yaliyomo - The Foundation for Civil Society
yaliyomo - The Foundation for Civil Society
yaliyomo - The Foundation for Civil Society
- No tags were found...
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
YALIYOMO

UTANGULIZI .........................................................................................................................3

1. MAELEZO YA FOUNDATION............................................................................................4

1.1 Dira .........................................................................................................................4

1.2 Lengo........................................................................................................................4

1.3 Misingi......................................................................................................................4

2. Maelezo ya maana ya maneno tunayotumia: Tunavyomaanisha katika

maneno tunayotumia ...............................................................................................5

3. Nani anaweza kuomba ruzuku...............................................................................6

3.1 Matawi ya mashirika makubwa.................................................................................7

3.2 Makundi yanayoshirikiana.........................................................................................7

4. Programu ya ruzuku.................................................................................................7

5. MAENEO YANAYOFADHILIWA NA FOUNDATION..........................................................8

5.1. Ushiriki wa kutunga sera na kutekeleza (sera)............................................................8

5.2 Kuimarisha utawala bora na haki za binadamu (utawala)...........................................9

5.3 Kuimarishwa kwa Uwezo wa Asasi za Kiraia...........................................................10

6. MAENEO AMBAYO HAYATAFADHILIWA NA FOUNDATION.........................................11

7. Jinsi ya kutuma maombi ..........................................................................................12

7.1 Nyaraka zinazotakiwa.............................................................................................12

7.2 Matawi ya mashirika makubwa...............................................................................13

7.3 Makundi yanayoshirikiana.......................................................................................13

7.4 Ufadhili wa mradi mkubwa, wenye washirika wengi...............................................13

8. WADHAMINI..................................................................................................................14

8.1 Nani anastahili kuwa mdhamini wa maombi yako.................................................14

8.2 Maoni ya wafadhili..................................................................................................15

9. Mara ngapi waweza kutuma maombi.................................................................15

9.1 Kama umeshawahi kupata fedha kutoka Foundation siku za nyuma........................15

9.2 Utumaji wa maombi ya ruzuku...............................................................................15

10. Nini kinatokea katika maombi yako.....................................................................15

10.1 Vigezo vya tathmini.................................................................................................16

10.2 Asasi yako..............................................................................................................16

10.3 Mradi wako.............................................................................................................16

10.4 Mambo yako ya kifedha..........................................................................................17
10.5 Kama maombi yako hayakufanikiwa (kukubaliwa)...................................................17

11. Mwongozo wa bajeti...............................................................................................18

11.1 Gharama za usafiri..................................................................................................18

11.2 Malazi na gharama za chakula................................................................................18

11.3 Kupitisha matumizi kwa kutumia risiti tu.................................................................19

11.4 Malipo ya ushiriki....................................................................................................19

11.5 Honoraria/Tunzo isiyodaiwa....................................................................................19

11.6 Gharama za uendeshaji & utawala / Mishahara / Mtaji............................................19

12. Uangalizi/ UFUATILIAJI..............................................................................................20

13. Jinsi ya kujaza fomu za maombi ya ruzuku.......................................................20

14. MASUALA unayostahili kuyajua.............................................................................25

14.1 Maombi ya ruzuku..................................................................................................25

14.2 Masharti ya ruzuku..................................................................................................25

15. Viambatisho................................................................................................................26

15.1 Kiambatisho 1: Wadhamini wa Ufadhili..................................................................26

15.2 Kiambatisho II: Mpango wa Mafunzo .....................................................................27

15.3 Kiambatisho III: Muundo wa Upangaji wa Bajeti.....................................................28

15.4 Kiambatisho lV: Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini.................................................29
UTANGULIZI

Tunawakushukuru kwa kuonyesha nia ya kushirikiana na Foundation for Civil Society. Kila kitu

unachotaka kujua kuhusu ruzuku na namna ya kuomba kipo katika mwongozo huu. Tafadhali

yasome maelezo haya kwa makini kabla ya kujaza fomu yako.

Ndani ya mwongozo huuutapata maelezo juu ya nani anaweza kuomba ruzuku, nini tunakiangalia

katika kufikiria maombi husika, namna ambavyo maombi yako yatashughulikiwa, na namna ya

kujaza fomu ya maombi. Fomu za maombi zinapatikana katika lugha za Kiingereza na Kiswahili.

Wafanyakazi wa Foundation wanao wajibu wa kutoa ufafanuzi wa vipengele vya fomu ya maombi

vinavyoleta utata na hali ya maombi yako kwa njia ya simu, nukushi, barua au barua pepe.

Kama unataka kujadili swali lolote linalohusu fomu yako, tafadhali ipigie kwanza ofisi yetu ili iweze

kupanga muda wa mkutano na mmoja wa wafanyakazi wa Foundation. Nafasi za miadi zinapatikana

Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 8:00 - 9:30 alasiri.

Fomu za maombi zinapatikana kati ya Jumatatu hadi Ijumaa toka saa 2.30 asubuhi - 10.00 jioni.

Kama huwezi kufika katika ofisi zetu kwa ajili ya kuchukua fomu za maombi unaweza kupiga simu,

kuandika barua pepe au kutuandikia barua ya kawaida na tutakutumia kifurushi cha fomu. Pia fomu

za maombi zinapatikana katika tovuti ya Foundation www.thefoundation-tz.org.

Foundation utaipata kupitia

The Foundation for Civil Society

Haidery Plaza, Ghorofa ya tano,

Mtaa wa Upanga/Kisutu,

S.L.P 7192,

Dar-es-Salaam,

Tanzania.

Simu: 022 - 2138530 / 2138531 / 2138532, 0754 - 005708

Nukushi: 022 - 2138533.

Barua pepe: information@thefoundation-tz.org

Tovuti: www.thefoundation-tz.org
1. NINI MAANA YA FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY

Foundation for Civil Society (Foundation) ni asasi huru iliyoanzishwa Tanzania kama Kampuni

isiyozalisha faida, inayofadhiliwa na wabia wa maendeleo wenye mawazo yanayofanana, na

kuongozwa na Bodi iliyo huru.

1.1 Dira

Dira ya The Foundation ni ‘Tanzania ambayo wananchi wake wamewezeshwa kutambua haki zao

na kushiriki katika michakato ya mabadiliko ambayo itaboresha hali zao za maisha.’

1.2 Dhima

Kuwawezesha wananchi kupitia utoaji wa ruzuku, kuwezesha kuundwa kwa mitandao na kuwezesha

utamaduni wa kujifunza pasipo ukomo katika Sekta ya Asasi za Kiraia.

1.3 Maadili ya Msingi

The Foundation inaahidi kutekeleza maadili yafuatayo:

Haki

Tutafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba huduma zetu haziwi za kibaguzi na kuzingatia

misingi ya usawa kuwa ndio mwongozo wa kazi zetu.

Uadilifu

The Foundation na wafanyakazi wake watatenda na kuhubiri uadilifu, katika miundo yake

yote, na katika shughuli zetu zote. Tutaendeleza sera ya ‘Kutovumilia Hata Kidogo’ aina zote

za rushwa, za ndani na nje ya Foundation.

Uweledi

Tutaukuza na kuuendeleza utamaduni ambapo wale wote wanaokutana nasi watahudumiwa

kwa uweledi, upole na heshima wakati wote. Tutajenga na kujivunia utamaduni wenye misingi

ya ubora na ufanisi, na kuwawezesha wale wote wanaofanya kazi na The Foundation waige

mfano huo katika shughuli zao zote.

Uwazi na Uwajibikaji

Tutakuwa wazi, hatutaficha na tutakuwa waaminifu. Tutawasilisha kwa uwazi yale yote

tunayoyafanya kwa kuzingatia itifaki za kutunza siri. Tutawajibika kwa vitendo vyetu na kwa

wale tunaowahudumia.

Usawa wa Jinsia

Tutajitahidi kuhakikisha kwamba masuala ya jinsia yanaingizwa kama ajenda rasmi katika

shughuli zetu zote, na tutawasaidia wapokearuzuku na wabia wetu waone umuhimu wa

kuzingatia jinsia.

Foundation haina nia ya kuwa mwakilishi wa asasi za kiraia au kuzungumza kwa niaba yao, bali

kujenga uwezo wa asasi hizo kwa kutumia utaratibu ulio ratibiwa vyema kukiwa na viwango vya

juu vya uwajibikaji, uwazi, ubora na matokeo.
2. Maelezo ya maana ya maneno yaliyotumika

Uwajibikaji

Utetezi

AZAKi

Consortium

Mjumbe

Katiba

Mali iliyowekwa wakfu

(endowment)

Usawa wa jinsia

Utawala

Rasilimali

Mabadiliko/ matokeo

ya muda mrefu

Uchukuaji wa dhamana kwa matendo yanayofanyika katika utendaji wa

shughuli stahiki.

Mchakato wa kushawishi mabadiliko ya sera, utetezi unaweza kutumika

kuelezea udhaifu wa sera, au mapungufu yaliyopo katika sera au sera

ambazo zipo lakini hazifuatwi.

Asasi zilizoundwa nje ya mfumo wa serikali ambazo huwezesha

wananchi kueleza mawazo yao na kuyafanyia kazi kwa pamoja kufikia

lengo lililokusudiwa. (Yaani Asasi za Kiraia).

Ni muunganiko wa makundi tofauti ambayo yanashirikiana kufikia lengo

ambalo ni moja.

Mwanachama au mmoja wa wafaidika wanaowakilishwa na asasi au

binafsi.

Hati ya kisheria yenye vipengele vifuatavyo:

- Jina la taasisi, madhumuni ya uwepo na malengo.

- Maelezo ya kufikiwa kwa malengo.

- Maelezo ya namna ya taasisi inavyoongozwa na kusimamiwa.

- Maelezo ya jinsi watu wanavyojiunga katika taasisi.

- Sahihi za viongozi na siku ya asasi kupitisha katiba.

Kiasi cha fedha kinachotolewa kwa kampuni au asasi kwa lengo la

kuzalisha fedha badala ya kutumia mara moja. Faida inayopatikana

sehemu inatumika kuendeshea mhimili muhimu wa asasi husika na

faida iliyobaki inagawiwa tena kutokana na sheria za ufadhili wa fedha

ili kuhakikisha uongezekaji wa ukuaji kwa ajili ya riba zaidi na shughuli

za baadaye za asasi husika.

Ni pale ambapo mwanaume na mwanamke wanakuwa na nafasi sawa

na kuelewa vizuri haki zao za binadamu na umuhimu katika kushiriki

na kupata faida za maendeleo ya kitaifa, kisiasa, kiuchumi, kijamii na

kitamaduni kwa kuzingatia haki za binadamu.

Sheria na kanuni zinazotakiwa kufuatwa katika uendeshaji na utekelezaji,

na ushirikiano wa nje wa asasi mbalimbali na serikali.

Shughuli unazofanya ambazo zitaleta huduma zinazokusudiwa na mradi.

Tofauti ya muda mrefu ambayo imechangiwa na mradi huo katika

kuyabadili maisha ya watu.
Wanachama

Isiyoendeshwa kwa

Mabadiliko

Matokeo ya awali

Sera

Mtandao wa usalama

Mtaji jamii

(Social capital)

Foundation

Makundi yaliyo katika

hali hatarishi

Watu wanaohusika na asasi fulani. Asasi pia zinaweza kuwa

wanachama.

