Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Mamilioni ya makundi tete ya watu hutegemea

mifugo kuendeshea maisha yao na kujikimu.

Mifugo na mazao yake hugharimia mahitaji

ya msingi ya kila siku na huwapatia fedha

wakati wa shida.
Picha kwa hisani ya Anita Swarup Picha kwa hisani ya Steve Sloan

Watu Bilioni moja wanaishi kwa kipato cha chini ya dola kwa siku

Karibia milioni 700 ya watu hutegemea mifugo kuendesha maisha yao. Fedha inayopatikana kutokana na mauzo ya

mifugo na mazao yake hugharamia elimu na huduma za afya. Wanyama hutoa samadi na hukokota zana za kilimo, hivyo

kusaidia uzalishaji wa mazao, kutoa ajira na fursa za kibiashara. Mifugo husaidia majukumu muhimu ya kijamii na

kiutamaduni kama vile utoaji wa mahari. Vifo vya wanyama kwa sababu ya magonjwa huathiri maisha ya wafugaji,

familia na jamii ulimwenguni. Pale ambapo umaskini na mazingira havitoi njia nyingine, kuku, mbuzi, kondoo, ng’ombe

na nguruwe humaanisha maisha, shule, mavazi, biashara, na chaguo la heshima na wito. Licha ya uhusiano wa karibu

kati ya afya za wanyama wafugwao na afya za binadamu, kati ya wanyama wafugwao na maisha ya binadamu, ni 4% tu

ya misaada ya kimataifa huelekezwa kwenye mahitaji ya kilimo kwenye nchi zinazoendelea.

Dira na Dhamira ya GALVmed

Dira

> Kulinda wanyama, kuokoa maisha ya watu

Dhamira

> Kuletamaendeleo ya kudumu ya huduma ya

utabibu wamifugo kwa wafugajimasikini katika nchi

zinazoendelea

> Kuendeleza, kuandikisha na kuzindua dawa 4 hadi

6 za chanjo,madawa yamifugo au vifaa vya

kuchunguzamagonjwa ifikapomwaka 2015 ili

kukidhimahitaji ya wafugajimasikini

> Kushirikiana namashirika wenza yaliyopo katika nchi

zinazoendelea ili kuhakikisha utaratibu en delevu wa

utoaji wa vifaa vipya kwa wafugaji masikini

> Kutoa mfano bora na wenye mafanikio juu ya

ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi na

kuendelea kuongoza kiukanda, hivyo kuhakikisha

utoaji wa vifaa vipya baada ya mwaka 2015

Kuwa na shauku kubwa na kuzingatia utoaji wa vifaa vipya

Si shirika tu bali ni utekelezaji wa kazi

Utendaji kazi

Kwa kushirikiana na uwanda mpana wa mashirika

mengine, GALVmed (Global Alliance for Livestock

Veterinary Medicines) inatengeneza chanjo, vifaa vya

kuchunguza magonjwa na madawa ya mifugo,

yanayopatikana kirahisi na kwa bei nafuu kwa

mamilioni ya watu wanaotegemea mifugo.

Kwa kuunga mkono Malengo ya Milenia, GALVmed

inatafuta njia za kupambana na magonjwa yenye

madhara makubwa na yale yaliyosahauliwa. Pale

ambapo chanjo thabiti ipo, lakini upatikanaji wake ni

mgumu, GALVmed na wabia wake hufanya kazi ya

kuongeza uzalishaji na kushughulikia udhaifu katika njia

za usambazaji. Hata hivyo, kwamagonjwamengine vifaa

vipya vinahitajika. GALVmed inapokea na kutumia

matokeo mazuri ya utafiti kutoka popote pale

ulimwenguni na unaolenga uzalishaji na kutumika

katika nchi zinazoendelea, pale inapobidi.

