12.07.2015 Views

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

Read - bunge .parliament.go. tz

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

BUNGE LA TANZANIA_______________MAJADILIANO YA BUNGE_______________MKUTANO WA NANEKikao cha Thelathini na Tano – Tarehe 28 Julai,2012(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)D U ASpika (Mhe. Anne S. Makinda) AlisomaDuaHATI ZILIZOWASILISHWA MEZANIHati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII:Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kwa Mwaka waFedha 2012/2013.

HOJA ZA SERIKALIMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikalikwa Mwaka 2012/2013 - Wizara ya Nishati na MadiniMajadiliano yanaendeleaSPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea namajadiliano. Kama nilivyowaambia, leo tutajadilianampaka saa tano na nusu tutakuwa tumemalizaOrodha ya waliomba kuchangia. Halafu saa tano nanusu hadi saa sita tutatoa dakika 15 kwa ManaibuWaziri, saa sita mpaka saa saba atapewa mtoa hojaWaziri, saa saba mpaka saa nane Kamati yaMatumizi. Kwa hiyo, nitawaita waliochangia maramoja.MHE. DEO H. FILIKUNJOMBE: Mwongozo wa Spika.SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mwongozo wakatihatuna kitu kilichotokea hapo awali tumeomba Dua tu,naomba matumizi ya mwongozo yawe sahihi kwasababu tumesoma Dua tu basi.MHE. DEO H. FILIKUNJOMBE: Aya ya 68 (7)inazungumzia jambo ambalo limetokea wakati uliopitaBungeni ambalo jana wakati Mheshimiwa Kafulilaanachangia alitumia neno kwamba nchi hii imebakwana mafisadi. Mwenyekiti aliyekuwa anaongoza Bungealimtaka Mheshimiwa David Kafulila neno aliondoekwamba neno hilo ni matusi na la kufedheheshaBunge.

Mheshimiwa Spika, mimi nimesoma literature nenomoja linapotumika kuna dictionary meaning nacontextual meaaning. Ukienda kwenye dictionary yacontextual meaning neno kubakwa siyo tusi.Nimesoma usiku nimetafakari sana, na nimeonakubakwa maana yake nini katika dictionary yacontextual meaning neno kubakwa ni kupokwa, nikuzidiwa na kulemewa.Kwa matumizi haya Mheshimiwa Kafulila alikuwasahihi na ukitazama michango ya Wabunge humundani wote kwa pamoja jana kwa mara ya kwanzamatendo yetu, maneno yote yalikuwa yanaashiriakwamba nchi hii imebakwa na mafisadi.Mheshimiwa Spika, sasa naomba mwongozowake, maana itafika mahali sasa Wabungewataogopa maneno ambayo yanamanisha yanatakakutupatia uzito wa kauli zao. (Makofi)SPIKA: Usinihutubie mwongozo unaniomba nifanyenini?MHE. DEO H. FILIKUNJOMBE: Ndio mwongozowangu, kwa maana neno hili linatumika tunasikiaDemokrasia imebakwa na tunalitumia kila sikutunaomba mwongozo wako mimi nataka neno hililirudi.SPIKA: Basi ukae mdogo wangu imeshatosha.

Waheshimiwa Wabunge sifa ya mtu yeyotemwenye hulka ya kuitwa mtu ni kile kinachotokamdomoni kwake kisichokuwa na nidhamu ndiokinachomfanya mtu aonekane. Unaweza kuwa mtuumevaa vizuri kabisa, unapendeza lakini kinachotokamdomoni ndio kinakufananisha na wewe unavyowezakusema.Kuna maneno mengine hapa ukisema ni sawasawa wewe umejivua nguo unaona hiyo. Kwa hiyo,ninachokisema hulka ya kiongozi hata kama neno hilolina tafsiri nyingi lakini angalia unamwambia nani?Huyo atakayesoma dictionary unayosema ni naniatakayesoma na humu dictionary hazipo na mbayazaidi ni kwamba Mwenyekiti anapotoa maamuzi kunatabia watu wanasimama na kuanza kubisha, jamanikanuni zetu ni kali mno.Tunapenda sana kuelimishana lakini ni kali mno.Ubishani na Mwenyekiti siyo tabia ya Bunge loloteduniani kote. Kwa hiyo, mimi nasema neno lile hatakama umesoma dictionary, hatuna dictionary hiyolakini linamweleza mtu mwenyewe. Tunaendelea.(Makofi)MHE. SUBIRA KHAMIS MGALU: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kupata nafasi asubuhi ya leo kuwezakuchangia hoja hii ya Wizara ya Nishati na Madini.Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu kwakunijalia afya njema na kuweza kusimama ndani yaBunge lako Tukufu na mimi kuweza kutoa mchangowangu.

Napenda niwatakie kheri ya mwezi waRamadhani Waislam wote nchini. Pia napendakuwashukuru sana wananchi wa Mkoa wa Pwani hasawanawake kwa kuweza kuendelea kuniunga mkono.(Makofi)Mheshimiwa Spika, awali ya yote nianzekuipongeza Wizara hii pamoja na viongozi wakekuanzia Waziri, Manaibu Waziri, Katibu Mkuu naWatendaji wote wa Wizara hii kwa maandalizi mazuriya Hotuba ambayo imewasilishwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba pia niipongeze Wizarakwa utekelezaji wa shughuli mbalimbali za mwaka2011/2012 hasa ambazo zimefanyika katika Mkoa wetuwa Pwani. Kwa mfano kukamilika kwa msongo waumeme wa kV 33 kwa Kata ya Mbwewe.Lakini sambamba na hilo kwa mara ya kwanzaMakao Makuu ya Wilaya ya Rufiji yamepata umeme.Lakini pamoja na hayo pia niipongeze Wizara naniiombe iendelee kutekeleza miradi ambayoinaendelea ya kusambaza umeme katika Kata yaMagindu Wilaya ya Kibaha katika Kata yaKimanzichana Wilaya ya Mkuranga mradi huuuendelee.Pia katika Kata ya Kiwangwa wananchi waKiwangwa walimpa kura nyingi za Udiwani wa CCMkutokana na imani ya kwamba mradi ule wakusambaza umeme na nguzo zimefika. Kamatunavyofahamu eneo lile linaongoza kwa uzalishaji wamatunda, tunategemea wadau mbalimbali baada ya

kufika nishati ya umeme wanaweza wakajengaviwanda na hatimaye wananchi nao wa Mkoa waPwani hususan katika maeneo niliyoyataja wawezekufanya shughuli za kujiletea uchumi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, pia niipongeze REA kwakuweza kutangaza tender ya kusambaza umemeunaokwenda katika Kijiji cha Nyamisati Kata ya Salaleambako kuna shughuli mbalimbali za uchumi kule.Kuna shule inayosomesha watoto yatima, kwa hiyo,ninadhani kufika kwa nishati hiyo itatusaidia sana.(Makofi)Mheshimiwa Spika, hivi karibuni tumeshuhudia najana Bunge lilijielekeza zaidi katika kutetea maslahi yaWatanzania. Jana Bunge lako Tukufu lilikwendasambamba na dhamira yako ambayo wakatitunakuchagua ulisema una nia ya kujenga Bunge mojajana dhamira hiyo imeanza kuonekana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, jana yamejitokeza makundimbalimbali yanayoona sheria ya manunuzi ya Ummakatika mkataba wa kusambaza mafuta kwa ajili yaIPTL wako wanaona kwamba Wizara imekiuka kanuni,wako wanaona kwamba mtazamo ule ulikuwa sawasawa.Mheshimiwa Spika, mimi naomba niunge mkonona nina uhakika hakuna kanuni ya manunuziiliyovunjwa. Nasema hivyo kwa sababu gani, kwambakatika Serikali yako manunuzi ambayo unatakiwa kwamfano sekta ya madawa lazima dawa ununue MSD,

Pia utengenezaji wa magari lazima utengenezekwenye karakana ya Serikali (TEMESA).Lakini pia hii PUMA (BP) ni kampuni ya Serikali inaasilimia 50. Hivi ni ubaya gani Serikali kuiwezesha taasisiyake inayomiliki asilimia 50 na ambayo taasisi hiyoMwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PUMA niMtanzania Ndugu Kelvin Felix ni dhambi gani? (Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini kinachosikitisha hata walewaliokuwa wanasema kanuni imevunjwa viongoziwawajibike hawataji kanuni gani ndani ya sheria yamanunuzi iliyovunjwa. Taifa limepata hasara ya kiasigani. Lakini kwa wale ambao tunaona kanunihaijavunjwa tunaambiwa taifa limeokoa kiasi chabilioni tatu (3) kwa muda wa wiki mbili. (Makofi)Mheshimiwa Spika, inasikitisha imefika wakatiBunge letu linatumika ndivyo sivyo. Tabia hii imeanzakuota mizizi tumeona Bunge la mwezi wa nne wakatitunajadili namna gani viongozi wawajibike, tulifanyamaamuzi. (Makofi)Lakini leo anaposimamishwa mtendaji kamatizinatumia mamlaka yake vibaya wanataka wakutanewajadili, alivyoteuliwa huyo mtendaji mbonahawakukutana.Kwa nini tunaingilia muhimili wa Serikali leo,alipopewa nafasi alivyoteuliwa hatukukutana kujadilikwa nini ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa shirika hilo.Lakini Serikali inapoamua hebu simama pisha

uchunguzi tujiridhishe Kamati zinaitana ili wajadili kunanini? (Makofi)Mheshimiwa Spika, tumechoka na ujasiri huu wakifisadi. Tunaomba Mheshimiwa Spika, utumie mamlakayako, tunaomba ifike wakati tuzi-review hizi kanunikama unaunda Kamati na endapo inatokea Kamatihizo hazitimizi wajibu wake, zivunjwe. Leo Kamatizingine hazina heshima, zipo Kamati zinatuhumiwaWatanzania hawaelewi zinatuhumiwa lakini watuwanaendelea na kazi.Hivi imani ya Watanzania itatoka wapi? Watuwanateuliwa kwenye Kamati wanaonekana kabisaushahidi upo, wanakwenda kuomba rushwa eti Bajetitupitishe Katibu Mkuu amewataja ushahidi anao kwanini wasichukuliwe hatua? (Makofi)Mheshimiwa Spika, usitulee Wabunge, chukuahatua hata kama ni sisi tunahusika, tuchukulie hatuahaiwezekani kanuni hii iseme eti kamati iliundwa ikaemiaka miwili na nusu hata kama kamati hiyo ikivurundaikae tu, tuzi-review hizo kanuni za Wabunge. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nchi hii ina changamoto nyingi,Serikali kila siku inatuhumiwa inanyanyasika kumbe kwamaslahi binafsi, leo tumewagundua. WaheshimiwaWabunge wenzangu nawaomba watu ambaowametajwa na hata kwenye vyombo vya habarivimetajwa, sasa tuwasusie michango yao kwenye partcaucus zetu kwenye Bunge, tujue michango yaoitakuwa ya maslahi binafsi.

Mheshimiwa Spika, haiwezekani kumbe watutunawaona wanapata sifa wanachangiawanaonyesha uchungu kumbe wanachangiawanakumbuka maslahi yao. Hivi ni binadamu ganiumechaguliwa na wananchi kuja kuisimamia Serikali,Serikali gani unayosimamia hiyo? (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa kweli Watanzaniawamesikitika, lakini baya zaidi vinanunuliwa mpakavyombo vya habari havizingatii weledi vinaandikataarifa tu Mkataba wa PUMA lakini hawatupi upandemwingine wa shilingi, nini kimeokolewa zingetumikakwa ajili ya kununulia madawa, madawati, kujengazahanati na kadhalika. (Makofi)Mheshimiwa Spika, mimi nasema naunga mkonohoja lakini ninawaomba Waheshimiwa Wabunge,tusitumike tuache kuwa na ma-agent wa mafisadi.Nawaomba watendaji wa Wizara hii waendelee kuzibamianya hiyo hata kama kwa kuvunja Kanuni ili mraditaifa hili linafaidika. Sisi Wabunge tutawaunga mkonona wale ambao tumewagundua kwanza tutawasusiamkichangia tutawazomea, kwenye part caucastutawazomea. Hamna chenu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)MHE. MOZA ABEDI SAIDY: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niwezekuchangia katika Wizara ya Nishati na Madini.

Kwanza kabisa napenda kuungana na Waislamwenzangu wote katika mfungo huu wa mweziMtukufu wa Ramadhani.SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Kigwangalla ulivyovaasiyo. Naomba ujiangalie, huruhusiwi kuwa nabaraghashia na koti na kanzu hiyo inaruhusiwa. Lakinivingine ulivyovaa hapana. Endelea Mheshimiwa Moza.(Makofi)MHE. MOZA ABEDI SAIDY: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Pia napenda kutoa pole kwa wale woteambao waliokutwa na maafa kwa namna moja amanyingine Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemumahali pema peponi na marehemu wotewaliotutangulia mbele ya haki.Mheshimiwa Spika, naomba kutoa mchangowangu mimi katika suala moja la ardhi kwani ni sualamtambuka na juu ya ardhi kuna watu chini ya ardhikuna vingi vilivyomo hata mali ambazo ni madini.Mheshimiwa Spika, nije moja kwa moja kwenyesuala la madini. Kuna kitu kimoja ambachokinatushangaza kidogo. Katika harakati nzima zakuweza kufambua madini haya wanavumbua vijanawetu ambao ni wazawa katika eneo husika ambaowanayagundua madini, wakishavumbua madini hayobasi wanakuja wawekezaji wengine, Serikaliinawaondoa wao inawaweka wawekezaji, wenyewewazawa halisi wanakuwa hawana kipato chochotewanakuwa kama vile watumishi katika eneo lao.Mifano tunayo mingi katika nchi hii.

Mfano huko Arusha katika uchimbaji wa madini yaTanzanite, tumegundua kwamba sasa hivi mkataba uleuko na Makaburu. Hata madini haya yanauzwa kwanembo ya Makaburu. Tuangalie katika nchi yetu yaTanzania uchumi huu ni wa kwetu wenyewe wananchiwa Tanzania, ardhi ni ya kwetu Tanzania, vijana wakwetu Tanzania, lakini wananyanyaswa vibaya mnovijana wetu ambao ndio wazawa wanaogunduamadini haya. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ningependa kuuliza Serikali inampango gani ya kuwaweka katika hali nzuri yakimaisha inayoweza kustawisha katika kupata uchumimzuri katika nchi yao na madini yao? Tunao wasomiwakubwa katika nchi hii kwa mfano Profesa IbrahimLipumba ambaye anaweza akasimamia uchumi huuwa nchi kama iwapo kuna sehemu ipo kunalegalega.Tusiwe wachoyo wa fadhila tuwe pia watu ambaotuna uwezo wa kuwatumia watu ambao wana elimuna ambao wanaweza wakaiongoza pia nchi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia suala lamapato ya madini, kwa kweli katika mapato ya madinihivi karibuni tumeona madini ya dhahabu na madinimengineyo yamepanda bei kitaifa. Lakini siamini kamakweli sisi tunaweza tukawa tunanufaika katika hali hiyo.Yapo mashaka makubwa tokea huko mwanzo. Piatuna wasiwasi na Hati Miliki. Hati Miliki hizi kwa niniSerikali haitoi kwa hawa wawekezaji wadogowadogo? Inatoa kwa wawekezaji wakubwa, kwa niniinakuwa wawekezaji ambao wanatoka nje, ambaosiyo Watanzania wanapewa nafasi kama hizi wanakuja

kuendelea kututawala na wanasomba mpaka udongowetu.Hivi tufikirie wananchi tuliopo hapa Tanzaniatutabaki maskini mpaka sehemu ya kukaa katikamaeneo yetu tutakuja kubaki na mashimo tu. HebuSerikali sasa ifikie hatua ya kufikiria kwamba kama kunauwezekano watalaam tunao hapa hapa nchiniTanzania hii kazi ifanyike hapa hapa katika nchi yetu yaTanzania na tusingoje kwamba tusubiri watu kutoka njeili wao wawe na uwezo mkubwa wa kuweza kutufanyiashughuli hizi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nihame moja kwa moja nasuala ambalo ni la umeme, nije kwenye suala laTANESCO. Kwa kweli ni hali ambayo inasikitisha hukonyuma tulipotokea. Lakini sasa hivi naona kwambashaka inakuwa inaondoka. Maadam tunao Mawaziriwetu ambao walioteuliwa juzi tu na Mheshimiwa Raiskwamba wasimamie suala hili la Nishati na Madini.Tunajua kwamba Tanzania tutanufaika kwa ajili yaowao. Wametutoa shaka, wasi wasi na mimi sina wasiwasi nawaunga mkono percent mia kwa mia.(Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tumegunduakwamba Serikali imeweza kugundua kwamba kunanjama nyingi ambazo zimejitokeza za hujuma nyingi zamafuta, haya mafuta ya umeme yanakuwayanahujumiwa na watu wengi hata na wafanyakaziwenyewe na inasadikiwa mafuta haya yanapikiwahata chipsi, samaki yanakaangiwa. Sasa sijui kama

Serikali ina taarifa hii na kwamba inawezekana yakawana athari gani katika maisha ya wanaadamu.Tunalo suala la ajira kwa vijana, TANESCOimekuwa na ubaguzi mkubwa kwa huyu MkurugenziMtendaji huyu Ndugu William Muhando. Kwa kweliukiangalia familia nzima ya TANESCO imekuwa imejikitakatika sehemu kubwa imekuwa ni ya kifamilia. Hakunawatoto wa kimasikini ambao wanaweza pale hatakama wamesoma waende pale wakafanye kazi nahata wakifanya kazi ndani ya siku mbili, tatu utakutakwamba wanabambikizwa kesi, hii imetokea maeneomengi, haya yalianzia kwenye maeneo ya Mpwapwa,Kiteto na maeneo mengine hali kadhalika vitu kamavilishawahi kujitokeza, hii yote ni mtu Meneja anamtakakuwa Ndugu yake asimamie yeye kuwa Mhasibu auyeye ndiyo kila shughuli ambazo za umeme anazotakayeye wawe wao tu kifamilia, kiukoo. Kwa kwelitumegundua mambo mengi ambayo kweli yanawezakujitokeza katika suala la umeme.Bili za umeme zimekuwa kubwa mno. Utakuta mtuanabambikizwa kesi ya bili aende akalipie ya mtuambaye anaesaga mashine au ya mtu ambayeanapasua mbao wakati ni mkazi tu anaekaa katikanyumba.Je, kwa mtindo huu si tunahamisha sisi wenyewewateja? Kwa hiyo, suala hili kwa kweli lifikiriwe kwaundani zaidi. Mita za umeme zimekuwa zinalipiwa kwagharama kubwa mno na nashukuru sasa hivi Serikaliimetangaza kwamba bei hiyo sasa hivi itakuwaimeshapungua na ipungue kwa asilimia kutoka kwenye

hiyo asilimia iliyopo mpaka ikifike hata asilimia tatu (3)angalau tuwe tunapata hata wateja wawe wengi.Kwa kuwa suala la umeme ni suala ambalokwamba linatakiwa liwe mbadala kwa sababuwananchi wengi huko Vijijini wanatumia kuni, gesi,huenda ikawa basi na hata umeme pia wawewanatumia. Bei ya umeme ipunguzwe, iwe chini yahapo.Mheshimiwa Spika, pamoja na kuyaongea haya,kwa kweli kuna suala ambalo linasikitisha mno kuonakwamba mwananchi wa kawaida kuambiwa kwambaalipie nguzo ya umeme kwa bei ya shilingi laki tano aumita ya umeme. Hivi ile bili tu ya shilingi elfu mbili auelfu moja inamshinda, hivi kweli huko tunakokwendakweli tutafika katika nchi yetu ya Tanzania?Mimi nalaani kitendo kikubwa kinachotokea chamafisadi wa TANESCO ambao wamejilimbikizia mali nawakawa wanawafanya wananchi kama watumishiwao, naomba mali zao zote wale wote ambaowamegundulikana na suala hilo, wataifishiwe mali zaoili suala lirudi katika nchi yetu ya Tanzania kwamba liwena msimamo na haki iwe sawa kwa wote. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nashukuru. (Makofi)MHE. JOHN SHIBUDA MAGALLE: MheshimiwaSpika, nashukuru kupata fursa hii ili na mimi niwezekuchangia katika hoja ya Wizara ya Nishati na Madini.Jambo la kwanza ni kwamba nina masikitikomakubwa sana, tusipoangalia umoja wa fikra kati ya

Bunge na Serikali usipoimarishwa, Taifa hili litakuwalimeathirika sana kupata faida kuwepo Mihimili hii kwaustawi na maendeleo ya jamii, kwa ustawi namaendeleo ya uchumi.Mheshimiwa Spika, kwa hiyo una deni kubwa sanala kuhakikisha ya kwamba Bunge letu hili pamoja na sisiWabunge tunakuwa ni watu waadilifu kwa maslahi yanchi hii. Kama pana shutuma, pana kusutwaWabunge, ni vyema hawa wanaosutwa wakatolewamajina yao, wakafahamika kuliko kukaatunanung’unika, tunalalamika. Kama tutaendelezamchezo wa kusutana na kutuhumiana kwa hisia,nadharia, vionjo, porojo ni hatari kubwa sana kamatunaweza tukaoneana pale ambapo hakuna ukwelina pale palipo na ukweli basi ukweli utekelezeke,mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.Mheshimiwa Spika, sekta ya nishati na madini nisekta muhimu sana katika kuhakikisha kwambapanakuwa na ustawi na maendeleo ya uchumi. Sektaya uchumi inategemea sana kuhakikisha kwambapana nishati ya kutosha. Kipindi hiki CCM naishauriielekeze Serikali yake kuhakikisha kwamba nishatiinaimarishwa na kama Serikali ilivyotangaza kupitiaWizara hii, vitendo vionekane vya kutuhakikishia yakwamba kuna mabadiliko yanayotarajiwa. Serikaliihakikishe ya kwamba inatunga taratibu za kuhakikishainaondoa mfumo batili wa kuagiza mafuta katikamaeneo ambako ndiko kwenye mazalio ya shutumana rushwa.

Mheshimiwa Spika, tuhakikishe ya kwambaumuhimu wa nishati una faida kubwa sana kwauchumi wetu pamoja na kuhakikisha ya kwambapalipo na uchumi endelevu, hapo hapo pia hatamapato ya Taifa yanakuwepo, wajasiliamali wanapatarasilimali na wanapata nguvu ya kuendelea. CCM naSerikali yake itambue ukweli wa kwamba utangulizi wakuhakikisha kwamba nishati inayopatikana na iliyokuwaikipatikana, ulikuwa ni udhaifu mkubwa kwa sababu yashutuma za rushwa, basi mfanye upembuzi, msiwekifuniko, mhakikishe ya kwamba mnapambanua naWatanzania mnawaambia dhuluma ya hujumailiyotendeka kutokana na fikra hasi za watumishi hasiwasio na uzalendo na uaminifu kwa Taifa hili.Mheshimiwa Spika, ahadi ya Serikali ya kwambamgao hautokuwepo, naomba Serikali hii ijiimarishe. Je,Mheshimiwa Waziri umekaa na Waziri wa Fedhaakakuakikishia kwamba atakusaidia kukupamashirikiano? Je, mtandao uliokuwa ni batili kwa usatwina maendeleo ya nchi haupo katika Wizara ya Fedhahivyo ukapata kikwazo, tafakari, chunguza, makepamoja na Mheshimiwa Waziri Mkuu atoe mashirikianoyakinifu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, namwomba MheshimiwaWaziri aielekeze TANESCO ihakikishe inakagua nguzozilizooza katika kipindi hiki cha kiangazi na ihimarishemfumo wa kusafirisha umeme wa njia kutokaShinyanga hadi Maswa, Meatu, Bariadi.

Maswa kila siku tuna mgao kipindi cha masika,ninaomba, nakuomba Mheshimiwa Waziri, kama kaulihiyo wananchi wa Maswa waienzi, ni wewe uhakikisheya kwamba sasa unasimamia TANESCO la sivyo huo nimradi wao wa over time.Mheshimiwa Spika, asiejua maana, hajui maana.Waziri na Katibu Mkuu mmerithi majambo ambayohayakuwa yenu. Kama mmerithi watu wabovu,hakikisheni mnatumia JIK sugueni muaondoe walewote ambao ni watu hatarishi kwa ustawi namaendeleo, msioneane aibu. La sivyo mtakujakujikuta kwamba hao watu ambao mtawaacha,watakapobainika ya kwamba wamepona,watajiimarisha na watakuwa ni vichugu na watakuwani dhoroba ya kuwamaliza nyinyi kwa sababu alieumialazima anakuwa na makovu ya hasira na anakuwa natabia ya kusigana.Mheshimiwa Spika, katika jamii yetu, lazima mjuekwamba kuna makuwadi wa mabwenyenye ambaohutafuta madalali wa kutia kitanzini waadilifu nawaaminifu wa watumishi. Waziri lazima atambue yakwamba kuna watu wa mbegu za ubadhilifu, watumbegu ubadhilifu, huwa hawakomi ndiyo maanawahenga wakasema kunguru hafugiki, sasa tambuenina muyaondoe yote ambayo ni makunguru kwasababu kunguru hata ukimpa ubwabwa, haweziakakaa akafugika. (Makofi)Mheshimiwa Spika, viharifu na vihusisho vinashutuma kwamba baadhi ya Wabunge ni najisi kwamasilahi ya nchi yetu. Hao Wabunge ambao ni najisi,

naomba ili Watanzania wajue basi watambulishwekwamba hawa ni najisi na kwa utukufu wa Bunge laTanzania, lakini tusiichi kwa hisia. (Makofi)Mheshimiwa Spika, natambua ya kwamba kunawatu ambao wanapendwa kuitwa watwana, vibaruana maboi ya unyonyaji.Kwa hiyo, napenda kusema ya kwamba lazimatuhakikishe ya kwamba tunapambana na watuambao ni makandarasi wa fitna na ni wataalamelekezi wa Itifaki za kubadilisha utu wa binaadamu.Hakikisheni hawa wanaondoka.Je, Serikali itawaambia nini Watanzania wajengesuluhu na Serikali ya CCM kuhusu kwamba kuna watuambao wamedhulumu mabilioni ya fedha.Je, kama hii basi ndiyo ninyi mmekuwa maabaraya kutambulisha dhuluma hizo, basi nawaombamhakikishe kwamba ninyi mnakuwa ndiyo Bima yakuthaminika Serikali na ninyi ndiyo mnakuwa Bima yakusadikika kwa Serikali. Mheshimiwa Waziri utukufuwako na Katibu Mkuu pamoja na timu yako, hivi sasanyie mnaonekana ni watu ambao mmekuja nautukufu. Kwa hiyo, kabla watu hawajawatengua udhuwa maadili yenu hakikisheni ya kwambamnawamaliza. (Makofi)Mheshimiwa Spika, tembo hubeba viroboto, lakiniviroboto haviwezi kubeba tembo.

Je, wale tembo wanaobeba viroboto mna hakikaya kwamba mmewapiga risasi wakafa? Maanayangu mazalia ya hao vimelea ambao ni watudhulumati, kwa masilahi ya nchi. Je mmehakikisha yakwamba mmewajua wote na kama mmewajua wote.Je, mnataka kuatamia funiko la vundo ambalo kwaWatanzania wamekuwa wakiumia nalo? Je, hasarangapi Tanzania imepata?Naomba shutuma hizo mzifanyie kazi kwaniViongozi ambao wanakataliwa hata na Imani yamadhehebu yao mkiwastiri sijui hao mnataka kufanyanini. Ikiwa Viongozi wa madhehebu ambayo ni batilihuumbuliwa na madhehebu yao. Naomba na Serikaliiwaumbue, iwatangaze hao watu ambao ni najisi kwaSerikali. Imani bila matendo mema, imani hufa.Kwa hiyo, naomba Bunge hili vile vile lifanye hivyohivyo. Natambua ya kwamba Bunge hili hivi sasalinataka kuwa kama butcher ya kuchinjia ubadhilifuwa watu. (Makofi)Kuna mtu mmoja ambaye amechinjwa humundani kupitia Wabunge ambao walistiri watuwanaodaiwa na Bodi ya Pamba, naiomba Serikaliitangaze makosa ya Mheshimiwa Mtunga, DG wa Bodiya Pamba, Bunge lako hili na watu ambaowamejigeuza kuwa watwana wa mabwenyenye,makuwaidi wa naizesheni tuhakikishe ya kwambawanachukuliwa hatua na wanaposema humu, wawewanatambulisha ushahidi sio kuzusha maneno ya jumlajumla na kubambikiza watu naomba na Bunge lisiwena dhana hiyo.

Mheshimiwa Spika, naomba Wabunge tutumievyema na dhamana tulizonazo kwa sababutusipoangalia utakaso na utukufu wa Bunge utakuaumeingia shari na wananchi wataanza kushangaa.Je, tukimbile wapi? Naomba wafanyabiasharawahalifu wa madeni ya kudhulumu sekta ya pambawashughulikiwe.Mheshimiwa Spika, hakuna dini inayosemadhulumati iitikiwe amen. Kwa hiyo, naomba na kushaurikwamba hivi sasa Serikali ijielekeze na mhakikishe yakwamba mnashindanisha uhadilifu kwani ujinga naujinga tukiushindanisha, uzaliwa chizi. Kwa hiyo,naomba hilo tuliondoe na siasa isiwe gulio la kuuzavionjo vya maneno ambayo ni batili kwa mstakabali tukujitafutia umaarufu binafsi.Mheshimiwa Spika, ni kitu gani kinaunda sumakuya kuvutia Wabunge wako waanze kuwa na vitendoambavyo si sahihi. Fanya utafiti, uchunguzi, ujue kunamatatizo gani yanayokabili sekta yako ya Wabunge,hatimaye wanaingia katika masuala ya rushwa nakutuhumiwa. Wewe la sivyo utaonekana Bunge lakolimeacha legacy mbovu. Malighafi ya uwoto waumanamba ni vitendo ambavyo vinasababisha mtuuwe mtwana. Kwa hiyo, naomba uhakikishe yakwamba wananchi ambao walikuwa wanaaminikwamba Uongozi wako utajenga legacy au urithi mzurikwa masilahi ya vijana, basi tuhakikishe ya kwambatunashinda vizuri.

Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Katibu Mkuuupatanyifu wa matendo yenu unahitajika nautaheshimika sana pale mtakapoendeleza vita hiyohata kwenye mikataba ya madini. Watu wanaoishikatika maeneo ya madini Kahama , Geita nakadhalika, ni watu dhalili, lakini Katiba inasemarasilimali ya Tanzania itumike kwa masilahi ya nchi naWatanzania wote. Katiba ya nchi inazungumzia hivyohivyo pamoja na Katiba ya CCM, mbona ninyi wana-CCM ambao ni asilia yangu hamtaki kuhakikishaSerikali yenu inatii Katiba pamoja na Katiba ya CCM?Ndugu zangu nawashauri, vyombo vya dola vitoemashirikiano ya kuhakikisha ya kwamba Katiba ya nchiinaheshimika, CCM ongezeni kasi ya uadilifu ilimhakikishe kwamba Serikali yenu sasa inayoitwaimeokoka baada ya kuwa katika tingatinga namatetemo ya kushtumiwa kisiasa.Mheshimiwa Spika, hakuna mabaya yanayowezakumfikia mtenda mema. Kwa hiyo, nahakikishakwamba Mheshimiwa Waziri pamoja na Katibu Mkuuna timu yako, Mwenyezi Mungu yuko pamoja nanyimtastirika na naomba Imani ya dini zenu muiendelezena nawaomba kila mtu ambaye ana Imani ya dinihususani mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani,tuhakikishe matendo yetu basi yanakuwa na uzalendo,uaminifu na utiifu kwa masilahi ya Taifa. Aidha, udhibitiwa dhuluma uliopo ndani ya jamii yetu hivi sasaunanyima hakika kuthaminika wongozi wa Serikali.

Vile vile naomba kusema ya kwamba ikiwawananchi wanapata ruzuku katika umeme, basi na beiya pamba vile vile ambayo pia ni nishati na madini,tuhakikishe kwamba bei ya pamba Serikali inapewa.Mheshimiwa Rais Kikwete, sikiliza kilio chawakulima wa pamba kwa sababu pia ni madini na ninishati.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,ahsante sana. (Makofi)MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Spika,naomba nimshukuru sana Mwenyezi Mungu kwakunipa uhai na kunipa fursa ya kuzungumza Bungenileo hii katika mazingira ambayo Mwenyezi Munguamejidhihirisha na kweli naomba sasa tukumbuke natukubali kwamba Mwenyezi Mungu na aitwe Mungu.(Makofi)Niliwahi kusema hapa Bunge kwambatumwogope Mungu, nakushukuru Mungu umeanzakujidhihirisha. Hii tabia iliyokwisha kuanza kujengekaingeiyumbisha sana Serikali. Hawa waliokaa hapambele wanafanya maamuzi, hakuna Waziri asie amuana kwa vyovyote vile unapoamua, wakowatakaokubali, wako ambao hawatakubali.Kwa kawaida tunategemea mtu ambayeamekuwa aggrieved na maamuzi yaliyofanyika nawatendaji wa Serikali, kuna mkondo ambaoumewekwa na wakati mwingine imetajwa kabisa

kwamba mtu ambaye hajaridhika aendeMahakamani, amekosa tenda, amekosa hili.Mtindo ambao ulikwishakuanza kujengekakwamba mtu anakosa jambo fulani, anakwenda kwaWabunge baadhi yao, anawarubuni, anawa- mobilize,wanakwenda Bungeni kusema vitu sasa tumeanzakuona kwamba si wote wanaopaza sauti kwambakuna jambo fulani limefanyika kwamba wanakuwawana dhamira ya kweli.(Makofi)Mheshimiwa Spika, tukienda hivyo, MheshimiwaKaimu Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri Mkuu na Raiswananisikia hakuna Serikali au hakuna Waziri ambayeatakuwa salama kama pale ambapo wanaamua,halafu watu wanakuja ku- mobilize Wabunge, wanapileup pressure na mambo yanakwenda ambavyoyanaweza yakaenda. (Makofi)Nampongeza sana sana Ndugu yangu Maswi,Mheshimiwa Waziri Prof. Muhongo kwa kufanyamaamuzi mazuri ya kijasiri ya kuhakikisha kwambawanaokoa rasilimali za nchi hii.Mheshimiwa Spika, nakuomba Ndugu yanguMaswi jipe moyo na tumia kitabu cha Wafalme, kitabucha kwanza, mlango wa nane (8) mstari wa 44-45;watashindwa na watakuwa wanaumbuka mmojabaada ya mwingine. Leo hawatajwi na naombamsiwataje, Mwenyezi Mungu ana namna yake yakuwataja, time will tell. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nizungumziemanufaa ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo yamigodi, tumekuwa tukilalamikia sana suala hili,ninawaomba sana wawekezaji ambao tunao kwenyemaeneo yetu kwamba sasa muda umefika wa kukaachini na niwaombe sana serioulsly kampuni ya AfricaBarrick Gold, tumekuwa na changamoto nyingi, waondiyo wawekezaji wakubwa kwenye sekata hii, lakinikwa bahati mbaya sana wao ndiyo wamekuwawamwisho kwenye kila jambo ambalo linalengakunufaisha wananchi.Mwaka 2008 Mheshimiwa Rais aliteuwa Kamati yaBomani na mimi nilikuwa Mjumbe, yalikujamapendekezo mengi mazuri, moja wapo ni lilelinalosema kwamba mrabaha uongezwe kutokaasilimia 3 hadi asilimia 4, kampuni zingine zimekubalilakini kampuni iliyokuwa inasuasua kukubali ni hiikampuni ya Barrick.Sehemu zote tulizozunguka duniani kampuni hizi zamigodi zimefanya uwekezaji mkubwa, tulikwendaKalgurie, Australia, kule Barrick wamejenga barabaraya lami kutoka Perth kilomita 720, leo tunawaambiakatika mazingira haya ambayo wako Kahama kwazaidi ya miaka 30 ijayo, washirikiane na Serikali kujengabarabara ya lami kutoka Kahama Mjini hadi Kakolawanasema hilo ni jukumu la Serikali. Mbona Australiawamefanya? Umefika wakati sasa wa mikataba hiituitizame. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala la Service Levy,Sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 inaziruhusuHalmashauri kutengeneza by- laws itakayoziwezeshakutoza ushuru wa 0.3 asilimia ya gross turn over.Mikataba ya Migodi, Mgodi wa Bulyanhulu, Buzwagiambayo ilifungwa baada ya Sheria hiyo kuwepo.Mheshimiwa Spika, sheria inazuia Halmashaurikutoza ushuru huo, badala yake inasema zitalipwadola 200,000. Sheria hiyo au Mkataba huo au Mikatabahiyo, imevunja Sheria ya Serikali Tawala, Kamati yaBomani ililiona na tukaishauri Serikali, irekebishe.Tunashukuru Serikali, ililiona na ikaliingiza kwenye Sheriaya Madini ya Mwaka 2010. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nawapongeza sana Resolute,wamekubali kuanza kurekebisha suala hilo. Sisitunawadai Africa Barrick Gold, dola za Kimarekanimilioni 11.7 ambazo zinatokana na Service Levy, tokaMgodi wa Bulyanhulu ulipoanza uzalishaji mwaka 2001na toka Mgodi wa Buzwagi ulipoanza uzalishaji mwaka2009. Wamekuwa wakilipa dola 200,000 ambazo ni farlesser than what we real deserve. Niwaombe Barrick,waoneshe sasa kweli spirit kwamba, wao ndio industryleader kwenye nchi hii na wanapoendelea kuwawakaidi kama ambavyo wamekuwa, niiombe Serikali,Profesa Mhongo na Timu yako kwamba, endeleenikuwa wakali dhidi ya watu hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wananyemelea kuanza Mgodimpya pale Mwakitolyo na wameshaanza kunyemeleakuanza Mgodi mpya pale Nyanzaga. Endapohawatakubali kufanya marekebosho ya mapungufuyaliyokuwepo toka zamani, kulipa Service Levy,kusaidia wananchi wanaoishi jirani na migodi,musiendelee kuwapa leseni za kufanya kazi watuhawa, wapeni wengine.Tunategemea kwa sababu wao ndio wakokwenye industry ndio waliwekeza kuliko wengine,wawe mfano. Tunawaambia rekebisheni mikataba,lipeni service levy, hawataki. Tunawaambiarekebisheni mikataba, lipeni ushuru au royalty kutoka 3kwenda 4 wanakuwa wazito. Katika mazingira hayowananchi wetu wataendelea kuteseka. Mimininaiomba Serikali, iendelee kusimama imara. (Makofi)Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mahusianoya migodi na wananchi, limekuwepo tatizo kubwasana la maeneo ya wachimbaji wadogowadogo,nilisema wakati fulani mwaka 2007, enzi zile Waziri niKaramagi kwamba, haiwezekani nchi nzima Kampunimoja, directly au indirectly, ikawa na leseni za utafitinchi nzima. Wilaya ya Kahama, ambayo ina madinikaribu kila sehemu, haina eneo hata moja lawachimbaji wadogowadogo. Maeneo yoteyameachiwa wawekezaji wakubwa, wakifanya utafitina hakuna wanachokifanya. Nakupongeza sanaMdogo wangu Mheshimiwa Masele, juzi nilipokuwanyumbani Segese, walikuwa wananiuliza kwamba.“Kaliza nanalia kamasele?” yaani wakimaanishaMasele anakuja lini kwetu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wamesikia kazi nzuri aliyoifanyaNg’anzo, wamesikia kazi nzuri aliyoifanya Geita.Naomba mdogo wangu Mheshimiwa Naibu Waziri,simama hivyo hivyo, njoo na Kahama. Tunaombaeneo letu la Mwazimba, tunaomba eneo letu laMasabi, tunaomba eneo letu la Nyangalata,tunaomba eneo letu la Nyamakwenge, ambayo yoteyametolewa leseni kwa wachimbaji wakubwa nawachimbaji wadogo kila wakisogea, wanatimuliwa. Ilanikuombe tu, uwe na tahadhari, maamuzi haya yakuwanyang’anya wakubwa au kuwanyima wakubwaukawapa wadogo, yana hatari zake. Ushahidi upo nawewe ni mtu mzima, nafikiri umenielewa.(Makofi/Kicheko)Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie suala laumeme vijijini. Nawashukuru sana REA, wamefanyakazi nzuri, mwaka jana wamepeleka umeme kwenyevijiji vya Ntunguru,Mwakata, pamoja na Mpera. Sasahivi nashukuru kwamba, wamekubali kupeleka umemekwenye vijiji vingine. Nikuombe Mheshimiwa Waziri nabahati nzuri umesema uko transparent, haujataja vijijiambavyo vitapatiwa umeme kwa Mwaka huu waFedha tunaouanza. Tunajua vijiji vipo, lakini hujavitaja.Kweli, umetoa ramani, lakini pamoja na macho yangukuwa mazuri, ile ramani ilikuwa haioneshi vijiji vyangu.Tunaomba utupe orodha, usipofanya hivyo, unatoanafasi ya kuchakachua, atakuja mtu mwenye nguvupale REA ataondoa kijiji hiki ataweka kijiji kingine. Lakiniukishalitoa likajulikana kwamba, Wilaya ya Kahama,Jimbo la Msalala, Vijiji vinavyopata umeme ni hivi,haitakuwa rahisi kuchakachua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini naomba pia, Wizara yaNishati na Madini, Mradi wa Umeme wa kwendaBukombe, ambao ni wa siku nyingi sana, ambaounapita kwenye Vijiji vyangu, Vijiji vya Longuya, Vijiji vyaIkinda, Vijiji vya Shilela, Vijiji vya Segese, mradi huouanze. Umechelewa sana na ninaamini kwamba,wananchi kwa kweli, wamefika mahali wanaelekeakukata tama. Niombe Serikali, kama mlivyokwishakuanza, muoneshe ujasiri huo huo.Mheshimiwa Spika, kwa kumalizia, nizungumzesuala lile lile la mahusiano kati ya Mgodi na wananchi.Kumekuwepo na malalamiko ya wananchiwalioondolewa eneo la Kakola, eneo la Bulyanhulu,mwaka 1996. Wananchi hao wamekuwa na madai,wananchi 4,176 wanadai nyumba 2,330, mashambazaidi ya hekta 34, visima 72, mialo 31 na mali zingine.Walikwenda Mahakamani, Mahakamani kule kutokanana kutokuwa na uwezo kesi imeendelea milele, hadileo haijakwisha. Mwaka 2009 wakaomba kwamba,tuzungumze tulimalize suala hili nje ya Mahakama; nabahati nzuri, tulizungumza na Mheshimiwa Waziri Mkuupamoja na aliyekuwa Waziri wa Madini wakati ule namazungumzo yakawa yameanza. Niwaombe, kamawalivyoonesha nia njema watu wa Resolute kuleNzega, kulimaliza suala hili, hebu tukae pamojatulizungumze, tuweze kuona namna ya kulimaliza. Nikwa njia hiyo tu, huu mzimu, hili bundi, litaondoka.Mheshimiwa Spika, kutokulitatua suala hili, Barrickatakapokuwepo pale na wananchi watakuwepo pale,manung’uniko yatakuwepo milele. Na kwa vyovyote

vile, hayatakuwa na manufaa kwa mgodi wala kwawananchi. Ikumbukwe, dawa ya deni ni kulilipa. Wakowatu walifanya mambo ya ajabu kule Kenya, miaka ya1800 sasa wanadai fidia.Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, naungamkono hoja hii. Ahsante sana. (Makofi)MHE. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaSpika, nashukuru sana na mimi kuweza kupata nafasikuweza kuchangia hoja katika Wizara hii. Kwanzakabisa, napenda kuipongeza Wizara na uongozi wakewote kwa ujumla, kwa namna ambavyo imejiwekeamikakati ya kuweza kuwapunguzia wananchimatatizo.Mheshimiwa Spika, lakini pili, kwa masikitikomakubwa napenda kueleza kwamba, Bunge letu hilina Wabunge wote walioko humu ndani, tumesahaumajukumu yetu ya msingi ambayo tunapaswa humundani, kuja kusimamia Serikali na kutetea hoja zaSerikali, au kuchangia katika hoja za Serikali, ili tuwezekuona ni namna gani tunaweza tukawasaidiawananchi, ambao kwa imani yao kubwawametuchagua kuja kuwatetea na kuwakilishamawazo yao hapa Bungeni.Mheshimiwa Spika, nalisema hili kwa sababu,Bunge hili, limekuwa ni Bunge la kujadili Muongozo,limekuwa ni Bunge la kujadili Taarifa na mambomengineyo yanayohusu Kanuni; sasa tunakuwa kanakwamba, hatukupata Semina wakati tunaingia humu

Bungeni. Kwa kweli, ni aibu, ni vema tukawawakilishavyema wananchi katika kujadili matatizo yao. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini pili, nasikitika sanamaana naogopa wanasema samaki mmoja akioza,huenda wote wakaoza. Sasa ninaogopa hili lisijelikatokea katika Bunge hili, kwa Wabunge wote.(Makofi)Mheshimiwa Spika, kama kweli, hizi tuhumazinazotolewa na wapo Wabunge waliohusika, basiSheria ifuate mkondo wake. Hawa ni sawa na akinaYuda, kama akina Yuda waliomsaliti Yesu. Sasa hawani akina Yuda, wanaowasaliti wananchiwaliowachagua. Wananchi, wamewachagua kwaimani kubwa kabisa kwamba, waje kuwakilishamawazo yao na kuweza kusaidiana katika kuletamaendeleo katika jamii tunazoishi.Lakini sasa, kama kiongozi, maana MheshimiwaMbunge ni Kiongozi; ukirudi Kijijini kule, ni Mheshimiwa,Mheshimiwa, Mheshimiwa, kila unakopita. Sasa kamautakuwa unaitwa Mheshimiwa, Mheshimiwa,utakuwaje Mheshimiwa ambaye, unakubali kabisakweli kweli, kupoteza mwelekeo wako, kupoteza dirayako, kupoteza vision yako uliyowaambia wananchi,unakuja kuchukua rushwa kwa ajili, ya kukwamishamiradi ya maendeleo? (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa kweli, ni aibu, aibu, aibusana. Waliofanya hivyo, kwa kweli, hapa sasa hivinajua nafsi zao zinawasuta. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunakemea rushwa,tunakemea nini. Je, tunategemea kweli, Mkurugenziwa TAKUKURU, Mzee Dkt. Hosea, atafanya kazi yakevizuri kweli? Kama sisi wenyewe Viongozi, ndiotunakuwa vyanzo vya kuchukua rushwa? Kwa kweli, niaibu sana. Wananchi huko kwa kweli, wanapiga simu,wanasikitika mno. Kwa hiyo, ninaomba kabisa katikahilo kwa kweli, ulivalie njuga. (Makofi)Mheshimiwa Spika, napenda niende kwenye hojamoja kwa moja. Napenda kuongelea suala lawachimbaji wadogowadogo. Wachimbajiwadogowadogo wamekuwa wakinyanyasika sana.Wachimbaji wadogowadogo ni masikini, wachimbajiwadogo wadogo hawana vifaa vya kutendea kazi.Katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati,inaonesha kuna pesa na kuna vitu ambavyovinatakiwa kupewa hawa wachimbaji wadogowadogo. (Makofi)Sasa sielewi ni utaratibu upi kwa sababu, hataBajeti ya mwaka jana ilisomeka hivyo hivyo, lakini hivininavyoongea wachimbaji wadogowadogo, hasawanaotoka eneo la Mpanda, Ibindi, Machimboni,Katesunga, hawajapata vifaa hivi hata siku moja.Sasa ninaomba, katika majumuisho yako MheshimiwaWaziri, uwaeleze wananchi wa Ibindi, Katesunga,Machimboni, Magamba, ni namna gani wanawezawakapata hiyo mikopo na ni namna gani wanawezakupata vifaa hivyo vya kutendea kazi.Mheshimiwa Spika, lakini lingine napendakuongelea kuhusu hili suala la mrahaba wa 4%.

Napendekeza, hii pesa ya mrahaba, itengewe akauntiyake maalum, ili iweze kuelekezwa hasa katika kutatuamatatizo ya jamii, kwa mfano, ikaelekezwa kwenyemashule, ikaelekezwa mahospitalini ambako ndiko sisiwote tunakotegemea kwamba, bila kurekebisha afya,ina maana kwamba, huyu mtu hataweza kufanya kaziyake vizuri, hataweza kujiletea maendeleo. Kamahatutaweza kuboresha shule zetu vizuri ni wazi kabisakwamba, hatutakuwa na product nzuri hapobaadaye. Kwa hiyo, ninaomba hii pesa kamainawezekana ikatengewa akaunti yake maalum, iliiweze kujulikana inafanya kazi gani hasa katika kuletamaendeleo kwa jamii.Mheshimiwa Spika, lakini lingine katika hilohilo,Mheshimiwa aliyetoka kuzungumza, ameongeleakwamba, kuna makampuni ambayo yanagomakulipa. Inakuwaje kampuni imekuja hapa, ikasainimkataba, leo Serikali, inaiambia ifanye hivi, inakataaand then mnaanza negotiation? Sheria ziko wapi?Makampuni kama haya yanayokataa kushiriki katikashughuli kama hizo ama kama mmejiwekea mkatabani wazi kwamba, hafai aondoke, hakuna sababu yakumbembeleza mtu, madini yetu hayaozi. Kwa hiyo,tunaomba kabisa kama mtu anashindwa ku-complyna Sheria za nchi na mikataba hiyo mnayoiweka, kamani mizuri kama ni mibovu, basi muipitie upya ili kila kitukijulikane na huyo anayekataa atoke. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naongelea suala la malipo yaleseni kwa wenye viwanja vidogo, ambao niwachimbaji wadogowadogo. Hivi karibuni nimekuwanikisikia kwamba, kuna Waraka umeandaliwa kwa ajili

ya kupandishwa kodi ya leseni kwa wachimbajikutokana na eneo alilonalo. Kodi hii ilianza, ilikuwakama 80,000/= ikapandishwa ikaja kama laki moja nakidogo, ikapanda tena ikawa kama laki mbili.Sasa hivi, inasemekana kwamba, watalipa milionimoja kwa mwaka. Sasa huyu mchimbaji mdogoambaye hujamwezesha katika vifaa vya kuchimbia,vifaa vya kjutafutia yale madini. Atapataje hiyo milionimoja, ili aweze kulipia ile leseni yake? Hii si njama yakutaka kuwanyang’anya viwanja vyao? Kamandivyo, je, mnafanyaje kuhusu hilo?Kwa kweli, katika kodi hiyo, naomba muangalieupya na muangalie ni namna gani, huyu mchimbajimdogomdogo mtakavyoweza kumsaidia.Mheshimiwa Spika, katika hilohilo la leseni,kumekuwa na makundi nimeongelea sana hili. Baadhiya wafanyabiashara, ambao ni investors, wanakujamoja kwa moja Wizarani, mnawapatia leseni kwakuangalia ramani. Mnasema hapa Katesunga hapa,Mpanda, kuna hii plot, unampatia yule mtu leseni,anakwenda kule. Anafika kule kwa Afisa Madini,anamwambia leseni yangu ni hii. Kwa kweli, tunatakasasa, leseni zote zianzie kwa wananchi kule chini na sikutoka Wizarani kwenda kule kwa wananchi. Hii yote nikujaribu kuleta migogoro na kuwafukuza wananchikatika maeneo yao, ili muwape hao investors, wakatiwao ndio wamezaliwa katika hayo maeneo na wanahaki kabisa ya kuendelea kuchimba katika yalemaeneo. Suala la msingi ni kuwawezesha, kuwapavifaa, ili waweze kujiongezea vipato.

Mheshimiwa Spika, suala la nguzo za kusambazaumeme. Kwa kweli, kama tutamwambia mwananchialipie nguzo, kutoka point moja kwenda nyingine,tunamwonea. TANESCO ilifanye hili suala yenyewe,TANESCO inajiendesha kibiashara, mwananchi huyokila mwezi analipia umeme, sasa ni kwa nini napokutoa nguzo kutoka pale kuileta hapa, mnamwambiamtu ailipie, kazi ya TANESCO ni nini? Sisi tunasematunataka mwananchi awe na maisha bora? (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba hilo nalolizingatiwe na liangaliwe upya namna ambavyotunaweza tukampunguzia mwananchi wa kawaida,gharama za kuvuta umeme, ili aweze na yeye kuwa naumeme nyumbani kwake, kwani tunaelewa faida zaumeme katika kujiletea maisha bora. Kwa hiyo, nivema hasa wananchi wa vijijini, tukawafikiria marambili.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,napenda kuunga mkono hoja. (Makofi)MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika,naomba nichukue fursa hii kukushukuru sana kwakunipa na mimi nafasi kuchangia mchango huu.Naomba niwapongeze Mheshimiwa Waziri na ManaibuWaziri na Katibu Mkuu na Maafisa wote wa Wizara hii,kwa kufanya kazi yao vizuri na kuandaa vizuri Bajetiyao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wabunge wengi,wamezungumzia hapa kwa uchungu mambo mengi,Wataalamu wa kutumbua majipu ya majungu ya siasawametumbua vyakutosha. Lakini jambo hili, wengiwamelizungumza katika hotuba hii ya Waziri, lakinilazima tulitafutie wakati kwa sababu, limedhalilishasana Bunge letu, jambo hili. (Makofi)Mheshimiwa Spika, na kwa mujibu wa Kanuni ya53 (2), kinasema, naomba kunukuu: “Bila kuathirimasharti ya Katiba na ya Kanuni hizi, Waziri auMbunge mwingine, anaweza kutoa hoja nakupendekeza kwamba, suala lolote lijadiliwe Bungenina hoja hiyo, itaamuliwa kwa mujibu wa masharti yaKanuni hizi.”Mheshimiwa Spika, naomba Wabunge wenzangumniunge mkono, kwamba, nitoe Hoja, baada yaBunge, utafutwe wakati muafaka, tulijadili suala hili, ilikama tuamue waliohusika wachukuliwe hatua auKamati ivunjwe au iendelee kama ilivyo, kwa mudamuafaka. Naomba kutoa Hoja. (Makofi/Kicheko)MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika,naafikiki.(Hoja ilitolewa iamuliwe)SPIKA: Waheshimiwa, naomba niwaambieni, huyuanachangia hoja, hajatoa hoja. Mheshimiwa VitaKawawa, huo siyo utaratibu… (Makofi/Kicheko)

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika,naomba kuendelea baada ya kuungwa mkono.SPIKA: Naomba munisikilize basi. Sasa hivi,unachangia tu, utaratibu wa kutoa hoja hauko hivyo.Kwa hiyo, tunaendelea. Endelea kuchangia.(Makofi/Kicheko)MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana. Nawashukuru Wabunge wote,waliounga mkono hoja yangu. (Makofi/Kicheko)Mheshimiwa Spika, naomba niendelee kwakutoa shukrani sana kwa Serikali. Kamailivyozungumzwa katika Hotuba ya Bajeti, umeme wajenereta katika Wilaya yetu ya Namtumbo natunategemea wakati wowote umeme huo utaanza.Mheshimiwa Spika, lakini pia, jenereta lilewalituambia ni la muda. Tunategemea umeme wagridi, ambao utaunganishwa kutoka Makambako.Lakini, katika umeme huo naishukuru sana Serikali,ulikuwa umeme wa KV 132, lakini nimefanya mapitio nasasa kuna makaa ya mawe Ngaka, ambayoyanategemea kuzalisha mpaka Mega Watts 400. Kwahiyo, wameona waweke msongo wa Kilo Volt 220.Tunaishukuru sana Serikali kwa kufanya maamuzihayo.Mheshimiwa Spika, tunaiomba Serikali, sasa. Kwakuwa, Namtumbo ulikuwa unakuja umeme wa gridi,baada ya kuwa umeshafika Songea, wa msongo waKilo Volt 33, tunaomba nao uongezwe transmission

yake kwa sababu, kutakuwa na mradi wa uraniambao peke yake tu, utahitaji matumizi ya more than20 Mega Watts za umeme. Kwa hiyo, tunaombanayo Serikali iongeze uwezo wa msongo huoutakaokuja Namtumbo.Mheshimiwa Spika, Waziri, ametueleza hapamakaa ya mawe ya Ngaka na kampuni ile ambayoinategemewa kuzalisha umeme wa makaa ya mawewa Mega Watts 400, ambayo wataanzia kwa MegaWatts 200, yenye thamani kwa kuanzia dola zamarekani 400.Sasa nilikuwa nataka kujua pia kwa Wizarainvestment hii ya dola 400 pia imechanganya natransmission line kuja mpaka Songea, au laah na kamasivyo tunaomba Serikali mpango wake ukoje wakuweka Bajeti ya kuweka transmission line?Kama hawa wenzetu ambao ni wawekezajiwatawekeza dola hizo milioni 400 kwa kuwekamtambo wa kuzalisha umeme sisi kama Serikalitumejipangaje kuweka fedha za kuweka transmissionline mpaka kutawanya na distribution line katika wilayaya Mbinga Songea, Namtumbo na Tunduru, tunaombaSerikali Waziri anapokuja kujumuisha aje atuelezempango huo ukoje.Mheshimiwa Spika, lingine nilikuwa natakakuzungumza nchi yetu tuna miradi mikubwa hii ya gesiinayokuja na yurani. Sasa nilikuwa nataka tujiulize natutafute majibu tumejiandaa vipi kusomesha vijanawetu zaidi watakaofanya kazi moja kwa moja katika

kazi ya usimamizi wa kitaalam katika machimbo nausafirishaji wa yurani, tumejiandaa vipi tunaombaWaziri aje atueleze na tuangalie pia wataalamtulionao.Lakini pia tumejiandaa vipi kusomesha zaidiwataalam wa kusimamia uzalishaji wa gesi asiliakusimamia mitambo yake vituo vya usafirishaji, na piausambazaji katika mtandao wa gesi katika vituo namajumbani.Tumesomesha vipi vijana wetu na je, tuna data zawataalam wangapi wa Kitanzania tulionao nchinikatika sekta hii na walio nje, na je, sasa hivi kwa miradihii mikubwa wataalam hao watatutosha katika kipindihiki tulichonacho?Lazima tufanye kazi hiyo kwa nguvu zotetumeanza lakini pia tuongeze nguvu kwa harakatuwapeleke vijana wetu katika nchi ambazo zenyevyuo zoefu za kusomesha wataalam wa gesi na yuraniili waweze sisi tusijekuwa watazamaji tu, tuwezekufanya kazi hiyo sisi wenyewe hapa nchini naWatanzania vijana wetu waweze kufanya kazi hiyo.(Makofi)Mheshimiwa Spika, awamu ya kwanza yamwalimu Nyerere tulipopata uhuru ilikuwa hainawasomi hata kidogo, lakini wao waliamua kwamakusudi kabisa ku-invest kwenye human capitalwalisomesha sana, mpaka leo tunao wakina Prof.Mhongo leo tunampigia makofi na sifa zote. (Makofi)

Kwa hiyo na sisi lazima tufanye maamuzi yamakusudi ya kusomesha vijana wetu hawa, lazima kwasababu ya hali halisi tuliyonayo na teknolojia tuliyonayosasa hivi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba kufahamu nimesikiakwamba katika haya makampuni ambayoyamegundua gesi hii ujazo wa cubic feet trillion 25mpaka 28 ni kwamba wana lessen walikuwa na lessenau wana lessen za pamoja za utafiti na uchimbaji kwaajili ya kwenda sokoni. Kwa sheria ile ya mwaka 1980nasema hivyo kwanini sheria ya uchimbaji gesi namafuta kama ni hivyo je, kwa sera na sheriatunayotaka kuitunga sasa hivi ya gesi makampuni hayayatahusika kwa sheria hii mpya na gesi auwataendelea na sheria ile ya zamani ya mwaka 1980.Na kama wataendelea na sheria ile ya mwaka 1980itakuwa ni kifo kingine cha kwetu kwenye madini haya.(Makofi)Naomba sana tufahamu hili Mheshimiwa Wazirianapokuja kwamba je, au tutaanza ku-negotiate naokama tulivyoanza ku-negotiate nao kama tulivyoanzaku-negotiate na wale wanaochimba madini yadhahabu. Wana mikataba ipi kwamba tutakapotungasera na sheria hii mpya na wao watakuwa ndani yakeau watasimamia ile sheria ya zamani. Tunaomba sanaMheshimiwa Waziri anapokuja atueleze hivyo, tusianzetena kulumbana na kama tulivyokosea katikamikataba ya nyuma.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nataka kumwungamkono Mheshimiwa Zungu juzi alizungumza kuhusianana mradi wa gesi kuweka kwenye stock market hasawa bomba hili, ili wananchi na wao wawezekuchangia, hili ni suala jema sana tukiwezeshawananchi kuwa na share katika mtandao wa bombala gesi basi pia tunawezesha pia mapato kwa Serikali.Naomba hii mtandao wa gesi tufikirie pia bombahili kuwa public entity Watanzania wenyewe wawezekuwa na share angalau asilimia 60, Serikali asilimia 30,lakini mtu yeyote wa nje asilimia zao zisizidi kumitunaomba sana hili Serikali iweze kulifikiria. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nilikuwa na mchango wanguni huo lakini naomba ufikirie ile hoja ili niweze kuungamkono ili tuweze kulifanyia kazi ahsante sana. (Makofi)SPIKA: Usije ukafikiria ulikuwa na hoja soma kanuniya 54 na 55 ndiyo inakupa ruhusu wewe kuleta hoja.Sasa nitamwita Said Mussa Zuberi na MheshimiwaWambura ajiandae kwa sababu hawa ndiyowachangiaji wa kwanza. Mwongozo wa Spika kuhusunini.MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA: MheshimiwaSpika, nimesimama kwa mujibu wa kanuni ya 68(7)nikitaka kuomba mwongozo wako kuhusiana na jambolilitokea hapo awali, wakati Mheshimiwa Ezekiel Maigeakichangia na hata aliyemfuatia Dkt. PudencianaKikwembe akichangia walisema kwamba migodi hailipiushuru wa huduma.

Lakini ninavyofahamu mimi kwa mujibu wa sheriailiyotengeneza Halmashauri ya mwaka 1982 sherianamba saba na ile sheria ya fedha za Halmashauri yamwaka 1982 namba tisa ambazo zote zinatoaprecedence kwa Halmashauri kukusanya ushuru wahuduma kwenye Business Enterprises ambazo zikokwenye maeneo husika. Mikataba ya midini imekujakuingia miaka ya 90 na kuendelea…SPIKA: Usijadili Mwongozo hatujadili kwa sababuunajadili sasa nataka mwongozo siyo kujadili.MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA: Sasamwongozo wangu ni kwamba sheria zilitungwa miakaya mwanzoni ya 80 mikataba ya madini imekujakusainiwa baadaye sheria zikiwepo na zikitaka Serikaliyaani Halmashauri husika zikusanye ushuru wa huduma.Sasa mwongozo wangu ni kwamba naombaunipe mwongozo kama sheria mama ambayoilitungwa tena kabla ya mikataba kusainiwa inawezaikawa over redden na mkataba tu ambao umesainiwabaina ya pande hizi mbili. Huo ndiyo mwongozo ninaoutaka kwako Mheshimiwa Spika. (Makofi)MHE. SAIDI MUSSA ZUBERI: Mheshimiwa Spika,kwanza kabisa nimshukuru Mwenyezi Mungu kwakunijalia uzima na afya njema, la pili ni kuunga mkonohoja asilimia mia moja. (Makofi)

Tatu niwapongeze Waziri pamoja na Manaibuwake wawili na Katibu wake Mkuu niwaambie you aredoing well carry on. (Makofi)Nimpongeze tena Waziri na Wizara yake kwautandikaji wa bomba la gesi kuelekea kule kwetuZanzibar. Tunaomba hili suala lifanyike ikiwezekanaharaka iwezekanavyo ili na sisi tuweze kupata matundahaya.Mheshimiwa Spika, nije moja kwa moja kwenyesuala la sakata la umeme, uwezo wa TANESCO naumeme ambao kwamba tunaupata. Totally capacityni megawatt 1,327, kama ile mitambo inafanya kazisawasawa. Matumizi yetu ni megawatt 800 ili tuwe namgao tunatakiwa chini ya 800 yaani 600 na kuendelea.Kwa maana hiyo kama alivyosema Waziri kwambahakuna sababu ya Tanzania kuwa na mgao waumeme, hili mimi nimelikubali kufuatana na takwimuzinavyoonyesha. Sasa tunachotakiwa tujiulize kwaninikipindi hicho cha nyuma tulikuwa na tatizo hili. (Makofi)Nashukuru sasa hivi tuna mwezi wa pili tangukuingia hawa hali imekuwa nzuri isipokuwa hali yahewa ilitaka kuchafuka kidogo tu. Lakini tunamshukuruMungu kwamba bado tunaendelea vizuri kwa sababuvyombo vya habari vilishaanza kuandika kwambamgao unakuja lakini vyombo hivyo vikaweka mambosawa kwamba hakuna mgao. (Makofi)Mheshimiwa Spika, sasa mimi nilikuwa natakaniende moja kwa moja kwenye haya masuala ya

uhujumu uchumi, hii inaonekana dhahiri kwambakatika Taifa letu tuna wadudu sijui tuwaite mchwa auwatu wa aina gani ambao hawa kazi yao waokuharibu kila kinachotengenezwa kwa maslahi yao.(Makofi)Wamewaweka wananchi katika hali ya unyongekatika muda mkubwa sana uliopita, hawa ni watuwachache na mimi niwashauri tu wananchi kwa kuwasasa hivi tuko kwenye suala la Katiba basi ni wakatimuafaka baada ya kuzungumzia vizuri suala laMuungano na Serikali mbili basi wasisahau kuwekasheria ipitishwe sheria ya kuhakikisha hawa watuwahujumu uchumi tunatakiwa sasa tuwaue tena kwarisasi. (Makofi)Wapitishe na nafasi hiyo wananchi wanayo wakatindiyo huu, hatuna muda mwingine na lazima twendekufuatana na hali za nyakati, wakati wa mwalimuNyerere umeshapita, wakati ule ilikuwa watuwakiambiwa tu kwa maneno wanasikia lakini sasa hiviwatu wanaambiwa walikuwa wakiambiwa kwenyemaandamano mpaka wanapelekewa washawashapamoja na mabomu sasa tujue kwamba haliimeshabadilika lazima tuwe na sheria ya uhakikakwamba hawa wanapigwa risasi na zile risasiwanazinunua. (Makofi)Kama hilo haliwezekani kama ni kitanzi basi hiyokambana ya kunyongewa nao wanainunua nawafanyaji wa kazi hizo wanawalipa na fedha wanazowamezichukua fedha nyingi fedha za kufanyia hivyozipo. Mimi naona wakati umefika na wala tusije

tukashawishiwa sijui wakaja Amnesty International hakisijui za binadamu haki za nani wasije wakatusumbuahawa. (Makofi)Juzi hapa Waziri wa Mambo ya Nje alisimama palena akazungumza kuhusu suala la ushoga, ulimwengumzima umesikia au mabwana wakubwa ambao kamawanasema wanaongoza ulimwengu wamesikiakwamba hatulitaki na tumesema kwamba tutafungamikanda kuhakikisha kwamba hili jambo lisifanyike hukukwetu hata kama watatuzuilia misaada. (Makofi)Basi na hili tuje tuwaambie kufuatana na halitunayokwenda nayo na nyakati tulizonazo sasa hivitunastahiki kuwa na sheria hii ya kuua waambiwe navigezo vipo na kama watashindwa kuwaeleza miminitawaambia kwa sababu hawa ni wahujumu uchumimimi nasema moja kwa moja wao wenyewe ni wauajiau kwa kuwa hawaandikwi kwenye magazeti? Waowenyewe ni mauaji.Sasa mimi naona labda nitoe rai tu kwamba niwakati sasa wa kukusanya data na kuwaelekezakwamba sasa tunakwenda tunakuelezeni kwaninitunazungumza hivi unapozimwa umeme labda kwamasaa mawili tu au matatu hasara gani na watuwangapi wanapoteza maisha kwenye nchi hii au kwakuwa magazeti hayaandiki? (Makofi)Kuna watu wanakuwa wako kwenye mashine kuleMuhimbili, umeme unapozimwa watu wanakufa kulekwa kuwa hawaandikwi kwenye vyombo vya habari,kuna dawa zinazohitajika zipate aidha joto la wastani

au baridi ya wastani zisitetereke, umeme ukizimwazinakosekana ina maana kuna watu wanapatainjection au vipi kwa kufikiriafikiria kwamba labdazimeharibika au hazijaaribika na kuna nyinginezinaharibika kabisa.Umeme huu unapozimwa viwanda vina collapse,kuna kuwa hakuna ajira na wanaofanya kaziviwandani ni watu wa hali ya chini, kipato chaokinatetereka na kinapotetereka kipato chao hatanyumba zao zinatetereka na kusababisha watotoaliokuwa nao kuanza kuwa na utapiamlo, watoto naowanakufa hawa. (Makofi)Wapewe data kama hizi waambiwe halafu sasawatueleze na nahakika wakiambiwa wanawezawakasema hao watu wa haki za binadamu wakisemakweli kumbe sasa kuna lazima ya kuweka sheria hii kwasababu wanakufa wengi na wala hatujamalizia hapo.Huo umeme wenyewe unapozimwa ukienda kama Dares Salaam pamekaa kama kwenye hekalu la mfalmenani huyu…MBUNGE FULANI: Solomoni.MHE. SAIDI MUSSA ZUBERI:Anakuwa urooo!Unasikia ni mivumo ni noise (makelele) yanakuwamengi, kiasi kwamba hata watu nao wanatakakupokea simu mjini pale unatafuta uchochoro wapiujifiche kwa ajili ya yale majenereta.

Sasa tutizame nao masuala ya mazingirayanavyoharibika na wakisemwa watu wa palewakapimwe wale wote wale wameathirika na umemewa majenereta wao, au kwa kuwa haziwekwi takwimuhizi, mimi naona ni afadhali kuepusha kuuwa maelfu yawatu lakini tukawauwa watu wasizidi 200. (Makofi)Halafu hawa watakaa sawa hawa, tukianza naowatano kumi mpaka kumi na tano basin chi hii itatuliana inawezekana ikarudia kule kule kwa mwalimuNyerere. Lakini sasa hivi wanachezea tu sheria kwasababu wanajua tena sio wao tu peke yao na zamanihawa mwalimu Nyerere hawa aliwaita wahujumuuchumi, baadaye wakaitwa maghabacholi halafuwakaitwa mafisadi, au sasa hivi tuwaite mafia, kwasababu sasa hivi wana dalili zote walishakuja mpakahumu Bungeni ni mafia hawa. Wanataka sasa hivimpaka kuturubuni mpaka Wabunge walishafikaBungeni sasa hawa ni mafia hawa kitu ambachokwamba wao hawajakifanya sasa jamani badotuendelee tu kukaa nao basi mimi naishauri kamaSerikali tunapoweka sheria hiyo tusiwaandike kwenyemagazeti, wakifikia wakati wa hukumu tunawahukumutu kisailensa hivyo hivyo kwa sababu wao wenyewe nisailensa killer hawa tunawauwa tu tusiwaeleze.(Makofi/Kicheko)SPIKA: Mhh!MHE. SAID MUSSA ZUBERI: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge naomba pianiwatambue wageni waliopo hapa ndani kwanzakabisa ni wageni wa Mheshimiwa Samuel Sitta, Waziriwa Afrika Mashariki, ambao ni Waheshimiwa Madiwaniyuko Mheshimiwa Jafari Kanikila, yuko MheshimiwaDiwani Ahmed Mohamed, huyu siyo diwani huyu nihakimu Nduguta ambaye ni mgunduzi wa dhahabuUrambo, karibu sana na tumefurahi kuwaoneni.(Makofi)Tuna wageni wengine wa Mheshimiwa StephenMasele Naibu Waziri wa Nishati na Madini, kutokaShinyanga Mjini, ambao ni Waheshimiwa Madiwanikutoka Manispaa ya Shinyanga wanaoongozwa naKatibu wao Mheshimiwa Shella Mashaneti,Waheshimiwa Madiwani karibuni sana. (Makofi)Tuna wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chamacha Mapinduzi wilaya na sekretarieti ya wilayawakiongozwa na Mwenyekiti Ndugu Alhaji Salum hukohuko Shinyanga nadhani karibuni. Kuna afisa Elimumanispaa ya Shinyanga Honorata Yuhubikaameambatana na Kamati ya shule maalum Luhachijana wawakilishi wa wanafunzi walemavu, karibuni sana.Wapo na wanafunzi wenye ulemavu, ahsante sanakaribuni sana. (Makofi)Halafu anacho kikundi cha madereva taxi waManispaa ya Shinyanga wakiongozwa na NduguKennedy Nyangi Mwenyekiti wa hawa maderevayuko wapi? Ahsante sana. (Makofi)

Halafu yupo na mjomba wake Masele ambaye niMr. Bonda Kinga na Mrs. Elizabeth Bonda wasimamehawa walipo. (Makofi)Pia ile club ya kulenga shabaha walewanaambiwa kwamba kesho mabasi yataondokatarehe 29 yatakuwepo saa mbili mabasi yakuwachukuwa wale ma-club rangers wale waMakutopora. Kwa hiyo, wale wanachama wakulenga shabaha wa kulenga shabaha basi saa tatumabasi yanaondoka yatakuwepo saa mbili hapa. Nakama mnalenga shabaha basi msichelewa.Waheshimiwa sasa namwita MheshimiwaAnastazia Wambura halafu atafuatiwa heshimiwa Prof.Peter Msolla na Mheshimiwa Naomi Kaihula piaajiandae.MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangiaasubuhi ya leo ili na mimi niweze kutoa mchangowangu katika hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nishati naMadini.Awali ya yote naomba nichukue nafasi hiikumshukuru sana Mwenyezi Mungu ambayeametujaalia uhai kwa sababu ni wengi walipendawaione siku ya leo lakini hawakuweza. Lakini vilevile sikwamba tunastahili sana sisi kuwepo hapa lakiniMwenyezi Mungu ameweza kutujaalia uhai.

Mheshimiwa Spika, nianze kwanza kumpongezaWaziri Mhongo ambaye ni Waziri wetu wa Nishati naMadini, Manaibu Waziri Simbachawene pamoja naMheshimiwa Masele pamoja na Katibu Mkuu waWizara ya Nishati na Madini kwa kazi nzuri ambayowameifanya katika kipindi kifupi sana cha kuwepokwao katika nyadhifa zao. Nawapongeza sana.(Makofi)Lakini pamoja na pongezi hizi kuna salamu zapekee kabisa kutoka Mkoa wa Mtwara. Salam hizi nishukrani kwa mambo makubwa matatu, kwanza niuzinduzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kupitiaSongosongo kuja Dar Es Salaam lakini vilevilewanashukuru sana kwa mgao wa Transformer 37ambazo zitapelekwa katika Wilaya za Mkoa waMtwara yaani Wilaya ya Nanyumbu ambayo ilikuwahaina umeme kabisa, Wilaya ya Tandahimba, Masasi,Newala, Mtwara Vijijijini pamoja na Mtwara.Wanashukuru sana kwa hilo lakini vilevile wanashukurusana kwa kuhakikisha kwamba sasa hivi TANESCOimeboresha miundombinu ya Umeme na kwambajambo hili limepelekea sasa umeme haukatikikatikihovyo.Mheshimiwa Spika, tulikuwa na tatizo kubwa sana,Mtwara na Lindi tulikuwa na Umeme wa gesi lakinitatizo kubwa lilikuwa ni kukatika mara kwa marakutokana na miundombinu ambayo ni chakavu.Wananchi wanashukuru sana na wanawaombeabaraka tele kwa Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Spika, uzinduzi wa bomba la gesiulifanyika tarehe 21 Julai, 2012 katika Kata yaMadimba. Lakini ajabu ni kwamba kuna vikundi aukikundi tusema ambacho kimezuka na sasa hivikimeanza kuwarubuni wananchi kwamba waukataehuu mradi.Tulielezwa wazi na ni jambo ambalo ni la ziadaambalo Wizara ililifanya siku hiyo ya kuelimishawananchi kuhusu faida kubwa sana za mradi wabomba la gesi na faida mojawapo ambayo tulielezwani kwamba Serikali itakuwa inaokoa trilioni 1.5 shilingi zaKitanzania kila mwaka na ni dhahiri kwamba hizi pesazitakwenda kusaidia katika sekta ya Nishati, Elimu, Maji,Afya na kadhalika.Lakini sasa kinachoshangaza ni hiki kikundiambacho kinapita kuwarubuni watu wakatae.Ninawaomba sana wananchi wa Mtwara ambaowaliupokea mradi huu kwa mikono miwili nawamekubali kabisa kutoa ushirikiano wao wasikubalikurubuniwa. Naomba kikundi hiki kikiwafikia wasemehatudanganyiki na wakumbuke kwamba mkataapema pabaya panamwita. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kuna faida nyingine ambazotulielezwa kwamba zitakuwepo, mojawapo ni ile yakupunguza gharama za uzalishaji viwandaji kwakutumia umeme wa gesi lakini pia hata magariyatakapokuwa yakitumia nishati ya gesi, gharama zanauli kwa wananchi au kwa abiria zitapungua nanitaafurahi sana kwa hili na ninaomba tu wananchiwatambue kwamba maisha bora ambayo

tunaambiwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi huundiyo mwanzo wake.Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii tenakuipongeza Serikali kwa jitihada ambazo imeonyesha,jitihada za kuondoa kabisa mgao wa umeme katikanchi yetu na tumeona wazi kwa sababu kipindi kamahiki mwaka jana kulikuwa na matatizo makubwa nakulikuwa na mgao mkali sana katika nchi yetu na hiiilipelekea hata kukwamisha Bajeti ya Nishati naMadini.Mheshimiwa Spika, mimi naiomba sana Serikaliyetu ya Chama cha Mapinduzi, chonde chondekwamba ule muda wa kuwafurahisha watu sasaumekwisha na sasa hivi tumebaki na muda wa kuwasurprisewatu na kwa kweli wananchi wanashangaa nawanapiga simu sana wakiuliza hivi ni kweli mgaoutakwisha? Hawaelewi na hawaamini! Kwa hiyo,ninachotarajia ni kwamba hivi karibuni penginetutakuwa na surprise nyingine katika kuhakikishakwamba tunaboresha mapato yanayotokana naNishati na Madini na pia tunapunguza migogoro aukuimaliza kabisa katika maeneo ya migodi. Lakinivilevile tuhakikishe tunaboresha hali za wachimbajiwadogo wadogo. Hizi ndizo surprise ambazotunatakiwa tuwape wananchi wetu.Ninaomba niungane na wenzangu kuwalaaniwale wote ambao hawaitakii nchi yetu mema kwamambo mazuri yanayofanyika, wale ambaowanajitahidi sana kuipeleka nchi yetu katika mwendowa kasi. Kiongozi anapojitahidi kukimbia utashangaa

mmoja anamtega kwa kamba ili kumwangusha. Namimi nachukua nafasi hii kuwalaani sana wanaofanyahivi.Lakini kwa upande wa hili suala ambalo watuwanalilalamikia la kuhusiana na sheria ya manunuzi,naomba kurejea maandiko matakatifu ambayoyanamsimulia Bwana Yesu kipindi kile alipomponyamgonjwa siku ya Sabato na Mafarisayo na Walimu waSheria wakaanza kumtuhumu kwamba amefanya kazisiku ya Sabato. Lakini aliwaeleza yafuatayo naakawaambia kwamba hivi ni nani kati yenu ambayePunda wake atatumbukia shimoni siku ya Sabatoasiweze kumtoa eti kwa sababu tu ni siku ya Sabato?Ni kengele ya pili?SPIKA: Ya kwanza!MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika,hiki kitendo ambacho viongozi wetu wa Wizarawamekifanya cha kuwasaidia wananchi wetukuondokana na giza bila kuitisha tender, miminikifananishe na kitendo cha kumponya mgonjwa sikuya Sabato na pia kitendo cha kumwokoa Punda sikuya Sabato. Kwa kweli hawana makosa na ninaombatuwaunge mkono kwa nguvu zote. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kabla sijamalizia mimi niiombeSerikali iangalie mambo yafuatayo kupitia Wizara yaNishati na Madini. Kuna tatizo kubwa sana la bilibandia kwa wananchi, wananchi wengiwanapelekewa bili ambazo si halisi ni kubwa kuliko

matumizi. Naomba sana Serikali ilifuatilie hili iliwananchi waweze kulipa kulingana na walichotumia.Lakini kingine ni kwamba hili wimbi la vifaa bandiavya umeme ambavyo vimezagaa zagaa madukanivinapelekea mioto na hasara kubwa….MBUNGE FULANI: Ni moto!MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika,nasikia ni moto na siyo mioto.Moto na hasara kubwa kwa wananchi wetu nakinaturudisha nyuma sana kimaendeleo, naombaSerikali au Wizara ishirikiane na TBS ili kusudi kuwezakudhibiti matatizo haya ya vifaa bandia vya umeme.Mheshimiwa Spika, jambo la tatu ambalonaliomba ni umeme unaotolewa wakati mwingine nahata juzi nadhani tumeona hapa, umeme ulikatika natukaahirisha Bunge, sijui sababu ilikuwa ni nini lakinikuna maeneo ambayo nyumba moja utaona nyingineina umeme na nyingine haina. Lakini kumbe uwezo wazile mita ni tofauti na umeme unaopelekwa pale nikidogo kwa hiyo, naomba sana TANESCO wanaposupplyumeme wa-supply umeme ambao unatosha.(Makofi)Mheshimiwa Spika, tatizo lingine ni la uzembe kwawafanyakazi wa TANESCO. Mara nyingi zinakuwazikitokea hitilafu lakini wanapoitwa wafanyakazi waTANESCO wanakuwa ni wazito sana na utakutayanatokea maafa bila sababu yoyote.

Mheshimiwa Spika, kabla sijamalizia naombanichukue nafasi hii kuwashukuru sana wanawake waMtwara kwa kuniunga mkono siku zote na kushirikianana mimi.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja naahsante.SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Peter Msolaatafuatiwa na Mheshimiwa Naomi Mwakyoma Kaihulana Mheshimiwa Mikidadi ajiandae.MHE. PROF. PETER M. MSOLLA: Mheshimiwa Spika,kwa niaba ya wananchi wa Kilolo kwanza napendanitoe shukrani zangu za dhati kwako wewe mwenyewekwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia hoja hiiiliyowasilishwa jana na hoja ambayo ni muhimu sanakwa uchumi wa nchi yetu.Pili, napenda kuwapongeza sana MheshimiwaWaziri, Manaibu Waziri, Katibu Mkuu, Wakurugenzi wotebila kumsahau Dkt. Mwakahesya wa REA ambaye sisiwatu wa Kilolo kwa kweli tumenufaika sana na kaziambazo amezifanya.Tatu, napenda kuipongeza sana Wizara kwakupunguza gharama za kuunganisha umeme ambayoilikuwa ni tatizo kubwa kwa watu wengi sana.Gharama za kuunganisha umeme kwa kweli zilianziajuu sana zilikuwa zaidi ya shiilngi 700,000/= na hatimayezikaja shilingi 455,000/= na kwenye hotuba ya juzi kwa

vijijini kwamba gharama hizi sasa zimepunguzwa hadikufikia shilingi 177,000/=.Tunaipongeza sana Wizara kwa sababu hiiitawezesha watu wengi na hasa walio vijijini ambao nimaskini kuunganishiwa umeme ikizingatiwa kwam basehemu nyingine hata kuni sasa hivi hazipatikanikutokana na kuharibika kwa mazingira. Hii ni nyenzonzuri kwa utunzaji wa mazingira lakini vilevile kwakuwawezesha wananchi walio wengi ili wawezekupata nishati ya uhakika.Punguzo hilo kama mlivyoanzia juu kutokashilingi 700,000/= mpaka shilingi 455,000/= na baadayeshilingi 177,000/= ni matarajio yangu kwambamtaendelea kuliangalia jambo hili na kuzidi kupunguzaili kusudi watu wengi zaidi waweze kunufaika kwasababu hata hiyo shilingi 177,000/= kwa vijijini bado nigharama kubwa.Katika maeneo ya sehemu za Kilolo watu wengisana walipoona umeme umefika wamejiandikisha.Maeneo waliyojiandikisha ni Ruaha Mbuyuni,Mtandika, Mahenge na sehemu nyingine mbalimbalilakini tatizo lao limekuwa ni uwezekano wa kuwezakulipa hiyo gharama kubwa ambayo ilikuwepo awalikabla ya kutangaza tangazo hili juzi na ndiyo maananasema kwamba tuendelee kuangalia hili ili kusudituweze kuendelea kupunguza gharama za kuwafikishiaumeme wananchi walio wengi sehemu za vijijini.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana tulipitishampango wa maendeleo wa miaka mitano kamasehemu ya Tanzania Development Division 2025 nalengo kubwa la mpango wa miaka mitano mwaka2011/2012 hadi mwaka 2015/2016 ilikuwa ni kuwekajitihada za makusudi za kukuza uchumi ili hatimayetufikapo mwaka 2025 Tanzania iwe ni nchi yenyeuchumi wa kati na iondokane na kutegemea uchumiwa kilimo na badala yake itegemee zaidi viwandayaani a shift from an agriculture based economy to anindustrial based economy na hivi ndiyo nchi nyingizilivyofanya, hazikukwepa kilimo lakini hatimayewakaingia kwenye viwanda vidogovidogo nabaadaye vikubwa na uchumi wa nchi ukaendelea.Lakini hili liliwezekana tu pale ambapo walikuwana nishati ya kuaminika na kwa kufuatana namwenendo tunaokwenda nao inawezekana kwambanishati inaanza kuwa ya kuaminika na kamatulivyohakikishiwa na Mheshimiwa Waziri kwambamambo ya kukatakata umeme sasa yatakuwa nihistoria. Kwa hiyo, hii sasa ni fursa ya sisi kukuzaviwanda vyetu. Tuanze na viwanda vidogovidogo vyakusindika mazao yetu ili kuongeza thamani nahatimaye tuweze kupata masoko mazuri.Najua tuliwahi kufanya semina na Wizara katikaukumbi wa Pius Msekwa juu ya Power System MasterPlan ya nchi hii, mengi yalizungumzwa. Lakini miminingeomba Wizara ipitie tena hii Power System MasterPlan ili kusudi waweze kuona ni namna gani wanawezakuiboresha ili kusudi tuweze kuwa na umeme au nishatiya kuaminika kwa muda wote. (Makofi)

Tuna vyanzo vingi sana sana lakini hatujavitumiavizuri, ni matarajio yangu kwamba hii Power SystemMaster Plan na itakuwa vizuri kama WaheshimiwaWabunge ambao wanazungumza na wananchiwengi waweze kupata nakala hiyo ili kusudi wawezekujua ni nini nchi yetu inajitahidi kufanya ili kuboreshanishati katika nchi yetu.Mheshimiwa Spika, napenda sasa nirejee kwenyeJimbo langu la Kilolo, kwanza nishukuru kwa jitihadakubwa zilizofanywa na Wizara hii kwa kutupatiaumeme katika baadhi ya maeneo.Mwaka 2009 umeme ulivutwa kutoka IringaTagamenta ukapelekwa Kilolo na hatimaye kufikampaka Kidabaga na umeme huu ulizinduliwa naMheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya M. Kikwete tarehe27 Oktoba, 2009. Toka wakati huo umeme huuumepita katika vijiji saba na shule za sekondari tatu bilakushushwa na watu hawajanufaika bado, ukianzia kijijicha Ihimbo, Utengule, Luganga Kibaoni, Luganga,Lulanzi, Lusinga, Ilamba, Maria Consolata SecondarySchool, Udzungwa Secondary School, na DabagaSecondary School, wote hawa wanaziangalia wayazikiwa zimepita juu bila kunufaika nao. (Makofi)Lakini vilevile mwaka 2011/2012 umemeumevutwa kutoka mji mdogo wa Ilula kuelekea RuahaMbuyuni mpakani na Morogoro. Umeme huu tokaumevutwa umepita Vijiji vya Ikokoto, Kitonga,

Mahenge, Mtandika, Kidika, Ruaha Mbuyuni na jiranikijiji cha Msosa bila wananchi kuweza kunufaika naumeme huo.Ombi langu, baada ya kazi kubwa hii ambayoimefanywa na umeme huu tayari gharama zakuunganisha zimeteremshwa, naomba sasa Wizaraitupie jicho la huruma katika vijiji hivyo ambavyonimevitaja ili vinufaike na umeme huu unaopitakwenye vijiji hivi. Upatikanaji wa umeme huoutahamasisha ujasiriamali na usindikaji wa vyakula namazao mbali mbali. (Makofi)Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayomachache napenda kutamka kwamba naungamkono hoja hii nikiwa na matumaini makubwakwamba watu wa Kilolo watanufaika na mpangouliopo na Bajeti iliyowasilishwa na Wizara hii ya Nishatina Madini. Ahsante sana. (Makofi)SPIKA: Ahsante sana, sasa nitamwita MheshimiwaNaomi Kaihula, atafuatiwa na Mheshimiwa FatumaAbdallah Mikidadi na Mheshimiwa Profesa KulikoyelaKahigi ajiandae.MHE. NAOMI M. KAIHULA: Mheshimiwa Spika naWabunge wote ahsanteni sana.Mimi nina machache ambayo napendakuzungumzia kuhusu hii Bajeti ya Wizara ya Nishatina Madini.

Kwanza kabisa napenda nimshukuru MwenyeziMungu kwamba kweli Mwenyezi Mungu huwa anajibuna majibu yenyewe tumeanza kuyaona hapa hapaduniani kabla ya kufa, kama ambavyo maranyingine nilisema hapa kwamba tunahitajikuombewa na kusudi Mungu atuongoze jinsi yakufanya kazi za wananchi waliotutuma humu Bungeni.Kwa yaliyokuwa yakizungumziwa kuanzia jana naleo naona kabisa mkono wa Mungu upo. Tunaanzakuzungumzia mambo ambayo tunataka na ambayoMungu anataka tufanye kazi ambayo tulipewa nawananchi kwa heshima na taadhima. NamshukuruMungu kwa ajili ya jambo hili.Pia napenda sasa hivi tumekwishaanza kuelewanakwamba Upinzani siyo ugomvi na kwamba Upinzaniupo hapa kwa ajili ya kuwasukuma na kuwachokonoawale watawala, upande mwingine ili waweze kufanyayale mambo ambayo wananchi wanayataka.Nimeona sasa tupo pamoja tunaendelea. Kwa hiyo,napenda niwapongeze pia Wapinzani wotewakiongozwa na Chama cha Demokrasia naMaendeleo, kwamba sasa tunakwenda pamoja.(Makofi)Mheshimiwa Spika, sasa nataka kuchangia katikaBajeti hii. Nina mambo mawili, matatu ambayonilikuwa napenda kuyazungumzia zaidi. Jambo lakwanza moja ambalo pia ningependa kulisisitizianinawapongeza kwa kweli Wizara hii ya Nishati naMadini, uongozi uliochaguliwa mpya na MheshimiwaRais wa Jamhuriu ya Muungano wa Tanzania, Dkt.

Jakaya Mrisho Kikwete, kwa sababu wameonekanakwamba wamekuwa na ujasiri na wakaweza kufanyakazi hiyo. Nawapongeza sana sana kwa hilo.(Makofi)Mheshimiwa Spika, sasa kwa upande wa umemekama mlivyofanya ni kweli tunawashukurummepunguza bei za umeme kwa faida ya wananchi.Lakini pia tungekuwa tunawaomba kwambamngeenda hatua nyingine kubwa zaidi.Baada ya kupunguza hizo bei za kuunganishaumeme majumbani, tulikuwa tunaomba sasa mfikiriesuala la umeme wenyewe upo juu sana, kiasikwamba hata watu wengi wa kawaida wanashindwahata kuutumia umeme wenyewe, na huenda pia ndilolinalopelekea watu wengine wakaanza kujiunganishiaumeme isivyo halali.Kwa hiyo, nilikuwa nawaomba sana mkae chinitena kwa maarifa na hekima kabisa kama mlivyofanyakupunguza bei za kuunganisha umeme majumbanimfanye hili suala muone jinsi ambavyo mtawezakufanya kuweza kuwafikia watumiaji mmoja mmoja nawale wa chini kupunguza hizi bei za umeme. Lakinipia ninawapongeza kwa dhati na ninaomba Munguawabariki kwa hilo mwendelee.Mheshimiwa Spika, ni kwamba TANESCO limekuwaShirika letu na limekuwa na matatizo mengi, na kwakweli katika majadiliano yetu tumeona kwambalimetetereka. Lakini pia kuna jambo nzuri ambaloMungu ametuonyesha kwamba lilikuwa linatetereka

kwa ajili ya mambo ya ufisaidi. Sasa kwa ajili yamambo hayo ya ufisadi ambayo sasa hivi yanaelekeakuwa wazi na yataendelea kuwa wazi. Tulikuwatunaomba hivi Wizara haya mambo ya IPTL kwa kwelisisi watu ambao ni wa kawaida layman hatujaonavizuri, hatujui yameishia wapi, wataendelea kutuibiafedha mpaka lini. Hawa watu wa DOWANS mpakaleo hatujajua wameishia wapi? Mambo ya Richmondhatujaelewa yataishia wapi?Tulikuwa tunaomba kwa vile mmekuwa na hekimamkafanya mambo mazuri mpaka tukafikia hapo tuliposasa. Tunaomba tujulishwe wazi wazi je, DOWANSimeishia wapi, IPTL itaishia wapi, Richmond iliishiawapi? Ili kusudi tuweze kufuatana na nyietunapokwenda kuweka sawasawa suala hili la umemekupitia hawa TANESCO. Hili tunaliomba sanamtusaidie kuweka mikakati mizuri.Mheshimiwa Spika, pamoja na hilo ningependakuzungumzia pia suala nzima la nishati kuhusu gesi.Kweli tunafurahi kuhusu gesi lakini pia badohatujafanya masuala mengi ya msingi, masuala kamaya sera, masuala kama ya sheria hizo. Lakinininachoomba sasa hivi tusiende haraka sana kwambamimi niweke gesi hapa hilo kweli litakuja.Lakini kwanza nilikuwa nafikiri tungeomba hizosera zije. Lakini hizo sera pia Serikali ihakikishie kwambawatu wengi ambao wana experience wameonakatika sehemu nyingine duniani waweze kuchangiakwa uwazi kabisa hata kama ni kuweka kwenyemagazeti, kwenye TV na kadhalika ili watu waletewe

waone ni jinsi gani gesi inaweza ikawa laana ama gesiinaweza kuwa na faida. Baada ya hapo ndiyo tuanzesasa kulizungumzia kama Katiba. Kwa sababu tusifanyemakosa yale yale tuliyofanya kwenye madini.Kwa hiyo, naomba sana tutakapokuja kutungasera ya gesi tuwe wazi, tusiikimbize kimbize na mwishoikawa ni sheria imepita halafu inakuja kutokea kamamasuala ya NSSF na wafanyakazi. Kwa hiyo,tunaomba kwamba sera ya gesi ije haraka na vituvingine ili tuweze kuona jinsi gani tutakwenda mbele.(Makofi)Mheshimiwa Spika, baada ya hapo ningependakuzungumzia suala la lingine la madini. Napata utatasana inasemekana kwamba haya madini karibuni nchinzima yamekwishauzwa. Inasemekana kwambawajanja kama huko walikotoka walikwishajipangiasehemu za madini na wengine wenyeji wa hapa nchinina wengine wakapeana hizo forty percent, au tenpercent. Sasa kama wamekwishapeana auimekwishagawiwa yote na sasa wana leseni zaopengine ni za miaka 90 au 99. Maana yaketunachekesha sana vitu vingine tukianza kufikiri.Sasa tunazungumzia suala la wachimbaji wadogowadogo, hawa wachimbaji wadogo wadogotutawagawia nini na inaelekea kama tunawarubuni tuyaani hatusemi ya ukweli. Kwa sababu kama sehemuzote za madini wanazo watu, wengine wanazo waponje wamekaa, wale wachimbaji wadogowanavyokwenda kule kuchimba anakuja mtu

anasema hii ni sehemu yangu kama kawaidawanawaambia waende mahakamani.Mheshimiwa Spika, lakini tujue kwambaMahakama yenyewe ni watu, mahakama naowanaweza wakala rushwa na mara nyingi wanashindawenye fedha. Tumeona kabisa, sasa hili tutalifanyaje?Naomba hili pia tulifikirie siyo kwa Wizara tu, hata sisitunavyokwenda ku-move tufikirie itafika wakatiambapo itabidi Bunge hili kwa makusudi kabisa liletesheria ya kuvunja hata sheria yake. Kwa sababu kamani hivyo inaelekea kwamba hakutakuwa na ufumbuzikwa sababu vita vitatokea daima milele.Mheshimiwa Spika, kwa sababu wale wachimbajiwakubwa hawatakubali kuachia yale watakimbiliaMahakamani, na wachimbaji wadogo ndiyo nchi yaoMungu aliwapa ardhi yao, madini yao ndivyoambavyo wataishia. Kwa hiyo na wenyewewatakwenda kuchimba lazima sivyo watakuwawanapiga risasi kama walivyokuwa wanaapigwa hukoBulyakhulu na huko mahali pengine. Kwa hiyo, hilisuala pia naomba tuambiwe.Je, inakuwaje ile mikataba iliyowekwa ambayowameng’ang’ania wale wakubwa wenye fedha ilituweze kuweka sawa mtafanya namna gani?Tungependa pia hili tupate jibu na tuone tunaendajenalo.Mheshimiwa Spika, sasa naona kwamba mambomuhimu ambayo nilikuwa nataka kuzungumzia ni hayo.Mwishowe, napenda nizungumze hivi kutokana

kwamba tumepata mafisadi wengi wapo, wenginehumu humu wengine sehemu nyingine.Mimi nilikuwa nasema hivi, kusema kuwauaitakuwa siyo kweli kama tunataka kufanya kwelituwafilisi. Hatua ya kufanya kweli ni kuwafilisi halafumnawatangaza, mkishawafilisi hata watu wenginewataona hawatafanya kile kitendo kwa sababuukiwaachia zile mali wanatumia zile mali kuharibusystem, wanatumia zile zile mali kwa ufisaidi kufanyanini, kwa hiyo mnakuwa hamwendelei.Kwa hiyo, kinachohitajika hapa ambapo wenginetunawafahamu, mnawafahamu na system ipo kwa ajilihiyo ihakikishie inawapata wote na kuwafilisi na hizomali zao kutumika kwa ajili kurekebisha madhara namakosa waliyofanya. Mimi hilo ndilo pendekezo langu.(Makofi)Mheshimiwa Spika, ninashukuru, napendakuwasilisha.SPIKA: Ahsante sana. Sasa nitamwitaMheshimiwa Fatuma Mikidadi na Mheshimiwa Prof.Kahigi ajiandae na Mheshimiwa Josephat Kandege.MHE. FATUMA A. MIKIDADI: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangiamada hii ambayo ipo mezani petu leo. Mimininaungana na wenzangu wote waliosema kwambasuala hili tulichunguze likoje, tupate jibu. Siwezi kurudiatena maneno waliyoyasema, lakini ninasema

ninaungana nao na ninaunga mkono hoja hii mia kwamia.Mheshimiwa Spika, ninaanza na kusema kwambalazima twende na wakati na tusingoje wakatiutubadilishe. Kwa nini niseme hivyo, nimesema hivyokwa sababu Tanzania tumegundua gesi. Sasa kwa ninituendelee kupata tabu wakati Tanzania tumegunduagesi. Hatuwezi kukaa tukangojea masuala ya mvuainyeshe ili tupate umeme. Masuala ya Mtera sasa basigesi imegunduliwa na ndiyo maana nimesema twendena wakati tusingoje wakati utubadilishe.Mheshimiwa Spika, kwa sababu tuna vyanzo vingivya gesi, tuna vyanzo vya nishati, nchi nzima sasatufumbuke, vyanzo vile vya gesi tuanze kuvitumia.Mheshimiwa Spika, tunayo gesi asilia Lindi, tunayogesi asilia Mtwara, tunayo gesi asilia Kinyerezi hivi vyoteni vyanzo vya gesi tu. Si hilo tu tunayo makaa yamawe Kiwira, tunao umeme wa upepo Singida, Makaaya Mawe Ludewa, tunacho Chuma cha Liganga. Hivivyote ni vyanzo vya gesi kwa nini tunakuwa na gizamiaka yote hii? Tangu umeme umeanza mwaka 1908Tanzania ambao uliletwa na Wajerumani mpaka leohatujafika popote kuhusu umeme.Mheshimiwa Spika, tunaomba sana sasa twendena wakati tusingoje wakati utubadilishe tutumie hivivyanzo tulivyokuwa navyo kupata umeme Tanzania.Hilo lilikuwa suala la umeme.