Fedha zinazopatikana na kuwekwa katika shughuli kwa ajili ya umma si

kwa ajili ya mtu binafsi.

Kitu ambacho kitaonyesha tofauti moja kwa moja katika utoaji huduma

kwa watu na asasi, na mafanikio ambayo asasi itayapata.

Mabadiliko ya moja kwa moja ambayo huduma yako itatoa kwa wale

wanaofaidika na mradi.

Sera ni muongozo, kanuni au maamuzi ambayo yanaziongoza au

yanayoonyesha shughuli za watu au makundi ya watu. Sera zinaweza

kuwepo katika maumbo na ukubwa wa aina zote, katika ngazi ya kijiji

hadi mkoa, ngazi za kitaifa na kimataifa.

Juhudi za jamii za kujihami na kujitoa kwa wale waliopo katika mazingira

magumu miongoni mwao.

Sheria na wajibu ulio ndani ya majukumu ya kijamii yanayowawezesha

watu kufikia malengo yao binafsi na yale ya kijamii.

Foundation for Civil Society.

Wale watu ambao wamebaguliwa kutokana na mazingira yao

na wapo hatarini. Wanaweza kuwa wazee, watoto, wenye VVU/

UKIMWI, wakimbizi yatima n.k.

3. Nani anaweza kuomba ruzuku

Tunakaribisha maombi kutoka kila pembe ya nchi yetu. Asasi yako inaweza kuomba ruzuku kutoka

Foundation kama ni:

• Asasi isiyo ya Kiserikali (NGO)

• Asasi ya Kijamii (CBO)

• Chama cha Kitaalamu

• Chama cha Wafanyakazi

• Chombo cha Habari

• Chama cha Ushirika 2

• Chama cha Kidini 3

1 - 2 Foundation inaweza kutoa ruzuku kwa vyombo vya habari, vyama vya ushirika kama fedha zinazoombwa kwa ajili ya mradi hazichangii

kuwapatia wao faida, kulipa madeni, kulipa gharama za uendeshaji, na mradi umelenga kuisaidia

3 Kumbuka kuwa makanisa na misikiti sio sehemu ya asasi za kidini
Na kama:

• Taasisi yako imesajiliwa Tanzania Bara au Visiwani.

• Kama umeandikishwa kama chama kisichotengeneza faida.

• Una katiba au kanuni za uendeshaji ambazo zinatambuliwa kisheria zikiwa zinaeleza wazi

madhumuni ya asasi yako na namna ambavyo unaiendesha.

• Asasi yako ina akaunti ya benki ambayo imekuwa na watia saini/sahihi zaidi ya mmoja.

(i) Foundation inaweza kutoa ruzuku kwa vyombo vya habari vyama vya ushirika kama

fedha zinazoombwa kwa ajili ya mradi hazichangii kuwapatia wao faida, kulipa madeni,

kulipa gharama za uendeshaji, na mradi umelenga kuisaidia jamii.

(ii) Taasisi ambazo zinajishughulisha na fedha kama kuweka na kukopa katika ngazi za vyama

vya ushirika au wakopeshaji wadogo au wale ambao wanashughulika na uwezeshaji wa

kifedha kwa lengo la uzalishaji watatakiwa kujieleza kwa undani zaidi kama watataka fedha

kutoka Foundation kwa lengo la kufanya shughuli nyingine zaidi ya zile wanazozifanya.

(iii) Foundation for Civil Society haitoi ruzuku kwa AZAKi za kimataifa (INGOs).

3.1 Matawi ya mashirika makubwa

Asasi ambayo ni tawi la asasi kubwa inaweza kuomba ruzuku kama itaonyesha wazi kwamba

inajiendesha bila kutegemea makao makuu yake.

3.2 Makundi yanayoshirikiana (consortia)

Foundation inashawishi asasi mbalimbali kufanya kazi kwa pamoja ili kutatua tatizo moja. Na kama

asasi mbili au zaidi zitaomba ruzuku kwa pamoja zitachukuliwa kama kundi la asasi.

4. Programu ya ruzuku

Jedwali lifuatalo linaonyesha kiasi cha ruzuku kinachotolewa, tarehe ya mwisho ya kupokea maombi,

na kipindi hadi utoaji wa ruzuku. Kuna aina nne za ruzuku ambazo zinatolewa na Foundation.

Aina ya ruzuku na tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi

Aina ya Ruzuku Kiwango

cha juu

kwa

mwaka

Muda wa

juu wa

ruzuku

Muda wa

mwisho wa

kuomba

Ruzuku Kubwa

(SG)

Ruzuku ya

kiwango cha

kati (MG)

Ruzuku ndogo

(RDG)

Ruzuku ya

Usajili (RDG)

Shilingi

Milioni

125

TZS

Milioni 45

Milioni

7.5

Laki mbili

(200,000)

Miaka 3 Machi 1

Julai 1

October 1

Miaka 3 Machi 1

Julai 1

Oktoba 1

Mara

moja

Mara

moja

Machi 1

Julai 1

Oktoba 1

Machi 1

Julai 1

Oktoba 1

Taarifa kwa

walioleta

fomu za

maombi

Kama ikipitishwa

fedha hutolewa

katika kipindi cha

Wiki 16 Wiki 24

Wiki 8 Wiki 16

Wiki 8 Wiki 16

Wiki 8 Wiki 16
Tunashauri uwasilishaji wa fomu za maombi mapema zaidi kabla ya tarehe wa mwisho

Idadi ya maombi yanayoweza kushughulikiwa katika kila mkupuo mmoja ina kikomo kutokana na

wingi wa mahitaji. Maombi yatapewa kipaumbele kulingana na yalivyowahi kufika kwa msingi wa

“Kuwahi kufika, kuwahi kushughulikiwa”, na utapewa taarifa kama fomu yako haitashughulikiwa

katika muda ambao umeombea.

Waombaji wa ruzuku wanaruhusiwa kutuma maombi kupitia tovuti moja kwa moja LAKINI wanatakiwa

kuhakikisha kwamba wanatuma pia fomu zilizotiwa saini na viambatanishi vya muhimu.

Maombi yanayofika ofisini baada ya tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kupita hayatashughulikiwa na

yatarudishwa kwa muombaji.

Ushiriki katika ufadhili wa pamoja

Foundation ipo tayari kuchangia sehemu ya ufadhili kwenye mradi mkubwa ambao umefadhiliwa

pia na wafadhili wengine. Unachotakiwa kufanya ni kuonyesha wazi ni sehemu gani Foundation

inaombwa kusaidia.

5. MAENEO YANAYOFADHILIWA NA FOUNDATION

The Foundation for Civil Society itafadhili maombi yote ambayo yamelenga kufanya shughuli

mbalimbali kusaidia watu maskini na wenye mahitaji na hasa katika maeneo lengwa yafuatayo:

5.1. Ushiriki katika utungaji wa sera na utekelezaji wake

Sera inaweza kuelezwa kama kanuni ambazo kwazo serikali, vyama vya siasa, kampuni za biashara

na asasi za kiraia, n.k. huongoza utekelezaji wa shughuli zake kwa umma au sheria katika utekelezaji

wake. Kwa maneno mengine Sera ni mpango wa utendaji au maelezo ya nia na mawazo.

Wajibu wa asasi za kiraia ni muhimu ili kuruhusu sauti za watu zisikike katika mchakato wa

kutunga sera. Foundation inasaidia miradi na asasi ambazo zinaiwezesha jamii kujihusisha katika

kutengeneza, kushirikiana na kutangaza sera; na ufuatiliaji na utekelezaji wa sera. Foundation

itatoa ruzuku kwa miradi na asasi ambazo zitaiwezesha jamii kujihusisha katika kutengeneza,

kushirikiana na kuitangaza sera, pamoja na ufuatiliaji na utekelezaji wa sera. Foundation itafadhili

miradi itakayowezesha sekta ya asasi za kiraia kuchangia katika kuimarisha uwezo wa wananchi

kushiriki ipasavyo katika michakato ya sera ili waweze kuchangia katika jitihada za kupunguza

umasikini. Miradi iliyoandikwa vyema yenye sifa zifuatazo itafikiriwa kupata ruzuku:

• Ile yenye uwezekano wa kuongeza kuzingatiwa kwa sera, sheria na kanuni za maendeleo ya

taifa,

• Ile yenye uwezekano wa kupunguza vikwazo vya kisera, kisheria na usimamizi vinavyoathiri

utoaji mzuri wa huduma,

• Ile inayoweza kuchochea mabadiliko ya sera na utendaji ili kushughulikia mahitaji ya makundi

yaliyo hatarini na pembezoni,

• Ile inayoweza kuwahusisha na kushirikisha jamii, hususani wanawake, watoto, watu wenye

ulemavu, masikini, makundi yaliyo hatarini na yaliyotengwa, katika kupanga vipaumbele kwa

ajili ya kuunda sera katika ngazi zote.

• Miradi ambayo inaweza kuongeza ufahamu wa wananchi kuhusu ubaguzi wa kijinsia, kutafsiri

sera za jinsia na kuwezesha ushiriki wa wanawake na watu waliopo katika makundi mengine
ya waliotengwa, katika kupanga vipaumbele vya uundaji wa sera katika ngazi zote.

• Miradi yenye uwezekano wa kuinua uelewa wa wananchi juu ya sera na athari zake katika

maendeleo.

• Miradi inayoweza kuongeza ushiriki wenye tija wa wananchi katika michakato ya sera (kutunga,

kutekeleza na kufuatilia)

• Miradi inayoweza kuchangia kuongezeka kwa rasilimali zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji

wa sera maalumu.

• Miradi inayoweza kuleta uraghibishi katika uwajibikaji na kujipanga vizuri kwa mikutano

ya vijiji, kamati za maendeleo za kata na baraza kamili la madiwani la wilaya ili kuruhusu

ushirikishwaji wa mwananchi na michakato ya sera ya mahali husika.

• Miradi inayohakikishia kuzingatiwa kwa sera za kitaifa na kimataifa zinazoshughulikia mahitaji

ya makundi maalumu.

Mifano ya shughuli zilizopo chini ya ushiriki katika utungaji wa sera na utekelezaji wake ni pamoja na:

• Ufuatiliaji wa miradi shirikishi ya kupunguza umasikini, ambayo inalinganisha na kutofautisha

habari juu ya umasikini na kuzisambaza eneo pana

• Kupanga mipango ndani ya jamii juu ya jinsi mabadiliko ya sera fulani yanavyoathiri maisha

yao na jinsi watakavyoitikia

• Ushiriki wa jamii katika kupanga vipaumbele kwa ajili ya sera za kitaifa

• Kuinua ufahamu wa umma juu ya masuala ya sera

5.2 Kuimarisha utawala bora na haki za kiraia

Azaki ni vyombo muhimu vya kuhakikisha kwamba taasisi za umma zinafanya kazi katika mazingira

ya uwazi na kwamba watu wanaelewa kuhusu haki zao. Foundation husaidia asasi zote ambazo

zinaamsha uelewa wa watu kuhusu haki zao na majukumu ya serikali, kuimarisha ushirikiano kati

ya asasi zinazofanya kazi katika masuala ya haki za binadamu katika ngazi za chini na kitaifa na

kuongeza upatikanaji wa haki kwa wananchi wote wa Tanzania.

