21.06.2013 Views

HOTUBA ILIYOTOLEWA NA PROFESA

HOTUBA ILIYOTOLEWA NA PROFESA

HOTUBA ILIYOTOLEWA NA PROFESA

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

HOTUBA ILIYOTOLEWA NA

PROF. JOHN HABWE WA CHUO KIKUU CHA

NAIROBI KATIKA SIKU YA MWISHO WA

MWAKA KATIKA SHULE YA UPILI YA

TAREHE 12- APRILI 2013

Utangulizi

MAUTUMA

KAUNTI YA LUGARI

Wageni waalikwa, walimu, halmashauri ya shule ya

Mautuma, wazazi, wanafunzi, mabibi na mabwana. Nina

furaha isiyo kifani kupata fursa hii ya kuzungumza nanyi

katika siku hii muhimu ya muktano wa mwaka. Furaha

yangu inatokana na umaarufu wa shule hii, nafasi yake

katika kaunti ya Lugari nzima na taifa la Kenya kwa jumla.

Na kwamba shule hii ndiyo tegemeo letu la siku za usoni

Ninapopata fursa ya kuzungumzia suala la elimu kama leo

ninapata ugumu fulani kwa sababu ya wepesi wa suala

lenyewe na kwa wakati huo mmoja ugumu wa suala hilo .

Maswali hunijia akilini mara moja.

1) Je, elimu bado ni muhimu katika wakati huu?

2) Je, ni kweli mtoto anaweza kuasi elimu na mambo

yakamwendea sawa?

3) Je, kijana asipopata elimu atashughulika na nini na vipi?

4) Je,jamii ingali na nia ya kujitolea mhanga kufanya lolote

almradi kusomesha vijana?

5) Je, kesho ya msichana katika juhudi hizi ni ipi?

6) Je, elimu bado imefungwa kwenye suala la kazi?

Tunapowazia maswali haya kwa makini ndipo tunapopata

changamoto kubwa ya kushughulika na juhudi ya kutafuta

elimu kutwa kucha. Lakini safari hii ya kutafuta elumu ina

matatizo na changamoto zake chungu nzima. Ni kama njia

ndefu inayoelekea mgodini kuliko na almasi, dhahabu na

fedha lakini yenye mikosi, majukumu na wakati mwingine

hata kuvunja moyo.Lazima niseme elimu na sawa na

JUHUDI. Pia elimu ni kitu ambacho kimejikita kwenye

neno UTEUZI. Ni kitu cha hiari lakini ambacho kina

fanaka ukikiteua mradi uwe na subira na uvumilivu.

Mwanafunzi lazima aweze kuhiari kusoma na mzazi awe

na hiari kumsomesha mwanawe.Ikiwa wana hiyo hiari

lazima waweze kutafakari na kutekeleza mambo yafuatayo:

a) Nidhamu na maadili

Ulimwengu una maendeleo makubwa. Maendeleo haya

yamelifanya gumu zaidi suala la nidhamu na maadili

ambalo tayari lilikuwa gumu hapo awali. Mtandao umeleta

mawasiliano ya haraka miongoni mwa vijana. Licha ya

manufaa yake kuna madhara yake pia. Suala la madawa ya

kulevya limekuwa sugu hapa nchini Kenya linaathiri vijana

wetu- wake kwa waume.

Wanafunzi wetu wengi wamejipata katika vita hivi vya

kijamii ambapo maadili yanamomonyoka kwa wepesi wa

ajabu.Ningependa kuwauliza swali. Je,wanafunzi

wanaweza kupita mtihani bila kuwa na maadili mema?

Haiwezekani! Kupita mitihani kunakwenda moja kwa moja

na maadili mema na nidhamu sio shuleni tu bali nyumbani

pia. Sio sasa tu bali hata katika maisha ya baadaye. Walimu

wamekabiliwa na shida kubwa ya kupambana na

wanafunzi wasio na maadili mema ili kuwafanya waache

ili wasiweze kuwaambukiza wanafunzi wengine kusumba

ya kiburi, usodai, udanganyifu, dharau , ulevi, nk. Lakini

changamoto na shida kubwa ya walimu hasa wale walio

katika idara ya ushauri shuleni ni kwamba, wazazi

wametekeleza jukumu lao la kawaida katika kuinua hali ya

maadili ya watoto wao. Licha ya kutotekeleza jukumu hili

wazazi pia wanaudhika watoto wao wakirekebishwa. Kazi

ya wazazi imekuwa ni kuwatendekeza watoto wao kwa

kuwaita “ Mummy” na “Daddy” na kudhani ati watoto wao

ni watu wazima.

b) Kuhimili Mwalimu

Walimu wengi wanataka wanafunzi wapite mitihani yao.

