwa kuanza matibabu ya kupunguza makali ya VVU nakurefusha maisha. Kwa kuwa matibabu haya yalikuwa ghali,niliamua kumshirikisha hali hii ngumu bosi wangu, Katibu Mkuuwa Baraza la Makanisa la Zambia. Alinisaidia kupata dawa kupitiaufadhili wa serikali. Kwa hakika nilisaidiwa. Nilipopimwa nakuonekana na VVU nilikuwa na uzito kwa kilo 51, lakini sasanina uzito wa kilo 90. Na chembechembe nyeupe za damu(CD4) zangu zimeongezeka na kuwa 470. Ninamwona daktarikila mwezi kwa ajili ya uchunguzi na kujitunza mwenyewe kwasababu ninajua hali yangu.Nimewashirikisha watu wengi hadithi yangu, si kwamba ninapendakuwa na VVU au ninaifurahia hali hii - lakini nimeona nimuhimu kuwatia nguvu wengine wanaojikuta katika hali kamailiyonikuta. Nimenyanyapaliwa na kukataliwa katika maisha. Lakinininajua kwamba Mungu ananipenda. Ana nafasi ya mwishokatika maisha yetu na hakika ameahidi kuungana nasi ili kuvunjaunyanyapaa, ukimya na fedheha ya VVU na Ukimwi.10 UTANGULIZI


Duara za TumainiNi mtandao wa kusaidia watu waishio au walioathiriwa na VVU naUkimwi. Vikundi vya masaidiano vimeundwa katika jiji lote la Lusaka,na kazi itatawanywa katika miji mingine ya Zambia pia. Kwa kawaidavikundi hukutana katika makanisa na mikusanyiko ya kiroho, lakinipia hata majumbani. Kazi hii ilianzishwa na Baraza la Makanisa la Zambia.Joy Lubina ni mshauri wa saikolojia ya jamii na Ackim Sakala nimwalimu. Wote wawili wanajulikana vyema kati umma wa wazambiakwa sababu wamekuwa na ujasiri wa kuwa wazi kuhusu hali zao. Kupitiamikutano mingi katika mtandao wa kiimani wa makanisa na katikamahojiano ya televisheni na redio pamoja na magazeti wanawashaurina kuwatia moyo wengine kuvunja ukimya na unyanyapaa juu ya VVU/Ukimwi.Ujasiri wa Kuwa WaziUshuhudaNA ACKIM SAKALA, MTENDAJI KATIKA DUARA ZA MATUMAINI, ZAMBIANilianza kuugua mwaka 1998. Nilikuwa na maumivu makaliya tumbo, madaktari hawakuweza kujua kilichokuwa kikisababishamaumivu. Niliwekwa katika matibabu ya vidonda vyatumbo japokuwa sikuwa navyo. Kabla ya hapo mwaka 1995 –nilimpoteza rafiki wa karibu. Alikufa akiwa mwembamba sanana dalili zote za Ukimwi. Baadaye, mwaka 1996 nilipoteza rafikimwingine katika namna hiyo hiyo.Katikati ya mwaka 2003 nilionyesha dalili zote kama za rafikizangu waliokwisha fariki. Ni wakati huo nilipoamua kuchukuahatua. Kati ya mwaka 1998 na 2002 nilishapoteza uzito kutokakilo 70 hadi kilo 41. Nilishapata malaria za mara kwa mara, kutokajasho usiku na vipele – hizi ni baadhi ya dalili.UpimajiIlikuwa ni June 2002 wakati nikiwa mjini nilipoona Kituo Kipyacha Upimaji na Ushauri ambapo kitu fulani kiliingia akilinimwangu. Niliamua kwenda kupima. Nilipitia katika ushauri,upimaji na kuonekana nimeathiriwa na VVU.Nikiwa nashuka ngazi baada ya kupima nilipata kwikwi iliyodumumuda wa siku sita, usiku na mchana. Nilichunguzwa na nikaonekananilikuwa na kifua kikuu na nikaanza tiba ya kifua kikuukuanzia mwezi June 2002 mpaka Februari 2003. Nilishaongezekauzito hadi kilo 65. Mtu niliyekuwa nimemweleza hali yangubaada ya kupima alikuwa ni mke wangu. Baadaye niliwaambiadada na kaka zangu na rafiki wachache niliowaamini. Tangu nilipopimwanikawa mgonjwa sana. Mke wangu alizingatia katikakunihudumia, lakini ninajua kwa hakika alikuwa akiogopa kuambukizwa.Baada ya miezi sita alikwenda kupima VVU. Tangu hapoamekuwa akienda kupima kila baada ya miezi mitatu. Bahati, kilamara amekuwa anaonekana kutokuwa na VVU.Kuishi Kwa Uwazi Kama FamiliaHaijawa rahisi kuishi na virusi. Nilizaliwa June 24, 1961, katikafamilia ya watoto tisa – wanne wa kiume na watano wa kike.Baada ya kuoa tulipata watoto watano, watatu wa kike na wawiliwa kiume. Mkubwa kwa sasa ana miaka 16 na mdogo ana miaka4. Miaka miwili ya kwanza sikuwaambia watoto wanguchochote, lakini baada ya kupata mazoezi kimatibabu mwaka2004 niliamua kuwa wazi kuhusu hali yangu. Niliombwa kuelezakidogo kuhusu maisha yangu katika kituo cha televishenicha taifa, na kabla ya hapo niliwapeleka binti zangu wawiliwakubwa katika ushauri. Hivi ndivyo hali yangu ilivyowekwawazi kwa watoto wangu. Ninaelewa haijawahi kuwa rahisi kwabinti zangu walio shule za sekondari kuwa na baba aliye naVVU – kama ambavyo haikuwa rahisi kazini kwangu na katikajumuiya yangu. Lakini ilinilazimu kukumbana na unyanyapaana fedheha na kusaidia kuvunja ukimya kwa kuongea kuhusuhali yangu kwa uwazi.MatibabuNilianza kupata matibabu ya kurefusha maisha (ART) kwa sababunilipata kifua kikuu. Baada ya miezi minne niliambukizwahoma ya uti wa mgongo. Miezi sita baadaye, nilipokwendakupimwa chembechembe nyeupe za damu (CD4) zilikuwachini hadi 270 lakini nilipokwenda kupima miezi sita baadayekipimo kilionyesha 324. Hivi karibuni nitakwenda kwa ajili yakipimo kingine, na ninatumaini zitakuwa zimeongezeka kwakuwa ninajisikia mwenye afya nzuri zaidi kuliko pale mwanzo.Baada ya kuwa nje ya kazi kwa mwaka mmoja, nimerudi katikakazi yangu ya ualimu na kama mwamuzi wa mpira wa miguu.Tabia ya Maisha Yangu LeoKwa sasa ninaishi maisha yenye kujali. Ninaamini mimi ni uumbwajiwa Mungu na kwamba ninaishi kwa makusudi ya Mungu.Ninaamini ninaweza kusaidia kuvunja ukimya ndani ya kanisana katika jumuiya kwa sababu ya nafasi yangu kama mwalimukatika jamii.Ninaweza kuongea kuhusu hali yangu ndani ya kanisa na katikaumma kupitia Duara za Tumaini, mtandao ulioundwa na Barazala Makanisa la Zambia. Kupitia Duara za Tumaini ninapatamasaada wenye thamani na mahitaji yangu binafsi yanatimizwa.Sote tunajaribu kuvunja unyanyapaa na fedheha na kutianamoyo kuwa wazi juu ya hali zetu ili kuwasaidia wengine.UTANGULIZI 11


NorwayUnyanyapaa na UtuMawazo, Uzoefu na Mtazamo Juu yaWatu Waishio au Walioathirika kwa VVUKatika kuitikia wito juu ya mtazamo wa kithiolojia kuhusu unyanyapaaunaohusiana na VVU na UKIMWI, Baraza la Kikristo laNorway liliwaalika watu waishio na VVU kuhudhuria katika majadiliano.Waliungana na wafanyakazi kutoka katika makanisa,seminari na taasisi zingine za Kikristo. Majadiliano yalifanyikaAksept, katikati ya jiji la Oslo mahali lilipo kanisa la wale walioathirikakwa VVU na Ukimwi. Mikutano ya namna hii iliendeleakwa miezi kadhaa, katika makundi madogo na makubwa. Mitazamoifuatayo inafafanua mtiririko wa maongezi tuliyoshirikishanaOslo na ni jaribio la kushirikishana yale yaliyojitokezakatika majadiliano yetu. Yanaeleza uzoefu kuhusu unyanyapaana uhitaji wa kuelewa nini maana ya kuwa mwanadamu.Mazingira ya UnyanyapaaNchini Norway, watu waishio na VVU wanakumbana na unyanyapaakwa mapana sana. Japokuwa tabia za unyanyapaahazionyeshwi kwa maneno, ziko dhahiri kwa wale waishio naVVU. Mtu mmoja alisema “watu wanakuchukulia tofauti: wanakukwepana wanakusengenya. Ujumbe hupokelewa vyemakama vile ambavyo ungesemwa kutoka juu ya mapaa ya nyumba.”Hata katika taasisi za afya, “mahali ambapo tunategemeakupata utaalamu na kupokelewa bila upendeleo,” kumekuwepotaarifa za mara kwa mara za wagonjwa wenye VVUwanaoachwa katika foleni au kukataliwa huduma za upasuaji.Kwa mujibu wa muathirika wa ubaguzi wa aina hii “inatokea,kwa sababu macho, mioyo na fikra zao zimefungwa!”Kwa mujibu wa watu waishio na VVU, uzoefu wa unyanyapaakatika jamii mara nyingi umesababishwa na kujinyanyapaa,ambako husababisha kufichika kwa hali zao kwa wengine.Wakati mwingine woga huu wa kukataliwa hauwezi kuthibitishwana watu wengine wanaweza kuonyesha hisia zisizotarajiwaza upendo na kukubalika katika kueleza hali zao kuhusianavirusi. Hata hivyo kinyume chake ni kweli. Mama mmoja akasemaanaogopa kusema na anajisikia hawezi kuwaambia rafikizake kuwa mwanae wa kiume ana VVU kwa sababu anaogopa“kupoteza heshima yake.” Kuna woga wa kujihalalishia kuwawatoto watanyanyapaliwa, au kwamba mtu atapoteza misaadainayohitajika ya marafiki na familia yake.Hivyo “ katika hali ya kutoaminika wapo wengi ambao hujitenga,wakikaa nyumbani bila kutoka nje”: hali ya mahusianoinayoweza kuwa useja wa kujitengenezea, inayoweza kusababishakufadhaika na wakati mwingine kujiua.Utambulisho na LawamaMasuala ya utambulisho yanaoneka kuwa na utata hasa yanapohusuVVU. Hii kwa sehemu ni kwa sababu ya dalili za lawamazinazoambatana nayo. Kama mshiriki mmoja alivyosema.“Ninaposema nina VVU, ninasikia sauti inayosema, ‘kwanini unavyo?’ Tofauti na kansa, VVU inaonyesha kuwa ni kituulichojitakia.” Kwa kukumbana na mitazano hii, kuishi na VVUkunaweza kumfanya mtu akaweka moyoni sura anayoumbiwana wengine, na kuigeuza kuwa ni sahihi juu yake mwenyewe.Hivyo virusi kuwa kielelezo cha utambulisho wa mtu. “Kusemakuwa mtu ana VVU ni kitu tofauti na kusema mtu anaishi naVVU au ni VVU halisi, akasema mtu mmoja. “Ndiyo”, mwingineakakubali: “Hiyo ni tofauti yenye maana sana kwa sababu ‘ni’inahusika na utambulisho wa jumla wa mtu; ambapo kamaukisema una virusi, inakuwa kitu tofauti na wewe, kitu ulichonachona siyo namna ulivyo. Hii ina maana kuwa haifungamanina utambulisho wako.” “Ina maana kuwa” akasema mwingine,“Lugha hiyo ni muhimu, pamoja na jinsi tunavyozungumzakuhusu sisi wenyewe.”KutengwaKadiri mazungumzo yalivyoendelea, iliendelea kuonekana dhahirikuwa uzoefu wa watu wenye VVU ulitoa mwanga katika mtazamowetu na maana ya kuwa mwanadamu katika jamii yetu.“Siwezi kumwambia yeyote nina VVU kwa sababu ninaogopawatanihurumia” alisema mtu mmoja; watahusiana nami katikanjia tofauti; watakuwa waangalifu kile wanachoniambia.”“Ninajisikia mdogo sana.” Alisema mshiriki mwingine. “Kamawangeweza kubaini kuwa mimi ni mtu halisi mwenye malengona mwenye rasilimali: lakini vyote wanavyoona ni virusi.” Washirikiwalieleza juu ya ukuta wa kutofahamu wanaokumbananao kila wakati wanapojaribu kueleza kuwa hata wao ni wanadamuwenye mahitaji ya kawaida ya kibinadamu. Washiriki wengiwalielezea hisia za kudharauliwa na kuhukumiwa.Hii ni kwa sababu watu wanaangalia zaidi virusi (ambavyo nivya kibaolojia) na kutolea sababu zenye utashi (si za kibaiolojia).Si kwamba watu wenye VVU ni watenda dhambi kidogokuliko wengine, lakini pia si watenda dhambi wakubwa kulikowengine. Uovu na ubaya vinaishi duniani, na sote tuna uovuna ubaya. Hiki ndicho tulichonacho kimsingi, alisema mshirikimmoja. “Lakini tatizo ni kwamba kuna mfano au sura kamilifuambayo watu hudhani ni lazima wafanane nayo,” alisema12 UTANGULIZI


utanguliziHivi ‘kuwa tofauti’ ina maana gani, basi? ‘Tofauti ina maanishakutoweka kwa wazi kutoka sura halisi ya kawaida tuliyonayowote, katika mazingira yetu ya ndani. Tukihusianisha sura hiina mwanadamu halisi, hivyo tumeelemea katika kufanya hukumuzisizo sahihi juu ya wale wasioikubali. Na tunajiwekambali nao. Lakini fulani ana mapungufu katika ubinadamukwa sababu tu ni wa tofauti.” Kuna utofauti mkubwa miongonimwetu, kwa namna ile ile kwamba kuna tofauti ndani ya kilamtu na kila mmoja miongoni mwetu.Hofu na Kukataamshiriki mwingine; ‘ kutwisha mzigo wa ubaya kwa watu fulanini njia ya kulinda ‘sura kamilifu’ tunayopenda kuwa nayo juuyetu wenyewe. Na ndipo sura hizi timilifu na maumbo zinaletaugumu kwetu sisi kujiona na kuwaona wengine kama tulivyo:tunaumba makundi yasiyo sahihi na kupoteza mawasilianona maisha yetu wenyewe, kwa mwelekeo wetu wenyewe kufanyayaliyo sahihi na mabaya.’ Kama suluhisho wale wanaotakakurejesha maadili katika jamii huanzisha visingizio vya“kubeba dhambi”, kama ilikuwa; na kama ikitokea tusikataeukweli kuhusu jamii, tunakataa kitu cha muhimu kuhusu sisiwenyewe kama wahusika.”Mfumo GonganishiMakundi haya bandia huumba tofauti kati ya watu. “Lakinitatizo ni, ‘alisema mshiriki mmoja’, pia yanasababisha tofautihata ndani ya watu. Hivyo mmoja anakwepa kujihusisha yeyemwenyewe na watu wengine kama tulivyo (au walivyo). Ambapomifumo gonganishi hutokea.: mtu anasema kitu hiki, namwindine anafanya au kuishi kwa namna tofauti. Jambo ambaloni unafiki. Watu wanaliona hili, na ndiyo sababu baadhi yawatu wanaacha kwenda kanisani. Lakini ‘kuwa mwanadamu’ inamaanisha ni kujifunza kuwa sisi wenyewe, si kuendana na surahalisi ambayo hata hivyo ni bandia. Tusilazimishane kuwa kamasisi wenyewe na tusihukumiane kwa sababu ya kuwa tofauti.”Upinzani mwingi juu ya nini ni tofauti ni matokeo yahofu.”Lakini kila mtu anaogopa kitu fulani,” Alisema mtummoja. “inahusiana na kuishi. Tunaogopa vitu vinavyotishiamaisha yetu. Na tunajitahidi kukiweka kando chochote kinachotishiamaisha yetu.” “Lakini woga mwigi unahusiana naujinga, na upendeleo,” alisema mwingine. “Sote tuna upendeleona kukata tamaa. Lakini ni lazima nikubaliane na ukwelihuu na nifanye kitu fulani kuhusu hiki, kama kurekebisha mitazamoyangu mibovu au kuchunguza mapendo yangu.”Kwa uhakika ni kwamba kuhukumiana kwa sababu ya tofautizetu ni kukataa ukweli thabiti kuhusu hali za kibinadamu,ambao ni kuwa sisi sote tu tofauti, lakini kwa namna fulani,sisi sote ni sawa.Biblia yenyewe imetumika mara nyingi kuridhia ubaguzi.“Kwa mfano, ‘Wamebarikiwa walio maskini wa roho’ wakatifulani imeonekana kama ujumbe unaoonea unaowaambiamaskini au watu wanaoteseka, ‘kwa kuwa unavyoteseka auukiwa maskini hapa duniani, basi utakwenda mbinguni utakapokufa.’Lakini pengine maana yake ni kwamba, kwa sababuya mateso yao, upendeleo maalum hutolewa kwa wale waliokatika mazingira magumu, wagonjwa au waliobaguliwa au- kwa namna yetu – kuishi na VVU au Ukimwi.”Ni kama machoyao yamefunguliwa na kuona kitu cha muhimu.” ‘Mtuhulazimishwa kujishughulisha yeye mwenyewe, kunyenyuamawe mazito yeye mwenyewe, kama yalivyo na kutafutakilichojificha chini yake.”Hivyo Agano Jipya limekuwa ni maandiko ya kinabiina ukombozi, ikiongelea udhaifu wetu na uwezo wetu,dhambi zetu na mazuri, kufanana kwetu na tofauti zetu: nakusisitiza kuwa yote haya ni sehemu ya nini maana ya kuwamwanadamu.UTANGULIZI 13


Baadhi ya Madokezo kwa VitendoUzoefu kutoka kwenye kundi Lililopo OsloMahaliUmuhimu wa kuwa na sehemu salama kwa mazungumzo marakwa mara umesisitizwa. Mjini Oslo, Aksept, kituo kwa ajili yayeyote aliyeathirika kwa VVU, mfululizo wa maongezi ulifanyikakati ya watu walioambukizwa VVU na walioathirika kwa VVUna Ukimwi kwa namna moja au nyingine. Wazo na hamasa yakufanya aina hii ya mazungumzo ilitokana na mtaala wa mafundishokuhusu mbinu za Kujifunza Biblia iliyotengenezwakatika kituo cha Ujamaa kilichopo Piertermartzburg, Afrikaya Kusini. Mazungumzo yaliendelea kwa miezi kadhaa, katikamakundi madogo na makubwa. Kutokana na uzoefu katikamazungumzo haya – yote hasi na chanya – tulifikia katika mitazamoya msingi na mashaka yaliyo muhimu ili kufanya mazungumzohaya kuwezekana. Vipengele hivi vifuatavyo vimeonyeshwakwa mifano kwenye mikutano yetu Oslo.1. Kuanza kwa UzoefuKatika mazungumzo yetu tulifikia katika uzoefu halisi wa maishaya watu waliotengwa na kunyanyapaliwa jinsi yalivyokuwa nakipaumbele tangu tulipoanza. Lakini mara nyingi, wakati mtazamowetu wa kualika jumuia katika mazungumzo ya aina hiikatika Kanisa na miradi ya kithiolojia, imekuwa ni rahisi kuwekaajenda za mikutano ambazo hazikidhi uzoefu halisi na mahitajiya msingi ya washiriki. Katika kujaribu kulikwepa hili, tuliandaamkutano wa kwanza kwa misemo mitatu ya ufunguzi.I. Unyanyapaa ni dhambiII. kujamiiana ni kuzuriIII. Kanisa lina UkimwiWanawake wawili wenye Ukimwi walitoa madokezo ya utan-gulizi na waliulizwa kujibu maswali yafuatayo: “Unadhani ajendaya kanisa juu ya Ukimwi ni nini?” na “Nini iwe ajenda ya kanisakuhusu Ukimwi?”2. Kutengeneza Nafasi SalamaTulipokutana kwa mara ya kwanza, tulichelewa kuanza mkutano,ili kuona kama wengi wa wale waliokuwa wamesaini kujakama wangekuja. Wengi hawakuonekana. Kulikuwa hali yakusita. Tutakuta mtazamo gani kwenye kikundi? Washiriki wengiwalikuwa hawajamwambia yeyote kuwa walikuwa na VVU.Lakini ilikuwa wazi walipojieleza wao wenyewe, waliokuwepopale kwa sababu ya kazi zao katika kanisa na waliokuwepo palekwa sababu VVU ilikuwa sehemu ya maisha yao wenyewe. Huuulikuwa mwanzo usio sawia, ingeweza kutisha kwa baadhi nailisisitiza umuhimu wa kuwa na nafasi salama.3. MahaliSehemu ya mkutano wetu haikuwa isiyo eleweka. Majadilianoyetu daima yalifanyika Aksept. Hili limekuwa ni muhimu katikakutengeneza mfumo salama kadiri inavyowezekana kwa walewaliosema juu ya uzoefu wao wenyewe katika kuishi na VVU.4. WashirikiIli kuumba ujasiri mkuu kwa ajili ya kushirikishana uzoefu,mkutano wa pili ulikuwa wa siri, hasa kwa watu waishio naVVU. Baadaye tuliruhusu mazungumzo kwa washiriki wengizaidi, lakini pia tulikuwa na vikundi vidogo vya mazungumzoambapo watu wangelizungumza zaidi juu ya mawazo yao na14 UTANGULIZI


utanguliziUtaratibu katikaKujifunza BibliaNorwayBiblia Kitabu KitakatifuHatua ya Kwanza Katika Maisha YetuBiblia ni kitabu kitakatifu kwa Wakristo wote. Ni muhimukatika maisha ya binafsi ya Mkristo na katika kuielewajamii. Wengi wanaamini kuwa wale waliosoma Biblia wanaaina fulani ya kanuni inayofungua maandiko mbalimbalina kwamba haijalishi namna wanavyoyaelewa maandiko.Tunaelewa kuwa ufahamu wa kithiolojia ni muhimu katikakujifunza Biblia, lakini tunaamini pia kuwa uzoefuwetu wa kila siku ni muhimu kwa kuelewa ujumbe uliomokatika maandiko ya Biblia. Wakristo Amerika ya Kusini naAfrika ya Kusini wametufumbua macho juu ya umuhimukwa watu wa kawaida katika kusoma Biblia. Kanuni yamsingi ya kujifunza biblia ni kuiainisha Biblia na maishaya kila siku kwa kila mmoja wetu, kwa ushawishi kuwakuna uhusiano kati ya yale Biblia inasema na yale watuwanakumbana nayo.Utaratibu unaoelezewa hapa umesimamia katika taratibuzinazotumika katika kituo cha Ujamaa kilichopo Pietermaritzburg,Afrika ya Kusini. Vikundi vya kujifunzaBiblia huko vimepangwa kutokana na tofauti za watu,pamoja na watu waishio na VVU na Ukimwi. Hawa wanajifunzaBiblia kwa kufuata uzoefu wa watu wenye VVU.Kwa njia hii maandiko ya Biblia yanatoa mtazamo mpyana wa ndani. Tunaamini utaratibu wao wa kujifunza bibliaunaweza kutusaidia kuangalia kwa uwazi mahusianoyaliyomo kati ya maandiko ya biblia na VVU na Ukimwi naunyanyapaa.Mafunzo ya Biblia Yanayomhusisha MtuKama kiongozi wa kikundi cha kujifunza Biblia, jukumu lakozaidi ni kama muwezeshaji na si mwalimu. Washiriki wasielekezwemaana ya andiko. Wafike katika maana ya andiko kutokanana mazingira yao. Baadhi ya watu hudhani wanajua zaidiya wengine! Na kuna wengine wasioamini kuwa tafsiri zaowenyewe zina umuhimu wowote. Kwa mfano: “Wewe ni mchungaji,huwezi kutueleza maana ya andiko hili?” Ni muhimukuwa uweke wazi kwa washiriki wote kuwa uzoefu wao nimuhimu katika kuelewa andiko. Uchunguzi wa maandiko yaBiblia si njia inayotakiwa kufuatwa kwa ubinafsi. Ni suala latabia katika kusoma Biblia. Kadiri unavyozoea na kuridhikana utaratibu huu wa kujifunza Biblia, unaweza kujiweka hurukutoka kwenye maswali. Uchunguzi wa maandiko ya biblia unawezakuelezwa kama tabia nne unapojifunza maandiko:1. Kusoma Biblia katika mtazamo wa mazingira ya wasomajiwenyewe na changamoto zinazowakabili.2. Kusoma Biblia pamoja na wengine.3. Kusoma Biblia kwa ufasaha na kwa undani.4. Kusoma Biblia ukiwa na wazo la kufanya siku ya kila mtu namabadiliko kijamii.Tabia Nne za Msingi1. Soma Biblia katikaMazingira ya Msomaji MwenyeweUtaratibu unaotumika hapa ni wa jumla na unaweza kutumikakwa mada yoyote inayokufurahisha. Tunashauri kuanzamajadiliano kwa maswali yanayosaidia kila mtu katika kundikushirikisha uzoefu ambao utaweza kukusaidia kuelewaujumbe wa maandiko ya biblia. Kuhusu VVU na Ukimwikama mada, kuna watu ambao hawajui ni kwa namna ganiilivyo kuishi na VVU. Japokuwa unaweza ukawa huna VVUwewe mwenyewe, tunaamini kuwa unao uzoefu ambao unawezakuutumia.2. Soma Maandiko Mkiwa PamojaBaada ya kushirikisha uzoefu unaohusiana na mada, somenimaandiko ya Biblia. Ni muhimu mkisoma kwa pamoja, kwasauti. Kusoma kwa pamoja kunakuwezesha kuielewa kamakikundi.Ni vyema kuchagua maandiko ambayo yanahusiana kwakaribu na mada kadiri inavyowezekana. Inawezekana ukaonakuwa Biblia haijishughulishi na mwelekeo wa mada16 UTANGULIZI


