25.07.2022 Views

Ulu ul Azmi minna Rusulun Juzuu Al Thaniya

Al Mustakshif Abu Manal Danah Ulu ul Azmi minna Rusulun Juzuu Al Thaniya

Al Mustakshif Abu Manal Danah Ulu ul Azmi minna Rusulun Juzuu Al Thaniya

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

1


2

‏﴿أُوْلُواْ‏

الْعَزْمِ‏ مِنَ‏

الر ُّسُلِ‏

الجزء ال ثن

تجميع وانتاج

المستكشف أبومنال دانا

UuLU AL A’AZMI MINA ALRRUSUL

AL JUZUI AL THANI

WENYE AZMA THABIT ZAIDI

MIONGONI MWA MITUME

SEHEMU YA PILI

KIMEKUSANYWA NA KUTAYARISHWA NA AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH

KIMECHAPISHWA NEW DELHI – INDIA.

MWAKA 1445 AL HIJRA – 2024 C.E


3

‏﴿ِسْ‏ مِ‏ ا‏ ِ الرحمْ‏ ‏َنِ‏ الرحِيمِ﴾‏

إن َّ الحَْمْدَ‏ هللِ َِّ‏ نحَْمَدُهُ‏ ونَسْتَعِينُهُ‏ وَنَسْتَغْفِرُهُ‏ وَنَعُوذُ‏ ابِ‏ هلل َِّ‏ ‏ِمنْ‏ شُرُورِ‏ أَنْفُسِ‏ نَا وَمِ‏ ‏ْن

سَيِّئَاتِ‏ أَعْمَالِنَا،‏ مَنْ‏ يَهْدِهِ‏ اهلل َُّ‏ فَلاَ‏ مُضِل َّ لَهُ‏ وَمَنْ‏ يُضْلِلْ‏ فَلاَ‏ هَادِيَ‏ لَهُ‏ وَأشْهَدُ‏

أنْ‏ لاَ‏ إِلَهَ‏ إِلا َّ اهلل َُّ‏ وَحْدَهُ‏ لاَ‏ شَرِيكَ‏ لَهُ‏ وَأشْهَدُ‏ أن َّ محَُم َّدًا عَبْدُهُ‏ وََر سُولُهُ‏

Inna Al-hamda Lillaahi nahmaduhu wanasta’eenahu wa nastaghfiruhu, wa

na’oodhu billaahi min shuroori anfusinaa wa min sayi’aati a’maalinaa. Man yahdih

Illaahu falaa mudhilla laahu wa man yudhlil falaa haadiya lahu. Wa ashhadu an laa

ilaaha ill-Allaahu wahdahu laa shareekallahu, wa ashhadu anna Muhammadan

‘Abduhu wa Rasooluhu.

Tafsir: Kwa jina la Allah, ambae anastahiki shukrani zote, tunaemuomba msaada na

msamaha wake. Tunajilinda kwa ulinzi wa Allah na kila maovu ya Nafsi zetu na

mambo mabaya yetu. Kwani kwa hakika mtu yeyote yule alieongozwa na Allah basi

hakuna atakaempotoa, na aliepotoshwa na Allah basi hakuna atakaemuongoa.

Nnashuhudia kua hakuna anaepaswa kuabudiwa isipokua Allah pekee asiekua na

mshirika, na nnashuhudia kua Muhammad (Salallahu A’layhi wa Salam) ni Mja wake

na ni Mtume wake.

يَقُولُ‏ اللهُ‏ عَز َّ وَجَ‏ َّل

‏﴿َي ُّهَا ال َّذِينَ‏ ءَامَنُواْ‏ ات َّقُواْ‏ اهلل ََّ‏ حَق َّ تُقَاتِهِ‏ وَلاَ‏ تمَُوتُن َّ إِلا َّ وَأَنتُم م ُّسْلِمُونَ‏ ﴾

Ya ayyuha alladhina amanoo ittaqoo Allaha haqqa tuqatihi wala tamootunna illa

waantum muslimoona (Surat Al Imran 3:102)

Tafsir: Enyi mlioamini! Muogopeni Allah (kwa kutekeleza maamrisho yake na

kuachana na makatazo yake) kama anavyostahiki kuogopewa. [Mtiini, mshukuruni

na daima mkumbukeni], na msife isipokua mkiwa katika hali ya kua ni Waislam.


4

‏﴿يَأَي ُّهَا الن َّاسُ‏ ات َّقُواْ‏ رَب َّكُمُ‏ ال َّذِى خَلَقَكُمْ‏ مِنْ‏ ن َّفْسٍ‏ وَحِ‏ دَةٍ‏ وَخَلَقَ‏ مِنْهَا زَوْجَهَا

وَبَث َّ مِنْهُمَا رِجَالاً‏ كَثِيراً‏ وَنِسَآءً‏ وَات َّقُواْ‏ اهلل ََّ‏ ال َّذِى تَسَآءَلُونَ‏ بِهِ‏ وَالأَْرْ‏ ‏َح ا مَإِ َّنا هلل ََّ‏

﴾ كَا نَعَلَيْ‏ ي ب كُمْرَقِ‏ اً‏

Ya ayyuha alnnasu ittaqoo rabbakumu alladhi khalaqakum min Nafsin wahidatin

wakhalaqa minha zawjaha wabaththa minhuma rijalan kathiran wanisaan

waittaqoo Allaha alladhii tasaaloona bihi waal-arhama inna Allaha kana

AAalaykum raqeeban (Surat An Nisaa 4:1)

Tafsir: Enyi Watu! Mcheni Mola wenu aliekuumbeni kutokana na Nafsi moja (Adam),

na kutokana nae (Adam) akamuumba Mke wake (Hawwa), na kutokana nao (Adam

na Hawa) akawaumba Wanaume na Wanawake wengi na muogopeni Allah ambae

ana haki juu yenu, na msivunje udugu, kwani kwa Hakika Allah ni mwenye uangalifu

mkubwa juu yenu.

‏﴿َي ُّهَا ال َّذِينَ‏ ءَامَنُواْ‏ ات َّقُواْ‏ اهلل ََّ‏ وَقُولُواْ‏ قَوْلاً‏ سَدِيداً۞يُصْلِحْ‏ لَكُمْ‏ أَعْمَلَكُ‏ مْ‏ وَيَغْفِ‏ ‏ْر

لَكُمْ‏ ذُنُوبَكُمْ‏ وَمَن يُطِعِ‏ اهلل ََّ‏ وَرَسُولَهُ‏

فَقَدْ‏ فَازَ‏ فَوْزاً‏ عَظِيماً‏ ﴾

Ya ayyuha alladhina amanoo ittaqoo Allaha waqooloo qawlan sadeedan, Yuslih

lakum aAAmalakum wayaghfir lakum dhunoobakum waman yutiAAi Allaha

warasoolahu faqad faza fawzan AAadhiman (Al Ahzab 33:70-71)

Tafsir: Enyi Mlioamini! mcheni na muogopeni Allah, na (daima) semeni kauli za

ukweli ulionyooka, atakuongozeni kufanya mema na kukusameheni dhambi zenu. Na

kwa hakika yeyote yule ambae anaemtii Allah na Mtume wake (Salallahu A’layhi wa

Salam) basi atakua ni miongoni mwa waliofuzu kwa mafanikio makubwa sana.

Allahuma Ij’Aalna minna al faizin fawzan A’adhimah…Aamin

أَمَا بَعْدُ‏


5

قَالَ‏ رَسُولِ‏ اهلل َِّ‏ صَل َّى اللهُ:فَإِن َّ أَصْدَقَ‏ الحَْدِيثِ‏ كِتَابُ‏ اهلل َِّ،‏ وَأَوْثََق الْعُرْي كَ‏ لِمَ‏ ةُ‏

الت َّقْوَى،‏ وَخَيْرَ‏ الْمِلَلِ‏ مِل َّةُ‏ إِبْرَاهِيمَ،‏ وَخَيْرَ‏ الس ُّنَنِ‏ سُنَنُ‏ محَُم َّدٍ‏ صَل َّى اللهُ‏ عَلَيْهِ‏

وَسَل َّمَ،‏ وَأَشْرَفَ‏ الحَْدِيثِ‏ ذِكْرُ‏ اهلل َِّ‏ تَعَالىَ‏ ، وَأَحْسَنَ‏ الْقَصَصِ‏ هَذَا الُْق رْآ ‏ُن

Qala Rasul Allahi Salallahu A’alayhi wa Salam: fa'inn 'asdaqa alhadith kitab alllahi,

wa'awthaq al’aAuryi kalimat alttaqwaa, wakhayr almilal millat 'Ibrahima, wakhayr

alssunan sunan Muhammad Sala Allahu Alyhi wa Salam, wa'ashraf alhadith dhikr

allah taalaa, wa'ahsan alqasas hadha al Quran.

Amesema Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam kua: Kwa hakika hadith za kweli

kabisa ni za Kitabu cha Allah Subhanah wa Ta’ala, na kauli nzito ni kauli zenye

Taqwa, na Mila bora ni Milat Ibrahima, Na Sunna bora ni Sunna za Muhammad

(Sala Allahu Alyhi wa Salam) na Maneno Matukufu ni Dhikr Allah Ta’ala na Visa

bora ni hii Qur’an.

وَ‏ يَقُولُ‏ اللهُ‏ عَز َّ وَجَ‏ َّل

‏﴿وَبِٱلحَْقِّ‏ أَنْزَلْنَاهُ‏ وَبِٱلحَْقِّ‏ نَزَلَ‏ وَمَآ أَرْسَلْنَاكَ‏ إِلا َّ مُبَشِّ‏ راً‏ وَنَذِيراً۞وَ‏ قُرْآً‏ فَرَقْنَاهُ‏ لِتَقْرَأَهُ‏

عَلَى ٱلن َّاسِ‏ ٰ عَلَى مُكْثٍ‏ وَنَز َّلْنَاهُ‏ تَنْزِيلاً۞قُلْ‏ آمِنُواْ‏ بِهِ‏ أَوْ‏ لاَ‏ ۤ تُؤْمِنُواْ‏ إِن َّ ٱل َّذِينَ‏ أُوتُواْ‏

ٱلْعِلْمَ‏ مِن قَبْلِهِ‏ إِذَا ٰ يُتْلَى عَلَيْهِمْ‏ يخَِر ُّونَ‏ لِلأَذْقَانِ‏ سُج َّداً۞وَيَ‏ قُولُونَ‏ سُبْحَانَ‏ آ رَبّ‏ نَ‏ نِإ

كَانَ‏ وَعْدُ‏ رَبِّنَا لَمَفْعُولاً۞وَيخَِر ُّونَ‏ لِلأَذْقَانِ‏ يَبْكُونَ‏ وَيَزِيدُهُمْ‏ خُشُوعاً۞قُلِ‏ ٱدْعُواْ‏

ِ

ٱهلل ََّ‏ أَوِ‏ ٱدْعُواْ‏ ٱلر َّحمَْٰنَ‏ أًَّ‏ م َّا تَدْعُواْ‏ فَلَهُ‏ ٱلأَسمَْآءُ‏ ٱلحُْسْنىَٰ‏ وَلاَ‏ تجَْهَرْ‏ بِصَلاَتِكَ‏ وَلاَ‏

تخَُا فِ‏ ا تْهبَِ‏ وَ‏ ٱبْتَغِ‏ بَينَْ‏ ذٰلِكَ‏ سَبِيلاً۞وَقُلِ‏ ٱلحَْمْدُ‏ هللِ َِّ‏ ٱل َّذِى لمَْ‏ يَت َّخِ‏ ذْ‏ وَلَداً‏ وَلمَ‏ يَكُ‏ ‏ْن

ل َّهُ‏ شَرِيكٌ‏ فىِ‏ ٱلْمُلْكِ‏ وَلمَْ‏ يَكُنْ‏ ل َّهُ‏ وَليِ‏ ٌّ م َّنَ‏ ٱلذ ُّ لِّ‏ وَكَبرِّْهُ‏ تَكْبِيراً‏ ﴾


6

Wabialhaqqi anzalnahu wabialhaqqi nazala wama arsalnaka illa mubashshiran

wanadheeran, Waqur-anan faraqnahu litaqraahu AAala alnnasi AAala mukthin

wanazzalnahu tanzeelan, Qul aminoo bihi aw la tu/minoo inna alladheena ootoo

alAAilma min qablihi idha yutla AAalayhim yakhirroona lil-adhqani sujjadan;

Wayaqooloona subhana rabbina in kana waAAdu rabbina lamafAAoolan;

Wayakhirroona lil-athqani yabkoona wayazeeduhum khushooAAan; Quli odAAoo

Allaha awi odAAoo alrrahmana ayyan ma tadAAoo falahu al-asmao alhusna wala

tajhar bisalatika wala tukhafit biha waibtaghi bayna dhalika sabeelan, Waquli

alhamdu lillahi alladhee lam yattakhidh waladan walam yakun lahu shareekun fee

almulki walam yakun lahu waliyyun mina aldhdhulli wakabbirhu takbeeran (Surat

Al Isra 17:105-111)

Tafsir: Na kwa haki tumeiteremsha chini (Hii Qur’an) na kwa haki imeshuka, na

tumekutuma wewe (Muhammad) si kwa chochote isipokua kwa ajili ya kuweka wazi

na kuonya. Na hii Qur’an ambayo tumeigawa (katika aya na sura tofauti) ili upate

kuisoma kwa watu kwa makusudio. Na tumeishusha hii (Qur’an) kwa vituo (tofauti).

Sema (Ewe Muhammad): ‘Iaminini au msiiamini. Kwani kwa hakika wale waliopewa

Ilm kabla yake (Ilm ya Ahl Al Kitab kina Abd Allah Ibn Salam, Salman Al Farsi n.k)’

waliposomewa, walianguka chini kwa nyuso zao kwa Unyenyekevu wa Kusjudu. Na

wakasema: ‘Utukufu ni wa Allah Pekee. Ahadi ya Mola wetu ni lazime iwe ni yenye

kutekelezwa’. Na wakaanguka kwa nyuso zao wakilia machozi na hii ilizidisha

Unyenyekevu wao. Sema (Ewe Muhammad) Muombeni Allah, au muombeni Ar

Rahmani, au kwa jina lolote (Katika Majina yake Matukufu), kwani kwake yeye ndio

kwenye umiliki wa Majina Matukufu, na Salini bila ya kufanya kelele au kwa sauti ya

chini, bali fuateni njia ya baina yake (hali hizo mbili). Na semeni, shukrani zote

anastahiki Allah ambae hana mtoto, na wala hana mshirika katika Ufalme wake, na

ni asiekua (na uhitaji wa) Msaidizi wala Mlinzi. Na Mkuzeni kwa Takbir.

ALLAHU AKBAR!


7

YALIYOMO

YALIYOMO ....................................................................................................... 7

VITABU VILIVYOTANGULIA VYA AL MUSTAKSHIF ABU MANAL

DANAH: ......................................................................................................... 13

UTANGULIZI ................................................................................................. 14

SURA YA KWANZA ........................................................................................ 20

MUONGOZO, MANUFAA, TIBA NA REHMA ZILIZOMO NDANI YA

QUR’AN. ........................................................................................................ 20

HIKMA NA BARAKA NDANI YA QUR’AN ..................................................... 28

MAFUMBO NA MITHALI ZILIZOMO NDANI YA QUR’AN. .......................... 35

AINA ZA KALIMAT (KAULI) NDANI YA QURÁN .......................................... 52

MANUFAA YA KUTAWANYIKA NA KUTEMBEA ARDHINI KULINGANA NA

QUR’AN. ........................................................................................................ 56

UMUHIMU WA HIJRA KATIKA ISLAM ......................................................... 66

MAUMBILE YA NYOYO ZA IBN ADAM: AL QALB, AL FUAD, AL LUBB, AL

SADR NA AN NAFS KATIKA QURÁN ............................................................ 74

AL QALB ........................................................................................................ 75

AL FUAD ........................................................................................................ 87

AL LUBB ........................................................................................................ 89

AL SADR......................................................................................................... 90

MAANA YA AQL, HIJR, HILM, NNUHA NA BALU. ....................................... 95

NAFS - MAUMBILE YAKE NA UHIBITI WAKE. .......................................... 101

NAFS AL AMMARAH BI ALSUI (NAFS SHAHWANIYYAH) ......................... 104

NAFS AL MULHIMAH ................................................................................. 105

NAFS AL LAWWAMAH. ............................................................................... 106

NAFS AL MUTMA’INAH .............................................................................. 107

NAFS RADHIYATAN .................................................................................... 111

NAFS MARDHIYAH. .................................................................................... 112

NAFS AL KAMILAH ..................................................................................... 112


8

KUSUDIO LA ALLAH SUBHANAH WA TA’ALA KUTUMA MITUME KWA

WAJA WAKE. ............................................................................................... 114

MITUME NA MANABII WALIOTAJWA KATIKA QURÁN. ........................... 124

MAANA YA MIUJIZA. .................................................................................. 137

SURA YA PILI............................................................................................... 146

HISTORIA YA MZEE IMRAN BABU YAKE NABII ISA IBN MARYAM BINT

IMRAN .......................................................................................................... 147

UHARAMU NA UTUKUFU WA DAMU KATIKA UISLAM. ......................... 149

ADHA YA DAMU YA KIMAUMBILE YA MWANAMKE................................ 179

KUKARIBIANA KIMAPENZI BAINA YA MKE NA MUME KATIKA

UISLAM ........................................................................................................ 185

KUZALIWA KWA MARYAM BINT IMRAN ................................................... 200

KAFFALA – ULEZI WA MARYAM BINT IMRAN. ........................................ 203

HAKI ZA YATIMA, MUNQATI NA LAQIT KATIKA UISLAM ...................... 210

AYAT AL QURSY - NYAKATI NA MATUKIO YA VIUMBE MBELE YA ALLAH

SUBHANAH WA TA'ALA .............................................................................. 247

SURAT AL MAA’UN – UMUHIMU WA KUJALI MAYATIMA, MASIKINI NA

SALA KATIKA DINI YA KIISLAM. ............................................................... 257

UMUHIMU WA UNYENYEKEVU KATIKA SALA NA DUA.......................... 300

KULELEWA KWA MARYAM BINT IMRAN NA NABII ZAKARIYAH ............ 364

KUZALIWA KWA NABII YAHYA IBN ZAKARIYAH ...................................... 373

SABABU YA KUSHUSHWA KWA SURAT MARYAM .................................... 383

HARFU MUQATTAA’AT NA KISA CHA NABII ISA. .................................... 389

MAANA NA FAIDA YA BIISMI ALLAHI ALRRAHMANI ALRRAHIM .......... 401

KAF – HA – YA – A’AYN – SAD ................................................................... 411

UJUMBE WA NAJRAN, THUMAMAH IBN UTHAL – UTHIBITSHO WA

WASIOKUA WAISLAM KURUHUSIKA KUINGIA MSIKITINI ..................... 419

MAUMBILE YA ISA IBN MARYAM NI MITHLI YA NABII ADAM. ............... 431

UTUKUFU WA KUTUNUKIWA UJA UZITO MARYAM BINT IMRAN ........ 441

KUZALIWA KWA NABII ISA IBN MARYAM ................................................ 463


9

KUZUNGUMZA KWA HOJA KWA ISA IBN MARYAM UTOTONI. .............. 470

HIJRA YA MARYAM BINT IMRAN NA NABII ISA BAINA YA MISRI NA

NASIRA......................................................................................................... 477

ANSARU ALLAH – AL HAWARIYINA .......................................................... 480

AL MAIDAH ................................................................................................. 488

UTHIBITISHO WA ISA IBN MARYAM KUA SI MUNGU. ............................ 497

KUPANDISHWA MBINGUNI KWA ISA IBN MARYAM NA KIFO CHA

MARYAM BINT IMRAN. ............................................................................... 503

ISA IBN MARYAM NA MARYAM MAJDALANIYAH ..................................... 512

WANAFUNZI WA NABII ISA IBN MARYAM KATIKA SURAT YASIN .......... 513

VITHIBITISHO VYA WANAZUONI JUU YA KUPANDISHWA JUU

MBINGUNI RUHI ALLAHI ISA IBN MARYAM WAKATI AKIWA HAI. ........ 521

TAQDIM WA TAAKHIR KATIKA QUR’AN .................................................. 527

ISA IBN MARYAM NA MAHDI, DAJJAL, JUJ WA MAJUUJ NA DHUL

QARNAYN. ................................................................................................... 532

KAULI ZA ISA IBN MARYAM A’LAYHI SALATU WA WASALAM

KATIKA AL RISALAT AL QUDSIYYAH. .................................................. 544

KAULI ZA NABII MUHAMMAD SALALLAHU ALYHI WA SALAM

KUHUSIANA NA NABII ISA ALAYHI SALAM. ............................................. 556

KAULI ZA ALLAH SUBHANAH WA TAALA JUU YA NABII ISA IBN

MARYAM. ..................................................................................................... 557

MAELEZO YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM

KUTOKA KATIKA YALE WALIORITHI MAYAHUDI NA WAKRISTO.......... 558

SURA YA TATU ............................................................................................ 561

IMAM AL ANBIYAI WAL ALMURSALINA MUHAMMAD SALALLAHU

A’LAYHI WA SALAM .................................................................................... 562

ASILI YA UARABU NA YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA

SALAM. ........................................................................................................ 563

NDOTO YA ABD UL MUTTALIB NA KISIMA CHA ZAMZAM ..................... 569

ABDULLAH IBN ABD UL MUTTALIB BABA YAKE RASUL ALLAH

SALALLAHU AAYHI WA SALAM ................................................................. 574


10

BARAKAH BINT THALABAH UMM AYMAN MAMA MLEZI WA RASUL

ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM .................................................. 579

AMINAH BINT WAHB MAMA MZAZI WA RASUL ALLAH SALALLAHU

ALAYHI WA SALAM ..................................................................................... 580

KIFO CHA ABDULLAH NA KUZALIWA KWA RASUL ALLAH SALALLAHU

ALAYHI WA SALAM. .................................................................................... 582

THUWAYBAH AL ASLAMIYAH MAMA MNYONYESHAJI WA PILI WA RASUL

ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM .................................................. 587

HALIMA BINT ABU DHUAYB AL SADIYA MAMA ALIEMNYONYESHA WA

RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM ...................................... 589

MIUJIZA YA UTOTONI MWA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA

SALAM WAKATI AKIWA KWA HALIMA BINT ABU DHUAYB .................... 591

INSHIRAH SADR YA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM. ... 595

TAFSIR YA SURAT AL INSHIRAH. .............................................................. 599

KIFO CHA AMINAH BINT WAHB MAMA YAKE RASUL ALLAH SALALLAHU

ALAYHI WA SALAM. .................................................................................... 608

USAFI WA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM NA USAFI WA

WAZEE WAKE. ............................................................................................. 611

RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM NA UMMU AYMAN

KATIKA NYUMBA YA ABU TALIB NA FATMA BINT ASAD ........................ 619

RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM NA HILF AL FUDUL ... 624

SAFARI YA KIBIASHARA YA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA

SALAM KATIKA ARDHI YA SHAM. ............................................................. 628

NDOA YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’ALAYHI WA SALAM NA

KHADIJA BINT KHUWAYLID RADHI ALLAHU ANHA. ............................. 637

MUHAMMAD AL AMIN SALALLAHU ALAYHI WA SALAM NA UJENZI WA

AL KAABAH. ................................................................................................ 641

RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM NA ALI IBN ABI TALIB 644

MAISHA YA UTUME WA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA

SALAM NA UPINZANI KUTOKA KWA WATU WAKE. ................................ 649

MAISHA YA DAR AL ARQAM NA HIJRA YA ABISINIYAH .......................... 668

DAMU YA KWANZA YA MASHAHIDI WA KIISLAM. .................................. 675


11

KUSILIMU KWA UMAR IBN AL KHATTAB RADHI ALLAHU ANHU ......... 689

KIFO CHA ABU TALIB NA KHADIJA BINT KHUWAYLID RADHI ALLAHU

ANHA ........................................................................................................... 696

SHAQQ AL QAMAR - MUUJIZA WA KUPASUKA KWA MWEZI................. 705

SIFA ZA UPEKEE WA KIMAUMBILE WA NABII MUHAMMAD SALALLAHU

ALAYHI WA SALAM: .................................................................................... 708

SAFARI YA ISRA NA MIRAJ. ........................................................................ 723

MAUMBILE YA BURAQ NA MIUJIZA YA SAFARI YA ISRA NA MIRAJ. ..... 734

MUSAB IBN UMARY BALOZI WA KWANZA WA UISLAM NA

MAKUBALIANO YA AQABAH. .................................................................... 747

DARJA ZA MASAHABA WA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA

SALAM. ........................................................................................................ 752

KUZALIWA KWA BAHR UL ILM ABDA ALLAH IBN ABBAS RADHI ALLAHU

ANHU. .......................................................................................................... 755

HIJRA YA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM ..................... 756

MUHAMMAD SALALLAHU ALAYHI WA SALAM, ALI IBN ABI TALIB NA

SUHAYB AL AL RUMI RADHI ALLAHU ANHUM NDANI YA ARDHI YA

QUBA ........................................................................................................... 769

MASJID TAQWA - MSIKITI WA MWANZO KUJENGWA NA RASUL ALLAH

SALALLAHU ALAYHI WA SALAM. .............................................................. 773

KUWASILI KWA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM KATIKA

MJI WA MADINAH AN NABI. ...................................................................... 777

MAKUBALIANO BAINA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM

NA WATU WA MADINAH ............................................................................ 784

KUWASILI KWA UMMU AYMAN KATIKA MJI WA MADINAH AN NABI. .. 787

RASUL ALLAH SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM NA MSAFARA WA

BIASHARA WA ABU SUFYAN ...................................................................... 791

YAWM AL FURQAN – SIKU YA VITA VYA BADR. ...................................... 797

KHALID IBN WALID NA VITA VYA UHUD, KHANDAK NA MUTAA. ........ 811

MAKUBALIANO YA SULHU AL HUDAYBIYYAH ........................................ 821

KUSILIMU KWA KHALID IBN WALID. ....................................................... 832


12

SAYFU ALLAH KHALID IBN WALID RADHI ALLAHU ANHU NA VITA VYA

MUTAH ........................................................................................................ 836

FAT-H MAKKIYAH - UFUNGUZI WA MJI WA MAKKAH. .......................... 838

WAKE WA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM. ........ 844

UMM AL MU’MININ SAWDAH BINT ZUMAH ........................................... 852

UMM AL MU’MININ AISHA BINT ABU BAKR AS SIDDIQ ........................ 853

UMM AL MU’MININ HAFSAH BINT UMAR IBN AL KHATTAB. ............... 855

UMM AL MU’MININ ZAYNAB BINT KUZAYMAH. .................................... 857

UMM AL MU’MININ RAYHANA BINT ZAYD ............................................. 859

UMM AL MU’MININ HIND UMMU SALAMAH. ........................................ 860

UMM AL MU’MININ MAYMUNA BINT HARITH IBN HAZAN AL

HILALIEH .................................................................................................... 862

UMM AL MU’MININ ZAYNAB BINT JAHSH. ............................................. 865

UMM AL MU’MININ RAMLA BINT ABU SUFYAN – UMMU HABIBA. ..... 867

UMM AL MU’MININ JUWAYRIYAH BINT HARITH. ................................... 870

UMM AL MU’MININ SAFIYYHA BINT HUYAY IBN AKHTTAB. ................ 871

UMM AL MU’MININ MARIA BINT SHAM. .................................................. 873

SURIYYAH NA MILK AL YAMIN KATIKA UISLAM ..................................... 875

MFUMO WA UTUMWA NA MATEKA WA VITA KATIKA UISLAM. ............ 880

AAL, AHL, ZAWJ NA QAWWAM KATIKA UISLAM. .................................... 888

WANAWAKE WALIO JIPENDEKEZESHA KINDOA NA WALIOCHIKA WA

NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM. .......................... 907

MAVAZI YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM. ...... 912

HIJA YA KUAGA YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA

SALAM. ........................................................................................................ 914

KHUTBA YA KUAGA YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA

SALAM. ........................................................................................................ 920

KIFO CHA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM. ........ 923

MAUTI, BARZAKH NA KABURI KATIKA AYA NA HADITH ....................... 942


13

KUHIFADHIWA NA KURAHISISHWA KWA QUR’AN. ............................... 980

MARUDIO YA VITABU VILIVYOTUMIKA KATIKA KITABU

HIKI: ....................................................................................................... 998

MARUDIO YA MITANDAO ILIVYOTUMIKA KATIKA KITABU

HIKI......................................................................................................... 999

VITABU VILIVYOTANGULIA VYA AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH:

1- IJTIHAD NA TAQLID HISTORIA YA UISLAM: MAIMAMU NA MADHHAB

YAO KATIKA UISLAM - TOLEO LA KWANZA - MWAKA - 1435 AL HIJRA

(2014).

2- IJTIHAD NA TAQLID HISTORIA YA UISLAM: MAIMAMU NA MADHHAB

YAO KATIKA UISLAM - TOLEO LA PILI - MWAKA - 1437 AL HIJRA

(2016).

3- IJTIHAD NA TAQLID HISTORIA YA UISLAM: MAIMAMU NA MADHHAB

YAO KATIKA UISLAM - TOLEO LA TATU - MWAKA 1439 AL HIJRA

(2018).

4-TAFSIR SURAT YUSUF – AHSAN AL QASAS - MWAKA 1441 AL HIJRA

(2020).

5-ULU UL AZMI MINNA RUSULUN JUZUU AL AWWAL – WENYE AZMA

THABIT MIONGONI MWA MITUME JUZUU YA KWANZA – MWAKA 1443

AL HIJRA(2022)


14

UTANGULIZI

‏﴿لَقَدْ‏ كَ‏ انَ‏ فىِ‏ قَصَصِ‏ هِ‏ مْ‏ عِبْ‏ رَةٌ‏ لأُوْ‏ لىِ‏

ٱلأَلْبَابِ‏ مَا كَانَ‏ حَدِيثاً‏ يُفْتَرَ‏ ‏ٰى وَلَٰكِن

ّ كُل شَيْءٍ‏ وَهُدًى وَرَحمَْةً‏ لِّقَوْمٍ‏ يُؤْمِنُونَ‏ ﴾

تَصْدِيقَ‏ ٱل َّذِى بَينَْ‏ يَدَيْهِ‏ وَتَفْصِيلَ‏ ِ

Laqad kana fee qasasihim AAibratun li-olee al-albabi ma kana hadeethan yuftara

walakin tasdeeqa alladhee bayna yadayhi watafseela kulli shay-in wahudan

warahmatan liqawmin yu/minoona (Surat Yusuf 12:111)

Tafsir: Kwa Hakika katika Visa vyao, kuna mafunzo kwa watu wenye kufahamu,

Haikua (hii Quran) Hadith ya kughushi, bali ni Usadikisho wa Vitabu (Zabur,

Tawrat, Injil n.k vilivyopo vya Allah) wenye maelezo ya kina juu ya kila kitu na

Muongozo na Rehma kwa Ummah wa Walioamini.

‏﴿ٱلحَْمْدُ‏ هللِ َِّ‏ رَبِّ‏ ٱلْعَالَمِينَ‏ ﴾

Alhamd Lillah Rabbi Al Aálamin!

Awali namshukuru Allah Subhanahu wa Ta’ala na kumuombea Rehma na Amani M-

bora na Mtukufu wa viumbe, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam.

Pili namshukuru Allah Subhanahu wa Ta’ala kwa kutujaalia kua ni wenye kuingizwa

kwenye Rehma zake kwa kujaaliwa kupata Muongozo wake na hivyo kua ni wenye

kumuamini yeye na Mtume wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam, na kwa

kunineemesha neema hii yenye manufaa na kisha kuniwezesha kua ni mwenye uwezo

wa kujaribu kuandika kwa mara nyengine tena. Namuomba Allah Subhanahu wa Ta’ala

atunufaishe kwa yale mambo yenye manufaa ndani ya kitabu hiki na pia yale


15

yaliyokuwemo katika maisha yetu na pia atuepushe na yale yasiyokua na manufaa

nasi..Aamiin.

Tunapoiangalia Qurán ambayo ni kitabu kitukufu cha Allah Subhanah wa Ta’ala basi

tunaona kua ndani yake imezungumzia mambo mengi sana yenye manufaa katika maisha

ya Ibn Adam, ikiwemo maamrisho, makatazo na pia visa kadhaa ndani yake, na pale

iliposhuka na kuelezea baadhi ya visa vya Manabii na Mitume basi ilikua na ujumbe wa

kumpa nguvu, utulivu na kumliwaza mpokeaji wake ambae ni Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam na vile vile Waislam wote kwa ujumla na hivyo tuweze

kutafakkar na kua na ustahmilivu na subra katika mitihani tutayo kumbana nayo katika

kipindi cha mpito cha uhai wa hapa Ulimwenguni kwa ujumla, ambapo hatukuletwa kwa

ajili ya kucheza, kwani tumeletwa kwa ajili ya kumuabudu Mola wetu na kua katika

mapigano dhidi ya Iblis na pia dhidi ya Matamani ya Nafsi zetu.

Kwani ukweli ni kua katika kipindi cha karne yetu tunayoishi basi Waislam wengi

wamekua ni wenye kuishi kimazoea badala ya kua ni wenye kuishi kulingana na Ilm ya

dini yao kwa kutumia njia na mifano iliyoainishwa ndani ya Quran na Sunnah, na

Waislam hivyo kua katika hali na mazingira yanayosikitisha Kidini, Kielimu, Kiafya,

Kiufahamu, Kimamlaka, Kiuchumi, n.k na hivyo ni kuonekana kua ni dhalili na wenye

kukosa subra, ustahmilivu mkubwa pale inapokosekana msaada wenye manufaa kwao

katika kutatua matatizo yao ambayo mengi hua ni yenye kutokana na mapambo ya

kidunia kiasi ya kua wanafikia kuitumia Dini yao kwa ajili ya manufaa yao ya kidunia na

hivyo kua ni wenye kukaribia kuingia katika ile hali ambayo imeelezewa na aya ifuatayo:

‏﴿وَمِنَ‏ الن َّاسِ‏ مَن يَعْبُدُ‏ الل َّهَ‏ ٰ عَلَى حَرْ‏ فٍ‏ ۖ فَإِنْ‏ أَصَابَهُ‏ خَيْرٌ‏ اطْمَأَن َّ بِهِ‏ ۖ وَإِنْ‏

أَصَابَتْهُفِ‏ ْنَةٌ‏ انقَلَبَ‏ ٰ عَلَى وَجْهِهِ‏ ا خَسِ‏ ل ‏َر د ُّ ن ْيَا وَالآْ‏ خِ‏ رَةَ‏ ۚ ذَٰلِكَ‏ هُوَ‏ الخُْسْرَ‏ انُ‏

الْمُبِينُ‏ ﴾

Wamina alnnasi man yaAAbudu Allaha AAala harfin fa-in asabahu khayrun

itmaanna bihi wa-in asabat-hu fitnatun inqalaba AAala wajhihi khasira alddunya

waal-akhirata Dhalika huwa alkhusranu almubeenu.(Surat Al Hajj 22:11)

Tafsir: Na miongoni mwa watu ni wale ambao Wanamuabudu Allah wakiwa

Ukingoni, hivyo kama akifikwa na Mema basi hua ni mwenye kuridhia, lakini

akifikwa na Mitihani basi hua ni mwenye kugeuza uso wake (hua na shaka na hivyo

hua ni mwenye kukosa Imani na Mola wake) hula hasara hapa Duniani na Akhera.

Huko hua ni kula hasara sana kuliko wazi.


16

Ama kuhusiana na ayah hii basi anasema Jarra Allah, Sultan Al Balagha Imam Abu Al

Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Neno ‘Harfin’ lililotumika katika ayah hii linamaanisha

hali ya mtu ambae hayupo katikati ya dini, yaani yupo pembeni kabisa kama vile

mtu anaeenda vitani kisha akakaa kwenye mstari wa nyuma kabisa huku akisubiri

watu wakishinda basi akimbilie ngawira na wakishindwa basi awe ni wa mwanzo

kukimbia’

Yaani hawa ni watu ambao Imani zao zimekua dhaifu na ingawa wanamuabudu Allah

Subhnah wa Ta’ala lakini hata hivyo hawana Imani thabit katika nyoyo zao kwani Nuru

ya Dini yao katika nyoyo zao ni dhaifu kiasi ya kua akipata mtihani mdogo tu basi

anaweza kua ni mwenye kuangukia katika hali mbaya ya kuiuza dini yake na hivyo kua

ni miongoni mwa wenye sifa ya unafiq.

Allah Subhanah wa Ta’ala ni mwenye kuwapima waja wake kwa kuwapa mitihani katika

mazingira tofauti kama alivyotuonesha kupitia katika viza vilivyomo ndani ya Qur’an

hivyo unapofuatilia njia na mifano iliyomo ndani ya Qurán basi unaona kua ingawa

Qurán imezungumzia visa vingi katika sura zake mbali mbali ambapo hapo hapo hakuna

kujirudia rudia kwa visa hivyo wala kupingana kwa visa hivyo katika kuvielezea kwake,

lakini kuelezewa kwa visa hivyo kamwe hakukuwa ni kwa ajili ya kutuelezea historia au

kutuburudisha kwa hadith zake tu, bali ni kwa ajili ya kutoa mifano yenye mafunzo na

pia yenye maonyo kwa kutuonesha namna Allah Subhanah wa Taála anavyowapenda,

anavyowahurumia na kuwajali waja wake wanaomtii kumshukuru na namna

anavyowaonya kabla ya kuwaadhibu wale wenye kumuasi na kumkufuru na ndio maana

akawa ni mwenye kutuhimiza kumtii kwa kutuambia:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ ٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَلْتَنظُرْ‏ نَفْسٌ‏ م َّا قَد َّمَتْ‏ لِغَدٍ‏ وَٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏

خَبِيرٌ‏ بمَِا تَعْمَلُونَ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo ittaqoo Allaha waltandhur nafsun ma qaddamat

lighadin waittaqoo Allaha inna Allaha khabeerun bima taAAmaloona (Surat Al

Hashr 59:18)

Tafsir: Enyi Mlioamini! Muogopeni Allah na tekelezeni majukumu yenu juu yake. Na

kila mmoja wenu aangalie ni nini Nafsi yake imetanguliza kwa ajili ya kesho. Na

Muogopeni Allah. Kwani Kwa Hakika Allah ni mwenye habari juu ya kila

mnachokifanya.


17

Hivyo mbali ya kua Allah Subhanah wa Taála ni mwenye kutuonya na kutuhimiza

kutekeleza majukumu yetu juu yake kupitia katika kitabu chake kitukufu lakini pia ni

mwenye kutuongoza ndani yake kama alivyosema:

بِكُل

ّ

‏﴿وَمَا كَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ لِيُضِل َّ قَوْماً‏ بَعْدَ‏ إِذْ‏ هَدَاهُمْ‏ حَتى َّ ٰ يُبَينِّ‏ َ لهَُم م َّا يَت َّقُونَ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ ِ

شَيْءٍ‏ عَلِيمٌ‏ ﴾

Wama kana Allahu liyudhilla qawman baAAda idh hadahum hatta yubayyina

lahum ma yattaqoona inna Allaha bikulli shay-in AAaleemun (Surat At Tawba

9:115)

Tafsir: Na si juu ya Allah kuwapotosha watu baada ya kuwaongoza hadi

akawabainishia ni jambo gani la kujiepusha nalo. Hakika Allah ni mwenye kujua juu

ya kila kitu.

Anasema Imam Ibn Al Mundhir Al Nishapuri kua: ‘Ilikua ni kawaida ya Sahaba Abd

Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu, kuwasomesha darsa Wanafunzi wake katika

kila siku ya Alkhamis na kisha baada ya kumaliza darsa basi hua ni mweye kusema:

‘Yeyote yule miongoni mwenu anaetaka kua Mwanazuoni basi na aombe dua juu

ya hilo. Na asiombe chochote baada ya hilo kwa sababu Mwanazuoni na

MWanafunzi wako sawa kimalipo. Enyi watu mimi sikhofu kua nyie mtaulizwa juu

ya kile ambacho Allah Subhanah wa Taála amekuwekeeni wazi juu yenu, kwani

amesema: ‘Wama kana Allahu liyudhilla qawman baAAda idh hadahum hatta

yubayyina lahum ma yattaqoona inna Allaha bikulli shay-in AAaleemun’ yaani, Na si

juu ya Allah kuwapotosha watu baada ya kuwaongoza hadi akawabainishia ni

jambo gani la kujiepusha nalo. Hakika Allah ni mwenye kujua juu ya kila kitu.’ ’

Hivyo ni wajibu wetu kuachana na kuepukana na kuishi kimazoea na badala yake

tujitahid kushikamana na njia na mifano iliyomo ndani ya Qur’an, na Sunnah za Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam na pia kushikamana na ufafanuzi wa Wanazuoni wa

skuli za Madhhab na mitazamo yao juu ya Vitu viwili hivyo ambavyo ndio vyanzo vya

Hukmu na Sharia vinavyotuongoza kidini katika njia iliyonyooka na hivyo kua ni wenye

kudumu katika njia ya uongofu.

Mpangilio wa Kitabu hiki kimegawika katika sura mbili ambapo katika Sura ya Kwanza

inazungumzia juu umuhimu wa kuisoma, kuifahamu na kuizingatia Qur’an kwa kina ili

kuweza kua ni wenye kunufaika na Mafunzo, Hikma na Busara zilizomo ndani yake na

nimeyaelezea haya kabla ya kuingia katika Sura ya Pili ambamo ndani yake ndio mna


18

Visa vya Manabii na Mtume Watano Waliokua na Azma kubwa zaidi katika Maisha yao

na kujaribu kufafanua historia zao, mitihani yao, subra na ustahmilivu wao uliotokana na

kua na Nuru ya Iman kwa Mola wao katika Vifua, Nyoyo na Nafsi zao na kua na

misimamo imara na hivyo kua ni mifano bora kwetu kutokana na yaliyomo ndani yake.

Na ingawa Mitume hao wako watano ambao ni Nabii Nuh Alayhi Salam, Nabii Ibrahim

Alayhi Salam Nabii Musa Alayhi Salam, Nabii Isa Ibn Mayram Alayhi Salam na

Muhammad Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, lakini hata hivyo katika kitabu cha

Juzuu ya kwanza sikuweza kuwaeleza Mitume hao wote, kwani nimewaelezea Mitume

watatu tu ambao ni Nabii Nuh Alayhi Salam, Nabii Ibrahim Alayhi Salam Nabii Musa

Alayhi Salam.

Na hii ni kwa sababu ya kua kama ningewaelezea wote kwa pamoja katika kitabu kimoja

basi Kitabu kingekua kikubwa sana yaani kingekaribia kurasa 2000, hivyo nimeona bora

nikigawe mara mbili kwa kutoa juzuu ya kwanza ili kurahisisha usomaji, na uzingatiaji

wa ujumbe uliomo ndani yake kwanza, na Alhamd lillah Allah Subhanah wa Ta’ala

ameniwezesha kutoa Juzuu ya pili ambayo ndani yake nimemuelezea Nabii Isa Ibn

Maryam Alayhi Salam na Nabii Muhammad Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na

hivyo namshukuru Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kuniwezeshe kutekeleza ahadi yangu

hii.

Hivyo kama tukizingatia mafunzo yaliyomo ndani yake basi tutakua ni wenye kunufaika

na mengi sana hususan katika wakati huu wa mitihani ndani ya Uhai wetu, kwani

kitatuongezea Imani kwenye Nafsi na Nyoyo zetu na kutupa Muongozo stahiki katika

kupigana vita dhidi ya uadui wa ndani kutoka katika Nafsi zetu na uadui wa nje

unaotokana na Shaytan na wafuasi wake wanaotuzunguka katika mazingira yetu kwani

anasema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

‏﴿ٱهلل َُّ‏ نَز َّلَ‏ أَحْسَنَ‏ ٱلحَْدِيثِ‏ كِتَاابً‏ م ُّتَ‏ شَاهبِ‏ اً‏ م َّثَانىِ‏ َ تَقْشَعِر ُّ مِنْهُ‏ جُ‏ لُودُ‏ ٱل َّذِينَ‏ يخَْشَوْنَ‏

رَب َّهُمْ‏ ثمُ َّ تَلِينُ‏ جُلُودُهُمْ‏ وَقُلُوبُهُمْ‏ إِلىَٰ‏ ذِكْرِ‏ ٱهلل َِّ‏ ذٰلِكَ‏ هُدَى ٱهلل َِّ‏ يَهْدِى بِهِ‏ مَن

يَشَآءُ‏ وَمَن يُضْلِلِ‏ ٱهلل َُّ‏ فَمَا لَهُ‏ مِنْ‏ هَادٍ‏ ﴾

Allahu nazzala ahsana alhadeethi kitaban mutashabihan mathaniya taqshaAAirru

minhu juloodu alladheena yakhshawna rabbahum thumma taleenu julooduhum

waquloobuhum ila dhikri Allahi dhalika huda Allahi yahdee bihi man yashao

waman yudlili Allahu fama lahu min hadin (Surat Az Zumar 39:23)


19

Tafsir: Allahu ameshusha hadithi bora kabisa, Kitabu (Quran) chenye sehemu ndani

yake zinazofanana kwa wema na usahih. Ngozi za wale wenye kuomuogopa Allah

zinatetemeka (Wanapoisikia Qurán). Na kisha Nyoyo zao na ngozi zao hulainika

kutokana na kumkumbuka Mola wao. Huo ni Uongofu wa Allah. Ambae humuongoza

amtakae na anaepotoshwa na Allah basi hakuna atakaemuongoza.

Namuomba Allah Subhanah wa Ta’ala awe ni mwenye kunifanikishia malengo yangu

ya kufikisha ujumbe katika kuvielezea Visa vya Ulu ul Azmin Minna Rusul Juzuu ya

Kwanza na hii ya Pili na kuinufaisha Nafsi yangu na kuwanufaisha Waislam wengine

wote kwa ujumla kutokana na Mafunzo, Hikma, Busara na Miongozo inayopatikana

ndani yake kulingana na Aya za Quran Tukufu, Sunnah na Hadith za Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na pia kulingana na Mitizamo ya Wanazuoni tofauti

waliotumia mda wao na Ilm yao katika kuelezea namna walivyofaham juu ya visa vya

Mitume hao husika na hivyo kua ni wenye kutunufaisha nasi. Na muomba Allah

Subahanh wa Ta’ala awalipe kwa jitihada zao na awazidishie ziada katika amali zao.

Na vile vile namuomba Allah Subhanah wa Ta’ala anisamehe kwa makosa na kasoro

zitakazojitokeza katika jitihada yangu hii kwani ukamilifu ni wake yeye tu, na ni yeye

pekee ndie mwenye kuijua nia yangu katika utekelezaji wa haya nnayoyafanya.

Amiin ya Rabb!


20

SURA YA KWANZA

MUONGOZO, MANUFAA, TIBA NA REHMA ZILIZOMO NDANI YA QUR’AN.

Bila ya shaka katika aya za Qur’an nilizoanza nazo ndani ya kitabu hiki na nyenginezo

nyingi zilizomo ndani ya Qura’an tumeona kua Allah Subhanah wa Taála ametuwekea

wazi kua ndani ya kitabu chake mna muongozo wa kina wa kila kitu katika maisha yetu,

ikiwemo pia Muongozo dhidi ya matatizo mbali mbali ya kidunia na kiakhera, lakini hata

hivyo kamwe hatutoweza kuikimbia hali ya matatizo tuliyokua nayo wakati bado tukiwa

ni wenye kuutupa ufunguo unaofungua mlango wa utatuzi wa matatizo hayo, ufunguo

ambao si mwengine bali ni Qurán yenyewe ambayo ndani yake hamna Muongozo tu,

lakini pia mna Kinga, Rehma na Tiba pia ya maradhi tofauti kuanzia ya Kimwili,

Kinyoyo, Kinafsi, Kiroho n.k kama inavyoweka wazi aya ifuatayo:

‏﴿وَنُنَزِّلُ‏ مِنَ‏ ٱلْقُرْآنِ‏ مَا هُوَ‏ شِ‏ فَآءٌ‏ وَرَحمَْةٌ‏ لِّلْمُؤْمِنِينَ‏ وَلاَ‏ يَزِيدُ‏ ٱلظ َّالِمِينَ‏ إَلا َّ

خَ‏ سَاراً‏ ﴾

Wanunazzilu mina alqur-ani ma huwa shifaon warahmatun lilmu/mineena wala

yazeedu aldhdhalimeena illa khasaran (Surat Al Isra 17:82)

Tafsir: Na tumeiteremsha hii Qur’an ndani yake mkiwa na Tiba na Rehma kwa

Walioamini, lakini kwa Madhalimu haiwanufaishi na chochote isipokua Hasara.

Naam aya imetumia neno Shifaun ambalo ni lenye kutokana na neno Shafa. Na kwa

kilugha basi neno Shafa hua ni lenye kumaanisha Kuponya, Kutibu, Kurudisha Afya,

Kuridhisha, Kurudisha katika hali yake ya Asili au ya Kimaumbile, na ndio maana wenye

Lugha yao hua wanasema: ‘Shaf’ahu aAn Al Mas-alati’ kumaanisha kua

Amemuondolea Mashaka na kumridhisha Nafsi yake juu ya Jambo fulani.

Anasema Sultan al Mutakallimin Mujaddid ud Din Imam Abu Abd Allah Muhammad

Ibn Umar Ibn Al Husayn Al Taymi Al Bakri Al Tabaristan Fakhr Ad Din Al Razi Al

Shafii kuhusiana na ayah hii kua: ‘Quran ni Tiba ya Kitabia, Kijamii, Kiroho na

Kiafya pia. Na bila ya shaka baadhi ya Aya zake zimebainika kua ni Tibba ya

Maradhi tofauti ya Kimwili’


21

Ama kwa upande mmoja basi Hujjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Ibn

Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii anatuambia

kua miongoni mwa manufaa yanayohitajika kupatikana katika Quran basi ni kujua darja

za usomaji wake katika hali tofauti kwa kusema kua: ‘Amesema Amir ul Muuminina

Ali Ibn Abi Talib kua: ‘Yeyote yule atakaesoma Qur’an wakati akiwa amesimama

kwenye Sala basi anapata thawabu 100 kwa kila herufi moja ya Qur’an, na

atakaesoma Qur’an wakati akiwa amekaa kitako ndani ya Sala basi hua ni mwenye

kupata thawabu 50 kwa kila herufi, yeyote yule atakaesoma Qur’an nje ya Sala

akiwa katika hali ya kua na udhu basi hua anapata thawabu 25 kwa kila herufi, na

kwa kila atakaesoma Qur’an bila ya udhu kutokana na kua ni mwenye kuihifadhi

Moyoni mwake basi atapata thawabu 10 kwa kila herufi’

Na kwa Upande mwengine basi Hujjat ul Islami Mujadid Ad Din Imam Abu Hamid

Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii basi

anatuwekea wazi namna ya kunufaika na Muongozo, Tiba na Rehma zilizomo ndani ya

Qur’an kwa kutubainishia umuhimu wa kuzifaham siri za ndani na za nje zinazotakiwa

kupatikana katika kisomo cha Qur’an ambazo ni:

1 – Unapoanza kusoma basi inatakiwa uhisi ukubwa na uwezo wa mwenye maneno

hayo ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala. Na athari hio unaweza kuihisi ndani ya

Moyo wako pale unapoanza kuhisi ukubwa wa Arshi na Mamlaka yake Duniani na

Mbinguni na kila kilichomo ndani yake wakiwemo viumbe vyake, Ibn Adam,

Majini, Wanyama, na Miti. Unatakiwa ukumbuke kua Muumbaji wa vitu vyote

hivyo ni Mmoja, na Vitu vyote hivyo vimo ndani ya mamlaka yake na uwezo wake.

Kuhisi Neema zake na Rehma zake basi kunakupelekea kua ni mwenye kutaka

kuzisoma aya zake na kuona ndani yake Sifa zake, Majina yake, Uzuri wake, Ilm

yake na Hikma zake.

Faham kua kama ilivyokua Qur’an inawezekana kuguswa na wale waliotoharika –

na hivyo kua ni iliyofichikana kwa wasiokua tohara – kwa kimaana na kisiri basi

ndio hivyo hivyo inavyofichikana kutokana na Nyoyo zisizokua Nadhifu.

2 – Unatakiwa utafakkar na kuzingatia maana yake wakati unapokua unaisoma

kama ukitaka kua ni miongoni mwa watu wenye kuisoma Qur’an. Unatakiwa

urudie kila ulichokisoma kwa ulimi wako wakati akili yako ilipokuwa haipo kwenye

kisomo cha aya husika. Kwani haitakiwi kuhesabu kisomo ambacho hakina

mazingatio ndani yake kua ni sehemu ya kufanya amali njema. Kwa sababu ubora

wa kisomo cha Qur’an hua ni katika kuzidisha mazingatio yake. Amesema Sayyidna

Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hakuna Ubora katika Amali njema pale

inapokua hakuna ufahamu juu ya Amali hio, na pia katika kisomo kisichokua na

Mazingatio.’


22

3 – Unatakiwa uwe ni mwenye kuvuna Matunda ya Ilm kutoka katika Matawi yake

na kuyatafutia kutoka katika asili yake zinakopatikana, huku ukiwa ni mwenye

kutafakkar. Usitafute Kinga kutoka katika sehemu ambayo unatafutia hazina, na

usitafute Hazina katika sehemu ambayo unatafutia Miski na harufu yake nzuri,

kwani katika kila Tunda basi hua lina tawi lake na kila hazina ina chanzo chake.

Jambo hili hua linarahisika pale unapojua kua kuna aina za aya za Quran

kulingana na kusudio la ujumbe wake kwa mfano:-

A - Aya ambazo zinazomzungumzia Allah Subhanah wa Ta’ala, Sifa zake na

Vitendo vyake. Hivyo tafuta ndani ya haya Ilm ya kujua Ukubwa na Ufalme wa

Allah Subhanah wa Ta’ala.

B – Aya ambazo zinazungumzia Muongozo wa njia iliyonyooka: Hivyo tafuta ndani

ya haya Ilm ya Rehma zake, Neema zake na Hikma zake.

C – Aya ambazo hua ni zenye kuzungumzia Maangamizo: Hivyo tafuta ndani yake

Ilm ya Uwezo, Ujabari na Utukufu wake Allah Subhanah wa Ta’ala.

D – Aya ambazo hua ni zenye kuzungumzia Maish ya Mitume: hivyo tafuta ndani

yake Ilm ya Huruma na Ukarim wake, Baraka, Neema na Misaada yake kwa waja

wake.

Hivyo kwa kila kusudio basi tafuta manufaa yaliyomo ndani yake kwa kadiri

inavyowezekana.

4 – Inakubidi ujilinde na kila kitu kinachozuia ufahamu wako kwa sababu kitu

hicho hua ndio pazia linalokuzuia kufaham kama alivyosema Allah Subhanah wa

Ta’ala:

‏﴿إِ َّ جَعَلْنَا عَلَى ٰ قُلُوهبِِمْ‏ أَكِن َّةً‏ أَن يَفْقَهُوهُ‏ وَفىِ‏ آذَاِِمْ‏ وَقْراً‏ وَ‏ إِن تَدْعُهُمْ‏ إِلىَٰ‏ ٱلهُْدَىٰ‏

فَلَنْ‏ يَهْتَدُو ۤ اْ‏ إِذاً‏ أَبَداً‏ ﴾

Inna jaAAalna AAala quloobihim akinnatan an yafqahoohu wafee adhanihim

waqran wa-in tadAAuhum ila alhuda falan yahtadoo idhan Abadan (Surat Al Kahf

18:57)

Tafsir: Na kwa hakika sisi tumejaalia katika nyoyo zao mapazia ili wasiifahamu

(Quran), na katika masikio yao uziwi. Na hata kama wewe ukiwaita katika uongofu

basi hawatoongoka Abadan.


23

Faham kua mtu mwenye ufahamu unaomtafuta Mola wake hua unapewa mitihani

ya aina mbili: Aidha hua unakua na mtihani wa kua na shaka na kukanusha ambao

hua ni wenye kuwajaribu wale ambao ni wenye Imani dhaifu. Au hua na mtihani

wa pazia linalojaa matamanio ya Moyo ambalo hua ni lile linalomfunika yule Mtu

mwenye kuiendekeza Dunia.

Ama kuhusiana na Mja ambae ni mwenye Iman na hivyo hua ni mwenye kua na

umakini katika Njia ya Mola wake, basi nao hua na Mapazia ya aina mbili. Ambapo

la kwanza ni vishawishi vya wasi wasi vinavompelekea kutofikiria hata juu ya kutia

katika Ibada husika, kwa mfano jee mwanzo wake ulikuaje Ibada hii, au bado niko

katika Ikhlas?, n.k. Aina ya pili ya vishawishi vya wasi wasi ni vile ambayo hua

vinakutoa katika umakini wa kutamka kwa usahih, na hivyo hukupelekea kua na

wasi wasi na kurudia tena kauli husika katika Ibada. Jambo hili hutokea ndani ya

Sala na nje ya Sala pia.

Jee itakuaje siri za Ufalme wa Allah Subhanah wa Ta’ala zipatikane na Moyo ambao

umakini wae upo katika kuhisi ni namna gani Midomo inafunga na kufunguka na

ni vipi Ulimi na Taya zinafanya kazi na hewa inapitaje baina yake?

Aina ya pili ya pazia linalokuwepo kwa Mja mwenye Imani ni pale mtu anapokua

hajui maana ya ndani ya kina cha aya za Qur’an. Kwani hali hii huuzuia ufaham

wake, kwani Allah Subhanah wa Ta’ala amemuamrisha Mja wake kua ni mwenye

kumuamini kulingana na hali ya vigezo tofauti ambavyo hua vipi katika ufahamu

wa juu juu na ufaham wa kina zaidi kama mfupa na nyama nyama iliyomo ndani

ya Mfupa kwa mfano: Allah Subhanah wa Ta’ala amewataka waja wake wawe ni

mwenye kuamini kua ni anaweza kuonekana, lakini hata hivyo kuonekana hua

kuna aina mbili ambazo ni:

Kama mtu atakua anaamini kua kumuona Allah Subhanah wa Ta’ala ni sawa na

kuoa kwa kutumia macho kama tunavyoona Ibn Adam Ulimwenguni basi

anategemea kujua nini juu ya siri ya Allah Subhanah wa Ta’ala pale aliposema:

‏﴿وَلَم َّا جَآءَ‏ مُوسَى ٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَل َّمَهُ‏ رَب ُّهُ‏ قَالَ‏ رَبِّ‏ أَرِنيِ‏ ۤ أَنظُرْ‏ إِلَيْكَ‏ قَالَ‏ لَن تَرَانىِ‏

وَلَٰكِنِ‏ انْظُرْ‏ إِلىَ‏ الجَْبَلِ‏ فَإِنِ‏ اسْتَقَر َّ مَكَانَهُ‏ فَسَوْفَ‏ تَرَانىِ‏ فَلَ َّما ٰ تجََل َّى رَب ُّهُ‏ لِلْجَبَِل

ٰ موسَى صَعِقاً‏ فَلَم َّآ أَفَاقَ‏ قَالَ‏ سُبْحَانَكَ‏ تُبْتُ‏ إِلَيْكَ‏ وَأََْ‏ أَو َّلُ‏ جَعَلَهُ‏ دَكّاً‏ وَخَ َّر

ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ ﴾


24

Walamma jaa moosa limeeqatina wakallamahu rabbuhu qala rabbi arinee andhur

ilayka qala lan taranee walakini ondhur ila aljabali fa-ini istaqarra makanahu

fasawfa taranee falamma tajalla rabbuhu liljabali jaAAalahu dakkan wakharra

moosa saAAiqan falamma afaqa qala subhanaka tubtu ilayka waana awwalu

almu/mineena (Surat Al Araf 7:143)

Tafsir: Na kisha akaja Musa katika eneo na mda maalum tuliompangia na

akazugungumza na Mola wake, (Nabii Musa)akasema : ‘Ewe Mola wangu Nioneshe

nipate Nikuone’ Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Huwezi kuniona, lakini

angalia Mlima, kama utabakia katika sehemu yake. Basi nawe utaweza utaniona’

Kisha alipouonesha Utukufu wake Mola wake kwa Mlima, akaujaalia kua ni wenye

kupukutika na kua vumbi. Na akaanguka nakupoteza faham Musa. Kisha

alipozindukana akasema: ‘Utukufu ni wako, Mimi Natubu kwako na hakika mimi ni

wa awali miongoni mwa Walioamini’

Na jee mtu huyo atafaham vipi kua haiwezekani kumuona kwa macho kama

tunavyoona katika Ulimwengu huu kwani jicho la kutizamia Ulimwengu hua

haliwezi kuona kila kitu, kila sehemu na kila upande, na jee atafaham vipi maana

ya maana ya maneno ya Allah Subhanah wa Ta’ala pale aliposema:

‏﴿لا َّ تُدْرِكُهُ‏ ٱلأَبْصَارُ‏ وَهُوَ‏ يُدْرِكُ‏ ٱلأَبْصَارَ‏ وَهُوَ‏ ٱلل َّطِيفُ‏ ٱلخَْبِيرُ‏ ﴾

La tudrikuhu al-absaru wahuwa yudriku al-absara wahuwa allateefu alkhabeeru

(Surat 6:103)

Tafsir: Hakuna Mtizamo utakaoweza kumuona yeye, lakini Mtizamo wake yeye huona

kila kitu. Kwani kwa hakika yeye ni Mpole na mwenye kujua kila kitu.

Aya ambayo inaenda sambamba na kauli yake isemayo:

‏﴿وُجُوهٌ‏ يَوْمَئِذٍ‏ ‏ َّضِرَةٌ۞‏ إِلىَٰ‏ رَهبَِّا ‏َظِرَةٌ‏ ﴾

Wujoohun yawma-dhin nadhiratun, Ila rabbiha nadhiratun (Surat Al Qiyamah

75:22-23)

Tafsir: Baadhi ya Nyuso siku hio zitang’ara, kutokana na kumuangalia Mola wao.


25

5 – Hutakiwi kua ni mwenye kufuatilia juu ya kupata Nuru ya Qur’an tu, lakini pia

unatakiwa upate hisia na athari zinazotakiwa kupatikana katika kuisoma Qur’an.

Hivyo usiisome aya bila ya kua si mwenye kujipamba na sifa zake. Kutokana na

kua na hali hio basi utakua ni mwenye kufaham na kuhisi athari ya kila aya

unayoisoma, kiasi ya kua rehma na usamehevu unapotajwa basi unakua unahisi

utulivu na furaha, na inapotajwa adhabu basi unahisi maumivu na khofu, kutokana

na kutajwa kwa Allah Subhanah wa Ta’ala, na Ukubwa wake na Sifa zake basi wewe

hua ni mwenye kuinamisha kichwa chako kutokana na Unyenyekevu unaouhisi

ndani ya mwili wako, kama vile mtu ambae unaetoweka kutokana na kumuona

Mola wako. Na wanapotajwa Makafiri na Utukufu wa Allah Subhanah wa Ta’ala

wa kua mbali sana na sifa ya kua na Mke na Mtoto basi wewe hua ni mwenye

kuinamisha kichwa chako na kupunguza sauti yako kama vile mtu anaejificha

kutokana na kuona haya isiyokua na kifani.

Athari hizi huonekana wazi kwenye viungo vya mwili wako kama vile kutokwa na

kilio kwa huzuni, kutokwa na jasho kwenye paji la uso kwa kuona aibu mbele ya

Mola wako, kutetemeka kwa furaha ya kuuona Utukufu wa Allah Subhanah wa

Ta’ala na kujisikia raha ndani ya viungo vyako, ulimi wako na sauti unapoona

habari njema ndani ya maneno yake Allah Subhanah wa Ta’ala na kua na khofu

unapoona ndani yake habari zenye kuonya. Kama ikiwa ni mwenye kufanikiwa kua

na hali ya hisia kama hivyo basi utakua ni mwenye kufanikiwa kupata Baraka za

Qur’an.

Kwa upande mwengine basi Shifaa na Rehma za Qur’an sio kua zinapatikana kutokana

na kuisoma na kuifanyia kazi tu lakini pia hua zinapatikana kwa kuisikiliza Qur’an

yenyewe pale inapokua inasomwa na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema

katika Qur’an:

‏﴿وَإِذَا قُرِ‏ ئَ‏ ٱلْقُرْآنُ‏ فَٱسْتَمِعُواْ‏ لَهُ‏ وَأَنصِتُواْ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تُرْحمَُونَ‏ ﴾

Wa-idha quri-a alqur-anu faistamiAAoo lahu waansitoo laAAallakum turhamoona

(Surat At Aaraf 7:204)

Tafsir: Kwa hivyo inaposomwa Quran isikilizeni, na mkae kimya kwa umakini ili

mpate kua ni wenye kurehemewa.

Abd Allah Ibn Masoud Radhi Allahu Anhu, anasema kuhusiana na ayah hii kua:

‘Inaposomwa Quran basi mnatakiwa mkae kimya huku mkiisikiliza kwa umakini

na kuitafakkari.’


26

Mtizamo wa Sahaba Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu ni mtizamo ambao

haujaachana na mtizamo wa Hujjat ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali. Hivyo tuiangalie ayah hii kulingana na mtizamo mwengine

ambao unatuthibitishia athari ya Qur’an katika miili yetu pale unapotulia na kuisikiliza,

na ili kufaham vizuri zaidi basi kwanza inabidi tufahamu kuhusiana na mawimbi ya

umeme yanayosambaza hisia za mawasiliano katika Ubongo wa miili yetu.

Katika kusafirisha hisia mbali mbali ndani ya miili yetu basi Ubongo hua unazalisha

nguvu ya mawimbi ya umeme ambayo nayo yamegawika katika aina nne. Aina ya

kwanza ni ilie inayoitwa Beta, aina hii huzalishwa pale mtu anapokua yuko katika hali

ya pirika pirika za kazi au jambo ambalo linahitaji umakini sana katika utekelezaji wake,

mawimbi haya hua na kasi ya mizunguko 15-40 kwa sekunde kulingana na namna

Ubongo unavyofanya kazi kwa ari katika wakati huo.

Aina ya pili ni ile iitwayo Alpha ambayo hua ni yenye kuzalishwa baada ya mtu husika

kumaliza jambo lililokua likimshughulisha akili yake, na hivyo kua kwenye hali ya

mapumziko ya ubongo na mwili, mawimbi haya ya Alpha hua yanatofautiana na Beta

kutokana na kua ni ya utulivu na hivyo hua ni yenye kasi ya mizunguko 9-14 kwa

sekunde, hali hii hua anayo pia mtu ambae amekaa na kutafakkari kitu kwa utulivu, au

akiwa anatembea taratibu kwa ajili ya kupata hewa nzuri na hivyo hua ni mwenye

kuridhika.

Aina ya tatu ya mawimbi hua ni ile inayoitwa Theta ambayo hua na kasi ya mzunguko

wa kati kwani hua na mizunguko 5-8 kwa sekunde, hali hii hua nayo yule ambae

ameshamaliza kazi, ameshapoa na kutulia na hivyo anakua ni mwenye kufikiria au

kukumbuka mambo mazuri mazuri yaliyopita au atakayoyapata baada ya yale

aliyoyafanya.

Aina ya mwisho ambayo ni aina ya nne ya mawimbi hua inaitwa Delta ambayo hua na

kasi ya mzunguko mdogo zaidi kwani hua na mizunnguko 1-4 kwa sekunde, na hali hii

hua nayo mtu pale anapokua anasinzia hadi anapoingia katika hali ya usingizi na kulala

fofofo!

Hivyo Mtu unaposikia Qur’an, ukanyamaza na kuisikiliza kwa umakini basi mzunguko

wa mawimbi ya Ubongo wako hua ni wenye kutoka katika hali iliyokuwepo na kuingia

katika hali ya Alpha ambayo ni ya kua mwenye kuridhika Kimwili, Kinafsi, Kiufaham

na Kiakili. Na hivyo kukupelekea kua na Muongezeko wa Imani ya Kiroho, ongezeko la

Uwezo wa Nguvu ya Kinga ya mwili, na ongezeko la uzalishaji wa seli mbali mbali za

mwili na hivyo kua ni tiba kwa Maradhi ya Saratani, huzidisha nguvu ya Akili katika

sehemu ya Ufahamu na kuhifadhi, Huimarisha mishipa ya Moyo na sambamba na hayo


27

basi usikilizaji wa Qur’an hukupunguzia Hisia za Khofu, Mshtuko, Wasi wasi, Uzito wa

mkusanyiko wa mawazo na hukupa utulivu wa kiakili kukupunguzia uvamizi wa maradhi

yanayotokana na mshtuko wa Moyo na mzunguko wa damu na utulivu wa kimwili pia

kwa ujumla kwani hata wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji basi hua ni wenye kupona

haraka maumivu yao pale wanapokua wanasikiliza Qur’an mara kwa mara.

Kwa upande mwengine basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anatuthibitishia

haya tena pale aliposema:

‏﴿ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ وَتَطْمَئِن ُّ قُلُوبُهُمْ‏ بِذِكْرِ‏ ٱهلل َِّ‏ أَلاَ‏ بِذِكْرِ‏ ٱهلل َِّ‏ تَطْمَئِن ُّ ٱلْقُلُوبُ‏ ﴾

Alladheena amanoo watatma-innu quloobuhum bidhikri Allahi ala bidhikri Allahi

tatma-innu alquloobu (Surat Ar Rad 13:28)

Tafsir: Wale walioamini na wakazipatia utulivu Nyoyo zao kutokana na kumkumbuka

Allah. Kwani kwa hakika ni katika kumkumbuka Alla ndiko kunakoupa Nyoyo

utulivu.

Ambapo anasema Imam Abu Muhammad Abd Allah Al Tustari kua: ‘Katika kufanya

(dhikr) huku ukiwa na (ʿilm) basi hua unapata utulivu (sukūn), na katika kufanya

Dhikr kwa Ufahamu (ʿaql) basi hua kunakuletea Utulivu mkubwa (ṭutmaʾīna).

Katika kufanya Dhikr huku ukiwa na (ʿilm) basi hua kunakuletea mapumziko ya

utulivu (sukūn), na Katika Kufanya Dhikr kwa ufahamu (ʿaql) Basi hua kuna

Utulivu mkubwa (ṭutmaʾīna) ’

Allah Subhanah wa Ta’ala anatuambia haya kwa sababu ni maumbile ya Nafsi za Ibn

Adam kua kila Nafsi zinapofikiria ya mapambo ya Kidunia, basi hua ni yenye kutaka

kuikimbilia na kujitumbukiza ndani yake na kutaka chengine zaid ya kile ambacho

kishaingia ndani yake. Lakini unapokua unamfikirira Allah Subhanah wa Ta’ala ambae

ndie Muumba basi hua hakuna kitu chengine chochote bora zaidi yake, hivyo kwako

wewe hua hakuna unachohitaji kwani kwake yeye kuna kila unachokihitaji na zaidi ya

utakachokihitaji kutoka kwake. Na hivyo hukupelekea kuyakimbia yasiyofaa na

kutokukukaribisha karibu yake, jambo hili hukupelekea kujawa na Imani na ari zaidi ya

kutekeleza maamrisho yake na kua ni mwenye kumtegemea yeye tu katika kila jambo

lako, na huo hua ni muongozo tosha kwa moyo na Nafsi yako, kama inavyosema aya

ifuatayo juu ya hayo.


28

‏﴿َٰي ُّهَا ٱلن َّاسُ‏ قَدْ‏ جَآءَتْكُمْ‏ م َّوْعِظَةٌ‏ مِّن ر َّبِّكُمْ‏ وَشِ‏ فَآءٌ‏ لِّمَا فىِ‏ ٱلص ُّدُورِ‏ وَهُدًى

وَرَحمَْةٌ‏ لِّلْمُؤْمِنِينَ‏ ﴾

Ya ayyuha alnnasu qad jaatkum mawAAidhatun min rabbikum washifaon lima fee

alssudoori wahudan warahmatun lilmu/mineena (Surat Yunus 10:57)

Tafsir: Enyi Watu! Kwa hakika yamekujieni Mawaidha kutoka kwa Mola wenu na

Tiba kwa ajili ya Vifua (Nyoyo) vyenu, na Muongozo kwa Walioamini.

Bila ya shaka tunapozungumzia Muongozo kwa Waumini wanaoishi katika hali ya

maisha ya Kiislam basi hatuwezi kukamilisha bila ya kugusia Hikma na Baraka

zinazopatikana ndani ya Muongozo huo kutoka kwa Mola wetu tuliobainishiwa ndani ya

kitabu kitukufu cha Qurán.

HIKMA NA BARAKA NDANI YA QUR’AN

Neno Hikma limetokana na asili ya neno Hakama ambalo kwa lugha ya Kiarabu hua ni

lenye kumaanisha Kuzuia, Kudhibiti, Kuamrisha, kua na Mamlaka, Kuhukumu, kua na

Hikma au Busara, kua na Uadilifu na kua na l’lm. Neno Hikma pia kimaana ndani yake

hua linajumuuisha tabia njema na kila sifa zilizo njema.

Tunapoiangalia Qurán basi tunaona pia kua ina sifa ya kua ni Uhkimat, yaani yenye

Kulindwa na Kudhibitiwa kutokana na Upotovu, na hivyo hua ni yenye kuweka bayana

kila lenye manufaa na kuweka bayana kila lisilokua na manufaa kwa kila Ibn Adam tena

bila ya kua na shaka yeyote ndani yake kutokana na asili yake. Kwani anasema Allah

Subhanah wa Taála kua;

﴿ بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ‏ ۞ حم ۤ ۞ وَٱلْكِتَابِ‏ ٱلْمُبِينِ۞‏ إِ َّ جَعَلْ‏ نَاهُ‏ قُرْآً‏ عَرَبِيّاً‏

ل َّعَل َّكُمْ‏ تَعْقِلُونَ۞‏ وَإِن َّهُ‏ فيِ‏ ۤ أُمِّ‏ ٱلْكِتَابِ‏ لَدَيْنَا لَعَلِي ٌّ حَكِيمٌ‏ ﴾


29

Bismi Allahi alRrahmani alRraheemi; Ha-meem, Waalkitabi almubeeni, Inna

jaAAalnahu qur-anan AAarabiyyan laAAallakum taAAqiloona, Wa-innahu fee

ommi alkitabi ladayna laAAaliyyun hakeemun (Surat Az Zukhruf 43:1-4)

Tafsir: Kwa jina la Allah mwingi wa Rehma na mwingi wa Huruma; Ha Mim. Na

(Naapa) kwa kitabu chenye kubainisha. Kwa hakika tumekijaalia Qurán kua katika

Lugha ya Kiarabu ili mpate kuzingatia. Na kwa Hakika hii (Quran) imo ndani ya

kitabu Mama mbele yetu, ni Kitukufu kilichojaa Hikma.

Anasema Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Qurán kimeitwa Umm ul Kitab

yaani Kitabu Mama kwa sababu hiki ni Kitabu ambacho ndio kilichotoa vitabu

vyote vya Mitume waliotangulia hapo kabla. Hivyo vitabu vyote vilivyotangulia

vimetokana na Kitabu Mama Qurán - Umm ul Kitab’

Umm ul Kitab si kitabu ambacho kilichojaa Hikma tu lakini pia ni kitabu ambacho

kimejaa Baraka ndani yake na juu ya hili basi linabainishwa na Qurán yenyewe pale

iliposema:

‏﴿وَهَٰذَا كِتَابٌ‏ أَنزَلْنَاهُ‏ مُبَارَكٌ‏ م ُّصَدِّقُ‏ ٱل َّذِى بَينَْ‏ يَدَيْهِ‏ وَلِتُنذِرَ‏ أُم َّ ٱلْقُرَىٰ‏ وَمَنْ‏

حَوْلهََا وَٱل َّذِينَ‏ يُؤْمِنُونَ‏ بِٱلآخِ‏ رَةِ‏ يُؤْمِنُونَ‏ بِهِ‏ وَهُمْ‏ عَلَى ٰ صَلاَهتِِمْ‏ يحَُ‏ افِظُونَ‏ ﴾

Wahadha kitabun anzalnahu mubarakun musaddiqu alladhee bayna yadayhi

walitundhira omma alqura waman hawlaha waalladheena yu/minoona bialakhirati

yu/minoona bihi wahum AAala salatihim yuhafidhoona (Surat Al AnAam

6:92)

Tafsir: Na hiki ni Kitabu (Qurán) ambacho kimeshushwa kikiwa kimejaa Baraka,

kuthibitisha vilivyotangulia kabla yake, ili upate kuuonya mji Mama (wa Makkah) na

iliyo pembeni yake, Wale ambao wanaamini juu ya Akhera wanaiamini (Qurán) na

wale ambao juu ya Sala zao wanahifadhi.

Neno Baraka kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kuongezeka, Kukua na pia

humaanisha Furaha. Neno Barakah linatokana na neno linalomaanisha sehemu ya mbele

ya Ngamia ambae amekaa chini na kuididimiza miguu ndani ya mchanga bila ya kutaka

kuondoka sehemu hio, na pia humaanisha msimamo thabiti wa mtu au kitu bila ya kurudi

nyuma kama vile anavyokua mtu shujaa anapobakia peke yake katika uwanja wa vita


30

dhidi ya maadui wote hivyo huamua kupigana hadi mwisho bila ya kukimbia mapigano,

Kua na msimamo, Kuishi, Kupewa heshima.

Hivyo Baraka hua ni muendelezo au muongezeko wa milele wa jema kutoka kwa Allah

Subhanah wa Taála wenye faida ndani yake ambalo hua halionekani kupungua kwake

bali hua linaonekana katika kuongezeka kwake bila ya kujua chanzo cha muendelezo au

muengezeko huo. Kwa mfano pale mtu anapotoa Sadaka na hivyo Baraka huingia katika

mali yake na kuonekana kwa muongezeko wa wingi wa Mali hio.

Anasema Allamah Abu Qasim Ibn Husein Ibn Mufadal Ibn Muhammad Raghib Al

Isfahani kua: ‘Baraka hua ni tofauti na Neema ambayo hua inamaanisha kitu au

jambo fulani maalum liwe kidogo au kikubwa kingi, na hua ni neema pale mtu

aliepewa anapokua na akili na ufahamu.’ Allah Subhanah wa Ta’ala amesema

katika Qurán:

‏﴿وَآاتَكُم مِّن ِ كُل مَا سَأَلْتُمُوهُ‏ وَإِن تَعُد ُّواْ‏ نِعْمَةَ‏ ٱهلل َِّ‏ لاَ‏ تحُْصُوهَا إِن َّ ٱلإنْسَانَ‏

لَظَلُومٌ‏ كَ‏ ف َّارٌ‏ ﴾

ّ

Waatakum min kulli ma saaltumoohu wa-in taAAuddoo niAAmata Allahi la

tuhsooha inna al-insana ladhaloomun kaffarun (Surat Ibrahim 14:34)

Tafsir: Na amekupeni nyinyi kila mlichotaka, na kama mkitaka kuzihesabu Neema za

Allah basi kamwe hamtoweza kuzihesabu. Kwa Hakika Mtu ni mwenye kujidhulumu

na mwenye kukufuru.

Hivyo tunapozungumzia kuhusiana na Allah, basi hua inazungumziwa kwa ujumla, na

kwa umoja kumaanisha: ‘Misaada na Fadhila zake Allah Subhanah wa Ta’ala'

anayoitoa kwa Waja wake. Na hua inajumuisha dalili zake, malipo yake, manufaisho

yake kwa Viumbe wake, Neema zake, Rehma zake, n.k.

Neno Barakah pia hua ni lenye kumaanisha al Ziyadah yaani Ziada, al Sa’adah yaani

Furaha, Al Du’a yaani Dua. Al Manfaáh yaani Manufaa, Al Baqah yaani Kinachobaki

Milele, Al Taqdis yaani Kitu kitukufu. Kwa hivyo Allah Subhanahu wa Taála anapotia

Barakah ndani ya kitu basi hata kama mwanzoni kitu hicho kilikua si chochote, lakini

baada ya kutiwa Barakah basi kitu hicho huanza kubadilika wingi, thamani yake,


31

manufaa yake na hata uzuri wake hupelekea kuzidisha idadi ya wingi wake. Barakah

kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala hua inakuja kutoka katika upande usiotegemewa

wala kufikirika na haihitaji wingi wa kitu.

Ama tunapozungumzia Barakah ndani ya Qurán kama ilivyoelezewa katika aya

tuliyoanza nayo ya Surat Al An Aam 6:92 na pia katika aya ifuatayo:-

‏﴿وَهَٰذَا كِتَابٌ‏ أَنزَلْنَاهُ‏ مُبَارَكٌ‏ فَٱت َّبِعُوهُ‏ وَٱت َّقُواْ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تُرْحمَُ‏ ونَ‏ ﴾

Wahadha kitabun anzalnahu mubarakun faittabiAAoohu waittaqoo laAAallakum

turhamoona (Surat Al AnAam 6:155)

Tafsir: Na hiki ni Kitabu (Qurán) ambacho kimeshushwa kikiwa kimejaa Baraka,

hivyo kifuateni na kuweni na Taqwa, ili muwe ni wenye kupata rehma.

Basi tunaona kua anasema Mujaddid ud Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Maana

ya Kitabun Mubarakan hua linamaanisha Kitabu chenye Rehma na Neema za Milele

kwa sababu hua ni chenye kuusia mema, malipo mengi zaidi na msamaha mkubwa

sana, na hapo hapo hua ni chenye kuonya kwa wanaomuasi Allah Subhanah wa

Ta’ala kwa kufanya Dhambi na Maovu’.

Ama kwa upande wa Imam Abu Al Thana’ Shihab ad-Dīn Sayyid Maḥmūd Ibn ‘Abd

Allāh Al Ḥusaynī Al Alusi Al Baghdadi basi yeye anasema kua: ‘Maana ya Kitabun

Mubarakan hua kunamaanisha Kitabu kilichojaaliwa kua na baraka nyingi ndani

yake, kwani kinajumuisha manufaa ya hapa Duniani na manufaa ya kesho Akhera

na kuweka wazi Ilm ya mambo ya sasa na yaliyotangulia’ (Ruh al-Ma'ani fi Tafsir al-

Qurán Al 'Adhim wa Sab'a Al Mathani)

Qurán imetumia aya zaidi ya 10 zenye kuzungumzia juu ya Baraka za Allah Subhanah

wa Taála katika vitu na mambo mbali mbali muhimu kwa Waislam kwa mfano: Mji wa

Makkah kama sehemu yenye nyumba ya awali ya kufanyia Ibada katika Surat Al Imran

3:96, Mji wa Jerusalem ulipotajwa Masjid Al Aqsa katika Surat Al Isra 17:1, Jangwa la

Sinai ambalo ni lenye Mlima Tur sehemu ambayo Allah Subhanhah wa Ta’ala

aliyozungumza na Nabii Musa, Ardhi ya Mji wa Sham sehemu ambayo waliozaliwa na

pia kuishi Mitume wengi zaidi katika Surat Al Anbiyah 21:71, Usiku wa Barakah

ulioshushwa Qurán katika Surat Ad Dukhan 44:3 na Surat Al Qadr.


32

Mti wa Mzaitun pia umetajwa kua na sifa ya kua Mubaraka katika Surat An Nur 24:35

ambapo matunda yake yanatoa mafuta ambayo hua ni yenye kutoa Nuru kali ya aina ya

Infra Red isiyoonekana kwa macho ya kawaida ya Ibn Adam lakini huweza kuonekana

kwa kutumia darubini maalum si hapa ulimwenguni tu lakini pia Nuru yake huweza

kuonekana hata kutoka katika kituo cha uchunguzi wa kisayansi cha angani. Mitume nao

pia ni miongoni mwa waliopewa sifa ya kua Mubaraka kama Nabii Nuh alipotajwa katika

Surat Hud 11:48, Nabii Ibrahim na Nabii Is-haq kama walivyotajwa katika Surat Saffat

37:113, Nabii Isa Ibn Maryam katika Surat Maryam 19:31. n.k

Neno Barakah ndio lililotoa neno Mubarik ambalo hua ni Isim fa'il yaani ni sifa ya

mweye kutoa Barakah ambae ni Allah Subhanah Allahu wa Taála pekee na ndio maana

Allah Subhanah wa Taála akawa na sifa ya kua na Tabarak ambayo ipo katika hali ya Al

Taqdis yaani ya Utukufu wa Kutoa Barakah pale aliposema katika Qurán:

ّ كُل شَيْءٍ‏

﴿ بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ‏ ‏۞تَبَارَكَ‏ ٱل َّذِى بِيَدِهِ‏ ٱلْمُلْكُ‏ وَهُوَ‏ ٰ عَلَى ِ

قَدِيرٌ‏ ﴾

Biismi Allahi AlRrahmani AlRrahim; Tabaraka alladhee biyadihi almulku wahuwa

AAala kulli shay-in qadeerun (Surat Al Mulk 67:1-2)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma na Mwingi wa Huruma; Ametukuka yule

ambae ndani ya mikono yake kuna Mamlaka, na ni yeye ambae ni mwenye uwezo wa

juu ya kila kitu.

Neno Tabaraka limetajwa ndani ya Qurán mara 9, ambapo aya zilizotaja na kutumia sifa

hii zimemsifia yule ambae tu ni pekee anaestahiki kua na sifa hio ya Al Mutabarik pekee,

ambae anatuwekea wazi juu ya hilo pale aliposema katika aya nyengine iliyotumia neno

Tabarakah Allahu ambayo inasema:

‏﴿إِن َّ رَب َّكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِى خَلَقَ‏ ٱلسَمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضَ‏ فىِ‏ سِ‏ ت َّةِ‏ أَ َّمٍ‏ ثمُ َّ ٱسْتَوَىٰ‏ عَلَ‏ ى

ٱلْعَرْشِ‏ يُغْشِ‏ ى ٱلْل َّيْلَ‏ ٱلن َّهَارَ‏ يَطْلُبُهُ‏ حَثِيثاً‏ وَٱلش َّمْسَ‏ وَٱلْقَمَرَ‏ وَٱلن ُّجُومَ‏ مُسَخ َّرَا ‏ٍت

أبَِمْرِهِ‏ أَلاَ‏ لَهُ‏ ٱلخَْلْقُ‏ وَٱلأَمْرُ‏ تَبَارَكَ‏ ٱهلل َُّ‏ رَب ُّ ٱلْعَالَمِينَ‏ ﴾


33

Inna rabbakumu Allahu alladhee khalaqa alssamawati waal-ardha fee sittati

ayyamin thumma istawa AAala alAAarshi yughshee allayla alnnahara yatlubuhu

hatheethan waalshshamsa waalqamara waalnnujooma musakhkharatin bi-amrihi

ala lahu alkhalqu waal-amru tabaraka Allahu rabbu alAAalameena (Surat Al Araf

7:54)

Tafsir: Hakika Mola wako ni Allah ambae yeye ndie alieumba Mbingu na Ardhi kwa

siku sita kisha akasimama juu ya Arshi, ni yeye ambae anauleta usiku kwa kuufunika

mchana kwa utaratibu usiosita, na Jua, na Mwezi, na Nyota zikiwa chini ya amri yake,

kwa hakika ni vyake viumbe na amri. Utukufu ni wake Allah Mola wa Ulimwengu.

Katika aya tuliyoianisha hapo juu ya Surat Al Araf 7:54 tunaona kua Allah Subhanah wa

Tabarak anatuwekea wazi kua Utukufu ni wake yeye tu kwani yeye ndie alietuumba sisi

viumbe na kila kitu kinachotuzunguka ulimwenguni na kuainisha Utukufu wake kwa kua

ndie mwenye Mamlaka ya kila kitu Mbiguni na Ardhini na kua ni yeye tu ndie aijuae

Siku ya Malipo na kutuhakikishia kua kwake yeye ndio marejeo yetu kama anavyosema

katika aya inayofuatia:

‏﴿وَتَبَارَكَ‏ ٱل َّذِى لَهُ‏ مُلْكُ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِندَهُ‏ عِلْمُ‏ ٱلس َّاعَةِ‏

وَإِلَيْهِ‏ تُرْجَعُونَ‏ ﴾

Watabaraka alladhee lahu mulku alssamawati waal-Ardhi wama baynahuma

waAAindahu AAilmu alssaAAati wa-ilayhi turjaAAoona (Surat Az Zukhruf 43:85)

Tafsir: Na Utukufu ni wa yule ambae mwenye mamlaka ya Mbiguni na Ardhini na

kila kilichomo baina yake, na yeye ndie mwenye kujua saa ya kiama na kwake yeye

ndio marudio yenu.

Hivyo ayah hii ya Surat Az Zukhruf 43:85 iko wazi kua ni jambo lisilokua na shaka kua

mwisho wetu Ibn Adam ni kufika tulikotoka yaani kwa Mola wetu lakini wakati bado

tupo safarini hapa ulimwenguni ndani ya Mamlaka yake kuelekea kwa Mola wetu basi

tunaweza kunufaika baada ya kufuata Muongozo wake na hivyo kupata Baraka na

Fadhila nyingi sana na za aina tofauti kutoka kwake Allah Subhanah wa Taála kama

inavyosema aya ifuatayo:


34

﴿َ أَي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ ۤ آمَنُو اْ‏ إِ‏ ن تَت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ يجَْعَل ل َّكُمْ‏ فُرْقَاً‏ وَيُكَفِّرْ‏ عَنكُمْ‏ ا سَيِّئَ‏ تِكُمْ‏

وَيَغْفِرْ‏ لَكُمْ‏ وَٱهلل َُّ‏ ذُو ٱلْفَضْلِ‏ ٱلْعَظِيمِ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo in tattaqoo Allaha yajAAal lakum furqanan

wayukaffir AAankum sayyi-atikum wayaghfir lakum waAllahu dhoo alfadhli

alAAaDheemi (Surat Al Anfal 8:29)

Tafsir: Enye Mlioamini! Kama mtamcha Allah basi atakujaalie Furqan na

kukufutieni Madhambi yenu na atakusameheni, na kwa hakika Allah ndie mmiliki

wa fadhila Kubwa.

Tunapoitafakkar ayah hii basi tunaona kua ayah imetumia neno Furqan ambalo maana

yake hua ni Muongozo unaotofautisha baina ya jema na ovu, na bila ya shaka neno hili

hua linafasirika vizuri zaidi pale tunapoiangalia maana ya aya ifuatayo ya Surat Al

Furqan:

‏﴿تَبَارَكَ‏ ٱل َّذِى نَز َّلَ‏ ٱلْفُرْقَانَ‏ عَلَى ٰ عَبْدِهِ‏ لِيَكُونَ‏ لِلْعَالَمِينَ‏ نَذِيراً‏ ﴾

Tabaraka alladhee nazzala alfurqana AAala AAabdihi liyakoona lilAAalameena

nadheeran (Surat Al Furqan 25:1)

Tafsir: Ametukuka yule ambae ameishusha Furqan (Qurán) kwa mja wake ili awe ni

muonyaji kwa viumbe.

Naam, neno Furqan linatokana na neno Faraqa ambalo kwa kiarabu hua linamaanisha

Kubagua, Kutofautisha, Kuamua au Kugawa, hivyo Furqan hua ni Uthibitisho, Hoja au

kitu kinachotofautisha baina ya Jema na Ovu, Nuru na Kiza, n.k.

Hivyo Qurán imepewa jina la sifa ya Furqan kwa sababu Quran ni yenye muongozo

wenye kubainisha na kutofautisha baina jema na ovu kwa kutumia njia tofauti za

kubainisha mambo kwa moja kwa moja, kwa mafumbo na njia ya mithali za aina tofauti

zenye mafunzo ndani yake.


35

MAFUMBO NA MITHALI ZILIZOMO NDANI YA QUR’AN.

Neno Mathala kwa kiarabu hua ni lenye kumaanisha Mithili ya kitu, Mfano, Mfanano,

Mfananisho, Sawasawa na kitu fulani, Muwakilisho, Msemo, Mithali n.k na baadhi ya

wakati neno hili hua linatumika kumaanisha Hoja!

Tunapoiangalia Qurán basi tunaona kua imetumia neno Mathala katika hali mbali mbali

mara 114 katika kutoa mafunzo yake ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala ameamua

kutumia pia njia za mithali au mifano ili sisi walengwa wenye kupewa ujumbe huo tupate

kutafakkar, kuzingatia na kufahamu kwa kina zaid mafunzo yanayotakiwa kupatikana

kutoka ndani ya kile kinachoelezewa juu yake kama anavyotueleza Allah Subhanah wa

Taála pale aliposema:

‏﴿وَلَقَدْ‏ صَر َّفْنَا فىِ‏ هَٰذَا ٱلْقُرْآنِ‏ لِلن َّاسِ‏ مِن ِ كُل مَثَلٍ‏ وَكَانَ‏ ٱلإِنْسَانُ‏ أَكْثَرَ‏ شَيْ‏ ءٍ‏

ّ

جَدَلاً۞‏

وَمَا مَنَعَ‏ ٱلن َّاسَ‏ أَن يُؤْمِنُو ۤ اْ‏ إِذْ‏ جَآءَهُمُ‏ ٱلهُْدَىٰ‏ وَيَسْتَغْفِرُواْ‏ رَب َّهُمْ‏ إِلا َّ أَن

أتَْتِيَهُمْ‏ سُن َّةُ‏ ٱلأَو َّلِينَ‏ أَوْ‏ ‏َْتِيَهُمُ‏ ٱلْعَذَابُ‏ قُبُلاً‏ ﴾

Walaqad sarrafna fee hadha alqur-ani lilnnasi min kulli mathalin wakana al-insanu

akthara shay-in jadalan; Wama manaAAa alnnasa an yu/minoo idh jaahumu

alhuda wayastaghfiroo rabbahum illa an ta/tiyahum sunnatu al-awwaleena aw

ya/tiyahumu alAAadhabu qubulan (Surat Al Kahf 18:54-55)

Tafsir: Na kwa hakika tumeelezea ndani ya hii Qur’an kila aina ya mithali kwa ajili

ya Watu. Lakini mtu hua ni mwenye kupenda kuliko (kiumbe) yeyote kujadili. Na

hakuna kinachowazuia watu kutokana na kutoamini wakati uongofu umewafikia na

kuomba msamaha kwa Mola wao. Isipokua ni kua na hali ya kufuata njia za watu

waliotangulia au wapewe adhabu itakayokabiliana nao uso kwa uso.

Bila ya shaka Ibn Adam ni kiumbe mwenye kupenda kujadili juu ya kila kitu kuliko

kiumbe mwengine yeyote yule wa Allah Subhanah wa Ta’ala, na hivyo hua si wenye

urahisi wa kujifunza kutokana na wanayoambiwa na mifano wanayoelezewa, na hivyo

hua ni wenye kuishi kwa kufuata mazoea ya wazee wao na waliowatangulia kabla yao,

kiasi ya kua kwa wengi wao inakua vigumu kwao kufumbuka macho kutokana na mazoea

hayo mpaka uwafikie ujumbe wenye kuonya na baadhi ya wakati hadi watu iwashukie


36

adhabu ya Mola wao juu yao. Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kutumithilishia

mifano kwa kutuambia kua:

‏﴿وَلَقَدْ‏ ضَرَبْنَا لِلن َّاسِ‏ فىِ‏ هَٰذَا ٱلْقُرْآنِ‏ مِن ِ كُل مَ‏ ثَلٍ‏ ل َّعَل َّهُمْ‏ يَتَذَك َّ رُونَ۞‏ قُرْآً‏ عَرَبِيّاً‏

غَيْرَ‏ ذِى عِوَجٍ‏ ل َّعَل َّهُمْ‏ يَت َّقُونَ‏ ﴾

ّ

Walaqad dharabna lilnnasi fee hadha alqur-ani min kulli mathalin laAAallahum

yatadhakkaroona; Qur-anan AAarabiyyan ghayra dhii AAiwajin laAAallahum

yattaqoona (Surat Az Zumar 39:27-28)

Tafsir: Na kwa hakika tumepiga kwa ajili ya watu ndani ya hii Qurán mithali za kila

aina ili (Watu) wawe ni wenye Kukumbuka. Qurán ya Kiarabu ambayo haina ubaya

wowote ndani yake ili wapate kua ni wacha Mungu.

Ingawa aya ya Surat Al Kahf 18:54 imetumia neno Sarafna ambalo hua ni lenye

kumaanisha Kuweka, kuelezea lakini ayah inayofuatia baada ya hio ambayo ni ya Surat

Zumar 39:27 na aya nyenginezo nyingi ambazo zimetumika katika njia ya kufunza kwa

kutoa Mithali hua zimetumia neno Dharaba ambalo kwa lugha ya Kiswahili hua

linamaanisha Dharuba. Hivyo Allah Subhana wa Taála ametumia neno Dharaba kwa

sababu kwa lugha ya Kiarabu neno Dharaba hua linamaanisha Kupiga kitu kwa nguvu

hadi kikatoa sauti, Kuponesha, Kutaja, Kufananisha, Kutafuta njia, Kufunga safari,

Kupigania kitu kwa ajili ya kupata faida au manufaa.

Hivyo aya zimetumia neno Dharaba kwa sababu zinatutaka tupiganie manufaa yaliyomo

ndani ya mithali hizo kama tukiwa hatujalala kiakili, na kama tumelala kiakili basi aya

zinatutaka tuzindukane kama vile watu waliopigwa dharuba yaani kibao usoni na hivyo

kua ni wenye umakini wa kuzingatia mithali tunazopigiwa na Mola wetu alietuumba

ambae ndie anaetujua maumbile yetu ndani nje.

Ndio maana ikawa mbali ya kua Qurán ni kitabu kilichaojaa Baraka lakini pia ni kitabu

ambacho tumeshushiwa Waislam kupitia kwa Rasul Allahi Salallahu A’layhi wa Salam

ili kitupe muongozo kwa ajili ya kumkumbuka Mola wetu na hivyo kutuwezesha kufuzu

katika maisha yetu ya hapa Duniani na ya kesho Akhera, hivyo hali hii ya kuletewa

muongozo kutoka kwa Muumba kwa ajili yetu ili tuufuate na kua na Ucha Mungu ni

fadhila kubwa sana kwa kila mmoja miongoni mwetu ambae atauamini na kuufuata

muongozo huo, kwani Allah Subhanah wa Taála alieuleta muongozo huo na kumpa kila

amtakae anatuambia katika Qurán kwa kusema:


37

‏﴿ذٰ‏ لِكَ‏ فَضْلُ‏ ٱهلل َِّ‏ يُؤْتِيهِ‏ مَن يَشَآءُ‏ وَٱهلل َُّ‏ ذُو ٱلْفَضْ‏ لِ‏ ٱلْعَظِيمِ‏ ﴾

Dhalika fadhlu Allahi yu/teehi man yashao waAllahu dhoo alfadhli alAAadheemi

(Surat Al Jumuah 61:4)

Tafsir: Hio ni Fadhila ya Allah ambayo humpa amtakae, ama kwa hakika Allah ni

mwenye fadhila kubwa sana.

Hivyo tusipotafakkar na kutoizingatia Qurán basi hatutonufaika na fadhila hizo zilizo

bora na tutakua kama watu waliotangulia kabla yetu waliotajwa katika aya inayofuata

baada ya hio ambayo nayo inasema kwa kumithilisha kua:

ُ

‏﴿مَثَلُ‏ ٱل َّذِينَ‏ حمُِّلُواْ‏ ٱلت َّوْرَاةَ‏ ثمُ َّ لمَْ‏ يحَْمِلُوهَا كَمَثَلِ‏ ٱلحِْمَارِ‏ يحَْمِلُ‏ أَسْفَاراً‏ بِئْسَ‏ مَثَل

ٱلْقَوْمِ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَذ َّبُواْ‏ آبَِتِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَٱهلل َُّ‏ لاَ‏ يَهْدِى ٱلْقَوْمَ‏ ٱلظ َّالِمِينَ‏ ﴾

Mathalu alladheena hummiloo alttawrata thumma lam yahmilooha kamathali

alhimari yahmilu asfaran bi/sa mathalu alqawmi alladheena kadhdhaboo bi-ayati

Allahi waAllahu la yahdee alqawma aldhdhalimeena (Surat Al Jumuah 62:5)

Tafsir: Mithili ya wale ambao wale waliopewa (Majukumu ya) Tawrat, lakini hapo

hapo wakashindwa kuyabeba (Majukumu hayo kwa kutekeleza amri zilizomo ndani

yake) hua ni kama mithili ya Punda aliebeba shehena za vitabu, Ni m-baya sana mfano

wa wale ambao wamekadhibisha aya za Allah na kwa hakika Allah hawaongozi watu

madhalimu.

Naam, hapa tunaona kua aya imetumia maneno Kamathali alhimari yahmilu asfaran –

Kama mithili ya Punda aliebeba Asfara, ambapo neno Asfara ni neno linalotokana na

neno Sifr la Kiarabu ambalo limetokana na neno Safara ambalo mbali ya kua hua

linamaanisha Safari lakini pa hua linamaanisha Kufagia, Kutawanyika, Kutembea,

Kufunua, Kupambazuka, Kuweka wazi kwa Maandishi yaani kwenye Kitabu na hivyo

neno Asfara lililotumika hapa hua linamaanisha Vitabu vikubwa vyenye kufunua macho

na ufahamu wa mtu kutokana na yaliyomo ndani yake kama ikiwa mtu huyo atavisoma,

atazingatia na kutafakkari yaliyomo ndani yake.

Na Alhamd Lillah sisi Waislam tumejaaliwa kua ni miongoni mwa waliochaguliwa

kupata fadhila bora kutoka kwa Allah Subhanah wa Taála hivyo tusipotafakkar na

kuzingatia Qurán basi hatutokua sawa na Punda tu aliebeba mzigo wa vitabu vyenye


38

thamani kubwa lakini asiejua thamani iliyomo ndani ya uzuito wa mzigo wake, bali

tutakua pia ni sawa na wale watu ambao wanaelezewa katika aya ya mithali ifuatayo:

‏﴿أُوْ‏ لَٰئِكَ‏ ٱل َّذِينَ‏ ٱشْتَرُواْ‏ ٱلض َّلاَلَةَ‏ بِٱلهُْدَىٰ‏ فَمَا رَبحَِتْ‏ تجَِّارَتُهُمْ‏ وَمَا كَانُواْ‏

مُهْتَدِينَ۞مَثَلُهُمْ‏ كَمَثَلِ‏ ٱل َّذِى ٱسْتَوْقَدَ‏ ‏َراً‏ فَلَم َّآ أَضَاءَتْ‏ مَا حَوْلَهُ‏ ذَهَبَ‏ ٱهلل َُّ‏

بِنُورِهِمْ‏ وَتَرَكَهُمْ‏ فىِ‏ ظُلُمَاتٍ‏ لا َّ يُبْصِرُونَ‏ ﴾

Ola-ika alladheena ishtarawoo aldhdhalalata bialhuda fama rabihat tijaratuhum

wama kanoo muhtadeena, Mathaluhum kamathali alladhee istawqada naran

falamma adhaat ma hawlahu dhahaba Allahu binoorihim watarakahum

fee dhulumatin la yubsiroona (Surat Al Baqara 2:16-17)

Tafsir: Hawa ni wale watu ambao, wameununua upotovu kwa bei ya uongovu, hivyo

biashara yao imekua haina faida, na hawakuongozwa. Mithili yao watu hao ni mithili

ya wale ambao wamewasha moto, kisha ukawamurikia katika maeneo yao, na kisha

Allah akauchuchukua mwangaza wao nao wakawa ni waliobakia katika kiza.

Yaani mithili yetu itakua sawa na watu ambao wamewekewa wazi uongofu lakini badala

ya kuutafakkar na kuufanyia kazi basi wao wakaachana nao hivyo kuendelea kupotoka

kwa kutokua na Shukrani, Yaqini na Ikhlas katika mambo yao, na hivyo kua ingawa

wamepata Nuru ya muangaza baada ya kua gizani, lakini kwa kutoujali muangaza huo

basi muangaza huo ukazimika na kutoweka kwani kila mtu unapokua na Shukran, Yaqini

na Ikhlasi kwa Mola wako basi ndivyo Nuru ya muangaza inavyozidi kuongezeka katika

Moyo wako, na unapokua na shaka na wasi wasi basi ndivyo inavyozidi kufifia nuru ya

muangaza huo na hivyo hutoweza kuongoka na hutoweza kua huru kutokana na

Matamanio ya Nafsi yako na upotovu wa Iblis.

Qurán inayaweka wazi haya pale Allah Subhnah wa Taála alipotoa mithali husika katika

aya ifuatayo:

‏﴿ضَرَبَ‏ ٱهلل َُّ‏ مَثَلاً‏ عَبْداً‏ مم َّْلُوكاً‏ لا َّ يَقْدِرُ‏ عَلَى ٰ شَيْءٍ‏ وَمَن ر َّزَقْنَاهُ‏ مِن َّا رِزْقاً‏ حَسَناً‏

فَهُوَ‏ يُنْفِقُ‏ مِنْهُ‏ سِ‏ رّاً‏ وَجَهْراً‏ هَلْ‏ يَسْتَوُونَ‏ ٱلحَْمْ‏ دُ‏ هللِ َِّ‏ بَلْ‏ أَكْثَرُهُ‏ ‏ْم

لاَ‏

يَعْلَمُونَ۞وَضَرَبَ‏ ٱهلل َُّ‏ مَثَلاً‏ ر َّجُلَينِْ‏ أَحَدُهمَُآ أَبْكَمُ‏ لاَ‏ يَقْدِرُ‏ عَلَى ٰ شَيْءٍ‏ وَهُوَ‏ ‏َكل ٌّ


39

عَلَى ٰ مَوْلاهُ‏ أَيْنَمَا يُوَجّ‏ ِ هه ُّ لاَ‏ ‏َْتِ‏ بخَِيرٍْ‏ هَلْ‏ يَسْتَوِى هُوَ‏ وَمَن ‏َْمُرُ‏ بِٱلْعَ‏ دْ‏ لِ‏ وَهُوَ‏

عَلَى ٰ صِرَاطٍ‏ م ُّسْتَقِيمٍ‏ ﴾

Dharaba Allahu mathalan AAabdan mamlookan la yaqdiru AAala shay-in waman

razaqnahu minna rizqan hasanan fahuwa yunfiqu minhu sirran wajahran hal

yastawoona alhamdu lillahi bal aktharuhum la yaAAlamoona, Wadharaba Allahu

mathalan rajulayni ahaduhuma abkamu la yaqdiru AAala shay-in wahuwa kallun

AAala mawlahu aynama yuwajjihhu la ya/ti bikhayrin hal yastawee huwa waman

ya/muru bialAAadli wahuwa AAala siratin mustaqeemin (Surat An Nahl 16:75-76)

Tafsir: Anakupigieni Allah mfano wa Mja ambae anamilikiwa na (Mja) mwenzake, na

hivyo akawa hana uwezo wowote, na Mtu mwengine ambae tumemjaalia riski nyingi

kutoka kwetu na hivyo akawa anatumia kwa siri na kwa uwazi, jee watakua sawa watu

hawa? Shukrani zote anastahiki Allah, lakini wengi wao hawajui. Na Allah anatoa

mfano wa watu wawili, ambapo mmoja wao ni bubu ambae hana uwezo wowote, na

hivyo kua ni mzigo kwa bwana wake, kwa kila upande amuelekezao hua hana faida

yeyote juu yake. Jee huyu hua ni sawa na yule anaeamrisha mema wakati mwenyewe

akiwa katika njia iliyonyooka.

Hayo ni maneno ya Muumba wa kila kitu na ndie pia alietuumba sisi na ndie anaetumiliki

na hivyo anatupa mithali zilizowazi kua bila ya shaka kitu ambacho kinamilikiwa na

hakina mamlaka yeyote basi hakiwezi pia kua na maamuzi yeyote isipokua kutekeleza

maamrisho ya Mmiliki na hivyo kuthibitisha kua Mwenye Mamlaka ya kila kitu

ulimwenguni ni Allah Subhanah wa Ta’ala na yeye pekee ndie anaestahiki Kuabudiwa

na Kushukuriwa kwani yeye ndie Muumba. Na juu ya hili basi kila mtu mwenye akili na

kutafakari hua ni mwenye kujua kua kuna tofauti baina ya Muumba na Kiumbe, pia baina

ya Mwenye uwezo na Asiekua na uwezo, Mwenye Nguvu na asiekua na nguvu, hivyo ni

ujinga ulio wazi pale inapokua Mtu hawezi kuona tofauti baina ya vitu viwili hivyo.

Kwa kua Allah Subhanah wa Ta’ala yeye ndie Muumba na Mmiliki wa kila kitu

Ulimwenguni iwe kikubwa au kidogo basi anawawekea wazi waja wake, kua yeye haoni

shida kututolea mifano hata kama ya mdudu Mbu, na zaid ya Mbu kiukubwa na pia zaidi

ya mbu kiudogo pia, pale aliposema katika Qurán:


40

‏﴿إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لاَ‏ يَسْتَحْىِ‏ أَن يَضْرِبَ‏ مَثَلاً‏ م َّا بَعُوضَةً‏ فَمَا فَوْقَهَا فَأَم َّا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏

فَيَعْلَمُونَ‏ أَن َّهُ‏ ٱلحَْق ُّ مِن ر َّهبِِّمْ‏ وَأَم َّا ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ فَيَقُولُونَ‏ مَاذَآ أَرَادَ‏ ٱهلل َُّ‏ هبَِ‏ ٰذَا مَثَلاً‏

يُضِ‏ ل ُّ بِهِ‏ كَثِيراً‏ وَيَهْ‏ دِى بِهِ‏ كَثِيراً‏ وَمَا يُضِل ُّ بِهِ‏ إِلا َّ ٱلْفَاسِ‏ قِينَ‏ ﴾

Inna Allaha la yastahyee an yadhriba mathalan ma baAAoodhatan fama fawqaha

faamma alladheena amanoo fayaAAlamoona annahu alhaqqu min rabbihim

waamma alladheena kafaroo fayaqooloona madha arada Allahu bihadha mathalan

yudhillu bihi katheeran wayahdee bihi katheeran wama yudhillu bihi illa

alfasiqeena (Surat Al Baqara 2:26)

Tafsir: Hakika Allah haoni haya kukupigieni mifano hata ya Mdudu Mbu au juu yake

zaidi wakati unapokua uko juu (mfano wa ukubwa wa huyo mbu). Ama wale wenye

kuamini, basi wanajua kua ni ukweli kutoka kwa Mola wao, ama kwa wale wasioamini

basi husema: ‘Ah Allah amekusudia nini juu ya mfano huu.’ Kutokana na mfano huo

basi huwapotosha wengi na kuwaongoza wengi. Na huwapotosha wale tu ambao ni

wenye kumuasi.

Naam, anasema Sultan al Mutakallimin Mujaddid ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi

kua: Allah Subhanah wa Taála haoni haya kutoa mfano wa kile alichokiumba, lakini

hapo hapo hua ni mwenye kuona haya juu ya kutojibu dua ya maombi ya mja wake

aliemuomba kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Allah

Subhanah wa Taála ni Hai na ni Mkarimu, kiasi ya kua anaona Haya kua mja wake

amenyanyua juu mikono yake kwa ajili ya kumuomba dua kisha yeye asimjibu dua

hio.

Katika kufafanua sehemu ya pili ya aya hii basi Sultan Al Balagha Imam Abu Al Qasim

Al Zamakhshari kua: Upotoshwaji hapa umenasibishwa na Allah Subhanah wa Taála

kwa sababu yeye ndie mwenye kutoa Mithali ambazo ndani yake hua kuna

muongozo kwa watu. Hivyo kwa wale watakaoufuata basi watakua ni wenye

kuongoka kutokana nao na wale watakaoukataa basi watapotoka. Anasema Malik

Ibn Dinar kua Siku moja alimtembelea mfungwa ambae alikua amefungwa

kutokana na kua na madeni mengi, na hivyo mtu huyo akamwambia Malik Ibn

Dinar kua: Hebu angalia namna tulivyofungiwa na kudhulumiwa haki zetu. Hivyo

Malik Ibn Dinar, akaangalia juu, na kuona kua kuna mkoba unaning’inia.


41

Hivyo nae akauliza: Jee ule ni mkoba wa nani? Ambapo yule mfungwa akajibu kwa

kusema: Ni wangu mie. Hapo Malik Ibn Dinar akaushusha mkoba ule chini ili

kuangalia mna nini ndani yake, na akaona kua mna Kuku na Halua, Hapo Malik

Ibn Dinar akasema: Ama hiki ndio kilichokufungisha. Yaani kuendekeza

matamanio ya Dunia na ya Nafsi.

Kwa upande mwengine basi, tunaona kua ayah hii ya mithali ya mdudu Mbu imetumia

neno BaAAoodhatan ambalo maana yake hua ni Mbu lakini mwishoni mwa jina hilo

kuna harfu Ta ambayo ni yenye kuonesha kua Mbu huyu si mbu yeyote yule, bali

ni Mbu jike kwani aya pia imetumia neno fawqaha yaani juu zaidi yake mbu jike.

Tunaweza kujiiuliza kwa nini labda Allah Subhanah wa Taála akatumia mfano wa

Mdudu mdogo huyu huku akibainisha kua haoni haya kummithilisha, kwa mtizamo wa

ghafla basi tunaweza kusema kua labda kutokana na uwezo wake Mbu jike wa kumdhuru

Ibn Adam na baadhi ya wakati kuweza kumsababishia hata kifo, kwani Mbu jike ndie

anaenyonya damu na kuitumia kwa ajili ya Mayai yao.

Lakini huo ni mtizamo wa juu juu tu, kwani mdudu Mbu ingawa ni mdogo kiumbo lakini

ana Miujiza mikubwa zaid inayostaajabisha. Kwani miongoni mwa sifa zao ni pamoja

na:

1-Kuna aina 2700 za Mbu.

2-Uzito wa Mbu hua ni baina 2-2.5 Milligram.

3-Mbu Jike katika uhai wake anaweza akanyonya lita milioni za Damu.

4- Mbu Dume huishi kwa muda wa siku 10-20 lakini Mbu Jike huishi kwa mda wa

siku 10-100.

5-Katika siku za kungára Mwezi basi Mbu huongezeka kwa mara 500 zaidi.

6-Mbawa za Mbu hua ni zenye kupiga mara 500 kwa kila sekunde moja.

7-Mbu ndio wadudu wanaoongoza kwa kuusababisha vifo Ulimwenguni.

8-Mbu hua wanapendelea damu ya watoto zaidi kuliko ya Watu wazima.

9-Mbu wanachukia mafuta ya ndimu kwa sababu hua yanawaumiza miguu yao.

10-Mbu anaweza akamfuatilia Mtu anaemtaka kumnyonya damu yake kwa umbali

wa futi 18.

11-Mbu wana Nyoyo tatu ambazo hufanya kazi sambamba.

12- Mbu wana Macho zaidi ya 100 kwenye kichwa chao.

13-Mbu wana Meno 48 katika midomo yao.

14-Mbu wana mbawa 3.

15-Mbu wana Sindano 6 katika pua zao, na kila Sindano ina kazi yake maalum.

16-Mbu wanaona kwa kutumia mionzi ya X-Ray na hivyo huweza kuona na

kuitaofautisha ngozi ya Ibn Adam na vitu venyine katika kiza.

17-Mbu wanauwezo wa kupima aina ya Damu wanayoihitaji kwa sababu hua

wanapenda zaidi damu ya Group O, na hua hawapendi damu ya Group A.

18-Mbu wanaweza kusikia harufu ya Ibn Adam kutoka umbali wa futi 100.


42

19-Mbu huwa wananyonya damu za viumbe wengine lakini hupendelea zaidi damu

ya Ibn Adam kwa sababu hua ni rahisi kuwanyonya, na hua wanaweza kugundua

harufu ya hewa ya Carbon Dioxide tunayoitoa mwilini ambayo hua imechanganyika

na Lacti Acid, Octenol, Uric Acid na Fatty Acid na hivyo hua wanajua kua kuna Ibn

Adam katika maeneo ya karibu.

20-Mbu hua wana chanjo ya ganzi ya kuondoa maumivu ambayo humpiga mtu

wanaetaka kumyonya damu mara tu wanapotua juu ya ngozi ya mtu ili mtu huyo

asihisi maumivu ya kutobolewa na kuingizwa sindano ya mbu na kisha kunyonywa

damu huyo.

21-Mbu hua wana pampu ambayo huwaongezea kasi ya kunyonya damu nyingi

zaidi pale wanapoifungua na kuanza kunyonya damu wanayoitaka.

Hio ni baadhi tu ya Miujiza mikubwa ya Mithali ya Mdudu Mbu, na bila ya shaka Qurán

haikutumia Mithali ya mdudu Mbu tu bali pia imetumia mithali ya Mdudu Nzi pale

iliposema katika aya ifuatayo:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱلن َّاسُ‏ ضُرِبَ‏ مَثَلٌ‏ فَٱسْتَمِعُواْ‏ لَهُ‏ إِن َّ ٱل َّذِينَ‏ تَدْعُونَ‏ مِن دُونِ‏ ٱهلل َِّ‏ لَن يخَْ‏ لُقُواْ‏

ذُابَابً‏ وَلَوِ‏ ٱجْتَمَعُواْ‏ لَهُ‏ وَإِن يَسْلُبْهُمُ‏ ٱلذ ُّابَ‏ بُ‏ شَيْئاً‏ لا َّ يَسْتَنقِذُوهُ‏ مِنْهُ‏ ضَعُفَ‏

ٱلط َّالِبُ‏ وَٱلْمَطْلُوبُ‏ ﴾

Ya ayyuha alnnasu dhuriba mathalun faistamiAAoo lahu inna alladheena

tadAAoona min dooni Allahi lan yakhluqoo dhubaban walawi ijtamaAAoo lahu wain

yaslubuhumu aldhdhubabu shay-an la yastanqidhoohu minhu dhaAAufa

alttalibu waalmatloobu (Surat al Hajj 22:73)

Tafsir: Enyi watu! Mnapigiwa mfano, hivyo usikilizeni kwa makini: Wale ambao

mnawaomba badala ya Allah, hawawezi kuumba hata Mdudu Nzi, hata kama

wakijikusanya pamoja kwa lengo hilo, na kama huyo Nzi akipokonya kitu kutoka

kwao, basi kamwe hawatokua na uwezo wa kumnyang’anya, wako dhaifu sana

waombaji na wanaoomba.

Hii ni mithali ambayo ndani yake Allah Subhanah wa Ta’ala anawapigia wale watu

wasiomuamini, mfano wa mdudu Nzi, mdudu ambae ni mdogo, asie na thamani,

asiependezesha sehemu anayotua kwa sababu hua ni sehemu yenye uchafu, na hata kama

haina uchafu basi Nzi akitua katika sehemu basi huwacha uchafu pale anapoondoka

katika sehemu husika, na pia huchukua kitu katika sehemu husika kiasi ya kua hakuna

Ibn Adam anaeweza kuona kwa macho yake kile alichokiwacha mdudu huyo wala


43

alichochukua mdudu huyo na hivyo hua haiwezekani kumpokonya alichochukua, kwa

sababu Nzi anapotaka kuchukua kitu fulani basi hutoa maji yenye kemikali ambayo

hukilainisha kitu hicho na kisha yeye hunyonya kilichomo ndani ya kitu husika na

kuondoka nacho kile cha ndani tu na hivyo hubakisha bua tupu yaani kile

kinachoonekana kwa mizamo wa nje na hivyo hua haonekani ni nini alichokichukua,

hivyo hua hakuna na uwezekano wa kupokonyeka kile alichokichukua.

Hapa haina haja ya kuzungumzia wingi wa wadudu Nzi, kwani kiaina tu basi kuna aina

90,000 za mdudu Nzi, ambao hua wanazaana kila baada ya wiki 2 huku kila Nzi jike hua

ni mwenye kutaga mayai 100. Na pia haina haja kuainisha juu ya maumbile ya Mbawa

zake mdudu Nzi ambapo kimaumbile hua zina hali ya upekee, ya kua na uwezo wa

kudhuru na uwezo wa kutibu.

Ambapo anasema Mujaddid ud Din Imam Shah Waliyu Allah Al Dahlawi katika Hujjat

Allah Al Baligha kua: Allah Subhanah wa Ta’ala anaweka wazi Hikma na Busara

zake katika kumuumba kwake Mdudu Nzi kua kila mdudu mwenye sumu basi hua

ni mwenye kujaaliwa kua na dawa ya kuondoa sumu hio kwa ajili ya kuulinda na

kuendeleza uhai wa mdudu huyo.

Ama kwa upande wa Shaykh al Akbar Imam Muhyi ad Din Abu Bakr Ibn Al Arabi basi

yeye anasema kua: Nzi mara zote hua ni mwenye kuliweka juu bawa lake lenye dawa

ili lisiguse kile kitu chenye umaji maji alichotulia juu yake, ili aweze kutumia Ubawa

huo kwa ajili ya kurukia anapotaka kuondoka kwa haraka katika sehemu hio, na

hii pia ni miongoni mwa Maumbile aliyojaaliwa kua nayo kutoka kwa Muumba,

ambapo sifa hii pia wanayo Sisimizi, Nyuki na Ndege wa aina ya Hud Hud. (Imam

al-Tahawi, Sharh Mushkil (8:343-344) Imam al-Khattabi, Ma`alim al-Sunan (4:459))

Ama hizi mithali za mdudu Nzi, Mbu na mithali nyenginezo zinathibitisha kua Allah

Subhanah wa Taála ndie Nuru ya kila kitu ulimwenguni yaani ni mwenye kuweka wazi

kile ambacho kilichokua hakijulikani na viumbe wake kama anavyosema yeye

mwenyeye katika aya ifuatayo:

‏﴿ٱهلل َُّ‏ نُورُ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ مَثَلُ‏ نُورِهِ‏ كَمِشْكَ‏ واةٍ‏ فِيهَا مِصْبَاحٌ‏ ٱلْ‏ مِ‏ صْبَاحُ‏ فىِ‏

زُجَاجَةٍ‏ ٱلز ُّجَاجَةُ‏ كَأَن َّهَا كَوْكَبٌ‏ دُرِّي ٌّ يُوقَدُ‏ مِن شَجَرَةٍ‏ م ُّبَارَكَةٍ‏ زَيْتُونَةٍ‏ لا َّ شَرْقِي َّةٍ‏ وَلاَ‏

غَرْبِي َّةٍ‏ يَكَادُ‏ زَيْتُهَا يُضِي ۤ ءُ‏ وَلَوْ‏ لمَْ‏ تمَْسَسْهُ‏ ‏َرٌ‏ ن ُّورٌ‏ عَلَى ٰ نُورٍ‏ يَهْدِى ٱهلل َُّ‏ لِنُورِهِمَن

ّ بِكُل شَيْءٍ‏ عَلَيِمٌ‏ ﴾

يَشَ‏ آءُ‏ وَيَضْرِبُ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱلأَمْثَالَ‏ لِلن َّاسِ‏ وَٱهلل َُّ‏ ِ


44

Allahu nooru alssamawati waal-Ardhi mathalu noorihi kamishkatin feeha

misbahun almisbahu fee zujajatin alzzujajatu kaannaha kawkabun durriyyun

yooqadu min shajaratin mubarakatin zaytoonatin la sharqiyyatin wala

gharbiyyatin yakadu zaytuha yudee-o walaw lam tamsas-hu narun noorun AAala

noorin yahdee Allahu linoorihi man yashao wayadribu Allahu al-amthala lilnnasi

waAllahu bikulli shay-in AAaleemun.(Surat Al-Noor 24:35).

Tafsir: Allah ni Nuru ya Mbingu na Ardhi, mithli ya Nuru yake ni kama Mishkat

(Mishkat ni sehemu kama kidirisha ambacho hujengwa maalum kwa ajili ya kuwekea

taa ukutani na hivyo kufanya muangaza wa taa hiyo uwe mkubwa zaid pale taa

inapokua ndani ya kidirisha hicho kuliko taa hiyo ikikaa katika sehemu iliyo wazi), na

ndani yake mna taa, na taa hiyo imo ndani ya kioo. Kioo ambacho kinang’ara kama

nyota ya Durriyun (aina ya nyota yenye kung’ara sana kama Lulu), (taa) ambayo

imewashwa kutokana na mti mtakatifu wa Mzaituni usio wa Mashariki wala

Magharibi, ambao mafuta yake hutoa mwangaza bila ya kuguswa (kuwashwa) na

moto wowote. Nuru juu ya Nuru! Allah humuongoza katika mwangaza wake yeyote

yule amtakae. Na Allah anaweka wazi mifano kwa Bani Adam, Na hakika Allah ni

mwenye kujua kila kitu.

Hapa tunaona kua aya hii imetumia kiunganishi ‘ka’ kinachotafsirika kwa lugha ya

Kiswahili kama ‘kama’ ambacho hujulikana kama Kaf at tashbih ambayo inayoleta

maana ya kushabihisha kitu kimoja kua kinafanana tu na kitu chengine lakini hata hivyo,

kitu hicho si kitu chenyewe kilichokusudiwa. Kutumika kwa Kaf at Tashbih katika aya

hii kunaonesha kutokuwepo uwezekano wa kuelezea sifa za Majina ya Allah Subhanah

wa Ta’ala hata kupitia kwa njia za kufananisha kwani yeye mwenyewe anasema kua:

‏﴿لَيْسَ‏ كَ‏ مِ‏ ثْلِهِ‏ شَ‏ ىْ‏ ءٌ﴾‏

Laysa kamithlihi shay-un (Surat Ash Shuraa 42:11)

Tafsir: Hakuna kitu chenye mithli yake.

Na vile vile akasema:

‏﴿وَلمَْ‏ يَكُ‏ نْ‏ ل َّهُ‏ كُ‏ فُواً‏ أَحَ‏ دٌ‏ ﴾

Walam yakun lahu kufuwan ahadun (Surat Al Ikhlas 112:4)

Tafsir: Hakuna anaefanana nae.


45

Hivyo ufananisho huu wa Sifa ya ‘Nuru ya Allah’ hauwezi kuonesha ukweli halisi

ulivyo, bali ufafanisho huu umetumika ili kufafanua kimaana kutokana na ufahamu wa

walengwa waliokusudiwa, kwa sababu ukweli halisi wa ‘Nur ya Allah’ ni ukweli ambao

hauwezi kufikirika kwa hali yeyote ya kiumbe yeyote yule na wala hauwezi kuelezeka

kwa lugha ya kiumbe chochote.

Hujjat ul Islami Mujaddid ud Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali katika kuielezea maana ya Al Nur anasema kua: Al Nur ni yule

anaeonekana kutokana na kuvifanya vitu vyote vionekane, kwani kila kitu

kinachoonekana chenyewe na kusababisha vitu vyengine vionekane hua kinaitwa

Nuru. Tukiangalia kwa mtazamo wa kua kila kilichokuwepo hupingana na

kisichokuwepo, basi kile kinachoonekana hakiwezi kulinganishwa na kitu chengine

isipokua tu na kile kilichokuwepo. Kwani hakuna kiza kilichokua cheusi zaidi

kuliko kile kiza cha kitu kisichokuwepo.

Kile kilichokua huru kutokana na giza la kutokuwepo, na kua na uwezekano wa

kutokuwepo, na huondoa kila kitu kutoka katika kiza cha kutokuwepo na

kukiingiza katika udhihirisho wa kuwepo, basi hua kinastahiki kuitwa Nuru.

Kuwepo ni Nuru iliyohuru isiyotegemea kitu inayomurika kila kitu kutokana na

asili ya Nuru yake Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani Allah Subhanah wa Ta’ala ni

Nuru ya Mbingu na Ardhi. Na kama ilivyokua hakuna hata muale mmoja wa

muangaza wa Jua ambo huonesha kua hio ndio chanzo cha muangaza wa Jua hilo,

basi vile vile hakuna hata chembe moja ya kitu kutoka katika vitu vilivyomo ndani

ya Mbingu na Ardhi, ambacho hakimpelekei mtu kukosa uhakika wa kutokana na

uwezekano wa kuwepo kwake bila ya kuhitaji kuwepo kwa yule aliesababisha

kuwepo kwa kitu hicho.

Hivyo kutokana na Nuru, hususan Nuru ya Allah, basi kila kitu hua kiko wazi, chenye

kuonekana, chenye kufahamika na hivyo kua ni chenye uhakika na chenye kua na yakini.

Ama kwa upande mwengine basi anasema Hasan Al Basr kua: ‘Mithali ya Nuru ya

Qurán ni Misbah (Taa). Misbah ambayo Sirajan (Moto au Muangaza) yake ni

Maarifah (Maarifa ya kuokoka Kinafsi) na Fatil (Utambi) yake ni Faraidh (FArdhi

za Dini) ambao Dhuhn (Mafuta) yake ni Ikhlas na Nuru yake (Ya Kiroho) ni ya

Ittisal (Kufikia Darja inayotakiwa kufikiwa). Hivyo kila Ikhlas ikizidi kiusafi basi

mwangaza wa Taa ndio hua unazidi Zaidi. Na kila fArdhi za dini zinapozidi basi

ndio unapopatikana uhakika (Haqiqa) na ndivyo Nuru inavyozidi.’

Allah Subhanah wa Taála anatupigia mifano myengine juu ya wale watu ambao

hawatomuamini yeye na hivyo kua ni wenye kumshirikisha kua ni wasiojua udhaifu

mkubwa sana wa kile wanachokiamini na kuona kua kinawanufaisha kwa kusema:


46

‏﴿مَثَلُ‏ ٱل َّذِينَ‏ ٱتخ ََّذُواْ‏ مِن دُونِ‏ ٱهلل َِّ‏ أَوْلِيَآءَ‏ كَمَثَلِ‏ ٱلْعَنكَبُوتِ‏ ٱتخ ََّذَ‏ تْ‏ بَيْتاً‏ وَإِ‏ َّن

أَوْهَنَ‏ ٱلْبُيُوتِ‏ لَبَيْتُ‏ ٱلْعَنكَبُوتِ‏ لَوْ‏ كَانُواْ‏ يَعْلَمُونَ‏ ﴾

Mathalu alladheena ittahadhoo min dooni Allahi awliyaa kamathali alAAankabooti

ittakhadhat baytan wa-inna awhana albuyooti labaytu alAAankabooti law kanoo

yaAAlamoona (Surat Al Anqabut 29:41)

Tafsir: Mithili ya wale ambao wanaoichukua Miungu myengine zaidi ya Allah, hua ni

mithli ya Buibui ambae hujijengea nyumba. Lakini kwa hakika! Hakuna nyumba

dhaifu kama nyumba ya Buibui, lau kama wao wangejua.

Katika aya hii ya Surat Al Anqabut ambayo ndio aya iliyotoa jina la Sura hii, basi tunaona

kua Allah Subhanah wa Taála anatutolea mfano wa Al Anqabut yaani mdudu Buibui

ambae anaelezewa Nyumba yake anayoijenga na kuishi kwa kutumia uzi laini wa Hariri

ambao anautoa ndani ya mdomo wake tena kwa wingi sana kiasi ya kua anaweza

akajenga nyumba baina ya miti miwili kwa kuurusha uzi huo kwa umbali mita 25 kutoka

upande mmoja hadi mwengine bila ya kuonekana kwa dalili ya kuishiwa kwa uzi wake

huo wa Hariri wala kuanguka chini kwa uzi huo kwani hunyooka kama waya katika

kutembea kwake kutoka upande mmoja kuelekea upande mwengine.

Uzi wa Buibui ni uzi wenye kutokana na Protein ambayo inatokana na madini ya Carbon,

Hydrogen, Oxygen na Nitrogen zinazozalishwa kwa wingi sana na mwili wake, na hadi

hii leo Wanasayansi na utaalamu wao wote bado hawajapata jibu juu ya uwezo wa Buibui

katika kuzalisha kwa wingi uzi huo bila ya kuishiwa na madini hayo hususan

ukilinganisha na ukubwa wa mwili wa mdudu Buibui.

Tunapoiangalia aya hii basi tunaona kua imetumia neno ‘Ittakhadha’ ambalo kwa kiarabu

hua ni lenye kumaanisha: Afanyae Kitu, Mwenye kuchukulia Kitu au Mwenye Kitu.

Lakini sasa neno Ittakhadha lililotumika hapa mwishoni mwake limeishia na harfu

‘ta’ na hivyo limekua katika hali ya Ittahadhat ambayo ni yenye kumaanisha jinsia

ya Kike.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala hapa anatuwekea wazi kua Buibui anaejenga nyumba

hua ni Buibui jike, na hivyo ni Buibui jike ndie anaedumu katika nyumba husika na wala

si Buibui dume. Jambo ambalo limethibitishwa pia na Wanasayansi wa Kijerumani

mnamo mwaka 1984 pale walipochapisha matokeo ya uchunguzi wao huo katika gazeti

la Cosmos Magazine la Ujerumani ambao umethibitisha hivyo. Hii ni kuthibitisha

miongoni mwa Miujiza mingi ya Qurán.


47

Ni maumbile ya Mdudu Buibui kua na uwezo wa kuzalisha uzi huu wa kujengea nyumba

yake ambapo nyumba hio hua na nyuzi aina tano tofauti, kuna nyuzi pana ambazo ndio

hua msingi wa nyumba na ndio anazotumia yeye katika kuzunguka na kuisimamia

nyumba hio, ingawa uzi huu ambao ndio msingi wa nyumba yake hua ni mpana lakini

upana wake haufiki hata upana wa milimita moja, Buibui pia hua anazalisha Uzi maalum

kwa ajili ya kuhifadhia Mayai yake, Uzi maalum kwa ajili ya kujilinda, na Uzi maalum

kwa ajili ya Kuhifadhia chakula chake na wadudu anaowakamata, na pia huzalisha uzi

mwengine ambao ni mwembemba zaidi kwa ajili ya hujenga ukuta ambao hua pia kama

mtego kwa ajili ya maadui zake na hapo hapo kwa ajili ya wadudu ambao hua ndio

chakula chake, na hivyo Buibui hua ni mwenye kusubiri katikati ya nyumba yake hado

pale nyuzi nyembamba zinapotetemeka na hivyo hujua kua upande fulani kuna mdudu

ameshaganda tayari, hivyo Buibui kwa kutumia nyuzi nene basi huelekea upande

uliotokea mtetemeko huo kwa kutumia nyuzi nene na kutembea hadi katika sehemu

aliyoganda mdudu kwenye mtego wake.

Kwa kimaumbile nyuzi zote hizi za aina mbili ingawa ni laini na nyembamba ambapo

nyuzi zenye uzito wa gramu 320 hua na uwezo wa kuzungushwa dunia nzima kutoka

pande moja hadi nyengine, lakini ni nyuzi ambazo hazina mfano wake katika uimara

wake, kwani nyuzi hizi hua na umadhubuti wa mara 100 zaidi ukilinganishwa na

umadhubuti wa uzi wa chuma cha pua ambacho ni chuma kigumu zaidi, mbali ya kua

Uzi wa Buibui ni madhubuti lakini pia uzi huo hua na uwezo wa kuvutika kwa mara nne

zaidi ya urefu wake wa kimaumbile bila ya kukatika na ukikusanywa pamoja hua na

ugumu mkubwa sana kwa mara 10 zaidi ya materiali ya Kevla ambayo hutumika kwa

ajili ya kutengenezea mavazi ya Bullet Proof yaani yanayovaliwa ili kuzuia risasi isitokee

upande wa pili na hivyo kuzuia zisiingie mwilini mwa Ibn Adam.

Si hivyo tu bali pia uzi huu wa Buibui hua ni wenye kujivuta na kupunguza urefu wake

kwa 50% unaponyeshewa na mvua na pia una uwezo wa kupitisha nguvu za mawasiliano

ya umeme haraka na kwa wingi zaidi kuliko kitu chochote kile kwani hata waya wa shaba

ambao ndio unaotumika kusafirishia umeme majumbani hua haufikii uwezo wa uzi wa

Buibui. Mbali ya kua na sifa zote hizo na nyenginezo lakini hapo hapo Allah Subhanah

wa Ta’ala anasema kua:

‏﴿وَإِن َّ أَوْهَنَ‏ ٱلْبُيُوتِ‏ لَبَيْتُ‏ ٱلْعَنكَبُوتِ‏ لَوْ‏ كَانُواْ‏ يَعْلَمُونَ‏ ﴾

Wa-inna awhana albuyooti labaytu alAAankabooti law kanoo yaAAlamoona (Surat

Al Anqabut 29:41)

Tafsir: Lakini kwa hakika! Hakuna nyumba dhaifu kama nyumba ya Buibui, lau kama

wao wangejua.


48

Kua hii ni nyumba ambayo mbali ya kua ni nyumba iliyojengwa kwa nyuzi zenye

umadhubuti wa hali ya juu kwa mdudu Buibui mwenyewe na wadudu wengine ambao

hua ndio chakula chake, lakini hapo hapo basi tunaona kua hakuna nyumba iliyo dhaifu

ndani na nje kama ilivyo nyumba ya Buibui, kwani mbali ya kua kwa nje inaweza

kuvunjwa na kuteketezwa mara moja na wale wenye uwezo zaidi ya Buibui na haiwezi

kumzuia Buibui huyo na madhara ya mvua wala ya jua kama tunavyojua lakini pia kwa

ndani ya nyumba hio basi hua na mazingira ya kutoishika kwa Buibui dume ambae yeye

kufariki kwake hutokea mara tu baada ya kumnyatia taratibu na kumuingilia Buibui jike

ambapo Buibui jike nae humgeuza Buibui dume huyo kua ni chakula chake huku wakiwa

katika hali ya kuingiliana. Jambo hili humpelekea Buibui jike kupata mayai ya akiba zaidi

kutoka kwa Buibui dume.

Na kwa baadhi ya Buibui basi pia Buibui jike hua ni mwenye kufariki mda mfupi tu mara

baada ya mayai kutoa watoto kwani watoto hao humgeuza mama kua ndio chakula chao

na ndio maana Buibui hutaga mayai takriban 3000 kwa mkupuo mmoja.

Bila ya shaka Allah Subhanah wa Ta’ala anatupigia mithali ili tupate kutafakkar ambako

nako kutatupelekea kufaham maana na makusudio ya mithali hizo kama alivyosema:

‏﴿وَتِلْكَ‏ ٱلأَمْثَالُ‏ نَضْرِبُهَا لِلن َّاسِ‏ وَمَا يَعْقِلُهَآ إِلا َّ ٱلْعَالِمُونَ‏ ﴾

Watilka al-amthalu nadhribuha lilnnasi wama yaAAqiluha illa alAAalimoona

(Surat Al Anqabut 29:43)

Tafsir: Na tunaipiga mifano hii kwa watu, lakini hakuna atakaefahamu isipokua wale

wenye kujua.

Allah Subhana wa Ta’ala anamalizia kuweka wazi juu ya aina mbali mbali za mifano na

mithali kwa ajili ya kuwanufaisha viumbe wake kwa kusema:

‏﴿وَلَقَدْ‏ ضَرَبْنَا لِلن َّاسِ‏ فىِ‏ هَٰذَا ٱلْقُرْآنِ‏ مِن ِ كُل مَثَلٍ‏ وَلَئِن جِ‏ ئْتَهُمْ‏ آبِيَةٍ‏ ل َّيَقُولَ‏ َّن

ٱل َّذِينَ‏ ۤ كَفَرُواْ‏ إِنْ‏ أَنتُمْ‏ إِلا َّ مُبْطِلُونَ‏ ﴾

ّ

Walaqad dharabna lilnnasi fee hadha alqur-ani min kulli mathalin wala-in ji/tahum

bi-ayatin layaqoolanna alladheena kafaroo in antum illa mubtiloona (Surat Ar Rum

30:58)


49

Tafsir: Na bila ya shaka, tumeipiga kwa ajili ya watu ndani ya hii Quran kila mifano,

lakini kama ukiwaletea wao vithibitisho basi wasioamini watasema kua: Hakika nyinyi

hamkua isipokua ni wenye kujishughulisha na mambo ya kipuuzi.

Hivyo bila ya shaka mifano na mithali hizo wamepigiwa Ibn Adam ili watumie akili zao

wapate kujiokoa na adhabu za Mola wao, kwani wasipotafakkar basi watakua ni watu

waliopotoka na wataingia Motoni, na hua si sawa watu Motoni na watu wa Peponi, kwani

watu wa Peponi hua si watu waliopotoka bali hua ni watu waliofuzu. Allah

anatukumbusha haya na kutuwekea wazi, thamani, uzito na umuhimu wa Qurán kwa

kutuambia:

‏﴿لاَ‏ يَسْتَوِي ۤ أَصْحَابُ‏ ٱلن َّارِ‏ وَأَصْحَابُ‏ ٱلجَْن َّةِ‏ أَصْحَابُ‏ ٱلجَْن َّةِ‏ هُمُ‏ ٱلْفَآئِزُونَ۞‏ لَ‏ وْ‏

أَنزَلْنَا هَٰذَا ٱلْقُرْآنَ‏ عَلَى ٰ جَبَلٍ‏ ل َّرَأَيْتَهُ‏ خَاشِ‏ عاً‏ م ُّتَصَدِّعاً‏ مِّنْ‏ خَشْيَةِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَتِلْكَ‏

ٱلأَمْثَالُ‏ نَضْرِبُهَا لِلن َّاسِ‏ لَعَل َّهُمْ‏ يَتَفَك َّرُونَ۞‏ هُوَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِى لاَ‏ إِ‏ لَٰهَ‏ إِلا َّ هُوَ‏ عَالمُِ‏

ٱلْغَيْبِ‏ وَٱلش َّهَادَ‏ ةِ‏ هُوَ‏ ٱلر َّحمَْٰنُ‏ ٱلر َّحِ‏ يمُ‏ هُوَ‏ ٱهلل َُّ‏ ۞ ٱل َّذِى لاَ‏ إِلَٰهَ‏ إِلا َّ هُ‏ وَ‏ ٱلْمَلِكُ‏

ٱلْقُد ُّوسُ‏ ٱلس َّلاَمُ‏ ٱلْمُؤْمِنُ‏ ٱلْمُهَيْمِنُ‏ ٱلْعَزِيزُ‏ ٱلجَْب َّارُ‏ ٱلْمُتَكَبرُِّ‏ سُبْحَانَ‏ ٱهلل َِّ‏ عَم َّا

يُشْرِكُونَ۞‏ هُوَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱلخَْالِقُ‏ ٱلْبَارِ‏ ئُ‏ ٱلْمُ‏ صَوِّرُ‏ لَهُ‏ ٱلأَسمَْآءُ‏ ٱلحُْسْنىَٰ‏ يُسَبِّحُ‏ ا لَهَُم فىِ‏

ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَهُوَ‏ ٱلْعَزِيزُ‏ ٱلحَْكِيمُ‏ ﴾

La yastawee as-habu alnnari waas-habu aljannati as-habu aljannati humu alfaizoona;Law

anzalna hadha alqur-ana AAala jabalin laraaytahu khashiAAan

mutasaddiAAan min khashyati Allahi watilka al-amthalu nadribuha lilnnasi

laAAallahum yatafakkaroona; Huwa Allahu alladhee la ilaha illa huwa AAalimu

alghaybi waalshshahadati huwa alrrahmanu alrraheemu; Huwa Allahu alladhee la

ilaha illa huwa almaliku alquddoosu alssalamu almu/minu almuhayminu

alAAazeezu aljabbaru almutakabbiru subhana Allahi AAamma yushrikoona;

Huwa Allahu alkhaliqu albari-o almusawwiru lahu al-asmao alhusna yusabbihu

lahu ma fee alssamawati waal-Ardhi wahuwa alAAazeezu alhakeemu; (Surat Al

Hashr 59:20-24)


50

Tafsir: Hawako sawa watu wa Motoni na Watu wa Peponi, kwani Watu wa Peponi

watakua ni waliofuzu. Lau kama tungeishusha hii Qurán kwa ajili ya Majabali, basi

kwa hakika ungeona namna Majabali yanavyonyenyekea na kumomonyoka kutokana

na kumuogopa Allah. Na hizi ni Mithali ambazo tunawapigia watu ili watafakkari!

Hakika yeye ni Allah ambae hakuna Mungu isipokua yeye. Mjuzi wa yasiyoonekana

na yanayoonekana. Yeye ni mwingi wa Rehma na Huruma. Yeye ni Allah ambae

hakuna Mungu isipokua yeye, yeye ndie Mfalme, Mtukufu, Asiekua na Kasoro,

Mwenye kuwahakikishia Usalama viumbe wake, Msimamizi wa Amani ya viumbe

wake wote, Muangalizi wa vitendo vya Viumbe wote, Mwenye uwezo Mkubwa sana wa

kulipa kwa kuadhibu kwa adhabu kali kabisa, Mwenye Uwezo Mkubwa wa kusimamia

mambo ya viumbe na kuwaweka chini ya khiari yake kama atakavyo, Mwenye Ukubwa

wa pekee usiokua na Kifani katika kila kitu. Utukufu ni wake yeye Allah ambae hana

mshirika. Yeye ni Allah ambae ndie Muumbaji, Muanzishaji wa kila kitu bila ya

kuhitajika kuwepo kwa kitu chengine katika kuanzisha kwake huko, Mwenye Kuumba

kwa namna na aina ya vitu atakavyo, kwake yeye ndio kwenye Umiliki wa Majina

Yenye Sifa Bora ambae anatukuzwa na kila kilichomo Mbinguni na kilichomo

Ardhini, na ni Mwenye Uwezo wa kila kitu na mwenye Hikma katika kila kitu

akifanyacho.

Baaada ya kutuwekea wazi hayo basi Allah Subhanah wa Taála anatupa mithali nyengine

hapo hapo kutuwekea wazi kua Viumbe walioumbwa na kupewa ukubwa wa mara 1000

zaidi yetu, yaani Milima basi hua inafahamu jukumu lake mbele ya Mola wake kiasi ya

kua kama ingeshushiwa Qurán basi bila ya shaka ingetetemeka na kububujika kutokana

na kua na khofu kwa Mola wake, lakini Ibn Adam asietumia akili yake na kutafakkar juu

ya Qurán basi basi hua ni mjinga mwenye kuipuuza na kutokua na khofu yeyote mbele

ya Mola wake kutokana na ujinga wake na kutojua majukumu yake.

Hivyo, basi Allah Subhanah wa Ta’ala anatoa mithali na visa ndani ya Qurán ili angalau

tupate kujifunza pale tutakapozingatia na kutilia maanani visa, mifano na mithali hizo na

ni kutokana na kutafakkar na kuzingatia kwake basi ndio tunapopata uongofu kwa

kufuata njia sahih tunazoelekezwa ndani yake na kuachana na njia potovu tunazokatazwa

kuzifuata kulingana na mifano hai tunayooneshwa kupitia katika njia zilizomo ndani ya

Kitabu chake Qurán na Sunnah za Nabii wake Muhammad Salallahu Aálayhi wa Salam

ikiwemo Mithali zinazoainisha kanuni za mawasiliano ya kauli kama isemavyo aya

ifuatayo:

‏﴿أَلمَْ‏ تَرَ‏ كَ‏ يْفَ‏ ضَرَبَ‏ ٱهلل َُّ‏ مَثَلاً‏ كَ‏ لِمَ‏ ةًطَيِّبَةًكَشََجر أ ةٍطَيِّبَةٍ‏ َ صْلُهَ‏ ا اثَبِتٌ‏ وَفَرْعُهَا فىِ‏

ٱلس َّمَآءِ‏ ۞ يُثَبِّتُ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ بِٱلْقَوْلِ‏ ٱلث َّابِتِ‏ فىِ‏ ٱلحَْيَاةِ‏ ٱلد ُّنْيَا وَفىِ‏ ٱ لآ خِ‏ رَةِ‏


51

وَيُضِل ُّ ٱهلل َُّ‏ ٱلظ َّالِمِينَ‏ وَيَفْعَلُ‏ ٱهلل َُّ‏ مَا يَشَآءُ۞‏ وَمَثلُ‏ كَ‏ لِ‏ ‏َمةٍ‏ ‏َخبِيثَةٍ‏ كَشَجَرَةٍ‏ خَبِيثٍَة

ٱجْتُث َّتْ‏ مِن فَوْقِ‏ ٱلأَرْضِ‏ مَا لهََا مِن قَرَارٍ‏ ﴾

Alam tara kayfa dharaba Allahu mathalan kalimatan tayyibatan kashajaratin

tayyibatin asluha thabitun wafarAAuha fee alssama/-I, Tu/tee okulaha kulla heenin

bi-idhni rabbiha wayadribu Allahu al-amthala lilnnasi laAAallahum

yatadhakkaroona, Wamathalu kalimatin khabeethatin kashajaratin khabeethatin

ijtuththat min fawqi al-Ardhi ma laha min qararin (Surat Ibrahim 14:24-26)

Tafsir: Jee hujaona namna Allah anavyopiga mifano, kauli nzuri hua ni kama mti

ambao asili yake (mizizi yake) iko thabit (imekomaa ardhini) na umechipua kuelekea

juu angani, huzaa matunda kila msimu kwa idhini ya Mola wake, na Allah anatoa

mifano kwa watu ili wapate kukumbuka. Na mithili ya kauli mbovu hua ni sawa na

mti uliong’oka na kua juu ya Ardhi ukiwa hauna uimara.

Bila ya shaka mfano wa Mti usiokua na mizizi Imara au mti ambao upo juu juu hua ni

mti usiokua na faida yeyote kwani hautoweza kutoa matunda, huu ni mfano mzuri ambao

pia unatuonesha kua amali za mtu asiekua ni mwenye kuamini basi hua hazina faida

kwake isipokua hapa hapa Duniani kwani Akhera hua hana malipo yeyote isipokua

hasara.

Anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alienda kwa Masahaba akawakuta wanazungumzia juu ya Kalimatan

Tayyibatan ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kalimatan

Tayyibatan ni kama Muumini ambae mizizi yake, imezama ardhini na Matawi yake

yako Mbinguni.’ Yaani amali zake hua zinanyanyuliwa Mbinguni na zinakubaliwa

Hivyo hii mithali ambayo Allah Subhanah wa Taála amemithilisha kwa Waumini

na Makafiri.

Na akasema Kalimatan Tayyibatan hua ni kauli za kweli zenye Ikhlasi ndani yake,

hua ni Shajaratin Tayyibatin yaani kama Mtende ambao mizizi yake ni madhubuti

ardhini na majani yake yamefikika Mbiguni. Vile vile ndivyo ilivyo amali za

Muumini ambazo zimepatikana kutokana na kuthibitisha kwa Kalimat at Tawhid

ambayo ni mzizi madhubuti wenye matawi yake Mbinguni yaani amali zake

zimenyanyuliwa juu Mbinguni na ni zenye kukubaliwa, isipokua labda ziwe ni

zenye kasoro (Ihdath) ndani yake.


52

Lakini hata hivyo Mzizi wa amali zake katika kumpwekesha Mola wake

hauondolewi, hivyo hii inakua kama vile ambavyo upepo unapovuma na

kuyumbisha majani ya Mtende tu, huku mizizi yake ikiwa madhubuti ardhini.

Na amezimithilisha kauli za Mtu asieamini na Shajara al Khabitha kwa kusema kua:

‘Wamathalu kalimatin khabeethatin kashajaratin khabeethatin’ kumaanisha mti wa

aina ya Hanzal (Matikiti ya Jangwani yasiyolika) ambao hakuna mti wenye ladha

mbaya sana kama huo, kwani hauna mizizi chini yake. Kama vile ilivyokua Kufr na

Unafiq ambao haustahmiliwi kesho Akhera. Hivyo katika hazina ya Allah

Subhanah wa Taála hakuna hazina nzito kama Kalimat Tawhid!’

AINA ZA KALIMAT (KAULI) NDANI YA QURÁN

Neno Kalimatan ni neno lililotokana na neno Kalama ambalo kwa Lugha ya Kiarabu hua

linamaanisha Kutoa Kauli, Kuzungumza, Kusema, Kuelezea kwa maneno, Kutoa

Mtizamo juu ya jambo Fulani, Kutoa habari au Amri, Ahadi, Kuwasilisha Ujumbe na pia

humaanisha Mtizamo au mawazo ambayo yamo ndani ya Ufahamu lakini bado

haujatamkwa.

Hivyo Qurán inatutolea mithali ya kauli njema kwa kutufunza pia umuhimu wa kanuni

za mawasiliano ya kufikisha ujumbe baina ya Mitume na watu wanaowapelekea ujumbe

katika jamii zao, Viongozi, Watawala, Wenye I’lm na wasiokua na I’lm, wafuasi wao na

wapinzani wao na kadhalika, kwa sababu kanuni za mawasiliano ya kufikisha ujumbe

kwa wahusika ni sehemu ya Iman na Ihsan ya dini ya Kiislam.

Kwani anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Al Islam

(Uislam) ni Hukm, Al Iman ni Wasl (Kuiwasilisha kwa Allah Subhanah wa Taa’la)

na Ihsan ni Thawab (Malipo). Hivyo Uislam ni Iqrar (kuthibitisha) ambako hua ni

kwenye kuonekana, lakini Iman hua haionekani, wakati Ihsan hua ni Taábud

(Ufanyaji Ibada)’

Hivyo ingawa neno Kalimah hua ni lenye kumaanisha pia Qawl (Kauli) lakini pia hapo

hapo hua linatofautiana kimaana pale tunapoona kua neno Kalimah hua linamaanisha pia

Mtizamo ambao umo ndani ya ufahamu wa Ibn Adam lakini haujatamkwa na ulimi, wala

kuoneshwa kwa njia yeyote ya ishara na hivyo hua ni mtizamo ambao haujaingia katika

hali ya Qawl.


53

Neno Qawl hua ni lenye kutokana na neno Qulu ambalo kwa kilugha hua linamaanisha

Kutoa kauli, Kusema, Kuzungumza, Kutamka, Kuelezea, Kuhadithia, Kunukuu na hua

pia linatumika katika kuainisha kitu au tukio halisi linalotokea bila ya kusikika sauti ya

maneno, kwa mfano pale mtu anaposema: ‘Qalat laha al aynayn samaAna wa ta’Atan’

yaani: ‘Yalimwambia yeye macho yangu nimesikia na nitatii’. Au pale wanaposema:

‘Imta'a ala hawdhu wa qala qatni’, yaani: ‘Lilijaa Hodhi hadi likasema imetosha’.

Neno Qala ndio lililotoa neno Qawlan ambalo humaanisha kutoa Kauli, Kusema,

Kuashiria au Kuelezea kwa kutumia njia ya kutoa sauti kama inavyosema aya ifuatayo

ambayo inakataza utumiaji wa kauli mbovu zisizokua na maana na hususan inapokua ni

kwa kupaza sauti, pale iliposema:

‏﴿م َّا يَفْعَلُ‏ ٱهلل َُّ‏ بِعَذَابِكُمْ‏ إِن شَكَرْتمُْ‏ وَآمَنْتُمْ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ شَاكِراً‏ عَلِيماً‏ ۞ لا َّ يحُِ‏ ُّب

ٱهلل َُّ‏ ٱلجَْهْرَ‏ بِٱلس ُّو ۤ ءِ‏ مِنَ‏ ٱلْقَوْلِ‏ إِلا َّ مَن ظُلِمَ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ سمَِيعاً‏ عَلِيماً‏ ﴾

Ma yafAAalu Allahu biAAadhabikum in shakartum waamantum wakana Allahu

shakiran AAaleeman, La yuhibbu Allahu aljahra bialssoo-i mina alqawli illa

man dhulima wakana Allahu sameeAAan AAaleeman (Surat An Nisaa 4:147-148)

Tafsir: Kwa nini Allah Subhanah wa Taála akuadhibuni nyinyi wakati Mmemshukuru

na Kumuamini. Na hakua Allah isipokua ni mwingi wa Kukubali, kuridhia na

kuthamini na Mwenye kujua kila kitu. Hapendi Allah uovu unaowekwa wazi kwa njia

ya kauli ya kupaza sauti, isipokua kwa yule aliedhulumiwa. Na hakika Allah ni mwingi

wa kusikia na mwingi wa ujuzi.

Naam aya mbili hizi zimetumia neno Shakartum na neno Jahara ambapo Hali ya

kuonesha Shukrani mbele ya Allah Subhanah wa Taála ni katika kumjua kwake na

Rehma zake ndani ya Nyoyo zetu, na kuthibitisha kwa njia ya Kauli na katika vitendo

vyetu. Sasa tunapozungumzia neno Shakartum ambalo ni lenye kutokana na Jina la Sifa

Tukufu ya Allah Subhanah wa Taála ambalo ni Shakir ambalo hua linamaanisha Mwingi

wa kukubali, kuridhia na kuthamini yale anayofanyiwa na Waja wake wanaompenda,

yaani hapa tunazungumzia kulingana na uhusiano baina ya Muumba kwa Kiumbe wake.

Ama tunapozungumzia kuhusiana na Kiumbe kwa Mja wake basi neno Shakir hua

linamaanisha Kukubali na kushukuru Rehma za Muumba juuu yake.

Hivyo aya inayofuatia ambayo ndio imetumia neno Jahara ambalo hua linamaanisha

kusema kwa Kupaza Sauti. Hivyo Allah Subhanah wa Taála anaweka wazi kua


54

hakubaliani na kauli mbovu zinazotolewa kwa kupaza sauti na Wanafiq, lakini hata hivyo

baadhi ya wakati mtu anapopandishiwa sauti basi inaruhusika kurudisha majibu ya kauli

hizo, hivyo aya hii inaweka wazi kua Allah Subhanah wa Taála anachukia Kauli mbovu.

Ambapo Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al

Qurtubi basi yeye anasema juu ya maana ya ayah hii ni kua: ‘Hapa kwanza inabidi

tuiangalie hali ya sharti la Illa yaani ‘Isipokua’, kisha ndio tunaangalia maana ya

aya yote kwa ujumla na hivyo kuona kua Ni mwenye kufanya Dhulma tu ndie

ambae hua ni mwenye kupaza sauti katika uovu.’

Allah Subhanah wa Taála anahoji kuhusiana na utumiaji bora wa mawasiliano ya kauli

katika Surat Fusilat kua:

‏﴿وَمَنْ‏ أَحْسَنُ‏ قَوْلاً‏ ممِّ َّن دَعَآ إِلىَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَعَمِلَ‏ صَ‏ ا لحِاً‏ وَقَا لَ‏ إِن َّنىِ‏ مِ‏ نَٱ لْمُسْلِمِينَ‏ ﴾

Waman ahsanu qawlan mimman daAAa ila Allahi waAAamila salihan waqala

innanee mina almuslimeena (Surat Fusilat 41:33)

Tafsir: Na ni nani mwenye kauli bora, zaidi ya yule anaewaita watu kwa Allah, na

akafanya mema na akasema: Hakika mimi ni Miongoni mwa Waisalam.

Katika kuilezea ayah hii basi anasema Hasan Al Basri kua: ‘Huyu hua ni mtu

anaependwa na Allah Subhanah wa Taála, ni mtu aliechaguliwa, na ndie

anaependwa na Allah Subhanah wa Taála zaid ya watu wote hapa duniani, kwani

yeye hua ni mwenye kuitikia wito wa Allah Subhanah wa Taála, na hivyo hua ni

mwenye kufanya mema na kusema kua: ‘Mimi ni miongoni mwa Waislam’ huyu

hua ndie Khalifa wa Allah hapa Ulimwenguni.’

Ama kwa upande wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi yeye

anasema kua: ‘Alie bora kwa Kauli ni yule ambae, anaewaongoza watu kumuelekea

Mola wao. Ibada zake na Sunna zake, na mwenye kujilinda juu ya makatazo ya

Mola wake, na anaeongoza katika Idama (Msisitizo) na Istiqama (Msimamo Thabit)

mbele ya Allah, na hivyo hua ni mwenye msimamo kutokana na khofu ya Khatma

yake. Na hua ni mwenye kua katika Tariqat al Wusta (Njia ya kati na kati), na kua

katika Jadda Mustaqima (Njia ilinyooka) ambayo ila atakaeifuta basi atakua

Salama, ambayo ni njia itakayompelekea kila atakae kua mbali nayo na kujawa na

Nadama (Majuto)’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari ametumia neno Tariqat Wusta

yaani Njia ya Msimamo wa Kati na Kati, kwani Ummah wa Kiislam unajulikana kwa


55

kua na sifa ya Ummatan Wasatan yaani Ummah wenye kufuata misimamo ya kati kati

bila ya kua ni wenye Ghuluw yaani kuvuka mipaka kwa kua na misimamo mikali katika

mambo yao na bila ya kua ni wenye Tafrit yaani kuvuka mipaka kwa kudharau mambo

yao.

Kwani Waislam ni wenye kutumia kauli nzuri, Allah Subhanah wa Ta’ala

anatuthibitishia kua walioamuamini yeye na wakawa wanafanya mema watakua ni wenye

kulipwa Pepo kwani wao ndio wale ambao walioongozwa kutokana na kauli njema kwa

kusema:

‏﴿إِن َّ اهلل َّ يُدْخِ‏ لُ‏ ال َّذِينَ‏ آمَنُوا وَعَمِلُوا الص َّ الحَِاتِ‏ جَن َّاتٍ‏ تجَْرِي مِنْ‏ تحَْتِهَا

يحَُل َّوْنَ‏ فِيهَا مِنْ‏ أَسَاوِرَ‏ مِنْ‏ ذَهَبٍ‏ وَلُؤْلُؤًا وَلِبَاسُهُمْ‏ فِيهَا حَرِيرٌ‏

الط َّيِّبِ‏ مِنَ‏ الْقَوْلِ‏ وَهُدُوا إِلىَ‏ صِرَاطِ‏ الحَْمِيدِ﴾‏

وَهُدُوا إِلىَ‏

الأَْنْهَاُر

۞

Inna Allaha yudkhilu alladheena amanoo waAAamiloo alssalihati jannatin tajree

min tahtiha al-anharu yuhallawna feeha min asawira min dhahabin walu/lu-an

walibasuhum feeha hareerun; Wahudoo ila alttayyibi mina alqawli wahudoo ila

sirati alhameedi (Surat Al Hajj 22:23-24)

Tafsir: Hakika Allah atawaingiza wale waliomuamini na wakafanya mambo mema

katika Bustani (Peponi) ambazo chini yake kuna mito ambamo watapambwa ndani

yake kwa makoja ya Dhahabu na Lulu na nguo zao zitakua za Hariri. Na

Wameongozwa kutokana na (utumiaji) bora miongoni mwa kauli na wakaongozwa

katika njia iliyonyooka.

Hivo ni baadhi tu ya mifano ya umuhimu wa kauli nzuri, iliyotajwa katika Qurán, lakini

tukifuatilia kwa makini basi tunaona kua Qurán imetumia asili ya neno Qulu katika hali

tofauti mara 1726 ikiwemo pale ilipotilia mkazo umuhimu wa kutovuka mipaka katika

mawasiliano baina yetu kwa njia ya kauli na kututaka kua na misimamo bora ya kati na

kati hata katika mazungumzo yetu na hivyo kuzijumuisha kauli tofauti katika aina 6 za

kauli bora ambazo ni:-

1. Qawlan Sadida

2. Qawlan Baligha

3. Qawlan Ma'rufan

4. Qalan Karima

5. Qawlan Layyina


56

6. Qawlan Maysura.

Katika kipindi ambacho Waislam tumezungukwa na mitihani katika kila upande ambayo

inayotupelekea kuhitaji kuthibitisha zaidi Imani na kumtegemea zaidi Allah Subhanah

wa Ta’ala katika maisha yetu na hivyo kuwa na uwezo wa kujilinda na madhara ya

viumbe na mitihani katika mazingira yetu na pia katika mazingira ya waliotangulia kabla

yetu, basi Qur’an haikutufunza namna ya kua na kauli nzuri tu bali pia Qur’an

imetuamrisha pia kujifunza kwa vitendo kwa kutumia njia ya kutembea katika maeneo

mbali mbali ardhini, kwani amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

‏﴿وَمِنْ‏ آَتِهِ‏ أَنْ‏ خَلَقَكُمْ‏ مِّن تُ‏ رَابٍ‏ ثمُ َّ إِذَآ أَنتُمْ‏ بَشَرٌ‏ تَنتَشِ‏ رُونَ‏ ﴾

Wamin ayatihi an khalaqakum min turabin thumma idha antum basharun

tantashiroona (Surat Rum 30:20)

Tafsir: Na Miongoni mwa Dalili mwake ni kua amekuumbeni nyie kutokana na

Udongo kisha mkawa katika Maumbo ya Watu Mliotawanyika na kutembea.

MANUFAA YA KUTAWANYIKA NA KUTEMBEA ARDHINI

KULINGANA NA QUR’AN.

Ni jambo lililowazi kua bila ya shaka Qurán imebeba kila aina ya ujumbe wenye manufaa

kwa ajili yetu ndani yake, na miongoni mwa mambo hayo yenye manufaa ni namna ya

kutembea ardhini kwa ajili ya kuzingatia hali na maumbile ya vitu mbali mbali vilivyomo

ndani yake na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akatutaka kutokua na Kibr katika

wakati wetu hapa Ulimwenguni kwani kufanya hivyo hakutotunufaisha wala

hakutotupelekea kuzingatia malengo ya kuumbwa kwetu na vinavyotuzunguka katika

mazingira yetu kama zinavyosema aya:

‏﴿وَلاَ‏ تمَْشِ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ مَرَ‏ حاً‏ إِن َّكَ‏ لَن تخَْرِقَ‏ ٱلأَرْضَ‏ وَلَن تَبْلُغَ‏ ٱلجِْبَالَ‏ طُولاً‏ ﴾

Wala tamshi fee al-Ardhi marahan innaka lan takhriqa al-ardha walan tablugha

aljibala toolan (Surat Al Isra 17:37)


57

Tafsir: Na msitembee juu ya Ardhi kwa madaha, kwani kwa hakika kamwe hamtoweza

kudidimia ndani ya ardhi, na wala hamtoufikia urefu wa milima.

Tunapoiangalia aya hii basi tunaona inatuonesha kua Ibn Adam tunatakiwa kua

wanyenyekevu na kamwe hatutakiwi kuishi maisha ya kujiona kwa kutembea kwa

madaha, kudunda au kwa ubabe kwani kufanya kwetu hivyo hakuto ipelekea Ardhi kua

ni yenye kutoboka na sisi kudidimia ndani yake na wala hakutopelekea kua warefu kiasi

ya kuufikia urefu wa milima, kwani kuna wengi waliokuja kabla yetu ambao nao walikua

wakijiona na kua na Kibr, lakini hata hivyo nao wakawa ni wenye kuacha kila kitu

Duniani kama walivyokikuta.

Na haya pia ndio maneno ambayo Luqman Al Hakim alitumia kumuusia Mtoto wake

kama inavyoelezewa katika Surat Luqman na aya zifuatazo:

‏﴿وَلاَ‏ تُصَعِّ‏ رْ‏ خَد َّكَ‏ لِلن َّاسِ‏ وَلاَ‏ تمَْشِ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ مَرَحاً‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لاَ‏ يحُِب ُّ كُل َّ مخُْ‏ تَالٍ‏

فَخُورٍ۞‏ وَٱقْصِدْ‏ فىِ‏ مَشْيِكَ‏ وَٱغْضُضْ‏ مِن صَوْتِكَ‏ إِن َّ أَنكَرَ‏ ٱلأَصْوَاتِ‏ لَصَوْتُ‏

ٱلحَْمِيرِ‏ ﴾

Wala tusaAAAAir khaddaka lilnnasi wala tamshi fee al-ardhi marahan inna Allaha

la yuhibbu kulla mukhtalin fakhoorin, Waiqsid fee mashyika waoghdud min

sawtika inna ankara al-aswati lasawtu alhameeri (Surat Luqman 31:18-19)

Tafsir: Na usigeuze uso wako kwa kujiona, na wala usitembee kwa madaha. Kwani

kwa hakika Allah hawapendi wenye kujivuna kwa fakhari. Na usiwe ni mwenye

haraka katika kutembea kwako, na punguza sauti yako, kwani sauti kubwa

inayochukiza ni sauti ya Punda.

Hivyo kabla ya mtu kua na Kibr na hivyo kutembea kwa madaha kutokana na uzuri wako,

mamlaka yako, mali zako, Ilm yako n.k basi inabidi kutafakkar ni nini kilichowafika wale

waliotangulia kabla yetu na hii ndio miongoni mwa sababu ambazo Allah Subhanah wa

Ta’ala akatuhimiza kutembea ardhini kwa unyenyekevu ili kupata kuona na kuzingatia

mazingira ya Ulimwengu katika aya takriban 14 ambazo zimetumia neno Nadhara.

Neno Nadhara kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kuona, Kuangalia, Kutizama

kwa kituo, Mtizamo, Kuchunguza, Kufikiria, Kusubiri, Kusubiri ili upate kuona au

kuthibitisha, Kufuatilia kwa umakini kwa kutumia macho, Kutafuta, Kuzingatia na pia

humaanisha Kutafakkar. Wenye Lugha yao hua wanasema Nadharat FiiHi yaani Angalia

Uone!


58

Neno Nadhara ndio lililotoa neno Undhuru ambalo ni lenye kumaanisha Angalia

Uzingatie, Ili kufahamu zaidi basi na tuangalie mfano unaofafanua wazi maana ya neno

Undhuru katika ifuatayo ambayo imetumia neno Undhurna:

‏﴿َأَي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ لاَ‏ تَقُولُواْ‏ رَاعِنَا وَقُولُواْ‏ ٱنْظُرَْ‏ وَٱسمَْعُواْ‏ وَ‏ لِلكَافِرِينَ‏ عَذَابٌ‏

أَلِيمٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo la taqooloo raAAina waqooloo undhurna

waismaAAoo walilkafireena AAadhabun aleemun (Surat Al Baqara 2:104)

Tafsir: Enyi Mlioamini! Msiseme (Kumwambia Rasul Allah Salallahu A’layhi wa

Salam) Raina semeni Undhurna na Sikilizeni! Na kwa Waliokufuru ni juu yao

Adhabu kali.

Ambapo tunaona kua anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Waarabu

walikua wakipenda kutumia neno Raina (lenye kumaanisha kua Tuangalie), hivyo

Mayahudi waliposikia Waarabu wakitumia neno hilo pamoja na Rasul Allah

Salallahu A’layhi wa Salam, basi nao wakalipenda, kwa sababu neno Raina hua ni

lenye kumaanisha matusi kwa lugha ya Kiyahudi, (Ambapo kwa Lugha ya Kiarabu

pia hua linamaanisha Mchungaji wa Wanyama wetu, na pia Mtu Mjinga na Laghai)

Hivyo Mayahudi wakasema: ‘Zamani tulikua tukimtukana Muhammad kisiri siri,

hivyo sasa hivi tunaweza kumtukana wazi wazi kwa kutumia hili neno Raina

ambalo limo katika Lugha yao.

Hivyo wakawa wanakuja mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na

kusema: ‘Ya! Muhammad Raina!’ kisha wanaanza kucheka! Siku moja walipokuja

akawepo Sa’ad Ibn Ubadah Radhi Allahu Anhu ambae ni miongoni mwa Ansari

mwenye kujua maana ya neno Raina kama walivyokua wakikusudia Mayahudi.

Hivyo Sa’ad Ibn Ubaidah Radhi Allahu Anhu akawaambia: ‘Enyi Maadui wa Allah!

Allah akulaanini nyie. Hakika mimi nnaapa kwa yule ambae ndani ya Mamlaka

yake imo Roho ya Muhammad Rasul Allah Salallahu Alyhi wa Salam. Kua kama

nikimsikia mtu yeyote yule anatumia tena neno hilo, basi Wa Allahi nitamkata

kichwa chake!’

Mayahudi hao nao wakapinga na kusema: ‘Lakini jee nyinyi hamtumii neno hilo?’

hivyo basi baada ya majibishano hayo ndio Allah Subhanah wa Taála akashusha

aya hio.’’


59

Hivyo neno Raina lina maana zenye utata ndani yake kwani hua halina maana ya

kutizama kwa ulazima wa kuona tu pekee. Lakini neno Undhurna maana yake ni kua:

‘Tuangalie kwa kituo ili Utuone au Tusubiri’, na ukweli ni kua kutokana na kua na

maana hio ya Kuangalia au Kutizama kwa ajili ya Kuona kwa kituo na mazingatio kwa

ajili ya kupata mafundisho na manufaa yaliyomo ndani ya kinachoangaliwa, basi Qurán

imetilia mkazo Kuangalia kwa ajili ya Kuona na Kutafakkar katika aya nyingi ndani yake

na kwa kuzungumzia mambo mengi ndani yake na hivyo kuzijumuisha pamoja aina tatu

muhimu za Safari kwa ajili ya Kuona ambazo ni:

Aina ya kwanza: Ni ile iliyoainishwa katika aya ambazo zimezungumzia Safari lakini

hazikutumia neno Undhuru, na hizi ni zile aya ambazo zinazungungmzia habari na Visa

vya Mitume na Manabii wakiwemo Nabii Nuh, Nabii Ibrahim, Nabii Musa, Dhul

Qarnayn, Al Khidhr, Nabii Yaqub, Nabii Yusuf, Nabii Sulaiman, Malqia Bilqis, Nabii

Yunus, Maryam Bint Imran, Nabii Isa, As-hab Al Kahf, Uzayr n.k.

Ambapo ndani yake zimewazungumzia watu wema hawa ambao ni miongoni mwa

mifano ya kuigwa mbele yetu. Haina haja kwetu sisi kuzianisha aya hizi kwa sababu

tutazizungumzia baadhi yake katika kurasa za mbele za kitabu wakati tukielezea maisha

ya Ulu ul Azmi Minna Rusul ambayo ndio mada kuu ya Kitabu chetu.

Aina ya Pili: Ni ile iliyoainishwa katika aya ambazo zinatuamrisha sisi kutembea ardhini

kwa malengo na makusudio ya kujifunza mambo mbali mbali tangu kuanzia kwa Viumbe

vya Ulimwenguni, Uwezo na Maajabu yao ya hadi kufikia katika kuona Uwezo Mkubwa

na Maajabu ya Muumba wa Ulimwengu wote na kila kitu kilichomo ndani yake. Aya hizi

hua zina malengo ya kututanua kiakili na kututayarisha kiufahamu na kutufunza juu ya

namna ya kukabiliana na mitihani na mambo mengine yaliyo mbele yetu kwa kua na

subra na ustahamilivu kama vile walivyokua wale waliotangulia kabla yetu ambao ni

miongoni mwa Waliomuamini Allah Subhanah wa Taála na pia miongoni mwa wale

ambao hawakumuamini, kwa mfano katika Surat Al Imran pale aliposema:

‏﴿قَدْ‏ خَلَتْ‏ مِنْ‏ قَبْلِكُمْ‏ سُنَنٌ‏ فَسِ‏ يرُواْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَٱنْظُرُواْ‏ كَيْفَ‏ كَانَ‏ عَاقِبَةُ‏

ٱلْمُكَذِّبِينَ‏ ﴾

Qad khalat min qablikum sunanun faseeroo fee al-Ardhi faondhuroo kayfa kana

AAaqibatu almukadhdhibeena (Al Imran 3:137)


60

Tafsir: Kwa hakika yamewafika mengi waliokuja kabla yenu (Walioamini na

Wasioamini), hivyo tembeeni katika Ardhi ili mpate kuona ni upi ulikua mwisho wa

wale waliokadhibisha.

Na mfano wa aya zinazohimiza kusafiri ili kupata vithibitisho juu ya Ukubwa wa Allah

na Uwezo wake katika Kuumba kwake ni pamoja ile isemayo:

‏﴿قُلْ‏ سِ‏ يرُواْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَٱنظُرُواْ‏ كَيْفَ‏ بَدَأَ‏ ٱلخَْلْقَ‏ ثمُ َّ ٱهلل َُّ‏ يُنشِ‏ ئُ‏ ٱلن َّشْأَةَ‏ ٱلآخِ‏ رَةَ‏ إِ‏ َّن

ّ ل شَ‏ يْ‏ ءٍ‏ قَدِيرٌ‏ ﴾

ٱهلل ََّ‏ ٰ عَلَى كُ‏ ِ

Qul seeroo fee al-Ardhi faondhuroo kayfa badaa alkhalqa thumma Allahu yunshio

alnnash-ata al-akhirata inna Allaha AAala kulli shay-in qadeerun (Al-Ankabut

29:20)

Tafsir: Sema: Tembeeni katika Ardhi na mpate kuona (namna Allah) alivyoanzisha

Uumbaji wake, na kisha Allah atawafufua viumbe kesho Akhera. Kwa Hakika Allah

ni muweza juu ya kila kitu.

Bia ya shaka Allah Subhanah wa Ta’ala hamuamrishi tu kila Ibn Adam kutembea ili

apate kujifunza kwa kuona lakini pia anatutilia mkazo zaidi sisi Waislam, tuliomuamini

juu ya jambo hilo. Aya inayofuatia pia ni miongoni mwa mifano mwa aya hizo.

‏﴿قُلْ‏ سِ‏ يرُواْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَٱنْظُرُواْ‏ كَيْفَ‏ كَانَ‏ عَاقِبَةُ‏ ٱل َّذِينَ‏ مِن قَبْلُ‏ كَانَ‏ أَكْثَرُهُمْ‏

م ُّشْرِكِينَ‏ ﴾

Qul seeroo fee al-ardi faondhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena min qablu

kana aktharuhum mushrikeena (Ar-Rum 30:42.)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad): Tembeeni katika Ardhi na mpate kuona ni upi ulikua

mwisho wa wale waliokuja kabla yenu. Walikua wengi wao ni Washirikina.

Aina ya Tatu: Ni ile iliyoainishwa katika aya ambazo zinawahoji wale ambao

hawatembei ardhini wakaona yaliyowafika wale walikuja kabla yao, ama kwa ujumla

basi aya za kundi hili la tatu zinawashutumu wale ambao hawakumuamini Allah


61

Subhanah wa Ta’ala, Mitume wake na vitabu vyake na hivyo kua ni wenye kupingana

na maamrisho ya Mola wao kutokana na ujinga wao kwa mfano pale Qurán iliposema:

‏﴿أَوَلمَْ‏ يَسِ‏ يروُاْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَيَنظُرُواْ‏ كَيْفَ‏ كَانَ‏ عَاقِبَةُ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَانُواْ‏ مِن قَبْلِهِمْ‏ كَانُواْ‏

هُمْ‏ أَشَد َّ مِنْهُمْ‏ قُو َّةً‏ وَآاثَراً‏ فىِ‏ ٱلأَ‏ رْضِ‏ فَأَخَذَهُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ بِذُنُوهبِِمْ‏ وَمَا كَانَ‏ لهَُ‏ م مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏

مِن وَاقٍ‏ ﴾

Awa lam yaseeroo fee al-ardhdhi fayandhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena

kanoo min qablihim kanoo hum ashadda minhum quwwatan waatharan fee al-

Ardhi faakhadhahumu Allahu bidhunoobihim wama kana lahum mina Allahi min

waqin (Surat Ghafir 40:21)

Tafsir: Jee hawakutembea juu ya Ardhi na wakaona, yalivyokua mabaki ya

waliotangulia kabla yao? Walikua na wingi wa kinguvu na kiathari walizoacha

ardhini zaidi yao. Lakini akawapa adhabu Allah kwa dhambi zao na hawakua na wa

kuwasaidia dhidi ya Allah.

Na vile vile ikasema tena katika Sura hio hio:

‏﴿أَفَلَمْ‏ يَسِ‏ يرُواْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَيَنظُرُواْ‏ كَيْفَ‏ كَانَ‏ عَاقِبَةُ‏ ٱل َّذِينَ‏ مِن قَبْلِهِمْ‏ ۤ كَانُواْ‏ أَكْ‏ ثَرَ‏

ن ‏ِم ْ‏ هُ‏ مْ‏ وَأَشَد َّ قُو َّةً‏ وَآاثَراً‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَمَآ أَغْنىَٰ‏ عَنْهُم م َّا كَانُواْ‏ يَكْسِ‏ بُونَ‏

Afalam yaseeroo fee al-Ardhi fayandhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena min

qablihim kanoo akthara minhum waashadda quwwatan waatharan fee al-Ardhi

fama aghna AAanhum ma kanoo yaksiboona (Surat Ghafir 40:82)

Tafsir: Jee hawakutembea juu ya Ardhi na wakaona, yalivyokua mabaki ya

waliotangulia kabla yao? Walikua wengi zaid yao na wenye uwezo mkubwa kinguvu,

na katika athari zao walizoacha katika ardhi, lakini hata hivyo kila kitu chao

walichokua nacho hakikua ni chenye kuwasaidia.

Hapa wale wasioamini wanatakiwa kutafakkar yale mambo ambayo yaliwafika watu

waliotangulia kabla yao ambao wao walikua ni wakubwa kimaumbile na kinguvu pia

kiasi ya kua athari zao walizoacha hadi hii leo bado zipo na zimekua ni miongoni mwa


62

maajabu ya Dunia, kwa mfano: Piramidi za Misri, Makasri, Ngome na Majumba

waliyoyajenga kwa kuchonga Milima ya mawe nchini Afghanistan, Iran, Iraq, Syria,

Jordan, Yemen n.k kwa kutumia utaalamu na zana ambazo hadi hii leo bado Wanasayansi

wa karne yetu hawajajua ni zana gani za karne hizo zinazochonga mawe kama zana za

karne yetu, kiasi ya kua ukiona athari zake basi lazima utastaajabu, kutokana na ukubwa

na umadhubuti wa Matofali, Mawe na Urefu wa Nguzo na Minara waliyojenga

kimpangilio kulingana na mpangilio wa nyota na sayari za angani, ambapo uzuri wa

Nakshi na mapambo yake baadhi miongoni mwa Majengo hayo hua ni kama yenye

kuonekana kama yamechongwa kwa kutumia mashine maalum za katika kipindi chetu

cha wakati wa maendeleo kutokana na unadhifu wake.

Lakini hata hivyo Ukubwa wao, Nguvu zao, Maarifah yao, Ujuzi wao, Utaalamu wao,

Mali zao, Majumba yao, Mafanikio ya athari zao walizokua nazo na kubakia hadi hii leo

basi vyote hivyo havikuwasaidia kitu, kwani kumsahau kwao Mola wao na kuenda

kinyume na maamrisho yake ndiko kulikosababisha kushushiwa adhabu kwao kupata

maangamizo yao kama inavyosema aya inayofuatia ya Surat Muhammad 47:10 ambayo

pia ni miongoni mwa mifano ya aya za Fayandhuru:-

‏﴿أَفَلَمْ‏ يَسِ‏ يرُواْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْ‏ ضِ‏ فَيَنظُرُواْ‏ كَ‏ يْفَ‏ كَ‏ انَ‏ عَاقِبَةُ‏ ٱل َّذِينَ‏ مِ‏ ن قَبْلِهِمْ‏ دَم َّرَ‏ ٱهلل َُّ‏

عَلَيْهِمْ‏ وَلِلْكَافِرِينَ‏ أَمْثَالهَُا﴾‏

Afalam yaseeroo fee al-ardi fayandhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena min

qablihim dammara Allahu AAalayhim walilkafireena amthaluha (Surat Muhammad

47:10)

Tafsir: Jee hawajatemea ardhini, na hivyo wakaona ni upi ulivyokua mwisho wa wale

ambao waliotangulia kabla yao (Waliokua wakifanya maovu) hakika aliwashushia

Allah juu yao maangamizo, na kwa makafiri yatawakuta mithili yake.

Ingawa Allah Subhanah wa Ta’ala anawataka Ibn Adam katika aya hizo za Safari zenye

malengo ya kujifunza lakini wale wajinga wasiojua miongoni mwetu wamekua katika

mstari wa mbele katika jitihada za kufuta athari za watu hawa waliotangulia kabla yetu

na ambao tumetakiwa kujifuza kutoka kwao tena kupitia katika aya zilizowazi kama

tunavyoona katika mifano ya aya hizo.

Inasikitisha kuona kua Watu wanaojiita Waislam tena walioamini kua wanavamia

miji ya Zamani ya Kihistoria na kisha kuvunja na kubomoa Majengo na Athari

mbali mbali za Kihistoria zilizozungumziwa kwenye Qurán, hususan katika Ardhi

ya Mashariki ya Kati kwani Miskiti mingi ya Kihistoria za watu Watukufu, kama


63

Mawalii, Masahaba, Maimamu n.k imeripuliwa kwa mabomu kwa mfano Masjid

Khalid Ibn Walid wa Mjini Homs nchini Syria, Mji wa Palmira, nchini Iraq mji wa

Nimrudh, nchini Libya mji wa Cyrene uliojengwa na Warumi miaka 630 kabla ya

Nabii Isa, nchini Yemen katika mji wa Barqaish, nchini Afghanistan, Lebanon,

Palestina, Miskiti na Maktaba za Mji wa Timbuktu, nchini Mali n.k

Watu hawa wasiojua hua wanatumia kisingizio cha ile hadith ya Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam isiemayo kua: ‘Msifunge safari kwa malengo ya kutembelea Miskiti

isipokua katika Misikiti Mitatu, Misikiti huu (Masjid An Nabbawi wa Madinah ),

Masjid Al Haram wa Makkah na Masjid Al Aqsa’(Sahih Bukharin a Muslim)

Huku ni kutofaham maana halisi ya Hadhith hio kwani anasema Al Hafidh Imam Zayn

Ad Din Abd Rahim Al Iraqi kua: ‘Miongoni mwa maana nzuri iliyobebwa na Hadith

hii, ni kukatazwa kwa malengo ya kutembelea Miskiti husika. Lakini, kutembea

kwa malengo ya Kutafuta I’lm, Kumtembelea Mtu Mtakatifu, Rafiki au Jamaa, au

kwa Malengo ya kufanya Biashara, Kuuburudisha Moyo, Kujizidishia Iman n.k

basi inaruhusiwa kwani hayo hayajajumuishwa ndani ya Hadith hii, na hili

linafafanulika vizuri zaidi na Hadith nyengine ya Abu Said Al Khudri ambae

anasema kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua : ‘Hairuhusiki

kwa mtu, kutembelea Miskiti kwa malengo ya Kusali ndani ya Msikiti huo, isipokua

kwa ajili ya Miskiti mitatu: Masjid Al Haram (Makkah), Masjid Al Aqsa na Misikiti

wangu huu (Masjid An Nabbawi wa Madinah ),’’’’((Musnad Imam Ahamd, Musannaf

Ibn Shaybah) Al Hashiyah Minhaj Al Tulab – Imam Al Jamal Shaykh Sulaiman Ibn

Mansur)

Na akasema Mujaddid Ad Din Imam Taj Ad Din Al Subki kua: ‘Hakuna sehemu juu ya

mgongo wa Ardhi ambayo iliyokua haina Utukufu wake, kwa ajili ya mtu

kutembelea sehemu hio kutokana na Utukufu husika, isipokua sehemu hizi (Masjid

Al Haram, Masjid Al Aqsa na Masjid An Nabbawi wa Madinah ). Na nnaposema

Utukufu wa sehemu husika, basi hua nnakusudia juu ya ule Utukufu uliothibitishwa

na Sharia za Kiislam. Ambapo Mtu hatakiwi kutembelea sehemu kwa ajili ya

Utukufu wa Sehemu hio husika, bali kwa sababu ya kutafuta I’lm, kwa kutembea,

au kwa sababu nyengine yeyote ile inayokubalika Kisharia. Wale ambao

wanaopinga juu ya hilo basi hua ni wenye kukosea katika Imani yao, kwani

kutembelea Msikiti husika hua kunatokana kwa ajili ya wale waliomo ndani ya

Msikiti husika, na si kwa ajili ya Msikiti husika. Hivyo Hadithi hii imepinga

kutembelea Miskiti kama Miskiti isipokua kwa ajili ya Miskiti Mitatu hio husika.

Lakini kufunga safari kwa sababu ya kumtembelea Mtu, au kwa sababu ya

kutafuta I’lm, basi hua si kwa sababu ya Msikiti huo, bali hua ni kwa ajili ya wale

waliomo kwenye Msikiti huo) (Hashiyah Minhaj Al Tulab – Imam Al Jamal Shaykh

Sulaiman Ibn Mansur)


64

Tumalizie sehemu hii kwa kuangalia aya ya Fayandhuru inayofuata ambayo kutokana

na ujumbe wake basi tunaona kua, Allah Subhanah wa Ta’ala anatuainishia tena

umuhimu wa kutembea pia kwa ajili ya kuona na kufahamu madhara yaliyowafika wale

waliokua ni wenye kupingana na Ujumbe wa Mitume wake kwani kupinga kwa watu hao

baada ya kuwekewa vithibitisho vilivyowazi hakukua na faida yeyote kwao wao na

badala yake ilikua ni kujitia maangamizo na hivyo kua ni wenye kujidhulumu wao

wenyewe, kama inavyoweka wazi aya ifuatayo:

‏﴿أَوَلمَْ‏ يَسيرُواْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَيَنظُرُواْ‏ كَيْفَ‏ كَانَ‏ عَاقِبَةُ‏ ٱل َّذِينَ‏ مِن قَبْلِهِمْ‏ كَانُ‏ و ۤ اْأَشَد َّ

مِنْهُمْ‏ قُو َّةً‏ وَأَاثَرُواْ‏ ٱلأَرْضَ‏ وَعَمَرُوهَآ أَكْثَرَ‏ ممِ َّا عَمَرُوهَا وَجَآءَتْهُمْ‏ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَاتِ‏

فَمَا كَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ لِيَظْلِمَهُمْ‏ وَلَٰكِن كَ‏ انُو ۤ اْ‏ أَنفُسَ‏ هُمْ‏ يَظْلِمُونَ‏ ﴾

Awa lam yaseeroo fee al-Ardhi fayandhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena min

qablihim kanoo ashadda minhum quwwatan waatharoo al-ardha waAAamarooha

akthara mimma AAamarooha wajaat-hum rusuluhum bialbayyinati fama kana

Allahu liyadhlimahum walakin kanoo anfusahum yadhlimoona (Surat Rum 30:9)

Tafsir: Jee hawatembei ardhini na kuona mwisho wa wale ambao waliotangulia kabla

yao, walikua wakubwa zaidi yao kinguvu, na wakawacha athari zao katika ardhi, na

wakaijaza Ardhi kuliko walivyofanya hawa, na wakaja kwao wao Mitume wenye

vitibitisho vilivyowazi. Hakika Allah hakuwadhulumu, bali wao ndio waliokua

wakijidhulumu.

Hakika watu hao waliotangulia walikua ni kama sisi yaani wenye Nyoyo, Macho na

Masikio na kadhalika lakini hata hivyo wao walikua ni miongoni mwa waliojidhulumu

kutokana na kutumia sivyo neema za viungo vyao hivyo muhimu walivyopewa na Mola

wao aya inayofuatia inaweka wazi juu ya jambo hilo.

‏﴿أَفَلَمْ‏ يَسِ‏ يرُواْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَتَكُونَ‏ لهَُمْ‏ قُلُوبٌ‏ يَعْ‏ قِلُونَ‏ هبَِآ أَوْ‏ آذَانٌ‏ يَسْمَعُونَ‏ هبَِا

فَإِن َّهَا لاَ‏ تَعْمَى ٱلأَبْصَارُ‏ وَلَٰكِن تَعْمَى ٰ ٱلْقُلُوبُ‏ ٱل َّتىِ‏ فىِ‏ ٱلص ُّدُورِ‏ ﴾

Afalam yaseeroo fee al-Ardhi fatakoona lahum quloobun yaAAqiloona biha

aw adhanun yasmaAAoona biha fa-innaha la taAAma al-absaru walakin taAAma

alquloobu allatee fee alssudoori (Surat Al Hajj 22:46)


65

Tafsir: Jee hawakutembea wao juu ya ardhi? Hawakua wao na nyoyo ambazo ni za

kufahamu na masikio ya kusikilizia? Kwa hakika sio macho yao yanayokua na upofu

wa kutoona bali ni nyoyo ndani ya vifua vyao ndio vilivyokua na upofu.

Moyo wa Ibn Adam unafahamu kulingana na mitizamo ya aina mbili aina ya kwanza ni

ya kuona kwa mtizamo wa ndani ya Moyo ambao ni kwa kupitia kwa njia ya hisia za

kuhisi kwa Moyo na mtizamo wa pili ni mtizamo wa kuona kwa mtizamo wa nje ya

Moyo, hivyo kutembea na kuona kwa mitizamo yote miwili hii, hua kuna manufaa zaid

kwani hupelekea kuuelimisha na kuupumzisha Moyo, Ufahamu na Akili ya Ibn Adam

kama anavyosema Mujaddid ad Din Imam Muhammad Idris al Shafii katika kitabu chake

cha Al Diwan kua:

Uache Mji wako kwa ajili ya kutafuta

Darja kwa kuelimika

Na Safiri. Kwani katika kusafiri kuna

faida Tano.

Kuiwepesishia Mzigo Nafsi na kujitafutia

Maisha yako.

Na I’lmu na Adabu na Marafiki bora.

Kama ikisemwa kua kusafiri ni Madhila

na Ugumu wa mambo.

Na urefu wa kuvuka Majangwa, ugumu

na matatizo.

Basi Kifo ni bora kwa Mtu kuliko

kubakia sehemu moja.

Katika Manyanyaso baina ya Usaliti na

Husda.

تغرب عن الأوطان في طلب العلى

وسافر ففي الأسفار خمس فوائد

تفريج هم واكتساب معيشةٍ‏

وعلمٍ‏ وآدابٍ‏ وصحبة ماجد

فإن قيل في الأسفار ذل ومحنة

وقطع الفيافي وارتكاب الشدائد

فموت الفتى خير له من قيامه

بدار هوان بين واش وحاسد

Naam neno Undhur basi limetumika pia tena katika Quran pale iliposema:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ ٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَلْتَنظُرْ‏ نَفْسٌ‏ م َّا قَد َّمَتْ‏ لِغَدٍ‏ وَٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏

خَبِيرٌ‏ بمَِا تَعْمَلُونَ‏ ﴾


66

Ya ayyuha alladheena amanoo ittaqoo Allaha waltandhur nafsun ma qaddamat

lighadin waittaqoo Allaha inna Allaha khabeerun bima taAAmaloona (Surat Al

Hashir 59:18)

Tafsir: Enyi Mlioamini, Muogopeni Mola wenu, na Nafsi ijichunguze juu ya kile

ilichokitanguliza kesho, na Mcheni Allah kwani kwa hakika Allah ana habari juu ya

kila mnachokifanya.

Aya inatuwekea wazi kua Ulimwengu tulionao unawakilisha siku ya leo katika Uhai wetu

na Ulimwengu wa Akhera unawakilishwa a siku ya kesho ambayo kwa hakika itakuwepo

kwa kila mmoja miongoni mwetu. Hivyo bila ya shaka kuna umuhimu wa kuziangalia

Nyoyo zetu na kufanya safari ndani yake kama anavyosema Mawlana Jalal Ad Din Al

Rumi kua: ‘Safari hukurudishia nguvu ya mwili, na mapenzi ndani ya Moyo wako.

Hivyo hata kama ikiwa huwezi kusafiri kuelekea kokote basi fanya safari ndani ya

sehemu za Moyo wako’

Hivyo amri ya Undhur imetumika kututaka Ibn Adam kutumia ipasavyo viungo vya miili

yetu yaani Miguu, Ufahamu wa Akili, Macho na mtizamo na ufahamu wa Moyo katika

kutafakkar na kuondoka kutoka katika hatua moja ya maisha duni ya kiimani na kuingia

katika hatua nyengine iliyobora zaid kiimani na hivyo kua ni wenye kupata ridhaa ya

Allah Subhanah wa Ta’ala kwa sababu hua ni wenye kufanya Hijra.

UMUHIMU WA HIJRA KATIKA ISLAM

Neno HIJRA linatokana na neno HAJARA la Kiarabu ambalo hua ni lenye kumaanisha

Kunyangánya kutoka kwa, Kupokonya kutoa kwa, Kuficha, Kudhibiti, Kukataza au

Kuzuia kuingia katika sehemu fulani, kuweka Kizingiti, Kusahaulika, Kuachana na kitu.

Neno Hajara ndio ililotoa neno Hijrun ambalo maana yake hua ni Kitu chochote

kilichokatazwa kufanywa, Ufahamu wa Ibn Adam, na pia likatoa neno Hajar ambalo

maana yake hua ni Jiwe, hivyo Jiwe limeitwa Hajar kwa sababu ya kutokana na kua na

maumbile ya Ugumu wenye kujidhibiti sana.

Neno Hajara ndio lilotoa neno Hijra ambalo pia hua ni lenye kumaanisha kuhama kutoka

katika sehemu moja isiyokubalika, au isiyowezekana kubakia na kuelekea katika sehemu

nyengine, ambapo hali hiyo ya kuhama hua inagawika katika sehemu mbili.


67

Ambapo kwanza ni kuhama kwa watu au mtu kutoka sehemu moja kwa ajili ya kuihami

nafsi yake au dini yake kuelekea sehemu nyengine yenye usalama zaid na aina hii ya

Hijra inazungumziwa na Allah Subhanah wa Taála ndani ya Qurán pale aliposema:

‏﴿وَمَن يُهَاجِ‏ رْ‏ فىِ‏ سَبِيلِ‏ اهلل َِّ‏ يجَِدْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ مُرَاغَماً‏ كَثِيراً‏ وَسَعَةً‏ وَمَن يخَْرُجْ‏ مِن

بَيْتِهِ‏ مُهَاجِ‏ راً‏ إِلىَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَرَسُولِهِ‏ ثمُ َّ يُدْرِكْهُ‏ ٱلْمَوْتُ‏ فَقَدْ‏ وَقَعَ‏ أَجْرُهُ‏ عَلىَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏

غَفُوراً‏ ر َّحِ‏ يماً‏ ﴾

Waman yuhajir fee sabeeli Allahi yajid fee al-Ardhi muraghaman katheeran

wasaAAatan waman yakhruj min baytihi muhajiran ila Allahi warasoolihi thumma

yudrik-hu almawtu faqad waqaAAa ajruhu AAala Allahi wakana Allahu ghafooran

raheeman (Surat An Nisaa 4:100)

Tafsir: Na yule ambae atakaehama kwa ajili ya Allah Subhanah wa Taála, basi atakuta

katika Ardhi sehemu nyingi sana za kuishi. Na yeyote yule atakaehama kutoka katika

nyumba kuhmia kwa Allah na Mtume wake na kifo kikamkuta basi atayakuta Malipo

yake yapo kwa Allah. Na kwa hakika Allah ni mwingi wa usamehevu na mwingi wa

Rehma.

Neno Hijra halikutumika katika Qurán kumaanisha kuhama kwa ajili ya kujinusuru

kutoka katika Ardhi moja kuelekea katika Ardhi nyengine tu lakini limetumika kuhama

kwa ajili ya kusimamia haki baina ya Mke Muadilifu na Mume Muadilifu pale Allah

Subhanah wa Ta’ala aliposema katika aya ifuatayo:

‏﴿ٱلرِّجَالُ‏ قَو َّامُونَ‏ عَلَى ٱلنِّسَآءِ‏ بمَِا فَض َّلَ‏ ٱهلل َُّ‏ بَعْضَهُمْ‏ عَلَى ٰ بَعْضٍ‏ وَبمَِآ أَنْفَقُ‏ واْ‏ مِنْ‏

أَمْ‏ وَالهِِمْ‏ فَٱل َّ صالحَِاتُ‏ قَانِتَاتٌ‏ حَافِظَاتٌ‏ لِّلْغَيْبِ‏ بمَِا حَفِظَ‏ ٱهلل َُّ‏ وَٱللا َّتِى تخََافُو ‏َن

نُشُوزَهُن َّ فَعِظُوهُن َّ وَٱهْجُرُوهُن َّ فىِ‏ ٱلْمَضَاجِ‏ عِ‏ وَٱضْرِبُوهُن َّ فَإِنْ‏ أَطَعْنَكُمْ‏ فَلاَ‏ تَ‏ بْغُواْ‏

عَلَيْهِ‏ ن َّ سَبِيلاً‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ كَ‏ انَ‏ عَلِيّاً‏ كَ‏ بِير اً‏ ﴾

Alrrijalu qawwamoona AAala alnnisa-i bima faddala Allahu baAAdahum AAala

baAAdin wabima anfaqoo min amwalihim faalssalihatu qanitatun hafidhatun

lilghaybi bima hafidha Allahu waallatee takhafoona nushoozahunna

faAAidhoohunna waohjuroohunna fee almadajiAAi waidriboohunna fa-in


68

ataAAnakum fala tabghoo AAalayhinna sabeelan inna Allaha kana AAaliyyan

kabeeran(Surat An Nisaa 4:34)

Tafsir: Wanaume ni Qawwamoona (wasimamizi) juu ya Wanawake kwa sababu Allah

amewafadhili baadhi yao (Wanaume) juu ya baadhi yao (Wanawake) kutokana na kile

wanachokichuma na kukitumia juu yao. Hivyo Wanawake wema ni watiifu (kwa Mola

wao na kwa Waume zao wenye kuwasimamia) na hujilinda wanapokua Waume zao

hawapo kile walivyoamrishwa na Allah kujilinda. Ama kwa Wanawake ambao

mnaona kua wanafanya maovu, basi waonyeni (kwanza), (kisha kama hawakusikia

basi) Fanyeni Hijra kutoka katika vitanda vyao, (Na kama hio haijasaidia basi)

wapigeni kidogo, lakini kama wakirudi katika utiifu wenu, basi msitafute njia za

kuwakera. Kwa hakika Allah ni alie Juu zaidi ya Kila kitu na ni Mkubwa sana.

Hapa tunaona kua kwanza aya imetumia neno Qawwam kwa kilugha hua linamaanisha

kusimamia au kuhudumia kitu kwa muda mrefu, hivyo tunapozungumzia kifamilia basi

neno hili hua linajumuisha jukumu la kusimamia kimwili, kimahitaji, kiheshima na

kimajukumu kwa upande wa kidunia na kiakhera.

Hivyo maana ya neno Qawwam hua kamwe haimaanishi kama vile wanavyofikiria watu

wengi kua maana yake ni kudhibiti, kuweka chini yake au chini ya mamlaka yake, kwani

kufikiria hivyo basi hua ni sawa na walivyokua wakifanya jamii za watu wa Jahiliyyah.

Katika kuielezea maana ya aya hii, basi Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam

Al Ghazali Al Thani Imam Fakhr al Din Al Razi anasema kua sehemu ya aya hii ya Surat

An Nisaa 4:34 ambayo ni: ‘Alrrijalu qawwamoona AAala alnnisa-i (Wanaume ni

wasimamizi wa Wanawake) ina uhusiano na sehemu ya aya nyengine kabla yake

isemayo:

‏﴿وَلاَ‏ تَتَمَن َّوْاْ‏ مَا

فَض َّلَ‏ ٱهلل َُّ‏ بِهِ‏ بَعْضَكُمْ‏ عَلَىٰ‏ بَعْ‏ ‏ٍض ﴾

Wala tatamannaw ma fadhala Allahu bihi baAAdhakum AAala baAAdhin’ (Surat

An Nisaa 4:32)

Tafsir: Na wala msitamani kile ambacho Allah amewafadhili baadhi yenu kuliko

wengine.

Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea kwa kusema: Aya ambayo tulisema kua

ilishushwa kwa sababu baadhi ya Wanawake walitoa kauli kuhusiana na Allah

kuwapendelea Wanaume katika Urithi. Hivyo Allah ameweka wazi katika ayah hii

kua amewafadhili tu Wanaume juu ya Wanawake kwa sababu Wanaume ni

Wasimamizi wa Wanawake. Kwani ingawa wote Mke na Mume wanafaidika na

matunda na haki zinazotokana na kua pamoja, basi Allah amemuamrisha


69

Mwanamme kumlipa Mwanamke sehemu ya ndoa yao, na kumhudumia katika

mahitaji ya kila siku, hivyo ongezeko la upande mmoja hukabiliana na ongezeko la

upande wa pili – na hivyo hua kama vile hamna pendeleo baina yao. Jambo hili

linaweka wazi mpangilio wa namna zilivyopangika aya.’

Hivyo darja ya Qawwam aliyokua nayo mwanamme kwa familia yake hua ni kuilinda,

kuisimania na kuwahudumia A’al, Ahl, Zawj au familia yake katika hali ya kiuadilifu, na

hapa msimamizi husika hua anatakiwa kuitumia fadhila hiyo aliyopewa na Allah

Subhanah wa Ta’ala, kwa kua na umakini, huruma, busara na subra katika kutekeleza

majukumu hayo, kwani vyenginevyo itakua ni kuenda kinyume na matakwa ya mfadhili

na mtoaji wa majukumu hayo na hivyo Mwanamme husika hupoteza haki ya kua na Darja

hiyo ya Qawwam.

Kwa upande wa pili basi tunaona kua Ayah hii ya Surat al Nisaa 4:34 imetumia pia neno

Hijra kwa kuwapa amri Wanaume wenye sifa ya Qawwam kwa wake zao kufanya Hijra

katika vitanda vya wake zao, pale inapokua Waume hao hawatekelezewi haki zao na

Wake zao wasiokua na utiifu kwao. Hivyo ayah hii inawapa haki Wanaume wenye sifa

ya Qawwam kuwapa adhabu Wake zao hao kwa kuwafanyia Hijra.

Ama juu ya Hijra hii basi kuna mitizamo tofauti kwani kuna wasemao kua Hijra hii

iliyomaanishwa hapa ni Hijra ya kutowaingilia Wanawake kwa muda fulani hadi

watakapojirekebisha. Na pia kuna wasemao kua Hijra hii inaamanisha kua wanaweza

kuwaingilia lakini wajizuie na kuwasemesha, na pia kuwapa mgongo wakati wa kulala

kama ikiwa watalala katika kitanda kimoja. Hizo ni miongoni mwa aina za Hijra

zilizotajwa ndani ya Qurán na ambazo Waislam tunatakiwa kuzifanya kwa kutumia

kiwiliwili katika kipindi cha uhai wetu hapa Ulimwenguni.

Ama tunapozungumzia Hijra ya pili basi hua ni ile ya kuhama kutoka katika hali moja

kuenda katika hali nyengine pia, lakini aina hii ya Hijra hufanywa kwa kutumia njia za

Kiroho, Kinafsi, Kiakili na Kifikra kama vile ambavyo Allah Subhanah wa Taála

alipomwambia Rasul Allah Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua awe na Subra

na anayofanyiwa na Makafiri huku akiwa ni mwenye kuachana nao na kutoshirikiana nao

kwa ukarimu na katika hali nzuri pale aliposema katika Surat Al Muzzamil:-

‏﴿وَٱصْبرِْ‏ عَلَى ٰ مَا يَقُولُونَ‏ وَٱهْجُرْهُمْ‏ هَجْراً‏ جمَِيلاً‏ ﴾

Waisbir AAala ma yaqooloona waohjurhum hajran jameelan (Surat Al Muzzamil

73:10)

Tafsir: Na kua na Subra (Ewe Muhammad) juu ya kile wanachokisema, na achana

nao kwa muachano mwema.


70

Hivyo Hijra hii ya aina ya pili yaani ya Kinafsi na Kiroho ni Hijra ambayo inajumuisha

pia kuhama kutoka katika hali ya kiza cha maasi na kuingia katika hali nyengine iliyo

bora zaidi ambayo ni hali ya kuingia katika Nuru, Muangaza na kua na Utiifu kwa Allah

Subhanah wa Taála na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Hijra ya aina hii ni Hijra ambayo inahimizwa na kutiliwa mkazo zaid kufanywa kwa kila

mmoja miongoni mwetu katika Dini ya Kiislam. Kwani hii hua ni hali ya kujidhibiti na

matamanio ya Nafsi dhidi ya kuiendekeza Dunia na hivyo kuzirudisha Nafsi katika

kumuelekea na kumtii Allah Subhanah wa Taála na Mtume wake Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam.

Umuhimu wa aina hii ya Hijra katika maisha yetu unathibitishwa na malengo ya

Muumba wetu kutuletea Qur’an ili iwe ndio muongozo wa kila kitu katika Maisha yetu

na hivyo kutakiwa kuifanyia kazi kama ipasavyo Qurán bila ya kuihama, kwani kuihama

Qurán hua ni kuenda kinyume na Imani ya Dini ya Kiislam na hivyo tutakua na masuali

ya kujibu mbele ya Mola wetu kama inavyosema Surat Al Furqan:

‏﴿وَقَالَ‏ ٱلر َّسُولُ‏ يٰرَبِّ‏ إِن َّ قَوْمِى ٱتخ ََّذُواْ‏ هَٰذَا ٱلْقُرْآنَ‏ مَهْجُوراً‏ ﴾

Waqala alrrasoolu ya rabbi inna qawmee ittakhadhoo hadha alqur-ana

mahjooran (Surat Al Furqan 25:30)

Tafsir: Na atasema Rasul, Ya Rabbi! Hakika kaumu yangu wameichukulia hii Qurán

kua ni Mahame.

Tunapozungumzia hali ya Qur-ána Mahjuran basi ingawa tunaona kua aya

inawazungumzia watu wa Kabila la Quraysh ambao ndio waliokua wakilalamikiwa

katika ayah hii kua hawakuiamini na waliichukulia Qurán kua ni kama hekaya za kale na

mashairi yasiyokua na maana yeyote. Lakini pia ayah hii inavizungumzia vizazi

vilivyofuatia baadae vikiwemo vizazi vilivyokuja kabla yetu, vizazi vyetu na vizazi

vitakavyokuja baada yetu. Vizazi hivyo ingawa ni vizazi vya Kiislam lakini hua

vimeifanya Qurán kua Mahjuran yaani iliyohamwa kwa njia nyingi sana ikiwemo,

Kutoisoma kabisa, Kuisoma lakini bila ya Kuitafakkar na Kuifaham, Kutochukua jitihada

yeyote ile ya kutaka kuifaham, Kutosimamia maamrisho yake, hukmu zake na Sharia

zilizomo ndani yake, Kutoitilia maanani n.k

Ukweli ni kua Waislam hatutakiwi kua ni wenye kuifanya Qurán kua Mahjuran bali

tunatakiwa Dunia ndio tuifanye kua ni Mahjuran, hivyo tunapaswa kufanya Hijra kutoka

kwenye matamanio ya Dunia na kuhamia ndani ya Qurán na kua ni wenye kufanikiwa

kwa kurudi kwa Mola wetu huku tukiwa ni wenye kufuzu kwa kua na Nyoyo zisizokua

na madoa ndani yake kwani Moyo ndio Msingi wa Mja kumjua Mola wake na hivyo ni

kiungo ambacho kinatakiwa kua kisafi na salama ndani nje na ndio maana Waislam


71

tukawa ni wenye kutiliwa mkazo wa kufanya Hijra ya kuachana na maasi na kurudi chini

ya utiifu wa Allah Subhanah wa Taála.

Kwani Anasema Allah Subhanah wa Taála kua:

‏﴿بَلَى ٰ مَنْ‏ أَسْ‏ لَمَ‏ وَجْهَهُ‏ هلل َِّ‏ وَهُوَ‏ محُْسِ‏ نٌ‏ فَلَهُ‏ أَجْرُهُ‏ عِندَ‏ رَبِّهِ‏ وَلاَ‏ خَوْفٌ‏ عَلَ‏ يْهِمْ‏ وَلاَ‏

هُمْ‏ يحَْزَنُونَ‏ ﴾

Bala man aslama wajhahu lillahi wahuwa muhsinun falahu ajruhu AAinda rabbihi

wala khawfun AAalayhim wala hum yahzanoon (Surat Al Baqar 2:112)

Tafsir: Bali yeyote yule ambae atausalimisha uso wake kwa Allah, akiwa ni mwenye

kufanya mema, basi malipo yake yapo kwa Mola wake na haina haja kwake kua na

khofu wala kua na huzuni.

Bila ya shaka aya iko wazi kua yeyote yule ambae atausalimisha uso wake na akajitolea

kwa ajili ya Mola wake pekee, na akajisafisha a kutokua na uchafu wa dhambi, akawa

Mcha Mungu, akawa ni mwenye I’lm ya kujua kila anachokifanya katika Ibada zake basi

hua ni mwenye kufanya mema katika mambo yake, basi hawatakua na khofu ya kua ni

wenye kufanyiwa Hajar (Kuachwa, au kusahaulika) na Mola wao kwani kwa hakika

Malipo yao watayakuta kwa Mola wao.

Ayah hii pia imetumia neno Wajh yaani Uso kwa sababu uso ndio sehemu muhimu ya

mwili wa Ibn Adam inayoonekana wazi na ndio inayomtambulisha mtu husika mbele ya

watu wengine na hivyo basi katika Lugha ya Kiarabu neno Wajh hua linawakilisha

muonekano wa mwili mzima wa Ibn Adam, na limetumika mara nyingi sana katika

Qurán kumaanisha kiwiliwili cha Ibn Adam.

Ayah hii pia imetumia neno Muhsin (Mwenye kuufanya Mema kwa kumtii Mola wale)

ambalo hua ni lenye kutokana na neno la Kiarabu Ihsan ambalo Kisharia maana yake hua

ni Kumuabudu Allah kama unamuona, na kama humuoni basi yeye anakuona, hivyo mtu

mwenye sifa ya Muhsin hua ni mtu ambae tayari ameshafanya Hijra ya kurudi kwa Mola

wake na hivyo katika kila analolifanya basi hua anamuona Mola wake na hivyo hua

hatakiwi kua na khofu ya kufanyiwa Hajar na Mola wake bali hua na ukaribu zaidi na

Mola wake kwa sababu mtu anapomkaribia Mola wake kwa hatua moja basi Allah

Subhanah wa Taála humkaribia mtu huyo kwa hatua mbili zaid, sasa katika hali kama

hii basi mtu huyu hua ni mwenye kufanya kila anachokifanya kwa Ihsan na hivyo hua ni

Muhsin katika matendo yake na hua ni Muhsin katika hali yake ya Kimaumbile kutokana

na jitihada zake kwa ajili ya Mola wake zinazotokana na muonekano wa nje wa viungo

vya mwili wake unaojumuishwa na Moyo wake na viungo vyengine vya ndani ya mwili

wake.


72

Mujaddid ad Din, Sultan al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaifafanua maana

ya Muhsin iliyotumika katika ayah hii kwa ile hadith isemayo kua:

‏”إِنم ََّا الأَْعْمَالُ‏ ابِلنِّي َّاتِ‏ “

Innama al aAmal bi alniyyati

Tafsir: Uhakika wa Amal hutegemea na nia yake.

Kwa kutuambia kua: Nia hua ni kitu ambacho kinatoka ndani ya kina cha Moyo

kutokana na Ikhlas iliyomo katika tendo jema husika, bila ya kuamua kua na

maamuzi juu ya tendo husika. Kwani siku zote mtu alieshiba kamwe hawezi

kuamua tu na kusema kua sasa hivi nna njaa, na akawa na njaa katika wakati

huo huo kama alivyoamua huku akiwa ameshiba, jambo hili hua haliwezekani,

bali mtu huyu humbidi kutafuta njia ya kukitamani chakula kutoka ndani ya

Moyo wake, na njia hio hujulikana kama Nia Sahih ambayo haipatikani hadi

pale mtu huyu atakapoweza kuuthibitishia Moyo wake na Ufahamu wake.

Hivyo Nia ya Muhsin hutokana na kujua na kufahamu malipo yanayotokana na

kitendo husika, huku kukijumuishwa I’lm iliyokuwemo katika kina cha Moyo

kua Allah Subhanah wa Taála ni mwenye uwezo juu ya kila kitu, na hivyo ndie

mwenye uwezo wa kutoa zawadi au kuadhibu na hakuna mwengine anaeweza

kufanya hivyo isipokua yeye. Kila Uthibitisho huu unapokua mkubwa na kua na

nguvu zaidi katika Nafsi na Moyo wa mtu husika kutokana na I’lm ya kujua

hayo basi ndivyo inavyozidi usafi wa Nia ya mtu husika.

Ama kwa upande wa Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn Muhammad

Al Ghazali basi yeye anasema kuhusiana mambo muhimu yanayohitajika katika

kufanikisha Amali njema za Muhsin ni kua:

1- Kua na Moyo Msafi katika kutekeleza Amali husika.

2- Kua na Ikhlas katika kutekeleza Amali husika.

3- Kuuhudhurisha Moyo na Ufahamu katika kutekeleza wa Amali husika.

4- Kua na Unyenyekevu mbele ya Allah Subhanah wa Taála.

5- Kua na Khofu mbele ya Allah Subhanah wa Taála.

6- Kua na Mapenzi Juu ya Allah Subhanah wa Taála.

7- Kua ni mwenye kuona Haya mbele ya Allah Subhanah wa Taála

8- Kua na Matumaini na kua ni mwenye kumuamini Allah Subhanah wa

Taála.

Ambapo mambo manane hayo hua yanafafanulika kwa kujumuishwa katika hali

zifuatazo:


73

1- Kua na Moyo Msafi na Ikhlas.

2- Kuuhudhurisha Moyo na Ufahamu katika kutekeleza Amali husika.

3- Kua na Unyenyekevu mbele ya Allah Subhanah wa Taála.

4- Kua na Khofu na Mapenzi mbele ya Allah Subhanah wa Taála.

5- Kuaona Haya, kua na Matumaini na Kua ni mwenye Kumtegemea Allah

Subhanah wa Taála baada ya kumaliza Amali husika.

Hujjat Islami Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali

anayafafanua majumuisho hayo kwa kusema kua:

1- Kua na Moyo Msafi na Ikhlas – Hii ni hali ambayo inajumuisha kuusafisha Moyo

kutokana na kua na Maradhi ya Nafsi na kua na Tabia Mbovu, katika hali pia Moyo

inabidi usafishwe na hivyo usiwe na nia au malengo yeyote ya kufanya jema kwa

ajili ya yeyote au chochote isipokua iwe kwa ajili ya Allah Subhanah wa Taála pekee

na hivyo Moyo wa Mtu husika hautakiwi kua na kitu chochote ndani yake isipokua

Muumba wa Moyo huo ambae ni Allah Subhanah wa Taála. Kiasi ya kua athari ya

Ikhlas ndani ya amali zake hua ni yenye kuonekana kuanzia kwenye Moyo wake na

hivyo hua ni zenye kuthibitishika katika kiwiliwili chake katika utekelezaji wa Amali

njema hizo. Ambapo hali ya juu kabisa ya kua na Moyo Msafi na Ikhlasi katika

matendo ya Mja hufikika pale inapokua Mja anafanya mambo mema kwa ajili ya

Mapenzi kwa Mola wake bila ya kutegemea Malipo kutoka kwake wala kua na khofu

au kutaka kuokoka kutokana na adhabu za Mola wake.

2- Kuuhudhurisha Moyo na Ufahamu katika kutekeleza Amali husika – Hii hua ni

ile hali ambayo inajumuisha ufanyaji wa amali njema huku Moyo na ufahamu ukiwa

unaenda sambamba na kauli na vitendo vya Mtu husika. Ambapo hapa hua

tunazungumzia mfumo mzima wa Ufahamu wa mtu katika kujua umuhimu wa jambo

analilofanya huku akiwa ni mwenye kumkumbuka Mola wake kimawazo, kikauli na

kivitendo katika kila hatua ya utekelezaji wa Amali husika.

3- Kua na Unyenyekevu mbele ya Allah Subhanah wa Taála – Hali hii inajumuisha

hali ya Kumnyenyekea, Kumtukuza, Kumkuza, Kumsifu Mola wako.

4- Kua na Khofu na Mapenzi mbele ya Allah Subhanah wa Taála – Hali hii

inajumuisha Al Taqwa (Taqwa), Al Khawf (Khofu) na Al Mahabbah (Mapenzi) kwa

Allah Subhanah wa Taála katika utekelezaji wa Amali husika. Na haya yote hua

yanategemeana na Ilm ya Mja juu ya Uwezo, Ukubwa, Malipo, Adhabu za Mola

wake wake na Wingi wa kasoro zake Mja huyo na wingi wa dhambi zake mbele ya

Mola wake. Kila mtu anaopokua anajua juu ya mambo haya basi ndio Khofu na

Mapenzi yanavyozidi kuongezeka kwa Mola wake.


74

5- Kuona Haya, kua na Matumaini na Kua ni mwenye Kumtegemea Allah

Subhanah wa Taála baada ya kumaliza Amali husika – Hali hii hua inajumuisha

Al Raja (Matumaini) na Tawakkul (kumtegemea Allah Subhanah wa Taála tu katika

kila kitu) baada ya kumaliza kutekeleza Amali husika. Kwani Mja anatakiwa kua ni

mwenye kuona haya kutokana na kua na kasoro nyingi katika Matendo yake na hivyo

anatakiwa kua na khofu ya kutokukubaliwa kwa Amali zake njema, lakini hapo hapo

anatakiwa kua ni mwenye kumtegemea Allah Subhanah wa Taála na kua na

matumaini kua atamkubalia amali njema zake hizo.

Ili kufahamu juu ya Hijra inayompelekea Mja kua na sifa ya Muhsin, basi na tuangalie

Maumbile ya Moyo ambacho ni kiungo kinachohusika moja kwa moja na utayarishaji

wa uthibitisho wa mtu husika kufanya Hijra kutoka katika hali ya kua ni mtu wa kawaida

na kuingia kuingia katika hali hio ya Muhsin, kwani tofauti na tunavyodhani sisi mimi na

wewe kua Moyo ni Moyo yaani ni Al Qalb, lakini tunapoiangalia Qurán basi tunaona

kua Moyo ni kiungo muhimu kilichogawika katika hali nne za darja tofauti kulingana na

mazingira ya Maumbile yake kama zilivyotajwa na Allah Subhanah wa Taála ndani ya

Qurán ambazo ni Al Qalb, Al Fuad, Al Lub na Al Sadr.

MAUMBILE YA NYOYO ZA IBN ADAM: AL QALB, AL FUAD, AL

LUBB, AL SADR NA AN NAFS KATIKA QURÁN

Maamrisho yote ya Dini ya Kiislam na Hukmu zake yamewekwa na Allah Subhnaha wa

Taála kwa ajili ya kusimamia Maslahi ya kila kiumbe kilichopo Ulimwenguni, lakini

Maslahi hayo huwezi kuyaona hadi pale utakapoisoma Dini ya Kiislam na kuifaham kwa

kutumia ufahamu wa Moyo na hapo ndipo utakapohisi athari zake ndani ya mwili wako

na pia ndipo utakapopata mantiki ya maamrisho hayo kama isemavyo aya ifuatayo ya

Surat Az Zumar ambao tushaiangalia katika Utangulizi:

‏﴿ٱهلل َُّ‏ نَز َّلَ‏ أَحْسَنَ‏ ٱلحَْدِيثِ‏ كِتَاابً‏ م ُّتَشَاهبِ‏ اً‏ م َّثَانىِ‏ َ تَقْشَعِر ُّ مِنْهُ‏ جُلُودُ‏ ٱل َّذِينَ‏ يخَْشَوْنَ‏

رَب َّهُمْ‏ ثمُ َّ تَلِينُ‏ جُلُودُهُمْ‏ وَقُلُوبُهُمْ‏ إِلىَٰ‏ ذِكْرِ‏ ٱهلل َِّ‏ ‏ٰذلِكَ‏ هُدَى ٱهلل َِّ‏ يَهْدِى بِهِ‏ مَن

يَشَآءُ‏ وَمَن يُضْلِلِ‏ ٱهلل َُّ‏ فَمَا لَهُ‏ مِنْ‏ هَادٍ‏ ﴾

Allahu nazzala ahsana alhadeethi kitaban mutashabihan mathaniya taqshaAAirru

minhu juloodu alladheena yakhshawna rabbahum thumma taleenu julooduhum


75

waquloobuhum ila dhikri Allahi dhalika huda Allahi yahdee bihi man yashao

waman yudhlili Allahu fama lahu min hadin (Surat Az Zumar 39:23)

Tafsir: Allahu ameshusha hadithi bora kabisa, Kitabu (Quran) chenye sehemu ndani

yake zinazofanana kwa wema na usahih. Ngozi za wale wenye kuomuogopa Allah

zinatetemeka (Wanapoisikia Qurán). Na kisha Nyoyo zao na ngozi zao hulainika

kutokana na kumkumbuka Mola wao. Huo ni Uongofu wa Allah. Ambae humuongoza

amtakae na anaepotoshwa na Allah basi hakuna atakaemuongoza.

Naam aya zimesema hivyo kwa sababu Moyo una maumbile ya kua ni kiungo kikamilifu

kinachojitegemea na hivyo kua na ufahamu wake na maamuzi yake yasiyotegemeana na

kiuongo chochote mwilini, na ndio maana Allah Subhanaha wa Taála akawa

ameuzungumzia Moyo katika hali tofauti na mara nyingi sana katika kitabu chake

kitukufu cha Qurán, hivyo na tuanze kwa kuangalia maana na matumizi ya neno Qalb

kama lilivyotumiwa katika Qur’an.

AL QALB

Neno Qalaba kwa Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kugeuka, Kugeuza kitu Juu Chini

au Mbele Nyuma au Ndani Nje, Kubadilisha, Kubadilika Hali au Muelekeo,

Kubadilishana Mmoja baada ya Mwengine. Neno Qalaba ndio lililotoa neno Qulub

ambalo maana yake hua ni Moyo, na tunapoiangalia Qurán basi tunaona kua imetumia

neno Qalaba mara 168 katika hali tofauti ikiwemo katika hali ya neno Qulubu ambalo

ndio lililotumika katika aya ya Surat Al Araf pale Allah Subhanah wa Ta’ala aliposema:

ن َّ ‏﴿وَلَقَدْذَرَأَْلجَِه مَكَثِير اًمِّنَ‏ ٱلجِْنِّ‏ وَٱلإِنْسِ‏ لهَُمْ‏ قُلُوبٌ‏ لا َّ يَفْقَهُونَ‏ هبَِ‏ ا وَلهَُمْ‏ أَعْينُ‏ ٌ

لا َّ يُبْصِرُونَ‏ هبَِا وَلهَُمْ‏ آذَانٌ‏ لا َّ يَسْمَعُونَ‏ هبَِآ أُوْلَٰئِكَ‏ كَٱلأَنْعَامِ‏ بَلْ‏ هُمْ‏ أَضَل ُّ أُوْلَٰئِ‏ كَ‏

هُمُ‏ ٱلْغَافِلُونَ‏ ﴾

Walaqad dhara/na lijahannama kathiiran mina aljinni waal-insi lahum quloobun

la yafqahoona biha walahum aAAyunun la yubsiroona biha walahum adhanun la

yasmaAAoona biha ola-ika kaal-anAAami bal hum adhallu ola-ika humu

alghafiloona (Surat Al Araf 7:179)


76

Tafsir: Na kwa hakika tumewaumba kwa ajili ya Jahannam wengi miongoni mwa

Majini na Watu. Wana nyoyo ambazo hawafahamu kutokana nazo, wana macho

ambayo hawaoni kutokana nayo, na wana masikio lakini hawasikii. Wao wako kama

Ngo’mbe lakini wao wamedhalilika zaidi, kwani hawa ndio wale ambao wamekubwa

na Mghafiliko.

Naam tunapoiangalia aya hii basi tunaona kua imetumia maneno yasemayo Walaqad

Dhara/na Li Jahannama yaani Na kwa hakika Tumewaumba kwa ajili ya Jahannam na

neno kwa ajili ya Jahannam limeunganishwa na harfu Laam. Ambayo ni Laam tofauti na

ile Laam ya LiyaAAbuduuni iliyotumika katika aya ifuatayo:

‏﴿وَمَا خَلَقْتُ‏ ٱلجِْن َّ وَٱلإِنسَ‏ إِلا َّ لِيَعْبُدُونِ‏ ﴾

Wama khalaqtu aljinna waal-insa illa liyaAAbudooni (Surat Adh Dhariyyat 51:56)

Tafsir: Sikuwaumba Majini na Ibn Adam isipokua kwa ajili ya kuniabudu mimi tu.!

Kwani Laam iliyotumika katika aya Surat Adh Dhurriyat 51:56 yaani Laam ya

LiyaAabuduuni hua inajulikana kama Laam Al Ghaayah yaani Laam inayoweka wazi

Kusudio la Kitu Fulani na Laam iliyotumika katika aya yetu ya Surat Al Aaraf 7:179

ambayo ni Laam ya Li Jahannama inajulikana kama Laam al Aqibah yaani Laam

inayoweka wazi kinachobakia baada ya tukio fulani.

Na ijapokua Wanazuoni wengi wanasema kua Laam zote mbili katika aya hizi ni Laam

Al Ghayah, lakini Laam ya LiyaAabuduuni hua pia inahesabika kua ni Laam al Tashrii

yaani Lam ya Kisharia wakati Laam ya Li Jahannama inahesabika kua ni Laam Al

Takwini yaani Laam ya Mfumo wa Kimaumbile.

Hivyo basi Laam iliotumika katika Li Jahannama ambayo ni Laam al Aqibah na hapo

hapo ikawa ni Lam Al Takwin imetumika ili kuweka wazi kua kutokana na Maumbile

yao viumbe viwili hivi yaani Ibn Adam na Majini basi wengi wataghafilika na

watashindwa kujizuia na matamanio ya Nafsi zao na hivyo kushindwa kwao kuzitumia

ipasavyo neema za Viungo hivyo walivyopewa na Mola wao ambavyo ni Macho,

Masikio na Nyoyo zao basi kutapelekea kutokea tukio la kuingizwa Motoni kwa wengi

miongoni mwao kutokana na makosa ya kutovitumia ipasavyo viungo hivyo kwa

kutokana na kughafilika, na ingawa kughafilika ni sehemu ya Maumbile ya Ibn Adam,

lakini hata hivyo hakuna Kughafilika kubaya kama kughafilika juu ya Mola Wako

aliekuumba!…Allahuma ajirna minna Naar!..Aamiin!


77

Hivyo tuungalie maumbile ya Al Qalb kulingana na mtizamo wa Kisayansi ili tupate

kujua kwani nini Allah Subhanah wa Ta’ala akasema:

‏﴿لهَُمْ‏ قُلُوبٌ‏ لا َّ يَفْقَهُونَ‏ هبَِا﴾‏

Lahum quloobun la yafqahoona biha – Wana Nyoyo Lakini hawafahamu kutokana

na Nyoyo hizo!

Mara nyingi sana Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qurán amekinasibisha kiungo cha

Moyo na Kuona, Kufaham na Kutafakkari pia kwa sababu kimaumbile Moyo ni kiungo

cha mwili ambacho kinajitegemea kwa kua na ufaham wenye nguvu ya upekee katika

mwili mzima wa Ibn Adam. Ufahamu wa Moyo wa Ibn Adam hua unafanya kazi zake

kimaumbile kwa kuishirikisha mifumo mikuu minne ya usafirishaji wa nguvu za hisia za

mwili wa Ibn Adam ambazo ni:

1- Mfumo wa Usambazaji wa hisia za sehemu tofauti za mwili.

2- Mfumo wa Viasili vinavyodhibiti maumbile ya ufanyaji kazi wa mwili

vinavyozalishwa na Moyo.

3- Mfumo wa Usambazaji Kemikali kupitia katika mapigo ya Moyo na

usambazaji Damu.

4- Mfumo wa Uzalishaji Nguvu za Kimaumbile za mwili za ufanyaji kazi wa

viungo vya Ibn Adam na nguvu za Mawimbi ya Mvutano wa Umeme wa

Sumaku za ndani ya Mwili na nje ya Mwili.

Kimaumbile Moyo wa Ibn Adam hua na uwezo wa kuzalisha nguvu za umeme zenye

asili ya mawimbi ya sumaku zenye nguvu mara 5000 zaid na nguvu kama hizo

zinazozalishwa na Ubongo wa Ibn Adam, nguvu hizo ambazo pia huweza kuhisika hata

nje ya mwili wa Ibn Adam kwa takriban umbali wa mita 3 hua na uwezo wa kusambaza

na kupokea na kuwasiliana na hisia mbali mbali kutoka katika ubongo wa mtu husika na

sehemu nyengine za mwili mzima wa mtu huyo na wakati huo hua na uwezo wa

kuwasiliana na nguvu zinazozalishwa na watu wengine zaidi ya wanane waliopo karibu

nae na hivyo hua na uwezo wa kuwaathiri watu hao walio karibu nawe kihisia.

Nguvu hizi zinazozalishwa na Moyo pia huweza kuwasiliana kihisia na kuathiri nguvu

za mvutano wa mawimbi ya umeme ya viumbe wengine waliokuwepo karibu yake mtu

ikiwemo Wanyama na Viumbe wengine wasioonekana wa Ulimwengu wa Al Ghayb. Na

ndio maana baadhi wakati mtu anaweza akakaa peke yake na ghafla akahisi kama mwili

unamsisimka, kwa sababu nguvu hizi za kimaumbile za Moyo hua na uwezo wa kuhisi

kutokea kuwepo kwa Viumbe wengine wasioonekana kama vile Majini ambao wao


78

Maumbile yao yana asili za nguvu hizi. Na ni kutokana na athari ya nguvu hizi ndio

Viumbe Majini hua na uwezo wa aidha kuwadhibiti Ibn Adam au kuwaogopa na

kuwakimbia Ibn Adam.

Moyo wa Ibn Adam una nyuroni 40000 ambazo kwa pamoja hua zinaunda kitu

kinachoitwa Akili ya Moyo, ambayo hua ni yenye uwezo wa kukumbuka kwa muda fupi

na kwa mda mrefu, kujifunza na kufanya maamuzi yake wenyewe bila kuitegemea akili

na hivyo hua na uwezo wa kuyadhibiti mapigo ya Moyo, athari ya Ufahamu wa Moyo

hua na uwezo wa kuubadilisha hata mtizamo wa ufahamu wa akili kihisia na kimaamuzi

katika mambo mbali mbali.

Kila Moyo unapopiga basi hua ni wenye kuzalisha nguvu za mawimbi ya umeme wa

sumaku na hivyo kusababisha athari mbali mbali za Moyo ikiwemo kuona kwa mtizamo

wa Jicho la Moyo, kuhisi kwa hisia za Moyo, ambapo hisia zote hizi zinapotokea ndani

ya Moyo hua zina athari kubwa zaidi ndani ya mwili wa Ibn Adam na zinazotofautiana

sana na zile zenye kutokea moja kwa moja kupitia katika akili ya Ibn Adam, ambapo

mawasiliano kutoka kwenye Moyo kuelekea kwenye Akili hua ni maradufu zaidi yana

umuhimu zaidi kwa ufanyaji kazi wa Mwili kuliko mawasliano ya kutoka kwenye Akili

kuelekea kwenye Moyo.

Hii inaonekana wazi pale Moyo unapobadilika hali yake kulingana na hisia na vitendo

tofauti vinavyosababishwa na ufaham wa akili na hivyo kuufanya Mwili wa Ibn Adam

kua dhaifu na kuishiwa nguvu, kwa mfano Ibn Adam anapokua na hasira, wasiwasi

mkubwa, mawazo mengi au khofu basi hali ya mapigo ya Moyo hubadilika na hivyo

hufanya mawasiliano na akili ambayo nayo baada ya kupata mawasiliano hayo basi hua

ni yenye kujua kua kuna hisia ambazo sio nzuri kwenye Moyo na mwili mzima kwa

ujumla na hivyo kusababisha akili kupungukiwa na uwezo wake wa kufanya kazi kwa

umakini na kufikiria ipasavyo.

Na hivyo kila Ibn Adam akiwa na hali kama hio mara kwa mara basi Moyo wake

hudhooofika, jambo ambalo hupelekea na viungo vyengine muhimu vya mwili

kudhoofika ikiwemo, Mafigo, Ini, Mapafu n.k na kusababisha madhara makubwa sana

mwilini ikiwemo mshtuko wa Moyo.

Mbali ya kua ni Moyo hua ni wenye nguvu za umeme zenye asili ya mawimbi ya sumaku

lakini pia hua ni wenye kusababisha uzalishwaji wa kemikali ambazo husababisha hisia

nzuri kwa Ibn Adam zikiwemo zile zinazojulikana kama Dopamine,Oxytocin,

Endorphines, Seratonin, n.k ambazo hua na jukumu la kukamilisha sifa ya maumbile ya

asili ya kila mtu yanayotokana na maana ya neno Al Ins. Neno Al Ins linatokana na neno

Anisa ambalo maana yake hua ni kua na Mazoea, Kupenda, Kua na Umoja kijamii, au

Kushikamana pamoja.


79

Hivyo Mtu ameitwa Insan kwa Lugha ya Kiarabu kwa sababu neno hilo hua linamaanisha

Kiumbe ambae Maumbile ya mwili wake yana sifa ya kuzalisha kemikali za Dopamine

na Oxytocin zinazosimamia hisia za Mapenzi, Matamanio, Mshikamano, Kusaidiana,

Kuhurumiana, n.k baina ya Mke na Mume, Baba na Mama, Kaka na Dada, Ndugu na

Familia, n.k kulingana na uhusiano wa hali ya hisia hizo zinazosababishwa kuzalishwa

kutokana na nguvu na uwezo wa Moyo na pia Ubongo wa Ibn Adam.

Kwani tunapozungumzia Oxytocin basi hua tunazungumzia kemikali ambazo kimaarufu

hua zinajulikana kama kemikali za ‘Mapenzi na Uaminifu’ na huzalishwa ndani ya miili

yetu baada ya kupatikana hisia zinazotokana na ufanyaji kazi wa viungo vya hisia za

Mwili za Kuona, Kusikia Sauti, Kuhisi Harufu au Kugusana na hivyo hutupelekea kua

na hali ya kujisikia kua na Raha, Upendo, Utulivu, Usalama, Amani pale tunapokua

karibu na wale tunaowapenda na hivyo kutuzidishia hisia za kutotaka kukosana au

kuachana na watu hao na kuwapenda, kuwajali, kuwafanyia ukarimu na kuwaonea

huruma.

Kemikali za Oxytocin pia hua ndizo zinazosimamia jukumu la kuvitayarisha viungo vya

mwili wa Mwanamme na Mwanamke katika kuingiliana kimwili, kwa ajili ya kuendeleza

vizazi na pia kwa ajili ya kuupa utulivu na kuupumzisha mwili kwa kuupa hisia za Raha

inayotokana na kitendo cha kuingiliana kimwili, ambayo hutegemeana na wingi wa

uzalishwaji wa Oxytocin kwani kila zinavyozidi kuzalishwa kwa wingi zaidi katika

wakati wa tendo hilo basi ndio inavyozidi kupatikana hisia za Raha ambayo haina mfano

wake katika tendo hilo kama anavyoelezea Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu

Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali pale aliposema kua:

‘Raha ya mda mfupi inayopatikana katika kuingiliana kimwili basi hua ni Raha

ambayo kamwe haiwezi kufananishwa na Raha nyengine, na kama ingekua ni yenye

kudumu basi ingekua ni moja kati ya dalili ya moja kati ya Raha za Milele

tulizoahidiwa Peponi’

Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali anatufafanulia zaidi pale aliposema: ‘Hikma ya Allah Subhanah wa

Ta’ala na Rehma zake zinaonekana pale unapoangalia katika kuweka Matamanio ya aina

aina mbili katika Maisha yetu. Matamanio ya kwanza ni ya muonekano wa kimaisha wa nje

pale mtu anapokua anaendeleza kizazi chake kupitia kwa watoto wake. Na muonekano wa

pili ni wa muonekano wa kimaisha ya ndani unaohusiana na maisha ya baadae kesho

Akhera. Kwani raha ya kuingiliana kimwili hua si yenye kudumu katika ulimwengu huu na

ni lazima iwe ni ya mda mfupi, na yenye kikomo kwa kumalizika mara tu baada ya kuihisi

raha hio kiasi ya kua humpelekea Ibn Adam kua na hamu ya kutaka raha hio iwe ni yenye

kudumu, na hivyo hii humfanya Ibn Adam kua ni mwenye kudumu katika Mema kiibada

ambayo yatampelekea kupata Raha kama hizo milele.’


80

Allah Subhanah wa Ta’ala anaelezea Miujiza ya ufanyaji kazi wa Oxytocin katika

maumbile yetu ambazo kuzalishwa kwake kunasababishwa na Moyo na Ubongo na

kutusababishia kua na hali ya Upendo na Utulivu baina yetu katika maisha yetu

aliposema:

‏﴿وَمِنْ‏ آَتِهِ‏ أَنْ‏ خَلَقَ‏ لَكُم مِّنْ‏ أَنفُسِ‏ كُمْ‏ أَزْوَاجاً‏ لِّتَسْكُنُو ۤ اْ‏ إِلَيْهَا وَجَعَلَ‏ بَيْنَكُ‏ م

م َّوَد َّةً‏ وَرَحمَْةً‏ إِن َّ فىِ‏ ذٰلِ‏ كََ‏ لآَتٍ‏ لِّقَوْمٍ‏ يَتَفَك َّرُونَ‏ ﴾

Wamin ayatihi an khalaqa lakum min anfusikum azwajan litaskunoo ilayha

wajaAAala baynakum mawaddatan warahmatan inna fee Dhalika laayatin

liqawmin yatafakkaroona (Surat Rum 30:21)

Tafsir: Na miongoni mwa alama zake ni kukuumbieni wake kwa ajili yenu kutoka

miongoni mwenu, ili mpate utulivu pamoja nao, na akakuwekeeni baina yenu mapenzi

na rehma. Kwa hakika katika hili kuna dalili kwa wale wenye kutafakkar.

Aya inatuwekea wazi kua: ‘Miongoni mwa Dalili za Utukufu, Uwezo na Rehma

kubwa za Allah Subhanah wa Ta’ala juu yetu ni kutujaalia Ibn Adam kua wa aina

moja lakini hapo hapo kua ni wenye maumbile mawili tofauti baina yetu kwani

kuna umbo la kijinsia ya Kiume na jinsia ya Kike, ambapo mbali ya kua kuna

utofauti wa Muonekano mzuri na wa kuvutia wa Umbo la nje baina ya jinsia mbili

hizo lakini pia kuna utofauti wa maumbile ya ndani ya miili katika mifumo ya

kiufanyaji kazi, kuanzia katika mfumo wa Hisia, Ufaham, Akili, Uzazi n.k.

Tofauti zote hizo za kimaumbile ni kwa ajili ya kutufanya kua ni wenye kuendana,

kuvaana, kutegemeana katika kutimiziana mahitaji ya kimwili na hivyo kua ni

wenye kupata utulivu wa nafsi zetu unaopatikana kutoka ndani ya uhusiano

unaokubalika kisharia na Allah Subhanah wa Ta’ala baina ya jinsia mbili hizo za

Kiume na Kike kwa ajili ya kuendeleza kizazi na pia kuistarehesha miili yetu na

akili zetu na hivyo ndani ya uhusiano huo kupatikana Furaha, Mapenzi, Huruma

na kutakiana mema baina ya Mume na Mke.’

Kwa upande mwengine basi, kemikali za Oxytocin zinapozalishwa na kuachiwa ndani ya

mwili wa Mwanamke basi hua pia ni zenye kuzidisha mtetemeko wa kizazi cha

mwanamke na hivyo kurahisisha manii ya Mwanamme kulifikia yai la Mwanamke na pia

hua ni zenye kuutayarisha mwili wa Mwanamke pale anapotaka kujifungua na kupelekea

kutanuka kwa njia ya Uzazi pale Mtoto anapotaka kuzaliwa na pia ndio zenye

kusababisha utayarishaji wa Maziwa baada ya mtoto kuzaliwa na kua tayari kwa ajili ya

kunyonya maziwa.


81

Ama kwa upande wa Dopamine basi inapozalishwa hua ni yenye kutupelekea kua na

hamu, ari maamuzi ya kutekeleza na kutimiza mahitaji yetu kijamii na matamanio yetu

kimaumbile na kihisia na hivyo hua inajulikana pia kama kemikali inayochangia

kuchochea kupatikana kwa hisia za kujisikia raha na hivyo kutupeleka kutaka kuongeza

bidii zaidi juu ya jambo lililotupa raha au manufaa na hivyo kua ni wenye kuridhika

kutokana na kutimiza malengo, mahitaji na matamanio yetu. Dopamine pia hua na

jukumu la kuhifadhi kumbukumbu ndani ya Ubongo, kusababisha umakini wa mtu katika

jambo husika, n.k

Hivyo basi Dopamine na Oxytocin hua ni zenye kufanya kazi pamoja sambamba ili

kuimarisha mshikamno wa uhusiano baina ya Mume na Mke, Kifamilia na Kijamii, n.k

kiasi ya kua Dopamine inapokosekana au inapokua imezalishwa kidogo basi hata kama

Oxytocin itazalishwe kwa wingi peke yake haitowezi kusababisha mshikamano huo

unaotakiwa kupatikana ili kua na ukaribu baina yetu na pia inapokosekana Oxytocin basi

Dopamine peke yake haiwezi kusababisha mshikamano huo.

Kwa upande wa Seratonin basi hua ni zenye kumfanya mtu kuuona Umuhimu na thamani

yake katika jamii au familia husika, hivyo Seratonin inapokua haijazalishwa mwilini basi

mtu husika hua ni mweye kujisikia mpweke na mwenye huzuni, mfano mtu

unaposhukuriwa baada ya kufanya jambo fulani basi shukrani hio husababishia

uzalishwaji wa Seratonin katika mwili na kumfanya mhusika awe ni mwenye kuridhika

kuona kua ni mwenye thamani na kukubalika, kwa sababu shukrani hua ni hali ya hisia

ya Moyo kuonesha kukubali thamani ya jambo jema ulilofanyiwa kutoka ndani ya moyo

wa mtu uliemfanyia wema huo.

Hivyo ushirikiano baina ya kemikali hizi za Oxytocin, Dopamine, Seratonin n.k ambazo

kuzalishwa kwake kunategemeana na mfumo wa ufanyaji kazi wa Moyo basi ndio

unaopelekea kuwepo kwa maingiliano ya watu na mshikamano katika Kifamilia na

Kijamii na hivyo huwapelekea watu unapowakosea kusema: ‘Ah unanitia uchungu ndani

ya Moyo!’ au unapowaambia maneno Qawlan Sadida basi husema ‘Maneno yako

yananigusa ndani ya Moyo!’ au ‘Hakika Mimi nampenda fulani kwa Moyo wangu wote’

n.k.

Hivyo ukweli ni kua Ibn Adam hua anautaja Moyo pale anapoathiriwa sana na kitu fulani

na hii ni kwa sababu kama kuhisi basi kabla ya kuhisi kwa ufahamu wa akili na Ubongo

basi kiungo kinachohisi kwanza hua ni Moyo, yaani hali ya hisia husika huanzia kwenye

Macho, au Masikio ambayo hupeleka habari kwenye Ubongo ambapo Ubongo nao

hutuma habari kwenye Moyo kisha Moyo hutoa maamuzi sahih juu ya jambo husika kwa

aidha kuzidisha kasi au kuyawacha katika hali yake ya kawaida mapigo ya Moyo na

sambamba hapo hapo Moyo hutoa habari zinazopelekea kuzalisha kemikali na

zinazosababisha mwili wa Ibn Adam kuchukua hatua stahiki kwa ajili ya jambo husika,

iwe kulia, kucheka, kupenda, kuchukia, kupigana, kukimbia, n.k.


82

Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anasema kua: ‘Al Qalb na Fuad

vinahifadhiwa ndani ya Sadr, hivyo Fuad inajumuisha Moyo mzima ambao

unajumuisha mishipa ya damu. Hivyo Qalb hua ni sehemu ambayo ndio kiti cha

hisia mbali mbali za upendo, chuki, hasira, ufahamu, n.k.’