Mheshimiwa Spika, suala la pili, ni suala la madini.Tanzania tunayo madini mengi sana. Kuna Mikoaambayo imepata ufadhili, kuna Mikoa ambayoimepata kuwezeshwa, lakini Mkoa wa Lindihatujawezeshwa, Mkoa wa Lindi nao una madinikadhaa, lakini hatujawezeshwa, kuna wachimbajiwadogo wadogo tu wamejaa lakini Mkoa mzima unamadini. Kila Wilaya ina madini, kwa nini na sisi Mkoawa Lindi hatuwezi kuwezeshwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nikikwambia hapa utashangaaWilaya ambazo zina madini katika Mkoa wa Lindi.Wilaya ya Liwale kuna dhahabu, Wilaya yaNachingwea kuna dhahabu, Wilaya ya Ruangwa kunagreen Tome line, kuna green garnet kuna dhahabuRungwa, lakini wachimbaji hawa hawasaidiwi. Kunarangi mbalimbali za kujengea nyumba zipo Rungwa,lakini hawawezeshwi.Mheshimiwa Spika, siyo hayo tu Lindi yenyewekama Lindi kuna Gypsum, kuna chumvi, kuna gesihatuwezeshwi. Kwa hiyo, naomba ile sera yakuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo Tanzania,naomba ifike Lindi iwasaidie wananchi wa Lindi iliwaweze na wao kunufaika kidogo.Mheshimiwa Spika, lingine madini ya chumvi,madini ya chumvi yasifananishwe na madini ya vito aumadini mbalimbali kama dhahabu, kwa sababuchumvi kama chumvi ambayo inachimbwa Mikoa yoteya Pwani ni chakula. Sasa tunaomba wakulima hawawa chumvi waweze kusaidiwa kwa sababu wanapatashida sana kwanza hawana soko. Pili, wanatozwa bei

kubwa sana ya ushuru. Sasa hivi haijulikani huyumkulima wa chumvi anaenda katika ofisi ya madini auofisi ya kilimo au ofisi ya ardhi yaani yupo yupo tu.Tunaomba sana waliangalie suala la wakulima wachumvi itamkwe kabisa wapo katika Wizara gani,wawajibike katika Wizara gani? Kwa sababu hukuwanaitwa ardhi wamekata mikoko, huku wanaitwaOfisi ya Madini leta fedha, sasa shughuli zimekuwanyingi mpaka watu hawaelewi. Tunaomba shughulizote za madini ziwekwe pamoja, madini ya chumvi ilitujue sasa inahusika na Wizara gani badala ya kuitwahuku na kule.Vilevile watafutiwe soko, chumvi sasa hivi hainasoko, imekaa tu kwenye godown Mtwara, Lindi, Tangana wapi huko naomba sana muwatafutie soko.(Makofi)Mheshimiwa Spika, madini hayo hayo ya chumviinabidi kabla haujayauza uwe umeweka madini joto.Sasa madini joto haya yaliwekwa na Serikali iliwananchi waweze kula ndani ya mwili yao ili kusaidiakuondoa magonjwa mbalimbali. Sasa tunaomba sisihaya madini joto basi Serikali iwawezeshe wakulima wachumvi ili waweze kuyapata bure au ipunguzwe bei yamadini joto. Kwa sababu bei sasa hivi ni aghali mno,haiwezi kununuliwa. Tunaomba mliangalie suala lamadini joto na ushuru mbalimbali upunguzwe katikamadini ya chumvi.Mheshimiwa Spika, TPDC: TPDC walipewa uwezowa kufanya kazi mbalimbali za gesi na kadhalika. Lakinivilevile walipewa kazi kwa ajili ya shughuli za umeme

vijijini. Sasa kwa nini hawafanyi hivyo au wanapatafedha kidogo? Kama walikabidhiwa shughuli zaumeme vijijini basi Serikali iwawezeshe, waongezeweBajeti yao ili wao waweze kuendeleza umeme vijijini.Tunaomba sana Serikali iwaangalie TPDC wawezekupewa msaada zaidi ili waendeleze umeme vijijini.Mheshimiwa Spika, umeme wa grid, umemeambao haupo katika grid kwa maana Mikoa ileambayo haipo katika grid inakuwaje, kwa sababumpaka sasa kuna Mikoa kadhaa ambayo haipo katikaumeme wa grid Tanzania. Tunaomba sana hiyo Mikoaninaijua ipo Kigoma, Rukwa, Ruvuma Kagera, Mtwarana Lindi wanatumia gharama kubwa sana kuwekamafuta kwenye generator. Tunaomba hapa baada yakugundulika umeme wa gesi na wao waingizwe katikagrid.Mimi sikushangaa kwa nini Mkoa wa Lindi naMtwara haupo katika umeme wa grid ni kwa sababuLindi na Mtwara kuna gesi na hao wenzetu ni jiranizetu gesi imeonekana tatizo ni nini? Tunaomba sanamtusaidie ili na sisi tuweze kunufaika. Hilo lilikuwa kuhusuumeme wa grid.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,nimalizie moja tu kwamba, sheria ya marekebishompya ya Nishati, Ibara ya 4(39) ilielekeza kwambabomba likipita katika kijiji fulani basi wananchi walewaweze kupatiwa umeme mpaka sasa sielewi bombahili lililotoka Kilwa kwenda Dar es Salaam hivi vijiji vyakatikati vimepatiwa umeme au bado nataka kupatajibu.

Kwa mfano, kuna Kilwa, kuna Jenga, Somanga,njia nne, Tingi, Nangukuru, Rufiji, Mkuranga naSongosongo penyewe. Tunataka kufahamu ni vijijivingapi tayari vimepatiwa umeme na vingine ni vipiambavyo ni bado na lini sasa hao watapatiwaumeme? Kwa sababu sheria ipo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hilo lilikuwa la mwisho, nasematena kwamba ninaunga mkono hoja mia kwa mia,mengine yote siwezi kuyarudia wenzanguwameyasema vya kutosha na imeeleweka. Sasatunangoja tu tuelezwe wahalifu ni nani?Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru. Mimi nimekwishachangia kwamaandishi, lakini nitasema machache ambayonitayasema kwa msisitizo. La kwanza, linahusu madinimimi ninavyoona kuna udhaifu katika sera ya madini,kuna udhaifu katika sheria ya madini, na kuna udhaifukatika mikataba ya madini.Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Wizara lazima irejeehizo sera, sheria na mikataba. Kuna udhaifu hatakatika kiwango cha kodi. Twende katika nchi nyinginekama Botswana, Zimbabwe, Guinea, Namibia nakadhalika tuangalie ni kiwango gani hasa ambachowawekezaji wanatozwa. Maana hapa tunasikiailikuwa asilimia tatu; sasa katika sheria ya mwaka 2010wakapandisha kidogo ikawa asilimia nne, lakini je

hicho ndicho wawekezaji wanatozwa kule Botswanaau Guinea? Kwa hiyo, inafaa tulifanyie kazi hilo.Mheshimiwa Spika, nimesema kwamba kunamatatizo katika sera na sheria. Tatizo la kwanzalinahusu utaratibu wa kugawa leseni za maeneo yamigodi. Toka mwanzo kabisa watu waliruhusiwakuchukua maeneo kiasi wanachotaka. Sasa hivininavyoongea huko Bukombe, Bukombe nzimaimeshachukuliwa. Nimesikia Mbunge wa Msalalaamesema kwamba kule Kahama nakokumechukuliwa.Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, toka mwanzokulikuwa na makosa yaliyofanyika. Maeneo kwa ajili yawachimbaji wadogo wadogo hayakutengwa. Hilondilo tatizo la msingi na hilo ndilo tatizo ambalo Wizaralazima ilishughulikie. Wakishalishughulikia hilo watakuwawametatua tatizo kubwa sana, watakuwawameondoa mgogoro ambao upo sasa hivi baina yawachimbaji wakubwa na wachimbaji wadogowadogo na pia watakuwa wameipatia sifa Serikali yaokwamba imetatua mgogoro mkubwa. Lakini hali ilivyosasa kuna mgogoro mkubwa huko Bukombe.Mheshimiwa Spika, kuna makundi ambayoyameungana, yakaunda ushirika, yamekwendakuomba leseni yakaambiwa kwamba hayo maeneoyameshachukuliwa. Sasa hivi wanahangaikawananipigia simu, wanasema Mbunge wetu tufanyenini? Pia kuna kundi lingine moja linaitwa Mkombozililipeleka maombi ya kupata leseni, likapewa eneo

ambalo liko kwenye Ziwa Victoria, yaani mambo yaajabu sana yanafanyika katika Wizara hii.Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ndugu yangu Profesabado ana kazi kubwa sana. Wizara hii imejaa ufisadi,imejaa ujanja ujanja. Sisi ambao tunakaa kwenyemaeneo ya madini hayo, tunafahamu hilo nawananchi kule wanafahamu. Kwa hiyo, naombakama ameanza hivi na watu wanamsifia sawa na miminamsifia, amefanya kazi nzuri na aendelee hivyo, lakinibado changamoto ni nyingi.Mheshimiwa Spika, kwenye kitabu chaMheshimiwa Waziri, kwenye ukurasa wa 91, amesemakwamba: “Natoa rai kuwa Serikali haitasita kufutamikataba kwa Kampuni zitakazoshindwa kutekelezampango kazi kwa muda uliopangwa kwa mujibu washeria”. Naomba atoe agizo sio rai liwe ni agizo, kwasababu hizi kauli za rai za kubembeleza bembelezahazitatufikisha kule tunakotaka kwenda na ndizozilizotufikisha hapa tulipofika.TAARIFAMHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika,napenda kumpa taarifa baba yangu Professa Kahigi,Wizara hii imeacha kubembeleza na ndiyo maanawanapigwa vita kwa mambo ambayo wanayafanya.Kwa hiyo, hawabembelezi tena wanafuata taratibu,wameziba mianya ya wala rushwa na ndiyo maanatunakwenda nao sambamba na ndio maanawanapigwa vita. Kwa hiyo, mambo ya kubembelezawalishaacha.

SPIKA: Profesa Kahigi naomba uendelee.MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: Taarifa hiyo…SPIKA: Nimesema endelea tu, achana na hiyo,endelea.MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: MheshimiwaSpika, nashukuru kwa taarifa, lakini sidhani kamaimeongeza chochote nilichokuwa nasema.Mheshimiwa Spika, nimeshamsifu kwa hatuaambazo amechukua, lakini ninachotaka ni kwamba,achukue hatua zaidi kwa sababu kusema kwambaameziba mianya ya rushwa sidhani kama amefanyahivyo, rushwa ni kitu kigumu sana kukishughulikia.Mifano, iko mingi hapa duniani sitaki kuitoa. Miminaendelea na mazungumzo yangu.Mheshimiwa Spika, ukurasa wa 106, namsifuProfesa anasema hivi, anatoa rai tena: “Kuwa migodiyote ianze kulipa kodi ya mapato bila ya kuletavisingizio.” Naomba asitoe rai, atoe agizo na ni vizuri,anapokwenda huko mbele anaagiza katika ukurasaunaofuata. Ni kwamba ule ukurasa wenye raihaukuwa na sababu yoyote kwa sababu huku mbeleanaagiza na ni hatua sahihi sasa hivi aagize naasimamie, kwa sababu tatizo kubwa ni usimamizi.Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie nishati.Nishati kama sekta ya madini pia imegubikwa natuhuma nyingi sana za rushwa na tunampongeza na

wenzake kwa jinsi walivyolishughulikia hili ambalolimekuwa likizungumzwa hapa Bungeni. Sitakikuzungumza zaidi kuhusu hilo, lakini ni kwambakushughulikia kitu kidogo sio kwamba umeziba nyufakama anavyosema Mheshimiwa binti yangu pale,hapana. Hiki ni kitu kidogo tu, rushwa ni kitu kikubwa;ukiondoa tu pingili moja, ni kwamba hujaimaliza hiyorushwa.Mheshimiwa Spika, lingine ambalo ningependakuongelea ni kwamba, watu hapa Bungeni walikuwawakililia umeme katika maeneo yao na mimi nimekuwani mmojawao kwa sababu Bukombe kwa miaka 50toka tupate uhuru haijawa na umeme mpaka leo.Angalau nashukuru Serikali kwamba kuna mpango wakupeleka umeme Bukombe na barua nimeshapatakutoka kwa Naibu Waziri anayeshughulikia NishatiMheshimiwa Simbachawene.Mheshimiwa Spika, lakini tunachoomba ratibaitekelezwe kama ilivyopangwa maana Bukombewamesubiri sana umeme kwa muda mrefu naninavyodhani sababu mojawapo kwa nini Bukombe ikonyuma kimaendeleo, ni kwa sababu haijawa naumeme katika kipindi chote cha miaka 50 toka tupateuhuru. Tunaomba hiyo ratiba itekelezwe.Mheshimiwa Spika, halafu pili, vile vijiji ambavyovinapitiwa na hizo nguzo, naomba vyenyeweviteremshiwe umeme na hasa katika maeneo yazahanati, shule za sekondari na maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, la mwisho ambalo ningependakuzungumzia kuhusu umeme ni kwamba, mwaka janakatika bajeti kulikuwa na miradi ambayo iliahidiwa naSerikali na kulikuwa na Mradi wa Taa za Mwanga BoraVijijini ambao ulikuwa utekelezwe Bukombe, Kahama,Biharamulo na Chato. Swali, mradi huu umefikia wapikatika utekelezaji wake kwa sababu hatujauona nawala hatujausikia tena toka wakati huo. Kuna mradi waTanzania Affordable Rural Electrification Plan ambaoulikuwa utekelezwe Bukombe na Kibondo. Mradi huoumefikia wapi?Mheshimiwa Spika, kwa hayo machache,nakushukuru kwa kunipatia hii nafasi, ahsante.SPIKA: Ahsante. Sasa nimwite MheshimiwaJosephat Kandege na Mheshimiwa Yusuph AbdallahNassir ajiandae.MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangiakatika hoja iliyo mbele yetu. Awali ya yote naombanimshukuru Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madinikwa namna ambavyo ameonesha Watanzaniatukiamua tunaweza kwa dhati na hasa pale ambapotukiamua kusimamia haki. Pia naomba niwapongezeManaibu Waziri, Mheshimiwa George Simbachawenepamoja na ndugu yangu Masele. (Makofi)Mheshimiwa Spika, baada ya kuwapongeza,naomba nijielekeze katika mambo machache, kwasababu kimsingi mengi yameshasemwa na

nisingependa nianze kurudia yale ambayoyalishasemwa.Mheshimiwa Spika, ukipitia hotuba yake inaoneshanuru mpya kwa Tanzania, inawezekana tukiamua.Lakini pia ameonesha jinsi ambavyo ile mikoa ambayoiko pembezoni inaweza ikafunguka kwa kuhakikishakwamba gridi ya Taifa inawafikia. Kwa hiyo,namwomba Mheshimiwa Waziri ahakikishe kwambaule umeme wa kutoka Nyakanazi kwenda Kigoma,Kigoma kwenda Katavi, Katavi/Sumbawanga,Sumbawanga/Tunduma,Tunduma/NjombeMakambako kule kwa Mheshimiwa Spika, halafu narudiIringa maana yake ni nini? Kwa ajili ya wawekezajitutakuwa tumefungua mikoa yote hiyo na uwekezajiambao tunatarajia kwa ajili ya maendeleo ya nchiutawezekana.Mheshimiwa Spika, lakini pia nilikuwa napitia kwaharaka haraka, bahati nzuri Profesa amechora mpakaramani kuonesha sehemu ambako miradiinatekelezwa. Namwomba ajaribu kurudia, atazamesehemu zipi ambazo zinaonesha kwamba badohazijapelekewa msukumo wa kutosha. Siku zotenilikuwa nikisema kwamba, ni vizuri Tanzaniatukaendelea kwa pamoja, ile biashara kwambasehemu zingine bado zionekane Profesa usikubalianena hii, wote twende kwa pamoja, maendeleo yawekwa Watanzania wote kwa ujumla.Mheshimiwa Spika, pia nimepitia nimekuta kunasehemu ambako Mheshimiwa anakiri kabisa kwamba,kuna vyanzo vingine vya umeme ambavyo lazima

tuvitumie na kila nikipata nafasi nitapiga kelele kwelikweli kwa sababu najua vyanzo hivi na Profesa nayeanajua makaa ya mawe ni chanzo ambacho ni rahisisana katika kuzalisha nishati hii.Mheshimiwa Spika, ukienda kule Rukwa kunachanzo kile cha Namwele ambacho yupo Mtanzaniamzalendo, yupo tayari kuzalisha anachotaka niguarantee kwamba TANESCO watanunua umeme huona kuingiza kwenye grid ya Taifa. Kwa hiyo, ni vizuritukawaunga mkono Watanzania wazalendo wenyenia thabiti ya kuhakikisha kwamba nchi hiitunaendelea.Mheshimiwa Spika, siku mbili tatu naaminiikiwezekana kwa Mheshimiwa Waziri kama siku sitahakupata usingizi. Hakupata usingizi kwa sababu yakile ambacho kilikuwa kikiendelea hapa. Lakini badoukifuatilia hawa ambao walikuwa wanatakakumkosesha usingizi ni wale ambao siku zotewamekuwa wakisema posho hawataki, kumbe wanaposho nzito wanazozitaka na sisi wengine wote nimashahidi. Hatuna posho nzito humu na ndiyo maanatumekuwa tukihangaika tupate posho hiyo ndogo kwasababu ndiyo halali. Watu wamekuwa wakisema,lakini wamejipambanua kwamba waadilifu, lakiniMwenyezi Mungu akitaka kukuangaza unaonekanadhahiri, huyu muadilifu kweli huyu, nyie mashahidi.Nadhani ujumbe utakuwa umefika kwa uzitonilioutarajia.Mheshimiwa Spika, naomba nichangie kuhusianana urani. Kuna maneno mengi sana yamesemwa na

inawezekana ni katika wale wenye nia mbayakuhakikisha kwamba Tanzania tunarudi nyuma badalaya kusonga mbele. Mtu akikwambia kuhusiana nahadithi ya urani utaona kama jambo baya kweli kweli.Kwenye Kamati yangu nimepata nafasi, nimetembeleakule Namtumbo. Ukiambiwa kwamba eti ni madinihatari kama vile ukisogelewa tayari yatalipuka, si sahihi.Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba nduguWabunge kwa ujumla wetu naomba tuunge mkono,tuhakikishe kwamba uchimbaji wa urani kwa ajili yamanufaa ya Taifa hili unafanyika na tusije tukaanzakupigana vita wenyewe kwa wenyewe. Ni MwenyeziMungu ametujalia, tuna kila sababu ya kuhakikishakwamba rasilimali hii tunaitumia kwa ajili ya manufaaya Watanzania walio wengi na si kwa wachache.Mheshimiwa Spika, nichangie kuhusiana nausambazaji wa umeme. Nimepitia katika kitabu chaMheshimiwa Waziri, ametaja sehemu kama mbili kwaMkoa wa Rukwa na hasa Jimbo la Kalambo. Napelekaumeme Makao Makuu ya Wilaya na Kasanga basi.Lakini ukija kutazama sehemu zingine naanza kusemani hii Tanzania ambayo bado tunaondoka kwapamoja, stahili hii ipo au haipo. Kwa hiyo nimwombeMheshimiwa Waziri, bado inawezekana huu siomsahafu hebu watazame namna ambavyowatapeleka miradi ya kutosha kwa mikoa hii ambayoilikuwa imeachwa nyuma na sisi tunataka tuinuke, weare sleeping quite for a long, ni wajibu wetu, ni hakikatutasimama, hebu tupeni uwezo. Msije mkatushikamikono halafu mkasema tunaendelea haiwezekani.

Mheshimiwa Spika, kwa jirani yangu MheshimiwaMipata pale, Makao Makuu ya Jimbo MheshimiwaMbunge hana umeme na wala siioni kamaimeandikwa sehemu yoyote. HaiwezekaniMheshimiwa Profesa ni vizuri akakaa tena akatazamasehemu zipi ambazo zinaonekana kuwa badohazijapewa hizo nafasi, fursa hii tuitumie na tufaidike nanamna ambavyo ameturahisishia ameshusha bei yakuunganisha umeme.Mheshimiwa Spika, nampongeza sana kwasababu mara ya mwisho nilisema hapa kwamba, hivileo sisi tunashindwa kuunganisha umeme baada yamiaka miwili bei ya kuunganisha umeme imepanda,tunataka mwananchi alipie kiwango cha juu, kosa lakenini ambalo linamsababisha mpaka aje alipie beikubwa? Kwa hiyo, namshukuru sana MheshimiwaWaziri kwa kuwa ameliona kosa hili. Naaminiungekuwa utaratibu mzuri, tukiamua kwambamwananchi kama inawezekana akaweka fedha leokwa kiwango cha leo, abaki anaidai TANESCOkupeleka umeme. Kwa hiyo, ile hadithi kwamba itafikakipindi bei ya umeme itapanda isiwepo. Ni wajibu waSerikali kuhakikisha kwamba huduma inatufikia sisiwote.Mheshimiwa Spika, pia naomba nimshukuruMheshimiwa Waziri kwa kutambua kwambatukitegemea chanzo kimoja hatuwezi kufika. Ni wajibuwa Wizara kuendelea kutafiti vyanzo vingine. Tanzaniatuna vyanzo vingi sana na tuutumie umeme kamabiashara ya kuweza kuuza baada ya kwambatumeshajitosheleza sisi wenyewe. Kwa hiyo, wataalam

waendelee kutafiti vyanzo viko vingi. Pale KalamboFalls maporomoko ya pili Afrika, wengi hawajui.Ukienda pale its amazing, you cannot imagine. Lakinitumeitumiaje fursa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziriatume wataalam wake wakatazame kama kunauwezekano wa kufua umeme, pale utapata mwingisana kwa ajili ya Taifa hili. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba niunge mkono hojakwa mara nyingine na nashukuru sana. (Makofi)SPIKA: Ahsante. Msemaji wetu wa mwishoatakuwa Mheshimiwa Yussuph Abdallah Nassir.MHE. YUSUPH A. NASSIR: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana, sikuwa na uhakika kama ningepatafursa ya kuchangia leo, lakini niishukuru meza yako kwautaratibu ulioutumia. Kwanza nianze kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kunipa siku hii ya leo. Nitumiefursa hii pia kuwatakia funga njema wale ambaohatujaonana, lakini pia niwashukuru WanakorogweMjini.Mheshimiwa Spika, kipindi cha wiki mbili zilizopitatumekuwa tuna kazi kubwa kuhusiana na Kamati ile yaKisekta ya Nishati na Madini kuangalia tasnia nzima yaWizara hii na kwa kuiangalia kwa dhati kabisa bilaunafiki, bila ya influence na hata bila ya kushawishiwakwa namna yoyote ile. Tulifanya kazi kubwa sisiwengine tuliobaki wakati Wajumbe wengine wakiwaChina kwa safari ya kikazi. Hotuba ya Kamati ya Nishatina Madini tuliifanyia kazi na tukairidhia wote, ni bahatimbaya mengi yaliyoandikwa mle ndani hayakupata

kusomwa hadharani, lakini kama ambavyo nilimshauriMwenyekiti wa Kamati akufahamishe kwamba hotubayake iingie kama ilivyo.Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii piakuupongeza uongozi mpya wa Wizara ya Nishati naMadini. Nimpongeze Katibu Mkuu aliyekaimu wakatiwa turbulence ya kipindi kilichopita na hatimayeakapata confirmation ya kuwa Katibu Mkuu sasa.Nichukue fursa hii pia kumpongeza Mheshimiwa Waziripamoja na Manaibu wake, lakini nataka niwekemsisitizo na nitakuwa na upendeleo hasa mdogowangu Stephen Maselle kwa kazi kubwa na umakinialioufanya wa kuweza kutudhihirishia sisi ndani yaKamati kuhusiana na yale yalikuwa yakiendelea.Mheshimiwa Spika, tulipata kukaa vikao vingi, sivema nikayasema yale yaliyojiri kwenye vikao. Lakinialiyesikia kasikia na mkubwa amekanyika.Inawezekana wengi tukafikiria utekelezaji wa Ilani yaChama cha Mapinduzi ni kuimba iyena iyena. Wakatiwa iyena iyena umekwisha, sasa ni wakati wa kuchapakazi na kuangalia misingi ya utendaji kazi iliyokuwasahihi. Tuache watu waimbe iyena iyena kwa nyakatizilizokuwa sawa, za uchaguzi na kampeni, lakini sasatuchape kazi. Mheshimiwa Waziri, Manaibu pamoja naKatibu Mkuu nawapongeza sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, sasa nijielekeze katika maeneoyanayohusiana na mafuta. Katika kipindi cha Januarimpaka sasa Watanzania walipata bahati mbaya yakupata nishati ya mafuta kwenye vyombo vyao vyausafiri ambavyo kwa kiasi fulani hayakuwa ya viwango

vile ambavyo nchi ilielekeza. Kukawa na vuta nikuvutebaina ya wafanyabiashara wadogo, wafanyabiasharawakubwa na hata na mwagizaji. Lakini tukajiuliza sisikama Kamati, nafasi ya mdhibiti iko wapi? Sasa wakatiMheshimiwa Mwenyekiti alipokuwa akisoma hotubayetu alishindwa kwa sababu ya wakati kuzungumziayale yaliyojiri katika malumbano yaliyokuwa yakitokeabaina ya Bodi ya waagizaji mafuta pamoja naMamlaka inayosimamia udhibiti kwa maana yaEWURA.Mheshimiwa Spika, kwa hesabu za haraka haraka,inawezekana kukawa kuna wind fall profit kubwaambayo aidha mwagizaji au msambazaji ameipata. Nivema basi tutumie fursa hii kwa kuangalia zile importratios na standard yetu ya mafuta, basi tuangalie nikodi kiasi gani ambayo tutaweza kuipata ili angalauwananchi waipate ile nafuu kwa kutumia mlangomwingine. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nataka nijikite kwenye suala lagesi. Tumewekeza kiasi cha rasilimali gesi tulichonachoni kikubwa, uwekezaji umeanza kujitokeza na kwamujibu wa taarifa na hotuba ya Mheshimiwa Waziriimetueleza wazi kabisa, umiliki wa bomba la gesikutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam na kuelekealitakakoelekea litakuwa chini ya Shirika la Maendeleoya Petroli. Tuipongeze sana Wizara pamoja na taasisihii. Lakini kubwa kwenye hotuba yake hakuelezea paleambapo bomba hili litakapofanya kazi TPDC ni taasisikubwa je, tumeishauri ianzishe kampuni tanzu?

Mheshimiwa Spika, nakumbuka kuna mahaliwamezungumzia cha kuwepo kwa GASCO, basi kwanini kuanzia sasa tusiipe uwezo ile GASCO tukaanzasasa kuwapa vijana wa Kitanzania fursa ya kuanzakuajiriwa kule, tukaanza sasa kuondoa lile kundi latukale wapi pale Mtwara kwa kuwafunza kazindogondogo angalau kwa kupitia kile chuo cha VETApale Mtwara, hata za kupita red oxide kwenye mapipehaya, washiriki hata kazi za kufunga pig kwasababu ni kazi zinazohitaji ujuzi tu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, gesi tumekuwa tukisemainaweza ikawa ni baraka au laana. Tumeshuhudiaresources na kwenye nchi nyingi kama Nigeria, OgonLand, tumeshuhudia pia vita vinavyoendelea kule DRCCongo vyote vinahusiana na rasilimali na kwa sababutuna matatizo ya kimpaka pale. Mashariki tuna mpakawa bahari na kusini tuna mpaka wa mto. Jambo loloteambalo linaweza kutokea Msimbati au Mnazi Bay nirahisi wale wafanya vurugu wakavuka mto nawakaenda upande wa pili. Ni vema sasa uwekezajihuu tuupe sura mpya ya ulinzi na usalama wa Taifa hili.(Makofi)Mheshimiwa Spika, ipo haja ya kuwa na naombanitumie neno kachero, tuwe na makachero wengisana kwenye maeneo haya ya kusini na tuwe namakachero wengi sana kwenye maeneo haya ya gesi.SPIKA: Ni kengele ya pili, ahsante sana.MHE. YUSUPH A. NASSIR: Mheshimiwa Spika, hiyo nikengele ya kwanza!

SPIKA: Basi malizia dakika hizo mbili.MHE. YUSUPH A. NASSIR: Mheshimiwa Spikaahsante. Suala la ulinzi na usalama halitakuwa namjadala. Lakini kadhalika pia ni kwa mara ya kwanzanimeweza kushuhudia muungano wa Vyama Visivyovya Kiserikali vingi ambavyo sasa vinaelekeza nguvuzake kusini. Tunajua Vyama Visivyo vya Kiserikaliumuhimu wake kwa jamii zetu, lakini ni vyema mtaalamahususi uwekwe na Serikali au hata Sheria itungwe naBunge letu. Kwamba vyama vitakavyojihusisha nauchochezi katika maeneo ambayo tuna rasilimali basivipigwe marufuku na hata ikiwezekana viongozi wakewafungwe.Nisingependa kuona Wamatumbi kule Mtwarawanashika pinde na mishale kwa ajili ya kuwamalizawenzao au wawekezaji ambao tunahangaika naohalafu ifikie mahali bomba lipigwe pancha,hatutakuwa tumeitendea haki nchi hii. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nataka niguse kidogo suala laumeme vijijini. Katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziriukurasa wa saba na wa nane amelizungumzia sana.Ameeleza wazi kabisa ni asilimia 6.5 ya Watanzaniawalioko vijijini ndiyo wanaopata umeme wakati wakaziwa vijijini, Tanzania nzima ni asilimia 75. Kamatulivyosema anatekeleza ilani ya Chama chaMapinduzi, basi aende kwa mchakamchaka ilikuhakikisha angalau asilimia 26 inafikiwa kabla ya 2015.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayomachache, nisipoteze muda mwingi, naunga mkonohoja hii. Nawapongeza sana viongozi na watendajiwakuu wa Wizara. Naomba kaka asafishetutamwombea aongeze idadi ya wafanyakazikupunguza ombwe lililopo la watendaji ndani yaWizara yake na wale tunaokuunga mkono kwa dhatitutaendelea kukuunga mkono ndani ya Kamati yakisekta kwa maana ya Chama ndani ya Bunge nahata ile Kamati ya Bunge ambayo inasimamia Wizarayako.Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kama ilivyo adawote mngependa kuzungumza na ningependakuwapa nafasi, lakini kila kitu sharti kifikie mwisho.Mpaka sasa hivi waliochangia mara mbili wamebakikaribu 36, waliochangia mara tatu na hawakufikiwa ni15 na aliyechangia mara nne ni mmoja tu. Kwa hiyo, nidhahiri kwamba wapo wengine wangeachwa tu.MICHANGO KWA MAANDISHIMHE. FAITH M. MITAMBO: Mheshimiwa Spika,nianze kwa kuunga mkono hoja na nichukue nafasi hiikumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Nishati naMadini kwa uadilifu wake mkubwa na umakini mkubwaanaoufanya na ambao ameuonesha katika kipindi hikikufupi cha uongozi wake.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,naomba niende katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri

wa Nishati na Madini ukurasa wa 57, Mheshimiwa Waziriametamka kwamba madini ya Uranium yanapatikanamaeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mto Mkuyu,ulioko Wilaya ya Liwale, Namtumbo na Tunduru.Ukurasa wa 136 jedwali linaonesha kwamba MkujuUranium project iko Wilaya ya Namtumbo peke yake.Mheshimiwa Spika, naomba binafsi kujiridhisha, je,ni kweli project hii ya Mkuju Uranium Project, Wilaya yaLiwale na Tunduru haihusiki? Je, Mheshimiwa Waziriyuko tayari kutuonesha mpaka au mwisho wa eneohilo la Mkuju Project ni wapi ili nasi Liwale tujiridhishekwamba hatumo? Kumeshaanza kutokea malalamikokatika Wilaya ya Liwale. Hata Mheshimiwa Wazirihataweza kutoa jibu leo, naomba nimtafute kwawakati mwingine ili niweze kupata majibu ya utata huu.Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii piakuipongeza Serikali kwa kupunguza gharama zakuunganisha umeme kwa wateja wadogo wadogo,wakati na wateja wakubwa. Ninachoomba kwaMheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini ni kwamba,punguzo hili la gharama za kuunganisha umeme,liende sambamba na upatikanaji wa vifaa vyakufanyia kazi hiyo, kama vile nguzo, nyaya za umeme,vikombe, transformers na kadhalika kwa sababukumekuwa na tatizo sana la upatikanaji wa vifaa hivyona hivyo hulifanya zoezi la kuwapatia wananchiwanaokusudiwa kupatikana umeme kukwama.Mheshimiwa Spika nimeshuhudia tatizo laupatikanaji wa nguzo, nyaya za umeme, vikombe nakadhalika. Katika Wilaya ya Liwale na mara nyingi

niliwasiliana na wafanyakazi wa TANESCO bilamafanikio. Wilaya ya Liwale ina wateja wengi sanakwa sasa ambao hawana umeme na wanatakakuunganishiwa umeme lakini kuna tatizo hilo la njaa.Namwomba sana Mheshimiwa Waziri alishughulikie nahili.Mheshimiwa Spika, sasa naomba niongelee sualala kuwaendeleza wachimbaji wadogo wadogo wamadini. Wilaya ya Liwale ina fursa kubwa sana yamadini na katika Mkoa wa Mtwara na Lindi, Wilaya yaLiwale ni Wilaya pekee ambayo ina aina ya madininyingi na kwa wingi na katika maeneo ambayoyanaonekana kuwa na madini, tayari kuna vitalu vyawatafiti na wachimbaji mbalimbali wakubwa navinaonekana kuwa na leseni za utafiti na uchimbaji.Sasa namwuliza Mheshimiwa Waziri wa Nishati,wachimbaji hawa wadogo wadogo ni maeneo ganiwatatengewa ndani ya Wilaya hiyo? Kama yapomaeneo bado hayana leseni za utafiti na uchimbaji,naomba Mheshimiwa Waziri atupe taarifa ili eneo hilolitengwe kwa ajili ya wachimbaji hawa wadogowadogo.Mheshimiwa Spika, ni muda mrefu nimeombakuwa na Ofisi Ndogo ya Madini Wilayani Liwale,wananchi wale wanateseka sana, kushughulikiamasuala yao ya leseni, uuzaji wa madini yao nakadhalika. Tunaomba sana tupate Ofisi ya Madini,Wilaya ya Liwale. Kwa sasa Ofisi za Madini ziko Mtwarana Tunduru na kumekuwa na urasimu mkubwa sanakatika Ofisi ya Madini Mtwara, katika kuwashughulikiawachimbaji hawa wadogo wadogo.

Mheshimiwa Spika, wachimbaji hawa wadogowadogo wana matatizo mengi ikiwa ni pamoja nakucheleweshwa leseni zao na documents nyinginezo,lakini pamoja na kuomba tupatiwe Ofisi Ndogo yaMadini ndani ya Wilaya ya Liwale ili na sisi tupunguziweadha ya kushughulikiwa matatizo yetu, namuombaMheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini aiangalie sanaOfisi ya Madini Mtwara kuna matatizo pale, ni kwa ninileseni zinachelewa? Ni kwa nini Ofisi hii ina-facilitatekuwanyang’anya wachimbaji wadogo wadogomaeneo yao.Mheshimiwa Spika, nizungumzie sasa masuala yagesi. Gesi inatoka Mkoa wa Lindi na Mtwara na gesihiyo sasa inachimbwa na kusafirishwa kuja Dar esSalaam kwa ajili ya uzalishaji wa umeme na matumizimengine. Ni huruma sana na itakuwa ni uonevumkubwa kama wananchi wa Mikoa hii ya Lindi naMtwara, Wilaya zote za Mkoa wa Lindi na Mtwarahazifaidiki na matunda ya gesi hii.Mheshimiwa Spika, Mikoa hiyo na Wilaya zake zotezinapaswa zifaidike na matunda ya gesi hiyo, ni aibusana Wilaya yoyote ile ya Mkoa wa Lindi na Mtwarakukosa umeme na huku gesi ikisafirishwa kwenda Dares Salaam, kuzalisha umeme na matumizi menginehuku ndani ya Mkoa wa Lindi kuna Wilaya ya Liwaleambayo haina umeme wa uhakika na ikiendeleakuhangaika na umeme wa generators, huku gesiikitokea ndani ya Mkoa huo wa Lindi. Sio umeme tu

hata mazao na manufaa yoyote yanayotokana nagesi hiyo, Wilaya zote zinapaswa kufaidika.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. CHIKU A. ABWAO: Mheshimiwa Spika,kwanza namwomba Mheshimiwa Waziri apokeepongezi zangu za dhati kabisa yeye mwenyewe, NaibuWaziri, Katibu Mkuu wa Wizara yake na Watendajiwake wote kwa ujumla. Kwa hotuba nzuri yenye kuletamatumaini makubwa ambayo yatapelekea kumalizatatizo la mgao wa umeme na kuhamasishaWatanzania wengi waweze kuingiza umeme kwenyemajumba yao kwa kupunguza gharama za kuingizaumeme majumbani, mijini na vijijini.Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizinamwomba afanyie kazi watumishi wanaohujumu nawanaolalamikiwa kuhusika kwenye tuhuma mbalimbaliambazo zimethibitika wachukuliwe hatua za kisheriaikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi kabisa ili wasijewakakuingiza katika matatizo, kumbuka mfichamaradhi kifo kitammaliza.Mheshimiwa Spika, pamoja na Mheshimiwa Wazirikujitahidi kuweka mkakati mzuri na kupunguzagharama za kuingiza umeme, bado tatizo la kulipianguzo inakuwa ngumu sana. TANESCO ni shirikalinaloendesha shughuli zake kibiashara, kitendo chakulipisha nguzo kinawafanya wakose wateja nahatimaye kupelekea shirika kufanya kazi kwa hasara. Ilibiashara ichanganye ni kufutilia mbali gharama zakulipia nguzo za umeme. Pia nampongeza sana kwa

hotuba yake iliyopelekea nitambue ameguswa sanana matatizo ya Wachimbaji wadogo wadogo, kitendocha kuamua kukutana nao na kuweka utaratibuendelevu wa kukutana kila mwaka naamini ni mwanzomzuri sana. Namwomba aendelee na utaratibu huo.Sambamba na hilo ajitahidi kuyafanyia kazimalalamiko atakayoyaona kuwa ni ya msingi na yanaukweli, akifanya hivyo amani itadumu.Mheshimiwa Spika, mwisho, namshukuruMheshimiwa Waziri, amenifariji sana katika hotuba yakepale uliposema hakutakuwepo tena na usiri katikamambo yote yatakayohusu Wizara yake. Naaminiataweka kila jambo bayana ikiwa ni pamoja namikataba yote ya madini ambayo imekuwaikilalamikiwa sana. Naamini kabisa akitekeleza kamaalivyoahidi atamaliza manung’uniko na atakuwa naamani katika kutekeleza mipango ya Wizara yake naakiwa na amani hakika ufanisi utakuwepo kwani akiwana amani ataipa akili yake motisha na ubunifu,atapata nafasi ya ubunifu na ubunifu utasaidia sanakuleta ufanisi katika kazi yake.Mheshimiwa Spika, naomba punguzo la kuingizaumeme lianze mara moja, huo mwezi wa kwanza ukombali sana na ajue kitendo cha kuweka hadi mwakanimwezi wa kwanza atakuwa amesimamisha biashara,wananchi wote wataona wasubiri hadi mwakani ndipowaombe kuingiziwa umeme hata wakiomba nakukubaliwa hawatakwenda kulipia hadi punguzolitakapoanza. Nafikiri ataona uzito wake miezi zaidi yamitano (5) ni hasara kubwa sana kibiashara.

Mheshimiwa Spika, namtakia Mheshimiwa Wazirikila la kheri katika utendaji kazi na mafanikio mema,wameanza vizuri Mwenyezi Mungu awasaidiewaendelee vizuri.MHE. SALIM HEMED KHAMIS: Mheshimiwa Spika,kwanza nampongeza Mheshimiwa Waziri, ManaibuMawaziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizarahii kwa kazi nzuri wanayofanya, kuifanya Wizara hii ifikiematarajio ya Watanzania. Kwa namna maalumniupongeze uongozi mpya chini ya Waziri Muhongokwa kufichua madudu yaliyokuwa yanaikwaza Wizarahii, tunategemea baada ya kudorora kwa muda mrefuWizara hii sasa itakuwa na matumaini ya Watanzania,pamoja na matumaini hayo, naomba nichangieyafuatayo:-Kwanza ni kuhusu madini, Tanzania imebarikiwakuwa na madini mengi, lakini wingi wakehaujawanufaisha Watanzania hata mahali palepanapochimbwa. Mirahaba inayotolewa badohaikidhi haja, Watanzania wanaobahatika kugunduamadini hawaaachwi kuendelea kuchimba na kufaidibadala yake haraka haraka wanaletwa wachimbajiwakubwa wao wanabaki manamba. Hii ni dhulumakubwa. Serikali lazima iwasaidie wagunduzi hawa kwakuwapa mitaji na utaalam ili nao wafaidi matunda yauhuru.Pili ni umeme; umeme ni muhimu kwa maendeleo,bila ya umeme wa uhakika hatutakuwa na wawekezajimakini, lakini hata wajasiriamali wetu wa ndani

watakuwa wakikatishwa tamaa na umemeusiotabirika. Hivi sasa tumeanza kujenga imani baadaya tamko la Wizara kuwa hapatakuwa na mgao tenawa umeme. Tunawapongeza kwa hili, hata hivyo beiya umeme bado ni kubwa hasa kwa Watanzania wakipato cha chini na kipato cha kati. Naiomba Serikaliieleze ni namna gani bei ya umeme itapungua iliWatanzania wengi waweze kuunga umeme ikitiliwamaanani kuwa ni asilimia ndogo tu ya Watanzaniawenye umeme majumbani kwao.Tatu, nichangie kuhusu umeme Zanzibar; Zanzibarinapata umeme, lakini kwa muda mrefu sasa Zanzibarkuna mgao wa umeme kila siku kwa maeneo kwamuda wa saa moja moja. Je, ni kwa sababu ganiTanzania Bara hakuna mgao, lakini Zanzibar kunamgao wa umeme? Naomba ufafanuzi.MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika, pamojana maoni na mapendekezo niliyowasilisha kupitiahotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, naomba kutoamchango ufuatao wa nyongeza hususan kuhusumasuala yanayohusu Jimbo la Ubungo:-Mheshimiwa Spika, mosi, kuhusu maombi yaumeme ya wananchi wa Mtaa wa Msakuzi juu yamradi wa umeme Kibamba Luguruni, Mtaa waMsamakuzi including Maswet Mosha ambao eneo laolilifanyiwa survey mwaka 2008 na kuahidiwakusambaziwa umeme ambapo alama au vizingiti vyanguzo viliwekwa. Mpaka sasa mradi huo

haujatekelezwa au hata baada ya TANESCO ngazizote husika kukumbushwa kwa miaka mbalimbali.Mheshimiwa Spika, pili, maombi ya kupewaumeme kwa wananchi wa Goba Matosa ambapoumeme ulipelekwa katika shule ya Lilian Kibo HighSchool. Hata hivyo, wakazi wa maeneo husika umemeumepita mbali yao. Pamoja na kupeleka barua zamaombi TANESCO kuanzia Julai, 2007(GB/MT/U/VOL.6/07) na Machi, 2010 (KIN/S/RM/P/S) namwaka 2011 nilikabidhi vielelezo vyote kwa TANESCOMakao Makuu.Mheshimiwa Spika, tatu, wananchi wa eneo laMringwa katika Mtaa wa Temboni (kwa Msuguri)ambao Kaya zaidi ya 1,000 zinaishi gizani. Mnamomwaka 2007 TANESCO ilituma wataalam na kufanyaSurvey katika eneo hilo na kuweka pegs maeneoambayo nguzo zilipita. Baada ya survey hiyowananchi waliahidiwa kuwa umeme umepangwakufanywa na Kampuni binafsi, mradi unaojulikanakama Kimara-Msigwa.Mheshimiwa Spika, nne, katika Kata ya Kwembekuna mradi wa maji unaofadhiliwa na BYC pamoja naTaasisi zingine ambazo zinashindwa kufanya kazi kwakuwa umeme ni mdogo. TANESCO wameshaandikiwakwa ajili ya kuweka Transfoma kubwa zaidi. Hata hivyo,majibu yamekuwa mpaka tusubiri eneo hilo lipangiwemradi. Ni muhimu TANESCO ikaharakisha kuwezeshawananchi wa eneo husika kupata maji kwa kuwekatransfoma yenye kuwezesha pampu kubwa ya majikufanya kazi. Aidha, Wizara ya Nishati na Madiniifahamu kuwa eneo husika linahitaji kuongezewa

nguvu kubwa ya umeme kwa kuwa kuna miradimikubwa imeanza kutekelezwa katika eneo husikamfano ujenzi wa Chuo Kikuu Muhimbili (MUHAS)Kwembe na Mloganzila na ujenzi wa Mji wa Viungani(satellite town) na Luguruni Kibamba.Mheshimiwa Spika, tano, Wizara imefikia hatuagani kwenye kusimamia upelekaji wa umeme katikamiradi ya Maji ya King’ongo, Saranga, Kilungule naMavurunza iliyotolewa na ahadi ya Rais Kikwete yaMei, 2010. Izingatiwe kwamba mwaka 2011, niliombaWizara ingilie kati kwa kuwa nguzo za umemezilisambazwa, lakini miradi ilisimama kutokana na kilekilichoelezwa kuwa ni uhaba wa vifaa na kuchelewakwa malipo ya Wakandarasi husika.MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA: MheshimiwaSpika, hongereni sana, bajeti yetu imepita kiulaini nakwa kishindo kuliko ilivyotarajiwa. Mmeanza kwahuruma ya Mungu na kuihurumia nchi endeleeni hivyohivyo.Mheshimiwa Spika, napendekeza yafuatayo:-Kwanza, leteni mapendekezo ya mapitio ya Sheriaya Madini ili yafuatayo yafanyiwe kazi:-(a) Kuondoa uwezekano wa uwepo wa fiscalstability clauses” kwenye mikataba ya madini;

(b) M-introduce kodi mpya za windfall gains taxna ring fencing (for tax purposes) ya miradi yamakampuni yanayochimba madini Tanzania;(c) Ku-charge capital gains na kubana mianyayote ya tax Avoidance strategies;(d) Ondoa exemptions kwenye sekta hii;(e) Weka lazima ya free carried interest na pia yashare za Serikali kwenye kila mradi uliopo nchiniTanzania; na(f) Badili au tafuteni namna nzuri ya kutwaaardhi toka kwa wananchi bila kuwaacha maskini napia bila fidia ama radhi nyingine.Pili, hakikisheni mnawabana wawekezaji wotewatekeleze maelezo ya Sheria ya Madini ya mwaka2010, kuwa waweke environmental rehabilitation bondili tuwe na uhakika kuwa watu wetu hawapatimadhara yatokanayo na uharibifu wa mazingirautokanao na shughuli za uchimbaji wa madiniMheshimiwa Spika, Tanzania must go beyond EITI,kwamba tutakapokuwa tunafanya marekebisho yaSheria ya Madini (kama nilivyopendekeza hapo juu)(tuongeze accountability na transparency zaidikwenye sekta za madini, gesi na mafuta, tuwekekipengele cha publicity kwenye mikataba (ilimchakato mzima wa kuondoa, kukabiliana na kusainiuwe wazi zaidi) pia wawekezaji wawe wanalazimikakisheria kufanya yafuatayo:-

- Ku-publish taarifa zao za mahesabu hapandani;- Kuwekeza kwenye soko la hisa la ndani;- Kuingiza fedha zao za mauzo yote hapandani na kufanya manunuzi yote kutokea ndani yaTanzania.Mheshimiwa Spika, kama hawatokubali hayawasipewe maeneo ya kuwekeza miradi mipyawaondoke na badala yake Serikali imiliki maeneo hayomapya na kupitia STAMICO ambaye atamiliki hisanyingi zaidi na atatafuta wabia kuongeza mtaji, ujuzi(technology) na management. Leo hii ResoluteTanzania Limited kwa mfano, imelipa Cumulative taxeszisizozidi TZS 150 bilioni toka imeingia Nzega na kuanzakuzalisha madini na kuuza. Uwekezaji wao ulikuwa TZS58 bilioni tu na baadaye wali-upgrade mitambo yaokwa kuongeza TZS Bil 26 nyingine. Walichovuna wao nizaidi ya ounce 1.99 milioni ya dhahabu yenye thamani(conservative rates) ya pesa isiyopungua trilioni mbili!Kweli tunaweza tukasema tunafaidika namna hii?Mheshimiwa Spika, Serikali imepewa dhamana yakuokoa nchi hii na wizi, dhuluma na ukandamizaji wamabeberu na kusaidia kuipaisha nchi hii kiuchumi kwafaida ya ndugu zetu, okoeni nchi hii!Mheshimiwa Spika, nashukuru na naunga mkonohoja.

MHE. BEATRICE M. SHELLUKINDO: MheshimiwaSpika, nampongeza Mheshimiwa Waziri Muhongo kwakuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara hii muhimu. However,I saw it coming ever since he came back from the bigpost in South Africa. Aidha nimpongeze kwa kazi nzurianayofanya katika mazingira mengi tata aliyoyakutanajua ataweza kurekebisha. Ninawapongeza Mawaziriwako wawili, Mheshimiwa Simbachawene naMheshimiwa Masele kwa kuteuliwa kuwa ManaibuWaziri. My belief is given that team nothing will goasunder.Vile vile kama Maswi is an asset, napendamuelewe kwa muda mrefu utendaji ndani ya Wizarahiyo na Serikali ulikuwa hautekelezi ipasavyo au kutoamaamuzi ya ukweli na uadilifu, kama mnavyofanyasasa kwa uwazi na kwa maslahi ya wasema kweli tupopamoja nanyi na Mungu yupo mbele yenu. Natakakuchangia, lakini nimeona licha ya muda kuwamchache, naweza kuja kuwaona na kupata majibuyote nitakayo, hivyo naomba mpokee hoja zanguchache.Mheshimiwa Spika, Kilindi ni moja ya Wilayaambapo zaidi ya asilimia 70 ni maeneo ya uchimbajimadini takribani miaka mitatu iliyopita, tuliahidiwakuwa na Ofisi ya Madini ya Wilaya badala yakutegemea Ofisi ya Handeni ambayo ni takribankilomita 110 toka Makao Makuu. Pamekuwepo namatatizo mengi yakiwemo malalamiko mengi ambapoyangetatuliwa endapo tungekuwa na Ofisi Wilayani.Ofisi tunayo, ningeomba sana sasa muangalieuwezekano wa kukamilisha suala hilo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu fedha zilizotengwa kwaajili ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo, naombasana angalau awamu hii, basi wachimbaji wadogo wakilindi wafikiriwe, nimekuwa nikifuatilia sana bilamafanikio, wengi wana maeneo lakini wanashindwakwani hawana vifaa (zana) na uelewa stahiki.Naomba sana sana elimu ya Sheria ya Madiniitaondoa dhana ya kufikiria kuibiwa kila mara nakupunguza kero ambazo hazina msingi.Mheshimiwa Spika, niwapongeze kwa reshufflezilizofanywa na Katibu Mkuu za watumishi kumuachamtumishi katika Ofisi ya Madini zaidi ya miaka mitano nitatizo kubwa kwani anajenga mazingira kuwa yeyendiye Alpha na Omega katika eneo husika. Inaumizaunapoona Afisa (RM) ana viwanja vya wachimbajiwadogo zaidi ya 80 kwa majina tofauti. Katika Ofisi yaHandeni napongeza sana mabadiliko, lakini badoyupo mmoja Elias wa muda mrefu ndiye anayesimamiamaslahi ya hao waliopita. Ukiua mende kwenyenyumba maliza wote, ukibakiza kidogo watazalianatena”.Mheshimiwa Spika, suala la umeme, nashukurukuwa kupitia Umeme Vijijini REA, tulipata umeme hadiMakao Makuu ya Kilindi Songe. Naishukuru Serikali kwaniaba ya watu wa Kilindi kwa hilo. Umeme umepitakuelekea Makao Makuu, njiani transfoma hakunaambapo nadhani pia wangenufaika na kazi hiyo nzuriya Serikali.

Mheshimiwa Spika, aidha Mashule hasa yaSekondari, Zahanati na vituo vya Afya vingepataumeme, nimejitahidi kufuatilia tangu mwaka 2010,ahadi ni nyingi bila mafanikio, kila mara nimekuwanikijibiwa kuwa transfoma zipo Mkoani, naombanisaidiwe kwa hili ili vijiji vyangu vifaidike kwani:-- Kukosa umeme kila mara kutokana na kuunguatransfoma na vifaa mbalimbali, ni vyema sasakuangalia ubora wa vifaa vinavyoletwa, aidha wengiwanatoa fedha kufungiwa umeme lakini vifaa hakuna.- Niliahidiwa kuanzia mwaka 2012 umemekuendelea toka Songe Makao Makuu hadi Gairo,Makao Mkuu ya Wilaya, vipi?MHE. MUHAMMAD IBRAHIM SANYA: MheshimiwaSpika, ni jambo la faraja na la kutia moyo kuona Serikaliyetu ina mipango kabambe ya kutandika bomba lagesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Dhamira hiyoni kuhakikisha kwamba mbali na kuunganisha umeme,lakini gesi hiyo itafikishwa majumbani na kutumika kwamatumizi ya kupikia.Mheshimiwa Spika, hii itasaidia sana kwakupunguza gharama za matumizi ya kuni na hasamkaa, wazo hili vile vile litapelekea kunusuru mazingirayetu ambapo watu wengi hukata miti na kutengenezamkaa kwa matumizi ya majumbani hongera kwa hilo,lakini vile vile ieleweke kuwa hiyo ni asilimia ndogo tuya matumizi ya gesi majumbani ukilinganisha naukubwa wa nchi yetu. Hivyo ni vyema katika mijimingine mikuu au hata vijijini nao wanaweza kufaidika

na mradi huu, ni dhahiri kuweka bomba na kusambazanchi nzima ni gharama kubwa nmo.Mheshimiwa Spika, hivyo basi, ni vyema Serikaliikatafuta njia mbadala nayo si nyingine ila kuuza gesihii ikiwemo ndani ya majiko ya gesi au mitungi ya gesi.Hapa watafaidika watu wote wa nchi nzima, hivyo nivyema Serikali ikaweka bei nafuu kwa majiko namitungi hii ili watu hasa wa vipato vya chini wawezekumiliki au kununua mitungi hii na kuanza kutumikahadi vijijini na sio vibaya mitungi ikapunguzwa bei kwaasilimia 50 na gesi yenyewe kuwa bei chini. Vile vilemitungi hii ifikishwe hadi Zanzibar, kwani kutandikwakwa bomba kwenda Zanzibar ni gharama kubwa ilanao wapate mitungi hii kwa bei nafuu.Mheshimiwa Spika, hii italeta faraja na Serikaliitaona faida zake katika suala zima la uhifadhi wamazingira na hii itapelekea hata kuweza kutunzamaeneo yenye vianzio vya maji kwa vile ukataji mitikiholela utapungua. Matumizi ya gesi ni bora kwa hizigas cylinder, kwa kuwa utatumia moto kwa mujibu wamatumizi yako, unapika chakula kikishawiva unazimajiko lako pale pale, ila mkaa utaendelea kuteketeamara baada ya upishi wako kwa vile hauzimwi kamajiko la gesi.Mheshimiwa Spika, mwisho tuwe makini nauvumbuzi wa uranium ni vyema tuwe makini na sualazima na uzito wa suala zima Kimataifa, sio vibaya niutajiri ambao Mungu ametujalia, ila naona tuwemakini, ni bora tujikite na gesi kwanza hadi tujue tijayake. Nchi ipo, watu wapo na tuanze kusomesha

vijana wetu ili tuwe na wataalam wa kutosha nawatayarishwe vyema na wao ndio watakaowezakumudu uchimbaji wa Uranium. Hatuna wataalam wakutosha kwa sasa, sio vibaya kwenda kidogo kidogo isbetter to be sure than to be sorry.MHE. JOHN M. CHEYO: Mheshimiwa Spika,nachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Wazirina Wafanyakazi wote kwa kazi nzuri inayoletamatumaini, aidha hotuba ya Wizara imetengeneza njiaya matumaini kwa Taifa letu, naomba kusisitizayafuatayo:-Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme, transmission nimuhimu, umeme ni nguzo muhimu katika Taifa kufikianchi kuwa ya uchumi wa kati katika muda mfupi, nchiyetu ni kubwa na naona pamoja na kupata njia zauhakika kama vile kutumia gesi na makaa ya mawe,juhudi za kuzalishwa umeme lazima ziendane nakuimarisha transmission. Kinachoonekana uzalishaji ukoupande mmoja southern corridor mpaka Dodoma,lakini mahitaji makubwa yako Kanda ya Ziwa. Nashaurimikakati ya transmission iwekwe wazi ili nasi tulio Kandaya Ziwa tupate matumaini mapya. Nasisitiza jambo hiliukizingatia kazi na nia nzuri ya kufikisha umeme vijijini.Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme vijijini,napongeza REA kwa kazi nzuri inayofanywa hataWilaya mpya yetu ya Itilima imekumbukwa na katikaJimbo langu vijiji vingi vimetajwa ingawa vimetajwaBungeni, basi vingebaki katika hansard. Natumainiatakupa taarifa rasmi kwa Wabunge wote, hakikaJimbo langu nasisitiza umeme. Nywalushu-Nkoma

wapewe kipaumbele ili tupate power ya kuvuta majikutoka bwawa la Nkoma, kwenda Kituo cha AfyaNywalushu ambacho kwa Wilaya mpya hii ya Itilima, hiindio hospitali ya Wilaya mpya Itilima. Jambo hililinajulikana kwa Mheshimiwa Rais aliyezindua lilebwawa mwaka 2006, Mheshimiwa Waziri Mkuu piakatika ziara yake mwanzo wa mwaka huu alishuhudiaumuhimu wa kuwa na umeme kwenye Kituo kipya chaAfya na kuwa na pampu ya maji.Mheshimiwa Spika, kuhusu madini, Tanzaniatumetunukiwa madini mengi sana nchi nzima, nami nimmoja wa wanakamati ya Bomani pamoja na KatibuMkuu wa Wizara Ndugu Maswi na changamoto katikasector hii ni nyingi na chanzo chake ni mtazamo hasikwamba anayegundua madini yanakuwa yakemineral right. Mgunduzi asiruhusiwe kuinyang’anya nchihayo madini kwa kisingizio analeta fedha yakuyachimba, ni ukweli usiopingika kwamba gharama simali ya mwekezaji bali ni mkopo. Dhamana yake ikiwamadini yetu The mineral right deposit certificate jambohili ni sawa na kumpa mtu vyumba vyako aweke rehanimawe unachopata ni kiduchu. Mtazamo huu naombaupya na kila mwekezaji lazima atoe hisa si chini yaasilimia 50 kwa Serikali itakayoshikilia kwa niaba yaWatanzania.Mheshimiwa Spika, urani ni madini yenye upekeemaalum, maoni yangu ni kwamba, tumeharakisha mnokukubali kwani ichimbwe na kuhamishiwe nchinyingine. Kwa nini tunawapa watu wengine nuclearcapability, madini haya ni defence material. Nashauri

sera maalum itumiwe na tusichimbe sana, tusubiriMataifa yanaelekea wapi katika madini haya.Mheshimiwa Spika, pamekuwa na mtindo wakukubali kutenga fedha lakini fedha haitolewi ni lazima,aidha, kisingizio kimekuwa fedha inatolewa kufuatanana mikataba ya ujenzi wa miundombinu ya umeme augesi, mikataba au michakato ya ununuzi ikichelewafedha zilizoidhinishwa na Bunge kwa mwaka huo nazozinachelewa na kwa kawaida muda wa bajeti ukiishanazo fedha zinatoweka na kuanza tena katika mwakawa bajeti. And eventually we remain with unfunded orunder funded projects, matokeo ya utaratibu huu wabajeti unafanya miradi mingi isitekelezwe kwa wakatiuliopangwa.Mheshimiwa Spika, nashauri fedha yote iliyotolewakwa mwaka husika ziwe ring formed na zitolewe kwaWizara na ziwekwe kwa deposit A/C ya mradi aumiradi. Tukifanya hivyo basi, miradi itakuwa fully fundedkatika uhai wote wa utekelezaji wa mradi.Mheshimiwa Spika, aidha, nashauri ukaguziufanyike kama migodi yote inachimbwa tu katikamaeneo yaliyoruhusiwa, ni wazi kwamba uchimbaji wachini ya ardhi siyo rahisi kuona kama mining inafanyikakwa eneo tu lile lililoruhusiwa na lina license,ikigundulika mwekezaji amevuka basi madini hayoyarudishwe kwa Watanzania au thamani ya fedha yamadini hayo ilipwe with interest.Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Simiyu tu umepatanickel na uchimbaji karibu umeanza, lakini kuna utata

mkubwa juu ya watu waliokutwa na mradi huu. Kamainavyojulikana Wilaya ya Busega, Wilaya ya Bariadi naItilima, mfano, Zanzui ina watu wengi sana na watuwana wasiwasi. Sheria inataka resetlement kabla yakuchimba, tunaomba mipango ya kuwapa watu hawamakazi mapya na sisi Wabunge tuelezwe kiuwazi.Mheshimiwa Spika, uongozi mpya wa Wizara hii,Mawaziri wote na Katibu Mkuu wanafanya kazi nzuri nanawapongeza na kuwaomba waendelee kwa ujasirina kwa kujua kwamba Bunge letu litaunga mkonomafanikio katika Wizara hii muhimu, Mungu awabariki.Mheshimiwa Spika, mwisho, nashauri kwa kuwatumefanikiwa kupata asilimia kubwa ya fedha zamaendeleo ya ndani, basi fedha hizi zitolewe kwawakati.MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika,nawapa hongera sana Mheshimiwa Waziri Mhongo,Naibu Mawaziri Simbachawene na MheshimiwaMasele, pamoja na ndugu Maswi Katibu Mkuu waWizara ya Nishati na Madini kwa kazi nzuri mliyofanyakwa kipindi kifupi cha nyadhifa zenu. NaipongezaSerikali kwa kuzindua mradi wa bomba la gesi na kwadhamira njema ya kumaliza mgao wa umeme.Mheshimiwa Spika, pamoja na kazi nzuriwanayoifanya naomba nichangie yafuatayo:-(1) Serikali ifuatilie suala la bili bandia kwa maanaya bili kubwa kuliko matumizi;

(2) Wizara ishirikiane na TBS kudhibiti vifaa bandiavya umeme vinavyoingizwa nchini ili kuzuia hasara namajanga ya moto;(3) Umeme unaosambazwa ulingane na uwezowa mita kwani unapokuwa mdogo zaidi ya mitahauwaki kabisa au unakatikakatika; na(4) TANESCO wakiitwa panapotokea hitilafuwafike mapema ili kuzuia maafa yasiwe yanatokea.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE:Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia katikamaeneo yafuatayo:-Mheshimiwa Spika, kuwawezesha wachimbajiwadogo kuanzisha vituo vya kisasa vya kuchimbamadini katika maeneo ya Rwamgasa-Geita, LondoniManyoni na Pongwe:-(a) Je, ni vigezo vipi vimetumika kuchaguamaeneo hayo tu?(b) Ni kwa nini vituo hivyo visiwepo maeneo yoteyenye madini kwa mfano Mpanda?Mheshimiwa Spika, Serikali imetenga jumla yashilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya kuwaendeleza wachimbajiwadogo wadogo ikiwa ni pamoja na kuwapa mikopokwa mwaka 2012/2013 na je, ni lini na kwa utaratibugani fedha hizo zitagawiwa?, Je fedha hizo zitagawiwa

kwa namna gani? Je, ni kwa maeneo yaliyotajwa tukwa mfano, maeneo ya Nyakuguru, Goronga, Gibasona Mogaviri, Kapalmsenga Mpanda, Ilagala, Ibaga naMpambaa, Isenyela (Chunya) na Makanya (Same),ama ni kwa maeneo yote yenye machimbo Tanzanianzima?Mheshimiwa Spika, katika taarifa ya MheshimwaWaziri, ukurasa 107, ameagiza Kampuni zotezilizochimba madini kwa miaka mitano na kuendelea,zianze kulipa kodi ya mapato bila kuleta visingizio? Je,agizo hilo linaanza lini? Je, mikataba na sheria hazipompaka makampuni hayo yawe na visingizio?Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. KAIKA S. TELELE: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja. Naipongeza sana Serikali kwa kutupatiaumeme wa Jenereta Makao Makuu ya Wilaya yaNgorongoro-Loliondo. Ahadi ya Mheshimiwa Rais yamwaka 2007 imetimia, naomba kufahamishwayafuatayo:-- Ni lini nguzo, nyaya na mita zitapelekwaLoliondo/Wasso ili kusambaza umeme huo?- Nini matokeo ya utafiti wa maji ya Mto Pinyinyikatika kufua umeme, utafiti ambao ulifanywa zaidi yamiaka 10 iliyopita.- Nini msimamo wa Serikali kuhusu uchimbaji nahatimaye ujenzi wa Kiwanda cha Soda Ash huko lake

Natron katika Kijiji cha Engaresero na bonde laEngaruka, Wilayani Monduli?Mheshimiwa Spika, Mgodi wa Naan katika Kijiji chaEnguserogambu ulimilikishwa kwa mchimbaji wa katiJumbe and Partners wa Mjini Arusha licha ya kwambawagunduzi wa madini hayo (spesertite) ni wachimbajiwadogo wa Kijiji cha Enguserosambu-Loliondo. Leseniya Jumbe and Partners (PML) itakwisha muda wakeDisemba, 2012.Mheshimiwa Spika, je, wachimbaji wadogo sasawatamilikishwa machimbo hayo?MHE. ENG. HAMAD YUSSUF MASAUNI: MheshimiwaSpika, nikiwa kama Mjumbe wa Bodi ya Puma Energy,nawapongeza sana kwa uamuzi wenu sahihi wakuamua kuitumia Kampuni hii ambayo ni miliki yaWatanzania kwa asilimia 50. Nataka nikuhakikishiekuwa Puma Energy itatoa ushirikiano na ni fursaambayo tumeshaiazimia kuitafuta kupitia kwenu. Hiindiyo faida ya kuwa na Mbunge angalau mmojakwenye Bodi za Mashirika ya Umma.Mheshimiwa Spika, tahadhari ni kwamba ili kaziyao nzuri isiharibike wasimamie TANESCO ifanyeyafuatayo:-(i) Waimarishe Transmission au Distributionnetwork;(ii)Ongezeni Access hasa vijijini;(iii) Punguzeni losses na ongezeni ufanisi;

(iv) Diversification; na(v) Intergrated water resources managementkwenye catchment areas.Mheshimiwa Spika, kuhusu gesi nashauriyafuatayo:-(a) GU MP na pia izingatie Zanzibar kwani badogesi ni suala la Muungano;(b) Gesi inufaishe watu;(c) Viwanda (vianzishwe viwanda vizito); na(d) Gesi iwe mbadala wa mafuta na ipelekwempaka vijijini watu watumie.MHE. BAHATI ALI ABEID: Mheshimiwa Spika,nampongeza Waziri na Naibu Mawaziri kwa hotuba hiinzuri sana na kwa ujasiri waliouonesha kwa makusudiwa kuwaletea maendeleo Watanzania kwani bila yaumeme wa uhakika viwanda vidogo vya wananchiwalipa kodi vitaendelea kusua sua.Mheshimiwa Spika, bila umeme wa uhakikawawekezaji wa viwanda vikubwa hawatawapata navijana wetu wataendelea kukosa ajira. Gesi itatuokoakwa kuwa na umeme wa uhakika na Wizaraitakaposimamia huu usambazaji wa mabomba ya gesikuja Dar es Salaam basi iangalie na jinsi Mabombahaya yatakavyokwenda mpaka Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii ndio jicho lamaendeleo ya nchi yetu kwani bila ya viongozi imarakama hawa walioteuliwa na Mheshimiwa Rais basiWizara hii haiwezi kwenda Mbele. Iko haja yakuangaliwa watendaji kwa macho mawili ili wasijewakawakwamisha kwa utendaji wao mbovutuliouzoea.Mheshimiwa Spika, baada ya hayo, naungamkono hoja.MHE. DUSTAN D. MKAPA: Mheshimiwa Spika, awaliya yote, napenda kuunga mkono hoja hii ya bajeti yaWizara ya Nishati na madini. Aidha, napendakumpongeza Waziri kwa hotuba yake nzuri, pamoja nayeye nawapongeza Manaibu, Katibu Mkuu naWatendaji wote kwa kuandaa bajeti hii.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii kwasababu kubwa maalum, kwanza ni kwa upatikanaji waumeme Wilayani Nanyumbu (Mangaka naMtambaswala) ndani ya mwaka huu wa fedha2012/2013. Naomba Wizara ihakikishe inatimiza ahadihii bila kukosa.Mheshimiwa Spika, pamoja na maeneoyaliyoainishwa kwenye barua hiyo naiomba Wizaraivipatie umeme vijijini ambamo umeme huo Mangakahadi Mtambaswala ili kuchochea maendeleo katikamaeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, tarehe 21 Julai kulifanyikauzinduzi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwarahadi Dar es Salaam, naipongeza Wizara na Serikali kwakubuni mradi huu mkubwa. Hata hivyo, inaonekanabado wengi wa wananchi wa Mikoa ya Mtwara naLindi hawaelewi kwa nini mradi huu utekelezwe,wanaambiwa na Wanasiasa uchwara kuwawanaporwa uchumi wao. Hivyo, naiomba Wizarakupitia vyombo vya habari magazeti na televisheni itoeelimu kwa wananchi wa maeneo haya ili wajue ni kwanini mradi huu upo na wao watanufaika vipi, ukweli nikwamba wananchi wameupokea kwa mtazamo hasi.Mheshimiwa Spika, wakati wa masika na majiramengineyo, nguzo za umeme zimekuwa zinaangukamara kwa mara, pengine ni nguzo zaidi ya tano auzaidi, hivyo kusababisha kero kubwa kwa wananchi.Naomba kadhia hii irekebishwe na nguzo zichimbiwechini ipasavyo.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaSpika, kwanza naanza kwa kumpongeza MheshimiwaProfesa Muhongo, Waziri kwa uwasilishaji wake mzuri nawenye weledi wa hali ya juu kabisa. Pili, nampongezakwa imani, uvumilivu na moyo wa kujitolea sanakiutendaji. Huu ni mfano wa kuigwa kwa maanahachoki na amekuwa mstari wa mbele katika kulileteaTaifa letu maendeleo kwa kipindi kifupi tangu kuteuliwakwake, lakini siachi kuwapongeza Naibu WaziriMheshimiwa George Simbachawene na MheshimiwaAugustine Massele kwa uwezo mkubwa aliouonesha

kwa kipindi kifupi tu ambacho wameingia katikaWizara husika.Mheshimiwa Spika, kama sote tunavyofahamu,Wizara hii ni kioo na roho ya uchumi wa nchi yetukatika nyanja za kiuchumi, majukumu yake ni mazito nayanahitaji umakini mkubwa sana katika utekelezaji. Niheri tuwaunge mkono na kusaidiana nao katikakurahisisha utendaji wao. Pamoja na hotuba yaokubeba karibu kila kitu na kujibu hoja nyingi, napendanami nitoe mchango wangu katika hotuba husika japokwa uchache.Mheshimiwa Spika, kama hotuba ya Waziriilivyoonyesha uvumbuzi wa gesi asili nchini umekuwa nimkubwa sana, hivyo naishauri Serikali iharakishe kuletaBungeni Sera ya Gesi hatimaye Sheria na Kanuni, hiiitasaidia sana kutoa mwongozo na namna bora yausimamizi wa sekta hii muhimu kwa uchumi wa nchiyetu. Pamoja na yote nasisitiza sana umuhimu washeria hizi kuzingatia maslahi ya wananchi wa maeneohusika lakini Taifa kwa ujumla.Mheshimiwa Spika, napendekeza pia sasa Wizarakupitia TPDC ihakikishe kuwa gesi inatumika kuinuasekta kama kilimo, viwanda na hata usafiri. Mudamrefu sasa tumekuwa tunaagiza kiasi kikubwa chambolea kutoka nje lakini imani yangu kuwa sasatuwekeze vya kutosha katika Viwanda vya Mboleakatika Mikoa ya Lindi na Mtwara.Mheshimiwa Spika, Serikali iwekeze vya kutoshakatika elimu kwa kuwapa kipaumbele vijana ambao

watakuwa tayari kushiriki katika fani za uchomeaji(welding), kuendesha mitambo, umeme na mitaala yaIT ili waweze kushiriki vema katika sekta hii adhimu.Kwa kuwa kwa kipindi cha miaka ya sabini nathemanini Serikali iliwekeza sana kwa kuandaawataalam na kuacha kuendelea kwa kipindi chamiaka ya tisini. Naishauri Serikali, wataalam wotewapewe mikataba maalum ili kuweza kuziba pengokwa kipindi hiki ambacho tunaandaa wataalam wetuwengine. Kutokufanya hivyo ni kupoteza uwekezajimkubwa na pia tutatoa fursa ya wataalam wotekutoka nje ya nchi.Mheshimiwa Spika, Sekta ya Gesi ni pana sanakiasi cha kusema ni mhimili mkubwa sana kwa uchumiwa nchi yetu. Naishauri Serikali itoe elimu ya kutoshakwa wananchi ili wapate kuelewa na kuepukaupotoshaji mkubwa unaofanywa na wasiopendamaendeleo, nashauri waandae hata majaridaambayo yatatoa elimu kwa umma.Mheshimiwa Spika, Serikali ichukue hatua zaharaka kuachana na utaratibu wa kukodi mitambo yauzalishaji umeme na kununua yake, lakini pia miradi yauzalishaji wa umeme kwa makaa ya mawe ipewekipaumbele cha kutosha nchini ili TANESCO ijiendeshekwa faida na kutoa unafuu kwa wananchi.Mheshimiwa Spika, Serikali ione umuhimu waushirikiano na nchi ya Trinidad and Tobago kwa kuwani wa kuenziwa na kuutilia maanani sana. Kwa kipindikirefu Balozi wao ameomba kutambuliwa na hajapewaithibati hii mpaka sasa.

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa naombanikushukuru kwa kunipa miradi mingi ya umeme kwavijiji katika Jimbo la Kilwa Kaskazini na kunipokeleamaoni yangu kwa kuamini kuwa yatafanyiwa kazistahiki. Nakutakia kila la heri na namwomba Munguatulinde sote.Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha nanaunga mkono hoja.MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Spika,kwanza nampongeza Waziri, Manaibu Waziri naWatendaji wote wa Wizara na Mashirika na wakalachini ya Wizara kwa kazi yao nzuri ya kuandaa bajeti hiiya Wizara ya Nishati na Madini. Naomba nitoe ushauriwangu kwa Serikali katika mambo sita kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Sheria ya Madiniya mwaka 2010, taarifa ya Jaji Bomani kuhusu sekta yaMadini ilitusaidia kutayarisha Sheria ya Madini yamwaka 2010, baadhi ya mambo mazuri katika Sheriampya ya Madini ni pamoja na:-- Kuongeza viwango vya mrabaha naunaotozwa kwenye gross badala ya netback value,tunashukuru Serikali imeweza kukamilisha mazungumzona kuziwezesha Kampuni zote za madini zenyemikataba kuanza kulipa mrabaha kwa matakwa yaSheria ya Madini ya mwaka 2010.- Serikali kuwa mwekezaji kupitia STAMICO nakuweza kupata Hisa (free carried interest na hisa za

kununua) kwenye migodi. Serikali ianzishe mazungumzona migodi iliyopo na itakayoanzishwa kama KabangaNickel, Dutwa Nickel, ARMZ Uranium, Panda hillPyrochloral na mingine ili kukabiliana kuhusu freecarried interests na hisa za kununua.- Migodi kuweka hisa zake kwenye Soko la MitajiDar es Salaam ili wananchi waweze kununua.Makampuni yote yalazimishwe kuweka hisa zakekwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam na wananchi nahasa Watanzania wenye uwezo wahamasishwekununua hisa hizo ili wawe wawekezaji kwenye sekta hiimuhimu.- Serikali kuzilazimisha kampuni za uchimbajimadini nchini kununua huduma na vifaavinavyopatikana nchini, ziandaliwe Kanuni na taratibuzitakazohakikisha kampuni hizi zinanunua bidhaa nahuduma za ndani. Kampuni zihamasishwe kuanzishamiradi ya wananchi kuwasaidia kuweza kuzalishabidhaa zenye ubora unaoweza kutumika migodini.- Kutoa fidia, kuwajengea makazi nakuwahamisha wananchi wanapisha ujenzi wa migodi(compensation, reallocation and resettlement), Wizaraya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Wizara yaArdhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi zirekebisheSheria ya Ardhi ili iweze kutekeleza matakwa ya sheriaya madini inayoanzisha suala la fidia lisiwe tatizo tena.Mheshimiwa Spika, pamoja na kutekelezamatakwa ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010, ni vizuripia Serikali ikakamilisha mapema marekebisho ya

Sheria ya Usonara na Sheria ya Baruti. Naiomba Serikalikutekeleza mambo hayo mapema ili kuhakikishayanayotokana na sekta ya madini yanaongezeka.Mheshimiwa Spika, kuhusu kuimarisha usimamiziwa sekta ya madini nchini, sekta hii ni sekta muhimusana ya uchumi nchini na inahitaji kuwa eneo lakipaumbele la Serikali ili kukuza uchumi wa Taifa kwaharaka. Kulingana na Sheria ya Madini ya mwaka2010, Idara ya Madini ni msimamizi mkuu wa Sekta yaMadini lakini haipewi kipaumbele na Serikali katikakupata watumishi wa kutosha na bajeti ya kutosha.Kwa hiyo, naishauri Serikali ishughulikie mambo mawiliyafuatayo:-- Ifanye Idara ya Madini kuwa Idarainayojitegemea kibajeti kama ilivyo Jeshi la Polisi auJeshi la Magereza, inahitaji kupewa Vote yake ili kwakutumia mtandao wa Idara ya Madini ulioenea nchinzima turahisishe usimamizi wa sekta ya madini. Kwakufanya hivyo, bajeti ya Idara, vitendea kazi, maslahiya wataalam na uwezo wa Idara kusimamia sekta yamadini vitaboreka; na- Ianzishe mpango maalum wa kuajiri wataalammbalimbali wanaohitajika kwenye Idara moja kwamoja kutoka vyuo vikuu kwa kipindi maalum, badalaya kuwatafuta wataalam hao kwenye soko. Mpangohuu utajaza pengo la uhaba wa wataalam kwenyeIdara ya Madini, kwa sasa nafahamu hali ya uhaba wawataalam kwenye Idara ya Madini ni mbaya sana.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kutunza dhahabu safikwenye hazina ya Taifa; niliwahi kushauri na nashauritena kuwa kutokana na bei ya dhahabu kuendeleakupanda kwenye soko la dunia karibu miaka 10 sasana itaendelea kupanda na kutokana na ukwelikwamba ni madini ya dhahabu yanayowakilishathamani ya fedha (sarafu) duniani ni wakati muafakasasa nchi yetu kuanza kutunza dhahabu kwenyehazina ya nchi yetu ili kuweza kurekebisha thamani yasarafu yetu inapoanguka.Mheshimiwa Spika, Marekani, mifano ya nchizinazotunza dhahabu kwa wingi katika hazina za nchizake ni pamoja na tani 8,000; Ujerumani zaidi ya tani3,000; Afrika Kusini zaidi ya tani 723 na Uingereza tani300; Swaziland tani 1,300; European Central Bank tani766. Yapo pia Mashirika ya Kimataifa kama Benki yaDunia zaidi ya tani 34,000 na IMF zaidi ya tani 4,000.Mataifa haya na nchi hizi ni mifano mahsusi ya nchizinazotumia dhahabu kujiwekea utajiri na kutunzathamani ya sarafu zao.Mheshimiwa Spika, napendekeza Wizara ya Nishatina Madini ishauriane na Wizara ya Fedha na Benki kuukuanzisha mchakato huu wa kutunza dhahabu kwenyeBenki Kuu ya Tanzania (sheria ya Benki Kuu inaruhusukufanya hivyo). Hii itatuimarisha kiuchumi, namna yakupata dhahabu, hii ni pamoja na kufanya yafuatayo:Kulipwa mrabaha na makampuni ya madini, sehemuya mrabaha katika dhahabu safi, kuanzisha utaratibumzuri wa kununua dhahabu hii kutoka kwa wachimbajiwadogo na Shirika la STAMICO kuwekeza kwenye

uchimbaji wa dhahabu na kuweka hazina ya dhahabuBenki Kuu ya Tanzania.Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo nchiniwanaweza kuwa na mchango mkubwa kwenyeuchumi wa Taifa letu wakitayarishwa na kuendelezwavizuri. Wachimbaji wadogo wa dhahabuwaendelezwe, wachimbaji wadogo hawa wanahitajikusaidiwa kupata mitaji, vitendea kazi na masoko ilishughuli zao za uchimbaji ziwe na tija. Naishauri Serikaliifanye mambo makuu yafuatayo:-- Iendelee na mchakato wa kuanzisha Mfukowa wachimbaji wadogo wa kisheria ili uwezekuchangiwa na wadau mbalimbali. Nakumbukamchakato huo wa kutayarisha Waraka wa Baraza laMawaziri ulikwishaanza, ukurasa wa 98, kifungu cha 172kwenye hotuba ya Waziri inaonesha kwamba Wizaraimetenga bilioni 2.5 (fedha za ndani) kwa ajili yawachimbaji wadogo, lakini haioneshi hatua iliyofikiwakuanzisha Mfuko huu muhimu. Serikali ilipe umuhimusuala hili kwa vile linaweza kuwakomboa wachimbajiwadogo. Mfuko huu uimarishwe uwe wa kisheria naunaweza kuchangiwa na wadau mbalimbali bada yakutenga fedha tu kutoka Serikalini;- Ishirikiane na sekta binafsi kuanzisha ununuziwa dhahabu yote ya wachimbaji wadogo ilikuhakikisha dhahabu hii haitoroshwi nje, tuige nchi yaGhana ambayo imeanzisha utaratibu wa kununuadhahabu na madini mengi mengine ya wachimbajiwadogo wote. Naomba Serikali ikajifunze Ghana, waowalianzisha mpango unaojulikana kwa jina la Precious

Minerals Marketing Corporation (PMMC) naumefanikiwa sana kuwaendeleza wachimbaji wadogohususan kuwapatia wachimbaji wadogo soko lamadini na kuongeza pato la Taifa la Ghana; na-Ihakikishe matumizi ya zebaki katika uchenjuaji wamadini ya dhahabu, kwa kuwasaidia na kuwaelekezawachimbaji wadogo namna ya kupata na kutumiavifaa vya tetorts na ama kutafuta njia mbadala yakuchenjua dhahabu bila kutumia zebaki kama vilekuyeyusha dhahabu eneo hilo hilo inapochimbwa.Mheshimiwa Spika, kuhusu mgawanyo waMrabaha; taarifa ya Jaji Bomani kuhusu sekta yaMadini ilishauri mgawanyo wa mapato yatokanayo namrabaha wa madini kati ya Serikali Kuu na Serikali zaMitaa vikiwemo vijiji vinavyozunguka migodi uwe kamaifuatavyo: asilimia 60 ya mrabaha iende kwenye Mfukowa Maendeleo ya Madini (the mineral developmentfund), asilimia 20 ya mrabaha iende kwenye Mamlakaya madini inayopendekezwa kuundwa katika sehemuya taarifa hii, asilimia 10 iende Wilaya yenye mgodi,asilimia saba iende kwenye Halmashauri nyinginekatika Mkoa wenye mgodi na asilimia tatu iendekwenye vijiji vinavyozunguka mgodi.Mheshimiwa Spika, bado naamini huu ulikuwa niushauri mzuri sana ambao ungesaidia sana wananchiwa kwenye maeneo ya madini kupata manufaa.Manung’uniko kutoka kwa wananchi wa maeneohaya kuhusu mgawanyo wa mapato ungemalizikakabisa.

Mheshimiwa Spika, nakumbuka nikiwa Kamishnawa Madini, Wizara wa Nishati na Madini ilishauri Barazala Mawaziri mapendekezo haya ya Kamati ya Raisyatekelezwe kwa kuacha fedha kidogo kwenyeHalmashauri na Vijiji husika na fedha zingine ziendeleekupelekwa Hazina kama inavyofanyika sasa. Bahatimbaya ushauri huo haukupokelewa, bado naaminisuala hili ni la manufaa sana kwetu, naomba Wizarailiangalie upya ili kuishauri Serikali tena kuwaachiaasilimia kidogo tu wananchi wa maeneo inakozalishwadhahabu.Mheshimiwa Spika, Wakala wa Ukaguzi wa Madini(TMAA); kazi yake kubwa ni kukagua uwekezaji ilimakampuni ya madini yaweze kulipa kodi ya mapatostahiki, ukurasa wa 65 kifungu namba 113 cha hotubaya Waziri wa Nishati na Madini kinaonesha kuwamafanikio makubwa ya wakala huu ni kuwezeshaKampuni ya Resolute kulipa shilingi bilioni 37.2 nakwamba kazi hii imefanywa kwa ushirikiano na TRA.Aidha, ukurasa 106 kifungu Na. 188, unaonesha kuwakazi kubwa ya TMAA ni kufanya kazi ya ukaguzi wauwekezaji ikishirikiana na TRA.Mheshimiwa Spika, hii inaonesha wazi kuwatumeunda wakala kufanya kazi zinazofanana na TRAna sehemu nyingine inaonesha TMAA inafanya kazi zilezile za Idara ya Madini, kwa mfano, tangazo la Wizarakuhusu kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji holela wamchanga katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwanikwenye gazeti la Habari leo la tarehe 11 Julai, 2012ukurasa wa saba (7) linadhihirisha wazi kuwa TMAAinafanya kazi za Idara ya Madini.

Mheshimiwa Spika, ukisoma malengo, majukumuna kazi za TMAA zilizoainishwa kwenye frameworkdocument ni zilezile za TRA, Idara ya Madini yaaniKamishna wa Madini kwa maana ya Mkaguzi Mkuu waMigodi na Makamishna Wasaidizi wa Kanda naWakaguzi wa Migodi wengine na sehemu ya biasharana uchumi, lakini pia ukaguzi wa mazingiraunaofanywa na TMAA unaingilia kazi halisi za NEMC nakitengo cha Mazingira cha Wizara.Mheshimiwa Spika, pamoja na sifa zotezinazotolewa juu ya utendaji wa TMAA, lakini tunawezakulisaidia Taifa zaidi tukipunguza matumizi kwakuhakikisha kazi hizo zinafanywa na Taasisi moja tu, nivema kujifunza na kuiga mifano ya nchi za Ghana,Canada, Marekani na Austaralia ambapo masuala yaukaguzi wa uwekezaji yanafanywa na Mamlaka zamapato za nchi hizo na masuala ya ukaguzi wa migodiukiwemo ukaguzi na ukusanyaji wa mrabahahufanywa na Idara zinazosimamia sekta ya madini.Mheshimiwa Spika, hali hii ya kuwa na Taasisikubwa inayofanya kazi zile zile za Taasisi zingine siyohekima ni kutumia fedha za Serikali vibaya. NaishauriWizara ishauriane tena na wadau wengine yaani TRA,NEMC na Idara ya Madini GST na hata TanzaniaNational Audit kuondoa mwingiliano huu. Ujuzi wawataalam wa TMAA tulioujenga ni muhimu sana kwaTaifa lakini unatakiwa kuwekwa mahali pake ili tupatethamani ya kazi yao (value for money).Mheshimiwa Spika, ahsante nashukuru na naombakuunga mkono hoja.

MHE. MBAROUK SALIM ALI: Mheshimiwa Spika,nichukue fursa hii kuipongeza safu ya uongozi yaWizara ya Nishati na Madini inayoongozwa naMheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo, kitendokilichofanywa na uongozi huo wa Wizara kwakugundua wizi mkubwa wa fedha za Serikali toka kwaShirika la TANESCO, huu ni mfano, ni jinsi gani Serikaliinavyopoteza pesa kwa watendaji wasioaminika.Nashauri Makatibu Wakuu wengine pia waige mfanowa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, ili nchiyetu itoke katika wimbi kubwa la umaskini.Mheshimiwa Spika, Wizara hii ni muhimu sana nabila utendaji wa ufanisi mkubwa wa Wizara hii, basiumaskini wa Tanzania hauwezi kuondoka. Hivyo basi,pamoja na Serikali kuongeza bajeti ya Wizara hii lakinibado ni kidogo na kuna haja kubwa ya kuongezewapesa ili waweze kutekeleza miradi mingi ya umeme,kama ripoti ya Kamati ilivyoainishwa sasa tuwe naslogan la Nishati Kwanza.Mheshimiwa Spika, Waziri katika uzinduzi wabomba la gesi alitamka kuwa kuna gesi nyingiiligundulika ambayo Tanzania inaweza kukusanya zaidiya trilioni 626.71. Huu ni utajiri mkubwa kwa nchi yetu,wasiwasi mkubwa ni jinsi gani nchi yetu imejipangakatika usimamizi wa rasilimali hii ya gesi na ili tuwezekusimamia vizuri, tunahitaji kuwa na mikakati endelevuili tuweze kuiendesha nishati hiyo vizuri. Hii ni pamojana kuwa na wataalam wa kutosha katika ngazi zote(downs stream and up stream). Sera na sheria za gesi

ni muhimu ziharakishwe ili ziweze kustawisha usimamizibora wa sekta hii ndogo ya gesi.Mheshimiwa Spika, suala la umeme vijijini bado nitete kwani kasi ya uwekaji wa umeme vijijini bado nindogo sana, fedha walizotengewa REA ni ndogo sanapamoja na kwamba zimeongezwa. Nashauri REAwawezeshwe zaidi ili wakala huu uweze kutekelezamiradi mingi ya umeme vijijini. Mwaka janatulipandisha kodi ya mafuta ya taa kwa azma kuwa,fedha hiyo ingekwenda katika Mfuko wa REA, tatizokubwa hilo halikufanyika na sasa kuna kadhia kubwaya mafuta ya taa vijijini na umeme pia hakuna.Mheshimiwa Spika, Wakala wa Geologia ni sektamuhimu sana, zaidi ya kutambua miamba, lakiniWakala huu pia wana uwezo wa kutambua majangakama tetemeko la ardhi, pamoja na umuhimu waWakala huu, lakini fedha wanazopata ni kidogo nakwa sababu hiyo wanakuwa hawana uwezo wakufanya kazi zao kwa ufasaha. Nashauri Wakala huuuwezeshwe zaidi na kupewa vifaa vya kisasa nanyenzo nyinginezo ili waweze kufanya kazi vizuri.Mheshimiwa Spika, niipongeze tena Wizara kwamabadiliko ya kiutendaji yanayoanza kuonekana nanaomba kuchangia hoja, lakini na kuunga mkonobajeti ya Wizara hii. Ahsante.MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Spika, awali yayote nimshukuru Mungu kwa kuniwezesha siku ya leokuweza kutoa mchango wangu wa maandishi,naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Nishati na

Madini kwa kuleta hotuba yenye matumaini kwaTanzania, hivyo hivyo kwa Watanzania kwa ujumlawake. Nchi yetu ni siku nyingi mara kwa maraimekuwa ikitumbukia kwenye kiza, kiza ambachoWatanzania walikuwa wakijiuliza nini hasakinachosababisha tatizo hili.Mheshimiwa Spika, imekuwa ni aibu nchi yetu kwamajirani zetu lakini hata dunia kwa ujumla. Nchi yetuimekuwa ikisifika duniani kote kwa jinsi MwenyeziMungu alivyoineemesha kwa rasilimali nyingi, leoimekuwaje nchi hii mara kwa mara iwe inatumbukiakwenye kiza?Mheshimiwa Spika, tuangalie majirani zetu Kenyailiwahi kupata mtikisiko wa umeme unaofanana na wanchi yetu wa kutumbukia katika mgao wa umeme wanchi yetu wa kutumbukia katika mgao wa umeme,lakini majirani zetu hawa Kenya tatizo hili halikuchukuamuda mrefu liliisha wakati majirani zetu hawa hawanarasilimali za kuweza kutushinda. Tatizo la kiza kwamajirani zetu lilisha kabisa hadi leo na walahawazungumzii tatizo la umeme kwenye nchi yao.Mheshimiwa Spika, leo Mheshimiwa Waziri waNishati na Madini baada ya muda mfupi tu kushikaWizara hii ameonesha kwa jinsi alivyo na nia yakuliondoa giza hili ambalo limekuwa sugu kwa nchiyetu, lakini pia ameonesha jinsi alivyo na uwezo katikasekta hii. Kwa kuwa tatizo hili limekuwa sugu la sikunyingi bila kujua tatizo ni nini na kwa kuwa sasa tatizolimejulikana kwamba kuna watu ambao kwa maslahiyao binafsi ndio ambao wanatusababishia tatizo hili la

nchi muda mwingi kuwa kwenye giza, jambo ambalolinatusababishia hasara kubwa kwa nchi yetu.Mheshimiwa Spika, vile vile wapo hataWaheshimiwa Wabunge ambao wanahusika auwanashirikiana na wahalifu hawa ambaowanaisababishia nchi yetu hasara kubwa, ni kwa niniwasitajwe hadharani hasa hapa Bungeni ili Watanzaniawote waweze kuwafahamu.Mheshimiwa Spika, wapo baadhi ya Wabungehapa Bungeni muda wote wanaosimama hujifanyawao ni waadilifu na waaminifu kwa nchi hii, vile vilekwa wananchi. Inasikitisha sana kuona Wabunge haohao kumbe ndio ambao wanasimama kwenye Bungehili na hata kwenye vyombo vya habari kuwezakuwatetea Mafisadi hao na Madhalimu hao kwa nchiyetu.Mheshimiwa Spika, nitamwomba MheshimiwaWaziri wakati wa kufanya majumuisho atuambie pindiKamati itakapoundwa kwa ajili ya kufanya uchunguziwa jambo hili zito na wakabainika baadhi ya Wabungekuhusika na kushirikiana na Mafisadi hawa, nini kauli yaSerikali.Mheshimiwa Spika, inasikitisha na inastaajabishakwamba zipo nchi nyingi ambazo zinategemearasilimali moja tu kwenye nchi hizo, lakini zimepigahatua na zinazidi kusonga mbele leo itakuwaje kwanchi yetu tuna rasilimali zote ambazo Mwenyezi Munguameziumba na kubwa zaidi tunayo rasimiali ambayohaipatikani dunia nzima yaani Tanzanite. Leo vipi nchi

hii baada ya kusonga mbele iwe tunarudi nyuma amasababu ni hii ya watu kama hawa ambao wanajalimaslahi yao kuliko maslahi ya nchi hii?Mheshimiwa Spika, sasa wakati umefika wakuweka mambo bayana, Mafisadi wote kuwekwahadharani na kutajwa kwa majina yao pamoja naWabunge hao wanaowatetea Mafisadi hao ili nchiisonge mbele.Mheshimiwa Spika, ahsante sana.MHE. AGRIPINA Z. BUYOGERA: Mheshimiwa Spika,napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza tenaMheshimiwa Rais kwa uteuzi alioufanya waWaheshimiwa Wabunge kwa mara ya kwanza.Mheshimiwa Spika, tangu nimekuwa Mbunge hiindio hotuba ya kwanza ya Wizara ya Nishati na Madiniambayo imekidhi matakwa ya Bunge kwa uwazi wautendaji.Mheshimiwa Spika, nawapongeza Mawaziri wotewa Wizara hii na napenda kumtia moyo Katibu Mkuu iliafanye kazi kwa kufuata Sheria, Kanuni na taratibu bilawoga wowote kwa kuwa atatatua kero za Watanzaniawote. Pamoja na pongezi zangu kwa Wizara naombanami nikumbukwe kwa niaba ya wananchi wa Jimbola Kasulu Vijijini kupatiwa umeme, hasa katika Kata zaTitye na Rungwe mpya ambako kuna maporomokomakubwa ya maji ambayo tunayatumia katika miradiya umwagiliaji wa kilimo cha mpunga na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, tunashukuru kupata umemeMakao Makuu ya Wilaya ya Kasulu, lakini katika Jimbola Kasulu Vijijini lenye Kata 19 hakuna Kijiji hata kimojaambacho kimepatiwa umeme.Mheshimiwa Spika, mMiradi mikubwa yote iliyokoWilaya ya Kasulu hususan miradi ya kilimo iko Jimbo laKasulu Vijijini, hivyo ni vyema kutupatia umeme wakutusaidia kufanikisha malengo ya Serikali ya kuondoaumaskini, miradi hiyo ni kama ifuatayo:-(1) Mradi wa Kilimo kwanza;(2) Mradi wa umwagiliaji; na(3) Mradi wa Kilimo cha miwa ili kuzalisha sukarina mazao mengi ya biashara na chakula.Mheshimiwa Spika, katika Kijiji cha Makere kunamadini ya chokaa ambayo yalitumika kujengamajengo yote ya Serikali katika Mkoa wa Kigoma,tangu wakati wa Mkoloni mpaka leo hii, lakini leo hiiwazalishaji au wachimbaji wadogo wanasumbuliwasana na Idara ya Maliasili na Utalii bila kujali leseni zao.Napenda kujua ni lini Wizara itakuja Kasulukuwatembelea vijana hao ili kuwapatia ushauri wakitaalam ili wachimbe chokaa kwa faida na ubora wabidhaa hiyo.Mheshimiwa Spika, Kata zinazohitaji umeme nikaribu zote kama nilivyotaja hapo juu. Je, ni lini REAwatakuja kutembelea huko? Kwa kuanzia niombe Kata

zifuatazo ziangaliwe: Kata ya Kitagata, Kata yaKurugongo, Kata ya Titye, Kata ya T/Mpya, Kata yaRusesa, Kata ya Kasangezi, Kata ya Muzye, Kata yaHeruushingoMheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Spika,naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwakunijalia uhai na uzima na leo hii nikaweza kuchangiakatika hotuba hii ya Wizara ya Nishati na Madini na pianampongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kwa kumchagua Waziri waNishati na Madini Mheshimiwa Sospeter Muhongo, ninaimani kubwa kuwa Wizara hii sasa itafanya kazi kwaufanisi mkubwa, tatizo kubwa lililoikumba Wizara hii niubadhirifu na ufisadi ambao watendaji wengi Wizaranina kwenye Taasisi zake hasa TANESCO, nashauri Waziriawafanyie utafiti sana watendaji wa TANESCO.Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali iangalie upyamikataba mibovu ya kufua umeme na mikataba yamadini. Hii ndio inayotia hasara Serikali kwa kiasikikubwa. Makampuni yanayochimba madiniyachunguzwe sana, hawa wana tabia ya kutoroshamadini bila Serikali kujua. Tabia hii inaitia Serikali hasarakubwa sana.Mheshimiwa Spika, gharama za umeme zimekuwani ghali sana, kiasi cha kuwa wananchi walio wengiwanashindwa kumudu gharama hizi za umeme.Naiomba Serikali iangalie upya gharama za umeme ili

wananchi wa kawaida weweze kumudu gharama hiziili na wao waweze kufaidika na umeme.Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali manufaa yagesi yainue uchumi wa nchi yetu na pia maisha yawatu yaweze kuboreka kwa neema hii ya gesiMwenyezi Mungu aliyotupa. Serikali iwe makini katikamikataba ya kuzalisha gesi tusije kuwa kama kwenyemikataba ya madini ambayo mpaka leo hii tunaionainavyoathirika katika nchi yetu hasa ile ya Barrick GoldMine.Mheshimiwa Spika, ukiumwa na nyoka ukiona ukutihuachi kushtuka, huu ni msemo wa Kiswahiliunaotuonesha athari ya mikataba hii mibovu, ni lazimatuogope isije ikatupata tena.MHE. GEORGE H. MKUCHIKA: Mheshimiwa Spika,napenda kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri ya kuvunagesi ya Mnazi Bay na kuzalisha umeme, matatizo yamgao wa umeme katika Mkoa wa Mtwarayamepungua na unapokatika ni masuala yamiundombinu tu siyo kwamba umeme haupo.Naipongeza Serikali kwa kutoa umeme toka Mtwarahadi Newala ambako imetuwezesha kusukuma majisaa zote na hatimaye kupunguza tatizo la upatikanajiwa maji kwa kiasi kikubwa.Mheshimiwa Spika, kwa miaka ya nyuma Serikaliiliahidi wananchi wa Mtwara kuwa kuna mradi maalumwa kuunganisha umeme majumbani kwa bei nafuuisiyozidi shilingi 70,000/= kwa nyumba. Wanasiasa nahasa Wabunge wa Mkoa wa Mtwara na Lindi

tuliwahamasisha wananchi kuwaandaa kwa shughulihii, bahati mbaya mradi huu ulikufa baada yawafadhili kujitoa. Naiomba Wizara ifanye mpango wakufufua mradi huu ili wananchi wa Mtwara ambaowanazalisha gesi waweze kunufaika.Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na urasimumkubwa kwa TANESCO kuunganisha umeme katikanyumba za watu hata pale ambapo umeme uko kwamfano, Kijiji cha Kikunga, Wilayani Newala kina umemekwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita. Tangu wakati huowatu wengi wamefanya wiring lakini bado kuingiziwaumeme. Jirani yake Kijiji hiki kimeungana na Vijiji vyaAmani na Pachoto, hakuhitajiki transformer, vijiji hivivimeomba kuunganishiwa umeme, lakini hakunahafua. Naomba vijiji hivi vishughulikiwe ipasavyo.Nashukuru kwa Vijiji vya Mtangalanga, Makonga naLengo, tayari vimetengewa fedha na za kupelekewaumeme. Naomba tuharakishe.Mheshimiwa Spika, mwisho wako wanaochocheawatu wa Mtwara wakatae kupeleka gesi Dar esSalaam. Wanasiasa tumewaeleza wananchi kuwa gesiinayobaki Mtwara inatosha kuzalisha umeme wa Mkoamzima. Ili wananchi waendelee kutuamini ni lazimatuongeze kazi ya kusambaza umeme vijijini ndani yaMkoa wa Mtwara.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. WARIDE BAKARI JABU: Mheshimiwa Spika,nampongeza Waziri wa Nishati na Madini kwauwasilishaji wake wa bajeti hii. Napongeza Wizara kwa

kupitia TANESCO na ZECO kwa makubaliano waliyofikiakupitia kero za Muungano, lakini nashauri yale mamboyaliyobakia kama bei ya distribution power kwa ZECOna mengineyo nayo yatafutiwe ufumbuzi, lakini piamakubaliano yaliyofikiwa ya kupunguza bei ya unitkwenye KVA, Pemba iwekwe sawasawa na Unguja ilikuwapunguzia mzigo wananchi wa Pemba.Mheshimiwa Spika, Bomba la gesi kutoka Mtwarampaka Dar es Salaam, nashauri Wizara ifikirie bombahilo kufikishwa Zanzibar kwa ajili ya matumizi yamajumbani kwani bei ya gesi ni rahisi kuliko umeme.Mheshimiwa Spika, Serikali itafute alternativesources za umeme kama geofarm, mawimbi ya Baharina mawimbi ya upepo kama ule unaotaka kuwepoSingida ili kuweza kuchangia umeme uliokuwepo.Mheshimiwa Spika, ahsante na naunga mkonohoja kwa asilimia mia moja.MHE. OMARY A. BADWEL: Mheshimiwa Spika,Wilaya ya Bahi haizingatiwi sana katika kupatiwa miradiya umeme vijijini na hivyo kuwa Wilaya ya mwisho kwaidadi ya kijiji kimoja tu ambacho kazi ya kupelekaumeme inaendelea katika Mkoa wa Dodoma.Mheshimiwa Spika, vipo vijiji ambavyo vipo karibuna umeme ulipo ambapo ni kati ya kilometa tatu hadisita tu lakini havijawekwa katika mpango wa kupatiwaumeme licha ya mimi binafsi na viongozi wote waWilaya kufanya juhudi ili vijiji hivyo viingizwe katikampango wa REA, lakini sijapata mafanikio. Naomba

Wizara iipe pia umuhimu Wilaya ya Bahi, vijiji vyakevipatiwe umeme.Mheshimiwa Spika, hapa chini nakuonesha vijiji naumbali toka chanzo cha umeme kilipo:-(a) Mpunguzi (Dodoma Mjini) - Chibelela (Bahi)kilomita tatu;(b) Chigongwe (Dodoma Mjini) - Kigwe ( Bahi)kilomita sita;(c) Ibugule (Bahi) - Mtitaa (Bahi) kilomita tatu; na(d) Mpamautwa (Bahi) Kijiji hiki umeme umepitalakini haujashushwa hadi leo, naomba ushushwe.Mheshimiwa Spika, natarajia majibu ya uhakika yaWilaya ya Bahi kupata umeme katika vijiji hivyo hapojuu.MHE. JAMES D. LEMBELI: Mheshimiwa Spika,napenda kuanza mchango wangu kwa kusemanaunga mkono hoja, lakini pamoja na kuunga mkonohoja nina machache yafuatayo:-Mheshimiwa Spika, Wizara ifuatilie kwa karibuutekelezaji wa ahadi ambazo zimetolewa naMakampuni ya Madini kwa wananchi wanaoishikandokando ya migodi. Ahadi hizo ni pamoja namalipo ya fidia kwa vifaa na mali za wananchi ambaowalihama maeneo kupisha uchimbaji. Kwa mfano,wananchi wa Vijiji vya Mwime, Mwendakulima naChapulwa hadi leo wapo baadhi ya wananchi ambao

ado wanadai malipo yao ya fidia, lakini mgodi waBuzwagi (viongozi) na Barrick Gold hawataki kutimizawajibu wao.Mheshimiwa Spika, Serikali ifuatilie kwa karibumahusiano yaliyopo baina ya wawekezaji migodi nawananchi kwa mfano pale Buzwagi hivi ni sahihi mgodikuwa na maji ambayo yanatumika kumwagilia hatabarabara wakati wanakijiji waliopo mita 100 tokakwenye uzio wa mgodi hawana maji na wanafuatamaji hadi kilomita tano. Je, haya maisha mazuri bainaya majirani?Mheshimiwa Spika, naomba sana Waziri na Naibuwafuatilie hali ya mahusiano yaliyopo baina ya migodina wananchi ili kuondoa tatizo ambalo likiruhusiwakuendelea litasababisha hata uvunjifu wa amani.MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaSpika, naomba kwa dhati ya moyo wanguniwapongeze wafuatao: Mheshimiwa Waziri, NaibuMawaziri wawili lakini pia Katibu Mkuu wa Wizara hii yaNishati na Madini kwa jinsi ambavyo wameanza kazikatika Wizara hii ambayo iligubikwa na jinamizi laubadhirifu wa mali ya umma, ufisadi uliokithiri narushwa ambayo ilitishia uhai, hususan ndani ya Shirika laUmeme (TANESCO).Mheshimiwa Spika, madini yamechangia pato laTaifa kwa asilimia 3.8 kwa sasa. Kwa kweli kutokana nahali halisi ya rasilimali ambayo tumejaliwa kuwa nayoya madini ambayo tumeyachimba na ambayotunatarajia kuyachimba, mchango wa rasilimali hii

haujaweza kuisaidia nchi hii kuondokana na dimbwikubwa la umaskini. Ni vyema udhibiti kutokana nautoroshaji wa madini yetu upewe kipaumbele, pia nivyema kuangalia upya mikataba yote na leseniambazo wamepewa wawekezaji hasa katika maeneoya wawekezaji na wachimbaji wadogo wadogo.Mheshimiwa Spika, ni vyema kuona ushauri wawananchi kwa kupitia Halmashauri zetu kushirikishwakuanzia hatua za awali ili kuondokana na matatizo namigogoro inayotokea.Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme, napongezakwa dhati operesheni inayoendelea sasa hivi nchinihususan katika Jiji la Dar es Salaam kwa wale woteambao wanajiunganishia umeme kinyemela nakulikosesha Shirika mapato. Hata hivyo, naiombaWizara iangalie vizuri suala hili kwani kuna uwezekanomkubwa wa wafanyakazi wa TANESCO ambao siowaaminifu, wanahusika moja kwa moja nauunganishaji, wizi na ubadhirifu huu ambao kwa sasahatia na hasara inawaangalia wananchi peke yao. Nivyema watendaji wote watakobainika kushirikiana nawanachi hao, wachukuliwe hatua za kinidhamu.Mheshimiwa Spika, deni wanalodaiwa Pan AfricaEnergy ni vyema lifuatiliwe na lilipwe harakaiwezekanavyo na madai yao wameeleza karibumabilioni ya shilingi, naomba Waziri ashauriane naCAG ili hesabu zao wanazosema zikaguliwe na ukweliuweze kujulikana.