Utaratibu wa VitendoZambiaKujifunza BibliaHatua zifuatazo zinaweza kufuatwa katika mifumo tofauti ya kujifunzaBiblia. Lakini mambo matatu mara nyingi ni ya muhimu:1. Maisha ya Kiroho – Kukosekana hili husababisha kukosekanakwa majadiliano kitaaluma.2. Kutumia Akili – Kukosekana kwa nidhamu kiakili na kufikirikwa kina husababisha “mawazo mazuri” yasiyo na msingi, piamitazamo isiyo sawia.3. Utashi – kukosekana kwa utashi wa kutii kunasababisha kutojifunzakwa vitendo.1. Soma Maandiko Kwa UangalifuFanya uchunguzi wa awali. Soma kipengele mara kadhaa, ikiwezekanakatika tafsiri tofauti. Andika kila wazo litakalokujia.Amua aina ya uandishi kama ni shairi, nathari, historia au hoja.2. Kujifunza kwa UndaniJaribu kuandika katika sentence moja kusudi la muhimu lililomokatika fungu la maandiko.3. Kugawanya MaandikoTafsiri za kisasa zimewekwa katika aya. Lakini inawezekanakuzigawanya aya hizi4. MiunganikoMaandiko mengi yameunganika. Ni lazima tujaribu kuvumbuamaunganiko kati ya aya. Maneno “sasa basi” na “basi” ni mfanowa hili: Warumi 6:1 na 8:1.5. VielelezoTunahitaji vielelezo kutusaidia katika mawazo yaliyofupishwa,kama mifano ya Yesu na namna alivyotumia maneno kamamwanga, chumvi nk.6. MarudioMwalimu yeyote mzuri anajua thamani ya marudio. Zingatiamlinganyo uliomo katika Zaburi: Ushairi katika Biblia ni wa marudio;mwandishi anaeleza ukweli katika njia moja na pia ukwelihuo huo katika mfumo mwingine. Mfano Zaburi 42:1-27. MhusikaWakati mwingine tabia hutajwa ili kusisitizia pointi. Jaribukutafuta zaidi kuhusu mtu huyo. Tofauti inaweza kuonekanamiongoni mwa wahusika, kwa mfano Mafarisayo na watozaushuru, Luka 18:9-14.8. Mtazamo Wetu Kwa Masuala Ya KisasaIwapo tunaiamini Biblia mtazamo wetu utakuwa tofauti kutokakwa ule wa wengine wengi. Kwa mfano hatutashawishikana hali au mazingira. Tutaichukulia biblia kama nisahihi katika hali zetu za sasa. Masuala fulani yameshughulikiwakwa uwazi. Matatizo mengine hayajashughulikiwa –tunatakiwa kuanzisha utaratibu tofauti wa kujifunza juu yamatatizo haya.9. Kutafuta KanuniKukuongoza kufikia MajibuKama wakristo ni lazima tuambatanishe maisha yetukwa Kristo, hivyo tutapata miongozo kwa masuala yenyeutashi kwa asili ya Mungu na kwa lipi Mungu amelidhihirishakuhusu makusudio yake kwa ajili yetu. Vipengelevifuatavyo vinaweza kuunda mfumo ambao utatuwezeshakufikia hitimisho kuhusu matatizo mengi yanaotokea sikuza leo:Upendo wa Mungu – Kumbukumbu la Torati7:6-8 Warumi 5:6-11Haki ya Mungu - Kumbukumbu la Torati32:4, Warumi 3:21-26Utakatifu wa Mungu – Mathayo 5:48Mungu ni Muumbaji – Mwanzo 1:2, Zaburi 8:5-8Mungu ni Mtunzaji – Mathayo 6:25-33Mungu ni Mkombozi – Waefeso 1:7Mungu ni Hakimu – Mathayo 25:31 – 46Sisi ni watumishi wa ulimwengu – Mwanzo 1:28-30Tunategemeana sisi kwa sisi – Mwanzo 4:9-11, Walawi 19:1810.Jinsi ya Kutumia KanuniKwanza kusanya taarifa nyingi kadiri inavyowezekanakuhusu tatizo la kushughulikia na amua kanuni ipiya biblia inahusika. Soma kwa uangalifu vifungu vyamaandiko vinavyoonekana kuoana. Tengeneza wasaakwa mazingira yanayobadilika tangu nyakati za Biblia.Iwapo kanuni inaonekana yenye kukinzana, kwanzaangalia tafsiri yako. Kama bado kuna mikinzano amuakanuni ipi ni ya juu. Kumbuka kutofautisha kwa uangalifukati ya mawazo yako mwenyewe na mafundishoya Biblia.18 UTANGULIZI


<strong>Mwili</strong> <strong>Mmoja</strong>Kwa maana mwili si kiungo kimoja bali ni vingi.Mguu ukisema kwa kuwa mimi si mkono, mimi siwa mwili, je! Si wa mwili kwa sababu hiyo? Na sikiolikisema kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili,je! Si la mwili kwa sababu hiyo? Kama mwili woteukiwa jicho ku wapi kusikia? Kama wote ni sikioku wapi kunusa? Bali Mungu amevitia viungo kilakimoja katika mwili kama alivyotaka. Lakini kamavyote vingekuwa kiungo kimoja mwili ungekuwawapi? Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja.Na jicho haliwezi kuuambia mkono , sina hajana wewe, wala kichwa hakiwezi kuiambia miguusina haja na ninyi. Bali zaidi sana vile viungo vyamwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwazaidi. Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyokuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshimazaidi, na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzirizaidi sana. Kwa maana viungo vyetu vilivyo nauzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanishamwili, na kukipa heshima heshima zaidi kile kiungokilichopungukiwa, ili kusiwe faraka katika mwili,bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe. Nakiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho,na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyotehufurahi pamoja nacho.1KORInTHO 12:14-26UTANGULIZI 19


20 KANISA


kanisaZambiaKanisa Lenya HurumaLiturjiaKatika kanisa la “Reformed” nchini Zambia mchungaji mmojaambaye ni mratibu wa VVU/UKIMWI, aliunda liturjia hii na kuitumiakwa baadhi ya vikundi vya watu waishio na VVU nchiniZambia.K = KiongoziW = Wote1. Wito Kwa Ajili ya KuabuduK: Bwana apewe sifa! Asifiwe, O watumishi wa Bwana, Lisifiwejina la Bwana! Libarikiwe jina la Bwana kuanzia wakati huu namilele.Kaka na Dada katika Yesu Kristo: Tumekutanika leo mbele zaMungu baba yetu mwenye huruma na upendo. Kwa hiyo kwamioyo ya unyenyekevu tumwabudu kwa maombi, nyimbo nasifa. AMINA2. Nyimbo za Sifa3. Maombi ya UfunguziW: Mpendwa Mungu, Tunalitukuza na kulisifu jina lako kwasababu ya upendo na ulinzi unaotupa kila siku katika maishayetu. Asante kwa upendo na ulinzi unaoendelea kutupa hataleo.Bwana tumekutanika kudai kupotea kwa asili ya kanisa lakokatika ulimwengu huu ulio katika maumivu kwa sababu yajanga la VVU na UKIMWI.Bwana kama kanisa tumekuwa kimya kwa masuala ya VVU naUKIMWI na kwa kufanya hivyo tumejitenga na huduma yakona watu wako walioathiriwa na ugonjwa huu. Tunaomba msamahawako.Bwana tunakuomba kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristokubadili mafundisho yetu na matendo kwa kaka na dada zetuwalioathirika au kutoathirika kwa VVU. Tupe moyo usiohukumubali unaopenda na kujali. Katika jina la Yesu tunaomba.AMINA.4. Wimbo5. Toba ya PamojaW: Tunakiri na kukubali kuwa sisi kwa namna fulani tumechangiaunyanyapaa na ubaguzi na kwamba makanisa yetuhayajawa salama au mahali pa ukaribisho kwa watu waishioau walioathiriwa na VVU na UKIMWI. Kwa nyakati fulani, Sakramentimekataliwa kwa watu waishio na VVU, ibada za mazishizimekataliwa kwa watu waliokufa kwa UKIMWI na hatujawafarijiwasio na matumaini. Tunakiri kuwa kanisa limekataa wakati lilipotakiwakukumbatia na kuhukumu lilipotakiwa kuonyeshaupendo, huruma na uangalizi. Tunatubu dhambi hizi. Kwa hiyotunajiweka sisi wenyewe katika kukubali kwa uaminifu kuvunjaukimya, kusema kwa uwazi na kwa ukweli kuhusu kujamihianaVVU na Ukimwi. AMINA.6. Kutangaza Msamaha na NeemaK: “Hili ni Agano nitakalo agana nao baada ya siku hizo, asemaBwana: Nitaweka sheria zangu katika mioyo yao na kuziandikakatika akili zao, sitazikumbuka dhambi zao na matendo yaomaovu milele.” Waebrania 10:16-17.7. Wimbo wa Kusifu na Shukrani8. Ombi la Ufunguzi wa Neno la MunguK: Mungu baba yetu neno lako ni taa kwa miguu yetu, bila hiyotunapotoka. Fungua macho yetu na masikio yetu ili tuwezekuona na kujua siri zilizofichwa katika neno lako. Baba, tufundishekupitia neno hili. Katika jina la Yesu Kristo tunaomba.AMINA.9. Kusoma Neno1 Korintho 12:14 – 2610. Mahubiri• Huu ni wito kwa kanisa dunia nzima kukubali kuwa janga laVVU na UKIMWI ni kama lake;• Kanisa lisikubali tu kuwa VVU vipo katikati yake, bali litoekwa ukamilifu na kukubali kwa uwazi na kuwajali kwa upendowalioathirika na kuathiriwa.11. Maombi Baada ya Mahubiri12. Wimbo wa Kufunga13. BarakaW: Mungu baba mwenye huruma na upendo atukuzwe milelena milele kupitia Yesu Kristo Bwana wetu. AMINA.KANISA 21


MSUMBIJIMtazamo Wa Kibiblia:Ugonjwa, Unyanyapaa Na Wajibu Wa KanisaKuwakumbatia WaliosahaulikaAgano la Kale linatuambia kuwa watu waliokuwa na ukomana kifua kikuu walisahauliwa na kutengwa na jamii ambamowaliishi (Walawi 13). Jamii kwa ujumla imerithi tabia hii ya kunyanyapaawatu wanaoteswa na magonjwa yanayochukuliwakuwa sugu. Lakini Bwana ni ndiye mwangalizi wa majira yotena sehemu kwa sababu anajua ali za watu wake katika magonjwana afya njema.Ni kwa sababu hii kanisa lazima lifanye kazi na watu walioathiriwaau kuathirika kwa VVU na UKIMWI ili kuwasaidia kuwana imani, kwa kuwa ni kwa imani milima huhamishwa, dhorubahupoozwa na miujiza kutendeka. Ni muhimu kuwakumbushawale wanaoteseka kuwa ni Mungu pekee ndiye anayeweza kukubalihali zote za kibinadamu na kwa kufanya hivyo tutawasadiakuponya hali zao za kiroho. (Waebrania 10:39). Kwa mtazamohuu imani huja kama silaha muhimu, ambayo ni muhimuna imara katika kuelewa changamoto ya VVU na UKIMWI. Bibliainatueleza kuwa Ayubu aliteseka sana lakini uvumilivu wakekatika imani ulimfanya kumshinda mwovu.(Ayubu 1:14-21)Katika maandiko, injili ya Yohana 8:1-11 inaelezea kisa katiya Yesu Kristo na mwanamke aliyezini. Ukweli kwamba Yesuhakuruhusu mwanamke apigwe mawe ni ishara iliyo wazi yaulinzi na kuwaangalia watu waliokataliwa na jamii.Mfano mwingine uliotolewa na Yesu Kristo unapatikana katikaInjili ya Mtakatifu Mathayo 8:1-3. Hapa ni pale Yesu alionyeshaupendo kwa kumgusa mtu mwenye ukoma, aliyekuwaametengwa kufuatana na sheria ya Musa.Kwa kumgusa mwenye ukoma Yesu Kristo alionyesha upendoalionao kwa kila mtu bila ubaguzi na alivunja desturi zakukataliwa na kubaguliwa kwa wanaoteseka kwa ukoma.Tukiongelea kithiolojia, katika mfano huu Yesu Kristo ameonyeshakuwa ugonjwa na udhaifu wa kibinadamu hauwakilishimatakwa ya Mungu.Katika baru yake kwa Warumi 3:10, Paulo anaonyesha ukwelidhahiri kwa wakristo wote kwa kueleza, “ hakuna mtu liye safi.Hata mmoja.” Kwa upande mwingine, Isaya 6:5 pia inaongeza,“Maana hata mimi ni mtu nisiye na midomo iliyo safi naninaishi kati ya watu wasio safi.” Kwa hiyo tendo la kusafishamidomo hutokea kama ishara ya shukrani kwa Mungu. Ni kwaneema yake tunachukuliwa kama wasafi. Hatuna haki ya kuwachekawengine. Hii ndiyo maana kuwanyooshea vidole watuwenye VVU na UKIMWI si haki bila kujali namna au sababu yakuathirika kwao.Mfano mwingine wa Yesu Kristo unapatikana katika Injili yaMarko 10:46-52. Hapa kipofu Batimayo, mwana wa Timayoaliyekuwa ametengwa na jamii yake katika mji wa Yeriko, baadaya kusikia kuwa Yesu wa Nazareti alikuwa akipita, alianza22 KANISA


kanisaMgahawa waKiekumeniakupiga kelele: “Yesu mwana wa Daudi Unihurumie!” Bila kujalimwitikio wa wafuasi wa Yesu na umati wa watu uliokuwaunamfuata, Yesu alisimama na kumwita Batimayo na kufanyaaone tena.Leo hii, Batimayo anamwakilisha dada au kaka aishiye na VVUna UKIMWI. Na kanisa na viongozi wake wameitwa kufunguamacho yao, kufikiri na kusikia sauti ya Batimayo, ambaye katikajamii ya leo ni watu waishio na VVU na UKIMWI, ambao witowao kwa matendo ni kwa kanisa na jamii kwa ujumla.Upendo na huruma vinaonyesha huduma ya Yesu na anakuwawa muhimu juu ya wote wale walioitwa kwa jina lake Kristo.Kwa hiyo, kama wakristo tumeitwa kupenda na si kuhukumu.Yesu mwenyewe alitupa mfano kwa namna alivyoonyesha upendona huruma kwa wale waliokuwa wakiteseka nyakati zake.Kwa yesu, Upendo lazima uonyeshwe katika “pendaneni ninyikwa ninyi kama unavyojipenda mwenyewe” na hurumia “ kwakusudio na kuteseka na mwingine”.Ni wajibu wa kanisa kuwa karibu na watu waishio na VVU naUKIMWI, ili weweze kuuona uso wa Mungu. Kanisa lina wajibuwa kuwafanya watu waishio na VVU na UKIMWI kuelewa kuwaMungu anampenda kila mtu. Ndiyo maana alimtoa mwanayeYesu Kristo, ili kwamba wale wanaoamini kupitia yeye wasiangamizwebali wawe na uzima wa milele.Kanisa limeitwa kuwa sauti ya kinabii na taasisiinayoponya, kama sehemu ya safari ya kupigavita unyanyapaa na kubaguliwa. “Café Ecuménico”ni jina lililotolewa kwa mradi unaoleta watuwenye au walioathiriwa na VVU na UKIMWI, uongoziwa kanisa, mtandao wa wachungaji waliokatika mapambano na VVU na Ukimwi na vyamavya kijamii. Malengo yake makuu ikiwa ni kulifanyakanisa kuwa wazi na sehemu salama kwamitazamo ya kawaida na mijadala juu ya VVU naUKIMWI.Mara moja kila mwezi, watu hukutana kujadilianamasuala yanayohusu VVU na janga laUKIMWI. Wanakutana chini ya mradi wa Kuzuiana kuondoa VVU na UKIMWI, kwa ubia na Barazala Kikristo la Msumbiji, Mtandao wa Wachungajikatika Kupambana na VVU/UKIMWI katika jiji najimbo la Maputo, chama cha watu waishio na VVUna UKIMWI kilichopo katika eneo liitwalo ‘CaniçoResidential Area’ na World Relief.Kwa sasa kuna zaidi ya wanachama 140 katikaChama cha watu waishio na VVU na UKIMWIpale Polana Caniço Residential Area na kama 30watumishi wa kanisa wanachama wa Mtandaowa Wachungaji katika Kupambana na VVU naUKIMWI. Wanahusika katika nafasi muhimu katikakuunda mtandao wa masaidiano. Baadhi yawachungaji wanatoka katika makanisa ambayosi wanachama wa Baraza la Kikristo la Msumbiji,inayoleta changamoto mpya katika “Café Ecuménico’.KANISA 23


kanisaUshauri wa Kichungaji na Kazi za Kikanisa Miongonimwa Watu Waishio na VVU na UKIMWIDenmarkKutengeneza JumuiaMpya Zenye TumainiNA Carina WøhlkKatika kipindi cha miaka michache, kusanyiko la watu wachacheambao wanaishi au wameathirika kwa VVU na UKIMWIlimeundwa ndani ya kanisa la Roho Mtakatifu katika jiji la Copenhagen,ambako kuna kituo kinachojishughulisha na VVUna UKIMWI. Uanzishwaji halisi wa kusanyiko ulitokea sambambana faragha kwa ajili ya watu wenye VVU na UKIMWI mwaka1999. Kusanyiko limeongezeka haraka na kimya – pamoja nakusanyiko la kuabudu na kusanyiko lingine maalum liabudulousiku.Juhudi za kuanzisha kusanyiko la wenye VVU zilianzishwa nawatu wenye VVU wenyewe. Walisema wanahitaji kuabudu nakukusanyika katika mazingira ya Kikristo. Ombi lao linaelewekaninapofikiria kuhusu upweke ambao mara nyingi ninauona kuhusianana huu ugonjwa hatari na unaounda desturi fulani. Katikaushauri wangu wa kichungaji, nimekutana na seti mbili zamatatizo yanayohusiana na upweke: hiari na usio wa hiari.Upweke wa hiari unatokea kwa watu wenye VVU, kutokanana matatizo mengi ya kijamii na viwewe vinavyohusiana naugonjwa walionao, wamechagua kujitenga na jamii. Wanatafutamaisha yao ya pekeee na jamii zao bila mahusiano yoyoteili kukwepa kupoteza mengi.Upweke usio wa hiari ni tatizo la watu wenye VVU ambao wamekataliwana kutengwa na jamii kwa sababu ya kuwa na VVU.Wamesukumwa mbali na hawajaribu kutafuta mahusiano najamii kwa kuogopa kulaumiwa na kutupwa.Kuushinda UpwekeKatika Warumi 14:7-8 Paulo anaandika, “Hatuishi kwa ajiliyetu wenyewe na hatufi kwa ajili yetu wenyewe. Kama tukiishi,tunaishi kwa ajili ya Bwana na kama tukifa tunakufa kwaajili ya Bwana: Kwa hivyo sasa, iwapo tunaishi au kufa, sisi niwa Bwana.”Maneno haya yanaweza kuongelea moja kwa moja juu yaupweke ambao watu wengi wenye VVU wanauona – kamaukumbusho kutoka kwenye injili kwamba hatujatengwa,hata kama wakati fulani inaonekana hivyo.Kwa jinsi ninavyoona, kanisa lina mchango kiasi fulani kuwezeshakuushinda upweke. Katika Ukristo, wanadamuwote wameumbwa kwa sura ya Mungu na wana thamani inayolingana.Tunaishikwenye mwili mmoja. Mtiririko huu wamawazo una maana kuwa unaunganika na kutegemeana nawanadamu wengine. Tunategemeana, ili maisha yaendelee.Lakini kwa hakika kuna tabia, hata katika kanisa kuwa kudhanibaadhi ya watu ni bora zaidi kuliko wengine na hii ni tishiokwa kanisa.Mwaka mmoja uliopita, baada ya safari yangu Zambia ambaponilijionea kwa mara ya kwanza ukubwa wa janga, nilihubirikatika Kanisa la Roho Mtakatifu. Katika mahubiri yangu nilitumiausemi “kanisa lina ukimwi” ili kuhamasisha mshikamanona roho ya uwajibikaji kwa wakristo. Usemi huu ulionekanani wa makosa. Wasikilizaji walisikia kitu kimoja tu; kwambakanisa linaumwa na kwamba ugonjwa unahusiana na ngono.Lakini msisitizo wangu ulikuwa na hakika ni kwamba VVUna Ukimwi unatuhusu sisi sote. Janga la Ukimwi ni changamotokwetu sisi sote. Kama wakristo ni lazima tuhusike namaumivu ambayo kaka na dada zetu katika kristo wanapitia.Lazima tuonyeshe huruma na kuwajibika kama tunataku kutoweshajanga hili.24 KANISA