Kwa upande mwengine basi tunaona kua Al Qalb yaani Moyo pia hua ni wenye uwezo

wa kuhifadhi hisia hizo na kukumbuka ndani yake tena kwa mda mrefu pia kama vile

ilivyokua kwa upande wa Ubongo, Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala

akatuelezea katika aya ifuatayo kwa kutuambia kua:

‏﴿ٱ ل َّ ذِي نَآ مَنُواْ‏ وَتَطْمَئِن ُّ قُلُوبُهُمْ‏ بِذِكْرِ‏ ٱهلل َِّ‏ أَلاَ‏ بِذِكْرِ‏ ٱهلل َِّ‏ تَطْمَئِن ُّ ٱلْقُلُ‏ وبُ‏ ﴾

Alladheena amanoo watatma-innu quloobuhum bidhikri Allahi ala bidhikri Allahi

tatma-innu alquloobu (Surat Ar Rad 13:28)

Tafsir: Wale wenye kuamini, na ambao nyoyo zao zinapata utulivu kutokana na

kumkumbuka Allah. Kwani ni katika kumkumbuka Allah ndio Nyoyo hupata utulivu.

Aya hii imekiambatanisha kiungo cha Moyo wa Ibn Adam na Hisia za Kufaham na

Kukumbuka kwani, imetumia maneno mawili ambayo ni Al Qalb liliopo katika hali ya

wingi ambalo ni Qulubu na kisha ikatumia neno Dhikri lenye kumaanisha Kukumbuka,

Kuhifadhi au kuweka kwenye Ufahamu, Kuonya, Kusifu, Kutukuza n.k hivyo aya

inaweka wazi Maumbile ya hali ya Utulivu unaopatikana ndani ya Moyo na Ufahamu

wake kutokana na Moyo husika kua na kumbukumbu ya kumkumbuka Allah Subhanah

wa Ta’ala. Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema tena kumwambia Mtume

wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

‏﴿إِن َّ فىِ‏ ذٰلِ‏ كََ‏ لآيَةً‏ وَمَا كَانَ‏ أَكْثَرُهُم م ُّؤْمِنِينَ۞‏ وَإِن َّ رَب َّكَ‏ لهَُوَ‏ ٱلْعَزِ‏ يزُ‏ ٱلر َّحِ‏ يمُ۞‏

وَإِن َّهُ‏ لَتَنزِيلُ‏ رَبِّ‏ ٱلْعَالَمِينَ۞‏

نَزَلَ‏ بِهِ‏ ٱلر ُّوحُ‏ ٱلأَمِينُ۞‏

عَلَى ٰ قَْلبِكَ‏ لِتَكُونَ‏ مِ‏ ‏َن

ٱلْمُنْذِرِينَ۞‏ بِلِسَانٍ‏ عَرَبيِ‏ ّ ٍ م ُّبِينٍ۞‏ وَإِن َّهُ‏ لَفِى زُبُرِ‏ ٱلأَو َّلِينَ‏ ﴾

Wa-inna rabbaka lahuwa alAAazeezu alrraheemu, Wa-innahu latanzeelu rabbi

alAAalameena; Nazala bihi alrroohu al-ameenu; AAala qalbika litakoona mina

almundhireena; Bilisanin AAarabiyyin mubeenin; Wa-innahu lafee zuburi alawwaleena;

(Surat Shu-ara 26: 191-196)


83

Tafsir: Na kwa hakika Mola wako ni Mwenye uwezo Mkubwa na ni Mwingi wa Rehma,

Na ka hakika hii (Qur’an)ni teremsho kutoka kwa Mola wa Ulimwengu wote.

Imeteremshwa kupitia kwa Ruhi Al Amiin (Malaika Jibril), Kwenye Moyo wako (Ewe

Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) Ili uwe ni mwenye kuonya. Kupitia katika

Lugha ya Kiarabu iliyowazi kabisa. Na Hii (Qur’an) imo ndani ya maandiko

(Zaburi, Tawrat na Injil) yaliyotangulia.

Hivyo kutajwa kwa Moyo katika ayah hii kua Qur’an imeteremshwa na kua ni kama

iliyogongwa muhuri kwenye Moyo wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ili isitoke,

kunatilia mkazo umuhimu wa kiungo hicho cha Al Qalb katika kuhifadhi kumbukumbu

kwake, kiasi ya kua aya imetoa kipaumbele zaidi kwa Ufahamu wa Moyo kuliko kwa

Ufahamu wa Ubongo na Akili.

Wanasayansi wamethibitisha haya ya kua Moyo unahifadhi kumbukumbu pale

walipofanya upasuaji wa upandikizaji wa Moyo uliofanyika mnamo mwaka 1988 nchini

Marekani kwa mgonjwa wa Moyo aitwae Claire ambae alipandikizwa Moyo na kisha

baadae aliandika kitabu Mabadilio ya Moyo ambacho ndani yake anaelezea yaliyomkuta

baada ya upandikizwaji wake huo wa Moyo kua alianza kupenda kunywa vilevi na

vyakula visivyokua na lishe na mambo mengine mengi ambayo yanayopendwa kufanya

na vijana walio tofauti na rika lake, kwani yeye alikua ni mtu mzima anaekaribia miaka

45-50 hivyo alikua hapendi kuyafanya mambo ya ujana ambayo keshayapita tayari kabla

ya kufanyiwa upadikizaji huo wa Moyo, yaani alibadilika tabia zake zote. Na kufikia

wakati ikawa anaota wazi wazi kua ana uhusiano wa kimapenzi na kijana mdogo kwake

kiumri wa Kiume aitwae Timothy. Claire alikua akihisi hisia za mapenzi makubwa sana

juu ya kijana huyu ambae hata hivyo alikua hamjui wala hajawahi kumuona katika

maisha yake, kwani yeye alikua akimuona ndotoni tu.

Hivyo Claire akaamua kufanya uchunguzi ambapo akagundua kua Moyo wake

aliopandikizwa ulikua ni wa Mtu aliekwisha fariki ambae alikua akijulikana kwa jina la

Timothy. Alipofuatilia kwa kina na kukutana na wazazi wa Timothy basi alithibitisha

kua kijana huyo ndie aliekua akimuona ndotoni pale alipooneshwa picha ya Timothy na

wazee wake, na wazee nao wakathibitisha kua Timothy ambae alifarikia akiwa na umri

wa miaka 18 alikua ni mwenye kupenda vilevi na vyakula vyote ambavyo Claire alikua

havipendi lakini akaanza kuvipenda baada ya kupandikizwa Moyo wa Timothy.

Mfano mwengine ni wa Mwanamme aitwae Graham wa Marekani pia ambae nae baada

ya kupandikizwa Moyo wa mtu mwengine basi akaanza kua na hisia za mapenzi na

Mwanamke aitwae Cheryl ambae alikua ni Mjane wa Mtu ambae alifariki baada ya kujiua

kwa kujipiga risasi na hivyo Moyo wake ukapandikizwa kwa Graham ambae alikua na

matatizo ya Moyo wake. Baada ya kupandikizwa na kutoka hospitali basi Graham

akamuoa Cheryl, ndoa ambayo ilidumu kwa miaka 12 kisha baada ya hapo, Graham


84

akajiua kwa kujipiga risasi kama alivyofanya yule mume wa mwanzo wa Cheryl ambae

Moyo wake ulipandikizwa kwa Graham.

Vile vile kuna mfano wa Professor wa Marekani aitwae Benjamin ambae nae alikua na

matatizo ya Moyo na mara tu baada ya kubadilishwa Moyo wake nakufanyiwa

upandikizwaji basi akawa ni mweye kuota ndoto zenye kutisha, kwani alikua anaota kua

anapigwa na Radi ambayo inamuunguza na kufikia kuuhisi ujuoto wa moto wake.

Professor Benjamin hakumwambia mtu yeyote juu ya ndoto hii isipokua Mke wake,

ambae nao akamuelezea Mke wa alietolewa Moyo huo baada ya kufariki kwake, na hivyo

Mke huyo akashtuka na akathibitisha kua mume wake alipigwa na Radi na baada ya

kupigwa na radi hio basi alifariki hapo hapo.

Ingawa huo ni mtizamo wa Kisayansi juu ya moyo na Maumbile yake tunapozungumzia

kuhusiana na Maumbile ya Moyo, lakini tunaporudi katika mtizamo wa I’lm ya Dini ya

Kiislam kupitia katika aya za Qurán basi tunaona kua: Mujaddid ad Din Hujjat ul Islami

Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhmmad Al Ghazali katika Ihya

Ulum Ad Din kua: ‘Al Qalb una sifa ya Latifah (Ni wenye uwezo na Sifa ya Kuona na

Kufaham mambo ambayo hayako wazi) na Rabbaniyyah (Utukufu wa Kimungu) na

Kiroho na ndio asili ya Ibn Adam. Al Qalb katika mwili wa Ibn Adam hua ni kiungo

kinachofaham, kinachotafakkari, kinachozingatia, kinachozungumziwa pale

unapozungumza na mtu, ndicho kinachoadhibu, ndicho kinacholaumu na ndio

kinachobeba Majukumu yote ya Ibn Adam. Al Qalb ni kama Mfalme wa mwili na

viungo vyengine ni kama Askari na wasaidizi’

Imam al Ghazali anaendelea kusema kua: ‘Heshima na Utukufu wa Ibn Adam, ambao

unawapita Viumbe wote walioumbwa na Allah Subhanah wa Taála unatokana na

Kumjua Allah Subhanah wa Taála, Al Qalb ni ndio unaojumuisha Ubora, Ukamilifu

na Uzuri wa Ibn Adam katika Ulimwengu huu na Malipo yake yatakayokuwepo

katika Ulimwengu unaofuatia. Ibn Adam Amejaaliwa kufaham na Kupata I’lm hii

kupitia kwa Moyo wake tu, na wala si kwa kutumia Viungo vyengine vyote

vilivyabakia. Kwani ni Moyo ndio unaomjua Allah, Unaofanya kazi kwa ajili ya

Allah, Unaojitahidi kwa ajili ya Allah, Unaomkaribia Allah, na kuweka wazi kile

inachokiona mbele ya Allah. Na viungo vyake vyote vya Ibn Adam vilivyobakia hua

ni wafuasi, watumwa na vifaa ambavyo Moyo huvitumia na kuviajiri.

Kwani ni Moyo unaokubaliwa na Allah ndio unaokua uko huru dhidi ya kila kitu

isipokua Allah Subhanah wa Taála, Moyo huwekewa pazia usimuone Allah

Subhnaha wa Taála pale Moyo huo unapokua umejaa kila kitu zaidi ya Allah, Al

Qalb ni ule ambao Mtu akiujua Moyo wake basi hua ni mwenye kuijua Nafsi yake

na akiijua Nafsi yake basi hua ni alimjua Mola Wake. Moyo ndio ule ambao Mtu

asipoujua Moyo wake, basi hatoijua Nafsi yake na hivyo hatomjua Mola wake.


85

Hivyo I’lm ya kuyajua maumbile ya Moyo na sifa zake ndio mzizi wa Dini na ndio

msingi wa njia ya yule mwenye kutamfuta Mola wake.’

Wenye kua na Ilm hio ya kumjua Mola wao ndio wale wanaoelezewa katika Aya

ifuatayo:

‏﴿م َّنْ‏ خَشِ‏ ىَ‏ ٱلر َّحمَْٰنَ‏ بِٱلْغَيْبِ‏ وَجَآءَ‏ بِقَلْ‏ بٍم ُّنِي بٍ‏ ۞ ٱدْخُلُوهَا بِسَلاَ‏ مٍ‏ ذٰ‏ لِكَ‏ يَوْمُ‏

ٱلخُُلُودِ‏ ﴾

Man khashiya alrrahmana bialghaybi wajaa biqalbin muneebin; Odkhulooha

bisalamin dhalika yawmu alkhuloodi (Surat Qaf 50:33-34)

Tafsir: Yule ambae anamuogopa mwingi wa Rehma katika Ulmwengu wa Ghayb, na

akaja na Moyo wenye kujirudia katika kufaya Toba. Wataambiwa: ‘Ingia ndani yake

kwa usalama, kwani hiya ni maisha ya Milele’

Watu hawa hua ni wenye kumuogopa Mola wao, wanapokua faragha hapa Duniani na

wanapokua mbele za watu pia, kabla ya hata hawajawa mbele ya Mola wao kesho

Akhera, ambapo hua wanamuogopa Mola wao kutokana na Rehma zake zaidi ya kitu

chochote, kiasi ya kua mbali ya kua ni mwenye kumjua Mola wake kutokana na Rehma

zake lakini hata hivyo hua si mwenye kufanya dhambi. Bila ya Shaka katika haya kuna

mafunzo mengi kwa kila mwenye Moyo wenye kutaka kuzingatia na hivyo ndivyo yenye

kusema aya ifuatayo:

‏﴿إِن َّ فىِ‏ ذٰ‏ لِكَ‏ لَذِكْرَىٰ‏ لِمَن كَانَ‏ لَهُ‏ قَلْبٌ‏ أَوْ‏ أَلْقَى ٱلس َّمْعَ‏ وَهُوَ‏ شَهِيدٌ‏ ﴾

Inna fee dhalika ladhikra liman kana lahu qalbun aw alqa alssamAAa wahuwa

shaheedun (Surat Qaf 50:37)

Tafsir: Kwa Hakika katika haya kuna ukumbusho kwa yule mwenye Moyo na akatoa

sikio lake kwa kusikiliza huku akiwa ni mwenye kushuhudia.


86

Kulingana na ufafanuzi huo basi ndio tunaona uzito na umuhimu wa majukumu ya Al

Qalb yaani Moyo pale Qurán ilipokua ikizungumzia siku ya Malipo siku ambayo

hakitomfaa kitu chake isipokua Qalbin Saliimin kwa kusema:

‏﴿يَوْمَ‏ لاَ‏ يَنفَعُ‏ مَالٌ‏ وَلاَ‏ بَنُونَ۞‏ إِلا َّ مَنْ‏ أَتَى ٱهلل ََّ‏ بِقَلْبٍ‏ سَلِيم﴾‏

Yawma la yanfaAAu malun wala banoona; Illa man ata Allaha biqalbin saleemin

(Surat Ash Shuara 26:88-89)

Tafsir: Katika siku ambayo haitomfaa mtu Mali wala watoto wake, Isipokua yule

atakaempa Allah Moyo ulio Salama.

Ama kuhusiana na aya hii basi anasema Sultan Al Balagha Imam Al Zamakhshari na pia

Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua, Qalbin Saliimin maana yake:

Hua ni Moyo ambao uko Salima yaani umejiweka huru na Kumshirikisha Allah

Subhanah wa Ta’ala na hivyo ukawa Aslama yaani na ukawa Salama, na ukawa

Salama yaani ukapata Usalama kutokana na Nyoyo za viumbe wengine, na Moyo

huo uka Istaslama yaani ukajisalimisha kwa Allah.’

Ama kwa upande wa Allamah Raghib Al Isfahani basi yeye anasema kua: Al Qalb hua

na maana ya Kugeuza kitu juu chini, au kukizungusha kitu, kama vile ambavyo

mtu unavyoigeuza Nguo, au unapogeukia upande mwengine tofauti na ule

ulioelekea. Hivyo maana yake hujumuisha hali ya kugeuka geuka, na ndio maana

Qurán inatumia neno Inqalib kumaanisha wale watu ambao wamegeuza muelekeo

wao, au waliokimbia kutoka katika uwanja wa vita, au hutumika kama jina

kumaanisha kitendo cha kupindua, na pia hutumika kumaanisha kwa mtu kurudi

tena kwa Allah Subhanah wa Ta’ala yaani baada ya kufariki kwa mtu huyo.

Allamah Raghib Al Isfahani anaendelea kufafanua kwa kusema kua: Jina hili la Al Qalb

hutumiwa kumaanisha Moyo wa Ibn Adam kwa sababu ya kua na maumbile ya

kugeuka geuka kila mara, au kama tunavyosema kua mtu yupo katika hali ya

mabadiliko ya Moyo pale anapokua anabadilika kihisia, kimtizamo, kimaamuzi.

Neno lenyewe Al Qalb, hua pia linajumuisha Nafsi, I’lm, Ushujaa, n.k.

Lakini hata hivyo Al Qalb hua si sawa na Ufahamu, bali Al Qalb mara nyingi hua

unajumuishwa na Ufahamu kama vile ambavyo unavyojumuishwa Mto wa maji


87

usiotembea, wakati ukweli ni kua ni Maji ya Mto ndio yanayotembea, lakini

kutembea huko hua kunajumuishwa na Mto kwa sababu Mto ndio wenye Maji.

Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia maneno Nuqallibu af-ida pale aliposema:

‏﴿وَنُقَلِّبُ‏ أَفْئِدَتَهُ‏ مْ‏ وَأَبْصَارَهُمْ‏ كَ‏ مَ‏ ا لمَْ‏ يُؤْ‏ مِ‏ نُواْ‏ بِهِ‏ أَو َّلَ‏ مَر َّةٍ‏ وَنَذَ‏ رُهُمْ‏ فىِ‏ طُغْيَاِِمْ‏

يَعْمَهُونَ‏ ﴾

Wanuqallibu af-idatahum waabsarahum kama lam yu/minoo bihi awwala

marratin wanadharuhum fee tughyanihim yaAAmahoona (Surat Al Anaam 6:110)

Tafsir: Na tutazigeuza Nyoyo zao na Macho yao (mbali na uongofu), kwani wamekataa

kuukubali kwa mara ya kwanza, na tutawaachia katika kupita kwao wakiwa na upofu.

Hivyo hapa Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia neno Nuqallibu Af-ida ambapo

kutokana na mtizamo mwengine basi hua tunaona kua jina jengine la Moyo hua ni Fuad.

AL FUAD

Neno Fuad linatokana na neno Fa’ada ambalo kwa Kiarabu hua linamaanisha Kuumizwa

Moyoni, Kupigwa Moyoni, Kuumwa na Moyo. Mbali ya kua neno Fa’ada limetoa neno

Fu’ad lakini pia neno hili ndio pia lililotoa neno Af’idah ambalo humaanisha Moyo au

Ufahamu.

Allamah Al-Raghib Al Isfahani anasema kua Al Fuad hua moja kwa moja linamaanisha

Qalb, likiwa na utofauti wa kua Moyo unaitwa Fuad kwa sababu ya kua pia na Maumbile

ya kua ni wenye kua na hisia ya kuripuka moto, kwani Fuad linatokana na kuoka Moto

nyama kwenye jiko au mkaa yaani juu ya Moto uwakao, kama mishikaki ambapo nyama

hio baada ya kuiva hua ni yenye kuitwa Faiid. Hivyo Moyo huitwa Fuad kwa ajili ya

kuainisha kwa kiasi gani mripuko wa Moyo wa mtu hua na uwezo wa kuathiri mambo

mengi katika maisha yake Ibn Adam.


88

Wakati Moto unapowaka ripuripu basi hua ni sawa na Moyo unapojaa jazba na hivyo

ndani yake hua na hisia za kutokua na utulivu na kuongezeka kwa mapigo yake na

hamasa, hali hii inawekwa wazi katika aya ya Qurán iliyotumia majina yote mawili ya

Moyo ambayo ni Qalb na Fuad pale Allah Subhanah wa Ta’ala anapotuelezea kisa cha

Nabii Musa baada ya Nabii Musa kutumbukizwa mtoni na kuokotwa na Asia bint

Muzahim Mke wa Fir’awn na kukabidhiwa mama yake Nabii Musa ili amnyonyeshe,

kwa kusema:

‏﴿وَأَصْبَحَ‏ فُؤَادُ‏ أُمِّ‏ مُوسَى ٰ فَارِغاً‏ إِن كَادَتْ‏ لَتُبْدِى بِهِ‏ لَوْلا ۤ أَن ر َّبَطْنَا عَلَى ٰ قَلْبِهَ‏ ا

لِتَكُونَ‏ مِنَ‏ ٱلْمُ‏ ؤْمِنِينَ‏ ﴾

Waasbaha fu-adu ommi moosa farighan in kadat latubdee bihi lawla an rabatna

AAala qalbiha litakoona mina almu/mineena (Surat Al Qasas 28:10)

Tafsir: Na ukawa mtupu (usiokua na mawazo yeyote isipokua mawazo juu ya Musa)

Moyo wa Mama yake Musa. Kiasi ya kua alikua tayari kuiweka wazi Siri yake (kua

Musa ni Mtoto wake) kama si sisi kuuthibitishia Moyo wake (kwa Iman), ili apate kua

ni miongoni mwa Walioamini.

Al Fuad pia hua unaitwa ni ufuniko wa hisia ulio juu ya Al Qalb, na hivyo kumaanisha

kua Al Qalb uko ndani zaidi na una umaalum zaidi kuliko sehemu ya juu ya Al Fuad.

Ingawa huu ni mtizamo wa Kilugha tu, lakini Wanazuoni wa U’lum ul Qurán wanasema

kua Al Fuad hua ni sehemu inayopatikana ndani zaidi ya Moyo kuliko Al Qalb kwani hio

ndio sehemu ambayo Nuru ya I’lm ya kumjua Allah Subhanah wa Taála huanzia na ndio

maana Allah Subhanah wa Taála akasema katika Qurán kua:

‏﴿وَلاَ‏ تَقْفُ‏ مَا لَيْسَ‏ لَكَ‏ بِهِ‏ عِلْمٌ‏ إِن َّ ٱلس َّمْعَ‏ وَٱلْبَصَرَ‏ وَٱلْفُؤَادَ‏ كُل ُّ أُولٰئِكَ‏ كَانَ‏ عَ‏ نْهُ‏

مَسْ‏ ؤُولاً‏ ﴾

Wala taqfu ma laysa laka bihi AAilmun inna alssamAAa waalbasara waalfu-ada

kullu ola-ika kana AAanhu mas-oolan (Surat Al Isra 17:36)


89

Tafsir: Na Msifuate kile ambacho hamkijui. Kwani bila ya shaka ya Macho, Masikio

na Nyoyo kila kimoja juu yake mtaulizwa.

Hivyo kwa kua Al Fuad ndio sehemu inayoanzia hisia mbali mbali ikiwemo Nuru ya Ilm

ya kumjua Allah Subhanah wa Taála huanzia basi bila ya shaka ndio tutakayoulizwa juu

ya namna tulivyoutumia, na hivyo hatutoulizwa juu ya Al Qalb, Al Sadr wala Al Lubb.

AL LUBB

Neno Al Lubb linatokana na neno la Kiarabu Labba ambalo hua ni lenye kumaanisha

Kujaaliwa kua na ufahamu wa kina, Moyo wenye huruma. Neno Labba ndio lililotoa pia

neno Albabun ambalo hua na maana ya Moyo, Sehemu ya kati kati ya kitu, Kiini au

Ufahamu wa Kitu, Sehemu ya kitu isiyokua na Doa wala Dosari yeyote, Moyo wa Ibn

Adam au wa Tunda kama vile Moyo wa Nanasi au Fenesi.

Hivyo neno Lubb ambalo wingi wake hua Albaab ambalo humaanisha ufahamu msafi

usiokua na dosari, Al Lubb pia humaanisha aina ya ufahamu ambao ni wenye kuona kitu

kwa kina au kwa mtizamo wa ndani kabisa ya Moyo. Na ukweli ni kua sehemu ya Al

Lubb ndio inayokaa Nuru ya Allah Subhanah wa Taála ndani ya Moyo wa Ibn Adam,

ambapo Ibn Adam mwenye Moyo wenye Nuru hio basi hua ni mtu asiekua na mapenzi

ya kitu chochote ndani ya Moyo wake isipokua mapenzi ya Allah Subhanah wa Ta’ala

pekee na hivyo hua na darja ya juu kabisa miongoni mwa Viumbe kiasi ya kua Viumbe

wote hua chini yake, wakiwemo Majini na Malaika.

Hivyo kila Lubb hua ni Ufahamu lakini si kila Ufahamu hufikia darja au uwezo wa

kufahamu wa Lubb na ndio maana Allah Subhanah wa Taála akasema katika Quran kua:

‏﴿يُؤّتِى الحِْكْمَةَ‏ مَن يَشَآءُ‏ وَمَن يُؤْتَ‏ الحِْكْمَةَ‏ فَقَدْ‏ أُوتِىَ‏ خَيرْ‏ اً‏ كَثِيراً‏ وَمَا يَ‏ ذ َّك َّرُ‏ إِلا َّ

أُوْ‏ لُواْ‏ ٱلأَلْبَابِ‏ ﴾

Yu/tee alhikmata man yashao waman yu/ta alhikmata faqad ootiya khayran

katheeran wama yadhdhakkaru illa oloo al-albabi (Surat Al Baqara 2:269)


90

Tafsir: Humpa hikma yule amtakae, na yule anaepewa hikma nae, basi kwa hakika

hua ni mwenye kupewa Kheri nyingi sana, na hawatokumbuka isipokua Ulu Albaab.

Kutokana na kua na maana hiyo basi ndio maana Allah Subhanah wa Taála akatumia

neno Ulu al Baab mara kadhaa katika Qurán ili kuweka wazi wale Waumini ambao wana

ufahamu mkubwa wa Kiakili, Kihisia na Kiimani, na hivyo kua ni wenye kujua, kuona

na kuhisi alama za Allah Subhanah wa Ta’ala na katika kila kitu na katika kila jambo.

Sehemu ya hali ya Moyo ya Al Lubb hua ni sehemu ambayo ina utulivu wa hali ya juu na

hivyo hua haina miripuko kama ya Al Fuad wala uwepezi wa Al Qalb na pia ni tofauti na

Al Sadr.

AL SADR

Neno Sadara kwa Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kurudi, Kuendelea Mbele, Kupita,

Kutokea, Kufikia, au Kupiga Kifua. Neno Sadara ndio lililotoa neno Sadrun ambalo

humaanisha Kifua, Sehemu ya juu ya mwili, Ufaham, Moyo. Na pia likatoa neno Sudur

ambalo maana yake hua ni Nyoyo au Vifua.

‏﴿َٰي ُّهَا ٱلن َّاسُ‏ قَدْ‏ جَآءَتْكُمْ‏ م َّوْعِظَةٌ‏ مِّن ر َّبِّكُمْ‏ وَشِ‏ فَآءٌ‏ لِّمَ‏ ا فىِ‏ ٱلص ُّدُورِ‏ وَهُدً‏ ى

وَرَحمَْةٌ‏ لِّلْمُؤْمِنِينَ‏ ﴾

Ya ayyuha alnnasu qad jaatkum mawAAidhatun min rabbikum washifaon lima fee

alssudoori wahudan warahmatun lilmu/mineena (Surat Yunus 10:57)

Tafsir: Enyi Watu! Hakika yamekujieni Mawaidha kutoka kwa Mola wenu, na ponyo

kwa yaliyomo ndani ya vifua vyenu. Muongozo na Rehma kwa Waumini.

Allah Subhanah wa Ta’ala anapozungumzia kuhusiana na Al Sadr basi hua anamaanisha

Moyo kuanzia nje yake hadi ndani kwenye kiini chake yaani Al Sadr hua unajumuisha

Ufahamu na Nguvu za uwezo wa Moyo katika kubeba hisia mbali mbali na kama

tunavyoona katika mfano wa aya iliyo hapo juu. Na ndio maana pale Allah Subhana wa

Ta’ala alipozungumzia kisa cha Nabii Musa katika Qurán basi anatuambia kua:


91

‏﴿قَالَ‏

رَبِّ‏ ٱشْرَحْ‏ لىِ‏ صَدْرِي﴾‏

Qala rabbi ishrah lee sadree (Surat Ta-Ha 20:25)

Tafsir: Akasema (Musa) Ewe Mola wangu nifunulie Moyo wangu kwa ajili yangu.

Aya inatuwekea wazi kua baada ya Nabii Musa kufahamu kua anataka kubebeshwa

mzigo mkubwa na mzito wa kueneza ujumbe wa Mola wake basi akajua kua atahitaji kua

na kifua kikubwa chenye ustahmilivu wa kubeba siri na kudhibiti hisia tofauti ikiwemo

hasira, huruma n.k yaani Al Sadr hua ni kama Sanduku ambalo ndani yake mna vitu

vilivyofichwa na pia kupingana na vishawishi vinavyotokana na minong’onezo ya

Shaytani kama vile iliyotumika katika aya ifuatayo:

‏﴿ٱل َّذِى يُوَسْوِسُ‏ فىِ‏ صُدُورِ‏ ٱلن َّاسِ‏ ﴾

Alladhee yuwaswisu fee sudoori alnnasi (Surat Nas 114:5)

Tafsir: Yule ambae anaenong’oneza ndani ya Nyoyo za Watu.

Shaytan kamwe hawezi kuinong’oneza Qulub bali hua ni mwenye kuinong’oneza Al

Sadr, kwa sababu Allah Subhanah wa Taála ameuumba Al Qalb kua ni kitu kitukufu na

kisafi kabisa, yaani hapa tunaona kua mfano wa Al Qalb kua kama sanduku lenye hazina

ndani yake, lakini pia ni kama Ngome ambayo huwezi kuifikia hadi kwa kupitia katika

njia za viungo vyengine vya Mwili kama Macho, Masikio, Ulimi n.k ambazo ni miongoni

tu mwa Neema nyingi zisizohesabika za Allah Subhanah wa Taála juu yetu ambazo mara

nyingi tunakumbushwa katika Qur’an ikiwemo katika aya ifuatayo:

‏﴿وَٱذْكُرُواْ‏ نِعْمَةَ‏ ٱهلل َِّ‏ عَلَيْكُمْ‏ وَمِيثَاقَهُ‏ ٱل َّذِى وَاثَقَكُم بِهِ‏ إِذْ‏ قُلْتُمْ‏ سمَِعْنَا وَأَطَعْ‏ نَا

وَٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ عَلِيمٌ‏ بِذَاتِ‏ ٱلص ُّدُورِ‏ ﴾

Waodhkuroo niAAmata Allahi AAalaykum wameethaqahu alladhee wathaqakum

bihi idh qultum samiAAna waataAAna waittaqoo Allaha inna Allaha AAaleemun

bidhati alssudoori (Surat Al Maidah 5:7)


92

Tafsir: Na kumbukeni Neema za Allah juu yenu, na makubaliano yake ambayo

mlikubaliana nae, pale mliposema: Tumesikia na Tunatii. Na Mcheni Allah kwani

kwa hakika Allah ni mwenye kujua yaliyomo ndani ya vifua.

Hivyo kutokana na Rehma zake Allah Subhanah wa Taa’la juu yetu basi hakumjaalia

Iblis kua ni mwenye uwezo wa kuingia ndani ya Qulub zetu, bali amemjaalia kua na

uwezo wa kuingia ndani ya Sudur, na hivyo ni sisi Ibn Adam kutokana na ujinga, kutojali

na kukosa shukrani kwa Mola wetu basi ndio tunajiachia na hivyo kumpa nafasi Iblis

kuingia ndani ya Qulub zetu kwa kupitia kwenye Sudur na kujaribu kutupotosha kwa

kupingana na Makubaliano tuliyokubaliana na Mola wetu, hili ni kosa ambalo kila mmoja

wetu ataenda kuulizwa juu yake kwani Allah Subhanah wa Taála anatuambia kua:

‏﴿إِن تَكْفُرُواْ‏ فَإِن َّ ٱهلل ََّ‏ غَنيِ ٌّ عَ‏ نكُمْ‏ وَلاَ‏ يَرْضَى ٰ لِعِبَادِهِ‏ ٱلْكُفْرَ‏ وَإِن تَشْ‏ كُرُواْ‏ يَرْضَهُ‏

لَكُمْ‏ وَلاَ‏ تَزِرُ‏ وَازِرَةٌ‏ وِزْرَ‏ أُخْرَىٰ‏ ثمُ َّ إِلىَٰ‏ رَبِّكُمْ‏ م َّرْجِ‏ عُكُمْ‏ فَيُنَبِّئُكُمْ‏ بمَِا كُنتُمْ‏ تَعْمَلُو ‏َن

إِن َّهُ‏ عَلِيمٌ‏ بِذَاتِ‏ ٱلص ُّدُورِ‏ ﴾

In takfuroo fa-inna Allaha ghaniyyun AAankum wala yardha liAAibadihi alkufra

wa-in tashkuroo yardhahu lakum wala taziru waziratun wizra okhra thumma ila

rabbikum marjiAAukum fayunabbi-okum bima kuntum taAAmaloona innahu

AAaleemun bidhati alssudoori (Surat Az Zumar 39:7)

Tafsir: Na kama mkikufuru, basi kwa hakika Allah si mwenye kuhitaji kitu kutoka

kwenu, na haridhii kufuru kutoka kwa Waja wake, na kama mkimshukuru basi

atakuridhieni. Hakuna mwenye mzigo atakaebeba mzigo wa mwenzake. Hivyo kwa

Mola wenu ndio marejeo yenu ambapo atakuambieni mliyokua mkiyafanya. Kwani

yeye ni mwenye kujua yale yaliyomo ndani ya Sudur.

Hivyo Moyo ndio wenye uuwezo wa kuchagua baina ya jema na ovu, jambo lililo sahih

na lisilo sahih kwa sababu kiungo hicho ndio makao makuu ya ufahamu wa Ibn Adam.

Hujjat ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali anasema kua: ‘Ingawa Moyo, Akili, Roho na Nafsi hua ni vitu

vyenye maana tofauti, lakini viungo hivi vyote kwa pamoja ndivyo vinavyowakilisha

kile ambacho kinachojulikana kama Viungo muhimu visivyoonekana vyenye uwezo

mkubwa wa Ibn Adam aliopewa na Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani hivi ndivyo

vinavyoyapadisha darja Maumbile ya Ibn Adam na kumtofautisha yeye na Viumbe

wengine’.


93

Na ndio maana kukawa kuna makubaliano ya Ijmaa juu ya utukufu, ukubwa na darja ya

Amali zinazofanywa na Moyo hua ziko juu zaidi kulingana na zile zinazofanywa na

kiwiliwili. Hivyo kuna umuhimu wa Ibn Adam kujisalimisha kwa Allah Subhanah wa

Taála kwa kutumia Nyoyo zao, Kumuamini Mola wao kwa kutumia Akili zao na kufanya

Ibada kwa kutumia Miili yao.

Anasema Imam Mahammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Fahamu kua Allah

Subhanah wa Taála alipotaka kuiweka wazi Ilm ya kujulikana kwake basi aliiweka

Ilm hio ndani ya Aql, kisha akaweka sharti kua hakuna Ibn Adam yeyote

atakaeweza kuifikia Ilm hio kwa njia yeyote ile isipokua kwa njia ya kutumia Aql,

Hivyo mtu yeyote yule alienyimwa Aql basi hua pia ni alienyiwa Ilm. Na kua na Aql

basi ni kua na Husn Al Nadhar (Hikma) mtazamo bora ya kujidhibiti juu ya kila

unachokifanya kwa ajili yako na kwa ajili ya Mola wako.’

Na kwa mtizamo huo basi tunaona kua Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al

Tustari anatufafanulia kua maumbile ya ndani ya Ibn Adam yanajumuisha hali ya

Kimaumbile ya Nafsi, Al Qalb, Aql na Al Ruh kama alivyosema katika maana ya aya

ifuatayo:

‏﴿فَٱلْمُلْقِيَاتِ‏ ذِكْ‏ راً‏ ﴾

Faalmulqiyati Dhikran (Surat Al Mursalat 77:05)

Tafsir: Na kwa Malaika Wanaoshusha Ukumbusho.

Ambapo ayah inazungumzia Ujumbe wa Qurán na kwa mtizamo wa Imam Abu

Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi tunaona anasema kua: Hii Qurán ni

Wahy, unaopita katika njia ya Ilham, ambayo inajumuisha Nafs Al Ruh, Aql na Qalb

na kuwekwa juu ya Nafsi ya Maumbile. Na hii hua ndio njia ya Dhikr al Khafiy

(Ukumbusho uliyofichikana).

Kwaini Allah Subhanah wa Ta’ala amesema katika Qur’an kua:

‏﴿فَمَن يُرِدِ‏ ٱهلل َُّ‏ أَن يَهْدِيَهُ‏ يَشْرَحْ‏ صَدْرَهُ‏ لِلإِسْلاَمِ‏ وَمَن يُرِدْ‏ أَن يُضِل َّهُ‏ يجَْعَلْ‏ صَ‏ دْرَهُ‏

ضَيِّقاً‏ حَرَجاً‏ كَأَنم ََّا يَص َّع َّدُ‏ فىِ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ كَذٰ‏ لِكَ‏ يجَْعَلُ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱلرِّجْسَ‏ عَ‏ لَى ٱل َّذِينَ‏ لاَ‏

يُؤْمِنُونَ‏ ﴾


94

Faman yuridi Allahu an yahdiyahu yashrah sadrahu lil-islami waman yurid an

yudhillahu yajAAal sadrahu dhayyiqan harajan kaannama yassaAAAAadu fee

alssama-i kadhalika yajAAalu Allahu alrrijsa AAala alladheena la yu/minoona

(Surat Al An Aam 6:125)

Tafsir: Ama kwa yule ambae Allah hutaka kumuogoza basi humfungulia kifua chake

kwa ajili ya Uislam, na kwa yule ambae hutaka kumdhalilisha basi humfungia kifua

chake na kua ni chenye kubana kama kwamba ni mwenye kupanda juu kuelekea

Angani. Hivyo ndivyo Allah anavyotoa adhabu kwa wale ambao hawakuamini.

Anasema Imam Muhammad Ibn Jarir Al Tabari Al Shafii kuhusiana na aya hii kua Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliulizwa: ‘Jee Moyo hufunguka vipi kwa ajili ya

Uislam?’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu: ‘Ni Nuru ya Allah

Subhanah wa Ta’ala ndio inayoingizwa ndani ya Nyoyo za Ibn Adam, hivyo Moyo

hua ni wenye kutulia na kufunguka.’

Na ingawa aya imetumia neno Harajan ambalo hua ni lenye kumanisha: Kubana kwa

matawi ya mti kiasi ya kua sehemu ya matawi hayo yaliyobanana haiwezi kufikika

na mtu wala na mnyama, lakini kwa upande wa Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi

Allahu Anhu alipoambiwa juu ya maana hiyo na mabedui ambao wao ni wataalamu

wakubwa wa lugha ya Kiarabu, basi Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu

akasema: ‘Huo hua ni Mfano wa Nyoyo za Wanafiq, kwani kamwe hakuna jema

linaloweza kuingia ndani ya Nyoyo zao.’

Na anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Allah

Subhanah wa Ta’ala ametofautisha baina ya Murid (Mja anaemtafuta Mola wake)

na Murad (Mja anaetafutwa na Mola wake) ijapokua Waja wawili hawa wote ni

kutoka kwake yeye mwenyewe Allah Subhanah wa Ta’ala. Lakini yeye Allah

Subhanah wa Ta’ala ni mwenye kutofautisha baina ya Khusus (Wenye sifa hususan

maalum) na Umum (Wenye sifa ya Ujumla) na hivyo kawatofautisha wale Murad

(wanaotafutwa na Allah Subhanah wa Ta’ala) katika ayah hii na nyenginezo’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anaendelea kutufafanulia kwa

kusema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni mwenye kuziangalia Nyoyo, zote

kwani nyoyo hua ziko mbele yake, hivyo anapoona Moyo fulani una unyenyekevu

juu yake basi huujalia jema atakalo juu yake Moyo huo, Kisha baada ya hapo

hufuata Nyoyo zenye kubadilika haraka na kurudi kwake yeye Allah Subhanah wa

Ta’ala. Hizo ni aina mbili za Nyoyo anazozijaalia mema.’

Na kisha Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari akasema: ‘Kila wakati

Allah anapouangalia Moyo na akauona kua ni wenye kua na hamu ya Ulimwengu

huu, basi huuchukia Moyo huo na kuchukia kwake huko, hua kunajionesha kupitia


95

katika kuuwachia Moyo huo pamoja na Nafsi ya Mtu huyo. Kwani Moyo

haumilikiwi na yeyote isipokua Allah Subhanah wa Ta’ala, na hivyo hautakiwi

kumtii yeyote isipokua Allah Subhanah wa Ta’ala. Hivyo kama ukiwa unaujali

Moyo wako basi Mfanye Mola wako awe ndie msiri wako.’

Hivyo kama vile ambavyo Quran ilivyotumia maneno Qalb, Fuad, Lubb na Sadr

kumaanisha Moyo basi pia tunapoiangalia neno Aql yaani Akili basi tunaona kua Qurán

imeitaja sehemu ya kiungo hiki katika hali tofauti lakini kimaana kuenda sambamba na

hali za Hijr, Hilm, Nuha na Balu.

MAANA YA AQL, HIJR, HILM, NNUHA NA BALU.

Neno Aql linatokana na neno Aqala la Kiarabu ambalo hua ni lenye kumaanisha.

Kufunga, Kuzuia, Kua na Busara, Kufahamu, Kulipia Fidya Mtu fulani. Kupanda juu ya

Kilele cha Mlima na pia hua ni lenye kumaanisha Kutumuia Ufahamu au Akili.

Ingawa kuna tofauti kimaandishi na kimatamshi lakini Quran ilipozungumzia Ufahamu

basi imetumia maneno kadhaa yenye kuenda sambamba kimaana na neno Aql, miongoni

mwao ikiwemo neno Naha ambalo hua ni lenye kumaanisha Kujizuia au Kufaham,

ambapo tunaona kua hali nyengine ya neno hili ni ile hali ya Nuhyatun ambayo hua ni

yenye kumaanisha kile kinachomzuia Ibn Adam kutovuka mipaka na kutofanya mambo

yasiyoingia akilini. Neno Nuha limetumika katika Qurán pale iliposema:

‏﴿أَفَلَمْ‏ يَهْدِ‏ لهَُمْ‏ كَمْ‏ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُمْ‏ مِّنَ‏ ٱلْقُرُونِ‏ يمَْشُونَ‏ فىِ‏ مَسَاكِنِهِمْ‏ إِن َّ فىِ‏ ذٰ‏ لِ‏ كَ‏

لآَ‏ ‏َتٍ‏ لأُِ‏ وْ‏ لىِ‏ ٱ ل ن ُّ هَ‏ ٰ ى ﴾

Afalam yahdi lahum kam ahlakna qablahum mina alqurooni yamshoona fee

masakinihim inna fee dhalika laayatin li-olee alnnuha (Surat Ta-Ha 20:128)

Tafsir: Jee si Muongozo kwao wao (Kujua) kua tumeviangamiza vizazi vingapi kabla

yao. Ambavyo wao wanatembea juu ya makazi yao? Hakika katika haya kuna mafunzo

kwa waliopewa Nnuha (Ufaham).


96

Quran imetumia pia neno Ahlam ambalo linatokana na neno Halama lenye kumaanisha

Ndoto, Muono na pia hua linamaanisha Ustahmilivu. Neno Ahlam hua pia linamaanisha

Kupea Kiufaham na maana hii inaonekana wazi pale Allah Subhanah wa Ta’ala ilipohoji

juu ya Makafiri kua na ufahamu wa kutafakkari, kutokana na kukanusha kwao lakini

hapo hapo kua na ufahamu tu si hoja bali hoja ni kua na ufahamu uliopea kwani huo ndio

ambao unamsababisha mtu kua na uwezo wa Kutafakari kwa kina na ndio maana Allah

Subhanah wa Ta’ala akauliza:

‏﴿أَمْ‏ أتَْمُرُهُمْ‏ أَحْ‏ لاَمُهُمْ‏ هبَِٰذَ‏ آ أَمْ‏ هُمْ‏ قَوْ‏ مٌ‏ طَاغُونَ‏ ﴾

Am ta/muruhum ahlamuhum bihadha am hum qawmun taghoona (Surat AT Tur

52:32)

Tafsir: Jee Ahlamuhum (Ufahamu wao) ndio unawaamrisha (kukuzulia ewe

Muhammad) au wao ni watu wanaopenda kuvuka mipaka?

Hivyo bila ya shaka ni kua ufahamu wao watu hao ambao ni Makafiri unaonesha kua

umepea lakini hata hivyo wanafanya hivyo kwa sababu ya kua na Kibri tu kutokana na

maumbile ya baadhi ya Ibn Adam wanapoona kua katika hali ya kua ni wenye

kujitosheleza ambayo hua ni sawa na ile hali inayoelezewa na aya ifuatayo:

﴿ كَلا َّ إِن َّ ٱلإِنسَانَ‏ لَيَطْغَى ٰ ۞ أَن ر َّآهُ‏ ٱسْتَغْنىَٰ‏ ﴾

Kalla inna al-insana layatgha; An raahu istaghna (Surat Al Alaq 96:6-7)

Tafsir: Hakika Ibn Adam hua ni mwenye kuvuka mipaka. Anapojiona kua

anajitosheleza.

Ama kuhusiana na jambo hili la kutotumia Ahlam kutokana na kua na Kibri basi mwisho

wake hua majuto katika siku ya Malipo kama inavyoweka wazi hivyo Quran kwa

kusema:

‏﴿وَقَالُواْ‏ لَوْ‏ كُن َّا نَسْمَعُ‏ أَوْ‏ نَعْقِلُ‏ مَا كُ‏ ن َّا فيِۤ‏ أَصْ‏ حَ‏ ابِ‏ ٱلس َّ عِيرِ‏ ﴾

Waqaloo law kunna nasmaAAu aw naAAqilu ma kunna fee as-habi alssaAAeeri

(Surat Al Mulk 67:10)


97

Tafsir: Na wao watasema: ‘Lau kama tungesikiliza au tungetumia akili zetu, basi

kamwe tusingekua ni miongoni mwa watu wa Motoni’

Mbali ya kua Neno Hajara ambalo ndio asili ya neno Hijra, lenye kumaanisha Kuhama

na ndio maana ambayo wengi sana ni wenye kuijua kutokana na tukio la Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kuhama kutoka katika Mji wa Makkah na kuhamia katika Mji

wa Madinah ambapo ndani ya tukio hili basi mna mafunzo mengi ikiwemo lile la

Umuhimu wa Nia katika kila Jambo analolifanya Muislam, kwani amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua:

‘Ama kwa hakika Amali Hutegemeana na Nia, na Kwa Hakika Kila mtu atalipwa

Kulingana na Nia yake, Hivyo yeyote Yule aliefanyq Hijra kwa Ajili ya Kidunia au

kwa ajili ya Mwanamke Basi Hijra yake hua ni kwa Ajili ya alichokifanyia

Hijra’(Sahih Bukhari)

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliyasema maneno ya Hadith hii kwa

ajili ya kuainisha Umuhimu wa Nia katika Kila Jambo. Na tunapoangalia hadith basi

tunaona kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anazungumzia Hijra kisha ndani

yake akainisha aina za Nia na Madhumuni ya Hijra.

Kwani katika Wakati huo, na hadi katika wakati wa leo pia Kuna watu hua ni wenye

Kufanya Hijra kwa ajili ya Dini yao, na kuna wanaofanya Hijra kwa ajili ya Dunia yao.

Na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kuhusiana na Wanawake kwa sababu

kuna Watu walifanya Hijra ya kutoka Makkah kuelekea katika Mji wa Madinah si kwa

sababu ya Dini yao wala si kwa sababu ya Mola wao na Mtume wake basi kwa sababu

tu ya Kusikia kua katika Mji wa Madinah kuna Wanawake wazuri zaid kuliko Wanawake

wa Makkah.

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Imam Maaruf Al Kharki kua: ‘Kila

kinapotokea Kitendo kinachofanywa na Ibn Adam basi hua ni chenye kutokana na

Nia Ndani yake, Hivyo Kama Nia ni Sahih basi na Kitendo hua Sahih. Na kama Nia

si Sahih basi na Kitendo hia si Sahih

Ambapo Nia Sahih juu ya Kitendo Sahih hua katika hali 3 zifuatazo;

1-Kama ikiwa Nia juu ya Kitendo Husika hua ni yenye kutokana na Kumuogopa

Allah Subhanah wa Ta'ala. Basi Kitendo hicho hua ni sawa na kufanya Ibada kwa

Mja huyo mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala.


98

2-Kama ikiwa Nia Juu ya Kitendo Hua ni yenye kutokana na Kuikimbilia Pepo ya

Allah Subhanah wa Ta'ala. Basi Kitendo hicho hua ni sawa na kufanya Biashara

kwa Mja huyo mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala. kwa ajili ya Akhera yake.

3-Kama ikiwa Nia juu ya Kitendo hicho hua ni yenye kutokana na Kuona aibu kwa

Mja Mbele ya Mola wake, na hivyo hua ni kutekeleza Wajibu wake na kuonesha

Shukrani kwa Mja huyo mbele ya Mola wake. Basi Kitendo hicho hua ni sawa na

Ibada ya Mtu mwenye Kujikomboa na Kutaka kujitafutia Uhuru unaotokana na

kua na uzito wa Majukumu yake mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Naam, Inasikitisha kuona kua wengi wetu pia leo hii hua tunafanya Ibada zetu nyingi

huku tukiwa na nia ya hali ya 3 yaani kwa sababu tu ya kujipunguzia Uzito wa

Majukumu.

Yaani kwa Mfano: Watu Wanafanya Ibada fulani kwa sababu tu ya Kumrishwa Na

Muumba kufanya Ibada hio, bila kutilia maanani kua kufanya kwao Ibada husika mbali

ya kua ni Jukumu lao lakini hua ni kwa ajili ya Manufaa yao wao wenyewe.

Na hivyo hatufanyi Vitendo kwa ajili ya Nia ya Aina ya kwanza yaani kwa Ikhlasi au

kwa ajili ya Nia ya Aina ya pili yaani kujitolea kufanya Bishara na Allah Subhanah wa

Ta’ala kwa ajili ya kuwekeza katika Akhera yetu, na hivyo kutokua ni wenye kufanya

Ibada kwa Kutumia Hisia na Ufaham juu ya kile tunachokifanya, na hii ndio maana

nyengine ya Hijr.

Kwani pia neno Hajara ndio asili ya neno Hijrun ambalo maana yake hua ni Kua na hisia

na Ufaham, mfano wa matumizi wa maana hii ni katika aya ifuatayo:

‏﴿هَلْ‏ فىِ‏ ذٰ‏ لِكَ‏ قَسَمٌ‏ لِّذِى حِ‏ جْرٍ‏ ﴾

Hal fee dhalika qasamun lidhee hijrin (Surat Al Fajr 89:5)

Tafsir: Hakika katika hayo mna vithibitisho kwa wale wenye Hijrin (Ufahamu).

Na tumalizie kwa kuangalia neno Balun ambalo nalo ni linaloenda sambamba kimaana

na neno Aql neno hili limetumika katika Qurán kumaanisha Moyo, Akili, Ufahamu, Nia

au Hali ya Ufahamu, Mawazo, Mtizamo au Jambo muhimu sana, miongoni mwa aya

zilizotumia neno hili ni pamoja na:


99

‏﴿وَقَالَ‏ ٱلْمَلِكُ‏ ٱئْتُونىِ‏ بِهِ‏ فَلَم َّا جَآءَهُ‏ ٱلر َّسُولُ‏ قَالَ‏ ٱرْجِ‏ عْ‏ إِلىَٰ‏ رَبِّكَ‏ فَاسْأَلْهُ‏ مَا ابَ‏ لُ‏

ٱلنِّسْوَةِ‏ ٱللا َّتِى قَط َّعْنَ‏ أَيْدِيَهُن َّ إِن َّ رَبىِّ‏ بِكَيْدِهِن َّ عَلِيمٌ‏ ﴾

Waqala almaliku i/toonee bihi falamma jaahu alrrasoolu qala irjiAA ila rabbika

fais-alhu ma balu alnniswati allatee qattaAAna aydiyahunna inna rabbee

bikaydihinna AAaleemun (Surat Yusuf 12:50).

Tafsir: Na akasema Mfalme: ‘Mleteni mbele yangu’. Lakini Wajumbe hao walipofika

mbele yake (Yusuf) basi akasema: ‘Rudini kwa bwana wenu na mmuulize: ‘Ni ipi hali

ya ufahamu wao wale Wanawake waliojikata viganja vyao?’ Hakika Mola wangu ni

mwenye kujua juu ya hila zao’

Ambapo aya hio Nabii Yusuf anauliza juu ya hali ya Akili, Ufahamu, Mawazo au

Mtizamo wa wale Wanawake waliompelekea yeye kua ni mwenye kuenda Jela bila ya

kua na makosa. Jee wametafakkar na kuona kua wao ndio wenye makosa? Jee Ufahamu

wao utakubali kua wao ndio wenye makosa? n.k.

Na mfano mwengine ni pale Firáwn alipomwambia Nabii Musa kama inavyoelezewa:

‏﴿قَالَ‏ فَمَا ابَلُ‏ ٱلْقُرُونِ‏ ٱلأُولىَٰ‏ ﴾

Qala fama balu alqurooni al-oola (Surat Ta-Ha 20:51)

Tafsir: Akasema (Firáwn): ‘Jee ni ni hali yao wale waliotangulia kabla yetu?’

Yaani Fir’awn anamhoji Nabii Musa kua kama kweli kuna Mungu, alieumba kila kitu na

kukipa muongozo, kwa nini watu hao basi hawakumuabudu Mola wao? Ufahamu wao

na akili zao ilikuaje ukawakoseshea uongofu? Jee walikua hawana Akili na Ufahamu?

Ina maana wameangamia au vipi?

Hivyo ukweli ni kua Qurán inazungumzia mambo mengi sana ambayo bila ya kufuatilia

basi hua ni yenye kuonekana kua ni ya kawaida, na ni pale tu tutakapoyafuatilia, na

kuyatafakkari basi ndipo tutakaponufaika na kupata Baraka zilizomo ndani yake, kwani

vyenginevyo basi tutakua ni miongoni mwa walioingia katika hali ya Sakara.


100

Neno Sakara kwa lugha ya Kiarabu kwa upande mmoja hua ni lenye maana sawa na neno

Aql ambayo ni Kuzuia, Kufunga, Kudhibiti, Kua katika hali ya kujilinda, n.k. Lakini kwa

upande mwengine wa kimaana basi neno Sakara hua ni lenye kupingana kimaana na neno

Aql, kwani tumeona kua Aql hua inamanisha kua na Akili, Kua na Ufahamu na pia kua

ni mweye Kutumia Akili wakati neno Sakara huani lenye kukanusha mtu kua na Ufaham,

yaani kua katika hali ya Kua ni kizingiti baina ya mtu na Ufahamu wake, Raha kubwa

sana au Maumivu Makali sana yanayotoa Akili, Kutokua na Ufahamu, Kutokua na Akili,

Kulaaniwa kiakili au Kulewa.

Anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Sakara hua ni

kitu chochote kile ambacho kinachoilevya Nafsi ya Ibn Adam hapa Duniani na

hivyo kumpelekea Ibn Adam huyo kua ni mwenye kuisahau Akhera yake’

Ndio maana Allah Subhanah wa Taála akatuzindua ili tusimsahau yeye na tusiisahau siku

ya mwisho ya Ulimwengu tunaoishi ambayo watu wataonekana kama wamelewa lakini

hawajalewa kama inavyosema aya ifuatayo:

ُ

‏﴿َٰي ُّهَا ٱلن َّاسُ‏ ٱت َّقُواْ‏ رَب َّكُمْ‏ إِن َّ زَلْزَلَةَ‏ ٱلس َّاعَةِ‏ شَيْءٌ‏ عَظِيمٌ‏ ۞ يَ‏ وْمَ‏ تَرَوْنَهَا تَذْهَل

كُل ُّ مُرْضِ‏ عَةٍ‏ عَم َّ آ أَرْضَعَتْ‏ وَتَضَعُ‏ كُل ُّ ذَاتِ‏ حمَْلٍ‏ حمَْلَهَا وَتَرَى ٱلن َّاسَ‏ سُ‏ ‏َك ارَ‏ ‏ٰى

وَمَا هُم بِسُكَارَىٰ‏ وَلَٰكِن َّ عَذَابَ‏ ٱهلل َِّ‏ شَدِيدٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alnnasu ittaqoo rabbakum inna zalzalata alssaAAati shay-on

AAadheemun; Yawma tarawnaha tadhhalu kullu murdhiAAatin AAamma ardaAAat

watadaAAu kullu dhati hamlin hamlaha watara alnnasa sukara wama hum bisukara

walakinna AAathaba Allahi shadeedun (Surat Al Hajj 22:1-2)

Tafsir: Enye Watu! Mcheni Mola wenu! Kwani Mtetemeko wa Ardhi wa Saa (Ya

Kiama) ni kitu kibaya sana. Katika Siku hio mtaona kila Mama anaenyonyesha

atamsahau Mtoto wake anaemnyonyesha, na mwenye Mimba ataiangusha (Itatoka

kwa Hamkani) Mimba yake, na Utawaona watu wakiwa katika hali ya kua ni Sukara

(Waliolewa), lakini hakuna atakaekua ni Sakara (kalewa), na kwa hakika Adhabu ya

Allah ni kali sana.

Naam aya inazungumzia hali itakavyokua katika saa ya mwisho ya Ulimwengu ambayo

itakuja kabla ya Siku ya Kufufuliwa, na ndio maana ikazungumzia juu ya kutoka kwa

Mimba kutokana na hamkani na tafrani zake siku hio, kwani hii ni siku ambayo

Ulimwengu utabadilika Maumbile yake na hivyo Jua litachomoza kutoka katika upande


101

wa Magharibi, Mfumo wa Nguvu wa Sayari utakwisha nguvu zake za Mvutano kutokana

na amri ya Mola wake alieuumba na hivyo kua ni wenye kusimama kwa ghafla moja.

Sayari, Nyota na Mwezi zitakosa muelekeo na kuanza kupukutika na hivyo Dunia

itashindwa kutulia kwenye mhimili wake nayo pia itakua ni yenye kutetemeka katika hali

nzito, yenye kasi kubwa isiyokua ya kawaida, na hivyo basi huenda baadhi ya Sayari na

vipande vyake vikaangukia Duniani. Hii ni hali ya hatari sana kwa Ibn Adam na ukweli

ni kua ni hali isiyoelezeka wala kufahamika kiufaham kwa ufahamu wa Ibn Adam kwani

hua ni yenye kuonesha kuwepo kwa Muumba na uwezo wake ambae ni Allah Subhanah

wa Taa’la.

Anasema Imam Musa Ibn Jafar Al Sadiq kua: ‘Lam Yakhaf Allaha Man Lam Yaaqil

Aani Allah – Yeyote yule asiemuogopa Allah Basi Hana Akili au Ufahamu juu ya

Allah.’

Kwa kumalizia juu ya hali za Maumbile na hali za Nyoyo na Akili na Ufahamu wa

Viungo hivyo basi na tuangalie hali hizo kulingana na mtizamo wa Imam Abu Abd Allah

Muhammad Ibn Ali Ibn Hasan Ibn Bashir Al Hakim Al Tirmidhi ambae yeye anasema

katika kitabu chake cha Bayan al Farq Bayn Al Sadr al Al Qalb wa Al Fuad wa Al Lubb

kua:

AL SADR – Ndio Sehemu inayokaa Nuru ya Uislam na pia hujulikana kama Nafs Al

Ammarah.

AL QALB – Ndio Sehemu inayokaa Nuru ya Iman na pia hujulikana kama Nafs Al

Mulhimah.

AL FUAD – Ndio Sehemu inayokaa Nuru ya Maarifah na pia hujulikana kama Nafs Al

Lawwamah.

AL LUBB - Ndio Sehemu inayokaa Nuru ya Tawhid na pia hujulikana kama Nafs Al

Mutma’inah.

Huo ni mtizamo wa Imam Al Hakim Al Tirmidhi, hivyo ili kuifahamu zaid basi na

tufafanue hizi aina nne za Nafsi zilizonasibishwa na hali nne za Nyoyo, ambapo tunaona

kua Neno Nafsi limetokana na neno Nafasa ambalo kwa lugha ya Kiarabu hua na maana

ya Kitu chenye Thamani, Katika kuomba, Kuliwaza, Kufurahisha.

NAFS - MAUMBILE YAKE NA UHIBITI WAKE.

Neno Nafs linatoka na neno Nafasa ambao kwa lugha ya Kiarabu hua ni lenye

kumaanisha Kitu Adimu na chenye Thamani Kubwa sana, kiasi ni hasara kubwa sana


102

kukitupa au kukipoteza na kama ukikipoteza basi bila ya shaka pengo lake hua kamwe

haliwezi kuzibika. Neno Nafasa hua pia ni lenye Kumaanisha Kuliwaza, Kuchangamsha

au Omba.

Subhana Allah! Bila ya shaka lugha ya Kiarabu ni lugha yenye kujitosheleza tena sana,

kwani tuunapoangalia maana ya neno Nafasa ambalo ndio lililotoa neno Nafsi basi neno

hilo moja tu kimaana limebeba Uzito mkubwa sana wa maana ya Nafsi kwa kina na

kutuonesha kua Nafsi ni kitu chenye Thamani kubwa sana na kilicho adimu sana kiasi ya

kua ukikipoteza basi hua umekula hasara kubwa sana na kamwe hutoweza kuliziba pengo

lake.

Neno Nafasa ndio lililotoa neno Nafsun ambalo maana yake hua ni Nafsi, Roho, Uhai,

Mtu alie hai, Ufahamu, Hisia za ndani za matamanio. Na pia neno Nasafa limetoa neno

Nafsi ambalo nalo pia maana yake hua ni Mimi mwenyewe Binafsi, Kitu chenyewe,

Damu, Kanuni za Msingi, Nia au Makusudio, Matamanio, Moyo, n,k

Nafsi hua ni kitu ambacho kimo ndani ya Miili ya Viumbe lakini hakionekani wala

hakikamatiki isipokua kwa Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ndie alietuumba. Hivyo

ingawa Nafsi haikamatiki wala haionekani lakini kimaumbile Nafsi hua inadhibitika na

kiumbe husika mwenye Nafsi hio kwani hua inajumuisha hali ya uhusiano wa ufanyaji

kazi wa hisia zote kamilifu za mwili wa kiumbe kwa kutumia Ufaham, Akili, Moyo na

Ubongo, n.k. Na ndio maana akatuusia Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema kua:

‏﴿وَٱذْكُر ر َّب َّكَ‏ فىِ‏ نَفْسِ‏ كَ‏ تَضَر ُّعاً‏ وَخِ‏ يفَةً‏ وَدُونَ‏ ٱلجَْهْرِ‏ مِنَ‏ ٱلْقَوْلِ‏ بِٱلْغُدُوِّ‏

وَٱلآصَالِ‏ وَلاَ‏ تَكُنْ‏ مِّنَ‏ ٱلْغَافِلِينَ‏ ﴾

Waodhkur rabbaka fee nafsika tadharruAAan wakheefatan wadoona aljahri mina

alqawli bialghuduwwi waal-asali wala takun mina alghafileena (Surat Al Isra 7:205)

Tafsir: Na Mkumbuke Mola wako katika Nafsi yako, kwa Unyenyekevu na kwa Khofu,

bila ya kupaza sauti Asubuhi na Jioni na Usiwe miongoni mwa wenye kughafilika.

Na kisha akatoa onyo juu ya watakaoshindwa kuzidhibiti Nafsi zao, na kuwaahidi wale

watakao weza kuzidhibiti Nafsi zao kwa kusema:


103

‏﴿فَأَم َّا مَن طَغَى ٰ ۞ وَآثَرَ‏ ٱلحَْيَاةَ‏ ٱلد ُّنْيَا ۞ فَإِن َّ ٱلجَْحِ‏ يمَ‏ هِىَ‏ ٱلْمَأْوَىٰ‏ ۞ وَ‏ أَم َّا مَنْ‏

خَافَ‏ مَقَامَ‏ رَبِّهِ‏ وَنَهَى ٱلن َّفْسَ‏ عَنِ‏ ٱلهَْوَىٰ‏ ۞ فَإِن َّ ٱلجَْن َّةَ‏ هِ‏ ىَ‏ ٱلْمَ‏ أْوَىٰ‏ ﴾

Faamma man tagha; Waathara alhayata alddunya; Fa-inna aljaheema hiya

alma/wa; Waama man khafa maqama rabbihi wanaha alnnafsa AAani alhawa; Fainna

aljannata hiya alma/wa (Surat An Naziat 79:37-41)

Tafsir: Ama kwa yule atakaevuka mipaka. Na akawa ni mwenye kupendelea Maisha

ya Dunia, Basi kwa Hakika Motoni ndio yatakapokua makazi yake. Ama kwa yule

atakae kua ni mwenye kua na khofu ya kusimama mbele ya Mola wake na akaizuia

Nafsi yake na Matamanio, Basi kwenye Bustani (Peponi) ndio yatakayokua makazi

yake.

Ili kufahamu zaidi juu ya udhibiti wa Nafsi na hali zake basi na tuangalie mtizamo wa

Sultan al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi ambae anatufafanualia kwa kusema

kua: Kimaumbile Nafsi hua ni kitu kimoja, lakini ni chenye hali nyingi

zinazotofautiana. Nafsi inapokua katika hali yake husika ya juu kabisa basi hua

katika hali ambayo ni yenye kusimamia hali yake hio na kuizidishia nguvu kwa

kuzidisha mwamko wake wa kuendelea kua katika hali husika.

Ama kwa upande wa Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad

Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii basi yeye anatuambia kua:

Kimaumbile Nafsi zimegawika katika aina mbili:-

1- Al Nufus Al Sahiha – Yaani Nafsi zenye Afya yake ya kimaumbile na hivyo hua

ni zenye kupeka Wahy na Ilham. Aina hii ya nafsi hua ni zenye kuonesha Miujiza

kwa sababu hua hazishuguliki na matamanio ya Kidunia. Hizi Hua ni Nafsi za

Maitume na Manabii ambao wao hua ni Madaktari wa Nafsi.

2- Al Nufus Al Maridha – Yaani Nafsi zenye maradhi ambazo nazo hua katika darja

tatu zifuatazo:

a) Nafsi zenye Maradhi kutokana na Matamanio ya Kidunia, lakini hua ni zenye

kutibika na kurudi katika hali yake ya kiafya ya kimaumbile kupitia katika

njia ya Kutafuta I’lm, Kutafakkar na Kuzingatia.


104

b) Nasi zenye Maradhi kutokana na hamu na ushawishi wa kuyakumbatia

Matamanio ya Kidunia na hivyo nafsi hizi hua ni zenye kua na Nuru. Ambayo

hua inaisaidida kuipigania Nafsi hii katika maisha yake yote ili kuirudisha

katika hali yake ya afya ya kimaumbile kwa kupitia katika njia ya I’lm

ambayo hua ni yenye kuyaangamiza Maradhi yaliyoikumba Nafsi hio bila

ya kutegemea.

c) Nafsi zenye Maradhi kutokana na kuharibika kwa hali ya kimaumbile ya nafsi

hio. Nafsi hii hua katika hali ambayo haiwezekani kutibika wala

kurekebishika na kurudi katika hali yake ya kimaumbile.

Wanazuoni wanasema kua Nafsi ziko katika hali 7 tofauti, ambazo ni Nafs al Ammara,

Nafs Al Lawwamah, Nafs Al Mulhimah, Nafs Al Mutma’inah, Nafs ar Radhiyah, Nafs Al

Mardhiyah na Nafs al Kamilah, ambapo kulingana na mtizamo wa Imam Al Hakim Al

Tirmidhi basi zinafafanulika kulingana na mifano ya aya zilizotaja hali za Nafsi ambazo

ni:

NAFS AL AMMARAH BI ALSUI (NAFS SHAHWANIYYAH)

Nafs Al Ammarah bi al Sui au Nafs Shahwaniyya (Nafsi ya Matamanio) hali ya Nafsi

ambayo inanasibishwa na hali ya sehemu ya hali ya Moyo inayokaa Nuru ya Uislam

yaani Al Sadr. Hali hii ya Nafsi hua ni yenye kumuelekeza Ibn Adam katika kufanya

maovu, hali hii inawekwa wazi katika Qurán pale ilipozungumzia juu ya kisa cha Nabii

Yusuf ambae alisema:

‏﴿وَمَآ أُبَرِّئُ‏ نَفْسِ‏ ي ۤ إِن َّ ٱلن َّفْسَ‏ لَأَم َّارَةٌ‏ بِٱلس ُّو ۤ ءِ‏ إِلا َّ مَا رَحِ‏ مَ‏ رَبيّ‏ ِ ۤ إِن َّ رَبىِّ‏ غَ‏ فُورٌ‏

ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Wama obarri-o nafsee inna alnnafsa laammaratun bialssoo-i illa ma rahima rabbee

inna rabbee ghafoorun raheemun (Surat Yusuf 12:53)

Tafsir: Nami Siiwachi huru Nafsi yangu, kwani kwa Hakika Nafsi ni yenye kuamrisha

kufanya maovu isipokua pale Mola wangu anapoingiza Rehma zake, Hakika Mola

wangu ni mwingi wa usamehevu na ni mwingi wa Rehma.


105

Nafsi inapokua katika hali ya Ammara bi Su yaani kuamrisha kufanya Maovu basi hua ni

yenye kuelemea zaidi na kuzama katika matamanio ya kidunia na ndio maana kwa

upande mwengine ikawa inaitwa Nafs Shahwaniyyah hivyo hakuna mwenye uwezo wa

kuiokoa Nafsi hio kutokana na Maovu yake isipokua kutokana na msaada wa Allah

Subhanah wa Taála alieiumba Nafsi hio, kama vile anavyosema Allah Subhanah wa

Ta’ala katika Qurán kua:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ لاَ‏ تَت َّبِعُواْ‏ خُطُوَاتِ‏ ٱلش َّيْطَانِ‏ وَمَن يَت َّبِعْ‏ خُطُوَاتِ‏ ٱلش َّيْطَ‏ انِ‏

فَإِن َّهُ‏ ‏َْمُرُ‏ بِٱلْفَحْشَآءِ‏ وَٱلْمُنْكَرِ‏ وَلَوْلاَ‏ فَضْلُ‏ ٱهلل َِّ‏ عَلَيْكُمْ‏ وَرَحمَْتُهُ‏ مَا ‏َز كَا مِنكُمْ‏ مِّ‏ ‏ْن

أَحَدٍ‏ أَبَداً‏ وَلَٰكِن َّ ٱهلل ََّ‏ يُزَكِّى مَن يَشَآءُ‏ وَٱهلل َُّ‏ سمَِيعٌ‏ عَلِيمٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo la tattabiAAoo khutuwati alshshaytani waman

yattabiAA khutuwati alshshaytani fa-innahu ya/muru bialfahsha-i waalmunkari

walawla fadhlu Allahi AAalaykum warahmatuhu ma zaka minkum min ahadin

abadan walakinna Allaha yuzakkee man yashao waAllahu sameeAAun AAaleemun

(Surat Nur 24:21)

Tafsir: Enyi mlioamini! Msifute hatua za Shaytan, na yeyote yule atakaefuata hatua

za Shaytan, basi (Shaytan) hua anamuamrisha kufanya maovu na kuasi. Na kama si

fadhila za Allah juu yenu na Rehma zake juu yenu, basi hakuna miongoni mwenu

ambae angelikua msafi asiekua na dhambi. Lakini Allah humsafisha amtakae na kwa

hakika yeye ni mwenye kuona na kujua.

Bila ya shaka Nafsi hii ya Al Ammarah bi al su hua ni Nafsi ambayo haina hali ya

kutafakkari, yenye ubiNafsi, na hivyo hua ni yenye kuendekeza Shahawa (Matamanio

yake) na kufanya mambo kwa kutumia nguvu bila ya kufikiria matokeo yake ya baadae,

na ikiachiwa bila ya kupata msaada wa Allah Subhanah wa Taála alieiumba basi hua ni

Nafsi yenye kuelekea katika mahala pabaya na hivyo hua ni yenye kujiangamiza kwa

kufuata muongozo wa Shaytani kutokana na kukosa muongozo wa Muumba ambao ni

muongozo wa Dini ya Kiislam, hali hii ya Nafsi hua ni tofauti na Nafsi Al Mulhima.

NAFS AL MULHIMAH


106

Nafs Al Mulhima hali ya Nafsi ambayo inanasibishwa na hali ya sehemu ya Moyo

inayokaa Nuru ya Iman yaani Al Qalb, hii hua ni hali ya Nafsi ambayo inapata Ilham

yaani Muongozo wa Kimaumbile kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala alieiumba Nafsi

hio. Aina hii ya Nafsi imetajwa katika aya ifuatayo:

‏﴿وَنَفْسٍ‏ وَمَا سَو َّاهَا۞فَأَلهَْمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا﴾‏

WaNafsin wama sawwaha, Faalhamaha fujooraha wataqwaha (Surat Ash Shams

91:7-8)

Tafsir: Naapa kwa Nafsi, Na kwa yule alieweka sawa kikamilifu. Kisha akaionesha ni

kipi kilicho kiovu juu yake na ni kipi kilicho sahih juu yake.

Nafs Al Mulhima hua ni Nafsi ambayo imekamilika kwa kua na Nuru ya Iman ya Dini ya

Allah Subhanah wa Ta’ala katika kumpwekesha kwake na hua ni yenye Maumbile ya

kutafakkar na kujua kua jambo fulani ni ovu na jambo fulani ni sahih, na hivyo hua ni

wenye kudumu katika kumtii Mola wake, na kuonesha shukran, ukarimu, upole, huruma,

unyenyekevu n.k na hii ni kutokana na Nafsi hio kua ni yenye kua na hisia za ndani kwa

ndani zenye ujumbe wa kuitia ari Nafsi hio kufanya Mema na kuiongoza katika njia iliyo

sahih, aina hii ya Nafsi hua ni tofauti na Nafs Al Lawwamah.

NAFS AL LAWWAMAH.

Nafs Al Lawwamah hali ya Nafsi ambayo inanasibishwa na hali ya sehemu ya Moyo

inayokaa Nuru ya Maarifah yaani Al Fuad. Hali ya Nafsi ambayo ni yenye kujua kasoro

zake za kimaumbile hivyo hua ni yenye kujilaumu laumu, na imetajwa katika ile aya

isemayo:

‏﴿وَلاَ‏ أُقْسِ‏ مُ‏ بِٱلن َّفْسِ‏ ٱلل َّو َّامَةِ‏ ﴾

Wala oqsimu bialnNafsi allawwamati (Surat Al Qiyama 75:2)


107

Tafsir: Na nnaapa kwa Nafsi yenye Lawama.

Nafs Al Lawwamah hua ni Nafsi ambayo ina maarifa na hivyo inafanya mambo kwa

kujua na kisha inajiangalia na kujilaumu, na hivyo kuipelekea mtu husika kujihisi ana

makosa, hujuta, hujisikia aibu na kuhisi bora hata asingefanya hayo aliyoyafanya na

hivyo kuamua kutorudia tena makosa husika, Mtu husika hua yuko katika Mapigano na

Nafsi yake kiasi ya kua baadhi ya wakati Nafsi inamshinda na kufanya Madhambi na

baadhi ya wakati hua anafanikiwa kuidhibiti Nafsi yake na kujizuia na kufanya

Madhambi.

Nafsi al Lawwamah hua ni Nafsi yenye Sifa za mtu Kujijua, Kua na khofu na Kutamani

kufanya mema, kuzisaidia Nafsi Nyengine, na hivyo kila hatua anayopiga mtu katika

kufanya mema huonekana ni hatua kubwa zaidi kuliko ile hatua aliyokua nayo mtu hapo

kabla na hivyo hua katika hali ya hatari ya kuingia kwenye Unafiq, kwani hali ya Nafsi

hii humfanya mtu ajione kua anajua, ameshafanya mema mengi sana na hivyo anastahiki

heshima kutoka kwa watu wengine wasiojua. Na hivyo hua na hali ambayo haiko salama

dhidi ya vishawishi vya Iblis, tofauti na Nafs al Mutma’inah.

NAFS AL MUTMA’INAH

Nafs Al Mutma’inah hali ya Nafsi ambayo inanasibishwa na hali ya sehemu ya Moyo

inayokaa Nuru ya Tawhid yaani Al Lubb. Neno Mutma’ina linatokana na neno

Tamana ambalo kwa kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kupumzika, Kutulia, Tegemea,

Kuweka kitu kwa Utulivu au kwa Ukimya, Kutuliza kwa Kiakili, KiNafsi na Kiroho.

Hali ya Nafsi hii hua imeegemea na kuelekea kwenye mambo ya Kiroho na uhalisia wake

wa Kimaumbile na hivyo hua na utulivu wa hali ya juu kabisa, Nafsi inapofikia katika

hali hii basi hua na sifa ya kutofanya makosa, kutokua na upotovu na hua ni yenye

kufanikiwa Duniani na Akhera hivyo hua ni yenye kupata utulivu, raha na furaha

kutokana na kumjua na kua na ukaribu na Mola wake. Allah Subhanah wa Ta’ala

anazitaja sifa za Nafsi za aina hii ya Nafsi kwa kusema kua:

‏﴿َٰي َّتُهَا ٱلن َّفْسُ‏ ٱلْمُطْمَئِن َّةُ‏ ﴾

Ya ayyatuha alnnafsu almutma-innatu (Surat Al Fajr 89:27)

Tafsir: Wataambiwa: Enyi nyinyi wenye Nafsi zenye utulivu.


108

Anasema Sultan al Mutakallimin Mujaddid ud Din Imam Al Ghazali Al Thani Imam

Fakhr ad Din Al Razi kuhusiana na Nafs Al Mutma’inah kua: ‘Ni Nafsi za watu wenye

I’lm ya Kumjua Mola wao na hua na Utiifu kwa Mola wao na hivyo kua na utulivu

na kuridhika. Na Jee ni kwa namna gani Nafsi hua ni yenye kupata Utulivu?

Nafsi hupata utulivu kutokana na njia mbili zifuatazo, ambapo njia ya kwanza ni

kupitia katika Moyo Kumkumbuka Alieuumba kama inavyoelezewa katika ile aya

isemayo:

‏﴿ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ وَتَطْمَئِن ُّ قُلُوبُهُمْ‏ بِذِكْرِ‏ ٱهلل َِّ‏ أَلاَ‏ بِذِكْرِ‏ ٱهلل َِّ‏ تَطْمَئِن ُّ ٱلْقُلُوبُ‏ ﴾

Alladheena amanoo watatma-innu quloobuhum bidhikri Allahi ala bidhikri Allahi

tatma-innu alquloobu (Surat Ar Rad 13:28)

Tafsir: Wale wenye kuamini, na ambao nyoyo zao zinapata utulivu kutokana na

kumkumbuka Allah. Kwani ni katika kumkumbuka Allah ndio Nyoyo hupata utulivu.

Njia ya pili ni kupitia katika kutafakkar ipasavyo, yaani wakati Ibn Adam mwenye

ufahamu anapo uangalia ulimwengu basi hua ni mwenye kuona kua mahitaji yake

yamefungamana na njia fulani ya uhakika ambayo kwa kutumia njia hizo basi hua

ni mwenye kupata mahitaji yake. Lakini hata hivyo kila anapoangalia asili ya

mshikamano wa njia hizo basi hua pia ni mwenye kuona kua njia hizo zenyewe, pia

hua ni zenye kutegemea njia nyengine au sababu nyengine.

Na kila anapoendelea kufuatilia zaidi basi ndivyo anavyozidi kuona kua njia hizo

zimeshikamana na njia nyengine, hivyo hivyo hadi kufikia mwisho wake hua ni

mwenye kulifikia sababisho la kila kitu kilichopo au Wajib al Wujud (Wajibu wa

Kuwepo) yaani Allah Subhanah wa Ta’ala. Na hivyo husimamia hapo kwa sababu

ya kua mfuatiliaji hua ni mtu mwenye Yaqini basi hua hakuna haja kwake

kufuatilia zaidi baada ya kumfikia yule ambae hakuna kitu chochote

kisichowezekana kwake, hali hii huleta utulivu ndani ya Nafsi ya mhusika.

Hali hii inatuwekea wazi kua mtu yeyote yule ambae atapendelea kua na I’lm juu

ya Kidunia kuliko I’lm ya Kiakhera basi mtu huyu hua ni mtu asiekua na utulivu,

hali ambayo hua ni tofauti na ya yule ataependelea kua na I’lm ya Kiakhera zaidi

kuliko I’lm ya Kidunia ambae yeye hua na Nafsi yenye utulivu.

Katika kuielezea Nafs al Mutma’inah basi tumegusia Wajib Al Wujud hivyo kabla ya

kuendelea zaid basi kidogo tufafanue nini maana ya Wajib al Wujud, ambapo ukweli ni

kua ni vigumu kuelezea maana ya Wujud kwa kimaana kama inavyomaanishwa na Lugha

ya Kiarabu lakini tutajaribu kufafanua ili tufahamu japo kwa juu kuhusiana na Wujud


109

kama inavyotokana na neno Mawjud kwani kulingana na mtizamo wa Aqidat al Wujud

yaani Imani ya Sifa ya Kuwepo imegawika katika sehemu tatu:-

WAJIB AL WUJUD yaani hali ya Wajibu wa Kuwepo, hali ambayo hua inaelezea na

kuthibitisha Wajibu wa Kuwepo kwake Allah Subhanah wa Taála ambae ndie Muumba

wa kila kitu. Ambapo kuwepo kwake hua kupo bila kutegemea kitu chengine chochote,

na kuwepo kwake hua ni Wajibu kwa ajili ya vitu vyengine vyote vilivyokuwepo ili

viwepo. Hali hii pia hujulikana kama Wahdat al Wujud au Upekee wa kuwepo kwake

bila ya kua na Mshirika.

Na tunapozungumzia sifa hii ya upekee ya Wajib Al Wujub ya Wajibu wa Kuwepo kwake

Allah Subhanah wa Ta’ala basi hua pia tunazungumzia Kutaka kwake, kwani kutokana

na hali ya viumbe wake kua ni wenye hali na mambo maalum, yaani mazingira yao,

maumbile yao, ukubwa wao, wakati wao, n.k basi hali hio ya kutaka kwake inatuonesha

kua ni mwenye Kua na Maamuzi na kufanya maamuzi hua kunaendana na Matakwa. Vile

vile hua pia tunazungumzia I’lm yake, kwani maamuzi hayo hua hayatokani na kutojua

bali hua yanatokana na kujua, na pia tunazugumzia Uwezo wake, kwani asiekua na

uwezo basi kamwe hua hawezi kufanya kitu chochote hususan tunapozungumzia kufanya

kitu bila kutegemea kitu chengine chochote.

Na bila ya shaka sifa zote hizi tatu yaani Kutaka Kwake, Ilm yake na Uwezo wake

haziwezi kuwepo bila ya kuwepo kwa Sifa ya Kua Hai kwake, ambako nako kunaenda

sambamba na Kua na Upekee na Kutokua na Mshirika, kwani kutokua na upekee kwake

na kua na Mshirika basi hua ni kwenye kupelekea kuwepo kwa mapingano na mvutano

katika mpangilio wa Viumbe vyake kwani kuwepo Maumbaji zaidi ya Mmoja basi

hupelekea upinzani baina ya Waumbaji na matokeo yake hakutokua na Kiumbe chochote

kama anavyosema mwenye Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qurán:

‏﴿لَوْ‏ كَانَ‏ فِيهِمَآ آلهَِةٌ‏ إِلا َّ ٱهلل َُّ‏ لَفَسَدَاتَ‏ فَسُبْحَانَ‏ ٱهلل َِّ‏ رَبِّ‏ ٱلْعَرْشِ‏ عَم َّا يَصِفُو نَ‏ ﴾

Law kana feehima alihatun illa Allahu lafasadata fasubhana Allahi rabbi alAAarshi

AAamma yasifoona (Surat Al Anbiyah 21:22)

Tafsir: Lau Kama ndani yake (Mbinguni na Ardhini) ingekua kuna na Miungu zaidi

ya Allah, basi vyote (Mbingu na Ardhi) vingekua vishafisidika (vishaangamia),

Utukufu ni wake Allah pekee, Mola wa Arshi, yuko mbali na wanavyomsifia.

Yaani kama ingekua kuna mshirika wake Allah Subhanah wa Taála basi bila ya shaka

ingekua kuna mvutano baina yao, kwani aidha wangekua wana nguvu moja au wana

nguvu tofauti kwani kama mmoja angakua dhaifu basi ingebidi kwa kuadiwa ni mwenye


110

nguvu, na kama wote wangekua na nguvu sawia basi mmoja angataka inyeshe mvua

mwengine angekataa, mwengine angeamua Duniani uingie usiku na mwengine angetaka

uchelewe kuingia, kwani fahali wawili hawakai zizi moja.

Na akathibitisha Allah Subhanah wa Taála jua ya Wahdat ul Wujud kwa hoja kusema

kua,

‏﴿مَا ٱتخ ََّذَ‏ ٱهلل َُّ‏ مِن وَلَدٍ‏ وَمَا كَانَ‏ مَعَهُ‏ مِنْ‏ إِلَهٍ‏ إِذاً‏ ل َّذَهَبَ‏ كُل ُّ إِلَٰهٍ‏ بمَِا خَلَقَ‏ وَلَعَلاَ‏

بَعْضُهُمْ‏ عَلَى ٰ بَعْضٍ‏ سُبْحَانَ‏ ٱهلل َِّ‏ عَم َّا يَصِفُونَ‏ ﴾

Ma ittakhadha Allahu min waladin wama kana maAAahu min ilahin idhan

ladhahaba kullu ilahin bima khalaqa walaAAala baAAdhuhum AAala baAAdhin

subhana Allahi AAamma yasifoona (Surat Al Muuminun 23:91)

Tafsir: Kamwe hakua Allah ni mwenye mtoto na kamwe hakukua na Mungu

mwengine zaidi yake, (Kama angekua na Washirika) basi kila Mungu angechukua

alichokiumba, na baadhi yao wangejaribu kuwazidi nguvu wengine. Utukufu ni wake

Allah pekee, alie mbali na wanavyomsifia.

Na pia akatoa hoja nyengine tena Allah Subhanah wa Taála juu ya Wahdat ul Wujud kwa

kusema:

‏﴿قُلْ‏ ل َّوْ‏ كَ‏ انَ‏ مَعَهُ‏ آلهَِةٌ‏ كَمَا يَقُولُونَ‏ إِذاً‏ لا َّبْتَغَوْاْ‏ إِلىَٰ‏ ذِى ٱلْعَرْشِ‏ سَبِيلاً‏ ﴾

Qul law kana maAAahu alihatun kama yaqooloona idhan laibtaghaw ila dhee

alAAarshi sabeelan (Surat Al Isra 17:42)

Tafsir: Waambie (Hao Makafikri): ‘Kama kungekua kuna Miungu wengine pamoja

nae kama wanavyosema wao, basi bila ya shaka (Miungu hao) wangetafuta njia ya

kua karibu na Mola wa Arshi Tukufu’

Ama kwa upande mwengine basi tunaona kua Umoja wa kuwepo kwa Muumba mmoja

unaonekana wazi pale tunapoona kua Maumbile ya Ulimwengu yalivyo, ambapo tunaona

kua kanuni za kisayansi zinaonesha kua Duniani kuna nguvu za kimaumbile za kifizkia

ambazo zinaenda sambamba bila kuzidiana ambazo ni nguvu za kifizikia zilizo dhaifu,

nguvu za kifizikia zilizo imara, nguvu za umeme za sumaku (Electromagnetic Forces)

na nguvu za kuvuta chini ardhini (Gravitational Forces). Bila ya kuwepo kwa nguvu hizi


111

sambamba basi ingakua vigumu kuata mawasiliano ya anga za nje. Hivyo kuwepo kwa

umoja huu wa nguvu za kimaumbile unathibitisha Wahdat ul Wujud.

MUMKIN AL WUJUD yaani hali ya Uwezekano wa Kuwepo, hali ambayo hua

inaelezea na kuthibitisha Uwezekano wa Kuwepo kwa Viumbe walioumbwa ambao

wanaweza wakawa wapo na pia wanaweza wakawa hawapo. Viumbe hawa Walioumbwa

hua hawana uhuru wa kuwepo na hivyo basi kuwepo kwao hua hakuna ulazima. Allah

Subhanah wa Taála amewajaalia kua wapo kutokana na Kutaka kwake, Uwezo wake,

Nguvu zake, I’lm yake na kama angetaka basi bila ya shaka viumbe hivyo

visingekuwepo. Kwani Viumbe hua vipo kutokana na Allah Subhanah wa Taála kutaka

kua viwepo yaani viumbe kuwepo kwa viumbe hivyo kunategemea kuwepo kwake yeye

ambae kuwepo kwake yeye hakutegemei kuwepo kwa kitu chengine.

MUSTAHIL AL WUJUD yaani hali ya Kutowezekana Kuwepo, ambako kunajumisha

kuwepo kwa ushiriki wa Majina, Sifa na Vitendo vya Allah Subhanah wa Ta’ala jambo

ambalo haliwezekani si kulingana na mtizamo wa Maandiko tu bali pia kulingana na

Ufahamu na Mantiq.

Sultan al Mutakallimin Mujaddid ud Din Imam Fakhr ad Din Al Razi anaendelea

kutuelezea kuhusiana na Nafs Al Mutma’inah kua Hivyo watu wenye hali ya Nafsi ya

Al Mutma’inah (Yaani Nafsi iliyotulia baada ya kutafakkar na kufuatilia hadi

wakalifikia sababisho la kitu yaani Wajib Al Wujub na hivyo kua na ukaribu na Mola

wao) basi wao ndio ambao watakaoambiwa katika wakati watakapo ondoka hapa

Duniani kua:

‏﴿َٰي َّتُهَا ٱلن َّفْسُ‏ ٱلْمُطْمَئِن َّةُ‏ ۞ ٱرْجِ‏ عِى إِلىَٰ‏ رَبِّكِ‏ رَاضِيَةً‏ م َّرْضِي َّةً‏

Ya ayyatuha alnnafsu almutma-innatu IrjiAAee ila rabbiki radhiyatan

mardhiyyatan (Surat Al Fajr 89:27-28)

Tafsir: Enyi wenye Nyoyo zenye utulivu! Rejeeni kwa Mola wenu huku mkiwa

Mmeridhika na Mola wenu na huku mkiwa ni Mmeridhiwa na Mola wenu.

Hivyo Allah Subhanah wa Taála anazitaja Nasf al Mutma’inah katika Surat Al Fajr

89:27-28 huku akiziainisha kua ni zenye sifa mbili kuu ambazo ni Radhiyatan na

Mardhiyah ambapo ndani yake ndio tunapata Nafs Radhiyatan na Nafs Mardhiyatan:

NAFS RADHIYATAN


112

Hii ni hali ya Nafsi ambayo ipo katika Mutma’ínah yaani katika hali ya utulivu na

kuridhia hukmu za Allah Subhanah wa Taála juu yake kiasi ya kua hakuna kitu ambacho

kinazifurahisha Nafsi hizi isipokua kua na Maridhia na majaaliwa ya Mola wake, hivyo

mtu mwenye Nafsi ya aina hii hua anajua kua majaliwa ya Mola wake juu yake

yanatokana na kile kilichoridhiwa na kufurahiwa na Mola wake.

NAFS MARDHIYAH.

Hali hii ya Nafsi ambayo ipo pia katika hali ya Mutma’inah hua ni hali ambayo ina Amani

kutokana na kutofanya dhambi, hii hua ni Nafsi ambayo haina matamanio ya Dhambi,

kwani Matamanio yake ni ya halali tu, hivyo Nafsi za watu hawa hua hazina sifa ya

kutofanya dhambi tu lakini pia hazitamani kufanya mambo maovu, kwani wao hutamani

yale tu ambayo Allah Subhanah wa Taála ameyaridhia na hivyo kua ni wenye kuachana

na yale ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala hakuyaridhia.

NAFS AL KAMILAH

Hii hua ni hali ya Nafsi ambayo pia hua inajulikana kama Nafs Al Nuraniyyah yaani Nafsi

yenye Nuru au Nafsi Al Muhhibah yaani Nafsi ya mwenye Kupenda au ya Urafiki wa

Karibu sana ambayo hua haipo katika hali ya Mutma’ainah tu bali pia hua ipo katika

Darja ya Ubora yaani Maqam al Ihsan na hii hua ni darja ambayo iko juu kabisa ya darja

zote, kwani mwenye Nafsi hii hua ni mwenye kufikia katika Darja ya ukaribu wa ambao

unajulikana kama qaba qawsayni aw adna yaani baina ya mipinde miwili au karibu zaid,

nyuma ya Nyayo za Rasul Allah Sallalahu Alayhi wa Salam. Hizi ni Nafsi za watu ambao

wameelezewa katika aya ifuatayo:

‏﴿أَي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ مَن يَرْتَد َّ مِنكُمْ‏ عَن دِينِهِ‏ فَسَوْفَ‏ ‏َْتِى ٱهلل َُّ‏ بِقَوْمٍ‏ يحُِب ُّهُمْ‏

وَيحُِب ُّونَهُ‏ أَذِل َّةٍ‏ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ أَعِز َّةٍ‏ عَلَى ٱلْكَافِرِينَ‏ يجَُاهِدُونَ‏ فىِ‏ سَبِيلِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَلاَ‏

يخََافُونَ‏ لَوْمَةَ‏ لا ۤ ئِمٍ‏ ذٰلِكَ‏ فَضْلُ‏ ٱهلل َِّ‏ يُؤْتِيهِ‏ مَن يَشَآءُ‏ وَٱهلل َُّ‏ وَاسِ‏ عٌ‏ عَلِيمٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo man yartadhdha minkum AAan deenihi fasawfa

ya/tee Allahu biqawmin yuhibbuhum wayuhibboonahu adhillatin AAala


113

almu/mineena aAAizzatin AAala alkafireena yujahidoona fee sabeeli Allahi wala

yakhafoona lawmata la-imin dhalika fadhlu Allahi yu/teehi man yashao waAllahu

wasiAAun AAaleemun(Surat Al Maidah 5:54)

Tafsir: Enye Mlioamini! Yeyote yule atakaerudi nyuma miongoni mwenu kutoka

katika Dini hii, basi Allah atawaleta watu ambao atawapenda nao watawapenda, Nao

watakua wanyenyekevu kwa wale walioamini,na wakali kwa waliokufuru, watapigana

kwa ajili ya Allah na kamwe hawatoogopa lawama kutoka kwa wanaolaumu. Hii nio

fadhila ya Allah nae humpa amtakae miongoni mwa waja zake. Hakika Allah ni

mwenye kuwatosheleza Waja wake na ni mwenye kujua kila kitu.

Na pia pale alipoelezea tena Allah Subhanah wa Taála kwa kumwambia Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam awaambie waja wake kua:

‏﴿قُلْ‏ إِن كُنتُمْ‏ تحُِب ُّونَ‏ ٱهلل ََّ‏ فَٱت َّبِعُونىِ‏ يحُْبِبْكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ وَيَغْفِرْ‏ لَكُمْ‏ ذُنُوبَكُمْ‏ وَٱهلل َُّ‏ غَفُورٌ‏

ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Qul in kuntum tuhibboona Allaha faittabiAAoonee yuhbibkumu Allahu wayaghfir

lakum Dhunoobakum waAllahu ghafoorun raheemun (Surat Al Imran 3:31)

Tafsir: Sema kama kweli mnampenda Allah basi nifuateni mimi na Allah

atakupendeni na atakusameheni dhambi zenu. Hakika Allah ni mwingi wa usamehevu

na ni mwingi wa Rehma.

Hivyo hii ni hali ya darja ya kua na ukamilifu wa kua ni Mtumwa wa Allah Subhanah wa

Ta’ala kwa kupitia katika ukamilifu wa kufuata mafunzo ya Rasul Allah Salalahu Alayhi

wa Salam, hivyo yule ambae amejaaliwa kuifikia darja hii hua ni mwenye kujaaliwa

kujua mapenzi kamilifu juu ya Allah Subhanah wa Ta’ala na Rasul Allah Salallahu

A’lahi wa Salam kwani hua wenye kujua kwa yakini kusudio la kuumbwa kwao.

Hivyo kutokana na kuwepo kwa utofauti wa Kimaumbile wa Nafsi za Ibn Adam basi

ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ndie Muumba akaamua kutuma Mitume

na Manabii kwa waja wake wenye kusudio maalum.


114

KUSUDIO LA ALLAH SUBHANAH WA TA’ALA KUTUMA MITUME

KWA WAJA WAKE.

Ili kujua nia na kusudio la Allah Subhanah wa Ta’ala kutuma Mitume kwa waja wake

kila baada ya muda fulani ulimwenguni basi kwanza inabidi tukumbuke kua Allah

Subhanah wa Taála amewaumba Ibn Adam kua ndio watawala wa Ulimwenguni na

alipotuumba alituumba katika umbo lililo bora kabisa kuliko viumbe wote kama

anavyosema katika aya ifuatayo:

‏﴿لَقَدْ‏ خَلَقْنَا ٱلإِنسَانَ‏ فيِ‏ ۤ أَحْسَنِ‏ تَقْوِيمٍ‏ ﴾

Laqad khalaqna al-insana fee ahsani taqweemin (Surat At Tin 95:5)

Tafsir: Kwa hakika tumemuumba mtu katika Taqwiim bora kabisa.

Naam aya hii ya Surat At Tin 95:5 ni miongoni mwa aya ambazo zinanukuliwa sana na

Waislam ulimwenguni lakini ni wachache wenye kuijua maana halisi ya ayah hii, kwa

sababu wengi sana hua wanazungumzia ubora wa muonekano wa nje wa mwili wa Ibn

Adam, lakini ukweli ni kua aya inaweka wazi ubora uliokamilia usiokua na kasoro wa

mwili wa Ibn Adam, ubora ambao unajumuisha mfumo mzima wa ufanyaji kazi

kikamilifu wa umbo la nje la mwili wa Ibn Adam ukishirikiana na ufanyaji kazi wa

mifumo yote kamilifu ya ndani ya mwili wa Ibn Adam ambayo inajumuisha Mfumo wa

Ubongo na Ufahamu wake, Mfumo wa hisia wa Uti wa mgongo na hisia zake tofauti

ikiwemo hisia za njaa, joto, baridi, matamanio, mapenzi, furaha, huzuni, maumivu n.k

Ubora huo unajumuisha pia mfumo kamilifu wa mzunguko wa Damu ndani ya Moyo na

ufahamu wake. Tunapozungumzia Moyo basi hua tunazungumzia kiungo ambacho ni

chenye ufahamu mkubwa na wa kina unaojitegemea kinguvu na kiuwezo kama

tulivyoona hapo kabla ambavyo vyote hivyo ni tofauti na uwezo wa ufahamu wa akili na

ufaham wa viumbe wengine kama Malaika na Majini.

Hivyo kamwe hatukukamilishwa kwa kujaaliwa kua na maumbile bora labda kwa ajili

ya kumhudumikia kwa kumtafutia riski au kumfanyia jambo lolote lile Muumba wetu

ambae ni Allah Subhanah wa Taála kwani yeye ni Muumba hivyo ni mwenye

kujitosheleza juu ya kila kitu na ni mwenye kua na uwezo wa kuwatosheleza viumbe

wake wote aliowaumba, hivyo Ibn Adam tumeumbwa kwa maumbile bora ili tupate

kutafakkar na kumjua, kumuabudu, kumshukuru na kumnyenyekea Allah Subhanah wa

Taála kama alivyotuwekea wazi kwenye Qurán kwa kusema:


115

‏﴿وَمَا خَلَقْتُ‏ ٱلجِْن َّ وَٱلإِنسَ‏ إِلا َّ لِيَعْبُدُونِ۞‏ مَآ أُرِيدُ‏ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ‏ وَمَآ أُرِيدُ‏ أَن

يُطْعِمُونِ‏ ﴾

Wama khalaqtu aljinna waal-insa illa liyaAAbudooni, Ma oreedu minhum min

rizqin wama oreedu an yutAAimooni (Surat Adh Dhariyyat 51:56-57)

Tafsir: Sikuwaumba Majini na Ibn Adam isipokua kwa ajili ya kuniabudu mimi tu.!

Sitaki kutoka kwao Riziki wala sitaki wanipe chakula.

Anasema Allamah Abu Qasim Ibn Husein Ibn Mufadhal Ibn Muhammad Raghib Al

Isfahani kuhusiana na neno LiyaA’Abuduuni lililotumika katika aya hii kua: ‘Ubudiyya –

Utumwa hua ni kuuonesha unyenyekevu. Na Ibada hua ni kutilia mkazo, kwani

Ibada ndio mpaka wa unyenyekevu, na hakuna anaestahiki unyenyekevu au

kuabudiwa isipokua yule ambae ni mwenye uwezo wa kujaalia kila kitu ambae ndie

anaestahiki kuabudiwa ambae ni Allah Subhnahah wa Ta’ala na ndio maana

akasema:

‏﴿وَقَضَى ٰ رَب ُّكَ‏ أَلا َّ

ۤ تَعْبُدُواْ‏ إِلا َّ إِ َّهُ‏ ﴾

Waqadha rabbuka alla taAAbudoo illa iyyahu (Surat Al Isra 17:23)

Tafsir: Na Mola wako amejaalia kua usimuabudu yeyote isipokua yeye’

Ama tunapozungumzia kuhusiana na LiyaA’Abuduuni basi hua kuna Ibada za aina mbili:

1. Unyenyekevu wa Ulazima – Ambao hua ni hali inayojumuisha kila kitu cha Mja

kinachohusiana na Muumbaji kutokana na kutokua na kitu na hivyo kua na uhitaji wa

Mja kwa Muumba ambae ni Allah Subhanah wa Taála.

2. Unyenyekevu wa Khiari – Ambao hua ni hali inayojumuisha hali moja kati ya mambo

ya matatu yafuatayo:


116

a) Unyenyekevu wa yule mtu ambae hayuko huru (yaani ni mtumwa alie chini ya

mtu mwengine, iwe kiutumwa, kiutumwa wa kileo ambao hua ni wa kikazi au

kifungo)

b) Unyenyekevu wa yule mtu ambae yuko huru lakini hua ni anaemtumikia Allah

Subhanah wa Taála (Ambalo ndio kusudio la uhalisia wa kila Kiumbe)

c) Unyenyekevu wa yule mtu ambae yuko huru lakini hua ni mwenye kumtumikia

Allah Subhanah wa Taála katika kuabudu na kihuduma, yaani anaemtumikia Allah

Subhanah wa Ta’ala kwa Ikhlasi na hivyo utumwa wake ni katika uhai wa Maisha

haya na kila kinachohusiana nayo. [Imam Raghib Al Isfahani, Mufradat Alfadh Al

Qurán, 542]

Hivyo Allah Subhanah wa Taála anatuwekea wazi kua hakutuumba sisi Ibn Adam na

Majini isipokua kwa ajili ya Kumuabudu na kumnyenyekea yeye peke yake, kwa sababu

yeye ndie Mola wetu alietuumba na kuendelea kutulea tangu tulikotoka, hapa tulipofikia

na hadi tutakapoelekea katika mwisho wetu kwa kutujaalia afya, nguvu, uwezo, rizki,

familia na kadhalika kwa kila mmoja miongoni mwetu kabla ya kuufikia mwisho wetu

ambao hakuna anaeujua miongoni mwetu isipokua yeye Mola wetu kama alivyosema

katika aya ifuatayo:

‏﴿وَهللِ َِّ‏ غَيْبُ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَمَآ أَمْرُ‏ ٱلس َّاعَةِ‏ إِلا َّ كَلَمْحِ‏ ٱلْبَصَرِ‏ أَوْ‏ هُوَ‏

أَقْرَبُ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ ٰ عَلَى ِ كُل شَيْءٍ‏ قَدِيرٌ۞‏ وَٱهلل َُّ‏ أَخْرَجَكُم مِّن بُطُونِ‏ أُم َّهَاتِكُمْ‏ لاَ‏

تَعْلَمُونَ‏ شَيْئاً‏ وَجَعَلَ‏ لَكُمُ‏ ٱلْس َّمْعَ‏ وَٱلأَبْصَارَ‏ وَٱلأَفْئِدَةَ‏ لَ‏ عَل َّكُ‏ مْ‏ تَشْكُرُونَ‏ ﴾

ّ

Walillahi ghaybu alssamawati waal-Ardhi wama amru alssaAAati illa kalamhi

albasari aw huwa aqrabu inna Allaha AAala kulli shay-in qadeerun; WaAllahu

akhrajakum min butooni ommahatikum la taAAlamoona shay-an wajaAAala

lakumu alssamAAa waal-absara waal-af-idata laAAallakum tashkuroona (Surat An

Nahl 16:77-78)

Tafsir: Na kwa Allah ndiko kwenye umiliki wa Ulimwengu usioonekana wa Mbiguni

na ardhini, na amri juu ya wakati si chochote bali ni kama kupepesa kwa jicho au

karibu zaidi. Kwa hakika Allah ni mwenye uwezo juu ya kila kitu. Na Allah ndie


117

aliekutoeni katika matumbo ya uzazi wa mama zenu wakati nyinyi mkiwa hamjui kitu,

na akakupeni Masikio, Macho na Moyo ili mpate kua ni wenye kushukuru.

Tunapozungumzia juu ya Ibada ya kumuabudu Allah Subhanah wa Taála katika Dini ya

Uislam basi hua hatuzungumzii tu Kusali, Kufunga kutoa Zakkah na Sadaka bali hua

tunazungumzia utekelezaji wa Majukumu yote tuliyoamrishwa na Allah Subhanah wa

Taála katika wakati wa uhai wetu wote tunapokua hapa Ulimwenguni, tangu kuingia

kwetu hadi kutoka kwetu, kwani sisi tumekuja hapa Duniani kwa ajili ya Mola wetu na

hivyo kua katika hali ya mapigano ya kutafuta mafanikio yetu ya baadae dhidi ya

vichochezi vya Iblis na Nafsi zetu zitakazopelekea kuachana na lengo la kuumbwa kwetu,

hivyo hatukuja Duniani kwa ajili ya mchezo jambo ambalo linawekwa wazi na aya

zifuatazo:

‏﴿لَقَدْ‏ خَلَقْنَا ٱلإِنسَانَ‏ فىِ‏ كَبَدٍ‏ ۞ أَيحَْسَبُ‏ أَن ل َّن يَقْ‏ دِرَ‏ عَلَيْهِ‏ أَحَ‏ دٌ‏ ﴾

Laqad khalaqna al-insana fee kabadin, Ayahsabu an lan yaqdira AAalayhi ahadun

(Surat Al Balad 90:5-6)

Tafsir: Kwa hakika tumemuumba Ibn Adam katika hali ya Harakati na Mapigano, Jee

anajihesabu kua hakuna mwenye kuweza kumdhibiti juu yake?

Aya zinatuwekea wazi kua Ibn Adam ameumbwa kwa ajili ya kua katika hali ya

mapigano yenye kudumu na kuendelea katika kipindi cha uhai wake wote, harakati na

mapigano ambayo yanaanzia tangu kutafutwa kwake na Wazee wake, hadi kupatikana

kwake anapozaliwa, anapokua kwake, anapoidhibiti Nafsi yake na hadi katika wakati wa

kutolewa Roho yake, yeye yupo katika hali ya harakati na mapigano ambayo yanatakiwa

yampelekee kua na unyenyekevu juu ya Mola wake ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala,

Lakini wapi kila anavyokua na kupata afya, uwezo, mali na kadhalika basi ndio kwanza

anapozidi kujiona kua hakuna kama yeye. Hivyo jee kweli anafikiria kua hakuna

atakaemdhibiti? Suali hili linatiliwa mkazo kwa kuulizwa tena katika aya ifuatayo pale

Qurán iliposema:

‏﴿أَيحَْسَ‏ بُ‏ ٱلإِ‏ نسَانُ‏ أَن يُتْ‏ رَكَ‏ سُدً‏ ى﴾‏

Ayahsabu al-insanu an yutraka sudan (Surat Al Qiyama 75:36)

Tafsir: Hivi anajihesabu mtu kua ataachwa bila kuhukumiwa?


118

Hivi jee kweli inawezekana kiumbe Ibn Adam kiachiwe tu bila ya kudhibitiwa na

Muumba wake juu ya majukumu yake kwa Mola wake na kwa viumbe wenzake? Bila ya

kuamrishwa kua lipi alifanye na kukatazwa lipi asilifanye na jee anafikiria kua

hatohesabiwa na kuhukumiwa kwa kila analolifanya hapa Ulimwenguni? Na kama

anafikiria hivyo basi huyu ni kiumbe ambae hakumuamini Mola wake kwani anaamini

kua Allah Subhanah wa Ta’ala alieumba kila kitu hana habari na kila kiumbe chake na

wala hajui kitu chochote juu yake, jambo ambalo haliingii akilini.

Kwani Allah Subhnah wa Ta’ala ambae ndie alieiumba Dunia na kuipamba kwa ajili ya

Waja wake ili wasipate shida katika mazingira yao na hapo hapo wasighafilike juu yake

basi anasema katika Qur’an kua:

‏﴿زُيِّنَ‏ لِل َّذِينَ‏ كَ‏ فَ‏ رُواْ‏ ٱلحَْيَاةُ‏ ٱلد ُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ‏ مِنَ‏ ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ وَٱل َّذِينَ‏ ٱت َّ قَواْ‏ فَوْقَهُمْ‏

يَوْمَ‏ ٱلْقِيَامَةِ‏ وَٱهلل َُّ‏ يَرْزُقُ‏ مَن يَشَآءُ‏ بِغَيرِْ‏ حِ‏ سَابٍ‏ ‏۞كَانَ‏ ٱلن َّاسُ‏ أُم َّةً‏ وَاحِ‏ دَةً‏ فَبَعَ‏ ‏َث

ٱهلل َُّ‏ ٱلن َّبِيِّينَ‏ مُبَشِّ‏ رِينَ‏ وَمُنذِرِينَ‏ وَأَنزَلَ‏ مَعَهُمُ‏ ٱلْكِتَابَ‏ بِٱلحَْقِّ‏ لِيَحْكُمَ‏ بَينَْ‏ ٱلن َّاسِ‏ فِيمَا

ٱخْتَلَفُواْ‏ فِيهِ‏ وَمَا ٱخْتَلَفَ‏ فِيهِ‏ إِلا َّ ٱل َّذِينَ‏ أُوتُوهُ‏ مِن بَعْدِ‏ مَا جَآءَتْهُمُ‏ ٱلْبَيِّنَاتُ‏ بَغْياً‏

بَيْنَهُمْ‏ فَهَدَى ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ لِمَا ٱخْتَلَفُواْفِي هِمِ‏ نَٱ لحَْقِّ‏ ‏ِإبذْنِهِ‏ وَٱهلل َُّ‏ يَهْدِى مَن

يَشَآءُ‏ إِلىَٰ‏ صِرَاطٍ‏ م ُّسْتَقِيمٍ‏ ﴾

Zuyyina lilladheena kafaroo alhayatu alddunya wayaskharoona mina alladheena

amanoo waalladheena ittaqaw fawqahum yawma alqiyamati waAllahu yarzuqu

man yashao bighayri hisabin; Kana alnnasu ommatan wahidatan fabaAAatha

Allahu alnnabiyyeena mubashshireena wamundhireena waanzala maAAahumu

alkitaba bialhaqqi liyahkuma bayna alnnasi feema ikhtalafoo feehi wama ikhtalafa

feehi illa alladheena ootoohu min baAAdi ma jaat-humu albayyinatu baghyan

baynahum fahada Allahu alladheena amanoo lima ikhtalafoo feehi mina alhaqqi biidhnihi

waAllahu yahdee man yashao ila siratin mustaqeemin(Surat Al Baqara

2:212-213)

Tafsir: Yamependezeshewa kwa waliokufuru Maisha ya Duniani na hivyo huwafanyia

maskhara walioamini, na wale wanaomcha (wanaotii maamrisho ya Allah Subhnaha

wa Ta’ala na kukaa mbali na makatazo yake), watakua juu yao katika siku ya Kiama,

Na Allah humruzuku amtakae bila ya kiasi. Walikua watu ni umma mmoja kisha Allah


119

akawatumia Manabii wenye Kubainisha na Kuusia, na pamoja nao akawatumia

Maandiko kwa haki ili watoe hukumu baina ya Watu katika mambo waliyotofautiana,

na hawakuhitilafiana navyo (Vitabu hivyo) isipokua wale waliokwishapewa baada ya

kubainishiwa kutokana na chuki baina yao, kisha akawaongoza Allah wale

walioamini kutokana na kile walichohitilafiana kuwaelekeza katika haki kutokana na

Idhini yake. Na kwa hakika Allah humuongoza amtakae katika njia iliyonyooka.

Kutokana na maneno ya aya hio basi ndio maana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akawa ni mwenye kupenda kuisoma dua ifuatayo katika wakati wa usiku anaposali Salat

Dhuha.

‏(الل َّهُم َّ رَب َّ جِ‏ بْرَائِيلَ‏ وَمِيكَائِيلَ‏ وَإِسْرَافِيلَ،‏ فَاطِرَ‏ ال َّسمَوَاتِ‏ وَالأَرْضِ‏ ، عَالمَِ‏ الْغَيْ‏ ‏ِب

وَالش َّهَادَةِ،‏ أَنْتَ‏ تحَْكُمُ‏ بَينَْ‏ عِبَادِكَ‏ فِيمَا كَانُوا فِيهِ‏ يخَْتَلِفُونَ،‏ اهْدِنيِ‏ لِمَا اخْتُلِ‏ ‏َف

فِيهِ‏ مِنَ‏ الحَْقِّ‏ إبِ‏ ذْنِكَ‏ ، إِن َّكَ‏ تَهْدِي مَنْ‏ تَشَاءُ‏ إِلىَ‏ صِرَاطٍ‏ مُسْتَقِيمٍ)‏

(Allahumma Rabb Jibrail wa Mikail waI'iisrafila, fatir alssamawat wal'ardhi,

aA’alim alghayb walshshahadati, 'ant tahkum bayn aIibadik fima kanuu fih

yakhtalifuna, ahdini lima akhtulif fih min alhaqq bi'idhnika, 'innak tahdi man

tasha' 'iilaa sirat mustaqimin)

Tafsir: Ya Allah Rabbi wa Jibril, na Mikail na Israfil, Muanzilishi wa Mbingu na

Ardhi, Mwenye kujua yaliyofichikana na yaliyowazi, hakika wewe ni mwenye

kuhukumu baina ya waja wako juu ya kile walichokhitilafiana, niongoze kutokana na

kile walichohitilafiana niwe katika Haki kwa idhini yako, kwa hakika wewe ni mwenye

kuwaongoza uwatakao katika njia iliyonyooka.

Hii ni Dua muhimu sana ambayo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua

akimuomba Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ni mola wa Malaika Jibril, Mikail na Israfil

kwa ajili ya uongofu wa Hapa Duniani na kesho Akhera, kwani hakuna usalama katika

siku ya malipo kesho Akhera hadi uwe ni mwenye kujihakikishia kua upo kwenye njia

iliyonyooka ambayo ndio njia ya waliofuzu kama anavyosema Allah Subhanah wa

Ta’ala:


120

‏﴿إِن َّ اهلل َّ يُدْخِ‏ لُ‏ ال َّذِينَ‏ آمَنُوا وَعَمِلُوا الص َّ الحَِاتِ‏ جَن َّاتٍ‏ تجَْرِي مِنْ‏ تحَْتِهَا

يحَُل َّوْنَ‏ فِيهَا مِنْ‏ أَسَاوِرَ‏ مِنْ‏ ذَهَبٍ‏ وَلُؤْلُؤًا وَلِبَاسُهُمْ‏ فِيهَا حَرِيرٌ‏

الط َّيِّبِ‏ مِنَ‏ الْقَوْلِ‏ وَهُدُوا إِلىَ‏ صِرَاطِ‏ الحَْمِيدِ﴾‏

الأَْنْهَاُر

۞ وَهُدُوا إَِلى

Inna Allaha yudkhilu alladheena amanoo waAAamiloo alssalihati jannatin tajree

min tahtiha al-anharu yuhallawna feeha min asawira min dhahabin walu/lu-an

walibasuhum feeha hareerun; Wahudoo ila alttayyibi mina alqawli wahudoo ila

sirati alhameedi (Surat Al Hajj 22:23-24)

Tafsir: Hakika Allah atawaingiza wale waliomuamini na wakafanya mambo mema

katika Bustani (Peponi) ambazo chini yake kuna kuna mito ambamo watapambwa

ndani yake kwa makoja ya Dhahabu na Lulu na nguo zao zitakua za Hariri. Na

Wameongozwa kutokana na (kutumia) bora miongoni mwa kauli (Dhikr Allah, Lâ

ilâha ill-Allâh, Alhamdu lillâh, Kusoma Qur’an, Kuamrishana Mema n.k) na

wakaongozwa katika njia iliyonyooka.

Hivyo bila ya shaka Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ametujaalia mahitaji yetu yote

hapa Ulimwenguni ni mwenye kujua na kuona kila kitu juu yetu hivyo ni wajibu wetu

kumuamini na kumtii na kufahamu kua bila ya shaka baadae kuna kuhesabiwa amali zetu

na ambapo kwa watakaoamini na kujichunga basi watakua ni miongoni mwa waliofuzu

na wale wasioamini na kucheza basi watakua ni miongoni mwa waliokula hasara kwani

mwisho wake watafikia mahali pabaya sana kama inavyosema Qurán:

‏﴿يُثَبِّتُ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ بِٱلْقَوْ‏ لِ‏ ٱلث َّابِتِ‏ فىِ‏ ٱلحَْيَاةِ‏ ٱلد ُّنْيَا وَفىِ‏ ٱلآخِ‏ رَةِ‏ وَيُضِل ُّ ٱهلل َُّ‏

ٱلظ َّالِمِينَ‏ وَيَفْعَلُ‏ ٱهلل َُّ‏ مَا يَشَآءُ‏ ‏۞أَلمَْ‏ تَرَ‏ إِلىَ‏ ٱل َّذِينَ‏ بَد َّلُواْ‏ نِعْمَةَ‏ ٱهلل َِّ‏ كُ‏ فْ‏ راً‏ وَأَحَ‏ ل ُّواْ‏

قَوْمَهُمْ‏ دَارَ‏ ٱلْبَوَارِ۞جَ‏ هَ‏ ن َّمَ‏ يَصْ‏ لَْونَهَ‏ ا وَبِئْسَ‏ ٱلْقَرَارُ۞وَجَعَلُواْ‏ هللِ َِّ‏ أَنَدا د اًلِّيُ‏ ضِل ُّواْ‏ عَن

سَبِيلِهِ‏ قُلْ‏ تمََت َّعُواْ‏ فَإِن َّ مَصِيرَكُمْ‏ إِلىَ‏ ٱلن َّارِ۞قُل لِّعِبَادِىَ‏ ٱل َّ ‏ِذينَ‏ آمَنُواْ‏ يُقِيمُواْ‏ ٱلص َّلاَةَ‏

وَيُنْفِقُواْ‏ ممِ َّا رَزَقْنَاهُمْ‏ سِ‏ رّاً‏ وَعَلانِيَةً‏ مِّن قَبْلِ‏

أَن ‏َْتِىَ‏ يَوْمٌ‏ لا َّ بَيْعٌ‏ فِيهِ‏ وَلاَ‏

خِ‏ لاَلٌ‏ ‏۞ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِى خَلَقَ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضَ‏ وَأَنزَلَ‏ مِنَ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ مَآءً‏ فَأَخْرَجَ‏ بِِه


121

مِنَ‏ ٱلث َّمَرَاتِ‏ رِزْقاً‏ ل َّكُمْ‏ وَسَخ َّرَ‏ لَكُمُ‏ ٱلْفُلْكَ‏ لِتَجْرِىَ‏ فىِ‏ ٱلْبَحْرِ‏ أبَِمْرِهِ‏ وَسَخ َّرَ‏ لَ‏ ‏ُكُم

ٱلأَنْهَارَ۞‏ وَسَخ َّر لَكُمُ‏ ٱلش َّمْسَ‏ وَٱلْقَمَرَ‏ دَآئِبَينِْ‏ وَسَخ َّرَ‏ لَكُمُ‏ ٱلْل َّيْل

َ

ٱ ل ن ‏َو َّ هَا رَ‏ ‏۞وَآاتَكُم مِّن ِ كُل مَا سَأَلْتُمُوهُ‏ وَإِن تَعُد ُّواْ‏ نِعْمَةَ‏ ٱهلل َِّ‏ لاَ‏ تحُْصُوهَا إِ‏ َّن

ٱلإنْسَانَ‏ لَظَلُومٌ‏ كَف َّارٌ‏ ﴾

Yuthabbitu Allahu alladheena amanoo bialqawli alththabiti fee alhayati alddunya

wafee al-akhirati wayudhillu Allahu aldhdhalimeena wayafAAalu Allahu ma

yasha/o; Alam tara ila alladheena baddaloo niAAmata Allahi kufran waahalloo

qawmahum dara albawari; Jahannama yaslawnaha wabi/sa alqararu;

WajaAAaloo lillahi andadan liyudhilloo AAan sabeelihi qul tamattaAAoo fa-inna

maseerakum ila alnnari, Qul liAAibadiya alladheena amanoo yuqeemoo alssalata

wayunfiqoo mimma razaqnahum sirran waAAalaniyatan min qabli an ya/tiya

yawmun la bayAAun feehi wala khilalun; Allahu alladhee khalaqa alssamawati

waal-ardha waanzala mina alssama-i maan faakhraja bihi mina alththamarati

rizqan lakum wasakhkhara lakumu alfulka litajriya fee albahri bi-amrihi

wasakhkhara lakumu al-anhara; Wasakhkhara lakumu alshshamsa waalqamara

da-ibayni wasakhkhara lakumu allayla waalnnahara; Waatakum min kulli ma

saaltumoohu wa-in taAAuddoo niAAmata Allahi la tuhsooha inna al-insana

ladhaloomun kaffarun (Surat Ibrahim 14:27-34)

Tafsir: Allah atawapa msimamo wenye kauli thabit wale wanaomuamini hapa Duniani

na Akhera, na Allah atawapotosha wale wenye kujidhulumu na Allah hufanya kile

akitakacho. Jee hujawaona wale ambao wamebadilisha Neema za Allah kua ni Kufuru

na kuwasababishia watu wao kukaa katika sehemu ya maangamizo? Jahannama ndio

utakaowaunguza! Na kwa hakika ni sehemu mbaya sana kukaa ndani yake, na

wanajaalia Miungu myengine dhidi ya Allah ili kuwapotosha watu kutokana na

muongozo wake, Waambie: Kuleni Raha!kwani kwa hakika mtakapofikia mwisho

wenu ni Motoni. Waambie (Ewe Muhammad) waja wangu walioamini! Kua

wasimamishe Sala, na watoe kutokana na kile tulichowaruzuku kwa siri na kwa

dhahir, kabla ya kuwasili siku ambayo itakua hakuna kupatana wala kupendeleana.

Allah ni yule ambae alieumba Mbigu na Ardhi na akashusha maji kutoka mbiguni,

na kutokana nayo akatoa matunda kua ni rizki kwa ajili yenu, na akazifanya Meli kua

kwa ajili ya matumizi yenu, ili muweze kuelea (kusafiri) juu ya Bahari kutokana na

amri yake na Mito kua kwa ajili yenu. Na akalifanya Jua na Mwezi kua daima ni yenye

kupita katika njia zake kwa ajili yenu, na akajaalia Mchana na Usiku kua ni kwa ajili

yenu. Na akakupeni kila kitu mlichohitaji. Na kama mtazihesabu Neema za Allah juu

ّ


122

yenu, basi kamwe hamtoweza kuzihesabu. Ama kwa Hakika Mtu ni mwenye

kujidhulumu na ni mwenye kukufuru

Allah Akbar! Wa Alhamd lillah! wa La Illah Ila Allah! Allah Subhanah wa Ta’ala ambae

ndie Mola wa Ulimwengu wote na kila kilichomo ndani yake, anatuwekea wazi namna

anavyotupenda sana waja wake na hivyo bila ya shaka yeye ni mwenye kutuonea huruma

kutokana na udhaifu wa Nafsi zetu na matamanio ya Ulimwengu huu wa mpito na

kututahadharisha juu ya siku ya Malipo siku ambayo itakua hakuna kupatana wala

kupendeleana.

Naam, kutokana na Ukarimu wake juu yetu kwa kutujaalia kila aina ya Neema

tunazozihitaji basi pia akatujaalia kutumwagia Rehma zake juu yetu Ibn Adam, kwa

kutupa nafasi ya kuomba msamaha wake kwa kila atakaeamua kurudi kwake, na pia kwa

kutuma Mitume kwa kila baada ya mda ili kutukumbusha waja wake juu yake, Mitume

hao ni kutoka miongoni mwa watu wa jamii husika ili watoe muongozo, maonyo na

kuwausia watu juu yake pale watu hao wanapopotoka kutokana na njia iliyosahih ya

kuelekea kwake kabla ya yeye kuamua kuwashushia wanaopotoka adhabu kali isiyoweza

kustahmilika kutokana na maumbile yetu Ibn Adam, kama inavyosema Qurán katika aya

zifuatazo.

‏﴿م َّنِ‏ ٱهْتَدَىٰ‏ فَإِنم ََّا يَهْتَدِ‏ ى لِنَفْسِ‏ هِ‏ وَمَن ضَل َّ فَإِنم ََّا يَضِل ُّ عَلَيْهَا وَلاَ‏ تَ‏ زِرُ‏ وَازِرَةٌ‏ وِزْرَ‏

أُخْرَىٰ‏ وَمَا كُن َّا مُعَذِّبِينَ‏ حَتى َّ ٰ نَبْعَثَ‏ رَسُولاً‏ ۞ وَإِذَآ أَرَدَْ‏ أَن ن ُّهْ‏ لِكَ‏ قَرْيَةً‏ أَمَرَْ‏

مُتْرَفِيهَا فَفَسَقُواْ‏ فِيهَا فَحَق َّ عَلَيْهَا ٱلْقَوْلُ‏ فَدَم َّرَْهَا تَدْمِيراً‏ ﴾

Mani ihtada fa-innama yahtadee linafsihi waman dhalla fa-innama yadhillu

AAalayha wala taziru waziratun wizra okhra wama kunna muAAadhdhibeena

hatta nabAAatha rasoolan, Wa-idha aradna an nuhlika qaryatan amarna

mutrafeeha fafasaqoo feeha fahaqqa AAalayha alqawlu fadammarnaha tadmeeran

(Surat Al Isra 17:15-16)

Tafsir: Ama kwa yule atakeongoka basi hua ni mwenye kuiongoa Nafsi yake, na

mwenye kupotoka basi hua ni mwenye kuipotosha Nafsi yake, na hakuna mbebaji

atakaebeba mzigo wa mwenzake. Na sisi kamwe hatuadhibu hadi inapokua tayari

tumeshatuma Mjumbe (kuonya). Na tunapoamua kuuangamiza Mji basi hua

tunatuma amri kwanza (kwa watu husika kua wamtii Allah Subhanah wa Taála) kwa

baadhi miongoni mwao ambao wamepewa vizuri katika uhai huu. Na kisha wakavuka

mipaka kutokana na kupewa huko, basi hapo ndio kauli (ya adhabu) inawahalalikia


123

juu yao. Na kisha baada ya hapo ndio tunauangamiza (Mji au Ummah husika) kabisa

kabisa.

Anasema Sultan al Mutakallimin Mujaddid ud Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi juu ya

ayah hii kua: ‘Wakati Allah Subhanah wa Taála anapotaka kuuangamiza mji

kutokana na dhambi za watu wake, basi hua haharakishi katika kuungamiza mji

husika kwa sababu ya kuwepo kwa madhambi hayo, bali huwaamrisha wenye

uwezo miongoni mwa watu hao kuachana na dhambi husika, kwani wenye uwezo

wanapofanya dhambi hizo wao basi wale wasiokua na uwezo nao huwafuata katika

hayo. Hivyo wanapo kataa kuachana na dhambi husika basi ndio huadhibiwa kwa

adhabu husika, na wamelengwa wenye uwezo kwa sababu wao ndio ambao

wanatakiwa zaid kumshukuru Allah Subhanah wa Taála kwa kuwapendelea kwa

neema alizowajaalia. Hivyo baada ya onyo la kwanza basi huwapa nafasi watu hao

kwa kuwaonya tena mara kadhaa, na wakiendelea kudumu katika dhambi hizo basi

na Adhabu husika huwashukia watu hao.’

Mbali ya kua Allah Subhanah wa Ta’ala anatuambia katika Qurán kua hashushi adhabu

hadi atume Mitume wake kuonya ili wawaonye watu na kuwarudisha watu katika njia

moja ya haki ya kimaumbile ya kumpwekesha Allah Subhanah wa Taála lakini pia hapo

hapo, inatuwekea wazi kua kila Ummah wa wakati husika ulikua ni wenye kutumia

Hukmu na njia tofauti zilizokua zikiendana na Nyakati husika, kwa mfano tunapoiangalia

kitabu cha Zabur cha Nabii Daud basi tunaona kua mbali ya kua kilikua kinabashiria

mambo yatakayotokea katika miaka ya baadae lakini pia kilikua ni kitabu kilichokua

hakina Sharia wala Hukmu ndani yake, lakini kilikua kinazungumzia mambo ya Halali

na Haram tu basi ndani yake.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala katuwekea wazi kua Qurán ndio kitabu kilichokuja

kubatilisha vitabu vyote vya Mitume wengine vilivyokuja kabla yake na hivyo

kumwambia Mtume wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kua Qurán ndio

chenye kauli ya mwisho na chenye uthibitisho juu ya vitabu vyote walivyopewa Mitume

waliotangulia kabla yake, na yaliyoteremshwa ndani ya Qurán ndio yanayotakiwa

kufuatwa badala yake kwa kusema:

‏﴿وَأَنزَلْنَآ إِلَيْكَ‏ ٱلْكِتَابَ‏ بِٱلحَْقِّ‏ مُصَدِّقاً‏ لِّمَا بَينَْ‏ يَدَيْهِ‏ مِنَ‏ ٱلْكِتَابِ‏ وَمُهَيْمِناً‏ عَ‏ لَيْهِ‏

ٍ

ّ

فَٱحْكُم بَيْنَهُم بمَِآ أَنزَلَ‏ ٱهلل َُّ‏ وَلاَ‏ تَت َّبِعْ‏ أَهْوَآءَهُمْ‏ عَم َّا جَآءَكَ‏ مِنَ‏ ٱلحَْقِّ‏ لِكُل جَعَلْنَا


124

مِنكُمْ‏ شِ‏ رْعَةً‏ وَمِنْهَاجاً‏ وَلَوْ‏ شَآءَ‏ ٱهلل َُّ‏ لجََعَلَكُمْ‏ أُم َّةً‏ وَاحِ‏ دَةً‏ وَلَٰكِن لِّيَبْلُوَكُمْ‏ فىِ‏ مَآ

آاتَكُم فَاسْتَبِقُوا الخَيْرَاتِ‏ إِلىَٰ‏ اللهِ‏ مَرْجِ‏ عُكُمْ‏ جمَِيعاً‏ فَيُنَبِّئُكُم بمَِا كُنتُمْ‏ فِيهِ‏ تخَْتَلِفُونَ‏ ﴾

Waanzalna ilayka alkitaba bialhaqqi musaddiqan lima bayna yadayhi mina

alkitabi wamuhayminan AAalayhi faohkum baynahum bima anzala Allahu wala

tattabiAA ahwaahum AAamma jaaka mina alhaqqi likullin jaAAalna minkum

shirAAatan waminhajan walaw shaa Allahu lajaAAalakum ommatan wahidatan

walakin liyabluwakum feema atakum faistabiqoo alkhayrati ila Allahi

marjiAAukum jameeAAan fayunabbi-okum bima kuntum feehi takhtalifoona

(Surat Al Maidah 5:48)

Tafsir: Na kwako wewe tumetuma Kitabu kwa Haki na Ukweli, kuthibitisha vitabu

vilivyotangulia kabla yake na chenye uongofu na uthibitisho zaidi juu yake. Hivyo toa

hukumu baina yao kutokana na alivyoteremsha Allah, na kamwe usifuate matamanio

yao, yatakayokutoa katika Haki iliyokujia wewe. Kwa kila mmoja miongoni mwenu

amebainishiwa Sharia na njia iliyowazi. Kama Allah angelitaka basi angekujaalieni

nyie kua Ummah mmoja. Lakini (mipango yake) ni kukujaribuni nyinyi juu ya kile

alichokujaalieni, hivyo jitahidini kwa kukimbilia katika kufanya mema. Marejeo ya

kila mmoja wenu ni kwa Allah. Ni yeye ndie ambae atakaekuonesheni ukweli juu ya

kile mnachohitilafiana.

Ama kuhusiana na aya hii basi anasema Qatadah kua; ‘Ingawa watu wa Mataifa yote

ya hapo awali yalikua yakifuata Dini Moja inayompwekesha Allah Subhanah wa

Ta’ala pekee, lakini wote walikua na Shariah tofauti’. Hapa sasa umefika wakati wa

kuwaangalia Mitume na Manabii hao waliotangulia na kutajwa katika Qurán.

MITUME NA MANABII WALIOTAJWA KATIKA QURÁN.

Kwa lugha ya kiarabu neno ‘Nabi’ lina maana ya habari au ripoti. Hivyo mtu huitwa

‘Nabi’ (Nabii) kwa sababu hua anatoa habari kuhusiana na Mola wake na pia hua

anapokea habari kutoka kwa Mola wake kupitia kwa Malaika Jibril. Kwa kishariah

neno ‘Nabi’ yaani Nabii, humaanisha mtu alie na sifa ya ubora ambayo

amehamasishwa kwa kupitia njia za Wahy kufanya vitendo vyake bila ya


125

kuamrishwa kuwafikishia watu wengine ujumbe wa Wahy huo na hivyo mtu huyo

huutekeleza ujumbe huo yeye mwenyewe binafsi.

Na ‘Rasul’ (Mtume) humaanisha mtu alie na sifa ya ubora ambayo amehamasishwa

kwa kupitia njia za Wahy kufanya vitendo vyake na kuamrishwa kuueneza na

kuwafikishia watu wengine ujumbe wa wahy huo. Hivyo kila Rasul (Mtume) hua ni

lazima kua Nabi (Nabii) lakini si lazima kwa kila Nabi (Nabii) kua ni Rasul (Mtume).

Katika kulifafanua zaidi hili basi na tuangalie mtizamo wa Imam Jaffar As Sadiq ambae

yeye anasema kua: Manabii wamegawika katika makundi manne:

1 - Nabii ambae hua anapokea Wahy na Ilham lakini hua hana jukumu la kueneza

ujumbe ulio ndani ya Wahy au Ilham husika kwa watu wengine.

2 - Nabii ambae hua anaona na kusikia ujumbe anaoletewa katika wakati ambao

akiwa macho wazi yaani hajalala na hayuko usingizini au katika wakati macho

yakiwa ameyafunga yaani akiwa usingizini lakini nae pia hua hana jukumu la

kueneza ujumbe huo kwa watu wengine.

3 - Nabii ambae hua ni Nabii Al Mursal ambae yeye hua anapokea ujumbe na

kuamrishwa kuutanaza ujumbe husika kwa baadhi ya watu tu.

4 - Nabii ambae hua ni hua anapokea Wahy na kutumwa kuueneza ujumbe huo kwa

watu wote kwa ujumla.

Anasema Hujjat ul Islami Mujaddid ud Din Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali kua: Kama ilivyokua kwa viumbe Ibn Adam kutofautishwa

na wanyama wengine kwa wao Ibn Adam kupewa Nafsi yenye Ufahamu, basi ndio

hivyo hivyo walivyotofautishwa Ibn Adam wengine na Mitume na Manabii kwani

Nafsi na Roho za Mitume na Manabii hutofautiana na za watu wa kawaida kwa

sababu wao hua ni waliopewa Uongofu na Ufahamu wenye kuongoka zaidi tofauti

na watu wengine, kwani Uongofu wao huwaongoza katika njia ya Allah Subhanah

wa Taála. Kama vile ilivyokua mwendo wa kutembea wa Ibn Adam kua ni tofauti

na ni Miujiza kwa Wanyama wengine basi ndio hivyo hivyo inavyokua kwa miendo

ya Mitume kuelekea kwa Mola wao kwani miendo yao hua ni tofauti na ni Miujiza

kwa Ibn Adam wengine.

Hivyo kushushiwa kwa Mitume na Manabii kwa watu hua ni Rehma kubwa sana kutoka

kwa Allah Subhanah wa Ta’ala. Tukiangalia historia ya Ulimwengu tunaona kua

ustaarabu Ulimwenguni ulianzia katika maeneo ya Mashariki ya kati baina ya nchi za

Misri, Syria, Iraq na Uarabuni, na hii ni kwa sababu maeneo hayo ndio maeneo ambayo


126

yalikua na idadi kubwa ya jamii za watu katika kipindi cha mwanzoni mwa maisha ya

Ulimwenguni kuliko maeneo mengine, hivyo idadi hiyo kubwa ya jamii za watu

waliokua wakiishi katika maeneo hayo kulipelekea kutumiwa kwa Mitume na Manabii

wengi katika maeneo hayo.

Mitume na Manabii hao walikua na miongoni mwa wenye sifa kuu zifuatazo:

1. Mitume na Manabii walitoka miongoni mwa Bani Adam, hawakutoka miongoni

mwa Majini au Malaika.

2. Mitume na Manabii walikua na sifa za uaminifu, ukweli, kutokufanya dhambi.

Hua hivi ili madai yao yakubaliwe na kupandishwa darja ya juu.

3. Mitume na Manabii walikua na sifa za kua na ufahamu uliokamilia, uhakika na

uongofu.

4. Mitume na Manabii walikua ni lazima wafikishe kwa watu wao ujumbe wote wa

Wahyi walioamriwa kuufikisha, hawakuficha kitu chochote.

5. Mitume na Manabii walikua ni Wanaume.

Ama kuhusiana na sifa ya tano, basi kuna kutofautiana kuhusiana na mtizamo wa

waliopewa Unabii kua ni Wanaume tu, kwani kwa tizamo wa Wanazuoni wanaofuata

mitizamo ya Aqida ya Maturidi basi wao wanaosema kua waliopewa Utume walikua ni

Wanaume tu.

Ama kwa upande wa Wanazuoni wanaofuata mtizamo wa Aqida ya Ashari basi wao

wanasema kua miongoni mwa waliopewa Unabii walikuemo pia Wanawake.

Kwa upande wa wafuasi wa Maturidi ambao ndio wanaosema kua waliopewa Unabii

walikua ni wanaume tu, basi wao wanasimamia katika uthibitisho wa aya ambayo

imetumia neno “Rijalan”, ambapo kwa mtizamo wao basi ni kua neno hilo hua

linamaaisha kua ni Mwanamme, aya hio ni ile isemayo kua:

‏﴿وَمَآ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ‏ إِلا َّ رِجَالاً‏ ن ُّوحِ‏ ى إِلَيْهِمْ‏ فَاسْئَلُواْ‏ أَهْلَ‏ الذِّكْرِ‏ إِن كُنتُمْ‏ لاَ‏

تَعْلَمُونَ﴾‏


127

Wama arsalna qablaka illa rijalan noohee ilayhim fais-aloo ahla aldhdhikri in

kuntum la taAAlamoona. (Surat al-Anbiya 21:7)

Tafsir: Na hatukutuma kabla yako Rijalan yeyote isipokua watu ambao

tuliwahamasisha, hivyo uliza wenye kujua ikiwa wewe hujui.

Lakini hata hivyo miongoni mwa Wanazuoni wenye I’lm ya Tafsir ambao ni wafuasi wa

Aqida ya Ashari wanasema katika kutafsiri aya hii kua neno 'Rijalan’, lililotumika hapa

linajumuisha Wanaume na Wanawake, hivyo miongoni mwa Manabii pia wapo Manabii

wanawake. Miongoni mwa Wanazuoni wenye mtizamo huo ni pamoja na Imam Abu

Hasan Al Ashari, Imam Fakhr Ad Din Al Razi (Katika Al Durr Al Mukhtari), Imam Al

Suyuti (Katika kitabu chake cha Al Ashbah wal Nazair), Imam Kamal al Humam (katika

kitabu cha Husun al Uswah), Imam Ibn Hazm, Imam Al Mubarkafuri (katika kitabu cha

Tuhfat al Awhathi) n.k.

Wanazuoni hao wanasimamia katika hoja ya vithibitisho ambavyo miongoni mwao ni

pamoja na pale Allah Subhanahu wa Ta’ala aliposema kuhusiana na Yuhanz ambae ni

mama yake Nabii Musa kua: ‘Na tukamshushia Wahyi mama yake Musa’, katika Surat

Al Qasas isemayo:

‏﴿وَأَوْحَيْ‏ نَآ إِلىَٰ‏ أُمِّ‏ مُوسَ‏ ى ٰ أَنْ‏ أَرْضِ‏ عِيهِ‏ فَإِذَا خِ‏ فْ‏ تِ‏ عَلَيْهِ‏ فَأَلْقِيهِ‏ فىِ‏ ٱليَمِّ‏ وَلاَ‏ تخََاِفى

وَلاَ‏ تحَْزَنيِۤ‏ إِ َّ رَآد ُّوهُ‏ إِلَيْكِ‏ وَجَاعِلُوهُ‏ مِنَ‏

ٱلْمُرْسَلِ‏ ‏َين ﴾

Waawhayna ila Ummi Moosa an ardhiAAeehi fa-idha khifti AAalayhi faalqeehi fee

alyammi wala takhafee wala tahzanee inna raddoohu ilayki wajaAAiloohu mina

almursaleena (Surat Al Qasas 28:7)

Tafsir: Na tukamshushia Wahyi mama yake Musa (kumwambia): ‘Mnyonyeshe

(Musa), lakini ikiwa utakhofia juu yake, basi mtie mtoni na wala usiwe na khofu yeyote

wala huzuni. Kwani kwa hakika sisi tutamrudisha kwako wewe na tutamfanya kua ni

miongoni mwa Mitume yetu’.

Na uthibitisho uliomo katika Surat Maryam, pale Allah Subhanahu wa Ta’ala aliposema:


128

‏﴿وَٱذْكُرْ‏ فىِ‏ ٱلْكِتَابِ‏ مَرْيمََ‏ إِذِ‏ ٱنتَبَذَتْ‏ مِ‏ نْ‏ أَهْ‏ لِهَ‏ ا مَكَ‏ اً‏ شَ‏ رْقِياً‏ ۞ فَٱتخ ََّذَ‏ ‏ْت مِن

دُوِِم حِ‏ جَاابً‏ فَأَرْسَلْنَآ إِلَيْهَآ رُوحَنَا فَتَمَث َّلَ‏ لهََا بَشَراً‏ سَوًِّ‏ ۞ قَالَ‏ ‏ْت إِنيّ‏

بِٱلر َّحمَْٰنِ‏ مِ‏ نكَ‏ إِن كُ‏ نتَ‏ تَقِيّاً‏ ۞ قَالَ‏ إِنم ََّآ أََْ‏ رَسُولُ‏ رَبِّكِ‏ لاًّهَبَ‏ لَكِ‏ م غُلَ‏ اًزَكِيّاً‏ ﴾

ِۤ أَعُوذُ‏

Waodhkur fee alkitabi maryama idhi intabadhat min ahliha makanan sharqiyyan;

Faittakhadhat min doonihim hijaban faarsalna ilayha roohana fatamaththala laha

basharan sawiyyan; Qalat innee aAAoodhu bialrrahmani minka in kunta taqiyyan;

Qala innama ana rasoolu rabbiki li-ahaba laki ghulaman zakiyyan (Surat Maryam

19:16-19)

Tafsir: Na ametajwa katika kitabu, Maryam, wakati alipojitenga kutokana na familia

yake katika sehemu inayoelekea upande wa Mashariki; Akaweka pazia kabla yao,

kisha tukamtumia Ruhi (Malaika) wetu alietokea mbele yake katika umbo la mtu

aliejaa heshima; Nae akasema: ‘Hakika mimi ninajilinda kwako na kwa Mwingi wa

Rehma, ikiwa unamuogopa Allah’; Nae (Malaika) akasema: ‘Mimi ni mjumbe kutoka

kwa Mola wako, (kukubashiria kua) utapata mtoto alie mwema’.

Kwani Allah Subhanahu wa Ta’ala alimchagua Maryam bint Imran na akamuamrisha

Malaika Jibril Alayhi Salaam kumshushia Wahyi wa kumbashiria habari njema kama

inavyofafanuliwa zaidi katika Surat Al Imran kwa kusema:

‏﴿وَإِذْ‏ قَالَتِ‏

ٱلْمَلاَئِكَةُ‏ يمَٰرْيمَُ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ ٱصْطَفَاكِ‏ وَطَه َّرَكِ‏ وَٱصْطَفَاكِ‏ عَلَى ٰ نِسَآِء

ٱلْعَالَمِينَ‏ ﴾

Wa-idh qalati almala-ikatu ya Maryamu inna Allaha istafaki watahharaki

waistafaki AAala nisa-i alAAalameena (Surat Al Imran 3:42)

Tafsir: Na (kumbuka) wakati Malaika aliposema: ‘Ewe Maryam! Kwa Hakika Allah

amekuchagua wewe na kukutakasa, na kukuchagua kua juu zaid ya Wanawake wote

wa Ulimwenguni’.

Na vile vile pale Allah Subhanahu wa Ta’ala alipomjumuisha Maryam bint Imran ambae

ni Mama yake Nabii Isa katika hali ambayo amewajumuisha Manabii wengine kwa

kusema katika Surat Al Imran:


129

‏﴿إِن َّ ٱهلل ََّ‏ ٰ ٱصْطَفَى آدَمَ‏ وَنُوحاً‏ وَآلَ‏ إِبْرَاهِيمَ‏ وَآلَ‏ عِمْرَانَ‏ عَلَى ٱلْعَالَمِينَ‏ ﴾

Inna Allaha istafa adama wanoohan waala ibraheema waala AAimrana AAala

alAAalameena (Surat Al Imran 3:33)

Tafsir: Hakika Allah amemchagua Adam, Nuh, familia ya Ibrahim na familia ya

Imran kua juu ya Alamin (Majini na Bani Adam wa wakati huo).

Na pia katika Surat Maryam pale Allah Subhanahu wa Ta’ala aliposema:

‏﴿أُولَٰئِكَ‏ ٱل َّذِينَ‏ أَنْعَمَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلَيْهِم مِّنَ‏ ٱلن َّبِيِّينَْ‏ مِن ذُرِّي َّةِ‏ ءادَمَ‏ وَممِ َّنْ‏ حمََلْنَا مَعَ‏ نُو ‏ٍح

وَمِن ذُرِّي َّةِ‏ إِبْرَاهِيمَ‏ وَإِسْرَائِيلَ‏ وَممِ َّنْ‏ هَدَيْنَا وَٱجْتَبَيْنَآ إِذَا تُتْلَى ٰ عَلَيْهِمْ‏ آَتُ‏ ٱلر َّحمَْٰ‏ ‏ِن

خَ‏ ر ُّو اْ‏ سُج َّداً‏ وَبُكِيّاً‏ ﴾

Ula-ika alladhina anAAama Allahu AAalayhim mina alnnabiyyeena

min dhurriyyati adama wamimman hamalna maAAa noohin wamin dhurriyyati

ibraheema wa-isra-eela wamimman hadayna waijtabayna idha tutla AAalayhim

ayatu alrrahmani kharroo sujjadan wabukiyyan (Surat Maryam 19:58)

Tafsir: Wao ni wale ambao Allah amewaneemesha kutoka katika miongoni mwa

Mitume, kutoka katika kizazi cha Adam, na wale tuliowachukua pamoja na Nuh, na

miongoni mwa kizazi cha Ibrahim na Israel na miongoni mwa wale tuliowaongoza na

kuwachagua. Wakati aya za mwenye wingi wa Rehma zinaposomwa, husujudu na

kulia.

Ambapo miongoni mwa kizazi cha Adam ni Idris, na miongoni mwa wale tuliowachukua

pamoja na Nabii Nuh katika Safina ni kizazi cha wazee waliomtoa Nabii Ibrahim, na

miongoni mwa kizazi cha Ibrahim ni Is-haq, Yaqub na Ismai’l na miongoni mwa Bani

Israel ni Mama yake Musa, Musa, Harun, Zakariyah, Yahya, Maryam na Isa Ibn Maryam.

Wanazuoni wanasema kua katika wanawake hao pia yumo Hawa mke wa Nabii Adam,

na vile vile Sarah aliekua mke wa Nabii Ibrahim, kama ilivyoelezewa katika Qurán kwa

kutumia njia ya kauli ya Sarah pale alipozungumza na Malaika walipokuja kumtembelea

Nabii Ibrahim na yeye akiwepo na kuwabashiriwa mtoto kama inavyoelezewa katika aya

ifuatayo:


130

‏﴿قَالَتْ‏ يٰوَيْلَتَا ءَأَلِدُ‏ وَأََْ‏ عَجُوزٌ‏ وَهَذَا بَعْلِى شَيْخًا إِن َّ هَذَا لَشَىْءٌ‏ عَجِ‏ يبٌ‏ ۞

ۤ قَالُو اْ‏ أَتَعْجَ‏ بِينَ‏ مِ‏ نْ‏ أَمْ‏ رِ‏ ٱهلل َِّ‏ رَحمَْةُ‏ ٱهلل َِّ‏ وَبَرَكَاتُهُ‏ عَلَيْكُمْ‏ أَهْلَ‏ ٱلْبَيْ‏ ‏ِت إِن َّهُ‏ حمَِيدٌ‏ مج َِّيٌد ﴾

Qalat ya waylata aalidu waana AAajoozun wahadha baAAlee shaykhan inna hadha

lashay-on Aaajeebun; Qaloo ataAAjabeena min amri Allahi rahmatu Allahi

wabarakatuhu AAalaykum ahla albayti innahu hameedun majeedun (Surat Hud

11:72-73)

Tafsir: Akasema (kwa kushangaa) ‘Ole wangu! Nitapata mtoto wakati mimi ni

kikongwe, na huyu hapa mume wangu ni kizee’. Nao (Malaika) wakasema: ‘Unaona

ajabu juu ya yale aliyoyakadiria Allah? Rehma za Allah na Baraka zake ziwe juu yenu,

Enyi familia ya Ibrahim. Hakika yeye (Allah) Mwenye kustahiki sifa zote na mwenye

Kushinda.’

Na pia habari hiyo kuelezewa kwa njia ya kuonesha picha ya vitendo katika Surat Adh

Dhuriyyat:

‏﴿فَأَقْبَلَتِ‏ ٱمْرَأَتُهُ‏ فىِ‏ صَر َّةٍ‏ فَصَك َّتْ‏ وَجْهَهَا وَقَالَتْ‏ عَجُوزٌ‏ عَقِيمٌ‏ ۞ قَالُواْقَا لُواْ‏

كَذٰ‏ لِكِ‏ قَالَ‏ رَب ُّكِ‏ إِن َّهُ‏ هُوَ‏ ٱلحَْكِيمُ‏ ٱلْعَلِيُم

Faaqbalati imraatuhu fee sarratin fasakkat wajhaha waqalat AAajoozun

Aaaqeemun; Qaloo kadhaliki qala rabbuki innahu huwa alhakeemu alAAaleemu

(Surat Adh Dhuriyyat 51:29-30)

Tafsir: Kisha Mke wake (Sarah) akakabiliana nao, na akajipiga vibao usoni na

kusema: ‘Kikongwe alie Mgumba!’. Nao (Malaika) wakasema: ‘Kadhalika hivyo

ndivyo asemavyo Mola wako. Hakika yeye ni mwingi wa Hikma, na ni Mjuzi wa kila

kitu.’

Na miongoni mwa Wanawake hao pia ni pamoja na Asiyah Bint Muzahim aliekua mke

wa Fir’awn, kutokana na kua ni mfano bora miongoni mwa wenye kuamini kama

isemavyo Qurán:


131

‏﴿وَضَرَبَ‏ ٱهلل َُّ‏ مَثَلاً‏ لِّل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ ٱمْرَأَةَ‏ فِرْعَوْنَ‏ إِذْ‏ قَالَتْ‏ رَبِّ‏ ٱبْنِ‏ لىِ‏ عِنَدكَ‏ بَيْتاً‏ ‏ِفى

ٱلجَْن َّةِ‏ وَنجَِّنىِ‏ مِن فِرْعَوْنَ‏ وَعَمَلِهِ‏ وَنجَِّنىِ‏ مِنَ‏ ٱلْقَوْمِ‏ ٱلظ َّالِمِينَ‏ ﴾

Wadharaba Allahu mathalan lilladheena amanoo imraata firAAawna idh qalat

rabbi ibni lee AAindaka baytan fee aljannati wanajjinee min firAAawna

waAAamalihi wanajjinee mina alqawmi aldhdhalimeena. (Surat At Tahrim 66:11)

Tafsir: Na Allah anatoa mfano kwa wale walioamini: Mke wa Fir’awn, pale

aliposema: ‘Mola wangu! Nijengee mimi nyumba kwako wewe Peponi, na uniokoe

kutokana na Fir’awn na amali zake, niokoe kutokana na watu madhalimu’

Ambapo aya inayofuatia baada ya hiyo inamsifia tena Maryam Bint Imran kwa kusema:

‏﴿وَمَرْيمََ‏ ٱبْنَةَ‏ عِمْرَانَ‏ ٱل َّتيِ‏ ۤ أَحْصَنَتْ‏ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِ‏ يهِ‏ مِن ر ُّ وحِنَا وَ‏ صَد َّ قَتْ‏

بِكَلِمَاتِ‏ رَب َّهَا وَكُتُبِهِ‏ وَكَانَتْ‏ مِنَ‏ ٱلْقَانِتِينَ‏ ﴾

Wamaryama ibnata AAimrana allatee ahsanat farjaha fanafakhna feehi min

roohina wasaddaqat bikalimati rabbiha wakutubihi wakanat mina alqaniteena

(Surat At Tahrim 66:12)

Tafsir: Na Maryam Bint Imran ambae alijihifadhi sehemu zake za Siri. Kisha

tukampulizia Roho kutoka kwetu, na akathibitisha Kauli ya Mola wake na Vitabu

vyake, na alikua ni miongoni mwa wenye Kumcha Mungu.

Hivyo kutokana na vithibitisho vyao hivyo tunaona kua Wanawake pia kama Wanaume

hua na sifa na uwezo wa kua miongoni mwa wenye kupokea Wahyi na hivyo hua kuna

uwezekano wa kua Manabii na vile vile kua ni miongoni mwa mifano bora inayofaa

kuigwa, ingawa hawakutajwa kua na Unabii kwa majina, kwani Allah Subhanahu wa

Ta’ala anasema kua kuna Mitume aliowataja majina na kuhadithia visa vyao katika

Qurán na vile vile pia kuna Mitume na Manabii ambao hakuwatajwa kwa majina katika

Qurán, kama inavyoelezea aya ifuatayo:


132

‏﴿إِ َّ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ‏ كَمَآ أَوْحَيْنَآ إِلىَ‏ نُوحٍ‏ وَٱلن َّبِيِّينَ‏ مِن بَعْدِهِ‏ وَأَوْ‏ ‏َحيْنَآ إِلىَٰ‏ إِبْرَهِيَم

وَإِسمَْعِيلَ‏ وَإْسْحَقَ‏ وَيَعْقُوبَ‏ وَالأَْسْبَا ‏ِط وَعِيسَ‏ ٰ ى وَأَي ُّوبَ‏ وَيُونُسَ‏ وَ‏ ‏َهرُونَ‏ وَسُلَيْمَ ‏َن

وَءَاتَيْنَا دَاوُودَ‏ زَبُوراً‏ ۞ وَرُسُلاً‏ قَدْ‏ قَصَصْنَهُمْ‏ عَلَيْكَ‏ مِن قَبْلُ‏ وَرُسُلاً‏ لم َّْ‏ نَْقصُصْهُ‏ ‏ْم

عَلَيْكَ‏ وَكَل َّمَ‏ اهلل َُّ‏ مُوسَى تَكْلِيماً‏ ۞ ر ُّسُلاً‏ م ُّبَشِّ‏ رِينَ‏ وَمُنذِرِينَ‏ لِئَلا َّ يَكُونَ‏ لِلن َّا ‏ِس

عَلَى ٱهلل َِّ‏ حُج َّةٌ‏ بَعْدَ‏ الر ُّسُلِ‏ وَكَا ‏َن ٱهلل َُّ‏ عَزِيزاً‏ حَكِيماً﴾‏

Inna awhayna ilayka kama awhayna ila noohin waalnnabiyyeena min baAAdihi

waawhayna ila ibraheema wa-ismaAAeela wa-ishaqa wayaAAqooba waal-asbati

waAAeesa waayyooba wayoonusa waharoona wasulaymana waatayna dawooda

zabooran; Warusulan qad qasasnahum AAalayka min qablu warusulan lam

naqsus-hum AAalayka wakallama Allahu moosa takleeman; Rusulan

mubashshireena wamundhireena li-alla yakoona lilnnasi AAala Allahi hujjatun

baAAda alrrusuli wakana Allahu AAazeezan hakeeman (Surat An Nisaa 4:163-165)

Tafsir: Hakika tumekushushia Wahyi wewe kama vile tulivyomshushia Nuh na

Manabii waliofuata baada yake. Na pia tulimshushia Wahyi Ibrahim, Isma`il, Ishaq,

Ya`qub, na Al-Asbat (kizazi cha watoto 12 wa Nabii Ya`qub) `Isa, Ayyub, Yunus,

Harun, na Sulayman; na Daud tukampa Zabur. Na Mitume ambayo tumekutajia wewe

kabla, na Mitume ambayo hatukukutajia, na Musa aliezungumza moja kwa moja na

Allah. Mitume kama wabebaji ujumbe mwema na maonyo pia, ili watu wawe hawana

kisingizio baada ya (kutumiwa) Mitume. Hakika Allah ni mwenye uwezo na ni mwingi

wa Hikma.

Na vile vile akasema tena Allah Subhanah wa Taála:

‏﴿وَلَقَدْ‏ أَرْسَلْنَا رُسُلاً‏ مِّن قَبْلِكَ‏ مِنْهُم م َّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ‏ وَمِنْ‏ ‏ُهمْ‏ م َّن لم َّْ‏ نَقْصُ‏ ‏ْص

قُضِى

عَلَيْكَ‏ وَمَا كَانَ‏ لِرَسُولٍ‏ أَن ‏َْتِىَ‏ آبِيَةٍ‏ إِلا َّ إبِِذْنِ‏ ٱهلل َِّ‏ فَإِذَا جَآءَ‏ أَمْرُ‏ ٱهلل َِّ‏ َ

بِٱلحَْقِّ‏ وَخَسِ‏ رَ‏ هُنَالِكَ‏ ٱلْمُبْطِلُونَ‏ ﴾


133

Walaqad arsalna rusulan min qablika minhum man qasasna AAalayka waminhum

man lam naqsus AAalayka wama kana lirasoolin an ya/tiya bi-ayatin illa bi-ithni

Allahi fa-itha jaa amru Allahi qudhiya bialhaqqi wakhasira hunalika almubtiloona

(Surat Al Ghafir 40:78)

Tafsir: Na kwa hakika sisi tulituma Mitume kabla yako (Ewe Muhammad), ambapo

baadhi yao tumekuhadithia juu yao na baadhi yao hatukuhadithia juu yao, na

haikuwahi kutokea kwa Mtume yeyote yule kupewa aya zetu isipokua kwa idhini ya

Allah, Hivyo inapokuja amri ya Allah basi jambo hilo litaamuliwa kwa haki na

wataofuata vyenginevyo watakua ni waliopotea.

Ama kwa upande mwengine basi Abu Dhar Radhi Allahu Anhu anasema kuhusiana na

idadi ya Mitume na Manabii katika hadith ifuatayo ambayo ni ndefu kidogo lakini yenye

mafunzo mengi ndani yake kua: ‘Siku moja niliingia Msikitini nikamkuta Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akiwa amekaa peke yake. Hivyo nikamuuliza: ‘Ya Rasul

Allah (Salallahu Alayhi wa Salam) Niambie kuhusiana na Ibada ya Sala ambazo

umetuamrisha?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Sala ni Ibada bora. Hivyo Sali kwa

wingi zaid kwa kadiri utakavyoweza’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Ibada ipi ni Bora zaid?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Kumuamini Allah na kupigana

Jihad kwa ajili yake.’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni yupi Mumuumini bora?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Muumini bora ni yule alie m-bora

katika tabia zake’

Abu Dhar akauliza; ‘Jee ni Muumini yupi aliekua salama?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Muumini alie salama ni yule ambae

Waislamu wenzake watakua salama kutokana na ulimi wake’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Ni yupi Muhajirina (Mhamiaji) bora?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Mhamiaji bora ni yule alie yahama

maovu yake’


134

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni Sala ipi ndio Bora?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Sala bora ni ile yenye Kisimamo

Kirefu’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni Funga ipi ndio Bora?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Funga bora ni Funga za FArdhi

ambazo zinazolipwa kikamilifu. Kwani Allah hutoa Malipo makubwa zaid’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Kafara ipi ndio bora zaidi?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Ya yule aliechinja na kuimwaga

damu kwa mikono yake’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Kuachia huru kuopi ndio bora zaid?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Mtumwa alie ghali kuliko wote na

alie m-bora kwa watu wake’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Sadaka ipi ndio bora zaidi?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Yenye jitihada za asiekua na kitu

na yenye kutolewa kwa siri kwa mwenye shida’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni ipi aya yenye uzito zaidi uliyowahi kushushiwa?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Ayat Al Kursiy’ kisha Rasul Allah

Salallahu Aályhi wa Salam akaongezea kwa kusema: ‘Abu Dhar! Mbingu 7 si chochote

mbele ya Ayat Kursy bali ni kama chembe ya mchanga katika sehemu ya Ardhi na

Kursy si chochote mbele ya Arshi bali ni chembe ya mchanga katika sehemu ya

ardhi’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee Kuna Mitume Mingapi?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Manabii 124000’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni wangapi miongoni mwao walikua ni Mitume?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Mitume 313, wengi sana na

wazuri sana’


135

Abu Dhar akauliza: ‘Jee ni Nabii gani wa Mwanzo?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Nabii Adam’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee nae alikua ni Mtume pia?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Naam, Allah alimuumba kwa

mikono yake, kisha akampulizia Roho yake, na akamuweka sawasawa’, kisha Rasul

Allah Salallahu A’layhi wa Salam akaongezea kwa kusema: ‘Abu Dhar! Wanne

miongoni mwao walikua ni Wasyria: Adam, Shith, Idris ambae ndie wa kwanza

kuandika kwa Kalamu na Nuh. Wanne miongoni mwao walikua ni Waarabu: Hud,

Shuayb, Salih na Mtume wako (Rasul Allah Salallahu Aályhi wa Salam). Ya Abu

Dhar! Mtume wa Mwanzo miongoni mwa Bani Israil ni Musa na wa Mwisho ni Isa,

Mtume wa Mwanzo ni Adam na wa Mwisho ni Muhammad.’

Abu Dhar akauliza: ‘Ya Rasul Allah! Jee Allah ameshusha vitabu vingapi?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Vitabu 104: Kwa Shith 50, kwa

Idris 30, kwa Ibrahim 10, kwa Musa 10 kabla ya kumshushia Tawrat, na kisha

akashusha Tawrat, Zabur, Injil na Furqan.’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee mlikua mna nini katika Suhufi Ibrahima?’ (Maandiko ya

Nabii Ibrahim)

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Visa vyenye mafunzo na Wasia

kama vile: ‘Enyi Wenye Kibr! Wafalme wenye kufanya dhulma, sikukuchagueni

nyie mjikusanyie mali, nimekuchagueni ili msimamie matatizo ya wenye

kudhulumiwa, mimi mwenyewe sikatai maombi ya mwenye kudhulumiwa, hata

kama aliefanyiwa dhulma huyo atakua ni mtu asieniamini’ na ‘Mtu mwenye akili

huugawa mda wake katika sehemu zifuatazo: Sehemu moja kwa ajili ya

kuwasiliana na Mola wake ambapo ndani yake atachukua sehemu ya amali zake,

Sehemu nyengine kwa ajili ya kutafakari uumbaji wa Allah Subhanah wa Taála, na

sehemu nyengine kwa ajili ya kujitafutia riski yake. Na mtu mwenye akili

hajishughulishi isipokua katika mambo matatu: Matayarisho kwa ajili ya Akhera

yake, Kufanya kazi kwa kujitafutia Riski yake na Kufurahia kile ambacho

hakijaharamishwa. Na mtu mwenye Ufahamu humbidi kuutumia vyema mda wake

kwa kujishughulisha na mambo yanayomhusu, kuulinda ulimi wake, kwani kila

anaegundua kua kauli zake ni sawa na vitendo vyake basi hatozungumza isipokua

mazungumzo yaliyo muhimu na kua na maana’’

Abu Dhar akauliza: ‘Na jee ni nini kilichoandikwa ndani ya Suhufi Musa?’(Maandiko

ya Nabii Musa)


136

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Ibar (Maneno yenye kuonya) kama

vile: ‘Inashangaza kwa yule mtu ambae ana uhakika wa kifo lakini akawa ni

mwenye kuzikimbilia anasa’’

Abu Dhar akauliza: ‘Jee na sisi tunayo maneno kama hayo katika kitabu chetu?’

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Naam!’ Kisha Rasul Allah Salallahu

A’layhi wa Salam akasoma aya zifuatazo:

‏﴿قَدْ‏ أَفْلَحَ‏ مَن تَزَك َّى ٰ ۞ وَذَكَرَ‏ ٱسْمَ‏ رَبِّهِ‏ فَصَل َّى ٰ ۞ بَلْ‏ تُؤْثِرُونَ‏ ٱلحَْ‏ يَاةَ‏ ٱلد ُّنْيَا۞‏

وَٱلآخِ‏ رَةُ‏ خَيْرٌ‏ وَأَبْقَى ٰ ۞ إِن َّ هَٰذَا لَفِى ٱلص ُّحُفِ‏ ٱلأُولىَٰ۞‏ صُحُفِ‏ إِبْرَ‏ اهِيمَ‏

وَمُوسَى ٰ ﴾

Qad aflaha man tazakka; Wadhakara isma rabbihi fasalla; Bal tu/thiroona

alhayata alddunya; Waal-akhiratu khayrun waabqa; Inna hadha lafee alssuhufi aloola;

Suhufi ibraheema wamoosa(Surat Al Aála 87:14-19)

Tafsir: Ama kwa hakika amefuzu yule anaejitakasa, Na akalikumbuka jina la Mola

wake na kisha akasali. Lakini nyinyi mnakumbatia maisha ya Dunia. Ijapokua maisha

ya akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. Hakika haya yametajwa katika Suhufi

zilizotangulia, Suhufi za Ibrahim na Musa.(Al Anwaa wa Al Taksim Al Hafidh Imam

Abu Hatim Abd Rahman Muhammad Ibn Idris Al Razi Ibn Hibban Al Basti)

Ama kuhusiana na aya hizi 5 za Surat Al Aála, basi anasema Ikrimah Mawla Abd Allah

Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Qad aflaha man tazakka – Kwa hakika amefuzu

yule aliejitakasa, ambapo aliefuzu kwa kujitakasa ni yule ambae ni mwenye

kumpwekesha Allah Subhanah wa Taála tu.’

Na akasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua kua: ‘Wadhakara isma

rabbihi – ‘Na akilikumbuka jina la Mola wake’ - hua kunamaanisha ukamilifu

unaopatikana ndani ya Nafsi ya mtu kutokana na kumjua Allah Subhanah wa

Taála. Na neno fasalla ‘Na kisha akasali’ basi linamaanisha Ukamilifu wa Mwili na

viungo vyake katika kumtii Mola wake’

Ama kuhusiana na ‘Bal tu/thiroona alhayata alddunya; Waal-akhiratu khayrun

waabqa’- basi amesema Muhaqiq Al Faqih Imam Shihab Ad Din Abu Abbas Ahmad

Ibn Muhammad Ibn Ali Ibn Hajar Al Haytami Al Makki Al Shafii kua: Amesema


137

Abu Musa Al Ashari kua amesema Rasul Allahi Salalahu A’layhi wa Salam kua:

‘Yeyote yule anaeipenda Dunia hii basi ataidhuru Akhera yake, na yeyote yule

anaeipenda Akhera yake basi ataidhuru Dunia hii, hivyo mnatakiwa muipendelee

Akhera yenu ambayo ni ya kudumu dhidi ya Dunia hii ambayo ni ya mpito.’

Na akasema Malik Ibn Dinar kua: ‘Kama ingekua Dunia hii ni Dhahabu lakini ni

yenye kupita na kutoweka na Akhera ni Tambara bovu lenye kudumu, basi Akhera

inatakiwa ipewe kipaumbele zaidi, Jee hali itakuaje pale ambapo Dunia hii ni

Tambara bovu la mpito na Akhera ni Dhahabu ya Milele?’

Na juu ya ‘Inna hadha lafee alssuhufi al-oola; Suhufi ibraheema wamoosa’ - Basi

anasema Imam Al Shanqiti kua: ‘Maneno haya yanaonesha kua Ibar – Maonyo ni

maunganisho yanayounganisha Vitabu na Maandiko yaliyopita katika mnyororo

mmoja’

Baada ya ufafanuzi huo kuhusiana na maana, sifa na tofauti baina ya Mitume na Manabii

basi na tuangalie kuhusiana na dalili na alama za Mitume wa Allah Subhanahu wa Ta’ala

ambazo hujulikana pia kama Miujiza.

MAANA YA MIUJIZA.

Miujiza hua ni maajabu ya Allah Subhanahu wa Ta’ala ambayo hua yanavunja Sharia’h

za kawaida za kimaumbile kupitia katika njia au mikono ya Mitume wake, ili kuthibitisha

Uaminifu na Ukweli wa Mitume wake. Muujiza unaweza kua katika njia ya kauli kama

vile Qurán au kwa njia ya vitendo.

‘Allamah Muhammad Sarfaraz Khan Safdar anasema kua: ‘Kilugha neno Mu’jizat hua

linatokana na neno ‘Ajz (Ajizi, au kutokua na uwezo), ambalo ni kinyume na neno

Qudrah (uwezo), na ‘ta’ [ambayo ni tāʼ marbūṭah kwa kilugha na huashiria kua ni

herufi ya mwisho katika neno na hutamkwa kwa kuhemewa ‘-a’ bila ya ‘t’, kihistori

herufi hii ilikua ikitamkwa kama ‘ha’ na ndio maana ‘ta marbutah hua inaonekana

kama ‘ha’] iliyoko mwishoni mwa neno hilo hua inaonesha msisitizo. Neno Mu‘jizat

hua ni sifa kama lilivyo neno Ayah (Alama, Dalili), n.k. Ni Allah Subhanahu wa

Ta’ala ambae hutengeneza ‘Ajz (Ajizi) ndani ya Mu‘jizat na hivyo kiukweli ni kua

huwaondolea uwezo wale wanaopinga. Mu’jizat hua unatoka kwa Allah Subhanahu


138

wa Ta’ala pekee, lakini hupitia katika mikono ya Mtume. Mtume hua hana uwezo

juu ya Miujiza yake. (Hidayat al-Murtab Ila Tariq al-Sawab fi Tahqiq al-Mu’jizat)

Mujaddid ud Din Imam Al Ghazali anasema kuhusiana na Miujiza kua: ‘Sababu

inayofanya Mu‘jizat kua inadhihirisha ukweli wa Mitume, ni kua katika kila kitu

ambacho Bani Adam hawezi kukifanya au hawezi kutoa mfano wake basi hua ni

lazima kimefanywa na Allah. Kila jambo hili linapohusishwa na changamoto za

Mtume, basi hua kama Allah Subhanahu wa Ta’ala anathibitisha kwa kusema,

‘Hakika wewe ni wa Kweli.’’(Ihya ‘Ulum al-Din)

Mujaddid ud Din Imam Fakhr Al Din Razi anasema kuhusiana na Miujiza kua,

‘Kutokana na aya nyingi kua zinazounga mkono ukweli tuliouzungumzia basi

tunaona kua, wakati Allah Subhanahu wa Ta’ala alipozungumzia kuhusiana na

Makafiri kua walitaka Miujiza mingi mikubwa mikubwa (Al Mu’jizat Al Qakhirah)

kutoka kwake yeye, Allah Subhanahu wa Ta’ala alisema katika maelezo yake:

‏﴿وَقَالُواْ‏ لَن ن ُّؤْمِنَ‏ لَكَ‏ حَتى َّٰ‏ تَفْجُرَ‏ لَنَا مِنَ‏ الأَْرْضِ‏ يَنْبُوعًا ۞ أَوْ‏ تَكُ‏ ونَ‏ لَكَ‏ جَ‏ ن َّةٌ‏

مِّن نخ َِّيلٍ‏ وَعِنَبٍ‏ فَتُفَجِّ‏ رَ‏ الأَْنْهَرَ‏ خِ‏ لَلَهَا تَفْجِ‏ يرًا ۞ أَوْ‏ تُسْ‏ قِ‏ ‏َط ٱلس َّمَآءَكَمَا

زَعَمْتَ‏ عَلَيْنَا كِسَفًا أَوْ‏ أتَْتِىَ‏ بِٱهلل َِّ‏ وَٱلْمَ‏ لائِكَ‏ ۤ ‏ِة أَوْ‏ يَكُونَ‏ لَكَ‏ بَيْتٌ‏ مِّن

زُخْرُفٍ‏ أَْو تَرْقَ‏ ٰ ى فىِ‏ الس َّمَآءِ‏ وَلَن ن ُّؤْمِنَ‏ لِرُقِيِّكَ‏ حَتى َّ تُنَزِّلَ‏ عَلَيْنَا كِتَاًاب ن َّقْرَءُهُ‏ قُ‏ ‏ْل

قَبِيلاً‏ ۞

سُبْحَنَ‏ رَبىِّ‏ هَلْ‏ كُنتُ‏ إَلا َّ بَشَرًا ر َّسُولاً﴾‏

Waqaloo lan nu/mina laka hatta tafjura lana mina al-Ardhi yanbooAAan; Aw

takoona laka jannatun min nakheelin waAAinabin fatufajjira al-anhara khilalaha

tafjeeran; Aw tusqita alssamaa kama zaAAamta AAalayna kisafan aw ta/tiya

biAllahi waalmala-ikati qabeelan; Aw yakoona laka baytun min zukhrufin aw tarqa

fee alssama-i walan nu/mina liruqiyyika hatta tunazzila AAalayna kitaban

naqraohu qul subhana rabbee hal kuntu illa basharan rasoolan. (Surat Al Isra 17:90-

93)

Tafsir: Na wao husema: ‘Hatutokuamini hadi pale utakaposababisha maji kutoka

ardhini kwa nguvu kwa ajili yetu; Au wewe una bustani ya Mitende na Mizabibu, na

usababishe maji kutoka kwa nguvu baina yao kwa wingi; Au usababishe Mbingu

kutuangukia vipande vipande kama ulivyojidai, au utuletee Allah na Malaika wake

mbele yetu uso kwa uso; Au una nyumba ya Zukhruf (iliyopambwa kwa Dhahabu) au


139

upae juu mbiguni, na hata hivyo hatutokuamini katika kupaa kwako hadi pale

utakaposhuka na kitabu ambacho tutakisoma’. Sema: Ametukuka Mola wangu! Mimi

sikua yeyote isipokua ni Bashar (mtu), alietumwa kama Rasul.

‘Yaani kwa maneno mengine, Bani Adam kua kiumbe chenye sifa za Utume,

kunamaanisha kua amekamilika katika vitendo vyake na kauli zake, na anaweza

kuwatibu Bani Adam wengine ambao waliokua hawana sifa mbili hizo; lakini si

lazima kua kutokana na kua na sifa hii (ya Utume) basi akawa na uwezo wa

kukutoleeni mambo [Mu’jizat] ambayo nyinyi mnamtaka akutoleeni’. (Matalib

‘Aliyyah, Mawlana Shibli Nu’mani)

Miujiza hua na sifa zifuatazo:

1. Hutokana kwa Allah Subhanah wa Ta’ala.

2. Huvunja Sharia’h za kawaida za kimaumbile katika kutokea kwake.

3. Hua na hali isioweza kuelezeka.

4. Hupitia kwa Mtume husika ili kuthibitisha Utume huo.

5. Hua inayoendana na madai yanayodaiwa.

6. Hua haipingani na madai yanayodaiwa.

7. Hua haizidishi wala haipunguzi kiasi cha madai husika.

A’llamah ‘Abd Al Rahman Ibn Khaldun anasema kuhusiana na Miujiza kua, ‘Miongoni

mwa alama za Mitume ni kufanya Miujiza ambayo huthibitisha ukweli wao.

Miujiza hua ni vitendo ambavyo mithili yake hua kamwe haiwezekani kufanywa na

Bani Adam. Na ndio maana ikaitwa Miujiza (Mu’jizat). Kwani hua haimo ndani ya

uwezo wa Bani Adam bali imo nje ya uwezo wao. Kuna utofauti wa mitazamo

kuhusiana na namna gani inavyotokea na namna gani huthibitisha ukweli wa

Mitume. Wachunguzi wa mitizamo ya kidini (Mutakallimun) wamesimamia katika

misingi ya Imani ya kua, Miujiza hua ni mambo ambayo hutokea kwa kutaka, na

hivyo husema kua Miujiza hutokea kutokana na uwezo wa Allah Subhanah wa

Ta’ala, na si kupitia katika vitendo vya Mitume wake. Mu’tazila wao wana mtizamo

wa kua vitendo vyote vya Bani Adam hutokana na Bani Adam mwenyewe, lakini

hata hivyo Miujiza hua haimo katika aina hizo za vitendo vinavyofanywa na watu.

Kulingana na Skuli za Madhhab yote, nafasi ya Mitume katika kufanya Miujiza hua

ndani ya mipaka ya ‘Changamoto zinazoendelea’ (Tahaddi) ambayo yeye huitoa

kutokana na amri ya Allah. Yaani Mtume hutumia Miujiza kabla ya kutokea

kwake, kama kithibitisho cha ukweli wa madai yake. Hivyo wao hua wanachukua

nafasi ya maelezo ya wazi kutoka kwa Allah kudhihirisha kua Mtume fulani ni wa

Kweli’.(Al Muqaddimah)

Ingawa Qurán haikuwataja Mitume wote lakini imetaja na kuhadithia visa na Hadith za

baadhi ya Mitume, ambao idadi yao ni 25 tu, na imefanya hivyo kwa sababu ndani ya


140

visa na Hadith hizo kuna mafunzo na mifano bora ya kuigwa katika uhai wa kila Bani

Adam, kama vile vile anavyosema mwenyewe Allah Subhanah wa Taála:

‏﴿وَكُلاًّ‏ ن َّقُص ُّ عَلَيْكَ‏ مِنْ‏ أَنْبَاءِ‏ ٱلر ُّسُ‏ ‏ِل مَا نُثَبِّتُ‏ بِهِ‏ فُؤَادَكَ‏ وَجَآءََك

وَمَوْعِظَةٌ‏ وَذِكْرَىٰ‏ لِلْمُؤْمِنِ‏ ‏َين ﴾

‏ِفى هَٰذِهِٱ لحَْ ُّق

Wakullan naqussu AAalayka min anba-i alrrusuli ma nuthabbitu bihi fu-adaka

wajaaka fee hadhihi alhaqqu wamawAAidhatun wadhikra lilmu/mineena (Surat

Hud 11:120)

Tafsir: Na vyote tunavyokuhadithia kuhusiana na habari za Mitume ni kwa ajili ya

kuupa nguvu moyo wako kutokana navyo. Na ndani yake hii (Qurán) umekujia ukweli

na pia mawaidha na ukumbusho kwa walioamini.

Sababu nyengine za kutajwa kwa visa vya Mitume na Manabii hao 25 ndani ya Qurán

hua ni pamoja na kuudhibitishia ukweli wa utukufu wa Utume na kazi ya aliyeshushiwa

Qurán hiyo ambae ni Mtume wa Mwisho Muhammad Rasul Allah Salallahu A’layhi wa

Salam, kuthaminisha thamani ya Ummah wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam dhidi ya Úmma za watu wa Manabii na Mitume waliotangulia, kuzihuisha njia za

Maisha ya Mitume na Manabii hao walizokua wakipita ili ziendelee kuwepo, kufahamika

na kufuatwa kwa milele.

Tunapoiangalia Qurán basi tunaona kua imewataja Mitume mbali mbali na tofauti

kulingana na mazingira yao waliyokabiliana na mitihani mbali mbali. Kwa mfano

tunapoiangalia Surat Al An Aam basi tunaona kua imetaja Mitume ambao

imewatafautisha kwa kua na sifa zifuatazo:

Nabii Nuh Alayhi Salatu wa Salam basi yeye ametajwa kua ni Nabii na Mtume wa

mwanzo kupingana na Jamii ya watu wanaoabudu Masanamu.

Nabii Is-haq na Nabii Yaqub Alayhim Salatu Salam basi wao wametajwa kua ndio

waanzilishi wa watu wa Bani Israil.

Nabii Daud na Nabii Sulayman Alayhim Salam wote wawili wametajwa kwa

kutofautishwa na Mitume wengine kwa kua na sifa ya Utume, Mali na Utawala wa

Mamlaka ya Kifalme.


141

Nabii Ayub na Nabii Yusuf Alayhim Salam wametajwa kwa kutofautishwa kwa

kujaribiwa kwa Mitihani na Ustahmilivu wao.

Nabii Musa na Nabii Harun Alayhim Salam wao wametajwa kwa kutofautishwa

kwa kua na uwezo na nguvu za kudhoofisha nguvu za Utawala wenye Nguvu kubwa

sana Kimamlaka.

Nabii Zakariyah, Nabii Yaqub, Nabii Isa Ibn Maryam na Nabii Ilyas Alayhim Salam

basi wao wametajwa kwa kutofautishwa kwa kua ni mfano wa kuigwa katika Ucha

Mungu, Ilm yao ya Kiroho na Kujitolea Muhanga.

Na vile vile tunapoangalia kwa upande wa Shaykh Al Akbar Imam Muhammad Ibn Ali

Ibn Muhammad Abu Bakr Muhyi Al Din Ibn Al Arabi Al Hatimi Al Ta’i Al Andalusi Al

Mursi Al Dimashqi ambae yeye ni mtaalamu wa I’lm Tasawwuf basi tunaona kua yeye

amewataja Mitume, Manabii na watu wengine Watukufu waliotajwa katika Qurán na

Hadith na kuwaainisha kulingana na aina za Hikma za ujumbe wa Allah Subhanah wa

Ta’ala zinazopatikana katika kuhadithiwa habari zao na hivyo tunaona kua:-

1. NABII ADAM – HIKMAH ILAHIYYAH – Hikma ya Uungu.

2. SHITH – HIKMAH NAFTHIYYAH – Hikma ya Matarajio.

3. NABII IDRIS – HIKMAH QUDUSIYYAH– Hikma ya Utukufu.

4. NABII NUH – HIKMAH SUBUHIYYAH – Hikma ya Kupandisha Darja.

5. NABII SALIH – HIKMAH FATIHIYYAH – Hikma ya Ufunguzi wa Kila Jambo.

6. NABII HUD - HIKMAN AHADIYYAH – Hikma ya Umoja wa kutokua na

Mshirika

7. NABII IBRAHIM – HIKMAH MUHAYMIYYAH – Hikma ya Upendo.

8. NABII LUT – HIKMAH MALIKIYYA – Hikma ya Uwezo wa Kiutawala.

9. NABII ISMAIL – HIKMAH ALIYYAH – Hikma ya Kujisalimisha.

10. NABII IS-HAQ – HIKMAH HAQQIYAH – Hikma ya Ukweli.

11. NABII YAQUB – HIKMAH RUHIYYAH – Hikma ya Kiroho.

12. NABII YUSUF – HIKMAH NURIYYAH – Hikma ya Nuru.

13. NABII SHUAYB – HIKMAH QALBIYAH – Hikma ya Kimoyo.

14. NABII UZAYR - HIKMAH QADARIYYAH – Hikma ya Makadirio.

15. NABII DAUD – HIKMAH WUJUDIYAH – Hikma ya Kua Hai.

16. NABII SULAYMAN – HIKMAH RAHMANIYYAH – Hikma ya Rehma.

17. NABII YUNUS – HIKMAH NAFASIYYAH – Hikma ya Sehem ya Kuvuta Hewa.

18. NABII AYYUB – HIKMAH GHAYBIYYAH – Hikma ya Ghayb.

19. NABII ILYAS – HIKMAH INASIYYAH – Hikmah ya Ukaribu

20. NABII MUSA – HIKMAH ULUWIYYAH – Hikma ya Mafanikio.

21. NABII HARUN – HIKMAH IMAMIYYAH – Hikma ya Uongozi

22. LUQMAN AL HAKIM – HIKMAH IHSANIYYAH – Hikma ya Tabia Njema.


142

23. NABII ZAKARIYYAH – HIKMAH MALIKIYYAH – Hikma ya Mamlaka.

24. NABII YAHYA – HIKMAH JALALIYYAH – Hikma ya Sifa Njema.

25. NABII ISA – HIKMAH NUBUWIYYAH – Hikma ya Unabii.

26. KHALID IBN SINAN – HIKMAH AS SAMADIYYAH – Hikma ya Kila kitu

kurudi Kwake.

27. NABII MUHAMMAD SALALLAHU ALAYHI WA SALAM – HIKMAH

FARDIYAH – Hikma ya Umoja wa Upekee

Ambapo anasema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

‏﴿وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ‏ مِن ر َّسُولٍ‏ إِلا َّ نُوحِ‏ ي ۤ إِلَيْهِ‏ أَن َّهُ‏ لا ۤ إِلَٰهَ‏ إِلا َّ أََْ‏ فَٱعْبُدُونِ‏ ﴾

Wama arsalna min qablika min rasoolin illa noohee ilayhi annahu la ilaha illa ana

faoAAbudooni (Surat Al Anbiyah 21:25)

Tafsir: Na sisi hatukutuma kabla yako (Ewe Muhammad) Mitume isipokua

tuliwashushia ujumbe kua Hakuna anaestahiki kuabudiwa ila mimi hivyo Niabuduni.

Kwa upande wa Imam Baddiuzzamman Said Nursi basi yeye anasema kua miongoni

mwa sababu ambazo zinamepelekea kuwepo kwa takriri au kurudiwa kwa Visa Vya

Manabii na Mitume katika sura tofauti za Quran hua kunatokana na kuonesha Miujiza

yake Allah Subhanah wa Ta’ala ambayo ni yenye malengo makuu yafuatayo:

1-Kuelezea sehemu za visa ambazo zimetajwa katika sehemu nyengine maalumu

kulingana na mazingira maalum, na hivyo ingawa hiii hua si Takriri lakini

huonekana kua kama ni Takriri kwa sababu ya mazingira ya muonekano wake.

2-Kuweka wazi ufasaha na uwazi wa aya za Qur’an, kwani katika baadhi ya sehemu

kisa husika hua kimetajwa kwenye sura husika kwa aya chache lakini katika baadhi

ya sura kimetajwa kwa kina na kwa aya nyingi.

3-Kuweka wazi uthibitisho wa Utume wa Rasul Allah Sallahu A’layhi wa Salam,

kubainisha kuwepo kwake Mungu mmoja tu ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala,

kutoa mafunzo ya kua Allah Subhanah wa Ta’ala ana uwezo juu ya kila kitu

ikiwemo kuwaadhibu wanaomuasi, kuwaonya wasiomuamini kwa kuwawekea wazi

yaliyowafika wale waliotangulia kabla yao. Kiasi ya kua kila Takrir iliyotumka basi

hua imetumika kwa ajili mazingira husika na katika wakati husika ili kufikisha

ujumbe husika.


143

4-Kumliwaza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na pia kuwaliwaza Waislam

ambao walikua wanakumbana na matatizo na mitihani mingi sana katika kipindi

hiki cha mwanzoni mwa Uislam, kwa mfano tunapoangalia kisa cha Nabii Musa na

Nabii Ibrahim basi tunaona kua vilikua vinarudiwa kwa sababu ya kuwaonesha

Waislam waliokua kwenye mitihani dhidi ya Makafiri kua lazima mwanzoni

wanaowaamini Mitume hao hua wanapata misukosuko lakini baadae hua kuna

uongofu na uokovu kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala.

Na pia kwa upande mwengine tunapoangalia mifano ya kuangamizwa kwa jamii za

Watu wa Nabii Lut na Fir’awn kutokana na Uasi wao basi hua kunaonesha kua

haina haja na wala haitakiwi kwa Ibn Adam kua ni wenye kufanya dhambi dhidi

ya viumbe wenzao, dhidi ya Mola wao na hawatakiwi kumuuasi Mola wao.

5-Kuwapa Moyo Waumini kujidhibiti dhidi ya adui wao mkubwa ambae ni Shaytan

na dhidi ya Uadui wa Nafsi zao, na kuwawekea wazi malipo watakayoyapata pale

watakapofanikiwa kujidhibiti na maadui zao hao, na hapo hapo kuwavunja Moyo

wasiwe ni wenye kudumu katika dhambi.

6-Kuwafundisha Waumini Dua na namna ya kumkumbuka Mola wao, kufuata

Maamrisho yake, kumpwekesha na kuwasisitizia kua wao ni viumbe na watumwa

wa Allah Subhanah wa Ta’ala. Na hivyo kuwaonesha Malengo na Makusudio ya

kuumbwa kwao na kuumbwa kwa Ulimwengu wanaoishi ndani yake ambao nao

una kila kitu wanachokihitaji katika maisha yao hapa Ulimwenguni.

7-Kuwaponya watu wa kila aina kuanzia wenye ufahamu wa hali ya juu na wenye

ufaham mdogo, wenye Taqwa na waliopotoka, wenye kuikimbilia Akhera yao na

wenye kuikumbatia Dunia yao.

Lakini hata hivyo si kila mtu hua ni mwenye bahati ya kusioma Qur’an yote,

ambayo ni ponyo na ni dawa kwa kila mtu. Kwa hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala

aambae ndie mwenye kuweka Lulu, Hikma na Busara katika kila kitu akifanyacho

ndani yake, na ndie ambae mwingi wa Rehma na Huruma kwa waja wake basi

akaamua kuweka ndani yake Sura ambazo ni zenye kubeba malengo makuu ya

Qur’an. Kiasi ya kua kila sura imekua kama ni Qur’an ndogo na hivyo kua ni zenye

kumrahisishia kila mtu kunufaika nayo, ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala

akasema katika Qur’an

‏﴿وَلَقَدْ‏ يَس َّرَْ‏ ٱلْقُرْآنَ‏ لِلذِّكْرِ‏ فَهَلْ‏ مِن م ُّد َّكِرٍ‏ ﴾


144

Walaqad yassarna alqur-ana lildhdhikri fahal min muddakirin (Surat Al Qamar

54:17)

Tafsir: Na kwa Hakika (kutokana na kuishusha katika Lugha ya Ibn Adam)

Tumeifanya Qur’an iwe ni rahisi kwa ukumbusho. Lakini jee ni nani mwenye

kuufuata ukumbusho huo?

8-Imeelezewa katika hadithi na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Kila

aya ina kina cha maana kuna Muhkamat na Mutashabihat, yaani maana iliyowazi

na maana ya ndani ambayo inaweza kufahamika na wenye kujua tu. Hii hua ni

kama kina cha mzunguko wa kimaana, na kila kina cha mzunguko wa kimaana

umegawika sehemu nne kimaelezo, kialama, kimatawi na kiainisho. Kwa mtizamo

mwengine basi kila aya ya Qur’an ina matabaka ya kimaana, na mambo mengi

ndani yake, ikiwemo Hukmu, Manufaa na ainisho kwa malengo maalum. Hivyo

kutokana na sababu hio basi ndio maana kisa kimezungumziwa katika sehemu

moja na kisha kikazungumziwa katika seheu nyengine, ambapo katika sura moja

kimeelezewa kwa sababu fulani na katika sura nyengine kwa sababu tofauti.

Kutokana na hali hii basi hua hakuna takrir katika Qur’an, yaani hii ni kama vile

yalivyofanana macho na masikio ya watu, lakini ukweli ni kua yote yapo tofauti.

9-Kama ilivyokua mwili wa Ibn Adam unavyohitaji mahitaji tofauti ambapo baadhi

ya mahitaji hayo hua yanahitajiika kila mara kama uvutaji wa hewa kwa mfano,

na baadhi ya mahitaji huhitajika baada ya mda fulani kama kula, kunywa maji n.k

na baadhi hua ni yenye kuhitajika kila baada ya wiki, mwezi au mwaka mara moja

kama vile matumizi ya dawa. Na hivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa mahitaji ya kiroho

kwa upande wa Ibn Adam kila mmoja hua na njia zake za kufanya Dhikr Allah,

kuna kila wakati wasema wasemao Allah! Allah, kuna wasemao Biismi Allahi kuna

wasemao La Illah Ila Allah kila baada ya saa n.k kutokana na kuwepo kwa hali hii

basi Qur’an pia imekua na takrir ndani yake kwa kutokana na kuhitajika kwake

na umuhimu wake.

Kulingana makusudio hayo na mengineyo mengi ambayo hatukuyataja basi

tunaona kua ingawa ndani ya Qur’an kuna takrir za mara kadhaa lakini hata hivyo

kujirudia huko basi kamwe hakukua ni kwenye kusababisha kukosekana kwa

mvuto wa Qur’an kama vile ambavyo yaliyo maneno au mazungumzo ya Watu,

lakini kwa upande wa Qur’an hali imekua ni kinyume chake, kwani kila ukiisoma

basi ndio hamu yya kuizoma zaidi ndivyo inavyozidi kukua na kuongezeka, vile vile

Qur’an ni Nuru ya kila Muumini katika kila wakati wa maisha yake yote hapa

Ulimwenguni na imekua hivyo kwa karne na karne, na imekua ikisomwa tena na

tena katika sala zao, na imerahisishwa kwa watoto kuihifadhi, Qur’an ni tamu kama


145

maji ya Zam Zam kwa mtu alie katika wakati wa kukata roho. Na haya yote

yanaonesha miujiza ya Qur’an iliyopo katika kila hali.

Baada ya kuangalia takrir katika Qur’an ambazo zimetumika katika kuelezea visa vya

Mitume tofauti ambapo ingawa Mitume na Manabii wote wanatoka kwa Allah Subhanah

wa Ta’ala kwa ajili ya kuja kueneza ujumbe wake Muumba na kuwaongoza watu katika

njia iliyosahih, na hivyo kukumbana na mitihani mingi sana kutoka kwa watu

wanaowausia juu ya ujumbe huo lakini baadhi miongoni mwao walikua na sifa ya darja

ya juu zaidi kuliko wengine na hii ni kulingana na mitihani waliyoipata na namna

walivyokabiliana na mitihani hio, na hivyo basi kutoka na kua na sifa hizo basi Mitume

hawa walikua wakijulikana kama Ulu al A’zmi mina al Rusul.


146

SURA YA PILI

عيسى ابن

االله روحي مريم


147

HISTORIA YA MZEE IMRAN BABU YAKE NABII ISA IBN MARYAM

BINT IMRAN

Tunapozungumzia Kisa cha Nabii Isa Ibn Maryam Alayhi Salam, basi hua hatuwezi

kukikamilisha kisa hicho bila ya kugusia ndani yake kisa cha Mzee Imran, Maryam Bint

Imran, Nabii Zakarriyah na Nabii Yahya na hivyo moja kwa moja tunatua katika aya za

mwanzoni zilizozungumzia kisa cha Mzee Imran katika Surat ya tatu iliyomo ndani ya

Qur’an ambayo imetumia jina lake Mzee Imran ambayo ni Surat Al Imran.

Ambao neno Al Imran ni lenye kutokana na neno Amara ambalo hua linamaanisha Kuishi

Ndani yake, Kutengeneza kitu kilichoharibika, Kujenga, Kufanya ziara Takatifu na pia

humaanisha Kujaza watu au Wakaazi katika sehemu fulani ya Ardhi.

Neno Amara ndio ia lililotoa neno Umrun ambalo hua linamaanisha Umri, Kuishi kwa

Mda mrefu, au Utu Uzima, na likatoa neno Umrah yaani Ibada ya Hija Ndogo na pia

likatoa neno Maamur ambalo hua inamaanisha Sehemu inayotembelewa na viumbe

wengi mara kwa mara.

Neno Amara ndio pia lililotoa jina la Imran ambalo ni moja kati ya Majina ya watu

Wawili watukufu waliotajwa ndani yake Qur’an yaani Mzee Imran ambae ni Baba yake

Nabii Musa alieishi miaka 1400 kabla ya kuzaliwa Mzee Imran wa pili ambae ni Baba

yake Bi Maryam Bint Imran ambae ndie Mama yake Nabii Isa Ibn Maryam Bint Imran

na hivyo Mzee Imran huyu kua ni Babu yake Nabii Isa.

Ambapo kwa mara ya kwanza Mzee Imran Babu yake Nabii Isa ambae alikua ni Mkuu

wa Makuhani wa Jerusalem alitajwa katika Qur’an pale Allah Subhanah wa Ta’ala

aliposema:

‏﴿إِن َّ ٱهلل ََّ‏ ٱصْطَفَى ٰ آدَمَ‏ وَنُوحاً‏ وَآلَ‏ إِبْرَاهِيمَ‏ وَآلَ‏ عِمْرَانَ‏ عَلَى ٱلْعَالَمِينَ۞‏ ذُ‏ رِّي َّةً‏

بَعْضُهَا مِنْ‏ بَعْضٍ‏ وَٱهلل َُّ‏ سمَِيعٌ‏ عَلِيمٌ‏ ۞ إِذْ‏ قَالَتِ‏ ٱمْرَأَةُ‏ عِمْرَانَ‏ رَبِّ‏ إِنىّ‏ ِ نَذَرْتُ‏

لَكَ‏ مَا فىِ‏ بَطْنىِ‏ محَُر َّراً‏ فَتَقَب َّلْ‏ مِنىِّ‏ إِن َّكَ‏ أَنتَ‏ ٱلس َّمِيعُ‏ ٱلْعَلِيمُ‏ ﴾

Inna Allaha istafa adama wanoohan waala ibraheema waala AAimrana AAala

alAAalameena; Dhurriyyatan baAAdhuha min baAAdhin waAllahu sameeAAun


148

AAaleemun; Idh qalati imraatu AAimrana rabbi innee nadhartu laka ma fee batnee

muharraran fataqabbal minnee innaka anta alssameeAAu alAAaleemu (Surat Al

Imran 3:33-35)

Tafsir: Hakika Allah amempandisha (Darja) Adam na Nuh na Ibrahim na Imran juu

zaidi ya Walimwengu wengine, Vizazi vya baadhi miongoni mwa baadhi yao, Na

kumbuka aliposema Mke wa Imran: ‘Ewe Mola Wangu, hakika mimi nimeweka

Nadhiri kua Mtoto wangu aliemo tumboni mwangu nimemtolea kwa ajili ya

kukutumikia wewe, hivyo nikubalie kwani kwa hakika wewe ni mwingi wa kusikia na

ni mwingi wa kujua juu ya kila kitu.’

Anasema Imam Muhammad Ibn Is-haq kua: ‘Imraat ul Imran alikua akijulikana kwa

jina la Hannah Bint Faqudh, na Imran mwenyewe alikua ni chifu wa watu wa Bani

Israil na akijulikana kwa jina la Imran Ibn Sahim Ibn Amur Ibn Mishan Ibn Hizqil

Ibn Ahraf Ibn Buam Ibn Azaziyah Ibn Amasiyah Ibn Nawus Ibn Nutha Ibn Barid

Ibn Yahushafat Ibn Radim Ibn Ababa Ibn RajiAm Ibn Sulayman Ibn Daud Alayhi

Salatu wa Salam.

Ambapo Nabii Zakariyah na Mzee Imran walikua ni watu wawili waliowaoa

Mabinti wawili wa kike wa Mzee Faqudh ambao ni Hannah Bint Faqudh na Isha

Bint Faqudh. Hivyo Nabii Zakariyah alimuoa Isha Bint Faqudh ambae ndie mama

yake Nabii Yahya na Mzee Imran alimuoa Hanah Bint Faqudh ambae ndie Mama

yake Maryam Bint Imran.’

Ambapo Hannah hakuwa na uwezo wa kupata Mtoto hadi pale alipokua Mtu mzima na

kufikia hali ya kutokua na matumaini ya kupata hata ujauzito, na kama zinavyosema aya

kua familia yao ilikua ni yenye kupandishwa Darja maalum na Allah Subhana wa Ta’ala,

ambapo siku moja wakati Hannah alipokua amekaa chini ya Mti basi alimuona ndege

kiwa anamlisha kinda wake chakula, na tukio hili likamtia simanzi kwani akakumbuka

kama hata ndege wanakua na watoto wao, basi inakuaje yeye hadi anafikia umri huo na

mumewe Imran hajajaaliwa kupata mtoto?

Lakini anasema Imam Abd Rahman Muhammad Ibn Al Husayn Ibn Muhammad Ibn

Musa Ibn Khalid Ibn Salim Ibn Rahawiyah Al Sulami Al Nishapuri Al Shafii kua: ‘Yule

ambae hana Subra juu ya kile alichojaaliwa na Mola wake juu yake, basi hatokua

na Subra juu ya kupata Uongofu kutoka kwa Mola wake.’ Hivyo bila ya shaka kwa

Upande wa Mzee Imran na Bi Hanah Bint Faqudh hawakua ni wenye kuvunjika Moyo

na majaaliwa ya Mola wao juu yao.

Na hivyo Hannah Bint Faqudh akasema baada ya tukio la kumuona ndege huyo maneno

yafuatayo: ‘Ya Allah. Hakika mimi naweka Nadhiri kwako kua kama utanijaalia

kua ni mwenye kupata Mtoto wa kiume, basi nitamtoa Mtoto huyo kwa ajili yako,


149

na hivyo atakua ni mwenye kujitolea kufanya huduma za kuyatumikia Madhabahu

yako, kama sehemu ya kuonesha shukurani zangu juu yako.’

Hivyo baada ya kuweka Nadhiri hio basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamjaalia Mzee

Imran na Hannah Bint Faqudh kua ni wenye kupata mtoto, lakini bila ya kujua kua mtoto

huyo ni alikua ni Mwanamke, na wo walitaka Mtoto wa Kiume kwa sababu katika kipindi

hicho ilikua ni kawaid wa Wacha Mungu kuwateu watoto wao wa kiume wanapozaliwa

kua ni kwa ajili ya kumtumikia Mola wao kwa kuhudumia Madhabahuni ambayo ni

sehemu ya kutolea Kafara iliyopo ndani ya Majumba ya Ibada ya watu wa Bani Israil.

Hivyo watoto hao wa kiume hua wanakaa ndani ya Majumba hayo na kuhudumia Usafi

na usimamizi wa ndani ya Majengo hayo hadi pale watakapofikia umri wa miaka 15, na

kisha baada ya hapo hua ni wenye kua na hiari ya aidha kubakia ndani ya majengo hayo

na kua Watawa au kutoka nje na kuenda kuishi maisha yao ya kawaida, na jukumu hili

lilikua ni kwa ajili ya watoto wa kiume tu, halikuweza kua ni jukumu la watoto wa kike

kwa sababu ya maumbile yao Wanawake na sharia zao wafuasi wa Dini ya Kiyahudi kwa

wakati huo na mpaka hii leo kutokana na kua Wanawake hua ni wenye Maumbile ya

kutokwa na Damu ya Hedhi kwa kila mwezi na pia kutokwa na Damu ya Nifasi baada ya

kujifungua na kupata Mtoto.

UHARAMU NA UTUKUFU WA DAMU KATIKA UISLAM.

Tunapozungumzia kuhusiana na Damu basi hua tunazungumzia kitu ambacho ni kitukufu

katika Dini ya Kikristo, Kiyahudi, Kikristo, Kipagani n.k ambacho hua kinawakilisha

Roho au Uhai wa Kiumbe. Kwani Damu ndio kiungo pekee muhimu kilichomo ndani ya

Mwili wa Kiumbe ambacho kinajumuisha Mfumo mzima unaojitegemea ambao upo

katika maumbile ya mtiririko wenye wingi wa lita 5 kwa upande wa Ibn Adam.

Mfumo wa Damu hua ni wenye kufanya kazi ya kuisaidia mifumo myengine muhimu ya

ufanyaji kazi ya ndani ya mwili katika kusimamia utekelezaji wa majukumu yake mbali

mbali ndani yake, hivyo bila ya kua na Damu basi kiumbe husika hua hana uwezo wa

Kuishi Ulimwenguni. Kwa sababu Damu hua inategemewa na takriban na kila mfumo

wa mwili wa kiumbe husika ndani ya mwili ikiwemo mfumo wa chakula ambao ni wenye

kusafirisha, kuchuja, kutawanya na kuhifadhi vitu muhimu vinavyohitajika na mwili

vilivyomo ndani ya chakula husika na kisha kukitoa nje ya mwili kila kile kisichohitajika

ndani ya mwili husika.


150

Damu husaidia pia mfumo wa kusafirisha na kuisambaza Hewa safi inayoingia ndani ya

mwili kuanzia kwenye mapafu ambapo huinyonya na kisha kuisambaza katika kila

kiungo kinachohitajika ndani ya mwili, wakati ikiwa katika hli ya usafi na kisha huitoa

nje ya mwili hewa chafu, kwani ikibakia ndani yake basi hua ni yenye kusababisha

madhara katika mwili wa mtu husika.

Damu hua ndio kiungo ambacho mfumo wake hua na kazi ya kusafirisha na kuzalisha

kemikali (hormones) mbali mbali za hisia, ulinzi na ukuaji wa mwili wa Kiumbe na pia

husafirisha vitamins, glucose, aminoacids, madini mbalimbali virutubisho vyenginevyo,

na kisha hapo hapo Mfumo wa Damu hua ndio unaosimamia kutoa nje ya mwili kila kitu

kisichohitajika ndani ya mwili baada ya kuchujwa kwake.

Na pia Damu hua ndio inayosimamia mfumo wa kudhibiti hali ya joto ndani ya Mwili

kulingana na hali ya mabadiliko ya mazingira husika yaliyopo nje ya mwili wa kiumbe

husika, na pia kulingana na mabadiliko ya hali ya kimaumbile ya ndani ya mwili husika.

Kwani mwili unapokua umezidiwa na joto basi Mfumo wa Damu huifanya mishipa ya

Damu kua ni yenye kutanuka na kupanda juu karibu na ngozi na kuifanya sehemu ya juu

ya mwili yaani ngozi kua ni yenye kuachia na kutoa nje Joto la ndani ya mwili.

Na inapokua mwili umepungukiwa na joto na kuhisi baridi basi Mfumo wa Damu

huifanya mishipa ya Damu kua ni yenye kubana na kuingia ndani zaidi na hapo huanza

kutokea vipele pele vidogo dogo vingi kwenye ngozi huku nywele za ngozi hua ni zenye

kusimama, ambapo tukio hili hua ni lenye kuifanya misuli ya ndani ya mwili kua ni yenye

kubana na kutetemeka na kuufanya mwili kua ni wenye kuzalisha joto zaidi na huku

mishipa hio ya Damu iliyobana na kuzama zaidi hua ni yenye kuhifadhi joto lisitoke nje

ya mwili na hivyo lisipungue ndani ya mwili.

Ambapo kwa upande mwengine basi Mfumo wa Damu ndio unaozalisha Mfumo wa

Kinga ya mwili dhidi ya maradhi ya ndani ya mwili na nje ya mwili, na hili linaonekana

wazi pale mtu anapokua anaumwa basi joto la mwili hupanda kutokana na kua Mfumo

wa Damu hua ni wenye kuongeza ufanyaji kazi wake na hivyo hua ni wenye kuzalisha

zaidi Seli nyeupe za Damu ambazo hua zinajulikana kama Leukocytes kwa ajili ya

kuulinda mwili na kupigana na kila kinachoonekana kua ni chenye kutaka kusababisha

madhara kwa mwili.

Ambapo kwa upande wa nje ya mwili unapopata jeraha, kisha kuanza kutokwa na Damu

basi mfumo wa Damu pia hua ni wenye kushirikiana na Protein ili kusimamia uzuiaji wa

utokaji wa Damu hio ili isipotee kwa kuigandisha na kuikausha sehemu ya juu ya nje ya

mwili iliyojeruhiwa.


151

Kutokana na umuhimu huo basi wa Damu kwa mwili wa Kiumbe kua ni sawa na Uhai

wa kiumbe husika ambao hua unaanzia kutokana nayo kama alivyoelezea mwenyewe

Muumba kwenye Qur’an pale aliposema:

‏﴿خَلَقَ‏ ٱلإِنسَانَ‏ مِنْ‏ عَلَقٍ‏ ﴾

Khalaqa al-insana min AAalaqin(Surat Al Aala 96:2)

Tafsir: Aliemuumba Mtu kutokana na Aa’alaqin.

Ambapo neno Aa’alaqin linatokana na neno Aliqa ambalo hua linamaanisha, Kushikama,

Kunata, Kuganda. Kung’ang’ania na pia hua linamaanisha Kitu chenye Thamani na

hivyo kisichotakikana Kuachiwa au Kuachika.

Hivyo neno Aa’alaqin hua linamaanisha Maumbile ya kitu kilichoshikamana kama

Damu, Manii ya Mwanamme au Mayai ya Uzazi wa Mwanamke na pia humaanisha

Mshikamano wa Kimapenzi. Na ndio maana Wanazuoni wakalitafsiri neno A’alaqin kua

ni Mshikamano wa pande au tone la Damu, na hii ni kwa sababu Aa’alaqin kua ni Kitu

ambacho kinategemea Uhai wake kutokana na kushikama na Damu na Kuinyonya Damu

ambayo hua ni Chakula chake.

Kwani pia hata mwanzoni mwa Uhai wa Ibn Adam baada ya kukutana kwa Mayai ya

Uzazi ya Baba na Mama na kushikamana, basi mshikamano huo wakati ukiwa ndani ya

Fuko la Uzazi la Mama huanza kukua na katika hali ya maumbile ya kama kipande cha

Damu ambacho nacho hua kinakua kutokana na kutegemea Damu ya Mama kwa

kushikamana na sehemu ya Fuko la Uzazi la Mama.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anazielezea hatua zaidi za maumbile hayo ndani ya

Qur’an kwa kutuambia kua:

‏﴿وَلَقَدْ‏ خَلَقْنَا ٱلإِنْسَانَ‏ مِ‏ ن سُلاَلَةٍ‏ مِّن طِينٍ‏ ۞ ثمُ َّ جَعَلْنَاهُ‏ نُطْفَةً‏ فىِ‏ قَرَارٍ‏

‏ِعظَاماً‏

م َّكِينٍ۞ثمُ َّ خَلَقْنَا ٱلن ُّطْفَةَ‏ عَلَقَةً‏ فَخَلَقْنَا ٱلْعَلَقَةَ‏ مُضْغَةً‏ فَخَلَقْنَا ٱلْمُضْغَةَ‏

فَكَسَوَْ‏ ٱلْعِظَامَ‏ لحَْماً‏ ثمُ َّ أَنشَأَْهُ‏ خَلْقاً‏ آخَرَ‏ فَتَبَارَكَ‏ ٱهلل َُّ‏ أَحْ‏ سَنُ‏ ٱلخَْالِقِينَ‏ ﴾

Walaqad khalaqna al-insana min sulalatin min teenin; Thumma jaAAalnahu

nutfatan fee qararin makeenin; Thumma khalaqna alnnutfata AAalaqatan

fakhalaqna alAAalaqata Mudghatan fakhalaqna almudghata AAidhaman


152

fakasawna alAAidhama lahman thumma ansha/nahu khalqan akhara fatabaraka

Allahu ahsanu alkhaliqeena (Surat Al Muuminun 23:12-14)

Tafsir: Na kwa hakika tumemuumba Mtu kutokana na Udongo wa Mfinyanzi, Kisha

tukamjaalia kua katika Nutfah (Mchanganyiko wa maji ya uzazi ya Mwanamme na

Mwanamke) na tukayahifadhi ndani Hifadhio Maalum (Fuko la Uzazi la Mama). Na

kisha tukaumba kutokana na Nutfatan katika Aa’alaqatin (Pande la Damu) na kisha

tukalifanya pande la Damu kua ni pande laini laini la Nyama, na tukafanya kutokana

na pande laini laini la Nyama kuwepo na Mifupa laini, na kisha tukaivisha Mifupa

kwa Nyama na kisha tukaumba kutokana nayo kua kiumbeca mwisho(Ibn Adam).

Hivyo Utukufu ni wa Allah tu ambae ndie mbora wa Kuumba.

Na baada ya kutuwekea wazi maumbile hayo basi katika sehemu nyengine Allah

Subhanah wa Ta’ala anahoji na kufafanua tena kua:

‏﴿بِ‏ سْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ‏ ۞ هَلْ‏ أَتَى ٰ عَلَى ٱلإِنسَانِ‏ حِ‏ ينٌ‏ مِّنَ‏ ٱلد َّهْرِ‏ لمَْ‏ يَ‏ كُن شَيْئاً‏

م َّذْكُوراً‏ ۞ إِ َّ خَلَقْنَا ٱلإِنسَانَ‏ مِن ن ُّطْفَةٍ‏ أَمْشَاجٍ‏ ن َّبْتَلِيهِ‏ فَجَعَلْنَاهُ‏ سمَِيعاً‏ بَ‏ صِ‏ يراً‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Hal ata AAala al-insani heenun mina alddahri

lam yakun shay-an madhkooran; Inna khalaqna al-insana min nutfatin amshajin

nabtaleehi fajaAAalnahu sameeAAan baseeran; (Surat Al Insan 76:1-3)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma na Mwingi wa Huruma;Hivi Jee hakua

Mtu katika kipindi wakati akiwa si kitu chochote kinachoweza kuzunguzmiwa?Kwani

kwa hakika tumemuumba Mtu kutokana na Nutfah kwa ajili ya kumjaribu na hivyo

tukamfanya kua ni mwenye kusikia na kuona.

Hivyo tunapoziangalia aya basi tunaona kua zinazungumzia kuhusiana na hatua za

maumbile ya Ibn Adam yaani Mtoto anaezaliwa na Mtu kua ni kuanzia kwenye Nutfah,

kisha Aa’alaqin na kisha Mudghah. Ambapo amesema Abd Allah Ibn Masud Radhi

Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Maumbile

ya Mkusanyiko wa kila mmoja wenu unakusanyika ndani ya Fuko la Uzazi wa

Mama yake ndani ya siku 40, na kisha hua Aalaqah kwa siku 40, na kisha hua

Mudghah kwa kwa siku 40. Na kisha Malaika hua anatumwa kwa ajili ya

kumuandikia mambo manne: Riziki yake, Uhai wake; Amali zake na Kama atakua

mwema au Muovu, nakisha hupuliziwa Roho yake’’(Bukhari na Muslim)

Na ndio maana akasema Mujaddid Ad Din Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid

Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali kua: ‘Hairuhusiki kuitoa


153

Mimba kwa sababu kuitoa Mimba hua ni sawa na Kuua, hususan Mimba hio

inapopita umri wa siku 120, kwani kufanya hivyo hua ni kuitoa Roho iliyokwisha

ingizwa ndani ya mwili wake na mwili wake hua ni wenye kujitegemea’

Kwani hatua ya kwanza ya Mtoto hua ni pale Manii yanapoingia Ndani ya Fuko la

Uzazi na kuchanganyika na Maji ya Uzazi ya Mama na hivyo hua tayari ni yenye

kujitayarisha kwa ajili ya Uhai, hivyo ni kusababishia madhara hua ni haram

ambapo dhambi za kuitoa Nutfah katika umri wa siku 40 hua ni ndogo kuliko

dhambi za kuitoa Aalaqah inapokua baina ya siku 40-80 ambazo hua ni ndogo

kuliko dhambi za kuitoa Mudgha ambazo hua ni baina ya umri wa siku 80-120.’

Na ndio maana pia Mwanamke Mjamzito anapofanya kosa linalostahiki kuadhibiwa

adhabu ya Kifo basi kwa sharia za Kiislam hua hahukumiwi hadi pale atakapojifungua

na kisha kua ni mwenye kumyonyesha Mtoto wake kwa muda wa kunyonyesha ambao

ni miaka miwili.

Kwani inapofikia umri wa siku 120 basi hua tayari ni Dhambi za Kudhulumu Nafsi ya

Mtu na hivyo Kutoa Mimba kwa kipindi hiki hua hakuruhusiki isipokua kwa sababu

inayokubalika Kisharia kwa mfano pale inapokua Mimba inahatarisha Afya na Uhai wa

Mama Mjamzito.

Ambapo kwa upande wa Al Muhaqqiq Imam Ibn Hajar Al Haytami basi yeye anasema

katika Tuhfah Al Muhtaj kua: ‘Ni haram kuitoa Mimba pale wakati ambapo Nutfah

imeshakua tayari imeshafanya Istiqrar (katika siku za 40 za mwanzo)’ na kwa

Upande wa Shaykh Ul Islami Imam Shams Ad Din Al Ramli basi yeye anasema katika

Nihayat Al Muhtaj kua: ‘Inaruhusika kuitoa pale inapokua haijafikia siku 120 yaani

kabla ya kupuliziwa Roho kwa Mimba hio.’ Ambao huu pia ndio mtizamo wa

Madhhab Imam Abu Hanifa

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Qasim Ibn Juzay Al Qalbi Al Maliki basi yeye

anasema kua: ‘Pale inapokua Fuko la Uzazi limeshikamana na Manii basi hua

hairuhusiki kuingia baina yake na kukatisha muendeleo wake, na mbaya zaidi pale

inapokua tayari Mimba tayari imeshaanza kua pande la nyama, na mbaya zaidi

pale inapokua tayari imeshapuliziwa Roho yake kwani hii hua ni Kuua Nafsi

kulingana na Makubaliano ya Ijmaa.’ Na huu pia ndio Mtizamo wa Madhhab ya Imam

Ahmad Ibn Hanbal

Ambapo anasema Abu Hurayrah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wanawake wawili wa kabila

la Hudhayl walipigana, ambapo mmoja wapo akachukua Jiwe akampiga

mwenzake, na hivyo akamuuma Mtoto aliemo ndani ya Tumbo lake. Hivyo kesi hii

ikapelekwa mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi Alayhi wa Salam ambae akaamua

kua aliempiga mwenzake alipe Ghurra.’


154

Ambapo Ghura maana yake hua ni Malipo ya fidia yanayolipwa na Mtu ambae

amesababisha madhara kuharibika kwa Mimba ya Mtu. Ambapo Ghura hua inatakiwa

kulipwa ndani ya mwaka mmoja kwa wale waliodhurika kutokana na madhara hayo

wakati wakiwa ni wenye haki ya kurithi kutoka kwa Kiumbe kilichomo ndani ya Mimba

iliyoharibika, isipokua yule aliesababisha Madhara ya kutoka Mimba hio labda tuseme

Mama mwenyewe au Baba n.k basi hua hawezi kurithi na badala yake atalipa Ghura

ambayo hua ni malipo ya kutoa Ngamia watano ambayo hua ni sehemu moja kati ya 20

za Diya yaani fidya ya kumwaga damu bila ya kukusudia.

Kwani kwa upande wa Uislam ikawa hairuhusiki kuimwaga Damu ya Ibn Adam bila ya

sababu inayokubalika kisharia, kama vile ambavyo Allah Subhanah wa Ta’ala

alivyowaamrisha watu wa Bani Israil hapo kabla kwa kusema:

‏﴿مِنْ‏ أَجْلِ‏ ذٰلِكَ‏ كَتَبْنَا عَلَى ٰ بَنيِ‏ ۤ إِسْرَائِيلَ‏ أَن َّهُ‏ مَن قَتَلَ‏ نَفْساً‏ بِغَيرِْ‏ نَفْسٍ‏ أَوْ‏ فَ‏ سَادٍ‏

فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَكَأَنم ََّا قَتَلَ‏ ٱلن َّاسَ‏ جمَِيعاً‏ وَمَنْ‏ أَحْيَاهَا فَكَأَنم ََّا أَحْ‏ يَا الن َّاسَ‏ جمَِيعاً‏ وَلَقَ‏ ‏ْد

جَآءَتْهُمْ‏ رُسُلُنَا بِٱلّبَيِّنَاتِ‏ ثمُ َّ إِن َّ كَثِيراً‏ مِّنْهُمْ‏ بَعْدَ‏ ذٰلِكَ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ لَمُسْرِفُونَ‏ ﴾

Min ajli dhalika katabna AAala banee isra-eela annahu man qatala nafsan bighayri

nafsin aw fasadin fee al-ardhi fakaannama qatala alnnasa jameeAAan waman

ahyaha fakaannama ahya alnnasa jameeAAan walaqad jaat-hum rusuluna

bialbayyinati thumma inna katheeran minhum baAAda dhalika fee al-ardhi

lamusrifoona (Surat Al Maidah 5:32)

Tafsir: Kutokana na hilo basi tumewaamrisha watu wa Bani Israil kua kwa yeyote yule

atakaeiua Nafsi (ya Mtu) bila ya (sababu ya kuuliwa) Nafsi ya mtu mwengine, au

kufanya ufisadi Ardhini basi ni kama alieua Watu wote kwa pamoja. Na atakae

ihuisha Nafsi basi ni sawa na aliewahuisha watu wote kwa ujumla. Na kwa hakika

walikuja kwao wao Mitume wetu wakiwa na Vithibitisho vilivyo wazi, lakini wengi wao

baada yake waliendelea kufanya Israfu ardhini.

Na kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akakataza pia kumwaga Damu ya Mtu aliemuamini

Allah Subhanah wa Ta’ala kama ilivyosema aya:


155

‏﴿وَمَن يَقْتُلْ‏ مُؤْمِناً‏ م ُّتَعَمِّداً‏ فَجَزَآؤُهُ‏ جَهَن َّمُ‏ خَالِداً‏ فِيهَا وَغَضِبَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلَيْهِ‏ وَلَعَنَهُ‏

وَأَعَد َّ لَهُ‏ عَذَاابً‏ عَظِيماً‏ ﴾

Waman yaqtul mu/minan mutaAAammidan fajazaohu jahannamu khalidan feeha

waghadhiba Allahu AAalayhi walaAAanahu waaAAadda lahu AAadhaban

AAadhiman (Surat Al Maidah 4:93)

Tafsir: Na yeyote yule atakaemuua Muumini kwa makusudi, basi malipo yake ni

Jahanama atakapokaa milele, na Adhabu na Laana za Allah zitakua juu yake, na

ametayarishiwa kwa ajili yake Adhabu kali sana.

Hivyo ingawa Damu ya Ibn Adam hua hairuhusiki kumwagwa kutokana na Utukufu

wake lakini hata hivyo kwa upande mwengine basi pia hairuhusiki kuiuza Damu wala

kuinunua kama inavyofanywa kwenye Mahospitali mbali mbali leo hii Duniani.

Na hii ni kutokana na kauli ya Abu Juhayfa Radhi Allahu Anhu ambae alimnunua

Mtumwa ambae kazi yake ilikua ni kufanya Hijama na kisha akaamrisha kua vifaa vyake

vya kufanyia Hijama vivunjwe, alipoulizwa ni kwa sababu gani akaamrisha hivyo basi

alisema kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ameharamisha bei ya

Damu’(Sahih Bukhari)

Ambapo kutokana na hadithi hii basi Mujaddid Ad Din Shaykh ul Islami Al Hafidh Imam

Shihab Ad Din Ahmad Ibn Hajjar Al Asqalani basi amesema kua: ‘Kinachomaanishwa

hapa katika hadithi hii ni kua Ni Haram kuuza Damu kama vile ambavyo ilivyokua

Haram kuuza Nyama ya Mnyama aliekufa na Nyama ya Nguruwe na ni Haram

kuuza na kununua Damu kulingana na makubaliano ya Wanazuoni.’(Fat-h Al Barr)

Na Mujtahid Imam Abu Bakr Muhammad Ibn Ibrahim Ibn Al Mundhir Al Nishapuri basi

yeye anasema kua: ‘Kuuza Damu hua ni Haram na hivyo Makubaliano ya kuuziana

Damu hua hayajuzu kutokana na maneno ya aya isemayo:

‏﴿قُل لا َّ أَجِ‏ دُ‏ فىِ‏ مَآ أُوْحِ‏ ىَ‏ إِلىَ َّ محَُر َّماً‏ عَلَى ٰ طَاعِمٍ‏ يَطْعَمُهُ‏ إِلا َّ أَن يَكُونَ‏ مَ‏ يْ‏ تَةً‏ أَوْ‏

دَماً‏ م َّسْفُوحاً‏ أَوْ‏ لحَْمَ‏ خِ‏ نزِيرٍ‏ فَإِن َّهُ‏ رِجْسٌ‏ أَوْ‏ فِسْقاً‏ أُهِل َّ لِغَيرِْ‏ ٱهلل َِّ‏ بِهِ‏ فَمَنِ‏ ٱضْطُ َّر

غَيْرَ‏ ابَغٍ‏ وَلاَ‏ عَادٍ‏ فَإِن َّ رَب َّكَ‏ غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾


156

Qul la ajidu feema oohiya ilayya muharraman AAala taAAimin yatAAamuhu illa

an yakoona maytatan aw daman masfoohan aw lahma khinzeerin fa-innahu rijsun

aw fisqan ohilla lighayri Allahi bihi famani idhturra ghayra baghin wala AAadin

fa-inna rabbaka ghafoorun raheemun(Surat Al AnaAm 6:145)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam): ‘Sikuona katika

nilivyoshushiwa wahyi chochote kile kilichoharamishiwa kuliwa na mtu mwenye

kutamani kula isipokua itakapokua ni Maiti au ni Damu yenye kutiririka au Nyama

ya Nguruwe, kwani kwa hakika huo ni uchafu au ni kufanya uovu kwa kuchinja si

kwa ajili ya Allah, lakini atakaelazimika bila ya kua na hiari ya kufanya uasi na

kuvuka mipaka basi kwa hakika Mola wako ni mwingi wa Kusamehe na ni mwingi wa

Huruma.’

Ambapo aya imetumia neno Daman masfoohan yaani Damu iliyokua Masfuha. Na neno

Masfuuha limetokana na neno Safaha ambalo hua linamaanisha Kumwaga, Kutiririka au

Kumiminika.

Neno Safaha ndio pia lililotoa neno Musafihun ambalo hua linamaanisha Mtu

anaemmwagia mwenzake manii au anaemwagiwa manii nje ya ndoa yaani anaefanya

Usharati au Uzinifu.

Ambapo kwa upande wa Imam Muhamamd Yusuf Al Atfayyesh basi yeye anasema kua:

‘Neno Safaha hua linamaanisha Mchanganyiko wa kua na Ufahamu Dhaifu na

kutumia kitu katika njia za uovu.’

Na si Damu tu bali kila kiungo cha Ibn Adam hua hairuhusiki kukiuza wala kukinunua

kutokana na Utukufu wa Mwili wa Ibn Adam kama alivyosema Allah Subhanah wa

Taala kua:

‏﴿وَلَقَدْ‏ كَ‏ ر َّمْ‏ نَا بَنىِ‏ ءَادَمَ﴾‏

Walaqad karramna banee adama (Surat Al Israa, 17:70)

Tafsir: Na kwa hakika tumemkirimu Bani Adam.

Lakini hata hivyo hapa pia inabidi tufahamu kua ingawa hairuhusi kuuza wala kununua

viungo vya mwili vya Ibn Adam au Damu ya Ibn Adam lakini inaruhusika kufidia kwa

kutoa kiasi cha malipo na kumpa mtu anaehitajika Damu yake iongezewe kwa mtu

mwengine, kutokana na kua mtu huyo mwenye Damu hio ya ziada ni mwenye kukataa

kutoa Damu hio kwa ajili ya Ibn Adam mwenzake hadi pale atakapota malipo hayo, na


157

hivyo hua una dharura isiyikua na khiaria mabyo ndio iliyoelezewa na sehemu ya aya

isemayo:

‏﴿فَمَنِ‏ ٱضْطُر َّ غَيْرَ‏ ابَغٍ‏ وَلاَ‏ عَادٍ‏ فَإِن َّ رَب َّكَ‏ غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Famani idhturra ghayra baghin wala AAadin fa-inna rabbaka ghafoorun

raheemun(Surat Al AnaAm 6:145)

Tafsir: Lakini atakaelazimika bila ya kua na hiari ya kufanya uasi na kuvuka mipaka

basi kwa hakika Mola wako ni mwingi wa Kusamehe na ni mwingi wa Huruma.’

Na hivyo basi kutokana na hali ya malipo hayo basi mtu anaetoa malipo kwa ajili ya

Damu hio hua hana kosa na hapati dhambi kutokana na kulipia huko, ila mwenye

kupokea malipo hayo kwa ajili ya Damu hio basi hua ni mwenye kujibadilishia malipo

ya jambo jema kwa kupata malipo ya jambo ovu.

Naam hio ni kuhusiana na Damu ya Ibn Adam, ama tunapozungumzia kuhusiana na

Damu ya mnyama ambae ni halali kuliwa basi hua inakubalika kumwagwa Damu yake

pale inapokua kufanya hivyo hua ni kwa ajili ya kutoa kafara kwa ajili ya Allah Subhanah

wa Ta’ala

Imam Khalil Ibn Is-haq Al Jundi Al Maliki anatubainishia Hikma ya kuruhusiwa kwa Ibn

Adam kuchinja Wanyama kwa kusema kua: ‘Wakati Allah alipowakirimu Ibn Adam

kwa ufaham, basi aliwafanya Wanyama wengine kua ni wenye kuruhusiwa kua

chakula chake kwa ajili ya kuwaimarishia Miili yao Ibn Adam, kubainisha

Makadirio yake Muumba kupitia katika njia ya Nyama yao na kuwaonesha Ibn

Adam kua anawajali kwa kuwaweka wao juu zaidi yao Wanyama hao.’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anasema katika Qur’an kua:

‏﴿وَٱلْبُدْنَ‏ جَعَلْنَاهَا لَكُمْ‏ مِّن شَعَائِرِ‏ ٱهلل َِّ‏ لَكُمْ‏ فِيهَا خَيْرٌ‏ فَٱذْكُرُواْ‏ ٱسْمَ‏ ٱهلل َِّ‏ عَلَيْ‏ هَا

صَوَآف َّ فَإِذَا وَجَبَتْ‏ جُنُوبُهَا

فَكُلُواْ‏ مِنْهَا وَأَطْعِمُواْ‏ ٱلْقَانِعَ‏ وَٱلْمُعْتَر َّ كَ‏ ‏ٰذلِ‏ ‏َك

سَخ َّرَْهَا لَكُمْ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تَشْكُرُونَ۞لَن يَنَالَ‏ ٱهلل ََّ‏ لحُُومُهَا وَلاَ‏ دِمَآؤُهَا وَلَٰ‏ ‏ِكن يَنَالُهُ‏


158

ٱلت َّقْوَىٰ‏ مِنكُمْ‏ كَذٰ‏ لِكَ‏ سَخ َّرَهَا لَكُمْ‏ لِتُكَبرُِّواْ‏ ٱهلل ََّ‏ عَلَى ٰ مَا هَدَاكُ‏ مْ‏ وَبَشِّ‏ رِ‏

ٱلْمُحْسِ‏ نِينَ‏ ﴾

Waalbudna jaAAalnaha lakum min shaAAa-iri Allahi lakum feeha khayrun

faodhkuroo isma Allahi AAalayha sawaffa fa-idha wajabat junoobuha fakuloo

minha waatAAimoo alqaniAAa waalmuAAtarra kadhalika sakhkharnaha lakum

laAAallakum tashkuroona; Lan yanala Allaha luhoomuha wala dimaoha walakin

yanaluhu alttaqwa minkum kadhalika sakhkharaha lakum litukabbiroo Allaha

AAala ma hadakum wabashshiri almuhsineena (Surat Al Hajj 22:36-37)

Tafsir: Na Wanyama wa Kuchinja (Ngombe, Ngamia n.k) tumewajaalia wao kwa ajili

yenu kua alama ya Allah, ndani yake mna kheri nyingi. Hivyo tajeni Jina la Allah juu

yao wanapokua kwenye safu (kwa ajili ya kuchinjwa), kisha wanapoanguka (baada ya

kuchinjwa) kuleni kutokana nao na walisheni kutokana nayo Masikini wenye kuomba

na wasioomba. Hivyo tumewafanya kua chini yenu ili mpate kushukuru. Na si Nyama

yao wala Damu yao inayomfikia yeye (Allah Subhanah wa Ta’ala) bali ni Taqwa

kutoka kwenu ndio inayomfikia. Hivyo tumewafanya kua chini yenu ili mpate

kumkuza Allah, kutokana na Uongozi wake juu yenu, na (Ewe Muhammad) wape

habari njema wenye kufanya mema.

Ambapo aya zimetumia neno Budna lenye kutokana na neno Badan ambalo hua

linamaanisha, Kunona, Kua na Mwili Mkubwa, Kua na Mwili bila ya Roho. Neno Badan

ndio lililotoa neno Budun ambalo hua linamaanisha Mnyama wa Kuchinja au wa

Kutolewa Kafara. Ambapo ingawa neno Badan na neno Jism hua ni yenye kufanana

kimaana lakini hapo hapo neno Jism hua linamaanisha Mwili au Kiwiliwili lakini pale

kinapozungumziwa kuhusiana na hali ya muonekano wake na rangi yake, wakati neno

Badan hua linatumika pale inapozungumziwa kuhusiana na mkubwa wa kiumri.

Na ikatumia neno Sawaffa ambalo ni lenye kutokana na neno Saffa ambalo humaanisha

Safu, Kupanga Mstari au kwa mpangilio, hivyo baadhi ya Wanazuoni hua ni wenye

kulisoma neno hili katika hali ya Saafinah ambalo hua linamaanisha pia Hali ya kutembea

kwa miguu, au Kujifunga wenyewe na hivyo kumfanya Ngamia kua ni mwenye

kusimama kwa miguu mitatu, na hivyo kua ni mwenye kuchinjwa wakati akiwa

amesimama katika hali hio na kuangukia upande mmoja kutokana na kushindwa kujizuia

baada ya kutokwa na damu nyingi sana.

Ambapo neno Saafinah pia ndio lile lililotumika katika ya zinazoelezea kisa cha Nabii

Sulayman pale alipokua akiangalia Farasi wazuri sana waliokua wakipitishwa mbele


159

yake wenye kuvutia kutokana na muonekano wao na madaha yao ya kusimama kwa

miguu mitatu kama ilivyosema aya:

‏﴿إِذْ‏ عُرِضَ‏ عَلَيْهِ‏ بِٱلْعَشِ‏ ىِّ‏ ٱلص َّافِنَاتُ‏ ٱلجِْيَادُ‏ ﴾

Idh AAuridha AAalayhi bialAAashiyyi alssafinatu aljiyadu (Surat Sad 38:31)

Tafsir: Wakati walipooneshwa mbele yake katika wakati wa Alasiri, Farasi bora

wanaopendeza.

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Imam Muhammad Ibn Jarir At Tabari kua

‘Kuna baadhi ya Wanazuoni ambao wamelifaham neno Sawaaf kua linamaanisha

na sawa ya ile maana ya neno Khaalis yaani Ikhlasi.’

Ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye

anasema kuhusiana na maneno yasemayo kua: ‘Fa-idha wajabat junoobuha yaani na

kisha wanapoanguka’ kua Neno Wajabat hua ni sawa na neno Saqata ambalo

humaanisha Kuanguka, ambapo kwa upande wa Zayd Ibn Aslam Radhi Allahu Anhu

anasema kua: ‘Wanapoanguka na Kufa’ na hii ni kwa sababu Mnyama anaechinjwa

hua hairuhusiki kukatwa sehemu ya mwili wake, kunyonyolewa, kuchunwa ngozi n.k

bali hua inaruhusika kufanyiwa hivyo pale anapokua ameshachinjwa na hayuko hai.

Kwani katika kipindi cha wakati wa Uhai wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi

watu wa Madinah walikua na tabia ambayo inaelezewa na Abu Waqiy Radhi Allahu Anhu

kwa kusema kua: ‘Kabla ya kuja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika Mji

wa Madinah ilikua ni kawaida kwa watu kukata Nundu ya Ngamia na Mkia wa

Kondoo hivyo Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam akaema kua: ‘Chochote kile

kitakachokatwa kutokana na Mnyama wakati akiwa hai basi hua Maiti (isiyofaa

kuliwa).’(Imam At Tirmidhii)

Na kwa upande wa Imam Abu Maali Al Juwayni Al Haramayn ambae ni mwalimu wake

Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali basi yeye

anasema katka Kitabu chake cha Nihayat Al Matlab kua mpaka kuikata sehemu ya

Samaki aliekua mzima baada ya kuvuliwa kwake basi hua haifai kwa sababu hii hua ni

sehemu ya kumuadhibu kiumbe huyo, lakini hua haimharamishi Samaki huyo na wala

haiiharamishi sehemu yake hio kutokana na kuliwa.

Na amesema Jabir Ibn Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alitangazia katika mji wa Makkah katika mwaka ambao Mji wa Makkah

ulitekwa na Waislam kua: ‘Kwa Hakika Allah na Mtume wake ameharamisha


160

uuzwaji wa Pombe, Maiti, Nguruwe na Masanamu’ Hivyo mtu mmoja akauliza:

‘Ya Rasul Allah! Vipi kuhusiana na Mafuta ya Mnyama aliekua Maiti? Kwani

yalikua yanatumika kwa ajili ya kupakaza kwenye Majahazi. Kuzipaka Ngozi na

watu walikua wakitumia kwa ajili ya kuwashia Taa zao.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Mafuta hayo pia ni Haram. Kwani

Allah aliwalaani Mayahudi, kwani kwa hakika (Nyama ya Mnyama aliekufa) Maiti

iliharamishwa juu yao, na kisha wao wakaigeuza katika hali nyengine (kwa

kuichanganyana vitu vyengine) wanaiuza na kupata faida kutokana nayo.’(Bukhari

na Muslim)’

Ambapo hadithi hii inatubainishia uthibitisho wa kua hairuhusiki kukificha kitu

kilichokua haramu na kisha kukichanganya na kitu kilichokua halali au kukigeuza jina

na kisha kukiuza baada ya kukipendezesha, kwani hii hua pia ni sawa na vile zilivyosema

aya zifuatazo:

‏﴿إِنم ََّا حَر َّمَ‏ عَلَيْكُمُ‏ ٱلْمَيْتَةَ‏ وَٱلْد َّمَ‏ وَلحَْمَ‏ ٱلخَْنْزِيرِ‏ وَمَآ أُهِل َّ لِغَيرِْ‏ ٱهلل َِّ‏ بِهِ‏ فَمَنِ‏ ٱضْطُ َّر

غَيْرَ‏ ابَ‏ غٍ‏ وَلاَ‏ عَادٍ‏ فَإِن َّ ٱهلل ََّ‏ غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ۞‏ وَ‏ ت لاَ‏ َ‏ قُولُواْلَِما تَصِ‏ فُ‏ أَ‏ لْسِ‏ نَتُكُمُ‏ ٱلْكَذِ‏ ‏َب

هَٰذَا حَلاَلٌ‏ وَ‏ هَٰذَا حَرَامٌ‏ لِّتَفْتَرُواْ‏ ٰ عَلَى ٱهلل َِّ‏ ٱلْكَذِبَ‏ إِن َّ ٱل َّذِينَ‏ يَفْتَرُونَ‏ ٰ عَلَى ٱهلل َِّ‏

ٱلْكَذِبَ‏ لاَ‏ يُفْلِحُونَ‏ ﴾

Innama harrama AAalaykumu almaytata waalddama walahma alkhinzeeri wama

ohilla lighayri Allahi bihi famani idturra ghayra baghin wala AAadin fa-inna

Allaha ghafoorun raheemun; Wala taqooloo lima tasifu alsinatukumu alkadhiba

hadha halalun wahadha haramun litaftaroo AAala Allahi alkadhiba inna

alladheena yaftaroona AAala Allahi alkadhiba la yuflihoona(Surat AnNaml 16:115-

116)

Tafsir: Hakika (Allah Subhanah wa Taala) amekuharamishieni juu yenu Maiti na

Damu na Nyama ya Nguruwe na kilichochinjwa ambacho si kwa ajili ya Allah, lakini

kama (mtu) atalazimika bila ya kua na khiari wala kuvuka mipaka basi hakuna kosa

juu yake. Kwani kwa hakika Allah ni miwingi wa Kusamehe na ni mwingi wa Huruma.

Na wala msiseme kuhusiana na ndimi zenu zenye kukadhibisha kua hiki ni halali na

hiki ni haramu kuzusha dhidi ya Allah Uongo, hakika wale wanaozua Uongo dhidi ya

Allah hawatofuzu.


161

Imam Burhan Ad Din Abu Hassana Ali Ibn Ab Bakar Ibn Abd Jalil Al Farghani Al-

Marghinani Al Hanafi kua: ‘Malengo ya Kuharamishwa baadhi ya Vyakula hua ni

kutokana na umuhimu wa kuilinda heshima ya Mwili wa Ibn Adam kwa kuuzuia

kutokana na kudhalilika kunakotokana na kula vyakula vilivyoharamishwa’, yaani

makatazo hayo hua ni yenye kukatazwa kutokana na madhara ya vitu hivyo kwa mwili

wa Ibn Adam na pia utumiaji wa vyakula vilivyoharamishwa hua ndio sababu kuu

inayompelekea Ibn Adam kua ni mwenye kufanya maasi, na hivyo anapokua anajidhibiti

basi humpelekea mtu husika kua ni mwenye kupendelea kufanya mema zaidi.

Hivyo vile vyakula vilivyoharamishwa vimeharamishwa kwa sababu ya madhara yake

na vilivyohalalishwa vimehalalishwa kutokana na faida zake na kuamrishwa kugawiana

na wengine pia wasiokua na uwezo navyo wapewe ili nao wanufaike navyo kama

ilivyoamrishwa kwenye aya zetu za Surat Al Hajj 22:36-37 ambazo ndani yake mna

maneno yasemayo;

‏﴿فَكُلُواْ‏ مِنْ‏ هَ‏ ا وَأَطْعِ‏ مُواْ‏ ٱلْقَانِعَ‏ وَٱلْمُعْتَر َّ ﴾

Fakuloo minha waatAAimoo alqaniAAa waalmuAAtarra (Surat Al Hajj 22:36)

Tafsir Hivyo kuleni kutokana nao na walisheni kutokana nayo Masikini wenye

kuomba na wasioomba.’

Ambapo maana ya maneno haya na amrisho liliomo ndani yake basi ndio msingi uliotoa

Hukmu ya Fiqh kua Nyama ya Mnyama anaechinjwa inatakiwa igaiwe katika sehemu

tatu ambapo sehemu moja hua ni kwa ajili ya Mchinjaji, sehemu ya pili kwa ajili ya Watu

wa karibu au Marafiki na sehemu ya tatu ni kwa ajili ya Masikini.

Na anasema Hujjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad

Ibn Muhammad Al Ghazali kua; ‘Allah Subhanah wa Taala amewataka Viumbe wake

kufuata maamrisho yake na hivyo kua ni wenye kula kile ambacho ni kisafi, kizuri,

kikamilifu chenye kunufaisha na chenye ladha tamu’ ambapo sifa zote hizi

zimejumuishwa kwenye neno Tayyib kama ilivyoelezewa kwenye aya ifuatayo:

‏﴿قُلْ‏ مَنْ‏ حَر َّمَ‏ زِينَةَ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱل َّتيِ‏ ۤ أَخْرَجَ‏ لِعِبَادِهِ‏ وَالْط َّيِّبَاتِ‏ مِنَ‏ ٱلرِّزْقِ‏ قُلْ‏ هِىَ‏ لِل َّ ذِينَ‏

آ مَنُو اْفىِٱ لحَْيَا ةِٱلد ُّنْيَا خَالِصَةً‏ يَوْمَ‏ ٱلْقِيَامَةِ‏ كَذٰ‏ لِكَ‏ نُفَصِّلُ‏ ٱلآَتِ‏ لِقَوْمٍ‏ يَ‏ عْلَمُونَ‏


162

‏۞قُلْ‏ إِنم ََّا حَر َّمَ‏ رَبىَِّ‏ ٱلْفَوَاحِ‏ شَ‏ مَا ظَهَرَ‏ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ‏ وَٱلإِثمَْ‏ وَٱلْبَغْىَ‏ بِغَيرِْ‏ ٱلحَْ‏ قِّ‏ وَأَن

تُشْرِكُواْ‏ بِٱهلل َِّ‏ مَا لمَْ‏ يُنَزِّلْ‏ بِ‏ هِ‏ سُلْطَاً‏ وَأَن تَقُولُواْ‏ عَلَى ٱهلل َِّ‏ مَا لاَ‏ تَ‏ عْلَمُونَ‏ ﴾

Qul man harrama zeenata Allahi allatee akhraja liAAibadihi waalttayyibati mina

alrrizqi qul hiya lilladheena amanoo fee alhayati alddunya khalisatan yawma

alqiyamati kadhalika nufassilu al-ayati liqawmin yaAAlamoona; Qul innama

harrama rabbiya alfawahisha ma dhahara minha wama batana waal-ithma

waalbaghya bighayri alhaqqi waan tushrikoo biAllahi ma lam yunazzil bihi

sultanan waan taqooloo AAala Allahi ma la taAAlamoona (Surat Al A’raf 7:32-33)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad): ‘Ni nani alieharamisha Vizuri vya Allah, ambavyo

amevitoa kwa ajili ya Viumbe wake na (Tayyibati) vizuri na visafi miongoni mwa riziki

zake’ Sema: ‘Hivi ni wa ajili ya wale walioamini katika maisha ya Dunia hii, lakini ni

kwa ajili yao tu katika siku ya Malipo.’ Hivyo ndivyo tunavyoelezea dalili zetu kwa

wale wenye kufaham. Sema: ‘Hakika aliyoyaharamisha Mola wangu ni mambo

machafu iwe ya dhahiri au ya siri, dhambi na kuvuka mipaka dhidi ya Ukweli au Haki

na kumshirikisha Allah kwa kile ambacho hakukipa mamlaka yake. Na kusema

kuhusiana na Allah juu ya mambo msiyoyajua.’’

Hapa tunaona kua aya zimetumia neno Tayyiba ambalo ni lenye kutokana na neno Tabba

ambalo hua ni lenye kumaanisha Kua Vizuri, Kupendeza, Kukubalika, Kuhalalika, Kua

na Usafi, Kufurahisha, Kuvutia kwa utamu.n.k

Hivyo basi tunapozungumzia kuhusiana na Tayyibati mina al Rizqi basi ndani yake

mnaingia kila kitu ambacho si kizuri na kinavutia, kisafi na kitamu tu lakini pia ndani

yake mnaingia kila chenye manufaa na mwili wa Ibn Adam, kukitumia bila ya kua na

kibri au kufanya israfu au kikimbilia baada ya kukikosa, kwani amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Yeyote yule mwenye chembe ya Kibri ndani ya

Moyo wake basi hatoinga Peponi.’

Mmoja kati ya Masahaba akauliza: ‘Ya Rasul Allah! Kama mtu anapenda Nguo zake

na Viatu vyake viwe vizuri ’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kwa

hakika Allah ni Mzuri na hivyo anapenda vilivyo vizuri. Kibri hua ni kusimama

dhidi ya Haki na Ukweli na kuwaangalia watu kwa chini.’

Na akasema tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Allah anapomjaalia Mja

wake fadhila zake basi hua ni mwenye kupenda kuona uzuri wa athari yake neema

hio juu ya mja huyo.’(Imam At Tirmidhii)


163

Hata hivyo kwa upande mwegine basi Mtu kua na vitu vizuri hua hakumaanishi kua ndio

mtu huyo anao ukaribu na Allah Subhanah wa Ta’ala na ndio maana Umar Ibn Al

Khattab Radhi Allahu Anhu akawa ni mwenye kusema kua: ‘Tungekula Vyakula vizuri

lakini Qur’an imesema:

‏﴿وَيَوْمَ‏ يُعْرَضُ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ عَلَى ٱلن َّارِ‏ أَذْهَبْتُمْ‏ طَيِّبَاتِكُمْ‏ فىِ‏ حَيَاتِكُمُ‏ ٱلد ُّنْيَ‏ ا

وَٱسْتَمْتَعْتُمْ‏ هبَِا فَٱلْيَوْمَ‏ تجُْزَوْنَ‏ عَذَابَ‏ ٱلهُْونِ‏ بمَِا كُنتُمْ‏ تَسْتَكْبرُِونَ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ بِغَيرِْ‏

ٱلحَْقِّ‏ وَبمَِا كُ‏ نتُمْ‏ تَفْ‏ سُقُ‏ ونَ‏ ﴾

Wayawma yuAAradhu alladheena kafaroo AAala alnnari athhabtum tayyibatikum

fee hayatikumu alddunya waistamtaAAtum biha faalyawma tujzawna AAathaba

alhooni bima kuntum tastakbiroona fee al-ardhi bighayri alhaqqi wabima kuntum

tafsuqoona(Surat Al Ahqaf 46:20)

Tafsir: Na katika siku ambayo wale waliokufuru watadhihirishiwa Moto (na

kuambiwa) Nyinyi mlipewa vitu vizuri katika maisha yenu ya Duniani na mkastarehe

kutokana navyo. Hivyo leo mtalipwa kwa Adhabu yenye kunyanyasisha kwa sababu

mlikua na Kibri katika ardhi bila ya kua na haki yeyote na kutokana na kua ni waasi

na wenye kufanya maovu.