Mheshimiwa Spika, kuhusu gesi asilia, naiombaWizara yafuatayo:-- Kuwekeza kwa kuwapatia elimu wazawakuhusiana na uchimbaji, usafirishaji na hata uuzaji wagesi;- Gas Company ifufuliwe haraka iwezekanavyokwani itasaidia kuratibu shughuli zote zinazohusiana nasekta hii;- Sera ya Gesi pamoja na Sheria zake ziharakishwena ziwe wazi hasa kwa Halmashauri zote ambazo zikokatika Mikoa ya Kusini ambapo bomba la gesi linapita,lakini pia kwa wadau ambao wanahusika na sekta hii;na- Ni dhambi kubwa iwapo Wizara itatoa misamahaya kodi kwa wawekezaji katika sekta hii ya gesi (tusijekurejea makosa ambayo yamefanyika katika madini).MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: Mheshimiwa Spika,ni dhahiri kwamba Wizara hii imepata Waziri, ManaibuWaziri na Katibu Mkuu ambao ni waadilifu na waaminikwa nchi yao na kwa wananchi wa Tanzania. Ni wazikwamba matendo maovu yaliyokuwa yakitendekandani ya Wizara hii ni ukweli kwamba yalikuwayakipangwa kwa makusudi. Yaliyojitokeza kwa Wizaraya Nishati na madini ni somo kwa Wizara nyingine zotena kama zitashindwa kupata somo kwa kuiga Wizarahii ni vyema na wao wakawajibika kwa sababuwatakuwa bado hawajaweza kupambanua maovu nawaovu.

Mheshimiwa Spika, Tanzania si nchi ya kuwa ombaomba, lakini imefikia hatua hiyo kutokana na tabia yawatu waliokuwa hawana uchungu na nchi piahawaangalii maslahi ya Watanzania walio na kipatocha chini. Leo Wizara hii ndani ya kipindi cha miezimitatu imekuwa na uwezo wa kukusanya billioni sitakwa mwezi, jambo ambalo miaka yote lilikuwa halipo.Tuna wajibu wa kupata maelezo ya kina kutoka kwaSerikali ni kwa nini Wizara hii chini ya Waziri Muhongoiweze kukusanya bilioni sita kwa mwezi, lakini miaka yanyuma zisipatikane?Mheshimiwa Spika, pato la Taifa limeongezekakwa mwezi kupitia Wizara hii, suala la ukataji waumeme limechukuliwa ahadi na Waziri kwambahalitokuwepo, tujiulize ni kwa nini nyuma yalikuwayakijitokeza matatizo hayo. Ni dhahiri kwambakulikuwa na ubadhilifu mkubwa uliokuwa ukitendekabaina ya viongozi na watendaji wa Wizarawaliokuwepo na nikisema viongozi sikusudii viongozi waSerikali tu, lakini wanakuwa na maslahi mawili; moja,kupata maslahi ya kisiasa kwa ajili ya kuteka mawazona fikra za Watanzania waione Serikali iliyopomadarakani kuwa ni kandamizi. Pili, kupata maslahi yakifedha na kujikusanyia fedha isivyo halali hukuwakipinga maslahi mengine yaliyo halali.Mheshimiwa Spika, umeme ni ukombozi wamwanadamu, umeme ni ajira, umeme ni hazina naumeme ni suluhu ya kuondoa umaskini katika nchi.Hata hivyo, gharama za umeme zimepanda kwaupande wa Zanzibar. Je, kama Mtanzania aliyeko

Zanzibar anapandishiwa bei ya umeme kinyume naMtanzania aliyeko bara hii si njia moja ya kuuvurugaumoja wetu? Mheshimiwa Waziri anatoa kauli ganikuhusiana na hili?.Mheshimiwa Spika, nguzo moja ya umemeZanzibar ni milioni moja na laki mbili, hivyo mwananchiutamfikiaje umeme huo kama gharama ya nguzo iweya mwananchi, waya ziwe za mwananchi na vifaavingine vyote viwe vya mwananchi na mwananchihuyo huyo analipia umeme kila mwezi, ni kwa nini basihili lisiangaliwe kwa Tanzania nzima mwananchiasiachiwe gharama ya kuunganisha umeme na kulipiagharama za umeme tu.MHE. HERBERT J. MNTANGI: Mheshimiwa Spika,naomba kuwapongeza sana Mheshimiwa Waziri naWaheshimiwa Manaibu wote na watendaji kwahotuba nzuri yenye mwelekeo wa uhakika wakuboresha sekta ya nishati na madini. Napendakumshauri Mheshimiwa Waziri na Manaibu Wazirikufufua mapendekezo yaliyokuwepo mezani, Serikalinikwa miaka 14 (kumi na nne) iliyopita bila kutekelezwa.Mheshimiwa Spika, kuhusu kuanzishwa upyakampuni ya GASCO; Kampuni hii iliundwa na kusajiliwana Mtendaji wake Mkuu kuandaliwa mwaka 1998/1999ili kusimamia usambazaji na mauzo ya gesi. Mtendajiwake leo ni marehemu ndugu Thomasi Masili.Uvumbuzi wa gesi asilia unaongezeka huko Mtwara,Lindi na Mkuranga, sio busara kuachia usimamizi warasilimali hii mikononi mwa Kampuni za Wageni. Siokosa kuingia ubia lakini chini ya mikataba yenye

dhamira njema, nimeona dhamira ya Wizara juu yaGASCO, naomba itekelezwe.Mheshimiwa Spika, kuhusu kuanzishwa kwaKampuni ya KILAMCO; kama ilivyokuwa GASCO chiniya TPDC pia iliundwa na kuandikishwa kampuni yaKILAMCO. Lengo lake pia ni matumizi ya Gesi ya MnaziBay kwa ajili ya kuzalisha mbolea, ni vema Kampunihiyo ikaanzishwa ili kuzalisha mbolea na kutumia vizurihazina kubwa ya gesi asilia.Mheshimiwa Spika, kuhusu kurejesha Kampuni yaCOPEC: kutokana na umuhimu wa matumizi ya mafutaKitaifa siyo busara nchi yetu kuachia jukumu lausambazaji wa mafuta mikononi mwa Kampuni zakigeni, tusihadaike kwamba kampuni hizozimeandikishwa Tanzania na hivyo ni za TanzaniaKampuni ya Umma-COPEC itakuwa kiongozi wa beidira za mafuta nchini.Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme wa dharuraMW 422; lazima tujiulize swali hili, ilikuwaje IPTL kupewamkataba mrefu wa zaidi ya miaka 20 wakati lengo laawali lilikuwa kupata umeme wa dharura? Gharamaza umeme wa dharura kutoka makampuni ya nje nighali sana, tuweke dhamira ya kweli kutekeleza miradiifuatavyo iliyopo ndani ya bajeti ya mwaka 2012/2013kama ifuatavyo:-(i) Mchuchuma 600MW(ii) Ngaka 400MW

(iii) Ruhudji(iv) RusumoJUMLA358MW75MW1433MWMheshimiwa Spika, ukamilisha wa miradi hiyopamoja na gesi ya Ubungo 105MW uende sambambana kuondoa umeme wa dharura ifuatayo:-(i) Symbion 137MW(ii) Aggreko 100MW(iii) IPTL 80 MWJUMLA317MWMheshimiwa Spika, tusiruhusu kupandikizakuongeza muda wa mikataba hiyo na tuchambueuhalali uliowezesha IPTL kupata mkataba wa mudamrefu. IPTL itumie gesi kuendesha mitambo yao. Kwakuwa mkataba unaipa jukumu TANESCO kununuamafuta ya kuendesha mashine zao, basi ijengwe hojaya kutumia gesi asilia badala ya mafuta mazito IFO.Nakumbuka mwanzo kabisa mitambo hiyo iliendeshwakwa mafuta ya ndege JET AI, naomba Wizaraichunguze hilo ili kusaidia kujenga hoja.Mheshimiwa Spika, kuhusu utekelezaji wa mradiwa Stigler’s Gorge 2100 MW; dhamira ya mpango wamradi huu ilikuwepo zaidi ya miaka 20 iliyopita.Hatukuanza kuutekeleza hata kwa awamu tatu kama

ilivyopendekezwa ndani ya muda huo leo. Tungekuwatayari tunazo 2100 MW za ziada na walakusingekuwepo na upungufu huu unaolieleza Taifa letu.Tumechelewa lakini tuthubutu na tuanze kwa dhatimwaka 2012/2013. Mapato ya mauzo ya gesiyachangie gharama za utekelezaji wa mradi huu.Mheshimiwa Spika, kuhusu Miradi ya UmemeMCC.1; Muheza tuna mpango kwa Vijiji 17, kumekuwana ucheleweshwaji wa miradi hii sasa kwa zaidi yamiaka mitano. Inaanza kufanana na miradi ya Benkiya Dunia ya Maji kwa Vijiji 10. Wizara isimamie ilikuboresha uharaka wa utekelezaji wa miradi hii,utekelezaji kwa uteuzi wa Wakandarasi umeanzaMuheza, lakini kasi ni ndogo, yapo malalamikokwamba Vijiji vilivyoteuliwa awali vimebadilishwa bilakushirikisha jamii.Mheshimiwa Spika, naomba Wizara ifuatie hiliambalo nimetumiwa ujumbe leo asubuhi tarehe28/7/2012.Mheshimiwa Spika, Mradi kati ya Wahisani waSweden na Halmashauri ya Wilaya ya Muheza juu yateknolojia mpya ya umeme; naishukuru sana REA naMkurugenzi wake Daktari Mwakahesya kwa kusaidiakuwezesha mradi huo kuanza. Balozi wa Tanzanianchini Sweeden amefika Muheza mwezi Machi, 2012kuona kama Halmashauri ya Wilaya ya Muhezaitaweza kuchangia utekelezaji wa mradi huo.Napenda kusema kwamba uwezo wa Halmashauri nimdogo na hivyo kuomba REA kuweka nguvu, kusaidia

kwa kuwa mradi huu upo katika majaribio na Tanzaniaimeteuliwa kuwa sehemu ya majaribio.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika,naomba kuchangia hoja ya Nishati na Madini.Napenda kuchukua fursa hii na kwa dhati kabisakumpongeza kaka yangu Mheshimiwa Muhongo,Waziri na Manaibu wake wote hasa MheshimiwaMassele kwa kazi ya uzalendo aliyoifanya kwa niabaya Wizara kutembelea maeneo ya migodi na kuongeana wananchi ingawa hakuongea na wananchi wote.Mfano, kuna sehemu walikwenda, asiende tu kuleLyamongo na kuacha sehemu ambazo zina kerokubwa kama Kata ya Matongo.Mheshimiwa Spika, Hivyo Mheshimiwa Waziritungependa Wananchi hawa pamoja na wadau wamadini kwa maana ya wachimbaji wa madini wadogowadogo, wa kati na wakubwa ili kusiwepo namalalamiko toka pande yoyote ile kwa maana yawananchi na wachimbaji.Mheshimiwa Spika, vile vile nachukua fursa hiiadhimu pia kumpongeza Katibu Mkuu wa WizaraMheshimiwa Eliakim Maswi.Mheshimiwa Spika, sasa nizungumzie suala zima lawachimbaji wadogo wadogo. Katika hotuba yamwaka 2012/2013, Wizara imeainisha kuwa inatengamaeneo ya Itandula, Wilayani Tarime lenye ukubwa wahekta 37. Lakini Wizara haikutamka wazi kuwa ni leseni

ngapi ndogo ndogo zimetolewa kwa wachimbajiwadogo wadogo na ni wangapi ambao leseniwalizopatiwa na wazawa na wengine kutoka nje yamaeneo ya machimbo?Mheshimiwa Spika, vile vile ningependa kujuakama leseni zimetolewa kwenye maeneo ambayo si yakwao, je, wamewalipa fidia wamiliki halali wa maeneohayo? Maana kumekuwepo na malalamiko mengisana juu ya watu kudai wana leseni za uchimbaji nakutanabaisha maeneo ambayo kuna watu wanamilikina kufanya shughuli zao za kilimo. Mfano, katika ziaraya Mheshimiwa Massele, kuna kundi la watu walidaiwana leseni za kuchimba katika meneo 13, maeneo yaMarera, Mwenyekiti wa kikundi hiki anaitwa DavidMakoma na hili suala lilipingwa mbele ya MheshimiwaMassele. Hivyo, napenda kujua hatua iliyochukuliwa iliwananchi hawa wanyonge ambao hawana uwezowa kuchimba madini basi wapewe fidia mbadala.Mheshimiwa Spika, napenda kujua hayo maeneomengine yaliyotajwa kama Mosabiri, Nyakunguru naGorongila. Gibaso ni kwa ajili ya wale wanaotakaleseni tu au pia kwa ajili ya ile ahadi ya Serikali yakuwapa maeneo wananchi wa maeneo ya migodiambapo baada ya uwekezaji wamekosa ajira nawakaahidi sio tu kuwapa maeneo bali kutoa elimusambamba na mitaji ili waweze kujiendeleza.Ningependa kupewa majibu katika hayo.Mheshimiwa Spika, ni dhahiri tumekuwatukishuhudia mauaji ya vijana wetu ambao ni nguvukazi ya Taifa letu wakija katika harakati za kujitafutia

fedha ili waweze kujikimu kimaisha kama kusomeshawatoto na kutunza familia, sasa wamebaki bila ujira nahuku wakifa au kuwa vilema.Mheshimiwa Spika, vile vile kumekuwepo namalalamiko mengi sana juu ya fidia na maramwananchi anapokuwa hajaridhika na fidia na hivyokugoma kupisha kwenye eneo lake hutishiwa na hatakupelekwa jela mahabusu huku nyumba na mazaokatika maeneo yao kubomolewa na kuharibiwa. Je, hiini haki? Mfano ni kwa ndugu Daniel Samwel Nyamaheambaye alipigwa na kupelekwa rumande ambapoalikaa na alipotoka alikuta Barick wamezungushia uzioeneo lake huku wakibomoa nyumba zake takribani tisapamoja na kuharibu mazao, bila hata kulipwa fidiaambayo wamekubaliana. Hii sio haki kabisatukumbuke wananchi hawa wanapisha ardhi yenyedhahabu ambapo walitakiwa kulipwa fidia pamoja naresettlement ambazo kwa upande wa wananchi waNyamongo hawafanyiwi hivyo.Mheshimiwa Spika, hii ni dhuluma, nina imani nasafu ya uongozi wa Wizara na uzalendo wao, hivyo nidhahiri kuwa wakati umefika wa kuwatendea hakiwananchi hawa wanyonge ambao wamekuwawakidhulumiwa kwa muda mrefu ili tuweze kuwa namahusiano mazuri na wachimbaji. Pia wachimbajiwanawajibika kufanya au kutoa huduma za kijamii ilikubadili mandhari ya maeneo husika. Maeneo yamadini yanasikitisha sana, inabidi siyo tu kunufaishaeneo la uchimbaji tu bali na Wilaya nzima hasa MakaoMakuu ya Wilaya pamoja na Kata jirani ili viweze ku-

eflect uwepo wa uchimbaji madini katika maeneohusika.Mheshimiwa Spika, mwisho nizungumzie juu yafedheha ya ubadhirifu ndani ya TANESCO na katikaIdara zingine za Mashirika ya Umma, tunaomba hatuambadala zichukuliwe na hatua mbadala sio tukuwafungulia kesi bali kuwafilisi mali zote ili kurejeshafedha zote zilizohujumiwa ambazo ni kodi yawananchi. Huu ugonjwa umekuwa ukitufilisi sana, watuwachache wanajineemesha huku Tanzania tukibakikuwa maskini.Mheshimiwa Spika, napenda kujua ni kwa kipindicha muda gani au miaka mingapi tuhuma ya kukatwaumeme imekuwa ikifanywa? Vile vile ningependakujua ni kiasi gani cha fedha kwa ujumla ambachoTaifa limeingia kwa kukatiwa umeme? Hii ni kuhusufedha walizojipatia hao wahujumu uchumi, achiliambali zile ambazo wananchi wamepata hasara kwaukosefu wa nishati hii muhimu kwa maendeleo ya nchiyetu.Mheshimiwa Spika, vile vile napenda kusisitizaumuhimu wa umeme vijijini kwani asilimia kubwa yaWatanzania wanaishi vijijini (75%) ambapo shughulikubwa ni kilimo ambapo nishati ya umeme ni kiini chaumwagiliaji, usindikaji wa mazao na kadhalika.Ukiangalia Vijiji vingi vya Mkoa wa Mara na hususanTarime na Rorya havina umeme, hivyo naomba vipewevipaumbele.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Spika, nianzekuchangia kwa upande wa Machimbo ya Madinikatika Jimbo la Mbozi Magharibi eneo la Sante, Kataya Ivuna kuna shughuli ya uchimbaji wa madiniunaendelea ambapo wananchi na mimi kamamwakilishi wa wananchi sifahamu. Hivyo basi ilikuweka sawa na kutahadharishwa mgogoro ambaounaweza kutokea, tunaomba tupatiwe maelezokuhusu uchimbaji madini katika eneo hilo, madini yaaina gani? Leseni wewe umepewa na nani? Shughulihiyo imewekezwa kwa muda gani? Pia wananchiwatafaidikaje na mradi huo wa machimbo ya madinihayo?Mheshimiwa Spika, kuhusu Miradi ya Umeme, kwakuwa katika Jimbo la Mbozi Magharibi ambalo kwasasa ndiyo Wilaya mpya ya Momba hatujawahi kabisakuwa na umeme kabisa katika Kata zote 14 tangutupate uhuru. Hivyo basi tunaiomba Serikali ihakikishekuwa kwa mwaka huu wa fedha angalau baadhi yamaeneo tupate umeme hali ambayo itatuwezeshakusukuma maendeleo katika Wilaya yetu ya Momba.Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, kwanzanaipongeza Serikali kwa kupunguza gharama za bei yauzalishaji wa umeme. Kwa kweli katika jambo hili Serikaliyetu imechangia moja kwa moja kusaidia Mtanzania.Hivyo, napenda kuishauri Serikali ielekeze nguvu zakezaidi katika kuongeza upatikanaji wa vifaa vya

uzalishaji wa umeme kwani ni dhahiri kutokana napunguzo hilo, wananchi wengi wataitikia wito wakujiunganishia wenyewe.Mheshimiwa Spika, jambo lingine nataka kuishauriSerikali juu ya kuongeza uangalifu katika suala lakuwafuatilia watendaji wa TANESCO, inatokana kamamtandao mkubwa wa uharibifu wa watendaji kwa niaya kujinufaisha binafsi. Ubinafsi katika shirika hiliumepelekea TANESCO kubeba jukumu la madenimakubwa, hii ina athari kubwa kwa uchumi wa Taifa hilina ina athari kubwa kwa maendeleo ya wananchi wakawaida.Mheshimiwa Spika, mwisho, naishauri Serikaliiongeze nguvu zaidi katika kusambaza huduma hiimuhimu vijijini. Hivi sasa idadi ya Watanzania wanaoishivijijini tunasaidia pia kasi ya uharibifu wa mazingira yetuambayo kwa sasa asilimia 95% ya Watanzania vijijiniwanatumia nishati ya kuni katika kuendeleza maishayao. Hii ni hatari sana na sababu kubwa ya janga hili nikutokana na nishati ya umeme kutopatikana katika vijijivyetu.Mheshimiwa Spika, ahsante.MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: MheshimiwaSpika, nianze kwa kuwapongeza Waziri, Naibu Mawazirina Wataalam wa Wizara, kwa hotuba nzuri nailiyowasilishwa vizuri. Nampongeza pia Msemaji waKambi Rasmi ya Upizani na Kamati, kwa maoni yaoyenye lengo la kuimarisha Sekta ya Madini na Nishati.

Mheshimiwa Spika, pia niipongeze Wizara kwahatua ilizochukua kuhakikisha kuwa nchi haiingizwikwenye giza lisilokuwa na sababu za msingi. Waziri nawasaidizi wake wote waendelee kuchukua hatua ilihatimaye Taifa letu liondokane na mgogoro wa nishatiambao umelikumba Taifa kwa muda mrefu. Mamboyafuatayo ambayo yamekuwa yakiwaumiza wananchiwazalendo yafanyiwe kazi mara moja:-(i) Miradi isiyotekelezeka. Miradi ya namna hiihuonesha kuwa Wizara ni ya kisanii, si sifa nzuri hatakidogo;(ii) Mikataba mibovu ya nishati (gesi na mafuta).Tuangalie mahali pengine wanafanyaje;(iii) Umeme usiokuwa na uhakika; na(iv) Tuhuma za ufisadi uliokithiri ngazi za juuWizarani.Mheshimiwa Spika, Mambo hayo yafanyiwe kazikwa makini ili Taifa lisonge mbele.Mheshimiwa Spika, niongelee pia nishati jadidifukwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi, nchi nyingiduniani zimejielekeza kwenye nishati jadidifu. Mbali nakwamba tunahitaji nishati ya kutosha kwa matumizibinafsi, viwandani na sehemu nyingine inabidi Wizaraianze kuandaa sera makini ya nishati jadidifu hasakuhusu joto ardhi, jua, upepo, biogesi, makaa yamawe safi na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, sasa nitajielekeza kwenyeJimbo langu la Bukombe, nashukuru kwamba sasaSerikali imeamua kupeleka umeme Bukombe,wananchi wa Bukombe wanachopenda ni kwa Serikalisasa kufuata ratiba kikamilifu ili mradi utekelezwe kwawakati.Mheshimiwa Spika, lingine ni kwamba, vijiji vyoteambako nguzo na nyaya za umeme vitapita, vipatiweumeme na vijiji vingine ambavyo havijapata basinavyo vifikiriwe ili mwaka ufuatao 2013/2014 viwekwekwenye utaratibu wa umeme wa REA.Mheshimiwa Spika, niongelee pia miradi mingineya umeme ambayo Bukombe iliahidiwa mwaka jana2011/2012. Katika hotuba ya bajeti ya mwaka jana(2011/2012), ukurasa wa 115 na ukurasa wa 117 miradiifuatayo ilibainishwa:-(1) Mradi wa taa za mwanga bora vijijini(community-based power trading) mradi huu ulipaswakutekelezwa Chato, Biharamulo, Kahama na Bukombe.(2) Mradi wa Tanzania Affordable RuralElectrification Plan. Huu ulipaswa kutekelezwaBukombe na Kibondo.Je, miradi hii imefika wapi kiutekelezaji au ilikuwa nimiradi hewa? Naomba majibu.Mheshimiwa Spika, pia nitaongelea tatizo moja laukorofi wa baadhi ya wawekezaji kutofuatasheria/mikataba katika sekta hii, wawekezaji hawa

wamekuwa wagumu kutimiza wajibu wa kijamii waMashirika na hata kulipa kodi. Nampongeza Wazirikwa kuliona hili na kuanza kuchukua hatua wakati wakuwabembeleza umekwisha.Mheshimiwa Spika, licha ya kupitia mikataba, Serana sheria na kuziba mianya yote, Wizara inapaswakusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mikataba husikakwani ukorofi wa kibeberu wa hawa wawekezajiunahitaji uangalizi na ufuatiliaji wa karibu.Mheshimiwa Spika, mifano ya ukorofi ni mingi naWizara inaifahamu:-(a) Ukweli kwamba Barrick Gold haijatekelezavipengele vya Sheria mpya ya Madini ya 2010.Wawekezaji wote waitwe na waambiwe kuwa fungateimekwisha.(b) Kumekuwa na kelele nyingi za malalamikokuhusiana na wawekezaji wa Mgodi wa Nyamongo.Ilifikia hatua Mheshimiwa Nyangwine alisema atashikamapanga na sasa wawekezaji wameanza kutekelezakidogo kidogo, lakini bado waongeze kasi kwani wanaTarime wamechoka kuibiwa na kunyonywa namwekezaji.Mheshimiwa Spika, Wizara iendelee kuwa namsimamo imara, isiendelee kuwabembelezawawekezaji.Mheshimiwa Spika madini, Sera ya Madini yaMwaka 1997 na Sheria ya Madini ya 2010, kwa kiasi

kikubwa viliwapendelea wawekezaji kwa kuwaandaliamazingira mazuri ili wawekeze bila matatizo.Wachimbaji wadogo wadogo hawakutengewamazingira mazuri na hapakuwa na mipango thabitiyoyote ya mafunzo, mikopo au mpango wowote wakupewa zana. Siku hizi kuna makundi ya watuyaliyounda Ushirika wa Uchimbaji Madini, mathalanihuko Bukombe, ambayo yamekosa maeneo yakuchimba dhahabu kwa sababu maeneo mengi yanaleseni. Hali hii inawakatisha tamaa wananchi wenyenia ya kushiriki katika kuvuna rasilimali ya dhahabu.Ninashauri yafuatayo:-Mheshimiwa Spika, kama nilivyopendekezamwaka jana, wachimbaji wadogo watengewemaeneo pembezoni mwa migodi mikubwa kuondoatatizo la migogoro baina ya wachimbaji wakubwa nawachimbaji wadogo. Kadhalika, hatua za makusudizichukuliwe kufuta liseni za maeneo ambayohayajaendelezwa (rai iliyotolewa kwenye Hotubaukurasa wa 91 liwe ni agizo). Kwa mfano, ukiangaliaramani ya madini ya Wilaya ya Bukombe, karibu Wilayanzima imejaa leseni lakini maeneo yaliyoendelezwa nimachache sana. Wizara isahihishe jambo hili ilituondoe malalamiko kuwa watu fulani walijipendeleakupata leseni huku wananchi wenyeji wakibakihawana kitu.Mheshimiwa Spika, Kituo cha Mafunzo kwawachimbaji wadogo kilichopendekezwa chaRwamugasa Kiharakishwe kuanzishwa, kitawasaidiasana wachimbaji wadogo kwa sababu wengi hawanamaarifa ya kutosha kuhusu uchimbaji na hatari zake.

Mheshimiwa Spika, suala la kuwezeshwa kifedha nimuhimu. Kama ilivyoelezwa katika Hotuba, utaratibuwa kutoa mkopo uandaliwe kwa makini ili wachimbajiwadogo wanufaike.Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara kwa kauliyake (ukurasa 106 – 107), inayosisitiza kuwa migodi yoteinaanza kulipa kodi bila visingizio. Wizara ifuatilie kwakaribu utekelezwaji wa agizo hili. Kadhalika, ifanyeutafiti katika nchi nyingine mathalani Botswana,Guinea, Ghana na Zimbabwe ili kuangalia waowanaendeshaje usimamizi wa Sekta ya Madini naviwango vya kodi, kama kodi yetu kwa migodi bado nindogo basi kuna haja ya kuirejea na kuirekebisha.Mheshimiwa Spika, jambo lingine linahusumazingira; Wizara ifuatilie kwa makini suala hili. Maranyingi wawekezaji lengo lao ni faida, lazimawafuatiliwe kuhusu athari za kimazingira za shughulizao. Je, Wizara ina mipnago yoyote ya kufuatilia athatiza kimazingira za shughuli za wachimbaji wadogowadogo? Nauliza hili kwa sababu yaelekea hakunampango wowote ule.Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, Sekta yaMadini kwa muda mrefu imekumbwa na tuhuma zaufisadi. Wizara ijitahidi kulishughulikia tatizo hili. Je,suala la Jairo limefikia wapi mbona Serikali ipo kimyakuhusu Maazimio ya Bunge kuhusu jambo hili?MHE. MBAROUK SALIM ALI: Mheshimiwa Spika,nichukue fursa hii kuipongeza safu ya Uongozi ya

Wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa naMh.Professor Sospeter Muhongo. Mh.Spika kitendokilichofanywa na uongozi huo wa Wizara kwakugundua wizi mkubwa wa fedha za serikali toka kwashirika la TANESCO. Huu ni mfano ni jinsi gani serikaliinavyopoteza pesa kwa watendaji wasioaminika.Nashauri Makatibu wakuu wengine pia waige mfanomzuri wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini;ili Nchi yetu itoke katika wimbi kubwa la umaskini.Mheshimiwa Spika, Wizara hii ni muhimu sana nabila utendaji na ufanisi mkubwa wa Wizara hii basiumaskini wa Tanzania hauwezi kuondoka. Mh.Spika,hivyo basi pamoja na serikali kuongeza bajeti yaWizara hii lakini bado ni kidogo na kuna haja kubwa yakuongezewa pesa ili waweze kutekeleza miradi mingiya umeme. kama ripoti ya Kamati ilivyoainisha sasatuwe na Slogan la Nishati KWANZA.Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri katikauzinduzi wa bomba la gesi alitamka kuwa kuna gesinyingi iligundulika ambayo Tanzania inawezakukusanya zaidi ya trilion 626.71. Mh.Spika huu ni utajirimkubwa kwa Nchi yetu. Wasiwasi mkubwa Mh.Spika nijinsi gani Nchi yetu imejipanga katika usimamizirasilimali hii ya gesi. Na ili tuweze kusimamia vizuritunahitaji kuwa na mikakati endelevu ili tuwezekuiendesha Nishati hiyo vizuri, hii Mh.Spika ni pamoja nakuwa na wataalamu wa kutosha katika ngazi zote(downstream and upstream). Mh.Spika pia sera nasheria za gesi ni muhimu ziharakishwe ili ziwezekustawisha usimamizi bora wa Sekta hii ndogo ya gesi.

Mheshimiwa Spika, Suala la umeme vijijini bado nitete kwani kasi ya uwekaji wa umeme vijijini bado nindogo sana. Mh.Spika fedha walizotengewa REA nindogo sana pamoja na kwamba zimeongezwa;nashauri REA wawezeshwe zaidi ili wakala huu uwezekutekeleza miradi mingi ya umeme vijijini. Mwaka janatulipandisha kodi ya mafuta ya taa kwa azma kuwafedha hiyo ingalienda katika mfumo wa REA. Tatizokubwa, hilo halikufanyika, na sasa kuna kadhia kubwaya mafuta ya taa vijijini na umeme pia hakuna.Mheshimiwa Spika, Wakala wa Geologia ni Sektamuhimu sana. Zaidi ya kutambua miamba lakiniwakala huu pia wana uwezo wa kutambua majangakama tetemeko la ardhi. Mh.Spika pamoja naumuhimu wa wakala huu lakini fedha wanazopata nikidogo; na kwa sababu hiyo wanakuwa hawanauwezo wa kufanya kazi zao kwa ufasaha.Mheshimiwa Spika, nashauri wakala huuuwezeshwe zaidi na kupewa vifaa vya kisasa nanyenzo nyinginezo ili waweze kufanya kazi vizuri.Mheshimiwa Spika, niipongeze tena Wizara kwamabadiliko ya kiutendaji yanayoweza kuonekana nanaomba kuchangia hoja hii na kuiunga mkono bajetiya Wizara hii.Mheshimiwa Spika, Ahsante.MHE. DUNSTAN L. KITANDULA: Mheshimiwa Spika,naomba nianze kwa kuunga mkono hoja ya Wizara yaNishati na Madini kuhusiana na Makadirio na Matumizi

ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Aidha,nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri, NaibuMawaziri, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hii NduguEliakim Chacha Maswi kwa kazi nzuri wanayoifanyakatika Wizara hii. Naamini sasa tutaona utendaji waTPDC na taasisi nyingine zilizopo chini ya Wizara hiiukiimarika.Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa umeme wauhakika mjini una uhusiano wa moja kwa moja najitihada zetu kama Taifa katika kupambana naumaskini. Nishati ya umeme ni nyenzo muhimu kwasekta za uzalishaji mali, ukuzaji wa ajira, kuongezakipato kwa wananchi wanaojiajiri katika sekta rasmi nazisizo rasmi, upatikanaji wa huduma bora na afya,upatikanaji wa huduma ya uhakika ya maji safi nasalama, elimu mashuleni na vyuoni na upashanajihabari kupitia simu, internet, redio na televisheni.Mheshimiwa Spika, katika ukurasa wa saba wahotuba ya Mheshimiwa Waziri tunaelezwa kuwa niasilimia 18.4 tu ya Watanzania ndio ambao tumewezakuwaunganishia umeme. Aidha, kati ya hao ni asilimia6.6 tu ya Watanzania waishio vijijini ndiowameunganishiwa umeme. Hii inamaanisha kwambaasilimia 68.4 ya Watanzania waishio vijijinihawajaunganishwa kwenye umeme.Mheshimiwa Spika, kwa maana nyingine nikisemakwamba sera zetu zinafifisha uibuaji na utumiaji fursa zakiuchumi zilizopo katika maeneo ya vijijini, tumezuiafursa ya wananchi vijijini kuongezea thamani mazao

yao na tumedumaza maendeleo ya viwanda katikamaeneo yaliyokosa umeme. Kwa hali hii hatupaswikushangaa tunapoona wimbi kubwa la watu kukimbiliamijini kutafuta ajira. Wimbi hili la watu wanaokimbiliamijini, hususan vijana tunalitengeneza sisi wenyewekutokana na kutoweka mazingira wezeshi kiuzalishaji nahuduma muhimu vijijini.Mheshimiwa Spika, Taifa haliwezi kusema kuwalinapiga hatua za kimaendeleo endapo zaidi yaasilimia 50 ya watu wake wanatengwa kutumia fursazilizopo kuwaendeleza. Kama kweli tunayo dhamira yadhati ya kuondoa umaskini vijijini, hatuna budikuwekeza katika kupeleka umeme vijijini, kwa sababukupeleka umeme vijijini tutaibua fursa nyingi zakiuchumi na uzalishaji wa ajira.Mheshimiwa Spika, kule Mkinga hususan katikaKata za Kigongoi na Bosha tunazalisha Karafuu, Iliki,Pilipili Manga, Mdalasini na sasa tumeanza kufufua zaola kahawa ambalo lilikuwa limetelekezwa. Kwa mudamrefu wananchi wameshindwa kufaidika na ukulimawa mazao haya kutokana na kuuza mazao kwa bei yachini. Kwa sasa amejitokeza mwekezaji ambaye yukotayari kuweka Kiwanda cha kuayongezea thamanimazao haya ikiwemo kuzalisha mafuta ya Makonyo.Hata hivyo, fursa hii kupotea kutokana na kukosekanaumeme katika Kata ya Kigongoi inayojumuisha Vijiji vyaVuga, Hemsambia, Mgambao Shashui, Kidundui,Kwekuyu na Bombo Mbuyuni.Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 1987 wakatiJimbo la Uchaguzi la Mkinga likiwa sehemu ya Wilaya

ya Muheza na hatimaye kupatiwa hadhi ya kuwaWilaya kamili, Serikali imekuwa ikiwaahidi wananchi waMkinga kuwapatia umeme katika vijiji mbalimbali.Aidha, kuanzia bajeti ya mwaka 2007/2008 nakuendelea Serikali imekuwa ikivionesha Vijiji vya Mkingakuwa katika mpango wa kuwapatia umeme kupitiaREA kama ifuatavyo:-(a) Daluni – kazi ya kupeleka umeme Kijiji chaDaluni inahusisha ujenzi wa njia ya umeme ya msongowa kilovoti 11, umbali wa kilomita 10, uwekaji watransfoma ya KVA 50 na njia ndogo ya msongo wa volti230/400 zenye urefu wa kilomita mbili; na(b) Gombero – kazi ya kupeleka umeme Kijiji chaGombero inahusisha ujenzi wa njia ya umeme yamsongo wa kilovoti 33 umbali wa kilomita 19, uwekajiwa transforma mbili na ujenzi wa njia ndogo za umemeza msongo wa volti 230/400 za urefu wa kilomita mbili.Mheshimiwa Spika, hata hivyo, licha ya kuwemokatika bajeti kwa miaka yote hii, ukamilishaji wa ahadiya Serikali kuvipatia vijiji hivi umeme haujafanyika nasasa imejengeka hofu miongoni mwa wananchi kuwavijiji hivi huenda vikaachwa katika kupatiwa umeme.Namwomba Waziri atuambie, kwa mwaka huuutekelezaji wa miradi hii utafanyika au ni hadidthi ile ileya miaka nenda rudi ya kuwemo katika bajeti naorodha ya miradi itakayotekelezwa na REA lakinihakuna utekelezaji.Mheshimiwa Spika, aidha, kwa nyakati tofauti(Mkutano wa Tisa, Kikao cha Kumi na Nne, 2007 na

Mkutano wa Kumi na Nne, Kikao cha Sita, 2009) Serikaliimekuwa ikitoa ahadi katika Bunge lako kuwa tayarikazi za awali za kuufanyia tathmini mradi huuzimekamilika, ikiwa ni pamoja na kubaini gharama,tayari TANESCO imekwishawasilisha REA maombi yaJumla ya Shilingi Bilioni 3.76 kwa ajili ya kufikisha umemeDaluni na Gombero na kwamba wakati wa kupelekaumeme kwenye vijiji hivyo itahakikisha kuwa vijiji vilivyojirani na maeneo hayo (Vuga, Hemsambia, Bwiti,Magati, Mapatano, Bantu, Machimboni, Jirihini, VundeManyinyi na Dima) navyo vinapatiwa umeme.Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya kazi kubwa yakuanzisha skimu ya umwagiliaji katika Kata yaMwakijembe, skimu ambayo itakuwa ukombozi nakichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi na pato lawatu wa Mkinga. Je, Serikali haioni busara yakuijumuisha Kata hii katika kuipatia umeme kutokeaDuga ambapo si mbali sana. Aidha, kwa busara hiyohiyo naiomba Serikali ifikirie uwezekano wa kupelekaumeme kwenye Kata ya Bosha, Kata ambayo inazofursa nyingi za uwekezaji katika kilimo. Kwa sasa tayariyupo mwekezaji ambaye ameonesha nia ya kuwekezakatika kilimo cha maua katika shamba la Kwamtili. Vilevile naiomba Wizara kupitia REA ifikirie uwezekano wakuzipatia umeme wa Solar Shule za Wilaya ya Mkingazilizopo nje ya mfumo wa umeme wa Gridi ya Taifa.Mheshimiwa Spika, kukosekana upatikanaji wanishati ya umeme ya uhakika kwa maendeleo ya Taifani kiashiria kimojawapo cha umaskini. Takriban asilimia75 ya Watanzania wanaishi vijijini na wanategemeakilimo kuendesha maisha yao ya kila siku. Aidha, ili

kukidhi mahitaji yao ya nishati, ukataji miti kwa ajili yakupata kuni na uchomaji wa mkaa kimekuwa ndiochanzo kikuu cha nishati vijijijni. Matumizi haya ya kunina mkaa yanachangia sana katika kuongezeka kwakasi ya uharibifu wa mazingira.Mheshimiwa Spika, wakati takwimu zikioneshaTanzania kuwa na ekari 33 milioni za misitu, uharibifu wamisitu unakadiriwa kusababisha upotevu wa hekta500,000 za misitu kwa mwaka; kati ya hizo hekta300,000 sawa na kilometa za mraba 3,320 za misituhupotea kutokana na uchomaji wa mkaa kila mwaka.Takwimu za Benki ya Dunia zinaonesha kuwa kwamwaka takribani tani 1,000,000 za mkaa hutumikanchini; huku Dar es Salaam ikiwa ndio kinara wamatumizi hayo kwa asilimia 50.Mheshimiwa Spika, vile vile tafiti zinabainisha kuwakwa kasi hii ya ukataji miti kwa ajili ya kuni na uchomajimkaa, nchi yetu katika kipindi kisichozidi miaka kumiijayo itashuhudia misitu yetu ikiwa imekwisha. KamaTaifa lazima tufanye jitihada kuhakikisha kuwatunainusuru misitu yetu kwa kuwapatia wananchivyanzo mbadala vya nishati. Lazima tuhakikishetunakuwa na mipango itakayotuwezesha kuitumiavyema hazina yetu ya gesi kuzalisha umemeutakaopatikana kwa bei ambayo hata mtu wa kijijiniataweza kuimudu. Ni vyema vile vile tuongeze kasi yakufikisha Gesi majumbani mwa watu wengi ili wawezekuitumia.Mheshimiwa Spika, fedha tunazotenga kwa ajili yaREA hazitoshi na mbaya zaidi hata hizo kidogo

zinazotengwa hazitolewi zote, lazima bajeti ya nishatiijielekeze katika kuhakikisha kuwa REA inapata fedhaza kutosheleza mahitaji ili iweze kufikisha huduma yaumeme kwa haraka vijijini ambako asilimia 75 yaWatanzania inaishi. Tukifanya hivyo tutaweza kuzuiauharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji mitiovyo.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja nikiaminikwamba, Serikali itazifanyia kazi changamotonilizoainisha na ushauri nilioutoa.MHE. ABDULLA JUMA SAADALLA: MheshimiwaSpika, kwanza naunga mkono hoja kwa asilimia miamoja.Mheshimiwa Spika, nizungumzie gesi Zanzibar.Nchi yetu imepewa na Mungu baraka ya kuwa ndiomkombozi wa Mtanzania, napendekeza sambambana usambazaji wa uwekaji wa bomba la gesi Tanzaniabara, utafiti, upembuzi na ufadhili vifanywe kwa kuonani kwa namna gani bomba hili litafika Zanzibar kwafaida ya wananchi wanaoishi Zanzibar. Jambo hililitazamwe wazi wazi ndani ya Sera mpya ya gesiitakayoundwa. Napendekeza kuwa katika uwekezajiwa gesi, lazima wananchi wamilikishwe hisa zauwekezaji tangu mwanzo wa uwekezaji.Mheshimiwa Spika, sasa nichangie kuhusu umemewa upepo, hili ni jambo la msingi na tunatarajialitasaidia sana katika kuongeza umeme ndani ya gridiya Taifa.

Mheshimiwa Spika, nafahamu kuwa hatuazimeshaanza kuchukuliwa ila wananchi wapewe fidiazao, hati miliki za ardhi na Kijiji lazima zitolewe na Wizaraya Ardhi, mbali na fidia Resettlement ya DisplacedVillagers ifanywe.Mheshimiwa Spika, kuhusu Compliance MonitoringUnit, Mheshimiwa Spika, naungana na Wabungewengine kuwa process ya kumkabidhi mwekezaji ardhiya kuchimba madini basi lazima kuwe kuna chombocha kufuatilia Compliance ya Sheria za uwekezajiikiwemo MoU baina ya wananchi, Serikali namwekezaji.Mheshimiwa Spika, kuhusu urani na wachimbajiwadogo wadogo; tunafahamu kuwa Serikaliimeshaandaa utaratibu mzuri wa kuchimba urani,sawa na sera ya uchimbaji pamoja na marejeo nakanuni zilizofadhiliwa na Mantra. Hili halina tatizo lakinituwe makini na mwekezaji huyu, lazima tujikite katikauwekezaji rasilimali watu ili wasome sheria, ufundi,uchimbaji, usambazaji, usafirishaji na utupaji wa urani.Pia Sera ya Madini inaruhusu wachimbaji wadogowadogo (small scale miners) wachimbe kuchangiamgodi mkubwa wa Karibu.Mheshimiwa Spika, naomba Sera isiruhusu smallscale miners kuwepo kuhusiana na Uranium.Nafahamu watu wataona kuwa huu ni utajiri wa bure,lakini madhara yake ni makubwa na ikiwezekana hataulinzi wa maeneo ya machimbo, processing, usafirishajina kadhalika. Muhimu kuepukana na Briefcase Bomb.

Mheshimiwa Spika, nawapa hongera sana kwaasilimia mia moja.MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Spika, kuhusumradi wa bomba la mafuta kutoka Dar es Salaamkwenda Mwanza (pipeline). Utafiti wa mradi ulianziamwaka 1983, Technical feasibility 1988 na economicfeasibility 1989 na mradi ulipata idhini ya utekelezajikutoka Ikulu tarehe 17 Julai, 1989. Ilipofika mwaka1997 mradi huu ulipata Baraka za Mheshimiwa Rais(Benjamin Mkapa), faida za mradi huu zinajulikana kwauchumi wa Kanda ya Ziwa na kwa niaba ya watu waKanda, naomba kupata kauli ya Serikali kwambautekelezaji wa mradi huu utaanza lini?MHE. UMMY A. MWALIMU: Mheshimiwa Spika,nianze kwa kuunga mkono hoja. Pili, pongezi kwaMheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri na Katibu Mkuukwa kazi nzuri ya kusimamia sekta hii muhimu kwamaendeleo ya Watanzania. Ni imani yangu na yawatu wengi kuwa mtasimamia ipasavyo Wizara hiimuhimu ili iweze kuchangia ipasavyo maendeleo yakiuchumi na kijamii.Mheshimiwa Spika, nauomba uongozi wa Wizara,Waziri, Naibu Mawaziri na Katibu Mkuu kuendeleakuhakikisha kuwa daima maslahi ya nchi ndioyanakuwa msingi mkuu wa maamuzi yoteyatakayofanywa na Wizara.Mheshimiwa Spika, nishati na maendeleo yawanawake; ningependa Wizara ihakikishe inatekelezakwa vitendo Sera ya Taifa ya Nishati (revised 2003)

katika masuala ya nishati na usawa wa jinsia hasakuhakikisha nishati ya kisasa inapatikana kwa matumiziya nyumbani hasa vijijini ili kuwapunguzia mzigowanawake na wasichana.Mheshimiwa Spika, wanawake ndio watafutajiwakubwa wa kuni kwa ajili ya kupikia, pia ndiowanaohakikisha kunakuwepo nishati kwa ajili yalighting. Karibu asilimia 85 ya nishati inayotumikamajumbani inatokana na kuni au mkaa. Hali hiiitaendelea hadi lini? Wanawake wengi pia vijijiniwanapoteza maisha wakati wa kujifungua kutokanana kukosekana kwa huduma za nishati ya kisasa(umeme katika vituo vya afya).Mheshimiwa Spika, wakati umefika sasa kwaWizara kuhakikisha upatikanaji wa huduma za nishatiya kisasa unapewa jicho la jinsia. Nipatiwe maelezo nimipango au mikakati gani ipo au imewekwa yakuhakikisha usawa na jinsia na upatikanaji wa hudumaza nishati ya kisasa kwa Watanzania hasa wanawakewalio vijijini. Rejea Sera ya Taifa ya Nishati, Rev. 2003Policy statements No. 60, 61, 62 na 63.MHE. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Spika, nianzekuchangia kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, bajeti ndogo ya REA; ni vyemaiongezwe ili usambazaji wa umeme vijijini uwezekwenda kwa kasi. Hususan kusambaza katika shule zoteza sekondari na vituo vya kutolea huduma ya afyaWilayani, Serengeti.

Mheshimiwa Spika, wale wote watakaopatikanana kuhujumu uwepo wa umeme wachukuliwe hatuakali za kisheria. Ni vyema kwa makusudi kabisa wotewatakaobainika na kuhujumu umeme iwe mfano,wachukuliwe hatua kulingana na Sheria ya WahujumuUchumi na takwimu zilizotolewa ni kiasi gani kimepoteakutokana na kukatika au mgao wa umeme.Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogowasaidiwe, wachimbaji waliojitolea katika Wilaya yaSerengeti kama Park Nyigoti, Majimoto, Ringwani(Kalambo) na Borenga hawajawezeshwa na wenginewanajiita watafiti, lakini hakuna uwazi, haowanachimba na ku-process madini au wanatafiti kwelina kama kweli wanatafiti hivi hakuna ukomo wakutafiti?MHE. MHONGA S. RUHWANYA: Mheshimiwa Spika,Serikali iwainue wachimbaji wadogo wadogo kwakuwapa mafunzo juu ya masuala yote yahusuyouchimbaji pamoja na mafunzo juu ya utunzajimazingira, lakini pia wapewe mikopo ya vifaa vyakuchimbia. Najua kuna juhudi zimeanza kufanyika zakuwainua wachimbaji wadogo wadogo lakini badokuna malalamiko mengi, wao ndio huwa wa kwanzakugundua yalipo madini, lakini mara nyingihuondolewa kwa mabavu na maeneo yaowanapewa wachimbaji wakubwa. Hatawanapohamishiwa maeneo mengine, si rahisi wawezekushindana na wachimbaji wakubwa bila kuwezeshwa.Mheshimiwa Spika, leseni za wachimbaji wadogowadogo zinachelewa sana kupatikana,

wanazungushwa sana. Bei ya leseni nazo zimepandasana. Serikali iangalie na ione umuhimu wa kupunguzabei kwani sasa hivi wachimbaji wana malalamikomakubwa.Mheshimiwa Spika, kuhusu gesi asilia, Sheria yaGesi na Sera ya Gesi pamoja na bomba la gesi. Nchiyetu imejaliwa gesi nyingi sana, nashauri Sera na Sheriaya Gesi iletwe mara moja Bungeni. Sheria itasaidiakudhibiti ufisadi na udhaifu katika sekta hii, pia kuepukamigogoro inayoweza kuhatarisha usalama wa nchi.Ujenzi wa bomba la gesi ni hatua muhimu na kubwa,lakini ni vema Serikali ilete au iweke wazi mkataba huoili wananchi waelewe hali halisi na tuhakikishe maslahiya Taifa yanalindwa na hii itasaidia kuondoa aukuepusha migogoro inayoweza kuhatarisha usalamawa nchi.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa bomba la gesi nihatua muhimu na kubwa, lakini ni vema Serikali ilete auiweke wazi mkataba huo ili wananchi waelewe halihalisi na tuhakikishe maslahi ya Taifa yanalindwa na hiiitasaidia kuondoa au kuepuka matatizo ya awaliyaliyoko kwenye mikataba ya madini iliyopo sasa. Vilevile lazima wananchi wa Lindi na Mtwara wawebeneficiaries wa kwanza wa mradi husika na Serikaliitueleze rasmi jinsi mikoa hiyo itakavyofaidika.Mheshimiwa Spika, bei ya mafuta ya taa sisuluhisho la uchakachuaji wa mafuta; maisha yawananchi maskini wa vijijini na wa mijini wanaathirikana bei ya mafuta ya taa, hali hii imeongeza ugumu wamaisha ukizingatia mfumuko wa bei unazidi kila

kukicha. Serikali itueleze kwa nini EWURA wanaingiagharama ya kununua vinasaba vingine vinavyowekwana EWURA wakati inaelezwa kwamba uchakachuajiunaendelea wakati solution ilikuwa kupandisha bei yamafuta ya taa? Kama imegundulika solution hiyoimefeli, basi bei ya mafuta ipunguzwe ili wananchiwapone na adha ya mfumuko wa beiunaosababishwa na bei za mafuta kupanda.Mheshimiwa Spika, uwekezaji katika Sekta yaMadini, naishauri Serikali kuweka hadharani ripoti yataarifa zote zilizowahi kutolewa kuhusiana na uwekezajikatika uchimbaji wa madini nchini kuanzia mwaka 1995hadi 2010 na kama Serikali imefaidika na nini kutokanana uwekezaji huo ili kama kuna upungufu mkubwatunao uwezo wa kuendelea au kubadili sheria.MHE. ABIA M. NYABAKARI: Mheshimiwa Spika,mimi ni mjumbe wa Kamati ya Nishati na Madini,naunga mkono hoja kwa asilimia 99 na asilimia mojachukueni maneno ya Mheshimiwa Mussa Zungu Azzanaliyochangia mfanyie kazi.Mheshimiwa Spika, viongozi hawa wa Nishati naMadini wameteuliwa, wamedhalilishwa vya kutoshawana makovu ya vidonda ndugu walivyopata tokakwa ndugu zao Wabunge. Mungu alisema: “Angalieninawatuma katikati ya mbwa mwitu, nanyi iweni wenyebusara na wapole kama hua.” Nawapongeza kwakuvumilia adha mnayoipata.Mheshimiwa Spika, macho yangu hayajaaminikama kweli katika Bunge hili kuna watu wenye kejeli,

kiburi na jeuri na wenye majivuno, lakini naaminiMwenyezi Mungu atawalipa sawasawa na mapenziyake.Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa SospeterMuhongo, Waziri na kundi lake, Naibu MawaziriMheshimiwa George Simbachawene na MheshimiwaStephen John Masele wote wa Nishati na Madinipamoja na Commando Eliakim Maswi, Katibu Mkuu waNishati na Madini kwa kudhalilishwa hivyo, Mungumwenyewe atakitwaa kitambaa na kuyafuta machozikutokana na majaribu mnayopata kutokana nauaminifu wenu. Si hivyo tu, bado mtakumbana nauchafu, ufisadi, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira,fitina, faraka, uzushi, husuda na watu wenye hila namidomo ya upotoshi, iweni makini mchague yakunena, ombeni hekima kama Mfalme Suleiman.Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa RaisJakaya Mrisho Kikwete kwa zawadi hii nzuri ambayoameiteua iwatumikie Watanzania, Naamini sasaSerikali imepata viongozi wenye uwezo katika Wizarahii, wenye fikra sahihi na matendo thabiti katikakuliendesha gurudumu la Taifa ili kuleta maendeleokatika jamii.Mheshimiwa Spika, nawaombeni sana viongozihawa wa Nishati na Madini kuwa macho na vituo vingivinavyoota kama uyoga na wakati wenginewanafunga vituo vyao au kuendesha kwa shida na sihivyo tu naombeni muwe macho kwenye bomba lamafuta (mita).

Mheshimiwa Spika, kuhusu REA; mtakapokuwamnataka kuanza zoezi hilo anzieni Rukwa jamani, Laelana Kasanga na katika mpango ujao msisahau Kilando,Wampembe, Kate, Muze, na Ilemba. Maeneo hayoyamechangamka na watu wanaokaa maeneo hayowanao uwezo wa kulipia bill za umeme. Pamoja nayote hayo msisahau Kaseya na mpakani kuna Ofisi zauhamiaji, Polisi, TRA, Forodha, Mifugo na Afya ilikuwavuta watu waweze kujenga majengo yakibiashara paweze kuonekana kama Tunduma vile.Mheshimiwa Spika, mgema ukimsifia tembo hulitiamaji na kwa nini nawapongeza? Ni mwanzo mzurimlioanza nao. Simamieni kwa makini ushushaji wa meliza mafuta kwa muda muafaka na kuhakikishamnajipanga kudai madeni ya TANESCO na kulipamadeni ya bilioni 319 ili kuonesha ufanisi wenu kuwa niwa hali ya juu, pia hakikisheni mnajenga Ofisi zakununua madini ya Watanzania.Mheshimiwa Spika, kulikuwa na taarifa ya kupoteaumeme kila siku milioni 4.1 kwa ajili ya uchakavu wamiundombinu: Je, Wizara inatuambiaje?- Meli za mafuta zimekuwa zinakaa bandarini siku45 kwa sababu gani? Kuzuia matatizo haya ya kiinimacho mnajipangaje?- Kwa nini tunadaiwa billion 319 wakati pesailikuwa inakusanywa?

- Kwa nini TANESCO imepewa hati safi ya ukaguziwa mahesabu na CAG wakati kuna madudu haya?Huyu naye aingizwe kwenye golikiki.- Watu hao binafsi ambao walikuwa hawalipibilioni 240 na Taasisi hizo ni zipi ambazo hazilipizichunguzwe kuna nini?Mheshimiwa Spika, Mwalimu Nyerere, baba waTaifa alisema uhuru na kazi, fanyeni kazi kwa upendo,furaha na amani, uvumilivu, utu, wema, fadhila,uaminifu na muwe wapole kiasi mtakuwa juu ya sheriawala hazitawahukumu.Mheshimiwa Spika, anayesema kwa nini mafutayalipanda bei Tanzania, hata Nigeria inayochimbamafuta yenyewe yalipanda toka Naira 65 hadi kufikiaNaira 200 kufuatana na anguko la uchumi katika sokola dunia.Mheshimiwa Spika, mwisho nasema, pendanenininyi kwa ninyi kwanza. Mheshimiwa Rais atambuewatu wa Musoma wana asili ya utawala bora hatakama ni elfu 20 awaweke wainue Taifa letu, asisahauwatu wa Kigoma kama nao ni waaminifu, japokuwakila mwenye kupata cheo huitwa mtu wa Mrundi.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja.MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Mheshimiwa Spika,suala la umeme Same Magharibi, katika Jimbo langukuna vijiji vingi ambavyo vimepitiwa na umeme (high

tension), lakini hakuna transfoma na low tension line(LT). Vijiji ambavyo naviombea LT line ni hivi hapa:Vudee Msanga, Bangalala, Mabilioni, Ishindo, Njoro naGonjanza. Aidha, Vijiji ambavyo havina umeme kabisani Saweni, Gavao, Rindini, Hezamu na Ndolwa.Naomba kupata majibu ni lini nitaletewa umemekatika maeneo niliyoyataja.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE: Mheshimiwa Spika,kwanza, naomba kumshukuru Mungu, kwa kunipatiazawadi ya uhai ili nami pia niweze kuchangia katikaHotuba hii.Mheshimiwa Spika, kipekee, nawapongezaViongozi wote wa Wizara hii muhimu kwa nchi yetu kwakuanzia na Mheshimiwa Waziri na Manaibu wake.Mheshimiwa Spika, Jimbo la Mtera pamoja nakuwa na chanzo muhimu cha maji ya Bwawa la Mteraambalo hutumika kuzalisha umeme kwa maendeleoya nchi yetu, jambo la kutia huzuni ni kwamba, katikavijiji 76 ni vijiji viwili tu ndivyo vina umeme ambaoumeletwa na Wamisionari wa Kanisa la Kiangrikana,bila wao tungekuwa 0 kwa 0. Hata hivyo, naishukuruSerikali kwa kunipatia umeme kwenye vijiji vitatu vyaMlowa Barabarani, Makangwa na Iringa Mvumi. Kwaawamu hii, kwa kuwa nguzo zimewekwa marundo kwamarundo, naomba kazi hiyo ifanyike kwa kasi sana,tusiache nguzo ziliwe na mchwa. Ombi langu kwakoMheshimiwa Waziri ni kuwa awamu ya pili vikumbukweVijiji vya Fufu, Manzase na Mloda.

Mheshimiwa Spika, kwa Tarafa ya Mvumi,tusisahau Kata ya Muungano katika Vijiji vyaMuungano na Ilolo, ambako umeme umepita karibusana. Naomba pia tupatiwe umeme katika Kijiji chaNdembwe kwenda Kata ya Handali kwa ajili yaSekondari ya Kata, Tarafa ya Mpwayungu kutokaMpunguzi.Mheshimiwa Spika, Jimbo la Mjini kupitia Kata yaMwitikila, Jimbo la Bahi mpaka Naguloo hadiMpwayungu, umeme ukiwaka utakuwa ukombozimkubwa kwa Wananchi wa Jimbo la Mtera.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja asilimiamia kwa mia.MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Spika,Kampuni ya Shanta Mining imekuwepo katika maeneoya Kinyamberu, Samberu na Mhimbi katika Kata yaMang‘onyi ya Jimbo la Singida Mashariki tangu mwaka2005. Kwa kipindi chote hicho, Kampuni hiyo imetwaamaeneo ya wananchi kwa nguvu bila ya kupataridhaa ya maandishi ya wenye ardhi na bila yakuwalipa wananchi hao fidia ya haki timilifu na yawakati mwafaka.Mheshimiwa Spika, yote hii ni kinyume cha Sheriaya Madini, 2010, Sheria ya Ardhi za Vijiji, 1999 na Kanuniza Ardhi za Vijiji za Mwaka 2001.Mheshimiwa Spika, mwaka 2006, Mkuu wa Mkoawa Singida aliunda Tume ya Uchunguzi wa Madai ya

Wananchi iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Singidawakati huo Ndugu Florence Horombe. Tume hiyo ilitoaripoti iliyothibitisha kwamba, Shanta Mining ilikuwaimeingilia maeneo ya wananchi bila ya kufuatataratibu za kisheria na bila ya kuwalipa fidia. Hadi sasamapendekezo ya Tume ya Horombe kuhusu malipo yafidia kwa wananchi hayajatekelezwa, licha ya ShantaMining kuyakalia maeneo yao kwa miaka saba sasa.Namwomba Waziri atoe Kauli ya Serikali ni liniwananchi wa maeneo tajwa ya Kata ya Mang‘onyiwatalipwa fidia yao halali na malimbikizo ya riba yamiaka yote ambayo Shanta Mining imekalia maeneoyao isivyo halali.Mheshimiwa Spika, tarehe 20 Januari, 2012, Waziriwa Nishati na Madini wakati huo Mheshimiwa WilliamNgeleja, alitoa leseni ya uchimbaji ML 455/2012 kwaShanta Mining. Leseni hiyo ni ya muda wa miaka kumina inaeleza kwa maeneo ya leseni hiyo ni Misughaa naMponda Kaskazini. Maeneo yote mawili yapo katikaKata ya Misughaa ya Jimbo la Singida Mashariki. Hatahivyo, kwa miaka yote ambayo Shanta Miningimeendesha shughuli za utafiti, haijawahi kufanya kazihizo katika Kata ya Misughaa bali miaka yotewamekuwa Kata ya Mang‘onyi na vijiji vyake ambavyosiyo maeneo ya leseni ML 455/2012. Naomba Wizaraichukue hatua za dharura kuhakikisha Shanta Mininginaenda kwenye eneo la leseni yake.Mheshimiwa Spika, Mashapo ya Mang‘onyiyanakadiriwa kuwa na wakia 120,000 za dhahabuzilizothibitika. Hiki ni kiasi kidogo ukilinganisha namashapo ya migodi mingine ya dhahabu hapa nchini.

Hii ndiyo sababu maisha ya leseni hii kuwa miaka kumibadala ya muda wa kawaida wa miaka ishirini natano. Kwa sababu hizi, ni busara maeneo haya yadhahabu yaachiwe kwa wachimabji wadogo iliwananchi wa vijijini nao wapate ajira yenye kipatokikubwa kama uchimbaji wa dhahabu na shughuli zakiuchumi zinazohusiana na wachimbaji wadogowadogo.Mheshimiwa Spika, moja ya maeneo ambayoyamesababisha makubwa ya kigeni kutolipa kodi stahilikatika Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia nigharama za uendeshaji (general and administrationcosts). Katika Mikataba yote kati ya Serikali naMakampuni ya Sekta hizi, gharama za uendeshajihuwa zinatolewa katika mahesabu ya mapato kwa ajiliya kugagatua kiwango cha kodi kinachotakiwakulipwa na makampuni haya.Mheshimiwa Spika, Mashirika kama Shirika laMaendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), hayana uwezowa kiutendaji kuelewa na/au kudhibiti gharama zauendeshaji za makampuni ya uwekezaji. Matokeoyake ni kwamba, gharama hizi zinakuwa kubwa namakampuni yanakuwa hayalipi kodi stahiki kwa nchiyetu.Mheshimiwa Spika, naomba Wizara ichukue hatuaza muda wa kati na za muda mrefu za kuelimisha idadikubwa ya Watanzania katika fani za kitaalam zamafuta na gesi asilia ili tuwe na kada ya wataalamwatakaotuwezesha kufahamu mbinu za makampunizinazoyasaidia kutolipa kodi.

MHE. MWANAMRISHO TARATIBU ABAMA:Mheshimiwa Spika, katika kuichangia hoja hii ya Wizaraya Nishati na Madini, nitazungumzia kuhusu wachimbajiwadogo. Wachimbaji wadogo wanateseka sana. Je,Serikali inawapangia nini wachimbaji wadogo ambaomaeneo yao yamechukuliwa na wachimbajiwakubwa?Mheshimiwa Spika, nimeona katika bajeti yakowachimbaji wadogo wamepangiwa mikopo shilingibilioni 2.5 pesa za ndani na dola za marekani milioninne na shilingi bilioni 6.4 ni fedha za nje.Mheshimiwa Spika, kawaida mdogo hufunikwa namkubwa kwa maslahi ya mtu au watu. Mikopo hii nilazima kuhakikisha ina wafikia walengwa, kwani kunawachimbaji wengine huwa hawataki kuchimba ilahutaka kuhodhi maeneo halafu wanayauza kwawachimbaji wakubwa.Mheshimiwa Spika, Wizara Nishati na Madini chiniya Waziri na Naibu Mawaziri, wazidi kuwa makinikuliokoa Taifa hili la Watanzania.Mheshimiwa Spika, pili, uwepo utaratibu ambaoutakuwa unawatambua na kuepuka wachimbajiwadogo kugombana na wachimbaji wakubwa ilikuepuka kuchangia maeneo.Mheshimiwa Spika, wachimbaji waongezewethamani kwenye madini yao, kwa kujengewa viwandavya kuongezewa thamani madini yao, kupatiwa

mashine za kukatia madini na Serikali ishughulikie bei zamashine hizo, wachimbaji wadogo watafutiwe masokoya kuuza thamani zao. Serikali iwatafutie kipimo chamadini na kama kipo basi wauziwe kwa bei nafuu iliwakimudu.Mheshimiwa Spika, ahsante.MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika,napenda kutumia nafasi hii kwa njia ya maandishi,kuwapongeza Waziri wa Nishati na Madini -Mheshimiwa Prof. Muhongo, Naibu Waziri wa Nishatina Madini anayeshughulikia nishati - NheshimiwaGeorge Simbachawene, Naibu Waziri wa Nishati naMadini - Mheshimiwa Stephen Masele, Katibu Mkuumtani wangu Eliakimu Maswi na Watendaji wotewalioshiriki kuandaa Bajeti hii nzuri, yenye mwelekeowa kurudisha heshima ya Wizara ya Nishati na Madini.Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiofichika kuwa,Wizara kupitia Waziri na Naibu Mawaziri, wakishirikianana Katibu Mkuu Maswi, wamefanya kazi nzuri kwakufuatilia Taasisi zake na kugundua Taasisi ya TANESCOimefanya ubadhirifu mkubwa wa kufuja fedha kwakutoa tender kwenye makampuni ambayo yalikuwayanauza mafuta kwa bei ya juu sana, yaani lita Shilingiza Kitanzania 1,800 wakati ilikuwepo kampuni iliyokuwainataka kuuza kwa bei ya shilingi 1,500.Mheshimiwa Spika, hivi kweli Mtendaji wa kuliokoaTaifa na uzalendo wa juu; ninaomba WaheshimiwaWabunge wenzangu muwaunge mkono Watendajiwenye uzalendo kama Ndugu Eliakim Maswi. Kutafuta

taarifa mbalimbali kwa maslahi ya nchi siyo vibaya balitusitumiwe na mtu au kikundi cha watu kwa maslahibinafsi. Tabia hii tutakuwa hatuwatendei hakiWatanzania wanaotegemea sana uwakilishi wetu, vilevile tutakuwa tunawavunja moyo Watendaji naMawaziri wetu. Ninapenda kumtia moyo NduguMaswi, akaze buti kazi yake ni ya mfano wa kuigwa.Mheshimiwa Spika, ninaipongeza Serikali kwakutenga shilingi bilioni 140 kwa ajili ya kupeleka umemevijijini. Pamoja na pongezi hizi, napenda kuendeleakuiomba Serikali ili ujenzi wa umeme vijijini uendeharaka ni vyema fedha zilizotokana na kuongeza kodiya mafuta ya taa ambazo zimetokana na kudhibitiuchakachuaji ya shilingi billion 300 zipelekwe REApamoja na fedha zilizokuwa zinapatikana kwa ajili yavinasaba sasa vinasaba vitoke kwani uchakachuajihaupo tena baada ya kupandisha bei ya mafuta yataa nazo ni shilingi bilion kumi kwa mwaka ziende REA.Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiofichika kasi yakupeleka umeme vijijini itaonekana haraka sana.Ninasubiri majibu mazuri kutoka kwa MheshimiwaProfesa Muhongo, Waziri mwenye dhamana na NaibuMawaziri wote wawili, wakati wakijibu hoja zaWabunge. Umeme ukifika kwa Watanzania woteutasaidia akina mama kuondokana na kupikia mkaana kuni hadi wanakuwa na macho mekundu nawanauwawa kwa kudhaniwa wachawi.Mheshimiwa Spika, napenda kurudia rai yangukuwa kuna umuhimu wa pekee kwamba, Serikali ifanyebidii kutengeneza Sera na Sheria kabla ya kuanza

shughuli za gesi ili kuondokana na mikataba mibovu,jambo litakaloleta tija ya uzalishaji kupitia gesi asilia.Mheshimiwa Spika, endapo gesi itasimamiwaipasavyo, Taifa litapata shilingi trilioni 600; hii itatoshakutekeleza Miradi yote kwani Bajeti ya Serikali sasa nishilingi trilioni 15 tu. Itaondoa umaskini na wananchiwote watanufaika kuanzia Mkoa wa Mtwara na Mikoayote nchini.Mheshimiwa Spika, vile vile napenda kuishauriSerikali kuanzisha Mfuko wa Mapato ya Gesi nautumike kutekeleza Miradi ya Maendeleo nchi nzima.Hii itaturahisishia kujua gesi imechangia kwa kiwangogani kuwaletea Watanzania maendeleo.Mheshimiwa Spika, vile vile mipango ianze sasa yakujenga viwanda vinavyotumia gesi; mfano, Kiwandacha Mbolea, Kiwanda cha Kemikali na kadhalika iliuzalishaji na matumizi vianze mara moja miaka mitanompaka minane ijayo.Mheshimiwa Spika, napenda kuipongeza Serikalikwa kuendesha semina ya madini Singida na maeneomengine nchini. Ninapenda kukiri kuwa, semina hiyoimesaidia sana kuwapa uelewa wachimbaji wadogo,watendaji wa vijiji na wananchi wanaozungukwa namigodi. Ninaiomba Serikali iongeze fedha zakuendesha semina na kuwawezesha fedha za kununuavitendea kazi. Tukiwakopesha wachimbaji, itasaidiawachimbaji kufaidi matunda waliyopewa na Mungu.

Mheshimiwa Spika, ninaishauri Serikali ihakikishemikataba yote ya madini inawekwa wazi na iwe yenyekuwanufaisha Watanzania.Mheshimiwa Spika, ninasisitiza kuwa service levyitokanayo na migodi iwe asilimia 0.3 kama sheriainavyosema, hatuna sababu ya kuyumba.Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba Serikalimaeneo yote yaliyoahidiwa kupelekewa umemeMkoani Singida, itekelezwe kama ilivyopangwa.Mheshimiwa Spika, namshukuru Mwenyekiti wanguwa Kisekta, kwa kushiriki katika kutusaidia kuishauriKamati masuala ya kitaalam, nasi kuyashauri mashirikaili kuimarisha ufanisi.Mheshimiwa Spika, napenda kumalizia kwakuunga mkono hoja.MHE. MKIWA A. KIMWANGA: Mheshimiwa Spika,nami napenda kuchangia hoja iliyoko mbele yetu.Kwanza, napenda kuwapongeza Waziri, MheshimiwaMuhongo na Naibu Waziri; Mheshimiwa Masele naMheshimiwa Simbachawene, kwa kuteuliwa katikaWizara hii. Ni matumaini yetu kuwa upele umepatamkunaji.Mheshimiwa Spika, napenda kuwaambia kuwa,Watanzania watakuwa na imani nanyi kwa jinsimlivyoanza kazi, tunawaombea Mwenyezi Munguawape afya na nguvu zaidi ili mtuondoe tulipo.

Mheshimiwa Spika, naomba Waziri aniambiejambo moja wakati wa majumuiisho; Geita katika Kataya Mtakuja, eneo la Nyakabale, kuna ardhi ambayoGGM waliihitaji na uthamini ukafanyika kwa ushirika katiya Watendaji na Wawakilishi wa GGM, lakini cha ajabuwakati wa malipo ya fidia, mtu mwenye migomba 200alilipwa migomba 50, miti ya mbao 300 kalipwa 70 namambo mengi ambayo wamelipwa kwa kupunjwa.Hiyo ni miaka minane iliyopita, lakini wakazi haowamefuatilia mpaka wamekaa chini. Katika Bunge laSaba niliuliza swali lakini jibu nilipewa kuwa GGM kwasasa hawahitaji eneo hilo tena.Mheshimiwa Spika, Wizara haijaenda hata sikumoja kuwaambia hawahitaji eneo hilo. Pia NaibuWaziri aliyepita nilimwomba tuongozane aendeakawaambie wananchi kuwa pesa waliyopewa walelakini ardhi bado ni mali yao, alikubali lakinihatukuenda nae huko.Mheshimiwa Spika, hebu tazama leo ni miakaninane shughuli za maendeleo hazifanyiki. Naombaniulize kama baada ya Bunge hili tutaongozana naWaziri au Naibu Waziri ili tukawafariji watu hawa?Naomba kauli kutoka Wizarani ili wananchi hawawaweze kufanya shughuli zao za maendeleo.Mheshimiwa Spika, napenda nimwulize Waziri;miaka minane wananchi hawa hawafanyi shughuli zamaendeleo; ni nani atawalipa gharama ambazohawakufanya kilimo, hawakuendeleza makazi na hatakuziba maeneo nyumba zao zimebomoka?

Mheshimiwa Spika, kauli ya Waziri kwa wananchihao. Naomba matamko yenu sana tena sana iliWakazi wa Nyakabale wawe na amani.Mheshimiwa Spika, ahsante.MHE. MAHMOUD HASSAN MGIMWA: MheshimiwaSpika, sina shaka na utendaji wa Waziri na NaibuMawaziri waliopo kwenye Wizara hii.Mheshimiwa Spika, pamoja na imani kubwaniliyokuwa nayo kwa Waziri na Manaibu wake, badokuna matatizo makubwa sana katika Wizara katikamaeneo ya Nishati na Madini.Mheshimiwa Spika, nikianza na umeme ni tatizokubwa sana na la kushangaza sana katika Tarafa yaKibengu, iliyopo Wilaya ya Mufindi katika Jimbo laMufindi Kaskazini.Mheshimiwa Spika, Bwawa la Kihansi lipo Tarafa yaKibengu, yenye Kata tatu; Kata ya Mapanda, Kibenguna Ihalimbo zenye vijiji 17. Vyanzo vikuu vya maji vipokatika vijiji hivi na bwawa hili linatoa megawatt 184kweneye Gridi ya Taifa.Mheshimiwa Spika, wananchi katika Tarafa hii,waliombwa zaidi ya miaka 15 iliyopita na Serikali kupitiaTANESCO, kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji nawananchi katika Jimbo langu walikubali nawaliahidiwa kupewa umeme kama mbadala. Chakusikitisha, leo ni zaidi ya miaka 15.

Mheshimiwa Spika, hitaji la Tarafa ya Kibengu nimegawatt mbili; hili linatusikitisha sana, tumemwonaNaibu Waziri, tumekutana na Uongozi wa TANESCOnikiwa na Madiwani wangu kutoka katika Tarafa hii yaKibengu, lakini cha kusikitisha tunapewa ahadi nzurizisizotekelezeka.Mheshimiwa Spika, nimeshawasiliana na NaibuWaziri, Mheshimiwa George Simbachawene, kwenyehili nataka nitoe angalizo Serikali inatakiwa itoe jibu iliwananchi wajue hatima yao.Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee,naomba nichukue fursa hii, kuishukuru sana Serikali yaChama cha Mapinduzi kwa kutekeleza ahadi katikaKata ya Ifwagi sasa umeme unawaka.Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi zangu,naomba sana Serikali hasa TANESCO, itekeleze ahadiyake ya kupeleka umeme katika vijiji vya Mfikilwa naIkongosi. Pia wapeleke umeme kwenye Taasisi za Shuleya Sekondari ya Ifwegi na kwenye Gereza la Isupilo.Mheshimiwa Spika, sehemu nyingine ambayoSerikali inatakiwa kutusaidia ni katika Vijiji vya Ludilo naIlasa. Kuna Mradi wa Mwinga Hydro Electricity kwa ajiliya vijiji 13 katika Wilaya ya Mufindi. Kwa masikitikomakubwa sana, vijiji hivi ambapo umeme unapitavimeachwa. Tumeongea mara nyingi na Uongozi waTANESCO na Wizara, lakini mpaka leo hakunakinachoendelea.

Mheshimiwa Spika, napenda kusikia kauli yaSerikali kuhusu suala la umeme katika vijiji hivi.Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni la Kata yaRungemba, ambalo lilitakiwa kuwa tayari umemeunawaka na wananchi katika maeneo hayawameshalipwa fidia zaidi ya mwaka, lakini kwamasikitiko makubwa, kazi ya kuweka umeme katikaeneo hili bado haijaanza mpaka leo. Naomba kusikiatamko la Serikali lini wataanza kazi ya kupeleka umemekatika eneo hili.Mheshimiwa Spika, nataka nirudie tena, nina imanikubwa sana na uwezo wa Waziri, Mheshimiwa Prof.Sospeter Muhongo na Naibu Mawaziri wake;Mheshimiwa George Simbachawene na MheshimiwaStephen Masele, kwa gia kubwa waliyoanza nayokatika uchapakazi katika eneo hili la Nishati na Madini.Mheshimiwa Spika, nampongeza sanaMheshimiwa George Simbachawene, kwa utendajiwake na pia nampongeza sana Mheshimiwa StephenMasele, kwa ujasiri na uadilifu wake katika kusimamiahaki katika maeneo ya Madini aliyoyatembelea katikaNyanda za Ziwa na Melelani.Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba majibukwenye hoja zangu.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii.

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA: Mheshimiwa Spika,naomba nianze kwa kuunga mkono hoja nakumpongeza Waziri na Timu yake yote Wizarani, kwamatayarisho na uwasilishaji mzuri wa Bajeti.Mheshimiwa Spika, nitajikita katika masuala mawilikatika mchango wangu; Sekta ya Gesi na Umemevijijini.Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa juhudiza kutafuta gesi na mafuta. Ugunduzi wa gesi Mtwarana Lindi ni habari njema kwa Taifa letu; hivyo, nimuhimu Serikali ikawekeza sana katika Sekta hiiambayo ndiyo itakuwa mojawapo wa ufumbuzi waPato la Taifa.Mheshimiwa Spika, ni muhimu sana Serikali harakaiweke Sera Mahususi ya Gesi na Sheria ili zibainishenamna gani Serikali inaweza kusimamia kwa makinirasilimali hii muhimu ya gesi.Mheshimiwa Spika, ninaiomba Serikali ielekeze auiongeze jitihada zake kufikisha umeme vijijini ilikuchochea maendeleo hasa katika Sekta ya Kilimo.Mheshimiwa Spika, Serikali kwa mwenendo huuwa kutenga bajeti kidogo, itachukua muda kufikishaau kukamilisha mpango wake wa kufikisha umemevijijini. Hivyo basi, Serikali haina budi kuongeza bajeti yaumeme vijijini.

Mheshimiwa Spika, naipongeza sana Serikali kwauamuzi wake wa kupunguza gharama za kuunganishaumeme kwa karibu asilimia hamsini.Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hojana kukumbushia umalizaji wa Mradi wa Umeme Vijijinikatika Wilaya ya Ulanga.MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Spika, sinabudi kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi waRehema, Mwenye Kurehemu, ambaye ameniwezeshakuwa na uhai na afya hasa katika Mwezi huu Mtukufu,awajalie wale wote ambao wameshikamana nayo herikubwa ndani yake; amina.Mheshimiwa Spika, nianze na suala la madini.Pamoja na kuwa madini ni neema ya nchi yetu, lakiniinaonekana kutosaidia ipasavyo wananchi hasasehemu ambayo inachimbwa madini hayo.Mheshimiwa Spika, mahusiano mabaya kati yawawekezaji na wananchi, yanasababishwa na Sera naMipango mibaya ya madini, hivyo, hupelekeawananchi kukosa fursa muhimu na huduma muhimukatika vijiji vyao. Utakuta mahusiano mabayayanasabaisha maafa makubwa sehemu mbalimbaliambazo zinatoka madini. Wananchi kukosa imani naViongozi wao na Serikali yao, Vijana wanakosa ajira nakubaki yatima katika nchi yao, vijana wanapojaribukuokota baki ya mawe ambayo yameshapembuliwadhahabu, wanauwawa kwa risasi pasipo huruma.

Mheshimiwa Spika, mahusiano mabayahusababisha uduni wa maisha ambamo wanazalishamadini, wananchi wanakosa elimu bora, matibabubora, maji safi na salama, umeme na barabara safi,wanakosa huduma muhimu zote lakini Dhahabu,Almasi Tanzanite, Rubi na nyinginezo vinaondoka.Mheshimwa Spika, Wananchi wanabaki na athariya umaskini na uchafuzi wa mazingira katika vijiji; hii nihatari na athari kubwa kwa nchi yetu.Mheshimiwa Spika, matatizo yanayowakumbawachimbaji wadogo ni sana. Miongoni mwa matatizohayo ni urasimu mkubwa wa kutafuta leseni. Hili nitatizo kwa wachimbaji wadogo na kupelekea kutumiagharama kubwa katika ufuatiliaji. Eneo moja kutolewaleseni mbili, bajeti hawafikii wachimbaji wadogo, zanaduni katika uchimbaji, kukosa umeme maeneo yauchimbaji, vitisho vinavyotolewa na baadhi yaviongozi, elimu na soko bora kwa thamani ya mali zao.Mheshimiwa Spika, naomba Serikali iangalie kwaumakini sana na kuboresha wachimbaji wadogowadogo. Kwa mujibu wa Waziri wa Nishati na Madiniwakati wa uzinduzi wa bomba la mafuta toka Mtwarahadi Dar es Salaam, Tanzania ina utajiri wa gesi yenyethamani ya shilingi trilioni 626.71, sawa na bajeti yamiaka 40 ijayo. Wasiwasi uliopo kwa watu walio wengisasa hivi ni namna tutakavyotumia vizuri utajiri huukuinua uchumi wa nchi. Mambo ya kuzingatia ilitunufaike ni lazima Serikali iweke wazi mikatabaendelevu, uwezo wa kuvuna rasilimali hii hasawataalam wa ndani na mengine yafananayo na hayo.

Mheshimiwa Spika, utajiri wa gesi usiwe laana kwanchi yetu. Nchi nyingi zenye rasilimali kama gesi,madini na mafuta, zimeingia kwenye lindi la migogoro.Kama Taifa, tuwe makini sana ili kwa umoja wetu,Mwenyezi Mungu atuepushie mbali utajiri wa gesi usiwelaana bali ulete baraka. Nchi kama Nigeriawalipogundua mafuta, kwa vile hawakujiandaanamna ya kufaidika na baraka hii, walijikuta wakiingiakatika migogoro ya wenyewe kwa wenyeweikiambatana na fujo na maandamano ya watu wamakundi mbalimbali ya kijamii.Mheshimiwa Spika, mimi naomba Serikali iwemakini tusifike huko.Mheshimiwa Spika, ahsante.MHE. HIGHNESS S. KIWIA: Mheshimiwa Spika, Mradiwa Umeme kupitia MCC ambao kimsingi kwa taarifa zaawali kwa upande wa Kata zangu za Sangabuye(Kayenze) na Buswelu ulipaswa uwe umekamilikakatika maeneo hayo, lakini mpaka sasa utekelezajiwake haujaanza. Kwa mujibu wa mkataba wamkandarasi, kwa maeneo aliyokuwa amepangiwa,alipaswa kazi hiyo awe ameanza kufikia mwezi wa tisamwaka huu.Mheshimiwa Spika, naomba nipewe ufafanuzi nasababu zilizopelekea Mradi huo wa Umeme kupitiaMCC kutokuanza na kukamilika hadi sasa?MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja. Sina haja ya kurudia kutoa

pongezi, kwani walizopewa zinatosha sana,ninachotaka kusema nami naungana na wotewaliotoa pongezi kwani wanastahili.Mheshimiwa Spika, namshukuru Waziri, Naibuwake, Katibu Mkuu wake na Watendaji wote, kwakuwapatia umeme wa uhakika wananchi wangu waMtwara Vijijini na kutuhakikishia kupata service levy yaasilimia 0.3.Mheshimiwa Spika, napenda kuihakikishia Wizaraya Nishati na Madini ushirikiano katika kutekeleza Mradiwa Bomba la Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.Mheshimiwa Spika, naiomba Wizara kuhakikishakuwa inasimamia maslahi ya Wananchi wa MtwaraVijijini na Mtwara kwa ujumla. WahakikishieniWananchi wa Mtwara umeme wa uhakika, kazikwenye Sekta ya Gesi na kuhamasisha wawekezajikujenga viwanda Mtwara na pia watumie hudumakutoka Mtwara.Mheshimiwa Spika, mwisho, naunga mkono hoja.MHE. GREGORY G. TEU: Mheshimiwa Spika,nampongeza Waziri, Naibu Mawaziri na Katibu Mkuu.Mheshimiwa Spika, yahusu kuendeleza usambazajiumeme katika Makao Makuu ya Wilaya na Vijijihususan katika Jimbo la Mpwapwa – Dodoma.Mheshimiwa Spika, naupongeza sana Wakala waNishati Vijijini (REA), kwa kazi nzuri wanayofanya kule

Jimboni Mpwapwa, ingawa bado kuna maeneokadhaa ambayo kwa bahati mbaya, hayakuainishwawakati maandalizi. Maeneo haya yamerukwa nakuachwa katikati, umeme utakapowaka maeneohaya yatakuwa yameachwa bila umeme.Mheshimiwa Spika, napendekeza Wakala waNishati Vijiji (REA) wanaoendelea na kazi hivi sasaJimboni Mpwapwa, wasiondoke katika Jimbo laMpwapwa bila kukamilisha usambazaji umeme katikamaeneo yaliyoachwa siyo makusudi bali maelekezohafifu ya awali. Kuondoka na kurudi tena kwa awamunyingine, itakuwa gharama kubwa sana ukizingatiamitambo mikubwa inayotumika.Mheshimiwa Spika, maeneo yanayohusika nakasoro hii ni haya yafuatayo:-(a) Kata ya Matomondo (Jimbo la Mpwapwa),vijiji husika ni Chisalu, Tambi, Mlembule, Mwenzele,Mbori na Makuputa;(b) Kata ya Lupeta (Jimbo la Mpwapwa), vijijihusika ni Bumila na Chang‘ombe;(c) Kata ya Chunyu/Nghambi (Jimbo laMpwapwa), vijiji husika ni Kazania na Kiyegeya; na(d) Kata ya Maze (Jimbo la Mpwapwa), vijijivinavyohusika ni Isinghu, Kwamshango na Chiseyu.Mheshimiwa Spika, inawezekana Wizara inaoutaratibu wake ambao sipingani nao. Ninachoshauri ni

kwamba, REA wakiondoka katika eneo ambako wapohivi sasa, kurudi tena baadaye (Awamu ya Pili),gharama zitakuwa kubwa ni kheri wamalizie kabisakisha waondoke.Mheshimiwa Spika, nawapongeza sana REA kwakazi nzuri wanayoifanya.MHE. ZAHRA ALI HAMAD: Mheshimiwa Spika, Serani Dira, bila ya Dira mwelekeo wa safari unakuwamgumu kufika. Wizara inachelewa kukamilisha Sera yaGesi, naomba ikamilike ili kuonesha njia ili yale makosamakubwa ambayo tulifanya nyuma kama ya madinitusiyarudie tena, yanatia aibu na si aibu tu balikudidimiza uchumi wa nchi yetu, ambapo asilimiakubwa ya wananchi wetu ni maskini, wasiotimiza miloangalau miwili kwa siku. Naomba Sera itekelezweharaka sana ili lengo letu liweze kufikiwa.Mheshimiwa Spika, naungana na WaheshimiwaWabunge wote ambao walichangia kuwa kwa vilemashine za kutengenezea vito ni za gharama sana,basi ni vizuri uchimbaji huo wakaachiwa wenyewe.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja na kumtakia Waziri na Manaibu wakeheri na fanaka.Mheshimiwa Spika, ahsante sana.MHE. PROF. JUMA A. KAPUYA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja kwa asilimia mia kwa mia.

Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri, ambayekwa muda mfupi ameweza kuielewa Wizara yake vizurina kuhimili changamoto zake.Mheshimiwa Spika, naenda moja kwa mojakwenye hoja ya umeme vijijini. Kwa kweli REAwanajitahidi, nimevutiwa kuona kuwa robo ya Vijiji vyaWilaya ya Kalina vimetajwa lakini Waziri umeacha vijijivifuatavyo: Kijiji cha ulindwanoni ambacho ndipoyapo Makao Makuu ya Wilaya ya Kaliua. Kwenye Kijijihiki cha Ulindwanoni ndiko ambako na nyumbaatakayoishi Mkuu wa Wilaya wa Kaliua ilipo. Naombasana kijiji hiki nacho kijumuishwe.Kijiji cha Usinge kutokana na wingi wa watu pale,takriban karibu watu 20,000 na pia kutokana na watukujishughulisha sana na ujasiriamali wenye kuhitajinishati ya umeme, mpaka wamefikia kubuni mbinu zaowenyewe za kuwa na nishati hii ya umeme, lakiniwakati mwingine kwa mbinu ambazo siyo salama.Tulishapata ajali ya moto ambao uliunguza soko zimana maduka yaliyokuwa yamezunguka soko hilo.Mheshimiwa Spika, kutokana na hali hii ndiyomaana Tume ya Wataalam ilipokuja kufanya feasibilitystudy walipendekeza kijiji hiki kipewe jenereta.Naomba sana kijiji hiki kipewe jenereta hii. Vile vilenamwomba Mheshimiwa Waziri akitembelee Kijiji hikicha Usinge kama ambavyo Waziri aliyekutanguliaalivyokuwa amewaahidi wananchi hawa.

Mheshimiwa Spika, katika feasibility study hiyo hiyovijiji vifuatavyo viliwekwa katika utaratibu wa kupatiwaumeme:-(a) Kata ya Ugunga: Vijiji vya Ugunga,Tuombemungu, Limbula, Limbula Siasa na Mkuyuni;(b) Kata ya Igagala: Vijiji vya Imalampaka,Kamsekwa, Mtakuja, Kazanaupate, Wachawaseme naKombe; na(c) Kata ya Kazaroro: Vijiji vya Imalamihayo,Kazaroho, Igwisi, Usangi, Lukalanga, Usimba, Nsimbo naKasungu.Mheshimiwa Spika, naomba sana vijiji hivivizingatiwe katika utekelezaji.Mheshimiwa Spika, mwisho, pale Kijijini Kasungu,Kata ya Kaliua, palitokea explosion kubwa sana wakatikampuni moja ya Wazungu walipokuwa wanachimbakisima ikabidi wakimbie baadaye wakaliziba shimo hilo.Tunahisi panaweza kuwa na gesi, naomba Waziri ajeafanye utafiti wa kina mahala hapa maana huendanasi tunaweza kuwa na neema hiyo ya gesi.Mheshimiwa Spika, namalizia kwa kumpongezatena Mheshimiwa Waziri na kumtakia utendaji kazimwema.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia kwa mia.

