Energiewende ya Ujerumani

globalenergiewende

Energiewende ya Ujerumani


Energiewende ya Ujerumani

Tunabadilisha mfumo wa nishati nchini Ujerumani


02 | Energiewende ya Ujerumani

Energiewende – tunabadilisha mfumo wa nishati nchini Ujerumani

Karibu!

Tumefurahi kuwa ungependa kujua kuhusu Energiewende, mradi muhimu sana kwa maisha ya

baadaye nchini Ujerumani.

Tumeamua kuzibadilisha njia zetu za utoaji nishati kuwa ya vyanzo visivyoisha kama vile jua

upepo na vinginevyo kama hivi. Tumeamua pia kuwa waangalifu zaidi katika kutumia nishati.

Kwa njia hii, Ujerumani inachukua jukumu muhimu katika kulinda hewa.

Energiewende ni jawabu tosha la swali kuhusu jinsi tunavyoweza kufanya usambazaji wa nishati

kuwa salama, nafuu na endelevu. Fursa hii ya kipekee ya Ujerumani, kama eneo la biashara

na uwekezaji, itafungua nafasi mpya za biashara, endeleza ungunduzi, toa nafasi za kazi, kuza

uchumi na itaifanya Ujerumani iache kutegemea uingizaji wa mafuta na gesi kutoka nchi

nyinginezo kwa kiasi kikubwa.

© iStock/SilviaJansenx © Paul Langrock

1971

Serikali ya Ujerumani ilizindua mpango wake wa kwanza wa utunzaji wa mazingira.


© dpa/Westend61/Werner Dieter

Energiewende ya Ujerumani | 03

Kwa nini tumepanga onyesho hili? Mara kwa mara serikali ya

Ujerumani huulizwa maswali mengi kuhusu Energiewende. Maswali

haya mengi sana hutoka duniani kote mpaka jina ‘energiewende’

lenyewe limeanza kutumika katika lugha nyingine mbalimbali.

Tunalifurahia hilo. Vilevile, watu wengi hushangaa kwa sababu ya

upana wa mradi na vitu mbalimbali vinavyojumuishwa. Katika

onyesho hili, tunapania kuonyesha majukumu haya pana pamoja na

changamoto zinazohusika.

Onyesho hili pia litaonyesha kuwa mchakato wetu wa kubadilisha

mfumo mzima wa utoaji nishati nchini Ujerumani hautakamilika

kwa siku moja. Mchakato mzima wa kuubadilisha mfumo wa utoaji

nishati uliopo kwa sasa kuwa mfumo wa nishati endelevu utafanywa

hatua kwa hatua hadi kufikia mwaka wa 2050. Katika kuufanikisha

mchakato huu, tutaongozwa na mwongozo madhubuti na malengo

wazi ya ubora wa kiwango cha juu.

Energiewende ina mizizi ya utendakazi wa kimataifa. Tunakaribisha

mazungumzo ya kina na majirani zetu wa Ulaya na washirika

wengineo wa kimataifa tukilenga ushirikiano na suluhisho kutoka

nchi mbalimbali. Tunahitaji kuwapo na ushirikiano katika kutoa

suluhu ya kupunguza uzalishaji wa CO2 ili kuzuia ongezeko la joto

duniani na kuunda vyanzo vya nishati ambavyo ni salama, endelevu

na nafuu.

Kwa kugeuza mfumo wake wa nishati kuwa salama, nafuu na

endelevu, Ujerumani inaonyesha jinsi inavyozingatia kwa uzito

wajibu wake wa kuyaboresha maisha ya wanadamu na kuifanya

dunia mahali bora zaidi. Tunakukaribisha uungane nasi tunapoingia

katika mfumo huu mpya wa nishati endelevu. Tunatumai utafurahia

onyesho na kuwa litakuwezesha kupata mengi ya kuwaza na kujadili.

1972

Mmoja kati ya mitaa ya kwanza kutumia nishati ya miale ya jua ulijengwa katika mji mdogo wa Penzberg, kusini mwa Ujerumani.


04 | Energiewende ya Ujerumani

Ufanisi wa nishati

Kutumia nishati

kwa ufanisi zaidi

Matumizi ya umeme, joto na mafuta kwa ufanisi huokoa pesa, huongeza uzalishaji unaoweza

kutegemewa na huchangia katika utunzaji wa hali ya mazingira ya nchi. Ujerumani

inalazimika kuingiza kiwango kikubwa cha vyanzo vya nishati kutoka katika nchi nyingine.

Uingizaji huu umepanda kiasi kwamba karibu asilimia sabini ya mahitaji yote ya nishati,

kutoka asilimia hamsini kama ilivyo kuwa katika miaka ya sabini, hutegemea uingizaji huu.

Hiyo ndiyo sababu ya iliyoufanya ufanisi wa nishati na uzinduzi wa nishati endelevu kuwa

misingi mikuu ya Energiewende.

Watu nchini Ujerumani wameelewa kuhusu umuhimu wa ufanisi wa nishati katika miongo

kadhaa iliyopita. Changamoto ya kwanza ya dharura ya dunia ya mafuta ya mwaka wa 1973

ilikuwa kishawishi kikubwa. Iliwaathiri Wajerumani waliokuwa wakiyategemea mafuta

asili ya ardhini. Serikali ya Ujerumani iliingilia kati kwa kuzindua kampeni ya habari

kuhusu utunzaji wa nishati na kwa kuweka vikwazo vya uendaji mbio wa magari kwenye

barabara. Tangu wakati huo, sheria nyingine zimeweka mikakati ya ufanisi wa nishati na

© dpa/Jörg Carstensen © dpa/Westend61/Werner Dieter

1973

Vita ya Yom Kippur (Oktoba 1973) vilisababisha hali ya dharura ya mafuta duniani.

Ujerumani ilianzisha mikakati ya watu kuende kwa Jumapili nne bila kutumia gari ili kuokoa nishati.


Energiewende ya Ujerumani | 05

Viwango vilivyolengwa vya kupunguza

matumizi ya nishati Ujerumani

Viwango vilivyolengwa vya kupunguza matumizi ya kimsingi ya nishati

ikilinganishwa na mwaka wa 2008a

Uchumi unakua wakati matumizi ya nishati yanapungua

Ukuaji wa uchumi na matumizi msingi ya nishati

1,958 15,202

2,355

14,766

2,783

13,293

-20% -50% -7,6%

1990

2000

2015

2020 2050

Iliyofanikiwa

kufikia mwaka wa

2015

Jumla ya pato la taifa kwa mabilioni ya euro.

Zaidi ya asilimia 1.4 kila mwaka kwa wastani

tangu mwaka wa 1990.

Matumizi ya kimsingi ya nishati kwa petajouli

asilimia -0.5 kila mwaka kwa wastani tangu 1990.

"Kilowati bora zaidi ni ile ambayo hatuitumii"

Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Shirikisho

kuitekeleza kwa fanaka. Mikakati hii inajumuisha vipengele vitatu

muhimu: matumizi ya fedha yaliyolengwa, kutoa habari mwafaka na

mwongozo kuhusu matumizi ya nishati pamoja na kuweka malengo

thabiti ya kupunguza matumizi ya nishati.

Kwa sababu hii, maelfu ya washauri wa nishati hutekeleza ukaguzi

wa nishati kote nchini Ujerumani na huwaonyesha wapangaji, wenye

nyumba na mashirika njia bora za kuokoa nishati na pia huwaeleza

watu kuhusu mipango ya fedha ya nishati ya nchi.

Mkakati huu unazaa matunda – matumizi ya nishati Ujerumani

yamepungua tangu mwaka wa 1990 ingawa uchumi wake umekua

kwa kiwango kikubwa . Viwanda vya Ujerumani sasa vimepunguza

matumizi ya nishati kwa zaidi ya asilimia kumi ikilinganishwa na

matumizi ya awali lakini uzalishaji wake umeongezeka marudufu.

Maendeleo ya kiufundi huwezesha jamii na mashirika kutumia

nishati kwa ufanisi zaidi. Vifaa vya nyumbani vya stima sasa hutumia

chini ya asilimia 75 ya umeme vikilinganishwa na vifaa vya miaka

15 iliyopita. Mabadiliko katika desturi za kila siku pia huokoa nishati.

Nchi zote za Jumuiya ya Ulaya zimekubali kupunguza matumizi ya

kimsingi ya nishati kwa asilimia 20 kufikia mwaka wa 2020 na kwa

angalau asilimia 27 kufikia mwaka wa 2030. Ujerumani imejiwekea

azimio la kuyapunguza matumizi ya kimsingi ya nishati kwa asilimia

20 kufikia mwaka wa 2020. Iliongeza mikakati ya kuokoa nishati

kupitia Mpango wa Utendakazi wa Kitaifa wa Ufanisi wa Nishati wa

Desemba 2014. Kwa kutumia mikakati iliyowekewa jamii, viwanda,

biashara na usafiri, lengo ni kupunguza matumizi ya nishati kwa

asilimia 1.5 kila mwaka kufikia mwaka wa 2020.

Uongezeko mkumbwa wa ufanisi wa nishati

Jumla ya uzalishaji kutokana na gigajouli moja (GJ):

+63%

1 GJ

€128.80

1 GJ

€205.50

1990 2015


06 | Energiewende ya Ujerumani

Joto

Joto ya kupendeza,

endelevu na fanisi

Ufanisi wa Energiewende pia unategemea kukipunguza kiasi cha nishati inayohitajika

kupasha joto, kupunguza joto na kuchemsha maji katika majengo, na kiwango ambacho

nishati endelevu inatimiza matumizi mengineyo. Kupasha joto kunachukua zaidi ya nusu ya

nishati inayozalishwa nchini Ujerumani. Karibu theluthi mbili ya hii hutumika kupasha joto

na kuchemsha maji katika nyumba za jamii milioni 40 za nchi.

Kupunguza matumizi ya nishati

ya kupasha joto

Viwango vilivyolengwa vya kupunguza matumizi ya

nishati ya kupasha nyumba joto

Petajouli 1944

zilitumika na nyumba za jamii milioni 40 Ujerumani kwa matumizi ya kupasha

joto na maji moto mwaka wa 2013.

Hii ni sawa na:

-20% -11,1% 14% 13,2%

2020

Iliyofanikiwa Iliyofanikiwa

kufikia mwaka kufikia mwaka

wa 2015 2020 wa 2015

mafuta

Matumizi ya kupasha joto

(ikilinganishwa na 2008)

Kiwango cha nishati endelevu

katika matumizi ya kupasha joto

Lita bilioni 56

za mafuta.

Mara tano

ya matumizi ya nishati ya

sekta ya ndege Ujerumani.

Matumizi ya nishati ya

Uswidi

© dpa/Jacobs University Bremen © dpa

1975

Sheria ya Utoshelezaji wa Nishati iliongeza viwangu vya nishati ya akiba inayostahili kuwekwa

na kuweka kikomo rasmi cha kasi ya magari kwenye barabara za Ujerumani. Serikali ya

Ujerumani ilizindua kampeni ya mawasiliano kuhusu utunduizi wa nishati.


Energiewende ya Ujerumani | 07

Hiyo ndiyo sababu Serikali ya Ujerumani inataka kupunguza

matumizi ya nishati ya msingi kutoka mafuta na gesi katika majengo

kwa asilimia 80 kufikia mwaka wa 2050. Kutimiza lengo hili ni lazima

majengo yawe na utunduizi zaidi wa nishati, wakati nishati endelevu

inapochukua nafasi kubwa zaidi katika kupasha na kupunguza joto.

Lengo ni kuwa nishati endelevu itachukua asilimia 14 ya kupasha

na kupunguza joto kufikia mwaka wa 2020. Kwa njia hii, Ujerumani

inatimiza malengo ya Ulaya. Agizo la sasa la Umoja wa Ulaya kuhusu

utendakazi wa nishati katika majengo linaeleza kuwa majengo yote

mpya barani Ulaya lazima yawe "majengo yanayokaribia kujimudu

kinishati" kuanzia mwaka wa 2021.

Ujerumani iligundua kwa haraka kiwango cha nishati kinachoweza

kuokolewa katika majengo. Kitambo, kama mwaka wa 1976, Serikali

ya Ujerumani ilianza kutekeleza Sheria ya Kuokoa Nishati, Sheria ya

kwanza ya Kuhifadhi Joto kutokana na dharura ya mafuta. Vipengele

vyake vimeendelea kusasishwa mara kwa mara na kujumuisha

maendeleo katika ufundi. Chini ya Sheria ya Joto ya Nishati Endelevu,

imekuwa ni lazima nyumba zote mpya zisimamie kiwango cha

chini cha matumizi yake ya nishati kupitia nishati endelevu kuanzia

mwaka wa 2009. Hii inaweza kutimizwa kwa kutumia nishati ya

miale ya jua pamoja na bwela la gesi au mafuta au kuweka mfumo wa

kupasha joto wa nishati endelevu kama vile pampu ya joto au bwela la

vidonge.

Hata hivyo, asilimia 70 ya majengo ya makazi ya watu nchini

Ujerumani zimedumu kwa zaidi ya miaka 35 – kumaanisha kwamba

zilijengwa kabla ya Sheria ya kwanza ya Kuhifadhi Joto kutekelezwa.

Hii inamanisha kwamba majengo mengi hayajakingwa vilivyo na

mara nyingi hupashwa joto na mabwela yaliyozeeka na nishati

za ardhini kama vile mafuta na gesi. Nyumba ya jamii ya wastani

Ujerumani hutumia kama kilowati 145 kwa mita mraba ya nyumba

kila mwaka kupasha joto, sawa na lita 14.5 za mafuta. Nyumba mpya

fanisi zaidi zinahitaji asilimia kumi ya hiyo pekee. Matumizi ya

kimsingi ya nishati katika nyumba nzee yanaweza kupunguzwa kwa

asilimia 80 kwa kufanya marekebisho ya kuboresha njia za utunduizi

wa nishati na kuanza kutumia nishati endelevu. Yaani, pana haja ya

kuwapo kwa kinga ya baridi iliyo bora zaidi, vitu vipya vya ujenzi,

mifumo ya kisasa ya kupasha na kupunguza joto na teknolojia bora

ya kuyadhibiti matumizi ya nishati. Katika mwaka wa 2015 pekee,

karibu euro bilioni 53 zilitumika katika kufanikisha ufanisi wa

nishati. Serikali ya Ujerumani hutoa misaada na mikopo ya riba ya

chini kama vishawishi.