Na kwa upande wa Hasan Al Basr basi yeye amesema kuhusiana na wale ambao ni wenye

kuyakimbilia mazuri ya Dunia ili wayapate hata kwa kutumia njia za haramu kua: ‘Allah

Subhnaha wa Ta’ala alipomtuma Mtume wake aliemchagua, ambae hakua ni

mwenye kufunga Mlango wake. Hakutafuta Mlinzi kwa ajili yake, hakua ni mwenye

kufanya dhulma, alikua ni mwenye kukaa chini ardhini, na alikua akila chakula

chake akiwa katika hali hio ya kukaa kitako chini, aliekua akiramba vidole vyake

baada ya kulaa kwake, hakua akivaa nguo za hariri, aliekua akipanda Punda na

kukubali Mtumwa wake kua ni abiria mwenzake juu ya Punda wake. Na alikua

akisema: ‘Yeyote yule mwenye kuachana na Sunnah zangu hua si wa miongoni

mwangu’’

Hasan Al Basr anaendelea kusema kua: ‘Na Sasa hivi tuna watu ambao wameachana

na Sunnah zake, hawa ni wale wapotovu ambao ni wenye kula Riba na kula vitu

vyengine vilivyoharamishwa, wajinga, na walionekana kua ni wajinga na

kuchukiwa na Mola wao, wanaamini kua hakuna ubaya katika kila chakula bora


164

wanachokimbilia kukitia mikononi mwao, wakayapamba majumba yao kwa

mapambo bora kabisa huku wakidai kusoma aya isemayo kua:

‏﴿قُلْ‏ مَنْ‏ حَر َّمَ‏ زِينَةَ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱل َّتيِ‏ ۤ أَخْرَجَ‏ لِعِبَادِهِ‏ وَالْط َّيِّبَاتِ‏ مِنَ‏ ٱلرِّ‏ زْقِ‏ ﴾

Qul man harrama zeenata Allahi allatee akhraja liAAibadihi waalttayyibati mina

alrrizqi (Surat Al A’raf 7:32)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad): ‘Ni nani alieharamisha Vizuri vya Allah, ambavyo

amevitoa kwa ajili ya Viumbe wake na (Tayyibati) vizuri na visafi miongoni mwa riziki

zake’

Hasan Al Basr anaendelea kusema kua: ‘Watu hawa hawajui kua Vitu hivyo ni kwa

ajili ya Marafiki wa Shaytan’

Naam..hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala ametujaalia vilivyo vizuri na kuwaweka chini

yetu wanyama wa chakula kwa ajili ya kua ni miongoni mwa vyakula vyetu vilivyo halali

yetu ambavyo hata hivyo inabidi vipatikane kwa njia ya uhalali na kisha ndio tupate

kuonesha shukrani kwake kwa kupitia njia ya kutoa kafara ya kumwaga damu ya

Wanyama hao kwa ajili yake yeye Muumba na hivyo basi hua hairuhusiki kula nyama ya

Mnyama aliechinjwa isipokua awe ni aliechinjwa kulingana na sharia za Kiislam,

ambayo inaanzia kwa mnyama huyo kutajiwa jina la Allah Subhana wa Ta’ala juu yake

katika wakati wa kuchinjwa. Kama inavyosema aya:

‏﴿فَكُلُواْ‏ ممِ َّا ذُكِرَ‏ ٱسْمُ‏ ٱهلل َِّ‏ عَلَيْهِ‏ إِن كُنتُمْ‏ آبَِتِهِ‏ مُؤْمِنِينَ‏ ﴾

Fakuloo mimma dhukira ismu Allahi AAalayhi in kuntum bi-ayatihi mu/mineena

(Surat Al Anaam 6:118)

Tafsir: Na Kuleni kile ambacho kimetajiwa Jina la Allah juu yake kama kweli nyinyi

ni wenye kuamini aya zetu.

Ambapo amesema Jundub Ibn Sufyan Al Bajali Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mara moja

sisi tulichinja Wanyama kua Kafara pamoja na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, hivyo baadhi ya Watu wakachinja kabla ya Sala ya Iddi, na baada ya Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kumaliza kusali, basi akaona kua wamechinja

kabla ya sala hivyo akasema: ‘Yeyote yule aliechinja Mnyama kabla ya Sala basi na

achinje tena badala yake na wale ambao hawakuchinja mpaka baada ya kumaliza

kusali basi na wchinje kwa kutaja jina la Allah’’(Sahih Bukhari)


165

Kwani nyama ambayo haikuchinjwa kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni sawa

na Maiti, ambayo ni Nyama iliyoharamishiwa kuliwa kama ilivyosema aya zenye

kubainisha vilivyoharamishwa kuliwa kwa kusema:

‏﴿حُرِّمَتْ‏ عَلَيْكُمُ‏ ٱلْمَيْتَةُ‏ وَٱلْد َّمُ‏ وَلحَْمُ‏ ٱلخِْنْزِيرِ‏ وَمَآ أُهِل َّ لِغَيرِْ‏ ٱهلل َِّ‏ بِهِ‏ وَٱلْمُنْخَنِقَةُ‏

وَٱلْمَوْقُوذَةُ‏ وَٱلْمُتَرَدِّيَةُ‏ وَٱلن َّطِيحَةُ‏ وَمَآ أَكَلَ‏ ٱلس َّبُعُ‏ إِلا َّ مَا ذَك َّيْتُمْ‏ وَمَا ذُبِحَ‏ عَلَى

ٱلن ُّصُبِ‏ وَأَنْ‏ تَسْتَقْسِ‏ مُواْ‏ بِٱلأَزْلاَمِ‏ ذٰلِكُمْ‏ فِسْقٌ‏ ٱلْيَوْمَ‏ يَئِسَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ مِن دِينِكُ‏ ‏ْم

فَلاَ‏ تخَْشَوْهُمْ‏ وَٱخْشَوْنِ‏ ٱلْيَوْمَ‏ أَكْمَلْتُ‏ لَكُمْ‏ دِينَكُمْ‏ وَأَتمَْمْتُ‏ عَلَيْكُمْ‏ نِعْمَتىِ‏

وَرَضِيتُ‏ لَكُمُ‏ ٱلأِسْلاَمَ‏ دِيناً‏ فَمَنِ‏ ٱضْطُر َّ فىِ‏ مخَْمَصَةٍ‏ غَيْرَ‏ مُتَجَانِفٍ‏ لإِثمٍْ‏ فَإِن َّ ٱهلل ََّ‏

غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Hurrimat AAalaykumu almaytatu waalddamu walahmu alkhinzeeri wama ohilla

lighayri Allahi bihi waalmunkhaniqatu waalmawqoodhatu waalmutaraddiyatu

waalnnateehatu wama akala alssabuAAu illa ma dhakkaytum wama dhubiha

AAala alnnusubi waan tastaqsimoo bial-azlami dhalikum fisqun alyawma ya-isa

alladheena kafaroo min deenikum fala takhshawhum waikhshawni alyawma

akmaltu lakum deenakum waatmamtu AAalaykum niAAmatee waradheetu

lakumu al-islama deenan famani idhturra fee makhmasatin ghayra mutajanifin liithmin

fa-inna Allaha ghafoorun raheemun(Surat Al Maidah 5:3)

Tafsir: Mmeharamishiwa juu yenu Maiti na Damu na nyama ya Nguruwe na kile

ambacho kimechinjwa si kwa ajili ya Allah, na kilichonyongwa au kupigwa kwa

kipigo cha nguvu, au kwa kuangukia Kichwa, au kwa Kutobolewa na Pembe za

Mnyama mwengine, na kile kilichobakia baada ya kuliwa na Wanyama wengine

isipokua kama mtawahi kukichinja (kabla hakijafa). Na kile ambacho kimechinjwa

kwa kutolewa kafara kwenye Madhabahu ya Masanam. Na pia kutumia mishare

kwa ajili ya kutafuta bahati au kutoa maamuzi, yote hayo ni Uasi. Leo hii

Wasioamini wote wameishiwa na matumaini juu ya Dini yenu, hivyo msiwe na

khofu nao, bali kuweni na khofu nami. Leo hii nimeikamilisha Dini yenu,

nimekamilisha fadhila zangu juu yenu na nimeuchagua Uislam kua ndio Dini yenu.

Lakini kwa yule ambae atakumbana na Njaa kali (basi anaweza kula hivyo


166

vilivyokatazwa), bila ya (kua ni mwenye) kuelemea kwenye dhambi, na kwa hakika

Allah ni mwingi wa Kusamehe na ni mwingi wa Rehma.

Ambapo iliposhuka aya hii basi Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu basi alilia sana

kutokana na kujua kua umewadia mda wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kuondoka Duniani kwani ameshatimiza wajibu wake wa kufikisha ujumbe wake kutoka

kwa Mola wake kwa ajili ya viumbe wake. Na bila ya shaka hili lilikua sahih kwa sababu

mara baada ya kushuka aya hii basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliishi kwa

mda wa siku 81 tu.

Ama kuhusiana na hukmu ya katazo hili liliomo ndani ya aya hii basi anasema Imam

Aḥmad Ibn Mūsá Ibn Marduwayh kua: ‘Suday Ibn Ajalan Radhi Allahu Anhu ambae

pia ni marufu kama Abu Umamah alichaguliwa na Rasul Allah Salallahu A’layhi

wa Salam akawausie watu wake kuhusiana na ujumbe wa Imani ya Dini Kiislam,

na wakati alipokua akiwausia juu ya ujumbe huo basi watu hao wakamletea Sahani

iliyojaa Damu ambayo ilikua imepikwa, nao watu hao wakamkaribisha. Lakini

akawaambia kua yeye ameharamishiwa kula chakula hicho na akawasomea aya hii.

Na kisha akaendelea kuwausia kuhusiana na ujumbe wa Dini ya Kiislam. Lakini

nao wakakataa, na kisha akawaomba maji kwani alikua ana kiu kubwa sana, lakini

nao wakakataa kumpa maji hayo na kumwambia kua bora wamwachie afe kwa kiu

kuliko kumpa maji. Abu Umamah anasema kua: ‘Mimi nilikua na kitambaa,

nikajifunika kichwa na kulala kutokana na joto kali. Wakati nikiwa nimelala akaja

mtu huku akiwa amebeba bakuli zuri sana ambalo uzuri wake hakuna anaeweza

kuufikiria, ambalo ndani yake mlikua mna kinywaji kitamu sana kisichoweza

kufikirika utamu wake. Akanipa kinywaji hicho nami nikanywa, na kutokana

nacho basi mimi nikaamka. Na Wa Allahi sikuona kiu tena! Na wala sikukihitaji

tena kile kitambaa baada ya kunywa kinywaji hicho.

Kisha nikawasikia wale watu wakiwa wanasema: ‘Angalieni, huyu mtu alikuja

kwenu kutoka katika jamii ya watu wa Milimani, lakini hamkumpa hata kinywaji’

hivyo wakanipa mie kinywaji cha Maziwa yaliyochanganywa na Maji, lakini nami

nikawaambia kua: ‘Hakika mimi sihitaji kinywaji chenu tena kwani Allah

amenipatia kinywaji. Na nikawaonesha tumbo langu, na watu wote hao wakaingia

katika Uislam. ’’ (Imam Ibn Abi Hatim, Imam Ibn Marduwayh, na Imam Al Hakim)

Ambapo aya zinaamrisha kuchinja na kumwaga Damu ambayo ni haram kuliwa kama

ilivyokatazwa na Allah Subhanah wa Ta’ala na ndio maana ikaamrishwa kuchinja kabla

ya kumla Mnyama kwa sababu Mnyama anapochinjwa kwa kukatwa Mishipa yake

mikuu ya Damu na bomba ya hewa basi Damu yote iliyomo ndani ya mwili wake hua ni

yenye kutoka kwa kutiririka kwa pamoja bila ya kubakia ndani ya mishipa ya damu


167

iliyomo ndani mwili wa Mnyama husika kutokana na kua Damu hua ni yenye

kusukumwa na Moyo.

Na ndio maana ikawa haitakiwi kumchinja mnyama kwa kumtenganisha kichwa na

kiwiliwili katika wakati wa kuchinja, bali kichwa kinatakiwa kutenganishwa na

kiwiliwili mara baada ya kumalizika kutoka kwa Damu ndani ya Mwili wa Mnyama, kwa

sababu kikitengenishwa kichwa mbali na kiwiliwili basi utokaji wa Damu

unaosababishwa na mapigo ya Moyo hua ni wenye kusita, na kisha Damu ya mnyama

hubakia ndani ya Nyama jambo ambalo hupelekea Nyama hio kua ni yenye kuweza

kuharibika mapema sana, na pia kua ni yenye kusababisha madhara kwa mlaji.

Ambapo hali hua tofauti wakati anapopigwa na kitu kizito au kunyongwa kwani katika

tukio hilo basi damu ya Mnyama husika, hua si yenye kutoka ndani ya mwili wake na

badala yake hua ni yenye kubakia ndani ya Mwili huo na kufanya mapande na kugandana

na nyama ya mnyama husika na hivyo kusababisha Nyama hio pia kua isiyoruhusika

kuliwa.

Na amesema Shaykh ul Islami Imam Muhammad Ibn Ahmad Ibn Zakariyah Al Ansari

kua amesema: ‘Muhyi Ad Din Abu Zakarriyah Sharaf An Nawawi kua: ‘Baadhi ya

Wanazuoni wamesema kua Hikma ya kutakiwa kuchinja hua ni Anhar Al Dam

yaani kuimwaga Damu yote na kutofautisha Uhalali wa Nyama na Mafuta na kile

kilichoharamishwa kwa Mnyama aliekufa kutokana na kubakiwa na Damu ndani

ya miili yao’(Asna Matalib)

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi

kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ameharamisha Nyama ya mnyama alieuliwa kwa

kunyonga au kwa kupigwa kwa kipigo cha dharuba kwa sababu ya kukosekana

Umuhimu wa kutoka na kumwagika kwa damu ya mnyama husika.’

Na Imam Abu Bakar Ahmad Ibn Ali Al Razi Al Jassas akasema kua: ‘Mtizamo wa Abd

Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu kuhusiana na Mnyama alieuliwa kwa kipigwa

silaha ya aina ya Banduqah (ambayo hua ni silaha kama jiwe, dongo la Duara au

chuma cha Duara), hua haruhusiki kuliwa’

Kwani amesema Imam Ahmad Ibn Hanbal kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua: ‘Msile mlichokipiga kwa Banduqah isipokua kama itakua

mliwahi kukichinja.’’ na huo ni mtizamo wa Imam Al Shafii, Imam Abu Hanifa na pia

Imam Malik.

Na amesema pia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kurusha Mawe

hakutomuua anaewindwa na wala hakutomuua Adui lakini kunaweza kuvunja

meno, au kutofoa Jicho.’(Sahih Imam Bukhari)


168

Na akasema Abd Allah Ibn Abbs Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam amekataza Sharita ya Shaytani. Ambayo ni Mnyama aliechinjwa kwa

kukatwa wazi huku Mshipa ya Damu ikiwa haijachinjwa na kisha akaachiwa kua

afe’(Sunnan Abu Daud)

Ambapo Adi Ibn Abi Hatim Radhi Allahu Anhu alimwambia Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua: ‘Ya Rasul Allah! Hakika mimi hua nnawinda kwa kutumia

Upinde ambao hauna manyoya nyuma yake jee Nyama yake ni halali?’ Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Unaweza ukala nyama yake kama ikiwa Ncha

ya Upinde imemtaboa, kwani aliepigwa na kuuliwa kwa ujiti wa upinde usiokua na

ncha hua ni mawqudha(aliegongwa mpaka akafa) hivyo msimle’(Bukhari na Muslim)

Na amesema Abaya Ibn Rafa’a Ibn Rafth Ibn Khadij kua: ‘Sisi tulikua na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam katika maeneo ya Dhul-Hulaifa, na hivyo watu walikua

na njaa na walikua wameteka Ngamia na Kondoo. Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam alikua Nyuma ya Watu, ambao walikua wakihangaikia kuchinja Wanyama

na kuwatia kwenye vyombo na kuwapika. Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam akaamrisha vyombo viachiwe na akaanza kugawa wanyama waliotekwa,

kuhusiana na Kondoo kumi kua sawa na Ngamia mmoja. Hapo Ngamia mmoja

akakimbia, na watu wakaanza kumkimbilia mpaka wakachoka. Katika wakati huo

kulikua na Farasi kidogo. Hivyo mtu mmoja akachukua Upinde na akampiga nao

Ngamia huyo na Allah akamsimamisha Ngamia huyo kutokana na Upinde huo.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Baadhi ya Wanyama hawa hua

ni kama Wanyama wa Mwituni, hivyo wakiwa hawadhibitiki basi wafanyieni kama

hivi (kwa kuwapiga upinde) kabla ya kuwagawanya Wanyama hao kwa Jeshi basi

Babu yangu akasema: ‘Tunaweza tukakutana na maadui baadae na hatutokua na

Visu, jee tunaweza kuwachinja Wanyama kwa kutumia Ncha za Mipinde?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Tumieni chochote kile kitakacho

sababisha kumwagika kwa damu, na kisha mleni Mnyama kama akiwa ametajiwa

Jina la Allah juu yake. Msimchinje Mnyama kwa Meno au kwa Kucha, na

nitakuambieni kwanini, kwa sababu Meno hua ni Mifupa (haiwezi kukata vizuri)

na Kucha zinatumiwa na Wahabeshi (na hivyo msiwaige kwani ni Makafiri)’’(Sahih

Bukhari)

Mbali ya kua aya hii imezungumzia kuhusiana na aina ya Nyama iliyoharamishwa kuliwa

na umuhimu wa kumwagwa Damu ya Mnyama husika lakini pia imezungumzia

kuhusiana na Azlami ambalo ni neno lililotokana na neno Zalama lenye kumaanisha

Kuzunguka zunguka, Kutembea, Kutoa zawadi ambayo ni ndogo sana, Kukata kitu na

kukifanya kua butu.


169

Na hivyo neno Azlami hua linamanisha Upinde ambao umekatwa hauna ncha wala

manyoya hivyo kua hauna mbele wala nyuma, ambao hua ni wenye kutumiwa na watu

waliokua wakiangalia na kubashiri kua kama mambo yatakua ama la, yana kheri ama la

n.k ambapo watu walipokua wanashaka juu ya jambo basi walikua wakienda kwenye

Majumba yao ya Ibada ambapo ndani yake hua kuna sehemu ambayo imewekwa Mipinde

hio, ambayo imeandikwa maneno yasemayo Naam, La, Mungu karidhia, Mungu

hakuridhia n.k

Hivya mtu huyo mwenye shaka juu ya jambo lake basi huenda kwenye mipinde yenye

kujibu kuhusiana na jambo husika kwa mfano kilimo, biashara, ndoa, vita, safari n.k na

akiingiza mkono kwenye sehemu iliyowekwa mipinde hio na akitoa ulioandikwa kua

Mungu ameridhia basi hua ni mwenye kufanya jambo hilo, na kama akitoa ambao

umeandikwa Mungu hakuridhia basi huachana na jambo hilo, n.k

Ambapo Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al

Qurtubi kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua amekubaliana na Fa’al

hua hakuhusiani na njia za kubashiria. Kwani Fa’al hua ni kuangalia kutokana na

neno jema ambalo mtu analisikia pale anapokua anaumwa, kwa mfano: ‘Ya Salim

ambalo humaanisha ‘Ewe uliesalimika na kua mzima na mwenye Afya’ na hivyo

mtu hua ni mwenye kuangalia kutokana na kusikia hali yake kutokana na

kuambiwa kua ni mwenye afya na hivyo hua ni mwenye matumaini ya kupona

haraka.

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakukubaliana kuhusiana na

kuangalia kuhusiana na hali ya ubaya wa kitu hali ambayo hua inajulikana kama

Tiyara ambayo hua ni kuangalia kutokana na Ndege anaeruka au Mwanamke

anaepita, n,k. Kwani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua ni mwenye

kupenda kushikamana na matumaini na kuangalia jambo kulingana na mtizamo

wa muonekano mzuri wa jambo husika na wala si kulingana na mtizamo wa

muonekano mbaya wa jambo husika.’

Ambapo anasema Jabir Ibn Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alikua akitufundisha sisi kufanya Istikhara katika kila jambo,

kama vile alivyokua akitufundisha Qur’an kwani alikua akisema: ‘Wakati mmoja

wenu anapokua na nia ya kufanya jambo, basi na asali Rakaa 2 zisizokua za Fardhi

na kisha aseme maneno ya Dua (ifuatayo):


170

الل َّهُم َّ إنيِّ‏ أَسْ‏ تَخِ‏ يرُكَ‏ بِعِلْمِ‏ كَ‏ , وَأَسْتَقْ‏ دِرُكَ‏ بِقُدْ‏ رَتِكَ‏ , وَأَسْ‏ أَلُكَ‏ مِ‏ نْ‏ فَضْ‏ لِكَ‏ الْعَظِيِم

فَإِن َّكَ‏ تَقْدِرُ‏ وَلا أَقْدِرُ,‏ وَتَعْلَمُ‏ وَلا أَعْلَمُ,‏ وَأَنْتَ‏ عَلامُ‏ الْغُيُوبِ‏ , الل َّهُ‏ م َّ إنْ‏ كُ‏ نْ‏ ‏َت

تَعْلَمُ‏ أَن َّ هَذَا الأَمْرَ‏ ‏(هنا تسمي حاجتك)‏ خَيْرٌ‏ ليِ‏ فيِ‏ دِينيِ‏ وَمَعَاشِ‏ ي وَعَاقِبَةِ‏

أَمْرِي أَوْ‏ قَالَ‏ : عَاجِ‏ لِ‏ أَمْرِي وَآجِ‏ لِهِ,‏ فَاقْدُرْهُ‏ ليِ‏ وَيَسِّرْهُ‏ ليِ‏ ثمُ َّ ابَرِكْ‏ ليِ‏ فِيهِ,‏ الل َّهُ‏ َّم

وَإِ‏ نْكُنْ‏ ت تَ‏ َ‏ عْلَمُ‏ أَن َّ هَذَا الأَمْرَ‏ ‏(هنا تسمي حاجتك)‏ شَر ٌّ ليِ‏ فيِ‏ دِينيِ‏ وَمَعَاشِ‏ ي

وَعَاقِبَةِ‏ أَمْرِي أَوْ‏ قَالَ‏ : عَاجِ‏ لِ‏ أَمْرِي وَآجِ‏ لِهِ,‏ فَاصْرِفْهُ‏ عَنيِّ‏ وَاصْرِفْنيِ‏ عَنْهُ‏ وَاقْدُرْ‏ ليِ‏

الخَْيْرَ‏ حَيْثُ‏ كَانَ‏ ثمُ َّ ارْضِنيِ‏ بِهِ‏

‘Ya Allah, hakika mimi natafuta msaada wako kwa kupitia katika Ilm yako,

natafuta msaada wako kupitia katika uwezo wako, natafuta msaada wako kupitia

katika fadhila zako, kwani kwa hakika wewe ni mwenye kujua kile nisichokijua

mimi, ni mwenye kujua yaliyofichikana, Ya Allah kama unajua juu ya jambo hili

(Hapa unataja jambo lako) lina kheri kwangu, kwa dini yangu na mwisho wa khatma

yangu, basi nipe uwezo nalo na unirahisishie juu yake, na tia baraka ndani yake.

Lakini kama unajua kua jambo hili (Hapa unataja jambo lako) halina wema juu

yangu na kwa dini yangu na kwa riziki yangu na mwisho wangu basi niepushe nalo

jambo hili na nipe uwezo juu ya lile lililo bora nami, kutoka kokote kule

litakalokuwepo na nitie ridhaa juu yake.’’

Aya pia imezungumzia kuhusiana na kuruhusika kuliwa vilivyoharamu pale inapokua

kuna ulazima wa kufanya hivyo kwani aliulizwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam:

‘Jee ni wakati gani vile vilivyo haramu vinaweza kua halali?’ Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akajibu: ‘Pale inapokua huna chakula cha Mchana, na ukakosa cha

Jioni, na ikawa huwezi kupata hata mboga za Majani basi unaweza kula.’

Na anasema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakika Allah anapenda

anaporuhusu kitu basi kikubalike kama vile anavyochukia kuasiwa’ (Sahih Ibn

Hibban)

Ambapo ili mtu awe ni mwenye kuruhusika kula kisichoruhusiwa basi inabidi awe katika

mazingira ya hali zifuatazo;


171

1-Mtu huyo lazima awe katika hali isiyokua ni ya kupata msaada na hivyo inambidi

ale kwa sababu hana njia nyengine ya kufanya ya kuokoa maisha yake na ya

wanaomtegemea.

2-Mtu huyo lazima awe hana nia ya kuvunja sharia za Allah Subhanah wa Ta’ala

kutokana na kula kwake huko kwani anfanya hivyo kwa sababu hana njia nyengine.

3-Mtu inapombidi kula chakula ambacho hakiruhusiwi kula basi hatakiwi kula

chakula hicho mpaka akashiba yaani anatakiwa ale kidogo tu kwa ajili ya

kupunguza njaa tu.

Hivyo ingawa Damu imeharamishwa lakini kwa upande mwengine basi tunaona kua sio

Damu yote iliyoharamishwa kwani amesema Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu

kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu A’layi wa Salam kua: ‘Aina mbili za Maiti

zimehalalishwa juu yangu ambazo ni Samaki na Nzige, na aina mbili za Damu

zimehalalishwa juu yangu ambazo ni Ini na Wengu.’(Mishkat Al Anwar)

Hivyo tunapozungumzia kuhusiana na Uhalali wa umwagaji wa damu ya mnyama

anaechinjwa kukubalika kuliwa hua ni kufanya Ibada ya kuonesha Shukran mbele ya

Allah Subhanah wa Ta’ala kwa ajili ya kutujaalia Nyama ya mnyama huyo kua ni

chakula chetu basi tunaona kua Wanazuoni wanakubaliana kua ili mnyama huyo awe

halali kuliwa na Muislam basi inabidi kuwepo na utekelezwaji wa Masharti muhimu

matano yafuatayo:

1-Tasmiyah – yaani kutajwa kwa Jina la Allah Subhnah wa Ta’ala katika wakati wa

kuchinjwa kwa Mnyama huyo.

2-Kumsalia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

3-Kumuelekeza Kibla Mnyama huyo wakati wa Kumchinja.

4-Takbir – yaani kusema Allahu Akbar.

5-Kuomba Dua ya kukubaliwa kwa Ibada hio ya kuchinja.

(Imam Shihab Ad Din Ahmad Ibn Husein Ibn Ahmad Abu Shujaa Al Isfahani katika Ghayat

At-Taqrib Fi Fiqh Al Shafii)

Ambapo ingawa tunapozungumzia kuhusiana na Tasmiyah basi tunaona hii ni kutokana na

uthibitisho wa ile aya isemayo:

‏﴿فَكُلُواْ‏ ممِ َّا ذُكِرَ‏ ٱسْمُ‏ ٱهلل َِّ‏ عَلَيْهِ‏ إِن كُ‏ نتُمْ‏ آبِ‏ َ تِهِ‏ مُؤْ‏ مِ‏ نِينَ‏ ﴾

Fakuloo mimma dhukira ismu Allahi AAalayhi in kuntum bi-ayatihi mu/mineena

(Surat Al Anaam 6:118)


172

Tafsir: Na Kuleni kile ambacho kimetajiwa Jina la Allah juu yake kama kweli nyinyi

ni wenye kuamini aya zetu.

Na pia kutokana na pale aliposema tena Allah Subhnah wa Ta’ala kua:

‏﴿وَلاَ‏ أتَْكُلُواْ‏ ممِ َّا لمَْ‏ يُذْكَرِ‏ ٱسْمُ‏ ٱهلل َِّ‏ عَلَيْهِ‏ وَإِن َّهُ‏ لَفِسْقٌ‏ وَإِن َّ ٱلش َّيَاطِينَ‏ لَيُوحُ‏ ونَ‏ إِلىَۤ‏

أَوْ‏ لِيَآئِهِ‏ مْ‏ لِيُجَ‏ ادِلُوكُ‏ مْ‏ وَ‏ إِنْ‏ أَطَعْتُمُوهُمْ‏ إِ‏ ن َّكُمْ‏ لَمُشْ‏ رِكُونَ‏ ﴾

Wala ta/kuloo mimma lam yudhkari ismu Allahi AAalayhi wa-innahu lafisqun wainna

alshshayateena layoohoona ila awliya-ihim liyujadilookum wa-in

ataAAtumoohum innakum lamushrikoona (6:121)

Tafsir: Na wala msile kile ambacho hakikutajiwa Jina lake juu yake, kwani ni Dhambi

na uasi na kwa hakika Shaytani huwanongo’neza marafiki zake kukugombanisheni

na kama mkiwatii basi mtakua ni washirikina.

Ambapo Wanzuoni wanasema kua asili ya kushushwa kwa aya hizi zenye amrisho hili

basi ni kutokana na kua kuna baadhi ya Wauza Nyama wa Makkah, waliposilimu walikua

wakishukiwa na Waislam kua walipokua wakichinja basi walikua wakitaja majina ya

Miungu yao ya zamani ndani ya Nyoyo zao. Hivyo Waislam wakasita kununua Nyama

katika Maduka yao ya kuuzia Nyama.

Na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akashusha aya iamrishayo kutamkwa kwa jina la

Allah katika kuchinja, na hivyo amrisho hili kua ni sharti litakalowapelekea wenye

Maduka hayo ya Nyama wasiwe ni wenye kutaja jina la Miungu wengine. Na hata kama

Wauza maduka hao wa Nyama au wachinjaji hao wakiwa si Waislam lakini wakataja jina

la Allah Subhanah wa Ta’ala katika kuchinja kwao.

Kwani kwa upande wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, Imam

Mujahid Ibn Sulayman, Ikrimah Mawla Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, Imam

Abd Rahman Al Suddi na wengineo basi wanasema kua aya ya Surat Al Maidah 5:5

imebainisha kua Nyama iliyochinjwa na Mayahudi na Wakristo hua ni halali kwa

Waislam pale iliposema:


173

‏﴿ٱلْيَوْمَ‏ أُحِ‏ ل َّ لَكُمُ‏ ٱلط َّيِّ‏ بَاتُ‏ وَطَعَامُ‏ ٱل َّذِينَ‏ أُوتُواْ‏ ٱلْكِتَابَ‏ حِ‏ ل ٌّ ل َّكُمْ‏ وَطَعَامُكُمْ‏ حِ‏ ل ٌّ

له َُّمْ‏ وَٱلْمُحْصَنَاتُ‏ مِنَ‏ ٱلْمُؤْمِنَاتِ‏ وَٱلْمُحْصَنَاتُ‏ مِنَ‏ ٱل َّذِينَ‏ أُوتُواْ‏ ٱلْكِتَابَ‏ مِن قَبْلِكُمْ‏

إِذَآ آتَيْتُمُوهُن َّ أُجُورَهُن َّ محُْصِنِينَ‏ غَيْرَ‏ مُسَافِحِ‏ ينَ‏ وَلاَ‏ مُت َّخِ‏ ذِ‏ ي ۤ أَ‏ ‏ْخدَانٍ‏ وَمَن يَكْفُْر

بِٱلإِيمَانِ‏ فَقَدْ‏ حَبِطَ‏ عَمَلُهُ‏ وَهُوَ‏ فىِ‏ ٱلآخِ‏ رَةِ‏ مِنَ‏ ٱلخَْاسِ‏ رِينَ‏ ﴾

Alyawma ohilla lakumu alttayyibatu wataAAamu alladheena ootoo alkitaba hillun

lakum wataAAamukum hillun lahum waalmuhsanatu mina almu/minati

waalmuhsanatu mina alladheena ootoo alkitaba min qablikum idha

ataytumoohunna ojoorahunna muhsineena ghayra musafiheena wala

muttakhidhee akhdanin waman yakfur bial-eemani faqad habita AAamaluhu

wahuwa fee al-akhirati mina alkhasireena (Surat Al Maidah 5:5)

Tafsir: Leo mmehalalishiwa kila kilicho kizuri na kisafi, na chakula chao (watu wa)

Ahl al Kitab ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao, kama vile (ilivyokua

halali kwenu) Wanawake wasafi walioamini na Wanawake wasafi wa watu wa Ahl al

Kitab wa kabla yenu, pale mtakapowapa ujira (mahari) wao mkiwa ni wenye kutafuta

usafi na wala si wenye kuendekeza matamanio na wala mkiwa hamkuwachukua kua

ni wapenzi wa siri na atakaeikufuru imani, basi amali zake hua zimepotea na katika

akhera atakua ni miongoni mwa waliokula hasara.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din, Sultan Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi

kuhusiana na aya hii kua: ‘Ili kuifaham aya hii (Surat Al Maidah 5:5) basi inabidi

uangalie aya iliyofuatia kabla ya aya hii (Surat Al Maidah 5:3) ambayo imesemwa

ndani yake:

‏﴿ٱلْيَوْمَ‏ يَئِسَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ مِن دِينِكُمْ‏ فَلاَ‏ تخَْشَوْهُمْ‏ وَٱخْشَوْنِ‏ ٱلْيَوْمَ‏ أَكْمَلْتُ‏ لَكُ‏ مْ‏

دِينَكُمْ‏ وَأَتمَْمْتُ‏ عَلَيْكُمْ‏ نِعْمَتىِ‏ وَرَضِيتُ‏ لَكُمُ‏ ٱلأِسْلاَمَ‏ دِيناً‏ فَمَنِ‏ ٱضْطُر َّ فىِ‏ مخََْمصَةٍ‏

غَيْرَ‏ مُتَجَانِفٍ‏ لإِثمٍْ‏ فَإِن َّ ٱهلل ََّ‏ غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Alyawma ya-isa alladheena kafaroo min deenikum fala takhshawhum waikhshawni

alyawma akmaltu lakum deenakum waatmamtu AAalaykum niAAmatee


174

waradheetu lakumu al-islama deenan famani idhturra fee makhmasatin ghayra

mutajanifin li-ithmin fa-inna Allaha ghafoorun raheemun(Surat Al Maidah 5:3)

Tafsir: Leo hii Wasioamini wote wameishiwa na matumaini juu ya Dini yenu, hivyo

msiwe na khofu nao, bali kuweni na khofu nami. Leo hii nimeikamilisha Dini yenu,

nimekamilisha fadhila zangu juu yenu na nimeuchagua Uislam kua ndio Dini yenu.

Lakini kwa yule ambae atakumbana na Njaa kali (basi anaweza kula hivyo

vilivyokatazwa), bila ya (kua ni mwenye) kuelemea kwenye dhambi, na kwa hakika

Allah ni mwingi wa Kusamehe na ni mwingi wa Rehma.

Hivyo Mujaddid Ad Din, Sultan Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi anamalizia

kwa kusema kua : ‘Ambapo fadhila zilizozungumziwa hapa ni juu ya Dini na kila

kitu kinachohusiana na Dini, na hivyo basi Allah Subhanah wa Ta’ala

anatubainishia kua pia ametukamilishia fadhila za kila kitu tunachokihitaji’

Na kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye anasema

kua: ‘Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu basi yeye alisema kua: ‘Msile vile

ambavyo vilivyochinjwa na Banu Taghrib kwani mimi nnaamini kua wao

hawakuchukua chochote kutokana na Ukristo isipokua Kulewa.’

Na kulingana na mtizamo wa Abu Darda Radhi Allahu Anhu, Ubaidah Ibn Samit Radhi

Allahu Anhu, Imam An Nakhai, Imam Sufyan Ath Thawry, Imam Abu Hanifa, Imam

Malik n.k basi ni kua Nyama iliyochinjwa na watu wa Ahl al Kitab hua ni Haram pale

inapokua hawakutaja jina la Allah Subhanah wa Ta’ala katika wakati wa kuchinja kwao.

Lakini pia kwa upande mwengine basi pia kuna ile hadith isemayo kua: ‘Amesema Aisha

Radhi Allahu Anha kua: ‘Kuna watu walikuja kwa Rasul Allah Salallau A’layhi wa

Salam ambao walisema kua: ‘Ya Rasul Allah (Salallahu Alayhi wa Salam) kuna

watu miongoni mwa Waarabu, ambao walitupa sisi Nyama ambayo hatujui kama

waliitamkia Jina la Allah juu yake ama la.’ Rasul Allah Salallau A’layhi wa Salam

akasema: ‘Itamkieni Jina la Allah Kisha ileni.’’’(Sahih Bukhari na Muslim, Imam Taqiy

ud Din Al Hisni Al Husayni katika Kifayat Al-Akhyar)

Hivyo tunapozungumzia kuhusiana na suali la Tasmiyah katika kuchinja na kumwaga Damu

ya Mnyama kwa njia za Kiislam basi tunaona kua kuna hali tano zifuatazo:

1-Kichinjo cha aliesema Tasmiyyah, ambae Dhabiha yake ni halali wa Makubaliano ya

Ijmaa.

2- Kichinjo cha aliesahau Tasmiyyah ambae Dhabiha yake ni Halali kulingana na Mtizamo

wa Madhhab ya Imam Al Shafii, Hanafi na Madhhab ya Imam Malik.

3-Kichinjo cha yule ambae hakusahau Tasmiyyah lakini kwa hakufanya Makusudi.


175

Ambapo kwa upande wa Madhhab ya Imam Al Shafii, basi anasema Mujaddid al Din Imam

Muhammad Idris Al Safii kua: ‘Wakati Muislam anapomwachia Mbwa wake au Ndege

wake aliefundishwa kuwinda, basi mimi hua nnapendelea (Tasmiyah Mustahab) kua

alitamke jina la Allah Subhanah wa Ta’ala. Lakini hata kama akisahau kulitamka na

kisha Mnyama wake huyo akamuua Mnyama anaewindwa basi anaweza kumla. Na hii

ni kwa sababu hata mtu akisahau kulitaja jina la Allah wakati anapochinja basi hua

anaruhusika kumla Mnyama huyo, kwa sababu Muislam hua ni mwenye kuchinja kwa

ajili ya Allah, hivyo hata akisahau kutaja jina la Allah basi hamna tatizo na hivyo basi

Mnyama alieuliwa na muwindaji Muislam kwa kutumia Mnyama wake hua sawa na

mauaji yanayofanywa kwa kuchinja kwa mkono’(Kitab Al Umm)

Kisha Mujaddid Ad Din Imam Muhammad Idris Al Shafii akamalizia kwa kusema: ‘Kama

ikiwa Muislam amesahau kutaja jina la Allah basi Mnyama wake aliechinja

anaruhusika kuliwa, lakini kama akiwa amewacha kulitaja kwa makusudi basi kichinjo

hicho hua hakifai kuliwa.’

Ambapo kwa upande mwengine basi kutokana na kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alisema katika Hadithi tuliyoiangalia kua ‘Itamkieni Jina la Allah Kisha ileni.’ na Imam

Al Shafii amesema kua Tasmiyyah ni Mustahab basi anasema Imam Abu Hasan Ali Ibn

Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al Shafii: ‘Ash Shafii amesema kua: ‘Wakati

Muislam anapomwachia Mbwa wake aliefundishwa kuwinda, basi mimi hua

nnapendelea (Tasmiyah Mustahab) kua alitamke jina la Allah Subhanah wa Ta’ala.

Lakini hata kama akisahau kulitamka na kisha Mnyama wake huyo akamuua Mnyama

anaewindwa basi hamna tatizo juu yake, na hii ni kwa sababu kutaka jina la Allah kwa

mnyama anaewindwa au anaechinjwa ni Sunna na wala si Wajib, na hivyo kama mtu

akiwa hakulitaja kwa makusudi au kwa kusahau basi Kichinjo chake ni Halali, na huu

ndio mtizamo wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na Abu Hurayra Radhi

Allahu Anhu, na miongoni mwa Wanafiqh wa Mwanzoni wenye Mtizamo huu pia ni

Ataa na Malik’(Al Hawi Al Kabir Fii Madhhab Al Imam Al Shafii)

Ambapo kwa upande wa Shaykh ul Islami Imam Abu Zakarriyah Sharraf An Nawawi basi

anasema kua : ‘Tasmiyyah ni Mustahab katika kuchinja au katika kutumia kifyatulio

katika wakati wa Kuwinda, au katika wakati wa kumtuma Mbwa au kama yeye. Na

kama Tasmiyyah ikiachwa kwa makusudi au kwa kusahauliwa basi Dhabiha inakua

Halali na kama ikiachwa kwa makusudi basi inakua ni Makruh, na huo ndio mtizamo

sahih wa Madhhab ukiwa na hali ya Makruh inayopendekezwa (Tanzih) bila ya kua na

Makruh ya kuharamishwa (Tahrim)’

Na akasema tena Shaykh ul Islami Imam Abu Zakarriyah Sharraf An Nawawi kua: ‘Katika

Madhhab yetu kufanya Tasmiyyah hua ni Sunnah katika kila jambo, hivyo kama

ikisahauliwa au ikiachwa kwa makusudi basi kichinjo hua halali na hakuna kosa juu

yake.’


176

Ambapo kwa upande wa Imam Muhammad Ibn Ahmad Al Khatib Ash Shirbini basi yeye

anasema: ‘Na Tasmiyyah si Wajibu, na mtu kama akiiwacha kwa makusudi au kwa

kusahau basi (Kichinjo) hua ni Halali’(Al Mughni Al Muhtaj)

4 - Kichinjo cha yule ambae hakuitaja Tasmiyyah kutokana na kuona kua haina maana

wala uzito wowote (Istikhaf).

Hapa inabidi tujue kuhusiana na maana ya neno Istikhfaf ambalo maana yake hua ni ile

inayotokana na neno Khaffa ambao hua linamaanisha Kua na Ufaham Mdogo, Kutokua na

Uzito, Kuchukulia Jambo kua ni Jepesi na pia humaanisha Kudharau jambo kwa wepesi wake.

Ambapo neno Istikhfaf hua linaenda sambamba kimaana na neno Istihza ambalo hua

linatokan na neno Hazza ambalo hua linamaanisha Kukichukulia kitu kwa wepesi, Kutokipa

kitu Uzito na Kutokitilia maanani na pia humaanisha Kufanya Mzaha.

Hivyo kwa upande wa Madhhab ya Imam Al Shafii basi neno Istikhfaf na neno Istihza hua

yanatumika sambamba kimaana kumaanisha kukichukulia kitu kwa wepesi, yaani kama vile

ambavyo Shaykh ul Islami Imam Shams Ad Din Al Ramli aliposema kua: ‘Imam An

Nawawi anasema katika Minhaj yake kua: ‘Kuritadi hua kunamaanisha kukata

mawasiliano na Uislam kwa nia, kwa kauli au kwa kitendo cha kukufuru, bila kuangalia

kama mtu alisema kauli ya kukufuru kwa Istahzai, au kutokana na Ukaidi wake tu au

kutokana na kuamini’ yaani kama vile mtu anapoambiwa kua Kata Kucha zako, nae

akajibu kua: ‘Sitokata Kucha hata kama ni Sunnah’’

Hivyo mfano huu hua ni sawa na mchinjaji atakaposema: ‘Sitosema Tasmiyyah japo kua ni

Sunnah’ na hivyo mtu atakaefanya hivyo basi basi atakua ni mwenye kosa la kufanya Istihzai

ambayo pia ni Istikhfaf na hivyo hali yake hua ni sawa na ni mwenye kufanya Kufr kutokana

na kulichukulia jambo hili kwa wepesi na kua ni la mzahaha na lisilokua na uzito wala maana

na hivyo basi kichinjo chake hicho hua si Halali ni Haramu na hakiruhusii kuliwa.

5- Kichinjo cha yule ambae ndie kawaida yake kutoitaja Tasmiyyah (Tahawun)

Neno Tahawun linatokana na neno Tawahin ambalo maana yake hua ni Kinu cha kusagia

Nafaka ambacho kua kinasaga kutokana na Mzunguko wake wa kijirudia rudia, hivyo neno

Tawahun hua maana yake hua ni mtu mwenye kawaida ya kutofanya kitu fulani mara kwa

mara kwa kurudia kutofanya kila wakati.

Hivyo tunapozungumzia Muislam ambae hua ni mwenye kawaida ya Kuchinja bila ya

kufanya Tasmiyyah ambapo hii hukmu yake kwa upande wa Madhab ya Imam Al Shafii

basi hua inaruhusika kula kichinjo chake, kama vile ambavyo ilivyoelezewa katika hali

ya tatu ya kichinjo kulingana na uthibitisho wa hadith ya Mama Aisha Radhi Allahu

Anha.

Huo ni mtizamo wa Madhhab ya Imam Al Shafii kuhusiana na kuchinja ambapo kwa

upande mwengine basi tunaona kua Wanazuoni wa Baraza la Wanazuoni wa Fiqh wa


177

Islamic Fiqh Assembly of the Organization Of Islamic Conference basi wao

wamekubaliana kuhusiana na mtizamo wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi

Allahu Anhu, Imam Mujahid Ibn Sulayman, Ikrimah Mawla Abd Allah Ibn Abbas, Imam

Abd Rahman Al Suddi ambao wasema kua aya ya Surat Al Maidah 5:5 imebainisha kua

Nyama iliyochinjwa na Mayahudi na Wakristo hua ni halali kwa Waislam pale iliposema:

‏﴿ٱلْيَوْمَ‏ أُحِ‏ ل َّ لَكُمُ‏ ٱلط َّيِّبَاتُ‏ وَطَعَامُ‏ ٱل َّذِينَ‏ أُوتُواْ‏ ٱلْكِتَابَ‏ حِ‏ ل ٌّ ل َّكُمْ‏ وَطَعَامُكُمْ‏ حِ‏ ل ٌّ

له َُّمْ‏ وَٱلْمُحْ‏ صَنَاتُ‏ مِنَ‏ ٱلْمُؤْمِنَاتِ‏ وَٱلْمُحْصَنَاتُ‏ مِنَ‏ ٱل َّذِينَ‏ أُوتُواْ‏ ٱلْكِتَابَ‏ مِن قَْبلِكُ‏ ‏ْم

إِذَآ آتَيْتُمُوهُن َّ أُجُورَهُن َّ محُْصِنِينَ‏ غَيْرَ‏ مُسَافِحِ‏ ينَ‏ وَلاَ‏ مُت َّخِ‏ ذِي ۤ أَخْدَانٍ‏ وَمَن يَكْفُرْ‏

بِٱلإِيمَانِ‏ فَقَدْ‏ حَبِطَ‏ عَمَلُهُ‏ وَهُوَ‏ فىِ‏ ٱلآخِ‏ رَةِ‏ مِ‏ نَ‏ ٱلخَْاسِ‏ رِينَ‏ ﴾

Alyawma ohilla lakumu alttayyibatu wataAAamu alladheena ootoo alkitaba hillun

lakum wataAAamukum hillun lahum waalmuhsanatu mina almu/minati

waalmuhsanatu mina alladheena ootoo alkitaba min qablikum idha

ataytumoohunna ojoorahunna muhsineena ghayra musafiheena wala

muttakhidhee akhdanin waman yakfur bial-eemani faqad habita AAamaluhu

wahuwa fee al-akhirati mina alkhasireena (Surat Al Maidah 5:5)

Tafsir: Leo mmehalalishiwa kila kilicho kizuri na kisafi, na chakula chao (watu wa)

Ahl al Kitab ni halali kwenu na chakula chenu ni halali kwao, kama vile (ilivyokua

halali kwenu) Wanawake wasafi walioamini na Wanawake wasafi wa watu wa Ahl al

Kitab wa kabla yenu, pale mtakapowapa ujira (mahari) wao mkiwa ni wenye kutafuta

usafi na wala si wenye kuendekeza matamanio na wala mkiwa hamkuwachukua kua

ni wapenzi wa siri na atakaeikufuru imani, basi amali zake hua zimepotea na katika

akhera atakua ni miongoni mwa waliokula hasara.

Na pia kulingana na hadith tuliyoiangalia isemayo kua: ‘Amesema Aisha Radhi Allahu

Anha kua: ‘Kuna watu walikuja kwa Rasul Allah Salallau A’layhi wa Salam ambao

walisema kua: ‘Ya Rasul Allah (Salallahu Alayhi wa Salam) kuna watu miongoni

mwa Waarabu, ambao walitupa sisi Nyama ambayo hatujui kama waliitamkia Jina

la Allah juu yake ama la.’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema:

‘Itamkieni Jina la Allah Kisha ileni.’’’(Sahih Bukhari na Muslim.)(Imam Taqiy-ud-Din

Al-Hisni Al-Husayni katika Kifayat Al-Akhyar)

Hivyo basi Wanazuoni hao wa Baraza la Wanafiqh la Islamic Fiqh Assembly of the

Organization Of Islamic Conference wamesema katika kikao chao cha 95 (Resolution no


178

95) kua: ‘Inaruhusika Kwa Mgeni wa Kiislam au Muislam anaeishi kwenye Nchi

isiyokua ya Kiislam kula Nyama za Wanyama waliochinjwa na Watu wa Ahl Al

Kitab pale inapokua Wanyama hao ni Halali kuliwa. Hivyo Waislam wanatakiwa

kuhakikisha kua Nyama hio haijachanganyika na vitu ambavyo ni

vilivyoharamishwa katika Uislam, na kuchinjwa kwenyewe pia kuwe kumefanyika

kwa njia za Kiislam’

Hii ni pale inapokua kuna uwezo wa kufuatilia kuhusiana na uchinjaji, lakini inapokua ni

vigumu kuhusiana na kujua kwake basi hali ya uchinjaji hua inachukuliwa kua ni yenye

utata juu yake, kwani haijulikani kua ulikua wa kihalali ama la. Na kutokana na kutokua

na uhakika huo basi, inabidi ihesabiwe kua ulikua ni wa Kihalali…Wallahu Aaalam!

Hio ni kuhusiana na Damu ya Ibn Adam na Damu ya Wanyama wa chakula, hivyo na

tuangalie kuhusiana na Damu ya kimaumble ya Mwanamke ambayo ndio sababu ya

Imraat Imran yaani Hannah Bint Faqudh kua ni wenye kusema kama ilivyosema aya:

‏﴿إِذْ‏ قَالَتِ‏ ٱمْرَأَةُ‏ عِمْرَانَ‏ رَبِّ‏ إِنىّ‏ ِ نَذَرْتُ‏ لَكَ‏ مَا فىِ‏ بَطْنىِ‏ محَُر َّراً‏ فَتَقَب َّلْ‏ مِنىِّ‏ إِ‏ ن َّكَ‏

أَنتَ‏ ٱلس َّمِيعُ‏ ٱلْعَلِيمُ‏ ﴾

Idh qalati imraatu AAimrana rabbi innee nadhartu laka ma fee batnee muharraran

fataqabbal minnee innaka anta alssameeAAu alAAaleemu (Surat Al Imran 3:35)

Tafsir: Na kumbuka aliposema Mke wa Imran: ‘Ewe Mola Wangu, hakika mimi

nimeweka Nadhiri kua Mtoto wangu aliemo tumboni mwangu nimemtolea kwa ajili

ya kukutumikia wewe, hivyo nikubalie kwani kwa hakika wewe ni mwingi wa kusikia

na ni mwingi wa kujua juu ya kila kitu.’

Tunapoiangalia aya yetu hii basi tunaona kua Imraat Imran amedhamiria kumfanya

mtoto wake awe Muharraran. Ambapo neno Muharraran ni neno linalotokana na neno

Harra ambalo hua linamaanisha Kua Huru, Mtu alie huru, Mtu ambae yuko huru

kutokana na Utumwa na hivyo hua ni mwenye kumtumika Allah Subhanah wa Taa’ala

tu. Hivyo neno Muharrarah linamaanisha kua Mtu alie huru kutokana na mambo ya

kidunia kwani ni mtu aliejitolea kwa Ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala peke yake.

Kwa maana hio basi mtoto aliekua akimtaka Imraat Al Imran alikua anatakiwa asiwe ni

mtoto mwenye kua na Adha.


179

ADHA YA DAMU YA KIMAUMBILE YA MWANAMKE.

Anasema Imam Ahmad Ibn Hanbal kua: ‘Amesema Anas Ibn Malik Radhi Allahu

Anhu kua: Mayahudi walikua wakijitenga na Wanawake zao katika kipindi cha

wakati wa siku zao za Mwezi, kiasi ya kua walikua wakikata hataa kukaka nao

pamoja kwenye Meza zao katika wakati wa kula, hivyo Maansari nao wakaathirika

na jambo hilo na wao pia wakaanza kufanya hivyo hivyo kwa wake zao. Hivyo Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaulizwa kuhusiana na jambo hilo na hivyo Allah

Subhana wa Ta’la akamshushia Rasul Allah Salallah Alayhi wa Salam aya hii

ambayo inasema:

‏﴿وَيَسْأَلُونَكَ‏ عَنِ‏ ٱلْمَحِ‏ يضِ‏ قُلْ‏ هُوَ‏ أَذًى فَٱعْتَزِلُواْ‏ ٱلنِّسَآءَ‏ فىِ‏ ٱلْمَحِ‏ يضِ‏ وَلاَ‏

تَقْرَبُوهُن َّ حَتى َّ ٰ يَطْهُرْنَ‏ فَإِذَا تَطَه َّرْنَ‏ فَأْتُوهُن َّ مِنْ‏ حَيْثُ‏ أََمرَكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ يحُِ‏ ُّب

ٱلت َّو َّابِينَ‏ وَيحُِب ُّ ٱلْمُتَطَهِّرِينَ‏ ﴾

Wayas-aloonaka AAani almaheedhi qul huwa adhan faiAAtaziloo alnnisaa fee

almaheedhi wala taqraboohunna hatta yat-hurna fa-idha tatahharna fa/toohunna

min haythu amarakumu Allahu inna Allaha yuhibbu alttawwabeena wayuhibbu

almutatahhireena (Surat Al Baqara 2:222)

Tafsir: ‘Na wanakuuliza kuhusiana na Hedhi waambie kua: ‘Ni Adha, hivyo kaeni

mbali na Wanawake wanapokua katika Hedhi na msiwakaribie mpaka wawe tohara.

Na kisha watakapojitoharisha basi waingilieni katika sehemu aliyokuamrisheni Allah,

kwani kwa hakika Allah anawapenda wenye kufanya toba na wenye kujitoharisha.’’

Hii ni miongoni mwa aya 2 ambazo zimetumia neno Mahiidh ambalo ni lenye kutokana

na neno Hadhat ambalo hua linamaanisha Kua katika Njia yake, Kua katika Siku zake,

Kua katika Hedhi, Kutoka Damu kwenye Fuko la Uzazi, hivyo neno Mahiidh hua

linamanisha Wakati wa Kutoka Damu, Sehemu ya Kutoka Damu.

Ambapo Shaykh Al Akbar Imam Muhyi Ad Din Abu Bakar Ibn Arabi amesema kua:

‘Kuna aina nane za majina ya Mwanamke mwenye Hedhi ambayo ni Haidh, Aarik,

Farik, Tamis, Daris, Kabir, Dhahik na Tamith.’


180

Na pia ikatumia neno Adha ambalo hua linamaanisha Kuudhi, Kuumiza, Kuharibika,

Kunyanyasika, Kudhuru, Kusababisha Maumivu ya Mwili na pia humaanisha

Kusababisha maumivu ya Kihisia.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia neno Adha katika aya hii kwa sababu kama

linavyoonesha maana yake neno hilo katika mitizamo tofauti basi ndio hali anayokua

nayo Mwanamke wakati akiwa kwenye Hedhi na hii ni kwa sababu kama tulivyosema

hapo kabla kuhusiana na Moyo wa Ibn Adam kua ni wenye kusababisha uzalishwaji wa

kemikali mbali mbali ikiwemo zile ambazo husababisha hisia nzuri kwa Ibn Adam

ambazo zinazojulikana kama Dopamine, Oxytocin, Endorphines, Seratonin,n.k ambazo

hua na jukumu la kukamilisha sifa ya maumbile ya asili ya kila mtu yanayotokana na

maana ya neno Al Ins. Neno Al Ins linatokana na neno Anisa ambalo maana yake hua ni

kua na Mazoea, Kupenda, Kua na Umoja kijamii, au Kushikamana pamoja.

Hivyo kila Kemikali hizi zikizalishwa kwa wingi basi Mwili wa Ibn Adam husika hua na

hisia za kujisikia vizuri zaidi, raha zaidi, kua na furaha zaidi na pia kutaka kua karibu na

Ibn Adam wenzake zaidi. Na kila zikipungua ndani ya mwili basi hali ya Ibn Adam

husika hua na hali ya kinyume chake, yaani mtu hua ni mwenye kutaka kua peke yake,

hua mnyonge, mwenye huzuni, mwenye kukerea kirahisi, asiekua na furaha n.k.

Na tunapozungumzia wakati wa Mahiidh kama ilivyotajwa kwenye aya yaani katika

kipindi hiki cha wakati wa Hedhi basi Maumbile ya mwili wa Mwanamke hua ni yenye

kupunguza uzalishwaji wa kemikali za Estrogen. Progesteron na Serotonin na hivyo

kemikali hizi zinapokua zimepungua ndani ya mzunguko wa Damu basi mwili wa

Mwanamke husika hua na mabadiliko ya kihisia yanayosababishwa hisia maumivu ya

kuumwa na Kichwa, Mgongo, Tumbo, Kutopata Usingizi vizuri, Maumivu ya Maziwa

kutokana na kua ni yenye kuvimba, n.k hali ambayo humpelekea mwanamke husika kua

ni mwenye kukosa raha na utulivu wa kihisia na kimwili.

Katika aya hii basi Allah Subhnah wa Ta’ala anatubainishia kwa kusema Huwa adhan

yaani ‘Ni Adha’ Na hivyo moja kwa moja kutuonesha kua anatutahadharisha kua Hiki

ni kitu ambacho kina madhara ndani yake na hivyo kua ni mwenye kututayarisha na

amrisho litakalofutia baada ya tahadhari hio ambalo linasema faiAAtaziloo alnnisaa fee

almaheedhi wala taqraboohunna hatta yat-hurna yaani ‘Hivyo kaeni mbali na

Wanawake wanapokua katika Hedhi na msiwakaribie kwa kuwaingilia mpaka wawe

tohara.’

Na katika amrisho hili basi tunaona kua ndani yake mna katazo lenye neno La Taqrabu

ambalo ni lenye kutokana na neno Qaraba ambalo hua linamaanisha Kukaribia, Kufikia

Karibu, Kua na Ukaribu katika Uhusiano au Katika Mahusiano iwe ya Udugu, ya Urafiki

au ya Kimapenzi.


181

Ambapo neno Qaraba ndio lililotoa neno Qurban ambalo humaanisha Mnyama

anaemwagwa Damu yake kwa kuchinjwa kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala kwa

ajili ya Kuutafuta Ukaribu wa Allah Subhanah wa Ta’ala.

Hivyo basi katazo ili halimaanishhi kua Waislam Wanaume wanatakiwa Kujitenga na

kukaa mbali na Wake zao, au Waislam wanawake wanataiwa wakae mbali na Waume

zao, kwani maana ya La Taqrab inayotumika hapa ni ile yenye maana ya kua

‘Msiwakaribie Kiuhuisano wa Kimapenzi wa Kuingiliana Kimwili’

Na ndio maana baada ya kushushwa aya hii basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akasema: ‘Kila kitu kinaruhusika isipokua kuwaingilia tu.’ Hivyo Mayahudi

waliposikia kuhusiana na aya hii basi wakasema: ‘Hakika hii ni tofauti na kila kitu

kuhusiana na vile tunavyofanya sisi’

Baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kusema hivyo basi Usayd Ibn Hudayr

Radhi Allahu Anhu na Abbad Ibn Bishr Radhi Allahu Anhu basi wakamuuliza Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kwa kusema kua: ‘Kama ikiwa Mayahudi wamesema hivyo

(kua wanajitenga na wake zao wanapokua katika siku zao na hawakai nao hata katika

chumba kimoja), hivi kwanini na sisi tusiruhusiwe kuwaingilia Wanawake wetu ili

kuwachochea zaidi na kuwatia wazimu zaidi? (Kua sisi tuko tofauti na nao)’

Waliposema maneno hayo basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikasirika sana

kiasi ya kua walidhani kua huenda akaamua kuwaadhibu. Hivyo hapo hapo wakatoka nje

na kisha wakarudi kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kumletea zawadi ya

Maziwa ili kumpunguzia hasira zake, na kisha wakaondoka tena. Na walipoondoka basi

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akatuma watu wakawaite Usayd na Abbad Radhi

Allahu Anhum na kisha akakaa na kunywa nao Maziwa hayo ili wasidhani kua

amewakasirikia.

Ambapo tunaporudi katika katazo hili basi pia tunaona kua limewataka Wanaume

kutokua na uhusiano wa kimpenzi na Wake zao wanaokua katika Hedhi kwa sababu ya

Madhara yake lakini halikusema ni nani anaedhurika na hivyo halimaanishi kua ni

Wanaume tu ndio wanaodhurika na Mahiidh au ni Wanawake tu, bali hii inamaanisha

kua Madhara haya yanawadhuru wote pale watakapokaribiana kwa kuingiliana kimwili

katika wakati huo.

Na ili tufahamiane vizuri basi bora na tuangalie kile kinachotokea katika mwili wa

Mwanamke katika wakati huo, ambae kimaumbile hua na Mifuko ya Mayai ya uzazi

inayojumuisha sehemu ya juu ya viungo vya Uzazi vya Mwanamke. Mifuko hii ya mayai

ya Uzazi ambayo iko miwili hua imeunganishwa kwa mrija au njia zilizo juu ya Mfuko

wa Uzazi, kwa kulia kwake na kwa kushoto kwake hua ni yenye kutoa Yai kila mwezi

mara moja ambako kunasababishwa na Kemikali zinazozalishwa na sehemu ya Ubongo


182

inayosimamia mfumo wa Uthibiti wa Kemikali mbali mbali za Mwilini ambao unaitwa

Pituitary Gland ambazo huzitaarifu Kemikali zilizopo juu ya Mifuko ya Mayai ziitwazo

Estrogen na Progesteron ambazo huzalishwa zaidi katika kipindi kwa Yai la Uzazi kwa

ajili ya kufanya mandalizi ya kuachia yai la Uzazi kuanzia siku 13-15 baada ya mzunguko

wa Hedhi iliyotangulia hapo kabla.

Hivyo Yai hilo linapoachiwa hua linaanza safari yake kupitia kwenye mirija ya Usafiri

wa Yai la Uzazi kuelekea kwenye Mfuko wa Uzazi kwa ajili ya matayarisho ya kuandaa

mazingira ya kulea mtoto, kwani kama yai hilo likikutana na yai la Uzazi la Mwanamme

basi Mfuko wa Uzazi hulipokea na kuligandanisha na Ukuta mpya maalum wa Mfuko

wa Uzazi wa Mwanamke ambao nao pia hua umeandaliwa baada ya kuongezeka

uzalishwaji wa kemikali za Estrogen ambazo hujenga Ukuta mpya huo na Progesteron

ambazo huuimrisha Ukuta kwa ajili ya matayarisho ya kumlea na kumkuza mtoto ndani

ya mfuko wa Uzazi.

Hivyo katika wakati huu ukuta huo wa Mfuko wa Uzazi wa Mwanamke hua na maumbile

ya kua na ukuta kama ukungu laini wa Damu iliyotolewa na mishipa ya Damu ya ukuta

wa Fuko la Uzazi ambayo ni nyepesi na isiyoweza kuganda ambayo kwa kawaida wingi

wake hua hauzidi vijiko vitatu, na hua na idadi ndogo ya kemikali za Protein, Chuma,

Prothromin, Thrombin na Fibrinogen, na hivyo hua tofauti na damu ya kawaida kwani

hii Damu hua ni maalum kwa ajili ya kusimamia jukumu la kulikuza yai la uzazi la

Mwanamke lililokutanishwa na yai la Mwanamme kwa ajili ya kupatikana mtoto.

Ambapo ili yai la Uzazi la Mwanamme likutane na yai la Uzazi la Uzazi la Mwanamke

wakati linapomwagwa ndani ya sehemu za Uzazi za Mwanamke basi inabidi Mayai ya

Mwanamme husika yawe na wingi usiopungua mayai milioni 15 hadi milioni 250 kwa

mililita moja ya kila mmwagiko mmoja wa Manii na hua na kasi ya kuogelea isiyopungua

micrometer 25 kwa sekunde moja.

Na hii ni kwa sababu ndani ya Mfumo wa njia ya Uzazi ya Mwanamke hua kuna kemikali

zenye acid ambazo kazi yake ni kusimamia ulinzi na uimarishaji wa mfumo huo wa

Mwanamke ili Viungo vya Uzazi vya Mwanamke visidhurike. Hivyo Mwanamme

anapomwaga mayai yake, basi hali hua kama majeshi ya upande wa Mwanamme na

upande wa Upande wa Mwanammke yamekutana na kukabiliana kwa mapigano

uwanjani, yaani Mayai ya Mwanamme yanatakiwa kulikimbilia Yai moja la

Mwanammke lililotolewa kwenye mfuko wa Mayai ambalo linakimbilia kuja kwenye

Mfuko wa Uzazi.

Hivyo katika mapigano hayo, kemikali za acid za ulinzi wa sehemu ya Uzazi wa

Mwanamke ambazo kimaumbile hua na mtizamo wa kua kila kitu kinaingia kutoka nje

ya mwili wake hua kina madhara na hivyo hakitakiwi kifike kwenye Mfuko wa Uzazi wa

Mwanamke na inabidi kizuiwe kisisababishe madhara, basi hua zinapingana na Mayai ya


183

Uzazi wa Mwanamme ambayo mbali ya wingi wake lakini linatakiwa yai litakalowahi

mwanzo tu kuingia kwenye yai la Uzazi la Mwanamke. Hivyo mamilioni kati ya

mamilioni hayo ya mayai ya Mwanamme hua ni yenye kubakia njiani kutokana na

kutofanikiwa kwake, kwani ni mwenye nguvu tu na afya ndie atakaeufikia Mfuko wa

Uzazi wa Mwanamke na ndie atakaelifikia yai la Uzazi la Mwanamke.

Na akilifikia tu basi kwa usalama wake hua ni mwenye kuingiza kichwa chake ndani,

kisha mkia wake hukatika na yai hilo la kike hutengeneza ukuta ili lisiingie ndani yake

yai jengine la Uzazi la Mwanamme, na kama yakiwahi kuingia mawili kwa pamoja basi

yai hilo la uzazi la Mwanamke hua ni lenye kubeba watoto pacha, n.k. Na kama mayai

ya Mwanamme yakiwa kidogo yaani tunazungumzia chini ya milioni 15 kwa kila

umwagaji mmoja au hayana nguvu na kasi basi hua inamaanisha kua Mwanamme husika

hana uwezo wa kupata mtoto.

Tunapoangalia matukio haya ya maumbile ya mfumo wa Uzazi wa Mwanamme na

Mwanamke na purukushani zinazotokea ndani ya Miili yao wakati wa kutafuta Mtoto

basi ndio tunaona maana halisi ya maneno ya ile aya isemayo:

‏﴿لَقَدْ‏ خَلَقْنَا ٱلإِنسَانَ‏ فىِ‏ كَبَدٍ‏ ﴾

Laqad khalaqna al-insana fee kabadin (Surat Al Balad 90:4)

Tafsir: Kwa Hakika Tumemuumba Mtu katika Kabad

Ambapo ingawa kwa upande wa Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu, Abd Allah

Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, Imam Mujahid Ibn Sulayman na Ikrimah Mawla Abd

Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi tunaona kua wao wanasema: ‘Neno Kabad

linamaanisha Kusimama sawia, yaani tofuti na wanyama wengine wasioweza

kusimama sawia.’

Lakini pia neno Kabad hua linamaanisha Kujeruhi kwenye Ini, Kumuumiza Mtu mpaka

akasikia Maumivu makali sana, Kukusudia Kitu, Kukumbana na Matatizo, Mapigano,

Purukushani, Kukutana na Kikwazo au Kizingiti, Kua katikati ya mapigano n.k.

Na hivyo basi kwa mtizamo huo hua unaamaanisha kua Mtu ameumbwa akiwa katika

hali ya mapigano tangu katika kutafutwa kwake Mtoto mpaka kupatikana kwake, kukaa

ndani ya fuko la uzazi la mama yake, kutoka ndani ya tumbo la mama yake, kulelewa

kwake mpaka kukua kwake, mpaka kufa kwake hua yuko katika hali ya kupiga hatua

moja hadi nyengine kutoka katika mapigano mbali mbali maishani mwake ikiwemo

mapigano ya kujidhibiti na matamanio ya Nafsi yake.


184

Hivyo Damu ya Hedhi hua ni yenye kumtoka Mwanamke pale inapokua Mfuko wake wa

Mayai ya Uzazi umeachia Yai la kila mwezi ambalo halikuweza kukutana na Yai la Uzazi

la Mwanamme na hivyo Yai hilo hua haliwezi kugandanishwa na Ukuta wa Mfuko wa

Uzazi na hivyo Ukuta wake huo laini wa Ukungu wa Damu uliotayarishwa kwa ajili ya

kulihudumia Yai la Uzazi, Na hivyo mfumo wa Yai la Uzazi huanza kupunguza uzalishaji

wa Kemikali Estrogen za kuukuza Ukuta huo na kupunguza uzalishaji wa kemikali za

Progesterone za kuuimarisha ukuta huo kunakopelekea kubana na kukaza kwa Mishipa

midogo midogo ya Damu ya Ukuta wa Uzazi ambako nako kunakosababisha maumivu

ya tumbo na kushuka kwa joto la Mwili wa Mwanamke husika na kupungua kwa kasi ya

mapigo ya Moyo na kasi ya mzunguko wa Damu.

Na kutokana na matukio haya ya kimwili yanayojumuisha kupunguzwa kwa uzalishaji

wa kemikali zinazouimarisha ukuta huo wa Damu basi ukuta huo hukosa uimara wake

na kidogo kidogo ukuta huo huanza kuporomoka, na kuweka wazi kua hakuna ujauzito,

hivyo na hivyo Ukuta wa Damu na Yai na Maji maji mengine yaliyoandaliwa kwa ajili

ya kuulinda Ujauzito, na hivyo kua vitu vyote hivyo vilivyoandaliwa kwa ajili ya uja

uzito hua havihitajiki tena Mwilini na hivyo inabidi vitoke nje.

Hivyo Damu zilizojumuisha ukuta huo unaoporomoka pamoja na sehemu ya Yai la Uzazi

la Mwanamke ambalo halikufanikiwa kutungwa na Yai la kiume kwa wakati huo huanza

kutoka nje ya Mwili na kujulikana kama Damu ya Hedhi.

Hivyo hii hua ni sehemu ya kimaumbile ya namna Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke

unavyojitayarisha kwa ajili ya kuendeleza kizazi, na inapokua hakuna mafanikio hayo

basi Mfumo huo hua ni wenye kujisafisha wenyewe kimaumbile, kwa ajili ya

matayarisho ya kutoa yai jengine la Uzazi katika mwezi unaofuatia na kutayarisha ukuta

mwengine mpya kwa ajili ya kulea yai hilo jipya la Uzazi la Mwanamke husika kama

litakutana na yai la Uzazi la Mwanamme.

Subhnah Allah w Allahu Akbar! Ukiyaangalia haya na kuyatafakar basi ndio unaona

maana ya ile aya isemayo:

‏﴿لَقَدْ‏ خَلَقْنَا ٱلإِنسَانَ‏ فيِ‏ ۤ أَحْسَنِ‏ تَقْوِيمٍ‏ ﴾

Laqad khalaqna al-insana fee ahsani taqweemin (Surat At Tin 95:5)

Tafsir: Kwa hakika tumemuumba mtu katika Taqwiim bora kabisa.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala amesema kua ‘Huwa Adhan aiAAtaziloo alnnisaa fee

almaheedhi wala taqraboohunna hatta yat-hurna yaani ‘Hio ni Adha Hivyo kaeni


185

mbali na Wanawake wanapokua katika Hedhi na msiwakaribie kwa kuwaingilia

mpaka wawe tohara.’

Kwa sababu ya kua hali iko wazi kama tulivyoelezea kua mabadiliko haya ya kimaumbile

hua yanasababisha kukosekana kwa utulivu wa kihisia na utulivu wa kimwili kwa

Mwanamke na kwa baadhi ya Wanawake hua wanapungukiwa na Nguvu pia, na ndio

maana Allah Subhnah wa Ta’ala akawaamrisha kua wasifunge wala wasisali wanapokua

katika Hedhi.

Hivyo tunapoangalia kuhusiana na kukaribiana kimapenzi baina ya Mume na Mke katika

hali ya kawaida bila ya kugusia suali la wakati wa Hedhi basi bila ya shaka ili Mume na

Mke waridhishane kimapenzi basi kwanza lazima kuwe na utulivu baina yao, na

inapotokea kua mmoja wao kua hana utulivu, au hajapata utulivu katika wakati wa

kujitayarisha na tendo la kuingiliana, basi hua ni kinyume na maamrisho ya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam.

KUKARIBIANA KIMAPENZI BAINA YA MKE NA MUME KATIKA

UISLAM

Amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua

‏﴿هُن َّ لِبَاسٌ‏ ل َّكُمْ‏ وَأَنتُمْ‏ لِبَاسٌ‏ له َُّن َّ﴾‏

Hunna libasun lakum waantum libasun lahunna (Surat Al Baqara 2:187)

Tafsir : Wao (Wake zenu) ni Lîbas kwenu na nyie (Waume zao) ni Lîbas kwao.

Neno Lîbas kwa kiarabu lina maana ya Stara, Hifadhi, Nguo au Vazi, na kama

inavyojulikana kazi ya vazi kua ni kuvaliwa ili kuulinda na kuuhifadhi mwili wa Bani

Adam na athari za nje kama vile jua, baridi, mvua n.k, kusitiri sehemu za siri ambazo ni

aibu kuzionesha, kuupendezesha mwili n,k basi ndio vile vile, wanavyositiriana na

kuheshimiana na kulindana Mume na Mke kutokana na matamanio ya nje yaliyokatazwa.

Na hivyo hali ya Libasi inatakiwa kua ndio iwe hali inayowapelekea Mume na Mke kua

ni wenye kusaidiana katika kupendezeshana na kuridhishana pale wanapokua pamoja na

katika kutaka kutimiza matamanio ya kukaribiana kimapenzi baina yao katika njia

inayoruhusika kisharia ambayo ni bila ya kuudhiana, kudhuriana wala kukirihishana,


186

kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kila mchezo anaocheza

Mtu hua hauna maana isipokua Kutunga Shabaha kwa upinde, Kumfundisha

Farasi na Kucheza na Mke wake’(Imam Ibn Majah)

Na amesema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua: ‘Mtu hatakiwi atimize haja yake (ya kumuingilia mke wake)

kutoka kwa mke wake kama (anavyofanya) Mnyama bali baina yao kuwe na

kuchezeana kwa mabusu na maneno’’(Imam Al Daylami)

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ameusia hivi kwa sababu inakua ni

Adha na Maumivu kwa viungo vya siri vya Mwanamke kukaribiwa na kuingiliwa bila

ya kutayarishwa kwa sababu Allah Subhanah wa Ta’ala katika kukamilisha Uzuri wa

mwili wa Mwanamke basi amemjaalia Mwanamke kemikali maalum ziitwazo Bartholin

Glands ambazo hua na kazi ya kuzirowanisha sehemu za Siri za Mwanamke kwani

Mwanamke anapotayarishwa basi mwili wake huanza kuzalisha Madini ya Nitric Oxide

ambayo hua na kazi ya kuongeza Mzunguko wa damu katika sehemu mbali mbali za

mwili ikiwemo katika sehemu za siri za Mwanamke.

Na hivyo muongezeko huo wa Nitric Oxide hua ni wenye kuzifanya sehemu hizo kua ni

zenye kuzisababishia Bartholin Glands kuzirowanisha sehemu hizo huku ukuta wa ndani

wa sehemu hizo ukiwa ni wenye kuongezeka ukubwa wake kwa kuelekea ndani ya Mwili

wake, na kukisukuma kizazi ndani zaidi ya mwili ili kutosheleza eneo la kupokea na

kuzivaa Sehemu za Siri za Mwanamme, na hapo hapo kutosababisha adha, maumivu na

madhara kwa Mfuko wa Uzazi wa Mwanamke.

Na hivyo inapotokea hali hio Mwanamke hua na hisia ya kuhisi kile kinachotokea ndani

ya Mwili wake katika sehemu ya ndani ya sehemu ya Siri kwani hua kama na hali kama

ya kuhisi kua ndani yae ana kama ukuta wa pango au uwazi fulani ambao hua inabidi

ujazwe kitu au kuzibwa na hivyo Mwanamke hua na hamu ya kutotaka kitu chochote

isipokua ya kutaka Nikah yaani kuzivaa sehemu za siri za Mwanamme na hapo basi ndio

hua inaruhusika kumuingilia na hivyo kupatikana kwa hisia za raha na starehe ambayo

haiwezekani kupatikana kama ikiwa kuna Adha na Maumivu hivyo ili kusiwe na adha na

maumivu kwa Mwanamke basi ni lazima kwanza atayarishwe.

Ambapo Imam Muhamad Ibn Muhammad Murtada Al Zabidi katika Ufafanuzi wa Ihya

Ulum Ad Din ya Hujjat Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammd Ibn

Muhammad Al Ghazali katika mlango wa ndoa ambapo amesema kua ‘Kuingiliana

Kimapenzi baina ya Mume na Mke kunatakiwa kuanze na maneno laini laini na

Kubusiana’ basi Imam Al Zabidi anasema kua: ‘Kubusu haimaanishi kua Mume

ayabusu Mashavu na Midomo tu bali pia anatakiwa ayapapase Maziwa na Chuchu


187

na kila sehemu ya mwili wa Mke wake’(Idhaf Al Sada Al Muttaqin Bi Sharah Ihya

'Ulum al-Din )

Na ndio maana akasema Allama Muhammad Abd Rauf Al Munawi kua : ‘Kupapasana,

kuchezeana na Kubusiana kwa mapenzi kabla ya kuingiliana (Baina ya Mume na

Mke) ni Sunnah Muakkadah, na ni Makruh kufanya vyenginevyo’(Faidh al-Qadir)

Hivyo bila ya kuwepo kwa matayarisho basi aidha haitowezekana kutokea kwa tendo

hilo au itawezekana lakini hakutokua na utekelezwaji wa haki na usawa baina ya watu

wawili hao katika tendo hilo, kwani mmoja hua amemvunjia haki yake mwenziwe na

hivyo hii hua ni sawa na ubakaji yaani Nikah bil Ikrah yaani Kuingilia kwa Chuki.

Ambapo neno Nikah basi ndio lile lilitumika katika ile aya isemayo:

‏﴿ٱلز َّانىِ‏ لاَ‏ يَنكِحُ‏ إِلا َّ زَانِيَةً‏ أَوْ‏ مُشْرِكَةً‏ وَٱلز َّانِيَةُ‏ لاَ‏ يَنكِحُهَآ إِلا َّ زَانٍ‏ أَوْ‏ مُشْرِكٌ‏

وَحُرِّمَ‏ ذٰلِكَ‏ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ ﴾

Alzzanee la yankihu illa zaniyatan aw mushrikatan waalzzaniyatu la yankihuha illa

zanin aw mushrikun wahurrima dhalika AAala almu/mineena(Surat Nur 24:3)

Tafsir: Mzinifu wa Kiume hamuingilii isispokua Mzinifu wa Kike au Mshirikini wa

Kike na Mzinifu wa Kike Haingiliwi ila na Mzinifu wa Kiume au Mshirkina wa Kiume

na hili limeharamishwa kwa Waumini.

Ambapo ayah hii imetumie aneno Nikah ambalo hua linamanisha Kufunga Kitu kwa

Kamba, kwa Kufuli au kwa Kukiziba kwa Kuingiza kitu chengine kwenye uwazi wake,

Kuunganisha, na pia hua linamaanisha Kuoa.

Hivyo wengi hua wanaitafsiri ayah hii kua Mzinifu wa Kiume hua kamwe hamuoi

isipokua Mzinifu wa Kike au Mshirikina na Mzinifu wa Kike Haolewi isipokua na

Mzinifu mwenzake wa Kiume au Mshirikina, na hili limeharamishwa kwa Waumini,

hivyo kwa upande mmoja hii hua si Tafsir sahih kwa sababu kuna Wanaume ambao

walikua wazinifu na baadae wakaoa Wanawake ambao ni wasafi, na pia kuna Wanawake

ambao walikua wazinifu baadae wakatulia kutokana na Kuolewa na Wasiokua wazinifu

waliowapenda, na kama tunavyojua kua Qur’an haisemi uongo, hivyo kama tukiitafsiri

kua watu hawa hawaoani isipokua wenyewe kwa wenyewe basi itakua inamanisha kua

hata huyu mwanamke Msafi alieolewa na Mtu aliekua Mzinifu hapo kabla basi nae

huenda akawa ni Mzinifu au na huyu Mwanamme pia baadae akawa Mzinifu. Jambo

ambalo si sahih.


188

Hivyo mbali ya kua Nikah ni neno linalotumika kumaanisha Kuoa, lakini pia hua

linamanisha Kuingilia na ndio maana Ubakaji au Kumuingilia Mwanamke kwa Nguvu

hua kunaitwa Nikah bil Ikrah yaani ni Kuingilia kwa kukirihisha au kwa chuki yaani bila

ya ridhaa ambayo hua pia ni sawa na Hirabah yaani yaani Kuchukua kitu kwa Nguvu au

kwa njia ya vitisho vya kutumia nguvu.

Kwani anasema Mujaddid Ad Din Imam Muhammad Idris Al Shafii kua: ‘Kama ikiwa

Mtu ana Mke mmoja au Suria ambae hua anamuingilia, basi anatakiwa kua ni

mwenye kumugopa Allah, na hivyo asimsababishie Madhara katika wakati wa

kumuingilia.’ (Kitab Al Umm)

Ambapo Imam Abu Sharaf Zakariyyah An Nawawi anasema kua: ‘Kama haiwezekani

kwa Mume kumuingilia Mke wake bila ya kumsababishia Madhara basi hua

haikubaliki kumuingilia’(Sharh Muhadhdhab)

Na ingawa kuna baadhi wanaweza wakatumia kisingizio cha Hadith ikiwemo ile ya Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam isemayo: ‘Nnaapa kwa yule ambae Maisha yangu

yapo Mikononi mwake kua: ‘Hakuna Mume anaemwita Mke wake kwa ajili ya

Kuingiliana Kimwili na Mwanamke akamkataa isipokua Allah Hua ni mwenye kua

na Ghadhabu nae (Mke) hadi Mume atakaporidhika nae’(Sahih Muslim)’

Ambapo ingawa hadith hii inamaanisha kua hairuhusiki kwa Mke kumkatalia Mumewe

anapomwita Kitandani kwa ajili ya Kukaribiana nae na kuingiliana kimwili, lakini pia

anasema Imam Abu Sharaf Zakariyyah An Nawawi kua: ‘Hadithi hii inamaanisha kua

ni Haram kwa Mke kumkatalia Mume wake pale anapomtaka bila ya kuwepo

sababu inayokubalika kisharia, na Hedhi haiwezi kukubalika kua ni sababu

inayokubalika kisharia kwa sababu Mume anayo haki ya Kustarehe nae wakati

akiwa na nguo zake mke huyo’

Lakini hata hivyo kama tukiiangalia hadithi hii kwa makini basi tunaoona kua Hadith hii

ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam imesema kua: ‘Allah Hua ni mwenye kua

na Ghadhabu nae (Mke) hadi Mume atakaporidhika nae’ hivyo maneno haya

yanamaanisha kua inapotokea hali kama hii basi Mume anatakiwa ajidhibiti, na awe na

Subra, au amsamehe Mkewe kwa sababu kama ingekua sio hivyo basi Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam angesema badala yake kua ‘Mume anayo haki ya

Kumuingilia mke wake huyo kwa Nguvu’ na kama hivyo ni sahihi basi Rasul Allah

Salallau Alayhi wa Salam anayo haki ya kusema hivyo na Allah Subhanah wa Ta’ala

anao uwezo wa kudhihirisha hilo na hadithi haikusema hivyo na haikudhihirishwa hivyo

na wala na aya hazikusema hivyo.

Hivyo mbali ya kua hairuhusikia kumuingilia mke wakati anapokua katika siku zake au

anapokua katika siku za Nifasi lakini pia Mke anayo haki ya kukataa kuingiliwa na


189

Mumewe kwas sababu zinazokubalika Kisharia, kwa mfano Anaumwa, au Mumewe

anamnyanyasa na hivyo Mke kutokua na raha wakati anapokua karibu ya Mumewe, au

anamchukia na hawezi kua nae pamoja, au hua anamdhuru katika kumuingilia kwake, au

mwanamke amechoka na yuko taabani, au hayuko katika hali ya kujisikia kuingiliana

kimwili na hivyo Mwili wake hauwezi kutayarishika kwa ajili ya kuingiliwa na hivyo

kumuingilia huko huweza kusababisha madhara kwa mwili wake.

Kwani amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

‏﴿لاَ‏ يُكَلِّفُ‏ ٱهلل َُّ‏ نَفْساً‏ إِلا َّ وُسْعَهَا﴾‏

La yukallifu Allahu nafsan illa wusAAaha(Surah Al Baqarah, 2:286)

Tafsir: Haikalifishi Allah Nafsi isipokua juu ya kile kilichomo ndani ya mipaka yake

Nafsi hio.

Hivyo Wanaume wa Kiislam wanatakiwa wajue kua Wake zao sio mashine za kufanyia

Mapenzi kwamba unaweza kumuingilia katika kwa matamanio ya nafsi yake katika

wakati uutakao na vyoyote atakavyo bila ya kujali hali yake ya kimaumbile aliyokua nayo

Mke katika wakati huo kwa sababu na wao ni Watu ambao wametokana nasi, kama

zinavyosema aya:

‏﴿وَمِ‏ نْ‏ آَ‏ تِهِ‏ أَنْ‏ خَ‏ لَقَ‏ لَكُم مِّنْ‏ أَنفُسِ‏ كُمْ‏ أَزْوَاجاً‏ لِّتَسْكُنُو ۤ اْ‏ إِلَيْهَا وَجَعَلَ‏ بَيْ‏ نَكُم

م َّوَد َّةً‏ وَرَحمَْةً‏ إِن َّ فىِ‏ ذٰلِ‏ كََ‏ لآَتٍ‏ لِّقَوْمٍ‏ يَتَفَك َّرُونَ‏ ﴾

Wamin ayatihi an khalaqa lakum min anfusikum azwajan litaskunoo ilayha

wajaAAala baynakum mawaddatan warahmatan inna fee Dhalika laayatin

liqawmin yatafakkaroona (Surat Rum 30:21)

Tafsir: Na miongoni mwa alama zake ni kukuumbieni wake kwa ajili yenu kutoka

miongoni mwenu, ili mpate utulivu pamoja nao, na akakuwekeeni baina yenu mapenzi

na rehma. Kwa hakika katika hili kuna dalili kwa wale wenye kutafakkar.

Hivyo basi Wanawake nao wanachoka na wanahisia za kimaumbile kwani ni Ibn Adam

na wala si viumbe Majini labda ambao wanastahmili kwa mda mrefu na kua na nguvu na

uwezo zaidi ya Ibn Adam, na ndio maana akasema Mujaddid Ad Din Imam Muhammad


190

Idris Al Shafii kua: ‘Ama kuhusiana na Kuingiliana basi ni jambo linalohusiana na

starehe na hivyo mtu hatakiwi kulazimishwa’(Kitab Al Umm)

Na Uislam ni Dini ya Uadilifu na Haki hivyo ni yenye kusimamia haki za Wanawake na

Wanaume hususan katika Ndoa na miongoni mwa mifano ya haya ni ile hadith ya Abd

Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu inayomuelezea Mke wa Thabit Ibn Qays Radhi

Allahu Anhu aitwae Jamila, ambapo tunapomzungumzia Thabit Ibn Qays basi hua ni yule

Sahaba ambae iliposhuka ile aya isemayo:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ لاَ‏ ۤ تَرْفَعُواْ‏ أَصْوَاتَكُمْ‏ فَوْقَ‏ صَوْتِ‏ ٱلن َّبىِ‏ ِّ وَلاَ‏ تجَْهَرُواْ‏ لَهُ‏ ٱ بِ‏ لْقَ‏ وْ‏ لِ‏

كَجَهْرِ‏ بَعْضِكُمْ‏ لِبَعْضٍ‏ أَن تحَْبَطَ‏ أَعْمَالُكُمْ‏ وَأَنتُمْ‏ لاَ‏ تَشْعُرُونَ‏ ﴾

Ya ayyuha allatheena amanoo la tarfaAAoo aswatakum fawqa sawti alnnabiyyi wala

tajharoo lahu bialqawli kajahri baAAdhikum libaAAdhin an tahbata aAAmalukum

waantum la tashAAuroona (Surat Al Hujurat 49:2)

Tafsir: Enyi Mlioamini Msinyanyue Sauti zenu juu ya sauti ya Nabii (Muhammad

Sallahu Alayhi wa Salam) na wala msizungume nae kama mnavyozungumza

miongoni mwenu, ili amali zenu zisije zikawa ni za bure wakati nyinyi mkiwa hamjui.

Basi Thabit Ibn Qays Radhi Allahu Anhu akasema kua: ‘Mimi ndie nilietajwa kwenye

Ayah hii, kwani nanyanyua sauti yangu mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, hivyo amali zangu zote zimekua ni za bure, nami nimekua ni mtu wa Motoni’

hivyo akabakia nyumbani kwake na hakutoka huku akimuomba Msamaha Allah

Subhanah wa Ta’ala na kulia machozi, Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipopata

habari hii basi akamtuma mtu kumuliza Thabit Ibn Qays Radhi Allahu Anhu kwanini

akawa katika hali hio?

Ambapo Thabit Ibn Qays Radhi Allahu Anhu akaanza kuelezea dhmabi zake moja baada

ya moja, na kasha kasemakua: ‘Hakika nnakhofia mimi kua nitakua ni miongoni mwa

watu ambao amefutiwa mema yake yote’ hapo Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam

akamwambia Thabit Ibn Qays Radhi Allahu Anhu kua: ‘La Takhaf, kwani kwa hakika

wewe ni mtu mwenye kuendesha maisha yako katika njia yenye kusifika, na utakua

shahidi hapo baadae na Allah Subhanah wa Ta’ala atakuingiza Peponi.’

Hivyo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mke wa Thabit Ibn

Qays Ibn Shammas, Jamilah ambae ni dada yake Abdulla Ibn Ubbay, alikuja kwa

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kusema: ‘Ya Rasul Allah Salallahu Alayhi


191

wa Salam Hakika mimi sina lalamiko baya dhidi ya Thabit Ibn Qays kuhusiana na

Dini yake wala Tabia zake, lakini sasa sitaki mimi kufanya jambo la Kikafiri wakati

nikiwa Muislam’’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuuliza Jamilah: ‘Hivi Jee

utamrudishia Bustani yake?’ kwani Mahari yake yalikua ni hio Bustani aliyopewa,

hivyo nae akasema: ‘Naam’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akamuamrisha Thabit Ibn Qays kwa kusema kua: ‘Chukua Bustani yako na kisha

mpe Talaka moja.’(Fath al-Bari.)

Ambapo kwa upande mwengine basi siku moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alikua amekaa na Al Ababs Ibn Abd Ul Muttalib Radhi Allahu Anhu na hivyo akasema:

‘Ya Al Abbas, hivi Jee haistaajabishi namna Mugheeth anavyompenda Barirah na

namna Barirah anavyomchukia Mugheeth?’

Ambapo Barirah ambae alikua ni Mtumwa aliolewa na Mugheeth ambapo wote wawili

walikua ni Watumwa, hivyo Aisha Radhi Allahu Anha akamnunua Barirah na kisha

akamuachia Huru, na Kiislam Mwanamke aliekua Huru hua hawezi kuolewa na

Mwanamme ambae ni Mtumwa, hivyo Barirah akawa na haki ya hiari ya kuamua kubakia

na Mughith au kuachana nae. Na ingawa Mughith alikua akimpenda sana Barirah kiasi

ya kua kila Mtu katika Mji wa Madinah alikua anajua juu ya Mapenzi hayo Makubwa

sana ya Upande mmoja, lakni hata hivyo kutokana na haki aliyokua nayo Barirah basi

nae akaamua kuitumia haki yake hio ya hiari na akataka kuachana na Mughith.

Ambapo kama alivyosema Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam kumwambia Ami yake

Al Abbas Ibn Abd Ul Muttalib Radhi Allahu Anhu kua ‘Ya Al Abbas, hivi Jee

haistaajabishi namna Mugheeth anavyompenda Barirah na namna Barirah

anavyomchukia Mugheeth?’ kwani kila mtu pia katika Mji wa Madinah alikua akijua

Barirah alikua hampendi Mughith. Hivyo Barirah alipopata uhuru wake basi akasema:

‘Alhamd Lillah, hakika mimi nimeshachoka na ndoa hii na nimepata nafasi ya

kutoka ndani yake, hivyo natoka’

Baada ya Barirah kuamua kutoka ndani ya Ndoa hio basi Mughith akawa anapita huku

akilia kwa huzuni na kulalamika na kumuomba kila mtu anaehisi kua atamsaidia katika

kumuusia Barirah ili arudi kwenye ndoa yake lakini jitihada zake hizo hazikufua dafu,

kwani Barirah alikua hataki hata kumtizama Mughith wala kuzungumza nae. Hivyo

Mughith akaamua kuenda kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kumuomba

amsaidie kumrudisha Barirah katika maisha yake ya ndoa pamoja nae.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuonea huruma Mughith na hivyo akamwita

Barirah na kumwambia bora arudi kwa Mughith kwani anampenda sana, na anaumia na

kuhuzinika Moyo wake kwa ajili yake, ambapo Barirah akamwambia Rasul Allah


192

Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Hivi Jee unaniamrisha au unamuombea’ Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akajibua: ‘Namuombea’ hivyo Barirah akajibu: ‘Kwa hali

hio basi mimi simtaki.’ Na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakuweza

kumlazimisha Barirah kurudi kwenye ndoa yake na Mughith.

Hivyo tunapozungumzia kuhusiana na mshikamano wa Uhusiano wa Mapenzi basi

lazima kuwe na maelewano yenye kushikamanisha Nyoyo zinazopendana na hivyo

inapotokea hali hio ya mshikamano kama huo basi hua hakuna kitu

kitakachopelekea kuvunjika kwa mshikamano huo, isipokua kile kitakachokua ni

chenye nguvu zaidi ya mshikamano huo, hivyo kama ikiwa mshikamano huo kua ni

wenye kutokana na sababu ya kitu fulani au malengo fulani basi mshikamano huo

wa hisia hizo za mapenzi nao hua ni wenye kutoweka pale sababu ya hio

inapotoweka au malengo hayo yasipofikiwa.

Kwani amesema Aisha Radhi Allahu Anha kua: ‘kulikua kuna Mwanamke mmoja

ambae alikua akienda kwa Quraysh na kuwachekesha, na alikuja Madinah pia na

kukaa kwa Mwanamke mmoja na akawa pia anawachekesha Watu’ hivyo Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akauliza: ‘Hivi jee Fulani bint Fulani anakaa na

nani?’ ambapo Aisha Radhi Allahu Anha akasema: ‘Anakaa pamoja na Fulani Bint

Fulani ambae ndie anaewachekesha watu’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Nafsi ziko kama Askari

walioshikamana, wale wanaoafikiana nao basi ndio hua pamoja nao na wale

wasiofikiana nao basi hawawezi kua pamoja nao’(Musnad Imam Ahmad Ibn Hanbal)

Na ndio maana akasema Allah Subhanah wa Ta’ala ndani ya Qur’an kua:

‏﴿ٱلخَْبِيثَاتُ‏ لِلْخَبِيثِينَ‏ وَٱلخَْبِيثُونَ‏ لِلْخَبِيثَاتِ‏ وَٱلط َّيِّبَاتُ‏ ٱ لِلط َّيِّبِينَ‏ ل ‏َو ط َّيِّبُو نَ‏ لِلْط َّيِّبَا تِ‏

أُوْلَٰئِكَ‏ مُبَر َّءُونَ‏ ممِ َّا يَقُولُونَ‏ لهَُم م َّغْفِرَةٌ‏ وَرِزْقٌ‏ كَ‏ رِيمٌ‏ ﴾

Alkhabeethatu lilkhabeetheena waalkhabeethoona lilkhabeethati waalttayyibatu

lilttayyibeena waalttayyiboona lilttayyibati ola-ika mubarraoona mimma

yaqooloona lahum maghfiratun warizqun kareemun(Surat Nur 24:26)

Tafsir: Mabaya hua ni kwa Watu wabaya, na Watu wabaya hua ni wenye kua na

Mabaya, Mazuri hua ni kwa Watu wazuri na Watu wazuri hua ni wenye Mazuri, kwani


193

wao (Wazuri) hua hawana makosa katika Mabaya wayasemayo kwani hua ni wenye

kusamehewa, na hupata Malipo yaliyo bora.

Ambapo baadhi ya Wafasiri wametafsiri aya kwa kusema kua Wanawake wabaya hua

ni kwa Wanaume wabaya, na Wanaume Wabaya hua ni kwa Wanawake Wabaya,

Na aya imetumia maneno Alkhabeethatu lilkhabeetheena waalkhabeethoona

lilkhabeethati ambayo yametokana na nenno Khabutha ambalo hua ni lenye kumaanisha

Kutokua na Rutba Au Kutokua na Faida, Kua Mbaya, Kua Ovu, kutokua na Thamani,

Kua na Uchafu wa maneno au vitendo.

Hivyo Waislam tunatakiwa kua wasafi na wenye sifa nzuri katika mahusiano yetu kwa

ujumla na wala tusiwe ni wenye kuudhiana, kukirihishana na kulazimishana na

kusababishiana madhara iwe kwa maneno au kwa vitendo baina ya Ibn Adam kwa

Ujumla, na kutokana namaamrisho hayo basi ndio maana tukaambiwa kua tusiwakaribie

Wanawake kwa kutaka kuwaingilia kimapenzi wakati wanapokua kwenye Mahiidh hadi

watakapokua tohara yaani wasafi.

Kwani mbali ya kua Mwanamke kua katika kiindi hiki hua na mabadiliko ya Mfumo wa

kihisia za kimaumbile na kimwili kwa kujisikia hali ya uchovu na kutokua na nguvu za

mwili kama kawaida yake na kuhisi maumivu katika sehemu tofauti za mwili wake

kulingana na maumbile ya Mwanamke husika, na hivyo tendo hili kua ni Adha kwake

lakini pia kwa upande wa Kiafya basi tendo hili hua ni lenye kuwadhuru wote

Mwanamme na Mwanamke yaani aliekatatazwa asikaribie kimapenzi na aliekatazwa

kukaribiwa kimapenzi.

Na hii ni kwa sababu katika wakati huu ukuta wa Mfuko wa Uzazi hua katika hali ya

udhaifu na usiokua na ulinzi Imara na hivyo huweza kusababisha madhara makubwa sana

kwa upande wa Mfuko huo, kwa Mayai ya Uzazi wa Mwanamke, Mirija ya Uzazi wa

Mwanamke na huweza kusababisha kutowezekana kupatikana kwa uja uzito wa

Mwanamke au pia kusababisha ujauzito wa aina ya Ectopic yaani mimba kutunga nje ya

mfuko wa Uzazi, ambapo aidha huweza kutunga kwenye Mirija ya Uzazi, kwenye Mayai

ya Uzazi, n.k na hivyo kusababisha utokwaji wa damu nyingi sana na pia husababisha

matatizo mkubwa ikiwemo yatakayosababisha kutolewa Kizazi, na pia maradhi mengine

mbali mbali ya maambukizi ikiwemo maradhi ya Mkojo, Kibofu cha Mkojo, Mafigo, n.k

Na kwa upande wa Mwanamme basi kumkaribia Mwanamke katika wakati wa Hedhi

humplekea Mwanamme kutoweza kuingiliana nae Mwanamke kwa sababu ya hali ya

Damu inayotoka, na hata kama ataweza basi pia Damu hio huweza kumsababishia

maradhi kwenye sehemu zake za siri na kwenye njia ya Mkojo na kwenye Mfumo wa

Mayai ya Uzazi ya Kiume.


194

Ambapo amesema Imam Al Qaffal Al Shashi amesema kua: ‘Aya imetumia neno Wa

La Taqrabuhuna ambapo neno La Taqrab linamaanisha Usifanye kitu lakini

ukisema La Tuqrib basi hua inamaanisha Usikaribie, hivyo hii inamaanisha kua:

‘Msiwaingilie Wanawake zenu’’

Hivyo bila ya shaka Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ni Muumba ni mwenye kujua kitu

na kutokana na kujua kwake kutokana na hikma zake basi ndio maana akakataza

kuwakaribia kwa kuwaingilia kimwili tu Wanawake katika siku hizo, na vyengine vyote

inaruhusika, kula nao, kukaa nao, kuwakumbatia, kuwabusu na kustarehe na kila sehemu

ya mwili wake isipokua baina ya Kitovu na Magoti. Kwani amesema Aisha Radhi Allahu

Anha kua: ‘Wakati mimi nilipokua niko kwenye siku zangu, nilikua namchana

Nywele zake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na alikua akiniegemea kwenye

mapaja yangu huku akiwa anasoma Qur’an.

Na Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al

Qurtubi amesema kua :‘Amesema Ibrahim Ibn Masruq kua: ‘Mimi nilimuuliza

Aisha: ‘Jee ni kipi kilicho halali yangu juu ya mke wangu anapokua yuko kwenye

Hedhi?’Aisha akajibu: ‘Kila kitu isipokua sehemu zake za Siri.’’

Hivyo kuna makubaliano ya Wanazuoni juu ya jambo hili ni kwamba atakaeenda

kinyume na amrisho hili basi hua ni mwenye kufanya dhambi na ingawa hatakiwi kutoa

fidya au kupewa adhabu yeyote lakini hua ni wajibu wake kufanya toba kwa Mola wake.

Kwa upande mwengine pia tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea wazi kua

hairuhusiki kuwaingilia Wanawake wanapokua wenye Hedhi pale alipomalizia kwenye

aya hio kwa kusema:

‏﴿فَإِذَا تَطَه َّرْنَ‏ فَأْتُوهُن َّ مِنْ‏ حَيْثُ‏ أَمَرَكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ يحُِب ُّ ٱلت َّو َّابِينَ‏ وَيحُِ‏ ُّب

ٱ لْمُتَطَهِّري نَ‏ ﴾

Fa-idha tatahharna fa/toohunna min haythu amarakumu Allahu inna Allaha

yuhibbu alttawwabeena wayuhibbu almutatahhireena (Surat Al Baqara 2:222)

Tafsir: ‘Na kisha watakapojitoharisha basi waingilieni katika sehemu

aliyokuamrisheni Allah, kwani kwa hakika Allah anawapenda wenye kufanya toba na

wenye kujitoharisha.’


195

Ambapo aya hii imetanguliza masharti mawili ya kutumizwa kabla ya kufikia hatua ya

kuwaingilia Wanawake waliokua na Hedhi ambayo ni kwanza Wamalize siku zao, pili

Wajitoharishe.

Ambapo kuhusiana na umuhimu wa kujitoharisha basi amesema Allah Subhanah wa

Ta’ala kua:

‏﴿إِذْ‏ يُغَشِّ‏ يكُمُ‏ ٱلن ُّعَاسَ‏ أَمَنَةً‏ مِّنْهُ‏ وَيُنَزِّلُ‏ عَلَيْكُم مِّنَ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ مَآءً‏ لِّيُطَهِّرَكُمْ‏ بِهِ‏ وَيُذْهِبَ‏

عَنكُمْ‏ رِجْزَ‏ ٱلش َّيْطَانِ‏ وَلِيَرْبِطَ‏ عَلَى ٰ قُلُوبِكُمْ‏ وَيُثَبِّتَ‏ بِهِ‏ ٱلأَقْدَامَ‏ ﴾

Idh yughashsheekumu alnnuAAasa amanatan minhu wayunazzilu AAalaykum

mina alssama-i maan liyutahhirakum bihi wayuthhiba AAankum rijza alshshaytani

waliyarbita AAala quloobikum wayuthabbita bihi al-aqdama (Surat Al Anfal 8:11)

Tafsir: Kumbuka wakati alipokufunikeni kwa usingizi kua kama ulinzi kutoka kwake,

na akajaalia Maji kumwagika kutoka Mbinguni kwa ajili ya kukusafisheni na

kukuondeleeni athari za uchafu wa Shaytan na kukutieni nguvu nyoyo zenu na

kuithibitishia uimara miguu yenu.

Ambapo neno Rijz hua linamaanisha Uchafu, Uchafuzi wa kugusana au kuingiliana kwa

kitu kilichokua kichafu kuchanganyika na kilichokua kisafi.

Na ikatumia neno Shaytan ambalo mbali ya kua ni lenye kumaanisha Kuasi, Kua mbali

kutokana na Rehma za Allah, Kiumbe kilichomuasi Allah Subhanah wa Ta’ala, Kiumbe

mwenye Kutoutaka na hivyo kua ni mwenye kuukimbia Ukweli, na pia humaanisha

Uovu.

Hivyo Kujitoharisha kwa kutumia Maji hua ni sehemu ya kujiondolea na kujisafisha

kutokana na madhara ya athari mchafuko unaotokana na nguvu za mionzi isiyoonekana

katika mazingira tunayoishi katika maisha yetu pamoja na viumbe wengine

wanaoonekana na wasioonekana, kwani kimaumbile kila kiumbe hai Duniani hua ni

chenye kuzalisha, kuathiri na pia kuathirika na mawimbi ya mionzi ya nguvu za mvutano

wa Sumaku miongoni mwetu.

Na haya tunaweza kuyaona na kuyajua pale tunapochunguza na kuuangalia mfano mmoja

tu ambao ni wa Mfumo wa Moyo wa Ibn Adam ambao hua unafanya kazi zake

kimaumbile kwa kuishirikisha mifumo mikuu minne ya usafirishaji wa nguvu za hisia za

mwili wa Ibn Adam ambazo ni:


196

1- Mfumo wa Usambazaji wa hisia za sehemu tofauti za mwili.

2- Mfumo wa Viasili vinavyodhibiti maumbile ya ufanyaji kazi wa mwili

vinavyozalishwa na Moyo.

3- Mfumo wa Usambazaji Kemikali kupitia katika mapigo ya Moyo na

usambazaji Damu.

4- Mfumo wa Uzalishaji Nguvu za Kimaumbile za mwili za ufanyaji kazi wa

viungo vya Ibn Adam na nguvu za Mawimbi ya Mvutano wa Umeme wa

Sumaku za ndani ya Mwili na nje ya Mwili.

Kimaumbile Moyo wa Ibn Adam hua unazalisha nguvu za umeme zenye asili ya

mawimbi ya sumaku zenye nguvu mara 5000 zaid na nguvu kama hizo zinazozalishwa

na Ubongo wa Ibn Adam, kwani Ubongo nao katika kufanya kazi kwake basi hua

unazalisha pia nguvu za mawimbi ya sumaku, ambapo nguvu za mfumo wa Moyo

huweza kuhisika hata nje ya mwili wa Ibn Adam kwa takriban umbali wa mita 3 hua na

uwezo wa kusambaza na kupokea na kuwasiliana na hisia mbali mbali kutoka katika

ubongo wa mtu husika na sehemu nyengine za mwili mzima wa mtu huyo na wakati huo

hua na uwezo wa kuwasiliana na nguvu zinazozalishwa na watu wengine zaidi ya wanane

waliopo karibu nae na hivyo hua na uwezo wa kuwaathiri watu hao walio karibu nawe

kihisia.

Moyo wa Ibn Adam una nyuroni 40000 ambazo kwa pamoja hua zinaunda kitu

kinachoitwa Akili ya Moyo, ambayo hua ni yenye uwezo wa kukumbuka kwa muda fupi

na kwa mda mrefu, kujifunza na kufanya maamuzi yake wenyewe bila kuitegemea akili

na hivyo hua na uwezo wa kuyadhibiti mapigo ya Moyo, athari ya Ufahamu wa Moyo

hua na uwezo wa kuubadilisha hata mtizamo wa ufahamu wa akili kihisia na kimaamuzi

katika mambo mbali mbali.

Kila Moyo unapopiga basi hua ni wenye kuzalisha nguvu za mawimbi ya umeme wa

sumaku na hivyo kusababisha athari mbali mbali za Moyo ikiwemo kuona kwa mtizamo

wa Jicho la Moyo, kuhisi kwa hisia za Moyo, ambapo hisia zote hizi zinapotokea ndani

ya Moyo hua zina athari kubwa zaidi ndani ya mwili wa Ibn Adam na zinazotofautiana

sana na zile zenye kutokea moja kwa moja kupitia katika akili ya Ibn Adam, ambapo

mawasiliano kutoka kwenye Moyo kuelekea kwenye Akili hua ni maradufu zaidi yana

umuhimu zaidi kwa ufanyaji kazi wa Mwili kuliko mawasiliano ya kutoka kwenye Akili

kuelekea kwenye Moyo.

Nguvu hizi zinazozalishwa na Moyo pia huweza kuwasiliana kihisia na kuathiri nguvu

za mvutano wa mawimbi ya umeme ya viumbe wengine waliokuwepo karibu yetu

ikiwemo Wanyama na Viumbe wengine wasioonekana wa Ulimwengu wa Al Ghayb. Na

ndio maana baadhi wakati mtu anaweza akakaa peke yake na ghafla akahisi kama mwili

unamsisimka, kwa sababu nguvu hizi za kimaumbile za Moyo hua na uwezo wa kuhisi


197

kutokea kuwepo kwa Viumbe wengine wasioonekana kama vile Majini ambao wao

Maumbile yao yana asili za nguvu hizi.

Na ni kutokana na athari ya nguvu hizi ndio Viumbe Majini hua na uwezo wa aidha

kuwadhibiti Ibn Adam au kuwaogopa na kuwakimbia Ibn Adam. Kwani tunazalisha

nguvu za Mawimbi ya Umeme ambazo ni zenye maumbile kama ya viumbe Majini

ambao sisi Ibn Adam kamwe hua hatuwezi kuwaona kwa sababu wao hawana maumbo

bali wako katika Hali kama ya mionzi ya Xray, ya Ultra Sound, ya Simu, ya Radio, ya

Tv n,k na hivyo hua pia na uwezo wa kimaumbile wa kuingia ndani ya Miili yetu Katika

Nyoyo, Ufaham, Mishipa ya Damu, Ubongo n,k bila ya sisi kuhisi kama vile ambavyo

inaweza kuingia ndani ya Miili yetu mionzi ya Xray, Ultra Sound.n.k.

Kwa hivyo kujitoharisha kwa Maji hua kunapelekea Ibn Adam kua msafi na kujiondolea

mchafuko wa athari mbali mbali zenye madhara ya Kiroho, Kimwili na Kihisia za mionzi

isiyoonekana inayotuzunguka kwenye mazingira yetu ikiwemo athari za maingiliano ya

nguvu za kimaumbile baina ya viumbe mbali mbali ikiwemo Majini katika Miili yetu na

pia kwa kuizima nguvu ya Mionzi ya viumbe Shaytani wanaotaka kutudhibiti kwa

kutokea ndani ya Miili yetu kimaumbile.

Ampapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua : ‘Maneno

yasemayo Min haythu amara kumullah yana maana nyingi nyingi na maana

iliyoelezewa hapa inamaanisha kua Mtu anaweza kumuingilia Mke wake kwa

kulala, kwa kusimama, kwa juu kwa chini, kwa kukaa, katika sehemu

iliyoamrishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Ambapo Allah Subhanah wa Taala anatubainishia wazi baada ya aya hio kwa kusema

kuhusiana na Wake zetu kwa kutumia neno Haratha ambalo ni lenye kumaanisha

Kulima, Kupanda Mbegu, Kuotesha Kitu, Kukata Kitu, Kuvuna, Kutifua Ardhi kwa ajili

ya kuotesha Mbegu au Mimea, Kukisoma kitu kwa undani zadi, Bustani, Mazao, Shamba

na pia humaanisha Mke.

Allah Subhanah wa Ta’ala amesema katika aya iliyotumia neno Harthun:

‏﴿نِسَآؤُكُمْ‏ حَرْثٌ‏ ل َّكُمْ‏ فَأْتُواْ‏ حَرْثَكُمْ‏ أَنى َّٰ‏ شِ‏ ئْتُمْ‏ وَقَدِّمُواْ‏ لأَنْفُسِ‏ كُمْ‏ وَٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَٱعْلَمُو ۤ اْ‏

أَن َّكُمْ‏ م ُّلاَقُوهُ‏ وَبَشِّ‏ رِ‏ ٱلْمُ‏ ؤْ‏ مِ‏ نِينَ‏ ﴾


198

Nisaokum harthun lakum fa/too harthakum anna shi/tum waqaddimoo lianfusikum

waittaqoo Allaha waiAAlamoo annakum mulaqoohu wabashshiri

almu/mineena (Surat Al Baqara 2:223)

Tafsir: Wake zenu ni Mashamba yenu, hivyo yaendeeni Mashamba yenu mtakavyo na

tangulizeni (kufanya mema) kwa ajili ya Nafsi zenu na muogopeni Allah, na jueni kua

mtakutana nae na Wabashirie (habari Njema) Waumini.

Tunapoiangalia aya hii katika kutumia kwake neno Harthun basi tunona kua inamaanisha

kua Mume hua ni Mkulima, Mke hua ni Shamba. Manii Hua ni Mbegu na Mtoto

anaepatikana kutokana na mchanganyiko wa Makadirio na Majaaliwa ya Allah Subhanah

wa Ta’ala na Jitihada za Mkulima katika kulihudumia Shamba lake hua ndio Matunda

yanayotokana na Shamba hilo.

Ambapo anasema Imam Bukhari kua amesema Nafi’i Mawal Ibn Umar Radhi Allahu

Anhu kua: ‘Wakati Ibn Umar alipokua akiisoma Surat Al Baqara alipoifikia aya hii

basi aliniuliza: ‘Jee unajua aya hii ilishushwa kwa sababau gani?’ nami nikasema :

‘La’ Hivyo nae akasema: ‘Ilishushwa kuhusiana na kadha na kadha kadha’ kisha

Imam Bukhari akaendelea kusema: ‘Amesema Abd Samad kutoka kwa Baba yake

kutoka kwa Ayyub kutoka kwa Nafi’i kua Ibn Umar amesema kua Aya hii

inamaanisha vyovyote vile mnavyotaka’ ’

Ambapo Imam Abu Daud amesema kua Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu

amesema kua: ‘Ibn Umar kuna kitu hakufaham. Kwani kulikua na kabila fulani la

Ansari ambao walikua ni Makafiri, na kuna kabila la Mayahudi ambao walikua ni

watu wa Ahl al Kitab, na wao Maansari walidhani kua Mayahudi walikua wako juu

zaidi kiilm. Hivyo wakawa wanawaiga Mayahudi katika wanayoyafanya.

Wakawaamrisha wasiwaingilie wake zao isipokua kwa upande mmoja (yaani

wanapokua wamelala chali) kwa sababu hii ndio njia ambayo inawafunika zaidi

Wanawake. Hivyo watu hawa wa Ansari wakawaiga kufanya hivyo Mayahudi.’

‘Wakati Maquraysh walikua wamezoea kuwavua nguo zote Wanawake wao na

kustarehe nao wakiwa chali na wakiwa kifudifudi. Hivyo wakati Muhajjiruna

walipokuja katika Mji wa Madinah na kuoa Mwanamke wa Kiansari basi Mtu

alikua anamuingilia katika hali hio na Mwanamke hakupenda na akamwambia:

‘Sisi tunaingiliwa kwa upande mmoja tu hivyo fanya hivyo au achana na mimi’

Habari hii ikaenea katika Mji wa Madinah na kumfikia Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam, hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akaishusha aya hii ‘Nisaokum

harthun lakum fa/too harthakum anna shi/tum’’ yaani ‘Wake zenu ni Mashamba

yenu, hivyo yaendeeni Mashamba yenu mtakavyo’ Kumaanisha kua Wake zenu ni


199

mashamba yenu Waingilieni wakiwa wamelala chali au wakiwa kifudifudi kwa

kupitia sehemu ambayo anayozaliwa mtoto’

Kwani amesema Khuzaymah Ibn Thabit Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul

Allahu Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Allah haoni haya sana kusema Ukweli’

mara tatu, kisha akasema: ‘Msiwaingilie Wanawake kwenye tupu zao za

Nyuma.’’(Imam Ibn Majah)

Imam Abu Hasan Ali Ibn Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al Shafii anasema

kuhusiana na Hadithi hii ambayo ni Mutawattir yaani iliyonukuliwa na Masahaba wengi

sana kiasi ya kua inakua vigumu Masahaba hao kukubaliana kusema Uongo kua: ‘Hii ni

kwa sababu ya kua kuna Makubaliano ya Masahaba juu ya hili, kwani imenukuliwa

na Ali Ibn Abi Talib, Abd Allah Ibn Abbas, Abd Allah Ibn Masud na Abu Dardaa

Radhi Allahu Anhum.’(Kitab Al Hawi Al Kabir Fi Fiqh Madhhab Shafii)

Ambapo wengine miogoni mwa Masahaba walionukuu hadithi hii ni pamoja na Sayyidna

Ali Ibn Abi Talib, Abu Darda, Abd Allah Ibn Amr Al As, na Abu Hurayrah Radhi Allahu

Anhum. Na huo pia ndio mtizamo wa Imam Said Ibn Musayyib, Abu Bakr Ibn Abd

Rahman, Mujahid Ibn Sulayman, Ikrimah Mawla Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu

Anhu, Imam Muhammad Idris Al Shafii, Imam Ibn Al Mundhiri Al Nishapuri.

Ama baada ya hapo Allah Subhanah wa Taala anatupa ukumbusho kwa kutuambia kua

mbali ya kuturuhusu kustarehe na wake zetu lakini tusimsahau yeye hata tunapokua

kwenye kilele cha starehe hizo kwa kusema:

‏﴿وَقَدِّمُواْ‏ لأَنْفُسِ‏ كُمْ‏ وَٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَٱعْلَمُو ۤ اْ‏ أَن َّكُمْ‏ م ُّلاَقُوهُ‏ وَبَشِّ‏ رِ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ ﴾

Waqaddimoo li-anfusikum Waittaqoo Allaha waiAAlamoo annakum mulaqoohu

wabashshiri almu/mineena (Surat Al Baqara 2:223)

Tafsir: Na tangulizeni (kufanya mema) kwa ajili ya Nafsi zenu na muogopeni Allah,

na jueni kua mtakutana nae na Wabashirie (habari njema) Waumini.

Hivyo tunapoangalia kuhusiana na kwa upande wa Maisha ya wafuasi wa Dini ya

Uyahudi basi hua kuna mtizamo tofauti kuhusiana na Damu, kwani kwa upande wao ni

kitu kitukufu na ndio maana hata nyama zao wanazochinja ambazo ingawa huchinjwa

kama wanavyochinja Waislam lakini baada ya kuchinjwa inabidi Nyama hio itiwe

Chumvi na ikaushwe Damu yote na kisha ndio inaweza kuitwa Kosha ambayo ndio aina

ya Nyama wanayoruhusika kuitumia kwa ajili ya kula..


200

Ambapo kwa upande wa Wanawake na Hedhi na maumivu na Maradhi yanayotokana na

damu ya Hedhi, basi kwao wao ilikua katika wakati kama huo ambao Mwanamke

anapoingia kwenye siku zake basi hua kuna hali inayojulikana kama Niddah ambayo hua

inamaanisha Utenganishwaji au Utolewaji ambao hua ni kutangenishwa na familia zao

kwa mda wa siku 7 ambazo Wanawake hao huchukulikwa na kuwekwa kwenye Jengo

maalum lililojengwa kwa ajili yao.

Ndani ya Jengo hilo ambalo linajulikana kama Jumba la wasiokua tohara hua

hawaruhusiwi kutoka kurudi majumbani mwao mpaka zipite siku 7, katika kipindi hiki

wanapokua kwenye Jengo hilo hua hawaruhusiwi kujipamba ambapo baada ya siku hizo

basi hua tayari wameshakua Tohara moja kwa moja bila ya kujitoharisha kwa kukoga au

kwa kutayamam pale inapokua hakuna maji kama ilivyo kwa upande wa Uislam, na

ingawa hua wanaruhusiwa kurudi Majumbani mwao, lakini hua hawaruhusiwi kuingia

kwenye Majumba ya Ibada hadi pale watakapopeleka ndege wawili kwa Kasisi wao kwa

ajili ya kutoa Kafara ambayo baada ya kuchinjwa kwake basi ndio inahesabika kua

wanaweza kuingia kwenye Majumba ya Ibada na kua mbele ya Mungu wao.

Kutokana na mazingira hayo basi ndio maana Hannah Bint Faqudh alikua akitegemea

kua Mtoto wake atakua ni wa kiume ili maisha yake yote mtoto huyo yawe ndani ya

Mahekalu ya Kuabudia, kwani kama akiwa mwanamke basi lengo lake hilo halitoweza

kufanikiwa kwani kuna kipindi Mtoto huyo itabidi awe ni mwenye ulazima wa kutolewa

kutoka kwenye Jumba la Ibada na kutengwa kutokana na Niddah.

KUZALIWA KWA MARYAM BINT IMRAN

Hivyo baada ya kunadhiria kwake huko Hannah Bint Faqudh basi akaendelea na uja uzito

wake, ambapo kati kati ya uja uzito huo basi Allah Subhnah wa Taala ambapo mtihani

Hannah Bint Faqudh ambao ni wa kondokewa na Mumewe yaani Mzee Imran ambae

alifariki Dunia, na hivyo Hannah akawa na huzuni kwani Mtoto huyo atakua ni mwenye

kukua bila ya baba yake.

Baada ya kupita Mtihani huo basi Allah Subhana wa Ta’ala akamjaalia kua ni mwenye

kujifungua baada ya mda wake kufika ambapo mara tu baada ya kujifungua basi Hannah

Bint Faqudh akaona kua mtoto aliejifungua alikua ni Mwanamke badala ya Mwanamme

aliemtegemea kumpata kwa ajili ya kutimiza nadhiri yake aliyoiweka na hivyo akaomba

radhi kwa Mola wake kama inavyobainisha aya:


201

‏﴿فَلَم َّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ‏ رَبِّ‏ ِ إِنىّ‏ وَضَعْتُهَآ ٰ أُنْثَى وَٱهلل َُّ‏ أَعْلَمُ‏ بمَِا وَضَعَتْ‏ ٱ وَلَيْس ل ذ َّكَرُ‏

ٰ كَٱلأُنْثَى ِ وَإِنىّ‏ سمَ َّيْتُهَا مَرْيمََ‏ ِ وِإِنىّ‏ أُعِيذُهَا بِكَ‏ وَذُرِّي َّ تَهَا مِنَ‏ ٱلش َّيْطَانِ‏ ٱلر َّجِ‏ يمِ‏ ﴾

َ

Falamma wadhaAAat-ha qalat rabbi innee wadaAAtuha ontha waAllahu aAAlamu

bima wadaAAat walaysa aldhdhakaru kaalontha wa-innee sammaytuha maryama

wa-innee oAAeedhuha bika wadhurriyyataha mina alshshaytani alrrajeemi(Surat

Al Imran 3:36)

Tafsir: Kisha alipomzaa akasema: ‘Ewe Mola wangu hakika mimi nimejifungua Mtoto

Mwanamke.’ Na Allah ni mwenye kujua zaidi juu ya kile alichojifungua: ‘Na

Mwanamme sio kama Mwanamke na kwa hakika mimi nimemwita Maryam. Na kwa

hakika nnaomba hifadhi yake kutoka kwako na kizazi chake kutokana na Shaytan

aliefukuzwa’

Amesema Abu Hurayra kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua :

‘Bila ya kumjumuisha Maryam na Mtoto wake basi hakuna Ibn Adam ambae

amezaliwa bila ya kuguswa na Shaytan katika wakati wa kuzaliwa, na ambae halii

kutokana na kuguswa na Shaytan’’

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi

kwa lugha yao basi neno Maryam maana yake hua ni Mja au Mtumwa au Mwenye

Kuabudu na hivyo basi Hanah Bint Faqudh anaweka wazi kuhusiana na kutimiza nadhiri

yake kupitia kwa Mtoto huyu kwa kuanzia na jina lake ‘Maryam’ hata kama ni

Mwanamke.

Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea

kutuambia kua aya hii inatafsirika katika hali mbili ambazo ni kua kwanza, kama itakua

tutaisoma aya hii kwa kusema: ‘WaAllahu aAAlamu bima wadaAAatu yaani Na Allah

ni mwenye kujua zaidi ju ya ile lichojifungua’ basi maneno yasemayo ‘Walaysa

aldhdhakaru kaalontha’ yatakua yanamanisha kua ni maneno aliyoyasema Hannah Bint

Faqudh yaani Imraat Al Imran.

Na hivyo basi hapa itakua Hannah Bint Faqudh hamaanishi kua kwake yeye basi bora

angepata Mtoto wa Kiume, bali alikua akimaanisha kua: ‘Hakika mimi nilitaka mtoto

wa Kiume lakini Allah Subhanah wa Ta’ala amenijaalia mimi Mtoto wa Kike, na

Mtoto wa kiume ambae niliemtaka hawezi kua kama mtoto huyu wa kike ambae

alienijaalia Allah Subhnah wa Ta’ala, kwani hata huyu pia ni bora’ na hii ni kwa

sababu Hannah Bint Faqudh alikua ni mwenye kuujua uwezo wa Mola wake juu yake


202

ambae ni mwenye kujua ni kipi bora kwa ajili yake, na hivyo hua ni mwenye kujaaliwa

na Mola wake kile kilichobora zaidi kwake,

Ambapo kama kama itakua tutaisoma aya hii kwa kusema: ‘WaAllahu aAAlamu bima

wadaAAat yaani Na Allah ni mwenye kujua zaidi ju ya kile alichojifungua’ basi

maneno yasemayo ‘Walaysa aldhdhakaru kaalontha’ yatakua yanamaanisha kua ni

maneno aliyoyasema Allah Subhanah wa Ta’ala.

Na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala kua ni mwenye kumjibu Hannah Bint Faqudh kwa

kumaanisha kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ni mwenye kujua ni kipi bora zaidi

kuhusiana na mtoto huyu wa kike aliezaliwa ambapo hapo baadae Maryam na

Mtoto wake wa kiume watakua ni wenye kuanza kua ni Muijiza kwa Ulimwengu

huu’ ambapo hata hivyo Hannah Bint Faqudh alikua hajui juu ya hilo kwani mtizamo

wake yeye ni wa kiumbe Ibn Adam ambao umejaa muonekano wa mazingira ya ufahamu

wa kimaumbile ya Ibn Adam na ndio maana akawa ni mwenye kuomba samahani kwa

Mola wake, kutokana na kuona kua malengo yake aliyonadhiria yatakua hayafanikiwi

kutokana na kutokujua kua Binti huyo ni bora zaidi kuliko mtoto mwengine yeyote yule

ambae angempata badala yake.

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala anatuambia kuhusiana na kilichofuatia baada ya hapo

kwa kusema katika aya ifuatayo baada ya hio kua:

‏﴿فَتَقَب َّلَهَا رَب ُّهَا بِقَبُولٍ‏ حَسَنٍ‏ وَأَنبَتَهَا نَبَااتً‏ حَسَناً‏ وَكَف َّلَهَا زَكَرِ َّ كُل َّمَ‏ ا دَخَلَ‏ عَلَيْهَا

زَكَرِ َّ‏ ٱلْمِحْرَابَ‏ وَجَدَ‏ عِندَهَا رِزْقاً‏ قَالَ‏ يمَٰرْيمَُ‏ أَنى َّٰ‏ لَكِ‏ هَٰذَا قَالَتْ‏ هُوَ‏ مِنْ‏ عِندِ‏ ٱهلل َِّ‏

إنًّ‏ ٱهللًَّ‏ يَرْزُقُ‏ مَن يَشَآءُ‏ بِغَيرِْ‏ حِ‏ سَابٍ‏ ﴾

Fataqabbalaha rabbuha biqaboolin hasanin waanbataha nabatan hasanan

wakaffalaha zakariyya kullama dakhala AAalayha zakariyya almihraba wajada

AAindaha rizqan qala ya maryamu anna laki hadha qalat huwa min AAindi Allahi

inna Allaha yarzuqu man yashao bighayri hisabin(Surat Al Imran 3:37)

Tafsir: Hivyo akamkubalia Mola wake kwa mkubalio ulio bora. Na akamfanya akuwe

katika makuzi mazuri na kumuweka chini ya usimamizi wa Zakarriyah. Hivyo kila

akiingia kwenye Mihrab (kumuangalia) alikua akimkuta na Riziki yake, hivyo

akasema: ‘Ewe Maryam, Umepata wapi yote haya?’ akasema (Maryam): ‘Hivyo ni

kutoka kwa Allah’ kwani kwa hakika Allah humruzuku amtakae bila ya hesabu


203

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamkubalia Hannah Bint Faqudhi maombi yake hayo

kwa mkubalio ulio bora kabisa na Maryam akawa ni mwenye Uzuri wa kimaumbile na

ubora wa kipekee usiokua na kuzidi ukubwa wa kitu chochote wake wala wa kupungua

kwenye mwili alikua ni mwenye kuvutia kuliko wote katika Wanawake wa wakati wake.

Uzuri wake huo ulikua ni wenye kuonekana dhahiri tangu wakati alipozaliwa kiasi ya

kua mtu alivutiwa nae na alipopelekwa kwa Makuhani kwa ajili ya kuombewa basi

walipomuona kila mtu ambae aliekua na uhusiano na Mzee Imran alikua anataka kua

ndio awe mlezi wake Mtoto huyo. Na Makuhani wakataka wamlee wao kwani ni mtoto

wa Mzee Imran ambae ndie aliekua Kiongozi wao Makuhani hao.

Hivyo Nabii Zakariyah ambae ni Mume wa Isha Bint Faqudh ambae ni Mama yake

Mdogo Maryam akasema kua yeye anastahiki kua ndie mlezi zaidi kwa sababu Mke wake

ni Mama yake mdogo Maryam.

KAFFALA – ULEZI WA MARYAM BINT IMRAN.

Hivyo jamii ya watu hao ikaamua kua wakarushe kalamu zao Mtoni na hivyo Kalamu ya

yule ambae haitozama kwenye maji ya Mto huo basi ndie atakaekua na Bahati ya kumlea

Mtoto huyo. Hivyo wakaondoka watu 19 pamoja na Nabii Zakariyyah hadi katika Mto

Jordan, na kisha wakachukua Kalamu zao ambazo ndio walizokua wakiandikia Tawrat,

na walipofika kwenye Mto huo basi wakazirusha Mtoni moja baada ya nyengine. Na hii

ni kutokana na kama ilivyolezewa katika aya ifuatayo ambayo Allah Subhnah wa Ta’ala

anamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kusema:

‏﴿ذٰلِكَ‏ مِنْ‏ أَنْبَآءِ‏ ٱلْغَيْبِ‏ نُوحِ‏ يهِ‏ إِلَيكَ‏ وَمَا كُنْتَ‏ لَدَيْهِمْ‏ إِذْ‏ يُلْقُونَ‏ أَقْلاَمَهُمْ‏ أَي ُّهُمْ‏

يَكْ‏ فُلُ‏ مَرْيمََ‏ وَمَا كُ‏ نْتَ‏ لَدَ‏ يْهِ‏ مْ‏ إِذْ‏ يخَْتَصِ‏ مُونَ‏ ﴾

Dhalika min anba-i alghaybi nooheehi ilayka wama kunta ladayhim idh yulqoona

aqlamahum ayyuhum yakfulu Maryama wama kunta ladayhim idh yakhtasimoona

(Surat Al Imran 3:44)

Tafsir: Haya ni katika habari za Ghayb tunakushushia juu yako, na wewe hukua mbele

yao waliporusha Kalamu zao (kuamua) ni yupi amtunze Maryam na hukua mbele yao

walipokua wakihasimiana.


204

Ambapo aya hii inatuonesha kuruhusika kufanya Bahati Nasibu ya aina hii ambayo ni

Bahati Nasibu ya Qurah (kupiga Kura), hivyo hapa haikusudiwi kua ile ya Kamari, kwani

kuna Bahati Nasibu ya Kamari na kuna Bahati Nasibu ya Bahati Nasibu yaani ya Qurah

ambapo Mujaddid Ad Din Shaykh Ul Islami Imam Ibn Hajar Al Asqallani na pia Imam

Abu Hasan Ali Ibn Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al Shafii wanaelezea Bahati

Nasibu ya Qurah ambayo ndio inayokubalika kisharia kwa kusema kua: ‘Bahati Nasibu

(Qurah) iliyokua ikifanywa ilikua kuna majina yanaandikwa kwenye vitu na kisha,

huitwa Mtu ambae ni Mgeni achague, na yule aliechaguliwa jina lake basi hua ndie

alieshinda na ndie atakaechaguliwa. ’

Na pia akasema Shaykh Islami Imam Abu Abd Allah Badr Ad Din Muhammad Ibn Abd

Allah Ibn Bahadir Al Zarkashi Al Shafii.: ‘Vyovyote vile itakafanywa (Qurah) Bahati

Nasibu basi hua inakubalika.’

Na kwa kua tumezungumzia Bahati Nasibu inayokubalika na Bahati Nasibu

isiyokubalika ambayo ni ya Kamari basi tuwekeane wazi zaidi kuhusiana na tofauti yake,

ambapo ‘Bahati Nasibu ya Kamari hua ni ile ya Watu kua wanatoa Kitu au

Wanalipia au Wanatuma Ujumbe wa Simu, na hivyo kua ni wenye kulipia asilimia

fulani inayokatwa kwenye simu zao kutokana na Ujumbe huo kwa ajili ya

kujumuishwa kwenye Mchuano wa Kuchaguliwa, ambapo kwa upande wa ujumbe

wa Simu hua zawadi haitolewi mpaka ifikie idadi fulani ya ujumbe uliotumwa

ambao utafikisha malengo ya kiasi cha pesa kinachotakikana kwa ajili ya kutoa

zawadi husika na hivyo kutokana na hali basi hili hua ndio jambo ambalo

lisilokubalika kisharia, kwani hua ni aina ya Kamari.’

Hivyo Mayahudi hawa akiwemo mzee Imran wakafanya Bahati Nasibu hio, na anasema

Imam Abd Rahman Al Suddi kua: ‘Ziliporushwa Kalamu hizo basi Kalamu ya

Zakariyyah ikaibuka juu a kusimama wima kama vile iliyorushwa kwenye Tope na

kisha ikaganda, huku Kalamu nyengine zote zikiwa ni zenye kuchukuliwa na

mkondo wa maji ya mto huo.’ hivyo Nabii Zakarriyah akawa ni mwenye kushinda

mashindano hayo na kua ni mwenye kubeba jukumu la kua ndie Mlezi wa Maryam Bint

Imran.

Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Waanbataha nabatan hasanan

wakaffalaha zakariyya kullama dakhala AAalayha Zakariyya yaani Na akamfanya

akuwe katika makuzi mazuri na kumuweka chini ya usimamizi wa Zakarriyah’

Ambapo aya imetumia neno Nabata ambalo mara nyingi hua linatumika

inapozungumziwa Miti na Mimea mbali mbali inayoota Ardhini kwani neno hili hua

linamaanisha Kuchipua, Kuota, Kukua, Kutoa Majani au Kunawiri bila ya kuonekana

athari ya kile chakula chake inachokula Mimea hio ambacho ni chenye kutokana na

Hewa, Maji na Udongo.


205

Ambapo tunapozungumzia Mtoto wa Ibn Adam basi hua inamaanisha Kukua katika

Mazingira yanayotokana na kuhudumiwa juu ya kila kitu, na hii ndio hali aliyokua nayo

Maryam kwani alikua na kila kitu ambacho anakihitajia ijapokua kitu hicho hakipatikani

kwenye maeneo ya ardhi hio au hayapatikani kwa sababu ya kua si msimu wake wa

kupatikana kitu hicho.

Na pia ikatumia neno Kaffala lenye kumaanisha Kulea Mtoto ambae si wa kuzaa yaani

wa Mtu mwengine, Kujali, Kusimamia, Kutunza, Kudhamini au Kuchunga ambapo neno

Kaffala ndio lililotoa neno Dhul Kifl ambalo ni jina lenye kumaanisha Mtu mwenye kua

na sehemu kubwa sana ya I’lm ambae amejitolea kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala

tu pekee.

Hivyo aya haikutumia asili ya neno Rabba lenye kumaanisha kua Mlezi ambae pia ni

Mzazi, kua Bwana kua Mmiliki, Bosi, Kutawala, Kumiliki, Kusimamia kwa kulea kutoka

hatua moja mpaka kuingia kwenye hatua nyengine, Kutunza, n.k. Neno Rabba ndio

lililotoa neno Rabb ambalo hua linamaanisha Muumba, Mtawala, Mfalme wa Kila kitu

cha Kimaumbile, Mwanzilishi na Msimamizi wa kila kitu tangu mwanzo hadi mwisho,

na hivyo kutubainishia kua Ibn Adam ni Kiumbe ameumbwa katika hatua zisizokua na

mipaka kimaendeleo.

Hivyo aya imetumia neno Kaffala kwa sababu neno hili kimaana hua pia linawakilisha

Kumuondolea Mzigo au Uzito mtu ambae ni mwenye kuhitaji kuwekwa chini ya

Uangalizi, Udhamini na uhifadhi na yule mwenye kubeba jukumu la Uangalizi huo

kisharia ambae hua ni Kafil juu ya yule mwenye kuhitaji kusimamiwa, kutokana na kua

ni mwenye sifa ya kua ni Yatima.

Ambapo miongoni mwa haki anazostahiki kuzisimamia Kafil basi ni lazima kwake

yeye ahakikishe kua anasmami majukumu yafuatayo:

Malezi Mazuri Kulingana na Imani ya Dini ya Kiislam: Ni wajibu wake Kafil

kuhakikisha kua anamsimamia na kumlea na kumtunza Yatima kulingana na malezi

yanayotokana na Mafunzo ya Kiislam kulingana na Maamrisho ya Qur’an na Hadith za

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuhusiana na malezi ya Mtoto.

Kwani tunapozungumzia Malezi Mazuri Kulingana na Dini ya Kiislam juu ya Mayatima

basi ili yakamilike Malezi hayo Ndani yake inabidi kuwe na Miongoni mwa Hali

zifuatazo ambazo hua ni Jukumu la Mlezi:

1-Kila Mlezi mwenye kubeba Jukumu la Kulea Mtoto ambae ni Yatima basi

anatakiwa Ahakikishe kua Anamlea Mtoto Husika katika Malezi ya Kiislam kama

ilivyoamrishwa na Allah Subhanah wa Ta'ala na Mtume wake Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam Hivyo Mtoto Huyo anatakiwa amsimamie katika kumtekelezea


206

Mahitaji yake muhimu kama ya Chakula, Malazi, Mavazi, Usimamizi wa Mirathi

yake n.k

2-Anaebeba Jukumu la Kulea Mayatima basi hua ni Wajibu wake kuhakikisha kua

Watoto au Mtoto wanapata haki yao ya Kupata Elimu ya Dini ya Kiislam kwa ajili

ya Dunia yao na Kwa Ajili ya Akhera yao, na pia ahakikishe kua Yatima au

Mayatima hao Wanapata Elimu ya Kidunia kwa ajili ya kuendeleza na Kuboresha

Maisha yao Duniani hapo baadae.

3-Mwenye Kubeba Jukumu la Kulea Watoto Mayatima au Yatima anatakiwa

ahakikishe kua Watoto au Mtoto Wanaishi katika Mazingira yaliyojaa Imani,

Upendo, Huruma na Tabia Njema Ndani yake Ili watoto hao wasije wakaharibika

kutokana na kurithi tabia zisizokua za Kiislam kutokana na kutofunzwa Akhlaki

na maadili ya Kiislam na hivyo, kua na Mitizamo mikali ya Dini yake au Kutokua

na Iman ya Dini yake, ma hivyo kukosa kua ni mwenye Huruma na Upendo kwa

Watoto wenzake na viumbe wengine katika maisha yake.

4-Wenye kulea Watoto Mayatima au Yatima hawatakiwi kubeba uzito wa Mzigo

wa zaidi ya Uwezo wao kama vile ilivyo kwa wengi miongoni mwa baadhi ya Watu

kiasi ya kua Matokeo yake Watu kuanza kutumia kisingizio cha Watoto hao na

kuanzisha Usumbufu na maaudhi kwa wenzake kutokana na kuwatumia watoto

hao kua ni chanzo cha kuingizia mapato kwa Kuomba Omba ovyo hapa na pale, wa

ajili ya kuwatekelezea mahitaji yao.

Kwa Sababu mbali ya Kua Uislam Umekataza Kuomba, kulingana na Aya na pia

Kulingana na Hadith za Rasul Allah A'alayhi wa Salam kwa Sababu katika Kuomba

Omba hua wanawasababishia Dhambi Waislam wenzao wanaowaomba. Na hii pia ni

kwa Sababu si kila mwenye Kutoa basi hua ni mwenye kutoa kwa Nia na Moyo Msafi,

kwani kuna wanaotoa kwa kinyongo, kuna wanaotoa kwa Unafiq, kuna wanaotoa kwa

kujikalifisha, kuna wanaotoa kwa kujionesha n.k.

Ambapo amesema Qabisah Ibn Mukharik Al Hilali Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi

nilingia kwenye Deni kwa ajili ya kupatanisha watu wawili na hivyo nikaenda kwa

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kumuomba msaada kutokana na deni hilo,

hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kua: ‘Subiri pamoja nasi

mpaka tuletewe Zakkah na kisha nitaamrisha upewe kitu chochote’ kisha Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaema: ‘Ewe Qabisah! Fahamu kua kuomba

Msaada hakuruhusiki isipokua katika hali tatu zifuatazo:

‘Kwa Mtu ambae ameingia kwenye Deni kwa sababu ya kupatanisha pande mbili,

kwani huyu anaruhusika kuomba mpaka amalize deni hilo, na kisha ajizuie

kuomba;


207

Kisha yule mtu ambae aliefikwa na Msiba ambao umemuangamizia Mali yake yote,

huyu hua anaruhusika kuomba hadi pale atakapokaa sawa;

Na kisha yule ambae ni Masikini sana, na hivyo watu watatu wenye Busara

miongoni mwa watu wake, wakathibitisha kua amefikwa na Umasikini na

anastahiki kuomba hivyo hapa hua anaruhusika kuomba msaada hadi pale

atakapotokana na hali hio.’

‘Hivyo Vyenginevyo zaidi ya hali hizi basi Mtu haruhusiwi kuomba, Ewe Qabisah!

Ni Haram kuomba Msaada, na anaeomba kisha akawa ni mwenye kula kutokana

na alichoomba basi hua anakula Haram’(Sahih Muslim, Musnad Imam Ahmad, Sunan

An Nasai, Sunan Abu Daud.)

Akasema tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hairuhusiki kumpa

Sadaka mtu ambae ni Mwenye uwezo au kwa yule ambae ni mwenye Nguvu na

Afya’(Imam At Tirmidhii)

Na siku moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimpa Umar Ibn Al Khattab Radhi

Allahu Anhu zawadi, hivyo Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akasema

kumwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Ya Rasul Allah bora mpe

mtu mwengine mwenye shida nayo zaidi yangu

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Yule ambae anaeomba

wengine kwa ajili ya kujiongezea Mali yeye mwenyewe basi hua ni sawa na

anaeomba Makaa ya Moto (wa Jahannam) hivyo mwache mwenye kuomba aombe

kidogo au zaidi: ‘Chukua, kisha kaa nayo au igawe kama Sadaka, na chochote kile

kitakachokuja kwako katika hali kama hii bila ya wewe kua ni mwenye Tamaa au

Kuomba basi pokea lakini kitakapokuja katika hali ya mazingira mengine basi

usikikimbilie kwa kukitamania’’(Sahih Muslim)

Na ndio maana akasema Imam Nur Al Din Abu Al Diya `Ali Ibn Al Shabramilisi Al Shafii

kua: ‘Kama Mtu Mmoja atampa Mtu fulani Sadaqa yake kwa kudhania kua Mtu huyo

ni fulani, na kisha akagundua kua mtu huyo sie aliemdhania basi Mtu alietoa Sadaka

anaruhusika kuichukua mwenyewe sadaka yake hio.’ (Hashiyyat Al Shabramilisi ala

Nehayat al-Muhtajj)

Ambapo kitu kinachotolewa katika Njia kama hizi hua hakina Barka ndani yake kwa

anaetoa na pia kwa anaepokea na Bila ya Shaka unapopokea kitu kama hiki basi unaweza

ukawasababishia matatizo mbalimbali wle unaowalea ikiwemo ya Udhaifu wa Kiimani

wale unaowalea.


208

Hivyo kama vile ambavyo Riziki yako inavyotakiwa iwe ya halali na isiwe iliyopatikana

kutoka kwa mtu ambae amekupa kwa kinyongo, kwa shingo upande, bila kuridhia au bila

ya Moyo Msafi na Nia safi n.k

Ambapo amesema Abu Kabshah Al Anmari Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alisema kua: ‘Nnaapa juu ya vitu vitatu ambavyo

nakutakeni nyinyi myahifadhi maneno yangu juu yake kua: ‘Sadaqah inayotolewa

katika Mali hua haipunguzi Mali husika, Mtu anaepatwa na Mitihani na akawa na

Subra juu yake, basi Allah Subhanah wa Ta’ala humpa Uwezo (na kumpandisha

Darja) na Mtu anaeanza Kuomba kua Allah Subhanah wa Ta’ala atamsababishia

mtu huyo kua na umasikini.’’’(Imam At Tirmidhi)

Ambapo tunapoangalia kuhusiana na Upande wa Fiqh basi kuna hali tatu tofauti

kuhusiana na Maumbile ya Kuomba, ambazo ni:

1- Hairuhusiki Kuomba: Kua imekatazwa kwa mtu kua ni mwenye kuwaomba watu na

huu ni mtizamo wa wengi miongoni mwa Wanazuoni, ambapo miongoni mwao ni

pamoja na Imam Muhammad Idris Al Shafii, Imam Ahmad Ibn Hanbal, Imam Abd Al

Barr Al Maliki, Imam Al Qurtubi, Imam Al Sannani, Imam Al Sarkhasi, Imam Al Kasani,

Imam Al Razi, Imam Al Shibrini, Imam Ibn Qudamah n.k ambapo kwa upande wa

Madhhab ya Imam Abu Hanifa basi wanasema kua : ‘Hairuhusiki kumpa mtu

anaeomba Msikitini’

Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kuomba Pesa hua si

sawa na Mtu anaeomba Makaa ya Motoni’(Sahh Muslim) na pia akasema kua:

‘Kuomba ni Jambo baya sana wenye Uso wa Mtu isipokua pale mtu anapokua

anaemuomba ni Mtawala wake au ni kitu cha muhimu sana’(Imam At Tirmidhi)

Ambapo kwa upande wa Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Al Ghazali kua:

‘Tunapozungumzia kuhusiana na kuomba basi kua tunaona hua ni kulalamika kwa

kubainisha Umasikini wa Muombaji kua amepungukiwa na Rehma za Allah

Subhnah wa Ta’ala. Na pia huonesha kua na unyenyekevu kwa mwengine zadi ya

Allah Subhnah wa Ta’ala wakati Waumini wanatakiwa wawe wanyenyekevu kwa

Allah Subhanah wa Ta’ala tu na mara nyingi hua inasababisha kero kwa

anaeombwa, na hii ni kwa ababu labda hua hawataki kutoa na hivyo hua ni wenye

kutoa kwa ajili ya kujionesha au kwa njia ya kuona aibu au kwa njia ya Unafiq. Au

huwabidi kutoa ili wasionekane kua ni Mabakhili. Hivyo kuomba kumekatazwa

kwa anaepokea’

Na wa Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye anasema kua: ‘Ingawa hairuhusiki

kuomba, lakini hua inakubalia pale inapokua anaeomba hua hajidhalilishi mbele


209

ya anaemuomba na hamsababishii kero yule anaemuomba, kwani ikiwa ni hivyo

basi hairuhusiki kabisa.’

Ambapo Imam An Nawawi amesema kuhusiana na Hadith hi kua: ‘Kuomba

kumekatazwa kwa sababu vyenginevyo basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

asingehimiza kuachana nako kuomba’

2- Ni Makruh Kuomba: Hujjat ul Islami Imam Mujaddid Ad Din Abu Hamid

Muhammad Al Ghazali anasema kua: ‘Ni Makruh kuomba ndani ya Msikiti lakini sio

Sadaqa isipokua pale inapokua Imam anatoa Khutba, na hii hua inakatazwa kwa

sababu wale wanaoomba hua wanafanya lile lililokatazwa na hawatakiwi kusaidiwa

kufanya hivyo.

Ambapo kwa upande wa Imam Zakariyah Al Ansari basi yeye anasema kua: ‘Kuomba

Msikitini haipendekezwi na hua inakirihisha na kuwapa wanaoomba hua kuna

malipo na hakukirihishi bali kuna katazwa, kama alivyosema Imam Al Shafii kua:

‘Kumuomba mtu kwa Jina la Allah au kwa ajili ya Allah kunakirihisha, yaani kwa

mfano kusema; ‘Nakuomba kwa jina la Allah, au Nakuomba kwa ajili ya Allah’ na

hivyo kuwapa watu kama hao wanaosema hivyo hua haipendekezwi’’

3- Inaruhusika Kuomba: Wengi miongoni mwa Wanazuoni wanakubaliana kua

kuomba kwa yule ambae atafanya hivyo kwa ajili ya kutatua matatizo yanayotokana na

kula hasara ya kupoteza Mali au Roho kwa kufiwa au kwa kutakiwa kulipa pesa za fidiya,

au kwa ajili ya kutatua ugomvi baina ya pande mbili, basi hua wanaruhusika kuomba

hadi pale watakapofanikiwa kutatua matatizo yao kama ilivyoelezewa kwenye hadith ya

Qabisah.

Hivyo kutokana na hali hii inayobainisha Ubaya wa kuomba basi Mtu unatakiwa uwe

makini zaid pale unapokua Una jukumu la Kuwalea watoto Mayatima kwani ukifanya

sivyo na kuanza kuomba basi badala ya Kupata Thawabu ya kulea Mayatima basi hua

unapata Dhambi badala yake.

Kwa Upande Mwengine pia ndani yake Jukumu hili pia hua pia inaingia ile hali ya Mtu

Kulea Mtoto wa Ndugu yake, au Baba yake Mdogo au Mama yake mdogo n.k Pale

inapokua Mzee wa Mtoto huyo hana Uwezo wa Kumhudumia Mtoto huyo, na Hivyo Mtu

husika anaechukua Jukumu la Ulezi huamua Kubeba jukumu hilo kwa ajili ya Kumsaidia

Ngugu yake huyo Ulezi wa Watoto wake kutokana na yeye kua na uwezo zaidi yake. Na

ndio maana jana nikasema Kua Mtu asiekua na Uwezo wa Kulea Mayatima basi hatakiwi

Kuikalifisha Nafsi yake kwa kubeba Jukumu asiloliweza kwani atakua anapata dhambi

badala yake.


210

Hivyo asiekua na Uwezo anaruhusika Kulea Yatima Lakini wa Jamaa yake pale inapokua

hakuna Njia nyengine ya kufanya yaani hakuna Mtu mwengine zaid yake na hivyo yeye

atapata Malipo zaid kutoka kwa Mola wake. Kutokana na Kua huo ni Mtihani kwake

ambao inabidi awe na Subra nao kwa Upande mwengine basi Mtu mwenye uwezo

anaruhusika Kubeba Jukumu la Kulea Mtoto iwe ni mwenye Uhusiano nae kama Jamaa

yake ama la.

Hata Kama Mzee wa Mtoto huyo atakua Bado yuko hai au wako hai, Lakini itakua Bora

zaid pale atakapomlea Mtoto ambae Mzee wa Mtoto huyo aliekua hai lakini hana Uwezo

wa Kiuchumi wa Kumlea Mtoto huyo.

Ambapo Jukumu hilo la Kumlea Mtoto huyo hua ni sawa na Uzito wa Jukumu la kumlea

Yatima, Laqit na Munqati, Kwani humbidi kumtekelezea Haki zake zote kama

tulivyoeleza hapo kabla na tunapoangalia Mfano mzuri wa jambo hili basi tunauona

katika tukio alilolifanya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika kipindi cha Uhai

wake kabla ya Kupata Utume wake pale alipoamua kumsaidia ulezi Ami yake yaani Abu

Talib Radhi Allahu Anhu kwa kuamua kumlea Ali Ibn Abu Talib Radhi Allahu Anhu

kama tutakavyoona hapo baadae kwenye kitabu hiki.

HAKI ZA YATIMA, MUNQATI NA LAQIT KATIKA UISLAM

Neno Yatima linatokana na neno Yatama ambalo hua linamanisha Kua Yatima, Kua bila

ya Baba katika wakati ambao mtu hajafikia umri wa miaka 15, Kua bila ya Mama kwa

Mnyama, na kwa upande wa Mwanamke hua ni Yatima pale anapokua hana Mume

kutokana na kua hajafikia Umri wa Kuolewa au Mjane wa Kufiwa na Mumewe au wa

Kuachwa, Kua peke yake, Kufifia, na pia humaanisha kua Mchovu.

Ambapo Imam Raghib Isfahani basi yeye anasema kua: ‘Yatima hua ni Kitu au Mtu

ambae yuko peke yake, alietengwa na hana mtu yeyote. Kwa mfano Durra Al Yatima

hua linamaanisha Lulu kubwa sana iliyoghali na isiyokua na mpinzani kwa

thamani. Na hivyo neno Yatima hua linamaanisha pia Kitu chenye thamani kubwa

zaidi ukilinganisha na vyenzake, Mtu aliewapita wenzake katika mambo

mbalimbali, Mtoto asiekua na Baba hua anaitwa Yatima na Mtoto asiekua na Mama

hua anaitwa Munqati (yaani Mtu aliekatiwa Mama yake)’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala katika ya hii anatuonesha umuhimu na utukufu wa

Yatima ambae hapa anawakilishwa na mtoto wa kike aitwae Maryam Bint Imran ambae

amefiwa na Baba yake, kama vile aliyoelezea kwenye Surat Adh Dhuha kuhusiana na


211

Yatima ambae si mwengine yeyote isipokua Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam

kwa kusema:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٰ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞وَٱلض ُّحَى ٱ ‏۞َو ل ل َّيْ‏ لِإِذَا سَ‏ جَ‏ ٰ ى ‏۞مَا وَد َّ عَكَ‏ رَب ُّكَ‏ وَمَا

قَلَى ٰ ‏۞وَلَلآخِ‏ رَةُ‏ خَيْرٌ‏ ل َّكَ‏ مِنَ‏ ٱلأُولىَٰ۞وَلَسَوْفَ‏ يُعْطِيكَ‏ رَب ُّ ‏َك

فَتَرْضَى ٰ ‏۞أَلمَْ‏ يجَِ‏ دْ‏ ‏َك

يَتِيماً‏ فَآوَىٰ‏ ‏۞وَوَجَدَكَ‏ ضَآلاًّ‏ فَهَدَىٰ‏ ‏۞وَوَجَدَكَ‏ عَآئِلاً‏ فَأَغْنىَٰ‏ ‏۞فَأَم َّا ٱلْيَتِيمَ‏ فَلاَ‏

تَقْهَرْ‏ ‏۞وَأَم َّا ٱلس َّآئِلَ‏ فَلاَ‏ تَنْهَرْ‏ ‏۞وَأَم َّا بِنِعْمَ‏ ةِ‏ رَبِّكَ‏ فَحَ‏ دِّثْ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi, Waaldhdhuha; Waallayli idha saja, Ma

waddaAAaka rabbuka wama qala; Walal-akhiratu khayrun laka mina al-oola;

Walasawfa yuAAteeka rabbuka fatardha; Alam yajidka yateeman faawa;

Wawajadaka dhallan fahada; Wawajadaka AAa-ilan faaghna; Faamma alyateema

fala taqhar; Waamma alssa-ila fala tanhar; Waamma biniAAmati rabbika

fahaddith(Surat Adh Dhuha 93:1-13)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma. Naapa kwa wakati

wa Dhuha (baina ya Asubuhi na kabla ya Adhuhuri) Na Kwa Usiku unapoingia na

kutulia. Hajakuacha Mola wako wala hajakuchukia; Na kwa hakika yatakayokuja ni

bora kwako kuliko ya Awali yaliyotangulia. Na kwa hakika uwezo kamilifu atakupa

Mola wako na Utaridhika. Jee hakukuona wewe kua ni Yatima akakupa makazi? Na

hakukona wewe kua umepotea akakuongoza? Jee hakukuona wewe huna kitu

akakutajirisha? Hivyo na Yatima usimdidimize. Na mwenye kuomba usimfukuze. Na

kuhusiana na Neema za Mola wako zihadithie.

Ambapo katika Sura hii basi Allah Subhanah wa Ta’ala anaanza na:

ٰ ‏﴿وَٱلض ُّحَى ٱ ‏۞َو ل ل َّيْ‏ لِإِذَا سَ‏ جَ‏ ٰ ى ﴾

Waaldhdudha; Waallayli idha saja (Surat Adh Dhuha 93:1-3)

Tafsir: Naapa kwa wakati wa Dhuha (baina ya Asubuhi na kabla ya Adhuhuri) Na

Kwa Usiku unapoingia na kutulia.


212

Ambapo neno Dhuha ni lenye kutokana na neno Dhahiya lenye kumaanisha Kupigwa na

Nuru ya Mionzi ya Jua, Kudhurika kutokana na Mionzi ya Jua, Kufunuliwa au Kuachiwa

wazi, Kuonekana wazi na Jicho au na Ufaham. Hivyo neno Dhuha linamaanisha Wakati

au Mda unaofuatia mara tu bada ya kuchomoza Jua, Mwangaza Kamili wa Jua, sehemu

ya siku ambayo tayari Jua lishapanda na liko juu.

Na neno Saja hua linamaanisha Kua na Utulivu, Kua Kimya, Kutulia, Kufunikwa,

Kutandazwa kwa kugubikwa na kiza.

Na hivyo basi maneno ya aya 2 hizi yanatubainishia Kiapo cha Allah Subhnah wa Ta’ala

anachokiapia kutokana na Maumbile ya Wakati na umuhimu wa Wakati katika kuwepo

kwake, kwani wakati wa kitu hua ni kulingana na hali ya kuwepo kwake kitu hicho

kulingana na matukio na hali ya mabadiliko ya kitu na ndio maana Shaykh Al Akbar

Muhyi Ad Din Imam Abu Bakr Ibn Arabi Al Maliki Al Qurtubi akasema kua: ‘Wakati

wa kitu hua ni katika kuwepo kwake’.

Hivyo tunapoangalia hali ya mabadiliko ya wakati Uhai wa Ibn Adam hua kama wakati

wa siku mwanzo wake huanzia Asubuhi na mwisho wake hua Usiku, na aya imeainisha

wakati na kubainisha matukio na mabadiliko ya hali ya kimaumbile yanayotokea baina

ya Asubuhi na kabla ya Mchana na Usiku unapoingia na Kiza kinapotanda na kinapotulia,

na hivyo kuwapa viumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala wakati wa kupata utulivu wa

kujipumzisha baada ya matukio ya harakati za kujitafutia Riziki Mchana kutwa.

Na kwa kua Sura hii inamzungumzia Rasul Allahu Salallahu Alayhi wa Salam basi

inatuonesha kua Allah Subhanah wa Ta’ala ameapa kwa wakati kuthibitisha na

kusisitizia umuhimu wa wakati kuainisha mabadiliko ya kimaumbile ya Rasul Allahu

Salallahu Alayhi wa Salam kwa kuanzia na wakati wa Dhuha na hivyo kuwakilisha

kipindi cha wakati wa pirika pirika za maisha ya Utotoni wa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam na kisha ikamalizia na wakati Usiku unapoingia na kutulia kuwakilisha wakati

wa baadae wa Rasul Allah Salallahu A’alayi wa Salam utakavyokua hapa Duniani na

Kesho Akhera, na haya yote yanawekwa wazi na aya zilizomo ndani yake Sura hii

ambapo aya zinendelea kwa kusema:

‏﴿مَا وَد َّعَكَ‏ رَب ُّكَ‏ وَمَا قَلَى ٰ ﴾

Ma waddaAAaka rabbuka wama qala (Surat Adh Dhuha 93:3)

Tafsir: Hajakuacha Mola wako wala hajakuchukia;


213

Ambapo sababu ya kushushwa kwake inaelezewa na hadith ya Jundub Ibn Sufyan Radhi

Allahu Anhu ambae anasema:

‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua anaumwa na hivyo hakua ni mwenye

Kusali Qiyam Al Layl kwa siku 2-3. Kutokana na hali hio basi kuna Mwanamke

alikuja kwake na kumwambia: ‘Muhammad, natumai kua Shaytan wako

amekuacha na kukukimbia, kwa sababu sijamuona mimi karibu yako kwa siku 2-

3 hivi.’(Sahih Muslim)

Na kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye anasema

kua huyu hakua ni Mwanamke yeyote yule isipokua alikua ni Arwa Bint Harb ambae ni

maarufu kama Ummu Jamil ambae ni dada yake Abu Sufyan Radhi Allahu Anhu na ni

mke wa Abu Lahab ambae ni Ami yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Ambapo kwa upande wa Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam Fakhr Ad Din

Al Razi basi yeye anahoji kwa kusema kua: ‘Hivi jee ilikua kuna umuhimu wa Allah

Subhanah wa Ta’ala kusema kua hamchukii Rasul Allah Salallahu Alahyi wa

Salam?’ kisha Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi

anajibu hoja hio kwa kusema: ‘Bila ya shaka La! bali hii ni kutokana na tuhuma

zilizoshutumiwa hivyo imebidi ibainishwe, yaani hii ni kama vile ambavyo mtu

anapoambiwa kua Mfalme anamchukia, hivyo Mfalme anapotaka kulipinga hilo

basi humwambia mtu huyo kua; ‘Hakika mimi sikuchukii wewe wala si sikupendi,

na hivyo karibuni nitakupa darja ambayo itakuridhisha kutokana na kua pamoja

nami.’’

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala anamuahidi Mtume wake Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kwa kumwambia kua:

‏﴿وَلَلآخِ‏ رَةُ‏ خَيْرٌ‏ ل َّكَ‏ مِنَ‏ ٱلأُولىَٰ‏ ﴾

Walal-akhiratu khayrun laka mina al-oola (Surat Ad Dhuha 93:4)

Tafsir: Na kwa hakika yatakayokuja hapo baadae ni bora kwako kuliko ya yale ya

Awali yaliyotangulia hapo kabla.

Na hivyo kuainisha umuhimu wa kua na Subra na kutokata tamaa juu ya kile

anachokitaka ambapo bila ya shaka hii pia ni kwa sababu Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam mwenyewe alikua ni mwenye kupendelea yajayo kesho Akhera ambayo ni

yenye kudumu milele ukilinganisha na ya leo ya mpito ya Kidunia, kwani siku moja

alikua amelala kwenye Jamvi, na kutumia bega lake na mkono wake kua ndio mto wake


214

hivyo aliponyanyuka basi bega lake likawa limefanya alama ya jamvi hilo alilolalia na

akawa anajisugua sugua ili alama hio iondoke.

Hivyo Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu akamwambia Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kama atawaruhusu basi watamtengenezea tandiko laini, na hivyo Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Mimi niifanye nini Dunia hii? Wakati

mfano wangu kwa Dunia hii ni sawa na mpanda Farasi alie safarini katika siku ya

joto kali kisha akafika chini ya mti na kukuta kivuli na hivyo akaamua kupumzika,

na kisha akaondoka kwenye sehemu hio na akaenda zake. ’

Kwani amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

‏﴿زُيِّنَ‏ لِل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ ٱلحَْيَاةُ‏ ٱلد ُّنْيَا وَيَسْخَرُونَ‏ مِنَ‏ ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ وَٱل َّذِينَ‏ ٱت َّقَواْ‏ فَ‏ وْقَهُمْ‏

يَوْمَ‏ ٱلْقِيَامَةِ‏ وَٱهلل َُّ‏ يَرْزُقُ‏ مَن يَشَآءُ‏ بِغَيرِْ‏ حِ‏ سَابٍ‏ ﴾

Zuyyina lilladheena kafaroo alhayatu alddunya wayaskharoona mina alladheena

amanoo waalladheena ittaqaw fawqahum yawma alqiyamati waAllahu yarzuqu

man yashao bighayri hisabin (Surat Al Baqara 2:212)

Tafsir: Yamependezeshwa kwa waliokufuru maisha ya Dunia na yamedharaulishwa

kwa wenye Kuamini, na kwa wale watakao kua na Taqwa basi watakua juu yao katika

Siku ya Malipo, na Allah ni mwenye kumruzuku amtakae bila ya hesabu.

Naam..hiki ni kigongo katika Vigongo Vinavyoumiza wale wenye Akili na kutafakkari,

hivyo kama hujakihisi basi Jipekue ndani ya Moyo wako ili ujijue Imani, Akili na

Ufaham wako umeenda Wapi?

Kwani tunatakiwa tutanabahi ili tufahamu kua Ingawa kweli Sisi tunajihesabu kua ni

Waislam lakini jee Tunapoiangalia Dunia hii tunaionaje? Inatuvutia na Kupendeza

kwenye Macho na Nyoyo zetu au Inadharaulika na kuonekana kua ni Dhihaka kwenye

Macho na Nyoyo zetu?

Ambapo kulingana na Aya basi tunaona kua: Hata waliotangulia walijiona kua Wamefika

hapa Duniani, walikua na Mamlaka makubwa na yenye Nguvu, walikua na Ulinzi

Mkubwa, Majumba Makubwa na Magari ya Kifahari n.k Lakini waliondoka na kuacha

kila kitu hapa hapo Duniani


215

Naam.. Hio ndio Hali ya Wasiojua kua Wakati wao uliopita na waliokua nao si chochote

kwani yote yaliyotokea ndani yake hayana thamani, yenye Thamani ni yale Yajayo katika

Wakati utakaokuja.

Kwani alisema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Ni kawaida ya Ibn Adam

kua ni mwenye kusema: Mali zangu Mali zangu, Lakini Jee Hivi Kuna Mali yako

gani zaidi ya ile ambayo tayari Umeshaila na Kuimaliza? zaidi ya ile ambayo tayari

Umeshaivaa na Imeshachakaa? zaidi ya ile ambayo Umeshaitumia na

Imeshamalizika? Hivyo Kilochobakia hakitakua chako kitakua wengine pale wewe

utakapokua hupo(Sahih Muslim)

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anamthibitishia

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuhusiana na kutimizwa kwa ahadi hio kwa

kumwambia kua:

‏﴿وَلَسَوْفَ‏ يُعْطِيكَ‏ رَب ُّكَ‏ فَتَرْضَى ٰ ﴾

Walasawfa yuAAteeka rabbuka fatardha.(Surat Adh Dhuha 93:5)

Tafsir: Na kwa hakika uwezo kamilifu atakupa Mola wako na kisha Utaridhika

Kwani neno Sawfa ni lenye kutokana na neno Safa ambalo hua linamaanisha Kua na

Harufu, Kua na Subira, Kuakhirisha, Kumpa mtu uwezo kamilifu wa kufanya atakavyo.

Hivyo neno Sawfa hua linamaanisha Ahadi yenye uhakika kamilifu itakayotekelezwa

hapo baadae.

Ambapo Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema

kuhusiana na aya hii kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alioneshwa Hazina

zote ambazo watafunuliwa watu wa Ummah wake baada yake. Jambo hili

lilimfurahisha sana, kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia Aya hii na

akamjengea makasri 1000 Peponi, ambao kila moja likiwa na Mke na wafanya kazi

watakaomfaa yeye.’(Imam At Tabari)

Ama kwa upande wa Bab Al Ilm Amir u Muuminin Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu

basi yeye anasema kua: ‘Hii inamaanisha atapewa Uombezi autakao juu ya Ummah

wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa namna atakavyoridhia’ Bab Al Ilm

Amir u Muuminin Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu alisema pia kua: ‘Watu wa Iraq

walikua wakiichukulia kua aya ya Surat Az Zumar isemayo:’


216

‏﴿قُلْ‏ يٰعِبَادِىَ‏ ٱل َّذِينَ‏ أَسْ‏ رَفُواْ‏ عَلَى ٰ أَنفُسِ‏ هِ‏ مْ‏ لاَ‏ تَقْنَطُواْ‏ مِن ر َّحمَْةِ‏ ٱهلل َِّ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ يَغْفِرُ‏

ٱلذ ُّنُوبَ‏ جمَِيعاً‏ إِن َّهُ‏ هُوَ‏ ٱلْغَفُورُ‏ ٱلر َّحِ‏ يمُ‏ ﴾

Qul ya AAibadiya alladheena asrafoo AAala anfusihim la taqnatoo min rahmati

Allahi inna Allaha yaghfiru aldhdhunooba jameeAAan innahu huwa alghafooru

alrraheemu(Surat Az Zumar 39:53)

Tafsir: ‘Sema: ‘Enyi Waja wangu ambao mliovuka mipaka dhidi ya Nafsi zenu (Kwa

kufanya maasi), msikate tamaa na Rehma za Allah kwani kwa hakika Allah

anasamehe Dhambi zote kwani kwa hakika yeye ni mwingi wa Kusamehe na ni mwingi

wa Rehma’’

Kua ndio tegemeo lao kubwa, lakini sisi Watu wa Ahl Al Bayt tunaamini kua aya

iliyobeba matumaini yote ni ile isemayo: Walasawfa yuAAteeka rabbuka fatardha -

Na kwa hakika uwezo kamilifu atakupa Mola wako na kisha Utaridhika’

Kwani Mbali ya Kua Amir ul Muuminin Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu amesema

kuhusiana na aya hii ya 6 kua inabashiria kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

Atapewa Nafasi Kamilifu ya kuuombea Ummah wake katika siku ya Malipo pale

atakapokua katika Mahal Al Shufaa.

Lakini pia kwa upande mwengine basi anasema Imam Abu Muhammad Abd Allah Sahl

Al Tustari kua: ‘Aya Hii inamaanisha Kua Allah Subhanah wa Ta'ala amemridhia

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Hivyo katika Siku ya Malipo atampa pia

Darja ya Kipekee ambayo ni ya kua katika sehemu inayojulikana kama Mahal Al

Shafaa katika Darja ya Maqaman Mahmudan’

Kwani Maqaman Mahmudan hua inamaanisha Sehemu Tukufu kuliko zote kufikika kwa

Ibn Adam ambayo hakuna atakaeweza kuifikia isipokua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kwani sehemu ya Daraja hio hua ni katika Upande wa Kulia wa Arshi ya Allah

Subhanah wa Ta'ala.

Ambapo neno Maqaman hua ni lenye Kutokana na neno Qama ambalo hua linamaanisha

Kusimama, Kunyanyuka, Kutulia tuli katika hali ya kusimama, Kustahmili, Kunyanyuka

kwa heshima.

Hivyo Neno Maqam hua linamaanisha Kukaa au Kusimama Katika sehemu fulani au

katika Darja fulani.


217

Na Neno Mahmuda hua ni lenye kutokana na neno Hamida ambalo humaanisha Kusifu,

Kutukuza, Kushukuru kutokana na sifa na Darja ya Anaeshukuriwa.

Neno Hamida ndio lilolotoa Hamd ambalo hua ni lenye kutumika kwa Ajili ya Allah

Subhanah wa Ta'ala katika kuonesha Shukran, Utukufu na Unyenyekevu Kuelezea

Upekee anaostahiki Kushukuriwa Allah Subhanah wa Ta'ala.

Hivyo neno Mahmuda hua linamaanisha Mwenye kusifika kwa Sifa Nzuri na

Kuheshimika. Na neno Mahmud ndio lililotoa Jina Muhammad ambalo ni la Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam lenye kumaanisha Mwenye Sifa Nzuri na Heshima Kubwa.

Ambapo amesema Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kuhusiana na

Maqaman Mahmudan kua: ‘Ni Darja ambayo atapewa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam katika siku ya Malipo, ambayo hii ni siku ambayo Watu watakua kama

walivyozaliwa bila ya nguo wala viatu, huku wakiwa wanasubiri kuhesabiwa Amali

zao. Halafu baada ya kusubiri baada ya mda mrefu, basi Rasul Allah Salallahu Alayi

wa Salam ataruhusiwa kuwaombea watu wake, hii sehemu atakayosimama

kuwaombea watu wake ndio inajulikana kama Maqaman Mahmuda’

Hivyo basi kwa maana hio basi aya hii pia hua inamaanisha kua Allah Subhanah wa

Ta'ala anamwambia Mtume wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kile

nilichokutayarishia Ewe Muhammad ni bora kuliko ulichonacho sasa hivi Unabii

wako na Utume wako, kwani mimi nimekutayarishia Mahal Al Shafaa na Maqaman

Mahmudan’

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala anamkumbusha juu ya yale yaliyopita juu yake Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kumwambia kwa njia ya kumhoji na kumthibitishia

hali aliyokua nayo ya Uyatima katika wakati huo wa utotoni mwake na namna Allah

Subhanah wa Ta’ala alivyomsaidia kwa kusema:

‏﴿أَلمَْ‏ يجَِدْكَ‏ يَتِيماً‏ فَآوَىٰ‏ ﴾

Alam yajidka yateeman faawa; (Surat Adh Dhuha 93:6)

Tafsir: Jee hakukuona wewe kua ni Yatima akakupa makazi?

Ambapo katika kuhoji kwake basi Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia neno Yajid

linalotokana na neno Jada ambalo hua linamaanisha Kuona kile kilichopotea, Kupata

Kitu kilichopotea, Kupata Kitu au Kuona. na pia akatumia neno Awa ambalo hua


218

linamaanisha Kuwajibisha au kusababisha kupata sehemu ya Makazi salama na yenye

utulivu, Kutulia, Kustaafu au Kupumzika, Kupata au kupewa Ukaribisho wenye utulivu.

Na hivyo Aya kua ni yenye kumuwekea wazi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alikua chini ya Uangalizi wa Mola wake katika kila hatua ya Maisha yake kuanzia katika

kipindi ambacho alipofiwa na Baba yake kabla ya kuzaliwa kwake an hivyo kua ni

Yatima, na akalelewa na Mama yake chini ya usimamizi wa Babu yake na kisha kufiwa

na Mama yake alipokua na umri wa miaka 6 na alipofiwa na Babu yake huyo alipokua

na umri wa miaka 8 na hivyo akalelewa na Ami yake, na pia pale alipofariki watu wa

Makkah walipotaka kumuua na Allah Subhanah wa Ta’ala akampa Awa katika Mji wa

Madinah .

Na hivyo pia aya ni kutuwekea wazi umuhimu wa Mayatima kua ni wenye kustahiki

kupata Awa yaani Kupewa sehemu ya Makazi, Kupewa sehemu ya kukaribishwa kuishi

ili apate utulivu asijihisi mnyonge au yuko peke yake au anaonewa kwa sababu mzee

wake hayuko n.k. kama tunapoona katika mfano wa hadith ifuatayo:

Anasema Mujaddid Ad Din Al Hafidh Imam Shihab ad Din Imam Ibn Hajar Al Asqalani

kua: ‘Siku moja baada ya Salat al Idd basi Rasul Allahi Salallahu Alayi wa Salam

alikutana na Mtoto (Zuhayr Al Saghir) ambae alikua amevaa nguo mbovu mbovu,

huku akiwa amekaa peke yake analia, wakati watoto wengine wakiwa wanacheza

kwa furaha. Hivyo Rasul Allah Sallallahu Aalayhi wa Salam akamkaribia Mtoto

huyo na kumwambia: ‘Mbona umekaa peke yako huku ukiwa unalia? Kwa nini

huendi kucheza na wenzako?’

Yule Mtoto ambae alikua hajui kua Mtu anaezungumza nae kua ni Rasul Allah

Saalallahu Alayhi wa Salam huku akiwa na kilio cha kwikwi akasema: ‘Oh..Sayyid,

hakika mimi Baba yangu amefariki, na Mama yangu ameolewa tena na Mume

mwengine, ambapo Baba yangu wa Kambo amenifukuza Nyumbani kwake, hivyo

nna njaa, sina nguo wala makazi, na leo hii nnaona wenzangu wakiwa na Wazee

wao jambo ambalo imenikumbushia Baba yangu ndio maana nikawa nnalia’

Baada ya kusikia maneno hayo ya Zuhayr Al Saghir basi Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akatokwa na machozi na kumkumbatia Mtoto huyo na kisha

akabusu kichwa chake na kumwambia: ‘Ewe Mtoto Mdogo, usiwe na huzuni kwani

unaweza kuniita mimi kua ni Baba yako, na Aisha ni Mama Yako, Ali kama Ami

yako, Hasan na Husein kama ndugu zako na Fatma kama Dada yako.’

Hapo uso wa Zuhayr Al Saghir ukang’ara kwa Nuru ya furaha, kutokana na kua

tayari ni mwenye kuingizwa kwenye familia ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam. Akachukuliwa hadi nyumbani kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akamvisha Nguo nzuri na wakala pamoja nae, kisha Zuhayr Al Saghir akatoka na


219

kuenda kucheza na watoto wenzake ambao walishangaa kumuona katika kama hali

hio.

Hivyo nao wakamuuliza: ‘Hapo kabla ulikua unalia na sasa hivi umekua na furaha,

kwanini?’ Zuhayr Al Saghir akajibu: ‘Hapo kabla nilikua nna njaa, lakini sasa hivi

nimeshiba, na nilikua Yatima lakini sasa hivi nna Baba kwani Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam ndie Baba yangu, Aisha ni Mama yangu, Ali ni Ami yangu, Fatma

ni Dada yangu na Hasan na Husein ni ndugu zangu’’ (Asbab Al Wurud - Fat-h Al

Barr)

Naam..hivyo kisha baada ya aya hio ya Surat Adh Dhuha 93:7 basi Allah Subhanah wa

Ta’ala anamhoji tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa njia ya kumthibitishia:

‏﴿وَوَجَدَكَ‏ ضَآلاًّ‏ فَهَدَىٰ‏ ﴾

Wawajadaka dhallan fahada (Surat Adh Dhuha 93:7)

Tafsir: Na jee hakukona wewe kua umepotea akakuongoza?

Ambapo hii ni aya ambayo imetumia neno Dhallan ambalo lina maana kadhaa pia

ikiwemo Kua katika Giza, Kupotea, Kutoweka, Kusahau, Kupotoka, Kuchukuliwa akili

kutokana na mawazo ya kitu fulani, Kupenda kitu na kukifikiria sana.

Na hii ni hali ambayo ilikua kama vile ambavyo alivyokua Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kabla ya kupewa Utume na Mola wake kama inavyoeleza aya ifuatayo:

‏﴿وَكَذٰ‏ لِكَ‏ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ‏ رُوحاً‏ مِّنْ‏ أَمْرَِ‏ مَا كُنتَ‏ تَدْرِى مَا ٱلْكِتَابُ‏ وَلاَ‏ ٱلإِيمَانُ‏

وَلَٰكِن جَعَلْنَاهُ‏ نُوراً‏ ن َّهْدِى بِهِ‏ مَن ن َّشَآءُ‏ مِنْ‏ عِبَادَِ‏ وَإِن َّكَ‏ لَتَهْدِ‏ ۤ ي إِلىَٰ‏ صِرَا ‏ٍط

م ُّسْتَقِيمٍ۞صِرَاطِ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱل َّذِى لَهُ‏ مَا فىِ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَمَا فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ أَلاَ‏ إِلىَ‏ ٱهلل َِّ‏ تَ‏ صِيرُ‏

ٱلأُمُورُ‏ ﴾

Wakadhalika awhayna ilayka roohan min amrina ma kunta tadree ma alkitabu

wala al-eemanu walakin jaAAalnahu nooran nahdee bihi man nashao min

AAibadina wa-innaka latahdee ila siratin mustaqeemin; Sirati Allahi alladhee lahu


220

ma fee alssamawati wama fee al-ardhi ala ila Allahi taseeru al-omooru (Surat Ash

Shura 42:52)

Tafsir: Na kadhalika tumekushushia wewe Ruhan (Wahy au Rehma) kutoka katika

Maamrisho yetu, wakati wewe ulikua hujui ni nini Kitabu wala Imani, lakini sisi

tukaijaalia hii (Qur’an kua) Nuru ambayo kutokana nayo tunamuongoza tumtakae

miongoni mwa waja wetu. Na kwa hakika wewe (Muhammad Salallahu Alayhi wa

Salam) unaongoza (Watu) katika njia iliyonyooka. Njia ya Allah ambae kwake yeye

kuna umiliki wa kila kilichomo Mbinguni na Ardhini. Na kwa hakika kila kitu mwisho

wake kinaenda kwa Allah.

Neno Dhallan kwa upande mwengine hua pia linamaanisha Mti ambao uliokua uko peke

yake Jangwani. Kwani anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi kua: ‘Waarabu walikua wakikuta Mti uko peke yake

katika sehemu ya ardhi basi walikua wakiuita Dhallan na alikua wakiutumia kua

kama ni alama katika njia za safari zao.’

Hivyo kutokana na maana hii basi Allah Subhanah wa Ta’ala alimuita Rasul Allah

Salallahi Alayhi wa Salam Dhallan kwa sababu Rasul Allah Salallahi Alayhi wa Salam

alikua ni mtu ambae katika jamii yake alikua yuko peke yake kivyake vyake katika

kuutafuta ukweli kuhusiana na Mola wake, na alimchagua kua Kiongozi wa Watu na

hivyo yeye kua ni Alama inayoongoza watu njia sahih.

Ambapo tunapolitumia neno Dhallan kwa kumaanisha Kupenda kitu na kukifikiria sana

basi tunaona kua aya inamanisha kua: ‘Jee hatukukuona sisi kua unapenda sana

Uongofu nasi tukakuongoza?’

Ambapo kwa upande wa Shayh ul Islami Imam Muhammad Tahir Ibn Ashur basi yeye

anasema kua: ‘Dhallan hua ni hali ambayo Mtu hua anajihisi kua amepotea na

amechanganyikiwa kiasi ya kua hajui afuate njia gani’

Na kwa upande wa Jarrah Allah Sultan Al Balagha Imam Abu Qasim Al Zamakhshari

kua: ‘Inasemekana kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua pamoja na

watu wake kwa mda wa miaka 40, hivyo kama ikiwa hii inamaanisha kua yeye

hakua ni mwenye kujua kuhusiana na Ilm iliyoshushwa hapo awali katika vitabu

vilivyotangulia basi itakua ni sahih.

Lakini kama itakua inamaanisha kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua

amepotoka na anafuata njia za wazee wake, basi maana hii itakua sio sahih. Na hii

ni kwa sababu Allah Subhanah wa Ta’ala kua ni mwenye kuwaongoza Mitume wake

wote na kuwalinda kutokana na kuabudu Masanam kabla ya hata kuwapa Utume’


221

Na kisha Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kwa kumhoji tena Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kwa njia ya kumthibitishia:

‏﴿وَوَجَدَكَ‏ عَآئِلاً‏ فَأَغْنىَٰ‏ ﴾

Wawajadaka AAa-ilan faaghna (Surat Ad Dhuha 93:8)

Tafsir: Na Jee hakukuona wewe huna kitu akakutajirisha?

Ambapo neno Ailan ni lenye kutokana na neno Ala ambalo hua linamaanisha Kuyumba,

Kugeuka, Kudharau, Kufanya Dhulma, Kufanya Kosa, Kumpa Mtu wakati Mgumu, Kua

na Shida, Kua na Familia kubwa, Kuihudumia Familia, Kumlisha Mtu Masikini.

Ambapo neno Aailan limetumika tena katika ile aya maarufu sana ya Surat An Nisaa

ambayo ni yenye kukataza kua na zaidi ya wake wanne, tunaona kua iliposhuka kukataza

Waislam kua na zaidi ya wake wanne haikukataza kua na Suria bali ilikua ikikhiyarisha

kwa wale watakaokosa kua na uadilifu basi waoe mke mmoja au wabakie na ‘Milk al

Yamin’ (Kilichomo ndani ya umiliki wa kisharia wa mkono wa kulia) yaani wale

wanaomilikiwa baada ya kutekwa vitani au baada ya kua ni miongoni mwa

wanaomilikiwa katika hali ya Utumwa katika wakati huo, hivyo aya hii imesema kua:

ٰ ٱلْيَتَامَى فَٱنكِحُواْ‏ مَا طَابَ‏ لَكُمْ‏ مِّنَ‏ ٱلنِّسَآءِ‏ مَثْنىَٰ‏

‏﴿وَإِنْ‏ خِ‏ فْتُمْ‏ أَلا َّ تُقْسِ‏ طُواْ‏ فىِ‏

‏ٰذلِكَ‏ أَدْ‏ نىَٰ‏

وَثُلاَثَ‏ وَرُابَعَ‏ فَإِنْ‏ خِ‏ فْتُمْ‏ أَلا َّ تَعْدِلُواْ‏ فَوَاحِ‏ دَةً‏ أَوْ‏ مَا مَلَكَتْ‏ أَيمَْانُكُمْ‏

﴾ أَلا َّ تَعُولُواْ‏

Wa-in khiftum alla tuqsitoo fee alyatama fainkihoo ma taba lakum mina alnnisa-i

mathna wathulatha warubaAAa fa-in khiftum alla taAAdiloo fawahidatan aw ma

malakat aymanukum dhalika adna alla taAAooloo. (Surat An-Nisaa’ 4:3).

Tafsir: Na ikiwa mnakhofu kua hamtoweza kuwafanyia haki mayatima, basi oeni

Wanawake wengine mnaowataka, wawili, au watatu, au wanne; lakini ikiwa

mnakhofu kua hamtoweza kuwafanyia uadilifu basi oeni mmoja tu, au wale

mnaowamiliki mikononi mwenu (Mliowateka vitani na Watumwa). Kufanya hivyo hua

ni kukaribia kujilinda kutokana na kutokua waadilifu.


222

Na hivyo basi kwa upande mwengine maneno dhalika adna alla taAAooloo mbali ya

kua hua yanatafsirika Kufanya hivyo hua ni kukaribia kujilinda kutokana na kutokua

waadilifu. Lakini pia hua yanatafsirika kua: Kufanya hivyo hua ni njia bora ya

kujilinda kutokana na kufanya Dhulma. Na vile vile hua pia yanatafsirika kua:

Kufanya hivyo hua ni njia bora ya kujilinda kutokana na kua na familia kubwa.

Na ndio maana ikawa kuna baadhi ya Wanazuoni wakawa wameitafisiri aya hii isemayo:

‏﴿وَوَجَدَكَ‏ عَآئِلاً‏ فَأَغْنىَٰ‏ ﴾

Wawajadaka AAa-ilan faaghna (Surat Ad Dhuha 93:8)

Tafsir: Na Jee hakukuona wewe huna kitu akakutajirisha?

Ambapo hali inayozungumziwa hapa ni hali ya Umasikini aliyokua nayo kabla ya

kuingizwa Bi Khadija Bint Khuwaylid Radhi Allahu Anha ndani ya maisha yake na Allah

Subhanah wa Ta’ala na hivyo kumtajirisha Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, kua

maneno haya pia yanamaanisha pia kua: ‘Jee Hatukukuona wewe ukiwa na familia

kubwa kuihudumia hivyo tukakusaidia kukuongezea baraka?’ na pia: ‘Jee

hatukukuona wewe kua unashida ya Kiroho, Kinafsi kutokana na kutojua ufanye nini

kuhusiana na wayafanyayo watu wako kwa ujahili wao nasi tukakusaidia

kukuongezea Ilm?’

Neno Aailan limetumika tena katika aya ifuatayo pale iliposema:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُو ۤ اْ‏ إِنم ََّا ٱلْمُشْرِكُونَ‏ نجََسٌ‏ فَلاَ‏ يَقْرَبُواْ‏ ٱلْمَسْجِ‏ دَ‏ ٱلحَْرَامَ‏ بَ‏ عْدَ‏ عَامِهِمْ‏

هَٰذَا وَإِنْ‏ خِ‏ فْتُمْ‏ عَيْلَةً‏ فَسَوْفَ‏ يُغْنِيكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ مِن فَضْلِهِ‏ إِن شَآءَ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ عَلِيمٌ‏ حَ‏ كِيمٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo innama almushrikoona najasun fala yaqraboo

almasjida alharama baAAda AAamihim hadha wa-in khiftum AAaylatan fasawfa

yughneekumu Allahu min fadhlihi in shaa inna Allaha AAaleemun hakeemun(Surat

At Tawba 9:28)

Tafsir: Enyi Mlioamini, hakika ya Washirikina ni Najisi hivyo msiwaruhusu

kuukaribia Masjid Al Haram baada ya mwaka huu na kama mtakua mnaukhofia


223

Umasikini, basi Allah atakutajirisheni kutokana na fadhila zake akitaka, Hakika Allah

ni mwenye kujua kila kitu na ni mwenye Hikma nyingi sana.

Hivyo maneno wa-in khiftum AAaylatan yanamaanisha Na kama mtakua mnaukhofia

Umasikini. Ambapo amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakika ya

Utajiri hua ni Utajiri wa Moyo, Na Umasikini hua ni Umasikini wa Moyo.’ Na akasema

tena: ‘Mtu Tajiri hua si yule ambae mwenye Mali nyingi bali ni yule mwenye Moyo

ulioridhika’

Kisha baada ya Allah Subhanah wa Ta’ala kutoa hoja na vithibitisho vyote hivyo vya

yale matukio muhimu sana na mabadiliko yaliyotokea hapo kabla ndani baina ya wakati

wa uhai wake Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam na yatakayotokea baadae kama

alivyoanza mwenyewe Allah Subhanah wa Ta’ala na Waaldhdudha; Waallayli idha

saja yaani Naapa kwa wakati wa Dhuha (baina ya Asubuhi na kabla ya Adhuhuri) Na

Kwa Usiku unapoingia na kutulia.

Na hivyo kutubainishia umuhimu wa wakati kulingana na hali ya matukio na hali ya

mabadiliko ya kitu basi Allah Subhanah wa Ta’ala anamuusia Mtume wake Salallahu

Alayhi wa Salam kuhusiana na Mayatima kama vile ambavyo alivyokua Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam chini ya usimamizi wa Allah Subhanah wa Ta’ala kwa

kusema kua:

‏﴿فَأَم َّا ٱلْيَتِيمَ‏ فَلاَ‏ تَقْهَرْ‏ ﴾

Faamma alyateema fala taqhar .(Surat Adh Dhuha 93:8)

Tafsir: Hivyo na Yatima usimdidimize

Ambapo neno Taqhar linatokana na neno Qahara lenye kumaanisha Kukandamiza,

Kuvunjia Haki, Kudidimiza, Kufanyia au Kuenda kinyume na matakwa, Kudhibiti,

Kuzidi kinguvu, Kua Juu Ya kitu, Kua Katili , Kua mshindi dhidi ya mwengine.

Na hivyo aya kua ni yenye kutuwekea wazi kutowanyanyasa Mayatima, na kutuamrisha

kuwafanyia wema na kua wakarimu nao, ambapo anasema Abu Ummamah Radhi Allahu

Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Yoyote yule atakae

mpapasa kichwa Yatima kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala basi atapata

thawabu kwa kila Nywele utakaokua chini ya Mkono wake, na mimi na mtu huyo

atakaemhurumia Yatima basi tutakua kama hivi (kisha Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akabana kidole chake cha kati na cha shahada na kuwaonesha

Masahaba zake) Peponi’’


224

Na kutokana na Hadith hii basi Abd Alla Ibn Umar Radhi Allahu Anhu akawa kila siku

akikutana na Yatima basi humpapasa kichwa chake na kumpa kitu chochote kizuri

alichokua nacho.

Na pia anasema Al Hasan kua: ‘Kila wakati ilipokua Abd Allah Ibn Umar Radhi

Allahu Anhu anakula basi alikua anawaita Mayatima wote wa Mtaa wake, kiasi ya

kua siku moja wakati anajitayarisha kula basi akamwambia Mtumwa wake kua

amuitie Mayatima wote wa mtaani, ambapo Yatima mmoja akakosekana kwani

alikua hayupo. Hivyo Mayatima waliokuwepo wakakaa na Abd Allah Ibn Umar

Radhi Allahu Anhu na wakaanza kula’

‘Na kila siku baada ya kula basi Abd Allah Ubn Umar Radhi Allahu Anhu alikua

akipewa Sharbati tamu sana aliyokua akiipenda. Hivyo katika siku hio Abd Allah

Ibn Umar Radhi Allahu Anhu akala na Mayatima wake chakula chote hadi

wakamaliza. Kisha baada ya kumaliza Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu

akachukua Bilauri akawa anataka kunywa Sharbati yake na mara akatokea yule

Yatima ambae alikua akitafutwa na akawa haonekani Hivyo Abd Allah Ibn Umar

Radhi Allahu Anhu alipomuona Yatima huyo basi akarudisha chini bilauri hio ya

Sharbati na kisha Akampa Yatima huyo huku akimwambia: ‘Kunywa hii kisha

mimi ndio nitajua kua sikukufanyia Taqhar.’

Na Allah Subhanah wa Ta'ala ameusia kuhusiana na Mayatima na Kutonyanyaswa kwa

sababu si tu kuwanyanyasa na kuwakandamiza hua ni sawa kukadhibisha Dini kama

tulivyoona kwenye Surat Al MaAu'n.

Lakini Kutowanyanyasa Mayatima hua ni sawa na kua na Taqwa na Kumpenda Allah

Subhanah wa Ta'ala na Mtume wake Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo hua ni sifa ya

Watu wa Peponi, Kwani mongoni mwa Watu wa Peponi ni wale watu ambao Allah

Subhanah wa Ta'ala amewataja kwenye Qur'an kwa kusema:

‏﴿إِن َّ ٱلأَبْرَارَ‏ يَشْرَبُونَ‏ مِن كَأْسٍ‏ كَانَ‏ مِزَاجُهَا كَافُوراً۞عَيْناً‏ يَشْرَبُ‏ هبَِ‏ ا عِبَادُ‏ ٱهلل َِّ‏

يُفَجِّ‏ رُونَهَا تَفْجِ‏ يراً۞يُوفُونَ‏ بِٱلن َّذْرِ‏ وَيخََافُونَ‏ يَوْماً‏ كَانَ‏ شَر ُّهُ‏ مُسْتَطِير اً‏ ﴾

Inna al-abrara yashraboona min ka/sin kana mizajuha kafooran; AAaynan

yashrabu biha AAibadu Allahi yufajjiroonaha tafjeeran; Yoofoona bialnnadhri

wayakhafoona yawman kana sharruhu mustateeran; (Surat Al Insan 76:5-7)


225

Tafsir: Hakika ya Waja Wema Watakunywa Kutoka kwenye Gilasizenye Maji kutoka

Katika Mto wa Peponi wa Kafuran. (Kafura ni) Chemchem Watakazokunywa

Kutokana nazo Waja wa Allah na Kuyasababishia Maji hayo Matamu Kutoka kwa

Kufoka kwa wingi bila ya kua na upungufu wala mwisho wake. Hao ndio Wale Ambao

waliotekeleza Nadhiri na Ahadi zao Na wakawa na Khofu na Siku Ambayo Itakua

Shari yake ni Iliyoenea na Kutapakaa.

Ambapo aya zinatubainishia kua Miongoni mwa watu wenye Sifa za kua ni Waja Wema,

basi ni wale wenye Sifa za kua ni wenye kutekeleza Nadhiri na Ahadi zao, kutokana na

kumuogopa Allah Subhanah wa Ta'ala na kuiogopa Siku ya Malipo siku ambayo Ubaya

au Shari yake itakua ni Kubwa na nzito kuliko Kheri yake

Kwani hii ni siku ya Malipo ambayo Watu watakimbiana Baba atamkimbia Mama na

Watoto wake, Mama atawakimbia Watoto wake, Ndugu atawakimbia Ndugu zake na kila

anaekimbia wenzake basi na yeye hua anatafutwa na kufukuziwa na hao anaowakimbia,

kwani kila mtu anataka kuiokoa Nafsi yake, kutokana na kujua kua yule anaemkimbia

ndie aliekua na jukumu la kumsimamia lakini hakumsimamia kwa hivyo atamkimbilia ili

amlaumu na kumdai kua ampunguzie Uzito wa Madhambi yake kwa kutotekeleza

majukumu yake Juu yake katika kumsimamia kwake.

Hivyo bila ya shaka siku hio, shari yake itakua ni Mustatiiran yaani itaenea kila shemu

na kwa kila mtu kama nuksi au laana fulani na hivyo kila mmoja atakua anaona tafrani

kutokana na uzito wa Mashakil yake..Ya Allah tustiri na Mitihani ya Siku hio ambayo

Sharruhu Mustatiiran..Amiin

Kwani ingawa hali itakua hivyo kwa wengi lakini kwa wachache haitokua hivyo na

wachache hao ni wale ambao Waja wema wenye sifa ya kua ni Abrar, wenye sifa ya kua

ni wenye Kutimiza Ahadi zao, Nadhiri zao, wenye sifa ya kutumia kwa kutoa Neema

walizoneemeshwa na Mola wao, mbali ya kua wanazipenda Neema hizo, lakini

wakadhihirisha Mapenzi yao kwa Mola wao kwa kuzitoa Neema hizo kwa ajili ya Mola

wao kwa kuwasaidia Masikini, Mayatima na Asir yaani Wasiokua huru.

‏﴿وَيُطْعِمُونَ‏ ٱلط َّعَامَ‏ عَلَى ٰ حُبِّهِ‏ مِسْكِيناً‏ وَيَتِيماً‏ وَأَسِ‏ يراً‏ ﴾

WayutAAimona alttaAAama AAala hubbihi miskeenan wayateeman waaseeran

(Surat Al Insan 76:8)

Tafsir: Na Wakawa ni Wenye Kuwalisha Chakula kwa kutokana na mapenzi ya

Kumpenda kwao Allah Subhanah wa Ta’ala, kwa kuwasaidia Masikini Mayatima na

Mateka.


226

Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Sadaqa Bora hua ni ile

ambayo unayoitumia wakati ukiwa na Afya Njema, Wakati ukiwa unaipenda Mali

Yako na Huku Ukiwa Unakhofia Umasikini’

Ambapo Jarah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari anasema kua: ‘Ndani ya maana

ya neno Asir yaani Wafungwa, Mateka au wasiokua huru basi wanaingia pia wale

ambao wamefungika kwa Matatizo ikiwemo wenye Madeni.’

Kwani Allah Subhanah wa Ta'ala anaendelea kutueleza kuhusiana na hao wanaosaidia

Masikini, Mayatima na Wenye Matatizo ya kutokua huru kwa kuwapa msaada kwa

Ikhlasi kua hua ni sawa na wenye kusema:

‏﴿إِنم ََّا نُطْعِمُكُمْ‏ لِوَجْهِ‏ ٱهلل َِّ‏ لاَ‏ نُرِيدُ‏ مِنكُمْ‏ جَزَآءً‏ وَلاَ‏ شُكُوراً۞فَوَقَ‏ اهُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ شَر َّ ذٰلِكَ‏

ٱلْيَومِ‏ وَلَق َّاهُمْ‏ نَضْرَةً‏ وَسُرُوراً۞وَجَزَاهُمْ‏ بمَِا صَبَرُواْ‏ جَن َّةً‏ وَحَرِيراً‏ ﴾

Innama nutAAimukum liwajhi Allahi la nureedu minkum jazaan wala shukooran;

Inna nakhafu min rabbina yawman AAaboosan qamtareeran; Fawaqahumu

Allahu sharra dhalika alyawmi walaqqahum nadhratan wasurooran(Surat Al Insan

76:9-11)

Tafsir: (Wanasema) ‘Hakika ya kukusaidieni kwetu ni kutokana na kutaka hesabu

kwa Allah, kwani sisi hatutaki Kutoka kwenu Malipo wala Shukurani; Kwani kwa

hakika sisi tunakhofia kutoka kwa Mola wetu siku ambayo ni nzito itakayozifanya

Nyuso kua na muonekano mbaya kabisa’; Hivyo Allah atawaokoa Watu hao na shari

ya Siku hio na kuwapa Muonekano wenye Nuru na furaha( katika siku hio)

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala anamuusia tena Mtume wake Salallahu Alayhi wa

Salam kuhusiana na kuwajali Masikini wasiokua na kitu, kama vile ambavyo alivyokua

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kabla ya kumuoa bi Khadija Radhi Allahu Anha

kwa kusema kua:

‏﴿وَأَم َّا ٱلس َّآئِلَ‏ فَلاَ‏ تَنْهَرْ‏ ﴾

Waamma alssa-ila fala tanhar; (Surat Adh Dhuha 93:10)

Tafsir: Na mwenye kuomba usimfukuze.


227

Ambapo neno Tanhar limetokana na neno Nahara ambalo hua linamaanisha

Kusababisha Mchirizi, au Njia ya Maji au Mkondo wa Maji kupita katika nja yake.

Kutiririka bila matatizo, Kukukemea, Kufukuza, Kukasirikia na pia humaanisha Kufanya

kitu katika wakati wa Mchana.

Na mbali ya kua wengi wanaitumia aya hii kwa ajili ya watu wanaoomba kuhusiana na

rizki zao, lakini aya pia aya hii inawazungumzia wale ambao ni wenye kuomba kuhusiana

na yale wasiyoyajua kuhusiana na Ilm ya Dini yao, kwani amesema Allah Subhanah wa

Ta’ala kua:

‏﴿إِن َّ ٱل َّذِينَ‏ يَكْتُمُونَ‏ مَآ أَنزَلْنَا مِنَ‏ ٱلْبَيِّنَاتِ‏ وَٱلهُْدَىٰ‏ مِن بَعْدِ‏ مَا بَي َّن َّاهُ‏ لِلن َّاسِ‏ فىِ‏

ٱلْكِتَابِ‏ أُولَٰئِكَ‏ يَلعَنُهُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ وَيَلْعَنُهُمُ‏ ٱللا َّعِنُونَ۞إِلا َّ ٱل َّذِينَ‏ ‏َاتبُواْ‏ وَأَصْ‏ لَحُواْ‏ وَبَي َّنُواْ‏

فَأُوْلَ ئِ‏ كَأَتُوبُ‏ عَلَيْهِمْ‏ وَأََ‏ الت َّو َّابُ‏ الر َّحِ‏ يمُ‏ ﴾

Inna alladheena yaktumoona ma anzalna mina albayyinati waalhuda min baAAdi

ma bayyannahu lilnnasi fee alkitabi ola-ika yalAAanuhumu Allahu

wayalAAanuhumu allaAAinoona; Illa alladheena taboo waaslahoo wabayyanoo

faola-ika atoobu AAalayhim waana alttawwabu alrraheemu (Surat Al Baqara 2:159-

160)

Tafsir: Hakika ya wale ambao wamekaa kimya kuhusiana na walichoshushiwa

kutokana na ubainisho na uongofu baada ya kua tumewawekea wazi ndani ya kitabu

basi hao wamelaaniwa na Allah na wamelaaniwa na wenye kulaani. Isipokua wale

ambao watatubu na wakafanya mema na wakabainisha (kile walichokificha), hivyo

hawa ndio nitakaowakubalia toba zao na kwa hakika mimi ni mwingi wa kusamehe

na ni mwingi wa huruma.

Na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Yeyote yule atakaeulizwa kuhusiana

na Mada na llm na yeye akawa anajua kuhusiana nayo kisha akaificha basi katika

Siku ya Malipo atafungwa hatamu ya Moto mdomoni mwake.

Na ndio maana Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu akasema kua: ‘Kama hii ingekua sio

aya ya Qur’an basi nisingenukuu hadithi yeyote’

Na akasema Imam Abu Hanifa kua: ‘Anapokujia Mtu mwenye kuomba kutaka kujua

kuhusiana na Ilm ya Dini yake basi Mtu huyu unatakiwa umpokee kwa

kumtandikia Zulia la Dhahabu chini ya miguu yake.’


228

Ambapo hata hivyo basi sio kila aina ya Ilm unakua ni mwenye kuitoa kwa sababu ya

kua unayo, kwani baadhi ya wakati unaweza ukasababisha madhara kwa wasiofaham na

kwa baadhi wanaweza wakawa hawakuamini, kama alivyosema Abd Allah Ibn Masud

Radhi Allahu Anhu kua: ‘Haiwezekani kua usitoe Ilm kwa wale wasiopea kilm na

kiufaham miongoni mwao isipokua watakua na shaka juu yake’

Na akasema Ali Ibn Abi Talib Radhi Allah Anhu kua: ‘Zungumza Na watu kulingana

na Uwezo wa Ufaham wao, au unataka Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume wake

Salallahu Alayhi wa Salam wakanushwe?’

Ambapo tunapozungumzia kuhusiana na upande wa wanaoomba Riziki basi Imam

Ibrahim An Nakhai amesema kua: ‘Waombaji ni wafanyakazi wa Posta wa Akhera,

ambao hua wanakuja kwenye Mlango wako na kusema: ‘Hivi Jee kuna kitu

chochote kile ambacho unataka kukituma Akhera?’’

Ambapo kwa upande mwengine basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua

akiwapa vitu watu wanaoomba kwa ustaarabu na pia alikua akiwapa wale wanaoomba

kwa kukirihisha, kwani alikua akisema kua: ‘Wamenifanya mimi nichague baina ya

kutoa vitu vizuri na baina ya kua bakhili kwa kutumia maneno yanayokirihisha,

wakati mimi si bakhili.’

Na Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al

Qurtubi amesema kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

Wapeni Msikini japo kidogo pale wanapoomba, au waondoeni kwa maneno mazuri,

kwa sababu inawezekana Masikini huyo akawa ni Malaika wa Allah Subhanah wa

Ta’ala amekuja kukujaribuni namna mnavyotumia neema mlizoneemeshwa na

Allah Subhanah wa Ta’ala’

Na akasema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Yeyote yule atakeotoa kwa

ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala kitu atakachoombwa basi Allah Subhanah wa

Ta’ala atamuandikia Thawabu 70 kwa alichotoa’ na pia akasema kua ‘Mtu

atakaeomba kwa kusema kua anaomba kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala basi

hua amelaaniwa. Na mtu atakaemkatalia mtu anaeomba kwa kusema kua anaomba

kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala basi hua amelaaniwa pia, kwani mtu huyo

atakua amefanya Uovu’ kwani: ‘Ni Pepo tu pekee ndio inayoombwa kwa ajili ya

Allah Subhanah Wa Ta’ala’(Fatawa Al Hindi)

Ambapo maneno haya ya Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam yanamaanisha

kua: Haitakiwi kua Mtu aombe kitu kwa kuapa kwanza kwa jina la Allah Subhanah

wa Ta’ala au kwa kutumia kisingizio cha jina la Allah Subhana wa Ta’ala kua

anaomba kitu Fulani kutokana na shida aliyokua nayo, na mtu atakaemkatalia mtu

huyo mwenye kuomba kwa anjia hio hua amelaaniwa kwa sababu hua ni mwenye


229

kukataa kufanya jambo la kutoa msaada kwa ajili ya Allah Subhana wa Ta’ala

wakati anao uwezo wa kusaidia.

Kwani amesema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakika Malaika Jibril amenishushia mimi kwenye

Moyo wangu kua, hakuna Nafsi itakayokufa hadi pale itakapokua Nafsi hio

imemaliza Riziki yake iliyopangiwa, hivyo muogopeni Allah na tafuteni Riziki zenu

kwa njia njema, kama ikiwa Riziki imekawia basi basi msiitafute kwa kutumia njia

zitakazopelekea kumuasi Allah, kwa sababu Riziki kutoka kwa Allah hua kamwe

haiwezekani kupatikana kwa njia yeyote ya kumuasi kwake.’’(Al Targhib wa Al

Tarhib)

Na ingawa kuna vithibitisho hivyo lakini hata hivyo inabidi tujue kua Waombaji hawa

waliokusudiwa hapa sio wale ambao wanapita katika Maduka kila Ijumaa kwa ajili ya

kuomba, au wanapita katika kila mlango kwa ajili ya kuomba, au wanaosimama

mabarabarani kwa ajili ya kuomba, kwani hawa sio waliokusudiwa hapa kwa sababu ni

masikini kwa sababu unakuta mtu kijana na nguvu zake anapita akiomba, na kuna

wengine wanawake wari hawana kazi yeyote isipokua kuomba yaani imekua ndio ajira

yao ya kujitafutia maisha.

Ambapo amesema Abu Dardaa Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah

Salallahu Alyhi wa Salam kua: ‘Bila ya Shaka Riziki ya Mtu hua ni yenye kumfuata

Mtu kama vile ambavyo Kifo kinavyomfuata Mtu husika’’ (Al Targhib wa Al Tarhib)

Na akasema Abu Said Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallah Alyhi

wa Salam kua: ‘Hata kama mtu atakua ni mwenye kuikimbia Riziki yake basi Riziki

yake hio itamkuta tu kama vile kitakavyomkuta Kifo chake’’(Al Targhib wa Al

Tarhib)

Na akasema Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alipata Tende, ambapo akatokea Masikini akamuomba na akampa Tende

hio huku akisema kwa kumwambia: ‘Angalia kwani kama hii hukuifuata basi

ingekufuata wewe’’

Hivyo tunapozungumzia kuhusiana na Waombaji yaani wenye shida kutokana na

kutokua na uwezo, basi Qur’an imewalezea kwa kutumia maneno mawili ambayo ni

Fuqara na Masaakin ambayo ingawa ni tofauti lakini hata hivyo hua yanaingiliana

kimaana.

Kwani neno Fuqara hua ni lenye kutokana na neno Faqura ambalo hua linaaamansha

Mtu Aliekua Maskini, Mtu Mwenye Shida Kubwa na Nyingi sana. Hivyo neno Fuqara

hua linatumika kumaanisha Mtu ambae anawategemea watu wengine kwa ajili ya


230

mahitajio yake ya kimaisha kutokana na sababu mbali mbali za kimaumbile ikiwemo

Uzee, Ulemavu au kutokana na mitihani mbali mbali ya kimaisha, na ndio maana neno

Faqira hua pia linamaanisha Kuzidiwa na Mithani ambayo huweza kumpelekea Mtu

kuhisi uzito wa maumivu ya Mtihani huo ndani ya Uti wa Mgongo, na neno Faqiratun

hua linamaanisha Mtihani wa Kuvunjika Mgongo.

Ambapo kwa upande wa neno Masakin hua linatokana na neno Sakana ambalo hua

linamaanisha Kutulia, Kukaa Kimya, Kusimama tulii. Hivyo neno Masakin hua

linamaanisha Mnyenyekevu, Mtulivu, Masikini, Mtu anaestahiki kusaidiwa kutokana na

Udhaifu au Unyenyekevu wake.

Neno Sakana ndio pia lililotoa neno Sikin yaani Kisu ambacho Kimeitwa hivyo kwa

sababu Kisu ndio chanzo cha Kukifanya Kiumbe Kitulie baada ya Kuchinjwa kwake.

Ambapo kwa upande wa Imam Muhyi Ad Din Imam Abu Zakarriyah Yahyah Sharaf An

Nawawi basi yeye anasema kua: ‘Maneno haya mawili Fukara na Masakin hua yana

maana moja yanapokua yametumika katika sehemu tofauti, lakini yanapotumika

katika sehemu moja hua yana maana tofauti.’

Na Wanazuoni wametofautiana katika maana ya maneno haya mawili kutokana na

yalivyotumika hapa kwani kwa upande wa Wanazuoni wa Madhhab ya Imam

Muhammad Idris Al Shafii na wafuasi wa Madhhab ya Imam Ahmad Ibn Hanbal basi

wao wanasema kua: ‘Fukara hua ni tu mwenye shida zaidi kuliko Masikini na hii ni

kutokana na mpangilio wa maneno haya yaliyotajwa kwenye aya hii, kwani

mwanzo ametajwa Fukara na kisha baadae ndio akatajwa Masikini.’

Na kwa upande wa Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Abu Hanifa na Madhhab ya Imam

Malik Ibn Anas basi wao wanasema kua: ‘Maskini ndie mwenye shida zaidi kuliko

Fukara.’

Kwa kumalizia kuhusiana na Fukara na Masikini basi tunaona kua:

Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Abu Hanifa basi wao wanafafanua maana mbili hizi

kwa kusema: ‘Masikini hua ni mtu ambae hana kitu kabisa. Fukara hua ni mtu

ambae anacho kitu kidogo ambacho hata hivyo hakimtoshi kwa mahitaji yake ya

kila siku.’

Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Malik Ibn Anas basi wao wanafafanua maana mbili

hizi kwa kusema: ‘Masikini hua ni mtu ambae hana kitu kabisa na hivyo hua

anaomba watu msaada. Fukara hua hana kitu hata kidogo lakini hata hivyo haombi

kwa watu.’


231

Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Muhammad Idris Al Shafii basi wao wanafafanua

maana mbili hizi kwa kusema: ‘Fukara hua ni mtu ambae hana kitu kabisa. Maskini

hua ni mtu ambae anacho kitu kidogo ambacho hata hivyo hakimtoshi kwa mahitaji

yake ya kila siku.’

Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Ahmad Ibn Hanbal basi wao wanafafanua maana mbili

hizi kwa kusema: ‘Fukara hua ni mtu ambae hana hata kitu kitachomtosheleza hata

nusu ya mahitaji yake. Maskini hua ni mtu ambae anacho kitu kidogo ambacho ni

zaidi ya nusu ya mahitaji yake na hivyo hua hakimtoshi kwa mahitaji yake ya kila

siku.’

Naam, tunarudi kwenye aya yetu ya mwisho ya Surat Adh Dhuha ambapo tunaona kua

Allah Subhanah wa Taa’ala baada ya kumtolea hoja na vithibitisho Mtume wake

Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam na kumuuisia basi anamwambia

‏﴿وَأَم َّا بِنِعْمَ‏ ةِ‏ رَبِّكَ‏ فَحَدِّثْ‏ ﴾

Waamma biniAAmati rabbika fahaddith .(Surat Adh Dhuha 93:11)

Tafsir: Na kuhusiana na Neema za Mola wako zihadithie.

Anasema Abu Al Ahwas kua amesema Baba yake kua: ‘Mimi nilikua nimekaa na Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam na akaniona kua nimevaa nguo chakavu, hivyo

akaaniuliza: ‘Hivi Jee wewe huna pesa?’ nami nikasema: ‘Nnazo nyingi tu’ Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaniambia : ‘Wakati Allah Subhanah wa Ta’ala

anapokujaalia kitu basi wacha athari yake ionekane juu yako.’’(Imam Abu Abd Allah

Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi)

Na amesema Imam Muhammad Ibn Jarir At Tabari kua: ‘Tangu enzi za zamani sisi

tumesikia kutoka kwa Waislam kua moja kati ya njia ya Kumshukuru Allah

Subhanah wa Ta’ala ni kutangazia Neema hizo.’

Ambapo siku moja Imam Abu Firas Abd Allah Ibn Ghalib Al Huddani Al Basri alisema

kumwambia rafiki yake: ‘Alhamd lillah Hakika mimi nimesali sana na nimesoma

sana Qur’an pia’ hivyo Rafiki yake huyo akasema: ‘Hivi inakuaje mpaka mtu kama

wewe anakua anasema kama hivyo?’ hivyo Abu Firas Abd Allah Ibn Ghalib Al

Huddani Al Basri akasema: ‘Bila ya Shaka kwani Allah Subhanah wa Ta’ala

amesema:’ Waamma biniAAmati rabbika fahaddith’


232

Ambapo anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al

Ansari Al Qurtubi kua: ‘Kusema Allahu Akbar baada ya kusoma Surat Adh Dhuha ni

Sunnah na hii ni kwa sababu amesema Imam Muhammad Idris Al Shafii kua:

‘Inapendekezwa baada ya kusoma Sura hii basi Mtu na aseme Allahu Akbar!’na

kuna wasemao kua inapendekezwa kusema: ‘Allahu Akbar, La ilaha illa Allahu, Allahu

Akbar.’

Na amesema Imam Ibn Muflih Al Hanbali kua: ‘Imam Ahmad anachukulia kua ni

jambo lenye kupendekezwa kusema Takbir kuanzia baada ya mwisho wa Surat Adh

Dhuha mpaka mwishoni mwa kila Sura za mwishoni wa Qur’an. Na hii imetajwa

na Ibn Tamim na wengineo, na hii ni namna walivyokua wakisoma watu wa

Makkah ambapo Imam Ul Qiraah Abu Hasan Muhammad Ibn Ahmad Al Bazzi

amenukuku kutoka kwa Ibn Kathir ambae nae amenukuu kutoka kwa Mujahid

ambae nae amenukuu kutoka kwa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu ambae

nae amenukuu kutoka kwa Ubbay Ibn Qaab Radhi Allahu Anhu ambae nae

amenukuu kutoka kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ’ na pia kuhusiana na

jambo hili basi amesema Imam Abu Abdullâh Muḥammad Ibn Abdullah Al Hakim

katika Mustadrak Al Hakim na Imam Abū Muḥammad Al Ḥusayn Ibn Masʻūd Ibn

Muḥammad Al Farrā' Al Baghawi pia.

Ambapo kwa upande mwengine tunapoiangalia Qur’an basi tunaona kua inaelezea visa

vya Mitume ambao waliokua pia na sifa ya Laqit. Ambapo neno Laqit linatokana na neno

Laqatta ambalo hua linamaanisha Kitu Kilichookotwa, Kitu kilichokusanywa baada ya

kuanguka, Kitu kilichochukuliwa, Mabaki ya Punje za Nafaka na pia humaanisha Kitu

ambacho hakitakiwi na hivyo kimetupwa na mtu mmoja na kuokotwa na mwengine.

Na tunapochunguza hali ya Laqit ndani ya Qur’an basi hua tunaoneshwa mfano wa kisa

cha Nabii Yusuf na Nabi Musa ambapo kwa Nabii Yusuf alitupwa na kuigizwa Kisimani

kutokana na Wivu wa kina Al Asbati yaani Kaka zake Nabii Yusuf na kisha akaokotwa

na kutolewa Kisimani na hivyo tukio hili kua ni sehemu ya maandalizi ya kuja kubebea

jukumu lake alilotayarishiwa na Mola wake. Na kutupwa Nabii Musa ambae alitupwa

Mtoni na Mama yake kutokana na maamrisho ya Mola wake ili kumuokoa kutokana na

mitihini ya mazingira yake na pia kumuingiza katika njia ya kukulia katika mazingira

yatakayorahisisha jukumu lake atakalopewa na Mola wake pia, kama ilivyosema aya:


233

‏﴿إِذْ‏ أَوْحَيْنَآ إِلىَٰ‏ أُمِّكَ‏ مَا يُوحَى ٰ ‏۞أَنِ‏ ٱقْذِفِيهِ‏ فىِ‏ ٱلت َّابُوتِ‏ فَٱقْذِفِيهِ‏ فىِ‏ ٱلْيَمِّ‏ فَلْيُلْقِهِ‏

ٱلْيَم ُّ بِٱلس َّاحِ‏ لِ‏ ‏َْخُذْهُ‏ عَدُو ٌّ لىِّ‏ وَعَدُو ٌّ ل َّهُ‏ وَأَلْقَيْتُ‏ عَلَيْكَ‏ محََب َّةً‏ مِّنىِّ‏ وَلِ‏ تُصْنَعَ‏ عَلَىٰ‏

عَيْنيِ‏ ۤ ﴾

Idh awhayna ila ommika ma yooha, Ani iqdhifeehi fee alttabooti faiqdhifeehi fee

alyammi falyulqihi alyammu bialssahili ya/khudhhu AAaduwwun lee

waAAaduwwun lahu waalqaytu AAalayka mahabbatan minnee walitusnaAAa

AAala AAaynee (Surat Al Ta-Ha 20:38-39)

Tafsir: Tulipomshushia Wahyi Mama yako juu yako juu ya tuliyomshushia,

tukamwambia Mtie ndani ya Tabut na kisha kitie ndani ya Mto, kisha Mto

utakichukua mpaka ukingoni, na atachukuliwa na adui yangu na adui yake. Na

nitakupamba kwa mapenzi kutoka kwangu, ili uwe ni mwenye kulelewa kutoka chini

ya uangalizi wangu.

Hii ni mifano ya hali ya Mitume walipokua Laqit walipokua wadogo ambapo

tunapozungumzia hali ya kua Laqit kwa Mtoto wa kawaida basi hua ni hali ambayo hatari

zaidi kuliko hali ya kua Yatima kwa sababu Yatima hua ni Mtoto ambae hana Baba lakini

anae Mama au ndugu na jamaa hivyo kama hakumtaka huyu basi atamtaka yule, wakati

hali ya Laqit hua ni hali ya Mtoto ambae hatakiwi kutokana na Mzee wake mtoto huyo

kua ni mwenye khofu ya umasikini kutokana na kutokua na kitu au kutokana na kuogopa

kutengwa kwa Uzinifu na hivyo humuacha na kumtupa mtoto katika sehemu bila ya

kumjali, na kutokana na hali kama hii basi Laqit anapokua Mchanga na kutupwa hua

hana Jina wala Nasaba tofauti na Yatima ambae hua na Nasaba.

Hivyo katika Surat Adh Dhuha basi Allah Subhanah wa Ta’ala anatufunza kwa

kutuonesha ndani yake Qur’an mifano hai ya kuwajali na kuwalea na kuwahudumia

Mayatima na Laqit kwa kutumia njia ya kufanya Kafala neno ambalo ni lenye maana

pana kama yalivyo maneno mengine Lugha ya Kiarabu na Allah Subhanah wa Ta’ala

amelitumia neno Kafala mara kadhaa ikiwemo pale aliposema:

‏﴿م َّن يَشْفَعْ‏ شَفَاعَةً‏ حَسَنَةً‏ يَكُنْ‏ ل َّهُ‏ نَصِيبٌ‏ مِّنْهَا وَمَن يَشْفَعْ‏ شَفَاعَةً‏ سَيِّئَةً‏ يَ‏ كُنْ‏

ّ ل شَ‏ يْ‏ ءٍ‏ م ُّقِيتاً‏ ﴾

ل َّهُ‏ كِفْ‏ لٌ‏ م َّنْ‏ هَ‏ ا وَكَ‏ انَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٰ عَلَى كُ‏ ِ


234

Man yashfaAA shafaAAatan hasanatan yakun lahu naseebun minha waman

yashfaAA shafaAAatan sayyi-atan yakun lahu kiflun minha wakana Allahu AAala

kulli shay-in muqeetan (Surat An Nisaa 4:85)

Tafsir: Na yeyote yule atakaeingilia jambo kwa nia nzuri basi atalipwa Malipo

yanayonasibiana kutokana nalo, na yeyote atakaieingila jambo kwa nia mbovu basi

(yakun lahu kiflun) atabeba jukumu litokanalo. Na Allah ni mwenye uwezo juu ya kila

kitu.

Na kisha akasema tena pale alipozungumzia kuhusiana na kesi aliyoletewa Nabii Daud

kua:

‏﴿إِن َّ هَذَآ أَخِ‏ ى لَهُ‏ تِسْعٌ‏ وَتِسْعُونَ‏ نَعْجَةً‏ وَلىَِ‏ نَعْجَةٌ‏ وَاحِ‏ دَةٌ‏ فَقَالَ‏ أَكْفِلْنِيهَا

وَعَز َّنىِ‏ فىِ‏ ٱلخِْطَابِ‏ ﴾

Inna hadha akhee lahu tisAAun watisAAoona naAAjatan waliya naAAjatun

wahidatun faqala akfilneeha waAAazzanee fee alkhitabi (Surat Sad 38:23)

Tafsir: (Alipoambiwa Nabii Daud) Hakika huyu Kaka yangu ana Kondoo tisini na

tisa, wakati mimi ninae mmoja tu, na anasema: ‘Akfilniiha –Nipe nimlee, na amenizidi

kwa maneno’

Na pale alipoinasibisha Kafala na Rehma kwa kusema:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ ٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَآمِنُواْ‏ بِرَسُولِهِ‏ يُؤْتِكُمْ‏ كِفْلَينِْ‏ مِن ر َّحمَْتِهِ‏ وَ‏ يجَْعَل ل َّكُمْ‏

نُوراً‏ تمَْشُونَ‏ بِهِ‏ وَيَغْفِرْ‏ لَكُمْ‏ وَٱهلل َُّ‏ غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo ittaqoo Allaha waaminoo birasoolihi yu/tikum

kiflayni min rahmatihi wayajAAal lakum nooran tamshoona bihi wayaghfir lakum

waAllahu ghafoorun raheemun (Surat Al Hadid 57:28)

Tafsir: Enyi Mlioamini (Nabii Musa na Nabii Isa) Muogopeni Allah na Muaminini

Mtume wake, nae atakupeni Kiflayni min Rahmatihi (Atakutunzeni Mara Mbili

kutokana na Rehma zake) na atakupeni Nuru ambayo mtatembelea (katika njia

iliyonyooka) na atakusameheni na Allah ni Mwingi wa Kusamehe na Mwingi wa

Rehma.


235

Ambapo amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kuna watu wa aina

tatu ambao ndio watakaopata Malipo mara mbili:

1-Yule Mtu ambae anamiliki Mtumwa, akamsomesha, akamfundisha tabia njema

na kisha akamuachia huru na kisha akamuoa basi atalipwa mara mbili.

2-Yule Muumini ambae alikua ni wa Ahl Al Kitab, na akawa ni Muumini wa kale

na akamuamini Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi atalipwa mara mbili.’

3-Na yule Mtumwa ambae ni mwenye kusimamia haki za Allah na akawa ni

Muaminifu kwa mwenye mali pia basi atalipwa mara mbili.’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Baina ya Wakati wenu na

wakati wa waliotangulia kabla yenu kuna Sala ya Asr na Maghrib, na mfano wenu

kulinganisha na mfano na Mayahudi na Wakristo basi hua ni sawa na Mtu ambae

amewaajiri Wafanyakazi na kusema; ‘Jee ni nani atakaefanya kazi kwa ajili yangu

kwa nusu siku kwa malipo ya siku kamili?’

Mayahudi wakafanya kazi kwa nusu siku kwa malipo ya siku nzima. Kisha Allah

Subhnah wa Ta’ala akauliza: ‘Jee ni nani atakaefanya kazi kuanzia Adhuhuri hadi

Al Asr kwa malipo ya siku nzima’ Hivyo Wakristo wakafanya kazi kuanzia

Adhuhuri hadi Al Asr.’ Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akasema:‘Jee ni nani

atakaefanya kazi kwa ajili kuanzia Al Asr mpaka Maghrib kwa malipo ya siku mbili

zaidi yake?’

‘Hivyo enyi Waislam nyinyi ndio mtakaofanya kazi baina ya Al Asr na Maghribi

kwa malipo ya siku mbili, na bila ya shaka mtalipwa mara mbili zaidi.’ Hivyo

Mayahudi na Wakristo wakakasirika na kusema: ‘Jee itakuaje sisi tufanye kazi na

kulipwa kwa chini zaidi?’ Allah Subhanah wa Ta’ala akauliza: ‘Jee mimi

nimekudhulumuni haki yenu?’ nao wakajibu : ‘La!’ Allah Subhanah wa Ta’ala

akasema: ‘Hizi ni fadhila zangu namfadhili nimtakae’(Imam Ibn Hibban)

Ambapo kutokana na hadithi hii basi na nyenginezo Wanazuoni wa Madhhab ya Imam

Abu Hanifa wamependekeza kua wakati baina ya sala ya Al Asr na Maghrib uwe mfupi

kuliko mda wa baina ya sala ya Adhuhuri na Al Asr, na hivyo Sala ya Al Asr hua

wanaichelewesha.

Hivyo Allah Subhnah wa Ta’ala anatutambulisha kisa cha Maryam Bint Imran kua kama

ni mfano wa Kaffala ili kutuelezea kuhusiana na umuhimu wa kuwajali Mayatima na sifa

anayostahiki kua nayo Kafil yaani mtu mwenye jukumu la kuwasimamia Mayatima,

ambapo katika kisa hiki basi umechaguliwa mfano wa Nabii Zakarriyah na Isha Bint

Faqudh, kwani amesema Allah Subhanahh wa Ta’ala ktika Qur’an kua:


236

‏﴿وَٱبْتَلُواْ‏ ٰ ٱلْيَتَامَى حَتى َّ ٰ إِذَا بَلَغُواْ‏ النِّكَا حَ‏ فَإِنْ‏ آنَسْتُمْ‏ مِّنْهُمْ‏ رُشْ‏ داً‏ فَٱدْفَعُواْ‏ إِلَيْهِمْ‏

أَمْوَالهَُمْ‏ وَلاَ‏ أتَْكُلُوهَآ إِسْرَافاً‏ وَبِدَاراً‏ أَن يَكْبَرُواْ‏ وَمَن كَانَ‏ غَنِيّاً‏ فَلْيَسْتَعْفِفْ‏ ن وَمَ‏

كَانَ‏ فَقِيراً‏ فَلْيَأْكُلْ‏ بِٱلْمَعْرُوفِ‏ فَإِذَا دَفَعْتُمْ‏ إِلَيْهِمْ‏ أَمْوَ‏ الهَُمْ‏ فَأَشْهِدُواْ‏ عَلَيْهِمْ‏ وَكَفَ‏ ٰ ى

يباً‏ ﴾ بِٱهلل َِّ‏ حَسِ‏

Waibtaloo alyatama hatta idha balaghoo alnnikaha fa-in anastum minhum rushdan

faidfaAAoo ilayhim amwalahum wala ta/kulooha israfan wabidaran an yakbaroo

waman kana ghaniyyan falyastaAAfif waman kana faqeeran falya/kul

bialmaAAroofi fa-idha dafaAAtum ilayhim amwalahum faashhidoo AAalayhim

wakafa biAllahi haseeban (Surat An Nisaa 4:6)

Tafsir: Na wajaribuni (Kiakili na ufaham wao) Mayatima hadi wawe wamebaleghe na

kufikia umri wa kuoa, na mkiwaona wana ufaham mzuri, basi wapeni mali zao, na

wala msizitumie kwa Israfu kutokana na kua na khofu kua watakua wakubwa. Na

kama ikiwa mmoja miongoni mwenu ni Tajiri basi asichukue malipo. lakini kama

akiwa Fukara basi na wacha na achukue kinachostahiki, na kisha mtakapowakabidhi

Mali zao basi kuwe na shahidi juu yao na kwa hakika anatosheleza Allah Kuchukua

Mahesabu.

Ambapo aya imetumia neno Bala ambalo linamaanisha Kujaribu, Kufanyia Mtihani iwe

kwa ajili ya Kupandisha Darja au kwa Kuadhirisha, Kuthibitisha, Kusimama. Kufadhili,

Hivyo aya inatubainishia kua kwa kila mwenye kufanya Kaffal yaani kulea basi baada ya

kufika mda wa kumalizika kipindi cha kulelewa Mayatima yaani wamesha baleghe basi

wanatakiwa kujaribiwa ufaham wao kuangaliwa kama wanao uwezo wa kusimamia Mali

zao, ambapo kwa upande wa Imam Abu Hanifa na Imam Malik basi mtizamo wao

kuhusiana na Umri stahiki kwa mtoto kua tayari ameshakua mkubwa hua ni miaka 17 wa

Mwanamke na miaka 18 wa Mwanamme.

Ambapo kwa Wanafunzi wa Imam Abu Hanifa ambao ni Wanazuoni wa Madhhab ya

Hanafi kma Imam Muhammad Abu Yusuf basi yeye anaendana sambamba na mtizamo

wa Imam Al Shafii na Imam Ahmad Ibn Hanbal kuhusiana na suali hili kwani wao

wanasema kua Umri wa mtoto kua Mkubwa ni miaka 15 bila ya kutofautisha baina ya

Mwanamme na Mwanamke.


237

Na hii ni kutokana na hadith isemayo: ‘Amesema Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu

Anhu kua: ‘Mimi nilipendekeza kwa Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam kua

niende kupigana katika vita vya Uhud nilipokua na umri miaka 14, lakini

hakuniruhusu. Hivyo nikapendekeza kwake tena niende kwenye vita vya Khandak

nilipokua na umri wa miaka 15 na akaniruhusu’(Sahih Muslim)

Na anasema Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Kwa upande wa

Imam Abu Hanifa basi kama Mtoto huyo itabidi akabidhiwe Mali zake bila ya

kujali kua kama ataweza kuisimamia ama la pale anapotimia umri wa miaka 25,

lakini Wanafunzi wake wametofautiana nae, kwa kusema kua kama Mtoto huyo

atakua bado hajaonesha kua amekua kiakili basi hastahiki kupewa jukumu la

kusimamia Mali zake.’

Ambapo kwa upande wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye

anasema kua: ‘Mtizamo wa kua kama Mtoto huyo atakua bado hajaonesha kua

amekua kiakili basi hastahiki kupewa jukumu la kusimamia Mali zake, basi ndio

pia Mtizamo wa Imam Al Shafii’

Hapa kuna baadhi wanaweza wakajiuliza hivi kwa nini Wanafunzi wa Imam Abu Hanifa

wakabadilisha Mtizamo na kuenda kinyume na Mtizamo wa Imam wao mkuu? Ambapo

jibu la suali hili kwa kirefu linapatikana katika kitabu changu cha Ijihad na Taqlid

Historia ya Wanazuoni na Madhhab yao katika Uislam, ambacho kinapatikana

mtandaoni kwa bure kama sadaqa. hivyo hapa tutazungumzia kwa juu juu tu ili kwa wale

ambao hawajakipata basi nao wanufaike.

Hivyo hii ni kwa sababu Imam Al Shafii alisoma kwa Imam Malik na kwa MWanafunzi

mkuu wa Imam Abu Hanifa kisha na yeye akamsomesha Imam Hanbal.

Sasa katika wakati wa kipindi cha uhai wake Imam Al Shafii basi kukatokea Mvutano

wa Kifiqh baina ya Madhhab ya Imam Abu Hanifa na Madhhab ya Imam Malik wakati

Maimamu wao hao wakuu wameshafariki na Imam Al Shafii akaombwa Autatue mzozo

huo.

Hivyo Imam Al Shafii akautatua kwa kuyatoa kasoro Madhhab hayo mawili kwa

kuziainisha Tofauti zao kwenye Vitabu viwili tofauti kimoja ni Ikhtilafi Al Maliki na

chengine ni Ikhtilafi Al Iraqiyyin (Hanafi). Kisha akaandika kitabu chake yeye na

kufafanua njia sahih ya kufuatwa katika Fiqh kiitwacho Al Risala. Na kutokana na

kuaandika Al Risala basi ndio Imam Al Shafii akawa anajulikana kama ni Baba wa Usul

Fiqh


238

Na Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Maliki na Imam Abu Hanifa wakivipitia vitabu

vyao walivyoandikiwa na Imam Al Shafii na kisha wakakipitia kitabu cha Imam Al Shafii

cha Al Risala na wakakubaliana na Mtizamo wa Imam Al Shafii.

Kwa hivyo sasa hapa ndio ikatokea Mitizamo miwli kwa Madhhab haya mawili kwani

kwa upande wa Madhhab ya Hanafi basi kuna mitizamo ya kabla ya kuja kwa Imam Al

Shafii ambayo ndiyo Mitizamo ya Imam Abu Hanifa Mwenyewe. Na kwa Madhhab ya

Imam Malik pia kuna Mitizamo wa kabla ya kuja Imam Al Shafii ambao ndio Mitizamo

ya Imam Malik mwenyewe.

Sasa unaposikia kua katika Madhhab kuna mitizamo miwili basi mmoja ni wa zamani

usiokua na Nguvu na wa pili ni mtizamo mpya yaani baada ya kuja Imam Al Shafii ambao

ni wenye Nguvu zaidi. Kwa mfano kama tulivyoona kwenye mfano wa upande wa

Madhhab ya Imam Abu Hanifa na Imam Malik kuhusiana na umri wa Kukabidhiwa mali

zake Yatima.

Hivyo inabidi tusijichanganye Kama vile ambavyo kwa mfano wanavyojichanganya

watu wasiojua pale wanaposikia kua katika Madhhab ya Imam Abu Hanifa na Madhhab

ya Imam Malik kuna mitizamo miwili ya kuhusiana na Muandamo wa mwezi. Ambapo

wa kwanza ni wa zamani na usiokua na nguvu ambao ni kabla ya kuja Imam Al Shafii ni

kua Mwezi Mmoja kwa Dunia nzima.

Halafu kuna mtizamo wa pili ambao ni Mpya ambao ndio unaokubalika ambao ni wenye

nguvu ambao ni wa baada ya kuja Imam Al Shafii na kuwakosoa na kuwaonesha kasoro

zao nao wakakubali ambao ni kua Kila sehemu na Muandamo wa mwezi wake.

Na ndio maana ukasikia kua kuna makubaliano ya Wanazuoni kuhusiana na Muandamo

wa kila Machweo na Muandamo wake kwa sababu Wanazuoni wa Madhhab mengine

wamekubaliana juu yake baada ya kuthibitishiwa na Mujaddid Ad Din Imam Muhammad

Idris Al Shafii.

Ila sasa ili kuyafaham haya inabidi usome historia za Maimamu hawa Uwafaham

Ipasavyo na Madhhab yao uyafaham ipasavyo na njia wanazotumia katika kutoa hukmu

zao katika Qur'an, Hadith, Sunna na Qiyas au Makisio na uzifaham ipasavyo.

Kisha ndio utajua kua hata Kiakili haifai kufuata Mtizamo ambao ni wa zamani na

usiokua na nguvu. Kwani ingawa ukweli ni kua zamani Qur'an ilikua inaandikwa

kwenye Ngozi kwenye Magome, na hata hadith pia zilikua zimeandikwa katika sehemu

tofauti lakini ukaja mtizamo mpya na Masahaba wakakubaliana kua ikusanywe pamoja

kwenye Mas-haf moja na Hadith zikusanywe pamoja na hivyo leo hii kila mtu anafuata

Mtizamo huo mpya kwani ndio unaokubalika zaidi na ndio unaonufaisha zaid.


239

Lakini ingawa watu hukubaliana kua hata nguo, Vyakula Matibabu, simu n.k za zamani

hazikubaliki, Lakini inashangaza kuona kua kuhusiana na Muandamo wa mwezi watu

bado wameng'ang'ania Mtizamo wa Zamani na usiokubalika wa kua Dunia Si Mviringo

bali ni Mraba.

Na bila ya shaka kuna baadhi wanaweza wakajiuliza ilikuaje mpaka Imam Al Shafii

akaweza kuwathibitishia Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Abu Hanifa kwa mfano, kwa

sababu Wanafunzi wa Imam Abu Hanifa ambao nia Imam Abu Yusuf na Imam Ash

Shaybani ni walimu wa Imam Al Shafii.

Sasa inakujae mpaka Walimu anakubali kua kweli sisi hapa tumekosea? Na sio hao tu

hata Imam Malik mwenyewe kuna wakati katika uhai wake alikubali mbele ya Imam Al

Shafii kua kweli hapa nimekosea na wewe uko sahih, na hili tunaliona pale wakati Imam

Al Shafii akiwa bado mdogo akisoma kwa Imam Malik.

Ambapo siku moja Al Shafi’i alikua amekaa chini ya miguu ya Imam Malik

akisomeshwa, alikuja mtu na kumwambia Imam Malik: ‘Hakika mimi nimeshamuacha

mke wangu jee nifanye nini?’

Imam Malik akamuuliza jee ilikuaje? Yule mtu akajibu: ‘Mimi kazi yangu ni kuuza

ndege, hivyo dukani kwangu alikuja mnunuzi akataka kumnunua ndege aina ya

Kasuku, alipofika akaniuliza kama yule Kasuku analia ama la, nami nikamuapia

kua kama halii basi mke wangu awe ameachika, kwani yule Kasuku alikua akilia,

hivyo yule mnunuzi akamnunua yule Kasuku lakini baada ya siku kadhaa

alimrudisha na kusema kua yule kanga halii.’

Imam Malik akajibu, ‘Hakika umeshamuacha mke wako, hivyo usimkaribie’. Al

Shafi’i akaingilia kati na kusema: ‘Subiri kwanza nikuulize. ‘Jee, baina ya kulia na

kunyamaza kwa kanga wako kupi ni kukubwa zaidi?’’

Yule muuzaji akajibu, ‘Kulia kwake ni kukubwa zaidi kuliko kunyamaza kwake’.

Al Shafi’i akajibu ‘Basi mkeo hajaachika’.

Hapo Imam Malik akaingilia kwa kusema ‘Ya Al Shafi’i unajuaje?’.

Al Shafi’i akajibu ‘Kwa sababu ulinidadithia kua kutoka kwa Al Zuhri, kutoka kwa

Abu Salam Ibn Abd al Rahman, kutoka kwa Umm Salama ambae amesema kua

Fatma bint Qayis alisema ‘Ya Rasul Allah! Abu Jahm na Muawiyah wote wawili

wameniposa’


240

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salaam akajibu ‘Muawiyah hana pesa, na Abu

Jahm hatui mzigo chini kutoka kwenye bega lake (kwa Safari), akiwa na maana:

Hali yao ya kila mara; Kwa Waarabu hutumia hali ya kila mara kutokana na

utokeaji wa mara kwa mara kwa kitu au jambo. Hivyo kwa kua Kasuku wake

alikua akilia hapo kabla kwa mda mrefu kulingana mda alionunuliwa ambao alikua

ni mwenye kunyamaza. Hivyo basi hii inamaanisha Kasuku wake huy bwana

analia’.

Imam Malik akaridhika na kumwambia Al Shafi’i ‘Naam uko Sahih!’.

Na ndio nikasema kua inabidi uwasome hawa Wanazuoni uwajue ndani nje na kisha ndio

utafaham, kua katika Moja kati ya Jambo ambalo Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Abu

Hanifa na Imam Malik walikua wanakosea katika mifumo yao ya Fiqh ilikua ni katika

Hadith au kauli ambayo ni ya Mtu mmoja.

Hii inaitwa Habar Al Wahid, kwani wao walikua hawaitumii ipasavyo, na bila ya shaka

Fatwa ya Mwezi ya Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua kila sehemu

na Muandamo wake pale yeye alipokua anakaa Makkah na kuukataa Muandamo wa Syria

kwa sababu Matlai yao ni tofauti, ni moja kati ya Habar Al Wahid yaani habari au kauli

ya Mtu mmoja.

Lakini sasa alipokuja Imam Muhammad Idris Al Shafii akawaambia kua Hii Habar al

Wahid ni Habari ambayo inastahiki kutumiwa kua pia kama chanzo cha kutolea Hukmu

za Sharia za Kiislam.

Kama mfano wa habari Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua kila sehemu na

Muandamo wake pale yeye alipokua anakaa Makkah na kuukataa Muandamo wa Syria

kwa sababu Matlai yaani Machweo yao ya Jua ni tofauti, na kisha akasema kua ‘Hivi

ndivyo alivyotufundisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.’

Hivyo kauli hii ya Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu ni moja kati ya Habar Al

Wahid yaani habari au kauli ya Mtu mmoja ambayo inakubalika kutoa Humu ya Kisharia.

Hivyo Imam Muhammad Idris Al Shafii akawaambia kua Hii Habar al Wahid ni Habari

ambayo inastahiki kutumiwa kua pia kama chanzo cha kutolea Hukmu za Sharia za

Kiislam kwa sababu Masahaba walikua wanaitumia na ilikua inakubalika kwao wao.

Kisha Imam Al Shafii akasema kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kua: Allah Subhanah wa Ta’ala humnawirisha yule Mja ambae amesikia maneno

yangu kisha akayakumbuka, akayahifadhi na kisha akayasogeza mbele zaidi kwa

wengine.’


241

Imam Al Shafii anaendelea kusema kua: ‘Inawezekana Mtu huyo anaeyasogeza mbele

akawa ana Ilm ya Fiqh lakini akawa ni Mwanafiqh, na anaweza akawaa ni

Mwanafiqh lakini akayasogeza mbele zaidi maneno hayo kwa wanaojua zaid yake.

Na Moyo wa Muislamu kamwe hauwezi kua na kinyongo kwa watu wa aina tatu’

1-Mwenye Ikhlasi katika kumtumikia Allah Subhanah wa Ta’ala.

2-Mkweli na Muamninifu kwa Waislam.

3-Mwenye Kuthibitisha katika jamii kua yeye anasimamia Maslahi ya Waislamu

na Kuwakinga na Upotovu.

Kisha Imam Muhammad Idris Al Shafii akatoa Mfano wa matumizi ya Habar Al Wahid

kwa kusema kua: ‘Abu Talha Radhi Allahu Anhu na wenzake waliivunja Mitungi

yao yote ya Pombe baada ya kuambiwa na Mtu kua Kuna aya imeshuka

inayoharamisha Pombe.’

Hivyo Abu Talha Radhi Allahu Anhu na wenzake hawakuhoji kweli au Uongo, imeshuka

jana au leo, bali wao waliposikia tu basi hapo hapo wakavunja Mitungi yao yote na

kumwaga Pombe iliyomo ndani yake yote.

Kisha akatoa na mfano mwengine ambao ni ule unaohusiana na iliposhuka aya ya 144 ya

Surat Al Baqara iliyoamrisha kua Sasa hivi Waislam wasikielekee Kibla cha Bayt ul

Maqdis bali waelekee Kibla cha Makkah pale iliposema:

‏﴿قَدْ‏ نَرَىٰ‏ تَقَل ُّبَ‏ وَجْهِكَ‏ فىِ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ فَلَنُوَلِّيَن َّكَ‏ قِبْلَةً‏ تَرْضَاهَا فَوَلِّ‏ وَجْهَكَ‏ شَطَْر

ٱلْمَسْجِ‏ دِ‏ ٱلحَْرَامِ‏ وَحَيْثُ‏ مَا كُنْتُمْ‏ فَوَل ُّواْ‏ وُجُوِهَكُمْ‏ شَطْرَهُ‏ وَإِن َّ ٱل َّذِينَ‏ أُ‏ وتُواْ‏ ٱلْكِتَا ‏َب

لَيَعْلَمُونَ‏ أَن َّهُ‏ ٱلحَْق ُّ مِن ر َّهبِِّمْ‏ وَمَا ٱهلل َُّ‏ بِغَافِلٍ‏ عَم َّا يَعْمَلُونَ‏ ﴾

Qad nara taqalluba wajhika fee alssama-i falanuwalliyannaka qiblatan tardhaha

fawalli wajhaka shatra almasjidi alharami wahaythu ma kuntum fawalloo

wujoohakum shatrahu wa-inna alladheena ootoo alkitaba layaAAlamoona annahu

alhaqqu min rabbihim wama Allahu bighafilin AAamma yaAAmaloona (Al-

Baqarah 2:144)

Tafsir : ‘Kwa hakika! Tumeona muelekeo wa uso wako kuelekea Mbinguni, Hakika

tutakuelekeza katika Qiblah ambacho kitakuridhisha. Hivyo geuzia uso wako kuelekea

Al Masjid Al Haram. Na kokote kule mliko basi geuzeni Nyuso zenu katika muelekeo


242

huo. Kwa hakika wale waliopewa Kitabu wanajua kua (kugeuzia kwenu muelekeo

kuelekea Al Kaabah) Haki kutoka kwa Mola wao na Allah hakughafilika na

wanayoyafanya.’