Iwapo tutakuwa pamoja, tunaweza kuuondoa ugonjwa nachuki miongoni mwetu. Kanisa linatakiwa kujifungua kwa ajiliya kusanyiko linaloweza kumkumbatia kila mmoja. Na katikakusanyiko hili tunaweza kusababisha uwezekano wa kuwawazi, kama vile tulivyo.Kuanzisha Mtandao wa SharikaKusanyiko la wenye VVU katika Kanisa la Roho Mtakatifu nimfano wa mtandao wa kijamii na kiroho kwa ajili ya watu walioathirikakwa VVU na Ukimwi. Kwa kuanzia, mtandao ulikuwadhaifu na wa kificho. Huduma mara ya kwanza zilitolewa kwawatu wenye VVU tu, kwa sababu wanachama wake hawakutakakujulikana. Kulikuwa hali ya kutengwa, lakini sababu ilikuwauzoefu uliokuwepo wa kuhukumiwa na Wakristo wenzao.Kadiri muda ulivyokwenda, Wakristo wenye VVU wamewezakuaminiana na kuwa wazi. Wameanza kujisikia huru na kuanzakuaminiana na kutegemeana kuhusuanana wahudumu na kusanyiko lote ndani yakanisa.Leo hii, ibada ni kwa wote walioathiriwana VVU/UKIMWI na si kwa wale walioambukizwatu. Hii ina maana kwamba walewalioathiriwa, familia zao na marafiki, wafiwa,walioajiliwa kati kazi inayohusiana namasuala ya UKIMWI nao wanakaribishwa.Kusanyiko la wenye Ukimwi halijafikia kiwangoambacho litaweza kugonga kengelena kufungua milango wazi, lakini malengoyamekuwa ni kuchangamana.Mara nne kwa mwaka, Januari, Aprili, Julai na Oktoba, ibadakwa wenye VVU huchukua sura ya Sakramenti takatifu ikifuatiwana chakula cha pamoja. Ni muhimu kwamba mikusanyikohii iwavutie washiriki wengi – kwa kawaida zaidi ya 20.Wanafanya aina mbili cha kusanyiko – mezani pa Bwana zakatika meza ya chakula.Washiriki wanapata wasaa wa kuhusiana - na watu wenginena Mungu. Alama ya muhimu kwa Ukristo, msalaba, unatuonyeshaumuhimu wa kutoka nje kwa ajili ya uzima.Wanadamu wanahitaji msingi ulio imara na mahusiano yakaribu. Hii inatumika si kwa wale wenye VVU, ambao wamepotezasana na mahusiano yaliyovunjika, kukataliwa sana,ndiyo, pengine hata hisia za kuwa wamekataliwa na Mungu.Ni matumaini yangu kuwa, kadiri muda unavyoenda, kutakuwana utashi mwingi kila mahali kuwakumbatia wale waishiona VVU na Ukimwi. Tunahitaji Kusanyiko la Kikristo lililowazilenyewe.KANISA 25


kanisaLiturjiaNorwayKuwa <strong>Mwili</strong> <strong>Mmoja</strong>Katika mazungumzo Oslo, Noway, yaliyowahusisha watuwaishio au walioathirika kwa VVU, moja ya mambo ya muhimuilikuwa kwamba ‘sisi sote ni wabeba mazuri na maovu.’ Tunatengenezamakundi yasiyo sahihi na kutosema kwelikuhusu sisi wenyewe ikiwa tunabebesha mizigo ya uovu watuwengine. Japokuwa tu watu tofauti kama watu sote ni sehemuya mwili mmoja. Hii ni sehemu ya liturjia hii. Maneno ya utangulizina malalamiko ni nukuu za mazungumzo. Ni vyema kuwafanyawatu tofauti wengine kusoma maandiko tofauti.K = KiongoziM = MsomajiW = Wote1. UtanguliziK: Unachomfanyia mwingine, unajifanyia mwenyewe na sisisote. Katika ufahamu wa ndani, sisi ni mtu mmoja. <strong>Mwili</strong>mmoja. Tunapomharibu mtu mmoja, tunaharibu kitu fulanindani yetu pia na kama madhara kitu fulani katika ubinadamu.Lakini hii haimanishi kuwa sisi wanadamu tunafanana.Kunatofauti kubwa miongoni mwetu, katika njia sawakwamba tofauti ipo ndani ya kila mtu kati yetu.2. WimboM1: Nimeumizwa na kuchoshwa kwa maswali mengi! Nihitaji la kibinadamu kuwa na mwandani; Nina mahitaji pia,hamu ya kuwa na watoto, hamu ya kuwa na mume.M2: Baadhi ya watu wanaona virusi pekee, hawanioni mimi!M2: Ninaogopa sana kukataliwa au kuvunjwa moyo. Sidhubutukuwa katika mapenzi.M2: Kwa nini inaonekana kama vule Mungu anakasirika ninapojitahidikufanya vizuri?M1: Nimemtafuta Mungu anayenipenda, asiyenihukumuna ambaye anaweza kunisaidia kukubali VVU na kuwa hurukuokana na mashutumu. Sikumpata kanisani. Umekuwa niutafiti wa upweke.W: Mpaka lini, Ee Bwana? Utanisahau milele?4. Ukiri wa Pamoja Ulio SahihiSoma kutoka upande mmoja wa madhabahu:M: Tunakiri kwamba sisi ni sehemu ya vyote alivyoumbaMungu na aliviona kuwa ni “vizuri sana” kwamba sote tunasehemukatika ya vizuri hivyo na ndani yetu uzuri unakaa.Tunakiri kwamba mtu wentu wa ndani, na miili yetu pia, mahitajiyetu na hamu yetu vyote ni sehemu ya sura ya Mungundani yetu.Tunakiri kuwa sote tuna thamani na kwamba tuna thamani kwasababu sote ni uumbaji wa Mungu, kwa sababu tupo na tunaishi3. MalalamikoWasomaji wawili kutoka nyuma ya madhabahu:W: Lini, Ee Bwana Utanisahau milele?M1: Ni kama vile watu wananikwepa, wananisengenya,wananichukulia kama vile ni wa tofauti. Wanadhani nimeharibikiwa.Nimetengwa.M2: Sithubutu kumweleza mtu ye yote kuwa nina VVU, kwasababi sifahamu wengi watalipokeaje.5. Kimya au Wimbo6. Uthibitisho waKushiriki Katika UharibifuSoma kutoka upande mwingine wa Madhabahu:M: Tunakiri kushiriki katika kuunda makundi na kutenga baadhiya watu wakati tunawaingiza wengine.26 KANISA


Tunakiri hisia zetu, kwamba tunaogopa yale yasiyozoelekana kwamba tumechangia tabia ya watu kujiona wametengwa,wamenyamazishwa na kubaguliwa.Tunakiri kuwa tumejihusisha zaidi na hadhi ya mtu na kuwatofauti zaidi kuhusu hali zao za ndani, umuhimu wao na ubinadamuwao wa kawaida.Tunakiri kuwa kuwa mara nyingine tunaona baadhi ya watuau vikundi fulani vya watu kuwa ni waovu na kwamba hatuonikuwa sisi ni sehemu ya uovu na wema.Tunakiri kutotenda haki kuwa wenye nguvu, afya na matajirikati yetu wanapewa kipaumbele, wanahudumiwa vizurina kwa njia hiyo tunapata hata zaidi.Tuangalia kwa huruma, tusamehe, tusafishe na tufanye watakatifu.7. Kimya au Wimbo8. Ukiri kwa Usawa Wetu KibinadamuSoma kutokea katikati ya madhabahuM: Tunakiri kuwa sehemu yetu ya ubinadamu imeumizwana kujeruhiwa, i uchi na kudhalilika.Tunakiri kuwa tu sawa kibinadamu. Ambapo hakuna hatammoja aliye juu au chini ya wenzake, hakuna aliye mwemaau mbaya zaidi ya wengine. Tunakiri kuwa sisi ni tofauti,aina na maumbile tofauti ambayo vyote ni sehemu ya ubinadamummoja: kwamba sisi ni sehemu ya mwili mmoja,kanisa moja – ambako wa mwisho ni wa kwanza na ambakonguvu ni ya yule aliye mnyonge.9. Ukiri Kwa Upendo wa MunguK. Unapendwa, zaidi ya unavyofahamu – unapendwa, umesamehewana kukombolewa.10. Kusoma MaandikoLuka 13:10-1711. Ukiri wa ImaniW: Tunaamini katika Mungu aliye Upendo;: aliyetuumba kwaupendo; anayeteseka tunapoteseka na aliye kazini dunianikwa ajili ya mema.Tunaamini katika Mungu ambaye hatumi magonjwa aumateso mengine kama adhabu kwa dhambi.Tunaamini katika Yesu Kristo, aliyejichukulia miili na damuyetu; aliyetuonyesha namna Mungu alivyo; anayewawekawatu juu ya sheria na kanuni; atusafishaye na kutuwekahuru kufuata njia ya upendo.Tunaamini kuwa Yesu Kristo hawezi kumilikiwa au kutawaliwana yeyote na kudhibitiwa na sheria na taratibu.Tunaamini katika Roho Mtakatifu ambaye hatuondoi katikamiili yetu au maisha ya duniani na ambaye hawafanyibaadhi ya watu waumini wazuri kuliko wengine.Tunaamini kuwa sote ni sehemu ya kanisa, na kwambasote ni jumuia inayong’ara, katika kanisa hili hakuna hatammoja ambaye kwa maana amewekwa nje, katika kanisahili watu hupata msaada kukubali na kujipenda wenyewe nakupenda jirani zao.Tunaamini katika kanisa ambalo halinyanyapai, halibagui,halitengi au kumhukumu yeyote.Tuamwamini Mungu. Msaada kwa kutoamini kwetu.12. Kutafakari MaandikoHapa ni baadhi ya miongozo:Katika Luka 13:10-17 tunakutana uso kwa uso na Munguambaye anapinga mamlaka na kulegeza vifungo vya watuwaliofungwa. Ni Mungu ambaye si tu kwamba yuko kazininyakati za kazi kuanzia saa tatu hadi kumi na moja, ie ndaniKANISA 27


ya taratibu fulani, bali ni nguvu ambayo haifungwi au kudhibitiwa.Mungu mwenyewe huvunja taratibu za maandikokwa sababu watu na huruma ni muhimu sana kuliko sheria.Lengo la sheria ni muhimu sana kuliko utii kwa sheria fulani.Asili ya Mungu ni Upendo na makusudi yake kutokanana maneno yake na matendo ni kulegeza vifungo, kuwainuawaliokandamizwa na kuwaweka watu huru; Munguanaponya na kuokoa.Kisa hiki na hadithi zingine kuhusu Yesu zinaweza kukusaidiakuondoa mitazamo ya Mungu inayomhusisha naukandamizaji, kulipiza visasi na kuadhibu, na badala yakekuelekeza katika kiini hasa cha injili – Upendo wa Mungukwa ajili ya kila mtu.Ukristo na injili vina umuhimu kiasi kwamba nyakati fulanizinaonekana kuwa havijatumika ipasavyo. Vinaweza kuwavyombo vizuri vyema sana kwa maisha yetu: vinaweza kutuwekahuru na kutusafisha katika kila kitu ndani yetu namazingira yetu yanayo tukandamiza. Yanaendana na haliya kutokuwa mkamilifu kibinadamu, inayoumba hukumuna fadhaa na ambayo huwashusha watu chini. Vina sisitizaumuhimu wa kujipenda na kuwapenda majirani.13. Maombi ya Mwombaji• Mungu wa kila mwanadamu, tupe uwezo na ujasiri kutambuana kukataa kila aina ya unyanyapaa, kutengwana kubaguliwa. Tusaidie kupinga upendeleo na tupeuwezo wa kutambua uwepo wako ndani ya kila mtu.Ndani ya mioyo yetu tunawaleta kwako wale ambaotunawafahamu wanapitia hali ya kutengwa.• Mungu wa Upendo, jifunue kwetu na tusaidie kushuhudiakwako kwa ukweli. Tuondoe na vishawishi kutumiavibaya ili kuwaumiza wengine, au kuhudumiwabadala ya kuhudumia Tusaidia kushirikiana upendoulioleta kwetu na kujitahidi kuondoa mitazamo mibovukuhusu wewe.• Mungu, chanzo cha maisha na uzima, tusaidie kuichungamiili yetu, maisha yetu na sisi wenyewe. Tupeujasiri na nguvu ya kupingana na dharau, ubaguzina ukatili kwa wanawake, na kukomesha udhalimuunaotokea ndani na nje ya ndoa. Daima tusaidie kuwaangaliawatu wenye upungufu kuliko sisi na kuongeakuhusu VVU kwa lungha zinazoonekana kuwa zaheshima, upendo, msamaha na urafiki.• Mungu wa Utatu, zifanye sehemu zetu za kukutanikamahali pa kujumuika wote, ambapo ujuzi wetu nathamani ya kila mtu unathaminiwa. Tusaidie kuwa vileambavyo ndani yetu tayari tuko: wanachama wa mwilimmoja. Tusaidie kumwona mtu kabla ya sheria, virusina ugonjwa. Tunaomba kwa ajili ya kanisa linalowezakufanya maisha kuwa mazuri na yanayowezekana kwaajili yetu sote, linaloweza kuwa mkondo wa nguvuzako za uponyaji humu duniani.14. Maombi ya Baraka na KutawanyikaK: Bwana awabariki na kuwatunza.Bwana awaangazie uso wake na awarehemu; Bwana awasamehena kuwapa amani yake.Mwende kwa amani: kwa ujasiri na furaha; mkielewa kuwamnapendwa; daima mkielewa na kila mahali kwamba ninyi nimwili wa Kristo.Mwende kwa amani na mmtumikie Bwana wa uzima.28 KANISA


Jamii ilikuwa inapanga kumhukumu mwanamke aliyekuwa amekutwa akifanyamapenzi nje ya ndoa; mwanaume aliyekuwa naye ilikuwa asihukumiwe.Walimleta kwa mwalimu aliyekuwa mjini wakati huo. Mwalimu hakupingampango wao. Kwa urahisi alisema yeyote asiye na dhambi awe wa kwanzakurusha jiwe. <strong>Mmoja</strong> baada ya mwingine, kuanzia mkubwa hadi mdogo,waliondoka. Kwa hiyo jaribio la kugawa na kutenga lilitenguliwa, siyo kwamuujiza, lakini kwa ufunuo wa msingi ambao wote tunashiriki. Kwa njia hiisote ni mwili mmoja.ANGALIA YOHANA 8:2-11kanisaNorwayMwanamke AliyekuwaApigwe MaweWakati tunatafakari juu ya kuhusishwa kwa kanisa inakuwamuhimu Pia Kuangalia na kuchunguza sababu za msingi kwanini unyanyapaa na kubaguliwa kunachukua nafasi katika jamiizetu na unajisikiaje ikiwa wewe ndiye unayenyanyapaliwa.Funzo hili la Biblia pamoja na hadithi ya Zakayo katika Luke19:2-10, inaweza kutusaidia kufanya hili1. Soma Andiko Kimtazamo wa Haliyako na Changamoto Zinazokukabili.• Unaweza kusema kuhusu wakati ambao ulitendewa isivyohaki?• Au kuhusu wakati ambao ulilaumiwa kwa sababu ya jamboambalo hukutenda?• Ulitaka nini kifanyika ulipoona kuonewa?2. Soma Andiko PamojaSoma hadithi ya mwanamke ambaye ilikuwa apigwe mawe,Yohana 8:1-11, pamoja. Hili linaweza kuwa andiko lenye nguvusana, hasa awaliokandamizwa. Hisia kali zinaweza kuibuka unapofanyiakazi andiko hili.3. Soma Andiko kwa Umakini na kwa UndaniAndika maneno ya muhimu kwenye ubao. Jiulize maswali yajumla kuhusu andiko kwanza.• Andiko linahusu nini?• Nini kimekushtua kuhusu andiko hili?• Ni vipi andiko hili linahusiana na kutendewa isivyo haki?Halafu angalia kwa undani kwenye andiko:• Tunamkuta nani katika hadithi?• Tunajifunza nini kuhusu watu kwenye andiko?Inaweza kusaidia pia kuangalia mahusiano ya watu katikaKujifunza Biblia Kuhusu Unyanyapaaandiko, pia katika mtazamo wa kijamii, kisiasa, kidini na kiuchumi.Kwa mfano:• Unadhani waandishi walimtendeaje mwanamke?• Unadhani kwa nini waandishi walimleta mwanamke kwa Yesu?• Unadhani waandishi walimkamata mwanamke wapi wakatiakifanya uzinzi?• Unadhani Kwa nini hatusikii lolote kuhusu mwanaume aliyekuwaakifanya naye uzinzi?• Unadhani kwa nini hakuna amri inayosema mwanaumeapigwe mawe?• Nini Yesu anakifanya anapokutana na waandishi na mwanamke?• Kwa nini waandishi wanaondoka bila kumpiga mawe mwa ­namke?• Nini Yesu anadhihirisha kuhusu Mungu?Baada ya kuwa umelichunguza andiko kwa uangalifu, nimuhimu kuangalia maisha na hali yako mwenyewe.• Unaweza kujiona kwenye andiko?• Unajiona ukiwa na nani?• Je, uliwahi kupitia hali kama hiyo?• Nani unadhani anapitia hali kama hiyo leo?4. Soma Andiko Ukiwa naMtazamo wa Kufanya MabadilikoKujifunza Biblia hakumaliziki mpaka unapokuwa umeona kileunachoweza kufanya kuleta tumaini lililo kwenye andiko katikasiku zetu za leo.• Tunaweza kufanya nini kuwazuia watu hasa wanawake, katikaaina hii ya ukandamizaji?• Tunawezaje kufanya maisha bora kwa watu wanaopitiaukandamizaji huu?KANISA 29


kanisaKuonyesha Upendo na Uangalizi katikadenmarkPumziko Lenye TumainiMazingira Muafaka Kirohona Carina WøhlkPumziko ama kurudi nyuma kunaweza kuelezewa kama mkakatiwa kujitoa. Kijeshi neno hili halina maana ya kushindwa.Inaweza kuonyesha haja ya kusimama na kufikiri juu ya halifulani iliyojitokeza.Kuwa na mapumziko ni desturi ya muda mrefu ndani ya kanisa.Neno pumziko ndani ya kanisa lina maana kuwa ni wakatina mahali kwa ajili ya ukimya na kutafakari, Pumziko ni wasaawa kujitoa ili kupumzika na kukusanya nguvu.Yesu Kristo mwenyewe anatupa uwezekano wa kuwa napumziko. Katika Marko 6:31 Yesu anawaambia wanafunziwake, “ Twendeni mahali pasipo na watu tukapumzike”. Yesumwenyewe anatafuta wasaa wa kutafakari - hebu fikiria bustaniya Getsemane. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa nahamu ya kuwa na mapumziko na nguvu na mtazamo ambaovinaweza kuwapa watu wa dunia ya leo.Tangu mwaka 1991 nimeshirikiana na rafiki kutoka Chamacha Kitaifa cha Kilutheri cha UKIMWI katika kuwa na mapumzikokwa ajili ya watu walioathiriwa kwa VVU na UKIMWI – hiini kusema kuwa wale walioambukizwa pamoja na ndugu najamaa wa wanaoishi na VVU au waliokufa kwa UKIMWI. Mapumzikohufanyika katika kituo cha mapumziko kaika mazingiramuafaka.Changamoto mojawapo inoyohusiana na mapumziko imekuwani kutafuta uhusiano sahihi kati ya mazungumzo nautulivu. Mapumziko ya kwanza yalifanzika katika ukimya, natulitumia sauti zetu pale tulipoomba na kuimba. Kwa baadhiya washiriki hii iliwasababishia wasiwasi. <strong>Mmoja</strong> wa washirikialijisikia kama vile akili imenyenyuliwa na hakujua namna yakuendana na hisia na mawazo ya wasiwasi yaliyomjaa.UkimyaIlikuwa wazi kwangu kuwa watu wengi wenye VVU wanauhusishaukimya pamoja na kifo. Watu wanaoishi katika mazingiraya kutengwa na upweke kwa sababu ya hali zao ki-VVU wana-hitaji kuongea na si kuwa kimya. Ni muhimu sana kushirikianana kukutana na wenye virusi. Kwa kuangalia hali zao wenyewekwa wengine, watu wenye VVU wanaweza kujifunza mikakatimipya ya kuondoa ugonjwa.Miaka ya hivi karibuni tumetengeneza uwiano kati ya maongezina ukimya katika njia maalum. Tumehakikisha kuwa tunawezakutumia njia mbili zilizo zoeleka. Ya kwanza ni katika maongezina nyingine ni kwa wale wanaohitaji ukimya na ambaowanahitaji kuangalia zaidi mhitaji yao ya ndani. Kuongezeakila mshiriki ana njia moja ambayo anaweza kuitumia kutafutaamani na ukimya.Tunawapa motisha washiriki kuwa wawe kimya katika kipindikuanzia kuanzia ibada ya jioni mpaka wakati wa kifungua kinywaasubuhi inayofuata. Siku ya mwisho kabla ya ibada yakufunga tunakula kifungua kinywa kimya, tunawasiliana kwatabasamu, kukumbatiana na ishara.Mbiu ya PumzikoMbiu ya mapumziko kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa“Mwanga katika giza”, “Ujasiri kuishi”, “Wasiwasi au woga”,“Ukaribu”, “Furaha ndani ya uzima” “Makosa na msamaha”, na“Ifanyike”. Kila mwaka baada ya pumziko fomu maalumu yakutathmini hutumwa na tunawaomba washiriki kupendekezambiu kwa ajili ya mwaka ujao. Kwa njia hii washiriki wenyewekwa hamasa wanaijaza na kuamua kuyaweka mambo ya muhimukatika form.Pumziko lina mbiu maalum. Hufanyika mwishoni mwa wiki,kuanzia ijumaa mchana mpaka jumatatu saa sita mchana.Vifungu viwili vya maandiko katika Biblia vinavyohusiana nambiu ya mwaka huo huchaguliwa. Vifungu hivyo hujadiliwa,kimoja Jumamosi na kingine Jumapili.Pumziko hufungwa Jumatatu kwa ibada na sakramenti. Hudumahii hukusanya mawazo na hisia kwa msisitizo na mazungumzokwa mbiu ya mwaka husika imetekelezwa.Sakramenti na matumizi ya amani ki-liturjia katika ibada hu-30 KANISA


WimboUlio Kimyasisitiza wajibu wa pumziko la kuumba kusanyiko. Washirikiwanaweza kwenda njia tofauti wakijua kuwa hawajaachwa pekeyao.Mungu yuko pamoja nao – na kuna wengine wanaoshirikiuzoefu wao na kuusambaza nchi nzima.Siku mbili nzima tunazozitumia kwenye pumziko zina vipindivitatu vya kuabudu katika muundo wake: maombi yaasubuhi, tafakuri juu ya maandiko ya Musa na kusoma jioni.Mambo haya matatu ndiyo ya lazima kufanyika kwa kila siku.Kuwa pamoja katika pumziko, peke yake inatosha. Ni muhimukwamba mpango mzima usiwe wa kuchosha. Ni lazima kufikirihitaji la washiriki la kupumzika na mlo pamoja na dawa. Kwakuongeza ni lazima kuwe wasaa wa maongezi na matembezi.Ibada yenye MsisimkoKila mwaka kati ya watu 20 na 30 hushiriki katika pumziko –Mashoga na wasio mashoga walio na VVU, familia, marafiki nawale waliopoteza wapendwa wao kwa UKIMWI. Kwa ufupi Mapumzikoni wasaa wa muhimu na ibada yenye msisimko waroho kwa wale wenye VVU na familia zao. Fomu nyingi za tathminikwa miaka mingi zimethibitisha umuhimu wa mapumziko,kiroho na kijamii.Labda faida kubwa ya mapumziko haya ni kwamba zimetianguvu uanzishwaji wa jamii zinazomwabudu Mungu kwa ajiliya watu waishio au walioathirika kwa UKIMWI. Baada ya pumzikola kwanza, wazo lilitolewa la kuwa na huduma kwa washiriki.Kwa miaka jamii hii imeongezeka na ina watu 30.Hamu inayojirudia mwaka baada ya mwaka kwa ajili ya mapumzikona jamii ya wanaoabudu walioathirika kwa VVU naUKIMWI inasisitiza namna ilivyo muhimu kwa kanisa kuwakubalikundi hili la watu katika ibada zake. Kanisa la kikiristo nilazima lifike kwa wanyonge ili kuwavuta katika Upendo.Sijawahi kudhani kuwa imani ni kuhusu kile unachofanyakanisani. Imani ni sehemu ya maishayako, maisha yako ya kila siku. Wala sijawahi kufikirikuwa unaweza kuwasiliana na Mungu kwakuomba kabla ya kwenda kulala au kuomba neemakabla ya kula. Maombi ni wasaa mzuri sana tulionaokatika kuwasiliana na Mungu kwa ukaribu,na inaweza kutumiwa katika hali zote na nyakatizote – mchana na usiku. Nafikiri inapendeza sanakuomba kwa pamoja kanisani – kwa mfano kusemasala ya Bwana- lakini nafikiri ni muhimu kuwana mahusiano binafsi na Mungu.Ninajisikia huzuni ninapoona watu wanaopayukakwa sauti zao kufanya maombi hapa na paleau hebu tukae chini na tukunje mikono yetu naooh, ni kwa namna gani imani yetu ni kubwa ausisi ni wakristo safi. Ni muhimu kukumbuka kujitunzakila wakati, katika mazingira yoyote uliyomo,katika maisha yako yote.Sisemi kuwa maombi ni ya thamani au kwambahakuna nguvu ya kutosha kuwa katika uelewakuwa mtu fulani anaomba kwa ajili yako nakwamba upo katika mawazo ya watu kwa namnaya upendo. Nimeona matunda ya hili – lakinikwa ajili ya mahusiano yako binafsi na Mungu, nimuhimu usijifariji mwenyewe kuwa ni kitu unachowezakufanya unapopiga magoti pembezonimwa kitanda chako kabala hujazima taa.Ni wasaa tulionao kila wakati na ni kitu ninachokionakuwa cha thamani sana na muhimu paleninapoimba. Nafikiri ni katika kuimba nimekuwana ukaribu zaidi, ukaribu sana na Mungu. Nimejisikiakuwa kuimba imekuwa ni njia yangu ya kuomba– njia yangu ya kukiri imani yangu. Baadhi ya watuhuiita ushuhuda na wanaruhusiwa kufanya hivyo.Imani haina kitucha kufanya juu ya ufafanuzi. Imanihakika ni kitu rahisi na kilicho kimya na kilmelalapale kama uzi katika maisha yangu.USHUHUDA WA JASPER, ALIYEKUFA KWA UKIMWI, DENMARKKANISA 31