Ni kiasi gani cha nishati kinachotumika

katika majengo?

Viwango kamili vya matumizi ya nishati katika Ujerumani

Majengo mapya hutumia tuu asilimia kumi

Matumizi ya kupasha joto kwa jumla kila mwaka kwa lita kwa kila mita

mraba ya nyumba kwenye aina tofauti za majengo.

37.6 %

majengo

Majengo yasiyorekebishwa

lita 15 hadi 20

Majengo nzee yaliyo rekebishwa

lita 5 hadi 10

29.5 %

kupasha joto

5.5 %

kwa maji moto

2.6 %

kwa taa.

Majengo mapya

lita 7

Nyumba zisizopashwa joto

lita 1.5

1977

Serikali ya Ujerumani iliweka viwango vyake vya kwanza vya ufanisi wa nishati

majengoni katika Sheria yake ya Kukinga Baridi.


08 | Energiewende ya Ujerumani

"Mwisho wa enzi ya

mafuta umeanza."

Dieter Zetsche, Mkurungezi Mkuu, Daimler AG

© dpa/Paul Zinken

1979/1980

Vita vya Iran na Iraq vilisababisha hali ya

dharura ya pili ya mafuta duniani.

1984

Enercon ilizindua mtambo wa kwanza wa kisasa

wa upepo kutengenezwa kwa wingi Ujerumani.


Energiewende ya Ujerumani | 09

Usafiri kwa kutumia umeme

Kuendesha gari kwa

kutumia umeme

Magari ndiyo bidhaa muhimu sana ambayo Ujerumani huuza nje.

Sekta ya magari huajiri zaidi ya watu 750,000 hivyo kuifanya kuwa

moja kati ya sekta zinazoajiri watu wengi zaidi nchini. Wakati huo

huo, sekta ya usafiri hutumia kiwango kikubwa cha nishati, kama

theluthi moja ya matumizi ya jumla ya nishati nchini Ujerumani.

Hiyo ndiyo sababu Serikali ya Ujerumani inajizatiti kupunguza

matumizi ya nishati katika sekta hii.

Tayari yamekuwapo mafanikio ya kiwango fulani. Kwa mfano, idadi

ya kilomita ambazo magari ya kubeba bidhaa na wasafiri yanayoenda

kila mwaka iliongezeka karibu marudufu kati ya miaka ya 1990 na

2013 lakini matumizi ya mafuta yalipanda kwa asilimia tisa pekee

katika kipindi hiki.

Ili kutunza matumizi ya nishati zaidi, Ujerumani inategemea

teknolojia madhubuti ya magari na mpango wa kuanza kutumia

magari ya umeme katika siku zijazo, ukilenga magari, malori, mabasi

ya usafiri wa umma na pikipiki. Nchi inalenga kuwa soko kuu la

kimataifa ya usafiri kwa kutumia umeme kufikia mwaka wa 2020. Ili

kuyatimiza malengo haya, Serikali ya Ujerumani inakuza ubunifu wa

soko na teknolojia kupitia idadi kubwa ya mipango.

Magari yanayotumia nishati ya betri yanachukuliwa kama ongezo

muhimu kwa magari ya umeme wa betri. Miradi ya haidrojeni na

betri za nishati ilipangwa kupokea euro bilioni 1.4 kutoka kwa serikali

kufikia mwaka wa 2016. Basi zinazotumia mfumo unaojumuisha

haidrojeni tayari zinatumika kwenye usafiri wa umma katika mijini

mikubwa kadhaa ya Ujerumani.

Pamoja na mifumo ya uendeshaji magari inayotunza tabianchi,

mitindo mipya ya usafiri kama vile kushiriki gari sasa imeanza

kupata umaarufu. Kushiriki gari hupunguza idadi ya magari kwenye

barabara na hupunguza athari za mafuta ya gari. Watu milioni 1.2

kwa sasa wamesajiliwa katika mashirika 150 yanayotoa huduma za

kushiriki magari nchini Ujerumani.

Viwango vinavyolengwa na hatua zilizochukuliwa katika sekta ya usafiri nchini Ujerumani

Kupunguza matumizi ya mwisho ya nishati

+1%

-10%

Yaliyotimizwa kufikia

mwaka wa 2015

Mwaka wa 2020

(ukilinganishwa na

mwaka wa 2005)

Watu milioni 80.9

walikuwa wakiishi Ujerumani

Kusambaza usafiri kwa kutumia umeme

Ujerumani mwaka wa

2015

Magari milioni 61.5

yalikuwa yamesajiliwa Ujerumani

Kuongeza ufanisi wa nishati

Ni kiasi gani cha nishati kinachohitajika kuendesha gari kilomita 100?

100 km

66.1 megajouli

1990

100 km

35.6 megajouli

2013

Magari 25000

yanayotumia umeme

Usafiri kwa kutumia

umeme katika mwaka wa

2015

Mwaka wa 2020

Kiwango kinacholengwa cha

usafiri kwa kutumia umeme

Magari milioni 1

+

Magari 130400

yanayotumia mfumo wa

mchanganyiko

1986

Mkasa mbaya ulitokea katika tanuri ya Kiwanda cha Kuzalisha Nishati kupitia

Nyuklia, Chernobyl Ukraini.

Wizara ya Shirikisho ya Mazingira, Uhifadhi wa Viumbe na Usalama wa

Nyuklia ilizinduliwa nchini Ujerumani.

1986

Gari la kwanza linalotumia miale

ya jua lilipewa idhini ya kutumia

barabara nchini Ujerumani.


10 | Energiewende ya Ujerumani

Nishati endelevu

Umeme kutokana

na nguvu ya jua na upepo

Ubunifu wa nishati endelevu pamoja na ufanisi wa nishati ni nguzo ya Energiewende.

Nishati za upepo, miale ya jua, maji, mimea na mvuke ni vyanzo asili vya nishati ambazo

hazidhuru tabianchi na ambazo zinasaidia Ujerumani kutotegemea sana mafuta ya ardhini na

zinatekeleza wajibu muhimu katika utunzaji wa tabianchi.

© aleo solar AG/Flo Hagena

Matumizi ya nishati endelevu yameendelea sana katika sekta ya umeme. Tangu mwaka wa

2014 nishati endelevu imekuwa chanzo muhimu zaidi cha nishati katika mkusanyiko wa

nishati nchini Ujerumani, ikitoa theluthi moja ya nishati inayotumiwa nchini. Miaka kumi

awali, nishati endelevu ilichangia asilimia tisa tu ya mahitaji ya nishati. Ufanisi huu ulitokana

na kutengwa kwa fedha kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya nishati. Mchakato huu ulianza

mwaka wa 1991 na upitishaji wa Sheria ya Usambazaji Umeme kwenye Gridi, ambayo ilileta

viwango vya bei ya stima vya kudumu na ununuzi wa lazima kwa nia ya kufungua soko kwa

teknolojia mpya. Hii ilifuatwa na Sheria ya Vyanzo vya Nishati Endelevu ya mwaka wa 2000.

Sheria hii inavipengele vitatu muhimu: viwango vya bei vilivyodhaminiwa vya teknolojia

anuwai, usambazaji wa umeme kwenye gridi unaopewa kipaumbele, na mfumo wa gharama

za ziada unaowezesha gharama za ziada zinazotokea kugawanywa kwa watumiaji wote wa

umeme.

Nishati endelevu ndizo vyanzo muhimu sana

vya nishati katika mkusanyiko wa umeme

Kiwango cha nishati endelevu katika matumizi yote ya umeme

Upepo ndiwo unatoa umeme mwingi kutoka

vyanzo endelevu

Kiwango cha nishati endelevu mwaka wa 2015

3.4%

1990

6.2%

2000

17.0%

Nishati ya upepo

42.3%

Mimea na samadi

28.8%

2010

31.6%

2015

Fotovolti

20.7%

Umeme wa

nguvu za maji

10.1%

1987

Westküste, shamba la kwanza la kuzalisha umeme kupitia upepo,

lilizunduliwa. Lilikuwa na mitambo 30.


© dpa

Energiewende ya Ujerumani | 11

Nishati endelevu huimarisha uzalishaji wa nishati na utunzaji wa tabianchi

Viwango vinavyolengwa vya 2015

Wastani Viwanda vya uzalishaji umeme

milioni 1.6

kutokana na fedha za Sheria

ya Vyanzo vya Nishati Endelevu

Saa za terawati 196.2

za umeme uliozalishwa

sawa na kiwango cha umeme

unaozalishwa nchini Ukraini

Tani milioni 156 –

kwa usawa wa CO 2

zimeokolewa

sawa na jumla ya gesijoto iliyotolewa New Zealand, Ureno na Latvia mwaka wa 2013.

Tangu kupitishwa kwa Sheria ya Vyanzo Endelevu vya Nishati,

uwekezaji wa kila mwaka umekuwa ukipanda kila mara hasa katika

mashamba mapya ya umeme wa upepo, viwanda vya Fotovolti na pia

viwanda vya kuchoma makaa na gesi ya mimea. Kiwango kikubwa

cha matumizi ya nishati kimesababisha kuwapo kwa sekta mpya

iliyo na zaidi ya 330,000 za kazi nchini Ujerumani pekee. Imekuza

utengezaji fanisi kwa wingi wa teknolojia ya nishati endelevu hivyo

kuwezesha upungufu wa bei duniani kote. Kwa mfano, mfumo wa

miale ya jua katika mwaka wa 2014 uligharimu asilimia 75 chini ya

gharama yake ya miaka mitano mbeleni. Saa ya kilowati ya umeme

wa miale ya jua ilipokea sawa na senti za euro 50 za kuwekeza mwaka

wa 2000 - sasa inapokea kati ya senti saba na kumi na mbili za euro.

Ingawa Ulaya ya Kati inapata jua kwa kiasi cha wastani, nishati ya

miale ya jua imekuwa chanzo muhimu cha umeme nchini Ujerumani.

Mifumo ya fotovolti sasa inachangia zaidi ya asilimia 20 ya umeme

unaotokana na nishati endelevu.

Kwa sasa nguvu ya upepo ndiyo chanzo muhimu sana cha umeme wa

nishati endelevu. Umeme kutoka vinu vya upepo katika nchi kavu

sasa unagharimu kati ya senti za euro 4.7 na 8.4 kwa saa ya kilowati -

kwa wastani.

Changamoto kuu inayoikabili nchi ya Ujerumani ni kuendeleza

ukuaji wa nishati ya upepo na miale ya jua ili vyanzo hivi viendelee

kuwa nafuu na viongeze utoaji unaoweza kutegemewa zaidi. Hiyo

ndiyo sababu Serikali ya Ujerumani imepanga upya utoaji wa fedha

kwa nishati endelevu katika sekta ya umeme. Upanuzi unalenga

teknolojia nafuu za nishati ya upepo na miale ya jua. Upanuzi wa kila

mwaka wa teknolojia mahususi unafanya hali kuwa rahisi kupanga na

kuelekeza maendeleo ya nishati endelevu. Wasimamizi wa viwanda

vya nishati endelevu sasa wanalazimika kuuza kiwango cha ziada cha

umeme kwenye soko, kama wasimamizi wengine wa viwanda, hivyo

kuchukua jukumu zaidi la kufanikisha mfumo wa utoaji nishati.

Kufikia mwaka wa 2017, fedha zinaotolewa kwa viwanda vyote

vinavyozalisha zaidi ya kilowati 750 zimekokotolewa kupitia tenda za

teknolojia maalum. Hii inaathiri karibu asilimia 80 ya uzalishaji wa

kila mwaka. Pia kuna tofauti za kimaeneo katika uzalizaji wa nishati

Wakati kuna upungufu katika gridi ya umeme, viwango vya tenda

hupungua. Hatua hizi zitawezesha ufanisi wa nishati endelevu katika

sekta ya umeme kuendelea.

1990

Serikali ya Ujerumani ilizindua mpango wa mapaa elfu moja kusimamia

fedha za viwanda vya fotovolti (PV). Ujerumani ya Mashariki na Magharibi

ziliungana tena. Jopo la Kiserikali la Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC)

lilichapisha ripoti yake ya kwanza ya ukadiriaji kuhusu tabianchi duniani.

1991

Sheria ya Kusambaza Umeme kwenye Gridi inawalazimu

watoaji wote wa nishati nchini Ujerumani kununua

umeme unaozalishwa kutokana na nishati endelevu.


12 | Energiewende ya Ujerumani

Gharama

"Je, Energiewende itakuwa ghali

sana kwa raia wa Ujerumani?"

Hapana, mojawapo ya malengo ya Energiewende ni kuhakikisha kwamba kuna nishati nafuu

katika siku zijazo. Nguzo zake mbili, ufanisi wa nishati na ukuzaji wa uzalishaji wa nishati

endelevu zinalenga kupunguza utegemeaji wa uingizaji wa nishati, kuongeza uzalishaji wa

nishati unaohakikika na kuuwezesha uwekezaji wenye fanaka nchini Ujerumani.

Familia inatumia kiasi gani kwa nishati kila mwezi?

Ulinganishaji wa matumizi ya kila mwezi kati ya mwaka wa 2003 na 2013

Kupasha joto na maji moto

66

96

Kupasha joto na maji moto

Kupika

Taa na umeme

10

22

176

euro

260

euro

23

41

Kupika

Taa na umeme

Mafuta

78

100

Mafuta

2003 2013

Bei ya mafuta ghafi imepanda kwa kiasi kikubwa katika mwongo uliopita. Mwaka wa 2014

gharama ya mafuta ya kupasha joto ilipanda ikawa karibu marudufu nchini Ujerumani kuliko

ilivyokuwa miaka kumi mbeleni. Tokeo moja ni kuwa, mwaka wa 2013 watumiaji walitumia

asilimia nane ya nishati kwa matumizi yao ya kibinafsi ikilinganishwa na miaka ya mwisho

ya tisini ambapo walitumia chini ya asilimia sita. Kupasha joto, maji moto, kupika na mafuta

kutoka vyanzo vya nishati ya mafuta ardhini vinavyoingizwa ndivyo sehemu kubwa ya bili za

© dpa/Philipp Dimitri © dpa/McPHOTO‘s

1992

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira na Maendeleo

mjini Rio de Janeiro ulipitisha kanuni za maendeleo endelevu.


