12.07.2015 Views

Untitled - World Council of Churches

Untitled - World Council of Churches

Untitled - World Council of Churches

SHOW MORE
SHOW LESS
  • No tags were found...

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

© WCC – EHAIA, 2005WCC – EHAIA,P.O. BOX 52802 – 00200,NAIROBI, KENYA.Toleo la Kwanza la KiswahiliMhariri Mkuu:Jacinta M. MaingiMhariri wa ToleoWilfred AmalembaWahariri:Paul M. William WambuaPeter NgigeMtafsiriAngeline Mdari (Mrs.)MwandishiBrigitta RubensonMchora PichaElijah NjorogeMpangaji wa KurasaFasons Business Systems LtdKimechapishwa Nchini Kenya


UTANGULIZIMaelezo yaliyo katika kijitabu hiki ni kwa ajili ya kutoamuongozo kwa wahudumu wa afya kuelewa wazi zaidiUkimwi ulivyo, ambao hadi hivi sasa hauna tiba walachango. Ndipo umekwisha kuenea katika sehemu nyingiduniani.Mnamo mwezi Juni 1986 Baraza la Makanisa Duniani(W.C.C.) lilianda kongamano ili kutokea na njia zinazowezakuyahusisha makanisa kukabiliana na janga la Ukimwi.Mapendekezo ya kongamano hilo yalidhihirisha kwambamakanisa yangeweza kuchangia kwa namna tatu:i) kwa malezi ya kiroho;ii) kuwahudumia jamii; na,iii) kuelimisha namna ya kuepuka Ukimwi.Kijitabu hiki kinachangia mapambano hayo.Njia kuu ya kueneza virusi vya Ukimwi, ama kwa kifupi,V.V.U, ni kwa kupitiakujamiiana, iwapomna virusi hivi kwamtu mmoja amawote wawiliwanaojamiiana. Kwahivyo ueneaji wakeunategemea tabia yamtu binafsi. Basimafunzo ya namna


ya kuepuka ndio tu ngao ya kukomesha ueneaji wa V.V.U.Ni lazima kuwe na mabadiliko kwa tabia na mienendokuhusu kujamiiana. Kujamiiana kuwe ni kwawanaoaminiana. Maambukizo ya V.V.U yanategemea sananamna mtu anavyoishi maisha. Walakini pia hutegemea haliya kiafya ya mtu wakati anapoambukizwa. Kuwepo aukutokuwepo kwa huduma za kimsingi za afya vile vilehuchangia sana ueneaji wa maambukizi. Kwa hiyo shughuliza kuwatunza waathirika na zile za kuzuia ueneaji wa V.V.Uzitambuliwe ni baadhi ya jitihada za afya ya kimsingi.Wahudumu wa afya wana wajibu kuwajalia kwa upendo nahuruma walioathirika. Wanastahili kuwa na elimu ifaaokuhusu Ukimwi ili kuwashauri walioathirika jinsi ya kuishikwa matumaini na namna ya kutoeneza V.V.U. Cha muhimuzaidi ni kuwahimiza waathirika washirikishe jamii habarizozote wanazozifahamu kutokana na hali yao. Ieleweke wazikuwa ni wajibu wa kila mmoja kuzuia kuenea kwa V.V.U.Kwa mara ya kwanza Ukimwi uligunduliwa AmerikaKaskazini, Ulaya, na Kusini mwa Sahara barani Afrika kwawakati mmoja. Tangu wakati huo Ukimwi sasa umeeneaduniani kote. Idadi ya watu wenye virusi ni dhihirisho yahatua ambayo ambukizo limepiga na wengi wa waathirikawataugua Ukimwi kati ya miaka tano na zaidi.