32 ujinsia wa binadamu


Nitatoa mkono wangu na mguu ili kuwa na kikundi cha Mduara wa Matumaini.Ninaweza kuwashirikisha watu hawa siri zangu za ndani kabisa nabado wakanipenda. Nilipougua kwa mara ya kwanza ilikuwa ni kikundihiki kilichonipa nguvu ya kuendelea mbele. Katika kundi hilo tuliongeleajuu ya maisha na pia tulipata mgeni aliyekuja kutufundisha juu yalishe, vipengele vya sheria, tiba mbadala na programu nyingi zingine. Nilipomsikiamwezeshaji akielezea hadithi yake jinsi alivyogundua yunaVVU, nilijiweka katika nafasi yake na kumwelewa. Hii ilinipa nguvu kutambuakuwa sikuwa peke yangu. Maisha yangu yaliokolewa kutokana nahili. Ndiyo maana najua ni jinsi gani hili ni muhimu kwa watu wengine.MJUMBE WA MDUARA WA MATUMAINI KITONGOJI CHA GARDENujinsia wa binadamuZambiaKujifunza Biblia Juu ya Ujinsia wa Binadamu, Unyanyapaa na VVUUbaba, Jinsia na YesuUtangulizi• Kwa mawazo yetu wenyewe dhambi ni nini?Kwa kirahisi tu, ngono ni tofauti ya kimaumbile baina ya wanawakena wanaume. Inahusu ukweli kuwa tunazaliwa wa-kujamiiana kuliko wanaume?• Je wanawake wanaonekana kuwajibika zaidi na dhambi zanawake ama wanaume. Kwa upande mwingine, ujinsia unahusuhisia za kijinsia, tabia zake na mahusiano yake. Ni uhusuano kiutamaduni yanayoamuliwa na desturi• Je tunatambua kuwa ujinsia wa kibinadamu ni maadili yabaina ya wapenzi wawili ama wale wanaotarajia kuwa wapenzi. • Je ujinsia ni kipawa toka kwa Mungu ama laana toka kwaLakini katika jamii mbalimbali, suala la ujinsia linalolinganishwa Shetani?na dhambi limejengeka ndani ya maadili ya kiutamaduni. • Ujinsia una faida gani kwa wanaume na wanawake?Mtazamo wa Kibiblia-Mwanamke aliyekamatwa akizinikatika hadithi hiyo tunaona jinsi dhambi ya kujamiiana ilivyosimikwakatika utamaduni na desturi za Kiebrania. Mafarisayowaliitunza sheria ya Musa, yaani torati. Walimletamwanamke waliyemkamata akizini ili kumjaribu yesu. Jibulake kwa maswali yao liliwapa changamoto kubwa washitakiwake. Yesu akasema, yeyote kati yenu asiye na dhambi awewa kwanza kumtupia jiwe. Alimlinda yule mwanamke. Washitakiwake waliondoka mmoja baada ya mwingine wakiwawamevunjika. Yesu akamwagiza yule mwanamke asifanyedhambi tena naye akasamehewa.• Je tunafanyaje kwa wale wanaoshutumiwa leo?• Je tunawapa changamoto ile ile waliopata wenzetu?• Je tunasamehe ama bado tunabeba mitazamo ile ile?Tafakuri• Tungependa kujua kwa nini yule mtu aliyehusika na tukiohilo hakuwa na wasi wasi wowote.HitimishoHadithi kutoka Yohana 8:3-11 inazungumzia hadhi: “Musa alituamurutuwapige mawe wanawake wa jinsi hii.” Uanaumena hali zinazofanana zimeshamiri katika kanisa leo. Dhambiya ujinsia imenyanyapaliwa kama DHAMBI ILE. Yesu aliwapachangamoto wanaume wa Kiebrania katika jibu lililotolewa.Yesu alifahamu shabaha yao katika kuwabagua wanawake.Tunamsikia Yesu akisema:• Ujinsia ni kipawa kutoka Mungu – Mwanzo 1:27-28• Ujinsia unabeba daraka fulani• Unahitaji kuwajibika kikamilifu kwa watu wa jinsia zote• Zaidi ya yote unahitaji kupendana (Efe 5:25-32; Col.3:12-13)Maadili ya kijamii na mafao yake yamejengwa katika mitazamoiliyojengeka kwa wengi katika jamii ambazo kwa upandemwingine zinaendeleza mifano ya watu kama wababe nawenye nguvu, na wanawake ama wasichana kuonekana kamawale wasio na nguvu, na hii inategemea majukumu ya kanisakuondosha udhalimu wa kijamii na ubaguzi wa kijinsia.ujinsia wa binadamu 33


ujinsia wabinadamuUjinsiaZambia- Kipawa na wajibuUtaratibu wa Ibada juu ya Ujinsia3. Somo la UfunguziI Korintho 7:3-124. Wimbo wa Sifa5. Maombi ya KufunguaK: Mtakatifu Mungu uliye haiAmbaye tumetokana na mkono wako wa kiufundiTunakushukuru kwa kipawa hiki cha ujinsia,Tunakushukuru kwa kazi zako kuu,Utuongoze ili tuweze kuikubali miili yetuNa kwamba tuweze kuuelezea ujinsia wetu katika njia ya kuwajibikazaidi.Tuongoze kukubali kuwa sisi ni hekalu la Roho MatakifuUtusamehe tunapoupungukia na kuupunguzia makali uumbajiwakoUtufundishe ili tusitumie vibaya uwezo wetu wa kuvutia ki-Utaratibu huu wa ibada uliandaliwa na kutumiwa na Duara mapenziza Matumaini huko Busokolo mjini Lusaka, Zambia. Duara za Utupe ujasiri wa kupinga mifumo yote inayogeuza miili ya binadamukwa biasharamatumaini ni vikundi vya misaada kwaajili ya wanoishi na VVUna UKIMWI.Kwa Roho wako, utuwezeshe kufurahia ujinsia wetuK: KiongoziTunaomba kwa Jina la Yesu KristoM: MsomajiK: Sasa tuzingatie kwa muda kidogo na kuleta mbele ya mawazoyetu mabaya ambayo tumeyatenda katia eneo la ujinsia.1. Msafara na nyimbo zikiimbwa.6. Sala ya Toba2. Salamu na Ukaribisho wa WageniK: Katika nafasi zetu na katika majukumu kama watu binafsiK: Ndugu kaka na dada zangu, tumekusanyika hapa leo kusherehekeauzuri wa uumbaji wake Mungu na huu ndio uzuri jafikiria na kuyafanya yale yote tunayopaswa kuyafanya kuelezea– baba, mama, walezi wa kiroho, viongozi wa vijana n.k. hatu-wa ujinsia wetu. “Kwa hiyo Mungu aliumba wanadamu kwa uzuri na fumbo la ngono, ujinsia na mahusiano mazuri. Kwa wingimfano wake.Kwa sura na mfano wake aliwaumba; mwanaume tumedumu katika mambo hasi yanayohusu ngono na hivyo kuupagaishaujinsia. Mungu tunaomba msamaha wako.na mwanamke aliwaumba….Kisha Mungu akaona kila kitu alichokitendakuwa ni chema.” Kwa hiyo, kwa maombi na sifa fikrana matendo, tumwabudu Mungu wa milele. Amina7. Wimbo8. Masomo Mwanzo1:27, 2:249. Mwongozo wa Mahubiria. UtanguliziWakati mamilioni ya watu wanaishi ama wameathiriwa kibinafsina VVU na UKIMWI, ugonjwa huu ni mojawapo ya matatizomakubwa sana katika zama zetu. Taasisi za kidini kwa ujumla namakanisa yote kwa pamoja yana nafasi kubwa ya kupambana nakuenea kwa ugonjwa huu kutoka mtu mmoja kwenda mwingine.Mungu aliumba wanadamu wakiwa na hisia zenye nguvuza ujinsia ambazo wanadamu wanaweza kuzitumia vizuri amavibaya. Hisia hizi zenye nguvu zinaweza kubebwa maishani nakufanyiwa kazi kwa njia ya kuwajibika. Kazi moja ya kanisa ni kuzungumziajuu ya maadili na uwajibikaji na kusaidia kupunguzamazingira hatarishi kupitia elimu. Ukristo umenyanyapaa ngonona kuifanya dhambi juu ya dhambi zote na kumbe imani ya Kibib-34 ujinsia wa binadamu


lia inaielewa dhambi kuwa ni dhambi.Tunaposherehekea ujinsia wetu, tunafanya yafuatayo:• Tunakubali kwamba Mungu aliwaumba wanadamu wote –waume kwa wake – katika sura ya Mungu, na kwa kufanya hivyoalitupa kipawa cha kuthaminiwa, kufurahiwa na kuenziwa.• Kuukubali ujinsia kama sehemu maalum ya utambulisho wetuinadumisha ushirikiano baina ya watu na kuleta starehe.• Tunakumbushwa kuwa pamoja na uwezo wa kuboresha mapenzina furaha katika uhusiano wa kibinadamu ujinsia unawawekawatu wazi baina yao wenyewe na pia mbele ya nguvuza kijamiib. Mafunzo yaliyotolewa• Uumbaji wa wanadamu kama mwanaume na mwanamkehaukuwa wa kubahatisha;• Kujamiiana katika ndoa ulikusudiwa na Mungu kutoa mafunzoya kisaikolojia, kimwili, kihisia, na ukamilifu wa kijamiina kiroho, zaidi ya kuzaa na kuongezeka tu.• Ikiwa familia ya Kikristo haiwezi kutoa majibu kwa vijanachipukizi, basi itawapoteza hao kwa watu wengine watakaoweza.Ikiwa kanisa litakaa kimya, nalo litawapoteza pia.10. Maombi• Omba kwamba Mungu atupe hekima kufundisha kuhusukile kilicho sawa na salama juu ya ngono, matendo ya kujamiiana,na mahusiano kwa kuzingatia VVU na UKIMWI• Kuwaombea wanawake na watoto waliodhalilishwa• Kutoa shukrani kwa ajili ya uongozi wa Mungu, ulinzi,na nia kwamba tuishi maisha yenye maendeleo namanufaa.11. Matoleo - Huku nyimbo ikiimbwa12. Sala ya kuombea Matoleo13. Baraka ya KufungaK: Bwana Mungu wa amani mwenyewe awatakase ninyi nyotekikamilifu; na roho zenu nafsi na mwili zihifadhiwe bila lawamahata kuja kwake Bwana Yesu Kristo. Neema ya Bwana wetuYesu Kristo iwe pamoja nanyi Amina.14. Wimbo wa KutawanyikaUjinsia wa kibinadamuUjinsia wa mwanadamu kwa hakika ni kipawa toka Mungu amabacho Kinapaswakufurahiwa na wapenzi wawili. Kipawa cha ujinsia kinaendelea kuwepondani tya watu wanaosihi na VVU na kinatakiwa kutumika na si kukandamiza.Ujinsia ni uumbaji wa ajabu wa Mungu, na unapaswa kufurahiwa nawote wanaoshi na VVU na wale wasio navyo.Duara zenye a Matumainiujinsia wa binadamu 35


norwayKutoka kujifunza Biblia Yoh 8:2-11Nani AnayedirikiKurusha Jiwe la Kwanza?Kila mwaka ibada katika Siku ya UKIMWI duniani ndani ya KanisaKuu la Kilutheri mjini Oslo Norway, hutayarishwa huko Aksept -Kituo cha Kimisheni cha Kanisa Jijini Oslo kwa wote wale ambaowameathiriwa na VVU. Mwaka 2002 mahubiri yaliandaliwa kwakushirikiana na wateja wa Aksept. Ifuatayo ni taarifa ya mchakatona mahubiri yaliyotolewa katika ibada hiyo.Unyanyapaa, ubaguzi, na ujinsiaMchakato ulianza kwa wasaa wa kubungua bongo kutafutamasomo na maandiko ambao ulionekana kuwa wa kufaa ulifanyikakwa wakati muafaka na ulioenda sambamba na walewalioshiriki mijadala husika. Kumbukumbu toka katika mikutanohiyo iliweka msingi wa kuandika mahubiri hayo. Shabaha ilikuwakuendesha mazungumzo baina ya wanadamu na Mungu - mahubiriyanayosikiliza, yanayoelewa, yanayofariji na yanayoletachanga moto. Mbinu iliyotumika inaweza kuwa msaada kwa kupatamfano wa mahubiri na hata kuwa mahubiri yenyewe. Zaidi,inatupatia undani wa kufikiri na hata kufanya mazungumzo katiya wale walioathirika kwa VVU, mchungaji na kifungu cha Biblia.1. Kubungua bongo kwa mara ya kwanza:Watu wanaoishi na VVU walioko Aksept walipata fursa ya kukutanamara mbili kwa kazi ya kikundi na kusema kitu juu ya kilewanachodhani kuwa ni muhimu kuelezea katika siku ya UKIWI Duniani mwaka huu. Asubuhi ya kwanza ilikuwa pamoja na“mjadala wa mwanzo juu ya maadili, dini, na falsafa kituoni.Hizi ni baadhi ya kumbukumbu zilizonakiliwa daftariniMatakwa na fikra juu ya ibada• ujinsia ungekuwa somo kuu mwaka huu• kanisa limehamishwa mbali sana na ukweli linapozungumziangono• hata msimamo wetu kuhusu ujinsia ni mgumu kuutekeleza• ingelikuwa sahihi kuendesha ibada ya mseto ya madhehebuyote ya kidini katika siku kama hii! VVU na UKIMWI umetuathirisote.Tunataka kusema nini kwa Mungu, Mahubiri yanaweza kuwakama mazungumzo kati ya Mungu na wanadamu• hitaji la dawa ya kuukomesha UKIMWI• kukubalika zaidi kutoka watu wengi. Ni lazima Mungu afunguemacho ya watu• haja ya kupata mtu wa kumpenda. Wale wenye VVU wanahitajikupata nafasi ya kupenda.• mzigo moyoni kwa watoto wanaozaliwa na VVU• Kwa nini mimi? ni vigumu kuikubali hadhi ya mtu; kughasighasimtu humkasirisha!• haja ya kumsaidia mhusika kurejea mahala pa kazi. Watubado wanakutana na ubaguziWale wanaoishi na VVU hawaundi kikundi cha watu wenye36 ujinsia wa binadamu


ujinsia wa binadamuUnyanyapaa awali ya yole, ni mfumo wa kulinda.Inaunganishwa na fikra kuwa kuna kitu ambachohakipo sawasawa kinachotutisha. Maranyingi; kitu ambacho hatukijui ama cha kigeni.Hofu yetu yaweza kuwa na sababu kamili amayaweza kuwa haina msingi wowote. Hata hivyo,tumejitungia mawazo na mifano juu ya vile tunavyoviaminikuwa ni hatari. Haya ni mawazoambayo huenda hatuyaelewi vilivyo, kwani unyanyapaahujenga mizizi yake katika fahamuzetu zizlizolala –katika mitazamo na mawazotulio nayo, lakini tusiyoyazungumzia na hatakuyakubalia. Ili tuweze kuhakiki sura hizi, tunahitajiutashi na ujasiri wa kujaribu misimamoyetu dhidi ya ukweli, na kuzifanyia tathminiukizipima na mtazamo wetu juu ya ubinadamutunaodai kuwa nao. Lakini huu unaweza kuwamchakato wenye shida nyingi hivyo fursa zinazojitokezazinahitaji kuimarishwa kwa makusudikabisa na nafasi salama zikipatikanaKUTOKA TAFAKURI ZA KITHIOLOJIA MJINI OSLOya UKIMWI Duniani yanaweza kufuata mwelekeo kwamba walewote wanaoishi na VVU si waaminifu kwa wake ama waumezao. Hii yenyewe ni mtazamo wenye kunyanyapaa.4. Mahusiano yanayowezekanaKwa upande mwingine, kifungu kinachokoza vyama vingi. Katikamkutano wa pili, majuma mawili yaliyofuata, tafakuri ilifanywakwa kifungu toka Yohana 8:2-11.Mwanamke huyu alikuwa tayari amekwisha hukumiwa nawale watu waliomleta kwa Yesu. Hao Mafarisayo na Waandishiwalikuwa na hatia gani? Je waliiona akisi yao wenyewendani ya mwanamke yule? Lazima tujikague wenyewe kablaya kuhukumu wengine.Waandishi na Mafarisayo walionyesha mtazamo hafifu kuelekeawanawake. Je mwanamke yule anajua nini kinachoendelea?Mwanaume naye, Je yuko wapi? Inawezekana hakufanyakitu chochote kabisa. Alikuwa ni mwathirika tu katika jamii iliyomilikiwana wanaume. Je mwanamke huyo alikuwa na VVU?Je alikuwa ameshitakiwa kwa kumuambukiza mtu? je mwanamkealijiamulia mwenyewe kujihusisha na shughuli iliyokuwaimetengwa kwa ajili ya wanaume? Je alikuwa akifanya biasharaya ngono? Ama alikuwa mwanamke aliyempenda mwanaumena akawa mwathirika wa ndoa ya nguvu. Kuna kila uwezekanohapa. Kifungu hakituelezi chochote kuhusu mwanamke yule.Naye hasemi chochote cha kujitetea.Tunajifunza zaidi kuhusu wanaume waliompeleka kwa Yesu.Walitaka kumtega mtego Yesu, ama kwa kumlazimisha aifuatesheria na kanuni au kuthibitisha kuwa alikwisha jitenga na kanuni,sheria na desturi za Kiyahudi. Wanathiolojia na watauwawaliifahamu sheria, walikuwa mafundi katika hiyo. Kulinganana sheria, mwanamke yule alipaswa kupigwa mawe! Nao walikuwatayari kufanya hivyo. Je walikuwa wamemwelewa vibayaYesu wakidhani kuwa yu upande wao?Lakini wanaume hawa walikuwa na nini katika dhamiri zao?Kwa nini walikuwa na hamaki sana? Je walikuwa kinyume nawanawake walioendesha maisha yao wenyewe ya kujamiiana?Je walikuwa ni wandume waliokuwa wamefadhaishwana mambo? Je walikuwa wametimiza matendo mangapi yaudhalilishaji wa ujinsia? Hatuelezwi chochote lakini tunawezakutumia dhana zetu....Kifungu hiki kinaangaliwa kwa kuhusiana na VVU na kinanyanyapaajinsi kilivyo: VVU havihitaji kuzungumziwa pamojana kutokuwa mwaminifu. Zaidi ya hayo ngono si pekee inayasiliamoja ama kabila moja. wanawake na wanaume, vijanakwa wazee, wenyeji wa Norway na wageni, mashoga na wasiomashoga, n.k.Katika Siku ya UKIMWI Duniani dhamira mbili kuu zilijitokeza:). Unyanyapaa/ ubaguzi na2.Ujinsia. Katika mkutano wa kwanza tulifanya kazi kutafutakifungu cha Biblia kitakachokuwa msingi wa kutafakari juuya maudhui haya mawili. Hivyo ilipendele zwa kufanya rejeakwa Wasamaria - Wasamaria walikuwa kundi lililonyanyapaliwana kubaguliwa wakati wa Yesu. Lakini kuna rejea chache zinazohusikana ujinsia katika kifungu kile. Wimbo wa Sulemanipia ulitajwa, lakini hautaji chochote juu ya unyanyapaaji. Hatimayetuliishia na hadithi juu ya mwanamke aliyepatikana nazinaa.2. Yoh 8:2-11 Inasomwa3. Mwanamke aliyepatikana na ZinaaHatukuwa tumeridhika na kifungu hiki pia, kwa sababu kiliunganishaujinsia na utendaji dhambi. Kifungu hicho pia kingewezakuonekana kama kinanyanyapaa; kwa nini ni mwanamketu peke yake aliyekamatwa katika tendo hilo? Nini kilimtokeamwanaume yule (lazima tudhanie kuwa kuna mwanaume aliyehusika)?Pia, mashirika na vyama katika siku kama hii, Sikuujinsia wa binadamu 37


ngono. Wengi wanatazamia kukutana na mtazamo wa jinsi hiihata katika sekta ya huduma ya afya. wapo wengi walio na VVUambao hawatadiriki kufanya ngono na wengine kwa sababu yakuogopa kuwaambukiza wengine, pia wanafikiri hawafai tena nahakuna atakayetaka kufanya ngono na yule ambaye ana VVU.Wengi wameeleza juu ya matukio yanayofanana kiasi fulanina lile la mwanamke katika kifungu cha Biblia. Wengine wamejiwekawazi kwenye vyombo vya habari kwa kuwa walijiachia wenyewena kufanya ngono na mtu fulani, lakini tofauti na hadithihii leo watu wapo tayari kuliko kawaida kutupa mawe, hasa kwakuwatwika majukumu makubwa watu wanaoishi na VVU zaidiya wale wasio navyo. Je mawe haya hufananaje?“Umepata kile unachokistahili.” “Usinikaribie!” Umeleta aibukatika ukoo wako!” hii ni baadhi ya ya jinsi mawe hayo ‘yalivyo’,na yanauma zaidi ya mawe halisi.Sababu kubwa ya kuwanyanyapaa watu wanaoishi na VVU nikuwa VVU vimeunganishwa na mambo mengi ambayo yamekwishakuhukumiwa kuwa ni dhambi katika utamaduni wetu:ujinsia, ukahaba, matumizi ya madawa ya kulevya, ushoga,uasherati, na kadhalika.Watu wametupa mawe katika mazingira ya jinsi hiyo kwa karnenyingi, ijapokuwa kuna hadithi kama ile ya Yohana Sura ya 8.6. Wanadamu kama Viumbe wenye UjinsiaJe tufanye nini ili tuondokane na hawa wenye uchu wa kuyatupamawe yao? Tunawapata hao ndani yetu wenyewe, ikiwatutazichunguza nafsi zetu.Huenda inasaidia kuzungumzia ujinsia katika njia iliyo wazi naya moja kwa moja kama inavyowezekana si tu kwa jinsi inavyopaswakuwa ama jinsi gani mtu anavyotaka kuwa.Ujinsia si kile kitu alicho nacho mtu: ni vile mtu alivyo. Ujinsiani jambo kubwa na gumu ikiwa pamoja na VVU ama bila VVU.Ni vigumu mtu kuishi katika viwango vyake vya kimaadili. Ujinsiunajumuisha yote mafanikio na mapungufu. Ni jambo la kimbinguna pia linafadhaisha. Linaweza likawa na utata nje amandani ya ndoa. Hakuna furaha itakayokuwa bora zaidi, hakunaitakayokuwa wazi zaidi.Ni vigumu kuzungumzia juu ya ujinsia wa mtu binafsi, yotehasa kuhusu nyakati za furaha na zile nyakati ambazo mtu angependazisitokee. Inauma sana kujisaliti mwenyewe, kwa sababuwapo watu wamesimama mstarini tayari kutupa mawe.Wengi ambao wana VVU wanapitia ukweli kwamba virusi vyujinsiawa binadamuoleta maambukizi ama kueneza ugonjwa. Lakini kila kitu kinachohusikana ngono tayari kina hatia. Dhambi kwa hakikainakuwa dhana potovu katika mantiki hii kwa sababu ngonoyenyewe si dhambi. Lakini ngono inapata ugumu tunapoingizaVVU. Ngono ilikuwa na ugumu hata kabla ya VVU watu wenginewameacha kufanya ngono baada ya kupata VVU. Mwanamkekatika kifungu hicho alihukumiwa na jamii yake yote, nasisi pia tunahukumiwa na jamii yetu nzima. Mtu ameondolewahaki yake ya kuishi kwa kuwa tu ana VVU. Watu wanasema“wamepata kile walichokistahili”: “Ni hukumu ya Mungu”, badounasikia wachungaji na mashehe wakizungumza namna hiyo.<strong>Mmoja</strong> katika kikundi alisikia kisa cha mwanamke aliyeuawakwa sababu ya uzushi usio na kweli!Dhambi ni nini? Ni kwa jinsi gani tutauhudumia “Ujinsia uliomzuri”. Ni vibaya wakati wengine wanapoelezea na kuamuadhambi ni kitu gani. Inapaswa kuwa jukumu la mtu binafsi,kwa sababu kile ambacho wengine wanaamini kuwa si sawachaweza kuwa sawa kwa mwingine. Je vipi kuhusu wale ambaobado hawajaolewa? Lakini kutokuwa mwaminifu ni dhambi;kwani daima mtu mmoja huumia mwishoni.Je ina maana gani kutupa mawe leo? Ni matendo ya hukumu,kujiweka juu ya wengine na kuwatenga wengine. Nchi 183hazitoi vibali vya kuingia nchini kwa watu wenye VVU. Lakinitumewahukumu pia wale waliotuambukiza? Je tumewatoleataarifa? Ama sivyo? Ngono ni tukio ambalo wahusika wotewawili wanawajibika wakati uhusiano ni wenye usawa. Itakuwajeikiwa utakamatwa katika hali ya kufanya ngono, na labdaukimwambukiza mwingine na VVU “Kama ningejua nimemwambukizamwingine nimpendaye - ningeweza kuimudu halihiyo.”Je mwanamke alipokea jibu? Je amesaidiwa? Hata nami sikuhukumu!Haya ni maneno yenye maana sana. “Nenda nausifanye dhambi tena.” Je hiyo ina maana hakuna ngono tena?Ama ina maana: “Ondoka hapa na uishi maisha ya ‘kawaida’kuanzia sasa? Ondoka na ujitunze mwenyewe; epuka ubaya,usiruhusu mtu akudhuru tena.”Je ni kipi kinacholeta mabadiliko katika mitazamo? Ufahamu,ujuzi wa mtu binafsi:”Ingeweza kuwa mimi.”5. UbaguziKuna mambo mengi ambayo tunaweza kuyatambua. Watu wenyeVVU mara nyingi wanakutana na mtazamo huu: usifanye38 ujinsia wa binadamu