© dpa/Jens Büttner

Energiewende ya Ujerumani | 13

Familia nchini Ujerumani kwa jumla hutumia pesa ngapi kwa nishati?

Matumizi mwaka wa 2013 kwa mabilioni ya euro

€bilioni

127.5

47.0

11.4

20.2

48.8

Kupasha joto na maji moto

Kupika

Taa na umeme

Mafuta

familia za nishati nchini Ujerumani. Ingawa bei za mafuta zilishuka

mwisho wa mwaka wa 2014 na zikawa nafuu kwa watumiaji wa

mafuta nchini Ujerumani, hakuna anayeweza kuitegemea hali hii

katika siku zijazo kwa sababu bei na upatikanaji wa nishati ya mafuta

ardhini hutegemea siasa za kimataifa.

Ni kweli Energiewende ina gharama zinazotokea. Mabilioni ya euro

yamewekezwa ili kuzindua muundo msingi mpya wa nishati na

kuzifanikisha hatua za ufanisi wa nishati. Hii inamaanisha kwamba

uzinduzi wa nishati endelevu ulichangia katika ongezeko la jumla la

bei za umeme ambazo familia katika Ujerumani zimekuwa zikilipa

katika miaka ya hivi karibuni. Katika mwaka wa 2007, kwa wastani,

watumiaji wa umeme walilipa senti za euro 21 kwa kila saa ya kilowati

ya umeme. Sasa wanalipa kama senti za euro 29. Kwa kila saa ya

kilowati ya umeme, watumiaji wanashiriki bei ya ukuzaji wa nishati

endelevu kupitia gharama za ziada za Sheria ya Vyanzo Endelevu

vya Nishati. Kwa sasa gharama ya ziada ya umeme imepungua

chini ya senti za euro 6.9. Hata hivyo, kiasi ambacho umma unalipa

kinategemea vigezo mbalimbali vinavyotawala bei. Kwa mfano, bei

katika soko la umeme imeshuka kwa kiasi kikubwa kwa sababu

ya idadi inayoongezeka ya nishati endelevu sokoni. Ni muhimu

kutambua kwamba pamoja bei zote mbili zimekuwa zikipungua

polepole katika kipindi cha miaka minne iliyopita – bei ya ziada ya

Sheria ya Vyanzo Endelevu vya Nishati na bei ya soko la umeme. Kwa

sababu hiyo, bei za wastani za umeme kwa familia zimekuwa thabiti

katika kipindi hiki.

Pana haja ya wenyeji wa Ujerumani na wanaotegemea uchumi wake

kutopata ongezeko la gharama ya uchumi. Hili linawezekana tu

iwapo bei ya nishati itadhibitiwa ipasavyo. Bei ya nishati ikipanda

basi hata bei za bidhaa nyinginezo pia huathirika. Hali hii huchangia

kutokwepo kwa usawa wa kimashindano ya kibiashara miongoni

mwa mashirika mbalimbali yanayozalisha bidhaa hizo. Hiyo ndiyo

sababu Ujerumani imeachilia kampuni maalum zinazotumia nishati

kwa wingi kutolipa bei ya ziada ya Sheria ya Vyanzo Endelevu vya

Nishati. Hata hivyo, kampuni hizo zinazoruhusiwa kutogharamia bei

hiyo ya ziada lazima ziwekeze zaidi katika ufanisi wa nishati.

1994

Gari ya kwanza ya umeme ya kutengenezwa

kwa wingi inazinduliwa kwenye soko.

1995

Mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko

ya Tabianchi uliandaliwa Berlin, hivyo kuashiria mwanzo wa

mazungumzu ya kupunguza athari za gesijoto duniani kote.


14 | Energiewende ya Ujerumani

Utunzaji wa tabianchi

Kupunguza athari za gesijoto

Utunzaji wa tabianchi na Energiewende zinategemeana. Zote zinalenga kudhibiti athari za

mabadiliko ya tabianchi kwa watu, mazingira na uchumi kwa kiwango endelevu. Kutokana

na ukadiriaji wa Jopo la Kiserikali la Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC), ongezeko la joto duniani

lazima lidhibitiwe isije ikapita selsi 2 zaidi ya jinsi hali joto ilivyokuwa kitambo katika enzi

iliyotangulia kuanzishwa kwa viwanda duniani. Hii inamaanisha kwamba ni kiasi mahususi

tu cha gesijoto ambacho kinaweza kuwa hewani. Kwa vile anga ina asilimia 65 ya kiasi hiki,

juhudi kubwa za dunia na nchi za kupunguza athari za gesijoto zinahitajika.

Dayoksidi ya Kaboni, ambayo inasababishwa kwa kiwango kikubwa na uchomaji wa mafuta ya

ardhini ndiyo inayoathiri sana mabadiliko ya hewa. Nchini Ujerumani na duniani kote, zaidi

ya theluthi moja ya gesijoto hutokea kwenye viwanda vya kuzalisha nishati. Hii ndiyo sababu

tunashikilia kwamba matumizi ya nishati endelevu ni njia muhimu sana ya kutunza hewa.

Malengo ya tabianchi na hatua zilizochukuliwa

Upungufu wa gesijoto uliopangwa na uliotimizwa

Nani anatoa gesijoto?

Hesabu zote ni sawa na mamilioni ya tani za CO 2

mwaka wa 2014

Tarajio

la 2020

-20% -24,4%

Mafanikio

kufikia mwaka wa

2014

Ulaya

(EU-28)

Tarajio

la 2020

angalau

-40% -27%

Mafanikio

kufikia mwaka wa

2014

Ujerumani

Tani milioni 902

...

358

84

160

35

181

72

12

Sekta ya kawi

Nyumbani

Usafiri

Biashara, huduma

Viwanda

Ukulima

Nyingine

© dpa/Luftbild Bertram © dpa/MiS

1996

Ulaya iliamua kuachilia huru masoko yake ya gesi na umeme ambayo mbeleni yalikuwa ya kitaifa pekee.

Tume ya Ulaya ilichapisha mikakati yake ya kwanza ya pamoja ya Ulaya kuhusu uzalishaji wa nishati endelevu.


© iStock/ querbeet

Energiewende ya Ujerumani | 15

Ujerumani imepunguza utoaji wa gesijoto kwa kiwango gani?

Hesabu zote ni kwa kiwango sawa na mamilioni ya tani ya CO 2

1,250

1990

1,121

1995

1,046

2000

994

2005

910

2010

902

2014

Kwa kusahihisha Mkataba wa Kyoto (Kyoto Protocol) wa 1997,

Ujerumani ilikubali kupunguza gesijoto kwa asilimia 21 ikilinganishwa

na viwango vya 1990, kufikia mwaka wa 2012. Hatua muhimu

zilikuwa tayari zimechukuliwa. Kufikia mwaka wa 2014, Ujerumani

tayari ilikuwa imetimiza mahitaji ya kuweka punguzo la asilimia 27.7.

Uzalishaji wa thamana ya euro bilioni moja kutoka kwenye kampuni

za Ujerumani sasa hutoa tu nusu ya gesijoto iliyotoa mwaka wa 1990.

Ujerumani imepanga kuongeza juhudi zake na kupunguza gesijoto

kwa angalau asilimia 40 kufikia mwaka wa 2020. Lengo lake ni

kwamba, kufikia mwaka wa 2050 itakuwa imepunguza gesijoto

kwa kati ya asilimia 80 hadi 95 ikilinganishwa na viwango vya

1990. Lengo hili la kupunguza gesijoto ya taifa liko kwenye sera

za kulinda hewa ya Ulaya na ya kimataifa. Viongozi wa serikali za

Ulaya wameamua kupunguza utoaji wa gesijoto katika nchi zao

kwa asilimia 20 kufikia mwaka wa 2020 na angalau kwa asilimia 40

kufikia mwaka wa 2030. Nchi 195 zilisahihisha Mkataba wa Paris

mwezi wa Desemba 2015. Wakitumia viwango wanavyolenga vya

kubadilika kwa tabianchi, nchi hizi zinataka kudhibiti ongezeko la

joto duniani kwa kiwango kilichopungua selsi 2 katika karne hii.

Kampuni za kufanya biashara ya gesijoto ambazo zimechangia

pakubwa uchafuzi wa mazingira sasa zimepewa masharti ya kiasi

cha gesijoto zinaweza kuachilia hewani. Hii juhudi muhimu ya Ulaya

ya kupambana na kubadilika kwa tabianchi. Wote ambao hutoa

gesijoto kwa kiwango kikubwa lazima washiriki katika mfumo,

ambao unasimamia sehemu kubwa ya utoaji wa CO 2

kutoka viwanda

na sekta ya kawi. Kampuni lazima ziwe na kiwango walichokubaliwa

cha utoaji wa gesijoto kwa kila tani ya gesijoto ambayo kila mojawapo

ya kampuni hizo hutoa. Ikiwa kiwango walichokubaliwa hakitoshi

wanaweza kununua zaidi au kuwekeza katika teknolojia za kutunza

tabianchi. Hatua hii inazuia utoaji wa CO 2

mahali ambapo ni nafuu

zaidi. Lengo ni kupunguza utoaji wa gesijoto kwa asilimia 43 kufikia

mwaka wa 2030 ikilinganishwa na viwango vya mwaka wa 2005

katika sekta zote kwenye mfumo wa kuuza gesijoto.

Serikali ya Ujerumani imeanzisha Mpango wa Utendakazi wa

Tabianchi 2020 na Mpango wa Utendakazi wa Tabianchi 2050 ili

kuwezesha Ujerumani kutumiza malengo yake ya taifa ya kupunguza

gesijoto. Mpango wa Utendakazi wa Tabianchi unajumuisha mikakati

kadhaa ya kuboresha utunduizi wa nishati na kufanya usafiri,

viwanda na kilimo kuchunga tabianchi zaidi. Mpango wa Utendakazi

wa Tabianchi una malengo ya muda mrefu ya kupunguza CO 2

kwa

sekta maalum kama vile sekta ya nishati au viwanda.

1997

Mkataba wa Kyoto wa kupunguza gesijoto duniani ulipitishwa.

Tangu wakati huo, nchi 191 zimeutilia saini mkataba huo.


16 | Energiewende ya Ujerumani

Nishati ya nyuklia

Kusimamisha matumizi

ya nishati ya nyuklia

Matumizi ya nishati ya nyuklia kuzalisha umeme yamezua hisia kali nchi Ujerumani kwa

miongo kadhaa. Wajerumani wengi hawezi kukadiria kiwango cha hatari cha teknolojia.

Wana wasiwasi kuhusu athari inayoweza kutokea kwa watu na mazingira kutokana na

ajali kwenye matanuri ya nyuklia. Hofu ilithibitishwa na ajali iliyotokea mji wa Ukraini wa

Chernobyl mwaka wa 1986 ambayo ilichafua maeneo ya Ujerumani. Katika mwaka wa 2000,

Serikali ya Ujerumani iliamua kupiga marufuku matumizi ya nishati ya nyuklia kuzalisha

umeme na ikaamua kutumia vyanzo endelevu kuzalisha nishati. Makubaliano yaliyoafikiwa

na wamiliki wa viwanda vya nyuklia yaliweka muda wa makataa wa kutumika kwa viwanda

vya nyuklia na yakaupiga marufuku ujenzi wa viwanda mpya.

© dpa/Uli Deck

Mpango ulisasishwa mwaka wa 2010. Viwanda vilivyoko vingetumika kwa muda mfupi ili

kuziba pengo mpaka wakati ambapo nishati ya nyuklia ingeweza kusitishwa na nafasi yake

kuchukuliwa na nishati endelevu. Kutokana na ajali ya tanuri la nyuklia mjini Fukushima,

Japani, mwezi wa Machi 2011, Serikali ya Ujerumani iliubatilisha uamuzi huu.

Viwanda vya nishati ya nyuklia nchini Ujerumani zitafungwa lini?

Mpango wa kupunguza uzalishaji wa viwanda vya nishati ya nyuklia nchini Ujerumani kufikia mwisho wa mwaka wa 2022

Jumla ya uzalishaji wa viwanda vya nishati ya nyuklia

Fukushima

43%

Nov. 2003

Mei 2005

Ago. 2011

57%

Mei 2015

Des. 2017

Des. 2019

Des. 2021

Des. 2022

2000 2005 2010 2015 2020

1998

Ujerumani ilipitisha sheria ya kuyaachilia huru masoko yake ya gesi na umeme.


Energiewende ya Ujerumani | 17

© dpa/Jens Wolf

Viwanda vya nyuklia nchini

Ujerumani zinapatikana wapi?

Viwanda vilivyosimamishwa na vinavyotumika

Kiwango kikubwa kilichozalishwa kwa mwaka

Kiwango kikubwa cha umeme kilichozalishwa kwa mwaka kwa kipimo cha

saa za terawati (TWh)

Unterweser

2011

Lingen

1997

Philippsburg 1

2011

Emsland

2022

Mühlheim-Kärlich

2001

Biblis A + B

2011

Brunsbüttel

2011

Stade

2003

Obrigheim

2005

Brokdorf

2021

Krümmel

2011

Grohnde

2021

Würgassen

1994

Grafenrheinfeld

2015

Neckarwestheim 2

Philippsburg 2

2022

2019

Isar 1

Neckarwestheim 1

2011

2011

Gundremmingen B

2017

Isar 2

Gundremmingen C

2022

2021

Rheinsberg

1990

Greifswald

1990

Mwaka ambapo kiwanda kiliratibiwa

kusimamishwa

Mwaka ambapo kiwanda kilisimamishwa

Viwanda vilivyosimamishwa

Viwanda vinavyotumika

171 TWh

viwanda vyote vya nishati ya

nyuklia nchini Ujerumani mwaka wa

2001

196 TWh

nishati zote endelevu

mwaka wa

2015

Bunge la Ujerumani lilipitisha sheria ya kusimamisha matumizi ya

nishati ya nyuklia kuzalisha umeme haraka iwezekanavyo. Viwanda

kadhaa za umeme vililazimika kuusimamisha uzalishaji wa umeme

punde tu sheria hii ilipoanza kutumika. Matumizi ya viwanda

vilivyosalia yatakomeshwa kufikia mwisho wa mwaka wa 2022. Kwa sasa

viwanda vinane vya nyuklia bado vinatoa umeme nchini Ujerumani.