Utawala bora unaweza kufafanuliwa kama ifuatavyo:

• Kuheshimu kikamilifu haki za binadamu,

• Jamii inayothamini wajibu na majukumu yake ya kiraia,

• Utawala wa sheria,

• Ushiriki athirifu,

• Ubia unaohusisha watendaji wengi pamoja na wingi wa vyama vya siasa

• Uwazi

• Michakato inayowajibika ndani na baina ya taasisi

• Sekta za umma, binafsi na asasi za kiraia zilizo na ufanisi na zenye kutimiza majukumu yao,

• Uhalali, upatikanaji wa maarifa, habari na elimu,

• Uwezeshaji wa watu kisiasa, usawa, uendelevu, misimamo na maadili ambayo inajenga

kuwajibika, mshikamano na kuvumiliana.

Foundation itatoa ruzuku kwa miradi ambayo itawezesha taasisi za serikali, umma na binafsi kuwa

wazi zaidi, kuwajibika na kuheshimu utawala wa sheria na haki za binadamu. Mahususi, Foundation

itafadhili miradi ambayo itahakikisha wananchi wanafahamu haki na wajibu wao, waweze kudai

uwajibikaji kutoka katika rasilimali za umma na hivyo miradi itakuwa na athari chanya katika

maeneo yafuatayo:

• Kuongezeka kwa uwezo wa wananchi, wake kwa waume, kupata habari juu ya shughuli za
Mamlaka za Serikali za Mitaa ambazo zinagusa jamii (katika eneo lile),

• Kuongezeka kwa uwajibikaji wa kijamii kwa mamlaka husika za umma na binafsi,

• Kuongezeka kwa ushiriki wa watu katika mikutano ya kijiji au serikali za mitaa,

• Kuhakikisha kwamba rasilimali za umma na vitegauchumi vinasambazwa kwa usawa na kwa

ufanisi na kusimamimiwa katika ngazi za vijiji na mitaa,

• Kuhakikisha panakuwepo na sheria na kanuni zinazotosheleza ambazo zinadhamini

kuheshimiwa kwa haki za binadamu

• Kuhakikisha kwamba mipango na bajeti za taifa na wilaya zinajumuisha na kushughulikia

mahitaji ya makundi maalumu

• Kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoripoti kuridhishwa na mfumo wa sheria

• Kuongezeka kwa ushiriki wa wananchi katika programu za elimu ya uraia na mpiga kura

• Kuimarisha uwajibikaji kati ya wananchi na viongozi wao waliowachagua, kama vile Madiwani

na Wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Mifano ya shughuli chini ya Utawala Bora na Uwajibikaji ni pamoja na:

• Mikutano ya hadhara juu ya sera za taifa

• Vipindi vya radio juu ya masuala ya utawala bora kama vile rushwa

• Michezo ya kuigiza shirikishi inayoamsha uelewa wa haki za binadamu

• Mafunzo ya viongozi wa asasi za kiraia na serikali za mitaa juu ya mabadiliko katika wajibu

na majukumu chini ya maboresho ya serikali za mitaa.

5.3 Kuimarishwa kwa Uwezo wa Asasi za Kiraia

Nia ya The Foundation for Civil Society ni kuhakikisha kwamba Asasi za Kiraia zinakuwa nguzo

imara ya kuleta mabadiliko; kufanikisha malengo yake yaliyokusudiwa na inatekeleza wajibu wake

wa utetezi kwa vipaumbele vya maendeleo. Tunapenda kuona sekta ya asasi za kiraia yenye ari,

ubunifu, inayotimiza majukumu yake, endelevu na inayowajibika; ambayo inachangia kikamilifu

katika kuleta mabadiliko ya kudumu katika maendeleo nchini Tanzania. Tunaelekeza nguvu zetu

katika maendeleo ya asasi moja moja na mitandao. Lengo la itikadi hii ni kuzifanya asasi za kiraia

zionekane na ziweze kutekeleza kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yaliyo chanya.

Kama sehemu ya uimarishaji wa uwezo wa asasi za kiraia, The Foundation itahakikisha uwepo wa

muunganisho miongoni mwa asasi za kiraia katika kupeana habari na kujifunza, na kuwezesha

utetezi imara uweze kufanyika. Wakati huo huo, asasi moja moja zinahitaji kukua ili ziweze kufanya

utetezi ulio na tija.

Mahususi The Foundation itafadhili maombi ambayo yanachangia katika mambo yafuatayo:

• Kuboresha uwezo wa utawala, usimamizi na utendaji wa AZAKi na mitandao nchini

Tanzania

• Kuongezeka kwa uwiano wa AZAKi zenye mifumo imara ya usimamizi wa fedha yenye vyanzo

vya fedha vinavyotosheleza na endelevu,

• Kuongezeka kwa kuunganisha mitandao miongoni mwa AZAKi ili kuhakikisha upatikanaji rahisi

na kupeana habari, na kuwa na sauti ya pamoja katika masuala mbalimbali ya maendeleo,

• Kuongezeka kwa uwezo wa AZAKi katika kuwa na utaalamu maalumu wa sekta mbalimbali

na kutumia mbinu za uweledi katika masuala ya maendeleo,

• Kuboreka kwa AZAKi katika kujiingiza kwenye masuala ya sera.

• Kuboreka kwa uwezo wa AZAKi katika kuandika mapendekezo ya miradi

• Kuongezeka kwa uwazi, kujihusisha, ushiriki na uwajibikaji kwa walengwa wao

10
• Kuongezeka kwa hadhi ya kisheria ya asasi moja moja na mitandao.

Mifano ya shughuli zilizopo chini ya Uimarishaji wa Asasi za Kiraia ni pamoja na:

• Kuimarisha mitandao

• Kujenga uwezo

• Kuunda na kusaidia mitandao ya wilaya

• Mafunzo ya stadi katika uchambuzi wa sera na utetezi kwa ajili ya wafanyakazi

Katika maeneo yote hapo juu, kuwahusisha masikini na makundi maalumu ni muhimu. Ubunifu

unahimizwa sana. The Foundation inapendelea miradi ambayo inatumia mbinu za kuwafikia watu

wengi zaidi, k.m. kutumia vyombo vya habari kuhakikisha idadi kubwa ya wananchi inalengwa na

miradi inayofadhiliwa.

6. MAENEO AMBAYO HAYATAFADHILIWA NA FOUNDATION

Foundation inaweza kutoa ruzuku kwa asasi ambazo zimeanzishwa si kwa nia ya kupata faida au

kwa ufupi hazizalishi kwa nia ya kupata faida. Hata kama mradi ulioombea si wa faida, hutakuwa na

nafasi ya kupata ruzuku kama katiba yako haionyeshi wazi kwamba asasi yako kimeanzishwa kwa

ajili ya huduma na wala si kwa kutengeneza faida. Kama unadhani kwamba asasi yako itakabiliwa

na sharti kama hili tafadhali pata ushauri kutoka kwetu kabla hujaandika maombi ya ruzuku.

The Foundation haitatoa ruzuku kwa hili/haya yafuatayo:

• Fedha za kutunisha mfuko

& msaada wa masomo au

utaalamu

• Mradi au shughuli ambazo

zipo nje ya Tanzania

• Mradi au shughuli ambazo

tayari zimemalizika

• Miradi ambayo inatoa

ruzuku kwa taasisi nyingine

• Bakshishi kwa ajili ya

wafanyakazi wa asasi

• Miradi inayozalisha faida

/ shughuli za ukopeshaji

fedha

• Maombi ya ruzuku kutoka kwa wataalamu

wa kuchangisha fedha au washauri ambao

wanajitegemeza kwa niaba ya asasi

• Watu binafsi

• Vyama vya siasa

• Mradi ambao unapendelea dini fulani

• Sekta binafsi (Labda iwe chama

kisichotengeneza faida)

• Asasi ambazo zina madeni makubwa

• Warsha, vingivevyo ziwe katika mpango

mkubwa wa shughuli ambazo zimeungana

zinaeleza kwa uwazi matokeo yake

• Gharama ambazo hazikutarajiwa

• Utoaji wa huduma za kijamii

ZINGATIA: Taasisi zote ambazo huendesha shughuli za utoaji mikopo kama vyama vya kuweka

na kukopa, taasisi za kifedha zinazotoa mikopo hata ile midogo au wale ambao biashara ya fedha

ndio mhimili wao mkubwa wanatakiwa kuwasilisha mchakato ambao umeweka wazi na wenye

ushawishi mkubwa kuhusu mradi wao kama watataka kushughulikia masuala nje na utaratibu wao

wa kawaida wa biashara ya fedha. Foundation haitatoa fedha kwa ajili ya kukopesha watu binafsi

au makundi.

11
7. Jinsi ya kutuma maombi

Tafadhali hakikisha kwamba unapata fomu halisi zinazohusiana na ruzuku yako au umeweza

kupata kielelezo cha maombi kwa mahitaji yako. Vyote tunavyotaka kujua kutoka kwako vipo

katika Mwongozo huu wa maombi ya ruzuku. Tafadhali hakikisha kwamba umejaza nafasi zote

unazopaswa kujazwa katika fomu. Fomu ambazo hazijakamilika hazitashughulikiwa na zitarejeshwa

kwako mwenyewe.

Unatakiwa kutumia fomu au muundo ulioelekezwa na Foundation iwe katika mfumo wa nakala ya

karatasi au ya kwenye kompyuta. Fomu zote zinatakiwa kuwasilishwa ama kwa uasili wake kama

ni nakala ngumu (ya kwenye karatasi) au kutumia fomu iliyopo katika mtandao wa Foundation.

Kumbuka kuwa wote wale watakaojaza fomu kwa kutumia njia ya mtandao, ni lazima pia kupeleka

fomu zilizotiwa saini katika nakala ngumu pamoja na nyaraka nyingine zinazotakiwa kuambatana

nazo.

Kama utaona kwamba hakuna nafasi ya kutosha katika fomu yako ya maombi, tafadhali usitumie

zaidi ya karatasi mbili za ziada kukamilisha majibu ya maswali. Karatasi zaidi zinaweza kutumika

katika mapendekezo ya bajeti na mipango ya mafunzo kama ni lazima.

7.1 Nyaraka zinazotakiwa

Ili maombi yako yaweze kufikiriwa tunahitaji nyaraka zifuatazo:

(i) Nakala mbili za fomu zako zikiwa zimekamilishwa,

(ii) Nakala mbili za cheti cha usajili wa asasi,

(iii) Nakala mbili za hati za kisheria zinazohusu asasi yako,

(iv) Nakala mbili za taarifa za kibenki zinazoelezea mwenendo wa akaunti yako angalau kwa

kipindi cha miezi sita iliyopita. Moja inatakiwa kuwa halisi ikiwa na muhuri na saini ya

benki,

(v) Nakala mbili za maelezo yaliyoandikwa na bodi ya wadhamini au miniti ya mkutano

inayoonyesha kwamba wamepitisha fomu hiyo unayoiwakilisha Foundation na wamekubaliana

na mradi,

(vi) Majina ya wadhamini wawili ambao wanaweza kuzungumza kuhusu asasi yako kwa

kujiamini,

(vii) Majina mawili ya Wadhamini wa ufadhili wa zamani katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita

na namna ya kuwapata (anuani) hasa kwa Ruzuku ya Kati na Ruzuku Kubwa. Kielezo cha

wafadhili kinaambatanishwa hapa kama Kiambatanisho 1,

(viii) Nakala mbili za taarifa ya fedha ya mwaka wa karibuni (kama una maombi ya Ruzuku ya Kati

ya shilingi zinazofikia milioni 35),

(ix) Nakala mbili za taarifa ya fedha iliyokaguliwa na kupewa cheti cha ripoti safi kwa miradi

ambayo inachukua miaka mingi (Kama unaomba zaidi ya shilingi milioni 35).

