You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
JARIDA MAALUM
Toleo la 2 Mei, 2020
Ofisi ya Waziri Mkuu
1
ASANTENI
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli
amewapongeza waislam wote nchini
kwa kumaliza mfungo wa mwezi
Mtukufu wa Ramadhani na
anawashukuru kwa namna walivyoshiriki
kuliombea Taifa....
-
2
UTOAJI MICHE YA CHIKICHI BURE
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa,
amesema upandaji wa zao la
michikichi utaanza rasmi
Oktoba mwaka huu.....
JARIDA LA MTANDAONI
RAIS DKT MAGUFULI AWASHUKURU WATANZANIA
Asema hatasahau namna watanzania walivyoliombea Taifa
Ataka tuendelee na dua, kila mmoja kwa imani yake
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza
waislam wote nchini kwa kumaliza mfungo wa
mwezi Mtukufu wa Ramadhani na anawashukuru
kwa namna walivyoshiriki kuliombea Taifa hasa
katika kipindi hiki cha kukabilia na ugonjwa wa
COVID-19.
Hayo yamesemwa leo (Jumapili, Mei 24, 2020) na
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati akizungumza
na waumini wa dini ya kiislam mara baada
ya kumaliza kuswali sala ya Eid El Fitri katika Msikiti
wa Gaddafi, jijini Dodoma. Pia Rais Dkt. Magufuli
amewashukuru waumini wa dini nyingine nchini
kwa kushiriki kikamilifu kwenye kuliombea Taifa.
“Leo hii tunamalizia dua ya kumshukru Mwenyezi
Mungu, jambo hili Mheshimiwa Rais anasema
hatasahau kwa viongozi wote wa dini kuwa
pamoja kuliombea Taifa. Pia Mheshimiwa Rais
amesema tuendelee na dua zetu, kila mmoja kwa
imani yake wakati wote ili Mwenyezi Mungu aendelee
kutuondoa katika janga hili ambalo limeleta
mtikisiko duniani kote.”
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi
Watanzania wote kwa ujumla waendelee kushirikiana
katika kulifanya Taifa liwe la amani na utulivu
.
“Dini zetu zinatutaka kila mmoja aendelee
kuomba, nchi hii imekuwa na utulivu sana na
mfano duniani kwa nchi zinazotaka amani.”
“Tuendelee na tabia hii na vingozi wa dini
endeleeni kusisitiza suala la amani, Serikali
inawasisitiza muendelee na shughuli zenu, sisi
tutahakikisha tunaendelea kulinda amani, fanyeni
kazi, mkulima lima na kwa walio viwandani nao
waendelee kufanya kazi.”
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema wananchi
wanatakiwa waendelee kuchukua tahadhari dhidi
ya ugonjwa wa COVID-19, ambapo amewasisitiza
wasiwe na hofu na waendelee kufanya kazi kwa
bidii.
Akizungumzia kuhusu hali ya ugonjwa wa
COVID-19 ilivyo kwa sasa nchini, Waziri Mkuu
amesema katika hospitali ya Amana yupo
mgonjwa mmoja, Mloganzila yupo mmoja,
Temeke hatuna mgonjwa aliyethibitishwa, Kairuki
hakuna mgonjwa, Rabiansia hakuna mgonjwa,
Regency hakuna mgonjwa, Aga Khan yuko
mgonjwa mmoja, Lulanzi Kibaha wapo wagonjwa
16 na Dodoma Mkonze mpaka leo asubuhi wapo
wagonjwa tatu.
Awali, Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh
Mustafa Rajab, amempongeza Rais Dkt Magufuli
Inaendelea Uk.2
1 JARIDA MAALUM
kwa kuwapa Watanzania moyo wa kishujaa na
ujasiri katika kukailiana na ugonjwa wa COVID-19
kwa kuwataka wamwombe Mwenyezi Mungu ili
aliepushe Taifa na janga hilo, wakati Mataifa na
viongozi wengine duniani yakikumbwa na taharuki.
“Hakuna mkombozi zaidi ya Mwenyezi Mungu,
shida zetu, matatizo yetu na hata tukijaribiwa kwa
maradhi au mtihani wa aina yoyote Mwenyezi
Mungu anatupa ushujaa wa kukabiliana nao. Hofu
ya maradhi ni kifo hivyo tusiwe na hofu tumtegemee
Mwenyezi Mungu kama Rais wetu anavyotusisitiza.”
2
Amesema wananchi hawana sababu ya kuwa na
hofu kwani tayari Rais Dkt. Magufuli alitangaza
siku tatu kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi
Mungu aliepushe Taifa na corona na viongozi wa
dini zote waliitikia wito na waliongoza maombi
ambayo yamejibiwa na sasa huo ugonjwa umepungua
nchini.
