08.03.2015 Views

jamhuri ya muungano wa tanzania - Tanzania Education Network ...

jamhuri ya muungano wa tanzania - Tanzania Education Network ...

jamhuri ya muungano wa tanzania - Tanzania Education Network ...

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

HOTUBA YA MKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO

ILIYOTOLEWA KATIKA UFUNGUZI WA JUKWAA LA

MAZUNGUMZO YA UGHARIMIAJI WA ELIMU TANZANIA

BLUE PEARL HOTEL, DAR ES SALAAM

16 SEPTEMBA, 2010

2

Mheshimiwa Mwenyekiti wa TEN/MET

Mheshimiwa Mratibu wa TEN/MET

MAOFISA WA IDARA MBALIMBALI ZA TEN/MET

WANACHAMA WA TENMET

WAWAKILISHI WA WIZARA, TAASISI NA IDARA ZA

SERIKALI

Wawakilishi wa Asasi zisizo za Kiserikali,

Wawakilishi wa Mashirika ya Wafadhili,

Wageni Waalikwa,

Mabibi na Mabwana,

Ninayo furaha na heshima kubwa kupewa fursa hii ya

kufungua jukwaa hili na mdahalo unaozungumzia

mambo yanayohusu ugharimiaji wa elimu.

Ninakumbuka kuwa tarehe 24 mwezi wa nne mwaka

huu, tuliadhimisha kwa ushirikiano kilele cha Kampeni

ya Kuadhimisha Juma la Elimu la Kimataifa kwenye

viwanja vya Mnazi Mmoja. Natambua kuwa kampeni hizi

za elimu za kimataifa hufanyika kila mwaka, na

zinaratibiwa na Shirika la Kimataifa la Kampeni za Elimu

2

3

(Global Compaign on Education - GCE ). Nafahamu pia

kwamba, kwa mwaka huu Kauli Mbiu ni „Ugharamiaji

wa Elimu’ (Financing Education) pamoja na ujumbe

usemao “Elimu ni Kitega Uchumi, Wekeza Sasa kwa

Manufaa ya Kesho”

Kuanzia mwezi wa nne mwaka huu, kwa pamoja

tumeshirikiana katika kuhakikisha kuwa ujumbe wa

ugharimiaji wa elimu unawafikia viongozi wote

wanaohusika katika utoaji wa maamuzi yanayohusu

ugharimiaji wa elimu. Ujumbe huu umetumwa katika

ngazi ya kitaifa hadi kimataifa.

Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru wadau wa

elimu wote mliofika kushiriki kwenye jukwaa hili la

mazungumzo ya pamoja kati ya Serikali na Mashirika

Yasiyo ya Kiserikali. Nafurahi kuwa mnatambua na

kutilia maanani maneno yaliyosemwa na viongozi

waliotangulia kuwa “Nchi tunayoijenga ni moja

Tanzania, Kwa nini tugombanie fito?” Kwa utambuzi

huu, nasema Ahsanteni sana.

Napenda nianze kwa kutoa pongezi zangu za pekee na

za dhati kwa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET)

3

4

kwa juhudi zenu mnazozifanya kila mwaka katika

maadhimisho haya ambayo hufanyika duniani kote kwa

lengo la kuboresha masuala mbalimbali ya elimu

hususan upatikanaji wa elimu bora kwa watu wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika kipindi cha miaka 15

iliyopita, Serikali ya Tanzania imeongeza tija na nia

thabiti ya kuboresha elimu katika ngazi zote kwa kuweka

Sera ya Elimu na Mafunzo, 1995 ambayo ipo katika

mchakato wa kuhuishwa, Mpango wa Maendeleo ya

Sekta ya Elimu, mipango mingine na mikakati maalum

inayoongoza utoaji elimu kwa wananchi. Miongoni mwa

mipango mingineyo na mikakati iliyopo ni Mpango wa

Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM), Mpango wa

Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES), Mpango wa

Maendeleo ya Elimu ya Juu (MMEJ) na Mpango wa

Maendeleo ya Elimu ya Wananchi. Aidha, Mpango wa

Maendeleo ya Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi upo

katika mchakato wa utayarishaji. Pia Serikali inatekeleza

Mkakati wa Maendeleo na Menejimenti ya Walimu na

Mkakati wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya

Mfumo Rasmi.