UKIMWI NI NINI?Ukimwi ni kifupi cha:Upungufu waKingaMwiliniUkimwi ni hali mbaya ya afya inayoambukizwa kwa kupitia‘virusi’ na dalili zake huwa zinadhihirika kwa njia t<strong>of</strong>auti.Kwa mara ya kwanza Ukimwi uligundulika mwaka 1981.Tangu wakati huo, Ukimwi umeenea kwa kasi sana koteulimwenguni. Habari kuhusu kuenea kwake zinazidikulundika kutoka maeneo mbali mbali duniani na karibukila nchi waleo ina watu walioambukizwa V.V.U aukuathirika na Ukimwi.VVU NI NINI?Virusi Vya Ukimwi ni kirefu cha V.V.U. Virusi hivivinasababisha upungufu wa kinga mwilini.Virusi vya Ukimwi ni vya kipekee. Havifanani na virusivingine vya kawaida. Hii ni kwa sababu virusi hivi huzaanakwa njia maalum na ya kipekee. V.V.U vilitambuliwa kwamara ya kwanza mnamo mwaka wa 1983, huko mjini Paris,Ufaransa, na mchunguzi mmoja wa kisayansi.Virusi hivi hushambulia chembechembe nyeupe katika damuna kupunguza uwezo wao wa kutoa kinga mwilini. Uharibifu


huo ni wa kudumu. V.V.U hupatikana kwa wingi zaidikwenye damu, majimaji ya uzazi, na maziwa ya mama.NI NANI ANAYEWEZA KUAMBUKIZWA?Ye yote yule aliye na V.V.U anaweza kuambukiza hata bilayeye kufahamu, kwani, huenda asiwe na dalili zozote zakudhihirisha hali yake ya afya. Mtu huweza kuishi na virusihivi mwilini mwake kwa miaka mingi bila kufahamu.Wakati huu, virusi huwa bado havijashambulia sehemukubwa ya kinga mwilini ndipo aanze kuugua. Miezi kadhaa


aada ya kuvamiwa na virusi, mwili huandaa kinga dhidi yavirusi hivyo. Uwepo wa virusi hivi hutambuliwa kwakuchunguzwa kitaalam.VIRUSI HUENEZWAJE?Virusi vya Ukimwi huenezwa kupitia damu au majimaji yauzazi. Vinaweza pia kuenezwa na mama aliyenavyo wakatiwa mimba, wakati anapojifungua au kwa kumnyonyeshamtoto mchanga maziwa yake.Mwanzoni virusi hivi huwa havina nguvu sana; lazimavizaane sana ndipo aliyeambukizwa atambue kwambaanavyo. Vinginevyo, idadi ya virusi huongezeka mtuanapoambukizwa mara kadhawa kadha.Virusi huenezwa kwa njiazifuatazo:• kwa kujamiiana namtu aliyenavyo;• kudungwa sindanoiliyochafuliwa navyo;• kuongezwa damuiliyochafuliwa navyo;na,• kutoka kwa mama mjamzito aliyenavyo


kumuambukiza mtoto akiwa bado tumboni, wakatianapojifungua au wakati wa kumnyonyesha mtoto.NI KWA NJIA ZIPI AMBAZO V.V.U HAVIENEZWI?Virusi havienezwi katika kushirikiana kwa njia za kawaida,kwa mfano:• kwa kushikana mikono;• kuishi pamoja;• kucheza pamoja; na,• kula na kunywa pamoja.Pia, V.V.U haviwezi kuenezwa na:• chakula;• maji;• vyombo vya chakulana vinywaji;wadudu; au,• mahali pa kujisaidia(msalani).


JINSI YA KUZUIA KUENEA KWA V.V.UAwali ye yote wapaswa kufahamu kuwa hakuna chanjo yakuzuia kuambukizwa V.V.U wala tiba ya Ukimwi. Kila mtuanapaswa kufahamujinsi ya kujikingadhidi ya V.V.U nakuishi maisha yakuwajibika. Katikasuala hili inabidijamii yote kuhusika.Hivyo elimu ya afyani ya maana kabisa.NI KINA NANI WANASTAHILI KUARIFIWA?Kila mtu