1 Chanzo, Benki ya Dunia, 2007 Picha ya jalada la mbele, kwa hisani ya Getty Images
Changamoto za uwepo na upatikanaji wa huduma za afya za wanyama

Uvumbuzi

Changamoto za

kiufundi

Uhaba wa taarifa

kuhusu bidhaa

zinazofaa

Mipango

iliyopotoka

kimawazo

Shughuli za GALVmed

> Kutoa kipaumbele kwenye magonjwa yenye madhara makubwa yanayoathiri zaidi wafugaji maskini

> Kuelewa vipingamizimuhimu vinavyojitokeza katika uvumbuzi wa vifaa vipya vinavyoweza kupunguza

madhara yamagonjwa katika nchi zinazoendelea

> Kubaini rasilimali na kuziba mapengo muhimu ya kiutaalam

Kupanga na kusimamiamiradi ya kuendeleza afya yamifugo

> Kupanga na kusimamiamiradi ya kuendeleza afya ya mifugo

Sifa za GALVmed

> Kulenga njia za kuwapatia vifaa vipya vinavyofaa watu wenye uwezo mdogo

> Msimamo (kutimizamalengo, viwango)

> Uwazi katika taratibu na utoaji maamuzi

> Uongozi katika ushirikiano na utendaji kazi

Ujuziwa GALVmed

> Ujuzi wa hali ya juu wa kiufundi

> Umahiri katika kutengeneza na kusajili madawa ya mifugo

> Usimamizi wamiradi nambinu za kutoa ushauri

> Ujuzi wa agenda za maendeleo

> Ujuzi wa kuchangisha fedha

> Kuanzisha Ushirikiano

Maendeleo

Ukosefu wa fedha

kwa ajili ya utafiti

wa masuala ya

maendeleo

Ubunifumbovu,

usimamizi mbaya

wa utafiti

Usajili

Uwepo wa taratibu

nyingi za kisheria na

zisizoeleweka

Ukosefuwa utaratibu

unaohakikisha

viwango vya ubora

Mamlaka tofauti za

serikali

GALVmed inavyoshughulikia changamoto hizi

Uzalishaji

Ukosefu wa mvuto

wa kibiashara

Mchakato wenye

gharama kubwa

Ukosefuwa

utaratibuwa

maendeleo

Uendeshaji wa

Kibiashara

Ukosefuwa soko la

mauzo

Ukadiriaji mbaya wa

mahitaji au matakwa

Ukubwa wa vifurushi

usio sahihi

Ukosefu wa ufahamu

au elimu juu ya

matumizi sahihi

Ugawaji

endelevu

Ugawaji usiokuwa na

msimamo

Vifaa vya magendo

Ukosefuwa njia za

kuzuia uigaji wa

uvumbuzi

Vifaa na utekelezaji

usio bora

Dhima yetu ni kuwezesha na kuongoza katika kukabiliana na changamoto hizi kwa kuwa na ubia ambao

unamwezesha mfugaji maskini kuweza kupata huduma za afya kwa wanyama. GALVmed inashughulikia udhaifu

katika mlolongo, kutoka kwenye uzalishaji wa bidhaa hadi kumfikia mnyama.

Picha kwa hisani ya Stuart Brown

GALVmed ni nini?

GALVmed ni shirikisho la kiulimwengu lisilo la

kibiashara na ni la ubia wa sekta binafsi na sekta ya

umma. Ina wanachama, wadau na washirika ambao

ni pamoja na:

Shirika la Chakula na Kilimo la UmojawaMataifa (FAO)

Shirika la Afya yaWanyama Duniani (OIE)

Umojawa Afrika (AU-IBAR)

Umoja wa Ulaya

Serikali za Nchi Zinazoendelea

Kituo cha Utafiti wa Kilimo kwa ajili ya Maendeleo ya

Kimataifa cha Ufaransa CIRAD

Shirika la Kimataifa la Afya ya Wanyama (IFAH)

Asasi za Kiraia kama vile FARM-Africa, Africare,

VETAID, Mercy Corps, NESPOD na BAIF

Wamaasai waishio Kaskazini mwa Tanzania waliiambia GALVmed

Hakuna Chanjo ya

Ndigana kali –

Hakuna Ng’ombe.