Mikakati inayohitajika ili kuondoa taka nururishi ya nyuklia pia

inaangazia changamoto zilizoko katika matumizi ya nishati ya

nyuklia. Ili kuwalinda watu pamoja na mazingira, uchafu huu lazima

uhifadhiwe kwa njia salama mbali na viumbehai kwa kipindi kirefu

sana. Wataalamu wanaamini njia bora ya kufanya hivyo ni kuuhifadhi

uchafu wa nyuklia chini kabisa kwenye miundo ya jiolojia.

Ujerumani haitaki kusafirisha nje taka zake nururishi. Lakini

kutafuta mahali mwafaka pa kuhifadhia taka hizi kunakumbwa na

matatizo kwani watu wanaoishi katika maeneo ya karibu na kampuni

hizo, kwa desturi, hupinga kuhifadhiwa kwa taka hizi maeneo

yanayoonekana kwamba ni mwafaka au maeneo yale yaliyokwisha

kukaguliwa kufikia sasa.

Hiyo ndiyo sababu Ujerumani sasa inachukua mwelekeo mpya.

Inahusisha matabaka yote ya jamii kwenye shughuli za utafutaji wa

maeneo mwafaka kwa njia ya kisayansi iliyo wazi. Lengo ni kupata

eneo la uhifadhi wa mwisho wa taka nururishi ya kiwango cha juu

kufikia mwaka wa 2031. Eneo linastahili kutoa usalama wa juu zaidi

kwa kipindi cha miaka milioni moja.

Tayari Ujerumani ina sehemu iliyopitisha kwa uhifadhi wa mwisho

wa chafu nururishi ya kiwango cha chini au wastani, eneo la

kuhifadhi la Konrad ambalo limeratibiwa kufunguliwa mwaka wa

2022.

2000

Tume ya Ulaya ilibuni mkakati wa kwanza wa pamoja wa nishati

endelevu, ufanisi wa nishati na ulinzi wa tabianchi bara la Ulaya.

Sheria ya Vyanzo Endelevu yaanza kutumika Ujerumani. Ikawa

ndiyo nguzo ya ukuzaji wa nishati endelevu nchini Ujerumani.

2000

Serikali ya Ujerumani iliamua kusitisha matumizi ya

nishati ya nyuklia. Viwanda vya nishati ya nyuklia

kuruhusiwa kutumika kwa hadi miaka 32 pekee


18 | Energiewende ya Ujerumani

© dpa/Jens Büttner

2002

Sheria ya kwanza ya Kutunza Nishati ilianza kutumika. Iliweka viwango

vya ufanisi wa jumla wa majengo mapya na majengo yaliyotumika.


Energiewende ya Ujerumani | 19

Ajira na uchumi

"Je, watu wengi hawatapoteza kazi

kwa sababu ya Energiewende?"

Uwekezaji wa juu kwenye aina zote za viwanda

vya nishati endelevu

Uwekezaji wa kila mwaka kwenye viwanda vya uzalishaji umeme nchini

Ujerumani kwa mabilioni ya euro

Kazi kutokana na nishati endelevu

Kazi nchini Ujerumani mwaka wa 2015

142,900

Nishati ya upepo

330,000

Kazi

113,200

42,200

Mimea na samadi

Nishati ya miale ya jua

4,.6

2000

27.3

2010

15.0

2015

17,300

6,700

Nishati ya mvuke

Umeme wa nguvu za maji

6,700

Utafiti

Energiewende ina athari kadhaa zenye manufaa. Inaendeleza

ubunifu, inapunguza gharama za uingizaji wa nishati kutoka katika

nchi za nje, inapunguza uchafuzi wa mazingira na utoaji wa gesijoto

na kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini Ujerumani.

Idadi kubwa ya mapato ya ukuzaji wa nishati endelevu na maboresho

ya nishati ya majengo yanasalia katika eneo la karibu kwa vile kazi ya

mikono inayohitajika kama vile kuweka na kuhifadhi inafanywa na

kampuni zinazopatikana katika eneo linalohusika.

Ukuzaji wa nishati endelevu na uwekezaji kwenye ufanisi wa nishati

unasababisha taaluma na kazi mpya kati sekta zitakazokua. Mikakati

ya ufanisi wa nishati iliyotekelezwa kwenye biashara, viwanda na

majengo pekee imesababisha kazi 400,000 mpya na uwekezaji kwenye

nishati endelevu umeongeza marudufu idadi ya wafanyakazi kwenye

sekta hiyo katika kipindi cha miaka kumi.

Baadhi ya kazi mpya zinachukua nafasi ya kazi kwenye viwanda

ambazo mafuta ya ardhini yana umuhimu mkubwa, hasa mafuta,

gesi na uchimbaji wa mawe ya makaa na pia uzalishaji wa umeme.

Kumekuwa pia na mabadiliko ya jumla ya utendakazi. Kwa mfano,

kuachilia huru masoko ya nishati ya Ulaya kumeongeza mashindano.

Hii inamaanisha kwamba kampuni hizo lazima ziwe bora zaidi katika

utendakazi wake. Mambo haya yote yanaleta mabadiliko kazini. Idadi

ya wafanyakazi katika sekta ya kawi ya desturi imepunguka katika

miaka ya hivi karibuni kutokana na hayo.

2003

Ulaya ilianza kutumia mfumo wa biashara

unao na uzito wa kisheria wa gesijoto.

2004

Sekta ya nishati endelevu iliwaajiri

watu 160,000 nchini Ujerumani.


20 | Energiewende ya Ujerumani

Mwendo wa dunia katika matumizi ya nishati endelevu

"Energiewende yaweza

kutekelezwa nchini Ujerumani

– lakini kwa nchi ambazo

uchumi wao si thabiti kama

Ujerumani, itakuwaje?"

© dpa/epa Business Wire

Energiewende si anasa lakini ni mradi ambao unaendeleza maendeleo endelevu na yenye faida

kwa kuzindua ubunifu, kukuza uchumi na kuzindua kazi katika sekta mbalimbali za siku zijazo.

Bei za teknolojia bunifu za nishati endelevu kama vile upepo, miale ya jua zimepungua kwa

kiwango kikubwa duniani kote katika miaka ya hivi karibuni. Uwekezaji katika utafiti na

ukuzaji wa hatua za kwanza na pia fedha za kusaidia nishati endelevu kupata pengo la soko

kwenye nchi tofauti zilizokomaa kiuchumi, hasa Ujerumani kulichangia pakubwa kushusha bei.

Zaidi ya nchi 140 zinataka kukuza nishati endelevu

Nchi zilizo na sera na malengo ya nishati endelevu

Zaidi ya njia moja ya usaidizi

Bei ya kusambaza umeme kwenye gridi/

malipo ya juu

Utoaji tenda

Kuhifadhi nishati ya kibinafsi

Ukosefu wa sera na data

Kutokana na kushuka kwa gharama za uwekezaji na kushuka kwa gharama za uendeshaji,

nishati endelevu sasa zaweza kupata soko bila usaidizi wa kifedha katika baadhi ya maeneo

duniani. Kwa mfano, mashamba ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo na viwanja

vikubwa vya umeme wa miale ya jua kule Amerika ya Kusini na Kaskazini zinatoa umeme

kwa bei nafuu zaidi kuliko viwanda vinavyotumia mafuta ya ardhini. Nchi kama vile Uchina,

Brazil, Afrika Kusini na India zinaongoza katika ukuzi wa nishati endelevu. Lakini ukuzi

2005

Biashara ya kununua na kuuza gesijoto

ilianza Ulaya. Nchi zote za Umoja wa

Ulaya zinashiriki katika mpango huu.

2007

Jumuiya ya Ulaya ilipitisha mswada wa tabianchi na nishati wa 2020 ulio na

makubaliano ya ukuzaji wa nishati endelevu, uhifadhi wa hewa na ufanisi wa nishati.

Louis Palmer alianza safari ya kuzunguka dunia kwa gari aina ya Solartaxi, gari

linaloendeshwa kwa nishati ya miale ya jua pekee. Safari yake ilichukua miezi 18.


Energiewende ya Ujerumani | 21

© dpa

Viwanda vingi vya nishati endelevu zinapatikana wapi duniani?

Uwezo wa viwanda kuzalisha umeme kufikia mwaka wa 2015

Mimea na samadi

1 | Marekani

2 | Uchina

1 | Uingereza

2 | Ujerumani

3 | Ujerumani Upepo kwenye 3 | Denmaki

bahari

Nishati ya mvuke

1 | Marekani

2 | Filipino

1 | Uchina

2 | Marekani

3 | Indonesia Upepo kwenye 3 | Ujerumani

nchi kavu

Umeme wa

nguvu za maji

1 | Uchina

1 | Uchina

2 | Brazil

2 | Ujerumani

3 | Marekani Fotovolti

3 | Japani

huu wakati mwingine unazuiwa na nchi kutoa ruzuku ya mafuta

ilikudumisha bei nafuu kwa wateja. Ruzuku hizi za karibu dola

bilioni 325 kila mwaka ni marudufu ya fedha zinatumika kukuza

nishati endelevu. Kama ruzuku hizi zingetumika kwenye mipango ya

kuboresha ufanisi wa nishati, fedha ambazo zingekuwako zingekuwa

mara tatu ya jinsi zilivyo sasa.

Kama vyanzo vya eneo, nishati endelevu hupunguza kutegemea kwa

kiwango uingizaji wa mafuta nchini na bei ya mafuta ya ardhini

isiyotabirika sokoni. Vyanzo hivyo pia vina nafasi muhimu ya kutimiza

ongezeko la matumizi ya nishati kwenye nchi zinazokomaa na

zinazoendelea bila kuongeza gesijoto au kuchafua mazingira ya eneo.

Katika maeneo yaliyo na miundu mbinu duni, ambapo umeme

unazalishwa na jenereta ghali za dizeli, nishati endelevu ndiyo njia

mbadala ambayo ni nafuu. Viwanda vya umeme wa miale ya jua na

mashamba ya kuzilisha umeme kupitia upepo zinaweza kujengwa

kwa haraka ikilinganishwa na vyanzo vingine na vinahitaji muda

mfupi wa kupangwa na kujengwa ikilinganishwa na viwanda vya

makaa ya mawe na nyuklia ambayo hujengwa kwa muda mrefu mno.

Nishati endelevu ghalibu huwa chanzo cha kwanza cha umeme kwa

watu. Hii ndiyo sababu nyingine nchi nyingi zimezundua mipango ya

misaada ya nishati endelevu.

Ujerumani inaunga mkono sera endelevu, bunifu na nafuu ya nishati

na inashiriki ufafanuzi kuhusu tajriba yake katika kufanikisha

mchakato wa Energiewende na nchi nyingine na hushirikiana

kwa karibu na majirani wake wa Ulaya na washirika wengineo wa

kimataifa. Ujerumani pia ina majukumu muhimu katika taasisi na

mashirika ya viwango mbali mbali. Pia ina makubaliano mengi ya

nishati na nchi kama vile India, Uchina, Afrika Kusini, Nigeria na

Algeria.

2008

Ujerumani ilizindua pasipoti ya nishati ya majengo ambayo inatoa habari

kuhusu matumizi ya nishati kwenye majengo na ufanisi wake.

Sheria ya Nishati Endelevu ya Joto iliamrisha kuwa kiwango fulani cha

kuzalisha joto lazima kitolewe na vyanzo endelevu katika majengo mapya.

2009

Shirika la Nishati Endelevu la Kimataifa

(IRENA) lilianzishwa na nchi 75.


22 | Energiewende ya Ujerumani

Gridi ya umeme

Gridi mahiri

© dpa/Stefan Sauer

Miundu msingi mipya na fanisi inahitajika ili kubadilisha mfumo wa nishati nchini

Ujerumani. Hii inamaanisha kwamba nyaya mpya za umeme na mifereji mipya ya gesi

lazima iwekwe na pia kuwapo kwa mabadili ya mfumo wa utoaji nishati kwa jumla. Wakati

viwanda vya nishati ya nyuklia nchini Ujerumani zitakapo fungwa, viwanda vya nishati

endelevu ziliopo hasa kaskazini na mashariki mwa Ujerumani vitajaza pengo hiyo. Nishati

hii inahitajika kusini mwa Ujerumani. Viwanda vingi vya nyuklia vinapatikana kusini

mwa Ujerumani, ambapo kuna watu wengi na mashirika makubwa ya viwanda. Njia mpya

za umeme zilizo na teknolojia mahususi na fanisi zitasafirisha umeme uliozalishwa na

mashamba ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo kaskazini na mashariki mwa Ujerumani

moja kwa moja hadi kusini.

Gridi ya umeme ya Ujerumani

ni kilomita milioni 1.8 kwa urefu

Gridi ya umeme inasambazwa wapi?

Nyaya mpya za umeme zilizopangiwa kuongezwa kwenye gridi

ya Ujerumani ya upeo wa volti ya umeme

BREMEN

KIEL

HAMBURG

SCHWERIN

Miradi iko katika hali ya kupangwa

Miradi imewasilishwa ili kupata idhini

Miradi imeidhinishwa au gridi kujengwa

Miradi iliyokamilika

HANNOVER

BERLIN

POTSDAM

MAGDEBURG

DÜSSELDORF

ERFURT

DRESDEN

WIESBADEN

Hii ni sawa na urefu wa mara

45

ya mizingo ya dunia kwenye ikweta.

MAINZ

SAARBRÜCKEN

STUTTGART

MÜNCHEN

Soko la ndani la nishati ya Ulaya ndiyo sababu ya pili iliyochangia kupanuliwa kwa gridi

nchini Ujerumani. Miundo msingi bora zaidi inahitajika katika nchi wanachama na nje ya

mipaka ili umeme uweze kusambazwa bila pingamizi kote katika Ulaya na umeme uwe nafuu

kwa watumiaji. Wasimamizi wa gridi za kusafirisha umeme barani Ulaya watoe mpango wa

pamoja wa kukuza gridi kila baada ya miaka miwili. Miradi yote ya Ujerumani imejumuishwa

katika mpango huu.