MHE. DKT. BINILITH S. MAHENGE: MheshimiwaSpika, nawapongeza sana Waziri, Mheshimiwa Prof.Muhongo na Manaibu wake wote wawili, kwa kazi nzurisana ya kuokoa mabilioni ya fedha yaliyotaka kuliwana wajanja wachache; hongereni sana.Mheshimiwa Spika, Mradi wa Umeme wa Rumakali– 222 MW, umo kwenye mpango wa kati wa kuzalishaumeme 2017, lakini nimeangalia Kitabu cha Hotuba yaWaziri sijaona hata setensi moja inayoelezea kuhusuMradi huu. Wananchi waliokuwa wanasikiliza Hotubawanahoji kwamba, Mradi huu umechakachuliwatayari? Naomba ufafanuzi.Mheshimiwa Spika, umeme vijijini; nimewakilishamaombi Wizarani na kwa Waziri (Naibu), kuhusu vijijivilivyopitiwa na nguzo za umeme toka Mbeya kujaMakete. Vijiji hivi ni Kitulu, Ujuni, Nkenja, Isapulano naLuvulunge. Vijiji hivi vitaendelea kulinda nguzo mpakalini? Naomba ufafanuzi.Mheshimiwa Spika, ninaleta maombi Wizarani naREA kuhusu upelekaji umeme Kata ya Ipelele na Iniho(Makete). Wataalamu walikwenda kupima, napendakujua upelekaji wa umeme utaanza lini?Mheshimia Spika, Miradi ya Umeme wa Maji:Tumepeleka maombi ya Mradi wa MaporomokoMadogo Madogo katika Vijiji vya Ipelela na Iniho.Wataalam wamekwisha kwenda kupima eneo hili,ningependa kujua nini hatima ya Mradi huu waUmeme? Naomba ufafanuzi.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mshimiwa Spika,napenda kusisitiza juu ya kuwanyonga wahujumu wauchumi nchini. Kwa kuanza na hao ambaowamekuwa wakisababisha mgao wa umeme ndani yaTANESCO kwa makusudi na kisha tuingie Bungenikuwakamata na kuwanyonga Wabunge wotewanaohusika kuunga mkono upuuzi unaofanywa naWatendaji wachache Serikalini.Mheshimiwa Spika, kamwe TANESCO na Taifahavitaweza kuendelea kwa kuwalinda watu wotewanaowatetea watu kama akina Mhandisi Mhando,ambao wanataka kununua mafuta kwa bei ya juu.Hawa si wenzetu hata kidogo.Iwapo mnaogopa kunyonga, tutunge Sheria namimnipatie cheo cha kuwa Mnyongaji Mkuu tena kwarisasi hadharani baada ya mtu kupatikana na hatia yauhujumu uchumi. Hakuna sababu ya kupoteza mudakila siku kulumbana Bungeni na nje ya Bunge kumbekuna watu wachache wana maslahi yaowanayoyajua; hili halikubaliki.Mheshimiwa Spika, naomba majibu wakati wamajumuisho ni lini utaletwa Muswada Bungeni wakunyonga wahujumu uchumi?Mheshimiwa Spika, nawasilisha.MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Spika,asubuhi nilipotoa mchango wangu wa maandishinilisahau kuwa Serikali iliahidi kupeleka umeme katikaTarafa ya Simbay (Makao Makuu), kupitia Wareta,

Dirma na Simbay kutoka Nangwa. Pamoja nakwamba, Mradi umeanza kutekelezwa, lakiniumechukua muda mrafu; ni takriban miaka miwili,naomba kasi ya utekelezaji iendelee. Vilevile kulikuwana Mradi wa Kupeleka Umeme Masakta, Masagarodana Getesam, lakini ulisimama kutokana na ujenzi waBarabara ya Minjingu – Singida. Ujenzi wa barabaraumekamilika; hivyo, naomba umeme sasa upelekweREA, waliniahidi kuweka umeme wa solar katika Shulezetu za Sekondari za Kata.Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Hanang nitashukurukama shule zetu zitanufaika na umeme ulioahidiwa.MHE. SYLVESTER M. KASULUMBAYI: MheshimiwaSpika, Jimbo la Maswa Mashariki na Wilaya ya Maswakwa ujumla wake, umejaliwa kuwa na utafiti warasilimali za mifugo, pamba, alizeti, mbaazi, mpunga naardhi nzuri inayokabiliwa na ukame na ina utitiri mwingiwa madini ya aina ya dhahabu, almasi, chuma, shaba,nikel na mengine mengi kama yanavyoonekana katikaQDS 49/2, QDS 49/1, QDS 49/3, QDS 49/4, QDS 50/1,QDS 50/3 na QDS 35/3.Mheshimiwa Spika, ninaiomba Serikali kwa kupitiaWizara ya Nishati na Madini, wakati wa kuhitimisha ionehaja ya kuiwekea mgawo wa umeme Wilaya hii katikaVijiji vyake vya Ipililo, Bushashi, Ngulinguli,Mwabayanda, Isageng‘he, Mbalagane, Mwakidiga,Mwadila, Mandang‘ombe na Gula.Mheshimiwa Spika, vijiji hivyo vikigawiwa umeme,Maswa itaanza kuvitumia vipaumbele vyake vya

kuimarishia uchumi kwa kuzitumia rasilimali nilizozitaja.Umeme utasukuma uanzishwaji wa usindikaji wa ngoziambazo zinapatikana kwa mamilioni ya tani, viwandavidogo vya alizeti, uanzishaji wa kiwanda cha nyama,ng‘ombe wanapatikana wa wingi uanzishaji wakiwanda cha nguo, pamba huzalishwa kwa mamilioniya tani katika Wilaya ya Maswa.Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Maswa iliyopatiwautajiri wa madini ya aina nyingi, wananchi kwa kutakakuyavuna madini hayo, wameamua kujiunga katikaUmoja wa Wachimbaji Madini Wadogo Wadogo waWilaya ya Maswa ambao umeshasajiriwa BRELA.Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo hawawameviomba vibali vijiji vinavyohusika ili waanzekuchimba madini hayo na hivyo ninaiomba Wizara yanishati na Madini iwatengee maeneo ya kuchimbamadini hayo kufuatia maabara ya madini iliyokoDodoma kuthibitisha kuwa sampuli zilizotumwa nawachimbaji zilithibitisha kuwepo kwa Dhahabu, Almasi,Shaba, Chuma, Nikel na mengine mengi.Mheshimiwa Spika, wachimbaji hawa wadogoninaomba wapatiwe leseni ili waingie katika ajira isiyorasmi na hivyo waweze kuujenga uchumi wa Maswana kuchangia kuongeza Pato la Taifa.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii.MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Spika,nampongeza Waziri, Manaibu wake; MheshimiwaSimbachawene na Mheshimiwa Masele, wakishirikiana

na Kamanda Maswi kama Katibu Mkuu.Nawapongeza sana, nakumbuka miaka ya 1995 kamasijakosea huyu Katibu Mkuu alikuwa Mwanachamawetu wa NCCR-MAGEUZI; hongera sana.Mheshimiwa Spika, walifanyika uamuzi wakizalendo, kuthibitisha kuwa huenda kwa muda mrefutumekuwa tukinunua mafuta kwa bei isiyo stahili; hivyo,napendekeza uchunguzi ufanyike tuweze kujua tangumwaka 2006 tumenunua mafuta kwa bei isiyo stahilikwa kiasi gani na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yawahusika. Kama tumeweza kushusha bei ya mafutakutoka shilingi 1800 mpaka 1400 ni ushidi kwamba,kuna hasara kubwa tumepata.Mheshimiwa Spika, ni muhimu kujua na kushirikikaribu katika tafiti za gesi. Zipo zinatumia dola milionimoja kwa siku, gharama hizi ni kubwa sana na zitakujakutuathiri baadaye wakati wa uzalishaji (overexpenditure concept).Mheshimiwa Spika, mfumo wa kupata au kununuaumeme kutoka makampuni ya kukodi ni hasara kubwa.Nimefanya uchunguzi kwa kampuni chache tu zaAGREKKO, SONGAS, IPTL, SYMBION, toka 2002 hadi 2012tumepoteza zaidi ya shilingi trilioni moja. Hizi nigharama ambazo tumezilipa pasipo kununua umeme.Hii mikataba haifai; hivyo, nashauri uangaliwe utaratibuwa kuondokana nazo.Mheshimiwa Spika, napongeza kwa maendeleoya ujenzi wa bomba la gesi, lakini tukumbuke kuwa ilikupunguza gharama ni muhimu tupate mitambo yetu

mipya, baada ya kupata gesi tuweze kufua umemekwa kutumia mitambo yetu wenyewe.Mheshimiwa Spika, napongeza majibu ya NaibuWaziri, Mheshimiwa Simbachawene, kwa uamuzi waWizara kuiingiza Wilaya Mpya ya Uvinza kwenyeMpango wa REA, kuhakikisha tunatumia ziada yaumeme unaopatikana Kigoma Mjini, kuhakikishaWilaya Mpya ya Uvunza inapata umeme ndani yamwaka huu wa fedha. Mradi wa Malagarasi utaletaMapinduzi ya Kilimo na Viwanda na hivyo huduma nabiashara na nchi za Burundi, Congo DRC na Zambia.Mheshimiwa Spika, hoja ya Mwadui; mchakatomzima wa uchimbaji, usafirishaji wa uuzaji wa almasibado unahodhiwa sana mwekezaji; hivyo, Serikalihaina uhakika wa mapato na thamani ya almasi. Kwamaelezo zaidi, rejea Ripoti ya Uchunguzi iliyofanywa naKamati ya PAC na kuwasilishwa hapa Bungeni Agosti 6,2004 bila kujadiliwa kutokana na nguvu za kifisadizilizokielemea Kiti na Bunge wakati huo.MHE. ALBERT O. NTABALIBA: Mheshimiwa Spika,kwanza, naipongeza Wizara na Mawaziri wote katikaSekta hii ya Nishati na Madini, kwa Hotuba nzuri sana,yenye matumaini makubwa kwa Watanzania.Mheshimiwa Spika, napenda kutoa ushauri kamaifuatavyo:-Tunaomba REA wapewe fedha zaidi ili kusambazaumeme vijijini kwenye Jimbo langu la Manyovu, ndikokuliko na Wilaya Mpya ya Buhigwe ambayo matumaini

ya kupewa umeme yameoneshwa ndani ya Hotubahii. Tunaomba tupewe kipaumbele cha umeme kwawananchi wote wa vijiji vyote.Mheshimiwa Spika, Jimbo la Manyovu, kunaHospitali ya Heri Mission, yenye umeme. Rai yangu nikwamba, REA waangalie namna ya kusaidia ili umemehuo uweze kusaidia taasisi za karibu na wananchi waliokaribu na chanzo hicho. Ninawaomba REA wafike nakutoa ushauri na kutuarifu juu ya hatua ya kufanya.Mheshimiwa Spika, ninaomba vijiji vitakavyopataumeme Kigoma, Jimbo la Manyovu, Wilaya Mpya yaBuhigwe, isisahaulike. Nilitaka kujua katika vijiji 25 nivingapi ndani ya Jimbo la Manyovu.Mheshimiwa Spika, tunaomba ukaguzi wa mita zaluku uendelee kuchunguzwa ili zisimwonee mteja auTANESCO.Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara kwakuokoa shilingi bilioni sita za ununuzi wa mafuta. Nasikama Wabunge, tunawapongeza Wizara kwa hatuahiyo.Mheshimiwa Spika, mwisho, nawatakia mafanikiomema na ninaunga mkono hoja.MHE. LOLESIA J. M. BUKWIMBA: Mheshimiwa Spika,napenda kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini,kwa Hotuba nzuri aliyowasilisha Bungeni leo.Nawapongeza Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu wa Wizarana Watumishi wa Wizara.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati na Madini niWizara muhimu sana katika maendeleo ya nchi yetu.Kwa kuwa na Nishati hata uchumi unakua kwa kasi,kwani nishati ya umeme ni kichocheo kikubwa chakukua kwa uchumi. Nichukue fursa hii kuishukuruWizara na Serikali kwa ujumla, kwa Mradi wa MCC,unaofanya kazi ya kupeleka umeme katika Mikoa sitaya Tanzania, Geita ikiwa ni mojawapo. Kwa sasanguzo zinasimikwa kwa kasi sana hasa katika Jimbo laBusanda kule Bukoli, Nyarugusu, Rwamgasa, Katoro,Bukondo, Chigunga na Nyachiluluma. Ninaombanipate taarifa ya utekelezaji hasa kujua ni lini umemehuu utawaka. Sambamba na hili, naiomba Serikaliihakikishe umeme huu unapelekwa katika Sektamuhimu katika jamii mfano katika Shule za Sekondari,Vituo vya Afya na Zahanati.Mheshimiwa Spika, katika Hotuba, ukurasa wa 51imezungumzia kuwa uchimbaji mdogo ni mojawapo yavyanzo muhimu vya ajira, lakini sijaona Wilaya ya Geitakutengewa maeneo kwa ajili ya uchimbaji mdogo.Ninaomba wakati wa majumuisho, nipate maelezo juuya wananchi wangu wa Nyarugusu, Nyaruyeye naBuziba kwamba wametengewa maeneo wapi?Mheshimiwa Spika, maeneo niliyoyataja wananchiwake wamekuwa na kilio cha muda mrefu sana juu yakutotengewa maeneo ya uchimbaji. Sera Mpya yaMadini ya 2010 imebainisha wazi kabisa kwamba,Serikali itatenga maeneo kwa ajili ya wachimbajiwadogo. Sasa basi naiomba Serikali iwaangalie

wananchi hawa, iwatengee maeneo ya uchimbajihasa katika maeneo niliyoyataja.Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni kuhusu mikopona mitaji. Ukurasa wa 52 wa Hotuba umezungumziakwamba, Serikali ilitenga shilingi bilioni 119 mwaka2011/12 na kwamba, fedha hizi zimetumika kwa ajili yaukopeshajii na ukodishaji wa vifaa kwa wachimbajiwadogo maeneo ya Rwamgasa, Wilayani Geita.Naomba kujua hao wananchi waliopewa hizo fedha niakina nani na wamepata fedha kiasi gani? Hililitanisaidia kuwapa ufafanuzi wananchi hasawachimbaji wadogo wa Geita.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika,naomba kutoa mawazo yangu katika hoja hii kamaifuatavyo:-Napenda kumpongeza sana Waziri na Manaibuwake, kwa kuteuliwa kwao kushika Wizara hii. KamaMheshimiwa Rais alivyo na imani nanyi, ndivyo naminilivyo na imani na ninyi. Mungu awasimamie mfanyekazi vizuri kwa niaba ya Watanzania na faida kwa nchi.Pia naomba Katibu Mkuu akaze boot, Munguatamsaidia pamoja na Watendaji wote.Mheshimiwa Spika, kwanza, nipongeze utaratibuwa kupeleka umeme vijijini. Nawaomba tu msipunguzekasi kwani ndiko kundi kubwa la vijana lilipo ambalohalina ajira, kwa kupeleka umeme vijijini vijana wengi

watajiajiri; hivyo, nami naomba niombee baadhi yamaeneo.Mheshimiwa Spika, katika Kata ya Ndago,inasikitisha kwamba, umeme umeishia NdagoMadukani tu, lakini ukienda mbele kuna Shule yaSekondari ya Kata (Ndago Sekondari), ambayoinahitajii umeme lakini pia ndiko anakoishi (nyumbani)kwa Mbunge huyu anayeandika mchango huu. Kwamiaka mingi nimekuwa nikiomba angalau ufike paleshuleni, ombi hilo halijazaa matunda mpaka leo. Hivyo,naomba sana tupeleke umeme Kijiji cha Kibaya,Ndago Sekondari.Mheshimiwa Spika, maomba umeme upelekweUrughu – Kata na Mtekente - Kata katika Wilaya yaIramba.Mheshimiwa Spika, nashukuru kwamba, Bajeti hiiitapelekea kupata umeme katika Wilaya Mpya yaMkalama. Niombe tu isichukue muda mrefu pamojana Ikungi kwani kwenda kwa haraka kutapelekeamaendeleo ya haraka katika Wilaya hizi mpya.Mheshimiwa Spika, kutokana na tatizo la majikatika Mji wa Singida, Mkoa ulipata Mradi wa Majikatika Kata ya Mwankoko, ambao ungemaliza tatizo lamaji. Tatizo kubwa ilikuwa ni umeme ambao TANESCOwanatakiwa wapeleke ili kuwasha mitambo yakupampu maji hatimaye kusambaza kwa Wakazi waMji wa Singida.Mheshimiwa Spika, naomba nitoe shukrani zanguza dhati kabisa kwa Mheshimiwa Waziri, ambaye mara

aada ya kumpa ki-note cha kumweleza tatizo hili,alinijibu kwa barua rasmi ya tarehe 10 Julai, 2012,yenye kumbukumbu Na. CBD,248/324/02/94. Kwelihapa namshukuru sana Mheshimiwa Waziri, naombawahusika tafadhali msimwangushe kama alivyoahidikutekeleza Mradi huu katika mwaka huu wa fedha wa2012/2013.Mheshimiwa Spika, suala la ugawaji wa viwanjavya madini naona bado lina utata hasa katika kutoaleseni. Hivi ni kwa nini Serikali isiweke utaratibu, marawanapotoa leseni waende kwa wananchi husikakupitia Serikali husika ili wamtambulishe mwekezaji waeneo husika kutoa masharti mapema kuliko ilivyo sasa,kwani mwekezaji anapoomba leseni, Serikali bila kujalikama eneo lile lina wachimbaji wadogo wadogo amahakuna, wao wanatoa tu leseni. Kweli wachimbajiwadogo wanaweza wakawa hawajavamia eneohusika, lakini ni vyema kutoa taarifa mapema na kamawameshavamia pia wapewe utaratibu mapema.Mheshimiwa Spika, naomba sana Serikali ikapimemadini yanayochimbwa katika Tarafa ya Ndago,Luzelukulu na Mbelekese, kisha iniletee majibu hapaBungeni. Pia nitapenda kujua ni mwekezaji ganiamepewa leseni na ni ya kuchimba ama ya utafiti nakijiji husika au kata wananufaikaje.Mheshimiwa Spika, napongeza sana Maonesho yaVito yaliyofanyika Arusha Mount, Meru Hotel. Yalifanasana na wanunuzi walikuwa wengi na watu wetuwaliuza na wengine walirudisha fedha bila kupata vito,hivyo inaonesha ni jinsi gani soko lilikuwa zuri.

Mheshimiwa Spika, nashauri Maonesho yoteyaboreshwe na iwe kila mwaka, lakini tuwaandaewatu wetu vizuri ili angalau kuwa na soko la uhakika natutoe elimu ya kutosha waache kupunjwa.Mheshimiwa Spika, naomba kama itakuwavyema, endapo madini yetu ya asili ambayo dunianikote hayapo ni hapa tu, yaani Tanzanite,tuyatengenezee utaratibu ama Sheria kwamba yaweni Nyara ya Taifa, yaani kama ilivyo pembe za ndovuna kadhalika kuwa na utaratibu ili kuwadhibiti watuwanaopora na kuyapunguza thamani madini yetu.Mheshimiwa Spika, namwamini Mheshimiwa Waziri,akae na Watendaji wake aone jambo hili, kama litafaachukua huo ushauri najua utapata ushindani, lakinibaadaye vizazi vijavyo vitakushukuru.Mheshimiwa Spika, mwisho, nashukuru kwamwaliko wa Wizara nilioupata kwenda kushirikiMaonesho ya Vito vya Thamani Arusha. Nilijifunzamengi na nimewasaidia sana wajasiriamali wangu(vijana) wa madini kupata contact na soko moja kwamoja. Ahsanteni sana.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya,naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.MHE. HAJI JUMA SEREWEJI: Mheshimiwa Spika,nakupongeza kwa kuniruhusu kuchangia kwamaandishi. Kwanza, namshukuru Mola wangu kwakunipa uzima na kuweza kuchangia hoja hii.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii asilimiamia kwa mia.Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri, kwaHotuba yake inayowapa matumaini Watanzania.Nawapongeza pia kwa kupunguza bei ya umeme kwawananchi ambao wanataka kuingiza umeme.Mheshimiwa Spika, hivi sasa kuna vyanzo vingi vyakuleta umeme hapa Tanzania kama vile makaa yamawe na gesi asilia. Kwa hiyo, naomba Serikali vile vijijivilivyo na vyanzo hizo basi lazima vionekane harakakwa kupatiwa umeme.Mheshimwa Spika, hivi sasa Mtwara kuna gesi yakutosha kwa umeme na tayari kazi imeshaanza chiniya Wachina; kwa hiyo, sehemu ile vijiji vyake vipateumeme.Mheshimiwa Spika, Ngaka kuna makaa ya maweambayo yameshaanza kuchimbwa na kupelekwa njeya nchi; kwa hiyo, nashauri Vijiji na Wilaya yakewafaidike na umeme wa mkaa wa mawe ili wafaidikena umeme kwa mali inayotoka sehemu yao.Mheshimiwa Spika, nazidi kuunga mkono hoja napia nazidi kukushukuru wewe.Mheshimiwa Spika, ahsante.MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: MheshimiwaSpika, mimi nachukua fursa hii kuchangia Hotuba yaWaziri wa Nishati na Madini.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kero za wananchiwaliozungukwa na migodi; wananchi waliozungukwana migodi wamekuwa wakiishi katika mazingiramagumu licha ya kuwa na rasilimali nyingizilizowazunguka. Pamoja na hayo, kumekuwa naahadi hewa nyingi wanazopewa na wawekezaji kamavile kuwajengea shule, kuwachimbia visima, kujengazahanati na kadhalika, lakini yote hayo yamekuwahayafanyiki, zaidi ya kuwachia mashimo na mahandakiyenye kuhatarisha maisha yao na ardhi hiyo haifai tenakwa kilimo. Yote hayo kumekuwa na kesi nyingi zaunyanyasaji wa wananchi hao pindi wanaposogeamaeneo ya migodi ikiwemo kupigwa, kujeruhiwa,kuuwawa, kupigwa risasi za moto na kesi hizozimekuwa hazijulikani hatima yake.Je, kwa nini Serikali hawafuatilii ahadi zawawekezaji kwa wananchi ili ziende sambasamba nautekelezaji wao?Je, mpaka sasa ni kesi ngapi zimeshatolewahukumu kuhusu unyanyasaji wa wananchi katikamigodi?Mheshimiwa Spika, ni hatua gani zilizochukuliwakwa wawekezaji waliotoa ahadi kwa wananchizisizotekelezeka?Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara hii haionisasa hivi ni wakati mwafaka wa kuweka mikataba yaowazi ili kila mwananchi ajue, kwa sababu ni rasilimaliya Taifa na mikataba hiyo iandikwe kwa Lugha ya

Taifa ili mwananchi aelewe ili kuondoa migogoro bainaya wananchi na Serikali?Mheshimiwa Spika Serikali ina mpango gani wakuwafidia wananchi ambao ardhi yao imeharibikwana wawekezaji ambayo haifai kwa kilimo wala kwashughuli zozote za maendeleo?Mheshimiwa Spika, Serikali hii imekuwa ikiwapuuza,kuwadharau na kuwanyanyasa wachimbaji wadogowadogo na kuwakumbatia wewekezaji wakubwakutoka nje, ambao wamekuwa wakikwepa kulipa kodihata Serikalini. Nchi nyingine huwawezeshawachimbaji wadogo wadogo, aidha kwa kundi kubwaau vikundi vidogo vidogo kuwa wawekezaji wazawakwenye maeneo yao. Wachimbaji hawa wadogowadogo hawana elimu na wala Serikali haijatengabajeti ya kutosha ya kuwasaidia wachimbaji.Kutokana na Serikali kutotaka kutoa elimu kwawachimbaji wadogo wadogo kwa makusudi,inasababisha wachimbaji wadogo wadogo kuharibumazingira.Je, lini Serikali itaona kuna umuhimu wa kutoaelimu ya kutosha kwa wachimbaji wadogo wadogo iliwaweze kujiajiri wenyewe na kupunguza tatizo la ajirakwa Serikali?Je, lini Serikali itaona kuna umuhimu wakuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo kuwawawekezaji wazawa na kuwatafutia masoko yauhakika?

Mheshimiwa Spika, tatizo la uchakachuaji wamafuta, limekuwa likiongezeka siku hadi siku.Inaonekana uvumbuzi wake ni mgumu kupatikana,pengine kuna mahusiano mazuri baina ya wachimbajina watu husika. Muda mrefu kumekuwa hakuna hatuazozote zinazochukuliwa dhidi ya wachakachuaji hao,lakini ikiwa itatumika sheria ya kuweka mipira yenyekuonesha nishati hiyo katika vituo vya mafuta tofauti nasasa hivi mipira hiyo ni meusi, hata mtu kufanyaubadhirifu ni rahisi kwa wenye vituo. Kumekuwa navituo vya mafuta vinavyojengwa holela kwenyemakazi ya watu na kuwasababishia usumbufuwananchi hao na kuhatarisha maisha yao.(a) Je, Serikali na Wizara ina utaratibu gani wakukagua visima vyote vya mafuta na kuhakiki vilivyobora ili kuepusha uchakachuaji wa mafuta?(b) Je, mpaka hivi sasa ni vituo vingapivilivyopata adhabu kutokana na kuchakachua mafutaau pampu?(c) Je ni mara ngapi kwa mwaka vituo vya kuuziamafuta vinakaguliwa?Mheshimiwa Spika, kumekuwa na usumbufumkubwa wanaoupata wananchi katika maombi yakufungiwa mita mpya au kubadilisha mita. Tatizolingine ambalo linawakera wananchi ni kununuaumeme katika njia ya mtandao wa simu za mkononi nakutoupata umeme huo kwa muda unaotakiwa aukukosa kabisa na kupoteza pesa zao.

(a) Je, Wizara ina mikakati gani ya kuhakikishakuwa usumbufu wanaoupata wateja wa kufungiwamita umekwisha?(b) Wizara na Serikali wana mikakati ganikukomesha wizi huo kwa wananchi wanaonunuaumeme bila kupata umeme na bila ya kurudishiwapesa zao?MHE. SALEH A. PAMBA: Mheshimiwa Spika, naungamkono hoja. Nampongeza sana Waziri, MheshimiwaMuhongo, Naibu Mawaziri; Mheshimiwa Masele naMheshimiwa Simbachawene, kwa uteuzi wao. Tunamatumaini makubwa kwao.Mheshimwa Spika, nawapongeza tena kwaHotuba nzuri sana, yenye kuleta matumaini mapyakwa Sekta hii ya Nishati na Madini. Ninayo maoniyafuatayo:-Mheshimiwa Spika, tunamshukuru MwenyeziMungu, kwa kutupatia gesi ya kutosha. Gesi iliyopohapa nchini inatosha kwa zaidi ya miaka 100.Kinachotakiwa ni kuwa na Sheria nzuri na usimamizi waSekta ya Nishati. Gesi isaidie pia maendeleo yamaeneo ambayo gesi inatoka. Makampuni ya gesiyasaidie maendeleo ya maeneo hayo, hatutakiscenario ya Delta kama ya Nigeria hapa.Mheshimiwa Spika, gesi hii isiishie Dar es Salaampekee, ifike katika Mikoa mingine kama Tanga,Morogoro ili kukuza uchumi.

Mheshimiwa Spika, ninataka kujua hatua iliyofikiwakatika kupeleka umeme katika Kata ya Mkaramo. Kwakuwa kila kitu kimekamilika; michoro, upembuzi yakinifuna gharama ni shilingi 742,000,000; je, kazi hiyo itaanzalini?Mheshimiwa Spika, namwomba Profesa na Timuyake waendelee na uzi huo huo, tupo pamoja nao.MHE. MOZA A. SAIDY: Mheshimiwa Spika, kwakuwa ardhi ni suala mtambuka, tunafahamu kwamba,kwenye ardhi kuna kila kitu chini ya ardhi na juu yaardhi. Mungu katupenda, nasi tumshukuru kutupaTanzania.Mheshimiwa Spika, nianze na suala zima la ardhina vilivyopo juu kwamba, ardhi ni rasilimali watu,wanyama, mimea, mito, maziwa madogo na baharikuu zote zapendeza na misitu. Ardhi ni rasilimali kwetu,yahitaji kutunzwa kwa hali na mali. Ndani yake mnaardhi, chini kuna mali pia. hebu tuone harakati zaugunduzi wa madini mara zote wachimbaji wadogoambao ni wazawa wa eneo husika kinachosikitisha nibaada ya kugunduliwa wale wachimbaji wadogowanaondolewa na Serikali na kupewa wawekezaji; hivini nani katuroga? Mifano ni mingi, mikataba mibovuiangaliwe upya.Mheshimiwa Spika, Madini ya Tanzanite kuleArusha yaligunduliwa na wazawa, lakini kwa sasamachimbo yote yako chini ya Makaburu, hata madiniya Tanzanite kwa sasa katika Soko la Kimataifa

yanauzwa kwa Nembo ya Makaburu. Kwa sasamadini yanapatikana maeneo mengi, ikiwemo Rubby.Dhahabu imegundulika Kondoa, Dodoma na ainanyingi zaanza kuonekana huko. Nafikiri baada yamuda mfupi, wananchi hawa wataondolewa katikamaeneo haya na kuletwa wawekezaji, harufu ipo.Mheshimiwa Spika, niongelee mapato yatokanayona madini. Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamati ya Bungeya Nishati na Madini ya 2012/13, bei ya dhahabu namadini mengine imepaa kwa kiasi kikubwa katika Sokola Kimataifa. Siamini sisi kama Taifa tumewezakwendana na kasi ya mabadiliko ya bei hii. Tumezidikuruhusu makampuni yafaidi rasilimali zetu bilampangilio, tunachofaidi zaidi ya mrabaha ni mapatoyatokanayo na kodi ya makampuni (Corporate Tax).Serikali ieleze faida tunayoipata kutokana na madinihasa baada ya kupanda kwa bei.Mheshimiwa Spika, kwa nini wachimbaji hawanahati miliki au hawawezeshwi kupata hati miliki yamaeneo ya uchimbaji? Kasumba hii ya kuendeleakuwasujudu wawekezaji hasa wa nje, kuwawezeshakupata hati miliki huku tukiwaacha watu wetu itaishalini? Tuna vijana wetu wengi wasomi na ndiyowanaovumbua madini hayo.Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inaingiahasara kubwa sana ya kulipia gharama za kusimamiakesi ambazo tulipoteza au tulishindwa.Mheshimiwa Spika, umeme ni kero kubwa kwenyemaeneo yetu. Kama tatizo ni maji mbona Tanzania ina

maeneo mengi ya kuwekeza maji tukapata umeme.Kama tatizo ni maji umeme asilia si upo kwa niniwananchi wasipatiwe mafunzo ya jumla wakapataumeme?Mheshimiwa Spika, watu wetu wengi ni maskinihawawezi kulipia gharama za umeme kwani utakutamtu ana nyumba ya vyumba vinne na kadhalika,analipia bili kubwa kuliko mwenye mashine ya kurandambao au mashine ya kusaga nafaka. Unajiulizamwanzo alikuwa analipia bili ndogo ghafla inapandamara mbili ya hapo; hivi kwa mtindo huo tutapatawateja wengi?Mheshimiwa Spika, mita za umeme zinazolipiwaTANESCO kwa bei kubwa mno hufanya mtu wakawaida kujenga nyumba na kushindwa kuweka mita;alipie nguzo, achangie; hivi kwa kipato gani hicho?Sasa umefika wakati Serikali iangalie masuala haya nakutoa elimu kwa umma ni kiwango gani watuwachangie?Mheshimiwa Spika, mafuta ya umemeyanahujumiwa na wafanyakazi wenyewe wa TANESCOna kuwauzia wafanyabiashara na kusadikiwa wapowanayoyatumia kwa kukaangia chipsi, samaki namatumizi mengine. Je, mafuta haya hayana madharakwa binadamu?Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. JOYCE J. MUKYA: Mheshimiwa Spika,naomba nichangie kwa maandishi kuhusu Bajeti yaWizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka 2012/2013.Mheshimiwa Spika, naanza na mgao wa umeme;hili limekuwa tatizo kubwa sasa na kwa muda mrefuhakuna taarifa yoyote inayotolewa hasa katika Jiji laArusha. Wiki mbili zilizopita kulikuwa na kukatika sanakwa umeme ila kinachosikitisha zaidi ni kujulikana kwataarifa hizi za baadhi ya watu Serikalini, kukata umemekwa makusudi kabisa, kwa kipindi cha muda fulani ili tukununua mafuta kwa ajili ya ku-run equipments. Hapohapo kuna deal ya ufisadi, hivyo kunufaika namanunuzi hayo kupitia makampuni ya mafutayaliyoshindikana au kupewa tender hiyo kwa ajili yamaslahi ya baadhi ya watu binafsi, ambao sitakikuwataja hapa kwani Kanuni zetu za Bunge haziruhusukutaja majina ya watu moja kwa moja.Mheshimiwa Spika, athari za kukatika umeme aumgao linavyoweza kuiathiri jamii na nitatoa mifano aukuzungumzia zaidi hospitalini.Mheshimiwa Spika, pengine nikiongea kwa mifanohalisi tunayokutana nayo katika maisha, nadhariainaweza kusaidia kuona uhalisia na kusababisha watuwaseme basi imetosha na hasa hao ambaowamekuwa wakileta mgao feki. Katika hili tukifikiriaumeme kwa njia mbadala zaidi ya mwanga, tutapatasababu nyingine ya kuendelea kuhamasishamapambano kwa maisha bora. Mfano, hospitalini nakatika mazingira ya theatre kuna emergency auoperation iliyokuwa inaendelea kisha unaambiwa

mgao umeanza na umeme utarudi baada ya 12 nawagonjwa wote uliokaa nao hali mbaya kila mmojaanalia maumivu makali na imagine nchi ambayowafadhili wamenunua Pls za kutosha kisha kwa sababuuhifadhi ni mbovu jamani.Mheshimiwa Spika, angalia suala zima la uhifadhiwa damu, inaelekea kuna maeneo ambayo kunajenereta kama sehemu za mjini lakini mahali kamaKibakwe, Longido, Katesh na kadhalika na Wilaya zapembezoni hili litawezekana vipi?Mheshimiwa Spika, tatizo la kuhifadhi maitilinawapa wakati mgumu sana wahudumu wamortuary zetu.Mheshimiwa Spika, wagonjwa waliopo nchi nzima,mtu anajua kafika hospitali, anategemea kuponabaada ya kuwekewa mashine ya oxygen kwa ajili yakumwongezea hewa, but ghafla umeme unakatika naanaambiwa hautarudi baada ya 12 hrs.Mheshimiwa Spika, tatizo hili linasababisha vifoambayo hata Mwenyezi Mungu hakuviita bado. Kwahali hii maisha bora yatatokea wapi jamani?Tutapunguza lini vifo visivyo vya lazima kwa wananchiwetu, halafu unasikia ni mkakati wa baadhi ya watu iliwafaidike na fedha.MHE. HAMAD ALI HAMAD: Mheshimiwa Spika,naomba nianze mchango wangu na suala la madini.

Mheshimiwa Spika, sasa ni miaka mingi sana nchiyetu inafanya kazi hii ya uchimbaji wa madini, lakinikinachosikitisha na kushangaza ni kuwa, kwa mudawote huo Serikali na Wananchi kwa ujumla tumekuwahatufaidiki na rasilimali hii ambayo Mungu ametujalianayo.Mheshimiwa Spika, siyo siri na ni ukweli kwamba,hata wale wananchi ambao wanaishi katika maeneoyanayotoa madini, hawafaidiki na maisha yaoyanaendelea kuwa duni.Mheshimiwa Spika, Tanzania tumegeuka kivuli chamvumo, kivuli kinafaidisha walio mbali. Tumekuwatukishuhudia wageni ambao tunawaita wawekezaji,wanafaidika kwa kuchukua madini yetu na kwendakufaidisha nchi zao na familia zao huku wakiiachaTanzania na watu wake tukiwa duni. Kama hiyohaitoshi, baadhi ya wawekezaji wanatoa rushwa kwabaadhi ya wenye mamlaka na wanawafunguliaakaunti nje ya nchi na kuwawekea mamilioni ya dola iliwapate nafasi ya kuendelea kuihujumu nchi.Mheshimiwa Spika, kama tulipoteza kwenyemadini sasa itoshe. Naomba niseme kwamba, gesi hiitulionayo kama hatutakuwa makini, hili ni bomuambalo tunatembea nalo na tusipokuwa makinitukalichezea litaturipukia.Mheshimiwa Spika, Nigeria walipopata mafutakwa kuwa hawakuwa wamejiandaa, waliingia katikavita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na Serikalikukosa kuzingatia kwamba, mafuta yalikuwa ni mali ya

watu wote na hivyo wachache tu ndiyo waliokuwawanafaidika.Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hii kuombakwamba, kwa kuwa Watanzania wote kuanzia Rais,Mawaziri, Wabunge na hata Wananchi; Wakulima naWafugaji walioko Mijini na Vijijini, wote wamewekamatumaini yao katika gesi hii iliyopo nchini. NaiombaSerikali iwazingatie zaidi wale wananchi ambao wapokatika maeneo ambayo gesi imepatikana na tuachekutoa nafasi ya wachache kujinufaisha wao na familiazao ili kuiondoa nchi yetu na matatizo yanayowezakutokea kama yalivyowapata wenzetu wa Nigeria.Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Zanzibar nakoimeonekana kuwepo kwa mafuta na gesi, naombaWaziri utakapofanya majumuisho uwaelezeWazanzibari msimamo wa Serikali ya Muungano iliwaanze kazi ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta nagesi kwa maslahi yao na Watanzania kwa ujumla.Mheshimiwa Spika, naomba kauli ya Serikali juu yajambo hili ili kazi hii iweze kuanza kwa upande waZanzibar.Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.MHE. JUMA SURURU JUMA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja kwa asilimia mia kwa mia.Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo ya Waziriwa Nishati na Madini, imebainika kuwa kuna upotevuwa fedha unaofanywa na Watendaji wa TANESCO,kwani iliarifiwa kwamba, TANESCO inakusanya jumla ya

shilingi bilioni 60 mpaka 70 kwa mwezi na jumla yashilingi bilioni 10 mpaka 15 ikiwa ni matumizi ya mwezi.Je, fedha nyingine zilizobakia zinakwenda wapi?Kutokana na sababu hizo, tunaomba Wizara itoeufafanuzi halisi wa fedha zinazobakia baada yamatumizi hayo. Pia ninaishauri Wizara ikaze buti katikasuala la mapato na matumizi ya TANESCOMheshimiwa Spika, naiomba Wizara ihakikishekwamba katika nchi yetu hii hakutakuwa na mgao waumeme na siku ikitokea kukatokea mgao wa umemebasi Uongozi wa Wizara uwajibike bila yakushurutishwa.MHE. SAID MUSSA ZUBEIR: Mheshimiwa Spika,kwanza kabisa, naunga mkono hoja asilimia mia kwamia. Pili, nampongeza Waziri na Naibu Mawaziri, kwamwanzo mwema, ujasiri na utendaji kazi wa hali ya juuna ushupavu walionao. Mnatakiwa mjichunge nakujilinda na watu ambao walikuwa na maslahi binafsina sasa inaonekana kufikia tamati.Mheshimiwa Spika, nawashauri mpitie upyaMikataba ya Madini na ile itakayoonekana ina harufuya ufisadi na haina maslahi na nchi ni bora ifutwe maramoja au ipitiwe upya.Mheshimiwa Spika, nahitimisha kwa kutaka kauli yaMheshimiwa Waziri, kwa kuwa gesi ni kati ya masualaya Muungano je, ni lini Sera ya kutandika bomba hilokuelekea Zanzibar itaanza?

MHE. ABDALLA HAJI ALI: Mheshimiwa Spika,Mwenyezi Mungu ni mkubwa, muweza wa mamboyote na ni mwenye Rehema kwa waja wake.Mheshimiwa Spika, aidha, nakupongeza wewebinafsi kwa Uongozi wako mahiri na imara katika Bungehili.Mheshimiwa Spika, katika mchango wanguningependa kutoa nasaha zangu kwa Waziri wa Nishatina Madini, Manaibu wake na Watendaji wote.Mheshimiwa Spika, takriban Wabunge wote nawananchi mbalimbali wamekuwa wakimpongeza Raiskwa kusadifu vyema katika uteuzi wa Waziri wa Nishatina Madini. Hivyo, namwomba Waziri aitunze heshimahii ambayo Rais kampatia Waziri.Mheshimiwa Spika, Waziri na Makamu wake wawiliwamejitwika jukumu zito na sote tunakiri kwamba, kaziyao ni nzito na ngumu sana, lakini kwa umahiri nauadilifu wa Waziri, Wananchi wamejenga matumainina wana imani nao na dalili njema zimeanzakujitokeza mapema. Wananchi wanafurahia kauli zaWaziri hata pale aliposema kwamba, hakuna sababuya mgao wa umeme uwezo tunao.Mheshimiwa Spika, pia wananchi wanafurahiasana kwa kupunguziwa gharama za kuunganishaumeme vijiji na mijini; tunaipongeza Wizara naWatendaji wote juu ya hili.Mheshimiwa Spika, Hotuba ya Waziri imekuwa nzurina bora sana, kwani ni Hotuba pekee ambayo

imeliunganisha Bunge lako na Wabunge wote, bilakujali itikadi za vyama vyao, wamekuwa wamoja katikakumwunga mkono Waziri na Wasaidizi wake juu yajambo hili. Hii imedhihirisha ile dhana ya kulitakaBunge liwe la kisasa na liwe Bunge moja ili kukidhi hajana matakwa ya wale ambao wametuchagua ilikuwawakilisha hapa Bungeni.Mheshimiwa Spika, Waswahili wanasema: “Mtimwema hupozwa na matunda yake.” Maana nikwamba, mti ukizaa matunda mema hupopolewakana kwamba kuzaa umefanya makosa. Hivyo, Wazirina Manaibu wake ni watu makini na ni watu safi. Je,Watendaji wa chini wakoje?Mheshimiwa Spika, ili kuitunza heshima hii ya Raiskwa kuwateuwa nyinyi na kumfanya Rais uteuzi wakeuwe wa mafanikio na ninyi pia mwendelee kung‘arakama mlivyoanza, basi ni wakati sasa wa kuisafishaWizara yenu na kuwaondoa wale wote ambaohawawajibiki kwa maslahi ya umma baliwanajinufaisha wenyewe na kuididimiza nchi.Mheshimiwa Spika, namwomba Waziri na Manaibuwake, wasimamie haki na Mungu atawapa nguvu juuya jambo hili, msitishwe, msirubuniwe, msihongeke,msiyumbishwe na wala msiogope. Nawaomba huoufisadi unaotajwa mpambane nao na mhakikishe hatamkifika kusulubiwa basi na waliosababisha muwemmekwisha wasulubu.Mheshimiwa Spika, kama Rais alivyowaamini na sisitujenge imani kubwa juu yao na nawasihi sana

watende kazi zenu kwa umakini mkubwa ili wasijekumwangusha Mheshimiwa Rais.Mheshimiwa Spika, namwomba Mungu awapenguvu na uvumilivu Mheshimiwa Waziri na Timu yakekatika kazi zao.MHE. NASSIB SULEIMAN OMAR: Mheshimiwa Spika,kwanza, nampa pongezi nyingi Waziri, Naibu Mwazirina Katibu Mkuu wa Wizara hii, kwa kazi nzuriwanayofanya. Pia nawapongeza sana kwa kugunduanjama za kuliweka Taifa hili katika giza kwa azma yakupata utajiri wa haraka.Mheshimiwa Spika, tumamshukuru Mungu kwakutujalia kugundua gesi nyingi katika nchi yetu.Tunaloliomba Wazanzibari ni kuwa mipangoitayarishwe ili gesi hiyo baadaye ifike Zanzibar, kamaulivyofika umeme. Hatua hii itasaidia sana kupunguzamatumizi ya makaa na kuni na hivyo kuhifadhimazingira ya nchi yetu.Mheshimiwa Spika, baada ya bei ya mafuta yataa kupandishwa, uchakachuaji wa mafutaumepungua kwa kiwango kikubwa. Serikali piaimeweza kuokoa zaidi ya shilingi bilioni 40.00 kwamwezi. Tatizo kubwa lililobaki ni mafutayanayokwenda nje ya nchi, wafanyabiasharawasiokuwa waaminifu hutumia nafasi hii kwakuyabakisha mafuta hayo hapa nchini, yaani mafutahayavuki mipaka yetu kwenda nchi za jiraniyalikokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, naiomba EWURA na TRAwajipange na kujitayarisha ili kulidhibiti suala hili, kwanifedha nyingi sana zinapotea kwa njia ya kushushashehena za mafuta nchini. Njia za kufanya ni kuwekapetroli kuhakikisha magari ya mafuta yanashushashehena zao nje ya nchi.MHE. ZARINA S. MADIBA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja. Napenda kuwapongezaMheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri na Watendaji wotewakiongozwa na Katibu Mkuu. Nina imani kubwa sanana Timu hiyo ya Wizara na ninaamini itawezakuikomboa nchi yetu kiuchumi kwani umeme ni nyenzokubwa sana katika uchumi wa nchi yetu.Mheshimiwa Spika, Wizara hii ni ngumu sana kwaniimegubikwa na ufisadi wa muda mrefu sana hadiwamefanya ni haki yao kula rushwa. Ninawaombamsiwe na wasiwasi kabisa, tupeni taarifa ya ukweli hataikibidi kvunja kanuni kwa maslahi ya wananchi.Mheshimiwa Spika, Serikali sasa inafaa kuangaliahizi Sheria au Kanuni kama hii ya Manunuzi. Kanuni naSheria hii imekuwa ikitumiwa vibaya kukandamizaufanisi wa sehemu mbalimbali na kulinda ufisadi. Sisikwenye viwanda vya nchini tumekuwa tukilalamikiaSheria hii. Tunaomba Mheshimiwa Waziri wa Fedhasasa aone umuhimu wa kuiangalia Kanuni au Sheria hiiya manunuzi ili zile Kanuni zinazolinda ufisadizirekebishwe na zile zinazoshindilia viwanda vyetu piazibadilishwe.

Mheshimiwa Spika, mafuta ya taa ni njia moja kuuya chanzo cha nishati vijijini. Mafuta ya taa yamekuwayakitumika pia kwenye vitotozi (incubator) vijijini,ambazo zinawasaidia akina mama kufuga kisasa.Kutokana na bei ya mafuta ya taa kupanda, akinamama hawa wamelazimika kuviachia vitotozi hivyo nakupata hasara. Wanawake hao waliweza kutotoavifaranga 100 kila mwezi na kupata vifaranga zaidi ya1,000 kwa mwezi, ukilinganisha na vifaranga 352 kwamwaka. Ninaomba bei ya mafuta ya taa iangaliweupya.Mheshimiwa Spika, kuna hoja ya kusaidiawachimbaji wadogo wadogo. Naomba nieleweinterest ya ndugu zangu kuwa washiriki. Ninaona jinsiwanavyohangaika kwa kutumia nyenzo duni. Vijanahao wakisaidiwa wanaweza kuchangia Pato la Taifa.Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziriameyasema mengi mazuri kwenye Hotuba yake, nikitanzi watu wana expectation kubwa sana na ninyi.Niwaombee kheri, amani na msiogope tupo pamojananyi.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Spika,nachangia hoja katika eneo la kodi za migodi yamadini kwa Halmashauri za Wilaya ambazo zinamigodi. Sheria ya Fedha ya Halmashauri za Wilaya yaMwaka 1982 inataja vyanzo vya fedha kwaHalmashauri na moja ya vyanzo hivyo ni asilimia 0.3 yamapato ya migodi. Wakati huo huo Mgodi una

mkataba na Serikali ambao una kipengele ambachokinazuia mgodi kulipa asilimia 0.3 ya mapato yake nabadala yake unataka ulipe dola laki mbili tu kwamwaka. Dola laki mbili kwa mwaka ni pesa kidogosana, ukilinganisha na mapato ambayo migodiinapata na asilimia 0.3 ya mapato ni kiwangoambacho Migodi inaweza kulipa bila kuathiri mapatoau faida.Mheshimiwa Spika, rai yangu ni kwamba, Sheria yaFedha ya Serikali za Mitaa ya Mwaka 1982 ilitungwa naBunge na hivyo inapaswa iwe kubwa na itawale ile yaMkataba wa Mgodi na Serikali. Kipengele chaMkataba wa Mgodi na Serikali kinachozuia migodikulipa asilimia 0.3 ya mapato yake yote ya mwaka nabadala yake kulipa dola laki mbili tu kwa mwakakiondolewe kabisa na migodi yote ianze kulipa asilimia0.3 ya mapato yake kwa mwaka kama ushuru wahuduma.MHE. FATUMA A. MIKIDADI: Mheshimiwa Spika,nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa kusoma vizuriHotuba na kwa kuchapa kazi vizuri. Ninaunga mkonohoja kwa asilimia mia kwa mia.Mheshimiwa Spika, hoja yangu ya kwanza niumeme. Tunataka umeme Lindi, Newala, Kilwa, Liwalena Ruangwa kwani gesi ipo, tatizo ni nini?Mheshimiwa Spika, TPDC wapewe pesa za kutoshaili waweze kusambaza umeme vijijini.

Mheshimiwa Spika, tunaomba wachimbajiwadogo wasaidiwe katika Mkoa wa Lindi nako kunaMadini ya kutosha. Wilaya zote katika Mkoa wa Lindikuna madini kama ifuatavyo: Wilaya ya Ruangwakuna Green Garnet, Green Tomaline, Safaya, Dhahabuna Unga wa Rangirangi; Wilaya ya Nachingwea kunaDhahabu na Safaya; Wilaya ya Lindi kuna Gypsum naChumvi; Wilaya ya Kilwa kuna Gypsum, Gas naChumvi; na Wilaya ya Liwale kuna Dhahabu, Safayana Madini ya Vito.Mheshimiwa Spika, tunaomba wasaidiwe mikopoili waweze kuchimba madini watu wapate ajira.MHE. OMARI R. NUNDU: Mheshimiwa Spika, naanzakwa kuipongeza Wizara kwa Hotuba nzuri na pia kwamatayarisho mazuri ya Hotuba na kazi za Wizara.Kwanza, nampongeza kwa kutuhakikishia kuwa mgaowa umeme hautakuwepo tena; hii ni faraja kubwa. Pianinaipongeza Wizara kwa kupunguza tozo lakuunganisha umeme, kitu ambacho kitachocheauchumi wetu.Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono kuongezabajeti ya usambazi wa umeme vijijini. Hapa ninaombaWizara ivipatie umeme mapema vijiji vyote ambavyomiundombinu ya umeme tayari ipo, vijiji ambavyovimepitiwa na nyaya za umeme. Katika Vijiji vyaKibafuta, Chongohani, Mkembe, Machui, Kisimatui,Pande A na Pande B.Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Tanga umebainikakuwa na Madini ya Vito vya Thamani vya aina nyingi

ali Vito hivyo vinauzwa nje na nyakati nyingine kupitianchi jirani kwa sababu Tanga hakuna Kituo chaKuboresha Vito hivyo. Ninaiomba Serikali ilifanyie kazisuala la kuanzisha Kituo hicho.Mheshimiwa Spika, imedhihirika kuwa Mmea waMkonge una matumizi mengi pamoja na uzalishaji waumeme; ni wazi kuwa jitihada za dhati zikifanywa basivijiji vingi vilivyoko kwenye Mashamba ya Mkonge naMiwa vitafaidika hivyo.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. ABDULKARIM E. H. SHAH: Mheshimiwa Spika,kwanza, naomba nimpongeze Waziri wa Nishati naMadini, Mheshimiwa Profesa Muhongo (Mb), ManaibuWaziri wake; Mheshimiwa Simbachawene (Mb) naMheshimiwa Maselle (Mb). Pia pongezi zangu zimfikieNdugu Maswi, Katibu Mkuu, kwa ujasiri wake na Timuyake yote. Nawapongeza Watumishi wote wa Wizarana Idara zake walio waaminifu.Mheshimiwa Spika, naomba sasa niulizie ulempango wa kupeleka mashine za kuzalisha umemekatika Wilaya ya Mafia umefikia wapi na pia mchakatomzima wa usambazaji umeme vjijini nao upo katikamchakato gani au umefikia wapi?Mheshimiwa Spika, naomba sana Wizara inisaidiekutoa taarifa kuhusu michakato hiyo miwili niliyoisema.

MHE. SAMIA SULUHU HASSAN: Mheshimiwa Spika,kwanza, naunga mkono hoja.Mheshimiwa Spika, Wizara imeonesha mwelekeomzuri katika Sekta ya Nishati. Naomba jitihada zakuondoa ufisadi kwenye Sekta hii ziendelee hatua kwahatua. Nashauri nguvu pia ielekezwe upande wamadini kwani nako pia kuna ufisadi wa kutisha.Mheshimiwa Spika, Viongozi wa Wizara wajiepushena vishawishi vya matamanio kwa WabungeWanawake wenye sifa dhaifu na baadayekuwashushia heshima na haiba yenu.MHE. ALLY KEISSY MOHAMED: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.Mheshimiwa Spika, naiomba Wizara ichunguzemafuta yote yanayopelekwa kwenye mitambo yote yaTANESCO nchi nzima na hasa iliyopo Dar es salaam.Yanapelekwa mafuta hewa kabisa, idadi ya mafutasiyo halali, ni wizi ilhali shahili. Pia zabuni za nyaya zaumeme kupewa mtu binafsi kwa upendeleo wakatikuna kiwanda ambacho Serikali ina hisa wala huwahawajulishwi kabisa hiyo ni rushwa ya wazi kabisa nadalili ya kuuwa viwanda vyetu.Mheshimiwa Spika, naomba umeme unaotokaKigoma Mpanda – Sumbawanga – Iringa upitie kwenyeVijiji vya Kasu, Lyazumbi, Paramawe, Mwai, Mtenga,Mashete na Londokazi. Vijiji hivyo vyote vipo njianikatika Barabara ya Mpanda – Sumbawanga. Pianaomba ahadi ya Naibu Waziri aliyekuwepo

Mheshimiwa Adam Malima katika ziara yake yaNamanyere Nkasi, alituahidi kutuongezea nguzo kwakilomita tano.Mheshimiwa Spika, naomba pia umeme kwendaBandari ya Kipili na Kirando utekelezwe haraka sana.Kwa sasa vinasaba haitakiwi kwa kuwa mafuta ya taana dizeli bei sawa ila hiyo shilingi sita kwa lita itolewamara moja.MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Spika,awali ya yote, napenda kumpongeza MheshimiwaWaziri na Naibu Mawaziri wote wawili, kwa kazi nzuriwaliyoanza nayo ambayo inaleta matumaini.Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali itekelezemipango hii yote mizuri tuliyosomewa katika Hotuba yaWaziri. Naishauri Serikali idhibiti uchimbaji wa Tanzaniteambayo ni madini yanayopatikana Mererani Mkoa waManyara. Madini haya hayawanufaishi Watanzaniawengi, yamekuwa yakisafirishwa zaidi Kenya. NaiombaSerikali idhibiti uuzwaji huu holela ili Watanzania wengiwaweze kufaidika.Mheshimiwa Spika, tatizo la umeme limekuwalikisumbua sana, hali inayopelekea hali ya maishakuwa ngumu, kusimama kwa uzalishaji viwandani,vijana kukosa ajira maana wengine wamejiajiri kwenyeshughuli mbalimbali zinazotumia umeme kwa mfanosaloon na nyinginezo.Mheshimiwa Spika, tumeona wenzetu Thailandwanakabiliana na tatizo la umeme kwa kutumia miwa,

takataka. Naishauri Serikali iangalie ni jinsi ganitutakabiliana na tatizo hili hasa pale kina cha majikinapopungua.MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Spika,naipongeza Serikali kwa kazi kubwa inayofanya katikakushughulikia tatizo la umeme. Pia isimamie vyemaujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Kilwa hadi Dar esSalaam.Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwakusimamia vyema Mradi wa Umeme katika Jimbolangu la Kisarawe. Nawashukuru sana Watendaji waWizara na TANESCO. Namshukuru Ndugu Mramba waTANESCO na Watendaji wenzake, kwa kuona umuhimuwa kusimamia Mradi wa Umeme Kisarawe hadiMsanga.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Spika,nawapongeza Mheshimiwa Waziri, Manaibu wotewawili, Katibu Mkuu na Timu nzima, kwa lengo nadhamira ya dhati ya kufanya re-formation Wizarani.Nawashukuru kwa kupunguza gharama zakuunganisha umeme hasa vijijini. Nikipata fursa yakuzungumza nitagusia, lakini pia ningependa kujuadestination na beneficiaries wa Sub-station ya KIA.Mheshimiwa Spika, la pili, ningeomba Miradi yoteya Umeme (On Going Projects), iliyokuwa Arumeruiendelee kama ilivyopangwa kwenye ramani, mingiimesimama kwa sasa. Finally, ninaunga mkono jitihada

zote chanya zenye lengo la kuipatia REA fedha zaidikwa ajili ya kutekeleza Miradi yote hususan ya Phase II ilina vijiji vyangu vya Arumeru vipate kufikiwa na umeme.Tungependa kufahamu Wizara inategemeakukamilisha lini Miradi ya REA Phase II?Mheshimiwa Spika, nawatakia kila la kheri katikamkakati wa kufanya re-formation Wizarani na siyotransformation.MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika,naipongeza Wizara kwa hatua za mwisho zakukamilisha Mradi wa Umeme wa Mwandoya. Kwakuwa Wizara inatekeleza Mradi wa Kupeleka UmemeMakao Makuu ya Wilaya ya Itilima; na kwa kuwakutoka Itilima kwenda Mwandoya (Makao MakuuJimbo la Kisesa) ni kilometa 40 tu: Je, Serikali wakatiinatekeleza Mradi wa Itilima itaunganisha naMwandoya ili pia kuunganisha na Makao Makuu yaMkoa wa Simiyu?Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri kwa agizola kutaka Kampuni zote zilizochimba madini kwa miakamitano na kuendelea, zianze kulipa kodi ya mapatobila kuleta visingizio. Nampongeza kwa ujasiri huo.Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri ameagizawafunge migodi na waondoke, lakini hajasema ni liniagizo hili litaanza kutekelezwa na hatuaatakazochukua kwa wale watakaokaidi. Naombaafafanue.

Mheshimiwa Spika, kuendeleza uchimbaji mdogowa madini katika aya ya 171, maeneo yaliyotengwakwa ajili ya uchimbaji mdogo yenye jumla ya hekta105,163 na kwamba Serikali itatoa bilioni 8.9kuendeleza wachimbaji wadogo. Kwa nini Serikalihaijatenga maeneo ya wachimbaji wadogo katikamgodi wa Mwadui katika Vijiji vya Maganzo nakadhalika?MHE. SALUM KHALFAN BARWANY: MheshimiwaSpika, idadi ya Watanzania wanaotumia nishati yaumeme ni kiasi kidogo sana, kwani taarifa inayoelezwahapa ni asilimia 17 tu ya Watanzania wote na zaidi yaasilimia 83 nchini hawapati umeme. Hii ni dhahirikabisa tupo nyuma kama Taifa katika matumizi yaumeme.Mheshimiwa Spika, pamoja na Mikoa ya Mtwarana Lindi kuiokoa nchi hii kwa kuwa na nishati yaumeme, bado hatuoni katika Gridi ya Taifa na Wazirihajasema lolote katika hili.Hatuna Wataalamu wa kutosha katika taaluma yaGesi nchini; ni vyema tukawa na Chuo cha Wataalamuwa Gesi ambao watadhibiti rasilimali. Sera ya Sheria yaGesi ni muhimu kuletwa kwa haraka, haikuwa vizurikuanza Mikataba kabla ya Sera na Sheria hiyo. NatakaSerikali ifanye haraka kuleta Sera hiyo katika Bunge laTisa, Novemba, 2012.Mheshimiwa Spika, gharama ya kuunganishaumeme kupunguzwa ni vyema katika Mikoa ya Kusini.Wizara ingeifikiria zaidi Mikoa hiyo kupatiwa ahueni ili

wajisikie wao hasa wameisaidia Nchi badala ya Tshs.177 kama ilivyokubalika katika Km. 4 katika maeneo yaMtwara, eneo liongezwe.Mheshimiwa Spika, Mataifa mengi Dunianiyameingia kwenye vurugu baada ya kupatikanamadini katika Mataifa haya. Tukiruhusu Mataifa ya Njekumiliki rasilimali hii, Mikataba inatufunga hata tukihitajikufanya marekebisho tunashindwa.Mheshimiwa Spika, ushauri wangu tumiliki hisa kwaasilimia kubwa na ikiwezekana asilimia zote zimilikiwena Serikali.Mheshimiwa Spika, suala la Gesi ya Mikoa ya Lindina Mtwara hatutarajii tu kupata umeme wa kuwashala hasha, hatutarajii tu kupewa ahadi ya kujengewashule, zahanati na barabara hapana. Tunahitajiindustrialised area, eneo la kiuchumi na uchumiendelevu. Automaticaly, hayo tunayoahidiwa yatakujayenyewe baada ya uchumi wetu kuimarika, uchumiunaojitegemea.Mheshimiwa Spika, tunajiuliza kwa nini Kituo chaGesi kijengwe Bagamoyo badala ya kujengwa Mtwaraau Lindi? Miji hii kwa nini isiwe Miji ya Gesi kwa maanaya Miji ya Viwanda?Mheshimiwa Spika, tuna sifa na vigezo vyote vyakuwa Miji ya viwanda; kwa nini Dar es Salaam? TunaNatural Habours ambazo zingeweza kusafirisha gesiyetu katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kugundulika kwa gesi Mikoa yaKusini, Lindi ikiwa ni mojawapo inatarajiwa kutoamwanga na matumaini ya miaka mingi ijayo. Nasemahivi kwa kuzingatia kwamba Mikoa hii imekuwa nyumana imetengwa kwa muda mrefu sana kimaendeleo.Gesi hii sasa iwe ni Mwanga Kusini, ilete baraka Kusini,ilete dira mpya Kusini na zaidi ya yote ibadili taswiranzima ya Mikoa hii ya Kusini. Ni vema Serikali ikawekamkakati wa kuanzisha Ukanda wa kiuchumi imarakatika Mikoa hii ili iweze kuleta manufaa ya kwelibadala ya kuishia kutoa maji, madawati na mengineyafananayo. Naungana na watu wengiwanaotahadharisha kuwa gesi hii ilete baraka na silaana, tujipange.Mheshimiwa Spika, tangu wiki hii ianze,kumekuwepo na ushabiki, shutuma na nyinginezinazofanana miongoni mwa Wabunge kuhusiana natuhuma ndani ya Wizara hii. Kitendo hiki kinaletaudhalilishaji mkubwa kwa Bunge mbele ya jamii.Naishauri Wizara iyafanyie kazi mawazo yoteyaliyotolewa hasa yale yanayohusu Wizara ili kuepukaaina yoyote ya ubadhirifu. Hiki ni kiashiria toshakwamba wapo watumishi ndani ya Wizarawaliokubuhu kwa rushwa kiasi kwamba wanapataujasiri wa kuligawa Bunge kwa kuwashawishi baadhi.Mheshimiwa Spika, wakati Bunge linajitahidikujisafisha, Wizara nayo ijipange kujiimarisha. Waziri,Manaibu Waziri wote na Katibu Mkuu watumie sifa,baraka na moyo waliopewa na Wabunge kulileteaTaifa manufaa. Waangalieni wasije wakalewa sifawakapoteza mwelekeo.

MHE. KURUTHUM J. MCHUCHULI: MheshimiwaSpika, awali ya yote, napenda kumpongezaMheshimiwa Waziri, Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu naTimu ya Watendaji wote, kwa kutuletea BungeniHotuba yenye kurudisha matumaini mapya kwaWatanzania.Mheshimiwa Spika, namwomba MheshimiwaWaziri atueleze ahadi yake ya kuwa mgao wa umemeTanzania basi! Je, amejipanga kiasi gani kwani Wizarayake imezungukwa na Ufisadi?Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati na Madiniiliwaahidi Wakazi wa Wilaya ya Rufiji wanaoishi katikamaeneo ya karibu na mpaka wa Nyamisati kuwaumeme wataupata kupitia REA. Je, ni lini Wananchihawa watapatiwa nishati hii muhimu ili nao wawezekujikwamua kiuchumi?Mheshimiwa Spika, Wananchi wangu wanaoishimaeneo ya Ikwiriri wanalalamika kuwa Meneja waTANESCO katika Tarafa ya Ikwiriri na Watendaji wakewana tabia ya kuwaongezea gharama za ankara yaumeme tofauti na matumizi wanayotumia.Mheshimiwa Spika, je, utaratibu huu ni sahihi?Namwomba Mheshimiwa Waziri atusaidie Wanarufijiwanyonge.Mheshimiwa Spika, nawasilisha.

MHE. RASHID ALI OMAR: Mheshimiwa Spika, awaliya yote, nachukua fursa hii kumshukuru kwa dhatiMwenyezi Mungu, kwa kunijaalia mimi na Wabungewenzangu kuwepo katika Bunge lako hili tukiwawazima wa afya na kutuwezesha kutekelezamajukumu yetu ambayo ni muhimu sana kwa Taifaletu.Mheshimiwa Spika, katika mchango wangu wamaandishi, naomba kwa heshima ya Bunge lako,nianze kwa kukushukuru wewe binafsi, kwa kuendeshavikao kwa umahiri na umakini, kwa hekima na busara;Mungu akusaidie zaidi.Mheshimiwa Spika, pili, shukrani zimwendee Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wetu wa Jamhuri yaMuungano, kwa uteuzi wake wa Uongozi wa Juu waWizara hii ya Nishati na Madini, kwa kumteua Waziri,Naibu Mawaziri na Katibu Mkuu mpya. Wotewanaonesha kila dalili za uchapaji kazi unaohitajika;kwa mfano, kwa muda mfupi waliweza kugundua nakuokoa shilingi bilioni sita ambazo zilikuwa zipoteekabisa.Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa zaMheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wauzinduzi wa bomba la mafuta toka Mtwara hadi Dar essalaam, inaonesha Tanzania inao utajiri wa gesi yenyethamani ya Shilingi trilioni 626.71 za Tanzania. Hiitunaweza kuikadiria kwamba ni kiasi cha bajeti yetuisiyopungua miaka 35 - 40 ijayo. Hofu na wasiwasiwangu ni namna gani tutakavyousimamia na kuutumiautajiri huu ili kuinua uchumi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ili tunufaike na utajiri huu nilazima utajiri huu usiwe wa laana. Nchi kama Nigeriawalipogundua mafuta kule kwao kwa vilehawakujiandaa vyema juu ya namna gani ya kufaidikana neema hii, walijikuta wakiingia katika migogoro yawenyewe kwa wenyewe, ikiambatana namaandamano ya watu wa makundi mbalimbali yakijamii, yaliyoleta uvunjifu wa amani na kusababishavifo vya watu.Mheshimiwa Spika, naomba niishauri Serikali naWizara hii tuwe na tahadhari juu ya mgao wa neemakwa wale wadau walio katika maeneoyatakayozalisha madini hayo.Mheshimiwa Spika, miongoni mwa madiniyanayotarajiwa kuvunwa kwa wingi ni Uranium. LazimaSerikali na Wizara iangalie madhara kiafya yabinadamu na madini haya.Mheshimiwa Spika, naomba niishukuru Serikali, nidhahiri kwamba Mheshimiwa Rais Kikwete ametuteuliaWaziri na Watendaji Wakuu wenzake wa Wizara mahiri.Sisi Wabunge wa Bunge lako tutashikamana naMheshimiwa Profesa Muhongo na wenzake(Watendaji) wa Wizara, kuchambua na kuchunguzauzembe, ubadhirifu na ufisadi katika Wizara hii muhimuinayosimamia maisha ya watu wa nchi hii.Mheshimiwa Spika, naomba niishauri Serikali kuwa,sisi Wabunge tuko pamoja nanyi, lakini atakaebainikakuhujumu uchumi wetu, achukuliwe hatua kali.

Mheshimiwa Spika, kama Serikali itakusudiatunaweza kuondoa hujuma na kulipeleka Taifa letupazuri. Ahsante.MHE. ALI KHAMIS SEIF: Mheshimiwa Spika, katikaHotuba ya Waziri, ukurasa wa 9 kifungu cha 15,imeelezwa kuwa kuna maendeleo katika Sekta yaMadini kuhusiana na migodi hulipa mrabaha waasilimia nne. Bahati mbaya mgodi uliotajwa kulipamrahaba huo wa asilimia nne ni Geita Gold Minepekee. Ninataka kuelewa kwa nini Mgodi wa NorthMara wa Barrick na Bulyankuru na migodi minginehaikuorodheshwa katika walipaji wa mrabaha huompya?Mheshimiwa Spika, STAMICO imeingiamakubaliano ya ubia na Tanzania AmericanInternational Development Corporation (2000) Limitedkatika suala la madini kwa asilimia 45 kwa 55. PiaSTAMICO wemeingia Mkataba wa Makubaliano yaUbia na Obtala Resources Limited kwa hisa ya asilimia50 kwa 50. Kitendo hicho ni kizuri na kitawafanyaWatanzania waweze kushiriki kwenye suala la madini.Mheshimiwa Spika, tatizo lililopo la Serikali yetu nijuu ya kuchangia asilimia zetu zinazotuhusu, wakatiwote huwa hatuchangii ipasavyo, matokeo yake yalemazuri yanayotegemewa huwa hayapatikani.Mheshimiwa Spika, Wizara hii ielewe kuwa nchiyetu inakabiliwa na tatizo kubwa la kugeuka jangwakulingana na ukataji mkubwa wa miti kwa ajili ya nishati

ya kupikia, aidha kwa kupikia kuni au mkaa, kwasababu wananchi wanahitaji kuni kwa kupikia chakulana kwa vile hakuna nishati mbadala ya kupikia nilazima wategemee misitu kwa kupikia.Mheshimiwa Spika, Wizara imeajiandaa vipi katikakupata nishati mbadala ili nchi yetu iepukane nakuingia kwenye jangwa?Mheshimiwa Spika, uzoefu uliopo katika nchi yetuni kuingia katika mikataba isiyo na tija kwa wananchi.Hilo limedhihirika katika Mikataba ya Migodi yaUchimbaji wa Dhahabu. Hivi imeshapatikana na Uraniipo tayari pengine mwaka 2013 itachimbwa. Kwa hofuya mikataba ya nyuma; je, Serikali ipo katika nafasigani katika Mkataba wa Uchimbaji wa Urani na gesi?Je maslahi ya nchi yamezingatiwa au maslahi yawawekezaji tu ndiyo yaliyozingatiwa?Mheshimiwa Spika, ahsante.MHE. HAROUB MOHAMED SHAMIS: MheshimiwaSpika, awali ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu,kwa Neema na Rehema zake nyingianazaonineemesha; ni wajibu kutamka Alhamdulillah.Mheshimiwa Spika, kabla sijatoa mchango wangu,nachukua fursa hii kumpongeza Raisi wetu mpendwa,Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa upeoalionao wa kuweza kumwona na kumteua ProfesaSospeter Muhongo, kuiongoza Wizara hii. Pianampongeza kwa dhati Profesa Muhongo, kwa uwezo,

idii, juhudi, maarifa na zaidi uzalendo wake kwa nchiyetu. Nawapongeza pia Naibu Mawaziri; MheshimiwaMasele na Mheshimiwa Simbachawene na KatibuMkuu, Bwana Eliakim C. Maswi. Napenda kuwaambiakazeni buti na Wabunge tupo pamoja nanyi.Mheshimiwa Spika, Wizara hii ina jukumu na dhimakubwa kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu nawananchi mmoja mmoja kwa ujumla. Nishati yaumeme ni nyenzo muhimu sana kwa maisha ya kila sikuna maendeleo yao na ya nchi. Serikali kupitia Wizarahii na hasa kwa timu hii mpya, iwe makini sana ili nchiipate umeme wa uhakika kuondoa aibu ya mgao.Nchi kama Tanzania, iliyojaaliwa vyanzo vingi vyaumeme kuliko nchi zote Barani Afrika isipokuwa Congotu (DRC), ni aibu sana kukosa umeme wa uhakika.Mheshimiwa Spika, tatizo lililothibitika la ukosefu waumeme nchini ni hujuma za kifisadi za makusudizilizokuwa zikifanywa na Wizara na Taasisi zake! Hotubaya Wizara hii imetoa matumaini, lakini Serikali kupitiaWizara hii isimamie Sera zilizopitishwa na ikataevishawishi vya kifisadi kwa maslahi ya nchi hii. Wizaraisimamie upunguaji wa gharama za umeme ambazo nikubwa sana kwa sasa, kiasi ambacho watu wa kipatocha chini ambao ni asilimia 75 ya Watanzaniawanashindwa kuzimudu.Mheshimiwa Spika, wakati umefika sasa Serikalikuileta Bungeni Mikataba yote ya Uzalishaji Umeme ilikubaini mikataba yote mibovu na ama tuirekebishe autuifute kabisa. Wakati wa kuwaachia wawekezaji

kuzalisha umeme ambao haununuliki kwa Mikataba yaKifisadi sasa umepita.Mheshimiwa Spika, ni wakati mwafaka pia kuiletaBungeni Mikataba ya Madini ili tuiangalie na tuisaidieSerikali kuishauri namna ya kuirekebisha. Mapato yanchi kutokana na madini hayaridhishi! Hatuazichukuliwe, bado hatujachelewa sana. Bunge niMhimili muhimu sana kati ya Mihimili mitatu ya Dola.Serikali sasa iwe karibu na Bunge ili kuliendeleza TaifaLetu. Wakati wa Serikali kufanya maamuzi yasiyo natija utaliangamiza Taifa hili, ambalo mimi binafsinajivunia.Mheshimiwa Spika, Serikali itoe maamuzi kwaMadini ya Vito kama Tanzanite, Saphire, Ruby nakadhalika yachongwe nchini. Hii itasaidia kuongezaajira kwa vijana wetu, lakini pia kongeza thamani yamadini yenyewe na hivyo kuongeza mapato. Ni aibukwa madini ya Tanzanite, yenye jina la nchi yetu,kuchongwa Nairobi Kenya na hivyo kutoa taswirakama madini hayo ni ya asili ya Kenya. NamwombaMheshimiwa Waziri alishughulikie jambo hili ipasavyo.Mheshimiwa Spika, ahsante sana.MHE. ESTER AMOS BULAYA: Mheshimiwa Spika,Serikali ihakikishe Kampuni ya Tanzanite One, kablahaijaingia Mkataba mpya kuzingatia yafuatayo:-- Ihakikishe inakamilisha ahadi zake zakupeleka maendeleo kwenye jamii inayozungukamgodi huo, kuna malalamiko hawajatimiza ahadi hizo.

- Tanzanite hawajalipa mrabaha wa dolamilioni mbili; nini hatima ya fedha hizo?- Kampuni ya GGM nayo imekwepa kulipa(Service Levy) tangu mwaka 1999 wakati Sheriainawataka kulipa asilimia 0.3 ya mapato katikaHalmashauri.- Mmejipanga vipi kuhakikisha mnawadhibitiMafisadi waliojipanga kuhujumu Miradi ya Gesi iliwaendelee kuuza mafuta mazito?- Watu wenye leseni ambao wamekumbatiamaeneo lakini hawayafanyii kazi wanyang’anywe.Tunajua wapo vigogo wenye maeneo lakinihawayaendelezi huku wachimbaji wadogowanahangaika.- Serikali mmejipanga vipi kuwasaidia vijana,wananufaika na madini yao kwa kuwawezesha kwamakundi kupata vifaa vya kuchimbia ili na wao wawewabia.- Mungu awabariki wote, mwendelee kuwawazalendo, tutawaunga mkono. Ulinzi wenu nimuhimu sana.MHE. DEO H. FILIKUNJOMBE: Mheshimiwa Spika,kwa niaba ya wananchi wa Ludewa, ninayo furaha naheshima kubwa kutokana na utendaji mzuri wa Wazirina Manaibu Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara yaNishati na Madini. Waziri wa Nishati na Madini na Katibu

Mkuu, fanyeni kazi, simameni imara. Sisi Wabungemakini tupo nyuma yenu, tutawapigania na tunaungamkono jitihada zenu.Mheshimiwa Spika, bajeti hii ya Nishati na Madini nibajeti yangu ya kwanza kuiunga mkono, ni bajetiinayotoa nuru mpya ya matumaini kwa Watanzania.Kwa mara ya kwanza, ninaunga mkono hoja.Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali ili kuhakikishatunakuwa na umeme wa kutosha unaotokana na maji,Mashamba ya Mbarali Farms na Kapunga Farms namashamba mengine makubwa yote yafungwe maramoja katika Bonde la Usangu ili Mtera Dam lijae nakutoa umeme mwingi. Ni ujinga kulima upstream,wakati hydroelectric scheme ipo down stream.Mheshimiwa Spika, wakulima wa mpungawapelekwe Bonde la Rufiji - Down Stream, the GreatRuaha and below Stigler’s Gorge isiyo Kilombero, if weplan to harness the gorge too for power.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. TEREZYA L. HUVISA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.Nawapongeza sana Waheshimiwa Mawaziri kwa kazinzuri wanayoifanya hasa nawapongeza kwa kuamuakupunguza bei za kuunganisha umeme kwa wananchihasa wa vijijini. Kitendo hicho kitasaidia sanakusambaza nishati ya umeme vijijini ili kuinua hali yauchumi nchini, maana viwanda vidogo vidogovitaweza kuanzishwa vijijini. Vile vile uwepo wa umeme

kwa wananchi kutatoa fursa ya kupata nishatimbadala kwa mahitaji ya nyumbani na viwandani.Mheshimiwa Spika, hali hiyo ikiimarika Sheria yaMazingira itakuwa imetekelezeka kwa sababu kuni namkaa havitatumika kwa ajili ya nishati ya kupikia.Naomba miradi yote hasa ya uchimbaji madiniizingatie Sheria ya Kuhifadhi Mazingira. Ni vizuri watoajileseni ya uchimbaji washirikiane vizuri na Baraza laHifadhi ya Mazingira ili kutekeleza vizuri Sheria yaUchimbaji pamoja na ya Mazingira.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: Mheshimiwa Spika,naomba nichukue nafasi hii kuchangia hoja katikaWizara ya Nishati na Madini. Kwanza, nampongezasana Waziri na Serikali kwa kuliweza tatizo lakutokuwepo au kuzimika kwa umeme mara kwa mara.Natambua changamoto zinazoikabili Wizara lakiniinaonesha sasa kuwa Wizara na Serikali wana kusudiola dhati katika kudhibiti na kushughulikia matatizo yaWizara husika.Mheshimiwa Spika, hoja yangu ya kwanza nikuhusu kutokuwa na wataalam wazalendowatakaoweza kuzifanya kazi za kitaalam katikamachimbo au migodi yetu pamoja na uhaba wawataalam uliopo namwomba Waziri aje na mikakati yakuwapeleka vijana kujifunza utaalam ili kuwezakufanya kazi katika machimbo yetu.

Mheshimiwa Spika, naomba kuongelea gharamaza mwanzo kwa wateja wapya wanaohitaji umeme,gharama ziko juu sana na kuweka umeme umbali wakuhitaji nguzo moja tu unahitajika kulipa si chini yashilingi 1,400,000 na baada ya gharama hizo badounahitaji kuendelea kulipia umeme. Nashauri Serikalikuchukulia suala la umeme kama la kibiashara na kwahiyo wao wafanye gharama zote ili wananchi wabakiena gharama za kununua umeme tu. Kuwatozawananchi gharama hizo ni kuwaonea nakuwabebesha mzigo usiokuwa wa kwao.Mheshimiwa Spika, nichangie pia kuhusuusumbufu wanaopata wateja wapya wa TANESCOwanapohitaji kupatiwa umeme. Pamoja na gharamana kuwa na uwezo wa kulipa gharama hizo wanapatausumbufu mkubwa sana na kukaa hadi miaka mitatuwakiwa wanafuatilia umeme, naomba Waziri aletemkakati wa kuwapatia haraka umeme wateja wapya.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. MASOUD ABDALLA SALIM: Mheshimiwa Spika,madini mbalimbali yanayochimbwa nchini badohayaleti faida kwa wakazi waliomo katika maeneoyanayochimbwa madini hayo, imekuwa ni vigumukuamini wengi walio karibu na maeneo ya uchimbajihali zao za maisha ni mbaya tofauti na matarajio.Mheshimiwa Spika, Serikali ina mkakati gani waziada wa kulazimisha Makampuni ya Madini kupelekahuduma za msingi na za lazima kwa maeneo ya karibuya vijiji vilivyozungukwa na madini?

Mheshimiwa Spika, wananchi waliozungukwa naMgodi wa Buhemba kule Mara na Tanzanite kuleArusha hawajapata manufaa yoyote. Kiwango chagesi kilichogundulika Lindi na Mtwara iwe ni chachu yakuboresha maisha na kupunguza umaskini katika Mikoaya Kusini, isiwe wananchi wa Lindi na Mtwara, wawe niwaangalizi wa bomba la gesi linalotoka Mtwara - Dares Salaam.Mheshimiwa Spika, kazi ya kuwapelekea umemevijijini iongezewe kasi ili angalau ifikie asilimia 65, kwanikasi ya maendeleo itafikiwa ikiwa Serikali itaongeza kasiya kupeleka umeme vijijini.Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali iondoe malipoya bei ya nguzo za umeme kwa wateja, si vizuri hatakidogo, Serikali kutoza bei ya nguzo za umeme wakatinguzo hizo ni uzalishaji unaotokea hapa Tanzania.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. MESHACK J. OPULUKWA: Mheshimiwa Spika,huko Meatu kuna shule inaitwa Shule ya SekondariKimali, naiomba Wizara ifikishe umeme katika shule hiiambayo iko Kilomita nne tu kutoka ilipo Grid ya Taifa.Mheshimiwa Spika, badala ya punguzo la bei yakuunganisha umeme kuanza Januari, 2013, sasa ianzeAgosti, 2012 ili kuwawezesha watu wengi zaidikuunganisha umeme kabla ya Christmas na mwakampya.

Mheshimiwa Spika, ahsante.MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika,kwanza, nampongeza Waziri, Manaibu Waziri, KatibuMkuu na Watumishi wote wa Wizara hii. Nashauriyafuatayo:-Kwanza, eneo likigundulika lina madini basi wenyeeneo husika washirikishwe kwenye mkataba namwekezaji, mathalani hisa asilimia 51 kwa 49. Hiiitasaidia kuwapa wazawa wetu uwezo mkubwa wakimapato na hatimaye kuongeza mapato ya Serikalina hivyo kukuza uchumi wa Taifa.Pili, maeneo yote yanayovunwa madini,husababisha uharibifu wa mazingira, suala la EIAlipewe kipaumbele na fidia kwa uharibifu wamazingira, lengo la saba la Milenia lizingatiwe.Tatu, kwa kuwa suala la Shirika la TANESCOlinaonesha wazi kwamba, kuna udhaifu mkubwa wakiutendaji ndani ya shirika hili, basi ni vema menejimentiikafumuliwa na kuundwa upya. Pia Bodi yaWakurugenzi wa Shirika la TANESCO ivunjwe maramoja. Aidha, wote walioshiriki katika kulihujumu Shirikahili mkondo wa Sheria uchukue nafasi yake, uchunguziuanzie tangu mwaka Juni, 2006.Nne, suala la gesi asilia lifanyiwe kazi harakaiwezekanavyo kwa kutunga sera na sheria itakaotoamiongozo na usimamizi wa rasilimali hii kwa maendeleoendelevu kwa Taifa letu.

MHE. GREGORY G. TEU: Mheshimiwa Spika,naipongeza Wizara hii kwa kazi nzuri waliyoanzakuifanya baada ya kuwapo mabadiliko, wakatimwingine mabadiliko huleta neema.Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia katikaeneo la madini yanayopatikana kama Wilaya yaMpwapwa. Maeneo yanakopatikana madinimbalimbali ni haya yafuatayo: Winza (Kibakwe),Izomvu, Mwenzele, Mlembule (Mpwapwa) nakadhalika.Mheshimiwa Spika, mpaka sasa kuna kasi kubwasana ya wachimbaji wakubwa wakiwemo wagenikuendelea na uchimbaji wa madini katika maeneoniliyotaja hapo juu bila ya utaratibu wa kisheria, hivyokuwasaidia wananchi na wachimbaji wadogo waliopokatika maeneo husika. Hali hii inawafanya wananchiwanaoishi katika maeneo hayo kushawishika kuuzamaeneo ambayo wana uhakika kuwa maeneo hayoyana madini.Mheshimiwa Spika, hali hii inaifanya Serikalikupoteza mapato, hususan Halmashauri ya Wilaya yaMpwapwa licha ya kuwa na madini kiasi cha kutoshalakini inakosa mapato. Vile vile wachimbaji wadogowanazidiwa na wachimbaji wakubwa (binafsi)wanaokuja na kunyemelea maeneo na wenginekuhodhi maeneo makubwa kwa kuyanunua au nakumiliki. Je, Wizara inachukua hatua gani kwakuyatambua, maeneo yote yenye madini na kuyalindayasivamiwe na wachache katika Wilaya hii yaMpwapwa? Je, Wizara itasaidiaje kuifanya

Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuweza kujipatiamapato na ajira kwa vijana? Je, Wizara inadhibiti vipiuharibifu huu unaoendelea pamoja na kuharibumazingira.MHE. DKT. CHARLES J. TIZEBA: Mheshimiwa Spika,nampongeza Waziri, Manaibu Waziri na Katibu Mkuukwa kazi nzuri wanayofanya. baada ya pongezi,naomba kuchangia katika mambo yafuatayo:-Mheshimiwa Spika, ni kweli kwa mtazamo waharaka haraka umeme wa kuzalishwa kwa gesi ni rahisikuliko matumizi ya mafuta. Mtazamo huu kwa hakikasiyo sahihi sana, kwani unaendekeza tabia sahihi sana,kwani unadekeza tabia ya kutotafuta suluhisho rahisina la kudumu. Gesi siyo renewable na hivyo iko sikuitakwisha.Pili, gesi hii ingeelekezwa kwenye matumizimengine ambayo yangechochea kukua kwa uchumina kupunguza kasi ya mahitaji ya pesa za kigeni namazingira, kama nishati mbadala.Mheshimiwa Spika, nachelea iko siku wajukuuwetu watatuuliza, iweje tuliamua kuchoma nishati mojaili kupata nishati nyingine? Nashauri tuwekeze zaidikwenye joto ardhi kupata umeme, Solar Source, Windna njia nyingine ambazo ni renewable. Hatujawekaumuhimu wa kutosha kwenye makaa ya mawe. Sualala kuchoma gesi kufufua umeme liwe la mpito(transitional short term measure) na ipewe muda waukomo wa ufuaji umeme kwa kuchoma gesi.

Mheshimiwa Spika, naomba mradi wa umeme waMCC unaoendelea kujengwa huko Sengeremauharakishwe, maana awali ilitarajiwa kuwa umemeutakuwa umewashwa ifikapo mwezi Mei, 2012. Hadisasa hakuna transformer hata moja, imefungwa nawananchi wanaendelea kuhoji, lini umemeutawashwa?Mheshimiwa Spika, katika mradi wa REA piaambao uko katika hatua za awali za utekelezaji,naomba Kisiwa cha Kome kipewe kipaumbele cha juuili kuleta imani kwa wananchi wa Visiwani (vipatavyo38 Jimboni Buchosa) kwamba Serikali yao ya Chamacha Mapinduzi inawajali na mipango ipo ya kuwapatiamiundombinu kwa ajili ya maendeleo yao.Mheshimiwa Spika, iko teknolojia ya kufua umemekwa upepo katika maeneo yaliyojitenga kama vileVisiwa, mashamba makubwa au vituo vya kitafiti mbalina maeneo ya makazi. Teknolojia hii bado ni siri hukoMarekani, na endapo Wizara itahitaji habari zaidi juu yajambo hili, basi nitaitafuta kwenye taarifa zaidi awezekupata maarifa hayo.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. ANNAMARYSTELLA. J. MALLAC: MheshimiwaSpika, nakushukuru kwa kupata nafasi hii ya kuchangiaWizara hii muhimu kwa maandishi. Nianze kwakumtanguliza Mwenyezi Mungu aliye na asili ya memayote.

Mheshimiwa Spika, nchi yetu ina Mikoa na Wilayaambazo zina madini yanayoendesha maisha ya watuikiwa kama ni sehemu ya ajira kwao, na ni waziwachimbaji wadogo wadogo hufaidika sanakunyoosha maisha yao kama wanapata msaadakutoka Serikalini.Mheshimiwa Spika, misaada tunayoiongelea nikama kutengewa maeneo ya wachimbaji wadogowadogo, kuhakikisha usalama, kuwekewa huduma zaafya katika maeneo ya machimbo yao na kutafutiwasoko.Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Katavi na Rukwa piatuna neema ya kuzungukwa na madini mbalimbalikama dhahabu, shaba na grina. Pia kuna wachimbajiwadogo wadogo ambao wanakidhi maisha yao kwauchimbaji wao mdogo. Lakini vijana badowanahangaika maeneo ya kuchimba, kwani Serikalihaijawatengea maeneo vijana bali wanajichanganyakatika maeneo ambayo yamemilikiwa na wachimbajiwenye pesa zao, ndipo wanakwenda wanachimbamabaki au masalio walimochimba.Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali kupitia Wizarana Waziri mwenye dhamana ahakikishe Wizaraimetenga maeneo rasmi kwa vijana wachimbajiwadogo wadogo ili waepukane na usumbufuwanaopata wa kukandamizwa na watu auwachimbaji wakubwa wenye pesa ili vijanawajikwamue katika umasikini na kupata maisha yenyeunafuu kupitia madini, tofauti na sasa maeneo mengiyameshikwa na Waarabu, Wachina na kadhalika.

Serikali pamoja na kukaribisha wawekezaji, inapashwakuwapa kipaumbele wazawa na hasa vijana.Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikisema akinamama wapewe kipaumbele, na daima akina mamawamekuwa wakijitoa katika sekta mbalimbalikuhakikisha wanajishughulisha ili kukabiliana nachangamoto na ushindani wa ajira. Kuna mtandao waakina mama wanaohamasisha matumizi ya nishatimbadala ya makaa ya mawe badala ya kuni. Wizaraya Nishati na Madini imeshafanya utafiti wa suala hili laakina mama hawa na wakathibitisha kwa maandishikuwa suala hili la kutumia nishati hii mbadala ni nzuri naendelevu na yenye faidia kwa Taifa letu. Akina mamahawa waliiomba Wizara Fedha, tena kwa mkopo, iliwaanzishe zoezi hilo Mkoa wa Rukwa na Wizarailiwajibu kuwapatia pesa hizo toka bajeti ya mwaka2011/2012, lakini mpaka hivi leo akina mama hawawamekuwa wakipigwa porojo tu. Sasa hapatunajenga au tunabomoa?Naiomba Wizara kupitia Waziri wa Wizara hiikuchukua hatua ya kuwasaidia akina mama hawawalioonesha nia na njia ya kupambana na umasikinina kuliingizia pato Taifa kupitia Nishati hii ili watimize niana azma yao, kwani suala lao lina faida na tija kwaTaifa letu, maana hata maeneo ambayo ni ya kwao,Serikali imekuwa ikiwazungusha kwa kuwawekeavikwazo ambavyo havina sababu za msingi.Mheshimiwa Spika, tuweke vipaumbele kwenyemambo yenye faida kwa Watanzania.

Mheshimiwa Spika, umeme bado ni tatizo kubwa,sehemu nyingine, mfano, Mkoa wa Katavi badotunatumia majenereta ambayo ni ya muda mrefu sanakiasi kwamba wakazi wanapata umeme kwa mgao nakwa wafanyabiashara inayotegemea umeme ni shida.Mheshimiwa Spika, Serikali sasa ijitahidi kuhakikishawachimbaji wadogo wadogo wanatengewa maeneoya uchimbaji na wanapata maji safi na salama,barabara, wanatafutiwa soko na mikopo.Mheshimiwa Spika, ahsante.MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: MheshimiwaSpika, nianze kwa kumpongeza Rais kwa kuteua teamnzuri ya Mawaziri kuongoza Wizara hii muhimu sana.Nakupongeza Mheshimiwa Waziri Prof. SospeterMuhongo, tuna imani naye, lakini pia Mheshimiwa Raisamempatia vijana mahiri kumsaidia MheshimiwaGeorge Simbachawene na Mheshimiwa StephenMasele. Wizara hii ni strategic sana katika uchumi wetu.Umeme hautakiwi kukatika katika viwanda vyetuambavyo tunataka viwe msingi wa nchi yenye uchumiwa kati (medium income country) ifikapo mwaka 2025.kwa mujibu kwa dira yetu ya maendeleo, vinahitajiumeme wa uhakika ili kufanya kazi zake vizuri.Baba wa Taifa aliwaambia Watanzania kwamba,madini ndiyo tegemeo kubwa la Watanzania naakasema wakati huo kwamba, tusingeanzakuyachimba mpaka wakati ambao tungekuwa nawataalam wetu (geologists) ili waweze kuzungumzalugha moja na wawekezaji.

Mheshimiwa Spika, Watanzania wanaaminikwamba kauli hiyo ya Baba wa Taifa ni sahihi na hivyowanategemea kwamba Serikali itakuwa makini sanakatika kusimamia Sekta hii ya Madini.Mheshimiwa Spika, Serikali inabidi iwasimamievizuri wawekezaji ili Watanzania wafaidike na madiniambayo ni zawadi ya Mwenyezi Mungu.Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ngara imebarikiwakuwa na madini mengi hasa dhahabu ambayohayajachimbwa. Wajerumani waliacha maandishiyanayosema, Ngara ni Wilaya tajiri kuliko zote kwadeposits za madini.Mheshimiwa Spika, sasa hivi Wilaya ina mgodi waKabanga Nickel. Mgodi huu ni wa pili kwa ukubwaduniani baada ya ule wa Canada (interms of deposit).Naiomba Wizara iwe karibu na wawekezaji katikamradi huu wa kujiandaa kuwapatia umeme wamegawati 30 zinazohitajika mgodi utakapoanzakufanya kazi. Pia Serikali iwe makini wakati wamchakato wa kuwahamisha wananchi na kuwaresettleili kupisha mgodi. Wakati wa kampeni zaUchaguzi Mkuu mwaka 2010, Mheshimiwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa Wilayani Ngaraalitoa ahadi ya kuupatia Mji mdogo wa Rulengeumeme wa generator pamoja na vijijivinavyouzunguka Mji wa Ngara.Mheshimiwa Spika, naiomba Wizara isaidiekuhakikisha Mji wa Rulenge unapata umeme huo kwa

kutumia Shirika la kueneza umeme vijijini REA. REAwamepiga hatua nzuri kwa kuwekeana Mkataba naHalmashauri ya Ngara kuhusu umeme wa Rulenge.Mheshimiwa Spika, naiomba pia Wizara isimamieumeme wa ORIO, Kampuni ya Holland. Kampuni yaORIO ilishawekeana Mkataba na TANESCO ili kuwekagenerator mbili kwenye Kituo cha TANESCO cha Ngaraili kusambaza umeme katika Miji midogo ya Mugomana Benaco na vijiji vya Kabaheshi, Nyamahwa naKashinga mpaka sasa generetor hizi hazijafungwa.Mheshimiwa Spika, maporomoko ya RusumoWilayani Ngara kwenye mpaka wa Tanzania naRwanda yana uwezo wa kutoa umemd wa Megawati90 na ni mradi wa nchi tatu; Rwanda, Burundi naTanzania, na kila nchi itapata Megawati 30. NaiombaWizara ihakikishe mradi huu haukwami na unaendeleaharaka. Umeme wa Rusumo utaziwezesha Wilaya zaNgara, Biharamulo na Kibondo kupata umeme wagrid. Mgodi wa Kabanga Nickel pia utafaidika naumeme huu.MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mheshimiwa Spika,naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Nishati naMadini kwa kuleta hotuba nzuri ya Wizara hii na kazinzuri anayoifanya. Nina imani naye na ninamhakikishiasupport yangu ya hali na mali. Nampongeza kwa kaulinzuri aliyoitoa Mtwara kuhusu TANESCO kulipia madeniyake na kukataza mawazo ya Makampuni ya gesikuweka rehani visima vyetu vya gesi kutokana namadeni ya TANESCO.

Mheshimiwa Spika, nawapongeza Manaibu Waziriwa Wizara ya Nishati na Madini – Mheshimiwa GeorgeSimbachawene na Mheshimiwa Stephen Masele kwakuonyesha umahiri mkubwa katika kutekelezamajukumu yao kwa umakini sana pamoja na kwambawamekaa muda mchache katika nafasi zao. Pongezizangu pia ni kwa Katibu Mkuu - Ndugu Eliakimu Maswikwa msimamo wake madhubuti wa kulinda na kuteteafedha za umma. Tunamwombea kwa MwenyeziMungu aendelee kumtia nguvu na ujasiri.Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Waziri waNishati na Madini - Mheshimiwa Prof. Muhongo kwa jinsialivyonipa msaada wa haraka wakati nilipompelekeasuala la umeme Vijiji vya Jimbo la Karagwe.Nimefurahishwa na kasi yake. Pia namshukuruMkurugenzi Mtendaji (REA) - Ndugu Mwakahesya naNdugu Msofe kwa kunikaribisha na kunisikiliza ofisinikwao siku ya Jumamosi. Hakika ni wasikivu nawameonyesha wanajali.Mheshimiwa Spika, umeme Jimbo (Wilaya) yaKaragwe, Vijiji ninavyoviombea umeme viko makundimawili. Mradi unaoendelea umekwepa vijiji vifuatavyo:Omurusimbi, Rukale, Misha, Ruhita, Rubale, Kibogoizi,Rugu, Kasheshe, Bujala, Nyakasimbi, Kahanga, Kijiji chaIhembe Na. 2, na Vitongoji; Rwanda/Kashambi.Mheshimiwa Spika, vijiji tajwa hapo juu vimerukwakatika mradi wa umeme vijijini unaoendelea waBisheshe, Nyaishozi na Ihembe. Naomba REA wapelekeumeme katika vijiji hivi ikiwemo na Vitongoji vya Karehena Kamuli katika Kijiji cha Nyakahanga ambako ndiko

umeme huu unakotokea, lakini wamesahauliwa. PiaShule za Sekondari, Zahanati, Makanisa, Mfano, Parokiaya Nyaishozi zimesahauliwa.Mheshimiwa Spika, umeme huu umepitabarabarani na kuingia ndani mita 100 tu. Vijiji vyanguvingi viko nje ya barabara kuanzia kilomita moja nanusu hadi tano kwa kila kijiji. Naomba mradi uingiendani waliko wanavijiji wanyonge, kwani baada yamradi kukabidhiwa TANESCO, wananchi walio wengihawataweza kulipia umeme huo.Mheshimiwa Spika, kuna ahadi za MheshimiwaRais alizozitoa mwaka 2005 na 2010 kuvipelekeaumeme vijiji vya Jimbo la Karagwe. Vijiji hivyo ni kamaifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, Vijiji vyote vya Tarafa yaNyabiyonza, Kijiji cha Chamuchuzi, Kijumbura, Kaiho,Kanywamagana, Kanogo, Chabuhora, Kandegesho,Nyakakika, Kayungu, Nyabweziga, Kakulaijo, Kibondo,Nyabiyonza, Nyakaiga, Bukangara, Ahakishaka,Kafunjo, Kamagambo, Rwenkorongo, Kiruruma,Biyungu, Nyakagoyagoye, Nyamieli na Nyakaswa.Mheshimiwa Spika, hivi vijiji vyote vimepakana,hivyo ni rahisi kuvifika. Ni ahadi ya muda mrefu.Naomba bajeti hii ya mwaka 2012/2013 umemeuwashwe.Mheshimiwa Spika, vijiji vingine ni Ihanda, Rukole,Chonyonyo, Omuchime Rulavo, Chanika, Runyaga,Ruhanya, Kinyinya, Katwe, Katembe, Kituntu,

Rwambaizi, Nyakahita, Kanoni, Kigarama Juu,Kigarama Chini, Bwera, Igurwa, Kibona na Kagutu.Mheshimiwa Spika, hivi vijiji ambavyo viko maeneoyanayopakana, hivyo ni rahisi vyote kufikika.Mheshimiwa Spika, vijiji vilivyopo Mji mdogo waKayanga ni Kijiji cha Nyakahanga, Bujuruga, KayangaVijijini na miti. Hivi viko ndani ya mamlaka ya Mji mdogowa Kayanga, lakini havina umeme.Mheshimiwa Spika, Vijiji vya pembezonivinavyohitaji kuangaliwa kwa jicho la huruma pia ni Kijijicha Omukakajinja, Rugela na Nyarugando (vijiji vyotehivi viko Kata moja ya Rugela). Naomba vipeweumeme.Mheshimiwa Spika, pia vipo vijiji vya pembezonivya Kata ya pembezoni ya Kihanga navyo ni Kijiji chaKishoju, Mulamba, Kihanga, Katanda, Kibwera naMushabaiguru.Mheshimiwa Spika, Jimbo la Karagwe ni Jimbolinalopakana na Uganda na Rwanda. Limeathirika nawakimbizi, vita vya Uganda, gonjwa la Ukimwi, Meli yaMV. Bukoba kuzama na hivyo kuathiri shughuli zauchumi. Hivyo basi, wananchi hawa wanahitaji hurumaya Serikali kuwainua kiuchumi na kijamii.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika,naanza kwa kuunga mkono hoja hii kwa asilimia miamoja.Mheshimiwa Spika, niendelee kwa kupongeza kazinzuri inayofanywa na Katibu Mkuu pamoja na Waziri naManaibu wote. Hatua inayoendelea hivi sasa yakuhakikisha Wizara inakuwa safi, naiunga mkono kwaasilimia mia moja. Ushauri wangu ni kwamba, zoezi lakuhakikisha Watendaji wabadhirifu wanaondoka,liendelee kwa nguvu hiyo hiyo na lisirudi nyuma hatakidogo, kwani Wizara hii imekuwa na uozo kwa mudamrefu.Mheshimiwa Spika, hatua hii inahitaji ujasiri, hivyonawaombea kwa Mungu ujasiri alionao uendeleehivyo hivyo, katu asiogope kwa kuwa naaminiMwenyezi Mungu amewaweka hapa ili watukomboeWatanzania.Mheshimiwa Waziri, tunamshukuru Mungu kwauwepo wenu na daima tutakuwa wote kwa hali zote.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika,kwanza nataka nimpongeze Mheshimiwa Waziri waNishati na Madini, Naibu wake na Katibu Mkuu kwa kazinzuri wanayoifanya ya kuhakikisha tatizo la umemelimeondoka. Tumekuwa na tatizo la umeme kwa mudamrefu sana kiasi cha kukata tama, lakini sasa inaelekeakuwa historia. Hongereni sana, endeleeni hivyo.