(x) Kama maombi yako yana kipengele cha mafunzo, unatakiwa pia kuleta:

Nakala mbili za mpango wa mafunzo. Mpango wa mafunzo hayo ni lazima uelezwe kwa

kina malengo ya mafunzo, kundi linalohusika, vigezo vilivyotumika kuwapata washiriki wa

mafunzo, wasifu wa walimu na mchanganuo wa mafunzo yenyewe, vitu ambavyo vitafundishwa

kwa washiriki. Kielezo cha mpango wa mafunzo/Kongamano kimeambatanishwa hapa kama

Kiambatanisho II,

(xi) Kwa asasi ambazo hazikusajiliwa kama asasi za kiraia chini ya Sheria ya Asasi Zisizo za

12
Kiserikali (NGO Act) kuwa na Hati ya Kukubalika (Certificate of Compliance) kutoka kwa

msajili wa NGOs itasaidia zaidi.

Zingatia: Kama asasi hazitafikia masharti yanayostahiki hazitafikiriwa.

7.2 Matawi ya mashirika makubwa

Kama AZAKi yako ni tawi la asasi kubwa ni lazima utoe:

• Nakala mbili za taarifa kutoka makao makuu kwamba wanajua mradi huo na wanakubaliana

na fomu za maombi ya ruzuku unayopeleka Foundation.

Pia lazima uwe katika nafasi ya kuthibitisha kwamba tawi lako lina haya yafuatayo:

• Kamati ya menejimenti inayojitegemea,

• Ina akaunti ya Benki,

• Ina hesabu za kila mwaka,

• Ina kauli juu ya mapato na matumizi yake.

Zingatia: Kama ruzuku itapitishwa itachukua miezi 4 kutoka mwisho wa tarehe ya maombi hadi

kupatikana kwa fedha. Unatakiwa kuhakikisha kwamba mpango wako wa utekelezaji hauanzi katika

kipindi cha miezi minne tangu umepeleka maombi yako.

7.3 Makundi yanayoshirikiana (Consortia )

Kama mpo AZAKi tofauti lakini mnaomba ruzuku kama kundi linaloshirikiana ambalo linatambulika

na kusajiliwa kisheria na lina katiba inayojitegemea iliyotengenezwa na wanachama wake, maombi

ya ruzuku yataangaliwa kama maombi ya taasisi nyingine zinazotaka ufadhili.

Lakini kama unaomba kwa niaba ya kundi ambalo halikusajiliwa kisheria lakini lina wanachama

wanaotaka kufanyakazi pamoja kufikia lengo fulani lazima kufanya yafuatayo:

• Lazima asasi moja ichaguliwe kama kiongozi ili kufanya kazi kwa niaba ya wenzake

wanaohusika na mpango mzima;

• Jaza fomu kwa ajili ya kundi lote (Hii ifanywe na AZAKi inayoongoza);

• Mkubaliane kwamba ruzuku hiyo italipwa kwa asasi kiongozi ambayo itawajibika kutekeleza

masharti ya ruzuku;

• Ni lazima kuwasilisha maelezo ya AZAKi nyingine kuonyesha kukubaliana na fomu hiyo.

Mkitaka ruzuku kama kundi (consortia) ni lazima ueleze wazi nafasi ya kila kundi katika utekelezaji

wa mradi husika.

ZINGATIA: Kundi linaweza kupeleka maombi mara moja tu kwa muda husika. Lakini wanachama

wa kundi wanaweza kuomba ruzuku kwa miradi mingine ambayo haihusiki na mradi ulioombewa

ruzuku kwa kupitia kundi walilopo. Na katika hili waombaji ni lazima waeleze wazi kabisa tofauti

za maombi yao kutoka katika maombi ya kikundi( consortia)

7.4 Ufadhili wa mradi mkubwa wenye washirika wengi

Kama utaomba ufadhili kwa mradi mkubwa wenye wafadhili wengi ni lazima utoe uthibitisho

ufuatao:

• Nakala mbili za barua za kuthibitisha ufadhili kutoka kwa washiriki wote wa mradi husika.

Barua hizo zieleze wazi kabisa kiwango cha fedha ambazo zinatolewa na wafadhili hao,

13
muda ambao fedha zitawakilishwa na fedha hizo zitafanya nini katika mradi husika. Ni lazima

ueleze wazi shughulia ambayo unataka ifadhiliwe na Foundation.

Kumbuka

Tafadhali hakikisha kwamba unaambatanisha nakala mbili kwa kila hati unayowasilisha ambayo

inatakiwa kuambatana na maombi yako. Pia kumbuka kuandika jina la asasi yako na anuani juu

ya kila hati inayoambatana na fomu za maombi. Hii itatusaidia kuhakikisha kwamba nyaraka

husika zote zipo pamoja na maombi ya ufadhili.

8. WADHAMINI

Tutakuwa tunawasiliana na wadhamini na wafadhili wengine ambao umetujulisha katika maombi

yako ya ruzuku.

Ndio kusema unapotupatia anuani ya wafadhili wako wa sasa na waliotangulia na namba yako ya

utambulisho tuliyokupa hakikisha haya yafuatayo yapo sahihi:

• Taarifa zilizomo zipo sahihi,

• Wahusika wameambiwa juu ya maombi yako,

• Wahusika wanaweza kupatikana kwa njia ya simu ili kusaidia kujibu baadhi ya maswali kutoka

Foundation katika kipindi cha wiki tatu tangu kuwasilisha kwako kwa fomu za maombi. Kama

mhusika hawezi kupatikana kwa simu hakikisha kwamba unatoa anuani yake ya posta na

anuani ya barua pepe, na kuwasilisha maombi yako mapema zaidi.

Maombi yote ya ruzuku lazima yawe na wadhamini wawili.

8.1 Nani anastahili kuwa mdhamini wa maombi yako

Mdhamini lazima awe mtu mkweli ambaye unamfikiria kuwa mwaminifu na mtu ambaye anaaminika

na maamuzi yake yanaweza kuaminika. Hao wawili lazima wawe wanajua asasi yako si chini ya

mwaka mmoja na wawe na uwezo wa kubadilishana mawazo juu ya uwezo na uzoefu wa asasi

husika. Ni lazima wawe wanaelewa vyema shughuli za asasi yako, menejimenti na fedha.

Wadhamini hawapaswi kuwa:

• Watu wa familia yako, ndugu au marafiki au yoyote ndani ya asasi,

• Kiongozi wa asasi yako au alikuwa mfanyakazi wa zamani au wa sasa,

• Mtu ambaye kwa sasa unashirikiana naye katika shughuli za asasi au zako,

• Watu ambao unaweza kuwahusisha baadaye na shughuli za mradi unaouombea fedha.

Tafadhali hakikisha kwamba wadhamini wako wanayotaarifa ya wewe kuwaweka katika fomu za

kuomba ruzuku Foundation na kwamba utawatumia kama wadhamini na waambie mradi ambao

umeuombea ruzuku.

ANGALIA: Ni lazima ueleze wazi uhusiano ulionao na wadhamini husika katika maombi yako.

Tunatarajia kwamba utatumia nafasi yako vyema ya kuchagua wadhamini wako. Kama wadhamini

wataonekana hawafai basi maombi yako hayatafikiriwa.

14
8.2 Maoni ya wafadhili

Wafadhili ni wale ambao walishawahi kukupatia ruzuku katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Orodhesha wafadhili wote bila kujali kama tutawauliza au la. Ni vyema kuorodhesha wafadhili

wako wote wa zamani katika fomu ya kuombea ruzuku. Kama mtu unayemfahamu katika Asasi

iliyowafadhili amebadilishwa, tafadhali elezea hili na itakuwa ni vema kama utatueleza nafasi hiyo

kwa sasa imeshikwa na nani na jina lake kama inawezekana.

Kielelezo cha wadhamini wafadhili kimeambatanishwa na kutambulishwa kama kiambatanisho I.

Inatakiwa kueleweka mapema kwamba waombaji wa ruzuku watatakiwa kutengeneza muhtasari

wa ufadhili ambao ulitolewa na wadhamini hao na kuelezea mabadiliko ambayo yamepatikana

katika jumuiya ikiwa ni matokeo ya utekelezaji wa mradi huo hivi karibuni.

9. Mara ngapi waweza kutuma maombi

AZAKi hairuhusiwi kuomba ufadhili zaidi ya mmoja katika kipindi kimoja. Kama utapeleka maombi

zaidi ya moja katika kila programu, maombi yote yatakataliwa. Inatakiwa utambue kwamba AZAKi

inaweza kupokea ruzuku ya aina moja tu kwa kipindi kutoka Foundation.

AZAKi yoyote ile ambayo imepeleka ombi lake la ufadhili la aina yoyote ile inashauriwa kusubiri

majibu kutoka Foundation kwa ombi lake la kwanza kabla ya kutuma maombi mengine. Hii itasaidia

kuona kwamba mambo yote yaliyoelezwa yanashughulikiwa inavyostahili.

9.1 Kama umeshawahi kupata fedha kutoka Foundation siku za nyuma

Ombi lako la zamani ni lazima liwe limeshughulikiwa na kufungwa rasmi kabla ya ombi jipya

kufikiriwa.Tathmini ya mradi wako ni lazima iwe imefanywa na Foundation kabla ya kuanza kufikiria

ombi jipya.

Utatakiwa kuonyesha matokeo ya mradi wa kwanza, kuelezea mafanikio, mambo ambayo mmejifunza

kutoka katika ruzuku yako ya kwanza, kutafakari uzoefu uliopatikana kutokana na utekelezaji wa

mradi na kuelezea kwanini unataka kuendelea na mradi huo au kuupanua zaidi .

9.2 Utumaji wa maombi ya ruzuku

Mara tu utakapokuwa umekamilisha kujaza maombi yako ya ruzuku na kuambatanisha na hati

zinazostahili unatakiwa kutuma maombi yako hayo kwa anuani ambayo imeonyeshwa ndani ya

kitabu hiki. Maombi hayo yanatakiwa kufika katika ofisi za Foundation kabla ya muda wa mwisho

wa kupokea maombi kutimia. Maombi pia yanaweza kuwasilishwa kwa kutumia tovuti kwa kutumia

anuani ya barua pepe iliyomo ndani ya mwongozo huu.