Sheikh Rajab aliongeza kuwa baada ya Mwenyezi
Mungu kukubali dua hizo na Rais, Dkt. Magufuli,
kutenga siku tatu za kumshukuru Mwenyezi
Mungu ambazo zinaisha leo, wananchi hawana
budi waendelee kumshukuru na kamwe wasishiriki
kwenye kufanya maasi. “Tuwe ni watu wenye
kushukuru neema tunazojaaliwa na Mwenyezi
Mungu na kamwe tusiwe wenye kuzikufuru
JARIDA MAALUM
MAJALIWA: TUTATOA MICHE YA CHIKICHI BURE KWA WANANCHI
Asema lengo ni kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa mafuta
Upandaji kuanza rasmi Oktoba
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, amesema upandaji wa zao la michikichi utaanza
rasmi Oktoba mwaka huu na kama kuna mtu mmoja mmoja au kikundi wanataka
kulima chikichi, waandae mashamba yao na miche ya awali watapewa bure.
“Serikal imedhamiria tulime zao hili kwa wingi na
tuwasaidie wakulima kwani tunatumia pesa
nyingi sana kununua mafuta ya mawese kutoka
nje. Tukilima kwa wingi tutajitosheleza na hatutaagiza
mafuta kutoka nje.”
Waziri Mkuu amesema kwa sasa Tanzania haitaagiza
mbegu za michikichi kutoka sehemu yoyote
duniani na badala yake itazalisha mbegu zake
yenyewe. “Tayari tuna miche milioni 1.8 na wataalamu
wetu wanaendelea kuzalisha.”
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Mei
23, 2020) baada ya kukagua kitalu cha miche ya
michikichi cha Halmashauri ya Kigoma Ujiji
pamoja na kitalu cha JKT Bulombora akiwa katika
ziara ya kikazi mkoani Kigoma.
Vile vile, Waziri Mkuu amemwagiza Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma Brigedia Mstaafu, Emmanuel
Maganga, ahakikishe JKT Bulombora wanapewa
ardhi waliyoomba kwa ajili ya kupanua kilimo cha
michikichi.
“Michikichi Kigoma ndio uchumi, tunataka wakulima
wengi walime zao hili na Kigoma ndio chanzo
cha zao la michikichi, Kigoma ndio iliyotoa chikichi
kwenda nchi nyingine.”
Amesema Ilani ya CCM ya 2015-2020 imeelekeza
kuwa kufufuliwa kwa zao hilo na Serikali imetekeleza
hilo kwa kuanzia Kigoma na kisha
yatafuatia maeneo mengine ya nchi.
Inaendelea Uk.4
3
JARIDA MAALUM
Waziri Mkuu amesema kwa sasa Tanzania haitaagiza
mbegu za michikichi kutoka sehemu yoyote
duniani na badala yake itazalisha mbegu zake
yenyewe. “Tayari tuna miche milioni 1.8 na wataalamu
wetu wanaendelea kuzalisha.”
“Michikichi Kigoma ndio
uchumi, tunataka wakulima
wengi walime zao hili na
Kigoma ndio chanzo cha zao la
michikichi, Kigoma ndio iliyotoa
chikichi kwenda nchi
nyingine.”
Amesema Ilani ya CCM ya 2015-2020 imeelekeza
kuwa kufufuliwa kwa zao hilo na Serikali imetekeleza
hilo kwa kuanzia Kigoma na kisha
yatafuatia maeneo mengine ya nchi.
Waziri Mkuu amesema awali kituo cha utafiti wa
zao hilo kilikuwa jijini Dar es Salaam, Serikali
ikaona haiwezekani na kuamua kukihamishia
Kihuinga, mkoani Kigoma.
Amesema wataalam walihamishiwa Kihinga na
tayari wameshazalisha zaidi ya miche milioni 1.8 na
kazi iliyobaki ni kuwapa wananchi ili waweze
kupanda kwenye mashamba yao.
Pia, Waziri Mkuu amewaagiza Maafisa Kilimo
wawasaidie wakulima kulima zao hilo kitaalamu
pamoja na wale wenye michikichi ya zamani jinsi
ya kuitoa na kupanda michikichi hizi mpya,
Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi wajiwekee
utaratibu wa kupalilia mashamba yao ili michikichi
iweze kustawi na wahakikishe hawachomi
moto mapori kwani utaharibu michikichi yao.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka Wananchi
nchini kote waendelee kuchukua tahadhari juu ya
ugonjwa wa COVID-19 na wafuate masharti ya
wataamu. Hata hivyo amesema idadi ya wagonjwa
wa COVID-19 imepungua sana nchini.
Naye, Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Omar
Mgumba, amesema anamshukuru Waziri Mkuu
kwa maelekezo yake ya kuagiza miche ya michikichi
igawiwe bure kwa wananchi. “Tumetumia sh.
bilioni 10.8 kwa ajili ya zoezi hili, na hizi ni jitihada
za Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.”
4 JARIDA MAALUM
KATIBU MKUU
Ofisi ya Waziri Mkuu
2 Mtaa wa Relini, S.L.P 980
40480 Dodoma,
Baruapepe: ps@pmo.go.tz, Simu:+255262322480
Fax:+255262324534, Tovuti: www.pmo.go.tz