Wasimamizi wa Gridi nchini Ujerumani hufanya ukadiriaji wao wenyewe, kuangazia mbele

miaka 10 hadi 20 ili kubashiri ni nyaya gani za umeme zitakazohitajika na nchi. Mapendekezo

yao hukaguliwa na mamlaka ya nchi, Shirika la Shirikisho la Mtandao Umma hujumuishwa

vilivyo kwenye mchakato huu. Shirika hutumia njia ya majadiliano kufikia suluhisho bora ya

kutimiza mahitaji ya watu, mazingira na uchumi.

2009

Sheria ya Kupanua Gridi ya Umeme ilipitishwa ili kuuharakisha

mchakato wa kuidhinisha nyaya mpya za umeme wa volti ya juu.


Energiewende ya Ujerumani | 23

© dpa/euroluftbild.de/Hans Blossey

"Energiewende kwa Ujerumani ni kama mradi

wa kusafirisha mtu wa kwanza kwenye mwezi."

Frank-Walter Steinmeier, Waziri wa Shirikisho wa Mambo ya Nje, 2015

Gridi ya kusambaza pia inahitaji kusasishwa ili itumike kutoa nishati

endelevu. Awali ilipangiwa kusafirisha umeme kwa watumiaji

tu, inafanya kazi kama njia ya kuelekea upande mmoja. Lakini

sasa, karibu viwanda vyote vya miale ya jua na vinu vingine vya

upepo vinasambaza umeme kwenye gridi ya kusafirisha. Umeme

usiohitajika sasa unaelekezwa nyuma. Pia, umeme uliozalishwa kwa

nishati endelevu hubadilika kulingana na hali ya hewa. Viwanda vya

miale ya jua ni fanisi sana jua inapotokea lakini utoaji wake hupungua

sana wakati kuna mawingu. Gridi za kusafirisha umeme lazima

ziboreshwe. Zahitajika kuwa gridi mahiri ili ziendelee kuwa thabiti

hata wakati uzalishaji wa umeme unageuka. Kwenye gridi mahiri

kuna mawasiliano kati ya wahusika wote, hawa ni watu na mashirika

yanayo zalisha, safirisha, hifadhi na kusambaza au kutumia umeme.

Kuzalisha na kutumia basi kunaweza kusimamiwa kwa ufanisi zaidi

na kurekebishwa kwa muda mfupi.

Jinsi gridi mahiri inavyofanya kazi

Picha rahisi ya wahusika, miundo msingi na njia za mawasiliano

Mtandao wa kusafirisha,

gridi ya usambazaji

Kusimamia na kuwasiliana

Mita mahiri

Wazalishaji wa umeme

Nishati endelevu na nishati ya desturi

Watumiaji

Jamii, viwanda na biashara

Soko

Nishati, huduma na biashara

Njiani

Katika nchi jirani za

Umoja wa Ulaya

Usafiri

Magari, usafiri wa

umma wa eneo

Hifadhi

Betri, mifumo ya kuhifadhi

2010

Serikali ya Ujerumani ilipitisha Mbinu ya Nishati, mkakati wa muda mrefu wa

mahitaji ya nishati ya Ujerumani mpaka mwaka wa 2050. Umoja wa Ulaya

ulipitisha agizo la utendakazi wa nishati katika majengo. Kuanzia mwaka wa 2021,

majengo yote mapya yalihitajika kuwa "majengo yanayokaribia kujimudu kinishati".

2010

Shirika la Nishati ya Ujerumani (DENA) lilichapisha matokeo

ya utafiti kuhusu upanuzi wa gridi unaohitajika kwa nishati

endelevu kutoa karibu asilimia 40 ya umeme nchini Ujerumani.


24 | Energiewende ya Ujerumani

Usalama wa uzalishaji

"Je, uzalishaji waweza kukidhi

matumizi wakati umeme mwingi

unatokana na nishati ya upepo

na miale ya jua?"

© dpa/Moravic Jakub

Wajerumani waweza kutarajia kuwa na umeme wa kutosha katika siku zijazo. Uzalishaji wa

umeme nchini ni kati ya zile bora zaidi ulimwenguni. Kwa jumla ya muda wa saa 8760 kwa

mwaka, umeme unapotea kwa wastani wa dakika 13 pekee. Kwa upande mwingine, upoteaji

wa umeme umepunguka hata zaidi katika miaka ya hivi majuzi, iwapo kuwa kiwango

kinachoongezeka cha umeme kinazalishwa na upepo na miale ya jua.

Makatizo ya umeme ni nadra sana Ujerumani

Wastani wa muda wa makatizo ya umeme kwa dakika mwaka wa 2013

10,0 Lasembagi

11,3 Denmaki

12,7 Ujerumani (2015)

15,0 Uswizi

15,3 Ujerumani (2013)

23,0 Uholanzi

68,1 Ufaransa

70,8 Uswidi

254,9 Polandi

360,0 Malta

Makatizo ya umeme ni nadra sana kusababishwa na mabadiliko ya uzalishaji wa umeme. Sana

sana hutokea kwa sababu za nje au makosa ya watu. Hii ndiyo sababu iliyokuwepo wakati

wa katizo kubwa la umeme nchini Ujerumani mnamo Novemba 4 mwaka wa 2006. Katizo

hili la umeme ambalo lilidumu kwa karibu saa mbili lilisababishwa na katizo la kawaida

lililopangwa la nyaya ya stima. Hatua hii ilisababisha uongezeko mkumbwa wa umeme

kwenye nyaya nyingine ulioleta matokeo ya mfuatano kwenye gridi ya Ulaya. Tangu tokeo

hili, mikakati ya usalama nchini Ujerumani na nchi jirani za Ulaya imeboreshwa hata zaidi.

Kwa mfano, Ujerumani imeweka viwanda vya ziada vya nishati vya kudumu ili kuzuia

ukosefu. Viwanda hivi vinakuwa na umuhimu zaidi wakati wa miezi ya baridi pale matumizi

yanapokuwa ya juu zaidi na vinu vya upepo vya Ujerumani vinazalisha umeme zaidi. Iwepo

gridi za umeme zinazidiwa kwa sababu zinasafirisha kiwango kikubwa cha umeme kutoka

kaskazini hadi kusini mwa Ujerumani, viwanda hivi vya ziada vinakidhi matumizi kusini.

2011

Ajali kubwa ilitokea katika kiwanda cha nyuklia mjini Fukushima, Japani. Ujerumani iliamua kukomesha

matumizi ya nishati ya nyuklia kuzalisha umeme kufikia mwaka wa 2022, mbele ya ilivyopangwa awali.

Viwanda vinane nzee vyafungwa mara moja. Tume ya Ulaya ilichapisha Mpango wa Nishati wa mwaka

2050, mkakati wa kudumu wa kulinda tabianchi na uzalishaji wa nishati barani Ulaya.


Energiewende ya Ujerumani | 25

© dpa/euroluftbild.de/Hans Blossey

Nishati endelevu tayari zatoa zaidi ya asilimia 60 ya umeme nchini

Ujerumani katika saa maalum, na kiwango hiki kitaendelea

kuongezeka katika miaka ijayo. Nishati endelevu anuwai huweza

pia kutumiwa ili kujaliza pengo linaloachwa na mbinu nyingine.

Miradi ya majaribio imeonyesha kuwa kuchanganya uzalishaji wa

umeme kutoka aina mbali mbali za viwanda kunawezekana, hivyo

kuviwezesha kutoa umeme unaoweza kuaminika zaidi. Wakati

ambapo hakuna jua au upepo, viwanda badilifu vya nishati ya

kawaida vinajaza pengo. Viwanda vya gesi hufanya kazi vyema sana

wakati kama huo, lakini viwanda vya kuhifadhi nishati na viwanda

vya mimea na samadi vinaweza pia kutoa umeme kwa haraka. Lakini

mpango ni kwamba mifumo ya kuhifadhi nishati itajaza pengo

wakati wa vipindi kama hivyo katika siku zijazo.

Watumiaji wa umeme pia wana jukumu muhimu. Wanaweza kupewa

motisha ya kutumia umeme wakati uzalishaji ni mwingi kama wakati

wa upepo mwingi. Watumiaji wa kiwango cha juu - viwanda au

bohari baridi za kuhifadhi kwa mfano – wanaweza kupunguza mzigo

kwa mfumo wote kwa njia hii.

Changamoto kubwa ni namna ya kuleta mabadiliko katika soko la

umeme. Ujerumani imeanza mchakato wa mabadiliko kwenye sekta

hii na imetekeleza mikakati ya kwanza. Mabadiliko ni muhimu.

Washikadau kwenye soko la umeme lazima wajipange kukabiliana

na mabadilko ya umeme unaozalishwa na upepo na miale ya jua.

Wakati huo huo, lazima pia kuwe na mashindano kati ya machaguo

mbalimbali ili kudumisha bei nafuu.

Upanuzi wa gridi ya kimataifa na ushikanishaji wa masoko ambayo

awali yalikuwa ya kimaeneo barani Ulaya pia huchangia katika

kudhibiti machaguo mbalimbali nchini Ujerumani.

Uzalishaji wa umeme kutokana na nishati endelevu unabadilikaje?

Uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo vyote vya nishati na matumizi ya umeme nchini Ujerumani katika mwaka wa 2016.

100 GW

80 GW

kizazi na matumizi ya umeme

60 GW

40 GW

20 GW

0 GW

Januari 10 7 Februari Machi 6 Aprili 3 Mei 1

Januari 24 Februari 21 Machi 20 Aprili 17

Mei 29 Juni 26 Julai 24

Mei 15 Juni 12 Julai 10

Agosti 21 Septemba 18 Oktoba 16 Novemba 13 Desemba 11

Agosti 7 Septemba 4 Oktoba 2 Oktoba 30 Novemba 27

Desemba 25

Viwanda vya umeme vya kawaida

Jua Upepo Umeme wa nguvu za maji ya mto Mimea na samadi Matumizi ya umeme

2012

Mkataba wa Kyoto uliongezwa muda hadi 2020 katika

Mkutano wa Tabianchi wa Umoja wa Mataifa mjini Doha.


26 | Energiewende ya Ujerumani

Hifadhi

Nishati inayopatikana

© dpa/Hannibal Hanschke

Kufikia mwaka wa 2050, Ujerumani inataka kupata asilimia 80 ya umeme kutoka nishati

endelevu, hasa vinu vya upepo na mifumo ya fotovolti (PV). Mawingu yanapotea kwa ghafla

au upepo unapopunguka bila ilani, nchi inahitaji mfumo wa umeme ambao unaweza badilika

haraka kwa hali kama hizo. Mifumo ya kuhifadhi nishati inatoa suluhisho. Wakati kuna

upepo mwingi na miale ya jua ya kutosha, mifumo inaweza kuhifadhi umeme, ambao inaweza

kutumiwa wakati kuna upungufu wa nishati, giza au anga yenye mawingu.

Kuhifadhi nyumbani: betri

Mchanganyo wa mfumo wa fotovolti (PV) na betri kwa matumizi

ya binafsi na ya kusambaza kwenye gridi.

Hifadhi ya kujazwa: kwa kutumia mabwawa asili

Picha ya mfumo wa hifadhi ya kujazwa

Bwawa la juu

Mfumo wa fotovolti (PV)

Injini /

jenereta

Transforma

1.

2.

Hifadhi ya betri

Mtambo wa pampu

Bwawa la chini

Kujizalishia mwenyewe:

matumizi ya moja kwa

moja ya umeme kutokana

na miale ya jua au betri

Usambazaji wa umeme

usiotumika kwenye gridi

1.

Kuhifadhi nishati

Umeme (wa kupindukia) huendesha mitambo.

Maji huelekezwa kwenye bwawa la juu.

2.

Kuachilia nishati iliyohifadhiwa

Maji hutiririka chini na kuendesha tabo.

Tabo huzalisha umeme na kuusambaza kwenye gridi

Mifumo 32000 ya kuhifadhi nishati kwenye betri inatumika

Uwezo wa kuzalisha GW 9.2; uwezo wa GW 4.5 unaongezwa

Kuna njia nyingi za kuhifadhi. Njia za kuhifadhi nishati kwa muda mfupi, kama vile kwa

kutumia betri, kapasita na mifumo ya gurudumu tegemeo, ni njia ambazo zinaweza kutumiwa

kupokea na kutoa nishati ya umeme mara kadhaa kwa siku lakini uwezo wake ni mdogo.

Ujerumani hutumia hasa viwanda vya kuhifadhi vilivyojazwa ili kuhifadhi umeme kwa muda

mrefu zaidi. Viwanda hivi, baadhi yao ambayo yuko Lasembagi na Austria, kwa sasa vina

uwezo wa karibu gigawati 9 zilizounganishwa kwenye gridi ya Ujerumani. Ingawa hii imeipa

Ujerumani hifadhi kubwa zaidi ya kujazwa katika Umoja wa Ulaya, kuna uwezekano mdogo

tu wa upanuzi. Hivyo, Ujerumani inashirikiana kwa karibu na nchi ambazo zina uwezo

mkubwa wa kuhifadhi. Austria, Uswizi na Norwe ndizo nchini muhumu zaidi.

2013

Ujerumani ilipitisha Sheria ya kwanza ya Mpango wa Mahitaji ya

Shirikisho kuhusu upanuzi muhimu wa mtandao wa kusafirisha umeme.

Gari la kwanza lililobuniwa kwa matumizi ya umeme pekee lilianza

kutengenezwa kwa wingi Ujerumani.

2013

Kiwanda cha kwanza kikubwa

cha kugeuza nishati kuwa gesi

kilianza kutumika Ujerumani.


Energiewende ya Ujerumani | 27

© Paul Langrock

Hifadhi ya hewa iliyobanwa ni chaguo lingine la kuhifadhi nishati

kwa muda mrefu zaidi. Inatumia nishati isiyotumika kubana hewa

kwenye nafasi chini ya ardhi kama mapangoni katika makuba ya

chumvi. Ikihitajika, hewa iliyobanwa inaendesha jenereta, hivyo

kuzalisha umeme.