enyewe vimekuwa ni ishara ya usafi katika ujinsia; inafunuadhana kwamba mtu husika hakuishi maisha yaliyonyooka.Kana kwamba kila mtu huishi maisha hayo.7. Unyanyapaa na UbaguziNi jambo la kuzingatia kwamba Kanisa ambalo limerithi hadithihii ya mwanamke aliyepatikana na kosa la zinaa halijawezakuwaelimisha waumini wake na kubadili utamaduni wakewa kuhukumu, angalau kuupunguza kidogo. Badala yake,tunayo historia ya kanisa ambapo watupa mawe wamepewauhuru wa kufanya mambo yao watakavyo. Wakati umefikaambapo tabia hii ya unyanyapaaji na ubaguzi itambulike kwajinsi ilivyo, yaani kama dhambi kinyume cha Mungu na injili.Kama ujinsia ni zaidi ya kuzaa tu - na ndivyo ilivyo - basi lazimauwe kitu ambacho kila mmoja ana haki nacho, si kwa wateulewachache tu - bila kusahau umuhimu wa kuwajibika. Hapapawe mahala pa kuanzia kwa mazungumzo yote juu ya jinsitunavyoweza kuishi pamoja kama viumbe wenye ujinsia. Natutakaposhirikisha kila mmoja katika hili ndipo tutakapowezakuondoa mipaka ile ya ubaguzi tuliyojiwekea. Na inaenda bilakusema kuwa hii lazima ijumuishe watu ambao wanaishi naVVU.Unyanyapaa upo wazi. Watu wanaoishi na VVU wamekataliwavibali vya kuingia nchini katika nchi 183 za dunia, madaktariwa meno wamekataa kuwatibu, marafiki wao wamewasutahata wafanyakazi wenzao mahala pa kazi. Yote hayayanajengeka na kuwa mitazamo kinyume cha ujinsia ambayoyanalingana na kutupiwa mawe.8. ”Hata mimi sikuhukumu!”Hii ndiyo injili: “Hata mimi sikuhukumu.” Baada ya kulibainihili: kwamba hakuna mtu aliye bora kuliko wengine inapokujakatika maisha ya ujinsia, nini hatua ya baadaye? Sisi tutaishijepamoja katika katika maisha yetu ya ujinsia? Tutawezaje kuzuiakuumizana? Tutawezaje kumheshimu kila mmoja? Tutawezajekuvumilia fumbuzi zingine, na kadhalika?Yesu alimwambia yule mwanamke hatimaye kuwa - “usitendedhambi tena.” - hii haina maana kufanya ngono siku zijazo.Zaidi ni suala la kujiangalia mwenyewe kwa siku zijazo. Hii nichangamoto! Hatutaukwepa mjadala juu ya haki na kile kisichohaki. Lakini tunaepushwa na unafiki ambao watu wengine nibora kuliko wengine katika eneo hilo.Je ina maana gani kuwa binadamu? Kuwana VVU ama kutokuwa navyo, maishayote na maisha ya kila mmoja ni maishayaliyo hatarini, kila maisha ni maishayaliyowazi. Ndani ya tofauti zote, kilamtu yu tupu na katika maana halisi yaneno, amejeruhiwa.Tunakumbushwa juu ya hili kila mara.Hata hivyo, tunajaribu kulikataa, nakuliweka mbali, tunajaribu kujishawishiwenyewe na wengine kwamba tukosalama, wazima na sisi si wa kufa.Ushirika wa kweli unawezekana tu palewatu wanapokuja pamoja na kutambuakuwa kila maisha yao binafsi yapo wazikwa jambo lolote - si kama ufahamu tulakini kama taarifa ya uwazi unaomkabilimtu yeyote kuweza kukutana najambo lolote yumkini hata kupata majeraha.Kisha ipo nafasi ya kukutana bainayetu, tupo katika ngazi moja na hivyotunaweza kuzungumza.KUTOKA TAFAKURI ZA KITHIOLOJIA MJINI OSLOujinsia wa binadamu 39


kujamiianaKweli zilizopo katikasura nzima ya UKIMWIdenmarkMaana, Kifona Upotevuna Elizabeth Knox-SeithKatika utamaduni wa magharibi, kifo huonekana kama tukiola kushindwa – na kuwa mgonjwa, yaani kuwa katika hatari yakufa, kunakuwa kulingana na ufahamu wa ndani namna mojaisiyo ya kupendeza sana ya adhabu. Kwa kuwa tumejaribu sanakutokomeza kifo kama sehemu mojawapo ya mzunguko wetuwa maisha, hivyo kuwa mgonjwa, ambayo ni kama kuwa katikamchakato wa kufa kunakuwa tishio katika utu wetu wa ndani.Ni lazima tusife: chochote na kitokee sisi ni lazima tuishi –milele ama kwa muda mrefu tunaoweza. Hili lenyewe hugeuzaugonjwa kuwa tukio la kushindwa.Ili tuweze kuelezea kuwa kifo ni sehemu asilia ya mzungukowa maisha yetu mara nyingi tumetafuta sababu binafsi za mtukuwa mgonjwa. Tunasema, ni mtu mwenyewe ndiye aliyekosea,aliyeshindwa kimaadili. Mtu huyu amefuata tabia ambayoni sahihi na haki kama ataugua. Ugonjwa na kifo una maana nzitosana katika utu wetu wa ndani kwani vyote vinaashiria kuwahatuna haki ya kuishi. Pale mateso yanapotufikia, yanatuambiajapo si moja kwa moja kuwa tumepoteza maana yetu kama wanadamu,yaani haki yetu ya kuishi.Kwa njia moja, namna hii ya kufikiri inafanya vitu kuwa rahisikwa wote wanaoishi na wote wenye afya. Wale wanaoumwa wanaweza,ikiwa tu watabadili mtindo wao wa kuishi na kuachiliawanayoyaita kuwa ni “makosa”, matumaini ya kupata tena hakiyao ya kuishi na hivyo kupona kutoka ugonjwa walio nao – nawale walio na afya njema wanaweza wakati ule ule kwa ushindikutangaza kuwa wale wanaoishi maisha yenye haki na sahihinao watapewa haki ya kuishi mileleLakini ugonjwa kama UKIMWI unaumbua udhaifu ambao kilamwanadamu na kila jamii hata ile iliyo duni kabisa inaupitiawanapokaribiwa na ukweli kama vile kifo. Katika maudhui yakukata tamaa UKIMWI huchipua swali, kwa nini mimi? Kwa ninimimi nifikiwe na haya? Kwa nini mimi nipoteze maisha? UKIMWIumeweka wazi kuwa kifo kinaweza kuingia katika umri wowotena kwamba tiba ya kisasa haithibitishi ongezeko la maisha yamilele. Na kama swali halinihusu mimi, linaweza kumhusu kakayangu, dada yangu, rafiki yangu wa kike, rafiki yangu wa kiume,mwanangu ama dada yangu, baba yangu ama mama yangu.Ikiwa mtu fulani aliye karibu yetu akaangukia eneo la hatari basiswali hilo huwa halisikiki tena katikati ya maumivu tulio nayo40 ujinsia wa binadamu


Uzoefu wa upendo, kukubalika na msaada baina ya vikundi vya hudumaambapo upendo wa Mungu hudhihirika inaweza kuwa nguvu kubwa yauponyaji. Uponyaji unalelewa pale makanisa yanaposhiriki maisha ya kilasiku mahali ambapo watu hujisikia salama kusimulia habari na shuhudazao. Kupitia ibada za kweli, makanisa husaidia watu kuingia eneo la uponyajila Mungu. Makanisa yana huduma muhimu sana katika kuhimiza majadilianona changanuo za habari, kusaidia kutambua matatizo na kuungamkono ushiriki kuelekea mabadiliko yenye maendeleo katika jumuia.Japhet Ndhlovu– uwezekano wa kumpoteza huyo “fulani” unakuwa ndiyo kigezokitakachotawala juhudi za dhati za kutafuta maana halisi yamambo hayo yote.Kuambiwa UkweliTaarifa ya kuambiwa kwamba una VVU huleta mshutuko kwakaribu kila mtu kwani ni kama pigo kubwa ambalo hubadilimaisha yao kabisa. Kila mmoja ambaye amekwisha pimaVVU na UKMIWI anajua jinamizi ambalo mtu hupitia, hasapale mtu anaposubiri majibu yake. Hata mtu angejaribu kujiandaanamna gani kupokea majibu hayo imekuwa vigumukujiandaa. Hata kwa wale wanaofikiri kwamba hatari ya kuambukizwani ndogo kusubiri ni zoezi ambalo wangependakutokuwa nalo. Haishauriwi pia kuchukua vipimo ikiwa haunamtandao wenye nguvu unaokuzunguka. Kukabiliwa na hatariya kupata maambukizi ya VVU ni kukabiliwa na maswali yamsingi mengine bado kufikiriwa, na kama utaachwa pekeyako ukiwa na matarajio mbalimbali na mashaka mengi yanayohusikainaweza kukuletea madhara binafsi.Shauku ya kuhukumu ni sehemu maarufu ya mfumo wa kihisiakuhusu VVU na UKIMWI, yote kwa wote walioambukizwana kwa familia zao. Je majirani wasema nini ikiwa watagunduaya kwamba mwanangu….? Je mama na baba yangu watasemanini, ikiwa watafahamu kuwa nime….? Daima nimekuwabinti mzuri …..Je watafikiri nini sasa….?Picha zinacheza mbele ya macho ya akili zetu mara tu mazungumzoyanapogeukia VVU na UKIWMI – na swali litakaoulizwaambalo daima haliulizwi kwa sauti ni, Je ameambukizwanamna gani?Ngono bado ni eneo ambalo limezungukwa na fumbo, matarajiona hofu - na hakuna mipaka katika mawazo ambayohufufuliwa na hoja kama hii hasa pale mtu anapogunduakuwa mtu aliye karibu nao ameambukizwa.Maswali ya hatia siku zote hubakia nyuma tu – na hivyoni muhimu kumkamata ngombe dume katika pembe zakena kusema hilo haliwezekani kutofautisha baina ya “hatia”na “wahanga wa VVU’ wasio na hatia. Wote wamo katikamtumbwi ule ule, bila kujali wameambukizwaje. Kwambamtu anaweza kuwa na uzoefu binafsi wa hatia na fedhehaunaohitaji kushughulikiwa, ni jambo lingine – lakini uzoefuhuo unaweza kuwa na ugumu pia, tena bila kuzingatia virusivilipatikanaje. Mama atakayeruhusu mtoto wake apewedamu kabla damu hiyo haijapimwa, anaweza kuwa na mzigomkubwa sana kuubeba wa hatia – na ni lazima asaidiwe kwanamna ile ile ambayo yule aliyeambukizwa na mpenzi wakewa kiume angehitaji kusaidiwa ili kushughulikia hasira anayowezakuwa nayo dhidi ya mpenzi wake na nafsi yake. Matukioya kujisikia hatia na kuona aibu mara nyingi ni matokeoya kutoikubali hasira. Huyo ni ngombe ´ dume mwingineanayepaswa kukamatwa pembe, na hiyo inahitaji juhudi zakutosha –lakini huwa ni amani sana pale ngombe dume huyoanapokuwa ameondoshwa njiani. Mafahali wanaweza kuongozwakwa kuzikamata pembe zao kwa wakati muafaka,lakini hiyo ina maana ya kuwepo mapambano daima. Kamawataruhusiwa kubaki hasara itakayopatikana itakuwa sawana ile katika duka la vyombo vya udongo.Shauku kwamba watu wote wana uzoefu kutokana nakuogopa yasiyojulikana, kifo na njia ile ambayo ugonjwahusika utafuata, mara nyingi kwa muda mrefu. Kwa mtualiye na VVU, kisichojulikana hujulikana, ama kitajulikanahatua moja baada ya nyingine na muda ukiendelea. Kwa kawaidawale ambao wapo karibu ya watu wenye VVU hujikutawakiwa na shauku kubwa kuliko hata wahanga wenyewe,hasa kwa sababu wao wenyewe hawaupitii mchakato huona wanaweza kudhania tu jinsi gani yalivyo mateso hayo.Hofu ya kitu gani kitatokea ni kubwa zaidi kuliko hofu aliyonayo mtu wakati jambo limekwisha tokea na linaendelea kuwepo– na kwamba watu wengi wanaoishi na VVU wanawezakusema sambamba kuwa ni nafuu wanapozifikia awamuza ugonjwa waliougopa hapo awali. Hii haina maana kuwashauku inapotea- daima kuna kitu kipya kinachoweza kutokea:awamu mpya za ugonjwa unaoambaa katika upeo wamaisha halisi huku ukileta tishio japo kwa mbali.Kuishi na VVU na UKIMWI ni tendo jepesi la kuweka uwianobaina ya uwezo wa kuachilia mambo na uwezo wa kudhibiti– si tu katika ujinsia bali katika maisha pia. Hili ni tendo la kujengauwiano ambalo linaboresha ufahamu wa mtu wa ninimaana ya kuwa binadamu.ujinsia wa binadamu 41


42 SURA ZA MUNGU


sura za munguKuwa sehemu ya matumaini yaKiulimwengu katikati ya matesodenmarkImaniNimekuwa muumini kwa muda mrefu kadiri ninavyokumbuka,lakini kama vile ilivyo kwa watu wengi imani yangu imepitia awamumbalimbali na migogoro mbalimbali.Kwa muda mrefu kabla sijaambukizwa na VVU, nilipitia kipindikizima cha kuchanganyikiwa kuhusu dini, na sikuwa na uzoefumwingi wa maisha ya kihisia. Baada ya kugundua kuwa nina VVUkidogo ama zaidi nimerejea tena kule nilikoanzia. Nimewahikuwa na mashaka na mtazamo wangu wote juu ya Kristo, mtazamowangu kama fikra niliyonayo. Lakini katika kipindi hichocha migogoro ya kimaisha ndipo nilipogundua ya kuwa nilikuwanina VVU. Tangu hapo nimerejea kwa namna fulani katika imaniniliyokuwa nayo wakati wa utoto. Ninakumbuka matukio kadhaanikingali mtoto, moja ni uhusiano wenye kina pamoja na Yesu.Uhusiano wa jinsi hiyo umenipatia nguvu –na ni chanzo cha maishamapya ya kupumzika katika imani yangu.Baada ya kugundua kuwa nina VVU, nilipitia vipindi kadhaa vyamitafaruku ya kihisia. Mawazo juu ya dhambi na hatia moyoni,kama inavyotokea kwa wengi wetu – kujisikia kwamba mimi ndiyeniliyeusababisha ugonjwa huu. Kisha fedheha iliyofuata baadayekama matokeo ya hali hiyo. Nilipambana na hali hiyo kwa mwakammoja na vita hiyo ilinifanya nijione mtu wa kuogofya sana.Nilikuwa nimejilaumu sana mwenyewe. Nilikuwa na hakimundani yangu, ambaye daima aliniambia nimejisababshiamwenyewe ugonjwa ule. Kwa mwaka wote ule nilizidi kujisikiafedheha, mwenye hatia na mwenye dhambi. Ingawa niliendelea,kupambana na hali zote hizo. Nilikosa baraka ya ushirika waKikristo ambao ungenisaidia kushinda hatia, fedheha na dhambimoyoni mwangu. Ina sumbua sana pindi unapogundua vema yakwamba una VVU kwani unaanza kupata dalili ndogo ndogo hapana pale, na hiyo hukuvunja pole pole.Nilimaliza mapambano yangu ndani ya mwaka mmoja kwajuhudi zangu mwenyewe. Yote kwa sababu nilikosa na mtu wakunisaidia kufanya hivyo.MaombiMaombi yamenisaidia katika vipndi vyote vya shida yangu.Nilipogundua ya kuwa nina VVU, mchakato ulianza, na katikahatua fulani niligundua kuwa yanipasa nianze kuomba tena.Hii ilikuja yenyewe tu. Nilijitenga mwenyewe katika nyumbamoja mikoani na nikaanza kipindi kirefu cha maombi. Nilitakakuomba - na maisha katika utu wangu wa ndani yakaanza,kama inavyokuwa unapoanza kuomba. Huu ni ulimwenguwa ndani ambao unaendelea kujifungua wenyewe na kuletahali ya ushirikiano. Nilishi katika hali yangu ya hofu ya kufa nakupata maambukizi ya UKIMWI na pole pole nikaanza kugunduakuwa haikuwa sababu yangu kupata ugonjwa huo. Haikuwasababu kwamba nilistahili adhabu. Nimeupata ugonjwa huukwa sababu zingine kabisa.Hivyo nilipata nguvu mpya ya kisaikolojia na nafasi ya kutoshapia. Niligundua kuwa nimeendelea kuwa na furaha zaidi?Maombi yaliwezesha furaha ipatikane na niliweza kukusanyanyenzo mbalimbali na nguvu ambazo ningetumia kwa mudauliobaki.ilikuwa kama chemichemi ya furaha ilikuwa ikitiririkandani yangu. Sasa nilikuwa nimekutana na kitu kingine na kamaMkristo ningeweza kusema kikawaida kabisa kuwa nimekutanana Yesu Kristo ama Mtakatifu. Mungu alinigusa, aliugusa moyowangu, ….na aliufungua moyo wangu,ili kwamba niweze kusikiafuraha ya msingi katika kuwa hai, furaha ya kuwa mwanadamuna kuishi na wanadamu wengine. Hofu yangu ilipungua,na sasa ikiwa nitakufa ama nitaugua kukawa na maana kidogosana. Hakunisumbua tena. Cha maana zaidi kikawa hali iliyopokwa sasa kwani nilikuwa nimekutana na ulimwengu wa ndaniuliokuwa umejaa na vingi sana, na hii ikanipa nguvu zaidi nauwezo wa kuishi, kiasi kwamba mipango yangu kwa ajili yasiku zijazo ikaanza tena kuwa na maana.Imani yangu ya ndani kabisa ni kuwa, watu wote wanaoteseka,watahusika na kubeba maumivu ya ulimwengu wote– mateso ambayo Kristo aliyapitia, hasa alipoona dhambi zoteulimwenguni katika historia yote – zote mara moja. Imaniyangu ni kuwa kila mwanadamu anayeteseka hushiriki katikakubeba mateso haya ya pamoja, ambayo wanadamu wote wanashirikiana.Kwangu mimi, hii ina maana kwamba katika saburiniliyo nayo na ugonjwa wangu ninashiriki katika mateso hayaya kiulimwengu. Hivyo kwa njia moja ninayashiriki mateso yaKristo, hii inanipa nguvu na furaha kubwa.USHUHUDA WA BJARNE, ALIYEKUFA KWA UKIMWiSURA ZA MUNGU 43


ZAMBIAtafakuri ya BibliaMatendo ya Uponyaji ya Yesuna japhet NdhlovuMatukio ya Kibiblia juu ya uponyaji alioufanya Yesu inajumuishamaelezo ya kutosha juu ya watu walioponywa, na jinsi walivyoupokeakuwatambua rasmi wale waliotupwa na ulimwengu kwa sababumoja hadi nyingine. Kwa utaratibu wa kudumu alikutana nawatu katika maeneo yao ya kuhitaji na kuyashughulikia mahi-uponyaji huo. Mwanamke yule asiyekuwa safi na taji hayo. Yesu anaelezwa kama mpiganaji, ambaye mara kwamwenye hali duni, mwenye ukoma aliyedhalilishwa na kudhihakiwa,mtu yule aliyepooza na kutengwa, omba omba asiyeona– hawa wote walikutana na kukumbatiwa na upendo waajabu toka kwa Mungu. Mara tu baada ya kujisikia kupendwana kukubalika, hali hii huwa tishio kwa wenye nguvu waliopo,desturi, na watu ambao wamewapuuza, kuwakataa, na hatakuwakandamiza.Baada ya mahubiri ya Petro kwa watu zaidi ya wakati waPentekoste mlemavu mmoja mwenye umri wa miaka 40 aliyelalalangoni mwa Hekalu aliponywa. Naye Petro akatangazakuwa nguvu ya Yesu ya ufufuo ambayo ilifanya kazi kurejeshamambo yote, ilimponya yule mlemavu na kwamba huyu Yesualipaswa kuabudiwa kama Bwana juu ya wote. Watawala wenyehofu wakawakamata Petro na Yohana. Walielewa kwambauponyaji huu si jambo jema la kawaida tu lililotendeka, balichangamoto dhidi ya mamlaka yao, na wito mpya wa utii nashambulio kwa mfumo uliopo.Uzito aliokuwa nao Yesu alipokabiliana na magonjwa unatolewakielelezo katika kisa cha uponyaji wa mtu aliyekuwa namkono uliolemaa (Mk 3:1-6). Uponyaji huu unapata umuhimukatika siku ya Sabato, kwani katika fikra ya Kiebrania kutomponyamtu yule kungemwacha katika hali inayokaribia kufa.Mapambano dhidi ya ugonjwa ni mapambano ya kuwaokoawale ambao wameumizwa na nguvu ya mauti na hatari zake.Kwa kuwa ugonjwa unapingamana na nguvu ya muumba yakuokoa, lazima urekebishwe na uumbaji kurejeshwa. Yesu nimkombozi ambaye rehema za Mungu zinapatikana. Kilichokipya katika huduma yake ni kwamba wenye kunufaika na hurumaza Mungu si viongozi wa kidini na wasomi wa sheria lakinini wale wanaochukuliwa kama walio nje, masikini, walemavu,wagonjwa, na wale waliofiwa. Yesu alijiweka huru kufikiwa nakila mmoja aliyemhitaji, akipuuza mipaka iliyozoeleka na hivyomara kwa nguvu alizo nazo anapingana na mamlaka yale ambayoyamewaweka watu katika hali ya unyonge. Chochote kilekilichowafunga watu lazima kikabiliwe na nguvu inayowezeshahayo kuharibiwa. Kwa jinsi hiyo wagonjwa waliponywa, walemavuwakapewa nguvu mpya ya utendaji na walionyanyaswakufunguliwa.Wakati yesu alipowakaribisha wagonjwa na walemavu kwamikono meupe aliwasilisha mfano wenye nguvu kwa wafuasiwake. Namna ambayo makanisa na washirika wake wanakabilianana changamoto ya VVU na UKIMWI ni kielelezo cha kiwangocha umakini walio nao katika kumfuata Yesu. Itikio lenye upendona huruma - la mikono iliofunguliwa- linatakiwa tokakwa watu wa Mungu. Ni daraka ambalo Yesu Kristo alilitoa, kwamfano maelezo juu ya Hukumu katika Matt 25:31-46. Zaidi,itikio kama hilo ni ishara ya neema na upendo wa Mungu, sikatika maudhui ya UKIMWI tu bali kwa jumuia yote kwa ujumla.Inatangaza kwa ajili ya wote kusikia na kuona kwamba utawalawa Mungu unaanza kutambulika na kuanza kupata sura yakeduniani.Kuwakubali katika upendo wale wanaoishi na VVU inatangazakuwa nguvu ya Mungu ya kuokoa inachukua hatamu dhidi yamauti na nguvu yake ya kuharibu. Huruma kwa hakika ndiyowito wa awali walio nao watu wa Mungu katika janga lililosababishwana wimbi la VVU na UKIMWI.Ni ufahamu gani wa undani ambao imani ya Kikristo inatupatiakatika hatua hii ya ukomavu wa kuwepo kwa UKIMWI. Baadhiya maandiko ya Agano Jipya yanaashiria kile tunachoaminikuwa lazima kijumuishwe katika harakati kamilifu za Kikristo zakupinga ukimya, fedheha, na unyanyapaa kwani haya yote yanahusishwana maambukizi ya VVU na UKIMWI, hatua ambayoni muhimu leo kama ilivyokuwa mara tu baada ya UKIMWI kutambuliwa.44 SURA ZA MUNGU