10. Nini kinatokea katika maombi yako

Mara tu utakapowasilisha maombi yako ya ruzuku utapatiwa namba ya rejea ambayo ni namba

ya utambulisho ikiwa ni kama kutambua kuwasilishwa kwa maombi yako ya ruzuku. Tafadhali

usipige simu au kuulizia maombi yako mpaka siku uliyoambiwa kuulizia. Tafadhali tupatie muda wa

kuangalia maombi yako kwa mujibu wa mwongozo huu kabla hatujakupa jibu.

15
Kila maombi hupitia hatua kadhaa za kuangaliwa kabla ya kufikiwa kwa maamuzi. Uteuzi wa

asasi zinazostahili kupata ruzuku hufanywa na manejimenti ya Foundation. Matokeo ya uteuzi huo

huwasilishwa kwa bodi ya wakurugenzi ya Foundation.

Matokeo hayo yatawasilishwa kwa wadau walioomba kwa njia ya barua, tovuti na magazeti.

10.1 Vigezo vya tathmini

Foundation huangalia kila ombi kwa kutazama vipengele ambavyo tayari vimewekwa katika kufikia

kuamua AZAKi fulani kupewa ruzuku. Kama sehemu ya mchakato wa kupitia maombi unaweza

kuletewa ombi la kutoa maelezo ya ziada. Lakini pamoja na kuulizwa maswali ya ziada na

wafanyakazi wa Foundation kamwe usifikiri kwamba nafasi yako ya kupewa ruzuku imeongezeka

kutokana na maswali hayo.

Kama asasi yako inastahili kuomba ruzuku, tambua kwamba maombi yako yataangaliwa kwa

kuzingatia vigezo vifuatavyo:

10.2 Asasi yako

Vigezo hivi vinatusaidia kuangalia muundo na menejimenti ya asasi yenu. Tunahitaji kuwa na

uhakika na:

• Kuwa asasi yako ina muundo wa kiutawala ambao ni thabiti na unaowajibika,

• Kwamba unaweza kabisa kupangilia fedha za asasi na kuzidhibiti,

• Kwamba asasi yako ina njia za wazi kabisa za kupanga na kuendesha shughuli zake,

• Shughuli za asasi ziko wazi kwa wote na inakazania kutoa haki sawa kwa kila mtu,

• Kwamba asasi yako inaonyesha wazi kwamba ina uzoefu na utaalamu wa kufanya shughuli

iliyosababisha uwepo wake,

• Kwamba asasi yako ina mahusiano na asasi nyingine zenye malengo kama yako,

• Kwamba asasi yako inajiendesha kwa kulingana na misingi ya Foundation,

10.3 Mradi wako

Vipengele vilivyotajwa hapa chini vinasaidia kutathmini mapendekezo ya mradi wako. Hivyo

tunahitaji kuwa na uhakika na:

• Kwamba tatizo lililoainishwa katika mradi unaoombewa ruzuku kuwa ni kweli ni hitaji kuu la

kundi lililolengwa (wafaidika au jamii husika),

• Kwamba mradi uliouibua umepangwa vilivyo na una wafanyakazi wanaostahiki,

• Kusudio la mradi wako linaonyesha wazi kabisa haja iliyopo,

• Mpango wako unaweza kufuatiliwa kwa urahisi kwa kutumia taarifa za awali zilizopo na

kwamba inapimika kwa kutumia viashiria vilivyo madhubuti,

• Mchanganyiko wa shughuli zinazolengwa kufanyika kama zinaweza kuleta mabadiliko ya

msingi yaliyoainishwa na kutarajiwa (matokeo ya awali na mabadiliko),

• Mradi wako unachangia kufikia dira, lengo la Foundation na angalau na moja kati ya maeneo

makuu ya Foundation.

16
Matokeo na mabadiliko yatakayoletwa na mradi wako sharti yawe:

Maalumu - Je Matokeo & mabadiliko yana mwelekeo maalum

Yanayopimika

Yanatekelezeka

Sahihi

Muda maalumu

Endelevu

- Je mabadiliko unayoyataka yanaweza kuangaliwa kwa kuona hali halisi

iliyopo sasa

- Je mabadilkiko yanawezekana katika muda uliopo

- Je matokeo & mabadiliko vinafanana na wazo la mradi ulioombewa ufadhili

Je yanawiana na mapendekezo yako ya washiriki uliowapendekeza

- Je unaweza kutambua muda ambao utaona matokeo & mabadiliko

- je matokeo & mabadiliko yataendelea kuonekana hata baada ya mradi

kumalizika

10.4 Mambo yako ya kifedha

Vigezo vifuatavyo vinatusaidia sisi kutambua namna unavyodhibiti fedha zako. Tunahitaji kuwa na

uhakika na:

• Kwamba asasi yako inaendeshwa vyema kifedha na inahitaji kupewa ruzuku,

• Akaunti ya benki ya asasi yenu ina waweka sahihi zaidi ya mmoja.

Mapendekezo ya bajeti ya mradi wako yawe kama ifuatavyo:

Ya kina:

Kila shughuli lazima ioneshe gharama zake kwa kina. Shughuli zote

zilizoorodheshwa katika fomu yako ya maombi lazima ziwe zinaeleza

bajeti kwa undani zaidi .Ni lazima katika maelezo yako utoe kwa

muhtasari kidogo shughuli husika (Itafanyika wapi na kwa namna gani,

lini itafanyika, watu wangapi watashiriki katika shughuli hiyo), na kueleza

gharama yake kwa undani zaidi.

Za kweli:

Sahihi:

Yanayostahiki:

Thamani ya fedha:

Mifumo ya fedha:

kwamba mahitaji yaliyoorodheshwa katika bajeti ni ya gharama za kweli

na yanatosheleza.

Vifaa husika vinaakisi bei halisi na vimejumlishwa kwa usahihi

Kwamba bajeti iliyopangwa ndiyo inayostahiki kwa asasi husika kwa

kuzingatia ukubwa wa asasi na uzoefu wake

Kama bajeti imezingatia gharama na inakidhi. Maombi ambayo

yataonyesha matokeo mazuri na makubwa kwa gharama ndogo

yataangaliwa kwa makini zaidi na kupewa kipaumbele.

Foundation inatarajia kupata maombi kutoka kwa AZAKi zenye mfumo

bora wa menejimenti na fedha na hivyo kuwa na rekodi za mapato na

matumizi na kwa njia hiyo kudhibiti fedha.

Kielelezo cha bajeti kimo ndani ya Mwongozo huu kama kiambatanisho III

17
10.5 Kama maombi yako hayakupita

Kama Foundation inaamua kwamba haitatoa ruzuku kwa asasi yako basi utapatiwa taarifa kwa njia

ya posta wiki nane baada ya kupita kwa muda wa mwisho wa kuwasilisha maombi katika kipindi

husika. Utapata barua inayokueleza wazi kwa nini Foundation imeshindwa kukubaliana na ombi

lako la kutaka ruzuku. Ni vyema kama utaisoma barua hiyo kwa uangalifu unaostahili.

Kama mtaamua kutuma maombi tena kwa Foundation kwa mradi huo huo itawapasa kujaza tena

fomu mpya na kuhakikisha mambo yote yaliyoelekezwa katika barua mnayatekeleza.

11. Mwongozo wa bajeti

Unatakiwa kuwasilisha bajeti katika muundo ambao ni wazi na rahisi kuelewa kwa mujibu wa

maelekezo ambayo yapo katika mwongozo huu (Angalia muundo katika kiambatanisho III). Bajeti

yako ni lazima ionyeshe wazi kwamba kiasi kilichoombwa kwa ajili ya mradi husika kimezingatiwa.

Wakati unatengeneza bajeti, kuwa na uhakika na kitu ambacho umepanga kukifanya, namna

utakavyofanya na kiasi gani cha fedha kinachotakiwa kwa mradi husika.

Foundation haitakaa kuzungumza nawe kuhusiana na kilichomo au kiasi kilichopo katika bajeti

yako au yaliyomo ndani mwake ambayo yamewasilishwa katika barua yako ya maombi. Hivyo ni

muhimu sana kuwasilisha bajeti yenye kila kitu, sahihi na inayoonyesha dhahiri thamani ya fedha.

Tengeneza bajeti kwa kuzingatia gharama halisi na kuwa na wastani katika maombi .Ni vyema katika

hili ukatambua kwamba si lazima kupata kiasi cha fedha cha kiwango cha juu ambacho kipo.

Maombi yako hayatafikiriwa iwapo bajeti yako haikutoa taarifa za kina na haioani na maelekezo na

viwango vilivyotolewa katika mwongozo wa bajeti.

11.1 Gharama za usafiri

Safari zote lazima zifanywe katika hali ya kuzingatia unafuu wa njia ya usafiri na uiweke bajeti hiyo

kama ni lazima watu wasafiri kwa umbali mrefu kushiriki katika shughuli za mradi.

11.2 Malazi na gharama ya chakula

Gharama zote za malazi na chakula ni lazima zithibitishwe kwa kutumia risiti katika taarifa ya

matumizi ya fedha ya robo mwaka. Foundation haitapitisha bajeti ya matumizi bila kuwa na risiti

halali za matumizi ya fedha. Tunahimiza asasi husika kulipa gharama hizi moja kwa moja badala ya

kuwalipa washiriki.

Ufuatao ni mwongozo unaostahili kutumika kwa ajili ya malazi na chakula:

Eneo Malazi Posho ya kujikimu

Majiji, Zanzibar, Dodoma, Bagamoyo Mjini 32,000 13,000

Manispaa 22,000 13,000

Mikoa na miji mikuu ya wilaya 11,000 9,000

Maeneo mengine yote 5,000 6,000

18
11.3 Kupitisha matumizi kwa kutumia risiti peke yake

Wakati unandaa bajeti yako, tafadhali kumbuka kwamba tumekupatia mwongozo wa kiwango cha

juu ambacho kinaweza kutumika kwa ajili ya usafiri, malazi na posho ya kujikimu.

Gharama zote za usafiri, malazi na posho ya kujikimu ni lazima kulipwa kwa wale ambao wanatoka

nje ya mji unakofanyika mradi husika (kwa wale washiriki ambao hawaishi katika eneo ambalo

zinafanyika shughuli husika). Washiriki ambao ni wakazi wa eneo ambako ndiko mradi unakofanyika

hawaruhusiwi kupewa malipo haya.

11.4 Malipo ya ushiriki

Hairuhusiwi kulipa malipo ya ushiriki kama motisha (posho za vikao) kwa ajili ya kushiriki katika

warsha au mikutano mingine.

11.5 Bakshishi (Honoraria)

Bakshishi (Honoraria) inaweza kulipwa kwa mtu wa nje ambaye ametoa au amefanya kazi fulani

ya huduma katika mradi. Chagua watu wako wa kukuendeshea mambo kwa kuzingatia bajeti yako

na njia mbadala ya kupunguza gharama za matumizi. Honoraria kamwe isilipwe kwa wafanyakazi

wenye mshahara katika AZAKi yako. Zingatia kwamba kama honoraria zako, posho ya kujikimu na

malazi yapo juu maombi yako yanaweza kukataliwa.