Ambapo ya hii ilishuka katika mwezi 15 Shaaban ya mwaka wa pili Al Hijra wakati wa

Sala ya Dhuhr hivyo Masahaba wakasali na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

katika Msikiti wake, na wakiwa hawakuelekea katika Kibla cha Jerusalem katika Masjid

Al Aqsa kama ilivyokua kawaida yao hapo kabla, bali walisali huku wakiwa wameelekea

katika Kibla kipya cha Makkah kilichoamrishwa kwenye aya hii, kisha baada ya sala

mmoja kati ya Watu wa ukoo wa Banu Salama akawa anarudi nyumbani akapita kwenye

Masjid Al Quba akawakuta Waislam wanasali sala ya Al Asr wakiwa wameeleka Bayt al

Maqdis.

Hivyo Muislam huyo kutoka katika ukoo wa Banu Salama akanadia Msikitini humo kwa

kusema kua: ‘Imeshuka aya inayosema kua Kibla cha Waislam sasa hivi ni kuelekea

katika Al Kaabah Mjini Makkah’ Na hapo hapo Masahaba waliomo kwenye Sala hio

wakageukia Katika Upande wa Mji wa Makkah, huku wengine walikua katika Kurukuu.

Ambapo huu ndio Msikiti pekee ambao ndani yake ilisaliwa Sala ambayo nusu yake watu

waliianza kuisali huku wakiwa wameelekea kibla cha Jerusalem na nusu yake

wakaimalizia huku watu wake wakiwa wamelekea kibla cha Makkah, na ndio maana

ukawa unaitwa Masjid Qiblatayn.

Tafakkar! Kwani Masahaba hawa hawakukata Sala, wala hawakuuliza kasema nani

kuhusiana na habari hio? Na kama jee ni kweli au ni Uongo? Kwani mtu aliesema

hawakumuona wao wamesikia sauti tu inawataarifu juu ya habari al wahid hio, wakati

wakiwa ndani ya Sala.

Nadhani japo kidogo itakua tumefahamiana kuhusiana na kwanini ikawa kuna tofauti

kwenye Madhhab haya Mawili ya Imam Abu Hanifa na Imam Malik ya mitizamo ya

Fiqh ya zamani na Mipya katika kesi kama hizi za umri Yatima kukabidhiwa mali yake,

Mwandamo wa mwezi, Itiqaf, n.k Hivyo Wanazuoni waliofuatia wa Madhhab hayo

wakakubaliana kufuata Mitizamo mipya.

Hivyo baada ya Surat An Nisaa 4:6 kuzungumzia kuhusiana na Ukabidhiwaji wa Mali

zao Mayatima basi ikakataza utumiwaji wa mali za Mayatima kwa israfu ambapo Imam

Muhammad Al Shafii anasema kua: ‘Mtu yeyote yule anaesimamia mali ya Yatima

basi anaweza kuchukua kutokana nayo kua kama sehemu ya malipo yake, na hua

hain hja ya kuzirudisha’ Ambapo pia ndio mtizamo wa Imam Hasan Al Basr, Imam

Ibrahim An Nakhai, Imam Ibn Attiyah na hii ni kutokana na uthibitisho wa ile hadithi

ambayo inasema: ‘Kuna mtu alimwambia Rasul Allah Salallahu Alayi wa Salam kua:

Hakika mimi sina njia ya kujipatia Riziki, lakini nina Yatima chini ya usimamizi


243

wangu’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Unaweza kutumia mali

yake Yatima lakini bila ya kufanya Israfu, au kuutumia msingi wenyewe na wala

usiokoe mali yako kutokana na kutumia mali yake’(Sahih Ibn Majah, Imam Ibn

Marduwayh, Imam An Nasai, Imam Ahmad, Imam Ibn Hibban na Imam Abu Daud.)

Ambapo kwa upande wa Amir ul Muuminin Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu

basi yeye alisema: ‘Mimi hua naichukulia Mali ya Bayt ul Maal kama

ninavyoichukulia mali ya Yatima, wakati ninapokua na kitu basi hua najitenga

nayo, na ninapokua sina kitu basi hua nnachukua kama mkopo, na kisha

ninapopata hua narudisha’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea visa hivi vya watoto wenye sifa za

Uyatima na Laqit ndani ya Qur’an kupitia kwa watu Watukufu na wenye darja kubwa

sana mbele yake na juu yetu ambao ni Mitume na Manabii kwa ajili ya kutufundisha

umuhimu wa kuwajali katika kuwalea na kuwahudumia ili watoto hao wakulie katika

hali na mazingira bora yatakayowaongoza katika maisha yao hapa Duniani na kesho

Akhera, kutokana na muongozo wa malezi ya mlezi husika, kwani kufanya hivyo hua ni

kuonesha kua na Subra na Ucha Mungu na malipo yake mbele ya Allah Subhanah wa

Ta’ala ni makubwa sana kama zinavyosema aya:

‏﴿إِن َّ ٱلأَبْرَارَ‏ يَشْرَبُونَ‏ مِن كَأْسٍ‏ كَانَ‏ مِزَاجُهَا كَافُوراً۞عَيْناً‏ يَشْرَبُ‏ هبَِ‏ ا عِبَادُ‏ ٱهلل َِّ‏

يُفَجِّ‏ رُونَهَا تَفْجِ‏ يراً۞يُوفُونَ‏ بِٱلن َّذْرِ‏ وَيخََافُونَ‏ يَوْماً‏ كَانَ‏ شَر ُّهُ‏ ‏ُمسْتَطِيراً۞وَيُطْعِمُوَن

ٱلط َّعَامَ‏ ٰ عَلَى حُبِّهِ‏ مِسْكِيناً‏ وَيَتِيماً‏ وَأَسِ‏ ا يراً۞‏ إِنم ََّ‏ نُطْعِمُ‏ كُمْلِوَ‏ جْهِٱ هلل َِّ‏ لاَ‏ نُرِيدُ‏ مِنكُ‏ ‏ْم

‏َك

جَزَآءً‏ وَلاَ‏ شُكُوراً۞إِ َّ نخََافُ‏ مِن ر َّبِّنَا يَوْماً‏ عَبُوساً‏ قَمْطَرِيراً۞فََوقَاهُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ شَر َّ ذٰلِ‏

ٱلْيَومِ‏ وَلَق َّاهُمْ‏ نَضْرَةً‏ وَسُرُوراً۞وَجَزَاهُمْ‏ بمَِا صَبَرُواْ‏ جَن َّةً‏ وَحَرِيراً‏ ﴾

Inna al-abrara yashraboona min ka/sin kana mizajuha kafooran; AAaynan

yashrabu biha AAibadu Allahi yufajjiroonaha tafjeeran; Yoofoona bialnnadhri

wayakhafoona yawman kana sharruhu mustateeran; WayutAAimona alttaAAama

AAala hubbihi miskeenan wayateeman waaseeran; Innama nutAAimukum liwajhi

Allahi la nureedu minkum jazaan wala shukooran; Inna nakhafu min rabbina

yawman AAaboosan qamtareeran; Fawaqahumu Allahu sharra dhalika alyawmi

walaqqahum nadratan wasurooran; Wajazahum bima sabaroo jannatan

wahareeran (Surat Al Insan 76:8-12)


244

Tafsir: Hakika ya Wacha Mungu, watakunywa kutoka kwenye Gilasi Kafuran (Kinyaji

kinachotokana na Chemchem ya Peponi),Chemchem ambayo watakunywa Waja wa

Allah na kuisababisha kufoka kwa wingi zaidi, hawa ni wale waliotimiza Nadhiri zao

na wanaoiogopa siku ambayo Shari yake itaenea, Ni wanaotoa Chakula mbali ya kua

ni wenye kukipenda, kwa Masikini, Na Mayatima na Mateka; (Wakiwaambia

kua)’Hakika sisi tunakulisheni nyinyi kwa kutaka Malipo ya Allah tu, hatutaki Mlipo

kutoka kwenu waa shukurani. Kwani sisi tunaogopa kutoka kwa Mola wetu ile siku

Ngumu na Nzito ambyo itazifanya Nyuso ziwe ni zenye kukunjana; Hivyo Allah

amewaokoa wao kutokana na shari ya siku hio na kuwapa muonekano mzuri wa

furaha, Na Malipo yo kutokana na Subira yao itakua ni Pepo na Nguo za Hariri.’

Aya inatuwekea wazi kua Watu wenye Taqwa na Waja wema hua ni wale ambao ni

wenye Huruma na Ukarimu na wenye kuamini kua kufanya kwao hivyo hua ni kwa ajili

ya Akhera yao kwani watahurumwa na kukirimiwa na Mola wao kesho Akhera, kutokana

na huruma na ukarimu wao kama vile wao walivyofanyiwa ukarimu na Mola wao hapa

Ulimwenguni, na ndio maaana akasema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

‘Peponi Kuna Mlango unaoitwa Furaha, ambao hawatoingia ndani yake isipokua

wale waliokua wakiwafurahisha Watoto’ (Imam Ad Daylami)

Amesema Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam: ‘Hakuna yeyote yule mwenye

kuwahudumia Mayatima basi atakua pamoja nami Peponi kama hivi – Huku

akionesha vidole vyake viwili cha shahada na cha kati vikiwa pamoja’ (Imam

Bukhari)

Hivyo Muislam yeyote yule atakaeendana kinyume na mtizamo huu na hivyo kua si

mwenye kuwajali Mayatima basi atakua ni miongoni mwa watu wenye sifa ya kua ni

Wanafiq.

Ambapo alisema Hasan Al Basr kua: ‘Hakuna anaeuogopa Unafiq isipokua yule Mtu

ambae ni Alieamini kweli, na hakuna anaejihisi kua amesalimika na Unafiq

isipokua yule ambae ni Mnafiq na Hakuna asieuogopa Unafiq isipokua Mtu huyo

hua ni Mnafiq.’

Ambapo Hasan Al Basr alisema hivi kwa sababu ya kua Unafiq ni Sifa ambayo haifai

kua nayo Muislam. Kwani Sifa ya Unafiq ni Sifa ambayo inachukiza mbele ya Allah

Subhanah wa Ta'ala na Mtume wake Salallahu Alayhi wa Salam kutokana na kua

Madhara yake ni Makubwa kuliko Madhara ya Mtu alie Kafiri. Na hii inawekwa wazi na

ile aya ambayo inasema;


245

‏﴿وَمِنَ‏ ٱلن َّاسِ‏ مَن يَقُولُ‏ آمَن َّا بِٱهلل َِّ‏ وَبِٱلْيَوْمِ‏ ٱلآخِ‏ رِ‏ وَمَا هُم بمُِؤْمِنِينَ۞يخَُ‏ ادِعُونَ‏ ٱهلل ََّ‏

وَٱل َّذِينَ‏ آمَنُوا وَمَا يخَْدَعُونَ‏ إِلا َّ أَنْفُسَهُم وَمَا يَشْعُرُونَ۞فىِ‏ قُلُوهبِِم م َّرَضٌ‏ فَزَادَهُمُ‏ ٱهلل َُّ‏

‏ِض

مَرَضاً‏ وَلهَُم عَذَ‏ ابٌ‏ أَلِيمٌ‏ بمَِا كَانُوا يَكْذِبُونَ۞وَإِذَا قِيلَ‏ لهَُمْ‏ لاَ‏ تُفْسِ‏ دُو اْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْ‏

ۤ قَالُو اْ‏ إِنم ََّا نحَْنُ‏ مُصْلِحُونَ۞أَلا إِن َّهُمْ‏ هُمُ‏ ۤ ٱلْمُفْسِ‏ دُونَ‏ وَلَٰكِن لا َّ يَشْعُرُونَ‏ ﴾

Wamina alnnasi man yaqoolu amanna biAllahi wabialyawmi al-akhiri wama hum

bimu/mineena, YukhadiAAoona Allaha waalladheena amanoo wama

yakhdaAAoona illa anfusahum wama yashAAuroona; Fee quloobihim maradhun

fazadahumu Allahu maradhan walahum AAadhabun aleemun bima kanoo

yakdhiboona; Wa-idha qeela lahum la tufsidoo fee al-ardi qaloo innama nahnu

muslihoona(Surat Al Baqara 2:8-11)

Tafsir: Na Miongoni mwa Watu kuna wale wasemao kua Wamemuamini Allah na

Siku ya Mwisho lakini hawakuamini wanadhani kua Wanamhadaa Allah na

Walioamini na Lakini Hawamhadai yeyote Isipokua Nafsi zao lakini wao Hawalioni

hilo kwani Ndani ya Nyoyo zao Wana Maradhi na Kisha Allah Akawaongezea

Maradhi Na Juu yao kuna Adhabu kali sana kutokana na Wanayoyakadhibisha

Wanapoambiwa Msifanye Ufisadi kwenye Ardhi hua Wanasema kua kwa Hakika Sisi

ni wenye Kutafuta Usuluhisho.

Hizi ni miongoni mwa aya za Mwanzoni mwanzoni mwa Surat Al Baqara, Sura ambayo

kwanza imeanza kufunguliwa kwa kuwazungumzia Waumini walioamini na Sifa zao

kama vile ambavyo imemalizia kufungwa kwa aya zake za Mwisho katika kuelezea Sifa

za Waumini pia na hivyo kuonesha na kusisitizia Umuhimu wa Kuamini Nguzo 6 za

Imani ya Dini ya Kiislam.

Ambapo kutokana na Kua na Sifa hio basi hata Sahaba Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu

Anhu aliusia kua: Katika wakati atakapofariki na Kuzikwa basi katika Upande wa

Kichwani kwake asomewe Kichwa cha Surat Al Baqara yaani aya 5 za Mwanzo za

Surat Al Baqara (2:1-5) na Miguuni mwake asomewe Kifungio cha Surat Al Baqara

yaani aya mbili za Mwishoni za Surat Al Baqara (2:285-286)

Hivyo katika Aya hizi za Surat Al Baqara 2:8-11 basi Allah Subhanah wa Ta'ala

anawazungumzia Wanafiq na Ubaya wao Kua ni Wenye Kufanya Hadaa kwa Maneno

yao, yaani ni wenye Kusema Uongo lakini hawajui kua Kufanya kwao Hadaa huko hua

ni Kujihadaa Nafsi zao, ambazo zina Maradhi ambayo wanayaendekeza na hivyo Allah


246

Subhanah wa Ta'ala akawazidishia Maradhi zaid ili apate kuwachoma vizuri kesho

Akhera kutokana na Unafiq wao kama zinavyosema aya:

‏﴿وَمَن يُشَاقِقِ‏ ٱلر َّسُولَ‏ مِن بَعْدِ‏ مَا تَبَين ََّ‏ لَهُ‏ ٱلهُْدَىٰ‏ وَيَت َّبِعْ‏ غَيْرَ‏ سَبِيلِ‏ ٱلْمُؤْمِنِ‏

نُوَلِّهِ‏ مَا َّ ٰ تَوَلى وَنُصْلِهِ‏ جَهَن َّمَ‏ وَسَآءَتْ‏ مَصِيراً‏ ﴾

‏َين

Waman yushaqiqi alrrasoola min baAAdi ma tabayyana lahu alhuda wayattabiAA

ghayra sabeeli almu/mineena nuwallihi ma tawalla wanuslihi jahannama wasaat

maseeran (Surat An-Nisa 4:115)

Tafsir : Na yeyote yule akayebisha na kumpinga Mtume, baada ya kua ameoneshwa

wazi njia iliyonyooka, na akafuata njia nyengine isiyokua ya walioamini,

Tutamuelekeza katika njia aliyochagua, na tutamchoma motoni - na huo hua ni

mwisho mbaya sana’

Na hii ni kwa sababu Miongoni mwa Sifa zao watu hao Wanafiq basi hua ni wenye

Kufanya Ufisadi Ardhini au Kusababisha Madhara katika Uislam. Lakini wanapoambiwa

kua hivyo wafanyavyo kua sivyo kwani hua wanaharibu badala ya kutengeneza basi wao

hua hawakosi Kisingizio kwa kusema kua Hivyo wafanyavyo wao hua si Kuharibu, si

Kusababisha Ufa katika Uislam bali ni Kujenga Uislam. Na bila ya shaka katika hili wako

wengi Sana, na wanaingia Waliokuwemo na wasiokuwemo kutokana na Watu kutojua

kwao na kupenda kufuata Mkumbo.

Kwani ndani yake ndio unakuta Waislam wenye Sifa ya Unafiq ambao wanawafanyia

Ufisadi Waislam wenzao katika Ardhi za Kiislam kama Yemen, Syria, Falestina,

Aghanistan, Iraq n.k kwa kuwasababshia mapigano na kusaidia uasi katka ardhi za

Waslam wenzao kwa manufaa yao ya kidunia na hivyo kuua Waislam wasiokua na hatia

na kusababisha madhara makubwa sana katika jamii za Kislam.

Na kisingizio chao? Wanasema Innama Nahnu Muslihoona na ambapo suluhisho lao

wao hua ni kuwaweka wale wanaoendana na Mitazamo yao na kusimamia maslahi yao,

ya kidunia ya kutaka kudumu zaidi madarakani, na hivyo ua ni wenye utafuta wafusi

wengi kwa kutumia njia za kuwashawishi watu wafuate mitizamo yao na hivyo kuanzisha

aina nyengine ya Unafiq wa kuwagawa Waislam katika jamii zao, kwa kutengeneza

makundi ya wale Waislam ambao wanaojitenga na wenzao katika Miandamo ya Mwezi

ya ardhi zao wanazoishi kwa ajli ya kuwafuta wao na kuwaimarishia mamlaka na itiqadi

zao.


247

Na hivyo kutokana nao basi takriban katika kila ardhi za Waislam sasa hivi kuna makundi

ya wanaofuata Muandamo wa mwezi wa Saudia na kuna wafuatao Muandamo wa nchini

mwao, hivyo kutokana na kuwepo kwa Unafiq katika Jamii za Kiislam basi ndani ya kila

nchi ambayo watu wanasali sala zao katika wakati mmoja basi kuna Ramadhani mbili na

sikukuu nne tofauti, na hao wanaofuata Muandamo ambao si wa ardhi zao basi nao wao

wanasema pia Innama Nahnu Muslihoona yaani Kwa Hakika sisi ni Wenye Kutafuta

Suluhisho.

Kutokana na kutofahamu kwao basi watu hawa hua hawajui kuhusiana na Maumbile ya

Matokeo na Nyakati baina ya Viumbe na Muumba, na hivyo hawajui ukubwa wa uwezo

wa Allah Subhanah wa Ta’ala na kwa sababu labda hawajaifaham maana ya Ayat al

Kursy.

AYAT AL QURSY - NYAKATI NA MATUKIO YA VIUMBE MBELE YA

ALLAH SUBHANAH WA TA'ALA

Ayat Al Qursy ambayo ilishuka katika mji wa Madinah na mbali ya kua Ayat al Kursiy

kua inajulikana kama Ayat Al Arshi lakini hua pia inajulikana kwa majina yafuatayo:

1-Sayyidat Ayi Al Qur’an.

2-Al Ruqqyat.

3-Ayyati Al Haris.

4-Wa Al Muhsanati.

5-Wa Al Junnati.

6-Wa Al Waqqiyati.

7-Wa Al Kafiyyati.

8-Wa Al Sharifati.

9-Wa Al Aadhimati.

10-Wa Ashraf Ayati.

11-Wa Aadham Ayati.

12-WatudaAai fii al Tawrati Ayyati Allah.

Hivyo tunapozungumzia Ayat Al Kursiy basi hua tunazungumzia kuhusiana na maneno

Matukufu ya Allah Subhanah wa Ta’ala yaliyomo katika aya tukufu kuliko zote ambayo

ni yenye kusema kua:

‏﴿ٱهلل َُّ‏ لاَ‏ إِلَٰهَ‏ إِلا َّ هُوَ‏ ٱلحَْى ُّ ٱلْقَي ُّومُ‏ لاَ‏ أتَْخُذُهُ‏ سِ‏ نَةٌ‏ وَلاَ‏ نَوْمٌ‏ ل َّهُ‏ مَا فىِ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏

وَمَا فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ مَن ذَا ٱل َّذِى يَشْفَعُ‏ عِنْدَهُ‏ إِلا َّ إبِِذْنِهِ‏ يَعْلَمُ‏ مَا بَينَْ‏ أَيْدِيهِمْ‏ وَمَا


248

خَلْفَهُمْ‏ وَلاَ‏ يحُِيطُونَ‏ بِشَيْءٍ‏ مِّنْ‏ عِلْمِهِ‏ إِلا َّ بمَِا شَآءَ‏ وَسِ‏ عَ‏ كُرْسِ‏ ي ُّهُ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏

وَٱلأَرْضَ‏ وَلاَ‏ يَؤُودُهُ‏ حِ‏ فْظُهُمَا وَهُوَ‏ ٱلْعَلِى ُّ ٱلْعَظِيمُ‏ ﴾

Allahu la ilaha illa huwa alhayyu alqayyoomu la ta/khudhuhu sinatun wala

nawmun lahu ma fee alssamawati wama fee al-ardhi man dha alladhee yashfaAAu

AAindahu illa bi-idhnihi yaAAlamu ma bayna aydeehim wama khalfahum wala

yuheetoona bishay-in min AAilmihi illa bima shaa wasiAAa kursiyyuhu

alssamawati waal-ardha wala yaooduhu hifdhuhuma wahuwa alAAaliyyu

alAAadheemu (Aya Al Qursy - Surat Al Baqara 2:255)

Tafsir: Allah! La ilaha illa Huwa Hakuna anaestahiki Kuabudiwa Isipokua Yeye (Yeye

Allah Subhanah wa Ta'ala) Ni Mwenye Uhai wa Milele na ndie Mwenye Kujisimamia

juu ya Kila kitu na ndie Msimamizi juu ya Kila kitu (Yeye ndie ambae) Haimpitii Hali

ya Kusinzia wala ya Kulala Usingizi Kwake yeye Ndio kwenye Umiliki wa Kila

Kilichomo Mbinguni na Ardhini Jee Ni Nani yule Ambae atakaeweza Kuingilia

Mambo yake (Allah Subhanah wa Ta'ala) Bila ya Idhini yake? (Allah Subhnah wa

Ta'ala) Kwani yeye (Allah Subhanah wa Ta'ala) Ni mwenye Kujua juu ya kila kitu

Kabla ya kutokea kwake na Baada ya Kutokea kwake na Hakuna atakaekua na

Chochote kutokana na Ilm yake Isipokua kwa kile akitakacho (kijulikane) Na Arshi

yake (Ukubwa wake) Imeenea Mbinguni na Ardhini na wala hachoki katika

kuvihifadhi na kuvisimamia vitu (Vilivyomo ndani yake Mbinguni na Ardhini) Na

Yeye ndie Aliejuu Kidarja na Kiutukufu hakuna alie zaidi yake

Hii ni Aya ambayo ndani yake inabeba ujumbe Mzito sana, kwani inaelezea mambo

mengi ambayo wengi hatuyajui kutokana na Ufinyu wa Ufaham wetu. Na aya inathamani

na manufaa Makubwa Sana ambayo pia wengi wetu hatuyajui na hatuyathamini, kwa

sababu ni kawaida ya yule asiekijua kitu basi kua ndie asiekithamini.

Hivyo basi tunafahamishana ili angalau tupate kuyajua baadhi ya Mambo hayo, kwani

hatuwezi kuelezana yote, kwa sababu tukitaka kuelezana yote basi hatuwezi kuyamaliza

yote leo hii ambapo Miongoni mwa Mambo tusiyoyajua sisi Waislam wa leo Kuhusiana

na Aya hii basi ni Sifa Tukufu na Majina Matukufu ya Allah Subhanah wa Ta'ala.

Na hivyo tunashindwa Kufaham na Kuelewa Ukubwa wa Uwezo wa juu ya kila kitu wa

Allah Subhanah wa Ta'ala kama ilivyobainisha Ayat Al Kursiyu. Na Ukweli ni kua Hili

sio Jambo Dogo la Kulidharau au la kutokukumbushana kwa sababu linaweza

kumpelekea Mtu kua ni Mnafiq na kila mtu anajua sehemu ya Mnafiq baada ya Kufariki

kwake na kesho Akhera kama zinavyoonesha Aya na Hadith.


249

Na kutokana na kutojua Uwezo na Ukubwa wa Allah Subhanah wa Ta'ala na Maana ya

maneno ya Ayat Al Kursiyyu basi ndio maana unakuta watu wanaulizana Kuhusiana

kwanini baadhi ya Matukio Muhimu ya Kiislam yawe yatofautiane kiwakati Duniani na

hivyo Wasiojua kua ni wenye Kutaka kua lazima yawe ni yenye kutokea katika hali ya

Umoja Duniani kote, Ambapo hapa tunachukulia mfano wa Usiku wa Laylat Al Qadr,

Funga ya Arafa, Idd, n.k

Ambapo Mara nyingi watu wanashindwa kufaham kua Moja kati ya Sifa za Allah

Subhanah wa Ta'ala ni Al Hakim yaani ni Mwingi wa Hikma, pia ni Al Aadil yaani ni

Mwingi wa Uadilifu. Na Tunapozungumzia kuhusiana na sifa za Hikma na Uadilifu basi

ndani yake ndio tunaona kua Allah Subhanah wa Ta'ala hua ni Mwenye Kufanya kila

kitu chake kwa Hikma zake na kukisimamia kwa Uadilifu wake. Hivyo hua ni Mwenye

Kumlipa Mja wake kwa Uadilifu kulingana na Amali yake

Kwani tunapoiangalia Aya Al Kursiy basi tunaona hizi sifa 2 za Al Hayyu Al Qayyum,

ambayo ni sifa zinatupa Majibu ya Masuali yetu yote haya wanayoulizana wale wasiojua.

Kwa Sababu tunapozungumzia Al Hayy kwa Ufaham wa Kibinadam basi hua

inamaanisha kua Ni Mwenye Kuishi Milele, na tunapozungumzia Kuishi basi hua

tunazungumzia kuwepo kwa kitu husika, na tunapozungumzia kuhusu Milele basi hua

tunazungumzia hali ya Kitu kua katika Kutokua na Mwanzo wala mwisho na kutokana

na kutokua na Mwanzo wala mwisho basi kitu hicho hua katika kila sehemu kipo na kila

wakati kipo.

Hivyo tunapozungumzia kuhusiana na Sifa hii ya Allah Subhanah wa Ta'ala basi hua

inatubainishia kua kwake yeye hua Hakuna Mipaka ya kuwepo kwake na pia hakuna

mipaka ya kutokuwepo kwake katika ila sehemu na katika kila wakati.

Yaani alikuwepo, yupo na atakuwepo kwa Mda wote na Katika sehemu yeyote kabla ya

kuwepo kwake sehemu hio na baada ya kuwepo kwake sehemu hio na hii ni kwa Sababu

yeye ndie Muumba

Kwani kwa Kiumbe Jambo hili hua haliwezekani kwa sababu kiumbe hua na mipaka ya

Wakati wa kuwepo kwake ambao hua ni hali inayolingana na mazingira yake na tukio la

kuwepo kwake katika sehemu husika.

Kwani Sifa ya pili ya Jina Tukufu la Allah Subhanah wa Ta'ala liliopo ndani ya aya hii

baada ya Sifa ya Al Hayyu, basi ni sifa ya Al Qayyum. Ambapo hii ni Sifa ambayo yenye

Kumaanisha kua yeye Allah Subhanah Wa Ta'ala ni Mwenye Kujisimamia kila Kitu juu

yake, ambapo sifa hii hua inaenda Sambamba na sifa ya Al Ghaniyuu.


250

Yaani ni Tajiri mwenye kila kitu na asiehitaji kitu chochote kutoka kwa yeyote, ambapo

hapo hapo katika kua na Utajiri wake huo basi kwake yeye hakipungui kitu chochote

katika Kutoa kwake kwa ajili ya kuwapa Viumbe wake. Hivyo kwa upande mwengine

hii hua ni sawa na hali ya Sifa Al Qayyum kwani katika Kusimamia kwake juu ya viumbe

wake basi hua ni mwenye Kusimamia kwa Ukamilifu kila kitu alichokiumba tangu

kuanzia kabla ya kuwepo kwake kitu hicho mpaka kutokea kwake na pia baada ya

kutoweka kwake kitu hicho Hapa Duniani na kesho Akhera pia.

Na hii yote ni kwa sababu ya hii sifa ya Al Hayyu yaani Mwenye Kuishi Milele. Hivyo

Kwa Kuangalia kwa juu juu maana ya Sifa za Majina Matukufu haya mawili tu, ya hii

Ayat Al Qur'siy basi hua tunaona wazi kua, Allah Subhanah wa Ta'ala anaweza wa

Kumsimamia Kila Kiumbe wake katika Kila kitu chake na katika sehemu na mazingira

yake na katika kuwepo kwake kiumbe huyo.

Kwani kila Mtu mwenye Kuamini basi anajua kua, unapokua Unasali Basi hua

umesimama Mbele ya Allah Subhanah wa Ta'ala. Ambapo kutokana na Sifa ya Al Hayyu

Al Qayyum yaani ya Kua na Uhai wa Milele na kua ni Mwenye Kusimamia kila kitu basi

Allah Subhanah wa Ta'ala hua mbele ya kila Mtu na anamsimamia na kumuangalia

katika Sala yake yote iwe Mtu huyo Anasali Chumbani kwake, Ukumbini kwake,

Msikitini, Jela, kwenye Ndege, kwenye Boti n.k

Na hii ni kwa Kila Mtu na ni kwa kila wakati na kwa sehemu Duniani na Mbinguni kwa

upande wa kila Malaika. Hivyo Basi hii haimaanishi kua Kama Mtu anafanya Ibada

Nyumbani kwake basi hua hayuko Mbele ya Mola wake na hivyo pia hua hayuko mbele

ya Usimamizi wake

Hivyo hali hii huwepo pia pale tunapozungumzia kuhusiana na Funga ya Arafah, Usiku

wa Laylat al Qadr, Ramadhan, Idd, Ashura, n.k basi haimaanishi kua kwa sababu ya

kutokea matukio hayo Mtukufu katika Muda ambao ni tofauti na wakati ni tofauti na siku

ni tofauti kutokana na utofauti wa Muandamo wa Mwezi ambao umesababishwa

kutokana na Hikma zake Allah Subhanah wa Ta'ala ambae ni mwingi wa Hikma kua

isiwezekane kwa Mtu kulipwa Malipo ya Ibada alizofanya katika Siku husika na Mahala

husika kulingana na Mazingira yake husika.

Kwa Sababu asiekua na Uwezo wa Kusimamia Hali hio hua Ni Kiumbe, lakini si

Muumba wa Kila ambae ni Allah Subhanah wa Ta'ala ambae yuko mbali Sana tena Sana,

tena Sana na Sifa za Viumbe wake, kwani yeye Allah Subhanah wa Ta'ala ni mwenye

uwezo wa Kusimamia kila kitu kwa Ukamilifu na kwa Uadilifu katika kila wakati na kila

sehemu kulingana na Maumbile ya Ulimwengu na kila kitu kilichomo ndani yake ambae

yeye ndie alieviumba na kuviumbia mazingira yake husika kutokana na Hikma zake

kulingana na Maslahi ya Viumbe wake.


251

Hivyo kutokana na Sifa zake mbili hizi tu, Tukufu basi Allah Subhanah wa Ta'ala anao

uwezo wa Kusimamia Kikamilifu na Kiuadilifu kila kitu cha Viumbe wake katika kila

sehemu kulingana na wakati wake Viumbe hao na kulingana na Mazingira yao viumbe

hao Ardhini na Mbinguni.

Na Ndani yake Usimamizi huo, ikiwemo pia Ibada husika za Waja wake kulingana na

wakati wao na sehemu zao, hivyo hii haimaanishi kua aliefanya Ibada husika

inayotegemeana na nyakati za Muandamo wa Mwezi kwa kufuata Muandamo wa sehemu

aliyokuwepo kua hayuko sahih na atakosa Malipo sahih kutokana na kua ametofautiana

na waliofanya Ibada husika wa Saudia labda tukuchukulie mfano kwa waliokesha kwa

kufuata nyakati za Usiku wa Laylat Ul Qadr au kwa Mahujaj waliokuwepo kwenye Siku

ya Arafah na hivyo kua ni wenye kuangaliwa kwa Jicho la Rehma na Allah Subhnah wa

Ta’ala kutokana na sehemu na mazingira yao hapo kabla ya kufunga yeye jana yake.

La, Kwani kutokana na kua Allah Subhanah wa Ta'ala ni mwenye sifa ya Al Hayyu Al

Qayyum, basi bila ya shaka kwa Hikma zake na Uadilifu wake huwaangalia pia kwa jicho

la Rehma wale waliokesha au waliofunga siku ya pili yake kulingana na Wakati wao na

hali Mazingira yao kua ni yenye kutofautiana na mazingia ya sehemu nyengine kiasi ya

kua kwao wao haiwezekani iwe siku hio ndio siku ya Arafa, au Laylat al Qadr kwani

haya yanayotokana na Hikma zake katika Kuumba kwake na Kukadiria kwake kwa

Rehma zake, Maslahi na manufaa ya Viumbe wake.

Hivyo Siku husika au tukio husika iwe la Funga ya Arafa, Laylat ul Qadir n.k hua ni

Moja Mbele ya Allah Subhanah wa Ta'ala tu, na hii ni kutokana na kua yeye ni Al Hayyu

al Qayyum

Lakini kwa upande wa Viumbe hutofautiana na hii ni kulingana na Mazingira yao na

Maumbile yao hapa Ulimwenguni, kwani viumbe hua wana mipaka ya kisehemu na ya

kinyakati katika kuishi kwao ambayo hua hawawezi kuivuka kutokana na maumbile yao

na Maumbile ya Ulimwengu wao, kwa namna walivyoumbiwa na Mola wao ambae ni Al

Hayyu al Qayyum.

Ambae anao uwezo pia wa kuwajaalia viumbe wake hao kua wote wawe na Usiku mmoja

na Mchana mmoja na Muandamo mmoja Ulimwengu mzima lakini hakufanya hivyo

kutokana na Hikma zake na pia kulingana na Maslahi ya Viumbe wake ndani ya

Ulimwengu wake.

Hivyo kwa wasiojua na kutofaham haya kutokana na udogo wa ufaham wao na kutotaka

kujua zaidi kwao basi wao huona kua kufnya kwao hivyo wafanyavyo kua ni wenye

kutafuta Suluhisho la kutaka Umoja wa Uislam wa Kidunia tena kwa kuanzia na

kuwatimizia haki zao wale Waislam ambao wako mbali nao kimasafa kwanza, badala ya

kuanza kulitafuta suluhisho hilo kwa kuanzia Majumbani mwao kwenye familia zao,


252

kisha kwa majirani zao, kisha katika mitaa yao, kisha katika miji yao, na kisha ndio

unawatafuta wale wa kuwatekelezea haki zao wa Kimataifa.

Kwani hivi ndivyo ambavyo alivyoamrisha Allah Subhanah wa Ta’ala pale alipoweka

mpangilio maalum wenye kusimamia malengo ya kuboresha maslahi ya Umoja wa

Kiislam kwa utekelezaji wa haki za wanaostahiki upewa kipaumbele kwanza katika

kufanyiwa wema na ukarimu kama alivyoanisha katika aya ifuatayo:

‏﴿وَٱعْبُدُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَلاَ‏ تُشْرِكُواْ‏ بِهِ‏ شَيْئاً‏ وَبِٱلْوَالِدَيْنِ‏ إِحْسَاً‏ وَبِذِى ٱلْقُرْبىَٰ‏ وَٱلْيَتَامَ‏ ٰ ى

وَٱلْمَسَاكِينِ‏ وَٱلجَْارِ‏ ذِى ٱلْقُرْبىَٰ‏ وَٱلجَْارِ‏ ٱلجُْنُبِ‏

‏َوٱبْنِ‏ ٱلس َّبِيِل

وَٱلص َّاحِ‏ بِ‏ بِٱلجَنْبِ‏

وَمَا مَلَكَتْ‏ أَيمَْانُكُمْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لاَ‏ يحُِب ُّ مَن كَانَ‏ مخُْتَالاً‏ فَخُوراً‏ ﴾

WaoAAbudoo Allaha wala tushrikoo bihi shay-an wabialwalidayni ihsanan

wabidhee alqurba waalyatama waalmasakeeni waaljari dhee alqurba waaljari

aljunubi waalssahibi bialjanbi waibni alssabeeli wama malakat aymanukum inna

Allaha la yuhibbu man kana mukhtalan fakhooran (Surat An Nisaa 4:36)

Tafsir: Na muabudu Allah na wala usimshirikishe, na wafanyie wema Wazazi wako,

na Ndugu zako, na Mayatima na Masikini, na Jirani yako wa Karibu kiudugu na jirani

yako wa Mbali, na Rafiki yako wa Karibu, na Msafiri na Mtumwa wanaomilikiwa na

Mikono yenu. Kwani kwa hakika Allah hawapendi wenye kujiona na kua na Ufakhari.

Ambao aya hii kwanza Allah Subhanah wa Ta’ala ameanza kwa kuainisha kua haki ya

kwanza ya kusimamiwa ni ya Allah Subhanah wa Ta’ala, kisha inakuja haki ya Wazee

kisha ndugu zako ndani ya familia yako na kisha, kisha haki ya Mayatima na kisha ya

Masikini, na kisha haki ya Majirani wa karibu na wa mbali na wasafiri na watumwa.

Hivyo inakuaje Mtu unajiita Muislam halafu katika wakati wa kutekeleza haki ya Allah

Subhanh wa Ta’ala kwa mfano ya Kufunga mwezi wa Ramadhani basi wewe baada ya

kufuata mpangilio wa aya hii kwa kuanza kutekeleza haki ya Wazee wako na Ndugu

zako, na Mjirani zako basi wewe unaanza moja kwa moja na kutekeleza haki ya watu

mbao uko nao kwa umbali wa maelfu ya kilomita?

Kisha mtu unakula mwezi wa Ramadhani na kujigamba na kujiona na kujisifu kua wewe

huwezi kufuata Muandamo wa mwezi wa eneo ulilokuwepo pamoja watu wa jamii yako

ambao unaosali nao Sala tano pamoja na hivyo kushindwa kujumuika nao katika kufunga

au kufungua na kujumuika katika kusheherekea sikukuu moja ya Kiislam kwani lazima

usheherekee kivyako na kisha hua unaona fakhari kufanya hivyo.


253

Wakati hapo hapo aya hii imemalizia kwa kusema: ‘Innah Allaha la yuhibbu man kana

mukhtalan fakhooran’ yaani Kwani kwa hakika Allah hawapendi wenye kujiona na

kua na Ufakhari.

Inasikitisha kua watu hawa kwa ujinga wao basi hawajui kua katika kufanya kwao hivyo,

yaani kufuata Muandamo wa mwezi wa sehemu tofauti na jamii yao huku wakiwa

wanaona fakhari basi, kwa upande mmoja hua ni wenye kukosa Subra, kuwavunjia haki

zao watu wao katika jamii yao na kwa upande wa pili hua ni wenye kusababisha

kuvunjka kwa umoja wa Kiislam katika jamii husika ambapo hili hua ni jambo ambalo

hua ni lenye kufanywa na wale watu wenye sifa zenye malengo ya Unafiq ambayo ni

kuuvunja nguvu Uislam, na hivyo wewe kua ni mwenye kuyatekeleza malengo hayo na

kukupeleka kua ni miongoni mwa Wanafiq.

Na ndio maana aliusia Harith Al Muhasibi kwa kusema kua: ‘Ni hasara kwetu kama

ikiwa tutapoteza vitu vitatu ambavyo ni Muonekano Mzuri wa Sura zetu

unaojumuisha kua na heshima, Kauli nzuri zinazojumuisha na Uaminifu na Umoja

wa Kindugu wenye Nguvu Unaojumuisha Kutosalitiana’

Na tumeona mara kadhaa kua baada ya Allah Subhanah wa Ta’ala kuhimiza usimamiwaji

wa haki zake basi hua ni sambamba mwenye kusisistiza kusimamiwa kwa haki za wazee,

na pia kuna aya hadithi kadhaa zinazohimiza usimamiaji wa haki ndugu, Mke, Mume,

Watoto na familia wa ujumla na pia ziko zinazozungumzia haki za majirani zako ambapo

miongoni mwao ni pamoja na zile ambazo zinasema:

Amasema Salman Ibn Amr Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua: ‘Kutumia kwa ajili ya Maskini hua ni Sadaqa, lakini kutumia

kwa ajili ya Masikini ambae ni wa karibu yako hua ni sadaka ya mara mbili zaid,

ambapo Sadaka ya aina ya kwanza hua ni kwa kutokana na kuunganisha udugu na

Sadaqa ya pili hua ni kutokana na kile ulichokituma ambacho ni sadaqa ya kawaida

(Imam At Tirmidhii)

Ama kuhusiana na haki ya Jirani basi Amesema Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam

kua: ‘Migogoro ya kwanza itakayo hukumiwa katika siku ya Malipo basi ni ile

migogoro ya haki baina ya Mtu na Jirani yake.’ ambapo Ummu ul Muuminin Aisha

Radhi Allahu Anha alimuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Ya Rasul Allah!

Wakati mimi nnao Majirani wawili, jee ni Jirani yupi anaestahiki kupewa zawadi?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Yule Jirani ambae uko karibu nae

zaidi.’(Sahih Muslim)

Na amesema Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Jibril aliendelea kuniusia mimi kuhusiana na kua


254

na uhusiano mzuri na Jirani hadi nikafikiria kua mwishowe huenda

akawajumuisha katika mirathi’(Sahih Bukhari)’

Ambapo anasema Miqdad Ibn Aswad Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam aliwauliza Masahaba zake kwa kusema: ‘Hivi mnafikiriaje

kuhusiana na Zinaa’ Ambapo Masahaba wakasema: ‘Bila ya shaka ni Dhambi

iliyokatazwa na Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume wake Salallahu Alayhi wa

Salam na itakayobakia kua hivyo hadi katika Siku ya Malipo’ Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akasema: ‘Basi ni bora kwa Mtu awe ni mwenye Kuzini na

wanawake 10 kuliko kuzini na mke wa jirani yake’

Kisha akawauliza tena Masahaba zake: ‘Jee mnafikiriaje kuhusiana na Wizi?’’

Masahaba wakasema ; ‘Bila ya shaka ni Dhambi iliyokatazwa na Allah Subhanah

wa Ta’ala na Mtume wake Salallahu Alayhi wa Salam na itakayobakia kua hivyo

hadi katika Siku ya Malipo’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Basi ni

bora kwa Mtu kuiba kwenye nyumba 10 kuliko kuiba kwenye Nyumba ya Jirani

yake’(Imam Ahmad)

Na ukweli ni kua Mfano wa Unafiq wa aina kama hii uko katika hali nyingi sana ambazo

wasiojua hua hawazioni na hata wakivishwa Miwani basi bado Mtu atakua haoni kwa

sababu Allah Subhanah wa Ta'ala tayari ameshaweka wazi kama tulivyoona kwenye aya

tulizoziangalia

Kwani wengi wetu hua wanadhani kua Unafiq hua ni ule ulioainishwa kwenye Hadith ya

Abd Allah Ibn Amr Radhi Allahu Anhu ambayo inasema: ‘Sifa nne akiwa nazo mtu

basi Mtu huyo hua ni Mnafiq, na yeyote yule atakae kua nayo japo moja kati ya

hizo basi hua na maumbile ya Unafiq hado atakapochana nayo ambazo ni:

Akiaminiwa basi husaliti, Akisema basi hudanganya, Akitoa ahadi hua hatekelezi

na Akipigana au Kugombana basi huvuka mipaka.’(Sahi Bukhari)

Lakini unafiq hua uko katika aina mbili ambazo ni Unafiq wa Maneno na Vitendo na

Unafiq wa Imani, ambapo ingawa Unafiq wa Amali na maneno hua haumtoi mtu kutoka

kwenye Imani ya Dini ya Kiislam lakini maneno na vitendo vyake vinapozidi kua na

Unafiq basi wingi wake huo huweza kumpelekea Mtu kuingia kwenye Unafiq wa Imani

na hivyo kumungamiza mtu husika.

Kwani Ubaya wa Unafiq na Madhara yake yanapokosa Tiba kutokana na Mnafiq kuona

kua yeye yuko Sahih basi hua ni Mwenye kusababisha Madhara Makubwa zaid kwa

Kuambukiza Maradhi hayo mpaka kwenye Kizazi chake na hivyo kupelekea

kuidhoofisha na kuiharibu kwa kuidhuru Jamii husika ya Kiislam.


255

Na kwa kua Watu hawa hua ni waliomo ndani ya Jamii husika ya Kiislam basi ni wale

wenye Ilm na kujua tu ndio wanaowajua kua hawa ni Wanafiq. Kwani hata Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alisema: Tahadharini na Moyo wa Muumini Mwenye

Kujua. Naam..bila ya Shaka Kwani wenye kujua hua ni wenye Kuona kwa Jicho la

Mtizamo wa Moyo!

Na ndio maana ingawa mimi si mwenye kujua lakini hua Namuomba Allah

Subhanah wa Ta'ala Aniepushe na Ujinga wa Kutojua zaidi na pia na ujinga wa

kutofuata wenye kujua na hivyo kua ni mwenye kufuata wasiojua badala yake. Kwa

sababu hakuna ujinga Mkubwa zaidi kuliko kua na Ujinga wa kutojua na kisha

hapo hapo ukawa pia ni mwenye kufuata wale Wajinga Wasiojua na kisha pia kua

Hujui kua unawaofuata ni wale Wajinga wasiojua.

Kwani unapokua katika hali kama hii halafu ukawa unajiita kua ni Muislam basi hali

yako inakua kama vile alivyosema Allah Subhanah wa Ta'ala katika aya zenye

Kumithilisha ambazo zinasema;

‏﴿مَثَلُهُمْ‏ كَمَثَلِ‏ ٱل َّذِى ٱسْتَوْقَدَ‏ ‏َراً‏ فَلَم َّآ أَضَاءَتْ‏ مَا حَوْلَهُ‏ ذَهَبَ‏ ٱهلل َُّ‏ بِنُورِهِمْ‏

وَتَرَكَهُمْ‏ فىِ‏ ظُلُمَاتٍ‏ لا َّ يُبْصِرُونَ۞صُم ٌّ بُكْمٌ‏ عُمْيٌ‏ فَهُمْ‏ لاَ‏ يَرْجِ‏ عُونَ‏ ﴾

Mathaluhum kamathali alladhee istawqada naran falamma adhaat ma

hawlahu dhahaba Allahu binoorihim watarakahum fee dhulumatin la yubsiroona;

Summun bukmun AAumyun fahum la yarjiAAoona(Surat Al Baqara 2:17-18)

Tafsir: Mithili yao Watu hao ni Kama Mithali ya Wale Ambao waliowasha Moto (Ili

wapate Muangaza wa kuona njia) Na Kisha Moto Unapowaka kuwaangazia Basi

Anaichukua Allah Nuru yao Na Kisha Huwawacha Kwenye Giza Na Huku wakiwa Si

wenye Kuona (Hivyo watu jao hua) Ni Viziwi, Mabubu na Vipofu Wala Hawarudi

(kwenye Njia iliyokua Sahih)

Nadhani aya ziko wazi kua hali ya Wanafiq hua ni wenye Kujiona kua wako sahih katika

Mambo yao na husema kua Wanajenga Uislam kumbe hua wanauvunja badala yake na

wanapoambiwa kua Wanafuata wasiojua basi hali yao hua ni:

Summun - Viziwi - Yaani Hua Wabishi hawakusikii wala hawakusikilizi hata

uwasomeshe vipi.


256

Bukmun - Mabubu Yaani Watapigwa na Mshangao na kukushangaa wewe Badala

yake kama vile anavyokua Bubu ambae hawezi kusoma Midomo yako unaposema

na Wala hawezi kusoma Alama za Vitendo vyako hivyo hakujibu kua amekubali

kua Kakosea.

Aumyun - Vipofu Yaani Hawaoni Ukweli wa Unayowaonesha.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala pia anawaelezea katika aya isemayo:

‏﴿وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ‏ تُعْجِ‏ بُكَ‏ أَجْسَامُهُمْ‏ وَإِن يَقُولُواْ‏ تَسْمَعْ‏ لِقَوْلهِِمْ‏ كَأَن َّهُمْ‏ خُشُبٌ‏

م ُّسَن َّدَةٌ‏ يحَْسَبُونَ‏ كُل َّ صَيْحَةٍ‏ عَلَيْهِمْ‏ هُمُ‏ ٱلْعَدُو ُّ فَٱحْذَرْهُمْ‏ قَاتَلَ‏ هُ‏ مُ‏ ٱهلل َُّ‏ أَ‏ َّنى

يُؤْفَكُونَ‏

Wa-idha raaytahum tuAAjibuka ajsamuhum wa-in yaqooloo tasmaAA liqawlihim

kaannahum khushubun musannadatun yahsaboona kulla sayhatin AAalayhim

humu alAAaduwwu faihdharhum qatalahumu Allahu anna yu/fakoona (Surat Al

Munafiqun 63:4)

Tafsir: Na kama ukiwaangalia basi miili yao inakuvutia, na wanapozungumza basi

utasikiliza maneno yao, wao ni kama mapande ya Mbao yaliyoenegemzwa ukutani,

wanadhani kua kila kilio ni dhidi yao. Wao ndio Maadui hivyo tahadhari nao, Laana

ya Allah juu yao, wamepotea sana.

Naam kwani Wanafiq hua hawana ufaham, wanavutia kimuonekano, na kimaneno lakini

kiakili hua hawana maana yeyote kama mbao ambazo zimeegemezwa ukutani zikiwa

zinaharibika

Kwani hio ni kwa juu juu tu kuhusiana na Madhara ya Unafiq wa Wanafiq Dhidi ya

Uislam Waislam, Unafiq wa Wanafiq dhidi ya Waislam Wenzao, katika kuvunja Umoja

wa Waislam, Kuwakandamiza Waislam, Kuwadhulumu Waislam n.k

Kwani Amesema tena Hasan Al Basr kua: ‘Muislam hubakia kua ni Muislam pale

anapokua anajiusia Nafsi yake na kuendelea kujichunga kwa kujihesabia Kasoro

zilizomo ndani ya Nafsi yake’

Na akasema Imam Yusuf Ibn Asbati kua: ‘Unyenyekevu Ni kumuona na Kumfikiria

Ibn Adam mwenzako kua ni mbora zaidi yako mbele ya Mola wako’


257

SURAT AL MAA’UN – UMUHIMU WA KUJALI MAYATIMA,

MASIKINI NA SALA KATIKA DINI YA KIISLAM.

Allah Subhanah wa Taa’la anatuambia kuhusiana na yule Mtu asiefanya vile alivyofanya

Nabii Zakarriyah pamoja na Makuhani wenzake katika kukimbilia kuchukua majukumu

ya ulezi wa Mtoto Yatima basi hua ni sawa na wale wenye kukadhibisha siku ya Malipo

ambapo ndani yake kuna Makafiri na pia kuna wanaojiita kua ni Waislam lakini

hawatekelezi majukumu yao Kiislam, na hivyo kua ni hua ni wenye sifa za Unafiq.

Na ili kuangalia hayo na kuweza kuyafaham vizuri basi moja kwa moja na tuingie

kwenye Surat Al Maaun ambayo ni Moja kati ya Sura ndogo miongoni mwa Sura ndogo

za Qur'an, kwani ina aya 8 tu, tukiijumuisha ndani yake na Biismi Allahi Rahmani Rahim.

Hivyo kama tunavyoiona Udogo wake lakini hii ni Sura ambayo ina Ujumbe Mzito sana

ndani yake. Kwani ni Sura ambayo inazungumzia Sifa za wale ambao ni Wenye

Kuikanusha Dini ya Kiislam. Ambapo kwanza inabidi tujue kua tunapozungumzia

kuhusiana na hali ya Kukadhibisha na Kukikubali kitu basi hua ni hali mbili tofauti

zinazopingana kimaana.

Ambapo hali ya kwanza hua ni hali ya Kukikubali Kitu, na hii hua ni hali ya Kuthibitisha

Hali ya kitu, iwe katika kuwepo kwake au katika kuonekana kwake kua kitu hicho kweli

kipo na kama kina manufaa ama la. Na mara nyingi ili kitu kikubalike basi hubidi

kionekane Uzuri wake au Manufaa yake.

Ambapo kukithibitisha kitu hua ni kazi rahisi sana kuliko kazi ya Kukadhibisha kitu

ambayo ndio hali ya pili yenye maana ya Kutokikubali kitu, na hivyo hua ni hali ya

kinyume ya hali ya kwanza ya Kukikubali kitu. Ama tunapozungumzia Ugumu wa

Kukikadhibisha Kitu basi mara nyingi hua ni kazi kubwa zaid, kwani ili ukikadhibishe

kitu basi hukubidi kwanza uthibitishe hicho kitu kama kipo au hakipo.

Na baada ya kuthibitisha kua kipo basi inabidi utafute kasoro zake, na ili ujue kasoro ya

kitu basi inakubidi Uingie ndani ya hicho kitu ukifaham ndani nje kisha ndio unaweza

ukakitoa kasoro zake kulingana na Ufaham wako. Ambapo hapo hapo ndani ya kitu

husika basi wewe unaetafuta kasoro basi huenda ukagundua kasoro kulingana na

Mtizamo wako, lakini kumbe kulingana na Mtizamo wa aliekitengeneza kitu hicho basi

hio unayoiona wewe kua ni kasoro juu ya kitu hicho, basi hua ndio Ubora wa kitu hicho

ambao huwezi kuujua mpaka akufafanulie yule aliekitengeneza kitu hicho, kisha na

wewe uwe tayari kukubaliana na Mtizamo wake.


258

Hivyo tunapoiangalia Surat Al Maaun basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta'ala ambae

ndie alieanzisha Dini ya Uislam ambayo ni Njia ya Mfumo wa Maisha ambayo inatakiwa

kufuatwa na Viumbe wa Allah Subhanah wa Ta'ala katika kuishi kwao hapa

Ulimwenguni kwa ajili ya manufaa yao hapa Duniani na Akhera na kwa manufaa ya

Viumbe wengine hapa Ulimwenguni. Basi tunaona Kua Allah Subhanah wa Ta'ala

Anautetea Mfumo wake huo aliouweka kwa ajili ya Viumbe wake hapa Duniani kua ni

Mfumo bora ambao hautakiwi kukadhibishwa.

Na hivyo basi Mfumo huo ambao ni wa Njia ya Maisha ya Kiislam hua hauwezi

kukadhibishwa isipokua na Watu wa Aina Mbili.

Ambapo wa kwanza ni Makafiri yaani wanaomkadhibisha kabisa Allah Subhanah wa

Ta'ala na kisha wa pili ni Wanafiq Ambao wao ni wenye Kuwadanganya Ibn Adam

wenzao na pia Kuzidanganya Nafsi zao kua Wameamini lakini kumbe ni wenye

Kukadhibisha Kutoka ndani ya Imani ya Dini ya Kiislam.

Kwani Surat Al Maun inaweka wazi Ubaya wa Wanafiq kwa kuwanasibisha na wale

ambao ni wenye Kuikadhibisha/Kuipinga Dini ya Allah Subhanah wa Ta'ala, na Ubaya

zaidi ni kua Ukabidhishaji huo unatoka Ndani ya Nafsi za Wafuasi wa Dini ya Kiislam.

kama zilivyobainisha aya zifuatazo zilizobainisha sifa 6 za wale wenye kukadhibisha

Dini na Siku ya Malipo ambapo sifa 2 kati yake ni za wale wasiowajali Mayatima na

Maskini, na sifa 4 zilizobakia ni za Waislam wa Kuchovya ambapo aya zinasema:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞أَرَأَيْتَ‏ ٱل َّذِى يُكَ‏ ذِّبُ‏ بِٱلدِّينِ۞فَ‏ ذٰ‏ لِكَ‏ ٱل َّذِى يَدُع ُّ

ٱ لْيَتِي مَ‏ ‏۞وَلاَ‏ يحَُض ُّ ٰ عَلَى طَعَامِ‏ ف ٱلْمِسْكِينِ۞‏ َوَيْلٌ‏ لِّلْمُ‏ صَلِّ‏ ينَ‏ ۞ ٱل َّذِينَ‏ هُمْ‏ عَن

صَلاَهتِِمْ‏ سَ‏ اهُونَ۞‏ ٱل َّذِينَ‏ هُمْ‏ يُرَآءُونَ‏ ۞ وَيمَْنَعُونَ‏ ٱلْمَاعُونَ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Araayta alladhee yukadhdhibu bialddeeni;

Fadhalika alladhee yaduAAAAu alyateema; Wala yahudhdhu AAala taAAami

almiskeeni; Fawaylun lilmusalleena; Alladheena hum AAan salatihim sahoona;

Alladheena hum yuraoona; WayamnaAAoona almaAAoona (Surat Al Maun 107:1-

7)

Tafsir: Kwa Jina La Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma, Hivi Jee

Umemuona wewe yule ambae anakadhibisha Dini? Huyu ni yule ambae ni mwenye

kumfukuza Yatima; Na kisha yule ambae hahimizi kulisha Masikini; Na Kisha Ole

Wao wale Wenye Kusali. Wale Ambao juu ya Sala zao Sahuna (Wanazidharau na


259

kuzichelewesha kwa kutosali katika wakati wake). Wale wenye kufanya Mema ili

waonekane, na Wenye kukataa Maaun (Kutoa japo kitu kidogo).

Tunapoiangalia aya ya kwanza ya Sura hii basi tunaona kua iko katika hali ya kuhoji kwa

kutumia neno Araayta ambalo ni lenye kutokana na neno Raa ambalo hua ni lenye

kumaanisha Kuona, Kufikiria, Kua na Mtizamo au Kudhania.

Na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia nneno Araayta hapa wa ajili ya kututaka

tuwe makini na kile anachotaka kutuonesha au kutubainishia kwenye aya zinazofuatia

baada ya hio, ambapo mwishoni mwa aya hii basi Allah Subhanah wa Ta’ala anatuwekea

wazi kua hilo jambo analotaka kutubanishia basi lina madhara makubwa sana ambayo

yanaweza kumpelekea Mtu kupoteza Imani yake.

Ili kufaham uzito wa kauli hii basi na tuchukulie mfano wa kua Kuna watu wamekaa

chini ya Mti halafu akaja mtu na kuja kusimama kwa mbali kidogo mbele yao, kisha mtu

huyo ambae anaona kila kitu chao watu hao basi akawaambia: ‘Hivi jee mmemuona

huyo Nyoka hapo alie juu yenu?’

Hivyo jee hali itakuaje kwa watu waliokuwepo chini ya Mti huo? Naam..hivyo hali hii

basi inatuonesha namna hali inavyotakiwa iwe kwa kila Muumini mwenye kuoneshwa

na kutakiwa kuyaangalia na kukaa mbali nayo yale ambayo yanayotakiwa kujihadhari

nayo na aya hii.

Halafu pia imetuma Neno Dana ambao kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Dini,

Kukubali Imani ya Dini, Kuamini Iman ya Dini, Kutumikia, Kuhukumu au Kuhudumia.

Neno Dana pia hua ni Jina la Mtoto wa Kike ambalo hua linamaanisha Lulu Kubwa Sana.

Ambapo neno Dana pia limetoa neno Dayn ambalo hua linamaanisha Deni au Mkopo.

Na pia neno Dana ndio lililotoa Neno Dinun ambalo humaanisha Malpo, Mamlaka,

Usimamizi, Shariah, Hukumu ya Kidini, Ushindi na pia hua linamaanisha Utiifu.

Hivyo tunapoiangalia maana ya neno Dana kimatumizi basi hua inategemea na sehemu

na sehemu kwa mfano katika ile hadith isemayo:

Alisema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Al Dinu Nasihat’ yaani Dini ni

Nasiha au kunasihiana. Hivyo Masahaba wakamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salaam : ‘Juu ya nini?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Juu ya Allah

Subhanah wa Ta’ala, na Kitabu chake na Mtume wake na juu ya viongozi wa Dini

ya Kiislam na Juu ya Waislam wa Kawaida.’ (Sahih Muslim)


260

Na neno Dana pia hutumika katika Kumaanisha Kitendo Chochote Kile iwe Kizuri au

Kibaya. Na hii ndio maana iliyotumika kwenye ile Hadith ambayo ni Mursal, yaani

Hadith ambayo imenukuliwa na Tabiina kutoka kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam bila ya kupitia kwa Sahaba ambayo inasema kua: ‘Amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua Wema hauharibiki, Dhambi haisahauliki, Deni halifi

hivyo kua kama utakavyo kwani Kama Tadiinu Tudan’ ambapo maneno Kama

Tadiinu Tudani hua yanamaanisha kua Kama utakavyofanya basi nawe ndivyo

utakavyofanyiwa.

Hivyo ingawa wengi miongoni mwa Wafasiri hapa hua wanatafsiri kwa kusema kua:

Araayta alladhee yukadhdhibu bialddeeni hua inamanisha Hivi jee umemuona yule

ambae ni mwenye kuikadhibisha Siku ya Malipo?

Lakini pia kwa kua Neno Al Diin lililotumika hapa linatokana na neno Dana ambalo

maana yake ni kama tulivyoifafanua hapo awali tunapozungumzia Mtu anaeikadhibisha

Dini ya Kiislam hua pia ni mwenye kukadhibisha Siku ya Malipo, na anaekadhibisha

siku ya Malipo basi hua pia ni mwenye Kuikadhibisha Imani ya Dini ya Kiislam

Hivyo basi kimaana tafsiri hizi mbili hua zimetokana na neno moja na hivyo pia

zinaendana sambamba kimaana ambapo kwa upande wa wengi sana waliotafsiri neno Al

Diin katika aya hii kua Ni siku ya Malipo basi wao wamechukua Mtizamo wa Bahr Ul

Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu.

Na sio kama mimi sikubaliani na tafsiri hio, La. Bali nimetafsiri hivyo kama

walivyotafsiri wengine wachache kwa sababu hua napenda Watu wajue na Mitizamo

tofauti. Kwani alisema Imam Abu Hanifa kua Mwenye kujua Mitizamo tofauti na sababu

zake basi ndie mwenye kujua vizuri zaid.

Naam..hivyo tunapoangalia aya yetu hii ya kwanza ya Surat Al Maaun basi tunaona kua

hapa Allah Subhana wa Ta'ala anamwambia Mtume wake Salallahu Alayhi wa Salam.

Na hapo hapo anatuambia sisi Waislam mimi na wewe Ili tupate kutafakkar kuhusiana

na jambo tunalouliziwa na Mola wetu ambalo ni:

Araayta alladhee yukadhdhibu bialddeeni; - Hivi Jee Unamjua yule ambae Ndie

anaekadhibisha Dini (Ya Kiislam au Kuwepo kwa Siku ya Malipo)?

Bila ya shaka hili si suali dogo, bali ni suali kubwa na zito sana na hivyo basi Allah

Subhanah wa Ta'ala anatutanabahisha Umuhimu wa kutafakkari Suali hili na hivyo

kututaka kua tunaposikia maneno yake haya basi tunatakiwa tuache kila kitu

tunachofanya na kuondoa kila kitu katika Ufaham wetu, ili tupate kujua ni nani hao

wenye Sifa ambayo ni yenye kuenda Kinyume na Maamrisho yake ambayo ndio Nguzo

ya Imani ya Dini ya Kiislam.


261

Na hapo hapo kututaka sisi mimi na wewe Kukaa mbali na wenye Sifa hizo zenye

kuangamiza ikiwemo ile ya kutowajali Mayatima na Masikini ambazo tumeshaziangalia

hapo kabla na ndio sababu ya kuitafsiri Surah hii ya Al Maun,

Hivyo miongoni mwa Watu wanaokadhibisha Dini na Siku ya Malipo basi ni wale wenye

Kuwafukuza na kutowajali Mayatima na Masikini kama zilivyosema aya:

‏﴿فَذٰ‏ لِ‏ كَ‏ ٱل َّذِى يَدُع ُّ ٱلْيَتِيمَ‏ ﴾

Fadhalika alladhee yaduAAAAu alyateema; (Surat Al Maun 107:2)

Tafsir: Huyu ni yule ambae ni mwenye kumfukuza Yatima;

Ambapo tunaona kua aya hii imetumia neno Da’Aa ambalo hua linamaanisha Kusukuma.

Kufukuza, Kutumia Nguvu katika kupingana na Kitu. Allah Subhanah wa Ta’ala

ameitumia tena neno hili pale aliposema katika ya zifuatazo:

ف َوَيْ‏ ي لٌ‏ َوْمَئِذٍلِّلْمُ‏ كَ‏ ذِّبِ‏ ينَ‏ ‏۞ٱل َّذِينَ‏ هُمْ‏ فىِ‏ خَوْضٍ‏ يَلْعَبُونَ۞يَ‏ وْمَ‏ يُدَع ُّونَ‏ إِلىَٰ‏ ‏َرِ‏

جَ‏ هَ‏ ن َّمَ‏ دَ‏ عًّا﴾‏

﴿

Fawaylun yawma-idhin lilmukadhdhibeena; Alladheena hum fee khawdhin

yalAAaboona; Yawma yudaAAAAoona ila nari jahannama daAAAAan(Surat At

Tur 52:11-13)

Tafsir: Ole wao katika Siku hio wale wanaokadhibisha; Ambao wanajiingiza kwenye

kucheza mambo ya Kiupuuzi. Hio ni siku ambayo watakaposukumwa kwa nguvu

kwenye Moto kwa Msukumo mbaya sana.

Hivyo hili ni neno tofauti kimaana na lile neno Da’a ambao hua linamaanisha Dua, Kuita,

Kuomba, Kukaribisha, Kusali, Kuomba Dua, Kulia kwa ajili ya Kutaka kitu, kama vile

lilivyotumika katika aya ifuatayo:

‏﴿وَقَالَ‏ رَب ُّكُمْ‏ ٱدْعُونيِ‏ ۤ أَسْتَجِ‏ بْ‏ لَكُمْ‏ إِن َّ ٱل َّذِينَ‏ يَسْتَكْبرُِونَ‏ عَنْ‏ عِبَادَتِى

سَيَدْخُلُونَ‏ جَهَن َّمَ‏ دَاخِ‏ رِينَ‏ ﴾


262

Waqala rabbukumu odAAoonee astajib lakum inna alladheena yastakbiroona

AAan AAibadatee sayadkhuloona jahannama dakhireena (Surat Ghafir 40:60)

Tafsir: Na amesema Mola wenu: ‘Niombeni Nitakujibuni. Kwani kwa hakika wale

wanaozifanyia Kibri Ibada zangu, wataingia Motoni kwa Muadhirisho.’

Hivyo maneno Fadhalika alladhee yaduAAAAu alyateema basi hua yanamaanisha ‘Huyo

ni yule ambae ni mwenye kumfukuza Yatima’ yaani baada ya kumuita Yatima kwa upole

na kumuonea Huruma basi hua ni mwenye kumfukuza, kutotaka kua karibu nae au kua

na ukaribu nae kutokana na kutomuonea huruma, kwani yeye hua hajali hali ya Mtoto

huyo kua ni mwenye kuhitaji Msaada, Ukarimu, Upendo na Huruma kwani hua ni

mwenye udhaifu kutokana na kua hana wazee kama vile ilivyokua kwa watoto wengine

ambao ni wenye kutetewa haki zao, kusimamiwa mambo yao, kutunzwa na kuhudumiwa

na wazee wao katika kila hitajio lao.

Na kutokana na kua Uislam ni Dini ya Uadilifu, Ukarimu. Upendo, Upole na hivyo kua

ni yenye kusimamia Maslahi ya Viumbe hapa Duniani kulingana Maamrisho na Sharia

za mwenyewe Muumba wa Dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, basi yeyote yule

atakaemfukuza Yatima hua ni mwenye Kukadhibisha Dini.

Kama ilivyosema Aya ya Mwanzo kushuka ambayo inayowazungumzia watu hao kwa

kuwabainishia Allah Subhanah wa Ta’ala anawaona kwani anaangalia na kuona kila kitu

kwa urahisi mkubwa sana na kwa umakini mkubwa sana na kuona kila kitu juu yao,

katika aya zilizotumia neno Rasada ambalo hua linamaanisha Kukaa Kwa Kuangalia kitu

kwa umakini mkubwa sana ndani nje bila ya kukosa kuona chochote juu ya kitu hicho

kinachoangaliwa, na hivyo kua na uwezo wa kukivamia na kukifanya vyovyote kitu

hicho kinachoangaliwa;

Ambapo hizi si aya nyengine bali ni zile ambazo anasema Imam Muqatil Ibn Sulayman

kuhusiana nazo kua: ‘Aya zilishushwa kuzungumzia Khalaf Ibn Ummayah ambae

alikua akimlea Yatima aitwae Qudamah Ibn Maz'un’ pale aya ziliposema:

‏﴿إِن َّ رَب َّكَ‏ لَبِٱلْمِرْصَادِ۞فَأَم َّا ٱلإِنسَانُ‏ إِذَا مَا ٱبْتَلاَهُ‏ رَب ُّهُ‏ فَأَكْرَمَهُ‏ وَنَع َّمَهُ‏ فَيَقُولُ‏ ِ رَبيّ‏ ۤ

أَكْ‏ رَمَنِ۞وَأَم َّآ إِذَا مَا ٱبْتَلاَهُ‏ فَقَدَرَ‏ عَلَيْهِ‏ رِزْقَهُ‏ فَيَقُولُ‏ رَبيّ‏ ِۤ أَهَ‏ انَنِ۞كَلا َّ بَل لا َّ تُكْرِمُونَ‏

ٱ لْيَتِي مَ﴾‏


263

Inna rabbaka labialmirsadi; Faamma al-insanu idha ma ibtalahu rabbuhu

faakramahu wanaAAAAamahu fayaqoolu rabbee akramani; Waamma idha ma

ibtalahu faqadara AAalayhi rizqahu fayaqoolu rabbee ahanani; Kalla bal la

tukrimoona alyateema. (Surat Al Fajr 89:14-17)

Tafsir: Kwa hakika Mola wako ni mwenye kuwaangalia kwa uangalifu mkubwa sana,

ama kuhusiana na Mtu pale anapojaribiwa na Mola wake, kwa kumkirimu na

kumneemesha, basi hua ni mwenye kusema: ‘Mola wangu amenikirimu’ Lakini

anapomjaribu kwa kumbania riziki yake, basi hua ni mwenye kusema: ‘Mola wangu

amenidhalilisha’ (Wataambiwa) La Bali Nyinyi Mlikua Hamuwakirimu Mayatima.

Na hivyo aya kua ni zenye Kuonya kuhusiana na Kutowajali Mayatima, kuwavunjia Haki

zao na kuzitumia sivyo Mali zao. Na pia kutowarudishia Mali zao baada ya kufikia Mda

wao wa kurudushiwa Mali hizo.

Ambapo amesema Allah Subhanah wa Ta'ala katika Surat An Nisaa kua:

‏﴿إِن َّ ٱل َّذِينَ‏ ‏َْكُلُونَ‏ أَمْوَالَ‏ ٱلْيَتَامَى ٰ ظُلْماً‏ إِنم ََّا ‏َْكُلُونَ‏ فىِ‏ بُطُوِِمْ‏ ‏َراً‏ وَسَيَصْلَ‏ وْنَ‏

سَعِيراً‏ ﴾

Inna alladheena ya/kuloona amwala alyatama dhulman innama ya/kuloona fee

butoonihim naran wasayaslawna saAAeeran (Surat An Nisaa 4:10)

Tafsir: Kwa Hakika Wale ambao wanaokula Mali za Mayatima kwa Dhulma basi kwa

Hakika Wanakula Ndani ya Matumbo yao Moto na Watachomwa kwenye Moto Mkali

Sana.

Kwani tunapoiangalia Aya yetu hii basi tunaona kua ni Miongoni mwa Aya ambazo

zinawazungumzia wale Watu ambao ni wenye Kulea Mayatima na hivyo kua pia ni

Wenye kusimamia Mali walizorithi Mayatima hao kutoka kwa Wazee wao waliofariki.

Ambapo Msimamizi au Mtunzi au Mlezi wa Yatima husika hua pia na Jukumu la

kuisimamia Mali hio ya Mirathi kama vile ambavyo walivyoachiwa kuwasimamia

Mayatima hao. Hivyo basi kama vile ambavyo Uislam unavyoamrisha Kuwasimamia

Mayatima Kiuadilifu basi ndio hivyo hivyo unavyotakiwa usimamizi juu ya Mali zao.


264

Ambapo amesema Abu Said Al Khudri Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wakati Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alipoenda katika Safari ya Miraj basi alikutana na Watu

ambao Wana Midomo Mirefu kama ya Ngamia

Na inaposemwa kua ni Midomo mirefu basi haimaanishwi kua ni Umbo la Mdomo

linalojumuisha na Mifupa Ya Kidevu na Meno yake, La. bali hua inamaanishwa Nyama

Mbili ziliopo kwenye Milango ya Midomo yetu, ambazo umuhimu wake hautokani na

kua n kw ajili ya kunyonyea ziwa la Mama tu tunapokua wadogo lakini pia zina aina

tofauti za umuhimu wa kimaumbile.

Kwani katika Viungo vya Mwili wa Ibn Adam ambavyo ni vyenye Hisia kali sana basi

ni Nyama hizi mbili za Midomo. Kwani Nyama mbili hizi za Midomo ni miongoni mwa

Nyama ambazo laini za Ibn Adam kwa sababu ni Nyama za Ndani ya Mwili zilizoumbwa

na Allah Subhanah wa Ta’ala kua ziwe Nje kwa sababu ya matumizi yake kwa mwili wa

Ibn Adam na pia hapo kua ni pambo la wake, na hivyo zina Viunganishi vya vyanzo vya

hisia Milioni Moja vinavyosafirisha hisia moja kwa Moja kwenye Ubongo.

Na wingi wa Hisia zake unaonekana pale unapompapasa Mtu taratibu katika sehemu hizo

kwa kidole kikavu juu yake, wakati nyama hizo zina ukavu basi mtu huyo lazima

Atajiramba Midomo yake. Kutokana na kua ni viungo vyenye hisia kali sana basi

Midomo pia hua na kazi ya kurekebisha joto la mwili kwa kulipunguza na kulitoa nje au

kulihifadhi zaid pale inapohitajika na ndio maana ikawa unapoona baridi basi mtu hua

unabana midomo yako, na pia ndio mana Watu wanaoishi kwenye nchi za Baridi yaani

Wazungu wakawa na maumbile ya Midomo myembamba kwa ajili ya kuhifadhi zaidi

Joto la mwili wao katika kipindi cha baridi kali, na watu wenye kuishi kwenye ardhi za

nchi Joto hua na maumbile ya kua na Midomo minene.

Na kutokana na kua ni kiungo chenye Hisia Kali sana cha Mwili wako, basi ndio maana

ikawa mtu katika kuonesha wingi wa hisia za Mapenzi yako na pia kupokea wingi wa

Hisia hizo basi hua Kiungo hicho hua kinatumia kwa ajili ya kusafirisha na kuwasilisha

Hisia za Mapenzi kwa njia ya Kunyonya au Kubusu iwe Mkono, Paji la Uso, Pua, Shavu,

Mdomo Mwengine, Shingo, Ziwa n.k

Kwani pia kuwasilisha hisia kwa kiungo cha Mdomo hua kuna athari kubwa na nyingi

zaid tofauti na viungo vyengine. Kwa upande mwengine wa mfano mzuri wa kuhisi wingi

wa hisia hizo basi fikiria pale unapokua unakula chakula kisha ukakosea na ukajitafuna

tu Mdomo kwa Bahati mbaya au ukaungua kutokana na umoto wa chakula, hua inakuaje

hali yako.

Na si hivyo tu, ingawa kila Mtu ana maumbile yake Nyama hizo lakini pia Allah

Subhanah wa Ta'ala amejaalia Kila Ibn Adam kua na Alama za peke yake za Midomo


265

yake, yaani kama vile ambavyo kila Mtu ana alama zake peke yake za Vidole vyake basi

na Lips pia zina alama ya peke yake.

Naam..Hivyo Abu said Al Khudri Radhi Allahu Anhu anatuambia katika Hadith hio kua:

‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliona katika Safari yake ya Miraj kua

Kuna Watu wana Nyama za Midomo Mirefu kama ya Ngamia, na Wanavutwa

kutokana nazo

Na kisha Wakawa Wanalishwa Mawe ya Moto ambayo Yanaingizwa Midomoni

Mwao na Kutokea kwenye Tupu zao za Nyuma’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipomuuliza Malaika Jibril: ‘Jee ni Kina nani

hao?’

Basi Malaika Jibril akajibu: ‘Hao ni wale watu ambao ni wenye Kula Mali za Yatima’

Ambapo Ukali wa Adhabu yake basi kidoogo hua unaweza kuonekana pale Mtu

unapokula Pili pili kali sana, ambazo kimaumbile hua zina kemikali inayojulikana kama

Capsaicin ambayo hua iko katika hali ya mafuta mafuta yanayokaa kwenye Moyo wa

pilipili na sehemu ya nje ya Kokwa za pilipili, ambapo unapozigusa hizo basi hupelekea

nyama au ngozi yako kua na hisia ya kuzidi kwa joto katika sehemu uliyoigusisha katika

mwili wako, na hivyo sehemu hio ya mwili wako hua ni yenye kua na hisia za kuwaka

moto.

Moto ambao huupelekea Moyo wako kuzidisha mapigo yake na hivyo kuzalisha kemikali

nyenginezo mwilini mwako ikiwemo kemikali za Endorphins ambazo hua ni zenye kazi

ya kupunguza hisia za maumivu ndani ya Mwili wako, na hivyo kemikali hizi pia hua na

kazi ya kukufanya uhisi hisia za raha ya aina fulani ambayo ndio inayowafanya

wanaopenda Pilipili kuona chakula kua hakina Ladha bila ya kula na pilipili, ambapo wa

upande mwengine basi kemkali za Endorphins hua pia ni zenye kuhusika pia kukupa

hisia za raha inayopatikana katika wakati wa kuingiliana kimwili.

Na tunapozungumzia Kemikali hizi za Capsaicin basi ukali wake hua haupungui isipokua

kwa kutumia Maziwa ya baridi, na mbali ya kemikali ya Capsaicin lakini pia Pilipili hua

zina Vitamin C, Vitamin K, Vitamin B, Vitamin A, Madini ya Shaba na Potassium

ambazo husaidia katika kuujenga Mwili na kuulinda na maradhi mbali mbali.

Hivyo hapa hatuzungumzii mfano wa ukali wa Moto wa Duniani, bali tunazungumzia

mfano wa Ukali wa Maumivu ya kawaida tu ya joto la Pilipili, inapokuwashia Moto

Mdomoni au unapochukua kisha ukajipaka katika sehemu za Siri au katika sehemu

yeyote utakayojigusa Mwilini basi hali yake hua ni ya tafrani, isiyokua na kifani, Sasa

Jee hali yako itakuaje wakati umeshavutwa Nyama zenye hisia kali sana za Mdomo wako


266

Kisha Unalishwa Mawe Ya Moto yanaingia ndani ya Tumbo lako, yanautokotesha

Utumbo wako mpaka unachemka halafu inabidi Uyatoe Mawe hayo ambayo bado

yamoto.

Na hio ndio maana ya kua: Wanaokula Mali ya Yatima hua hawali chochote isipokua

Wanakula Mawe ya Moto, na hivyo ndivyo watakavyolishwa katika Siku ya Malipo

na Ndivyo watakavyoyatoa ndani ya Matumbo yao na kuyala tena na kuyatoa tena

kwa mfululizo..Allah atustiri na Adhabu kama hizo.

Kwani kwa upande mwengine basi anasema Imam Abd Rahman Al Suddi kua: ‘Mtu

yeyote yule anaekula Mali ya Yatima, Basi katika Siku ya Malipo atafufuliwa huku

akiwa anatokwa na Moto Mdomoni, Puani na Masikioni, Kiasi ya Kua Watu

watajua kua huyu alikua ni Mtu aliekua akila Mali ya Yatima.’

Na inaposemwa kua Mtu atatoka Moto basi haimaanishi kua hali yake itakua kama

Dragon au Mvuta sigara yaani hahisi Madhara ya Moshi wa sigara. La.

Bali hua inamaanisha kua Mtu anaungua mdomo kama alienyweshwa Uji uliotoka moja

kwa moja jikoni, lakini sasa hapa hali ni mbaya zaidi kwani, inakua katika kila sehemu

ya kiungo chake kinatoka Moto, Mdomoni, Machoni, Masikioni, Puani na kwenye

sehemu zake za Siri anaungua na kuwiva lakini Nyama za sehemu zake hizo zinaota tena

na tena na kuungua tena na tena. Yaani haya ni Maumivu yasiyosita wala kua na

Mwisho...Allah atustiri

Naam hio ndio maana ya aya yetu hio ya kwanza ya Surat An Nisaa 4:10 juu ya Adhabu

za Watakaokula Mali za Yatima kwani hua ni Dhulma Kubwa tena Sana, kwani Allah

Subhanah wa Ta'ala ametuwekea wazi katika aya ya Surat An Nisaa 4:10, kuhusiana na

adhabu ya kila anaekula Mali ya Yatima kua ni Mwenye Kujijazia Mawe ya Moto

Tumboni mwake, na kama tulivyoona pia kwenye Hadith.

Kwani sijui mimi na wewe tumehisi nini baada ya Kuifaham aya hio, kwa sababu Ingawa

Masahaba walikua wanawapenda Mayatima kutokana na Kuona Mfano Bora Wa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam namna alivyokua hakuwajali Mayatima.

Lakini iliposhuka Aya hii basi Masahaba waliingiwa na Khofu kutokana na Imani yao na

Taqwa mbele ya Allah Subhanah wa Ta'ala kiasi ya kua ilifikia hali Hata Chakula

alichopakuliwa Yatima basi wakawa wana hiyari wasikile hata kama Yatima huyo

ameshakula au ameshiba. Na hii ni kutokana na kuogopa Kuvutwa Midomo yao na

Kujazwa Mawe Moto ndani ya Matumbo yao.

Na Ndio Wenye Kujua hua Wanalia wanaposoma baadhi ya Aya kutokana kuhisi Uzito

wa Aya ndani ya Nyoyo zao.


267

Na hii ni kulingana na Mtu na Mtu kwani kuna wanaolizwa na aya za Adhabu na kuna

wanaolizwa na aya zinazosuta Nafsi, n.k Hivyo kama mimi na wewe tunasoma Qur'an

halafu hakuna hata aya moja ambayo inayoweza kutuliza na kutokwa na Machozi, basi

inabidi tujijue kua tuna kasoro tena kubwa sana.

Yaani aidha tuna Udhaifu wa kiimani na hivyo tuna Unafiq kwani hatujali na wala

hatugusiwa na maana ya Maneno hayo Matukufu, Au tunasoma Qur'an lakini hatujui

maana yake na hivyo haituathiri inavyotakiwa ituathiri, Hivyo tujiangalie kisha tujaribu

kutafuta Utatuzi wa Kasoro hizo.

Hivyo baada ya aya hio ya Surat An Nisaa 4:10 basi kama tulivyosema kua Masahaba

waliathiriwa na aya ifuatayo:

كَيْل

‏﴿وَلاَ‏ تَقْ‏ رَبُواْ‏ مَالَ‏ ٱلْيَتِيمِ‏ إِلا َّ بِٱل َّتىِ‏ هِ‏ ىَ‏ أَحْ‏ سَ‏ نُ‏ حَ‏ تى َّ ٰ يَبْ‏ لُغَ‏ أَشُد َّ هُ‏ وَأَوْ‏ فُواْ‏ ٱلْ‏ َ

‏َولَوْ‏ بِٱلْقِسْطِ‏ لاَ‏ نُكَلِّفُ‏ نَفْساً‏ إِلا َّ وُسْعَهَا وَإِذَا قُلْتُمْ‏ فَٱعْدِلُواْ‏ كَ‏ انَ‏ ذَا قُرْبىَٰ‏

وَٱلْمِيزَانَ‏

وَبِعَهْ‏ دِ‏ ٱهلل َِّ‏ أَوْ‏ فُواْ‏ ذٰ‏ لِكُ‏ مْ‏ وَص َّاكُ‏ مْ‏ بِهِ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تَذَك َّ رُونَ‏ ﴾

Wala taqraboo mala alyateemi illa biallatee hiya ahsanu hatta yablugha ashuddahu

waawfoo alkayla waalmeezana bialqisti la nukallifu nafsan illa wusAAaha wa-idha

qultum faiAAdiloo walaw kana dha qurba wabiAAahdi Allahi awfoo dhalikum

wassakum bihi laAAallakum tadhakkaroona(Surat Al Anaam 6:152)

Tafsir: Na Wala Usiikaribie Mali ya Yatima isipokua Kwa ajili ya Kuiboresha, hadi

pale atakapofikia umri wa kua mkubwa. Na toeni kwa ukamilifu na pimeni kwa

uadilifu, sisi hatuikalifishi Nafsi isipokua kwa uwezo wake. Na mnaposema basi

kuweni na uadilifu hata kama ikiwa anaehusika ni mtu wa karibu yenu. Na timizeni

ahadi kwa Mola wenu, hii anakuamrisheni ili mpate kukumbuka.

Ambapo anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kuhusiana nayo

kua: ‘Watu waliosadiki, hua ni wenye kusema katika hali nne, Hua wanazungumza

maneno kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala, kwa Kupitia katika Ujumbe wa

Allah Subhanah wa Ta’ala, kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala au Maneno

ambayo yanaendana na Maneno ya Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Ambapo kuna watu pia ambao huzungumza na Nafsi zao na kwa ajili ya Nafsi zao,

na hivyo hawa hua ni waliohifadhiwa kutokana na kuzungumza kauli sizo. Na kuna

watu ambao hua wanazungumzia watu wengine na hivyo hua ni wenye kuzisahau


268

Nafsi zao, hivyo hua ni wenye kuzusha na kua ni wenye kupotoka. Na upotofu hua

ni ule waliouzusha.

Hivyo achaneni na Mazungumzo kwa ajili ya kutafuta Ilm. Na mzungumze yale tu

ambayo ni Muhimu. Na hivyo utakua ni mwenye kuhifadhika kutokana na

madhambi ya mazungumzo. Na hivyo aya inatuamrisha kuhusiana na Uadlifu wa

maneno kua Usiseme hadi pale itakapokua unaogopa kua kama hukusema basi

utapata dhambi’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anaendelea kutuambia kua:

‘Yeyote yule Mwenye kua na dhana basi hatokua na Yaqini, na yeyote yule

atakaezungumzia jambo lisilomhusu basi huondokewa na Imani. Na yeyote yule

anaejihusisha na jambo jengine lolote lile lisilokua ni kwa ajili ya Mola wake basi

huondokewa na Ucha Mungu, na anaeondokwa na vitu vitatu hivi basi hua ni

mwenye kuangamia, kwani atahesabiwa kua ni miongoni mwa maadui wa Allah

Subhanah wa Ta’ala.’

Na kisha baada ya hapo basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamalizia kwa kusema:

‏﴿وَأَن َّ هَٰذَا صِرَاطِى مُسْتَقِيماً‏ فَٱت َّبِعُوهُ‏ وَلاَ‏ تَت َّبِعُواْ‏ ٱلس ُّبُلَ‏ فَتَفَر َّقَ‏ بِكُمْ‏ عَ‏ ن سَبِي لِهِ‏

ذٰلِكُمْ‏ وَص َّاكُمْ‏ بِهِ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تَت َّقُونَ‏ ﴾

Waanna hadha siratee mustaqeeman faittabiAAoohu wala tattabiAAoo alssubula

fatafarraqa bikum AAan sabeelihi dhalikum wassakum bihi laAAallakum

tattaqoona(Surat Al Anaam 6:153)

Tafsir: Na kwa hakika hii ndio Njia Sahih, hivyo ifuateni na wala msifuate nyengine

kwani zitakufarakisheni kutoka katika njia yake, anakuamrisheni hivyo ili mpate kua

Wacha Mungu.

Ambapo anasema Imam Muhammad Ibn Jarir At Tabari kua: ‘Amesema Abd Allah Ibn

Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Siku moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alichora Mstari Ardhini na kisha akasema: ‘Hii ndo njia ya Allah’ kisha akachora

mistari myengine kushoto kwake na kulia kwake kisha akasema: ‘Hizi ni njia

ambazo mbeleni mwake amekaa Shaytani akiwavutia watu ndani ya muelekeo

wake’ na kisha akasoma aya hii (ya Surat Al Anaam 6:153)’


269

Na kwa upande mwengine basi amesema Ardab Ibn Sarriyah Radhi Allahu Anhu kua:

‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alituusia sana sisi kiasi ya kua machozi yalijaa

kwenye Macho yetu na Nyoyo zetu zikailinika, hivyo tukasema: ‘Ya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam hakika huu ni ujumbe ambao unajaza macho yetu, hivi

jee ungependa kutuusia zaid?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hakika mmi nimekuachieni

Weupe ambao Kiza chake hua ni kama Mchana wake, hivyo hakuna atakaeteleza

isipokua yule ambae atakaejiangamiza mwenyewe. Hivyo yeyote yule atakeishi

baada yangu. Atashuhudia tofauti nyingi. Ambapo ni juu yenu itakua kuhusiana na

Sunnah zangu, na Sunnah za Makhalifa wangu waongofu na ni juu yenu utiifu wenu

hata kama (Kiongozi wenu) atakua ni Mhabeshi Mwenye pua iliyolala, shikamaneni

na haya hata kwa kutumia meno yenu. Kwani Muumini hua kama Ngamia

aliefungwa hatamu hua anaenda kokote kule anakoongozwa.’’(Imam At Tirmidhi)

Ambapo anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Fuateni

Sunnah na njia za Watu wema waliotangulia. Kwani mimi nna khofu kua utafika

wakati ambao Watu watakua wanachukia kuambiwa kua wamfuate Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam katika kila Jambo, hivyo watu wataachana na wale

wanaowausia juu ya hilo na watawaadhirisha.’

Na hivyo sasa Masahaba ndio wakaona kua amrisho hili liliomo kwenye aya hizi za

(Surat Al Anaam 6:152) sasa limekua lina balaa zaid, kwani hata kusogelea Tusiisogelee!

Hivyo anasema Imam Ahmad Ibn Musa Ibn Marduwayh kua: ‘Baada ya tukio hili basi

Kuna Sahaba alimfuata Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kumsikitikia kwa

kumwambia: ‘Ya Rasul Allah! Hakika mimi sina njia ya kujipatia Riziki yangu.

Lakini sasa nnae Yatima nnaemlea’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamwambia Mtu huyo kua: ‘Unaweza

Kutumia Mali ya Yatima lakini bila ya Kuifuja wala kuifanyia Israfu, kwa

kutoutumia Msingi wake na wala Kujikusanyia Mali kutokana na Msingi wa Mali

yake hio.’

Ambapo Maneno haya ya Imam Ibn Marduwayh ni yenye kutokana na Hadith Sahih

ambayo imo pia kwenye Musnad Imam Ahmad, Sunnan Imam Abu Daud, Sunan An

Nasai, Sunnan Ibn Majah na Sahih Ibn Hiban.

Ambapo tunapoangalia maana ya Hadith hii basi ndani yake tunakutana na maana

inayoendana sambamba na Mtizamo wa Amir ul Muuminin Umar Ibn Al Khattab Radhi

Allahu Anhu, Atah Ibn Abi Rabbah, Ikrimah Mawla Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu

Anhu, Ibrahim An Nakhai, na pia ndio Mtizamo wa Hasan Al Basr na wa Mujaddid Ad

Din Imam Muhammad Idris Al Shafii pia kua: ‘Mtu ambae ni Masikini na kisha akawa


270

anamhudumia Yatima ambae ana Mali aliyorithi kutoka kwa Mzee wake, basi Mtu

hua haruhusiki kutumia Mali hio isipokua tu kiasi ya kile ambacho ni kidogo

ambacho anaweza kukitumia kwa ajili ya kua kama ni Ujira wake tu, na hivyo hiki

kidogo anachochukua kua kama Ujira wake basi hua hana ulazima kukirudisha.’

Ambapo kwa upande wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, Umm ul

Muuminin Aisha Radhi Allahu Anha, Imam Amr Ibn Al Shabi, Imam Abu Aliyah basi

wao wanasema kua:

Kinachoruhusika Kutumiwa na Kafil yaani Mtu anaemsimamia Yatima kutokana

na Mali yake basi hua ni vitu vile ambavyo ni Muhimu kwa ajili ya Matumizi ya

Nyumbani, kwa Mfano Vyakula, Matunda, Mboga Mboga, Maziwa na vitu kama

hivyo, hivyo Mtu hua anaruhusiwa kuvitumia lakini sio kwa Fujo wala kwa Israfu,

atumie kwa kiasi chake Nyumbani kwake, kua kama ni Malipo yake kutokana na

Kulea kwake

Lakini kuna vitu vya Thamani kama Dhahabu, Fedha, Almasi, Pesa Nyingi n.k basi

hua hairuhusiki kuchukua isipokua labda kama ukiwa na nia ya kua hicho

unachochukua kua unakichukua kua kama ni Mkopo na hivyo baadae

Utakirudisha.

Kwani Allah Subhanah wa Ta'ala pia amesema katika Surat An Nisaa kua:

‏﴿وَٱبْتَلُواْ‏ ٰ ٱلْيَتَامَى حَتى َّ ٰ إِذَا بَلَغُواْ‏ النِّكَاحَ‏ فَإِنْ‏ آنَسْتُمْ‏ مِّنْهُمْ‏ رُشْداً‏ فَٱدْفَ‏ عُواْ‏ إِلَيْهِمْ‏

أَمْوَالهَُمْ‏ وَلاَ‏ أتَْكُلُوهَآ إِسْرَافاً‏ وَبِدَاراً‏ أَن يَكْبَرُواْ‏ وَمَن كَانَ‏ غَنِيّاً‏ فَلْيَسْتَعْفِفْ‏ ن وَمَ‏

كَانَ‏ فَقِيراً‏ فَلْيَأْكُلْ‏ بِٱلْمَعْرُوفِ‏ فَإِ‏ ذَا دَفَعْتُمْ‏ إِلَيْهِمْ‏ أَمْوَالهَُمْ‏ فَأَشْهِ‏ دُواْ‏ عَلَيْهِمْ‏ وَكَفَ‏ ٰ ى

يباً‏ ﴾ بِٱهلل َِّ‏ حَسِ‏

Waibtaloo alyatama hatta idha balaghoo alnnikaha fa-in anastum minhum rushdan

faidfaAAoo ilayhim amwalahum wala ta/kulooha israfan wabidaran an yakbaroo

waman kana ghaniyyan falyastaAAfif waman kana faqeeran falya/kul

bialmaAAroofi fa-idha dafaAAtum ilayhim amwalahum faashhidoo AAalayhim

wakafa biAllahi haseeban (Surat An Nisaa 4:6)

Tafsir: Na wajaribuni (Kiakili na ufaham wao) Mayatima hadi wawe wamebaleghe na

kufikia umri wa kuoa, na mkiwaona wana ufaham mzuri, basi wapeni mali zao, na


271

wala msizitumie kwa Israfu kutokana na kua na khofu kua watakua wakubwa. Na

kama ikiwa mmoja miongoni mwenu ni Tajiri basi asichukue malipo. lakini kama

akiwa Fukara basi na wacha na achukue kinachostahiki, na kisha mtakapowakabidhi

Mali zao basi kuwe na shahidi juu yao na kwa hakika anatosheleza Allah Kuchukua

Mahesabu.

Kwa upande mwengine basi pia inabidi tujue unapokua na Imani basi kwako wewe kua

tahadhari hua ni bora zaid, na ndio maana kwa Upande wa Sayyidna Umar Ibn Al Khattab

Radhi Allahu Anhu basi yeye alikua akisema:

‘Hakika Mimi hua naichukulia Mali ya Ummah kua ni sawa na Mali ya Yatima,

yaani pale nnapokua na kitu basi hua siigusi Mali hio na nnapokua sina kitu na na

shida sana basi hua nnachukua kua kama Mkopo, na hivyo nikipata basi hua

nnarudisha’

Na hii ni kutokana na wasia wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae alimuusia

Abu Dhar Radhi Allahu Anhu kwa kumwambia: ‘Ewe Abu Dhar! Hakika mimi nauona

Udhaifu wako ndani yako, hivyo napendelea kwa ajili yako kile ambacho

nnakipendelea kwa ajili ya Nafsi yangu, Kua kamwe usikubali kua kiongozi baina

ya watu wawili na wala usikubali kuisimamia Mali ya Yatima.’(Sahih Muslim)

Kwani ili uifaham maana ya Hadith hii basi inabidi kwanza Umjue Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam na Sifa zake ambapo Allah Subhanah wa Ta'ala amemsifia kua ni

Kiumbe bora na ni mwenye Rehma na Huruma kwa Walimwengu pale aliposema katika

Qur'an:

‏﴿وَمَآ أَرْسَلْنَاكَ‏ إِلا َّ رَحمَْةً‏ لِّلْعَالَمِينَ‏ ﴾

Wama arsalnaka illa rahmatan lilAAalameena(Surat Al Anbiyah 21:107)

Tafsir: Na Hatukukutuma wewe isipokua kua ni Rehma kwa Ulimwengu.

Na pia pale ilipothibitisha Qur'an kwa kusema:

‏﴿لَقَدْ‏ جَآءَكُمْ‏ رَسُولٌ‏ مِّنْ‏ أَنفُسِ‏ كُمْ‏ عَزِيزٌ‏ عَلَيْهِ‏ مَا عَنِت ُّمْ‏ حَرِيصٌ‏ عَلَيْكُمْ‏ بِٱلْمُؤْمِنِ‏ ينَ‏

رَءُوفٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾


272

Laqad jaakum rasoolun min anfusikum AAazeezun AAalayhi ma AAanittum

hareesun AAalaykum bialmu/mineena raoofun raheemun(Surat At Tawba 9:128)

Tafsir: Kwa Hakika Amekuja Kwenu Mtume Kutokana na Miongoni mwa Nafsi zenu

(yaani si katika Maumbile yeyote yale isipokua katika Maumbile ya Kiibinadam kama

mlivyo nyinyi) Mna thamani kubwa sana ya Kimapenzi kwake yeye, Hataki Mdhurike

au Muwe na Ugumu wa Mambo yenu. Kwani Anajali sana Juu yenu kwa Waumini ni

Mwenye Kuwaonea Huruma na Mwingi wa Rehma.

Hivyo hizi ni aya mbili ambazo zinazomuelezea Rasul Allah Salallahu Alayhu wa Salam

kwa Kifupi lakini hapo hapo kwa Mapana Makubwa Sana.

Na hapa sitaki kushuka katika kufafanua kwa sababu nikishuka tutachukua Mda mrefu

kwani Mada yake inahitaji Kitabu Kizima, Ila kwa ufafanuzi mfupi tu basi katika wakati

wa Kukusanywa Qur'an basi Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu alikua

haikubali aya ya Qur'an mpaka apate Uthibitisho wa Mashahidi walioihifadhi aya hio

tena Mashahidi hao wawe Masahaba wacha Mungu na wenye Ilm kweli.

Lakini aliposomewa aya hii basi hakutaka hata shahidi bali aliikubali Moja kwa Moja

kwani alisema kua: ‘Aya hii ya Surat at Tawba ni aya inayomuelezea Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kama alivyo.’ hivyo hapa tunaona kua Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam ambae ni mwenye sifa ya kua ni mwenye Rehma kwa

Waumini basi anamuusia Sahaba wake kua asikubali Kusimamia Mali ya Yatima.

Hapa kwanza nataka tufahamiane kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

hakumuusia Sahaba wake huyo ambae ni Abu Dhar Radhi Allahu Anhu kua Asilee

Yatima bali alimuusia kua asikubali kusimamia Mali ya Yatima. Ambapo hivi ni vitu

viwili tofauti na bila ya shaka Kulea Yatima hua ni Kazi rahisi zaid na ni Jukumu Jepesi

zaidi kuliko Kusimamia Mali ya Yatima

Kwani baada ya Kumjua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi tunatakiwa pia

tumjue Sahaba Abu Dhar Al Ghifari Radhi Allahu Anhu. Ambapo kwa juu juu basi Abu

Dhar Al Ghifari Radhi Allahu Anhu alikua ni Mtu wa 5 Kuingia katika Dini ya Uislam.

Halafu alikua ni Miongoni mwa Masahaba ambao wana Ucha Mungu na Muaminifu

mkubwa Sana.

Kiasi ya Kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisema kua: ‘Mbingu hazijawahi

kumfunika chini yake Mtu Muaminifu Kama Abu Dhar’ (Imam At Tirmidhi)

Na Abu Dhar Al Ghifari Radhi Allahu Anhu alikua ni Mtu wa mwanzo kabisa Miongoni

mwa Waislam kua ni mwenye Kutumia salam ya Asalaam Alaykum


273

Hivyo mimi na wewe leo hii tukisema Salaam Alaykum, basi na Abu Dhar Al Ghifari

Radhi Allahu Anhu nae anapata sehemu ya Thawabu zake kutokana na kua sisi ni wenye

kumuiga yeye kutokana na maamkizi hayo kwani yeye ndie wa Mwanzo, na kulingana

na Hadith basi atakaeanzisha Jambo jema basi kila likifanywa na Yeye hua anapata

Thawabu zake bila ya kumpunguzia Mfanyaji.

Na anaeanzisha ovu pia anapata dhambi za kila afanyae Ovu hilo. Sasa Fikiria kil

Ukisema Asalaam Alaykum basi wewe una thawabu 10 na Abu Dhar Radhi Allahu Anhu

anapata 10. Na hii tangu Mwanzo wa Uislam mpaka leo..Jee tunazungumzia Salam

ngapi? Zenye Thawabu 10, 10,10 mara ngapi?

Naam..hio pia ni kwa ufupi kuhusiana na Abu Dhar Radhi Allahu Anhu. Hivyo

tukiiangalia Hadith hii ya Wasia kuhusiana na Mali ya Yatima basi tunaona kua wasia

huo unatoka kwa M-bora wa Viumbe, Mwenye Rehma na Huruma kwa Ulimwengu na

Wauamini, unaelekea kwa Mtu ambae hakuna Muaminifu zaidi yake chini ya Mbingu

ambae anaambiwa na M-bora wa viumbe kua hakika yeye pia anaweza akafeli Mtihani

wa Mali ya Yatima.

Ya Allah!...Hivi Kama itakua Abu Dhar Radhi Allahu Anhu ambae hakuna anaemfikia

kwa Uaminifu anaambiwa kua asikubali Kusimamia Mali ya Yatima kutokana na

Ukubwa wa Jukumu la Mali hio na Uzito wa Mitihani yake, Jee hali itakuaje kwangu

mimi na wewe?

Na kisha akasema tena Allah Subhanah wa Ta'ala:

كَيْل

‏﴿وَلاَ‏ تَقْ‏ رَبُواْ‏ مَالَ‏ ٱلْيَتِيمِ‏ إِلا َّ بِٱل َّتىِ‏ هِ‏ ىَ‏ أَحْ‏ سَ‏ نُ‏ حَ‏ تى َّ ٰ يَبْ‏ لُغَ‏ أَشُد َّ هُ‏ وَأَوْ‏ فُواْ‏ ٱلْ‏ َ

وَٱلْمِيزَانَ‏ بِٱلْقِسْطِ‏ لاَ‏ نُكَلِّفُ‏ نَفْساً‏ إِلا َّ وُسْعَهَا وَإِذَا قُلْتُمْ‏ فَٱعْدِلُواْ‏ وَلَوْ‏ كَ‏ انَ‏ ذَا قُرْبىَٰ‏

وَبِعَهْ‏ دِ‏ ٱهلل َِّ‏ أَوْ‏ فُواْ‏ ذٰ‏ لِكُ‏ مْ‏ وَص َّاكُ‏ مْ‏ بِهِ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تَذَك َّ رُونَ‏ ﴾

Wala taqraboo mala alyateemi illa biallatee hiya ahsanu hatta yablugha ashuddahu

waawfoo alkayla waalmeezana bialqisti la nukallifu nafsan illa wusAAaha wa-itha

qultum faiAAdiloo walaw kana dha qurba wabiAAahdi Allahi awfoo thalikum

wassakum bihi laAAallakum tadhakkaroona(Surat Al Anaam 6:152)

Tafsir: Na Wala Usiikaribie Mali ya Yatima isipokua Kwa ajili ya Kuiboresha , hadi

pale atakapofikia umri wa kua mkubwa. Na toeni kwa ukamilifu na pimeni kwa

uadilifu, sisi hatuikalifishi Nafsi isipokua kwa uwezo wake. Na mnaposema basi


274

kuweni na uadilifu hata kama kiwa anaehusika ni mtu wa karibu yenu. Na timizeni

ahadi kwa Mola wenu, hii anakuusieni ili mpate kukumbuka.

Kwani anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wakati Allah

Subhanah wa Ta'ala aliposhusha aya hizi Mbili basi Kila Mtu miongoni mwa

Masahaba aliekua na Yatima alijitenga na Yatima aliekua nae Watu wakawa

Wanakula na Kunywa Tofauti na Mayatima wao, na Baadhi walikua hawali

Chakula alichopikiwa Yatima wake, hadi akile Mwenyewe Yatima huyo, na baadhi

ya Wakati hufikia Chakula cha Yatima husika Kuharibia kutokana na kutoliwa

(Imam An Nasai)

Naam..hivyo ndivyo Walivyokua Masahaba wakishikamana na Maamrisho ya Allah

Subhanah wa Ta'ala. ‘Ambapo Hali hii iliendelea mpaka sasa Masahaba Wakaona

huu ushakua Mtihani mkubwa Sana, kwa sababu wao wamefaham kua Yatima

akiwekewa Chakula basi kisiliwe mpaka aje kula mwenyewe.’

Hivyo Wakamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam juu ya Uzito wa

Maneno ya Aya hizi Juu yao.’

Na baada ya Kulalamika huko basi Allah Subhanah wa Ta'ala akawashushia Amrisho

lenye ufafanuzi ndani yake kupitia kwa Mtume wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam katika aya iliyotumia neno Salaha tulilolifafanua maana yake hapo kabla ambalo

liko katika hali ya Islahun pale Allah Subhanah wa Ta'ala aliposema katika Qur'an kua:

‏﴿وَيَسْأَلُونَكَ‏ عَنِ‏ ٱلْيَتَامَى ٰ قُلْ‏ إِصْلاَحٌ‏ له َُّمْ‏ خَيْرٌ‏ وَإِنْ‏ تخَُالِطُوهُمْ‏ فَإِخْوَانُكُمْ‏ وَٱهلل َُّ‏

يَعْلَمُ‏ ٱلْمُفْسِ‏ دَ‏ مِنَ‏ ٱلْمُصْلِحِ‏ وَلَوْ‏ شَآءَ‏ ٱهلل َُّ‏ لأَعْنَتَكُمْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ عَزِيزٌ‏ حَكِيمٌ‏ ﴾

Wayas-aloonaka AAani alyatama qul islahun lahum khayrun wa-in tukhalitoohum

fa-ikhwanukum waAllahu yaAAlamu almufsida mina almuslihi walaw shaa Allahu

laaAAnatakum inna Allaha AAazeezun hakeemun(Surat Al Baqra 2:220)

Tafsir: Na Wanakuuliza (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) Kuhusiana na

Yatima: ‘Waambie (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) kua Islahun (Kua

Na Wema na Uadilifu) Juu ya Mali zao ni Bora na Kama Mkichanganyika nao (katika

mambo yenu) Basi wao Ni Ndugu zenu na Allah Ni Mwenye Kumjua Fisadi Na

Mwenye Islahi (Mwenye wema na Uadilifu) Na Kama angetaka Allah Basi

angekuwekeeni Ugumu hakika Allah ni Mwenye Uwezo Mkubwa Sana na ni Mwenye

Hikma Kubwa sana.


275

Neno Salaha kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kua Sahih, Kua Mzuri, Kua

Muadilifu na pia umaanisha Suluhu. Neno Salaha ndio lililotoa Neno Islah ambalo hua

linamaanisha Kuweka Kitu Sawa, Kuboresha Kitu, Kukifanya Kitu Kiwe Kizuri.

Na pia likatoa neno Salih ambalo ni Jina la Nabii wa Allah Subhanah wa Ta'ala

alietumiwa watu wa Thamud ambalo hua linamanisha Mtu Mwema. Na pia ndio lililotoa

neno Muslihuna yaani Watu wenye Kufanya Mema, au wenye Kusuluhisha mambo.

Ambapo aya inatuwekea wazi kuhusiana na kuwafanyia Wema juu ya mali zao, kama

ilivyokua ni jukumu la kila mtu kua anatakiwa kua na Uadilifu katika usimamizi wa Mali

yake basi ndio hivyo hivyo anavyotakiwa kua na uadilifu juu ya Mali ya Yatima.

Yaani kama itakua matumizi ya Mali hio itakua ni kwa ajili ya mambo sio, yaani

mambo ya maasi na kufanya israfu basi matumizi hayo hua hayaruhusiki.

Na kama ikiwa matumizi hayo ni kwa ajili ya mambo mema na kutafuta ridhaa ya

Allah Subhanah wa Ta’ala na katika kutekeleza wajibu wa Kidini juu ya Mali hio

au juu ya Yatima hao, kwa mfano kuitolea Zakkah Mali hio unapowadia mda wake,

basi utumiaji huo wa Mali hio hua ni wa Wajibu pia na kufanya hivyo hua ni

kusimamia na kuwatekeleza Mayatima hao haki yao juu ya Mali yao.

Na inapokua matumizi hayo yatakua hayana ulazima lakini haitoathiri Mali yao

kwa mfano kutoa Sadaka kutokana nayo basi inaruhusika, lakini kama ikiwa utoaji

huo wa Sadaka utaathiri Mali ya Mayatima hao kutokana nayo basi haitoruhusika

kuitolea Sadaka mali hio, kwani kufanya hivyo itakua ni sawa na kuwavunjia haki

yao Mayatima hao.

Na katika kututilia msisitizo wa kutoruhusika kufanya Dhulma na kuwavunjia haki

Mayatima na Mali zao katika Uislam basi ndio Allah Subhanah wa Ta’ala ndio

akashusha aya isemayo:

‏﴿وَلاَ‏ تَقْرَبُواْ‏ مَالَ‏ ٱلْيَتِيمِ‏ إِلا َّ بِٱل َّتىِ‏ هِىَ‏ أَحْسَنُ‏ حَتى َّ ٰ يَبْلُغَ‏ أَشُد َّهُ‏ وَأَوْفُواْ‏ ابِ‏ لْعَهْدِ‏ إِ‏ َّن

ٱلْعَهْ‏ دَ‏ كَ‏ انَ‏ مَسْ‏ ؤُولاً‏ ﴾

Wala taqraboo mala alyateemi illa biallatee hiya ahsanu hatta yablugha ashuddahu

waawfoo bialAAahdi inna alAAahda kana mas-oolan (Surat Al Isra 17:34)


276

Tafsir: Na wala usiikaribie Mali ya Yatima isipokua kwa ajili ya kuiboresha, hadi pale

watakapofikia umri mkubwa wa kubaleghe, na tekelezeni ahadi kwani kwa hakika juu

ya ahadi Mtaulizwa

Kwani hapo zamani hali ilikua kama anavyosema Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas

Radhi Allahu Anhu kua:

Hapo zamani Katika Zama za Kijahiliya Watu walikua hawawapi Mali zao Watoto

wadogo wa Kike na wa Kiume, hivyo Siku Moja kuna Ansar aliekua akiitwa Aus

Ibn Thabit Radhi Allahu Anhu ambae alifariki Dunia. Na kuacha Watoto wawili wa

Kike na Mmoja wa Kiume.

Hivyo baada ya kufariki Aus Radhi Allahu Anhu basi, wakatokea Watoto wa Kiume

wa Baba mdogo Aus Radhi Allahu Anhu na kisha wakachukua Mali zake zote

alizowacha ambazo ni za Urithi wa watoto wake. Hivyo Mke wake Aus akawaambia

Watoto hao wa Kiume wa Baba yake Mdogo Aus Radhi Allahu Anhu kua:

Kama Mnachukua Mali zote basi bora waoeni Mabinti zake ambao nao pia

Wanaasili ya Damu moja nanyi, lakini nao wakakataa

Hivyo mke huyo wa Aus Radhi Allahi Anhu akakimbilia kwa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kushtaki, Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawaita

Watu hao wawili ambao ni watoto wa Kiume wa Baba mdogo wa Aus na

kuwaambia: ‘Msichukue Mali ya Mayatima kwani nimepokea Wahy kua watoto

wote wa Kike na Kiume wa Mfiwa hua wanapewa urithi wao’ (Imam Al Sabuni katika

Tafsir Ayat al Ahkami Al Quran)

Hivyo katika enzi za Ujahiliya Watu hawakua tu wakiwanyang'anya Mayatima Urithi

wao kama kwenye Mfano tuliouangalia wa Kifo cha Aus Ibn Thabit Radhi Allahu Anhu.

lakini pia Watu walikua wakichukua Mali za Mayatima na kuzibadilisha na zao wao au

kwa kuzichanganya na Mali zao wao, na kisha baadae huwapa Mayatima zile mali zenye

thamani ya chini zaidi ya Mali zao. Kwa Mfano Watu walikua wakichukua Kondoo

walionona wa Mayatima na kisha huwarudishia Mayatima hao Kondoo wagonjwa au

waliokonda badala yake.

Hivyo kutokana na Matukio kama haya basi Allah Subhanah wa Ta'ala akashusha ile aya

isemayo:


277

‏﴿وَآتُواْ‏ ٱلْيَتَامَى ٰ أَمْوَالهَُمْ‏ وَلاَ‏ تَتَبَد َّلُواْ‏ ٱلخَْبِيثَ‏ بِٱلط َّيِّبِ‏ وَلاَ‏ أتَْكُلُو ۤ اْ‏ أَمْوَالهَُ‏ مْ‏ إِلىَٰ‏

أَمْ‏ وَالِكُمْ‏ إِن َّهُ‏ كَ‏ انَ‏ حُ‏ وابً‏ كَ‏ بِيراً‏ ﴾

Waatoo alyatama amwalahum wala tatabaddaloo alkhabeetha bialttayyibi wala

ta/kuloo amwalahum ila amwalikum innahu kana hooban kabeeran (Surat An Nisaa

4:2)

Tafsir: Na Wapeni Mayatima Mali zao Na Wala Msizibadilishe (Mali zenu nyie) Mbaya

kwa Nzuri (Zao wao)Na Wala Msile Mali zao kwa (kuzijumuisha) na Mali zenu Kwani

Kwa Hakika Kufanya Hivyo ni Dhambi Kubwa sana.

Hii ni ay ambayo imetumia neno Huban ambalo ni tofauti kimaana na neno Hubban

kwani Neno Hubban ni lenye kutokana na neno Hubb ambalo hua linamaansiha Mapenzi,

Upendo au Kitu ambacho kinavutia na kupendezesha. Ambapo neno Huban lililotumika

kwenye aya hii katikati lina harfu waw na hivyo kua ni lenye kumaanisha Kuvuka

Mipaka, Kufanya Dhambi, Kufanya Jambo lisilofaa, Kufanya Uhalifu au Kufanya

Maangamizi.

Ambapo anasema Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Katika

Wakati ambao Sahaba Abu Ayub Al Ansari Radhi Allahu Anhu alipokua anataka

Kumtaliki Mke wake, aitwae Umm Ayub Radhi Allahu Anha hivyo Abu Ayub Al

Ansari alienda kuomba Ushauri kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, kama

amuwache Mke wake huyo ama la.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamwambia Abu Ayub Al Ansari

Radhi Allahu Anhu kua: ‘Ama kwa hakika kwako wewe kumuacha Umm Ayoub

basi itakua ni Huuban Kabiran’Ambapo Abu Ayub Al Ansari Radhi Allahu Anhu

alipoambiwa hivyo basi akaachana na Mawazo hayo ya kuachana na Mke wake

huyo.

Hivyo kulingana na Kauli hii ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi maneno

Huuban Kabiran haikumaanisha kua Kumuacha Umm Ayub Radhi Allahu Anha yatakua

Mapenzi makubwa sana kwani kama mtu ana mapenzi Makubwa sana na Mke wake basi

hua hataki Kumuacha.

Hivyo hapa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akimaanisha kama ilivyokua

ikimaanisha Aya kua Kufanya hivyo hua ni Kosa Kubwa Sana.


278

Na hivyo kwa maana hio basi Aya inatuwekea wazi kua Kula Mali ya Yatima au

Kumbadilishia Mali yake Nzuri na Kumpa Mbovu basi hua Ni Kosa La Dhambi Kubwa

linaangamiza. Kama tulivyoona katika aya tuliyoiangalia juzi ya Surat An Nisaa 4:10

tulipozungumzia Kuhusiana na Mdomo na Kujaza Matumbo Moto.

Na pia kama alivyoonya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kusema katika

hadith kua: Jiepusheni na Mambo Saba yenye Kuangamiza ambayo ni:

1-Kumshirikisha Allah Subhanah wa Ta'ala.

2-Kufanya Uchawi.

3-Kuua Mtu bila ya Sababu inayokubalika Kishariah.

4-Kula Riba.

5 –Kula Mali Ya Yatima.

6-Kukimbia kutoka kwenye Uwanja wa Vita vya Jihad kwa Ajili ya Allah Subhanah

wa Ta'ala.

7-Kuwasingizia Uchafu Wanawake ambao ni Wasafi.

(Imam Al Bukhari)

Hivyo kuhusiana Mayatima basi ukweli ni kua kila mmoja anatakiwa awe na ufahamu

juu Haki zao. Kwani kutofaham juu ya haki zao hua ni Ujinga wa Kutojua Dini yako na

kukufanya wewe kua na Uyatima wa Kutokua na Ilm ya Dini yako.

Kwani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisema kuwaambia Masahaba zake kua:

‘Yatima hua si Mtu ambae Hana Baba wala Mama Bali Yatima hua ni Mtu Ambae

Ni Mjinga asiekua na Ilm’(Imam Ibn Majah)

Na katika hili basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anatuwekea wazi kua Mtu

aisekua na Ilm hua ni mwenye Ugumu wa Maisha yake kutokana na Ujinga Wake. Kwani

Ilm humsaidia na kumrahisishia Mtu Maisha yake hapa Duniani na Kesho Akhera kama

vile Yatima anavyosaidiwa na Mzee wake.

Kwani unapokua huna Ilm basi unaweza pia ukawa ni miongoni mwa wanaokadhibisha

Dini kutokana na ujinga wao ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kutuelezea

aina nyengine ya Watu hao wanaokadhibisha Dini kwa kuwaambatanisha pamoja na

wasiowakirimu Mayatima pale aliposema:


279

‏﴿كَلا َّ بَل لا َّ تُكْرِمُونَ‏ ٱلْيَتِيمَ۞وَلاَ‏ تحََاض ُّونَ‏ عَلَى ٰ طَعَامِ‏ ٱلْمِسْكِينِ‏ ﴾

Kalla bal la tukrimoona alyateema; Wala tahadhdhoona AAala taAAami

almiskeeni (Surat Al Fajr 89:17-18)

Tafsir: (Wataambiwa) La Bali Nyinyi Mlikua Hamuwakirimu Mayatima. Wala

hamkuwa ni wenye kuamrisha kuwapa chakula Maskini.

Ambapo katika Surat Al Maun basi alisema:

‏﴿وَلاَ‏ يحَُض ُّ عَلَى ٰ طَعَامِ‏ ٱلْمِسْكِينِ‏ ﴾

Wala yahudhdhu AAala taAAami almiskeeni; (Surat Al Maun 107:3)

Tafsir: Na kisha yule ambae hahimizi kulisha Masikini.

Aya mbili hizi zimetumia asili ya Neno Hudhdhu ambalo hua linamaanisha Kuhimiza,

Kutia Ari au Mwaamko au Kuchochea au Kuamrisha.

Kama tuko makini na kutafakkari basi itakua tunaona kua Aya mbili hizi, kwa kua ni za

Mwanzoni kushuka katika Kipindi cha Mwanzoni mwa Utume basi ingawa hazikua ni

zenye Kukemea sana juu ya Makosa hayo Mawili ya Kutowakirimu Mayatima na

Masikini, kwani zilikua zinaweka wazi tu kua haya ni Mambo Mabaya sana.

Hivyo tunapoziangalia aya hizi za Surat Al Maun, basi tunaona kua kimaana zunaenda

sambamba na aya tulizoziangalia za Surat Al Fajr, lakini hata hivyo aya hizi zinatofauti

kimaana.

Kwani aya hizi za Surat Al Maun zimekuja na Tangazo zito sana tena lenye Onyo la kua

kwa Kila anaejihesabu kua Ameamini lakini akawa anafanya Makatazo yaliyomo Ndani

ya Tangazo hilo, basi Moja kwa Moja Mtu huyo atakua ni Mwenye Kuikadhibisha Dini,

mwenye Kuikadhibisha Siku ya Malipo.

Na Hivyo hata kama anasali basi mbele ya Waislam wenzake Muislam huyo atakua ni

mwenye Kusimamisha Nguzo za Dini ya Kiislam lakini ndani ya Moyo wake hua ni

mwenye kuvunja Nguzo ya Imani ya Dini ya Kiislam.


280

Ili kufahamu vizuri hapa basi na tuchukulie Mfano kwamba Mtu anaumwa na Malaria,

kisha Labda akaambiwa na Daktari kua Dawa yake ni kua amalize dozi ya Vidonge

Viwili vya dawa kwa siku tatu.

Hivyo Mtu huyo akawa hakuamini kua Dawa hio itamsaidia, na hivyo akawa ni mwenye

kuchukua hizo dawa alizopewa kisha badala ya kula Vidonge viwili basi yeye akameza

vidonge vya siku moja tu. Hivyo bila ya Shaka Mtu huyo hatoweza kupona kwa sababu

amevunja Nguzo moja ya Imani ya Kumuamini Daktari wake. Sasa Homa ikimzidi sijui

atamlaumu nani, kwa kukosa kwake Imani.

Ambapo tunapozungumzia Kuikadhibisha Dini kulikotajwa kwenye Aya hii ni

kutoaamini na hivyo kutokukubaliana na kile kilichoamrishwa na Allah Subhanah wa

Ta'ala. Sasa hii hua ni hali ya Muislam kua ni Mnafiq kama tutaitafsiri aya hii kwa

kutumia maana ya Kukadhibisha Dini, yaani sehemu ya Dini kua anaiamini lakini

sehemu nyengine haiamini.

Ama kama tutaitafsiri aya hii kwa maana ya kusema kua ni mwenye Kuikadhibisha siku

ya Malipo. Basi bila ya shaka, hapo ndani yake wanaingia pia wale ambao si Waislam

pia, kwani Muislam hua anaamini Siku ya Malipo lakini asiemuamini Allah Subhanah

wa Ta'ala basi hua haamini juu ya siku ya Malipo.

Ambapo hii sifa ya Kutohimizana kuwaonea huruma na kuwasadia Masikini kwa Pesa,

Chakula, Nguo n.k Imewekwa wazi kabisa kua ni sifa ya yule Mtu ambae si Mwenye

kumuamini Allah Subhanah wa Ta'ala pale alivyosema Allah Subhanah wa Ta'ala katika

Surat Al Haqqah kua Mwenye Uwezo wa Kuwasaidia Masikini kisha akawa

hajawasaidia basi katika Siku ya Malipo atakua ni mwenye kusema:

‏﴿يٰلَيْتَهَا كَانَتِ‏ ٱلْقَاضِيَةَ۞مَآ أَغْنىَٰ‏ عَنىِّ‏ مَالِيَهْ۞ه َّ لَكَ‏ عَنىِّ‏ سُلْطَ‏ انِيَهْ‏ ﴾

Ya laytaha kanati alqadhiyatu; Ma aghna AAannee maliyah; Halaka AAannee

sultaniyah(Surat Al Haqqah 69:27-29)

Tafsir: Ya Laiti (Bora Kifo) kingekua Ndio Mwisho wangu; Haukunifaa Utajiri wa

Mali yangu; Yamekimbia kutoka kwangu Mamlaka yangu

Yaani Mtu Ataomba asingefufuliwa baada ya Kufariki kwake, kwani haumfai Utajiri

wake wala Mamlaka yake, na baada ya kuonesha kwao Majuto hayo katika siku hio basi

Allah Subhanah wa Ta'ala atawaambia Malaika wa Motoni ambao Ukubwa wao na

Nguvu zao basi hakuna hata kiumbe mmoja anaeweza kupingana nao.


281

Kwani hawa uwezo wao ni pamoja na Kuwasimamia Majini ambao, Ukubwa wao zaidi

ya Mlima wa Kilimanjaro, sasa hao ni Majini na Miili yao na watadhibitiwa kama

Vifaranga vidogo vidogo, jee hali itakuaje kwa Ibn Adam anaekadhibisha Dini na hivyo

Kumuasi Mola wake, itakuaje hali yake siku hio ambayo Allah Subhanah wa Ta'ala

anatoa Amri kuwaamrisha Malaika hao Dhidi ya Kila Kiumbe aliemuasi kwa kusema:

‏﴿خُذُوهُ‏ فَغُل ُّوهُ۞ثمُ َّ ٱلجَْحِ‏ يمَ‏ صَل ُّوهُ۞ثمُ َّ فىِ‏ سِ‏ لْسِ‏ لَةٍ‏ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ‏ ذِرَاعاً‏

فَاسْ‏ لُكُوهُ‏ ﴾

Khudhoohu faghulloohu; Thumma aljaheema salloohu; Thumma fee

silsilatin dharAAuha sabAAoona dhiraAAan faoslukoohu (Surat Al Haqqa 69:33-

35)

Tafsir: Mkamateni Kisha Mfungeni Minyororo, Kisha Ndani ya Moto Mkali Sana

Mtupeni, Kisha Mfungeni Kwa Mnyororo Wenye Urefu wa Dhiraa Sabiini;

Kwani wengi Hua ni wenye kupenda kurushiana vipande vya picha za filamu za Kwenye

Whatsapp ambazo zinaonesha namna Watu Wanaojionesha wanavyowachoma kwenye

Moto kwa kuwafanya Mshikaki Kuku, Mbuzi, Kondoo, Ngo'ombe, n.k Huku akiwa

anazungushwa zungushwa, na anapowiva Mnyama huyo basi Nyama yake hua laini sana

na hivyo kua ni tamu nzuri kwa ajili ya kuliwa.

Hivyo kila mmoja anatakiwa afahamu kua kama atakua ni Mwenye Kumuasi Mola wake

basi haya maneno tunayokumbushana katika aya hizi yanamaanisha kua Mtu huyo katika

siku ya Malipo nae atakua kama inavyochomwa Mishikaki ya nyama za Wanyama hao.

Ambapo Wanazuoni wanasema kua Hii Minyororo inayozungumziwa ambayo Mtu

Muasi atafungwa nayo siku hio yenye Ukubwa wa Dhiraa 70 basi Kwanza utaingizwa

Puani kwenye tundu ya kwanza na kutokea Mdomoni. Kisha unaingizwa kwenye tundu

ya pili ya Pua na kutokea kwenye njia ya haja kubwa, kisha unatumbukizwa ndani ya

shimo la Moto wa Jahannam, kisha kama anavyogeuzwa Kuku au Kondoo basi na yeye

ndivyo atakavyogeuzwa.

Ila sasa Ubaya ni Kua Hawa Wanyama tunaowachoma sisi Wanakua washachinjwa na

hawana Uhai, lakini sisi tukimuasi Allah Subhanah wa Ta'ala basi tutafanywa Mishkaki

huku tukiwa hai…Ya Allah, Tustiri na Adhabu ya Moto huo..Allahuma Aaamiin


282

Kwani Allah Subhanah wa Ta'ala anajua kua Watu watajiuliza kwanini Watapewa

Adhabu hio, hivyo ili watu wasiulize basi yeye anaweka wazi kwa kusema kua huyo

atakaefanywa hivyo ni yule ambae:

‏﴿إِن َّهُ‏ كَانَ‏ لاَ‏ يُؤْمِنُ‏ بِٱهلل َِّ‏ ٱلْعَظِيمِ۞وَلاَ‏ يحَُض ُّ عَلَى ٰ طَعَامِ‏ ٱلْمِسْكِينِ‏ ﴾

Innahu kana la yu/minu biAllahi alAAadheemi; Wala yahudhdhu AAala taAAami

almiskeeni; (Surat Al Haqqa 69:34-35)

Tafsir: Hakika huyu Hakua ni Mwenye Kuamini Juu ya Allah Subhanah wa Ta'ala

Mwenye Utukufu Na Hakua ni mwenye Kuhimiza Kuwalisha Masikini.

Kwani Muislam anaponeemeshwa Neema ya Mali na Allah Subhnah wa Ta’ala basi hua

anatakiwa aitumie ipasavyo kwa ajili ya kumridhisha Allah Subhnah wa Ta’ala kwa

kuwasaidia watu wengine katika Jamii yake, kwani Mali hio aliyopewa hakuipata

kutokana na jitihada zake bali ameipata kutokana na majaaliwa ya Mola wake ambae

ndie Mmiliki wa kila kilichomo Mbinguni na Ardhini.

Ambapo siku moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliwahoji Masahaba zake kwa

kusema: ‘Hivi jee ni nani miongoni mwenu ambae Mali atakazowaachia waarithi

wake anazipenda zaidi kuliko Mali zake?’ Masahaba wakasema: ‘Hakika sisi

tunazipenda zaidi Mali zetu’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema

kuwaambia Masahaba zake kwa kusoma aya ifuatayo:

‏﴿وَمَا لَكُمْ‏ أَلا َّ تُنفِقُ‏ واْ‏ فىِ‏ سَبِيلِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَهللِ َِّ‏ مِيرَاثُ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ لاَ‏ يَ‏ سْتَوِى

مِنكُم م َّنْ‏ أَنفَقَ‏ مِن قَبْلِ‏ ٱلْفَتْحِ‏ وَقَاتَلَ‏ أُوْلَٰئِكَ‏ أَعْظَمُ‏ دَرَجَةً‏ مِّنَ‏ ٱل َّذِينَ‏ أَنفَقُواْ‏ مِن

بَعْدُ‏ وَقَاتَلُواْ‏ وَكُلاًّ‏ وَعَدَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱلحُْسْنىَٰ‏ وَٱهلل َُّ‏ بمَِا تَعْمَلُونَ‏ خَبِيرٌ‏ ﴾

Wama lakum alla tunfiqoo fee sabeeli Allahi walillahi meerathu alssamawati waalardhi

la yastawee minkum man anfaqa min qabli alfathi waqatala ola-ika

aAAdhamu darajatan mina alladheena anfaqoo min baAAdu waqataloo wakullan

waAAada Allahu alhusna waAllahu bima taAAmaloona khabeerun (Surat Al Hadid

57:10)


283

Tafsir: Inakuaje mpaka nyinyi hamtoi kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala? Wakati

kwa Allah ndiko kwenye umiliki wa mirathi ya Mbinguni na Ardhini. Hawako sawa

miongoni mwenu wale ambao ni wenye kutoa na wenye kupigana kwa ajili ya Allah

kabla ya Ushindi. Kwani hawa wako juu zaidi kidarja kuliko wale waliotoa na kisha

kupigana baada yake. Lakini kwa wote basi Allah ameahidi malipo mema na Allah ni

mwenye kujua juu ya kila mnachokifanya.

Yaani Aya inawahoji walioneemeshwa mali kwa ajili ya kuzisimamia kwa mda mfupi

katika maisha yao hapa Duniani na mwenye Utajiri wa Milele na wa kutohitajia kitu

chochote ambae si mwengine isipokua ni Allah Subhanah wa Ta’ala kua kwanini

hawatumii neema hio ya mali na kisha wakanufaishwa zaidi na yule aliewapa mali hio

kwa kulipwa Pepo kutokana na kutumia kwao kwa ajili yake hapa Ulimwenguni?

Na pia aya hii inazungumzia tofauti baina ya Darja ya Masahaba waliotumia Mali zao

kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala na waliopigana kwa ajili ya Allah Subhanah wa

Ta’ala kabla ya Kutekwa kwa Mji wa Makkah na Waislam na Darja ya Masahaba

waliotumia Mali zao kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala na waliopigana kwa Ajili ya

Allah Subhanah wa Ta’ala baada ya kutekwa kwa Mji wa Makkah na Waislam.

Ambapo neno Sadaqah hua ni lenye kumaanisha Kua mkweli, kua Muaminifu, Kusema

Ukweli, Kuthibitisha Ukweli, Kuamini, Kusadiki, Kua na Imani, na pia Kutoa kitu kwa

ajli ya Kusidia. Hivyo kutubainishia kua ni wale tu wenye kumuamini Allah Subhnaha

wa Ta’ala na kua ni wenye Taqwa na kuamini juu ya siku malipo na kuhesabiwa ndio

wenye Kutoa Sadaqah.

Na kutokana na kumuamini Mola wao na kuamini juu ya hayo basi hua ni wenye kutoa

miongoni mwa vile vinavyostahiki kutolewa kulingana na maamrisho yake Allah

Subhnah wa Ta’ala kwa kujali uzuri na ubora wa anachotoa kama alivyosema katika aya

ifuatayo:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُو ۤ اْ‏ أَنْفِقُواْ‏ مِن طَيِّبَاتِ‏ مَا كَسَبْتُمْ‏ وَممِ َّآ أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ‏ ٱلأَرْضِ‏

وَلاَ‏ تَيَم َّمُواْ‏ ٱلخَْبِيثَ‏ مِنْهُ‏ تُنْفِقُونَ‏ وَلَسْتُمْ‏ آبِخِ‏ ذِيهِ‏ إِلا َّ أَن تُغْ‏ مِ‏ ضُواْ‏ فِيهِ‏ وَٱعْلَمُ‏ و ۤ اْ‏ أَ‏ َّن

ٱهلل ََّ‏ غَنيِ ٌّ حمَِيدٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo anfiqoo min tayyibati ma kasabtum wamimma

akhrajna lakum mina al-ardhi wala tayammamoo alkhabeetha minhu tunfiqoona

walastum bi-akhidheehi illa an tughmidoo feehi waiAAlamoo anna Allaha

ghaniyyun hameedun (Surat Al Baqara 2:267)


284

Tafsir: Enyi mlioamini, toeni (Sadaqa) kutokana na kile mlichokichuma kwa halali na

kutokana na vile tulivyovizalisha kwa ajili yenu kutoka ardhini. Na wala msitoe kile

ambacho ni kibaya wakati nyinyi wenyewe hamtokubali kukipokea isipokua (labda

mtapokea) mkiwa mmefumba macho. Na Allah ni Tajiri anaejitosheleza na mwenye

kustahiki kusifiwa.

Na si kwa kujaalia Ubora na Uzuri tu lakini kutoa kulingana na uwezo wake mtu, bila

kujali kingi, kikubwa au kidogo kwani mtoaji hua ametoa kwa ajili ya kutafuta radhi za

Allah Subhanah wa Ta’ala ambae si mwenye kudharau kilichotolewa kabla ya kuangalia

Nia ya alietoa kisha ndio kuangalia kilichotolewa kama alivyosema katika aya ifuatayo:

‏﴿ٱل َّذِينَ‏ يَلْمِزُونَ‏ ٱلْمُط َّوِّعِينَ‏ مِنَ‏ الْمُؤْمِنِينَ‏ فىِ‏ الص َّدَقَاتِ‏ وَال َّذِينَ‏ لاَ‏ يجَِدُونَ‏ إِلا َّ

جُهْدَهُمْ‏ فَيَسْخَرُونَ‏ مِنْهُمْ‏ سَخِ‏ رَ‏ ٱهلل َُّ‏ مِنْهُمْ‏ وَلهَُمْ‏ عَذَابٌ‏ أَلِيمٌ‏ ﴾

Alladheena yalmizoona almuttawwiAAeena mina almu/mineena fee alssadaqati

waalladheena la yajidoona illa juhdahum fayaskharoona minhum sakhira Allahu

minhum walahum AAadhabun aleemun (Surat At Tawba 9:79)

Tafsir: Ama wale ambao ni wenye kuzikejeli Sadaqa zilizotolewa na Waumini na wale

wasioweza kutoa isipokua kwa ikhlasi, basi Allah atawaadhirisha na kuwakejeli

nawatapata Adhabu kali sana

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Aya hii ilishuka pale

baada ya Abd Rahman Ibn Awf alipotoa Waqiah 40 za Dhahabu (Kumpa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kama Sadaqah yake kwa Uislam) na Sahaba

mwengine akatoa sehemu ndogo ya punje za Nafaka. Hivyo Wanafiq wakasema:

‘Wa Allahi Abd Rahman hakukusudia kufanya chochote isipokua kufanya Riya

katika kutoa kwake, na kuhusiana na yule mwengine basi Allah Subhanah wa Ta’ala

hana haja ya kimchango chake kidogo’’

Ambapo mtizamo mwengine ni ule usemao kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam aliitisha mchango wa Sadaqa, hivyo akatokea Mtu mweusi mwenye

muonekano usiopendeza akiwa na Ngamia wake mzuri sana na kumtoa Sadaqa.

Hivyo mmoja kati ya Wanafiq akasema: ‘Hakika Ngamia wake ni Mzuri kuliko

yeye mwenyewe’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamsikia na

akasema: ‘La, Bali yeye ni Mbora zaidi ya Ngamia wake na ni mbora zaidi yenu.’’


285

Ambapo amesema Abu Hurayrah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah

Alayhi wa Salam kua: ‘Kama mmoja wenu atatoa Sadaqa yenye ukubwa wa Kokwa

moja ya Tende kutokana na kichumo chake cha halali basi Allah Subhanah wa

Ta’ala huipokea kwa mkono wake wa kulia. Na kisha huyakuzisha malipo yake

kama vile mmoja wenu anavyomlea mtoto wa Farasi wake, hadi malipo hayo

yakawa makubwa sana kama Mlima’’(Imam Bukhari)

Kwani amesema pia Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

‏﴿آمِنُواْ‏ بِٱهلل َِّ‏ وَ‏ رَسُولِهِ‏ وَأَنفِقُواْ‏ ممِ َّا جَعَلَكُم م ُّسْتَخْلَفِينَ‏ فِيهِ‏ فَٱل َّذِينَ‏ آمَ‏ نُواْ‏ مِنكُمْ‏

وَأَنفَقُواْ‏ لهَُمْ‏ أَجْ‏ رٌ‏ كَ‏ بِيرٌ‏ ﴾

Aminoo biAllahi warasoolihi waanfiqoo mimma jaAAalakum mustakhlafeena feehi

faalladheena amanoo minkum waanfaqoo lahum ajrun kabeerun (Surat Al Hadid

57:7)

Tafsir: Aminini Allah (Subhanah wa Ta’ala) na Mtume wake (Salallahu Alayhi wa

Salam) na tumieni kutokana na kile tulichokujaalieni kua na Ukhalifa juu yake. Na

kwa wale walioamini miongoni mwenu na wakatumia tulichowapa basi watakua na

Malipo makubwa sana.

Hivyo ili tunufaike zaidi basi inabidi tujue ni Masikini gani ambao tusipohimizana

kuwalisha na kuwasaidia basi tutakua na masuali mazito ya kujibu, kwa sababu kwa

upande mmoja basi hali iko kama tunavyoona kua Uislam unakataza kuomba, hivyo jee

hawa Masikini wanaozungumziwa hapa ni Masikini wa aina gani?

Hivyo jibu la suali hili tunalipata pale tunapoangalia maneno ya Imam Abu Jafar

Muhammad Ibn Jarir At Tabari ambae anatuambia kua : ‘Amesema Abu Hurayra Radhi

Allahu Anhu kua : ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Masikini

wa kweli hua si yule ambae anaenda na kuwaomba watu kwa ajili ya Tende moja

mbili, au kwa kula chakula cha tonge moja au mbili, bali ni yule ambae anaeona

haya kuomba, soma kama unataka aya isemayo:


286

‏﴿لِلْفُقَرَآءِ‏ ٱل َّذِينَ‏ أُحصِرُواْ‏ فىِ‏ سَبِيلِ‏ ٱهلل َِّ‏ لاَ‏ يَسْتَطِيعُونَ‏ ضَرْابً‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ يحَْ‏ سَبُهُمُ‏

ٱلجَْاهِلُ‏ أَغْنِيَآءَ‏ مِنَ‏ ٱلت َّعَف ُّفِ‏ تَعْرِفُهُم بِسِ‏ يمَاهُمْ‏ لاَ‏ يَسْأَلُونَ‏ ٱلن َّاسَ‏ إِلحَْافاً‏ وَمَا

تُنفِقُواْ‏ مِنْ‏ خَيرٍْ‏ فَإِن َّ ٱهلل ََّ‏ بِهِ‏ عَلِيمٌ‏ ﴾

Lilfuqara-i alladheena ohsiroo fee sabeeli Allahi la yastateeAAoona dharban fee alardhi

yahsabuhumu aljahilu aghniyaa mina alttaAAaffufi taAArifuhum

biseemahum la yas-aloona alnnasa ilhafan wama tunfiqoo min khayrin fa-inna

Allaha bihi AAaleemun (Surat Al Baqara 2:273)

Tafsir: (Sadaka hua ni) Kwa Mafukara ambao wamezuilika kwa ajili ya kujitolea kwa

ajili ya Allah, na hawawezi kutembea Ardhini (kwa ajili ya kufanya kazi au biashara),

na wale wasiowajua huwadhania kua ni Matajiri kutokana na kujiheshimu kwao.

Unaweza kuwajua kutokana na alama yao, hua hawawaombi watu kwa kukera, na

chochote kile mtakachotumia kwa ajili ya kheri basi Allah anajua juu yake’

Katika aya hii Allah Subhanah wa Ta'ala anatubainishia kua Wanaostahiki kupewa

Sadaqa kua ni wale ambao ni wenye sifa ya kua ni ‘Uhsiruu fii Sabli Allahi’ yaani

Wamezuilika kwa ajili ya kujitolea Katika Njia ya Allah.

Na tunapozungumzia kuhusiana na ‘Uhsiruu fii Sabli Allahi’ basi hua ni yenye

kuwaelezea wale Watu wenye Kuzuilika kutokana na kufanya Kazi zao za Kujitafutia

Maisha kwa sababu ya kua ni wenye Kujitolea kwa ajili ya Kupigania Njia ya Allah

Subhanah wa Ta'ala na hivyo basi tunapoyaangalia Maneno haya basi tunaona kua Ndani

yake wanaingia Wale watu ambao hua ni wenye kuacha yao na kisha wakawa ni wenye

kujitolea kwa Ajili ya Allah Subhanah wa Ta'ala.

Ambapo tunapowazungumzia watu wa aina hii basi wengi wetu hua ni wenye

kuwasahau, kwani hawa hua si wengine isipokua ni wale Maimamu wa Miskitini,

Wahudumu wa Miskitini, Walimu wa Madrasa wanao wanaowasomesha Watoto wa

Kiislam Dini yao, Wanafunzi wanotafuta Ilm ya Dni ya Kiislam, Waislam waliojitolea

kwa Ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala, na kisha wakawa na hali mbaya ya Maisha n.k

Hivi jee leo hii Wazee wangapi wanawalipia ipasavyo watoto wao Madrasa na hivyo

katika Kulipa kwao Ipasavyo kua ni wenye Kuwafikishia Sadaqa yao stahiki Walimu wa

Madrasa kutokana na kujitolea kwao kwa ajili ya Allah, Kama ilivyosema Aya?


287

Au Jee ni Waislam Wangapi katika Kutoa Kwao Misaada na Sadaqa hua

Wanawakumbuka Walimu wa Madrasa? Au ni Waislam wangapi katika Kutoa kwao

Misaada na Sadaqa hua wanawakumbuka Maimamu wa Miskiti wanaowasalisha, au

Waadhini, au Wahudumu wa Miskitini, n.k?

Kwani hawa wote wanajumuishia katika watu waliotajwa kwenye aya hii kua wanatakwa

wapewe kipaumbele katika kupewa Sadaqa kwa sababu ni mongoni mwa walio katika

hali ya Uhsiruu Fii Sabili Allah.

Na kisha kwa upande mwengine basi tunaona kua katika aya yetu hii kua Allah Subhanah

wa Ta'ala anatubainishia kua Wanaostahiki Sadaqa ni wale ambao ni wenye sifa ya kua

ni AlttaAAaffufi.

Ambapo neno alttaAAaffufi hua ni lenye kutokana na neno A'affa lenye kumaanisha

Kujizuia, Kujihifadhi, Kujidhibiti kutokana na kile ambacho kimekatazwa, Kujizuia na

kile ambacho ni Haram. Ambapo Neno TaA'affuf hua linamaanisha Kua na Heshima,

Kuona Haya au Kujizuia.

Na ili tufaham vizuri zaid kuhusiana na maana ya Neno hili na hivyo Kufaham sifa za

Masikini Stahiki kama ilivyozungumzia Aya basi na tuangalie mifano ifuatayo ambapo

mfano wa kwanza ni ule wa aya ambayo inasema:

‏﴿وَلْيَسْتَعْفِفِ‏ ٱل َّذِينَ‏ لاَ‏ يجَِدُونَ‏ نِكَاحاً‏ حَتى َّ ٰ يُغْنِيَهُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ مِن فَضْلِهِ‏ وَٱل َّذِينَ‏ يَبْتَغُونَ‏

الْكِتَابَ‏ ممِ َّا مَلَكَ‏ تْ‏ أَيمَْانُكُمْ‏ فَكَ‏ اتِبُوهُمْ‏ إِنْ‏ عَلِمُتُمْ‏ فِيهِمْ‏ خَيرْ‏ اً‏ وَآتُوُهمْ‏ مِّن م َّالِ‏ ٱهلل َِّ‏

ٱل َّذِي ۤ آاتَكُمْ‏ وَلاَ‏ تُكْرِهُواْ‏ فَتَيَاتِكُمْ‏ عَلَى ٱلْبِغَآءِ‏ إِنْ‏ أَرَدْنَ‏ تحََص ُّناً‏ لِّتَبْتَغُواْ‏ عَرَضَ‏ ٱلحَْيَاِة

ٱلد ُّنْيَا وَمَن يُكْرِههُن َّ فِإِن َّ ٱهلل ََّ‏ مِن بَعْدِ‏ إِ‏ كْ‏ رَاهِهِن َّ غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

WalyastaAAfifi alladheena la yajidoona nikahan hatta yughniyahumu Allahu min

fadlihi waalladheena yabtaghoona alkitaba mimma malakat aymanukum

fakatiboohum in AAalimtum feehim khayran waatoohum min mali Allahi alladhee

atakum wala tukrihoo fatayatikum AAala albigha-i in aradna tahassunan

litabtaghoo AAarada alhayati alddunya waman yukrihhunna fa-inna Allaha min

baAAdi ikrahihinna ghafoorun raheemun(Surat An Nur 24:33)

Tafsir: WalyastaAAfifi (Na Wajizuie Kwa Kujihifadhi na Yaliyokatazwa) Wale Ambao

hawana Uwezo (Wa Kifedha) Kwa ajili ya Kuoa hadi Pale Watakapowezeshwa na


288

Allah kutokana na Fadhila zake (Neema zake) Na miongoni mwa mnaowamiliki

wakitaka kuandikiwa mkataba wa uhuru wao, waandikieni hivyo, ikiwa mnawajua

kua ni waaminifu. Na wapeni baadhi ya mali zenu zinazotokana na utajiri wa Allah

aliokupeni juu yenu. Na msiwalazimishe kufanya ukahaba, ikiwa wanataka usafi, ili

mpate kunufaika kidunia. Lakini ikiwa mmoja wenu atawalizimisha (kufanya

ukahaba), basi baada ya kulazimishwa huko, Allah ni mwenye kusamehe na ni mwingi

wa rehma (Atawasamehe wanawake hao kutokana na kulazimishwa kwao kufanya

dhambi hiyo).

Kwani hii ni aya ambayo inafafanuliwa na ile Hadith ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam isemayo kua: ‘Ndoa ni sehemu ya Sunnah yangu, yeyote yule asietekeleza

Sunnah yangu basi hua si Miongoni mwangu. Hivyo Oaneni kwani kwa Hakika

mimi nitajisifia wingi wenu kiidadi mbele ya Ummah Nyengine. Hivyo kila mwenye

uwezo na Aoe na asiekua na Uwezo basi na Afunge, kwani funga humzuilia Hamu

yake’(Imam Ibn Majah)

Na akasema tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kuna watu wa aina tatu

ambao msaada juu yao hua wenye kusaidia kusimamia jukumu la Allah. Kumsaidia

yule anaetaka kuoa, kumlipia Mtumwa ili awe huru na Kumlipia Mtu anaepigania

kwa ajili ya njia ya Allah’(Imam Ibn Majah, Imam At Tirmidhii)

Nadhani tumefahamiana maana ya aya yetu kulingana na Ufafanuzi wa Hadith hii na

tunapoangalia mfano wa pili wa aya iliyotumia neno A’affa basi tunakutana na ule wa

mfano wa aya ya Tabbaruj ambayo inasema:

‏﴿وَٱلْقَوَاعِدُ‏ مِنَ‏ ٱلنِّسَآءِ‏ ٱل َّلاَتِى لاَ‏ يَرْجُونَ‏ نِكَاحاً‏ فَلَيْسَ‏ عَلَيْهِن َّ جُنَاحٌ‏ أَن يَضَعْنَ‏

ثِيَابَهُن َّ غَيْرَ‏ مُتَبَرِّجَاتِ‏ بِزِينَةٍ‏ وَأَن يَسْتَعْفِفْنَ‏ خَيْرٌ‏ له َُّن َّ وَٱهلل َُّ‏ سمَِيعٌ‏ عِلِيمٌ‏ ﴾

WaalqawaAAidu mina alnnisa-i allatee la yarjoona nikahan falaysa AAalayhinna

junahun an yadaAAna thiyabahunna ghayra mutabarrijatin bizeenatin waan

yastaAAfifna khayrun lahunna waAllahu sameeAAun AAaleemun(Surat An Nur

24:60)

Tafsir: Na Kwa wale (Wazee waliopitiliza Umri wa Kutokua na Matamanio ya

Kuingiliana) Miongoni mwa Wanawake ambao Hawategemei Kurudi Katika Maisha

ya Ndoa basi Hua Hakuna Makosa Juu yao kama Wakiwacha Nguo zao bila ya

Kutoonesha Mapambo yao lakini kama YastaAaffifna (watajizuia na Kuihifadhi) basi

hua ni kheri kwao, Na Allah ni Mwingi wa Kusikikia na Mwingi wa Kujua


289

Ambapo aya hii ya Surat An Nur 24:60 inabainisha kua kwa Wanawake ambao washakua

Wazee na hawavutii tena Miili yao na hawana Matamanio ya Kimwili na hivyo hawana

haja wala hamu ya kutaka kuolewa tena basi wanaruhusika kutojihifadhi, kwa kuvaa

nguo za kawaida tu bila ya kujitanda, ila kama Wanawake hao YastaAAfifna (watajizuia

na Kuihifadhi) basi hua ni bora kwao, na kwa hakika Allah Subhanah wa Ta’ala ni

mwingi wa kusikia na kujua.

Yaani Hili ni Onyo kua Wanawake wasichukue Kisingizio cha Kua anajiona kua

ameshakoma Hedhi Labda na hivyo hataki Kuolewa akasema kua hana hata hamu ya

Matamanio ya Kimwili lakini Hapo hapo Mwili wake Unavutia Wazee wenzake au vijana

pia wanaopenda Wazee na hivyo Mwanamke huyo akauwacha wazi Makusudi Mwili

wake huo bila ya kujistiri ipasavyo ili kuonesha Uzuri wa Maumbile Uonekane wazi.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta'ala katika Onyo hili basi anaweka wazi kua yeye ni

mwenye kusikia yanayosemwa na Nyoyo za kila Kiumbe wakiwemo Wanawake hao na

mimi na wewe pia.

Hivyo anajua Nia yako ni ipi, na hata kama Mwanamke akiwa hana nia hio ya kujionesha

lakini pia hapo hapo tumesema kua kuna wazee wa Kiume ambao wanapenda Wazee

wenzao, na pia kuna Vijana ambao wanavutiwa na Wanawake wazee kwani hua

wanasema kua Ng’ombe hazeeki Maini. Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta'ala

akasema kua Kama Wanawake hao watajiheshimu na kujihifadhi basi ni kheri kwao.

Hivyo hii ni mifano ya maana ya neno AlttaAAaffufi. Lililotumika kwenye ya 273 ya

Surat Al Baqara inayoelezea aina za watu Masikini wenye kustahiki kupewa Sadaqah,

kwani hawa hua ni wenye kujiheshimu, wenye kukinai na wenye kuridhika na Majaaliwa

ya Mola wao juu yao na hivyo hua ndio wenye kujua maana ya ile aya isemayo:

‏﴿وَأَن َّهُ‏ هُ‏ وَ‏ أَغْنىَٰ‏ وَأَقْنىَٰ‏ ﴾

Waannahu huwa aghna waaqna(Surat An Najm 53:48)

Tafsir: Na kwa hakika ni yeye (Allah Subhanah wa Ta’ala) ndie mwenye kutoa kingi

kinachotosheleza (kinachotajirisha) na kidogo kinachokinaisha.

Naam bila ya shaka, kwani ukijua maana ya maneno ya aya hii na kuyatafakkari basi

utakua ni Mtu mwenye Kutosheka na pale Allah Subhanah wa Ta'ala anapokumwagia

Rehma na Neema zake kwa wingi, na hivyo utakua ni mwenye kuonesha Shukrani kwa

kuzitumia ipasavyo neema hizo katika njia ya Kukunufaisha wewe na Viumbe wenzako


290

Na hapa ndani yake haiingia Mali tu au pesa, bali pia ndani yake inaingia Afya, Cheo,

Madaraka, Mamlaka, Umoja katika jamii yako ya Kiislam n.k. Naam..hio ni katika hali

ya Aghna yaani ya Kutajirishwa au Kutoshelezwa na Neema kutoka kwa Mola wako.

Ambapo tunapoangalia kwa upande wa Aqna basi hua ni Kukinai yaani pale unapopewa

Kitu kiasi chako, au kidogo zaidi ya mahitaji yako, na kisha ukawa na mtizamo wa kua

kwako wewe ni muhimu kupata hicho ulichopata kuliko kukosa kabisa kwani angalau ya

kua wewe umepata hicho kidogo kwani kuna wengine hawakupata. Na katika kukinai pia

ndani yake mnaingia kila Rehma na Neema ya kila kitu ulichopewa na Mola wako, na

hivyo kua ni mwenye kuridhika na Mjaaliwa yake juu yako kwa ni yeye ndie mwenye

kujua kilicho bora kwako, hivyo kua na Subra kwako na kushukuru basi hua ni bora

kwako

Hivyo hii ndio hali waliyokua nayo watu Masikini waliozungumziwa kwenye aya yetu

ya Surat Al Baqara 2:273, Hua ni wenye sifa ya AlttaAaffuf ya Kujizuia na kua na Subra

kwani wanajua kua vyovyote vile itakavyokua basi wao wamekinai kwani kutokana na

makadirio ya Allah Subhnah wa Ta’ala hio ni kheri kwao.

Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Watu wa Peponi ni wa

aina tatu:

1-Mtu mwenye Mamlaka na akawa Muadilifu, na mwenye kutoa Sadaqah na

Muongofu.

2-Mu mwenye huruma na Moyo Mlaini kwa Ndugu zake na Waislam wenzake.

3-Mtu aliekua msafi na asieomba Msaada ingawa ana watoto wengi’(Imam Muslim)

Kwani anasema Abu Said Al Khudri Radhi Allahu Anhu kua: ‘Safari Moja sisi tulikua

tuna hali mbaya sana. Hivyo kuna Mtu akaniambia kua nikaonane na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kumuomba msaada

Hivyo Nami nikafuata Ushauri huo na kutoka hadi kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam lakini nilipofika tu kwake basi nikamsikia anasema kua: ‘Mtu yeyote yule

atakaefanya TaAaffuf kujizuia kutokana na Kuomba basi Allah Subhanah wa

Ta'ala atamuokoa Mtu huyo kutokana na Kuomba, Mtu yeyote yule atakaemuomba

Allah Subhanah wa Ta'ala riziki kutoka kwake, basi Allah Subhanah wa Ta'ala

atamruzuku Mtu huyo. Lakini Hata Hivyo Mtu akituomba basi tusimkatalie

Kumpa pale inapokua tunao Uwezo wa Kumsaidia.’

Abu Said Al Khudhri Radhi Allahu Anhu anaendelea kusema kua Hivyo Nami

nikaiambia Nafsi yangu kua: ‘Kwanini mimi nisifanye TaAaffuf (Kujizuia Kuomba),


291

na hivyo Allah Subhanah wa Ta'ala akanijaalia Mimi kupata Uokovu wa Kua si

miongoni mwa wenye Kuomba?

Hivyo nami nikarudi Nyumbani na tangu siku hio basi nikaiahidi Nafsi yangu kua:

‘Hakika mimi sitomuomba Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa chochote

Kile hadi utakapofika Mwisho wetu hata kama Dunia itatuangukia juu yetu au

itatuzamisha ndani yake, Isipokua kwa yule atakaenusuriwa na Allah Subhanah wa

Ta'ala miongoni mwetu.’

Naam, ndani ya tukio hili tunatakiwa tuzingatie namna Masahaba walivyokua Wakiishi

na kufuata Maamrisho ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika kufanya

Ta'aAaffuf, yaani kujizuia kutokana na waliyokatazwa na Allah Subhanah wa Ta'ala na

pia na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Kwani anasema Mujaddid Ad Din, Sultan Al Mutakallimin Imam Al Mushaqiqin, Imam

Al Ghazali Al Thani Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Al Husayn Ibn Umar Fakhr

Ad Din Al Razi kuhusiana na aya hii ya 273 ya Surat Al Baqara kua:

‘Aya inatubainishia kua Masikini hawa waliotajwa hapa ni huwezi kuwajua

kutokana na Muonekano wao bali utaweza kuwajua kutokana na Roho na Nyoyo

zao, kwani kama vile ambavyo haiwezekani kuonekana kwa Khofu ya Mwili wa

Mnyama wa Mwituni pale anapokua katika hali ya kua ni mwenye kumuona Simba

na kumuogopa.

Na hii ni kwa sababu sio Wanyama wengi ambao tayari wameshawahi kukumbana

na Nguvu na purukushani za Simba anapovamia. Hivyo ndivyo pia inavyokua hali

ya Watu hawa, ambao huweza kujulikana kutokana na Utulivu wa Nyoyo na Roho

zao ambayo hua ni katika hali ya Upekee wa Kimaumbile ambao ndio

zinazowadhihirisha sifa zao.’

Kwani Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea kutubainishia kwa njia

ya kuhoji kua: Kama imeshawekwa wazi kua hali yao ya Al TaaAaffuf - yaani ya

Kujizuia Kuomba ndio Alama yao basi inakua inamaanisha nini kua Hawawaombi

watu kwa njia ya Kukera?

Naam..kwa sababu kuna watu wasiokua na TaAaffuf hua wanaomba kama Ruba yaani

akikuganda kwa ajili ya kukuomba basi hakuganduki mpaka umpe sadaka yake, yeye

hafikirii kua labda na wewe hua una matatizo yako, la, kwani hua ana ubinafsi wa

kujifikiria yeye tu kiasi ya kua Ukimuona tu au ukiona simu yake basi unaanza kusema

Astaghfir Allah!. Kwa sababu unakua unajua kua sasa hivi nafikwa na Mtihani ambao ili

kuuepuka basi inabidi niseme Uongo, au nafikwa na Mtihani huu kwa sababu ya

Madhambi yangu..nk.


292

Na hii ndio hali ambayo Waislam hatutakiwi kua nayo, yaani ya Mtu kua anaomba mpaka

anawakera wale anaowaomba, na hivyo kujipatisha dhambi za bure Muombaji na pia

kumsababishia dhambi mwenye kutoa Msaada, kwa sababu tayari mtu keshakua anatoa

kwa kusikitika inamaana kua yeye hapati thawabu kwa kutoa kwake na wewe unapata

dhambi kwa kumsababishia Udhia mwenzako.

Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Watu wa aina tatu

hatozungumza nao Allah Subhanah wa Ta’ala katika siku ya Malipo, wala

hatowaangalia na wala hatowasafisha:

1-Wenye Kibri

2-Wenye kutoa Sadaqa huku wakiwa ni wenye kulalamika na kukumbushia juu ya

ukarimu wao.

3-Wale wanaouza bidhaa na kuapa uongo’(Imam At Tirmidhii)

Hivyo Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea kutupa Majibu ya suali

lake ambalo wengi huenda walijiuliza kua. ‘Kama Aya imesema kua wanajizuia

Kuomba, sasa inakuaje kua hapo hapo inasema Hawaombi kwa kukera?’

Ambapo jibu la suali hili ni kua: ‘Kinachoelezewa hapa hua sio Sifa yao watu hao kua

ni wenye kuomba kwani Tayari aya imeshasema kua Watu hawa wanafanya

TaaAaffuf yaani Wanajizuia na Kuomba. Hivyo basi haya Maneno yasemayo kua

Hawawaombi watu kwa kukera yanawalenga wale Wanaoomba kua hawatakiwi

kuomba hadi kufikia hali ya kua ni wenye Kukera.’

Mujaddid Ad Din Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea kutufafanualia kwa kusema kua:

‘Yaani hapa hali inakua kama vile ambavyo Mtu umekaa kwako, kisha wakaingia

watu wawili, Ambapo mmoja wao akiwa ni Mtu Mwema na mwengine ni Mtu

Muovu, kisha wewe ukawa ni mwenye kumsifu yule Mtu Mwema kwa kusema kua:

‘Mashaa Allah, Una sifa nzuri zilizo Njema sana’

Na kisha hapo hapo ukamwambia na yule Mtu Muovu kwa kusema: ‘Lakini na

wewe pia si Muovu’ Ambapo katika kusema kwako huko kumwambia Mtu huyo

Muovu kua na yeye si Muovu, basi hua kunamaanisha kua Mtu huyo ni Muovu.’

Na amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Allah Subhanah wa Ta'ala

hapendezewi na Mambo Matatu:

1-Mazungumzo yasiyokua na Maana.


293

2-Kufanya Israfu katika Mali.

3-Kuomba Omba watu kwa Kukera’ (Imam Muhammad Ibn Jariri At Tabari)

Ambapo anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Abd Allah Al Hakim al

Nishapuri kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, Alipohimiza kutoa Sadaqa

basi mmoja kati ya Masahaba akasema: ‘Ya Rasul Allah Mimi nna Dinar Moja!

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hio Itumie kwa ajili ya Nafsi

yako’

Kisha Mtu huyo akasema: ‘Na Nikiwa nna moja zaidi?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Itumie kwa ajili ya Mke wako’

Mtu Huyo akasema: ‘Na Kama nikiwa na Moja zaidi?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Itumie kwa ajili ya Watoto wako’

Kisha Mtu huyo akasema: ‘Na kama nikiwa na moja zaid?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hio sasa unajua vizuri ni nani

anaestahiki zaidi’

Naam..hivyo aya inatuonesha kua Kila utakachokua nacho na kukitumia basi Allah

Subhanah wa Ta'ala anajua juu yake, na anajua juu ya nia yako. Ambapo hadithi hii

inatuonesha ni nani anaestahiki kupata sadaqa yako kutoka kwako kulingana na Uwezo

wako.

Na Ndio Maana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamwambia Sahaba wake huyu

kua kwanza aanze na Nafsi yake, Kisha kwa ajili ya Mkewe, kisha kwa ajili ya Watoto

wako, kisha ndio utoe Sadaqa kwa watu wengine. Na hivyo sio Unatoa sadaka

kuwasaidia Omba omba ili watu wakuone halafu Watoto wako Nyumbani wanalia Njaa.

Hii inakua ni Dhambi badala ya Thawabu Au Unatoa halafu Ukaombe ili Utoe tena, Au

huna kisha unapewa kisha nawe Unatoa ili upewe tena. Hii pia hua haifai

Kwani amesema tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Sadaqah bora ni ile

inayotumiwa kutokana na ziada, mkono wa Juu (Unaotoa) ni bora kuliko wa chini

(Unaopokea) na anza (kwa kumpa) yule mwenye familia kubwa zaidi’ (Imam

Bukhari)


294

Na katika Hadith nyengine pia basi amesema Abdallah Ibn Jabir Radhi Allahu Anhu kua:

‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua amekaa na Masahaba zake mara

akaja mmoja miongoni mwa Masahaba huku akiwa na Kipande cha Dhahabu,

kama yai na kisha akasema: ‘Ya Rasul Allah Pokea hiki kua ni kama Sadaqa yangu,

na nnaapa kua sina kitu chengine Hapa Duniani zaidi ya hii Dhahabu.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akageukia upande wa pili. Ambapo Sahaba

huyo akamfuata upande huo aliogeukia, hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam akageukia tena Upande Mwengine.

Sahaba huyo akamfuata Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika upande huo

huo tena, Huku akimpa Dhahabu hio.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaichukua Dhahabu hio halafu akaitupa

huku akisema: ‘Mtu anakuja kwangu mimi akiwa na kile tu anachokimiliki na

kutaka kukitoa Sadaqa halafu baada ya kukitoa anakaa chini na Kuanza Kua

Omba Omba..Sadaka Inatakiwa itoke kwenye Kilicho cha ziada!’ (Imam Muhammad

Ibn Jarir At Tabari)

Ambapo kwa upande mwengine basi ingawa haipendekezwi kuwapa Sadaqa watu

wasiokua na sifa stahiki ya kusaidiwa lakini hapo hapo, kama itakua kutoa sadaqa huko

kutasaidia kubadilisha aina za hali za watu hao basi hua inakubalika kwa mfano kama

inavyowekwa wazi na hadithi ifuatayo:

‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kuna mtu alisema kua:

‘Nitatoa Sadaqah’ hivyo siku ya pili akatoka na kumpa Sadaqah Mwizi, na watu

wakasema, : ‘Amempa Sadaqah Mwizi’ hivyo mtu huyo akasema: ‘Ya Allah,

Alhamd lillah kua nimempa Sadaqah Mwizi.’

Na siku ya pili usiku akampa pesa Mwanamke mzinzi na watu wakasema, :

‘Amempa Sadaqah Mzinzi’ hivyo mtu huyo akasema: ‘Ya Allah, Alhamd lillah kua

nimempa Sadaqah Mzinzi.’ na siku ya tatu asubuhi akampa pesa Tajiri na watu

wakasema : ‘Amempa Sadaqah Tajiri’ hivyo mtu huyo akasema: ‘Ya Allah,

Alhamd lillah kua nimempa Sadaqah Mwizi, Mzinzi na Tajiri.’

Hivyo akaambiwa: ‘Ama kuhusiana na Sadaqah aliyopewa Mwizi, basi labda

itamfanya asiibe, Ama Sadaqah aliyopewa Mzinifu basi Labda itamfanya Asizini

na aliyopewa Tajiri basi labda itamfanya awe ni mwenye kuingiwa na ari na hivyo

kutoa kutokana na kile alichoneemeshwa na Allah.’’(Sahih Bukhari na Sahih Muslim)

Hivyo baada ya Allah Subhanah wa Ta’ala kuwazungumzia wale wasiohimizana kutoa

na kuwasadia Masikini katika aya 3 za mwanzo za Sura hii ya Al Maun na kuwajumuisha


295

kua ni miongoni mwa wanaokadhibisha Dini basi Allah Subhnah wa Ta’ala anaendelea

kwa kujumuisha ndani yake kwa kuwazungumzia Wanafiq ambao ni wale wenye sifa ya

Aaan Salatihim Sahun kama zinavyosema aya;

ف َوَيْلٌ‏ لِّلْمُ‏ ﴿ صَلِّ‏ ينَ‏ ۞ ٱل َّذِينَ‏ هُمْ‏ عَن صَلاَهتِِمْ‏ سَاهُونَ‏ ﴾

Fawaylun lilmusalleena; Alladheena hum AAan salatihim sahoona; (Surat Al Maun

107:4-5)

Tafsir: Na Kisha Ole Wao wale Wenye Kusali. Wale Ambao juu ya Sala zao Sahuna

(Wanazidharau na kuzichelewesha kwa kutosali katika wakati wake).

Ambapo aya hizi zimewajumuisha watu waliomo kwenye makundi yafuatayo:

Wale wasiosali Kabisa.

Wale wanaosali lakini si ndani ya wakati wake Sala hio bali ni nje ya wakati wa

Sala.

Wale wanaosali lakini hawasimamishi Nguzo za Sala.

Wale ambao hawana Kushuu ndani ya Sala.

Ambapo kulingana na mtizamo wa Sa’ad Ibn Abi Waqqas Radhi Allahu Anhu basi yeye

anasema kua: ‘Kilichokusudiwa hapa si kukosekana kwa Khushuu bali ni kulingana

na kudharau wakati wa Sala mpaka unapokua umepita.’

Na kwa upande wa Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, basi anasema

kua: ‘Hii inahusiana na Kutosali kabisa, jambo ambalo lilikua linafanywa na

Wanafiq, yaani walikua wanasali wanapokua pamoja na watu lakini wanapokua

peke yao hua hawasali’

Na kwa upande wa Imam Mujahid Ibn Sulayman, Imam Qatadah Al Sadusi, na Jabir Ibn

Zayd basi wao wanasema kua: ‘Hii inahusiana na wale ambao ni wenye kuzidharau

Sala zao kwa kusali pale tu wanapopenda kusali na wasipotaka basi hua hawasali’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amewazungumzia wale ambao ni wenye

kuzidharau Sala zao kua ni Wanafiq ambao wamezungumziwa na aya ifuatayo:


296

‏﴿إِن َّ ٱلْمُنَافِقِينَ‏ يخَُادِعُونَ‏ ٱهلل ََّ‏ وَهُوَ‏ خَادِعُهُمْ‏ وَإِذَا قَامُو ۤ اْ‏ إِلىَ‏ ٱلص َّلاَةِ‏ قَامُواْ‏ كُسَالىَٰ‏

يُرَآءُونَ‏ ٱلن َّاسَ‏ وَلاَ‏ يَذْكُرُونَ‏ ٱهلل ََّ‏ إِلا َّ قَلِيلاً‏ ﴾

Inna almunafiqeena yukhadiAAoona Allaha wahuwa khadiAAuhum wa-idha

qamoo ila alssalati qamoo kusala yuraoona alnnasa wala yadhkuroona Allaha illa

qaleelan(Surat An Nisaa 4:142)

Tafsir: Na kwa hakika Wanafiq wanataka kumfanyia hadaa Allah, lakini Allah ndie

anaewahada wao. Na wanaposimama kusali hua wanasimama kwa uvivu ili

waonekane na watu, na hawamkumbuki Allah (Ndani ya Sala zao) isipokua kidogo tu.

Ambapo amesema Anas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua: ‘Hio ni Sala ya Mnafiq, hua ni mwenye kusubiri hadi Jua

linapotua baina ya ncha mbili za pembe za Shaytan, halafu ndio haraka sana

hukimbilia kudonoa ardhini mara nne na hivyo hua ni mwenye kumkumbuka

Allah kwa mda mfupi sana’(Sahih Muslim)

Ambapo amesema Ata’ Ibn Dinar kua: ‘Alhamd lillah kua Allah Subhanah wa Ta’ala

amesema katika aya hizi kua ‘Wale ambao ni wenye kua na dharau ndani ya Sala

zao, bali amesema: ‘Wale wenye kudharau Sala zao’ kwani hakuna hata mmoja

miongoni mwetu ambae si mwenye kukosa au kupungukiwa na umakini kwenye

Sala.’

Na Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari amesema kua: ‘Hali hii hua

inaonekana na wengi sana miongoni mwa wale ambao ni wenye kujidai kua wao ni

Waislam (lakini huku Nyoyo zao zikiwa zimezongwa na Matamanio ya kidunia),

Unapokua pamoja nao basi utaona kua hawana wanachokizungumzia isipokua

Dunia yao, na hivyo hua hawamkumbki Allah Subhanah waTa’ala isipokua kidogo

tu.’

Ambapo Allah Subhana wa Ta’ala amezungumzia tena kuhusiana na Unafiq wa wale

wanaosali kwa kusema tena katika Qur’an:

‏﴿وَمَا مَنَعَهُمْ‏ أَن تُقْبَلَ‏ مِنْهُمْ‏ نَفَقَاتُهُمْ‏ إِلا َّ أَن َّهُ‏ مْ‏ كَ‏ فَ‏ رُواْ‏ بِٱهلل َِّ‏ وَبِ‏ رَسُولِهِ‏ وَلاَ‏ ‏َْتُونَ‏

ٱلص َّلواَةَ‏ إِلا َّ وَهُمْ‏ كُسَالىَٰ‏ وَلاَ‏ يُنفِقُونَ‏ إِلا َّ وَهُمْ‏ كَارِهُونَ‏ ﴾


297

Wama manaAAahum an tuqbala minhum nafaqatuhum illa annahum kafaroo

biAllahi wabirasoolihi wala ya/toona alssalata illa wahum kusala wala yunfiqoona

illa wahum karihoona(Surat At Tawba 9:54)

Tafsir: Na kitu gani kinachosababisha kisikubaliwe kile wanachokitoa wao isipokua

ni kua wao hawakumuamini Allah na Mtume wake (Salallahu Alayhi wa Salam). Na

hawaji kusali isipokua wanakua katika hali ya uvivu, na hawatoi kitu isipokua wakiwa

katika hali ya kukirihishwa.

Tunapoziangalia aya hizi basi tunaona kua katika kuelezea sala za Wanafiq hao

wanapokua wanasali basi aya mbili hizi zote zimetumia neno Kusala ambalo hua

linamaanisha Kua Mvivu, Kuregea, kutokua na Umakini, kua Mzito, Kua na Ajizi.

Ambapo hii hua ni sifa mbaya sana yenye madhara makubwa kwa Muislam kua Kaslan

basi amesema Malik Ibn Anas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallau Alayhi wa

Salam alikua akiomba Dua kwa kusema: ‘Allahumma inni a'udhu bika minal-'ajzi,

wal-kasali, wal-jubni, wal-hirami, wa a'udhu bika min 'adhabil-qabr wa a'udhu bika

min fitnat al-mahya wal-mamat’’ yaani Ya Allah hakika mimi natafuta hifadi yko

kutokana na Kua na Ajizi, Kua Kaslan (Mvivu), kutokana na kua Mwoga na kua

na Uzee, kutokana na Adhabu ya Kaburi na kutokana na Mitihani ya Maisha na

Mauti’(Sahih Bukari)

Na ndio maana kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari akasema

kua: ‘Aya imetumia neno Kusala ambalo wingi wake hua ni Kaslan yaani watu

ambao ni Wavivu, na hivyo basi Muumini wa kweli hatakiwi kua ni mwenye kusema

kua alikua ni Kaslan kuhusiana na mambo mema ya kheri ambayo hakuyafanya.’

Na kwa upande wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye anasema

kuhusiana na maana ya aya hizi kua: ‘Hawa ni wale watu ambao hua ni wenye kusali

katika Sala za Jamaa wanapokua mbele za watu lakini wanapokua peke yao hua

hawasali, na hivyo kutuwekea wazi kua, vitendo vya Ibada inatakiwa viwe ni vyenye

kutoka kwenye Nyoyo na hapo ndio vitamridhisha Allah Subhanah wa Ta’ala. Na

hivyo kama havikufanywa kutokana na ndani ya Nyoyo basi hua havina manufaa

yeyote, bali hua ni vyenye kua na madhara badala yake.’

Ambapo amesema Abu Qatadah Radhi Allahu Anhu amesema kua : ‘Amesema Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakuna Mwizi mbaya kuliko yule anaejiibia

kutoka kwenye Sala zake.’ Abu Qatadah Radhi Allahu Anhu akauliza: ‘Itakuaje Mtu

ajiibie kutoka kwenye Sala zake?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema

kua: ‘Kwa kutorukuu na kusjudu ipasavyo’(Mustadrak Al Hakiim)


298

Kwa upande wa Hudhayfah Ibn Al Yaman Radhi Allahu Anhu basi yeye alisema kua:

‘Jihadharini na Khushuu ya Mnafiq’ na alipoulizwa: ‘Ndio nini Khushuu ya

Mnafiq?’ basi Hudhaifah Ibn Al Yaman Radhi Allahu Anhu alisema: ‘Wakati Kiwili

wili kinapokua na Khushuu lakini Moyo ukiwa hauna Khushuuu. ’

Hudhayfah Ibn Al Yaman Radhi Allahu Anhu alisema pia kua ‘Kitu cha Mwanzo

ambacho kitaondoka kwenye kwenye Dini yenu hii ni Khushuu, na kitu cha Mwisho

ambacho mtakipoteza kwenye Dini yenu ni Sala, ambapo mtamuona Mtu anasali

lakini akiwa hana jema ndani yake na kisha itafikia wakati mtakua mnaingia

Misikitini na hamto muona hata mtu mmoja wenye Khushuu ndani yake.’

Na Abu Abd Allah Al Ashari Radhi Allahu Anhu amesema kua : ‘Amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam Mtu anaesali bila ya kurukuu na kusjudu ipasavyo hua

ni sawa mtu mwenye njaa sana. Kisha akala kokwa moja au mbili za Tende. Hua

hamsaidii kitu kabisaa’(Imam At Tabarani)

Kwani Sala ndio Msingi wa Jengo la Dini ya Kiislam, hivyo kama Ukiwa na Umakini

katika Kuusimamia Ujenzi wa Msingi huo na ukawa Imara basi hata ujengewe Ghorofa

ngapi za Mitihani Juu yake basi bado Uislam wako Utakua Imara. Na pia ndivyo

utakavyokua Imara Uislam wa wale waliochini yako kama utawasimamia katika Sala

zao.

Na hii ni kutokana na ile aya ya Surat Al Ankabuut ambayo inasema:

‏﴿ٱتْلُ‏ مَا أُوْحِ‏ ىَ‏ إِلَيْكَ‏ مِنَ‏ ٱلْكِتَابِ‏ وَأَقِمِ‏ ٱلص َّلواَةَ‏ إِن َّ ٱلص َّلواَةَ‏ تَنْهَى ٰ عَنِ‏ ٱلْفَحْشَآءِ‏

وَٱلْمُنْكَرِ‏ وَلَذِكْرُ‏ ٱهلل َِّ‏ أَكْبَرُ‏ وَٱهلل َُّ‏ يَعْلَمُ‏ مَا تَصْنَعُونَ‏ ﴾

Otlu ma oohiya ilayka mina alkitabi waaqimi alssalata inna alssalata tanha AAani

alfahsha-i waalmunkari waladhikru Allahi akbaru waAllahu yaAAlamu ma

tasnaAAoona (Surat Al Anqabut 29:45)

Tafsir: Wasomee (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) Kile tulichokushushia

kutoka ndani ya Kitabu, Na simamisha Sala, kwani kwa hakia Sala Inazuia ufanyaji

Dhambi za Matamanio na Maasi ya Kufr, na kumkumbuka llah ni kukubwa kimalipo

na Allah ni mwenye kujua juu ya Mnayoyafanya.

Hivyo bila ya shaka kama Msingi wa Jumba la Imani ya Kiislam kwa upande wa Sala

zako ukiwa Mbovu basi bila ya shaka Nyumba ya Imani yako itakua ni yenye


299

Kuporomoka, na hivyo kuna hatari ya kuangukia kwenye Unafiq na pia kwenye kua ni

Miongoni mwa wenye Kukadhibisha Dini na Siku ya Malipo na hivyo bila ya shaka

Hutakua na Mwisho Mwema.

Kutokana na aya hizi na hadith basi ndio tunaona umuhimu wa kutoona Uvivu katika

kufanya Ibada na pia kutuonesha umuhimu wa kua na Unyenyekevu kwenye Ibada kwani

kutokana nao Unyenyekevu huo yaani Khushuu ndio hupatikana mafanikio ya Dunia na

Akhera kama anavyosema Hasan Al Basr pale alipousia:

‘Tafuteni Utamu unaopatikana katika Mambo matatu. Jambo la kwanza ni utamu

wa ndani ya Sala, Utamu wa Kufanya Dhikr Allah na Utamu wa Kusoma Qur’an,

kwani Utamu wake vitu hivi hupatikana ndani yake, na ukiupata ndani yake basi

fahamu kua Mlango wa Peponi uko wazi kwa ajili yako, na kama ukiukosa basi

Mlango wa Peponi umefungwa kwa ajili yako.’

Ambapo katika hadith nyengine basi tunaona kua amesema Abu Said Al Khudhri Radhi

Allahu Anhu kua kuhusiana na kua na umakini na unyenyekevu ndani ya Sala kua:

‘Wakati mmoja wenu anapoenda miayo ndani ya Sala, basi na ajizuie kwa kadri

atakavyoweza, ili shaytan asiingie ndani ya mdomo wake’(Sahih Muslim)

Na akasema tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Sala Tano ambazo Allah

Subhanah wa Ta’ala amezifaridhisha, basi kila atakaetia udhu ipasavyo kwa ajili

yake na kisha akasali kwa wakati wake, na akarukuu kikamilifu huku akiwa na

unyenyekevu, basi imeahidiwa na Allah Subhanah wa Ta’ala kua atasamehewa,

lakini kwa yeyote yule ambae hatofanya hivvyo basi hua hakuna ahadi hio kwa ajili

yake yaani kama Allah akitaka atamsamehe na kama akitaka atamuadhibu’(Sunan

Abu Daud)

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anaendelea kutuambia katika Hadith nyengine

kuhusiana na kudharau Sala kwa kusema: ‘Hakika Mja anaweza kusali na kisha

akawa hakupata chochote kutokana nayo Sala hio isipokua sehemu ya 10 ya Sala

hio, au 9 au 8 au 7, au 6 au 5 au Robo au Nusu’(Musnad Imam Ahmad)

Ambapo amesema Hasan Al Basr kua: ‘Kama itakua huijali Sala yako, basi utakua

unajali nini zaidi yake? Kwa sababu kila unapokua unaijali Sala yako basi ndio

unavyojaaliwa kuyarekebisha maisha yako, hivi jee hamjasikia kua Sala

imeambatanishwa na Mafanikio? Pale inaponadiwa ‘Hayya aAala Al Salah Hayya

Aala al Falah!’ yaani ‘Njooni katika Sala, Njooni katika Mafanikio’ hivi jee

Utamuombaje Allah Subhanah wa Ta’ala akupe Mafanikio wakati hutimizi wajibu

wako kwake?’


300

Hivyo ili nasi tupate mafanikio kwenye Sala na Dua zetu kama alivyojaaliwa mafanikio

ya dua zao Hannah Bint Faqudh na Nabii Zakarriyah basi na tuangalie umuhimu wa

kujaribu kua na Unyenyekevyu kwenye Ibada.

UMUHIMU WA UNYENYEKEVU KATIKA SALA NA DUA

Anasema Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali kua: ‘Hivi Jee ni watu wangapi ambao hua ni wenye

kuwaheshimu Wafalme na kuogopa Mamlaka yao ingawa hawahitaji kitu

chochote kutoka kwao? Lakini hata hivi kwa upande wa Allah Subhanah wa

Ta’ala bsi hua ni wajibu kwa Mja kua ni mwenye kutegemea malipo kutoka kwake

kutokana na kumtukuza kwake na kumuomba kwake kwenye Sala, kama vile

ambavyo Mja huyo hua anakhofu kutokana na Adhabu yake Allah Subhanah wa

Ta’ala kutokana na makosa yake Mja huyo.’

Hivyo ili mtu afahamu maana ya yale ayasemayo ndani ya Sala wakati anapokua ndani

ya sala basi hua ni wajibu wake mtu huyo kujifunza na kujikumbusha maana ya maneno

hayo ya ndani ya Sala na hivyo awe ni mwenye kujilinda na kila kitu ambacho ni chenye

kumpelekea kumuondolea Unyenyekevu ndani yake, kwani kila mja anapokua ni

mwenye kufaham kwa kina maana ya maneno yaliyomo ndani ya Sala basi ndio

anavyojua zaidi kuhusiana na maana ya Sala na jukumu la Sala yake juu yake.

Kwa kuanzia na kujua ni nini maana ya neno Sala ambapo tunapoangalia maana ya neno

Sala basi hua tunaona kua ni lenye kutokana na Mzizi wa herufi Sad-Lam-Waw ambalo

hua ni lenye kumaanisha Kuumia au kua na maumivu katika sehemu ya Chini ya

Mgongo, Kuifanya Sehemu ya Kati ya Mgongo kua ni yenye kupinda kwa kuingia ndani

na pia humaanisha Kusali au Kuomba Dua.

Baada ya kujua maana hio basi hua ndio utaona namna gani unatakiwa uwe muonekano

wa mwili wako katika kila hatua ya kitendo chako unapokua ndani ya Sala. Kwani

hutakiwi kua ni mwenye Kusimama, na Kurukuu, na Kusjudu na Kukaa kama Mtu ambae

ni mwenye Mamlaka Makubwa na Kujiona, na wala hutakiwi vitendo vyako vionekane

kama vya Mtu ambae kama alieonewa au aliechoka na yuko taabani hajiwezi, bali

unatakiwa uwe ni mwenye muonekano wa Mtumwa ambae anampenda sana na

kumheshimu na Kumti mmiliki wake kutokana na Ukarimu na Huruma ya Mmiliki wake

huyo alie mbele yake.


301

Ambapo hapa Mtumwa hua ni wewe unaesali na Mmiliki hua ni Allah Subhanah wa

Ta’ala ambae ndie yuko mbele yako, Hivyo unaposimama basi Nyoosha Mgongo wako

na Mwili wako mzima uwe umenyooka, huku Uso wako ukiwa unaangalia chini mbele

yako katika sehemu unayosujudia huku miguu yako ikiwa umeitanua kwa nyanda moja

baina yake, hivyo usiitanue kama mtu anaetaka kucheza Sumo wala usiibane kama askari

alieambiwa akaze miguu.

Unapoingia kwenye Sala na Kusema ‘Allahu Akbar’ na unaponyanyua mikono hadi

usawa wa Mabega, na kisha unapoifunga mikono yako Kifuani mkono wa kulia juu ya

mkono wa kushoto chini ya Moyo wako hua unamaanisha kua umeirembea kwa mikono

yako Dunia yote na kila kitu chake kutoka ndani ya mwili wako na kisha kuujaza Moyo

wako, Roho yako, Nafsi yako na Ufahamu wako umakini na yakini kua uo mbele ya Mola

wako kwa ajili ya Maombi yako.

Unapo rukuu na kushika Magoti yako basi pia nyoosha mgongo wako sawasawa kiasi ya

kua kama itawekwa gilasi ya Maji juu ya Mgongo wako basi itakaa bila ya kuanguka

yaani usiupinde mgongo wako ukatokeza juu kama Upinde, na hakikisha Miguu yako

imenyooka sawasawa sawa bila ya kupinda kwenye sehemu za magoti yako, huku

mikono yako ikiwa imeshika magoti yako na vidole vyako vikiwa vimetanuka.

Ukisjudu pia usiupinde Mgongo bali nyoosha Mgongo wako ukae sawasawa kiasi ya kua

kama mtu atakuwekea gilasi ya maji maji kwenye uti wako wa mgongo basi gilasi ya

maji hayo haitoanguka kutoka mgongoni mwako.

Unaposjudu basi kwanza ni magoti yako ndio yanayotakiwa kua yaguse ardhi, kabla ya

mikono yako na kisha mikono na kisha ndio paji la uso huku ukihakikisha kua paji lako

la uso na pua yako vinagusa sehemu unayosjudia huku miguu magoti na viganja vya

mikono tu vikiwa vimegusa chini, hivyo mikono usiilaze chini yote kama anavyoilaza

paka au mbwa wakati anapolala, na wala usikunje ngumi wakati wa kusjudu bali kunjua

huku ukiwa umevibana vidole vyako na hapo hapo mikono yako usiitanue sana kama

ndege anaetaka kuruka na hivyo kua ni mwenye kuwakera wenzako kutokana na

kutanuka kwa mikono yako, bali iweke mikono yako katika mtanuko wa kiasi ikiwa

sawa na mabega yako, huku ukihakikisha kua vidole vya miguu yako pia vikiwa

vimeelekea Kibla.

Hivyo hapa kuna utofauti wa namna vinayotakiwa kukaa vidole vya mikono katika

wakati wa Kurukuu ambapo hua inakubidi kuviachanisha na katika wakati wa kusujudu

unatakiwa kuvibana.

Unapokaa Attahiyyat basi pia nyoosha mgongo na wala usiupinde mpaka ukafanya

kibyongo na tumbo likaingia ndani kama unavyopindika Upinde unapovutwa kwa ajili

ya kuachia Mshale uliomo ndani yake, na wala usiupinde Ubavu wako mpaka ukawa


302

unamuegemea mwenzako kiasi ya kua kama akiondoka basi huendaa ukaanguka

kutokana na kushidwa kujizuia kwako kutokana na kumuegemea.

Huku mguu wako wa Kushoto ukiwa umeukalia na wa Kulia ukiwa umebakia kama

ulivyokua katika wakati wa Kusjudu. Na ni Suna kusali huku ukiwa miguu chini bila ya

soksi wala khuf.

Hii ni hali unayotakiwa kua nayo Mtu katika muonekano wa vitendo vya viungo vya

kiwiliwili chako, ambapo mbali ya kua na hali hio, lakini kiufaham, kiakili kinafsi na

kimoyo ili mtu uwe na unyenyekevu ndani ya Sala yako basi unatakiwa uwe katika hali

zifuatazo:

Hudhur Al Qalb - Kuuhudhurisha Moyo ndani ya Sala. Yaani kuufanya Moyo wako

uwe huru kutokana na kila kitu isipokua kile ambacho uko katika kutaka kukifanya

katika wakati huo, yaani Ibada ya Sala yako. Hivyo ili uweze kuhudhurisha Moyo wako

kwenye Sala basi hua inakubidi kufuta kila kitu unachokifikria katika ufaham wako

katika wakati huo kabla ya kuinga kwenye Takbir ya ufunguzi wa kuingia Ndani Sala.

Al Tafahhum – Kufaham kila kitendo unachofanya na kila neno unalosema ndani

ya Ibada ya Sala. Kwani kufahamu maana ya kila kitendo na maana ya kila neno hua

ni kwenye kuhudhurisha pia Moyo katika kurahisisha Kufaham kila hatua ya Sala kama

inavyotakiwa, kwani hii ndio ambayo inayokufanya uwe na uwezo wa kuachana na kila

Ovu.

Al Taadhim – Utukuzaji wa Allah Subhanah wa Ta’ala ambae unasimama mbele

yake katika wakati wa Ibada yako. Hili ni jambo muhimu sana katika Sala yako,

Kwani hata kama ukiwa umehudhurisha Moyo wako kwenye Sala na pia unafahamu

kila unachokifanya ndani yake basi kamwe huwezi kupata hali ya unyenyekevu kama

ikiwa hukua ni mwenye kuhisi Ukubwa na Utukufu wa yule ambae umesimama mbele

yake na hivyo hutokua na hali inayotakikana kupatikana kutokana na kua ni mwenye

kumkumbuka Mola wako kwa kuona na kuhisi kua yuko mbele yako.

Al Haibah – Heshima ya hali ya juu inayotokana na kuvutiwa kwa kujawa

Mapenzi na Utiifu wa Hali ya Juu. Hii hua ni hali ambayo hua inapatikana baada ya

kufanya Taadhim, kwani hua ni hali ya heshima inayotakana na kua na Mapenzi na

Unyenyekevu uliojaa Taqwa kutokana na kujua ukubwa na uwezo wa Allah Subhanah

wa Ta’ala.

Al Rajaa – Matumaini yaani kua na Matumaini ya kupata malipo Mema kutokana

na kutekeleza Ibada yako hio ya Kumkumbuka na kumtukuza Allah Subhanah wa

Ta’ala ndani yake.


303

Al Haya – Kuona Haya yaani kukubali na kujiona kua wewe kama kiumbe basi una

kasoro nyingi na kubwa sana kutokana na Udhaifu wako mbele ya Mola wako

aliekuumba ambae kwa wakati huo yuko mbele yako.

Ambapo anasema Hudhayfah Ibn Al Yaman Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi nilisali

pamoja na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika usiku mmoja, kisomo

chake kilikua kirefu na alipokua akisoma aya yenye Tasbih basi alikua akisema

Subhana Allah na alipokua akisoma aya inayouliza Suali basi huuliza Suali,

anaposoma aya inayoomba ulinzi kutoka kwa Allah basi nae huomba Ulinzi kwa

Allah Subhanah wa Ta’ala’(Sahih Muslim)

Na akasema tena Hudhayfah Ibn Al Yaman Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi nilisali

pamoja na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika usiku mmoja, alipokua

akisoma aya yenye kutaja Rehma basi alikua akiomba Rehma za Allah Subhanah

wa Ta’ala na alipokua akisoma aya inayotaja Adhabu za Allah Subhanah wa

Ta’ala basi huomba msamaha, anaposoma aya inayoomba ulinzi kutoka kwa

Allah basi nae huomba Ulinzi kwa Allah Subhanah wa Ta’ala na anaposoma Aya

zinazomuelezea Allah Subhanah wa Ta’ala husema Subhaan Allah’(Taadim Qadr

Al Salah)

Ambapo katika hadith nyengine basi amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kua: ‘Wakati Imam anaposema Aamiin basi na nyinyi itikieni Aamiin kwani kila

anaeitikia Aamiin na kisha ikaendana sambamba na Amiin ya Malaika basi mtu

huyo hua ni mwenye kusamehewa Dhambi zake zote zilizopita (Imam Bukhari)’

Tunapoangalia mfano wa wenye kua na unyenyekevu ndani ya Sala basi miongoni mwao

hua ni mfano wa Sahaba wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aitwae Abbad Ibn

Bishr Radhi Allahu Anhu ambae siku moja wakati Jeshi la Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam lilipokua katika bonde la kuelekea katika maeneo ya Najd basi Rasul Allahu

Salallahu Alayhi wa Salam aliamua kupiga kambi katika eneo moja ambalo aliliona kua

linafaa kwa ajili ya kambi hio, na hivyo akawauliza Masahaba jee nani atakua Mlinzi wa

kambi katika usiku wa siku hio.

Ambapo Abbad Ibn Bishr na Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu ambao ni marafiki na

ni ndugu wa Uislam uliotokana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kumkutanisha

Ansar Abbad Ibn Bishr Radhi Allahu Anhu na kumkabidhi Amar Ibn Yasir Radhi Allahu

Anhu ambae alikua ni Muhajjirina alipohamia Madinah basi wao wakaamua kua ndio

wataolinda kambi kwa usiku wa siku hio.

Hivyo Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu akalala katika sehemu ya kwanza ya usiku huo

ili baadae aamke kisha ampishe Abbad Ibn Bishr Radhi Allahu Anhu ili nae alale huku


304

yeye akiendelea na kusimamia ulinzi. Baada ya Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu

kulala basi Abbad Ibn Bishr Radhi Allahu Anhu akatia udhu wake na kisha akaanza kusali

Qiyam Al Layl na baada ya kumaliza kusoma Surat al Fatiha basi akatiririka na Surat Al

Kahf ambayo ina aya 110.

Wakati yuko katikati ya Sura hio huku akiwa amezama kwenye Utamu wa Ladha ya

kisomo chake na Utulivu wa Sala yake wakati akiwa mbele ya Mola wake, basi mara

hapo hapo bila ya kujijua akajikuta kua yuko pia mbele ya ya Adui yake miongoni mwa

maadui wa Uislam ambae alikua amejificha kwenye moja kati ya Majabali ya Bonde hilo

na hivyo Adui huyo akachomoa Upinde wake na kuanza kutunga Shabaha yake kwenye

mwili wa Abbad Ibn Bishar Radhi Allahu Anhu ambae alikua ndani ya Sala yake mbele

ya Mola wake.

Kwa hivyo ghafla Abbad Ibn Bishr Radhi Allahu Anhu akashtukia Mshale wa Upinde

umezama kwenye mwili wake, ambapo kwa hali ya kawaida basi kwa kila Ibn Adam

anaefikwa na tukio kama hili basi lazima awe ni mwenye kuhisi maumivu yake, lakini

hata hivyo Abbad Ibn Bishr Radhi Allahu Anhu hakua ni mwenye kuhisi Maumivu ayo

kutokana na namna alivyozama kwenye ladha ya Utamu wa Ibada yake huku akiendelea

na kisomo chake, na mara akisikia akasikia mshindo wa mshale wa pili ukizama katika

sehemu nyengine ya Mwili wake, na wakati anamalizia Kisomo chake mara akahisi

muingio wa mshale wa tatu kwenye nyama ya mwili wake.

Abbad Ibn Bishr Radhi Allahu Anhu akamalizia kisomo chake kisha akaichomoa Mishale

hio mitatu, kisha akaelekea kwenye rukuu na kisha akanyanyuka na kisha akaelekea

kwenye Sijda aksjudu sijda ya kwanza akakaa kitako na kisha alipoelekea kwenye sijda

ya pili nguvu zikamuishia akaanguka n kumuta rafiki yake Ammar Ibn Yasir Radhi

Allahu Anhu, na kumwambia: ‘Amka uendelee na Ulinzi kwani kwa hakika mimi

nimeshambuliwa na kujeruhiwa.’

Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu akaamka na alipomuona ndugu yake huyo akiwa

katika hali kama hio ya kua ni mwenye kuanguka huku akitokawa na damu tele basi

alishtuka na kumuuliza ndugu yake huyo kwa kusema: ‘Subhana Allah! Kwanini

hukuniamsha mara tu wakati ulipopigwa mshale wa kwanza?’

Abbad Ibn Bishr Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Kwa sababu siku hisi kutokana na kua

nilikua niko katikati ya kisomo cha Surat Al Kahf na utamu wake ukanizidi ndani

ya Moyo wangu kiasi ya kua nilishindwa kukikatisha Kisomo hicho. Na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam pia aliniamrisha kua niihifadhi kwenye Moyo Sura hio,

hivyo kwangu mimi Kifo ni bora kuliko kukikatisha kisomo cha Sura hio’

Kwa upande mwengine basi baada ya kufariki Amir ul Muuminin Abu Baqr As Siddiq

Radhi Allahu Anhu basi Amir Ul Muuminina Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu


305

basi alimuuliza Asma Bint Uways Radhi Allahu Anha ambae ni Mkewe Abu Baqr As

Sadiq Radhi Allahu Anhu kwa kusema: ‘Hivi Jee Abu Baqr alikua akifanya Ibada

katika hali gani anapokua nyumbani?’

Asma Bint Uways Radhi Allahu Anha akajibu: ‘Alikua akitia Udhu katika wakati wa

Sala ya Tahajjud, na kisha huanza kusali, na alipokua akisoma Qur’an ndani yake

basi alikua akilia, na wakati wa Kusjudu alikua akilia, na alipokua akiomba Dua

pia alikua akilia’ baada ya kusikia sifa hizo basi Amir Ul Muuminina Umar Ibn Al

Khattab Radhi Allahu Anhu nae akaanza kulia.

Ambapo kwa upande wa Amir ul Muuminin Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu basi

ilikua kila ukiingia wakati wa Sala alikua akionekana kua ni mtu mwenye khofu na uso

wake hubadilika rangi, na alipoulizwa kwanini hali yake imekua hivyo basi alisema: ‘Wa

Allahi, umefika wakati tuliojiaminisha kuibeba Amana’ na kisha husoma aya

ifuatayo:

﴿ إِ َّعَرَ‏ ضْنَا الأَْمَانَةَ‏ عَلَى ٱلس َّمَاوَا ‏ِت وَٱلأَرْضِ‏ وَٱلجِْبَاِل فَأبَينَْ‏ أَن يحَْمِلْنَهَا

وَأَشْ‏ فَقْ‏ نَ‏ مِنْ‏ هَ‏ ا وَحمََلَهَ‏ ا ٱلإِنْسَا ‏ُن إِن َّهُ‏ كَ‏ انَ‏ ظَلُوماً‏ جَ‏ هُ‏ ولاً‏ ﴾

Inna AAaradhna al-amanata AAala alssamawati waal-ardhi waaljibali faabayna an

yahmilnaha waashfaqna minha wahamalaha al-insanu innahu kana dhaluuman

jahuulan; (Al Ahzab 33:72)

Tafsir: Kwa hakika tuliipa Amana, Mbingu na Ardhi na Milima lakini vikaikataa

kuichukua; kwa sababu ya kuogopa: lakini Mtu akaichukua: Hakika alikua ni

mwenye kujidhulumu na ni mjinga;

Ambapo ili tuifaham vizuri zaidi maana aya hii basi ni vizuri kuanza na aya zilizotangulia

kabla yake ambazo zinasema:

‏﴿َي ُّهَا ال َّذِينَ‏ ءَامَنُواْ‏ ات َّقُواْ‏ اهلل ََّ‏ وَقُولُواْ‏ قَوْلاً‏ سَدِيداً‏ ‏۞يُ‏ صْلِ‏ حْلَكُ‏ مْ‏ أَعْمَلَكُ‏ مْ‏ ‏َويَغْفِْر

لَكُمْ‏ ذُنُوبَكُمْ‏ وَمَن يُطِعِ‏ اهلل ََّ‏ وَرَسُولَهُ‏ فَقَدْ‏ فَازَ‏ فَوْزاً‏ عَظِيماً۞‏ إِ َّ عَرَضْنَا الأَْمَانَةَ‏

عَلَى ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَٱلجِْبَاِل فَأبَينَْ‏ أَن يحَْمِلْنَهَا وَأَشْفَقْنَ‏ مِنْهَا وَحمََلَهَا

ٱلإِنْسَانُ‏

إِن َّهُ‏ كَانَ‏ ظَلُوماً‏ جَ‏ هُولاً‏ ﴾


306

Ya ayyuha alladhina amanoo ittaqoo Allaha waqooloo qawlan sadeedan, Yuslih

lakum aAAmalakum wayaghfir lakum dhunoobakum waman yutiAAi Allaha

warasoolahu faqad faza fawzan AAadhiman; Inna AAaradhna al-amanata AAala

alssamawati waal-ardhi waaljibali faabayna an yahmilnaha waashfaqna minha

wahamalaha al-insanu innahu kana dhaluuman jahuulan. (Al Ahzab 33:70-71)

Tafsir: Enyi Mlioamini! mcheni na muogopeni Allah, na (daima) semeni kauli za

ukweli ulionyooka, atakuongozeni kufanya mema na kukusameheni dhambi zenu. Na

kwa hakika yeyote yule ambae anaemtii Allah na Mtume wake (Salallahu A’layhi wa

Salam) basi atakua ni miongoni mwa waliofuzu. Kwa hakika tuliipa Amana, Mbingu

na Ardhi na Milima lakini vikaikataa kuichukua; kwa sababu ya kuogopa: lakini Mtu

akaichukua: Hakika alikua ni mwenye kujidhulumu na ni mjinga.

Ambapo kutokana na aya hizi basi tunaona kua ingawa wengi wetu miongoni mwa

wasiojua hua ni wenye kuona kua kipimo cha Mafaniko ya Mtu hapa Duniani kua ni kua

mwenye kumiliki Mali au Mamlaka, lakini hata hivyo ukweli ni kua hicho sio kipimo

sahihi kwani hiki kilichotajwa hapa kwenye aya hii yaani cha Kua na Taqwa na

kumogopa Allah Subhanah wa Ta’ala ndio kipimo pekee kinachoonesha Mafanikio ya

Mtu, na sio hapa Duniani tu bali pia na Akhera.

Na ndio maana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawa ni mwenye kupendelea

sana katika Khutba zake Kuanza na aya nne za Taqwa ambapo ndani yake mna aya za

70-71 za Surat Al Ahzab kwa mpangilio ufuatao:

‏﴿َي ُّهَا ال َّذِينَ‏ ءَامَنُواْ‏

ات َّقُواْ‏ اهلل ََّ‏ حَق َّ تُقَاتِهِ‏ وَلاَ‏ تمَُوتُن َّ إِلا َّ وَأَنتُم م ُّسْلِمُو ‏َن ﴾

Ya ayyuha alladhina amanoo ittaqoo Allaha haqqa tuqatihi wala tamootunna illa

waantum muslimoona (Surat Al Imran 3:102)

Tafsir: Enyi mlioamini! Muogopeni Allah (kwa kutekeleza maamrisho yake na

kuachana na makatazo yake) kama anavyostahiki kuogopewa. [Mtiini, mshukuruni

na daima mkumbukeni], na msife isipokua mkiwa katika hali ya kua ni Waislam.

Ambapo tunapoziangalia aya hizi zinazozungumzia kuhusiana na umuhimu wa Taqwa

basi tunaona kua Allah Subhana wa Ta’ala amesema ndani yake kwa kuanza na Ya

Ayyuha Alladhina Amanoo yaani Enyi Mlioamini kisha akasema kwa kumalizia pamoja

nayo Ittaqoo Allaha yaani Muogopeni Allah na katika aya nyengine ya Surat An Nisaa

4:1 ambayo ni miongoni mwao aya 4 hizo basi amesema Ya Ayyuha Al Nassu yaani

Enyi Watu kisha akasema kwa kumalizia pamoja nayo Ittaqoo Rabbakumu yaani

Muogopeni Mungu wenu. Kama tutakavyoona katika kufafanua hapo mbele.


307

Ambapo anasema Imam Abu Muhamamd Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘‘Ittaqoo

Rabbakumu’ yaani ‘Muogopeni Mungu’ wenu wanaambiwa wale ambao ni wenye

Kutaka kuchuma Malipo kwani wao hua ni wenye kutafuta Neema na Rehma na

hivyo watu hawa hua wanatafuta kitu kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala’

‘Na ‘Ya Ayyuha Alladhina Amanoo Ittaqoo Allaha yaani Enyi Mlioamini Allah’ hua

wanaambiwa wale ambao ni wenye Kumjua Allah Subhanah wa Ta’ala kwani wao

hua ni wenye kutaka kuipata Siri ya Allah Subahanh wa Ta’ala na hivyo wao hua

ni wenye kutafuta njia ya Kumpata mwenyewe Allah Subhanah wa Ta’ala’

Hivyo kua na Taqwa hua kuko katika hali tatu. Ambapo kwanza hua ni katika

Kuuogopa Moto wa Allah Subhanah wa Ta’ala ambao umetayarishwa kwa ajili ya

Makafiri na hivyo kwa Walioamini hua ni wenye kuepukana nao kwa kua na Subra

na kujizuia kutokana na Maovu na kumtii Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume

wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo hua ni wenye kuingizwa

kwenye za Allah Subhanah wa Ta’ala na kupata Ridhaa ya Mola wao kama

zinavyosema Aya:

‏﴿وَٱت َّقُواْ‏ ٱلن َّارَ‏ ٱل َّتيِ‏ ۤ أُعِد َّتْ‏ لِلْكَافِرِينَ۞وَأَطِيعُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَٱلر َّسُولَ‏ لَعَ‏ ل َّكُمْ‏

تُرْحمَُونَ۞وَسَارِعُو ۤ اْ‏ إِلىَٰ‏ مَغْفِرَةٍ‏ مِّنْ‏ ر َّبِّكُمْ‏ وَجَن َّةٍ‏ عَرْضُهَا ٱلس َّمَاوَاتُ‏ وَٱلأَرْضُ‏ أُعِد َّتْ‏

لِلْمُت َّقِينَ‏ ﴾

Waittaqoo alnnara allatee oAAiddat lilkafireena; WaateeAAoo Allaha

waalrrasoola laAAallakum turhamoona; WasariAAoo ila maghfiratin min

rabbikum wajannatin AAardhuha alssamawatu waal-ardhu oAAiddat

lilmuttaqeena(Surat Al Imran 3:131)

Tafsir: ‘Na uogopeni Moto ambao umetayarishwa kwa ajili ya Makifiri. Na mtiini

Allah na Mtume wake ili mpate kuingizwa kwenye Rehma; Na kimbilieni katika

Usamehevu wa Mola wenu na kwa ajili ya Pepo ambayo upana wake ni kama ilivyo

Mbingu na Ardhi ambayo imetayarishwa kwa ajili ya wenye Taqwa’

Pili hua ni katika Kumcha Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo Mja hua ni mwenye

kuonesha Shukran kwa Neema na Rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala juu yake.

Na Tatu hua ni katika kumcha Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kutomshirikisha,

bila ya kutegemea Malipo kutoka kwake.


308

Ambapo hali ya Kwanza ya Kumcha Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni hali ya Watu

waliokua ni wa Chini miongoni mwa waja wake, hali ya Pili hua ni hali ya waliokua

Kati na kati na hali ya Tatu hua ni ya waliokua Juu yaani Waliotangulia na hawa

wenye hali ya Tatu ndio wale waliotajwa kwenye aya ifuatayo:

‏﴿وَلْتَكُنْ‏ مِّنْكُمْ‏ أُم َّةٌ‏ يَدْ‏ عُونَ‏ إِلىَ‏ ٱلخَْيرِْ‏ وَ‏ ‏َْمُرُونَ‏ بِٱلْمَعْرُوفِ‏ وَيَنْهَوْنَ‏ عَنِ‏ ٱلْمُنْكَرِ‏

وَأُوْ‏ لَٰئِكَ‏ هُمُ‏ ٱلْمُفْ‏ لِحُونَ‏ ﴾

Waltakun minkum ommatun yadAAoona ila alkhayri waya/muroona

bialmaAAroofi wayanhawna AAani almunkari waola-ika humu almuflihoona

(Surat Al Imran 3:104)

Tafsir: Na kuweni miongoni mwenu na kundi la Watu ambao watakua ni wenye

kuwaita watu kwenye Kheri kwa Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya, na hawa

ndio wale watakaokua wamefuzu.

Kwani Hawa ni watu ambao wanasimama kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala

tu. Hawa hua hawarudi nyuma wala hawazuiliki kutokana na kusimamia na

kuamrisha maamrisho ya Mola wao na kuyakataza makatazo yake na hua

hawamtegemei yeyote katika jambo lolote, kwani hua ni wenye kuona kasoro zao

na udhaifu wa Nafsi zao na hivyo wanatumia uhai wa Maisha yao kwa ajili ya

kutafuta Ridhaa ya Mola wao.

Na hivyo hua Wanafanya Matendo yao kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala,

wanausia juu ya Dini ya Allah Subhanah wa Ta’ala na ni wenye kuwaita Viumbe

warudi kwa Allah Subhanah wa Ta’ala, hivyo biashara yao imewanufaisha na

hawajutii juu ya makubaliano yao na Mola wao.

Hawa hua ni wale watu ambao hua wamesimama kwenye Yakini na hivyo wamekua

huru kutokana na Hiari zao na Uwezo wao na wameachana na Matamanio ya Nafsi

zao, wanamjua Allah Subhanah wa Ta’ala na wanamtegemea na kumuomba na

kujitahidi kwa ajili ya Mola wao tu.

Wao hua kamwe hawafikirii kuhusiana na Mitizamo ya watu juu yao, kwani

kwenye Nyoyo zao wana urafiki na Mola wao, kwenye Macho yao wanaona Ufunuo

wa Nafsi zao na hivyo hua ni wenye kukiona kila kitu kama kilivyo katika Maumbile

ya uhakika wake. Kwani wakati wengine hua wanaangalia Maumbile kwa mtizamo

wa Viumbe basi wao hua wanaangalia Maumbile kwa Mtizamo wa alieumba. Hawa

ndio waliochaguliwa na Allah Subhanah wa Ta’ala na kuainishwa kwa alama ya

Ufalme wake.


309

Ingawa kwa kimaumbile Mja hua anatamani kitu chengine na Muumba hua

anataka kitu chengine, lakini hapo hapo wote kwa pamoja hua wanataka kitu

kimoja na hii ni kutokana na makubaliano yao baina yao. Na hii ndio maana ya ile

kauli isemayo kua: ‘Pale Mja anapojali kuhusiana na anayoyajali Mola wake basi

Allah Subhanah wa Ta’ala humuondolea khofu kuhusu Dunia na Akhera yake’

Hivyo Umoja hua ni kumuangalia yule alie Mmoja tu na kujua kua yeye ni Mmoja

tu pekee, na hivyo kila kitu hua kinatoka katika sehemu Moja ambayo ni ya

kutokana nae na Makadirio yote hua ni kutokana nae.

Ama kuhusiana na Kutofautiana na Shariah, basi hua kuna aina mbili. Ambapo

aina ya kwanza hua ni katika Kanuni za Sharia na aina ya pili hua katika Matawi

ya Sharia.

Ambapo kutofautiana kuhusiana na Kanuni basi hua ni kubaya sana na ni hatari

sana, na hii ni kwa sababu hapa hua kuna hali ya pande mbili tu, kuna hali ya

upande ulio Sahih na hali ya upande usiokua Sahih na ndio maana Allah Subhanah

wa Ta’ala akabainisha njia ya upande uliokua Sahih na kusema:

‏﴿وَأَن َّ هَٰذَا صِرَاطِى مُسْتَقِيماً‏ فَٱت َّبِعُوهُ‏ وَلاَ‏ تَت َّبِعُواْ‏ ٱلس ُّبُلَ‏ فَتَفَر َّقَ‏ بِكُمْ‏ عَ‏ ن سَبِي لِهِ‏

ذٰلِكُمْ‏ وَص َّاكُمْ‏ بِهِ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تَت َّقُونَ‏ ﴾

Waana Hadha siratee mustaqeeman faittabiAAoohu wala tattabiAAoo alssubula

fatafarraqa bikum AAan sabeelihi dhalikum wassakum bihi laAAallakum

tattaqoona (Surat Al Anaam 6:153)

Tafsir: Na hii ndio njia yangu iliyonyooka hivyo ifuateni na wala msifuate njia

nyengine kwani zitakupotosheni kutokana na njia yake, na hivyo ndivyo anavyo

kuamrisheni ili mpate kua wacha Mungu.

Ama kuhusiana na hali ya pili ya kutofautiana kwenye Matawi ya Sharia basi hua

ni sawa na kua na makundi mawili tofauti ambayo hua ni yenye kuelekea Safari

moja yenye lengo moja lakini kila mmoja akachukua njia yake na kuifuata, hivyo

ingawa watu hawa hua ni wenye kufuata njia tofauti lakini mwisho wake hua ni

wenye kukutana kwenye lengo moja kuu la safari yao, hivyo kutofautiana huku hua

kuna Rehma pia ndani yake, na hii ndio maana ya yale maneno yasemayo kwenye

aya ifuatayo:


310

‏﴿وَجَاهِدُوا فىِ‏ ٱهلل َِّ‏ حَق َّ جِ‏ هَادِهِ‏ هُوَ‏ ٱجْتَبَاكُمْ‏ وَمَا جَعَلَ‏ عَلَيْكمْ‏ فىِ‏ ٱلدِّينِ‏ مِنْ‏

حَرَجٍ‏ ﴾

Wajahidoo fee Allahi haqqa jihadihi huwa ijtabakum wama jaAAala AAalaykum

fee alddeeni min harajin (Surat Al Hajj 22:78)

Tafsir: Na jitahidi kupigania kwa ajili ya Allah kwa haki kama inavyostahiki kupigania

kwani amekuchagueni na hakukujaaleni katika Dini kua na ugumu.

Na pia pale aliposema:

‏﴿يُرِيدُ‏ ٱهلل َُّ‏ بِكُمُ‏ ٱلْيُسْرَ‏ وَلاَ‏ يُرِيدُ‏ بِكُمُ‏ ٱلْعُسْرَ‏ ﴾

Yureedu Allahu bikumu alyusra wala yureedu bikumu alAAusra (Surat Al Baqra

2:185)

Tafsir: Allah anakutakieni urahisi na hataki kukufanyeni Ugumu.

Kisha Rasu Allah Salallahu Alayhi wa Salam hufuatia kwa aya ifuatayo:

‏﴿يَأَي ُّهَا الن َّاسُ‏ ات َّقُواْ‏ رَب َّكُمُ‏ ال َّذِى خَلَقَكُمْ‏ مِنْ‏ ن َّفْسٍ‏ وَحِ‏ دَةٍ‏ وَخَلَقَ‏ مِنْهَا ‏َزوْجَهَا

وَبَث َّ مِنْهُمَا رِجَالاً‏ كَثِيراً‏ وَنِسَآءً‏ وَات َّقُواْ‏ اهلل ََّ‏ ال َّذِى تَسَآءَلُونَ‏ بِهِ‏ وَالأَْرْحَامَ‏ إِن َّ اهلل ََّ‏

﴾ كَا نَعَلَيْ‏ ي ب كُمْرَقِ‏ اً‏

Ya ayyuha alnnasu ittaqoo rabbakumu alladhi khalaqakum min Nafsin wahidatin

wakhalaqa minha zawjaha wabaththa minhuma rijalan kathiran wanisaan

waittaqoo Allaha alladhii tasaaloona bihi waal-arhama inna Allaha kana

AAalaykum raqeeban (Surat An Nisaa 4:1)

Tafsiri: Enyi Watu! Mcheni Mola wenu aliekuumbeni kutokana na Nafsi moja

(Adam), na kutokana nae (Adam) akamuumba mke wake (Hawwa), na kutokana nao

(Adam na Hawa) akawaumba Wanaume na Wanawake wengi na muogopeni Allah


311

ambae ana haki juu yenu, na msivunje udugu, kwani kwa Hakika Allah ni mwenye

uangalifu mkubwa juu yenu.

Hivyo: ‘‘Ittaqoo Rabbakumu’ yaani ‘Muogopeni Mola wenu’ wanaambiwa wale watu

wa kawaida ambao Ucha Mungu wao hua unatokana na kua ni wenye kuziona

Neema na Rehma za Allah Subhanah w a Ta’ala na msukumo wao hutokana na

kutumia Neema na Rehma hizo kwa Miili yao kwa ajili ya kumtumkia Mola wao’

‘Na ‘Ya Ayyuha Alladhina Amanoo Ittaqoo Allaha yaani Enyi Mlioamini Muogopeni

Allah’ hua wanaambiwa wale ambao ni wenye Kumjua na kumjali Allah Subhanah

wa Ta’ala na hivyo Ucha Mungu wa hua unatokana na kua ni wenye Kumuangalia

Allah Subhanah wa Ta’ala na malengo yao hua ni kupatikana kwa utulivu ndani ya

Nyoyo zao kutokana na Kumshuhudia Mola wao’

Ambapo amrisho hili la kumuogopa Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni kwa ajili ya

Waja kulifanya kua ndio ngao yao ya kujizuia wasifikiwe na Makatazo ya Mola

wao. Ambao kwanza hua ni mwenye kutafuta Ulinzi katika kifungo cha Tawhid na

kuepukana na Shirk.

Pili hua ni kutafuta Ulinzi katika Utiifu na kukaa mbali na njia ya Uasi.

Tatu hua ni kutafuta Ulinzi kwa Tahadhari na kuyakimbia yenye kua na shaka

ndani yake.

Hivyo yeyote yule atakaepanda Ngazi hizi za Kumcha Allah Subhanah wa Ta’ala

basi ataufikia Uokovu, na asiepanda Ngazi hizo basi atakua amekula hasara kama

zinavyofafanua aya pale ziliposema:

‏﴿وَيُنَجِّ‏ ى ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِينَ‏ ٱت َّقَوْاْ‏ بمَِفَازَهتِِمْ‏ لاَ‏ يمََس ُّهُمُ‏ ۤ ٱلس ُّو ءُ‏ وَلاَ‏ هُمْ‏ يحَْزَنُونَ۞ٱ هلل ََُّخا لِ‏ قُ‏

ِ كُل شَيْءٍ‏ وَهُوَ‏ ٰ عَلَى كُل وَكِيلٌ۞ل َّهُ‏ مَقَالِيدُ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَٱل َّ ذِيَن

ّ شَيْءٍ‏

ِ

كَ‏ فَرُواْ‏ بِآَ‏ تِ‏ ٱهلل َِّ‏ أُوْ‏ لَٰئِكَ‏ هُ‏ مُ‏ ٱلخَْاسِ‏ رُونَ‏ ﴾

ّ

Wayunajjee Allahu alladheena ittaqaw bimafazatihim la yamassuhumu alssoo-o

wala hum yahzanoona; Allahu khaliqu kulli shay-in wahuwa AAala kulli shay-in

wakeelun; Lahu maqaleedu alssamawati waal-ardhi waalladheena kafaroo bi-ayati

Allahi ola-ika humu alkhasiroona. (Surat Az Zumar 39:61-63)


312

Tafsir: Na atawaokoa Allah wale ambao wenye Taqwa kwenye sehemu zao za

waliofuzu, na hawatoguswa na Ovu na wala hawatokua na Huzuni. Allah ndio

Muumba wa kila kitu na yeye ndie Msimamizi wa kila kitu. Kwake yeye ndiko kwenye

funguo za Mbingu na Ardhi na wale waliozikufuru aya za Allah wao ndio watakaokula

hasara.

Na pia pale ziliposema tena aya katika Surat At Talaq:

‏﴿وَمَن يَت َّقِ‏ ٱهلل ََّ‏ يجَْعَل ل َّهُ‏ مخَْرَجاً۞وَيَرْزُقْهُ‏ مِنْ‏ حَيْثُ‏ لاَ‏ يحَْتَسِ‏ بُ‏ وَ‏ مَن يَتَوَك َّلْ‏ عَلَى

ّ لِكُل شَيْءٍ‏ قَدْراً‏ ﴾

ٱهلل َِّ‏ فَهُوَ‏ حَسْبُهُ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ ابَلِغُ‏ أَمْرِهِ‏ قَدْ‏ جَعَلَ‏ ٱهلل َُّ‏ ِ

Waman yattaqi Allaha yajAAal lahu makhrajan; Wayarzuqhu min haythu la

yahtasibu waman yatawakkal AAala Allahi fahuwa hasbuhu inna Allaha balighu

amrihi qad jaAAala Allahu likulli shay-in qadran (Surat At Talaq 65:2-3)

Tafsir: Na atakae Muogopa na kutekeleza Majukumu ya Allah juu yake basi (Allah

Subhanah wa Ta’ala) atamjaalia njia ya kutoka katika kila tatizo. Na atamruzuku

kupitia katika njia ambazo hatozitegemea, na atakaemtegemea Allah (Subhanah wa

Ta’ala) basi atamtosheleza, hakika Allah atamfanikishia Jambo lake. Kwani kwa

hakika Allah amejaalia makadirio juu ya kila kitu.

Kwani baada ya aya hio ya Surat An Nisaa 4:1 basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam ndio hua anamalizia na aya ya Tatu ya Taqwa ambayo hua ni iliyobeba Qawlan

Sadida yaani Kauli Iliyonyooka ambayo inasema.

‏﴿َي ُّهَا ال َّذِينَ‏ ءَامَنُواْ‏ ات َّقُواْ‏ اهلل ََّ‏ وَقُولُواْ‏ قَوْلاً‏ سَدِيداً‏ ‏۞يُ‏ صْلِ‏ حْلَكُ‏ مْ‏ أَعْمَلَكُ‏ مْ‏ وَيَغْفِ‏ ‏ْر

لَكُمْ‏ ذُنُوبَكُمْ‏ وَمَن يُطِعِ‏ اهلل ََّ‏ وَرَسُولَهُ‏

فَقَدْ‏ فَازَ‏ فَوْزاً‏ عَظِيماً‏ ﴾

Ya ayyuha alladhina amanoo ittaqoo Allaha waqooloo qawlan sadeedan, Yuslih

lakum aAAmalakum wayaghfir lakum dhunoobakum waman yutiAAi Allaha

warasoolahu faqad faza fawzan AAadhiman (Al Ahzab 33:70-71)

Tafsir: Enyi Mlioamini! mcheni na muogopeni Allah, na (daima) semeni kauli za

ukweli ulionyooka, atakuongozeni kufanya mema na kukusameheni dhambi zenu. Na


313

kwa hakika yeyote yule ambae anaemtii Allah na Mtume wake (Salallahu A’layhi wa

Salam) basi atakua ni miongoni mwa waliofuzu kwa darja kubwa sana.

Ambapo tunapoziangalia Aya zote hizi na mpangilio wake basi tunaona kua

zinazungumzia kuhusiana na kutilia mkazo Taqwa na hivyo ndani yake zimetaja neno

Taqwa mara 4.

Ambapo aya hii inatubainishia kua Kufuzu kwa Walioamini hapa Duniani na Akhera

hakupimwi kulingana na Mamlaka uliyokua nayo, Pesa ulizokua nazo, Mali ulizokua

Nazo, Uzuri uliokua Nao, Nguvu ulizokua nazo, Umaarufu uliokua nao n.k kwani

ukipimwa kulingana na vipimo hivyo basi utakua Dhaluman Jahulan katika Kipimo cha

Kufuzu kwako na hivyo ili usiwe Dhaluman Jahulan basi hua Kipimo kinachotumika

hua ni kutokana na Taqwa yako Mbele ya Mola wako.

Hivyo hii ni Aya ambayo Imefunika Kila Kitu katika aya hizi 4 ambazo hua zinajulikana

kama Aya za Taqwa kwani zimezungumzia kuhusiana na Taqwa ndani yake mara 4.

Ambapo kwa upande wa Hujjat ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad

Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii basi yeye anasema kua:

‘Qur'an ina Aya 741 ambazo zina Sifa Ya Kua ni Lulu za Qur'an kwani ni Aya

zinazomuonesha Ibn Adam Njia Sahih ya Kuifuata katika Maisha yake

Na pia Qur'an ina aya 763 ambazo zina sifa ya Kua ni Mataji ya Hazina za Qur'an

kwani hua zinazungumzia kuhusiana na Sifa za Allah Subhanah wa Ta'ala.’

Na miongoni mwa Lulu 741 za Qur'an basi 4 kati yao ni aya hizi za Taqwa ambazo pia

hua ni aya za Tawhid

Ambapo anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Qawlan

Sadida hua ni maneno ya Tawhid ambayo ndio msingi wa Dini ya Kiislam na Ndio

Nguzo kubwa ya Kujisalimisha na kuingia ndani yake. Mwanzo wa Ilm za Dini yote

ni Tawhid. Msingi wa kujua kila kitu ni Tawhid. Ukuta baina ya Imani na Kufr ni

Tawhid, Tofauti baina ya Rafiki na Adui ni Tawhid, Kidhibiti cha baina ya Mbingu

7 na Ardhi 7 ni kupitia katika Tawhid. Nuru ya Viumbe vya Ulimwengu wa Dhahir

na Ulimwengu wa Al Ghayb ni Tawhid na hali ya Maumbile ya Ulimwengu mzima

wa Al Dhadhir na wa Al Ghayb unatokana na Nuru ya Tawhid. Na Lulu ya Mwanzo

ya Irfan ni Tawhid na mwanzo wa Kujua baada ya Kuitafuta Hakika ni Tawhid’

‘Hivyo unapoiweka Tawhid katika sehemu yake basi mtazamo wako hua ni wenye

kuchukua na kupata Muonekano wa Uongufu, Ulimi wako huanza kua ni Hazina

ya Hikma na Busara, Usikivu wako hua ni Chaza yenye Lulu ya Amanah na


314

Uaminifu. Moyo wako hua ni sehemu kuu ya Kutafakkar na Kuzingatia na Nafsi

yako hua ni sehemu ambayo Matamanio huweka Soji lake tayari kwa ajili ya

kupandwa na kudhibitiwa.’

‘Tawhid hua ni nauli ya kuingia Peponi na Tawhid hua ni yenye kutosheleza kua ni

Ibada, kwani Tawhid hua ni Bei ya kuingia Peponi na inatosheleza kila kila kitu

katika matendo yote ya Ibada. Tawhid hua si kumpwekesha Allah Subhanah wa

Ta’ala peke yake bali Tawhid hua ni kujihesabu kua wewe uwe ni mmoja tu ambae

ni kwa ajili yake Allah Subhanah wa Ta’ala’

Anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Wakati Allah

Subhanah wa Ta’ala anapompa mtu mafanikio katika kuweza kufanya mema basi,

hii hua ni Dalili kua Mtu huyo kua ni mwenye kusamehewa na Allah Subhanah wa

Ta’ala’

Hivyo hali ya kua na Taqwa hua inaenda sambamba na kua na Uwezo wa kusimamia

jukumu la Amanah na hivyo pia kua na mafanikio. Neno Amanah linatokana na mzizi wa

herufi za kiarabu Alif-Mim-Nun, ambalo maana yake ni kua katika hali ya amani,

usalama, ulinzi, uaminifu na kua na imani na kitu. Usalama na amani wa sehemu fulani

huweza hupatikana kutokana na ulinzi na uaminifu wa yule anaeyatawala mazingira

hayo. Hivyo tunapozungumzia maana ya Amanah Kiislamu basi hua tunazungumzia kitu

kinachotegemeana na Khalifah anaetawala Ulimwenguni ambae ni Bani Adam.

Tukiangalia kwa undani zaid basi tunaona kua neno Amanah limetumika katika Qur’an

kutoa maana yenye kina kirefu zaidi. Kwani inaelezea kuhusiana na haki ya Bani Adam

na majukumu yake dhidi ya Bani Adam wenzake, mazingira yake na pia viumbe vyengine

vyote vilivyoumba na Allah Subhanahu wa Ta’ala. Kila kitu alichojaaliwa kupewa au

kuamrishwa kiumbe Bani Adam afanye, hata kama ikiwa ni kwa manufaa yake, basi hua

ni Amanah na hivyo huhitajiwa kuchungwa na kutumiwa kulingana na Sharia’h za yule

aliempa Amanah hiyo ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala. Kwani ni wajib unapopewa

Amanah aidha kuirudisha kama ilivyokua, kwa aliekupa ama kuitumia kulingana na

matakwa au muongozo wa aliekupa Amanah hiyo.

Ambapo amesema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kuuliwa katika njia ya Allah Subhanah wa

Ta’ala hua ni kwenye kufuta Dhambi zote isipokua dhambi za Amanah, kwani mtu

mwenye kupewa Amana na kisha akawa hakujiaminisha, basi ataletwa katika siku

ya Malipo, na kuambiwa ikabidhishe amana kama ulivyopewa.

Nae atasema: ‘Ya Rabb Dunia haipo tena’ ataambiwa: ‘Ikabidhishe Amanah’ nae

atasema tena: ‘Ya Rabbi Dunia haipo tena (nitaikabidhisha vipi mie?)’ hapo

wataambiwa Malaika: ‘Muingizeni katika Hawwiyah (Moto Mkali sana)!’ hivyo


315

Mtu huyo atachukuliwa na kutupwa kwenye Moto wa Jahannam. Kisha atazama

hadi chini ya kina cha chini cha mwisho kabisa cha Moto huo.

Na chini yake huko ndani ya Hawwiyah ataikuta Amana yake hio, na kisha ataibeba

na kuiweka juu ya mabega yake. Na kuja nayo juu hadi kwenye kingo za Moto huo

na kutaka kutoka nayo, lakini atateleza na itamponyoka na kutumbukia tena hadi

chini ya kina cha Moto huo, na tukio hili litakua ni lenye kujirudia Milele.’

Ambapo kuhusiana na mtizamo wa Fiqh juu ya Amanah tunazopeana Ibn Adam basi

Wanazuoni wametofautiana kuhusiana nazo pale inapokua mtu aliekabidhiwa Amanah

husika ikawa imempotea mbali ya kua alikua akisimamia ipasavyo, kwani kwa upande

wa Wanazuoni wa Madhhab ya Imam Al Shafii basi wanasema kua itabidi Mtu huyo

aliekabidhiwa aitafute nyengine kisha aikabidhi kwa aliemkabidhi au alipe fidya

kulingana na matakwa ya mwenye Amanah, ambapo kwa Upande wa Madhhab ya Imam

Abu Hanifa basi wao wanasema kua haina haja kukabidhi nyengine wakati ile ikiwa

imepotea kwa bahati mbaya.

Na amesema Zayd Ibn Wahab kua : ‘Hudhayfah alituambia sisi kua: ‘Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alituambia sisi kuhusiana na mambo mawili ambapo

mimi nimeliona moja likiwa tayari limeshatokea, huku nikiwa nasubiri na la pili

litokee’

Kwani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisema: ‘Amanah (Uaminifu)

imeshushwa ndani ya mizizi ya Nyoyo za Watu. Na kisha watu hao wakajifunza

Qur’an na wakajifunza Sunnah’ na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akatuambia kuhusiana na namna itakavyo ondolewa Amanah kwa kusema: ‘Mtu

atakua ni mwenye kusinzia na Uaminifu wake utaondolewa kutoka kwenye Moyo

wake na hivyo athari yake itakua kama kovu ndogo yenye rangi ya kiza kiza na

kisha atasinzia tena na itaondolewa tena na athari yake kua kama suguru gumu

linaouathiri mkono wa mtu kutokana na kufanya kazi ngumu za sulubu. Au kama

cheche ya Moto ambao hua mnaizima kwa kuipiga piga na kuikanyaga kwa miguu.

Na hivyo mtamuona mtu huyo kua ni mfano wa kuigwa, ingawa hakuna kitu chenye

thamani ndani yake mtu huyo, na kisha watu watakua wanahudumiana lakini

hakuna hata mmoja mwenye kujali kua na uaminifu kiasi ya kua watu watakua

wanasema kuhusiana na atakaekua na Uaminifu kua: ‘Kuna mtu miongoni mwa

watu fulani ambae ni Muaminifu’ na itasemwa kuhusiana na mtu kua: ‘Ni Mtu

Hodari sana, Ni Mtu Mwenye akili sana, ni Mtu mzuri sana.’ Lakini Mtu huyo

hatokua na Iman ndani ya Moyo wake hata Chembe.’

Kwani pia mara kadhaa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amekua akisema katika

Khutba zake kua: ‘Hakuna Imani kwa mtu ambae si Muaminifu Kiamana na hakuna

Dini kwa yule ambae asietimiza Ahadi.’


316

Kutokana na aya ya 72 ya Surat Al Ahzab tunaona kua Allah Subhanahu wa Ta’ala

aliikabidhi Amanah kwa viumbe vyengine ikiwemo Mbingu, Milima na Ardhi lakini

viumbe hivyo vikaikataa Amanah hiyo kutokana na uzito wake na hivyo kuogopa kua

baadae vitashindwa kuitekeleza.

Anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na kukataa Mbingu,

Ardhi na Milima juu ya amanah hio kua: ‘Kukataa kwao huko hakui sawa na kukataa

kwa Ibilis, kwa sababu kukataa kwa Ibilisi kulikua ni kukataa kutii amri, lakini

kukataa Kulikotajwa hapa kunatokana na khiyari kwani vitu hivi viliulizwa

kwanza kabla ya kutakiwa kubeba Amanah, Na pili kukata kwa Ibilisi unatokana

na Kiburi lakini kukataa kwa vtu hivi kunatokana na Unyeneyekevu.’

Lakini hata hivyo Amanah hiyo alipopewa Bani Adam, yeye akaipokea kwa mikono

miwili. Hivyo kulingana na Mtizamo huu wa Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu

Anhu basi tunaona kua Amanah inayozungumziwa hapa si nyegine isipokua ni Sala.

Lakini kwa upande wa Ubay Ibn Qaab Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua: ‘Kila

kitu ulichojaliwa na Mola wao ni Amanah hata Uchi wa Mwanamke kwake yeye

Mwanamke hua ni Amanah.’

Na kwa upande wa Abd Allah Ibn Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu basi yeye amesema

kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala alipomuumba Mwanamme basi alimwambia

kuhusiana na Uchi wake kua ni Amanah na hivyo asiutumie isipokua kwa njia za

Halali.’

Na Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua: ‘Amanah

iliyokusudiwa hapa hua ni Mali na kila kitu ambacho ulichoneemeshwa na Allah

Subhanah wa Ta’ala hua ni Amanah na ulichoamrishwa Kiislam pia.’

Ambapo kwa upande wa Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, Imam

Qatadah Al Sadusi na Imam Said Ibn Jubayr basi wao wanasema kua: ‘Amanah

iliyokusudiwa hapa hua ni majukumu ya Maamrisho ya Allah Subhanah wa Ta’ala

juu yetu na Makatazo yaliyomo ndani ya mipaka aliyoiweka ndani yake.’

Ambapo tukimuangalia Imam Abu AMuhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi

yeye anasema kua: ‘Amanah hua ni utiifu juu ya Allah Subhanah wa Ta’ala katika

kutekeleza Maamrisho yake ya Fardhi aliyoyaamrisha kupita katika njia ya Dini

yake.’

Na Kwa Upande wa Imam Abu Qasim Al Qushayri basi yeye anasema kua: ‘Amanah

hua ni kusimamia na kutumiza kile ambacho ni wajib kulingana na kanuni za Fiqh,


317

na pia hua tunaweza kusema kua ni Imani ya Kumpwekesha Allah Subhanah wa

Ta’ala na kujilinda kwa ajili ya kutovuka nje ya mipaka yake aliyoiweka ndani ya

maamrisho yake’

Swali la kujiuliza ni kua Jee ilikuaje Bani Adam akaikubalia Amanah ambayo viumbe

vyengine waliikataa?

Tukiangalia Tafsir ya Imam Ibn Kathir basi tunaona inasema kua, Wakati Allah

Subhanahu wa Ta’ala alipovipa Amanah viumbe vyake yaani Mbingu, kisha Ardhi

na kisha Milima ilikua si katika hali ya kuvilazimisha viumbe hivyo kubeba jukuma

la Amanah hiyo, bali ilikua ni katika hali ya hiari na hivyo alivipa pia uamuzi wa

kuchagua, kwani hali hiyo ulikua katika hali ya kuulizwa: ‘Jee mtakua tayari

kuyatekeleza masharti ya Amanah hii kutoka kwetu ili mpate malipo yake?’, viumbe

vyote hivyo vikauliza: ‘Malipo gani hayo?’, na wakaambiwa : ‘Ikiwa mtaweza

kutekeleza masharti ya Amanah hii, kutokana na juhudi zenu zote, mtaliwa malipo

bora, hususan kupata ukaribu zaid mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala, lakini

ikiwa hamtoweza kutekeleza masharti yake, basi mtapata adhabu kali sana.’

Hivyo baada ya kusikia masharti ya amana hiyo viumbe vyote hivyo vikubwa vikajibu

kwa kusema: ‘Mola wetu, hata sasa hivi sisi tuko chini ya amri yako, lakini sasa hivi

(kutokana na kupewa uamuzi wa kuchagua) tunajisikia kua tuko dhaifu sana

kuubeba mzigo huo mzito na hatutoweza kutekeleza masharti yake, ama kuhusiana

na malipo sisi hatuyataki, na kuhusiana na adhabu hatuwezi kuistahmilia.’

Tukiangalia kwa upande wa Tafsir ya Imam Al Qurtubi, tunaona kua, baada ya viumbe

vitatu hivyo yaani Mbingu, Ardhi na Milima kupewa Amanah hiyo na kuikataa, basi

Allah Subhanah wa Ta’ala akamuambia kiumbe Insan au mtu: ‘Tumeipa Amanah yetu

kwa Mbigu, Ardhi na Milima lakini ikaweka wazi kutoweza kwao kubeba jukumu

zito la Amanah hiyo, Jee vipi wewe utaibeba Amanah hii ukijua uzito wa majukumu

yake?’, Mtu akauliza, ‘Ya Rabbi ni majukumu gani hayo’, na majibu yakawa: ‘Kama

ikiwa utafanikiwa kutekeleza majukumu ya Amanah hiyo kadri uwezavyo (yaani

kua mtiifu kadri utakavyoweza) utalipwa (kwa kuupata ukaribu wa Allah na

fadhila zake juu yako na pia kuishi milele Peponi) na kama ukishindwa kutekeleza

majukumu ya Amanah hiyo basi utaadhibiwa’. Hivyo Adam (akiwa na hamu kubwa

sana ya kupata kua na ukaribu na Allah na pia ridhaa yake) akakubaliana na

majukumu hayo na hivyo kuibeba Amanah hiyo.

Ni jambo lililowazi hapa kua, tukio la kupewa Amanah lilitokea kabla ya tukio la

ahadi, yaani lile tukio la kuulizwa kwa watu wote : ‘Jee mimi si Mola wenu?’, kwani

swali hilo la ahadi lililoulizwa hapo linatokana na kukubaliana kubeba Amanah na


318

kutekeleza majukumu yake. Kwani ili kua Khalifah ardhini, basi kitu cha muhimu

na cha lazima ni uwezo wa kulibeba jukumu la Amanah.

Kama ilivyokwisha kadiriwa na Allah Subhanah wa Ta’ala, kua Allah Subhanahu

wa Ta’ala alikua ameshaamua kumteua Adam kama Khalifah wake katika ardhi na

ukhalifa huu huweza kukabidhiwa yule atakaeweza kubeba jukumu la kutii

maamrisho ya muumbaji – kwa sababu lengo la ukhalifa ni kua hukmu na Sharia’h

za Allah Subhanahu wa Ta’ala zitumike ardhini na hivyo viumbe vya Allah

Subhanahu wa Ta’ala vishawishiwe kutekeleza hukmu na Sharia’h hizo. Kutokana

na utofauti wa viumbe Adam akakubali kubeba jukumu la Amanah hiyo – ijapokua

alikua akifahamu kua kuna uwezekano wa kutokea kwa baadhi ya watu miongoni

mwa viumbe hivyo, kutokua na uwezo kubeba Amanah hiyo. (Mazhari na Bayan ul

Qur’an)

Ambapo kuhusiana na tukio la ahadi linalozungumziwa hapa ni lile lililotajwa kwenye

aya isemayo:

‏﴿وَإِذْ‏ أَخَذَ‏ رَب ُّكَ‏ مِن بَنيِ‏ ۤ آدَمَ‏ مِن ظُهُورِهِمْ‏ ذُرِّي َّتَهُمْ‏ وَأَشْهَدَهُمْ‏ عَلَى ٰ أَنفُسِ‏ هِمْ‏

أَلَسْتُ‏ بِرَبِّكُمْ‏ قَالُواْ‏ بَلَى ٰ شَهِدَْ‏ أَن تَقُولُواْ‏ يَوْمَ‏ ٱلْقِيَامَةِ‏ إِ َّ كُن َّا عَنْ‏ هَٰذَا

غَافِلِينَ۞أَوْ‏ تَقُولُو ۤ اْ‏ إِنم ََّآ

أَشْرَكَ‏ آابَؤَُ‏ مِن قَبْلُ‏ وَكُن َّا ذُرِّي َّةً‏ مِّن بَعْدِهِمْ‏ أَفَتُهْلِكُنَا بمَِا

فَعَلَ‏ ٱلْمُبْطِلُونَ۞وَكَذٰ‏ لِكَ‏ نُفَصِّلُ‏ ٱلآَتِ‏ وَلَعَل َّهُمْ‏ يَرْجِ‏ عُونَ‏ ﴾

Wa-idh akhadha rabbuka min banee adama min dhuhoorihim dhurriyyatahum

waashhadahum AAala anfusihim alastu birabbikum qaloo bala shahidna an

taqooloo yawma alqiyamati inna kunna AAan hadha ghafileena; Aw taqooloo

innama ashraka abaona min qablu wakunna dhurriyyatan min baAAdihim

afatuhlikuna bima faAAala almubtiloona; Wakadhalika nufassilu al-ayati

walaAAallahum yarjiAAoona (Surat Al Araf 7:172-173)

Tafsir: Na Kumbuka pale Alipochukua Mola wako Kutoka kwa Ibn Adam kutoka

kwenye Migongo yao Vizazi vyao Na Kuwashuhudisha kwa Nafsi zao (Kwa

Kuwauliza): ‘Jee Mimi Sie Mola wenu?’ Wakasema : ‘Naam!’ Tunashuhudia; hivyo

Msije mkasema katika siku ya Malipo kua : ‘Sisi hatukua na habari juu ya hili’ au

Msije mkasema: ‘Waliokushirikisha ni Wazee wetu waliotangulia kabla yetu na sisi ni

vizazi vyao tu vilivyofuata baada yao. Hivyo utatuangamizaje sisi kutokana na


319

waliyofanya wabatilishaji?’ na hivyo ndivyo tunavyofafanua Aya zetu ili wapate

Kurudi (kwa Mola wao)

Neno Dhahara kwa Kilugha hua linamaanisha Dhahiri, Kutokea, Kuonekana,

Kutofautika, Kufunguka, Kuchomoza, Kuweka wazi, Kudhihirisha, Kujua, Kupanda

Kushinda na pia humaanisha Kudharau.

Neno Dhahara ndio lililotoa neno Adhuhuri ambalo Humaanisha wakati ambao Jua

lishachomoza na lishaupita katika Usawa wa Kichwa. Na pia neno Dhahara hua

linamaanisha Mgongo au Kumuumiza Mtu Mgongoni.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta'ala pia hakutuficha bali ametuwekea wazi kuhusiana na

tukio hilo na hii ni kwa sababu tukio hili lilitokea wakati sisi tukiwa katika hali ya

Vinasaba ndani ya Migongo ya wazee wetu na wao ndani ya migongo ya wazee wao

ndani ya mapazia ya Ulimwengu usioonekana maelfu ya miaka na miaka ndani yake.

Ambapo Anasema Jarrah Allah Imam Abu Qasim al Zamakhshari kua: Tukio hili la

Kiapo lilitokea katika hali ya Kiroho, pale tulipotakiwa na Allah Subhanah wa

Ta'ala kua Tuwe na Tukawa.

Na anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kuhusiana na aya hii

kua: Allah Subhanah wa Ta'ala aliwachukua Mitume na Manabii wote kutoka

kwenye Sehemu za Siri za Adam. Kisha akatoa katika kila Mtume na Nabii kizazi

cha Ummah wake vikiwa katika hali ya Uqul (Akili). Kisha akachukua Ahadi

kutoka kwa Mitume kwanza kama alivyosema katika aya ifuatayo:

‏﴿وَإِذْ‏ أَخَذَْ‏ مِنَ‏ ٱلن َّبِيِّينَْ‏ مِيثَاقَهُمْ‏ وَمِنْكَ‏ وَمِن ن ُّوحٍ‏ وَإِبْرَاهِيمَ‏ وَمُوسَى ٰ وَعِيسَى ٱبْ‏ ‏ِن

مَرْيمََ‏ وَأَخَذَْ‏ مِنْهُمْ‏ مِّيثَاقاً‏ غَلِيظاً﴾‏

Wa-idh akhadhna mina alnnabiyyeena meethaqahum waminka wamin Nuuhin wa-

Ibraheema waMuusa waAAeesa ibni Maryama waakhadhna minhum meethaqan

ghaleedhan (Surat Al Ahzab 33:7)

Tafsir: Na Kumbuka tulipochukua kutoka kwa Manabii Ahadi zao Kutoka kwako (Ewe

Muhammad) na kwa Nuh na kwa Ibrahim na kwa Musa na kwa Isa Ibn Maryam Na

Tumechukua kutoka kwao Ahadi nzito sana.


320

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anaendelea kutuambia kua:

‘Ahadi walioitoa Mitume hawa ni kua Watafikisha Ujumbe wa Allah Subhanah wa

Ta'ala kuhusiana na Maamrisho Yake na Makatazo yake, Kisha baada ya Mitume

hio kutoa ahadi hio basi Allah Subhanah wa Ta'ala akavikusanya Vizazi vyote vya

Ibn Adam kuanzia mwanzo hadi mwisho wake kisha akawauliza Ibn Adam hivi jee

mimi sie Mola wenu?