Hakuna ng’ombe –

Hakuna Wamaasai

Taasisi za utafiti na za elimu za nchi zilioendelea na

zinazoendelea, ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Kimataifa

ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), Chuo cha Mifugo cha

Onderstepoort (OVI); Watengenezajiwa chanjo za

wanyama, Vifaa vya Kibiologia vya Onderstepoort

(OBP); Taasisi ya Taifa UtabibuwaMifugo, Ethiopia

(NVI); Taasisi ya Taifa ya Utibabu wa Mifugo Botswana

(BVI); Learned Society, Chama cha Wataalamu wa

Mifugo Uingereza; Chuo cha UtafitiMifugo cha Tamil

Nadu, Taasisi ya Utafiti ya Moredun (MRI), pamojab na

washiriki binafsi kamamashirika ya afya ya wanyama:

Pfizer,Merial, Intervet, CEVA Animal Health; kampuni

za uchunguzi wa magonjwa, IDEXX na Indian

Immunologicals Limited.

GALVmed haiwezi kutatua matatizo yote peke yake, ila

ni mojawapo ya sululisho. Mwanzoni GALVmed ilianza

shughuli zake Novemba 2005, na kuanzia Septemba

2008 ilianza kukuza muundo wake pamoja na utendaji

wake wa kazi. Baada ya hapo, imefanya juhudi kubwa

za kuongeza zanaa zake kwa kusudi maalumu ya

kuendeleza uchunguzi wa magonjwa, dawa za chanjo

na madawa ya kukabili magonjwa ya mifugo.
Picha kwa hisani ya Anita Swarup

GALVmed inatiliamkazomagonjwamuhimu

ambayo yanahusiana zaidi na utaratibu wa

kupunguza umasikini na kuboresha ustawi wa

maisha katika maeneo yaliolengwa. Magonjwa

haya yamegawanywa katika makunde manne:

magonjwa ya ng’ombe, ya wanyama wadogo

wanaocheua, nguruwe na ndege, ijapokuwa

kuna magonjwa yanayoathiri makundi yote. Vifo

vya wanyama vinavyosababishwa na magonjwa

vinawaacha wafugaji wengi wawe katika hali

mbaya, kwa hiyo dawa za chanjo na matibabu ni

muhimu katika uchumi wao na zinachangia

kudumisha afya za wafugaji na familia zao.

Marry, Kiongozi wa Chama cha Wanawake Kijiji cha Mairowa,

Longido, Tanzania

Magonjwa yanayotiliwa mkazo na GALVmed

Kwa sababu ya dawa ya

chanjo, Nimefanikiwa kupata

ndamawengi ambao

ninawauza na kuweza kulipa

ada ya shule. Ninaweza

kutenga pesa za ada ya shule

kwa sababu ninajua kwamba

Ndama wana afya nzuri

Ng’ombe

Ndingana kali

Ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya Ng’ombe

Ugonjwa wa Hemorrhagic Septicaemia

Ugonjwa wa Nagana

Wanyama wadogo wanaocheua

Virusi vyamaradhi vinavyoambukizambuzi na

kondoo

Ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya Mbuzi

Kondoo & Mbuzi

Ndui ya kondoo na mbuzi

Nguruwe

Ugonjwa waminyoo ya nguruwe

Ugonjwa wa homa ya nguruwe

Homa yamafua ya nguruwe

Ndege

Ugonjwa wa Mdondo wa Kuku

Mafua Makali ya Ndege

Magonjwa yanayoathiri makundi yote

Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa

Picha kwa hisani ya Steve Sloan

Kutafuta Ufumbuzi wa Matatizo

Magonjwa ya kipaumbele ambayo GALVmed na wabia

wake wanayashughulikia ni:

Ndingana kali (East Coast Fever) Ndigana inaua kadiri

ya ng’ombe milioni moja kila mwaka Afrika, ingawa

chanjo yake ambayo hutengenezwa na Taasisi ya

Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo iliyopo Nairobi imekuwepo

tangu mwaka 1970. Hivi sasa, chanjo hiyo haipatikani

kirahisi na idadi ya mwisho ya dawa ilitegenezwamwaka

1996. Tiba ya ugonjwa huu imetimizamafanikio ya tiba

kwa asilimia 98% nchini Tanzania, na kwa kushirikiana

na ILRI, GALVmed inafanya mpango wa kuweza

kurahisisha upatikanaji wa chanjo kwa bei rahisimara tu

itakaposajiliwa. Usajili unahitaji msimamo thabiti wa

majaribio ili kuhakikisha usalama wa dawa na

kuhakikisha uwezekano wa kufanya biashara na

kuanzisha mtandao wa ununuzi na kutoa huduma ili

kuwapatia kipato watu waliopo katika nchi

zinazoendelea. Mpaka sasa GALVmed imefanikiwa

kusajili dawa ya chanjo nchini Kenya, Tanzania na

Malawi.

Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (Rift Valley Fever)

ni ugonjwa unaoambukizwa na mbu na unaua binadamu

pamoja na wanyama. Kwa sababu huwa inatokea kila

baada yamiaka 5 hadi 7, wafugaji wenyemapatomadogo

wanasita kuchanjamifugo dhidi ya ugonjwa huu. Kama

wafugaji wakichanganya chanjo dhidi ya ugonjwa huu na

chanjo zamagonjwamengine kama vile Ugonjwa wa

Mapele ngozi au Ndui ya Kondoo/Mbuzi, wafugaji

watapatamafanikiomakubwa.

Ugonjwawa Mdondo wa Kuku (Newcastle Disease)

inaua kadiri ya asilimia 100% ya kuku,mabata. Katika

bara la Afrika tu,milioni 589 ya kuku wako katika hatari

ya kuambukizwa na ugonjwa huo ambao unaweza

Kimani Merendei, Tanzania

Dawa ya chanjo dhidi ya

Ndigana Kali inanipa amani.

Maisha yangu yamezidi kuwa

mazuri. Nataka watoto wangu

wapate kazi mjini auwawe na

ng’ombe au mashamba ya

kisasa.

kuambukiza kuku ambao nimuhimu kwamaisha ya

mamilioni ya wananchi wenye uwezomdogo. Chanjo

dhidi ya ugonjwa huu unapatikana kwa wafugaji

wanaofanya biashara, lakini ukubwa wa kifurushi na

mahitaji ya frigi inakuwa ngumu kwa wafugajimasikini

kupata dawa hizi za chanjo. GALVmed inashirikiana na

washiriki wenza katikambinu za kukabilimasuala haya.

Ugonjwa wa minyoo ya nguruwe (Porcine Cysticercsis)

ni ugonjwa ulionea Afrika, Amerika ya Kusini na Asia.

Nguruwe walioambukizwa inabidi wauzwe kwa bei

rahisi au inabidi wauwawe. Ugonjwa huu pia unaweza

kuathiri binadamu na kusababisha uvimbe katika

ubongo wa binadamu, na inasemekana ugonjwa huu

unasababisha vifo 50,000 kwamwaka katika nchi

zinazoendelea, na pia husababisha kati ya asilimia

20 – 50% ya ugonjwa wa kifafa duniani ambao huwa

unajitokeza baada yamuda, na kuletamadharamakubwa

katikamaisha ya watu. GALVmed na washiriki wenza

wanafanya jitihada za kuhakikisha kwamba dawa za

chanjo na madawa yanayohitajika dhidi ya ugonjwa huu

wa nguruwe, hii ikiwa ni njiamojawapo ya kupunguza

hatari ya kumuambukiza binadamu.