Mheshimiwa Spika, napenda nitoe shukrani zanguza dhati kwa Serikali kwa kusaidia tatizo la umemekuzidi ghafla au kupungua ghafla jambo ambalolilikuwa linawatia hasara sana wananchi wa Mkoa waDar es Saalam. Serikali imefunga transformer mpyakatika Mkoa wetu, hongereni sana.Mheshimiwa Spika, pamoja na wingi wa pongezi,sasa niishauri Serikali yangu sikivu ya Chama chaMapinduzi kwamba, Serikali inapata gharama kubwaya kuwaunganishia wananchi umeme toka eneo hadieneo, katikati kuna nyumba nyingi ambazo hazinaumeme kabisa, hii ni hasara kwa TANESCO.Mheshimiwa Spika, nini kifanyike? TANESCO niShirika ambalo linatakiwa aliendeshwe kibiashara zaidina liajiri wabunifu ambao watalifanya Shirika letu letuliendeshwe kibiashara na kifaida zaidi. Ni wajibu waTANESCO kushawishi wananchi walio eneo la katikakatiya mtu anayepelekewa umeme wakubali kufungiwaumeme hata kwa kulipa gharama kwa awamu mbiliau tatu, lakini Shirika litakuwa limevuna. Tuacheubinafsi, tuangalie uzalendo. TANESCO badala yakukusanya kwa nyumba moja, itakusanya nyumbanyingi na Shirika litapata angalau fedha za kujiendeshabadala ya sasa kusubiri ruzuku ya Serikali.Mheshimiwa Spika, tumekuwa tukiishauri TANESCOibadilike hata kiutendaji, siku moja kuchukua vijanawaka-promote umeme na kufanya ukaguzi wanyumba hadi nyumba kuhakiki matumizi ya umeme nawale ambao hawana umeme washawishike kutumiaumeme. Hakika tutapata ongezeko la kipato, kwani

promotion na advertsment ni party ya biashara na nilazima kutengewa fungu katika shughuli yoyote yabiashara.Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali katika suala lamafuta ya mitambo kwamba, pamoja na juhudi zaSerikali kujenga bomba la gesi kwa kusaidia wananchikupata umeme wa gharama nafuu, lakini katika kipindihiki cha mpito, Serikali isifanye makosa kwa kununuamafuta ya gharama za juu.Mheshimiwa Spika, napongeza juhudi zaMheshimiwa Waziri na Manaibu wake na Katibu Mkuukwa kuokoa Shilingi bilioni tatu kwa kila wiki mbili naShilingi bilioni sita kwa mwezi. Fedha hizi ni nyingi sanana zitatusaidia kufanyia shughuli mbalimbali zamaendeleo. Hongereni sana na nawaunga mkonokwa asilimia mia kwa mia.Mheshimiwa Spika, ni vyema sasa wanasheria waSerikali ndani ya Wizara waangalie Procurement Act nayale maeneo yanayofuka ufisadi yaletwe Bungeniturekebishe haraka, sheria hii isiwe kikwazo chamaendeleo.Mheshimiwa Spika, bei ya mafuta mazito ni ndogosana, wakati nje ya Tanzania (Ghuba) Falme zaKiarabu iko chini sana. Wizara kama imefanikiwa kuonaufisadi wa kununua mafuta kwa bei kubwa, suala laPuma na TANESCO iwe changamoto kwetu, Serikaliiagize mafuta kwa gharama zake toka nje na tujetutumie katika mitambo yetu wenyewe. Tufanyemajadiliano na kampuni yetu ya Puma ambayo

asilimia 50 ni yetu, kutafuta njia ya majadiliano pasipokuwaletea hasara.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia kwa mia, bajeti ya Wizara ipitishwe.MHE. NYAMBARI C. M. NYANGWINE: MheshimiwaSpika, nianze kwa kumpongeza Waziri wa Nishati naMadini na Wizara hii kwa kuchapa kazi vizuri pamojana uadilifu anaouonyesha katika kulitumikia Taifa letu.Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwapongezaManaibu Mawaziri wote wawili wa Wizara hii kwauchapaji kazi wao, bila kumsahau Katibu Mkuu waWizara. Kwa hakika nguvu za Waziri, Manaibu Mawaziripamoja na Watendaji wengine wa Wizara hiiwakiunganisha pamoja, nina imani kuwa wanawezakufanya lolote la maana katika nchi hii.Mheshimiwa Spika, binafsi siungi mkono hoja hiikwa kuwa kuna mambo mengi sana ambayoyanahitaji fikra zaidi kuyatatua kuliko nguvu. Pia kwahistoria mbaya sana ya Wizara hii kuhusu eneo laNyamongo (ambalo ni North Mara) lililoko WilayaniTarime, bado hakuna ufumbuzi wowoteuliokwishapatikana.Mheshimiwa Spika, hoja zangu hazitakuwa tofautina za mwaka 2011, kwani hadi sasa utekelezaji wa yaleniliyoyaongelea kwenye bajeti ya mwaka 2011 badounasuasua ingawa umenza taratibu. Hivyo namwombaWaziri anijibu maswali yafuatayo:-

Suala la umeme wa REA ni hakika na ukweli uliowazi kuwa umeme huu wa REA ukifika katika vijiji vyotevya Tanzania, nchi ya Tanzania itapiga hatua mbelezaidi kwa maendeleo.Mheshimiwa Spika, ni lini ahadi ya Waziri Mkuu waTanzania - Mheshimiwa Mizengo Peter Kayanza Pindaya kukipatia umeme Kituo cha Kurya cultural Centrekilichoko Kijiji cha Msanga, Kata ya Goronga, Tarafa yaIngwe, Wilaya ya Tarime itatekelezwa?Mheshimiwa Spika, mradi wa REA katika vijiji vyaNyamwigura, Rozana, Kemakorere, Nyarero,Nyamwaga, Keisangura, Tagare, Muriba, Kumwika,Kobori, Itivyo, Mangucha, Kegonga, utakamilika? Huumradi ni maarufu kama mradi wa umeme wa ItivyoWilayani Tarime.Mheshimiwa Spika, kwanini gharama za kuingizaumeme katika nyumba ambazo ziko karibu na mradihuu zisipunguzwe ili kuwawezesha wananchi masikinikujiwekea umeme katika nyumba hizo? Je, mradi waREA katika vijiji vya Security Road Wilayani Tarime tokaRorya Susuni Kubiterere, Remagwe, Nyabisaga, Borega,Ganyange, Kimusi hadi Nyantira utaanza na kukamilikalini? Je, mradi wa REA katika Vijiji vya Nyakunguru,Kibasuka Nyarwana Weigita, Kembwi, Manga hadiKomaswa utaanza lini na utakamilika lini?Mheshimiwa Spika, napenda kuleta ombi maalumkwamba, kwa kuwa Wilaya ya Tarime ina rasilimali zakutosha kwa wananchi wake kuweka umeme katikanyumba zao, naiomba Wizara ihakikishe kuwa mradi

wa REA unaanza mara moja katika Vijiji vya Kata zoteza Tarime zikiwemo za Nyandoto, Gorong’a, Itiryo,Nyanungu, Kiore, Kibasuka, Bumera, Kitare, Magoto nakadhalika.Mheshimiwa Spika, je, Serikali kupitia Wizara hiiinasema nini juu ya umeme unaokatikakatika kutokanana mgawo wa kutengenezwa na Watendaji waliokoWizarani? Je, Serikali kupitia Waziri wa Wizaraamewachukulia hatua gani?Mheshimiwa Spika, vitendo vya rushwavimeshamiri sana kwenye Shirika la TANESCO. Je,Serikali inalifahamu hilo? Kama inalifahamu,imejipanga vipi ili kuondoa aibu hii? Kuna tetesi kuwakuna baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri yaMuungano wanapokea rushwa toka kwa Watendajiwa TANESCO. Je, Serikali inalifahamu hilo? Imechukuahatua zipi? Halikadhalika, kuna tetesi kuwa baadhi yaWabunge wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madiniwanajihusisha na biashara isiyo halali na TANESCO. Je,Waziri anasemaje kuhusu hilo?Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kuwa, nchiyetu ya Tanzania imebarikiwa kupata maliasili yamadini ya kila aina, mfano almasi, dhahabu, uranium,tanzanite na mengine mengi ambayo hayana hatamajina. Je, sekta ya madini inalinufaishaje Taifa hili?Mheshimiwa Spika, iuna tetesi kuwa makuadi wamadini (madalali) ndio wanaonufaika na Sekta hii yaMadini kuliko nchi. Waziri anasema nini juu ya hilo?Waziri amejipanga vipi kurekebisha mikataba mibovu

ambayo viongozi wenye uroho walisaini kwa pupa nasasa inaliangamiza Taifa na hivyo kuifanya Tanzaniakuwa kichwa cha mwendawazimu au shamba la bibina babu katika Sekta hii ya Madini? Je, mrahaba mpyaambao nasikia ni 4% ni halali kwa Taifa hili? Kama siyohalali, ni nini kifanyike? Kwa nini tusigawane 50% kilapande baada ya kutoa gharama ya uzalishaji? Ni nanianayedhibiti na kuangalia uzalishaji wa kiasi gani chadhahabu katika migodi yetu?Mheshimiwa Spika, gesi ni bahati ya pekeeambayo Mwenyezi Mungu muumba wa Mbingu naNchi ametujalia. Nasikia ina thamani ya Shilingi trilioni600. Huu ni utajiri ambao kwa kweli nchi yetu imejaliwa.Mheshimiwa Spika, Serikali imejipanga vipi kuvunahiyo gesi? Serikali imejipanga vipi ili kuhakikisha kuwaasilimia 60 ya gesi hiyo yote inalinufaisha Taifa? Serikaliinatoa mafunzo gani kwa wananchi ili kuwaandaa kwamatumizi ya gesi katika majumba yao? Je, Serikali inamkakati gani wa kuwaandaa Watanzania ili wawezekununua magari yanayotumia gesi na siyo petrol waladiesel?Mheshimiwa Spika, wafanyabiashara wengi wamafuta hasa petrol huchanganya nishati hiyo na maji,mafuta ya taa na kadhalika. Hali hii inapelekeauharibifu mkubwa wa magari. Kwa mfano, kampuni yaBig Bon inaongoza kwa kufanya mchezo huu. Je, Wazirikupitia Wizara yake analijua hilo? Je, amechukuahatua gani hadi sasa? Je, haoni kuwa EWURAimeshindwa jukumu na wajibu wake, hivyo ivunjwe ilikianzishwa chombo kingine badala yake?

Mheshimiwa Spika, mgodi wa dhahabu NorthMara, maarufu kama mgodi wa Nyamongo WilayaniTarime, ni mgodi ambao umegubikwa na changamotonyingi sana. Je, Wizara inasaidiaje kutoa fidia halali kwawanaohamishwa ili kupitisha uwekezaji katika eneo laNyamongo? Kwa nini fidia hizo zimechelewa kulipwahadi sasa? Kwa nini mwekezaji hajatekeleza ahadizilizopo kwenye mikataba, za kutoa huduma za kijamiikama vile maji, umeme, shule, barabara na afya?Wizara inasaidiaje kufanikisha suala hili?Mheshimiwa Spika, sakata la maji ya Mto Tigiti(maji yenye sumu) lilitikisa Bunge hili kwa muda sasa.Kwa nini hadi sasa wale wote walioathirika katika majiya Mto huu hawajalipwa fidia? Je, NEMC iliishauriSerikali kuhusu suala hili? Je, Kamati za Kudumu zaBunge za Nishati na Madini na ile ya Ardhi, Maliasili naMazingira, ilitoa ushauri gani kwa Serikali kuhusu sakatahili?Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara hiiimefikia hatua gani ya kuwaelekeza wachimbajiwadogo wadogo? Fedha zilizotengwa na mgodi kwaajili ya wachimbaji wadogo wadogo takribani US$5,000,000 iliwekwa katika akaunti gani? Kama zikoWizarani, kwa nini hazitumiki? Kama hazijatolewa namwekezaji, Serikali inasema nini? Je, ujenzi wa ukuta(fence) katika eneo la mgodi, utarudisha mahusianomema kati ya mwekezaji na wananchi wanaozungukamgodi huo? Kwa vipi? Je, hilo ndilo suluhusho lakudumu?

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na ahadi kemkemtoka kwa mwekezaji kuwa mpango kabambe wakujenga barabara ya Nyamwaga Road itokayo TarimeMjini – Kemakorere – Nyamwaga - Nyamongo hadi MtoMara yenye umbali wa takribani kilomita 53 kwakiwango cha lami. Je, kupitia Wizara hii, Serikali inatoaushauri gani juu ya utekelezaji wa ahadi hizi? Ni linimgodi utaanza kulipa Halmashauri loyalty ya US$1,000,000 badala ya US$ 200,000 ambayo inalipwa kwasasa? Je, kodi ya huduma, yaani services levy, inalipwaipasavyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime?Mheshimiwa Spika, uharibifu wa mazingira katikamgodi wa dhahabu wa North Mara, yaani Nyamongo,ni kero kwa wananchi wa eneo husika. Je, Serikalikupitia Wizara hii, inatoa ushauri gani juu ya milipuko yabaruti maji ya sumu na kadhalika, ambayohuwakumba mara kwa mara watu wa eneo husika?Mheshimiwa Spika, Vijiji vyote vya Kata zaNyangoto na Kemambo vilivyoko Nyamongovinanufaika na asilimia moja ya mgodi isipokuwa kijijikimoja cha Mrito. Kwa nini kijiji hiki hakijaingizwakwenye mradi wa vijiji vinavyonufaika na mgodi?Mheshimiwa Spika, tatizo la ajira katika mgodi waNorth Mara linatatuliwaje? Ni lini mgodi utapima Mji waNyamongo na Mji wa Nyamwaga kama ahadi nyingizinavyoelekeza? Je, mgodi una mpango wowote wakujenga nyumba za kisasa katika Miji hii miwili? Ni linimgodi utajenga Chuo cha Ufundi (VETA) katika eneola Nyamongo ili kukamilisha ahadi ya mgodi? Je,

mauaji yasiyo na kikomo huko Nyamongo yatakomalini?Mheshimiwa Spika, wananchi wa Tarime wanakaajuu ya dhahabu, wanatembea juu ya dhahabu nahata wanalala juu ya dhahabu, lakini wanakabiliwa naumasikini uliokithiri? Je, Serikali inasema nini juu ya hilo?Mheshimiwa Spika, kwanini wananchi wengi waTarime hawashirikishwi katika suala la biashara nahuduma nyingine kwenye mgodi?Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.MHE. HEZEKIAH N. CHIBULUNJE: Mheshimiwa Spika,napenda kumpongeza sana Waziri wa Nishati naMadini pamoja na Naibu Mawaziri wote wawili.Wameanza vizuri na mipango yote waliyoiainishainatutia matumaini makubwa juu ya uongozi wao.Aidha, napongeza sana timu yenu ya utendajiikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara kwa utendajimahiri na umakini sana. Napenda pia nipongezehotuba nzuri ya bajeti ya Wizara, na ninaiunga mkonohoja.Mheshimiwa Spika, kwa vile Wizara ilikwishatoaahadi ya kutelemsha umeme kwenye maeneoyanayopitiwa na nguzo za umeme na yale ya karibuna maeneo yaliyo na umeme, naomba kwa maranyingine kupata kauli ya Serikali juu ya ahadi hiyo kwavijiji vya Msange kilometa nne toka Chamwino Ikulu,Chinangali – Mwegamile kwenye njia kuu ya umemetoka Dodoma kwenda Kongwa na Mpwapwa.

Kitongoji cha Mpera kilometa mbili ndani ya Kijiji chaChamwino Ikulu. Maeneo haya yalikwishatathiminiwana TANESCO na uongozi wa Wizara uliowatanguliakupitia kwa Waziri na Naibu Waziri. Walikwishakutanana wananchi wa maeneo hayo na kuwapa ahadi yakupatiwa umeme. Naiomba kauli ya Serikali kwa maranyingine juu ya ahadi hiyo kwa wananchi wa vijiji hivyo.Mheshimiwa Spika, napenda kuishukuru sanaSerikali kwa kupanga kunipatia umeme kupitia mradiwa MCC kwenye Kata za Manchali, Majeleko naChilonwa zilizoko kwenye Jimbo langu la Chilonwa.Pamoja na shukurani hizo, naomba Serikali iwajulishewananchi na Taasisi mbalimbali ambazo ziko karibu namaeneo ambayo umeme huo utapitia iwapowatasambaza umeme huo pia. Maeneo yanayohusikani Shule ya Sekondari Manchali, Shule ya MsingiChalinze, Shule ya Sekondari Chilonwa. Kwa vilemaeneo haya yapo kwenye njia ya umeme huu wamradi wa MCC, naomba kuleta ombi kwa Serikalikuangalia uwezekano wa kuzifikishia umeme Taasisi hiziili ziweze kutoa huduma kwa wananchi wanaohusikana Taasisi hizi.Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa narudiakuwapongeza Waziri pamoja na Naibu Mawaziri nakuwaunga mkono. Naomba kupewa majibu ya hojazangu hizo mbili.Mheshimiwa Spika, nawasilisha.MHE. ABDULAZIZ M. ABOOD: Mheshimiwa Spika,kuna baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa

yakilalamikiwa na wananchi wengi wa Jimbo laMorogoro Mjini kwa muda mrefu sasa. Kuna Shirikahalijawatoa huduma hii muhimu ya nishati ya umemekatika jamii na hivyo kukwamisha shughuli mbalimbaliza kiuchumi na hata kulikosesha Shirika lenyewemapato makubwa.Mheshimiwa Spika, maeneo ambayohayajapatiwa huduma hii ni Kihonda (VETA), MtaaKilongo Kata ya Mkundi, Kayenzi Mtaa wa Sina Kata yaMafisa, Kola ‘A’ Missionary, Mtaa wa Area ‘K’ Kata yaK/Changani, Mtaa wa Mji Mwema, Kata ya Tungi naKata ya Mindu, Bingwa na Towelo Kata ya Mlimani.Sehemu hizi zina wananchi wengi sana waishio katikamaeneo mengi bila ya kuwa na umeme. Kwa mfano,Mtaa wa Kilingo Kata ya Mkundi pekee ina wakazikaribu 900 wanahitaji huduma ya umeme. KihondaVeta wakazi karibu 700 nao wanahitaji huduma hii.Mheshimiwa Spika, hivyo basi, ukitizama tathiminihii, ni wakazi wengi sana ambao hawajapelekewaumeme katika Jimbo la Morogoro Mjini ukizingatiaManispaa ya Morogoro inataka iwe Jiji. Kuna baadhiya maeneo, kwa mfano, Mafisa kuliwekwa nguzo, lakinicha kushangaza nguzo hizo ziliondolewa bila taarifayoyote, na wananchi wa maeneo hayo ndiowaathirika zaidi.Mheshimiwa Spika, pia kukua kwa Taasisi nyingizinazojihusisha na jamii ambazo zinakosa huduma hizo,na baadhi ya Taasisi hizo ni Vituo vya Kulelea WatotoYatima, Shule za Msingi na Sekondari, Vituo vya Afya,na wajasiriamali ambao wengi ni wanawake. Aidha,

kutopatikana kwa nishati hii, kunawadidimizawananchi kiuchumi.MHE. SYLVESTER M. KASULUMBAYI: MheshimiwaSpika, kwanza nianze kwa kukupongeza kwa kuteuliwakwako kuwa Mbunge na kwa kuteuliwa kuwa Waziri waNishati na Madini, Wizara iliyo nyeti sana katika ustawiwa uchumi wa nchi yetu.Mheshimiwa Spika, naomba nikuhabarishe kuwa,Jimbo la Maswa Mashariki pamoja na kuanzishwa rasmimwaka 2010, limo ndani ya Wilaya Kongweiliyoanzishwa na Wakoloni hapo mwaka 1927, miaka 85iliyopita.Mheshimiwa Spika, Jimbo hili ni miongoni mwaMajimbo yanayonyemelewa kwa kasi ya kumezwa najangwa kufuatia na ukame uliopo unaosababishauotaji wa miti kadri inavyopandwa kuwa hafifu sana,hali inayopelekea wanawake kukata minyaa ili kupatakuni na kukusanya vinyesi vya ng’ombe ambavyohuvitumia kama kuni mbadala ya kuwawezeshakupikia vyakula hali ambayo kazi ya kupika vyakulavyao huandamana na wingi wa moshiunaowasababishia macho yao kuwa mekundu.Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri katikakuanza kuwapunguzia adha hii inayowakabiliwananchi wa Jimbo la Maswa Mashariki ili nao waanzekutumia nishati itakayozuia ukataji wa miti na uokotajiwa vinyesi vya ng’ombe ili miti na vinyesi vya ng’ombekuvibakizia kazi ya kurutubisha ardhi na kuimarishautunzaji wa mazingira ya Jimbo la Maswa Mashariki.

Mheshimiwa Spika, hivyo, kutokana na umuhimuhuo, nakuomba vijiji vifuatavyo uone haja ya kuvigawiaumeme. Vijiji hivyo ni Kijiji cha Ipililo cha Kata ya Ipililo -Maswa (Simiyu), kijiji cha Ngulinguli cha Kata yaNgulinguli – Maswa (Simiyu), Kijiji cha Mwabayandacha Kata ya Mwigwa – Maswa (Simiyu), Kijiji chaIsageng’he cha Kata ya Sukuma – Maswa (Simiyu), Kijijicha Mbalagane cha Kata ya Lalago – Maswa (Simiyu),Kijiji cha Mandang’ombe cha Kata ya Lalago - Maswa(Simiyu), Kijiji cha Mwadila cha Kata ya Sukuma –Maswa (Simiyu), Kijiji cha Gula cha Kata ya Lalago –Maswa (Simiyu), Kijiji cha Mwakidiga cha Kata yaLalago - Maswa (Simiyu).Mheshimiwa Spika, ninayo matumaini makubwakuwa ombi hili Mheshimiwa Waziri atalifanyia kazi iliwakazi hao nao waweze kuanza kutumia nishati yaumeme katika kuwarahisisha kuujenga uchumi wa nchiyetu na kuachana na matumzi ya kuni na vinyesi vyang’ombe ili miti na vinyesi vya ng’ombe viendeleekuirutubisha ardhi yetu.Mheshimiwa Spika, naomba kukuwasilishia ombihili muhimu kwa Mheshimiwa Waziri. Naomba wakatiatakapokuwa anahitimisha hotuba yake ya bajeti,anijulishe kilichojiri dhidi ya ombi hili.MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Spika,napenda kutoa maoni yangu kuhusu hotuba ya Waziriwa Nishati na Madini, Mheshimiwa Sospeter Muhongokama ifutavyo:-

Mheshimiwa Spika, umeme ni wa muhimu sanakatika kuendeleza maisha ya Watanzania, kuendelezauwekezaji na kadhalika. Hata hivyo ni wananchiwachache sana wamenufaika na umeme. Hotuba yaNishati na Madini, ukurasa wa saba, ni aibu kwambamiaka 50 baada ya uhuru Watanzania waishio Vijijini, ni6.6% tu ndio wameunganishiwa umeme ikiwa ni 18.4%ya Watanzania wote waliounganishiwa umeme kwasasa.Mheshimiwa Spika, hivi karibuni imebainikakwamba kuna mpango wa kuviwekea rehani baadhiya visima vya gesi katika Kisiwa cha Songo Songo kwamadai ya mwekezaji kutafuta fedha katika Taasisi zaKimataifa nje ya nchi. Ningependa kuhoji, ni nini kauliya Serikali kuhusu hilo?Mheshimiwa Spika, ahadi ya kupatikana kwa kiasicha Megawati 3000 za umeme ilitolewa naMheshimiwa Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yakekwa Taifa ya kuukaribisha mwaka 2012, pale aliposemakwamba, ujenzi wa bomba la gesi toka Songo Songona pia toka Mtwara hadi Dar es Salaam, utaligeuzatatizo la umeme kuwa historia. Je, bomba hilo litakuwana uwezo wa kusafirisha gesi yenye futi za ujazo ngapina ni lini ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais itaanzakutekelezwa?Mheshimiwa Spika, mitambo iliyopo Dar es Salaaminayoendeshwa kwa kutumia gesi ya Songosongokama vile Songas, Symbion, mitambo ya Ubungo yaTANESCO, Jacobson ya TANESCO - Tegeta kwa ujumlawake inazalisha Megawati 522. Lakini gesi iliyopo ya

Megawati 400 haiwezi kukidhi Megawati hizo zote kwamara moja. Hii ina maana kwamba mashine zotezingepata gesi zingeweza kutembea na ku-produceumeme kwa wakati mmoja na hivyo kupunguzautegemezi wa umeme wa maji ambao katika hali halisi,kwa hivi sasa una upungufu mkubwa.Mheshimiwa Spika, hivi sasa kuna uwezo mkubwawa mitambo ya gesi kuliko gesi iliyopo. Serikaliiharakishe mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara naSongo Songo ili mitambo yote ya kuendesha gesiifanye kazi kwa wakati mmoja na hivyo kuepusha Taifana baa la mgao wa umeme.Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kwambaTANESCO hawakusanyi mapato ipasavyo nainavyostahili. Uzalishaji wa umeme haulingani namapato yanayokusanywa. Changamoto zifuatavyozinazorotesha utendaji na mafanikio ya TANESCO, wiziwa umeme kwa kutumia vishoka wa umeme. Upotevuwa umeme kutokana na miundombinu mibovu,wadaiwa wakubwa hawalipi kwa wakati na wenginehawalipi kabisa.Mheshimiwa Spika, TANESCO ingeweza kufanyayafuatayo ili kuboresha mapato yake. Eneo laDistribution wange-out source kuwapa Kampuninyingine, wao wadai tu malipo. Nchi nyinginewanafanya hivyo, mfano, Latin America na nchinyingine za Ulaya. Umeme mwingi unaopotea kwenyehightension kwa sababu ya miundombinu mibovu napia wizi (vishoka) wasakwe na kuadhibiwa,miundombinu iboreshwe kwa kuweka transmission lines

zenye uwezo mkubwa kutoka KV 220 na kuongezwahadi KV 400 au KV 600.Mheshimiwa Spika, kutokana na connection kuwanyingi, uwezo wa transfoma zilizopo umepungua, kwamfano, Dar es Salaam, zibadilishwe mapemaiwezekanavyo ili kuondoa usumbufu uliopo kwawatumiaji wa umeme.Mheshimiwa Spika, kwa haya machache,naomba kuwasilisha.MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: MheshimiwaSpika, awali ya yote, nampongeza Mheshimiwa Wazirikwa hotuba nzuri na uwasilishaji wake makini na kwaufasaha. Nawapongeza pia Naibu Mawaziri, KatibuMkuu, Viongozi na Watumishi wa Wizara kwa uandaajiwa hotuba yenye mwelekeo na matumaini.Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hiipia kuipongeza Wizara kwa usimamizi mzuri wa sera zaNishati na Madini. Mradi wa umeme vijijini ni mkomboziwa Watanzania wengi ambao wanaishi vijijini, nakichocheo kikubwa cha maendeleo ya nchi yetu.Wizara na hasa Waziri aendelee kusimamia kwaumakini utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini ilitupate mafanikio.Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Bagamoyo,tuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa Nishati yaUmeme kwa wananchi vijijini. Kuna vijiji kadhaaambavyo vinapitiwa na nguzo na nyaya za umeme,lakini vyenyewe havipati umeme. Mwaka 2008 Wizara

ilipitisha umeme mkabala na barabara ya Dar esSalaam mpaka Kitopeni (Bagamoyo). Katika barabarahiyo, kuna vijiji kadhaa vikiwemo Mapinga, Kerege,Zinga, Kiromo na Kitopeni. Tatizo ni kuwa wanaofaidikani wale tu ambao wapo jirani sana (labda mita 100 -300) na nguzo zilizopo. Nje ya hapo, gharama yakuvuta ni kubwa sana, wananchi wanashindwa.Maombi yetu katika laini hiyo ya Dar es Salaam –Bagamoyo. Wizara iongeze mtandao wa laini yaumeme ili wananchi wengi zaidi waweze kuvutaumeme kwa gharama nafuu.Mheshimiwa Spika, pia kuna vijiji kadhaa katikamaeneo mengine ambayo ama vinapitiwa na umeme,au viko karibu sana na umeme, lakini havipati hudumahiyo ya umeme. Hivi ni pamoja na vijiji katika Kata yaYombo (Yombo, Matimbwa, Chasimba na Kongo).Kata ya Kiromo ni Kijiji cha Buma ambacho kina idadiya wananchi wengi wanaotaka huduma hiyo. KatikaKata ya Zinga Vijiji vya Pande na Kondo vimesubirihuduma hiyo kwa miaka mingi na umeme upo karibuyao sana.Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Wazirianipe majibu, ni lini vijiji hivi katika Wilaya ambayoinapakana na Dar es Salaam vitapata huduma yaumeme?Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE.EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Spika,nashukru kwa fursa hii ya kuchangia hoja ya Waziri waNishati na Madini.

Mheshimiwa Spika, mchango wangu ni kamaifutavyo:-Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naombakuwapongeza Viongozi Waandamizi wote wa Wizarahii, yaani, Mheshimiwa Prof. Muhongo, Naibu Mawazirina Katibu Mkuu ambao wote ni wapya, kwakuaminiwa na kuteuliwa kushika dhamana za uongoziwalizonazo. Binafsi, nawafahamu vizuri utendaji wenu,na kwa kweli tayari mmeanza kuonyesha cheche zenu,labda kwa asiye na macho tu au mwenye lake jambondiye haoni. Aidha, nawapongeza kwa bajeti nzuriyenye kupeleka umeme Chela Ngaya, Bulige, Busangina Ntobo kama nilivyoomba, nitaachaje kuiungamkono? Hivyo naunga mkono hoja hii.Mheshimiwa Spika, pamoja na matumaini hayomakubwa, naomba Waziri na timu yake niwaongezeehadidu za rejea kwa kazi yao ya mwaka 2012/2013ambazo ni kero kwa Wanamsalala.Mheshimiwa Spika, Halmashariuri ya Wilaya yaKahama, ina madai ya jumla ya Dola 7,406,993ambazo ni ushuru wa huduma (service levy) ambayohaijalipwa na migodi toka migodi ya Bulyanhulu (2000)na Buzwagi (2009) ianze uzalishaji.Mheshimiwa Spika, mikataba ya uwekezaji yamigodi hii ilivunja sheria ya Serikali za Mitaa ya mwaka1982 inayoziruhusu Halmashauri kutoza ushuru huo kwaasilimia 0.3 ya pato ghafi la mwekezaji, badala yakemikataba hiyo iliweka ukomo wa Dola 200,000 kama

mbadala wa service levy ambayo ni ndogo kulikoservice levy yenyewe.Mheshimiwa Spika, Tume ya Bomani ambayo miminilikuwa Mjumbe pamoja na akina Maswi, ilionaupungufu huo na kushauri Serikali irekebishe Sheria yaMadini ya mwaka 2010, ikazingatia ushauri huo. Lakinihadi leo majadiliano, utekelezaji haujafanyika. Suala lakuongeza royalty toka 3% hadi 4% ambalo nalo limokwenye sheria mpya na linatokana na observation andrecommendation ya Tume ya Bomani limeanzakutekelezwa. Hili la service levy nalo ni budi litekelezwemwaka huu.Mheshimiwa Spika, kama Serikali ilivyounda Kamatindogo ya Bunge kufuatilia chenji ya rada Uingereza,wananchi wa Msalala wameunda Kamati ndogoninayoingoza nije kudai chenji yetu pia. NaombaWabunge wenzangu mtusaidie chenji yetu tulipwe.Naomba Mheshimiwa Waziri mtusaidi tulipwe.Mheshimiwa Spika, naipongeza REA kwakuendelea kutekeleza mradi wa umeme Mpera,Ntungulu na Mwakata Jimboni kwangu. Nashukuru piakwa kukubali maombi yetu ya kupeleka umeme Vijijivya Nyambula, Nyamigege, Busangi, Chela, Ngaya,Bulige na Ntobo. Naomba utekelezaji uanze wiki ijayo.Hata hivyo, naomba kuikumbusha Serikali kuhusu mradiwa umeme wa Bukombe ambao unanufaisha vijijivyangu vya Segese, Shilela, Nyikoboko, Lunguya naIkinda. Ahadi hii jamani imechelewa mno kutekelezwa,kwani ni ya mwaka 2008. Naomba nisikie na wananchi

wasikie mradi huu sasa, na kwa hakika kabisa, utaanzalini kutekelezwa?Mheshimiwa Spika, pamoja na Kahama kuwa namaeneo mengi ya madini, hakuna eneo hata mojalililotengwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Kilawanapogundua wanafukuzwa. Tunaomba wachimbajiwadogo walioko Masabi, Nyangalata, Nyamakwengena Mwazimba wasiendelee kuondolewa, waachiwemaeneo hayo. Tunaomba maeneo mwaka huu.Mheshimiwa Spika, kuna madai ya wananchi waKakola walioharibiwa mali zao mwaka 1996 wakati wakuanzisha mgodi wa Bulyanhulu. Bado wananchi haowapatao 200 wanadai. Wamehangaika Mahakamanihadi wameishiwa hata fedha za kuendesha kesi.Walishaomba tangu mwaka 2009 kwamba Serikali ioneuwezekano wa kumaliza suala hili kwa maelewano.Tunaomba sana ombi lao hilo lizingatiwe naikiwezekana tatizo hilo liishe mwaka huu.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,naomba kushukuru. Kama nilivyosema awali, naungamkono hoja ili Profesa Muhongo na timu yakewalimalize hili.MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja hii muhimu. Kwanza napendakumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa namna ambayokatika kipindi kifupi amefufua upya matumaini ya Taifaletu kujikomboa kutokana na mgawo wa makusudiuliokuwa ukikumbwa na kusimamiwa na watumishiwasio na huruma walioajiriwa katika Serikali na Shirika la

Usambazaji wa umeme nchini Tanzania (TANESCO). Nifaraja iliyoje kumpata kiongozi ambaye amewezakubaini uozo uliokuwa umegubika Sekta ya UmemeNchini? Tunamwombea heri Mheshimiwa Waziri naWasaidizi wake, changamoto zinazolikabili Taifa hili niza hali ya juu katika Sekta ya Umeme, licha ya kuwepokwa raslimali za kutosha zinazohusiana na uzalishaji waumeme, kwa mfano, maji, gesi, jua, upepo, joto ardhi,urani na makaa ya mawe.Mheshimiwa Spika, naishauri kwa moyo wa dhatiSerikali na Wizara yenye dhamana kwenye Sekta yaNishati na Madini, nchi sasa inakabiliwa nachangamoto ya mabadiliko ya tabianchi, kutokana nauharibifu wa mazingira, na ukataji miti kwa lengo lakuchoma mkaa unaouzwa Mjini kwa matumizimbalimbali ya nyumbani. Ni muhimu Wizara ije namkakati kabambe wa kuzalisha umeme kutokana namakaa ya mawe ambayo yanapatikana kwa wingiKusini mwa Tanzania huko Kiwira, Mchuchuma nakadhalika. Uzalishaji wa umeme utakapoongezeka, nivyema ukaenda sambamba na ujenzi wa njia zakusambaza umeme na kuupeleka vijijini.Umeme ukipatikana, uuzwe kwa bei nafuu ilikuepusha nchi yetu kugeuka jangwa. Aidha, kwa kuwanchi yetu imejaliwa kuwa na rasilimali ya gesi asiliakatika Mikoa ya Lindi na Mtwara, ni muhimu sasaSerikali ikaandaa mkakati kabambe wa kusambazagesi hiyo kwa kuanzia Majiji ya nchi hii ambayo ni Dares Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya na Arusha. Baadaya Majiji yetu kupatiwa huduma ya gesi, ifuate MajijiMakuu ya Mikoa na Wilaya.

Mheshimiwa Spika, mkakati huu utanusuru kwakiasi kikubwa misitu na miti inayochomwa kwa lengo lakupata mkaa unaotumiwa kwa kiwango kikubwa mjini.Chanzo kingine cha umeme ni kuanza mkakati wakujenga vinu vya kuzalisha umeme (nuclear readers),lengo ni kunusuru mazingira ya nchi yetu.Mheshimiwa Spika, naomba ahadi ya Serikali naWizara itoe msukumo wa kipekee katika kuyapatiaumeme maeneo yote ya Wilaya mpya ya Mbongwe ilikusukuma maendeleo kwa kasi zaidi.Mheshimiwa Spika, aidha, Wilaya ya Mbongweimejaaliwa kuwa na wingi wa madini ya dhahabukatika maeneo ya Ihenda, Nyakafuru, Lugunga,Bukandwe na Nyakasahuma, lakini tatizo lililopo nikwamba wachimbaji wadogo wadogohawajawezeshwa kupata nyenzo na miundo msingikatika kuwasaidia wachimbaji hawa kuongeza tijakatika shughuli zao. Naiomba Serikali iongeze jitihadaza kuyaainisha maeneo yanayofaa kwa shughuli zaoza uchimbaji ikiwemo kuwapatia lesenizitakazowawezesha kuyamiliki kihalali maeneowanayofanyia kazi. Hii ni kwa mujibu wa taratibu zakisheria.Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, napendakuchukua fursa hii kuipongeza Serikali kupitia Wizara yaNishati na Madini kwa uamuzi wake wa kuipatia Wilayayetu ya Mbongwe huduma ya umeme kupitia mradiwa electricity V na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Mheshimiwa Spika, naomba mchakatouharakishwe. Naunga mkono hoja.MHE. HUSSEIN MUSSA MZEE: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja kwa asilimia mia kwa mia. Sababuza kuunga mkono hoja ni kutokana na Serikali kulikabilitatizo la umeme angalau kwa mwaka huu hatujawana mgao mkali.Mheshimiwa Spika, napongeza Wizara ya Nishatina Madini, Waziri, Manaibu Mawaziri na Katibu Mkuu,kwa kazi kubwa wanayoifanya katika Wizara ya Nishatina Madini ya kuinusuru Wizara hiyo.Mheshimiwa Spika, katika mchango wangu,nitatoa masikitiko kwa umeme wa Zanzibar(miundombinu siyo mizuri) sijui ni nani, lakini naombaiangaliwe.Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi za Serikali zaujenzi wa bomba la gesi, lakini gharama za mafuta nikubwa sana. Naipongeza Serikali kwa kuokoa Shilingibilioni sita kwa mwezi, na naomba waangalie maeneomengine kuona jinsi ya kunusuru hali kama hiyo.Mheshimiwa Spika, Wizara imeokoa fedha nyingisana, wamefanya uzalendo mkubwa sana natunawaunga mkono asilimia mia kwa mia.MHE. BETTY E. MACHANGU: Mheshimiwa Spika,napenda kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini -Mheshimiwa Profesa Muhongo na Katibu Mkuu wake

Ndugu E. Maswi kwa kuteuliwa kushika nyadhifa hizi zaUwaziri na Ukatibu wa Wizara ya Nishati na Madini.Mheshimiwa Spika, Shirika la TANESCO, limekuwalenyewe, hakuna mshindani, na hivyo utendaji wakesiyo wa kufurahisha. Yapo mambo mengi yanafanywana Watendaji ya kuwahujumu Watanzania.Watanzania nao pia wanahujumu Shirika.Mheshimiwa Spika, kwa muda mchache, viongozihawa wameonyesha mafanikio, wameonyeshakufunga mirija ya wizi na matumizi mabaya na ufisadiwa Watendaji wa TANESCO. Ninashauri waendelee nawachukue hatua kwa wafujaji wa fedha ya umma.Kununua mafuta Purma, kuli-save Shilingi bilioni tatuambazo miaka mingine zilikuwa zinawekwa mifukoni.Wahusika wachukuliwe hatua za kisheria walipe fedhawanazofuja.Mheshimiwa Spika, kwa sababu imeonyeshaTANESCO kumbe inaweza kulipa madeni kwakukusanya zaidi ya bilioni 50 kwa mwezi naishauriSerikali iangalie uwezekano wa kuwapa Watanzaniaumeme wa uhakikia na endelevu kukatika kwa umememara kwa mara kumetesa watanzania kiuchumi nakijamii. Biashara nyingi zimedorora na maeneomengine ujambazi kutokea kwa sababu ya giza.Nashauri bei ya umeme pia iangaliwe ipungue kidogo.Mheshimiwa Spika, yako maeneo mengi nchiniambayo yana maporomoko madogo ambayo vijiji auprivate sector wanaweza kuzalisha umeme waMegawatt chache za kutosha Kijiji, Zahanati, Shule nakadhalika zilizopo, na umeme unaozidi wakawauzia

Serikali. Naishauri Serikali ifanye utafiti wa maeneokama haya ili umeme utakaopatikana utumike u-savemzigo mkubwa wa umeme wa grid, badala yake,umeme wa grid uelekezwe zaidi katika Miji mikubwa.Mheshimiwa Spika, viwanda vya sukari vinawezapia kupata umeme kutokana na residue zinayotokanana miwa. Kiwanda cha TPC Moshi kinatengenezaumeme wa Megawati 15. Wanatumia Megawati 10,Megawati mbili wanawapa Kijiji na Megawati tatuwanauzia TANESCO. Naishauri Serikali, viwanda vyotevyenye residue za aina hiyo waelekezwe watengenezeumeme kuipunguzia mzigo Serikali.Mheshimiwa Spika, Bwawa la Nyumba ya Mungulinalosaidia Kituo cha Umeme cha Hale Tanga, sasa hivihali yake imezidi kuwa mbaya. Kwa sababu Serikaliinahitaji kuzalisha umeme, nashauri Serikali ichukuehatua za ziada kuliweka sawa ili umeme wa kutoshauendelee kupatikana.Mheshimiwa Spika, wachimbaji wakubwa wadhahabu na madini mengine, kuna wakati wanatafitimaeneo na wanaona kuwa eneo hilo halina madini yakutosha kufungua mgodi. Nashauri maeneo kamahaya Serikali itoe leseni za Makampuni hayo naiwagawie wachimbaji wadogo kwa mpangiliomaalum.Mheshimiwa Spika, Kenya inajulikana kamaexporter mkubwa wa Tanzanite katika nchi za AfrikaMashariki, lakini mchimbaji na mwenye Tanzanite niTanzania. Nashauri Serikali, Tanzanite inayochimbwa

ikatwe hapa hapa Tanzania na kuwepo Umoja waWachimbaji ambao watathibiti uuzaji holela wa madinihayo.Mheshimiwa Spika, yapo maeneo hatarishiambayo Serikali inatoa prospective licence na wakatimwingine liseni za uchimbaji, mfano ni Msitu waShengena Wilayani Same. Eneo hilo ni hifadhi ya Taifana ni eneo ambalo ni hatarishi kwa maporomoko yaardhi (land slides). Maporomoko kama hayo mwaka2009 yaliua watu 24, wachimbaji, wanabeba udongona malori kupeleka Kenya ati una bauxite. Wakatiwanachimba mlimani, chini ya mlima kuna kaya zaidiya 3000. Je, Serikali haioni kuwa kuna haja kufanyautafiti wa maeneo kabla ya kutoa leseni za wachimbajihawa katika misitu ya Shengena?Mheshimiwa Spika, nashauri Serikali kwenyekuzalisha umeme ishirikishe pia wahandisi wazawa waumeme. Experience yao pia inaweza kusaidia hasakatika vyanzo vipya vya kuzalisha umeme.Wakishirikishwa, inawezekana pia wakasaidia kutoataarifa zozote za hujuma zinazopangwa na Watendajiwa TANESCO. Tunaishukuru Serikali kufanya utafiti nakugundua gesi huko Mtwara. Tunaishukuru kufungaMkataba na Kampuni ya China kujenga bomba lakusafirisha gesi mpaka Dar es Salaam na Tanga.Naishauri Serikali kwamba bomba hili lijengwempaka Arusha kwa sababu mapato mengi ya pato laTaifa yanatokana na utalii ambao unatoka Arusha naKilimanjaro. Kama wakazi wale wakipata gesiwataacha kukata miti, mazingira yataboreka na utaliii

utashamiri na pato la Taifa. Pili, nashauri Serikaliisimamie ujenzi wa bomba hili na bomba limilikiwe naSerikali na isiruhusiwe kampuni binafsi kumiliki labdakwa Mkataba unaofaa na siyo wa kinyonyaji.Mheshimiwa Spika, nashauri gesi iingizwe Dar esSalaam, iwe na bei nafuu ili kupunguza matumizi yamkaa (mazingira).Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Spika,Wilaya ya Kwimba ina vijiji vingi havina Nishati yaumeme na hata kama nishati hiyo wangepelekewa,kwa sababu nyumba zao ni za tembe na zimeezekwakwa nyasi.Mheshimiwa Spika, naomba Serikali ianzishe mradiwa kuhamasisha wananchi hao kuboresha nyumbazao kwa kushirikiana jambo ambalo limefanikiwaRwanda, kwa kuzingatia hali halisi ya vijiji.Napendekeza Wizara katika kitengo chake chahuduma za jamii, watoe mashine za kufyatulia matofalina mabati ili kuwawezesha wananchi kuwa nanyumba ambazo zitafaa kuweka nishati ya umeme nahata ile ya Solar.Mheshimiwa Spika, naomba Serikali itoe maelezojinsi gani bajeti hii ya Wizara inazingatia kuboreshamaendeleo ya wanawake kuanzia Wizarani na jamiikwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, maendeleo ya nchi yoyote sikuhizi yanapimwa kwa kuangalia jinsi ganiwanamwezesha mwanamke. Hili linazingatiwa sana nawenzetu wa nchi zilizoendelea kama Marekani. Bajetiza Wizara zote huzingatia matumizi kwa uwiano wakijinsia.Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziriatueleze jinsi Wizara yake inavyotekeleza majukumuyake kwa kutambua nafasi ya mwanamke katika jamii.MHE. HENRY D. SHEKIFU: Mheshimiwa Spika,naipongeza Wizara kwa jitihada zake za kupunguzamgao wa umeme.Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais wakati wakampeni mwaka 2001 aliahidi kuwasaidia wananchiwa Tarafa ya Mlola kupelekewa umeme.Mheshimiwa Spika, naishukuru REA na Wizara kwaujumla kuonyesha dalili na nia thabiti ya kupelekaumeme Tarafa ya Mlola kwa kutuma wataalamkwenda kupima (survey) ya kupeleka umeme vijiji vyaKata za Kwekanga, Malimbwi Kilole Ngwelo na Mlola.Katika Tarafa ya Mlola. Baada ya mashauriano nauongozi wa REA, tulikubaliana umeme sasa utokeekwenye msongo wa KV 33 kuanzia eneo la Malindikupitia eneo la Vijiji vya Mziragembei, Mghangaikuelekea Malimbwi na Tawi litoke hapa Mshangaikuelekea Kwakanga, Karenda, Kilole hadi Mbwei naMhezi ipatiwe tawi dogo na kutoka Mbwei umemeupelekwe Kijiji cha Ungo hadi Mlola.

Mheshimiwa Spika, naomba umeme kwenda Kataya Ngwelo upitie kijiji cha Makole kutokea Kwekanga.Kwa kufuata Mpango huo, vijiji vyote vya Kata nilizotajazitapata umeme wa uhakika wa msongo wa KV 33badala ya mpango wa awali kwamba umemeutakaopelekwa Tarafa ya Mlola hususan Kwekangaungetumia njia ya msongo wa KV 11 kutoka eneo laKwemakame.Mheshimiwa Spika, baada ya kupata umeme Kataya Kwekanga, Ngwelo, Malimbwi, Kilole na Mlola,naomba Serikali iangalie uwezekano wa kupelekaumeme Kata ya Makanya ambayo kipekee ndiyohaitaguswa na mpango wa sasa wa kupeleka umemeTarafa ya Mlola.Mheshimiwa Spika, kuchelewa kuunganishiwaumeme wananchi wa Kijiji cha Gare eneo la Kizaraambao waliomba umeme na kulipia mwaka 2002, hadileo hii mwaka 2012 hawajapata umeme. Nimewasilishaviambatanisho kwa Waziri wa Nishati na Madini -Mheshimiwa Profesa Muhongo. Naomba wananchihao wapate haki yao ya kupatiwa umeme.MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Spika,kumekuwepo na tatizo la muda mrefu la umeme kwaukosefu wa maji hasa kwenye bwawa la Mtera,kwamba maji yanapungua. Nilikuwa naulizia, MtoPangani ni lini uliwahi kupungua maji? Kwanini Serikaliisielekeze nguvu kubwa kwenye Mto Pangani ambaohuwa haukauki maji?

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Korogwe vijjini,kuna maeneo mawili ya nguvu ya umeme, lakini chakushangaza, kwenye Jimbo hilo ambalo vyanzo niviwili, vijiji havina umeme kabisa.Mheshimiwa Spika, Kampuni ya REA inasambazumeme vijijini. Je, ni kwanini hawajawahi kusambazaumeme hata kwenda kupima Korogwe Vijijini, badalayake inahusika Mjini tu?Mheshimiwa Spika, kuna vijiji ambavyo vimepitiwana umeme lakini vijiji havina umeme. Kwa mfano, Kataya Mnyuzi na Kijiji cha Kwamzindawa, Mkwakwani,Gereza la Lusanga Kata ya Kwagunda, Mngaza, Kataya Kerenge Kubaoni, Lusanga, Kwemazandu,Matalawanda Kata ya Magoma Mbuyuni Kikwajuni,Sekioga Kata ya Dindira, Kwefingo, Mgwashi Kata yaVugiri Bagamoyo, Makweli, Mlalo Kata ya Mkalamo,Masimbau. Naomba Serikali iangalie kwa undanisehemu hizi ukizingatia nguvu ya umeme inatokahapa.Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wadogowapewa maeneo maalum na hati ili wapate mikopoKalalani na Kigwasi kule kwenye Jimbo la Korogwevijijini.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwaasilimia mia moja.MHE. JUMA S. NKAMIA: Mheshimiwa Spika, kwanzanaunga mkono hoja ya Wizara hii ya Nishati na Madinikwa asilimia mia.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuunga mkono hoja,naomba sasa kuchangia kwenye maeneo yafuatayo:-Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imetengafedha za kupeleka umeme kwenye Wilaya Mpya yaChema katika mwaka huu wa fedha, naomba umemehuo utokee katika Kijiji cha Mondo ambapo kunaumeme wa grid ya Taifa ili upite katika vijiji vya Waida,Sori, Pongai, Cheku, Kelema na Paranga ambayo lichaya kuwa na idadi kubwa ya watu, pia ni kilomitachache kutoka Chema kuliko kuchukua umeme kutokaKondoa Mjini ambako ni mbali zaidi ya mara tatu nahakuna kijiji chochote kilichopo kati ya Kondoa naChemba kwa kufuata barabara kuu.Mheshimiwa Spika, umeme umefika katika Kijiji chaDalai ila kilometa nne tu kabla ya kufika katika Kijiji chaTandala ambacho kina watu zaidi ya 15,000 ambaowanahitaji umeme huo kwa udi na uvumba. NaiombaSerikali kupitia TANESCO kufikisha umeme katika kijiji hikiambacho hakihitaji hata nguzo zaidi ya 20.Mheshimiwa Spika, vijijini vya Mapanga naChuruku vina umeme ambavyo vipo kilomita chachekutoka Vijiji vya Kerikima Jangalo Itotwa na Mlongiaambavyo vina idadi kubwa ya wakazi wasiopungua40,000 ambao wanahitaji umeme.Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhimakubwa, naiomba Serikali kupeleka umeme katika vijijihivi ili wananchi wapate umeme na Serikali iongezemapato yake.

Mheshimiwa Spika, kwa mara nyingine tena,nampongeza Mheshimiwa Waziri Prof. Muhongo, NaibuMawaziri Boniface Simbachawene na Naibu WaziriMheshimiwa Stephen Masele kwa kuteuliwa kwao, nanaamini watakuwa kichocheo cha kuboresha nishatiya umeme na madini.Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha, naungamkono hoja.MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Spika,Kampuni ya Madini ya North Mara Gold Mine (BarrickMinning Company) kudhulumu Wilaya ya Serengeti.Kwa vile kuna beacons za eneo la umiliki la Madini laKampuni hii ya Barrick, lipo katika Wilaya ya SerengetiKata ya Kisaka Vijiji vya Borenga na Nyiboko, kwa ninihakuna mgao katika Wilaya ya Serengeti na piamchango wao katika vijiji hivyo?Mheshimiwa Spika, kwa vile kuna vyanzo vingi nambadala wa umeme kama gesi na maporomokokama Majimoto, Rorya (Panyakoo) na Tarime(Nyakunguru) kwa reserve kubwa sana ya gesi piakatika Mto Mara eneo la Balagonja kwa maporomokoya maji makubwa ni kwa nini usianzishwe mradimkubwa wa kufua umeme ili kupunguza kero yaupungufu wa umeme (17%) ili kufikia 2015, tufikie 30%.Mheshimiwa Spika, kwa vile bahati nzuri umemehuu wa grid umefika Tarime (Nyamongo) ni kwa ninibidii ya makusudi haifanyiki ili kusambaza umeme huokwenda Wilaya ya Serengeti?

Mheshimiwa Spika, ni kwa nini umeme wakuaminika hauletwi toka Uganda (Jinga) ili kuendeleakuongeza vyanzo vya kupata umeme na pia kupanuauhusiano wa Afrika Mashariki?Mheshimiwa Spika, je, Wizara ina mpango gani wakupunguza gharama ya umeme ili kutoa fursa yakupunguza uharibifu wa mazingira, kwa sababuumeme kuwa ghali inachangia sana kuharibu misitu namazingira?Mheshimiwa Spika, mrahaba ni kidogo sana (4%)Serikali itazame upya ili kupandisha pato kutokana namadini kutoka 14%.Mheshimiwa Spika, nashauri sheria ya madiniipitiwe kwa vile bado kuna kero nyingi.Mheshimiwa Spika, madini ya uranihayajafahamika vizuri kwa wananchi kwa vilewananchi wengi hawajui kwa kina juu ya hatari naathari za madini haya. Je, Serikali ina mpango gani ilikuelimisha wananchi na kuwalinda?Mheshimiwa Spika, kuongeza nguvu (voltageincrease) na kuweka transformer maeneo yaliyopewaumeme mwaka 2004; sehemu nyingine ni single phase:Je, REA (Wizara) ina mpango gani kuweka umeme wathree phase na kuweka transformers?MHE.MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika,kwanza, nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Nishati

kwa kazi kubwa anayoifanya ya kupambana naubadhirifu na ufujaji wa mali ya umma hasa katikaShirika la TANESCO. Namwomba Mheshimiwa Waziripamoja na Manaibu zake waongeze jitihada zakupambana na wale ambao hawaitakii mema nchi hii.Mheshimiwa Spika, suala la umeme vijijini, nimuhimu sana Wizara ikaweka kipaumbele kikubwakupeleka umeme vijijini, kwani tukitaka maendeleo yaharaka katika nchi hii, lazima umeme vijijini uwafikiewananchi walio wengi katika nchi ambao wengi waowanaishi huko. Tukiimarisha kupeleka umeme huko,wananchi wengi watakuwa na fursa ya kuwezakusindika mazao wanayoyazalisha katika maeneo yaowanaoishi.Mheshimiwa Spika, umeme wa grid ya Taifa katikaMikoa ya Pembezoni, Mikoa ya Rukwa, Katavi naKigoma haina umeme wa grid ya Taifa. TunaiombaSerikali kupitia Wizara, ilete umeme wa grid ya Taifa iliuweze kuinua uchumi katika Mikoa hiyo, kwani umemewa uhakika ukiwepo tutakuwa na uhakika wa kupatawawekezaji ambao watawekeza katika Nyanja yaKilimo, Madini, Uvuvi na kadhalika. Maeneo yetu yanavivutio, tatizo kubwa ni kukosekana kwa umeme wauhakika.Mheshimiwa Spika, mradi wa makaa ya mawe nimuhimu sana ukaimarishwa kwa kuweka mikakati yakusimamia mradi huu ufanye kazi ili uweze kutoaMegawati za kutosha kwa ajili ya kupeleka umemekatika maeneo ya nchi hii na kupata ziada ya kuuzanje ya nchi na kulipatia pato la Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, naiomba Wizara inihakikishieuwezekano wa kupata umeme katika maeneo ya ZiwaTanganyika maeneo ya Karema na Ikola. Eneo hili nimuhimu sana ukizingatia shughuli za eneo hili ni uvuviambao kama wakipata umeme upo uwezekanomkubwa wa kukuza uchumi katika eneo hili natulishapata wawekezaji katika sector ya uvuvi ambaowanataka kufanya shughuli za uvuvi na kujengaviwanda vya kuchakata samaki katika eneo hilo. Tatizokubwa ni ukosefu wa umeme.Mheshimiwa Spika, naiomba Wizara iweze kutoaumeme katika Kata Kata ya Kabungu na Mpandandogo kwani ziko karibu sana na maeneo ya Mjiniambako umeme upo, kwani tukisogeza umeme katikakata hizo, kuna uwezekano mkubwa wa kusaidia Shuleza Sekondari zilizopo katika Kata hizo na kuwasaidiajamii zifanye shughuli za kiuchumi vizuri.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Spika,naomba nichukue fursa hii kuchangia bajeti ya Wizaraya Nishati na Madini kwa njia ya maandishi. Awali yayote, naunga mkono bajeti hii ipite na kama kunamabadiliko, basi yawe yale ya kuongeza fedha na siyokupunguza.Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza, katika Wizarahii ni hoja ya kujipanga upya. Wizara na asasi zotezilizoko chini yake yawabidi kutambua kuwa kwa kiasikikubwa Maendeleo na Ustawi wa Taifa hili

unategemea uendeshaji na udhibiti wa sekta hii. Kwalugha ambayo labda haitapendeza kwa masikio yawatu wengine, tuko katika hali duni na kasi yamaendeleo hairidhishi Watanzania kwa sababu yakushindwa ku-manage sekta hii ya Nishati na Madini.Naunga mkono bajeti hii kwa matumaini kuwa masikioya Serikali kupitia Wizara hii yatasikia na kuwezakutekeleza yale yanayoshauriwa na yanayowastahiliwananchi wa Taifa hili. Nina imani na Viongozi naWatendaji wa Wizara hii mpaka hapo sasa tuanze.Mheshimiwa Spika, nafasi ya umeme katikakuchangamsha uchumi wa Taifa na mchango wa REA,utendaji wa REA katika uhai wake wa miaka mitanounaonekana na kuvuma nchi nzima. Miradi 119imejengwa yenye gharama ya Shilingi bilioni 257.67,84ikiwa imekamilika na miradi 35 ikiwa inaendelea hojayangu ni kuwa, kama Shilingi bilioni 260 zimelifanyaTaifa lizizime na kuona matumaini katika REA, basi kwamwaka mmoja wa bajeti kiasi kikubwa kitengwe ilihatua iliyotuchukua miaka mitano tuivuke kwa miezisita tu. Hiyo ndiyo busara ya mwana mikakati CharlesHandy. Mwanachura huwa asubiri dimbwi lipate jotojua likitoka, bali huchupa toka dimbwi moja kwendadimbwi lingine mpaka afikie dimbwi lenye jotoanalotaka. Watanzania vijiji tunawaombea umeme,siyo vibatari, na ndiyo maana tukaongeza kodi mafutaya taa. Tengeni Shilingi bilioni 600 tuingie kwenyedimbwi lenye maji yenye joto tulitakalo umeme vijijivyote. Inawezekana.

Mheshimiwa Spika, uongozi wa Wizara unapashwakuelekeza macho kwa mtoto huyu mzuri anayeanzakutambaa. Wapeni Mamlaka majukumu na njia zauwajibikaji Watendaji wa asasi hii. Kueni karibu na REA,fuatilia utendaji wao na pimeni malengo yao kwavipindi vifupi. Moja, hii itasaidia kuwapa msukumo wandani katika kutekeleza malengo; pili, itawaepusha nawatu wenye nia mbaya ambao bila kutafuna manenowatakuwa wananyemelea fedha nyingi zinazotengwana Serikali ili wazitafune. Tatu, ukaribu utatuwezeshakujua mapema kama train yetu imetokea kwenye relina hivyo kurudi kabla hata wasafiri wenginehawajajua. REA na value for money!Mheshimiwa Spika, Shirika la Umeme TANESCO nimuhimu, mbali ya kuzalisha na kusambaza umeme, hikini Chuo. Watanzania wanaoingia katika Taasisi hiiwana fursa sawa ya kujiendeleza na kupanda ngazibila kujali nasaba zao. Hoja yangu hapa ni kuwaTANESCO iimarishwe kwa mfumo ilionao kwa kutumiaSBUs katika kuleta ufanisi, lakini isimegwe vipande. Niukweli uliowazi ikimegwa vipande, walio wengiwatakimbilia generator, lakini zaidi Watendaji wazawawatabaki katika madaraja ya chini bila kujali wanaujuzi na utendaji uliotukuka kiasi gani.Mheshimiwa Spika, TANESCO ina tatizo laukusanyaji wa madeni yake. Moja, iwapo sheriazinazoendesha asasi hii zina upungufu, basi ziletweBungeni tuwape meno makali. Pili, kwa mtazamowangu watendaji wake wenye elimu na ujuzi wa ufundiwanapashwa kupigwa msasa wa sheria na biashara.Hoja yangu hapa ni kuwa mkusanya madeni awe na

elimu ya ufund,i uzoefu wa ufundi, na msasa wabiashara. Epukeni kuajiri watu wasioweza kutofautishavolt na watt kuja kufanya kazi ya biashara nakukusanya madeni. TANESCO ni asasi ya kiufundi, hivyoIdara zote zizungumze lugha ya ufundi. Tatu, ni kutumiamtindo wa total marketing katika kukusanya madeni.Mheshimiwa Spika, mtindo huu umetumika sanakatika nchi za Mashariki ya mbali ambazo Watanzaniatunapenda kuzisifia na kuzitolea mfano. Chini yamfumo huu, kila mfanyakazi ni mlinzi na mkusanyaji watozo za Shirika. Mfano, kwa Jiji la Dar es Salaam, Shirikalinapaswa kuhakikisha kila Mtaa au la, basi Mitaaminne mpaka mitano anaishi mfanyakazi katika mtaaau Kata. Kazi ya mtu huyu ni kusikiliza, kuchunguza nakutoa taarifa kwa jambo lolote lenye manufaa kwaShirika. Inapobidi, chini ya utaratibu maalum,wafanyakazi hawa wanaweza kupewa jukumu lakukagua malipo ya Ankara. Ni kheri katika Shilingi bilioni200 zilizoko mikononi mwa wateja zikalipwa mara mojana motisha wa asilimia tano kwa Watendajiwanaosimamia na kufuatilia.Mheshimiwa Spika, TANESCO inaendana namitambo ya kukodi. Tunapojenga bomba la gasi asili nivema basi tuelekezwe ni vipi tutaanza kuondoamitambo ya kukodi na kununua ya kwetu. Hoja hapa niratiba ya kuondoa kuwekea order na kuleta ya kwetutukizingatia kuwa utengenezaji wa mitambo uchukuemiaka miwili mpaka mitatu. Visingizio zaidi siku zambeleni visitumike kuwatupia watanzania mitambochakavu ambayo wenye nayo wamekuwa wakitutoza

capacity change kwa viwango vya juu sana.Tujipange kwa ajili ya kesho.Mheshimiwa Spika, mwisho, katika Sekta yaUmeme nizungumzie umeme utokanao na vyanzo vyamaji. Wakati umefika sasa Serikali kwa kutumia Wizara,Idara na Vitengo vyake vyote vinavyohusika na Mitona Maji kuhusika kwa nguvu zote katika kutunza hazinahii. Vyanzo vya maji, mito, misitu, hifadhi ya maji namabwawa, lazima yaangaliwe kitaalam na yalindwe.Mabwawa yaliyojengwa kwa gharama kubwa ni vematuyatunze ili yazalishe umeme kwa ufanisi, matumizi yamaeneo oevu na mito bila kuangalia matumizi namanufaa mapana ya maji, lazima yakemewe naSerikali kwa nguvu sana.Mheshimiwa Spika, nizungumzie sekta ya mafutajamii ya petrol au downstream activities. Mafuta nijukumu la Wizara ya Nishati. Nakiri kuwa, nimemwelezaMheshimiwa Waziri kwa mifano na amekubali kuwaupungufu katika sheria unaifanya sekta hii, ujumbena/au ikae bila uangalizi makini. Hii ni sekta nyetiinayohitaji uangalizi wa karibu wa Serikali. Siyo sahihikuamini kuwa sekta binafsi katika ushindani wa sasa,sheria na siasa zisizotabirika itaweza kuendeleza sektakwa kushamirisha shughuli pande zote za nchi.Mheshimiwa Spika, narejea msimamo wangu wakutaka kuwepo kampuni ya kitaifa (National OilCompany), iliyojengeka na kukua taratibu kuanzia chini(organic growth) akihusisha mizizi na matawi yawananchi. Hapa namaanisha Serikali za Mitaa,Halmashauri za Wilaya, Asasi za Serikali, Mashirika ya

Umma na Makampuni binafsi ambayo mikakati yao yautendaji ni kujinasibisha na Serikali. Sikubaliani namipango na mikakati ya kampuni COPEC. Hiki siyotunachohitaji, tunataka kujenga mtandao toka chini.Kampuni ya Taifa inayoendesha kwa namna fulanikituo kinachomilikiwa sehemu na Halmashauri ya Kilwaau Chama cha Ushirika cha KCU na Bukoba. Katika halituliyonayo, sioni kampuni binafsi inayokopa kwa riba yasoko na masharti ya kurudisha mkopo baada ya miakamitano ikajenge Kituo cha Mafuta Kisiwani Goziba aunyumbani Rutoto.Mheshimiwa Spika, lakini jambo lingine, kutokuwana kampuni ya kitaifa katika dunia hii iliyojaa mitikisikoya kiuchumi, ni hatari kwa uchumi na usalama wa nchi.Katika hali ya mtikisiko, busara kwa kampeni binafsi nikukimbia soko. Anayetaka mifano kwa hili, ana lakejambo.Mheshimiwa Spika, nizungumzie mfumo waununuzi wa mafuta kwa wingi, Bulle ProcurementSystem. Mfumo huu ukianzishwa kwa azimio la Bungeletu Tukufu na unaendeshwa na regulationszilizopitishwa na Waziri mwenye dhamana. Niliungamkono azimio na kupinga regulations na mpaka sasabado nazipinga. Muhimu hapa ni kuwa, yote yaleniliyoyapinga yameanza kutokea labda jambo mojaau mawili. Mafuta yana vitu vitatu muhimu; quality,availability na affordabilitiy. Hatukuwa na tatizo laupatikanaji wa mafuta kabla ya mfumo huu na sasahali ni ile ile ukiacha kidogo mafuta ya taa.

Mheshimiwa Spika, tatizo la bei liko pale pale namfumo haujaleta nafuu. Hii ni kutokana na kutokuwepomiundombinu sahihi, lakini pia kanuni za uendeshajikuwa na mapungufu upande wa uhakika wa kiasikilichoanzishwa kuna maboresho hasa kwa walewazembe wa kufanya kazi wanaopendelea kila kituwaletewe Mezani. Tumeshuhudia tofauti katika kiasikwa kulinganisha takwimu, bandari ya kupakia,kushusha na matankini. Umeibuka ugonjwa waupotevu wa mafuta katika mtandao wa mabombaKurasini, tatizo ambalo nilikuwa mmoja wa waganguziwake waliolidhibiti kwa mafanikio makubwa. Napendaniwapongeze watendaji waliokuja kunitaka ushaurijapo kwa uficho.Mheshimiwa Spika, tatizo kubwa ni ubora wamafuta yanayoingizwa nchini. Taarifa ya Mkemia Mkuuna EWURA zimethibitisha kuwa petrol iliyoingizwa nchinikati ya Januari na Machi ilikuwa na ethanol kupita kiasikaribu asilimia 10 zaidi. Vyombo vyetu vimeonyeshaupungufu TBS na EWURA mpaka baada ya kiliokikubwa. Lakini baya zaidi, regulations za Wazirimwenye dhamana zimekuwa kimya. Taifa naWatanzania wamepata hasara ambayo siyo Wizara auEWURA anayekuwa tayari kusema ni kiasi gani.Naishauri Serikali ilazimishe mamlaka husika kutamkakiasi cha hasara na walaji waombwe msamahatujipange upya.Mheshimiwa Spika, mbali na mapungufu katikaregulations, ni mtindo wa utendaji Serikalini ambapoIdara, Mamlaka na Mashirika kila kimoja kinajipangakama himaya inayojitosheleza na isiyohitaji ushirika toka

nje. Vyombo vinavyotawala au kuendesha Sekta niTPA, TBS, EWURA, PIC na Wizara yenyewe. Hawa wotekila asasi inasimama kama kiumbe kisicho na uhai,mfano, jiwe au chuma. Mfano, wa ethanol unatoshakuelezea mapungufu ninayoyasema, lakini kurejea kwamlundikano wa meli nje ni mfano mwingine. Iweje gatila Kurasini lipangiwe kupokea meli tisa kwa mwezi ili halimeli moja inatumia siku tatu mpaka nne kushushamzigo. Wakati huo huo kuna meli ya mafuta mazito(HFO), mafuta ya kula (VD) na wakati mwingine LPG.Mheshimiwa Spika, hoja yangu hapa ni kuwa,asasi ziongozwe na utumishi kwa umma yaani kuwapaWatanzania kile wanachotaka. Wasiongozwe na sheriazilizounda mamlaka hizo, bali sheria hizo wazitumiekutekeleza majukumu. Nashauri Sekta ya Mafuta ibakina idhibitiwe na Wizara ya Nishati na asasi nyinginewawe wawezeshaji.Mheshimiwa Spika, nimepitia nyaraka zamawasiliano za PIC, kuna hatari inalikabili Taifa, kunakauli zisizo rafiki, kauli za kutishiana na kusababishianahasara za mamilioni ya Dola za Kimarekani, kauli zakupelekana Mahakamani. Hoja yangu hapa ni: Je,iwapo PIC atapelekwa Mahakamani na kuamriwaalipe mfano Dola milioni 20. Fedha hizi atazitoa wapiau zilipwe kupitia kanuni ya bei ya mafuta? IwejeMuungano wa Makampuni binafsi utendaji waouwabebeshe mzigo Watanzania mbumbumbu? Unamapungufu katika hili (regulations) na katika Tanzaniayenye mmomonyoko wa maadili na Ulimwengu wawasaka faida, sintoshangaa kusikia PIC inashitakiwa,inashindwa kesi na walaji wanabebeshwa mzigo.

Dhamira ya Serikali ni nzuri, uamuzi wa Bunge ni sahihi,ila utekelezaji ulipuuza ushauri wa Kamati ya Nishati,Wabunge, na wale waliosema kwa nia njema.Mheshimiwa Spika, nichangie sekta ya gesi ya asili.Awali ya yote tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatuatuliyofikia. Gesi nyingi imevumbuliwa, imekubalikabomba la Mtwara lijengwe, lijengwe na makandarasiwengi kuhakikisha shughuli (kupunguza muda waujenzi) lakini zaidi limilikiwe na Serikali. Natoa pongezikwa hilo, kwani ilikuwa vita kali, mapambano yaupinzani wa waziwazi. Nayasema haya kuwakumbushaWaheshimiwa Wabunge, Serikali na wananchi kwaujumla kwamba ulikuwepo upinzani wa hatari, hivyotumeshinda pambano. Kwa kutambua hili,kutawafanya wale waliopewa dhamana watekelezemajukumu yao wakijua kuwa kunaweza kuwepo nguvupinzani zinazoweza kufurahia kukwamua kwa mradihuu muhimu.Mheshimiwa Spika, nizungumzie haja yamaandalizi ya kudhibiti matumaini ya Watanzania juuya neema hii. Pia nidokezee juu ya haja ya kutumiamapato ya gesi asilia kushamirisha shughuli zawananchi bila kuwaacha wakiwa tegemezi wa kupatakila kitu bure. Ni kutokana na maeneo haya Kamati yaNishati ikapendekeza kuundwa kwa ERA (EnergyRegulatory Authority), tuwe na timu ya watu sasawatakaoshinda na kulala wakiwaza juu ya nishati,neema ya gesi waioanishe na nishati zote, wabainisheneema na athari za nishati na vyanzo vyake nawajiandae leo kuidhibiti Sekta ya Nishati miaka 100ijayo. Hoja hapa ni kuwa, nachelea shughuli za

kushitukiza au dharura ambao sasa unataka kuwautamaduni wetu.Mheshimiwa Spika, nihitimishe mchango wangumdogo kwa kuzungumzia Sekta ya Madini. NaishauriSerikali ifuatilie kwa karibu na kutoa taarifa juu yamachimbo ya Kyerwa na Karagwe. Machimbo ya Tin-Kyerwa yalitekelezwa kwa misingi ya kiuchumi wakatihuo. Sasa ziko habari kuwa watu toka nchi jiraniwanasomba kifusi toka Kyerwa na kupeleka kwao. Ipotaarifa kuwa moja ya nchi jirani inao mtambo wakusafisha madini hayo na sehemu kubwa ya malighafiinatoka kwetu.Mheshimiwa Spika, hoja yangu ni kuwa Serikaliibebe jukumu la kubainisha manufaa ya rasilimali hii nakama kuna manufaa, tujenge kiwanda cha kusafishakatika Wilaya mpya ya Kyerwa.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. SAID A. ARFI: Mheshimiwa Spika, nimefarijikana hotuba ya Mheshimiwa Waziri ukurasa 82 kuhusuufuaji na usambazaji wa umeme Mpanda.Unafadhiliwa na Uholanzi kiasi cha Megawati 2.5.Napenda kushauri, ni wakati muafaka sasa wakati huuwa maandalizi ya mradi huu ukaenda sambamba nakufikisha umeme huo Kakese Mbugani na maeneo yajirani na ili idadi inayokusudiwa ifikiwe, ni lazima kujenganjia za kusafirisha umeme katika maeneo yote naviungo vya Mji wa Mpanda, kuanzia Ilembo, Kasimba,Nsemlwa, Kawajense, Shanwe na Misunkumilo.

Mheshimiwa Spika, nina matumaini makubwamapendekezo haya yatazingatiwa.MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika,napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwako na kwaMawaziri wenye dhamana juu ya Wizara hii. Awali yayote, napenda kumshukuru sana Mungu kwa kunipauhai na kuniwezesha kupata fursa ya kutoa mchangowangu mdogo sana katika Wizara hii hasa upande waNishati.Mheshimiwa Spika, napenda sana kuitumia kaulihii; “kama unashindwa kuvumbua usishindwe kuiga.”Mheshimiwa Spika, wote tunajua nyumba ni malina dhamana isiyohamishika na nyumba ndiyoinayofungiwa umeme.Mheshimiwa Spika, wenzetu Kenya walikuwawanao mpango mzuri sana wa kuwakopeshawananchi wake huduma ya ufungaji wa umemeuliokuwa ukijulikana kwa jina la Stima loan.Mheshimiwa Spika, mpango huu ulitoa mafanikiomakubwa sana kwa kuwapa wananchi wengi nishatihii na malipo ya mkopo wa kufungiwa umeme ulilipwakatika bili za mwezi kwa watumiaji na mikopo hiyoimelipwa vizuri sana.Mheshimiwa Spika, nimeona niliseme hili makusudikwa kuwa watu wetu wengi Mijini na Vijijini ambapohuduma ya umeme imefika, wanapata shida kubwa

sana kwa kuwa fedha yote wameitumia katika ujenziwa nyumba zao.Mheshimiwa Spika, kama Wizara kupitia Shirikalake la Umeme (TANESCO) likizingatia haya nakushirikiana na wataalamu wake walipo, basiwananchi wetu watapata nishati hii na itatusaidia sanakutunza mazingira yetu hasa kati matumizi ya kuni namkaa.Mheshimiwa Spika, bado matumizi ya mita za Lukuyanahitajika sana hasa katika Miji ya Musoma nakwingineko.Mheshimiwa Spika, katika Mji wangu wa Musoma,kuna shida kubwa sana la Meter za kusomea matumiziya umeme na pendekezo la wakazi wengi wa Mji wetuni kufungiwa mita za Luku ili kuepukana na folenikubwa inayokuwepo kwa sasa katika ulipaji wa bili zamwezi ambao umeonesha usumbufu mkubwa na hasabili za makadirio tofauti na Unit halisi inayotumika kwasasa.Mheshimiwa Spika, kabla ya kuunganishwa kwagridi ya Taifa, Mji wa Musoma ulikuwa na generator yakufua umeme ambayo tulikuwa tunatumia na ninauhakika Mheshimiwa Waziri anajua vizuri ma-jeneratorhaya yaliyokuwa yapo maeneo ya Nyakato MusomaMjini. Tungependa wakati wa majumuisho, basiMheshimiwa Waziri atusaidie kujua ma-generator hayoyako wapi kwa sasa na yanafanya nini?

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, napenda tukuwatia moyo Waziri na Manaibu wake, pia KatibuMkuu wa Wizara, kama mipango yao itatekelezekakwa kasi na kiasi kikubwa, basi kuna badiliko kubwasana kwa maisha na uchumi wa nchi, pia mwananchimmoja mmoja na hiyo ndiyo dira ya Taifa letu.Mheshimiwa Spika, nawatakia mafanikio memakatika utekelezaji wa bajeti hii.MHE. KASSIM K. MAJALIWA: Mheshimiwa Spika,kwanza naunga mkono hoja kwa asilimia mia kwa mia.Mheshimiwa Spika, napenda nitumie nafasi hiikuishukuru Wizara na Shirika la TANESCO kwa kukubalikuendelea na kazi ya kuboresha huduma ya umemeWilaya ya Ruangwa.Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mpango wa Wizarana Serikali ni kutoa huduma ya umeme hadi vijijini,Ruangwa bado inapata huduma isiyo ya uhakika yaumeme kwa sababu mbalimbali ikiwemo njia mbovuya mzunguko kutoka Mtwara, Tandahimba, Newala,Masasi, Nachingwea hadi Ruangwa.Mheshimiwa Spika, nimefanya mawasiliano naKatibu Mkuu kuomba ujenzi wa njia mpya fupi na yauhakika kwa kuunganisha Nyanganga hadi Nkowe(Ruangwa), njia inayotoa umeme wa uhakika iliRuangwa, pia Wilaya ya Nachingwea ipate umemewa uhakika utokao Lindi.

Mheshimiwa Spika, njia hiyo mpya itawezesha vijijivikubwa saba kupata huduma ya umeme (Nangangaya Ruangwa, Malolo, Michenga, Chimbila A, ChimbilaB, Nandagala, Namahema). Hatua ya awali iliyofikiwanaomba iongezwe uwezo ili TANESCO na Lindi ianzekazi ya ujenzi wa njia hiyo. Naomba pia kupatiwaumeme katika vijiji vikubwa vilivyo kwenye njia yaMbekenyera, Namichiga hadi Mandawa ambakowataalam wa TANESCO walishafika kwa hatua yaawali.Mheshimiwa Spika, kwa mpango huu nawashaurikuwa mpango wa kufikisha umeme Wilaya ya Liwalemfanye maunganisho Wilayani Ruangwa kwa sababuza kupunguza gharama.Mheshimiwa Spika, ahsante.MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Spika,umeme ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya jamiiyoyote ile hususan vijijini. Ni jambo la kusikitisha kuonabaada ya miaka 50 ya Uhuru ni asilimia 14.5 tu ndiowanatumia umeme. Kwa kweli hatua hii hairidhishi,naamini Serikali itafanya juhudi kubwa ili kufikia mwaka2015 angalau 30% ya Watanzania wapate umeme.Usambazaji wa umeme hapa nchini umekuwaukichukua muda mrefu kutokana na sababu nyingiikiwemo gharama kubwa za kuweka umeme, ughaliwa nguzo, lakini kubwa zaidi ni ubinafsi uliopo ambapowananchi husubiria wengine waweke nguzo ili wapateurahisi. Ni rai yangu basi mtu anapoweka nguzo, walewatakaoweka umeme baadaye kwa kupitia nguzo ilewamlipe yule wa awali. Hata hivyo, bado tunaitaka

Serikali ipunguze bei ya nguzo kutoka Sh. 900,000/=hadi Sh. 500,000/= ili wananchi waweze kuwekaumeme au nguzo ziwe bure na mwananchi alipie tuservice line.Mheshimiwa Spika, Watanzania wotewamefurahishwa sana na upatikanaji wa gas asilia kuleLindi na Mtwara. Habari hii njema siyo tu itakuza pato laTaifa, lakini pia itapunguza kwa kiasi kikubwa ukatajihovyo wa mti kwa ajili ya mkaa. Ni rai yangu kuwaSerikali itapunguza sana bei ya gesi hii ili wananchiwengi waweze kutumia gesi hii asili.Mheshimiwa Spika, Tanzania imebarikiwa kupatamadini ya aina nyingi pamoja na vito vya thamanikubwa ikiwemo Tanzanite, Almasi na nyingine nyingi.Mheshimiwa Spika, pamoja na madini na vitohivyo vyote, bado vinaliingizia pato la Taifa kwa chiniya 4%. Tunajiuliza, nini sababu ya pato hili dogo? Tatizoni nini? Nini sasa kifanyike ili Taifa liweze kupata patozaidi? Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusumchanga na udongo ulio na madini kupelekwa nje yanchi kwa ajili ya kufanyiwa tafiti. Je, ni lini Serikaliitakuwa na vifaa vya kisasa kuchunguza madini na vitohapa hapa nchini ili kuwaondoa wananchi wasiwasiwa kuchakachuliwa au kuibwa kwa rasilimali zake?MHE. AMOS G. MAKALLA: Mheshimiwa Spika,nianze kuwapongeza na kuwashukuru Waziri naManaibu wake wawili kwa kupokea maombi yangu yakupeleka umeme katika vijiji vya Kidudwe, Kunke,Lusanga, Ng’ambo, Kipala, Makumu, Mbuyeni, Melela,

Kibati na Poma. Naishukuru Serikali kwa kupokeamaombi yangu niliyoyatoa Bungeni katika bajeti yamwaka 2011/2012 na aliyekuwa Waziri wa Nishati naMadini - Mheshimiwa William Ngeleja, alinijibuamepokea maombi yangu na Serikali itatekeleza.Mheshimiwa Spika, nashukuru uongozi mpya chiniya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongokwa kunijibu na sasa nafurahi Vijiji na Kata hizo zipokatika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2012/2013.Naomba tu utekelezaji sasa wa upelekaji umememaeneo hayo ili kuchochea ukuaji wa uchumi nahuduma za jamii.Mheshimiwa Spika, naomba pia Wizara itembeleemachimbo ya dhahabu Matale kuwasaidiawachimbaji wadogo wametumia zana duni,wasaidiwe pia mitaji kwa ajili ya kununua zana zakisasa. Aidha, Serikal itabakiza eneo la madini Melela,Kata ya Melela ili kutoa ushauri na maelekezo kwawananchi wakazi, na athari ya hifadhi ya madini namipaka yake ili maeneo yasiyo na madini wananchiwapewe kwa ajili ya kilimo na fidia kwa walioathirikana utafiti wa madini.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. MWIGULU L. N. MADELU: Mheshimiwa Spika,nianze kwa kuipongeza sana Serikali kwa nia yake yadhati na jitihada ilizozifanya kuhakikisha wananchiwanapata umeme. Binafsi na kipekee nimpongezeMheshimiwa Waziri na Manaibu wake kwa jitihada na

uwezo mkubwa waliioonesha wa kumudu majukumuya Wizara.Mheshimiwa Spika, kwa nafasi hii nikumbushie tuahadi ya umeme katika Vijiji vya Maluga, Ng’anguli,Makunda, Kitusha, Kitukutu, Kizaga, Simbalungwala,Mkulu, Motomoto, Zinziligi, Kibaya, Songambele, Kibigiri,Kizonzo, Mseko, Malendi, Mgongo, New Kiomboi, Melina Kisiri.Mheshimiwa Spika, pia naomba ombi maalumkwa Waziri na Serikali kukiangalia Kijiji cha Kaseriakupata umeme kwa kupitia mpango ulioanza kupelekaumeme Sepuka, kwani vijiji hivyo vinapakana. Hiyoitakuwa imesaidia sana hata kufikisha umeme hadiKata ya Mbelekese.Mheshimiwa Spika, aidha, niombe Serikalikuwasilisha mswada wa maswala ya gesi ili nchi iingiekwenye biashara ya gesi ikiwa na sheria ya gesi. Hii nijambo muhimu sana kwa nchi yetu kwa wakati huu.Mheshimiwa Spika, vile vile naomba Serikaliiangalie upya Sheria ya Uchimbaji ili kusaidiawachimbaji wadogo wadogo kupewa leseni ilikuondoa migogoro migodini.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika,napenda kuchangia na kutoa ushauri wangu katikahoja hii ya Nishati na Madini. Kwanza kabisa, napendakukumbusha ahadi nyingi ambazo zimeahidiwa kuhusu

kupeleka umeme Jimboni Nyang’hwale, imekuwakama hadithi tu! Ahadi hizo tangu mwaka 1998 hadi2012 hakuna utekelezaji hadi leo, pamoja nawalioahidi ni viongozi wa ngazi za juu.Mheshimiwa Spika, mwaka 1998 Mzee Malecelaaliahidi, mwaka 1999 Naibu Waziri – MheshimiwaMalima aliahidi, mwaka 2005 Mzee Malecela aliahidi,mwaka 2009 Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete aliahidi,tarehe 6 Julai, 2012 Naibu Waziri – Mheshimiwa StephenJulius Masele aliahidi mbele ya wananchi katikaMkutano wa hadhara pale Kharumwa ambapo niMakao Makuu ya Wilaya mpya ya Nyang’hwale. PiaWaziri alishuhudia nguzo ambazo zimetupwa njianikama maonyesho zaidi ya miezi minane. Ni lini sasaumeme utawaka Jimboni Nyang’hwale?Mheshimiwa Spika, pili naomba kuchangia piakuhusu uchimbaji wa dhahabu unaofanywa naBlang’uru Gold Mine, uchimbaji huo ambaounafanyika katika eneo la Jimbo la Nyang’hwarekatika vijiji vya Iyenze, Mwasabuka, Nyamikonze naSTAMICO. Ni ukweli usio na shaka kabisa kwamba kunamadhara makubwa ambayo yamejitokeza hivi karibunibaada ya milipuko ya miamba inayofanywa na mgodihuo hivi karibuni, baadhi ya nyumba na majengo yaShule ya Msingi ya Iyenze zimepasuka vibaya na ardhipia imepasuka na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishatina Madini tarehe 6 Julai, 2012 katika ziara yakeamethibitisha kwa kuona kwa macho yake.Pia tarehe 6 Julai, 2012 Mheshimiwa Naibu Waziriwa Nishati na Madini ameweka jiwe la msingi la shule

mpya kabisa lenye madarasa manne na ofisi mbili nanyumba moja yenye familia mbili za walimu hapo kijijicha Mwasabuka. Kijiji cha Iyenze jiwe la msingi jengo laZahanati Iyenze, majengo yote yamefikia kufungwalenta, tarehe 24/07/2012 saa 12.00 asubuhi mlipukomkubwa ulitokea na majengo yote yamepata nyufanyingi sana na ardhi kupasuka. Je, hasara hiyo nahatari hiyo Serikali na mgodi huo unachukua hatuagani kufidia hasara hiyo na kuepusha madharamakubwa ambayo yanaweza kuangamiza wananchiwa maeneo hayo? Naomba kauli ya Serikali kwa hili.MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika,nawapongeza sana Waziri na Manaibu Waziri kwanzakwa kuteuliwa kuongoza Wizara nyeti kwa uchumi wanchi yetu. Lakini pili, kwa kushirikiana na Katibu Mkuu -Ndugu Maswi kuandaa bajeti ya Wizara yao nakuiwasilisha vyema hapa Bungeni.Mheshimiwa Spika, naomba niwashukuru Wizarapia kwa kusimamia vizuri mradi wetu wa umeme wagenerator Wilaya ya Namtumbo na sasa upo katikahatua inayoridhisha, ila tu nakumbusha tena mradi uleulikuwa uwe wa Megawati moja, lakini generatorinayoletwa ni ya Megawati 0.4. Mimi nina wasiwasi kwakuwa Wilaya ya Namtumbo ndiyo inayozalishamahindi, alizeti, ufuta na mpunga kwa wingi nawananchi wake wamehamasika kununua na kujengaviwanda vya kusindika mazao yao ili wawezekuongeza thamani yake na kuuza kwa beiitakayoweza kukuza uchumi wao. Hivyo, kwa umemewa Megawati 0.4 utakuja kusumbua kwakuwautakuwa mdogo kusumbua kwa kuwa utakuwa

mdogo. Ndiyo katika mawasiliano mbalimbaliniliyofanya ya mdomo nimekuwa nikijibiwa na mradiule ni wa muda, unakuja mradi wa kuunganishwakatika umeme wa grid ya Taifa lakini mradi ule wa sasawa generator ulikuwa wa Megawati moja, hata katikahotuba ya Waziri wa Nishati na Madini ya bajetizilizopita alizungumzia, akasema Serikali imetengafedha za kuweka umeme wa generator katika Wilayaza Namtumbo, Sumbawanga, Ngorongoro naalielezea Megawati zitakazopatikana Namtumbo,Megawati moja.Tunaomba Serikali katika bajeti ijayo mtutengeeMegawati 0.6 generator ili tuwe na umeme wa uhakikautakaoongeza pato la uzalishaji wa wananchi waNamtumbo wakati tunasubiri kuunganishwa katikaumeme wa grid.Mheshimiwa Spika, nawapongeza Viongozi Wakuuwa Wizara kwa kuokoa hela za Taifa katika manunuziya mafuta ya kuendeshea vinu vya kuzalisha umemekwa mafuta. Nawaunga mkono kwa hatua nzurimliyochukua.Mheshimiwa Spika, nchi yetu imegundulika kuwana madini mengi na yatakayoweza kuubadilishauchumi wa nchi yetu kwa haraka. Hivyo, ushauriwangu kwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madinina Wizara zinazohusika moja kwa moja na kuendelezarasilimali watu ambao watakuja kusaidia kusimamiamiradi hiyo sisi wenyewe Watanzania. Naombakufahamu, Wizara imejiandaaje kuona fursa hiituliyonayo, tuna wataalam wangapi vijana

watakaokuja kusimamia uzalishaji wa gesi na mtandaowake unaotarajiwa kuwa mkubwa na kuwa unafanyakazi kubwa? Naamini siyo tu kwa kuzalisha umemekatika vituo vya kuzalisha, bali pia utasambaza katikavituo vya gesi kwa ajili ya magari na pia kwa matumiziya nyumbani. Je, mpaka sasa tunao wataalamwangapi? Je, tuna mpango gani wa kuwapelekavijana wetu nje kwenye nchi zenye vyuo vyenye uzoefuwa kufundisha wataalam wa gesi kwa kusimamiauzalishaji na usambazaji wake ili wapate elimu hiyo kwaharaka waje kutusaidia ili tusiwe watazamaji tu wautaalam huo?Mheshimiwa Spika, naomba Wizara ishirikiane kwakaribu na sekta husika na uzalishaji wake kukamilikamchakato wa uanzishaji wa uzalishaji wa urani tulionaonchini ili tuweze kuongeza pato la Taifa. Lakini pia niushauri wangu kwamba ni vyema kupata piawataalam wetu wenyewe wa kusimamia uzalishajiwake na usafirishaji na uhifadhi wake. Ni jambo lamuhimu sana.Mheshimiwa Spika, naomba Wizara itazame,tunao wataalam wangapi katika eneo hilo napotential technical man and women ambao tunawezakuwaendeleza na kuja kufanya kazi hizo?Mheshimiwa Spika, naomba sekta husikazishirikiane kwa haraka kuona jinsi ya kutekeleza kwapamoja kupata wataalam wengi zaidi watakaokujakukabiliana na fursa tuliyopata ya madini.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. MODESTUS D. KILUFI: Mheshimiwa Spika,Wizara ya Nishati na Madini ni Wizara nyeti sana kwauchumi wa nchi yetu. Umeme ni chanzo kikuu chanishati kwa ajili ya kuendesha mitambo mbalimbali kwaajili ya viwanda na kutoa huduma mbalimbali kwenyetaasisi za umma. Aidha, nishati ya umeme imetoa ajirakwa Watanzania wengi.Mheshimiwa Spika, napenda nichukue nafasi hiikupongeza juhudi za Waziri wa Nishati na Madinipamoja na Wasaidizi wake, lakini bado juhudi kubwazaidi zinahitajika katika kupelekea umeme vijijiniambako ndiko Watanzania wengi waliko. Umemeukipelekwa vijijini utapunguza wimbi la vijana kukimbiliaMijini kwa sababu watakuwa na uwezo wa kubuni ajirambalimbali ambazo pia zitakuza uchumi wa Taifa kwakufanya rasilimali watu kutumika vizuri.Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Mbarali ni miongonimwa Wilaya zenye vijiji vingi ambavyo havina umeme.Nimekuwa nikiomba mara nyingi ili Mbarali nayoiingizwe kwenye mpango wa REA bila mafanikio.Nataka kujua ni lini mpango huu utaingizwa Wilaya yaMbarali ili vijiji vya Ilongo, Igalako, Sonyanga, Uturo,Ukwavila, Utengule ambavyo vimepitiwa na umemeunaopita kwenda Mbeya Mjini na wao wapate nishatihiyo muhimu. Kama hiyo haitoshi, zipo Kata zaMadibira, Mheshimiwa Rais alipotembelea alitoa ahadiya kupeleka umeme kutokana na shughuli kubwa yakilimo cha umwagiliaji na kuwa na mitambo ambayohaifanyi kazi kwa kukosa umeme. Aidha, zipo Kata zaRuiwa, Utengule, Luhanga, Igava, Ipwani, Mawindi na

Mwatenga hazina umeme pamoja na kuwa nahuduma mbalimbali za jamii.Mheshimiwa Spika, naleta ombi maalum kwamba,Gereza la Mbarali halina umeme, askari wamekuwawakifanya kazi katika mazingira magumu nyakati zausiku. Umeme haupo mbali sana na mahaliunapoweza kuunganishwa.Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio mengikatika Wizara hii, naomba juhudi kubwa zielekezwekwenye umeme wa gesi, nishati ya jua na makaa yamawe. Kwani umeme wa kutegemea majiumeathiriwa sana na hali ya hewa. Mfano, kumekuwana malalamiko sana kuwa kilimo cha umwagiliaji hasaMbarali kinaathiri maji kwenda bwawa la umeme laMtela, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa ni uhabawa mvua kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Kwanihata wakulima wa Mbarali baadhi ya maeneo mazaoyao yamekuwa yakikauka kwa kukosa maji. Isitoshe jinsimaji yanavyotumika, ipo mikondo mbalimbaliinayorudisha maji Mto Ruaha. Kipindi cha mvua nyingimaji huwa mengi na kipindi cha Mvua chache majihuwa machache.Mheshimiwa Spika, aidha, changamoto huwahazikosekani. Upo ufisadi ambao umekuwa ukiitafunaWizara hiyo kutokana na kuwa na baadhi ya viongozi(watendaji kutokuwa na uadilifu) pambana nao, tupopamoja hatukubali mpaka wote wenye tabia hiyowamalizike. Katika ufisadi huo, lipo tatizo la gharama zauunganishaji umeme na bei ya nguzo za umemeambazo zinaandaliwa hapa hapa nchini, lakini bei ni

kubwa mno, heri ukanunue nje ya nchi. Nalo hililiangaliwe.Mheshimiwa Spika, mikataba ya madiniiliyowekwa kifisadi ndiyo inayofanya Taifa kuingiahasara. Ingelifaa kutazamwa upya ikiwa ni pamoja nakuona mikataba ya nchi nyingine inayowekwa kwamanufaa ya Taifa.MHE. DKT. FESTUS B. LIMBU: Mheshimiwa Spika,napongeza juhudi kubwa na maarifa vinavyofanywana uongozi wa juu wa Wizara ukiongozwa na Wazirimwenyewe, Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu, NaibuKatibu Mkuu, Makamishina na kadhalika. Kasimliyoanza nayo Waheshimiwa Mawaziri, Katibu Mkuu,mwendelee nayo. Nina imani Watanzania walio wengina Waheshimiwa Wabunge wanaunga mkono.Kanyaga moto twende.Mheshimiwa Spika, mimi ni muumini mkubwa wagesi. Naamini gesi ndiyo itakayomkomboa Mtanzaniandani ya muda mfupi. Sekta hii itachangia kwa kiasikikubwa, kwa haraka na kwa uhakika katika maeneoyafuatayo kuwa na umeme wa uhakikausikokatikakatika, wa bei nafuu, itatuingizia fedha zakigeni, kwani tutauza nje gesi na hivyo kuimarishaShilingi ya Tanzania, itachangia kuongeza ajira,itahamashisha uanzishwaji wa viwanda (vya plastic) nahasa mbolea, itachochea utumiaji wa mbolea ya beiya chini kwa wingi ambayo itachangia kuongeza tijakatika Sekta ya Kilimo na hivyo kuchangia kupunguzaumasikini, fedha (mapato) zitakazopatikana kutokanana gesi zitaweza kuwekezwa katika maeneo na sekta

mbalimbali nchini kama vile afya, elimu, maji, kilimo,viwanda na kadhalika.Mheshimiwa Spika, naomba Wizara iwe makinisana katika kuchukua hatua ili kuhakiksha kuwahatufanyi makosa kama ilivyotokea kwenye sekta yetuya madini. Ni lazima tuhakikishe sera yetu ya madiniinakuwa nzuri, sheria nzuri na kanuni safi. Tusipofanyahivyo, vizazi vijavyo vitatulaumu sana na Munguatatulaani.Mheshimiwa Spika, nawatakia kila la kheri.Naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.MHE. JOSEPHINE GENZABUKE: Mheshimiwa Spika,nampongeza Waziri Mheshimiwa Prof. Sospeter M.Muhongo kwa hotuba yake nzuri. NawapongezaManaibu Waziri, Mheshimiwa George Simbachawene,Mheshimiwa Stephen J. Masele pamoja na KatibuMkuu wa Watendaji wa Wizara kwa kazi nzuriwanayoifanya.Mheshimiwa Spika, umeme uliopo Kasulu naKibondo ni mwingi sana kuliko matumizi. Hivyo,naomba wananchi wote ambao wameshalipia ilikuweza kusambaziwa nyaya kusudi wapatiwe umeme.Meneja wa TANESCO Kasulu hatendi haki hata kidogokwa sababu aliwalipisha wananchi pesa Sh. 200,000/=badala ya Sh. 69,000/= na kuwapatia risiti za Sh.69,000/= kwa kudai kuwa Sh. 200,000/= ni kwa ajili yakulipia nguzo. Baadhi ya wananchi wakatii na kutoapesa hizo. Cha kusikitisha, pamoja na kulipia gharamahizo, hawapatiwi umeme.

Mheshimiwa Spika, naomba wananchi haowaliokwishalipia wapewe umeme badala ya visingiziovilivyopo sasa, kuwa hakuna nguzo wala nyaya. Je,kama hakuna nguzo wala nyaya, kwanini Menejaaliwatapeli wananchi kwa kuchukua pesa zao?Mheshimiwa Spika, naomba wachimbaji wadogowadogo wawezeshwe ili waweze kupatiwa mitaji, vifaavya uchimbaji, na soko. Vijana wengi hawana ajira,hivyo wakiwezeshwa kupewa fursa wataweza kujiajiriwao wenyewe.Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba meneja waTANESCO Kasulu ahamishwe.Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya,naomba kuunga mkono kwa asilimia mia moja.MHE. DKT. SEIF S. RASHID: Mheshimiwa Spika,naomba kwanza niwasilishe pongezi nyingi za dhatikwa Serikali katika juhudi zake za kuongeza kiwangocha uzalishaji wa nishati na kuondoa uwezekano wamgao wa umeme nchini.Mheshimiwa Spika, niliomba Serikali kutoakipaumbele kwa uzalishaji wa umeme wenye unafuukwa mtumiaji ili wengi wetu tuweze kuitumia nishati hiikwa unafuu zaidi na kupanua wigo wa matumizi yanishati hii.Mheshimiwa Spika, nawasilisha ombi rasmi nakukumbusha ombi langu nililowasilisha mwaka 2011 ili

umeme uliofika Wilaya ya Rufiji uwanufaishe watuwengi zaidi badala ya wengi wao hivi sasa kuwa niwatazamaji tu.Mheshimiwa Spika, naomba Serikali kwanzakuvipatia umeme vijiji ambavyo vimepitiwa na umeme.Ni ahadi ya Mheshimiwa Rais wetu kuvipatia umemevijiji hivyo ikiwa ni pamoja na Kiwanga, Chimbi A, B, C,Utunge, Kitundu na Kindwitwi. Naomba kwenye vijijiambavyo vimeshapata umeme, lakini umeme huohaujasambazwa na imewaacha watu wengi wakiwawatazamji na hivyo kusababisha malalamiko tena hatakatika sekondari zetu pale Muhoro na Utetehawajapatiwa umeme. Naiomba Serikali kuwapatiaumeme watu wengi zaidi.Mheshimiwa Spika, niliomba umeme ambao upotayari katika Mji wa Ikwiriri usambazwe angalau kwaawamu kuelekea Mloka na hivyo kutoa fursa kwa vijijizaidi ya 14 kunufaika na mradi huo, ambao mwaka2011 nilijibiwa hapa Bungeni kwa mradi huo unahitajifedha nyingi kwa sababu ya umbali wake. Kwa vile vijijizaidi ya 14 vipo ndani ya hizo kilometa 100, wastani waumbali wa kilometa tano kutoka kijiji kimoja hadikingine. Mradi huu utaongeza uwezekano wakuwekeza viwanda vya kuongeza thamani ya mazaoya kilimo na kukuza utalii wa pori la Selous nakuchochea maendeleo ya dhati katika eneo hili.Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali kusambazaumeme kutokea Kijiji cha Nyamwage kuelekeaMbwara ambako pia kuna Sekondari na Kijiji cha jirani

yake cha Nambonji ambapo Kituo cha Afyakinajengwa hapo.Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kupta fursa yakuchangia kwa maandishi na kwa muhtasari, naiombaSerikali katika mambo haya matatu, kuwashushiaumeme vijiji ambavyo umeme umepita kwao katikaWilaya ya Rufiji Kiwanga, Chumbi, Utunhe, Kitondo,Kindwitwi, katika vijiji ambavyo vimepatiwa umemeusambazwe katika vijiji hivyo ili watu wengi wanufaikena umeme huo, kusambaza umeme kutokea Ikwiririkupitia vijiji 15 hadi kijiji cha Mloka kwa awamu nakutokea Nyamurage hadi Nambunjo kupitia Mbwara.Mheshimiwa Spika, nashukuru na naunga mkonohoja.MHE. AGGREY D. J. MWANRI: Mheshimiwa Spika,kwa niaba ya wananchi wa Jimbo langu la Siha,naomba kuchukua fursa hii kumpongeza sanaMheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo na Waziri waNishati na Madini kwa hotuba yake nzuri na yenyeuchambuzi wa kina kuhusu maendeleo ya Nishati naMadini katika nchi yetu. Napongeza sana jitihadaambazo Waziri na Naibu Mawaziri wake wameonyeshakatika kipindi cha muda mfupi waliokaa katika Wizarahii. Nawapongeza pia Manaibu Mawaziri wote wawili,Mheshimiwa George Simbachawene na StephenMasele kwa kazi ya hali ya juu ambayo wanaifanyakatika Wizara na hivyo kuinua kiwango cha ufanisi.Pongezi sana.