MAISHA YA KUWAJIBIKA NI YAPI?Katika jamii nyingi ishara ya utu uzima ni kuanzakujamiiana kwa wavulana na wasichana. Kwa hivyo vijanahuwa na msisimko mku wa kuanza kujamiiana mapema.Walakini si lazima kufanya hivyo ili kujihisi umekuwa mtumzima au usiyet<strong>of</strong>autiana na vijana wengine wa kawaida.Kutojamiiana ndiyo njia bora zaidi ya kujikinga. Kunazo njianyingi nyinginezo za kuonyesha upendo kama vilekubusiana, kupigana pambaja, kushirikiana katika shughuli,kutiana moyo na kupeana mawaidha mema.Kuimarisha uhusianomwema una<strong>of</strong>aahuchukua muda.Unaweza ukavunjwana kutoaminiana.Kujamiiana nawapenzi wengikunaweza kuonekanakama jambo lakusisimua walakinilinaweza kuletahasara kubwa. Kilamara mtu anapojamiiana kiholela ndipo anapozidi kuwakatika hatari kuu ya kuambukizwa V.V.U au magonjwamengine ya zinaa. Ili uwe salama, inapaswa uwe na mpenzimmoja mnaoaminiana.


Kwa hiyo:• Kila wakati unapojamiiana vaa mpira (condom)kujikinga dhidi ya V.V.U au magonjwa ya zinaa.Mpira wenyewe uwe wa hali ya juu na uvaliwe kwanjia inay<strong>of</strong>aa mda wote wa kujamiiana. Inapaswampira uvaliwe mara moja tu kisha utupwe kwa njiaifaayo.• Jiepushe na watu wanaojamiiana kiholela.Kutojamiiana hatakama ni kwa mdamrefu, hakudhuruafya ya mwanamkeau mwanamume.Kinyume na hayo,ukweli ni kwambahiyo ndiyo njiasalama kabisa yakuzuiakuambukizwa virusi na hata yale maradhi mengineya zinaa.• Epuka kudungwa sindano ila katika zahanatizinazotambulika ambapo una uhakika vyombo hivyoni salama.• Hakikisha ya kuwa vyombo au vifaa vya kutahiri,kutoboa masikio au kufanya urembo wa kuchanjangozi vimechemshwa na ni salama.


NI NANI YUKO HATARINI KUAMBUKIZWA?Ni kila mtu ambaye yuko hatarini ya kuambukizwa, hasa:a) Watu walioambukizwa magonjwa ya zinaa na walewalio na vidonda katika sehemu zao za siri.b) Watu wanaojamiianakiholela.c) Wanawake auwanaumewanaojamiiana nawateja wengi kwamadhumuni yamapato.d) Wagonjwawanaodungwasindano ambazo sio salama.e) Wagonjwa wanaoongezwa damu ambayohaijachunguzwa.


UKIMWI NA MIMBAMama aliye na virusi vya Ukimwi anaweza kumuambukizamtoto wake kabla hajajifungua, wakati anapojifungua, auanapomnyonyesha. Mimba inaweza kufichua dalili zaUkimwi. Baadhi ya hospitali namahabara zina utaalam wakuchunguza iwapo mtuameambukizwa. Kwa hivyo,mwanamke ambaye hanauhakika na ambaye anatakaapate mtoto anapaswaachunguzwe kwanza.Mwanamke ambaye anajua auanashuku kwamba ana V.V.Uanapaswa kuepuka kupatamimba ili aweze kudumishaafya bora kwa mda mrefuiwezekanavyo. Mume na mkewanashauriwa kutumia mpira(condom) wakati wote wanapojamiiana ili kukinga kushikamimba na hata ongezeko la maambukizi ya V.V.U.


