7-2-2012.pdf

bunge.parliament.go.tz

7-2-2012.pdf

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

ORODHA YA SHUGHULI ZA LEO

11 APRILI, 2012

MKUTANO WA SABA

KIKAO CHA PILI


ORODHA YA SHUGHULI ZA LEO

_______________

MKUTANO WA SABA

KIKAO CHA PILI – TAREHE 11 APRILI, 2012

I. MASWALI:

OFISI YA WAZIRI MKUU:

16. MHESHIMIWA HAMAD RASHID MOHAMED

(WAWI):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu:-

(a) Je, ni miradi mingapi na ya aina gani

inayohitaji uwekezaji wa ama ubia na sekta

binafsi au ya sekta binafsi peke yake;

(b) Je, ni utaratibu gani mwekezaji aufuate ili

asisumbuke kupata taarifa ya uwekezaji huo.

2


17. MHESHIMIWA DAVID ZACHARIA KAFULILA

(KIGOMA KUSINI):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu:- Mgogoro

wa ardhi kati ya wakazi wa Kata ya Ilagara na

Magereza unazidi kuwa mkubwa na kuhatarisha

amani kwa wakazi wa eneo hilo:-

Je, Serikali imechukua hatua gani kulipatia

ufumbuzi tatizo hilo ili wananchi husika waweze

kupata ardhi kwa ajili ya kilimo.

OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA

UMMA:

18. MHESHIMIWA SARA MSAFIRI ALLY

(VITI MAALUM):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya

Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma:- Tatizo la

ajira limekuwa likiongezeka kila mwaka nchini:-

Je, Serikali haioni kuwa huu ni wakati muafaka wa

kufuta ajira za mikataba kwa watumishi waliofikia

umri wa kustaafu hasa kwa fani zenye watalaam

wengi nchini ili kutoa fursa kwa vijana wenye sifa

na uwezo wa kupata ajira.

3


WIZARA YA KAZI NA AJIRA:

19. MHESHIMIWA ANGELLAH JASMINE KAIRUKI

(VITI MAALUM):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Kazi na Ajira:-

Mwezi Juni, 2011 Nchi yetu ilikuwa moja ya nchi

Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani waliosaini

Mkataba wa Kimataifa unaolinda Haki za

Wafanyakazi wa Majumbani:-

Je, mchakato wa kuridhia Mkataba huo umefikia

hatua gani.

WIZARA YA UJENZI:

20. MHESHIMIWA LAMECK OKAMBO AIRO

(RORYA):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi:- Mhe.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kampeni za

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 aliahidi ujenzi wa

barabara ya Mika – Utegi – Randa hadi Shirati

yenye urefu wa km. 40 kwa kiwango cha lami:-

4


(a) Je, ni lini ahadi hiyo itatekelezwa;

(b) Je, ni lini barabara ya Irienyi – Kinesi

itapandishwa hadhi kuwa barabara ya Mkoa

kama kikao cha RCC kilivyopitisha.

21. MHESHIMIWA MHONGA SAID RUHWANYA

(VITI MAALUM):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi:-

Kupanda kwa gharama za ujenzi kunaathiri sana

miradi ya maendeleo hasa katika Mikoa ya Kigoma

Rukwa na Tabora ambapo njia za usafirishaji ni

ngumu hali inayosababisha kupanda kwa bei za

bidhaa; mfano mfuko wa saruji Dar es Salaam ni

Shs.13,000=, wakati Kigoma ni Shs.19,500/= hadi

23,000/=:-

Je, kwa nini Serikali hutoa fedha za miradi kwa

kiwango sawa kwa Mikoa bila kuzingatia uhalisia

huo.

5


WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII:

22. MHESHIMIWA AL-SHAYMAA JOHN KWEGYIR

(VITI MAALUM):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Afya na Ustawi

wa Jamii:- Watu wengi wenye ulemavu wa ngozi

hususan watoto wadogo wamepoteza viungo vya

miili yao kwa kukatwa na watu wenye imani za

kishirikina wasio na huruma ili kujiongezea kipato

au utajiri hasa Mikoa ya Kanda ya Ziwa:-

Je, Serikali inawasaidiaje wale wote waliopata

ulemavu kwa kushambuliwa na majangili

wasiokuwa na huruma.

WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:

23. MHESHIMIWA RICHARD MGANGA NDASSA

(SUMVE):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Chakula

na Ushirika:- Halmashauri za Kanda ya Ziwa

Victoria zinapata gharama kubwa sana katika

usafirishaji wa Mahindi yanayofikia katika ghala la

Hifadhi ya Chakula lililopo Shinyanga ambalo

linahudumia Kanda yote ya Ziwa:-

6


Je, kwa nini Serikali isiyatumie maghala makubwa

yaliyopo katika stesheni za Bukwimba ili

kuzipunguzia mzigo Halmashauri hizo.