Mheshimiwa Spika, nampongeza kwa namna yakipekee Katibu Mkuu wa Wizara hii, Ndugu EliachimMaswi kwa jitihada zake za hali ya juu ambazo zimeletaufanisi mkubwa na wa hali ya kutoa matumaini kwaWatanzania. Aidha, nampongeza Dkt. Mwakiyesia -Mkurugenzi wa REA kwa utumishi wake wa kutukukakatika REA. Baada ya pongezi hizi, naomba kutamkakwamba ninaunga hoja hii mkono.Mheshimiwa Spika, naomba kukumbushia baruayangu nilivyomwandikia Mheshimiwa Waziri kuhusumiradi ya kusambaza umeme Wilayani Siha ambayoimechukua muda mrefu bila kukamilika. Miradi hii ni ileya West Kilimanjaro katika Kata ya Ngare-Nairobi naNdumeti Kata ya Livishi, Kijiji cha Nshere-hehe na MowoNjamu katika eneo la Kyaboo na Kijiji cha Mese, Kataya Nasai eneo la Omarinyi lililopo Kijiji cha KowokoKaskazini na eneo la Kikwe lililopo Kijiji cha KobokoKusini na vijiji vya Kishisha na Mae bado vina nguzozimelala chini na wananchi wamekuwa wanasubirikwa miaka mingi bila mafanikio.Mheshimiwa Spika, naomba sana, miradi hiiikamilishwe, kwani gharama kubwa imekwishatumikakuianzisha kwa kupika maeneo husika na kusimamishanguzo katika baadhi ya maeneo husika.Mheshimiwa Spika, mwisho, nakumbushia eneo laLawate kuelekea Kijiji cha Ngumbaru ambapo ndipostesheni ya kusambaza umeme ilipo katika kuhitimisharai yangu. Naomba kushauri REA iongezewe kiasi chafedha kinachopelekwa katika wakala hii, kwani kama

nilivyoeleza, wameonyesha jitihada za hali ya juu katikausambazaji wa umeme vijijini.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii.MHE. EDWARD N. LOWASSA: Mheshimiwa Spika,napongeza hotuba nzuri uamuzi wa kushusha gharamaza kuunganishwa umeme ni mzuri sana. Napongeza.Mheshimiwa Spika, harakisheni suala la sera naSheria ya Gesi yake kusema kwa uhakika sera hiyo nasheria hiyo italetwa lini Bungeni? Bila sera na Sheria yaGesi itakuwa hatuwatendei haki Watanzania.Mheshimiwa Spika, katika kuandaa sera,uangaliwe uwezekano wa kuunganisha uchumi nafedha zitakazotokana na gesi kusaidia ajira kwa vijanakwa kuwekeza katika kilimo na maeneo yatakayotoaajira kwa vijana. Tuangalie sana ili upatikanaji wa gesiusiwe a curse, bali a blessing.Mheshimiwa Spika, mwisho, kamilisheni usambazajiwa umeme Mto wa Mbu.MHE. RITA L. MLAKI: Mheshimiwa Spika, kwanzanampongeza sana Waziri, Katibu Mkuu na Watendajiwa Wizara kwa hotuba nzuri sana ya Wizara hii.Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia eneo lamadini. Nimesikitishwa kuona nchi yetu inachimbamadini ya thamani ya Dola za Marekani bilioni 2.2 nasisi kama nchi tunapewa Dola milioni 62 tu. NashauriSerikali tupitishe sheria ya kutuwezesha kununua hisa

katika migodi hiyo ili angalau nchi yetu iweze kunufaikana madini hayo.Pia ningeshauri STAMICO iwe na sheria nyingi zaidikatika migodi ya Buhemba na Backreef, wabia wawena minority shares.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja.MHE. LUCY P. OWENYA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kupata nafasi ya kuchangia.Mheshimiwa Spika, pamoja na Serikali kulielezaBunge lako Tukufu, utafiti umefanyika kuhusu uchimbajiwa madini ya urani kwamba hautaathiri mazingira: Je,utafiti umefanyika kuona ni kwa kiasi gani afya zawanadamu na wanyama wataathirika kwa uchimbajiwa madini hayo? Je, kuna uharaka gani wa kuchimbamadini haya wakati haya yaliyopo bado hatujawezakwa kiasi kikubwa kuhakikisha wananchi wanafaidikanayo?Mheshimiwa Spika, umeme wetu umekuwaukitegemea maji, lakini kwa sasa hivi pamekuwepo naukame sana kupelekea ukosefu wa mvua, hivyokuathiri mitambo inayotumia maji kama Mtua nakadhalika na mwaka huu mvua hazikunyesha zakutosha, hivyo kuna kila dalili lazima kutakuwepo namgao mkubwa wa umeme siku za karibuni. Je, kwampango wa muda mfupi, sababu siyo jambo lakushtukiza, TANESCO imejipanga vipi kuhakikisha watuwanapata umeme? Palikuwepo na ma-genetor karibia

kila Mkoa: Je, ni ma-generator mangapi yanafanyakazi katika kila Mkoa, ili yasaidie katika tatizo laumeme?Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu sasatumekuwa tukitumia umeme wa dharura kwa kutumiamitambo ya kukodi ambayo ina gharama kubwa naSerikali inapata hasara kubwa ya kulipa capacitycharges na hii inapelekea bei kubwa sana kwamtumiaji (mwananchi) kwa kulipa bei kubwa. Ni linitutamaliza hii system ya kutumia umeme wa dharura?Je, miaka yote hii, itachukuwa muda gani kujifunza?Mchakato wa kutumia umeme wa makaa ya mawena gesi asilia umefikia wapi? Kwa sababu kwa sasa huuumekuwa ni wimbo katika kila hotuba ya bajeti yaWizara hii.Mheshimiwa Spika, kuhusu matumizi ya gesi kwaajili ya matumizi ya nyumbani, naipongeza Serikali kwahili kwa sababu kwa kiasi kikubwa tutaokoa mazingirayetu. Lakini naomba kutoa tahadhari kwamba Serikaliitoe elimu kwa watumiaji kuhusu kulipuka na piapawepo na maandalizi ya kutosha. Kwa mfano, kilanyumba lazima iwe na fire extinguisher na Serikalilazima iwe na magari ya kutosha ya zimamoto pindipanapotokea moto, yaweze kwenda sehemu tofauti.Mheshimiwa Spika, pamoja na EWURA kusimamiana kuthibiti mafuta ya petrol yasiyo na ubora hayauzwikatika vituo vyetu, licha ya Serikali kuagiza mafuta kwapamoja (bull procurement system) bado bei ni ghalilicha ya kupandisha bei ya mafuta ya taa, badomafuta yanachakachuliwa. Je, Serikali inaweza kutoa

maelezo licha ya EWURA kufanya ukaguzi na licha yamafuta ya taa kupanda bei, bado uchakachuaji upo?Sababu ni nini? Kulikuwa hakuna haja ya kupandishamafuta ya taa bei na kuwatesa wananchi wenyekipato cha chini na kushindwa kununua mafuta nabadala yake wanaendelea kukata miti kwa ajili yamatumizi ya kuni za kupikia na mkaa na kupelekeakuharibu mazingira.MHE. JOSEPHINE T. CHAGULLA: Mheshimiwa Spika,kwanza kabisa, namshukuru sana Mwenyezi Mungukwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kupata nafasihii ili niweze kutoa mchango wangu wa maandishikatika hotuba hii iliyopo mbele yetu.Mheshimiwa Spika, nampongeza sanaMheshimiwa Waziri pamoja na Manaibu Waziri wakelakini pia naomba kuwapongeza watendaji wote waWizara hii ya Nishati na Madini kwa kuandaa vizurikabisa hotuba hii.Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa,naomba nimpongeze sana kaka yangu mpendwaKatibu Mkuu wa Wizara hii, Ndugu Maswi kwa kazi nzurikabisa anazozifanya pale Wizarani.Mheshimiwa Spika, Katibu Mkuu ni mfano wakuigwa kabisa na Watanzania wote. Uzalendo wake,usafi wake na uchapakazi wake, vinafaa kabisakusifiwa. Anafanya kazi nzuri sana. Mimi naomba sanaWaheshimiwa Wabunge wote tumpongeze kwa hilo nasiyo kumkatisha tamaa kama wanavyofanya watuwengine.

Mheshimiwa Spika, mimi namtaka MheshimiwaMaswi pamoja na Waziri na Manaibu Waziri wasongembele, kazi ni nzuri, endeleeni kufukuza watuwasiokuwa na uzalendo na nchi yetu, hata mkifukuzawote, tutaajiri watumishi wengine wapya. Vijana wengiwapo, hawana kazi, wamemaliza Chuo Kikuu,watafanya kazi. Napongeza sana kazi yenu ni nzurisana, songeni mbele.Mheshimiwa Spika, mchango wangu nauelekezazaidi kwa wachimbaji wadogo wa madini.Mheshimiwa Spika, nashauri Serikali iwawezeshekupata mikopo ili waweze kupata vifaa vya kisasa vyauchimbaji ukilinganisha na vya sasa wanavyotumia.Aidha, pia Serikali iwape mafunzo na seminawachimbaji wadogo hawa.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hivyo,naunga mkono hoja.MHE. AZZA H. HAMAD: Mheshimiwa Spika, kwanzanashukuru kupata nafasi ya kuchangia kwa maandishibajeti hii ya Wizara ya Nishati na Madini.Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara kwakuandaa hotuba nzuri yenye matumaini, lakini pamojana hayo, kuna mambo ambayo yanakera katika jamiiyetu kutokana na mambo ambayo Wizara hiiinayafanya.

Mheshimiwa Spika, mwananchi wa kawaidaaliyeko huko kijijini, ambaye hata hati ya kimila hana,anakuwa kama mkimbizi kwenye eneo lake, mfano,yanapogundulika kuwa eneo hilo lina madini bilakumshirikisha mwenye eneo, kibali cha utafiti kinatokamoja kwa moja Wizarani. Hata mwenye eneo hanataarifa yoyote au leseni ya uchimbaji anapewamwekezaji bila mwenye eneo kushirikishwa. Utaratibuhuu ni mbovu na ni unyanyasaji mkubwa kwa wenyemaeneo hayo.Uutakuta utafiti wenyewe unafanyikazaidi ya miaka 10, wanatafiti nini?Mheshimiwa Spika, Serikali haiwatendei hakiwananchi wetu na tunasababisha umasikini mkubwakwa wananchi kulipwa gharama ambayo haifanani namali inayotolewa katika eneo lake na inasababishahata wananchi wakakosa sehemu ya kulima.Mheshimiwa Spika, la mwisho, kwa umuhimumkubwa, Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anajibu,naomba anijibu ule utafiti unaofanywa na Kampuni yaBarrick katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga,Jimbo la Solwa Kata ya Mwakitolyo utakwisha lini?Kwani mwaka 2011 watu hawa walisemawamekamilisha utafiti na baada ya muda mfupiwanaanza kazi rasmi, lakini toka mwaka 2011 mpakaleo hii hakuna kinachoendelea zaidi ya utafiti. Badohaitoshi, kuna Kampuni nyingine ya Kichina nayo ipoHalmashauri ya Shinyanga. Wizara mnasemawanafanya utafiti, ule siyo utafiti ni uchimbaji, kituambacho kinafanya wananchi hawa washindwe hatakulima.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, lakininaomba majibu ya huo utafiti unaoendeleaMwakitolyo zaidi ya miaka kumi sasa.MHE. ISMAIL A. RAGE: Mheshimiwa Spika, awali yayote, napenda kuunga mkono hoja ya Wizara yaNishati na Madini.Mheshimiwa Spika, naomba Wizara kwa kupitiaEWURA wawe waangalifu sana katika kupunguza beiya mafuta, kwani mpaka sasa ukweli wananchi badohawaridhiki na bei za mafuta pamoja na kuanzishamfumo wa ununuzi wa Bulk ambao tulitegemeakupata nafuu.Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa sheria mama,sielewi kwa nini Makampuni yanalipa US $ 250,000 tukwa Halmashauri zinazohusika badala ya kulipa sourcelevy ya 0.03% kwa mujibu wa sheria. Naomba Waziriatakapojumuisha, atoe maelezo ya kutosha.Mheshimiwa Spika, katika suala la bei yakuunganisha umeme, nampa hongera sanaMheshimiwa Waziri, kwani nina imani kubwa hata hapobaadaye mambo yakiwa mazuri, basi wananchi waTabora watapata nafuu sana.Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Katibu Mkuukununua mafuta bila ya kufuata Sheria ya Manunuzi,mimi nataka kumpongeza na kumhakikishia kwamba,Wabunge wenye uchungu na nchi yao watamuungamkono hatua aliyochukua ya kuokoa Shilingi bilionitatu. Anastahili tunzo (honourable) na Mungu amjalie.

Mheshimiwa Spika, tunamwomba sanaMheshimiwa Waziri awe mwangalifu sana katikaMikataba ya Gesi ili Serikali iweze kufaidika na miradihii.Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba MheshimiwaWaziri aangalie Jimbo langu la Tabora Mjini ambalolina Kata 25; kati ya hizo, kuna Kata 11 za Mjini na Kata14 ni za Vijijini. Kwa hiyo Kata hizi naomba na zenyewezipatiwe umeme katika mpango wa Wakala wa REA.Nina imani na ofisi ya Waziri itatusaidia sana wakazi waTabora.Mheshimiwa Spika, naunga mkono Wizara yaNishati na Madini mia kwa mia. Ahsante.MHE. BRIG GEN. HASSAN A. NGWILIZI: MheshimiwaSpika, naunga mkono hoja ya Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka2012/2013 kwa asilimia mia moja. Hotuba ya Waziri ninzuri. Pamoja na changamoto nyingi zilizopo mbeleyake, ninaamini kuwa matarajio yote yanatekelezeka.Hata hivyo, katika Jimbo la Mlalo umeme ulikwishafikakatika Tarafa moja ya Mlalo. Umeme huo pia ulikuwaufikishwe kwenye Tarafa ya Mtae na Umba ilikukamilisha mradi huo. Kushindwa kutekelezwa kwamradi huo, imekuwa ni chanzo kikubwa chamalalamiko ya wananchi wa Jimbo hilo. InashauriwaMamlaka ya Umeme Vijijini (REA) ilishughulikie tatizo hiliharaka iwezekanavyo.Mheshimiwa Spika, ninawasilisha.

MHE. GOODLUCK J. OLE-MEDEYE. MheshimiwaSpika, nampongeza sana Mheshimiwa Profesa SospeterMuhongo, Waziri wa Nishati na Madini pamoja naMheshimiwa George Simbachawene na MheshimiwaStephen Masele, Naibu Mawaziri kwa kuteuliwa naMheshimiwa Rais kuongoza Wizara hii na kwa kazi nzuriwaliyokwishaifanya tokea wakabidhiwe kazi hiyo.Mheshimiwa Spika, nampongeza Bwana EliakimMaswi, Katibu Mkuu na Makamishna na Wakurugenziwa Idara mbalimbali Wizarani, Wenyeviti wa Bodi naWatendaji Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizarapamoja na watumishi wote, kwa jitihada wanazofanyakutekeleza sera na sheria za sekta za nishati na madiniili kuongeza mchango wa sekta hizo kwenye uchumiwa Taifa letu.Mheshimiwa Spika, napenda kutoa maoni naushauri kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, kwanza ni kuhusu Sera yaNishati. Upungufu wa umeme nchini umeathiri uchumina maendeleo ya jamii kwa ujumla kwa sababu yaviwanda na shughuli nyingine zenye kuhitaji umemekutofanya kazi kwa kiwango kilichopangwa. Nchi yetuimejaliwa kuwa na rasilimali ya madini ya uraniambayo ni chanzo muhimu katika uzalishaji wa nishatiya umeme. Kwa kutambua rasilimali hiyo tuliyo nayo, nivizuri tukapanga kushirikiana na nchi zenye uzoefukatika ujenzi na usimamizi wa vinu vya kuzalishaumeme wa nuklia ili kuzalisha umeme wa kutosha nchinzima na sehemu yote ya Afrika kusini mwa jangwa laSahara.

Mheshimiwa Spika, pili, utekelezaji wa mipango yaumeme vijijini, mwaka juzi Wizara iliwajulisha wananchiwa Wilaya ya Arumeru Magharibi kuwa imetenga kiasicha shilingi 7.5 bilioni kwa ajili ya kutekeleza miradi yaumeme kwenye kata tano kati ya 21 za Wilaya hiyo.Tulifarijika sana baadhi ya miradi ilipoanza kutekelezwailitupa matumaini kuwa sasa mipango ya wananchikuanzisha viwanda vidogo ili kutoa fursa za ajira,kuongeza thamani ya mazao yao pamoja nakuwezesha utekelezaji wa miradi ya maji namengineyo. Hata hivyo, inasikitisha kuona kuwamkandarasi ambaye ni TANESCO wamekuwa wakitoasababu mbalimbali za kuchelewa utekelezaji wa miradihii. Naomba Wizara itujulishe kuwa ina mpango ganiwa kutekeleza miradi hiyo na ni lini inatarajiwakukamilika?Mheshimiwa Spika, tatu, tarehe 26 April 2012,Naibu Waziri wa Nishati na Madini akifanya ziarakwenye Halmashauri ya Wilaya ya Arusha (ArushaDistrict Council) ambapo katika mikutano ya hadharakwenye Kata mbalimbali aliahidi kuwa Serikali itaingizakwenye Mpango wa kupatiwa umeme vijiji visivyokuwana umeme kwenye Halmashauri hiyo. Aidha,alimwagiza Meneja wa Mkoa wa TANESCO kuwawafanye upembuzi na kuwasilisha taarifa Wizarani ilishughuli hiyo ianze bila kuchelewa. NamwombaMheshimiwa Waziri awajulishe wananchi waHalmashauri ya Wilaya ya Arusha juu ya hatuailiyofikiwa katika kuwezesha vijiji vilivyo kwenye Wilayahiyo kupata umeme. Kwa taarifa kwa MheshimiwaWaziri kuwa Wilaya ya Arumeru inakabiliwa na tatizo la

muda mrefu la maji, moja ya sababu zinazokwazauendeshaji wa vyanzo vya maji ni ukosefu wa umeme.Kwa niaba ya wananchi wa Wilaya yangu, naombasana tusaidiwe kuondokana na adha hii.Mheshimiwa Spika, nne, leseni za madini. Uzoefuumeonesha kuwa leseni za uchimbaji madinimbalimbali ikiwemo mchanga, morum na vitombalimbali zimekuwa zikitolewa na MakamishnaWasaidizi wa Kanda bila kushirikisha wadau muhimuwakiwemo wamiliki wa ardhi yenye madini hayo. Ikomifano mingi kwenye Wilaya yangu ambapo uchimbajiumesababisha migogoro. Nashauri kuwa Wizara itoemwongozo kwa Makamishna Wasaidizi wa Kanda ilikuhakikisha kuwa wananchi wanaomiliki ardhi yenyemadini wanafaidika na rasilimali hizo kwa kuwa wabiaau kulipwa fidia inayostahiki ikiwa wataridhia utaratibuhuo.Mheshimiwa Spika, nawasilisha na narudia kusemanaunga mkono hoja kwa dhati.MHE. DKT. DAVID M. MALLOLE. Mheshimiwa Spika,napenda kuchangia kidogo katika nishati inayotokanana umeme wa jua (solar power). Zipo aina nyingi zanishati kama vile umeme wa maji, gesi, mafuta nakadhalika. Aina zote za nishati ni ngumu sana kuziweka.Umeme wa maji unahitaji ujazo wa maji mengi kwenyemabwawa, gesi inahitaji gharama kubwa ya kutandikamabomba ya gharama kubwa yatakayokwenda mailinyingi, umeme wa mafuta pia ni gharama kubwa,umeme wa jua hauna gharama kubwa sana. Ni rahisi

sana kutumia umeme wa jua kwa ajili ya mwanga, pasiza umeme, fridge, television na majiko ya kupikia.Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kutumia kampuniza ndani na nje, watangaze tenda za kusambazaumeme wa jua nchi nzima, kwenye majumba, hospitali,shule na taasisi nyingine nyingi ili kuokoa mazingira yaukataji misitu ovyo. Kampuni za umeme wa jua piazisambaze majiko ya umeme wa jua kwa mwendo wakasi sana nchi nzima. Kadiri muda unavyoendelea,Serikali pia itafikisha vyanzo vingine vya nishati nchinzima, mfano nishati ya umeme wa maji, gesi, makaaya mawe, mafuta na kadhalika.Mheshimiwa Spika, kama tutaendelea kufikiria njiakubwa za nishati mathalani nishati ya umeme wa maji,gesi na mkaa, tutachelewea sana na nchi nzimaitaathirika vibaya kwa kufyeka miti na kupanua jangwala Sahara Afrika ya Mashariki na Kusini mwa Afrika kwahasara yetu wenyewe na vizazi vijavyo. Tusambazeharaka nishati ya umeme wa jua, nishati nyinginezitafuata baadaye.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. MARIAM R. KASEMBE: Mheshimiwa Spika,nachukuwa nafasi hii kuchangia kwa maandishi kamaifutavyo:-Mheshimiwa Spika, nianze kumpongezaMheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kwake kuwaMbunge na Waziri wa Nishati na jinsi ambavyoameanza kuonyesha uzalendo katika utendaji kazi

wake, akisaidiana na Ndugu Eliakim Maswi ambaye niKatibu Mkuu wa Wizara, nawatakia kila la kheri, wazidikuwa wabunifu kufichua uovu ambao umekuwaukifanywa na viongozi na watumishi wasio na uzalendona nchi yetu. Pia nawapongeza Manaibu Mawaziri waWizara hii ambao ni kiungo kikubwa katika kumsaidiaMheshimiwa Waziri na kuleta ufanisi mzuri wa Wizara hii.Mheshimiwa Spika, Serikali ya Chama chaMapinduzi imefanya jitihada kubwa kufanya utafitikatika nchi yetu na kuweza kufanikisha kupata gesikatika Mkoa wa Mtwara huko Mnazibay. Jitihada hizi nikubwa sana na ni mafanikio ambayo Watanzania hasawananchi wa Mkoa wa Mtwara wana matumainimakubwa sana kwamba tatizo kubwa la umemeambalo tulikuwa nalo sasa ufumbuzi umepatikana.Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya uzinduzi waujenzi wa bomba la kusafirisha gesi toka Mtwara na Dares salaam. Hii ni hatua kubwa ya maendeleo. Rai yaWanamtwara ni kwamba tupewe kipaumbele katikakusambaza umeme vijijini ili kuwaondolea wananchiadha kubwa ambayo inawakabili kwa miaka mingisana. Hakutakuwa na faida kama gesi inatoka Mtwarakisha wananchi wanaendelea kuwa gizani. Gesi asili nimaendeleo, tunaomba Serikali ifanye jitihada zakuwekeza na kutafuta wawekezaji ambao watajengaviwanda Mkoani humo ili kuharakisha na kuchocheamaendeleo na kutoa ajira kwa wananchi wa Mkoa waMtwara na Tanzania kwa ujumla.Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Mtwara, ni Mkoaambao ulisimama kimaendeleo kwa miaka mingi,

upatikanaji wa gesi hii nina imani kubwa itaharakishamaendeleo katika sekta mbalimbali. Hivyo, naiombaSerikali na Wizara kwa ujumla katika zoezi la kusambazaumeme vijijini, iangalie maeneo ya taasisi kama vilezahanati, shule za msingi na shule za sekondari, misikitina makanisa na maeneo yenye huduma za jamiikusaidia kupeleka nguzo bure ili kuwapunguziagharama wananchi na kuwawezesha kuweka umemekatika taasisi hizo ili waweze kutoa huduma stahiki. Kwamfano, shule zitawawezesha vijana wetu kusoma nakuzitumia maabara katika shule za sekondari lakini hataumeme katika zahanati, wananchi watapata hudumabora na chanjo na akina mama wajawazito kujifunguabila kulazimika kutoa mchango wa mafuta wakati wakujifunga na kadhalika.Mheshimiwa Spika, TANESCO ni shirika ambalolinategemewa sana na wananchi mijini na vijijinikupata huduma za umeme lakini wananchiwamekuwa wakikosa imani na huduma wanazotoakwani wamekuwa wakitoa bili kubwa kwa wateja waokuliko matumizi yanayotumika lakini pia wananchiwamekuwa wakipeleka maombi ya kuwekewaumeme vijijini kwa miaka mingi lakini hawapati hudumahiyo.Mheshimiwa Spika, nina maombi yafuatayo kwaSerikali:-(a) Wananchi ambao watawekewa umemevijijini hasa Jimbo langu la Masasi wawekewe Lukukuepusha kupewa bili tofauti na matumzi yao;

(b) Vijiji ambavyo vilishapeleka maombi TANESCOwapewa kipaumbele katika kuwekewa umeme kamavijiji vya Nangose Temeke, Chikunja vilivyopo Wilaya yaMasasi; na(c) Upelekaji wa nguzo za umeme katika taasisivijijini, Serikali isaidie kwani hali ya wananchi vijijini niduni.Mheshimiwa Spika, natumaini maombi yanguyatapatiwa majibu yenye tija, kwa wananchi umemeni uchumi, umeme ni maendeleo.MHE. RASHIDI ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Spika,kwanza sina budi kumshukuru sana Mwenyezi Mungukwa kuniwezesha leo hii kuchangia kwa maandishi. Pianimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa hotuba yake mbeleya Bunge lako Tukufu.Mheshimiwa Spika, maendeleo ya Taifa loloteulimwenguni yanahitaji kuwepo kwa umeme wauhakika. Sasa ni vyema kabisa kujikita kwa nguvu zoteza kitaifa kupambana na mambo yafuatayo:-Mheshimiwa Spika, kwanza, kupata umeme wauhakika. Nchi nyingi sana zilizo makini wanaweka seraya umeme (power) kuwa ni jambo la kwanza la Kitaifa.Nasema hivi kwa sababu bila ya kuwa na umeme wauhakika, Serikali haiwezi kuleta mapinduzi ya viwandana kwa maana hiyohiyo hatuwezi kuleta mapinduzi yakilimo na hivyo uchumi wote wa Taifa utakuwa nimdogo. Kwa maana hiyo, naiomba Wizara hii kuliona

hili na kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa umemewa uhakika.Mheshimiwa Spika, pili, uchimbaji wa madini namikataba. Madini ni utajiri mkubwa katika Taifa letu.Jambo la msingi ni kuanza kujikita na kujipanga upyakupitia Sheria za Leseni za Uchimbaji pia kupitiamikataba ya wachimbaji ili mikataba hiyo iwe kwamaslahi ya Taifa.Mheshimiwa Spika, ndani ya Wizara hii, uko ufisadimkubwa sana. Mheshimiwa Waziri ni vyema sanakupitia kila sekta ili kuhakikisha ufisadi uliopo ndani yaWizara hii unakomeshwa kabisa.Mheshimiwa Spika, tatu, gharama za umeme.Bado gharama za umeme kwa watumiaji ni kubwamno, hailingani na pato la wastani la Watanzania. Sionisababu ya maana kwa nini nchi zilizoizunguka Tanzaniaumeme ni rahisi ukilinganisha na Tanzania. Pia mafutani rahisi katika Mataifa hayo kuliko Tanzania. Hiiinatokana na viongozi katika Wizara hii kukosauzalendo na hivyo kuangalia ubinafsi zaidi. Kwa hiyo,naiomba Wizara hii kupitia Waziri kupunguza gharamaza umeme mara moja.Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.MHE. DKT. TITUS M. KAMANI: Mheshimiwa Spika,napenda kumpongeza Waziri na Manaibu wake,Katibu Mkuu na timu ya Wizara iliyokubali nakudhamiria kuleta mageuzi ya nishati katika nchi yetuna pia kuifanya Tanzania inufaike na utajiri wake

mkubwa wa madini, naomba msilegeze uzi. Hatahivyo, naomba sana mliangalie suala la kupelekaumeme vijijini kwa uzito mkubwa. Hii ni kutokana naukweli kuwa taasisi za elimu zilizopo vijijini kama vileshule za sekondari zinatoa elimu yenye upungufu kwavitendo kutokana na kutokuwepo umeme kwamatumizi ya maabara.Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya bajeti yamwaka uliopita 2011/2012, Serikali iliahidi kukamilishautekelezaji wa miradi ya umeme Jimboni Busega(zamani Wilaya ya Magu) lakini hadi sasa miradi hiyoinaendelea kwa kasi ndogo sana. Miradi hiyo ni:-(i) Nassa – Nyamikoma – Kalemelaunaotekelezwa na kampuni ya Symbion;(ii) Lamadi - Bariadi kupitia vijiji vya Mkula naLutubiga. Kuna hospitali kubwa Mkula, watekelezaji nikampuni ya NAMIS ikasimamiwa na TANESCO Bunda;(iii)Nyashimo - Ngasamo kwa ufadhili waBenki ya Maendeleo ya Afrika; na(iv) Mwanangi – Badugu - Busani kwa ufadhili waADB ukisimamiwa na TANESCO Magu/Mwanza.Transforma tu ndiyo ilikuwa ikihitajika. Wananchi wanamatumaini sana kwa miradi hii, naomba ahadi isiishiekuwa hewa.Mheshimiwa Spika, Mji Mdogo wa Lamadi, licha yakuwa na umeme katika maeneo ya biasharakandokando ya barabara, kuna maeneo makubwa ya

makazi hayana umeme, hii ni pamoja na kijiji jirani chaLukungu ambapo wananchi kwa ushirikiano na wadauwa maendeleo tumejenga kituo kikubwa cha watotowenye mahitaji maalum ambacho hakina umeme.Tunaomba kupitia mipango ya Wizara ifanye harakakuvipatia umeme vijiji hivi ambavyo ndivyo kitovu chauchumi katika Wilaya mpya ya Busega.Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Busega, tunazotaarifa ya kuwepo hazina kubwa ya chokaa katikaKata za Shigala na Kabita, kampuni binafsi zimeanzakuchangamkia kukamata maeneo kwa kununua ardhikwa bei ndogo kwa wananchi. Tunaomba mwongozoharaka wa namna ya vijiji kuingia mikataba namakampuni haya ya wachimbaji. Hali kama hiiimejitokeza kwa kampuni ya Kichina katika kijiji chaNgongoko, Kata ya Malili. Tusipelekee wananchi wetukwenye umaskini.Mheshimiwa Spika, Serikali inazo taasisi nzuri sanaza madini GST, STAMICO na Chuo cha Madini, naombataasisi hizi ziimarishwe ili ziweze kulinufaisha Taifa.Ziongezewe rasilimali fedha, watumishi na vifaa iliwaweze kufanya vizuri hasa katika kipindi hiki ambaposekta ya madini inakua na kasi. Chuo cha Madiniambacho binafsi nimekitembelea, kinahitajikuboreshwa haraka ili kiweze kuongeza udahili kwakukiongezea mabweni, bwalo na madarasa. Piakipewe uwezo wa kuajiri Wakufunzi na kuwasomeshazaidi waliopo. Napongeza mpango wa kuanzishamtaala wa mafuta na gesi katika chuo hicho. Naombapia kiwe na mafunzo ya muda mfupi ili kuwafundisha

wachimbaji wadogowadogo nchini ili waboreshembinu za uchimbaji.Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Busega naBariadi Magharibi, kumegunduliwa pia hazina kubwaya madini ya nickel katika milima ya Ngasomo naDutwa. Hadi sasa hofu imeanza kutanda katika vijijivinavyozunguka maeneo haya jinsi gani wananchiwatafidiwa kwa kuondolewa katika maeneo yao.Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali isije ikaingiakwenye mtego wa wawekezaji na kuwalipa fidiakiduchu wananchi na kuwaachia umaskini.Ikiwezekana wananchi wapewe ubia katika migodi hii.Hivi sasa tayari hata zile kazi ndogondogozimeshapewa watu wa mbali na maeneo ya Ngasomoau Jimbo la Busega. Hii ni kinyume cha Sheria yaUwekezaji wa Madini. Naomba hali hii irekebishwemara moja na isiruhusiwe kutokea pale uwekezaji kamiliutakapotokea. Naomba sana eneo la Ngasomo naJimbo la Busega liepushwe kuwa Nyamongo nyingine.Pale Ngasomo pia kuna wachimbaji wadogowadogowa dhahabu. Wachimbaji hao hawagusi eneomuhimu la nickel lakini tayari wameanza kuhofishwa namwekezaji.Mheshimiwa Spika, nashukuru sana Waziri naNaibu wake kwa msimamo wa kulinda wachimbajiwadogowadogo kama alivyoongea nao kwenye kikaocha Dodoma na pale nilipowaleta kuongea nawataalam wa Wizara kwenye ofisi ya madini.

Mheshimiwa Spika, naomba sana Wizara isimamievizuri uwekezaji wa nickel pale Ngasomo.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. SABREENA H. SUNGURA: Mheshimiwa Spika,napenda kupata majibu kwa nini Afisa Madini waMkoa wa Kigoma anashindwa kukusanya na kuzibanakampuni zinazochimba madini katika Kata ya IlagalaMkoani Kigoma katika Halmashauri ya Wilaya yaKigoma na Kapala Msenga? Kwa kuwa ni zaidi yamiaka thelathini madini hayo hayalipiwi service levywala mrahaba, nataka kauli ya Waziri.Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itauunganishaMkoa wa Kigoma na gridi ya Taifa ili vile viwandaendelevu na ambavyo ni powerful viweze kuanzishwaMkoani humo.MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: MheshimiwaSpika, naomba kumpongeza Mheshimiwa Waziri naMheshimiwa Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watendajiwao wote kwa hotuba nzuri inayotekelezeka nainayotia matumaini.Mheshimiwa Spika, kwa shukrani za pekee,naishukuru Wizara ya Nishati ya Tanzania Bara kwakuisaidia Zanzibar kupata umeme wa uhakika kwakupitia Baharini kwa manufaa ya Wazanzibar wote.Mheshimiwa Spika, jambo zuru lazima lipongezwena kumsaidia mwenzio lazima ushukuriwe. Hivyo katikaukurasa 88 - 89 imetoa picha nzuri ya punguzo la

kuunganisha umeme mjini na vijijini kwa punguzokubwa. Huo ndio mwanzo mwema kwa Wizara nawateja wake na hii inaonesha kwamba sasa Wizaraimepata uongozi uliokomaa.Mheshimiwa Spika, hata hivyo, naomba Wizara yaNishati Tanzania Bara nayo kuishauri Serikali yaMapinduzi Zanzibar kufuata mfano huo mzuri wakuisaidia jamii ya Wazanzibar wakati ule mtapokuwana vikao vya pamoja vya mashirikiano baina yaTanzania Bara na Tanzania Visiwani.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Spika, kodi yamapato, kauli ya Waziri kuhusu migodi kulipa kodi yamapato, ni kauli ambayo haiwajawahi kutolewa nakiongozi yeyote wa Serikali na ni kauli ya kuungwamkono na kila Mtanzania mzalendo. Lazima kampunihizi zilipe kodi stahili, kodi na tozo zote, msimamo huuusitetereke hata kidogo.Mheshimiwa Spika, pamoja na hatuazinazochukuliwa na Serikali dhidi ya ubadhirifu katikaShirika la TANESCO, kuna masuala yanapaswakuangaliwa pia. Mfano wakati ni kweli kwambaTANESCO inapata Tanzania shilingi bilioni 60 naTanzania shilingi bilioni 70 kwa mwezi na kwambamishahara ni Tanzania shilingi bilioni 11 tu, badoTANESCO inatumia fedha nyingi sana kununua umemekutoka IPPs. Mfano taarifa ya CAG ya mwaka 2010inaonyesha kwamba wakati TANESCO walitumiaTanzania shilingi bilioni 39 kama ‘staff costs’, Shirika

lilitumia Tanzania shilingi bilioni 212 (45% of all revenuesfrom TANESCO) kununua umeme kutoka wauzajibinafsi. Suala hili halijitokezi kwenye hoja za Serikali,mikataba mibovu ndio kiama cha TANESCO, mikatabahii ipitiwe upya.Mheshimiwa Spika, Malagarasi Hydro. Mradi waumeme wa maporomoko ya Malagarasi, ni muhimusana kwa Mikoa ya Kigoma na Katavi. Naishauri Serikaliitekeleze mradi huu kwa haraka kwa kushirikisha taasisiza umma ndani ya nchi. Mradi huo pia unapaswakuwianishwa na mradi wa ‘transmission’ ili umemeutakaozalishwa Malagarasi uweze kuingia kwenye gridau kuweza kuusambaza kwenye Mkoa wa Kigoma naKatavi.Mheshimiwa Spika, Mererani, ninashauri kwambaeneo la Mererani liwe eneo maalum la Kiserikali kamailivyo machimbo ya Almasi kule Botswana. Nashaurikwamba Botswana model itumike kwenye Tanzanite ilikuwezesha nchi kufaidika na madini hayo ya vito. Kwakuwa leseni ya Tanzanite One imemalizika na Sheria yaMadini ya mwaka 2010, imetaka vito kumilikiwa naWatanzania, nashauri Watanznia hao wawe Serikali auShirika la Serikali. Tuunde ‘Debtswave’ yetu kwenyeTanzanite ili kulinda, kuhifadhi na kudhibiti biashara yavito vya Tanzanite. Leseni zote za Tanzanite ziwe chiniya Serikali na iundwe kampuni yenye hisa za Serikali50% na ‘strategic investor’ 50%, Botswana modelitatusaidia Mererani.MHE. ABDUL J. MAROMBWA: Mheshimiwa Spika,awali ya yote, napenda kuunga mkono hoja iliyo

mbele yetu. Katika hotuba hii yenye uwazi mkubwa,imeonekana dhamira sahihi ya viongozi wa Wizarakatika kuisimamia. Nawaomba viongozi wa Wizarawaweze kusimamia ipasavyo haya yote yaliyoandikwaili yatekelezwe kwa ukamilifu.Mheshimiwa Spika, pamoja na kuunga mkonobado kuna changamoto nyingi ambazo inabidiSerikali/Wizara iziangalie kwa mapana yake ilikuhakikisha kuwa kasoro hizo zinamalizika. Miongonimwa changamoto hizo ni hizi zifuatazo ambazozinahusu Jimbo la Kibiti na Wilaya ya Rufiji kwa ujumlawake.Mheshimiwa Spika, wakati wa uwekwaji wabomba la gesi toka Somanga na Dar es Salaammwishoni mwa miaka ya 1990, Songas kwa kushirikianana Wizara ya Nishati na Madini waliingia mikataba navijiji vyote ambavyo bomba hili litapita kwambawatapewa huduma mbalimbali za kijamii pamoja naumeme. Naishukuru Serikali kuwa hilo limefanyikaingawa si kwa asilimia mia. Kwa mfano, katika Jimbo laKibiti, bomba la gesi limepita kwenye vijiji zaidi ya nane(8) lakini hadi leo hii ni vijiji vitatu tu kati ya vijiji 68 vyaJimbo la Kibiti vina umeme. Vijiji hivyo ni Kibiti Mchukwi(Mchukwi hospital) pamoja na Bungu. Hata hivyo, vijijivyote hivyo vitatu mahitaji ya umeme ni makubwamno na wananchi waliounganishiwa umeme si zaidi ya2%.Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali iangalie sualahili kwani maombi ya kuunganishwa umeme yapomengi kwa Afisa wa TANESCO Ikwiriri lakini utekelezaji

ado hauridhishi. Kwa mfano, mwezi May mwaka huukatika kijiji cha Kibiti, nguzo 12 zimeteremshwa lakinikinachoendelea hakijulikani, nguzo hizi zitaendeleakutosimikwa hadi lini? Nini sababu zinazosababishakuchelewa kwa mradi huu ambao tayari Serikaliilikwishaukubali?Mheshimiwa Spika, kwa kuwa umeme umefikaKibiti sekondari, ni vizuri kwa Serikali kuwaunganishiaumeme wananchi wa Kinyanya na Mtawanya badalaya umeme huo kutumika kwa shule hiyo pekee.Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni katika kijiji chaMchukwi, ni kweli umeme umepita katika kijiji hiki lakinini hospital ya Mchukwi pekee imepata umeme. Ni vizuribasi wananchi wa kijij cha Mchukwi A piawakaunganishwa kwani kuna shule mbili ya msingi nasekondari, zahanati pamoja na nyumba za wananchi,maombi tayari yapo TANESCO.Mheshimiwa Spika, katika mkataba wa Songas,vijiji vya Kata ya Mjawa (Jaribu Mpakani, Uponda naMjawa) vilivyopitiwa na bomba la gesi navyoviliahidiwa kupatiwa umeme lakini hadi sasa vijiji hivyovyenye wakazi zaidi ya elfu kumi na tano havijapataumeme. Mwaka jana aliyekuwa Mkurugenzi waTANESCO aliahidi kuwa; kwa umeme umefika Bungukm.8 toka Jaribu Mpakani, TANESCO itapeleka umemehapa kwa mwaka wa fedha 2012/2013 lakini hakunachochote kinachoendelea. Naiomba Serikali iangalieupya suala hilo kwa kuwapelekea umeme kabla yakuanza kupitisha bomba la gesi linguine. Wananchi waKata hii wamechoka na ahadi hewa zinazotolewa na

Serikali kuhusu kupelekewa umeme. Wananchi hawawamesema hawatakubali kupitisha bomba llinginekama umeme hautapelekwa.Mheshimiwa Spika, suala lingine ni upelekaji waumeme Nyamisati kwa kuwa tender ilikwishatangazwa,nilitaka kujua hadi sasa wamefikia wapi? Lini utekelezajiwake utaanza?Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. ENG. ATHUMANI R. MFUTAKAMBA:Mheshimiwa Spika, Jimbo la Igalula mwezi June 201lilithibitishiwa na Bunge (iko kwenye Hansard) na piahotuba ya Rais, Mheshimiwa Dkt. Jakaya MrishoKikwete ahadi aliyoitoa tarehe 29/10/210, Ilolwansimba,Uyui, Tabora kwamba Wizara kupitia Wakala waUmeme Vijijini (REA), vijiji vifuatavyo vitapatiwa umeme.Goweko, Nsololo, Imalakaseko, Kigwa A, Kigwa B naIgalula. Naomba sasa kwa niaba ya wananchi waIgalula kupitia bajeti hii, mradi hii ya umeme ikamilike.Mheshimiwa Spika, mitambo ya Kinyerezi II - Mw240, gharama dola za Marekani milioni 432 (691.2bilioni). Hii gharama ni kubwa kwa ukokotoaji wakimkataba, uhandisi, ununuzi, manejiment (EDCContract). Sheria ya Dole Gumba (Rule of Thumb) nikwamba Kimataifa MW 1 (kwenye EDC) ni sawa na$milioni moja. Hivyo basi MW 240 ni sawa na $240milioni angalau $300 lakini siyo $432 labda kama kunaziada ya miundombinu, Wizara itoe maelezo.

Mheshimiwa Spika, bei ya mwisho ya umeme kwamlaji hukokotolewa kwa kuangalia maeneo mawili,capacity charge, inaangalia gharama za ujenzi wamitambo kama ulipaji mkopo au urudishwaji wauwekezaji (return on investment), utility charge(gharama au malipo kufuatana na kiasi cha umememteja anavyotumia). Hivyo basi, kama gharama yaujenzi ni kubwa ($432m) maana yake umemeunaozalishwa utakuwa ghali kwa kipindi cha uhai wamradi (project life cycle), bei hii itazamwe kwa makini iliumeme ukuze uchumi na siyo kuwa mzigo kwabiashara/viwanda na watumiaji wa majumbani.Mheshimiwa Spika, madini mengi yanayochimbwanchini yanaongezewa thamani Jaipur India(Tanzanite), Thailand (vito) na kwingineko, ajira na patokubwa vinapotea nchini. Wizara ishirikiane na Wizara zaViwanda na Biashara na Masoko na Wizara yaUwekezaji na Uwezeshaji ili viwanda hivi vijengwe hapanchini kwa ubia na makampuni ya nje. Mikatabaiingiwe na maduka makubwa katika majiji makubwaDuniani ili vito, mikufu, bangili, pete, herein, vidani,shanga vitengenezwe hapa Tanzania na kufaidishahata wachimbaji wakubwa na wadogo hapa nchinina wachenjuaji madini na masonara, bei zitawekwahapa Tanzania. Matangazo kwa bidhaa hizi sasayatasomeka katika mitandao, magazeti, television nasehemu za maduka ya mitindo Duniani mfano Paris,New York, London, Dar es Salaam, Hongkong, LosAngeles, Bervelly Hills na Casablanca.Mheshimiwa Spika, Loya, Tura, Nsololo, Goweko niKata zilizo Jimboni Igalula. Ziko kila dalili za gesi, petrol

(Iwembele swamps), madini ya dhahabu, almas na vitokatika maeneo haya. Naomba Wizara ifuatilie maeneohaya ili wachimbaji wakubwa na wadogo wawezekufaidika.Mheshimiwa Spika, fedha za vinasaba sasa simuhimu kwa sababu ya bei ya mafuta ya taa sasa ikojuu hivyo, hakuna uchakachuaji. Shilingi bilioni mbilinaomba ziletwe Igalula kupitia REA na kupelekaumeme vijiji zaidi ya sita vya Tura, Malongwe, Loya,Lutende, Miyenze na Miswaki (Mpyagula), shilingi bilionisita zipelekwe Majimbo mengine yanayohitaji umeme.Mheshimiwa Spika, Wizara iendelee kufanya kazikwa karibu zaidi kwa miradi ya Mchuchuma, makaa yamawe-umeme), Liganga (chuma) inayoongozwa naWizara ya Viwanda na Biashara na Masoko na ujenziwa bwawa la Stiegler’s Gorge MW 1200 chini ya Wizaraya Kilimo, Chakula na Ushirika. Wizara itumie utaalamna uzoefu na taasisi zake (TANESCO) ili umemeuzalishwe kitaalam na kufaidisha nchi na wananchi.Ikibidi miradi ya umeme ishughulikiwe na Wizara mamaya Nishati na Madini.Mheshimiwa Spika, Kiwira, deni la shilingi 40 bilioni,mabenki shilingi 37 bilioni yalipwe. Management fee yashilingi 8 bilioni isilipwe kwani imeshindwa utekelezaji wamajukumu yake. Wahusika waitwe mbele ya Kamati yaNishati na Madini kutoa ufafanuzi kuhusu Kiwira Coal naTanpower Limited.

Mheshimiwa Spika, kampuni ya Pan African Energyilipe $20.1 milioni pamoja na riba wanazodaiwa naSerikali, kodi waliyokwepa.Mheshimiwa Spika, wananchi wapewe sharestujenge bomba la gesi.MHE. CAPT (MSF) JOHN Z. CHILIGATI: MheshimiwaSpika, awali ya yote, nampongeza Mheshimiwa Waziri,Manaibu Waziri na Watendaji wote wa Wizara hii, kwakazi nzuri wanayoifanya katika kusimamia utekelezajiwa shughuli chini ya Wizara hii. Pamoja na pongezi hizi,ninayo maoni na mapendekezo yafuatayo:-Mheshimiwa Spika, kwanza ni mradi wa umemeManyoni – Bahi. Naishukuru Wizara hi kupitia REA kwakwanza kutekeleza mradi huu. Chini ya mradi huu, vijijivyote 15 vinavyopitiwa na nguzo vinatakiwa kupataumeme lakini wakati mradi unakaribia kumalizika kamavijiji vitatu vimerukwa kuwekewa transformer, vijiji hivyoni Sukamahela, Mbwasa na Maweni. Je, kurukwa kwavijiji hivi ni bahati mbaya au imekusudiwa iwe hivyo?TANESCO waliahidi kuwa dosari ingerekebishwa lakinihakuna hatua iliyochukuliwa na REA wanajiandaakukabidhi mradi huu wakati vijiji hivyo havijaingizwakatika mpango wa kupata umeme. Naiomba Wizaraiwasukume REA warekebishe dosari ya kuruka vijiji vitatukabla hawajakabidhi.Mheshimiwa Spika, mbili, mradi wa umeme Iringa -Singida (400kv). Mradi huu umepita katika Tarafa tatuza Wilaya ya Manyoni, Kintiku, Kilimatinde na ManyoniMjini. Wananchi wanaopitiwa na mradi, mali zao

zimefanyiwa tathmini na baadhi wamelipwa. Hatahivyo, kuna wananchi 61 ambao ama hawajalipwakabisa au wamelipwa kwa kupunjwa kwa vile baadhiya mali zao hazikuingizwa katika ripoti ya uthamini.TANESCO wameandikiwa barua na MkurugenziMtendaji wa Wilaya ili walipe fidia hizo lakini badohawajalipa na wananchi hao 61 wanayo malalamikomakubwa.Mheshimiwa Spika, tatu, mradi wa umeme waupepo Singida. Mradi huu wa kutengeneza umemekupitia upepo (50 Mw) na wa pili 100 Mw, unaripotiwakila mwaka katika hotuba ya Wizara hii, sasa ni mwakawa tatu lakini utekelezaji hauonekani. Haya nimakampuni binafsi, kama kuna vikwazovinavyochelewesha mradi kuanza basi Wizara iingiliekati ili kuweka mazingira yatakayowezesha mradi huukuanza.Mheshimiwa Spika, nne, umeme wa jua (solarenergy). Hotuba ya Wizara haikutoa uzito kuhusuchanzo hiki cha umeme. Wizara itafaa iweke mpangomahsusi wa kuwezesha chanzo hiki cha umemekutumika hasa vijijini. Tatizo la chanzo hiki ni bei kubwaya vifaa vyake. Serikali iondoe kodi katika vifaa hivyo iliwananchi wa kawaida vijijini waweze kuvinunua nakunufaika na umeme wa jua.Mheshimiwa Spika, tano, wachimbaji wadogo wamadini (Londoni). Tunashukuru kwa Serikali kuwekautaratibu wa kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogowa Londoni kupitia kampuni ya Tan Discovery MineralConsillincy. Tatizo lililopo sasa ni utoaji na utengaji

maeneo kwa wachimbaji wadogo. Tunaomba Serikaliitenge maeneo mahsusi kwa ajili ya wachimbajiwadogo na kuwapa leseni.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii.MHE. ROSWEETER F. KASIKILA: Mheshimiwa Spika,namshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema yoteanayotujalia. Nikushukuru nawe binafsi kwakutuelekeza tunapopotoka wakati wote ndani na njeya vikao. Nimshukuru Waziri mwenye dhamana,Manaibu Mawaziri, Katibu na Watendaji wote katikaWizara hii, kwa hotuba nzuri lakini kwa mipango yaomizuri ya 2012/2013 ambayo inaonyesha sasainakwenda kuleta mapinduzi ya maendeleo Tanzaniana hasa kwa wananchi wa Mkoa wa Rukwa.Mheshimiwa Spika, umeme wa genereta (Rukwa).Mkoa wa Rukwa specifically Sumbawanga Mjini, tanguenzi na enzi wamekuwa wakitumia umeme mdogokutoka Mbala na Zambia ambao umekuwa haukidhihaja na kwa hiyo ukawa supplement na umeme wagenerator ambao umekuwa ukitumika kwa matumiziya nyumbani ambapo pia imekuwa ikifika sasa nneusiku unakatika mpaka kesho yake (mara nyingi), marachache umeme umekuwa ukiendelea kuwaka mpakaasubuhi.Mheshimiwa Spika, umeme huu hautoshi kuletamaendeleo Mkoa wa Rukwa. Katika mgao wa fedhaza Serikali, Mkoa wa Rukwa tumekuwa tukiwa karibu namwisho mwa orodha ya Mikoa yote kwa vigezoambavyo ni kutokuwa na vivutio vya maendeleo.

Maendeleo ya Mkoa wa Rukwa hayatakuwepo kwakuendelea kuwa na umeme wa generator ambao piauna serve population ndogo sana ya SumbawangaMjini na siyo kwa wakazi wote wa Sumbawanga Mjini.Mheshimiwa Spika, utajiri wa Mkoa wa Rukwa,hakuna Mkoa tajiri hapa nchini kama Mkoa wa Rukwalakini ndio Mkoa maskini kuliko yote hapa nchini.Nasema hivyo kwa sababu, kilimo Mkoa wa Rukwaunalima mahindi kwa kiwango cha kulisha Mikoa yotehapa nchini. Si hayo tu, hata alizeti, ufuta, karanga namaharage. Mkoa unatakiwa kusaga na kusindikaunga, mafuta, maharage na kadhalika. Mkoaunatakiwa kusindika minofu na samaki wa ZiwaTanganyika na Rukwa. Mkoa unatakiwa kuchimbamadini ya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na makaaya mawe tuliyonayo.Mheshimiwa Spika, umeme wa grid ya Taifa. Mkoawa Rukwa kwa muda mrefu tumeahidiwa umeme wagrid ya Taifa unaotoka Nyakanazi -Kigoma - Katavi -Rukwa – Tunduma - Mbeya – Makambako – Iringa. Nikwa kuupata umeme huu na barabara itakapoisha,tutakapojengewa kiwanja cha ndege, tutawezakupata wawekezaji ambao wameshaanza kuonyeshania pamoja na wawekezaji wenyeji, tutaanzisha nakuendeleza viwanda vikubwa vitakavyoletamaendeleo makubwa kwa wananchi wa Mkoa waRukwa na kuinua uchumi wa Mkoa wa Rukwa naTanzania kwa ujumla. Viwanda hivyo vitasaga nakusindika unga wa mahindi, ngano, mafuta ya alizetina ufuta na kadhalika. Vitasindika minofu na samaki

watamu wa Ziwa Tanganyika na Rukwa, vitachimbamadini ainaaina pamoja na makaa ya mawe.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Spika,napenda kuchukua fursa hii kuipongeza Wizara yaNishati na Madini, kwa kazi nzuri inayofanywa kwa bidiina kwa utaalamu. Nampongeza Waziri, NaibuMawaziri, Katibu Mkuu, Wakuu wa Mashirika chini yaWizara pamoja na watumishi wote.Mheshimiwa Spika, naomba kumuuliza Waziri,Naibu Mawaziri na Katibu Mkuu, atueleze ni liniwatatekeleza ahadi ya vijiji au maeneo 10 kwa Wilayakuunganishiwa umeme? Mbona utekelezajiunasuasua?Mheshimiwa Spika, napenda kuona mikatabaiangalie pale inapotokea prospecting rightszinavyouzwa kwa bei kubwa kuliko gharama yaprospecting. Tuangalie Uganda ilivyonufaika baada yakudai haki yake Mahakamani, prospecting rights yamafuta ya petrol yalivyouzwa kwa faida kubwa ili nasitunufaike.Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri tuone kuwaresource for equity production sharing iangaliwe.Wawekezaji wanapokuja na mitaji iwe ndiyo share yaona nchi yetu shares zake zitokane na resources zetukama gesi, dhahabu, mafuta na kadhalika. Inabidituangalie upya dhana inayotumika. Ikiwa hatunafedha za kufanya prospecting, tunaweza kuruhusu

wawekezaji wafanye prospecting lakini baada yahapo gharama hizo ziwe capitalised ama sivyotutafute fedha zetu kufanya prospecting.Mheshimiwa Spika, ahsante.MHE. DKT MARY M. MWANJELWA: MheshimiwaSpika, awali ya yote, naunga mkono hoja hii nakumpongeza Mheshimiwa Waziri, Manaibu Waziri wawilipamoja na Katibu Mkuu, Ndugu Maswi ambaye kwakweli kwa uzalendo wake na kwa maslahi ya nchi,amethibitisha kuwa anaweza. Pamoja na pongezi hizohapa juu hata hivyo ningetaka haya machache kwaleo nipatiwe majibu ya kina.Mheshimiwa Spika, mgodi wa Kiwira Coal Mine.Naipongeza Serikali kurudisha mgodi huu STAMICO.Kwa mantiki hiyo, ninaamini STAMICO watatumiazabuni ya uwazi kwa kuzingati sifa na vigezo ili kumpatambia anayestahili na kufaa.Mheshimiwa Spika, ninataka kujua katika historiaya kuingia ubia kati ya Serikali na Tanpower Resourcesilizingatia vigezo gani? Maana imepelekea mgodi huukuwa idle na kizungumkuti kwa Serikali kudhaminikampuni hii katika mkopo wa shilingi bilioni 16.9 nakushindwa still pamoja na riba kufikia shilingi bilioni32.19. Nahitaji kujua fedha analipwa nani kwa maslahiya nani na kwa nini? Vinginevyo waliohusika wotewachukuliwe hatua kali za wazi za kisheria na pesa hizoziende katika shughuli za kijamii kama afya, umemevijijini na elimu - vitendea kazi.

Mheshimiwa Spika, naomba nielezwe mikakati yaSTAMICO juu ya kuendeleza mgodi huo wa Kiwira niipi? Katika ripoti nzima ya hotuba ya Mheshimiwa Wazirisijaona mahali popote juu ya Mlima Kabulu ambao nisehemu ya mgodi wa Kiwira na hazina yake ni kubwakuliko ya Kiwira Coal Mine. Naomba nipatiwe maelezoya kina taratibu gani zilitumika katika kutenganishaleseni hizi mbili na what is the way forward on this?Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwakuongeza mrahaba royalty toka 3% to 4% namakampuni ya madini yenye mikataba kufanya hivyo.Hata hivyo, ningeshauri Serikali tena i-negotiate namakampuni yanayo exist na yenye mikataba iliSTAMICO iwe na hisa huko kama entity ya Serikali kulikokusubiri makampuni mapya ambayo hatuna uhakikanayo.Mheshimiwa Spika, pamoja na mrahaba lakini piakama Taifa katika madini tunategemea sanacorporate tax. Kodi hii inalipwa kijanjajanja tu hivyokulipotezea Taifa pato. Makampuni ya madini kilabaada ya muda fulani yanauza ama kubadilishamajina kwa nini? Corporate social responsibility zamakampuni ya madini in addition haziendani namapato wanayopata. Huu ni ujanjaujanja tu hivyoSerikali kutonufaika ipasavyo. Capital gain taxinakwenda wapi?Mheshimiwa Spika, sekta ya madini ni muhimusana katika Taifa hili. Nchi yetu ni mojawapo ya nchitajiri katika Afrika kwa madini lakini ndio nchimojawapo maskini Afrika, kwa nini? Mchango wa sekta

hii muhimu ya madini umekuwa sio wa kuridhishakutokana na upungufu mbalimbali kama unnecessarylobbying ambapo Taifa linapoteza mapato, mikatabamibovu na kadhalika. Nini mkakati wa Serikali katikakurudisha hali nzuri ya sekta hii ya madini in order?Tanzania inapenda sana wawekezaji na inaheshimulakini hii imekuwa nchi inayopoteza to the extreme,inatakiwa iwe win-win situation.Mheshimiwa Spika, Tume ya Mzee Bomani narecommendation zake zimefika wapi? Tunaboreshajesekta without this good governance withtransparency? Misamaha ya kodi - ubelievable!Mheshimiwa Spika, biofuel, kwa sasa Tanzania serayake haipo, isitoshe kwa muda huu tunapitia jambo lagesi ambalo nchi tunatakiwa kuwa makini sana,tuondokane na makosa yaliyotokea huko nyuma forwin-win situation, vinginevyo hao wawekezaji kamawanakuja kutunyonya bila national interest basi wasije,madini asili hayaozi. Biofuel haina faida kwaWatanzania, imeacha Watanzania devastated due totheir land grabbing na uongo kwa wawekezaji hao.Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha, naungamkono hoja.MHE. LAZARO S. NYALANDU: Mheshimiwa Spika,nampongeza Mheshimiwa Waziri na Manaibu Mawaziriwake kwa hotuba nzuri ya bajeti na naomnba kuungamkono hoja hii.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara kupitia REAwasaidie kupeleka umeme katika maeneo hayamuhimu Jimboni Singida Kaskazini. Maeneo kama yaIlongero - Msange – Mangida. Umeme huu uunganishepia shule za sekondari zifuatazo zilizo katika njia hii,Maghoja sekondari, Murigha girls sekondari,Madasenga sekondari pamoja na Mji Mdogo waMsange.Mheshimiwa Spika, eneo linguine ni Singida – Mgori– Ngimu - Pohama pamoja na shule zifuatazoMwanamwema sekondari, Ngimu sekondari naPohama sekondari.Mheshimiwa Spika, tunaomba Wizara iharakishemchakato wa kupatikana kwa umeme wa upepo kwakuanzisha mradi wa umeme Singida. Wananchi waSingida wanasubiri kwa hamu kuanzishwa kwa mradihuu na kusaidia kuleta ajira.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA: Mheshimiwa Spika,naipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayotia tumaini kwaWatanzania haswa suala la umeme. Umeme ni kitumuhimu sana kwa Taifa letu lakini uwezo wa wananchikumudu gharama ya kuingiza majumbani umeme nakulipa ankra za umeme ni kazi kubwa kulinganisha nakipato na hata aina ya nyumba za wengi wanazokaa,miundombimu haitoi nafasi nzuri ya wao kuwekaumeme huo.

Mheshimiwa Spika, nashauri Serikali ni vema ikawana mpango mbadala kwa wale wasioweza kufungaumeme wa TANESCO watumie solar na hizo solarzitolewe na REA na wananchi walipie polepole bilahivyo Serikali nia yake ya kuangaza nchi hii itakwamana hii itazua matabaka kwa wale walionacho nawasionacho.Mheshimiwa Spika, Wanamissenyi wengiwameshafanya taratibu zote za kuingiza umememajumbani lakini mpaka leo maeneo mengihawajapata umeme. Naomba kujua lini umeme huoutaletwa? Japo nimepokea barua ya kuwekewaumeme katika vijiji 24, lini kazi hiyo itaanza?MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika,nawapongeza Waziri na Naibu Mawaziri kwa kazi nzuriwanayofanya.Mheshimiwa Spika, Serikali inashughulikiajemashimo yanayoachwa wazi na wachimbaji wadogona wakubwa wa madini? Inasikitisha sana unapoonamashimo makubwa yameachwa, nini hatma yake?MHE. WILLIAM V. LUKUVI: Mheshimiwa Spika,kwanza naunga mkono hoja. Hatua za kupunguzagharama za kuunganisha umeme vijijini naiungamkono sana. Naomba ianze kutekelezwa haraka ilikupunguza gharama za maisha ya wananchi wa vijijini.Mheshimiwa Spika, nawapongeza sana REA kwakazi na kasi ya utendaji uliotukuka na mimi nitashiriki

kikamilifu katika kuisema REA ili iendelee kupata fedhanyingi za kutosha.Mheshimiwa Spika, naamini ratiba ya kuwekaumeme Tarafa ya Pawaga ili kuwasaidia wananchiwakulima wa mpunga kukoboa mchele kwa kutumiaumeme lakini pia kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Raisaliyoitoa mwaka 2009 na mwaka huu 2012alipotembelea Pawaga, itatekelezwa mwaka huu2012/2013.Mheshimiwa Spika, nawatakia kila la kheri KatibuMkuu na Watendaji wote, Mheshimiwa Waziri naManaibu wake katika kutekeleza Ilani ya Chama chaMapinduziMHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Spika,awali ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu kwakunijalia afya njema na kuweza kuchangia hoja hii.Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali,nawapongeza Mheshimiwa Waziri, Manaibu Mawazirina Watendaji wote wakiongozwa na Katibu Mkuu,Ndugu Eliakim Maswi.Mheshimiwa Spika, naipongeza sana Wizara yaNishati na Madini kwa uamuzi wa kupunguza gharamaza kuunganisha umeme hasa maeneo ya vijijini kwaasilimia 61.1. Aidha, naipongeza sana REA kwakuendelea na kazi ya kusambaza umeme katikamaeneo mbalimbali ya vijijini. Vilevile naipongezaSerikali kwa kukamilisha taratibu za mkopo kwa ajili yaujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara na Dar es

Salaam, ni kweli bomba la gesi litaleta mapinduzi yauchumi katika nchi yetu.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii.MHE. MANSOOR S. HIRAN: Mheshimiwa Spika,kwanza kabisa, naomba nichukue nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Sospeter Muhongokuteuliwa kuwa Mbunge na Mheshimiwa Rais na piakuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambayo niWizara nyeti. Pia nichukue nafasi hii kumpongezaMheshimiwa Masele na Mheshimiwa Simbachawenekwa kuteuliwa kuwa Manaibu Waziri wa Wizara hii.Naomba nimpongeze Waziri kwa kusimamia vizuriTANESCO na kuhakikisha mgao hakuna, pia kufuatiliaufisadi ndani ya TANESCO.Mheshimiwa Spika, umeme vijijini, MheshimiwaWaziri, wananchi wa Wilaya ya Kwimba hususanitaarifa ya Mwanashimba, upembuzi yakinifu (feasibilitystudy) ulishafanyika kuhusu upelekaji wa umeme MjiMdogo wa Hungumalwa na ginnery za Sangu naMwamala. Naomba mwaka huu umeme ufike, pia hiini ahadi ya Ilani ya Uchaguzi.Mheshimiwa Spika, leseni za madini, naombanichukue nafasi hii kuipongeza Wizara kwa maamuzi yakufuta leseni ambazo hazijafanyiwa kazi kwa mudamrefu. Pia sio hiyo tu kuna makampuni yamehodhimaeneo makubwa sana wakati uwezo wake wakuyatumia maeneo yote hayo haina lakini amelaliamaeneo ambayo wananchi wengi wanatakawayafanyie kazi.

Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hii kushauriyafuatayo kwa huu uagizaji wa mafuta ya pamoja.(i)EWURA wapange cap price kwenye mauzoya mafuta ya diesel inayouzwa kwenyemigodi hii;(ii) Mafuta ya Jet-AI, yanayouzwa kwenyeviwanja vya ndege yapangiwe cap price nausimamiwe kwa karibu. Hiyo Jet-AI inaweza kuuzwakama kerosene na huku tunafahamu Jet-AI hailipi kodi;(iii) Market share ya makampuni ya mafutaitumike na EWURA ya mafuta ambayo wanayapangiakwenye cap price; na(iv) Mafuta ya transit yalipe windfall tax wakatiwanataka ku-localize.Mheshimiwa Spika, TANESCO, napongeza kwamaamuzi ya Wizara ya kupunguza gharama yakuunganisha umeme vijijini na mjini. Napongeza piakwa maamuzi ya kusimamisha uongozi wa juu waTANESCO kwa sababu ya ufisadi.Mheshimiwa Spika, gesi, naipongeza Serikali kwakuamuwa kujenga bomba ya kusafirisha gesi kutokaMtwara kuja Dar es Salaam.hii.Mheshimiwa Spika, mwisho, naunga mkono hoja

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono hoja kwa asilimia mia kwa mia.Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwetekwa kumtafuta Waziri wa Nishati na MadiniMheshimiwa Profesa Sospeter M. Muhongo na kumteuamtu huyu muhimu kwa Taifa letu hili. Hakika kwa dhatikabisa Wizara imepata watu na siyo watu wamepataWizara. Nawapongezeni sana Waziri na Manaibu wotewawili Simbachawene, Masele, hakika kabisa Wizaraimepata watu na mafiga matatu kweli yamekamilikakatika Wizara hii.Mheshimiwa Spika, natoa angalizo (ulinzi),kutokana na mafisadi waliopo katika nchi hii, watuwafuatao wapewe ulinzi mkali sana; Waziri wa Nishatina Madini, Mheshimiwa Profesa Sospeter MwijarubiMuhongo, Katibu Mkuu wa Wizara, Ndugu Eliakim C.Maswi na Manaibu Waziri wote wawili ili wawezekutenda kazi yao vizuri.Mheshimiwa Spika, naomba Waziri atakapokuwaanafafanua hoja, anieleze juu ya mambo yafuatayo:-Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itapeleka umemeLaela, Mji Mdogo kupitia vijiji vyote toka Sumbawangahadi Laela? Waziri atakumbuka Mji huu ndiyoumependekezwa kuwa Makao Makuu ya Halmashauriya Kwela, naomba nipatiwe majibu. Aidha,atakumbuka Jimbo lote la Kwela hakuna hata kijijikimoja kilicho na umeme.

Mheshimiwa Spika, umuhimu wa kupeleka umemeUkanda wa Ziwa Rukwa. Ukanda huu umekuwaukisahaulika katika huduma muhimu japokuwa ni eneolenye uchumi mkubwa na shughuli zinahitaji sanaumeme. Eneo hili lina tarafa mbili kubwa, Tarafa yaMtowisa na Tarafa ya Kipeta. Pia inavyo vijiji 50 vikubwana kata saba (7) kubwa za mfano wa miji midogo kwamajina kama ya Mfinga, Muze, Mtowisa, Milepa,Ilemba, Kaoze, Kipeta.Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Wazirianipatie maelezo ni lini maeneo hayo yatapatiwaumeme? Vilevile naomba majibu ni lini kijiji chaSakalilo kitapatiwa umeme ili mradi wa umwagiliaji uwena manufaa kwa wananchi kwa kufunga mashine zakukoboa mpunga?MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika,naanza kwa kuunga mkono hoja iliyoletwa mbele yetu.Aidha, baada ya kuunga mkono hoja, naombanichangie baadhi ya maeneo kama yafuatayo:-Mheshimiwa Spika, kwanza ni uwepo wa umemewa uhakika na uunganishaji wa Mikoa isiyo kwenyegridi ya Taifa. Ni ukweli usiopingika kwamba bilaumeme wa uhakika, hakuna maendeleo kwani bilaumeme hakuna uwekezaji unaoweza kufanyika.Naipongeza Serikali kwa kulitambua hili na kuanzampango wa kuunganisha umeme wa gridi ya Taifakuanzia Nyakanazi kwenda Kigoma, Kigoma kwendaMpanda, Mpanda kwenda Sumbawanga,Sumbawanga kwenda Tunduma, Tunduma kwenda

Makambako, Njombe hadi Iringa. Njia hii niliyoitajaitachangamsha ukuaji wa uwekezaji na kuchocheaukuaji wa uchumi kwa Mikoa ya Iringa, Kigoma, Katavi,Ruvuma, Mbeya na Njombe.Mheshimiwa Spika, pamoja na nia njema yaWizara ya kuhakikisha kwamba nishati ya umeme yauhakika inasambazwa nchi nzima, ni vizuri vyanzovingine vya kuzalisha umeme zisipuuzwe. Katikamchango wangu wa kuzungumza na kuandika,niliainisha chanzo cha nishati kutoka makaa ya maweya Namwele yaliyopo Rukwa yakichimbwa namzalendo ambaye yuko tayari kuzalisha umeme nakuingiza kwenye gridi ya Taifa ili mradi apate uhakikakwamba kiasi cha umeme utakaozalishwa utanunuliwana TANESCO. Naomba Mheshimiwa Waziri mwenyedhamana atoe majibu kwamba mpango huu nautayari wa mzalendo huyu unaachwa hivihivi tu natukawa tunawavutia wawekezaji wa kutoka nje yanchi?Mheshimiwa Spika, Jimboni kwangu kuna chanzocha nishati kinachotokana na joto la ardhi. Hivyo,naiomba Wizara itume watalaam ili kufanya uchunguziwa kitaalam.Mheshimiwa Spika, pili napenda kuzungumziasuala la kusambaza umeme Wilaya zote nchini.Kwanza, napenda kupongeza nia njema ya Wizara yakuhakikisha kwamba Makao Makuu ya Wilaya zotezinafikiwa na nishati ya umeme. Pamoja na nia njemahii, napenda Wizara ikatoa kipaumbele kwa mijiambayo ni Makao Makuu ya Wilaya zote Tanzania.

Inatia unyonge pale ambapo Waheshimiwa Wabungewa baadhi ya Majimbo wanaongelea na kuomba vijijivyao vipatiwe umeme wakati baadhi yetu hatunaumeme hata Makao Makuu ya Wilaya achilia mbaliMakao Makuu ya Tarafa na Makao Makuu ya Kata. Ilituhakikishe maendeleo yanafika katika maeneo yetuyote ya nchi ni bora tukazingatia Makao Makuu yaWilaya zote zinafikiwa na umeme.Mheshimiwa Spika, tatu, ahadi za Mheshimiwa Raisna Makamu wa Rais. Kazi nzuri iliyoanzishwa na uongozimpya wa Wizara kwa maana ya Mheshimiwa Waziri naKatibu mpya ni vizuri pia wakakumbuka ahadi zaMheshimiwa Rais na Makamu wake ili kuendeleakuwajengea heshima viongozi wetu hawa kwawananchi. Naliandika hili kumkumbusha MheshimiwaWaziri kwamba katika Jimbo langu la Kalambo tulipatabahati ya kutembelewa na Mheshimiwa Makamu waRais aliyefika Tarafa ya Kasange mwambao mwa ZiwaTanganyika na kutuzindulia Soko la Kimataifa la Samakila Kasange na kujionea umuhimu wa kupatiwa umemekatika bandari na soko lile. Naiomba Wizara kuwekakatika mpango wa utekelezaji wa kufikisha nishati hiimuhimu kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Makamu waRais.Mheshimiwa Spika, nne, bulk procurement, uwekajiwa vijinasaba pamoja na ethanol. Bunge tulilazimikakupandisha bei ya mafuta ya taa ili kukabiliana nauchakachuaji wa mafuta ya diesel na petrol.Inashangaza pamoja na hatua hii eti bado vinasabavimewekwa ili kuyatambua mafuta, huu ni wizi wa

mchana, ukomeshwe mara moja na Wizara badala yakuendelea kufuja pesa za walipa kodi wa nchi hii.Mheshimiwa Spika, katika mkataba wa kununuamafuta kwa pamoja, kuna kipengele kimewekwa chakuongeza ethanol. Kipengele hiki kimekuwa kikitumikavibaya kwa kuongeza ethanol nyingi hivyo kuwa naathari kwa mtumiaji na chombo chake na hasaukizingatia tabia ya ethanol inapokaribiana na maji nabei halisia ukilinganisha na bei ya petrol kwenye soko,ni vizuri clause hii ikaondolewa ili kuondoa malalamishikwa watumiaji.MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika,naunga mkono na ninampongeza Waziri, Katibu Mkuu,Bwana Maswi, najua vizuri utendaji wake wa kaziuliyotukuka tangu akiwa Hazina, naipongeza pia timuya Manaibu Waziri. Waziri simamia misingi ya haki,usitetereke, safisha nyumba yako imejaa uchafu, anziaWizarani shuka kwenye taasisi zilizo chini ya Wizara.Waziri simama kwa miguu yako, tembelea miguu yakouwe na msimamo, usiyumbishwe na nguvu ya pesa,yapo majaribu utapambana nayo ukizubaayatakuteka. Wizara hiyo imefukuzisha mpaka WaziriMkuu, pana mambo hasa upande wa mafuta, gesi nabaadaye uranium. Simama kidete na Munguakuongoze siku zote katika maamuzi yenye hekima nabusara ili tuijenge nchi yetu.Mheshimiwa Spika, naungana na Waziri katikamaelezo yote ya hotuba yake, naomba wajipangekwa utekelezaji ili bajeti ijayo waweze kutueleza

utekelezaji wa haya wameyatekeleza kwa asilimiangapi?Mheshimiwa Spika ukurasa wa 105 – 187,umezungumzia migodi kulipa kodi ya mapato, nchiinatakiwa inufaike na rasilimali zake na si kunufaishawawekezaji pekee, lisimamie ili migodi iweze kulipakodi stahili.Mheshimiwa Spika, naomba kukumbushia ahadiya TANESCO kuhusu kupeleka umeme kupitia Wakalawa Umeme Vijijini (REA) katika maeneo ya Tallo, Ibindo,Kadashi, Nyashama, Maligisu na Kabila Centre. Serikaliimekuwa ikiniahidi tangu bajeti ya mwaka jana nanimekuwa nikiuliza maswali ya mara kwa mara namara ya mwisho niliambiwa mradi huo unasubirikutangazwa ambapo zabuni ilikuwa zifunguliwe Meimwaka huu, je, umefika katika hatua gani? Pia kupitiaREA ilitaka iunganishe umeme kutoka Montare,Ishingisha, Mhulya, Ngulle na Nyamatale Wilaya yaKwimba. Waungwana siku zote ukiahidi tekeleza ahadikwani Serikali inaponiahidi Bungeni wananchi wanguwanasikia, lakini nami nikienda kufanya mikutanoyangu naahidi kufuatilia kauli ya Serikali.Mheshimiwa Spika, Waziri na Katibu Maswi nimajembe yenye uhakika, najua hawawezi kufanyamiujiza lakini wanaweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi,nidhamu katika maeneo wanayoyaongoza, watu sasawanafikia kutokujali wanatumia nyadhifa zaokujinufaisha, hawajali maslahi au dhamanawaliyokabidhiwa.

Mheshimiwa Spika, mimi ndiye niliyemwondoaaliyekuwa DG, Dokta Rashidi kwa matumizi mabaya yamadaraka. Tupo pamoja kama mtasimamia vizurirasilimali zetu tulizozawadiwa na Mwenyezi Mungu.Mheshimiwa Spika, nawatakia kila la kheri siyolazima wakati unahitimisha kuvitamka vijijinilivyoviainisha, naweza nikapewa majibu hata kwamaandishi.Mheshimiwa Spika, nawasilisha.MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: MheshimiwaSpika, kwanza napenda kuzungumzia kuhusu leseni zauchimbaji madini kwa wachimbaji wadogowadogo.Nchi yetu ya Tanzania imebarikiwa kuwa na ardhikubwa yenye madini ya aina mbalimbali mfanodhahabu, almasi, tanzanite, uranium, bauxite nakadhalika lakini cha kushangaza maeneo yote yenyemadini yamegawiwa kwa wachimbaji wakubwawenye mitaji mikubwa na kuwa ni laana kwawachimbaji wadogowadogo ambao wamezaliwakatika maeneo hayo. Badala ya kuwanufaishawananchi husika wenye eneo hilo maeneo ya madiniyamegawiwa kwa wawekezaji tena wengi wakiwa niwa kigeni, wawekezaji hawa hupewa leseni za utafitina hata kabla ya kumaliza utafiti wengine huanzakuchimba madini na kuyasafirisha nje kwenye nchi zao.Ni kwa nini Serikali haiwapi wachimbajiwadogowadogo leseni za kuchimba madini ili naowaweze kunufaika na rasilimali ya nchi yao?

Mheshimiwa Spika, pili ni kuhusu fidia kwawananchi. Kumekuwa na migogoro mikubwa yawananchi wanaoondolewa kwenye maeneo yaoyenye madini na ulipaji wa fidia kutokufanywa kamainavyostahili. Wananchi wangu mfano wa Mkoa waSingida, Wilaya ya Singida Vijijini, Mang‘onyi naSumbaru - Ikungi wanalalamikia unyanyasaji nausumbufu mkubwa wanaoupata toka kwa kampuniya Shanta Mining Co. Ltd. ambayo pamoja na kupewaeneo kwa kukiuka utaratibu bado kampuni hiihaijawalipa wananchi husika fidia waliyokuwawanadai. Nashauri Serikali ifuatilie mgogoro huu kati yaShanta Mining na wananchi wa Mang‘onyi Singidakuona uhalali wa wawekezaji hawa, ni matatizoambapo yamepelekea hata kujeruhiana hasa katikakijiji cha Sumbaru.Mheshimiwa Spika, tatu, faida ya umeme waupepo Mkoani Singida. Mkoa wa Singida pamoja nakuwa na hali ya nusu jangwa, umebarikiwa kuwa naupepo mwingi ambao una manufaa makubwa katikakuzalisha umeme wa upepo. Umeme wa upepoutasaidia sana katika utunzaji wa mazingira hasa katikaMkoa huo ambao ni jangwa na hivyo utapunguzauharibifu wa mazingira kwa kukata miti kwa ajili ya kunina mkaa. Naiomba Serikali iharakishe mchakato wakuleta umeme wa upepo ili kuokoa mazingira yetu navilevile kuinua kipato cha wananchi wa Mkoa waSingida ambacho kiko chini sana.Mheshimiwa Spika, nne, kashfa ya ununuzi wamafuta kwenye makampuni ya IPTL, SONGAS nakadhalika. Kwa kuwa kumekuwa na manung‘uniko

mengi na ukosefu wa maadili katika kutunza fedha aumatumizi ya fedha za umma, ni vizuri sasa ukafanyikauchunguzi mahsusi kupitia ofisi ya CAG ili kubaini nihasara kiasi gani TANESCO inapata katika ununuzi wamafuta ya kuendesha mitambo ya kufua umeme.Imeonekana kwamba kuna watu wasio waaminifukwenye Shirika ambao wanapenda umeme wadharura kwa maslahi binafsi wanayoyapata kwenyemakampuni husika.Mheshimiwa Spika, hii inapelekea hasara kubwasana na hivyo kupoteza fedha nyingi za walipa kodi wanchi hii. Kwa mfano, manunuzi ya mafuta toka IPTL naSymbion kwa mwezi yanakadiriwa kuwa ni shilingi bilioni42 na haya manunuzi yatagharimiwa kwa miezi mitano(5) kuanzia sasa. Sasa kwa manunuzi haya yamabilioni ya shilingi tutegemee nini kwenyemustakabali wa uhai wa Shirika la TANESCO na Taifakwa ujumla? Nashauri Serikali pia kufuata Sheria yaManunuzi ya Umma katika manunuzi yake.Mheshimiwa Spika, tano, wawekezaji wamakampuni ya uchimbaji madini. Nchi yetu haijawezakufaidika kwenye sekta ya madini kwani faidainayopatikana haitoshelezi kulingana na kiasi chamadini yanayochimbwa nchini. Makampuni yauchimbaji madini yamekuwa yakichukua mchanga nakuupeleka kwao kuufanyia utafiti ili kuona kama kunamadini. Swali, ni nani anafuatilia mchanga huo nakujiridhisha kwamba kiasi kinachotolewa namakampuni hayo ni cha kweli? Ni kwa nini uchunguzihuo usifanyike hapahapa nchini ili kujiridhisha sisi wenye

nchini? Huu mtindo haufai na badala yakeumeendelea kuliletea Taifa hasara kubwa.Mheshimiwa Spika, kama haitoshi, makampuni yamadini hayajafanya vya kutosha kutokana na kilewanachovuna. Wananchi walioondolewa kwenyemaeneo ya madini wameendelea kuwa maskini, kwasababu wawekezaji hawa wanatakiwa waendelezemaeneo waliyoyakuta na sio kufanya vituvidogovidogo kama ujenzi wa shule zisizokwisha.Mheshimiwa Spika, tunataka uwazi wa mikataba,miradi ya maendeleo kama shule za kisasa, umeme,barabara, hospitali, maji na nyumba bora za kuishiwafanyakazi. Ni kwa nini Tanzania haifanyi kama AfrikaKusini ilipotoa eneo lake lenye dhahabu kwawawekezaji na leo tunashuhudia mji mzuri ubaoitwaEgol the place of Gold? Kwa nini wachimbaji wamadini wa Tanzania wanaacha mashimo tu nakuchafua vyanzo vya maji kama ilivyotokea kuleNyamongo Mkoani Mara? Serikali ije na majibu yakutosha.Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.MHE. MATHIAS M. CHIKAWE: Mheshimiwa Spika,natangulia kuunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziriwa Nishati na Madini.Mheshimiwa Spika, naomba kumshauriMheshimiwa Waziri kuhusu suala la umeme vijijini.Wilaya ya Nachingwea ina umeme Makao Makuu yaWilaya kisha umeme huo unatoka Nachingwea na

kuelekea Rwangwa, ukipita juu ya vijiji kadhaa bila vijijihivyo kufaidi umeme huu. Naomba umeme ushukekatika vijiji vya Matangini, Ikungu, Rupota, Ruponda naMarambo. Wananchi hawaelewi kwa nini umeme huuupite tu juu bila kuwanufaisha wanakijiji hawa.Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hilo, narudiakuunga mkono hoja ya Waziri wa Nishati na Madini.MHE. RAMADHANI HAJI SALEH: Mheshimiwa Spika,napenda nichukue fursa hii kumshukuru MwenyeziMungu, Mwingi wa Rehma ambaye ametufikisha katikaBunge lako Tukufu tukiwa hali ya uzima.Mheshimiwa Spika, niaze kuchangia bajeti hiikatika upande wa madini. Tanzania ni nchi yenyemadini mengi lakini hadi leo bado hatujafaidika narasilimali hiyo. Kwa kuwa bado hatujachelewa katikakulinda rasilimali hiyo, Serikali ichukue hatua yakurekebisha Sheria ya Madini ili wawekezajiwasiondoke na madini na kutuachia mashimo.Mheshimiwa Spika, naomba nijikite katika upandewa gesi. Kama tutaitumia gesi vizuri, Tanzania itapatafedha nyingi na itaweza kupunguza hata deni la nje.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. HAMOUD A. JUMAA: Mheshimiwa Spika,mchango wa madini katika bajeti ya Taifa ni mdogosana. Hii inaleta hisia kwamba haya madini (utajiri) huutulionao ni wa kazi gani wakati wanaonufaika ni watuwengine tofauti kabisa. Hakika sisi kama Taifa au nchi

yetu imegeuka kabisa na kuwa shamba la bibi.Wawekezaji kutoka nje wameshatusoma nakutufahamu kiundani udhaifu wetu na sasa wanatumiaudhaifu wetu huu kuchuma mali yetu na kuondoka.Kila mtu anajua kwamba tunaibiwa katika sekta yamadini lakini cha kushangaza hatuoneshi mikakati yakuondoa hali hii. Wizara na Serikali kwa ujumlaimejipangaje kuhakikisha kwamba tunaepuka balaahili?Mheshimiwa Spika, suala la umeme wa uhakikalimekuwa kizungumkuti kisichoeleweka. Hadi sasa kunagiza nene katika Wizara hii ya kuondolewa kwaMtendaji Mkuu wa TANESCO na tuhuma za uwepo wamikataba ya kijanja kuhusu tenda za kusambazamafuta. Inaonekana wazi kuwa Wizara hii iko katikahali ngumu sana (haijatulia). Kutokana na mambo yotehaya, tusitegemee maendeleo yoyote kuletwa naWizara hii iliyoko katika hali tete. Maamuzi magumuyanahitajika ili kubadili hali hii na kunusuru nchi yetu.Mheshimiwa Spika, tusipojipanga vizuri katika sualazima la sera, uongozi, mikakati na kadhalika, utajiri wagesi unaoleta matumaini makubwa kwa kila Mtanzaniautageuka kuwa laana, watu wengi wanatahadharisha,nami naungana nao kutahadharisha juu ya jambo hili.Hatutapenda kuja kujuta baadaye kwani Waswahilihusema majuto ni mjukuu. Ni lazima sote tujielekezekatika kuwa na sera, mipango na sheria zitakazotulindana kutuongoza katika kuifaidi rasilimali hii kwa amani nautulivu. Tusipofanya hivi, itageuka laana na hakunaatakayefaidi.

Mheshimiwa Spika, sasa ni wakati wa kutamka bilawoga “Mikataba Mibovu Basi”, jamani imetosha sasa.Wataalam wetu nao ifike mahali waone kuwauzalendo ni muhimu sana, ubinafsi haufai kabisa katikamikataba ndani ya sekta ya madini. Mikataba mibovuinaashiria ulafi, ubinafsi, rushwa na mengine mengi kwawatumishi wasio waaminifu. Waziri na Manaibu wakewote ni wapya katika Wizara hii, tumieni nafasi hiyokujenga upya Wizara yenye kuleta tija na matumainikwa Watanzania.Mheshimiwa Spika, suala la uharibifu wa mazingirautokanao na uchimbaji wa madini nalo lisifumbiwemacho. Tunahitaji Tanzania endelevu kwa vizazi vingivijavyo. Siku hizi kuna dhana maarufu ya maendeleoendelevu ambayo huwezi kuitenga na utunzaji wamazingira. Ni lazima tuwe na mikakati thabiti yakunusuru mazingira yetu kwani madini yanaweza kuishaila mazingira yatabakia hadi mwisho wa nyakati.MHE. DKT. AUGUSTINE L. MREMA: MheshimwaSpika, naunga mkono hoja hii, ingawa Waziri ni mgeni,lakini kwa muda mfupi tumeridhika na hatuaanazochukua za kupambana na ufisadi katika Shirika laTANESCO na Wizara kwa ujumla.Mheshimiwa Spika, namwomba Waziri atatuesuala la kukatika umeme katika Wilaya za Rombo naMoshi Vijijini. Kukatikakatika kwa umeme mara kwamara kunaleta kero kubwa. Najua kuna kazi nzuriinayofanyika Makuyuni, Himo katika Jimbo langu laVunjo. Naomba wakati wa majumuisho uwaelezewananchi wa Rombo na Moshi Vijiji kutokana na

uwekezaji unaoendelea pale Makuyuni, Himowatanufaika lini na vipi?Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Vunjo kunamaeneo mengi ambapo TANESCO walipeleka nguzoza umeme katika maeneo hayo lakini kwa zaidi yamiaka mitano nguzo ziko palepale hazijachimbiwaardhini na wala hawajapeleka nyaya katika maeneohayo.MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika,naanza kwa kuunga mkono hoja. NampongezaMheshimiwa Rais Jakaya kwa uteuzi makini wa viongoziwa Wizara hii ya Nishati na Madini.Mheshimiwa Spika, pongezi kwa Waziri naManaibu Waziri wote wawili, kwa maoni yangu,naridhishwa na timu hiyo tangu imepatikana na kwamajukumu ya muda mfupi yaliyotekelezwa lakini piakwa namna mlivyopanga hotuba hii ya bajeti ya2012/2013. Katika utekelezaji wa bajeti hii kwa2011/2012, kulikuwa na changamoto nyingi mfanokukosekana kwa nishati ya umeme hata hivyo juhudi zakuridhisha zilifanyika kupunguza upungufu huo.Mheshimiwa Spika, Wizara ilikuwa inatekelezamradi wake kupeleka umeme Wilayani Nkasi kutokaSumbawanga ambapo vijiji vyote vya njiani vingewezakunufaika. Kazi nzuri ilifanyika na tumeahidiwa kupataumeme wakati wowote kuanzia sasa, hata hivyo kunachangamoto zifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, wananchi wa vijiji vya Nkundi,Kipande, Kantawa, Mihindikwa, Kasu, Chala naKacheche katika Jimbo la Nkasi Kusini wanalalamikasana kuwa miundombinu iliyoandaliwa njiani katika vijijihivyo haijaruhusu kuwapatia umeme wale waliokomita chache tu ndani ya kijiji yaani miundombinuhaijasambazwa katika vijiji hivyo. Inaonyesha niwananchi wachache tu ndiyo watakaobahatikakupata nishati hii muhimu ambayo wameisubiri miakamingi. Waziri hebu fanya wote watakaohitaji umemewapate katika vijiji vilivyopitiwa na umeme.Mheshimiwa Spika, umeme huu utawaka lini hasaMjini Namanyere, wananchi wanasubiri kwa hamuahadi ya Rais wao ambaye aliwaahidi kupata umemeharaka iwezekanavyo. Japokuwa kazi inaendeleavema, tunaomba umeme uwake.Mheshimiwa Spika, mpango wa mwaka 2012/13.Katika mpango huu, nimeona nia njema ya Wizarakuboresha upatikanaji wa nishati mijini na vijijini.Naomba pia nipongeze kupunguza gharama zauingizaji umeme mijini na vijijini kwa 25% hadi 70%. Kwapunguzo hili, lazima Waziri apongezwe.Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni uwazi naukakamavu Waziri anaotoa katika kutumikiaWatanzania. Mgao haukubaliki, ni kauli ya kwanzakutolewa na Wizara hii. Kama itakuwa ndivyo, sifa hiiitaendelea kutukuka kwa muda mrefu. Kama hakunaumeme viwanda havifanyi kazi, watu watakosa ajira,nchi itakuwa giza, kodi hakuna na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, uthibiti wa leseni za madini.Nakupongeza nalo vilevile kuona uwezekanokuongeza zaidi mrabaha toka 4% ili makampuniyanayochimba wachangie zaidi. Vilevile nashauri kwakuwa uchumi wetu unakuwa kwa haraka, maeneostrategic kwa madini yanaweza kubaki kwa wazalendo(wawekezaji), hata kama hawana uwezo, Serikaliiwachangie kidogokidogo hadi hapo nchiitakapokuwa na uwezo.Mheshimiwa Spika, REA, naomba umeme MakaoMakuu ya Jimbo la Nkasi Kusini, Tarafa ya Kate. Umemeunaoenda Namanyere umepita kijiji cha Nkundi,ukitoka Kundi kupelekwa Kate ni kazi ndogo kwaniunakuwa unapitia vijiji vya Kalundi, Myula, Ntalamila nahatimaye Kate.Mheshimiwa Spika, mwamko wa Ziwa Tanganyika,Mji Mdogo wa Wampembe wakipata umemetutaweza kusindika samaki aina ya migebuka ambayokwa sasa tunapeleka Zambia. Ni aibu Ziwa Tanganyikaambalo tunalimiliki kwa sehemu kubwa kuliko nchiyoyote, mazao yake yanasindikwa Zambia ambapo ninchi ambayo inahodhi eneo dogo sana, tatizo niumeme kukosekana kule mwambao.MHE. AMINA ABDALLAH AMOUR: MheshimiwaSpika, pamoja na kuwa uchumi wa nchi yetu sasa hiviumeelekezwa kwenye gesi na madini na pamoja nakuchangia pato la taifa lakini bado pato hili halijamfikiaMtanzania. Mimi tatizo kubwa ninaloliona ni kwambahatuna sera inayotueleza juu ya usimamizi wa hii gesina madini ili tuweze kusimamia vizuri kwa kuwa

tunaambiwa tu kuna sheria fulani lakini hatuna mfumomaalum kuwa hizi sheria zinatakiwa zisimamiwe na nchiyenyewe, matokeo yake hizi taasisi zinazoundwa kamaSTAMICO na nyingine zinafanya kazi kama Idara yaSerikali. Tatizo hili naliona ni la msingi, naiomba Serikaliilishughulikie na kulipatia ufumbuzi.Mheshimiwa Spika, kuhusu wachimbajiwadogowadogo ambao ni Watanzaniawananyanyaswa sana na wachimbaji wakubwaambao ni wageni. Cha ajabu, Serikali huwahaiwachukulii hatua hawa wachimbaji wakubwa naSerikali kila siku inakuwa na kigugumizi kutoa adhabu.Leo ukisikia mgodi umevamiwa na Watanzania hatuakali zinachukuliwa na pale wanapotunyima dhahabuzetu Serikali haichukui hatua. Nachukua nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati naMadini, Mheshimiwa Stephen Julius Masele kwa kuwezakuwatetea wachimbaji wadogowadogo, huu ndiouzalendo, umethubutu, umeweza bado kusongambele.Mheshimiwa Spika, mikataba, naishauri Serikaliipitie upya mikataba na ile iliyokuwa mizuri ambayoinawapa haki Watanzania na Tanzania iendelee na ilemikataba mibovu ifutwe mara moja bila kujali mkatabawa nani na unamalizika lini.Mheshimiwa Spika, tunao Watanzania ambaowamesoma na hawana kazi yoyote, ni boratuwawezeshe na hii kazi waifanye wao ya kujazamikataba pamoja na kufanya utafiti kuliko hawa

wageni ambao hawana lolote kwani 90% yainformation wanapata kwa hawa Watanzania.Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, MheshimiwaWaziri tunataka tuone hii gesi inapunguza ukali wamaisha.MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE: Mheshimiwa Spika,napenda kuchukua nafasi hii kwanza kumpongezaWaziri wa Nishati na Madini kwa ujasiri wake nakuthubutu kusema wazi katika hotuba yake juu yamigodi kulipa kodi ya mapato (ukurasa 106-107).Hongera sana na hakikisha hilo linatekelezwa kwavitendo.Mheshimiwa Spika, madini, nchi yetu imebarikiwasana kuwa na rasilimali madini, hii isiwe “balaa” kwanchi yetu bali iwe “baraka” kwa nchi yetu na watuwake.Mheshimiwa Spika, Serikali iweke mikataba wazi,mikataba yenye manufaa kwa nchi. Sekta hii yamadini imegumbikwa na “usiri” mkubwa na wananchikuteseka katika nchi yao.Mheshimiwa Spika, Serikali inapaswa kuwawekeamazingira bora wachimbaji wadogo, iwawezeshe kwakuwanunulia vyombo vya kisasa ili waweze kujipatiariziki yao.Mheshimiwa Spika, Serikali ihakikishe kupimamaeneo yote ya migodi hasa migodi mipya kama

mgodi wa Murus Endabash Gold Mining Karatu. Sheria,kanuni na taratibu zote zifuatwe na mikataba iwe wazi.Mheshimiwa Spika, sambamba na baraka yamadini tuliyonayo, Serikali ihakikishe uharibifu wamazingira unaotokana na uchimbaji wa madiniunadhibitiwa.Mheshimiwa Spika, haiingi akilini kwa mwekezajikudai kuwa anapata hasara miaka 5 – 7 na badoanaendelea kuchimba bila kulipa kodi, hili likome maramoja.Mheshimiwa Spika, kwa habari ya gesi,chondechonde, Serikali isitoe msamaha wa kodi.Baraka ya kuwa na Gesi kwa nchi yetu ni ukombozitosha kwa uchumi wetu na kwa maisha yaWatanzania. Naitaka Serikali kuhakikisha kuwamikataba inayofanywa katika mradi huu wa gesi iwena tija/manufaa kwa Watanzania, angalizo, tusijetukafanya kama kwa madini.Mheshimiw Spika, nishati, nampongeza Waziri natimu kwa hatua wanazochukua kusafisha Wizara, keepit up.Mheshimiwa Spika, umeme ni muhimu sana kwamaendeleo ya nchi katika nyanja zote. NapendaSerikali iniambie ni lini itakamilisha upelekaji wa umemeEndamarariek, Karatu kazi ambayo inafanywa kwanamna ya ajabu. Wananchi walijitolea kuchimbianguzo na hatimaye TANESCO ilifunga nyaya mwanzona mwisho wakaacha sehemu ya katikati na mara zote

wamekuwa wakidai watakamilisha hadi leo badohaujakamilika.Mheshimiwa Spika, REA, napenda kujua ni liniSerikali itapeleka umeme Tarafa ya Mbulumbulu wakatiambapo REA ilishafanya upembuzi yakinifu kuhusuupelekaji wa nishati hii Mbulumbulu.Mheshimiwa Spika, napenda kuishauri Serikalikutumia nishati ya umeme wa upepo na umeme wajua (solar pawer) hasa kwa shule zetu za Serikali za Katana Zahanati katika vijiji vyetu. Serikali iwekeze zaidikatika eneo hilo.MHE. MAGDALENA H. SAKAYA: Mheshimiwa Spika,pongezi kwa Waziri, Manaibu Waziri na watendaji wotewa Wizara hii kwa kuandaa hotuba hii na kuleta hapaBungeni. Kwa dhati, napongeza kazi nzuri ambayoimeanza kuonekana ndani ya Wizara hii chini yaProfesa Sospeter Muhongo, mtaalam na professionalna wasaidizi wake. Wote tumpe nafasi awezekutekeleza mipango mizuri iliyopangwa na kusaidiaWatanzania. Huyu ni mtendaji sio mwanasiasa.Mheshimiwa Spika, tumekuwa tukiomba miakayote hapa Bungeni Serikali ilete mikataba mikubwakama vile umeme, madini, gesi, makaa ya maweWabunge tupate fursa ya kuipitia ili ilete tija kwaWatanzania. Ni kwa nini Serikali bado inafanyamikataba hii kuwa siri? Kwa nini mikataba muhimukama hii inakuwa siri hata kwa wawakilishi? Ni ninikinafichwa huko?