Kugeuza nishati kuwa katika hali ya gesi ni njia mpya ya kuhifadhi

nishati kwa muda mrefu. Mbinu hii inatumia mchakato wa

elektrolisisi mbapo umeme hugeuzwa kutoka katika hali ya nishati

endelevu kuwa haidrojeni au gesi asili sanisi. Manufaa ya mbinu hii

ni kuwa haidrojeni na gesi asili zinaweza kuhifadhiwa, kutumiwa

mara moja au kusambazwa kwenye gridi ya gesi ya asili. Gesi hizi ni

rahisi kusafirisha na zinaweza kutumika kwa njia nyingi. Viwanda

vya nishati vinaweza kuzirejesha kuwa umeme na joto kama

inavyohitajika, na watumiaji wanaweza kuzitumia kupika, kupasha

joto au kuendesha gari.

Lakini mifumo mingi ya kuhifadhi nishati bado ni ghali mno, kwa

hivyo Serikali ya Ujerumani inarahisisha utafiti na maendeleo

kwenye suala hili. Katika mwaka wa 2011, serikali ilizindua

mkakati wa kuwekeza kwenye hifadhi. Tangu mwaka wa 2013, pia

imekuwa ikiwekeza kwenye mifumo midogo anuwai ya kuhifadhi

inayohusiana na fotovolti (PV). Kurekebisha upungufu mdogo kwa

haraka kwenye gridi ya umeme ni njia mpya ya kutumia betri.

Uzinduzi kwenye soko wa mifumo hii ya betri utaendeleza utafiti na

ubunifu na kupunguza gharama.

Hata hivyo, wataalamu wanasema matumizi ya mifumo mipya ya

kuhifadhi mwanzoni yatakuwa machache. Gharama nafuu za mifumo

ya teknolojia zote za kuhifadhi zitapatikana tu baadaye wakati nishati

endelevu zitakapo kuwa sehemu kubwa ya uzalishaji nishati. Katika

muda mfupi au muda wa kati, machaguo mengineyo ndiyo afadhali kwa

kuwa ni nafuu zaidi. Machaguo haya yanajumuisha upanuzi wa gridi au

kudhibiti uzalishaji na matumizi ili kutumia nishati kwa ufanisi.

Kugeuza umeme kuwa gesi

Kwa kutumia elektrolisisi na kutengeneza methani; matumizi yanayoweza kutokea

Uzalishaji wa kupindukia

wa nishati endelevu

ELEKTROLISISI

KUTENGENEZA METHANI

H 2

CH 4

H 2

H 2

Mtandao wa gesi asili

Mifumo ya kuhifadhi gesi

Matumizi ya viwanda Usafiri

Uzalishaji umeme Utoaji joto

Miradi 15 ya majaribio inayoendelea; miradi 6 inayojengwa au iliyopangwa

2014

Ujerumani ilibadilisha Sheria ya Vyanzo Endelevu vya Nishati. Sheria sasa inajumuisha malengo ya ukuzaji wa kila mwaka na inalazimisha ushirikiano

kwa soko. Umoja wa Ulaya ulikubaliana kuhusu malengo ya nishati na tabianchi kufikia mwaka wa 2030: kupunguza viwango vya gesijoto kwa asilimia

40, kuongeza kiwango cha nishati endelevu kuwa angalau asilimia 27 na kupunguza matumizi ya nishati kwa angalau asilimia 27. Ujerumani ilipitisha

Mpango wa Utendakazi wa Taifa wa Ufanisi wa Nishati na ilizindua Mpango wa Utendakazi wa Tabianchi wa 2020. Zikiwa na kiwango cha asilimia 27.4

katika uzalishaji wa umeme, nishati endelevu zakuwa chanzo muhimu zaidi cha nishati nchini Ujerumani kwa mara ya kwanza.


28 | Energiewende ya Ujerumani

Raia na Energiewende

"Je, raia watanufaikaje kutoka

Energiewende?"

Energiewende inaweza tu kufanikiwa ikiwa inaungwa mkono na umma – hii itaiwezesha sana

nishati kuendelea kuwa nafuu kwa wateja. Umma pia itanufaika moja kwa moja kutokana na

urekebishaji wa uzalishaji wa nishati. Watu wengi hutafuta ushauri kuhusu jinsi ya kuitunza

nishati nyingi zaidi nyumbani mwao.

Watu wanaobadilisha mfumo wa zamani wa kupasha joto au wanaofanya marekebisho ya

kuwezesha utunduizi wa nishati hufaidika na mikopo ya riba ya chini na misaada ya serikali.

Wale ambao wanatafuta fleti ya kukodisha hupokea habari kiotomatiki kuhusu kiwango cha

nishati inayotumia na gharama zake. Na wakitaka kununua mashine mpya ya kufua nguo,

kompyuta au taa, lebo inawaonyesha ukadiriaji wa utunduizi wa nishati wa bidhaa.

Ni viwanda vingapi vinavyomilikiwa na umma?

Uwezo wa kuzalisha nishati unaopatikana kwa vikundi vya wamiliki kwa asilimia.

46.6%

Raia

(wamiliki binafsi 25.2%; mashirika ya ushirika ya

nishati 9.2%; uwekezaji wa umma 11.6%)

12.5%

Wazalishaji nishati

41.5%

Wawekezaji

(wawekezaji wa mashirika na wawekezaji wakubwa)

© dpa/Westend61/Tom Chance © dpa/Bodo Marks

2015

Tume ya Ulaya iliwazilisha mkakati wa mpango wa kuunganisha nishati. Hatua hii ililenga sehemu tano: usalama wa

uzalishaji, soko la nishati la ndani lililounganishwa kabisa, ufanisi wa nishati, kuondelea uchumi kaboni na utafiti wa nishati.

Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Umoja wa Mataifa wakutana mjini Paris, ambapo nchi 195 zinakubaliana kuzuia

ongezeko la joto duniani kwa zaidi ya selsi 2.


dpa/Marc Ollivier

Energiewende ya Ujerumani | 29

Umma pia inahusika kwenye sekta ya desturi ya nishati. Umeme

na joto hasizalishwi tu na wazalishaji wadogo na wakubwa lakini

pia raia ambao wana paneli zao za miale ya jua na wanaowekeza

kwenye mashamba ya kuzalisha umeme kupitia upepo na viwanda

vya kutengeneza gesi kutoka mimea na samadi. Mifumo mingi ya

fotovolti (PV) kati ya milioni 1.5 iliyowekwa Ujerumani iko kwenye

paa za nyumba za watu. Raia wamewekeza kwenye karibu nusu ya

tabo za upepo nchini Ujerumani na karibu nusu ya uwekezaji kwenye

nishati ya mimea na samadi inafanywa na wakulima.

Wale ambao hawawezi kuweka au kulipia teknolojia yao binafsi ya

nishati endelevu wanaweza kuungana na watu wengine. Karibu

mashirika 900 ya nishati yaliyo na wanachama zaidi ya 160,000

yanawekeza kwenye miradi ya Energiewende. Uwekezaji huanzia euro

100 pekee.

Zaidi ya hayo inapokuja kwa mambo halisi ya Energiewende, raia

wanachama wanaweza kutoa maoni. Kwa mfano wanaweza kueleza

hisia na mapendekezo yao wakati shamba mpya la kuzalisha umeme

kupitia upepo linapangwa kwenye eneo lao. Umma hutekeleza

jukumu kubwa kwenye majadiliano kuhusu mipango ya nyaya

za kusafirisha umeme ambazo zitasafirisha kiwango kikubwa

cha umeme kote nchini Ujerumani. Raia wanakaribishwa katika

mazungumzu kutoka mwanzo wakati mahitaji ya upanuzi wa gridi

yanapo kadiriwa ili kutoa maoni yao. Pia wanashiriki katika hatua

nyingine zote za mipango ikiwa ni pamoja na uamuzi wa njia halisi

ambayo nyaya ya kusafirisha umeme itapitia. Mbali na hayo, raia

hupokea habari za kina kuhusu miradi ya kusafirisha umeme kutoka

Shirika la Mtandao la Shirikisho na wasimamizi wa gridi kabla ya

mikakati rasmi.

Shughuli hizi zina ungwa mkono na juhudi ya Mazungumzu ya

Umma kuhusu Gridi ya Umeme ambayo ina ofisi za maeneo na

ambayo huwa na matukio ya umma kwenye maeneo ambayo miradi

ya upanuzi imepangwa. Pia inakuwa kama pahali pa marejeo ya

mambo yote kuhusu upanuzi wa gridi. Kwa kuanza majadiliano

katika hatua za kwanza, ni rahisi zaidi kutekeleza miradi ya nishati na

kuongeza ukubalifu wa miradi na umma.

Je, watu wanawezaje kunufaika nyumbani na Energiewende?

Machaguo ya mbinu za utunduizaji wa nishati na matumizi ya nishati endelevu kwenye nyumba iliyojengwa

miaka ya sabini

Punguzo la nishati la -13%

kukinga paa dhidi ya baridi

60-70% ya umeme wa matumizi binafsi

mfumo wa fotovolti (PV) ulio na hifadhi ya betri

Punguzo la nishati la -10%

glasi tatu za dirisha

Punguzo la -22% la nishati

kukiga ukuta wa nje dhidi ya baridi

Punguzo la nishati la -80%

balbu za LED badala ya balbu za kawaida

Punguzo la -5% la nishati

kinga ya dari dhidi ya baridi

Punguzo la -15% la nishati

uboreshaji wa mfumo wa kupasha joto

100% ya joto ya matumizi binafsi

bomba ya joto ya kupasha joto na maji moto

2016

Mkataba wa Tabianchi wa Paris ulianza kutekelezwa Novemba 4 baada

ya kuidhinishwa na mabunge ya nchi 55 za kwanza.

Ujerumani yaboresha msaada kwa nishati endelevu. Kufikia mwaka wa

2017, mialiko ya tenda kupitia kwa njia zote za teknolojia imetolewa.


30 | Energiewende ya Ujerumani

Faharasa

Ada ya kusambaza kwenye gridi

Ada ya kusambaza kwenye gridi

Sheria ya Vyanzo Endelevu vya Nishati

inawadhaminia wasimamizi wa viwanda

vya nishati vinavyotumia miale ya jua au

upepo ada ya chini ya umeme wanaozalisha

katika kipindi mahususi. Tarehe inayotumika

kuamua ada ni mwaka ule kiwanda cha nishati

kinapozinduliwa. Ada hushuka kila mwaka

vile teknolojia inavyoboreka na matumizi pana

ya teknolojia husaidia gharama za uwekezaji

kushuka kila wakati. Nchini Ujerumani

utaratibu wa mnada (Angalia Mnada)

utachukua mahali pa ada za sasa za kudumu za

kusambaza kwenye gridi katika miaka ijayo.

Ada ya ziada ya Sheria ya Vyanzo Endelevu vya

Nishati / mfumo wa ada ya ziada

Watumiaji wote nchini Ujerumani husimamia

ada za ziada za nishati inayozalishwa kutokana

na vyanzo endelevu vya nishati kupitia ada ya

ziada ya bei ya umeme, kwa mujibu wa Sheria

ya Vyanzo Endelevu vya Nishati. Kiwango cha

ada ya ziada hutokea katika utofauti kati ya

ada zinazolipwa wasimamizi na mapato kutoka

mauzo ya umeme kwenye soko la nishati.

Biashara zilizo na mahitaji makubwa ya umeme

hazilipishwi ada ya ziada kamili.

Betri

Betri ni vifaa vya kielektro-kemikali vya

kuhifadhi nishati. Zikiunganishwa na mzunguko

umeme, zinaachilia chaji na umeme unapita.

Betri zinazowekwa chaji upya hutumika kwenye

bidhaa kama vile simu za mkononi na magari

yanayotumia umeme. Betri zinazowekwa chaji

upya zinatumika pamoja na vyanzo endelevu ya

nishati, kwa mfano kwenye miradi ya fotovolti

(PV). Hapa zinarejelewa kama mifumo ya betri

ya kuhifadhi. Betri zaweza kuhifadhi tu kiasi

kidogo cha chaji ya umeme, kulingana na uwezo

wao (unaopimwa kwa saa za ampea – ah).

Betri za nishati

Betri za nishati ni viwanda vidogo sana vya

nishati ambavyo hugeuza nishati ya kemikali

kuwa nishati ya umeme, hivyo kuzalisha

umeme. Zinatumika kwa mfano kuyaendesha

magari ya umeme au kwenye maeneo

ambayo hayajaunganishwa kwenye gridi ya

umeme. Nyenzo zinazohitajika ni haidrojeni

na oksijeni pekee. Mfumo huu wa kuzalisha

nishati hausababishi gesijoto, mbali mvuke

tu. Haidrojeni inayohitajika kuzalisha nishati

yaweza kutengenezwa kwa umeme kutoka

vyanzo vya nishati endelevu (angalia nishati

hadi gesi) Lakini betri za nishati ambazo

hutumia nyenzo tofauti kama vile methanol pia

ziko.

Biashara ya kununua na kuuza gesijoto

Barani Ulaya CO 2

inathamana ya soko. Sekta

ya nishati na viwanda vikubwa lazima zitoe

hati kwa kila tani ya gesijoto wanayosababisha.

Ikiwa hawana hati za kutosha inawabidi

kununua kwenye soko maalum. Wakipunguza

gesijoto wanayosababisha, wanaweza kuuza

hati wasizohitaji. Kwa kuwa idadi ya hati

zinazopatikana kile mwaka zinapunguka,

mashirika yana kishawishi cha kuwekeza

kwenye mikakati ya kuokoa nishati au kutumia

vyanzo vingine vya nishati ambavyo havidhuru

mazingira sana.

Gesijoto

Gesijoto hubadilisha hewa ya anga kwa njia

ambayo mwanga unaoakisiwa kutoka dunia

haurudi angani lakini huakisiwa na hewa ya

anga kwenye dunia, hivyo kuchangia kwa

kiwango kwa ongezeko la joto duniani. Athari

hii ni sawa na nyumba ya kioo na hupasha dunia

joto. Gesijoto inayajulikana sana ni dayoksidi ya

kaboni, ambayo husababishwa hasa kutokana

na kuchomwa kwa mafuta ya ardhini kama

vile mafuta, gesi na makaa ya mawe. Gesijoto

zingine ni pamoja na methani na CFC.