11.6 Gharama za uendeshaji & utawala / Mishahara

Unaweza kabisa kubajeti sehemu fulani ya fedha zako kwa ajili ya kujiendesha na hii isizidi asilimia

30 ya fedha zilizoombwa kutoka Foundation. Hii ni sawasawa na kutoa msaada katika gharama

za uendeshaji na inatakiwa kuendesha gharama zote za msingi za kuendeshea AZAKi (kama vile

gharama ya pango, vifaa vya ofisi, mishahara, gharama za magari, muda wa wafanyakazi wa utawala,

na huduma za azaki ambazo haziko mahsusi kwa ajili ya mradi). Bajeti yako isiongeze gharama za

huduma za kiutawala kwa zaidi ya asilimia 30. Kwa wale ambao wataomba chini ya asilimia hizo

wataangaliwa vyema kwani inaonekana wao wanatambua thamani ya fedha.

Kumbuka

Ukiwa unakamilisha fomu yako ya maombi tafadhali kumbuka:

• Jaza maombi ya ruzuku kwa kuzingatia uzoefu wa AZAKi na mipango yake.

• Tunaangalia kwa makini sana juu ya mawazo yako na si maneno tu unayotumia katika

fomu yako ya maombi ya ruzuku. Kama tutahisi kwamba maombi yako ya mradi

yameandaliwa na mtaalamu wa masuala ya utunishaji mfuko, huenda tukakutoa kwani

hustahili.

• Unatakiwa kutupatia taarifa za kweli na takwimu zinazounga mkono ombi lako.

• Unatakiwa kuwa na uhakika juu ya mradi wako na kitu unachoweza kufanikiwa.

• Andaa bajeti yako kwa kuzingatia gharama halisi kwa kutumia mwongozo uliopewa.

Usiweke bei ya juu ya vifaa au kupandisha gharama.

• Usiambatanishe na taarifa za ziada ambazo hazikuombwa.

• Zingatia maelekezo uliyopewa katika Mwongozo huu na maelezo ya mwongozo

kwenye fomu yako kwa ukamilifu.

19
12. Ufuatiliaji

Miradi yote ambayo imepewa ufadhili na Foundation itafuatiliwa na kukaguliwa kila mara. Unatarajiwa

kuwasilisha kwa Foundation taarifa za robo mwaka za fedha na nadharia ya mwenendo wa mradi kama

makubaliano ya mkataba yanavyodai. Ukaguzi huo utafanyika katika shughuli ambazo zimekubaliwa

na katika taarifa zao za robo mwaka za maendeleo ya mradi na ripoti za fedha. Mpango wa kuripoti

na muundo wake vitatolewa kwako mara tu baada ya kutia saini mkataba huo. Kielelezo cha mpango

wa ufuatiliaji wa mradi kipo humu kwenye mwongozo kama Kiambatanisho IV.

13. Namna ya kujaza fomu za maombi ya ruzuku

Kipengele hiki kina maelekezo yanayohusu jinsi ya kujaza fomu za maombi. Lengo la sehemu hii

ni kusaidia waombaji kuwa na elimu ya kutosha kuhusu maelekezo yanayotakiwa katika ujazaji wa

fomu. Ni matumaini yetu kwamba waombaji wataona eneo hili kuwa na msaada mkubwa kwao.

Tutashukuru kama waombaji watatutumia maoni au taarifa zao za mrejesho ambazo zitatusaidia

kuboresha zaidi huduma zetu katika sekta ya AZAKi za Tanzania.

Fomu za kuombea ruzuku zina sehemu nne kama ifuatavyo:

• Sehemu ya 1: Taarifa ya mradi,

• Sehemu ya 2: Muundo wa uendeshaji,

• Sehemu ya 3: Angalia kama maombi yako yamejazwa vyema na kukamilika,

• Sehemu ya 4: Kipengele cha makubaliano.

Sehemu ya 1: Taarifa ya mradi

1.1. Jina la Mradi: Muombaji hapa anatakiwa kuandika jina la mradi. (kwa mfano: Mradi wa

udhibiti wa VVU na UKIMWI).

1.2. Maeneo yanayofadhiliwa

Hapa mwombaji anatakiwa kuonyesha ni eneo lipi kati ya maeneo yanafodhaliwa na

Foundation ambapo mradi wake anauombea. Yaani mradi wake unaangukia katika wazo gani

linaloshughulikiwa na Foundation.

1.3. Lengo kuu la mradi: katika kipengele hiki muombaji anatakiwa kuandika taarifa kwa ufupi

juu ya mafanikio ya mradi huo kwa upana wake, yaani mafanikio ya mradi katika ngazi za

maendeleo ya kitaifa na ya kisekta (Mathalani, Kuboresha hali ya kiafya kwa wananchi wa

wilaya XXX kwa kufanikiwa kushawishi wananchi kukabiliana na matatizo ya UKIMWI kwa

namna endelevu zaidi).

1.4. Muhtasari wa mradi: Toa maelezo ya kwa ufupi juu ya y mradi unalenga kufanikisha nini

katika kipindi chote cha utekelezaji wake kwa walengwa wa eneo husika.

Kwa mfano: Mradi utahakikisha unakuwa endelevu katika kukabiliana na tatizo la VVU na

UKIMWI na magonjwa ya zinaa kupitia mpango wa CBHC, Uhamasishaji na ushiriki wa jamii

(Community mobilization and participation), BCCI, Kuishauri jamii (Community Counseling),

Msaada kwa Vijana( support for Youths) PLWHA na kushawishi upimaji hiari na ushauri nasaha.

20
Pia mradi utaangalia athari za malaria kama ugonjwa nyemelezi ambao huharakisha vifo vya

wagonjwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI au kuongeza mzigo kwa familia zilizoathirika

na ugonjwa wa UKIMWI. Shughuli za mradi zitatekelezwa kwa ushirikiano wa karibu kati ya

serikali ya Tanzania (kama: MOH na MOEC) Wilaya na serikali za vijiji na NACP. Utekelezaji

wa mradi utasimamiwa na wizara ya Afya (MOH) kupitia mpango wake wa Kuzuia na Kudhibiti

VVU/UKIMWI/Magonjwa ya zinaa MTP III) na NACP.

Lengo kuu la kimaendeleo: Ni kuboresha afya za wakazi wa wilaya XXX kwa kuwashawishi

kuwa na mpango endelevu wa kukabiliana na UKIMWI. Masuala makuu yatakayoangaliwa:

Kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI; kuhudumia na kuwasaidia wananchi wanaoishi

na viurusi vya UKIMWI; Kuhudumia na kuwasaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika

mazingira magumu na kuwa na mtandao wa elimu na utetezi kuhusu VVU/UKIMWI.

1.5. Maelezo ya tatizo linalohitaji ufumbuzi kupitia mradi huu - Nini hasa kinakushawishi uone

kuwa mradi huu unahitajika (Toa amelezo ya kitu ambacho kinatakiwa kubadilishwa kwa

kundi husika kwa kutekeleza mradi huo).

(Kwa mfano: Kwa mujibu wa ripoti ya National AIDS Control Program (NACP) asilimia 90

ya wananchi wanaelewa kuhusu ukimwi. Ukweli huu hata hivyo unagongana na kasi ya

maambukizi, inayosababisha kuwepo kwa idadi kubwa inayotisha ya wagonjwa wengi wa

ukimwi. Janga hili limesambaa kwa kasi katika maeneo ya vijijini na mwaka 1997, zaidi ya

asilimia 10 ya wanawake waliokuwa wakihudhuria kliniki za uzazi katika baadhi ya maeneo

ya vijijini walibainika kuwa na virusi vya ukimwi.

Idadi ya wagonjwa wa ukimwi kama ilivyoripotiwa na NACP kwa upande wa Tanzania

Bara ilipanda kutoka 25,503 mwishoni mwa mwaka 1990 kufikia 88,667 mwaka 1996. Kiasi

cha aislimia 80 ya waliokutwa na ugonjwa ni wale wenye umri wa miaka 20-44. Tanzania

ni nchi iliyo kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo imeathiriwa vibaya na janga hili ikiwa na

wastani wa maambukizo ya asilimia 10 kwa watu wazima. Utafiti zaidi wa Tanzania National

AIDS Control Program (NACP) Tanzania Bara unaonyesha kupanda kwa wagonjwa kutoka

25,503 mwishoni mwa miaka ya 1990 kufikia 88,667mwaka 199. Kulikuwa na wagonjwa

14,112wa ukimwi kwa mwaka 2001 na hivyo kusababisha idadi ya wagonjwa kufikia 144498

toka 1983. Na zaidi ya asilimia 80 ya watu waliokutwa na ugonjwa huo ni watu wa umri wa

miaka 20 – 44. Kuna wastani wa watu 2229770 wenye ukimwi ambao umri wao ni kuanzia

miaka 15 na kuendelea. Magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya zinaa (STIs) yaliyoripotiwa

mwaka2001 yalikuwa 211291 na 149222 kwa mwaka 2000 na 39385 mwaka 1999 (Taarifa

ya VVU/UKIMWI STI surveillance report NACP 2002). Kutokana na hali hiyo Wizara ya afya

nchini Tanzania imebuni mkakati wa kukabiliana na hali hiyo unaoitwa (MTP – III) ukiainisha

harakati mbalimbali zinazofanywa na taifa kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuzingatia

takwimu za mwaka 1998 hadi 2002).

Itambulike wazi kuwa maandiko mazuri ya kauli ya tatizo lazima yawe na mambo yafuatayo:

• Kueleza kwa uwazi kabisa hali ambayo inastahili kubadilishwa kwa utekelezaji wa mradi

kwa kuzingatia ukweli wa mambo ulivyo,

• Itaonyesha kwa wazi kabisa nani na nini kimeathirika,

• Kuhalalisha uwepo wa tatizo,

21
• Kuelezea tatizo ambalo linalhusiana na nia ya kuanzishwa kwa asasi,

• Kuelezea ukubwa wa tatizo katika jamii husika.

1.6. Muda wa mradi: Muda wa utekelezaji wa mradi. (Mfano: Mradi huu utatekelezwa kwa miezi

24).

1.7. Katika kipengele hiki muombaji anatakiwa kuonyesha kiwango cha fedha anachohitaji kutoka

Foundation (kwa mfano. Sh. 249,000/=).

1.8. Maelezo yanatakiwa kutolewa kama ufadhili unaoombwa ni wa kushirikiana yaani kama

Foundation inatakiwa kugharamia sehemu tu ya ruzuku.

1.9. Uchanganuzi wa Bao la Mantiki (Logical Framework Analysis).

Lengo mahususi la mradi:

Hapa muombaji anatakiwa kuandika matokeo anayoyatarajia katika mradi wake yaani faida yake

kwa maendeleo ya wananchi, muda wa mradi utakapokuwa umekwisha. Wananchi watakuwa

wamefaidi nini. Kumbuka kwamba vipengele vyote vya mradi vitachangia matokeo hayo.

Viashiria vya mabadiliko:

Hapa mwombaji anatakiwa kutoa maelezo mwishoni mwa mradi kuonesha kuwa mafanikio

yamepatikana na manufaa yake ni endelevu.

Matokeo ya awali:

Hapa mwombaji anatakiwa kuandika matokeo ya moja kwa moja yatakayotolewa (bidhaa na

huduma za mradi) ambazo zaidi zipo chini ya usimamizi wa menejimenti.