Mheshimiwa Spika, Serikali baada ya kuunda timuya kuunda Tume ya kuangalia mikataba ya madinihapa nchini, ilibadilisha sheria/marekebisho yavipengele vya sheria kwa lengo la kufanya sekta yamadini inufaishe Taifa na Watanzania wote. Serikaliieleze ni kwa nini viwango vipya vya mrahaba wamadini vilivyopendekezwa kisheria havijatekelezwampaka leo 2012? Sheria iliainisha jinsi ya kuwezeshawachimbaji wadogo waweze kuchimba kitaalam nakunufaika na kazi wanayoifanya, kuwapimia maeneoyao ya uchimbaji mdogomdogo na kupatiwa hatimiliki. Ni kwa nini mpaka leo bado wachimbajiwadogowadogo wanahangaika na kulalamikakuondolewa kwenye maeneo yao?Mheshimiwa Spika, kuna kikundi cha wachimbajiwadogowadogo wako Ilejoa, Tarafa ya Ulyankuru,Urambo, wamepewa leseni za utafiti kwa miaka zaidiya sita. Mwaka 2010 walipoanza kuchimba madiniwameingia viongozi wakubwa wamepewa lesenikwenye eneo hilohilo wakiongozwa na Mbunge waeneo hilo na sasa wale vijana wanaambiwawaondoke. Wizara imewanyima leseni ya kuendeleana uchimbaji kundi la Tumaini. Ni kwa nini Wizara inatoaleseni mpya ndani ya eneo ambalo lina leseni nyingineya uchimbaji?Mheshimiwa Spika, pamoja na nchi yetukugundulika madini ya uranium katika maeneo mengikama Bahi, Kondoa, Namtumbo, na kadhalika, badokama Taifa hatujapenda kuingia kwenye utafiti nauchimbaji wa uranium kwa manufaa ya Taifa. Hatunautaalam wa kutosha (capacity building) kwa watu

wetu hapa nchini kuweza kuingia kwenye explorationya madini hayo.Mheshimiwa Spika, Serikali inategemea zaidiwawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza kwenyeuchimbaji. Tunao uzoefu wa kutosha kwa jinsi ambayomigodi ya almas, dhahabu, tanzanite na kadhalikainavyodhulumu haki za Watanzania. Wakati madiniyakivunwa na kusafirishwa nje, wanaoishi kuzungukamigodi yote ni maskini wa kutupa. Je, hili sio somotosha kwa Serikali iliyoko madarakani?Mheshimiwa Spika, ni nini kinachoisukuma Serikalikukurupuka hadi kwenye hifadhi zetu kuanza uchimbajiwa uranium wakati ikijua fika hatuna uwezo wakusimamia? Je, Serikali inataka kuchimba kila kilichokoardhini kwa wakati mmoja huu sio ulafi?Mheshimiwa Spika, kuanzia Awamu ya Kwanza yaRais, marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere alijua tunazorasilimali nyingi sana ardhini kama madini, gesi, mafutana kadhalika, kwa nini Serikali baada ya kujifunzakutokana na makosa isijikite kwanza kujenga uwezo wandani? Tuwe na wataalam professionals ndani ya nchiyetu watakaosimamia rasilimali zetu kwa manufaa yaTaifa hili?Mheshimiwa Spika, matokeo ya gesi, umeme,mafuta ya taa, moto poa kuwa ghali sana na hivyowananchi wengi kushindwa kutumia kama nishati, nihatari sana kwa uhai wa misitu yetu. Asilimia 80% yaWatanzania wanatumia mkaa kupikia wakati speed yakupanda miti ni ndogo sana na hata ikipandwa

inakauka kutokana na kukosa mvua ya kutosha. Gesikg.15 ni Tshs.65,000 – 75,000, tunaelewa vipato vyawatu wetu. Serikali ipunguze bei ya nishati za kupikiakunusuru nchi na jangwa.MHE. ABDALLAH SHARIA AMEIR: MheshimiwaSpika, kwanza kabisa, napenda kumshukuru MwenyeziMungu kwa kuniwezesha kuwa Mbunge wa Bunge hili.Pili, napenda kuipongeza Wizara hii na Mawaziri naKatibu Mkuu wake kwa kazi nzuri na kubwa ndani yaWizara hii kwa faida ya nchi kwa jumla.Mheshimiwa Spika, mimi binafsi ninaomba kuungamkono hoja hii kwa asilimia mia moja, kwa sababuWizara hii chini ya uongozi mpya, unaonekana ukotayari kufanya kazi kwa ajili ya wananchi na kuimarishaChama changu cha CCM.Mheshimiwa Spika, ninamuomba MheshimiwaWaziri aendelee kuwabana viongozi watendajiwasiofaa kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania,hasa wafanyakazi wadogo kwani hawa ndio chachuya matatizo ya TANESCO kuonekana Shirika hili kuwahalifai mbele ya Watanzania kwani wao ndio madalalikwa wakubwa wao katika kutengeneza rushwa za kilasiku katika Shirika TANESCO.Mheshimiwa Spika, mimi binafsi, nampongezatena Waziri kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi kifupi.Namwombea Mwenyezi Mungu aendelee kuwapahekima Mawaziri wetu wote wa Wizara hii na MtendajiMkuu wa Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, namwomba Waziri kuangaliakwa jicho la huruma umeme vijijini, hizo shilingi bilionitatu zilizookolewa TANESCO zipelekwe kwenye mradiwa umeme vijijini.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii asilimiamia moja.MHE. SARA M. ALLY: Mheshimiwa Spika, naombakuchangia hoja zifuatazo:-Mheshimiwa Spika, kwanza ni vituo vya kuuzamafuta kufunguliwa bila utaratibu maalum. Ukiangaliamaeneo ya Kibaha, Dar es Salaam na Morogoro Mjinihasa maeneo ya kituo cha mabasi ya Msamvu, utaonakumekuwepo na vituo vingi ambavyo vinahatarishausalama wa watu wanaofanya shughuli karibu namaeneo hayo.Mheshimiwa Spika, inashangaza kuona vituo vyamafuta vimelundikana eneo moja wakati maeneomengine hasa Mikoani hakuna vituo vya kutosha.Mfano mzuri ni kipindi cha mgogoro wa mafutaambapo magari mengi yaliyokuwa yanayofanyasafari ndefu za Mikoani mfano Singida – Dar es Salaam,yalipata tabu kwani vituo vilivyoko barabarani nivichache sana ukilinganisha na vile vilivyokuwa Kibahana Morogoro Mjini na kusababisha abiria kupatamatatizo. Nashauri uwekwe utaratibu maalum wautoaji wa vibali kwa wanaotaka kuanzisha vituo vyamafuta hii ni kuepuka mlundikano wa vituo vyamafuta.

Mheshimiwa Spika, pili, kasi ya kuandaa sera,sheria na gas master plan iongezwe ili Watanzaniawaweze kutoa maoni yao na kujiridhisha namnawakavyofaidika na rasilimali ya gesi. Aidha, wananchiwahamasishwe kuwekeza kwenye sekta ya gesi nakununua hisa kwenye sekta ya gesi.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Spika,kwa kuwa umeme ni muhimu katika kuinua uchumi waTanzania, nimefurahishwa sana na plans zakutekelezwa kwa mwaka 2012/2013.Mheshimiwa Spika, katika Jimbo la Mufindi Kusinindilo Jimbo pekee linalozalisha nguzo za umeme nchinilakini vijiji vyake vingi havina umeme. Naomba umemekatika vijiji vya Mbalamaziwa – Malangali hadiIhowanza; Mtambula – Kiliminzowo – Iramba; Ihomasa –Udumuka – Kilolo; Nyigo – Ihawaga; Rugolofu; Nyololo -Maduma – Matanana - Bumilayinga. Naiomba sanaWizara kwa vijiji hivyo vilivyovitaja hapo juu ni muhimusana kuwa na umeme. Pia Rais alipotembelea Jimbola Mufindi Kusini aliahidi kuwa vijiji vya Mbalamaziwa –Malangali - Ihowanza watapewa umeme.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. PHILIPA G. MTURANO: Mheshimiwa Spika,Profesa Muhongo, Mheshimiwa Maswi, MheshimiwaMasele na Mheshimiwa Simbachawene, kazeni buti,kazi yenu imeonekana kwa muda mfupi tumliokabidhiwa Wizara. Big up, tuko nyuma yenu,

msiogope vitisho, tunawaombea kila iitwapo leo, bigup!Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY: Mheshimiwa Spika,katika kuchangia, nimegawa mchango wangu kamaifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, kuhusu nishati, kwanzanapenda kuchangia kuhusu umeme. Bajeti ya REA(Sh.157 bilioni) iongezwe, ni ndogo sana. NaipongezaTANESCO kwa kupunguza gharama ya kuunganishaumeme hasa katika maeneo ya vijiji. Hii itachocheakukua uchumi vijijini, itasaidia viwanda vidogokuanzishwa vijijini, shule na zahanati zitapata umemekwa ajili ya maabara na majokofu.Mheshimiwa Spika, pili ni gesi, bei ya uzalishaji nausambazaji wa gesi idhibitiwe ili kuzuia ubandishaji nakuhujumiwa bei na “supply” ya gesi.Mheshimiwa Spika, tatu, ni mafuta, bei ya mafutaya taa ilipandishwa kwa ajili ya kudhibiti uchakachuajiwa mafuta, hili linatekelezwa. Kwa hiyo, bei ya mafutaya taa itazamwe upya ili kupunguza matumizi yamkaa.Mheshimiwa Spika, nne, makaa ya mawe,naishauri Serikali kuwekeza katika kampuni ya Kiwira ilikuwapatia wananchi bidhaa hii ya umeme kwa beirahisi.

Mheshimiwa Spika, sehemu nyingine ambayonapenda kuiongelea ni kuhusu madini. NaishauriSerikali katika kutoa leseni ama kutafuta au kuchimbamadini, ishirikishe Halmashauri ya Wilaya ya eneohusika pamoja na Serikali ya kijiji kupata uhakika waumiliki wa ardhi na kulinda uharibifu wa mazingira.Mapato yanayotokana na leseni yasitufanyetukaharibiwa mazingira. Sheria ya Madini, Ardhi na ileya Serikali ya Mitaa zinahitaji kuoanishwa (harmonized)ili kuondoa mgogoro uliopo.Mheshimiwa Spika, Serikali itekeleze uamuzi wakewa kukataza kusafirishwa madini yasiyosafishwa(unprocessed raw minerals) hasa dhahabu natanzanite.Mheshimiwa Spika, mwisho, idadi ya wanafunzi 30– 50 wanaotegemewa kusomeshwa katika fani ya gesini wachache sana.Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Muhongona Manaibu Mawaziri, Simbachawene na Masele,mnafanyakazi nzuri.MHE. SUSAN L.A KIWANGA: Mheshimiwa Spika,napenda nipate majibu ya Serikali, je, ni mkakati ganiunaofanywa na Wizara wa kuhakikisha Watanzaniawanapewa elimu/taarifa za rasilimali za madinimbalimbali zilizopo katika maeneo yao?Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali kushushaumeme kwa Kata 23 za Wilaya Kilombero, Wilayaambayo ina miradi/migodi miwili (2) ya umeme na

mingine inayotarajiwa kuanzishwa lakini Kata takribani15 hazina umeme na zilizo na umeme ni baadhi yavijiji.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa kilimoMorogoro Kusini Mashariki, Kata ya Pangawe ambapounaendeshwa na Wakorea, ziko tetesi kwamba kunamadini na wanachimba bila Serikali kujua, naombaWizara ifuatilie.Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Kilombero pamojana kuwa na migodi miwili (2) ya umeme, lakiniHalmashauri haipati mrahaba wowote. Naombamajibu kama Halmashauri inastahili au la.Mheshimiwa Spika, Jimbo/Wilaya ya Kilombero, niWilaya iliyoteuliwa na Rais kuwa ghala la chakula.Hivyo ni muhimu sana kupatiwa umeme ili wananchiwanaozalisha nafaka waweze kusindika na kukuzakipato.Mheshimiwa Spika, kwa mara ya kwanza nawapapongezi Waziri Mheshimiwa Muhongo na Katibu waWizara, Ndugu Maswi kwa utu na uzalendo wao katikakuokoa kodi za Watanzania zilizokuwa zinaliwa namafisadi. Mungu awabariki na awape ujasiri, lakinimuikumbuke Wilaya ya Kilombero katika kuwashushiaumeme ambapo wamebaki kuangalia nguzo tu kwamiaka mingi. Watanzania wanateseka muwaokoe.MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, awaliya yote, napenda kuchukua nafasi hii kupongezauteuzi wa Waziri mpya wa Nishati na Madini, pamoja

na Manaibu Waziri wawili (2), naamini wataitendeahaki Wizara hii muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu.Mheshimiwa Spika, pili, napenda kuchukua fursahii kupata ufafanuzi toka kwa Waziri juu ya maagizoyaliyotolewa na Naibu Spika wakati wa majumuisho yaWizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,maagizo husika yalitaka Wizara ya Nishati na Madini,wakati wa kupitisha makadirio ya mapato na matumiziitoe maelezo juu ya mkataba ulioingiwa tarehe 23Machi, 2007 kati ya Uranium Resources PLC na WesternMetals Limited na Game Frontiers of Tanzania Limited.Mkataba ambao, pamoja na mambo mengineunamhalalishia Game Frontiers Limited kupata malipotoka kwa makampuni yanayofanya utafiti katika kitalucha uwindaji katika kijiji cha Mbarang‘andu. NikiaminiWizara ilipata muda wa kulipitia suala hili kwa umakinimkubwa hivyo kuweza kutoa ufafanuzi stahiki kwaBunge hili Tukufu.Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kuwa, mmiliki wakampuni ya Game Frontiers of Tanzania, Ndugu MohsinM. Abdallah, ni mmoja kati ya watu waliotajwa naTume ya Kuchunguza Kero ya Rushwa Nchini, iliyokuwaikiongozwa na Jaji Joseph Sinde Wariobawakituhumiwa kuwa washirika wa kulipwa katikarushwa kubwa na ukwepaji mkubwa wa kodi.Mheshimiwa Spika, tatu, napenda kuchangiakuhusiana na gharama kubwa ambazo Wizarainatumia kwa kukodisha/kutumia Mawakili binafsi.Niungane na mapendekezo ya Msemaji Mkuu waKambi ya Upinzani, wa kuitaka Serikali itoe msimamo

juu ya ushiriki wa Mkono & Company Advocatesambao huligharimu Taifa hili mabilioni ya shilingi kwamwaka. Halikadhalika, naomba Mheshimiwa Wazirialieleze Bunge hili Tukufu, kampuni binafsi ya Mkono &Company Advocates ambayo inasemekana ilianzakazi ya ushauri kwa TANESCO dhidi ya IPTL tokeamwaka 2007.Mheshimiwa Spika, mwaka 2010 Bunge hili Tukufulilipiitisha Sheria ya Madini, ambapo pamoja namambo mengine, sheria husika pamoja na mambomengine, ilizungumzia suala la machimbo ya vito katikavifungu 8(3) na 8(4) na kutoa mamlaka ya uchimbajimadini husika kwa wazalendo (Watanzania) na paleambapo utaalam na uwekezaji mkubwa sanaunahitajika kuwe na ubia (50/50) baina ya Watanzaniana wageni. Taarifa zilizopo zinaonyesha kwambakampuni ya Tanzanite One inakaribia kumaliza mudawake wa mkataba, naomba kauli ya Serikali kuhusianana utekelezaji wa sheria husika.Mheshimiwa Spika, imekuwa ni jambo la kawaidasana kwa watu kuhodhi maeneo makubwa yenyemadini pasipo kuyaendeleza. Naomba Wizara kwakuwa imejitabainisha kama ni Wizara ya uwazi naukweli ituletee orodha ya watu wote wenye leseni zauchimbaji nchini, lakini hawajayaendeleza.MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika,napenda kuzungumzia kuhusu mikataba mibovu,nashauri Serikali (Waziri na Manaibu wako) mpitie kwaupya mikataba yote ya madini na mfanyie kazi taarifazote za kamati ambazo zimewahi kukusanywa juu ya

sekta ya madini na mfanyie kazi mikataba yote mibovumtupilie mbali kwa maslahi ya wananchi.Mheshimiwa Spika, pili ni nguzo za umeme,nashauri Serikali msiuze nguzo za umeme kwawananchi, muwakopeshe ili wengi waweze kuvuta nakuunganisha umeme kwenye nyumba zao.Mheshimiwa Spika, tatu, REA (umeme vijijini), badoWatanzania 86% hawana umeme hususan vijijini.Mheshimiwa Waziri mpango huu wa umeme vijijiniutatekelezwa lini kwa vijiji visivyo na umeme? Wakatiwa majumuisho tuambiwe ni fedha kiasi ganizimetengwa kwa ajili ya REA ikiwezekana tuambiwekatika bajeti hii ni vijiji vingapi vitapatiwa umememwaka huu.Mheshimiwa Spika, nne, ofisi za TANESCO, nashauriisibaki kwenye Makao Makuu ya Mkoa kwaniwananchi wote wanashindwa kusafiri kwenda MakaoMakuu ya Mkoa. Nashauri TANESCO wafungue ofisi kilaMakao Makuu ya Wilaya ili kurahisisha ulipaji wa bili zaumeme ili kupunguza gharama za nauli kwaWatanzania.MHE. JUMA A. NJWAYO: Mheshimiwa Spika,napenda kwanza kutoa pongezi kwa MheshimiwaWaziri wa Wizara hii na Manaibu wake pia Katibu Mkuu,kwa kazi nzuri za kukabiliana na changamoto zilizomokwenye Wizara hii.Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo ya awalihapo juu, napenda kushauri yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, mosi, naiomba Serikali kuwamakini sana na tasnia ya gesi na mafuta kwani nchinyingi hapa duniani wamejikuta badala ya kuwachanzo cha uchumi, mafuta na gesi yameleta adhana usumbufu kwa wananchi kukosa amani. Ni vyematuwe makini, wasikivu na waelekevu kwa maoni namatakwa ya wananchi wetu.Mheshimiwa Spika, pili, Wizara ya Nishati na Madiniifanye “advocacy” ya gesi kwa wananchi wa Mikoa yaKusini yaani Mtwara na Lindi juu ya kiasi cha gesikilichopo, umuhimu wa bomba la gesi kulipeleka Dar esSalaam na kwa vipi Mtwara/Lindi bado watanufaikana rasilimali hiyo. Haitoshi kwa viongozi pekee waMtwara kupata uelewa kama ilivyofanyika kwenyeBaraza la Ushauri la Mkoa (RCC) siku chache zilizopitana kuacha wananchi bado hawajui mengi. Ni lazimaWizara iongeze wigo wa kutoa uelewa kwa wananchihuku viongozi (sisi) wa Mkoa wa Mtwara tukishirikikuwaelimisha wananchi.Mheshimiwa Spika, tatu, TANESCO ni chanzokikubwa cha matatizo ya Wizara hii. Dawa yake niWizara kuisimamia kwelikweli na pia kuanzisha Shirikalingine la Umma ili lifanye kazi kama competitor nahivyo kuzalisha ushindani wa maendeleo. Shirika hiloliwe la kizalendo na litakalojikita vijijini tu kwa sasapengine “REA” ingefaa pia kufanya kazi ya TANESCOvijijini.Mheshimiwa Spika, nne, katika mapango wausambazaji umeme katika Mikao ya Mtwara na Lindi,

napenda kupata orodha ya vijiji vya awalivitakavyoanza kunufaika na mradi huu kwa ajili yarejea mbalimbali.Mheshimiwa Spika, mwisho, naunga mkono hojahii huku nikiwatakia viongozi na watendaji wa Wizara hiiufanisi wa kimaendeleo, ahsante sana.MHE. RIZIKI OMAR JUMA: Mheshimiwa Spika,naomba nianze mchango wangu kwa kumpongezaMheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini yeye naManaibu wake na watendaji wake wa Wizara kwa kazinzuri wanayoifanya na kusimamia kwa umakinimkubwa vyanzo vingi vya umeme vilivyopo Tanzania.Mheshimiwa Spika, pili, naomba Serikali ifanyeharaka kuandaa Sera ya Madini kwani vinginevyo haliya madini yetu Tanzania itaendelea kudhoofika.Mheshimiwa Spika, mikataba mibovu ipitiwe tenakwa ajili ya uhakiki, lakini ikiwezekana iandikwe upya ilikuondoa huu utata uliopo kwani inawezekana wizi huuukaendelea.Mheshimiwa Spika, pamoja na kupunguzagharama za kuunga umeme, tunaipongeza sanaWizara ila naomba basi ile kazi ya kusambaza umemevijijini iongezeke ili Watanzania waishio huko naowaweze kufaidika na huduma hii kama wenzao. Pianaomba sana ile gharama ya matumizi ya umeme (beiya umeme) basi ipunguwe kwani imepanda kiasiambacho watu wengi watashindwa kumudu huduma

hii, tafadhali Mheshimiwa Waziri tuendelee kuwasaidiaWatanzania.Mheshimiwa Spika, suala la wachimbajiwadogowadogo, naomba tuwasaidie ili nao wawezekujikomboa kwa kupata stahili zao ipasavyo kwaniwanasumbuliwa sana na hawa wawekezaji wakubwa.MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Spika, awali yayote, naunga mkono hoja.Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Lindi, ni Mkoa wamwisho katika maendeleo ya miradi lakini hatupaswikuwa wa mwisho, hii inatokana na ubaguzi wa miradiya umeme iliyopelekwa ikilinganishwa na Mikaomingine. Katika hotuba ya ofisi ya Waziri Mkuu, ukurasawa 37 ambapo unaelezea kwamba Serikali imepelekaumeme vijijini katika Mikoa 16, Lindi na Mtwara haipoje? Kulikoni!Mheshimiwa Spika, kwa mtazamo huo, inakatishatamaa kuona Lindi ipo nyuma katika kila mradi,inasikitisha! Kwa mfano, tunahitaji umeme Nanganga –Nachingwea; Nanganga – Ruangwa; Ngongo – Milola;Nachingwea – Liwale; Nangurukuru – Liwale;Nangurukuru – Mbwemkulu na Mchingwa – Kitomanga.Maeneo haya niliyoyataja, yanaunganisha barabaraza Mikoa hiyo, zinaleta changamoto ya maendeleohivyo naomba Wizara itoe kipaumbele ili kuwe naufanisi katika maendeleo haya ya pamoja.Mheshimiwa Spika, madini, Mkoa Lindi, napendakutoa angalizo kubwa kutokana na ofisi ya Kanda ya

Madini kuwa Tanga kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.Naomba ibadilishwe iende Lindi au Mtwara kurahisishakazi ya utoaji leseni.Mheshimiwa Spika, watendaji wa Wizarakujihusisha na ufisadi wa kugawa vitalu kwa wageni nawao kuwa madalali wa vitalu, kama Wizara haitakuwamakini, nchi itaingia kwenye hasara kubwa. Kitendocha wageni kupewa maeneo kinyemela na wengiwao kuwa vinara wa uharibifu na kuipeleka nchikubaya.Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani kwakumalizia na kuunga mkono hoja.MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, nichukuenafasi hii kumpongeza Waziri, Mheshimiwa ProfesaSospter Muhongo, Naibu Waziri, Mheshimiwa GeorgeSimbachawene na Mheshimiwa Stephen Masele,Katibu Mkuu na watendaji wote wa Wizara hii kwakuwasilisha bajeti ya Wizara yao hapa Bungeni.Mheshimiwa Spika, Wizara hii ni nyeti na inachangamoto kubwa sana.Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogowamekuwa na matatizo makubwa kutokana nachangamoto nyingi sana wanazokumbana nazo katikamradi wa uchimbaji. Ni vyema Serikali ingeanzishamfuko ambao ungeweza kuwasaidia katika kupatamitaji na kununua vifaa vya uchimbaji.

Mheshimiwa Spika, vilevile wachimbaji hawawadogo hawana elimu ya kutosha ya kuendelezamiradi yao. Hivyo Serikali ingetenga pesa kwa ajili yakusaidia kuwapatia elimu.Mheshimiwa Spika, pia wachimbaji hawawanakabiliwa na tatizo kubwa la kuvamiwa nawachimbaji wakubwa na mbaya zaidi wapowawekezaji wenye maeneo mengi na badohawafanyi kazi yoyote. Hii inawanyima fursawawekezaji wadogo ambao ni wazawa.Mheshimiwa Spika, Shirika la TANESCO linakabiliwana matatizo makubwa sana hasa wananchikulilalamikia sana Shirika, kwanza kukatikakatika bilataarifa kwa umeme, kuongezewa gharama za bili kwamalipo ya umeme, kuna baadhi ya watendajiwamekuwa na mtandao wa kulihujumu Shirika kwakuwaunganishia umeme visivyo halali, kunapotokeatatizo la hitilafu katika eneo fulani ukitoa taarifahuduma haipatikani kwa uharaka.Mheshimiwa Spika, pia Serikali ingeangaliagharama za kufunga umeme katika majumba yao.Wananchi wengi wanashindwa kutumia huduma hiikutokana na gharama kubwa na usumbufu wa kupatahuduma hiyo.Mheshimiwa Spika, pengine Serikali ingelengakutumia rasilimali tulizonazo kama milingoti ya umeme.Wilaya ya Mufindi katika Mkoa wa Iringa kuna msituambao unatoa hiyo milingoti, je, ni kweli milingoti hiyoikitoka nje ya nchi ni bei rahisi kuliko inayotoka hapa

kwetu? Ni vyema sasa hili lingeangaliwa ili kuendeleakukuza uchumi kwa kutunza rasilimali zetu wenyewe.Mheshimiwa Spika, Wakala wa Nishati vijijini – REAilianzishwa, lengo kubwa ilikuwa kuboresha,kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa matumiziya nishati bora vijijini. Pamoja na mpango huu mzuri,Serikali ingekuwa na mkakati wa kuhakikisha vijiji vyotevinapata umeme. Sababu vijiji vingi sana havinaumeme na hata havina uhakika kama lini umemeutafika na bajeti ya Wakala huu iongezwe iliwaendelee kufanya kazi kwa kasi zaidi.Mheshimiwa Spika, madini, kwa kuwa nchi yetuimeanza kuzalisha gesi tena ya kutosha, je, gesi hiyoinayozalishwa ni kiasi gani na kiasi gani kinafika kutokainapozalishiwa hadi Ubungo kwenye mitambo? Kwasababu gesi nyingi inapotea njiani wakati wakuisafirisha hadi kwenye mitambo Ubungo.Mheshimiwa Spika, je Serikali haioni ilishauriwavibaya na wataalam, kwani umeme ungezalishwapalepale jirani na sehemu inapozalishwa gesi iliyenyewe isafirishe umeme badala ya kusafirisha gesi?Je, haioni kama umeme ungeanzia kule inakotoka gesivijiji vingi vingefaidika kwa kupata umeme?Mheshimiwa Spika, niwapongeze Waziri, KatibuMkuu na timu yake kwa kazi nzuri waliyoifanya kwakipindi kifupi toka wapate madaraka.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ENG. GERSON H. LWENGE: Mheshimiwa Spika,naomba kumpongeza sana Profesa Muhongo, Waziriwa Nishati na Madini pamoja na Manaibu Mawaziriwake na uongozi mzima wa Wizara hii kwa hotubanzuri sana na naunga mkono.Mheshimiwa Spika, nianze mchango wangu katikaeneo la umeme. Nchi hii imekuwa na mgogoro wamikataba iliyoingia na nchi hii katika kutafuta umemewa dharura, je, dharura huwa ya miaka mingapi?Naomba sana Profesa uone namna ya kuifutamikataba hii ambayo si endelevu, mkataba wowotekama hamna namna ya kutoka au kuisha basi huo nimkataba mbovu na ifike muda tuachane nayo.Mheshimiwa Spika, Shirika la Umeme Vijijini liendeMikoa yote, tupewe ratiba ya vijiji vyangu vya Jimbo laNjombe Magharibi vikiwemo Ulembwe, Egagala,Makoga, Kipengale, Wangana, Uhekule, katika Tarafaya Imalinyi, vijiji vya Itulalumba, Ihanja, Dulamu,Palagawamu, Kirinto, Kanani, Mambegu, Ludungazikiwemo sekondari za ulembwe, Makuga, PhilijioMagula, Wamike, Ludunge na Ilembula.Mheshimiwa Spika, naomba REA wafike Wilayampya ya Wagungumbe na hasa Makao Makuu yaWilaya hiyo ya Igwachanya na watupe ratiba ni liniumeme utapatikana katika vijiji hivyo na Makao Makuuya Wilaya ambapo umeme upo hauna nguvu nasasa ni mji, maeneo mengi hayana umeme. Pia paleIlembule ni mji mdogo, maeneo mengi hayanaumeme.

Mheshimiwa Spika, eneo la madini nalo lina mengiyanatakiwa kufanyiwa kazi. Mikataba ya uchimbajimadini iwe yenye maslahi kwa Taifa kuliko kuwa kwakikundi kidogo. Napendekeza mikataba hiyo ipitiweupya kwa lengo la kuboresha na kulinda maslahi yaTaifa.MHE. ABDULSALAAM SELEMAN AMER: MheshimiwaSpika, naunga mkono hoja.Mheshimiwa Spika, kwanza napendakuwapongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Mawazirikwa uteuzi weo huu katika Wizara nyeti yenyemsukosuko katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu.Mheshimiwa Spika, ombi langu kwao ni kukazabuti, kwa juhudi wanazozifanya katika Wizara hii naMwenyezi Mungu awalinde.Mheshimiwa Spika, ombi langu kuhusu REA,naomba waibane Wizara ya Fedha kupata pesaambazo Bunge lilipitisha katika kodi ya kerosene iliwaweze kufanya kazi yetu vizuri kupitia REA iliwananchi walio vijijini nao wapate haki yao ya umeme.Mheshimiwa Spika, kwa kupitia REA, naomba sanawaweze kutupatia umeme vijiji vilivyo jirani na mtambowa Kidatu. Toka mradi huo uanze zaidi ya miaka 20iliyopita kuna baadhi ya vijiji kama Kidogobasi,Msowero, Iwembe, Rumango, Vidunda na Kidezo.Naomba msaada wake Mheshimiwa Waziri iliwananchi waliozunguka mradi huo wapate umeme

huo. Nyaya zinapita mbele yao na kwenda Miji yambele, wao wanaambulia kulinda na kuona nguzo nawaya zinapita mbele yao.Mheshimiwa Spika, chonde chonde ombi languhilo Mheshimiwa Waziri alipe kipaumbele angalaukelele za mitambo ziwapoze kwa kuwapatia umemekwani ni haki yao kimsingi.Mheshimiwa Spika, nashukuru.MHE. SAID J. NKUMBA: Mheshimiwa Spika,nachukua fursa hii kumpongeza Waziri, Naibu Mawazirina Katibu Mkuu kwa namna Wizara ilivyoanzakushughulikia matatizo sugu ya upatikanaji wa nishatiya umeme.Mheshimiwa Spika, miradi ya kupeleka nishati yaumeme vijijini na ile miradi ya kupeleka nishati yaumeme kwenye Makao Makuu ya Wilaya ni jambo laukombozi kwa wananchi wetu. Katika sehemu hiinaomba maeneo ya Sikonge ambayo kwa mudamrefu yamekuwa yakiomba nishati hii bila mafanikiompaka sasa.Mheshimiwa Spika, naiomba Wizara iangalie eneola Kiyombo lililoko Kata ya Kipiri jirani na Kata yaMgandu Wilaya ya Manyoni.Mheshimiwa Spika, kwa kuwa upo mradiunaoendelea pale Mgandu, naiomba Wizara iwekeuendelezo wa mradi huu kwenye maeneo yote mpakaKilumbi, Mwamagembe na Rungwa.

Mheshimiwa Spika, eneo la Tarafa ya Sikonge,naiomba Wizara iangalie uwezekano wa kushushaumeme maeneo ya Mpombwe, Mkolye na Mlogolokwenye njia ya kuelekea Sikonge toka Tabora. Aidha,Kata ya Chabutwa na Ipole pamoja na Kata yaMibono na Usunga ni maeneo ya Kata zenye mahitajiya nishati hii muhimu.Mheshimiwa Spika, mwisho, niiombe Wizara Kataya Mole ipelekewe umeme kama ambavyo Serikaliimekuwa ikiahidi.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii.MHE. PROF. PETER MSOLLA: Mheshimiwa Spika,nampongeza Waziri, Manaibu Waziri, katibu Mkuu naWakurugenzi wa Wizara kwa kuwasilisha bajeti nzuri nayenye kuleta matumaini kwa Watanzania.Mheshimiwa Spika, aidha, naipongeza Wizara kwadhati kwa kupunguza gharama za uunganishajiumeme kwa asilimia kubwa jambo ambalo lilikuwa nitatizo kubwa kwa Watanzania walio wengi na hususanwale waishio vijijini.Mheshimiwa Spika, hivi karibuni kuna tatizo labaadhi ya wananchi wanaojiunganishia umememajumbani bila kufuata taratibu. Je, Wizara inamkakati gani wa kupambana na tatizo hili ambalosehemu nyingine vitendo hivi vimesababisha moto nakuleta hasara kubwa?

Mheshimiwa Spika, nasikitika kueleza kwambalicha ya umeme kuvutwa kutoka Iringa kwendaKidabaga (Kilolo) mwaka 2009, vijiji saba na sekondaritatu zimepitwa bila umeme kuteremshwa. Aidha,umeme kutoka Ilula hadi Ruaha Mbuyuni, WilayaniKilolo umekwisha vutwa, lakini umeme haujawashwana vijiji nane havijapata umeme licha ya watu wengikujiandikisha kupata umeme. Ni lini umemeutapatikana katika vijiji na shule hizi?MHE. NAOMI MWAKYOMA KAIHULA: MheshimiwaSpika, kwa mara nyingine tena naomba nichangie kwauchache hoja hii ya umuhimu mkubwa kwa wananchiwa Tanzania.Mheshimiwa Spika, bila ya unafiki wa Chama auvipi naomba nipongeze sana uteuzi wa ProfesaSospeter M. Muhongo ambaye umahiri na umakiniwake umejidhihirisha katika hotuba yake yenyeufasaha wa hali ya juu.Mheshimiwa Spika, baada ya hapo, naombakusisitiza baadhi ya mambo ambayo yeye kamakiongozi mkuu wa Wizara hii ya Nishati na Madinianapaswa kuyazingatia katika utendaji wake wakuikomboa nchi kutokana na janga kubwa la ufisadiwa madini na umeme.Mheshimiwa Spika, tatizo kubwa la uchumi waTanzania ni uhujumu wa uchumi unaofanywa nasyndicates ambazo zimesukwa kitaalam sana kiasi chakufanya iwe vigumu sana kutambua nani anafanyanini na ana maslahi gani katika masuala ya mikataba.

Mheshimiwa Spika ili nchi hii upone inahitaji watuau viongozi wajasiri wa kutoa maamuzi magumu kamayaliyofanywa na Waziri kutupilia mbali makubalianoyasiyokuwa na maslahi kwa wananchi.Mheshimiwa Spika, suala linalohitajika pia ni hatuazaidi ya kutambua wahujumu hawa na kuchukuliwahatua za kuwafilisi badala ya kuwaacha tu, waweexposed ili wawe mfano kwa wale wenginewanaotaka kufuata mfano wao.Mheshimiwa Spika, suala la gesi si la mchezotunahitaji Sera haraka na Sheria mbalimbali ili tuwezekuisimamia vizuri sekta hii.Mheshimiwa Spika, jambo lingine muhimu nikwamba tunaomba ramani inayoonesha vitalu namgao wake kwa watu mbalimbali, ufanyiwe mkakatiwa kuipitia ikiwezekana Bunge lihusishwe katikakutengua sehemu zote za madini zilizomilikishwa bilampangilio wa fisadi kwa wageni irudishwe kwawananchi.Mheshimiwa Spika, ni muhimu sana kwa Taifa sasahivi kuona kuwa vijana wetu wanafanyiwa mkakati wakumiliki vitalu kwa kudhaminiwa na Serikali yao. Piatuhakikishe kwamba wananchi wanaohamishwakwenye sehemu za madini, pia wanachukua hisakatika sehemu wanazozihama na wahakikishiwekuhamia kwenye nyumba yenye miundo mbinu yamsingi kama maji, barabara, umeme na kadhalika.

Zaidi zaidi iwe ni marufuku kuwamilikisha wageni ardhibali wakodishiwe tu kwa kushirikiana na wazalendo.Mheshimiwa Spika, naamini kuwa uongozi waMheshimiwa Muhongo utayatafakari na kuyazingatiamapendekezo niliyoyatoa hapo juu.Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika,kuhusu utoaji na usimamizi wa leseni za madini, Serikaliinaeleza kuwa kupitia Hotuba ya Waziri shughuli zautoaji wa leseni za madini nchini zimeendeleakuimarika na kuboreshwa. Sikubaliani na Serikali katikahoja au taarifa hii kwa kuwa katika migodi mipyainayoibuka utoaji wa leseni za uchimbaji kwawachimbaji wadogo, umekuwa na urasimu na doublestandard au double allocation ya plot za uchimbajihivyo kupelekea wazawa au wenyeji wa eneoinapogundulika madini hawapewi nafasi za awali zaumiliki wa maeneo ya uchimbaji. Mfano, wa eneolenye matatizo kama niliyoainisha hapo juu ni eneojipya la uchimbaji lililopo Endabash – Karatu.Tunaomba Wizara iingilie kati na kumaliza matatizoyaliyopo eneo hilo jipya la uchimbaji.Mheshimiwa Spika, kuhusu kuendeleza uchimbajimdogo wa madini unaofanywa na wachimbajiwadogo, mojawapo ya vyanzo muhimu vya ajiranchini hususan maeneo ya vijijini. Hivyo basi, Serikali nivema iwape nafasi ya kwanza wachimbaji hawawadogo leseni kwa wakati ikiwa ni pamojakuwaanishia maeneo sahihi ya uchimbaji.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kutokana na halingumu ya uchumi inayowakabili vijana hawa, Serikaliianzishe Mifuko Maalum kwa ajili ya kuwapatia mitaji namikopo wachimbaji hawa ili wapate vifaa vyauchimbaji, jambo ambalo litasaidia wachimbaji hawakatika kumudu gharama za ukodishaji wa zana, hivyokuwafanya vijana hawa kuendelea na kazi hii ambayohuwapatia ajira.Mheshimiwa Spika, Wizara iendelee kutoamafunzo kwa wachimbaji wadogo ili kufahamu mbinumbalimbali za kukabiliana na changamotowanazokutana nazo sambamba na kuimarisha afyazao na usalama wao, hasa waweze kujikinga namaambukizi ya UKIMWI, hii ikiwa na utunzaji wamazingira katika migodi ili kupunguza uharibifumkubwa wa mazingira unaofanyika katika maeneo yamigodi hapa nchini.Mheshimiwa Spika, kuhusu nishati ya mafuta,Serikali lazima ichukue hatua za dhati dhidi yaupatikanaji wa bei ya mafuta ya taa. Mafuta hayahutumiwa na wananchi walio wengi wa kipato chachini, jambo ambalo humzidishia mwananchi mzigomkubwa na kusababisha bidhaa za kuni na mkaakuwa kubwa na kupelekea uharibifu mkubwa wamazingira, Serikali ituambie ina mkakati gani wakumpunguzia mwananchi mzigo.MHE. ALPHAXAD K. LUGOLA: Mheshimiwa Spika,kwanza nampongeza Rais kwa kuwateua Waziri naManaibu wachapa kazi ambao wameanza kwa

muda mfupI kuonesha kwamba nchi yetu inamwelekeo wa kutatua matatizo ya mgao wa umemepamoja na matatizo katika sekta ya madini.Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizonapenda kusema yafuatayo:-Mheshimiwa Spika, gharama za kuunganishaumeme Vijijini pamoja na kuwa sasa 170,000/=, badowananchi wetu vijijini kutokana na kipato chao kuwakidogo hawataweza kuzimudu. Nashauri kuwawananchi waunganishiwe umeme na gharama yakuunganishiwa ziwe zinalipwa kidogo kidogo kupitiaankara ya mwezi hadi fedha ziishe. Naomba majibu.Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wadogoJimboni Mwibara wanahitaji semina na mafunzo yamuda mfupi kwa ajili ya kujua angalau kwa uchache,sekta ya madini ili wajue namna ya kutafuta masoko,kupata vifaa na zana za uchimbaji, taratibu zamasuala ya leseni za utafiti na kadhalika. Aidha,nashauri Wizara iwasaidie kwa kuwapatia vifaa kamacrashers na mercury. Naomba majibu.Mheshimiwa Spika, umeme vijijini Mwibara ambaommetenga fedha, ni vema mkazingatia suala la fidiakwani hatujafidiwa kwa wale ambao waliathirikawakati wa kupitisha umeme kutoka Bunda kwendaUkerewe. Naomba majibu.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Spika,nachukua fursa hii kumpongeza sana MheshimiwaProfesa Sospeter Muhongo kwa juhudi kubwaaliyoionesha kwa kipindi kifupi alichofanya kazi katikaWizara hii. Nawapongeza Naibu Mawaziri, Katibu Mkuukadhalika na wafanyakazi wote wa Wizara hii kwajitihada zao za kuhakikisha kwamba wawekezajiwanakoma kutuibia katika migodi na kadhalika.Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizonaomba kuchangia mambo machache kamaifuatavyo:-Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara kwakuokoa sh. Bilioni 6,282,900,000/= kila mwezi baada yauamuzi wa kuvunja mkataba wa Tanesco na kampuniya Oryx na Camel Oil. Nawapongeza sana. NaishauriWizara kuendelea kupitia mikataba mbalimbali ndaniya Wizara inawezekana yakagundulika mengi zaidi.Mheshimiwa Spika, madini ya uraniyamegunduliwa Namtumbo, Manyoni na Bahi na hivikaribuni mradi utaanza kutekelezwa.Mheshimiwa Spika, wananchi wanaozungukwawalioko kwenye maeneo yenye madini ya uranihawajaelimishwa athari za madini hayo, naiombaSerikali kwanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusumadini ya urani kabla ya kuchimbwa kwani ni madiniyenye athari kubwa kwa afya ya wanadamu, mimeana wanyama.

Mheshimiwa Spika, naomba kujua mradi waumeme wa upepo umefikia wapi, kwani ni umemewenye gharama nafuu.Mheshimiwa Spika, umeme unaopotea njianikutokana na uchakavu wa miundombinu ni mwingi.Serikali ina mpango gani wa kutengenezamiundombinu kabla ya kuingiza MW nyingizinazotarajiwa.Mheshimiwa Spika, mradi wa kufua umeme waStigler’s Gorge MW 2100 ni wa muda mrefu sana nawananchi hawaelewi ni kwa sababu gani haujaanzakutekelezwa. Bajeti ya mwaka 2011/2012 tulielezwakuwa mradi huu utakamilika mwaka 2014. Bajeti hii ya2012/2013, Mheshimiwa Waziri hajasema mradi huuutakamilika lini? Kama Serikali haina fedha za kutoshani bora kuwa na miradi michache inayotekelezekakuliko kubeba miradi mingi tusiyoweza kutekeleza.Mheshimiwa Spika, nina imani na Serikali kuwamradi wa gesi asilia itawanufaisha wananchi bilakuzongwa na kelele za wananchi kwamba, tunaibiwana wawekezaji. Serikali irudishe imani kwa wananchikwamba kuibiwa na wawekezaji hakupo tena.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kwa sababutulikubaliana kwamba saa tano na nusu tunawaitawanaojibu hoja kwa dakika ishirini ishirini kwa kila NaibuWaziri, halafu Waziri mwenyewe atapewa dakika 50.Hiyo itatupeleka mpaka saa saba, halafu tutaingia

kwenye Kamati ya Matumizi. Kwa hiyo, namwita NaibuWaziri Mheshimiwa Maselle.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELLE): Mheshimiwa Spika, nakushukurukwa kunipa fursa hii. Nianze kwa kumshukuru MwenyeziMungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kusimamakatika Bunge lako Tukufu. Niwatakie heri Waislam wotewanaoshiriki ibada hii ya Ramadhan Mbaraka. Pianatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwakupoteza wapenzi wao katika ajali ya meli iliyotokea 18Julai, 2012 huko Zanzibar.Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zanguza dhati kwa Mheshimiwa Rais Daktari Jakaya MrishoKikwete kwa kuniamini kuitumikia Wizara hii kamaNaibu Waziri wa Nishati na Madini kuisimamia sekta yamadini. Kwa mara nyingine ameonesha imani yake najinsi anavyothamini vijana wa Taifa hili na kuidhihirishafalsafa yake ya kuwaandaa vijana kupata uzoefu wauongozi kwa manufaa ya baadaye ya Taifa letu.Mheshimiwa Spika, pia nichukue nafasi hiikumpongeza Mheshimiwa Makamu wa Rais, WaziriMkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda kwa maelezo namiongozo yake mbalimbali ambayo wamekuwawakinipatia tangu nimeingia katika Bunge hili.Nimshukuru sana Waziri wangu Mheshimiwa ProfesaSospeter Muhongo kwa kuniongoza vyema nakuhamishia uprofesa wake kwangu.

Mheshimiwa Spika, pia nimshukuru sana kwa dhatiNaibu Waziri mwenzangu, kaka yangu MheshimiwaGeorge Simbachawene, Katibu Mkuu Eliakim Maswi,Makamishna, Wakurugenzi na watumishi wote waWizara kwa ushirikiano walionipa katika utekelezaji wamajukumu yangu na wamenifanya nizoee mazingiramapya ya kazi kwa haraka. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nikupongeze wewe binafsi kwakusimamia na kuliongoza vyema Bunge letu. Kwangunaamini kwamba wanawake na wasichana wengihapa utaendelea kuwa mfano bora kwao.Nakumbuka ulivyonipigania nichaguliwe kuwaMakamu wa Rais kijana zaidi kuwahi kutokea katikaBunge la Afrika kabla ya kujitoa hatua za mwishonikufuatia uteuzi wangu katika nafasi hii. (Makofi)Mheshimiwa Spika, niwashukuru pia MheshimiwaNaibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Mawaziri, ManaibuWaziri, Katibu wa Bunge na kwa kipekee kabisaniwashukuru Wabunge wote kwa ushirikiano wao mzurikwangu, nasema ahsante sana. (Makofi)Mheshimiwa Spika, wananchi wa Mkoa waShinyanga ndiyo waliyoniwezesha kuwemo katikaBunge lako Tukufu, hivyo napenda kutumia nafasi hiikuwashukuru kwa ushirikiano wao mkubwawanaoendelea kunipa na kuniwezesha kutekelezamajukumu yangu. Naahidi kuendelea kushirikiana naokatika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabilina kuleta maendeleo ya kweli katika Mkoa waShinyanga na Taifa kwa ujumla. Familia yanguimeendelea kuwa mhimili mkubwa wa utendaji mzuri

wa kazi zangu. Kwa namna ya pekee napendakumshukuru mke wangu mpenzi Pauline kwa kunipamoyo na watoto wetu Lisa na Fernando.Mheshimiwa Spika, napenda sasa nichangie hojahii ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madiniiliyowasilishwa jana hapa Bungeni kwa kujibu baadhiya hoja za Waheshimiwa Wabunge, majibu yanguyatajibu hoja zilizoelekezwa kwenye sekta ya madini.Mheshimiwa Spika, Wabunge wengiwamechangia kwenye suala la mrabaha na mapatoyote yanayotokana na sekta ya madini kwakuwatambua, najua wengi wamechangia.Mheshimiwa Ezekiel Maige, Mheshimiwa HamisKigwangala, Mheshimiwa Selemani Zedi, MheshimiwaDeogratias Ntukamazina, Mheshimiwa Daktari MaryMwanjelwa na wengine wote waliochangia katikaeneo hili.Mheshimiwa Spika, ni kweli Watanzania wengiwamekuwa na kilio cha siku nyingi kwamba sekta yamadini pengine haichangii vizuri kwenye pato la Taifana tungependa tupate zaidi ya hiki tunachokipata.Napenda kukiri katika Bunge lako Tukufu kwambaSerikali imejitahidi kupiga hatua kubwa muhimu katikakuongeza mapato yanayotokana na sekta hii yamadini ukilinganisha na kule tulikotoka.Mheshimiwa Spika, utakumbuka kwamba sekta hiihasa uwekezaji mkubwa wa madini una umri wa miakaisiyozidi 15 hapa nchini. Kwa hiyo, kweli kule mwanzotulikosa uzoefu na sasa Watanzania wengi

wameendelea kuelewa na kujifunza na Sheria 2010baada ya Tume ya Bomani na maoni mbalimbali yawadau likiwemo Bunge lako Tukufu ililetamapendekezo ambayo Sheria ile imeboresha mambomengi ambayo kwa sasa kwa kweli yanalinufaishaTaifa kwa kiwango. Lakini sisi kama Wizara hatujaridhikabado tunataka tupate zaidi ya hapo.Mheshimiwa Spika, mrabaha ulikuwa ukilipwaasilimia tatu ya net, lakini sasa tumeanza kupokeaasilimia nne baada ya majadiliano na makampunimakubwa ya migodi japokuwa majadiliano hayakuwamepesi, lakini tunashukuru vijana wazalendowanaofanya kazi kwenye migodi hiyo kwakuwatambua Ndugu Deo Mwanyika wa Barrick, VicePresident Bwana Gerald na Bwana Victor kwaushirikiano ambao wametoa katika Wizara yetukuhakikisha kwamba Serikali kama vijana wazalendowa Taifa hili wanatoa msaada wa kuona kwambawananufaika zaidi katika sekta hii ya madini.Mheshimiwa Spika, sasa Watanzania wengiwanafikiri tunapopata mrabaha asilimia nne ya growthya mapato yote wanayopata wanafikiri ndiyo hicho tutunapata. Hili tumekutana nalo sehemu mbalimbali,wanafikiri ile sasa asilimia 96 inakwenda wapi? Inamaana huyu mwekezaji anaondoka na asilimia 96.Ndugu zangu Watanzania sio hivyo.Mheshimiwa Spika, mrabaha sio kodi, mrabahakama vile mahari inayolipwa kwenye familia baada yakumtunza binti na anapoolewa. Ni kama shukrani kwamaana kwamba Taifa hili limebarikiwa kuwa na

asilimali hizo. Lakini tunazo kodi mbalimbali ambazoTaifa linapata.Mheshimiwa Spika, ningependa Watanzaniawaelewe kwamba sio asilimia nne ya mrabaha ndiyotunachokipata peke yake. Naomba nizitaje kodizingine ambazo tunazipata kama Serikali ikiwemoPAYE, kuna kodi ya withholding tax, kodi ya zuio, kodiya VAT, stamp duty, import duty excise duty, corporatetax, income tax, road toll, local levy na kodi zingine.Kwa hiyo, hizi kodi zingine ambazo zipo kwa mujibu waSheria ukizikokotoa zote Serikali inapata mpaka wastaniwa asilimia 52 ya mapato yanayotokana na uzalishajiwa migodi ya hapa nchini. (Makofi)Mheshimiwa Spika, migodi mikubwa tanguimeanza shughuli za uzalishaji mpaka sasa imewezakulipa Serikalini, jumla ya bilioni 951 katika Serikali Kuu.Lakini kuna suala ambalo wengi wamezungumza,nitazungumza baadaye kidogo la service levy. Kwelikwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1982, LocalGovernment Finance Act, 1982 inaeleza wazi na kuipamamlaka Halmashauri kukusanya mapato kiwangokisichozidi 0.3 percent na hiyo ndiyo Sheria mama.Mheshimiwa Spika, sasa kwa bahati mbaya kamanilivyosema inawezekana tulivyoanza, tulikuwahatujapata uzoefu wa kutosha migodi hii ilikuwa hailipihiyo na mgodi wa kwanza Resolute ulianza mwaka1997, ukafuatiwa na GGM mwaka 1999, lakini kwakipindi chote hicho hawakulipa service levy kwenyeHalmashauri zetu, wanakofanya kazi na hoja yao

ilikuwa kwamba Halmashauri hazijatayarisha by lawsna GN ambayo ilifuata mwaka 2006.Mheshimiwa Spika, tumekuwa na vikao vingi sanana migodi hii na kwa kweli kama Mheshimiwa ProfesaKahigi alivyosema kwamba sio kutoa rai tumeshaagizana naagiza tena migodi yote lazima izingatie Sheriamama. Kisingizio cha kusema kwamba GN haikuwepo,by laws hazikuwepo, lakini hakuna GN na by lawsambazo zinaweza kufuta Sheria mama. Kwa hiyo, nihaki yetu kama Watanzania, Halmashauri zetu ni hakiziweze kulipwa madeni yote ya nyuma kama stahiliyetu kwa mujibu wa Sheria. (Makofi)Mheshimiwa Spika, tayari nimeshaanzamazungumzo tangu nilipoingia Wizarani mwezi waTano na migodi hii mikubwa napenda kukirimazungumzo hayakuwa mepesi, yalikuwa mazito.Lakini nataka kulihakikishia Bunge lako Tukufu naWatanzania kwamba tumeweza ku-cross deal la GGMkulipa madeni yote ya nyuma tangu walipoanza.Wataalam wetu wamesha-establish ni kiasi gani chapesa ambazo walikuwa wanakwepa kulipa tanguwalipoanza mpaka mwaka 2005 ambapo GN ilitoka.Mheshimiwa Spika, vile vile tumeweza kupatasuluhisho la mgogoro uliodumu muda mrefu waResolute na ulimhusisha hasa ndugu yanguMheshimiwa Kigwangala, amepambana kuhakikishakwamba Halmashauri ya Nzega inapata kile kituambacho inastahili.

Vita hiyo tumeweza kuishinda kwa pamoja naninawashukuru sana kwa ushirikiano walionipa katikamajadiliano yale na migodi hii imeenda kukaa kwenyebodi zao kuhakikisha kuwa madeni yote ya nyumaambayo walikuwa hawalipi kuanzia 1997 mpaka 2005yanalipwa.Mheshimiwa Spika, nimemsikiliza MheshimiwaMaige, amezungumzia pia Bulyan’hulu. Nataka nimpetaarifa tu kuw, kesho nitakuwa na kikao na Bulyan’hulukwa maana ya Barrick, kwa wembe ule ule kuhakikishakuwa haki ambayo ilikuwa imepotea siku nyingiinapatikana. Kwa hiyo, niwahakikishie ndugu zetu kulekwenye Halmashauri kuwa, nina hakika Barrick ilitoamfano wa kukubali kwenda mapema ku-immigratekutoka mrabaha wa asilimia tatu kwenda asilimia nnena ilionekana kulaumiwa na migodi mingine. Migodihiyo mingine nayo imekuwa ya kwanza kukubali kulipamadeni ya nyuma. Natumaini na Barrick naowatakubali kulipa madeni ya nyuma. (Makofi)Kwenye Sheria Mpya ya 2010, yapo mamboambayo yameboreshwa ambayo Watanzania wengihawayaelewi. Huko nyuma migodi hii ilipokujakuwekeza tukiri kuwa ni uwekezaji mkubwa sana.SPIKA: Naomba jielekeze kwenye mike, kadiriunavyokwenda pembeni mike inakuwa mbali.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELE): Mheshimiwa Spika, ni uwekezajimkubwa. Sasa migodi ilipokuwa ikija ilikuwa inaletamkopo wa asilimia 100, kwenye Sheria mpya

tumeboresha kuwa debit na equity lazima iwe asilimia70 kwa asilimia 30. Kwa hiyo, inatusaidia kupunguzamuda wa kulipa Corporate Tax, kwa sababu watuwengi wamekuwa wakizungumza migodi mingi nahailipi Corporate Tax lakini hiyo ilitokana na investmentambazo wameweka pale sasa ile payback periodinakuwa ni ndefu sana kama umekuja na mkopo waasilimia 100. Kwa hiyo, unapopunguza mkopo kwakutumia utaratibu mpya kwenye Sheria yetu nikwamba, inapunguza ule muda wa payback, kwahiyo, migodi mingi imeanza kulipa Corporate Tax,nafikiri kama kuna mgodi ambao haujalipa ni Buzwagi.Hiyo inakwenda sambamba na kurekebisha,reinforce, hii migodi. Barrick zamani walikuwawanachuliwa kama Barrick Tanzania. Kwa hiyo, kamaBuzwagi imeanza leo na Bulya’nhulu imeanza zamanina inapata faida, Tulawaka au Buzwagi ikiwa inapatahasara, hasara ile inabebwa na Bulya’nhulu; kile kitukimerekebishwa kila mgodi utasimama wenyewe. Kwahiyo, kama Bulya’nhulu inapata faida ni faida kwaBulya’nhulu lakini pia Sheria imerekebisha rehabilitationbond hasa mgodi unapokuwa unaelekea kwenyekufungwa, kunakuwa na ile closure planimerekebishwa wataweka bond kiasi kisichopunguaDola milioni thelathini kama security ya Serikali ikitokeakuwa migodi ile haitafanya chochote katika uwekezajiambapo wamechimba mashimo.Mheshimiwa Spika, procurement and servicetumepigia kelele sana kuwa migodi inanunua vyakulanje, mchicha na kila kitu, sasa hivi Sheria yetuinawalazimisha wanunue ndani ili kutoa kipaumbele

kwa makampuni ya ndani na kuweza kutoa supplykatika migodi hii. Hili la service levy linakwendasambamba na makampuni mengine ambayoyamekuwa yanatoa zile huduma, sub-contracting.Ninapenda kutoa rai kwa Halmashauri zote nchinizinazotoa huduma ndani ya migodi, zinapaswa kulipaservice levy kwa sababu msingi wa service levy pia nikuchangia huduma ambayo wanaitumia katikamaeneo husika. Kama wanatumia barabara zetu,wanakanyaga, wanatumia ofisi zetu, kwa hiyo, naowanapaswa kulipa. Nawapongeza Kampuni ya BPambayo sisi Serikali tuna share, wao wanalipa kuleGeita na makampuni mengine yote yanapaswa kulipa.Mheshimiwa Spika, lakini kwenye migodi mipyaitakayoanza na kwa Sheria mpya, tumeweka kuwalazima Serikali tutakuwa na shares zisizopungua asilimia15 na hii itatokana na powers zetu za ku-negotiate.Kwa hiyo, mgodi wowote mpya utakaoanza kablahatujatoa leseni, sisi tunakuwa na share zisizopunguaasilimia 15 kama free carried interest na ambayotutakuwa tunapata gawio mwisho wanapopata faida.Ukiachia mbali kodi ambazo tutapata WaheshimiwaWabunge, napenda hili lieleweke vizuri na Watanzaniawaweze kuona tumepiga hatua kubwa sana tokatulipoanza mpaka sasa, lakini dhamira yetu kamaWizara tupate zaidi ya hapo.Utatuzi na usuluhishi wa migogoro maeneo yamigodi: Kumekuwa na migogoro mingi sana kwenyesehemu za migodi na nimefanya ziara katika baadhi yamaeneo ya Kanda ya Ziwa na Arusha. Migogoro mingiimetokana na aidha baadhi ya watumishi wenye

tamaa ya kutaka kushiriki katika shughuli hizi za madini.Kulikuwa na mgogoro kule Ushirombo, Halmashauriilikuwa inataka kuchukua leseni, tukaushughulikia.Kubwa zaidi, nilitaka kuzungumzia hapa tabia iliyotakakujitokeza ya migodi kushiriki vitendo vya kuua raia.Mheshimiwa Spika, sisi kama Serikali hatuwezikuvumilia mauaji ya wananchi yatokee na tuna wajibuwa ku-guarantee usalama wa Watanzania wotewanaoishi maeneo ya migodi na pia tuna wajibu waku-guarantee usalama wa makampuni ya uwekezaji.Kwa hiyo, sote kwa pamoja tumekaa vikao kuonanamna nzuri ya kufanya kuhakikisha tunapata njiasahihi ya ku-deal na migogoro na kuuwa isiwe kimbiliola kwanza. Kwa hiyo, ndugu zangu maeneo ya Geita,Nyamongo, Mheshimiwa Nyambari Nyangwine,umekuwa ukipiga kelele sana, Amar Kassu kumekuwana mgogoro kule wa Geita - Bulya’hulu wameingiakatika eneo la Wilaya ya Nyang’hwale. Hili napendaniliweke wazi kuwa, tulipoomba taarifa katika Mgodiwa Bulyanhulu hawakutoa taarifa sahihi namnawalivyokwenda kule chini kuvuka mpaka wa Kahamana kuingia upande wa Geita wakati ule ikiitwa na sasainaitwa Nyang’hwale. Kwa hiyo, Wilaya yaNyang’hwale inazo sababu zote za msingi za ku-claimhaki yoyote inayopatikana kutokana na mapato kamaWilaya zingine zenye migodi.Vijiji ambavyo vipo karibu na mgodi ule vimondani ya leseni ya Barrick, Kwa hiyo, tunaangalia nakesho kwenye mazungumzo yetu tutajadili namna yakuwafidia kama Mheshimiwa Mbungealivyopendekeza, ikiwezekana wale wananchi

wafidiwe wahamishwe pale na Nyang’hwale, kamaWilaya ianze kuangalia ni namna gani nayo itanufaikana uwekezaji ule. Kwa sababu underground mgodi waBulya’hulu umeshafika Wilaya ya Nyang’wale kwa zaidiya kilometa moja.Wachimbaji wadogo ndiyo imekuwa focus yetukama Wizara, tunatambua mchango wa Watanzaniana kuwa nchi hii itajengwa na Watanzania wenyewe.Sisi kama Wizara, ninamshukuru Mheshimiwa Waziri,ameshaelekeza kuwa lazima tuwasaidie wachimbajiwadogo wa maeneo ya Nyarugusu, Mgusu,Ushirombo, Ushokerahela, Misungwi na Igalula kule kwandugu yangu Mheshimiwa Mfutakamba na akinaMheshimiwa Lolesia Bukwimba, Mheshimiwa CharlesKitwanga, Mheshimiwa Moza Abedi Said, MheshimiwaEzekiel Maige na Mheshimiwa William Ngeleja, wotewamezungumzia suala hili.Nataka niseme kuwa, hiki ni kipaumbele chetu natumeshaanza kuwatengea maeneo wachimbajiwadogo. Nchi yote imegawanywa, ukiangalia kwenyeramani utaona sehemu zote zina leseni. Kwa Sheria yaMadini hasa eneo la leseni ya utafiti, inapomalizamuda wake yule mwenye leseni anatakiwa aachieeneo nusu kwa Kamishna wa Madini. Kamishnaataangalia kama hilo eneo linafaa kwa matumizi yawachimbaji wadogo, tunawagawia. Kwa hiyo, lesenizote tulizotangaza ambazo hazijatimiza masharti naambazo tumetangaza kwa mujibu wa Sheria,ninawaomba wenye leseni hizo wafuate masharti;vinginevyo, tutazifuta kwa mujibu wa Sheria natutazigawa kwa wachimbaji wadogo.

Mheshimiwa Spika, ndugu zangu kwa eneo hiloieleweke hivyo na ule mgogoro wa kuwa wachimbajiwadogo wanagundua halafu mwekezaji anakuja,shida kubwa pale ni elimu. Unapokuwa unamiliki ardhihaitoshelezi kuwa ndiyo tayari unamiliki leseni yauchimbaji na haimzuii mtu mwingine kuja ku-applyleseni ya uchimbaji katika eneo hilo. Kwa hiyo,nawaomba ndugu zangu Watanzania, mnaoonakwenye maeneo yenu ya asili yana madini, nendenimkaombe leseni, mnapochelewa mtu mwingineakiomba leseni ya utafiti na wewe unapokwendakuomba unakuta tayari lile eneo kuna mtu amekwishaapply, utaratibu ni kuwa, anayeanza ku-apply ndiyoanayehudumiwa. Kwanza, ni suala la elimu;tunaendelea kuitoa ili watu waelewe kumiliki ardhi siyoleseni ya uchumbaji na kumiliki leseni ya uchimbaji siyokumiliki ardhi. Lazima umfuate mtu mwenye ardhimkubaliane naye na aridhike, kwa maana ya kucompensatena upate consent yake. Kwa hiyo,kwenye suala la compensation kumekuwa namalalamiko mengi na hili ndugu zangu tukiri kuwaSheria yetu ya Ardhi inafidia surface.Mtu akikuta madini sehemu anaangalia kama unashamba, una mihogo, miembe, nyumba, ndiyoanafidia surface. Kwa hiyo, nafikiri Bunge hili na sisiWizara tutapenda kupokea mapendekezo na ushaurituone namna wenzetu wa ardhi wanavyoweza kureviewSheria yao ili kama kuna uwezekano tuanzekufikiria na kule chini kuna nini, kwa sababu inakuwa nikelele kuwa mtu anapisha uwekezaji, analipwa mihogoyake na chini anaacha dhahabu. Hilo

tumekwishaliona na tunalifanyia kazi, lakini zaidi, Sheriaya Ardhi inatakiwa iangalie kwenye compensation.Mheshimiwa Spika, Udhibiti na Utoroshaji waMadini. Mimi nilikuwa muumini wa udhibiti na utoroshajiwa madini na nilipokuwa kwenye Kamati ya PACnilikuwa ninagombana sana na Kamishna. Watanzaniawengi tunaamini kwamba, udhibiti ule haukosawasawa lakini ninataka kuwahakikishia ndugu zangukuwa, nilikuwa ninagombana kwenye ukaguzi, lakininimefuatilia nimeona kwa umakini na ndiyo nikajakugundua Agency yetu ya TMAA, inafanya kazi kubwasana ya kubaini upungufu mbalimbali. Haya madeniya nyuma tunayozungumza, TMAA ndiyo iliyofanya zilehesabu na kugundua Tanzanite One Arusha walikuwawana-under declare mrababa kuanzia 2004 – 2008,jumla ya Dola za Kimarekani milioni mbili na nusuzilikuwa hazijalipwa. Hivi sasa tunavyozungumza,ninapenda kulihakikishia Bunge lako kuwa, pesa zilezimelipwa baada ya kukabana na Tanazanite One.Niseme tu kwamba, Mheshimiwa Kahigi alisema kuwa,tunatoa rai siyo tu rai tuko serious na tunakabakwelikweli. (Makofi)(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wamzungumzaji)SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, kengele ya pili.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELE): Mheshimiwa Spika, baada yakusema haya, kwa heshima kubwa, ninawashukuru

sana Waheshimiwa Wabunge, kwa kipekee kabisa kwajinsi walivyotupa nguvu ya kuchapa kazi.Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja.(Makofi)NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, nianze kwakumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa zawadi ya uhai nakuniwezesha leo hii kuwepo na kuongea mbele yenu.Kwanza, ninawatakia Waislamu wote, RamadhaniKareem.Naomba kutumia fursa hii, kuungana naWatanzania wenzangu, kuwapa pole ndugu zetu wotewaliopoteza maisha katika ajali ya meli iliyotokeaZanzibar, tarehe 18 Julai, 2012. Mwenyezi Mungu,azilaze roho za marehemu wote mahala pema peponina wale waliopata madhara waweze kupata nafuu.Kwa namna ya pekee, naomba nimshukuru Raiswangu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kwakuniteua kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini,ninayeshughulikia Nishati. Ninaomba kumwahidi naniwaahidi Watanzania wote kwamba, nitakuwamwadilifu na nitatumia umakini mkubwa katikakufanya kazi yangu na sitamwangusha MheshimiwaRais. (Makofi)Pia nashukuru sana kwa ushirikiano ninaopewa namafundisho na Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa maleziyake na Mawaziri wote, kwa namna wanavyonisaidiakatika kutekeleza wajibu wangu. Ninapenda

kuwashukuru Waheshimiwa Mawaziri na NaibuMawaziri wote walioteuliwa. Kwa kuwa ni mara yanguya kwanza kusimama hap, nawapongeza naWaheshimiwa Wabunge, kwa kuchaguliwa pia.(Makofi)Mheshimiwa Spika, ninawashukuru Wananchi waJimbo la Kibakwe, kwa ushirikiano wanaonipa na hasakatika kipindi hiki ninapotekeleza majukumu yangu yaUnaibu Waziri na Jimbo pia. Ninapenda kuwaahidikuwa, sitawaangusha na nitafanya kila linalowezekanakuleta maendeleo katika Jimbo letu la Kibakwe.(Makofi)Mheshimiwa Spika, ninawashukuru WaheshimiwaWabunge wote, wa Vyama vyote, kwa ushirikianowanaonipa hadi kufikia hatua hii, kwa kuniwezeshakukulia ndani ya Bunge hili. Nikiri kwamba, kisiasa miminimekulia ndani ya Bunge hili; nawashukuruni nyotekwa ushirikiano huu.Mheshimiwa Spika, ninakushukuru wewe binafsikwa malezi yako na hata kuniwezesha leonikaonekana kuwa ninastahili kufanya kazi hii yaUnaibu Waziri na kumsaidia Mheshimiwa Rais. Mwisholakini siyo kwa umuhimu, nawashukuru familia yanguyote na hasa mke wangu Mariana, kwa kunitia nguvuna ushauri katika kutekeleza majukumu yangu.Nachukua nafasi hii ya mwisho katika kushukurukumshukuru sana Mheshimiwa Profesa Muhongo, kwanamna ambavyo anatufanya tufanye naye kazi kwaraha sana. Ukifanya kazi na Profesa unapaswa kuwa

na kasi na kufanya maamuzi na kuthubutu kila wakatina yeye yupo tayari kukusahihisha; Mheshimiwa Waziriwangu ninakushukuru sana. Namshukuru sana piandugu yangu Mheshimiwa Masele, kwa ushirikianoanaonipa, lakini pia Katibu Mkuu wetu Ndugu Maswina Makamishna wote Wizara ya Nishati na Madini,tuendelee kuchapa kazi, tumepata support kubwa yaWatanzania. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kabla sijaingia kwenye hojazilizochangiwa na Wabunge, labda niseme nimetafsirinini leo na jana, kwa muda ambao nimekuwepo katikaBunge kwa miaka takriban saba. Nimeona kitu tofautikwamba, sasa sauti ya Mwenyezi Mungu,imejidhihirisha ndani ya Bunge hili. Kwangu mimi siyosababu ya kujidai, siyo sababu ya kujiona, ninaweza autunaweza Wizara yetu lakini ninaamini kupitia kwenu,Mwenyezi Mungu ameamua kujitokeza na hivyotutajitahidi kufanya kazi kwa niaba ya Watanzaniakuhakikisha kuwa wanaona ile furaha waliyoitarajiawakati wote.Wizara yetu ina mambo mengi makubwa; niWizara ambayo inakamata Uchumi. Ukizungumziaumeme unazungumzia Uchumi wa Nchi. Ukizungumziaumeme unazungumzia uhai na usalama wa Uchumi.Ukizungumzia umeme unazungumzia uhai na usalamawa kisiasa na uhai na usalama wa kijamii. Kwa hiyo,umeme ndiyo kila kitu katika nchi. Wabunge wengiwamechangia kwa hisia mbalimbali; wenginewamesema mambo mengi lakini niseme tu kwamba,haya yote mliyoyasema kwetu sisi ni changamoto tupu;yote yalikuwa yanatusaidia ili kutekeleza majukumu

yetu. Kubwa kuliko yote ambalo limesemwa naWabunge wengi ni lile linalohusu TANESCO na masualaya umeme kwa ujumla; hili limesemwa na takribanWabunge wote.Mheshimiwa Spika, wapo waliochangia kwakuandika, wapo waliochangia kwa kuzungumzaBungeni na wapo ambao kwa kupiga makofi tu huo nimchango tosha, lakini wapo ambao kwa hisia zao tuutaona ni mchango tosha kabisa. Mimi ninaaminikuwa wote humu ndani mmechangia kwa kiasikikubwa jambo hili, kwa hiyo, sihitaji hata kutaja majinakwa kuwa wote nina register rasmi kuwa mmesemajambo linalohusu TANESCO na umeme. Labda nisememambo mawili, matatu, katika sehemu hii.Tulipoingia pale Wizarani tukiongozwa naMheshimiwa Profesa Muhongo, mimi nimwite jembe;tulipoanza kazi kazi yetu kubwa tulianza na TANESCO.Tuliwaita TANESCO ofisini kwetu asubuhi, mchana najioni, lakini kila wakitueleza hatuwaelewi tukasemakuwa labda elimu tunatofautiana hapa mimi sielewi tu.Ukiuliza mapato yanayopatikana huelewi, ukiuliza kunamatatizo gani huelewi, lakini kila unapokaa siku mbiliunaombwa kukubaliana na mgao wa umeme namkizungumza mezani mgao unatoweka. Kumbeumeme wa Tanzania ni suala la kuzungumza mezanihalafu mnakubaliana kuwa unakuwepo mgao auhaupo; hii haikubaliki. (Makofi)Mheshimiwa Spika, hii haiwezi kukubalika naninaamini kwa Waziri wangu Mheshimiwa ProfesaMuhongo na ndugu yangu Mheshimiwa Masele na

Katibu Mkuu Maswi, nawaambieni na niwahakikishienihakuna kitu; wafikirie formation mpya, lakini kwa hilohawawezi. Hisia zilikuwa ni kubwa zinazohusu bei yaumeme, lakini wananchi wengi na Wabungemmefurahia sana juu ya kupunguza gharama zauwekaji umeme. Sisi tunafurahi pia, lakini jambo hilitumelifanya kwa kazi kubwa kweli kweli, limetuchukuatakriban vikao 10 mpaka 15 kuzungumzia kuhusujambo hili tunaambiwa haiwezekani, lakinitunamshukuru Mungu wa Haki leo limewezekana.(Makofi)Kazi kubwa ni kututia moyo ili tuweze kulisimamia,lakini pia kuna suala ambalo Waheshimiwa wengiwamelizungumza; Mheshimiwa Anna KilangoMalecela, Mheshimiwa Joseph Selasini, MheshimiwaAlphaxard Lugola, Mheshimiwa David Kafulila,Mheshimiwa Magale Shibuda na Mheshimiwa EzekielMaige kwamba tuibane TANESCO. TANESCO ndiyo kilakitu; kwa hiyo, kwa kuwa ninyi ndiyo mnaagaliaaccountability ya Serikali kama Bunge, mkituruhusutuwe tunaingilia kwa kibali chenu kinachofanyika ndaniya TANESCO hatutashindwa. Umeme unaibwaTANESCO na wanaoiba wanajulikana hawafanywichochote. Wizi mkubwa wa umeme acha wa vishoka,upo wizi wa kutumia mita hizi za LUKU, mtu anakuwa naunits nyingi haijulikani anazipata wapi. Kwa hiyo, hayayote ni matatizo makubwa ambayo yapo. Nguzozinatoka Mufindi hapa Nchini tunanunua kwa shilingi270,000; kwa nini?Kwa hiyo, nasema sisi tumejipanga, tunaogopa tukwa sababu tatizo ni kubwa sana, tusije tukakurupuka,

tunaenda tukiwa very analytical. Tunataka twendekwa hatua, tumeanza na hatua hii lakini tutaendakimoja baada ya kingine na ninawahakikishieniWatanzania wataonja raha ya maisha. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba nielezee suala la gesi.Suala la gesi nalo limechangiwa na Wabunge wengikwa hisia kubwa, lakini walioongoza kwa hili pamoja naKamati zote mbili ni Wabunge wanaotoka Mikoa yaMtwara na Lindi, wamelisemea jambo hili sana.Wanataka kuona manufaa ya gesi katika maeneoyao. Ni vizuri nikawataja ambao ni Mheshimiwa HawaGhasia, Mheshimiwa Murtaza Mangungu, MheshimiwaJuma Njwayo, Mheshimiwa George Mkuchika,Mheshimiwa Dunstan Mkapa, Mheshimiwa JeromeBwanausi, Mheshimiwa Anna Abdallah, MheshimiwaAgnes Hokololo, Mheshimiwa Anastazia Wambura,Mheshimiwa Mathias Chikawe, Mheshimiwa KassimMajaliwa, Mheshimiwa Faith Mitambo, MheshimiwaFatma Mikidadi, Mheshimiwa Salum Khalfan Barwany,Mheshimiwa Riziki Omary Juma, Mheshimiwa RizikiLulida, Mheshimiwa Diana Mwatuka, MheshimiwaMaulida Anna Komu, Mheshimiwa Mariam Kasembe,Mheshimiwa Jabir Marombwa na Wabunge wenginewengi wamelizungumzia jambo hili.Mheshimiwa Spika, nataka niwahakikishiekwamba, jambo hili Serikali imejipanga kuhakikisha gesiinasaidia Taifa, lakini gesi inayotoka Mtwara na Lindi nilazima na maeneo ambako gesi inatoka waone utamuhuo. Kwa hiyo, tuwahakikishie kwamba tumejipangana tunatambua kuwa zipo ahadi nyingi zilizotolewa naSerikali, wakati wa kuzitekeleza sasa umefika na kama

mnabisha angalieni tunafanya nini kuanziatutakapopitisha Bajeti yetu leo. Tusaidieni tupitishebajeti na tunawahakikishia kwamba, tutaanzakuchukua hatua. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ninawafahamisha Wabungehawa kwamba, yaliyofanywa kule ni mambo mengi,sasa hivi tuna transfoma 37 tulizozipeleka kule, hapotuna uhakika wa vijiji vingi sana kupata umeme. Pia vijijivyote vinavyopitiwa na bomba lile tunataka viwe naumeme. Hapa kama Serikali hatuzungumzii suala laumeme kwamba wapate umeme, kwa sababu gesiinatoka kule tunataka tuzungumzie na miundombinumingine yote, kama barabara na viwanda kwa ujumlawake. Kwa sababu mtu akiweka viwanda kule Mtwarani dhahiri kwamba, ataweza kuzalisha kwa bei ndogo,kwa sababu umeme wa kule utakuwa na special tariff.Pamoja na hali ilivyo sasa, leo hii umeme uliopoMtwara bado ni mwingi na tunahitaji kuuendeleza zaidikwa matumizi na bado uchumi wa Mtwara upo chinikwa sababu bado tunahitaji kuweka viwanda. Kwahiyo, nachukua nafasi hii kwa niaba ya Serikali kutoawito kwa wawekezaji mahali popote kwendakuwekeza pamoja na kwamba nchi nzima panafaa,lakini Mtwara na Lindi panafaa zaidi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, gharama ya umeme wa Kusinina mipango ya umeme kwamba REA haipo kule Kusini,jamani ninyi watu wa Kusini ni Special Zone,msizungumzie habari ya REA. Ninyi mnazungumziaSpecial Program ya Serikali, namna ya kupandishahadhi na maisha ya watu kwa kupitia umeme,barabara na kila kitu. Ninawaomba sana Wabunge

wote wa Lindi na Mtwara, Jumatatu, saa saba, baadaya Bunge, tukutane ili tuweze kufundana vizuri natuoneshane ni nini Serikali inataka kufanya katika Mikoayenu.Mheshimiwa Spika, lilizungumzwa pia suala lakukatika umeme katika Majimbo mbalimbali. Matatizohaya yanatokana na uchakavu wa laini na Mzee waVunjo na Rombo Mheshimiwa Selasini alisema hili naWabunge wengi wamesema katika maeneo yaokwamba, sehemu hizo umeme unakatika sana.Naomba niwahakikishie kwamba, kama tutaibanamianya ya fedha inayopotea TANESCO, kamatutabana matumizi na mikataba mibovu na kamakweli tutahakikisha tunaifanya TANESCO ikae mahalipanapotakiwa, marekebisho ya vitu hivi ni madogosana na ya hela kidogo sana. Kwa hiyo, marekebishohaya yatakuja na mimi niwahakikishie kwamba,tutarekebisha sehemu zenye umeme ili uweze kutulia.Mheshimiwa Spika, yapo mengine yaliyosemwa naMheshimiwa David Kafulila, Mheshimiwa Kabwe Zitto,Mheshimiwa Gosbert Blandes na MheshimiwaDeogratias Ntukamazina kwamba, Mikoa ya Kigoma,Katavi na Rukwa, ule Mradi ambao tunautarajia wanjia ya electricity five, ninyi kule mpo salama isipokuwatu bado Serikali hatujafikia kwenye stage za kupatafedha. Tungeweza kusema stage tulizofikia lakini siyovizuri kusema jambo ambalo lipo kwenye process. Kwahiyo, program ile itatusaidia, lakini itaenda sambambana Mradi wa Malagarasi wa 42 Megawatts na MrongoKigakata 16 Megawatts. Hii itaenda pamoja katikapackage hiyo.

Mheshimiwa Spika, pia nizungumzie suala zima lachangamoto za utekelezaji wa mfumo wa uagizajimafuta kwa pamoja. Mfumo huu wa uagizaji wamafuta umetusaidia sana Serikali katika kuhakikishaangalau tunadhibiti mapato na kupata mapatomakubwa. Mfumo huu wa kuagiza mafuta kwapamoja umeisaidia hata TRA kukusanya fedha nyingiza kutosha. Mfumo huu umetusaidia kudhibitiuchakachuaji, lakini pia nirudie kusema hata sualazima la vinasaba ambalo Wabunge mmelisema sanahapa.Mkataba wa Vinasaba unaisha mwezi wa nanemwishoni; tuache uishe tukae tutafakari tutashaurianana Bunge tuone njia bora ni ipi ya kufanya, kwasababu imeelezwa hapa na hoja hii ni ya msingikwamba, vinasaba vinaongeza gharama ya mafuta.Hatuwezi kukataa moja kwa moja, tutaangalia the bestway.Mheshimiwa Spika, yapo mawazo pia katikaWizara kwamba, kwa nini tusitafute njia ya usafirishajiwa mafuta kwa kutumia monitoring ya magari yaelectronic. Siku hizi teknolojia zimepanda, unawezaukafunga vifaa na wanaosafirisha mafuta na exportikajulikana au under escort, kwa namna yoyote iletutakubaliana lakini dhamira ya Serikali ni kupunguzagharama kwa mwananchi wa kawaida. Kwa sababugharama ya mafuta huwa inahamia kwa mwananchiwa kawaida.

Mheshimiwa Spika, suala zima la kufufua Kampuniya Mafuta ya OPEC, Serikali imeshaanza kuchukuahatua na tunadhani kufanya downstream business yamafuta ni muhimu kwa Serikali. Kuwa na kampuniinayoshiriki na Private Sector ni muhimu kwa sababuinatusaidia kupata information ya industry ya mafutainakwendaje, ingawa kuna gharama lakini hatuazimeshaanza kuchukuliwa.Mheshimiwa Spika, lilizungumzwa suala lingine lakwamba, Serikali inachukua hatua gani kuhusu tatizo lakuingiza nchini mafuta yasiyokidhi viwango. Niseme tukwamba, EWURA wameshauri, TBS uwezo wao wakupima mafuta kama tulivyoweza kupata taarifambalimbali ni mdogo, wanapima vipimo vichache tukati ya vipimo vingi wanavyotakiwa kuvipima. Kwahiyo, tumeshauri EWURA wenyewe waanzishe maabarawaweze kupima wenyewe mafuta. Pia tunafikiriaurekebishaji wa Kanuni za Uagizaji wa Mafuta kwaPamoja ili kuhakikisha tunaziba mianya katikakutekeleza mfumo huo.Mheshimiwa Spika, uandaji wa Sera ya Gesitunawahakikishia kwamba, mwezi huu tisa Seraitakuwa imekamilika na mchakato wa consultationunaanza mapema kabisa baada ya Bunge hili. Kwahiyo, niwahakikishie kwamba, Sera ya Gesi itakujamapema na kwa hiyo hadi Bunge linalokuja Sheriainaweza ikawa Mezani kwa ajili ya kujadiliwa. Hapondipo tutakapotakiwa kusema ni namna ganitunaweza kulinda maslahi yetu.

Mheshimiwa Spika, wapo wengine wameletadhana hapa kwamba, eti Serikali tumeshaingiamikataba mibovu. Nataka niwahakikishie kwamba,katika gesi bado hatujapoteza, tukijilinganisha sisi nanchi za wenzetu, kwa mfano, Afrika Kusini, sisitumewazidi. Ukiangalia fiscal regime comparison yakwetu sisi Tanzania ambao hatujaanza hata kufanyaproduction, tupo at 72 percent ya Government take,Serikali inachopata ni 72 percent. Kwa hiyo, tunawazidiAfrika Kusini, tunawazidi Mozambique, tunawazidiNamibia na pengine tunaweza tukaenda zaidi yahapo kwa sababu suala la biashara ya gesi, investmentinapoanza inakuwa kidogo, mzani una-balance lakinikadiri miaka inavyokwenda na tunavyozidi kuzalisha,Serikali inazidi kuwa na hisa nyingi zaidi na baadayeinaweza ikawa na hisa nyingi kuliko hata kampuni.Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tusiwe na wasiwasihatujapoteza, we are in 72 percent of Governmenttake. Tukae tusubiri Sera ije, tufikirie tuweke namnagani. 72 percent siyo mbaya, huko kwingine AfrikaKusini wenyewe wapo kwenye almost 30 percent.Mheshimiwa Spika, najua muda wangu ni mdogona pengine siyo rahisi kujibu hoja zote. NiwahakikishieWabunge yale maombi yao yote ya Vijiji vyao namaeneo inapopita Miradi ya REA na marekebishowanayotaka, kama kuna maombi mapya, sisi Wizarayetu haina usiri, njoo tukae tukubaliane umeme upitewapi, wapi uliruka na wapi tufanye nini. Niwahakikishiekwamba, Wizara imeagiza transfoma 370, kazi yatransfoma hizo ni kwa ajili ya kutatua matatizo ya waleambao nyaya zinapita juu. Wananchi wanauona

umeme unapita, tunataka kote kwenye maeneo hayoambako umeme unapita juu transfoma 370 ni kushushatu kila mahali. (Makofi)Mheshimiwa Spika, ninaamini target ya Serikali yaChama cha Mapinduzi itafikiwa, asilimia 30 yaWatanzania watakuwa na umeme.Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hiikuwashukuru sana, kama nilivyosema, siyo rahisi sanakutumia muda huu wa dakika 20 kujibu hoja hizi zote,maana ili nijibu hoja zote nilipaswa nisome karatasizote, siyo rahisi sana. Kwa hiyo, niwahakikishie tukwamba, tutatoa majibu yote, tutaweka kwenyepigeon hall na pengine wale Wabunge ambaowanataka kupata ufafanuzi wa mambo yao, thisMinistry should be a friendly Ministry. Wabunge muwena urafiki na Wizara hii; mmeanzisha ukombozi waTanzania katika Wizara yetu, sisi hatutawaangusha. Nichangamoto kwetu kuhakikisha kwamba, tunafanyakazi nzuri kwa Watanzania na kuhakikisha kwamba,tunakuwa karibu na Wabunge maana mmeamuakutuonesha maajabu ya Mungu kupitia Wizara yetu.Tunawaahidi huduma iliyotukuka na uaminifu mkubwana Mwenyezi Mungu atatusaidia katika hili.Mheshimiwa Spika, nisingependa kengeleinigongee, nawashukuru Wabunge wenzangu,naomba kuunga hoja mkono. (Makofi)SPIKA: Ahsante, sasa nitamwita mtoa hoja.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika,nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu,Mwingi wa Rehema, kwa kuniwezesha kufika siku ya leoninapohitimisha hoja yangu kuhusu Makadirio yaMapato na Matumizi kwa Mwaka 2012/13.Mheshimiwa Spika, natoa shukrani za dhati kwaMheshimiwa Selemani Zedi, Mwenyekiti wa Kamati yaKudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na MheshimiwaJohn Mnyika, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni. Kwa namna ya kipekee kabisanaomba niwashukuru sana Wabunge wote bila kujaliitikadi zetu, tumepokea, tumejadili na kutoa maelekezokwa Wizara yangu. Maelezo na ushauri wenu nichachu ya utendaji ambao wenzangu wanapaswakuanza kuuekeleza mara moja.Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hoja hii,Wabunge wamepata nafasi ya kuchangia kwamaandishi ambao jumla yao ni 194. Waliochangia kwakuzungumza ni 30.Mheshimiwa Spika, nitaanza kuwatambua kwamajina muda si mrefu, ambaye sitamtaja jina lakeanisamehe kwa dhati kwani sikukusudia ilanikikumbushwa nitataja jina lake kabla sijahitimishahoja yangu.Mheshimiwa Spika, orodha ya Wabungewaliochangia kwa kuzungumza ni kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Mussa Zungu Azzan, Mbunge wa Ilala,Mheshimiwa Said Bungala, Mbunge wa Kilwa Kusini,

Mheshimiwa Rachel Mashishanga Robert, Mbunge waViti Maalum, Mheshimiwa Hasnain Mohamed Murji,Mbunge wa Mtwara Mjini, Mheshimiwa ShaffinAhmedali Sumar, Mbunge wa Tabora Kaskazini,Mheshimiwa Diana Mkumbo Chilolo, Mbunge wa VitiMaalum, Mheshimiwa Christopher Ole Sendeka,Mbunge wa Simanjiro, Mheshimiwa Anne KilangoMalecela, Mbunge wa Same Mashariki, MheshimiwaJoseph Roman Selasini, Mbunge wa Rombo,Mheshimiwa Gosbert Blandes, Mbunge wa Karagwe,Mheshimiwa Hamis Missanga, Mbunge wa SingidaMagharibi, Mheshimiwa Vick Kamata, Mbunge wa VitiMaalum, Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, Mbungewa Nyang’hwale, Mheshimiwa Lolesia Bukwimba,Mbunge wa Jimbo la Busanda, Mheshimiwa Dkt. HamisKigwangalla, Mbunge wa Nzega, MheshimiwaAlphaxard Lugola, Mbunge wa Mwibara naMheshimiwa Subira Mgalu, Mbunge wa Viti Maalum.Mheshimiwa Spika, Wabunge wenginewaliochangia ni Mheshimiwa Moza Abedi Saidy,Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa John ShibudaMagalle, Mbunge wa Maswa, Mheshimiwa EzekielMaige, Mbunge wa Msalala, Mheshimiwa PudencianaKikwembe, Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa VitaKawawa, Mbunge wa Namtumbo, Mheshimiwa SaidMussa Zubeir, Mbunge wa Fuoni, Mheshimiwa MarthaUmbulla, Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa FatmaAbdallah Mikidadi, Mbunge wa Viti Maalum,Mheshimiwa Prof. Kulikoyela Kahigi, Mbunge waBukombe, Mheshimiwa Abia Nyabakari, Mbunge waViti Maalum na Mheshimiwa Joseph Kandege Mbungewa Jimbo la Kalambo.

Mheshimiwa Spika, kwa kuokoa muda na kwakuwa Majimbo yenu mnayafahamu, naomba nisitajeMajimbo.Mheshimiwa Spika, orodha ya Wabungewaliochangia kwa maandishi ni kama ifuatavyo:-Mheshimiwa Dkt. Charles Tizeba, MheshimiwaAnna MaryStella Mallac, Mheshimiwa DeogratiasNtukamazina, Mheshimiwa Gosbert Blandes,Mheshimiwa Lucy Mayenga, Mheshimiwa MariamKisangi, Mheshimiwa Nyambari Nyangwine,Mheshimiwa Hezekia Chibulunje, Mheshimiwa Abdul-Aziz Abood, Mheshimiwa Sylvester Kasulumbayi,Mheshimiwa Rebecca Mngodo, Mheshimiwa ShukuruKawambwa, Mheshimiwa Ezekiel Maige, MheshimiwaAugustino Massele, Mheshimiwa Hussein Mussa Mzee,Mheshimiwa David Kafulila, Mheshimiwa BettyMachangu, Mheshimiwa Leticia Nyerere, MheshimiwaHenry Shekifu, Mheshimiwa Stephen Ngonyani,Mheshimiwa Juma Nkamia, Mheshimiwa Dkt. Kebwe S.Kebwe, Mheshimiwa Moshi Kakoso, MheshimiwaCharles Mwijage, Mheshimiwa Said Amour Arfi,Mheshimiwa Vincent Nyerere, Mheshimiwa MajaliwaKassim Majaliwa, Mheshimiwa Susan Lyimo,Mheshimiwa Amos Makalla, Mheshimiwa MwiguluMadelu, Mheshimiwa Hussein Nassor Ama, MheshimiwaVita Kawawa na Mheshimiwa Modestus Kilufi.Mheshimiwa Spika, wengine ni Mheshimiwa Dkt.Festus Limbu, Mheshimiwa Josephine Genzabuke,Mheshimiwa Dkt. Seif Seleman Rashid, Mheshimiwa

Aggrey Mwanri, Mheshimiwa Edward Lowassa,Mheshimiwa Rita Mlaki, Mheshimiwa Lucy Owenya,Mheshimiwa Josephine Chagulla, Mheshimiwa AzzaHamadi Hilal, Mheshimiwa Ismail Rage, MheshimiwaBrig. Jen. Hassan Ngwilizi, Mheshimiwa Goodluck Ole-Medeye, Mheshimiwa David Malole, MheshimiwaMariam Kasembe, Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah,Mheshimiwa Dkt. Titus Kamani, Mheshimiwa SabreenaSungura, Mheshimiwa Fakharia Khamis Shomar,Mheshimiwa Kabwe Zitto, Mheshimiwa Abdul JabiriMarombwa, Mheshimiwa Athumani Mfutakamba,Mheshimiwa Deo Filikunjombe, Mheshimiwa Capt. JohnChiligati, Mheshimwia Rosweeter Kasikila, MheshimiwaMary Nagu, Mheshimiwa Mary Mwanjelwa,Mheshimiwa Lazaro Nyalandu, Mheshimiwa AssumpterMshama, Mheshimiwa Margaret Sitta, MheshimiwaWilliam Lukuvi, Mheshimiwa Mansoor Hiran,Mheshimiwa Ignas Malocha, Mheshimiwa JosephKandege, Mheshimiwa Richard Ndassa, MheshimiwaChristowaja Mtinda, Mheshimiwa Mathias Chikawe,Mheshimiwa Abuu Hamoud Jumaa, Mheshimiwa Dkt.Augustine Mrema, Mheshimiwa Desderius Mipata,Mheshimiwa Amina Abdallah Amour, MheshimiwaMch. Israel Natse, Mheshimiwa Magdalena Sakaya,Mheshimiwa Abdallah Sharia Amer, Mheshimiwa SaraMsafiri Ally, Mheshimiwa Mendrad Kigola, MheshimiwaPhilipa Mturano, Mheshimiwa Mustapha Akunaay,Mheshimiwa Susan Kiwanga, Mheshimiwa HalimaMdee, Mheshimiwa Pauline Gekul, Mheshimiwa JumaNjwayo, Mheshimiwa Riziki Lulida na Mheshimiwa RitaKabati.