GALVmed pia imeanza kujishughulisha namagonjwa

mengine, kama vile Ugonjwa wa Homa yaMapafu ya

Ng’ombe ambao ni ugonjwa wamlipuko usiokuwa na

mpaka na huletamadharamakubwa Afrika; Ugonjwa wa

Homa yaMapafu yaMbuzi ni ugonjwa unaoweza kuua

kati ya asilimia 60 – 100% yambuzi walioambukizwa, na

Virusi vyamaradhi vinavyoambukizambuzi na kondoo ni

ugonjwa unaothiri uchumi na ulianza kujitokeza

mwanzoni wamwaka 1980.
Picha kwa hisani ya Meritxell Donadeu Picha kwa hisani ya WRENmedia

Mtizamo wa Biashara wa GALVmed

Ukweli

Bilioni 1.1 yawatuwanaishi kwa pato la chini ya dola 1

kwa siku

(Bill & Melinda Gates Foundation)

Karibu bilioni 2.5 yawatuwanaishi kwa pato la chini ya

dola 2 kwa siku

(Bill & Melinda Gates Foundation)

Bilioni 1.02 yawatu hawana chakula cha kutosha – idadi

hii ni zaidi yawananchiwanaoishi Amerika, Kanada

pamoja na Jumuia ya Ulaya

(FAO 19 June 2009)

Licha yaMalengo yaMaendeleo yaMilenia, idadi ya watu

wasio na lishe bora duniani imeongezeka na

kufikiamilioni 75mwaka 2007 namwaka 2008 kufikia

milioni 40, na sababu kubwa ni ongezeko la bei ya

chakula

(FAO 9 Dec 2008)

Kati yawatotomilioni 9.7, asilimia 53%yawatoto

wanakufa kwa kosefuwa lishe bora katika nchi

zinazoendelea kilamwaka – mtotommoja kila sekunde 6

(FAO 2004)

Ni asilimia 4%tu yamsaadawa kimataifa ndiyo

inatumika katika shughuli za kilimo duniani

(World Bank, 2007).

Malengo muhimu

> Uongozi

> Mtizamo

> Mikakati

> Ushirikiano

> Utaratibu waMaendeleo

> Kutafuta njiampya

> Usimamizi + Ukadiriaji

Lengo la 1

Kuandaa nyenzo za kufanya maamuzi kwa kuzingatia

takwimu juu ya athari za kiuchumi na kijamii na

uelewa wa masoko

Lengo la 2

Kutengeneza chanjo dhidi ya magonjwa 6 ya

wanyama ambazo ni muhimu katika kupunguza

umasikini na maisha ya watu

Lengo la 3

Kushughulikia Utumiaji, Upatikanaji, Ugawaji

mlolongo wenye faida na kuelezea juu ya maendeleo

endelevu

Lengo la 4

Kurahisishamawasiliano + mtandao katika ngazi zote

ili kuwe na uwezo wa kufuatiliamabadiliko yamipango

na utekelezaji
Wasiliana na GALVmed:

Ofisi ya Uingereza:

Doherty Building, Pentlands Science Park, Bush Loan, Edinburgh EH26 0PZ, UK

Simu: +44 (0)131 445 6264

Nukushi: +44 (0)131 445 6222

Barua peper: info@galvmed.org

Ofisi ya Afrika:

Ghorofa ya Kwanza, Tawi la Magharibi, A.K.D. House II, Fairgrounds, Kitalu No. 54478,

Gaborone – Botswana, S.L.P. 45108, Gaborone

Simu: +267 3121 202/203/209

Barua pepe: info@galvmed.org

www.galvmed.org

Kwa sasa inafadhiliwa na:

GALVmed imesajiliwa kama shirikisho la kiulimwengu la kimsaada na lisilo la kibiashara linalohusisha ubia wa sekta ya umma, sekta binafsi na serikali.

Imesajiliwa Scotland kama shirika la msaada SC039197 Imesajiliwa kama shirika la msaada England na Wales: 1115606

Jina la usajili: Global Alliance for Livestock and Veterinary Medicines

Imesajiliwa England na Wales Na. 5393391, kwa ukomo wa udhamini

Ofisi ya usajili: Maclay Murray & Spens, One London Wall, London EC2Y 5AB, UA