V.V.U HUENEZWA KWA KUNYONYESHA?Utafiti unabainisha kwamba virusi vya Ukimwi huendavikapatikana kwenye maziwa ya mama. Basi, kuna hatari yamtoto mchanga kuambukizwa anaponyonya. Lakini, kwavile kuna hatari kuu ya mtoto kuambukizwa magonjwamengine kwa kupewa maziwa kwa chupa, mama aliye naV.V.U anashauriwa kumnyonyesha mtoto kwa mda upataomiezi sita. Baada ya hapo, ampe chakula cha kutafuna.Imebainika kwamba katika mpangilio huo hatari ya mtotokuambukizwa V.V.U hupungua.UKIMWI NA KUCHANJWASindano ndizo hutumika katika shughuli za kuchanja watuili wasiambukizwe nabaadhi ya maradhi.Katika hali hiyo, vifaahivyo vinawezakuchangia uenezaji waV.V.U. Iwapo sindanozitachemshwa kwadakika ishirini kabla ya kuchanja mtoto, hatari ya kuenezavirusi katu haipo. Inapaswa sindano zinazotumika maramoja zitiwe katika sanduku na kutupwa kwa njia yausalama. Daima juhudi ifanywe kuzuia damu isipenye ndaniya bomba la sindano wakati wa kudunga.


KUKAGULIWA KWA DAMUMtu anayeshuku kwamba ana virusi vya Ukimwi anastahilikukaguliwa damu ili ukweli ubainishwe. Namna mbilimuhimu za kukagua damu ni ELISA na ile ya matokeo yaharaka. Kwa kawaida mwili huchukua kati ya miezi 2 hadi 6ili kujitengenezea kinga.Kutoonyesha ishara hiyo siodhihirisho kwamba mtuhajaambukizwa virusi.Kabla ya kukaguliwa damu,mtu anastahili kushauriwa ilikumuandaa apokee matokeo.Iwapo ana V.V.U ushauriutahusu jinsi atakavyo badilimienendo na kuishi kwamatumaini. Ikiwa hanaV.V.U mtu huyu atashauriwa kuepuka tabia zinazowezakuhatarisha maisha yake katika siku za usoni. Ukimkaguamtu damu ni haki yake apewe matokeo, kwani asipopewa,hatajua hatari aliyonayo kwake mwenyewe na kwa wengine.MTU ALIYE NA V.V.U YAMPASA AFAHAMUYAFUATAYO:Mtu anayefahamu au kushuku ana V.V.U anapaswakuzingatia yafuatayo:1. Epuka kabisa kueneza virusi vya Ukimwi kwa njiazifuatazo:-


a. Hakikisha kwamba hauenezi V.V.U kwa:i. Kutojamiiana bila matumizi ya mpiraii. Kutochangia utoaji wa damu2. Jikinge dhidi ya magonjwa ya zinaa.3. Hakikisha usivute sigara au kujiingiza katika uleviwa aina yeyote.4. Kula lishe bora.5. Hakikisha unapata tiba kwa magonjwa yafuatayo:a. Kifua kikuub. Malariac. Magonjwa ya zinaa.


UNAVYOWEZA KUMTAMBUA MTU ALIYE NA V.V.UBaadhi ya waathirika hushambuliwa na homa, kikohozi aumaumivu makali kooni. Baada ya hapo huenda wasionyeshedalili zozote kwa muda mrefu. Dalili za Ukimwihut<strong>of</strong>autiana sana katika nchi mbali mbali ulimwenguni.Ishara na dalili zingine hua zaidi kakitka sehemu mojakuliko nyingine. Ishara kama vile kupoteza uzanihudhihirika sana barani Afrika. Huko Marekani isharainayojitokeza sana ni kichomi kikali, ilhali barani Asia kifuakikuu hudhihirika sana.Ishara na dalili za Ukimwi ni sawa na zile za magonjwamengine. Kwa hivyo ni kupitia kwa ukaguzi wa damu tukunaweza kubainisha iwapo mtu ana V.V.U au Ukimwi. Kwakumtazama mtu huwezi kujua ikiwa ana V.V.U amaUkimwi.KUDHIBITISHA KUWA MTU ANA UKIMWIIli kudhibitisha kuwa mtu mzima ana Ukimwi inastahilidalili kuu mbili na moja ndogokudhihirika. Kwa mtoto mdogo ni dalilikuu mbili na mbili ndogo zinazodhihirika.Dalili Kuu• Kupoteza zaidi ya asili mia kumi yauzani wa mwili kwa mtu mzima.• Kuvia au kukua pole pole sana kwamtoto mchanga.