Gridi ya umeme – gridi ya upeo wa volti – gridi

ya kusafirisha

Gridi ya umeme ndiyo mbinu ya kusafirisha

umeme. Nchini Ujerumani na nchi zingine

nyingi gridi huwa na viwango vinne ambavyo

hutumiwa na volti tofauti: volti ya juu kabisa

(220 au 380 kV), volti ya juu (60 kV hadi 220 kV),

volti ya wastani (6 hadi 60 kV) na volti ya chini

(230 au 400 V). Gridi ya volti ya chini hutumikia

wapokeaji kama vile nyumba binafsi. Mitandao

ya volti ya upeo hutumia volti iliyo karibu mara

1000 zaidi na husafirisha kiwango kikubwa cha

umeme kwa masafa marefu. Mitandao ya volti

ya juu husambaza umeme hadi mitandao ya

wastani au mitandao ya chini. Mitandao ya volti

ya wastani husambaza umeme zaidi lakini pia

hutumikia wateja wakubwa kama vile viwanda

na hospitali. Nyumba binafsi hupokea umeme

wao kutoka gridi ya volti ya chini.

Gridi mahiri

Gridi mahiri ni mtandao wa usafirishaji

ambapo vipande vyote huwasiliana na

vingine, kuanzia wazalishaji, kupitia nyaya na

mifumo ya kuhifadhi hadi kwa mtumiaji. Hii

hutokea kupitia usambazaji wa kiotomatiki

wa data za kidijitali. Mawasiliano ya haraka

husaidia kuepusha vikwazo na uzalishaji wa

kupindukia wa umeme na kusawazisha nishati

inayozalishwa na mahitaji ya washikadau.


Energiewende ya Ujerumani | 31

Usambazaji wa umeme wa nishati endelevu

unaobadilika hasa unahitaji suluhisho kama

hii. Na wakati huo huo gridi mahari huwezesha

udhibiti wa mahitaji kwa njia ya mifumo

inayobadilika ya ada za umeme.

Hifadhi ya hewa iliyobanwa

Hifadhi ya hewa iliyobanwa hutumia nishati ya

umeme kuhifadhi hewa kwa kutumia shinikizo

kwenye mfumo wa mapango chini ya ardhi.

Hewa iliyobanwa yaweza kuachiliwa kama

inavyohitajika kupitia tabo, hivyo kuzalisha

nishati. Teknolojia hii haijatumiwa sana kufikia

sasa. Lakini inaonekana kama njia inayoweza

kutumika kuhifadhi nishati isiyotumika

iliyozalishwa na vyanzo endelevu vya nishati.

Mapango ya chumvi yaliyorekebishwa

yasiyopitisha hewa yanachukuliwa kuwa pahali

salama pa kuhifadhia nishati. Ujenzi huu una

changamoto za kijiolojia ambazo zinabidi

kutatuliwa. Kwa sababu mfumo ukipatikana

ukiwa na kasoro hauwezi kurekebishwa.

Vile vile ni muhimu mkazo wa mawe

yanayozunguka usiathiriwe.

Hifadhi ya kujazwa

Hifadhi ya kujazwa au viwanda vya hifadhi

ya kujazwa ni njia ambayo imejaribiwa na

kutumiwa katika kuhifadhi nishati. Nishati

isiyotumika kwenye gridi inatumika kusafarisha

maji kwenye bwawa la juu. Nishati ya ziada

ikihitajika, maji huachiliwa ili kuendesha tabu

ambayo huzalisha umeme.

Jengo linalokaribia kujimudu kinishati

Majengo yanayokaribia kujimudu kinishati

yanaashiria majengo yanayotumia nishati

ndogo sana. Kuanzia mwaka wa 2021, majengo

yote mpya katika Jumuiya ya Ulaya lazima

yatafuata kiwango kilichowekwa. Kanuni

zinalenga majengo ya umma kuanzia mwaka

wa 2019. Nchini Ujerumani matumizi ya msingi

ya nishati ya majengo kama hayo hayastahili

kupita 40 kWh kwa mita mraba kwa mwaka.

Jumla ya matumizi ya umeme

Kuhesabu matumizi ya jumla ya umeme katika

nchi, umeme unaozalishwa kwenye nchi na umeme

unaoingizwa kutoka nje hujumlishwa. Umeme

unaouzwa nje hutolewa kutoka hesabu hii.

Umeme unaozalishwa nchini

+ umeme unaoingizwa

- umeme unaouzwa nje

----------------------------------------------

= Jumla ya matumizi ya umeme

Kapasita

Kapasita zinaweza kuhifadhi umeme kwa muda

mfupi. Kapasita ina vipande viwili kama vile

sahani na mipira ya chuma. Kipande kimoja kina

chaji chanya na kipande kingine hasi. Vipande

hivi viwili vikiunganishwa, umeme husafirishwa

mpaka chaji zinaposawazika.

Kilimbikizi umeme cha gurudumu tegemeo

Kilimbikizi umeme cha gurudumu tegemeo

Vilimbikiza umeme vya magurudumu tegemeo

vinaweza kuhifadhi umeme usiotumika kwenye

gridi kwa muda mfupi. Nishati ya umeme

huhifadhiwa kimashine. Mota ya umeme

huendesha gurudumu tegemeo. Nishati ya

umeme hugeuzwa kuwa nishati ya kuzunguka.

Kuirejesha, gurudumu huendesha mota ya

stima inapo hitajika. Kama betri, gurudumu

tegemeo zinafaa kwa ujenzi wa vipande. Ufundi

wa msingi umefahamika tangu Enzi za Kati hata

kama haukuhusishwa na nishati ya umeme enzi

hizo. Magurudumu haya tegemeo yamebuniwa

kwa ajili ya kuhifadhi nishati kwa muda mfupi

wakati wa uzalishaji mwingi. Nishati ambayo

inaweza kurejeshwa haraka kwenye gridi.

Kiwanda cha nishati ya dharura

Viwanda vya nishati ya dharura hutumika

wakati vizuizi vinapotokea kwenye usafirishaji

wa umeme. Kwa vile vinastahili kuwashwa na

kuzimwa kwa haraka, viwanda vya gesi ndivyo

vinavyofaa zaidi kwa madhumuni haya.

Kiwango cha ufanisi wa nishati

Kiwango cha ufanisi wa nishati huashiria

thamani inayotokea (kiwango cha thamani

ya huduma na bidhaa zinazopatikana katika

nchi kila mwaka) kwa kila kitengo cha nishati

kinachotumika. Katika uchumi, nishati ya

msingi ndiyo inayotumika kama kigezo cha

hesabu.

Kushiriki gari

Kushiriki gari ni hali ya watu kadhaa kutumia

gari moja kusafiri. Kwa sababu hii, kwa

kawaida, hawa huwa wateja wa kampuni

inayomiliki magari hayo. Wakihitaji gari,

wanaweza kukodisha moja. Kushiriki gari ni

tofauti na huduma za desturi za kukodisha gari

kwa vile gari inaweza kuhifadhiwa muda mfupi

tu kabla ya kutumika na kwa muda mfupi wa

matumizi kama vile dakika 30. Jumuiya nyingi

zimeandaa sehemu maalum za kuegesha

magari yanayotumika tu katika huduma za


32 | Energiewende ya Ujerumani

kushiriki gari. Pia jumuiya zinaweza kuruhusu

magari yanayoshirikiwa kutumia njia maalum

za mabasi.

Mabomba ya joto

Mabomba ya joto hufyonza nishati ya joto

kutoka eneo, kwa mfano kutoka sehemu za

chini. Joto hili hutumika kuchemsha maji moto

au kupasha majengo joto. Umeme wanaohitaji

waweza kuzalishwa kutoka vyanzo endelevu

vya nishati. Friji hufanya kazi kwa dhana hii -

hupata baridi ndani lakini nje hutoa joto.

Marekebisho ya Ujenzi

Hatua za ufanisi wa nishati zilizotekelezwa

kwenye majengo zikijumuisha kuondoa kabisa

sehemu dhaifu ambapo nishati hupotelea

zaidi ya inavyohitajika ikilinganishwa na hali

ya teknolojia kwa sasa. Hatua zinazoweza

kuchukuliwa ni pamoja na kukinga ukuta na

paa dhidi ya baridi na kuweka dirisha mpya

zilizokingwa dhidi ya baridi. Chaguo nyingine ni

kusasisha mfumo wa kupasha joto.

Mashirika ya ushirika ya nishati

Mashirika ya ushirikiano kama

tunavyoyafahamu nchini Ujerumani ni dhana

ambayo imepata mizizi kuanzia karne ya 19.

Friedrich Wilhelm Raiffeisen na Hermann

Schulze-Delitzsch wote walipata wazo

wakati mmoja ya kuanzisha mashirika ya

ushirikiano ya kwanza nchini Ujerumani.

Dhana ni kwamba watu kadhaa waliyo na

maslahi sawa ya biashara waungane na

hivyo waongeza ushawishi kwenye soko,

kwa mfano kama shirika la ushirikiano la

ununuzi. Nchini Ujerumani aina hii ya biashara

husimamiwa na sheria tofauti. Mashirika

ya ushirikiano katika shughuli za kuzalisha

umeme yamekuwepo kwa muda. Mwanzo

wa kusambaza umeme Ujerumani, maeneo

ya mashambani hayangeweza kwenda kwa

mwendo wa miji mikumbwa hivyo yakaanzisha

mashirika ya ushirkiano ya nishati ili kuzalisha

umeme wao wenyewe. Baadhi ya mashirika

haya ya ushirkiano yangali yapo. Mfumo wa

ushirikiano umepewa mwendo mpya kutokana

na Energiewende. Wengi wanaohusika ni watu

binafsi wanaosimamia ujenzi wa viwanda

vya kuzalisha umeme kupitia miale ya jua au

upepo.

Matumizi ya mwisho ya nishati

Nishati ya mwisho ni ile ambayo inamfikia

mtumiaji. Vitu kama vile upotezi wakati wa

kusafirisha umeme na upotezi mwingine

unaohusiana na ufanisi wa viwanda vya

nishati hutolewa kutoka hesabu hii. Lakini,

upotezi unaotokea kwa watumiaji kama vile

joto kwenye kifaa cha kuwasilisha umeme

zinajumuisha kwenye matumizi kamili ya

nishati.

Mfumo wa kuchoma marisawa

Marisawa ni vidonge vidogo au miti

iliyotengenezwa kutoka vipande vya au

unga wa mbao uliobanwa. Huchomwa

kwenye mifumo maalum ya kupasha joto.

Kubanwa huvipa uzito wa juu wa nishati,

lakini vinachukua sehemu ndogo ya hifadhi

vikilinganishwa na mbao kwa mfano. Mifumo

ya kuchoma vidonge haiathiri tabianchi kwa

vile vinatoa dayoksidi ya kaboni inayolingana

na ile dayoksidi ambayo mumea ulifyonza.

Mkataba wa Kyoto

Mjini Kyoto, Japani mwaka wa 1997, Nchi

Wanachama wa Mkataba wa Mfumo kuhusu

Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC) walikubali

malengo ya kupunguza gesijoto kufikia

mwaka wa 2012. Kituo cha marejeleo ni

viwango vya mwaka wa 1990. Zaidi ya nchi

190 zimehalilisha Mkataba. Kipindi cha pili

cha makubaliano hadi 2020 kilikubaliwa

katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu

Mabadiliko ya Tabianchi mjini Doha. Mkataba

wa Kyoto uliutangulia Mkataba wa Paris wa

Tabianchi wa Desemba 2015 ambapo kufikia

hapo nchi 196 wanachama wa UNFCCC

walikubaliana kuhusu kiwango cha juu cha

kuongezeka kwa joto duniani, cha chini ya selsi

mbili.

Mnada

Kuanzia mwaka wa 2017 minada itafanywa

ili kuamua viwango vya bei zitakazotumika

kwenye miradi mipya ya viwanja vya kuzalisha

umeme kupitia upepo au miradi kubwa

ya fotovolti (PV). Miradi kadhaa itapigwa

mnada kwa wakati mmoja na wanaotaka

kuhusika watawasilisha zabuni ya mradi

husika ilikuamua orodha ya bei itakayotumika

mwanzo. Bei halisi ya umeme kutoka vyanzo

endelevu vya nishati sasa itaamuliwa baada ya

orodha ya bei ya kuamrishwa. Katika mwaka

wa 2015, minada mitatu ya miradi mikumbwa

ya fotovolti(PV) ilifanyika ili kufanya majaribio

na kuboresha mchakato.

Nishati endelevu

Nishati endelevu zinajumuisha nishati ya

upepo, nishati ya jua (fotovolti (PV), na joto ya

jua), joto ya ardhini, nguvu za maji na nishati

ya bahari. Katika nishati ya nguvu za maji kuna

utofautishaji: miradi midogo ya nguvu za maji

huhesabiwa kama nishati endelevu katika

takwimu nyingi, lakini viwanda vikubwa vya

kuzalisha umeme wa nguvu za maji vilivyo na

uwezo wa megawati 50 au zaidi hazihesabiwi.

Kando na vyanzo desturi vya nishati kama

vile makaa ya mawe, mafuta, gesi, nishati ya

nyuklia, vyanzo vya nishati endelevu havitumii

nyenzo asili zinazoisha ili kuzalisha umeme.

Tofauti moja ni mimea na samadi, ambayo

huchukuliwa kutodhuru tabianchi ikiwa

haitumii nyenzo ghafi zaidi kushinda zile

ambazo zitakua katika kipindi hicho.

Teknolojia ya joto ya ardhini hukosolewa mara

kwa mara. Uingiliaji kwenye jiolojia waweza


Energiewende ya Ujerumani | 33

kusababisha mitetemeko ya ardhi au kuenua

ardhi kwa kiwango ambacho majengo yaliyo

juu yake hayakaliki.

Nishati hadi gesi (elektrolisisi, methani)

Nishati hadi gesi ni teknolojia inayowezesha

uhifadhi wa muda mrefu wa nishati ya

umeme isiyotumika. Kwa michakato miwili

umeme hugeuzwa kuwa gesi ambayo

inaweza kuhifadhiwa kwenye hifadhi ya

gesi na kusafirishwa kupitia gridi ya gesi.