4

5

Mipango hii iliibuliwa ili kukidhi mahitaji ya kuongeza

fursa za upatikanaji wa elimu iliyo bora kwa watanzania

wote. Mipango na mikakati mbalimbali ilitekelezwa kwa

madhumuni ya kuitikia matamko ya kitaifa yaani

MKUKUTA na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025.

Vile vile kutekeleza matamko ya kimataifa ambayo taifa

lilikuwa limeyaridhia na kukubali kuyatimiza. Baadhi ya

matamko haya ni kama vile; Tamko la Dakar 2000 Elimu

kwa Wote na Malengo ya Maendeleo ya Milenia. Haya

yote yanazitaka nchi wanachama kuunga mkono jamii

za kimataifa katika kuboresha upatikanaji wa elimu bora

kwa wote ikiwa kama haki ya msingi ya kila

mwanadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Matunda ya jitihada za

Serikali katika kuboresha upatikanaji wa elimu, yako

wazi kwa sasa. Chini ya MMEM na MMES

tumeshuhudia mapinduzi makubwa katika upatikanaji

wa elimu kwa watoto wengi zaidi wenye umri wa

kwenda shule za msingi na wale wote wanaofaulu

5

6

kuendelea na masomo ya sekondari. Baada ya juhudi

kubwa za Serikali na jamii kuchangia katika kujenga

shule nyingi za msingi na sekondari, hasa maeneo ya

vijijini ambako kulikuwa na changamoto kubwa, hivi

sasa vijana wengi zaidi (wa kike na kiume) wanapata

fursa za kujiunga na elimu ya msingi na

sekondari.Mpaka mwaka 2010 wapo wanafunzi

8,419,305 (wasichana 4,216,038) wa shule za msingi

kutoka 5,981,338 (wasichana 2,929,3300) na 1,638,699

(wasichana 728,528) wa sekondari 2010 kutoka

wanafunzi 323,318 (Wasichana 147,263) mwaka 2001.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kama nilivyosema hapo

mwanzo kwamba, kauli mbiu ya kampeni ya

kuadhimisha wiki ya Elimu ya Kimataifa ni “Ugharimiaji

wa Elimu” (Financing Education) na ujumbe ni

“Elimu ni Kitega Uchumi, Wekeza Sasa kwa Manufaa

ya Kesho, elimu kwa watanzania ni muhimu sana hasa

katika mbio zetu za kupambana na maadui watatu;

ujinga, maradhi na umaskini. Silaha pekee ya

kuwashinda maadui hawa wote watatu ni elimu bora.

Maana elimu kama inavyobainishwa na Sera ya Elimu

6

7

na Mafunzo ni mchakato ambao mtu hupata maarifa na

ujuzi wa kujitambua na kujiweka sawa katika

kupambana na mazingira na mabadiliko ya mara kwa

mara ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Aidha, elimu ni

kama njia kuu ya mtu kuweza kutambua uwezo wake

kamili.

Hivyo basi, Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ni suala

muhimu sana kwa kila mtu bila kujali umri, jinsia, rangi

wala dini. Na kwa kutambua hilo Serikali imekuwa

ikihakikisha inapandisha bajeti ya sekta ya elimu.

Mwaka 2007/08 bajeti ya sekta ya elimu ilikuwa ni trilioni

1.1 ma mwaka 2010/11 imefikia trilioni 2.2 Lengo ni

kuziwezesha taasisi zote za elimu kuanzia ngazi ya

elimu ya awali hadi vyuo vikuu kupata rasilimali

zinazotakiwa ili kuhakikisha watanzania wengi wanapata

maarifa na ujuzi bora wa aina mbalimbali ili waweze

kuyamudu maisha na mazingira yao na kuchangia

maendeleo ya haraka katika jamii zao. Hii ni kutokana

na ukweli kwamba, fursa ya elimu kwa watanzania ni

namna pekee ya kuwapa dhana na silaha za

kukabiliana, si tu na mitego ya ujinga, umaskini na

7

8

maradhi, bali pia mitego ya ukoloni mamboleo, na

ushindani wa kimataifa.