• Kuharisha mfululizo kwa zaidi ya mwezi mmoja.• Kuwa na homa zaidi ya mwezi mzima.Dalili Ndogo• Kukohoa kwa mda mrefu.• Mwasho wa ngozi.• Kuvimba kwa tezimwilini.• Maambukizo ya marakwa mara kwa watoto.• Kuwa na vidonda aina yaHerpes Zoster ambavyo haviponi kwa mtu mzima.• Kushambuliwa na vidonda aina ya Herpes Simplexkwa mtu mzima.JINSI YA KUMSAIDIA MTU ALIYE NA UKIMWIHadi waleo, hamna tiba ya Ukimwi, ijapokuwa zipo dawa zakuzuia V.V.U visizaane kwa kasi, zinazojulikana kama ARV.Muathirika ashauriwe kutumia dawa za kienyeji iwapo zipo.Waathirika wanapaswa kupata matibabu mara tuwanaposhambuliwa na maradhi mengine. Kila juhudiifanywe ili wawe na raha.


KUTIBU ISHARA AU DALILI ZA MAGONJWAKuharishaHili ni tatizo la kawaida mno hasa miongoni mwa watotowadogo. Jambo kuu la kuzingatia ni kupungukiwa na majimengi. Mpe mgonjwa:• Myeyusho wa chumvi na sukari.• Myeyusho maalum wa ORS• Vinywaji.• Tiba za kienyeji.• Usimpe mtoto dawa za kuangamiza vijidudu auvidonge vya kuzuia kuharisha.Vindonda vya mdomoni na kooni• Paka dawa ya urujuani.• Sukutua mdomo kwa kutumia maji yenye chumvi.• Tumia dawa za kienyeji.VilengelengeMpe asprini au paracetamol.HomaHii ni dalili ya kawaida kwa watoto na watu wazima.• Mpe mgonjwa vinywaji.• Muoshe mgonjwa na maji ya joto kiasi.• Mpe mgonjwa asprini au paracetamol


Kikohozi; Kichomi Kikali; Vidonda Masikioni; KifuaKikuuMgonjwa apatiwe dawa ya kuangamiza vijidudu.Mgonjwa apelekwe hospitali au zahanati apate tibainayostahili.Mwasho wa ngoziMgonjwa apelekwe hospitali auzahanati apate tiba inayostahili.


UTUNZAJI WA MUATHIRIKA WA UKIMWIKumbuka kwamba watu walio na virusi au walewalioathirka Ukimwi wanahitaji kushiriki pamoja katikajamii. Pumzi na hata ngozi yao haiambukizi V.V.U nawanahitaji kutangamana katika hali zote. Ni jambo lamuhimu kuelimisha jamaa ya muathirika ukweli kuhusuUkimwi ili wasije wakamuogopa.Mara tu muathirika anap<strong>of</strong>ahamu ukweli kuhusu hali yake,anahitaji kushauriwa kikamilifu ili aweze kukabiliana nahisia za woga, wasiwasi na hasira. Wahudumu wa afya nafamilia ya mgonjwa wanahitaji kujiandaa. Waathirikahuhitaji mtu aliye mvumilivu na tayari kuwasikiliza na