Hatua ya kwanza hutumia umeme kugeuza

maji kuwa oksijeni na haidrojeni kupitia

elektrolisisi. Haidrojeni inayotolewa yaweza

aidha kusambazwa kwenye gridi ya gesi moja

kwa moja kwa viwango vinavyodhibitiwa au

kugeuzwa hadi gesi kwa hatua ya pili (uundaji

methani) Uundaji methani hujumuisha

kuongeza dayoksidi ya kaboni kwenye

haidrojeni ilikuzalisha methani na maji.

Methani ndiyo sehemu kubwa ya gesi asili na

inaweza kusambazwa kwenye gridi ya gesi bila

tatizo.

Nishati ya msingi/matumizi ya nishati ya

msingi

Nishati ya msingi ni jumla ya nishati

inayopatikana kutoka vyanzo vya nishati kama

vile makaa ya mawe, mafuta, jua au upepe.

Kugeuza hadi nishati ya mwisho (angalia

matumizi ya mwisho ya nishati) husababisha

upotezi, kiwango kikitegemea chanzo asili

ya nishati, kwa mfano wakati wa uzalishaji

umeme na usafirishaji. Matumizi ya nishati

ya msingi basi huwa juu kuliko matumizi ya

nishati ya mwisho.

Sehemu za kupanulia

Sehemu za kupanulia husaidia ukuzaji wa

vyanzo vya nishati endelevu kutabirika

zaidi, huboresha uunganisho kwenye gridi

ya nishati na huweka gharama za ziada kwa

watumiaji zikiwa chini. Sheria ya Vyanzo

Endelevu vya Nishati huwa na sehemu tofauti

ya kupitia kwa kila aina ya teknolojia ya

nishati endelevu. Uwezo mpya ulioongezwa

ukipita thamani ya juu katika mwaka wowote,

ruzuku za chini kidogo zitatumika mwaka

unaofuata. Ongezeko likikosa kufika kiwango

kilichotarajiwa katika sehemu iliyotengwa, ada

za usaidizi zinapunguzwa kwa kiwango kidogo

au zinabaki zilivyo.

Soko moja la Ulaya

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ni

soko moja na kuwapo kwa soko hili moja

kunahakikisha kwamba kuna usafarishaji huru

wa bidhaa, huduma, mitaji na kwa kiwango

fulani, watu kati ya mipaka ya nchi. Kwa

mfano, hakuna ushuru wa forodha au kodi

nyingine zinazotozwa bidhaa na huduma

zinazosafirishwa nje ya mipaka. Umeme,

mafuta, gesi pia husafirishwa kutoka nchi moja

hadi nyingine. Lakini miundu misingi iliyopo

ya umeme na gesi haitoshelezi shughuli za

soko moja ya nishati ya Ulaya. Kanuni sawa za

kupita mipaka bado zinahitajika. Changamoto

hizi mbili zinatarajiwa kutatuliwa katika miaka

michache ijayo ili kuhakikisha bei sawa za

umeme katika Umoja wa Ulaya na kuongeza

umeme unaoweza kutegemewa.

Taka nururishi

Taka nururishi hutokea wakati nishati ya

nyuklia inatumika kuzalisha umeme. Nyenzo

nururishi hugeuzwa kuwa viini vingine kwenye

tangi ya nishati iliyo na vyuma. Baada ya

muda fulani, viini hivi haviwezi kutumika

tena, lakini bado ni nururishi. Kwanza ni

isotopu za elementi za urani, plutoni, neptuni,

aidini, caesini, strontini, americini, kobolti

na nyingine. Muda unavyoenda viini vingine

nururishi hutokea vile viwango vya kuoza

vinavyoendelea. Lazima taka ihifadhiwe salama

kwa kipindi kirefu ilikuepuka madhara kwa

binadamu na mazingira. Nyenzo nururishi zaidi

lazima zihifadhiwe kwa uthabiti kwa angalau

miaka milioni moja. Taka nururishi ya wastani

huhitaji mikakati michache ya ulinzi na taka

nururishi hafifu haihitaji mikakati ya uzito ya

ulinzi. Lakini hii pia lazima ihifadhiwe kwa

uthabiti kwa muda mrefu.

Usawa na CO 2

Usawa na CO 2

ni thamani ya kulinganisha

athari ya kiini cha kimekali na athari ya

gesijoto, kwa kawaida katika kipindi cha miaka

100, ambapo gesi ya dayoksidi ya kaboni (CO 2

)

ina thamani ya moja. Ikiwa kiini kina usawa wa

CO 2

25, utoaji wa kilo moja ya nyenzo hii ina

madhara mara 25 zaidi ya utoaji wa kilo moja

ya CO 2

. Kumbuka: Usawa wa CO 2

hauelezi

chochote kuhusu mchango wa kiini kwa

mabadiliko ya tabianchi.

Ufanisi wa nishati

Ufanisi wa nishati unaeleza kiwango cha

utendakazi kikilinganishwa na nishati

iliyotumika au kiwango cha nishati

kinachohitajika ili kupata kiwango fulani cha

utendakazi. Jinsi nishati inavyo kuwa na ufanisi,

ndivyo matokeo yanavyoweza kutimizwa

kwa kutumia nishati chache. Kwa mfano

jengo lililo na kiwango cha juu cha ufanisi wa

nishati litahitaji nishati chache kupasha joto

au kupunguza joto likilinganishwa na jengo la


34 | Energiewende ya Ujerumani

ukubwa sawa lililo na kiwango cha chini cha

ufanisi wa nishati. Uzalishaji viwandani na

usafiri ni sehemu zingine ambazo ufanisi wa

nishati unashika umuhimu zaidi. Mikakati ya

ufanisi wa nishati huvutia biashara inapookolea

biashara pesa nyingi zaidi ya zile zilizotumika

kuiweka. Watumiaji binafsi pia wanaweza

kusaidia kuokoa nishati kwa kutumia vifaa

vilivyo na ufanisi zaidi wa nishati. Katika nchi

nyingi, friji, televishoni, mashine za kufua,

nk. huwa na lebo ya matumizi ya nishati ili

kuwezesha watumiaji kuona kwa haraka ufanisi

wa nishati wa kifaa.

Vipindi vya giza

Vipindi ambavyo nguvu za upepo na miradi

ya fotovolti (PV) haiwezi kuzalisha umeme

vinajulikana kama vipindi vya giza. Hali mbaya

kabisa ni ya usiku wenye giza wa mwezi mpya

bila upepo. Wakati wa vipindi hivi, vyanzo

vingine vya nishati au nishati iliyohifadhiwa

awali lazima itumike kukidhi matumizi ya

umeme.


Energiewende ya Ujerumani | 35

Orodha ya marejeo

AG Energiebilanzen e.V. (2016):

Energieverbrauch in Deutschland im Jahr 2015.

Agora Energiewende (2015): Agorameter –

Stromerzeugung und Stromverbrauch.

Auswärtiges Amt (2015): Hotuba ya Frank-

Walter Steinmeier akizindua Mazungumuzo ya

Mpito wa Nishati mjini Berlin.

BMWi und BMBF: Energiespeicher –

Forschung für die Energiewende.

Bundesamt für Strahlenschutz (2016):

Kernkraftwerke in Deutschland:

Meldepflichtige Ereignisse seit

Inbetriebnahme.

Bundesministerium für Umwelt, Naturschutz,

Bau und Reaktorsicherheit (2015):

Atomenergie – Strahlenschutz.

Bundesministerium für Wirtschaft und

Energie (2014): Die Energie der Zukunft. Erster

Fortschrittsbericht zur Energiewende.

Bundesministerium für Wirtschaft und

Energie (2014): Zweiter Monitoring-Bericht

„Energie der Zukunft“.

Bundesministerium für Wirtschaft und

Energie (2015): Die Energie der Zukunft.

Fünfter Monitoringbericht zur Energiewende.

Bundesministerium für Wirtschaft und

Energie (2015): Eckpunkte Energieeffizienz.

Bundesministerium für Wirtschaft und

Energie (2015): Erneuerbare Energien

in Zahlen. Nationale und Internationale

Entwicklung im Jahr 2014.

Bundesministerium für Wirtschaft und

Energie (2015): EU-Energieeffizienz-Richtlinie.

Bundesministerium für Wirtschaft und

Energie (2016): Bruttobeschäftigung durch

erneuerbare Energien in Deutschland und

verringerte fossile Brennstoffimporte durch

erneuerbare Energien und Energieffizienz.

Bundesministerium für Wirtschaft und

Energie (2016): Energiedaten: Gesamtausgabe.

Kufikia Novemba 2016.

Bundesministerium für Wirtschaft und

Energie (2016): Erneuerbare Energien auf einen

Blick.

Bundesnetzagentur (2015): EEG-Fördersätze

für PV-Anlagen. Degressions- und

Vergütungssätze Oktober bis Dezember 2015.

Bundesnetzagentur; Bundeskartellamt (2016):

Monitoringbericht 2016.

Bundesregierung (2015): Die

Automobilindustrie: eine Schlüsselindustrie

unseres Landes.

Bundesverband CarSharing (2016): Aktuelle

Zahlen und Daten zum CarSharing in

Deutschland.

Bundesverband der Energie- und

Wasserwirtschaft (2014): Stromnetzlänge

entspricht 45facher Erdumrundung.

Bundesverband der Energie- und

Wasserwirtschaft e.V. (2016): BDEW zum

Strompreis der Haushalte. Strompreisanalyse

Mai 2016.

Baraza la Wasimamizi wa Nishati barani

Ulaya (2015): Ripoti 5.2 ya kutathmini ya CEER

kuhusu Uendelevu wa Uzalishaji wa Umeme -

Sasisho la data.

Deutsche Energie Agentur GmbH (2012):

Der dena-Gebäudereport 2012. Statistiken

und Analysen zur Energieeffizienz im

Gebäudebestand.

Deutsche Energie Agentur GmbH (2014):

Der dena-Gebäudereport 2015. Statistiken

und Analysen zur Energieeffizienz im

Gebäudebestand.

Deutsche Energie-Agentur (2013): Nishati hadi

Gesi. Eine innovative Systemlösung auf dem

Weg zur Marktreife.

Deutsche Energie-Agentur (2015):

Pilotprojekte im Überblick.

Deutscher Bundestag (2011): Novelle des

Atomenergiegesetzes 2011.

DGRV – Deutscher Genossenschaftsund

Raiffeisenverband e.V. (2014):

Energiegenossenschaften. Ergebnisse

der Umfrage des DGRV und seiner

Mitgliedsverbände.

EnBW (2015): Pumpspeicherkraftwerk Forbach

– So funktioniert ein Pumpspeicherkraftwerk.

entsoe (2014): Mpango wa miaka 10 wa

Kuendeleza Mtandao 2014.

Tume la Mazingira Ulaya (2016): Ukadiriaji wa

kila mwaka wa Umoja wa Ulaya wa gesijoto

1990-2014.

Filzek, D., Göbel, T., Hofmann, L. et al. (2014):

Kombikraftwerk 2 Abschlussbericht.

GWS (2013) Gesamtwirtschaftliche Effekte

energie- und klimapolitischer Maßnahmen der

Jahre 1995 bis 2012.

IEA (2016): Muhtasari wa Hali ya Nishati

Duniani katika mwaka wa 2016, Novemba 2016.

Jopo la Kiserikali kuhusu Mabadiliko kwenye

Tabianchi (2014): Mabadiliko kwenye Tabianchi

2014. Ripoti ya Usanisi.

Shirika la Kimataifa la Nishati Endelevu

(2015): Ada za Kuzalisha Nishati Endelevu

mwaka wa 2014.

IRENA (2015): Ada za kuzalisha nishati

endelevu mwaka wa 2014.


36 | Energiewende ya Ujerumani

KfW (2015): Energieeffizient bauen und

sanieren. KfW-Infografik.

Kraftfahrt-Bundesamt (2016):

Fahrzeugbestand in Deutschland.

Merkel, A. (2015): Hotuba ya Waziri Mkuu wa

Shirikisho, Merkel, katika hafla ya mwaka mpya

ya Bundesverband Erneuerbare Energie e.V.

(BEE) mnamo 14 Januari 2015.

Ratgeber Geld sparen (2015): Kühlschrank

A+++ Ratgeber und Vergleich. Kufikia Novemba

2015.

REN21 (2016): Nishat endelevu 2016. Ripoti ya

Hali ya Dunia 2016.

Statistische Ämter des Bundes und der Länder

(2014): Gebiet und Bevölkerung – Haushalte.

Statistisches Bundesamt (2014):

Bevölkerungsstand.

Statistisches Bundesamt (2015): Preise.

Erzeugerpreise gewerblicher Produkte

(Inlandsabsatz) Preise für leichtes Heizöl,

schweres Heizöl, Motorenbenzin und

Dieselkraftstoff. Lange Reihen.

Statistisches Bundesamt (2015):

Umsätze in der Energie-, Wasser- und

Entsorgungswirtschaft 2013 um 1,6%

gesunken.

Statistisches Bundesamt: Umweltökonomische

Gesamtrechnungen, Werte für 2015 on

https://www.destatis.de/

trend:reseach Institut für Trend- und

Marktforschung, Leuphana Universität

Lüneburg (2013): Definition und Marktanalyse

von Bürgerenergie in Deutschland.

Umweltbundesamt (2015):

Emissionsberichterstattung Treibhausgase

Emissionsentwicklung 1990-2013 –

Treibhausgase.

Umweltbundesamt (2015): Nationale

Trendtabellen für die deutsche

Berichterstattung atmosphärischer Emissionen

1990-2013.

Umweltbundesamt (2015): Presseinfo 14/2015:

UBA-Emissionsdaten 2014 zeigen Trendwende

beim Klimaschutz.

Umweltbundesamt (2016): Treibhausgas-

Emissionen in Deutschland.

Umweltbundesamt (2016): UBA-

Emissionsdaten für 2015 zeigen Notwendigkeit

für konsequente Umsetzung des

Aktionsprogramms Klimaschutz 2020.

Zetsche, D. (2009): Hotuba kwenye Majadiliano

ya Usafiri Duniani, Stuttgart, Januari 2009.


© dpa/Catrinus Van Der Veen

Chapa

Auswärtiges Amt

Werderscher Markt 1

10117 Berlin

Simu.: +49 30 1817-0

www.diplo.de

Mhariri/usanifu

Edelman.ergo GmbH, Berlin

Diamond media GmbH, Neunkirchen-Seelscheid

More magazines by this user