Ibn Adam wakaitikia kua Ndie, ambapo huu ulikua ni Mtihani Juu ya Ibn Adam

na baada ya Kujibu Suali hilo na hivyo kua ni wenye Kuoa si mtihani huo basi

wakarudishwa ndani ya sehemu za Siri za Adam. Na ndio maana akawatuma kwa

ajili ya Kuwaongoa kwa kuwakumbusha Makubaliano yao Ibn Adam kwake yeye

Na ni kwake yeye Allah Subhanah wa Ta'ala kwenye Ilm ya kujua kuhusiana na

siku ya tukio hilo la Ahadi Na pia ni kwake yeye ndiko kwenye Ilm ya kujua ni nani

atakubaliana nayo ahadi hio na kuitimiza na ni nani atakaeikataa na kuikadhibisha

hakitofika Kiama hadi pale itakapokua tayari kila Mtu aliekubali na kuthibitisha

ahadi hio kua ni mwenye Kuishi Duniani’

Naam Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari aliulizwa kuhusiana na

Utiifu na Uovu mbele ya Allah Subhanah wa Ta'ala, ambapo nae akajibu kwa kusema

kua: ‘Ama kwa hakika miongoni mwa Dalili za Uovu hua ni Kukataa Utukufu wake

Allah Subhanah wa Ta'ala. Na katika Dalili za Utiifu hua ni Kutanuka kwa Kifua

na Moyo na kujaa Nuru ya Imani, na hivyo Moyo wako hua ni wenye kujazwa na

ulinzi wa kufanya Utiifu na mafanikio ya kuachana na Dunia.’

Kwani kuhusiana na Uovu na Utiifu wa mtu Mbele ya Allah Subhanah wa Ta'ala basi:

Amesema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: Makadirio ya Maumbile ya Mtu hua ni Kuwekwa

ndani ya tumbo la Uzazi la Mama yake kwa siku 40. Kisha hua ni katika pande la

Damu kwa siku hizo hizo, na kisha hua katika pande la Nyama katika Siku hizo

hizo. Kisha Allah Subhanah wa Ta'ala huamrisha kuandikwa kwa Amali, Riziki,

Kifo na Utiifu au Uasi wa Mtu huyo, Kisha Mtu huyo Hupuliziwa Roho yake.’

‘Hivyo Miongoni mwenu kuna mtu ambae atafanya Mema mpaka atafikia dhiraa

moja kukaribia kuingia Peponi halafu kile kilichokadiriwa kimfike kitatokea na

kuamua matokeo yake na ataanza kufanya Maovu ya watu wa Motoni. Na

Miongoni mwenu kuna mtu atafanya maovu mpaka itabakia dhiraa moja tu baina

yake na Moto na kisha kilichokadiriwa juu yake kitatokea na ataanza kufanya

Mema.’(Sahih Bukhari)


321

Hii ni hadith inayomaanisha kua Mbali ya kua Ibn Adam walikubali kua Allah Subhanah

wa Ta'ala ndio Mola wao na hivyo Watakua watiifu kwake, lakini hapo hapo kuna watu

wataenda Motoni na wengine wataenda Peponi.

Na hii ni kulingana na Amali zake Mtu husika kua ataenda Peponi kutokana na kutaka

kwake Mtu huyo kuenda Peponi kwa kufuata Maamrisho ya Mola wake. Na atakae enda

Motoni ataenda Motoni kutokana na Makosa yake. Kwani ndani ya Maumbile ya Uhai

wa kila Ibn Adam basi kuna kitu kinaitwa Qadar na kuna Kuna Kitu kinaitwa Qadha.

Ambapo tunaopozungumzia Qadha basi hua ni ile hi ambayo Allah Subhanah wa Ta'ala

ameibanisha katika Aya isemayo:

‏﴿بَدِيعُ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَإِذَا ٰ قَضَى أَمْراً‏ فَإِنم ََّا يَقُولُ‏ لَهُ‏ كُنْ‏ فَيَكُونُ‏ ﴾

BadeeAAu alssamawati waal-ardhi wa-idha qadha amran fa-innama yaqoolu lahu

kun fayakoonu.(Surat Al Baqara 2:117)

Tafsir: Muumbaji wa Mbingu na Ardhi, anapotaka kitu kiwe, hukiambia kua na hua.

Ambapo Mujaddid Ad Din, Shaykh ul Islami Al Hafidh Imam Shihab Ad Din Ibn Hajar

Al Asqallani anasema kuhusiana na aya hii kua: ‘Qadhaa hua inahusiana na Makadirio

ya Ujumla kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta'ala ya Milele.’

‘Na Qadar hua inahusiana na Maelezo juu ya Qadha na Utekelezaji wake katika

Maisha ya Mtu husika katika Wakati husika.’

Naam..kutokana na Maana hio basi hua tunaona maana ya maneno ya Hadith yetu

isemayo kua tayari kuna Makadirio ya Mtu mwema na Muovu hua yanamaanisha kua

Allah Subhanah wa Ta'ala ni mwenye kujua Mwanzo wa kitu kama kua kwake katika

kukua kwake na mwisho wake kutokana na Ilm yake.

Na hii ni kwa sababu Kitakachompeleka Mtu Peponi au Motoni hua ni Matendo yake

ambayo hua yanabainishwa na Ilm ya Allah Subhanah wa Ta'ala juu ya mtu husika kwa

kutumia njia ya Qadar.

Ambapo neno Qadar hua linamaanisha Makadirio, Ilm, Ufaham, Kipimo kikamilifu,

Uwezo, Makisio, Maamuzi, Sharia, Mpangilio, Mandalizi. n.k

Ambapo amesema Allah Subhanah wa Ta'ala katika Qur'an kua:


322

‏﴿بَدِيعُ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَإِذَا ٰ قَضَى أَمْراً‏ فَإِنم ََّا يَقُولُ‏ لَهُ‏ كُنْ‏ فَيَكُونُ‏ ﴾

BadeeAAu alssamawati waal-ardhi wa-idha qadha amran fa-innama yaqoolu lahu

kun fayakoonu.(Surat Al Baqara 2:117)

Tafsir: Muumbaji wa Mbingu na Ardhi, anapotaka kitu kiwe, hukiambia kua na hua.

Kwani Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu katika kipindi cha Utawala wake

katika wakati alipokua wakienda katika Vita vya Siffin na Jeshi lake basi aliulizwa: ‘Ya

Amir ul Muuminin! Jee hii kuenda kwetu kwenye Vita hivi kunatokana na Qadha

na Qadar ya Allah Subhanah wa Ta'ala?

Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akajibu: ‘Naam! hakika mimi nnaapa

kwa Allah Subhanah wa Ta'ala ambae ndie aliejaalia Miti na Majani yaote na

akavipa Uhai Viumbe vyake, kua Katika kila kitu basi ndani yake hua mna Qadha

na Qadar ya Allah Subhanah wa Ta'ala’

Ambapo aliemuuliza suali Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akasema:

‘Kama ni Hivyo, basi itakua kila tunachikifanya hua tunakifanyia kazi bure’

Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akasema: ‘La sio hivyo! Kwani Allah

Subhanah wa Ta'ala hua anakulipa wakati ukielekea kupigana kwa ajili yake na pia

hukulipa wakati unaporudi baada ya kupigana, na hii ni kwa sababu hakuna

aliekulazimisha kufanya hivyo bali umefanya hivyo kutokana na hiari yako

mwenyewe.’

Hivyo Sayyidna Ali Radhi Allahu Anhu akaulizwa tena: ‘Hivi Sio Qadar na Qadha ndio

inayotuongoza sisi kufanya haya tunayofanya?

Amir ul Muuminin Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu Akasema: ‘La! Hivi

wewe unafikiria kua Qadha imekuganda wewe na Qadar imeshikamanishwa na

wewe? Sio hivyo, Kwani kama ingekua kama hivyo basi ingekua hakuna Malipo ya

Thawabu wala Malipo ya Adhabu, na ingekua hakuna haja ya Pepo wala vitisho

vya Jahannam, wala Sharia wala Makatazo. Hivyo Allah Subhanah wa Ta'ala

asingewaaadhibu wale wanaofanya dhambi na wala asingewasifu wale wanaofanya

mema. Hivyo Wale wanaofanya Mema wangekua hawastahiki kusifiwa kwani ni

sawa na wale wanaofanya Maovu. Na wanaofanya Maovu wangekua haina haja juu

yao Kulaaniwa kwani ni sawa na wanaofanya Mema’


323

‘Hivyo Maneno hayo ya wanaosema kua kila tunalofanya linatokana na sisi

kuongozwa na Qadha na Qadar hua ni Maneno ya Wasioamini, yaani wapiganaji

wa Jeshi la Shaytani, Wanafiq na wasiouona Ukweli. Hao ni Walioangamia na ni

wenye kuabudu Moto walio katika Ummah huu. Kwani Allah Subhanah wa Ta'ala

amewapa Watu Maamrisho kutokana na kua ni mwenye kuwapa Uhuru wa

kuchagua’

‘Na amekataza Mambo kwa ajili ya kuwataka wakae nayo mbali mambo hayo.

Amekifanya kila kitu kua na Urahisi katika Maamrisho yake, na wala

hakuwalazimisha watu kumuasi kwa kutumia nguvu wala uwezo wake juu yao. Na

wala hakuwatuma Mitume bure bure tu!, Hakuiumba Ardhi na Mbingu na kila

kilichomo ndani yake kwa kucheza bure bure’

‘Hivyo Mawazo ya mtu kama huyo anaefikiria hivyo hua ni Mawazo ya Mtu

asieamini, hawaoni hata aibu na Moto wa Jahannam uwe juu yao. ‘

Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akaulizwa tena: ‘Haya hebu Tuambie

Jee Qadha na Qadar hua zinatuongoza kwenye nini?’

Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Qadha na Qadar ni Matakwa

na Makadirio ya Allah kama alivyosema katika Qur'an:

ٰ ‏﴿وَقَضَى رَب ُّكَ‏ أَلا َّ ۤ تَعْبُدُو اْ‏ إِلا َّ إِ َّهُ‏ وَبِٱلْوَالِدَيْنِ‏ إِحْسَاً‏ ي إِم َّا َ‏ بْلُغَن َّ عِندَكَ‏ ٱلْكِبَرَ‏

أَحَدُهمَُا أَوْ‏ كِلاَهمَُا فَلاَ‏ تَقُل له َُّمَآ أُفٍّ‏ وَلاَ‏ تَنْهَرْهمَُا وَقُل له َُّمَا قَوْلاً‏ كَرِيماً‏ ﴾

Waqadha rabbuka alla taAAbudoo illa iyyahu wabialwalidayni ihsanan imma

yablughanna AAindaka alkibara ahaduhuma aw kilahuma fala taqul lahuma offin

wala tanharhuma waqul lahuma qawlan kareeman (Surat Al Isra 17:23)

Tafsir: Na Ametaka Mola wako Kua Usimuabudu Yeyote isipokua yeye, na kuwafanyia

wema Wazee wawili na kama mmoja wao au wote wawili kati yao ama wa akiwa wazee,

basi usiwaambie hata uf! Na wala usiwakripie na zungumz nao kwa Kauli zenye

Ukarimu. (Surat Al Isra 17:23)

Naam..aliemuuliza Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akasema: Ya Amir ul

Muuminin Hakika wewe ni Mtu ambae mtu anaweza kutegemea Radhi za Allah

Subhanah wa Ta'ala kupitia kwa kutii Maamrisho yako, kwani kwa hakika


324

umetubainishia jambo ambalo linawachanganya wengi katika Dini yetu, hivyo

Allah Subhanah wa Ta'ala akulipe kwa hayo.

Hivyo ili tufaham zaid basi inabidi tuingie kwenye Fani ya Ilm ambayo inajulikana kama

Ilm Al Kalam ambapo ndani yake tunakutana na Kanuni inayosema kua: ‘Ilm ya Kitu

husika hua juu ya kile kinachojulikana’ hivyo kutokana nayo basi bila ya shaka Allah

Subhanah wa Ta'ala hua ni Mwenye Kujua ni nani Miongoni mwetu Ibn Adam ataenda

Motoni na ni nani ataenda Peponi.

Yaani tuchukulie mfano wa vile sisi tunavyojua kua kipindi hiki cha mwezi huu Sala ya

Alfajir hua inaingia saa ngapi na ya Magharibi inaingia saa ngapi na hivyo hua tunajua

kua ikifika saa kumi na nusu jioni basi Magharibi hua haijaingia na saa kumi Usiku basi

Alfajiri bado haijaingia. Hivyo hata Ukiamka na Ukiadhini wewe saa tisa Usiku basi

huwezi kusali Alfajiri wala kusalisha Sala ya Alfajiri kwa sababu mda wa Sala ya Alfajiri

haujafika. Hivyo hii hua ni hali ya Qadha kwa sababu Allah Subhanah wa Ta'ala ametaka

iwe hivyo.

Lakini sasa tunapozungumzia kuhusiana na Qadar yaani Makadirio basi hua kuna aina

ya hali mbili:

Ambapo hali ya kwanza hua ni kuhusiana na yale mambo ambayo yako nje ya

uwezo wa Kiumbe na hivyo kiumbe hua hana hiari nayo. Kwa mfano Siku, Wakati,

wa Kuzaliwa kwake, Wazee wake, Ndugu zake, Nchi atakayozaliwa, Siku na wakati

wa Kifo chake n.k

Hivyo hii hua ni kama kwa upande wa Sala Kiumbe unakua huna hiari, kwani

ukifika wakati wake basi huwezi kuuzuia usiingie, na ukitoka wakati wake basi

huwezi kuurudisha.

Ambapo hali ya pili ya Qadar hua ni Katika yale ambayo ingawa ni Jukumu lake

Kiumbe lakini anakua na hiari juu yake kutekeleza ama la.

Hivyo na hapa tuchukulie tena Mfano wa Sala, Kua Tayari Mda wa Kusali Maghribi

umeshaingia hivyo ni Jukumu lako kusali na hivyo kua na sifa ya Kaslan (Kuona Uvivu)

au Saahun (Kudharau) hua ni Hiari yako. Na kutokana na hii Hiari basi ndio maana Allah

Subhanah wa Ta'ala akatuwekea Malaika Kiraman Katibin wawili Raqib na Atid kwa

ajili ya kutuandikia kwenye Vitabu vyetu kuhusiana na Qadar yaani Makadirio yaliyomo

ndani ya uwezo wa Hiari yetu Kimatendo.

Hivyo kama ukitekeleza Jukumu lako ipasavyo basi Malaika wataandika ipasavyo na

utalipwa na Mola wako ipasavyo. Na kama hukutekeleza Jukumu lako na ukadharau na


325

kuona Uvivu basi bila ya Shaka Utaandikiwa Ipasavyo na Utaadhibiwa na Mola wako

ipasavyo.

Ambapo kwa upande mwengine basi tunapoangalia hadith nyengine ya Qadha na Qadar

katika kitabu cha Sahih Muslim basi tunaona kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

aliwaambia Masahaba zake kua : ‘Hakuna hata mmoja Miongoni mwenu isipokua

Allah Subhanah wa Ta'ala anajua iko wapi Nafasi yake Mtu huyo katika Pepo au

Motoni’

Masahaba wakauliza: ‘Ya Rasul Allah! Hivyo Jee kwanini basi sisi tunafanya Mema?

Kwanini tusitegemee hali hio?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu: ‘La Endeleeni kufanya Mema kwani

kila mmoja kati yenu atajikuta kua kwake yeye inakua rahisi kufanya mambo hayo’

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salama akasoma Aya zifuatazo:

‏﴿إِن َّ سَعْيَكُمْ‏ لَشَتى َّ ٰ ‏۞فَأَم َّا مَ‏ نْ‏ أَعْ‏ ٰ طَى ‏َو ٱت َّقَ‏ ٰ ى۞‏ وَ‏ صَد َّ قَ‏ بِٱ لحُْسْ‏ نىَٰ‏ ‏۞فَسَنُيَسِّ‏ رُهُ‏

لِلْيُسْرَىٰ‏ ‏۞وَأَم َّا مَن بخَِلَ‏ وَٱسْتَغْنىَٰ‏ ‏۞وَكَذ َّبَ‏ بِٱلحُْسْنىَٰ‏ ‏۞فَسَنُيَسِّ‏ رُهُ‏ لِلْعُسْرَىٰ‏ ﴾

Inna saAAyakum lashatta; Faamma man aAAta waittaqa; Wasaddaqa bialhusna;

Fasanuyassiruhu lilyusra; Waamma man bakhila waistaghna; Wakadhdhaba

bialhusna; Fasanuyassiruhu lilAAusra(Surat Al Layl 92:5-10)

Tafsir: Jitihada zenu katika Matendo yenu yametofautiana (Kimalengo na

kimakusudio), Hivyo kwa Yule atakaetoa (Sadaqa) na Kutekeleza Wajibu wake kwa

Allah; Na Akaamini Katika mema hayo; Basi sisi Tutamrahisishia Njia ya Kufanya

mema hayo; Na Atakae kua Bakhili na Kujiona kua Anajitosheleza; Na

Akakadhibisha Juu ya Mema hayo; Basi Tutamrahisishia Njia hio ya kufanya Maovu

hayo.

Hivyo tujitahid kutekeleza Majukumu yetu katika Kumtii Mola wetu na Kufanya Mema,

na kisha bila ya shaka Allah Subhanah wa Ta'ala ataturahisishia Njia ya Kufanya Mema

zaidi, kwani kufanya kwetu mema na kuachana na makatazo yake hua kunaonesha kua

tuna Adabu na Utiifu mbele ya Mola wetu.


326

Kwani anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Kwa

hakika miongoni mwa dalili ya kupotoka hua ni kukataa Ufalme wake Allah

Subhanah wa Ta’ala. Na kwa hakika miongoni mwa dalili za Utulivu na furaha ya

Moyo hua ni kutanuka kwa Moyo wako kutokana na kujaa Imani na hivyo kua ni

mwenye kujaaliwa utajiri wa Moyo wako, na kupata hifadhi ya kua na Utiifu kwa

Mola wako na Kuachana na Ulimwengu (Zuhd).

Kwani yeyote yule atakaejaaliwa kua na Adabu baina yake na Mola wake basi hua

ni mwenye kujaaliwa kusafishwa Moyo wake na hivyo hua ni mwenye furaha na

utulivu, na hakuna kitu chengine chochote kizuri kama kua na Adabu mbele ya

Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anatuambia kua: ‘Ni jambo la

kawaida pale Watu wanapokabidhiana Amana basi hua ni wenye kuweka Alama

ya muhuri juu ya amana hio, na wanapoitaka kuichukua wenyewe amanah hio

basi hukagua alama ya muhuri huo, na hivyo kama alama hio ko kama ilivyokua

katika wakati wa makabidhiano basi aliekabidhiwa hua ni mwenye kupongezwa

kutokana na uaminifu wake.

Hivyo nawe umekabidhiwa Amanah pale Allah Subhnah wa Ta’ala alipokuuliza:

‘Jee mimi sie Mola wako?’ na kutokana na suali hilo basi ikawa umepigwa muhuri

kwa kuitikia kwako pale uliposema: ‘Naam bila ya shaka na wewe Ndie Mola

wangu’

Na unapofika mwisho wa Uhai wako hapa Duniani basi utapelekewa kwenye

Makazi ya Vumbi na Malaika atakuja na kukuuliza: ‘Hivi Jee ni Nani Mola

wako?’ Suali hili hua ni katika hali ya kuangalia Muhuri wako upo au haupo.’

‘Hivyo ewe Ibn Adam, Muhuri umewekwa kuanzia tangu juu ya kichwa chako

hadi kwenye Miguu yako. Huo haukua Muhuri wowote isipokua Muhuri wa

Mapenzi (Mihr) ya Mola wako juu yako. Kuonesha kua Wewe ni wake Allah

Subhanah wa Ta’ala na yeye ni kwa ajili yako’

Kwani Milima haikua na uwezo wa ya kuweza kubeba uzito wa Amanah hii, na

wala Ardhi pia, hivi jee hamjaona namna Allah Subhanah wa Ta’ala

alivyothibitisha katika Qur’an pale aliposema:


327

‏﴿لَوْ‏ أَنزَلْنَا هَٰذَ‏ ا ٱلْقُرْآنَ‏ عَلَى ٰ جَبَلٍ‏ ل َّرَأَيْتَهُ‏ خَاشِ‏ عاً‏ م ُّتَصَدِّعاً‏ مِّنْ‏ خَشْيَةِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَتِلْكَ‏

ٱلأَمْثَالُ‏ نَضْرِبُهَا لِلن َّاسِ‏ لَعَل َّهُمْ‏ يَتَفَك َّرُونَ‏ ﴾

Law anzalna hadha alqur-ana AAala jabalin laraaytahu khashiAAan

mutasaddiAAan min khashyati Allahi watilka al-amthalu nadhribuha lilnnasi

laAAallahum yatafakkaroona (Surat Hashr 59:21)

Tafsir: Lau Kama tungeishusha Qur’an juu ya Jabali basi kwa hakika ungeliona

linavyonyenyekea na kububujika kutokana na kumuogopa Allah Subhanah wa

Ta’ala. Na hio ni Mifano tunayowapigia watu ili wapate kutafakkari.

Hivi Jee mmemuona Malaika, ambae Mabawa yake akiyatanua Upana wake hua

yanauweka upeo wa Macho mawili Chini yake, lakini hata hivyo huyo Malaika nae

hana uwezo wa kuibeba Amanah hio, halafu fikiria kua Maskini Ibn Adam ambae

ngozi yake imetandazwa juu ya Mifupa yake, kama Mpiganaji Shupavu asiekua

na Woga na kunywa Mvinyo wa Mitihani kutoka ndani ya Gilasi la rafiki wa

Karibu, na hivyo kua haathiriki na mabadiliko yeyote yanayomtokea juu yake.

Jee unajua kwa nini? Kwa sababu yeye Ibn Adam ni Mmiliki wa Moyo, na Moyo

ndio wenye kubeba kile itu ambacho Mwili hauwezi kubeba yaani Nuru ya Allah

Subhanah wa Ta’ala. Hivyo wakati Adam aliechaguliwa, ambae ni mwenye

Maajabu ya Viumbe vyote na upekee wa Matamanio yake alipooona basi alipoona

kua Mbingu na Ardhi zimekataa kubeba Amanah hio basi yeye akatoka mbele

kama Ibn Adam na kuchukua jukumu la kubeba Amanah hio na kusema kua:

‘Hakika viumbe hawa wameangalia juu ya uzito wa jukumu la Amanah na hivyo

wakakataa, lakini mimi nimeangalia Ukarimu wa Mwenye Kuweka Dhamana na

ndio maana nikaichukua.’

Ambapo hapa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anamaanisha kua:

‘Jukumu la Kuibeba Amanah hio halichukuliwi na kubebwa kutokana Nguvu bali

hubebwa kutokana na hisia za Ari na Msukumo wa Kimaumbile wa Nafsi.’

Kwani amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kuhusiana na Maumbile ya Nafsi na

Msukumo wake kua kama zinavyosema aya:


328

‏﴿وَنَفْسٍ‏ وَمَا سَو َّاهَا۞فَأَلهَْمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا۞قَدْ‏ أَفْلَحَ‏ مَن زَ‏ ك َّاهَا۞وَقَدْ‏

خَابَ‏ مَن دَس َّاهَا﴾‏

Wanafsin wama sawwaha; Faalhamaha fujooraha wataqwaha; Qad aflaha man

zakkaha ; Waqad khaba man dassaha (Surat ash Shams 91:7-10)

Tafsir: Nnaapa Kwa Nafsi na kwa yule (Mwenyewe Allah Subhanah wa Ta’ala)

alieiweka sawa kiukamilifu, na Kisha akaionesha kwa kuitia Msukumo juu ya kile

kilichokua sicho juu yake na kilichokua ndicho juu yake. Kwa hakika Amefuzu

atakaeitakasa (Nafsi yake) na kwa hakika ameangamia yule atakaeiendekeza.

Ambao tunaona kua zetu zimetumia neno Lahama ambalo hua ni lenye kumaanisha

Kumeza Kitu, Kumeza Funda la Maji au la Chakula, ambapo neno Lahama ndio lililotoa

neno Ilham ambalo hua linamaanisha Maumbile ya Kiumbe Hisia za Unyama ndani

yake, Hali ya Kiumbe Kua na Ukaribu Mkubwa na wa haraka wenye Msukumo kutoka

kwa Muumba yaani Allah Subhanah wa Ta’ala, na pia humaanisha Ujumbe kutoka kwa

Muumba yaani Allah Subhanah wa Ta’ala.

Na ikatumia pia neno Fajara ambalo hua ni lenye kumaanisha Kumwagia Maji, Kuvunja,

Kuchimba, Kuchimbia, Kufuata upande mwengine usiotakiwa, Kusababisha kuenea na

Kumwagika na pia humaanisha Kufurika na kumwagika.

Ambapo neno Fajara ndio lililotoa neno Fajrun ambalo hua linamaanisha Kuvunjka kwa

Usiku na Kuingi kwa Asubuhi. Na pia likatoa neno Fujjar ambalo hua linamaanisha

Uovu, Utovu wa Nidhamu au Kufanya Makosa.

Na pa katua neno Waqaya ambalo hua ni lenye kumaanisha Kulinda, Kuhifadhi,

Kukiweka kitu chini ya Ulinzi ili kisidhurike na uovu au Madhara, kua Salama, Kua na

Ngao na pia humaanisha Kusamamia Jukumu. Ambapo neno Waqaya ndio liliotoa neno

Taqwa ambalo humaanisha Kujilinda, Kukaa mbali na Maovu, Kusimamia Jukumu, na

pia humaanisha Kujizuia

Na hivyo basi maneno Faalhamaha fujooraha wataqwaha hua yanamaanisha kua Moja

kati ya sifa za Ukamilifu wa Kimaumble wa Nafsi uliojaaliwa na Allah Subhanah wa

Ta’ala basi ni kua imepewa Ukaribu mkubwa sana na wa haraka wenye Msukumo

kutoka kwa Allah Subhnah wa Ta’ala wa kuoneshwa njia isiyokua sahih na hivyo ya


329

kuachana nayo na pia kuoneshwa Jukumu lake ambalo hua ni lenye kusimamia na

kuihifadhi Nafsi isidhurike kwa kufanya Makosa.

Hivyo yule atakaeisafisha na kuisimamia Nafsi hio na ikawa ni yenye kufuata njia yake

ya kimaumbile na hivyo kutofuata upande usiotakiwa basi atakua amefuzu, na yeyote

yule atakaeiendekeza na kushindwa kuisimamia basi atakua amepotoka na hua ni

miongoni mwa walioangamia.

Na ndio maana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawa ni mwenye kupenda

kuomba Dua isemayo: ‘Ya Rabb, Ipe Nafsi Taqwa yake, kwani kwa hakika wewe

ndie Msimamizi wake na Ndie Mmiliki wake, Na Isafishe kwani wewe ni M-bora

Miongoni mwa wenye Kusafisha.’

Kwani kila Ibn Adam atakuja kuulizwa juu ya Nafsi yake kama zinavyosema aya:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ ٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَلْتَنظُرْ‏ نَفْسٌ‏ م َّا قَد َّمَتْ‏ لِغَدٍ‏ وَٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏

خَبِيرٌ‏ بمَِا تَعْمَلُونَ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo ittaqoo Allaha waltandhur nafsun ma qaddamat

lighadin waittaqoo Allaha inna Allaha khabeerun bima taAAmaloona (Surat Al

Hashir 59:18)

Tafsir: Enyi Mlioamini Mcheni Allah na kila mmoja aiangalie Nafsi yake imetanguliza

nini (kwa Mola wake) na Mtiini Allah, kwani kwa hakika Allah ni mwenye kua na

habari juu ya kila mnachokifanya.

Ambapo katika Aya hii basi Allah Subhanah wa Ta’ala anatoa onyo kuhusiana na siku

ya Malipo kua kila mmoja atakuja kuulizwa kuhusiana na mambo matatu ambayo ni

kuhusiana na: Juu ya yale anayodaiwa na Nafsi yake; Anayodaiwa kulingana na

Anayoyajua baina yake na Mola wake, na yale anayodaiwa juu ya Ufaham wake.

Na ndio maana akasema Hasan Al Basr kua: ‘Ibn Adam anapofariki basi Ibn Adam

wenzake huulizana juu ya Ibn Adam huyo aliefariki kwa kusema: ‘Jee amewacha

Nini?’ ambapo kwa upande wa Malaika basi wao hua ni wenye kuulizana juu ya

Ibn Adam huyo aliefariki kwa kusem kua: ‘Jeea ametanguliza nini’’

Hivyo ni jukumu la kila Muumini kua ni mwenye kujitahidi kua ni mwenye kutekeleza

maamrisho ya Allah Subhanah wa Ta’ala na kufanya mema kwa ajili ya kutanguliza kwa

Mola wake na wakati huohuo sambamba akiwa ni mwenye kusimamia jukumu lake la


330

Amanah aliyokubali kuichukua kutoka kwa Mola wake, ambapo inabidi awe hivyo ili

aweze kua miongoni mwa wenye kuthibitisha juu ya kukubali kwake kubeba jukumu la

Aamana hio na hivyo kua pia ni mwenye kuisimamia na kutimiza Ahadi hio aliyoitoa

mbele ya Mola wake na kushuhudia kama zinavyothibitisha aya pale ziliposema:

‏﴿َوٱ ل َّ ذِي نَهُمِْ‏ لأَمَا َ هتِ‏ ‏ِمْوَ‏ عَهْ‏ دِ‏ هِمْرَا عُو نَ‏ ‏۞وَال َّ ذِينَ‏ هُمْ‏ بِشَهَادَاهتِِم قَائِ‏ مُونَ‏ ﴾

Waalladheena hum li-amanatihim waAAahdihim raAAoona; Waalladheena hum

bishahadatihim qa-imoona (Surat Al Maarij 70:32-33)

Tafsir: Na wale ambao juu ya Amana zao na Ahadi zao wametimiza, Na wale ambao

Shahada zao wamezisimamisha.

Ambapo wenye kuzisimamisha shahada hua ni wale ambao hawakumshirikisha Allah

Subhanah wa Ta’ala baada ya kushuhudia na hivyo hawatokua ni wale ambao

wametajwa mwishoni mwa maneno ya aya yetu yasemayo:

‏﴿إِن َّهُ‏ كَانَ‏ ظَلُوماً‏ جَهُولاً﴾‏

Innahu kana dhaluuman jahuulan – Kwa hakika alikua ni mwenye kujidhulumu na

mjinga.

Ambapo neno Dhaluma maana yake ni kua aliejidhulumu Nafsi yake na neno Jahula

linamaanisha kutokujua matokeo yake, na kutokana na maneno haya basi kwa ujumla

inaonekana kua Mtu analaumiwa kua ni mjinga kwa kujidhulumu kutokana na kukubali

kubeba Amanah kubwa yenye jukumu zito ambayo inazidi uwezo wake.

Lakini kutokana na maelezo yaliyowazi kutoka katika Qur’an, basi tunaona kua hivi

sivyo ilivyokusudiwa kwa sababu neno ‘Mtu’ linamaanisha Adam au Bani Adam wote.

Sasa Adam yeye kama Nabii, basi ana ulinzi wa Allah wa kutofanya dhambi. Hivyo

mzigo wa jukumu alioubeba aliubeba kihalali na kiuhakika, na matokeo yake ndio

akapewa cheo cha kua Khalifah wa Allah na akatumwa ardhini.

Adam alifanywa kua kiumbe cha kusujudiwa na Malaika, hivyo na Akhera pia, makazi

yake yatakua yapo juu kuliko hata yale ya Malaika. Na ikiwa neno ‘Mtu’ linamanisha

Bani Adam, basi katika mtizamo huu pia kuna Maelfu ya Mitume watukufu na Mamilioni

ya watu wema wa Allah (Awliya Allah) hata Malaika huwaiga - wale waliokubalika

kutokana na mambo yao katika maisha kiasi ya kua waliweza kuidhibiti na kuibeba


331

Amanah hiyo ya Allah. Kutokana na msingi huu uliowekwa na roho za watu wema kama

hawa ambao walipata haki ya kihalali na kiasili ya kubeba amana hiyo nzito kiasi ya kua

Qur’an yenyewe imetangazia kua Bani Adam ni kiumbe bora kuliko viumbe wote pale

iliposema:

Walaqad karramna banee adama (Surat Al Israa, 17:70)

Tafsir: Na kwa hakika tumemkirimu Bani Adam.

‏﴿وَلَقَدْ‏ كَ‏ ر َّمْ‏ نَا بَنىِ‏ ءَادَ‏ مَ﴾‏

Aya hii inaonesha kua Adam hana makosa na vile vile Bani Adam hawana makosa pia.

Hivyo Mufassirin, wanaotafsiri wamesema kua meneno haya ‘Kwa hakika alikua ni

mwenye kujidhulumu na mjinga’, hayana maana ya kutoa lawama, au kulaumu, bali yapo

katika hali ya kuelezea hali ya tukio miongoni mwa wengi kati ya Bani Adam. Kiasi ya

kua, ikiwa hali ya wengi miongoni mwa Bani Adam wakajidhihirisha kua ni Dhaluman

(waliojidhulumu) na Jahulan (wajinga wasiojua matokeo ya mwisho) basi hua ni

walioshindwa kutekeleza haki na matakwa ya Amanah hiyo na wataingia katika hasara

kubwa. Bani Adam hua wanasifika hivyo kwa sababu hivi ndivyo hali halisi ilivyo kwa

idadi kubwa sana miongoni mwao.

Hivyo maana ya aya hiyo ni kua, kwa sababu Bani Adam amekubali kubeba jukumu la

Amanah hiyo, basi matokeo yake yamewagawa Bani Adam katika makundi mawili:

Kundi la kwanza ni la wasioamini, wanafiq na wengineo ambao wanapinga na pia

kuenda kinyume na maamrisho ya Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo wakawa ni

miongoni mwa waliolipoteza jukumu la Amana hiyo na matokeo yake ni kua

watapata adhabu kali baadae, hawa ndio ambao waliojidhulumu kutokana na

ujinga wao.

Kundi la pili ni wale walioamini na wakatekeleza maamrisho ya Allah Subhanah wa

Ta’ala, matokeo ya watu hawa ni kuingizwa katika Rehma na Usamehevu wa Allah

Subhanahu wa Ta’ala, hawa ndio watakaokua miongoni mwa waliofuzu.

Na hivi ndivyo ilivyotafsiriwa maana ya maneno Dhaluman na Jahula na wengi

miongoni mwa wafasiri – Kua maneno haya hayawajumuishi Bani Adam wote kwa

ujumla kua wana sifa hiyo. Bali inawazungumzia wale walioshindwa kutekeleza

majukumu ya Amanah waliyopewa na matokeo yake basi ni kama inavyosema aya

inayofuatia baada ya hio kua:


332

لِّيُعَذِّبَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱلْمُنَافِقِينَ‏ وَٱلْمُنَافِقَاتِ‏ وَٱلْمُشْرِكِينَ‏ وَٱلْمُشْرِكَاتِ‏ وَيَتُوبَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلَى

ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ وَٱلْمُؤْمِنَاتِ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ غَفُوراً‏ ر َّحِ‏ يماً‏ ﴾

LiyuAAadhdhiba Allahu almunafiqeena waalmunafiqati waalmushrikeena

waalmushrikati wayatooba Allahu AAala almu/mineena waalmu/minati wakana

Allahu ghafooran raheeman (Al Ahzab 33: 73)

Tafsir: Hivyo Allah atawaadhibu Wanafiq wa kiume na wanafiq wa kike na Al

Mushrikûn (wanaume na wanawake wanaomshirikisha). Na Allah atawasamehe

Waumini wa kweli wa kiume na wa kike. Na hakika Allah ni mwingi wa Usamehevu

na ni mwingi wa Rehma.

Na kwa upande wa Imam Zayn Al Abidiin Ali Ibn Husayn Ibn Ali Ibn Abi Talib Radhi

Allahu Anhu ambae alikua anapenda sana kusali, kiasi ya kua anaweza akabakia katika

kusjudu kwa saa nzima. Hivyo siku moja alikua Nyumbani kwake, Nyumba yake ikawa

inawaka Moto, na yeye alikua kwenye Sijda. Watu wakatoka ndani ya Nyumba hio huku

wakinadia Moto! Moto!

Wakatoka watu wote na vitu vyao, na walipofika nje wakajiona kua wako peke yao bila

ya kuwepo Imam Zayn al Abidin Radhi Allahu Anhu. Watu hao wakanza kuulizana yuko

wap na wakajawa na khofu, wasiwasi na huzuni kubwa sana.

Lakini baada ya mda Moto ukaisha na kuzimika, watu wakaingia ndani na kumkuta Imam

Zayn Al Abidin bado akiwa kwenye Sijda huku akiwa hajadhurika hata kidogo kutokana

na Moto huo hivyo wakamsubiri mpaka alipomaliza Kusali na alipomaliza basi

wakamuuliza:‘Ya Zain Al Abidin hivi hukusikia wewe watu walipokua wakinadia

Moto Moto!?’

Imam Zayn Al Abidin akasema: ‘Bila ya shaka nilisikia lakini sasa akili yangu yote

ikakimbilia kufikiria kwenye Moto wa Jahannam badala ya kukimbilia kufikiria

Moto wa Duniani, hivyo khofu yangu ikazama kwenye moto wa Akhera kwani ndio

mkali zaidi, ikanibidi nibakie kwenye Sijda kumuomba Mola wangu aniepushe na

Moto wa Jahannam.’

Na anasema Imam Husayn Al Karabisi ambae ni mWanafunzi wa Imam Muhammad

Idris Al Shafii kua: ‘Imam Al Shafii alikua akisali katika sehemu ya robo tatu ya

Usiku na alikua akisoma aya zaidi ya 50, na wakati mwengine zaidi ya aya 100. Na

katika kisomo chake alikua katika kila aya ya Rehma akiomba Rehma kwa Mola

wake, na katika kila aya ya Adhabu alikua akiomba Maghfira baada yake, na hivyo

kua ni mwenye kujumuisha pamoja ndani ya sala yake Matumaini yake juu ya Mola

wake na Khofu yake juu ya Mola wake. ’

﴿


333

Ambapo kwa upande wa Imam Malik Ibn Anas muanzilishi wa Madhhab ya Imam Malik

basi yeye alikua katika wakati wa Sala zake basi kila akisoma Surat Takathur akifika

katika aya ya mwisho isemayo:

‏﴿ثمُ َّ لَتُسْأَلُن َّ يَوْمَئِذٍ‏ عَنِ‏ ٱلن َّعِيمِ‏ ﴾

Thumma latus-alunna yawma-idhin AAani alnnaAAeemi (Surat Takathur 102:8)

Tafsir: Na kisha Mtaulizwa katika siku hio kuhusiana na Neema Mlizopewa.

Basi Imam Malik alikua anairudia aya hii na kuirudia huku akilia sana kutokana na

kuguswa na maana ya maneno aya hii. Na vile vile kwa upande wa Imam Sufyan Ath

Thawry yeye alikua pia na hali kama hii ya kurudia na kuirudia rudia aya huku akilia

wakati anaposali pale anapofikia katika aya ya ya 5 ya Surat Al Fatiha isemayo:

‏﴿إِ َّ كَ‏ نَعْبُدُ‏ وإِ َّ كَ‏ نَسْتَعِينُ‏ ﴾

Iyyaka naAAbudu wa-iyyaka nastaAAeenu(Surat Al Fatiha 01:05)

Tafsir: Hakika wewe tu ndie tunaekuabudu na ni wewe tu ndie tunaekuomba

Msaada.

Na alipoulizwa kwanini hua ni mwenye kuiruda rudia aya hii huku akilia basi Imam

Sufyan Ath Thawry alisema: ‘Kwa sababu sisi tunasema kua tunamuadudu Allah

Subhanah wa Ta’ala na kumtegemea lakini ukweli ni kua sisi hua tunategemea

Dinari na Dirham.’

Na alisema Said Ibn Muadh kua: ‘Hakika mimi nna sifa tatu ambazo hua nna hamu

sana kushikamana nazo mda wote, na hapo nitakua mzuri sana. Wakati wa kusali

hua sifikirii kitu chochote isipokua Sala nnayoisali, nikisikia hadith yeyote kutoka

kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi hua sina shaka nayo na

nnapohudhuria kwenye Maziko basi hua sifikirii chochote isipokua Maziko hayo

na kile kinachotakiwa ndani yake.’

Hivyo tunapozungumzia kuhusiana na Khushuu au unyenyekevu basi hua ni kitu

muhimu sana kuwemo ndani ya Sala, kwani bila ya kua nayo khushuu ndani yake basi

tutakua hatujatofautiana na Wanafiq ambao wao juu ya Sala zao wana hali ya Sahuun

na Kaslan, na ndio maana katika kujaribu kujitofautisha na hali yao basi ikawa

inapendekezwa kujitenga na kila kitu ambacho kitapelekea kukuondolea umakini wako

kwenye Ibada ya Sala kama alivyosema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pale


334

alipoingia kwenye Jengo la Al Kaabah na kusali rakaa mbili, lakini kabla ya kusali basi

aliona kua pembeni kuna pembe mbili za Kondoo.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam baada ya kumaliza kusali Sala yake basi

alimwambia Uthman Al Hajabi kua: ‘Nilisahau kukwambia kua uzifunike hizo

pembe mbili, kwa sababu haitakwi ndani ya Nyumba kua na kitu ambacho

kitamshughulisha mtu mwenye kufanya Ibada.’(Imam Abu Daud)

Na ndio maana pia akasema Imam Abu Sulayman Hamd Ibn Muhammad Al Khattabi

Al Shafii kua: ‘Ama kuhusiana na kusali nyuma ya watu ambao watakua

wanazungumza, basi kwa upande wa Imam Al Shafii na Imam Ahmad Ibn Hanbal

basi wao wanasema kua ni Makruuh, na pia kua mazungumzo yao hayo hua

yanamshughulisha mfanyaji Ibada.’

Na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliwaambia Masahaba zake kua: ‘Hakika

nyinyi nyote mnapokua mnasali basi hua mnazungumza na Mola wenu, hivyo

msishughulishane na msinyanyue sauti zenu mnapokua mnasoma au ndani ya

Sala’(Musnad Imam Ahmad)

Ambapo katika wakati wetu huu wa leo ndani yake watu wenye kua na sifa ya Sahuuna

na Kaslan basi hua wanaingia pia wale watu ambao hua wanaingia Misikiti huku

wakiwa na simu zao, bila ya kuzizima au bila kuondoa mlio wa sauti na kuziweka

kimya, hivyo hii pia hua ni miongoni mwa aina ya Unafiq.

Na nnasema hivi kwa sababu Muislam huyo hua hajali yuko katika sehemu gani, kwani

kuingia kwake Msikitini hua ni kutokana na mazoea tu, yaani kama vile ambavyo Mtu

ambae hua ni mwenye mazoea ya kila siku kuenda katika majengo ya kufanyia mazoezi

na hivyo ukifika mda hua anaenda kuinama na kuinuka na kujinyoosha kwa dakika

kadhaa na kisha anatoka.

Na hivyo kutokana na kuendekeza Matamanio na Mapambo ya Kidunia basi Muislam

huyu hua ni mwenye kuyakumbatia na kuingia nayo matamanio yake na mapambo yake

Msikitini wakati akiwa mbele ya Mola wake, na matokeo yake Matamanio hayo na

mapambo ya Dunia yaliyomo ndani ya Mfuko wake wa Kanzu au wa Suaruali yanaanza

kumwita kwa mlio wa simu uwe wa mziki au mwengineo wakati yeye akiwa

anamsujudia Mola wake, na hivyo baada ya kuitwa huko na simu yake hio basi akili

yake hua kwa haraka sana ni yenye kuruka kutoka kwenye Sala na faham za kua yuko

mbele ya Mola wake na kuhamia kwenye Mapambo ya kidunia yaliyomo mfukoni

mwake.


335

Hapo hapo Muislam huyo hua ni tayari ni mwenye kuonyesha Dharau mbele ya Mola

wake, kujitoa kwenye Khushuu ya Sala yake na pia kuwatoa kwenye Khushuu za Sala

zao wenzake anaosali nao pamoja na kuwashughulisha kwa kuendekeza kuyakumbtaia

matamanio ya Dunia yake.

Hivyo inatakiwa kila mmoja wetu kujua kua unapokua unasali hua si kua upo mbele ya

Hakimu ambae haoni wewe umetia nini mfukoni mwako au unafikria nini ndani ya

Moyo wako, bali hua uko mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala ambae ni mwenye kuona

kusikia na kujua kila kitu juu yako na juu ya viumbe vyote na vitu vyengine vyote

vilivyokuzunguza katika mazingira yako na hivyo basi kama hukuzima sala yako hua

unakua ni miongoni mwa wenye kumvunjia heshima na kumuonesha dharau Mola wako

na hivyo kua ni miongoni mwa Fawaylun lil Mussalina alladhiina hum Aan Salatihim

Sahuuna na pia miongoni mwa Waidha Kamu Salati Qamu Kusala na kwa maana hio

hua hua ni mwenye kusali huku ikimilaani Sala yake hio.

Na kuhusiana na wale wenye sifa ya Alladheena hum yuraoona ambao ni wenye kufanya

Riya. Kwani wenye kufanya Riya hua ni tofauti ni wenye kufanya Unafiq, na tofauti yao

ni kua Mnafiq hua hana imani kabisa na hivyo hua ni mwenye kuficha hali ya kutoamini

kwake kwa kujionesha kufanya Ibada, ambapo kwa upande wa Mwenye kufanya Riya

basi yeye hua ni Mwenye kuamini na mwenye kufanya Mema lakini hua ni mwenye

kuyaonesha kwa watu mema yake hayo ayafanyayo.

Na bila ya shaka ni wale wenye Ikhlasi tu ndio wenye kujua kuhusiana mna Kujionesha,

wengineo wote hua hawajui na hivyo hua wanaona ni jambo la kawaida tu kufanya mema

kisha wakawa wanasifiwa nao wakwa ni wenye kujisikia raha kutokana na kusifiwa

kwao.

Na ndio maana Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari akwa ni mwenye

kuusia kwa kusema kua: ‘Tafuteni Ikhlasi ya matendo yenu kuanzia ndani kutoka

katika Nia yenu kwani ni pale tu unapokua na Ikhlasi ya kwenye nia ndio hua ni

mwenye kujua kuhisiana na Riya’

Na akasema tena Imam Abu Muhamamd Sahl Abd Allah Al Tustari kua: ‘Mja hatoonja

ladha ya Imani hadi pale atakapoachana na mambo yafuatayo: Yaliyokua Haram

kwake,Yaliyokua na Shaka, Ujinga, Vyenye Kulevya na Kujionesha. Na kisha

akawa n mwenye kushikamana na mambo yafuatayo: Kua na Ilm, Kua na usahihi

katika Matendo mema yake, Kua na Moyo Safi, Kua na Ulimi wenye Hikma, Kua

na Tabia Njema kwa watu na kua na Ikhlasi kwa Mola wake hua hajioni kwani hua

anajua Kasoro zake. ’

‘Na kwa hakika yule mwenye Kufanya Toba basi hua ni mwenye kukaa mbali na

Dhambi na hua ni Mtifu kwa Mola wake, Kwani yule mwenye Utiifu kwa Mola


336

wake hua si mwenye haja ya Kujionesha kwani hua daima yuko katika

Kumkumbuka Mola wake, na mwenye kumkumbuka Mola wake’

Kwani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliwauliza Masahaba zake kwa kusema

kua: ‘Hivi Jee nikuambieni ni kipi ambacho mimi nna kikhofia zaidi ya Masih

Dajjal?’

Masahaba Wakauliza: ‘Ni kitu gani hicho Ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hakika Mimi nnakhofia zaidi Shirk

Iliyofichikana, Ambayo ni ya kumuona Mtu akiwa Anasimama kwa ajili ya Kusali

lkisha anaipamba Sala yake kwa ajili ya wengine Ili waione’ (Sunnan Ibn Majah)

Kwani tunappzungumzia kuhusiana na Kujionesha katika Ibada kua ni Kwenye

Kumaanisha Kukadhibisha Dini na Siku ya Malipo na hivyo kua na Sifa ya Unafiq basi

hua haimaanishi katika Sala tu bali pia na katika Ibada nyenginezo kama vile alivyosema

Allah Subhanah wa Ta'ala katika Qur'an:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ لاَ‏ تُبْطِلُواْ‏ صَدَقَاتِكُم بِٱلْمَنِّ‏ وَٱلأَذَىٰ‏ كَٱل َّذِى يُنْفِقُ‏ مَالَهُ‏ رِ‏ آئَ‏ ءَ‏

ٱلن َّاسِ‏ وَلاَ‏ يُؤْمِنُ‏ بِٱهلل َِّ‏ وَٱلْيَوْمِ‏ ٱلآخِ‏ رِ‏ فَمَثَلُهُ‏ كَمَثَلِ‏ صَفْوَانٍ‏ عَلَيْهِ‏ تُرَابٌ‏ فَأَصَابَهُ‏ وَابِ‏ ‏ٌل

فَتَرَكَهُ‏ صَلْداً‏ لا َّ يَقْدِرُونَ‏ ٰ عَلَى شَيْءٍ‏ ممِّ َّا كَسَبُواْ‏ وَٱهلل َُّ‏ لاَ‏ يَهْدِى ٱلْقَوْمَ‏ ٱلْكَافِرِينَ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo la tubtiloo sadaqatikum bialmanni waal-adha

kaalladhee yunfiqu malahu ri-aa alnnasi wala yu/minu biAllahi waalyawmi alakhiri

famathaluhu kamathali safwanin AAalayhi turabun faasabahu wabilun

fatarakahu saldan la yaqdiroona AAala shay-in mimma kasaboo waAllahu la

yahdee alqawma alkafireena (Surat Al Baqara 2:264)

Tafsir: Enyi Wale ambao Mlioamini msitoe Sadaqa Zenu Kwa Kukumbusha juu ya

kutoa Kwenu au Kwa Kufanya Adha Kama yule Ambae anatumia mali yake Ili

Aonekane na Watu Huku akiwa Hamuamini Allah Na Siku ya Malipo Kwani Mfano

wake hua kama mfano wa Jiwe Gumu ambalo Juu yake Kuna Vumbi Likanyeshewa

Mvua Kubwa Sana Na kisha ikaliwacha Likiwa Wazi na Tupu Hawawezi Kufanya

chochote Juu ya kile walichokichuma na Allah Hawaongozi watu Makafiri.

Kwani tunapoiangalia Aya hii basi bila ya shaka tunaona kua ni Aya inayoenda

Sambamba kimaana na Aya ya kwanza ya Sura yetu isemayo Araayta Alladhii

Yukadhdhibu BiAlddin yaani Jee Uemuona Yule ambae ni Mwenye kukadhibisha Dini?


337

Kwani nayo pia baada ya kuainisha Kasoro za Wenye Kutoa na kisha Kujionesha na

Kusimbulia kwa Maneno kua wao Wametoa na Kukumbusha Namna walivyosaidia na

kusimbulia, kua Hawana kitu na hivyo hua ni Sawa Na Waliokadhibisha Dini na Siku ya

Malipo na hivyo Hawakumuanini Allah Subhanah wa Ta'ala na siku ya Malipo.

Ambapo Watu hawa hua Hawana Kitu na Allah Subhanah wa Ta'ala anatutolea Mfano

wa Kua Katika Kutoa kwao basi hali yao hua Kama Jiwe la Gumu na Kubwa kama Mlima

wa Safwa lililovaa Koti la Vumbi Kubwa halafu Jiwe hilo likanyeshewa Mvua Kubwa

Sana.

Ambapo katika kiweka wazi maana halisi ya aya hii basi Allah Subhanah wa Ta’ala neno

Wabilun ambalo ni lenye kutokana na neno Wabala ambalo hua linamaanisha Mvua

Kubwa Sana na yenye Matone Makubwa na Mazito sana ya Maji kiasi ya kua kama

yakikupiga basi hua yanaweza kukusababishia Madhara. Na hivyo aya kua ni yenye

kuweka wazi kua Jiwe hilo mbali ya ukubwa wake na maumbile yake ya kua na mapango

na michongoko lakini likishukiwa Wabilun basi hua ni lenye Kuvuliwa Koti lake lote la

Vumbi liliopo Juu yake na katika kila Michongoko na mapango yake na hivyo kua tupu

kiasi ya kua hata uzito wake hupungua, yaani hivyo ndivyo pia Unavyopungua Uzito wa

Kile unachokitoa baada ya Kusimbulia na Kujionesha.

Ambapo kwa upande mwengine ambao ni kulingana na Mtizamo wa Imam Muhammad

Ibn Jarir At Tabari basi yeye anasema kuhusiana na Aya hii kua:

Amesema Amr Ibn Hurayth kua: ‘Kuna Mtu alienda katika Vita Vya Jihad, na kisha

hakua ni Mwenye Kufanya Dhambi yeyoye Ndani yake lakini akawa ni mwenye

Kurudi Vitani huku akiwa hana Malipo yeyote mbele ya Mola wake’

Hivyo Amr Ibn Hurayth akaulizwa: ‘Itakuaje Hali hio?’

Amr Ibn Hurayth akasema: ‘Hii hua ni Hali ya Muislam ambae Alienda katika Vita

vilivyoamrishwa na Allah Subhanah wa Ta'ala na kisha alipofika Vitani akawa ni

mwenye Kumlaumu Kiongozi wake kwa kusema: ‘Hakika Mimi sitoenda Tena nae

Vitani Kiongozi huyu!’

Huyu hua ni Mtu ambae Hua hana Kitu katika Malipo ya Waliopigana Jihadi, na huyu

ndie yule ambae Allah Subhanah wa Ta'ala anamzungumzia kwa kusema: Enyi Wale

ambao Mlioamini msitoe Sadaqa Zenu Kwa Kukumbusha juu ya kutoa Kwenu au Kwa

Kufanya Adha Kama yule Ambae anatumia mali yake Ili Aonekane na Watu Huku

akiwa Hamuamini Allah Na Siku ya Malipo

Ya Allah! Huu ni Mtihani mkubwa Sana kwani Ukiangalia Ndani yake aya hii basi hua

Wanaingia pia Wale Ambao Wasiofuata Mitizamo ya Viongozi wao wa Dini Katika


338

Jamii zao Kiibada na Kuwakosoa na kisha badala yake Wakawa wanawafuata Kiibada

Viongozi wa Nchi Nyengine walio Mbali kabisa na Jamii zao kwa mfano kuhusiana na

Miandamo ya Mwezi. Na hii ni kwa Sababu Tunapozungumzia Riya na Kujiona na

Kujionesha katika Ibada basi tunazungumzia Bahari pana sana yenye kina kirefu sana.

‘Kwani Hakuna Mwenye Kujua kuhusiana Ujinga isipokua yule ambae ni Mwenye

Kua na Ilm.’

Ambapo anasema Shufay Ibn MaAati ambae alikua ni Tabiina amesema kua: ‘Siku Moja

Mimi Niliingia katika Mji wa Madinah na nikamuona Mtu ambae alikua

amezungukwa na watu Hivyo nikauliza Huyu Ndie Nani?’

Nami nikaambiwa kua: ‘Huyu ndie Abu Hurayra’

Hivyo baada ya kusikia Jina lake basi nami nikamsogelea Mtu huyo na kumsogelea

hadi nikamfikia katika wakati ambao watu walikua wameshapungua. Nami

nikamwambia: ‘Nakuomba kwa Al Haqq na najua kua Unasema Ukweli, hivyo

tafadhali niambie Jambo ambalo umelisikia Moja kwa Moja kutoka kwa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu akaniambia

mimi kua: Bila ya Shaka nitakuambia wewe kile ambacho mimi nimekisia Moja

kwa Moja kutoka kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na nikakifaham

ipasavyo’.

Lakini sasa kabla ya kuniambia kitu hicho basi Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu

akazimia.

Kisha baada ya Mda akapata ufaham na kizidukana na kisha kuniambia:

‘Nitakuambia Jambo ambalo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliniambia

mimi Nyumbani kwake wakati ilipokua hakuna mtu yeyote ndani ya Nyumba yake’

Kisha Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu akazimia tena, na kisha akapata faham na

kuzindukana, kisha akasema: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ameniambia

kua: Allah Subhanah wa Ta'ala atawafufua Watu katika siku ya Malipo na

kuwakusanya na atakuja kuwahukumu. Na kila mtu atakua amepiga Magoti’

Subhana Allah! Ya Allah!

Kwani hapa ndio Unaona kwanini Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu akawa ni

mwenye Kuzimia kwa Khofu ya Ujumbe uliomo kwenye Manano aliyoyasema

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, ambapo Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu

anaendelea kwa kusema: ‘Mtu wa Mwanzo kuitwa atakua ni Mtu alieisoma Qur'an

na Mtu aliepigana Jihadi na kuupata Ushahidi na Tajiri aliepewa Mali na Allah

Subhanah wa Ta'ala.’


339

Na Kisha Allah Subhanah wa Ta'ala atamuuliza Mwanazuoni wa Qur'an kwa

kusema: ‘Hivi Jee Mimi sikukufundisha wewe kile ambacho nilikishusha kwa

Mtume wangu.’

Ambapo Mwanazuoni huyo atasema: ‘Naam..Bila ya Shaka Ndio ewe Mola wangu.’

Allah Subhanah wa Ta'ala atauliza: ‘Hivyo Jee ulitumia vipi Ilm Uliyojifunza?’

Mwanazuoni huyo atasema: ‘Nilitumia usiku wangu na Mchana katika Kuisoma’

Allah Subhanah wa Ta'ala atasema: ‘La Hakika wewe Unasema Uongo!’

Na Malaika nao watasema: ‘Hakika wewe Unasema Uongo! ’

Allah Subhanah wa Ta'ala atasema: ‘Kwani wewe Ulifanya hivyo kutokana na

kutamani kua Watu waseme kua fulani ni Mwanazuoni na Watu wamesema Juu ya

hilo kuhusiana nawe’

Kisha ataitwa Mtu aliepewa Mali na kuulizwa: ‘Hivi Jee Mimi sikukuneemesha

wewe kwa Mali kiasi hukua na haja ya Kumuomba yeyoye?’

Aliepewa Mali atasema: ‘Naam..Bila ya Shaka Ulinineemsha ewe Mola wangu’

Allah Subhanah wa Ta'ala atauliza: ‘Hivi Jee Ulitumiaje Mali hio?’

Aliepewa Mali atasema: ‘Hakika Mimi niliitumia kwa ajili ya Kuunga Udugu, Kwa

kuitumia kwa ajili ya Ndugu na Jamaa zangu na Nikatoa Zakkah na Sadaqa.’

Allah Subhanah wa Ta'ala atasema: Hakika wewe Ni mwenye Kusema Uongo

Na Malaika watasema: ‘Hakika Umesema Uongo!’

Kisha Allah Subhanah wa Ta'ala atasema: ‘Wewe Uliitumia kwa sababu ya Kua na

hamu ya Kuonekana kua ni Mkarimu Na hivyo watu wakusifie, na Wamekusifia

Juu yako’

Kisha Ataulizwa Mpiganaji Jihadi aliefariki na Kupata Ushahidi: ‘Hivi wewe

Ilikuaje Mpaka Ukauliwa?’

Mpiganaji huyo atasema: ‘Ewe Mola wangu Uliamrisha kua watu wapigane Jihadi

kwa ajili yako, hivyo na mimi nimepigana na kuuliwa kwa ajili yako.’


340

Allah Subhanah wa Ta'ala atasema: Hakika wewe Unasema Uongo

Na Malaika watasema Hakika wewe Umesema Uongo!

Allah Subhanah wa Ta'ala atasema: ‘Hakika wewe Ulipigana na Kuuawa kwa

Sababu ulikua unataka watu waseme kua wewe ni Shujaa mahiri sana, na Watu

wamesema hilo kuhusiana nawe’

Kwani Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu anaendelea kusema kua: ‘Hapa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akanipiga Goti langu na kisha akasema: 'Hawa

ndio watakaokua Watu wa Mwanzo Kutumbukizwa Motoni kua kama kuni za

Moto huo’

Hivyo kila mmoja wetu anatakiwa azingatie kua hii hali ya inayohusiana na hawa watu

watatu hawa waliotajwa kwenye Hadithi hii ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam,

basi itamkuta pia kila Mmoja wetu, kwani tutaulizwa katika Kila Jambo letu tulifanya

kwa ajili gani?

Na kama hatutokua na Ikhlasi katika nia basi sote tutakua ni Miongoni mwa Alladhiina

Hum YuraaUna - Wenye Kujionesha katika Amali zao kwani amesema Allah Subhanah

wa Ta’ala kua:

‏﴿مَن كَانَ‏ يُرِيدُ‏ ٱلحَْيَاةَ‏ ٱلد ُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ‏ إِلَيْهِمْ‏ أَعْمَالهَُمْ‏ فِيهَا وَهُمْ‏ فِيهَا لاَ‏

يُبْخَسُونَ۞أُوْلَٰئِكَ‏ ٱل َّذِينَ‏ لَيْسَ‏ لهَُمْ‏ فىِ‏ ٱلآخِ‏ رَةِ‏ إِلا َّ ٱلن َّارُ‏ وَحَبِطَ‏ مَا صَنَعُواْ‏ فِ‏ يهَا

وَابَ‏ طِلٌ‏ م َّا كَ‏ انُواْ‏ يَعْمَ‏ لُونَ‏ ﴾

Man kana yureedu alhayata alddunya wazeenataha nuwaffi ilayhim aAAmalahum

feeha wahum feeha la yubkhasoona; Ola-ika alladheena laysa lahum fee al-akhirati

illa alnnaru wahabita ma sanaAAoo feeha wabatilun ma kanoo yaAAmaloona

(Surat Hud 11:15)

Tafsir: Yeyote yule anaetaka Maisha ya Kidunia na Mapambo yake tutamlipa malipo

ya amali zake ndani yake kikamilifu bila ya kumpunguzia. Hao ni wale ambao hawana

sehemu yao Akhera isipokua Moto na ni bure matendo yayo waliyoyafanya ndan yake

(Duniani na ni batili waliyokua wakiyafanya.

Kwani anasema Mujaddid Ad Din, Shaykh Ul Islami Muhyi Ad Din Imam Abu Zakarriyah

Sharaf An Nawawi kua:


341

Kujionesha hua kuko katika aina Mbili, Ambazo aina zote huzifanya Amali kua

hazina thamani

Aina ya Kwanza hua ni Kufanya Ibada kwa ajili ya kupata ukaribu na Allah

Subhanah wa Ta'ala huku ukiwa ni Mwenye Kutegemea Kusifiwa na Watu

Aina ya Pili hua ni Kufanya Ibada kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta'ala ili kupata

Kusifiwa na Watu.

Kisha Imam An Nawawi anaendelea kutuambia kua: ‘Hakuna Mtu anaeweza

Kuifahamu Riya na kuyafaham Maumbile yake kwa Namna yalivyofichikana,

Isipokua kwa yule Mtu ambae ni Mwenye kuitafuta Ikhlasi, kwani Mtu huyo hua

ni mwenye Kujitahidi Kuufaham Uhalisia wa Kujionesha ili aweze kua ni Mwenye

Kujua Uhalisia wa Ikhlas.’

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari basi yeye

anasema kua: ‘Hakuna Kitu Kigumu kwa Nafsi kama Ikhlasi na hii ni kwa sababu

Nafsi yenye Matamanio hua haiwezi kua na Ikhlasi.’

‘Na hii pia ni kwa sababu hisia za Nafsi kupenda Riya au Kujionesha hua zina

Nguvu kubwa sana kiasi ya kua huweza Kupenya ndani ya Imani imani ya Mtu.’

‘Ambapo ndani ya Imani ya Mtu hua ndio kwenye Chanzo cha Ibada za Fardhi,

hivyo basi Imani ya Mtu huweza kughilibika na kua ni ya Unafiq kutokana na

Kujionesha.’

‘Na hii huonekana wazi pale Mtu anapokua kwa Muonekano wa nje anaonekana

hana kasoro kutokana na Mtizamo wa kila mtu juu yake, lakini sasa hua ni Allah

Subhanah wa Ta'ala pekee ndie Mwenye kujua Mtizamo wa Ndani wa Mtu huyo na

mtizamo huo wa ndani ya Moyo wake unapokua tofauti na Mtizamo wa nje basi

Mtu huyo Tayari hua ni Mwenye Kufanya Riya au Kujionesha na hivyo hua ni

Mnafiq.’

‘Hivyo Basi Kitendo cha Mtu yeyote yule kitakachofanywa na kikawa ni tofauti na

Mtizamo wa Moyo wake basi hua ni kitendo cha Kujionesha kwa sababu ya

kutokana na Athari ya Watu wengine Juu yako basi hua ni Shirk.’

Kwani ili tuijue zaid Ikhlasi ili tuweze kukimbia Kujionesha basi na tumuangalie Imam

Abu Qasim Al Junayd ambae yeye anatuambia kua: ‘Ikhlasi hua ni Kitendo ambacho

ndani yake hakitafutwi kitu chochote isipokua kutafutwa Ukaribu wa Allah

Subhanah wa Ta'ala popote pale kitakapofanyika Kitendo hicho.’


342

Siku moja Amir ul Muuminin Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu alimkuta Sahaba

Muadh Ibn Jabal Radhi Allahu Anhu akiwa amekaa kwenye Kaburi la Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam huku akiwa analia, Sayyidna Umar Radhi Allahu Anhu

akamuuliza Muadh Ibn Jabal Radhi Allahu Anhu: ‘Ya Muadh mbona Umekaa hapo

huku ukawa unalia?’

Ambapo Muadh Ibn Jabal Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Hakika mimi simlilii Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam bali nnalia kutokana na kukumbuka Maneno yake

ambayo aliniambia alipokua katika sehemu hii hii kua hata sehemu Ndogo tu ya

Kujionesha hua ni Shirk’

‘Na hivyo wale watu watakao kua na Taqwa basi watakua na thamani kubwa sana

mbele ya Allah Subhanah wa Ta'ala ambao watakua:

Watakapokua hawapo katika sehemi basi Watatafutwa. Watakapo kua wapo

katika sehemu basi Hawatojulikana kama ndio wao. Hao ndio Taa za Ilm na

Viongozi wa Uongofu.’

Ambapo alisema Hasan Al Basr kua : ‘Hakika mimi nimeishi na Masahaba 70

waliopigana Vita vya Badr na kama Leo Hii Watafufuka basi Kama Nyinyi

Mtawaona Wanavyoishi basi Mtawaona kua ni Wenda Wazimu kutokana na Khofu

yao Juu ya Allah Subhanah wa Ta'ala’

‘Na Wao wakikuoneni Nyinyi Leo hii Mnavyoishi basi watasema kua Nyinyi

Hamkumuamini Allah Subhanah wa Ta'ala na hawatokujueni isipokua kwa

Kukuoneni Kibla Chenu katika Wakati mnaposali.’

Na bila ya shaka ingawamaneno haya ya Hasan Al Basr aliyazungumza kuwaambia watu

wa Jamii yake ndani ya Miaka 100 ya kwanza ya Uislam, lakini maana yake natgusua

tena sana hadi sisi leo hii. Hivyo ili kufaham zaid maana aliyokua akiikusudia Hasan Al

Basr basi hakuna mifano mizuri kuliko ile inayoonesha namna watu Wema waliotangulia

Kabla yetu walivyokua Wakiichukulia maana ya aya tunayoinglaia yasemayo Alladhiina

hum Yuraauuna - Wale ambao ni wenye Kujionesha Katika Amali zao.

Na hivyo kua ni wenye Kuogopa sana na Kuikimbia hali ya YuraaAuna kwani mfano wa

Kwanza tunakutana na Mfano wa Imam Sufyan Ath Thawry ambae yeye alikua akiingia

kwenye Mtaa na kisha akaona Mbele yake kuna watu wanaomjua, basi alikua

akibadilisha Njia, kwa Sababu ya Kuogopa kua huenda Watu hao wataanza kuoneshana

kua huyu ndio Imam Sufyan Ath Thawry Mcha Mungu Mkubwa sana.


343

Na hivyo Sufyan Ath Thawry alikua akiogopa kua huenda Kuoneshana kwao huko

kuhusiana nae huenda kukamfanya Ajisikie na Kujiona na hivyo kuhesabiwa na Mola

wake kua yeye ni Miongoni mwa wenye Kujiona katika Amali zao.

Mfano wa Pili tunachukua Mfano wa Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad

Din Imam Al Shafii Al Thani Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii ambae Darja yake kwa leo basi hakuna

anaemfikia kwani ni sawa na Mitume wa Bani Israil, kitabu chake cha Ihya Ulum Ad Din

tu kinathibitisha ukubwa wa Ilm yake na Darja yake kwani ni Imamu ambae anakubalika

na Kunukuliwa na Madhhab yote ya Kiislam ya Hanafi, Malik, Shafii, Hanbal, Ibadhi na

Shia pia, na ili kuyajua haya basi inabidi umsome na umjue kwa kumfanyia utafiti wa

kina.

Ambapo katika wakati wa kipindi cha Uhai wake basi alipofikia Umri wa miaka 40 alikua

tayari vitabu vyake vinasomwa kwenye Ulimwengu mzima wa Kiislam, hii ilikua ni hali

ambayo kwake yeye ilikua ni ya Mtihani kwani alikua kama Mfalme kwa namna watu

wanavyomkubali, hivyo akaingiwa na khofu kutokana na kuona huenda hli ho

ikabatalisha amali zake njema Mbele ya Mola wake, hivyo akaamua kujitolea kwa ajili

ya Mola wake kwan ialihisi kua md wake wote alikua akiwatumikia Waislam kwa

kuwanufaisha kwa Ilm Yake bila ya kumuangala Mola wake.

Hivyo Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani

Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al

Shafii akamua kuhama kutoka kwenye Mji wake wa Baghdad hivyo akaiweka familia

yake chini ya Usimamizi wa Kaka yake ambae ni Imam Ahmad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Ghazali na kumkabidhi fedha za matumizi yao kwa mda atakaokua hayupo

pamoja nao.

Kisha Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani

Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al

Shafii akaaga na kuondoka na kutembelea sehemu mbali mbali za Ardhi za Kiislam bila

ya kujulikana kua yeye ni nani, wala kujitambulisha na alikua akifikia katika Mji basi

alikua akifikia Miskitini na kua ni mfanyaji usafi wa Msikiti anaoufikia na kila siku

husafisha kuanzia ndani, nje mpaka vyooni, na alikua hakai mda mrefu katika Mji

anaofikia kwani kuna baadhi ya Miskiti ilikua inasomeshwa darsa kupita katika Vitabu

vyake, hali hii ilikua ikimfanya kujihisi kua huenda akaanza kujiskia ndani ya Nafsi yake

na kumkosesha Unyenyekevu mbele ya Mola wake.

Katika safari zake Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii

Al Thani Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al

Tusi Al Shafii alihama kutoka katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Damascus wa Banu


344

Ummayad baada kua ni mfanyaji Usafi wa Msikiti huo, kisha jioni moja wakati Darsa

inaendelea basi Imam Mkuu wa Msikiti huo anaesomesha Darsa aliulizwa Suali kisha

nae kajibu kwa kusema kua Kuna mitizamo tafauti juu ya hili ambapo kwa mfano Hujjat

ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Al Ghazali amesema kuhusiana na suali kua..

Ambao Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani

Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al

Shafii hapo hapo akanyanyuka na kuondoka na kuhama katika Msikiti huo kutokana na

kua na Khofu ya kua asije akaingia na hali ya kujiona kua ananukuliwa na Imam huyo

kwenye darsa hio, ambapo ili ujue ukubwa wa Ilm ya Imam huyo wa Msikiti huo aliekua

akimnukuu Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani

Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al

Shafii basi pia inabidi ujue kua tuapozungumzia Msikiti wa Banu Ummayad ambao ni

Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Damascus nchini Syria basi hua tunazungumzia Msikiti

ambao ndani yake umetoa na unatoa Wanazuoni wakubwa na darsa zake zinasomeshwa

na Maimamu wakubwa wa fani za Ilm mbali mbali za Dini ya Kiislam, kwani hata Imam

na Nawawi ametoka kwenye Msikiti huo na pia amesomesha kwenye Msikiti huo.

Vile vile katika wakati wake huo ambapo ulikua ni wa kipindi cha muda wa Miaka 10

ambayo mwisho wake alimalizia katika Masjid Aqsa na ndimo alimoandika kitabu chake

cha Ihya Ulum Ad Din, basi Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam

Al Shafii Al Thani Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al

Ghazali Al Tusi Al Shafii alifikia safari moja katika Msikiti ambao aliendelea kufanya

Usafi kama kawaida yake, ambapo siku moja wakati akiwa amelala kwa kujipumzisha

ndani ya Msikiti huo, huku Maimamu wa Msiiti huo wakiwa wanaendelea kusomesha

Darsa, basi akaja Mtu na kuwauliza suali Maimamu hao, huku yeye akisikia suali hilo

ambapo nao wakashindwa kutoa jawabu la suali hilo.

Hivyo wakati alieuiza suali aliposhindwa kupata jibu na akuamua kutoka Msikitini basi

akapitia karibu na sehemu aliyokua amejinyoosha Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az

Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad

Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii huku akiwa na muonekano unaosikitisha

kwenye Uso wake kutokana na kutopata ufumbuzi wa sual lake hilo. Hivyo Hujjat ul

Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani Imam Abu Hamid

Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii akamuita mtu

huyo na kumpa jibu la suali lake hilo.

Ambapo Mtu huyo akaanza kucheka kwa sauti na kusema: ‘Unafikiria kua mimi sikujui

wewe? Wewe si mfagiaji tu na mpigaji deki wa Msikiti huu, hivyo inakuaje inajidai

unajua jibu lake wakati wale pale unaowaona ni Maimamu wa Msikiti huu

wameshindwaa kutoa jibu lake, hivi jee unafikiria nitaweza kukuamini mimi?’


345

Baada ya kusema hivyo basi wale Maimamu walioulizwa suali basi wakaja karibu kutaka

kujua imekuaje mpaka yule mtu akawa anasema hivyo? Na walipofika na kumuuiza Mtu

huyo imekuaje basi yule Mtu akasema: ‘Kuhusiana na lile suali nililokuulizeni na

mkashindwa kulijibu basi huyu mfanya usafi hapa Msikitini amesema kua jibu lake

ni kadhaa wa kadhaa’ hivyo wale Maimamu wakaangaliana na kutafakari kisha

wakatabasamu na kusema: ‘Naam…huyu bwana itakua yuko sahih kuhusiana na

suali lako hili..Sahih’

Kisha wakamgeukia Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii

Al Thani Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al

Tusi Al Shafii huku wakiwa wamejwa na mshangao na kumuuliza: ‘Ah! Hivi wewe

umejuaje juu ya jibu lake? kwani wewe ni nani? Mbona una Ilm kubwa kiasi

hicho?’.

Ambapo hapo hapo bila ya kujibu Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din

Imam Al Shafii Al Thani Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad

Al Ghazali Al Tusi Al Shafii basi akanyanyuka kisha kisha kaenda kuchukua vitu vyake

na kuhama kutoka katika Mji wenye Msikitini huo, kwa khofu ya kutotaka kujulikana

kua yeye ni nani ili asiipe Nafsi yake nafasi ya kua ni yenye kumkosesha Unyenyekevu

kutokana na kua ni mwenye kujiona.

Naam...ukiangalia Mifano hii basi unaona uhalisi wa maneno ya Imam Hasan Al Basr

kua sisi leo hii mtu akifanya hivyo basi ataonekana ni Mwenda wazimu...lakini watu

hawa walikua wakipigana Vita na Matamanio ya Nafsi zao ili zisiweze kua na hisia za

Kujiona na hivyo kua na Ikhlasi katika Ibada zao.

Kwani mfano mwengine ni ule wa Imam Yahya Ibn Muadh ambae yeye alikua akienda

Katika Ibada ya Hija basi alikua akienda peke yake na kivyake vyake.

Alipoulizwa kwanini hakuondoka na Misafara ya Mahujaji wakienda Makka katka Ibada

ya Hijjah basi alisema kua: ‘Kuondoka na Msafara wa Mahujaji kwangu mimi hua

si chochote isipokua ni Kujionesha katika Ibada’ Na sio yeye tu bali pia Imam Abu

Ubayd alikua akisema hivyo hivyo.

Naam hivyo ndivyo watu waliotangulia kabla yetu walivyokua wakiogopa Riya au

Kujionesha katika Kila kitu chao.

Hivyo Jee Kama watu hawa watafufuliwa leo hii na kisha wakatuona mimi na wewe

tunaojiita kua ni Waislam na namna tunavyoishi watasema Tumeamini kweli?


346

Wakati kila mtu anataka ajulikane kua yeye anafuata Saudia, au anajua zaidi leo amesali

Msikiti fulani au amaeenda Umra Makkah au Kuhiji na Selfie na Video kwenye Insta,

Facebook na whatsapp n.k tunatuma

Kwani Jee na sisi mimi na wewe leo hii tukiwaona watu kama hawa hatutosema kua ni

Wendawazimu au Wanajifanya wacha Mungu Sana kwa namna wanavyomuogopa Allah

Subhanah wa Ta'ala na kuikimbia Riya na kupigana vita na Matamanio ya Nafsi zao kwa

nguvu zao zote ili wawe na Ikhlasi katika Ibada zao?

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi

kua; ‘Kuna mtu alimwambia mwenzake ambae alikua amekaa kwa mda mrefu

katika kusjudu, hivyo akamwambia baada ya Kusali kua: ‘Ingekuwa Vizuri zaidi

kama Sijda yako hiyo ungeifanya Nyumbani kwako.’ Na hii ni kwa sababu Riya hua

vigumu kuonekana na mtu aifanye kwani hua ni sawa na Sisimizi mweusi aliepo

kwenye Jiwe Jeusi tena katika Usiku wa kiza.’

Anasema Imam Jamal Al Islam Abu Qasim Ibn Hawarin Ibn Abd Al Malik Ibn Talha Al

Qushayri kua: ‘Kwa miaka mingi kulikua kuna Shaykh ambae alikua kila siku

anawahi kwenye Safu ya mbele katika Msikiti ambao alikua akisali kila siku. Siku

moja akapatwa na dharura na hivyo akachelewa kuenda Msikitini na ikambidi asali

katika Safu ya Nyuma kabisa. Kisha baada ya siku hio akawa hakuonekana tena

Msikitini hapo’

Ambapo baada ya mda alipoonekana njiani na akaulizwa kwanini siku hizi

haonekani Msikitini basi Shaykh huyo akajibu kwa kusema kua: ‘Siku zote mimi

nilikua nikisali kwenye Safu ya Mbele, kwa takriban mwaka mzima na nilikua

nahisi kua nilikua nna ikhlasi katika kusali kwangu huko. Lakini katika siku

ambayo nilichelewa kusali, basi niliona aibu kua huenda kuna mtu ataniona nikiwa

nasali katika safu ya nyuma.’

‘Kutokana na tukio hili na kuhisi kwangu huko basi nikajua kua katika kusali

kwangu kote basi mimi sikua na Ikhlasi ndani ya Sala zangu nilizosali Msikitini,

kwani nilikua na khofu juu ya namna watakavyonifikiria Waislam wenzangu, hivyo

nikaamua bora niwe nasali Nyumbani.’

Na ndio maana kwa upande wa Hujjat ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn

Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali katika Fatwa zake basi akasema : ‘Kama ikiwa

Mtu atakua anaona kua anaposali peke yake hua anakua na unyenyekevu zaidi basi

kwa mtu kama huyo hua ni bora kwake kusali peke yake nyumbani kwake.’

Mujaddid Ad Din Shaykh ul Islam Imam Abu Zakarryah Sharaf An Nawawi anasema kua:

‘Ni vigumu sana kwa Mtu kua ni Mwenye uwezo wa kuijua Riya, na kuyajua


347

maumbile ya uficho wake, hivyo ili mtu uwe ni mwenye kua na uwezo wa kujiua

Riya basi inabidi kwanza ujue uhalisi wa Ikhlasi’(Bustani Al Arifin.)

Ambapo amaesema Imam Abu Qasim Al Junayd kua: ‘Ikhlasi hua ni kitendo ambacho

ndani yake hakitafutwi kitu chochote isipokua Ukaribu wa Allah Subhanah wa

Ta’ala Popote pale kitakapofanyika kitendo hicho.’

Ambapo alisema Imam Abu Yazid Al Bistami kua: ‘Hakika mimi nilikua mhunzi wa

Nafsi yangu kwa Muda wa miaka 12, ambapo baada ya miaka mitano nikakiona

kioo cha Moyo wangu, na kisha baada ya mwaka nikaanza kuuchunguza Moyo na

Nafsi yangu, na nikaanza kuona ufuniko kwenye Moyo wangu, hivyo nikatumia

miaka 12 kuukata ufuniko huo, halafu ghafla nikaona ufuniko juu ya Nafsi yangu

na hivyo nikatuma miaka 5 kuukata na kisha baada ya hapo ndio nikapata Ufunuo,

na baada ya hapo ikawa nikiwangalia viumbe basi hua nawaona kua ni wafu (yaani

hawawezi kumnufaisha wala kumdhuru, hawawezi kumpungizia wala

kumuongezea chochote) na hivyo nikaanza kumkuzisha Mola wangu mara nne zaid.

Na akasema Imam Abu Said Al Kharaz kua: ‘Ikhlasi haiwezi kua Ikhlasi isipokua pale

inapokua na Usadikisho na Subra ndani yake, na Subra haiwezi kua ni Subra

sipokua pale inapokua na Ikhlasi na Usadikisho ndani yake na Usadikisho hauwezi

kua Usadikisho isipokua pale utakapokua na Ikhlasi na Subra ndani yake.’

Na akasema tena Imam Abu Qasim Al Junayd kua: ‘Mtu mwenye kufanya Ibada kwa

Ikhlasi hua ni mwenye kubadilisha Ufanyaji wa Ibada zake mara 40 kwa siku,

ambapo Mtu mwenye Unafiq hua ni mwenye kudumu na hali yake hio hio kwa

Miaka 40 ’ yaani Mtu huyo huyo hua si mwenye kuridhika na namna ya kufanya Amali

hio hio moja katika hali moja tu kila siku, bali hua ni mwenye kutafuta njia ya kuboresha

Amali zake katika kila hali, ambapo katika hili ndio tunaona umuhimu wa kutafuta Ilm

yaani mtu hutakiwi kua ni mwenye kutosheka na I’lm uliyokua nayo tu kama walivyo

wengi miongoni mwa Waislam wa leo, bali unatakiwa uwe ni mwenye kutafuta Ilm zaid

na kutafakkari zaidi ili kuboresha amali zako kwa Ikhlasi.

Kwani anasema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an kua:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞تَنزِيلُ‏ ٱلْكِتَابِ‏ مِنَ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱلْعَزِيزِ‏ ٱلحَْكِيمِ۞إِ َّ أَنزَلْنَآ إِلَيْكَ‏

ٱلْكِتَابَ‏ بِٱلحَْقِّ‏ فَٱعْبُدِ‏ ٱهلل ََّ‏ مخُْلِصاً‏ ل َّهُ‏ ٱلدِّينِ۞أَلاَ‏ هللِ َِّ‏ ٱلدِّي ‏ُن ٱلخَْالِصُ‏ وَٱل َّذِينَ‏ ٱتخ ََّذُواْ‏


348

مِن دُونِهِ‏ أَوْلِيَآءَ‏ مَا نَعْبُدُهُمْ‏ إِلا َّ لِيُقَرِّبُوَ‏ إِلىَ‏ ٱهلل َِّ‏ زُلْفَى ۤ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ يحَْكُمُ‏ بَيْنَهُمْ‏ فىِ‏ مَا

هُمْ‏ فِيهِ‏ يخَْتَلِفُونَ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لاَ‏ يَهْدِى مَنْ‏ هُوَ‏ كَاذِبٌ‏ كَف َّارٌ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi;Tanzeelu alkitabi mina Allahi alAAazeezi

alhakeemi; Inna anzalna ilayka alkitaba bialhaqqi faoAAbudi Allaha mukhlisan

lahu alddeena; Ala lillahi alddeenu alkhalisu waalladheena ittakhadhoo min

doonihi awliyaa ma naAAbuduhum illa liyuqarriboona ila Allahi zulfa inna Allaha

yahkumu baynahum fee ma hum feehi yakhtalifoona inna Allaha la yahdee man

huwa kadhibun kaffarun (Surat Az Zumar 39:1-3)

Tafsir: Kwa Jina La Allah mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma. Teremsho la Kitabu

(Qur’an) ni kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala mwingi wa Utukufu mwingi wa

Hikma. Kwa hakika tumekushushia wewe (Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam)

kwa Haki. Hivyo Muabudu Allah pekee kwa Ikhlasi kwa ajili ya Dini yake (bila ya

kujionesha wala kumshirikisha). Kwani kwa hakika Dini ni kwake yeye Allah tu pekee.

Na wale ambao ni weye kuchukua zaidi yake Wasaidizi na (kisha wakasema): ‘Sisi

hatuwaabudu isipokua kwa ajili ya kutukaribisha karibu ya Allah’ basi kwa hakika

Allah atahukumu baina yao juu ya yale waliyokhtilafiana. Kwa hakika Allah

hawaongozi wale ambao ni wenye kukadhibisha na Makafiri.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua tunapozungumzia

kuhusiana na neno kwa Haki basi hua linamaanisha hali mbili ambapo maana ya kwanza

ni kua Kitabu kinachozungumziwa hapa yaani Qur’an kimeshushwa huku kikiwa ni

chenye kubeba Ukweli ndani yake. Na maana ya pili ni kua. Kitabu hicho kimeshushwa

kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kwani hakuna uwezekano wowote wa kua

kimeandikwa na Ibn Adam.

Kwani Imam Hasan Al Basr alikua na Rafiki yake aitwae Farazdaq. Na Farazdaq alikua

na Mke ambae pia alikua akimjua Hasan Al Basr. Hivyo ikatokea kipindi ambacho

Mkewe Farazdaq alikua anaumwa sana kiasi ya kua alikua akijua kua hatoweza kupona

kutokana na Maradhi hayo, hivyo akausia kua atakapofariki basi Imam wa Kuongoza

Sala ya Maiti juu yake awe ni Hasan Al Basr. Hivyo Mke huyu wa Farazdaq hakuchukua

mda mrefu isipokua alifariki Dunia na hivyo ulipowadia wakati wa kusaliwa basi Imam

Hasan Al Basr akaambiwa kuhusiana na namna alivyousia Maiti huyo kabla ya kufariki

kwake.

Hivyo Hasan Al Basr akaongoza Sala ya Maiti ya Mke huyo wa Rafiki yake kisha

akamuombea Dua na wakaenda Kumzika Makaburini kama kawaida. Baada ya kuzika


349

basi Hasan Al Basr akamuuliza Farazdaq: ‘Hivi Jee umejitayarisha vipi kwa ajili ya

Siku hii?’

Farazdaq akajibu: ‘Nimetayarishia Kauli ya Shahada’

Imam Hasan Al Basr akasema: ‘Bila ya Shaka Shahada ndio Nguzo Kuu ya Hema

lakini Jee vipi kuhusiana na Kamba za Hema?’

Kwani anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na Kauli hii

ya Imam Hasan Al Basr kua:

Katika Kila hema linalojengwa basi hua linahitaji Nguzo na Kamba ya Kuzuilia Turubali

la Hema husika na kisha Hema ndio litasimama hivyo Shahada hua ni Nguzo na Amali

njema hua ndio Kamba

Naam..hivyo kwa Muislam Mbali ya kua ni Mwenye kutakiwa kua ni mwenye kutamka

Shahada lakini pia Ili Uislam wake Usimame na uwe katika hali ya Msimamo Thabit

basi Muislam huyo hua ni Menye Kuhitajika Kufanya Mema kwa Kumtii kwa Ikhalsi

Mola wake aliemuumba.

Ambapo aya hizi za Surat Az Zumar 39:1-3 zinatuwekea wazi kua:

Ibn Adam anatakiwa amuabudu Allah Subhanah wa Ta’ala peke yake tena kwa

Ihklasi.

Ibn Adam anatakiwa asifuate Dini Nyengine yeyote isipokua Dini Ya Kiislam kwani

hio ndio Dini ya Allah Subhanah wa Ta’ala na ambayo yeye Muumba ameamrisha

kua ndio ifuatwe

Ibn Adam asifanye Amali njema yeyote bila ya kua na Ikhlasi ndani yake yaani

Amali hio isiwe kwa ajili ya mwengine yeyote isipokua ni kwa ajili ya Allah

Subhanah wa Ta’ala.

Kwani Vyengine Atakua ni Miongoni mwa wenye Kujionesha na hivyo kua ni Miongoni

mwa Alladhiina hum YuraAuna yaani ni mwenye kujionesha na hivyo Ibn Adam huyo

atakua ni sawa na Alitayarisha Kujenga Hema huku akiwa na Turubali na Nguzo tu, bila

ya kua na Kamba ya Kushikamanisha Turubali hilo na Nguzo hio.

Na hivyo katika Siku ya Malipo Mtu atakua na Mlima wa Amali Njema, lakini Allah

Subhanah wa Ta'ala atamwambia kuhusiana na amali zake hizo kua:


350

Hakika wewe Ulisali katika siku fulani kwa sababu tu ya kuambiwa kua Umesali lakini

mimi Ndio Mola wako ambae hakuna mwengine zaid yake Ulifunga siku fulani kwa

sababu ya fulani lakini mimi ndie Mola wako hakuna mwengine zaid yangu, Ulitoa

Sadaqa kwa sababu ya Kuonekana,n.k

Na kisha Mlima wake huo wa Amali zake njema zote alizofanya Utaporomoka kama

vile ambavyo unavyoona inavyopangwa Chungu ya Machungwa na kisha ikaanza

kuondolewa Chungwa moja baada ya moja kuanzia Chini ya chungu hio ya Machungwa

Na hivyo atakua hana pa kujihifadhi kwani Amejenga Hema bila ya kua na Kamba na

hivyo Hema limepeperuka na atajuta badala yake kwani akiangalia anaona Adhabu Kali

inamsubiri huku aliyoyategemea yote yametoweka

Amesema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua: ‘Kinyongo hakitouvamia Moyo wa yule Muislam ambae

atakaethibitisha kua na mambo matatu yafuatayo: Ikhlasi mbele ya Allah

Subhanah wa Ta’ala katika vitendo vyake, Kutoa Ushauri wa kweli kwa wenye

Madaraka na Kushikamana na Waislam katika jamii yake.’’(Imam At Tirmidhii)

Ambapo amesema Imam Dhu Nun Al Misri kua: ‘Ikhlasi hua ni yenye kukamilika pale

inapokua Mtu una usadikisho ndani yake na ni mwenye subira ndani yake. Na

Usadikisho hukamilika pale inapokua kuna Ikhlasi na Udumisho ndani yake. Na

hua kuna alama tatu za mtu mwenye Iklasi: Kwanza Mtu hua ni mwenye kuona

kua kusifiwa kwake na kulaumiwa kwake kutoka kwa Ibn Adam wenzake kua ni

sawasawa. Pili mtu huondokewa na hisia za kua ni mwenye kufanya Mema pale

anapokua anafanya Mema hayo. Tatu hua ni mwenye kusahau na kutojali

kuhusiana na Malipo kutokana na anayoyafanya.

Na hivyo Ikhlasi hua ni siri baina ya Mja na Mola wake, kwani hata Malaika hua

hawajui kitu chochote kutokana nayo, na hivyo hua hawawezi kuandika kwenye

daftari la Matendo ya Mja wanaemuandikia.’

Ambapo kwa upande wa Abu Uthman Al Maghribi basi yeye anasema kua: ‘Ikhlasi hua

ni hali ambayo Nafsi hua hajisikii raha kua nayo. Hii hua ni Ikhlasi ya wale watu

ambao ni wa kawaida. Ama kuhusiana na Ihlasi ya watu waliochaguliwa na Allah

Subhanah wa Ta’ala basi hua inawajia si kwa hutokana na kutaka kwao, bali

mambo mema yao hua ni yenye kutokana na Ikhlasi yao lakini hua hawana habari

nayo na wala hawayahesabu kua ni mema, hio ndio Ikhlasi ya waliochaguliwa’

Ambapo kwa upande wa Imam Al Ruwaym basi yeye amesema kua: ‘Ikhlasi katika

Mema hua ni kua Mtu anafanya Mema bila ya kutaka Malipo hapa Dunani wala


351

kesho Akhera na wala hataki kukirimiwa na Malaika wawili Munkar na Nakir wa

Kaburini.’

Na anasema Mmoja kati ya Wanafunzi wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah

Al Tustari kua: ‘Ijumaa Moja mimi nilienda kwa Imam Sahl Al Tustari mda Mfupi

kabla ya kuanza Sala ya Ijumaa na nilipofika baada ya kugonga Mlango wake na

Kuitikiwa basi nikaingia ndani lakini ghafla nikashtuka na kusita, hapo hapo

mlangoni kwani mbele yangu niliona kua kuna Nyoka.

Lakini hata hivyo Imam Al Tustari ambae alikua ukimbini kwake akaniambia:

‘Ingia ndani Usiwe na Khofu, kwani hakuna Ibn Adam atakaepanda Darja yake

Kiimani kama atakua anaogopa Viumbe wenzake hapa Ardhini’

Hivyo nami taratibu nikaingia ndani, nikamsalimia, nae akanishika Mkono na

kuniuliza: ‘Leo ni Ijumaa, hivi jee Unataka kwenda Msikitini pamoja Nami?’

Hivyo nami nikajibu: ‘Nataka lakini sasa tatizo ni kua tumeshachelewa kwani

kutoka hapa tulipo hadi katika Msikiti wa Ijumaa basi ni safari ya Siku nzima

nzima hivyo hatutowahi Sala ya Ijumaa’

Imam Al Tustari akatabasam na kisha akaubana Mkono wangu, na kufumba na

kufumbua mimi nae tukawa tuko mbele ya Msikiti wa Ijumaa. Hivyo tukaingia

ndani Msikitini na kisha tukasali Sala ya Ijumaa pamoja na watu wengine. Kisha

baada ya Ibada ya Sala ya Ijumaa tukatoka nje mimi na Imam Al Tustari ambae

akasimama na kisha akwa anawaangalia watu waliokua wakitoka Msikitini baada

ya Sala ya Ijumaa hio kisha akaniambia: ‘Ma-shaa Allah! Msikiti una Watu wengi

Sana wanaosimamia La Ilaha Illa Allah, lakini inasikitisha kuona kua Ndani yake

Miongoni mwa hawa wanaotoka basi ni Wawili watatu tu ndio wenye Ikhalsi, kwani

takribn wengine wote ni wenye Kujionesha’

Naam huyo ni Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari ambae ni Miongoni

mwa Mawalii wa Allah Subhanah wa Ta'ala. Ambae alizaliwa mwaka mmoja kabla ya

kufariki Imam Muhammad Idris Al Shafii, yaani mnamo mwaka 203 Al Hijra na alisoma

pamoja na Imam wa Hadith Imam Abu Daud na alikua pamoja na Dhu Nun Al Misri.

Ambapo Imam Adh Dhahabi alisema kuhusiana na Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd

Allah Al Tustari kua: ‘Imam Al Tustari alikua ni Shaykh Al Arifin yaani Shaykh wa

wenye Kujua.’

Ambapo alisema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Mtu

yeyote yule atakaemfumbia Jicho Allah Subhanah wa Ta'ala kwa sekunde Moja tu,

basi kamwe Mtu huyo hatokua ni Miongoni mwa Walioongoka’


352

Naam..sijui jama tumeifaham kauli hii ama la, lakini kama hatujaifaham basi inabidi

tufaham kua Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anamaanisha kua:

Ibn Adam hutakiwi kumfumbia jicho lako Mola wako hata kwa sekunde moja

kwani kufanya hivyo hua kunamaanisha kua ni Kumsahau Mola wako na kujidai

kua kama hayuko na hivyo ukawa unafanya yako, kwani ukifanya hivyo basi hua

inamaanisha kua tayari umeshapotea njia na hivyo sasa unaanza kutokwa na

Ikhlasi na kuanza kufanya Mambo yako kwa ajili ya Viumbe wenzako badala ya

Mola wako.

Hivyo kutokana na Mtizamo na ufafanuzi huu wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd

Allah Al Tustari basi tunaona kua Unapokua Unafaham maana ya Tawhid au

Kumpwekesha Allah Subhanah wa Ta'ala bila ya kumshirikisha basi hua kunakufanya

wewe usiwe ni mwenye Kujionesha, kwa sababu unakua unajua kua wengine wote

hawastahiki Kile ambacho anastahiki Mola wako kutoka kwako.

Hivyo hapa inabidi rutafakkari na kuulizana tena kua kama ikiwa Imam Abu Muhammad

Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari alisema kuhusiana na Watu walioishi katika Mwaka wa

Karne ya 2-3 ya Kiislam kua Wengi ni wenye Kusema La Ilaha Illa Allah, lakini hawana

Ikhlasi na Badala yake ni wenye Kujionesha Hivi Jee itakuaje hali yetu leo hii sisi mimi

na wewe?

Kwani alisema Imam Ali Ibn Sahl kua: ‘Mtu unapokimbilia kufanya Mema basi hua

ni dalili ya kupata Kasi kutoka kwa Mola wako. Unapojizuia Kufanya Maovu basi

hii hua ni Dalili ya kua ni Mwenye Tahadhari. Unapokua Unahifadhi Siri za Moyo

wako na Mioyo ya wengine basii hii hua ni dalili ya Kupata Ufunuo, na Unapokua

unajionesha basi hua Unathibitisha Ujinga wako. Na yeyote yule asiesimamisha

vizuri msingi wa Jitihada zake katika kujiboresha Kiimani basi kamwe hatofikia

Malengo stahiki yanayotakiwa kufikiwa Kiimani’

Na Imam Sufyan At Thawri alimuandia barua rafiki yae aliekua akiishi Syria aitwae

Abbad Ibn Abbad Al Khawwas Al Arsufi na kumwambia: ‘Faham kua uko katika

waati ambao Masahaba wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam walikua

hawataki kukutana nao, na wao walikua na I’lm ambayo sisi leo hii hatuna kwani

wao walikua na vyanzo vya llm ambavyo sisi hatuna. Hivyo itakuaje hali yetu sisi

kuufikia wakati huu huku tukiwa hatuna Ilm kubwa kiasi hicho? Hatuna Subra?

Hatuna wasaidizi katika kufahamishana lipi Jema, lipi Ovu miongoni mwa watu na

Duniani kwa ujumla? Hivyo chukua lile lililo sahih ushikamane nalo.

Na nami nakuusia wewe kubakia kutokua na Umaarufu, kwani huu ni wakati wa

kubakia katika hali ya kutojulikana na kutojionesha, kwani wacha Mungu hua ni

wenye kuogopa kujionesha, na kua ni wenye kutegemea kupata Ikhlasi katika Ibada

zao, Na usijichanganye na watu, kwani ilikua watu wakikutana hua ni wenye


353

kunufaishana katika akhera yao lakini leo hii hakuna hali hio katika kukusanyika

kwa watu. Hivyo ni bora zaid kutojichanganya nao.’

Na kwa upande mwengine basi kuhusiana na maneno yasemayo:

‏﴿ٱل َّذِينَ‏ هُمْ‏ يُرَآءُونَ‏ ﴾

Alladheena hum yuraoona (Surat Al Maun 107:6)

Tafsir: Wale wenye kufanya Mema ili waonekane.

Hapa inabidi tufahamu kua aya hii haiendani kinyume na ile aya ambayo tuliyoiangalia

hapo kaba ya Surat Adh Dhuha ambayo inasema:

‏﴿وَأَم َّا بِنِعْمَ‏ ةِ‏ رَبِّكَ‏ فَحَ‏ دِّثْ‏ ﴾

Waamma biniAAmati rabbika fahaddith.(Surat Adh Dhuha 93:11)

Tafsir: Na kuhusiana na Neema za Mola wako zihadithie.

Ambapo kuhusiana na maana ya maneno haya basi kwanza tumuangalie tena Thabit Ibn

Qays Radhi Allahu Anhu alikua ni Muandishi wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na hivyo alikua ni mtu mwenye kupenda kuonekana kua amependeza kila wakati, na

hivyo iliposhushwa ile aya isemayo:

‏﴿وَلاَ‏ تُصَعِّرْ‏ خَد َّكَ‏ لِلن َّاسِ‏ وَلاَ‏ تمَْشِ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ مَرَحاً‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لاَ‏ يحُِب ُّ كُل َّ مخُْتَالٍ‏

فَخُورٍ‏ ﴾

Wala tusaAAAAir khaddaka lilnnasi wala tamshi fee al-ardhi marahan inna Allaha

la yuhibbu kulla mukhtalin fakhoorin, (Surat Luqman 31:18)

Tafsir: Na usigeuze uso wako kwa kujiona, na wala usitembee kwa madaha. Kwani

kwa hakika Allah hawapendi wenye kujivuna kwa fakhari.

Basi Thabit bin Qays Shammas Radhi Allahu Anhu hakutoka nje akawa ni mwenye kukaa

ndani kwake tu na kulia kwani alihisi kua ayah hii inamzungumzia yeye katika wakati

anapotoka hukua akiwa amevaa mavazi yake mazuri na ya kupendeza, lakini sasa


354

akaanza kuona kua kupendeza kwake imekua kunamuonesha kua ni mwenye kujiona na

kua na fakhari

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipoipata habari hii ya Thabit bin Qays

Shammas Radhi Allahu Anhu basi akatuma mtu ili akaulizwe kwanini amekua akijifungia

ndani na kulia tu na kufaya Istighfar?, na hivyo Thabit bin Qays Shammas Radhi Allahu

Anhu akajibu: ‘Hakika mimi napenda nikitoka niwe nimevaa nguo Nzuri’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hakika wewe sie ulietajwa

kwenye Ayah hii, kwani wewe ni mwenye kuishi Maisha mazuri na utaendelea

kuishi Maisha vizuri, na Allah Subhanah wa Ta’ala atakuingiza Peponi.’

Na hata Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akiwashauri watu wake wanaotoka

kwenye kufikisha ujumbe wa Dini ya Kiislam mbele ya Makafiri kua ni wenye kuvalia

nguo nzuri ili kuuwakilisha Uislam katika hali hali ya ubora wake.

Hivyo inaruhusika kuonesha Neema ulizojaliwa kupewa na Mola wako bila ya kua na

kibr au kujiona pia baadhi ya mambo katika kufanya Ibada za fardhi kwa ajili ya kuwatia

ari Waislam wawe ni wenye kufanya mema kama inavyosema aya ifuatayo:

‏﴿إِن تُبْدُواْ‏ ٱلص َّدَقَاتِ‏ فَنِعِم َّا هِىَ‏ وَإِن تخُْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا ٱلْفُقَرَآءَ‏ فَهُوَ‏ خَيْرٌ‏ ل َّكُ‏ مْ‏

وَيُكَفِّرُ‏ عَنكُم مِّن سَيِّئَاتِكُمْ‏ وَٱهلل َُّ‏ بمَِا تَعْمَلُو نَ‏ خَبِيرٌ‏ ﴾

In tubdoo alssadaqati faniAAimma hiya wa-in tukhfooha watu/tooha alfuqaraa

fahuwa khayrun lakum wayukaffiru AAankum min sayyi-atikum waAllahu bima

taAAmaloona khabeerun(Surat Al Baqara 2:271)

Tafsir: Na kama Mkizidhihirisha Sadaka zenu (katika kutoa kwenu) basi ni bora,

Lakini kama mkifanya siri na kuwapa Masikini basi hua ni Kheri kwenu. Na Allah

atakusameheni katika madhambi yenu, na Allah ni mwenye kujua juu ya yale

mnayoyafanya.

Ambapo hapa aya imetumia neno FaniAaimma linalotokana na neno Naa’ama ambalo

hua linamaanisha Neema, Kuishia Maisha yasiyokua na Shida, Kua na Raha katika

Maisha, Kutokua na Mashakil. Neno Naa’ama linapoongezewa harfu Mim mbele yake

hua linatoa neno NaA’amma ambalo linamaanisha kuvumishi cha sifa ya Kua na hali ya

Ubora.


355

Na pia imetumia neno Khayrun linalotokana na neno Khara ambalo hua linamaanisha

Kupata Utajiri, Kustawi au Kunawiri Kimaisha, Kua Bora, Kua Na Kheri na Manufaa

na Faida zaidi, Kua katika hali nzuri inayopendelewa zaidi, Inayokubalika zaidi. Neno

Khara ndio lililotoa neno Khayran ambalo hua linamaanisha Ucha Mungu zaidi.

Hivyo basi ingawa maneno haya Naama na neno Khara yanafanana kimaana lakini neno

Khayrun linamaanisha kua ni Kitu bora zaid, na hivyo aya inatuthibitishia kua Kutoa

Sadaqa dhahiri mbele za watu ni Bora pale inapokua Mtu anafanya hivyo kwa Ikhlasi

yaani bila ya kua na nia ya kujionesha mbele za watu lakini hata hivyo mtu anapokua ni

mwenye Kutoa kwa Faragha au kisirisiri hua ni kufanya Ucha Mungu zaidi na hivyo

kunapendekezwa zaidi.

Naam..hivi jee tumeziona namna aya mbili hizi ambazo zimo ndani ya Sura Moja ambayo

ni Surat Al Baqara 2:164 na 2:171 namna zilivyokaa na namna zinavyosema?

Kwani ndani yake mpangilio wa aya hizi na mada inayozungumziwa ndani yake na

maana ya aya zinavyosema kwa kuanzia na aya ya 164:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ لاَ‏ تُبْطِلُواْ‏ صَدَقَاتِكُم بِٱلْمَنِّ‏ وَٱلأَذَىٰ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo la tubtiloo sadaqatikum bialmanni waal-adha (Surat

Al Baqara 2:264)

Tafsir: Enyi Wale ambao Mlioamini msitoe Sadaqa Zenu Kwa Kukumbusha juu ya

kutoa Kwenu au Kwa Kufanya Adha.

Na aya ya 2:171 ambayo inasema:

‏﴿إِن تُبْدُواْ‏ ٱلص َّدَقَاتِ‏ فَنِعِم َّا هِىَ‏ وَإِن تخُْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا ٱلْفُقَرَآءَ‏ فَهُ‏ وَ‏ خَيْرٌ‏ ل َّكُمْ‏ ﴾

In tubdoo alssadaqati faniAAimma hiya wa-in tukhfooha watu/tooha alfuqaraa

fahuwa khayrun lakum (Surat Al Baqara 2:271)

Tafsir: Na kama Mkizidhihirisha Sadaka zenu (katika kutoa kwenu) basi ni Bora zaid,

Lakini kama mkifanya siri na kuwapa Masikini basi hua ni Ucha Mungu zaidi.

Basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta'ala anabainisha hikma zake ktika aina mbili za

Ufanyajji wema kwa Ujumla ambazo ni:


356

1-Ufanyaji wa Wema unaofanywa na Mtu na kisha Kutoa Maneno ya Kujisifu na

Kukumbusha Wema au Msaada Uliofanya na Mtu husika na Kusimbulia. Ambao

hua si wa Ikhlasi bali ni wenye kua na Kibri na Kujionesha ndani yake na hivyo

haufai na hua ni Makosa kufanya hivyo kwani hua Unajifutia Malipo ya Mema

yako yote uliyoyafanya.

2-Ufanyaji Wema unaofanywa na Mtu Kwa Ikhalsi Hadharani na bila ya Kujiona

au Kusimbulia ambao hua ni Bora, na pia wa Siri siri ambao hua ni Uchamungu.

Huu hua ni Ufanyaji wema Unaohimizwa na Kupendekezwa kwani una Malipo

Makubwa.

Naam..kwa maana hio basi Muislam Unatakiwa uwe katika hali moja tu katika kila kitu

chako, yaani hali ya Kua ni Mwenye kumkumbuka Mola wako kutokana na neema zake

alikupendelea na kukujaalia wewe zaid ya wengine.

Hivyo Ukitoa Msaada, Kumfanyia Mtu wema au Ukifanya wema basi hutakiwi Uhesabu

Fadhila unazowafanyia Wengine labda kua Mimi Nimekufanyia wewe hiki na hiki, au

Nimekusaidia hili na Lile, au Kama sio Mimi basi asingejua Kitu au asingekua Vile au

Nishasomesha Sana, Nishafanya Dhikr Sana n.k

Kwani ukishasema hivyo basi unakua tayari Unasimbulia na Kujionesha na kua ni

Mwenye Adha pia kwa viumbe wenzako na kwa Mola wako. Na hivyo unaporomosha

Amali njema zako na kujifisidi na kujidhulumu Nafsi yako bila ya Kujijua.

Kama vile alivyoambiwa Abu Dhar Radhi Allahu Anhu pale alipomuuliza Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Ya Rasul Allah! Jee ipi Sadaqa ni bora zaid?’Rasul

Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Kumpa Sadaqa Mtu mwenye kuhitaji

kisirisiri na kumsaidia Mtu anaejitahidi kutafuta Riziki yake.’’

Ambapo anasema Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Itakapokua mtu anasali kikamilifu anapokua

hadharani na akafanya hivyo hivyo anapokua faragha, basi Allah Subhanah wa

Ta’ala hua ni mwenye kusema: ‘Kwa hakika huyu ndio Mja wangu wa

Kweli’’’(Mishkat Masabih)

Hapa vile vile inabidi tufahamiane pia kua tunapozungumzia kuhusiana na wale wenye

sifa ya Alladheena hum yuraoona yaani ambao ni wenye kufanya Riya. Basi ndani yake

hawaingii wale ambao ni wenye hali ya Mtu kujisikia hisia za Raha ndani ya Nafsi yake

kutokana na Kufanya Mema kwani hali hii ya hisia hizi hua si miongoni mwa Riya kwani

hii hua ni hali ya hisia ambayo mtu husika anakua anaipata pale anapokua anafanya

Jambo jema husika ambayo hua ni Ibada kwa ajili ya Mola wake tu.


357

Na hivyo Moyo wake hua umefunguka na kutanuka na Akili na Ufahamu wake hua

umezama ndani ya Ibada hio na hivyo hua ni mwenye kujihisi kua yuko yeye na Allah

Subhanah wa Ta’ala wake katika wakati huo, na hisia hizi humpa Mtu husika hisia ya

kama kuna Mto unaotiririsha hisia za Raha na Utulivu ndani ya Moyo wake na Mwili

wake, na hii ndio maana ya ile aya inayosema:

‏﴿ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ وَتَطْمَئِن ُّ قُلُوبُهُمْ‏ بِذِكْرِ‏ ٱهلل َِّ‏ أَلاَ‏ بِذِكْرِ‏ ٱهلل َِّ‏ تَطْمَئِن ُّ ٱلْقُلُوبُ‏ ﴾

Alladheena amanoo watatma-innu quloobuhum bidhikri Allahi ala bidhikri Allahi

tatma-innu alquloobu(Surat Ar Rad 13:28)

Tafsir: Wale walioamini na Nyoyo zao zikapata utulivu kutokana na Kumkumbuka

Allah, Kwani katika Kumkumbuka Allah Hupatika Utulivu wa Nyoyo.

Na anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kuhusiana na aya hii

kua: ‘Katika kumkumbuka Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kutumia Ilm basi hua

kunapatikana (Sukun) Utulivu ndani yake, na katika kumkumbuka Allah

Subhanah wa Ta’ala kwa kutumia Ufahamu basi hua kunapatikana (Tutma’inina)

utulivu ndani yake’

Hivyo Mja yeyote yule anaesema kua anafanya Dhikr basi hua anaingia katika moja kati

ya hali mbili zifuatazo: Kuna wale ambao Wanaomuogopa Allah Subhanah wa Ta’ala

kikweli na hivyo hua hawaondokewi na hali hio, hivyo hawa hua ndio wanoihisi hali

ya Mapenzi makubwa na uzito wa hisia hizo ndani ya Nyoyo zao, hawa hua ndio

wanaofanya Dhikr Allah na ndio wanaoishi kwa ajili ya Mola wao, Akhera yao, Ilm

na Sunnah.

Halafu kuna wale ambao wanaosema kua wanahisi uzito wa hisia hizo, furaha na

raha katika kila hali. Hawa hua ndio wenye kuishi kwa ajili ya Ibilisi, Dunia hii,

Ujinga na Bidaa, hawa ndio watu wabaya zaidi.

Kwani siku moja Hasan Ibn Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu aliambiwa: ‘Watu

wanasema kua wewe ni mwenye kujiona’ ambapo nae akajibu: ‘Hakika mimi si

mwenye kujiona bali ni mwenye kujiheshimu na kuijua thamani yangu, kwani hii

hali niliyokua nayo mimi inahusiana na kujiheshimu kunakoenda sambamba na

unyenyekevu na kujitosheleza ambako hakuathiriki kutokana na Umasikini’

Ambapo anasema Jarrah Allah Imam Al Zamakhshari kua: ‘Kuna tofauti baina ya

kujiona na kujiheshimu, ambapo ni wale wenye kua na Ilm hua ni wenye kuweza

kutofautisha baina ya sifa ya kujiona na sifa ya kujiheshimu Nafsi yako.’


358

Na kwa upande wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye anasema

kua: ‘Kujiheshimu na Kujithamini hua si sawa na Kujiona na Kua na Kibr, kwani

kujiheshimu hua ni Wajibu wa Muumini ambae hua hatakiwi kuidharau thamani

yake.

Wakati Kujiona hua kunatokana na Mtu kutoijua thamani yake na huku

Kujiheshimu hua kunatokana na Mtu kua ni mwenye kuijua Thamani yake, hivyo

hali ya kujiheshimu hua inakaribiana kimaana na Kujiona isipokua hua

zinatofautiana kiuhalisia.’

Ama kuhusiana na maneno yasemayo WayamnaAAoona almaAAoona

‏﴿وَيمَْنَعُونَ‏ ٱلْمَاعُونَ‏ ﴾

WayamnaAAoona almaAAoona(Surat Al Maun 107:7)

Tafsir: Na Wenye kukataa Maaun (Kutoa japo kitu kidogo).

Basi neno MaAun hua linamaaanisha Kusafiri masafa marefu kwa kasi kubwa sana.

Mtiririko wa Maji, Kutoa Kitu kirahisi, Kutoa Sadaka, Zaka, Kua na Ukarim wa kusaidia

au kutoa vitu vidogo vidogo vyenye maana kimatumizi kama Sindano, Uzi, Chumvi,

Kibiriti n.k kwa ajili ya kuwapa Majirani wanapokua na shida navyo.

Ambapo kwa upande wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye

anaema kua: ‘MaAun ni vitu vidogo vidogo vinavyotumika Nyumbani’ ambapo kwa

upande wa Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua: ‘MaAun

ni Vitu vidogo vidogo ambavyo watu huazimana kama Nyundo, Ndoo, mkoba, n.k’

Imam Bukhari basi yeye anasema kua neno hili linamaanisha Ma’ruf Kullun yaani Kila

Jambo Jema, na baadhi ya Wanazuoni wametafsiri manemo haya WayamnaAAoona

almaAAoona kua ni yenye kumaanisha kua: Watu hawa ni wenye kukataa kutoa

Zaka.

Hivyo aya zinatuonesha kua baada ya kuzungumzia Ubakhili wa Kiibada yaani katika

Sala basi aya zinazungumzia kuhusiana na Ubakhili wa Mali kwa kuwataja wale ambao

ni ‘WayamnaAAoona almaAAoona’ yaani Na Wenye kukataa Maaun (Kutoa japo kitu

kidogo) kwani kama ikiwa mtu anashindwa kutoa vitu ambavyo havina thamani juu yake

basi atategemewaje katika kutoa vitu vyenginenyo, kama Sadaka, Zakah, n.k?


359

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimwambia Bibi Aisha Radhi Allahu Anha kua:

‘Ewe Aisha Hakika Allah Subhanah wa Ta'ala ni Mpole na Mkarimu na ni mwenye

Kupenda Upole na Ukarimu hivyo hua ni Mwenye Kulipa kwa Ukarimu Kile

ambacho hakitolewi kwa Ugumu na hua Halipi chengine zaid yake’(Sahih Muslim)

Na akasema tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Yeyote yule

atakaemrahisishia Muislam mwenzake matatizo yake ya Kidunia, basi Allah

Subhanah wa Ta'ala atamuokoa Mtu huyo kutokana na matatizo yake ya Kiakhera.

Yeyote yule atakaemsaidia Muislam Mwenzake kulipa Deni lake ambalo hawezi

kulilipa basi Allah Subhanah wa Ta'ala atamrahisishia Matatizo yake hapa Duniani

na Kesho Akhera Yeyote yule atakaeficha Siri za za Muislam Mwenzake basi Allah

Subhanah wa Ta'ala atamfichia Siri zake kesho Akhera’(Sahih Muslim)

Ambapo Siku moja Aisha Radhi Allahu Anha Alimuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kuhusiana na vitu ambavyo havitakiwi kukataliwa, Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akasema: ‘Maji, Moto na Chumvi.’ Hivyo Aisha Radhi Allahu Anha

akasema: ‘Kwa hakika tunafahamu kuhusiana na umuhimu wa Watu kua ni wenye

kuhitaji Maji, lakini jee ni vipi kuhusiana na Moto na Chumvi.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Mtu anaetoa Moto atapata malipo

ya kutoa Sadaqa kwa kila kitakachopikwa na na Moto huo, na mtu anaegawa

Chumvi atalipwa kua ametoa Sadaka katika kila chakula kitakachopikiwa na

kutiwa ladha na Chumvi hio. Na mtu anaempa Muumini maji funda moja katika

sehemu ambayo haina matatizo ya Maji basi hua ni sawa na mtu aliemuachia huru

Mtumwa. Na mtu atakaempa funda moja la Maji Muumini katika sehemu ambayo

haina maji basi hua ni sawa na alieokoa Uhai wa Mtu.’(Al Mishkat)

Hadith inatuonesha kua kumpa Muislam mwenye kiu Funda moja la Maji katika sehemu

isiyokua na Maji basi hua ni Sawa na Kumuachia Huru Mtumwa ambacho ni tu kidogo

sana. Lakini Jee tunajua Thamani ya Kuamchia Huru Mtumwa?

Naam Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kama Muislam

akimuachia Huru Mtumwa basi Allah Subhanah wa Ta'ala atamuokoa Muislam

huyo na Moto kwa kila sehemu yake ya Mwili kutokana na Kuuokoa Mwili wa

Mtumwa huyo kutokana na Utumwa’ (Sahih Al Bukhari)

Ambapo kuhusiana na kumpa maji mtu katika sehemu ambayo Maji hakuna kua ni sawa

na kumpa uhai mtu basi amesema pia Allah Subhanah wa Ta’ala kuhusiana na kumpa

Uhai mtu mmoj kua ni:


360

‏﴿مِنْ‏ أَجْلِ‏ ذٰلِكَ‏ كَتَبْنَا ٰ عَلَى بَنيِ‏ ۤ إِسْرَائِيلَ‏ أَن َّهُ‏ مَن قَتَلَ‏ نَفْساً‏ بِغَيرِْ‏ نَفْسٍ‏ أَوْ‏ فَ‏ سَادٍ‏

فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَكَأَنم ََّا قَتَلَ‏ ٱلن َّاسَ‏ جمَِيعاً‏ وَمَنْ‏ أَحْيَاهَا فَكَأَنم ََّا أَحْ‏ يَا الن َّاسَ‏ جمَِيعاً‏ وَلَقَ‏ ‏ْد

جَآءَتْهُمْ‏ رُسُلُنَا بِٱلّبَيِّنَاتِ‏ ثمُ َّ إِن َّ كَثِيراً‏ مِّنْهُمْ‏ بَعْدَ‏ ذٰلِكَ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ لَمُسْرِفُونَ‏ ﴾

Min ajli dhalika katabna AAala banee isra-eela annahu man qatala nafsan bighayri

nafsin aw fasadin fee al-ardhi fakaannama qatala alnnasa jameeAAan waman

ahyaha fakaannama ahya alnnasa jameeAAan walaqad jaat-hum rusuluna

bialbayyinati thumma inna katheeran minhum baAAda dhalika fee al-ardni

lamusrifoona (Surat Al Maidah 5:32)

Tafsir: Kutokana na hayo tuliyowaamrisha watu wa Bani Israil basi ni kua kama Mtu

akiiua Nafsi moja bila ya kulipiza kisasi cha Kuua basi hua ni sawa na alieua

Ulimwengu Mzima na Mtu yeyote atakaokoa uhai wa Mtu mmoja basi hua ni sawa na

alieokoa Uhai wa watu wa Dunia nzima. Na kwa hakika walikuja kwao wao Mitume

wetu na mabainisho yetu, lakini hakika wengi miongoni mwao baada yake wakawa ni

wenye kuendelea kufanya israfu.

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Mtu alieamini (Allah Subhanah

wa Ta'ala) hua ni Mkarimu, kwani hakuna Jema kwa yule Mtu ambae Si Mkarimu

wala si Mwenye Urafiki’ (Musnad Imam Ahmad)

Na akasema tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Ukarimu hauwezi

kuonekana katika kitu chochote isipokua Utaongeza Uzuri wa Kitu hicho. Na

Hauwezi kukosekana katika Kitu chochote isipokua Utakitia Dosari kitu hicho

kutokana na kukosekana kwake’(Imam Muslim)

Siku Moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliwauliza Masahaba zake kwa

kusema: ‘Hivi Jee nikuambieni juu ya yule Mtu ambae ataharamishiwa na Moto?’

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam mwenyewe akajibu kwa kusema kua: ‘Ni

yule Mtu ambae anakaribika, Mkarimu na mwenye Misimamo ya kati na

kati’(Imam At Tirmidhii)

Kwani amesema Aisha Radhi Allahu Anha kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam aliomba Dua kuwaombea Watu wa Ummah wake kwa kusema: ‘Ya Allah!

Yeyote yule atakaekua na huruma juu ya Ummah wangu basi mimi nakuomba

wewe kua uwe na Huruma juu yake Mtu huyo, na yeyote yule atakaekosa huruma


361

juu ya Ummah wangu basi mmi nakuomba wewe umfanyie ugumu katika mambo

mambo yake.’’ (Musnad Imam Ahmad)

Naam, Allah Subhanah wa Ta’ala anafananisha hali ya mtu asiemjali Yatima ambae hua

pia ni Maskini kua ni sawa na mtu ambae anakadhibisha kuwepo kwa siku ya Malipo, na

kuamini kuwepo kwa siku ya Malipo hua ni sehemu ya Nguzo za Imani ya Dini ya

Kiislamu, na kwa maana hiyo basi mtu anaemfukuza na asiemjali Yatima basi hua ni

sawa na mtu ambae amevunja Nguzo ya Imani ya Dini yake na hivyo kua si Muislam, na

hata kama alikua ni Muislam basi atakuja kujuta katika siku ya Malipo pale atakapopewa

kitabu chake kwa mkono wa kushoto kama zinavyosema aya:

‏﴿وَأَم َّا مَنْ‏ أُوتِىَ‏ كِتَابَهُ‏ بِشِ‏ مَالِهِ‏ فَيَقُولُ‏ يٰلَيْتَنىِ‏ لمَْ‏ أُوتَ‏ كِتَابِيَهْ۞وَ‏ لمَْ‏ أَدْ‏ رِ‏ مَا

حِ‏ سَابِيَهْ۞يٰلَيْتَهَا كَانَ‏ ‏ِت

ٱلْقَاضِيَةَ۞مَآ أَغْنىَٰ‏ عَنىِّ‏ مَالِيَهْ۞ه َّلَكَ‏ عَنىِّ‏ سُلْطَانِيَهْ۞‏

‏ِذرَاعاً‏ فَاسْ‏ لُكُوهُ۞‏

خُذُوهُ‏ فَغُل ُّوهُ۞ثمُ َّ ٱلجَْحِ‏ يمَ‏ صَل ُّوهُ۞ثمُ َّ فىِ‏ سِ‏ لْسِ‏ لَةٍ‏ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ‏

إِن َّهُ‏ كَانَ‏ لاَ‏ يُؤْمِنُ‏ بِٱهلل َِّ‏ ٱلْعَظِيمِ۞وَلاَ‏ يحَُض ُّ عَلَى ٰ طَعَامِ‏ ٱلْمِسْكِ‏ ينِ‏ ﴾

Waamma man ootiya kitabahu bishimalihi fayaqoolu ya laytanee lam oota

kitabiyah; Walam adri ma hisabiyah; Ya laytaha kanati alqadhiyatu; Ma aghna

AAannee maliyah ; Halaka AAannee sultaniyah, Khudhoohu faghulloohu;

Thumma aljaheema salloohu; Thumma fee silsilatin dharAAuha

sabAAoona dhiraAAan faoslukoohu; Innahu kana la yu/minu biAllahi

alAAadheemi; Wala yahuddu AAala taAAami almiskeeni (Surat Al Haaqah 69:25-

34)

Tafsir: Na ama yule atakepewa Kitabu Chake kwa Mkono wa Kushoto basi atasema:

‘Natamani bora nisingepewa hesabu yangu’; Na kamwe nisingejua ikoje Hesabu

yangu; Ya Laiti! huu(bora) ungekua ndio mwisho wangu’. ‘Mali zangu hazikunifaa

kitu’, ‘Yako wapi Mamlaka yangu?; (Itaamrishwa)’Mkamateni na Mfungeni’; ‘Kisha

Mtupeni Ndani ya Moto Mkali sana’; ‘Kisha Mfungeni kwa minyororo ambayo

ukubwa wake ni dhiraa 70’; ‘Kwani kwa hakika alikua Hamuamini Allah Mtukufu’;

‘Na hakua ni mwenye kuhimiza kuwalisha Maskini’

Hivyo Allah Subhaanah wa Ta’ala anatuonesha umuhimu wa kuwajali Mayatima na

kutufunza namna ya kutekeleza majukumu ya kuwalea na kuwasimamia Mayatima

kupitia katika kisa hiki cha Maryama Bint Imran pale alipolelewa na Nabii Zakariyyah

kua ni sehemu ya Kufanya wema, na kua ni sehemu ya kutekelezea Mamrisho ya Allah


362

Subhnah wa Ta’ala na hivyo kua ni sehemu ya kutokadhicshisha Dini na Kuwepo kwa

siku ya Malipo na hivyo kutokua na sehemu ya Unafiq ndani ya Moyo wako.

Na mtu unapokua huna Unafiq ndani ya Moyo wako, na hivyo kua ni mwenye Ikhlas

katika kila jambo lako basi Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni mwenye kukujaalia Kiflayni

kutoka katika Rehma zake kama alivyosema katika Qur’an:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ ٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَآمِنُواْ‏ بِرَسُولِهِ‏ يُؤْتِكُمْ‏ كِفْلَينِْ‏ مِن ر َّحمَْتِهِ‏ وَ‏ يجَْعَل ل َّكُمْ‏

نُوراً‏ تمَْشُ‏ ونَ‏ بِهِ‏ وَيَغْفِرْ‏ لَكُمْ‏ وَٱهلل َُّ‏ غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo ittaqoo Allaha waaminoo birasoolihi yu/tikum

kiflayni min rahmatihi wayajAAal lakum nooran tamshoona bihi wayaghfir lakum

waAllahu ghafoorun raheemun(Surat Al Hadid 57:28)

Tafsir: Enyi Mlioamini Muogopeni Allah na Muaminini Mtume wake, nae atakupeni

Kiflayni min Rahmatihi (Atakutunzeni Mara Mbili kutokana na Rehma zake) na

atakupeni Nuru ambayo mtatembelea (katika njia iliyonyooka) na atakusameheni na

Allah ni Mwingi wa Kusamehe na Mwingi wa Rehma.

Kwa sababu Allah Subhanah wa Ta’ala ni mwenye kuona na kujua kila kilichomo ndani

ya Nyoyo za Waja wake kabla yake na baada yake na hivyo pia ni mwenye kujua ni kipi

kile anachostahiki Mja wake na matokeo yake baada ya kukipata kwake na hivyo ndio

mana akasema kua atamppa yule anaemtii Kiflayni min Rahmatihi, kama alivyopewa

Hana Bint Faqudh alipoomba ajaaliwe Mtoto wa Kiume, lakini badala yake akajaaliwa

Mtoto bora wa kike ambae nae akatoa mtoto bora wa Kiume hivyo hapa kuna Rehma

mbili kubwa ambazo ziliambatana sambamba zilizotokana na Maombi ya Hannah Bint

Faqudh kutokana na kua na Usafi wa Nafsi na Moyo wake katika kuomba kwake katika

wakati wa tukio au haja husika.

Kwani amesema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Dua bora

ambayo hua ni rahisi kujibiwa hua ni ile dua iliyoombwa kwenye wakati wake’

Ambapo anasema Imam Jamal Islam Abu Qasim Abd Al Karim Ibn Hawazin Al

Qushayri kuhusiana na Uombaji wa Dua kua: ‘Faida ya Kuomba Dua ni katika

kubainisha shida yako ijulikane mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala, na hivyo hua

si kumfanya Allah Subhanah wa Ta’ala kufanya atakavyo juu yako. ’


363

Imam Jamal Islam Abu Qasim Abd Al Karim Ibn Hawazin Al Qushayri anaendelea

kutuambia kua: ‘Dua ya Mtu wa Kawaida Hua inabainishwa kwa maneno yake. Dua

ya Wacha Mungu hua inabainishwa na Vitendo vyake na Dua ya Mawalii wa Allah

Subhanah wa Ta’ala hua inabainishwa na hali yake aliyokua nayo.’ Na ‘Dua Bora

ni ile inayoombwa katika wakati wa Huzuni.’

Siku moja Nabii Musa katika kuishi kwake alikutana na mtu ambae alikua akiomba Dua

kwa unyenyekevu sana, hivyo Nabii Musa akasema kumwambia Allah Subhanah wa

Ta’ala kua: ‘Ya Allah, Hakika kama Shida yake ingekua imo ndani ya mikono yangu

mie basi ningemtekelezea’

Hivyo Allah Subhnah wa Ta’ala akamwambia Nabii Musa kua: ‘Ewe Musa Hakika

mim ni mwenye huruma zaidi yako juu yake. Na ingawa yeye ananiomba mimi

lakini Moyo wake uko pamoja na Kondoo wake, hivyo mimi hua simjibu Mja ambae

Moyo wake Unafikiria kitu chengine zaidi yangu.’

Hivyo Nabii Musa kamfuata mtu huyo na kumwambia alivyosema Allah Subhanah wa

Ta’ala kisha mtu huyo akamgeuzia Allah Subhnah wa Ta’ala Moyo we wote na

akajibiwa Dua yake.

Na Imam Jafar As Sadiq aliulizwa siku moja na Wanafunzi wake kwa kuambiwa: ‘Hivi

kwa nini sisi hu ni wenye kuomba Dua lakini Dua zetu hazikubaliwi?’ Imam Jafar

As Sadiq akajibu: ‘Kwa sababu hua Mnamuomba yule ambae hamna Ilm Juu yake.’

Ambapo kwa upande mwengine basi Imam Yahya Ibn Said Al Qattani alimuona Allah

Subhanah wa Ta’ala ndotoni katika usingizi wake na hivyo akamwambia: ‘Ya Rabb,

mimi nimekua nikikuomba sana lakini sijaona kujibiwa maombi yangu.’ Hivyo

Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Imam Al Qattani kua: ‘Ewe Mja wangu

Yahya, hii ni kwa sababu mimi napenda kusikia sauti yako.’

Na pia kwa upande wa Imam Al Wasiti aliombwa aombe Dua ambapo nae akasema:

‘Hakika mimi nna khofu ya kua kama nikiomba Dua basi Allah Subhanah wa Ta’ala

atasema: ‘Kama ikiwa utaniomba kile kitu ambacho nimeshakukadiria basi itakua

umenitilia shaka, na kama ikiwa umeniomba kitu ambacho sikukukadiria basi

itakua hukunitukuza kama inavyostahiki, lakini kama utaridhika basi kwa mda

muwafaka nitakupa kila nilichokukadiria’’

Na akasema Imam Muhammad Ibn Khuzaymah kua: ‘Mimi nilikua katika Mji wa Al

Iskandriyah (Alexandria, Misri) wakati Ahmad Ibn Hanbal alipofariki, na nikawa

nimejawa na Huzuni sana. Hivyo usiku nilipolala nikamuona Ahmad Ibn Hanbal

akiwa anacheza cheza, hivyo nikamuuliza Ahmad Ibn Hanbal. ‘Ewe Abu Abd


364

Allah! Hivi hivyo unavyofanya ndio nini?’ Nae akajibu: ‘Hii ndio hali ya Mja

anaekua Peponi’

‘Nami nikamuuliza: ‘Allah amekufanya nini?’ Ahmad Ibn Hanbal akasema:

‘Amenisamehe makosa yangu yote na amenivisha Taji kichwani mwangu na kunipa

vitu vya dhahabu na kuniambia kua: ‘Hakika hii ni kutokana na wewe kua ni

mwenye kusema kua Qur’an ni Maneno yangu’

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Ewe Ahmad Ibn Hanbal hebu niombee

kama vile ambavyo alivyokufundisha Sufyan Ath Thawry ulipokua Duniani’

Ahmad Ibn Hanbal akasema: ‘Ya Rabb, Ewe Mola wa kila kitu, kutokana na uwezo

wako juu ya kila kitu nakuomba unisamehe juu ya kila kitu na usiniulize chochote

kile juu ya kila kitu’ hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Ewe Ahmad ingia

Peponi’ hivyo nami nikaingia.

KULELEWA KWA MARYAM BINT IMRAN NA NABII ZAKARIYAH

Anasema Imam Muhammad Ibn Is-haq kua: ‘Amesema Allah Subhanah wa Ta’ala

kua:

‏﴿وَأَنبَتَهَا نَبَااتً‏ حَسَناً‏ وَكَف َّلَهَا زَكَرِ َّ كُل َّمَا دَخَلَ‏ عَلَيْهَا زَكَرِ َّ ٱلْمِحْرَابَ‏ وَجَدَ‏

عِندَهَا رِزْقاً‏ قَالَ‏ يمَٰرْيمَُ‏ أَنى َّٰ‏ لَكِ‏ هَٰذَا قَالَتْ‏ هُوَ‏ مِنْ‏ عِندِ‏ ٱهلل َِّ‏ إنًّ‏ ٱهللًَّ‏ يَرْزُقُ‏ مَن

يَشَآءُ‏ بِغَيرِْ‏ حِ‏ سَابٍ‏ ﴾

Waanbataha nabatan hasanan wakaffalaha zakariyya kullama dakhala AAalayha

zakariyya almihraba wajada AAindaha rizqan qala ya maryamu anna laki hadha

qalat huwa min AAindi Allahi inna Allaha yarzuqu man yashao bighayri

hisabin(Surat Al Imran 3:37)

Tafsir: Na akamfanya akuwe katika makuzi mazuri na kumuweka chini ya usimamizi

wa Zakarriyah. Hivyo kila akiingia kwenye Mihrab (Kumuangalia na kumpelekea

Mataji yake) alikua akimkuta na Riziki yake, hivyo akasema: ‘Ewe Maryam, Umepata

wapi yote haya?’ akasema (Maryam): ‘Hivyo ni kutoka kwa Allah’ kwani kwa hakika

Allah humruzuku amtakae bila ya hesabu.


365

Hivyo Nabii Zakarriyah akamchukua Mtoto huyo na kumteua Isha Bint Faqudh

ambae ni Mama yake Nabii Yahya kua ndie Mlezi wa Mayam Bint Imran na

kumsimamia juu ya kila kitu, kisha alipokua mkubwa basi Nabii Zakarriyah

akamjengea Maryam Bint Imran Mihrab yaani Chumba maalum cha Kuishi na

kufanyia Ibada kwa ajili yake katika upande wa Mashariki na kuweka mlango

wake juu hivyo mtu hawezi kuingia ndani yake mpaka atumie ngazi, na kila siku

alikua akimpelekea mahitaji yake, chakula, kinywaji na mafuta ya kujipaka, na

kisha huondoka na kumuacha huku akiwa ni mwenye kuufunga mlango huo kwa

kufuli na ufunguo huondoka nao.

Kama zinavyosema Aya kuhusiana na sehemu hio ya Masharii kua:

‏﴿وَٱذْكُرْ‏ فىِ‏ ٱلْكِتَابِ‏ مَرْيمََ‏ إِذِ‏ ٱنتَبَذَتْ‏

مِ‏ نْ‏ أَهْ‏ لِهَ‏ ا مَكَ‏ اً‏ شَ‏ رْقِياً﴾‏

Waodhkur fee alkitabi maryama idhi intabadhat min ahliha makanan sharqiyyan

(Surat Maryam 19:16)

Tafsir: Na ametajwa katika kitabu, Maryam, wakati alipojitenga kutokana na familia

yake katika sehemu inayoelekea upande wa Mashariki.

Ambapo neno Mihrab linatokana na neno Haraba amblo hua linamaanisha Kuharibu

Kitu, Kukifanya Kitu kua hakifai na Hakina Maana, ambapo neno hili ndio lililotoa neno

Harb ambalo hua linaamaanisha Vita au Mapigano, na hivyo Mihrab hua ni sehemu ya

pembeni ya ndani ya Nyumba au chumba ambacho mtu hua anakaa ndani yake peke yake

kwa ajili ya kua na Mola wake na hivyo kua ni mwenye kupigana vita na Iblisi kwa ajili

ya Nafsi yake na Mola wake.

Hivyo Nabii Zakrriyah ambae alikua pia ni mwenye kazi ya Useremala basi alikua kila

siku alikua akienda kwenye Mihrab hio kumuangalia Maryam Bint Imran na Nabii

Zakarriyah alikua akimkuta tayari Maryam Bint Imran ana chakula ndani ya Mihrab hio,

ambacho hua ni mchanganyiko wa kila aina ya Vyakula vizuri na vitamu, kiasi ya kua

kuna baadhi ya vyakula vya msimu basi vilikua vinakutikana ndani ya Mihrabu hio

anayoishi Maryam Bint Imran hata kabla ya msimu wake kufika kwa mfano vyakula vya

wakati wa kiangazi vilikua vinapatikana katika wakati wa Masika na vya wakati wa Vuli

vinapatikana katika wakati wa Kipupwe na kuna vyengine vilikua ni kutoka sehemu za

mbali ambavyo ingawa mimea yake ilikua haioti katika maeneo ya Jerusalem lakini

chumbani kwake Maryam Bint Imran vilikua vinapatikana.

Jambo hili lilimshangaza sana Nabii Zakarriyah hivyo akamuuliza Maryam Bint Imran

kama zinavyosema aya:


366

‏﴿قَالَ‏ يمَٰرْيمَُ‏ أَنى َّٰ‏ لَكِ‏ هَٰذَا قَالَتْ‏ هُوَ‏ مِنْ‏ عِندِ‏ ٱهلل َِّ‏ إنًّ‏ ٱهللًَّ‏ يَرْزُقُ‏ مَن يَ‏ شَآءُ‏ بِغَيرِْ‏

حِ‏ سَابٍ‏ ﴾

Qala ya maryamu anna laki hadha qalat huwa min AAindi Allahi inna Allaha

yarzuqu man yashao bighayri hisabin(Surat Al Imran 3:37)

Tafsir: Hivyo akasema (Nabii Zakrriya kwa kuuliza): ‘Ewe Maryam, Umepata wapi

yote haya?’ akasema (Maryam): ‘Hivyo ni kutoka kwa Allah’ kwani kwa hakika Allah

humruzuku amtakae bila ya hesabu.

Ama kuhusiana na tukio hili basi anasema Jafar Ibn Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua:

‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua anakaa kwa mda wa siku kadhaa

bila ya kua na chakula hadi inafikia wakati inakua taabu juu yake, hivyo alikua

akienda kwa nyumbani kwa Wake zake na ilikua hakuna kitu chochote ndani yake.

Hivyo akaenda kwa Fatma na kumwambia: ‘Ewe Binti yangu Kipenzi, jee unacho

chakula chochote kile? Kwa sababu mimi nnaona njaa’ Fatma akajibu: ‘Wa Allahi

naapa kwa Baba yangu na kwa Mama yangu, Sina Chakula.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipoondoka, basi mara Mfanyakazi wa

Fatma akaleta Bakuli ambalo ndani yake mlikua na Vipande vya Mikate viwili na

Nyama kidogo, hivyo Fatma akalipokea Bakuli hilo na kisha akalifunika na

kusema: ‘Naomba kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anirahisishie mimi

na familia yangu kupitia hili’ kwani wote walikua ni wenye shida ya chakula.

Hivyo Fatma akawatuma Hasan na Husein kwa Babu yao, na mara Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akaja kwa Fatma na alipofika basi: ‘Naapa kwa ajili

yako, kwa Baba yangu, kwa Mama yangu kua Allah Subhanah wa Ta’ala

ametuletea kitu ambacho nami nimekihifadhi kwa ajili yako’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akachukua Bakuli hilo na kulifunua. Subhana

Allah! Bakuli hilo lilikua limejaa Mikate na Nyama. Na hapo Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akamuona Fatma kua ni mwenye muonekano wa

mshangao mkubwa sana, nae Fatma akajua kua ni Miujiza ya Allah Subhanah wa

Ta’ala hivyo akamshukuru na kumtukuza Allah Subhanah wa Ta’ala na kumsalia

Mtume wake Salallahu Alayhi wa Salam’


367

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akauliza: ‘Vimetokea wapi hivi ewe Binti

yangu?’ na Fatma akajibu:

‏﴿هُوَ‏ مِنْ‏ عِندِ‏ ٱهلل َِّ‏ إنًّ‏ ٱهللًَّ‏ يَرْزُقُ‏ مَن يَشَآءُ‏ بِغَيرِْ‏ حِ‏ سَابٍ‏ ﴾

Huwa min AAindi Allahi inna Allaha yarzuqu man yashao bighayri hisabin (Surat

Al Imran 3:37)

Tafsir: ‘Hivyo ni kutoka kwa Allah’ kwani kwa hakika Allah humruzuku amtakae bila

ya hesabu’

Na hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Sifa zote anastahiki Allah

Subhanah wa Ta’ala ambae amekufanya wewe kua ni sawa na Mwanamke wa Watu

wa Bani Israil, kwani nae pale alipopewa Riziki yake na alipoulizwa kuhusiana nayo

basi alijibu:

‏﴿هُوَ‏ مِنْ‏ عِندِ‏ ٱهلل َِّ‏ إنًّ‏ ٱهللًَّ‏ يَرْزُقُ‏ مَن يَشَآءُ‏ بِغَيرِْ‏ حِ‏ سَابٍ‏ ﴾

Huwa min AAindi Allahi inna Allaha yarzuqu man yashao bighayri hisabin(Surat

Al Imran 3:37)

Tafsir: Hivyo ni kutoka kwa Allah’ kwani kwa hakika Allah humruzuku amtakae bila

ya hesabu’

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawaita watu wote ndani ya nyumba

hio Fatma, Hasan, Husein na wake zake wote Rasul Allahu Alayhi wa Salam wakala

mpaka wakashiba, huku bakuli hilo likiwa limebakia kama lilivyokua hapo awali,

Fatma akaamrisha kua sehemu nyengine iliyobakia wagaiwe Majirani zake wote.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala alitia baraka yake kwenye bakuli lenye Mikate

miwili na Nyama kidogo na kua ni bakuli lenye Mikate na Nyama ya kushiba kila

mtu.

Hali ya Maryam Bint Imran kulelewa na Nabii Zakariyah iliendelea kwa mda hadi

ikafikia wakati Nabii Zakaria akawa ni Mtu Mzima sana. Hivyo akawaambia Makuhani

wa Bani Israil kua. Hakika mimi tayari nimeshakua Mtu mzima sana kua ni mwenye

kumsimmia Maryam Bint Imran, hivyo jee ni nani miongoni mwenu atakaeweza

kunisadia jukumu langu hili?


368

Hivyo watu hao wakakubaliana kua kuna Mtu mmoja miongoni mwa watu wa Bani Israil

ambae anaitwa Yusuf Ibn Yaqqub Ibn Mathan Ibn Amur Ibn Mishan Ibn Hizqil Ibn

Ahraf Ibn Buam Ibn Azaziyah Ibn Amasiyah Ibn Nawus Ibn Nutha Ibn Barid Ibn

Yahushafat Ibn Radim Ibn Ababa Ibn RajiAm Ibn Sulayman Ibn Daud ambae ni Mcha

Mungu na yeye alikua ni Fundi Seremala na alikua ni Ibn Ami yake Maryam Bint Imran

na hivyo anastahiki kutokana na kua na sifa na vigezo kua ndie Al Kaffal wa Maryam

Bint Imran.

Hivyo Maryam Bint Imran akawa chini ya uangalizi wa Yusuf Ibn Yaqqub na baada ya

mda kupita basi Nabii Zakarriyah akaona kua miaka inaenda kwani katika kipindi hiki

alikua tayari ana umri wa miaka 300 na yeye hana ndugu wala jamaa wala mtoto, kwani

jamaa zake aliokua nao kwa wakati huo walikua ni Isha ambae Mke wake na Maryam

Bint Imran tu, hivyo akaamua kumuomba Mola wake ili apate Mtoto mwema ambae

atakaeweza kuendeleza kizazi chake, na kumrithisha majukumu yake hivyo akasema

kama zinavyosema aya:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞ك ۤ هيع ۤ ص ۤ ۞ ذِكْرُ‏ رَحمَْةِ‏ رَبِّكَ‏ عَبْدَهُ‏ زَكَرِ َّ ‏۞إِذْ‏ ‏َدَىٰ‏ رَب َّهُ‏

نِدَآءً‏ خَفِيّاً۞قَالَ‏ رَبِّ‏ إِنى َّ وَهَنَ‏ ٱلْعَظْمُ‏ مِنىِّ‏ وَٱشْتَعَلَ‏ ٱلر َّأْسُ‏ شَيْباً‏ وَلمَْ‏ أَكُنْ‏ بِدُعَآئِ‏ ‏َك

رَبِّ‏ شَقِيّاً۞وَإِنىّ‏ ِ خِ‏ فْتُ‏ ٱلْمَوَالىَِ‏ مِن وَرَآئِى وَكَانَتِ‏ ٱمْرَأَتِى عَاقِراً‏ فَهَبْ‏ لىِ‏ مِن

ل َّدُنْكَ‏ وَلِيّاً۞يَرِثُنىِ‏ وَيَرِثُ‏ مِنْ‏ آلِ‏ يَعْقُوبَ‏ وَٱجْعَلْهُ‏ رَبِّ‏ رَضِيّاً‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Kaf-ha-ya-AAayn-sad;Dhikru rahmati

rabbika AAabdahu Zakariyya; Idh nada rabbahu nidaan khafiyyan; Qala rabbi

innee wahana alAAadhmu minnee waishtaAAala alrra/su shayban walam akun

biduAAa-ika rabbi shaqiyyan; Wa-innee khiftu almawaliya min wara-ee wakanati

imraatee AAaqiran fahab lee min ladunka waliyyan; Yarithunee wayarithu min ali

yaAAqooba waijAAalhu rabbi radhiyyan.(Surat Maryam 19:1-6)

Tafsir: Kwa Jina Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma. Kaf-Ha-Ya-Aayn-Sad;

Zinatajwa Rehma za Mola wako kwa Mja wake Zakarriyah. Alimpomnadia Mola wake

mnadio wa Siri. Aliposema: ‘Ewe Mola wangu hakika mimi mifupa yangu imekua

myepesi kwangu na Mvi zimeenea kwenye kichwa changu, na kamwe sikua kwenye

Dua zangu kwako ewe Mola wangu kua ni mwenye kuvunjika Moyo, Na nnakhofia

jama zangu baada yangu kwani mke wangu ni Tasa, Hivyo nipe mimi kutoka kwako

Msaidizi, ambae atanirithi mimi na atarithi kutoka katika familia ya Yaqub na mjaalie

Ewe Mola wangu kua ni mwenye kuridhiwa nae.’


369

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Kuna sababu

nyingi ambazo zinaweza kuelezewa kwanini Nabii Zakariyyah akaomba Dua kwa

Siri, kwa mfano labda alikua akiomba Dua katika wakati wa Usiku Mkubwa Sana

na hivyo hakutaka kuwakera watu wengine, au kwa sababu kuomba dua kwa sauti

ndogo hua ni sehemu ya kuonesha Ikhlasi, au kwa sababu alikua na khofu kua watu

watamsikia na kuanza kumsimanga kwa kutafuta mtoto wakati akiwa na umri

mkubwa, n.k’

Ambapo katika kuomba kwake Nabii Zakarriyah basi Qur’an inatuonesha namna ya

kuomba Dua kua Kwanza unatakiwa ukubali udhaifu wako kwa kuutaja mbele ya Mola

wako ili kuonesha kukubali na kuthibitisha uwezo wake na ukubwa wake na kua

unathamini rehma na neema zake juu yako na hivyo unahitaji kutoka kwake.

Na katika kuomba kwake basi tunaona kua Nabii Zakarriyah ametumia neno Waliyyan

ambalo hua linatokana na neno Waliya ambao hua lina maana nyingi ikiwemo Karibu,

Fuata, Karibia. Neno Waliya ndio lililotoa neno Walin ambalo humaanish Mlinzi, Rafiki

Msaidizi, Rafiki Anaelinda au Kutetea, na pia hua linamaanisha Mrithi au Msimamizi na

pia hua linamaanisha Ibn Ami, Baba Mdogo, Baba Mkubwa n.k

Ambapo kwa upande mwengine basi Allah Subhanah wa Ta’ala anatuelezea ni Waliyyan

gani ambae Nabii Zakarriyah alikua akimtaka pale alipoelezea tukio hili katika Surat Al

Imran pale aliposema:

‏﴿هُنَالِكَ‏ دَعَا زَكَرِ َّ رَ‏ ب َّهُ‏ قَالَ‏ رَبِّ‏ هَبْ‏ لىِ‏ مِنْل َّدُنْ‏ كَذُرِّي َّةًطَيِّبَةً‏ إِن َّكَ‏ سمَِيعُ‏ ٱلد ُّعَآءِ‏ ﴾

Hunalika daAAa zakariyya rabbahu qala rabbi hab lee min ladunka dhurriyyatan

tayyibatan innaka sameeAAu aldduAAa/-I (Surat Al Imran 3:38)

Tafsir: Wakati kiwa huo Zakariyyah akamuomba Mola wake (na) Kusema: ‘Ewe Mola

Wangu nipe mimi kutoka kwako Kizazi Kizuri kwani kwa hakika wewe ni mwenye

kusikia Dua’

Na hivyo kumaanisha kua Nabii Zakarriyah alikua anataka ajaaliwe Mtoto wa Kiume

kutoka kwa Mola wake, ambae ataendeleza majukumu yake na ya Babu yake ambae ni

Nabii Yaqub, kwani watu wa Bani Israil wote asili yao ni kutoka kwa Nabii Yaqub ambae

yeye nie Mtu wa kwanza kua ni mwenye kuitwa Israil kutokana na kua alikimbia kutoka

kwao baada ya kutishiwa kuuliwa na Kaka yae, na hivyo kawa ni mwenye kutembea

Usiku usiku na mchana kua ni mwenye kujificha. Hivyo kutokana na kutembea kwake

usiku basi ndio kawa na sifa ya kua ni mwenye Sara bil Layl – Israil.


370

Anasema Jarrah Allah Sultan Al Balagha Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kuhusiana

na maneno ya Surat Maryam 19:6 yasemyo kua kua: ‘Nabii Zakkariyah amesema:

‘Yarithunee wayarithu min ali yaAAqooba waijAAalhu rabbi radhiyyan’ yaani ‘ambae

atanirithi mimi na atarithi kutoka katika familia ya Yaqub na mjaalie Ewe Mola

wangu kua ni mwenye kuridhiwa nae’, hivyo Nabii Zakarriyah alisisitiza kwa

kusema min ali YaAaquuba kwa sababu si kila aliekuwemo kwenye kizazi cha Nabii

Yaqub alikua ni Nabii na hivyo kua ni mwenye Ilm ambayo inastahiki kurithiwa’

Aya pia zinatuthibitishia umuhimu wa uomba kupata watoto wema kwani ndio chanzo

cha kupata manufaa hapa Duniani na kesho Akhera. Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala

akamwambia Nabii Zakarriyah kwa kusema kama zisemavyo aya:

‏﴿فَنَادَتْهُ‏ ٱلْمَلا ۤ ئِكَةُ‏ وَهُوَ‏ قَ‏ ائِمٌ‏ يُصَلِّى فىِ‏ ٱلْمِحْرَابِ‏ أَن َّ اهلل ََّ‏ يُبَشِّ‏ رُكَ‏ بِ‏ يَحْيَى ٰ مُصَدِّقاً‏

بِكَلِمَةٍ‏ مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَسَيِّداً‏ وَحَصُوراً‏ وَنَبِيّاً‏ مِّنَ‏ ٱلص َّالحِِينَ‏ ﴾

Fanadat-hu alMala-ikatu wahuwa qa-imun yusallee fee almihrabi anna Allaha

yubashshiruka bi Yahya musaddiqan bikalimatin mina Allahi wasayyidan

wahasooran wanabiyyan mina alssaliheena; (Surat Al Imran 3:39-41)

Tafsir: Na kisha Malaika wakanadia huku yeye akiwa amesimama akisali katika

Mihrabu: (wakasema)‘Hakika Allah anakubashiria (Mtoto) Yahya kuthibitisha Kauli

kutoka kwa Allah (Nabii Isa), na mja mwema mwenye cheo, na msafi asiekua na

dhambi na Nabii na Miongoni mwa Waja wema’

Hapa tunaona kua katika kumsifu kwake Yahya basi Allah Subhanah wa Ta’ala kua

atakua ni mwenye kuthibisha Unabii wa Nabii Isa, na pia Nabii Yahya ni mwenye sifa

ya kua ni mwenye Darja, Cheo cha Unabii na ni Miongoni mwa waja wema wenye sifa

ya kua ni Hasur, ambapo aya ametumia neno Hasur ambalo ni lenye kutokana na neno

Hasara au Hasira ambalo hua linamaanisha Kuzuia, Kubana au Kufungwa.

Neno Hasara ndio lililotoa neno Hasir ambalo hua linamanisha Jela, Kifungoni au

Gerezani. Hivyo neno Hasur lililotumika hapa linamaanisha kua ni Msafi ambae

haendekezi matamanio ya kutaka Wanawake.

Na kutokana na aya hii basi tunaona kua baadhi ya Wanazuoni wanasema kutooa

kama mtu unaweza kujizuia basi ni bora na inaruhusika, yaani hii inakua kama hali

ya Shaykh ul Islami Muhyi Ad Din Imam Abu Zakarriya Sharraf An Nawawi ambae

ni miongoni mwa Maimamu ambao hawakuoa na ndani yake anaingia pia Imam


371

Bukhari, Imam Abu Qasim Al Zamakhshari, Imam Muhammad Ibn Jarir At Tabari,

Imam Abd Allah Ibn Abi Najih, Imam Bishr Ibn Harith Al Hafi, Imam Abu Sad Al

Sam’ani, Imam Mulla Ali Al Qari, Shaykh Ibn Taymiyah. nk

Ambapo amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Enyi Vijana,

yeyote yule mwenye uwezo basi na aoe kwani kufanya hivyo hua ni sehemu ya

kuinamish mtizamo wa macho na kulinda kwa usafi, ama kwa wale wasiokua

na uwezo basi na wafunge kwa sababu funga hua inaangamiza Matamanio.’

Na akasema tena Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kua: ‘Mambo manne

yalikua ni Sunna za Mitume, Kuona haya, Kujitia Mfuta Mazuri, Kusugua

Meno na Kuoa.’(Imam At Tirmidhii)

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anasema tena katika Qur’an kua:

‏﴿وَلَقَدْ‏ أَرْسَلْنَا رُسُلاً‏ مِّن قَبْلِكَ‏ وَجَعَلْنَا لهَُمْ‏ أَزْوَاجاً‏ وَذُرِّي َّةً‏ وَمَا كَانَ‏ لِ‏ رَسُولٍ‏ أَن

ّ لِكُل أَجَلٍ‏ كِتَابٌ‏ ﴾

‏َْتِىَ‏ آبِيَةٍ‏ إِلا َّ إبِِذْنِ‏ ٱهلل َِّ‏ ِ

Walaqad arsalna rusulan min qablika wajaAAalna lahum azwajan wadhurriyyatan

wama kana lirasoolin an ya/tiya bi-ayatin illa bi-idhni Allahi likulli ajalin kitabun

(Surat Rad 13:38)

Tafsir: Na Kwa Hakika tumetuma Mitume kabla yako na tukawajalia kua ni wenye

kuoa na kupata watoto na haikua kwa Mitume kuleta uthibitisho isipokua kwa Idhni

ya Allah. Kwani kwa kila kitu kimeandikiwa kwenye Kitabu.

Hivyo Nabii Zakarriyah akasema:

‏﴿قَالَ‏ رَبِّ‏ أَنى َّٰ‏ يَكُونُ‏ لىِ‏ غُلاَمٌ‏ وَقَدْ‏ بَلَغَنىِ‏ ٱلْكِبَرُ‏ وَٱمْرَأَتِى عَاقِرٌ‏ قَالَ‏ كَذٰ‏ لِكَ‏ ٱهلل َُّ‏

يَفْعَلُ‏ مَا يَشَآءُ۞قَالَ‏ رَبِّ‏ ٱجْعَلْ‏ لىِّ‏ ۤ آيَةً‏ قَالَ‏ آيَتُكَ‏ أَلا َّ تُكَلِّمَ‏ ٱلن َّاسَ‏ ثَلاَثَةَ‏ أَ َّمٍ‏ إِلا َّ

رَمْزاً‏ وَٱذْكُرْ‏ ر َّب َّكَ‏ ير كَثِ‏ ٱ اًوَسَبِّحْ‏ بِ‏ ى لْعَِش ‏َوٱ لإِبَْكا رِ‏ ﴾


372

Qala rabbi anna yakoonu lee ghulamun waqad balaghaniya alkibaru waimraatee

AAaqirun qala kadhalika Allahu yafAAalu ma yasha/o; Qala rabbi ijAAal lee

ayatan qala ayatuka alla tukallima alnnasa thalathata ayyamin illa ramzan

waodhkur rabbaka katheeran wasabbih bialAAashiyyi waal-ibkari; (Surat Al Imran

3:40-41)

Tafsir: Akasema (Nabii Zakarriyah): ‘Ewe Mola wangu jee nitapataje Mtoto wakati

mimi tayari ni Mzee na mke wangu ni Tasa?’ Allah Akasema: ‘Kadhalika Allah

hufanya vile atakavyo’ Akasema (Nabii Zakarriyah): ‘Ewe Mola wangu nijalie dalili’:

Akaambwa Dalili yako hua hutozungumza na watu kwa siku 3 isipokua kwa kutumia

alama za mikono. Na mkumbuke Mola wako kwa wingi na mtukuze mchana na

asubuhi.

Ambapo aya zinatuonesha kua kulingana na maneno ya Nabii Zakarriyah, basi hakua ni

mwenye kua na shaka juu ya kukubaliwa kwa maombi yake bali alikua yuko katika hali

ya kuhoji kutokana na kutaka kupata muongozo wa kujua njia gani atumie? Wakati Mke

wake ni Tasa na yeye ni Mzee, au itabidi afanye kama alivyofanya Nabii Ibrahim kuoa

Mwanamke mwengine kijana? Na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamhakikishia kwa

kumwambia kua atakavyo Allah Subhanaha wa Ta’ala basi ndivyo itavyokua yaani

atapata mtoto katika umri aliokua nao, bila ya kurudishiwa yeye ujana na bila ya kuhitaji

kuoa mke mwengine kijana.

Ambapo kuna badhi ya Wafasiri wanasema kua Nabii Zakarriyah aliuliza hivi kwa

sababu ilichukua mda wa takriban miaka 20 baina ya kuomba kwake Dua na kupokea

majibu ya Dua yake hiyo. Na kuna wasemao kua hoja hii alitoa kwa ajili ya kumtaka

Allah Subhnah wa Ta’ala amfafanulie vizuri zaidi kuhusiana na tukio hili.

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala anambainishia Nabii Zakarriyah kua kwake yeye ni

mwenye uwezo juu ya kila kitu, kwani hata Nabii Zakarriyah aliumbwa kutokana na kua

tone la manii ambalo halina thamani yeyote kama isemavyo aya:

‏﴿قَالَ‏ كَذٰ‏ لِكَ‏ قَالَ‏ رَب ُّكَ‏ هُوَ‏ عَلَى َّ هَينٌِّ‏ وَقَدْ‏ خَلَقْتُكَ‏ مِن قَبْلُ‏ وَلمَْ‏ تَكُ‏ شَيْئاً‏ ﴾

Qala kadhalika qala rabbuka huwa AAalayya hayyinun waqad khalaqtuka min

qablu walam taku shay-an;(Surat Maryam 19:9)

Tafsir: Kadhalika hivyo ndivyo asemavyo Mola wako: ‘Ni rahisi kwangu mie. Kwani

kwa hakika nimekuumba wewe hapo kabla wakati ulikua si chochote.’


373

Kisha Nabii Zakarriyah akaomba aoneshwe dalili ya kutokea kwa jambo hilo, ambapo

akambiwa kua hatokua na uwezo wa kuzungumza na watu kwa mda wa siku tatu ijapokua

hatokua na tatizo lolote, kama zinavyobainisha aya:

‏﴿قَالَ‏ رَبِّ‏ ٱجْعَل ليِ‏ ۤ آيَةً‏ قَالَ‏ آيَتُكَ‏ أَلا َّ تُكَلِّمَ‏ ٱلن َّاسَ‏ ثَلاَثَ‏ لَيَالٍ‏ سَوًِّ۞فَ‏ خَرَجَ‏

عَلَى ٰ قَوْمِهِ‏ مِنَ‏ ٱلْمِحْرَابِ‏ فَأَوْحَى ٰ إِلَيْهِمْ‏ أَن سَبِّحُواْ‏ بُكْرَةً‏ وَعَشِ‏ يّاً‏ ﴾

Qala rabbi ijAAal lee ayatan qala ayatuka alla tukallima alnnasa thalatha layalin

sawiyyan; Fakharaja AAala qawmihi mina almihrabi faawha ilayhim an sabbihoo

bukratan waAAashiyyan(Surat Maryam 19:10-11)

Tafsir: Akasema (Zakarriyah) ‘Nijaalie Dalili.’ (Allah Subhanah wa Ta’ala)Akasema:

‘Dalili yako ni kua hutozungumza na Watu kwa Usiku Mitatu huku ukiwa mzima

ulietimia’. Akatoka kwa watu wake kutokea kwenye Mihrabu akawaambia kwa

kutumia alama za mikono kumtukuza Allah Asubuhi na Jioni.

Naam hii ni miongoni mwa Aya ambazo zinathibitisha kuruhusika kutumika kwa Alama

za mikono na ishara katika Sharia za Dini ya Kiislam, kwani hii pia hua ni kama vile

ambavyo alivyofanya Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam pale alipomuuliza

Mtumwa kuhusiana na kama anamjua yeye Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ni

nani? Ambapo Mwanamke huyo akamuoneshea Kidole Rasul Allah Salallahu Alyhi wa

Salam na kisha akaoneshea kidole hicho Mbinguni. Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam akasema kua: ‘Huyu Ni Muislam’

Na pia katika hadithi nyengine pale alipomuuliza Mtumwa huyo: Jee unajua Allah

Subhanah wa Ta’ala yuko wapi? Ambapo Mtumwa huyo akaonesha Kidole Juu

Mbinguni.

Hivyo Nabi Zakarriyah akatoka nje ya Mihrabu ambapo watu hao hua wanamsubiri kwa

ajili ya kumsabihi Allah Subhanah wa Ta’ala na kisha akawasalisha lakini akawa hawezi

kutoa sauti, hivyo akawa nazungumza nao na kuwafahamisha na kuwasalisha kwa

kutumia alama za mikono, kwani hio ndio ilivyokua dalili ya kujaaliwa kupata mtoto

aliemuomba ambae ni yule aitwae Yahya.

KUZALIWA KWA NABII YAHYA IBN ZAKARIYAH


374

‏﴿يٰزَكَرِ َّ إِ َّ نُبَشِّ‏ رُكَ‏ بِغُلاَمٍ‏ ٱسمُْهُ‏ يحَْيىَٰ‏ لمَْ‏ نجَْعَل ل َّهُ‏ مِن قَبْلُ‏ سمَِيّاً‏ ﴾

Ya zakariyya inna nubashshiruka bighulamin ismuhu yahya lam najAAal lahu min

qablu samiyyan (Surat Maryam 19:7)

Tafsir: Akasema Allah Subhanah wa Ta’ala kua: ‘Ewe Zakarriyah hakika sisi

tunakubashiria wewe Kijana jina lake Yahya ambalo hatukumjaalia yeyote hapo

kabla’

Ambapo kwa upande wa Imam Qatadah Al Sadusi basi yeye anasema kua: ‘Allah

Subhanah wa Ta’ala hakuwahi kumpa Mtu yeyote yule jina hili isipokua Nabii

Yahya, hata kama ikiwa Ibn Adam aliwahi kufanya hivyo.’

Na kwa upane wa Bahar Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu anhu basi yeye

anasema kua: ‘Hakuna Mwanamke aliekua katika hali ya Uzee na Utasa wa Isha kua

atapata mtoto kama huyo’

Na kwa upande wa Imam Mujahid Ibn Sulayman basi yeye anasema kua: ‘Maana ya

Samiyya iliyokusudiwa hapa hua ni sawa na ile ambayo hua inamaanisha kama

linavyomaanisha neno Shabiha ambalo maana yake hua ni kushabihiana kama vile

lilivyotumika katika aya ifuatayo:’

‏﴿ر َّب ُّ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَمَا بَيْنَهُمَا فَٱعْبُدْهُ‏ وَٱصْطَبرِْ‏ لِعِبَادَتِهِ‏ هَلْ‏ تَعْلَمُ‏ لَهُ‏

سمَِيّاً‏ ﴾

Rabbu alssamawati waal-ardhi wama baynahuma faoAAbudhu waistabir

liAAibadatihi hal taAAlamu lahu samiyyan (Surat Maryam 19:65)

Tafsir: Mola wa Mbingu na Ardhi na kila kilichomo ndani yake, hivyo muabuduni na

dumuni katika kumuabudu jee mnamjua nani mwenye sifa kama yeye?

Hivyo Isha akashika Mimba na kua na ujauzito wa Mtoto huyo ambae aliekua akijulikana

kwa jina la Yahya, ambapo mtoto huyo alipozaliwa alikua ni Mwema na Mcha Mungu

sana kwani tangu utotoni alikua akimuabudu Mola wake na kuwapita watu wazima

waliokua wakubwa zake, na pia alikua ni mwenye kuwausia watu wake kuhusiana na

Mola wake yeye pamoja na Baba yake yaani Nabii Zakariyah.

Ambapo anasema Allah Subhanah wa Ta’ala kuhusiana nae kua:


375

‏﴿يٰيَحْيىَٰ‏ خُذِ‏ ٱلْكِتَابَ‏ بِقُو َّةٍ‏ وَآتَيْنَاهُ‏ ٱلحُْكْمَ‏ صَبِيّاً۞وَحَنَاً‏ مِّ‏ ن ل َّدُ َّ وَزَكَوٰةً‏ وَكَانَ‏

تَقِيّاً۞وَبَرّاً‏ بِوَالِدَيْهِ‏ وَلمَْ‏ يَكُن جَب َّاراً‏ عَصِيّاً۞وَسَلاَمٌ‏ عَلَيْهِ‏ يَوْ‏ مَ‏ وُلِدَ‏ وَيَوْمَ‏ يمَُوتُ‏ وَيَوْمَ‏

يُبْعَثُ‏ حَياً‏ ﴾

Ya yahya khudhi alkitaba biquwwatin waataynahu alhukma sabiyyan; Wahananan

min ladunna wazakatan wakana taqiyyan; Wabarran biwalidayhi walam yakun

jabbaran AAasiyyan; Wasalamun AAalayhi yawma wulida wayawma yamootu

wayawma yubAAathu hayyan.(Surat Maryam 19:12-15)

Tafsir: Ewe Yahya shikamana na Kitabu (Taurat) kwa nguvu na tukampa Hikma

wakati akiwa mtoto mdogo, Na tukamfanya kua ni mwenye Huruma na akawa Msafi

na Mwema. Na akawa Mtiifu kwa wazee wake na wala hakua Jabari na mwenye kuasi

kwa Mola wake. Na salamu iwe juu yake katika Siku Aliyozaliwa, katika Siku

Atakayokufa na katika Siku Atakayofufuliwa.

Hivyo mtoto huyo ambae ni Nabii Yahya alikua ni Mja mwema tangu katika kipindi cha

utotoni mwake, na kua nimiongoni mwa Manabii ambao walipewa Unabii Utotoni na

kua mtiifu kwa Mola wake na kwa Wazee wake, na kuingizwa kwenye usalama na Allah

Subhanah wa Ta’ala katika siku ya kuzaliwa wake, siku ya kufa kwake na katika siku ya

Kufufuliwa kwake.

Anasema Imam Sufyan Ibn Uyayna kua: ‘Maneno yanayoainisha siku hizi tatu katika

aya hii yanamaanisha siku tatu ambazo Ibn Adam anakua na khofu na wasiwasi

sana ambazo ni Siku ya Kuzaliwa, Siku ya Kufa na Siku ya Kufufuliwa.’

Siku moja Nabii Yahya alimuomba Allah Subhanah wa Ta’ala : ‘Ya Allah hakika mimi

nilikua nataka unioneshe Ibilisi akiwa katika maumbile yake kama alivyoumbwa

na nataka anijibu masuali yangu yote nitakayomuuliza bila ya kunificha kitu

chochote.’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Ibilis: ‘Nenda kwa Mja wangu Yahya

Ibn Zakarriyah katika hali ya maumbile kama ulivyoshuka kwa mara ya kwanza

kutoka Mbinguni kuelekea Ardhini, na usimfiche juu ya kitu chochote kile

atakachokuuliza.’

Hivyo Ibilisi akaenda kwa Nabii Yahya akiwa kama alivyokua wakati aliposhuka kutoka

Mbinguni kwa mara ya kwanza, na alipofika kwa Nabii Yahya akajitambulisha kwa


376

kusema: ‘Ewe Nabbiyu Allah Yahya hakika mimi ni Ibilisi, Mola wangu amenituma

nije kwako kama nilivyoshuka mara ya kwanza kutoka Mbinguni.’ Nabii Yahya

akamuangalia Ibilis na akamuona kua na maumbile yenye kutisha huku akiwa na ndege

ndege wadogo wanamzunguka juu kichwani mwake, na katika sehemu zake za Siri kuna

vijumba vijumba vya ndege hao, na kwenye mguu wake kuna vikuba vya fedha.

Na hivyo Nabii Yahya akamuuliza Iblisi: ‘Hivi kwanini una videge vinavyoruka ruka

juu ya kichwa chako?’ Ibilisi akasema: ‘Kwa kuwatumia wao hua nnaziteka nyara

akili za Ibn Adam’Nabii Yahya akasema: ‘Na hivyo vikuku kwenye mguu?’ Ibilisi

akajibu: ‘Hua nnavipiga piga hivi kwa ajili ya watu hadi Ibn Adam hao waimbe na

kucheza mziki.’

Nabii Yahya akamuuliza Iblisi:‘Jee ni katika wakati gani hua unawadhibiti Ibn

Adam?’ Ibilisi akasema: ‘Pale anapokua ameshiba’ Nabii Yahya akamuuliza Iblisi:

‘Hivi jee umeona kitu chochote kile kwangu ambacho hakiridhishi ndani ya Nafsi

yangu?’ Ibilisi akasema: ‘La, Sijaona’ Nabii Yahya akauliza: ‘Hata mara moja?’

Ibilisi akasema: ‘Naam ilitokea mara moja pale ilipotokea, ulipokua umefunga na

kisha ukawa umeshiba baada ya kula sana iftari, ambapo katika usiku wa siku hio

hukuweza kuuhuisha usiku wako ama ilivyo kawaida yako.’

Hivyo Nabii Yahya akasema: ‘Basi Bila ya shaka sitokula tena Mpaka nikashiba’ Na

Ibilisi nae akasema: ‘Hakika nami, sitomwambia ukweli Ibn Adam tena’

Nabii Yahya alikua ni Mtu ambae anaependwa na kukubalika sana miongoni mwa Watu

wa Bani Israil, na katika wakati wa kipindi cha wakati huo kulikua na Mfalme ambae

alimuoa mjane mmoja ambae alikua na binti yake mdogo, hivyo binti huyo alipokua

mkubwa alikua mzuri sana na hivyo Mfalme huyu akataka kumuoa binti huyo huku

akiwa sambamba na Mama yake lakini akawa haijulikani uhalali wa Ndoa hio.

Ambapo anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Nabii Isa

Bint Maryam alimtuma Nabii Yahya Ibn Zakarriyah akiwa na miongoni mwa

Wanafunzi wake 12, kuwafundisha watu wa Bani Israil, na miongoni mwa mambo

aliyowakataza ilikua ni kutooana ndugu, hivyo Mfalme akawa anataka kumuoa na

hivyo Mfalme akawa anamtimizia matakwa yake yote’

Hivyo mama wa binti huyo akamwambia Mfalme huyo inabidi atafutwe Nabii Yahya

auliziwe juu yake. Nabii Yahya alipoitwa akasema kua Ndoa hio haikubaliki kisharia,

wakati Makuhani wao walisema kua inakubalika kutokana na kua na hofu juu ya Mfalme

huyo. Mfalme huyo akakasirika na kusema kua Nabii Yahya hataki Mfalme amuoe Bint

huyo, na binti nae akasema kua haiwezekani kwake kuolewa na Mfalme hadi


377

atakapouliwa Nabii Yahya na Baba yake, yaani Nabii Zakarriyah. Hivyo Mfalme

akaamua kutekeleza matakwa hayo.

Nabii Yahya akakamatwa na kisha akauliwa kwa kukatwa Kichwa, ambapo sehemu

iliyodondokea Damu yake basi ilikua ikichemka kama yanavyochemka maji ya Moto.

Na kila sehemu hio ikifukiwa basi bado damu inachemka tena kwa wingi zaidi.

Kwa upande wa Nabii Zakarriyah alipopata habari hio na kujua kua na yeye pia

anatafutwa basi akakimbia, na wakati anakimbia akakutana na Mti ambao akauombea

mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala kua mtu huo ufunguke ili aingie na patae nusra ndani

yake, ivyo mti ukafunguka na Nabii Zakariyyah akainga ndani yake.

Watu waliokua wakimtafuta Nabii Zakarriyah wakashindwa kumjua wapi alipojificha,

hivyo akatokea Iblisi na kuwaambia kua amemuona Nabi Zakariyyah wakati alipoingia

kwenye mtu huo. Na hata hivyo watu wa Bani Israil hawakuweza kumuamini Ibilisi

lakini nae akawathibitishia kwa kuwaonesha kipande cha Kilemba cha Nabii Zakarriyah

ambacho kilikua kimetokeza nje ya Mti huo.

Hivyo watu wa Bani Israil wakaamua kuukata mti huo, katikati kwa msumeno wakati

Nabii Zakarriyah akiwa ndani yake. Walipokua wanaukata wakamkuta Nabii Zakarriyah

ndani yake lakini nao hawakusita bali waliendelea kuukata na kumata pamoja nao Nabii

Zakarriyah aliekua ndani yake, Nabii Zakarriyah akaanza kulia huku akitaka kunadia

kumuomba msaada Mola wake. Lakini mara akatokea Malaika Jibril na kumwambia

Nabii Zakariyyah kua: ‘Ewe Zakarriyah Mola wako anakuambia kua, Kua na Subra

kwani ukilia na kuomba msaada basi matabaka 7 ya Ardhi yataangamia kwa ajili

yako, hivyo bora kaa kimya tulia na kua na ustahmilivu’

Hivyo Allah Subhanh wa Ta’ala akaamua kuwapa Adhabu kwa kuwatumia watu wa Bani

Israil Jeshi la watu ambao watawaangushia Mamlaka yao na kuwafanya Watumwa.

Hivyo sambamba katika wakati wa kipindi hiki katika ardhi ya Iraq kulikua kuna Mfalme

ambae alikua anaitwa Sennercherib na Jemedari wake Mkuu alikua akijulikana kwa jina

la Nebuchadnezer.

Hivyo Mfalme Sennerceherib akamuamrisha Nebuchadnezar atayarishe Jeshi ili

akawavamie watu wa Bani Israil, hivyo walipofika katika Mji wa Jerusalem wakakuta

Mji Umezungushiwa Ukuta Mkubwa sana na wakashindwa kuuvamia mji huo hivyo

wakaweka kambi nje, ambapo walikaa kwa masiku kadhaa bila ya mafanikio na

wakaamua kua waondoke na jeshi lao na kurudi Iraq.

Na walipokua wanajitayarisha kuondoka akatokea Bibi Kizee mmja wa Bani Israil na

kuwauliza: ‘Hivi yuko wapi kongozi wa Jeshi Hili?’ Bibi huyo akapelekwa kwa

Nebuchadnezer na alipofika basi akasema: ‘Hakika mimi nimesikia kua mnataka


378

kuondoka kabla ya kuuteka mji huu’ hivyo Nebuchadnezer akasema: ‘Naam..kwa

sababu tumeshakaa kwa mda mrefu na hatuwezi kuuteka kutokana na huu ukuta

na Wanajeshi wangu wameshaishiwa na subira na pia mahitaji yetu yanamalizika

hivyo hatuna njia isipokua kuondoka bila kufanikisha Lengo letu.’

Yule Bibi akasema: ‘Hakika mimi nilikua nafikiria hivi jee kama nikikuambieni

jambo la kufanya cha kufanya na mkafanikiwa kuingia ndani ya Mji huu, mtaahidi

kunipa kile nikitakacho? Na kisha mtamuua ninaetaka auliwe? Na mtamuachia

huru nitakaetaka aachiwe?’

Nebuchadnezar akasema: ‘Naam, tunaahidi kufanya kama utakavyo kama

ukitusaidia’ Yule Bibi akasema: ‘Sawa, hivyo utakapoamka asubuhi, basi ligawe

Jeshi lako katika makundi manne aambpo kila kundi litakaa katika upande mmoja

wa Mji. Halafu nyanyueni mikono na mseme: ‘Ya Allah hakika wewe ni mwenye

kujua juu ya kila kitu, hivyo tuongoze kwa yule aliemuua Yahya Ibn Zakarriyah’

na wakishasema hivyo basi ukuta huu mnauona mkubwa na Imara utaanguka chini

mara moja’

Hivyo ilipowasili Asubuhi basi Nebuchadnezer akaligawa Jeshi lake katika makundi

manne, kisha akaliamrisha lifanye kama vile alivyoambiwa na yule Bibi na hapo hapo

Ukuta huo ukaanguka, na jeshi lake inakinga ndani ya Mji huo kutoka katika pande nne

tofauti, walipofika ndani basi yule bibi akamwambia Nebuchadnezer: ‘Wachinje watu

wa Bani Israil juu ya sehemu hii mmoja baada ya mwengine mpaka nikwambie

basi’

Hivyo katika sehemu hio wakachinjwa Watu wa Bani Israil mmoja baada ya mwengine

mpaka wakafikia watu 70000. Na hapo sehemu hio ikasita kuchemka, yule Bibi akasema:

‘Basi imetosha kwani akichinjwa Nabii wa Allah, basi Allah hua haridhiki hadi pale

itakapokua yule aliemchinja Nabii huyo na kila ya yule aliefurahia jambo hilo

achinjwe pia.’ Na kisha baada ya hapo wakalivunja Jengo la Asahraa liliomo ndani ya

Ardhi ya Al Quds na akawateka watu wa Bani Israil na kufanya Watumwa

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anaelezea namna Mayahudi walivyokua wakiwaua

Mitume waliotumiwa kwa kusema:


379

‏﴿وَلَقَدْ‏ آتَيْنَا مُوسَى ٰ ٱلْكِتَابَ‏ وَقَف َّيْنَا مِن بَعْدِهِ‏ بِٱلر ُّسُلِ‏ وَآتَيْنَا عِيسَى ٱبْنَ‏ مَرْ‏ يمََ‏

ٱ ب لْ‏ أ َيِّنَا َ تَِو ي َّدَْهُ‏ بِرُو حِ‏

ٱلْقُدُسِ‏ أَفَكُل َّمَا جَآءَكُمْ‏ رَسُولٌ‏ بمَِالاَتَهْوَىٰ‏ أَنُْفسُكُمْ‏ ٱسْتَكْبَرْتمُْ‏

فَفَرِيقاً‏ كَذ َّبْتُمْ‏ وَفَرِيقاً‏ تَقْتُلُونَ‏ ﴾

Walaqad atayna moosa alkitaba waqaffayna min baAAdihi bialrrusuli waatayna

AAeesa ibna Maryama albayyinati waayyadnahu biroohi alqudusi afakullama

jaakum rasoolun bima la tahwa anfusukumu istakbartum fafareeqan

kadhdhabtum wafareeqan taqtuloona (Surat Al Baqara 2:87)

Tafsir: Na kwa hakika tulimpa Musa Kitabu na baada yake tukatuma Mitume wengine,

na tukampa Isa Ibn Maryam vithitibitisho vilivyokua wazi na takamthibishia kwa Ruhi

Al Qudus (Malika Jibril) hivi jee kila wakija Mitume na kile ambacho hakiendani na

Matamanio ya Nafsi zenu Mtafanya Kibri? Na mkawakadhibisha baadhi yao na

mkawaua baadhi yao.

Ambapo amesema Abu Ubaidah Ibn Jarrah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Watu wa Bani Israil waliua kwa kila siku

Mitume 43 na Wacha Mungu 170 ambao walikua wanawaamrisha kufanya mema.’’

Na akasema tena Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an kua:

‏﴿فَبِمَا نَقْضِهِمْ‏ م َّيثَاقَهُمْ‏ وَكُفْرِهِم آبََ‏ تِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَقَتْلِهِمُ‏ ٱلأَنْبِيَآءَ‏ بِغَيرِْ‏ حَقٍّ‏ وَقَوْلهِِمْ‏

قُلُوبُنَا غُلْفٌ‏ بَلْ‏ طَبَعَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلَيْهَا بِكُفْرِهِمْ‏ فَلاَ‏ يُؤْمِنُونَ‏ إِلا َّ قَلِيلاً‏ ﴾

Fabima naqdihim meethaqahum wakufrihim bi-ayati Allahi waqatlihimu alanbiyaa

bighayri haqqin waqawlihim quloobuna ghulfun bal tabaAAa Allahu

AAalayha bikufrihim fala yu/minoona illa qaleelan (Surat An Nisaa 4:155)

Tafsir: Na kutokana na kuvunja kwao Miadi yao na kuzikufuru aya za Allah, na katika

kuwaua Mitume bila ya haki, na kutokana na kusema kwao: ‘Nyoyo zetu zimefunikwa

(Hatukifaham wanachokisema Mitume), La bali Allah ameweka muhuri kwenye

nyoyo zao kutokana na kukufuru kwao, kwani hawakuamini isipokua kidoogo tu’


380

Ambapo wanasema Wanazuoni wamesema kua Allah Subhanah wa Ta’ala aliwajaalia

watu hawa wa Bani Israil kua ni wenye kufikwa na Mitihani na hivyo waliuawa watu

70000 badala yake kutokana na kumuua Nabii Zakarriyah na watu 70000 kutokana na

kumuua Nabii Yahya.

Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kutakua na Hijra baada ya

Hijra, hivyo watu bora Duniani ni wale ambao wakaishi katika Ardhi ya Hijra ya

Nabii Ibrahim’(Mustadrak Al Hakim)

Na amesema Al Azdi Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alitutuma sisi tukatafute Ngawira kwa miguu, lakini hatukupata kitu Hivyo

tukarudi ambapo nae aliona namna tulivyokua tumechoka kutokana na

muonekano wa Nyuso zetu

Hivyo akasimama na kisha akasema: Ya Allah Usiwaachie peke yao kwa Ajili yangu

pale nitakapokua Dhaifu kwa ajili yao Usiwaachie peke yao kwa ajili yao pale

watakapokua Dhaifu kwa ajili ya Watu wao, pale watakapozuiliwa Mema kwa ajili

yao

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaweka Mkono juu ya kichwa

changu na kusema: Ewe Ibn Hawalah! Kama ukiona Ukhalifa umeingia kwenye Al

Quds, halafu ikafuatia Mitetemeko ya Ardhi, kisha Mitihani, na mambo mengi

Makubwa yakafuatia, basi Wakati uliobakia utakua karibu kwa watu kuliko huu

mkono wangu kwenye Kichwa chako’ (Mustadrak Al Hakim)

Na amesema Imam Abu Muhammad Al Hasan Ibn Hibat Allah Ibn Abd Allah Ibn Asakir

kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Hili jambo (la Ukhalifa)

litafuata baada yangu hapa Madinah , kisha katika Ardhi ya Sham, Kisha Hijaz,

Kisha Iraq, Kisha Mjini (Istanbul) Kisha Bayt ul Maqdis hivyo likifika Baytu ul

Maqdis basi itakua limefikia sehemu yake hivyo hakuna watu watakaoliondoa

kutoka katika Mji wao ambao watalipata tena jambo hilo.’

Naam..Ama kuhusiana na Hadithi hizi zote zinazungumzia kuhusiana na Ukhalifa wa

Kiislam katika Ardhi husika, na Historia inaonesha kua sehemu zote zilizotajwa katika

Hadith juu ya Ukhalifa wa Kiislam kua ni tayari Ukhalifa ushawahi kutawaliwa..isipokua

Bayt ul Maqdis yaani Jerusalem.

Kwani amesema Allah Subhanah wa Ta'ala katika Surat Al Isra kua:


381

‏﴿وَقَضَيْنَآ إِلىَٰ‏ بَنىِ‏ إِسْرَائِيلَ‏ فىِ‏ ٱلْكِتَابِ‏ لَتُفْسِ‏ دُن َّ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ مَر َّتَينِْوَلَ‏ ت َعْلُ‏ ن َّ عُلُوّاً‏

كَبِيراً۞فَإِذَا جَآءَ‏ وَعْدُ‏ أُولاهمَُا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ‏ عِبَاداً‏ ل َّنَآ أُوْلىِ‏ أبَْسٍ‏ شَدِيدٍ‏ فَجَاسُواْ‏

خِ‏ لاَلَ‏ ٱلدَِّرِ‏ وَكَانَ‏ وَعْداً‏ م َّفْعُولاً‏ ﴾

Waqadhayna ila banee isra-eela fee alkitabi latufsidunna fee al-ardhi marratayni

walataAAlunna AAuluwwan kabeeran; Fa-idha jaa waAAdu oolahuma

baAAathna AAalaykum AAibadan lana olee ba/sin shadeedin fajasoo khilala

alddiyari wakana waAAdan mafAAoolan(Surat Al Isra 17:3-4)

Tafsir: Na Tumewatakia Bani Israil katika Kitabu kua Mtafanya Ufisadi Ardhini mara

mbili na mtakua madhalimu na wenye Kibri kikubwa sana kisha Itapokamilika Ahadi

ya kwanza baina yake tutatuma Dhidi yenu waja wetu wenye nguvu kubwa (wa Kivita)

Wataingia Mpaka Ndani kabisa ya Majumba yenu na Ilikua ni Ahadi iliyotimizwa.

Ambapo anasema Imam Said Ibn Jubayr kuhusiana na aya hizi kua: ‘Aya hizi

zinazungumzia tukio lililowakuta Watu wa Banii Israil walipotawala na kuja juu

sana kisha Wakavamiwa na Nebuchadnezer. Ambae aliangamiza kila kitu chao

Bani Israil katika Mji wa Jerusalem na kisha akawaua baadhi yao na waliobakia

akawachukua na kuenda Nao katika Ardhi ya Babylon na kuwafanya Watumwa

wa utawala wake kwa mda wa miaka 70. Na kisha baada ya miaka 70, Utawala wa

Uajemi Ukauvamia Utawala wa Nebuchadnezer na Kuuangusha, na kisha

ukawaachia Huru watu wa Bani Israil nao wakarudi tena Jerusalem.’

Naam..Allah Subhanah wa Ta'ala anaendelea kuliezea tukio kwa kusema katika Surat Al

Isra kua:

‏﴿ثمُ َّ رَدَدْ‏ َ لَكُ‏ مُ‏ ٱلْكَ‏ ر َّةَ‏ عَلَيْهِ‏ مْ‏ وَأَمْ‏ دَ‏ دْ‏ َ كُ‏ م أبَِمْ‏ وَالٍ‏ وَ‏ بَنِينَ‏ وَجَ‏ عَلْنَاكُ‏ مْ‏ أَكْثَرَ‏ نَفِير اً۞إِنْ‏

أَحْسَنْتُمْ‏ أَحْسَنْتُمْ‏ لأَِنْفُسِ‏ كُمْ‏ وَإِنْ‏ أَسَأْتمُْ‏ فَلَهَا فَإِذَا جَآءَ‏ وَعْدُ‏ ٱلآخِ‏ رَةِ‏ لِيَسُوءُواْ‏

وُجُوهَكُمْ‏ وَلِيَدْ‏ خُ‏ لُواْ‏ ٱلْمَسْجِ‏ دَ‏ كَمَا دَخَلُوهُ‏ أَو َّلَ‏ مَر َّةٍ‏ وَلِيُتَبرُِّواْ‏ مَا عَلَوْاْ‏ تَتْبِ‏ يراً‏ ﴾

Thumma radadna lakumu alkarrata AAalayhim waamdadnakum bi-amwalin

wabaneena wajaAAalnakum akthara nafeeran; In ahsantum ahsantum li-


382

anfusikum wa-in asa/tum falaha fa-idha jaa waAAdu al-akhirati liyasoo-oo

wujoohakum waliyadkhuloo almasjida kama dakhaloohu awwala marratin

waliyutabbiroo ma AAalaw tatbeeran(Surat Al Israa 17:6-7)

Tafsir: Na Kisha tukakurudushieni nyie ushindi juu yao watu hao (wa Nebuchadnezer)

Na Tukakusaidieni kwa Mali na Watoto Na tukakujaalieni Uwezo mkubwa wa

Kunguvu (Nasi tukasema) Kama Mtakua Wema basi Mtakua wema kwa ajili ya Nafsi

zenu Na Kama Mkiasi basi ni kwa hio (Nafsi yenu pia) Na Kisha Itakapokuja Ahadi

ya Pili Kuzihuzunisha Nyuso zenu (Kwa tutakalokuleteeni) Na Kuingia (Maadui zenu)

Msikitini (Al Quds) Kama walipoingia mara ya kwanza na kukuangamizeni kwa

Muangamizo mkubwa utokanao na mikono yao.

Kwani aya mbili hizi zinazungumzia kuhusiana na tukio kubwa litakalotokea baada ya

Watu wa Bani Israil ambalo ni la pili baada ya lile lililowakuta kutoka kwa Mfalme

Nebuchadnezer, ambapo baada yake walirudi tena Jerusalem na juu ya hili basi tunaona

kua kuna mitizamo tofauti, kwani ukweli ni kua kabla na baada ya tukio la

Nebuchadnezer na Mayahudi kurudi Jerusalem basi Mayahudi waliasi tena mara kadhaa,

na wakaletewa Mitume na Manabii Kadhaa.

Ambapo mara ya moja wapo ni wakati wa Miaka 170 kabla kipindi cha Nabii Zakarriyah,

Nabii Yahya na Nabii Isa, basi akatokea Mfalme wa Uturuki, akawavamia na kuwaua na

kuwateka waliobakia. Na kisha baada ya hapo watu wa Bani Israil waliookoka baada ya

kukimbia wakarudi Jerusalem na wakavamiwa na Utawala wa Roman Empire.

Na pia katika kipindi cha Miaka minane kabla ya kuzaliwa Nabii Isa Alayhi Salam, na

kisha miaka ya baadae Watu wa Bani Israil wakaasi dhidi ya Utawala wa Roman Empire,

ambapo katika Uasi huo basi Watu wa Bani Israil wakashambiliwa na kuuliwa tena na

kutekwa. Hivyo kutokana na Uasi wao kwa Mola wao basi Allah Subhanah wa Ta'ala

amewaahidi kua Watarudi Jerusalem, ambapo Watapigwa tena kwa pigo kubwa zaidi.

Na tumeona Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika hadith alisema kua Ukhalifa

Utaingia Jerusalem kisha ndio kitafuata Kiama. Hivyo bila ya shaka, kuna pigo kubwa

zaid ambalo linawasubiri Mayahudi, ambalo litapelekea kuwepo kwa Ukhalifa wa

Kiislam katika ardhi ya Jerusalem, na kwa kua hatujafika huko, basi na turudi katika kisa

chetu ambacho ndani yake kinamjumuisha kwa pamoja, Nabii Zakarriyah, Nabii Yahya,

Maryam Bint Imran na kuzaliwa kwa Nabii Isa Ibn Maryam kama ilivyozungumziwa

ndani ya Surat Maryam.


383

SABABU YA KUSHUSHWA KWA SURAT MARYAM

Tunapozungumzia kisa cha Nabii Isa Ibn Maryam basi hua tunazungumza kisa ambacho

kwa upande mmoja Allah Subhanah wa Ta’ala amekizungumzia ndani ya Kitabu chake

Kitukufu kwa ajili ya kumtia Moyo zaid na kumfunza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam na Masahaba zake juu ya yale yaliyotokea kwa Mitume waliofuatia kabla ya kuja

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ili awe ni mwenye kua na subra na ustahmilivu

zaidi kutokana na madhila makubwa anayofanyiwa yeye na wafuasi wake wa Dini ya

Kiislam katika ardhi ya Makkah kutokana na Chuki dhidi yao kutoka kwa watu wa Kabila

la Quraysh.

Kwani kwanza watu wa Quraysh walianza kuwaadhibu wale Masahaba ambao walikua

ni dhaifu miongoni mwa waliokua wakiamini Imani ya Dini ya Kislam, kwa kuwaadhibu

Wanawake wake kwanza kwa mfano kuna Mwanamke ambae alikua akijulikana kwa jina

la Zimmira Radhi Allahu Anha ambae walimtesa sana, na kuna aitwae Al Nahdiya au

Hakima Bint Habib ibn Kuwayb, Radhi Allahu Anha ambae walimpiga mpaka akopeteza

Nuru ya Macho yake, bila ya shaka hatuwezi kumsahau Sumayyah Bint Khayat Radhi

Allahu Anha ambae ndie mtu wa kwanza kupata ushahidi baada ya kua ni Muislam wa

kwanza kuuliwa kutokana na Imani yake.

Halafu wakahamia kwa Watoto ambao ni vijana kama Musab Ibn Umayr Radhi Allahu

Anhu ambae likua ni Sahaba kijana mwenye kuvutia kuliko vijana wote wa Kiume wa

mji wa Makkah, kwani kila Mwanamke wa Mji wa Makkah alikua anatamani kuolewa

nae, na hii pia ni kutokana na kua Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu alikua na wazee

ambao ni matajiri sana na walikua wanaompenda sana, na hivyo alikua anavaa vizuri na

kupendeza kuliko watu wote katika mji wa Makkah.

Lakini aliposilimu tu na kuamua kuingia kwenye Dini ya Kiislam basi mambo yake

mazuri yote haya yalitoweka, kwani alifungiwa ndani kwa mda wa miaka mitatu na

kuzuiliwa asitoke nje kwani akitoka basi ataonana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, na alipoachiwa na kuonekana kua hana muelekeo wa kuachana na Iman ya Dini

ya Kiislam basi alipokonywa kila kitu chake, na akawa ni mwenye kuonekana kama

Omba omba anaevaa matambara mabovu badala yake, lakini hata hivyo haya yote

hayakumfanya Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu kua ni mwenye kuachana na Imani

yake hio mpya kwani hali ilikua ni kinyume chake. Na matokeo yake Musab Ibn Umayr

Radhi Allahu Anhu akawa ndie Balozi wa kwanza wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam katika Mji wa Madinah na alifanikiwa kuupata ushahidi katika Vita vya Badr.


384

Na alikuwemo pia Talha Ibn Ubayd Allah Radhi Allahu Anhu ambae alikua ni mwenye

Umri wa miaka 15, pale alipoingia kwenye Uislam ambapo mama yake alikua akimfunga

kamba na kutembea nae sokoni kama mbuzi huku akimtukana, na Makafiri wakimpiga

na kumlaani ni nzima.

Alikuwemo pia Imran Ibn Husein Radhi Allahu Anhu ambae alificha tukio la kusilimu

kwake, na hivyo siku moja Baba yake Imran akaenda katika Dar Al Arqam ambayo ni

Nyumba ya Arqam Ibn Abi Arqam Radhi Allahu Anhu ambae ni Sahaba mdogo kijana

wa umri wa miaka 14 ambae aliirithi kutoka kwa Baba yake, Nyumba hii ilikuwepo

katika upande wa Kaskazini chini ya Kilima cha Safa ambamo ndani yake walikua

wakikutana Masahaba pamoja na Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam kwa siri

kusomeshana Qur’an.

Na hivyo mzee Husein alipoingia ndani basi Masahaba walimficha Imran kwa kumkalia

ili asionekane na Baba yake kisha akaja kudhuriwa lakini badala yake Mzee Husein

alipoingia ndani basi alienda moja kwa moja kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na akasilimu, na baada ya kusilimu basi Imran akatoka chini ya miguu ya Masahaba

waliokua wamemkalia na akamkimbilia Baba yake na kukumbatia kwa furaha na

mapenzi yake juu ya Baba yake, huku yeye na Masahaba waliobakia wakilia kwa wingi

wa Imani na hisia zilizowaja Nyoyoni mwao baina yao.

Ambapo kwa upande wa pili kisa hiki kiliteremshwa na kuzungumziwa ndani ya Qur’an

kwa ajili ya kua ni kama Silaha na Kinga kwa ajili ya Waislam dhidi ya Maadui zao hao.

Kwani kisa hii kilikua ndio Silaha na kinga pekee ambayo iliwafanya Waislam wawe

washindi dhidi ya Makafiri wa Makkah pale walipozidiwa na hivyo kuamua kukimbilia

uhamishoni katika ardhi ya Uhabeshi, hivyo bila ya shaka Allah Subhanah wa Ta’ala

ambae ndie m-bora wa kupanga na kukadiria, aliamua kukishusha kisa hiki kabla ya

kufanyika kwa Hijra hio mnamo mwishoni mwa mwaka wa 4 baada ya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kushushiwa Utume.

Hivyo mwanzoni mwa mwaka wa 5 wa Utume, basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam akawaambia Masahaba zake kua wahamie Uhabeshi, kwani ndani ya Ardhi hio

kuna ‘An Najash’ yaani ‘Mfalme’ ambae anajulikana kwa jina la An Najash Ashama Ibn

Abjar ambae ni Muadilifu na hakuna anaepata madhara kutokana nae kama

wanavyoelezewa miongnoni mwa Ahl Al Kitab wenye sifa ya Uadilifu pale iliposema

Qur’an katika aya ifuatayo:


385

‏﴿وَمِنْ‏ أَهْلِ‏ ٱلْكِتَابِ‏ مَنْ‏ إِنْ‏ أتَْمَنْهُ‏ بِقِنْطَارٍ‏ يُؤَدِّهِ‏ إِلَيْكَ‏ وَمِنْهُمْ‏ م َّ نْ‏ إِن أتَْمَنْهُ‏ بِدِينَارٍ‏

لا َّ يُؤَدِّهِ‏ إِلَيْكَ‏ إِلا َّ مَا دُمْتَ‏ عَلَيْهِ‏ قَآئِماً‏ ذٰلِكَ‏ أبَِن َّهُمْ‏ قَالُواْ‏ لَيْسَ‏ عَلَيْنَا فىِ‏ ٱلأُمّ‏ يَِّين ِ

سَبِيلٌ‏ وَيَقُولُونَ‏ عَلَى اهلل َِّ‏ ٱلْكَذِبَ‏ وَهُمْ‏ يَعْلَمُونَ‏ ﴾

Wamin ahli alkitabi man in ta/manhu biqintarin yu-addihi ilayka waminhum man

in ta/manhu bideenarin la yu-addihi ilayka illa ma dumta AAalayhi qa-iman thalika

bi-annahum qaloo laysa AAalayna fee al-ommiyyeena sabeelun wayaqooloona

AAala Allahi alkadhiba wahum yaAAlamoona (Surat Al Imran 3:75)

Tafsir: Na miongoni mwa watu wa Ahl ul Kitab kuna yule ambae hata kama

akiaminiwa Qantri (Mali nyingi sana) basi atakurudishia mwenyewe, na miongoni

mwao ni yule ambae ukimuamini Dinari moja basi hatokurudishia, isipokua pale

inapokua unamdai kwa mfululizo, na hii ni kwa sababu wamesema: ‘Hakuna tatizo

kwetu sisi kusaliti na kuchukua mali ya wasiojua’ na wanasema kuhusiana na Allah

uongo na wanajua juu ya hilo.

Hivyo Masahaba 10 Wanaume na Masahaba wa 4 Wanawake wakahamia kisiri siri,

ambao ni Sad Ibn Abi Waqqas, Jahsh Ibn Riyab, Abd Allah Ibn Jahsh, Jafar Ibn Ab Talib,

Uthman Ibin Affan na mkewe Ruqayyah Bint Rasul llah Salallahu Alayhi wa Salam, Abu

Hudhayfah Ibn Utbah na Mkewe Sahla Bint Suhayl Zubayr Ibn Awwam, Musab Ibn

Umair, Abd Rahman Ibn Awf, Abu Salama Abd Allah Ibn Al Asad na mkewe Ummu

Salamah Hind Bint Abi Umayyah, Uthman Ibn Mazun, Amr Ibn Rabiah, Laylat Bint

Asmah Radhi Allahu Anhum.

Masahaba hawa walisafiri kwa kutumia Jahazi kutoka katika mji wa Shuaiba na kufikia

katika mji wa Adulis, na ingawa leo hii hua liko katika ardhi ya maeneo ya Eritrea lakini

katika wakati huo eneo hilo lote lilikua linajulikana kama Abissiniyah yaani Ethiopia. Na

kisha baada ya hapo ukafuatia msafara wa Masahaba 83 ambao ni Wanaume na

Masahaba 18 ambao ni Wanawake wakahamia pia.

Ambapo anasema Ummu Salamah Radhi Allahu Anha kua: ‘Wakati sisi tulipohamia

katika Ardhi ya Uhabeshi, basi tuliishi na miongoni mwa Majirani bora ambae ni

An Najashi, tulitekeleza Ibada zetu kwa usalama na amani, tulimuabudu Allah

Subhanah wa Ta’ala bila ya kubughudhiwa na hatukuwahi kusikia tu chochote kile

ambacho hatukikipenda. Hivyo habari hizi zilipowafikia watu wa Quraysh basi

wakaazana kupanga njama zao dhidi yetu.’


386

Yaani watu wa Kabila la Quraysh la Makkah waliamua kuwatuma Wajumbe maalum

wawili ambao ni vijana mahiri kwa kua na sifa ya kujadiliana na kushawishi kidiplomasia

hawa hawakua vijana wowote isipokua walikua ni Amr Ibn Al Aas ambae mbali ya kua

ni mwenye hikma na busara sana miongoni mwa Vijana wa Quraysh lakini pia alikua ni

Kijana Mpiganaji mahiri sana, ambapo pamoja nae akatumwa Abd Allah Ibn Abi Rabii

ambae pia alikua ni mfanya biashara maarufu anaejulikana mpaka Abissiniyah.

Wajumbe wawili hawa walipewa jukumu la kuwatumia zawadi wajumbe wa Baraza la

washauri la An Najash kwa ajili tu ya kumshauri An Najash awarudishe Waislam hao

katika Mji wa Makkah, hivyo Amr Ibn Al Aas akamwambia An Najash kua: ‘Kwa

hakika katika Ardhi yako kuna watu waliotoka kwetu ambao wameasi na

wamewakimbia watu wao, baada ya kuachana na Imani ya wazee wao na wamekuja

kuishi katika ardhi yako na kuendeleza Imani ya Dini yao mpya, lakini hawakuingia

kwenye Dini yako, hivyo tungependa uturuhusu kuwarudisha kwetu katika familia

zao kwani kuna watu wao ambao wanasikitika na kuhuzunika kutokana na

kuondoka kwao.’

Baada ya Amr Ibn Al Aas kumalizia kuelezea kuhusiana na matakwa ya watu wa

Quraysh, mbele ya An Najash na baraza lake la Washauri, basi washauri hao

wakamuunga mkono Amr Ibn Al Aas, kua kama hali ya watu hao ni hali ya waasi

waliosababisha machafuko katika ardhi yao, na wamekimbia na kukimbilia Abissiniya

basi bila ya shaka inabidi watu hao warudishwe kwao, ili wasije wakaleta machafuko

kutokana na Imani ya Dini yao hiyo mpya ambayo pia ni tofauti na Imani ya Dini ya

Utawala wa An Najash, lakini hata hivyo kwa upande wa An Najash kutokana na Uadilifu

wake basi mara tu baaada ya kusikiliza hoja hizo basi akasema: ‘La, kamwe sitoweza

kuwaruhusu watu hawa ambao ni Majirani zangu kwa watu wawili hawa, hata

kama watu hai watakua wanampango ya siri dhidi ya Utawala wangu, hadi pale

nitakapowata na kuzungumza nao na kusikiliza kuhusiana na majibu yao kutokana

na hoja na shutuma zenu. Na hakika ni wajibu wangu mimi kua na uhusiano mzuri

nao kwani nao wana uhusiano mzuri nami.’

Na kisha baada ya hapo An Najash akaamrisha kua Waislam hao waletwe mbele yake,

kwa ajili ya kufanya mahojiano nao. Masahaba hao wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam walipopata habari ya wito huo basi basi wakakaa na kuulizana namna ya kujibu

suali hilo la na Najash, kwa kusema: ‘Hivi jee sisi tutamwambia nini sisi An Najash?’

na hivyo wakakubaliana kua watamchagua kijana Mdogo ambae nae pia ni mahiri kwa

ufahamu wa Lugha na mwenye kujaa Hikma na Busara katika kuzungumza kwake.

Huyu hakua kijana mwengine yeyote isipokua alikua ni ingawa Jafar Ibn Abi Talib Radhi

Allahu Anhu alikua ni Ibn Ami wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam lakini

pia alikua ni miongoni mwa Masahaba watano waliotoka katika ukoo wa Banu Hashim

waliofanana sana kisura na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ambapo


387

miongoni mwa waliofanana nae pia wakiwemo Hasan Ibn Ali Ibn Abi Talib (mjukuu wa

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam), Abu Sufyan Ibn Al Harith, As Sayb Ibn

Ubayd (Babu wa babu yake Imam Muhammad Idris Al Shafi’i) na Qutham Ibn Al Abbas

Radhi Allahu Anhum.

Hivyo Masahaba wakamchagua Jafar Radhi Allahu Anhu ambae babu yake ndie

aliekabiliana na Jeshi la Abraha katika mwaka wa Tembo pale Abraha ambae ndie

aliekua Gavana wa Yemen anaemuwakilisha Mtawala wa Abissiniya hapo kabla

alipotaka kulivunja Al Kaabah, na akaangamizwa na Allah Subhanah wa Ta’ala, ambapo

kujitambulisha kwake Jafar mbele ya An Najash basi kutambanishia An Najash kua

anazungumza na nani, hivyo Jafar atasema ukweli kama ulivyo kwa kusema: ‘Bila ya

shaka tutamwambia kama alivyotuamrisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

bila ya kujali kitakachofuata baada ya hapo.’

Na hivyo walipowasili kwa An Najash basi wakamkuta An Najasha akiwa na Makasisi

wake na Vitabu vyao pamoja na Wajumbe wa Baraza lake la Washauri, ambapo nae

baada ya kuwakaribisha basi akawauliza Masahaba hao kwa kusema: ‘Nimesikia kua

nyinyi mna Dini mpya ambayo ni tofauti na Dini ya asili ya watu wenu, hivyo nilikua

nataka kujua hivi jee hii dini yenu ni Dini gani, na kwanini kutokana nayo mkawa

mmewaasi wazee wenu? Na hapo hapo mkawa hampo kwenye ufuasi wa Dini yetu’

Hivyo anasema Umm Salamah Radhi Allahu Anha kua: ‘Mzungumzaji wetu alikua ni

Jafar Ibn Abu Talib ambae alisema: ‘Ewe Mfalme, sisi tulikua ni watu wajinga,

tuliokua tukiishi kama wanyama wa mwituni, mwenye nguvu miongoni mwetu

aliishi kwa kuwatumia wasiokua na nguvu. Tulikua hatuna sheria yeyote, na tulikua

hatuna mamlaka isipokua wenye nguvu dhidi ya wasiokua na nguvu. Tulikua

tukiabudu masanamu yaliyotengenezwa kutokana na udongo au miti, na hatukujua

ni nini maana ya heshima wala nini maana ya Utu.

Halafu Mungu akatushushia Rehma zake, akatutumia Mtume kutoka miongoni

mwetu, ambae anafahamika kutokana na ukweli wake na uaminifu wake, tabia

zake ni mfano wa kuingwa miongoni mwetu, na ni mwenye kutoka katika ukoo bora

miongoni mwa Waarabu. Akatuita katika kumuabudu Mungu mmoja, na

akatukataza kuyaabudia Masanamu, akatuamrisha kusema ukweli, kuwalinda

wasiokua na nguvu, Masikini, Wanyonge, Wajane na Mayatima.

Ametuamrisha kuwaheshimu Wanawake na kua tusiwasingizie mambo ya uongo.

Wengi miongoni mwa watu wetu bado ni wenye kua na Miungu mingi na

wanachukia maamuzi yetu ya kujiunga na Imani mpya ambayo inayoitwa Uislam.

Hivyo wameanza kututeketeza, na ni katika kukimbia mauaji yao ndio tukafuata

usalama katika Ufalme wako.’


388

Maneno haya yalikua ni yenye sifa ya Qawlan Sadidah na hivyo ujumbe wake ulifika

ndipo na kama unavyotakwa ufike na kuacha athari inayotakiwa ndani ya Moyo wa An

Najash na kumbakisha akiwa ni mwenye fikira na hisia kubwa sana An Najash, hivyo

akasema kumwambia Jafar Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hivi Jee unao

uthibitisho wowote ule kutoka kwenye Kitabu cha huyo Mtume wenu?’ ambapo

Jafar Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akajibu: ‘Naam!’ An Najash akasema: ‘Nisomee’

Hivyo Jafar Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kuanza kumsomea An Najash Surat

Maryam, kuanzia mwanzo wake hadi katika aya ya 34, kama tutakavyoona katika Tafsir

yake na hivyo kutokana na kusikiliza kwake kisomo cha Jafar Ibn Abi Talib Radhi Allahu

Anhu na maana ya tafsir yake basi kulimpelekea An Najash kutokwa na machozi, hadi

Ndevu zake zikaroa kwa machozi, na Makasisi wa An Najash nao wakajaza vitabu vyao

machozi, kutokana na Aya hizo, kisha An Najsha akasema: ‘Naapa kwa jina la Mungu

kua Hiki Kitabu chenu na Kitabu cha Musa vimetokana na Chanzo kimoja, Wa

Allahi mimi sitokuslimisheni bali nitakubakisheni kwenye ardhi yangu na

sitokusalitini na sitokurudisheni mkateswe na maadui zenu.’

Umm Salamah Radhi Allahu Anha anaendelea kusema kua: ‘Baada ya Amr Ibn Al Aas

kuondoka na Abd Allah Ibn Rabiah kuondoka mbele ya An Najash basi Amr Ibn

Al As akasema: ‘Wa Allahi nnaapa mimi kua kesho nitawakilisha maelezo ambayo

yataung’oa Mzizi wa Kila kitu katika maisha yao’ ambapo Abd Allah Ibn Rabia Radhi

Allahu Anhu akasema: ‘Haina haja kwa sababu hata hivyo hawa watu wetu wana

haki za Nasaba ya Kifamilia Nasi, hata kama ikiwa wamepingana nasi’ hivyo Amr

Ibn Al Aas akasema: ‘Wa Allahi nitamjuulisha An Najash kua Hawa Waislam

wanasema kua Isa Ibn Maryam ni Mja.’

Hivyo Siku ya pili yake Asubuhi Amr Ibn Al Aas akamwambia An Najash kua: ‘Ewe

An Najash hakika hawa watu wanasema sivyo kuhusiana na Isa Ibn Maryam, hivyo

hebu waite uwaulize upate kujua Jee wanasemaje juu yake?’ naam, maneno haya

yalimshtua An Najash, kwa sababu alikua ameshawakubalia Waislam na kuwaahidi

usalama watakapokua katika ardhi yake, lakini sasa kama inakuwa wanasema sivyo

kuhusiana na Isa Ibn Maryam basi itabidi asiwaonee huruma kwani hata watu wake

hawatoweza kumfaham na watasababisha machafuko na hivyo nae atapata upinzani

mkubwa sana, hivyo akaamrisha kua Waislam hao waitwe tena mbele yake.

Waislam walipoitwa basi wakulizwa: ‘Hivi Jee Dini yenu inasemaje nyie kuhusiana

na Isa Ibn Maryam’

Hivyo Jafar Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Hakika sisi tunasema kile

ambacho amekisema Mtume wetu kutokana na Kitabu alichokuja nacho ambacho

kinasema kua: ‘Isa Ibn Maryam ni Mja wa Allah, Ni Mtume wake, Ni Ruhi ambae


389

ameumbwa na yeye, Ni Kauli yake ambayo imepitia kwa Maryam Bint Imran,

ambae ni Bikira’

Baada ya kusikia hivyo basi An Najash akainama na kuchora mstari chini kwa

fimbo yake kisha na kisha akasema: ‘Isa Ibn Maryam hakuvuka juu ya kile

mnachokisema hata kwa upana wa mstari wa fimbo hii.’ Kisha akawageukia

Waislam na kuwaambia: ‘Wallahi Naapa kua mko huru kuabudu mtakavyo katika

ardhi yangu, na yeyote yule atakae kubughudhini basi atapata adhabu kali juu yake

na pia atalipa fidya ya dhahabu juu ya yeyote yule atakaembughudhi miongoni

mwenu’

Ummu Salamah Radhi Allahu Anha anaendelea kusema kua: ‘Hivyo Amr Ibn Al Aas

na Abd Allah Ibn Rabiah wakaondoka huku wakiwa wameadhirika sana, huku sisi

tukiwa tumebakia na kuishi katika makazi mazuri pamoja na jirani yetu An

Najash.’

Naam..hivyo hio ndio sababu na malengo ya kushushwa Surat Maryam ambayo ni yenye

98 ambazo takriban zote ni zenye kumalizikia na harkah ya Fat-ha tein na hivyo kuifanya

kua ni miongoni mwa Sura ambazo zina mpangilio mzuri sana na wa kuvutia sana

kimtiririko katika kuisoma kwake.

Ambapo anasema Ummu ul Muuminina Aisha, Abd Allah Ibn Zubayr, Bahr ul Ilm Abd

Allah Abbas Radhi Allahu Anhum kua: ‘Surat Maryam ni Sura iliyoshuswa katika Mji

wa Makkah’ na Imam Muqatil Ibn Sulayman amesema kua: ‘Surat Maryam yote

Imeshushwa Makah isipokua Aya yake 58 ya Sijda ndio iliyoshushwa katika Mji

wa Madinah ’ na Kwa upande wa Imam Al Suyuti basi yeye amesema kua : ‘Surat

Maryam yote imeshushwa Makkah isipokua Aya yake 58 na aya ya 71 ndio

zimeshushwa Madinah ’

HARFU MUQATTAA’AT NA KISA CHA NABII ISA.

Neno MuqattaA’at ni neno lililotokana na neno Qata’a ambalo kwa Lugha ya Kiarabu

hua linamaanisha Kukata, Kutengenisha, Kugawa, Kutofautisha. Hivyo Harfu

MuqattaA’at hua inamaanisha herufi za Lugha ya Kiarabu ambazo zinapoandikwa na

zinaposomwa hua zinasomwa kwa kutengenishwa kwa mfano herufi Kaf Ha Ya Aain

Saad ambalo ndio neno la mwanzo baada ya aya ya ufunguzi ya Biismi Allahi Rahmani

Rahim wa Surat Maryam ambayo ni Sura ya 19 iliyomo ndani ya Qur’an, na herufi hizi

kwa baadhi pia hua wanaziita kua ni Huruf al Mutafarriqa yaani Herufi zilizotenganika.


390

Ambapo ingawa kuna Wanazuoni wasemao kua neno كٓھیعٓصٓ‏ Kaf Ha Ya Aain Saad ni

miongoni mwa yale maneno yanayojumuishwa katika Harfu MuqattaA’at (Harfu

zilizokatwa au zilizofupishwa) ambazo hua hakuna anaejua maana yake isipokua

mwenyewe Allah Subhanah wa Taála.

Lakini kwa upande wa Mujaddid ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Fakhr Ad Din Al

Razi amesema kua: ‘Haiwezekani kua Allah Subhanah wa Taála, aingize kitu ndani

ya Kitabu chake Qur’an ambacho sisi hatutokifaham maana yake. Na kwa sababu

yeye Allah Subhanah wa Taála ndie alietuamrisha sisi kukitafakkar kitabu chake

kwa lengo la kutupa uongofu kutokana nacho. Hivyo basi lengo hili la kuitafakkari

Qur’an halitoweza kufikiwa kama ikiwa hatutoifaham maana yake, kwani lengo

hili huweza kufikiwa pale tu baada ya kufaham maana yake. (Mafatih al Ghayb,

Tafsir al Kabir)

Baadhi ya wenye kujua wamesema kua Harfu hizo MuqaattaAt zinamaanisha:

‏.الله Mimi) au neno Allah ‏,أنا)‏ Inayowakilisha neno Anā ‏:(ا)‏ Alif

Hā ‏:(ه)‏ Inayowakilisha neno Al-Hādī ‏,الھادي)‏ Muongozi) Inayowakilisha neno Huwa

‏.(‏Yeyeھو)‏

Ḥā ‏:(ح)‏ Inayowakilisha neno Al-Ḥamīd ‏,الحمید)‏ Kushukuriwa).

Ṭā ‏:(ط)‏ Inayowakilisha neno (Ewe).

یقین Inayowakilisha neno (Ewe) au Yaqin ‏:(ي)‏ Yā

Kāf ‏:(ك)‏ Inayowakilisha neno Al-Kāfī ‏,كافي)‏ Anaetosheleza).

‏(التف Herufi ya pili katika Neno Allah) au (Latif ‏,الله)‏ Inayowakilisha neno Allāh ‏:(ل)‏ Lām

Mīm ‏:(م)‏ Inayowakilisha neno Al-ʿAlīm ‏,العلیم)‏ Herufi ya mwisho ya neno Alim) au

inayowakilisha neno Al-Majīd ‏,المجید)‏ Mshindi).

Nūn ‏:(ن)‏ Inayowakilisha neno Al-Qalam (Inayowakilisha neno "Kalamu au Peni") au

) نر (Nur

Sīn ‏:(س)‏ Inayowakilisha neno As-Samī' ‏,السمیع)‏ Mwenye Kusikia).

A’in ‏:(ع)‏ Inayowakilisha neno Al-ʿAlīm ‏,العلیم)‏ Mwenye Kujua).

Ṣād ‏:(ص)‏ Inayowakilisha neno As-Ṣādiq ‏,الصادق)‏ Mkweli).

Qāf ‏:(ق)‏ Inayowakilisha neno Al-Qādir ‏,القادر)‏ Mwenye Kukadiria).

‏.(رائي / رأى / رؤیا / یرى / بصی رKuona Inayowakilisha neno Al Raa (Mwenye ‏:(ر)‏ Rā

Qurán ina Surah 29 zilizoanzia na Huruf MuqattaA’at ambapo 3 kati yao zina herufi

1, 9 kati yao zina herufi 2, 13 kati yao ina herufi 3, 2 kati yao zina herufi 4 na 2 zina

herufi 5, Sura hizo ni:

Nambari Namba ya Surah Jina la Sura Huruf-a-MuqattaA’at

1 38 Surat Saad صٓ‏ Saad


391

2 50 Surat Qaaf قٓ‏ Qaaf

3 68 Surat Al Qalam نٓ‏ Nun

4 40 Surat Al Ghafir حمٓ‏ Ha Mim

5 41 Surat Al Fusilaat حمٓ‏ Ha Mim

6 43 Surat Az Zukhruf حمٓ‏ Ha Mim

7 44 Surat Ad Dukhan حمٓ‏ Ha Mim

8 45 Surat Al Jathiyyah حمٓ‏ Ha Mim

9 46 Surat Al Ahqaaf حمٓ‏ Ha Mim

10 20 Surat Ta-Ha طھ Ta-Ha

11 27 Surat An Naml طسٓ‏ Ta Sin

12 36 Sura Yasin یسٓ‏ Ya-Sin

13 10 Surat Yunus الر Alif Lam Ra

14 11 Surat Hud الر Alif Lam Ra

15 12 Surat Yusuf الر Alif Lam Ra

16 14 Surat Ibrahim الر Alif Lam Ra

17 15 Surat Al Hijr الر Alif Lam Ra

19 29 Surat Al Anqabut المٓ‏ Alif Lam Mim

20 30 Surat Ar Rum المٓ‏ Alif Lam Mim

21 31 Surat Luqman المٓ‏ Alif Lam Mim

22 32 Surat As Sajda المٓ‏ Alif Lam Mim

23 2 Surat Al Baqara الم Alif Lam Mim

24 3 Surat Al Imran الم Alif Lam Mim

18 26 Surat Ash Shuara طسۤ‏ مۤ‏ Taa Sin Mim

25 28 Surat Al Qasas طسٓمٓ‏ Taa Sin Mim

26 7 Surat Al Araf المٓصٓ‏ Alif Lam Mim Sad

27 13 Surat Rad المٓر Alif Lam Mim Ra

28 19 Surat Maryam كٓھیعٓصٓ‏ Kaf Ha Ya Aain Saad

29 42 Surat Ash Shuraa حمٓ‏ عٓسٓقٓ‏ Ha Mim Aain Sin Kaf

Tunapoangalia Harfu MuqattaAat kulingana na mitizamo ya Wanazuoni wenye Ilm ya

Tasawwuf katika Fani ya Ruhaniyya basi wao wanasema kua Harfu hizo ambazo ni zipo

mwanzo mwa sura 19 tulizoziangalia hapo juu kua zimezigawa harfu za lugha ya Kiarabu

nusu kwa nusu, kwani hizo zinaitwa Al Huruf Al Nuranniyah (Yaani Herufi zenye sifa

ya kua na Nuru) ambazo ziko 14. Na Herufi zilizobakia hua zinaitwa Al Huruf al

Dhalamiyyah ambazo nazo zimegawika sehemu mbili.

Sehemu ya kwanza ni yenye herufi 7 zenye sifa ya darja ya juu na sehemu ya pili ni zenye

darja ya chini. Herufi hizi hua zina athari yake kinguvu, ambapo katika Surat Al Fatiha

tunaona ina herufi zote hizo herufi 7 zenye darja ya chini ambazo hujulikana kama

Sawaqit al Fatihah.


392

Herufi hizo ni zenye kunasibishwa na Majina Matukufu ya Allah Subhanah wa Taála na

hivyo kua ni zenye kufanyiwa Dhikr kila moja katika siku yake kwa mpangilio ufuatao:

‏-’‏Faف Al Fardan lenye kumaanisha Mwenye Upekee. Ambalo ni jina la Dhikr ya siku

ya Jumaatatu.

Jimج – Al Jabbar lenye kumaanisha Mwenye Nguvu na Ujabari wa kipekee ambalo ni

jina la Dhikr ya siku ya Jumanne.

Shinش – Al Shahid lenye kumaanisha Mwenye Kushuhudia kila kitu ambalo ni jina la

Dhikr ya siku ya Jumatano.

‏-’‏Thaث Al Thabit lenye kumaanisha Mwenye Uthabiti wa Kipekee ambalo ni jina la

Dhikr ya siku ya Alkhamis.

Dha – Al Dhahir lenye kumaanisha Mwenye Kuonekana dhahir kwa dalili zake ظ

ambalo ni jina la Dhikr ya siku ya Ijumaa.

Kha’ – Al Khabbir lenye kumaanisha Mwenye Habari juu ya Kila kitu ambalo ni jina خ

la Dhikr ya siku ya Jumamosi.

Zay – Al Zakiy lenye kumaanisha Mwenye Utukufu wa Juu kabisa ambalo ni jina la ز

Dhikr ya siku ya Jumapili.

Ama kwa upande wa Dhu Nun Al Misri basi yeye anasema kua: ‘Majina Matukufu ya

Allah Subhanah wa Ta’ala, ni mharakisho wa dua ambayo ikiombwa kupitia katika

Majina hayo basi Dua hio hua ni yenye Kujibiwa Haraka. Na ndani yake mna

Herufi 7 na katika Ummu ul Kitaab yaani Surah Al Fatiha ambayo ni Sura yenye

Aya 7 basi herufi zote za Kiarabu zimo katika aya isipokua ث Tha’ (500), ج Jim (3),

’ (80) Fa’ ف (900), Dha’ ظ (300), Shin ش (7), Zal ز (600), Kha’ خ

Ama katika kitabu cha Manbah Usul Al Hikma basi Imam Al Sanusi mara kadhaa

amekua akitumia herufi hizo katika Dua zake kwa kuanzia na neno Wa Bi Haqqi ث Tha’

. (80) Fa’ ف (900), Dha’ ظ (300), Shin ش (7), Zal ز (600), Kha’ خ (3), Jim ج (500),

Kwa upande wa Shaykh Al Akbar Imam Abu Bakr Ibn Al Arabi basi yeye anasema kua:

‘Inabidi Mjue Harfu Muqataa’at zote, zilizoanza mwanzoni mwa Sura za Qur’an ni

majina ya Malaika na nimezitaja katika baadhi ya matukio, ambapo kamwe

haijawahi kutokea kwangu kuzitumia bila ya kutokea Malaika ambae alinielezea

mie juu ya Jambo nisilolijua. Kwa kifupi hawa ni Walimu wangu. Hivyo nikiita

moja kati ya Harfu hizo basi hua ni sawa na kumuita mmoja kati ya Malaika ambae

nae hutokea na kunisaidia kama ninavyohitaji’

Ambapo:

Harfu Siku yake Msimamizi wake Jina Maalum

Kha ‏(‏‎600‎‏)خ

Jumapili Rawfa’il Khabirخبیر


393

Shin ‏(‏‎300‎‏)ش

Jumatatu Jibril Shakirشاكر (7) Zal ز

Jumanne Samsama’il Zakiyزكي ‎900)Dhal‏)ظ Jumatano Mika’il

Dhahirظاھر Tha ‏(‏‎500‎‏)ث

Alkhamis Sirfaya’il Thabitثابت ‎3)Jim‏)ج Ijumaa ‘Anya’il

Jabbarجبار Fa ‏(‏‎80‎‏)ف

Jumamosi ‘Azra’il Fatirفاطر Shaykh Al Akbar Imam Abu Bakr Ibn Al Arabi anaendelea kutuambia katika Al-Durr al

Maknūnfī 'Ilm al-Ḥurūf, kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala alimfundisha Nabii wake

Adam Jina tukufu kuliko yote. Kisha baada ya hapo Nabii Adam akamfundisha

mtoto wake Seth ambae nae akamfundisha Nabii Idrisa Alayhi Salaam. Nabii Idrisa

Alayhi Salaam alikua ni mwenye kupokea vitabu 30 kutoka kwa Allah Subhanah

wa Ta’ala na akapewa I’lm ya herufi, na siri za Hikma, Nambari na mambo

mengineyo, na yeye ndie aliyekua ni wa mwanzo kuandika kwa kutumia Kalamu.

Nabii Idrisa aliandika kitabu kiitwacho Kanzu Al Asrar (Hazina ya Siri), ambacho

Thabit Ibn Qurta Al Harani ameandika kukielezea juu yake. Na mimi nilipokutana

nae Nabii Idrisa baada ya kupata ufunuo, basi nikamuuliza, ufunuo zaidi juu yake

ambapo nae akasema: ‘Ufunuo huu ni ile ambayo iliyohifadhiwa nje ya Kitabu

kwani myengine yote iliyobakia imefichika na imefungwa ndani yake. Kisha

akanifunulia baadhi ya Siri zisizojulikana ambazo hakuna mtu mwenye kuzijua juu

yake. Ilm hii ya Herufi baadae ikarithiwa na watu 40 tu wa Haramisa wa Misri’’

Kwani baadhi wanaweza kujiuliza kwa nini kila nikiandika herufi basi hua ninaandika

nambari mbele yake kwa mfano ‏’‏Thaث (500), ج Jim (3), خ Kha’ (600), ز Zal (7), Shinش

‏’‏Faف (80) n.k, kwani hii ni kulingana na mtizamo wa Ilm (900), Dha’ ظ (300),

Ruhaniyyah ambapo harfu hizi zimepewa thamani ya uzito wa kiidadi kama ifuatavyo.

الف 1 ب 2 ج 3 د 4 ه 5 و 6 ز 7 ح 8 ط 9 ى 10 ک 20 ل 30 م 40 ن 50 س 60 ع 70 ف 80

ص 90 ق 100 ر 200 ش 300 ت 400 ث 500 خ 600 ف 700 ض 800 ظ 900 غ 1000.

Na wenye Ilm Ruhaniyyah hua wanatumia uthibitisho wa kua kila kitu kina idadi yake

kinambari kutokana na ile aya ambayo inasema:

‏﴿لِّيَعْلَمَ‏ أَن قَدْ‏ أَبْلَغُواْ‏ رِسَ‏ الاَتِ‏ رَهبِِّمْ‏ وَأَحَ‏ اطَ‏ بمَِا لَدَ‏ يْهِ‏ مْ‏ وَأَحْ‏ صَى ٰ كُ‏ ل َّ شَ‏ يْ‏ ءٍ‏

عَدَداً‏ ﴾

LiyaAAlama an qad ablaghoo risalati rabbihim waahata bima ladayhim waahsa

kulla shay-in AAadadan (Surat Al Jinn 72:28)


394

Tafsir: Na huwalinda (Mitume) hadi ahakikishe kua wamefikisha ujumbe wa Mola

wao. Na yeye (Allah) amekizunguka na amekilinda kila kitu katika idadi.

‘Ambapo aya imetumia neno Ahata lenye kutokana na neno Ha-Ta linalomaanisha

Kuangalia, Kulinda, Kuzunguka, Kugubika, au Kujua kitu kwa Undani, na pia

ikatumia neno Ahsa ambalo linalotokana na neno Ha-Ssa ambalo hua ni lenye

kumaanisha Kupiga Changarawe au Kijiwe kimoja kimoja, Kuhesabu kwa

Umakini, Kutia Nambari, Kuhesabu Kiidadi, Kujua au Kufahamu Idadi ya Kitu’.

Ama kwa upande mwengine basi Imam Muhammad Ibn Is-haq amesema kua amesema

Imam Muhammad Ibn Saib Al Kalbi kua amesema Abu Salih, kua amesema Jabir Ibn

Abd Allah Ibn Riyab: Abu Yasir Ibn Akhtab, pamoja na baadhi ya Mayahudi

walipita mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae nae alikua akisoma

Surat Al Fatiha, kisha akasoma Alif Lam Miim, Dhalika Al Kitab La Rayba Fihi

Hudda lil Mutaqqin.

Hivyo (Abu Yasir Ibn Akhtab) akamfuata ndugu yake Huyayy Ibn Akhtab ambae

alikua amekaa na Mayahudi wenzake na kuwaambia: ‘Wallahi! Nimemsikia

Muhammad akisoma kile alichoteremshiwa, Alif Lam Miim, Dhalika Al Kitab La

Rayba Fihi Hudda lil Mutaqqin.’ Huyayy akamuuliza: ‘Umemsikia akisoma maneno

hayo?’ Abu Yasir akajibu; ‘Naam!’ Hivyo Mayahudi hao wakaondoka wote kwa

pamoja hadi kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kumuuliza: ‘Jee Jibril

amekuteremshia maneno yasemayo Alif Lam Miim, Dhalika Al Kitab La Rayba Fihi

Hudda lil Mutaqqin?’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Naam.’

Mayahudi wakasema: ‘Allah ameleta Mitume kabla yako, lakini sisi kamwe

hatujawahi kusikia miongoni mwao ambae ametaarifiwa juu ya mda wa Mamlaka

isipokua wewe. Na mda wa uhai watakaoishi watu wa Ummah wako kwani, Alif ni

1, Lam ni 30, Mim ni 40, na hio jumla yake ni 71. Hivyo hio ni miaka 71, sasa jee

tunataka kumfuata Mtume ambae Mamlaka yake mwisho wake ni Miaka 71 na

uhai wa Watu wake mwisho wao ni miaka 71?’

Kisha wakamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Ya Muhammad Jee

kuna jambo jengine uliloshushiwa zaidi linalofanana na hili?’ Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam.’ Mayahudi wakauliza: ‘Jee ni lipi?’ Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Alif Lam Mim Sad.’ Mayahudi wakasema:

‘Hio ni zaidi, kwani Alif ni 1, Lam ni 30, Mim ni 40, Sad ni 90 hivyo hapa

inamaanisha miaka 161.’

Mayahudi wakauliza: ‘Ya Muhammad jee kuna jengine zaid?’ Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam. Alif Lam Ra.’ Mayahudi wakasema:

‘Alif ni 1, Lam ni 30 na Ra ni 200. Hio hua ni miaka 231’.


395

Wakauliza tena: ‘Ya Muhammad jee kuna jengine zaid?’ Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akasema: ‘Alif, Lam, Mim, Ra’. Mayahudi wakasema: ‘Alif ni 1,

Lam ni 30, Mim ni 40 na Ra ni 200. Hio ni miaka 271.’

Kisha Mayahudi hao wakaondoka na kusema: ‘Ya Muhammad hakika sisi

tumechanganyikiwa juu ya mambo yako haya, kwani hatujui juu ya mda wa

Mamlaka yaliopewa Ummah wako kama utakua ni mrefu ama la.’

Mayahudi hao wakaambiana: ‘Twende zetuni’ kisha wakaondoka kwa pamoja

huku Huyay akimwambia Abu Yasir pamoja na Rabbi wao kua: ‘Na ni nani

atakaeweza kujua kwani huenda miaka hio yote 71, 61, 100, 231, na 271 hua ni 734

ni kwa ajili ya Ummah wa Muhammad, na bado kuna myengine ambayo

hayakuhesabiwa.’(Tarikh Imam Bukhari, Durr al Manthur na katika Al Itiqan Fi Ulumu

Ul Qur’an Imam Al Suyuti, Tafsir Imam Ibn Kathir Maktabah Qurtubah Al Qahira.)

Kwa upande wa Suhayli basi yeye anasema: ‘Inaonekana kua jumla ya idadi ya herufi

MuqataaAt zote zilizorudiwa ndio Urefu wa Mamlaka ya Ummah huu.’

Ama kwa upande wa Imam Abu Al Khayr Shams Al Din Muhammad Ibn Muhammad

Ibn Muhammad Ibn Ali Ibn Yusuf Al Jazari Al Shafii basi yeye anasema katika ushairi

wake wa Al I’lm Hukm Al Qiraat kua:

والبیت ھو أبیاتھا قاف وزاي في العدد....من یحسن التجوید یظفر بالرشد

وقاف في العدد = 100 و زاي = 7

آي عدد الآبیات 107 بیت والله أعلم

‘Na Nyumba yake ni Nyumba za Qaf na Zay katika Idadi..Na anaekiboresha kisomo

chake cha Tajwid kwa kutumia muongozo wa Jaffar,

Na Qaf kiidadi ni 100 na Zay 7 hivyo idadi ya nyumba yake ni 107.

Na Allah ni mwenye kujua zaid (Mandhumat Al Muqaddimat, Imam Ibn Al Jazari)

Vile vile tunapoangalia miongoni mwa Wanazuoni katika kuitafsiri Surat Ar Rum basi

anasema Imam Abu Shamah Shihab Ad Din Abd Rahman Ibn Ismail Ibn Ibrahim Ibn

Uthman Ibn Abi Baqr Ibn Ibrahim Ibn Muhammad Al Maqdisi kua: Alisema Imam Abu

Al Hakam Abd Salam Ibn Abd Al Rahman Ibn Mohammad Ibn Barrajan katika

kuitafsiri Surat Ar Rum:


396

‏﴿ال ۤ م۞‏ ٱ غُلِبَ‏ تِ‏ ل ُّرو مُ‏ ﴾

ۤ

Alif, Laam, Miim, Ghulibati Alrum (Surat 30:1-2)

Tafsir: Alif Laam Miim; Warumi wameshindwa.

Kua: ‘Jerusalem itakua chini ya Mamlaka ya Utawala wa Roman Empire hadi

katika mwaka 583 Al Hijr kwani katika mwaka huo ndio watakaposhindwa na

kupinduliwa. Na Jerusalem itakua chini ya Mikono ya Uislam hadi mwisho wa

Dunia. Na hii ni kulingana na idadi iliyomo ndani aya hii’. Na hivyo ndivyo

ilivyotokea. (Tarikh Al Khulafa, Imam Al Suyuti, Al Itiqan Fi Ulumu Ul Qur’an Imam Al

Suyuti)

Tafakkar! Kwani Imam Ibn Barrajani alichukua idadi ya neno Ghulibat yaani

watashindwa ambalo kiidadi ni 1432 na hivyo wenye kushindwa hua ni wenye kula

hasara hivyo akatoa neno Al Rum ambalo kiidadi ni 277, hivyo akapata jawabu ya 1155

kisha akajumlisha na nambari ya Sura ambayo ni 3 na kisha akajumlisha na nambari ya

aya ambayo ni 2 akapata jawabu ya mwaka 1187 Christian Era.

Ingawa hio ni mitizamo mbali mbali pale tunapozungumzia harfu Al MuqattaAat kupitia

katika Ilm ya Ruhaniyya lakini pia kuna mtizamo wa pili nao una ufafanuzi tofauti juu

yake, ufafanuzi huo unawekwa wazi na mfano ufuatao: Katika kipindi cha Utawala wa

Khalifa Al Mutawakkil ambae alikua ni mtawala wa Mamlaka ya Al Abbas, basi

aliandikwa barua na Mtawala wa Rumi ambayo ilikua inasema: ‘Hakika mimi

nimesikia kua katika kitabu cha Dini yenu mna Sura ambayo ina herufi zote

isipokua herufi 7 (Sawaqit al-Fatiha: ث Tha’ (500), ج Jim (3), خ Kha’ (600), ز Zal

‏’‏Faف (80)) ndani yake. Na kama Surah hii ikisomwa (900), Dha’ ظ (300), Shinش (7),

basi humpatia Pepo yule aisomae. Hivyo mimi nilikua nataka kujua ni Sura gani

hio na kwa nini herufi hizi hazimo ndani yake’

Suali la barua hii lilimchanganya sana Khalifa Abu Al Faḍhl Jaʽfar ibn Muḥammad Al

Muʽtaṣim Billāh maarufu kama Al Mutawakkil, hivyo ikambidi kumtafuta Imam Ali An

Naqi ambae alikua akiishi katika Ardhi ya mjini Samara. Imam Ali An Naqi alipoulizwa

juu ya suali hilo basi akajibu: ‘Sura hio ni Surat Al Fatiha, na herufi hizo hazimo

ndani yake kwa sababu kila moja kati ya Sawaqit hizo zinawakilisha maneno yenye

maana maangamizo katika kauli ya Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Khalifa al Mutawakkil akamuuliza Imam Ali An Naqi juu ya herufi 7 za Sawaqit, ambapo

Imam Ali An Naqi nae akajibu: ‘Herufi ya kwanza ni herufi Thaث ambayo


397

inawakilisha maangamizo yaani Thubur, herufi ya pili ni ج Jim ambayo

inawakilisha Moto wa Jahannam yaani Jahim. Herufi ya tatu ni خ Kha ambayo

inawakilisha Ubaya yaani Khubth au Hasara yaani Khusr. Herufi ya nne ni ز Zal

ambayo inawakilisha Zaqqum ambao ni mti wa Motoni ambao Matunda yake ni

yenye sumu na machungu yasiyokua na mfano wake. Herufi ya tano ni ش Shin

ambayo inawakilisha Shaqawa. Herufi ya sita ni ظ Dhal ambayo inawakilisha

Dhulma na herufi ya saba ni ف Fe ambayo inawakilisha Afat yaani Mitihani na

maangamizo kwa ujumla.’

Kwa upande wa wataalamu wa Lugha wanasema kua kila herufi ya Kiarabu hua ina

maana pekee inayojitegemea kwa mfano: Herufi Alif inapokua peke yake inatumika

kuuliza Suali, herufi Mim inawakilisha kuuliza juu ya kitu au Mtu na pia humaanisha

wingi katika kiwakilishi, Herufi Lam huwakilisha Kukataa, n.k hivyo basi kulingana na

mtizamo huo hua tunaona kua Neno Alif Lam Mim hua linamaanisha hali ya Mahojiano,

Kupinga au Kuuliza masuali, yaani kupinga baadhi ya mambo na kuafikiana baina ya

mambo yanayopingana. Sultan Al Mutakallimi Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al

Razi anasema pia kua: ‘Waarabu walikua wakitumia herufi ‏'ع'‏ kumaanisha Pesa,

herufi ‏'غ'‏ kumaanisha Mawingu, herufi ‏'ن'‏ kumaanisha Samaki, n.k’

Katika kuunga mkono maana hizo basi tuangalie mifano ifuatayo ambapo tunapoangalia

moja kati ya mashairi ya Walid Ibn Uqba Ibn Abu Mua’yit basi tunaona kua anasema:

Qultu Laha Qifiy faqalat Qaf.

قلت لھا قفي فقالت قاف

Tafsir: ‘Nilimwambia yeye (Mwanamke): ‘Kaa Kidogo’, nae akajibu: ‘Qaf. Ambapo

herufi ya mwisho ambayo ni Qaf imetumika kuwakilisha neno: Waqaftu ambaloوقفت

maana yake ni Kusimama. Mfano mwengine ni ule wa Imam Abu Abd Allah

Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi ambae anatoa mfano

kwa kusema kua Waarabu hua wanasema:

كف لنا السیف شا

Qafa Lana al Sayf Shin yaani: ‘Unatutosha sisi Upanga kua Sha’ ambapo Herufi Shin

imetumika kumaanisha neno Shafii. Na wengine hua wanasema kua inamaanisha neno

Shahidan’

Kwa upande wa Imam Abu Talib Al Makki basi yeye anasema kua: ‘Sayyidna Ali Ibn

Abi Talib Karamah Allahu Wajh alikua akiomba dua kwa kwa maneno yasemayo:

‘Ya Kaf, Ha, Ayn, Sad, hakika mimi nakuomba kupitia kwako uninusuru na Dhambi


398

zenye kuangamiza, kuondokewa na Baraka, kuondokewa na mvua, au kuzidiwa na

Maadui zangu. Ya Allah! Tulinde dhidi ya Nafsi zetu.’’ Ambapo harfu Kaf

inawakilisha Jina la Allah Subhanah wa Ta’ala la Al Kafi, Ha ni Al Hadi, Ya ni Al Yaqin,

A’ayn ni Al A’lim na Sad ni Al Ssadiq.

Ama tunapomuangalia Imam Tahir Ibn Ashur katika kuitafsiri Surat Yasin basi amesema

kua neno Ya Sin ambazo ni Harfu mbili za Ye na Sin hua linamaanisha Ya Sayyid yaani

Ewe Bwana (wa Mitume).

Ambapo Imam Hamid Al Din Abu Hasan Ahmad Ibn Abd Allah Al Kirmani basi yeye

anasema kuhusiana na Surat Ta-Ha kua: ‘Ta-Ha maana yake ni Mwezi Mweupe kwani

Harfu Ta ina uzito wa idadi ya 9 na harfu Ha ina thamani ina uzito wa idadi ya 5 na

ukijzijumlisha kwa pamoja unapata 14 kumaanisha mwezi 14 muandamo.’(Al

Gharaib)

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari ambae yeye anatuambia kua: ‘Kila

Kitabu ambacho Allah Subhanah wa Ta’ala alikishusha basi kina mfumo wa siri

ndani yake, na mfumo wa siri wa Qur’an umo katika herufi ambazo ndio ufunguzi

wa Sura husika, kwa sababu Herufi hizo ndizo ni Majina na Sifa zake. Kama

anavyosema Alif Lam Mim (2:1, 3:1, 29:1 na 31:1), au Sad (38:1) au Alif Lam Ra

(10:01, 11:1,) n,k. basi harfu hizi zinapojumuishwa pamoja, zinatoa jina Tukufu la

Allah Subhanah wa Ta’ala. Kwa mfano Alif, Lam, Ra, Ha, Mim na Nun basi hua

tunapata jina la Al Rahman. Ambapo kwa Abda Allah Ibn Abbas na Dahhaq Ibn

Muzahim basi wao wamesema kua Alif Lam Min hua inamaanisha: ‘Mimi ni Allah

na Nnajua’.

Ambapo kwa Upande wa Ali Ibn Abi Talib Karama Allahi Wajh basi yeye anasema kua:

‘Haya ni Majina ambayo, yapo katika hali ya herufi zilizotawanyika. Lakini kama

ikichukuliwa herufi moja kutoka katika kundi kila kwa mpangilio wa kua ni tofauti

na herufi iliyokaribu yake herufi hio, na zikakusanywa pamoja kiidadi basi hua ni

zenye kuunda jina la mwingi wa Rehma. Hivyo kama ikiwa jina hili litajulikana na

kisha likatumiwa katika maombi ya Dua basi litakua ni jina lenye Nguvu sana kiasi

ya kua Dua ya muombaji kwa kupita jina hilo itakua ni yenye kukubaliwa.’’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anaendelea kutufafanulia kwa

kutuambia kua: ‘Nimepokea Hadith kutoka kwa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu

Anhu ambae anasema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ameapa kua kitabu chake

hiki, alichomshushia Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam, ni kitabu

ambacho kipo chini ya uangalizi wake. Hivyo akasema: ‘Alif Lam Mim. Hiki ni

Kitabu..ambapo Alif hua inamanisha Allah, Lam inamaanisha Jibril na Mim hua

inamaanisha Muhammad, hivyo basi hapa inaonesha kua Allah Subhanah wa


399

Ta’ala, amekula kiapo kwa ajili yake yeye mwenyewe, na kwa ajili ya Malaika wake

Jibril, na kwa ajili ya Nabii wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam.’’’

Tumalizie kwa kuangalia upande wa Imam Jafar As Sadiq kupitia kwa Sufyan Ath

Thawry ambae anasema kua: ‘Mimi nilimuuliza Imam Jafar As Sadiq: ‘Ya Ibn Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam, jee ni nini maana maneno ya Allah Subhanah wa

Ta’ala katika kusema kwake Alif, Lam, Miim na Alif, Lam, Miim, Saad na Aliif, Lam,

Ra na Aliif, Lam, Miim, Ra na Kaf, Ha, Ya, Ayn, Saad na Ta, Ha na Ta, Siin na Ta,

Siin, Miim na Ya, Siin na Saad na Ha, Miim na Ha, Miim, `Ayn, Siin, Qaaf and Qaaf

na Niin’’

Imam Jafar As Saddiq akajibu: ‘Ama kuhusiana na Alif-Lam-Mim iliyo mwanzoni

mwa Surat Al Baqara basi hua inamaanisha Mimi ni Allah Mfalme na Alif-Lam-

Miim iliyo mwanzoni mwa Surat Al Imran basi hua yenye kumaanisha Mimi ni Allah

Mtukufu na Alif-Lam-Miim-Saad humaanisha Mimi ni Allah Muamuzi wa Kila kitu

na Mkweli. Alif-Lam-Ra hua inamaanisha Mimi ni Allah Mwenye Wingi wa

Usamahevu. Maana ya Alif-Lam-Miim-Ra hua inamanisha Mimi ni Allah Mwenye

Kuhuisha, Mwenye Kufisha, Mwenye Kutoa Rizki. Maana ya Kaf-Ha-Ya-Ayn-Sad

hua ni Mimi Mwenye Kutosheleza, Mwenye Kuongoza, Mwenye Kuhifadhi,

Mwenye Ilm, Mwenye katika Ahadi zake.

Ama kuhusiana na Ta-Ha basi hili ni jina miongoni mwa Majina ya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam. Na hua linamaanisha Ewe Mwenye Kuutafuta ukweli

na Kuongoza katika njia ya Ukweli. Hatujakuteremshia Qur'an ili usifanikiwe

katika njia yako, bali tumekuteremshia kwa sababu ya kukuboreshea Hali yako.