kuwatia moyo. Wanahitaji kuhimizwa kuishi na kushirikikatika maisha ya kawaida kwa uwezo wao.Ukimwi hupunguza kinga mwilini. Muathirika akishaanzakuwa na ishara na dalili za Ukimwi mwili wake huzidikudho<strong>of</strong>ika. Hata hivyo, mtu anaweza kuishi kwa mdamrefu kutoka alipoambukizwa hadi kuugua na hatimayekufa na ni muhimu sana kumsaidia kuishi vyema kwa mdahuo wote.Watu wengi huogopa kifo kwa sababu siri yake haijulikani.Waathirika wanahitaji nafasi ya kuieleza hali yao kwa mtuwanaye muamini na yutayari kuwasikiliza. H<strong>of</strong>u nawasiwasi wao hupungua wanapojieleza.MUATHIRIKA APATE USAIDIZI WAPI?Hospitali au zahanatiWagonjwa wenye homa kali, kuharisha na maumivuwanahitaji utunzaji katika zahanati kwa mda fulani.Wanahitaji tiba na uuguzi ufaao.NyumbaniMgonjwa ambaye anaweza kutunziwa nyumbani aruhusiweili jamaa walioelimishwa barabara wampokee na kumsaidiainavyowezekana.Kuuguza mgonjwa katika hospitali au zahanatiHakuna sababu ya kumtenga mgonjwa, kwa kusudi lakutoeneza V.V.U. Hata hivyo, huenda ikalazimu kumtengaasiambukizwe magonjwa mengine.


Taratibu za usafiYapasa waathirika wasaidiwe kuishi katika mazingira safi.Maisha hayo yawezekana bila ya hatari. Hata hivyo, kunamambo machache ya kukumbuka:• Nguo chafu hasa zenye damu zaweza kueneza virusi.• Vidonda vinavyotokwa damu au vidonda vinginevyote vyaweza kueneza virusi.Kwa hiyo matandiko na nguo zilizochafuka zinastahilikulowekwa katika myeyuko wa klorin kabla ya kufuliwa. Nimuhimu kwa wahudumu wavae glavu (mifuko ya kuvaliamikono) wanapowashughulikia wagonjwa na kisha wafungevidonda vinavyotokwa damu. Pale vifaa hivyo haviwezikupatikana, sabuni itumiwe kuisafisha mikono.


KUUGUZA MGONJWA NYUMBANIMuathirika wa Ukimwi anahitaji kutunzwa kimwili, kirohona kiakili. Kwa vile hakuna tiba,utunzaji bora unawezakutolewa na jamaa.Nyumbani, muathirikayupo katika mazingiraanayoyaelewa na hujihisikuwa salama. Mtu aliyena Ukimwi anastahili:• Kupumzika yakutosha.• Kutumia vinywajina lishe bora.• Kushirikiana najamaa na marafiki.• Kutovuta sigara au kulewa.Ni muhimu kuielimisha jamaa ya muathirika kuhusuUkimwi ili wasiogope kumhudumia. Wanapaswa kujua jinsiya kujikinga dhidi ya V.V.U kwa kutogusa majimajiyanayotoka mwilini mwa mgonjwa. Wanastahilikushirikiana naye ili kumuonyesha upendo. Kumgusahakuambukizi V.V.U ila ni onyesho la kumfariji.Katika jamii ambapo V.V.U vinaenea, yapasa kila mtu kuishimaisha ya tahadhari. Huwezi kumtambua mtu mwenyeV.V.U kwa kumtazama tu kwa hivyo jikinge. Jamii ambayo


inaelewa kuhusu Ukimwi barabara inafahamu kwambakumgusa mgonjwa sio hatari na kwamba wagonjwa huhitajiusaidizi.JAMAA ZA MUATHIRIKA WA UKIMWI WANAPASWAKUJUAKabla ya kumleta muathirika wa Ukimwi nyumbani, jamaawatakaomtunza wanapaswa kuelewa yafuatayo:• V.V.U havienezwi kwa kushirikiana kijamaa.• V.V.U havienezwi kwa kugusana.• Waathirika wanahitaji vyakula bora vyenye nguvu,protini na vitamini.• Waathirika wanahitaji kuguswa na kukumbatiwa.• Kujamiiana na mtu aliye na Ukimwi kuna hatari yakuambukizwa virusi.• Damu na majimaji ya uzazi ya muathirikahuambukiza.• Nguo na vyomboambavyo vimeguswana maji au damukutoka mwilini mwamgonjwa vilowekwekwenye myeyuko waKlorin ikiwezekana,kisha vioshwe kwamaji moto kwakutumia sabuni.