24. MHESHIMIWA MODESTUS DICKSON KILUFI

(MBARALI):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Chakula

na Ushirika:-

(a) Je, ni lini Serikali itamaliza mgogoro kati ya

wananchi wa KAPUNGA ambao shamba lao

la Small Holders lenye ukubwa wa hekta 800

na eneo la makazi hekta 1070 Wilayani

Mbarali ambalo kwa pamoja alipewa

Mwekezaji wa NAFCO KAPUNGA badala ya

hekta 5500 alizostahili kupewa;

(b) Je, Serikali inatoa tamko gani kwa Mwekezaji

wa NAFCO KAPUNGA aliyechoma kwa

kemikali mazao ya Mpunga ya wananchi zaidi

ya ekari 449;

(c) Je, Serikali itakuwa tayari kusimamia malipo

ya fidia ya mazao ya wananchi yaliyoharibiwa

na mwekezaji huyo.

7


WIZARA YA KATIBA NA SHERIA:

25. MHESHIMIWA MESHACK JEREMIAH

OPULUKWA (MEATU):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Katiba na

Sheria:- Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa

Umma wa Mwaka 2007 hauwatambui Mawakili wa

Serikali walioajiriwa kwenye Wizara pamoja na

Idara za Serikali kama Mawakili wa Serikali bali

Maafisa Sheria:-

(a) Je, Serikali itafuta lini Waraka huo wa kibaguzi

na Mawakili wote walioajiriwa kama Mawakili

wa Serikali kuendelea kuitwa hivyo na si

Maafisa Sheria;

(b) Je, Serikali itawalipa lini Maafisa Sheria posho,

mishahara na stahili nyingine sawa na

Mawakili wa Serikali waliopo Ofisi ya

Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kama

taaluma nyingine zinavyofanya Serikalini.

8


26. MHESHIMIWA AUGUSTINO MANYANDA

MASELE (MBOGWE):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Katiba na

Sheria:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatizo la

malipo ya Wazee wa Mabaraza ya Mahakama za

Mwanzo Wilayani Bukombe na Jimbo la Mbogwe

ambao hawajalipwa posho zao tangu walipokuwa

wakifanya kazi Wilaya ya Kahama, kabla ya

kugawanywa.

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:

27. MHESHIMIWA RIZIKI OMAR JUMA

(VITI MAALUM):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Elimu na

Mafunzo ya Ufundi:- Katika mwaka wa fedha

2010/2011 Serikali ilisema itatekeleza mpango wa

ufundishaji kwa njia ya TEHAMA; lakini katika

utekelezaji wa mpango huo kunahitajika mambo

muhimu kama umeme, vifaa kama vile Kompyuta,

majengo ya kuwekea vifaa hivyo n.k:-

Je, Serikali imetekeleza mpango huo kwa kiwango

gani hasa kwa kuhakikisha umeme, vifaa na

majengo vinapatikana.

9


28. MHESHIMIWA MENDRAD LUTENGANO

KIGOLA (MUFINDI KUSINI):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Elimu na

Mafunzo ya Ufundi:- Katika matokeo ya darasa la

saba mwaka 2011 watoto wengi walifutiwa

matokeo ya mitihani yao ambapo miongoni mwao

watoto 361 wanatoka Wilaya ya Mufindi kwenye

shule za vijijini na wanaitegemea elimu hiyo kama

mtaji wao wa maisha:-

(a) Je, Serikali haioni kuwa haijawatendea haki

watoto hao pamoja na uamuzi wa kurudia

mitihani hiyo;

(b) Je, kwa nini watoto hao ambao hawajafikisha

miaka 18 wapewe adhabu kubwa hivyo;

(c) Je, Serikali inachukua hatua gani kwa

watendaji wanaosababisha ufujaji wa mitihani.

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI:

29. MHESHIMIWA RITTA ENESPHER KABATI

(VITI MAALUM):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya

Ndani ya Nchi:- Askari wa Kikosi cha F.F.U Kihesa

Mkoani Iringa wanakabiliwa na tatizo la uchakavu

wa nyumba za kuishi:-

10


(a) Je, Serikali ina mpango wowote wa kuboresha

makazi ya Askari hao;

(b) Je, Serikali iko tayari sasa kutenga fedha

katika bajeti yake ya mwaka 2012/2013 kwa

ajili ya kuboresha nyumba za Askari hao.

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII:

30. MHESHIMIWA PHILEMON KIWELU

NDESAMBURO (MOSHI MJINI):

Atamuuliza Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na

Utalii:- Mlima Kilimanjaro ulio katika Mji wa Moshi

ni kivutio Kikuu cha Utalii kinacholiingizia Taifa

fedha nyingi za kigeni kuliko Hifadhi yoyote

Tanzania:-

(a) Je, kwa nini Serikali inaupa kipaumbele Mji wa

Arusha kama kituo cha kupanda Mlima

Kilimanjaro badala ya Mji wa Moshi;

(b) Je, hii siyo kuhujumu Mji wa Moshi ambao

uchumi wake unazidi kudidimia baada ya

viwanda vyake kufa.

11


II. MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI:

(Kusomwa Mara ya Pili, Kamati ya Bunge Zima

na Kusomwa Mara ya Tatu)

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria

Mbalimbali za Biashara wa Mwaka 2011 [The

Business Laws (Miscellaneous Amendments) Bill,

2011].

DODOMA DKT. T.D. KASHILILAH

11 APRILI, 2012 KATIBU WA BUNGE

12

More magazines by this user
Similar magazines