Ama juu ya maana ya Ta-Sin basi maana yake hua ni Mimi ndie Mwenye Madai ya

Kutekelezewa na ndie Mwenye Kusikia Kila Kitu. Ama kuhusiana na Ta-Sin-Miim

basi hua inamaanisha Mimi Ndie mwenye Madai, mwenye Kuona Kila Kitu, ndio

wa Mwanzo na Ndie wa Mwisho.

Ama kuhusiana na Yasin basi nalo pia ni jina la Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam na hua linamaanisha Ewe Mwenye Kusikiliza Uteremsho wetu na Qur'an

iliyojaa Hikma, Kwa Hakika wewe ni Mjumbe Wetu Katika Njia Iliyonyooka. Ama

kuhusiana na Saad basi ni Chemchem inayotiririka kutoka chini ya Arshi ya Allah

Subhanah wa Ta'ala na ndio kutokana na maji ya Chemchem hii basi ndio rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam alitilia Udhu wake pale alipopelekewa juu

Mbinguni katika Usiku wa Miraj. Na ndio Chemchem ambayo Malaika Jibril

huenda kujitumbukiza kila siku, kisha hutoka na kujikunuta Maji yote yaliyomo

kwenye mbawa zake. Na hakuna hata tone moja linalopukutika kutokana na maji

hayo kutoka kwenye mbawa zake isipokua Allah Subhanah wa Ta'ala hua ni

mwenye kuumba Malaika ambae hua ni mwenye kumtukuza na kumisfu Allah

Subhanah wa Ta'ala kwa mda wote mpaka siku ya Malipo.


400

Ama kuhusiana na Ha-Mim basi hua inamaanisha Mwenye Kustahiki Kusifiwa na

Kutukuzwa. na Ha-Miim-Ayn-Sin-Qaf basi hua linamaanisha Mstahmilivu,

Mwenye Kulipa Malipo Bora kwa Wafanyao Mema, Mwenye Kujua Kila kitu,

Mwenye Kusikia Kila Kitu, Mwenye Uwezo wa Kila Kitu na mwenye Nguvu Juu ya

Kila kitu. Na Qaf hua inamaanisha Mlima ambao ni wenye Kuizunguka na

Kuifunika Dunia na kupitia katika Mlima huu ndio Allah Subhanah wa Ta'ala

akaitandaza Dunia kwa ajili ya Ibn Adam kuishi ndani yake. Ama Kuhusiana na

Nun basi huu ni Mto wa Peponi ambao Allah Subhanaha wa Ta'ala aliuambia

ujikusanye na uwe mgumu na akatoa Kalamu na Wino kutokana nao, kisha

akaiambia Kalamu hio: 'Andika!' nayo ikaandika kwenye Al Lawh Al Mahfudh kila

kitu kilichotokea na kitakachotokea hadi siku ya Malipo. Na Kalamu hio ni yenye

Nuru ya Allah Subhnaha wa Ta'ala na Lawh ni yenye Nuru ya Allah Subhanah wa

Ta'ala.'

Sufyan Ath Thawry akamwambia Imam Jafar As Sadiq: 'Ewe Ibn Rasul Allah! Hebu

Nielezee juu kikamilifu juu ya Amri ya Lawh na Kalamu na Wino wake na

nifundishe kile ambacho Allah Subhanah wa Ta'ala amekufundisha.' Imam Jafar

As Sadiq akasema: 'Ewe Ath Thawry, kwa hakika kama wewe usingekua mtu

anaestahiki kujibiwa basi mimi nisingekujibu. Hivyo fahamu kua Nun ni Malaika

anaeielekeza Kalamu, na Kalamu ni Malaika anaeielekeza Al Lawh, na Al Lawh ni

Malaika anaemuelekeza Malaika Israfil na Israfil anamuelekeza Mikail na Mikail

anamuelekeza Jibril na Jibril anawaelekeza Mitume wote Sala na Salamu ziwe Juu

yao' Sufyan Ath Thawry anasema kua, kisha Imam Jafar As Sadiq akaniambia:

'Haya nenda zako ewe Ath Thawry kwani hakuna kizingiti juu yako kutokana na

Ilm niliyokuachia kwako'’

Tunaporudi kwa Sultan Al Mutakallimi Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi

Al Shafii, na pia Imam Abu Jafar Muhammad Ibn Jarir at Tabari Al Shafii basi tunaona

kua wanasema pia kua: 'Harfu MuqataA'at zilikua pia ni zenye umuhimu wa kutaka

kuwaonesha Makafiri wa Mji wa Makkah utofauti na maajabu ya Qur'an na hivyo

iwavutie, kwani wao walikua ni wenye kuapa kua kamwe hawatosikiliza Qur'an.

Hivyo basi Maajabu ya Harfu hizi yaliwafanya wawe na hamu ya kutaka kujua

kuhusiana na Qur'an ambayo tayari walikua hawako tayari kuisikiliza.'

Na ndio maana pia akasema Sultan Al Balagha Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari na

Imam Nasir Ad Din Al Baydawi kua: 'Malengo ya Harfu MuqataA'at ni kuwawekea

wazi Makafiri kua Qur'an ina herufi ambazo na wao pia hua ni wenye kuzitumia

katika Lugha yao lakini hata hivyo wakawa ni wenye kushindwa kutoa mithili ya

sura moja tu ambayo itafanana na japo moja kati ya Sura 114 za zilizomo ndani ya

Qur'an'


401

Hivyo kwa njia moja au nyengine basi hua haishangazi kwanini Wanazuoni wakawa

wana mitizamo tofuati juu ya herufi hizi kwa sababu Qur'an tukufu ina aya Mutashabihat

ambazo hua ni zenye maana nyingi ndani yake na hii hua ni yenye kuweka wazi Ukubwa

usiokua na mwisho wa I'lm ya alieteremsha Qur'an ambae ni Allah Subhanah wa Ta'ala.

Hivyo basi ni jambo la kawaida kwa Harfu Muqata'Aat kua ni zenye siri ndani yake na

pia kua na maana tofauti kulingana na mitizamo wa Wanazuoni tofauti juu yake.

Hivyo kabla ya kuingia katika Surat Maryam basi na tuangalie maana ya Biismi Allahi

Al Rahmani Al Rahim:

MAANA NA FAIDA YA BIISMI ALLAHI ALRRAHMANI ALRRAHIM

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ الر َّحمَْنِ‏

الر َّحِ‏ يمِ﴾‏

Biismi Allahi AlRahmani AlRahiim.

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma.

Hii ni aya ya mwanzo ya Qur’an na pia ni Utangulizi na Ufunguzi wa kila kitu

kinachofanywa na kila Mtu aliemuamini Allah Subhanah wa Ta’ala. Anasema Mujaddid

Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Al Mushakikin Shaykh ul Islami Imam Fakhr Ad

Din Al Razi kuhusiana na ayah hii kua: ‘Harfu Ba iliyopo mwanzoni mwa ayah hii hua

inamaanisha Ilsaq (kiunganishi) ‘Kwa’ ambacho kinaunganisha uanzaji wa kitendo

na jina la Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Neno Allah kwa lugha ya Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Jina Tukufu ambalo ni la

Muumba wa Kila kitu, kilichomo kwenye Ulimwengu unaoonekana na usioonekana,

ambae ni Mmiliki wa kila kitu Mbinguni na Ardhini, ambae ndie mmiliki wa Sifa nzuri

zote na Majina Matukufu yote. Hivyo Majina yote Matukufu ya Allah Subhanah wa

Ta’ala na sifa zake Tukufu ambazo kwa ufahamu wa Ibn Adam hua haziwezi

kufafanulika kikamilifu na ipasavyo kama inavyobidi kuelezewa zilizotajwa ndani ya

Qur’an ni yenye kuweka wazi maana ya jina la Allah Subhanah wa Ta’ala kulingana na

Ufahamu wa Ibn Adam.

Anasema Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din, Zuhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani

Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al

Shafii kua: 'Allah ni Jina la yule ambae yupo hai, ambae ni mwenye sifa za kua ni


402

Muumba na Mlezi juu ya kila kitu alichokiumba. Yeye ni mwenye upekee pale

tunapozungumzia usahihi wa kuwepo kwake, na bila ya shaka hakuka kitu

chengine chochote kile kilichokuwepo ambacho kinaweza kupewa sifa stahiki ya

kuwepo kwake kitu hicho kutokana na utukufu wa kuwepo kwake. Kwani kile

ambacho inabidi kiwepo kulingana na sifa ya kutoweka kwake, kwani kila

kinachokuwepo basi lazima kitoweke. Iipokua kuwepo kwake Allah Subhanah wa

Ta'ala.'

Inabidi ujue kua Jina hili ‘Allah’ ni Jina Kubwa na Tukufu kuliko yote katika ya

Majina 99 ya Allah Subhanah wa Ta'ala, kwa sababu jina hili ndilo linalojumuisha

sifa zote za Allah Subhanah wa Ta'ala. Kwani kila jina lake moja hua na maana

moja, kama Alimu, Qawiyum, Qayyum n.k lakini jina hili la 'Allah' ni jina maalum

la Allah Subhanah wa Ta'ala. Hakuna mwenye kutumia jina la Allah isipokua Allah

mwenyewe. Iwe kwa njia ya moja kwa moja au kwa njia nyengine, wakati majina

mengine kama Al Qadir, Al Alim, ArRahman n,k yanaweza kutumika kwa njia

nyengine. Lakini jina la Allah halitumiki kwa yeyote yule isipokua yeye na ndio

maana likawa ndio jina Tukufu kuliko yote.'

Imam Jamal Islam Abu Qasim Abd Al Karim Ibn Hawazin Al Qushayri basi anasema

kua: 'Kilugha harfu Ba katika Neno Biismi Allahi hua kinawakilisha kiunganishi

yaani Bi-llah humaanisha Kupitia kwa Allah Subhanah wa Ta'ala. Ambapo mambo

mapya hua ni yenye kubainishika na kupitia kwake yeye basi viumbe vilivyoumbwa

huwepo. Na hua kamwe hamna katika viumbe vipya vilivyoumbwa (hadith

makhluq) au mshikamano wa matukio yanayotokea sambamba (Hasl Mansuq), au

kutokana na kitu kinachoonekana au kinacho hisika kihisia kwa athari zake, n.k.

Au kitu chochote kutokana na jiwe au udongo au majani au miti au alama

zinazobakia ardhini (Rasm) au mabaki yaliyosimama (Talal) au hukmu yeyote au

sababu ambayo inayoonekana kuwepo kwake.

Ambapo hua haviwezi kuwepo isipokua kwa kuwepo mwenye Hakika ya kuwepo.

Na Hakika hio hua ni katika Mamlaka yake. Ambayo Mwanzo wake hua ni kutoka

kwake na Mwisho wake hua ni kurudi kwake. Kupitia kwake yeye basi yule

anaetangazia Tawhid Allah basi hua ni mwenye kupata na anaepinga hua ni

mwenye kukosa Iman. Kupitia kwake yeye basi yule anaekubali hua ni mwenye

kujua na kupitia kwake basi yule mwenye kuasi hua ni asiejua na kubakia nyuma.

Allah Subhanah wa Ta’ala amesema ‘Biismi Allahi’ hakusema ‘Bi Allahi’. Na

kulingana na mitizamo ya baadhi ya watu basi husema kua hii ni njia yakutafuta

Baraka kupitia katika kumtaja jina lake. Na kulingana na wengine basi basi hua ni

kutokana na tofauti ya maneno haya ‘Biismi Allahi’ na Kiapo ‘Bi Allahi’. Na

kulingana na baadhi ya Wanazuoni basi pia tunaona kua wanasema kua ni kwa

sababu ya ‘Ism’ jina basi ndio kitu hua ni chenye kinaitwa ‘Musamma’.


403

Ama kulingana na mtizamo wa watu wenye Ilm ya Ruhaniyyat ya Kiroho ya ‘Irfan’

basi ili kupata usafi wa Moyo kutokana na mshikamano na kuikomboa Nafsi

kutokana na vikwazo ili neno ‘Allah’ lipate kuingia ndani ya moyo uliokua msafi na

nafsi iliyosafika.

Baada ya kuitaja ayah hii, basi baadhi ya watu hua wanakumbushwa kutokana na

harfu ‘Ba’ ambayo ni yenye kutokana na Wema au Ukarimu (Birr) na Mawalii

wake na harfu ‘Sin’ ni kutokana na Siri ‘Sirr’ baina yake na wale aliowachagua na

kutokana na harfu ‘Mim’ kutokana na neno Rehma zake ‘Manna’ kwa waja wake

wenye Uwalii (Ahl Al Walaya). Ambao hua wanajua kua kutokana na Rehma zake

basi hua wenye kujua Siri zake, na kutokana na Rehma zake juu yao hua ni wenye

kutekeleza maamrisho yake, na kutokana nae Allah Subhanah wa Ta’ala basi hua

ni wenye kujua uwezo wake.

Na kwa upande mwengine basi kuna wasemao kua: kutokana na kusikia Biismi

Allahi hua ni wenye kukumbushwa kutokana na harfu ‘Ba’ inayotokana na neno

Wema au Ukarimu (Baraa) ya Allah Subhanah wa Ta’ala na harfu ‘Sin’ kutokana

na neno Salama na kutokua na kasoro na harfu ‘Mim’ inayotokana na neno

Utukufu wake Mkubwa (Majid) katika Utukufu wa kuelezewa kwake. Wengine hua

ni wenye kukumbushwa kutokana na harfu ‘Ba’ kutokana na Uzuri wake wenye

Upekee (Baha) na harfu ‘Sin’ kutokana na neno Kung’ara kwa Nuru yake (Sana),

na harfu ‘Mim’ kutokana na Mamlaka yake ‘Mulk’.

Ama kwa upande wa Imam Abd Razak Al Kashani basi yeye anasema kua: ‘Kupitia

katika kutojidhihirisha, basi yule alie na hali ya Al Wahid (Upekee) basi hujionesha

kupitia katika hali ya Al Wahidiyyah (Umoja). Hivyo hapa hali ya Al Ayan Al

Thabitah (Utibitisho) ambayo hua ni utambulisho kwa Ulimwengu kujionesha

katika hali hii. Uthibitisho huu huendelea kujionesha katika sifa za kiumbaji.

Kutokana na kutokea na hali hio ya kujionesha basi, hali hio ya Al Tajalli Al

Shuhudiyy (kujidhihirisha wazi na kushuhudiwa) hupelekea kutokea maumbile ya

jina yaani Asmaiyyah.

Katika hali kama hii basi jina na sifa za Muumba hua ni zenye kuonekana wazi.

Hivyo basi jina hili la Allah hua ni jina ambalo huonesha sifa za Muumba, na jina

lake tukufu la Allah hua linaitwa Al Asm al Adhim. Kwa hivyo jina hili la Allah hua

ni jina la mwanzo katika majina yake yote, na hivyo hivyo ndivyo hali inavyokua

kwa sifa zake zote tukufu, kwani jina la Allah linajumuisha majina yake yote

Matukufu na sifa zake zote tukufu.

Jina la Allah hua linayaunganisha pamoja majina yake yote matukufu na sifa zake

zote tukufu, na hivyo Hadhrat Ilahiyyah (hudhihirisha sifa ya Uumbaji) hua inakua

inakaa juu ya Majina yake yote Matukufu


404

Ama kwa upande wa Shaykh Al Akbar Imam Ibn Arabi basi yeye anasema kua: ‘Jina la

Allah hua linawakilisha hali ya kuwepo kwake Muumbaji kupitia katika njia ya

Hikma na Busara, kwa mfano: Jina la Muumba (Al Asm Al Alam) hua linatokana

na vitu vilivyopewa majina. Kwa hivyo basi jina la Muumba hua linaashiria Tanzih

(Kutokuwepo Muingiliano) baina ya muumbaji na viumbe. Na jina la Muumba

hubainisha Ithbat (Uthibitisho) ya maumbile ya Sifa Tukufu. Hata hivyo hali ya yule

aliepo hua hairuhusu kugawanyika kiidadi kwa sababu Muumbaji ni Qiyam al Adad

(Alie mmoja Kiidadi). Majina ya muumbaji hua ni yenye cheo cha kuthibitisha sifa

tukufu, kwa mfano Al Alim (Mwenye kujua juu ya kila kitu), Al Qadir (Mwenye

uwezo wa kukadiria juu ya kila kitu) Al Murid (Mwenye uwezo wa Kutaka kila

kitu), Al Samiu (Mwenye Kusikia kila kitu) Al Basir (Mwenye Kuona Kila kitu),

n.k.’

Anasema Allaamah Abu Bishr Ibn Amr Ibn Uthman Ibn Qanbar Al Basr maarufu kama

Al Sibawayh anasema kua: ‘Herufi Alif na Lam yaani Al ambazo haziwezi

kutenganishwa peke yake mwanzoni mwa jina la Allah basi hua ni Muuganiko wa

Jina hilo na wala halitokani na Neno au Jina lolote. Kwani Jina Allah kamwe

haliwezi kua ni kifupi cha Al-Ilah kama wanavyodhani baadhi ya watu. Hivyo Jina

la Allah ni Jina kamili la Muumba na hivyo halina ushabihiano na Jina jengine

lolote la lugha yeyote. Hivyo basi Jina la Allah halitakiwi kutafsiriwa kwa lugha

yeyote bali linatakiwa kubakia katika hali yake ya asili kama lilivyo yaani Allah!’

Ama kwa upande wa Imam Nasir Ad Din Al Baydawi anasema kua: ‘Muongozo huu

wa kuanza na kila kitu na Biismi Allahi unamfunza Muumini kutafuta Baraka

kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala katika kila jambo lake katika maisha yake.’

Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam Al Mushakiqin Shaykh ul Islami Imam

Al Ghazali Al Thani Imam Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na ayah hii kua: ‘Biismi

Allahi hua inamfunza Muislam kuomba msaada kwa Allah Subhanah wa Ta’ala

kupitia katika Neema na Baraka zake katika kila kitu chake na hivyo hua ni yenye

kumfanya Muislam kuanza kila kitu chake na Dhikr Allah. Na ndio maana katika

kufanya kila kitu chako basi kuisoma ayah hii hua inapendekezwa na hua na hali

ya Mandub katika Sharia za Fiqh’

Katika kufafanua zaid maana aliyoinisha Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin Imam

Al Mushakiqin Shaykh ul Islami Imam Al Ghazali Al Thani Imam Fakhr Ad Din Al Razi

anaielezea hali ya Biismi Allah kulingana na Sharia za Fiqh na matumizi yake kwa

kusema kua:

1) Biismi Allah hua ni Fardhi: kuitamka pale Muislam anapotaka kuchinja mnyama

kwa ajili ya kula au anaporusha Upinde, Mshale, Risasi wakati wa kuwinda au

anapomuachia Mnyama wa kuwindia katika wakati wa kuwinda.


405

Na pia ni Fardhi kwa Mtizamo wa Madhhab ya Imam Muhammad Idris Al Shafii

kuisoma katika Sala unaposoma Surat Al Fatiha au Mwanzoni mwa Sura nyengine

yeyote isipokua Surat At Tawba ile kwa sababu Biismi Allah hua ni Moja kati ya aya ya

mwanzo katika kila Sura isipokua Surat At Tawba. Na kuisoma kwa Biismi Allahi kwa

Sala za Kutoa Sauti hua ni Wajib kwa kila Sura isipokua Surat At Tawba au unapoanza

katikati ya Sura. Kusoma Biismi Allahi kwa Sauti hua kunaulainisha Moyo wa Msomaji.

Kwani anasema Imam Abu Zakariyyah Sharaf An Nawawi kua: ‘Mtu anaetaka kusoma

basi asome Biismi Allah Rahmani Rahim mwanzoni mwa kila Sura isipokua Surat

Baraa’ah (At Tawba), kwa sababu wengi miongoni mwa Wanazuoni wamesema kua

hii ni aya popote pale itakapoandikwa ndani ya Mus-haf. Na imeandikwa mwanzoni

mwa kila Sura isipokua katika Surat At Tawbah. Hivyo kama atasoma mwanzoni

mwa kila Sura isipokua Surat At Tawba basi hua na uhakika kua amesoma Qur’an

nzima au Sura nzima. Na kama atakua hakusoma Biismi Allah basi atakua

ameiacha sehemu ya Qur’an na hii ni kutokana na mtizamo wa wengi miongoni

mwa Wanazuoni’

2) Biismi Allah hua ni Sunnah kuitamka wakati wa kusoma Surat Al Fatiha katika Sala

kulingana na mtizamo wa Madhab ya Hanafi ambao ni mtizamo wa Imam Abu Hanifa,

Imam Ibn Al Hammam na Imam Al Halabi.

3) Biismi Allah hua si Mustahab wala si Sunnah na wala si Makruh kuitamka katika

wakati wa kusoma Surat Al Fatiha katika Sala kulingana na Mtizamo wa Imam Abu

Yusuf.

4) Biismi Allah hua ni Makruh kuitamka katika wakati kuisoma Surat At Tawba

ambayo haina Biismi Allahi mwanzoni mwake, ila kwa Mtizamo wa Imam Al Ramli basi

hua ni Sunnah kuitamka unapoanza kati kati ya Sura hio ama kwa upande wa Mujaddid

Ad Din Al Hafidh Imam Shihab ad Din Imam Ibn Hajar Al Asqalani basi hua ni Sunnah

kuisoma mwanzoni mwa Surat Tawbah na ni Makruh kuisoma wakati unapoanza kati

kati ya Surat At Tawba.

Na pia hua ni Makruh kuitamka katika wakati wa kufanya mambo ambayo yana shaka

ndani yake kwa mfano kama kuvuta sigara.

5) Biismi Allah hua ni Mubah kuitamka wakati wa kuanza kutembea, kukaa kitako au

kusimama.

6) Biismi Allah hua ni Haram Kuitamka katika wakati wa kufanya mambo ya Haram,

Kuitamka wakati unapokua na Janaba, Unapokua na Hedhi au Nifasi pale unapokua na

nia ya kuisoma aya za Qur’an isipokua haiwi haram pale inapokua unafanya hivyo kwa

sababu yua kutabarruk au kwa ajili ya kufanya Dhikr.


406

Ama kwa upande wa Shaykh Muhammad Al Amin Ash Shanqeeti basi yeye anasema

kua: ‘Wanazuoni wametofautiana juu juu ya Biismi Allahi kua ni aya mwanzoni

mwa kila Sura au ni aya mwanzoni wa Surat Al Fatiha tu au ni aya kamili

inayojitegemea kama aya nyengine ama la.

Ama kulingana na aya isemayo:

‏﴿إِن َّهُ‏ مِن سُلَيْمَانَ‏ وَإِن َّهُ‏ بِسْمِ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱلر َّحمَْٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ‏ ﴾

Innahu min Sulaymana wa-innahu bismi Allahi alrrahmani alrraheemi(Surat An

Naml 27:30)

Tafsir: Hii ni kutoka kwa Sulayman na hakika inasema Biismi Allahi Rahmani Rahim

Basi bila ya shaka hii ni moja kati ya aya za Qur’an na hii ni kulingana na

makubaliano ya Ijmaa. Ama kuhusiana na Surat Baraat (At Tawbah) Basi Biismi

Allahi sio miongoni mwa aya za Sura hio, lakini kuna kutofautiana kuhusiana na

hayo mambo mengine, kwani baadhi ya Wanazuoni wa Usul wamesema kua Biismi

Allahi si miongoni mwa Aya za Qur’an na baadhi wamesema kua ni miongoni mwa

Aya ya Surat Al Fatiha tu. Na pia wako wanaosema kua Biismi Allahi ni Aya

Mwanzoni mwa kila Sura, na huu ni Mtizamo wa Imam Muhammad Idris Al Shafii.

Baada ya kuangalia mitizamo hio basi tunaona kua kuna umuhimu mkubwa sana kua

unapoanza kufanya kitu chako na kauli ya Biismi Allahi katika kila jambo lako jema na

linaloruhusika Kisharia hua pia ni mwenye kuonesha Shukrani kwa Mola wako kutokana

na kukujaalia Neema zake zisizohesabika kutoka kwake, katika uhai wako hapa

Ulimwenguni na hivyo hua ni mwenye kuukubali uwezo mkubwa wa Mola wako juu ya

kila kitu alichokujaalia, huku yeye akiwa si mhitaji wa kitu chochote kutoka kwako.

Kwa maana hiyo basi Muislam anapokua ni mwenye kuzoea kuanza kufanya jambo kila

jambo lake kwa Biismi Allahi basi hua ni mwenye kujichunga sana, katika mambo yake,

na hivyo hua si mwenye kutaka kuingiza mambo yasiyofaa ndani ya jambo hilo, au

mambo ya haram na hivyo kumharibia jambo lake hilo, kwani kusema Biismi Allahi hua

kunamkumbusha Muislam kua anaanza kufanya jambo ambalo lake hilo ambalo litapita

katika njia za halali na hivyo kupata Baraka na Neema zaidi kutokana na kua limo ndani

ya Maamrisho ya Mola wake na pia kwa kua hua haliendani kinyume na maamrisho ya

Mola wake.

Na ndio maana akasema Al Ghawth Al Adham Al Qutb Muhyi Ad Din Shaykh Abd Al

Qadir Al Jilani kua:


407

‘Biismi Allah hua ni Hazina ya wale Ambao ni wenye kukumbuka.

Biismi Allah hua ni Muhimu sana na ni ulinzi wenye nguvu kwa walio dhaifu.

Biismi Allah hua ni Nuru kwa wenye kupenda na ni furaha kwa wenye kua na hamu.

Biismi Allah hua ni Liwazo kwa maumbile ya Nafsi zetu.

Biismi Allah hua ni Ukombozi wa Miili yetu.

Biismi Allah hua ni Nuru inayong’arisha vifua vyetu.

Biismi Allah hua ni Mfumo wa kanuni unaoendesha kila jambo katika maisha yetu.

Biismi Allah hua ni Taji la kila mwenye kujiamini.

Biismi Allah hua ni Taa ya wenye kufikia malengo yao.

Biismi Allah hua ni Maridhio ya mahitajio ya mwenye kuhitaji.

Biismi Allah hua ni Jina la yule ambae anaempandisha darja mja mmoja na

kumshusha darja Mja mwengine.

Biismi Allah hua ni Jina la yule ambae anaeuhifadhi Moto wa Jahannam kwa ajili

ya kuwachoma maadui zake kama malipo yao na anauhifadhi Uzuri wa Pepo kwa

ajili ya miadi ya Marafiki zake.

Biismi Allah hua ni Jina la Yule ambae yuko peke yake asiekua na Mshirika.

Biismi Allah hua ni Jina la Mwenye kuishai milele bila ya kua na Mwisho.

Biismi Allah hua ni Jina la yule ambae mwenye uwezo wa Upekee bila ya kuhitaji

usaidizi.

Biismi Allah hua ni Dua ambayo hua ni utangulizi wa kila Sura katika Qur’an.’

Naam, tunapoangalia kwa upande wa I’lm Ruhaniyyat basi wanasema Wanazuoni wenye

I’lm hio kua: ‘Kuna Majina 3000 ya Allah Subhanah wa Ta’ala. Ambapo kati ya hayo

basi Majina 1000 ni yenye kujulikana na Malaika pekee, Majina 1000 mengine

pekee yanajulikana na Manabii, Majina 300 yametajwa kwenye Tawrat, Majina

300 yametajwa kwenye Injeel, Majina 300 Yametajwa kwenye Zabur na Majina 99

yametajwa kwenye Qur’an Tukufu. Hivyo Majina yote hua ni 2999. Jina moja

lililobakia linajulikana na Allah Subhanah wa Ta’ala ambae amemjuulisha Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam juu ya Jina hilo na limo katika Biismi Allahi Ar

Rahmani Rahim. Hivyo mwenye kuisoma aya hio basi hua ni sawa na mwenye

kupata malipo ya aliesoma majina hayo 3000’

Baada ya kuangalia maana na matumizi ya Jina la Allah kwa kifupi kulingana na

mitizamo ya wanazuoni mbali mbali basin a tuangalie maana ya jina la pili liliomo katika

Biismi Allahi Rahmani Rahim ambalo ni Rahman na Rahim, ambayo ni majina

yanayotokana na mzizi mmoja wa neno Rahima ambalo hua ni lenye kumaanisha

Kupenda, Kua na Upole, Kua na Huruma, Kua na Ukarimu, kua na Wema, Kua na

Rehema.

Na kama kawaida tunapozungumzia Sifa za Majina Matukufu ya Allah Subhanah wa

Taa’ala kimaana basi hua tunajaribu tu kuelezea kulingana na mtizamo wa ufahamu wa

Ibn Adam, kwani ukweli ni kua kama anavyosema Mujaddid Ad Din Hujjat Ul Islami


408

Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali kua kwa

vyovyote vile tutakavyojaribu kuelezea maana ya Majina Matukufu ya Allah Subhanah

wa Ta’ala basi kamwe hatutoweza kuelezea maana yake kikamilifu kama inavyostahiki,

yaani tuchukulie mfano wa hili neno Rahman ambalo limetumika kwenye aya ifuatayo:

‏﴿قُلِ‏ ٱدْعُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ أَوِ‏ ٱدْعُواْ‏ ٱلر َّحمَْٰنَ‏ أًَّ‏ م َّا تَدْعُواْ‏ فَلَهُ‏ ٱلأَسمَْآءُ‏ ٱلحُْسْنىَٰ‏ ﴾

Quli odAAoo Allaha awi odAAoo alrrahmana ayyan ma tadAAoo falahu al-asmao

alhusna (Surat Al Isra 17:110)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad): Muombe Allah au Muombe Mwingi wa Rehma,

vyovyote vile utakavyomuomba kwani kwake yeye ndiko kwenye Umiliki wa Majina

Matukufu.

Naam, ayah hii ya Surat Al Israa inaweka wazi umuhimu wa kumuomba Allah Subhanah

wa Ta’ala kwa kutumia Majina yake Matukufu ambapo Jina la Al Rahman linamaanisha

Yule ambae ni mwenye Rehma nyingi sana kupita kiasi na hivyo kutokua na mfano wake

katika Rehma zake, kwani yeye si mwenye kua na Rehma pekee tu bali pia hua ni

mwenye kusababisha Rehma zake kuwafikia wale awatakao miongoni mwa waja wake

waliomuamini kama inavyosema aya ifuatayo:

‏﴿هُوَ‏ ٱل َّذِى يُصَلِّى عَلَيْكُمْ‏ وَمَلاَئِكَتُهُ‏ لِيُخْرِجَكُمْ‏ مِّنَ‏ ٱلظ ُّلُمَاتِ‏ إِلىَ‏ ٱلن ُّورِ‏ وَكَانَ‏

بِٱلْمُؤْمِنِينَ‏ رَحِ‏ يماً‏ ﴾

Huwa alladhee yusallee AAalaykum wamala-ikatuhu liyukhrijakum mina

aldhdhulumati ila alnnoori wakana bialmu/mineena raheeman (Surat Al Ahzab

33:43)

Tafsir: Ni yeye ambae ndie mwenye kukusalia na Malaika wake, ili akutoe kutoka

katika kiza na kukuingiza katika Nuru. Na ni yeye ambae kwa Waumini ni Mwingi wa

Rehma.

Kulingana na aya hizi basi tunaona kua Ar Rahman maana yake ni mwenye sifa ya kua

na Rehma na Ar Rahim maana yake hua ni kutoa Rehma. Na kulingana na mtizamo wa

Shaykh Al Akbar Imam Muhyidiin Ibn Al Arabi basi yeye anasema kua kuna: ‘Neno Ar

Rahma lina athari mbili ambapo ya kwanza ni Athar bi al Dhat na Athar bi al Sual.


409

Na tunapozungumzia Athar bi al Dhat basi hua tunazungumzia athari inayotokana

na bainisho la Rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala kupitia katika sifa za Rehma

hizo. Kwani kimaumbile basi viumbe vyote vilivyopo hua ni vyenye kuanisha sifa

ya kuwepo kwa Rehma zake. Ama kwa mtizamo mwengine basi tunapozungumzia

Athar bi al Sual basi hua tunazungumzia athari ya Rehma ilivyogaiwa kwa viumbe.

Hususan kwa viumbe Ibn Adam ambao wao hua ni wenye kupewa Rehma

kulingana na jithada zao, kwa mfano pale wanapoomba kama inavyosema aya

ifuatayo: ’

‏﴿إِن َّهُ‏ كَانَ‏ فَرِيقٌ‏ مِّنْ‏ عِبَادِى يَقُولُونَ‏ رَب َّنَآ آمَن َّا فَٱغْفِرْ‏ لَنَا وَٱرْحمَْنَا وَأَنتَ‏ خَيْرُ‏

ٱلر َّاحمِِينَ‏ ﴾

Innahu kana fareequn min AAibadee yaqooloona rabbana amanna faighfir lana

wairhamna waanta khayru alrrahimeena (Surat Al Muuminun 23:109)

Tafsir: ‘Bila ya shaka walikua ni miongoni mwa Makundi ya Waja wangu ambao

walikua wakisema: ‘Ewe Mola wetu! Hakika sisi tumekuamini, Hivyo tusamehe, na

utuingize katika Rehma zako, kwani kwa hakika wewe ni m-bora wa wenye kua na

Rehma.’

Yaani kutokana na jitihada hizo za kumuomba Mola wao basi Allah Subhanah wa Ta’ala

hua ni mweye kuwaingiza watu hao kwenye Rehma zake, kwani watu hao hua

wanajulikama kama Ahl al Hadhrah yaani watu ambao wameingia kwenye hadhara ya

Mola wao.

Sultan Al Mutakkalimin Mujaddid Ad Din Imam Al Ghazali Al Thani Imam Fakhr Ad

Din Al Razi kua: ‘Katika Biismi Allahi’ kuna harfu 19, ambazo ni sawa na idadi ya

Malaika wa Jahannam ambao ni 19 hivyo kila unaposema Biismi Allahi basi unakua

na matumaini ya kuvuka kizuizi cha adhabu ya kila mmoja kati ya Malaika hao 19

wa Moto.’ (Na huo pia ndio mtizamo wa Mujaddid Ad Din Shaykh ul Islami Al Hafidh

Imam Ibn Hajar Al Asqalani katika kitabu chake Al Majmaa Al Muasisi na pia Imam Abu

Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi katika Ahkam

Al Quran na Mujaddid Ad Din Imam Abd Rahman Al Suyuti katika Al Durr al Mandhur)

Tunaingia katika maana ya Biismi Allahi Ar Rahmani Al Rahim ambapo tunaona kua

Hujjat Al Islami Mujaddid Ad Din Az Zuhruf ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn

Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali anasema kua: ‘Katika ayah hii basi tunaona

kua ndani yake mmejumuishwa Ilm yote inayohusiana na Sifa za Majina Matukufu

za Allah Subhanah wa Ta’ala, na Ilm ya Sifa za Ar Rahmani Ar Rahim


410

zimejumuishwa kwani hizi ni Sifa ambazo zimezipita Sifa zote Tukufu Kiuwezo na

Kiilm. Na Sifa mbili hizi hua ni zenye kuleta hali ya hisia nzuri na zinazovutia

tofauti na nyengine ambazo hua zinaamsha Ghadhabu au Khofu.’

Ama kulingana na mtizamo wa Shaykh Al Akbar Imam Ibn Arabi basi tunaona kua yeye

anasema kua: ‘Jina la Al Rahman hua ni Sifa yenye kujumuisha ukubwa kamilifu wa

Hikma zake kuhusiana na Ulimwengu mzima kulingana na mapokezi ya mwanzoni

mwa yule alie wa mwanzo. Al Rahim hua ni Sifa inayojumuisha ukubwa kamilifu

kimaana kwa ajili ya Ibn Adam kuhusiana na Mwishoni mwa yule alie wa mwisho.

Na hii ni kwa sababu wanasema wenye kujua kua: Ya Rahman hua ni kwa ajili ya

Dunia na Akhera na Ya Rahim hua ni kwa ajili ya Akhera. Hii inamaanisha

kuunyanyua Ukamilifu wa Ibn Adam na kuwakirimu kwa hali zote za ki ujumla na

kimahsusi kwa kila mmoja, na ni kudhihirisha Sifa ya Allah.’

Ama kwa upande wa Imam Nasir Ad Din Al Khayr Abd Allah Ibn Umar Al Baydawi

anasema kua: ‘Maneno haya mawili Al Rahmani Al Rahim hua yanathibtisha

thamani ya mubalagha (kutoa maana yenye uzito mkubwa wa kitu) kuhusiana na

Rehma. Kwani sifa ya Al Rahman hua ni yenye kujumuisha jumla ya Rehma za

Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kila kitu katika Ulimwengu huu, kwa Waumini na

wasiokua Waumini, kuhusiana na hali ya Maisha, Riziki, Afya, Akili, Ufahamu, n.k.

na Al Rahim hua inajumuisha Sifa za Allah Subhnah wa Ta’ala anaetoa fadhila zake

kwa Waumini, kwa kuwaongoza katika Uongofu, Imani, Kufanya Mema na

kuachana na Maovu katika uhai wa Ulimwenguni, na hapo hapo kuwalipa furaha

ya Milele na mafanikio ya kweli kesho Akhera.’

Ama kwa upande wa Amir ul Muuminin Fi Al Hadith Imam Abdullah Ibn Mubarak basi

yeye anasema kua: ‘Al Rahman maana yake ni yule Mwenye Kujibu kama ikiwa

utamuuomba, na Al Rahim maana yake hua ni yule mwenye Hasira kali usipo

muomba’

Na pia kuna wasemao kua Al Rahman maana yake hua ni kutoa riski kwa Viumbe wake

na Al Rahim ni mwenye Kusamehe Dhambi za Walimuamini. Hivyo basi mtegemee

Allah Subhanah wa Ta’ala katika kutafuta riski yako, na mtegemee yeye katika

kusamehe kasoro zako. Kwani kimaumbile Ibn Adam hua ni mwenye hali tatu zifuatazo:

‘Kwanza ni hali ya kutokuwepo kwa kiumbe kinachohitaji kuwepo. Pili ni hali ya

kuishi kwa kiumbe anaetaka kuwepo Milele na Tatu ni hali ya mtu anaehitaji

Usamehevu katika uhai wa Akhera, hivyo mja hua ni mwenye kumhitaji Mola wake

na Sifa zake katika kutafakkari majina haya ambayo ni: Allah ambae ndie Mwenye

kumjaalia Mja huyo kuwepo kwake, Al Rahman ambae ndie anaetoa Riski kwa ajili

ya Mja wake kuendelea na Uhai wake na Al Rahim ambae ndie mwenye Kusamehe

Kasoro na makosa ya Mja katika siku ya Malipo’


411

Anasema Baddiuzzamman Said Nursi katika Risale Nuri kua: ‘Kauli ya Biismi Allahi

imejaa Baraka ya hazina kiasi ya kua kutokana na kukuunganisha na Allah

Subhanah wa Taa’ala basi hukubadilishia udhaifu wako na umasikini na

kukuingiza katika ukumbi wa Allah Subhanah wa Ta’ala. Hivyo mtu anaeanza

jambo lake na Biismi Allahi basi hua ni mwenye kufanya jambo lake kwa jina la

Mola wake na hivyo hua ni sawa na anaejiunga na Jeshi na kisha akawa ni mwenye

kufanya mambo hayo chini ya ngao ya jina la Taifa husika. Hua si mwenye kua na

khofu na yeyote, kwani hufanya kila jambo lake kwa jina la Shariah husika na hivyo

kua na ngao imara dhidi ya yeyote atakaepingana nae’

Hivyo Jafar Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu alianza kuisoma Surat Maryam kwa

kuanza na Biismi Allahi Al Rahmani Al Rahim akatiririka na aya ya kwanza ya Sura hio

yasemayo Kaf-Ha-Ya-AAayn-Sad.

KAF – HA – YA – A’AYN – SAD

﴿ كهيعص﴾‏

Kaf-Ha-Ya-AAayn-Sad (Surat Maryam 19:1)

Tafsir: Kaf-Ha-Ya-AAayn-Sad

Kama tunavyoona kua hizi ni Harfu MuqattaaAt, ambapo Kaf ni harufi inayojitegemea,

Ha ni herufi inayojitegemea, Ya ni Herufi inayojitegemea, Aaayn ni herufi

inayojitegemea na Sad ni herufi inayojitegemea.

Ambapo kuna miongoni mwa Wanazuoni wasemao kua herufi hizi tano za Surat Maryam

zinajumuisha miongoni mwa Majina Matukufu ya Allah Subhanah wa Ta’ala (Min Al

Asmaaihi Al Husna). Na ndio maana Nabii Zakarriyah alikua akianza Kuomba dua zake

kwa kutumia herufi hizi tano, na hii ni kwa sababu kila Dua hua ina Siri yake peke yake

ambayo katika kuomba kwake hua ni yeye kumkaribisha Muombaji mbele ya Allah

Subhanah wa Ta’ala na kumfanya kua ni mwenye kukubaliwa maombi yake.

Ambapo Nabii Zakarriyah alikua akianza na Kaf-Ha-Ya-AAayn-Sad kwa sababu Harfu

Kaf inawakilisha Jina tukufu la Allah Subhanah wa Ta’ala ambalo ni Al Kafi yaani

Mwenye Kutosheleza na hii ni kutokana na namna Nabii Zakarriyah alivyokua akijihisi

udhaifu wake mbele ya Mola wake na hivyo kuonesha Unyenyekevu na kudhihirisha kua


412

huna atakaeweza kumtoshelezea mahitaji yake hapa Duniani isipokua Allah Subhanah

wa Ta’ala. Kwani Kaf pia ha inamanisha Hal Idhafa yaani Hali ya kuonesha Udhaifu.

Ambapo kuhusiana na Ha basi yeye ni Al Hadi yaani Muongozaji, ama kuhusiana na Ya

basi ni Yu/wiyi yaani Mwenye Kukaribisha Kimakazi, ama kuhusiana na Al Aaayn basi

ni Al Aalam yaani Ndie Chanzo cha Kila Kitu, ama kuhusiana na Sad basi ni Al Sadiq

yaani Mkweli mwenye kuaminika.

Na hivyo basi unaweza kuanza kusoma Dua yako kwa kusema kwa mfano unapokua na

uzito katika kipato ukaanza Dua yako kwa kusema: ‘Bismi Allahi ‘ar-Rahmani ‘ar-

Raheem, Kaf Ha Ya `Ayn Sad, Ha Mim `Ayn Sin Qaf, Iyyaka na`bud wa iyyaka

nasta`een. Allahu Lateefun bi `ibaadihi yarzuqu man yashaa..’ au unapokua unahitaji

usalama basi unaweza kuanza Dua yako kwa kusema Bismi Allahi ‘ar-Rahmani ‘ar-

Raheem, Bi Haqi Kaf Ha Ya `Ayn Sad, Kifayatuna Ha Mim `Ayn Sin Qaf, Himayatuna

Fasayakfikahumu Allahu wa Huwa Al SamiaAu Aaliimun.

بحق كهيعص كفايتنا ‏،حم عسق حمايتنا فسيكفيكهم الله وهو السمع العليم

Na pia maneno haya peke yake hua ni ulinzi wa Dua inayojitegemea ambapo unakua

unayasoma mara 313 au mara 11 kwani ‘Bismi Allahi ‘ar-Rahmani ‘ar-Raheem, Bi

Haqi Kaf Ha Ya `Ayn Sad, Kifayatuna Ha Mim `Ayn Sin Qaf, Himayatuna

Fasayakfikahumu Allahu wa Huwa Al SamiaAu Aaliimun.’ Maana yake hua ni ‘Kwa

jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma kwa haki ya Kaf Ha Ya `Ayn

Sad, Inatutosheleza Ha Mim `Ayn Sin Qaf, Ni Himaya yetu inayotulinda

(Fasayakfikahumu Allahu wa Huwa Al SamiaAu Aaliimun) Allah anakutoshelezeni

nyinyi Dhidi yao kwani kwa hakika yeye ni mwenye kusikia kila kitu na mwenye kujua

kila kitu.

Ambapo maneno yasemayo Fasayakfikahumu Allahu wa Huwa Al SamiaAu Aaliimun

ndio yale yaliyomo kwenye aya ambayo imesema kua:

‏﴿فَإِنْ‏ آمَنُواْ‏ بمِِثْلِ‏ مَآ آمَنْتُمْ‏ بِهِ‏ فَقَدِ‏ ٱهْتَدَواْ‏ و َّإِن تَوَل َّوْاْ‏ فَإِنم ََّا هُ‏ مْ‏ فىِ‏ شِ‏ قَاقٍ‏

فَسَيَكْفِيكَهُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ وَهُوَ‏ ٱلس َّمِيعُ‏ ٱلْعَلِيمُ‏ ﴾


413

Fa-in amanoo bimithli ma amantum bihi faqadi ihtadaw wa-in tawallaw fa-innama

hum fee shiqaqin fasayakfeekahumu Allahu wahuwa alssameeAAu alAAaleemu

(Surat Al Baqara 2:137)

Tafsir:Kisha kama wataamini mithili yake kile unachokiamini wewe basi watakua

wamongoka, lakini kama ikiwa watageuka basi watakua ni wanaopinga. Hivyo Allah

atakutosheleza wewe dhidi yao, na kwa hakika yeye ni mwenye kusikia kila kitu na ni

mwenye kujua kila kitu.

Ama kwa upande Amir Ul Muumin Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu basi alikua

akisikika akiwa anaomba Dua kwa kusema: ‘Kaf Ha Ya `Ayn Sad, Ighfirlii’ na kwa

Upande wa Imam Abd Rahman Al-Kalbi, Imam Mujahid Ibn Sulayman na Imam Al

Dahhak Ibn Muzahim basi wanasema kua: ‘Kaf ni yenye kumaanisha Karim, Ha ni Al

Hadi, Ya ni Mwingi wa Rehma Aayn ni Mwenye Kujua na Kuona na Sad ni Mkweli

Muaminifu’.

Na kwa upande mwengine anasema Imam Malik Ibn Dinar kua: ‘Katika Safari Moja

Mimi nilikua nikienda kwenye Ibada ya Hija, ambapo njiani nikakutana na mtu

ambae alikua hana Kipando wala Mzigo wowote. Nami nikamsalimia, kwa

kumwambia ‘Asalaam Alaykum wa Rahmat Allahi wa Barakatuh!’ nae akanijibu wa

kusema ‘Wa Alaykum Salam wa Rahmat Allahi wa Barakatuh!’’

Nami nikamuuliza: ‘Unatokea Wapi?’ nae akanijibu: ‘Kwa kinakotoka kila kitu’

nami nikamwambia: ‘Na Unaelekea Wapi?’ akanijibu kwa kusema: ‘Kwenye

Nyumba yake.’ Nikamuuliza: ‘Na jee iko wapi mzigo yako?’ nae akasema: ‘Kiko

Kwake kila kitu Changu’ hivyo nikamwambia kua: ‘Safari ni ndefu kama huna

chakula wala maji, jee unakitu chochote kile’ nae akasema: ‘Naam, nilipoanza

safari yangu nilichukuwa herufi tano’. Nami nikamuuliza: ‘Herufi gani hizo?’

Nae akasema: ‘Kaf-Ha-Ya-AAayn-Sad’ nami nikamuuliza : ‘Jee ni nini maana ya

Kaf?’ nae akajibu: ‘Kaf ni kua Yeye ni Al Kafi, yaani ni Mwenye Kutosheleza, ama

kuhusiana na Ha basi yeye ni Al Hadi yaani Muongozaji, ama kuhusiana na Ya basi

yeye ni Yu/wiyi yaani Mwenye Kukaribisha Kimakazi, ama kuhusiana na Aaayn

basi ni Al Aalam yaani Ndie Chanzo cha Kila Kitu, ama kuhusiana na Sad basi ni

Al Sadiq yaani yeye ni Mkweli.

Na hivyo yeyote yule ambae kufuatana na Mwenye Kutosheleza, Mwenye

Kuongoza, Mwenye Kukaribisha Kimakazi ambae ndie Chanzo cha Kila kitu na

ndie Mkweli basi hua si mwenye Kutokinai, hua si mwenye Kupotea njia, hua si

mwenye woga, na hua si mwenye kuhitaji chochote kua kama akiba katika Safari

yake’


414

Kisha Mtu huyo ulipoingia Usiku Akavua kanzu yake kwa ajili ya kujifunikia mwili

wake kabla ya kulala kwake, kisha akasema: ‘Dunia Uhalali wake ni katika

kuhesabiwa kwake yaliyofanyika ndani yake na Uharamu wake ni Katika Kulipwa

Malipo yake Kesho Akhera.’(Yaani ili kuishi Duniani basi inabidi uhesabiwe

uliyoyafanya ndani yake, na huwezi kulipwa uliyoyafanya ndani yake mpaka kwanza

uharamishiwe kuishi ndani yake kwa kufikwa na Mauti ili utoke Ulimwenguni uingie

Akhera.)

Na kisha mtu huyo akanyanyua Kichwa na Mikono juu na kusema: ‘Ewe

Usienufaika na Utiifu wa Waja juu yako, na wala usiedhurika na Uasi wa Waja juu

yako, Nijaalie mimi kua na kile ambacho Hakikunufaishi Na niepushe na Kile

Usichodhurika Nacho.’

Na tulipoingia kwenye Ihram na watu kuanza kuitikia: ‘Labbaika Allahuma

Labbaik, Labbaika La Sharka Laka Labbaik, Inna Alhamd Wa Niaamata Laka Wa

Mulk, Lasharika Laka Labbaik’ sikumuona kua yeye ni miongoni mwa Wenye

kuitikia. Hivyo nikamauuliza, vipi Mbona umekaa Kimya?

Nae akasema: Ewe Shaykh Hakika mimi nna khofu kua Huenda mimi nikaitikia

halafu yeye akaniambia: ‘La, Hakika mimi sitokuridhia, sitokusikia na wala

sitokuangalia’ kisha Mtu huyo akaondoka na sikumuona tena, katika macho yangu

hadi pale tulipofika katika maeneo ya Minna ambapo nilimuona akiwa analia sana

na kusema:

‘Ewe Kipenzi ulieridhika na Damu yangu, hakika Damu yangu ni halali juu yako.

Wa Allahi kama Roho yangu ingemjua yule nnaempenda zaidi yake, basi ingekaa

juu ya kichwa chake badala ya kwenye miguu yake.

Ewe Mama Yangu usinilaumu kwa mapenzi yangu juu yake, kwani usingelaumu

kama ungeujua uzuri wake.

Hakika watu wanaizunguka Al Kaabah bila ya ufahamu, lakini ya laiti kama

wangekua wanaizunguka kwa ufaham juu ya Mola wao basi wangehalalishiwa

Utukufu wao.

Ya Allah hakika watu wanafanya Hija, lakini mimi nna Hija ndani ya Makazi yangu

na hivyo naitolea Kafara Nafsi yangu na Damu yangu kwa ajili yako.

Ya Allah hakika watu wamechinja na kutafuta ukaribu nawe kwa kutoa Sadaka

kwa ajili ya kua ni zawadi kwako, lakini mimi sina chochote cha kutoa kwa


415

kunikaribisha karibu yako, isipokua hii Roho yangu ambayo ipo kwa ajili yako,

hivyo nakuomba nipokelee mimi kwa ajili yangu kwani tayari nimeiwaklisha mbele

yako.

Kisha akanyanyua juu Macho yake huku akiwa analia na kububujikwa na machozi

mengi sana, kisha ghafla akaanguka chini na kutulia tulii kwani alikua amekutana

na Malakat al Mauti.

Ambapo katika usiku wa siku hio, wakati nikiwa namfikiria yeye basi nilipolala

nikamuona usingizini, na nikamuuliza: ‘Vipi imekuaje?’ nae akasema: ‘Allah

amenijaaalia mimi kua ni sawa na Mashahidi wa Vita vya Badr na pia akaniongezea

Daraja’ nami nikamuuliza: ‘Kwanini akakuongezea Darja?’ nae akasema: ‘Kwa

sababu Mashahidi wa Badr wao waliuliwa kwa Mapanga ya Maadui zao, wakati

mimi nimeuawa kutokana na Mapenzi ya Mola wangu juu yake’

Na pia kuna mtizamo mwengine ambao ni ule unayoifafanua aya hii:

﴿ كهیعص﴾‏

Kaf-Ha-Ya-AAayn-Sad (Surat Maryam 19:1)

Tafsir: Kaf-Ha-Ya-AAayn-Sad

Kua Harfu Kaf hua inamanisha kua Allah Subhanah wa Ta’ala ni Al Kafi yaani ni

mwenye Kutosheleza kwa Mja wake ambapo hapa katika Kaf-Ha-Ya-AAayn-Sad basi

Mja aliejumuishwa ndani ya siri yake kimaaana maneno haya hua ni Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kama vile alivyosema katika Qur’an pale alipohoji kwa

kutumia neno Bikafin katika aya ifuatayo:

‏﴿أَلَيْسَ‏ ٱهلل َُّ‏ بِكَ‏ افٍ‏ عَبْدَ‏ هُ‏ وَيخَُوِّفُونَكَ‏ بِٱل َّذِينَ‏ مِن دُونِهِ‏ وَمَن يُضْلِ‏ لِ‏ ٱهلل َُّ‏ فَمَا لَهُ‏

مِنْ‏ هَادٍ‏ ﴾

Alaysa Allahu bikafin AAabdahu wayukhawwifoonaka bialladheena min doonihi

waman yudhlili Allahu fama lahu min hadin (Surat Az Zumar 39:36)


416

Tafsir: Hivi Jee Allah si mwenye Kutosheleza kwa Mja wake (Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam)? Lakini wao hua wanajaribu kuwatisha wale ambao

wanamshirikisha! Na anaepotoshwa na Allah basi hakuna wa kumuongoza.

Ambapo harfu Ha hua inamaanisha Hidaya yaani Muongozo kama vile alivyosema

katika aya ifuatayo:

‏﴿لِّيَغْفِرَ‏ لَكَ‏ ٱهلل َُّ‏ مَا تَقَد َّمَ‏ مِن ذَنبِكَ‏ وَمَا أتََخ َّرَ‏ وَيُتِم َّ نِعْمَتَهُ‏ عَلَيْكَ‏ وَيَهْدِيَ‏ كَ‏

صِرَاطاً‏ م ُّسْتَقِيماً‏ ﴾

Liyaghfira laka Allahu ma taqaddama min dhanbika wama taakhkhara

wayutimma niAAmatahu AAalayka wayahdiyaka siratan mustaqeeman (Surat Fath

48:2)

Tafsir: Amekusamehe (Wewe Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam)Allah katika

yaliyopita Katika Dhambi zako na yatakayokuja, na amekamiisha Neema yake juu

yako na amekuongoza katika njia iliyonyooka.

Ambapo neno Ya hua linaamanisha Yada yaani Mkono, Kuunga Mkono au Kutoa Mkono

katika kusaidi kitu au Jambo kama ilivyosema aya ifuatayo;

‏﴿وَٱذْكُرُو ۤ اْ‏ إِذْ‏ أَنتُمْ‏ قَلِيلٌ‏ م ُّسْتَضْعَفُونَ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ تخََافُونَ‏ أَني َ‏ تَخَ‏ ط َّفَ‏ كُ‏ مُ‏ ٱلن َّاسُ‏

فَآوَاكُمْ‏ وَأَي َّدَكُم بِنَصْرِهِ‏ وَرَزَقَكُمْ‏ مِّنَ‏ ٱلط َّيِّبَاتِ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تَشْكُرُونَ‏ ﴾

Waodhkuroo idh antum qaleelun mustadhAAafoona fee al-ardhi takhafoona an

yatakhattafakumu alnnasu faawakum waayyadakum binasrihi warazaqakum mina

alttayyibati laAAallakum tashkuroona (Surat Al Anfal 8:26)

Tafsir: Na kumbuka wakati mlipokua kidogo na mkichukuliwa kua ni dhaifu katika

Ardhi, na ulikua ukiogopa kua labda kuna watu watakuteka Nyara. Lakini yeye

akakupa (Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam) Makazi (Kwa kukuhamishia katika

Mji wa Madinah kutoka Makkah) na kukusaidia kwa nusura yake na akakuruzukuni

vizuri na vya halali ili mpate kushukuru.


417

Ambapo neno Harfu Ayn inamaanisha Aadha yaani Kukinga au Kuhifadhi kama

ilivyosema katika aya ifuatayo:

‏﴿يَۤ‏ أَي ُّهَا ٱلر َّسُولُ‏ بَلِّغْ‏ مَآ أُنزِلَ‏ إِلَيْكَ‏ مِن ر َّبِّكَ‏ وَإِن لم َّْ‏ تَفْعَلْ‏ فَمَا بَل َّغْتَ‏ رِسَالَ‏ تَهُ‏ وَٱهلل َُّ‏

يَعْصِمُكَ‏ مِنَ‏ ٱلن َّاسِ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لاَ‏ يَهْدِى ٱلْقَوْمَ‏ ٱلْ‏ ا ‏َك فِرِي نَ‏ ﴾

Ya ayyuha alrrasoolu balligh ma onzila ilayka min rabbika wa-in lam tafAAal fama

ballaghta risalatahu waAllahu yaAAsimuka mina alnnasi inna Allaha la yahdee

alqawma alkafireena (Surat Al Maidah 5:67)

Tafsir: Ewe Mtume (Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) Tangazia (Ujumbe)

ulioshushiwa kutoka kwa Mola wako, Na kwani kama hukufikisha basi utakua

hukufikisha Ujumbe wake. Na Allah atakuhifadhi wewe kutokana na Watu. Kwani

Allah hawaongozi watu wenye kumkufuru.

Na Harfu Sad hua ni yenye kumanisha Salat Ala Nabii kama vile ilivyosema Aya

ifuatayo:

‏﴿إِن َّ ٱهلل ََّ‏ وَمَلاَئِكَتَهُ‏ يُصَل ُّونَ‏ عَلَى ٱلن َّبىِِّ‏ ‏َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ صَل ُّواْ‏ عَلَيْهِ‏ وَ‏ سَلُِّمو اْ‏

تَسْلِيماً‏ ﴾

Inna Allaha wamala-ikatahu yusalloona AAala alnnabiyyi ya ayyuha alladheena

amanoo salloo AAalayhi wasallimoo tasleeman(Surat Al Ahzab 33:56)

Tafsir: Hakika Allah (Subhanah wa Ta’ala amemsamehe) na Malaika wake

wanamsalia (Wanamuombea asamehewe) Nabii (Muhammad Salallahu Alayhi wa

Salam) hivyo enyi Mlioamini nanyi msalieni kwa kikamilifu kama inavyotakiwa.

Na hii ni kwa kwa sababu iliyowekwa wazi na aya isemayo:


418

‏﴿وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ‏ فَإِن َّ اهلل ََّ‏ هُوَ‏ مَوْلاَهُ‏ وَجِ‏ برِْيلُ‏ وَصَالِحُ‏ الْمُؤْمِنِينَ‏ وَالْمَلاَئِكَةُ‏ بَعْدَ‏

ذٰلِ‏ كَ‏ ظَهِيرٌ‏ ﴾

Wa-in tadhahara AAalayhi fa-inna Allaha huwa mawlahu wajibreelu wasalihu

almu/mineena waalmala-ikatu baAAda dhalika dhaheerun (Surat At Tahrim 66:4)

Tafsir: Na hata kama mkidhihirisha (katika kushirikiana) pamoja Dhidi yake

(Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) basi kwa hakika Allah ndie Mlinzi wake na

Jibril, na wema Miongoni mwa Waumini na Malaika baada yake wamedhahirisha.

Ambapo neno Mawla lililotumika hapa ni lenye kutokana na neno Waliya ambalo hua

linamaanisha Kua Karibu, Kua na Ukaribu, Fuata au Karibia. Lakini hua linabadilika

maana kulingana na namna lilivyotumika, ambapo kwa namna lilivyotumika hapa katika

hali ya kwanza ambayo ni yenye kuzungumzia Uhusiano baina ya Allah Subhanah wa

Ta’ala na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi hua linamaanisha maana kamilifu

ya kua Allah Subhanah wa Ta’ala ni Msimamizi wa kila kitu juu ya Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam.

Ambapo lilipotumika kwa upande wa uhusiano wa Malaika Jibril na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam basi hua linamanisha Mfikishaji wa Jumbe wa Allah

Subhanah wa Ta’ala, na lilipotumika kwa upande wa uhusiano wa baina ya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na Waumini basi hua linamaanisha Wafuasi,

Wanaoshikamana nae kutokana na kile alichoshushiwa na Allah Subhanah wa Ta’ala

kupitia kwa Malaika Jibril, na lilipotumika kuhusiana na uhusiano baina baina ya Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Malaika wengine wa kawaida basi hua linamaanisha

Wanamuombea apate utulivu.

Hivyo Jafar akaendelea kutiririka na Surat Maryam mbele ya An Najash, kuanza kwenye

aya ya kwanza tuliyoifafanua ya Kaf-Ha-Ya-AAayn-Sad hadi kwenye aya 15, ambazo

zinazozungumia kuhusiana na Nabii Zakariyah na Nabii Yayha na Maryam Bint Imran

kama tulivyoona hapo kabla, kisha baada ya hapo akaendelea kusoma aya ambazo na

zenye kuelezea kisa cha kuzaliwa kwa Nabii Isa Ibn Maryam ambazo ndani yake ndio

Allah Subhanah wa Ta’ala anaelezea kuhusiana na kuumbwa na kuzaliwa kwake Nabii

Isa Ibn Maryam.


419

UJUMBE WA NAJRAN, THUMAMAH IBN UTHAL – UTHIBITSHO

WA WASIOKUA WAISLAM KURUHUSIKA KUINGIA MSIKITINI

Mnamo mwezi wa Dhul Hijja wa mwaka wa 10 Al Hijra wa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam, basi alipokea ujumbe wa watu 60 kutoka katika Mji wa Najran ambao walikua

ni Wafuasi wa Dini ya Kikristo. Mji wa Najran ni mji ambao upo kusini ya mji wa

Madinah kwa umbali wa kilomita 730, yaani hapa tunazungumzia maeneo ya karibu na

ardhi ya Yemen.

Ujumbe huu ulipokelewa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kukaribishwa

ndani ya Msikiti wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na wakaruhusiwa kusali

ndani yake ambapo walisali kwa kuelekea Kibla chao katika upande wa Mashariki kama

anavyosema Imam Muhammad Ibn Is-haq kua:

‘Amesema Muhammad Ibn Jafar Ibn Zubayr kua: ‘Ujumbe kutoka Najran ulikuja

kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na akaingia Msikitini baada ya kusali

sala ya Al Asr. Walikua wamefuatana na Msafara wa Ngamia ambao ulikua

unaongozwa na Ukoo wa Bani Al Harith Ibn Kab.

Ambapo Masahaba wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam walipowaona

wakasema kua hawakuwahi kukutana na Msafara kama huo baada yake. Na

ulipofika wakati wa kufanya Ibada yao, basi walisimama ndani ya Masjid Nabawi

na wakapiga kengele yao na kisha kufanya Ibada yao huku Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akiwaambia Masahaba zake kua: ‘Waacheni wafanye Ibada yao.’

Na wakasali huku wakielekea Mashariki’

Na kutokana na Uthibitisho huu basi tunaona kua Wanazuoni wametofautiana kuhusiana

na kuruhusika kwa wasiokua Waislamu kuingia Msikitini na hivyo pia kutokana na

kuruhusika huko basi kunamaanisha kua hata Wanawake wanapokua katika hali ya

kutokua Tohara hua wanaruhusika kuingia Msikitini iwe kwa ajili ya kutekeleza haja

fulani, kuenda kusoma Darsa n.k.

Ambapo pia wenye mtizamo huo hua wanatumia pia uthibitisho wa ile hadith ya Imam

Ibn Hazim ambayo inasema: ‘Amesema Umm Ul Muuminin Aisha Radhi Allahu Anha

kua: ‘Kulikua kuna Mtumwa Mweusi wa Kike wa ambae alikua anamilikwa na

Kabila Moja la Waarabu ambao walimuacha huru, hivyo Mwanamke huyo akaja

hadi kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na akasilimu, na akawa na hema

dogo ndani ya Msikiti’’(Al Muhalla Bi Al Athar)


420

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu kua:

‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikutana nae katika njiani katika Mji wa

Madinah , wakati akiwa katika hali ya kua na Janaba. Hivyo Abu Hurayrah Radhi

Allahu Anhu akakimbilia kuenda kukoga Janaba. Hivyo Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akaona kua Abu Hurayrah hayuko mbele yake kwenye Darsa lake,

na Abu Hurayrah Radhi Allahu Anhu aliporudi basi Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam akamuuliza Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu: ‘Ulikuwepo wapi ewe Abu

Hurayrah?’

Abu Hurayrah Radhi Allahu Anhu akajibu: ‘Ya Rasul Allah! Nilikua niko katika

hali ya kua na Janaba Hivyo sikutaka kukaa pamoja nawe hadi pale nitakapo kua

nimekoga na kujitoharisha.’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema:

‘Subhanah Allah! Muumini hua kamwe hawi Mchafu’’(Sahih Muslim)

Ambapo kuhusiana na ile hadithi isemayo kua: ‘Amesema Aisha Radhi Allahu Anha

kua amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Msikitini hua

hairuhusiki kuingia Mwanamke Mwenye Hedhi au yeyote yule ambae hayuko

tohara’(Sunnan Imam Abu Daud, Sunnan Imam Ibn Majah na Sunnan Imam Abu

Huzaymah)’

Basi kulingana na mtizamo wa baadhi ya Wanazuoni kuhusiana na hadithi hii wanasema

kua ni Hadith dhaif na huo ni mtizamo wa Imam Abu Sulayman Hamd Ibn

Muhammad Al Khattabi katika Maalim Sunnan Sharh Imam Abu Daud, Imam Abu

Zakarriyah Sharaf An Nawawi katika Al Majmua na Imam Ibn Hazim Al Andalus katika

Al Muhalla.

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Shaykh ul Islami Imam Abu Zakkariyah

Sharaf An Nawawi kua: ‘Kwa mtizamo wa Umar Abdul Aziz, Qatadah na Imam

Malik, basi ni kua hairuhusiki kwa Wasiokua Waislam, kuingia Msikitini’ (Sharh

Sahih Muslim)

Na huo pia ndio mtizamo wa Imam Abu Hasan Ali Ibn Muhammad Ibn Habib Al

Mawardi Al Shafii ambae yeye anasema kua kulingana na Mtizamo wa Imam Al Muzani

ambae ni mWanafunzi wa Imam Muhammad Idris Al Shafi basi ni kua: ‘Haikubaliki

kwa Wasiokua Waislam kuingia Msikitini na hii ni kwa sababu watu hawa hua kila

siku wamo katika hali ya kutokua tohara’ (Al-Hawi Al-Kabir)

Na kwa upande wa Imam Mansur Ibn Yunus Al Buhuti Al Hanbali basi yeye anasema

pia kua : ‘Haruhusiki kwa wasiokua Waislam kuingia Miskitini hata kama

wakipewa ruhusa na Waislam na hii ni kwa sababu amesema Allah Subhanah wa

Ta’ala kua:


421

‏﴿إِنم ََّا يَعْمُرُ‏ مَسَاجِ‏ دَ‏ ٱهلل َِّ‏ مَنْ‏ آمَنَ‏ بِٱهلل َِّ‏ وَٱلْيَوْمِ‏ ٱلآخِ‏ رِ‏ وَأَقَامَ‏ ٱلص َّلاَةَ‏ وَآتَى ٰ ٱلز َّكَواةَ‏

وَلمَْ‏ يخَْشَ‏ إِلا َّ ٱهلل ََّ‏ فَعَسَ‏ ى ٰ أُوْ‏ لَٰئِكَ‏ أَن يَكُ‏ ونُواْ‏ مِ‏ نَ‏ ٱلْمُ‏ هْ‏ تَدِينَ‏ ﴾

Innama yaAAmuru masajida Allahi man amana biAllahi waalyawmi al-akhiri

waaqama alssalata waata alzzakata walam yakhsha illa Allaha faAAasa ola-ika an

yakoonoo mina almuhtadeena (Surah At Taubah 9:18)

Tafsir: Kwa hakika wenye kuisimamia Misikiti ni wale ambao ni wenye Kumuamini

Allah na siku ya Malipo, Wanaosali na kutoa Zakkah, na wasiomuogopa yeyote

isipokua Allah, kwani hawa hukaribia kua ni miongoni mwa Walioongoka.

Kwa upande mmoja basi tunaona kua ayah hii inazianisha sifa za wale watu ambao

wanatakiwa kusimamia Miskiti na kua ni wenye amri Miskitini, kua wenye kutakiwa kua

ni wenye Kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala na Siku ya Malipo yaani wasiwe

Wanafiq, na kisha ikaendelea kuwataja wale ambao Wanaosali na Kuota Zakkah na

Wasiomuogopa yeyote ispokua Allah Subhanah wa Ta’ala. Kwani hao ndio wenye

kuukaribia Uongofu.

Ambapo tunapojiangalia sisi leo basi tunaona kua tuko katika Mtihani mkubwa sana

kuhusiana na kua na sifa stahiki za usimamizi wa Misikiti, kwani wengi sana

wanaosimamia Miskiti katika jamii zetu wanojita Wenyeviti, Makatibu na Maimamu pia

hawana Sifa hizi stahiki, na hivyo hua ni wenye kuifanya Miskiti kama ya Baba zao, ni

wenye kufanyana uchawi, kuoneana vijicho na kuhasidiana, kutambiana na kuoneshana

kwa ajili ya kupigania Maslahi yao ya Kidunia wanayojitafutia wanapokua viongozi wa

Miskitini.

Tunaporudi katika mada yetu basi hua unaona kua hii ni aya ambayo imetumia neno A’sa

ambalo humaanisha Kukaribia Kitu, Kua na Uwezekano wa kukifikia kitu, Labda,

Inawezekana, Inategemewa na pia humaanisha kuelezea hali ya Mtu ambae ni mwenye

Ari, Juhudi, Mategemeo, Khofu au Matamanio juu ya kitu fulani. Ambapo Imam

Muhammad Ibn Is-haq anasema kua; ‘A’sa inapotoka kwa Allah Subhanah wa T a’ala

basi hua ni Ahadi iliyothibitishwa.’

Na hivyo mtizamo wa kua hairuhusiki kwa Wasiokua Waislam pia ndio Mtizamo

unaokubalika zaid wa Madhhab ya Imam Ahmad Ibn Hanbal kama anavyosema Imam

Muhammad Ibn Abd Al Qawi Al Mardawi Al Hanbali katika kitabu cha Al Kashaf al-

Qina’a.


422

Ambapo kuhusiana na kutoruhusika kwao katika Masjid Al Haram basi Wanazuoni

wanasimamia katika ile aya isemayo:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُو ۤ اْ‏ إِنم ََّا ٱلْمُشْرِكُونَ‏ نجََسٌ‏ فَلاَ‏ يَقْرَبُواْ‏ ٱلْمَسْجِ‏ دَ‏ ٱلحَْرَامَ‏ بَعْدَ‏ عَ‏ امِهِمْ‏

هَٰذَا وَإِنْ‏ خِ‏ فْتُمْ‏ عَيْلَةً‏ فَسَوْفَ‏ يُغْنِيكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ مِن فَضْلِهِ‏ إِن شَآءَ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ عَلِيمٌ‏ حَ‏ كِيمٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo innama almushrikoona najasun fala yaqraboo

almasjida alharama baAAda AAamihim hadha wa-in khiftum AAaylatan fasawfa

yughneekumu Allahu min fadhlihi in shaa inna Allaha AAaleemun hakeemun

(Surah al-Taubah 9:28)

Tafsir: Enyi Mlioamini kwa hakika Washirikina ni wenye Najis hivyo msiwakaribishe

kwenye Masjid Al Haram baada ya mwaka huu. Na kama mnakhofu juu ya Umasikini

basi Allah atakutajirisheni kutokana na fadhila zake akitaka. Kwa hakika Allah ni

mwenye kujua juu ya kla kitu na ni mwingi wa Hikma.

Ambapo aya imetumia neno Najasa ambalo hua linamaanisha Uchafu, Kutokua na usafi,

Kutokua Tohara, Kitu kinachohitajika kusafishwa.

Na anasema Imam Raghib Al Isfahani kua: ‘Ndani yake hua mnajumuishika Uchafu

unaohisika kwa viungo vya hisia kama Macho, Mdomo, Pua Masikio au Mikono.

Na pia ndani yake hua mnajumuishika Uchafu ambao hua unfahamika kwa njia ya

Akili na Ufaham. Hivyo uchafu hua huo wa aina 3 ambazo ni:

Kwanza kuna Najis ya Kweli ambayo kila mtu anaihesabu kua hio kweli ni Najis.

Halafu kuna aina ya pili ya Najis ambayo ni ya Kisharia ambayo inasababisha

ulazima wa kutia Udhu au Kukoga baada ya kuingia kweye hali ya mazingira yake,

kwa mfano: kua na Janaba, Hedhi, Nifasi, Kutokwa na kitu katika tupu mbili n.k.

Na kisha kuna aina tatu ya Najis ambayo ni ya Uchafu wa Kimoyo ambao ndani

yake hua kuna Imani ya Kishirikina au Tabia mbaya. Hivyo hizi zote hua ni Najis’

Na kutokana na maana hii basi tunaona kua pale Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

aliposema kumwambia Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu kua Muumini hkamwe hawezi

kua Mchafu basi alikua akimaanisha kuhusiana na Uchafu wa Kiimani ndani ya Moyo

na Ufahamu. Kwani huo ndio Najis Kubwa zaidi. Ambapo kwa upande wa wasioamini

basi wao hua ni wenye Aina zote tatu za Najis


423

Hivyo kwa mtizamo wa Imam Qatadah Al Sadusi na Amir ul Muuminin Umar Ibn Abd

Al Aziz basi amesema kuhusiana na aya hii kua: ‘Ingawa ya hii imezungumzia

kuhusiana na Masjid Al Haram lakini aya inajumuisha eneo zima la ardhi takatifu

ya Mji wa Makkah.’

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Hanifa Nuuman Ibn Thabit basi yeye anasema kua:

‘Makafiri wanaruhusika kuingia katika Miskiti wanayoitaka na si lazima wawe na

sababu Maalum. Na wanaweza kuingia hata katika Masjid Al Haram kama

wakiruhusiwa na Waislam, yaani hii ya inawapa Waislam haki ya kuwazuia na

hapo hapo inawakatalia Makafiri kuingia.’

Ambapo hii hua ni sawa na Mtu kumwambia Mtu mwengine kua: ‘Sitaki kukuona

hapa mbele ya macho yangu’ na hivyo kua ni mwenye kuelezea kutopendezwa

kwake kuwepo kwa mtu huyo mbele yake katika sehemu aliyokuwepo lakini bila ya

kumharamishia mwenzake huyo kuingia katika sehemu hio.

Na kwa upande wa Mujaddid Ad Din Imam Muhammad Idrsis Al Shafii basi yeye

amesema kuhusiana na aya hii kua: ‘Aya hii imekataza Makafiri kutoingia kwenye

Masjid Al Haram, lakini haikuzungumzia juu ya Miskiti myengine yeyote. Na hivyo

hii inamaanisha kua inaruhusika kwa Wakristo na Mayahudi kuingia kwenye

Miskiti myengine lakini kwa sababu maalum’ ambao huu pia ndio Mtizamo wa

wafuasi wa Madhhab ya Imam Malik.

Na Hukmu hii hua ni kutokana na Uthibitisho wa Hadith ya kisa cha Thumamah Ibn

Uthal ambae alikua ni Chifu wa Banu Hanifa ambae alikua ni mmoja kati ya Machifu wa

Ardhi ya Yamamah. Na mnamo mwaka wa 9 Al Hijra Rasul Allah Sallahu Alayhi wa

Salam alituma Barua 8 kwa Viongozi tofauti wa eneo la Uarabuni na mipakani mwake,

ili kuwaelezea kuhusiana na Utume wake na pia kuhusiana na kuukubali Ujumbe huo wa

Allah Subhnah wa Ta’ala ambapo miongoni mwa waliopelekewa Barua hizo alikuwemo

pia Thumamah Ibn Uthal wa Yemen, nae akapingana na ujumbe wa Barua hio, na kisha

akasema kua atamuangamiza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Dini yake hio

mpya ya Uislam anayoitangazia.

Ambapo tunapozungumzia Mji wa Yamamah basi tunaona kua ni Mji ambao watu wake

walikua wakijisifa kutokana na mambo neema walizojaaliwa na Mola wao juu yao wani

walikua wakisema: Hakika sisi tumewapita Watu wa Duniani Mashariki na

Magharibi kwa Mambo Matano:

‘Tumewapita Kwanza kwa kua na Wanawake wazuri kuliko wote Ulimwenguni.

Tumewapita Pili kwa kua na Ngano Bora Zaidi Ulimwenguni.

Tumewapita Tatu kwa kua na Tende Tamu Sana.


424

Tumewapita Nne kwa kua na Wanyama wenye Nyama Tamu sana, na

Tumewapita Tano kwa kua na Maji Matamu na Mazuri sana yanayosafisha Koo

na Kifua.’

Hivyo kutokana na kua na hali ya mtizamo huo juu ya jamii yao basi Thumama Ibn Uthal

akaamua kupinga na kukataa matakwa ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na

hivyo ingawa hakuwaua Wajumbe hao ambao ni Masahaba wa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam waliompelekea ujumbe huo hapo hapo lakini alitafuta nafasi nyengine

ya kuwaua Waislam atakapokutana nao na alipopata nafasi mara ya pili ya kukutana na

Msafara wa Masahaba wa Rasul Allah Salallahu Alayhiwa Salam wakati alipokua

anaelekea katika maeneo ya Yamamah basi aliuvamia na kuwaua Masahaba wote. Hivyo

Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam alipopata habari hio basi akatangaza kulipiza

kisasi dhidi yake kua kokote atakapoonekana basi hukumu yake pia kua ni kifo.

Baada ya tukio hilo basi haukupita mda mrefu isipokua Thumamah akaamua kufanya

Umra ya kikafiri katika mji wa Makkah, akafunga safari kutoka Yamamah kwa bahati

mbaya au nzuri katika safari yake akapitia katika maeneo ya Mipaka ya Mji wa Madinah

na akakutana na Jeshi la Waislam lililokua likifanya doria kuilinda mipaka ya Madinah

bila ya kumjua na walipomhoji anafanya nini katika maeneo hayo basi akawa ana kibri

na hataki kujieleza, hivyo nao wakamkamata na kumpeleka katika Mji wa Madinah kwa

Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam.

Na walipofika basi wakamfunga kamba kwenye moja kati ya nguzo za ndani ya Msikiti

wa Nabii Salallahu Alayhi wa Salam huku wakimsubiri Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa

Salam aje kumhoji kisha atoe hukmu yake juu ya mtu huyo wasiemjua na asietaka

kujieleza. Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam alipoaingia Msikitini na kumuona

mtu huyo aliefungwa kwenye Nguzo ya Msikitini basi akawauliza Masahaba zake: ‘Hivi

jee mnamjua ni nani huyu mliemkamata na kumfunga hapa?’ Masahaba wakajibu:

‘La Ya Rasul Allah sisi hatumjui ni nani.’

Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akawaambia Masahaba zake kua: ‘Huyu si

mwengine bali ni Thumamah Ibn Uthal Al-Hanafi, na bila ya shaka mmefanya

jambo zuri sana kumkamata.’ Kisha Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akatoka

Msikitini humo na kuelekea Nyumbani kwake ambayo ni yenye kupakana na Msikiti

wake kiasi ya kua akikaa Chumbani kwake hua ni mwenye kuona Msikitini kwa kupitia

Dirishani mwa chumba chake.

Alipofika nyumbai kwake basi Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akawaambia

watu wake: ‘Tayarisheni chakula chochote mlichokua nacho, kisha mpelekeeni

Thumamah Ibn Uthal’ na kisha akaamrisha Ngamia wake akamuliwe Maziwa, na kisha

akaelekea kwa Thumama kwa ajili ya kuzungumza nae kwa kumtaka asilimu, lakini


425

Thumamah akakataa katu katu. Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akamwambia: ‘Unaiteteaje Nafsi yako?’

Thumamah Ibn Uthal akasema: ‘Kama unataka kuniua basi bila ya shaka utakua

umepata damu yenye thamani kubwa sana ya kuua, kutokana na ulichokamata.

Kama unataka kusamehe basi hakika mimi nitakua na shukrani kutokana na

usamehevu wako. Na kama unataka pesa nikulipe kua ni kama fidya kwako basi

taja kiasi ukitakacho nitakulipa kama utakavyo.’

Baada ya kupata majibu hayo basi Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akaondoka

na kumuacha Thumamah Ibn Uthal akiwa amefungwa hapo hapo kwenye nguzo ya

Msikitini kwa siku 2 mfululizo huku akiwa ni mwenye kupelekewa chakula na Maziwa

kama kawaida. Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuuliza tena kwa

kumwambia: ‘Unaiteteaje Nafsi yako?’

Thumamah Ibn Uthal akasema tena: ‘Kama unataka kuniua basi bila ya shaka utakua

umepata damu yenye thamani kubwa sana ya kuua, kutokana na ulichokamata.

Kama unataka kusamehe basi hakika mimi nitakua na shukrani kutokana na

usamehevu wako. Na kama unataka pesa nikulipe kua ni kama fidya kwako basi

taja kiasi ukitakacho nitakulipa kama utakavyo.’

Baada ya kutoa majibu hayo basi Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akawaambia

Masahaba zake: ‘Mfungueni na kisha muachieni aende zake.’ Hivyo Masahaba

wakamfungua na kumuachia huru Thumamah Ibn Uthal ambae nae akatoka nje ya

Msikiti kisha akapanda Ngamia wake na kuelekea nje ya maeneo ya ardhi ya Madinah .

Lakini alipofika katika maeneo yenye Mitende na Maji ya Baqii, ambayo baadae

ilibadilishwa kua ni sehemu ya kuzikia Masahaba wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, basi Thumamah akashuka kwenye Ngamia wake na kumnywesha maji na kisha

akajisafisha mwili wake kwa kukoga.

Kisha akampandia tena Ngamia wake na kurudi katika Mji wa Madinah mpaka ndani ya

Msikiti wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Masahaba wakashangaa kumuona

kua amerudi na kuulizana imekuaje. Lakini Thumamah Ibn Uthal akasimama mbele yao

na kusema: ‘Ashhadu An La Ilaha Illa Allah, wa ashhadu Ana Muhammad Rasul

Allah’

Na kisha Thumamah Ibn Uthal akatoka hadi kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na kusema: ‘Ewe Muhammad! Wa Allahi, ilikua hakuna Uso unaochukiza mbele ya

macho yangu kama uso wako. Lakini sasa hivi hakuna Uso wa mtu unaonivutia na

nnaoupenda kama uso wako. Hakika mimi nimewaua baadhi ya watu wako, hivyo

niko chini ya Rehma zako. Hivyo jee utanifanya nini?’


426

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Sasa hivi hakuna hatia dhidi yako,

kwani kuingia kwako katika Uislam kumefuta makosa yako yote uliyoyafanya hapo

kabla na hivyo kukupa nafasi ya kuanza upya maisha yako.’

Hivyo Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu akafurahi sana na kusema: ‘Wa Allahi!

Nitajiweka mimi mwenyewe Nafsi yangu, na Upanga wangu na yeyote yule

atakaekua chini yako na chini ya ufuasi wa Dini yako. Hivyo Ya Rasul Allah!

Hakika Wapanda Farasi wako waliponikamata basi nilikua nikielekea kufanya

Umra. Kwa hivyo unanishauri nifanye nini?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hamna tatizo nenda kafanye Umra

yako, lakini fanya kwa njia iliyoamrishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala’ na kisha

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamfahamisha Thumamah Radhi Allahu Anhu

namna ya kufanya Umra hio. Kisha baada ya hapo basi Thumamah Radhi Allahu Anhu

akatia nia yake na akafunga safari yake kuelekea katika kufanya Ibada ya Umra katika

njia ya Kiislam kama aliavyoamrishwa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Hivyo alipofika katika Bando la Mji wa Makkah akaanza kusoma Talbiyyah kwa sauti

kubwa sana hukua akisema: ‘Labbayk Allahumma labbayk. Labbayka la shareeka laka

labbayk. Innal hamda wa-n ni'mata laka wa-l mulk La shareeka lak.”

yaani ‘Naitikia, Allah wito wako, Naitikia kua hakuna mshirika dhidi yako. Naitikia

hakika wewe ni mwenye kustahiki shukrani zote na ni mmiliki wa Neema zote na

mmiliki wa Mamlaka juu ya kila kitu hakuna mshirika dhidi yako’

Kutokana na tukio hili basi Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu akawa ndie

Muislam wa Kwanza juu ya uso wa Ardhi kua ni mwenye kufanya Talbiyah huku

akiingia ndani ya mji wa Makkah. Ambapo ukubwa wa sauti ya Thumamah Ibn Uthal

Radhi Allahu Anhu uliwashtua Maquraysh wa Mji wa Makkah, na hivyo kujiuliza

kumetokea nini? Na walipomsikiliza maneno yake basi wakapandwa na hasira kubwa

sana na hivyo kujipanga na kutaka kumpiga anaesoma Talbiyah hio kabla ya kumjua

kutokana na chuki waliyokua nayo watu hao dhidi ya Uislam.

Hivyo ingawa watu wa Makkah walitoka na silaha zao kwa ajili ya kumshambulia mtu

huyo, lakini kutoka kwao huko hakukumshtua wala kumtia khofu Thumamah Ibn Uthal

Radhi Allahu Anhu kwani hali ilikua tofauti badala yake kwa sababu yeye alizidi kungiwa

na ari ufakhari na kuzidi kupaza sauti huku akiwa amejawa na hisia kubwa za mapenzi

juu ya Allah Subhanah wa Ta’ala, Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na dini yake

mpya aliyoiamini na kuingia siku kadha hapo kabla.

Hivyo miongoni mwa vijana wa Quraysh akanyayua Upinde wake akauweka baina ya

mikono yake na kuanza kutunga shabaha kwenye mwili wa Thumamah Ibn Uthal Radhi

Allahu Anhu, lakini hata hivyo miongoni mwa Wakubwa wanaomjua Thumamah Ibn


427

Uthal Radhi Allahu Anhu wakamzuia kijana huyo na kumwambia: ‘Laana iwe juu yako!

Ole wako uuwachie huo upinde wako kisha umpige kwenye mwili wake, hivi jee

unamjua ni nani huyo? Huyo ni Thumamah Ibn Uthal ambae ni Chifu wa

Yamammah, hivyo ukimdhuru tu basi watu wake watazuia misafara yetu yote ya

Kibiashara inayopita kwenye ardhi yao na matokeo yae tutapatwa na madhara

makubwa sana’

Ambapo Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu alipokaribia karibu basi Viongozi wa

Quraysh wakamfuta na kumuuliza: ‘Thumamah imekuaje, una wazimu au? Imekuaje

ukaachana na Dini ya Mababu zako ambayo ndio iliyokua Dini yako?’

Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Sikuachana na Dini ya Mababu

zangu, bali nimeamua kufuata Dini iliyokua bora zaidi ambayo ni Dini ya

Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam. Na Wallahi nnaapa kwa jina la Mungu wa

Jengo hili la Al Kaabah kua baada ya kurudi kwangu katika Ardhi yangu, basi

hakuna Ngano wala zao lolote litokanalo na ngano kua litakufikieni hadi pale

mtakapokua ni wenye kuifuata Dini ya Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam’

Na kisha baada ya hapo Thamamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu akafanya Umra ya

kwanza kufanywa kama ilivyoamrishwa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na

kisha baada ya kumaliza akachinja kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala.

Kisha akarudi katika mji wake na kuwausia watu wake juu ya Allah Subhanah wa Ta’ala

na kuwaamrisha kua wazuie mazao yanayotokana na ngano zao wasiwapelekee watu wa

Mji wa Makkah wa Quraysh. Tukio ambalo lilipelekea kupanda kwa hali ya maisha

katika Mji wa Makkah, na baadhi ya watu wakafariki kwa sababu ya njaa.

Hivyo watu wa Makkah wakamwandikia barua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam,

kumlalamikia kwa kumwambia kua: ‘Ewe Muhammad Tunasikitika kua umevunja

makubaliano yetu, kwani Makubaliano yaliyokuwepo baina yetu katika Mkataba

wa Hudaybiyah ni kua hatutakiwi kuvunjiana udugu baina yetu, lakini wewe

Muhammad umeenda kinyume na makubaliano hayo kwani umevunja Udugu

baina ya watu. Na pia umeua na kusababisha vifo kwa kutumia njia ya njaa. Kwani

Mtu wako Thumamah Ibn Uthal ametukatia njia ya usambazaji wa mahitaji ya

Ngano tunayoitegemea kwa ajili ya chakula chetu. Hivyo sisi tuna matumaini

kutoka kwako utamwambia Thumamah asitukatie njia za usambazaji wa Chakula

chetu.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliposomewa Ujumbe huo basi akamtuma mtu

aende Yamamah kwa Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu kumjuulisha kua inabidi

awaondolee vikwazo watu wa Mji wa Makkah, ambapo Thumamah Ibn Uthal Radhi


428

Allahu Anhu baada ya kupokea ujumbe huo basi akawaondoelea Watu wa Makkah

vikwazo hivyo.

Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu aliendelea kuishi pamoja na watu wake huku

wakiendelea kufuata Dini ya Kiislam na kumtumikia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam hadi kufariki kwake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambapo katika ardhi

ya Yamamah kukazuka Upinzani dhidi yake kutoka kwa Musallima ambae alitangazia

kua yeye ndie Mtume mpya baada ya kufariki Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na

hivyo baadhi ya watu wakaanza kumfuata na kumuamini Musallima Al Kadhdhab.

Kwani Musallima alikua akiwaambia Watu wake kua: ‘Hivi Nyinyi Mnajifikiriaje?

Yaani kitu kilichowafanya Watu wa Quraysh kua ni Bora zaidi yenu? Wakati wao

wako kidogo kuliko sisi, na Ardhi yetu ni Nzuri na Kubwa sana kuliko Ardhi yao.

Hivyo bila ya shaka Jibril ananishukia mie pia kama vile ambavyo alivyokua

akimshukia Muhammad’

Na kutokana na Kauli hio basi Musallima alikua hapingi kua Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam hakua Mtume La! Alikua anakubalia kua Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kua alikua ni Mtume, ila sasa na yeye pia anashirikiana nae katika Utume huo.

Hivyo Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu akawaambia watu wake wa Banu Hanifa

kwa kusema kua: ‘Enyi watu wa Banu Hanifa jihadharini na kosa hili la kufuata

upotovu mkubwa sana. Kwani hakuna Muongozo kama Muongozo wa Allah

Subhanah wa Ta’ala. Hivyo wa Allahi hakuna kitakachomnufaisha yeyote yule

atakaefuata Upotovu huo (wa Musallimah) isipokua maangamizo. Kwani enyi watu

wa Banu Hanifah fahamuni kua hakuna Mtume atakaefuatia baada ya Muhammad

Salallahu A’alayi wa Salam na hakuna Mtu yeyote anaeshirikiana nae katika Utume

wake huo, na hivi jee mnafaham kua amesema Allah Subhanah wa Ta’ala katika

Qur’an kua:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞حم ۤ ‏۞تَنزِيلُ‏ ٱلْكِتَابِ‏ مِنَ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱلْعَزِيزِ‏ ٱلْ‏ عَلِيمِ۞غَافِرِ‏

ٱلذ َّنبِ‏ وَقَابِلِ‏ ٱلت َّوْبِ‏ شَدِيدِ‏ ٱلْعِقَابِ‏ ذِى ٱلط َّوْلِ‏ لاَ‏ إِلَٰهَ‏ إِلا َّ هُوَ‏ إِلَيْهِ‏ ٱلْمَصِيرُ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Ha-meem; Tanzeelu alkitabi mina Allahi

alAAazeezi alAAaleemi; Ghafiri aldhdhanbi waqabili alttawbi shadeedi

alAAiqabi dhee alttawli la ilaha illa huwa ilayhi almaseeru (Surat Ghafir 40:1-3)

Tafsir: Kwa Jina La Allah Mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma. Ha Mim. Teremsho

la Kitabu (Qur’an) ni Kutoka kwa Allah Mwenye Utukufu wa juu ya kila kitu na ni


429

mwingi wa Kujua juu ya Kila kitu. Mwenye Kusamehe Dhambi na ni mwenye Kukubali

Toba na ni Mkali wa Adhabu, na Mwingi wa Fadhila Hakuna Mungu isipokua yeye

na kwake yeye ndio marejeo yetu.

Hivyo rudini kwa Mola wenu, kwani jee mnawezaje nyinyi kufananisha maneno

haya matukufu ya Allah Subhanah wa Ta’ala na maneno ya Musayllima?’

Na kisha baada ya maneno hayo basi Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu

akawakusanya wote wale wanaokubaliana na msimamo wake wa kubakia kwenye

Uislam miongoni mwa watu wa Banu Hanifa na kuanza kujipanga kwa ajli ya kupigana

vita vya Jihadi dhidi ya Wanaopingana na Uislam wanaoongozwa na Musallimah Al

Kadhdhab aliejitangazia kua ni Mtume mpya ambae ndie mrithi wa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam.

Kwani hivyo ndivyo alivyojaribu Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu kuwatoa

kwenye Upotovu lakini wengi wao hawakumsikiliza. Hivyo akabakia nao kidogo wale

waliokua wakimsikiza kisha akamchagua Mmjoa na kumtuma kwa Amir Ul Muuminina

Abu Bakr Radhi Allahu Anhu kwa ajili ya Kuomba Msaada dhidi ya Wafuasi wa

Musallima.

Ambapo hiki kilikua ni kipindi cha Mwaka wa 11 Al Hijra. Hivyo baada ya Amir

Muuminin Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu kupata ujumbe huo basi nae

akaandika Barua 4.

Ambapo Moja ilirudi Yamamah kwa Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu ya

kumwambia kua astahamili kwanzi asifanye kitu hadi utakapomfikia msaada ambao uko

njiani unakuja.

Kisha ya pili akaituma kwa Shurahbil Ibn Hasan Radhi Allahu Anhu na kumwambia kua

anatakiwa apeleke Jeshi katika Ardhi ya Yamamah na akifika akutane Thumamah Radhi

Allahu Anhu na wasifanye chochote hadi afike Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu na

Jeshi lake.

Barua ya Pili ikatumwa kwa Ikrimah Ibn Abu Jahl Radhi Allahu Anhu ambae nae

akaambiwa apeleke Jeshi Yamamah na akifika akutane na Thumamah Radhi Allahu Anhu

na kisha asifanye Lolote Mpaka afike Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu.

Na Kisha barua ya nne ikatumwa kwa Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu na

Kuambiwa kua akishamalizana na Mitume wengine walioibuka maeneo ya Uarabuni basi

Aharakishe haraka sana kuelekea kwenye Mji wa Yamamah kwani Kuna Mtume

anaeitwa Musallimah kaibuka anatakiwa ashughulikiwe.


430

Na Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu akifika huko badi atakutana na Thumamah,

Shurahbil na Ikrima Radhi Allahu Anhum ambao wote wanamsubiri yeye tu na watakua

chini ya Uongozi wake

Kwani Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu aliwasili katika Mji wa Yamamah mnamo

mwezi 10 Shawwal Na mnamo Mwezi 11 Shawwal akawaongoza Waislam katika Vita

dhidi ya Musalima Al Kadhdhab.

Haya yalikua ni Mapigano Makali sana katika Historia ya Uislam. Na hapa ndio tunaona

Hikma na Busara na Imani za Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu kwani kama

angepigana peke yake basi asingechukua Mda isipokua angekua ni mwenye Kuangamia

yeye na Jeshi lake.

Lakini badala yake akaomba Msaada kwa Amir ul Muuminin Abu Baqr Radhi Allahu

Anhu ambae nae alitumia Busara, Hikma na Silaha Bora na Nzito kuliko zote alizokua

nazo ambayo ni Upanga wa Allah Subhanah wa Ta'ala yaani Khalid Ibn Walid Radhi

Allahu Anhu.

Kwani Amir Ul Muuminina Abu Baqr Radhi Allahu Anhu alimuuliza Amr Ibn Al Aas

Radhi Allahu Anhu kwa kusema: ‘Ewe Amr Ibn Al Aas hakika wewe Una Busara zaid

na kutoa Hukmu miongoni mwa Waarabu, hivi Jee Unasemaje kuhusiana na

Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu?’

Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Khalid Ibn Walid ni Mfalme wa Vita,

Rafiki wa Kifo, Mwenye Mvamio wa Simba na Subra ya Paka.’

Na Bila ya Shaka Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu hakukosea!

Kwani kwa upande mwengine basi Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu alipofika katika

Mji wa Yamamah basi akakumbuka maneno ya Kiongozi wake Amir Ul Muuminina Abu

Baqr Radhi Allahu Anhu kua: ‘Ewe Khalid, kumbuka kua Hutokutana na Watu

Matata kama watu wa Al Yamamah, kwani watapigana na wewe Kwa kila hali

Hivyo basi Usisahau kua katika kushambulia kwao wakikushambulieni kwa Mkuki

basi nanyi Jibuni kwa Mikuki

Wakikushambulieni kwa Upinde basi Nanyi Jibuni kwa Mipinde

Wakianza kutumia Mapanga! Basi fahamu kua Mmeingia katika hali ambayo ni ya

Mapigano yanayompelekea Mama kukimbia na Kumsahau Mtoto wake.’


431

Kwani hapa jambo ambalo inabidi tuliweke wazi, kwani wengi wanafaham sivyo

kuhusiana na Vita vya Jihadi, kua inaruhusika kuua waliokuwemo na wasiokuwemo

kama wanavyofanya wale wanaojiripua kwa kujitolea Muhanga. Ukweli ni kua kufanya

hivyo hua si sehemu ya Jihad fi Sabili Allah na ni kinyume cha Mamrisho ya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na pia makubaliano ya Wanazuoni, kwani Jihdi hua na

masharti yake ikiwemo kutoruhusiki kupiganwa pae inapokua hakuna kiongozi

Muadilifu katika Ardhi ya Waislam husika.

Na ndio maana Amir Ul Muuminina Abu Bakr Radhi Allahu Anhu akamwambia Khalid

Ibn Walid Radhi Allahu Anhu ambae ni Mpiganaji Mahiri kwa Silaha za aina zote, juu

ya vipando vyote, na pia hajawahi kushindwa, Hata kwa kutumia Silaha za Kimaumbile

ya Mwili wake.

Hivyo Amir Ul Muuminina Abu Bakr Radhi Allahu Anhu alimwambia Khalid Ibn Walid

Radhi Allahu Anhu kua: Mkuki kwa mkuki, upinde kwa upinde, upanga kwa upanga na

hivyo hii inamaanisha kua Kiislam hairuhusiki kumpiga mtu ambae hajashika Silaha.

Hio ni kwa Upande Mmoja, lakini kwa upande wa pili pia tunaona katika Wasia wa Amir

Ul Muuminina Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu kwa Khalid Ibn Walid Radhi

Allahu Anhu kwa kumwambia kua:

‘Ewe Khalid, Kama Mkiwakamata Askari wa Maaduie zenu basi kuweni na Rehma

na Huruma Juu yao.

Waoneeni Huruma Majeruhi wao.

Msiwaue Mateka wao.

Msiwatushie Kuwachoma Moto.

Na kuweni Makini katika kutekeleza Maamrisho yangu haya.

Salaam Alaykum wa Rahmat Allahi wa Barakatuh’

Naam...hayo ndio yaliyokua Maamrisho na ndio Sharia na Hukmu za Kiislam kuhusiana

na Vita Vya Jihadi na pia kuhusiana na Mateka wa Vita.

MAUMBILE YA ISA IBN MARYAM NI MITHLI YA NABII ADAM.

Tunaporudi katika ujumbe wa Najran uliomtembelea Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam baada ya kua ni Mmoja kati ya Jamii za watu ambao nao walitumiwa moja kati ya

miongoni mwa Barua 8 kama aliyopelekewa Thumamah Ibn Uthal Radhi Allahu Anhu

basi tunaona kua ujumbe huo ulikua ni wa watu 60 ambao ni wenye kuheshimika sana

katika Mji wa Najran ambao walichaguliwa maalum kwa ajili ya kujadiliana na Rasul


432

Allah Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo walikua wakiongozwa na Viongozi watatu wa

Dini ya Kikristo ambao ni:

1. Abu Harith Ibin 'Alqamah ambae ni Padri Mkuu wa Najran na Muwakilishi

Mkuu wa Kanisa Katoliki wa Urabuni ambae ndie aliepokea Ujumbe wa Mualiko

wa kuingia katika Uislam miongoni mwa mialiko minane aliyotuma Rasul llah

Salallahu Alayhi wa Salam kwa viongozi wa Uarabuni na maeneo mengine ya

Mipakani mwake.

2. Abdul Masih, Muwakilishi Mkuu wa Watu wa Najran ambae alikua akisifika

kwa kua na Hikma na Busara na uzoefu wa Kidiplomasia.

3. Ayham, ambae ni Chifu wa Mji wa Najran.

Hivyo ujumbe huo wa watu 60 ulipowasili Mjini Madinah ulikua umevalia Majoho ya

Hariri, Pete na Mikufu ya Misalaba ya Dhahabu shingoni mwao, wakaingia Msikitini na

kumsalimia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambapo ingawa Rasul Allah

Salallahu layhi wa Salam alipowaona hakuvutiwa na mavazi yao, jambo ambalo Watu

hao wa Najran walilihisi na wakajiuliza imekuaje ikawa hivyo.

Hivyo Ujumbe huo wawatu hao ukaamua kutafuta utatuzi wa hali hio na wakaulizia na

kushauriwa kua wazungumze na Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu ambae

nae aliwashauri kua hawatakiwi Kuingia Msikitini umo kukutakana na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam wakati wakiwa katika hali hio ya mavazi waliyokua nayo

kwani Uislam haupendekezi na umeharamisha kuvaliwa kwa Mavazi hayo, hivyo

wakibadilisha mavazi hayo na kuvaa mavazi ya kawaida basi Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam atawapa heshima yao.

Baada ya ushauri huo basi Ujumbe wa watu hao ukabadilisha Mavazi yao na mapambo

yao, na kuvaa mavazi ya kawaida, kisha wakaingia katika Masjid An Nabawi na

kumsalimia tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Ambapo nae akasalimiana nao

kisha wakampa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam zawadi walizokuja nazo kwa ajili

yake akazipokea. Ambapo anasema Imam Bayhaqi kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alisema kua: ‘Wa Allahi mwanzoni hapo kabla walipokuja walikua

wamefuatana na Shaytan.’’

Hivyo baada ya kusalimiana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi kabla ya

kuanza majadiliano yao basi Wajumbe ho wakasema kua umewadia Mda wa kusali,

hivyo wakaomba wasali na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawaruhusu wasali

ndani ya Msikiti wake huo. Nao wakasali huku wakielekea katika upande wa Mashariki

linakochomozea Jua.

Kisha baada ya kumaliza Ibada yao basi wakasogea karibu ya Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam na wakakaa nae na kuanza kujadiliana kuhusiana na alilowausia kwenye


433

Ujumbe wa barua yake kwa kuwaambia : ‘Nakukaribisheni katika Imani ya Dini ya

Kumpwekesha Mungu Mmoja bila ya kumshirikisha Mungu huyo wa Ulimwengu

na kila kilichomo ndani yake ambae ni Allah Subhanah wa Ta’ala ’ na waliposikia

ujumbe huo basi watu hao wa Najran wakataka kujua kuhusiana nae huyo Mungu aitwae

Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawasomea

Surat Al Ihlas kwa kusema:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞قُلْ‏ هُوَ‏ ٱهلل َُّ‏ أَحَ‏ دٌ‏ ‏۞ٱهلل َُّ‏ ٱلص َّمَدُ۞لمَْ‏ يَلِدْ‏ وَلمَْ‏ يُولَدْ۞وَلمَْ‏

يَكُ‏ نْ‏ ل َّهُ‏ كُ‏ فُواً‏ أَحَ‏ دٌ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Qul huwa Allahu ahadun; Allahu alssamadu;

Lam yalid walam yooladu; Walam yakun lahu kufuwan ahadun (Surat Al Ikhlas

112:1-5)

Tafsir: Kwa Jina la Allah mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma; Sema (Ewe

Muhammad Salallahu Allahu Alayhi wa Salam) kua: ‘Yeye ni Allah ni Mmoja tu,

Allah ni Mwenye Kujitosheleza, Hakuzaa wala hakuzaliwa, na Hakuna hata mmoja

anaefanana nae.’

Ujumbe wa Watu hao ukasema: ‘Kama Uislam unamanisha Imani juu ya Mungu

mmoja tu wa Ulimwengu basi sisi tayari tushamuamini zamani na tunatii

maamrisho yake’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawaambia: ‘Uislam unabeba baadhi ya

matendo mema yenu ndani yake lakini baadhi ya matendo yenu yanaonesha kua

nyinyi hamuuamini Uislam. Kwani inakuaje mnasema kua mnamuamini Allah

Subhanah wa Ta’ala na kumuabudu wakati mnaiabudu Misalaba na hamjizuii

kutokana na kula Nguruwe? Na mnaamini kua Allah Subhanah wa Ta’ala ana

Mtoto?’

Ujumbe wa Watu hao ukasema: ‘Sisi tunaamini yeye (Isa Ibn Maryam) kua ni Mungu

kwa sababu alikua akifufua waliokufa, aliponesha wanaoumwa, aliwafanya Ndege

aliowatengeneza kwa udongo kua ni walio hai na kuruka na hivyo haya yote

yanaonesha kua yeye ni Mungu.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawaambia: ‘La yeye Mja wa Allah Subhanah

wa Ta’ala na hivyi yeye ni kiumbe. Allah Subhanah wa Ta’ala alimuweka yeye ndani


434

ya Tumbo la Maryam Bint Imran, na hivyo Nguvu zake zote na uwezo amepewa na

Mola wake’

Ujumbe wa Watu hao ukasema: ‘Ndio! Yeye ni Mtoto wa Mungu kwa sababu

Maryam Bint Imran alimzaa bila ya kuolewa wala kuingiliwa na mtu yeyote. Na

kwa Mtoto hua ni lazima awe na Baba, kwa hivyo huyu lazima Baba yake atakua

ni Mungu. Hivyo kubaliana nasi na kisha sisi tutakufuata katika Dini yako, Au

wewe unafikiria kua ni nani atakua Baba yake Isa ewe Muhammad?’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akashusha aya zifuatazo:

‏﴿إِن َّ مَثَلَ‏ عِيسَى ٰ عِندَ‏ ٱهلل َِّ‏ كَمَثَلِ‏ آدَمَ‏ خَلَقَهُ‏ مِنْ‏ تُرَابٍ‏ ثمِ َّ قَالَ‏ لَهُ‏ كُن فَيَ‏ كُونُ‏

‏۞ٱلحَْق ُّ مِنْ‏ ر َّبِّكَ‏ فَلاَ‏ تَكُنْ‏ مِّنَ‏ ٱلْمُمْترَِينَ‏ ﴾

Inna mathala AAeesa AAinda Allahi kamathali adama khalaqahu min turabin

thumma qala lahu kun fayakoonu; Alhaqqu min rabbika fala takun mina

almumtareena; (Surat Al Imran 3:59-60)

Tafsir: Hakika Mithili ya Isa mbele ya Allah ni kama mithili ya Adam, ameumbwa

kutokana na Udongo kisha akaambiwa kua na akawa. Ni Ukweli kutoka kwa Mola

wako, hivyo usiwe miongoni mwa wenye kua na shaka.

Ambapo aya ni zenye kubainishia uhalisia wa Maumbile ya Nabii Isa, kua kutokana na

Miujiza ya maumbile yake basi pia hastahiki kuitwa Mungu wala Mtoto wa Mungu, na

hii ni kwa sababu maumbile ya Nabii Isa ni kama ya Nabii Adam, tena bado Maumbile

ya Nabii Adam yana Miujiza zaidi kwani yeye hana Baba wala Mama ambapo kwa

upande wa Nabii Isa basi angalau yeye anae Mama, kwa hivyo kama Nabii Isa atakua ni

Mungu hivyo jee Nabii Adam atakua ni nani? Na vile vile wakijiuliza suali hilo basi

itabidi pia wajiulize kuhusiana na Hawa ambae nae ametokana na Adam. Jee Mama yake

nae yuko wapi?

Hivyo hapa tunapoyaangalia Maumbile ya Viumbe watatu hawa basi hua tunaona kua

Allah Subhanah wa Ta’ala anaweka wazi kuhusiana na uwezo wake wa kua pale

anapokitaka kitu kua basi hua kwa kukiambia Kun fayakunu – Kua na Kitu kinakua. Na

hivyo ndivyo ilivyokua kwa Maumbile ya Nabii Adam kua bila ya kuwepo kabla yake

Mwanamme wala Mwanammke au Mama wala Baba, kwa Maumbile ya Hawa kutokana

na Nabii Adam ambalo na tukio la Mwanamke kutokana na Mwanamme lakini hapo hapo


435

kua bila ya kuwepo kwa Baba wala Mama na kisha kua kwa Maumbile ya Nabi Isa kua

kutokana na Mwanamke peke yake bila ya kushirikishwa Mwanamamme.

Ambapo anasema Hujjt u Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali kua; ‘Kuzaliwa kwa Mtoto yeyote yule hua kunaokana na

sababu mbili, ambapo sababu ya kwanza hua ni iliyowazi ambayo ni kutokana na

Manii ya Baba na Yai la Mama na Mfuko wa Uzazi wa Mama, ambapo sababu ya

pili hua ni ya Ghayb isiyoonekana na hivyo kua ni iliyofichika, na hii hua ni Kauli

ya Allah Subhanah wa Ta’ala ya kukiambia kitu Kun-Fayakunu kua na hivyo hua

kinakua. Hivyo basi kwa kua hapa kwa Nabii Musa hakukuwepo kwa asili ya

sababu ya kwanza ya Manii ya Baba basi bila ya shaka kuzaliwa kwake Nabii Isa

Ibn Maryam kunatokana na sababu ya pili ambayo ni Kun fayakunu.’

Kisha zinawabainishia wazi Watu hao wa Najran kwa kuwaambia kua Wasitilie shaka

kuhusiana na ukweli wa Maneno waambiwayo juu yake Nabii Isa na pia juu ya ukweli

wa kuhusiana na Maumbile yake Nabii Isa, ambapo hata hivyo Watu hao wa Najran

hawakukubaliana na ukweli huo, hata baada ya kubainishiwa ukweli huo na Rasul Allah

Salallahu A’layhi wa Salam baada ya kuupokea.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akashusha aya hii ya 61 ambayo inajulikana kama aya

ya Mubahala au aya ya Al Mula’anah. Neno Mubahila linatokana na neno Bahala ambalo

kwa lugha ya Kiarabu hua linamanisha Kulaani, Kuapiza, na pia hua linamaanisha

Kuomba Dua kwa Allah Subhanah wa Ta’ala kwa hali ya Unyenyekevu. Ambapo neno

Mubahala hua linamaanisha Mashindano ya Kuapizana, au Kulaanina au Kuombeana

Dua Mbaya, hivyo aya hio ni yenye kusema:

‏﴿فَمَنْ‏ حَآج َّكَ‏ فِيهِ‏ مِنْ‏ بَعْدِ‏ مَا جَآءَكَ‏ مِنَ‏ ٱلْعِلْمِ‏ فَقُلْ‏ تَعَالَوْاْ‏ نَدْعُ‏ أَبْنَاءََ‏

وَأَبْنَآءَكُمْ‏ وَنِسَآءََ‏ وَنِسَآءَكُمْ‏ وَأَنْفُسَنَا وأَنْفُسَكُمْ‏ ثمُ َّ نَبْتَهِلْ‏ فَنَجْعَلْ‏ ل َّعْنَةَ‏ ٱهلل َِّ‏ عَلَى

ٱلْكَاذِبِينَ‏ ﴾

Faman hajjaka feehi min baAAdi ma jaaka mina alAAilmi faqul taAAalaw nadAAu

abnaana waabnaakum wanisaana wanisaakum waanfusana waanfusakum thumma

nabtahil fanajAAal laAAnata Allahi AAala alkadhibeena (Surat Al Imran 3:61)

Tafsir: Hivyo yeyote yule atakaekua na hoja kwako juu ya Isa baada ya kukufikia Ilm

hii, basi waambie: ‘Wacha tuwaite Watoto wetu na Watoto wenu, Wanawake wetu na


436

Wanawake wenu, Sisi wenyewe na Nyinyi wenyewe kisha tusali na tuombe laana ya

Allah juu ya wale wanaokadhibisha’

Ambapo ndani yake aya hii basi tunaona Allah Subhanah wa Ta’ala kutokana na kujua

Maumbile ya viumbe wake Ibn Adam kua ni wenye kupenda Watoto wao, Wake zao na

familia zao kwa ujumla na hivyo hua yuko tayari kujihatarisha maisha yake kwa ajili ya

kuwaokoa watu wa familia yake kutokana na kuwapenda kwake, na hivyo kimaumbile

hua haiwezekani na ni vigumu kwa mtu kua ni mwenye kutaka kuhatarisha Maisha yake

na maisha ya familia yake kwa ujumla.

Na katika ya hii basi Allah Subhnah wa Ta’ala ametaja kwa mpangilio wa darja za watu

katika familia kwa namna wanavyopendwa kimaumbile, ambapo kama tulivyoona kua

kwanza Mtu hua ni mwenye kuwapenda Watoto wake, kisha Wake zake kisha ndio yeye

Mwenyewe na ndio utaona Mtu akiwa hana kitu kisha akajaaliwa kupata chakula basi

kwanza humpa Mtoto wake, kisha Mkewe kisha ndio atakula yeye kama kikibakia au

baada ya watoto basi atagawana na Mkewe, kwani asiefanya hivyo hua na kasoro ya

Kimaumbile ya kua na Ubinafsi ya kujijali na kujipendelea yeye kwanza katika kila kitu.

Hivyo ingawa waliokua wakihojiana hapa walikua ni Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam na Watu hawa wa Najran tu lakini Allah Subhanah wa Ta’ala anamwambia

Mtume wake kua yeyote yule ataekabisha juu ya maumbile ya Nabii Isa baada ya

kuwekewa wazi kila kitu kama zilivyosema aya, basi na wawajumuishe Watoto wa pande

zote zinazobishana, Wanawake wa pande zote zinazobishana, pamoja na wote

wanaobishana juu ya jambo hili kwa ni moja kisha wasali na kuomba laana ya Allah

Subhanah wa Ta’ala iwashukie wale wote wanaosema uongo pamoja na familia zao, na

hivyo kile kitakachotokea baada ya maombi hayo ya kulaaniana baina yao basi kiwe ni

Fundisho na Uthibitisho juu ya ni nani ambae yuko sahih katika madai yake juu ya Nabii

Isa Ibn Maryam.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akafikisha ujumbe wa Aya hii na

kukubaliana na watu hao wa Najran kua kesho yake In-sha Allah waje kwenye Mubahala

katika hali hio waliyokubaliana kama ilivyoelekeza Aya hii ya Mubahala. Na ilipofika

siku ya pili yake asubuhi basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akatoka huku akiwa

amefuatana na Hasan na Husayn ambao amewakamata mikono huku Fatma Bint Rasul

Salallahu Alayh wa Salam akiwa pamoja Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu wakiwa

wanafuata nyuma yake huku akielekea kwenye makabiliano ya Mubahala.

Na Abu Harth Ibn Alqamah alipoona hali hio basi akawaambia watu wake hao wa Najran

kua: ‘Wallahi hakika mimi nnaona kwenye Nyuso kama wangekua ni wenye

kumuomba Allah auondoe Mlima kutoka katika sehemu moja kuupeleka sehemu

nyengine basi Allah angewaondolea Mlima huo na kuupeleka katika sehemu hio

waitakayo. Hivyo msitoke kwenda kukabiliana nae katika Mubahala. ’ na hivyo watu


437

hao wa Najran wakakubaliana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua bora

watalipa Jizya yaani kodi kwa Waislam badala yake.

Ambapo anasema Imam Muhammad Ibn Jarir At Tabari kua: ‘Amesema Amr Ash

Shaabi kua: ‘Baada ya Wakristo hao kukubaliana makabiliano ya Mubahala basi

basi baadae waliomba Ushauri kutoa kwa miongoni mwa mmoja kati ya watu

wenye hikma miongoni mwao ambae aliwaambia kua kamwe wasikubali kuenda

kwenye Makabaliano hayo ya Mubahala.’’

Na kwa upande wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Sad Ibn Mani Al Basr basi

yeye anasema kua: ‘Wakristo hao walisema kumwambia Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam katika siku hio ya Mubahala kua: ‘Hakika sisi tunaona kua haina

haja na si sahih kukabiliana nawe kwenye Mubahala, hivyo unaweza kutuamrisha

unalotaka nasi tutakubaliana nawe ili kupatikane Usalama na Amani baina yetu’’

Ambapo amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Kama Abu Jahl

angemrushia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam Utumbo ya Ngamia basi

angezuliwa na Malaika mbele ya macho ya watu wote, na kama Mayahudi

wangetaka wafe baada ya kusema kua:

‏﴿وَقَالُواْ‏ لَن تمََس َّنَا ٱلن َّارُ‏ إِلا َّ أَ َّماً‏ م َّعْدُودَةً‏ ﴾

Lan tamassana alnnaru illa ayyaman maAAdoodatan (Surat Al Baqara 2:80)

Tafsir: Sisi hatutoguswa na Moto isipokua kwa siku kidogo tu’

Basi nao wangekufa na wangeiona sehemu yao kwenye Moto. Na kama Wakristo

wa Najran wangekabiliana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwenye

Mubahala huo, basi wangerudi Majumbani kwao na kisha wangekuta familia zao

na Mali zao zote kua zimeangamia badala yake.’

Hivyo baada ya watu hao wa Najran kukubali juu ya kulipa Jizya basi wakamuomba

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kua awape mtu mmoja anaeaminika miongoni

mwa Masahaba zake aende pamoja nao ili akawasaidie kupatanisha ugomvi uliopo baina

yao katika Mji wa Najran. Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akakubaliana

na maombi hayo. Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaandikiana nao

Mkataba wa makubaliano baina yao ambao uliandikwa na Abd Allah Ibn Abu Bakr Radhi

Allahu Anhu na kushuhudiwa na Abu Sufyan Ibn Harb Radhi Allahu Anhu, Ghilan Ibn

Amr Radhi Allahu Anhu, Malik Ibn Awf Radhi Allahu Anhu, Aqra Ibn Habis Radhi

Allahu Anhu na Mughira Ibn Shuba Radhi Allahu Anhu ambapo maelezo yaliyomo ndani

yake makubaliano hayo ilikua ni kama ifuatavyo:


438

Biismi Allahi Al Rahmani Al Rahim.

Haya ndio makubaliano ambayo Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam

amekubaliana na Watu wa Najran, kua ana Mamlaka juu ya Matunda yao, Mazao

yao, Dhahabu zao, Fedha na Watumwa wao. Na hivyo amewachia wao vyote hivyo

kwa malipo ya Hulla 2000 kwa mwaka, ambapo Hulla 1000 watalipa katika mwezi wa

Rajab na Hulla 1000 watalipa katika mwezi wa Safar ambapo kila Hulla 1 ni sawa na

Waqia moja yaani Dirham 4.

Mbali ya hivyo, lakini watu wa Najran watatakiwa kulipa gharama za Makazi na

Matamizi ya Wajumbe wangu kwa si zaidi ya siku 20 na Wajumbe wangu hao

hawatowekwa katika Mji wa Najran kwa zaidi ya Mwezi mmoja. Na pia watu wa

Najran watatakiwa kutoa Mkopo wa Ngao 30, Farasi 30 na Ngamia 30, kama

itahitajika pale utakapotokea Uasi nchini Yeman. Na hivyo kama ikitokea kupotea kwa

kitu chochote katika hivyo vitakavyo kopeshwa kwa watu wangu, basi watu wangu

watakua wanadaiwa vitu hadi pale watakapovirudisha.

Watu wa Najran watastahiki Ulinzi kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala na

Makubaliano ya Muhammad Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuwahifadhia

Maisha yao, Imani yao, Mali zao kwa wale waliokua hawapo na waliokuwepo na

Famlia zao na Mrafiki zao. Na hawatotakiwa kubadilisha Utamaduni wao, Dini yao,

wala Makasisi wao, wala Watawa wao wala walinzi wa Makanisa yao hawato

badilishwa kutoka kwenye sehemu za kazi zao.

Kwani kila walichokua nacho ni chao, bila ya kujali kama kikubwa au kidogo,

hawatoshukiwa na wala hawatofanyiwa mauaji ya kisasi, hawatotakiwa kukusanya

jeshi na wala hakuna Jeshi litakaloingia kwenye ardhi yao. Na yeyote yule miongoni

mwa atakaeomba haki yake hasi itabidi apewe kwani haki itasimamiwa miongoni

mwao, na yeyote yule atakae chukua riba kutokana na kile alichopewa hapo kabla basi

hatokua chini ya Usimamizi wangu. Na hakuna Mtu yeyote katka Mji wa Najran

ambae atahukumiwa kutkana na kosa la mwengine.(Yahya Ibn Adam Ibn Sulayman,

Kitab al Kharaj)

Ama kuhusiana na Mubahala ambalo ndio neno lililotoa Nabtahil lililotumika kwenye

ya Mubahala na pia likatoa neno Ibtihal basi alisema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu

Anhu kua: ‘‘Hii ni Ikhlas’ (shahada) huku akinyoosha kidole cha Shahada, na kisha

akanyanyua Mikono yake kukaribia usawa wa Mabega huku Viganja vikitizama

juu na akasema: ‘Hii ni Dua’ na kisha akanyoosha Mikono yake mbele na kusema:

‘Hii ni Ibtahil’’(Sunnan Al Kubra Imam Al Bayhaqi)

Ambapo:


439

Kunyoosha kidole cha Shahada hua kunamaanisha Tawhid yaani kumpwekesha

Allah Subhanah wa Ta’ala.

Hua inapendekezwa sana kua Kidole cha Shahada lazima kinyanyuliwe pale Mtu

anapotamka Shahada iwe kwenye Sala au nje ya Sala.

Kauli ya ‘La Ilaha’ yaani ‘Hakuna Mungu’, hua inakanusha Kumshirikisha Allah

Subhanah wa Ta’ala na kauli ya ‘Illa Allah’ yaani ‘Isipokua Allah’ hua inaashiria

Tawhid.

Ambapo anasema pia Imam Al Bayhaqi kua: ‘Kuna mtu miongoni mwa watu wa

Madinah alisema kua: ‘Kuna siku mimi nilisali pembeni ya Khifafa Ibn Imaa Ibn

Rukhsa Radhi Allahu Anhu, na aliponiona nikiwa nimenyoosha kidole changu cha

Shahada basi akasema: ‘Ewe Ndugu yangu kwanini wewe ukafanya hivyo?’ nami

nikasema kua: ‘Hakika mimi nimewaona Watu walio bora na Wanazuoni wakiwa

ni wenye kufanya hivi’ hivyo Khifafa Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Uko sahih,

kwani mimi nilimuona Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akiwa ni mwenye

kunyanyua kidole chake cha Shahada katika wakati wa kukaa At Tahiyyat. Ambapo

Makafiri wakamshutumu kua alikua anawafanyia Uchawi, lakini waongo, kwani

Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam alifanya hivyo kwa sababu kufanya hivyo

hua inamaanisha kushuhudisha Umoja wa Allah Subhanah wa Ta’ala.’’

Ambapo amesema Imam Ibrahim An Nakhai kua: ‘Inapendekezwa kunyoosha Kidole

cha Shahada katika wakati unaposema Shahada, na inakirihisha kunyoosha vidole

viwili’

Na Imam Abū Muḥammad Al Ḥusayn Ibn Masʻud Ibn Muḥammad Al Farra Al Baghawi

amesema pa kua: ‘Wengi miongoni mwa Watu wenye Ilm wakiwemo Masahaba wa

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, Tabiina na Tabii Tabiina walikua ni wenye

kunyoosha kidole cha shahada pale wanaposema Illa Allah katika Tashahud.’(Sharh

Al Sunnah)

Baada ya tukio hilo la Mubahala basi mnamo mwezi wa Rabiul Awwal 10 Al Hijra Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamtuma Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu na

jeshi la watu 400 katika Mji wa Najran kwa Banu Harith Ibn Kab na kumwambia kua:

‘Nenda katika Mji wa Najran na kisha wausie kuhusiana na Uislam, kama

wakikubaliana nao basi fanya kila linalostahiki, na kama wakipingana nawe basi

pigana nao.’

Hivyo Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu akatoka na jeshi lake hadi nje ya Mji wa

Najran. Kisha akapiga kambi katika maeneo hayo na kuwatuma Wajumbe wake


440

wakawausie watu wa Najran kuhusiana na Uislam kwa mda wa siku tatu. Na baada ya

siku tatu watu wote wa Najran wakaingia katika Uislam.

Baada ya watu hao kuingia kwenye Uislam basi Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu

akawafundisha watu hao kuhusiana na Dini ya Kislam, kisha akamuandikia barua Rasul

Allah Salallau Alayhi wa Salam kutaka kujua afanye nini baada yake.

Hivyo Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam akajibu barua hio kwa kusema:

Biismi Allahi Al Rahmani Al Rahim.

Kutoka kwa Muhammad Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kufikia kwa Khalid

Ibn Walid.

Al Salaam Alaykum!

Alhamd Lillah Ladhi La Ilaha illa Allah kwa lile ulilolifanya.

Nimepokea barua yako iliyoletwa na Mjumbe kutoka kwako, ambayo umesema ndani

yake kua watu wa Banu Harith Ibn Kab wamaeingia katika Uislamu bila ya upinzani,

wamemuamini Allah Subhanah wa Ta’ala ambae hana mshirika na wameshuhudia

kua Muhammad ni Mja na ni Rasul Allah na kua Allah Subhnah wa Ta’ala

amewaongoza kwenye njia iliyonyooka.

Wape habari ya kua watapata Malipo ya neema za Akhera kama ikiwa watafanya

kama alivyoamrisha Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume wake. Na watishe

kuhusiana na Adahabu za Akhera kama watafanya kinyume cha maamrisho ya Allah

na Mtume wake. Kisha unaweza kurudi huku ukwa na Mjumbe wao pamoja nao.

As Salaam Alaykum wa Rahmat Allahi wa Barakatuh.

Hivyo baada ya mda Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu akarudi na jeshi lake na

Ujumbe wa Najran katika Mji wa Madinah na moja kwa moja wakaenda kwa Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na kumfahamisha kua kweli wote wamekua Waislam na

hivyo Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam akamteua Qays Ibn Husayn ambae alikua

ni miongoni mwao ujumbe huo wa Najran kua ndio awe Gavana wao, na kisha baada ya

mda Ujumbe huo ukarudi katika Mji wa Najran huku ukiwa umesheheni zawadi kutoka

kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.


441

UTUKUFU WA KUTUNUKIWA UJA UZITO MARYAM BINT IMRAN

Tunapomuangalia Maryam Bint Imran basi tunaona kua ni Mwanamke ambae ni mwenye

sifa ya kumtii Allah Subhanah wa Ta’ala, mwenye kuachana na mambo ya kidunia na

kuyakmia mapambo ya Dunia, hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala amemchagua Maryam

Bint Imran kua ni mfano bora kwa Wanawake na pia kwa Wanaume kutokana na

Uchamungu wake, na hvo ndani yake kutuonesha mfano wa yale yanayoweza kutokea

pale Mtu unapokua Mcha na mitihani mbali mbali unayoweza kukumbana nayo kutoka

katika jamii unayoishi na hivyo kutakiwa kutorudi nyuma wala kutetereka katka

msimamo wako mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala na kukubaliana na Majaaliwa yake

juu yako.

Anasema Imam Abu Is-haq Ahmad Ibn Muhammad Ibn Ibrahim Al Thalabi Al Shafii

kua: ‘Wakati Maryam Bint Imran alipotimia umri wa miaka 15 basi alikua na

ujauzito wa Isa Ibn Maryam kwa mda wa siku 3. Ambapo pamoja nae katika

nyumba ya kufanyia ibada alikuwepo Yusuf ambae alikua ni Mtoto wa kaka yake

baba yake, ambae nae alikua pia ni mwenye kujitolea kwa ajili ya Mola wake. Yusuf

alikua ni mtu mstahmilivu na ni fundi Seremala ambae ni mwenye kuwasadia watu

katika kutengeneza fanicha zao. Yusuf na Maryam walikua na Jukumu la kuchota

Maji kutoka kwenye Pango lenye chemchem ya Mji na kisha huyapeleka katika

Jengo wanalofanyia Ibada Mayahudi.’

Ambapo mtu huyu anaetwa Yusuf basi hakua mtu mwengine yeyote isipokua ni yule

tuliemzungumzia hapo kabla ambae alikua pia ni Mlezi wake Maryam Bint Imran ambae

alikua anaitwa Yusuf Ibn Yaqub Ibn Mathan Ibn Amur Ibn Mishan Ibn Hizqil Ibn Ahraf

Ibn Buam Ibn Azaziyah Ibn Amasiyah Ibn Nawus Ibn Nutha Ibn Barid Ibn Yahushafat

Ibn Radim Ibn Ababa Ibn RajiAm Ibn Sulayman Ibn Daud.

Siku moja katika kipindi cha Kiangazi, Maryam Bint Imran kwani Allah Subhanahu wa

Ta’ala alimuamrisha Malaika Jibril Alayhi Salaam kujua na kuenda kwa Maryam bint

Imran kwa ajili ya kumshushia Wahyi na kumbashiria habari njema kama ilivyoelezewa

katika Surat Al Imran pale iliposema:

‏﴿وَإِذْ‏ قَالَتِ‏ ٱلْمَلاَئِكَةُ‏

يمَٰرْيمَُ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ ٱصْطَفَاكِ‏ وَطَه َّرَكِ‏ وَٱصْطَفَاكِ‏ عَلَى ٰ نِسَآِء

ٱلْعَالَمِينَ‏ ﴾


442

Wa-idh qalati almala-ikatu ya Maryamu inna Allaha istafaki watahharaki

waistafaki AAala nisa-i alAAalameena (Surat Al Imran 3:42)

Tafsir: Na (kumbuka) wakati Malaika aliposema: ‘Ewe Maryam! Kwa Hakika Allah

amekuchagua wewe na kukutakasa, na kukuchagua kua juu zaid ya Wanawake wote

wa Ulimwenguni’.

Hivyo alipofika kwenye Pango hilo basi akakutana na Mtu ambae alikua ni Malaika Jibril

ambae alimbashiria kuchaguliwa kwake na kupandishwa Darja ya Utakaso kutoka kwa

Mola wake na kuamriwa kua awe ni mwenye kudumu katika Ibada.

﴿ يمَٰرْيمَُ‏ ٱقْنُتىِ‏ لِرَبِّكِ‏ وَٱسْجُدِى وَٱرْكَعِى مَعَ‏ ٱلر َّاكِعِينَ‏ ﴾

Ya maryamu oqnutee lirabbiki waosjudee wairkaAAee maAAa alrrakiAAeena

(Surat Al Imran 3:42)

Tafsir: Ewe Maryam Muabudu Mola wako, na Umsujudie na Urukuu pamoja na

wenye kurukuu.

Ambapo aya imetumia neno Uqnut ambalo hua lintokana na neno Qanata ambalo hua

linamaanisha Kujitolea. Kua Mtiifu, Kufanya Ibada kwa Ikhlasi na Unyenyekevu. Na

hivyo basi kwa uande wa Imam Mujahid Ibn Sulayman basi yeye anasema kua: ‘Allah

Subhanah wa Ta’ala anamwambia Maryam Bint Imran kua anatakiwa awe ni

Mwenye kudumu katika Ibada za Mda mrefu’ na kua anatakiwa ashikamane na wale

Wacha Mungu waliojitolea katika kufanya Ibada kwa Ikhlasi na Unyenyekevu kwani

Ikhlasi na Unyenyekevu hua ni vyenye kumuondolea Ibn Adam hisia za Kujiona, Kibri

na kua na Chuki.

Ambapo wanasema Wanazuoni kua baada ya Maryam Bint Imran kuambiwa hivyo bsi

akawa anasimama usiua na uali hadi miguu yake ikawa ni yenye kuimba

Mbali ya hivyo basi amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

‘Wanatosheleza kwenu, Wanawake wa Ulimwengu ni Maryam Bint Imran, Khadja

Bint Khuwylid na Fatma bint Muhammad Salallahu layhi wa Salam.’ (Tirmidhi)

Na akasema tena Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Miongoni mwa

Wanaume wamekuwepo wengi waliokua ni wenye kuufikia ukamilifu. Lakini kwa

upande wa Wanawake basi hakuna alieufikia ukamilifu wa Maryam Bint Imran,


443

Asiyah Bint Muzahim mke wa Fir’awn na Aisha ambapo utukufu wao dhidi ya

Wanawake wengine basi hua ni sawa na Tharid na vyakula Vyengine.’

Ambapo Tharid hua ni Chakula ambacho ni kitamu sana na tunu cha kipindi cha Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kilichokua ni chenye mchanganyiko wa Mkate, Nyama

na Mchuzi wa Nyama kama wa Biriani.

Utukufu wake Maryam Bint Imran tunauona wazi pale tunapoangalia Qur’an na kuona

kua ingawa Qur’an imezungumzia habari za Wanawake kadhaa ndani yake kama Mke

wa Nabii Adam, Mke wa Nabii Nuh, Mke wa Nabii Ibrahim, Mke wa Nabii Lut, Mke wa

Waziri aliempa Mtihani Nabi Yusuf, Mke wa Fir’awn, Wanawake wawili wa Shuayb

ambao mmoja wao alimuoa Nabi Musa, Dada yake Nabii Musa, Malkia wa Sheba lakini

hakuna hata mara moja ambapo kuna sehemu iliyotaja majina ya Wanawake hao,

isipokua katika Kisa cha Maaryam Bint Imran tu, ambae ndie Mwanamke pekee alietajwa

kwa jina, na si hivyo tu bali pia Maryam Bint Imran ndie Mwanamke pekee ambae Jina

lake limetumika kua ni jina la moja kati ya Majina ya Sura za Kitabu kikufu cha Qur’an.

Na hii ni kwa makusudio ya kumsafisha Maryam Bint Imran kutokana na Utukufu wake

na kutokana upatikanaji wa Uja uzito wake na pia wa mtoto wake, na hivyo kuondoa na

kufuta kila chembe ya shaka au wasiwasi kuhusiana na Utukufu wake na Miujiza yake

juu ya Upatikanaji wa Mtoto wake, hivyo katajwa moja kwa moja ili watu wasijiulize

yeye au si yeye au ni mwengine, na hii inathibitishwa mara kadhaa kuhusiana nae

Maryam Bint Imran kama zinavyosema aya:

‏﴿وَٱذْكُرْ‏ فىِ‏ ٱلْكِتَابِ‏ مَرْيمََ‏ إِذِ‏ ٱنتَبَذَتْ‏ مِ‏ نْ‏ أَهْ‏ لِهَ‏ ا مَكَ‏ اً‏ شَ‏ رْقِياً‏ ۞ فَٱتخ ََّذَ‏ ‏ْت

دُوِِم حِ‏ جَاابً‏ فَأَرْسَلْنَآ إِلَيْهَآ رُوحَنَا فَتَمَث َّلَ‏ لهََا بَشَراً‏ سَوًِّ﴾‏

مِن

Waodhkur fee alkitabi maryama idhi intabadhat min ahliha makanan sharqiyyan;

Faittakhadhat min doonihim hijaban faarsalna ilayha roohana fatamaththala laha

basharan sawiyyan; (Surat Maryam 19:16-17)

Tafsir: Na ametajwa katika kitabu, Maryam, wakati alipojitenga kutokana na familia

yake katika sehemu inayoelekea upande wa Mashariki; Akaweka pazia kabla yao,

kisha tukamtumia juu yake Ruhi (Malaika) wetu aliejimithilisha katika umbo la mtu

aliekamilia na kujaa heshima.

Aya inasema kua ametajwa, amekubukwa, amekumbushiwa tena na kuendelea

kukumbushiwa ili msije mkamsahau Maryam Bint Imran, na kuendelea kuelezea hususn

juu ya yaliyotokea kwa kutumia neno Intabadhat ambalo linatokana na neno Nabadha.


444

Neno Nabadha hua linaamanisha Kurusha, Kurembea, Kufukuza, Kutenga kitu au

Kuweka Kitu pembeni kutokana na kutokua na thamani kwake au kutokana na kutotaka

kukihesabu. Hivyo neno Intabadhat hua linamaanisha Mwanamke aliejitenga. Na hivyo

kumaanisha Kua Maryam Bint Imran aliamua kujitenga kwa sababu ya kua alikua ni

mwenye kuingia kwenye siku zake na hivyo haruhusiki kuingia kwenye Mihrab.

Na ndio maana Imam Al Abd Al Rahman Al Suddi, Imam Muqatil Ibn Sulayman Al

Balkhi na Imam Al Hassan basi wao wanasema kua: ‘Maryam Bint Imran alikua

akikaa katika Mihrab pale anapokua Tohara, na anapokua katika siku zake basi

hua ni mwenye kuenda kwa Isha Bint Faqudh ambae ni Dada wa Mama yake, na

hukaa huko hadi anapokua tohara tena na kurudi kwenye Mihrab.

Hivyo siku moja wakati alipokua anataka kujitoharisha kutokana na hedhi basi

alichagua sehemu ya upande wa Mashariki yenye kupigwa na jua kwa sababu hiki

kilikua ni kipindi cha Kipupwe. Na kisha akaiziba sehemu hio kwa pazia baina yake

na baina ya watu wake na alipokua katika mazingira hayo akatokea Malaika Jibril,

na kumpa habari ya Ujumbe kutoka kwa Mola wake kuhusiana na Ujauzito wake,

na kisha Malaika Jibril akaipulizia Kanzu ya Maryam Bint Imran.’

Na kwa upande mwengine basi kuna wasemao kua Maryam Bint Imran alijitenga katika

upande huo wa Mashariki si kwa sababu ya kua alikua ni mwenye kuingia kwenye siku

zake, bali ni kwa sababu alikua ni mwenye kutaka kuupata Ukaribu zaidi kwa Allah

Subhanah wa Ta’ala katika Ibada zake. Kwani kufanya kwake hivyo hua ni kweye

kumuongezea Imani kwa kumkumbuka Allah Subhanah wa Ta’ala na kumpa nguvu zaid

katika kukabiliana na mitihani atakayokumbana nayo hapo baadae katika maisha yake

kwani hukuonesha Uwezo na Ukubwa wa Allah Subhanah wa Ta’ala.

Na hii ni kwa sababu Ibn Adam unakua hujichanganyi na mambo ya Kidunia na

kujulikana na watu wengi basi hali hii hua inakusaidia kutoathirika na athari mbaya na

zenye kuenda kinyume na maadili ya Kiislam katika jamii zinazowaathiri wengi

kutokana na kua ni wenye kuiga na kufuata mambo yasiyotokana na Imani ya Dini ya

Kiislam kutokana na kutokuwepo kwa vizuizi vya athari hizo katika jamii.

Ambapo kwa upande wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas na pia Abd Allah Ibn Masud

Radhi Allahu Anhum basi wao wanasema kua Maryam Bint Imran aliingia katika siku

zake za kupata hedhi mara moja tu na hakuwahi kuingia tena ndani yake, hivyo alipopata

hedhi katika mara hio na kisha ikasita basi basi akaelekea katika upande wa Mashariki

kwa ajili ya kujitoharisha, na kisbha akaweka baina yake na sehemu aliyokuweo ili watu

wasimuone ambapo hapo ndio Allah Subhanah wa Ta’ala akamtuma Malaika Jibril kwa

ajili ya kumbashiria juu ya Kupata uja uzito kwake ambao kutokana nao basi atakua ni

mwenye kupata mtoto mtakatifu yaani Isa Ibn Maryam.


445

Ambapo hapa katika aya hii basi Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia jina la Ruhi

ambalo hua ni lenye kutokana na neno Raha ambalo hua ni lenye kumaanisha Upepo,

Mamlaka, Roho. Pumzi au Hewa ya Uhai, Wahyi, Furaha na pia hua linamaanisha Qur’an

kwa sababu Qur’an hua ina sifa ya Kuhuisha Nyoyo. Hivyo neno Ruhina hua

linamaanisha Ruhi Wetu yaani Kiumbe mwenye Uhai anaemilikiwa na Ufalme wa Allah

Subhanah wa Ta’ala ambae ni Malaika Jibril.

Ambpapo unapomzungumzia Malaika Jibril basi tunaona kua ingawa ni mongoni mwa

Malaika wenye maumbo madogo miongoni mwa Malaika lakini hata hivyo Jibril ni

Malaika mwenye Darja kubwa sana mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo kua

ndio Mkuu wa Malaika na ndio maana akakabidhiwa madaraka ya kua ni Mwenye

kuwashushiwa Wahyi na Vitabu vyote Mitume wake Allah Subhanah wa Ta’ala.

Na hivyo Malaika Jibril amekua na sifa ya Jina la Ruhi Al Qudus yaani Roho Mtakatifu

yaani ni Kiumbe asiekua na Kasoro na asiefanya Makosa, Ruhi Al Amin yaani Roho

Inayoaminiwa na hivyo kua ni mwenye kuaminiwa na Allah Subhanah wa Ta’ala katika

kutuma ujumbe wake kwa Mitume na Manabii wake na kama tunavyoona kwa Maryam

Bint Imran, ambae ni mwenye kua na sifa ya Unabii pia, kama tulivyoelezea hapo kabla

tulipozungumzia maana na tofauti baina ya Mtume na Manabii.

Hivyo anasema Ikrimah Mawla Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kuhusiana na

tuko hilo kua: ‘Maryam Bint Imran alitokezewa na Malaika Jibril ambae alikua

katika umbo la kijana Mwanamme mweupe asiekua na ndevu mzuri mwenye

kuvutia na nywele za singa na mwenye heshima kubwa sana’ hivyo Allah Subhana

wa Ta’ala alimtuma kwake Malaika Jibril katika Maumbile hayo ili Maryam Bint Imran

asiingiwe na Khofu baada ya kumuona kijana huyo, na hivyo aweze kumsikiliza atakapo

mfikishia ujumbe wake huo kutoka kwa Mola wake.

Ambapo tukio lililotokea baada ya hapo basi linaelezewa na Allah Subhanah wa Ta’ala

katika Qur’an pale aliposema:

‏﴿قَالَتْ‏

إِنيّ‏ ِۤ أَعُوذُ‏ بِٱلر َّحمَْٰنِ‏ مِ‏ نكَ‏ إِن كُ‏ نتَ‏ تَقِيّاً‏ ۞

لاًّهَبَ‏ لَكِ‏ غُلَماً‏ زَكِيّاً﴾‏

قَالَ‏ إِنم ََّآ أََْ‏ رَ‏ ‏ُسولُ‏ رَبِّ‏ ‏ِك

Qalat innee aAAoodhu bialrrahmani minka in kunta taqiyyan; Qala innama ana

rasoolu rabbiki li-ahaba laki ghulaman zakiyyan (Surat Maryam 19:18-19)


446

Tafsir: Nae (Maryam Bint Imran) akasema: ‘Hakika mimi ninajilinda kwako na kwa

Mwingi wa Rehma, ikiwa unamuogopa Allah’; Nae (Malaika Jibril) akasema: ‘Mimi

ni mjumbe kutoka kwa Mola wako, kukuzawadia mtoto wa kiume alie mwema’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamjaalia Maryam Bint Imran kua na utulivu

alipotokewa na Malaika Jibril katika Maumbile ya Kijana Mwanamme Mzuri, Mwenye

Heshima, Utulivu na Kuvutia kiasi ya kua haikua rahisi kwa Maryam Bint Imran

kushtuka kutokana na muonekano huo wa Kijana huyo. Kwani kama angemtokea kwa

ghafla au kwa muonekano unaoshtua basi huenda Maryam Bint Imran angekua ni

mwenye kupiga kelele na kukimbia na kutotaka hata kuzungumza na kijana huyo.

Na hivyo Malaika Jibril kutokua na uwezo wa kumpa Ujumbe huo kwa namna

ilivyokusudiwa Umfikie ujumbe huo Maryam Bint Imran, na pia Malaika Jibril alikua na

hali ya Utulivu na heshima kubwa kimuonekano kwa sababu tukio hili la kwanza

linalotokea hapa la kuonekana kwa Malaika Jibril mbele ya Maryam Bint Imran si kubwa

na halina uzito zaidi ya lile litakalofuatia, ambalo ni la kufikisha Ujumbe wa kutokea

tukio la Tukufu la Miujiza ya kipekee ambalo halijawahi kutokea Ulimwenguni tangu

kuumbwa kwa Ulimwengu wala halitotokea tena baada ya kutokea kwake tukio hilo

katika mazingira haya aliyokua nayo Maryam Bint Imran.

Hivyo kutokana na muonekano huo wa Malaika Jibril basi ulimfanya Maryam Bint Imran

kua Mnyenyekevu zaid na kumjali na mwenye kumuonea huruma kijana huyo asiemjua

kutokana na kuwepo katika sehemu asiyostahiki kuwepo kijana huyo basi akamuusia kwa

moja kwa moja kurudi kwa Mola wake ambae yeye Maryam Bint Imran ndie aliekua

akimjali na kumtumikia maisha yake yote tangu kuzaliwa kwake, hivyo akakimbilia

kujihifadhi vizuri mavazi yake na kwa kutumia Qawlan Sadida yaani kauli ya moja kwa

moja iliyojaa utulivu bila ya kutaka kujuana nae Kijana huyo ni nani na amekuja kufanya

nini katika sehemu hio na akasema: ‘Hakika mimi ninajilinda kwako na kwa Mwingi

wa Rehma, ikiwa unamuogopa Allah’’.

Ambapo nae (Malaika Jibril) akatumia Qawlan Sadidan kwa moja kwa moja

kujitambulisha na kudhirisha Dhumuni la kuwepo kwake mbele ya Maryam Bint Imran

katika mazingira kama hayo, ambayo kweli hastahiki kuwepo Mtu mwengine zaidi yake

kutokana na Maryam Bint Imran kua ni mwenye kuichagua sehemu hio maalum kwa ajili

ya kua peke yake na ndio maana akaweka pazia kwa ajili ya kujistiri, hivyo akamtuliza

zaidi Maryam Bint Imran ili amfikishie ujumbe aliopewa na Mola wake kumfikishia kwa

kusema: ‘Mimi ni mjumbe kutoka kwa Mola wako, kukubashiria kua Allah Subhanah

wa Ta’ala ametangazia kukutunukia Mtoto alie mwema’.

Ambapo hapa aya imetuma neno Ahaba ambalo ni lenye kutokana na neno Wahaba

ambalo hua linamaanisha Kuzawadia, Kutunuku au Kutoa Kitu kwa ajili ya kumpa mtu

kama zawadi. Hivyo Malaika Jibril ametumia kauli hii ya Ahaba kumaanisha kua Allah


447

Subhanah wa Ta’ala amesema kua anataka kumtunukia Maryam Bint Imran zawadi

Tukufu ya Mtoto kwani hivyo ndivyo alivyoamrishwa na Mola wake

Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kuelezea kwa upande mwengine kwa kusema kua:

‏﴿إِذْ‏ قَالَتِ‏ ٱلْمَلا ۤ ئِكَةُ‏ يمَٰرْيمَُ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ يُبَشِّ‏ رُكِ‏ بِكَلِمَةٍ‏ مِّنْهُ‏ ٱسمُْهُ‏ ٱلْمَسِ‏ يحُ‏ عِيسَى ٱبْنُ‏

مَرْيمََ‏ وَجِ‏ يهاً‏ فىِ‏ ٱلد ُّنْيَا وَٱلآخِ‏ رَةِ‏ وَمِنَ‏ ٱلْمُقَر َّبِينَ‏ ﴾

Idh qalati almala-ikatu ya maryamu inna Allaha yubashshiruki bikalimatin minhu

ismuhu almaseehu AAeesa ibnu maryama wajeehan fee alddunya waal-akhirati

wamina almuqarrabeena; (Surat Al Imran 3:45)

Tafsir: Na (kumbuka) wakati aliposema Malaika: ‘Ewe Maryam, Allah

anakubashiria wewe habari njema za Kalimati (Maneno yake ya Kua na Akawa)

kutoka kwake, anaeitwa Al Massih Isa Ibn Maryam atakaeheshimiwa hapa Duniani

na Akhera na atakua ni miongoni mwa waliokaribu na Allah Subhanah wa Ta’ala.

Aya inatubainishia kua Malaika Jibril anamwambia Maryam Bint Imran kua Allah

Subhanah wa Ta’ala anambashiria yeye kuhusiana na Kalimati. Ambapo neno Kalimati

hua linatokana na neno Kalama ambalo hua linamaanisha Kusema, Kuzungumza,

Maneno, Sentensi, Lugha, Msemo, Amrisho, Hoja, Dalili, Bashirio, Utume, Ahadi au

Mawasiliano.

Na anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Ujio wa Nabii Isa

ulizungumziwa kwenye vitabu vyengine vilivyotangulia vya Mitume waliokuja

kabla yake, hivyo ulipowadia wakati wa kuja kwake basi ikasemwa kua hii ni

Kalimati iliyobashiriwa. Na hivyo kawa anaitwa Kalimati Allah.’

Ambapo kwa upande wa Imam Murtada Al Zabidi basi yeye anasema kua: ‘Nabii Ia

aliitwa Kalimati Allah kwa sababu Maneno yake yalikua ni yenye kuwasadia watu

katka kuwaongoza katika njia ya Allah Subhanah wa Ta’ala kutokana na thamani

yake kama vile ilivyokua kwa Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu ku ni mwenye

kuitwa Saifu Allah kutokana na Kuusaidia Uislam dhidi ya Makafiri kutokana na

Upanga wake’

Ambapo kwa Upande wa Shayh Al Akbar Imam Abu Bakr Ibn Arabi basi yeye anasema

kua: ‘Allah Subhanan wa Ta’ala aliposema kua: ‘Idha qadha amran fa-innama

yaqoolu lahu kun fayakoonu - Anapotaka kitu kiwe hua ni wenye kukiambia tu Kua

na Kikawa’ ambapo neno Kun hua si neno lenye Herufi mbili bali ni tatu, ambapo


448

harufi mbili ni za nje ambazo ni Kaf na Nun na herfu moja ni ya Ndani ambayo ni

Waw ambayo ipo baina ya Kaf na Nun. Kufichwa kwa herufi Waw kunatokana na

kutotamkika kwake kutokana na Nun, ambapo kufichikana huku kwa herufi Waw

baina ya herufi mbili hizi hua kunamaanisha kuwepo kwa Ulimwengu wa Ibn Adam

ambako ndiko kunakounganisha na kutofautisha baina ya herufi Kaf na Nun.’

‘Hivyo kuhusishwa kwa Isa na Maryam hua ni kuthibitisha kua Viumbe wote hua

ni wenye kutokana na Kauli ya Allah Subhanah wa Ta’ala ya KuN. Na hivyo Nabii

Isa hua ni muwakilishi wa uhalisia wa Kun na Maryam Bint Imran ambae ndie

alieamini katika Kalimati Allahi na Vitabu vyake na matokeo ya yote haya ni

kutokana na Neno hili Kun na maneno mengine ya Allah Subhanah wa Ta’ala.’

‘Hivyo neno KuN hua ni amrisho la Kuumba (Kalimat al Amr Al Taqwin), kwani

Allah Subhnah wa Ta’ala amesema kua Nabii Isa Ibn Maryam ni Kalimati Allah, na

kila kilichoumbwa hua ni kutokana na Kalimati Allah, na hivyo basi Allah Subhanah

wa Ta’ala hatumii neno zaid ya KuN katika Kuumba kwake, hili ni neno ambalo

linalobainisha kuwepo kwake na kuwepo kila kitu chake’

Katika aya hii pia Allah Subhanah wa Ta’ala anamwambia Maryam Bint Imran kua

Kalimati Allahi huyo atakua ni Masih atakaeitwa kwa jina la Isa Ibn Maryam. Ambapo

neno Masih hua ni lenye kutokana na neno Masaha ambalo hua linamaaisha Kupangusa,

Kufuta, Kupapasa kwa Utaratibu, Kupakaza Kitu, Kupaka kitu kwenye Mwili, Kupitisha

Mkono juu ya Kitu, Kupendeza, kua Nzuri na yenye Baraka na pia humaanisha Kufunga

safari ya Kutembea ardhini.

Hivyo Nabii Isa Bint Maryam ameitwa Masih kwa sababu alikua ameshaandikiwa kua

atakua ni mwenye Kutembea kwa unyenyekevu katika sehemu mbali mbali Ardhini kwa

ajili ya kufikisha Ujumbe wake kwa Makabila tofauti ya watu wa Bani Israil yaliyokua

yametawanyika katika sehemu mbalimbali ardhini ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala

amezizungumzia kua amewajaalia Isa Ibn Maryam na Maryam Bint Imran kua ni Makazi

kwa ajili yao pale aliposema katika aya ifuatayo:

‏﴿وَجَعَلْنَا ٱبْنَ‏ مَرْيمََ‏ وَأُم َّهُ‏ آيَةً‏ وَآوَيْنَاهمَُآ إِلىَٰ‏ رَبْوَةٍ‏ ذَاتِ‏ قَرَارٍ‏ وَمَعِينٍ‏ ﴾

WajaAAalna ibna maryama waommahu ayatan waawaynahuma ila rabwatin dhati

qararin wamaAAeenin(Surat Al Muuminuun 23:50)

Tafsir: Na tumemjalia Ibn Maryam na Mama yake kua ni Dalili. Na tukawapa makazi

katika Ardhi iliyojuu sehemu ya usalama na amani na chemchem.


449

Na kwa upande mwengine basi tunaona kua Neno Masih kwa Lugha ya Kiyahudi hua

linamanisha kua ni Mfalme au Muokozi anaetegemewa.

Kisha aya inatuonesha kua Allah Subhanah wa Ta’ala anambainishia Maryam Bint Imran

kuhusiana na Utukufu wa Tunukio la Mtoto atakaempata kua atakua ni miongoni mwa

Minna Al Mukarrabin yaani watakokua karibu nae Allah Subhanah wa Ta’ala na

kumalizia kwa kusema kua:

‏﴿وَيُكَلِّمُ‏ ٱلن َّاسَ‏ فىِ‏ ٱلْمَهْدِ‏ وَكَهْلاً‏ وَمِنَ‏ ٱلص َّالحِِينَ‏ ﴾

Wayukallimu alnnasa fee almahdi wakahlan wamina alssaliheena; (Surat Al Imran

3:46)

Tafsir: Na atazungumza na watu kutoka kwenye Kitenga cha Watoto wadogo na

Ukubwani na atakua ni miongoni mwa waja wema.

Ingawa kuna hadith ya Abu Hurayrah kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kua watoto watatu walizungumza kwenye Mikoba ya kubebea watoto ambao

ni Isa, Mtoto alieishi kwenye wakati wa Jurayj na Mtoto wa Mwanamke alietupwa

kwenye shimo la As-hab al Uhdud’

Ambapo tunapozungumzia Mtoto wa Kisa cha Jurayj basi amesema Abu Hurayrah Radhi

Allahi Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua hakuna

mtoto aliezungumza kwenye Mikoba ya kubebea watoto isipokua ni Isa Ibn

Maryam na sahaba yake Jurayj.’ Hivyo Abu Hurayrah Radhi Allahu Anhu akasema:

‘Ya Rasul Allah, Hivi jee huyu Sahaba wa Jurayj ndio nani?’

‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Jurayj alikua ni Mtawa ambae

alikua akiishi katika eneo la nyumba ya kitawa peke yake. Ambapo katika eneo

alilokua akiishi kulikua kuna Mfugaji ambae alikua akitembelea katika eneo hilo

na mmoja kati ya Wanawake wa Kijijini hapo alikua pia akitembelea eneo hilo kwa

ajili ya kumtembelea Mfugaji huyo.’

Hivyo siku moja akaja mama yake Jurayj wakati Jurayj akiwa ndani ya Sala na

kumwita: ‘Ewe Jurayj!’

Hivyo Juray akajiuliza: ‘Mama yangu au Sala yangu?’hivyo akona bora amaliza

Sala yake, kisha mama yake akaita tena: ‘Jurayj!’ Jurayj akajiuliza tena: ‘Mama

yangu au Sala yangu?’ na akaona kua bora amalize Sala yake. Mama yake akaita


450

tena mara ya tatu: ‘Jurayj!’ Jurayj akajiuliza tena: ‘Mama yangu au Sala yangu?’

na akaona kua bora amalize Sala yake.’

Hivyo baada ya kua Jurayj hakumjibu mama yake basi mama yake akasema: ‘Ewe

Jurayj, Namuomba Allah asikujaalie Ufe hadi pale utakapotizama nyuso za

Wanawake waovu’ na kisha mama yake Jurayj akaondoka.’

Na baada mda yule Mwanamke wa Mji huo, akaletwa mbele ya Mfalme wa mji huo

baada ya kujifungua Mtoto, ambapo akaulizwa Mwanamke huyo, ‘Huyu Mtoto

Baba yake ni Nani?’ ambapo yule Mwanamke akasema: ‘Baba yake ni Jurayj’

Mfalme akauliza: ‘Jurayj yule Mtawa?’ Mwanamke akasema: ‘Naam.’

Mfalme akaamrisha kwa kusema: ‘Nendeni mkaivunje Nyumba yake na kisha

mlete mbele yangu’

Hiyvo watu wakaenda kwenye Nyumba ya Jurayj na kuivunja vunja yote, na kisha

wakamkamata Jurayj na kufunga kamba mikono yake shingoni mwake na

kumpeleka mbele ya Mfalme, hivyo wakati anapelekwa mbele ya Mfalme basi

akawa ni mwenye kuwaona Wanawake waovu na kutabasam.

Alipofika mbele ya Mfalme basi Mfalme akamuuliza Jurayj: ‘Hivi Jee Unayajua

madai ya Mwanamke huyu?’ Jurayj akauliza: ‘Ana madai gani?’

Mfalme akasema: ‘Anadai kua wewe ndie Baba wa Mtoto wake.’ Jurayk

akamuuliza Mwanamke huyo: ‘Yuko wapi huyo Mtoto wako?’ Watu wakasema:

‘Yuko chubani mwake’ Hivyo Jurayj akapelekwa kwenye chumba cha Mtoto huyo

na alipomuona mtoto huyo basi akamuuliza: ‘Jee ni Nani Baba yako?’ Mtoto

akajibu: ‘Baba yangu ni Mfugaji’

Kutokana na Majibu hayo basi Mfalme akasema: ‘Jee tukujengee Nyumba tupya kwa

Dhahabu?’ Jurayj akasema: ‘La’ Mfalme akauliza: ‘Kwa Fedha?’ Jurayj akasema:

‘La’ Mfalme akauliza: ‘Jee tuijenge kwa kitu gani?’ Jurayj akasema: ‘Ijengeni

kama ilivyokua hapo mwanzo’ Hivyo Mfalme akaamrisha kua nyumba ya Jurayj

ijengwe upya kama ilivyokua hapo awali.

Kisha Jurayj akatabasamu, na alipotabasam basi Mfalme akamuuliza Jurayj: ‘Kitu

gani kilichokufanya uwe ni mwenye Kutabsam?’

Jurayj akajibu: ‘Kuna kitu ambacho nimekitambua, Laana ya Mama yangu

imenipitia’ na kisha akamuelezea Mfalme juu ya ya yaliyotokea(Imam Bukhari)


451

Ambapo katika Hadithi hii basi tunaona kua Ingawa Rasul Allah Salallahu A’layhi wa

Salam alisema kua: ‘Mtoto inabidi anatakiwa anasibishwe na Kitanda na hivyo

mzinifu hua hana Mtoto.’(Bukhari na Muslim)

Na hivyo hadithi hii ya kua Kitanda cha wana Ndoa hakizai Haramu kua ni yenye

kutumika katika kutoa Fatwa isemayo kua: ‘Mtoto wa nje ya Ndoa hua hawezi

kunasibishwa na nasaba ya Mwanamme aliezini na Mwanamke, hata kama Mzinifu

huyo Mwanamme akikubali kua Mtoto huyo ni wake’ ambao huu ndio mtizamo

Unaokubalika zaidi miongoni mwa Wanazuoni kwani una makubalino juu yake.

Lakini kwa upande mwengine basi tunaona kua kuna mitizamo miwili tofauti, kwani

mbali ya mtizamo huo wa kwanza kua haikubaliki kumnasibisha Mzinifu wa kiume na

Mtoto wa Zinaa hata kama Mzinifu akikubalikua ni wake lakini kwa upande mwengine

kuna Wanazuoni ambao wana mtizamo tofauti kuhusiana na jambo hili na hii ni kutokana

na uthibitisho wa Hadith hii ya kisa cha Jurayj.

Kwani anasema Imam Ibn Qudamah Al Maqdisi kua: ‘Kwa upande wa Wanazuoni

wakubwa wa Fiqh wa kizazi cha mwanzoni mwa Uislam katika kipindi cha Tabiina

kama Urwa Ibn Az Zubayr, Sulayman Ibn Yasir, Hasan Al Basr, Muhammad Ibn

Sirin, Ibrahim An Nakhai na Is-haq Ibn Rahawayh basi wao wanasema kua: ‘Kama

Mzinifu Mwanamme akikubali kua Mtoto ni wake basi inakubalika kunasibishwa

nae.’

Na huu pia ndio mtizamo wa Shaykh Ibn Taymiyyah na Imam Ibn Al Qayyim, Shaykh

Muhammad Rashid Rida na pia Shaykh Muhammad Ibn Uthaymin, na hii ni kwa sababu

ya uthibitisho wa Mtoto wa Hadithi ya Jurayj ambae amejinasibisha na Mfugaji Kondoo

kupitia katika njia ya Miujiza ya usemaji wa Mtoto huyo kwa idhini ya Allah Subhanah

wa Ta’ala japo kua Mtoto huyo alitokana na kitendo cha Zina,

Na hivyo hii inaonesha kua inakubalika kumnasibisha Mtoto na Baba yake huyo kama

Baba atamkubali hata kama ni wa Zina, na hii ni kwa sababu Malengo ya Shariyah za

Allah Subhnah wa Ta’ala ni kuhifadhi Kizazi na kusimamia haki za watoto na kuwalea

katika hali nzuri na ya uongofu.

Hivyo basi kama itakua mtoto husika atakua ni mwenye kukosa malezi ya Kiislam na

huduma za kijamii pale itakapokua anahesabiwa kua ni Mtoto wa nje, basi hua kulingana

na mtizamo wa Wanazuoni hawa basi tunaona kua inakubalika kumnasibisha na Baba

yake hata kama ni wa nje ya Ndoa kama Baba atakubali kua ni Mtoto wake kwa ajili ya

kusimamia Msalahi yake mtoto husika ya kidunia na Kiakhera.

Ambapo kwa upande wa Encyclopedia Ya Fiqh ya Kiislam inayochapishwa nchini

Kuwait basi inasema kua: ‘Imam Is-haq Ibn Rahawayh, ibn Taymiyyah na wengineo


452

ni wenye kua na mtizamo usemao kua: ‘Uhusiano wa kinasaba baina ya Mtoto wa

Zina na Mwanamme aliezini na Mwanamke ambae hajamuoa hua unathibitishwa

kwa sababu kuzini kwake nae kumethibitishwa tayari. Hivyo kama ilivyo katika

kunasibishwa kwa uhusiano wa Mama, basi na uhusuiano wa Mzinifu pia

unathibitishwa, na hivyo nasaba yake mtoto huyo kutopotea na kutodhurika

kutokana na kosa la aibu la dhambi ambayo halimhusu mtoto huyo, kama

anavyosema Allah Subhanah wa Ta’ala’’

‏﴿وَلاَ‏ تَزِرُ‏ وَازِرَةٌ‏ وِزْرَ‏ أُخْ‏ رَىٰ‏ ﴾

Wala taziru waziratun wizra okhra (Surat Al Isra 17:15 )

Tafsir: Na hakuna mbebaji atakaebeba mzigo wa mwenzake.

Ambapo mtizamo huu hua unalazimisha pia mirathi baina ya Mtoto na Mzinifu

huyo kuwepo kutokana na uthibitisho wa Nasaba, kwa sababu mirathi hua ni yenye

kusimamia misingi ya unasaba, na Wanazuoni hawa wamethibitisha hili katika hali

iliyotajwa.

Na mbali ya Hadith hio ya Jurayj lakini hata hivyo pia kuna hadithi isemayo kua

‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Watoto wanne

Wamezungumza ndani ya mkoba wa kubebea Watoto wachanga ambao ni : Mtoto

wa Msusi wa Fir’awn, Shahidi wa Nabii Yusuf, Mtoto wa kisa cha Jurayj na Isa Ibn

Maryam.’

Ambapo mbali ya hivyo lakini pia Allah Subhanah wa Ta’ala amemsifu Nabii Isa kabla

ya kuzaliwa kwake kua atakua ni mwenye kuzungumza hadi ukubwani mwake, katika

kipindi cha Kahlan ambacho ni kipindi baina ya Ujana na Utu Uzima. Kwani neno

Kahlan linatokana na neno Kahala ambalo hua linamanisha Kufukia Umri wa Kupea na

Kukomaa Kiakili yaani kuanzia baina ya miaka 30 hadi 60.

Na hii haimaanishi kua Nabii Isa atazungumza Ukubwani kama ilivyo kawaida ya

kuzungumza mimi na wewe kama tulivyo Ibn Adam wengine na hivyo kua hakuna mana

yeyote ndani yake maneno haya. La! Kwani aya haikumaanisha hivyo bali imeamaanisha

kua Nabii Isa atakua ni mwenye kuzungumzia kuhusiana na Kalimat Allah yaani maneno

ya Allah Subhanah wa Ta’ala tangu mara tu baada ya kuzaliwa kwake wakati yupo

kwenye Kitenga cha Mtoto Mchanga hadi atakapofikia ukubwani mwake.


453

Na hivyo hapa Allah Subhanah wa Ta’ala anabainisha kua Nabii Isa Ibn Maryam ataishi

na kupita umri wa miaka 40, na katka kipindi chote hicho basi atakua ni miongoni mwa

Minna al Salihiin yaani Waja wema wenye kufanya Mema.

Ambapo baada ya Malaika Jibril kumbainishia Maryam Bint Imran ujumbe wake huo

kuhusiana na Utukufu wa Tunukio hilo ambalo ni lenye Uzito mkubwa sana na hikma

kubwa sana ndani yake basi Maryam Bint Imran akatulia huku akitafakkari kuhusiana na

utukufu wa Tunukio hilo atakalojaaliwa kutokana na Utukufu wake mbele ya Allah

Subhanah wa Ta’ala na hivyo akawa ni mwenye kujawa na mshangao mkubwa zaidi

kutokana na Tunukio hilo kutoka kwa Mola wake.

Kwani ingawa tukio la mwanzo la kutokewa na Malaika Jibril mbele yake halikumshtua

wala kumshangaza sana Maryam Bint Imran lakini hata hivyo bashirio la ujumbe wake

zikamshtua na kumshangaza sana Maryam Bint Imran, kwa sababu ingawa yeye anamjua

Mola wake, na hivyo kujua kua ndie pekee mwenye uwezo wa kumjaalia kiumbe kua na

uwezo wa kupata Mtoto, lakini hua ni baada ya Mja huyo kua ni mwenye kuingiliana na

Mwanamme kama ni Mwanamke au kua ni Mwenye kuingiliana na Mwanamke kama

mja huyo ni Mwanamme, hata hivyo hajawahi yeye kusikia kua kuna Mwanamke ambae

amepata ujauzito bila ya kuingiliana na Mwanamme, sasa itakuaje kwa kwake yeye

ambae hana Mume, wala hajawa na hamu ya kua na Mume na wala hajawahi kua na

ukaribu wala kuingiliwa na Mwanamme yeyote kua ni mwenye kuja kupata Mtoto, bila

ya shaka haya ni masuali ambayo ni ya kimaumbile kwa kiumbe Ibn Adam hivyo

haishangazi kuona kua Maryam Bint Imran anauliza masuali haya kutokana na maumbile

yake.

Hivyo Maryam Bint Imran akadhidhirsha Mshangao wake huo wa kimaumbile baada ya

kutafakkar kwake na hivyo akauliza kama zinavyosema aya:

‏﴿قَالَتْ‏ أَنى َّٰ‏ يَكُونُ‏ لىِ‏ غُلاَمٌ‏ وَلمَْ‏ يمَْسَسْنىِ‏ بَشَرٌ‏ وَلمَْ‏ أَكُ‏ بَغِيّاً‏ ﴾

Qalat anna yakoonu lee ghulamun walam yamsasnee basharun walam aku

baghiyyan; (Surat Maryam 19:20)

Tafsir: Akasema (Maryam Bint Imran) kua: ‘Nitakua na Mtoto wa kiume mimi

wakati sijawahi kuguswa na mtu yeyote (Mwanamme) na wala mimi si Mwanamke

mwenye kutembea na Wanaume?’

Hapa tunaona kua Maryam Bint Imran anajitambulisha na kujitetea Mbele ya Malaika

Jibril kwa kusema kua yeye si Baghiya hivyo itakuaje apate Mtoto? ambapo neno

Baghiya hua ni lenye utokna na neno Bagha ambalo hua linamaanisha Kuvuka Mipaka,


454

Kufanya Uovu, Kuendekeza Matamanio, Kua Mwenye Kufanya Dhulma, Kutokua na

Haya, Kufanya mambo ya Aibu na pia hua inamanisha Kila Kitu ambacho si kitu Kiovu

tu kinachoonekana na kuhisikana na kuchukiwa na watu wengine lakini pia hua

kinamaanisha Kitu kiovu Kinachosababisha Madhara.

Neno Bagha ndio lililotoa neno Baghia ambalo hua linamaanisha pia linamaanisha kua

Uzinifu, Umalaya, Uasharati, Kuendekeza Matamanio.

Sultan Al Mutakkalimin Mujaddid Ad Din Imam Al Ghazali Al Thani Imam Fakhr Ad

Din Al Razi anasema kuhusiana na maneno haya ya Maryam Bint Imran kua: ‘Kwanini

hapa Maryam Bint Imran anasema kua yeye si Malaya? Jibu la suali hili ni kua

pale Maryam Bint Imran aliposema: ‘Sijawahi Kuguswa na Mwanamme’ alikua

akimaanisha kua: ‘Hajaolewa’ na hivyo ikabidi pia aongezee kwa kusema kua na

wala yeye si Mwanamke Malaya’

Hivyo baada ya kutoa hoja hio basi Malaika Jibril akasema kumwambia Maryam Bint

Imran kua:

‏﴿قَالَ‏ كَذٰ‏ لِكَ‏ قَالَ‏ رَب ُّكَ‏ هُوَ‏ عَلَى َّ هَينٌِّ‏ وَلِنَجْعَلَهُ‏ آيَةً‏ لِّلْن َّاسِ‏ وَرَحمَْةً‏ مِّن َّا وَكَانَ‏ أَمْ‏ راً‏

م َّقْضِيّاً‏ ﴾

Qala kadhaliki qala rabbuki huwa AAalayya hayyinun walinajAAalahu ayatan

lilnnasi warahmatan minna wakana amran maqdhiyyan; (Surat Maryam 19:21)

Tafsir: ‘Akasema (Malaika Jibril): ‘Kadhalika hivyo ndivyo alivyosema Mola wako:

‘Hivyo ni rahisi sana juu yangu mie’’Na tutamjaalia kua dalili kwa Watu na Rehma

kutoka kwetu, na ni Jambo ambalo tayari limeshatakiwa liwe’

Ambapo neno Hayyinun hua linatokana na neno Hana lenye kumaanisha Kua Rahisi,

Kua Jepesi, Kua na Udhaifu, Kufanyika kwa urahisi, Kua Kimya. Neno Hana pia ndio

lililotoa neno Ahana ambalo hua linamaanisha Kuchukiza, Kochokoza au Kuadhirisha.

Na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anabainisha kua kwake yeye kufanya hivyo

kumjaalia Maryam Bint Imran kupata Mtoto bila ya kukutana na Mwanamme hua ni

Jambo dogo na ni rahisi sana.

Kama vile alivyoweza kumjalia kupata Ujauzito Sarah Mke wa Nabii Ibrahim, Nabii

Zakarriya na Isha Bint Faqudh na pia Mzee Imran na Hannah Bint Faqudh pale


455

Wanawake wote hao walipokua tasa na waume zao wakiwa wazee sana. Allah Subhanah

wa Ta’ala anaendelea kumuelezea Nabii Isa Ibn Maryam katika aya hizi kwa kusema kua

Na atamjaalia kua ni dalili ya uthibitisho kwa Watu na Rehma kutoka kweke, kwani hilo

ni Jambo ambalo tayari limeshatakiwa liwe.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kumbainishia Nabii Muhammad Salallahu

Alayhi wa Salam juu ya habari za Ghayb kwa kina juu ya Maryam Bint Imran na

kubashiriwa kwake kushika Mimba ya Nabii Isa kua kunatokana na kutaka kwake yeye

iwe hivyo kwani yeye ndie Muumba wa kila kitu kama zinavyoendelea kufafanua aya za

Surat Al Imran kwa kusema:

‏﴿قَالَتْ‏ رَبِّ‏ أَنى َّٰ‏ يَكُونُ‏ لىِ‏ وَلَدٌ‏ وَلمَْ‏ يمَْسَسْنىِ‏ بَشَرٌ‏ قَالَ‏ كَذٰ‏ لِكِ‏ ٱهلل َُّ‏ يخَْلُقُ‏ مَا يَشَ‏ آءُ‏

إِذَا قَضَى ٰ أَمْراً‏ فَإِنم ََّا يَقُولُ‏ لَهُ‏ كُنْ‏ فَيَكُونُ‏ ﴾

Qalat rabbi anna yakoonu lee waladun walam yamsasnee basharun qala kadhaliki

Allahu yakhluqu ma yashao idha qadha amran fa-innama yaqoolu lahu kun

fayakoonu; (Surat Al Imran 3:47)

Tafsir: Akasema (Maryam Bint Imran): ‘Ewe Mola wangu itakuaje mimi niwe na

Mtoto, wakati sijawahi kuguswa na Mtu yeyote?’ Akasema (Allh Subhanah wa

Ta’ala): ‘Kadhalika hivyo ndivyo Allah anavyoumba atakacho, kwani anapotaka

jambo liwe basi hua ni mwenye kukiambia kitu hicho Kua na hivyo Kinakua’

Hapa tunaona kua kuna hali ya mtizamo tofauti ya mazingira ya mazungumzo

yaliyoelezewa na yale ya kwenye aya ya Surat Maryam 19:20 kwani wakati kule kulikua

kuna mazungumzo baina ya Maryam Bint Imran na Malaika Jibril katika aya hizi tunaona

kua moja kwa moja Maryam Bint Imran akiwa anazungumza na Mola wake yaani Allah

Subhanah wa Ta’ala kwa kurudisha hoja yake kwa Mola wake kutokana na maumbile

yake na hali ya mazingira yake anayoishi.

Na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anambainishia Maryam bint Imran kua katika tukio

hili, kutokana na Utukufu wake Maryam Bint Imran na utukufu wa Mtoto wake yaani Isa

Ibn Maryam basi kutakua na upekee wa Miujiza ya Kimaumbile juu ya kile

kilichokadiriwa kiwe kua kitakua, kama inavyotakiwa kiwe na hii ni kwa sababu ya

Malengo na makusudio ya hicho kinachotakiwa kiwe, yaani Tunukio la kile kilicho bora

asichokitarajia na bila ya shaka Allah Subhanah wa Ta’ala hakutuwacha tukawa ni wenye

kujiuliza bila ya kujua ilitumika njia gani kufanikisha hilo kwani Qur’an inatubainishia

njia iliyotumia katika kumtunukia kwake huko kutokana na maumbile yake katika aya

isemayo:


456

‏﴿وَمَرْيمََ‏ ٱبْنَةَ‏ عِمْرَانَ‏ ٱل َّتيِ‏ ۤ أَحْصَنَتْ‏ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ‏ مِن ر ُّوحِ‏ نَا وَصَد َّقَتْ‏

بِكَلِمَاتِ‏ رَب َّهَا وَكُتُبِهِ‏ وَكَانَتْ‏ مِنَ‏ ٱلْقَانِتِينَ‏ ﴾

Wamaryama ibnata AAimrana allatee ahsanat farjaha fanafakhna feehi min

roohina wasaddaqat bikalimati rabbiha wakutubihi wakanat mina alqaniteena

(Surat At Tahrim 66:12)

Tafsir: Na Maryam Bint Imran ambae alijihifadhi sehemu zake za Siri, kisha

tukampulizia ndani yake Roho kutoka kwetu, na akathibitisha Kauli ya Mola wake na

Vitabu vyake, na alikua ni miongoni mwa wenye Kumcha Mungu.

Tunapoiangalia Ayah hii basi tunaona kua imetumia neno Ahssanat ambalo hua

linamaanisha Kukilinda Kitu, Kukihifadhi kisipatikane, au Kisiharibiwe, Kukiwekea

Ngao au Ngome Imara.

Na pia ikatumia neno Farjaha ambalo hua linatokana na neno Faraja linalomaanisha

Kufungua, Uwazi, Ufa, Kutanua, Kuachia wazi sehemu iliyo baina ya Vitu viwili na pa

humaanisha Sehemu ya Siri ya Mwanamke baina ya miguu miwili.

Na hivyo Aya kua ni zenye kuweka wazi kua Maryam Bint Imran alikua ni mwenye

kujihifadhi na kujilinda kikweli hasa sehemu zake za Siri kwa sababu Allah Subhanah

wa Ta’ala sehemu hizo ni Amanah ambayo amekabidhiwa na kuamriwa kua kama

ataitumia basi na aitumie kulingana na masharti yake aliyoyashurutisha Allah Subhanah

wa Ta’ala juu ya Amanah hio.

Na kisha aya ikaendelea kubainisha namna alivyotunukiwa Maryam Bint Imran

kuhusiana na Tunu hio kwa kusema baada ya Ahsanat Farjaha kua Fanafakhna Feehi

Min Roohina yaani Kisha Tukampulizia Ndani yake Roho kutoka kwetu, ambapo hapa

hua kunamaanisha kua aidha Maryam Bint Imran alipuliziwa Roho hio kutoka kwa Allah

Subhanah wa Ta’ala ndani ya Mwili wake kwa Ujumla au kwa kupitia katika sehemu

zake za Siri ambazo zimehifidhiwa kama zilivyozungumziwa hapa au kama

walizozisema Wanazuoni yaani kwa juu baina ya Mabega na Shingo yake, wa Allahu

Aaalam.

Na ingawa hivyo ndivyo hali ilivyokua na haikuwahi kutokea kabla yake wala baada

yake kwa Ibn Adam wengine lakini hata hivyo tunapoangalia kwa upande mwengine basi

tunaona kua katika wakati wa kipindi chetu Wanasayansi wamegundua kua hali hii ya


457

uzazi hua inatokea pia kwa aina fulani ya Nyoka, Samaki na baadhi ya Wadudu ambao

wanao uwezo wa kushika Mimba na kupata watoto bila ya kuingiliana.

Baada ya Maryam Bint Imran kupiliziwa Roho hio ndani yake basi Allah Subhanah wa

Ta’ala anaendelea kumbainishia Maryam Bint Imran kuhusiana na Darja na majukumu

atakayokua nayo Nabii Isa baada ya kuzaliwa kwake kwa kuelezea kama ilivyosema

Surat Al Imran katika aya zifuatazo:

‏﴿وَيُعَلِّمُهُ‏ ٱلْكِتَابَ‏ وَٱلحِْكْمَةَ‏ وَٱلت َّوْرَاةَ‏ وَٱلإِنجِْيلَ‏ ﴾

WayuAAallimuhu alkitaba waalhikmata waalttawrata waal-injeela; (Surat Al Imran

3:48-51)

Tafsir: Na (Allah Subhanah wa Ta’ala) atamfundisha Kitabu na Hikma na Taurat na

Injil.

Ambapo katika aya hii tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anaahidi kua

atamfundisha Nabii Isa Ilm ya Kitabu, ambapo ndani yake ndio mna Ilm za vitabu

walivyoletewa Mitume wengine waliotangulia kabla yake, na hapa ndio tunaona kua kwa

upande mwengine basi tunapozungumzia somo la I’lm Ul Huruf ambalo linatokana na

Vitabu vya Nabii Idrisa Alayhi Salam basi Shaykh Al Akbar Imam Abu Bakr Ibn Arabi

ana mtizamo wa kua ni somo linalojulikana pia kwa jina la I’lm Issawi.

Na pia akaahidi kua atamfundisha na Hikma, ambapo kulingana na Bahr Ul Ilm Abd

Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi anasema kua: ‘Hikma iliyokusudiwa hapa

hua inamaaanisha Hukmu na Sharia za yaliyohalalishwa na yaliyoharamishwa.’

Na kuna wasemao kua Hikma iliyozungumziwa hapa hua inamaanisha Mitizamo tofauti

kuhusiana na Ilm ya Dini ya Kiislam kupitia katika Sunna za Mitume wengine wote

waliotangulia kabla yake.

Kisha aya ikamalizia kuhusiana na ahadi ya kupewa kwa Nabii Isa Ilm ya Taurat na Injil

ambapo ingawa Taurat alishushiwa Nabii Musa kwa ajili ya kuwaongoza Watu wa Bani

Israil lakini Allah Subhanah wa Ta’ala aliahidi kua atamfundisha Nabii Nabii Isa Taurat

pia na Hukmu zake, Hivyo Nabii Isa alikua na Ilm ya Taurat na Injil pia zote mbili

sambamba, ambapo tofauti yake ni kua Maamrisho na Makatazo yaliyokuwemo kwenye

Injil yalikua ni mepesi kuliko yale yaliyokuwemo kwenye Taurat.


458

Kisha aya zinaendelea kutuelezea namna Allah Subhnah wa Ta’ala alivyokua

akimwambia Maryam Bint Imran kuhusiana na Miujiza ya Allah Subhanah wa Ta’ala

kwa Ruhi wake Isa Ibn Maryam kua:

‏﴿وَرَسُولاً‏ إِلىَٰ‏ بَنىِ‏ ۤ إِسْرَائِيلَ‏ ِ أَنىّ‏ قَدْ‏ جِ‏ ئْتُكُمْ‏ آبِيَةٍ‏ مِّ‏ ن ر َّبِّكُمْ‏ أَنىّ‏ ِۤ أَخْ‏ لُقُ‏ لَكُ‏ مْ‏ مِّ‏ نَ‏

ٱلطِّينِ‏ كَهَيْئَةِ‏ ٱلط َّيرِْ‏ فَأَنفُخُ‏ فِيهِ‏ فَيَكُونُ‏ طَيرْ‏ اً‏ إبِِذْنِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَأُبْرِئُ‏ ٱلأَكْمَهَ‏ وٱلأَ‏ بْرَ‏ ‏َص

وَأُحْيِى ٰ ٱلْمَوْتَى إبِِذْنِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَأُنَبِّئُكُمْ‏ بمَِا أتَْكُلُونَ‏ وَمَا تَد َّخِ‏ رُونَ‏ فىِ‏ بُيُوتِكُمْ‏ إِن َّ ‏ِفى

ذٰلِكَ‏ لآيَةً‏ ل َّكُمْ‏ إِن كُنتُم م ُّؤْمِنِينَ‏ ﴾

Warasoolan ila banee isra-eela annee qad ji/tukum bi-ayatin min rabbikum annee

akhluqu lakum mina altteeni kahay-ati alttayri faanfukhu feehi fayakoonu tayran

bi-idhni Allahi waobri-o al-akmaha waal-abrasa waohyee almawta bi-idhni Allahi

waonabbi-okum bima ta/kuloona wama taddakhiroona fee buyootikum inna

fee dhalika laayatan lakum in kuntum mu/mineena (Surat Al Imran 3:49)

Tafsir: Na tutamfanya Isa kua Mtume wa watu wa Bani Israil (Mwenye Kusema)

‘Nimekuja kwenu nikiwa na Vithibitisho kutoka kwa Mola wenu. Hivyo

nitakutengenezeeni kutokana na udongo kua kama Ndege na kisha nitampulizia, na

atakua Ndege aliekua hai kwa idhini ya Allah (Subhanah wa Ta’ala). Na

nitamponesha aliezaliwa Kipofu na mwenye Ukoma na nitawakhuisha waliokufa kwa

Idhini ya Allah, na nitakuambieni mtakachokula na mlichohifadhi Majumbani

mwenu. Kwa hakika katika haya kuna Vithibitisho kama kweli nyinyi ni wenye

Kuamini’

Naam, hii ni miongoni mwa aya ambazo zinatuonesha na kuthibitisha kua Nabii Isa

alikua ni Nabii na Mtume wa watu wa Bani Israil kwa ajili ya kuja kuendeleza na

kusimamia maamrisho yaliyomo ndani ya Taurat na Injil, na hivyo Allah Subhanah wa

Ta’ala anawataka watu wa Bani Israil kutokana na vithibitisho vyake atakavyokuja

navyo basi wawe ni wenye kufuata maamrisho yake kama kweli wao ni wenye

kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala.

Ambapo ndani yake vithibitisho hivyo pia ni Miujiza ya kua na uwezo wa kutengenezea

Ndege wa Udongo na kisha atakapompulizia basi Ndege huyo atakua hai kwa Idhini ya

Allah Subhanah wa Ta’ala na kuruka hewani.


459

Ambapo hii ni kwa sabau Nguvu za Kiroho za Nabii Isa ni zenye uwezo mkubwa sana

kwa sababu maumbile ya Roho yake yanatokana na kupuliziwa tumboni Mama yake

moja kwa moja, hivyo ni mwenye kua na uwezo mkubwa wa kiathari katika uwezekano

wa kuwasiliana moja kwa moja na Roho za viumbe wengine tofauti na walivyo viumbe

wengine wa kawaida.

Kiasi ya kua kwake yeye Nabii Isa ilikua rahisi kuufinyanga Udongo na kisha

Kumuomba tu, idhini ya Allah Subhanah wa Ta’ala ya kua baada ya kuupulizia Udongo

bsi uingizwe ndani yake Roho ya ndege ambayo iliyokua tayari imeshaumbwa na

inasubiri kuingizwa kwenye mwili wake ndege huyo alioufinyanga Nabii Isa. Na hii pa

hua kwa waliokufa pia pale alipopewa uwezo wa Kuwafufua kutokan na Idhini ya Allah

Subhanah wa Ta’ala

Na pia atakua na uwezo wa Kumponesha Kipofu kwa njia ya kumuwekea mkono na

kumpangusa usoni mwake, na pia kuwaponesha wanaoumwa na Ukoma kwa

kuwapangusa sehemu za mwili zilizoathirika na Maradhi hayo ambapo nao watakua ni

wenye kupona kutokana na mpanguso huo wa mikono yake, na hili pia hua ni miongoni

mwa maana ya jina lake la Al Masih.

Hii ni Miujiza maalum kwa ajili ya Nabii Isa Ibn Maryam ambayo Allah

Subhanah wa Ta’ala alimjaalia kua na uwezo nayo, kulingana na mazingira yake

atakayokua akiishi katika jamii za watu wao waliokuwepo katika wakati huo,

kwani huu ulikua ni wakati wa umahiri mkubwa sana wa fani ya Utabibu,

ambapo hata hivyo mbali ya kua na Wataalamu wa fani ya tiba lakini hakukua

na watu wanaoweza kutibu maradhi kama hayo, ambapo hii inakua kama vile

ilivyokua katika wakati wa kipindi cha Nabii Musa wakati watu wa Misri na

Bani Israil walipokua wamebobea katika fani ya Uchawi, hivyo Allah Subhanah

wa Ta’ala akampa Nabii Musa Miujiza ya Fimbo na myengineo, ili kukabiliana

nao na kuwathibitishia watu wake ukweli wa Ujumbe wake.

Kisha Allah Subhnah wa Ta’ala anasema kuhusiana na Muujiza mwengine mkubwa

atakaouonesha Nabii Isa ni kua atakua ni mwenye Kufufua watu waliokufa,

kuwahalalishia baadhi ya mambo ambayo waliharamishwa watu wa Bani Israil ndani ya

Taurat, na hivyo kua ni mwenye kuthibitisha juu ya kile alichokuja nacho kwenye Injil

na hivyo kutilia mkazo kua watu hao wa Bani Israil kua wanatakiwa warudi kwa Mola

wao, kama zinavyosema aya:


460

‏﴿وَمُصَدِّقاً‏ لِّمَا بَينَْ‏ يَدَى َّ مِنَ‏ ٱلت َّوْرَاةِ‏ وَلِأُحِ‏ ل َّ لَكُمْ‏ بَعْضَ‏ ٱل َّذِى حُرِّمَ‏ عَلَيْكُمْ‏

وَجِ‏ ئْتُكُمْ‏ آبِيَةٍ‏ مِّن ر َّبِّ‏ كُ‏ مْ‏ فَ‏ ٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَأَطِيعُ‏ ونِ‏ ‏۞إِن َّ ٱهلل ََّ‏ رَبىِّ‏ وَرَب ُّكُمْ‏ فَٱعْبُدُوهُ‏ هَٰذَ‏ ا

صِرَاطٌ‏ م ُّسْتَقِيمٌ‏ ﴾

Wamusaddiqan lima bayna yadayya mina alttawrati wali-ohilla lakum baAAdha

alladhee hurrima AAalaykum waji/tukum bi-ayatin min rabbikum faittaqoo Allaha

waateeAAooni; Inna Allaha rabbee warabbukum faoAAbudoohu hadha siratun

mustaqeemun (Surat Al Imran 3:50-51)

Tafsir: (Na atasema Nabii Isa): ‘Nimekuja kuthibitisha kile ambacho kimekuja kabla

yangu kilchomo ndani ya Taurat na kukuhalalishieni sehemu ambayo imeharamishwa

kwa ajili yenu. Na nimekuja kwenu na Uthibitisho kutoka kwa Mola wenu. Hivyo

Muogopeni Allah na Nifuteni. Kwa hakika Allah ni Mola wangu na Mola wenu hivyo

Muabuduni (yeye peke yake msimshirikishe). Hii ndio njia iliyo sahih’

Ambapo hapa tunaona kua Nabii Isa atakua ni mwenye kuwahalalishia watu wa Bani

Israil baadhi ya vile vilivyoharamishwa kwenye Taurat na hivyo basi hii haimaanishi kua

Vitabu viwili hivi Taurat na Injil kua vinapingana la, bali kuna baadhi ya Maamrisho ya

Taurat yamekuja kubatilishwa na baadhi ya maamrisho yaliyomo ndani ya Injil. Na hivyo

kumaanisha kua Watu wa Bani Israil walikua wanatakiwa wawe ni wenye kufuata

mitizamo mipya iliyomo kwenye Injil.

Hivyo baada ya Maryam Bint Imran kubainishwa yote hayo, juu ya Utukufu na umuhimu

wa Majukumu ya Mtoto wake huyo na namna atakavyopatikana ndani ya mwili wake

basi Malaika Jibril akaipulizia Nguo yake Maryam Bint Imran na kuna Mtizamo usemao

kua Malaika Jibril alimpulizia Maryam Bint Imran kwenye Shingo yake na hivyo

Mpulizio huo ukaingia Mwilini mwake, na katika hali ya kimiujiza basi Mwili wake

ukabeba ujauzito wa Isa Ibn Maryam kama anavyosema Allah Subhana wa Ta’ala katika

Qur’an:

‏﴿فَحَمَلَتْهُ‏ فَٱنْتَبَذَتْ‏ بِهِ‏ مَكَاً‏ قَصِيّاً‏ ﴾

Fahamalat-hu faintabadhat bihi makanan qasiyyan (Surat Maryam 19: 22)


461

Tafsir: Na kisha ikatunga na kuibeba (Mimba hio ya Isa Ibn Maryam) na akajitenga

pamoja nae (Isa Ibn Maryam ndani ya Mwili wake) katika makazi ya kipekee.

Ambapo anasema Imam Wahb Ibn Munabih kua: ‘Wakati Mayram Bint Imran

alipobeba Ujauzito wa Isa Ibn Maryam basi dalili za ujauzito zikaanza kujionesha

na hivyo Maryam Bint Imran akahama kutoka Nasira na kuhamia katika maeneo

ya Bayt Al Lahm (Nyumba ya Nyama au Bethlehem) ili kua mbali na watu wake

wengine’

‘Na mara ya kwanza Maryam Bint Imran alipomhisi Isa Ibn Maryam ndani ya

mwili wake, ilikua yuko pamoja na Yusuf wakati walipokua wakielekea kwenye

Nyumba ya Ibada iliopo kwenye Mlima wa Zayuni, kwani wao ndio waliokua

wasimamizi wa Nyumba hio, na ilikua hakuna watu wacha Mungu zaidi yao. Hivyo

Yusuf alipojua kuhusiana na Ujauzito huo basi alishtuka sana, kwani hili lilikua ni

jambo la aibu sana kwake na kwa Maryam Bint Imran, na hakujua achukue hatua

gani.’

‘Kwani alipokua akitaka kumtuhumu, basi alishindwa kutokana na Ucha Mungu

wake, na kutokua na hali ya kutofanya makosa kwake, na kutokana na kua kila

wakati alikua pamoja nae, na hakuwahi hata mara moja kumuona akifanya

dhambi, hivyo alipoona kua ujauzito unaonesha basi akaamua kumwambia: ‘Kuna

jambo ambalo limo akilini mwangu kuhusiana nawe, na nimejitahid kulificha na

kujizuia lakini nimeshindwa, hivyo nimeona kua bora nilidhihirishe ili nipunguze

uzito kifuani mwangu. Hivyo niambe ewe Maryam, hivi Jee Mti huweza kuota bila

ya kupandikizwa kwa mbegu?’

Maryam akajibu: ‘Naam’

Yusuf akauliza: ‘Hivi Jee Mmea unaweza kuota bila Mvua?’

Maryam akajibu: ‘Naam!’

Yusuf akauliza: ‘Hivi jee inawezekana kuwepo kupatikana kwa Mtoto bila ya

kuwepo kwa Baba?’

Maryam akajibu: ‘Hivi Yusuf Jee wewe hujajifunza kua Allah Subhnah wa Ta’ala

aliisababisha Miti kukua bila ya kuwepo Mbegu zake katika siku aliyoiumba Miti

hio na hivyo Miti yote iliyofuatia ilitokana na mbegu zilizozalishwa na Miti hio?

Na Jee hukujifunza kua Allah Subhanah wa Ta’ala aliifanya Miti ikue bila ya

kuwepo Maji? Na kisha ndio makadirio ya Allah Subhanah wa Ta’ala yakafanya

Mvua kua ndo Uhai wa Miti baada ya kuiumba katika hali tofauti? Au wewe


462

unasema kua Allah Subhana wa Ta’ala hawezi kuiotesha Mimea hadi apate msaada

wa Maji?’

Hivyo Yusuf akasema: ‘La kwa hakika mimi sisemi hivyo bali nnasema kua: ‘Allah

Subhanah wa Ta’ala anaumba akitakacho na anapotaka kitu kiwe basi husema kwa

kukiambia tu Kua na Kinakua’’

Hivyo Maryam Bint Imran akasema: ‘Sawa ila Jee hukujifunza wewe kua, Allah

Subhanah wa Ta’ala alimuumba Adam na Hawa bila ya kuwepo kwa Mke na

Mume?’ Yusuf akasema: ‘Naam bila ya Shaka!’ kisha baada ya kujibu suali hilo

basi Yusuf ikamjia akilini kua kwa vyovyote vile itakavyokua basi hali aliyokua

nayo Maryam Bint Imran itakua ni moja kwa moja kutokana na Miujiza ya Allah

Subhanah wa Ta’ala juu yake Maryam Bint Imran, na hivyo haikubaliki kwake

yeye Yusuf kua ni mwenye kumuuliza Maryam Bint Imran kuhusiana na hali

aliyokua nayo.’

Hivyo habari hii ya Ujauzito wa Maryam Bint Imran kawa ni siri ndani ya familia yake

yaani baina yake yeye Yusuf na Nabii Zakarriyah mkewe ambae ni Isha Bint Faqudh

kwani watu wa Bani Israil wakijua basi watasema kua Yusuf amezini nae Maryam Bint

Imran kwa sababu mda wote wako pamoja na Maryam hakutani na Mwanamme yeyote

isipokua na Yusuf ambae ndie Mlezi wake.

Siku moja Maryam Bint Imran alienda kumtembelea Isha Bint Faqudh ambapo katika

kipindi hiki Isha bint Faqudh alikua na Ujauzito wa Nabii Yahya. Hivyo Maryam Bint

Imran aliposalimiana na Isha Bint Faqudh basi Isha Bint Faqudh akasema: ‘Hakika mimi

nnahisi kua hiki kilichomo ndani ya tumbo langu kinakiinamia kilichomo ndani ya

Tumbo lako.’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala alielezea habari hii ya Nabii Yahya kua ni mwenye

kumsadikisha Nabii Isa Ibn Maryam pale aliposema kumwambia Nabi Zakarriyah:

‏﴿أَن َّ اهلل ََّ‏ يُبَشِّ‏ رُكَ‏ بِيَحْيَى ٰ مُصَدِّقاً‏ بِكَلِمَةٍ‏ مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَسَيِّداً‏ وَحَصُوراً‏ وَنَبِيّاً‏ مِّ‏ نَ‏

ٱلص َّالحِِينَ‏ ﴾

Anna Allaha yubashshiruka bi Yahya musaddiqan bikalimatin mina Allahi

wasayyidan wahasooran wanabiyyan mina alssaliheena; (Surat Al Imran 3:39-41)


463

Tafsir: ‘Hakika Allah anakubashiria (Mtoto) Yahya kuthibitisha Kauli kutoka kwa

Allah (Nabii Isa), na mja mwema mwenye cheo, na msafi asiekua na dhambi na Nabii

na Miongoni mwa Waja wema’

Kisha baada ya hapo Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Maryam Bint Imran kua:

‘Ukijifungua miongoni mwa Watu wako basi watakusimbulia na kukufukuza na

kukupiga mawe na kutaka kukuua wewe na Mtoto wako, na hivyo bora hama

kutoka katika Mji huo.’

Ambapo kwa upande wa Imam Abd Rahman Al-Kalbi, basi yeye anasema kua: ‘Allah

Subhanah wa Ta’ala alimwambia Yusuf kua kama Maryam akijifungua basi watu

watamuua kwa sababu watasema kua amezini hivyo hameni’

Hivyo Maryam Bint Imran akamwambia Yusuf kuhusiana na mtizamo huo, na hivyo

Yusuf akamwambia Maryam bora wahame kwenye Mji huo wa Nasira (Nazareti) ulioko

Kaskazini mwa ardhi ya Falestina, waelekee katika Mji mwengine kusini mwa Ardhi ya

Falestina, na hivyo siku ya pili alfajir mapema kabla ya watu hawajaamka wakatoka

katika Mji huo na kuelekea katika ardhi ya Bethlehem.

KUZALIWA KWA NABII ISA IBN MARYAM

Tunapoangalia kitabu cha Biblia basi tunaona vinasema kua wakati Malaika Jibril

alipomshukia Maryam Bint Imran kumbashiria kuhusiana na kutunukiwa kwake Ujauzito

wa Isa Ibn Maryam na Allah Subhanah wa Ta’ala basi tunaona kua ilikua ni katika

kipindi cha mwishoni kabisa cha Kipupwe cha Mwezi wa Adar ambao ni mwezi wa 6

katika kalenda ya Kiyahudi ambao nao hua ni wenye kufuatiwa na Mwezi wa Nisan

ambao ni mwezi wa 7 wa Kiyahudi ambapo ingawa Mayahudi hua wanatumia Nambari

za miezi badala ya Majina kwani mfumo wa Majina ya Miezi iliyokua ikitumika katika

kipindi hicho ilikua ni yenye kua na asili ya watu wa Iraq katika Ardhi ya Babylon ambao

ndio waliouhamishia Jerusalem baada ya wao kua ni watawala wa ardhi ya Mayahudi, na

hivyo wakawa wanatumia Kalenda inayotokana na asili yao.

Hivyo ili tufaham zaidi basi na tuangalie inavyoonesha kwenye mpangilio wa Kalenda

ya Miezi ya Kislam, Kiyahud na Kikristo hapo chini:

KALENDA ZA MIAKA ZA DINI KUU DUNIANI

KIISLAM KIYAHUDI KIKRISTO

Muharram Tishri January

Safar Heshvan February


464

Rabi Al Awwal Kislev March

Rabi Al Thani Tebet April

Jummada Al Awwal Shebat May

Jummada Al Thani Adar June

Rajab Aviv/Nisan July

Shaban Iyar August

Ramadhan Sivan September

Shawwal Tamuz October

Dhul Qaadah Ab November

Dhul Hijjah Elul December

Kwa maana hio basi tunapoiangalia Kalenda hii basi tunaona kua kama Malaika Jibril

alimbashiria Maryam Bint Imran kutunukiwa mtoto katika mwezi wa Adar basi kama

ikiwa ujauzito huo ulichukua miezi 9, basi Nabii Isa alizaliwa mnamo mwezi wa Heshvan

au Kislev yaani mwezi wa February au March na ndio maana kuna baadhi ya watafiti

wanasema kua Nabii Isa alizaliwa tarehe 28 March.

Na pia kuna wasemao kua alizaliwa tarehe 6 April, na hii pia ni kutokana na Imani ya

watu waliotangulia hapo kabla ya Kua Mitume hua ni wenye kufariki katika siku ambayo

walizaliwa. Ambapo kwa upande wa Waislam tunaamini kua Nabii Isa hakufariki

kulingana na vithibitisho tutakavyoviangalia hapo baadae lakini alisulubiwa tarehe 6

April.

Na hapa ndio tunaona tofauti ya kwanini Wakristo wakawa ni wenye kusheherekea

sikukuu ya Kuzaliwa kwa Nabii Isa tarehe 25 December ambayo kwa mara ya kwanza

ilianza kusheherekewa mnamo mwaka 725 C.E baada ya Kusulubiwa Nabii Isa, na hii ni

kwa sababu ya kua ni tarehe 25 December hua ni siku yenye kujulikana kama siku ya

Jua.

Kwani hii hua ndio siku ambayo masaa ya siku yanaaza kuongezeka ukubwa, kwa sababu

katika nchi za Baridi basi kinapoingia Kipindi cha Baridi Mchana hua mfupi na Usiku

hua mkubwa, hivyo kuanzia tarehe 25 December ndio Jua hua linaanza kuongezeka

kutokana na mabadiliko ya Nyakati za Muangaza wa Jua, hivyo Mapagani waikua

wakisema kua hii ni siku ya kuzaliwa kwa Jua na kwa kua siku hii ilikua inasheherekewa

na Mapagani wengi wa Scandinavia, Rome, Mashariki ya Kati, India, China n.k

Hivyo Wakuu wa Kanisa wakaamua kua bora siku hii ya tarehe 25 December ambayo ni

siku ya Sikukuu ya Jua kua inasibishwe na kuzaliwa kwa Nabii Isa kutokana na kua wengi

miongoni mwao walikua wakiadhimisha siku hio na pia wao ni wenye Imani ya kua Nabii

Isa ni mwenye nguvu kama ya Jua kwa Ulimwengu na ndio maana hua wanamwita pia

kwa jina la Jua la Uongofu.


465

Hivyo katika Alfajiri moja ya mwaka wa 65 baada ya Mfalme Aleksandriyah kuiteka

Ardhi ya Babylon katika wakati wa baina ya Mwezi wa Heshvan na Kislev yaani baina

ya mwezi wa February na March basi Yusuf na Maryam Bint Imran wakatoka katika

ardhi ya Nasira (Nazaret) ambayo iko katika maeneo ya Kaskazini na kuelekea kusini

mwa ardhi ya Falestina, ambapo katika siku ya 5 ya safari walipochoka siku hio wakaona

kua bora Maryam Bint Imran apumzike kutokana na hali yake aliyokua nayo. Kutokana

na Maumivu ya uchungu aliyokua akiyahisi, hivyo wakapiga kambi katika sehemu

ambayo kulikua na Mtende uliokauka ambao haukua na Tende kwani hata majani yake

yalikua ni makavu, sehemu hii ilikua ikijulikana kama Bayt Al Lahm (Bethlehem).

Allah Subhanah wa Ta’ala anaielezea hali ilivyokua mara baada ya Yusuf na Maryam

Bint Imran walipofika katika eneo hili kwa kusema:

‏﴿فَأَجَآءَهَا ٱلْمَخَاضُ‏ إِلىَٰ‏ جِ‏ ذْعِ‏ ٱلن َّخْلَةِ‏ قَالَتْ‏ يٰلَيْتَنىِ‏ مِت ُّ قَبْلَ‏ هَٰذَا وَكُنتُ‏ نَسْياً‏

م َّنسِ‏ يّاً‏ ﴾

Faajaaha almakhadhu ila jidhAAi alnnakhlati qalat ya laytanee mittu qabla hadha

wakuntu nasyan mansiyyan; (Surat Maryam 19:23)

Tafsir: Yakamjia Machungu ya Uzazi yakampelekea kwenye shina la Mtende, na

akasema: ‘Ya Laiti! Bora ningekufa mimi kabla ya haya na nikawa sahauliko

lililosahauliwa zamani sana’

Ambapo tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anaielezea hali aliyokua akiihisi

Maryam bint Imran ndani ya Mwili wake Mtukufu kua ni Almakhadhu, ambalo ni neno

linalotokana na neno Makhadha ambalo hua linamaanisha Kuchanganya kitu kwa nguvu,

Kutikisa au Maumivu ya mwili yanayotokana na Uchungu wa Mja mzito.

Hii hua ni hali ambayo anaipata Mwanamke aliekua na ujauzito kutokana na Mwili wa

Mwanamke huyo kua tayari unataka kukitoa nje kiumbe kilichokuwemo ndani ya mwili

wake kutokana na kua Mda wa kutoka nje ya mwili wake na kuingia Duniani kwa kiumbe

huyo na kuishi maisha yake ya kujitegemea umewadia. Ambapo kwa kimaumbile basi

Mfupa wa kiuno wa Mwanamke hua ni mpana kuliko wa Mwanamme, na hii ni kwa

sababu ya kumuwezesha kubeba Mtoto ndani ya mwili wake na kukaa kwa urahisi.

Na kwa upande mwengine basi mifupa ya Mapaja ya Mwanamke pia kwa juu hua

imetanuka zaidi tofauti na ya Mwanamme, kutokana na upana wa Mfupa wa Kiuno chake

Mwanamke na mfumo wa mpangilio wa viungo vya mifupa yake katika maeneno hayo,

na hii pia humuwezesha Mwanamke kua na uwezo wa kubana zaidi miguu yake katika


466

wakati wa kukaa na pia pale inapohitajika kujilinda na madhara ya wanaotaka

kumuingilia kimwili bila ya ridhaa yake kwani kutanuka kwa viunganisho vya mifupa ya

mapaja yake kwa juu kuanzia kiunoni mwake kunapelekea kuingia ndani kwa viungo vya

mifupa ya magoti yake na hivyo kumuwezesha kirahisi kukutanisha magoti yake na

kubana mapaja yake, katika kukaa kwake na hapo hapo upana huo hua ni pambo la

kumfanya awe ni mwenye kuvutia maumbile yake mbele ya kiumbe mwenza wake yaani

Mwanamme.

Hivyo kutokana na sifa ya Ukamilifu wa Maumbile Ibn Adam, basi Allah Subhanah wa

Ta’ala ameujaala mwili wa Mwanamke kua ni wenye uwezo wa kujitayarisha kwa kila

hatua kwa ajli ya kubeba mtoto ndani yake na kisha kumtoa kwa kujifungua pale mda wa

kufanya hivyo unapowadia, kwa kumtayarishia njia Mtoto huyo ili atoke nje yake kwa

salama na amani, na hivyo mwili huo hua ni wenye kutanua mifupa ya nyonga na kiuno

huku fuko la uzazi likiwa na kazi ya kujibinya kwa kukaza na kuachia kwa ajili ya

kumsukuma mtoto aelekee kwenye njia yake ya kimaumbile kutoka nje ya Mwili, hii hua

ni hali ya maumivu inayofanana na kama maumivu ya kufungwa mpira na kukazwa sana

ndani ya fuko la uzazi, ambapo kwa baadhi hua wanainasibisha hali hii ya kujibinya kwa

fuko la uzazi la kumsukuma mtoto kuelekea chini katika njia yake kua kama vile mtu

unaekandamiziwa ndani kwa ndani ya tumbo lako na kitu chenye ncha kali sana.

Maumivu haya hua ni yenye kuchukua mda wa sekunde 45 hadi 60 ndani ya kipindi cha

kila dakika 10 kwa masaa kadhaa hadi pale njia ya kutokea mtoto yaani sehemu za Sri za

Mwanamke ziakapotanuka na kufikia kua na upana wa sentimita 10 ambapo utanukaji

wa kila sentimita moja huchukua saa moja mpaka mawili, inategemea na maumbile ya

Mwanamke na pia inategemea ni mtoto wa ngapi, kwani baada ya mtoto wa kwanza basi

mwili wa Mwanamke hua umeshazoea na hivyo hua haichukui mda mrefu kama masaa

matano ambapo hua na tofauti kubwa na pale inapokua ndio kwanza mara ya kwanza na

kwa mtoto wa kwanza kama hali ilivyokua katika wakati huu kwa Maryam Bint Imran.

Ambae kutokana na kuhisi maumivu hayo, kwa mara ya kwanza basi ndio maana akawa

ni mwenye kusema kutokana na machungu hayo kua: ‘Ya laytanee mittu qabla hadha

wakuntu nasyan mansiyyan yaani ‘Ya Laiti! Bora ningekufa mimi kabla ya haya na

nikawa sahauliko lililosahauliwa zamani sana’ (Surat Maryam 19:23) yaani alikua

anaona bora angekua ni mwenye kufariki kabla ya hata ya kufikiwa na jambo hilo

lililomtokea katika wakati huu, kwani bora angekua ameshakufa na ameshasahauliwa

zamani sana, kuliko kuhisi maumivu hayo anayoyahisi katika wakati huo.

Hali hii ya Maumivu ya kimaumble hua ni yenye kusababishwa na ufanyaji kazi kamilifu

wa Mifumo mbali mbali ya ndani ya Mwili wa Mwanamke katika utekelezaji wake wa

kimaumbile ikiwemo uzalishwaji wa kemikali muhimu zifuatazo:


467

Prostoglandin ambayo huzalishwa kabla ya kuzaliwa kwa mtoto kwa ajili ya kutayarisha

urahisi wa uzalishwaji wa kemikali nyeingine iitwayo Oxytocin. Katika mazingira haya

ya mwili basi kemikali za Oxytocin hua na kazi ya kuubinya mfuko wa uzazi na kumtoa

nje mtoto anapokua tayari kutoka na pia hua na kazi ya kuurudisha Mfuko wa uzazi katika

hali yake ya kawaida kwa ajili ya matayarisho ya kubeba mtoto mwengine, na hapo hapo

husaidia katika kuzalisha chakula cha Mtoto baada ya kuzaliwa kwake yaani Maziwa ya

Mama yake, na kusababisha hisia za mvuto wa mapenzi na kutotaka kuachana baina ya

Mama na Mtoto wake.

Katika kipindi hiki pia mwili wa mwanamke hua ni wenye kuzalisha kemikali ziitwazo

Relaxin ambazo huutanua mfuko wa Uzazi kwa ajili ya kujifungua na pia kulivunja chupa

la mtoto ndani ya fuko la Uzazi na kutanua mifupa ya kiuno cha Mama na hivyo

kusababisha Mtoto huyo kutoka kwa urahisi kutokana na Maji yaliyomo ndani ya chupa

la lililombebeba mtoto ndani ya fuko la Uzazi.

Na kuna pia kemikali ziitwazo Beta Endorphins ambazo hua ni zenye kuupoza mwili

kutokana na maumivu yote ya mwili aliyokua akiyahisi katika wakati wa kujifungua na

kuzima maumivu hayo mara tu bada ya mtoto kutoka nje ya Mwili wa Mama na

kumfanya Mama kua na hali ya hisia ya furaha baada ya kupata Mtoto huyo.

Kimaumbile mara baada ya Mama kujifungua basi mwili wa Mwanamke hua ni wenye

kulitoa nje chupa la Mtoto kutokana na sehemu liliyojiachia kwenye fuko la uzazi ili fuko

lake la uzazi lipate kupona haraka na pia kuzuia kutoka damu nyingi zaidi, na hivyo

katika kipindi hiki pia fuko la uzazi hua ni lenye kubana na kujikamua kidogo kidogo.

Na hivyo kumsababishia Mama aliejifungua kua ni mwenye kuhisi homa ya baridi baridi

kwa mda mfupi baada ya kujifungua kutokana na pia kua ni mwenye kupoteza maji

mengi na joto mwilini mwake. Na ili mtoto aweze kupata chakula chake basi mara baada

ya tukio hilo la kujifungua mwili wa Mama hua ni wenye kuendelea kuzalisha Kemikali

za Oxytocin na Prolactin kwa ajili ya kukijaza kifua cha Mama mtoto maziwa na hivyo

ndani ya siku tatu maziwa hua ni tayari yaliyojaa kwa ajili ya kumnyonyesha Mtoto wake

huyo ambayo nayo pia hua ni yaliyojaa Madini tofauti muhimu kwa ajili ya ulinzi wa

afya na ukuaji wa Mtoto huyo, kama vile Vitamin, Protein na Mafuta ambayo

yanahitajka ndani ya miezi 6 ya mwanzoni mwa maisha ya mtoto.

Hivyo kwa upande wa Maryam Bint Imran alipotokewa na hali hii ya uchungu, bila ya

kujua ni kitu gani kinachotaka kumtokea na kuanza kujuta kutokana na ukali wa

maumivu hayo ya kimaumbile na kisha kajifungua basi hakua ni mwenye kujua nini

afanye kwani alikua peke yake, hukua akiwa na wasi wasi zaidi juu ya kile kitakachofuta

baada ya kujifungua kwake Mtoto huyo, yaani watu wake watamchukuliaje? kwani Allah

Subhanah wa Ta’ala alimjaalia Maryam Bint Imran ujfungua wakati Yusuf akiwa


468

hayupo, ameenda katafuta mahitajio yanayohitajika kwa ajili ya kuandaa kambi ya

mapumziko ya mda mfupi katika maeneo hayo.

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hali ya tukio hili

kutokana na mpangilio wa Aya na maneno yake kua haikumchukua mda mrefu

kwa Maryam Bint Imran kuondoka Nyumba kabla ya kujifungua’.

Baada ya kujifungua basi Maryam Bint Imran akajikuta nguvu zimemuishia lakini hapo

hapo akasikia sauti kutoka chini yake ikisema kama zinavyosema aya:

‏﴿فَنَادَاهَا مِن تحَْتِهَآ أَلا َّ تحَْزَنىِ‏ قَدْ‏ جَعَلَ‏ رَب ُّكِ‏ تحَْتَكِ‏ سَرًِّ۞وَ‏ هُزِّى ۤ إِلَيْكِ‏ بجِِذْعِ‏

ٱلن َّخْلَةِ‏ تُسَاقِطْ‏ عَلَيْكِ‏ رُطَباً‏ جَنِيّاً‏ ﴾

Fanadaha min tahtiha alla tahzanee qad jaAAala rabbuki tahtaki sariyyan;

Wahuzzee ilayki bijidhAAi alnnakhlati tusaqit AAalayki rutaban janiyyan (Surat

Maryam 19:24-25)

Tafsir: Kisha akanadiwa kutoka chini yake (na kuambiwa): ‘Usiwe na Huzuni, kwani

amejaalia Mola wako chini yako kua na chemchem ya maji. Na litikise shina la Mtende

nalo litaangusha kwa ajili yako Tende zilizopea.’’

Ambapo maneno yasemayo Min Tahtiha kama yakisomwa kwa kuwekewa alama ya

kisra chini ya harfu Mim na kua Min Tahtiha basi anaesema maneno haya hua ni Allah

Subhanah wa Ta’ala kupitia kwa Malaika Jibril ambae kwa wakati huo alikua chini

karibu yake na kama yakisomwa kama Man Tahtaha kwa kuwekewa Fat-ha, basi itakua

yanamaanisha kua anaesema maneno haya atakua ni Isa Ibn Maryam kutokana na Idhini

ya Allah Subhanah wa Ta’ala baada ya kuzaliwa kwake ambae kwa wakati huo alikua

chini yake Maryam Bint Imran.

Ambapo aya zinatuonesha kuhusiana na tukio hili kua mbali ya kua ni wenye kutakiwa

kua wenye kumtegemea Allah Subhanah wa Ta’ala katika kila kitu lakini pia tunatakiwa

kufanya jithada tusibweteke kua kila kitu kitakuja wenyewe kutokana na Majaaliwa ya

Allah Subhanah wa Ta’ala. Kwani hapa tunaona hali aliyokua nayo Maryam Bint Imran

kutokana na maumivu aliyokua akiyahisi kiasi ya kua alikua akiomba kua bora angekua

ni miongoni wa waliosahauliwa kabisa, yuko taabani na hivyo kwake yeye basi hakuna

kitu anachokihitaji zaidi katika wakati huo isipokua kupumzika, lakini anapokea amri ya

kua hatakiwi kupumzika bali anatakiwa ajitafutie riski yake kwa kusukuma kisiki cha mti

mkavu wa Mtende, ambao nao utamuangushia Tende mbivu zilizopea.


469

Hapa inabid tujue kua Mtende si Mpapai na hivo labda utautikisa na Mapapai yataanguka,

Kwa Mtende ni Mti Mgumu kama Mnazi hivyo si rahisi kuweza kuusukuma na

kuangusha tende zake hata kwa Mwanamme alietimia kimaumbile, lakini hii pia ni

sehemu ya ya Miujiza yake Allah Subhanah wa Ta’ala kwa Maryam Bint Imran kua

aliweza kuutikisa nao ukamuangushia Tende hizo.

Ambapo kwa upande wa Bahr ul ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi

anasema kua: ‘Chem chem hio ilitokea baada ya Malaika Jibril au Isa Ibn Maryam

kupiga chini mguu wake na hivyo ikatokea chemchem hio, na Mtende huo ambao

ulikua mkavu ukawa ni wenye kua mbichi na wenye Tende zilizopea na kuanguka

baada ya kutikiswa kwake na Maryam Bint Imran.’

Ambapo anasema Imam Al Rabi Ibn Al Khaytham kua: ‘Hakuna kitu bora kwa

Mwanamke aliejufungua Mtoto baada ya kujifunga kama Tende zilizopea, na kwa

mgonjwa hakuna kitu bora kama Asali.’

Na Imam Amr Ibn Maymun amesema kua: ‘Hakuna kitu bora zaidi kwa Mwanamke

aliejifungua kuliko Tende zilizopea’ na kisha akasoma aya hizi za Surat Maryam

19:24-25

Kisha baada ya tukio hilo basi Yusuf akamuwashia Moto Maryam Bint Imran na

kumzungushia kwa ajili ya kumuongezea joto la mwili ambalo lilikua limeshuka baada

ya kujifungua kwake. Kwani alikua anatetemeka mbali ya kua alikua ni mwenye kufanya

mazoezi ya kuupasha Moto mwili kutokana na amrisho la kutikisa Mtende. Kisha baada

ya hapo akamvunjia Lozi 7 ambazo alikua nazo ndani ya Mkoba wake na kumpa.

Ambapo anasema Imam Wahb Ibn Munabih kua: ‘Katika siku ambayo alizaliwa Nabii

Isa basi Masanam yote yalianguka chini, na Mashetani wote walianguka chini na

kushtuka, bila ya kujua ni kwa sababu gani. Hivyo moja kwa moja wakakimbilia

kwa Ibilis laanat Allah. Ambae alikua amekaa kwenye Kiti chake cha Ufalme, ndani

ya kina cha bahari, na walikutana nae katika wakati wa saa sita mchana. Na

alipowaona wasaidizi wake hao wote kwa pamoja basi akashtuka na kuwauliza

kimetokea nini?’

Wasaidizi hao wakamwambia mkuu wao Ibilisi Laanat Allahi kuhusiama na yaliyotokea,

na kisha wakasema kua: ‘Kwa kipindi hiki hakuna jambo zuri zaidi kwetu la

kuwaangamizia Ibn Adam zaidi ya Masanam na kutokana na tukio hili basi tuna

khofu kua hii huenda ikawa inamaanisha hawatokua na ushawishi wa kuendelea

kuyaabudu Masanam tena, na tumefukua kila sehemu ya Bahari na Ardhi kwa ajili

ya kutaka kujua nini kimetokea lakini hatukuweza kugundua.’


470

Hivyo Ibilisi akasema: ‘Bila ya shaka hili litakua jambo kubwa sana, hivyo subrini

wacha nikafuatilie’ kisha Ibilisi akatoka na kukaa kwa muda wa takriban masaa matatu

akiwa anaelea juu angani, na kisha ghafla akaona kila ambacho hawakukiona wasaidizi

wake, kwani aliona sehemu katika Ardhi ambayo ilikua ina utofauti na sehemu nyengine

na akahisi kua imezungukwa na Malaika. Lakini hata hivyo akajaribu kuisogelea sehemu

hio ili aone kuna nini kilichotokea lakini jithada zake zikagonga ukuta kwa sababu

alishindwa kuisogelea kwani kila upande anaojaribu kusogelea basi anakutana na ukuta

usioonekana.

Na ndio maana akasemaa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Shaytan

amemgusa kila mtoto wa Ibn Adam aliezaliwa katikati ya kifua chake kwa kidole

chake, isipokua Isa Ibn Maryam kwani ambae alikua na ngao ya Allah Subhanah

wa Ta’ala kwani ilikua kila akimgusa basi alikua akigusa ngao’

Hivyo Ibilisi Laanat Allahi akarudi kwa wafuasi wake na kuwaambia kua: ‘Hakika mimi

nimezunguka Duniani, Mbinguni na Ardhini na Baharini ndani ya masaa matatu

na nikagundua kuzaliwa kwa Isa Ibn Maryam. Ambae ni mtoto hajawahi kubebwa

na Fuko lolote la uzazi, bila ya kujulikana kwake nami. Au kwa Mwanamke

kujifungua bila ya mimi kuwepo. Na nnatarajia kua watu wengi zaidi

watapotoshwa kutokana nae huyu aliezaliwa kuliko watakaoonglewa. Lakini hata

hivyo basi hakuna Mtume ambae atatupa ushindani zaidi kuliko huyu aliezaliwa

leo.’

Ambapo Imam Mujahid Ibn Sulaiman basi yeye anasema kua : ‘Wakati nilipokua peke

yangu na Isa ndani ya Tumbo langu basi alikua akinizungumzisha, na ilipokua kuna

mtu anaenizungumzisha mimi basi yeye alikua akimtukuza Allah Subhanah wa

Ta’ala ndani ya Tumbo langu, nami nilikua nikisikia. ’

KUZUNGUMZA KWA HOJA KWA ISA IBN MARYAM UTOTONI.

Amesema Imam Mujahid Ibn Sulayman kua: ‘Baada ya Allah Subhanah wa Ta’ala

kumtayarishia mazingira yake Maryam bint Imran na kumrahisishia kujifungua

kwake basi akamwambia kua

‏﴿فَكُلِى وَٱشْرَبىِ‏ وَقَرِّى عَيْناً‏ فَإِم َّا تَرَيِن َّ مِنَ‏ ٱلبَشَرِ‏ أَحَداً‏ فَقُوليِ‏ ۤ إِ‏ نىّ‏ ِ نَذَرْتُ‏ لِلر َّحمَْٰنِ‏

صَوْماً‏ فَلَنْ‏ أُكَلِّمَ‏ ٱلْيَوْمَ‏ إِنسِ‏ يّاً‏ ﴾


471

Fakulee waishrabee waqarree AAaynan fa-imma tarayinna mina albashari ahadan

faqoolee innee nadhartu lilrrahmani sawman falan okallima alyawma insiyyan

(Surat Maryam 19:26)

Tafsir: Hivyo kula na kunywa na kua na utulivu wa Jicho lako, na kama ukimuona

Mtu yeyote yule basi sema: ‘Kwa Hakika Mimi nimefunga kwa ajili ya Mwingi wa

Rehma na sitozungumza leo na mtu yeyote’

Ingawa aya imetumia neno Sawman ambalo ingawa hua linaamisha Kujizuia Kutokana

na kitu kilichokatazwa au Kufunga lakini Wanazuoni wametofautiana kuhusiana na

maana yake kwani kuna baadhi ya Wanazuoni ambao wamelitafsiri kama Samt yaani

Kukaa Kimya, yaani Kula kiapo cha Kutosema Kitu ambao pia ni Mtizamo wa Abd Allah

Ibn Masud Radhi Allahu Anhu na kuna wanaosema kua hii ni kwa sababu kuna baadhi

ya Funga za Kiyahudi hua ndani yake mnajumuishwa kujizuia Kusema kitu chochote kile

isipokua Dhikr Allah.

Ambapo kwa upande wa Imam Muhammad Ibn Jariri At Tabari basi yeye amesema kua

aya inamaanisha kua: ‘Maryam Bint Imran alikua anaamrishwa awataarifu watu

kuhusiana na kufunga kwake kwa kutumia alama za mikono’ ambapo

tunapozungumzia kuhusiana na kufunga kwa upande wa Kiislam basi tunaona kua

Hakukukatazwa kuzungumza ndani yake bali kumekatazwa kuzungumza maneno ya

Kipuuzi na yasiyokua na maana.

Na ndio maana siku moja Amir Ul Muuminin Au Bakr As Siddiq Radhi Allah Anhu

alipishana na Mwanamke ambae watu walikua wanasema kua ameapa kua hatozungumza

na Mtu yeyote ambapo nae akasema: ‘Hakika Uislam umebatilisha hilo.’

Amesema Imam Abd Rahman Al-Kalbi kua: ‘Yusuf alimbeba na kumpeleka Maryam

Bint Imran na Isa Ibn Maryam kwenye Pango, na akawawacha huko wa mda wa

siku 40 na kisha akatoka nao, wakati wanarudi katika Mji wa Nasira na Maryam

Bint Imran akiwa amembeba Isa Ibn Maryam mikononi mwake basi Isa Ibn

Maryam alisema kumwambia mama yake kua: ‘Ewe Mama furahia kwani mimi ni

Masih Mja wa Allah’’

Hivyo baada ya kupita siku 40 basi Maryam Bint Imran na Mtoto wake Mchanga ambae

ni Isa Ibn Maryam pamoja na Yusuf wakaanza safari ya kurudi katika Mji wa Nasira

ambako ndiko walikua wakiishi hapo kabla.

‏﴿فَأَتَتْ‏ بِهِ‏ قَوْمَهَا تحَْمِلُهُ‏ قَالُواْ‏ يمَٰرْيمَُ‏ لَقَدْ‏ جِ‏ ئْتِ‏ شَيْئاً‏ فَرًِّ‏ ﴾


472

Faatat bihi qawmaha tahmiluhu qaloo ya maryamu laqad ji/ti shay-an fariyyan

(Surat Maryam 19:27)

Tafsir: Kisha akamchukua Mtoto kwa Watu wake huku akiwa amembeba. Nao

wakasema: ‘Ewe Maryam kwa hakika umetuletea jambo ambalo halijawahi

kufanywa’

Hapa tunaona kua watu hawa wa Bani Israil wa Mji wa Nasira wanalielezea tukio hili

kutumia neno Fariyya ambalo ni lenye kumaanisha Kukata, Kugawa, Kusingizia Ubaya,

Kuzusha, La Kushangaza na Kustaajabisha ambalo halijawahi kusikika hapo kabla kwa

Ubaya au Uovu wake.

Na hii ni kwa sababu haijawahi kutokea kua Mtawa na Mtu Mcha Mungu awe ni mwenye

kua na sifa ya kutokewa au kufanya kama alivyofanya Maryam Bint Imran yaani kupata

Mtoto bila ya Kuolewa, na ndio maana hata Maryam Bint Imran mwenyewe

alipobashiriwa tunukio hili kutoka kwa Mola wake basi alisema kama vile ambavyo

walivyosema watu hawa kua:

‏﴿أَنى َّٰ‏ يَكُونُ‏ لىِ‏ غُلاَمٌ‏ وَلمَْ‏ يمَْسَسْنىِ‏ بَشَرٌ‏ وَلمَْ‏ أَكُ‏ بَغِيّاً‏ ﴾

Anna yakoonu lee ghulamun walam yamsasnee basharun walam aku baghiyyan;

(Surat Maryam 19:20)

Tafsir: ‘Nitakua na Mtoto wa kiume mimi wakati sijawahi kuguswa na mtu yeyote

(Mwanamme) na wala mimi si Mwanamke mwenye kutembea na Wanaume?’

Na hivyo kimaumbile pia hua ni jambo la kawaida kwa watu kutofahamu na hivyo kutaka

kujua ukweli juu tukio hilo, ambalo kwa mtizamo wa juu juu tu basi haiwezekani kupata

jawabu bila ya kufikiria vyenginevyo yaani itakuaje Mwanamke awe ni mwenye kupata

Mtoto bila ya Kuingiliwa na Mwanamme? Na kutokana na hali kua ni hivyo kimanitiki

hua kama Mwanamke amepata Ujauzito na Kujifungua basi hua inamaanisha kua hakuna

njia nyengine yeyote isipokua ameingiliwa na Mwanamme.

Na hivyo basi Watu hao wakasisitiza zaidi kua jambo hilo ni la kustaajabisha sana kwa

sababu kimaumbile baadhi ya mambo hua yanatokana kulingana na asili au urithi, lakini

kwa upande wake Maryam Bint Imran hakua na asili ya kua ni mwenye kuweza kupata

Mtoto bila ya kuolewa, kutokana na utukufu wake na pia Utukufu wa asili yake kifamilia

hivyo haiwezekani kua jambo hilo limetokea kutokana na kurithiwa kwa tabia mbaya

labda kutoka katika familia, au asili yake, kwani hakuna katika urithi wala asili na ndio


473

maana watu hao wakamwambia Maryam Bint Imran kwa kusema kama zinavyosema

Aya:

‏﴿ُٰخْتَ‏ هَارُونَ‏ مَا كَانَ‏ أَبُوكِ‏ ٱمْرَأَ‏ سَوْءٍ‏ وَمَا كَانَتْ‏ أُم ُّكِ‏ بَغِيّاً‏ ﴾

Ya okhta haroona ma kana abooki imraa saw-in wama kanat ommuki baghiyyan

(Surat Maryam 19:28)

Tafsir: Wakasema Watu hao: ‘Ewe Dada yake Harun, hakuwahi kua Baba yako ni

Mzinifufu, na wala Mama yako kua ni Malaya’

Ambapo anasema Al Mughira Ibn Shubah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alinituma mimi kwa watu wa Najran. Na wakasema:

‘Hivi umefikiria kuhusiana na hii aya uliyotusomea kwenye Qur’an isemayo: Ewe

Dada yake Harun wakati Musa alikua ni mwenye kuja kabla ya Musa? Hivyo

niliporudi nikamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam ambae nae alisema

kua: ‘Jee hukuwaambia wewe kua walikua wamezoea kuitana kwa majina ya

Mitume na watu wacha Mungu kabla yao?’

Ambapo anasema Imam Qatadah Al Sadusi kua: ‘Kabla ya kipindi hiki watu wa Bani

Israil walikua na mtu mwema ambae alikua akiitwa Harun ambae ni tofauti na

Harun kaka yake Nabii Musa, ambapo katika siku aliyofariki basi Jeneza lake

lilishindikizwa na watu 40000 ambao wote walikua wakiitwa Harun.’

Anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al

Qurtubi kua: ‘Kuna mitizamo tofauti kuhusiana na mda ambao uliopita baina ya

Nabii Musa Ibn Imran na Nabii Isa Ibn Maryam. Kwani Imam Muhammad Ibn

Saad amesema katika Tabaqat Al Saadi kua: ‘Abd Alla Ibn Abbas Radhi Allahu

Anhu amesema kua: ‘Baina ya Nabii Musa Ibn Imran na Isa Ibn Maryam kulikua

na miaka 1,700 na kamwe hakukua na fatra (kipindi ambacho hakukua na Mitume

kwa watu wa Bani Israil) baina yao, kwani katika kipindi hiki watu wa Bani Israil

walitumiwa Mitume 1000. Ambayo ni mbali ya idadi ya Mitume myengine

iliyotumwa kwa Ummah wa watu wengine. Na baina ya Nabii Isa Ibn Maryam na

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi kuna miaka 599’ ’(Tafsir Jamii Al Ahkami

Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi )

Ama kwa upande wa Mujaddid Ad Din Al Hafidh Imam Shihab ad Din Imam Ibn Hajar

Al Asqalani basi yeye anasema kua: ‘Wanazuoni wanakubaliana kua kipindi cha

Mayahudi na hadi kipindi cha kuwasili Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ni


474

zaidi ya miaka 2000. Na Kipindi cha Wakristo na Rasul Allah Salallahu Alayhi w

Salam ni miaka 600’ (Fa-th Al Baari, 4/449 Mujaddid ad Din Al Hafidh Imam Ibn Hajar

Al Asqalani)

Naam anasema Imam Al Sabuni Al Hanbali kua: ‘Harun huyu anaezungumziwa hapa

si Nabii Harun ambae alikua pamoja na Nabii Musa kwani bila ya shaka utofauti

wa kipindi walichoishi wao na Maryam bint Imran ni zaid ya miaka 1000.’ (Safwat

Al Tafaasir)

Ama kwa upande wa Sultan Al Mutakallimin Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al

Razi basi yeye ameifafanua ayah hii katika sehemu nne ambazo tunaweza tukazifupisha

kama ifuatavyo:

1. Harun huyu alietajwa katika aya hii alikua ni mtu ambae ni Mcha Mungu

miongoni mwa Bani Israil, hivyo wale watu ambao walikua ni wacha Mungu

walikua wakinasibishwa nae Harun huyu.

2. Harun huyu alietajwa katika aya hii, ndio yule yule Nabii Harun ambae ni kaka

yake Nabii Musa. Hivyo Marymam bint Imran alikua ni mwenye kutoka katika

kizazi cha Nabii Harun, kama vile abavyo mtu alietoka katika ukoo wa Hamdan

kwa mfano kua ni mwenye kuitwa: ‘Ewe ndugu yake Hamdan’ yaani yule

anaetoka katika kizazi cha Hamdan.

3. Harun huyu alikua ni mtu mwenye umaarufu katika mambo ya kufanya maasi.

Hivyo Maryam alizungumziwa hapa katika hali ya ‘Tashbiih’ yaani

kumshabihisha. Kwani Bani Israil wao walimuona Maryam Bint Imrankua

alikua amefanya maasi.

4. Harun huyu alikua ni kaka yake Maryam Bint Imran ambae alikua ni mtu

mwema na mwenye ucha Mungu, ambapo maana hii hua ni yenye kuendana

sana kimaana kwa sababu kuu mbili zifuatazo:

i. Hii ndio maana ya juu ya Aya, hivyo hakutokua na uhitaji wowote ule wa kuingia

ndani kutafuta maana inayoainishwa au iliyofichwa na ayah hii.

ii. Hii ilitumika kuonesha ‘Tawbikh’ yaani Karipio. Kwani hali hii ya karipio hua

ni kubwa zaidi pale linaponasibishwa na Ndugu kwani hili pia hua

linamkumbushia Wazee wake yule anaekaripiwa na adabu alizofundishwa na

Wazee wake hao. Kwani Ayah hii pia imewaainisha wazee wake waliomzaa


475

Maryam Bint Amran. (Mafatih Al Ghayb /Al Tafsir Al Kabir, Imam Fakhrudin Al

Razi)

Na akasema Imam Wahb Ibn Munabih kua: ‘Jina Harun lilikua ni la Mtu mmoja

miongoni mwa watu waovu sana katika jamii ya Watu wa Bani Israil na alikua

anachukiza sana kwa maovu yake ikiwemo Uzinifu, hivyo watu hawa wa Bani Israil

moja kwa moja wakamfananisha Maryam Bint Imran na Harun huyo kutoka na

tukio hili.’

Ambapo kutokana na maana ya kauli hii kulingana na Mtizamowa Imam Wahb Ibn

Munabih basi tunaona kua Watu hawa walimlaani Maryam Bint Imran kwa

kumfananisha na Harun huyo Muovu na kisha hapo hapo wakamkasirikia na kumkosoa

kua itakuaje afanye hivyo wakati wazee wake hawakua ni wenye sifa hizo, na hivyo hii

ni kauli yenye kuonesha namna Watu hawa walivyokua wakimjali na kumthamni

Maryam Bint Imran na kua wamechukizwa sana na kuvunjwa Nyoyo zao kutokana na

Aibu aliyowatia ambayo imevunja Imani yao juu yake, kwani thamani yake juu yao baada

ya tukio hili imeanguka chini yote.

Hivyo Maryam Bint Imran akafanya kama alivyoamrishwa na Mola wake ambae ndie

aliembebesha jukumu hilo zito juu yake lenye kumletea Mitiani hii anayokabiliana nayo

mbele ya watu wake, kwa kutoa ishara kama inavyobainishwa na Aya:

‏﴿فَأَشَارَتْ‏ إِلَيْهِ‏ قَالُواْ‏ كَيْفَ‏ نُكَلِّمُ‏ مَن كَانَ‏ فىِ‏ ٱلْمَهْدِ‏ صَبِيّاً‏ ﴾

Faasharat ilayhi qaloo kayfa nukallimu man kana fee almahdi sabiyyan (Surat

Maryam 19:29)

Tafsir: ‘Akaashiria juu yake (Mtoto wake wazungumze nae) Nao wakasema:

‘Tutazugumzaje sisi na Mtoto aliemo kwenye Mkoba wa kubebea Mtoto mchanga?’’

Lakini hata hivyo Maryam Bint Imran akaendelea kwa kufanya kama alivyoamrishwa na

Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kumuashiria Isa Ibn Maryam kua umefika wakati wa

Kujitetea na kudhihirisha Miujiza yake itakayodhibitisha kua yeye hakupatikana

kutokana na kama wanavyofikiria na kudhania watu hao wa Najran kwa kujitetea kwa

hoja zinazoshiria Miujiza ya Kuzaliwa kwake siku 40 tu zilizopita kama zinavyosema

aya:


476

﴿ قَالَ‏ ِ إِنىّ‏ عَبْدُ‏ ٱهلل َِّ‏ آاتَنىِ‏ َ ٱلْكِتَابَ‏ وَجَعَلَنىِ‏ نَبِيّاً‏ ۞ وَجَعَلَنىِ‏ مُبَارَكاً‏ أَيْنَ‏ مَا كُ‏ نتُ‏

وَأَوْصَانىِ‏ بِٱلص َّلاَةِ‏ وَٱلز َّكَ‏ ا وٰةَِم دُمْ‏ تُحَيّاً‏ ۞ وَبَرّاً‏ بِوَالِدَتِى وَلمَْ‏ يجَْعَ‏ لْنىِ‏ جَب َّاراً‏ شَقِيّاً‏

۞ وَٱلس َّلاَمُ‏ عَلَى َّ يَوْمَ‏ وُلِدْت ُّ وَيَوْمَ‏ أَمُوتُ‏ وَيَوْمَ‏ أُبْعَثُ‏ حَيّاً‏ ۞ ذٰ‏ لِكَ‏ عِيسَى ٱبْنُ‏

مَرْيمََ‏ قَوْلَ‏ ٱلحَْقِّ‏ ٱل َّذِى فِيهِ‏ يمَْتَ‏ رُونَ‏ ﴾

Qala innee AAabdu Allahi ataniya alkitaba wajaAAalanee Nabiyyan;

WajaAAalanee mubarakan aynama kuntu waawsanee bialssalati waalzzakati ma

dumtu hayyan; Wabarran biwalidatee walam yajAAalnee jabbaran shaqiyyan ;

Waalssalamu AAalayya yawma wulidtu wayawma amootu wayawma obAAathu

hayyan Dhalika AAeesa ibnu maryama qawla alhaqqi alladhee feehi yamtaroona

(Surat Maryam 19:30-34)

Tafsir: Akasema (Isa Ibn Maryam): ‘Hakika mimi ni Mja wa Allah ambae amenipa

Kitabu na kunijaalia kua ni Nabii. Na amenijaalia kua ni Barka popote pale

nitakapokuwepo na Kua ni mwenye kuusiwa juu ya Sala na Zakkah kudumu nazo

wakati niko hai. Na kumfanyia wema Mzazi wangu (Maryam Bint Imran) na wala

hakunijaalia kua ni mwenye Ujabari wa kutumia nguvu. Na Salama iko juu yangu

katika siku niliyozaliwa na siku nitakayokufa na katika siku nitakayofufuliwa. Huyo

ndio Isa Ibn Maryam Kauli ya haki ambae wao ni wenye shaka nae’

Aya inatuonesha kua ingawa Isa Ibn Maryam alikua na umri wa siku 40 lakini alikua na

uwezo wa kubainisha Hoja zake kutokana na kujaaliwa kwake na Allah Subhanah wa

Ta’ala kwa ajili ya kumtetea Mama yake na kujitetea kwa kujielezea yeye mwenyewe

kua yeye ni Mja wa Allah Subhanah wa Ta’ala sambamba kimaana maneno haya akiwa

anakanusha kua yeye pia si Mungu na wala si Mtoto wa Mungu kama wanavyodai au

watakavyodai watakaokuja baada yake.

Na kisha anabainisha kusudio la kutumwa kwake na Mola wake kwa watu wake hao kua

ni Ni mwenye Darja ya Unabii wa kuwaelekeza watu katika njia sahihi ya kumuelekea

Mola wao na kuwakataza Maovu na kuwaamrisha Mema na amekuja na Kitabu chake na

hivyo kua ni mwenye Barka popote pale atakapokuwepo Ulimwenguni. Na kamwe hakua

ni mwenye kujaaliwa kua na Kibri dhidi ya Maamrisho ya Mola wake na mbele ya Mama

yake.


477

Ambapo amesema Imam Abu Muhammad Abd Allah Sahl Al Tustari kua amesema Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kibriyah ni Vazi la Allah Subhanah wa Ta’ala

hivyo yeyote yule atakaeshindana na Allah Subhanah wa Ta’ala juu yake vazi hilo

na kulivaa, basi atatumbukizwa Motoni uso uso.’

Hivyo baada ya kujitetea kwake huko Nabii Isa Ibn Maryam basi habari zikafika kwa

Watawala ambao walikua ni wenye Mamlaka ya Ufalme ulio chini ya mwamvuli wa

utawala wa Roma Empire uliokua unaongozwa na Qaysar, ambae alikua akitawala

maeneo yote ya Mwambao wa Bahari ya Mediterenean, ambapo kwa wakati huu Mfalme

wa ardhi ya Israil alikua ni Mfalme Herod ambae alipanga kumuua Isa Ibn Maryam

kutokana na kubashiriwa na watu wake kuhusiana na kuzaliwa kwa Mtoto ambae ataleta

matatizo ya upinzani kwa Utawala wake na Utawala wa Roman Empire. Hivyo basi Allah

Subhanah wa Ta’ala akamwamrisha Maryam bint Imran na Yusuf kua umefika wakati

wa kuhama kutoka katika Ardhi ya Falestina kuelekea katika ardhi ya Misri.

HIJRA YA MARYAM BINT IMRAN NA NABII ISA BAINA YA MISRI

NA NASIRA

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Maryam Bint Imran na Yusuf kua

wahame na Isa Ibn Maryam kutoka katika Ardhi ya Falestina kuelekea katika Ardhi ya

Misri na hawatakiwa kurudi hadi pae atakapofariki Mfalme Herod, kwani Mfalme huyo

anapanga mipango ya kutaka kumuua Isa Ibn Maryam, hivyo alfajir ya siku ya pili basi

Yusuf akampakia Maryam Bint Imran na Isa Ibn Maryam kwenye Punda wake na kuanza

safari yao ya kuelekea katika ardhi ya Misri, hadi walipovuka katika maeneo yenye

Miinuko iliyokaribu na ardhi ya Misri ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala anaielezea kwa

kusema kua:

‏﴿وَجَ‏ عَلْنَا ٱبْنَ‏ مَرْيمََ‏ وَأُم َّهُ‏ آيَةً‏ وَآوَيْنَاهمَُآ إِلىَٰ‏ رَبْوَةٍ‏ ذَاتِ‏ قَرَارٍ‏ وَمَعِينٍ‏ ﴾

WajaAAalna ibna maryama waommahu ayatan waawaynahuma ila rabwatin dhati

qararin wamaAAeenin (Surat Al Muuminun 23:50)

Tafsir: Na tukamjaalia Ibn Maryam na Mama yake Dalili tukawapa makazi katika

sehemu iliyojuu iliyobakia na chemchem ya maji.

Ambapo neno Rabwatin hua linamaanisha Kuongezeka, Kukuza, Kutuna, Kujaa,

Kupanda Juu, Kuelea juu juu, Kukuza kitu, Kukuza Ufahamu kwa kusomesha. Ambapo

neno hili limetokana na neno Rabwa ambalo ndio lililotoa neno Riba na hivyo pia


478

kumaanisha Riba au Kitu chochote kinachoongezeka na kua ni cha ziada kutokana na

Mkopo au Kiasi kilichozidi zaidi ya vile kilichokua kabla ya kuwekezwa kwake.

Ambapo kwa upande wa Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu na Imam Ad Dahhaq basi wao

wanasema kua: ‘Rabwah hii inamaanisha eneo zima la Ramallah, Misri na Syria’

lakini kwa upande wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye amesema kua

:‘Hii inamaanisha ni Ardhi iliyonyanyua na kuwepo juu ya sehemu nyengine

zilizoizunguka’

Na kwa upande wa Imam Al Qazzaz basi amesema kua ni: ‘Sehemu ya Ardhi ambayo

inamwagiliwa Maji safi’ na Imam Abu Zayd basi yeye anasema kua hii ni Ardhi ya

Misri.

Na wengine wengi miongoni mwa Wanazuoni basi ni wenye kusema kua Maryam Bint

Imran alihamia katika Ardhi ya Misri na hii ni kwa sababu Ardhi ya Misri kwa wakati

huu ilikua iko mbali na mamlaka ya Mfalme Herod, na hivyo Maryam Bint Imran na Isa

Ibn Maryam alikaa katika ardhi hio ya Misri kwa Muda wa miaka 12 huku akiwa ni

mwenye kufanya kazi kuchuma Pamba mashambani.

Ambapo anasema Imam Muhammad Ali Al Baqr kua: ‘Wakati Nabii Isa alipozaliwa

basi alipokua na umri wa siku moja basi alikua akionekana kama ana umri wa

mwezi mmoja, hivyo baada ya miezi 9 alipelekewa Madrasa, na alipokaa darasani

basi Mwalimu wake akamwambia sema: ‘Biismi Allahi AlRahmani Al Rahim’ hivyo

nae akasema, kisha akaambiwa asome Abjad, hivyo Isa Ibn Maryam akamuuliza

Mwalimu wake kama anajua maana ya herufi za Abjad.’

‘Hivyo mwalimu akamsogelea Isa Ibn Maryam kwa ajili ya kutaka kumpiga bakora

Isa Ibn Maryam, lakini Isa Ibn Maryam akasema: ‘Tafadhal usinipige, kwani kama

unajua basi niambie na kama hujui basi niambie nikutafsirie.’ Hivyo Mwalimu

huyo akamwambia Isa Ibn Maryam kua: ‘Haya tuambie maana yake.’’ Isa Ibn

Maryam akasema:

‘ABJaD – Alif inamaanisha (La) Ilaha Illa Allah, Ba inamanisha Bazagha yaani

Mtandazo wa Nuru ya Allah, Jim inamanisha Jalalah yaani Ufalme wa Allah na Dal

inamanisha Dini.’