Lakini wanakosa nyenzo za kimsingi za kuwasaidia

kutekeleza kazi hii. Tunaweza kuuliza Je, inawezekana

mwalimu kusomesha Jumamosi bila chai au bila chakula

cha mchana?

Hapana! Haiwezekani! Taasisi nyingi zimeamua kumsaidia

mwalimu. Jinsi mbili ni muhimu katika kumhimili

mwalimu. Kwanza kwa kumheshimu. Pili kwa kumpa

usaidizi autakao. Na usaidizi huu ni muhimu zaidi ikiwa

wanafunzi anaoshughulika nao ni wale watakao msaada

zaidi “ slow learners” maarufu katika Kiingereza. Ninajua

wazazi wana mizigo mingi lakini ningependa

kuwakumbusha kuwa huu pia ni mzigo mwingine

unaotaka muushughulikie. Japo sasa ni mzito katika siku

za baadaye utakuwa mzito zaidi. Afadhali kumwelimisha

mwanao badala ya kumkimu na kumsaidia yeye na familia

yake uzimani wakati ambapo utakuwa huna nguvu au

uwezo.

c) Suala la Karo

Karo ndio msingi wa shule yoyote. Ningependa

kuwahimiza wazazi muilipe mapema iwezekanavyo ili

watoto wenu watunzwe vyema. Bila karo shule haiwezi

kutekeleza majukumu yake ya kimsingi kama vile kununua

chakula, kujenga na na kukarabati sehemu ambazo huwa

zimeharibika . Moja katika sifa za shule ambazo hupita

katika mitihani ni ulipaji wa mapema wa karo ili shule

ipange mikakati na mambo yake mengine mapema ya

kujiendesha. Hatungependa hali ambapo mkuu wa shule

badala ya kufundisha, kusimamia shule shughuli yake

nyingine iwe kuzunguka katika madeni na wadeni ili

kukopa maziwa, mkate, nyama ili kuendesha shule hali na

wazazi nyinyi mmekaa raha mustarehe. Ninajua uchumi

wetu umemwelemea mzazi na kumwia mzito lakini ombi

hili nalitoa kama rafiki yenu na pia kama mzazi

mwenzenu.

d) Kutambua vipawa vya watoto wetu

Wazazi wenzangu ningewaomba muwasaidie watoto wenu

kutambua vipawa vyao. Nyinyi ndio mnaokaa nao kuliko

hata walimu wala msiwalazimishe watoto wenu kufanya

mambo hawataki. Ikiwa watoto wenu wana utashi na

hajana na mambo fulani wasaidieni kuyapata. Msilazimishe

watoto wenu kuwa wahandisi kama wanataka kuwa

walimu. Wala msiwalazimeshe kusomea udaktari kama

wanataka kuwa marubani. Pia msiwalazimishe kuwa

mameneja ikiwa watakachokuwa ni wanamuziki. Acheni

wafanye kazi waitakayo. Lakini muhimu kwanza ni

kuwapa msingi wa elimu kwa kulipa karo mapema na

kuwasaidia katika kitu wanachokitaka kutegemea uwezo

wenu.

e) Kuwasikiliza na kuwa na wakati nao.

Wazazi wengi mimi nikiwa mmoja wao hawana muda na

watoto wao. Hii ni kwa sababu ya pilkapilka za kazi na

shughuli nyingine za maisha .Wazazi wengi hawajui tabia

za watoto wao hata wanapoingilia madawa ya kulevya

hushtuka. Kwa mfano, kuna wazazi wasiojua kama Watoto

wao wako kidato cha pili au tatu. Hii ndiyo sababu mzazi

anapoelezwa mwanawe anafanya jambo fulani anasema

kuwa mwanawe hawezi kufanya hivyo hali inayopelekea

ugumu katika kumsaidia na kumrekebisha. Tutengeni

muda na wanaetu ili wapate kusoma na kufaulu maishani.

Wasaalam,

Prof. Hamu Habwe

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!