NAMNA YA KUTUNZA VYOMBOVILIVYOCHAFULIWAVirusi vya Ukimwi vinaweza kuenezwa kwa njia ya sindanoiliyotumika kwa mtu aliyenavyo. Kwa hiyo ni lazima vifaavyote vichemshwe baada ya kutumiwa. V.V.U ni hafifu sanana huangamizwa na joto la nyuzi 56°C au kwa kulowekwakwenye maji yaliyo na madawa ya kawaida ya kuaangamizavijidudu.Zipo njia tatu za kuvisafisha vyombo.1. Kuvichemsha kwa dakika ishirini au zaidi.2. Kwa kutumia mvuke.3. Kuviloweka katika myeyusho wa maji yaliyo na dawaya kuangamiza vijidudu kwa mda wa dakika ishiriniau zaidi – myeyusho ukiwa umetengenezwaifuatavyo:a. Gram 5 za klorini kwa lita moja ya maji;b. Kiungo kimoja cha Jik kwa kila kumi za majic. Gram 700 za ethanol katika lita moja ya maji.Yapasa miyeyusho mipya itengenezwe kwa mahitaji ya kilasiku kwani uwezo wa myeyusho hupungua baada ya mda.Nguo zenye damu zapaswa kufuliwa kwa makini. Ilikuviangamiza virusi inafaa zifuliwe kwa sabuni na majimoto, kisha zianikwe juani. Virusi vya Ukimwi haviwezikuhimili joto la jua na hali ya ukavu.


NAMNA YA WAHUDUMU KUJITUNZAHatari ya wahudumu kuambukizwa V.V.U wanapotekelezakazi ni ya chini. Ni jambo la muhimu wahudumu haokutahadhari na kujikinga vilivyo ili wasiambukizwe.Vyombo ambavyo vimeguswa na damu ya mgonjwavinastahili kushughulikiwa kwa uangalifu mno. Ikiwezekanaglavu za mikono zivaliwe kila mara na wakati wa upasuajiglavu ndefu zaidi zivaliwe. Hapana haja ya kuvaa makotimarefu na vifuniko vya pua au glavu za mikono wakatiwahudumu wanapowauguza wagonjwa.Wahudumu wa afya wanastahili kushirikiana kwa uzoefu nahisia zao. Ni muhimu waungwe mkono na jamii, hasaviongozi wa dini na wazee.


A.R.V NI NINI?Ukimwi hauna tiba. Walakini, watu walioambukizwa V.V.Upamoja na wale walio na Ukimwi huathiriwa na magonjwamengine. Wakati ule utaratibu wa kinga mwiliniunapoharibiwa na V.V.U basi magonjwa kadha wa kadhahudhihirika. Ni sharti hayo magonjwa yatibiwe. Pia kuzaanakwa V.V.U ni sharti kupunguzwe. Kuna aina ya madawayanayotumiwa kudhibiti V.V.U na kutibu haya magonjwa.Madawa haya hasa hujulikana kama Antiretrovirals, amakwa kifupi, ARV.MATUMIZI YA ARV NI YAPI?Matumizi ya ARV sio tiba ya Ukimwi. Ilhali hutumiwa kwakudhibiti na kutibu magonjwa yanayo muathiri mtu aliye naV.V.U ama Ukimwi. Madawa haya yanastahili kutumiwa kilasiku katika maisha ya muathirika. V.V.U huzaana kwenyechembechembe nyeupe za binadamu. Ili kuzikatizazisizaane, madawa ya ARV hutumika.TIBA YA PAMOJA YA ARV NI IPI?Ili matumizi haya ya ARV yawe yenye manufaa, muathirikani budi atumie mchanganyiko wa haya madawa kwapamoja. Iwapo aina tatu au zaidi ya madawa hayayanapotumika kwa pamoja, mchanganyiko huo hujulikanakama HAART. Utumizi wa aina mbili ama zaidi ya ARV kwawakati mmoja hupunguza sana ukaidi wa V.V.U dhidi yamadawa.