‘HaWaZ – Ha inamaanisha Hawwiyah yaani sehemu ya chini kabia ya Moto, Waw

inamanisha Waylun yaani Ole wao watakaouingia Moto huo, na Za inamaanisha

Zafir yaani Harufu mbaya ya watu wa Motoni.’

‘HaTaYa – Inamaanisha Hattat yaani wenye Dhambi watakua chini zaid kuliko wale

wenye Kutubu.’


479

‘KaLaMaN – Ka Inamanisha Kalam - Maneno ya Allah Subhanah wa Ta’ala Lam n

yenye kukataa kua si yenye kuumbwa na hayana Mubadala yaani Mim ambayo ndio

Mubadala ya hayana Mbadala wake.’

‘SaFaS – ni Saun Bi Sain ambayo inamanisha Kipimo kwa kipimo Adhabu kwa

Adhabu.’

‘QaRaShaT – Ni Taqrishuhum yaani Allah Subhanah wa Ta’ala atachukua kutoka

hapa na pale katika siku ya Malipo’

Hivyo ilipofika wakati wa kuena kuchukuliwa katika siku hio kutoka Madrasa basi

Mwalimu akamwambia Maryam Bint Imran kua: ‘Mchukue Mtoto wako kwani ni

mwenye kujua kila kitu hivyo hahitaji kusoma kama watoto wengine.’

Ambapo anasema Imam Kaab Al Akhbar kua: ‘Isa Ibn Maryam alikua ni mwenye

muonekano wa Mtu ambae ni mwenye rangi ya kiza kuelekea kwenye Weupe,

Nywele zake zilikua hazina Mafuta kabisa na alikua ni mwenye kutembea miguu

chini bila ya viatu, alikua hana nyumba wala mapambo wala matumizi isipokua juu

ya kile anachohitajia katika siku husika tu. Usiku unapoingia alikua ni mwenye

kusimama na Kusali Usiku kucha na alikua ni mwenye kuwaponya Vipofu wenye

na Ukoma kwa idhini ya Allah na alikua akifufua waliokufa pia kwa idhini ya

Allah.’

Hivyo miaka 12 baada ya kuhamia katika ardhi ya Misri basi Allah Subhnaah wa Ta’ala

akaichukua Roho ya Mfalme Herod na kisha akamtaarifu Maryam Bint Imran n Yusuf

na Isa Ibn Marym kua Mfalme Herod ameshafarki na hivyo wanaweza kurudi katika Mji

wa Nasira, hivyo na wakarudi na wakawa ni wenye kuishi kwenye Mji huo kwa miaka

kadhaa hadi pale Isa Ibn Maryam alipotimiza umri wa miaka 30, yaani miaka 18 baadae.

Ambapo katika kipindi hiki basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia Wahyi Isa Ibn

Maryam na kumwambia kua umefika wakati wa kujidhihirisha kwa ajili ya kufikisha

ujumbe wake aliotumiwa na Mola wake kwa ajili ya watu wa Bani Israil.

Nabii Isa Ibn Maryam akaanza kutangazia ujumbe wa Allah Subhanah wa Taa’la kwa

kutumia silaha ya Miujiza yake akiwa ni mwenye kuponya waliokua wamepooza,

waliokua na Ukoma, waliokua na Majini na Mashetani na hata waliokua vipofu

aliwapanguza nyuso zao na wakawa ni wenye kuona, bila ya kuchukua malipo yeyote

kutoka kwao, kwani yeye alikua ni mwenye kutaka watu hao wawe ni wenye kuamini

Imani yake anayowausia tu juu yao basi, hivyo watu wakaanza kumpenda na kumfuata

katika Imani yake nae akazidi kua maarufu na kila mtu alikua ni mwenye kutaka kujuana

nae Al Masih Isa Ibn Maryam Ruhi Allah ambapo miongoni mwa waliokua wakimkubali

kuhusiana na ujumbe wake wakawa wanajulikana kama Ansaru Allah


480

ANSARU ALLAH – AL HAWARIYINA

Neno Ansar hua linamaanisha Nusura, Usaidizi, Uhifadhi, Ulinzi, Msaada au kitu

kinachosababisha Utulivu au Mliwazo pale kinapopatikana.

Ambapo kama tulivyoona kua Nabii Isa alikubalika na kupata wafuasi ambao walikua

tayari wako pamoja nae na hivyo wako tayari kwa ajili yake na kwa ajili ya Allah

Subhanah wa Ta’ala na hivyo watu hawa kua na sifa ya kua ni Ansaru Allah katika kisa

cha Nabii Isa pale aliposema katika kuwathibitishia watu wake kwa kuwaonesha njia

sahih kua:

‏﴿وَمُصَدِّقاً‏ لِّمَا بَينَْ‏ يَدَى َّ مِنَ‏ ٱلت َّوْرَاةِ‏ وَلِ‏ أُحِ‏ ل َّ لَكُمْ‏ بَعْضَ‏ ٱل َّذِى حُ‏ رِّمَ‏ عَلَيْكُمْ‏

وَجِ‏ ئْتُكُمْ‏ آبِيَةٍ‏ مِّن ر َّبِّكُمْ‏ فَٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَأَطِيعُونِ۞إِن َّ ٱهلل ََّ‏ رَبىِّ‏ وَرَب ُّكُمْ‏ فَٱعْبُدُوهُ‏ هَٰذَ‏ ا

صِرَاطٌ‏ م ُّسْتَقِيمٌ‏ ﴾

Wamusaddiqan lima bayna yadayya mina alttawrati wali-ohilla lakum baAAda

alladhee hurrima AAalaykum waji/tukum bi-ayatin min rabbikum faittaqoo Allaha

waateeAAooni; Inna Allaha rabbee warabbukum faoAAbudoohu hadha siratun

mustaqeemun; (Surat Al Imran 3:50-51)

Tafsir: Na nimekuja kuthibitisha kile ambacho kimekuja kabla yangu, kutoka katika

Tawrat na kukuhalalishieni sehemu ya kile ambacho mliharamishiwa na nimekuja

kwenu nikiwa na uthibitisho kutoka kwa Mola wenu hivyo Mtiini Allah na Nifuateni

mie. Kwani kwa Hakika Allah Ni Mola wangu na ni Mola wenu hivyo Muabuduni, hii

ndio njia iliyonyooka.

Hivyo baaada ya kutoa uthibitisho huo basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamjaalia Nabii

Isa kua na Wasaidizi ambao ni wenye kumkubali yeye Allah Subhanah wa Ta’ala na

kumkubali Nabii Isa Ibn Maryam kama zinavyosema aya pale Allah Subhanah wa Ta’ala

alipothibitisha kwa kusema:


481

‏﴿وَإِذْ‏ أَوْحَيْتُ‏ إِلىَ‏ ٱلحَْوَارِيِّينَ‏ أَنْ‏ آمِنُواْ‏ بىِ‏ وَبِرَ‏ سُ‏ ولىِ‏ ۤ قَالُو اْ‏ آمَن َّا وَٱشْ‏ هَ‏ دْ‏ أبَِ‏ ن َّنَا

مُسْلِمُونَ‏ ﴾

Wa-idh awhaytu ila alhawariyyeena an aminoo bee wabirasoolee qaloo amanna

waishhad bi-annana muslimoona (Surat Al Maidah 5:111)

Tafsir: Na wakati mimi (Allah) nilipowatilia ndani ya nyoyo zao Hawariyyina kua

waniamini mimi na kwa Mtume wangu basi wakasema: ‘Tumeamini na kushuhudia

kua sisi ni Waislam.’

Hapa tunaona kua aya yetu hii imetumia neno Awhaytu ambalo pia ni lenye kutokana na

neno Waha ambalo hua linamaanisha kua ni Wahyi, Maelekezo, Alama, Dalili, Uamsho

au Msukumo unaowekwa kwenye Moyo, Akili au Ufahamu na pia humaanisha

Mnong’onezo wa Siri.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anatueleze kua ni yeye ndie aliewatia Msukumo watu

hao nao wakawa ni wenye kumkubali na kumfuata Nabii Isa Ibn Maryam, na hivyo kua

n wenye kutaka kumsaidia Nabii Isa Ibn Maryam kwa kumunga mkono katika majukumu

yake aliyopewa na Mola wake ili ayafikishe kwa watu wake na hivyo watu hao ndio pia

wakawa wanaitwa Hawarriyin.

Na neno Hawariyiin ni neno lenye kutokana na neno Hara ambalo hua linamaanisha

Kurudi, Kurudia, Kuchanganyikiwa, Kugeuza Macho kutokana na kuchanganyikiwa na

kitu na hivyo kutokiona vizuri kitu hicho. Kua na Macho Makubwa mazuri na ya kuvutia.

Neno Hara ndio lililotoa neno Hur ambalo hua linamaanisha Kitu Kizuri Kisafi

kisichokua na Doa wala Uchafu, na hivyo kumaanisha Vumbe wa Wazuri na Wasafi wa

Peponi ambao ni wenye Jinsia ya Kike na ya Kiume, ambapo Hur wa kike hua ni kwa

ajili ya zawadi ya Waumini wa Kiume kutoka kwa Mola wao kutokana na yale Mema na

Mazuri waliyokua wakiyafanya kwa ajili ya Mola wao hapa Duniani.

Na Hur wa kiume hua ni kwa ajili ya zawadi ya Waumini wa Kike kutoka kwa Mola wao

kutokana na yale Mema na Mazuri waliyokua wakiyafanya kwa ajili ya Mola wao hapa

Duniani.

Hivyo neno Hawari hua linamaanisha Yule Mtu ambe alipewa Mitihani na Mola wake

na kisha akafuzu Mithani hio na kuonekana kua ni Muadilifu na ni Mtiifu wa Mola wake,

na hivyo basi katika aya yetu hua linamaanisha kutubainishia ukubwa wa Darja yao watu

hawa ambao walikua ni wasaidizi maalumu waliochaguliwa na Allah Subhanah wa


482

Ta’ala kwa ajili ya Nabii Isa Ibn Maryam na hivyo kua ni wenye kujisalimisha kwa

Allah Subhanah wa Ta’ala kama zinavyobainisha aya pale ziliposema:

‏﴿فَلَم َّآ أَحَس َّ عِيسَى ٰ مِنْهُمُ‏ ٱلْكُفْرَ‏ قَالَ‏ مَنْ‏ أَنصَارِ‏ ى ۤ إِلىَ‏ ٱهلل َِّ‏ قَالَ‏ ٱلحَْ‏ وَارِي ُّونَ‏ نحَْنُ‏

أَنْصَارُ‏ ٱهلل َِّ‏ آمَن َّا بِٱهلل َِّ‏ وَٱشْهَدْ‏ أبَِ َّ مُسْلِمُونَ‏ ﴾

Falamma ahassa AAeesa minhumu alkufra qala man ansaree ila Allahi qala

alhawariyyoona nahnu ansaru Allahi amanna biAllahi waishhad bi-anna

muslimoona (Surat Al Imran 3:52)

Tafsir: Na kisha alivyohisi Isa kutokana na Kutoamini kwao basi akasema: ‘Jee ni

nani Ansaru Allah’ wakasema Hawwariyyun kua: ‘Sisi ndio Ansari Allah,

tuliemuamini Allah na tunashuhudia kua sisi tumejisalimisha (kwa Allah Subhanah

wa Ta’ala)’

Na tunapoangalia watu hawa wenye sifa ya Hawariyun basi tunaona kua Wanazuoni

wanma kua walikua ni watu 12 Ambao ni: ‘Simioni. Pita, Andrew, James Ibn Zebede,

John Ibn Zebede, Philip, Bartholomew, Thomas, Matthew, James Ibn Alphaeus,

Labaeus Ibn Thaddaeus, Simioni Ibn Kanan na Judas Iscarioti’

Ambapo anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hawa

walikua ni Wavuvi ambapo Isa Ibn Maryam alikutana nao na kuwauliza: ‘Hivi jee

mnafanya nini?’ nao wakajibu: ‘Tunavua Samaki’ nae Isa Ibn Maryam akasema:

‘Hivi Jee hamtaki nyinyi kutembea pamoja na mimi ili tupate kuwavua Watu?’

Watu hao wakauliza: ‘Ndio vipi hivyo?’

Isa Ibn Maryam akasema: ‘Kwa Kuwaita kwa Ajili ya kumuelekea Allah Subhanah

wa Ta’ala’ nao watu hao wakauliza kwa kusema: ‘Kwani wewe ni Nani?’ Nabii Isa

akasema: ‘Mimi ni Isa Ibn Maryam ambae ni Mtume na Nabii wa Allah Subhanah

wa Ta’ala.’ Hivyo watu hao wakamuuliza : ‘Jee kuna Mtume baada yako?’ nae

akasema: ‘Naam Mtume kutoka Urabuni’’

Ambapo kwa upande wa Imam Ibn Arta basi yeye amesema kua: ‘Hawa walikua ni

Wafuaji Nguo na Wapakaji Rangi Vitambaa (Yuhawwirun)’ ambapo kwa upande wa

Imam Abd Allah Ibn Mubarak basi yeye anasema kua: ‘Hawa waliitwa Hawwariyun

kwa sababu walikua waking’ara kutokana na Nuru ya kufanya sana Ibada kwa ajili

ya Allah Subhanah wa Ta’ala’ na kwa upande wa Imam Ad Dahhaq Ibn Muzahim basi

yeye alisema kua: ‘Watu hawa walikua wanaitwa Hawwariyyun kwa sababu ya usafi

wa Ndani ya Nafsi na Nyoyo zao. Na walikua pia ni warithi wa Isa Ibn Maryam’


483

Ambapo amesema Imam Nasr Ibn Shaml kua: ‘Hawwariyyun ni miongoni mwa Watu

wema ambao watu hua wanawatumia kwa ajili ya kuomba Msaada wanapofikwa

na Mithani kama vile alivyosema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua : ‘Kila

Mtume hua na Hawwari wake, na Hawwari wangu mimi ni Al Zubayr’’

Na kwa upande wa Imam Qatadah Al Sadusi basi yeye anasema kua: ‘Hawwaryyun wa

Rasul Allah Salallahu Alyhi wa Salam walikua ni kutoka katika Ukoo wa Quraysh

ambao ni Abu Baqr As Siddiq, Umar Ibn Al Khattab, Uthman Ibn Affan, Ali Ibn

Abu Talib, Hamza Ibn Abd al Muttalib, Jafar Ibn Abu Talib, Abu Ubaydah Ibn

Jarrah, Uthman Ibn Mazun, Abd Rahman Ibn Awf, Saad Ibn Abi Waqqas. Talha

Ibn Abd Allah na Al Zubayr Ibn Awam Radhi Allahu Anhum’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anaelezea kuhusiana na Umuhimu wa watu wenye

darja ya Hawwariyyun pamoja na wafuasi wa Mitume katika Ummah zao, kua katika

siku ya Malipo wataulizwa Mitume kuhusiana nao wafuasi wao kua jee waliupokeaje

Ujumbe wa Mola wao juu yao kwa kusema:

‏﴿يَوْمَ‏ يجَْمَعُ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱلر ُّسُلَ‏ فَيَقُولُ‏ مَاذَآ أُجْبْتُمْ‏ قَالُواْ‏ لاَ‏ عِلْمَ‏ لَنَآ إِن َّكَ‏ أَنتَ‏ عَلا َّمُ‏

ٱلْغُيُوبِ‏ ﴾

Yawma yajmaAAu Allahu alrrusula fayaqoolu madha ojibtum qaloo la AAilma

lana innaka anta AAallamu alghuyoobi (Surat Al Maidah 5:109)

Tafsir: Katika siku ya Malipo wakati Allah Subhanah wa Ta’ala atakapowakusanya

Mitume na kuwaambia: ‘Hivi jee mlijibiwa nini (kutokana na watu wenu

mliowafikishia Ujumbe wenu)’ na wao watasema: ‘Hatuna sisi Ilm juu ya hilo, kwani

kwa hakika wewe ndie Mjuzi juu ya Kila kitu kilichofichakana’

Ambapo anasema Iman Abd Rahman Al Sudi kua: ‘Katika siku ya Malipo Mitume

watajibu kutokana na khofu baada ya kuulizwa suali hilo kua hakika sisi hatujui

walijibu vipi’ lakini baada ya hali ya khofu kutulia basi watatoa ushahidi dhidi ya

watu waliowafikishia Ujumbe wao’

Na akasema Sultan Al Balagha Imam Abu Al Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Kutokana

na kua ni wenye kujua kuhusiana na kuulizwa basi Mtume hao, na hivyo

kutokuwepo wazi kwa uwezekano wa kuadhbiwa ama la basi Mitume hao watajibu

kua wao hawajui kuhusiana na Ilm ya Ghayb, na hivyo kua ni wenye kumuwachia

Allah Subhanah wa Ta’ala atoe hukmu kulingana na Hikma zake, ambapo kwa


484

upande mwengine hii inamaanisha kua watadhihirisha kua Ilm yao mbele ya Mola

wao si chochote si lolote’

Yaani hii inakua kama walivyojibu Malaika pale alipoumbwa Nabii Adam kama

zinavyosema aya:

‏﴿وَعَل َّمَ‏ ءَادَمَ‏ الأَسمَْآءَ‏ كُل َّهَا ثمُ َّ عَرَضَهُمْ‏ عَلَى الْمَلَئِكَةِ‏ فَقَاَل أَ‏ نْبِئُ‏ وِنى

إِن كُ‏ نتُمْ‏ صَدِقِينَ‏ ۞

قَالُواْ‏ سُبْحَنَكَ‏ لاَ‏ عِلْمَ‏ لَنَآ إِلا َّ مَا عَل َّمْتَنَآ إِن َّ ‏َك أَن ‏َت

أبَِسمَْآءِ‏ هَؤُلاَِء

ٱلْعَلِيُم

ٱلحَْكِيمُ‏ قَالَ‏ يَاءَادَمُ‏ أَنبِئْهُم أبَِسمَْآئِهِمْ‏ فَلَم َّآ أَنْبَأَهُ‏ ‏ْم أبَِسمَْآئِهِم قَاَل أَقُلْ‏ ل َّكُمْ‏ إِنيّ‏ ِ

‏ِض وَأَعْلَمُ‏ مَا تُبْدُونَ‏ وَمَا كُنتُمْ‏ تَكْتُمُونَ﴾‏

أَعْلَمُ‏ غَيْبَ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْ‏

WaAAallama adama al-asmaa kullaha thumma AAaradahum AAala almala-ikati

faqala anbi-oonee bi-asma-i haola-i in kuntum sadiqeena; Qaloo subhanaka la

AAilma lana illa ma AAallamtana innaka anta alAAaleemu alhakeemu; Qala ya

adamu anbi/hum bi-asma-ihim falamma anbaahum bi-asma-ihim qala alam aqul

lakum innee aAAlamu ghayba alssamawati waal-ardhi waaAAlamu ma tubdoona

wama kuntum taktumoona; (Surat Al Baqara 2:31-33)

Tafsir: Wao (Malaika) wakasema: ‘Utukufu ni wako, Sisi hatuna I’lm isipokua ya kile

ulichotufundisha, hakika wewe ni mjuzi wa kila kitu na mwingi wa busara’. (Allah)

Akasema: ‘Ewe Adam watajie majina yake’, na alipowatajia majina ya vitu hivyo

(Allah akasema): ‘Jee sikukwambieni kua mimi najua mambo ya Ghayb

(yaliyofichika) Mbinguni na Ardhini, na nnajua kile mnachokiweka wazi na kile

mnachokificha’.

Ambapo tukio la kuulizwa kwa Malaika la Surat Al Baqara 2:31-33 limeshatokea kwani

lililotokea Mbinguni kabla ya Ibn Adam kushushwa Ulimwenguni na tukio la kuulizwa

Mitume la Surat Al Maidah 5:109 halijatokea na hivyo litatokea katika siku ya Malipo,

na kisha baada ya hapo Allah Subhanah wa Ta’ala atamkumbusha Nabii Isa Ibn Maryam

kuhusiana na neema alizomjaalia kwa idhini yake kama zinavyosema aya:

۞


485

‏﴿إِذْ‏ قَالَ‏ ٱهلل َُّ‏ يٰعِيسَى ٱبْنَ‏ مَرْيمََ‏ ٱذْكُرْ‏ نِعْمَتىِ‏ عَلَيْكَ‏ وَعَلَى ٰ وَالِدَتِكَ‏ إِذْ‏ أَي َّدت ُّ كَ‏

بِرُوحِ‏ ٱلْقُدُسِ‏ تُكَلِّمُ‏ ٱلن َّاسَ‏ فىِ‏ ٱلْمَهْدِ‏ وَكَهْلاً‏ وَإِذْ‏ عَل َّمْتُكَ‏ ٱلْكِتَابَ‏ وَٱلحِْكْمَةَ‏

وَٱلت َّوْرَاةَ‏ وَٱلإِنجِْيلَ‏ وَإِذْ‏ تخَْلُقُ‏ مِنَ‏ ٱلطِّينِ‏ كَهَيْئَةِ‏ ٱلط َّيرِْ‏ إبِِذْنىِ‏ فَتَنفُخُ‏ فِيهَا فَتَكُو ‏ُن

طَيرْ‏ اً‏ إبِِذْنىِ‏ وَتُبرِْىءُ‏ ٱلأَكْمَهَ‏ وَٱلأَبْرَصَ‏ إبِِذْنىِ‏ وَإِذْ‏ تخُْرِجُ‏ ٰ ٱلْمَوتَى إبِِذِْنى وَ‏ إِذْ‏ كَ‏ فَفْ‏ ‏ُت

بَنيِ‏ ۤ إِسْرَائِيلَ‏ عَنكَ‏ إِذْ‏ جِ‏ ئْتَهُمْ‏ بِٱلْبَيِّنَاتِ‏ فَقَالَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ مِنْهُمْ‏ إِنْ‏ هَٰذَا إِلا َّ

سِحْرٌ‏ م ُّبِينٌ‏ ﴾

Idh qala Allahu ya AAeesa ibna maryama odhkur niAAmatee AAalayka waAAala

walidatika idh ayyadtuka biroohi alqudusi tukallimu alnnasa fee almahdi wakahlan

wa-dth AAallamtuka alkitaba waalhikmata waalttawrata waal-injeela wa-idh

takhluqu mina altteeni kahay-ati alttayri bi-idhnee fatanfukhu feeha fatakoonu

tayran bi-idhnee watubri-o al-akmaha waal-abrasa bi-idhnee wa-idh tukhriju

almawta bi-idhnee wa-idh kafaftu banee isra-eela AAanka idh ji/tahum

bialbayyinati faqala alladheena kafaroo minhum in hadha illa sihrun mubeenun

(Surat Al Maidah 5:110)

Tafsir: (Kumbuka) Atakaposema Allah (katika siku ya Malipo): ‘Ewe Isa Ibn Maryam,

Unakumbuka Fadhila zangu juu yako na juu ya Mama yako pale nilipokuunga mkono

kwa Ruhul Qudus (Malaika Jibril) ili uwe ni mwenye kuzungumza na watu kutoka

kwenye Mkoba wa Mtoto Mchanga na Utakapokua Mkubwa, na nilipokufundisha

kuandika, na kukupa Hikma, na Tawrat na Injil. Na pale kile ulichokifanya kwa

udongo kwa umbile la Ndege, kwa idhini yangu nawe ukakipulizia na kikawa ndege

kwa Idhini yangu, na ukawaponyesha wale waliozaliwa vipofu kwa Idhini yangu, na

wenye maradhi ya Ukoma kwa Idhini yangu, na Kuwafufua waliofariki kwa Idhini

yangu, na nilipowazuia Bani Israil dhidi yako kutokna na kua umewajia na vithibitiso

vilivyo wazi kwao, na wasioamini miongoni mwao kua ni wenye kusema: ‘Hik si

chochote isipokua ni Uchawi uliowazi’’

Ambapo kuhusiana na maneno yasemayo kua Idh qala Allahu ya AAeesa ibna maryama

odhkur niAAmatee AAalayka waAAala walidatika idh ayyadtuka biroohi alqudusi -

(Kumbuka) Atakaposema Allah (katika siku ya Malipo): ‘Ewe Isa Ibn Maryam,

Unakumbuka Fadhila zangu juu yako na juu ya Mama yako pale nilipokuunga mkono

kwa Ruhul Qudus’ basi wanasema Wanazuoni kua hii ni Kuhusiana na Roho


486

aliyopuliziwa Isa Ibn Maryam ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala amempulizia ili iwe

na upekee wa kiheshima na huu ni mtizamo wa Imam Al Rab Ibn Anas.

Ambapo kwa upande mwengine basi kuna wanaosema kua maneno Ruhi Al Qudus yaani

Roho Mtakatifu yanamaanisha kua Utakatifu wa Roho ya Nabii Isa unatokana na kua

Maumble yake hayakutokana na Matamanio ya Kibinadamu kwa upande wa Mwanamme

na wala hayakutokana na hakukumbatiwa na Fuko la Uzazi linaloingia kwenye siku zake.

Ambapo kwa upande wa Imam Abd Rahman Al Suddi basi yeye anasema kua: ‘Ruh Al

Qudus hapa ni Malaika Jibril ambapo Isa Ibn Maryam amepewa Nguvu kutokana

nae Malaika Jibril, kwa sababu alikua ni rafiki wa karibu wa Malaika Jibril, alikua

akiimsadia, akitembea pamoja nae ardhini, na pia ndie aliepaa nae Mbinguni’

Kwani miongoni mwa sifa za Mailaka Jibril ni zile zilitajwa kwenye na maneno ya aya

isemayo:

‏﴿ذُو مِر َّةٍ‏ فَٱسْتَوَىٰ‏ ﴾

Dhoo mirratin faistawa (Surat An Najm 53:6)

Tafsir: Mwenye uwezo Mkubwa akasimama.

Anasema Bahr Ul Ilm Abdallah Ibn Abbar Radhi Allahu Anhu kua: ‘Neno Dhumirratin

hua linamaanishsa Muonekano Mzuri sana na wenye ukubwa wa kupendeza’ na pia

hua linamaanisha Kiumbe ambae asiekua na Kasoro Mwenye Nguvu Kubwa sana,

Ufahamu Mzuri sana na Afya na hivyo kumaanisha sifa ya Malaika Jibril. Na pia

humaanisha Ufaham Mzuri sana wa Mas’ala ya Fiqh na Sharia.

Ambapo anasema Imam Abd Rahman Al-Kalbi kua: ‘Siku Moja Malaika Jibiril

alimuona Ibili akitaka kumgusa na Kumdhuru Nabii Isa, hivyo Malaika Jibril

akampiga Ibisi kwa Ncha ya Ubawa wake ambao ulimpeperusha Iblisi hadi katika

Mlima uliopo India. Ni kutokana na Nguvu na Uwezo wake Malaika Jibril basi

amekua ni mwenye Kuwaadhiabu watu wa Thamud bila kuwacheleweshea Adhabu

yao mbali ya wingi wa idadi yao na Ukubwa wa Miili yao, na kutokana na uwezo

wake huo basi hu ni mwenye kusafiri kwa kasi kubwa sana kuenda na kurudi

Mbinguni na Ardhini.’

Ambapo kwa upande wa Imam Said Ibn Jubayr basi yeye anasema kua: ‘Ruhi Al Qudus

ni moja kati ya Majina Matukufu ya Allah Subhanah wa Ta’ala ambalo Isa Ibn

Maryam alikua kilitumia katika kuwahuisha watu waliokufa na kuwaonesha watu

Miujiza hio.’


487

Ama kuhusiana na Kitabu basi Wanazuoni wanasema kua ilikua ni Kitabu ambacho

chenye Juzuu 10 ambapo 9 kati yao pamoja na Hikma na Tawrat ilikua ni kwa ajili ya

Nabii Isa Ibn Maryam, ambapo Nabii Isa alikua amezihifadhi ndani ya Moyo wake.

Na anasema Imam Wahb Ibn Munabh kuhusiana Ndege kua : ‘Nabii Isa alikua

akifinyanga Ndege wa Udongo na kisha kumpulizia na akawa Ndege alie hai

kutokana na Idhini ya Allah Subhanah waa Ta’ala na alikua akifinyanga Ndege aina

ya Popo kwa sababu Ndege wa aina hio ni Ndege ambao waliokamilia kwani wana

Meno, Maziwa na pia hua wanaingia kwenye siku zao na hua hawatagi bali hua ni

wenye kuzaa. Na kisha baada ya kuruka kwao ndege hao basi huruka hadi katika

upeo wa Macho na kutoweka’

Ambapo kuhusiana na kuponyesha kwake Maradhi basi Nabii Isa alikua ni mwenye

kuponyesha wale ambao wasiowezekana kutibika kwani maradhi hayo yalikua ni wenye

kuwachanganya Matabibu kutokana na kutokuwepo uwezekano wa kutibika kwake kwa

kuwapangusa watu hao katika kiungo chenye Ugonjwa na kisha hua ni mwenye kusema

Biismi Allahi Rahmani Rahim na kiungo husika hua ni chenye kupona.

Imam Abd Rahman Al-Kalbi anasema kua Nabii Isa aliua na uwezo wa Kufufua kwa

kutumia majina Matukufu ya Allah Subanah wa Ta’ala ambayo ni : ‘Ya Hayyu Ya

Qayyum’

Ama kuhusiana na miongoni mwa waliofufuliwa na Nabii Isa baada ya kufariki kwao bas

yumo pia Al Adhar (Lazarus) ambae alikua ni rafiki yake Nabii Isa, ambapo Nabii Isa

alifunga safari kwa ajili ya kumtembelea rafiki yake huyo, lakn alipofika nyumbani

kwake akaambiwa kua Al Adhar ameshafariki mda mrefu uliopita, hivyo Nabii Isa

akaomba apelekewe kwenye Kaburi la Al Adhar na alipofika mbele yake basi akasema:

‘Ewe Allah, Mola wa Mbingu Saba na Ardhi saba, Hakka wewe ndie ulienituma

mimi kwa watu wa Bani Israil kuwaita kwa ajili ya kuifuata Dini yako, na

umewaambia Kua mimi nnaweza kuwahuisha Waliokufa kwa Idhini yako, hvo

nakuomba Ewe Mola wangu kua Mfufue Al Adhar’ Na hivyo Al Adhar akafufuka, na

kisha akawa ni mwenye kuishi na kisa akaoa na akajaaliwa kupata Watoto.

Miongoni mwa Sifa za Nabii Isa ni pamoja na kua nauwezo wa kutembea Juu ya Maji

Baharni bila ya kuzama ambapo amesema Imam Abu Mansur Al Khamshawi kua

amesema Muadh Ibn Jabal Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu

Alayh Wa Salam kua: ‘Kama mngekua mnamjua Allah Subhanah wa Ta’ala kwa

Ilm ya Yaqini basi mngefikia Darja ya Ilm ambayo hamna tena Ujinga baada yake

na ambayo hakuna alieifika.’ Hivyo Masahaba wakasema: ‘Hata wewe Ya Rasul

Allah?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam..Hata mimi’


488

Hivyo Masahaba wakasema: ‘Ya Rasul Allah! Hakika sisi tumesika kua Isa Ibn

Maryam alikua akitembea Juu ya Bahari’’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akasema: ‘Naam kama ikiwa Mtamcha Allah Subhanah wa Ta’ala na mkawa na

Imani zaidi basi pia angekua ni mwenye kutembea juu ya hewa’

Masahaba wakasema : ‘Ya Rasul Allah hakika sisi hatukufikria kua Mitume hua na

Kasoro pia’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hakika Allah

Subhanah wa Ta’ala ana darja zilizo juu zaidi kwa Mtu yeyote kuzifikia. ’.

Naam hio ni baadhi ya Miujiza ya Nabii Isa Ibn Maryam, ambapo hata hvyo ndan yake

mna Muujiza ambao hatujauzunguzma, kwani huu ni Muujiza ambao kutokana nna

upekee wake basi umepewa jina la Sura yake maalum ambayo ni Surat Al Maidah

inayoelezea ndani yake Muujiza wa Al Maidah kuanzia katika aya ya 112 ya Sura hio ya

5 ya Qur’an.

AL MAIDAH

Neno Maidah kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kukunuta. Kuondoa,

Kukereketwa, Kujaza au Kufunika Meza Funiko, Kitambaa au kwa Chakula, Kugawa

Chakula, Kutoa Riziki.

Neno Maidah ndio lililotoa neno Maidatun ambalo hua linamaanisha Kutandaza Meza

na Kuijaza Chakula juu yake, na pia humaanisha Kuujaza Ufahamu kwa Ilmu, kwani Ilm

hua ni chakula cha Ufaham.

Tunapokiangalia Kisa cha Nabii Isa Alayhi Salam basi Allah Subhana wa Ta’ala basi

tunaona kua amezungumzia kuhusiana na Neema na Muujiza wa Maidatun

aliyowatunukia watu wa Bani Israil pale aliposema katika Qur’an.

‏﴿إِذْ‏ قَالَ‏ ٱلحَْوَارِي ُّونَ‏ يٰعِيسَى ٱبْنَ‏ مَرْيمََ‏ هَلْ‏ يَسْتَطِيعُ‏ رَب ُّكَ‏ أَن يُنَزِّلَ‏ عَلَيْنَا مَآئِ‏ دَةً‏

مِّنَ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ قَالَ‏ ٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ إِن كُنْتُم م ُّؤْمِنِينَ۞‏ قَالُواْ‏ نُرِيدُ‏ أَن ‏ َّْكُل مِنْهَا وَتَطْمَئِ‏ َّن

َ

قُلُوبُنَا وَنَعْلَمَ‏ أَن قَدْ‏ صَدَقْتَنَا وَنَكُونَ‏ عَلَيْهَا مِنَ‏ ٱلش َّاهِدِينَ‏ ﴾

Idh qala alhawariyyoona ya AAeesa ibna maryama hal yastateeAAu rabbuka an

yunazzila AAalayna ma-idatan mina alssama-i qala ittaqoo Allaha in kuntum

mu/mineena; Qaloo nureedu an na/kula minha watatma-inna quloobuna


489

wanaAAlama an qad sadaqtana wanakoona AAalayha mina alshshahideena; (Surat

Al Maidah 5:112-13)

Tafsir: Na pale waliposema Al Hawariyyuuna: ‘Ewe Isa Ibn Maryam Jee anaweza

Mola wako kututeremshia sisi juu yetu Maidah Kutoka Mbinguni?’ akasema (Nabii

Isa): ‘Kuweni Wacha Mungu kama kweli nyinyi ni wenye kuamini.’ Nao wakasema:

‘Tunataka kula kutokana nayo kwa ajili ya kuzituliza Nyoyo zetu na kujua kua ni

ukweli unaotuambia na hivyo tutakua ni wenye kushuhudia.’

Aya zinatubanishia kua ndani yake watu hawa wa Hawariyyun kulikua kuna watu ambao

walikua wana hali ya kutaka kupima uwezo na nia ya Nabii Isa katika kua tayari

kufanikisha matakwa yao juu yake ili wapate kuzithibitishia Nyoyo zao zaidi, mbali ya

kua tayari wameshapandikiziwa dalili ya Imani kwenye nyoyo zao kutoka kwa Allah

Subhanah wa Ta’ala kuhusiana nae Nabii Isa, na ndio maana Nabii Isa akawaambia kua

wawe ni wenye kumcha Allah Subhanah wa Ta’ala kama kweli wameamini.

Ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye

anasema kua: ‘Ndani yake watu hawa kulikua kuna baadhi ya wachache ambao si

wenye Imani ya kweli nae, na walikua wakitafuta sababu ya kumtoa kasoro Nabii

Isa.’

Na kwa upande mwengine basi tunaona kua mbali ya kua neno Maidah hua inamaanisha

Meza iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwekewa Chakula cha Karamu juu yake lakini

kulingana na Mtizamo wa Wanazuoni basi wanasema kua neno hili Maidah katika aya

hii linamaanisha Aina ya Chombo kama Sufuria ambacho hua kinawekwa chini na

kuzungukwa na watu kwa ajili ya kula chakula kilichomo ndani yake. Na hivyo basi hua

linamaanisha Chakula.

Ama kwa upande wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye

anaelezea tukio hili la Hawariyyun kuomba washushiwe Maidah kwa kusema kua: ‘Isa

Ibn Maryam aliwaomba Wanafunzi wake wafunge kwa siku 30 na kisha waombe

Dua ambayo itajibiwa. Kwani kila afanyae kazi basi hulipwa ujira wake mwishoni

baada ya kumaliza kazi yake. Hivyo watu hao wakafunga na mwishoni mwa

Mfungo wao basi wakaomba kua washushiwe Maidah kutoka Mbinguni.’

Na amesema Amar Ibn Yasi Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua: ‘Maidah hii ilikua ikishuka ikiwa na Mkate na Nyama, na hii

ni kwa sababu walimuomba Nabii Isa chakula ambacho watakua wanakula bila ya

kukikinai’(Imam At Tirmidhi)

Na hivyo Nabii Isa akaahidi kua atawaombea chakula ambacho hawatakiwi kua na hiana

nacho, kwani wakati pale watakapokua hawakifichi au hawasalitiani miongoni mwao,


490

basi chakula hicho kitashuka kwa ajili yao, lakini wakiwa na hiana nacho basi

wataadhibiwa baada yake kutokana na hiana yao.

Hivyo baada ya watu hao kumaliza mda wa Ibada ya Kufunga kwao basi Nabii Isa Ibn

Maryam akanyanyua juu mikono na kumuomba Mola wake kwa kusema kama

zinavyosema aya:

‏﴿قَالَ‏ عِيسَى ٱبْنُ‏ مَرْيمََ‏ ٱلل َّهُم َّ رَب َّنَآ أَنزِلْ‏ عَلَيْنَا مَآئِدَةً‏ مِّنَ‏ ٱلس َّ مَآءِ‏ تَكُونُ‏ لَنَا عِيداً‏

ِ إِنىّ‏ مُنَزِّلهَُا عَلَيْكُ‏ ‏ْم

لِّأَو َّلِنَا وَآخِ‏ رَِ‏ وَآيَةً‏ مِّنْكَ‏ وَٱرْزُقْنَا وَأَنتَ‏ خَيْرُ‏ ٱلر َّازِقِينَ۞قَالَ‏ ٱهلل َُّ‏

فَمَن يَكْفُرْ‏ بَعْدُ‏ مِنكُمْ‏ ِ فَإِنيّ‏ ۤ أُعَذِّبُهُ‏ عَذَاابً‏ لا َّ أُعَذِّبُهُ‏ أَحَداً‏ مِّنَ‏ ٱلْ‏ عَ‏ الَمِينَ‏ ﴾

Qala AAeesa ibnu maryama allahumma rabbana anzil AAalayna ma-idatan mina

alssama-i takoonu lana AAeedan li-awwalina waakhirina waayatan minka

waorzuqna waanta khayru alrraziqeena; Qala Allahu innee munazziluha

AAalaykum faman yakfur baAAdu minkum fa-innee oAAadhdhibuhu AAadhaban

la oAAadhdhibuhu ahadan mina alAAalameena; (Surat Al Maidah 5:114-115)

Tafsir: Akasema Isa Ibn Maryam: ‘Ewe Allah, Ewe Mola wetu tushushie sisi Maidah

kutoka Mbinguni ili katika siku hii iwe ni Sikukuu kwa ajili ya wa Mwanzoni na wa

Mwishoni miongoni mwetu na iwe ni Dalili kutoka kwako, Turuzuku kwani wewe ni

m-bora wa kuruzuku. Akasema Allah (Subhanah wa Ta’ala): ‘Hakika mimi

nitakuteremshieni juu yenu(Maidah), lakini kama atakufuru baada yake mmoja wenu,

basi bila ya shaka nitamuadhibu yeye kama vile nitakavyomuadhibu kiumbe

mwengine yeyote’’

Hivyo baada ya Maombi hayo ya Nabii Isa Ibn Maryam kutoka kwa Watu wa Baani Israil

basi Allah Subhanah wa Ta’ala akajibu kwa kudhihirishwa kwa masharti ya kujibiwa

maombi hayo kua wanatakiwa waoneshe shukrani kutokana na kukubaliwa maombi yao

na kujaaliwa neema wanayoitaka, kwani kutoonesha shukrani hua kuna madhara

makubwa sana yanayotokana na adhabu ya alietoa Neema ambae ni Allah Subhanah wa

Ta’ala.

Ambapo tunapozungumzia kuhusiana na kuonesha Shukrani basi hua tunazungumzia

kuonesha Utiifu katika utumiaji wa neema hizo tulizokabidhiwa ambapo kutokana na

kuonesha kwetu huko utiifu basi hua pia ni wenye kudhihirisha shukrani zetu na

kuongezewa rehma za Allah Subhanah wa Ta’ala na ulinzi wake juu yetu kama

zinavyosema Aya:


491

‏﴿وَإِذْ‏ أتََذ َّنَ‏ رَب ُّكُمْ‏ لَئِن شَكَرْتمُْ‏ لأََزِيدَن َّكُمْ‏ وَلَئِن كَفَرْتمُْ‏ إِن َّ عَذَابىِ‏ لَشَدِيدٌ‏ ﴾

Wa-idh taadhdhana rabbukum la-in shakartum laazeedannakum wala-in kafartum

inna AAadhabee lashadeedun (Surat Ibrahim 14:7)

Tafsir: Na kumbuka wakati alipotangazia Mola wako kwa kusema: ‘Kama

Mtanishuruku basi nitakuzidshieni, lakini kama mkinikufuru basi kwa hakika adhabu

yangu ni kubwa sana.’

Kwani Nabii Daud alimwambia Allah Subhanah wa Ta’ala: ‘Ya Allah hivi nitawezaje

mimi kukushukuru wewe ipasavyo wakati katika kila nikikuonesha shukrani zangu

juu yako basi nawe hua unaniongezea Neema zaidi kutoka kwako?’ Allah Subhanah

wa Ta’ala akasema: ‘Hakika hivi sasa umenishukuru ipasavyo’

Ambapo anasema Imam Muqatil Ibn Sulayman kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala

akajibu maombi ya Nabii Isa na kumwambia nnakutumieni kile mlichokiomba. Na

yeyote yule atakaekula na kisha akawa si mwenye kuniamini basi nitamfanya kua

ni miongoni mwa Mifano na ni miongoni mwa laana kutoka kwangu na Onyo kwa

watu watakaokuja baadae’

Na baada ya watu wa Bani Israil kubainishiwa masharti hayo na Nabii Isa na kukubaliana

nayo basi mara wakashuka Malaika ambao walikua wamechukua Maidah ambayo ndani

yake mlikua mna Mikate 7 na Samaki 7 na kuwawekea mbele yao. Nao wakaanza kula

mmoja mmoja miongoni mwao tangu wa mwanzo wao hadi wa mwisho wao na kushiba

bila ya kupungua chakula hicho.

Ambapo anasema Imam Ata Ibn Saib kua: ‘Wakati Maidah hio iliposhushwa na

kuwekwa mbele yao watu wa Bani Israil, basi walikuja watu wengi sana na

wakaanza kutia mikono yao na kuchukua sehemu ya Maidah hio kwa ajili ya kula

na ilikua na kila aina za vyakula isipokua Nyama.’

Imam Qatadah Al Sadusi basi yeye anasema kua: ‘Wakati Maidah ilipokua ikishuka

basi ilikua na Matunda ya Peponi na ilikua inakuja Asubuhi na Jioni kwani ilikua

ni sawa na Manna na Salwa waliyopewa watu wa Bani Israil wa Nabii Musa.’

Amesema Salman Al Farisi Radhi Allahu Anhu kua: ‘Nabii Isa hakuwahi kua na

mpizani wala mtu aliekua na darja yake kwani hakua ni mwenye kuwafukuza

Mayatima, wala hakua ni mwenye kucheka, wala hakua ni mwenye kuwafukuza nzi


492

wanapotua mwilini mwake, hakua ni mwenye kukichukulia chochote kwa kujisifia,

hivyo Hawwariyyin walipomwabia kua wanataka Maidah washushiwe basi nae

akamuomba Mola wake ishuke Maidah hio.’

Baada ya Maidah hio kushushwa basi Nabii Isa akawa ni mwenye kulia huku akisema:

‘Ya Allah! Ewe Mola wangu, nijaalie mimi kua ni mwenye shukrani na ijaalie hii

Maidah iwe ni yenye kutufanya wenye kuonesha Shukrani, na wala usiijalie ikawa

ni mfano wa miongoni mwa Adhabu.’

Katika wakati huu watu wake hao wa Bani Israil walikua wamevutiwa na harufu nzuri

sana ya Maidah hio kiasi ya kua kila mmoja anataka kuionja kwa hamu kubwa kutokana

na harufu hio, hivyo Nabii Isa Ibn Maryam akawaambia watu wate wake kua: ‘Wacha

wabora Miongoni mwenu wawe ni wenye kuanza kuifunua Maidah hii, na waanze

kwa Biismi Allahi kabla ya kuanza kuila.’

Lakini Hawarriyyin wakasema: ‘La! Hakika wewe ndie mwenye kustahiki zaid

kuanza kuifungua Maidah hii na kwa kuanza kuila.’ Hivyo Nabii Isa Ibn Maryam

akanyanyuka akasali rakaa mbili ndefu na kisha akamuomba Mola wake tena kua asiijalie

kua ni Mtihani dhidi yao kisha akasema: ‘Bismi Allahi, Innaka Anta Khayrun Raziqiin’

Na hapo hapo akaifungua na Maidah ikawa aimejaa Vyakula na harufu yake nzuri ya

upekee na ya kuvutia ikahanikiza katika eneo lote hilo, ikawa kuna kila aina ya vitoweo

na kila aina ya mikate yenye Maziwa, yenye Siagi, yenye Asali, yenye Samli, yenye

mafuta ya Zaitun n.k

Watu wa Bani Israil wakawa ni wenye kula kutoka katika Maidah hio kwa mda wa siku

40. Ambapo kila siku asubuhi wanapokua na njaa na kutaka basi Maidah hua inatokea

na kila siku jioni baada ya kula na kushiba basi Maidah hio hua inatoweka, katika kipindi

hiki hakuna hata mtu mmoja aliekua akishinda na njaa wala alielala na njaa miongoni

mwao.

Ilipofika siku ya 40 miongoni mwa watu wa Bani Israil wenye uwezo wakapata habari

juu ya ya Maidah hio, hivyo nao wakawa wanakuja kula, lakini Allah Subhanah wa

Ta’ala akamwambia Nabii Isa kua: ‘Ifanye Maidah hii kua ni kwa ajili ya Masikini

na wala si kwa Matajiri’ hivyo Nabii Isa akafanya hivyo na akawazuia Matajiri

kutokana na kula vilivyomo ndani ya Miadah hio, na tukio hili liliwapelekea Matajiri

kuanzisha Fitna kuhusiana na ushukaji wa Maidah hio na kuanza kusambaza uvumi kua

wanashaka na Maidah hio, na hivyo kua ni wenye kuulizana na kuwauliza watu wa Bani

Israil kuhusiana na uhakika wa kushuka kwa Maidah hio kwa kusema: ‘Hivi Jee Maidah

hio mnaiona kua inateremka Kutoka Mbinguni au inatokea mbele yenu tu?’


493

Hivyo Nabii Isa akawaambia watu wake hao kua: ‘Jitayarisheni na Adhabu ya Mola

wenu kwani tayari mmeshavuka mipaka baada ya kutilia shaka Maamrisho yake’

Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Nabii Isa kua: ‘Bila ya shaka nilisema kua

yeyote yule asieamini juu ya kushuka kwake basi kwa hakika nitamshushia Adhabu

kubwa juu yake’

Hivyo Nabii Isa akasema:

‏﴿إِن تُعَذِّبْهُمْ‏ فَإِن َّهُمْ‏ عِبَادُكَ‏ وَإِن تَغْفِرْ‏ لهَُمْ‏ فَإِن َّكَ‏ أَنتَ‏ ٱلْعَزِيزُ‏ ٱلحَْكِيمُ‏ ﴾

In tuAAadhdhibhum fa-innahum AAibaduka wa-in taghfir lahum fa-innaka anta

alAAazeezu alhakeemu; (Surat Al Maidah 5:116-119)

Tafsir: Hakika kama utawaadhibu basi wao ni waja wako na kama utawasamehe basi

kwa hakika wewe ni Mwingi wa Uwezo na Mwingi wa Hikma’

Wanazuoni wanasema kua kua miongoni mwa watu waliokua na shaka baada ya kuona

Maidah hio walikua ni watu 330000 ambao siku ya pili asubuhi yake wote waligeuka kua

ni Nguruwe, ambao walitapakaa mitaani, na hivyo watu waliokua walioamini juu ya

kushuka kwa Maidah hio na kua wako salama basi wakawa na khofu kubwa sana,

wakamfuataNabii Isa kwani miongoni mwao walikau ni watu wa familia zao na walikua

wakiwaita kwa majina basi walikua wakiwafuata, lakini hawawezi kuzungumza baina

yao, na Nguruwe hao waliishi kwa mda wa siku 3 na kisha wakafariki wote.

Miongoni mwa Miujiza Nabii Isa Ibn Maryam ilikua pia ni kufufua kwake watu

waliokufa na kuwafanya wawe hai, ambapo mja kati ya matukio hayo ni kua siku kadhaa

alipokua akipita makaburini aliwahi kukutana na Mtu ambae alikua amekaa kwenye

Kaburi moja huku akiwa na huzuni kubwa sana, na hivyo kumuuliza imekuaje mpaka

ikawa kila siku anakaa hapo Kaburini? Ambapo mtu huyo akajibu kua aliezikwa hapo

alikua ni Mke wake ambae uzuri wake na maumbile yake yalikua mazuri sana, na yeye

alikua akimpenda sana.

Hivyo Nabii Isa Ibn Maryam akamwambia Mtu huyo kua: ‘Hivi Jee unataka nimuombe

Allah Subahanah wa Ta’ala amfufue?’ Yule Mtu akasema : ‘Naam’ hivyo Nabii Isa

Ibn Maryam akasali rakaa 2 na kisha akamuomba Allah Subhanah wa Ta’ala amfufue

Mtu huyo, na mara hapo hapo kaburi hilo likafunguka na akatoka Mtu ambae alikua

Mweusi na hivyo Nabii Isa Ibn Maryam akamuuliza Mtu huyo: ‘Wewe ni Nani?’

Ambapo Mtu huyo akasema: ‘Ya Rasul Allah hakika mimi ni Mtu ambae nipo kwenye

Adhabu kwa mda wa miaka 40, na katika wakati huu nimeambiwa Nijibu kwa

kufufuka nami nikajibu kwa kufufuka. Ya Rasul Allah hakika mimi nishaadhibiwa


494

kwa adhabu kali sana, hivyo kama Allah Subhanah wa Ta’ala atanirudsha Duniani

basi sitomuas tena, Hivyo nakuomba niombee.’

Hivyo Nabii Musa akamuonea huruma Mtu huyo na akamuombea, na kisha

akamwambia: ‘Haya Nenda zako.’ Mtu huyo akaondoka, ambapo yule mtu aliekua

amekaa kaburini analia akamwambia Nabii Isa Ibn Maryam kua: ‘Ya Rasul Allah hakika

mimi nilikosea kuhusiana na Kaburi la Mke wangu, sio hili alilotoka huyu bwana

bali ni hili hapa’

Hivyo Nabii Isa Ibn Maryam akamuomba tena Allah Subhanah wa Ta’ala na hapo hapo

Kaburi hilo jengine likafunguka na ndani yake akatoka Mwanamke Mzuri sana. Hivyo

Nabii Isa Ibn Maryam akamwambia Nabii Isa: ‘Jee unamjua huyu Mwanamke?’ yule

Mtu akasema: ‘Naam, huyu ndie Mke wangu’ hivyo Isa Ibn Maryam akamuomba Allah

Subhanah wa Ta’ala kua Mwanamke huyo aendelee kuishi, hivyo Mtu huyo na Mke

wake wakamshukuru Nabii Isa kisha wakaondoka.

Katika safari yao Mtu na mke wake huyo, basi wakapumzika chini ya Mti, na Mume

akalala, mara akapita Mtoto wa Mfalme na baada ya kumuona Mke huyo akampenda na

kuvutiwa nae, na akamuashiria Mke huyo amfuate, na Mke huyo akavutiwa na Mtoto wa

Mfalme na kuamua kumfuata.

Mwenye mke alipoamka bila ya kumuona Mke wake basi akaamua kumtafuta Mke wake,

na kwa bahati akamuona pamoja na Mtoto wa Mfalme na alipomkimbilia na kusema kua

ni Mke wake, basi Mtoto wa Mfalme akasema kua ni Mtumwa wake yeye, hivyo wakati

mvutano huo unaendelea mara akatokea Nabii Isa ambapo Mume wa Mke huyo

akamlalamikia kuhusiana na yaliyotokea, na Mke huyo alipotakiwa kurudi kwa Mume

wake basi akasema kua yeye ni Mtumwa wa Mtoto wa Mfalme na hamjui Mwanamme

huyo.

Hivyo Nabii Isa akamwambia Mke huyo: ‘Turudishe Amanah tuliyokupa.’ Na Mke

huyo akasema: ‘Bila ya shaka nitakurudishia’ na kisha hapo hapo Mke huyo akaanguka

chini na kufariki na hapo Nabii Isa akasema kumwambia yule Mume: ‘Hivi Jee umewahi

kuona Jambo la kustaajabisha zaidi ya yule Mwanamme? Allah Subhanah wa

Ta’ala alimpa Mtihani wa Kifo wakati akiwa ni Kafiri na kisha akamfufua na

akawa ni mwenye Kuamini’

‘Na jee umewahi kuona Mwanamke ambae Allah Subhanah wa Ta’ala alimuingiza

kwenye Mtihani wa Kifo huku akiwa Mwenye Kuamini lakini akawa Kafiri baada

ya kufufuliwa kwake?’

Nabii Isa aliwafufua watu wanane ambapo Watu wa Bani Israil wakamwambia Nabii Isa

kua: ‘Hakika wewe Isa ni mwenye kuwafufua watu ambao wamefariki Karibuni, na


495

hivyo hua hawajaondokewa na roho zao bado, kama kweli wewe na uwezo huo basi

tufufulie wale watu waliofariki zamani sana.’

Hivyo Nabii Isa akawaambia watu hao kua: ‘Sawa hivyo Jee mnataka nimfufue Nani?’

Watu hao wakasema: ‘Mfufue Sham Ibn Nuh’

Nabii Isa akasema: ‘Nionesheni Kaburi lake’ hivyo watu hao wakamuonesha Nabii Isa

Kaburi la Sham ambae ni Mtoto wa Nabii Nuh.

Nabii Isa Ibn Maryam alpofika kwenye Kaburi hilo basia akaomba Dua kisha akasema;

‘Ewe Sham, Fufuka kwa Idhini Ya Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Hivyo Sham akafufuka kutoka kwenye Kaburi hilo huku akiwa ni mwenye kusema: ‘Ya

Rasul Allah Hakika Mimi nipo chini ya Amri yako.’ Na watu wa Bani Israil

wakamuona kua ni mwenye Ndevu na Nywele Nyeupe, hivyo wakamuuliza: ‘Imekuaje

Na Mvi wakati ulipofariki ulikua Kijana’ na Sham akasema: ‘Hakika mimi nilisikia

Sauti ikiniamrisha Ninyanyuke, na hivyo kutokana na kua na khofu juu ya Siku ya

Malipo, na nikadhani kua ni sauti ya Israfil na hivyo Nywele zangu zikawa na rangi

nyeupe kwa khofu’

Nabii Isa akasema: ‘Vipi unasemaje? Unatakaa kuendelea kuishi au unataka kurudi

kaburini?’ Sham Ibn Nuh akauliza: ‘Ya Rasul Allah, jee kama nikiendelea Kuishi

halafu itakuaje nitakufa tena ama vipi?’ Nabii Isa akajibu: ‘Naam Mwisho wake

Utakufa’ Sham akasema: ‘Kwa maana hio basi hakika mimi sitoepukana na

Machungu ya Kifo’ Hivyo Sham akarudi tena Kaburini, ambapo wanasema wenye kujua

kua Sham alifariki miaka 4000 kabla ya kuja Nabii Isa Ibn Maryam.

Hivyo kutokana na Miujiza yake hii ya kufufua Watu na myengineo basi imewapelekea

Wakristo kusema kua Nabii Isa ni Mungu na pia ni Mtoto wa Mungu kama vile

wanavyoema Mayahudi kuhusiana na Uzayr kama inavyosema Qur’an;

‏﴿وَقَالَتِ‏ ٱلْيَهُودُ‏ عُزَيْرٌ‏ ٱبْنُ‏ ٱهلل َِّ‏ وَقَالَتِ‏ ٱلن َّصَارَى ٱلْمَسِ‏ يحُ‏ ٱبْنُ‏ ٱهلل َِّ‏ ذٰلِكَ‏ قَوْلهُُ‏ م

أبَِفْوَاهِهِمْ‏ يُضَاهِئُونَ‏ قَوْلَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ مِن قَبْلُ‏ قَاتَلَهُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ أَنى َّٰ‏ يُؤْفَكُونَ‏ ﴾

Waqalati alyahoodu AAuzayrun ibnu Allahi waqalati alnnasara almaseehu ibnu

Allahi dhalika qawluhum bi-afwahihim yudhahi-oona qawla alladheena kafaroo

min qablu qatalahumu Allahu anna yu/fakoona (Surat At Tawba 9:30)


496

Tafsir: Na wanasema Mayahud kua Uzayr ni Mtoto wa Allah na wanasema Manasara

kua Al Masih ni mtoto wa Allah, hii ni kauli kutoka kwenye Midomo yao, wanaiga

kauli za wale waliokufuru kabla yao. Laana ya Allah iwe juu yao kwani wako mbali

na Ukweli.

Na hivyo Allah Subhanah wa’a Ta’ala anatubainisha kwa vithibitisho kua wasemavyo

hiyo wako mbali na ukweli na hii ni kwa sababu Nabii Isa Ibn Maryam ni Nabii wake na

ni Mtume wake, na wala sio Mungu, hivyo kua na Mtizamo mwengine zaidi ya huo basi

hua ni kukufuru kama inavyosema Surat Al Maidah kua:

‏﴿ل َّ قَدْ‏ كَفَرَ‏ ٱل َّذِينَ‏ قَآلُو ۤ اْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ هُوَ‏ ٱلْمَسِ‏ يحُ‏ ٱبْنُ‏ مَرْيمََ‏ قُلْ‏ فَمَن يمَْلِكُ‏ مِنَ‏ ٱهلل َِّ‏

شَيْئاً‏ إِنْ‏ أَرَادَ‏ أَن يُهْلِكَ‏ ٱلْمَسِ‏ يحَ‏ ٱبْنَ‏ مَرْيمََ‏ وَأُم َّهُ‏ وَمَن فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ جمَِيعاً‏ وَهللِ َِّ‏ مُلْ‏ ‏ُك

ّ كُل شَيْءٍ‏ قَدِيرٌ‏ ﴾

ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَمَا بَيْنَهُمَا يخَْلُقُ‏ مَا يَشَآءُ‏ وَٱهلل َُّ‏ ٰ عَلَى ِ

Laqad kafara alladheena qaloo inna Allaha huwa almaseehu ibnu maryama qul

faman yamliku mina Allahi shay-an in arada an yuhlika almaseeha ibna maryama

waommahu waman fee al-ardhi jameeAAan walillahi mulku alssamawati waalardhi

wama baynahuma yakhluqu ma yashao waAllahu AAala kulli shay-in

qadeerun (Surat Al Maidah 5:17)

Tafsir: Kwa hakika wamekufuru wale ambao wasemao kua Allah ni Masih Ibn

Maryam, waambie (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam): ‘Jee ni nani

atakaeweza kua na umiliki wa pamoja na Allah juu ya kitu chochote kile kama (Allah

Subhanah wa Ta’ala) akitaka kumuangamiza Masih Ibn Maryam na Mama na kila

kitu hapa ardhini kwa pamoja? Kwani kwa Allah ndiko kwenye Umiliki wa Mbingu

na Ardhi na kla klichomo baina yake Mwenye uwezo wa Kuumba akitakacho, Allah

ana uwezo juu ya kila kitu.’

Ambao hii ni aya inayokataa na kukanusha kuwepo kwa ushirika baina ya Allah

Subhanah wa Ta’ala katika Mamlaka yake ya Umungu si kwa Nabii Isa tu bali pia na

kwa Maryam Bint Imran, na hivyo kubainisha kua hakuna tofauti baina ya Isa bn Maryam

na Maryam Bint Imran kwani wote ni viumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala.

Ambapo katiika aya hii basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala hakutumia jina la

Nabii Isa kama Isa Ibn Maryam, bali ametmia Jina la Sifa yake kuu ambayo inawapelekea

watu kua ni wenye kumdhania kua ni Mungu, yaani aya imetumia jina la Masih Ibn

Maryam ambalo tumesema kua linamaanisha Kupangusa, Kufuta, Kupapasa kwa


497

Utaratibu, Kupakaza Kitu, Kupaka kitu kwenye Mwili, Kupitisha Mkono juu ya Kitu,

Kupendeza, kua Nzuri na yenye Baraka, Kufunga safari ya Kutembea ardhini na pia

humaanisha Mfalme au Muokozi.

Na hivo kuanisha kua sifa yake hio ya kua na Uwezo wa kugusa Mgonjwa akapona na

ya Uokozi pia haimfanyi kua ni mwenye sifa za Kimungu, na kisha aya zinaweka wazi

kwa kuhoji kwa kusema kua: ‘Jee ni nani atakaeweza Kumzuia Allah Subhanah wa

Ta’ala kama akitaka kumuangamiza huyo Masih Ibn Maryam na Maryam Bint

Imran kama akiamua kuwaangamiza wao na kila kitu klichomo Ardhini?’

UTHIBITISHO WA ISA IBN MARYAM KUA SI MUNGU.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anawabainishia Wakristo na Mayahudi kua

wasishangazwe na Maumbile ya Isa Ibn Maryam kwani yeye ni Kiumbe kama viumbe

wengine, kwani nae Isa Ibn Maryam alibainisha juu ya hayo na hivyo wanaosema

kinyume na maneno yake mwenyewe Isa Ibn Maryam basi ni wenye kukufuru, kama

zinavyoendelea kubainisha tena Aya za Surat Al Maidah kua:

‏﴿لَقَدْ‏ كَ‏ فَ‏ رَ‏ ٱل َّذِينَ‏ ۤ قَالُواْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ هُوَ‏ ٱلْمَسِ‏ يحُ‏ ٱبْنُ‏ مَرْيمََ‏ وَقَالَ‏ ٱلْمَسِ‏ يحُ‏ ‏َبَنيِ‏ ۤ إِسْرَائِيل

ٱعْبُدُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ رَبىِّ‏ وَرَب َّكُمْ‏ إِن َّهُ‏ مَن يُشْرِكْ‏ بِٱهلل َِّ‏ فَقَدْ‏ حَر َّمَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلَيهِ‏ ٱلجَْن َّةَ‏ وَ‏ مَ‏ أْوَاهُ‏ ٱلن َّا ‏ُر

وَمَا لِلظ َّالِمِينَ‏ مِنْ‏ أَنصَارٍ۞ل َّقَدْ‏ كَفَرَ‏ ٱل َّذِينَ‏ ۤ قَالُواْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ اثَلِثُ‏ ثَلاَثَةٍ‏ ‏َومَا مِنْ‏ إِلَ‏ ٍٰه

إِلا َّ إِلَٰهٌ‏ وَاحِ‏ دٌ‏ وَإِن لم َّْ‏ يَنتَهُواْ‏ عَم َّا يَقُولُونَ‏ لَيَمَس َّن َّ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ مِنْهُمْ‏ عَذَابٌ‏ أَلِ‏ يمٌ‏ ﴾

َ

Laqad kafara alladheena qaloo inna Allaha huwa almaseehu ibnu maryama waqala

almaseehu ya banee isra-eela oAAbudoo Allaha rabbee warabbakum innahu man

yushrik biAllahi faqad harrama Allahu AAalayhi aljannata wama/wahu alnnaru

wama lildhdhalimeena min ansarin; Laqad kafara alladheena qaloo inna Allaha

thalithu thalathatin wama min ilahin illa ilahun wahidun wa-in lam yantahoo

AAamma yaqooloona layamassanna alladheena kafaroo minhum AAadhabun

aleemun; (Surat Al Maidah 5:72-73)

Tafsir: Kwa hakika wamekufuru wale ambao ni wenye kusema kua Allah Masihu Ibn

Maryam’ wakati Masih Ibn Maryam mwenyewe amesema: ‘Enyi watu wa Bani Israil

Muabuduni Allah ambae ni Mola wangu na ni Mola wenu, kwani kwa hakika


498

anaemshirikisha Allah, basi Allah amemharamishia Pepo na makazi yake yatakua ni

Motoni na kwa wenye kufanya Dhulma basi hakuna wa kuwanusuru.’ Kwa hakika

Wamekufuru wale ambao ni wenye kusema kua kwa hakika Allah ni wa tatu katika

Watatu. Na hakuna aliekua Mungu isipokua Mungu ambae ni Mmoja, na kama

hawakusita kutokana na wayasemayo, basi kwa hakika watakumbana wale wenye

kukufuru na adhabu kali sana.

Naam baada ya Allah Subhanah wa T a’ala kudhihirisha maneno ya Al Masih Isa Ibn

Maryam kwa watu wake wa Bani Israil na Manasara, na kukanusha Utatu wa Kimungu

na kuthibisha Umoja wake basi Allah Subhanah wa Ta’ala anawaonya na kuwausia kwa

kuwaambia kua anawataka wale wenye kuamini kinyume chake kama alivyosema yeye

kua yeye yuko tayari kuwasamehe kama watamuomba Msamaha kwani yeye ni mwenye

Sifa ya kua ni Mwingi wa Usamehevu na Mwingi wa Huruma, kama zinavyosema aya:

‏﴿أَفَلاَ‏ يَتُوبُونَ‏ إِلىَٰ‏ ٱهلل َِّ‏ وَيَسْتَغْفِرُونَهُ‏ وَٱهلل َُّ‏ غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ‏۞م َّا ٱلْمَسِ‏ يحُ‏ ٱبْنُ‏ مَرْيمََ‏ إِلا َّ

رَسُولٌ‏ قَدْ‏ خَلَتْ‏ مِن قَبْلِهِ‏ ٱلر ُّسُلُ‏ وَأُم ُّهُ‏ صِدِّيقَةٌ‏ كَاَ‏ ‏َْكُلاَنِ‏ ٱلط َّعَامَ‏ ٱنْظُرْ‏ كَيْفَ‏

نُبَينِّ‏ ُ لهَُمُ‏ ٱلآَتِ‏ ثمُ َّ ٱنْظُرْ‏ أَنى َّٰ‏ يُؤْفَكُونَ‏ ﴾

Afala yatooboona ila Allahi wayastaghfiroonahu waAllahu ghafoorun

raheemun; Ma almaseehu ibnu maryama illa rasoolun qad khalat min qablihi

alrrusulu waommuhu siddeeqatun kana ya/kulani alttaAAama ondhur kayfa

nubayyinu lahumu al-ayati thumma ondhur anna yu/fakoona (Surat Al Maidah 5:74-

75)

Tafsir: Hivyo jee hawatotubu kwa Allah na kuomba msamaha kwani kwa hakika Allah

ni mwingi wa Usamehevu na na mwingi wa Huruma. Hakua Masih Ibn Maryam

isipokua ni Mtume, kwa hakika wamekuja kabla yake Mitume. Na Mama yake alikua

ni aliesadiki wote walikua ni wenye kula Vyakula, angalia namna tunavyowabainisha

wazi Aya zetu lakini hata hivyo angalia wanavyopotoka.

Anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Aya hii

inatubainishia kua Mitume wote walikua ni Ibn Adam na hivyo hawakua na

Maumbile mengine yeyote ya Kimalaika wala ya Kijini’

Ambapo Sultan Mutakallimin Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye

anasema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala anawaelezea Isa Ibn Maryam na Maryam

Bnt Imran kua walikua n wenye Kula vyakula na hivyo basi kuthibitisha kua ni


499

wenye kujisaida pia’ hivyo jee inakuaje wenye sifa ya kua ni Watu kua ni wenye

kuhesabiwa kua ni Miungu?

Kwani Allah Subhanah wa Ta’ala hakuwahi kuwaletea watu hapo kabla Mitume ambao

ni wenye maumbile ya Majini au Malaika, bali hua daima ni mwenye kuwatumia Ibn

Adam wenzao na ndio maana akasema:

‏﴿وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ‏ إِلا َّ رِجَالاً‏ ن ُّوحِ‏ ي ۤ إِلَيْهِمْ‏ مِّنْ‏ أَهْلِ‏ ٱلْقُرَىٰ‏ أَفَلَمْ‏ يَسِ‏ يرُواْ‏ فىِ‏

ٱلأَرْضِ‏ فَيَنظُرُواْ‏ كَيْفَ‏ كَانَ‏ عَاقِبَةُ‏ ٱل َّذِينَ‏ مِن قَبْلِهِمْ‏ وَلَدَارُ‏ ٱلآخِ‏ رَةِ‏ خَ‏ يْرٌ‏ لِّل َّذِينَ‏

ٱت َّقَواْ‏ أَفَلاَ‏ تَعْقِلُونَ‏ ﴾

Wama arsalna min qablika illa rijalan noohee ilayhim min ahli alqura afalam

yaseeroo fee al-ardhi fayandhuroo kayfa kana AAaqibatu alladheena min qablihim

waladaru al-akhirati khayrun lilladheena ittaqaw afala taAAqiloona (Surat Yusuf

12:109)

Tafsir: Na Hatujawahi kutuma (Mtume) kabla yako isipokua ni watu miongoni mwao

kuwashushia wao. Hivi jee hawajatembea kwenye ardhi wakaona mwisho wa wale

waliokua kabla yao? Na kwa hakika makazi ya Akhera ni bora kwa wenye kua na

Taqwa. Jee hamna akili?

Aya imetumia neno Rijalan ambalo hua ni lenye kutokana na neno Rajila au Rajala

ambalo hua ni lenye kumaanisha Kutembea kwa miguu miwili, Kuhimiza kwa kutumia

miguu, Kuruhusu Mama kumnyonyesha Mtoto wake, Kuachia huru na Mama yake,

hivyo neno Rijalan humaanisha Mtu, ambapo Rijal hua ni Mwanamme.

Na Imani ya Dini ya Kislam ni yenye kusimamia kwenye msingi wa Imani ya

kumpwekesha Allah Subhnah wa Ta’ala pekee na hivyo haikubaliki kuwepo kwa Mungu

mwengine zaidi yake Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani kufanya hivyo hua ni kwenye

Kumtoa Muislam katika Imani ya Dini yake, na kutokana na kua watu wa Ahl Al Kitab

yaani Wakristo hua ni wenye kuamini kua Nabii Isa ni mwenye Sifa ya Kiumbe

sambamba na ya Kimungu basi Allah Subhanah wa Ta’ala anawabanishia ukweli watu

hao kwa kuwaonya kwa kusema kua:


500

‏﴿َٰهْ‏ لَ‏ ٱلْكِتَابِ‏ لاَ‏ تَغْلُواْ‏ فىِ‏ دِينِكُمْ‏ وَلاَ‏ تَقُولُواْ‏ عَلَى ٱهلل َِّ‏ إِلا َّ ٱلحَْق َّ إِ‏ نم ََّا ٱلْمَسِ‏ يحُ‏

عِيسَى ٱبْنُ‏ مَرْيمََ‏ رَسُولُ‏ ٱهلل َِّ‏ وَكَلِمَتُهُ‏ أَلْقَاهَا إِلىَٰ‏ مَرْيمََ‏ وَرُوحٌ‏ مِّنْهُ‏ فَآمِنُواْ‏ بِٱهلل َِّ‏ وَرُسُلِِه

وَلاَ‏ تَقُولُواْ‏ ثَلاَثَةٌ‏ ٱنتَهُواْ‏ خَيرْ‏ اً‏ ل َّكُمْ‏ إِنم ََّا ٱهلل َُّ‏ إِلَٰهٌ‏ وَاحِ‏ دٌ‏ سُبْحَانَهُ‏ أَن يَكُونَ‏ لَهُ‏ وَلَدٌ‏ ل َّهُ‏

مَا فىِ‏ ٱلس َّمَاوَا ‏ِت وَمَا فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ ٰ وَكَفَى بِٱهلل َِّ‏ وَكِيلاً۞‏ ل َّن يَسْتَنكِفَ‏ ٱلْمَ‏ سِ‏ يحُ‏ أَن

‏ْف عِبَادَتِهِ‏ وَيَسْتَكْبرِْ‏

عَنْ‏ ۤ ئِكَةُ‏ ٱلْمُقَر َّبُونَ‏ وَمَن يَسْتَنْكِ‏

يَكُونَ‏ عَبْداً‏ هللِ َِّ‏ وَلاَ‏ ٱلْمَلا

فَسَيَحْشُرُهُمْ‏ إِلَيهِ‏ جمَِيعاً‏ ﴾

Ya ahla alkitabi la taghloo fee deenikum wala taqooloo AAala Allahi illa alhaqqa

innama almaseehu AAeesa ibnu maryama rasoolu Allahi wakalimatuhu alqaha ila

maryama waroohun minhu faaminoo biAllahi warusulihi wala taqooloo

thalathatun intahoo khayran lakum innama Allahu ilahun wahidun subhanahu an

yakoona lahu waladun lahu ma fee alssamawati wama fee al-ardhi wakafa biAllahi

wakeelan Lan yastankifa almaseehu an yakoona AAabdan lillahi wala almala-ikatu

almuqarraboona waman yastankif AAan AAibadatihi wayastakbir

fasayahshuruhum ilayhi jameeAAan (Surat AnNisaa 4:171-172)

Tafsir: Enyi watu wa Ahl Al Kitab msivuke mipaka katika Dini yenu na wala msiseme

kuhusiana na Allah ispokua Ukweli, kwa hakika Masih Isa Ibn Maryam ni Mtume wa

Allah na ni Kauli yake ambayo alibeba Maryam, na Ruh kutoka kwake, hivyo

Muaminini Allah na Mitume wake na wala msiseme : ‘Utatu, Kusitisha kwenu ni bora,

kwani Allah ni Mmoja tu, Utukufu ni wake peke yake na yuko mbali yeye kutokana na

kua na Mtoto’ Kwake yeye ndio kwenye umiliki wa kila kilichomo Mbinguni na

Ardhini, Hakika llah ni mwenye kutosheleza juu ya usimamizi wa kila kitu. Kwani

kamwe Masih hatokua na fakhari ya kukataa kua yeye ni Mja wa Allah, na Wala

Malaika waliokaribu nae Allah Subhanah wa Ta’ala, na yeyote yule atakaekosa fahari

ya Uja wake (mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala) na akawa na Kibri basi (Allah

Subhanah wa Ta’ala) atawakusanya wote kwa pamoja mbele yake (katika siku ya

malipo).

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kutuambia kua atawauliza Mitume

kuhusiana na namna walivyopokewa na watu wao baada ya kuwafikishia Ujumbe wao,

kutoka kwake, ambapo mongoni mwao watakaoulizwa basi yumo pia Isa Ibn Maryam

ambapo hali itakua kama zisemavyo aya:


501

‏﴿وَإِذْ‏ قَالَ‏ ٱهلل َُّ‏ يٰعِيسَى ٱبْنَ‏ مَرْيمََ‏ أَأَنتَ‏ قُلتَ‏ لِلن َّاسِ‏ ٱتخ َِّذُونىِ‏ وَأُمِّىَ‏ إِلَٰهَينِْ‏ مِن

دُونِ‏ ٱهلل َِّ‏ قَالَ‏ سُبْحَانَكَ‏ مَا يَكُونُ‏ ليِ‏ ۤ أَنْ‏ أَقُولَ‏ مَا لَيْسَ‏ لىِ‏ بحَِقٍّ‏ إِن كُنتُ‏ قُلْتُهُ‏

فَقَدْ‏ عَلِمْتَهُ‏ تَعْلَمُ‏ مَا فىِ‏

نَفْسِ‏ ى وَلاَ‏ أَعْلَمُ‏ مَا فىِ‏ نَفْسِ‏ كَ‏ إِن َّكَ‏ أَنتَ‏ عَلا َّمُ‏

ٱلْغُيُوبِ‏ ‏۞مَا قُلْتُ‏ لهَُمْ‏ إِلا َّ مَآ أَمَرْتَنىِ‏ بِهِ‏ أَنِ‏ ٱعْبُدُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ رَبىِّ‏ وَرَب َّكُمْ‏ وَكُن ‏ُت عَلَيْهِ‏ ‏ْم

ل

ّ

شَهِيداً‏ م َّا دُمْتُ‏ فِيهِمْ‏ فَلَم َّا تَوَف َّيْتَنىِ‏ كُنتَ‏ أَنتَ‏ الر َّقِيبَ‏ عَ‏ لَيْهِ‏ مْ‏ وَأَنتَ‏ ٰ عَلَى كُ‏ ِ

شَيْءٍ‏ شَهِيدٌ‏ ﴾

Wa-idh qala Allahu ya AAeesa ibna maryama aanta qulta lilnnasi ittakhidhoonee

waommiya ilahayni min dooni Allahi qala subhanaka ma yakoonu lee an aqoola ma

laysa lee bihaqqin in kuntu qultuhu faqad AAalimtahu taAAlamu ma fee nafsee

wala aAAlamu ma fee nafsika innaka anta AAallamu alghuyoobi; Ma qultu lahum

illa ma amartanee bihi ani oAAbudoo Allaha rabbee warabbakum wakuntu

AAalayhim shaheedan ma dumtu feehim falamma tawaffaytanee kunta anta

alrraqeeba AAalayhim waanta AAala kulli shay-in shaheedun(Surat Al Maidah

5:116-117)

Tafsir: Na kumbuka wakati Allah Subhanah wa Ta’ala atakaposema (katika siku ya

Malipo); ‘Ewe Isa Ibn Maryam! Hivi jee uliwaambia wewe watu kua: ‘Nichukulieni

Mimi na Mama yangu kama Miungu wawili baada ya Allah?’ Atasema (Nabii Isa):

‘Utukufu ni wako Allah! Siwezi mimi kusema kile ambacho sina haki ya kusema juu

yake. Hivyo kama ningesema kitu kama hicho, basi kwa hakika wewe ni mwenye kujua

juu yake, kwani wewe ni mwenye kujua kile kilichomo ndani ya Nafsi yangu wakati

mimi si mwenye kujua kilichomo ndani ya Nafsi yako. Bila ya shaka ni wewe pekee

ndie mwenye kujua vilivyofichikana na visivyoonekana’’Hakika mimi sikuwaambia

isipokua kile ambacho uliniamrisha (niwaambie) kua: ‘Muabuduni Allah Mola wangu

na Mola wenu na mimi nilikua ni shahidi juu yao wakati nilipokua naishi pamoja nao.

Lakini uliponichukua Juu, basi wewe ndie uliekua Muangalizi juu yao na wewe ni

mwenye kushuhudia juu ya kila kitu’

Ambapo Aya zinatuwekea wazi kua wale wote wanaodai kua ni wafuasi wa Nabii Isa Ibn

Maryam, basi ni wafuasi ambao hawafanani na mafundisho yake, kwani wenye kuenda

kinyume na Maamrisho yake na hivyo hua ni wenye kufuata matamanio ya Nafsi zao na

matokeo yao wataingia Motoni badala yake, kwani Nabii Isa atatoa Ushahihi wake dhidi


502

yao na kuwakana kua wao sio wafuasi wake, kwa sababu hawakua ni wenye kushikamana

na usahih na ukweli wa Ujumbe wake juu yao.

Kwani Allah Subhanah wa Ta’ala anatubainishia kua Waumini wa kweli ni wale

waliokua na Msimamo katika Kuamini kwao kama zinazosema aya:

‏﴿مِّنَ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ رِجَالٌ‏ صَدَقُواْ‏ مَا عَاهَدُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ عَلَيْهِ‏ فَمِنْهُمْ‏ م َّن قَضَى ٰ نحَْبَهُ‏

وَمِنْهُمْ‏ م َّن يَنتَظِرُ‏ وَمَا بَد َّلُواْ‏ تَبْدِيلاً‏ ﴾

Mina almu/mineena rijalun sadaqoo ma AAahadoo Allaha AAalayhi faminhum

man qada nahbahu waminhum man yantadhiru wama baddaloo tabdeelan (Surat

Al Ahzab 33:23)

Tafsir: Miongoni mwa Waumini Mna watu walioamini kile walichokiahidi kwa Allah

juu yao, na kuna baadhi yao wanasubiri na hawajabadilika hata kidogo (Imani yao)

Ambapo katika kuhojiwa kwake Isa Ibn Maryam katika siku hio ya Malipo na Allah

Subhanah wa Ta’ala basi ataanza kujibu kwa Kumtukuza Allah Subhnah wa Ta’ala kwa

kusema kua Utukufu ni wake yeye peke yake, na hivyo kudhihirisha kua yeye Isa Ibn

Maryam kamwe hastahiki kupewa Utukufu wa kufanyiwa hivyo walivyofanya wanaojiita

kua ni wafuasi wake.

Na kuthibitisha kua kutokana na Maumbile yake basi yeye si mwenye uwezo wa kuona

na kujua kila kitu, bali ni Allah Subhanah wa Ta’ala pekee ndie mwenye uwezo huo na

ameona wazi juu ya kila alichokisema kuwaambia watu wake na kila alichokifanya kwa

ajili yao watu hao, na kisha anamalizia kwa kusema kua:

‏﴿إِن تُعَذِّبْهُمْ‏ فَإِن َّهُمْ‏ عِبَادُكَ‏ وَإِن تَغْفِرْ‏ لهَُمْ‏ فَإِن َّكَ‏ أَنتَ‏ ٱلْعَزِيزُ‏ ٱلحَْكِيمُ‏ ﴾

In tuAAadhdhibhum fa-innahum AAibaduka wa-in taghfir lahum fa-innaka anta

alAAazeezu alhakeemu; (Surat Al Maidah 5:118)

Tafsir: Hivyo kama utawaadhibu basi wao ni waja wako na kama utawasamehe basi

kwa hakika wewe ni Mwingi wa Uwezo na Mwingi wa Hikma’

Na hivyo Nabii Isa kua ni mwenye kuwarudisha watu wake hao alioambiwa awaongoze

na madai yao hayo kama yalivyokua Mbele ya Mola wake na kumuachia Maamuzi yake


503

juu yao watu hao, kua kama atataka kuwaadhibu basi ni haki yake kuwaadhibu watu hao,

na kama atataka kuwasamehe basi ni kutokana na Huruma, Rehma, Hikma na

Usamehevu wake Allah Subhanah wa Ta’ala.

Tunapoangalia Kwa upande mwengine basi amesema Abu Dhar Al Ghifari Radhi Allahu

Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisali na kuirudia aya hii ya Surat

Al Maidah 5:119 katika Qiyam Al Layl mpaka ikakaribia kuingia Alfajir, nami

nikamuuliza ni kwa sababu gani ambapo nae kaniambia kua: ‘Hakika mimi

nimeuombea Ummah Wangu na Wamepewa Uombezi wangu isipokua kwa wale

watakaomshirikisha Allah Subhanah wa Ta’ala’’

Na hi ni kwa sababu amesema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Surat An Nisaa kua:

‏﴿إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لاَ‏ يَغْفِرُ‏ أَن يُشْرَكَ‏ بِهِ‏ وَيَغْفِرُ‏ مَا دُونَ‏ ذٰلِكَ‏ لِمَن يَشَآءُ‏ وَمَن يُشْرِكْ‏ بِٱهلل َِّ‏

فَقَدْ‏ ضَل َّ ضَلاَلاً‏ بَعِيداً‏ ﴾

Inna Allaha la yaghfiru an yushraka bihi wayaghfiru ma doona dhalika liman

yashao waman yushrik biAllahi faqad dhalla dhalalan baAAeedan (Surah An Nisaa

4:116)

Tafsir: Kwa Hakika Allah hasamehe wenye kumshirikisha, lakini husamehe dhambi

nyenginezo kwa amtakae. Na anaemshirikisha Allah basi kwa hakika hua ni mwenye

kupotoka katika upotovu wa mbali sana.

KUPANDISHWA MBINGUNI KWA ISA IBN MARYAM NA KIFO CHA

MARYAM BINT IMRAN.

Anasema Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Isa Ibn Maryam

alikutana na Mayahudi ambao walipomuona basi nao wakamnadia wa kusema:

‘Anakuja mbele yetu Mchawi na Mtoto wa Mchawi, Msaliti na Mtoto wa

Msaliti’’na kisha baada ya hapo wakaanza kumtukana Isa Ibn Maryam. Hivyo Isa

Ibn Maryam akamuomba Allah Subhanah wa Ta’ala kwa kusema: ‘Ya Allah! Wewe

ni Mola wangu, na Mimi natokana na Ruhi wako, Nimeumbwa kwa Kauli yako, na

sikuja kwao kwa Hiari yangu, Ya Allah mlaani yule ambae ni mwenye kunitukana

mimi na Mama yangu’

Hivyo hapo hapo watu hao waliokua wakimtukana Nabii Isa wakageuka na kua Kima

wote. Hivyo Chifu wa Mayahudi alipoona tukio hili basi basi akaingiwa na khofu kubwa


504

sana kutokana na Maombi yake hayo. Hivyo wakajikusanya na kuanza kuhoji kuhusiana

na hali ya hatari ya uwezo wake huo wa kuwageuza Watu Kima, ghafla moja na kuona

kua bora wamalizane nae Isa Ibn Maryam kwa kumkamata na kumuua.

Lakini walipoamua kufanya hivyo basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamtuma Malaika

Jibril na kumwambia kua amlinde kwa yake ya Ukuta utakaomzunguka Nabii Isa ili

asidhuriwe na Mayahudi hao. Hivyo Mayahudi hao wakamteua mmoja miongoni mwao

aingie ndani ya ukuta huo kupitia kwenye Upenyo mdogo wa Ukuta huo ili akamuue

Nabii Isa, ambapo Mtu huyu aliechaguliwa alikua akiitwa Filitianus au Pilato.

Hivyo Filitianus alipoingia ndani kwenye upenyo wa Ukuta huo, akawa hakumkuta Isa

Ibn Maryam ndani yake, na akakaa kwa mda akimtafuta, huku Mayahudi wenzake

walioko nje wakidhani kua labda alikua akipigana nae Nabii Isa Ibn Maryam ndani yake,

lakini kumbe katika tukio la kuingia ndani kwake basi Allah Subhanah wa Ta’ala

akamjalia Filitianus kua na muonekano wa Mithili ya Nabii Isa Ibn Maryam badala yake,

na hivyo alipotoka nje basi Mayahudi wakadhani kua Filitianus ameuliwa na Isa Ibn

Maryam na hivyo Isa Ibn Maryam ndio ametoka nje baada ya kumuua Filitianus, hivyo

wakamkamata na kisha wakamuua na kumsulubu Filitianus huku wakidhani kua yeye

ndie Isa Ibn Maryam.

Ambapo kwa upande wa Imam Wahb Ibn Munabih basi yeye anasema kua: ‘Allah

Subhanah wa Ta’ala alimjaalia Isa Ibn Maryam kua ni mwenye kujua kua karibuni

ataondoka Ulimwenguni, hivyo nae akawa na khofu juu ya kuondoka kwake, na

akawaalika Wanafunzi wake na kuwatarishia Chakula cha Usiku na kuwaambia:

‘Kusanyikeni pamoja nami leo Usiku kwani ninakuhitajini.’

Ulipowadia Usiku wa siku hio, basi Isa Ibn Maryam akawatayarishia Wanafunzi

wake hao Chakula alichopika kwa ajili yao, wakala hadi wakamaliza na kisha

akawa ni mwenye kuwakosha mikono yao huku akiwausia juu ya Allah Subhanah

wa Ta’ala, huku akiwapangusa mikono yao kwa nguo yake. Ambapo hili lilikua ni

jambo ambalo halikuwavutia Wanafunzi wake. Na hivyo Nabii Isa akawaambia

Wanafunzi wake hao kua: ‘Hatokua miongoni mwangu yule ambae hakunifanyia

kile ambacho mimi nimemfanyia yeye’

Ambapo mimi nimekualikeni hapa leo hii, nimekulisheni na kukukosheni mikono

yenu kwa mikono yangu ili nanyi mpate kuona kutoka kwangu. Na kwa hakika

mnaona na kujua kua mimi ni mbora mongoni mwenu, hivyo haitakiwi kwa hata

mmoja miongoni mwenu kua ni mwenye kujiona kua yuko juu zaidi ya mwenzake,

hivyo ni wajibu wenu kwa kila mmoja miongoni mwenu kujitolea kwa ajili ya

mwenzake kama mimi nilivyojitolea kwa ajili yenu. Na baada ya haya nilikua

nataka kukuombeni kua mniombee kwa Allah Subhanah wa Ta’ala, huku mkiwa

na Ikhlasi kua Kifo kisinikaribe’


505

Hivyo baada ya hapo Wanafunzi wake hao wakaanza kumuombea Dua Nabii Isa

Ibn Maryam, lakini Allah Subhanah wa Ta’ala akawajaalia kua na usingizi mzito

sana, hivyo wakashindwa kuendelea na Dua hio na kuanza kusinzia na kulala

badala yake, hivyo Nabii Isa kawambia Wanafunzi wake hao: ‘Subhanah Allah

hamuwezi kunitekelezea maombi yangu hata kwa usiku mmoja?’

Ambapo Wanafunzi hao wakajibu: ‘Wa Allah hatujuia nini kimetukuta kwani

tmezoea kukesha katika Ibada pamoja nawe lakini leo hii inaonekana kua Usingizi

umekua mwingi kupita mipaka.’ Hivyo Nabii Isa akasema: ‘Basi Mchungaji

atandoka na Kondoo watabakia, na mmoja kati yenu miongoni mwenu atanisaliti

na kunuza kwa malipo ya fedha kidogo na kisha atakula fedha hizo bila kujali,

jambo ambalo litatokea kabla ya hata kuwika Jogoo wa kwanza wa Alfajiri.’ Kisha

Nabii Isa na Wanafunzi wake wakatawanyika kila mmoja akielekea katika sehemu

yake kuendelea na Usingizi wake.

Katika kipindi hiki Mayahudi walikua wakimtafuta Nabii Isa Ibn Maryam, na

njiani wakafanikiwa kumkamata Mwanafunzi wake Nabii Isa aitwae Simion,

ambae nae akamkana Nabii Isa kua si Mwalimu wake, na kisha alipoachiwa

akaanza kusikitika na kujilaumu kwanini akamkana Mwalimu wake, na kisha

akasikia Sauti ya Jogoo wa kwanza wa Alfajir na hivyo sauti hio ilimhuzunisha sana

kwani alikua akikumbuka maneno ya Isa Ibn Maryam kuhusiana na kusalitiwa

kwake.

Ilipoingia asubuhi basi Juda ambe ni mmoja kati ya Wanafunzi wa Isa Ibn Maryam

akaelekea kwa Mayahudi na kuwaambia kua wampe pesa za fedha 30 na kisha

atawapeleka katika sehemu aliyojificha Isa Ibn Maryam, na alipowapeleka na

kuingia ndani basi Mwanafunzi huyo akawa na muonekano wa Isa Ibn Maryam,

hivyo hao wakamkamata na kumfunga kamba na kisha wakamwambia kua: ‘Kama

kweli wewe unatibu wenye Ukoma na kufufua waliokufa, basi itakuaje uwe

simwenye kuweza kujifungua kutokana na kamba hizi tulizokufunga’ kisha

wakamtemea mate, wakamchoma na Miba na kisha wakamsulubu huku wakidhani

kua wanamsulubu Isa Ibn Maryam.

Ama kwa Upande wa Imam Qatadah Al Sadusi basi yeye anasema kua: ‘Mayahudi

walimuwekea Mlinzi Nabii Isa ili amfuate kila anapoenda ili iwe rahisi kwao

kumkamata pale itakapohitajika. Hivyo siku moja Isa Ibn Maryam akaelekea

Milimani na Mlinzi huyo akamfuata, na walipofika huko basi Allah Subhanah wa

Ta’ala akamchukua na kumpandisha Mbinguni Isa Ibn Maryam na kisha

akamvisha Myahudi huyo muonekano wa Nabii Isa, hivyo Mayahudi wenzake

walipotaka kumuua Nabii Isa basi wakamkamata yeye na Kumsulubu huku akiwa

ni mwenye kulalalamika kua yeye sie Isa Ibn Marayam.’


506

Allah Subhanah wa Ta’ala analielezea tukio hili katika Aya iliyotuma neno Makara

ambalo hua linamanisha Kupanga Njama, Kumuadhibi Mtu Muongo, Kupanga Njama

au Mbinu kwa kutumia Ustadi Mkubwa sana. Ambapo neno Makara ndio lililotoa neno

Makirin ambalo hua linamaanisha Mwenye Kuadhibu Mwishoni wenye kupanga Njama

baada ya kuwazidi kwa ubora wa mipango ya Kufanya Njama na hivyo kuwadhihirisha

ubya wa Njama zao waliopanga Njama, ambapo maneno haya yote yametumika kwenye

aya hio isemayo kua:

‏﴿وَمَكَرُواْ‏ وَمَكَرَ‏ ٱهلل َُّ‏ وَٱهلل َُّ‏ خَيْرُ‏ ٱلْمَاكِرِينَ‏ ﴾

Wamakaroo wamakara Allahu waAllahu khayru almakireena(Surat Al Imran 3:54)

Tafsir: Na wakapanga Njama, na Akapanga Allah, na Allah ni M-bora wa

Kuwaadhibu wenye Kupanga.

Kwani wakati Mayahudi wanapaga Njama zao za Kumuua Nabii Isa basi nae Allah

Subhanah wa Ta’ala ambae ni Mbora wa kupanga na kuadhibu kwa kila mwenye

kupanga njama zenye maovu ndani yake akapanga yake na kumbainishia Nabii Isa kwa

kusema:

‏﴿إِذْ‏ قَالَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٰ يٰعِيسَى ِ إِنىّ‏ مُتَوَفِّيكَ‏ وَرَافِعُكَ‏ إِلىَ َّوَمُطَهِّرُكَمِنَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَ‏ فَرُواْ‏

وَجَاعِلُ‏ ٱل َّذِينَ‏ ٱت َّبَعُوكَ‏ فَوْقَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ إِلىَٰ‏ يَوْمِ‏ ٱلْقِيَامَةِ‏ ثمُ َّ إِلىَ َّ ‏َمرْجِعُكُْم

فَأَحْكُمُ‏ بَيْنَكُمْ‏ فِيمَا كُنتُمْ‏ فِيهِ‏ تخَْتَلِفُونَ‏ ﴾

Idh qala Allahu ya AAeesa innee mutawaffeeka warafiAAuka ilayya

wamutahhiruka mina alladheena kafaroo wajaAAilu alladheena ittabaAAooka

fawqa alladheena kafaroo ila yawmi alqiyamati thumma ilayya marjiAAukum

faahkumu baynakum feema kuntum feehi takhtalifoona (Surat Al Imran 3:55)

Tafsir: Na akasema Allah (Subhanah wa Ta’ala): ‘Ewe Isa! Hakika mimi

nitakutimizia Ahadi niliyokuwekea, nitakunyanyua kwangu na kukusafisha kutokana

na wale ambao waliokufuru na nitawajaalia wle wanaokufuata kua juu ya

waliokufuru hadi katika siku ya Kiama. Na kisha mtarudi kwangu nami nitahukumu

baina yenu juu ya yale mliyokua mkikhitilafiana’


507

Ambapo aya imetuma neno Mutawaffika ambalo linatokana na neno Wafa ambalo hua

linamaanisha Kufikia Mwisho, Kutimiza Ahadi, Kurudisha Amanah, Kutekeleza Wajibu,

Kulipa Deni. Neno Wafa ndio lililotoa neno Wafat ambalo hua linamaanisha Kifo.

Ambapo kwa upande wa Raghib Al Isfahani basi yeye anasema kua: ‘Neno Rafa’a hua

linatumika kumaanisha Kunyanyua vitu Vilivyo hai na Kuvipandisha kutoka

katika sehemu moja na kuviweka kwenye sehemu nyengine’

Ambapo kwa Upande wa Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allah Anhu kua: ‘Neno

Mutawaffika linamanisha Mumituka (yaani Nitakusababishia Kifo)’ na kwa upande

wa Al Hasan Al Basri amesema kua; ‘Allah Subhanah wa Taála alimpaisha Mbinguni

Isa Ibn Maryam katika hali ya kimwili na kiroho.’

Hasan Radhi Allahu aAnhu anasema kua: ‘Rasul Allah Salallahu Aálayhi wa Salam

Aliwaambia Mayahudi kua: ‘Isa Ibn Maryam hajafariki, na atarudi Duniani kabla

ya Siku ya Kiama’’ (Imam Ibn Jarir Al Tabari)

Na kwa upande wa Imam Ibn Abi Hatim Abd Rahman Ibn Muhammad Ibn Idris Al Razi

basi yeye anasema kua: ‘Amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua:

Kabla ya Allah Subhanah wa Ta’ala kumnyanyua Isa Ibn Maryam Mbinguni, basi

Nabii Isa alienda kwa Wanafunzi wake’ ambao walikua ni 12 na alipofika alikua

kama ni mwenye nywele zinazotiririka Maji na akasema kuwaambia Wanafunzi

hao: ‘Kuna mmoja miongoni mwenu hatoniamini mimi kwa mara 12 baada ya

kuniamini kwake’ Kisha akawauliza Wanafunzi wake hao: ‘Jee ni nani miongoni

mwenu atajitolea kua muonekano wangu uonekane juu yake? Na kisha awe ni

mwenye kuuliwa baada yangu, na hivyo atakua ni mwenye kuingia Peponi pamoja

nami?’

Ambapo mmoja kati ya Wanafunzi wake ambae alikua ni kijana kuliko wote

akasimama na kusema kua yeye yuko tayari, lakini Nabii Isa Ibn Maryam

akamwambia akae chini, Nabii Isa akauliza tena atakakaejitolea lakini hakuna

aliesimama isipokua yule kijana alisimama tena. Nabii Isa akamwambia akae chini

tena, na kisha akauliza kwa mara ya tatu nani atajitolea kuchukua nafasi hio lakni

hakuna aliesimama, na yule kijana akasimama tena. Hivyo Nabii Isa akasema:

‘Wewe utakua ndie mwenye kuchukua Muonekano wangu.

Hivyo kijana huyo akawa na muonekano wa Nabii Isa na Nabii Isa akapaa angani,

hivyo Mayahudi walipoanza kumtafuta Nabii Isa wakamuona Kijana huyo na

Kumsulubu badala yake huku wakimdhani kua ni Nabii Isa. Ambapo wafuasi wa

Nabii Isa wakawa ni wasiomuamini Nabii Isa kwa mara 12 na wakagawika katika

makundi Matatu ambayo ni:


508

Yaqubiyah ambao wao wanasema kua: ‘Mungu alibakia pamoja nasi kwa mda

alioutaka na kisha akapanda Mbinguni’

An Nasturiya ambao wanasema kua: ‘Mtoto wa Mungu alikua pamoja nasi kwa

mda alioutaka na kisha Baba yake akamchukua juu Mbinguni. ’

Waislam ambao wanasema: ‘Mja na Mtume wa Allah alibakia pamoja nasi kwa

aliotaka Allah Subhanah wa Ta’ala na kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akampaisha

Mbinguni’

Ambapo makundi mawili ya Yaqubiyah na Nasturyia yameshikamana na

kupingana na Waislam na kuwaua, na hivyo tangu baada ya tukio hilo basi Uislam

ulifichikana hadi pale Allah Subhanah wa Ta’ala alipomleta Nabii Muhammad

Salallahu Alayhi wa Salam’

Ambapo amesema Imam Qasim Muhammad Hasham katika Tafsir Al Azizi kua: ‘Ummu

ul Muuminin Safiya Radhi Allah Anha alipotembelea Bayt ul Maqdis na baada ya

kusali aktika Masjid Al Aqsa basi alipanda katika Mlima Tur akasali pia na

akasema: ‘Huu ndio Mlima ambao Isa Ibn Maryam alinyanyuliwa kupandishwa

Mbinguni’’

Na kwa upande wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi anasema kua;

‘Neno Tawaffa hua linamaanisha Kukichukua kitu katika hali ya Ukamilifu, hivyo

hii inamaanisha kua Allah Subhanah wa Ta’ala alimyanyua Juu Nabii Isa katika

hali ya kiroho na kimwili ili Mayahudi wasifanikiwe kumdhuru, na ndio maana

Allah Subhanah wa Ta’ala akawambia Nabii Isa Ibn Maryam kama alivyosema

katika Surat Al Imran 3:55’

Ambapo kiunganishi wa harfu Waw baina ya Mutawaffeeka wa rafiAAuka ilayya

hayamaanishi kua hapa kuna mfuatano wa jambo moja baada ya jengine. Hivyo

aya inamaanisha kua Allah Subhanah wa Ta’ala anafanya mambo yote haya lakini

kuhusiana na wakati gani, wapi na sehemu gani basi hua inategemea na vithibitisho,

na hivyo hii kua ni ushahidi kua Isa Ibn Maryam yuko hai.

Na kwa upande wa Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al

Ansari Al Qurtubi basi yeye anasema kua: ‘Mfumo wa mpangilio na maana ya Harfu

Waw hivyo maana ya maneno ya aya hii Mutawaffeeka wa rafiAAuka ilayya itakua

Nitakunyanyua kwangu mie na nitakusafisha kutokana na wale wanaoikataa Imani

ya Dini na nitakuchukua wewe kwangu mimi baada ya kupaa kwako Mbinguni.


509

Ambapo maana ya kwanza ya neno Mutawaffeeka hua inamaanisha kua

Nitakunyanyua wewe kutoka kwa watu hao na kukupandisha juu kwangu mie, na

maana ya pili ya Mutawaffeeka hua inamaanisha Nitakufanya Ulale Usingizi

ambapo Usingizi hua ni pacha wa Kifo na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala

akatumia neno hilo kumaanisha Usingizi katika aya ifuatayo:

‏﴿وَهُوَ‏ ٱل َّذِى يَتَوَف َّاكُم بِٱلل َّيْلِ‏ وَيَعْلَمُ‏ مَا جَرَحْتُم بِٱلن َّهَارِ‏ ثمُ َّ يَبْعَثُكُمْ‏ فِيهِ‏ لِيُقْضَىٰ‏

‏’أَجَ‏ لٌ‏ م ُّ سَمًّى ثمُ َّ إِلَيْهِ‏ مَرْجِ‏ عُكُمْ‏ ثمُ َّ يُنَبِّئُكُم بمَِا كُنتُمْ‏ تَعْمَلُونَ‏ ﴾

Wahuwa alladhee yatawaffakum biallayli wayaAAlamu ma jarahtum bialnnahari

thumma yabAAathukum feehi liyuqda ajalun musamman thumma ilayhi

marjiAAukum thumma yunabbi-okum bima kuntum taAAmaloona (Surat Al

Anaam 6:60)

Tafsir: Na ni yeye ndie ambae yatawaffakum anaechukua Roho zenu katika wakati wa

Usiku(wakati mmelala) na ni mwenye kujua juu ya mliyoyafanya wakati wa Mchana

na kisha hukuamsheni ili mpate kutimiza wakati wenu mlioandikiwa, na kisha kwake

yeye ndio marudio yenu na kisha mtabainishiwa mliyokua mkiyafanya.

Ambapo kwa upande wa Imam Al Sabuni basi yeye anasema kua: ‘Hikma ya Allah

Subhanah wa Ta’ala kutoa tangazo hilo ni kumbashiria Nabii Isa kua atamuokoa

kutokana na Mayahudi na atamnyanyua Juu Mbinguni huku akiwa Mzima mzima

bila ya kufikwa na Matatizo yeyote’(Safwat al-Tafasir)

Na kwa upande wa Imam Zahid Al Kawthar basi yeye anasema kua: ‘Maana halisi ya

neno Raf’a hua ni kusafirisha Kitu kutoka chini kuelekea Juu, hivyo haina haja ya

kutafuta maana nyengine yeyote kuhusiana na maneno haya katika aya hii’

Ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye

anasema kua: ‘Neno Mutawaffika hua linamaanisha kua Nitakulinda kutokana na

Kuuliwa na Watu na hivyo nitakupa haki kamilifu ya Kufariki kifo cha

Kimaumbile, na wala si cha Kuuliwa.’

Na hii ni kwa sababu anasema Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua

maana ya ile aya isemayo


510

‏﴿وَإِن َّهُ‏ لَعِلْمٌ‏ لِّلس َّاعَةِ‏ فَلاَ‏ تمَْتَرُن َّ هبَِا وَٱت َّبِعُونِ‏ هَٰذَا صِرَاطٌ‏ م ُّسْتَقِيمٌ‏ ﴾

Wa-innahu laAAilmun lilssaAAati fala tamtarunna biha waittabiAAooni hadha

siratun mustaqeemun (Surat Az Zukhruf 43:61)

Tafsir: Na kwa Hakika Yeye atakua ni Alama ya kujulikana kwa Saa (Ya Kiama) hivyo

msiwe na shaka nayo na nifuateni Mimi katika njia hi iliyonyooka.

Ambapo aya inatuwekea wazi kua Kiama hakitofika (kwani neno Ilm hapa

limetumika kubainisha Shuruti la kua kitendo hakitotokea hadi kitokee kitnedo

chengine kwanza) Kabla ya Isa Ibn Maryam kurudi Duniani ambapo Aatamuua

Dajjal na Atafuata Qur’an na Atafanya Ibada ya Hija pia na kisha ndio kitakuja

Kiama

Ambapo kwa upande wa Imam Muqatil Ibn Sulayman basi nae amesema kua ‘Maneno

laAAilmun lilssaAAati linamaanisha Ukaribu wa wazi wa Saa ya Kiama utaonekana

mwishoni mwa Dunia baada ya Kushuka Nabii Isa’

Na kwa upande mwengine basi neno Wafa halikutumika tu kumaanisha Kifo ndani ya

Qur’an bali pia limetumika kumaanisha Kuitoa Roho moja kwa moja bila ya kuirudisha

Ndani ya Mwili, na pia limetumika kumaanisha Kuichukua Roho kutoka ndani ya Miwili

na kisha baadae kuirudisha tena Roho hio ndani ya Mwili kama ilivyobainisha aya

ifuatayo:

‏﴿ٱهلل َُّ‏ يَتَوَفى َّ ٱلأَنفُسَ‏ حِ‏ ينَ‏ مَ‏ وْتِهَا وَٱل َّتىِ‏ لمَْ‏ تمَُتْ‏ فىِ‏ مَنَامِهَا فَيُمْ‏ سِ‏ كُ‏ ٱل َّتىِ‏ قَضَىٰ‏

عَلَيْهَا ٱلْمَوْتَ‏ وَيُرْسِ‏ لُ‏ ٱلأُخْرَىٰ‏ إِلىَٰ‏ أَجَلٍ‏ م ُّسَمًّى إِن َّ فىِ‏ ذٰلِ‏ كََ‏ لآَ‏ تٍ‏ لِّقَوْمٍ‏

يَتَفَك َّرُونَ‏ ﴾

Allahu yatawaffa al-anfusa heena mawtiha waallatee lam tamut fee manamiha

fayumsiku allatee qadha AAalayha almawta wayursilu al-okhra ila ajalin

musamman inna fee dhalika laayatin liqawmin yatafakkaroona(Surat Zumar 39:42)

Tafsir: Allah ni (Yatawaffa) mwenye Kuchukua Roho katika wakati wa (Mawtiha) kifo

chao na wale (Lam Tamut) ambao hawakufa katika usingizi wao, kisha huzizuia za


511

wale awatakiao Kifo na nyengine huzirudisha tena kwa ajili ya Mda waliowekewa,

hakika katika haya una dalili kwa watu wenye kutafakari.

Ambapo amesema Abu Hurayra kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kua: ‘Mitume ni ndugu wenye kutokana na Mama tofauti, lakini ni wenye

kutokana na Baba mmoja, hua ni wenye kushushiwa Dini moja, hivyo mimi ni

karibu sana kwa Isa Ibn Maryam na yeye atashuka tena, na mtakapomuona basi

mtamjua kwani ni Mtu wa urefu wa kati na kati na mwenye rangi ya mwangaza

wenye wekundu, na nywele zake atakua amezipasua kati kama zenye kuyaangusha

matone ya Maji ingawa hazijaroa. Ataivunja Misalaba, atawaua Nguruwe, atagawa

Mali na kupigana na Watu kwa ajili ya Uislam hadi pale itakapokua hakuna Dini

nyengine ardhini’

Ni katika kipindi cha wakati wake ambapo ndipo atakapotokea Massih Dajjal Al

Kadhaab ambae atauliwa na kutakua na Usalama Ardhini kiasi ya kua Simba

watakua wanatembea pamoja na Ngamia, Chui na Ng’ombe, Mbwa Mwitu na

Kondoo na Wototo watacheza na Nyoka, na hawatodhuriana na ataishi ardhini kwa

miaka 40 na kisha atakufa na Waislam watamsalia na Kumzika’(Sunan Abu Daud)

Tukio la kupandishwa Mbinguni kwa Nabii Isa lilitokea katika Mwezi wa Ramadhani

katika usiku wa Laylat Ul Qadir wa mwaka wa 33 baada ya kuzaliwa Nabii Isa.

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala anabainisha kuhusiana na kitakachofuata baada ya

tukio hilo la Kuahidiwa Nabii Isa kua atapaishwa Mbinguni na kuepushwa na Kuuliwa

na Maadaui zake, na kisha waliokua hawakumuamini basi watalipwa hapa hapa Duniani

na watakaomini basi watalipwa kikamilifu kama ilivyolezewa katika aya nyengine tena

ambayo nayo pia imetumia neno lenye asili ya neno Wafa lakini likiwa katika hali ya

Fayuwafiihim Ujurahum lenye kumaanisha Kikamilishiwa Kikamilifu Malipo yao pale

ziliposema aya kua:

‏﴿فَأَم َّا ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ فَأُعَذِّبُهُمْ‏ عَذَاابً‏ شَدِيداً‏ فىِ‏ ٱلد ُّنْيَا وَٱلآخِ‏ رَةِ‏ وَمَا لهَُمْ‏ مِّنْ‏

ُّب

‏ َّصِرِينَ۞وَأَم َّا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُوا وَعَمِلُواْ‏ ٱلص َّ الحَِاتِ‏ فَيُوَفِّيهِمْ‏ أُجُورَهُمْ‏ وَٱهلل َُّ‏ لاَ‏ يحُِ‏

ٱلظ َّالِمِينَ۞ذٰلِكَ‏ نَتْلُوهُ‏ عَلَيْكَ‏ مِنَ‏ الآَتِ‏ وَٱلذِّكْرِ‏ ٱلحَْكِيمِ‏ ﴾

Faamma alladheena kafaroo faoAAadhdhibuhum AAadhaban shadeedan fee

alddunya waal-akhirati wama lahum min nasireena; Waamma alladheena amanoo

waAAamiloo alssalihati fayuwaffeehim ojoorahum waAllahu la yuhibbu


512

aldhdhalimeena; Dhalika natloohu AAalayka mina al-ayati waaldhdhikri

alhakeemi (Surat Al Imran 3:56-58)

Tafsir: Ama kuhusiana na wale waliokufuru basi Wataadhibwa Adhabu kali sana

Duniani na Akhera na hawatokua na wa Kuwanusuru. Na ama kuhusiana na wale

walioamini na wakafanya Mema basi fayuwaffeehim ojoorahum (watakamlishiwa

Kikamilifu Ujira wao), na Allah hawapendi wenye kufanya Dhulma. Haya

tunakusomea juu yako (Ewe Muhammad) kutoka katika Aya zetu na ukumbusho

wenye Hikma.

Na anasema Imam Wahb Ibn Munabih kua: ‘Wakati Allah Subhanah wa Ta’ala

alipomtaarifu Isa Ibn Maryam kuhusiana na kupaishwa Mbinguni basi, Isa Ibn

Maryam akawachagua Wanafunzi wake wawili ambao ni Simiun na Yahya na

kuwataka wakae karibu na Mama yake yaani Maryam Bint Imran kwa ajili ya

kumuangalia na kuwataka wasiachane nae.

Hivyo wakaamua pamoja na Andrew na Maryam Bint Imran kua waelekee kwa

Mfalme Marut ambae ni wa Ardhi ya Bizantiyum na kumtaka awe ni mwenye

Kumuabudu Allah Subahanh wa Ta’ala, ambapo kabla ya hapo basi Allah

Subhanah wa Ta’ala alimtuma Nabii Yunus kwenye Ardhi hio, na walipofika huko

basi Mfalme Marut akaamrisha kua Andrew na Simiun wasulubiwe.

Ambapo Yahya na Maryam Bint Imran wakakimbia, lakini hata hivyo walipofika

njiani wakazingirwa, na hapo hapo Ardhi ikapasuka na hivyo Maryam Bint Imran

na Yahya wakatumbukia ndani yake, na watu wa Mfalme Marut walipokaribia

eneo hilo wakajaribu kufukua katika sehemu hio walilozama Maryam Bint Imran

na Yahya lakini hawakukuta kitu. Hivyo Mfalme Marut alipohadithiwa hali

ilivyokua basi akaamini kua hio ni Miujiza ya Allah Subhanah wa Ta’ala na hivyo

akasilimu…lakini mwenye kujua zaid ni Allah Subhanah wa Ta’ala.

ISA IBN MARYAM NA MARYAM MAJDALANIYAH

Mongoni mwa watu wa Bani Israil katika kipindi cha Nabii Isa aliekua ni Mcha Mungu

na mwenye kumuamini sana Nabii Isa alikuwepo Mwanamke ambae alikua akijulikana

kwa jina la Maryam Majdalaniyah, ambae alikua akiishi katika kijiji cha Majladan.

Maryam Majdalaniyah, alikua ni Mwanamke Mzuri sana lakini alikua na tatizo la

ugonjwa wa kutokukoma kwa Hedhi yake na hivyo alikua ni mwenye kukataa kuolewa

kutokana na tatizo lake hilo ingawa wengi miongoni mwa watu wa Ban Israil walipeleka

posa zao kwa ajili ya kutaka kumuoa.


513

Hivyo Maryam Majdalaniyah, alipopata habari kua Nabii Isa anatibu Maradhi

yasiyotibka basi akatafuta nafasi ya kuonana nae Nabi Isa lakini Allah Subhanah wa

Ta’ala alipomjaaalia Maryam Majdalaniyah, kuipata Nafasi hio ya kukutana nae Nabii

Isa basi akashindwa kumuelezea Nabii Isa kuhusiana na tatizo lake hilo, lakini

akafanikiwa kumgusa mgongo wake Nabii Isa, na kutokana na tukio hilo basi Allah

Subhanah wa Ta’ala akamjaalia Maryam Majdalaniyah kua ni mwenye kupona maradhi

yake, na hivyo akawa anampenda na kumuamini zaidi Nabii Isa.

Ambapo kuna wasemao kua Maryam Majdalaniyah aliombwa na Nabii Isa kua

awakusanye Wanafunzi wake Nabii Isa Ibn Maryam kwa ajili ya Chakula chake cha

Mwisho kabla ya kuwatawanya Wanafunzi wake katika maeneo mbali mbali ya ardhi

kama alivyoamrishwa na Allah Subhnah wa Ta’ala ambapo miongoni mwao ni wale

waliotajwa kwa kupigiwa mfano kwenye Surat Yasin.

WANAFUNZI WA NABII ISA IBN MARYAM KATIKA SURAT YASIN

Amesema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Surat Yasin kua:

‏﴿وَٱضْرِبْ‏ لهَُمْ‏ م َّثَلاً‏ أَصْحَابَ‏ ٱلقَرْيَةِ‏ إِذْ‏ جَآءَهَا ٱلْمُرْسَلُونَ۞إِذْ‏ أَرْسَ‏ لْنَآ إِلَيْهِمُ‏

ٱثْنَينِْ‏ فَكَذ َّبُوهمَُا فَعَز َّزَْ‏ بِثَالِثٍ‏ فَقَالُو ۤ اْ‏ إِ َّ إِلَيْكُمْ‏ م ُّرْسَلُونَ‏ ﴾

Waidhrib lahum mathalan as-haba alqaryati idh jaaha almursaloona; Ith arsalna

ilayhimu ithnayni fakadhdhaboohuma faAAazzazna bithalithin faqaloo inna

ilaykum mursaloona; (Surat Yasin 36:13-14)

Tafsir: Na wapigie Mfano wa Watu wa Mji wakati walipokuja kwao Mitume. Wakati

tulowatumia Mitume wwili wakawakadhibisha wotehvyo tukawaongez na wa Tatu nao

kisha wakasema: ‘Kwa hakika sisi tumetumwa kwenu kama Mitume’

Nabii Isa aliwaambia Wanafunzi wake kua: ‘Enyi Hawarriyun umefika mda wa

kuondoka kwangu hivyo huu ni wasia wa mwisho juu yenu kutoka kwangu, ambao

ni kua Allah Subhanah wa Ta’ala atakutumeni nyie kwa jamii za watu, hvyo isihini

kwa heshima, kuweni wapole, wenye huruma na ukarimu. Mtakapokutana na

mithani basi kuweni na Subira. Ishini miongoni mwa watu kama wanavyoishi

Kondoo miongoni mwa Mbwa Mwitu na wala msishindane kwa ajili ya mambo ya


514

kidunia, katika kila jambo lenu msimsahau Mola wenu na daima kuweni ni wenye

kumtegemea yeye.

Nae atakusimamieni na kukupeni msaada atakupeni hoja na vithibitisho ambavyo

vitakavyokua vya nguvu. Katika maisha yenu mtakua na wapinzazni wa aina mbili

ambao ni Wafalme na Wanawake, hivyo iwachieni Dunia hii kwa wenye Mamlaka

nanyi mtakua Salama kutokana na Upinzani wao. Ama kuhusiana na Wanawake

basi fungeni na ishini katika njia ya Usafi, mtu akikupigeni kwenye shavu moja basi

mpeni na shavu la pili amalizie. Amkeni asubuhi mapema na sehemu yeyote ile ya

ardhi mtakayoelekea basi waiteni watu kwa Mungu wao kulingana na Lugha yao,

na Simiyun ndio kiongozi wenu.’

Simiyun akamuuliza Isa Ibn Maryam kwa kukema: ‘Hivi Jee mimi utanipeleka wapi,

Ya Rasul Allah?’ Nabii Isa akasema: ‘Nenda katika Ardhi ya Antakiya’ ambapo

Simiyun akasema: ‘Hakika mimi ni Mtu mzima sina nguvu, jee nitafanikisha vipi

jambo hilo?’ Hivyo Nabii Isa Ibn Maryam akasema: ‘Allah atakupa Nguvu’ Simiyun

akasema: ‘Ya Rasul Allah! Basi bora nipe wa kufuatana nao miongoni mwetu’. Nabii

Isa Ibn Maryam akasema: ‘Chagua uwatakao miongoni mwenu’ hivyo Simiyun

akamchagua Yahya.

Ambapo kwa upande wa Imam Muhammad Ibn Is-haq basi yeye anasema kua walioenda

katika mji wa Antakiya ambao ni watu waliotajwa kwenye Surat Yasin walikua ni Farud

na Marud, na kwa upande wa Imam Muqatil Ibn Sulayman basi yeye anasema kua

walikua ni Yuman na Malus, na kwa upande wa Imam Kaab Al Ahbari basi anasema kua

walikua ni Sadiq na Suduq na kwa upande wa Imam Wahb Ibn Munabih basi yeye

anasema kua hawa walikua ni Yahya na Yunus. Lakini kwa upande wa Imam Al Qarafi

Al Shashi basi yeye anasema kua hawa walikua ni Manabii wawili wa Allah Subhanah

wa Ta’ala.

Hivyo Simiyun na Yahya walipolala katika usiku wa siku hio, basi baada ya mda

wakaamka na kujikuta wapo nje kwenye sehemu iliyowazi tofauti na walivyolala hapo

awali, kwani walikua katika ardhi ya kigeni wasiyoifaham huku wakiwa ni kwenye eneo

ambalo ni lenye mandhari ya shamba wakafaham kua wamewasili kwenye ardhi

nyengine tofauti.

Hivyo asubuhi ya siku hio wakaona Lango la kuingilia kwenye mji ambao pia hawauijui,

hivyo wakaelekea kwenye Mlango wa Mji huo, na walipoulizia wakaambiwa kua huo ni

Mji wa Antakiya, na kabla hawajaingia ndani yake kwa ajili ya kuwausia watu wa Ardhi

hio kuhusiana na Allah Subhanah wa Ta’ala basi wakakamatwa na kutokana na

kushukiwa kua ni wapelelezi wa Maadui wa watu wa Mji huo.


515

lakini walipojitetea kua wao ni wafuasi wa Isa Ibn Maryam na kazi yao ni kutangazia

Dini ya Allah Subhanah wa Ta’ala Mwingi wa Rehma na mwingi wa Huruma basi

ingawa kuna baadhi waliowasikiliza na kuvutiwa na ujumbe wao lakini wengi zaidi

waliukataa na hivyo wakakumbana na upinzani mkubwa sana kama zinavyoelezea Aya

pale ziliposema:

‏﴿قَالُواْ‏ مَآ أَنتُمْ‏ إِلا َّ بَشَرٌ‏ مِّثْلُنَا وَمَآ أَنَزلَ‏ ٱلر َّحمَْٰنُ‏ مِن شَيْءٍ‏ إِنْ‏ أَنتُمْ‏ إِلا َّ

تَكْذِبُونَ۞قَالُواْ‏ رَب ُّنَا يَعْلَمُ‏ إِ َّ إِلَيْكُمْ‏ لَمُرْسَلُونَ۞وَمَا عَلَيْنَآ إِلا َّ ٱلْبَلاَغُ‏ ٱلْمُبِينُ‏ ﴾

Qaloo ma antum illa basharun mithluna wama anzala alrrahmanu min shay-in in

antum illa takdhiboona; Qaloo rabbuna yaAAlamu inna ilaykum lamursaloona;

Wama AAalayna illa albalaghu almubeenu; (Surat Yasin 36:15-17)

Tafsir: Wakasema (Watu hao kua): ‘Nyinyi ni Watu tu kama sisi, na hakushusha

Mwingi wa Rehma kitu chochote isipokua nyinyi ni wenye kusema Uongo’;

Wakasema: ‘Mola wetu ni mwenye kujua kua sisi ni Wajumbe tuliotumwa kwenu, Na

wajibu wetu ni kufikisha Ujumbe muhimu ulio wazi’

Hivyo ikawabidi watu hao wawadhihirishie watu wa Antakiya kua wayasemayo ni ya

kweli, kwani Mola wao ndie mwenye kujua zaidi ukweli huo juu yao, lakini tatizo sasa

wengi sana kati ya watu hao wakawa si wenye kutaka kufaham juu ya ujumbe huo

muhimu ulio wazi, na hivyo wakaona kua Wajumbe hao wanataka kuwagawanya watu

wao na kutengeneza ufa ndani ya jamii yao baina ya wanaowasikiliza na wasiowasikiliza,

hivyo wakasema wengi wao:

‏﴿قَالُو ۤ اْ‏ إِ َّ تَطَي َّرَْ‏ بِكُمْ‏ لَئِن لم َّْ‏ تَنتَهُواْ‏ لَنَرْجمَُن َّكُمْ‏ وَ‏ لَيَمَس َّ ن َّكُ‏ مْ‏ مِّ‏ ن َّا عَذَابٌ‏ أَلِيمٌ‏ ‏۞قَالُواْ‏

طَائِرُكُم م َّعَكُمْ‏ أَإِن ذُكِّرْتمُ‏ بَلْ‏ أَنتُمْ‏ قَوْمٌ‏ م ُّسْرِفُونَ‏ ﴾

Qaloo inna tatayyarna bikum la-in lam tantahoo lanarjumannakum

walayamassannakum minna AAadhabun aleemun; Qaloo ta-irukum maAAakum

a-in dhukkirtum bal antum qawmun musrifoona; (Surat Yasin 36:18-19)

Tafsir: Wakasema (Watu wa Antakiya): ‘Hakika sisi tunaona Tatayyarna (bashirio la

Uovu) kutoka kwenu, na hivyo kama hamjakoma basi tutakupigeni Mawe na mtafikwa

na Adhabu Kali sana kutoka kwetu.’Wakasema (Wajumbe hao): ‘Bashirio lenu Uovu


516

lkopamoja navyi! Kwani (mnasema hivyo) kwa sababu ya kukumbushwa Tu? Hakika

nyinyi ni watu waliovuka Mipaka.’

Ambapo aya metumia neno Tatayyarna ambalo ni lenye kutokana na neno Tara ambalo

hua linamaanisha Kuruka Angani, Kuelea juu ya hewa, Kukimbilia kufanya jambo kwa

papara, Nuksi, Mikosi au Jambo baya au Ovu, Ndege warukao Angani, Mdudu, Mtu

anaepaa kiakili na kiroho na hivyo hua si mwenye kujishusha chini kutokana na mambo

ya kidunia.

Neno Tara pia hua linamaanisha Mtu mwenye kufanya kwa haraka Kitendo

kitakachosababisha Madhara au Faida. Ambapo ilikua ni kawaida ya Watu wa zamani

kua wenye kua na Imani ya kuangalia namna Ndege wanavyokua wanaruka na kutua na

kisha hua ni wenye kubashiri wema au uovu wa jambo fulani kutokana kitendo cha Kutua

na Kuruka kwa ndege husika na kutokana na kitendo hicho basi ndio likapatikana neno

Tatayyar.

Na hivyo aya kutubainishia kua watu hawa wa Antakiya walikua wanawaona wajumbe

wao hao kua kama ni Nuksi na kua wanataka kuwasababishia Mikosi kwani haiwezekani

kua Allah Subhanah wa Ta’ala awatumie wao Watu kama Mitume, kwani ilikua ni

kawaida ya watu wasioamini kuamini kua kama kweli Allah Subhanah wa Ta’ala anataka

kuwaongoza watu basi atawatume watu wawaongoze wao, kwani wao ni wenye kujua

zaidi, hivyo wakawaonya Watu hao na kusema kua kama hawakukoma kuwaambia

maneno yanayotaka kuwasababishia mikosi basi watawapiga mawe Wajumbe hao.

Hakuchukua mda isipokua tukio la habari za mabishano haya baina ya Wajumbe hawa

na watu wa Antakiya, likamfikia Mfalme wa Antakiya ambae nae alikua pia si mwenye

kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala bali alikua ni mwenye kumuabudu Mungu wao

aitwe Artems, hivyo alipopata habari hio basi akaamrisha kua wajumbe hao waadhibiwe

kwa kusababisha vurugu kwenye Ardhi ya Antakiya na kisha wafungwe Jela.

Wakati wakiwa Jela basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamteua Mjumbe mwengine ili

aende akawongezee nguvu ili kuwathibitishia watu hao wa Antakiya kua Ujumbe wake

na Wajumbe wake ni wa Kweli, ambapo huyu alikua ni Mwanafunzi mwengine aitwae

Paul, ambae nae alipofika katika Mji huo basi akajaribu kutafuta njia ya kua na ukaribu

na Mfalme na bila ya saka Allah Subhanah wa Ta’ala akamrahisishia njia hio kwani ndani

ya Mda mfupi basi akafanikiwa kua ni mwenye ukaribu na Mfalme.

Baada ya Paul kuupata ukaribu huo basi siku moja wakati akiwa anazungumza na

Mfalme bas akamwambia Mfalme huyo kwa kusema: ‘Ewe Mfalme, nimesikia

kuhusiana na watu wawili ambao wako Jela na wanateswa kwa sababu ya kua ni

wenye kufuata Imani ya Dini tofauti na ya watu wako. Hivi jee umewasikiliza hoja

zao?’ Mfalme akajibu: ‘La Hasira zangu ziliingilia kati maamuzi yangu hayo’ Hivyo


517

Paul akasema: ‘Hivyo unaonaje kama tukitumia busara na kuwafanyia uadilifu wa

kuwaita na kuwasikiliza hoja zao?’

Hivyo Mfalme akatafakari kisha akakubaliana na mtizamo wa Paul, na kisha akaamrisha

watu wawili hao waitwe mbele yao, na walipofikishwa mbele yao basi Mfalme akasema

kumwambia Paul: ‘Haya wahoji tusikie hoja zao’ hivyo Paul akawauliza: ‘Jee ni nani

aliekutumeni kuja katika Ardhi ya nchi hii?’ ambapo nao wakajibu: ‘Sisi tumetumwa

na Mungu alieumba Ulimwengu na kila kitu kilichomo ndani yake.’

Paul akawauliza: ‘Jee Mna vithibitisho gani?’ nao wakajibu: ‘Tunavyo vithibitisho

vingi, ikiwemo kuponya wanaoumwa maradhi sugu na yasiyopoa na kuwaponesha

vipofu wasioona na kua ni wenye kuona kwa idhini ya Allah.’

Mfalme akaamrisha waletwe Vipofu, na kila mwenye maradhi Sugu ndani ya Ardhi yake

ili wawaponeshe, na walipoletwa wagonjwa hao basi wakaombewa na kupona. Mfalme

akashangaa kutokana na Miujiza hio, kisha Paul akamwambia Mfalme huyo: ‘Labda

tumuulize na Mungu wako kama anaweza kufanya Miujiza kama yaliyofanywa na

Mungu wa watu hawa.’ Mfalme huyo akamuangalia Paul kisha akasema: ‘Hakika

mimi siwezi kukuficha kutokana na kujua kua hakuna anaeweza kuyafanya haya,

isipokua hawa watu ni wachawi, hivyo wanataka kututoa kwenye Imani ya Mababu

zetu ambayo tumedumu nayo miaka na miaka.’

Na hivyo Paul alipojaribu kumfafanulia Mfalme kuhusiana na vithibitisho vya hoja za

Watu hao juu ya wa uwezo wa Mola wao watu hao walioponesha wagonjwa mbele yao

basi nae akaonekana kua kumbe yuko pamoja nao, hivyo akajumuishwa pamoja nao na

ikatoka amri kua kila anaewakubali na kuwafuata basi auawe pamoja nao.

Ambapo anasema Imam Wahb Ibn Munabih kua: ‘Mfalme huyo hakuwaamini

Wajumbe hao, na hivyo yeye na watu wake wakajipanga kwa ajili ya kuwaua

Wajumbe hao.’ Ambapo wakati anajiandaa kwa tukio hilo la kuwaua wajumbe wakiwa

kati kati ya Mji huo, katika sehemu ya uwanja wa kupitishia hukumu ya adhabu ya kifo

basi kwa mbali akatokea Mtu ambae alikua akiwakimbilia kwa ajili ya kuwakataza watu

hao wasifanye uovu wa dhulma hio ya kuwaua Wajumbe hao wa Allah Subhnah wa

Ta’ala kama zinavyosema aya:

‏﴿وَجَآءَ‏ مِنْ‏ أَقْصَى ٱلْمَدِينَةِ‏ رَجُلٌ‏ يَسْعَى ٰ قَالَ‏ يٰقَوْمِ‏ ٱت َّبِعُواْ‏ ٱلْمُرْسَلِينَ۞ٱت َّبِعُواْ‏ مَن

لا َّ يَسْ‏ أَلُكُمْ‏ أَجْ‏ راً‏ وَهُمْ‏ م ُّهْ‏ تَدُ‏ ونَ‏ ﴾


518

Wajaa min aqsa almadeenati rajulun yasAAa qala ya qawmi ittabiAAoo

almursaleena; IttabiAAoo man la yas-alukum ajran wahum muhtadoona(Surat

Yasin 36:20-21)

Tafsir: Na mara akaja Mtu kutoka mbali ya Mji akikimbilia akasema: ‘Eni watu

wangu Wafuateni Wajumbe hawa, wafuateni wale ambao hawakudaini Malipo kwani

wao wameongozwa’

Ambapo anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Jina lake

Mtu huyu lilikua ni Habib Al Najjar ambae alikua ni fundi Seremala.’ Ambapo

Imam Wahb Ibn Munabih anasema kua: ‘Habib likua ni mgonjwa mwenye maradhi

ya ukoma, na nyumba yake ilikua iko mwanzoni kabisa mwa Lango la kuingilia

kwenye mji wa Antakiya, na alikua ni Muumini mwenye ukarimu sana, alikua

akipata malipo ya kazi zake alikua akiyagawa sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni

kwa ajili ya familia yake na sehemu ya pili ni kwa ajili ya kutoa Sadaqa.

Aliposikia kuhusiana na kua watu wake wanataka kuwaua Wajumbe hao basi

aliwakimbilia kuwaonya kwani kabla yake alikua akimuamini Allah Subhana wa

Ta’ala laakini aikua akifanya Ibada zake kwa siri, na aliposikia kuhusiana na

ujumbe wa watu hao basi alidhihirisha Iman yake na kuwausia watu wake.’

Hivyo watu wa Antakiya walipomuona Habib anawatetea watu hao basi nao

wakamjumuisha pamoja nao na kumwambia: ‘Ala kumbe na wewe ni miongoni mwao

watu hawa wanaopingana na Imani ya Dini yetu na ni mwenye kuamini mitizamo

ya Imani ya Dini yao?’

Hivyo Habib akasema kama zinavyobainisha aya:

‏﴿وَمَا لىَِ‏ لاَ‏ أَعْبُدُ‏ ٱل َّذِى فَطَرَنىِ‏ وَإِلَيْهِ‏ تُرْجَعُونَ۞أَأَتخ َِّذُ‏ مِ‏ ن دُونِهِ‏ آلهَِةً‏ إِن يُرِدْنِ‏

ٱلر َّحمَْٰنُ‏ بِضُرٍّ‏ لا َّ تُغْنِ‏ عَنىِّ‏ شَفَاعَتُهُمْ‏ شَيْئاً‏ وَلاَ‏ يُنقِذُونَ۞إِِ‏ نيّ‏ ۤ إِذاً‏ ل َّفِى ضَلاٍَل

م ُّبِينٍ۞‏ ِ إِنيّ‏ ۤ آمَنتُ‏ بِرَبِّكُمْ‏ فَٱسمَْعُونِ‏ ﴾

Wama liya la aAAbudu alladhee fataranee wa-ilayhi turjaAAoona; Aattakhidhu

min doonihi alihatan in yuridni alrrahmanu bidhurrin la tughni AAannee

shafaAAatuhum shay-an wala yunqidhooni; Innee idhan lafee dalalin mubeenin;

Innee amantu birabbikum faismaAAooni; (Surat Yasin 36:22-25)


519

Tafsir: Jee kwanini nisimuabudu yule ambae alieanianzisha na ambae kwake yeye

ndio kwenye marudio yenu? Hivi nitachukuaje Miungu wengine ambao

hawatonisaidia kitu pale mwingi wa Rehma atakapoamua kunidhuru hawatonisaidia

kitu dhidi yake? Kwa hivyo basi nitakua kwenye upotovu. Hakika mimi nimemuamini

Mola wenu: ‘Hivyo nisikilizeni’

Lakini baada ya kusema maneno hayo basi watu wa Antakiya wakamvamia Habib na

wakamuua kama walivyowaua wale wengine ambao ni Wajumbe wa Allah Subhanah wa

Ta’ala ambapo anasema Imam Abd Rahman Al Suddi kua: ‘Watu hawa walimpiga

mawe Habib mpaka akafariki Dunia huku akiwa ni mwenye kusema: ‘Ya Allah

Waongoze watu wangu.’’

Ambapo amesema Imam Hasan Al Basr kua: ‘Walimtoboa Koo yake na kisha

wakamtundika kwenye mlango ya Mji huo na kisha wakamzika, hivyo Allah

Subhanah wa Ta’ala akamfaridhshia Pepo moja kwa moja na akaambiwa:

‏﴿قِيلَ‏ ٱدْخُلِ‏ ٱلجَْن َّةَ‏ قَالَ‏ يٰلَيْتَ‏ قَوْمِى ا يَعْلَمُونَ۞بمَِ‏ غَفَرَ‏ لىِ‏ رَ‏ بىِّ‏ وَ‏ جَعَلَنىِ‏ مِنَ‏

ٱلْمُكْرَمِينَ‏ ﴾

Qeela odkhuli aljannata qala ya layta qawmee yaAAlamoona; Bima ghafara lee

rabbee wajaAAalanee mina almukrameena; (Surat Yasin 36:26-27)

Tafsir: ‘Akaambiwa: ‘Ingia Peponi’ nae akasema: ‘Ya Laiti kama watu wangu

wangejua’ Alivyonisamehe Mola wangu na kunifanya kua ni miongoni mwa

Waliokirimiwa.’

Hivyo baada ya watu wa Antakiya kuwaua Mtume hao na kisha wakamuua Habib basi

Allah Subhanah wa Ta’ala akawaghadhibikia na kuwaadhibu kama zinayosema aya:

‏﴿وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَى ٰ قَوْمِهِ‏ مِن بَعْدِهِ‏ مِن جُندٍ‏ مِّنَ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ وَمَا كُن َّ ا مُنزِلِينَ۞نِإ

كَانَتْ‏ إِلا َّ صَيْحَةً‏ وَاحِ‏ دَةً‏ فَإِذَا هُمْ‏ خَامِدُونَ‏ ﴾

Wama anzalna AAala qawmihi min baAAdihi min jundin mina alssama-i wama

kunna munzileena; In kanat illa sayhatan wahidatan fa-idha hum khamidoona

(Surat Yasin 36:27-29)


520

Tafsir: Na hatukuwashushia Watu wa Kaumu yake baada yake Jeshi kutoka Mbinguni

na wala hatukuhitaji kua ni wenye kutuma. Kwani haikua ila Ukelele Mmoja tu nao

wakawa wameteketea.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anatuambia kua watu hawa wa Mji wa Antakiya

hawakuhitaji kushushiwa Jeshi kutoka Mbinguni kwani haikuhitajika kufanywa hivyo,

na hii ni kutokana na Muumbaji kua ni mwenye kujua udhaifu wa Viumbe wake na kila

kitu juu yao, kua pale anapotaka kuwaadhibu basi si lazima awatumie Adhabu

inayotokana na wingi wa kitu kinachoadhibu, kwani kwake yeye hakuna

kinachoshindikana, hivyo anaweza kutumia kitu kimoja tu kidogo ambacho ni chenye

kudharaulika sana lakini madhara yake yakawa ni ya mangamizo makubwa na ya hatari

sana.

Kwa mfano kama tulivyoona kwenye adhabu iliyowakuta watu wa Nabii Hud, ambao

tulisema kua walipigwa na Upepo wa hali ya Umoja wa Rihan wa Adhabu, hivyo basi na

watu hawa wa Antakiya aliamua pia kuwaadhibu kwa adhabu Moja ambayo ni yenye

kutokan na Sauti inayojulikana kama Sayhatun ambayo ni adhabu inayotokana na

Ukelele Mmoja mkubwa sana ambao matokeo yake hua ni kuwapelekea waliopigiwa

Ukelele huo kua hapo hapo ni wenye Kupoteza faham na kutoka Roho moja kwa moja

kutokn ana kuzimika kwa uhai wao, kwani Kuzimika ndio maana ya neno Khamidun

lililotumika kwenye aya yetu inayoelezea tukio hili lililowakuta watu wa Antakiya.

Ambapo wanasema Wanazuoni kua Allah Subhanah wa Ta’ala alimtuma Malaika Jibril

kua aende kwenye Lango kuu la kungilia kwenye Mji huo na kisha Anadie ndani ya Mji

huo kwa Ukele Mmoja tu, kua ndio iwe dhabu yao. Kwani kimaumbile Sauti hua

inasikika kutokana na kua ni yenye kua na Mtetemeko wa Mawimbi ya hewa ambao

hukusanywa katika sehemu ya nje ya sikio na kisha kusafirishwa hadi ndani kwa njia ya

Mawimbi ambayo huingia ndani sikioni na kugonga kwenye ngoma ya sikio, na kisha

kusukumwa ndani zaidi kwenye sehemu ya kati ya sikio kupitia kwenye mifupa laini ya

hisia ambayo huyapeleka mawimbi hayo kwenye mzunguko wa Tarumbeta au Koa ya

sikio ambayo ndani yake hua mna Majimaji ambayo yanapopokea mtetemeko huo wa

Hewa unaosababisha mawimbi kama ya bahari juu ya Maji hayo.

Mawimbi ya maji ya Sikio husababisha seli za Nywele ndogo ndogo sana za hisia za

Sikio zilizomo kwenye sehemu ya ndani yake kuichukua Sauti hio baada ya kuipima

udogo na ukubwa wa sauti kulingana na ukubwa wa Mawimbi ya Maji ya Sikio na kisha

kuisafirisha sauti hio hadi kwenye mapokezi ya sauti na kupelekwa kwenye mfumo wa

sauti wa Ubongo ambapo hutafsiriwa na Ufaham kua hii ni sauti ya aina fulani na

inamaanisha kitu fulani.

Hivyo kila sauti inavyokua kubwa basi na mawimbi yake hua ni makubwa pia na hua

inasafiri pamoja na Upepo ambao hua unaingia kwa kasi kubwa kwenye masikio na


521

kusababisha tabaka la hewa hio kuingia ndani ya Ngoma ya Sikio na Kuipasua kisha

hewa hio hukimbilia kwenye Mapafu kupitia kwenye Koo na hivyo kuyafanya Mapafu

kupasuka kutokana na ukubwa wa Nguvu ya Sauti ambapo nako hupelekea Mripuko wa

Moyo na kusababisha Kifo cha Ghafla.

Kwani tukio hili la kusikia hadi kutafsiriwa kwa sauti husika na ufaham hua ni lenye

kutokea ndani ya wakati ambao ukubwa wake ni sehemu moja kati ya sehemu kumi ya

sekunde moja, hivyo bila ya shaka Allah Subhanah wa Ta’ala ametuma neno

Khamiduuna kumaanisha kua kutokana na tukio la adhabu hii yenye maumivu makubwa

sana yasiyostahamilika ya miripuko na mipasuko ya viungo mbalimbali muhimu vya

ndani ya mwili lilielekea Watu hawa wote kua ni wenye Kuzimika kwa Ghafla moja Uhai

wao na hili ndilo lililowakuta watu wa Antakiya.

VITHIBITISHO VYA WANAZUONI JUU YA KUPANDISHWA JUU

MBINGUNI RUHI ALLAHI ISA IBN MARYAM WAKATI AKIWA HAI.

Amesema Rasul Allahi Salallahu Ala’ayhi wa Salam kua: ‘Katika kila baada ya miaka

100 basi wale wenye I’lm watakuja kuihifadhi hii Ilm ya Dini, na hivyo watakua ni

wenye kukanusha tafsiri za wajinga na uongo wa wenye kulaghai na wenye kuvuka

mipaka’ (Sunan Al Kubra , Mishkat Al Masabih, Bughya al Multamis)

Amesema tena Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam: ‘Ama kwa Hakika Allah

Subhanah wa Ta’ala atatuma kwa ajili ya Ummah huu kila baada ya miaka 100 mtu

ambae atakua ni mwenye kufanya Tajdid kwa ajili ya Dini yake’ (Sunan Abu Daud).

Na kulingana na mtizamo wa Imam Jalaluddin Al Suyuti katika kitabu chake Mirqat al

Saud ni kua: ‘Kuna makubaliano ya Wanazuoni wa Hadith kua Hadith hii ni Sahih’

Neno Tajdid kwa Kiarabu hua ni lenye kumaanisha Kurudisha upya, kurudisha kitu

katika hali yake ya awali au ya asili baada ya kitu hicho kua ni chenye kufanyiwa

marekebisho, au kusahaulika. Mtu ambae anaefanya kazi hii ya Tajdid hua anajulikana

kama Mujaddid.

Mujaddid maana yake hua mtu mwenye kufanya Tajdid. Hivyo kulingana na hadith

yetu hio ambayo ni hadith sahih basi Allah Subhanah wa Taála ameahidi kua katika kila

baada ya miaka 100 atajaalia kua na mtu ambae ni mwenye kufanya Tajdid na hivyo

kuirudisha Imani ya Dini ya Kiislam katika njia iliyosahih.


522

Anasema Shaykh Al Islam Imam Badr Al Din Abdal anasema: ‘Mujaddid hujulikana

kutokana na kuwepo kwa makubaliano yenye nguvu juu ya Mwanazuoni husika

kulingana na mtizamo wa Wanazuoni wenzake ambao wamenufaika sana na uwezo

wake mkubwa wa I’lm. Hudhihirika kutokana na sifa za ndani na za nje za I’lm ya

Dini ya Kiislamu zinazompelekea kuunga mkono na kulinda Sunnah za Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na pia kukabiliana na kuzishinda Bida’a.

(Risalah Mardhiyyah fi al-Nusrat Madhhab al-Asha'riyyah)

Imam As Suyuti ameorodhesha majina ya Wanazuoni wafuatao kua ni Mujaddid wa

karne zifuatazo katika kitabu chake kinachoitwa Tuhfat Al-Mujtahidin bi Asma' Al-

Mujaddidin.

Mujaddid wa karne ya kwanza ya ya Uislam: Amir al-Mu'minin Umar Ibn Abd al-

Aziz (682 - 720).

Mujaddid wa karne ya pili ya Uislam: Mujaddid Imam Muhammad Ibn Idris Al Shafi`i

(767 - 820).

Mujaddid wa karne ya tatu ya Uislam: Mujaddid Imam Abu Al Hasan Ali ibn Isma'il

Al-Ash'ari (874 –936). Ambae ni mfuasi wa Madhhab ya Imam Al Shafi’i.

Mujaddid wa karne ya nne ya Uislam: Mujaddid Imam Abu Bakr Muḥammad Ibn Al

Ṭayyib Al Baqillāni (930-1013), Ambae ni mfuasi wa Madhhab ya Imam Maliki.

Mujaddid wa karne ya tano ya Uislam: Mujaddid Imam Abu Hamid Ibn Muhammad

ibn Muhammad Al-Ghazali (445-505 A.H/1058–1111). Ambae ni mfuasi wa Madhhab

ya Imam Al Shafi’i kutoka Tus, Iran.

Mujaddid wa karne ya sita ya Uislam: Mujaddid Imam, Imām al-Mushakkikīn Abu

Abdullah Muhammad Ibn Umar Ibn al-Husayn at-Taymi al-Bakri at-Tabaristani Fakhr

ad-Din ar-Razi (544-606 A.H/1149-1209). Ambae ni mfuasi wa Madhhab ya Imam Al

Shafi’i kutoka Ray, Iran. na

Mujaddid Imam ad-Din Abu Al Qasim Abdul Karim Ibn Muhammad Ibn Abdul Karim

Ibn Al-Fadhl Ibn Hasan Ar Rafi'i Al Qazwini (557-623 A.H/1162-1226). Ambae ni

mfuasi wa Madhhab ya Imam Al Shafi’i kutoka Qazwini, Iran.

Mujaddid wa karne ya saba ya Uislam: Mujaddid Imam Muhammad Ibn Ali Ibn Wahb

Al Misri Al Maliki As Shafi’i maarufu kama Imam Ibn Daqeeq Al Eid (625-702 A.H).

Ambae ni mfuasi wa Madhhab ya Imam Al Shafi’i kutoka Misri.

Mujaddid wa karne ya nane ya Uislam: Mujaddid Imam, Al-Haafidh Shihabuddin Abu

ul Fadhl Ahmad Ibn Ali Ibn Muhammad maarufu kama Imam Ibn Hajar Al Asqalani.

Ambae ni mfuasi wa Madhhab ya Imam Al Shafi’i kutoka Asqalani, Palestina. na

Mujaddid Imam Sirajuddin `Umar Ibn Rastan Ibn Nasir Ibn Salih Ibn Ahmad Ibn

Muhammad Ibn Shihab Al Asqalani maarufu kama Imam Al Bulqini (724-810

A.H/1324-1403). Ambae ni mfuasi wa Madhhab ya Imam Al Shafi’i kutoka Bulqina,

Misri.


523

Mujaddid wa karne ya tisa ya Uislam: Mujaddid Imam, Hafidh Jallal Ad Din Abu

Bakr Abd Rahman Al Suyuti (849-911 A.H/1445-1505) Ambae ni mfuasi wa Madhab ya

Imam Al Shafi’i kutoka Al Qakhira (Cairo), Misri.

Wanazuoni waliofuatia baada ya Imam Al Suyuti wakaendeleza orodha hiyo kama

ifuatavyo:-

Mujaddid wa karne ya kumi ya Uislam: Mujaddid Imam Shams Ud Dîn Muhammad

Ibn Ahmad Al Ramli (919-1004 A.H). Ambae ni mfuasi wa Madhhab ya Imam Al Shafi’i

kutoka Al Ramlah, Misri.

Mujaddid wa karne ya kumi na moja ya Uislam: Mujaddid Imam Rabbani Al Alf Al

Thani Shaykh Ahmad Al Faruqi Al Sirhindi (1564-1624). Ambae ni mfuasi wa Madhhab

ya Hanafi kutoka Sirhind (Punjab) India.

Mujaddid wa karne ya kumi na mbili: Mujaddid Imam, Al-Qutb Abd Allah Ibn Alawi

Al Haddad (1634-1720). Ambae ni mfuasi wa Madhhab ya Imam Al Shafi’i kutoka

Hadhramawt, Yemen. na

Mujaddid Imam Shah Waliyu Allah Ad Dahlawi ambae ni mfuasi wa Madhhab ya Imam

Abu Hanifa

Mujaddid wa karne ya kumi na tatu ya Uislam: Mujaddid Imam Muhammad Amin

Ibn Abidin ash Shami (1198–1252 AH/1783-1836). Ambae ni mfuasi wa Madhhab ya

Hanafi kutoka Syria.

Mujaddid wa karne ya kumi na nne ya Uislam: Mujaddid Imam, Muhaddith al Akbar

Muḥammad Badr Al Dīn Ibn Yūsuf Al Marākishī Al Sibtī al Baybānī Al Dimashqī Al

Ḥasanī (1850-1935). Ambae ni mfuasi wa Madhhab ya Maliki kutoka Morocco. na

Mujaddid Imam Muhammad Zahid Ibn Hasan Al Kawthari (1879-1951). Ambae ni

mfuasi wa Madhhab ya Hanafi kutoka Uturuki.

Na zifuatazo ni kauli za Wanazuoni hao wenye Ilm ya juu na kufikia darja ya Mujaddid

Ad Din juu ya kurudi tena kwa Nabii Isa baada ya kupandishwa kwake mbiguni.

Mujaddid Imam wa Karne ya kwanza: Abdullah Ibn Abbas (618 – 687 AH) alisema

kua “Allah Subhanah wa Taála alimnyanyua Isa Ibn Maryam kumpelekea

Mbinguni.” (Imam Abu Bakr Ahmad Ibn Husayn Ibn Ali Ibn Musa Al Khosraji Al

Bayhaqi)

Mujaddid Imam wa Karne ya pili: Imam Abu ʿAbdullah Muhammad Ibn Idris al

Shafi‘i (767/150 – 820/204 CE/AH) Alisema kua: ‘Kama ilivyokua kwa Isa Ibn

Maryam alivyopandishwa juu Mbinguni, basi ndio hivyo hivyo atakavyoshushwa

Ulimwenguni kwa amri ya amri ya Allah Subhanah wa Taála ili kuja kueneza Dini

ya Allah Subhanah wa Taála, watu wenye Imani dhaifu wanaweza wakaona kua hii


524

haiwezekani. Lakini hili ni jambo rahisi pale tunapozungumzia Uwezo wa Allah

Subhanah wa Taála’

Mujaddid Imam wa Karne ya tatu: Abū Al-Hasan Alī Ibn Ismā’īl Al-Ash’arī

(874/260 – 936/324 CE/AH) anasema kua: ‘Kuna Makubaliano ya Ijmaa Ummat kua

Isa Ibn Maryam alinyanyuliwa juu mbinguni.’ (Al-Ash’ari’s al-Ibana ‘an Usul al-

Dina,)

Mujaddid Imam wa Karne ya nne: Abu Abd-Allah Muhammad ibn Abd-Allah al-

Hakim al-Nishaburi (933/321 – 1012/403 CE/AH) anasema katika kitabu chake cha

Mustadrak Al Hakim kua: Amesema Abd Allah Ibn Abbas kua kuhusiana na aya

isemayo:

‏﴿وَإِن مِّنْ‏ أَهْلِ‏ ٱلْكِتَابِ‏ إِلا َّ لَيُؤْمِنَن َّ بِهِ‏ قَبْلَ‏ مَوْتِهِ‏ وَيَوْمَ‏ ٱلْقِيَامَةِ‏ يَكُونُ‏ عَلَيْهِ‏ مْ‏

شَهِيداً‏ ﴾

Wa-in min ahli alkitabi illa layu/minanna bihi qabla mawtihi wayawma alqiyamati

yakoonu AAalayhim shaheedan (Surat An Nisaa 4:159)

Tafsir: Na hakuna miongoni mwa watu wa Ahl ul kitabi isipokua watamuamini kabla

ya mauti yake na katika siku ya Kiama atakua ni shahidi dhidi yao.

Ayah hii ni uthibitisho kua Isa ibn Maryam atakuja tena na watu wa Ahl al Kitabi

wote watamuamini kabla ya kufariki kwake. (Imam Al-Hakim, Al-Mustadrak)

Mujaddid Imam wa Karne ya Tano: Hujjat ul Islami Imam Abū Hāmid Muhammad

Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali ‘Qurán itafutika kutoka katika Nyoyo

za watu na hakuna mtu ambae ataikumbuka, hivyo watu watarudi tena katika enzi

za kuimba nyimbo na kuimba mashairi na hikaya. Kisha Masih Dajal atatokea na

Isa Ibn Maryam Alayhi Salatu wa Salam atashuka na kumuua. Wakati

yatakapotokea yote haya itakua kama vile hali ya mwanamke mjamzito

anakapokua katika hali ya uchungu, akisubiri kujifungua ’(Ihya Ulum Ad Din)

Akasema tena Hujjat Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazal kua: ‘Mitume wote wameoa, isipokua Isa Ibn Maryam yeye

hakua ni miongoni mwa Waliooa lakini ataoa katika wakati wa kipindi chake cha

pili atakapokuja Duniani’ (Ihya Ulum Ad Din Siri ya Ndoa)


525

Imam Abu Bakar Ibn Al Arabi yeye anasema kua: ‘Ingawa miaka zaidi ya 1000 imepita

tangu kuzaliwa kwa Isa Ibn Maryam, lakini ukweli ni kua yeye bado yuko hai

kiroho na kimwili mbele ya Allah Subhanah wa Taála’ (Sharh Jamii Al Tirmidhii)

Mujaddid Imam wa Karne ya Sita: Al Ghawth Shaykh Abd al-Qadir al-Jilani (1077

– 1166 CE) yeye anasema kua: ‘Isa Ibn Maryam, hakuoa, lakini mwisho wa Dunia

utakapofika basi Allah Subhanah wa Taála atamrudisha tena Duniani, na ataoa

binti wa Quraysh ambae atazaa nae mtoto wa kiume’(Al Malfuzat.)

Mujaddid ud Din Imam Fakhr Al Din Al Razi anasema kua:

‏﴿بَل ر َّفَعَهُ‏ ٱهلل َُّ‏ إِلَيْهِ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَزِيزاً‏ حَكِيماً‏ ﴾

Bal rafaAAahu Allahu ilayhi wakana Allahu AAazeezan hakeeman (Surat An Nisaa

4:158).

Tafsir: Bali alimnyanyua Allah kwake yeye, na kwa hakika Allah ni mwenye Uwezo

na ni mwingi wa Hikma.

Aya hii inatuwekea wazi kua Isa Ibn Maryam alinyanyuliwa mbinguni wakati

akiwa hai (Mafatih Al Ghayb/Tafsir al Kabir)

Ambapo neno Bal yaani Bali kimaana hua ni ni lenye kuonesha kukataa na kubatilisha

kitendo kilichofuatia kabla yake na hivyo kua ni lenye kuthibitisha kitendo kinachofuata

baada yake.

Mujaddid Imam wa Karne ya Nane: Imam Ibn Hajar Al-Asqalani (1372/773 – 1448/852

CE/AH) “Mahdi atatokana na Ummah huu, na Isa Ibn Maryam atashuka na kusali

nyuma yake’ na akasema tena pia kua; ‘Hakuna Mtume baina ya Isa Ibn Maryam na

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na yeye Isa Ibn Maryam hana kaburi’.

(Fath al-Baari)

Mujaddid Imam wa Karne ya Tisa: Jalaluddin Al-Suyuti (1445/849 – 1505/911

CE/AH) amesema kua “Mji Wa Jerusalem una utukufu wake kwa Waislam kwa

sababu, ni katika mji wa Jerusalem ndipo ambapo Isa Ibn Maryam alizaliwa, ni

katika mji wa Jerusalem ndipo Mitime wengi waliuliwa, ni katika Mji wa Jerusalem

ndio sehemu ambayo Isa Ibn Maryam alizungumza wakati akiwa ndani ya mkoba

wa kubebea mtoto mchanga, na ni katika mji wa Jerusalem ndio sehemu ambayo


526

alipandishwa juu mbinguni na ndipo atakaposhukia kutoka Mbinguni (Durr al-

Manthur)

Imam Al Suyuti amesema tena katika kuifafanua aya ifuatayo:

‏﴿إِذْ‏ قَالَ‏ ٱهلل َُّ‏ يٰعِيسَى ٱبْنَ‏ مَرْيمََ‏ ٱذْكُرْ‏ نِعْمَتىِ‏ عَلَيْكَ‏ وَعَلَى ٰ وَالِدَتِكَ‏ إِذْ‏ أَي َّدت ُّكَ‏

بِرُوحِ‏ ٱلْقُدُسِ‏ تُكَلِّمُ‏ ٱلن َّاسَ‏ فىِ‏ ٱلْمَ‏ هْ‏ دِ‏ وَكَ‏ هْ‏ لاً‏ ﴾

Idh qala Allahu ya AAeesa ibna maryama udhkur niAAmatee AAalayka waAAala

walidatika idh ayyadtuka biroohi alqudusi tukallimu alnnasa fee almahdi wakahlan

(Surat Al Maidah 5:110)

Tafsir: Alisema Allah Subhanah wa Taála kua: ‘Ewe Isa Ibn Maryam kumbuka neema

zangu juu yako na juu ya mzazi wako (Mama yako Maryam Bint Imran) nilipokusaidia

mimi na Ruh ul Qudus (Malaika Jibril) hivyo ukazungumza na watu wakati upo katika

mkoba wa mtoto mchanga na utakapokua’

Neno Kahlan lililotumika hapa linamaanisha kua Isa Ibn Maryam atashuka chini

kutoka Mbinguni kabla ya siku ya Kiama, kwa sababu alipandishwa juu Mbinguni

kabla ya kuufikia uzee (Tafsir al-Jalalayn, Surah al-Ma’ida)

Imam Suyuti ameandika katika Durr Manthur kua: Imam Ahmad, Imam Bukhari, Imam

Muslim na Imam Baihaqi wamesema kua amesema Rasul Allah Salallahu A’lahi wa

Salam kua: ‘Jee Itakuaje hali yenu, katika wakati ambao Isa Ibn Maryam atashuka

na kua miongoni mwenu na Imam wenu atakua ni kutoka miongoni mwenu?’

Mujaddid Imam wa Karne ya Kumi na Moja: Rabbānī Shaykh Ahmad Al-Farūqī Al-

Sirhindī Mujaddid Alf Thānī (1564 – 1624 CE) ambae amesema: “Isa Ibn Maryam

atashuka kutoka mbinguni na atakua ni mfuasi wa Nabii Muhammad Salallahu

Alayhi wa Salam, kwa kauli nyengine basi, atakua ni mwenye kufuata shariah za

Allah Subhanah wa Taála alizokuja nazo Rasul Allah Salallahu aAlayhi wa Salam.’

(Rasail Imam Rabbani)

Mujaddid Imam wa Karne ya Kumi na Mbili: Shah Waliullah Dehlwi (1703 – 1762

CE) ambae amesema ‘Hakuna mtu hata mmoja miongoni mwa Ahl Ul Kitab

atakaekua hai isipokua ataka ni mwenye kumuamini Isa Ibn Maryam pale

atakaposhuka tena kabla ya kuufariki kwake, hata na Mayahudi watakaokuwepo

katika wakati huo watamuamini’ (Fath ur Rahmaan Fii Tarjumatul Qura’an, 4:159)


527

Mujaddid Imam wa Karne ya Kumi na mbili; Muhammad ash-Shawkani (1759–1834

CE) amesema kua: ‘Isa ibn Maryam alinyanyuliwa juu Mbinguni na atashuka

mwishoni mwa Ulimwengu’ (Fath al-Qadir)

Mujaddid Imam wa Karne ya kumi na nne; Bediüzzaman Said Nursî (1878 - 1960) :

‘Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam aliainisha miongoni mwa Miujiza

mikubwa Ulimwenguni ni kushuka kwa Isa Ibn Maryam pale aliposema: ‘Isa ibn

Maryam atashuka kutoka mbiguni, na ataishi kulingana na Sharia yangu’’ (Rasail

Bediuzzaman)

Mujaddid Imam Muhammad Ash-Shanqeeti (1907 – 1973 C.E) amesema kua:

‘Qur’an na Sunna zinathibitishha kua Isa Ibn Maryam yuko hai na anaishi mbiguni

na atashuka kabla ya siku ya Mwisho’(Adwaa Ul Bayaan fii Tafsir Il Qurán bil Qurán)

Na bila ya shaka amesema Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Isa Ibn

Maryam atarudi katika Ulimwengu huu na kujumuika na Ummah wangu na hivyo

kua ni mwenye kufuata sharia yangu.’ (Sahih Bukhari na Muslim na Sunan Imam Ibn

Majah)

TAQDIM WA TAAKHIR KATIKA QUR’AN

Tunapozunguzumzia llm Al Maani na Ilm al Balagha katika Uumu ul Qur’an basi

tunaona kua katika baadhi ya aya ndani ya Qur’an zimetumia mfumo wa maneno

unaojulikana kama Taqdim na Ta’akhir yaani Kuzungumziwa kwa vitu viwili katika hali

ambayo kimoja hua kinawahi kukitangulia chengine katika kutajwa kwake, ijapokua

kimaumbile basi kile kilichotangulizwa hua ni cha Mwisho na kile kilichotajwa Mwisho

hua ni cha Mwanzo.

Hivyo pale inapokua Kitu husika kimetangulizwa kwa kutajwa mwanzo basi hua

kinajulikana kama Taqdim na kile kilichotajwa Mwisho hua kinajulikana kama Taakhir

yaani Kilichowekwa Mwisho katika mpangilio wa kutajwa kwake.

Ambapo hata hivyo mfumo huo wa mpangilio wa maneno hayo ya Taqdim na Taakhir

katika aya husika hua hayabadilishi maana na badaa yake hua ni wenye kuthibitisha

maana halisi iliyokusudiwa kubainishwa na Aya na hivyo kuifanya Qur’an kua na sifa za

upekee katika mpangilio wa maneno yake.

Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi anatuambia kua: ‘Ndani katika Qur’an

kuna hali ya matukio ambayo hua inajulikana kama Taqdim wa Taakhir


528

(Kubainisha hali ya Utangulizi wa Kitu na hali ya Mwisho wa Kitu) ambayo ni

mengi sana, kwa mfano pale aliposema Allah Subhanah wa Ta’ala:

‏﴿وَٱهلل َُّ‏ أَخْرَجَكُم مِّن بُطُونِ‏ أُم َّهَاتِكُمْ‏ لاَ‏ تَعْلَمُونَ‏ شَيْئاً‏ وَجَعَلَ‏ لَكُمُ‏ ٱلْس َّمْعَ‏

وَٱلأَبْصَارَ‏ وَٱلأَفْئِدَةَ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تَشْكُرُونَ‏ ﴾

WaAllahu akhrajakum min butooni ommahatikum la taAAlamoona shay-an

wajaAAala lakumu alssamAAa waal-absara waal-af-idata laAAallakum

tashkuroona (Surat An Nahl 16:78)

Tafsir: Allah amekutoeni nyie kutoka kwenye matumbo ya Mama zenu huku mkiwa

hamjui kitu na amekujaalieni Masikio, Macho na Nyoyo ili mpate kua ni wenye

kuonesha Shukurani

Ambapo hali ya Taqdim na Taakhir hapa katika aya ni pale tunapoona kua ingawa

Allah Subhanah wa Ta’ala anawaumba Ibn Adam wakiwa na Masikio, Macho na

Nyoyo wakati wakiwa Matumboni mwa Mama zao kabla ya kuzaliwa kwao, lakini

hapa ametaja kuzaliwa kwao kabla ya kutaja viungo hivyo walivyoumbwa navyo.

Ambapo mifano myengine ya hali hii ya Taqdim wa Taakhir tunaziona katika Qu’ran

pale Allah Subhanah wa Ta’ala aliposema kua:

‏﴿وَلاَ‏ تُعْجِ‏ بْكَ‏ أَمْوَالهُُمْ‏ وَأَوْلاَدُهُمْ‏ إِنم ََّا يُرِيدُ‏ ٱهلل َُّ‏ أَن يُعَذِّبَهُمْ‏ هبَِا فىِ‏ ٱلد ُّنْيَا وَ‏ تَزْهَقَ‏

أَنفُسُهُمْ‏ وَهُمْ‏ كَ‏ افِرُونَ‏ ﴾

Wala tuAAjibka amwaluhum waawladuhum innama yureedu Allahu an

yuAAadhdhibahum biha fee alddunya watazhaqa anfusuhum wahum kafiroona

(Surat At Tawbah 9:85)

Tafsir: Na wala Msione Ajabu juu ya Mali zao na Watoto wao kwani Allah anataka

kuwaadhibu kutokana nao hapa Duniani na hivyo Roho zao zitoke huku wakiwa ni

Makafiri.


529

Na hivyo aya hii intakwa ifahamike kama : ‘Fa la tu`jibuka amwaluhum wa la

auladuhum fi al-hayat al-duniya;innama yuridu Allahu li yu`adhdhibahum biha fi al-

`akhira’ yaani ‘Na Kisha Msistajabishwe na Mali na Watoto wanaowamiliki katika

maisha ya Duniani. Kwani Allah anataka kuwaadhibu kutokana nao Kesho

Akhera’

Ambapo huu ni mfano wa hali ya Taqdim Kutangulizwa kwa Kitu katika kubainishwa

kwake kwani Makafiri hua ni wenye Kuadhibiwa Akhera ambapo kwa upande wa aya

ifuatayo basi hua ni yenye mfano wa hali ya Taakhir yaani ya Kucheleweshwa Mwisho

kwani inasema:

‏﴿وَ‏ لَوْلاَ‏ كَلِمَةٌ‏ سَبَقَتْ‏ مِن ر َّبِّكَ‏ لَكَانَ‏ لِزَاماً‏ وَأَجَ‏ لٌ‏ م ُّسَمًّ‏ ى﴾‏

Walawla kalimatun sabaqat min rabbika lakana lizaman waajalun musamman

(Surat Ta-Ha 20:129)

Tafsir: Na kama si Kauli iliyotangulia kutoka kwa Mola wako na jambo lisiloepukika

basi ni jambo ambalo limeshaamuliwa litokee (Adhabu yao ingewafika hapa Duniani)

Ambapo inatakiwa ifahamike kama ‘Wa laula kalimatun sabaqat min rabbika wa

ajalun musamma lakana lizama’ yaani ‘Na Kama si Kauli iliyotangulia kutoka kwa

Mola wako kua litokee basi lisingeepukika (Adhabu ingetokea hapo hapo)’

Ambapo mfano mwengine ni ule wa aya ya Mirathi ambayo inasema:

‏﴿يُوصِيكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ فيِ‏ ۤ أَوْلاَدِكُمْ‏ لِلذ َّكَرِ‏ مِثْلُ‏ حَظِّ‏ ٱلأُنْثَيَينِْ‏ فَإِن كُن َّ نِسَآءً‏ فَوْقَ‏ ٱثْنَتَينِْ‏

فَلَهُن َّ ثُلُثَا مَا تَرَكَ‏ وَإِن كَانَتْ‏ وَاحِ‏ دَةً‏ فَلَهَا ٱلنِّصْفُ‏ وَلأَبَوَيْهِ‏ ِ لِكُل وَاحِ‏ دٍ‏ مِّنْهُمَا

ٱلس ُّدُسُ‏ ممِ َّا تَرَكَ‏ إِن كَانَ‏ لَهُ‏ وَلَدٌ‏ فَإِن لم َّْ‏ يَكُنْ‏ ل َّهُ‏ وَلَدٌ‏ وَوَرِثَهُ‏ أَبَوَاهُ‏ فَلِأُمِّهِ‏ ٱلث ُّلُثُ‏ فَإِن

ّ

كَانَ‏ لَهُ‏ إِخْوَةٌ‏ فَلِأُمِّهِ‏ ٱلس ُّدُسُ‏ مِن بَعْدِ‏ وَصِي َّةٍ‏ يُوصِى هبَِآ أَوْ‏ دَيْنٍ‏ آآبَؤُكُمْ‏ وَأَبناؤُكُ‏ ‏ْم

لاَ‏ تَدْرُونَ‏ أَي ُّهُمْ‏ أَقْرَبُ‏ لَكُمْ‏ نَفْعاً‏ فَرِيضَةً‏ مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ كَانَ‏ عَلِيماً‏ حَكِ‏ يماً‏ ﴾


530

Yooseekumu Allahu fee awladikum lildhdhakari mithlu hadhdhi alonthayayni fa-in

kunna nisaan fawqa ithnatayni falahunna thulutha ma taraka wa-in kanat

wahidatan falaha alnnisfu wali-abawayhi likulli wahidin minhuma alssudusu

mimma taraka in kana lahu waladun fa-in lam yakun lahu waladun wawarithahu

abawahu fali-ommihi alththuluthu fa-in kana lahu ikhwatun fali-ommihi alssudusu

min baAAdi wasiyyatin yoosee biha aw daynin abaokum waabnaokum la tadroona

ayyuhum aqrabu lakum nafAAan fareedatan mina Allahi inna Allaha kana

AAaleeman hakeeman(Surat An Nisaa 4:11)

Tafsir: Allah anakuamrisheni kuhusiana na Watoto wenu: Juu ya Mwanamme ni

sawa na sehemu ya Wanawake wawili. Lakini kama ikiwa kuna Watoto wa Kike peke

yao wawili au zaidi basi juu ya ni sehemu mbili kati ya tatu ya Mali ya Mtu, na kama

kuna mmoja tu basi juu yake yeye ni Nusu, na kwa Mzazi wa Mtu basi kila mmoja juu

yake ni Sehemu moja kati ya Sita ya Mali kama ikiwa amewacha Mtoto, lakini kama

ikiwa hakuacha Mtoto na Mzazi pekee anaerithi kutoka kwake basi juu ya Mama yake

ni sehemu moja kati ya tatu na kama ana Ndugu basi juu ya Mama ni moja kati ya

Sita, baada ya Wasia aliouacha (Kutekelezwa) au Deni (Kulipwa)

Ambapo ingawa Aya imetaja Kutekelezwa kwa Wasia kwanza lakini kwa upande wa

Hukumu za Fiqh basi kwanza hua ni Deni ndio linaloshughulikiwa mwanzo kabla ya

Wasia.

Mfano mwengine ni ule wa Aya inayosema:

‏﴿فَفَه َّمْنَاهَا سُلَيْمَانَ‏ وَكُلاًّ‏ آتَيْنَا حُكْماً‏ وَعِلْماً‏ وَسَخ َّرَْ‏ مَعَ‏ دَاوُودَ‏ ٱلجِْبَالَ‏ يُسَبِّحْ‏ نَ‏

وَٱلط َّيْرَ‏ وَكُن َّا فَ‏ اعِلِينَ‏ ﴾

Fafahhamnaha sulaymana wakullan atayna hukman waAAilman wasakhkharna

maAAa dawooda aljibala yusabbihna waalttayra wakunna faAAileena (Surat Al

Anbiyaa 21:79)

Tafsir: Na Tukamfahamisha juu yake Sulayman na kila mmoja wao tumempa Hikma

na Ilmu. Na tumeviweka chini yake Daudi, Majabali yanamsalimia na Ndege na ni

sisi wafanyaji wa hayo.

Ambapo kwa kikawaida basi Ilm huitangulia Hikma lakini katika ayah hii Hikma

imetajwa katika hali ya kuitangulia Ilm. Na mfano mwengine ni wa ile aya ya Surat Al

Mulk ambayo inasema:


531

‏﴿ٱل َّذِى خَلَقَ‏ ٱلْمَوْتَ‏ وَٱلحَْيَاةَ‏ لِيَبْلُوَكُمْ‏ أَي ُّكُمْ‏ أَحْسَنُ‏ عَمَلاً‏ وَهُوَ‏ ٱلْعَزِيزُ‏ ٱلْغَفُورُ‏ ﴾

Alladhee khalaqa almawta waalhayata liyabluwakum ayyukum ahsanu AAamalan

wahuwa alAAazeezu alghafooru(Surat Al Mulk 67:2)

Tafsir: Ni yeye ndie alieumba Mauti na Uhai ili akupimeni ni yupi miongoni mwenu

kua ni m-bora katika kufanya Mema, na yeye Ndie Mwenye Utukufu na ni Mwingi wa

Usamehevu.

Ambapo aya imetanguliza Maumbile ya Kifo kabla ya Maumbile ya Uhai wakati

kimaumbile kwanza hua kuna Uhai na kisha ndio hufuata Kifo.

Na mfano mwengine ni katika ile aya semayo:

‏﴿ٱلحَْمْدُ‏ هللِ َِّ‏ ٱل َّذِى أَنْزَلَ‏ عَلَى ٰ عَبْدِهِ‏ ٱلْكِتَابَ‏ وَلمَْ‏ يجَْعَل ل َّهُ‏ عِوَجَا﴾‏

Alhamdu lillahi alladhee anzala AAala AAabdihi alkitaba walam yajAAal lahu

AAiwajan(Surat Al Kahf 18:1)

Tafsir: Shukran zote anastahiki Allah yule ambae amemshushia Mja wake Kitabu na

hakuweka ubaya ndani yake

Inatakiwa ifahamike kua ‘Alhamd lillahi Aladhii anzala `al `abdihi al-kitab qayyiman

wa lam yaj`al lahu iwaja’ yaani ‘Shukran zote anastahiki Allah yule ambae

amemshushia Mja wake Kitabu kilichokamilia bila ya kukijaalia kua na kasoro.

Kutokana na kuwepo kwa hali hii ya Taqdim na Taakhir ndani ya Qur’an basi Imam

Qatada Al Sadusi basi yeye amesema kua: ‘Aya hii ya Surat Al Imran 3:55:

‏﴿إِذْ‏ قَالَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٰ يٰعِيسَى ِ إِنىّ‏ مُتَوَفِّيكَ‏ وَرَافِعُكَ‏ إِلىَ َّوَمُطَهِّرُكَمِنَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَ‏ فَرُواْ‏

وَجَاعِلُ‏ ٱل َّذِينَ‏ ٱت َّبَعُوكَ‏ فَوْقَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ إِلىَٰ‏ يَوْمِ‏ ٱلْقِيَامَةِ‏ ثمُ َّ إِلىَ َّ ‏َمرْجِعُكُْم

فَأَحْكُمُ‏ بَيْنَكُمْ‏ فِيمَا كُنتُمْ‏ فِيهِ‏ تخَْتَلِفُونَ‏ ﴾


532

Idh qala Allahu ya AAeesa innee mutawaffeeka warafiAAuka ilayya

wamutahhiruka mina alladheena kafaroo wajaAAilu alladheena ittabaAAooka

fawqa alladheena kafaroo ila yawmi alqiyamati thumma ilayya marjiAAukum

faahkumu baynakum feema kuntum feehi takhtalifoona (Surat Al Imran 3:55)

Tafsir: Na akasema Allah (Subhanah wa Ta’ala): ‘Ewe Isa! Hakika mimi

nitakutimizia Ahadi niliyokuwekea, nitakunyanyua kwangu na kukusafisha kutokana

na wale ambao waliokufuru na nitawajaalia wale wanaokufuata kua juu ya

waliokufuru hadi katika siku ya Kiama. Na kisha mtarudi kwangu nami nitahukumu

baina yenu juu ya yale mliyokua mkikhitilafiana’

Kua inatakiwa ifahamike kama ‘Rafiyuka ilayya wa Mutawafeeka’ yaani Allah

Subhanah wa Ta’ala anamwambia Nabii Isa kua ‘Nitakunyanyua kwangu na

kukutimizia Ahadi niliyokuwekea’

ISA IBN MARYAM NA MAHDI, DAJJAL, JUJ WA MAJUUJ NA DHUL

QARNAYN.

Neno Mahdi ni neno linalotokana na neno Hada au Huda ambalo kwa Kiarabu hua ni

lenye kumaanisha Kuongoza njia, Kuonesha njia kwa Ukarimu au Kuongoza njia

iliyokua Sahih. Hivyo tunapozungumzia neno Mahdi basi hua tunazungumzia mtu

mwenye sifa ya kua ni mwenye kuongoka na kua ni mwenye kuelekea katika njia sahih.

Mara nyingi unapozungumzia juu ya Mahdi basi watu hua ni wenye kujiuiza kwa

kutoweza kujua juu ya uhalisia wa huyu Mahdi ndio nani yaani ni Nabii Isa, au ni mtu

mwengine zaidi?

Jibu la suali hili linapatikana pale tunapoangalia na kuona kua: Kuna Hadith ambazo

zinathibitisha kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliwaombea Dua baadhi ya

Masahaba zake wawe ni miongoni mwa Mahdi, Kuna hadith zinazothibitisha kua familia

ya watu wa Ahl Al Bayt watatoa mtu kabla ya kipindi cha mwisho wa Dunia ambae nae

atakua na darja ya Imam Mahdi ambae yeye alipotajwa katika hadith basi ametajwa kwa

jina la Al Mahdi jina ambao linaweka wazi kua yeye ndie atakaekua na Darja ya upekee

na sifa inayostahiki ya kua ni Al Mahdi.

Yaani kama vile ambavyo tunavyosema kua Imam wa Hadith kua ni Hafidh wa Hadith

kwa mfano Al Hafidh Imam Al Baghawi, Al Hafidh Imam Al Sakhawi, Al Hafidh Imam

Al Qastallani, Al Hafidh Imam Ibn Al Mundhri, n.k. lakini hapo hapo watu wanaposema


533

Al Hafidh pekee bila ya kutaja jina la Imam husika basi moja kwa moja wenye kujua hua

wanajua kua aliekususdiwa hapo si Al Hafidh yeyote mwengine isipokua Mujaddid ad

Din, Shaykh ul Islami Al Hafidh Imam Shihab Ad Din Ibn Hajjar Al Asqalani.

Hivyo basi tunapozungumzia Mahdi basi na Nabii Isa Ibn Maryam ambae ni Nabii na

Mtume wa Allah Subhanah wa Ta’ala nae pia anajulikana kwa cheo cha Mahdi lakini si

Al Mahdi.

Miongoni mwa hadith ambazo zinathibitisha kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alitumia jina hilo katika dua zake kuwaombea Masahaba zake wawe na daraja hio ni ile

ambayo alimuombea dua Jarir Ibn Abdullah Radhi Allah Anhu, kwa kusema:

الل َّهُم َّ ثَبِّتْهُ‏ وَاجْعَلْهُ‏ هَادًِ‏ مَهْدًِّ‏

Ya Allah! Mjaalie msimamo thabit na umjaalie uongofu wenye darja ya Mahdi (Sahih

Bukhari)

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimuombea dua Muawwiyah Ibn Abu Sufyan

Radhi Allahu Anhu, kwa kusema:

Ya Allah! Mjaalie uongofu wa Mahdi (Jami’ Tirmidhi)

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimsifia Sayyidna Ali Ibn Abi Talib Karama

Allahu Wajh kwa kusema:

Mtamuona kua ni Muongofu na mwenye sifa ya Mahdi ambae atakuongozeni

katika njia iliyonyoooka (Al-Isaba fi Ma’rifatil Sahaba)

Ama kuhusiana na jina lake huyu mtu mwenye darja ya Al Mahdi, basi amesema Rasul

Allah Salallahu A’layhi wa Salam kua: ‘Kuna mtu atakaetoka katika familia yangu

ambae atakua jina lake kama jina langu, na jina la baba yake kama jina la baba

yangu.’(Sunan Abu Dawud)

Vile vile alisema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hata kama itabakia siku

moja tu kabla ya kufika Kiyama, basi Allah Subhanah wa Ta’ala atamtuma mtu

kutoka katika familia yangu ambae ataijaza hii Dunia haki na uadilifu kama vile

mwanzo ilivyokua imejaa dhulma.’(Sunan Abu Daud)


534

Ambapo amesema Jabir Ibn Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah

Salallahu Alayh wa Salam kua: ‘Ukifika wakati, basi Isa Ibn Maryam ghafla

atashuka miongoni mwa Waislam. Na utakusanyika mkusanyiko kwa ajili ya Sala

nae ataambiwa: ‘Ewe Ruhi Allah njoo mbele utusalishe’ lakini nae atasema: ‘La,

Imamu wenu atakuja mbele na atakusalisheni’ hivyo baada ya Sala ya Alfajr

Waislamu waatoka kwa ajli ya kupigana na Masih Dajjal, ambapo Dajjal

atakapomuona Isa Ibn Maryam basi atayeyuka kama inavyoyeyuka Chumvi

kwenye Maji, hivyo Isa Ibn Maryam atamsogelea na Kumuua, na hali itafikia kua

hadi kila Jiwe litakua linasema: ‘Ewe Ruhi Allah, kuna Yahudi amejificha nyuma

yangu’ hivyo hakuna Mfuasi wake hata mmoja ambae ataepuka kuuliwa’’(Musnad

Imam Ahmad)

Na amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Wakati Mahdi

atakaposalisha Sala ya Al Fajr pamoja na Waumini katika Bayt ul Maqdis, basi

atamtambulisha Isa Ibn Maryam ambae atakuwepo, nae Isa Ibn Maryam

atamshika bega Mahdi na kumwambia: ‘Adhana imeadhiniwa kwa ajili yako, hivyo

ni wajibu wako kusalisha’’(Al-Qawl Al-Mukhtasar Fi alamat Al-Mahdi Al-Muntazar)

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam amesema kua: ‘Naapa kwa jina la Allah

Subhanah wa Taála, ambae ndie alienituma mimi kua ni Mtume wa kweli, kua bila

ya shaka Isa Ibn Maryam atakuta katika Umma wangu watu ambao watachukua

nafasi ya Wanafunzi wake hapo atakaporudi katika kipindi cha mwisho wa Dunia’

(Al-Tirmidhi, Nawadir al-Usul fi Ma'rifat Ahadith al-Rasul)

Ambapo anasema Imam Sa’id Nursi Bediuzzaman kua: ‘Kushuka kwa Isa Ibn Maryam

na kujulikana kua yeye ndie Masih Isa Ibn Maryam kutajulikana kwa kupitia njia

ya kua na Nuru ya Imani, kwani si kila mtu atakua ni mwenye kujua kuhusiana

nae’

‘Na atakapokuja atakua ni mwenye kusali nyuma ya Imam Mahdi na kumfuata

kwake kunadhihirisha Umoja wa Mamlaka ya Qur’an na kua ni yenye kufuatwa.’

Kama inavyothibitishwa na aya ifuatayo:

‏﴿وَعَدَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ مِنْكُمْ‏ وَعَمِلُواْ‏ ٱلص َّ الحَِاتِ‏ لَيَسْتَخْلِفَن َّهُمْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ كَمَ‏ ا

ٱسْتَخْلَفَ‏ ٱل َّذِينَ‏ مِن قَبْلِهِمْ‏ وَلَيُمَكِّنَن َّ لهَُمْ‏ دِينَهُمُ‏ ٱل َّذِى ٰ ٱرْتَضَى لهَُمْ‏ ن وَلَيُبَدِّ‏ لَ‏ َّ هُْم


535

مِّن بَعْدِ‏ خَوْفِهِمْ‏ أَمْناً‏ يَعْبُدُونَنىِ‏ لاَ‏ يُشْرِكُونَ‏ بىِ‏ شَيْئاً‏ وَمَن كَفَرَ‏ بَعْدَ‏ ذٰلِ‏ كَ‏ فَأُوْلَٰئِكَ‏

هُمُ‏ ٱلْفَاسِ‏ قُون﴾‏

WaAAada Allahu alladheena amanoo minkum waAAamiloo alssalihati

layastakhlifannahum fee al-ardhi kama istakhlafa alladheena min qablihim

walayumakkinanna lahum deenahumu alladhee irtada lahum

walayubaddilannahum min baAAdi khawfihim amnan yaAAbudoonanee la

yushrikoona bee shay-an waman kafara baAAda dhalika faola-ika humu

alfasiqoona (Surat Nur 24:55)

Tafsir: Na anawaahidi Allah wale ambao Walioamini miongoni mwenu na wakafanya

Mema kua watakua ni Makhalifa wa Ardhini kama vile ambavyo alivyowafanya

waliotangulia kua ni Makhalifa na atawathibitishia kwa ajili yao Dini yao ambayo

ameiridhia na kuwapa wao baada ya khofu na Usalama wao: (kwa kuwaambia)

‘Niabuduni mimi msinishirikishe na yeyote’ Hivyo Mtu yeyote atakae kufuru baada ya

hapo basi atakua ni miongoni mwa Wapotovu.

Hivyo kuja kwa Mahdi na kurudi kwa Isa Ibn Maryam hua ni Rehma ya Allah Subhanah

wa Ta’ala kwa Waja wake wanaomtii na pia utimizwaji wa Ahadi yake kama

zinavyosema aya:

‏﴿وَمَن يَتَوَل َّ ٱهلل ََّ‏ وَرَسُولَهُ‏ وَٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ فَإِن َّ حِ‏ زْبَ‏ ٱهلل َِّ‏ هُمُ‏ ٱلْغَالِبُونَ‏ ﴾

Waman yatawalla Allaha warasoolahu waalladheena amanoo fa-inna hizba Allahi

humu alghaliboona(Surat Al Maidah 5:56)

Tafsir: Ama wale wanaotaka urafiki kwa Allah na Mtume wake na Walioamini, basi

kwa hakika ni Kikundi cha Allah ndio chenye kua na ushindi.

Ambapo pia tukio hili la kurudi kwa Nabii Isa Ibn Maryam na kushirikiana na Mahdi

kupigana na Dajjal litakua ni lenye kuenda sambamba na tukio la kufurika kwa Yajuj wa

Majuj ambao nao wataangamizwa kutokana na Dua ya Nabii Isa Alayhi Salam na hivyo

kuthibitisha ubainisho wa miongoni mwa dalili kubwa za mwisho za mwisho za Dunia,

kama anavyosema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an:


536

‏﴿حَتى َّ ٰ إِذَا فُتِحَتْ‏ ‏َْجُوجُ‏ وَمَأْجُوجُ‏ وَهُمْ‏ مِّن ِ كُل حَدَبٍ‏ يَنسِ‏ لُونَ۞وَ‏ ٱقْتَرَبَ‏

ٱلْوَعْدُ‏ ٱلحَْق ُّ فَإِذَا هِىَ‏ شَاخِ‏ صَةٌ‏ أَبْصَارُ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ يٰوَيْلَنَا قَدْ‏ كُ‏ ن َّا فىِ‏ غَفْ‏ لَةٍ‏ مِّ‏ ‏ْن

ّ

هَٰذَا بَلْ‏ كُن َّا ظَالِمِينَ‏ ﴾

Hatta idha futihat ya/jooju wama/jooju wahum min kulli hadabin yansiloona;

Waiqtaraba alwaAAdu alhaqqu fa-idha hiya shakhisatun absaru alladheena

kafaroo ya waylana qad kunna fee ghaflatin min hadha bal kunna dhalimeena(Surat

Al Anbiyah 21:96-97)

Tafsir: Hadi watakapofunguliwa Yajuj na Majuj, na kisha watatoka katika kila

sehemu kwa kasi. Na itakaribia Ahadi ya kweli na kisha utayaona Mtizamo wa Macko

ya wasioamini yakiwatoka na kusea: ‘Ole wetu hakika sisi tulikua tumeghafilika juu

ya hili na tumekua miongoni mwa Waliojidhulumu’

Katika kuelezea kwake tukio hilo basi aya zinasema kua hadi watakapofunguliwa Yajuj

na Majuj ‘min kulli hadabin yansiloona’ na neno Hadabin limetokana na neno Hadiba

ambalo hua linamanisha Mtuno, Mvimbo, Muinuko au Kilima.

Na hivyo maneno Min Kulli Hadabin hua yanamaanisha Kutoka katika kila Jamii, na

Sehemu na kutoka katika kila upande wa Dunia, na neno Yansiloona linatokana na neno

Nasala ambalo hua linamaanisha Kizazi, Kuzaliwa, Kutoka kwa wingi na kwa haraka

sana, na hivyo basi aya kua ni zenye kutubainishia kua tukio hili litakua ni la kutisha sana

kwa namna watakavyopotokea viumbe hawa ambao ni Yajuj wa Majuj, kiasi ya kua

itakua hakuna kwa kukimbilia kwa namna watakavyotoka kwa kasi kubwa sana na kwa

wingi sana.

Kwani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliwaambia Masahab zake kwa kusema:

‘Allah Subhanah wa Ta’ala atasema katika siku ya Malipo: ‘Adam’ na Nabii Adam

ataitikia: ‘Naam Ewe Mola wangu, hakika mimi niko chini ya Amri yako’ Hivyo

aitasema: ‘Waleteni watu wa Motoni.’ Nabii Adam atauliza: ‘Ndio wapi hao?’ Allah

Subhanah wa Ta’ala atasema: ‘Katika kila watu 1000 basi wao ni watu 999’ na

baada ya maneno hayo basi utawaona vijana wanakua wazee, waja wazito

wanajifungua, na utawaona watu kua kama wameleewa lakini hawakulewa bali

Adhabu ya Allah ni kali sana.’

Masahaba wakamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kusema: ‘Hivi jee

ni nani miongoni mwetu atakua ni mmoja kati yao kama ikiwa kila katika 1000 basi

999 watachukuliwa?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema:


537

‘Nakubashirieni kua kwa kila mmoja miongoni mwenu basi Yajuj wa Majuj ni

1000’(Sahih Bukhari)

Hivyo hii ni hadith ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam inayotuonesha namna

wingi wake Yajuj wa Majuj kulingana na wingi wake watakavyokua, hivyo bila ya shaka

itakua hamkani kubwa sana, ambapo kwa upande mwengine basi kuna hadithi ya An

Nawwas Ibn Sa’am Radhi Allahu Anhu ambae yeye anatuelezea hali itakavyokua katika

wakati huo kwa kusema kwa kutumia manano yafuatayo:

‘Asubuhi moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimzungumzia Dajjal, na

wakati tulipokua tukizungumzia kuhusiana na uovu na ubaya wake, basi Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kuhusiana na baadhi ya mambo ambayo

yanaonesha kua Kuja kwake itakua ni Mtihani mkubwa sana, Kisa chake kilitujaza

khofu kama kwamba Dajjal alikua amejificha Nyuma ya mashina ya Mitende na

wakati wowote atachomoza. ’

‘Tulipowasili mbele yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika wakati wa

Jioni basi akaona hali yetutuliyokua nayo na akatuuliza: ‘Vipi mbona mko hivyo?’

nasi tukasema: ‘Hakika wewe ulimzungumzia asubuhi, ambapo kuna baadhi ya

mambo uliyasema yalikua hayana athari kubwa katika uhatari wake, na kuna

mambo ambayo uliyasema ambayo yametuonesha sisi kua ni yenye kua katika hali

ya kua ni mtihani mkubwa sana kiasi ya kua tumekua na khofu sana na kufikiria

kua huenda ikawa Dajjal yuko karibu sana yetu yaani kama kwenye mashina ya

Mitende’’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Mtihani sio wa Dajjal tu, bali kuna

na mtihani myengine ambayo mimi nnaikhofia kua itakudhuruni zaidi kama

(Dajjal) akikutokeeni miongoni mwenu basi mimi nitakabaliana nae, na kama

akitokea na wakati mimi nikiwa siko miongoni mwenu basi kila mmoja wenu

atapingana nae kwa kadiri ya Ushujaa wake, na Allah Subhanah wa Ta’ala ni mlinzi

na Muongozaji wa Kila Muislam pale mimi nitakapokua sipo’

‘Nyinyi mtamjua (Dajjal) kutokana na kua ni mwenye kua ni kijana mwenye nywele

ngumu zenye kujipinda na mwenye Jicho moja lililoelekea Juu. Na kama ikibidi

nimfananishe na mtu basi namfananisha na Ab Al Uzza Ibn Qatan (Mmoja kati ya

watu wenye sura mbaya wa Kabila la Banu Khuza katika wakati wa Ujahiliya)’

‘Hivyo kama Muislam miongoni mwenu atakumbana nae basi anatakiwa asome aya

za mwanzoni za Surat Al Kahf dhidi yake. Dajjal atatokea katika maeneo yaliyokua

wazi ya Syria na Iraq na kusababisha tafrani kulia na kushoto: ‘Hivyo enyi waja

wa Allah kueni na msimamo dhidi yake.’


538

An Nawwas Ibn Sa’am Radhi Allahu Anhu anasema : ‘Nasi tukasema: ‘Ya Rasul Allah

hivi jee atatembea na kuyafanya hayo atakayoyafanya kwa siku ngapi Ardhini’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kwa siku 40, lakini siku moja

itakua ni sawa na Mwaka mmoja na siku ya pili sawa na mwezi mmoja, na siku

zitakazobakia itakua ni sawa na kama siku za kawaida’

An Nawwas Ibn Sa’am Radhi Allahu Anhu anasema : ‘Nasi tukasema: ‘Ya Rasul Allah,

hivyo hii siku moja ambayo itakua ni sawa na mwaka mmoja sisi tutasali sala 5 kwa

ajili ya siku moja tu?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘La bali

mtakua ni wenye kusali kwa kukadiria wakati wa sala tano kwa mwaka huo mmoja’

An Nawwas Ibn Sa’am Radhi Allahu Anhu anasema : ‘Nasi tukasema: ‘Ya Rasul Allah

Jee atakua ni mwenye kutembea Ardhini kwa kasi gani?’ Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akasema: ‘Kwa kasi ya kama Kiwingu kinavyosukumwa na Upepo

na atakutana na watu atakaowaambia wamfuate katika Imani yake potofu, nao

watamuamini na kuitikia wito wake, na kisha atayakusanya Mawingu na itanyesha

Mvua, ataiamrisha Ardhi na itaota majani na watalishia Wanyama juu yake, na

watakaporudi malishoni basi Nundu zao zitakua kubwa zaidi ya hapo kabla na

Maziwa yao yatajaaa na Mapaja yatanona’

‘Na kisha Dajjal atapita kwa watu wengine na kuwaita katika Kufuru yake, lakini

watu hao wataukataa wito wake, na hivyo atavunjika moyo na kuondoka, ambapo

baada ya kuondoka kwake basi Watu hao walioamini watapatwa na Mtihani wa

njaa na hawatokua na kitu. Halafu Dajjal atapita katika sehemu hio iliyo kame na

ataiambia Ardhi hio: ‘Toa nje Hazina zako’ na Ardhi hio itatoa Hazina zake kama

Nyuki wanavyomfuata Malikia wao, na kisha Dajjal atamwita mmoja kati wa watu

ambae ni kijana na kisha atamkata kwa upanga wake katika sehemu mbili na

sehemu mbili hizo zitatengenganishwa na kuwekwa katika masafa ya kama Mtunga

shabaha na Upinde wake na sehemu ya kutungia shabaha, na kisha Dajjal atamwita

Mtu huyo na vipande vyake vitaungana na Mtu huyo atakuja mbele yake huku

akiwa na tabasam na furaha’

Katika kipindi hiki Allah Subhanah wa Ta’ala atamtuma Isa Ibn Maryam, ambae

atang’arisha Mnara mweupe wa Mashariki ya Damascus akiwa amevaa maguo

mawili ya Rangi na mikono yake yote miwili kua ni yenye kukaa juu ya Mbawa za

Malaika wawili, na atakapoinama itakua kama anatiririka maji (kwenye nywele

zake) na atakaponyanyuka itakua matone yake yanang’ara kama Lulu halisi.

Mtu yeyote asieamini Allah akivuta pumzi atakayoitoa basi atakufa katika wakati

huo huo na pumzi zake akitoa zitafikia umbali wa upeo wa macho yake. Na kisha

atamtafuta (Dajjal) hadi atamtokezea kwa mbele yake katika Mlango wa Ludd (Wa

Bayt ul Maqdis) na kumua. Baada ya hapo Isa Ibn Maryam atakuja kwa watu


539

ambao Allah Subhanah wa Ta’ala amewalinda dhidi ya Dajjal. Atawagusa nyuso

zao na kuwabashiria bashirio jema la kua na darja za juu Peponi.

Wakati Isa Ibn Maryam atakapokua katika hali hio Allah Subhanah wa Ta’ala

atamshushia Wahyi na kumwambia: ‘Hakika mimi natuma watu ambao ni

miongoni mwa waja wangu ambao hakuna mikono miwili itakayoweza kupigana

nao, hivyo wakusanye waja wangu katika Mlima Tur’ hivyo Isa Ibn Maryam atatii

amri hio. ‘Na kisha nitawaachia Yajuj wa Majuj na wataporomoka kutoka katika

kila pande, ambapo wimbi lao la kwanza litapita Buhairah Tabariyyah (Bahari ya

Galileo au Tiberias yenye upana wa kilomita 53 na urefu wa kilomita 21 na kina

cha maji wa mita 42), ambapo litakunywa kila kitu ndani yake. Na kundi la pili

litakapopita hapo na kuona kua hakuna kitu litasema: ‘Hakika hapa kulikua kuna

Maji’

Watakapofika kwenye Mlima Khamar katika maeneo ya Bayt ul Maqdis basi Yajuj

wa Majuj watasema: ‘Tumeshaua kila mtu kwenye ardhi hivyo sasa hivi tuwaue

wale waliopo Mbinguni’ na kisha watarusha Mishale yao Mbinguni na Allah

Subhanah wa Ta’ala atairudisha mipinde hio ikiwa na Damu.

Rasul Allah Isa Ibn Maryam na watu wake watajihifadhi kwenye Mlima Tur, na

Waumini wengine watapata hifadhi katika maeneo yao yaliyohifadhika, watakua

na vyakula lakini haitochukua mda vitamalizika na kufikia hali kua kichwa cha

ng’ombe kitakua ni bora kuliko Dinari 100 za Dhahabu. Kisha Rasul Allah Isa Ibn

Maryam na Masahaba zake watamgeukia Allah (Na kumuomba Dua awasitiri

kutokana na Yajuj wa Majuj) na atatuma maradhi ya kuwaambukiza Yajuj wa

Majuj (na hivyo kua ni wenye Kuliwa na funza kwenye Shingo zao) na

wataangamizwa hadi mtu wa mwisho Miongoni mwao.

Rasul Allah Isa Ibn Maryam na Masahaba zake watatoka kwenye Mlia wa Tur na

kushuka chini na kukuta hakuna sehemu ya ardhi isipokua ina Maiti ya Yajuj wa

Majuj na kutakua kuna harufu mbaya sana. Rasul Allah Isa Ibn Maryam na

Masahaba zake watamgeukia Allah Subhanah wa Ta’ala (Kumuomba dua

awaondolee Mtihani wa maiti hizo nae atawajibu) na atawajibu kwa kuwatuma

ndege ambao shingo zao ukubwa wake kama shingo za Ngamia na kuchukua Maiti

hizo na kuzirembea anakotaka Allah Subhanah wa Ta’ala.

Baada ya hapo Allah Subhanah wa Ta’ala atashusha Mvua ambayo hakuna hata

Nyumba ya Udongo wala hema la Bedui, itakayakosa kunyesewa na mvua hio. Na

aradhi itakoshwa na kua Nyeupe kama kioo na kisha Allah Subhanah wa Ta’ala

ataiambia Ardhi: ‘Otesha Mimea yako na Matunda yako toa wingi wa vilivyomo

katika rehma yako’


540

Na kutakua na baraka sana kiasi ya kua Komamanga moja litatosheleza kua ni

chakula cha watu kadhaa, na gamba lake litatosheleza kua ni paa la kujilinda dhidi

ya Jua na Maziwa yatatosheleza kwa kila mtu kwani Maziwa kutoka kwa Ngombe

mmoja yatatosheleza Kabila zima na maziwa ya Mbuzi mmoja yatatosheleza kwa

Ukoo mzima (Miaka 40 baada ya kipindi cha neema hizi na usalama na Amani basi

ndio wakati wa Kiama utakaribia).

Allah Subhanah wa Ta’ala atatuma Upepo mzuri sana ambao utasababisha

kuifanya miili ya Waumini kua yenye kufa ganzi na kisha kila Roho ya Muumini

itatolewa. Na watabakia wabaya watupu miongoni mwa Ibn Adam, waovu na

wasioamini ambao watafanya mambo ya aibu na yasiyofaa ardhini kama Punda, na

ni dhidi yao ndio Saa ya Kiama itawafikia.(Imam Muslim)

Ama kuhusiana na Yajuj ya Majuj basi Allah Subhanah wa Ta’ala amewaelezea katika

kisa cha Dhul Qarnayn pale aliposema katika Qur’an:

‏﴿وَيَسْأَلُونَكَ‏ عَن ذِى ٱلْقَرْنَينْ‏ ِ قُلْ‏ سَأَتْلُواْ‏ عَلَيْكُم مِّ‏ نْهُ‏ ذِكْ‏ راً۞إِ‏ ‏ َّ مَ‏ ك َّن َّا لَهُ‏ فىِ‏ ٱلأَرْ‏ ضِ‏

وَآتَيْنَاهُ‏ مِن ِ كُل فَأَتْبَعَ‏ سَبَباً۞حَتى َّ ٰ شَيْءٍ‏ سَبَباً۞‏ إِذَا بَلَغَ‏ مَغْ‏ ‏ِربَ‏ ٱلش َّمْسِ‏ وَجَدَهَا

تَغْرُبُ‏ فىِ‏ عَينٍْ‏ حمَِئَةٍ‏ وَوَجَدَ‏ عِندَهَا قَوْماً‏ قُلْنَا يٰذَا ٱلْقَرْنَينِْ‏ إِم َّآ أَن تُعَذِّبَ‏ وَإِم َّآ أَن

ت َت َّ خِ‏ ذَفِي هِمْحُْسن اً‏ ‏۞قَالَ‏ أَم َّا مَن ظَلَمَ‏ فَسَوْفَ‏ نُعَذِّبُهُ‏ ثمُ َّ يُرَد ُّ إِلىَٰ‏ رَبِّهِ‏ فَيُعَذِّبُهُ‏ عَذَاابً‏

ن ُّكْ‏ راً۞وَأَم َّا مَنْ‏ آمَنَ‏ وَعَمِلَ‏ صَالحِ‏ اً‏ فَلَهُ‏ جَزَآءً‏ ٱلحُْسْنىَٰ‏ وَسَنَقُوُل

لَهُ‏ مِ‏ نْ‏ أَمْ‏ رَِ‏ يُسْ‏ راً۞ثمُ َّ

أَتْبَعَ‏ سَبَباً۞حَتى َّ ٰ إِذَا بَلَغَ‏ مَطْلِعَ‏ ٱلش َّمْسِ‏ وَجَدَهَا تَطْلُعُ‏ عَلَى ٰ قَوْمٍ‏ لم َّْ‏ نجَْعَل له َُّمْ‏ مِّن

دُوَِا سِ‏ ترْ‏ اً۞كَذٰ‏ لِكَ‏ وَقَدْ‏ أَحَطْنَا بمَِا لَدَيْهِ‏ خُبرْ‏ اً‏ ﴾

ّ

Wayas-aloonaka AAan dhee alqarnayni qul saatloo AAalaykum minhu dhikran ;

Inna makkanna lahu fee al-ardhi waataynahu min kulli shay-in sababan;

FaatbaAAa sababan; Hatta idha balagha maghriba alshshamsi wajadaha taghrubu

fee AAaynin hami-atin wawajada AAindaha qawman qulna ya dha alqarnayni

imma an tuAAadhdhiba wa-imma an tattakhidha feehim husnan; Qala amma man

dhalama fasawfa nuAAadhdhibuhu thumma yuraddu ila rabbihi

fayuAAadhdhibuhu AAadhaban nukran; Waamma man amana waAAamila

salihan falahu jazaan alhusna wasanaqoolu lahu min amrina yusran; Thumma


541

atbaAAa sababan; Hatta idha balagha matliAAa alshshamsi wajadaha tatluAAu

AAala qawmin lam najAAal lahum min dooniha sitran; Kadhalika waqad ahatna

bima ladayhi khubran (Surat al-Kahf 18:83-91)

Tafsir: Na wanakuuliza kuhusiana na Dhul Qarnayn waambie: ‘Nitakuambieni kitu

kutokana na ukumbusho juu yake’ Kwa hakika tumemueweka kwenye Ardhi na

tukampa njia (sababu) juu ya kila kitu; Hivyo akafuata Njia; hadi akafikia

(Magharibi) linakotua Jua akalikuta linatua kwenye chemchem ya maji ya tope

nyeusi, na akakutana karibu nayo watu Nasi tukasema: ‘Ewe Dhul Qarnayn Aidha

waadhibu au wafanyie wema’. Hae akasema: ‘Ama yule atakaefanya Dhulma basi

tutamuadhibu yake kisha atarudishwa kwa Mola wake ambae atamuadhibu kwa

adhabu kali zaidi; Na ama yule atakaeamini na Akafanya Amali njema basi atapata

malipo mema, na sisi tutazaungumza nae juua ya jambo letu (la Uongofu) kwa urahisi’

Na kisha akafuata Njia nyengine. Hadi akafikia katika sehemu inayochomoza Jua,

akalikuta linachomoza kwa watu ambao hatukuwajaalia chochote cha kujistiri

kutokana nalo; na kadhalika kwa hakika sisi ni wenye kujua kila kitu kuhusiana nae

(Dhul Qarnayn).

Ambapo amesema Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Dhul

Qarnayn alikua ni Nabii ambae Mshauri wake alikua ni Al Khidr ambae nae alikua

pia ni miongoni mwa Wanajeshi wa Dhul Qarnayn’

Na Imam Al Azraq basi yeye anasema kua: ‘Dhul Qarnayn aliingia katika Uislam

katika kipindi cha Nabii Ibrahim na aliwahi kufanya Tawwaf na Nabii Ibrahim na

Nabii Ismail na Nabii Ibrahim alimuombea Dua na Allah Subhanah wa Ta’ala

aliyasababisha Mawingu kua chini ya amri yake na hivyo alikua akienda nayo

atakako’

Na aliitwa Dhu Qarnayn kwa sababu alikua ni mwenye kutawala Ardhini kwa Karne

Mbili, na kuna wanaosema kua ni kwa sababu alitembelea na kutawala Pande zote mbili

za Dunia kuanzia Mashariki hadi Magharibi.

Ambapo Mujaddid ad Din, Shaykh ul Islami Al Hafidh Imam Shihab Ad Din Ibn Hajjar

Al Asqalani anasema kua Dhul Qarnayn alikua akiitwa Abdulla Ibn Dahhaq Ibn Mad, na

kuna wanaosema kua ni Mussab Ibn Abdulla Ibn Qattan, na kuna wasema kua ni

Mazuban Bin Marzaba na kuna wasemao kua ni Saib Ibn Maraid na pia kuna wasemao

kua ni Harmasa na Hardia.

Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kutuelezea kuhusiana na Dhul Qarnayn na ukuta

alioujenga kwa ajili ya kuwazuia na kuwadhibiti Yajuj wa Majuj kwa kusema:


542

‏﴿ثمُ َّ أَتْبَعَ‏ سَ‏ بَباً۞حَتى َّ ٰ إِذَا بَلَغَ‏ بَينَْ‏ الس َّد َّيْنِ‏ وَجَدَ‏ مِن دُوِِمَا قَ‏ وْماً‏ لا َّ يَكَادُونَ‏

يَفْقَهُونَ‏ قَوْلاً۞قَالُواْ‏ يٰذَا ٱلْقَرْنَينِْ‏ إِن َّ ‏َْجُوجَ‏ وَمَأْجُوجَ‏ مُفْسِ‏ دُونَ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَهَ‏ ‏ْل

نجَْعَلُ‏ لَكَ‏ خَرْجاً‏ عَلَى ٰ أَن تجَْعَلَ‏ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ‏ سَدّاً۞قَالَ‏ مَا مَ‏ َّكنىِّ‏

فِيهِ‏ رَبىِّ‏ خَيٌْر

فَأَعِينُونىِ‏ بِقُو َّةٍ‏ أَجْعَلْ‏ بَيْنَكُمْ‏ وَبَيْنَهُمْ‏ رَدْماً۞آتُونىِ‏ زُبَرَ‏ ٱلحَْ‏ ‏ِديدِ‏ حَتى َّ ٰ إِذَا سَاوَىٰ‏ بَينَْ‏

ٱلص َّدَفَينِْ‏ قَالَ‏ ٱنفُخُواْ‏ حَتى َّ ٰ إِذَا جَعَلَهُ‏ ‏َراً‏ قَالَ‏ آتُونيِ‏ ۤ أُفْرِغْ‏ عَلَيْهِ‏ قِطْراً۞فَمَا ٱسْطَاعُو ۤ اْ‏

أَن يَظْهَرُوهُ‏ وَمَا ٱسْتَطَاعُواْ‏ لَهُ‏ نَقْباً۞قَالَ‏ هَٰذَا رَحمَْةٌ‏ مِّن ر َّبىِّ‏ فَإِذَا جَآءَ‏ ‏َوعْدُ‏ رَبىِّ‏

جَعَلَهُ‏ دَك َّآءَ‏ وَكَانَ‏ وَعْدُ‏ رَبىِّ‏ حَقّاً۞وَتَرَكْنَا بَعْضَهُمْ‏ يَوْمَئِذٍ‏ يمَُوجُ‏ ‏ِفى

بَعْضٍ‏ وَنُفِخَ‏ ‏ِفى

ٱلص ُّورِ‏ فَجَمَعْنَاهُ‏ مْ‏ جمَْعاً‏ ﴾

Thumma atbaAAa sababan; Hatta idha balagha bayna alssaddayni wajada min

doonihima qawman la yakadoona yafqahoona qawlan; Qaloo ya dha alqarnayni

inna ya/jooja wama/jooja mufsidoona fee al-ardhi fahal najAAalu laka kharjan

AAala an tajAAala baynana wabaynahum saddan; Qala ma makkannee feehi

rabbee khayrun faaAAeenoonee biquwwatin ajAAal baynakum wabaynahum

radman; Atoonee zubara alhadeedi hatta idha sawa bayna alsadafayni qala

onfukhoo hatta idha jaAAalahu naran qala atoonee ofrigh AAalayhi qitran; Fama

istaAAoo an yadhharoohu wama istataAAoo lahu naqban; Qala hadha rahmatun

min rabbee fa-idha jaa waAAdu rabbee jaAAalahu dakkaa wakana waAAdu

rabbee haqqan; Watarakna baAAdahum yawma-idhin yamooju fee baAAdin

wanufikha fee alssoori fajamaAAnahum jamAAan (Surah al-Kahf 18:92-99)

Tafsir: Na kisha akafuata njia hadi akafika baina ya Milima miwili na akakuta kabla

yao(Milima hio)Kaumu ya watu ambao hawafaham Kauli, na wakasema: ‘Ewe Dhul

Qarnayn! Hakika Yajun na Majuj wanafanya ufisadi kwenye Ardhi, hivyo jee tukupe

ujira ili utujengee Ukuta baina yetu na baina yao?’; Akasema (Dhul Qarnayn):

‘Alichoniwekea (katika kunipa Mali, Mamlaka na Uwezo wa kinguvu) Mola wangu ni

bora; Hivyo nisaidieni uwezo wa wasaidizi, nami nijataalia baina yenu na baina yao

Kizuizi; Nipeni Vipande vya Vyuma’ na kisha alipoujaza Uwazi baina ya Kingo za

Milima miwili akasema: ‘Pulizeni’ hadi akaifanya ikawa (nyekundu) kama Moto kisha

akasema: ‘Nileteeni Shaba iliyoyeyuka kuimiminia juu yake’ hivyo Yajuj na Majuj

wakawa hawana uwezo wa kuivunja au kuitoboa; Duhl Qarnayn akasema: ‘Hii ni


543

Rehma kutoka kwa Mola wangu, Lakini itakapowadi Ahadi ya Mola wangu, basi

atauangusha chini, na ahadi ya Mola wangu ni ya kweli’ katika siku hio

(watakapotoka nje Yajuj wa Majuj), basi tutawaachia kuvamia kama mawimbi moja

baada ya jengine, na kisha Baragumu litapulizwa na tutawakusanya wote kwa pamoja.

Ambapo amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kwa hakika Yajuj wa

Majuj wanachimba kwenye Ukuta kila siku, hadi plae wanapoona kua Mwangaza

wa Jua unapita baina yake, na kisha Kiongozi wao hua ni mwenye kusema:

‘Twendeni zetuni, mtakuja kesho kumalizia’ na wakifika katika siku ya pili yake

basi huukuta Ukuta huo kua uko imara kuliko jana yake, hadi pale itakapofikia

ahadi ya Allah atakapotaka kuwaachia wawavamie Ibn Adam, basi kiongozi wao

atasema: ‘Twendeni zetuni, In-Shaa Allah mtakuja kesho kumalizia’ na hivyo

wakifika kesho yake wataukuta ukuta uko katika hali kama walivyouacha hapo

jana yake, na watachimba na kutoka ndani yake na kuwavamia Ibn Adam.

Watakunywa Maji yote watakayokutana nayo, na Ibn Adam watakimbilia kwenye

ngome zao, na Yajuj wa Majuj watarusha Mipinde yao Juu angani na itakaporudi

itarudi huku ikiwa ina wekundu kama wa Damu nao watasema: ‘Tumewashinda

watu wa Ardhini na wa Mbinguni pia’ kisha hapo Allah atatuma Mafunza kwenye

shingo zao ambao wataua wote.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Wallahi naapa kwa yule ambae

Roho ya Muhammad iko mikononi mwake, kua Viumbe hai wa Ardhini (wadudu

na wanyama wa ardhini) watanenepa kutokana na kula nyama na kunywa damu

zao’(Musnad Imam Ahmad)

Ambapo anasema Shaykh ul Akbar Imam Ibn Arabi kuhusiana na maneno ya Hadith hii

kua: ‘Hadithi hii ina Miujiza mitatu kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala ambayo

ni:

1-Allah Subhanah wa Ta’ala hakuwajaalia Yajuj wa Majuj uwezo wa kujua katika

ufahamu wao kua ni wenye kua na uwezo wa kuchimba kwenye ukuta huo kwa

masaa 24 bila ya kusita usiku na mchana, kwani kama wangejaaliwa hivyo basi basi

isingewachukua mda mrefu kutokana na nguvu na wingi wao kuumaliza Ukuta

huo.

2-Akili zao na Ufahamu wao umeghafilishwa na kutokua na haja ya kuuparamia

juu Ukuta huo, kwa kutumia vifaa na zana mbali mbali. Ingawa kulingana na

mtizamo wa Wahb Ibn Munabih ni kua watu hawa wanalima kwenye ardhi yao na

hivyo kumaanisha kua wanazo zana tofauti. Hivyo pia kama hawakughafilishwa

basi ingekua ni rahisi sana kwao wao kukusanya zana zao na kutafuta njia ya

namna ya kuuparamia ukuta huo na kutoka ndani yake.


544

3-Allah Subhanah wa Ta’ala hakuwajaaliwa kua ni wenye kujua kua wenye

kutakiwa kusema In-shaa Allah, kwani kauli hii itawajia katika ufahamu wao pale

utakapofika wakati walioandikiwa kua waseme hivyo kwa ajili ya kutimiza jambo

linalotakiwa kutokea.

Kwani amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

﴿ وَعْدَ‏ ٱهلل َِّ‏ لاَ‏ يخُْلِفُ‏ ٱهلل َُّ‏ وَعْدَهُ‏ وَلَٰكِن َّ أَكْثَرَ‏ ٱلن َّاسِ‏ لاَ‏ يَعْلَمُونَ‏ ﴾

WaAAda Allahi la yukhlifu Allahu waAAdahu walakinna akthara alnnasi la

yaAAlamoona (Surat Rum 30:6)

Tafsir: Hio ni Ahadi ya Allah, na havunji Allah Ahadi yake lakini wengi Miongoni

mwa watu si wenye Kujua.

KAULI ZA ISA IBN MARYAM A’LAYHI SALATU WA WASALAM KATIKA AL

RISALAT AL QUDSIYYAH.

Mujaddid ud Din Hujjat ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii alipokua akiishi katika msikiti wa Bayt ul

Maqdis katika Bab al Dhahab katika kipindi ambacho kilikua ni cha kutafuta ukaribu

zaid na Mola wake Allah Subhanah wa Taála basi alifanikiwa kuzipata na kuziandika

hadith za Nabii Isa Ibn Maryam A’layhi Salaam, katika kitabu chake kiitwacho Al Risalat

Al Qudsiyyah, miongoni mwa Hadith hizo ni pamoja na:

Allah Subhanah wa Taála alimwambia Isa Ibn Maryam: ‘Ya Isa Ibn Maryam baada

yako mimi nitatuma Ummah ambao hautokua na Huruma wala I’lm. Hivyo kuna

mambo watakayoyapenda na yatakapowafika basi watanitukuza na kunishukuru,

na kuna mambo watakayoyachukia na yatakapowafika, basi watakua na subra na

watanitegemea zaid mimi.’

Nabii Isa Ibn Maryam akauliza: ‘Itakuaje hali yao kua hivyo wakati watakua hawana

huruma wala I’lm?’

Allah Subhanah wa Taála akasema: ‘Hakika mimi nitawapa sehemu ya Huruma

zangu na Sehemu ya I’lm yangu.’


545

Allah Subhanah wa Taála akamwambia Nabii Isa Ibn Maryam: ‘Ya Isa Ibn Maryam!

Jiusie juu ya Hikma zangu, na ukinufaika nazo basi, basi wausie watu juu yangu na

vyenginevyo, basi jihadhari nami.

Allah Subhanah wa Taála alimshusia Nabii Isa Ibn Maryam katika maandiko asilia ya

Biblia kwa kumwambia kua: ‘Waambie Bani Israil kua, Mja yeyote yule atakaefunga

kwa ajili yangu basi nitamlipa mja huyo kwa kuufanya mwili wake uwe imara na

Akhera kumpa malipo bora zaidi’

Allah Subhanah wa Taála alimwambia Isa Ibn Maryam katika Biblia asilia kua: ‘Ya Bani

Adam nimekuumbeni na kukuleeni kimaisha nyinyi, lakini bado hua mnamuabudu

mwengine zaidi yangu, Enyi Waja wangu mimi nnakukaribisheni karibu lakini

nyinyi mnanikimbia. Mimi nna kukumbukeni lakini nyinyi mnanisahau, Hivi jee

Ya Ibn Adam mnarudi na kulala popote mnapotaka nyinyi?’

Allah Subhanah wa Taála alimwambia Isa Ibn Maryam katika Bibilia asilia kua: ‘Kila

mnavyokua na kupungua ufahamu wenu, basi mtalipwa na kuhesabiwa kila kitu

chenu.’

Imeandikwa katika Biblia asilia kua: ‘Usitafute I’lm ya kile usichokijua hadi pale

utakapokua ni mwenye kutekeleza kile unachokijua’

“Isa Ibn Maryam A’layhi Salaam aliwafufua kutokana na uwezo wa Allah Subhanah

wa Taála watu wanne ambao ni Al Adhir (Lazarus) ambae alikua ni Rafiki yake,

Mtoto wa kiume wa Mtu Mzima sana fulani, mtoto wa kike wa Mzee aitwae Al Ashir

na Sham ambae ni mtoto wa Nabii Nuh Alayhi Salaam.

Ama kuhusiana na Al Adhir basi alikua ni mwenye kufariki kwa muda mfupi kabla

ya Nabii Isa kumuomba Allah Subhanah wa Taála amfufue, na alipofufuliwa aliishi

akaoa na kupata watoto.

Ama kuhusiana na mtoto wa Mtu Mzima Mzee, basi Nabii Isa alikua akipita na

akamuona mtoto huyo akiwa ametiwa ndani ya Jeneza, Hivyo Isa Ibn Mayam

akamuomba Allah Subhanah wa Taála, amfufue na mtoto huyo wa kiume

alipofufuliwa basi akavaa nguo zake na kulibeba Jeneza lake na kurudi kwa watu

wake.

Ama kuhusiana na Bint wa Al Ashir, basi ulipita usiku mmoja tu tangu kufariki

kwake, hivyo Isa Ibn Maryam akamuomba Allah Subhanah wa Taála amfufue

ambapo alimfufua na akaolewa na kupata watoto.


546

Watu wa Bani Israil walioshuhudia Miujiza hii basi walimhoji Isa Ibn Maryam kwa

kumuambia kua : ‘Unawafufua waliokufa karibuni, hivyo inawezekana ikawa hawa

uliowafufua walikua hawajafa bali walikua ni wenye kuzimia tu, subiri tukuoneshe

kaburi la Sam mtoto wa Nuh utufufuie’

Isa Ibn Maryam akawaambia Bani Israil: ‘Nionesheni Kaburi lake’

Hapo watu wa Bani Israil wakamchukua hadi katika Kaburi la Sam Ibn Nuh. Isa Ibn

Maryam akaomba Dua na Allah Subhanah wa Taála akamfufua Sam Ibn Nuh huku

nywele zake zikiwa zimejaa mvi, hivyo Isa Ibn Maryam akamuuliza: ‘Imekuaje hadi

nywele zako zikawa ni zenye kujaa mvi, kwani katika kipindi chako ulichoishi

nywele za watu zilikua hazioti mvi?’

Sam Ibn Nuh akasema: ‘Ýa Ruhi Allah! Wakati uliponiita, nilisikisa sauti iliyokua

ikiniamrisha mimi kujibu ninayoulizwa na Ruh Allah na hivyo nikadhani kua Siku

ya Kiama imewasili, hivyo nikafufuka na nywele zenye mvi kutokana na khofu

niliyokua nayo’

Isa Ibn Maryam akamuuliza tena Sam Ibn Nuh: ‘Hebu niambie kuhusiana na maumivu

ya kutoka kwa Roho!’

Sam Ibn Nuh akajibu kwa kusema: ‘Ya Ruhi Allah! Kwa hakika uchungu wake bado

haujaondoka katika Roho yangu.’

Tafakkar! Kwani katika kipindi hicho alikua tayari ameshakaa kaburini kwa muda wa

miaka 4000. Kisha Sam Ibn Nuh akawageukia Bani Israil na kuwaambia: ‘Muaminini

kwani huyu ni kweli Mtume wa Allah’ lakini hata hivyo, baadhi wakamkubali Isa Ibn

Maryam na baadhi wakamkanusha na kusema kua huo ni uchawi.

Maryam bint Imran, alimchukua Isa Ibn Maryam akiwa mtoto na kumpelekea kwa wenye

ujuzi wa kazi za kutia na kutoa rangi nguo ili ajifunze kutoka kwao kazi hio. Baada ya

muda mwalimu wa Nabii Isa alifikwa na dharura na hivyo ikambidi asafiri lakini kabla

ya kusafiri, akamwambia Isa Ibn Maryam: ‘Mimi inanibidi nisafiri, na nina nguo

nyingi ambazo inabidi zitiwe rangi, hivyo itabidi unsaidie kuzutia rangi’.

Hivyo Nabii Isa Ibn Maryam akachemsha maji na kuzichanganya rangi zote pamoja na

kuzimimina ndani ya tangi na kuzichanganya nguo zote zilizokusudiwa kutiwa rangi

katika tangi moja na kusema: ‘Bismi Allahi Rahmani Rahim pakika Rangi’. Mara

mwalimu wake akaingia na kumkuta tayari ameshazichanganya nguo zote katika tangi

moja, wakati nguo inayotakiwa kua na rangi tofauti huingizwa katika tangi tofauti.


547

Hivyo baada ya kuona hali hio basi mwalimu huyo akasema: ‘Umeshaniharibia’. Lakini

hapo hapo Isa ibn Maryam akazitoa nguo hizo kutoka katika tangi hilo na kutoa kila nguo

ikiwa na rangi yake, kulingana na namna ilivyokususidwa, iliokusudiwa iwe kijani ikawa

kijani, nyekundu ikawa nyekundu na kadhalika. Hivyo Mwalimu wake huyo akashangaa

sana na akajua kua jambo hilo kamwe haliwezekani isipokua kutokana na uwezo wa

Allah Subhanah wa Ta’ala hivyo nae akawa ni miongoni mwa wenye kumuamini Isa Ibn

Maryam.

Siku moja Iblis alimfuata Nabii Isa kisirisiri kisha akasema: ‘La ilaha illa Allah’, ambapo

Nabii Isa Ibn Maryam akasema: ‘Ama kwa hakika hii ni kauli sahih lakini mimi

sitoitamka kwa ajili ya kukufuata wewe’

Alisema Isa Ibn Maryam: ‘Tuba (Bonde la Peponi) ni kwa ajili ya kila yule ambae

anajidhibiti kutokana na matamanio ya kidunia juu ya ahadi ambayo bado

haijatimia’ na akasema tena kua; ‘Tuba ni wa ajili wale wenye macho ambayo

hayalali na hayana nia ya kufanya dhambi na pale yanapoamka hua hayakusudii

kufanya dhambi’

Alisema Isa Ibn Maryam: ‘Enyi Wanafunzi wangu, yawekeni na njaa matumbo yenu

ili mmpate kumuona Mola wenu’

Alisema Isa Ibn Maryam: ‘Enyi Wanafunzi wangu, yawekeni matupu matumbo yenu

na miili yenu isipokua sehemu za siri zenu ili nyoyo zenu zimuone Mola wenu’

Maana ya kauli hii ni kua Ibn Adam tunatakiwa tufunge na kutosheka na mavazi

tuliyokua nayo bila ya kupenda fakhari ya kubadilisha kila mitindo ya mavazi inayoingia.

Isa Ibn Maryam alikaa kwa siku 40 huku akiwa anazungumza na Mola wake tu bila ya

kula kitu chochote, kisha likamjia wazo la mkate hapo akasita kuzungumza na Mola wake

na mkate ukatokea mbele yake. Isa Ibn Maryam akaanza kulia kutokana na kupoteza

utamu wa mazungumzo yake na Mola wake. Mara akaona kivuli cha mtu mzee kutoka

juu yake.

Isa Ibn Maryam akasema: ‘Allah akubariki ewe Walii wa Allah, Niombee kwa Allah

kwa ajili yangu kwani nilikua katika hali ya hiyo lakini mkate ukanijia katika

mawazo yangu na hali hio ikatoweka’. Yule Mzee akaomba dua kwa Allah Subhanah

wa Ta’ala akasema: ‘Ya Allah! Kama unajua kua mkate uliwahi kuingia katika

mawazo yangu tangu mimi kukujua wewe, basi usinisamehe. Kwa hakika mimi

nilikua nikila kile ambacho hukipata bila ya kukifikiria wala kukiwazia’


548

Isa Ibn Maryam alionya kwa kusema: ‘Tahadhari na kuangalia watu wa jinsia

nyengine kwani ni mbegu inayotosha kupandikiza matamanio ndani ya moyo, na

hutosheleza kua ni mtihani juu yako’

Isa Ibn Maryam aliulizwa: ‘Tuusie kuhusiana na jambo ambalo litatuingiza Peponi

kutokana na kulitekeleza kwake.’ Isa Ibn Maryam akajibu: ‘Kukaa kimya’, yule

alieuliza akasema: ‘Ama hio itakua haiwezekani’ Isa Ibn Maryam akajibu: ‘Basi

msizungumze chochote isipokua lililo Jema’

Isa Ibn Maryam alisema: ‘Mambo manne hayawezi kufikiwa bila ya uchovu, ambayo

ni mwanzo wa Ibada, Unyenyekevu, Kunyamaza kimya, Dhikr Allah kwa wingi

zaidi na kwa uchache’.

Isa Ibn Maryam hakua na mnyama wa kupanda wala nyumba ya kujihifadhia. Hakua ni

mwenye kuhifadhi kwa ajili ya kesho na popote pale unapomfikia usiku basi hulala hapo

hapo.

Isa Ibn Maryam alikaa na kujipumzisha chini ya kivuli cha ukuta fulani. Mwenye ukuta

akamwambia aondoke chini ya ukuta wake huo. Isa Ibn Maryam akanyanyuka na kisha

akamgeukia yule mwenye ukuta na kusema: ‘Sio wewe unaeniondoa, kwenye kivuli

hiki bali ni yule asiependa mimi nifurahie kivuli hiki ndio anaeniachia niondoke’

Alisema Isa Ibn Maryam: ‘Enyi Bani Israil, kunyweni maji safi, kuleni Mbaazi, na

Mkate wa Shayiri, lakini jihadharini juu ya Mikate ya Ngano kwa sababu kamwe

hamtoweza kurudisha shukrani zake kwa aliekupeni’

Akasema tena Isa Ibn Maryam: ‘Waangalie ndege, hawapandi Miti wala hawavuni

lakini wanahifadhi kwa sababu Allah Subhanah wa Taála anampatia riziki yake

kila siku, na ukisema kua sisi Ibn Adam tuna matumbo makubwa ukilinganisha na

Ndege, basi waangalie Ngómbe na utaona namna Allah Subhanah wa Taála

anavyomjaalia rizki yake.’

Katika safari zake Isa Ibn Maryam alipishana na watu watatu, ambao walikua

wamekonda hadi rangi yao imebadilika, hivyo akawasimamisha na kuwauliza: ‘Jee ni

kitu gani kilichokufanyeni muwe hivi.’

Wale watu wakajibu: ‘Khofu ya Jahannam’, hivyo Isa Ibn Maryam akasema: ‘Allah

Subhanah wa Taála amejithibtishia kuziondoa khofu zenu’. Kisha akaendelea na

safari yake, na njiani akakutana na watu watatu wengine ambao wamekonda zaidi ya

wale wa kwanza, akasimamisha na kuwauliza pia: ‘Jee ni kitu gani kilichokufanyeni

muwe hivi?’.


549

Ambapo wale watu wakajibu: ‘Matamanio ya kupata Pepo’. Hapo Isa Ibn Maryam

akasema: ‘Allah Subhanah wa Taála amejithibitishia kuwa atakupeni kile

mnachokitamani’. kisha akaendelea na safari yake na kukutana na watu watatu wengine

ambao wamekonda zaidi ya wale aliowapita, lakini nyuso zao zilikua ni zenye kungára

sana, hivyo akawasimamisha na kuwauliza pia: ‘Jee ni kitu gani kilichokufanyeni

muwe hivi?’. Wale watu wakasema: ‘Sisi tunampenda Allah Subhanah wa Taála’.

Hapo Isa Ibn Maryam akasema: ‘Nyinyi ni miongoni mwa waliokaribu nae.’

Isa Ibn Maryam aliamuona mtu ambae ni kipofu, bubu na amepooza nusu mwili katika

pande zote, na mwili wake umeshaanza kuoza kwa ukoma, lakini hata hivyo huyo mtu

anasema: ‘Alhamd lillah! Namshukuru Allah kwa kile ambacho ameniepusha mimi

na mitihani aliyowapa viumbe wake wengine’, Isa Ibn Maryam akamuuliza yule

mgonjwa: ‘Jee ni mitihani gani uliyoepushwa.’ Yule mzee akajibu: ‘Ya Ruhi Allah!

Allah amenijaalia mimi I’lm ya kumjua yeye ndani ya moyo wangu, hivyo niko

katika hali nzuri kuliko waliyokua nayo wengine’, hapo Isa Ibn Maryam akasema:

‘Uko Sahih, nipe mkono wako’, yule mtu akampa mkono wake Isa Ibn Maryam na pale

pale yakaonekana mabadiliko katika mwili wa yule mtu kwani alipona na kua na sura

nzuri kabisa na akawa ni Mwanafunzi wake.

Isa Ibn Maryam aliwauliza Wanafunzi wake: ‘Jee miti hua inaota wapi?’ Wanafunzi

wakajibu: ‘Ardhini’ hivyo Isa Ibn Maryam akasema: ‘Naam, hivyo kwa hakika Hikma

haiwezi kukua isipokua kwenye Moyo kama ilivyo Ardhi na miti’

Bani Israil walimuuliza Isa Ibn Maryam: ‘Ya Ruhi Allah, jee yupo mtu kama wewe leo

hii Duniani?’ Isa Ibn Maryam akajibu: ‘Naam, kwani yeyote yule anaefanya dhikr

Allah huku akiwa n mwenye kukaa kimya, na mtizamo wake ukawa ni wenye

Tafakkur, basi hua ni sawa nami’

Wakati kifo kilipokua kinatajwa mbele ya Isa Ibn Maryam, basi muonekano wake

hubadilika, hivyo aliwaambia Wanafunzi wake: ‘Enyi Wanafunzi wangu! Ombeni dua

kwa Allah ili airahisishe adhabu ya kifo juu yangu, kwa sababu mimi naogopa kifo

kiasi ya kua khofu yangu inataka kuniingiza kwenye kifo chenyewe’

Katika kutembea kwake Isa Ibn Maryam alilikuta fuvu la kichwa na taratibu akalisogeza

pembeni kwa mguu wake na kisha akasema: ‘Sema kutokana idhini ya Allah’, ambapo

fuvu hilo likasema: ‘Ya Ruhi Allah, ama mimi nilikua ni Mfalme wa jamii ya watu

fulani na katika wakati fulani, na wakati nikiwa katika Mamlaka ya Ufalme wangu

huku nikiwa na kofia ya Ufalme wangu na kuzungukwa na walinzi, askari na

wafanyakazi wangu, Ghafla Malaika wa Mauti akatokea juu ya kiti cha ufalme

wangu, na hapo kila kitu katika viungo vyangu vikaanza kupoteza uezo wake, na


550

Roho yangu ikanitoka na kufuatana na Malaika wa Mauti, kiasi ya kua nilitamani

kua watu wote hao walionizunguka wakati wote huo wangeondoka na kuniacha

mimi peke yangu.’

Alihoji Isa Ibn Maryam: ‘Jee ni Miili mingapi mizima, yenye nyuso za kupendeza na

ndimi zenye ufasaha wa lugha ya kuvutia zitakua ni zenye kupiga makelele baina

ya matabaka tofauti ya Moto?’

Aliulizwa Isa Ibn Maryam: ‘Ya Isa Ibn Maryam! Hebu tuelezee juu ya kile ambacho

sisi tukikifanya kitatupelekea kuingia Peponi’. Hivyo Isa Ibn Maryam akajibu: ‘Uzuie

Ulimi wako kwa kutozungumza kabisa’ watu wakasema: ‘Jambo hilo

halitowezekana’ Isa Ibn Maryam akasema: ‘Basi msizungumze isipokua juu ya lile

liliokua jema’

Isa Ibn Maryam alisema: ‘Kufanya Ibada kumegawika sehemu kumi, ambapo

sehemu tisa hua ni kukaa kimya na sehemu moja iliyobakia hua ni kukaa mbali na

watu.’

Isa Ibn Maryam alisema: ‘Yeyote yule asemae uongo kila wakati, basi utatoweka

uzuri wa haiba yake. Na Yeyote yule anaemwambia mtu kile anachopenda kusikia

yule anaezungumza nae, basi itavunjika heshima yake. Yeyote yule anaefikiria sana

basi basi mwili wake utadhoofika. Na Yeyote yule asiekua na tabia njema basi hua

ni mwenye kujiadhibu Nafsi yake mwenyewe.’

Siku moja Isa Ibn Maryam alipishana na Nguruwe njiani na kumwambia Nguruwe huyo:

‘Pita kwa Amani’. Watu wakamuuliza Isa Ibn Maryam: ‘Ya Ruhi Allah! Unasema nae

hivyo Nguruwe?’. Isa Ibn Maryam akasema: ‘Nnachukia kuuzoesha Ulimi wangu

kusema maneno yasiyofaa’

Isa Ibn Maryam alikua akitembea na Wanafunzi wake, njiani wakakutana na mzoga wa

mbwa. Wanafunzi wake wakasema: ‘Hakuna harufu mbaya kama ya Mbwa’. Isa Ibn

Maryam akasema: ‘Hakuna Weupe mzuri kama wa Meno yake’.

Isa Ibn Maryam pamoja na Wanafunzi wake walikutana na Wayahudi na kuanza

kuwausia lakini Wayahudi hao wakamtukana Isa Ibn Maryam, lakini hata hivyo Isa Ibn

Maryam akawajibu Wayahudi hao kwa kauli nzuri. Wanafunzi wake wakamuuliza:

‘Inakuwaje watu hawa wamekutukana na kisha wewe unawajibu kwa kauli nzuri

nzuri?’ Isa Ibn Maryam akasema ‘Kila mtu hutumia kile alichokua nacho’

Akasema Isa Ibn Maryam: ‘Enyi Ibn Adam msiyachukulie Maisha kua ni Mola wenu,

kisha nayo yakakuchukulieni kua ni Waja wake. Hifadhini mali zenu na yule ambae


551

hatozipoteza, kwa sababu yule anaeandamana na mali katika maisha haya hua ni

mwenye kuogopa kutoweka kwa mali hio, wakati yule ambae mwenye

kuiandamanisha na Allah mali yake hua ni si mwenye kuogopa kitu chochote juu

ya mali hio’

Isa Ibn Maryam alisema kuwaambia Wanafunzi wake: ‘Enye Wanafunzi wangu,

hakika mimi nimeigeuza Dunia hii juu chini, hivyo msiipambe juu yangu, kwa

sababu uovu wa Dunia hii ni kua Allah anadhulumiwa ndani yake kwa kutotiiwa

amri zake, na uovu huo ni mkubwa kiasi ya kua Akhera haitoweza kupatikana

isipokua kwa kuachana na Dunia, hivyo ivukeni tu Dunia na msiishi juu yake.

Fahamuni kua mzizi wa kila Dhambi hutokana na kuipenda Dunia. Matamanio ya

saa moja tu humrithisha mtu urefu uliojaa huzuni’

Isa Ibn Maryam akasema kuwausia Wanafunzi wake: ‘Hakika mimi nimeuangusha

ulimwengu huu na kuukalia juu ya mgongo wake, hivyo nanyi msiwaruhusu

Wafalme na Wanawake kukushindanisheni juu yake, ama kuhusiana na Wafalme

basi msishindane nao katika Dunia hii kwa sababu hawatokukaribieni pale

mtakapowaacha wao na Dunia yao, ama kuhusiana na Wanawake, *Jizuieni nao

kwa kufunga na kusali.’

*Kujizuia na Wanawake kuliko kusudiwa hapa, hakumaanishi kua Watu wasioe bali

kunamaanisha kua Watu wasipende Wanawake wasiokua halali yao kwa kuzini.

Miongoni mwa wasia wa Isa Ibn Maryam ni pale aliposema: ‘Maisha yanadai na

yanadaiwa. Hivyo yeyote yule atakaeyadai maisha ya Akhera basi Akhera humdai

hadi imalizike riski yake, na yeyote yule anaeyadai maisha ya Dunia basi Akhera

humdai hadi mwisho wake kitakapomjia kifo na kumkamata shingo yake.’

‘Kamwe haiwezekani katika moyo wa Muumin kua na mapenzi ya Maisha ya Dunia

pamoja na Maisha ya Akhera, kama vile ambavyo isivyowezekana kwa Maji na

Moto kuchanganywa katika Jagi moja’

Isa Ibn Maryam Aliulizwa ‘Kwa nini hutaki kua na nyumba itakayokutosheleza?’,

ambapo nae akajibu ‘Kutoweka kwa waliotangulia kabla yetu kunatosheleza’’

Katika safari za Isa ibn Maryam basi siku moja ilitokea na mvua kubwa sana, radi na

upepo mkali, hivyo akaamua kujificha mvua hiyo katika moja kati ya bustani ya karibu,

lakini akaona kua kuna mwanamke nae amejificha katika bustani hivyo akaamua

kutojificha, akatoka na kukimbilia mbele zaidi ambapo aliona kuna pango kubwa sana

akaingia ndani ya pango hilo, na ghafla akakutana na Simba, hivyo taratibu akamkaribia

na kuanza kumpapasa ili kumtuliza Simba huyo huku akisema: ‘Ya Allah! Kwa hakika


552

wewe umekijaalia kila kitu kua na sehemu yake ya utulivu lakini hukuniwekea

mimi sehemu hio.’

Allah Subhanah wa Taála akasema kumwambia Isa Ibn Maryam: ‘Sehemu yako ya

Utulivu ni kati kati ya rehma zangu. Nnaapa kua Katika Sku ya Malipo nitakujaalia

kuoa Hawra (Wake wa Peponi) 100 ambao nimewaumba kwa mikono yangu, na

utashehereka katika harusi hio kwa miaka 4000 ambapo siku moja katika miaka

hio hua ni sawa na uhai mzima wa mtu, na nitaamrisha kutolewe wito

utakaotangazia kua: Jee Wako wapi wale ambao walikua hawana kitu katika

maisha yao? Njooni katika sherehe ya Harusi ya Isa Ibn Maryam ambae nae aliishi

bila ya kua na kitu katika uhai wake’

Amesema Isa Ibn Maryam kua: ‘Waylun! (Ole wao) wale wanaoendekeza Dunia! Jee

hawaoni kua mtu anakufa kisha anawacha kila kitu kilichomo ndani yake? Jee

hawaoni kua Duania inawakimbia lakini nao wanaiamini? Wanaiamini Dunia huku

nayo inawavunja Moyo?.

Na Waylun! kwa wale wenye kujidanganya Nafsi zao, Inakuaje kua wanakifuata

kile wanachokichukia na kukikimbia kile wanachokipenda? Na kinawakimbilia kile

walichokwisha ahidiwa?

Waylun! Kwa wale ambao mawazo yao ni juu ya Dunia hii tu! Na amali zao ni za

Dhambi tu! Kwani Kesho watakua maarufu kutokana na Dhambi zao!’

Siku moja Isa Ibn Maryam na Wanafunzi wake walipita katika kijiji kimoja na kukuta

watu wakiwa wamekufa katika hali na sehemu mbai mbali za kijiji hicho, hivyo Isa Ibn

Maryam akawaambia Wanafunzi wake: ‘Ama kwa hakika watu hawa wamefariki

kutokana na Adhabu ya Allah Subhanah wa Ta’ala juu yao, kwa sababu kama

wangekua wamekufa kwa sababu nyengine yeyote ile basi wangekua wamezikwa!’.

Wanafunzi wa Isa Ibn Maryam wakamwambia Isa Ibn Maryam: ‘Ya Ruhi Allah! Kama

ni hivyo basi sisi tungependa kusikia habari zao.’ Hapo Isa Ibn Maryam akamuuomba

Allah Subhanah wa Taála awajaalie waujue ukweli juu ya habari ya watu hao, ambapo

akashushiwa Wahyi na kuambiwa kua inabidi arudi katika sehemu hiyo katika wakati wa

usiku ambapo ataweza kuwauliza juu ya habari yao na watu hao watamjibu masuali yake

juu yao, wakati wa Usiku ulipowadia Isa Ibn Maryam akapanda katika sehemu ambayo

iliyo juu kidogo na kuanza kunadia katika maeneo hayo wa kusema:

‘Enyi Wakazi wa Kijiji hiki.’ Mmoja kati ya Watu walifariki katika kijiji hicho akajibu:

‘Naam Ya Ruhi Allah! Tuko chini yako kusikiliza amri yako!’


553

Isa Ibn Maryam akamwambia mtu huyo: ‘Hebu tuambieni yaliyo kusibuni hadi

mkawa katika hali hii’

Yule Mtu akasema: ‘Hakika sisi hua tuko kwenye mapumziko katika wakati wa

usiku na hua tuko katika adhabu katika wakati wa mchana’.

Isa Ibn Mayam akauliza: ‘Jee ilikuaje hadi ikawa mko hivyo?’

Yule mtu akajibu: ‘Kwa sababu sisi tulikua tuiipenda sana Dunia na hivyo kua ni

wenye kumuasi Mola wetu kwa kuwatii wasiokua waadilifu miongoni mwetu.’

Isa Ibn Maryam akauliza: ‘Jee ni kwa kiasi gani mlikua mkiipenda Dunia?’

Yule mtu akajibu: ‘Kama vile ambavyo Mama ampendavyo mtoto wake, kwani hua

pale mama anapomkaribia mtoto wake basi mtoto humfurahia mama yake, na

mama anapokaa mbali na mtoto wake basi mtoto humlilia mama yake na huingiwa

na huzuni kwa kua mbali na mama yake’.

Hapo Isa Ibn Maryam akauliza tena: ‘Mbona ni wewe peke yako tu ndie unaejibu

masuali yangu? Jee ni kwa nini wenzako hawajibu masuali yangu?’

Yule mtu akajibu: ‘Kwa sababu wanavijinga vya mtoto ndani ya midomo yao

ambavyo vimezuiwa na mikono imara ya Malaika wa Motoni!’

Isa In Maryam akauliza: ‘Sasa imekuaje kua wewe ukawa ni mwenye kuweza

kunijibu?’

Yule mtu akajibu : ‘Ama mimi nilikua ni miongoni mwa watu hawa lakini kamwe

sikuwa ni mmoja kati ya watu hawa, na hivyo adhabu ilipokuja ilinikumba na mimi

pia, hivyo mimi nnaning’inizwa kwenye ukingo wa Jahannam, na sijui kama

nitatumbukizwa ndani yake ama nitaokolewa dhidi yake’

Hapo Isa Ibn Maryam akawaambia Wanafunzi wake: ‘Kula mkate uliotokana na

shayiri iliyosagwa na chumvi na kuvaa ngozi na kulala kwenye uchafu ni bora na

salama zaidi kwa Ulimwengu huu na Ulimwengu wa Akhera’

Isa Ibn Maryam aliambiwa: ‘Tufundishe Ilm ambayo itatupelekea sisi kupendwa na

Allah Subhanah wa Taála’ ambapo nae akajibu: ‘Uchukieni Ulimwengu huu na hapo

ndipo Allah Subahanh wa Taála akatapokupendeni’ Isa in Maryam akaendelea kwa

kusema: ‘Enyi mnaoupenda Ulimwengu huu kwa ajili ya kufanya mema, basi


554

fahamuni kua kuachana nao na kuondoka ndani yake hua ni bora zaidi na ndio kua

na Taqwa zaidi’

Isa Ibn Maryam alisema: ‘Enyi Wanafunzi wangu! Kuweni ni wenye kuridhika

kidogo Duniani, kwa kupata usalama wa Dini, kama vile ambavyo Wanaoipenda

Dunia wanavyokua wametosheka na udogo wa Dini na Usalam wao Duniani’

Isa Ibn Maryam Alisema : ‘Mimi Mkate wangu ni Njaa, Kauli yangu ni Khofu, Nguo

zangu ni Sufi, Sala zangu katika kipindi cha Baridi ni Alfajiri, Taa yangu ni Mwezi,

Chakula changu na Matunda yangu ni kila kitu kinachozalishwa na Ardhi,

Nnautumia Usiku wangu nikiwa sina kitu na Nnauamkia Usiku huo katika asubUhi

yake nikiwa Sina Kitu. Na Hakuna mtu alie Tajiri juu ya Ardhi kama mie ’

Nabii Isa Ibn Maryam alikua ni mwenye kuuona Ulimwengu katika hali ya uhalisia wake

ambao ni wa hali ya mwanamke Ajuza asiekua na meno lakini aliejaa mapambo ya

Wanja, Podari na Rangi za Mdomo tele. Hivyo aliuuliza Ulimwengu huo kwa kusema:

‘Jee tayari Umesholewa Mara ngapi?’ Ulimwengu ukamjibu: ‘Ama Siwezi

kuzihesabu mara nilizoolewa’. Isa Ibn Maryam akauliza: ‘Jee waliooana nawe wote

wamefariki au Wamekutaliki’. Ulimwengu ukajibu: ‘La Ni mimi ndie ambae

nimewateketeza kwa kuwaua wote’ Hapo Isa Ibn Maryam Akasema: ‘Adhabu ipo

kwa wale utakao oana nao, inakuaje kua wao hawajifunzi kutokana na yaliyowafika

waliotangulia? Inakuaje unawaangzamia mmoja baada ya mwengine lakini nao

hawana habari hio na kamwe hawakuchoki?’