sura za munguLabda, hakuna ugonjwa ambao ulikuwa wa kutisha sana katikaPalestina ya karne ya kwanza kama vile ukoma. Ukoma ulieneapolepole hadi kuufanya mwili uchukize na hivyo kunyanganywaumahiri wake. Kupata maambukizi hayo kulimaanishakutengwa ili kutogusana na mtu yeyote asiye na ukoma; ukomasi tu haukuwa na tiba bali pia ulikuwa ni hatari.Alipokutana na mwenye ukoma katika barabara kuu ya Galilaya,Yesu angeliweza kutamka neno la uponyaji kutokeambali, kama alivyofanya katika matukio mengine (k.m.Luka7:1). Lakini Yesu alichagua kuunyosha mkono wake na kumgusamwenye ukoma huku akimponya. Kwa kufanya hivyo,Yesu alizipinga desturi za kijamii na pia kutoujali ukoma katikahali yake halisi. Aliamua kuhatarisha afya yake na kibali chakembele ya jamii kwa kuweka mikono yake juu ya mtu aliyechokana maisha.Kwa nini Yesu alitenda kwa namna hii isiyokubalika kiafya nakijamii? Marko anatueleza ya kuwa Yesu alifanya hivyo kwasababu alisukumwa na huruma kwa tatizo la mwenye ukomayule.Uponyaji wa mwenye ukoma yule haukuwa tendo lililojitenga.Huruma iliambatana na maisha na huduma ya Yesu. Marakwa mara aliguswa na huruma alipoiona njaa, alipouona ujinga,ugonjwa, na hata alipokiona kifo. Kwa hiyo Yesu alikamatwana huruma wakati alipowaona watu wa kawaida katika hali yakupoteza shabaha ya maisha na kuwa kama “kondoo wasio namchungaji” (Math 6:34), wagonjwa na wasioona wakiwa miongonimwa makundi ya watu (Math 14:14; 20:34), na huzuni yawale waliopoteza wapendwa wao (Luka 7:13; Yohana 11:35).Bila kubakia tu katika eneo la hisia, huruma ya Yesu ilijielezayenyewe katika utendaji wake ndani ya huduma yake. Kutokanana huruma yake aliwafufua wafu (Yohana 11; Luka 7:14),aliwafundisha watu wengi (Marko 6:34), na kuponya wagonjwa(Math 14:14; 4:23; 9:23; 9:35; 19:2)Katika kuwahudumia wenye shida Bwana Yesu hakuogopakugusana nao. Alikamata mikono ya wagonjwa (Marko 1:31;Math 9:25) na wale waliofungwa na shetani (Marko 9:27). Vidolevyake viliwagusa wasioona (Math 20:34; Yohana 9:6; Math9:29), viziwi (Marko 7:33), na wasiosema (Marko 7:33). Chakushangaza kabisa zaidi ya yote, Yesu aliwagusa wenye ukoma– wale waliotengwa wa enzi zake (Math 8:3; Marjo 1:41; Luka5:12-13), na hivyo kuonyesha kina cha huruma yake.Huruma ya Yesu haikuwa na mipaka, ilivuka rafiki zake wotena hata kuwazunguka maadui zake. Akitarajia hatimaye kukataliwakwake katika taifa alilolipenda, Yesu aliulilia mji wa Yerusalemu(Math 23:37). Wakati wa kukamatwa kwake alipendakumponya askari ambaye sikio lake lilikuwa limejeruhiwa katikapurukushani iliyotokea (Luka 22:51). Yesu pia aliomba Babayake ajibu kwa rehema na msamaha kwa maaskari waliokuwawakimsulubisha (Luka 23:34). Kwa kufanya hivyo,Yesu aliishikatika yale aliyofundisha, kwamba huruma zielekezwe kwamtu yeyote bila kubagua, kama mfano ule wa Baba wa mbinguni(Math 5:43-45). Kama mmoja wa wafuasi wake wa awalialivyosema baada ya kuyatafakari maisha ya Yesu, “Kwani unaijuaneema ya Bwana wetu Yesu Kristo kwamba ingawa alikwatajiri lakini kwa ajili yetu akawa maskini ili kwamba kwa umaskiniwake tuwe matajiri” (2 Kor 8:9).Kulingana na Agano Jipya, Yesu si mfano mkubwa wa hurumapeke yake. Muhimu zaidi, yeye anabeba moyo wahuruma wa Mungu wa Biblia. Dhamira ya Mungu mwenyehuruma, inayoibuliwa kutokana na ufunuo wake mwenyewe,inapatikana katikati ya imani ya jumuia ya Kiebrania,baada ya kulifunua jina la kimungu kwa Musa mlimaniSinai, Yahweh alijieleza mwenyewe kama “Mungu mwenyeneema na huruma, si mwepesi wa hasira, mwenye upendona mwaminifu” (Kut 34:6). Mungu huyu anawahurumiawatu katika taabu zao, si kwa sababu ya sifa zao za kibinadamuila kwa sababu ya upendo wa Mungu na rehemazake nyingi. Tukumbuke kuwa Mungu ni mwenye neemahata katikati ya dhambi na uasi wa kibinadamu. Munguhakika ni mwenye neema na rehema katika mazingirahaya ya UKIMWI. Huruma za Mungu zinatungoza kufikiau t e n d a j i w a k i m u n g u u n a o o n y e s h w a Ya t i k a Ye s u K r i s t o .SURA ZA MUNGU 45


sura za munguKujifunza BibliaDenmarkSura Nne za MunguTokea tukio la kwanza la kujitokeza kwake, VVU na UKIMWI daimaumetafsiriwa kama adhabu toka kwa Mungu. Watu wengiwenye VVU wameikubali tafsiri hii, na hii huongeza matesojuu ya mateso. Dhana kwamba VVU na UKIMWI ni adhabu tokakwa Mungu inaashiria sura asilia ya Mungu kama nguvu inayoadhibuna kukaripia.Katika mafunzo ya Biblia yanayofuata tutazingatia visa vinnetoka Agano Jipya vinavyotupatia mbadala wa sura ya Munguyenye upendo na maendeleo.Msingi wa kawaida wa visa hivi vinne ni kuwa vina akisi suraya Mungu katika mwendo. Mungu husogea na huweza kusogezwa.Mungu si mgumu na si aliye mbali. Hukutana nasihapa, na pale tulipo.Luka 15:11-32Mfano wa Mwana MpotevuMungu anayekimbia na kukutana nasiHadithi ya Mwana mpotevu inatuonyesha sura yenye nguvuya Mungu kupitia mtazamo na matendo ya Baba. Mungu ndiyeanayetukumbatia – kwa dhati na kwa ukarimu. Anakimbia kutujiana kutuzungushia mikono yake, kama vile hadithi inavyosemahivyo ndivyo baba anavyofanya. Na kinachomhimizani ile nguvu ya upendo aliyonayo. Mwana mpotevu ni kielelezocha wale wanadamu walioko chini udongoni na pia nje yaulingo. Hii inaweza kumtokea mtu yeyote. Na mambo mengiyanaweza kutufanya tuzame chini kwa kuvunjika moyo.Maana inayotolewa na hadithi hii katika injili ni kuwa Munguhutupa uwezekano wa maisha mapya, yanayopewa kielelezona uzoefu tulioupata na undani wa kifahamu tulioupata katikasafari yetu kuelekea chini. Kipo kituo cha mageuzi katika kilamgogoro wa kimaisha, na kwetu sisi pia hata pale tulipovurugafursa zilizojitokeza kwa ajili yetu, zaidi kwetu tena hata paletunapoona aibu juu ya maamuzi na makosa yetu.Hadithi hii inatupa matumaini kwamba tunaweza kuendeleakuishi maisha yetu pamoja na hayo yote yanayotupata – nakwamba yupo Mungu na wapo wanadamu ambao wanasubirikutukaribisha jinsi tulivyo – bila kujali hali yetu ya kiafya naVVU ama historia ya maisha yetu.Maswali ya Kufikiria• Lini Mungu alikuja na kukutana nawe katika harakati za maishayako?• Unaweza kujifananisha na nani zaidi - mwana mpotevu amakaka yake mkubwa ambaye anadhani hakutendewa vizurina babaye?• Nani kati yao yuko mbali kabisa na baba yao?• Kuna uhusiano gani kati ya “msamaha” na “haki”?Luka 24: 13-35Simulizi ya Safari kulekea EmmauMungu anayetembea kando yetuHuzuni huleta ganzi katika fahamu zetu. Hivi ndivyo ilivyotokeakwa wanafunzi baada ya Yesu kufa. Ni wagumu kusikiliza,akili zao zimepumbaa, wasioona vizuri na walioyumbana kwenda mbali. Hawatambui kuwa Bwana aliyefufukaanatembea kando yao.Hadithi hii inaelezea sura ya Mungu aliyeshinda mateso iliaweze kuchukuliana nasi katika huzuni yetu. Yeye anatembeakatika barabara mbaya pamoja nasi – bila kutuacha tupotezelengo na mwamko. Hutubeza ili atuwezeshe kuonamambo yote katika mtazamo mpya. Upendo wake wenyenguvu unatufanya tuweze kuukabili ulimwengu unaotuzunguka– na kuendelea na maisha yetu. Anatutia moyo na kutupachangamoto ya kuishi. Hukutana nasi kwa maneno nakwa vitendo.Sura hii ya Mungu imepewa maana yake na dhana ya AganoLa kale ya Mungu aliye Imanueli, yaani Mungu pamoja nasi.Ndiyo. Mungu yu pamoja nasi, na amekuja na kukaa nasi. Yukaribu – hata pale tunapotoa machozi ma kukasirika kwa kutoonekanakwake.Maswali ya kufikiria• Mara ngapi katika maisha yako umejisikia kwamba ulitelekezwa?• Je inawezekana sura hii ya Mungu kuwa mfano mzurikwetu?• Je inawezekana kweli Mungu aliyetembea kando kando yetuatatufundisha jinsi ya kutembea pamoja na wanadamu wenzetuwenye mahitaji?• Je sura ya Mungu anayetembea pembeni mwetu inaletamaana gani kwa wale wanaokufa na UKIMWI?.• Wanafunzi walimtambua Yesu alipoumega mkate wakati wa46 SURA ZA MUNGU


chakula cha jioni. Je sakramenti ya Chakula cha Bwana inamaana gani kwa watu wenye huzuni?Yohana 13:1-17Hadithi ya Yesu akiwaosha miguu wanafunzi wakeMungu anayeinama chini kutugusaHadithi ya Yesu akiwaosha miguu wanafunzi wake inatupapicha ya Mungu aliye tayari kupiga magoti ili aweze kutukaribia.Utayari huu unafunuliwa katika kufanyika kwakemwili, ambapo Mungu Mwana anainama chini kutoka mbingunihadi chini, na katika tukio hilo kabla tu ya matukio yaIjumaa Kuu na Pasaka, ambapo Yesu anainama kuwahudumiawanafunzi wake. Kwa njia hii anaonyesha unyenyekevuna utayari kwa kugusana nao.Watu wengi wenye VVU ni wahanga wa chuki na hofu yakugusana kimwili. Wanajisikia kuwa ugonjwa wao unawalizimishakwenda magotini na kwamba watu wengine wanawadharauna kujitenga nao. Yesu akiwa tayari kunyooshamkono wake na kuwagusa na kuwainua walio wanyonge nimfano mzuri kwa Wakristo binafsi na hata kwa kanisa kwajumla.Maswali ya Kufikiria• Je lini ilikuwa mara ya mwisho kwako kupiga magoti ili kumfikiamtu mwingine?• Je umewahi kuwa, ama unahisi kuwa umekuwa mwenyehofu ya kuwagusa wengine?• Je unafikiri nini juu ya sura ya Mungu aikwa chini ameinamana kukushika miguu na mikono?• Je sura ya aina hiyo ya Mungu ina maana gani kwa wenyeVVU na UKIMWI?Yohana 9:1kkUponyaji wa mtu aliyezaliwa akiwa asiyeonaMungu anayejinyoosha kutufikia na kutuponyaKatika kisa hiki cha uponyaji, Yesu anaondoa muunganiko wowotekati ya hatia na hatima. Kwa kufanya hivyo pia anaondoa suraya Mungu kama yule anayehukumu ama kuadhibu, yeye anayetupatiatunachokistahili. Badala yake, katika uponyaji peke yake,anachora picha halisi ya Mungu anayetufikia kwa nia ya kutukamilishaWakati wanapokutana na yule asiyeona, wanafunzi wanakuwana tahadhari. Wanatafuta mtu wa kumtupia lawama. Watu wengiwenye VVU wanakutana na hali ya jinsi hiyo yenye utata wa kimaadilihata pale wanapojifungua na kueleza hali ya ugonjwawalio nao. Uonevu wa kawaida ni ule ambapo wale wenye VVU naUKIMWI wametengeneza vitanda vyao, na sasa ni lazima wavilalie.Katika hadithi hii Yesu anaweka wazi kuwa hatupati kile tunachokistahili.Hadithi hii ya Injili ni moja tu kati ya nyingi zilizomokatika Agano Jipya kuhusu uponyaji. Watu ambao wanumwa sanawanahitaji kupewa matumaini, lakini matumaini bandia yanawezakuleta maumivu makubwa. Hata hivyo hakuna uwezekano kwawale wenye UKIMWI kuponywa, lakini matumaini yanayoletwana Injili, ni sura na mfano wa Mungu mwenye upendo ambayeanaweza kutupatanisha sisi katika ukweli wa ugonjwa na kutupatianguvu ya kuishi – bila kujali yote yaliyopo.Maswali ya Kufikiria• Je unaamini kama kuna uhusiano baina ya kile tunachokifanyana kile kinachotutokea?• Je wakati wa miujiza umekwisha?• Je upatanisho na ugonjwa mkubwa unaweza kuleta uponyajiwa kiroho?SURA ZA MUNGU 47


Mfano wa Mwana mpotevuKujifunza Biblia Luka 15:11-321. UtanguliziKatika tamaduni nyingi za kiafrika, kama si zote uhusiano bainaya mtoto na mzazi hauwezi kuvunjwa kirahisi na kitu chochote.Hata dhambi na kifo haviwezi kusitisha uhusiano wa aina hiyo.Tunapohusisha mambo haya na Mungu muumbaji wa vyotewakiwemo wanadamu., tunagundua kuwa hakuna kinachowezakututenga na upendo wa Mungu. Je VVU na UKIMWI vinawezakututenga na Mungu jinsi hiyo mwenye kusamehe.2. TafakuriKatika kujifunza kwa upana kifungu hicho – ambacho kinawezakusomwa mara nyingi kutoka tafsiri mbalimbali ili kuwezakukielewa vizuri na kuukubali mfano huo – maswali yafuatayoyanaweza kusaidia:a. Maswali yanayohusu kifungu chenyewe:• Onyesha jinsi mfano huu unavyojibu hoja ya Mafarisayo katikaLuka 15:2• Baba, Mwana na Roho wanapenda kufanya nini na kuonanini kinatendeka?• Kama yule mtoto aliye mdogo katika kisa chetu angejihukumumwenyewe. Je! Baba angeweza kumpokea tena nyumbani?• Je mfano wa mwana mpotevu unatufundisha nini juu yauhusiano wetu na Mungu?• Je Mafarisayo walitaraji kujifunza nini kutokana na kisa hikicha kusisimua.ZambiaMungu Anayesameheb. Maswali yanayohusiana na VVU na UKIMWI:• Je unaona mweleko huo huo katika juhudi zetu za kukabilimaambukizi ya VVU?• Je kuna wakati ambapo tunawadharau wale wanaoishi naVVU kama watoto ambao wamepotea?• Je huenda tunawaangalia kama wenye dhambi waliopatamaambukizi ya virusi kwa kuendesha maisha ya kutojalichochote• Tutatambuaje chanzo cha maambukizi na kwa nini ni lazimatufahamu, je si kwa sababu zile zile za kutoa lawama.• Je Mungu anaangalia watu wanaoishi na VVU na UKIMWIkama wakosaji ambao hawawezi kusamehewa?c. Jinsi kifungu kinavyohusika na mazingira yetu:• Je tunaweza kuiona tabia aliyokuwa nayo kaka mkubwakatika kisa chetu miongoni mwa jamii ya Kikristokatika kuendekeza ukimya, fedheha, na unyanyapaaunaohusishwa na maambukizi ya VVU?• Hebu angalia herufi zilizotajwa katika kifungu nasomo gani linaweza kutolewa humo na kulitumia katikamapambano dhidi ya unyanyapaa unaombatanana VVU.• Tunapata kanuni zipi toka katika vifungu?• Jinsi gani Kanisa linaweza kuwa chemichemi ya upendona ukarimu?48 SURA ZA MUNGU


Sikuwahi kabisa kupitia maisha yaliyokamilika kamanilivyofanya baada ya kugundua ya kuwa nina VVU.Ili kukutana na nafsi yako mwenyewe - ni vigumu, nikazi kubwa, kitu ambacho ungependa kukiepuka kamaungeweza, na tunahitaji msaada wa kila moja wetukatika safari yote. .USHUHUDA WA RONNY, ALIYEKUFA KWA UKIMWI, DENMARKsura za munguMasomo mawili ya BibliaZambiaMungu wa UumbajiKatika semina ambayo iliendeshwa katika ukumbi wa Mt. PauloUCZ Kabwata mjadala ulifanyika ukijumuisha kundi la watuwalioishi na VVU. Wote hawa ni wanachama wa mtandao wakuhudumiana unaojulikana kama Mduara wenye Matumaini.Ifuatayo ni kumbukumbu ya majibu yao juu ya vifungu kadhaavya Biblia.Luka 15:1-11Kondoo aliyepotea na Sarafu iliyopoteaKifungu kilisomwa na kundi lote kutoka tafsiri mbalimbaliza Biblia ili kupata maana halisi ya kifungu kile.Baada ya kukisoma kifungu washiriki walipewa changamotoni kwa jinsi gani watajisikia kama waishio na VVU endapokifungu kingesomwa mbele yao.Yafuatayo ni majibu:• Kujisikia msamaha – Mungu husamehe• Kujisikia upendo – Mungu ni pendo• Kujisikia kukaribishwa – Mungu ni mkarimu• Kujisikia kuomba sana baada ya kupitia matatizo. Lazimatukumbuke kuwa yupo Mungu mwenyezi wa kumpelekeamaombi yetu. Kifungu kinatupatia hisia za kuwa na uhakikakiasi kwamba hata baada ya kupitia matatizo ama magumuyupo Mungu wa kutusamehe daima tunapochukua hatuazinazostahili.Wengine walidhani ya kuwa kifungu kilileta hali ya kujisikiakuhukumiwa tayari – mtu mmoja alisema: “ unapokisomakifungu hiki kwa mara ya kwanza utadhani sasa unahukumiwahasa ikiwa umeishi maisha yasiyokuwa na tahadharitena yaliyohususisha ngono.”Kundi lilithibitisha ya kwamba wamejifunza Mungu yupoili kusamehe na kuwasaidia kuanza maisha maisha mapyaambapo hawataangalia jinsi walivyopata ugonjwa bali kuishimaisha yasiyo na majuto.Mwanzo 27-28Mungu anaumba Mwanadamu kwa sura yakeKifungu kilisomwa kutoka tafsiri tofauti za Biblia ili kuielewakwa udani maana yake.Baada ya kusoma kifungu hicho tena, washiriki waliulizwanini kilikuwa kinaendelea katika fikra zao walipokuwa wakisikilizakifungu hicho. Yafuatayo ni majibu waliyotoa:• Mungu ni mkuu• Mungu ni mwenyezi• Mungu ni muumba hata kama tuna VVU, naye ametubariki• Tumeumbwa kwa sura ya Mungu na hivyo tunafananana Mungu na yote tunayoyapitia tuyaache mikononi mwaMungu kwani yeye ni muumba wetu. Muumba huyu anajuana kuvielwea virusi hivi sana.-Tunapaswa kuwa na shukrani na daima kumwomba Munguna kuendelea kumshukuru kwa maisha yetu.Jambo lingine waliloliona wanachama ni kuwa ikiwa Munguni muumba wetu –kwa nini tupitie mateso mengi – kwa ninituwe na VVU? Kwa nini asiviondoe virusi toka kwetu?SURA ZA MUNGU 49


Kujifunza Biblia kutoka Luka 13:10-17NorwayMwanamke MlemavuKatika mijadala mjini Oslo, iliyowahusisha watu wanaoishi naVVU ama kuathirika, kifungu hiki cha Biblia kikawa muhimusana kwa uelewa wetu juu ya kile kinachomaanisha kumwonamtu kando yetu na kutopagawa na amri na taratibu za kisheria.Miongozo ifuatayo inaweza kusaidia kujifunza kifungu hiki.1. Soma kifungu kwa kuzingatia mazingirayako mwenyewe na changamoto unazozikabili:Kabla ya kusoma kifungu cha Biblia uulize maswali kadhaa juuya jinsi washiriki wanavyomchukulia Mungu kuwa ni nani najinsi gani mazingira tofauti ya maisha yanavyoweza kutupatiasura tofauti ya Mungu. Kwa mfano:• Je unaweza kutueleza wakati ambapo ulifikiri Mungu amekuadhibu?Ulifanya nini?• Je umewahi kujisikia ya kuwa Mungu anakupenda paletu unapokuwa unastahili hivyo ama kamaunazitii amri zaMungu?• Je pamewahi kuwepo mazingira ya aina nyingine ambapoulikosa uhakika wa upendo wa Mungu, ukifikiria kuwa Munguanaweza kuwa amekasirika kidogo ama mgumu kumwamini?Turuhusu washiriki wafikirie juu ya jambo hili kwa muda kablahatujaanziasha mjadala wa vikundi. Ili kuweka mambo katikawepesi wa kutokuwaogofya wengine unaweza kuanza kwakuwaeleza juu ya tukio ambalo unadhani huenda lilikuwa adhabuya Mungu. Jaribu kuwasaidia watu kuelewa mifano nasura tofauti tunayobeba pamoja nasi daima. Unaweza pia kuziandikasura tofauti zilizotajwa katika karatasi pana ya ubaoni,kwa mfano: Mungu anayekasirika; Mungu mwenye hali zinazobadilika;Mungu anayehukumu na kuendelea.2. Kisome kifungu hicho kwa pamojaSoma hadithi juu ya mwanamke mlemavu katika Luka 13:10-17. kila mmoja asome sentensi ama andiko moja.3. Kisome kifungu kwa ufasaha na kwa kirefuAndika maneno ya msingi katika karatasi. Uliza maswaliya jumla juu ya kifungu hiki.• Kifungu hicho kinahusu nini?• Nini kinakugusa juu ya kifungu hiki?• Dhamira gani zimo katika kifungu hiki?Kisha angalia kwa makini katika kifungu:• Unakutana na nini katika hadithi?• Tunajifunza nini juu ya kifungu hikiInaweza pia kuwa na msaada mkubwa kuangalia mahusianobaina ya watu katika kifungu hicho, pia kutokakatika mitazamo ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi.• Je viongozi wa sinagogi wanahusiana vipi na matesoya mwanamke?• Je Yesu anahusiana vipi na viongozi wa sinagogi?• Je Yesu anahusiana vipi na Sabato?• Je viongozi wa sinagogi wanahusiana vipi na maishaya binadamu, hasa kulingana na alichosema Yesu?.• Je watu tofauti waliokuwepo walisema nini mwishoni?• Kuna thiolojia gani ya Yesu ya uelewa wa Mungu katikakifungu?• Unajisikiaje kulinganisha na kifungu?Baada ya kufanya kazi kwa karibu pamoja na kifunguhicho cha Biblia, ni vizuri kwamba myaangalie maishayenu na mazingira yenu.• Je unaweza kuitambua hali aliyokuwa nayo yule mwanamke?• Je umewahi kukutana na matukio kama yale yaliomtokeayule mwanamke?• Je kitu gani kingine unachodhani kinafanana na halialiyokuwa nayo yule mwanamke?• Je Unahusiana vipi na na wengine wanaofanana nayesiku hizi50 SURA ZA MUNGU