Kwa kuwa kuna daktari ambaye anauwezo wa kushaurikuhusu ARV, basi hamna haja ya wewe kujua majina yakitaalam ya mchanganyiko huu. Kwa hiyo, unashauriwakukitembelea kituo cha afya kilicho karibu na kinachotoamsaada wa ARV ili kupata mawaidha zaidi kuhusu matumiziya ARV.Mara nyingi, matumizi ya ARV hayaanzi wakati ule mtuanapodhihirika ana V.V.U. Matumizi haya haunzishwa palehesabu ya CD4 ni mia mbili (200) au chini yake. Ushauri wadaktari ndiyo utakao bainisha iwapo muathirika amehitimuhicho kiwango cha kutumia ARV.Matumizi ya ARV huambatana na lishe bora pamoja na tibaya magonjwa mengine yanayo muathiri mtu aliye naUkimwi. Sio jambo la busara kubadilisha matumizi hayabila kushauriana na daktari.Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limetoa muongozo wamatumizi ya ARV ulimwenguni. Muongozo huu huanza paledalili za Ukimwi zimedhihirika na uwezo wa kinga ya mwiliumepungua kwa kiasi kikubwa. Habari hii hupatikana kwakupitia ukaguzi katika mahabara unaobainisha kiwango chavirusi na pia hesabu ya CD4 katika chembechembe nyeupeza damu.


FAIDA YA MATUMIZI YA A.R.V1. Kuongezea maisha ya mtu aliye na V.V.U au Ukimwi.2. Kupunguza magonjwa mengine.3. Kumzuia mama aliye na V.V.U kumuambukizamtoto.4. Kupunguza gharama ya matibabu.5. Kuwawezeshawaathirika kuendeleakufanya kaziinavyopasa.6. Kuimarisha jamii.7. Kupunguza hasarakwa uchumi wa taifa.8. Kuwashawishi watuwote kutamani, kwahiari, kujua hali yaokuhusu V.V.U kwakutembelea kituo cha kutoa ushauri na kupimwa.9. Kupunguza unyanyapaa na kutengwa kwawaathirika wa V.V.U na Ukimwi.10. Kuwezesha utoaji thabiti wa huduma na elimumurwa kwa wahudumu wa afya.Waleo, serikali nyingi na hata vituo vya afya vya kibinafsivinatoa huduma ya ARV bure au kwa bei nafuu na ni jambola busara kutembelea kituo cha afya kilicho karibu nawe iliupate kujulishwa huduma iliopo.


KAMUSIV.V.U Virusi vya UkimwiUKIMWI Upungufu wa Kinga MwiliniARV Antiretroviral drugs: Madawa ya kulemezaV.V.U visizaane mwilini mwa muathirikaWCC <strong>World</strong> <strong>Council</strong> <strong>of</strong> <strong>Churches</strong> - Baraza laMakanisa UlimwenguniWHO <strong>World</strong> Health Organization – Baraza la AfyaUlimwenguniMuathirika Mtu aliyeambukizwa V.V.U ama aliye naUkimwi.Mahabara Mahali pa kitaalam pa kukagua aukuchunguza jambo kwa kutumia vifaa vyakisayansi na kitaalam.Zahanati Kituo kidogo cha afya kinachopatikanakijijiniChembechembenyeupe Viumbe vipatikanavyo katika damu ambavyohubuni kinga ya mwili dhidi ya virusi auvijidudu vinavyoambukiza maradhi aumagonjwaCondom Mpira ya plastiki ivaliwayo kwenye sehemuya siri kwa madhumuni ya kufanya ngonoama kujamiianaELISA Aina ya utaalam wa kukagua iwapo damuimeshambuliwa na V.V.UVCT Kituo cha kutoa ushauri kwa hiari nakupimwa


HAART Highly Active Antiretroviral Therapy –Matumizi ya madawa ya ARV yaliyoongezwanguvu.ART Antiretroviral Therapy – Matumizi maalumya madawa ya ARVCD4 Aina ya chembechembe nyeupe

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!