Viashiria vya matokeo:

Viashiria katika kiwango matokeo hupima kiasi na ubora wa matokeo na muda wa ufikishaji kwa

wahusika. Kanuni hizi hutumika pia wakati wa kuuangalia mradi na pia kuufanyia tathmini.

Shughuli

Hapa muombaji anatakiwa kuwasilisha kazi zitakazofanywa katika utekelezaji wa mradi na hivyo

kuleta matokeo.

22
Mpangilio wa namna ya kufanya kazi

Matokeo Viashiria vya matokeo Nguvu inayotolewa

kwa kila tokeo

Kupunguza

maambukizo

ya UKIMWI

kupitia mpango

endelevu wa

afya ya msingi

ya jamii,

msaada wa

kijamii, na

mabadiliko ya

kitabia ifikapo

Desemba 2009

• Mfumo wa

kubadilishana

taarifa za UKIMWI

inaanza kufanya

kazi ifikapo.

Desemba 2009

• Wengi wa vijana

wanaanza kufanya

ngono salama

katika wilaya X

ifikapo Desemba

2009.

Wananchi 40 kuwa

wameshafunzwa

masuala ya PRA ifikapo

Desemba 08.

Shughuli za kufanya kwa kila

tokeo

• Kutambua wanavijiji 40 ili

kufundwa ifikapo Oktoba

07.

• Kuwezesha mafunzo ya

PRA kwa jamii lengwa 40

ifikapo Januari 08.

• Kuandaa taarifa ya mafunzo

Februari 08.

Wanajamii 40

waliofunzwa wanaanza

shughuli za PRA katika

vijiji 21 kwenye wilaya

X ifikapo desemba 9.

• Kuwezesha ufuatiliaji na

tathmini baada ya mafunzo

Desemba 08.

Kuwa na wanavijiji

wa kujitolea 30

waliofunzwa VVU/

UKIMWI na BCCI

ifikapo Desemba 08.

• Kutambua watu

wa kujitolea 30 ili

wafundishwe ifikapo Machi

08.

• Kuwezesha mafunzo ya

HIV/AIDS na BCCI kwa

watu 30 waliotambulika

katika vijiji ifikapo April 08.

• Kuandaa taarifa ya mafunzo

ifikapo Mei 08.

• Kuwezesha ufuatiliaji na

tathmini baada ya mafunzo

ifikapo Oktoba 08.

Waelimisha rika 40

wakitoa elimu ya VVU/

UKIMWI kwa warika

21 katika vijiji 21 vya

wilaya X ifikapo Dec.

09.

• Kuwazuru waelimisha rika

katika kila robo mwaka.

23
1.10. Mpango wa ufuatiliaji wa Matokeo (Mfano)

Matokeo Viashiria Zilikotoka takwimu Muda wa

kukusanya data

Kupunguza kiwango cha

maambukizi ya VVU kwa

kupitia mpango wa afya ya

msingi, msaada wa kijamii

na mabadiliko ya kitabia

kufikia Desemba 2009.

Kuwepo kwa

mfumo wa

kubadilishana

taarifa za

ukimwi kufikia

mwaka 2009.

• Kumbukumbu ya

mahudhurio kituo cha

taarifa.

• Mchanganuo wa taarifa

za makundi lengwa.

• Taarifa za tathmini.

• Kila mwezi.

• Kwa miezi

mitatu (kila

robo mwaka).

• Kwa mwaka.

1.11. Walengwa: Idadi na mahali walipo

Taja idadi binafsi ya watu waliofaidika na mradi, vijiji, wilaya na mikoa

Sehemu ya 2: Maelezo ya Asasi (Shirika)

2.1. Jina la asasi: Jaza jina kama lilivyo katika katiba na usajili.

2.2. Jina ambalo unalitumia (Tofauti na lile la 2:1): Utajaza nafasi hii kama jina unalotumia tofauti

na lile la 2:1 hasa kama ni kifupisho.

2.3. Usajili: Hapa unatakiwa kuhakikisha kwamba unatoa taarifa zote za asasi ikiwemo aina ya

usajili, tarehe ya usajili na anuani.

2.4. Kama unaomba kama sehemu ya ubia au muungano wa asasi: Tafadhali orodhesha majina ya

AZAKi nyingine mnazoshirikiana au mtakazoshirikiana katika mradi huo. Na kama ni zaidi ya

sita basi tengeneza kiambatanisho mwishoni mwa ukurasa.

2.5. Mtu atakayekuwa anawasiliana na Foundation: Jaza jina la mhusika, nafasi yake na anuani za

mawasiliano atakazofanya baina yake na Foundation kwa niaba ya asasi.

2.6. Viongozi na wafanyakazi: Orodhesha majina ya viongozi wa asasi yako na nyadhifa walizonazo.

Wanaweza kuwa Bodi ya wadhamini, Kamati ya usimamizi, au bodi ya wakurugenzi.

2.7. Taarifa za kina za Akaunti ya benki: Mwombaji anatakiwa kutoa taarifa za akaunti ya benki

kama: Jina la akaunti, namba ya akaunti, aina ya akaunti, Jina kamili la benki iliyopo akaunti

hiyo, tawi lake, anuani ya tawi na majina ya watia saini na nyadhifa zao katika asasi.

2.8. Wadhamini huru: Wadhamini hawa wanatakiwa kuwa wakweli na ambao maamuzi yao si rahisi

kuyumbishwa au kupingwa na ni watu wenye heshima zao. Aidha, wanatakiwa wawe wamejua

asasi husika kwa mwaka mzima na wenye uwezo wa kuelezea asasi husika kiuwezo na kiuzoefu.

Wanatakiwa kuijua vyema asasi husika hasa shughuli zake, menejimenti na masuala ya kifedha.

KUMBUKA: Unatakiwa kueleza wazi uhusiano wako na wadhamini na Foundation inatarajia

kwamba utatumia busara zako vyema katika kumchagua mdhamini. Kama Mdhamini

ataonekana hafai maombi yako hayatafikiriwa.

Sehemu ya 3: Kifungu cha makubaliano

Hiki kinatakiwa kujazwa na mwenyekiti, Katibu au mweka hazina lakini hawatastahili kuwa watu

ambao wanawasiliana moja kwa moja na Foundation.

Sehemu ya 4: Angalia kama maombi yako yamekamilika

Waomba ruzuku wanashauriwa kutumia maelekezo yaliyopo katika mwongozo kuhakikisha

kwamba wanafanyakazi ya kujaza fomu za maombi kwa unadhifu, uhakika. Unatakiwa kujaza kila

kisanduku kabla ya kuwasilisha maombi.

24
14. Masuala unayotakiwa kuyajua

Tafadhali soma masuala yafuatayo kwa uangalifu zaidi. Ni sharti kwa kila mtu ambaye anataka

ruzuku kutoka Foundation akayasoma, kuyaelewa na kuyakubali:

14.1 Maombi ya Ruzuku

(i) Mwongozo huu na fomu za maombi zinatolewa bure.

(ii) Kwamba taarifa zilizomo katika mwongozo huu na fomu za maombi zinaweza kubadilika

kila inapobidi. Tuna haki ya kubadili kipengele chochote katika sera zetu, kanuni na

vigezo vya mchakato.

(iii) Fomu ya maombi ya ruzuku inaweza isiwe na taarifa zote zinazohitajika kuamua maombi

gani yanaweza kupewa ruzuku. Tunaweza kutaka taarifa zaidi kutoka kwako kuthibitisha

maombi yako. Pia tutataka taarifa kutoka mtu wa tatu kama vile wadhamini wako na

wafadhili wa sasa ulionao.

(iv) Maombi yanafanywa kwa matakwa ya mwombaji. Kutokana na hilo hatuwezi kushtakiwa

kwa hasara, uharibifu au gharama zinazotokana na mchakato mzima wa kuomba ruzuku,

kukataliwa kwa ruzuku au kushughulikia maombi yako.

(v) Uamuzi wa kutoa ruzuku bado ni haki ya Menejimenti ya Foundation for Civil Society,

na maamuzi yake ni ya mwisho na hayakatiwi rufaa.

(vi) Iwapo viongozi, Menejimenti au wafanyakazi wa Foundation watamjua mtu kati ya wale

walioomba ruzuku, wanatakiwa kutangaza mgongano wa maslahi na kujiondoa katika

kushughulikia shauri linalomhusu mtu huyo.

(vii) Maombi yako yatatupwa kama itabainika kwamba umedanganya au kutoa taarifa ambazo si

sahihi wakati wa mchakato wa kuomba ruzuku au kufungiwa baada ya kupokea ruzuku.

14.2 Masharti ya ruzuku

a. Wakati muda wa ruzuku umekwisha, hakuna ulazima wa aina yoyote kwa Foundation

kutoa ruzuku tena kwa mradi husika.

b. Fedha hazitatolewa mpaka asasi husika inatiliana saini mkataba na Foundation ambao

utaeleza wazi masharti ya fedha ya ruzuku.

c. Kama asasi haitafuata makubalino wakati wa utekelezaji basi ruzuku hiyo inaweza

kuondolewa, kusimamishwa au kufutwa muda wowote.

d. Tunaweza kutumia jina la asasi yako na mradi husika katika kujitambulisha kwa umma

na kazi zake na taarifa ya mradi wako na jina lake itakuwa ni kitu cha wazi kwa umma

na kitatangazwa. Hata hivyo huna ruksa ya kutumia jina au alama ya Foundation kwa

manufaa yako au ya asasi yako bila kibali cha maandishi kutoka kwa Foundation.

e. Maombi yote ya ruzuku ambayo yatakuwa yamepitishwa yatatangazwa katika magazeti

ya kitaifa kama sehemu ya sera za uwazi za Foundation.

f. Foundation itahakikisha inaipa taarifa serikali juu ya ruzuku zote ilizotoa kitaifa na ngazi

ya chini. Wote waliopokea ruzuku wanatarajiwa kutoa taarifa ya ruzuku zao kwa serikali

za mitaa kwa maandishi.

g. Mradi wako utaangaliwa na kukaguliwa na wafanyakazi wa Foundation, washauri wake

na wafadhili wake. Wale wanaopewa ruzuku wanatarajiwa kuweka kumbukumbu za

fedha zikiwemo vocha za matumizi kwa ruzuku zote wanazopewa.

h. Wapokea ruzuku wa The Foundation inawalazimu kuzingatia Kanuni za Maadili za

Mashirika Yasiyo ya Serikali (NGOs)zilizoambatishwa na mwongozo huu.

25
15. Viambatisho

15.1 Kiambatanisho 1 Wadhamini wa ufadhili

Jina la asasi ...........................................................................................................................................

Jina la Mfadhili Mtu wa kuwasiliana

naye

Taarifa za anuani ya

madhamini kama

simu, sanduku la

posta anuani ya

barua pepe

kiasi cha fedha

kilichowahi kutolewa

naye

jina la Mradi siku ya kuanza na

kumalizika

Zingatia: Kwa wale walioomba ruzuku ya Kati watatakiwa kujaza taarifa za wafadhili kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita

26
15.2 Kimabatanisho cha II: Mpango wa mafunzo

Malengo ya

mafunzo/

Warsha

Dondoo za mada

zitakazozungumziwa

Mbinu za

ufundishaji

zitakazotumika

Kundi lililolengwa Vigezo vilivyotumika

kupata washiriki

Elimu iliyotolewa

itakavyoweza kusambazwa

kwa makundi mbalimbali

27
15.3 Kiambatanisho III: Muundo wa upangaji wa Bajeti

JINA LA ASASI:…………………………………………………………………………….