Mheshimiwa Spika, wengine ni Mheshimiwa Eng.Gerson Lwenge, Mheshimiwa Abdulsalaam SelemaniAmer, Mheshimiwa Said Nkumba, Mheshimiwa Prof.Peter Msolla, Mheshimiwa Naomi Kaihula, MheshimiwaCecilia Paresso, Mheshimiwa Alphaxard Lugola,Mheshimiwa Felister Bura, Mheshimiwa LivingstoneLusinde, Mheshimiwa Tundu Lisssu, MheshimiwaMwanamrisho Taratibu Abama, Mheshimiwa DianaMkumbo Chilolo, Mheshimiwa Mkiwa Kimwanga,Mheshimiwa Mahamoud Mgimwa, Mheshimiwa Dkt.Haji Hussein Mponda, Mheshimiwa Yussuf Haji Khamis,Mheshimiwa Highness Kiwia, Mheshimiwa HawaAbdulrahman Ghasia, Mheshimiwa Gregory GeorgeTeu, Mheshimiwa Zahra Ali Hamad, Mheshimiwa Prof.Juma Kapuya, Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge,Mheshimiwa Moses Machali, Mheshimiwa AlbertNtabaliba, Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, MheshimiwaSaleh Pamba, Mheshimiwa Prof. Kulikoyela Kahigi,Mheshimiwa Maryam Msabaha, Mheshimiwa HamadAli Hamad, Mheshimiwa Dkt. Lucy Nkya, MheshimiwaMoza Abedi Saidy, Mheshimiwa Haji Juma Seleweji,Mheshimiwa Martha Moses Mlata, Mheshimiwa OmariRashid Nundu, Mheshimiwa Dustan Kitandula naMheshimiwa Fatma Mikidadi.Mheshimiwa Spika, wengine ni MheshimiwaSelemani Jumanne Zedi, Mheshimiwa Zarina ShamteMadabida, Mheshimiwa Juma Sururu Juma,Mheshimiwa Ally Keissy Mohamed, Mheshimiwa SamiaSuluhu Hassan, Mheshimiwa Catherine Magige,Mheshimiwa Abdulkarim Shah, Mheshimiwa Dkt. DalaliKafumu, Mheshimiwa Joshua Nassar, MheshimiwaSelemani Saidi Jafo, Mheshimiwa Luhaga Mpina,

Mheshimiwa Salum Khalfan Barwany, MheshimiwaKuruthum Mchuchuli, Mheshimiwa Khatib Said Haji,Mheshimiwa Rashid Ali Omar, Mheshimiwa HaroubMuhammed Shamis, Mheshimiwa Ali Khamis Seif,Mheshimiwa Haji Khatib Kai, Mheshimiwa Ester Bulaya,Mheshimiwa David Silinde, Mheshimiwa Mbarouk SalimAli, Mheshimiwa Meshack Opolukwa, MheshimiwaJames Mbatia, Mheshimiwa Dkt. Terezya Huviza,Mheshimiwa Deo Filikunjombe; huyu labda ameandikamara tatu tatu, Mheshimiwa Eugen Mwaiposa,Mheshimiwa Masoud Abdalla Salim, Mheshimiwa ChikuAbwao, Mheshimiwa Faith Mitambo, MheshimiwaJames Mbatia, Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla,Mheshimiwa John Mnyika, Mheshimiwa Dkt. AbdullaJuma Abdulla Saadalla, Mheshimiwa James Lembeli,Mheshimiwa Rajab Mbarouk Mohamed, MheshimiwaOmary Badwel, Mheshimiwa Luhaga Mpina,Mheshimiwa Kombo Khamis Kombo, MheshimiwaAgripina Zaituni Buyogela, Mheshimiwa Dkt. DavidMathayo David, Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmed,Mheshimiwa Ester Matiko, Mheshimiwa BeatriceShellukindo, Mheshimiwa Waride Bakari Jabu naMheshimiwa Herbert Mntangi.Mheshimiwa Spika, wengine ni MheshimiwaGeorge Huruma Mkuchika, Mheshimiwa Ezekia Wenje,Mheshimiwa Ummy Ally Mwalimu, Mheshimiwa MhongaSaid Ruhwanya, Mheshimiwa Dkt. Kebwe S. Kebwe,Mheshimiwa Muhammad Ibrahim Sanya, MheshimiwaAnastazia James Wambura, Mheshimiwa Dkt.Pudenciana Kikwembe, Mheshimiwa John Cheyo,Mheshimiwa Salum Barwany, Mheshimiwa Kaika Telele,Mheshimiwa Suleiman Nassib Omar, Mheshimiwa

Dunstan Mkapa, Mheshimiwa Murtaza Mangungu,Mheshimiwa Abdalla Haji Ali, Mheshimiwa Said MussaZubeir, Mheshimiwa Bahati Ali Abeid, Mheshimiwa Eng.Hamad Yussuf Masauni, Mheshimiwa Amina NassoroMakilagi, Mheshimiwa Zitto Kabwe, Mheshimiwa NassirYussuf, Mheshimiwa Jenista Mhagama na ndugu zanguwaliowakilisha hapa Mheshimiwa Steven Maselle naMheshimiwa George Simbachawene.Waheshimiwa Wabunge, napenda kusisitiza fursaniliyowapatia kwamba, huenda muda hautoshi namaswali mnayo mengi sana. Wizara yetu inatakakufanya kazi karibu sana na ninyi. Kwa hiyo,nimewaagiza wafanyakazi wote ambao wapo hapakwa ajili ya bajeti wakiwa na Wakuu wao wa Vitengo,kuanzia kesho watasikiliza hoja zenu ambazo mnazo.Kwa hiyo, kesho Jumapili, kati ya saa tatu asubuhimpaka saa saba, tafadhali kama una tatizo lolote hasaukiangalia ile michoro, tuliwapatia njooni ofisini kwetu,ofisi ipo nyuma ya Dodoma Hoteli. Watakaa hapahapa Jumatatu na Jumanne kuanzia saa mbili asubuhimpaka saa 12 jioni. Kwa hiyo, jamani wenye kiu yamaswali tunawakaribisha sana. (Makofi)Pili, napenda sasa niwaeleze kidogo tatizo ambalolimeleta mambo mengi, la TANESCO nadhani ni vizurimlisikie kutoka kwangu mwenyewe. Kabla sijalisemahilo, kuna vitu viwili ambavyo ni vya muhimu sana.Napenda niwaeleze Waheshimiwa Wabunge naWatanzania wote wanaotusikiliza hapa; alikuwepoMwanafilosofia mmoja, mwenyeji wa Scotland,walikuwa kwenye majadiliano mengi sana ya mambo

ya filosofia. Mwaka 1852 alisema nitayatafsiri kwaKiswahili baadaye.Alisema truth like a touch, the more it shock itshines, narudia tena hii ni lugha ya zamani kidogo, siyoKiingereza chepesi cha siku hizi. Truth like a touch, themore it shock it shines, yaani ukweli ni kama tochi aukurunzi yenye betri, ndani unavyozidi kuitingisha ndivyojinsi ambavyo mwanga unazidi kuwaka. Unajua tafsirihizi unamwachia mtu mwenyewe huwezi ukamtafsiria.(Makofi)Wa pili, alikuwepo Mwandishi maarufu sana waKimarekani alikuwa anaitwa Walter Lipman, tarehe 14Aprili, 1945 alikuwa Mwandishi wa New York HeradTribunal, Gazeti la New York lile, ni kubwa sana mpakasasa hivi bado lipo. Tarehe 14 Aprili, 1945 alisema haya:“The final test of a leader is that he lives behind him inother men the conviction and the will to carry on.”Naomba nirudie tena: “The final test of a leader is thathe lives behind him in other men the conviction andthe will to carry on.” Kwa maneno mengine, ukitakakujua mafanikio ya Kiongozi yeyote ni yule ambayeameacha kitu nyuma, amewaacha watu nyumaambao wanataka kuyaendeleza yale aliyoyaacha.Kwa siku chache nilizokaa hapa Bungeni, hapa nduguzangu mtakapokuwa mnafanya hii tafsiri kuna makundiya watu wawili; kuna kundi la Mwalimu Nyerere, kunakundi la Marehemu Sokoine na kuna kundi la Kawawa.Utakavyokuwa unafanya tafsiri, kuna kundi lingine laMobutu, kuna kundi la Bokasa na kundi la Abani.(Makofi/Kicheko)

Mimi nilipata bahati kusoma shule yetu ilikuwanzuri. Mimi kwetu ni Musoma Mjini pale, kwanza,Ndugu Maswi hata hatusikilizani lugha, yeye anatokaTarime mimi natoka Musoma Mjini. Huyu kijana Nyerereni mpwa wangu, kutoka kwao na kwetu ni nyumbatano tu, ni mpwa wangu wa karibu sana. MwalimuNyerere wakati nikiwa form one, mnamjua NeilArmstrong, mtu wa kwanza kutembea kwenye mweziilikuwa tarehe 20 Julai, 1969 na mimi nilikuwa form one,bahati nzuri nilisoma Shule ya Wamarekani tukaonaArmstrong anatua mwezini. Mwalimu alikuwa mwepesisana kutufanya wakati huo tusipoteze na kujidharau,alisema hivi: “Wakati wengine wanakwenda mwezini,sisi twende vijijini. Je, Wabunge na Serikali tulimsikilizaMwalimu? (Makofi)Sasa nije TANESCO. Mtu anayeitetea TANESCO auanayewaumiza TANESCO, msichukue the short historykama kile kitabu tulichokuwa tunakisoma; Short Historyof Tanganyika, chukua Long History. Hili Shirikalilianzishwa mwaka 1930, yalikuwa makampuni mawiliyakaja pamoja. Sasa toka mwaka 1930 hata kamainabadilisha watu wanaoiendesha hamuwezikulikubalia hadi leo hii, asilimia chini ya 20 yaWatanzania hawana umeme. Unatetea nini; unateteaupuuzi tu? (Makofi)Isitoshe ni kwamba, TANESCO ni asilimia 100, niShirika la Umma la Serikali. Yeyote anayejidanganyakwamba halitaingiliwa anapoteza muda, tutaliingilia tu.(Makofi)

Sasa basi kama ni hisa 100 na ninyi Watanzaniammejua mambo ya hisa siku hizi, sote hapa tumenunuahisa huku mbili, tatu, si kila mwisho wa mwakamnapata gawio (dividend)? Nitaongea na Wazirimwenzangu wa Fedha, tuanzie TANESCO na Mashirikayangu yaliyoko chini yangu nayapa maagizo, Januarimwakani lazima tufanye kikao. Wao watakuwawanatoa fedha ngapi kurudishia wenye hisa?Hamuwezi kuja hapa kila siku bajeti hazitoshi mnasemavyanzo mnapeleka kwenye bia badala ya kwendakuchukua hela TANESCO. (Makofi)Mwisho, muundo mpya wa kutatua matatizo yaWizarani kwangu; mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Bodi yaSTAMICO, nilikuwa Mwenyekiti wa Tume Teuleiliyokwenda kuchunguza vifo vya Mererani mwaka2002, lakini wengi nadhani hiyo ripoti yangu hamjaiona.Sasa tunakuja na mtindo mpya, lazima tubadilike.Nami nasema Wizara yangu haya mambo ya Tumesiyataki. Kitakachotokea kuanzia sasa tujaribu huumtindo tukishindwa tutarudi kwenye Tume, kama tatizolimetokea kwa sababu Wafanyakazi wa Wizarawanalipwa kwa ajili ya shughuli hiyo, watakwenda nakushughulikia hilo tatizo, watatengeneza ripoti halafututakuwa na kitu kinachoitwa public hearing, yaanihiyo Ripoti kama Ripoti ni watu wa Mererani,tutakwenda nayo na mimi mwenye nitakuwepoitawasilishwa tutaijadili tutamaliza hapo na Watanzaniawanasonga mbele. (Makofi)Sasa kwa sababu sitaki kukosa neno, naombanizungumzie utendaji wa Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO. Tangu kuteuliwa kuiongoza Wizara ya Nishati

na Madini, tumeona uwajibikaji usiokidhi matakwa yaKanuni za Utumishi katika uendeshaji wa Shirika la Ugavina Umeme nchini.Mheshimiwa Spika, TANESCO ni Shirika la Ummakwa asilimia 100; hivyo, linahitaji kuangaliwa kwa karibusana na kuchukua hatua za haraka ili kuwezeshaustawi wa Watanzania. Napenda kulihakikishia Bungelako Tukufu kuwa, tumeamua kwa dhati kabisakurejesha heshima ya Serikali katika eneo hili. (Makofi)Kama TANESCO watafanya kazi kulingana nataratibu, hatuna tatizo, kinyume chake lazimatuchukue hatua bila kusita. (Makofi)Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge,wameshauri tuongeze juhudi na turudishe heshimakatika TANESCO, nami nasema hili linawezekana kwakuwa tumedhamiria, nia tunayo na uwezo tunao.(Makofi)Uamuzi wa kumsimamisha Mkurugenzi MtendajiMkuu wa TANESCO, ulichukuliwa na Bodi yaWakurugenzi katika Kikao cha Dharura cha tarehe 13 -14 Julai, 2012. Kwa mujibu wa maelezo ya Bodi,amesimamishwa kutokana na tuhumu za ubadhirifu namatumizi mabaya ya madaraka. Bodi ya Wakurugenziimemwomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu zaSerikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma hizo.Mheshimiwa Spika, baadhi ya tuhuma zilizo dhahirina zitafanyiwa kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu waHesabu za Serikali ni pamoja na hizi hapa: Kwanza,kukiuka, maadili ya utumishi wa umma kwa kuingia

mkataba ambao yeye mwenyewe ana maslahi namke wake Eva akiwa Mkurugenzi. Aidha, Wakurugenziwengine ni watoto wake; Fred na Veronica William. Nikweli kabisa, kampuni yao iliyoanza kazi Aprili, 2012,kwa mtaji wa shilingi milioni kumi, miezi minanebaadaye ilipata mkataba wa zaidi ya shilingi milioni 880TANESCO. (Makofi)- Kuwepo kwa manunuzi mengi yasiyokidhivigezo ni tatizo lingine kubwa katika TANESCO. Wakatinafanya kikao na Wafanyakazi wa TANESCOwalioandika tuhuma zilikuwa zimejaa kasha. Moja,iliyonifurahisha sana na kunisikitisha ni kwamba,waliagiza spare part kutoka Uingereza wakalipia Pauni50,000 kumbe lilikuwa box la misumari.- Kukumbatia wafanyabiashara ambaowalichangia sana kushindwa kwake kutenganishamaslahi binafsi na maslahi ya Shirika.Waheshimiwa Wabunge, kuna Wabunge wawili,watatu siwezi kuwataja.WABUNGE FULANI: Wataje.WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Hawapo huko,wao walinipatia information nzuri nikaimeza; nikwamba, mimi mwenyewe nilikuwa najua kwambahizo nguzo ambazo tunapigia kelele zinatoka hapahapa nchini huko Iringa, zinasafirishwa kwendaMombasa halafu zinarudishwa nchini zikiwa nguzo zaSouth Africa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunao ushahidi usio na shakawa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge na Wajumbewa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,kufanya biashara na TANESCO. Ni kazi ngumu kwelikweli kumsimamia anayekupa biashara na hawezikukuheshimu kwa kuwa anakufahamu na anakufadhili.Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge, wameingiamkataba wa kuiuzia TANESCO matairi na kushinikizakubadili bei ya matairi hayo baada ya mkatabakufungwa na hili lilifanyika pamoja na kuwa matairihayo hayakuwa na viwango. (Makofi)Mheshimiwa Spika, naomba niwashauri nakuwaomba Waheshimiwa Wabunge, kwa dhati kabisa,waache kufanya biashara na TANESCO ili wawe nauhuru wa kuisimamia na kuiwajibisha paleinaposhindwa kutekeleza majukumu yake; kufanyavinginevyo ni kujiweka katika mazingira magumu sanaya kimaslahi.Mheshimiwa Spika, kuhusu pendekezo kuwaiundwe Tume Teule, ni maoni yangu kuwa hakunaumuhimu wa kufanya hivyo, kwa vile tayari CAGalishapewa kazi hiyo. Kwa hiyo, Watanzania namagazeti yote tufunge huu mjadala tufanye mambomengine ya muhimu. (Makofi)Mheshimiwa Spika, niruhusu nijibu hoja chachekwa kufuata maudhui yanayofanana. Nawashukurusana Naibu Mawaziri wa Madini, kwa kujibu vizuri hojaza Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, sasa niruhusu nijibu hojachache kwa kufuata maudhui yanayofanana.Nawashukuru sana Waheshimiwa Naibu Mawaziri waNishati na Madini kwa kujibu vizuri hoja zaWaheshimiwa Wabunge. Wamenirahisishia kazi. Nianzena Hoja za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati naMadini.Mheshimiwa Spika, Sera, Sheria na MpangoKabambe wa Gesi Asili. Umuhimu wa Sera, Sheria naMpango Kabambe uko wazi. Wizara imekamilishamaandalizi ya Sera hiyo na nadhani Naibu Waziriameieleza kwa ufasaha kabisa.Mheshimiwa Spika, hofu ya mgawo wa umeme.Hofu isiyo ya lazima imetanda miongoni mwetu nakukuzwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusuuwezekano wa kuwa na mgawo wa umeme. Nadhanina hili limeelezwa vizuri kwa sababu capacity yakuzalisha tunayo na matumizi yetu yako chini zaidi.Mheshimiwa Spika, TPDC kusitisha ugawaji wavitalu. Kuna ukweli kuwa Sheria na Sera za Gesizikikamilishwa, mikataba ya utafutaji inaweza kuwabora zaidi. Hata hivyo, Sera ya Nishati na Madini, Sheriaya Utafutaji wa Mafuta na Gesi ya mwaka 1980 naModel PSA, vinatosheleza mahitaji ya sasa. Pamoja nahayo, suala la ugawaji wa vitalu vya kutafutia mafutana gesi asili katika maeneo ya baharini, linaanzakuonekana kuwa tete. Hapa inabidi tuchukue hadharikubwa kwani ni vema tusichukue uamuzi wa kudumazautafutaji nchini kama tulivyofanya miaka ya nyuma.

Waheshimiwa Wabunge, niwaeleze kwambadunia ya leo hii, ni mambo ya ushindani. Siku nyinginenikiongea, nitawaeleza vigezo 12 ambavyo vinafanyanchi iweze kushindana na nchi zingine. Kwa hiyo, sisianayeshauri tusimamishe utafutaji wa mafuta,tutakuwa tumefanya kosa kubwa sana kwa sababuMsumbiji wanatafuta, Kenya wanatafuta, Congowanatafuta, Kenya wamegundua juzi mafuta kule juu,Uganda wamegundua mafuta, kwa hiyo WaheshimiwaWabunge, ni lazima tuendelee na zoezi la kutafutamafuta na gesi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, PAT kulipa Dola za MarekaniBilioni 20.1 na hizi nadhani Waheshimiwa ManaibuWaziri wameeleza vizuri na ukweli ni kwambatumeagizwa mikataba hiyo tuichunguze upya namikataba ya Songas tuipitie upya. Kwa hiyo, muwe naimani kwamba hiki kitu tunakifanyia kazi.Mheshimiwa Spika, Mfumo wa Uagizaji wa Pamojawa Bidhaa za Mafuta. Nadhani hii aya ya 161 yahotuba yangu, maelezo yanajitosheleza na hata hivyotunazidi kulifanyia kazi.Mheshimiwa Spika, baadhi ya hoja zilizotolewa naKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madinizimetolewa pia na Kambi Rasmi ya Upinzani. Ninatoamajibu kwa hoja zifuatazo:-Mheshimiwa Spika, kutayarisha wataalamwatakaohitajika katika sekta ya gesi. Mimi mwenyewenashukuru nimesema, pale Wizarani tumeanzisha

marshal plan, hata mkisoma kwenye kitabu chetuhicho kuna marshal plan. Tunataka kati ya mwaka huuna mwaka 2016 tuwe na vijana wataalam kati ya 30 na50 na isitoshe hawa watasomeshwa kwa hela zetu, zilepesa ambazo zilizokuwa zinaingia Wizarani, mnasemahamjui zinavyotumika na zile za kule TPDC, sasa sisikama Wizara tunatoa scholarships. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kusitisha uwekaji wa vinasabakwenye mafuta, Naibu Waziri ameliongelea.Mheshimiwa Spika, mikataba ya bomba la gesi laMtwara, tumeliongelea kwa kirefu sana.Mheshimiwa Spika, sasa nije kwenye hili laTANESCO na wizi wa TANESCO. Kuna jambo muhimukulisemea kwani halikubaliki ambalo ni wizi wa umemenchini kwa kutumia mitandao ya Luku isiyosajiliwa naTANESCO (ghost vending system). Katika zoezilinaloendelea la ukaguzi wa mita za TANESCO pamojana ukusanyaji wa madeni, tayari wateja watanowakubwa wamekamatwa na kufikishwa Polisi. Watejahao wamekutwa na unit za umeme ambazohazikununuliwa kihalali kupitia mtandao wa mauzo yaLuku wa TANESCO. Naelewa wapo wengi wa aina hii.Wateja ambao mpaka sasa tumethibitisha kwambawanaiba umeme ni pamoja na hawa:-(i)(ii)St. Marys International School;Access Bank iliyoko Tabata Matumbi;

(iii) Shree Shyam wenye duka linalojulikana kamaMalick Bhachool lililopo Mtaa waAggrey/Market Karikoo; na(iv) Akubu Paradise Hotel iliyopo Mtaa waMagira, Kariakoo.Mheshimiwa Spika, hawa wote; St. Mary’s nithamani ya shilingi milioni 10.5, Access Bank ni thamaniya shilingi milioni 13.8, Shree Shyam ni thamani yashilingi milioni 8.1, Philipo Gunda mwenye Hoteliinayojulikana kwa jina Akubu Paradise Hotel iliyopoMtaa wa Magira, Kariakoo huyu unit zake ni za thamaniya shilingi milioni 25.3. Baadhi ya wateja hawawamekwishafikishwa Polisi kwa ajili ya kutoa maelezona hatua zingine zitachukuliwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza mpango waSerikali wa kupunguza matumizi ya fedha za ummahasa katika ununuzi wa magari yenye gharamakubwa, napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufukwamba Wizara yangu itatekeleza kwa dhati agizo laMheshimiwa Waziri Mkuu la kudhibiti matumizi yamagari ya bei mbaya kuanzia mwaka huu wa fedha.(Makofi)Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji huo, ViongoziWaandamizi wa Wizara wakiwemo Makamishna naWakurugenzi waliokuwa wanahudumiwa na magari yagharama kubwa, wataanza kutumia magari yakawaida, ambayo ujazo wake hauzidi (CC) 3,000 nahizi ni gari zao za mkopo. Hili zoezi litatufanya tuwetunaokoa shilingi bilioni 1.4 kila mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sekta ya madini. Hapa NaibuWaziri ameongelea mambo ya corporate tax kwambatumeanza kulipa na hili la Merareni nalo limeongelewana Ndugu zangu wale rafiki zangu wa Tanzanite One,hili jambo liko mezani kwangu. Kwanza, tumeshatoa ileleseni ambayo ilikuwa ni special minning licenseimebaki mining licence ya kawaida na yenyewehaijatolewa kwa sababu hatuwezi kufanya naomaongezi mpaka wawe wamemaliza kulipa fedhazetu za nyuma. (Makofi)Waheshimiwa Wabunge, suala la Kiwiralimeongelewa kwa undani na mimi niseme kwa mudaniliokaa pale, tumelichunguza kwa undani sana, lakininiwaeleze tu kwa kifupi, iwapo tunataka mgodi huouchukuliwe na STAMICO na zile asilimia 70 ya hisazilizoko kwenye kampuni ya Kiwira, ni lazima tulipemadeni ya kule walipokopa fedha. Ukichukua deni,hata ukichukua urithi wa mzazi wako, nadhaniunachukua urithi wa nyumba na madeni yake. Kwahiyo, ndiyo hali halisi hiyo. Tunaweza tukawa wachungukweli lakini kurithi mali lazima urithi na madeni na uzurini kwamba wanaodai kwa wingi ni Mashirika ya Umma.Ni NSSF, PSPF pamoja na CRDB. Kwa hiyo, tukiwalipahao, hata hii mijadala mikubwa ya fedha zawafanyakazi, tutakuwa tumesaidia sana hayomashirika. Kwa hiyo, Ndugu zangu, kila kitu kinaendavizuri kwenye hilo.Mheshimiwa Spika, sasa kuna hili la kupelekamchanga nje, labda wakaoteshe kule, sawa inawezaikatokea miujiza ya kijiolojia lakini sidhani kama hiyo ipokwamba madini yanaota kwa sababu kama dhahabu

ya kule Mwanza ilitengenezeka miaka 2.7 billion yearsago. Kwa hiyo, ni process ndefu ya kutengenezamadini sio ya kuotesha mara moja kama uyoga. Hatahivyo, Waheshimiwa, kitu ambacho vilevile miminimeshaagiza na project inaanza nakubaliana na nyie.Katika ule mchanga, kuna madini tusiyoyafahamu nakwa vifaa vilivyoko hapa nchini, hatuwezi kuyafahamuna haya madini yamekuja kuwa na uthamani hivikaribuni, haya sasa yanaitwa technology metals austrategic metals.Mheshimiwa Spika, kuna ugomvi kati ya China naMarekani kwa sababu China ina-control 95% ya madiniya aina hiyo duniani, halafu anakuwa mjanja, hatumii,anakwenda nje, lakini ndiyo ujanja wa kibiashara. Sasanimeagiza, bahati nzuri katika mwanafunzi wangummoja ambaye alionekana kutimiza conditions zanguza kufanya utafiti, nimempatia Profesa Mruma ambayendiye CEO wa Geological Survey, tunaanzisha mradiwa, je, haya madini yako wapi? Hizo ramanitulizowapatia baada ya muda tuonyeshe hizi strategicmetals ziko wapi. Kwa hiyo, ni kitu kipya, hatuwezikulaumu technology inabadilika. Madini kama hayo nikama indium yaani hizi electronics zote mnazotembeanazo zinahitaji hiyo na wengine mnafahamu ule wizi wacoltan, ile coltan ni crom byte na tantalum. Iletantalum ni ya muhimu sana kwenye mambo yacomputers na semi-conductors. Halafu kuna menginekama palladium, haya yote ndiyo yanayotumikakutengeneza exhausts za pipe za gesi. Sasa ni kwelinakubaliana na hilo na sisi tunalifanyia kazi. Hayamambo mengine ya madini, mwenzanguameyaongelea kwa kirefu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine lililoulizwa na Kambi yaUpinzani hasa Mheshimiwa Mdee, huu mkataba wa siri,kweli tumeufuatilia mkataba wa siri, ule wa uchimbajiwa uranium. Sasa hapa ile kampuni ya kutokaAustralia, imeingia mkataba na kampuni ya Kitanzaniainaitwa Game Frontiers ambayo kazi yake ni kuwindakule karibu na Selous, lakini ukiangalia kwenye ramanikile kitalu kiko nje ya Selous. Sasa wakaingia mkatabawa kulipana, huo mkataba ni kwenye dola milioni sita(6 milioni) kila mwaka walipane halafu wakianzakuchimba vilevile malipo yatakuwepo. Sasa sijui kamaTRA ilipata chochote. Nimetuma watu Wizara ya Ardhikulifuatilia na nimetuma vijana kwenye field wakiwa naGPS waweze kuangalia kama kuna coordinates na hilokweli lipo na tunalifanyia kazi. (Makofi)Mheshimiwa Spika, mwisho kuna wenginewalisema kwamba, nadhani huyu ni MheshimiwaMnyika, alitoa pendekezo zuri sana kwamba inabidi nasisi tuanze kuwa na gold reserves, lakini hiyo ni kitumuhimu, hakuna nchi iliyoendelea na yenye uchumimzuri ambayo haina hazina ya dhahabu. Kama kunaMchumi anasema hatupaswi kuwa nayo, hata sisiambao siyo Wachumi tutaanza kuweka alama yakuuliza. (Makofi)Mheshimiwa Spika, niwaonyeshe tu kwa mfano,nchi kubwa duniani kama Marekani, Januari mwakahuu, Marekani reserve yake ya dhahabu ilikuwa ni tani8133.5, dhahabu waliyoweka reserve. Namba mbiliduniani ni Ujerumani, ina tani 3396.35 na tatu ni IMF, inatani 2811.1. Sasa Waheshimiwa Wabunge kama IMF

inayotushauri kila siku na yenyewe ina reserve, weweunayeshauriwa kwa nini usiwe na reserve? (Makofi)Mheshimiwa Spika, namba nne ni Italy, ina reserveya tani 2451.8. Ya tano ni France, ina tani 2435.4; ya sitani China, ina tani 1054 na sisi bingwa wetu Afrika Kusinianashika namba 29, ana tani 125. Niliangalia naMalawi alikuwa na tani 0.3, sasa hata Malawi itushindejamani? (Makofi)Mheshimiwa Spika, hitimisho, si rahisi kujibu kila hojailiyopokelewa. Hata hivyo, naahidi kuwa nitaandaamajibu ya hoja zote na kuyawasilisha kwaWaheshimiwa Wabunge kama kitabu. Nitashirikiana naBunge lako Tukufu ili kuhakikisha kuwa sekta ya madinina nishati zinaongeza mchango wake katika ukuaji wauchumi wa nchi na kamwe sitawaangusha. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kusema kwamba,iwapo Dira yetu ya Maendeleo ya 2015, inasemakwamba sisi tutoke kwenye nchi ambazo ni maskinitwende kwenye middle income country. Maana yakuingia kwenye nchi za katikati, ni kwamba kipatochako kinapaswa kuwa kati ya dola 3800 na dola12,500. Sasa kufika huko Waheshimiwa Wabunge, nilazima tuwe na umeme ambao ni zaidi ya megawatt3500. Kwa hiyo, tunaomba hili Bunge litusaidie tutimizemalengo yetu tuliyoainisha kwenye dira yetu yamaendeleo.SPIKA: Mheshimiwa Waziri, naomba usubiri kidogo.Kuna suala lilikuwa linazungumzwa hapa kwambamafuta yalivunja utaratibu, hukutupa faida ya hiyo kitu;

kwamba ununuzi wa mafuta sijui umevunja taratibu nanini. Naomba utumie dakika chache kueleza suala hilo.WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa Spika,utaratibu huo, kwanza Waheshimiwa Wabungetuangalie tu mantiki iliyo ya chini kabisa, simple logic.Mimi hapa ninaumwa njaa na sina fedha ya kununuliachakula, Mheshimiwa Mbunge hapa anasema Nduguyangu huwezi ukafa njaa, naomba nikusaidie. Niuamuzi wake either anipatie chakula au fedha. Hivikweli mimi ninayeumwa njaa nitamwekea masharti?Sasa TANESCO haina fedha, mafuta, lakini inatakaiweke masharti kwa anayempatia fedha. Kwa hiyo,nadhani hiyo tu kwanza haina mantiki. (Makofi)Mheshimiwa Spika, la pili ni hivi, ile siku ambayowaliweka mgao nchi nzima, mimi sikupewa taarifa,Manaibu Mawaziri hawakupewa taarifa, Katibu Mkuuhakupewa taarifa. Tukasema potelea mbali hakunasababu ya kukasirika, mimi nilikuwa nimeitwa na Mkuuwangu, Waziri Mkuu niwe Dar es Salaam siku ya ijumaa,tumefanya kazi mpaka karibu saa tisa usiku,tunaambiwa umeme umerudi, ndipo na mimi nikaendakitandani. Asubuhi nimesafiri kutoka Dodoma mpakaDar es Salaam, nikafika kwenye jengo la TANESCO paleUbungo, nikawapigia simu Waheshimiwa mmeshaendakuchukua mafuta? Walikuwa bado hawajaendakuchukua mafuta. Sasa fikirieni Waheshimiwa kamakweli ni mgao ambao ni halali na wana nia ya mafuta,mtu kasafiri kutoka Dodoma mpaka Dar es SalaamUbungo, watu wa Dar es Salaam hawajaendakuchukua mafuta, nadhani hiyo ni tafsiri ya ajabu sana.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa mbali ya hapo, ielewekekwamba, sisi fedha tulizowapatia hatujaingilia, hiyo yakusema tumeingilia Kanuni, Wizara haikuamka ikaendakuingilia fedha za TANESCO na kuingilia zile tenderingsystem zao, hayo ni kazi yao. Hatukuingia huko, sisitulikuwa tunawapatia wao, tunawasaidia. Kwa hiyo,siyo kweli kwamba tumekiuka, ingelikuwa tumekiuka nakama tungevuka mpaka, tukaingia ndani ya TANESCOna kuwalazimisha kwamba acheni hao, chukuenihawa PUMA, hatukufanya hivyo. Kwa hiyo na sisi kamaWizara kisheria, tuna haki ya kuweza kununuachochote kwa upande wetu na wale TANESCO wanahaki hiyo. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hakuna kosalimefanyika kwa sababu wao wana haki kisheria yakununua chochote kama wana hela zao na sisi hukutunaruhusiwa kisheria. Kwa hiyo, hiyo nayo haionyeshichochote tulichokiuka. (Makofi)Mheshimiwa Spika, kingine tena ni kwamba, hiiPUMA ni Kampuni yetu, tuna 50%. Sasa uangalie jinsiambavyo tunajimaliza wenyewe; kwanza tukinunuakwenye kampuni yetu kama ambavyowafanyabiashara wengine hapa wanaambizanakanunue kwenye maduka ya ukoo wako, utakuwaunaacha biashara ndani ya familia, moja hiyo. Kwakuwa, tuna 50%, inamaanisha kwamba, biashara hiyoikifanikiwa na sisi dividends, pato letu, gawio letu,tutafaidika! Lakini zile kampuni nyingine tukizipatia,hata kama zingekuwa na bei ya chini, hela hizo

tumepeleka lakini hizi za PUMA, faida yake badotutaipata kwenye gawio na isitoshe, yenyewe ndioimetoa bei ya chini. (Makofi)Mheshimiwa Spika, halafu uchunguzi wetuumeonesha kwamba, hata huyu anayeuza kwa1,850/= kwa lita, kumbe anaenda kununua PUMA naPUMA sio 1,500/= ni 1,460/=. Sasa hapa WaheshimiwaWabunge, kwanza tumeokoa shilingi bilioni tatu (3) kilabaada ya wiki mbili, inamaanisha shilingi bilioni sita (6)na isitoshe tumeongeza gawio letu wakati tukija kukaachini kuwekana sawa kimahesabu. Pia isitoshe huyuPUMA mpaka sasa hivi, Waheshimiwa, sisi hatujalipahata senti moja, ametudhamini kwa mkopo na sio kwelikwamba tumepeleka fedha, haijalipwa senti hatamoja kwa sababu, sisi ni wabia, ni kampuni yetu. Kwahiyo, kuna sababu nyingi sana ambazo zinaoneshakwa nini tumefanya tulivyofanya. (Makofi)Mheshimiwa Spika, lakini la mwisho kabisa, unajuamimi sikusoma Sheria, lakini ukiwa unasomasomavitabu na magazeti na nini, unaweza ukajikutaunakuwa Bush Lawyer. Ni kwamba, tumeenda kupatabarua na makubaliano kwa sababu, IPTL bado ipochini ya mufilisi. Imeandikwa kabisa na barua tunayona hiyo sisi ndio tulingoja ndio ingekuja kuniokoa mimina Maswi, kama hii kitu ingekuja hapa Bungeni. Ndiotulikuwa tumeificha, tunangoja, kama nondo yamwisho hiyo. (Makofi/Kicheko)Mheshimiwa Spika, hiyo barua inasema kwamba,atakayeinunulia IPTL mafuta ni Wizara. Kwa hiyo,Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote, hili

jambo nadhani limefikia tamati. Tusonge mbele natufanye kazi kwa manufaa mengine. (Makofi)Mheshimiwa Spika, sasa unajua mambo yakujifunza hayana mwisho, nilisharukia mambo menginekabisa, naomba kutoa hoja. (Makofi/Kicheko)WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU –TAMISEMI: Mheshimiwa Spika, Naafiki. (Makofi)MWONGOZO WA SPIKAMHE. EZEKIA D. WENJE: Mwongozo wa Spika!SPIKA: Naomba tuendelee, wakati wa uamuzihatufanyi mwongozo. Nimetoa maamuzi kwamba,tunaingia kwenye Kamati ya Bunge Zima.KAMATI YA MATUMIZIMATUMIZI YA KAWAIDAFUNGU 58 – WIZARA YA NISHATI NA MADINI(Hapa Wabunge wanaotaka kuuliza maswaliwalisimamakabla ya kifungu husika kusomwa)MWENYEKITI: Naomba mkae kwanza. Utaratibu nikwamba, atasoma kile kifungu kinachohusika, atasomaile hesabu inayohusika, halafu ndio mtasimama.Naomba uanze tena.

Kif. 1001- Administration and HRManagement … Shs. 8,027,554,000/=MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi.MWENYEKITI: Mkumbuke, tunaingia kwenye Sera,sio kijijini kwangu hakuna umeme, sijui kikaenda hapa,hivyo sivyo; Sera, Mheshimiwa!MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, katika mchango wangu wa maandishi,Serikali, imetenga jumla ya shilingi bilioni 8.9 kwa ajili yakuendeleza wachimbaji wadogo, ikiwa ni pamoja nakuwapa mikopo. Je, hii pesa, shilingi bilioni 8.9,itagawanywa kwa wachimbaji wote Tanzania amakatika maeneo ambayo yamewekwa kwa ajili yakugawanya viwanja kwa ajili ya wachimbajiwadogowadogo, ambayo imeoneshwa hapa kwenyehotuba ambayo ni kama maeneo 12 hivi?MWENYEKITI: Hebu uliza vizuri swali lako. Achakwenye Mafungu, wewe uliza Sera yenyewe ikoje?Ukiingia kwenye Mafungu, sisi hatujaingia huko.MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: MheshimiwaMwenyekiti, naulizia kwamba, Wizara imetengatakribani shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya kuendelezawachimbaji wadogowadogo. Je, pesa hiiinagawanywaje, kwa kufuata uwiano wa maeneoyote ya wachimbaji wadogowadogo?

MWENYEKITI: Sera ya Wizara, kuhusu wachimbajiwadogowadogo na viwanja, ndio unachotakiwakujibu, tafadhali!WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, fedha hizi ukisema uzigawe kwawachimbaji wadogowadogo mmoja mmoja, haziwezikutosha. Tulichokifanya, tumeagiza Mikoa yote kuwana Vyama vya Wachimbaji Wadogo na pia kuwa naChama cha Kitaifa. Kwa hiyo, tunapotoa mkopo kwawachimbaji wadogo, tutaelekeza kwenye vyama vyaoambavyo ndio vitakuwa vinawatambua wanachamawa vyama vile.MHE. ENG. HAMAD YUSSUF MASAUNI: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Maanambali ya kwamba mimi ni Mjumbe wa Bodi ya PUMAlakini Wizara hii ndio imenilea, ajira yangu ya kwanza,nilianzia hapa.Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wanguwa maandishi, nilizungumzia na bahati nzuriMheshimiwa Waziri na Naibu Waziri, walieleza kwamba,Mpango na Sera karibu zitafika hapa Bungeni. Sasanilitaka kujua tu kwamba, je, kwa kuwa bado suala lagesi tunapolizungumza sasa hivi ni suala la Muungano;Mipango hii na Sera hii, imezingatia ni jinsi ganiZanzibar, itafaidika? Kwa sababu, hata kama itaamuabaada ya mabadiliko ya Katiba, pengine gesi iondoke,lakini tunapozungumza sasa hivi gesi ni suala laMuungano. Kwa hiyo, naomba ufafanuzi katika hili?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI – MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Ni kweli kama anavyosemaMheshimiwa Masauni kwamba suala la gesi bado nisuala la Muungano kwa sasa hivi, suala la Katibainabakia vilevile; hatuwezi kusema chochote kile,labda tusubiri wakati huo tuone itakuwa nini.MHE. SAID MUSSA ZUBEIR: Mheshimiwa Mwenyekiti,mimi katika mchango wangu wa maandishi, nilikuwanataka nisikie chochote kuhusu Sera ya Gesi kwaupande wa Zanzibar lakini kwa bahati mbaya,sikumsikia Waziri akisema chochote, naomba majibu.MWENYEKITI: Hili liko sawasawa na lile lililopita?.MHE. SAID MUSSA ZUBEIR: Yes!MWENYEKITI: Sasa itakuwa ni kurudia, MheshimiwaMkiwa.MHE. MKIWA ADAM KIMWANGA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Katika mchango wangu wamaandishi, nilipenda kujua ni nini Sera ya Madini paleambapo wawekezaji wanakuja kuhitaji eneo na eneohilo likathamanishwa na wananchi wakazuiwa kufanyamaendeleo yao au kufanya shughuli zao za kijamii nabaada ya muda wawekezaji wale wakaahirishakuchukua eneo lile, takribani yapata miaka 8 au 7.Nimetolea mfano, Kata ya Mtakuja, Kijiji chaNyakabale; nilitaka nijue Sera inasema nini na ni ninihatma ya wananchi hawa?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera yaMadini iko wazi, mwekezaji anapokuja kutaka eneololote kwa ajili ya uwekezaji, wawekezaji wakubwakwanza wanaanza kwa kuomba leseni za utafiti naleseni ile anapoipata kwanza, kabla hajafanyachochote ni lazima apate ile right of entry; apeweconsent ya lile eneo ambalo anakwenda. Kwa hiyo,kwa suala la Nyakabale, tunafahamu kuna leseni paleya Mgodi wa GGM, wameshikilia baadhi ya maeneona kwa sasa tuko kwenye mazungumzo kwa sababuhawayatumii ili waachie maeneo hayo kwa ajili yawachimbaji wadogo.MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kwa kuzingatia Mikataba mingi yaKimataifa inayoweka msisitizo kumuendelezaMwanamke Duniani, naomba Wizara, kupitia kwaMheshimiwa Waziri, atupe maelezo ni jinsi gani bajetiya Wizara yake imezingatia kumwendelezamwanamke kielimu, kiuchumi na kijamii?NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELE): Mheshimiwa Mwenyekiti, sisikwenye Wizara yetu, maana najaribu kutafuta Serahapa, siipati sawasawa lakini tunatambua mchangowa wanawake katika sekta ya madini na tunasimamiakwenye ajira. Ukitembelea kwenye migodi, wanawakewanapewa nafasi na hata kwenye madini pia, kwenyenishati ya gesi, tumetoa kipaumbele pia wanawakewaweze kupata ajira.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Nilitaka kujua kwamba, baada yauwekezaji, wananchi wa kwenye migodi sehemumbalimbali Tanzania, imesababisha wakakosa ajira. Hiiimesababisha kushuhudia wananchi wanauwawa,wengine wanakuwa vilema, wengine wanapelekwagerezani. Mwaka jana mwezi wa Mei, 2011, Serikaliilisema mojawapo ya njia ya kutatua kero hiyo ya ajirakwa wananchi hawa wanaozunguka migodiitawatengea maeneo maalum pamoja na kuwapamitaji na mafunzo. Lakini katika hotuba ya Waziri,hakuainisha ni katika hatua zipi wamefikia, badalayake amesema tu watatoa leseni kwa wachimbajiwadogo na tunajua leseni za wachimbaji wadogo zinamasharti ambayo wananchi hawa hawawezi kutimiza.Kwa hiyo, napenda kupata kauli ya Serikali, kuhusukauli yao waliyoitoa mwaka jana.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli yaSerikali iliyotolewa mwaka jana, siwezi kufanyareference kwa sasa lakini ninachoweza kumuelezaMheshimiwa Mbunge ni kwamba, katika Sera yaMadini, inatoa kipaumbele, hata kwenye Sheriaambayo nimeieleza hapa wakati najibu hoja, inatoakipaumbele kwanza kwa ajira za vijana na hasakwenye maeneo ambayo yanazunguka migodi hiyo.Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa limetokea tatizokwamba kuna baadhi ya sifa ambazo zinahitajika kwavijana wa eneo lile, wanazikosa. Kwa hiyo, migodiinalazimika kwenda kupata vijana wa maeneo

mengine ambao wana sifa zinazokidhi mahitaji yamigodi.MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Katika mchango wangu wa maandishi,nilitaka kujua kuhusu uendeshaji wa Shirika la TANESCO.Kwa kuwa, tarehe 13 na 14, Bodi ilikaa na ikafanyamaamuzi dhidi ya Menejimenti na Bodi hiyohiyohaikuwa na usafi wa kuweza kufanya maamuziwaliyofanya dhidi ya Menejimenti; na kwa kuwa,baadhi ya Wajumbe, waliofanya maamuzi yakuwasimamisha hao Watendaji wa TANESCO, naowalikuwa na mgongano wa kimaslahi katika utaratibumzima wa kuendesha Shirika hilo. Nikaomba Wazirianipatie majibu, kwa nini asivunje Bodi ya TANESCOvilevile ili iweze kukaa pembeni wakati huu uchunguziunapofanyika ili haki itendeke kwa wote? Kwa sababu,Bodi ni chafu na Menejimenti ni chafu na hili ni Shirika laWatanzania wote. Kwa hiyo, nilitaka kupata majibukutoka kwa Waziri.WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, alichokisema Mheshimiwa Mbatia, ni kwelina sisi tunapenda kwenda taratibu na sio kwa jazba.Kwa hiyo, ukweli ni kwamba, tunakokwenda, inabidiBodi ivunjwe, lakini inabidi twende kwa taratibu badalaya kwenda kwa haraka. Nashukuru kwambaMheshimiwa Mbatia anayoyasema ni kweli kwambaBodi ina matatizo na Menejimenti ina matatizo,Menejimenti sehemu wameshasimamishwa, Bodiwanasema ikae pembeni, hata kabla ya haya yotekutokea, tulishaanza kuweka alama ya kuuliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niseme tu hivi,kwenye mashirika na kampuni zote ambazo ziko chiniya Wizara yangu na nilivyowaeleza kwambaMheshimiwa Rais ndiye anateua Mwenyekiti wa Bodina wale Wajumbe wa Bodi kama mlivyoona TPDC kwakujaribu kuwashirikisha Watanzania wote, uamuziwangu ni kwamba nitakuwa ninatangaza kwenyemagazeti Mtanzania yeyote anayejipima na kuonaana uwezo wa kuingia kwenye Bodi analeta maombiyake. Tumeshaanza kufanya kwa TPDC, naonammeona wameomba watu 72 na tutachuja. Kwa hiyo,yote yale badala ya kukaa mimi wale Wajumbe waBodi, ni mimi napaswa kuwateua, lakini nadhani kwakutenda haki kwa wataalam wa fani mbalimbali, siyovizuri mimi nijifungie mwenyewe chumbani halafuninateua rafiki zangu. (Makofi)Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hizo ndizotaratibu mpya za Wizara yangu na wote hata aweMbunge, awe tayari kushindana. Ukiona kwamba unaubavu wa kushindana, leta maombi. Ahsante.(Vigelele/Makofi)MHE. DKT. AUGUSTINE L. MREMA: MheshimiwaMwenyekiti, katika mchango wangu wa maandishikwa Wizara hii, nilimwomba Waziri afafanue seraambayo itatumika kule Vunjo, Moshi Vijijini na Rombokwa sababu ule umeme tunaotumia sasa hivi unamatatizo makubwa sana. Unatoka pale Kiyungi ukijaVunjo unazima, ukipata matatizo yanasambaa mpakaMoshi Vijiji mpaka Rombo. Sasa nataka kujua mpangokabambe, mpango mpya, sera ambayo itaweza

kutukomboa eneo hilo ili tuweze kupata umeme wakudumu ahsante.MWENYEKITI: Mheshimiwa Mrema, huwatunakuheshimu lakini hilo siyo suala la kisera.MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante sana. Madini ya nickel ni madinimuhimu sana katika utengenezaji wa ndege, chumacha pua. Sasa hotuba ya Mheshimiwa Waziri, ni hotubamuhimu sana na ni road map inayoonyesha dira lakininimesikitika kuona mgodi mkubwa ambao ni wa piliduniani katika deposit za nickel haukuguswa kabisa nahotuba hii. Sasa napenda kujua Mheshimiwa Waziri,Serikali ina mpango gani na mgodi wa KabangaNickel?WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, nami nimemuomba radhi, ukweli nikwamba hatukuweka kwenye hotuba lakininimeshaonana na watendaji wote na ile kampuniwamenieleza, ni kupitiwa lakini ni mgodi mzuri sana.Lakini usisahau Mheshimiwa Mbunge kwamba kwamuda fulani walisimamisha shughuli kwa sababu yamambo ya kifedha na kitu kimoja ambacho miminitakifuatilia kwenye Kabanga Nickel, kwanza ni mgodimkubwa kweli, halafu ile nickel na cobalt haiko tuupande wa Tanzania, inaenda mpaka kule Burundisehemu za Msongati. Kwa hiyo, kuna jambo mojanilikaa nikawauliza, hivi tukifika pale mpakani kamahuko kuna Burundi, Tanzania tutaonaje, lakini nadhanihilo wataalam wataifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ambachoniliongea na CEO, nilimueleza nadhani Kamishnaanayeshughulika na leseni, kabla ya kutoa ile leseni yakuchimba, kitu inachobidi tukifanyie kazi ni kwambayeye ameomba leseni ya nickel na copper peke yakelakini kutokana na rafiki yangu aliyekuwa anafanyaPhD yake upande wa Burundi, hiyohiyo inaonekanakuna vanadium, kuna PGE ambayo inathamani zaidikuliko nickel na copper. Kwa hiyo, nadhani nitatumawatu, nikachukue sample, tutaenda kwenye maabarakubwa duniani waweze kutueleza kama kweli yeyeanasema vanadium na PGE haipo ambayo inathamani kuliko nickel na copper.Mheshimiwa Mwenyekiti, isitoshe nimeongea naMheshimiwa Waziri anayeshughulikia mambo ya reli,kitendawili kingine ni kwamba wakishaanza kuzalisha,kuanza kuvuna nickel na copper, wao wanasafirishatani zaidi ya 250,000 na ukichukua reli yetu ya kati,nadhani ndiyo ujazo wake huo na yenyewe inasafirishakaribu tani 250,000 kwa mwaka. Kwa hiyo, vilevileinabidi tukae chini na Wizara inayohusikana na relikabla huo mradi haujaanza lakini tunaufuatilia natunajua ni mradi muhimu sana, samahani kwa kuwahaipo kwenye kitabu.MHE. EUGEN E. MWAIPOSA: MheshimiwaMwenyekiti, nishukuru kupata nafasi lakini kwenyemchango wangu wakati nilipokuwa nachangia kwamaandishi, nilimwomba Mheshimiwa Waziri anieleze auawaelezee Watanzania utaratibu au sera ya kupatawanachama wapya wa TANESCO. Nilimwelezea kwakirefu ni jinsi gani wananchi wengi wanaotaka umeme

wanapata usumbufu mkubwa hata baada yakukamilisha yale mahitaji yanayohitajika kwa mfanokujiandaa labda kujiandikisha katika kijiji husikawanakuwa 200 au 100 lakini wanakuwa wanakwendana kurudi hadi kufikia miaka mitatu. Kwa hiyo, natakatu kujua sera ya TANESCO ya kupata wateja wapyainasemaje kuhusu muda na utaratibu kwa ujumla?MWENYEKITI: Uenezaji wa umeme, MheshimiwaNaibu Waziri.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Ni kweli Mheshimiwa Mwaiposaanachokisema na hili linatokana na yale maandaliziyaliyokuwa siyo mazuri ya kukosa vifaa kama mita,wire, nguzo na vitu vingine na hii inatupelekea kwenyemsingi wa tatizo lenyewe la TANESCO lakini sisi kamaWizara tulishatoa tamko kwamba tunadhani mpakatarehe 30 Juni, Mheshimiwa Waziri aliagiza wawewamemaliza kuwafungia wateja wa zamani wote ilituanze kushughulika na hawa wapya. Tunafikiri kwasababu jana tumetaja tarehe ya kuanza kutumika hiviviwango vipya, tutakapofika kwenye viwango vipya,basi waanze wateja wapya wale wa zamani wotewawe wameshafungiwa. Hivi tunavyosema, TANESCOwana mita karibu 50,000 ambazo zimeingia, kwa hiyo,hakuna Mkoa ambako shughuli za ufungiaji watejahaziendelei, kila Mkoa wanaendelea kwa ushindani,kwa mfano hapa Dodoma hapa ni karibu wateja wotewameshafungiwa.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Katikamchango wangu wa maandishi, nilitaka kujua tu seraya Wizara kuhusiana na usambazaji wa gesi ambayoimepatikana katika nchi hii kwa miji ile mikubwa kamaMwanza, Mbeya, Arusha, maana miji imeonekanakwamba sasa inatumia mkaa kwa wingi na matokeoyake inakuwa inachangia kwa kiasi kikubwa…MWENYEKITI: Katika miji mikubwa?NAIBU WAZIRI WA NISHATI MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanzanimshukuru tumeanza kwa kiasi fulani, Dar es Salaamkuna mradi ambao unaendelea kusambaza Dar esSalaam lakini uendelezaji wa matumizi ya gesi ni jamboambalo tunalitarajia na hii itakwenda kwa kasi,itatusaidia kuokoa mazingira. Lakini yote hayayatatimia tu endapo kwanza lile bomba litakamilika nabomba lile tumepanga likamilike ndani ya miezi kumina nane kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambakotunaamini tutaanzia na hiyo program iliyokwishaanzana baadaye tutaona namna ya kusambaza gesisehemu zingine.MHE. AGRIPINA Z. BUYOGERA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Miminapenda kuuliza, katika mchango wangu wamaandishi, nilizungumzia suala zima la sera ya Serikalikuhakikisha inafikisha umeme vijijini. Nikaielekeza nakuishauri Wizara kwamba kule kijiji cha Titye tunamaporomoko makubwa sana ambayo tunayatumiahata katika kilimo cha umwagiliaji. Je, Wizara iko tayari

kuagiza wataalam wakapitie maporomoko yale nakuangalia ili kuweza kupata umeme katika maeneo yavijiji vya Titye, Lalambe na maeneo mengine? Ahsante.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,tunakushukuru. Ni kweli anachokisema MheshimiwaBuyogera. Kwanza, ndiyo sera ya Wizara yetu kwa sasakwamba tusitegemee tu kila mtu akasema grid, grid,vyanzo hivi vya maeneo husika ni vyanzo muhimu napengine kunaweza kukaanzishwa hata ushirika wawatumiaji wa vyanzo hivi. Kwa hiyo, REA wanafanyakazi nzuri, mpaka sasa wamesha-identify vyanzo zaidiya 50 nchini na wanaendelea kufanya hivyo nakwenye bajeti yetu mkisoma kwenye hotuba iletumetenga kiasi cha fedha kwa ajili ya identification nabaadaye kuendeleza. Baadhi ya maeneo tayaritumetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyanzo hivyovinavyojitegemea na wanaanzisha ushirika nawatumiaji na hata mkawa na tariff ya kwenu wa eneohilo. Kwa hiyo, niseme tu kwamba WaheshimiwaWabunge tuwe wa kwanza katika kuhakikisha kwambatunatunza mazingira ya maeneo yanayoweza kuwa navyanzo hivyo vya maporomoko ili vyanzo vile vitusaidiekuzalisha umeme katika maeneo yetu, wazo la grid,grid, ni wazo ambalo kwa kweli haliendani na wakatiwa sasa.MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Ukienda ukurasa 89 wa hotuba yaMheshimiwa Waziri, tunashukuru kwamba gharama zakuunganisha umeme zimepunguzwa kwa single phasekutoka shilingi milioni moja laki tatu mpaka laki tatu na

kwa nguzo mbili kutoka shilingi milioni mbili mpaka lakinne na hamsini vijijini lakini hatujaambiwa kwa waleambao nguzo zinazidi idadi hiyo hapo inakuwajegharama yake?NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,makadirio yetu haya yanatokana na ukweli kwamba niwajibu wa Shirika lenye kazi hii kufikisha hata karibu naumbali huo mdogo kwamba wakifikisha umbali ule,sasa ndiyo ibakie jukumu la mteja. Lakini mahaliambapo panazidi nguzo zikawa nyingi kumi, kumi nangapi panahitaji sasa program maalum. Huu ni umbalimkubwa ambao unahitaji kwa kweli kuwa na mpangomaalum lakini tunataka TANESCO tunaposemawamefikisha umeme basi angalau unazungumzianguzo moja, mbili au hakuna nguzo kabisa. Kwa hiyo,hapa ndiyo maana hatukusema chochote. Kwa hiyo,ni jukumu la TANESCO kusogeza kwa umbali huo.MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana. Nami naomba kuuliza kuhusu serainasemaje kuhusu umiliki wa nguzo kwa sababuunakuta mtu amevuta labda nguzo tatu halafuwengine wanakuja kuchukua umeme bila nguzoyoyote lakini yule mateja wa awali hapaticompensation yoyote. Naomba kujua sera inasemaje ilituweze kujua wanasaidiwaje wale waliovutamwanzoni? (Makofi)NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Mbunge analeta hoja ambayo kwa kweli

na sisi tumeijadili sana na ni kweli kwamba haina logickwamba mtu unavuta nguzo kwako tano halafu mtumwingine anakuja kuchukua pale na wewe ulilipiahalafu hurudishiwe fidia yako na hili kwenye sheria nasera zimetambua kabisa kwamba huyu mteja aliyevutakwa kiasi hicho wanaokuja wengine lazima wamlipe aushirika li-negotiate naye kuona namna gani wanawezakufidiwa. Kwa hili tumewaagiza TANESCO kwambawasifanye kiholela, lazima wafanye kwa mujibu wakanuni zilizopo na ni kanuni ambazo zipo kabisakwamba lazima wana-mediate pale kuhakikishakwamba huyu mteja naye anapunguziwa ule mzigoalioupata mwanzo.MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana. Katika mchango wangu wa maandishinilitaka kujua kwamba mwaka 1983 kuna mradi wabomba la mafuta ulianza kufanyiwa utafiti kutoka Dares Salaam kwenda Mwanza. Ilipofika mwaka 1998, Raisaliyekuwepo aliidhinisha huu mradi kuanzakutekelezwa, wa bomba la mafuta kutoka Dar esSalaam kwenda Mwanza kusaidia Kanda ya Ziwa lakinimpaka sasa huu mradi haujawahi kuanza. Sasanapenda kujua sera ya Serikali inasemaje kuhusu mradihuu wa bomba la mafuta kutoka Dar es Salaamkwenda Mwanza kusaidia Kanda ya Ziwa?NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru, tunajua kwamba ulikuwepo mradi huolakini kama unavyojua nchi imepitia vipindi mbalimbalivya kiuchumi na wakati mwingine sera za duniazinatukumba tunafikiri pengine hiki na hivi na hivi. Sisi

tunafikiri tulichukue hili tuweze kwenda kulifuatilia tuonekama bado ni viable au ni vipi, ahsante sana.MHE. FAITH M. MITAMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Katika mchango wangu wa maandishinimetaka kujua, katika kurasa wa 51 wa hotuba yaMheshimiwa Waziri ametamka mpango wakuwaendeleza wachimbaji wadogowadogo kwakuwapa mikopo, mitaji pamoja na kuwatengeamaeneo. Sasa swali langu ni kwamba maeneo mengikaribu Tanzania nzima, aidha yana leseni za utafiti amauchimbaji, hawa wachimbaji wadogowadogo wamadini watatengewa maeneo yapi wakati maeneomengi yameshachukuliwa?NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELE): Mheshimiwa Mwenyekiti, wakatinajibu hoja hapa nilieleza kwamba kweli maeneomengi yameshikiliwa na leseni za utafiti na makampunimakubwa na wale wadogo lakini Sheria ya Madiniinaeleza wazi kwamba leseni zile zinapo-expire,zinapofika mwisho yule mwenye leseni anapaswaaachie nusu ya eneo lile, hiyo ni kwa mujibu wa sheria.Kwa mantiki hiyo sasa, sisi tumekubaliana kwenyeWizara kwamba maeneo yatakayoachiwa nusututayaangalia kiwango cha mashapa yaliyopo palekama yanafaa kwa kupewa wachimbaji wadogo.Tunawahamasisha wachimbaji wadogo wawe kwenyeushirika ndiyo inakuwa rahisi kuwagawia maeneo kulikomtu mmoja mmoja kwa sababu maeneo kweli si mengisana na kwa mtu mmoja mmoja hayawezi kutosheleza.Kwa hiyo, tutatumia yale ambayo leseni za utafitizitafika mwisho na anapo-renew lazima afike mwisho.

MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru. Katika mchango wangu wamaandishi, nilikuwa nimependekeza kwamba pengineSerikali ituletee mapendekezo ya kubadilisha Sheria yaMadini ya mwaka 2010 ili tuweze kufuta possibility yakuwa na fiscal stability clause lakini pia tu-introducekodi nyingine mpya kama win for gain tax pamoja nakufanya ring facing, Serikali inasemaje kuhusu hilo?NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELE): Mheshimiwa Mwenyekiti,nililikaribisha hili nilivyokuwa nikijibu hoja kwamba yakomambo ambayo lazima sasa tuyaangalie tena. Kwamfano, amelizungumza hilo lakini pia tulizungumziacompensation, bado kuna mjadala mkubwaunaendelea kwenye maeneo mbalimbali yenyemadini na kama nchi sasa hivi ndiyo tunaelekeakwenye kufahamu vizuri hii industry ya madini. Kwahiyo, ninakaribisha mawazo hayo na kwa sababumchakato wa kuleta mabadiliko ya sheria humuBungeni unafahamika na sisi tutaliangalia nawataalam wetu.MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru. Imeonekana hujuma ndani ya Shirika laTANESCO, ni tatizo kubwa sana kiasi kwambakumekuwa na mgao wa umeme ambao sio wa lazimana hata Mheshimiwa Waziri amejaribu kueleza hatabaadhi ya Waheshimiwa Wabunge wamekuwawakijuhusisha na hujuma ndani ya Shirika la TANESCOkiasi kwamba Bunge leo hii linaonekana kuwa na sura

mbaya machoni pa wananchi wote ambao wamesikiamijadala ambayo imekuwa ikiendelea tangu jana.Sasa naomba ufafanuzi kutoka kwa MheshimiwaWaziri. Katika kutekeleza sera au falfasa ya ukweli,uwazi na uwajibikaji, ni kwa nini Waziri asilieleze Bungena umma wa Watanzania Waheshimiwa Wabungeambao wamejihusisha moja kwa moja kwenye suala lakuhujumu TANESCO na ku-support mambo ambayoyameonekana hayana tija kwa Taifa leo? Naombaufafanuzi ni kwa nini wasitajwe ili isionekane kwambaBunge zima wanashirika au ni sera ya Wizara kuwafichawahujumu wa uchumi ambao walistahili kunyongwahadharani ili kuweza kutoa fundisho kwa watuwengine? Naomba ufafanuzi. (Makofi)NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza niweke vizuri rekodi kwamba MheshimiwaWaziri hakusema kwamba wapo Wabungewanaohujumu TANESCO amesema wapo Wabungewanaofanya biashara na TANESCO na katika kufanyabiashara hakuna Mbunge anayezuiwa kufanyabiashara.Sasa tatizo ni kwamba, unafanya biashara nanani? Una maslahi gani huko unakofanya biasharaukiwa Mbunge? Hilo ndilo linalokuwa tatizo. Sasa kwamsingi huo, na kwa kuwa Waziri ameshasema naameshatoa wito kwamba anawaomba waachekufanya biashara, lakini hatuwezi kuzuia haki ya waokufanya biashara kwa sababu hiyo ni haki yao, ila tukwamba wanafanya biashara wakati huo wengine

wakiwa kwenye Kamati na wengine wakiwawanaisimamia hiyo hiyo Serikali, hapo ndipo kunamjadala, na hilo pia ni suala ambalo linahusu sanaBunge lenyewe kufanya maamuzi. Kwa hiyo, sisi kamaSerikali tunafikiri kwamba ni vizuri wakaacha tu kufanyahiyo biashara na TANESCO.MWENYEKI: Mheshimiwa John J. Mnyika.MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzanitulieleza umuhimu wa Wizara kusafisha Wizara naTaasisi zake na ninashukuru Mheshimiwa Waziri ametoakauli kuhusiana na TANESCO.Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, kwenyehotuba tulitaka vilevile kauli ya Serikali, kwani msingi wamatatizo kwenye Taasisi ya Wizara ya Nishati na Madinini pamoja na mambo ndani ya Wizara yenyewe; nakwa kuwa, kuliundwa Kamati mbalimbali za Bungekama Kamati iliyochunguza ukusanyaji wa pesamaarufu kama Kamati ya Suala la Jairo na Kamati yaMasuala ya Gesi ya Asili; na kwa kuwa, ndani ya taarifaza Kamati kuna Maazimio ya Bunge yaliyotokana nataarifa hizo, kuna hatua ambazo zilipaswa kuchukuliwaza kusafisha Wizara ikiwemo baadhi ya Watendaji waWizara.Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kupata kauli yaSerikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Kamati hizimbili muhimu ambazo zimekuwa zikisuasua kwa kipindikirefu.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, kuna mitindo mingi sana ya kufanya kazi,lakini mimi nadhani mtindo wangu huwa ni wakujiridhisha kwanza. Labda kidogo tunatofautiana,kwani Mheshimiwa, yeye ni mwanasiasa per se na sisikidogo sayansi huwa zinataka evidence. Sasa mimisiwezi kukurupuka tu nawatoa watu bila kuwa naevidence.Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbungekwamba kazi hii tunaifanyia kazi, lakini vilevile mtu asijeakaonewa, lazima tuwe na vithibitisho natunavyofanya kazi kwa mtindo wetu hatufanyi kazi kwaredio na magazeti, sisi huwa tunafanya kazi kwa kuonamatokeo. Naomba niseme kwamba tumeanza, na siyohivi, tumeshaanza na katika kikao changu nawafanyakazi wa Wizara tuliongea kwa kirefu na kwaundani sana Water Front na mwisho wake tulitakakuonyesha kwamba kweli mambo tuliyokubaliana,tumekubaliana nayo kwa uzalendo wa hali ya juu.Tulikula kiapo ambacho hatukutumia Biblia walaQuran. Baada ya kula kiapo tukaimba Wimbo wa Taifa,kwa hiyo, ambaye atakiuka kiapo chetu, basiyatampata hayo yanayopaswa kumpata.Kwa hiyo, tunachukua taratibu za kusafishaWizara, na zipo, lakini lazima twende kwa taratibuambazo hazitamwonea mtu yeyote.MWENYEKITI: Ahsante, tunaendelea naMheshimiwa Mgimwa.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Nataka kujua, Sera ya Wizarakuhusu kuvipatia vijiji vyote vinavyozunguka maeneoya miradi ya umeme kama vile Bwawa la Mtera naKihansi.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa swali la Mheshimiwa Mgimwa.Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya sasa ya Wizarana utaratibu tuliouandaa ni kwamba kupitia miradi yaREA, tutahakikisha maeneo yote ambayo ni wadau wakaribu sana wa vyanzo muhimu vya umeme nchini,wanapatiwa umeme, na hii unaiona inakwendasambamba na wenzetu ambako kunatoka bomba lagesi. Kwa wale wote ambao kunatoka gesi bombalinapita na wenyewe wanapatiwa priority ya kupataumeme, na kwa hiyo, tunaendelea na sehemu zotezenye vyanzo muhimu katika nchi wapate umeme kwasababu ndiyo wanaotazama maeneo yale. Kwa hiyo,tutajitahidi kama kwako Kihansi na Mtera ambako nikwangu nao wanapata privilege hiyo na wako katikampango mzima nafikiri tuwasiliane ili nikuonyeshe vijijitulivyoviainisha.MHE. ALHAJI MOHAMMED H. MISSANGA:Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipanafasi. Katika mchango wangu wa kuzungumza,nilijaribu kuikumbusha Serikali kwamba, kamakumbukumbu yangu iko sawasawa, Sheria ya REA yamwaka 2005 inaelekeza kwamba tozo ambazowatapewa REA ni 5% lakini hivi sasa tozo inayotozwa ni

3%. Kwa hiyo, nikasema, ili tuipe REA fedha za kutosha,ni angalau hili ambalo lipo kwenye sheria ya kutoa tozoya 5% litekelezwe wakati hatua nyingine zinafikiriwa.Je, Mheshimiwa Waziri unasemaje juu ya hilo?NAIBU WAZIRI WANISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli kwamba inawezekana tozo hiyo ni 5%, lakiniwakati mwingine tunasema isizidi 5%, maana sasaukisema uweke kabisa kwenye 5%, inabidi wakatimwingine uangalie economics za nchi na uangalie haliikoje. Kwa sababu hata mafuta yenyewe tusijetukayapandisha bei sasa yakawa tena hata wananchihawawezi kumudu na kuongeza gharama za maisha.Kwa hiyo, tunakwenda kwa umakini mkubwa,lakini pale itakapobidi, basi Serikali itafanya maamuziya kuongeza.MHE. DESDERIUS J. MIPATA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana. Katika mchango wanguwa maandishi, nilitaka kujua juu ya sera ya usambazajiumeme vijijini inayotekelezwa na REA, kwa niniwanapopita kwenye kijiji hata kama kuna watuwamejiandikisha, vizuri lakini hawasambazi kwa watuwote wenye kiu, wanaweka kidogo kwa watuwachache na kuendelea. Jambo hili linaleta usumbufuna watu wanakuwa wameshasubiri muda mrefu.Nilitolea mfano juu ya maeneo mbalimbaliyanayotoa umeme, kwa mfano, mradi unaotokaSumbawanga kwenda Namanyele, sasa hivi watu

wamejiandikisha na walisubiri sana muda mrefu ahadiya Mheshimiwa Rais, lakini sasa umeme unapita, lakiniinaonekana maeneo mengine yataachwa.Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua hilo!MWENYEKITI: Sera ikoje?NAIBU WAZIRI WANISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa swali la Mheshimiwa Mipata.Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba REAwanasambaza umeme na angalau tunakuwa nanyumba za kuanza nazo kwa walewatakaochangamka kujiandikisha mwanzo, lakini siyokwamba tunaishia hapo. Kwa hivi sasa kwa sababumazingira yamebadilika kwamba hata bei yakuunganishiwa umeme tumeishusha, hii yote ni kwa ajiliya kuwafanya wananchi wa maeneo ya vijijini ambakotunaamini kwamba uwezo wao siyo mkubwa, wawezekumudu gharama.Pia, kwa maeneo kwa mfano, kutokaSumbawanga kwenda Namanyele ambapo mradi huuumepita na kwamba vipo vijiji ambavyowamejiandikisha na umeme haujashushwa, tayaritumeshaliona hilo na tumeagiza transformer 370ambazo Wizara imeagiza na itawakabidhi TANESCO iliwaweze kushusha sehemu zote ambapo umemeunapita ili wananchi wasione tu waya zinapita juu.

MHE. MAGALLE J. P. SHIBUDA: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Wilaya ya Maswa ina ahadi yakusambaziwa umeme katika vijiji kwa zaidi ya miakamitano. Je, Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kufungasafari kwenda Maswa akatusaidie kukwamua vizuiovya kupata umeme vijijini kwa sababu ya urasimuuliojitokeza, ni wa kila mbuzi hula kwa urefu wa kambayake?MWENYEKITI: Mheshimiwa Shibuda sisitunazungumzia sera, sasa tena tukienda Maswa…MHE. MAGALLE J. P. SHIBUDA: Namwalika, maanayake ndiyo swali lenyewe lilikuwa …MWENYEKITI: Anasemaje?WABUNGE FULANI: Anamwalika!MWENYEKITI: Ah! Basi atakuja. Mheshimiwa Dkt.Kebwe.MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante kwa nafasi hii. Napenda nipatemaelezo ya Serikali katika maeneo ambayo kunamwingiliano kama Waziri alivyotoa maelezo, yaanimwingiliano wa Nyang’wale na Geita, lakini hakutoamaelezo kwamba baada ya hapo ni nini kinafanyikakatika nchi nzima ya kufanya mapping ikiwemosehemu ya mgodi wa North Mara jinsi ambavyoumeingiliana na Serengeti, lakini Serengeti haipatimapato katika kijiji cha Nyiboko pamoja na Borenga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba majibu.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELLE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwelikuna maeneo mengi sana nchini yanaingiliana kwasababu mtandao wa madini au miamba ya madinihaifuati mipaka ya kiutawala. Kwa hiyo, mambo hayamaamuzi yake mara nyingi huwa ni ya majadiliano nakama nilivyosema wakati najibu hoja kwambatutakuwa na kikao na Kampuni ya Barrick kwa ajili yakujadiliana na uongozi wote, wanaotoka katikamaeneo husika.Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nimetambuaalivyosema hili la Serengeti kuingiliana na Nyamongona lenyewe tutalitatua kwa majadiliano. Lakini piayapo matatizo katika mpaka wetu wa Kusini kati yetusisi na Malawi na lenyewe kuna Tume maaluminaendelea kulifanyia kazi ili kuangalia ile miambainayovuka upande wa pili wa Malawi na inayokujaupande wetu Tanzania. Kwa hiyo, haya yanatatuliwakwa majadiliano.MHE. REBECCA M. MNGODO: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Katika mchango wangu wamaandishi niliomba kupata msimamo wa Serikalikutokana na kwamba, baada ya kuzinduliwa bombala gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaamimebainika kwamba mwekezaji ameomba kuwekabaadhi ya visima vya Songosongo rehani ili kuombafedha katika taasisi za nje. Sasa ninapenda kujua, nikweli kwamba jambo hili lipo? Nini msimamo wa Serikali

kuhusu kuweka visima vya gesi vya Songosongo rehanijambo ambalo ni aibu na ni hatari sana kwa nchi yetu?WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, ni kweli kwamba kuna Kampuni moja ilitoapendekezo hilo na hii imetokana na kwamba TANESCOimetumia umeme wake mwingi na TANESCO ilikuwahailipi deni. Sasa kampuni inataka kuendelea nashughuli zake, kwa hiyo inataka kwenda kukopa fedhanje. Sasa kwenda kukopa fedha nje, ikatoa pendekezokwamba iweke kisima kimoja rehani ambacho kinagesi karibu milioni 880 billion cubic feet na vilevileakapendekeza kwamba assets zisizohamishika likiwemobomba la gesi la Dar es Salaam. Lakini kwa kifupi nikwamba, haikubaliki wala haitekelezeki, haiwezekani!Msimamo wa Serikali ni kwamba tumekataa nahaliwezi kufanyika hilo. (Makofi)MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Watanzania wanafahamu kwamba Taifa letukwa sasa linakwenda kuwa Taifa lenye uchumi wa gesina mafuta miaka michache ijayo, na kuna Makampunimengi kutoka duniani yanafanya tafiti za mafuta nagesi. Lakini changamoto kubwa katika eneo hili niuwazi kuhusu kiasi ambacho kinapatikana, lakini uwazikatika gharama ambazo wanazitumia. Zipo taarifa kwabaadhi ya Makampuni ikiwemo Mare and Prom, zinaover estimate, yaani zina report gharama kubwa sanaau zina inflate, wanatumia Dola za Kimarekani milioni60 lakini wanasema wanatumia Dola za Kimarekanimilioni 240.

Sasa nataka kujua, Serikali yetu inachukua hatuagani kuweza kudhibiti mwenendo wa Makampuniambayo yanafanya tafiti za mafuta na gesi nchini ilitusije kutumbukia katika tatizo lile lile ambalolinajitokeza kwenye Makampuni ya Madini?MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, tena kwa kifupikwa sababu nina dakika nne tu.WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, anachosema kinaweza kuwa ni kweli,kwani sina uhakika. Lakini lazima tufahamu kwambahaya Makampuni ambayo yanatafuta gesi na mafuta,ni hayo hayo Makampuni ambayo yanatafuta gesi namafuta popote duniani. Hicho ni kitu cha msingi, kwanisiyo tu yamekuja kwa ajili ya Tanzania.Jana niliagiza TPDC analysis ya matumizi ya kwao,Kampuni kwa Kampuni na mimi napenda kumkaribishaMheshimiwa Mbunge kati ya kesho, Jumatatu naJumanne, timu ya TPDC ipo hapa, ina hizo nyaraka,aweze kuja tujaadiliane ana kwa ana kwa sababu hiini ndefu sana.MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Nataka kujua sera ya zabunipamoja na utoaji wa leseni kubwa za madinizinapokuwa ni moja, tangu moja zikagawanywainakuwaje?Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wanguwa maandishi nilielezea mfano wa mlima Kaburu katikamgodi wa Kiwira. Nashukuru.

MWENYEKITI: Naomba ujibu kwa kifupi sana, kwaninina dakika chache sana.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELLE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwareference aliyoizungumza ya Kaburu, kuna taratibuzilikiukwa nyingi kwenye sera na sheria. Kwa hiyo,Mheshimiwa Waziri alipokuwa anajibu, alielezakwamba tumefaya uchunguzi na uchunguziunaendelea. Kwa hiyo, namwomba MheshimiwaMbunge, kwa hizi siku tulizozitoa baadaye tunawezatukampa ufafanuzi kwa sababu ni suala refu sana.MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Katika mchango wamaandishi niliieleza Wizara kwamba, miradi ya gesi nijambo muhimu sana katika ustawi wa uchumi nakukuza sekta nyingine katika nchi yetu.Mheshimiwa Mwenyekiti, umezuka upotoshajimkubwa sana kwamba miradi hii haielekei kuisaidianchi. Nilitaka Wizara ionyeshe jitihada za dhahiri kabisakuelimisha wananchi na hasa wa Mikoa ya Lindi naMtwara. Nini manufaa ya gesi katika uchumi wa nchiyetu na yale ambayo wao watanufaika nayo?NAIBU WAZIRI WANISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,tumeanza kufanya hivyo na tulikuwa tumeanza naMkuu wa Mkoa wa Mtwara na tunaendelea na kwakweli wananchi watambue kabisa kwamba gesi inamanufaa makubwa, inasababisha mbolea,

inasababisha uzalishaji wa umeme, inauzika yenyewekama bidhaa na kwa hiyo, kuna manufaa makubwana kwa kweli viwanda vitakua na kilimo kitakua kwasababu ya gesi.Kwa hiyo, nikubaliane na Mheshimiwa Mangunguna nimpongeze kwa jitihada kubwa anazofanya katikakutetea suala la gesi katika maeneo ya Mikoa ya Lindiya Mtwara.MHE. IGNAS A. MALOCHA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru. Katika mchango wangu wamaandishi nilieleza kuwa ni haki ya Mtanzania yeyotekupatiwa umeme, lakini nikaeleza kwamba yapomaeneo yanasahaulika kupelekewa umeme japokuwayana fursa nyingi za kiuchumi yanayoweza kusaidiaTaifa letu na nikatoa mfano wa Ukanda wa ZiwaRukwa na nikaiomba Serikali ijaribu kutuma wataalamukupita katika ukanda huo ili waweze kubaini fursazilivyo nyingi zinazoweza kusaidia uchumi wa nchi hii.MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, nitatumiakifungu namba 104 kuongeza dakika ili tumalize walewalioomba. Haya, Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli kwamba yapo maeneo yenye fursa nzuri namuhimu sana za kiuchumi kama maeneo yaumwagiliaji na maeneo ambayo yana rutuba. Sisikatika Sera ya Umeme ya Taifa, ni kwamba, maeneohayo yenye fursa za kiuchumi, kilimo cha umwagiliajina mabonde makubwa ni lazima yapelekewe umeme,

kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Malocha kwambahata Laela na hata maeneo ya mradi wa umwagiliajiakote tunapeleka umeme.MHE. DKT. TITUS M. KAMANI: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Katika uwekezaji wa migodimikubwa uliofanyika awali ambao ulishahamishawananchi, umewaacha watu wengi katika umasikini,lakini katika baadhi ya migodi, ni watu wanapambanana wawekezaji na hatimaye uuaji.Katika uwekezaji mkubwa ambao utakuja kamaambavyo nilitoa mfano wa Ngasamo ambapo kunaNickel nyingi, imeonekana kwamba wananchi sasahawatahamishwa mpaka wapewe thamani halisi yamaeneo yao pamoja na mali zilizopo ili wasiondokewakiwa masikini. Ahsante.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELLE): Mheshimiwa Mwenyekiti,Mheshimiwa Mbunge ameuliza, lakini alichokieleza nikama ametoa jibu moja kwa moja kwamba lazimakuwe na compensation kama wananchi walikuwepoeneo husika na lazima mwekezaji apate right of entry,yaani lazima apate kibali na makubaliano ya kufanyashughuli pale. Kwa hiyo, huo ndiyo utaratibu na sheriainaelekeza hivyo. Kwa hiyo, kilichopo ni kusimamia nakuhakikisha kwamba tusingoje madhara yatokee amakumkaribisha mwekezaji halafu baadaye ndiyotunageuka. Lakini lipo tatizo, kwani kuna watu ambaowanavamia maeneo ambayo mwekezaji anakusudiakufanya compensation. Wakihisi hivyo, wanawahikwenda kule kuchukua yale maeneo ili nao wafidiwe.

Kwa hiyo, wanasababisha usumbufu mkubwa kwawawekezaji.MHE. JOELSON L. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Kwa kuwa, katika aya ya 190 MheshimiwaWaziri ametoa agizo zito la kutaka kampuni zotezinazochimba madini kwa miaka mitano na kuendelea,ambazo hazijaanza kulipa kodi ya mapato, zianzekulipa bila visingizio na wale watakaoshihdwa, basiwafunge migodi na kuondoa. Lakini sasa swali nikwamba, Makampuni haya ni Makampuni gani kwamajina na amri yake hii inatekelezwa msimu gani sasa?Ni msimu huu wa fedha amri hii inaanza kutekelezwaau itatekelezwa kipindi gani?NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweliMheshimiwa Waziri ameagiza yote yaanze kulipacorporate tax. Hivi sasa Makampuni ya Barrick namengine yote kwa mfano, TULAWAKA, Bulyanhulu, naNorth Mara wanalipa, kasoro Buzwagi ambayouwekezaji wake siyo wa muda mrefu sana. Lakini piaMakampuni kama GGM na Resolute pia wanalipasambamba na Tanzanite one. Kwa hiyo, hii corporatetax inalipwa baada ya kuwa Kampuni imeanzakutengeneza faida. Tulichokuwa tunakipigania kwenyesheria ni kuhakikisha tunapunguza ule muda mrefu wapayback period, waanze kulipa mapato mapemakuliko ule muda ambao ulikuwa umekisiwa kule awali.Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini haya yote namabadiliko ya mikataba, zile MDAs yanafanyika kwamazungumzo na tumekwishakubaliana na haya

Makampuni kwamba, kuanzia mwezi Septemba, 2012tunaanza kukaa mezani kujadili upya kupitia Mikatabayote ya Madini.MHE. HASNAIN M. MURJI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru. Katika mchango wangu nilitaka kujuakwamba kulikuwa na sera ya kwamba sisi watumiaji waumeme wa gesi tulipoanza kutumia umeme wa gesimiaka minne iliyopita, kulikuwa na ahadi kwambaatakayetumia umeme huo wataunganishiwa kwagharama nafuu ya flat rate ya Sh. 70,000/= kwakutumia Kampuni ya Artumas, bahati mbaya Kampuniya Artumas sasa imefilisika na imekabidhi TANESCO nahiyo ahadi haijatekelezeka. Je, tukitaka kujua sasaTANESCO pia ahadi hiyo wataweza kuitekeleza? Siyokatika mradi huu wa bomba la gesi mpya, ni miakaminne iliyopita!NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,ni kweli Mheshimiwa Murji tumekwishaongea nayemara kwa mara juu ya jambo hili. Lakini ni kwelikwamba Serikali inafanya mambo makubwa sana kuleMtwara na Lindi kwa sababu hata huo umeme wa gesiambao wanautumia, Serikali inatoa fedha takribanShilingi bilioni tano kila mwaka kufidia gharama zauzalishaji wa umeme wa gesi, kwa sababu hakunanamna yote ambayo wananchi wale kwa matumiziyale madogo madogo wanaweza wakalipa zilegharama.Kwa hiyo, Serikali inafanya mambo makubwasana na ziada ya hapo sasa tumepanga kwenda zaidi

ya pale. Kwa hiyo, hili analolisema la kupunguzagharama za umeme kwa Sh. 70,000/= ilikuwa ni ahadiya wakati huo. Sasa tunakuja na mpango mkubwaambao sasa utashirikisha na Serikali imeamua kwelikabisa kuhakikisha kwamba inaweka vizuri kule Kusini.Kwa hiyo, tuta-accommodate mambo mengi. Kwahiyo, mimi nadhani hili liwe ni sehemu ya mazungumzoyetu tutakayoyazungumza Jumatatu, niliyoombakukutana na Waheshimiwa Wabunge wa Lindi naMtwara.MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Mimi kwenye mchango wangu wa maandishinilikuwa nimemweleza kwanza kwa kumpongeza kwamaonyesho yale makubwa ya vito vya thamaniyaliyofanyika Arusha na kwamba Wizara ilialikawanunuzi vito vya thamani kutoka sehemu mbalimbaliduniani, na walikuwepo pale wanaliuza na hatimayewanunuzi wengine walirudi na fedha zao. Sasa je, Serainasemaje kuhusu kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo hasa wale wa vito vya thamani ambaowamekuwa wakitembea na mawe mfukoni bila kujuathamani yao ili waweze kupata soko? Ahsante.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELE): Mheshimiwa Mwenyekiti, sheriainaelekeza kwamba madini ya vito ni lazima kwanzayachimbwe na wazawa. Lakini Arusha hasa kwenyeTanzanite one, kuna tatizo kubwa la utoroshaji waTanzanite na hii inafanyika baada ya wale wanunuziwa zamani waliokuwa wakitoka India, wamegeukakuwa sasa ni ma-broker. Sasa hawa watu wetuWaswahili wamekwishakosa biashara sasa hivi. Kwa

hiyo, nilikuwa Arusha kule na nimeshaagiza walewageni wote ambao wanajihusisha na biashara ya vitokama ma-broker, waondoke haraka. Niliwapa siku 14na nikaagiza kabisa vyombo vya Ulinzi na Usalamavifanye msako baada ya siku 14, kama kuna wanunuzitoka nje wanaofanya kazi ya u-broker waondoke.Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tumewekamkakati kama Wizara kuhakikisha tunaifanya Arushakuwa John stone Center ya Afrika na hilo tutalifanyakwa kujenga jengo maalum Centre nawafanyabiashara vijana wa Arusha wanaotembeaMitaani wawe na sehemu ambayo mnunuzi akijaanawakuta na siyo kwenye vichochoro vya Arusha.(Makofi)MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Diana Chilolo.MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Katika mchango wangu wa maandishinilifarijika sana kusikia maelezo ya Mheshimiwa Wazirikwamba ataharakisha kuleta Sera na Sheria pamojana Mpango wa Gesi hapa Bungeni ili aweze kusimamiamapato makubwa yatakayotokana na gesi. Sasanikawa nimemshauri Mheshimiwa Waziri kwamba,anaonaje hayo mapato makubwa yaliyotokana nagesi atengeneze mfuko wa mapato pekee yake wagesi ili Watanzania tuwe na historia kutokana na gesi tu,tumenufaika kiasi gani? Tumepata mapato gani?Tumefanya nini kutokana na fedha hizo?WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, hilo wazo, mbali na kwamba ameliuliza na

Kamati amependekeza, na sisi tunalo wakatitunatengeneza sera. Sera itakapokuja mbele yenu nabaada ya kupitiwa na watu wengi sana, ni lazimafedha zinazopatikana kutokana na gesi au mafutaziende kuzamishwa kwenye Mfuko wa Hazina,hatutajua zinatumikaje. Kwa hiyo, tutaweka SpecialFund, tutafuta jina lake kama ambavyo nchi nyinginewanafanya mfano, Norway na sehemu nyingine. Niwazo zuri sana, tumelichukua na sisi tunalo. (Makofi)MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana. Kumekuwa na malalamiko mengi sanakwa vijana wenzangu ambao wanafanya kazi kwenyeMakampuni ya migodi, mbali ya kwamba wanakosakazi zenye staha ambazo wengi wao wanapatawageni. Lakini malalamiko haya yamekwenda mbelezaidi na kudhalilishwa na wengi hata kuvuliwa nguokwa kisingizio cha kuondoa na mawe. Miminimefarijika kwamba kwenye hii Wizara, pia wapoMawaziri vijana akiwemo Mjumbe wa Baraza Kuu.Mwenzangu, Mheshimiwa Stephen Masele: Sasa je,mmejipanga vipi kuhakikisha vijana hawa waKitanzania wanaondokana na manyanyaso hayoambayo wamekuwa wakiyapata kwa muda mrefu?NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELE): Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa swali la Mheshimiwa Ester Bulaya. Nikweli kumekuwa na kesi nyingi zinaripotiwa zamanyanyaso, tumepokea kesi kutoka Arusha kwenyeMgodi wa Tanzanite One kwamba vijana wetu wengiwanapopita pale wanapita kwenye scanner nawanahisi kwamba ile scanner inaweza ikawa na

madhara kiafya. Lakini nilipozungumza na uongozi waMenejimenti ya mgodi ule wa Tanzania Onewakasema kwamba ile inawasaidia wao kujuavilivyomo mle ndani. Lakini tukazungumza kwambascanner zile au kuwapekua kwa njia ya physical kwaakinamama inakuwa shida kidogo.Mheshimiwa Mwenyekiti, ni suala ambalo kwakweli linahitaji majadiliano ya mara kwa mara baina yaSerikali na migodi hii kuhakikishia kwamba taratibu zakazi zinasimamiwa bila kunyanyasa jinsia ama Utaifa.(Makofi)MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kushauri pale alipoishia Mheshimiwa Machali,naendelea kidogo, kwamba; kutokana na messagezilizotumwa hapa Bungeni za kutisha, Waziri na KatibuMkuu watashindwa kufanya kazi inavyotakiwa.Tumetumiwa message karibu nusu ya WaheshimiwaWabunge hapa, wanamtisha na kwambawatamwondoa kwa vyovyote vile na watapambananaye mpaka mwisho, na baadhi ya WaheshimiwaWabunge walimdai Katibu Mkuu rushwa Shilingi milioni50 ili wakagawane kwenye Kamati zao. Huu ni ushahiditosha na sisi tukienda kule nje tunadharauliwaWaheshimiwa Wabunge wote, kwamba Wabunge niwala rushwa. Kwa hiyo, wametuchafua Wabungewote humu ndani. Kwa hiyo, naomba majina yatajwebila huruma yoyote, wanajulikana. Kwa nini tunaogopakuwataja? (Makofi)MWENYEKITI: Mheshimiwa Keissy, ahsante, hilolimekwishajibiwa. Tunaendelea.

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: MheshimiwaMwenyekiti, katika mchango wangu wa maandishi,katika ukurasa wa 10, niliishauri Serikali kutokana naTaarifa za Serikali kwamba kuanzia mwezi Januari,mwaka 2012, mpaka mwezi Machi, mafuta, jamii yapetrol gasoline yenye thamani ya dollar 210 yaliingianchini. Taarifa za Mkemia Mkuu wa Serikali zikasemaethanol in essence zaidi ya asilimia 10 ilikuwaimeongezwa kiasi ambacho kiliwapiga changa lamacho Watanzania kwa hasara ya karibu dollar 20.Nikamwomba Mheshimiwa Waziri atoe msimamo waSerikali, na kama hana la kufanya, awaombemsamaha Watanzania ambao waliuziwa kitu chenyethamani ndogo kwa bei ya thamani kubwa, yaani kwakutumia quotation za Mediteranian wakati ndani kunaethanol nyingi sana ambayo kwenye Soko la Duniainauzwa dollar 200 wakati ukweli wenyewe sisitumechanjiwa Dollar 1000 kwa tani.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nampongeza Mheshimiwa Mwijage, anafanyakazi nzuri sana kwenye Kamati, ameisaidia Kamatipamoja na Serikali kwa sababu yeye ni mtalaam wamasuala haya. Lakini pia nimpongeze kwa mchangowake katika page ya 10 zilizoandikwa mbele nanyuma, kwa hiyo, ni page 10 za maandishi.Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kulitokeamalalamiko ya mafuta mabaya ambayo ilibainikabaadaye kwamba ni ethanol ilikuwa imezidi na ethanolina bei ndogo. Kwa hiyo, sisi tunafikiria uchakachuaji

huku kwenye mafuta yakishashuka kumbeuchakachuaji unafanyika hata huko huko kablahajafika hapa nchini. Hili tumelipokea na tunalifanyiakazi na bado tunahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwaMheshimiwa Mwijage. (Makofi)MWENYEKITI: Mheshimiwa Kilufi hayupo,Mheshimiwa Lugola.MHE. ALPHAXARD K. N. LUGOLA: MheshimiwaMwenyekiti, mimi nataka kujua, kama Wizara ya Nishatina Madini inayo sera ya double standards katikakuwataarifu watanzania juu ya kinachoendelea hapaBungeni.Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati MheshimiwaWaziri anafanya majumuisho, aliweza kuwa na ujasiriwa kuwataja wale ambao wamehusika na kuihujumuTANESCO, akataja Eva kama Mke wa William Mhandokwa Watanzania, akamtaja Fred kwa Watanzania,akataja Makampuni yakiwemo na Shule za St. Mary’sna mengine kwa Watanzania wakawajua wanaibaumeme wa Tanzania, baadaye akaenda kwenye eneola Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Nishatina Madini na akasema kwamba wamejihusisha nakuuza matairi mabovu na wamejihusisha nakupandisha bei ya matairi. Kwa maana hiyo, alikuwaanawataja watu ambao wanaihujumu TANESCO.Nataka maelezo ni sera ya double standards kwaWizara hii kutaja baadhi ya Watanzania mbele waWatanzania, na wengine kutowataja hapa Bungeni, nisera ya double standards? Naomba majibu. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge hakuna chadouble standards hao wengine wana utaratibumwingine wa kushughulikiwa. Mheshimiwa ZainabKawawa.MHE. ZAINAB R. KAWAWA: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi.Mheshimiwa Mwenyekiti, itakumbukwa kwambamwanzoni mwa mwaka 2011 kwa maana ya mwishonimwa mwaka wa fedha uliopita, TANESCO iliongeza beiya umeme kwa asilimia 41. Ongezeko hili tunajuaathari zake limechangia pia wizi wa umeme, ongezekohili limechangia ugumu wa maisha, lakini kisingizio chaongezeko la umeme huu ni kutokana na gharama zamgao wa umeme. Sasa naiomba Wizara ituelezehapa, kutokana na udharura ule ule wa kuongezaasilimia 41 ya gharama ya umeme, ni lini sasaitaishusha asilimia hiyo 41 ya gharama ya umeme kwaudhararu huo huo kwa kuwa sasa imekwishapunguzagharama ya mafuta ya kuendeshea mitambo yaumeme kwa Shilingi bilioni sita kwa mwezi, lakini piaimepunguza gharama ya kuunganisha umememajumbani? Sasa ninaomba, sambamba na hayo,ituambie ni lini kwa dharura itapunguza hii asilimia 41 iliWatanzania turudi kule kule kulipa umeme kwagharama nafuu ambazo tulikuwa tunalipa siku zote?(Makofi)MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri naomba kwakifupi sana.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaMwenyekiti, naomba Mheshimiwa Mbunge akumbukehistoria ya nchi yetu, wakati tulikuwa na hoteli chachekule Arusha, Mwanza, hoteli zilikuwa za bei ya juu sana.Sasa hivi ukienda Kongo DRC hoteli ni chache, bei yakule wakikupatia hoteli ya Dola 500 huwezi kuamini.Hapa siri ni kwamba Watanzania watumiaji wakiwawengi bei itapungua. Kwa sasa hivi ni karibu asilimia 18ya Watanzania ambao wanatumia umemeukilinganisha na Kisiwa kidogo cha Mauritius ambachoni karibu asilimia 99.8 ambacho raia wake wanaumeme. Afrika Kusini ambaye economically ndiyogiant ya Afrika mwenye GDP ya zaidi ya Dola bilioni500, asilimia 75 ya raia wake wana umeme.Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge dhamira yetu nikushusha umeme na ndiyo maana tunakuja namikakati mingi sana ya uzalishali umeme na usambazajiwa umeme kusudi watu wakiongezeka, tukifikaangalau asilimia 50 na ile bei itapungua.MHE. BETTY E. MACHANGU: MheshimiwaMwenyekiti, ahsante. Hotuba ya Mheshimiwa Waziriimeainisha migodi nane mikubwa ambayo inawasilishamipango ya kufunga migodi closure plans, na hii italetaathari kubwa sana kwa ajira hapa nchini. Je, Serikaliina mpango gani licha ya mradi wa gesi na Urani naNickel, ina mpango wowote wa kufunga migodimingine mipya ya dhahabu au madini mengine?NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.STEPHEN J. MASELLE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza,ile mining closure plan haimaanishi kwamba migodiyote itafungwa kwa mara moja. Kila mgodi una maisha

yake. Kwa mfano, Bulyankhulu wanakwenda mpakamiaka 25, wapo wanaokwenda mpaka miaka 15. Kwahiyo, ina uhai tofauti. Kwa hiyo, kilichopo pale nimatakwa ya sheria kwamba kila mgodi lazima uwe naplan watakapokuwa wanataka kufunga, mambo ganiwatayafanya kwa ajili ya utunzaji wa mazingira namambo mengine mbalimbali. Kwa hiyo, zile ni hatuaambazo Wizara inazichukua kuhakikisha kwambainatimiza matakwa ya sheria. Lakini pia ipo migodimipya mingine ambayo ipo kwenye utaratibu wakuanzishwa kama Mheshimiwa Waziri alizungumziaKabanga Nickel kule Ngara, kuna Bariadi, kule kunaShanta mining Chunya na Singida pale kuna Shanta.Kwa hiyo, ipo migodi mingi ambayo ipo kwenyeprocess za mwisho katika utafiti na ipo njianikuanzishwa.Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tatizo la ajirahalitajitokeza sana kwa sababu bado kuna gunduzinyingi zinaendelea kufanyika.MHE. ALBERT O. NTABALIBA: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Kwakuwa, Taasisi za Serikali, Majeshi, Polisi, na Hospitalizimekuwa na matatizo makubwa sana kulipa bili zaumeme. Huku Serikali na Bunge wakiwaidhinishia hizobajeti za umeme kwenye bajeti zao: Je, ni lini sera yakuchukua fedha zote zinazopelekwa kwenye Taasisizikapelekwa moja kwa moja na Wizara? (Makofi)NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti,nikiri tu kwamba maswali mengine ni magumu. Lakini

hili kwa kweli jibu lake ni jepesi. Ni kweli kama fedhaimetengwa kwa ajili ya umeme katika Wizara,inakuwaje ngumu tena isilipwe. Lakini niseme basikwamba, kila Wizara itaangalia utaratibu wake, ila sisiWizara ya Nishati na Madini tutaamua kwa zile Taasisizetu zote kupeleka hela kama moja kwa moja aunamna gani, kwa sababu mchakato unavyokwendahuko pengine ndiyo inayopelekea pengine zisilipwe bili,lakini zinaonekana kwenye vitabu vya bajeti.MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, sasa mudauliobaki unaniruhusu kutumia guillotine ni dakika kumi.Katibu.(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipilitishwa na KamatiyaMatumizi bila mabadiliko yoyote)Kif. 1002 - Finance and Accounts … Shs.1,812,553,000/=Kif. 1003 - Policy and Planning … Shs.1,726,723,000/=Kif. 1004 - Internal Audit Unit … Shs. 845,173,000/=Kif. 1005 - Legal Services… … … Shs.4,825,302,000/=Kif. 1006 - Government CommunicationUnit … … … … … … … … Shs. 1,399,847,000/=Kif. 1007 - Procurement ManagementUnit... … … … … … … … Shs. 800,614,000/=Kif. 1008 - Environment ManagementUnit … … … … … … … … Shs. 587,358,000/=Kif. 1009 - Management InformationSystem.. ... ... ... ... ... ... ... .. Shs. 2,483,014,000/=Kif. 2001 - Minerals … … … … … Shs.32,655,213,000/=Kif. 2002 - Madini Institute … … Shs. 0Kif. 2004 - Tanzania Diamond Sorting Agency

(Tansort) … … Shs. 1,966,898,000/=Kif. 2005 - Eastern Zone … Shs. 1,141,724,000/=Kif. 2006 - Western Zone … Shs. 670,899,000/=Kif. 2007 - Lake zone … … Shs. 1,122,750,000/=Kif. 2008 - Northern Zone … Shs. 969,475,000/=Kif. 2009 - Southern Zone … Shs. 808,695,000/=Kif. 2010 - Central Western Zone Shs. 1,039,656,000/=Kif. 2011- Central Zone … … … Shs. 729,942,000/=Kif. 2012 - Southern Western Zone Shs. 943,308,000/=Kif. 3001 - Energy and petroleum Shs. 45,495,170,000/=(vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipilitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)MIPANGO YA MAENDELEOFUNGU 58 - WIZARA YA NISHATI NA MADINIKif. 1003 - Policy and Planning … Shs.700,000,000/=Kif. 1008 - Environment ManagementUnit … … … … … … … Shs.871,000,000/=Kif. 2001 - Minerals … … …. … Shs. 66,240,000,000/=Kif. 2002 - Madini Institute … … Shs. 3,500,000,000/=Kif. 2003 - Research and LaboratoryServices … … … … … … Shs. 1,500,000,000/=Kif. 3001 - Energy and Petroleum Shs. 458,379,861,000/=(vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipilitishwa na Kamati yaMatumizi bila mabadiliko yoyote)(Bunge lilirudia)

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaSpika, naomba kutoa taarifa kwamba Bunge lakoTukufu limekaa kama Kamati ya Matumizi na kuyapitiaMakadirio ya Matumizi ya fedha za Wizara ya Nishatina Madini kwa mwaka 2012/2013 na kupitia vifunguvyote kwa pamoja na kuvipitisha bila ya mabadilikoyoyote. Hivyo basi, naliomba Bunge lako Tukufuliyakubali makadirio haya.Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI:Mheshimiwa Spika, naafiki.(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)(Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madinikwa Mwaka 2012/2013 yalipitishwa na Bunge)SPIKA: Kwa hiyo, kwanza kabisa, naombanichukue nafasi hii kukupongeza Mheshimiwa Waziri naManaibu Waziri wako na Katibu Mkuu kwamba Wizarammeichukua siku za karibuni, lakini tunaona kabisaushujaa ulioko kule.Kwa hiyo, tunawapongeza wafanyakazi naWakurugenzi wote walioko chini ya Wizara hiyokwamba tunawahitaji sana kurudisha uadilifu katikanchi katika eneo linalohusika na sisi tunawaombeakheri tuweze kufanikiwa. Kwa hiyo, sasa nitamwitaMheshimiwa Vita Kawawa.

MHE. VITA M. KAWAWA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii sasa niwasilishehoja yangu kuhusu Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge(Kanuni ya 53(2), natumia pia kifungu kidogo cha55(3)(f).Mheshimiwa Spika, katika michango iliyokuwamingi ya Waheshimiwa Wabunge kwenye Wizara yaNishati na Madini, imeonyesha kwamba, baadhi yaWajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini na baadhiya Wabunge kuwa wamejihusisha na vitendo vyarushwa. Kwa kuwa suala hili na tuhuma hizi ni sualalinalohusu Maadili, na suala hili la Maadili linahusu piahaki, kinga na madaraka ya Bunge, kwa kutumiaKanuni ya 53(2) na Kanuni ya 55(3)(f) naomba kutoahoja kwamba, kwa kuwa tuhuma hizi ni nzito, zinagusaBunge lako Tukufu, na hivyo kulidhalilisha kwa ujumlawake, na kwa kuwa tuhuma hizo ni nzito na vigumukuzithibitisha, naomba utumie Mamlaka yakoyaliyoainishwa katika Kanuni ya 5(1), hivyo niombeBunge lako likubali kwa mujibu wa Kanuni ya 5(1)naomba niisome na nanukuu, Mamlaka ya Spika,kifungu cha 5(1):“Katika kutekeleza majukumu yake yaliyotajwakatika Ibara ya 84 ya Katiba, Spika ataongozwa naKanuni hizi na pale ambapo Kanuni hazitokuwa namwongozo, basi Spika atafanya kazi kwa kuzingatiaKatiba, Sheria nyingine za nchi, Kanuni nyingine zilizopo,maamuzi ya awali ya Maspika wa Bunge pamoja namila na desturi za Mabunge mengine yenye utaratibu

wa Kibunge unaofanana na utaratibu wa Bunge laTanzania.”Hivyo kwa mamlaka uliyonayo, naomba kwanzaukubali kuivunja na kuiunda upya Kamati ya Nishati naMadini na Kamati nyingine zilizopata kutuhumiwakuhusiana na rushwa. Pili, naomba jambo hililililolalamikiwa sana katika hotuba hii ya Nishati naMadini lifanyiwe uchunguzi na Kamati ya Haki, Kingana Madaraka ya Bunge ili ukweli wake ukibainika nahatua ziweze kuchukuliwa.Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.MHE. HERBERT J. MNTANGI: Mheshimiwa Spika,naafiki.(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naona hoja hiyoimeungwa mkono, halafu iko wazi, haina ubishimwingine. Kwa hiyo, kwa madhumuni hayo na piaametumia kifungu sahihi cha ile 55(3)(f) ambayo ni Hakina Kinga za Wabunge, hii haitolewi taarifa. Kwamaana hiyo basi, Waheshimiwa Wabunge, sio tu kwahoja hii, kwa siku zilivyokuwa zinakwenda, tabia yaWaheshimiwa Wabunge kwa maelezo hayaimebadilika. Nimeagiza Kamati yangu ya Haki, Maadilina Madaraka ya Bunge tutengeneze code of ethics namtu yeyote atakayetuhumiwa katika mazingira hayo,lazima sisi tuchukue hatua inayostahili, tena kubwa. Piatunataka siyo kwa yule Mbunge anayehusika tu,

tutakwenda na kwa yule mtu anayehusika. Kwasababu imejitokeza sasa hivi utakuta Mbunge hapaanatoka jasho kweli kweli, anatoa hoja, kumbeanafanya kazi ya mtu fulani.WABUNGE FULANI: Waambie!SPIKA: Ni imani yangu kabisa kwamba Serikali yetuna nchi yetu kwa ujumla inapita katika kipindi champito kama huo mpito wa Bunge, kama hamtakuwaimara na kuwa na msimamo wa kuweza kuisimamiaSerikali, kwa ukweli hatutaweza kwenda, na matumainiya wananchi ni wapi kama siyo Bunge? Mimi nasemakwa dhati kabisa, kitendo hiki kwa kweli hakikubalikindani ya Bunge hili. (Makofi/Kicheko)Hatuwezi kuisimamia Serikali hukutunapokeapokea, mnaisimamiaje Serikali kwa mtindohuu? Kwa hiyo, naamini kabisa Wabunge mkikaa vizurina tukafanya kazi yetu vizuri, mabadiliko makubwakatika uendeshaji wa Serikali yatatokea. Lakini wenzetumara wanakwenda huku, mara wajipendekeze, marawaombe hiki, mara waombe hiki, hatuwezi kwendahivyo. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge, kwamaamuzi haya, kwanza kwa kutumia Kanuni hiyo ya53, nalipeleka suala hili kwenye Kamati ya Haki, Kingana Maadili ya Bunge ili walifanyie uchunguzi na kuletataarifa hapa. Sasa hao mliokuwa mnawatakawatajwe, sasa hiyo Kamati itafanya kazi hiyo.(Makofi/Kicheko)Pili, kwa kutumia mamlaka niliyopewa na Kanuniya 113(3) na baada ya Wabunge kuunga mkono hoja

ya Mheshimiwa Vita Kawawa, naridhia ombi hilo. Hivyonitaivunja Kamati hiyo na nyingine ambazozitaonekana zina tabia hiyo.MBUNGE FULANI: Safi! Wakae bila Kamati hao.(Makofi/Kicheko)SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwanza kabisa,niwashukuru sana kwa kazi mliyoifanya sana wiki hii nakwa ushujaa ambao mmeufanya kabisa katika kipindihiki na kwa hiyo, natoa tangazo pia kwamba kunamchezo wa Kirafiki na NMB wanaohusika mwendemkacheze kwa ari mpya na nguvu mpya mtuleteeushindi kama kawaida na ile Klabu ya Kulengashabaha kesho waende. Vinginevyo, natakanawatakia week-end njema, naahirisha Kikao chaBunge mpaka siku ya Jumatatu saa tatu asubuhi.(Saa 8.33 mchana Bunge liliahirishwa mpaka Siku yaJumatatu, Tarehe 30 Julai, 2012 Saa Tatu Asubuhi)

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!