Dhumuni kubwa la ugharimiaji wa elimu ni kuhakikisha

kwamba kila mtanzania anapata elimu iliyo bora ambayo

itamwezesha kukabiliana na changamoto za maisha

katika mazingira anayoishi.

Pamoja na mafanikio mengi ambayo Serikali imeweza

kuyafikia katika kuboresha elimu nchini, imeweza

kuhamasisha na kuchangia katika ongezeko la majengo

ya shule za msingi na sekondari na kupelekea

ongezeko kubwa la uandikishwaji wa wanafunzi.

Kwa sasa hivi Serikali ikishirikiana na wadau mbalimbali

wa elimu, ipo kwenye mchakato wa kupitia Sera ya

Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995. Ni matarajio yetu

kwamba sera inayopitiwa itaweza kutoa ufumbuzi wa

changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu.

Mheshimiwa mwenyekiti, Pamoja na historia nzuri

ya mafanikio tuliyoyapata katika sekta ya elimu, bado

tuna changamoto kadhaa katika ugharimiaji wa elimu.

Changamoto hizi zimeviza kwa kiwango fulani utoaji

wa elimu bora kwa watanzania wote.

8

9

Baadhi ya changamoto hizo ni kuwepo na idadi kubwa

ya wanafunzi wahitaji kugharimiwa elimu

ikilinganishwa na uwezo wa serikali. Aidha, uainishaji

wa wahitaji wa kugharimiwa elimu pia ni changamoto.

Vile vile, bado hatuna mkakati mahususi wa kivitendo

unaoweza kuhamasisha na kuchangia elimu kwa

ujumla katika ngazi ya jamii. Kwa mfano, wanajamii

wapo tayari kuchangia fedha nyingi za harusi kuliko

mwanafunzi aliyekosa ada ya kulipa shuleni.

Maana ni ukweli ulio wazi kwamba, kama taifa

litaundwa na jamii kubwa yenye watu wasio na elimu,

maarifa na wenye ujuzi mdogo au hafifu; juhudi za

kujiletea “maisha bora kwa kila mtanzania”

zitakwama. Hii ni kwa sababu ni watu wachache tu

watakaochangia maendeleo ya nchi na sehemu

kubwa ya wananchi watakuwa sio wazalishaji wazuri

katika jamii. Katika mazingira haya ni dhahiri kuwa

familia nyingi zitaendelea kuwa duni hivyo kutishia

maendeleo ya taifa letu.

Mheshimiwa mwenyekiti, serikali ya awamu ya nne

imetoa kipaumbele ili kuhakikisha kwamba ugharimiaji

wa elimu kwa watanzania inapewa kipaumbele na

9

10

kwamba hii inajidhihirisha katika bajeti na mikakati

mingine ya Serikali ambapo sekta ya elimu hupewa

kipaumbele.

Nimalizie kwa kutoa wito kwa wadau wote wa elimu

hapa nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika

kufanikisha azma ya upatikanaji wa elimu kwa

watanzania wote kwa kuzingatia utoaji wa elimu bora.

Maana tukifanikiwa kuboresha elimu basi tutakuwa

tunafikia malengo ya MKUKUTA, Dira ya Maendeleo

ya Tanzania 2025, Elimu kwa Wote na Milenia. Kwa

jinsi hii, tutakuwa tumejenga msingi mzuri wa kuleta

maendeleo nchini.

Baada ya kusema hayo, natamka rasmi kufunguliwa

kwa Jukwaa la mazungumzo kuhusu ugharimiaji wa

elimu. Mazungumzo yanayolenga kuhakikisha

upatikanaji wa elimu bora kwa kila mtanzania, na

usawa katika utoaji wa elimu. Tuendelee

kuhamasisha uboreshaji na ugharamiaji wa Elimu kwa

vile ndiyo “Elimu kwa wote”.

10

11

Ninawashukuru sana kwa kunialika na asanteni

kwa kunisikiliza!

ONE GOAL ... ELIMU KWA WOTE

11

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!