S/No Shughuli zinazohusika na vinavyotakiwa Gharama

ya

mkataba

1.0 Maandalizi ya Mradi Waratibu 4, 2 kila

Wilaya … Siku 3

Gharama

za Jumla

QTR 1

Gharama za

Jumla QTR 2

Gharama za

Jumla QTR 3

Gharama

za Jumla

QTR 4

Mwaka

wa 1

Jumla

Mwaka

wa 2

Jumla

Mwaka

wa 3

Jumla

1.1 Nauli Waratibu 2 @ 10,000/= 20,000 20,000 0 0 0 20,000

1.2 Nauli Waratibu 2 @ 12,000/= 24,000 24,000 0 0 0 24,000

1.3 Posho kujikimu Waratibu 4 @ 11,000/= X Siku

2

1.4 Kuchapa barua ya mwaliko nakala 1 X

1,000/=

1.5 Kuchapa barua ya taarifa ya mafunzo nakala 1

X 1,000/=

1.6 Kuchapa barua ya mwaliko kwa viongozi

serikali nakala 1 X 1,000/=

1.7 Kurudufu (kutoa nakala) barua za kuhudhuria

mafunzo nakala 220 @ 50/=

1.8 Kudurufu barua za taarifa ya mafunzo

Wawezeshaji nakala 4 X 50/=

1.9 Kudurufu barua ya mwaliko Viongozi wa

Serikali 4 X 50/=

88,000 88,000 0 0 0 88,000

1,000 1,000 0 0 0 1,000

1,000 1,000 0 0 0 1,000

1,000 1,000 0 0 0 1,000

11,000 11,000 0 0 0 11,000

200 200 0 0 0 200

200 200 0 0 0 200

1.10 Bahasha Pcs 228 @ 50/= 11,400 11,400 0 0 0 11,400

1.11 stempu kutuma barua Pcs 228 X 400//= 91,200 91,200 0 0 0 91,200

Jumla ndogo Na.1 249,000 249,000 0 0 0 249,000

(Katika mstari wa 1.0, 2.0, 3.0 na nyingine katika kolamu ya Shughuli na pembejeo (Activity and Inputs) inaonyesha masuala mbayo yanatakiwa kufanyiwa kazi kwa ujumla wake bila kuacha,

inatakiwa ionyeshe nini kinatakiwa kufanywa, wapi, kw amuda gani na kwa ajili ya nani. Kutoka mstari wa 1.1 kuelekea chini katika kolam ya Shughuli na pembejeo (Activity and Inputs)

,kunaonyesha na kutengeneza hesabu ya gharama za jumla kwa kila pembejeo inayotakiwa; Inatakiwa ionyeshe wazi, idadi ya namba na gharama kwa kila pembejeo inatakiwa kwa ajili ya

kukamilisha Shughuli. Gharama halisi kwa kila kimoja inatakiwa ionyeshe kama Jumla ya thamani ya mkataba (Total Contract Value). Kwa gharama za jumla za Ruzuku ndogo ya QTR 1

inatakiwa iwe sawa na Jumla ya thamani ya mkataba ( Total Contract Value) , kwa miradi yenye miaka mingi na wafadhili wengi, makadirio ya wastani kwa kila mwaka lazima yaonyeshwe

chini ya kila mwaka 1, 2 na 3. na katika kila mwaka wa uendeshaji gharama zinatakiwa kugawanywa katika robo kwa kutegemea ni wakati gani shughuli hiyo itafanyika). Tunashauri bajeti

itengenezwe wakati mipango ya kazi imeshaandaliwa.

28
15.4 Kiambatanisho lV: Mpango wa ufuatiliaji na tathmini

Mabadiliko Maelezo ya lengo

viashiria vinavyoweza kutathminiwa (Idadi

ya viashiria kwa kila tokeo visizidi viwili (2])

Matokeo

Shughuli

Mabadiliko

Matokeo

Shughuli

Chanzo cha taarifa

(Data Source)

Namna ya

ukusanyaji wa

takwimu

Muda wa

kukusanya

takwimu hizo

29
15.5 Sera ya ‘Kutovumilia Rushwa Hata Kidogo’:

The Foundation for Civil Society inaendesha sera ya ‘Kutovumilia Rushwa Hata Kidogo’ kwa aina

zote za rushwa, ndani ya the Foundation na huduma zake, pia nje pamoja na wale wote ambao the

Foundation inaweza kuwa na mahusiano ya aina yoyote. Mfanyakazi yeyote wa the Foundation

atakayepatikana na hatia, kufuatia uchunguzi wa kina wa vitendo visivyofaa vya rushwa, atachukuliwa

hatua kali chini ya taratibu za kinidhamu za The Foundation.

Pale ambapo mwananchi yeyote atakuwa na sababu za kumtilia shaka mtu yeyote anayehusiana na the

Foundation, basi anatakiwa awasiliane na Mkurugenzi Mtendaji, akimwamini kabisa, na kumuarifu

juu ya masuala hayo mapema iwezekanavyo, kwa maandishi ikiwezekana, au kwa njia nyingine

zilizopo, akitoa ushahidi kadri awezavyo kusaidia madai yake mara tu atakapo tahadharishwa au

kufuatwa moja kwa moja.

Mkurugenzi Mtendaji atahakikisha kwamba jambo hili linachunguzwa kwa siri na kwa unyeti wake

ndani ya taratibu za the Foundation za malalamiko na kuhakikisha kutobainika kwa mlalamikaji,

ili kumlinda asiwekwe katika hatari. Mlalamikaji hatabaguliwa kwa aina yoyote ile kutokana na

kuwasilisha malalamiko ya kweli.

Baada ya hapo the Foundation itaendesha uchunguzi wa kina, ambao matokeo yake yatarejeshwa

kwa mlalamikaji yakiwa na maamuzi yaliyo kamili na yanayostahili.

Ikumbukwe kwamba uchunguzi wowote na matokeo yoyote yatazingatia sera ya malalamiko na

taratibu za the Foundation, hususani ikizingatia misingi ya haki na Sheria za Tanzania. Kwa taarifa

zaidi ya jinsi ya kuwasilisha malalamiko rejea Sera ya the Foundation ya Kushughulikia Malalamiko

(15.6), ambayo pia hupatikana katika tovuti yetu, www.thefoundation-tz.org

15.6 Sera ya Kushughulikia Malalamiko

The Foundation for Civil Society ina maadili 5 ya msingi, ambayo ni haki, uadilifu, uweledi, uwazi

na uwajibikaji, na usawa wa kijinsia. Katika misingi ya maadili haya, the Foundation inadhamiria

kutoa fursa kwa wanaopokea huduma zetu kutoa malalamiko kwenye masuala ya rushwa, tabia,

taratibu na kufanya maamuzi. Hivyo basi, the Foundation imetayarisha Sera hii ya Kushughulikia

Malalamiko ili itumike na wadau wetu wote. Lazima ieleweke kwamba Sera ya Kushughulikia

Malalamiko hairuhusu kwa namna yoyote ile ukataji wa rufaa kwa maamuzi yaliyofanywa na

the Foundation. Maamuzi kuhusu ruzuku yaliyofanywa na the Foundation ni ya mwisho, lakini

malalamiko dhidi ya maamuzi yataisaidia the Foundation kuboresha maamuzi/huduma zake za

baadaye. The Foundation itashughulikia malalamiko yote katika njia iliyo ya haki, bila upendeleo,

uwazi na kwa muda unaofaa.

The Foundation inakusudia kufanya yafuatayo:

• Kushughulikia malalamiko kwa uzito wake na kwa ufanisi

• Kutatua malalamiko haraka pale inapowezekana

• Kujifunza kutokana na malalamiko na kuchukua hatua za kuboresha huduma zetu

• Kumsaidia na kumlinda mlalamikaji

Unatakiwa ufanye nini unapokuwa na malamiko

Unapotaka kuwasilisha malalamiko kuhusu the Foundation, ruzuku iliyotolewa na the Foundation au

30
kuhusu mfanyakazi wa the Foundation, au Mjumbe wa Bodi, unaweza kufanya hivyo kwa maandishi,

kwa kutumia nukushi, barua pepe (malalamiko@thefoundation-tz.org), kwa simu au kwa kuja wewe

mwenyewe. Wale wanaopenda kuja kutoa malalamiko yao wenyewe watahitaji wapangiwe muda.

Iwapo malalamiko yako utayatuma kwa kuandika barua, nukushi au barua pepe, tafadhali onyesha

namba yako ya simu, iwapo jibu la awali kwa kutumia simu litafaa. Iwapo unatuma kwa baruapepe,

tafadhali onyesha iwapo unahitaji majibu kwa barua pepe, kama sivyo, tafadhali toa anuani

kamili ya posta. Tutakuomba uweke malalamiko yako katika maandishi, iwapo umewasiliana nasi

kwa mdomo. Tutaweza kukupatia msaada kwa hili iwapo ni lazima. Kwa mara ya kwanza wasilisha

malalamiko yako moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa the Foundation au iwapo inastahili

na katika mazingira yasiyo ya kawaida, kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi.

Utapokea uthibitisho kutoka kwetu kwamba malalamiko yako yamepokelewa. Iwapo hutapokea

uthibitisho ndani ya siku saba za kazi za kuwasilisha malalamiko yako, tafadhali wasiliana na

Mkurugenzi Mtendaji moja kwa moja.

Nini kinafuata baada ya hapo

Baada ya kupokea malalamiko yako, tutalenga kujibu mara moja, na mara zote ndani ya siku 14.

Iwapo hili haliwezekani, tutaeleza kwa nini na kukujulisha itachukua muda gani.

Iwapo hujafurahia majibu ya awali unayopata, wasiliana na Mkurugenzi Mtendaji tena na utafute

ufafanuzi. Kufuatia jibu la pili, iwapo bado hujaridhika, unashauriwa kumuandikia Mwenyekiti wa

Bodi ya Wakurugenzi.

Iwapo bado hujafurahishwa na matendo ya the Foundation, unaweza kumuomba Mwenyekiti wa

Bodi apeleke malalamiko yako kwa Waamuzi huru wachunguze malalamiko yako jinsi ambavyo

yalivyoshughulikiwa.

Usiri

Kwa ujumla walalamikaji wanahimizwa na the Foundation watamke majina yao na jinsi ya kuwapata,

wanapowasilisha malalamiko. Kwa kufanya hivyo wanahakikishiwa viwango vya juu kabisa vya

usiri na Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Bodi. Hata hivyo, katika mazingira yasiyo ya

kawaida, mlalamikaji anaweza kuamua kutoonyesha jina lake au maelezo ya jinsi ya kumpata na

anaweza kuwasilisha malalamiko yasiyo na jina. Hata hivyo, walalamikaji watambue kwamba

ushirikiano wa moja kwa moja na walalamikaji unawezesha kwa kiwango kikubwa kushughulika, na

kuirahisishia the Foundation kuchukua hatua za kutosha, za haki na endelevu ili kutatua mapungufu

yanayohusika.

31