sura za mungu4. Soma kifungu ukiwana wazo la kubadili mamboMasomo ya Biblia yaliyowekwa katika mazingira ya mahalihayamaliziki hadi utakapoona kile ambacho unawezakufanya kuleta upeo wa matumaini katika kifungu katikasiku zetu za leo.• Nani anayefanya mawasiliano hayo ama wapi tunapatasura ya Mungu ambayo Yesu anaiwakilisha leo?• Tutapambana namna gani dhidi ya sura zinazopotoshwaza Mungu.• Tutawezaje kueneza sura ya Mungu ambayo Yesuameleta?• Tutafanyaje maisha kuwa bora kwa watu walio katikahali kama ile aliyomo yule mwanamke?TafakuriMazungumzo mjini Oslo juu ya kifungu hiki yanaweza kupewamuhtasari ufuatao;Ukweli kwamba Yesu aliponya watu siku ya Sabato umekuwana maana kwa kuelewa moja ya sifa maalu sana za Mungu.Hapa tunakutana na Mungu anayepinga mamlaka na kufunguavifungo vya wale waliofungwa.“Ni Mungu yule ambaye si tu anapatikana kwa shughuli katiya saa 3 asubuhi na saa 11 jioni, bali yeye ni nguvu isiyowezakuwekewa mipaka ya utendaji.”Katika hadithi hii tunaona Mungu mwenyewe akivunja kanuniza maandiko ”kwa sababu Mungu ameweka watu na hurumajuu ya sheria. Kile ambacho Yesu amekimaanisha ni kwambakusudi la sheria ni muhimu sana kuliko kufuata vipengele binafsivya sheria yenye sura ya kutobatilika.” Au kama mshirikimmoja alivyosema , “Ni asili ya Mungu kupenda, na kusudila maneno na vitendo vyake ni kufungua vifungo vya watu,kuwainua waliokandamizwa, kuweka huru waliofungwa, nakuponya na kuokoa.”SURA ZA MUNGU 51


sura za munguMungu ni muumbaji mwenye upendo wa kudumu. Mungu ni Mungu anayesamehe.Ijapokuwa mtu anaweza kuwa na VVU, tunajua kwamba Mungu anatupendana anatuhudumia. Kwa kuwa yeye ni muumba wetu tumekubali halizetu za kiafya na kuendelea kumtafuta katika maisha yetu yote. Si wale wanaoishina VVU ama Mungu anayestahili kulaumiwa kwa ugonjwa huo kutokea.Upendo wa Mungu na kazi zake zinaweza kuwa zimedhihirishwa kupitiawalio baina yetu wanaoteseka. Mungu ni Mungu mwenye upendo kwa sababutuliumbwa kwa mfano wake na kubarikiwa naye.DUARA ZA MATUMAINI, ZAMBIAZambiaHakuna HukumuK - KiongoziW- Wote1. Ukusanyaji wa watumuziki ukichezwa2. Wito wa kuabuduK: Bwana anasema “Mimi ndiye nikuponyaye…uniangalie miminawe utapona.”Marafiki, tumekutana hapa mbele za Mungu mwenyezi, yeyeanayejali na mwenye huruma. Kwa hiyo kupitia maombi na sifana nyimbo tumwaabudu Mungu anayeishi milele na mwenyeupendo mwingi. Amen.3. Nyimbo za Sifa4. Sala ya kufunguaK: Baba, upendo wako unafanya kazi kupitia uumbaji wote.Mwana wa Mungu, katika mfano wako tutafanywa wapya. Rohomtakatifu, umeyagusa maisha yetu kwa matumaini. Pokeaibada yetu, utuchukue tena tukutumikie mbele zako: utuwekehuru ili tukutukuze leo.Bwana, katika uwepo wako tunakubali sehemu yetu katikadunia ambayo imechoshwa na maumivu. Katika zama zetu hizitunakutana na maumivu kwa njia mbalimbali. Tunapokutanaleo, wengi wanateseka kwa sababu ya wimbi la VVU na UKIMWI.Watu wanaoishi na VVU wananyanyapaliwa. Tunakuomba Bwanakwamba utatutumia sisi kama vyombo ambavyo upendowako unaweza kutiririka kuwafikia kaka zetu na dada zetu wanaoishina VVU.Bwana mwenye rehema, pale ambapo tumewanyanyapaarafiki zetu na pia sisi kwa sisi, utusamehe na uhuishe upendowako ndani ya mioyo yetu ili kwamba tuweze kuonyesha kujalina huruma kwa wale wanaoishi na VVU.Utuongoze katika ibada hii. Tunaomba tukutane na ushirikawa kweli baina yetu nawe na baina yetu sisi kwa sisi.Utusikie katika Jina la Mwanao Bwana wetu Yesu Kristo. Amina.5. Maombi ya TobaK: Bwana mwenye neema, kwa toba yetu yote ya imani ambayohutoweka utendaji unapohitajika, tumekiri kuwa tunakupenda nakwamba tunapendana sisi kwa sisi lakini bila shaka haikuwa hivyo.W: Tusamehe tunaombaK: Utusamehe kwa kutokutii kwetuW: Tumeshiriki maonevu, ukatili, na unyanyapaa dhidi ya walemiongoni mwetu wanaoishi na VVU, kwa hivyo kuwanyanganyawatu maisha yenye uzima tele na tumaini ulilotupa ndani ya MwanaoYesu Kristo.K: Kama jumuia yenye imani kwa Mwanao, hatujawaonyesha kakazetu na dada zetu wema wako.52 SURA ZA MUNGU


W: Uturehemu eeh BwanaK: Kama Kanisa, hatujawa na upendo baina yetu kama vile Kristoalivyotupenda: hatujasameheana kama tulivyosamehewa; hatujajitoleakutumikia ulimwengu ulioharibika kwa upendo.W: Tunakiri kuwa dhambi yetu kama kanisa katika jina la Bwana aliyejaaneema: Amina6. Tamko la MsamahaK: Marafiki, katika Yesu Kristo, hapa tuna uthibitisho wa upendowa ajabu wa Mungu. Ilikuwa wakati tukingali wenye dhambiYesu alikufa kwa ajili yetu. Pokea rehema za Mungu kwa Jina laMungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu.W: Neema ya ajabu jinsi gani ilivyo tamu ile sauti iliyoniokoafukara kama mimi, nilikuwa nimepotea hapo awali lakini sasanimepatikana, nilikuwa nisiyeona lakini sasa ninaona7. Maombi na ufahamu zaidiK: Bwana mwenye neema, neno lako linatupatia uzima telekatikati ya maumivu na mateso. Lnaleta matumaini wakati tumekatatamaa. Naomba uturuhusu sisi kuisikia sauti yako leotunaposoma neno lako takatifu na tunaomba liponye kuvunjikakwetu moyo. Katika Jina la Yesu Kristo tunaomba. Amina!8. Somo kutoka maandiko matakatifuYohana 8:1-119. Mwongozo wa Mahubiri• walimu wa sheria walimleta mwanamke na mtu anawezakushangaa yuko wapi mwanamume aliyekuwa akizininaye. Sheria ya Musa ilihitaji kuuwawa kwa wote wawili nasi mwanamke peke yake [law 20:10, Kumb. 22:22]• Waalimu washeria walitaka kumwaibisha yule mwanamkenakumnyanyapaa. Jambo ambalo ni baya sana kulifanya.Wale walioambukizwa VVU hawapaswi kunyanyapaliwa.• Baadhi yetu tunatenda kana kwamba hatujawahi kufanyadhambi siku za nyuma na kufikiri kuwa kaka zetu wanaoishina virusi wamefanya dhambi zaidi yetu. Sisi nasi niwenye dhambi pia.• Yesu hakumhukumu lakini alionyesha huruma na kwaneema kubwa alimwambia asitende dhambi tena.10. MaombiKwa uchaguzi wako mwenyewe.11. Nyimbo ya kufunga12. Maombi ya KufungaW: Neema ya Bwana wetu Yesu, Upendo wa Mungu babana ushirika wa roho Mtakatifu, uwe nasi leo na siku zote.Amina!SURA ZA MUNGU 53


sura za mungu“Ndani yake tunaishitunatembea na kuwa na uzima”NorwayUtaratibu wa Ibada Kwa VituoIbada hii ni matokeo ya mazungumzo yaliyofanyika Oslo juu yaunyanyapaa wa watu wanaoishi na VVU. Inatarajiwa kwambaibada yote itajumuisha mahubiri yatakayoelezea sura ya Munguna fikra juu ya ubinadamu.Utangulizi wa Utaratibuwa Ibada na maandalizi yakeUtaratibu wa Ibada sio mwongozo ulionyooka wa ibada. Wakatimwingi wa ibada wale ambao watapenda wanaweza kutafutanafasi ya kwenda katika vituo mbalimbali katika chumba kile.Vituo hivyo mbalimbali vinahusika na maisha ya binadamu nakile kinachofanyika mbele za Mungu ambaye ametuumba,ametukubali, na kutuweka huru.Ibada hii kimsingi si ile ya kawaida, kwa hiyo ni muhimukwamba waabuduo waandaliwe mapema ili kwamba wawena mawazo ya kile ambacho watakishiriki. Maandalizi hayayanaweza kufanyika katika vipindi vya mwanzo vya ibada,vijalida vya kanisa na kadhalika. Hii ina maana ya kuwafanyawatu wasijisikie ya kutengwa ama kubaguliwa. Ni muhimu kuwekaagenda kwa ibada ambayo inaelezea dhana iliyo nyumayake pamoja na maendeleo yake. Ibada hii ina mambo yanayofananana vituo asilia vya Msalaba.Vituo vilivyotajwa hapa ni mapendekezo yetu. Vinapaswakuandaliwa kabla ya ibada. Kwa kuwa wanahitaji nafasi yakutosha unaweza kuongeza ama kupunguza idadi kulinganana matakwa ya mahali mlipo na nafasi zilizopo. Katika mazingiramengi, idadi ya vituo vilivyoorodheshwa inaweza isiwehalisi. Kwa hiyo tunashauri ya kwamba ufanye uchaguzi. Lakinikituo tulichokiita Mahali pa Ajabu lazima kiingizwe, nibora sana kwanza kutafuta namna asili za kuelezea jambozitakazotuwezesha kupata alama kwa vituo mbalimbali. Tumeandaamapendekezo kadhaa ya rangi yatakayoweza kujumuishwakwa kutundika vipandev ya nguo zilizofumwa ukutaniama kuzilaza chini. Pia inawezekana kuruhusu vipandevyembamba vya nguo hizo vitoke katika vituo hadi Mahali paAjabu. Kuwepo pia na Biblia iliyo wazi katika kila kituo, hasaikiwa imefunguliwa katika moja ya vifungu vya Biblia vilivyopendekezwa.Kwa nyongeza kifungu kilicho kifupi kinawezakuandikwa katika karatasi na kuninginizwa juu ama kuwekwapembeni karibu na Biblia. Hii itasaidia kuona kituo kinamaanishanini. Hatushauri watu kutumia vikaratasi vidogo vyenyegundi. Muhimu sana: fanya mambo rahisi na yanayowezakutendeka. Haya tuliotoa ni ushauri tu, si mambo ya lazima:mazingira ya mahali lazima yazingatiwe na hayo yataashiriakile utakachopenda kujumuisha.Pia tumeshauri mahali utakapoweka vituo hivyo mbalimbalikatika chumba. Sehemu hizi pia zinategemea uchaguziwako. Uwezekano mwingine ni kuendesha ibada hiyoyote nje. Mlango wa kuingia “kanisani” unaweza kutumikapia kama eneo la madhabahu. Lakini si wazo zuri kuwa navituo vingine ndani na vingine nje ya jengo. Hii itawezakutafsiriwa kana kwamba vituo vingine ni muhimu zaidiya vingine.Shule ama jumba la parokia linaweza kutumika kama mahalapa kuabudia. Maandalizi ya ibada yanaweza kuwa nafasi nzuriya kuendesha warsha inayowahusu vijana na watu wazima.Muda unaweza kutumika kutafakari juu ya vituo na namna yakuvifikia, kushughulikia umoja wa ibada, kuandaa ramani nakutengeneza vituo, na labda kutafuta njia mbadala ya kuvitoleautambulisho. Unaweza, kwa mfano, kuambatanisha, uzoefubinafsi na visa vingine katika baadhi ya vituo. Ni muhimu hayanayo yawekwe kwa kifupi.54 SURA ZA MUNGU


Vituo• Mahali pa manunguniko na malalamikoUchungu, mawe, giza na rangi zinazon’gaa. Karibu na mlangowa kuingilia nyumba ya ibada. Zab 22:2• Mahali pa mazungumzoUwezekano wa kutua mizigo; toba. Pamewekwa nyuma yaeneo la kuabudia. Viti vimepangwa viwili Viwili. Meza zikiwana vikombe na chai ya moto. Mawe yakiwa na mishumaa inayowakajuu yake. Rangi ya kijani iliyoiva sana. Yohana 3: Nikodemoalikuja usiku kwa Yesu ili kusema……• Mahali pa UshirikaPamewekwa nyuma pembeni mwa chumba. Mshumaa unaowakaumewekwa katikati ambapo watu wanaweza kuketikatika mduara wakizunguka mwanga. 1 Kor 12;12-26 (mst.13);Filipi 2:1.• Mahali pa kicheko na furahaUkiambata moja ya kuta za nje. Manjano, rangi nyingi nyingi,pua nyekundu, ama mchoro wa msanii. Mwanzo 18:12; I Kor1:27a..• Mahali pa mwili na Ujinsiakuchua miguu ama mikono. Rangi zinazovutia kiupendopinki,maua, mitandio, shela iliyoandaliwa vizuri. Wimbo waSulemani Wimb.4:1; Luka 7:38b• Mahali pa thamaniLulu, nyota, kibahri. Kutoka Isaya 45:3: “ Nitawapa ninyi hazinagizani na katika utajiri wa maeneo ya maficho. Ili ujue kwambani mimi Bwana ninayekuita kwa Jina lako”.• Kijito cha majiNi kisima. Katika kituo cha ubatizo, ukiwa na mimea iliyohifadhiwakatika chungu, na mti. Mkondo wa maji wa kumwagiliamaua; maji baridi ya kunywa; karai la kuoshea. Rangi ya kibaharina kijani. Yohana 4:14; Ubatizo wa Yesu, Ufunuo 22:1 , 17;Zab 42:1• Mahali pa uwazi na maumivuKatikati, kuelekea nyuma ya eneo la kuabudia. Kitambaa chakufumwa rangi nyekundu (damu ya mzee) Uwezekano wa kusomashairi na vifungu vingine. Yeremia 30:17.• Mahali pa AjabuNi mahali pa mageuzi, hamasa ya maisha na nguvu. Katikati yasehemu ya kuabudu. Kuna mkate na divai. Rangi zote zawezakukusanywa hapa..• Mahali pa maombezi nakuwasha mishumaaNjiani kuelekea eneo la madhabahu. Fursa ya kuwasha mshumaana kuandika sala za maombezi katika vijikaratasi. Chunguama chombo kinachofanana. Rangi ya matumaini. Filipi 4:6• Mahali pa MapumzikoMbele ya madhbahu. Rangi nzito zenye joto, mito ya vitanda,blanketi, magodoro. Math 11:28• Mahali pa MapambanoNyuma ya madhabahu, ikiwezekana sambamba na ukutakuelekea madhbahuni. Mabango, karatasi ukutani za kuandikia.Rangi za mapambano. Zambarau. Ephe 6:12SURA ZA MUNGU 55


sura za mungu1. MsafaraWakati nyimbo inayostahili ikiimbwa. Washiriki wanabeba divaina mkate [mmoja], maji kwa ajili ya vijito vya maji na mshumaakwa ajili ya kila kituo. Kila mtu mmoja awe na mshumaa mmoja,unaobebwa katika mikono iliyofumbwa. Msafara utaelekeamadhbahuni.2. Salamu pamoja na Neno fupi la Biblia• Mdo 17:24-25; 27b – 28• Watu walio na mishumaa wataenda kwenye maeneo yaorasmi ama baada ya salamu au ama wakati wa utambulishopale kila kituo kitakapokuwa kinatajwa. Tunapofanyahivyo, vituo vilivyoko karibu vitajwe mwanzoni, ili kwambaushirika uone kwamba pale ndipo wabeba mshumaa wanapokwenda.Baada ya hapo vifuate vituo vilivyopo mwishonimwa eneo la kuabudia.3. Wimbo4. UtanguliziManeno ya ufunguzi na maelezo ya chumba. Andaa mazingiraya kiusalama ukizingatia kile kitakachotokea. Mambo yakutaja:• Haki ya kuwa kitu kizima• “Tazama Mtu yule”, weka nafasi kwa ajili ya maisha yote ambayoyanasaidiwa na Mungu• Vituo vyote vinatajwa, ama na mtu fulani anayesimulia tukiolililotokea linalomuunganisha na kituo kimojawapo kati yahivyo, ama kwa kuchukua baadhi ya mawazo kutoka katikamahubiri yaliyoandikwa mwishoni mwa orodha hii ya ibadailyopendekezwa. Ikiwa wabeba mshumaa wameelekea katikavituo vyao, basi wasimame pale kituo chao kitakapotajwahuku wakiendelea kubeba mshumaa wao.• Waeleze watu kwamba wanaweza kuendelea kukaa kimyakatika maeneo yao, au kwenda hadi vituo vyo vyote wanavyohitaji.Hakuna sababu ya kwenda kwenye vituo vingiiwezekanavyo. Ni vema kusiskiliza hisia zako.• Tangaza kama ibada ya Ushirika Mtakatifu itakuwepo amakaramu ya chakula chenye upendo ama kitu kingine chochotekufuatia ziara hadi vituo hivyo.• Kila kitu KIFANYIKE machoni pa Mungu, katika nyumba yakena kimwelekee Mungu anayetukubali na aliyetuumba jinsitulivyo.“Ndani yeke tunaishi,Utaratibu wa Ibadatunatembea na kuwa na huo uzima”• Sala ya kuhitimisha Utangulizi Asante sana, kwambatunaweza kuwa watu tuliokamilika nyumbani mwako: wewemuumba wetu: wewe Yesu, ambaye unatukubali na uliyetuwekahuru: wewe Roho Mtakatifu, unayetoa na kufanyaupya maisha ndani yetu.”5. Toba ya ImaniPendekezo Kanuni ya Nicea6. MuzikiMuziki wa ala ama wenye kuongoza kutafakari7. Ziara kutembelea VituoAngalau kwa nusu saa: ama tukiwa kimya na muziki wa mbaliukichezwa, ama katika ukimya ikiwa hilo haliogopeshi. Ikiwaukimya utachaguliwa, inaweza kuwa vizuri zaidi kuvunjaukimya mara mbili ama tatu kwa kutumia nyimbo za kutafakari.Hii inajenga hisia za ushirikiano katika chumba kizimawakati watu wakitembelea vituo kadhaa.8. Ushirika Mtakatifu au Mlo wa UpendoWakati watu wametawanyika chumbani, ibada inaendelea. Watuwanaweza kubakia pale walipo.• Wakati kuna Ushirika Mtakatifu: msherehekeaji anapiga magotikaribu na mkate na divai katika mlolongo wa kati wa vitikaribu na Mahali pa Ajabu na unaweza kuanza moja kwa mojana maneno maalum ya kuendesha ibada hiyo: Usiku ule aliposalitiwa….”• Kuonyeshana Ishara ya Amani: “Tusalimianeni sote katika upendowa Yesu/ “Amani ya Bwana wetu iwe pamoja nanyi.”• Ugawaji wa meza ya Bwana unaanzia Mahali pa Ajabu. Walewanaopenda wanaweza kupokea Ushirika Mtakatifu. Mkateambao umebarikiwa [si kuwekwa wakfu] unaweza kugawanywakwa wale ambao hawatarajii kupokea Ushirika. Ugawajihuo unaweza kufanyika kimya kimya ukiambatana na nyimboza kutafakari.9. Sala ya Bwana, Baraka ya kufunga na kutawanyikaKila mmoja anakusanyika katika katika duara ndani ya duara.Sala ya bwana inasemwa kwa pamoja, kisha Mchungajianatamka Baraka ya Kufunga Ibada10. Wimbo wa kuongoza msafara wa kutoka56 SURA ZA MUNGU


Mahubiri YaliyopendekezwaTupo hapa. Tumekuja kusimama mbele za Bwana ndani yauwepo wake Yeye Aliye Mtakatifu. Tumeupa kisogo ulimwengu.Ulimwengu ulio laini, mgumu, usio na haki, uliojaa anasa nawenye kupendeza. Tumesimama hapa, tukiangalia kwa uhakikanje. Lakini “Ulimwengu” haujatupa sisi visogo. Sie tungali tumeubebapamoja nasi, na ndani yetu fadhaa na hasira badozinakoroga mambo chini chini. Kutaka na kushindwa bado zinashindanabaina yao ili kutupotosha tusitafute kukutana naYeye Aliye Mtakatifu. Inawezekana mwili wetu huu wa kibinadamuunaweza kukumbuka uzoefu wa usiku ule ingawa roho zetuzina mwelekeo wa kulisahau hilo, ya kwamba kujivunia mambomazuri yaliyopita jana inahatarisha unyenyekevu ama kuletafedheha kwa wale wanaotishia heshima yetu binafsi.Tunajaribu kuwa kamili na tunaamini kuwa hii ni sawa nakusema tuwe kamili katika hali ile tunayopaswa kuwa nayo tunapomkaribiaMungu…ama je si hivi ndivyo inavyopaswa kuwa?Je kuwa kamili si kukubali tofauti zilizopo za mema na mabaya?Je si mtu binafsi kujipatia haki ya kuwa sehemu ya uumbaji napia kuwa sehemu ya ulimwengu unaoendelea kuhangaika?Ni pale tu tunapolikubali hili na kupeleka Kanisani vyote vile tulivyonavyo kama wanadamu, ndipo tunapoweza kukutana na YeyeAliye Mtakatifu. Hapo tunatoa nafasi kwa neema, kukaribishwatena kwa Mungu na furaha. Kila kitu kinawezekana kwa Mungu.Katika ibada hii tutaruhusiwa kuwa vile tulivyo, yaani binadamu.Ndani ya kila mmoja wetu kuna vyumba vya kutosha,na leo kuna vyumba vingi katika nyumba hii ya Bwana. Wakatimwingine ni vile vyumba vyenye furaha na shukrani ndivyovinavyotawala nafasi zilizopo ndani yetu. Ikiwa hivyo ndivyoilivyo kwako leo basi mfuate mbeba mshumaa hadi sehemuya furaha na kicheko. Ikiwa kwa upande mwingine ikiwa hii nisiku ambapo chumba cha aibu na hasira kinatawala, basi ufuatembeba mshumaa mwingine hadi sehemu ya malalamiko namanunguniko. Ikiwa mwili wako utahama kati ya kuwa na hajaya kuguswa na haja ya kupumzika, basi utembelee vituo vyotekile cha mwili, ujinsia na uhisia – na mahali pa mapumziko. Amaikiwa upo katika kipindi cha maisha yako unapoona kuwa kilakitu kimekauka ndani yako, kana kwamba unazunguka ovyokatika uwanda ulio kame, hivyo basi ufuate mbeba mshumaahadi kisima chenye maji yenye uhai au usafiri hadi mahali penginepanapofaa ambapo utaweza tena kuinuka katika umaarufuwako. Ama uchukue njia itakayokutoa toka sehemu ya mazungumzo,ambapo unaweza kujifungua na kujiachilia mwenyewekwa mambo yote yanayokuzuia usikutane na wengine, hadi sehemuya ushirikiano ambapo utapokea nguvu kwa kutiwa moyona wenzako. Kutoka hapo unaweza kuendelea mbele zaidi, amakwa wengine katika sehemu ya maombezi yenye kuombeanana uwashaji wa mishumaa, ama unaweza kujitupa mwenyeweuwanjani kupigania maisha bora katika mahali panapohusika.Mwisho, fuata barabara inayoongoza kutoka vituo vyote hadiMAHALI PA AJABU ambapo tunainua mikono yetu kama vyombovitupu na kupokea mkate na divai, ujasiri wa kuishi na nguvu yakutoka na kwenda ulimwenguni – pamoja na Mungu.Namna hii tunakuwa salama. Tukiwa ndani ya nyumba ya Mungutukionana ana kwa ana na yeye Aliye Mtakatifu, tunaweza kuwavile tulivyo. Kila kitu kinawezekana kufanyika - kwa Mungu.Kaa kimya kwa muda na ujisikie kile unachokihitaji leo. Labdainatosha kutembelea kituo kimoja – ama utapenda kukaa tu katikaviti vya kanisani wakati wote? Chochote ambacho ni sahihikwako bado ni sahihi tu.Katika nyumba ya Mungu tupo huru.Ndani ya Nyumba ya Mungu tunaishi nakutembea na kupatauhai wetu.SURA ZA MUNGU 57


Kila mwaka wakati wa majira ya baridi, kipindi cha faragha huandaliwakwa ajili ya watu wanaoishi na VVU na UKIMWI pamojana wapendwa wao. Watu huja pamoja kutafakari, kuomba,kuzingatia na kusaidiana – kwa ukimya na pia kwa kushuhudiana.Huu ni mfano wa utaratibu wa ibada ya pamoja:1. Nyimbo2. Sala ya AsubuhiTuombe,Mungu Bwana wetuTunakushukuru kwa ukimya huuKatika ulimwengu uliojaa kelele na purukushani.Asante kwa sababu upo hapaBwana, uende pamoja nasi katika siku mpya iliyo mbele yetu.Hatujui ikiwa siku hii itangaa na kupendezaAma itakuwa imezingwa zingwa na iliyo chungu.Lakini tunaamini na kutumaini kuwa wewe ni Mungu wa upendo,Kwamba utaenda pamoja nasi kila siku hadi mwisho wa nyakati,Ndiyo,hadi ndani ya umilele usio na mwisho,Kwamba unatupenda na kutusaidia bila kujali kinachotokea.Utusaidie tuwe na muda mzuri wa maombi leoUtujalie kuyasikia mapigo ya moyo wako. Amina!3. Somo la Biblia: Luke 24:13-354. KutafakariTunaweza kufuata njia nyingi katika maisha yetu. Tunawezakuchukua njia kuu ama zile za pembeni. Tunaweza kuchukuanjia za mkato ama kuchukua mizunguko. Tunaweza kupoteana kukengeuka. Tunaweza kusimama katika njia panda na kukosafikra ya kuchagua mwelekeo wa kufuata.Mwongozo wa Ibada wakati wa FaraghaSala ya AsubuhiDenmarkJuu ya UkaribuTunaweza kufuata njia nyingi katika maisha yetu. Kati ya hizozingine hutuongoza katika njia isiyo na mpenyo wa kutokea.Nyingine hutufikisha pale tunapotaka kufika. Na kisha vipo vijiaambavyo hatujawahi kukanyaga miguu yetu, njia ambazo hazijapitiwa,maeneo yenye fursa ambazo bado kuvumbuliwa.Hapo zamani palikuwepo mtu aliyefikia mwisho wa safariyake – mbinguni. Pamoja na Bwana aliona maisha yake yakipita.Alifurahi alipoona nyakati za kupendeza na alilia alipoonanyakati za kusiskitisha. Lakini aligundua ya kwamba katikanyakati zote njema, kulikuwa na fungu lingine la nyayo pembenimwa zile zake, kana kwamba kulikuwa na mwingine. Lakinikatika nyakati mbaya kulikuwa na nyayo za miguu miwilizikipasua njia katika safari ya maisha.Yule mtu alimwangalia Bwana na kumwuliza kwa kumkaripia,“kwa nini ulikuwa nami tu pale kila kitu kilipokuwa rahisi naminikiwa na furaha? Kwa nini hukutembea nami wakati mamboyalipokuwa mabaya zaidi?” Bwana akaligusa shavu lake nakumwambia“ Mtoto wangu mpendwa, wakati maisha yakoyalipokuwa hayavumiliki tena sikutembea pembeni mwakobali nilikubeba.Tunaweza kufuata njia nyingi katika maisha. Lakini muhimuzaidi ya njia tunazochukua ni watu wanaotembea pembenimwetu, wenzetu tulio nao katika safari yetu. Yesu Kristo si tukiongozi wetu bali yeye ni mwenzetu. Hatua kwa hatua anatuongozana anatusaidia katika mizigo yetu pale inapotuelemea.Yeye atatutegemeza, na kutuinua na kutuweka mabeganimwake na kutubeba ikiwa tutwekwa chini kwa lazima. Amina!5. Nyimbo6. AmaniAmani ya Mungu inapokelewakwa kukumbatiana katika upendowa kindugu.58 SURA ZA MUNGU


sura za munguSala ya MchanaKukaa Kimyana Kusikiliza1. NyimboPale ulipoketi Ukiwa na magamba yafedheha na uchafuWa mikono yako iliyo tupu bali imejawa namakovuJuu ya nafsi yako tupu na yenye makovuUnasimulia hadithi yako na unahesabuhasara uliyopataYule mtu aliyekuacha ama mtoto ambayeilibidi umwacheSumu iliyofurika ndani ya mwili wakoMto uliojaa ambao hakuna anayewezakuuzuiaAmbao hautaki kukoma katika kungurumakwakeHuku ikizipiga na kuharibu kingo zako zotelainiUnasema nataka kufa Mimi sisemi kituNina nyoosha mkono wangu na kuushikamkono wako ulio mgumu na usio na rahaSala ya Mchana2. MaombiKama ilivyo kwa wanafunzi wako njiani kwenda Emmaus.Nasi daima tunashindwa kuonaKwamba ni wewe Yesu, uliyejiunga nasi safarini. Lakini palemacho yetu yanapofungukaTunagundua kuwa ilikuwa ni wewe uliyeongea nasi sikuzoteHata kama wakati mwingine tulikugeuka na hatukusikianeno lolote ulilosema.Lakini hiki ni kielelezo cha imani tuliyonayo kwako: kwambatujaribu kupenda na kusamehe pamoja na weweIjapokuwa tumekuwa na mashaka, kwa sababu ya imaniyetu, wewe Yesu umekuwepo hapa daima, upendo wakoukiwaka kwa kina kirefu ndani ya mioyo yetu.Shukrani zetu zimfikie Mungu!Amina!3. Kusoma na KutafakariLuka 24:13 –35 ikisomwa polepole.4. Ukimya MfupiWashiriki wanachagua neno ama sentensi kutoka masomo,inayosambazwa kama kitambaa kilichorembwa kwa rangimchanganyiko na kutandikwa kanisani sakafuni.5. Ukimya6. Nyimbo7. Baraka ya Harunihii itasomwa wakati wote wameshikana mikono: Bwana tubarikina ututunze. Bwana ifanye sura yako in’gae juu yetuna uwe na neema juu yetu. Bwana ainue hari yake juu yetuna atupatie amani! Amina!SURA ZA MUNGU 59


“Bwana, uwe pamoja nasi hapa,karibu yetu wakati siku inapochomozana jua na mwanga wa nyota unapozizimakatika virindi vya giza la usiku.Roho yako isituache kabisa hadiutakapotupokea mbinguni”Anima!B.S. INGEMAN, NO. 366. KATIKA KITABU CHA NYIMBO CHA KIDENMARK CHA 1966Mahubiri katika Ibada ya FaraghaLuka 24:13-35DenmarkMungu anayetugusana carina WøhlkTumeogopa sana kugusana sisi kwa sisi. Ninyi mlio na VVU kwakiwango kikubwa mmekutana na hofu hii ya kutokuwa karibuna wenzenu katika mwili na nafsi yako – vyote pale wale wasioambukizwawamejiweka mbali nawe katika wasiwasi wao nakutokujua kwao, na wakati ambapo ninyi wenyewe mmewasukumawengine mbali nanyi kwa sababu mmekuwa na uoga wakupuuzwa na kukataliwa.Tumeogopa sana kugusana sisi kwa sisi, kwa sababu kugusanakimwili kunaanika udhaifu wetu na utofauti wetu. Hivyotunawapiga butwaa watu kwa mbali badala ya kuwaruhusuwatukaribie. Tunajiepusha kushirikiana na wengine. Marachache sana tumejitokeza mbele na kueleza habari zetu hususankuwa sisi ni akina nani. Hii inahitaji kujisikia kwa dhatindani yetu na ndani ya wengine pia, inahitaji ukaribu kwa Munguanayetukumbatia na na anayetupenda kupita mipaka yoteya ufahamu.Katika faragha hii tumeangalia asili na umuhimu wa ukaribu.Mbali na pilika pilika za maisha ya kila siku tumezingatia manenona fikra. Tumezungumza lugha ya maombi na tumekutana kilammoja na mwenzake katika ukimya. Sasa tunataka kutembeakidogo na wanafunzi katika barabara inayoelekea Emmaus –ilituweze kudaka na kuelewa vizuri ukaribu wa kimungu.Hadithi ya Emmaus inatupeleka hadi wakati na mahali – mahalipenye utupu – baada ya jeuri ya msalaba wa Kalvari.wawili katiya wanafunzi wa Yesu, wawili kati ya marafiki wawili wapendwa,wapo njiani kuelekea katika kijiji cha Emmaus. Walikuwa katikahali ya masikitiko makubwa huku wakienda. Ingawa ilikuwa ikingalini mchana, wao bado walikuwa gizani kabisa. Hawakuwezakuiona njia ya kuepuka maumivu yao. Kwa niniYesu, ambayealikuwa mwema sana, kuufikia mwisho mbaya wa aina hii? Jehakuwa ameahidi ya kuwa atakuwepo pale kwa ajili yao? Na kishaanaenda akiwa amewatelekeza bila kujali. Hawaelewi chochote –yaani hata yote yale ambayo imemlazimu Yesu kutaabika kwayo.Hawaoni maana yoyote katika kisirani hiki.Wanafunzi wa Yesu wamepotea. Wajipoteza wenyewe katikakujisikia kwao kupoteza. Wamempoteze mtu waliyempenda.napia wamepoteza imani yao katika maneno yake. Wasingewezakuamini tena ya kwamba yeye alikuwa yule aliyesema kuwandiye –mkombozi na Mwana wa Mungu matarajio yao yote namatumaini waliyokuwa nayo yalitoweshwa.Walimfuata mtu waliyeamini kuwa ni njia ya kwenda mbinguni– na kwamba njia hiyo ghafla imebadilika na kufikia mwishowake. Wamechanganyikiwa na kukata tamaa. WameondokaYerusalemu kwa huzuni na mshangao. Mino’ngono ilidai japokwa ukweli fulani kuwa kaburi la Yesu lilikuwa tupu. Lakini hiyoilionekana kuwa si kitu cha kuamini, kwani kilikuwa chemasana kuwa cha kweli.Ghafla, mtu wa tatu alifika katika eneo la tukio. Huyu alikuwani Bwana aliyefufuka, Yesu Kristo. Tunalijua hilo. Lakini wanafunzihawakumtambua. Yote wanayoyaona ni mgeni tu.Hawakukatishwa tamaa wanachokiona ni njonzi.Mtu aliwauliza kwa nini wapo chini sana. Wanaonekana kanakwamba wamepoteza rafiki yao wa karibu…wanafunzi walimwelezanini kilitokea Yerusalemu siku chache zilizopita. Wanamwelezajinsi ndoto zao zote zilivyoharibika na kuangukana sasa zimelala chini ya msalaba.Kwa uwezo mkubwa, yule mtu anawatafsiria unabii wa kale.Anawaelezea jinsi ilivyoandikwa katika maandiko kuwa imempasaMwana wa Mungu ateswe na kisha kuchukuliwa juukatika utukufu. Anajaribu kuweka sawa maoni ya wanafunzijuu yamambo yaliyotokea. Wanapokaribia kijiji walichokuwawakienda, yule mgeni alitangulia mbele kidogo kana kwambaalikuwa akiendelea. Lakini wanafunzi, waliofurahia kuwa nayena pia maneno yake yenye ufahamu, walimwomba akae nakula pamoja nao. Wakati wa chakula, muujiza ulitokea. Magambayalidondoka kutoka katika macho ya wanafunzi.Kwa muda mfupi tu wakati Yesu akiumega mkate, Karamu yaBwana ikawa imefanyiwa marejeo – lakini kwa namna nyingine.Sasa imekuwa wazi kuwa yule anayetoa ndiye anayepewa.Yesu Kristo amekufa na kufufuka. <strong>Mwili</strong> wake na damu yakeni moja pamoja na mkate na divai.Ni katika ushirika huu wakila siku, na si barua isiyo na uhai inayowapa wanafunzi imanikatika ufufuo. Ni kule kuambatana, na si mazungumzo, kinachofunguaakili zao. Wanafunzi wanamwona Yesu akiwa haikatika mwili kule barabarani, lakini haiwaingii vizuri. Wanasi-60 SURA ZA MUNGU


sura za mingukia anapotafsiri maandiko. Lakini hawamsikilizi kwa makini. Sikwamba wana mioyo migumu tu, bali wao ni wagumu kusikiana wazito kujifunza.Ni wakati ule tu wanapokuwa wanajiandaa kula, muda wanapoketipamoja na Yesu chakulani, ndipo wanapogundua namnagani mateso na utukufu vinaelea katika hadithi hii .Ufunuoni kuwa na macho yako wazi.Katika furaha ya kutambuliwa, Yesu anatoweka. Njia zaolazima zipishane kwa sasa, lakini wanafunzi hawasumbuliwitena na wasiwasi wa kutenganishwa na Yesu. Wamemwona nakugundua kuwa yeye ni nani. Wamemtambua na kumkubalikuwa yeye ni Mwana wa Mungu. Na kwamba anawaweka huruwarudie maisha yao na uhusiano na watu wengine. Mitumewaliokuwa wamekufa ganzi sasa wamepata nguvu mpya nakuwa watendaji.Hali za kimaisha ambazo hazitabiriki pia hazibadiliki haraka,lakini si ilivyo kwa imani ya wanafunzi. Hawana majuto tena.Hawapotezi mwelekeo tena. Sasa wanaweza kuiona maana yakile kilichotokea.Hadithi ya safari kuelekea Emmaus ni hadithi ya mchakato wahuzuni. Wanafunzi wanaenda katika safari ya ndani na ile ya nje.Wanasafiri kutoka mashaka na kukata tamaa hadi utendaji.Tunapowapoteza wale tuliowazoea, wakati vitu vinapoporomokabadala ya kuendelea mbele, wakati mioyo yetu inapovunjikana hakuna kitu cha kutushikilia, tunaelemewa na hisiaza kutokuwa na maana na kukata tamaa. Tunakuwa kama walewanafunzi wawili wakielekea Emmaus. Tunajiona wapwekena tuliotelekezwa na Mungu, na ndipo tunaililia mbingu “kwanini?”Lakini hata hivyo hatuwezi kuiona maana mahali pasipo namaana, ingawa pia hatuwezi kujenga mshikamano pale palipona maanguko, hatukuachwa peke yetu. Ipo njia ya kushindamateso. Yesu Kristo atajiunga nasi katika njia hiyo – hata paletunapomwona kama mgeni tu.Yeye atatutoa kutoka katika giza la mashaka na kukata tamaa.Atatupa ufahamu wa ndani ili tuweze kuiona hali yetu waziwazi.Atatumwagia upendo wake na kutujaza matumaini. Matumainihuleta nuru katika maisha. Matumaini huyaona maishayetu jinsi yalivyo – wakati huo huo ikiangalia mianya ya kuletamabadiliko.Tunaogopa sana kugusana sisi kwa sisi. Lakini tunaye Munguanayetugusa kwa uzuri wake mkubwa sana wa milele. Tunaogopasana kukaribiana. Lakini tunaye Mungu ambaye hutakatugusane naye: Mungu ambaye – kwa maana halisi- hujandani ya ngozi yetu, kwa sababu anatupenda.Tunaogopa sana kugusana sisi kwa sisi. Lakini katika maishayetu na uhusiano baina yetu, Mungu huja karibu – hata kamahatutaki chochote kutoka kwake na kinachomhusu. Yeye hujakaribu kwa upendo unaovuka mipaka yetu na kutuelemea kwanguvu zake. Amina!Mpendwa Mungu Baba,Asante sana kwa kuwa leo tulikuwa hapapamoja nawe na kila mmoja wetukatika faragha hii.Tunaomba:Uiweke mioyo yetu tayari kuupokeaupendo.Uyaweke macho yetu waziKupokea ufunuo wakoTuimarishe katika imaniKwa kuwa wewe ni BwanaJuu ya uzima na mautiJuu ya walio hai na walio wafu piaWewe ambaye u sala moja mbali,Uwe karibu nasi daima!Amina!Na sasa tuombe kwa muda mfupi tukiwa kimya…Sasa mnaweza kusimama, na pamoja na mitume tunajiombeana kumwombea kila mmoja.Neema ya Bwana wetu Yesu kristo, Upendo wa Mungu Baba, naushirika wa Roho MtakatifuUwe pamoja nasi soteAmina!SURA ZA MUNGU 61


Kuwasha MishumaaMungu, uliumba ulimwengu mmoja,usio na mipaka na migawanyiko.Tunatubu hakika kwamba ni kwa sababu yetu ulimwengu umepasuka na kumeguka.Tusaidie kurejesha umoja ulimwenguni,Na utuunganishe katika mapambano ya kuwapatia watu wote wenye VVU fursa sawa na haki wanazopate watu wengine.Mungu, tunaomba kwa ajili ya nchi zile ambazo mamlaka yamefumba macho yao na kutouoona ukweli unaodhihirishwa na VVU na UKIMWI.Tupatie ujasiri wa kuziweka wazi, ili kwamba hakuna mwingine yeyote anayehitaji kutolewa kafara katika madhabahu ya kukataa.Tunauwasha mshumaa kwa ajili ya umoja wa wanadamu wote.(Mshumaa unawashwa)Mungu tupatie ujasiri ili tufanyie kazi umojaMungu wewe ambaye ni chanzo cha utu na heshima yetu.Utuonyeshe wajibu tulionao kwa kila mmoja wetu.Utusaidie kujenga ulimwengu ambapo hakuna atakayefaidika na mateso na huzuni ya watu wengine,ulimwengu ambapo watafiti, wazalishaji wa madawa na sisi wenyewe tutakuwa makini kufahamu wajibu wetu wa kimaadili.Mungu tunaoomba kwa ajili ya ulimwengu ambapo maisha ndio hoja kubwa –si takwimu na faida.Tunawasha mshumaa kwa ajili ya vipaumbele sahihi katika jamii. (Mshumaa unawashwa)Mungu utupatie ufahamu wa ndani kutendea kazi hakiMungu, wewe uliyetuumba sawa bila kujali shughuli zetu za kutafuta maisha, ngazi za kijamii, utaifa ama mielekeo yetu ya ujinsia.Utuunganishe dhidi ya mipaka yote ya kijamii tuliyoiweka.Tunaomba kwa ajili ya waliojiajiri kutoa huduma ya ngono wanaonyonywa na kuishi chini ya ugumu wa kazi yao.Tunaomba kwa ajili ya wale wote wanaopambana kwa ajili ya haki ya kujilinda wenyewe dhidi ya VVU.Hao tunaomba wasikilizwe na kwamba wapate wasemaji wenye nguvu na ndugu halisi katika mapambano.Tunawasha mshumaa kwa ajili ya dunia ambayo haitakuwa na sisi na wao.(Mshumaa Unawashwa).Mungu tupatie mshikamano ili tuwe sauti kwa wasio na sauti.62 SURA ZA MUNGU


KumpendaMunguTumeshirikiana na wewe katikamaumivu yetu na kupoteza kwetu.Wewe ni tumaini letuKatika mateso yetu na kuhitaji kwetuTunaomba tupate amani katika kuaminikwamba wewe ni mwenye uwezomiongoni mwa walio wadhaifu.Utuonyeshe basi kuwa nguvuzako zinaweza kudhihirika katikatiya udhaifu wetu usio na kifaniMungu, unatuhudumia na umetuita tumtumikie kila mmoja bila kuhesabu gharama.Imarisha mwelekeo wetu na utayari wetu kumhudumia kila mmoja wetu.Tunaomba kwa ajili ya waajiriwa katika sekta za afya na za kijamii na kwa waliojitolea wanaofanya kazi miongoni mwa watu wanaoishi na VVU.Wasaidie kujua kuwa wanakutumikia wewe, Oh Bwana Mungu, na uwape ustahimilivu.Tunawaombea marafiki, jamaa na wapenzi wa wale ambao wana VVU, na wale waliofiwa kutokana na UKIMWI.Tunawasha mshumaa kwa ajili ya faraja kwa wale wanaomboleza. (mshumaa unawashwa)Mungu utupe moyo wa huruma wa kuwahudumia wale wanaoteseka.Mungu, umetuumba sisi sote kwa mfano wako na umetufanya kuwa waumbaji wenza wa ulimwengu wenye haki.Utusaidie katika mapambano dhidi ya ubaguzi, ujinga, na upumbavu,ili kwamba muda mfupi ujao tuweze kuona milima na mabonde ya ulimwengu unaowapatia heshima inayostahili wote wanaoishi na VVU.Mungu, uwakaribie wale ambao wamepoteza ajira zao, marafiki wao, familia na wapenzi wao kwa sababu ya hali yao ya VVU.Tunawasha mshumaa huu kwa ajili ya ulimwengu tukiwa na heshima na taadhima kwa watu wote. (Mshumaa unawashwa)Mungu utupatie dira tutakayowashirikishaWale waliopoteza matumaini yole.Mungu ambaye unatujua na kuyasikia maumivu yetu:Tunajua kwamba hakuna kitakacho tutenganisha na upendo wako.Tunaomba kwa ajili ya watu wote walio na VVU na wote ambao wameathiriwa na UKIMWI.Ambao wanaishi na shauku nyingi, wakiwa na majonzi na kujisikia kupotelewa.Mungu uliyeumba watu wote katika mfano wako, utusaidie kuwapo pale walipo wenzetu wanaoteseka.Tunawasha mshumaa kwa ajili ya dunia ambapo tunashirikiana mateso na kuchukuliana mizigo. (Mshumaa unawashwa)Mungu tupe upendo wako wa ziada ili tuweze kuelewa kwa kina zaidi maumivu na mategemeo ambayo ni sehemu ya binadamu.SURA ZA MUNGU 63


Sala Sikuya UKIMWI DunianiBabaYetu Uliye MbinguniKatika siku hii ya UKIMWI Dunianitunakuja kwako na kila kitukinacho tuponda ponda na kutusukumaTunaomba:Uwe pamoja na wanao na bintiwala wote wanaoishi na VVU na UKIMWI.Watoto wamekuwa yatima,wanawake wamekuwa wajane.Vizazi vinatoweka.Mungu utupe nguvu ya kukabiliwimbi la UKIMWI katikaupana na ukubwa wakeTuinue juu,ili tuweze kwenda ulimwengunina kupambana dhidi ya UKIMWIna ubaguzi wenye jeuri kubwa.Tusaidie kukabiliana na kujitangazia haki kwetubinafsi na mawazo yetu yasio sahihi kuhusu VVUna wale walioambukizwa.Fungua mioyo yetu kwaajili ya mabadiliko na upatanisho.Katika wema wako Munguwape mapumziko walewaliofariki kutokana nakwa wale wanaoishi na na VVUHili tunaliomba katikaJina la Yesu KristoBwana wetu.64 UTANGULIZI


<strong>Mwili</strong><strong>Mmoja</strong><strong>Mwili</strong> <strong>Mmoja</strong> ilianzishwa kwa pamoja na Kikundi cha KuwekaMikakati kilichokutana Lusaka 2004.Kutoka Zambia: Japhet Ndlovu, Joy Lubinga, MunalulaAkakulubelwa, Rose Malowa. Kutoka Msumbiji: Dinis Matsolo,Elias Massicame. Kutoka Norway: Jan Bjarne Sodal, EstridHessellund, Steinar Eraker. Kutoka Denmark: Carina Wøhlk,Birthe Juel Christensen. Kutoka EHAIA: Sue ParryWALIOCHANGIA KITABU CHA 2ZambiaMch. Japhet Ndhlovu, Katibu Mkuu wa wa Baraza la Makanisanchini Zambia. Akishirikiana na Duara za Tumaini. Joy LubingaMshauri Nasaha Masuala ya Akili na Jamii, Duara za Tumaini.Ackim Sakala. Mwalimu, Mwana harakati UKIMWI+. Duaraza Tumaini. Askofu Luckson Chibuye, Mch. Pearson Banda.Mratibu VVU na UKIMWI kutoka Kanisa la Reformed, Zambia.MSUMBIJIMch. Elias Zacarias Massicame, Mratibu wa Kitaifa wa VVU/UKIMWI katika Baraza la Makanisa Msumbiji akishirikianana Mch. Dinis Matsolo, Katibu Mkuu wa Baraza la MakanisaMsumbijiDENMARKMch. Birthe Juel Christensen, Afisa Habari, DanChurch Aid.Denmark. Mch. Carina Wøhlk, Chama cha Taifa cha UKIMWIcha Kilutheri. Preben Bakbo Sloth, HIV+ activist. ElizabethKnox-Seith, Mwana Soshiolojia MtamaduninorwayJan Bjane Sodal, Mratibu wa Mradi wa VVU/UKIMWI waBaraza la Kikristo Norway akishirikiana na watu waishioau walioathiriwa na VVU wanaokutana Aksept – Kituo chakanisa Mjini Oslo. Norway: Helge Fisknes, Oslo City Mission.Steinar Eraker, former pastor at Aksept, Mch. ElisabethTveito, Mjumbe wa Bodi katika Baraza la UKIMWI Norway,Mhariri-mwenza, na Estrid Hessellund, wa Toleo ‘Positive:Branding, Sexuality, HIV and AIDS. Verbum, Norway, 2005uk 16 na 29’TUNASHUKURU KWA RUKHSA YENU YA KUTUMIAYALIYOMO KTIKA TOLEO HILI LA SASA

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!