Nabii Isa Ibn Maryam alisema: ‘Wa Allahi ukweli nakuambieni kua: Mgonjwa hua

ni mwenye kukiangalia chakula na hua hahisi ladha yake kulingana na maumivu

aliyokua nayo, na hali hii pia ndio waliyokuaa nayo wanaoiendekeza Dunia, kwani

hua hawaihisi ladha ya kufanya Ibada na hawauoni utamu wake kutokana na kile

anachokitafuta Duniani. Wallahi ukweli nakuambieni mnyama wa kipando

anapokua hajapandiwa na wala hajafundishwa kupandiwa basi hubadilika na kua

mgumu kudhibitika pale anapotaka kupandiwa, na hivyo hivyo ndivyo ulivyo Moyo

unapokua haujazoeshwa kukumbuka juu ya kifo na kufanya Ibada basi nao pia

hugeuka na kua mgumu kupita kiasi. Wallahi ukweli nakuambieni kua kama ikiwa

mtungi wa maji haujatoboka basi hua tayari kua ni sehemu ya kuhifadhia asali,

Nyoyo pia ziko hivyo hivyo, kama ikiwa hazijatobolewa na matamanio na ubahili

haujauchafua Moyo na anasa haijautia ugumu moyo huo, basi bila ya shaka Moyo

huo utakua ni Mtungi uliojaa Hikma na Busara ’,

Isa Ibn Maryam Alisema: ‘Mfano wa yeyote yule anaeiendekeza Dunia hua ni sawa

na mtu mwenye kunywa maji ya bahari. Kwani kila anavyozidi kula basi ndivyo

anavojzididhishia kiua yake hadi kufikia kifo chake’


555

Isa Ibn Maryam alisema: ‘Katika Mali kuna maradhi matatu: Mtu kuipata kutoka

katika vyanzo visivyo halali. Na ikiwa kaipata kutoka katika vyanzo vya halali basi

ataitumia katika njia zisizo za halali.’ Wanafunzi wake wakamuuliza, ‘Vipi kama

akiwa atazitumia katika njia za halali?’ Isa Ibn Maryam akasema: ‘Basi

zitamshughulisha kiasi ya kua atamsahahu Mola wake.’

Isa Ibn Maryam alisema: ‘Wanazuoni waovu hua ni sawa na Jabali ambalo

limeanguka kutoka juu hadi kwenye mlango wa pango lenye kutoa maji, na hivyo

kuyaziba maji hayo huku likiwa haliyatumii maji hayo wala haliyaachii maji hayo

kutiririka kwa ajili ya manufaa ya vitu vyengine’

Isa Ibn Maryam alisema: ‘Mfano wa mtu anaetafuta Ilm kisha akawa si mwenye

kuifanyia kazi kwa vitendo hua ni sawa na mwanamke anaefanya zinaa kisiri siri

na kisha akawa na uja uzito. Na tumbo lake linapojitokeza na kua kubwa huanza

kuadhirika na kuona haya kutokana na ujauzito huo, hali hii ndio watakayokua

nayo watu wasioifanyia kazi Ilm yao, kwani Allah Subhanah wa Taalah

atawaadhirisha katika siku ya Malipo mbele ya watu wote.’

Isa Ibn Maryam alikutana na mtu mmoja aliejitambulisha kwake na Isa Ibn Maryam

akamuuliza: ‘Jee wewe unajishughulisha na nini?’ Yule mtu akajibu: ‘Mimi hua

nnajishughulisha na kufanya Ibada tu!’ Isa Ibn Maryam akamuuliza tena mtu huyo:

‘Jee ni nani anaekuhudumia katika kukutafutia mahitaji yako?’ yule mtu akajbu:

‘Nnahudumiwa na ndugu yangu’ Isa Ibn Maryam akamwambia mtu huyo: ‘Ama kwa

Hakika ndugu yako ni mwenye kufanya Ibada bora zaidi kuliko wewe.’

Allah Subhanah wa Ta’ala alimwambia Isa Ibn Maryam: ‘Kama ukiniabudu mimi kwa

Ibada zote za viumbe wa Ardhini na Mbinguni na ikawa hakuna mapenzi kwa ajili

ya jina la Allah na chuki kwa ajili ya jina la Allah basi Ibada yako hio

haitokunufaisha na kitu chochote.'

Isa Ibn Maryam aliwaambia Wanafunzi wake: ‘Tafuteni mapenzi ya Allah Subhanah

wa Taála kwa kuwachukia wafanyao maovu, ukaribu na Allah kwa kukaa mbali

nao, na tafuteni ridhaa ya Allah katika yale wayachukiayo wao.’ Wanafunzi

wakauliza: ‘Ya Ruhi Allah! Jee tukae na nani?’ Isa Ibn Maryam akajibu: ‘Kaeni na

wale ambao mtakapokaa nao watakukumbusheni juu ya Allah, na kukuzidishieni

mema yenu kutokana na kauli zao. Na wale ambao mambo yao yatakufanyeni

muipendelee Akhera yenu.’

Alisema Nabii Isa kuwaambia Wanafunzi wake kua: ‘Kaeni na njaa, na Kiu na Msivae

Nguo nzuri na Jichosheni ili Nyoyo zenu zipate kumjua Allah.’


556

KAULI ZA NABII MUHAMMAD SALALLAHU ALYHI WA SALAM

KUHUSIANA NA NABII ISA ALAYHI SALAM.

Amesema Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua: ‘Mtume wa kwanza ni

Adam na wa mwisho ni Muhammad. Mtume wa mwanzo wa Bani Israil ni Musa na

wa mwisho ni Isa Ibn Maryam. Na Mtume wa mwanzo kuandika kwa kutumia

Kalamu ni Idrisa’

‘Yahya Ibn Zakariyyah alimwambia Isa Ibn Maryam: ‘Wewe ni Ruhi Allah na

kauli yake (Kun) na wewe ni bora kuliko mimi’ Isa Ibn Maryam akasema: ‘Wewe ni

bora kuliko mie kwani Allah Subhanah wa Taála amekujaalia wewe Usalama lakini

mimi amenisalimia kwa usalama.’

‘Ndugu zangu, Mitume waliotangulia, idadi yao ni 8000. Kisha akafuatia Isa Ibn

Maryam na kisha nikafuatia miebaada yake.’

‘M-bora miongoni mwa Ibn Adam ni Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad. Na

Muhammad ni m-bora wao zaidi.’

‘Iblis humgusa kila Ibn Adam anaezaliwa na mama yake isipokua Maryam bint

Imran na mtoto wake ambae ni Isa Ibn Maryam.’

Isa Ibn Maryam alimuona mtu anaiba kitu, hivyo akamuuliza mtu huyo: ‘Umeiba nini?’

Yule mtu akajibu ‘La! Wa Allahi la ilaha illa huwa!’ yaani La Sijaiba! Naapa kwa

yule ambae hakuna Mungu isipokua yeye’. Hivyo Isa Ibn Maryam akasema: ‘Naam,

namuamini Allah na siamini macho yangu.’

Kauli hii inaashiria namna Isa Ibn Maryam alivyokua akithamini kiapo kupitia kwa yule

ambae hakuna anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokua yeye, kiasi ya kua alikua yuko

tayari kutoyaamini macho yake, kuliko kutoamini kiapo cha mtu alieapa kwa ajili ya

Allah Subhanah wa Ta’ala.

‘Adam yuko katika Mbingu ya Kwanza, na vitendo vya kizazi chake vinawekwa

wazi mbele yake, na Yusuf yuko katika Mbingu ya Pili, na watoto wawili wa dada

wawili, Yahya na Isa wapo katika Mbingu ya Tatu, Idris yupo katika Mbingu ya

Nne. Harun yupo katika Mbingu ya Tano, Musa yupo katika Mbingu ya Sita na

Ibrahim yupo katika Mbingu ya Saba.’


557

KAULI ZA ALLAH SUBHANAH WA TAALA JUU YA NABII ISA IBN

MARYAM.

Amesema Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua: ‘Allah Subahanah wa

Taála amesema: Ya Isa Ibn Maryam! Mimi ndie Mola wako na ndie Mola wa

Mababu zako waliotangulia, Jina Langu ni Ahad na ndie Ahad wa Pekee. Mimi ndie

pekee ninaeumba kila kitu na kila kitu kinatokana nami na hivyo kila kitu kitarejea

kwangu.

Ya Isa Ibn Maryam! Wewe ndie uliechaguliwa nami kutokana na amri yangu, na

umeumba kutokana na udongo umbo la ndege kutokana na idhini yangu, na

umekhuisha waliokufa kutokana na kauli yangu, hivyo kua ni mwenye kunihitaji

mimi na mwenye kua na khofu nami, kwani hakuna atakae kuokoa dhidi yangu

isipokua mimi.

Ya Isa Ibn Maryam! Nimekuchagua wewe kutokana na yule ambae ni Mwingi wa

Ukarimu na mwingi wa Rehma, nimeamua kukupa urafiki wangu kwa kukutumia

wewe furaha hivyo umebarikiwa wakati ulipokua mdogo na hadi utakapokua

mkubwa na popote pale utakapokuwepo. Mimi nnashuhudia kua wewe ni Mja

wangu na ni mtoto wa Mja wangu wa Kike. Hivyo niingize katika hali ya kua na

khofu nami katika nafsi yako, na uniweke katika ufahamu wako kwa kunikumbuka

mimi kwa ajili ya siku ya Malipo na nikaribie kwa kufanya Amali za ziada, na

nitegemee mimi kwani nitakutosheleza, na usimtegemee yeyote mwengine kwani

kufanya hivyo kutanifanya mimi nisikusaidie.

Ya Isa Ibn Maryam! Dumisha Dhikr kwa ulimi wako na uruhusu ukarimu wangu

uutawale Moyo wako.

Ya Isa Ibn Maryam amka kutoka katika nyakati za usahaulivu na kusanya kwa ajili

yangu mie ambae ndie pekee mwenye Hikma.

Ya Isa Ibn Maryam! Kua mwenye kuabudu kwa kunihitaji mimi na uue moyo wako

kutokana na khofu yake juu yangu.

Ya Isa Ibn Maryam! Ukhuishe Usiku kwa ajili ya kutafuta ridhaa yangu na kua na

kiu katika wakati wa mchana kwa ajili ya siku ya mahitaji yako mbele yangu.


558

MAELEZO YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA

SALAM KUTOKA KATIKA YALE WALIORITHI MAYAHUDI NA

WAKRISTO.

‘Muhammad Rasul Allah, Ni Mja wangu niliemchagua, hatokua tu si mpole wala

mpigaji kelele Masokoni. Hatoondoa Ovu kwa kutumia njia ya Uovu, bali atakua

ni mwenye kusamehe na kutotilia maanani maovu aliyofanyiwa. Atazaliwa katika

mji wa Makkah na atahamia katika mji wa Taba, na Utawala wake utakua katika

Ardhi ya Syria, yeye na kila atakaekua pamoja nae atakua ni mwenye kuvaa

mkanda kiunoni mwake, atahubiri Quran na Hadith na atatia udhu mikononi

mwake na miguuni mwake. ’

Amesema Isa Ibn Maryam: ‘Mliambiwa hapo kabla kua miaka kwa miaka, pua kwa

pua, nami nakuambieni msipingane na uovu kwa uovu. Lakini yeyote yule atakae

kupiga kibao shavu la kulia basi mpe na shavu la kushoto, na atakae kuchukulia

shati lako basi mpe na suruali yako, na yule atakae kutumia wewe kwa ajili ya

kutembea nae kwa maili moja basi tembea nae kwa maili mbili’

Kulikua na mtu ambae alikua ni mporaji aliekua akiwapora watu njiani kwa miaka 40,

hivyo wakati Isa Ibbn Maryam alipopishana na mtu huyu basi huyu mtu akasema

kuiambia nafsi yake: ‘Huyu ni Nabii wa Allah Subhanah wa Taála akiwa ni mwenye

kupita na MWanafunzi wake hivyo nami nitajiunga nao ili niwe mtu wa tatu

miongoni mwao’ Hivyo akajiunga nao kwa unyenyekevu huku akijaribu kua karibu na

yule mWanafunzi huku akiiambia nafsi yake: ‘Mtu kama mie sistahiki kutembea

pamoja na Mcha Mungu huyu’.

Yule MWanafunzi wa Nabii Isa Ibn Maryam nae akajiuliza katika Nafsi yake: ‘Ah kwa

nini mtu huyu anatembea karibu yangu kiasi hiki’ hivyo akaongeza mwendo kihatua

hadi akamfikia Nabii Isa na akawa ni mwenye kutembea pamoja nae ubavuni mguu kwa

mguu huku yule mwizi akiwa yuko nyuma yao. Hivyo Allah Subhanah wa Taála

akayaonesha haya yanayotokea kwa Nabii Isa Ibn Maryam kwa kumwambia kua tangu

walipoanza kutembea na yule mporaji basi Allah Subhanah wa Taála amemfutia dhambi

zake yule mporaji na pia amemfutia thawabu zake yule mWanafunzi wa Nabii Isa Ibn

Maryam. Hivyo Nabii Isa Ibn Maryam akawataarifu kilichotokea na hapo yule mporaji

akawa ni mWanafunzi wa Nabii isa Ibn Maryam.


559

Isa Ibn Maryam alisema: ‘Enyi Wanafunzi! Wakati nyinyi hua ni wenye kukhofia

Dhambi basi sisi Mitume hua ni wenye kuikhofia Kufr’

Isa Ibn Maryam alisema: ‘Enyi Wanafunzi wangu! Muogopeni Mola wenu, na

ipendeni Pepo na kuweni warithi wa ustahmilivu wakati wa Mitihani. Kila mtu

anatakiwa ajitenge na Dunia hii. Wa Allahi! Kula Majani na kulala kwenye uchafu

pamoja na mbwa hua si chochote katika kuitafuta Pepo’

Isa ibn Maryam alipokua akitembea njiani alimkuta mtu ambae alikua amelala huku

akiwa amejifunika guo lake na hivyo akaamua kumuamsha na kumwambia: ‘Ewe

ulielala! Amka na umkumbuke Mola wako Allah Subhanah wa Taála’, Ambapo yule

mtu alielala akasema: ‘Unataka nini kutoka kwangu wakati mimi nimeachana na

Ulimwengu na wamiliki wake?’ Hapo Isa Ibn Maryam akasema: ‘’Kama ni hivyo basi

endelea kulala ewe kipenzi changu’

Isa Ibn Maryam alisema: ‘Kwa Hakika mimi naupenda Umasikni na nnachukia

anasa’. Na ukweli ni kua Isa Ibn Maryam alikua akipenda kuitwa kwa jina la: ‘Ewe

Mtiifu na Mnyenyekevu’

Isa ibn Maryam alisema: ‘Kamwe msiangalie utajiri wa watu wa Duniani kwani

mng’aro wa utajiri wao utachukua mwangaza wa Imani yenu’

Aliambiwa Nabii Isa Ibn Maryam na Wanafunzi wake: ‘Ya Rasul Allah, ingekua vizuri

kama ungetuamrisha sisi kujenga Nyumba ya Kumuabudia Allah’, Isa Ibn Maryam

akajibu: ‘Nendeni kajengeni Nyumba hio kwenye maji Baharini’. Wanafunzi

wakauliza: ‘Jee Tutajengaje Nyumba katika sehemu iliyojaa maji?’ Isa Ibn Maryam

akajibu: ‘Na Jee itasimamishwa vipi Ibada katika sehemu iliyojaa mapenzi ya

Dunia?’

Katika kutekeleza moja kati ya maamrisho ya Allah Subhanah wa Taála kama

ilivyoelezewa katika Qurán pale iliposema:

‏﴿قَدْ‏ خَلَتْ‏ مِنْ‏ قَبْلِكُمْ‏ سُنَنٌ‏ فَسِ‏ يرُواْ‏ فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ فَٱنْظُرُواْ‏ كَيْفَ‏ كَانَ‏ عَاقِبَةُ‏

ٱلْمُكَذِّبِينَ‏ ﴾

Qad khalat min qablikum sunanun faseeroo fee al-Ardhi faondhuroo kayfa kana

AAaqibatu almukadhdhibeena (Al Imran 3:137)


560

Tafsir: Kwa hakika yamewafika mengi waliokuja kabla yenu (Walioamini na

Wasioamini), hivyo tembeeni katika Ardhi ili mpate kuona ni upi ulikua mwisho wa

wale waliokadhibisha.

Basi njiani Isa Ibn Maryam akakutana fuvu la kichwa la mtu aliekufa kwa mda mrefu,

hivyo akaingiwa na hamu ya kujua kilichomfika mwenye fuvu hilo, na kumuomba Allah

Subhanah wa Taála amfufue mwenye fuvu hilo ili azungumze nalo, ambapo Allah

Subhanah wa Taála akaliruhusu fuvu hilo na kuanza kusema:

"Ana Balwan Bin Hafs, Malikul Yaman. 'Ishtu alfa sanatin, waruziqtu alfa waladin,

waftadodtu alfa bikrin, wa fatahtu alfa madeenah. Famakaana kullu dhaalika illa

kanaaim. Faman sami'a qissotiy, fayaghtarra biddunya".

"Mimi ni Balwan Ibn Hafs aliekua Mfalme wa Yemen, Nimeishi miaka 1000,

niliruzukiwa watoto 1000 na niliwatoa bikra bikira 1000 na niliifungua Miji 1000,

na kisha hayakua haya yaliyonitokea ila ni kama ndoto. Hivyo yeyote yule

atakaekisikia kisa changu basi kamwe asihadaike na mapambo ya Dunia ".

Amesema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an kua:

‏﴿وَإِذْ‏ قَالَ‏ عِيسَى ٱبْنُ‏ مَرْيمََ‏ يٰبَنىِ‏ إِسْرَائِيلَ‏ إِنىّ‏ ِ رَسُولُ‏ ٱهلل َِّ‏ إِلَيْكُم م ُّصَدِّقاً‏ لِّ‏ مَا بَينَْ‏

يَدَى َّ مِنَ‏ ٱلت َّوْرَاةِ‏ وَمُبَشِّ‏ راً‏ بِرَسُولٍ‏ ‏َْتِى مِن بَعْدِى ٱسمُْهُ‏ أَحمَْدُ‏ فَلَم َّا جَاءَهُم

بِٱلْبَيِّنَاتِ‏ قَالُواْ‏ هَٰذَا سِ‏ حْرٌ‏ م ُّبِينٌ‏ ﴾

Wa-idh qala AAeesa ibnu maryama ya banee isra-eela innee rasoolu Allahi ilaykum

musaddiqan lima bayna yadayya mina alttawrati wamubashshiran birasoolin

ya/tee min baAAdee ismuhu ahmadu falamma jaahum bialbayyinati qaloo hadha

sihrun mubeenun(Surat As Saffat 61:6)

Tafsir: Na alisema Isa Ibn Maryam: ‘Enyi watu wa Bani Israil, hakika mimi ni Rasul

Allah niliyeshushiwa juu yenu kuthibitisha kabla yangu Tawrat na kukubashirieni juu

ya Mtume ambae atakuja baada yangu jina lake Ahmad ambae atapokuja na

Ubainisho basi watasema: ‘Huu ni Uchawi uliowazi’’

Ambapo bashirio hili la Isa Ibn Maryam kua atakuja Mtume baada yake aitwae Ahmad

lilikuja kudhihirika miaka 1400 baada ya kufariki kwake Isa Ibn Maryam katika ardhi ya

Bara Arabu iliyokua ikijulikana kama Bakka au Makkah.


561

SURA YA TATU

الإمام الأنبياء والمرسلين

محمد صلى االله عليه وسلم


562

IMAM AL ANBIYAI WAL ALMURSALINA MUHAMMAD SALALLAHU

A’LAYHI WA SALAM

Miaka 2000 Kabla ya kuzaliwa Nabii Isa Ibn Maryam basi Nabii Ibrahim Alayhi Salam

aliuombea Mji wa Makkah ambao ndio uliokua ni Mji anaoishi Mke wake Hajar na Mtoto

wao ambae ni Nabii Ismail Alayhi Salam basi Nabii Ibrahim A’layhi Salaam aliomba

kuwaombea watu wa familia yake hio kwa kusema:

‏﴿رَب َّنَا وَٱبْعَثْ‏ فِيهِمْ‏ رَسُولاً‏ مِّنْهُمْ‏ يَتْلُواْ‏ عَلَيْهِمْ‏ آَتِكَ‏ وَيُعَلِّمُهُمُ‏ ٱلْكِتَابَ‏ وَٱلحِْكْمَةَ‏

وَيُزَكِّيهِمْ‏ إِن َّكَ‏ أَنتَ‏ ٱلعَزِيزُ‏ ٱلحَكِيمُ‏ ﴾

Rabbana waibAAath feehim rasoolan minhum yatloo AAalayhim ayatika

wayuAAallimuhumu alkitaba waalhikmata wayuzakkeehim innaka anta

alAAazeezu alhakeemu. (Surat Al Baqara 2:129)

Tafsir: Ya Rabb! Watumie miongoni mwao Mtume, Mtume ambae atakaewasomea aya

zako na kuwaamrishia yaliyomo ndani ya kitabu (Qur’an) na Al-Hikmah (Kilichojaa

Hikma na I’lm ya Sharia’h za kiislam n.k), na uwatukuze. Kwa hakika wewe ni

muweza kila kitu na ni mwingi wa Busara.

Ambapo kwa hakika Allah Subhanahu wa Ta’ala alimkubalia dua hizo na kizazi chake

kikawa kinaongezeka na kukua kidogo kidogo, hatua kwa hatua, watu kutoka miji mbali

mbali wakaanza kusikia kuhusiana na mji huo na nyumba hiyo na wakawa wanakuja

kuutembelea na kufanya Ibada katika mji huo na kizazi cha Nabii Ibrahim A’layhi Salaam

na Nabii Ismai’l A’layhi Salaam, kikaendelea kua ndicho kinachoshika funguo za

nyumba ya Al Ka’abah na wasimamizi wa nyumba hiyo, na kuendeleza usimamizi huo

kizazi baada ya kizazi hadi kufikia kwa muanzilishi wa kabila la Quraysh, na ndani ya

kabila hilo pia, na baada ya mda mrefu kupita Allah Subhanahu wa Ta’ala akaijibu dua

ya Nabii Ibrahim A’layhi Salaam, iliyotajwa katika aya 129 ya Surat Al Baqara kwa

kumtoa katika miongoni mwa kizazi hicho mbora wa viumbe vyote, ambae si mwengine

bali ni Nabii na ni Mtume wa Mwisho ulimwenguni, Habib Allah Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam.


563

ASILI YA UARABU NA YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU

A’LAYHI WA SALAM.

Vitabu vya historia vinasema kua asili ya Waarabu imetokana na miongoni mwa makundi

aina tatu ya watu:-

1. Al Arab ul Baidah ( البائد ‏(العرب Waarabu waliopotea: Hawa ni wale watu waliokua

miongoni mwa kizazi kilichotoweka cha watu wa ‘Ad, Thamûd, Tasam, Jadis na

Imlaq ambao walikua wakiishi katika maeneo ya Al Ahqaf yaliyopo baina ya

Hadramawt na Oman ambao Mtume wao alikua ni Nabii Hud A’layhi Salaam.

2. Al Arab ul Ariba العاربة)‏ ‏(العرب Waarabu wenye Uarabu asilia: Hawa ni wale watu

waliokua ni miongoni mwa kizazi kilichotokana na Nabii Hud A’layhi Salaam

kupitia kwa Ya‘rub Ibn Yashjub Ibn Qahtan Ibn Hud ambao walikua wakijulikana

pia kama Waarabu wa Yarub wa Qahtan ambapo pia walikua wakitawala katika

maeneo ya Yemen.

3. Al Arab al Mustariba المستعربة)‏ ‏(العرب Waarabu waliopewa Uarabu kwa

kuchanganya vizazi: Hawa ni wale watu waliotokana na kizazi cha Nabii Ibrahim

A’layhi Salaam kupitia kwa Nabii Ismai’l A’layhi Salaam ambae alimuoa Sayyida

Bint Mudad ambae ni mtoto wa Mudad Ibn Amr aliekua kiongozi wa ukoo wa Banu

Jurhum wenye asili ya Al Arab ul Ariba na hivyo kizazi cha mchanganyiko baina ya

Nabii Ismai’l Ibn Ibrahim A’layhi Salaam na Sayyida Bint Mudad ndio ukawa ni

kizazi kinachojulikana kama Al Arab al Mustariba ambao pia hujulikana kama

Waarabu wa Adnan. Waarabu hawa wa Adnan ndio chanzo cha asili ya Ukoo wa

Quraysh.

ة

Kizazi hiki cha watoto wa Nabii Ismai’l A’layhi Salaam ambacho ndio asili halisi ya Al

Arab al Mustariba kilikua na watoto kumi na mbili ambao ni Qidar, Fidmah, Bana,

Buth, ‘Awil, Taqis, Masma’, Taima, Jasham, Haidir, Duma, Yatur, na Massa. Ambapo

kizazi cha Taima baadae kilihamia katika maeneo ya Madinah al Munawwara na kizazi

cha Massa kilihamia katika maeneo ya Yemen.

Watu wa kizazi cha Qidar ambacho kilitokana na mtoto wa kwanza wa Nabii Ismai’l

A’layhi Salaam kilikua ni chenye nguvu na uwezo na umuhimu mkubwa sana, kiasi ya

kua wametajwa pia katika vitabu vya Taurat, maandiko ya watu wa Ashur (Assyrian)

ambao ni wenye asili ya Babylon (Iraq kuelekea juu Uturuki), kimetajwa pia katika

historia za Wagiriki, Warumi na Wamisri kua ni watu wenye kukaa katika maeneo ya

Hijaz (Maeneo ya Uarabuni hususan maeneo ya nchi ya Saudi Arabia).


564

Kizazi hiki cha Qidar ndicho kilichotoa ukoo wa Quraysh ambao uliokua ni ukoo

mkubwa katika Mji Mtakatifu wa Makkah, na pia ulikua ni ukoo ambao ulikua ukitawala

mji huo kwani ndio uliokua ukisimamia na kushika ufunguo wa Al Kaabah, ingawa asili

ya ukoo huo ilikua inatokana na kizazi cha Nabii Ibrahim A’layhi Salaam kupitia kwa

Nabii Ismai’l A’layhi Salaam kupitia kwa Haidir na kupita vizazi na vizazi, lakini asili

ya kuanza kutumika kwa jina la jina la Quraysh ilianzia kwa Fihr Ibn Malik ambae pia

alikua akijulikana kwa jina la Quraysh ambalo ni neno la kiarabu lenye maana nyingi, na

miongoni mwao ikiwemo ‘Mwenye kutafuta na kukusanya’ na pia ‘Samaki mkubwa

wa baharini aina ya Papa’.

Fihr Ibn Malik aliitwa Quraysh kwa sababu yeye alikua ni mtu tajiri ambae aliekusanya

mali nyingi sana, ambazo hata hivyo alikua akizitumia kwa ajili ya kuwatafuta masikini

wa karibu wa eneo lake na kisha kuwasaidia katika kutimiza mahitaji ya maisha yao.

Ukoo wa Quraysh ulikua unafuata dini ya Uislam iliyoachwa na Nabii Ibrahim A’layhi

Salaam na Nabii Ismai’l A’layhi Salam, kizazi hadi pale Iblis laA’anatu Allahi Alayhi

alipofanikiwa kumpotosha Amr Ibn Luay ambae alikua ndie kiongozi wa mji huo katika

wakati huo, Amr Ibn Luay akateleza na kutoka katika njia ya maisha iliyoanzishwa na

Nabii Ibrahim A’layhi Salam.

Kwani kwa mara ya kwanza alifunga safari na kuelekea Sham kibiashara na alipofika

huko akawakuta watu wanaabudu masanamu, alivutiwa sana na jambo hilo kiasi ya kua

aliamua kununua masanamu na kurudi nayo katika mji wa Makkah na kuyaweka ndani

ya Al Kaabah na kisha kuwaamrisha watu wayatukuze na kuyaheshimu masanam hayo.

Miongoni mwa masanamu hayo lilikuwemo kubwa lao lilokuwa likiitwa Hubal, na

wengine wakiwa na majina ya Lata, Uzza, Manah, Wadd, Sawa, Yaghut, Nasr, Isaf, Naila

n.k.

Katika kipindi hiki mji wa Makkah ulikua hauna mfumo maalum wa uongozi uliokua

ukisimamia umoja na maslahi ya jamii ya watu wanaoishi maeneo hayo na vile vile

maslahi ya wageni wanaotembelea maeneo hayo kwa ajili ya biashara na pia kwa ajili ya

hija, ambayo ilikua si ya asili kama ilivyokua katika nyakati za mwanzoni, kwani hija hii

ilikua ni hija ambayo kila mtu alikua akienda kuhiji aidha na sanamu lake ama kwa ajili

ya sanamu lake maalum analoliamini kua linaweza kumtekelezea shida zake. Katika

kipindi hiki kila kitu kilikua kinaendeshwa kiukoo, kwa kila ukoo kujitegemea katika kila

kitu kwa ajili ya maslahi ya ukoo huo.

Hata hivyo baada kufikia wakati wa uongozi wa Qusay mambo yalianza kubadilika,

kwani yeye alijaaliwa akili na mbinu nzuri za uongozi. Hivyo alitumia akili yake na

kuanzisha mfumo wa uongozi ambao ulijenga umoja wa watu wa mji huo na hivyo

kuanza kuwanufaisha watu hao wa Makkah na vile vile kuwanufaisha wageni wanaoingia

na kutoka katika mji huo. Miongoni mwa yale aliyofanya ambayo bado yanaendelea

kufanyika hadi hii leo ni pamoja na:-


565

Kuunda baraza ambalo lilikua na kamati ya viongozi waliokua wakisimamia

makubaliano ya pamoja kiujumla. Aliunda Sharia’h ambayo ilikua ikitumiwa na kamati

hiyo katika mambo yao ya kiutawala, na akajenga nyumba pembeni ya Al Kaabah,

iliyokuaa ikitwa Daar un Nadwa ambayo ilikua ni nyumba ya baraza hilo kwa ajili ya

kukutana na kuzungumzia matatizo na kutatua mambo mbali mbali yanayowahusu watu

wa mji huo.

Aliunda mfumo wa kuwalipisha kodi wageni wanaoenda kwa ajili ya biashara na kwa

ajili ya kuhiji katika mji huo ili kuwanufaisha watu wa Makkah, na vile vile kuwanufaisha

watu wanaoenda kuhiji kwa kuwapatia huduma za chakula, maji na makazi.

Baada ya hapo Qusay akachukua na kuyasimamia majukumu yote yanayohusiana na:

1. Hijaba – Kuhifadhi funguo za Al Kaabah.

2. Nadwa – Kiongozi wa Daar un Nadwa (Baraza la mji Makkah).

3. Rifada – Kushughulikia chakula cha watu wanaohiji.

4. Saqaya – Kusimamia maji kwa ajili ya watu wanaohiji.

5. Liwa – Kuchagua kiongozi wa kuongoza vita.

6. Qiyada – Kiongozi wa Jeshi la Makkah.

Qusay alipofariki aliwacha watoto wawili ambao walikua ni Abd Darr na Abd Manaaf,

hivyo uongozi wa mji huo ulirithiwa na mtoto wake mkubwa aliekua akiitwa Abd Darr,

lakini kutokana na kua hakua na uwezo wala sifa nzuri zinazohitajika katika kutekeleza

majukumu hayo ya uongozi, akaamua kumuachia majukumu yake hayo ndugu yake

aliekua maarufu kama Abd Manaf lakini jina lake halisi lilikua ni Mughira, ambae alikua

ni mwenye sifa na uwezo wa majukumu hayo na hivyo aliendelea kuongoza hadi pale

alipofariki Abd Darr.

Baada ya Abd Darr kufariki, viongozi wa mji wa Makkah wakakutana na kukukubaliana

kua majukumu ya uongozi ya Abd Manaf, yagaiwe nusu ayabebe mtoto mkubwa wa Abd

Darr aliekua akiitwa Abd Shams na nusu yaliyobakia aendelee kuyatekeleza Abd Manaf.

Hivyo Abd Manaf akawa na majukumu ya kuwashughulikia watu wanaokuja kuhiji na

vile vile abakie kua kiongozi wa Jeshi la watu wa mji wa Makkah. Abd Shams yeye

(ambae alikua ni mtoto wa Abd Darr) akapewa jukumu la kusimamia Al Kaabah na

kiongozi wa wakati wa vita, na vile vile wote wawili kwa pamoja wakawa ni viongozi

wa baraza na kamati ya mji wa Makkah.

Baada ya Abd Manaf kufariki, majukumu yake yote yakahamia kwa mtoto wake wa

mwisho aliekua akiitwa Amr au maarufu alijulikana kama ‘Hashim’ yaani ‘Mkataji wa

Mikate’. Amr alikua na sifa za uwezo wa kuongoza tofauti na watoto wake wengine

kwani Hashim alikua ni kopi asilia ya Qusay (aliekua babu yake). Hili linaonekana wazi

pale ilipotokea katika wakati wa uongozi wake mji wa Makkah ulikumbwa na ukame

mkubwa sana, na hivyo Amr alitumia mali yake ili kununua chakula kutoka katika

sehemu zilizo nje ya mji wa Makkah kwa ajili ya watu wake wa mji wa Makkah.


566

Jambo hili la kununua mikate nje ya mji wa Makkah na kuwaletea watu wa mji wa

Makkah lilimpatia Amr jina la ‘Mkataji wa Mikate’. Hivyo Amr au Hashim alianzisha

misafara yake ya biashara iliyokua ikiwahudimia watu wa Makkah kwa kufanya biashara

kuanzia Yemen, Sham hadi Jerusalem, alisimamia mwenyewe mambo yote

yanayohusiana na usalama wa misafara yake hiyo inapokua njiani katika kila sehemu

kwa kujadiliana na kufunga mikataba na watu wa sehemu mbali mbali zinazopita

misafara yake.

Kutokana na cheo na ukarimu aliokua nao Hashim, watu wa Makkah wakaamua

kumuweka Hashim katika ngazi ya juu ya uongozi kuliko Abd Shams. Katika kuongoza

kwake mji wa Makkah, Hashim aliwahakikishia usalama wao na kuwahudumia watu

wote waliokua wakija Makkah kuhiji, hususan wale waliokua hawana uwezo na ambao

waliokua ni masikini na vile vile alishusha bei za vitu vyote katika msimu wa kuhiji.

Jambo ambalo lilimpelekea kupendwa sana na watu wa mji huo na pia wageni

wanaotembelea mji huo.

Baada ya kufariki Abd Shams, ikabidi uongozi kwa upande wake urithiwe na mtoto wake

mkubwa wa kiume aliekua akiitwa Umayyah. Lakini kutokana na kua Ummayah alikua

ni mtu mwenye kumuonea choyo na wivu Hashim kutokana na sifa alizokua nazo na

namna anavyoongoza, akaamua kumpiga vita Hashim na kutaka uongozi aliokua nao

Hashim avuliwe ili apewe yeye ambae ndie anaestahiki kwa sababu uongozi huo ulikua

ni wa baba yake ambae alikua ndie mtoto mkubwa katika familia.

Kutokana na hali hii kila mtu akawa anajua kua Ummayah alikua anataka utawala kwa

sababu ya Nafsi yake kupenda madaraka na hivyo alikua hafai, lakini Hashim alikua

akifaa kwa sababu alikua akiyatumia madaraka kwa ajili ya manufaa ya jamii ya watu

wa Makkah. Hivyo ili kutatua tatizo hili watu wa Makkah wakakutana na kuamua kupiga

kura, kwa masharti kua yeoyote yule atakeshindwa basi itambidi ahame katika mji huo

kwa miaka kumi. Matokeo ya kura hiyo yakaonesha kua Ummayah ameshindwa na hivyo

ikambidi ahame akahamie kaskazini ya Sham kwa miaka kumi halafu ndio arudi, na huu

ndio ukawa mwanzo wa kuwepo kwa upinzani baina ya ukoo wa Banu Hashim na ukoo

wa Banu Umayyah.

Hashim akaendelea kua kiongozi wa mji wa Makkah hadi pale alipofariki ambapo

uongozi wake ukarithiwa na mtoto wake wa kiume aliekua akiitwa Abd ul Muttalib

ambae jina lake halisi ni Shaibatul Al Hamd Ibn Hashim ambae nae alikua ni mtu

aliekulia na kufuata njia za kuongoza kwa uongozi bora ambao uliokuwepo kwa ajili ya

manufaa ya watu wa mji huo. Abd ul Muttalib alikua ni mtu mwenye kukubalika na

kuheshimika katika mji wa Makkah.

Ukoo wa Quraysh ulikua umegawika katika makabila makuu yafuatayo:-

Banu Abd Al Darr - kabila kutoka ukoo wa Quraysh.

Banu Abd Manaf - kabila kutoka ukoo wa Quraysh, ambao lilikua limegawika katika

makabila:-


567

• Banu Nawfal - kabila kutoka ukoo wa Banu Abd Manaf.

• Banu Muttalib - kabila kutoka ukoo wa Banu Abd Manaf.

• Banu Hashim - kabila kutoka ukoo wa Banu Abd Manaf, aliotoka Hashim, babu

yake mkubwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam.

• Banu Abd Shams - kabila kutoka ukoo wa Banu Abd Manaf, wazee wa Banu

Umayyah aliotoka Muawwiyah, Abu Sufyan na Uthman Ibn Affan.

Banu Makhzum - kabila kutoka ukoo wa Quraysh, aliotoka Khalid Ibn Al Walid (Saifu

Allah) na Ikrimah Ibn Abi Hisham.

Banu Zuhrah - kabila kutoka ukoo wa Quraysh, aliotoka Aminah Bint Wahb Ibn Abd

Manaf ambae ni mama yake Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na

Sahaba Sa'ad Ibn Abi Waqqas.

Banu Taym - kabila kutoka ukoo wa Quraysh, aliotoka Abu Bakr.

Banu Adi - kabila kutoka ukoo wa Quraysh, aliotoka Umar Ibn Al Khattab.

Banu Asad - kabila kutoka ukoo wa Quraysh, aliotoka Abd Allah Ibn Al Zubayr na mke

wa kwanza wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, Sayyida Khadijah Bint

Khuwaylid maarufu kama Khadija Al Kubra na pia Khadijah Amiral Qurayshi.

Banu Sahm - kabila kutoka ukoo wa Quraysh, aliotoka Amr Ibn Al Aas.

Banu Jumah - kabila kutoka ukoo wa Quraysh.

Katika kipindi hiki cha utawala wa Abd ul Muttalib, kulikua na baraza la kamati ya

uongozi wa mji wa Makkah uliokua na viongozi wa Quraysh (Sadat Quraysh) ambalo

lilikua ni lenye kuwajumuisha watu wafuatao:-

• Aaes Ibn Waeel (Banu Saham).

• Amr Ibn Hisham au Abu Jahl (Banu Makhzum).

• Abd Al Uzza au Abu Lahab (Banu Hashim).

• Abu Sufyan ibn Harb (Banu Umayyah).

• Akhnas Ibn Shariq (Haleef Banu Aadi).

• Aswad Ibn Mutlib (Banu Asad).

• Hakeem Ibn Huzaam (Banu Asad).

• Matum Ibn Aadi (Banu Nawfal).

• Mughirah Ibn Abd Allah (Banu Makhzum).

• Nabeeha Ibn Hujaj (Banu Jumah).

• Nazar Ibn Harris (Banu Abd Darr).

• Suhayl Ibn Amr (Banu Aamir).

• Umayyah Ibn Khalaf (Banu Jumah).

• Uqba Ibn Mui’t (Banu Abd Darr).

• Utba Ibn Rabi'ah (Banu Abdu Shams).


568


569

NDOTO YA ABD UL MUTTALIB NA KISIMA CHA ZAMZAM

Katika Mchana mmoja wa kipindi cha Kiangazi Siku moja wakati Abd Ul Muttalib akiwa

na umri wa maka 40 kamili basi alilala pembeni ya Al Kaabah kwenye kivuli cha Al

Kaabah basi akajiona kua amesimama kwenye Hajar na mara akasikia sauti ya mtu

asiemjua akiwa karibu yake akimuamrisha ndani ya usingizi wake kwa kusema: ‘Amka

ili upate kuchimba Tayyibah.’ Ambapo Neno Tayyiba maana yake hua ni Kitu Kizuri

chenye Manufaa kutokana na Usafi wake na Uhalali wake. Hivyo Abd ul Muttalib

akauliza: ‘Tayyibah ndio nini?’ lakini hata hivyo Mtu huyo hakumjibu suali hilo na

badala yake akatoweka Abd ul Muttalib akaamka huku akiwa amejawa na masuali

yasiyokua na jawabu akilini mwake, lakini hata hivyo akadharau na kuona kua labda

ilikua ni Adghathi Ahlami yaani ndoto isiyokua na mbele wala nyuma wala maana yeyote.

Lakini hata hivyo siku ya pili alipolala tena katika sehemu hio basi akasikia tena sauti ya

mtu asiemjua akiwa karibu yake akimuamrisha ndani ya usingizi wake kwa kusema:

‘Amka ili upate kuchimba Barra.’ Ambapo Neno Barra hua linamaanisha Kitu Kisafi

na Chenye Baraka. Hivyo Abd ul Muttalib akauliza: ‘Barra ndio nini?’ lakini hata hivyo

Mtu huyo hakumjibu suali hilo na badala yake akatoweka.

Ingwa hakua ni mwenye kujua kwanini anamuota mtu huyo anaemuamrisha kufanya

jambo asilolijua ndani ya Ndoto hizi ya mara ya pili na kisha mtu huyo kutoweka, lakini

amrisho hili la safari hii ya pili lilimfanya Abd Ul Muttalib kua ni mwenye kuamini kua

hizi ndoto zitakua zinamaanisha kua kuna jambo anatakiwa awe analifanya. Lakini hata

hivyo hakuweza kujua ni jambo gani, na kutojua kwake huko kulimpelekea kua ni

mwenye kujiuliza masuali mengi zaidi.

Na hivyo siku ya tatu alipolala tena katika sehemu hio basi akasikia tena sauti ya mtu

asiemjua akiwa karibu yake akimuamrisha ndani ya usingizi wake kwa kusema: ‘Amka

ili upate kuchimba Madnuna.’ Ambapo neno Madnuna maana yake hua ni kitu Kisafi

na chenye Thamani kubwa.

Hivyo Abd ul Muttalib akauliza: ‘Madnuna ndio nini?’ lakini hata hivyo Mtu huyo

hakumjibu suali hilo na badala yake akatoweka. Na tukio hili likamchnganya zaidi kwa

sababu mtu anaemuota hua hamtajii jina moja hilo hilo kila siku bali anamtajia majina

tofauti, na kwanini akilala nyumbani kwake usiku hua haoti ndoto hio, bali hua anaota

akiwa amelala kwenye Al Kaabah? N.k

Na ilipofika siku ya nne basi alipolala tena katika sehemu hio hio basi akasikia tena sauti

ya mtu asiemjua akiwa karibu yake akimuamrisha ndani ya usingizi wake kwa kusema:

‘Amka ili upate kuchimba Zamzam.’ Hivyo Abd ul Muttalib akauliza: ‘Zamzam ndio

nini?’ ambapo safari hii Mtu huyo hakuondoka bali alimjibu kwa kusema: ‘Zamzam ni


570

kisima cha Maji ambayo hayakauki wala hayasiti katika kutiririka kwake.

Kutokana na Maji Haya basi utakua ni mwenye kuweza kuwasaidia Mahujaji kwa

mahitajio yao ya Maji. Kisima kipo baina ya sehemu inayotiririka na kugawanyika

Damu ya Wanyama wa Kafara na baina ya sehemu inayozikwa mabaki ya vichinjo

hivyo. Hii ni sehemu ambayo hua wanakuja Kunguru na kupekua, na katika

sehemu hio kuna jumba la sisimizi pia. ’

Naam majibu haya yalimfurahisha sana Abd ul Muttalib hivyo mara tu baada ya kuamka

alikua ni mwenye kujawa na furaha, kwani kwa mara ya kwanza amepata ufumbuzi wa

tatizo lililokua likimtatiza ndani ya wiki hio nzima, ambao ni nini maana ya amrisho

alilokua akiamrishwa, na bila ya shaka mara kadhaa amewahi kusikia kuhusiana na

Kisima cha Maji ya Zamzam, lakini hakuna hata mtu mmoja ambae alikua ni mwenye

kujua kiko wapi kisima hicho.

Na hii ni kwa sababu katika kipindi cha kutoweka kwake kulitokea mapigano na hivyo

watu wa Banu Jurhum wakawa ni wenye kuukimbia Mji huo na hivyo wakatumbukiza

kila kitu chao ndani ya Kisima cha Zamzam, na kisha wakakifukia Kisima hicho. Hivyo

ilikua inajulikana kua kuna kisma cha Zamzam lakini hakuna anaejua kiko wapi, na hivyo

hii ndoto ilikua ikimbashiria yeye Abd Ul Mutallib kua ndie Mvumbuzi wa Kisima cha

Zamzam na anatakiwa akichimbe tena upya.

Hivyo Abd Ul Mutallib akanyanyuka kutoka katika sehemu aliyokua amelala huku

akitabasam na kuelekaa katika sehemu aliyoelekezwa ndani ya ndoto. Katika kuangalia

kwake sehemu hio basi akamuona Kunguru kwenye sehemu aliyoelekezwa ndani ya

ndoto yake na hivyo akatabasamu zaidi ndani ya Moyo wake, tabasam ambalo

lilionekana wazi juu ya Uso wake na kwenye mng’aro wa Macho yake, alipoisogelea

sehemu hio Kunguru huyo akaruka kuelekea angani na kumuacha Abd Ul Mutallib akiwa

ni mwenye kuizingatia na kuiwekea alama ndani ya ufahamu wake sehemu hio.

Kisha Abd Ul Mutallib akaondoka sehemu hio na akarudi tena siku ya pili yake huku

akiwa na Mtoto wake pekee kwa wakati huo aliekua akiitwa Harith ambae walipofika

katika sehemu hio basi wakaaza kuchimba kimya kimya, huku wakiwawacha watu wa

kabila la Quraysh wakiwa wamejawa na mshangao kutokana na tukio hilo bila ya kujua

nini kinachoendelea. Kwani Abd Ul Mutallib aliamua kulifanya tukio hilo la uchunguzi

kua ni siri kubwa sana, kwa sababu hakutaka wenzake wa kabila la Quraysh wajue juu

ya jambo hilo.

Kwani hii ilikua ni heshima kubwa kwake kama vile ambavyo ilivyokua heshima kubwa

kwa Babu wa Mababu zake alieuvumbe Mji wa Makkah ambae ni Nabii Ibrahim alipokua

pamoja na Mtoto wake Ismail walipokua wakiufukua Msingi wa Jengo la Al Kaabah kwa

ajili kulijenga upya jengo hilo. Hivyo na kwa upande wa Abd Ul Mutallib na Mtoto wake

Harith walifanya jambo lao hilo wakiwa wawili tu la kuchimbua Kisima cha Zamzam


571

Na baada ya kupita mda katika kuchimba kwao eneo hilo la ardhi hio, basi wakaanza

kuona dalili ya Ukuta wa Kisima hicho na hivyo wakazidi kujawa na furaha kua kile

wakitafutacho bila ya kukijua kiko wapi kwa miaka na miaka basi leo hii kimetokea na

kinaonekana dalili zake wazi chini ya macho yao, na hivyo Abd Ul Mutallib akajisikia

akisema: ‘Allahu Akbar… Allahu Akbar’

Ambapo tukio hili la kauli hii lilipelekea watu kusogea karibu zaidi kuona kuna maajabu

gani yaliyotokea, na haukuchukua mda mrefu isipokua Viongozi wengine wa Kabila la

Quraysh wakapata habari hio, hivyo nao haraka wakakimbilia kwenye eneo la tukio hilo,

na walipofika wakamwambia Abd Ul Mutallib: ‘Ewe Abd Ul Mutallib. Hiki kisima ni

cha Babu wa Mababu zetu sote ambae ni Ibrahim, hivyo bila ya shaka sisi pia tuna

haki ya juu ya Kisima hiki cha Zamzam, kwa hivyo nasi tunastahiki kushiriki katika

kukifukua Kisima hiki pamoja nawe.’

Abd Ul Mutallib akajibu: ‘La! Siwezi kukuachieni Mnisaidie kwani hili ni jukumu

langu mimi peke yangu kwani mimi ndie nilieamrishwa na kuoneshwa la kufanya

kwenye eneo hili.’

Ambapo hata hivyo watu hao wa Kabila la Quraysh hawakufurahishwa na Jibu hilo hivyo

nao wakasema: ‘Abd Ul Mutallib hakika wewe ni Mtu ambae hana mtu wa

kumtegemea isipokua huyu Mtoto wako mmoja, hivyo inakuaje unakua na hali

kama hii ya ukaidi wa kubishana na kupingana nasi?’

Bila ya shaka kauli hii ilimhuzunisha sana Abd Ul Mutallib kwani aliona kua tayari

anadharauliwa kutokana na kua na Mtoto mmoja tu hivyo akasema: ‘Kwa hivyo

mnanihukumu sio, kwa sababu niko peke yangu na sina Mtoto zaidi ya huyu

mmoja? Basi hakika mimi nnaapa kua kama Allah Atanijaalia kupata watoto 10

basi nitamtoa mmoja Kafara kwa ajili ya Al Kaabah.’

Ambapo maneno haya yalipotoka kwenye Moyo wake kupitia kwenye ulimi wake

yalikua ni Dua, Kiapo, Dhamira na pia Nadhiri mbele ya watu wake na Mungu wa jengo

la Al Kaabah. Na hivyo tukio hili halikuweza kuishia hapa, kwani hapo hapo akawacha

uchimbaji wake huo na kuwaambia watu hao kua: ‘Kama hamkubaliani nami basi

Mimi nataka tukamtafute mtu ambae atatatua kwa haki juu ya nani mwenye haki

zaidi ya kukifukua Kisima hiki na nataka mzozo huu utatuliwe na mtaalamu wa

Ilm ya kubashiri wa Banu Saad Ibn Huzaym wa Dimashq.’

Hivyo wakuu hao wa kabila la Quraysh wakakubaliana na rai hio na wakaamua kufunga

safari ya kuelekea katika Mji wa Syria katika siku ya pili yake, lakini Allah Subhanah wa

Ta’ala na makadirio yake basi akajalia kua walipofika njiani wakajishtukia kua maji yao

ya akiba waliyochukua yameisha yote, bila ya kujua yameisha ishaje isipokua kwa

wachache tu miongoni mwao ndio ambao waliobakiwa na maji ambayo ni kidogo sana.


572

Hali hii iliwapelekea kukaa na kujadiliana nini cha kufanya kwani hata hivyo hao

wachache waliokua na maji hayo basi walikua na ubinafsi wa kugawana Maji hayo na

wenzao miongoni mwao.

Na hakuna kitu kibaya na hatari zaidi kwa Msafara wa wasafiri wa Jangwani kuliko

kuishiwa na maji kwa msafara huo, hivyo baada ya kujadiliana basi Abd Ul Muttalib

akashauri kua bora kila mmoja achimbe Kaburi lake taratibu kisha aingie ndani yake kwa

ajili ya kusubri kifo chake, kuliko kuendelea na Safari kisha wakafa wote kwa pamoja.

Hivyo watu hao wakakubaliana na rai hio, na kisha wakaanza kujichimbia Makaburi yao.

Lakini ghafla Abd Ul Mutallib akapata wazo bora zaid akilini mwake, na hivyo

akawashauri wenzake kwa kuwaambia: ‘Mimi sasa hivi nadhani kua jambo bora zaidi

ni kutafuta Maji, kuliko kuchimba Makaburi, kwani huenda Allah akatuonesha

Maji.’ Hivyo watu hao wakakubaliana na wazo hilo, na kila mmoja akapanda kipando

chake kwa ajili ya kutafuta Maji, wakatoka Jangwani na kuelekea kwenye eneo la

tambarare, ambapo ghafla Ngamia wa Abd Ul Muttalib akajikwaa na jiwe ambalo nalo

lilipoondoka kwenye sehemu yake ya asili, basi ukatokea mbubujiko wa chemchem ya

Maji chini yake.

Abd Ul Mutallib alipoona mbubujiko huo wa Maji basi hakuamini macho yake, na hapo

hapo akashuka chini kutoka wenye Ngamia wake kwa ajili ya kuhakikisha juu ya kile

kinachoonekana na Macho yake, kama kua ni kweli anayoyaona ni Maji kweli ama la.

Na aliposegelea karibu eneo hilo akaona kua kweli hakua ni mwenye kudanganywa na

kile kilichoonekana na macho yake. Hivyo Abd Ul Muttalib akawaita wenzake kwa

kuwaambia: ‘Njooni Kwenye Maji, kwani Allah ametupatia Maji, kwa ajili yetu na

kwa ajili ya Wanyama wetu.’

Tukio hili la kupatikana kwa maji na Abd Ul Muttalib lilibadilisha mtizamo wa watu wa

Kabila la Quraysh juu ya Abd Ul Muttalib kwani tukio hili limedhihirisha ukubwa wa

Darja yake juu ya yao, na thamani ya ukubwa wa cheo chake juu yao na kukubalika zaidi

mbele yao hivyo wakasema:

‘Ewe Abd Ul Muttalib haka sisi hatuna haja ya kupingana na wewe sasa hivi kwani

umetudhihirishia kua unastahiki kua ndie mchimbaji pekee wa Kisima cha

Zamzam, hivyo tunaahidi kua hatutokusitisha wewe kuchimba Kisima hicho, na

hivyo haina haja ya kuelekea katika mji wa Dimashq kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi

wa lililokua tatizo letu, kwani limeshatatulika hivyo wacha turudi Nyumbani ili

ukaendelee na Uchimbaji wa Kisima cha Zamzam.’

Hivyo msafara huo ukageuza muelekeo wa Safari yao na kurudi nyumbani katika Mji wa

Makkah. Ambapo Imam Al Bayhaqi anasema kua: ‘Waliporudi katika Mji wa Makkah

basi Abd Ul Muttalib akaendelea kujenga Ukuta pembeni ya Kisima cha Zamzam,


573

lakini kuna watu miongoni mwa Wapinzani wake wakauvunja ukuta huo. Hivyo

akaujenga tena upya ukuta huo na kisha akaomba Dua kama alivyoamrishwa

kwenye ndoto kwa kusema: ‘Ya Allah, Hakika Mimi siyahalalishi maji haya kwa

ajili ya Mtu anaetaka kukoga, bali kwa ajili ya wale wanaotaka kunywa tu.’

Kisha akawaita watu wake na kuwataarifu kuhusiana na Ndoto yake, na Dua yake,

na kisha baada ya hapo, ikawa kila mtu anaetaka kufanya Israfu kwenye Kisima

hicho basi hua ni mwenye kuumwa sana badala yake.’

Wakati uchimbwaji au usafishwaji au Ufuwaji wa kisima cha Zamzam ukiwa unaendelea

basi ndani yake mlitolewa vitu vingi sana vya thamani vilivyotumbukizwa hapo kabla

ikiwemo sanamu la Mnyama aina Ghazali (Paa), Mapanga ya Kivita na Ngao za Dhahabu

vyote vikiwa katika hali nzuri kabisa, hivyo Watu wa kabila la Quraysh walipoona vitu

hivyo vya thamani basi wakaona choyo na kuhisi kua Abu Talib atafaidika zaidi. Hivyo

nao wakasema: ‘Ya Abd Ul Muttalib hakika na sisi pia tuna haki juu ya vitu hivi.’

Hivo Abd Ul Muttalib akasema: ‘Kwa hakika nyinyi hamna haki juu ya vitu hivi

lakini hata hivyo hamna tatizo kwani nitakua na huruma juu yenu, kwa kutoa

maamuzi baada ya kucheza bahati nasibu nanyi.’ Watu hao wakauliza: ‘Tutacheza

bahati nasibu gani?’

Abd Ul Mutallib akasema: ‘Tutabahatisha kwa kuangalia matokeo ya kuweka

majina ya kitakachotolewa kwa Hubal, ambapo ndani yake kitakachotolewa

mtakua na Alama mbili kwa ajili ya Al Kaabah. Alama mbili kwa Ajili yangu,

Alama mbili kwa ajili yenu, na Alama mbili kwa ajili ya kukosa sote.’ Na watu hao

wa Quraysh wakakubaliana na Mtizamo wa Bahati Nasibu hio.

Hivyo wakaenda kwa Hubal na kucheza bahati nasibu hio, wakaweka ndani yake alama

zao na matokeo yake Abd Ul Muttalib akashinda, hivyo Ghazali wa Dhahabu akaachwa

ndani ya Al Kaabah, na kisha Abd Ul Muttalib akayayeyusha Mapanga na Ngao za

Dhahabu na kisha akatengeneza pande kama bati la dhahabu kutokana nayo ambalo

akalitumia kwa ajili ya Mlango wa kuingilia ndani ya Jengo la Al Kaabah, na hivyo

akawa ni Mtu wa Mwanzo kulipamba Jengo la Al Kaabah kwa Dhahabu.

Baada ya tukio hilo basi alipita miaka 30 ambayo ndani yake miaka hio basi Allah

Subhanah wa Ta’ala alimjaalia Abd Ul Muttalib kuwa na watoto wengi wa kike na wa

kiume, ambao ni Harith, Hamza, Az Zubayr, Hajl, Al Muqqawwim, Dirar, Abu Lahab

Abd Ul Uzzah, Abu Talib, Abdullah, Al Abbas, Saffiyah, Ummu Al Hakkam Al Baydha,

Umaymah, Arwa na Barah.

Na mmoja miongoni mwao watoto wake hawa basi Abd ul Muttalib alikua akimpenda

sana kwa sababu alikua kua ni mtoto wake ambae ni mtoto wake bora na alie mzuri wa


574

sura na kitabia, mkweli na mwenye busara pia, mtoto huyu alizaliwa mwaka 545 C.E

miaka 25 kabla ya vita vya Tembo na alikua akiitwa Abdullah Ibn Abd ul Muttalib.

ABDULLAH IBN ABD UL MUTTALIB BABA YAKE RASUL ALLAH

SALALLAHU AAYHI WA SALAM

Abd Allah Ibn Abd ul Muttalib alikua ni mmoja kati ya Watoto 10 wa Mzee Abd Ul

Muttalib, ambapo mara tu baada ya kuzaliwa basi alikua na muonekano wenye upekee

unaovutia kwa kila mtu anaemuangalia. Hivyo watu wote wa Mji wa Makkah walikua ni

wenye kumpenda sana Abdullah kutokana na uzuri wa Maumbile na Nuru ya muonekano

wake.

Baada ya Abdullah kua mkubwa kidogo basi Abd Ul Muttalib akakumbuka kuhusiana na

Kiapo na Nadhiri aliyoiweka miaka 30 iliyopita wakati alipokua na Umri wa miaka 40

baada ya kuchekwa kua ana mtoto mmoja tu wakati akiwa anchimba Kisima cha

Zamzam, na kuapa kua kama akijaaliwa kua na watoto 10 basi mmoja atamtoa Kafara

kwa ajili ya Allah.

Hivyo Abd Ul Muttalib akawataarifu watoto wake na kuwaambia kua Mtoto mmoja

miongoni mwao itabidi awe ni mwenye kutolewa kafara kutokana na nadhiri hio

aliyoiweka miaka 30 iliyopita ambayo inabidi kutekelezwa, na bila ya shaka watoto wake

wote hao hawakua ni wenye kupinga juu ya hilo, bali waliuliza: ‘Hivyo Jee itaamuliwaje

kua ni yupi wa kutolewa kafara miongoni mwetu?’

Abd Ul Muttalib akasema: ‘Kila mmoja wenu itabidi achukue Upinde wa Mshale na

kisha auandike jina lake kisha anipe mie’ Hivyo watoto hao wote wakachukua upinde

kila mmoja na wake kisha wakaandika Majina yao na kumkabidhi Abd ul Muttalib, na

kisha wao wakabakia Nyumbani kwa ajili ya kusubiri matokeo ya Bahati nasibu hio,

huku watu wa kabila la Quraysh wakikusanyika mbele ya Hubal na kisha mishale hio ya

Upinde ikawekwa kwa Hubal, na kisha akaamrishwa mtu mmoja miongoni mwa watu

waliouwepo mbele hapo aende akatoe Upinde mmoja kwa Hubbal, mtu huyo alipoutoa

upinde huo na kusoma jina lililoandikwa kwenye upinde huo basi akasema: ‘Abdullah!’

Baada ya kusomwa upinde huo basi Abd ul Muttalib hakuamini masikio yake na hivyo

akamwita msomaji huyo na kumwambia ampe upinde huo ili ausome yeye mwenyewe,

na alipopewa na kuusoma akaona kua umeandikwa Abdullah, na kisha hapo hapo

akajisikia uchungu mkubwa sana kwani alikua akimpenda sana Abdullah kuliko Mtoto

wake yeyote, na si yeye tu peke yake ndie aliekua akimpenda kijana huyo bali Mji Mzima

wa Makkah Ulikua ukimpenda sana kijana huyo. kiasi ya kua bado kidogo Abd ul


575

Muttalib akatae kutekeleza Nadhiri hio, lakini akakumbuka ahadi aliyoiweka mbele ya

Allah na watu wake.

Hivyo Abd Ul Muttalib akageuka na kutoka kwenye Jengo la Al Kaabah kisha akaelekea

Nyumbani huku akiwa ni mnyonge na mwenye huzuni kubwa sana kutokana na

kuvunjika Moyo sana na matokeo ya bahati nasibu hio ya mshale huo, lakini hana budi

kwani lazima atimize nadhiri yake aliyoweka na hivyo alipoingia Nyumbani kwake

akawakuta Watu wa Nyumbani kwake wakiwa ni wenye kumsubiri ili wapate kujua juu

ya matokeo ya Bahati nasibu hio, hivyo nae akasema bila ya kuwatazama Watoto wake

hao kua: ‘Abdullah, Allah amekuchagua wewe kua ni mwenye kutakiwa kutolewa

kafara kwa ajili yake’

Habari hii iliwahuzunisha watu wote wa familia ya Abd Ul Muttalib lakini hata hivyo

haikua ni yenye kumuathiri Abd Allah mwenyewe kwani hata baada ya kusikia Jina lake

basi hakua ni mwenye kua na khofu wala huzuni, hivyo Abd Ul Muttalib akaukamata

mkono wa Abdullah na kisha akatoka nae nje kuelekea nae kwenye Al Kaabah.

Ambapo ingawa Abdullah alikua na maridhio kama ya Nabii Ismail alipoambiwa kua

anatakiwa kutolewa kafara kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala lakini kwa upande wa

watu wa Mji wa Makkah basi walikua ni wenye kujawa na simanzi na hivyo wakamuuliza

Abd Ul Muttalib: ‘Ewe Abd Ul Mutallib, unataka kumfanya nini Abd Allah?’

ambapo nae Abd Ul Muttalib akajibu: ‘Naenda kumtoa kafara kutimiza dhamira

yangu niliyoiweka hapo kabla’

Hivyo wakuu wa Quraysh wakasema: ‘Ewe Abd Ul Muttalib, inakuaje unataka

kufanya jambo hili? Wakati wewe ni mmoja kati ya watu wanaoheshimika katika

Mji huu? Hivi huoni wewe kua ukifanya hivyo basi watu wengine nao watafuata

mfano wako? Na hivyo watu wakiwatoa kafara watoto wao wa kiume basi

hakutokua na Wanaume katika Kabila letu?’

Kutokana na maneno hayo basi watu wote wa Mji wa Makkah wakawa ni wenye

kupingana na mtizamo huo wa Abd ul Muttalib, hivyo Al Mughira Ibn Abd Allah Ibn

Ibn Umar Ibn Makhzum ambae ni Mjomba wake Abdulla akasema: ‘Ewe Abd ul

Muttalib Wallahi, haiwezekani kwako wewe kumtoa kafara Mtoto wako ispokua

kama kutakuwepo na kisingizio kinachokubalika, hivyo hata kama itakubidi wewe

uwe ni mwenye kupoteza mali yetu yote kwa Ajili ya kuokoa Maisha yake basi kwa

hakika kwetu sisi ni bora kupoteza mali yote kuliko kumtoa kafara Abd Allah na

tuko tayari kujitolea kwa ajili yake.’

Kisha wakuu wa Quraysh wakasema: ‘Ewe Abd Ul Muttalib, mchukue Abd Allah na

kisha uende nae katika Mji wa Dimashq, ambapo kuna Mwanamke ambae anaitwa

Arrafa, Mwanamke huyu ni mwenye Hikma na Busara na Mtizamo wa kuona


576

Mbali sana kutokana na Muono wake, na kila Mtu kutoka Mashariki na Magharibi

ya Ardhi hua ni mwenye kuelekea kwake anapokua na Matatizo na ni mwenye

uwezo wa kutibu na kutatua matatizo mbali mbali. Hivyo kama akisema kua mtoe

Kafara Abdullah basi itabidi umtoe lakini akisema kua kuna njia nyengine

itakayotuepusha sisi kutokana na huzuni basi itabidi uitekeleze’

Shauri hili lilimpendezesha sana Abd Ul Muttalib na akaona kua ni bora kufanya kama

alivyoshauriwa na wenzake, hivyo akamchukua Abdullah na kisha wakafunga safari ya

kuelekea Syria kumtafuta Mwanamke huyo atakaewasaidia kutatua mtihani wao huo.

Lakini walipofika katika Mji wa Madinah basi wakapata habari kua Mwanamke huyo

hayuko katika Mji wa Dimashq bali ameelekea kwenye Mji wa Khaybar, hivyo nao

wakafunga safari hadi katika Mji wa Khaybar na kwa bahati nzuri wakakutana na

Mwanamke huyo aitwae Arrafa.

Na walipofika tu basi Abd Ul Muttalib akamuelezea hali ya mkasa wao ilivyokua tangu

mwanzo hadi mwisho na kisha baada ya kumaliza kuelezewa basi Arrafa akamuuliza

Abd Ul Muttalib: ‘Hivi Jee katika ardhi ya Mji wenu hua mnatoa fidya ya Ngamia

wangapi kwa ajili ya Mtu mmoja?’ Abd Ul Muttalib akajibu: ‘Hua tunatoa Ngamia

10’

Hivyo Arrafa akamwambia Abd Ul Muttaliab: ‘Vizuri sana, sasa rudini katika Mji

wenu na kisha katayarishe Ngamia 10, kisha wachukue Ngamia hao na Mtoto wako

kisha nendeni katika sehemu ambayo Mipinde ya Mishare hio hua inatolewa, halafu

muweke Mtoto wako katika upande mmoja na Ngamia 10 Upande mwengine. Kisha

andaa mipinde ya mishare miwili, mmoja kwa ajili ya Mtoto wako, na mwengine

kwa ajili ya Ngamia 10.

Kisha toeni Mshale wa Upinde kama kawaida na kama upinde utakaotolewa

utaonesha kua ni Ngamia basi utawachinja Ngamia na kumnusuru Mtoto, na kama

Upinde ukitoka utakua ni wa Mtoto basi itakubidi uongeze idadi ya Ngamia wa

Kafara hadi pale Mola wako atakaporidhika nawe, na hivyo kila ukitoka Upinde

wa Ngamia basi utawachinja Ngamia, na hivyo kwa njia hii utakua ni mwenye

kumnusuru Mtoto wako na hapo hapo utakua ni mwenye kumridhisha Mola wako’

Na bila ya shaka shauri hili lilimfurahisha sana Abd Ul Mutallib na kumridhisha, na hivyo

haraka sana yeye na Abdullah wakafunga safari kwa ajili ya kurudi katika Mji wa

Makkah. Na alipofika katika mji wa Makkah na kuelezea namna alivyofahamishwa basi

watu wa mji wa Makkah nao wakafurahia na kuunga mkono mtizamo huo.

Hivyo Abd Ul Mutallib akaamua kutafuta Ngamia wekundu wenye bei ghali kuliko wote,

kisha akawachukua Ngamia 10 miongoni mwao, na kisha akamchukua Abdullah na

kumuweka upande wa Hubal, na kisha ikachukuliwa mishale ya mipinde miwili na


577

mmoja ukaandikwa Abdullah na mwengine ukaandikwa Ngamia. Kisha mipinde hio

ikawekwa ndani ya sehemu yake ya kuchaguliwa na kisha akatumwa Mtu akachomoe

Mshale mmoja, na alipochomoa basi ukatoka Mshale ulioandikwa Abdullah.

Hivyo Abd Ul Mutallib akaongeza idadi ya Ngamia hao na kua Ngamia 20, ukawekwa

tena Mshale na kutolea na ulipotolea ukatolewa wa Abdullah tena, hivyo wakaongezwa

Ngamia 10 na wakawa Ngamia 30, ambapo mshale uliendelea kuwekwa na kutolewa

ukiwa na jina la Abd Allah kwa mara 10 hadi ikafikia Idadi ya Ngamia hao kua ni 100.

Ambapo watu wa Mji wa Makkah walikua ni wenye kupigwa na Mshangao sana

kutokana na tukio hili la upekee ambalo halijawahi kutokea kabla yake kwa kutakiwa

kuchinjwa Ngamia wengi zaidi, na pia halijawahi kutokea kwa kutokea Jina hilo hilo kwa

mara 10 mfululizo.

Na jambo la kushangaza basi ni kua baada ya idadi ya Ngamia kutimia 100, basi Mshale

huo ulipotolewa ukawa unaonesha kua na jina la Ngamia na hivyo kumaanisha kua

wanatakiwa wachinjwe Ngamia. Ambapo tukio hili liliwafurahisha sana watu wa Mij wa

Makkah kwani walikua wamepata afueni kubwa sana. Lakini Abd Al Muttalib akasema:

‘La itabidi turudie mara 3 kuhakikisha kua kweli hivyo ndivyo anavyotaka iwe

Allah’, na bila ya shaka ikafanywa kama alivyoamrishwa na mara zote 3 mishare

ikaashiria kua wanatakiwa wachinjwe Ngamia. Hivyo Abd Ul Muttalib akaridhia na

kuamrisha kuchinjwa kwa Ngamia hao 100, na hivyo Abdullah akawa amenusurika na

kutolewa Kafara. Ngamia hao wakachukuliwa hadi katika sehemu ya baina ya Safwa na

Marwa na kisha wakachinjwa na kutolewa sadaka.

Miongoni mwa waliokua wakiangalia tukio hili basi alikuwemo Mwanamke mmoja tajiri

na mwenye Ilm ya Kitabu ambae alikua akijulikana kama Ruqqiya, huyu alikua ni dada

yake Waraqah Ibn Nawfal. Ruqqiya aliwahi kusoma kwenye vitabu kuhusiana na kuja

kwa Mtume atakaetokea mwishoni mwa Dunia, hivyo alipomuangalia Abdullah na Nuru

aliyokua nayo Usoni basi akagundua kua Kijana huyo ana mbegu za Uzazi wa Mtume

huyo aliebashiriwa Vitabuni.

Jambo hili na alama aliyoiona Ruqqiya ilimvutia sana na akaona kua aitumie nafasi

aliyokua nayo kwa ajili ya kubeba mbegu hizo za Mtume huyo kutoka kwa Abdullah

kuingizwa kwenye fuko lake la uzazi kwa kuingiliana kimwili na Abdullah ili yeye awe

ndie mwenye utukufu wa kua ni Mama wa Mtume huyo, lakini hata hivyo

alimpomsogelea Abdullah na kumwambia kua anamtaka na atamlipa Ngamia 100 kama

waliochinjwa kwa ajili yake, basi Abdullah akakataa katakata na kumwambia Ruqqiya

kua:

‘Haram hua ina maumivu makubwa sana, kiasi ya kua hata maumivu ya kifo hua

hayaufikii ukubwa wake, lakini Halali haina maumivu na wala si chungu, hivyo

bora tafuta kile kilicho halali yako, kwani wenye kuamini hua ni wenye kuilinda


578

Imani yao ipasavyo, na haiwezekani kwao kufanya jambo ambalo hua linahesabika

kua ni kujivunjia heshima.’ Na kisha Abdullah akaondoka kurudi nyumbani huku

akimfuata baba yake.

Ambapo kwa upande mwengine basi Hisham Al Kalbi anasema kua: ‘Huyu alikua ni

mwanamke aitwae Fatmah Ibn Murrah na alikua ni mwanamke Mzuri sana na

Msafi miongoni mwa wasafi na mwenye Ilm ya Ahl al Kitab na baada ya kuona

dalili ya Nuru hio kwenye Paji la Uso la Abdullah basi akamtaka kimapenzi lakini

Abdullah akakataa.’

Ambapo Mwanamke huyu alimwambia hivyo Abdullah Ibn Abdul Muttalib kwa sababu

jambo hili lilikua linakubalika katika wakati huo wa enzi za Ujahiliya, kwani

tunapoiangalia mahusiano ya kimapenzi na Ndoa katika wakati wa Ujahiliya basi

tunaona kua kulikua na aina nne za mahusiano ya Ndoa ambazo ni:

1- Mahusiano ya Ndoa ambayo ndio yanayokubalika kwa Kisharia za Kiislam

ambapo Mwanamme anaenda Kumposa Mwanamke kupitia kwa Walii wake

Mwanamke huyo na wanapokubaliana basi yanatolewa Mahari na kufanyika

kwa Ndoa hio.

2- Mahusiano ambayo ilikua Mwanamme asiekua na utukufu kijamii

anamwambia Mke wake, kua nenda kalale na fulani Ibn fulani na kisha Mume

huyo hua si mwenye kumgusa Mke wake huyo hadi atakapohakikisha kua Mke

wake ni Mja mzito kutoka kwa Mwanamme aliemuamrisha aende akalale nae

Mke wake. Na walikua wanafanya hivi kwa sababu ya kuingiza utukufu wa

kizazi ndani ya familia ambayo haina utukufu katika jamii na hivyo kuupata

utukufu huo kutoka kwenye kizazi cha Mwanamme huyo mwenye utukufu

katika jamii.

3- Mahusiano ambayo Mwanamke yeyote anaetaka Mtoto basi anakua na

uhusiano na Wanaume wengi, ambao anaingiliana nao hadi anapata uja uzito

na akishajifungua basi huwaita Wanaume hao na kumchagua anaemtaka

mmoja miongoni mwao kua ndio Baba wa Mtoto wake na hivyo Mwanamme

aliechaguliwa hua hana hiari ya kukataa na wala waliobakia hua hawana uwezo

wa kupinga.

4- Mahusiano ambayo ni ya Mwanamke Malaya ambae hua anaweka bendera

kwenye nyumba yake kuashiria kua anafanya kazi hio, ambapo Wanaume nao

hua ni wenye kuenda kwa Wanawake hao, na kisha Mwanamke huyo

anapopata uja uzito kujifungua basi huitwa wale wote ambao aliigiliana nao, na

kisha anachaguliwa mtu na kuambiwa kua aague kuhusiana na huyo mtoto ni


579

wa nani kati ya watu hao, na anapoaguliwa Mwanamme huyo basi hapo hapo

Mwanamme huyo hua ndio Baba wa Mtoto huyo.

BARAKAH BINT THALABAH UMM AYMAN MAMA MLEZI WA

RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM

Mchana wa siku moja ya mwaka 569 C.E katika Ardhi hio Takatifu ya Mji wa Makka

katika Soko la Mji huo waliwasili Watumwa kutoka Ethiopia na hivyo kua ni wenye

Kuuzwa kwenye soko la Mji huo. Ambapo Miongoni mwa Watumwa hao alikuwepo

Binti mmoja Mwenye asili ya Kiafrika yaani alikua ni Mtu mweusi ambae alikua

akijulikana kwa jina la Barakah Bint Thalabah.

Haijulikani ilikua kuaje mpaka Binti huyu akajikuta yuko Sokoni akiuzwa kama

Mtumwa, ila kinachojulikana ni kua ingawa hii ilikua ni Bahati Mbaya sana kwake Binti

huyu kwa wakati huo, Lakini kutokana na Mipango ya Mbora wa Upangaji na Kukadiria

yaani Allah Subhanah wa Ta'ala basi alikua amelijaalia tukio hili kua ndio sababu ya

Kupanda Darja ya juu ya Binti huyu, kwani alimjaalia kua ni mwenye kutolewa

alikotolewa katika Bara la Afrika na kusafirishwa hadi katika Ardhi Takatifu ya Mji wa

Makkah.

Kwa ajili tu ya kuja kuuzwa na kununuliwa na kutolewa katika Madhila ya Utumwa na

si mtu mwengine yeyote isipokua Kijana Mtanashati, Mzuri wa Kitabia na Kimaumbile

mwenye umri wa miaka 24 aliekua akijulikana kama Abdulla Ibn Abd Al Muttalib ambae

ndie atakaekua Baba yake Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam.

Ambapo katika kipindi hiki ambacho Abdullah Ibn Abd al Muttalib anamnunua Baraka

basi Abdulla alikua bado hajamuoa Mke wake anaeendana nae kwa Utanashati wa

Kimaumbile na Kitabia aitwae Amina Bint Wahb ambae ndie Mama yake Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam.

Na haukuchukua Mda Mrefu tangu Barakah kuingia kwenye Nyumba hio isipokua

Abdullah Ibn Abd Al Mutallib alifikia umri wa kuoa, baba yake Abd ul Muttalib aliamua

kumtafutia Mwanamke bora kisura, msafi kitabia na kikabila alieweza kupatikana katika

mji wa Makkah kwa wakati huo, na Mwanamke huyo alipatikana kutoka katika kabila la

Banu Zuhra ambapo kulikua na Mwanamke aitwae Aminah Bint Wahb Ibn Abd Manaf.

Hivyo hii inamaanisha kua Barakah aliingia katika Nyumba ya Abdullah Ibn Abd

Muttalib kabla ya Kuingia kwa Amina Bint Wahb katika Nyumba hio. Ila sasa Barakah

alikua ni Mfanyakazi pekee wa Nyumba hio.


580

Hivyo Barakah akawa ni Mfanyakazi pekee na Rafiki wa Karibu wa Amina Bint Wahb

yaani mama yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na pia akawa ni Mtu ambae ni

rafiki yake wa karibu sana Amina Bint Wahb.

AMINAH BINT WAHB MAMA MZAZI WA RASUL ALLAH

SALALLAHU ALAYHI WA SALAM

Abd Ul Muttalib alipompata Bint huyo aitwae Amina Bint Wahb na kuridhika nae basi

akamwambia Wahb Ibn Abd Manaf ambae alikua ni Chifu wa kabila la Banu Zuhra kua

anataka kumpa posa ya Aminah kwa ajili ya Mtoto wa wake Abdullah, ambapo Wahb

Ibn Abd Manaf akasema:

‘Ewe Ibn Ami wangu, hakika sisi tumeshapokea Posa yako kabla yako, kwani

Mama yake Amina alipolala juzi usiku aliota kua kuna Nuru imeingia ndani ya

Nyumba yetu na kisha ikamurika Ardhini na Mbinguni kote, na mimi jana Usiku

nimemuota babu yetu Ibrahim ambae alikua akiniambia kua: ‘Hakika mimi

Nimemuozesha Abdullah Ibn Abd Ul Muttalib kwa Binti yako Amina, hivyo

atakapokuja basi ipokee Posa hio, na kutokana na ndoto hio basi nimekua najiuliza

tangu asubuhi leo nilipoamka Jee utakuja wakati gani? Na ndio umekuja’’ ambapo

baada ya kusikia habari hio basi Abd Ul Mutallib akasema: ‘Allahu Akbar! Allahu

Akbar!’

Hivyo Harusi hio tukufu ya watoto wa Machifu wawili wa Makkah Abd ul Muttalb na

Wahb Ibn Abd Manaf, ambao ni Abd Allah ambae alikua na umri wa miaka 24 na

Aminah ambae alikua na umri wa miaka 20 ikafanyika na watu wa Mji wa Makkah

wakafurahika sana. Hii ilikua ni harusi ambayo ilibadilisha Muelekeo wa Dunia kama

ilivyobashiriwa na ndoto ya Mama yake Amina Bint Wahb, kwani ndio ndoa ambayo

ndani yake alizaliwa Kiumbe bora kuliko viumbe wote, kiumbe ambae ni mwenye

jukumu la kuitoa Dunia kutoka kwenye kiza cha ujinga wa kutomjua Mola wao na

kuiingiza kwenye Nuru ya Dini ya Kiislam.

Siku kadhaa baada ya kufungwa Ndoa hii, basi Abdullah akakutana tena njiani na yule

mwanamke aiwate Ruqqiyah ambae alimtaka Abdullah, lakini cha kushangaza ni kua

safari hii Ruqqiyah hakua ni mwenye kumjali wala kumpapatikia Abdullah, hali hii

ilimshanganza sana Abdulla na hvyo akamuuliza Ruqqiya: ‘Imekuaje? Umepona ile

hali yako uliyokua nayo hapo kabla baada ya kuniona au?’

Ruqqiyah akajibu: ‘Naam katika siku zile uliua na Nuru kubwa sana Ambayo ilikua

imetapakaa kwenye paji lako la uso, na hivyo ilinichanganya sana kwa uzuri wake,

na uzuri wa muonekano wako, lakini sasa hivi ile Nuru siioni tena, imetoweka sijui

imeenda wapi’.


581

Kwani ni kweli Ruqqiya alikua haioni tena ile Nuru iliyokua kwenye paji la uso la

Abdullah kwa sababu Nuru ili ilikua tayari imeshahama kutoka kwa Abdullah na

kuhamia kwa Amin Bint Wahb ambae ndie aliembeba Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam ndani ya Tumbo lake la Uzazi.

Ambapo anasema Baraka kua: ‘Wiki mbili baada ya Abdullah Ibn Abd Al Muttalib

na Amina Bint Wahb kuoana basi jioni Moja alikuja Abd Al Muttalib na

kumtaarifu Abdullah kua ajitayarishe na Msafara wa Kibiashara unaoelekea

katika Ardhi ya Sham’

Taarifa hii ilimhuzunisha sana Amina kiasi ya kua alikua akilia huku akisema: ‘Itakuaje,

Itakuaje Mume wangu ndio kwanza tumeoana halafua anafunga safari kuelekea

Sham wakati mimi hata hina yangu ya harusi haijafutika kwenye Mikono yangu?’

Hivyo wakati ulipowadia wa Masafara wa Sham kuondoka basi Amina Bint Wahb

alianguka chini na kuzimia, kutokana na kua hali ya mapenzi ya kweli yaliyokuwepo

baina ya Abdullah Ibn Abd Mutallib na Amin Bint Wahb ambao ndio Baba na Mama wa

Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam.

Ambapo kwa upande mwengine basi Baraka anaendelea kusema kua: ‘Hakika mimi

nilipomuona Amina ameanguka chini na Kuzimia basi nililia kwa uchungu na

kusema: Masikini Sayyidati wangu’

Naam.. Baraka anaendelea kutuambia kua: ‘Niliposema Masikini Sayyidati wangu,

basi Amina akaufungua macho yake, akaniangalia huku machozi yakiwa

yanamtiririka na huku akijizuia kwa maumivi ya huzuni akasema: ‘Nipeleke

Kitandani Ewe Barakah’

Hivyo Amina akakaa Kitandani kwa mda Mrefu na kutokana na huzuni yake basi alikua

hazungumzi na mtu yeyote na wala hamuangalii mtu yeyote ambae anaekuja

kumtembelea na kumtizama hali yake isipokua Mzee Abd Ul Muttalib.

Kwani Barakah anaendelea kutuambia kua: ‘Miezi miwili baada ya Kuondoka

Abdullah, basi siku moja asubuhi Amina aliniita mimi na nilipomkaribia nikaona

kua uso wake Unang'ara kwa Nuru ya furaha kisha akaniambia:‘Ewe Barakah!

Hakika mimi usiku wa kuamkia Leo hii nimeona ndoto inayostaajabisha Sana’’

Baraka anasema: ‘Nami nikasema Itakua Ndoto inayobashiria wema Ewe Sayyidati

wangu.’


582

Baraka anaendelea kusema kua: ‘Amina akasema kua, Hakika mimi nimeona kwenye

Ndoto kua Kuna Nuru imetoka Tumboni mwangu na kisha Ikamurika na kutia

Nuru Milima yote na Mabonde yanayozunguka Mji wa Makka na nje yake’

Baraka anaendelea kusema kua: ‘Mimi nikamuuliza Amina: Jee hii inamaanisha kua

Unahisi kua una Uja uzito ewe Sayiddati Wangu?’

Hivyo Amina akajibu: ‘Naam, nna ujauzito ila sasa sihisi kama wanavyohisi

Wanawake wengine, kwani mimi nahisi kawaida tu’

Baraka akasema: ‘Ewe Sayyidati Wangu, Ama kwa Hakika Utapata Mtoto mwenye

Baraka kubwa sana na mwenye kuja na kila Jema na kheri ndani yake’

Kwani hii Ndoto ndio iliyokua ikibashiria kuzaliwa kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam, ambapo katika wakati huu wa kipindi chote hiki ambacho Abdullah Ibn Abd

ul Muttalib akiwa hayupo basi Amina Bint Wahb aliendelea kua na Huzuni kutokana na

kua mbali na Mumewe kipenzi.

KIFO CHA ABDULLAH NA KUZALIWA KWA RASUL ALLAH

SALALLAHU ALAYHI WA SALAM.

Hata hivyo ujauzito huo haukumtia wasiwasi wala kumletea matatizo yoyote, kwani mara

kwa mara ilikua usiku akilala usingizini humuona mtu anakuja na kumpa habari njema

za kile kilichokuwemo ndani ya tumbo lake la uzazi. Mara moja alipokua amelala

usingizini mtu huyo alimwambia ‘Una ujauzito wa kiongozi na Nabii wa Ummah

huu’, na karibu ya kujifungua akamwambia tena ‘Sema baada ya kujifungua sema ‘Ya

Allah, mlinde mtoto huyu kutokana na ubaya wa kila chenye ubaya’, halafu mpe

jina la Muhammad’.

Hivyo jukumu la kumliwaza na kumuondolea Mawazo hayo ya Kumfikiria na

Kumkumbuka Mumewe halikua chini ya usimamizi wa mtu yeyote yule lilikua chini ya

Baraka kwani Barakah ndie aliekua mtu wa karibu nae sana na hivyo alikua akijaribu

kumzungumzisha na kumchangamsha Aminah bint Wahb.

Jambo lilimsaidia Aminah katika wakati wa Mchana lakini kila inapoingia wakati wa

Usiku na kulala basi Aminah alikua akiweweseka Usingizini huku akitaja jina na

Mumewe kama anavyosema Barakah: ‘Katika kipindi hiki mimi nilikua nalala chini

ya Miguu yake Sayyidat wangu, na nilikua nikimsikia Usiku akinung’unika na

kuweweseka huku akilitaja jina la Mumewe ambae alikua hayupo, Kilio chake na

Kuweweseka kwake kulikua kunaniamsha Usiku na hivyo kunifanya niwe ni


583

mwenye kujaribu kumliwaza na kumtuliza na kumpa nguvu kutokana na hali

aliyokua nayo.’

Kwani katika kipindi hiki ndio Jeshi la Tembo la Abraham ambae aliekua Mfalme wa

Yemen alipoamua kuenda katika Mji wa Makkah kwa ajili ya Kulivunja Al Kaabah. Hii

ilikua mnamo mwaka huo huo wa 570, katika ardhi ya nchi ya Yemen iliyokua iko chini

ya utawala wa Mfalme wa Kikristo wa Abisinia (Ethiopia), mfalme huyu alikua na

Gavana wake anaesimamia eneo la Yemen ambae alikua anajulikana kwa jina la Abraha

Al Ashrah.

Abraha aliamua kuenda katika mji wa Makkah na jeshi la watu 60,000 pamoja na Tembo

13 ili kuivunja Nyumba tukufu ya Al Kaa’bah baada ya kujenga katika mji wake kanisa

refu na zuri kwa ajili ya kuwavuta zaid watu waliopo karibu na eneo analolitawala ili

waache kuenda Makkah katika Nyumba tukufu ya Al Ka’abah na badala yake waende

kuabudu katika Kanisa hilo, lakini hata hivyo watu wa Yemen walikataa kufanya hivyo

kwani woao taari wameshazoea kufanya Ibada ya Hija katika Mji wa Makkah, na badala

yake wakasubiri usiku kisha wakalitia Moto Kanisa hilo, hivyo akaona hakuna njia

nyengie isipokua kulibomoa Al Ka’abah.

Abrahah alipofika katika viunga vya mji wa Makkah, akapiga kambi na kisha akatuma

jeshi lake liende kuteka mali zote zilizokuwemo katika mji huo, na miongoni mwa mali

zilizotekwa walikuwemo Ngamia 200 wa Abd Ul Muttalib ambae ndie aliekua kiongozi

wa mji wa Makkah. Halafu akatuma wajumbe wenye ujumbe usemao kua hawakuja

kupigana vita bali wamekuja kwa nia ya kuibomoa nyumba ya Al Ka’abah, hivyo ikiwa

watu wa Makkah watamuachia aibomoe nyumba hiyo basi, itakua hakuna matatizo

ataibomoa halafu ataenda zake na jeshi lake, lakini ikiwa hawatomuachia kutimza nia

yake hio basi wajitayarishe na vita, na majibu ya ujumbe huo inabidi yatolewe na

kiongozi wa mji huo mbele ya Abraha tena kwa mdomo wake, hivyo ikabidi Abd ul

Muttalib aongozane na mjumbe huyo hadi kwa Abraha, kutoa jibu.

Na mara Mjumbe alipofika basi Abd ul Muttalib akamwambia mjumbe wa Abraha: ‘Sisi

hatuna nguvu wala uwezo wa kupigana na Abraha, na hii ni nyumba ya Allah, hivyo

kama Allah akitaka basi ataiepusha na msiba nyumba yake’ yule mjumbe

akamwambia Abd ul Muttalib kua itabidi amchukue ampeleke kwa Abraha ili ampe

mwenyewe ujumbe huo, hivyo wakaongozana hadi kwa Abraha, walipofika Abraha

akamuuliza Abd ul Muttalib ‘Unasemaje?’, Abd ul Muttalib akajibu ‘Nilikua nataka

unirudishie Ngamia wangu’

Abraha akacheka na kumwambia Abd ul Muttalib ‘Nilipokuona nilivutiwa nawe na

kukuheshimu, na nnajua namna watu mbali mbali wanavyokuheshimu lakini jibu

lako limekushusha hadhi mbele ya macho yangu: Yaani wewe unajali Ngamia wako


584

tu? Lakini husemi chochote kuhusiana na nyumba yenu tukufu ambayo

mnayoitukuza tangu enzi za mababu zenu?’.

Abd ul Muttalib akajibu ‘Mimi ni mmiliki wa hao Ngamia tu, hivyo nakuomba

unirudishie Ngamia wangu, ama kuhusiana na nyumba takatifu, basi nayo pia ina

mmiliki wake: Hivyo mmiliki wake atailinda yeye mwenyewe nyumba yake’.

Abd ul Muttalib akapewa Ngamia wake, na alipofika kwa watu wake akawaambia watu

wake waondoke wakakae mbali ili wasije wakaangamizwa au kudhuriwa na watu wa

Abraha mara tu baada ya Abraha kuivamia Al Ka’abah, na kisha akaenda katika Al

Ka’abah, na kusema ‘Ya Allah, mtu huilinda nyumba yake, hivyo nawe ilinde

nyumba yako, usiiwachie misalaba yao na ujuzi wao kuuzidi ujuzi wako, na ikiwa

unataka kuwaachia kufanya wanavyotaka basi ni hiari yako kuwaachia wafanye

watakavyo’, na kisha baada ya hapo akawachukua watu wake na kutoka nje ya mji wa

Makkah.

Tukio hilo liliwashtua wengi sana akiwemo Amina Bint Wahb ambae alikua na uja Uzito

wa Miezi kadhaa lakini Amina Bint Wahb akamwambia Abd Al Muttalib kua kwa hali

aliyokua nayo basi haina haja kwake yeye kutoka kwenye Mji huo kwani ana uhakika

kua Abrahah hatoweza kulivunja Al Kaabah kutokana na kua ni lenye kulindwa na Allah.

Ambapo kama alivyokua akihisi Aminah Bint Wahb ambae ndani ya tumbo lake alikua

amembeba Kiumbe Mtukufu ambae ni Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kua

Abraha hatofanikiwa kuingia katika Mji wa Makkah kutokana na Uangalizi wa Allah juu

ya Ardhi hio kutokana na utukufu wake, basi Jeshi la Abraha halikufanikiwa kuingia

kwenye ardhi hio.

Kwani Siku ya pili asubuhi Abraha na jeshi lake, wakajitayarisha kuelekea katika Al

Ka’abah lakini Tembo wao mkubwa ambae alikua akifuatwa na tembo wengine kila

akielekezwa kuelekea upande wa Al Ka’abah basi hugoma kuelekea huko, lakini

wakimgeuzia upande mwengine basi huelekea upande huo na kutaka kuondoka, hivyo

watu wa Abraha nao wakawa kila akianza kuondoka basi haraka humgeuzia upande wa

Al Ka’abah na hapo Tembo huyo kukaa chini na hugoma kabisa kunyanyuka badala yake.

Tembo huyo alipigwa na kufanywa kila kitu ili anyanyuke aelekee upande wa Al Ka’abah

lakini wapi.

Na mara ghafla likatokea kundi kubwa la ndege weusi ambao midomoni mwao na

kwenye kucha zao walikua wamechukua kokoto, na hapo ikaanza kunyesha mvua ya

kokoto, kokoto hizo hazikua kokoto za kawaida bali zilikua ni kokoto za mawe ya motoni

(Sijjil), na kila ndege alikua amekuja maalum kwa ajili ya mtu wake, ikawa hakuna kwa

kukimbilia wala kwa kujificha na kila mtu anaeguswa na kokoto hiyo, basi huanza


585

kumomonyoka sehemu mbali mbali za mwili wake, kwa kuanza kuachia kwa ngozi yake

na nyama huanguka na damu kuanza kumwagika kama vile inavyomwagika chem chem

ya maji, hii ni hali ambayo liendelaea hadi jeshi la Abraha likaangamia lote na kua kama

‘a`Asf, Ma'aakul’ yaani chakula kilichotafunwa tafunwa na kisha kikatemwa. Allah

Subhanahu wa Ta’ala anatuhadithia kisa hiki katika Qur’an kwa kusema:

‏﴿أَلمَْ‏ تَرَ‏ كَيْفَ‏ فَعَلَ‏ رَب ُّكَ‏ أبَِصْحَبِ‏

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ‏

ٱلْفِيلِ‏ ‏۞أَلمَْ‏ يجَْعَلْ‏ ‏َكيْدَهُمْ‏ فىِ‏ تَضْلِيلٍ‏ ۞ وَأَرْسَل

َ

عَلَيْهِ‏ مْ‏ طَيرْ‏ اً‏ أَابَ‏ بِيلَ۞تَرْمِيهِم بحِِجَارَةٍ‏ مِّن سِ‏ جِّ‏ يلٍ‏ ‏۞فَ‏ ‏َجعَلَهُمْ‏ كَ‏ عَصْ‏ فٍ‏ م َّأْكُولِ‏ ﴾

Bismillahi Rahmani Rahim.

Alam tara kayfa faAAala rabbuka bi-as-habi alfeeli; Alam yajAAal kaydahum fee

tadhleelin; Waarsala AAalayhim tayran ababeela; Tarmeehim bihijaratin min

sijjeelin; FajaAAalahum kaAAasfin ma/koolin (Surat Al Fil 105:1-5)

Tafsir: Jee umeona namna gani Mola wako alivyowafanyia watu wa Tembo, Jee

hakuwafanyia mipango yao kua ni yenye kudhalilika, Na akawashushia dhidi yao

ndege kwa makundi (Ababil). Kuwapiga kwa mawe ya Sijjil, na akawafanya kua kama

(`Asf, Ma'kul).

Kutokana na kisa hiki, Waarabu wakawa wanauita mwaka huu wa 570 kua ni A’m al Fil

yaani Mwaka wa Tembo. Mwaka ambao Allah Subhanahu wa Ta’ala aliiokoa Al

Ka’abah kutokana na madhara ya watu wenye jeshi la Tembo na pia akawaokoa watu wa

ukoo wa Quraysh kutokana na madhara ya Watu wa Tembo ambao walikua na nia ya

kuliangamiza Al Ka’abah.

Hivyo baada ya tukio hilo la kuangamizwa kwa Jeshi la Abraha na Tembo wake, basi

haukuchukua mda mrefu isipokua Msafara wa kwanza kutoka Sham uliwasili katika Mji

wa Makkah. Na Barakah alipopata habari tu ya kuwasili kwa Msafara huo basi haraka

sana akakimbilia katika Nyumba ya Mzee Abd Al Muttalib ili kupata habari za Bwana

wake yaani Abdullah kwa ajili ya kumpelekea Sayyidati wake yaani Aminah.

Lakini kwa siku hio hakupata habari yeyote hivyo akarudi kimya kimya kwa Amina Bint

Wahb bila ya kumwambia chochote kutokana na kuogopa kumzidishia Machungu

Sayyidati wake.


586

Lakini baadae Barakah akaenda tena kwa Abd Al Muttalib na hapa sasa ndio akapata

habari kua Abdullah amefariki njiani. Ambapo anasema Barakah kua: ‘Nilipopata

habari hio, Nilipiga Ukelele na kisha sijui kilitokea nini kwani Nilikimbia kwa kasi

sana hadi kwa Aminah huku nikilia, na Kupiga Makelele kua alieenda Safarini,

anaesubiriwa kwa Hamu hatorudi tena’

‘Amina aliposikia habari hizo nzito basi alizimia tena nami nikawa ni mwenye

kukaa nae ubavuni mwa kitanda chake huku akiwa katika hali ya Nusu hai nusu

mfu hakukua na Mtu yeyote ndani ya Nyumba ya Amina isipokua mimi.’

‘Hivyo nilikaa nae Usiku na mchana na Kumuuguza mpaka alipojifungua Mtoto

wake ambae ni Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam katika Usiku ambao Mbingu

zilikua zinameremeta kwa Nuru ya Allah na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alipozaliwa basi mtu wa mwanzo kumbeba Mikononi mwake alikua ni Mimi’

(Barakah).

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala analitaja tukio hili la kuja kwa Rasul Alah Salallahu

Alayi wa Salam kwenye Qur’an pale aliposema:

﴿َ أَهْلَ‏ ٱلْكِتَابِ‏ قَدْ‏ جَآءَكُمْ‏ رَسُولُنَا يُبَينِّ‏ ُ لَكُمْ‏ كَثِيراً‏ ممِّ َّا كُنْتُمْ‏ تخُْفُونَ‏ مِنَ‏ ٱلْ‏ كِتَابِ‏

وَيَعْفُواْ‏ عَن كَثِيرٍ‏ قَدْ‏ جَآءَكُمْ‏ مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏ نُورٌ‏ وَكِتَابٌ‏ م ُّبِينٌ۞يَْهدِى بِهِ‏ ٱهلل َُّ‏ مَنِ‏ ٱت َّبَ‏ ‏َع

رِضْوَانَهُ‏ سُبُلَ‏ ٱلس َّلاَمِ‏ وَيخُْرِجُهُمْ‏ مِّنَ‏ ٱلظ ُّلُمَاتِ‏ إِلىَ‏ ٱلن ُّورِ‏ إبِِذْنِهِ‏ وَيَهْدِيهِمْ‏ إِلىَٰ‏ صِرَاطٍ‏

م ُّسْتَقِيمٍ‏ ﴾

Ya ahla alkitabi qad jaakum rasooluna yubayyinu lakum katheeran mimma

kuntum tukhfoona mina alkitabi wayaAAfoo AAan katheerin qad jaakum mina

Allahi noorun wakitabun mubeenun; Yahdee bihi Allahu mani ittabaAAa

ridwanahu subula alssalami wayukhrijuhum mina aldhdhulumati ila alnnoori biidhnihi

wayahdeehim ila siratin mustaqeemin (Surat Al Maidah 5:15-16)

Tafsir: Enyi watu wa Ahl Al Kitab amekujieni Mtume mwenye kubainisha juu yenu

mengi mliyokua mkiyaficha katika Kitabu ijapokua hayatilii maanani mengi sana

(mliyoyaficha) kwa hakika Imekujieni kwenu Nuru na kitabu chenye Mabainisho.

Ambavyo anawaongozea Allah wale wakataofuata njia yake ya usalama, na kuwatoa

kutoka kwenye kiza kuwaingiza kwenye Nuru kwa idhini yake na kuwaongoza katika

njia iliyonyooka.


587

Ambapo aya hizi zinawazungumzia Mayahudi waliokua ni wenye kujaribu kuuficha

ukweli kuhusiana na yaliyoandikwa kwenye vitabu vyao juu ya ukweli wa vithibitisho

vya kuja kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambapo ndani yake aya hizi pia

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amewakilishwa na kunasibishwa na Nuru ya

Uongofu wa kuwatoa watu kwenye kiza cha kutofuata njia sahih ya kimaumbile

tuliyumbiwa Ibn Adam na kuwarudisha kwenye njia sahih iliyonyooka.

Hivyo baada ya tukio hili la kuzaliwa kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

lilitokea kwenye Nyumba ya Abu Talib katika mwezi 12 Rabi Al Awwal ya mwaka wa

Tembo, ambapo ni sawa na tarehe 8-6-570, na mkunga wake aliemzalisha alikua ni

Ashifa Bint Awf ambae ni mama yake Abd Rahman Ibn Awf, baada ya kuzaliwa kwake

akaitwa Babu yake yaani Abd ul Muttalib akamchukua na kumpa jina alilobashiriwa

Aminah Bint Whab yaani Muhammad.

Baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuzaliwa basi alinyonyeshwa kidogo

na Mama yake halafu akachukuliwa na kupelekwa kwa Bi Thuwayba ambae ndie aliekua

Mnyonyeshaji wake na mlezi wake wa pili baada ya Baraka ambae yeye kwa wakati huu

alikua ni mwenye kubakia na mzazi yaani Amina Bint Wahb.

THUWAYBAH AL ASLAMIYAH MAMA MNYONYESHAJI WA PILI

WA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM

Ni kawaida kwa desturi za Waarabu kua inapopatikana habari njema au nzuri basi watu

hua ni wenye kuonesha Ukarimu na Shukuran, hivyo katika siku aliyozaliwa Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam basi Thuwaybah ambae alikua ni Mtumwa wa Ami yake

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae aliekua akiitwa Abd Al Uzza Ibn Abd Ul

Muttalib maarufu kama Abu Lahab ambae alikua pia na mtoto wake aitwae Masruh

ambae ndie aliekua akimnyonyesha, hivyo Thuwaybah alipopata habari ya kuzaliwa kwa

Rasul Allah Salal Alayhi wa Salam basi alikimbilia kwa Bwana wake na kumpa habari

hio kwa kusema: ‘Hivi Jee umesika kua, Aminah amejifungua Mtoto wa kiume?

Kwa Ajili ya ndugu yako Abdullah?’

Hivyo baada ya kupokea habari hio basi Abu Lahab kutokana na furaha yake basi

akasema kumwambia Thuwaybah kua: ‘Nenda kwani kwa hakika nimekuachia Huru’

na hivyo baada ya hapo Thuwaybah akamnyonyesha kwa muda Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam.

Ambapo Thuwaybah alikua pia ni mwenye kumnyonyesha Abu Salamah Ibn Abd Al

Asad Radhi Allahu Anhu na pia alimnyonyesha Hamza Ibn Abd Ul Muttalib Radhi Allahu


588

Anhu ambae ni Ami yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo pia nae akawa

ni Ndugu yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa upande wa Unyonyweshaji.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Abu Fadhl Ibn Hajjar Al Asqalani kua:

‘Thuwaybah ambae ni Mtumwa alieachiwa huru na Abu Lahab na ametajwa na

Ibn Mandah kua ni miongoni mwa Masahaba, lakini kuna tofauti baina ya

mitizamo, kuhusiana na kama alikua Ni Muislam ama la. Kwani Abu Nuaym

Amesema kua: ‘Hatujui sisi kua kama alisilimu na kua ni Muislam ama la, bali kile

kinachosemwa kwenye Vitabu vya Historia ya Kiislam ni kua Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alikua akimheshimu na akimtembelea baada ya kumuoa Bi

Khadija, na alikua akimtumia zawadi kutoka katika Mji wa Madinah na baada ya

kutekwa kwa Mji wa Khaybar basi alifariki Dunia na kama alivyofariki mtoto wake

Masruh.’’

Ambapo maana ya maneno yasemayo kua Abu Lahab alimuacha huru na

akamnyonyesha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam yanamaanisha kua

alimuachia huru kabla ya kumnyonyesha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam,

lakini kile kilichoandikwa kwenye Vitabu vya historia vinaonesha kua hali ni

kinyume chake, ambacho ni kua Abu Lahab alimuachia huru kabla ya Hijra

ambalo hili ni tukio lililotokea mda mrefu baada ya kumnyonyesha Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam, na As Suhayl amesema kua Kuachiwa huru kwake

kulitokea kabla ya kumnyonyeha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambapo

maneno ya As Suhayl yanasema kua:

‘Al Abbas amesema kua, Wakati Abu Lahab alipofariki, basi mimi nilimuona

kwenye ndoto mwaka mmoja baadae hukua kaiwa na hali mbaya kabisa, nae

akasema: ‘Hakika mimi sijapata utulivu kutokana na Adhabu ambayo hua haisiti

isipokua katika siku ya Jumatatu.’ Na hii ni kwa sababu Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alizaliwa siku ya Jumatatu na Thuwaybah alimpelekea habari hizo

Abu Lahab ambae nao akamuachia huru Thuwaybah’’

Hata hivyo hapa inabidi tujue kua kwa Upande wa Shaykh Ul Islami Al Hafidh Imam

Ahmad Ibn Muhammad Al Qastallani, yeye anasema kuhusiana na riwaya hii kua:

‘Kuhusiana na Kauli hii kua kama inaweza kutumika kama uthibitisho wa kua Mtu

asiekua Muislam anaweza akawa ni mwenye kulipwa wema wake baada ya kufariki

kwake, basi kama ingekua hakuna muunganishi anaejulikana katika hadithi hii,

basi hii ingekua haina nguvu kuhusiana na hukumu iliyopo kuhusiana na kulipwa

kwa wasiokua Waislam baada ya kufariki kwao, ila hadith hii, ina muunganiko

mzuri na inakubalika.


589

Lakini hata hivyo, Ndoto hua haiwezi kutumika kua kama uthibitisho wa

kubadilisha maana au kuathiri hukumu ya kisharia hususan pale inapokua

inapingana na Qur’an kama inavyoonesha katika hadithi hii, na hivyo inawezekana

ikawa adhabu iliondolewa kwa Abu Lahab peke yake kutokana na tukio la

kumuchia huru Thuwaybah katika siku aliyozaliwa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam’(Imam Al-Zurqani, Sharh Mawahib Laduniya)

Mujaddid Ad Din Imam Abu Fadhl Ibn Hajjar Al Asqalani basi yeye anasema kua:

‘Hakika haya yaliyotokea yametokea kutokana na Rehma za Allah kutoka na

Ukubwa wake na Uwezo wake juu ya wale wasiomuamini kutokana na Ukarimu

wao kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, w Aallahu Aalam.’(Fat-h Al Barr)

Hivyo basi Thuwayba alimnyonyesha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kua

mlezi wake kwa mda wa wiki moja, hadi pale katika Mji wa Makkah alipowasili

Mwanamke wa Banu Bakr aitwae Halimah Bint Abi Dhuab Abdullah Ibn Al-Harith Ibn

Shaghna Ibn Jabir Ibn Razam Ibn Nasera Ibn Fasiya Ibn Nasr Ibn Sa’ad Ibn Bakr Ibn

Hawazin Ibn Mansour Ibn Ikramah Ibn Khasfah Ibn Qays Ibn ‘Ilan marufu kama

Halimah Al Saadiah.

HALIMA BINT ABU DHUAYB AL SADIYA MAMA

ALIEMNYONYESHA WA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA

SALAM

Hali ya hewa ya Mji wa Makkah ilikua ni ya Joto sana na yenye nyevu nyevu, hivyo

ilikua si hali ya hewa yenye mandhari mazuri kwa afya ya ukuaji wa Watoto. Ambapo

hali ilikua tofauti katika maeneo ya Jangwani kwani kulikua na mazingira ya Utulivu,

urahisi wa Maisha na pia usafi wa kimazingira, na watu waishio Majangwani nje ya Miji

hua na Utamaduni mzuri Lugha asilia na tabia njema zaidi kuliko watu wa Mjini.

Hivyo hali hii ya utofauti wa kimazingira uliwapelekea watu wa Mji wa Makkah wenye

uwezo wa kimaisha na Darja kua ni wenye kuwatafutia watoto wao wanyonyeshaji wa

maalum wan je ya Mji ambako hua ni wenye kukaa na watoto wao hao hadi kipindi cha

kumaliza kunyonya cha miaka miwili au zaid na hivyo watoto hao hua na afya njema

zaidi na miili imara zaidi kutokana na maziwa yenye afya zaidi ya wanyonyeshaji hao.

Miongoni mwa wanawake wa Makabila ya watu wa Jangwani wanaosifika kwa umaarufu

wa kazi kama hizo za kunyonyesha Watoto walikua ni Wanawake wa Kabila la Said Ibn

Bakr ambao walikua wanaishi upande wa kaskazini nje ya Mji wa Makkah, kwani hawa

walikua ni watu ambao ni wenye kuheshimika sana kutokana na Utamaduni wao, Tabia


590

zao, Lugha yao, Unyenyekevu wao na Ukarimu wao, na hivyo wengi miongoni mwa

Watu wenye Darja wa Mji wa Makkah walikua wakipenda kuwakabidhi watoto wao kwa

Wanawake wa Bani Bakr.

Ambapo katika mwaka aliozaliwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi kulikua

na ukame mkubwa sana katika maeneo ya ardhi waliyokua wakiishi wa wa Kabila la

Banu Bakr nje ya Mji wa Makkah. Hivyo wanawake wa Kabila hilo wakaamua kua

hakuna njia ya kujirahisishia kupata kipato cha kuongeza riziki zao isipokua kuelekea

katika Mji wa Makkah kwa ajili ya kutafuta Watoto wa Kunyonyesha na hivyo kua ni

wenye kujipatia kipato kwa ajili ya riziki yao.

Miongoni mwa wanawake hao alikuwemo pia Mwanamke mmoja ambae alikua akiitwa

Halima Bint Abu Dhuayb na alikua ameenda katika Mji wa Makkah akiwa amefuatana

na Mumewe ambae alikua akijulikana kwa jina la Harith, na walikua na Mtoto mchanga

wa kiume aitwae Abdullah na walipowasili katika Mji wa Makkah basi walikua

wamechelewa kwa sababu usafiri wa Halima aliopanda ulikua ni wa Punda ambae nae

alikua ni dhaifu na mwenye kutembea taratibu.

Na kutokana na utaratibu huo wa Punda wake Halima basi wlpofika katika Mji wa

Makkah basi wakakuta kua Watoto wote wenye wazee wameshachukuliwa na

wanyonyeshaj na hivyo wakashindwa kupata Mtoto wa kunyonyesha, lakini kwa bahati

nzuri wakaambiwa kua kwa Mzee Abd Ul Muttalib kuna Mtoto mmoja ambae alikua ni

Yatima ambae Wanawake wengine wa Banu Bakr walikataa kumchukua kwa sababu ya

Uyatima wake.

Hivyo Halima alipofika kwa Abd Ul Muttalib basi akajitambulisha kwa kusema kua yeye

ni mwanamke wa Banu Bakr anaeitwa Halimah. Na hapo Abdu Ul Muttalib akamwambia

Halima kua: ‘Ewe Halima hakika mimi nina Mtoto ambae ni Yatima,

nilimpendekeza kwa Wanawake wengine wa Banu Bakr lakini wamemkataa, hivyo

nakuomba kua Mnyonyoshaji wake Mtoto huyu na hivyo huenda akakuongezea

mali na bahati katika Maisha yako kutokana na kumlea kwako.’

Hivyo kwa kua Halima hakutaka kurudi Nyumbani mikono mitupu basi akakubaliana na

rai hio ya Abd Ul Muttalib, lakini kwanza ikambidi akubaliane na mumewe juu ya

maamuzi hayo, ambapo nae akakubaliana na mtizamo huo wa Mkewe, na kisha Halima

akarudi kwa Abd Ul Muttalib kumwambia kua amekubaliana na makubaliano ya kumlea

mtoto huyo na kisha wakaelekea nyumbani kwa Abd Ul Muttalib kwa ajili ya kumchukua

Mtoto huyo.

Hivyo Abd Ul Muttalib akamchukua Halima na kuenda nae hadi kwenye Nyumba ya

Aminah Bint Wahb na alipoingia ndani akapelekwa Moja kwa Moja hadi kwenye

Kitanda cha Mtoto huyo anaetegemewa kua ni mwenye kumlea yaani Rasul Allah


591

Salallahu Alayhi wa Salam, ambapo macho ya Halima yalipomuona Mtoto huyo na uzuri

wake na nuru inayoakisi kwenye paji lake la uso, akiwa amekumbatiwa na kitambaa cha

sufi cha rangi nyeupe na blanketi la kijani huku akitoa harufu nzuri iliyohanikiza chumba

kizima, basi hapo hapo Halima alijawa na tabasamu kubwa sana lililokua likidhihirisha

mapenzi makubwa ya ghafla yaliyotokea na kuzizamisha hisia za mapenzi yake yote ya

mwili wake kwenye kina cha Moyo wake kwa ajili ya mtoto huyo alielala usingizi mbele

yake.

Halima Bint Abu Dhuayb akashindwa kujizuia na kujidhibiti mwili na ufaham wake na

hivyo taratibu akajikuta akiwa anainama na kumchukua Mtoto huyo kutoa ndani ya

Kitanda chake na kumuingiza ndani ya mikono yake huku akiwa amejawa na mapenzi

na huruma kubwa sana, akamsogeza Mtoto huyo kifuani mwake na kisha akainamisha

uso wake na kumbusu kwenye paji la uso wake huku ukiwa umejaa furaha Moyo wake,

na hapo hapo Mtoto huyo akaamka na kuonesha uzuri wa macho yake kwa yule anaebusu

paji la uso wake.

Hivyo macho mazuri na matukufu ya M-bora wa viumbe Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam yakakutana na macho ya mlezi wake mpya ambae ni Halima Bint Abu Dhuayb

na hapo hapo yakafungamana pamoja maisha yao yenye kua na ahadi ya Miujiza, Rehma,

Neema na Baraka zisizotarajiwa ndani ya kipindi cha miaka 5 ijayo watakapokua pamoja.

MIUJIZA YA UTOTONI MWA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI

WA SALAM WAKATI AKIWA KWA HALIMA BINT ABU DHUAYB

Halima Bint Abu Dhuayb akajaribu kumnyonyesha Mtoto huyo mtukufu kwenye ziwa

lake la kulia ambalo hapo kabla ilikua halina maziwa mengi na ya kutosha, lakini mara

tu baada ya kulipachika ziwa hilo ndani ya Mdomo wa Rasul Aallah Salallahu Alayhi wa

Salam basi hapo hapo Halima akahisi hali ya mabadiliko katika Maziwa yake kwani

aliyahisi maziwa yake hayo yakiwa ni yenye kujaa Maziwa ambapo hii ilikua ni hali

ambayo hakuitegemea.

Halima akamnyonesha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hadi akashiba na kisha

akarudi kwa Mumewe na kumuelezea maajabu yaliyotokea, ambapo Harith mwenyewe

hakua ni mwenye kutegemea hali hio ya mabadiliko ya ghafla, hivyo akashangaa na

kujawa na furaha kwani inaonekana wamejaaliwa kupata Baraka kwa sababu hata mtoto

wao pia aliezaliwa karibuni aitwae Abdulla atapata Maziwa ya kutosha kutokana na tukio

hili, hivyo kuanzia siku hio Rasul Aallah Salallahu Alayhi wa Salam akawa

ananyonyeshwa Ziwa la kulia huku Abdulla akiwa ananyonyeshwa Ziwa la Kushoto la

Halima Bint Abu Dhuayb na hivyo tangu siku hio basi Abdullah Ibn Harith akawa ni

Ndugu yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam wa kunyonya.


592

Baada ya makubaliano hayo baina ya Abd Ul Muttalib na familia ya Halima Bint Abu

Dhuayb kuhusiana na ulezi wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi Halimah na

mtoto mpya mwenye baraka alieingia kwenye familia yao aitwae Muhammad Ibn

Abdullah yaani Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam wakamuaga Abd Ul Muttalib na

Aminah Bint Wahb na kisha wakaanza safari yao ya kutoka nje ya Mji wa Makkah.

Safari ilikua ndefu lakini hikua ni ya uchovu, na hivyo ulipofika wakati wa Magharibi

basi wakapiga kambi katika sehemu tulivu na yenye usalama na kumpumzika kwenye

hali ya utulivu mkubwa usiokua wa kawaida katika usiku huo, kiasi ya kua walipomka

Asubuhi yake basi Harith alipoenda kuwakama Maziwa Ngamia wake akaona

mabadiliko yasiyokua ya kawaida katika chuchu zao, kwani chuchu zilikua zimejaa

Maziwa mengi sana, hivyo akamwita Halima na kumwambia: ‘Ewe Halima hivi jee

unajua kua umechukua Ulezi wa Mtoto Mtukufu na baraka kubwa sana?’

Hivyo Halima akajibu kwa kusema: ‘Naam..Wa Allahi hata na mie naona ni hivyo

hivyo.’ Na hii ni kwa sababu Halima aliona mabadliko ya Punda wake pia ambae hapo

awali alikua ni dhaifu, lakini katika safari hii ya kurudi kwao basi Punda huyo alikua ni

mwenye nguvu na mwenye kutembea kwa mwendo wa haraka zaidi, kiasi ya kua

walipoanza safari baada ya asubuhi hio basi Punda huyo wa Halima aliwapita Wanyama

wengine wote na hivyo kua ni muongozaji wa Msafara na walipokua wanatembea basi

Watu waliulizana hivi huyu Punda alikua ndio yule yule au ni mwengine?

Na waliposhindwa kujizua basi wakamuuliza Halima: ‘Ewe Bint Abu Dhuayb, hivi kwa

nini umekua na haraka hivyo? Au umebadilisha Punda mwengine hivyo huyu ni

tofauti na yule uliepanda mwanzo?’

Halima Bint Dhuayb akajibu: ‘La Wallahi huyu ni Punda yule yule, tofauti ni kua

amekua na maajabu kwani sio mimi ninae muongoza, yaani hata sifaham ni kitu

gani kinachoendelea kwenye ufahamu wa Punda huyu.’

Kwani hakuna aliekua akijua kua mabadiliko ya ajabu ya Punda huyo yanatokana na kua

Punda huyo ni mwenye kujua kiumbe mchanga aliembeba kua ni M-bora wa Viumbe

ambae ni kipenzi cha Allah Subhanah wa Ta’ala yaani Nabii Muhammad Salallahu

Alayhi wa Salam.

Na walipofika Safari yao katika ardhi yao basi ingawa walipoondoka hapo awali ilikua

kuna Ukame na visima vya maji vimekauka na hali ya mazingira ya Ardhi yao

haikubadilika haraka sana, kwani maji yalikua bado yamekauka visimani, majani ya miti

yamepungua lakini Wanyama wa Halima walikua wanashiba na kutoa maziwa kwa wingi

zaidi mbali ya kua walikua wanalishiwa sehemu moja ya malisho na wanyama wa watu

wengine.


593

Watu wakaanza kuulizana kwa nini katika Wanyama wa Halima Bint Dhuayb wakawa

ni walionenepa na kutoa mziwa mengi zaidi wakati wanyama wake na wanyama wengine

wote wanalishwa kwenye eneo moja ambayo hata hivyo bado hali ya ukame iko vile vile?

Hivyo wakaanza kulaumiana kua huenda ikawa ni kwa sababu kukataa kwao kumlea

Yatima anaelelewa na Halimah.

Walipomfuata Halima na mumewe kumuuliza imekuaje mpaka Wanyam wao wakawa

na hali tofauti na ya wa kwake wakati wote wanalishwa kwenye eneo moja basi Halima

akasema: ‘Wa Allahi jambo hii halihusiani na Wanyam wala sehemu wanayolishiwa,

bali hii inahusiana na siri kubwa ya Allah mwenyewe, kwani ila kitu kilianza

kubadilika baada ya sisi kuanza safari ya kurudi kutoka katika Mji wa Makkah’ na

bila ya shaka Halima na Harith walikua ni wenye kujua kua Miujiza hii yote inatokana

na huyu mtoto Yatima wanaemlea yaani Muhammad Ibn Abdullah Salallahu Alayhi wa

Salam, hivyo nao wakwa ni wenye kumpenda zaid ya wanavyompenda na kumhifadhi

Mtoto wao waliomzaa.

Baada ya hali kuzidi kua ngumu katika maeneo hayo kutokana na ukame basi watu wa

maeneo hayo wakaamua bora wakusanyike kwa ajili ya kufanya maombi ya mvua kwa

Mungu wao. Hivyo wakakusanyika katika siku maalum katika eneo maalum kwa ajili ya

kufanya maombi hayo, na ingawa walikusanyika watu wote lakini kwa upande wa

Halima yeye hakutaka kuenda kwa sababu ya kua ni mwenye kutotaka kumuingiza juani

mtoto wake huyo anaemlea, kwani kwake yeye mtoto huyo ni Lulu ya jicho lake, hataki

hata kumtoa ndani mwake kutokana na baraka iliyojaa ndani yake wacha mbali

kumhangaisha kwa kumpeleka Milimani kupigwa na jua.

Hivyo baad ya majaribo kadhaa ya kuomba dua ya mvua bila ya mafanikio basi watu hao

wakakumbuka kua Halima ana Mtoto mwenye kua na baraka na Miujiza, hivyo

wakajadiliana kua wamuombe Halima aende nae Mtoto huyo kwenye Maombi yao hayo,

ambapo ingawa mwanzo Halima alikataa lakini mwisho ikambidi akubali kwa ajili ya

kuwasaida majirani zake, hivyo siku hio akamfunga funga vizuri Mtoto huyo kabla ya

kutoka nae kwa ajili ya kuelekea kwenye sehemu ya Maombi hayo ili asidhurike na Jua

kali linapiga ardhini.

Lakini cha kushangaza ni kuwa mara tu alipotoka nae kuelekea kwenye sehemu ya

maombi basi akajikuta kua kama mtu anaetembea chini ya mti mkubwa, na alipoangalia

juu basi akaona kua kuna Mawingu ambayo yalikua yakimfuata kwa juu yake na hivyo

kua ni yenye kumfayia kivuli yeye na Mtoto wake huyo. Halima akajawa na furaha ndani

ya Moyo wake kwani alikua akijua kua jambo alilolifanya la kutoka nae Mtoto huyo

kuenda nae kwenye maombi hayo na Miujiza yake basi bila ya shaka watu wake

watajibiwa maombi yao.


594

Na bila ya shaka baada ya kufika nae Mtoto huyo kwenye eneo husika basi na kuanza

kufanya maombi yao basi haikuchukua hata dakika isipokua walianza kuona kiwingu

kikubwa cha Mvua huku rasha rasha za mvua hio ikianza kuanguka anguka katika eneo

la ardhi yao, tukio ambalo liliwafanya watu hao kua ni wenye kuanza kushangiria na

kufurahia matokeo ya kukubaliwa kwa Maombi yao kutokana na utukufu wa Mtoto alie

Yatima anaelelewa na Halima ndani ya jamii yao miongoni mwao, na wakathibtisha kua

Mtoto huyo ni mwenye Barka na Miujiza, na wakaanza kumpenda sana na kufurahia kua

ni Mtoto Mtukufu kwenye Jamii yao.

Kutokana na Mvua hio basi hali ya mazingira ikaanza kubadilika katika maeneo ya Ardhi

yao, kwani ardhi iliyokua imekufa basi ikaanza kua ni yenye kuota majani na mimea

ikachipua na Wanyama wakawa ni wenye kushiba na kunawiri na kutoa maziwa yenye

kutosha na haop hapo kuanza kua ni wenye kuongezeka.

Ambapo kwa upande wa Mtoto huyo yaani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi

hali yake nae ikaanza kubadilika kila mda unavyoenda kutokana na kua ni mwenye kukua

tofauti kimaumbile na watoto wengine, kwani alianza kuzungumza akiwa na umri wa

miezi minane na kua ni mwenye kujiweza na kua na ukakamavu wa mwili wake

alipotimia umri wa miezi 10, huku kiwa ni mwenye uzuri wa kipekee unaovutia kwa kila

anaemuangalia na mwenye adabu na heshima kwa kila mtu katika jamii yake.

Baada ya kutimia miaka miwili basi ukawadia mda wa watoto waliokua wakilelewa na

kunyonyeshwa na watu wa Banu Sad kua ni wenye kurudishwa kwao wazee wao katika

Mji wa Makkah, hiki kilikua ni kipindi cha huzuni kubwa kwa Halima na familia yake

pamoja na jamii nzima y watu wake, kwani kwa hakika yeye hakua tayari kumrudisha

mtoto huyo kwa Mama yake, na wala watu wa mji huo hawakua tayari kumrudisha mtoto

huyo kutokana na Utukufu wake na manufaa na baraka yake juu yao watu hao.

Lakini ikawa hakuna nia nyengine ya kufanya kwani ahadi ni kua baadaa ya kumaliza

kipindi cha kunyonya mtoto basi inabidi arudishwe kwa wazee wake. Hivyo Halima na

mume wake wakafunga safari pamoja na Mtoto wao Muhammad Salallahu Alayhi wa

Salam kwa ajili yakurudi katika Mji wa Makkah kumkabidhi mtoto huyo kwa Aminah

Bint Wahb ambae alikua akimsubiri kwa hamu kubwa sana Mtoto wake pekee ndani ya

Maisha yake aliempata kutoka kwa Mume wake aliempenda kwa dhati, lakini hata hivyo

Allah kwa Hikma zake hakuwajaalia kua ni wenye kuishi pamoja kwa mda mrefu kwa

kumchukua Abdullah Ibn Abd Ul Muttalib na kumtanguliza katika Ulimwengu wa

Barzah hata kabla ya kuzaliwa Mtoto wake.

Aminah Bint Wahb alifurahia sana kuonana tena na Mtoto wake huyo ambae kipindi hiki

alikua amekua mkubwa lakini sasa, tatizo ni kua ingawa Amina Bint Wahb alikua na

hamu sana ya kua na Mtoto kutokana na kua mbali nae kwa mda mrefu na pia kutokana

na kumpenda kwake, lakini hata hivyo kipindi hiki Mji wa Makkah ulikua umekumbwa


595

na Mtihani wa maradhi ya Maambukizo, hivyo Aminah Bint Wahb akawa anakhofia juu

ya Afya ya Mtoto wake atakaporudishwa katika kipindi hiki katika Mji wa Makkah na

hivyo hali hii ikawa ni kheri kwa upande wa Halima nae akamwambia Aminah Bint

Wahb: ‘Hivi jee utaniruhusu mimi kuendelea kubakia na Mtoto wangu huyu

Muhammad kwa mda mrefu zaid? Kwani hata mimi nnakhofia kuhusiana na

Mripuko wa Maradhi haya usije ukamuathiri.’

Wazo hili kutoka kwa Halima Bint Dhuayb lilikua ni kama alikua ni mwenye kuona

anayoyawaza na kuyafikiria Aminah Bint Wahb hivyo bila ya kusita akaona kua kwa kua

mitizamo yao inaendana sambamba katika kusimamia Maslahi ya usalam wa Afya ya

Mtoto Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kutokana na mapenzi yao juu ya mtoto

huyo basi nae akaona kua bora kwa Muhammad kuendelea kubakia na Halima Bint Wahb

katika ardhi ya nje ya Mji wa Makkah kwa mda zaidi na Muhammad Salallahu Alayhi

wa Salam akawa ni mwenye kubakia na Halima Bint Dhuayb.

Baada ya kurudi katika ardhi ya Watu wa Banu Sad basi Mtoto Muhammad Salallahu

Alayhi wa Salam akaendelea kuishi na watu huku akiwa ni mwenye kua ni mwenye

maumbile ya Muono wa mbali, mwenye kutafakkari, mwenye kupenda kuangalia

Mbinguni kwani mwenye kujiuliza kuhusiana na Maumbile ya Mbingu yalivyo au

kujiuliza kuhusiana na kivuli kinachomfuata katika kutembea kwake katika wakati wa

jua kali na alipokua akichunga kondoo na wenzake basi alikua ni kama mwenye

kuzungumza na kufahamiana vizuri na Mifugo yake kutokana na Majaaliwa ya Allah

Subhanah wa Ta’ala juu yake ambapo yeye hana habari yeyote kuhusiana nayo juu yake,

ambayo ni kutayarishwa kwa ajili ya Neema ya Sharh Sadr.

INSHIRAH SADR YA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM.

Neno Sharaha hua linamaanisha Kufungua, Kukata, Kutanua, Kuweka wazi, Kufunua,

Kutandaza, Kufafanua, Kuelezea, Kurahisisha Kiuzito na Kiufaham.

Ambapo amesema Allah Subhanah wa Ta’ala katika aya zilizotumia neno hili kua:

‏﴿فَمَن يُرِدِ‏ ٱهلل َُّ‏ أَن يَهْدِيَهُ‏ يَشْرَحْ‏ صَدْرَهُ‏ لِلإِسْلاَمِ‏ وَمَن يُرِدْ‏ أَن يُضِل َّهُ‏ يجَْعَلْ‏ صَ‏ دْرَهُ‏

ضَيِّقاً‏ حَرَجاً‏ كَأَنم ََّا يَص َّع َّدُ‏ فىِ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ كَذٰ‏ لِكَ‏ يجَْعَلُ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱلرِّجْسَ‏ عَلَى ٱل َّذِينَ‏ لاَ‏

يُؤْمِنُونَ‏ ﴾


596

Faman yuridi Allahu an yahdiyahu yashrah sadrahu lil-islami waman yurid an

yudhillahu yajAAal sadrahu dhayyiqan harajan kaannama yassaAAAAadu fee

alssama-i kadhalika yajAAalu Allahu alrrijsa AAala alladheena la yu/minoona

(Surat Al AnAam 6:125)

Tafsir: Ama kwa yule ambae Allah hutaka kumuogoza basi humfungulia kifua chake

kwa ajili ya Uislam, na kwa yule ambae hutaka kumdhalilisha basi humfungia kifua

chake na kua ni chenye kubana kama kwamba ni mwenye kupanda juu kuelekea

Angani. Hivyo ndivyo Allah anavyotoa adhabu kwa wale ambao hawakuamini.

Anasema Imam Muhammad Ibn Jarir Al Tabari Al Shafii kuhusiana na aya hii kua Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliulizwa: ‘Jee Moyo hufunguka vipi kwa ajili ya

Uislam?’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu: ‘Ni Nuru ya Allah

Subhanah wa Ta’ala ndio inayoingizwa ndani ya Nyoyo za Ibn Adam, hivyo Moyo

hua ni wenye kutulia na kufunguka.’

Na ingawa aya imetumia neno Harajan ambalo hua ni lenye kumanisha: Kubana kwa

matawi ya mti kiasi ya kua sehemu ya matawi hayo yaliyobanana haiwezi kufikika

na mtu wala na mnyama, lakini kwa upande wa Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi

Allahu Anhu alipoambiwa juu ya maana hiyo na Mabedui ambao wao ni wataalamu

wakubwa wa lugha ya Kiarabu, basi Sayyidna Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu

akasema: ‘Huo hua ni Mfano wa Nyoyo za Wanafiq, kwani kamwe hakuna jema

linaloweza kuingia ndani ya Nyoyo zao.’

Na anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari kua: ‘Allah

Subhanah wa Ta’ala ametofautisha baina ya Murid (Mja anaemtafuta Mola wake)

na Murad (Mja anaetafutwa na Mola wake) ijapokua Waja wawili hawa wote ni

kutoka kwake yeye mwenyewe Allah Subhanah wa Ta’ala. Lakini yeye Allah

Subhaah wa Ta’ala ni mwenye kutofautisha baina ya Khusus (Wenye sifa hususan

maalum) na Umum (Wenye sifa ya Ujumla) na hivyo kawatofautisha wale Murad

(wanaotafutwa na Allah Subhanah wa Ta’ala) katika ayah hii na nyenginezo’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari anaendelea kutufafanulia kwa

kusema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala hua ni mwenye kuziangalia Nyoyo, zote

kwani nyoyo hua ziko mbele yake, hivyo anapoona Moyo fulani una unyenyekevu

juu yake basi huujalia jema atakalo juu yake Moyo huo, Kisha baada ya hapo

hufuata Nyoyo zenye kubadilika haraka na kurudi kwake yeye Allah Subhanah wa

Ta’ala. Hizo ni aina mbili za Nyoyo anazozijaalia mema.’

Na kisha Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abd Allah Al Tustari akasema: ‘Kila wakati

Allah anapouangalia Moyo na akauona kua ni wenye kua na hamu ya Ulimwengu

huu, basi huuchukia Moyo huo na kuchukia kwake huko, hua kunajionesha kupitia


597

katika kuuwachia Moyo huo pamoja na Nafsi ya Mtu huyo. Kwani Moyo

haumilikiwi na yeyote isipokua Allah Subhanah wa Ta’ala, na hivyo hautakiwi

kumtii yeyote isipokua Allah Subhanah wa Ta’ala. Hivyo kama ukiwa unaujali

Moyo wako basi Mfanye Mola wako awe ndie msiri wako.’

Ambapo pia tunaona kua aya imetuma neno Yas’adu ambalo hua linamaanisha

Kuhangaika Kupanda Juu na hii ni kwa sababu Mtu unapopanda juu kuelekea Angani

basi hua unaukandamiza Moyo wako kutokana na kua ni wenye Kudidimizwa chini

kunakotokana na Nguvu ya Mvutano ya Gravity kunakotokana na Mwili wako kua ni

wenye kupingana na nguvu huo katika wakati wa kuenda Juu, na hivyo aya hii hua pia ni

uthibitisho wa Miujiza ya Qur’an kua ni kitabu cha mwenyewe Muumba alieumba kila

kitu.

Ambapo hisia za kubanwa kwa Moyo na Kifua kwa upande wa Kiimani basi hua ni zenye

kuachia pale Ibn Adam anaposikia na kumjua Mola wake na hii ni kutokana na kua Moyo

huo hua ni wenye kuingia ndani yake Nuru ya Allah Subhanah wa Ta’ala, na hivyo kifua

na Moyo huo hua ni wenye kutanuliwa na Mwenyewe Muumba kutokana na Nuru yake

hio na kumrahisishia Mja wake katika kukimbilia na kupata ukaribu na Mola wake.

Mfano mwengine wa matumizi ya neno hili ni pale lilipotumika katika kuelezea Uhiari

wa Mtu katika Kutaka kuutanua na Kuufungua Moyo wake kwa ajili ya kuingiza kiza

cha Kufru ndani yake, kutokana na matamanio yake kama pale ziliposema aya:

‏﴿مَن كَفَرَ‏ بِٱهلل َِّ‏ مِن بَعْدِ‏ إيمَانِهِ‏ إِلا َّ مَنْ‏ أُكْرِهَ‏ وَقَلْبُهُ‏ مُطْمَئِن ٌّ بِ‏ ٱلإِيمَانِ‏ وَلَٰكِن م َّن

شَرَحَ‏ ابِلْكُفْرِ‏ صَدْراً‏ فَعَلَيْهِمْ‏ غَضَبٌ‏ مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَلهَُمْ‏ عَذَابٌ‏ عَظِيمٌ‏ ﴾

Man kafara biAllahi min baAAdi eemanihi illa man okriha waqalbuhu mutmainnun

bial-eemani walakin man sharaha bialkufri sadran faAAalayhim ghadhabun

mina Allahi walahum AAadhabun AAadheemun (Surat An Nahl 16:106)

Tafsir: Yeyote yule atakaemkufuru Allah baada ya kua ni mwenye Imani, isipokua yule

ambae amelazimishwa juu yake (kukufuru), huku Moyo wake ukiwa umetulia kwenye

Imani (ya kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala), lakini atakae ufungua Moyo wake

kwa Kufru basi ni juu yao Adhabu ya Allah na watapata Adhabu kubwa sana.

Ambapo katika aya hii tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anatuthibitishia kua Imani

ya Mtu hua ni yenye kuthibitishwa Ndani ya Moyo wake Mtu huyo na wala si kutokana

na maneno yake, kwani Mdomo hua ni wenye kubainisha tu yale yaliyomo ndani ya

Moyo wa Mtu husika na kuyathibitisha kwa maneno.


598

Na hivyo kutuwekea wazi kua kama itatokea Mtu atalazimishwa kufanya Ovu baada ya

kutishwa Uhai wake, basi hua hawezi kulaumiwa kutokana na ovu hilo, na hii pia ni kwa

sababu amesema pia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hesabu

husimamishwa kwa Ummah wangu juu ya jambo alilofanya Mtu kwa bahati

mbaya, kwa kusahau au kwa kile alicholazimishwa kukifanya.’

Ambapo anasema Imam Abu Hanifa kuhusiana na Hadithi hii kua: ‘Kusamehewa huko

kwa Ummah hua kunakubalika kua kama ni kisingizio katika siku ya Malipo na

katika baadhi ya mambo ya kidunia, ambapo hapa kwanza itabidi Qadhi

achunguze na kuangalia kwanza, kisha ndio anaweza kutomhukumu kama kweli

ama la, na pia kwa baadhi ya mambo ya kidunia hua haikubaliki kwa mfano mtu

anapomuua mtu mwengine kwa bahati mbaya basi kisharia hua hasamehewi bali

hua anatakiwa kulipa Fidiya’

Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi

anatufafanulia kuhusiana na maana ya aya kwa mifano pale aliposema: ‘Pale inapokua

Muislam anajua kua maneno yake yanaweza yakasababisha madhara kwa Waislam

wasiokua na hatia, basi hua inakubalika kutoa ushahidi wa Uongo, na hivyo katika

tukio kama hili basi hua haina haja ya kulipa fidia kutokana na kula kiapo cha

Uongo’

Na kwa upande wa Imam Ibrahim An Nakhai basi yeye ansaema ni bora kusema kua:

‘Wa Allahi, kama mimi ningesema Jambo hilo, basi Allah Subhanah wa Ta’ala

angekua na habari nalo’ na hivyo Msikilizaji hua ni mwenye kuichukulia kauli hio kua

inamaanisha kua Mtu huyo hakusema kuhusiana na jambo hilo, na hapo hapo hakusema

uongo katika kuapa kwake, kutokana na kua na nia ya kutosema Uongo. Na ndio maana

Imam Ibrahim An Nakhai alikua kama hataki kuonana na mtu ambae amemfuata

Nyumbani kwake basi huingia kwenye chumba chake cha kusalia na kisha humwambia

Mtumwa wake kua amwambie Mtu huyo kua: ‘Wallahi yuko Msikitini.’

Hivyo ingawa Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia neno Sharaha Sadran kumaanisha

Kukifungua Kifua kwa ajili ya kuingiza Kufru ndani ya Moyo wa Mtu kutokana na hiari

yake Mtu huyo, lakini mara nyingi zaidi Allah Subhanah wa Ta’ala ametumia neno hilo

Sharaha Sadran kumaanisha Kuingiza Imani na Ilm ndani yake kunakotokana na Hiari

na Jitihada za Mja katika kumkimbilia Mola wake na kutokana na Makadirio na matakwa

ya Allah Subhanah wa Ta’ala juu ya Mja wake, kama tunavyoona vile alivyoomba Nabii

Musa kwa Mola wake pale aliposema:

‏﴿قَالَ‏ رَبِّ‏ ٱشْرَحْ‏ لىِ‏ صَدْرِي﴾‏


599

Qala rabbi ishrah lee sadree (Surat Ta-Ha 20:25)

Tafsir: Akasema (Nabii Musa) Ewe Mola wangu nitanulie Kifua changu.

Ambapo katika aya hii tunaona kua Nabii Musa alikua ni mwenye kumuomba Allah

Subhanah wa Ta’ala juu ya Jambo hilo, lakini hali ilikua ni tofauti kwa upande wa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kama alivyobainisha Allah Subhanah wa Ta’ala pale

aliposema katika Surat Al Inshirah.

TAFSIR YA SURAT AL INSHIRAH.

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞أَلمَْ‏ نَشْ‏ رَحْ‏ لَكَ‏ صَدْ‏ رَكَ‏ ‏۞وَوَضَعْنَا عَنكَ‏ وِزْرَكَ‏ ‏۞ٱل َّذِيۤ‏

أَنقَضَ‏ ظَهْ‏ رَكَ‏ ‏۞وَرَفَعْنَا لَكَ‏ ذِكْرَكَ‏ ‏۞فَإِن َّ مَعَ‏ ٱلْعُسْ‏ رِ‏ يُسْ‏ راً۞إِن َّ مَ‏ ‏َع

يُسْ‏ راً۞فَإِذَا فَرَغْتَ‏ فَٱنصَبْ‏ ‏۞وَإِلىَٰ‏ رَبِّكَ‏ فَٱرْغَبْ‏ ﴾

ٱلْعُسْ‏ ‏ِر

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Alam nashrah laka sadraka; WawadhaAAna

AAanka wizraka; Alladhee anqadha dhahraka; Fa-inna maAAa alAAusri yusran;

Inna maAAa alAAusri yusran; Fa-idha faraghta fainsab; Wa-ila rabbika fairghab

(Surat Al Inshirah 94:1-8)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma; Hivi jee

hatukukifungua kifua chako kwa ajili yako? (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa

Salam) Na kukuondolea wewe Uzito wa Mzigo wako?; Ambao ulikua

unakukandamiza; Na kukupadishia Darja kutajwa kwako? Hivyo katika Ugumu

mmoja hua kuna Urahisi mara mbili, Bila ya shaka kwenye Ugumu mara moja kuna

Urahisi mara mbili, Hivyo unapomaliza mambo yako basi simama kwa ajili ya Mola

wako, Na umgeukie Mola wako kwa Maombi yako.

Na akasema Imam Malik Ibn Dinar kua: ‘Hakuna Mtihani Mkubwa ambao anaweza

kuupata Mtu kuliko kua na Ugumu wa Moyo, na pia kwa Ummah kama

kuondolewa Huruma ndani ya Nyoyo zao’

Kwani amesema Allah Subhanah wa Ta’ala katika Qur’an kua:


600

‏﴿أَفَمَ‏ ن شَ‏ رَحَ‏ ٱهلل َُّ‏ صَدْرَهُ‏ لِلإِسْلاَمِ‏ فَهُوَ‏ عَلَى ٰ نُورٍ‏ مِّن ر َّبِّهِ‏ فَوَيْلٌ‏ لِّلْقَاسِ‏ يَةِ‏ قُلُوبُهُمْ‏

مِّ‏ ن ذِكْ‏ رِ‏ ٱهلل َِّ‏ أُوْ‏ لَٰئِكَ‏ فىِ‏ ضَلاَلٍ‏ م ُّبِينٍ‏ ﴾

Afaman sharaha Allahu sadrahu lil-islami fahuwa AAala noorin min rabbihi

fawaylun lilqasiyati quloobuhum min dhikri Allahi ola-ika fee dhalalin

mubeenin(Surat Az Zumar 39: 22):

Tafsir: Hivi Jee aliefunguliwa Na Allah Kifua chake kwa Uislam na akawa kwenye

Nuru kutoka kwa Mola wake (ni sawa na asiekua katika Uislam?): Hivyo Ole wao

wale ambao Nyoyo zao zimekubuhu dhidi ya Kumkumbuka Allah, kwani kwa hakika

hao wako katika upotovu Mkubwa sana.

Hivyo ingawa Nabii Musa alimuomba Allah Subhanah wa Ta’ala kua amtanulie kifua

chake, lakini kwa upande wa Surat Al Inshirah basi aya zinatubainishia kua Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alijaaliwa kua ni mwenye kutanuliwa Moyo na kifua chake

na Allah Subhanah wa Ta’ala kwa ajili ya kumjaza Ilm na Imani juu yake Allah Subhanah

wa Ta’ala na hivyo kumtayarisha kwa ajili ya kua na maarifah na kujisalimsha kwa ajili

ya kumtii kikamilifu Mola wake.

Ambapo tunapozungumzia kuhusiana na tukio hili la Sharaha Sadr ya Rasul Allah

Salallah Alayhi wa Salam basi Wanazuoni wametofautiana juu ya kua ni wakati gani

lilitokea tukio hili kwani kuna wasemao kua inawezekana tukio hili lilitokea baadae

katika wakati wa Safari ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ya Isra na Miraj, na

pia kuna wanaosema kua tukio hili ni lile lilitokea wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam akiwa mdogo.

Ambalo linaelezewa na baadhi wanaosema kua lilitokea wakati Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alipokua kwa Halima Bint Dhuayb pamoja na Abd ullah wakati

walipokua wakichunga Kondoo karibu na Nyumba yao na kisha wakakaa kitako chini ya

kivuli cha Mti, ambapo hapo hapo usingizi ukampitia Abd Allah huku Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akiwa ni mwenye kufikiria kuhusiana na Muumbaji wa

Ulimwengu.

Mara Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaona kua Kondoo wao wameenda mbali

nao hivyo akaamua kuwafuata ilikuwarudisha karibu tena na Nyumbani, wakati

anawakimbilia Kondoo hao mara wakatokea Watu wawili ambao walikua wamevaa nguo

nyeupee ambao walikua wanamuangalia huku wakiwa ni wenye kutabasam tabasam


601

lenye kuvutia, huku mmoja wao akiwa amebeba Bakuli la dhahabu lililokua limejaa

Theluji mkononi mwake.

Watu hao wakamkaribia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kisha taratibu

wakamkamata na kumlaza juu ya Majani ambayo yalikua kama zulia huku wakiwa na

tabasamu, jambo ambalo halikumshtua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwani

aliadhani kua ni sawa ni wenye kutaka kucheza nae na hivyo hawatomdhuru kama ilivyo

kawaida ya Watu wenye kupenda watoto namna wanavyocheza na watoto.

Ingawa hali ilikua ni hivyo kulingana na mtizamo wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam lakini kwa upande wa Abdullah, ambae wakati tukio hili linatokea alikua

amezindukana, basi yeye alishtuka na hivyo haraka sana akakimbilia nyumbani kwa

Halima na kumwambia kuhusiana na aliyoyaona yanatokea huko nje, na hivyo habari

hizo ziliwafanya Halima na Harith waliokuwemo ndani ya Nyumba kuacha kila kitu

walichokua wanafanya na kukimbilia nje katika upande aliokua amelazwa Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na watu wawili hao kama alivyoelezea Abdullah.

Lakini walipofika katika eneo hilo hawakuwaona watu wawili hao, bali walimuona Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akiwa ni mwenye kunyanyuka huku akiwa na uso

uliosawijika kutokana na tukio lililomtokea ambalo hata hivyo yeye hakua ni mwenye

kujua ni kwanini likatokea, na hivyo wakaamua kumuuliza ni kitu gani kilichotokea

ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema:

‘Walikuja watu wawili waliokua wamevaa nguo nyeupee, ambao mmoja wao alikua

ameshika Bakuli la Dhahabu likiwa limejaa Theluji ndani yake, waliponikaribia

wakanilaza chini kwenye majani na kisha wakanizuia na wakanipasua Kifua

changu, wakautoa Moyo wangu na kuupasua pia na kisha wakatoa ndani ya moyo

wangu kitu cheusi kama damu iliyoganda na kisha wakakirembea na kisha

wakanisafisha Moyo wangu na Kifua changu kwa theluji na kisha wakaniacha na

wakaondoka’

Ambapo kuhusiana na tukio hili basi kuna wanaosema watu hawa pia walimtahiri Rasul

Allah Sallahu Aalyhi wa Salam, na pia kwa upande mwengine basi wapo wasemao kua

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alitahiriwa hapo kabla na Babu yake ambae ni

mzee Abd Ul Muttalib kwani ilikua ni kawaida ya Waarabu kutahiriana, kutokana na kua

jambo hilo ni lenye asili ya kutoka kwa Nabii Ibrahim kupitia kwa Nabii Imail.

Na kwa upande mwengine tunapoliangalia tukio hili basi kua na Hadithi pia ambayo

ndani yake anasema Ubay Ibn Kaab Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hakika Abu Hurayrah

alikua ni mwenye kupenda kumuuliza masuali Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kwani siku moja alimuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa


602

kusema: ‘Ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hivi jee ni alama gani ya

mwanzo iliyokuonesha wewe kuhusiana na Utume wako’’

‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akakaa kitako kisha na kisha akasema:

‘Ama Masuali yako Abu Hurayrah! Naam ilikua nilipokua nna umri wa miaka 10

wakati nilipokua Jangwani, na mara nikasikia kuna mtu anazungumza na mie

kutoka juu hivyo nilipoangalia Juu nikaona watu wawili ambapo mmoja wao alikua

akisema kumwambia mwenzake: ‘Ndie huyu?’’

‘Na kisha wakatua mbele yangu, na hakika mimi sijawahi kuona watu kama hao

mfano wake, hata nguo walizokua wamevaa zilikua tofauti kwangu mie,

wakanikaribi na kisha kila mmoja wao akanizuia kwenye bega langu, na mpaka

sasa hivi nahisi ubaridi wa mguso wao, ambapo mmoja akamwambia mwenzake:

‘Mlaze chini’ hivyo wakanilaza chini bla ya kutumia nguvu yeyote kisha mmoja

wapo akamwambia mwenzake: ‘Mfungue kifua chake’ nami nikafukunguliwa

Kifua bila ya kutoka Damu wala kuhisi Maumivu.’

‘Kisha mmoja akamwambia mwenzake: ‘Toa Udanganyifu na Wivu’ mwenzake

akatoa kitu kama kama damu nyeusi na akaikirembea. Kisha mwengine akasema:

‘Mpandikize ndani yae Rehema na Huruma’ na kisha mwenzake huyo akatoa kitu

kama alichokitoa hapo mwanzo lakini hiki kilikua na rangi ya Fedha. Na kisha

akanikamata kidole changu cha gumba cha Mguu na kusema: ‘Rudi kua kama

ulivyokua’ nami baada ya hapo nikawa kama nilivyokua mzima nakimbia huku na

kule nikiwa na Rehema kwa wadogo na kua na Huruma kwa wazee ’

Hivyo kuhusiana na maneno haya ya aya hizi yenye kuhoji kwa njia ya kuthibitisha

kuhusina na Sharh Sadr ya Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam kama zilizivyosema

aya:

‏﴿أَلمَْ‏ نَشْ‏ رَحْ‏ لَكَ‏ صَدْ‏ رَكَ‏ ﴾

Alam nashrah laka sadraka; (Surat Al Inshirah 94:1)

Tafsir: Hivi jee hatukukifungua kifua chako kwa ajili yako? (Ewe Muhammad

Salallahu Alayhi wa Salam).

Basi tunaona kwa upande wa Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi

yeye anasema kua: Allah Subhanah wa Ta’ala alimtanulia kifua Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kwa kumjaza Nuru ya Ujumbe wa Dini ya Kiislam


603

Na Imam Hasan Al Basr basi yeye anasema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala

alimtanulia kifua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kumjaza Ilm ya Dini

ya Kiislam na Hikma’ na pia kuna wanaosema kua maana ya maneno haya

yanamaanisha kua: ‘Hivi Jee sisi hatukukusafisha Moyo wako na hivyo ukawa

hauruhusu vishawishi vya Shaytan ndani yake?’

Na kisha aya za Surat Al Inshrah zinaendelea kusema:

﴿ وَوَضَعْنَا عَنكَ‏ وِزْرَكَ‏ ‏۞ٱل َّذِي ۤ أَنقَضَ‏ ظَهْ‏ رَكَ‏ ﴾

WawadhaAAna AAanka wizraka; Alladhee anqadha dhahraka; (Surat Al Inshirah

94:2-4)

Tafsir: Na kukuondolea wewe Uzito wa Mzigo wako?; Ambao ulikua

unakukandamiza.

Na kwa upande mwengine basi Abu Ubaydah Ibn Jarrah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Allah

Subhanah wa Ta’ala amemrahisishia Uzito katika kazi ya Mtume wake Salallahu

Alayhi wa Salam, ili asihisi uzito mkubwa, kutokana na Neema na Rehma zake juu

yake. Kwani jukumu lake la kuitangaza Dini ya Allah Subhanah wa Ta’ala kwa

Makafiri lilileta upinzani mkubwa na madhara makubwa sana, ambayo hata hivyo

yalivumiliwa na Waislam bila ya kutaka kulipiza Kisasi hapo baadae, na hii pia

ndivyo hali ilivyokua kwa upande wa Masahaba.’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abdallah Al Tustari Al Shafii anasema kua: ‘Maneno

haya yanamaanisha kua Tumekuondolea wewe kutokukubali Utulivu kutoka kwa

yeyote isipokua kutoka kwetu na kukupa wewe kua na utulivu na usalama kutokana

na kututetegemea kwa kila kitu’

Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi

anasema kuhusiana na aya hizi kua ni yenye maana na zile aya isemayo:

‏﴿لِّيَغْفِرَ‏ لَكَ‏ ٱهلل َُّ‏ مَا تَقَد َّمَ‏ مِن ذَنبِكَ‏ وَمَا أتََخ َّرَ‏ وَيُتِم َّ نِعْمَتَهُ‏ عَلَيْكَ‏ وَيَ‏ هْدِيَكَ‏

صِرَاطاً‏ م ُّسْتَقِيماً‏ ﴾

Liyaghfira laka Allahu ma taqaddama min dhanbika wama taakhkhara

wayutimma niAAmatahu AAalayka wayahdiyaka siratan mustaqeeman (Surat Al

Fat-h 48:2)


604

Tafsir: Amekusamehe juu yako Allah zilizotangulia miongoni mwa dhambi zako na

zitakazokuja na ametimiza neema yake juu yako na amekuongoza kwenye njia

iliyonyooka.

Anasema Imam Ashanqinti kua: ‘Hakuna kutofautiana juu ya Mitizamo ya

Wanazuoni kua Mitume wana ulinzi wa kutofanya dhambi.’

Ambapo alisema Abu Talib kumwambia ndugu yake Al Abbas kua: ‘Hakika mimi

nilimchukua (Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) chini ya uangalizi wangu na

sikuachana nae hata mara moja si usiku wala si mchana, na nilikua nikimlaza baina

ya watoto wangu katika sehemu ya kwanza ya usiku halafu katika sehemu ya pili

ya usiku nimekua nikimhamisha kwa tahadhari, na wala sijawahi kumsikia

akisema uongo, wala akicheka kwa sauti kubwa na wala sijawahi kumuona

akisimama kucheza na watoto wengine.’

Ambapo kwa upande wa Mujjadid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye

anasema kua: ‘Maneno WawadhaAAna AAanka wizraka; Alladhee

anqadha dhahraka yanamaanisha kuweka wazi hali aliyokua nayo Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kuhusiana na Jamii ya watu wake walivyokua kabla yeye

kupata Utume wake kama alivyosema Allah Subhanah wa Ta’ala katika aya

ifuatayo:

‏﴿فَلَعَل َّكَ‏ ابَخِ‏ عٌ‏ ن َّفْسَكَ‏ عَلَى ٰ آاثَرِهِمْ‏ إِن لم َّْ‏ يُؤْمِنُواْ‏ هبَِٰذَا ٱلحَْدِيثِ‏ أَسَفاً‏ ﴾

FalaAAallaka bakhiAAun nafsaka AAala atharihim in lam yu/minoo bihadha

alhadeethi asafan (Surat Al Kahf 18:6)

Tafsir: Na kisha labda utajimaliza Nafsi yako kwa huzuni zitokanazo na athar zao kwa

sababu ya kutoamini hizi hadithi.

Ambao hali hii hua pia ni sawa na ile hadithi ambayo ndani yake amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Mfano wangu mimi na watu wa Ummah wangu ni

sawa na Mtu aliewasha Moto unaomurika katika sehemu aliyokuwepo, lakini

jambo hilo linawasababishia wadudu wawe ni wenye kuangukia ndani ya moto huo.

Na hivyo Mtu huyo kua ni mwenye kujaribu kuwavuta wadudu hao wasiangukie

ndani ya moto huo, lakini wadudu hao hua wenye kumzidi mtu huyo na kujiingiza

ndani ya Moto huo. Hivyo hali yangu mimi ni ya kua ni mwenye kutafuta Njia ya

kukuepusheni nyinyi msiingie ndani ya Moto’

Ama kuhusiana na aya isemayo:


605

‏﴿وَرَفَعْنَا لَكَ‏ ذِكْرَكَ‏ ﴾

WarafaAAna laka dhikraka (Surat Al Inshirah 94:4)

Tafsir: Na kukupadishia Darja kutajwa kwako?

Ambapo neno Dhikr hua linamaanisha Kukumbuka, Kusheherekea, Kutaja, Kuweka

Akilini, Kuonya, Kusifiia, Kupandisha Darja, Kufanya kua maarufu.

Na hivyo aya hii inamaanisha kua Allah Subhanah wa Ta’ala amempandisha Darja Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika Kutajwa na kukumbukwa kwake katika mambo

muhimu na ya msingi kiasi ya kua anapotajwa Allah Subhanah wa Ta’ala basi hua kuna

na ulazima wa kumtaja na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa mfano kama vile

katika mjumuisho wa maneno ya Shahada ‘La Ilaha Illa Allah, Muhammad Rasulu

Allah’ ambayo hutamkwa katika sehemu mbali mbali ikiwemo pale Mtu anapothibitisha

kuingia katika Iman ya Dini ya Uislam, katika Adhana, Katika Iqama, Katika Sala n.k

Na pia katika safari yake ya Miraj basi Jina la Rasul Salallahu Alayhi wa Salam lilikua

likitajwa katika kila Mbingu pale Malaika Jibril alipokua akiomba ruhusa kuingia kupitia

kwenye Milango ya Mbingu hizo, na bila ya shaka ndani yake kukumbukwa huko kwa

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ni pale atakapopata darja ya kupanda kwenye

darja ya Maqaman Mahmuda, Kukabidhiwa Chemchem ya Al Kawthar n.k

Na kwa upande mwengine bsi tunaona kua katika kupandishwa kwake huko darja Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi hata maadui zake imekua vigumu kwao wao kua

ni wenye Kumdharau na kushindwa kujizuia kwa kutomsifu kwa sifa bora Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kutokana na Utukufu wake mbele ya Viumbe wote.

Kisha Allah Subhanah wa Ta’ala anaendelea kutuambia kua:

‏﴿فَإِن َّ مَعَ‏ ٱلْعُسْ‏ رِ‏ يُسْ‏ راً۞إِن َّ مَعَ‏ ٱلْعُسْ‏ رِ‏ يُسْ‏ راً‏ ﴾

Fa-inna maAAa alAAusri yusran; Inna maAAa alAAusri yusran (Surat Al Inshirah

94:5-6)

Tafsir: Hivyo katika Ugumu mmoja hua kuna Urahisi mara mbili, bila ya shaka

kwenye Ugumu mara moja kuna Urahisi mara mbili.


606

Kulingana na mfumo wa Lugha ya Kiarabu basi Nomino inaporudiwa katika kauli na

kisha ikawa imetanguliziwa na harfu Alif Lam kabla yake basi kila moja kati ya nomino

hizo hua zinahesabika kua ni Moja. Lakini pale inapokua Nomino hio inapokua

imerudiwa bila ya kutanguliziwa na Alif Lam, basi kila nomino moja hua inakua

inahesabika kua ni Moja na inayojitegemea.

Na katika aya zetu hizi mbili tunaona kua Nomino ‘Usr’ ambayo ni neno linalotafsirikia

kua ni Ugumu imerudiwa huku ikiwa imetanguliziwa na Alif Lam kabla yake yaani liko

katika hali ya Al Usr na hivyo hua linamaanisha kua ni hali ya Umoja ya Ugumu. Ambapo

neno Yusr ambalo linatafsirika kama Wepesi na hapa limetumiwa bila ya kutanguliziwa

Alif Lam kabla yake na hivyo kua ni lenye kumaanisha Wepesi mara mbili zaidi na hivyo

kumaanisha kua Katika kila Ugumu mmoja basi kuna Urahisi mara mbili yake.

Ambapo anasema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Kulikua kuna jiwe mbele

ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo akasema: ‘Kama ikiwa Ugumu

wowote utaingia kwenye jiwe hili basi utafuatia wepesi wake kwenye jiwe hili na

kuutoa Uzito huo’ na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akashusha aya isemayo: ‘Fainna

maAAa alAAusri yusran; Inna maAAa alAAusri yusran’’

Na akasema Hasan Radhi Allahu Anhu kua: ‘Siku moja Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alitoka nyumbani kwake huku akiwa na na hali ya furaha na kusema:

‘Fa-inna maAAa alAAusri yusran; Inna maAAa alAAusri yusran yaani Hivyo

katika Ugumu mmoja hua kuna Urahisi mara mbili, bila ya shaka kwenye Ugumu

mara moja kuna Urahisi mara mbili.’ (Dur Al Mandhur)

Kwani haiwezekani kua Mtu atafikwa na Ugumu tu katika kila kitu bila ya kupatikana

wepesi. Hivyo Allah Subhnaha wa Ta’ala amerudia Kauli hii ili Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam apate farijiko pale anapopata ugumu, na pia kwa kila Muislam anaepata

ugumu katka mambo yake basi anatakiwa ajue kua kuna Ahadi ya Allah Subhana wa

Ta’ala kua ‘Fa-inna maAAa alAAusri yusran; Inna maAAa alAAusri yusran yaani

Hivyo katika Ugumu mmoja hua kuna Urahisi mara mbili, bila ya shaka kwenye

Ugumu mara moja kuna Urahisi mara mbili.’

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abdallah Al Tustari basi yeye

anasema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala ameikuzisha hali ya Matarajio katika aya

hii kutokana na Ukarimu wake na ufichikano wa Rehma zake, na ndio maana

akautaja wepesi mara mbili’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisema: ‘Fa-inna maAAa alAAusri

yusran; Inna maAAa alAAusri yusran yaani Hivyo katika Ugumu mmoja hua kuna

Urahisi mara mbili, bila ya shaka kwenye Ugumu mara moja kuna Urahisi mara


607

mbili.’ Na hivyo kumaanisha Ufahamu wa Moyo na Akili kua ni Mambo mawili

mepesi ambayo ni yenye kuweza kuudhibiti ugumu mmoja ambao ni Nafsi na hivyo

kuirudisha katika hali ya Ikhlas’

Ama kuhusiana na

‏﴿فَإِذَا فَرَغْتَ‏ فَٱنصَبْ‏ ‏۞وَإِلىَٰ‏ رَبِّكَ‏ فَٱرْغَبْ‏ ﴾

Fa-idha faraghta fainsab; Wa-ila rabbika fairghab (Surat Al Inshirah 94:8-9)

Tafsir: Hivyo unapomaliza mambo yako basi simama kwa ajili ya Mola wako, Na

umgeukie Mola wako kwa Maombi yako.

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abdallah Al Tustari anasema kua: ‘Aya inamanisha

kua Unapomaliza Sala zako na kisha ukakaa kitako basi jitahidi kwa ajili ya Mola

wako na rudi katika hali ya awali ya kimaumbile kabla ya viumbe wengine ukiwa

na Mola wako peke yako na hivyo kuingia katika hali kua ni siri ndani ya siri’ kama

alivyosema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kwa hakika mimi hua nna

wakati ambao nnakua na Mola wangu. Hii hua ni katika wakati ambao hua

simshughulikii yeyote isipokua Mola wangu.’

Ambapo kwa Upande wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu basi yeye

ni mwenye kusema kuhusiana na maneno ya Aya hizi kua: ‘Yanamaanisha kua

Unapomaliza Kusali basi jishughulishe na Kuomba Dua’ ambapo kwa Upande wa

Imam Jabir Ibn Zayd basi yeye amesema kua: ‘Unapomaliza mapigano yako kwa ajili

ya Allah basi rudi kwenye Sala na maombi’.

Imam Mujahid Ibn Sulayman amesema kua hua yanamanisha kua: ‘Unapomalizia

mambo yako ya kidunia basi geukia katika upande wa pili wa kiakhera’, na akasema

Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Maneno

haya yanamaanisha kua fuatisha kwa kufanya mema zaidi baada ya kufanya

Mema’

Hivyo kulingana na Mtizamo wa baadhi ya Wanazuoni ni kua ilikua ni katika kipindi hiki

cha kukaa kwa Halima Bint Dhuyab ndio lilitokea tukio la kwanza la kutanuliwa kifua

kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae alikaa kwa Bi Halima Bint Dhuayb

kwa miaka mitano na kisha akarudishwa katika mji wa Makkah kwa Mama yake Mzazi

ambae ni Aminah Bint Wahb na kuendelea kuishi pia pamoja na Mama yake mlezi ambae

ni Ummu Ayman.


608

KIFO CHA AMINAH BINT WAHB MAMA YAKE RASUL ALLAH

SALALLAHU ALAYHI WA SALAM.

Baada ya Miaka mitano ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi alirudishwa katika Mji wa

Makkah basi akapokelewa kwa furaha mapenzi na Amina Bint Wahb pamoja na Barakah.

Na baada ya Mwaka Mmoja basi Bi Amina Bint Wahb akaamua kua anataka kutembelea

Kaburi la Mume wake Abdullah Ibn Abd Al Muttalib aliefariki miaka 6 iliyopita.

Ambapo kipindi hiki Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam alikua na umri wa miaka 6,

na Bi Aminah Bint Wahb aliamua kumchukua pia Mwanawe na Barakah katika safari

hio ndefu, na ingawa Abd Al Muttalib alijaribu kumnasihi Amina Bint Wahb kua

asifunge safari hio ndefu lakini Bi Amina bint Wahb alikua ni mtu wa misimamo na hivyo

akaamua kua hakuna atakemzuia kufanya ziara hio ya kutembelea Kaburi la Mume wake

Kipenzi ambae ndie pia baba wa Mtoto wake kipenzi.

Hivyo siku ya Safari ilipowadia Amina Bint Wahb, Baraka na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam wakapanda juu ya Ngamia mmoja kwenye Kibanda kilichojengwa juu

ya Mgongo wa Ngamia wao huku wakiwa ni wenye kufuatana na Msafara uliokua

ukielekea Katika Ardhi ya Sham.

Safari iliendelea huku Rasul Allah Alayhi wa Salam akiwa kwenye mikono ya Baraka.

Allah Subhanah wa Ta'ala akawajaalia Safari ya Utulivu na Salama mpaka walipofika

Katika Mji wa Madinah baada ya siku 10.

Walipofika katika Mji wa Madinah Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam na Barakah

wakaachwa kwenye Nyumba ya Mjomba wake Bi Amina Bint Wahb ya Banu Najjar na

kisha Bi Amina bint Wahb akawa anaenda Kaburini kwa Mumewe kila siku huku akiwa

ni mwenye kuhuzunika na kua na Majonzi makubwa sana.

Siku moja wakati Aminah Bint Wahb akiwa ameenda Makaburini huku Ummu Ayman

akiwa amebakia na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam huku wakiwa wamekaa mbele

ya nyumba waliyofikia, mara wakapita Rabi wawili wa Kiyahudi ambao walipomuona

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, basi wakasimama na kumwangalia kwa umakini

na mshangao. Jambo hili lilimsababishia Rasul Allah Salallahui Alayhi wa kunyanyuka

kutoka katika sehemu aliyokaa na kukimbilia ndani kutokana na kua na woga wa

Mtizamo wa watu hao.

Hivyo Mayahudi hao wakamkaribia Ummu Ayman na kumuuliza: ‘Huyu Mtoto uliekua

nae anaitwa nani?’


609

Ummu Ayman akashatuka, kwanini watu hawa walisimama na kumuangalia sana Rasul

Salallahu Alayhi wa Salam na kisha wakawa wanataka kujua jina lake.

Hivyo nae akawauliza: ‘Kwanini nyinyi mnataka kujua juu ya jina lake?’

Mayahudi hao wakasema: ‘Hakika sisi hatuna nia mbaya nae Mtoto huyo isipokua

huyu mtoto anaonekana kama ni Mtu ambae sisi tunamjua, hivyo jee jina lake ni

nani?’

Hivyo Ummu Ayman akasema: ‘Jina Lake ni Ahmad.’

Mayahudi hao wawili wakangaliana tena kwa mara ya pili huku wakiwa na mshangao

zaidi lakini wenye kuzijaza nyuso zao na tabasamu, kisha wakasema: ‘Jee unaweza

kumuita, tukamuangalia tukahakikisha zaidi?’

Hivyo Ummu Ayman akabakia anajiuliza imekuaje watu hawa wanataka kuhakikisha

zaidi juu yake, kwani kuna nini? Lakini kabla hajauliza suali hilo basi Mayahudi hao

wakaona muonekano wa Uso wake kua umekua ni wenye kujawa na wasi wasi, hivyo

nao wakamwambia Ummu Ayman: ‘Usiwe na khofu kwani sisi hatufikirii wala

hatutaki kitu chochote isipokua wema, na hivyo hatuna nia ya kumdhuru yeye au

mtu mwengine yeyote yule, hakika sisi tunampenda huyu Mtoto kwa ajili ya Allah.

Hivyo tafadhali muite aje japo kwa mda mdogo tu.’

Maneno haya kidogo yalimtuliza Ummu Ayman hivyo baada ya kutafakari basi akaingia

ndani na kutoka na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Ambapo alipotoka nae basi

Mayahudi hao wakainama na kumsujudia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na

kisha wakanyanyuka huku wakiwa na nyuso zilizojaa tabasamu na kuanza kumuangalia

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam tangu juu mpaka chini na kisha wakamgeuza na

kumuangalia mgongoni na kuambiana kwa kusema: ‘Huyu Mtoto ndio yule Mtume wa

Ummah Huu, atakuja kuhamia katika Mji huu. Kisha vitafuatilia Vita na Uhamiaji

na matukio mengi makubwa sana yatatokea katika Mji huu’ na kisha Mayahudi hao

wakamuaga Ummu Ayman na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kuondoka.

Na kisha baada ya Wiki Moja Bi Amina Bint Wahb na Barakah na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam wakafunga Safari kurudi katika Mji wa Makkah.

Ukweli ni kua hii ilikua ni safari yenye kuchosha Sana kuenda na Kurudi kwa Njia ya

Jangwani Hususan kwa Mwanamke. Na Msafara ulipofika katikati baina ya Madinah Na

Makkah basi Bi Amina Bint Wahb akapatwa na Homa Kali sana.

Msafara ukasimamishwa na hapo Bi Amina bint Wahb akazidi kuzidiwa hivyo

akamwamita Barakah na kumwambia: ‘Ewe Barakah hakika mimi sitoweza kuendelea


610

kuishi kwani mda wangu wa kuondoka Duniani umewadia, hivyo nakuachia Mtoto

wangu Muhammad chini ya Uangalizi wako, umlee kama mtoto wako kwani

alimpoteza Baba yake wakati akiwa tumboni mwangu na sasa hivi atampoteza

Mama yake mbele ya macho yake. Barakah kua nae Muhamamd na wala usiachane

nae.’

Barakah anasema: ‘Mimi nikaanza kulia kwa huzuni kwani nilihisi kua Moyo wangu

ulikua umevunjika vipande vipande Muhammad alipoona hali hio basi nae akaanza

kulia na kisha akamkumbatia Mama yake shingoni huku Amina akiwa ni mwenye

kutoka Roho yake’

Kwani tukio hili la Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuondokewa na Mama yake

mzazi ambae ni Aminah Bint Wahb lilitokea katika maeneo ya Al Abwa. Ambapo kipindi

hiki Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua na umri wa Miaka 6 tu akiwa hana

Baba wala Mama na Amina Bint Wahb akazikwa katika eneo hilo, na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akabakia na Baraka ambae ni Mama yake Mlezi

aliekabidhiwa na Mama yake Mzazi.

Subhana Allah!

Tunapokitafakkari kisa hiki mpaka hapa tulipofikia basi tunaona Hikma zake Allah

Subhanah wa Ta'ala katika Kila hatua ya Maisha ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kua lilikua linamtayarisha katika kukulia katika mazingira ya kubeba Majukumu

yake Matukufu aliyotayarishiwa na Fatiri Al Samawati wa Al Ardhi yaani Muumba wa

Mbingu na Ardhi.

Kwani kutokana Hikma zake basi Allah Subhanah wa Ta'ala alikua akimtayarisha Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kumuonesha Utukufu wake mbele ya Mola wake,

kua hakuna yeyote yule anaetakiwa amtegemee isipokua Allah Subhanah wa Ta'ala.

Yaani hapa inakua zaidi ya ile ya Nabii Musa ambae nae alifanyiwa kama hivi lakini

baadae akawekwa kwenye Jumba la Kifalme la Firawn, na Kulelewa na Wamisri wakati

yeye ni Muisrail na Nabii Musa alikua na Kaka na Dada na Mama mpaka Ukubwani.

Lakini kwa upande wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakua na Kaka wala Dada,

hakua na Mama wala Baba, bali alikua na Baraka ambae ni Mama Mlezi tu ambae nae

hakua Muarabu kama alivyokua yeye Mwenyewe.

Kwani kama tunakumbuka mwanzoni mwa Kisa basi tulisema kua ingawa Baraka

alijikuta anauzwa Kama Mtumwa na kujihisi kua ana Bahati mbaya sana, lakini kwa

upande wa Muumba yaani Allah Subhanah wa Ta'ala m-bora wa Kukadiria basi alikua

tayari amesha mkadiria Baraka Darja ya Juu kabisa miongoni mwa Waja wake.


611

Hivyo Bahati mbaya yake aliyoiona hapo mwanzo kumbe ilikua ndio Bahati ya Dhahabu

kwake kwa Sababu kutokana Baraka alitoka katika Darja ya Chini ya Kua Mtumwa na

Moja kwa Moja kupanda hadi kua Mama Mlezi wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam.

Na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam mpaka alipokua Mtu mzima basi alikua

akijivunia Mama yake huyo aitwae Baraka kwa kumwita Ummmi yaani Mama.

Ambapo Ndani ya Hili pia kuna Hikma ya Allah Subhanah wa Ta'ala kutufunza sisi kua

Ibn Adam wote ni wamoja, iwe Mswahili, Muarabu, Mhindi, Mzungu, n.k

Tusidharauliane na Hivyo Usiwe na Kibri na kumwambia Mwenzio; Unajua mimi Nani?

Kwani unaweza kumdharau na kumfanyia Kibr Mtu ambae mbele ya Muumba na Mtume

wake akawa na Darja kubwa Sana kutokana na Nuru ya Imani Moyoni mwake.

Na tusiichukulie mitihani tunayokumbana nayo Duniani kua ni kwa ajili ya Kutudidimiza

kwani hua ni kwa ajili ya kutusafisha na Kutupandisha Darja zaid kama tutakua na Subra.

USAFI WA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM NA

USAFI WA WAZEE WAKE.

Aliulizwa Imam Muhammad Abdur Rauf Bin Taj Al Arifin Ibn Ali Bin Zainal Abidin

Ibn Yahya Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Ahmad Ibn Makhluf Ibn

Abd Salam Al Hadadiy Al Munawiy Al Qahiriy Al Mishriy Al Shafii: ‘Hivi Jee Wazee

wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam wako Motoni ama la?’ ambapo Imam Al

Munawi akasema kua: ‘Wazee wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam walifariki

katika kipindi ambacho hukukua na Mtume na bila ya shaka hua hakuna Adhabu

pale inapokua hakushushwa Mtume’ kwani amesema Allah Subhanah wa Ta’ala

katika Kitabu chake Kitukufu kua:

‏﴿م َّنِ‏ ٱهْتَدَىٰ‏ فَإِنم ََّا يَهْتَدِى لِنَفْسِ‏ هِ‏ وَمَن ضَل َّ فَإِنم ََّا يَضِل ُّ عَلَيْهَا وَلاَ‏ تَزِرُ‏ وَازِ‏ رَةٌ‏ وِزْرَ‏

أُخْرَىٰ‏ وَمَا كُن َّا مُعَذِّبِينَ‏ حَتى َّ ٰ نَبْعَثَ‏ رَسُولاً‏ ﴾

Mani ihtada fa-innama yahtadee linafsihi waman dhalla fa-innama yadhillu

AAalayha wala taziru waziratun wizra okhra wama kunna muAAadhdhibeena

hatta nabAAatha rasoolan (Surat Al Isra 17:15 )


612

Tafsir: Yeyote yule Atakaejiongoa basi atakua amejiongoa kwa ajili ya Nafsi yake na

atakaepotoka basi atakua amejipotosha kwa ajili ya Nafsi yake, na hakuna mbebaji

atakaebeba mzigo wa mwenzake, na hatukua sisi wenye kuadhibu hadi kwanza pale

tutakapotuma Mjumbe.

Hii ni aya ambayo inatubainishia kua Allah Subhanah wa Ta’ala hatowaadhibu wale

watu ambao hawakufikiwa na Ujumbe wa Dini ya Kiislam, ambapo kwa upande wa Abu

Hurayrah Radhi Allahu Anhu basi yeye amesema kuhusiana na ayah hii kua: ‘Allah

Subhanah wa Ta’ala atawakusanya watu wote ambao waliishi baina ya Mitume

Miwili yaani baada ya kufariki kwa Mtume wa kwanza na wa kabla ya kuwasili

Mtume wa pili, ambapo ndani yake kundi hili watakuwemo pia watu walioishi huku

wakiwa hawana akili, Viziwi na Mabubu na kisha atawajaalia Mtume miongoni

mwao. Na kuwaamrisha kua waingie Motoni na hivyo wao watakua ni wenye

kusema: ‘Tutaingiaje Motoni wakati sisi hatukutumiwa Mtume?’’

Abu Hurayrah Radhi Allahu Anhu anaendelea kusema kua: ‘Wa Allahi kama

wangekubali kuingia basi Moto huo wangeuona kua baridi na salama juu yao, hivyo

wale ambao wangekua ni wenye kumtii Allah Subhanah wa Ta’ala Duniani basi na

hapa wangetii amri hio’

Ambapo tunapoangalia hali hii kwa upande wa Wazee wake Rasul Salallahu Allahyi wa

Salam basi tunaona kua Wanazuoni wanasema kua: ‘Hakukua na Mtu katika

mnyororo wa wazee wake Rasul Salallahu Allahyi wa Salam ambae alikua ni

mwenye kumshirikisha Allah Subhanah wa Ta’ala tangu kutokea kwa Nabii

Ibrahim, na hakuna alieuchafua Moyo wake kwa kumshirikisha Allah Subhanah

wa Ta’ala’

Kwani amesema Al Imam, Al 'Allamah, Al Hafidh Al Awhad Sheikh Al Islam Qadhi

'Iyad Ibn Musa Al Yahsubi kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kua: ‘Mimi nimetokana na mpangilio wa kizazi cha Waliosafi daima katika Mababa

na Mamama’’

Na Qur’an inawazungumzia watu wasioamini Allah Subhanah wa Ta’ala kua ni Wachafu

kama zinavyosema aya:


613

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُو ۤ اْ‏ إِنم ََّا ٱلْمُشْرِكُونَ‏ نجََسٌ‏ فَلاَ‏ يَقْرَبُواْ‏ ٱلْمَسْجِ‏ دَ‏ ٱلحَْرَامَ‏ بَعْدَ‏ عَامِهِمْ‏

هَٰذَا وَإِنْ‏ خِ‏ فْتُمْ‏ عَيْلَةً‏ فَسَوْفَ‏ يُغْنِيكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ مِن فَضْلِهِ‏ إِن شَآءَ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ عَلِيمٌ‏

حَكِيمٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo innama almushrikoona najasun fala yaqraboo

almasjida alharama baAAda AAamihim hadha wa-in khiftum AAaylatan fasawfa

yughneekumu Allahu min fadhlihi in shaa inna Allaha AAaleemun hakeemun(Surat

At Tawba 9:28)

Tafsir: Enyi Mlioamini, hakika ya Washirikina ni Najisi hivyo msiwaruhusu

kuukaribia Masjid Al Haram baada ya mwaka huu na kama mtakua mnaukhofia

Umasikini, basi Allah atakutajirisheni kutokana na fadhila zake akitaka, Hakika Allah

ni mwenye kujua kila kitu na ni mwenye Hikma nyingi sana.

Hivyo kutokana na kua Usafi ni tofauti na Uchafu na kua na Imani hua ni Usafi na

kutokua na Imani hua ni Uchafu basi inabidi kukubaliana kua hakukua na aliekua mchafu

miongoni mwa Wazazi wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, na ndio maana Allah

Subhanah wa Ta’ala akampandisha Darja Mtume wake huyo Salallahu Alayhi wa Salam

kama alivyosema katika Qur’an:

‏﴿لَقَدْ‏ جَآءَكُمْ‏ رَسُولٌ‏ مِّنْ‏ أَنفُسِ‏ كُمْ‏ عَزِيزٌ‏ عَلَيْهِ‏ مَا عَنِت ُّمْ‏ حَرِيصٌ‏ عَلَيْكُمْ‏ بِٱلْمُؤْمِنِ‏ ينَ‏

رَءُوفٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Laqad jaakum rasoolun min anfusikum AAazeezun AAalayhi ma AAanittum

hareesun AAalaykum bialmu/mineena raoofun raheemun (Surat At Tawbah 9:128)

Tafsir: Kwa hakika, amekujieni Mtume (Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam)

kutoka miongoni mwenu, Inamuuma sana kua nyinyi mdhurike au mpate matatizo,

ana wasiwasi juu yenu (ili mpate kuongoka, na mtubu kwa Mola wenu, ili mpate

kuingia Peponi na muokoke na moto) kwa Waumini Yeye (Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam) Ni mwingi wa Huruma na mwingi wa Rehma.


614

Ambapo amesema Imam Al Husayn Ibn Al Fadhl kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala

amempa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam Sifa mbili tukufu za majina yake

yeye Allah Subhanah wa Ta’ala ambazo ni Mwingi wa Huruma na ni mwingi wa

Rehma’,

Ambapo juu ya usafi wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi pia limeelezewa

na ile aya isemayo:

‏﴿لَقَدْ‏ مَن َّ ٱهلل َُّ‏ عَلَى ٱلْمُؤمِنِينَ‏ إِذْ‏ بَعَثَ‏ فِيهِمْ‏ رَسُولاً‏ مِّنْ‏ أَنْفُسِ‏ هِمْ‏ يَتْلُواْ‏ عَلَيْهِ‏ مْ‏ آَتِهِ‏

وَيُزَكِّيهِمْ‏ وَيُعَلِّمُهُمُ‏ ٱلْكِتَابَ‏ وَٱلحِْكْمَةَ‏ وَإِن كَانُواْ‏ مِنْ‏ قَبْلُ‏ لَفِى ضَلالٍ‏ م ُّبِينٍ‏ ﴾

Laqad manna Allahu AAala almu/mineena idh baAAatha feehim rasoolan min

anfusihim yatloo AAalayhim ayatihi wayuzakkeehim wayuAAallimuhumu alkitaba

waalhikmata wa-in kanoo min qablu lafee dhalalin mubeenin(Surat Al Imram 3:164)

Tafsir: Kwa hakika ametunuku Allah kwa Waumini pale alipotuma miongoni mwao

Mtume (Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) kutokana nao, akiwasomea aya zake

na kuwasafisha (Kutokana na dhambi zao) na kuwatukuza na kuwafahamisha Kitabu

chake na Hikma (Sunnah za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam), wakati hapo

kabla walikua kwenye upotovu mkubwa.

Ambapo kama tunavyojua kua haiwezekani kua kitu kinachosafisha kitu chengine kua ni

kichafu kwani badala ya kusafisha basi kitachafua zaidi, hivyo bila ya shaka kitu kisafi

ndio hua kina sifa ya kusafisha kile kilicho kichafu na hivyo usafi unaozungumziwa hapa

na ayah hii ni Usafi wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kutokana na asili yake na

yale aliyokuja nayo kutoka kwa Mola wake kwa ajili ya Waumini wa Dini yake, kama

alivyoomba Nabii Ibrahim Alayhi Salam pale aliposema.

‏﴿رَب َّنَا وَٱبْعَثْ‏ فِيهِمْ‏ رَسُولاً‏ مِّنْهُمْ‏ يَتْلُواْ‏ عَلَيْهِمْ‏ آَتِكَ‏ وَيُعَلِّمُهُمُ‏ ٱلْكِتَابَ‏ وَٱلحِْكْمَةَ‏

وَيُزَكِّيهِمْ‏ إِن َّكَ‏ أَنتَ‏ ٱلعَزِيزُ‏ ٱلحَكِيمُ‏ ﴾

Rabbana waibAAath feehim rasoolan minhum yatloo AAalayhim ayatika

wayuAAallimuhumu alkitaba waalhikmata wayuzakkeehim innaka anta

alAAazeezu alhakeemu (Surat Al Baqara 2:129)


615

Tafsir: Ewe Mola wetu! Watumie (Vizazi vyetu hivyo) kutoka miongoni mwao Mtume.

Ambae atawasomea aya zako na kuwaelimisha juu ya Kitabu chako na Hikma na wape

Utukufu. Kwani kwa hakika wewe ni mwenye uwezo juu ya kila kitu na ni mwingi wa

Hikma’

Ambapo amesema Imam Abu Muhammad Al Husayn Ibn Mas'ud Ibn Muhammad Al

Farra Al Baghawi kua: ‘Amesema Mujahid kua Maana ya neno Kitabu na neno

Hikma yaliyotajwa kwenye aya hii yanamaanisha kua: ‘Kitabu ni Qur’an na Hikma

hua inamaanisha Kuifaham Qur’an ambapo wengine wamesema kua neno Hikma

lililotumika hapa linamaanisha Hukmu. Na wengine wamesema kua ni Ilm

inayojumuishwa na kuifanyia kazi Ilm hio.’

Na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akasema katika njia ya kuonesha kua ni mwenye

kujibu Dua ya Nabii Ibrahim ya kuletewa kwa Watu wa Mji wa Makkah Mtu

akataewasafisha na kuwafundisha Hikma na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala kua ni

mwenye kudhihirisha majibu ya Dua yake hio katika aya zifuatazo:

‏﴿هُوَ‏ ٱل َّذِى بَعَثَ‏ فىِ‏ ٱلأُمِّيِّينَ‏ رَسُولاً‏ مِّنْهُمْ‏ يَتْلُو عَلَيْهِمْ‏ آَتِهِ‏ وَ‏ يُزَكِّيهِمْ‏ وَيُعَلِّمُهُمُ‏

ٱلْكِتَابَ‏ وَٱلحِْكْمَةَ‏ وَإِن كَانُواْ‏ مِن قَبْلُ‏ لَفِى ضَلاَلٍ‏ م ُّبِينٍ‏ ﴾

Huwa alladhee baAAatha fee al-ommiyyeena rasoolan minhum yatloo AAalayhim

ayatihi wayuzakkeehim wayuAAallimuhumu alkitaba waalhikmata wa-in kanoo

min qablu lafee dalalin mubeenin(Surat Al Jumuah 62:2)

Tafsir: Yeye (Allah Subhanah wa Ta’ala) ndie ambae aliemleta kutokana na watu

wasiojua Mtume kuwaletea juu yao Aya zake na kuwasafisha na kuwasomesha kitabu

chake na hikma ijapokua hapo kabla walikua wapo katika upotovu mkubwa

Na pia kama alivyosema tena Allah Subhanah wa Ta’ala kua

﴿ كَمَآ أَرْسَلْنَا فِيكُمْ‏ رَسُولاً‏ مِّنْكُمْ‏ يَتْلُواْ‏ عَلَيْكُمْ‏ آَتِنَا وَيُزَكِّيكُمْ‏ وَيُعَلِّمُكُمُ‏

ٱلْكِتَابَ‏ وَٱلحِْكْمَةَ‏ وَيُعَلِّمُكُم م َّا لمَْ‏ تَكُونُواْ‏ تَعْلَمُونَ‏ ﴾


616

Kama arsalna feekum rasoolan minkum yatloo AAalaykum ayatina

wayuzakkeekum wayuAAallimukumu alkitaba waalhikmata wayuAAallimukum

ma lam takoonoo taAAlamoona (Surat Al Baqara 2:151)

Tafsir: Kama tulivyokushushieni juu yenu Mtume kutoka miongoni mwenu

kukuleteeni Aya zetu na kukusafisheni na kukufundisheni Kitabu na Hikma nan a

kukufundisheni juu ya yale mliyokua hamyajui.

Ambapo amesema Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kuhusiana na maneno yasemayo

Rasoolan minhum na Rasulan Minkum kua yanamaanisha: ‘Kutokana na Wazee,

kutokana na Uhusiano wa Kindoa na Kizazi, kua hakuna Mchafu (wa Dhambi)

kutoka miongoni mwa Mababu zake tangu kuanzia kwa Nabii Adam, kwani Wazee

wake wote walikua ni waliooana Kisharia’

Ambapo Imam Ibn Qalbi basi alisema kua: ‘Hakika mimi nimeandika Kitabu chenye

Wazee 500 wa Kike wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na sikuwahi kukuta

yeyote miongoni mwao mwenye sifa mbaya ikiwemo uzinifu ambao ulikua

umetapakaa katika nyakati za Kijahiliyah’

Na akasema Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Maneno ya

Allah Subhanah wa Ta’ala yasemayo

‏﴿وَتَقَل ُّبَكَ‏ فىِ‏ ٱلس َّاجِ‏ دِينَ‏ ﴾

Wataqallubaka fee alssajideena (Surat Ash Shuara 26:219)

Tafsir: Na Unapogeuka (Ewe Muhammad) miongoni mwa Wanaosujudu.

Yanamaanisha kua Kutoka kwa Mitume na Mitume hadi nikakutoa kua kama

Mtume.

Hivyo ingawa Wazazi wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam waliishi katika kipindi

cha Ujahiliyah na hawakuishi katika kipindi cha uhai wa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam lakini hii haimaanishi kua Wazee wake hao hawatopata Uokovu katika siku ya

Malipo kwa sababu wao ndio waliobeba na kutoa Nuru ya Utume na walikua katika hali

ya usafi ambayo kupitia katika hali yao hio ndio kulikomtoa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kwa hekima za Allah Subhanah wa Ta’ala.

Hivyo baada ya kuzikwa kwa Amina Bint Wahb basi Barakah akarudi katika Mji wa

Makkah Huku akiwa na Mtoto wake wa kulea ambae ni Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, ambapo wakaenda moja kwa moja hadi kwa Babu yake Rasul Allah Salallahu


617

Alayhi wa Salam ambae ni Abd Al Mutallib na hivyo wote wawili wakahamia na kua ni

wenye kuishi ndani ya Nyumba hio kwa mda wa Miaka miwili huku Abd Ul Muttalib

akiwa ni mwenye kumpendekeza Abu Talib kua ni msimamizi wa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kama yeye atakua hayupo.

Wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipokua na umri wa miaka 7, basi

Mfalme wa Yemen aitwae Seif Ibn Dhi Yazin Al Himyari aliiteka sehemu ya Ardhi ya

Abisyniya, hivyo wakuu mbali mbali wa ardhi za Kiarabu wakaelekea katika ardhi ya

Yemen kwa ajili ya kumpongeza, ambapo miongoni mwao alikuwemo pia Abd Ul

Muttalib ambae nae alikua ameongozana pia na Mjukuu wake yaani Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam.

Na walipofika basi Mfalme Dhi Yazin akamuita kwa faragha Mzee Abd Ul Muttalib kwa

umuhimu wa kua ndie Kiongozi wa Mji wa Makkah na kumwambia: ‘Ewe Abd Ul

Muttalib, hakika mim nna maelezo ya siri ambayo inabidi nikueleze na hatakiwi

ajue mtu mwengine, na mimi sijawahi kumwambia mtu mwengine isipokua wewe

na hi ni kutokana na maubile ya Sifa na Tabia zako’

‘Hivyo jambo nitakalokuambia litabakia kua ni siri yako hadi pale Allah

atakapoamua kulidhihirisha, kwani imedhihirika kwangu mie kua kuna Mtoto

atazaliwa ambae atakua na alama mgongoni baina ya mabega yake mawili, ambae

atakua ni kiongozi atakua anafuatwa na Watu hadi siku ya Kiama. Na Mtoto huyo

sijajua kama ameshazaliwa ama bado, ila akizaliwa basi atakua ni Yatima, atafiliwa

na Baba yake na Mama yake, na kisha atalelewa na Babu yake na kisha Babu yake

huyo atafariki, na kisha Mtoto huyo atalelelewa na Ami yake.’

‘Na ingawa wako wengi watakaofanana nae lakini huyu atakua ni alietumwa na

Allah na hivyo atapata wafuasi ambao watampenda na kumuunga mkono sana kwa

kila kitu, nae atapingana na watu wengi, na wafduasi wa Dini mbali mbali na

kuwaadhirisha maadui zake na kuziteka sehemu bora za Ardhi Ulimwenguni, na

kuwafanya watu wawe ni wenye kumuabudu Allah tu mwingi wa Rehma. Ambapo

maneno yake yatakua ni ya Hekima, Busara na Uadilifu, atawaamrisha watu

kuachana na maovu nae hatofanya maovu na atawaamrisha kufanya mema na yeye

atakua ni mwenye kufanya mema. Nami nnaapa juu ya haya nnayoyasema kwa

Mugu wa Al Kaabah.’

Abd Ul Muttalib akasema: ‘Ewe Mfalme Dhi Yazin, hakika mimi nilikua nnae mtoto

wa kiume ambae alikua anaitwa Abdullah nilikua nampenda sana, hivyo

nikamuozesha kwa mwanamke bora katika jamii yangu, mke wake alikua anaitwa

Amina, na ndoa yao imetoa mtoto wa kiume ambae ana alama mgongoni mwake na

ana kila dalili ulizoziainisha, kwani Baba yake na Mama yake wameshafariki na


618

sasa hivi niko nae mimi na nimempendekeza alelewe na Ami yake nitakapofariki

mimi’

Mfalme Dhi Yazin akasema: ‘Basi hilo ndio nililokua nataka kukuambia, kwa hivyo

mtunze mjukuu wako kutokana na madhara ya Mayahudi na Manasara kwani ndio

watakaokua maadui zake wakubwa. Lakini Allah atamlinda dhidi yao, hivyo fanya

hii iwe siri yako bila ya kuwataarifu watu kwani tamaa yao ya uongozi itawapelekea

kupingana nae pia. Mimi nimeona haya kwenye vitabu ambamo ndani yake

mmesemwa pia kua Mji wa Madinah utakua ndio utakaompa usalama ambao

kutokana nao atapata ushindi mkubwa sana.’

‘Ila nnamkhofia kua atapatwa na matatizo makubwa, hakika mimi nnao uwezo wa

kuwaambia Waarabu wote wamfuate, ila mimi nnakukabidhi wewe jukumu hilo

kwani sina uhakika kama watu wako watakubaliana nalo jukumu hilo. Hivyo mimi

na wewe tutawasiliana tena juu ya jambo hili baada ya mwaka’

Kisha Mfalme Dhi Yazin akawazawadia Wajumbe aliokuja nao Abd Ul Muttalib zawadi

ya Watumwa 10 kila Mjumbe, Fedha, Vitambaa na Mafuta Mazuri.

Na ingawa Abd Ul Mutalib alikua ni mtu wa kawaida kwa muonekano wake likini alikua

si Mtu wa Kawaida mbele ya watu wake, kwani alikua ni kiongozi wa Kabila la Quraysh,

na ilikua ni kawaida ya Viongozi wa Kabila la Quraysh kila siku asubuhi kukutana

kwenye Al Kaabah kwa ajili ya kuzungumzia kuhusiana na Jamii yao, hivyo alikua

akifika basi hutandika chini nguo yake kisha huikalia, na alikua hamruhusu mtu yeyote

yule kuikalia nguo yake hio anayoitandikia chini isipokua Mjukuu wake yaani Rasul

Allah Sallah Alayhi wa Salam ambae alikua akienda nae kila siku kwenye Mkutano huo.

Kwani Abd Ul Muttalib alikua hataki Mjukuu wake huo kutokana na Dalili zake na

mabashirio mema juu yake awe ni mwenye kucheza na Watoto wengine, na alikua akikaa

nae pembeni yake kwenye mikutano hio ya baraza basi hua ni mwenye kusema kuhusiana

na Rasul Allah Sallah Alayhi wa Salam kua: ‘Huyu Mtoto wangu atakuja kua Mtu

Mkubwa sana.’

Lakini hata hivyo Abd Ul Muttalib hakujaaliwa kua ni mwenye kuishi na kuithibitisha

kauli yake hio kwani mbali ya kua baada ya Abd Ul Muttalib mbali kuagana na Mfalme

Dhi Yazin basi Mfalme Dhi Yazin hakuishi kwa mda mrefu akafariki Dunia. lakini pia

baada ya kumalizika miaka miwili basi Mzee Abd Al Mutallib nae akafariki Dunia.

Hivyo Barakah na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam wakahamia kwa Ami yake

Abu Talib ambae ni Ami yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na pia Baba yake

Sayyidna Jaffar Ibn Abu Talib Radhi Allahi Anhu na Sayyidna Ali Ibn Abu Talib Radhi

Allahu Anhu, hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikaa kwa Abu Talib kwa

takriban miaka 17 huku akiwa chini ya Uangalizi wa Baraka yaani Mama yake Mlezi.


619

RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM NA UMMU

AYMAN KATIKA NYUMBA YA ABU TALIB NA FATMA BINT ASAD

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipotimia umri wa miaka minane akawa

ni mwenye kuishi kwa Ami yake huyo Abu Talib aliependekezwa na Abd Ul Muttalib

kutokana na kua Abu Talib alikua ni mtu ambae mwenye huruma sana ingawa alikua ni

mtu masikini lakini ni mwenye uaminifu na mwenye kupendwa na watu wote wa kabila

la Quraysh na kamwe hakua ni mwenye kuishi maisha yake katika hali ya Kijahilia kama

walivyokua wakiishi watu wengine wa Mji wa Makkah.

Abu Talib alikua ni mtu mwenye kumiliki Ngamia wachache na alikua na ni mwenye

famila kubwa sana, kama vile ambavyo Ali Ibn Abu Talib alivyokua akimzungumzia

baba yake huyo kwa kusema: ‘Baba yangu alikua ni Kiongozi wa watu wa kabila la

Quraysh na ingawa alikua ni Masikini lakini hakuna mtu miongoni mwa watu wa

Quraysh aliekua anajiona ana darja ya juu zaidi yake’

Hivyo bila ya shaka Abu Talib alikua ni Mtu pekee ambae anatashiki kua ni msimamizi

wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Abu Talib alikua pia ndie Msimamizi wa Al

Kaabah na kuwagawia Maji Mahujaji wanaotembelea Mji wa Makkah lakini kutokana

na ugumu wa maisha yake basi akaamua kulihamishia Jukumu hili kwa ndugu yake

ambae ni Al Abbas. Abu Talib alikua ni mtu ambae anaempenda sana Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kuliko hata anavyowapenda watoto wake kiasi ya kua alikua

kila sehemu anayoenda au kukaa basi na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hua

yuko pembeni yake, hata wakati wa kula pia likua haiwezaki kwake kula bila ya kuwepo

Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam pembeni yake.

Na ingawa alikua ni mtoto mdogo lakini Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam alikua ni

mtoto ambae anapokaa na watu kula basi chakula hicho hua ni chenye barka kubwa sana

na ingawa hakua ni mtoto mwenye kupenda kula sana lakin pia hakua ni mtoto mwenye

kulalamika juu ya kua na njaa au kiu, kwani anasema Ummu Ayman kua: ‘Hakika mimi

sijawahi kumuona Mtume Muhammad Salallah Alayhi wa Salam akilalamika juu

ya Njaa au kiu katika wakati wa utoto wake. Kwani alikua akinywa funda moja la

maji ya Zamzam asubuhi na kisha kila tukitaka kumpa chakula alikua akisema kua

hakika yeye hana njaa kwani ameshiba’

Katika kipindi hiki cha Utotoni wakati akiwa anaishi kwa Abu Talib basi hali ya

mazingira ya Mji wa Makka ilibadilika tena na ikawa kuna ukame, baada ya kua mvua

haikunyesha kwa mda mrefu, hivyo watu wa kabila la Quraysh wakamwambia Abu

Talib: ‘Ewe Abu Talib, Watu wetu na wanyama wetu wanakufa kutokana na

Ukame, hivyo tuombee ili tuweze kupata Mvua kutoka kwa Allah.’


620

Hivyo Abu Talib akakubaliana na ushauri huo na akamchukua Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam na wakaenda hadi kwenye Al Kaabah, kisha Abu Talib akanyanyua

mikono juu na kuanza kuomba huku Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam akiwa

amesimama pembeni yake mkono wake wa kushoto ukiwa umekamata Kitambaa cha Al

Kaabah na mkono wake wa kulia ukiwa umenyoosha kidole cha shahada kuelekea

Mbinguni. Na haukuchukua mda isipokua Maombi hayo ya Abu Talib na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam yalijibiwa kwa kumwagika mvua kubwa sana na yenye

manufaa kwa watu wote wa Mji wa Makkah na maeneo ya Karibu yaliyokumbwa na

ukame huo.

Katika wakati huu ambao Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipokua akiishi kwa

Abu Talib basi ndani ya nyumba hio hakua ni mwenye kupendwa na Abu Talib tu bali

pia alikua akipendwa sana na Mke wake Abu Talib ambae alikua anaitwa Fatma Bint

Asad ambae nae pia aikua akmpenda zadi ya anavyowapenda watoto wake na hvyo alikua

akimuonesha kua yeye ni kama mama yake mzazi na hivyo kumfanya Rasul Allah

Salaahu Alayh wa Salam asijihisi kua ni Yatima.

Na hivyo mapenzi haya ya Fatma Bint Asad kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

yalimuathiri pia na yeye mwenye Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam kiasi ya kua

baadae alipokuja kuoa basi alimwita Mtoto wake wa kike kwa jina la Fatma kutokana na

mapenzi yake kwa mama yake huyu kipenzi, na mapenzi haya yalidhihirishwa wazi pale

baadae katika maziko ya Fatma Bint Asad ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam alivua Kanzu yake na kumzungushia nayo Fatma Bint Asad wakati alipokua

akimuweka kaburini huku akisema: ‘Leo Mama yangu amefariki, na baada ya Abu

Talib basi hakukua na mwanamke ambae alionesha mimi ukarimu na huruma

kama Mwanamke huyu, hivyo nimeifanya kanzu yangu hii kua ndio sanda yake

ambayo ndio itakayokua kanzu yake Peponi na nimemuwekea nayo ili ayapende na

kuyazowea maisha ya hapa kaburini.’

Wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipotimia umri wa maka 10 basi Abu

Talib alifunga safari nae kuelekea katika ardhi ya Sham, ambapo njiani walipofika

kwenye maeneo ya Ardhi ambayo linajulikana kama Busra, msafara wao ukasimama

kwenye eneo ambalo lilikua lina jengo la Makaazi ya Makasisi wa Kikristo ambao lilikua

linasimamiwa Mtawa aitwae Bahira.

Na Msafara huo uliposimama kwenye eneo lake basi Bahira akahisi kua kuna utofauti wa

hali ya muonekano wa kimazingira ya msafara huo na misafara myengine ilipokua

inakuja, hivyo akaamua kuwaalika watu wote waliomo kwenye msafara huo kwa ajili ya

chakula chake, ambapo watu wa msafara huo wakaingia na kujitayarisha kwa ajili ya

mualiko huo wa chakula lakini kwa kua Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam alikua

hana njaa sana kama kawaida ya maumbile yake, basi yeye akamuomba Abu Talib kua


621

bora abakie chini ya mmoja kati ya miti iliyopo nje ya Jengo hilo kwa ajili ya kusimamia

Ngamia wa Msafara huo.

Baaa ya watu wa Msafara huo kungia ndani basi Bahira akapita na kuwaangalia watu

wote waliomo kwenye Msafara huo kwenye nyuso zao, laini hata hivyo ikawa kama

hakuridhika na kile alichokiona kwenye nyuso hizo za watu wa Msafara huo, kwani

alikua anategemea kuona kile kilichomuonesha utofauti wa Msafara huo kabla ya

kuwasili kwake, hivyo akawauliza watu waliopo mbele yake kwa kusema: ‘Hakika mimi

nimemkaribisha kila mtu aliekuwepo pamoja nanyi kwenye Msafara wenu, hivyo

jee mna uhakika kua hamjamuacha mtu yeyote nje ya Msafara huu?’

Abu Talib akasema kua: ‘Kuna Mtoto mmoja aitwae Muhammad ambae yeye yuko

nje anasimamia Ngamia wa msafara wetu’

Bahira akasema: ‘Inabidi awepo kwani nae ni miongoni mwa walioalikwa kwenye

mualiko huu.’ Hivyo Bahira akatoka nje na kumuangalia Mtoto huyo, na alipofika nje

na kumuangalia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi akaona mti huo kua uko

katika hali ya kua kama ni wenye kuinama na ni wenye kumkumbatia Mtoto huyo. Na

hapo hapo akakiona kile ambacho alikua anakitegemea kukiona kwenye uso wa Mtoto

huyo ambayo ni Alama ya Nuru ya uso wa Mtoto huyo, na hivyo Bahira akafurahia sana

kuona alama ya Nuru hio.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akala pamoja na watu wake kwenye msafara huo,

na kisha baada ya kula chakula hicho basi Bahira akamwambia Abu Talib kua:

‘Mlipokua mnakuja kwenye msafara wenu, mimi niliona kiwingu ambacho kilikua

kinafuatana nanyi kwa ajili ya kukufanyieni kivuli msafara wenu, na pia kiwingu

hicho kilikuwepo juu ya Mti uliposimama msafara wenu ambao ndio alipokua

amekaa mtoto huyu.’

Kisha Bahira akamuangalia Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam Mgongoni na

akaona Alama ya Utume wa Mwisho ambayo ni alama ya mtokezo wa umbo la nusu

duara chini ya mfupa wa mabega ya Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam na akasema:

‘Hii ndio Alama inayoonesha kua huyu ndie Mtume wa mwisho alietajwa kwenye

Vitabu vyetu ambae Allah atamtuma kua ni Rehma kwa Walimwengu. Hivyo na

kushauri Abu Talib kua rudi nae nyumbani mtoto huyu kwani Mayahudi

wakimuona basi watajaribu kumuua Mtoto huyu.’ Na hivyo Abu Talib akaufanyia

kazi ushauri huo kwa kukatisha safari yao hio na kurudi nae Rasul Allah Salallahu

A’layhi wa Salam katika Mji wa Makkah.


622

Baada ya kurudi safari yao hio basi Rasul Allah Salallah Alayh wa Salam akawa ni

mwenye kumsaidia Abu Talib kuchunga Kondoo wake ingawa Abu Talib mwenyewe na

Fatma Bint Asad hawakupendelea jambo hilo. Lakini kutokana na kua yeye mwenyewe

lilimvutia sana basi wakamwamchia awe ni mwenye kuchunga Kondoo hao katika

maeneo ya ardhi ya Jiyad katika Mji wa Makkah, na pia baadae akawa ni mwenye kazi

ya kuchuma Matunda ya Siwak katika maeneo ya Marr Zahran.

Ambapo alisema Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam kua: ‘Mara kadhaa mimi

nilikua nataka kufanya mambo ambayo wanafanya watu wa zama za Kijahiliya,

lakini Allah Subhanah wa Ta’ala alinizua mimi kufanya mambo hayo, hivyo kuanza

hapo sikutaka kufanya yale mambo ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala alikua

hataki niyafanye hadi pale nilipopata Utume. Ama kuhusiana na mambo

niliyokusudia kuyafanya basi hali ilikua kama hivi:

Siku moja Usiku mimi pamoja na vijana wa Quraysh tulikua tunachunga Kondoo

wetu kwenye mmoja kati ya milima ya Makkah, hivyo nami nikapendekeza kwa

rafiki yangu kua kama atanisaidia kuangalia Kondoo wangu basi mimi nitaenda

pamoja na marafiki zangu wengine kwenye viburudisho vya usiku ambapo watu

hua wanakaa na kutoleana hadithi, hivyo rafiki yangu huyo akasema kua

ataniangalizia Kondoo wangu kwa ajili yangu, nami nikaelekea Mjini Makkah.’

Na nilipoziona tu Nyumba za Makkah na kusikia sauti za watu waliokua wakipiga

kelele kwa kuburudika, basi nikamuuliza mtu mmoja kuna nini? Nae akaniambia

kua kuna mtu anaoa na wanasheherekea harusi yao. Hivyo nami nikakaa karibu na

harusi hio na kuanza kuangalia kinachotokea. Na mara nikapitiwa na usingizi

sikuweza kuamka hadi lilipochomoza jua na niliporudi kwa rafiki yangu akaniuliza

ni nini nilichofanya nami nikamwambia sikufanya chochote na kumuelezea

kilichotokea katika usiku wa kabla yake.

Usiku wa siku nyengine tena, nikamuomba rafiki yangu ruhusa ya kuondoka, nae

akanikubalia, hivyo nikaondoka na kuelekea kwenye mji wa Makkah, nami

nikaona yale niliyoyaona hapo kabla, na nikakaa na kuangalia, na nikalala tena na

sikuweza kuamka hadi asubuhi yake, kisha nikarudi na kumuelezea rafiki yangu

kilichotokea, na tangu siku hio sikujaribu kufanya jambo hilo tena hadi nilipopata

Utume. (Imam Al Munawi)

Ilikua ni kawaida ya watu wa Quraysh kukutana kwa mwaka mara moja mbele ya

Sanamu la Buwana ambapo hua wanakaa na kuzungumza, Kunyoa nywele zao, Kuchinja

wanyama wao na kusheherekea sherehe kubwa kubwa, hivyo wakati mmoja ulipowadia

mda wa kufanya hivyo basi wakajitayarisha na kutaka kukusanyika pamoja na kutaka

kumchukua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pamoja nao, lakini hata hivyo Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akakataa.


623

Hivyo Abu Talib na familia yake yote kwa ujumla wakamchukua na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kuelekea kwenye sehemu hio, lakini walipofika wakagundua

kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hayuko pamoja nao, hivyo wakakasirika na

kuanza kumtafuta, na walipompata basi walimuona kua yuko katika hali mbaya sana ya

kua taaban, hivyo wakamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwanini akawa

yuko katika hali kama hio, hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema:

‘Nna khofu kubwa sana nisije nikadhurika’ Abu Talib akamwambia: ‘Hakika wewe

una sifa nzuri sana na hivyo hivyo Allah hawezi kuruhusu kua uwe ni mwenye

kudhurika, Hivyo hebu tuambie imekuaje?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hakika mimi nilipolikaribia ile

sanamu basi kuna mtu aliekua amevaa nguo nyeupe alitokea mbele yangu na

kunambia kua: ‘Ewe Muhammad Rudi unakotoka na kamwe usiliguse

Sanamu’’Hivyo tangu siku hio basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakuwahi

kuyasogelea Masanamu hayo.(Imam Ali Burhan Din A Halabi)

Huku Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, alikua ni kijana mwenye uso na

umbo la kuvutia si mrefu sana wala si mfupi sana alikua na nywele nyeusi, nyusi na kope

zilizofunika macho makubwa ya kupendeza yaliyoficha ndani yake sifa ya mamlaka na

uongozi juu ya watu wengine, pua yake ilikua ya kawaida na mdomo wake ulikua na

meno meupe yaliyopangika vizuri, kidevuni alikua na ndevu zilizojaa, shingo ndefu

inayopendeza na kifua kilichobebwa na mabega mapana, alikua ni mwenye ngozi nyeupe

na akitembea hutembea kwa mwendo wa ukakamavu wa mtu aliekua kama mtu anae

teremka kilimani hata kama anapandisha kilima, muonekano wa sura yake ni wa mtu

mwenye upeo wa kuona mbali ki mawazo, ki hikma na mwenye kutafakkar.

Kutokana na kua ni mwenye matayarisho ya Kuteuliwa na Allah Subhanah wa Ta’ala

kua Nabii na pia ni Mtume wa mwisho alieletwa na Allah Subhanahu wa Ta’ala ili

kuuweka sawa Ulimwengu na kuuelekeza katika njia iliyo sahih, kuitoa Dunia katika njia

iliyojaa giza, ujinga na kila aina ya dhulma na kuuingiza katika njia yenye Nuru, I’lm na

Uadilifu. Kama alivyosema Allah Subhanahu wa Ta’ala katika Qur’an.

‏﴿هُوَ‏ ٰ ۤ ٱل َّذِي أَرْسَلَ‏ رَ‏ سُولَهُ‏ بِٱلهُْدَىٰ‏ وَدِينِ‏ ٱلحَْقِّ‏ لِيُظْهِرَهُ‏ عَلَى ٱلدِّينِ‏ كُلِّهِ‏ و كَفَى بِٱهلل َِّ‏

َ

شَهِيداً‏ ﴾

Huwa alladhi arsala rasoolahu bialhuda wadeeni alhaqqi liyudhhirahu AAala

alddeeni kullihi wakafa biAllahi shaheedan. (Surat Al Fat-h 48:28)


624

Tafsir: Ni yeye alietuma Mtume wake kwa ajili ya njia ya Uongofu na Dini ya haki, ili

kuzifunika dini zote, na Allah anatosha kua Shahidi.

Ambapo miongoni mwa sifa zake basi alikua ni Al Amin yaani Muaminifu kama

anavyosema mwenye Allah Subhanah wa Ta’ala katika aya ifuatayo:

‏﴿وَمِنْهُمُ‏ ٱل َّذِينَ‏ يُؤْذُونَ‏ ٱلن َّبىِ‏ َّ وَيَ‏ قُولُونَ‏ هُوَ‏ أُذُنٌ‏ قُلْ‏ أُذُنُ‏ خَ‏ يرٍْ‏ ل َّكُ‏ مْ‏ يُ‏ ؤْمِنُ‏ بِٱهلل َِّ‏

وَيُؤْمِنُ‏ لِلْمُؤْمِنِينَ‏ وَرَحمَْةٌ‏ لِّل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ مِنكُمْ‏ وَٱل َّذِينَ‏ يُؤْذُونَ‏ رَسُولَ‏ ٱهلل َِّ‏ لهَُمْ‏ عَذَ‏ ابٌ‏

أَلِيمٌ‏ ﴾

Waminhumu alladheena yu/dhoona alnnabiyya wayaqooloona huwa odhunun qul

othunu khayrin lakum yu/minu biAllahi wayu/minu lilmu/mineena warahmatun

lilladheena amanoo minkum waalladheena yu/dhoona rasoola Allahi lahum

AAadhabun aleemun(Surat At Tawba, 9:61)

Tafsir: Na miongoni mwao mna watu wanaomuudhi Nabii (Salallahu Alayhi wa

Salam) na wanasema kua yeye ni mwenye kulipa sikio lake kila jambo: ‘Waambie

Hakika yeye anasikiliza yale yaliyo bora kwenu, Anamuamini Allah na Anawaamini

Waumini na ni mwenye rehma kwa wale walioamini miongoni mwenu, na kwa wale

wenye kumuudhi Mtume wa Allah (Salallahu Alayhi wa Salam) basi ni juu yao adhabu

kali.’

Ambapo aya hii inazungumzia sifa ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ya kua ni

mwenye kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala na Waumini wake pia na ni mwenye

huruma juu yao, ambapo hii pia ni kutokana kwake kua na ubora wa Tabia kiasi ya kua

alikua akijulikana pia kwa jina la Muhammad Al Amin, kutokana na kua ni mwenye kua

na Uaminifu hata kabla ya kua na darja ya Utume katika maisha yake.

RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM NA HILF AL

FUDUL

Eneo la Ukaz ni eneo maarufu sana kutokana na kua ni eneo linalojumuisha moja kati ya

masoko matatu makubwa na maarufu katika maeneo ya ardhi ya Uarabuni ambayo ni

Ukaz, Majanna na Dhul Majaz ambayo yote yalikua yakifanya kazi katika kipindi cha

wiki mbili za mwezi wa Dhul Qaidah. Ingawa Soko la Ukaz ambalo lipo mashariki ya


625

nje ya Mji wa Makkah na lilikua lipo ndani ya ardhi iliyopo baina ya Mji wa Nakhla na

Mji wa Taif ambayo ingawa ilikua inamilikiwa na Kabila la Banu Hawazin lakini soko

hilo lilikua likidhibitiwa na watu wa kabila la Banu Tamim.

Ambapo kama tunavyojua kua mwezi huu wa Dhu Al Qaidah, Dhu Al Hijjah, Muharram

na Rajab kua ni miongoni mwa miezi Mitukufu ambayo ilikua inaheshimiwa tangu

wakati wa kipindi cha Ujahiliyah na hivyo hua hairuhusiki kupigana vita ndani yake.

Hivyo ndani ya kipindi hiki cha Dhul Qaidah basi watu wa Uarabuni walikua ni wenye

kupumzika na kustarehe, na hivyo katika kipindi hiki soko la Ukaz hua ni lililojaa shamra

shamra za maonesho na starehe kila aina, ikiwemo mashindano ya Mashairi, Hadithi na

Mikasa, Kamari, Ulevi, Nyimbo na Ngoma zinazochezwa na Wanawake wa aina mbali

mbali, n.k

Na mbali ya kua madhumuni ya maonesho hayo ya soko la Ukaz ilikua ni kustarehe na

kutumia pesa zilizopatikana baada ya mzunguko wa mwaka wa kufanya kazi lakini

kutokana na kua ndani yake mlikua mna starehe za anasa za Ulevi basi ilikua lazima

kunatokea mapigano ndani yake ambayo yalikua yakijulikana kama mapigano ya Fijar.

Ambapo neno Fijar hua linatokana na neno Fajara linalomaanisha Dhulma, Maasi, Fujo

za Uovu, Kutokua na Aibu wala Haya, Kuzini, Kufanya Uasharati.

Na hivyo mapigano haya yalikua yakianzishwa na mambo yasiyokua na maana kama

inavyomaanisha maana ya jina la Mapigano hayo ya Fijar. Ambapo ndani ya miaka 10

yalitokea mapigano mara nne ambapo mnamo mwaka wa 10 baada ya kuzaliwa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi yalitokea mapigano ya mwanzo ya Fijar ndani ya

soko la Ukaz baada ya Mtu mmoja kutoka katika Kabila la Banu Ghifar kusema kua:

‘Mimi ndie Mtu anaeheshimka sana kuliko wote miongoni mwa watu wa Uarabuni’

Hivyo kutokana na kusema maneno hayo basi mmoja kati ya watu wa Kabila la Hawazin

ambao ndio wamilikia wa eneo hilo la Soko la Ukaz basi akachukulia kauli hio kua

Unyanyaso juu yake, na hivyo akatoa Upanga wake na kumpiga nao mtu huyo wa Kabila

la Banu Ghifar mguuni mwake na kumjeruhi, na hivyo hii ikawa ndio sababu ya kutokea

mapigano makubwa baina ya Makabila mawili hayo, katika Soko la Ukaz katika mwezi

wa Dhul Qaidah.

Ambapo mapigano ya pili yalitokea baadae baada ya Kijana wa kiume wa Kabila la Banu

Hawazin kumvua Hijab mwanamke wa Kabila la Quraysh, na hivyo kua ni mwenye

kumvunjia heshima Mwanamke huyo, kwani hata katika kipindi hicho basi Wanawake

wenye kujiheshimu walikua ni wenye kujitanda, tofauti na wanavyofikiria watu wengi

miongoni mwetu leo hii kua kujitanda na kujihifadhi kwa Mwanamke anapokua

hadharani hua ni kujikosesha uhuru wake Mwanamke. Hivyo watu wa Kabila la Quraysh

walipigana vita na watu wa Kabila la Banu Hawazin baada ya Mwanamke wa Quraysh

kuvuliwa Hijabu yake hadharani kwenye soko la Ukaz.


626

Mapigano ya tatu ya vita vya Fijar yalitokea baina ya Ukoo wa Banu Kinana na Ukoo wa

Watu wa Banu Hawazin baada ya mmoja kati ya watu wa Banu Kinana kukataa kulipa

deni kwa wakati alilokua akidaiwa na Mtu huyo wa Banu Hawazin

Na mapigano ya nne ya Fijar yalitokea katika kipindi cha wakati ambao Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alipokua na umri wa miaka 20, ambayo yalipiganwa baina ya

Watu wa Banu Kinana na watu wa Banu Qays baada ya Baraz Ibn Qays wa Banu Kinana

kumuua Urwa ambae ni mwenye kutokana na ukoo wa Banu Qays.

Hivyo katika wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipokua kijana wa umri wa

miaka 20, kulitokea mapigano hayo ambapo Abu Talib alimchukua Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Banu Kinana ambapo hata hivyo Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakua ni mwenye kupigana kwenye vita hivyo bali

alikua ni mwenye kusaidia katika kuokota Mishale ya Upinde wa Maadui kwa ajili ya

kumpa Ami yake yaani Abu Talib.

Ambapo katika kutafuta suluhu ya mapigano hayo basi pande hizo mbili zikakubaliana

kua inabidi wahesabiwe Maiti wa Pande zote kisha pande iliyoua watu wengi zaidi basi

itabidi ilipe fidya, na baada ya kuhesabiwa maiti hao basi ikagundulika kua kuna Maiti

20 zaidi za Banu Qays, hivyo watu wa kabila la Quraysh na Banu Kinana wakalipa fidya

kwa ajili ya watu hao 20 na kisha ndio ikapatikana suluhu.

Na kutokana na hali ya matukio hayo ya vita vya Fijar kua ni vyenye kuanzishwa na

mambo yasiyokua na maana na kupelekea kumwagika kwa damu nyingi sana, na kuvunja

umoja wa Makabila ya Waarabu na kusababisha uadui baina yao, na kukosekana kwa

usalama kwa Wageni wanaotembelea na kupita njia kwenye Mji huo, kiasi ya kua mara

moja Asl Ibn Wail ambae ni ni miongoni mwa watu wakubwa wa mji wa Makkah

alipotaifisha mali za mmoja kati ya Watu wa Kabila la Al Zabidi la Yemen.

Ambapo mtu huyo wa kabila la Al Zabidi alipojaribu kuomba msaada wa kwa watu wa

Makkah basi walimfungia Mlango yao, na hivyo nae akaamua kuelekea kwenye Mlima

wa Abu Qubays na kuanza kulalamika kwa kupaza Sauti kuhusiana na namna

alivyodhulumiwa na kunyanyaswa na Asl Ibn Wail na kukosa Msaada kutoka kwa watu

wa Makkah. Na hivyo baada ya tukio hili basi Viongozi wa Kabila la Quraysh wakaamua

kuunda Jumuiya ya Usuluhishi ambayo itakua ni yenye kusimamia haki za watu

waliodhulumiwa na hivyo kuepusha dhulma na umwagaji wa Damu katika maeneo ya

ardhi yao na jirani pia.

Muanzilishi wa Jumuiya hii alikua ni Zubayr, ambae alishirikiana na viongozi wa Banu

Hashim, Banu Muttalib, Banu Zuhra, Banu Asad, Banu Harith na Banu Taym ambapo

makao makuu ya Jumuiya hii yalikua ni kwenye Nyumba ya Abdullah Ibn Juda ambae

alikua ni Tajiri sana na ni mwenye kuheshimika na watu wote wa Mji wa Makkah na


627

maeneo ya Jirani. Na Jumuiya ilikua ikiitwa Hilf Al Fudul ambapo Hilf maana yake ni

Kiapo na Fudul maana yake ni Watu wenye Kuheshimika Kitabia.

Ambapo kwa upande mwengine basi kuna wanaosema kua Tukio hili la makubaliano

haya liliitwa Hilf Al Fudul kwa sababu, katika kipindi cha Uanzishwaji wa Mji wa

Makkah basi pia kulikua kuna makubaliano baina ya Fudayl wa Banu Jurhum na Fudayl

wa Banu Qatura ambayo yalikua ni ya kuhusiana na Kuzuia Uovu usifanyike ndani ya

Mji wa Makkah, hivyo kutokana na kua watu wa Quraysh walikubaliana pia kuhusiana

na tukio hilo basi Jumuiya hio ikawa inaitwa Hilf Al Fudul kumaanisha Kumbukumbu

ya makubaliano baina ya Fudayl wawili hao wa awali.

Malengo ya Jumuiya hio ya Quraysh yalikua ni kusimamia mambo yafuatayo:

1- Hakuna Mtu ambae atakaenyanyaswa na kuvunjiwa haki zake bila ya

kuangalia kama ni Mtu wa Mji wa Makkah ama la.

2- Hakutokua na Fursa ya kufanya dhulma wala kunyanyasa Mtu, na hivyo

kila atakaenyanyasa na kudhulumu basi atachukuliwa hatua za nidhamu

dhidi yake.

3- Kusimamia Haki za Waliodhulumiwa hadi wapate haki zao ili wasiokua na

uwezo wasdhulumiwe haki zao na wenye uwezo.

Ambapo wanachama wa Jumuiya hii walikubaliana kwa kulishana kiapo kwa kusema

kua: ‘Tutalinda Viapo vyetu hadi pale Bahari itakapokua haina maji ya kutosha ya

kurowanisha hata unywele, hadi Milima itakapobubujika na kupeperushwa, hadi

pale Istilam (Tukio la kupangusa au kilipungia mkono kwa mbali Hajar Al Aswad

wakati wa kuzunguka Al Kaabah) litakapofutwa’

Na jukumu la mwanzo kabisa la Jumuiya hii lilikua ni kuzirudisha kwa mwenyewe

mmiliki wa Mali za Myemen wa Al Zabidi aliepokonywa na Asl Ibn Wail.

Hivyo tukio hili lilitokea wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipokua na

Umri wa miaka 20 na hivyo ingawa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua ni

mdogo Kiumri ukilinganisha na Umri wa Viongozi hawa wakubwa wa Quraysh lakini

nae pia aliingizwa kwenye Jumuiya hii kutokana na Uaminifu wake na Uadilifu wake

katika kusimamia haki za Watu tofauti wa Mji wa Makkah na wa maeneo mengineyo

wanaojuana nae.

Ambapo anasema Abu Muhammad Abd Al Malik Ibn Hisham Ibn Ayyub Al Himyari Al

Mu'afiri Al Baṣri kua alisema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakika mimi

nilikuwepo katika nyumba ya Abdullah Ibn Juda wakati kiapo kilipothibitishwa,


628

na kwa mtizamo wangu basi ni kua kiapo hicho kilikua ni cha kupendeza kwangu

kuliko kumiliki Ngamia Mwekundu, na hata kama nikiitwa kuhudhuria katika

wakati huu wa Uislam basi nitakubali kuhudhuria.’

Kwani alisema pia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Fanyeni Makubaliano

ambayo ni yenye kusimamia haki za watu, ili wenye nguvu wasiwe na uwezo dhidi

ya wasiokua na nguvu’(Sunan Al Kubra)

SAFARI YA KIBIASHARA YA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI

WA SALAM KATIKA ARDHI YA SHAM.

Wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipotimia Umri wa miaka 24 alikua

tayari ameshaenda na misafara ya Kibiashara na Ami yake yaani Abu Talib katika Ardhi

ya Syria, na lakini hata hivyo safari hizo zilisita kwa sababu ya hali mbaya ya uchumi wa

Abu Talib kutokana na kua na Familia kubwa, vita baina ya makabila na vile vile hali ya

Ukame.

Katika kipindi hiki kigumu basi walioweza kudumu na Biashara walikua ni wale wenye

mitaji mikubwa tu ya biashara, ambapo mmoja miongoni mwao alikuwepo Mwanamke

Mzuri, anaehishimika katika Mji wa Makkah, huyu alikua Mwanamke anaejulikana kwa

jina la Khadija Bint Khuwaylid Ibn Asad ambae alikua ni mwanamke mwenye umri wa

miaka 39 ambae alierithi Utajiri wake kutoka kwa Baba yake Khuwaylid Ibn Asad ambae

alikua ni tajiri mkubwa sana na alifariki katika Vita vya Fujjar.

Khadija Bint Khuwaylid alikua ni Mwanamke alieachwa baada ya kuolewa mara mbili

ambapo mara ya kwanza ilikua ni pale alipoolewa na Abu Halah Ibn Zurara Ibn Al

Nabbash Al Tamimi ambae kutokana nae alipata watoto wawili, mmoja alikua akiitwa

Hind na mwengine akiitwa Hala, na baada ya kuachika kwenye Ndoa hio basi akaolewa

na Atiq Ibn Idd Ibn Umar Ibn Makhzum ambapo alipata mtoto mmoja aitwae Hind bint

Atiq.

Ambapo Hind Bint Atiq baadae aliolewa na Saffiy Ibn Ummayah Ibn Aabid Ibn Abdullah

Ibn Mahkzum ambapo katika ndoa hio wakapata Mtoto wa kiume waliemwita

Muhammad ambae Ukoo wake ukawa unaitwa Banu Tahirah, yaani Ukoo wa

Mwanamke aliekua Masafi ambae ni Khadija Bint Khuwaylid na hii ni kutokana na usafi

wa Khadijah Bint Khuwaylid, na akawa anaitwa Bint Tahira na pia alikua akiitwa kwa

jina la Amirat Al Quraysh yaani Malkia au kiongozi wa Kike wa Quraysh, na pia alikua

akiitwa Khadija Al Kubra yaani Khadija Mkuu wa Kike wa Quraysh na hii ni kutokana

na Uadilifu wake na namna anavyosimamia na kuendeleza Biashara zake ambazo zilikua

hazina Mpinzani kwa Ukubwa na wingi wa Mali zake, kwani alikua na uwezo wa

kubadilisha Vumbi akilitia mkononi mwake na kulifanya likawa Dhahabu badala yake.


629

Misafara ya kibiashara ya Khadija Bint Khuwaylid ilikua ikizunguka sana na kupata

umaarufu baina ya Makkah na Yemena na pia baina ya Makkah na Sham, na kutokana

na Ukarimu, Uadilifu na mafanikio yake basi Khadija Bint Khuwalid alikua akipendwa

sana na watu wa Mji wa Makkah hususan Wanawake na alikua kila anapoenda basi

lazima hua na Msafara wake wa Wanawake wanaopenda kua karibu yake.

Safari moja wakati Khadija Al Kubra alipokua akizunguka Al Kaabah pamoja na

marafiki zake, basi akatokea Myahudi mmoja ambae alisema: ‘Ewe Amirat Al Quraysh,

Jee unajua kua atatokea Mtume katika zama hizi? Hivyo yeyote yule anaetaka

kuolewa nae basi na aolewe.’ Ambapo hata hivyo Wanawake waliokua wamemzunguka

Khadija Al Kubra wakakasirika kusikia maneno hayo kutokana na kua Khadija Bint

Khuwaylid alikua ni mwanamke anaejiheshimu na tayari ameshakataa posa za Wanaume

kadhaa ambao walikua hawana vigezo stahiki mbele yake. Hivyo marafiki zake hao

wakamrushia Mawe Myahudi huyo nae akaondoka.

Ndani ya mwaka huu Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam watu wa Quraysh

waliandaa Msafara wa Biashara mkubwa sana wa kuelekea Sham, ambapo ndani yake

Msafara huu pia zilikuwemo Mali za Khadijah Bint Khuwaylid lakini alikua hajapata mtu

wa kuusimamia biashara hizo kwani alikua hajapata mtu stahiki wa kusimamia mali zake

zake hizo, hivyo akawa ni mwenye kutafuta mtu wa kusimamia Biashara zake hizo.

Habari za utafutwaji wa Msimamizi wa Biashara za Khadija Bint Khuwaylid kwenye

Msafara huo zilimfikia Abu Talib basi akamtaarifu Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kwa kumwambia: ‘Ewe Mtoto wa Kaka yangu, hakika wewe unajua kua mimi

si mwenye umiliki wa kitu wala mali yeyote kwani hali hii ya njaa na ukame

imekausha kila kitu katika mali zangu, kiasi ya kua hakuna sehemu ya kutegemea

kwa upande wangu, lakini kuna msafara wa Biashara unaoelekea Sham ambao

ndani yake pia mna Mali za Khadija Bint Khuwaylid’

‘Na Khadija Bint Khuwaylid anatafuta Msimamizi wa Mali zake kutoka kwenye

Kabila letu,na kama unavyojua ni kua Khadija ni mwanamke Tajiri sana na watu

wengi sana ni wenye kunufaika na Biashara zake, hivyo anahitaji mtu kama wewe

kua ni msimamizi wake, mtu anaeaminika, mkweli na muadilifu, hivyo kama

ukienda kuzungumza nae kuhusiana na kusimamia Mali zake katika Msafara huu

basi bila ya shaka atakufaham na kukukubali kutokana na sifa zako na Uaminifu

wako. Ingawa mimi sifurahii kukupeleka Sham kwa sababu ya kuogopa kuja

kudhuriwa kwako na Mayahudi, lakini hakuna njia nyengine ya kufanya kwa

upande wangu katika hali kama hii tuliyokua nayo isipokua kukuruhusu kuenda

pamoja na Msafara huo.’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Ewe Ami yangu, hamna tatizo

mimi niko pamoja nawe hivyo fanya lile unaloliona kua ni sahih’


630

Bila ya shaka alitakalo Allah Subhanah wa Ta’ala kua basi hua ni lenye kutokea na kua

bila ya kua na kipingamzi chechote, kwani ingawa mazungumzo haya walikubaliana

baina ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Abu Talib lakini hali ilikua ni kama

vile Khadija Bint Khuwaylid alikua akiwasikiliza, kwani wakati mazungumzo ya Watu

waili hawa yanaendelea basi na kwa upande wa Khadija Bint Khuwaylid nae likamjia

wazo la kujaribu kumuomba Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam awe msimamizi wa

Mali yake katika Msafara huu kua ndio yeye peke yake mwenye sifa za kusimamia Mali

yake, hivyo akamtuma mtu aende kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ili

amuombe aje mbele yake kwani anataka kuzungumza nae.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipofika mbele ya Khadija Bint Khuwalid na

kusalimiana nae basi Khadija Bint Khuwaylid akasema: ‘Nimekuita kwa sababu

nilikua nataka kupendekeza kutuma Mali zangu katika Mji wa Dimashq pamoja

nawe ili uwe msimamizi wake, kwani najua kua kwa hakika wewe ni Mtu mwema,

Muaminifua sana na Muadilifu, hivyo niko tayari kukulipa wewe malipo ambayo

kamwe sikuwahi kumlipa mtu yeyote kabla yake, hivyo jee unaonaje?’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu: ‘Bila ya shaka hii ni Rehma

ambayo Allah amekujaalia kuipata’ na hivyo kumaanisha kua amekubaliana na

mapendekezo hayo ya Khadija Bint Khuwaylid.

Na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliporudi nyumbani na kumuelezea Abu

Talib kuhusiana na yaliyotokea basi Abu Talib akamwambia Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua bora akapatane nae Khadija Bint Khuwaylid ili apate kujua atalipwa

kiasi gani, lakini hata hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kua

ameridhika na makubaliano hayo, hivyo Abu Talib akaona bora aende yeye mwenyewe

kwa Khadija Bint Khuwaylid ili akapatane nae kuhusiana na malipo hayo, hivyo akatoka

na kuelekea kwa Khadijah Bint Khuwaylid na alipofika akamwambia:

‘Ewe Khadija hakika sisi tumesikia kua umelipa Ngamia wawili kwa wasimamizi

wa Msafara uliopita hivyo na sisi kwa upande wetu hatuwezi kubaliana na kua

Muhammad asimamie Msafara wako isipokua kama utampa Ngamia si chini ya

wanne.’

Ambapo Khadija Bint Khuwaylid akamwambia Abu Talib: ‘Ewe Abu Talib hakika

wewe umeamua kupendekeza bei ya chini zaidi ya nilivyofikiria, kwani mimi

nilikua tayari kutoa zaidi ya hio’ hivyo Abu Talib akafurahia makubaliano hayo.

Hivyo Msafara ulipokua tayari basi Khadija Bint Khuwaylid akamteua Mtumwa wake

aitwae Maysara ambae alimwambia kua awe Msaidizi wa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kwa kumwambia: ‘Fuatana nae Muhammad kwenye msafara huu na ni

jukumu lako kumtii katika kila atakalokuamrisha, na wala usiende kinyume na


631

maamrisho yake, jitahid uwe ni mwenye kuja kunielezea kila kitu kitakachotokezea

kwenye msafara huu.’

Baada ya siku kadhaa za maandalizi ya msafara huo kumalizika basi Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akakabidhiwa Mali za Khadija Bint Khuwaylid hukua akiwa

na msaidizi wake ambae ni Maysara, ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akaagana na watu wa familia yake na Bi Khadija bint Khuwaylid na kisha Msafara huo

ukaanza safari yake.

Msafara huo ulikua ni msafara wa safari ndefu ambao hua ni yenye kuchukua mda wa

miezi mitatu hadi kuwasili katika Ardhi ya Sham, baada ya safari ya siku kadhaa kabla

ya kuwasili mwishoni mwa safari yake basi msafara huo ukawasili katika ardhi yenye

jengo la Makuhani wa Busra ambayo hapo awali Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alipokua mdogo alipofuatana na Babu yake ambae ni Abd Ul Muttalib basi alikutana na

Bahira, hivyo msafara huo ukasimama kwenye eneo hilo kwa mapumziko ya muda mfupi

ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasimama chini ya Mti ule ule

aliosimama katika wakati alipokua Mdogo na Babu yake.

Na katika kipindi hiki Bahira alikua ameshafariki na hivyo Msimamizi wa jengo lililopo

kwenye eneo hilo alikua ni Kuhani mwengine aitwae Nastura, ambae nae alishanganzwa

na tukio la kumuona Mtu asiemjua akiwa amekaa chini ya Mti huo mkubwa uliopo karibu

yake, hivyo akamuona Maysara ambae aliwahi kuonana nae hapo kabla katika misafara

kadhaa yenye mali za Khaidja Bint Khuwaylid na kumuliza: ‘Jee yule aliekaa chini ya

Mti wa Mzaituni ndie ni nani’

Maysara akasema: ‘Yule ni kijana anaeheshimaka sana katika Mji wa Makkah na

mwenye sifa za upekee miongoni mwa watu wa Kabila la Quraysh’

Nastura akakaa kimya na kutafakari kisha akasema: ‘Inashangaza sana kwani hakuna

mtu anaekaa chini ya Mti ule isipokua atakua ni Mtume’ hivyo akamuuliza Maysara:

‘Hivi jee macho yake yana wekundu ndani yake?’ ambapo Maysara akajibu: ‘Naam.’

Hivyo Nastura akasema: ‘Basi atakua ni Mtume, yaani ndie Mtume wa Mwisho’

Maneno haya yalimtia wazimu wa furaha Maysara kwani yalikua ni maneno

yasiyosahaulika, yalikua kama yaliyooteshwa kwenye ufahamu wake na hivyo kuganda

kwenye ufahamu wake. Kiasi ya kua hakujali hata baada ya msafara huo kuondoka na

kumalizia Safari yake katika Mji wa Dimashq na kufanya Biashara zake na kufunga safari

ya kurudi katika Mji wa Makkah kua mara hii mmiliki wake Bi Khadija Bint Khuwaylid

amepata faida kubwa sana baada ya kusimamiwa mali zake na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam katika Biashara yake aliyoifanya katika Mji wa Dimashq na pia katika

mzigo wanaorudi nao katika Mji wa Makkah, kwani kwake yeye habari ya faida haikua


632

na thamani wala maana yeyote kuliko yale maneno aliyoambiwa na Nastura kua

Muhammad ndie atakaekua Mtume wa Mwisho.

Kwani pia kuna jambo jengine ambalo lilimshangaza zaidi Maysara na kuthibitisha

maneno ya Nastura baada ya kuyatafakari na kuanza kumfuatilia Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam na kugundua kua pale wakati msafara huo unarudi katika Mji wa

Makkah basi mbali ya kua hali ya Jangwani ilikua ni ya Jua kali lakini kwa upande wao

ilikua kama kuna kivuli katika kila sehemu wanayopita na hivyo kutokua ni wenye

kuathiriwa na Ujoto wa Jua hilo, na hivyo Maysara akajaribu kujizuia kwa kutowaambia

wasafiri wenzake kutokana na ugunduzi wake huo, kwani alikua anasubiri kufikisha

habari hio njema kuliko zote kwa mtu mmoja tu pekee ambae ni mmiliki wake yaani ni

Khadija Bint Khuwaylid.

Msafara huo ulipokaribia katika Mji wa Makkah basi Khadija Bint Khuwaylid nae

akakugundua kua Msafara huo ulikua ukifuatwa na Kiwingu ambacho ni chenye kuupa

Kivuli Msafara huo, ambacho kilisimama pia karibu ya Nyumba yake pale Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alipokaribi na kukabidhi mzigo wa Mali alizonunua kutoka

katika Mji wa Dimashq kwa ajili ya kuja kuuzwa kwenye Mji wa Makkah.

Na bila ya shaka Maysara nae alipofika mbele ya Khadija Bint Khuawaylid na kumpa

habari juu ya kila kilichotokea na alichosikia kutoka kwa Nastura na kisha kuongezea

yale aliyoyaona kwa uchunguzi wake mwenyewe kua hakuna Mtu muaminifu, mkweli

na mwenye barka kwenye Biashara kama Muhammad Salallahu Aalyhi wa Salam na

uthibitisho unaonekana wazi juu ya mali alizokuja nazo ambazo wingi wake na fadiya

yake ni tofauti na hali ya biashara ya Bi Khadija Bint Khuwaylid ya hapo kabla ya

Misafara yake yote ya kibiashara.

Ambapo mara baada ya kuelezewa kila kilichotokea basi Bi Khadija Bint Khuwaylid nae

akakumbuka maneno ya yule Yahudi aliesema katika ile sikua liyokua akizunguka Al

Kaabah na marafiki zake, na hivyo hakuweza kufikiria tena kuhusiana na faida

iliyopatikaan kwenye Biashara yake, kwani kilichogangda akilini mwake ni Ukweli wa

maneno aliyoyasikia kabla yake ambayo ni kuhusiana na Mtume wa mwisho katika

wakati wa uhai wake, ambae tayari yuko chini yake katika usimamizi wa Biashara zake.

Hivyo bila ya kupoteza mda basi Khadija Bint Khuwaylid akatoka moja kwa moja hadi

kwa mtoto wa Mjomba wake aitwae Waraqah Ibn Nawfal ambae ni mwenye Ilm ya Ahl

al Kitab na kisha akamuelezea kuhusiana na yaliyotokea, ambapo baada ya kusikia habari

hio basi Waraqah akakaa kimya huku akitafakkar juu ya habari hizo na kisha akasema:

‘Kama unayoyasema ni kweli basi Muhammad atakua kweli ndie Mtume wa

mwisho atakaetumwa kwenye Ummah huu, ambae mimi pia nilikua nikijua

kuhusiana na kua atakuja na nilikua namsubiri ila sikuwa ni mwenye kujua kua

ndio ameshawasili.’


633

Ambapo kauli hii ilimfurahisha sana Khadija Bint Khuwaylid, kwani mbali ya kua alikua

ni mwenye kuvutiwa na uzuri wake, uaminifua na uadilifu wake, kiasi ya kua alikua

tayari kumlipa zaidi ya mara mbili yake katika kusimamia biashara zake lakini pia habari

hii ya kua yeye ndie Mtume wa mwisho ilimuathiri sana ndani ya Moyo wake hivyo

akatamani kua Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam awe ndie Mume wake kutokana

na upekee wa sifa zake, mbali ya kua kwa mda mrefu hakua ni mwenye kufikria

kuhusiana kua na haja kuolewa tena maishani mwake, lakini ghalfa moja mfumuko wa

matukio haya yaliyojitokeza mbele ya macho yake na ufaham wake yalimpeleka kua ni

mwenye kujikuta akiwa amezama kwenye bahari ya hisia nzito za kimaumbile za

mapenzi ndani ya Moyo wake.

Ambapo kimaumbile hizi hua ni hisia zisizokua na maana pale inapokua ni za upande

mmoja tu, kwani ili hisia hizi zikamilike basi inabidi kuwepo kwa hali ya uwiano wa

makubaliano wa ndani ya nyoyo baina ya pande mbili ya hisia za Mwanamke na

Mwanamme, kwani vyenginevyo basi anaependa bila ya kupendwa hua ni mwenye

kuumizwa na athari ya mapenzi yake kwa yule asiekua na hisia za kumpenda juu yake.

Kwani kwa lugha ya Kiarabu mapenzi hua yanafafanulika na kuelezewa kwa maneno

mengi, ikiwemo:

1. Hawa – hii ni hali ya mwanzo ambayo hua ni hali ambayo unauteka nyara Moyo na

hivyo hua ni wenye matamanio mengi sana na ya ghafla na ndio maana Waarabu wakawa

wananasibisha hali hii na Hawa al Najm yaani Mapenzi yanayofanana na Kuanguka kwa

Nyota.

2. Wadd – Baada ya Hawa basi hali inyofuatia hua ni ile inayoitwa Wadd ambayo hua ni

hali ya kupenda kwa kuendelea na kwa uaminifu.

3. Hubb – Baada ya Wadd ndio hua inafuatia hali ya Hubb ambayo hua ni hali ya Mapenzi

ya kimaumbile kunakotokana na kua na Mapenzi yaliyo safi ambayo ndani yake basi yule

anaependa hua hana khiari wala uthibitisho wa kuwepo kwa khiari ya anaependwa.

4. Ishq – ambayo hua ni hali ya kudhibitiwa na matamanio yanayotokana na mapenzi

yaliyouzunguka Moyo wa anaependa. Kwani neno Ishq hua ni lenye kutokana na neno

Ashaqa ambalo hua ni lenye kumaanisha Kupanda, Kuzunguka, Kuzonga katika Miti

tofauti, na hivyo Ishq hua ni hali ya kuzongwa wa Moyo wa anaependa kiasi ya kua hua

haoni mwengine zaidi ya yule anaempenda.

Ambapo mara nyingi hua linatumika neno Hubb, ambapo neno Hubb hua ni lenye

kutokana na harfu 2 za Kiarabu ambazo ni:


634

1- Hu Ambayo unapoitamka basi hua inasababisha mdomo kuachana na kutanuka,

na

2- Bb Ambayo unapoitamka basi hua inasababisha Midomo Kufunga na Kuungana.

Neno Hubb ambalo linamaanisha Hisia za Mapenzi au Kupenda hua linaweka wazi kua

‘Moyo wa Mtu unapopenda hua unatanuka na kisha unamuingiza mhusika

anaependwa na Moyo wa huyo unaopenda ndani yake katika kina chake, na

kumbakisha anaependwa ndani ya kina cha Moyo wa anaependa, kama vile kitu

kilichoingizwa Mdomoni kisha Mdomo Ukafumbwa na kilichoingizwa ndani yake

ikawa kimemezwa, bila ya kutakiwa kutoka ndani yake kama vile linavyoonesha

neno Hubb katika wakati wa kulitamka kwake.’

Na hivyo basi neno Hubb ambalo ndio lililotoa neno Mahabba hua linatumika kuelezea

Mapenzi ambayo ni yenye kudumu kiasi ya kua anaependwa hua hawezi kusahaulika

ndani ya Akili na Moyo wa anaependa, na hivyo hisia hizo hua ni zenye usafi usiokua

na shaka ndani yake wala kuchujwa na hisia nyengine zozote. Na ndio maana Allah

Subhanah wa Ta’ala akasema katika Qur’an kua:

‏﴿وَمِنَ‏ ٱلن َّاسِ‏ مَن يَت َّخِ‏ ذُ‏ مِن دُونِ‏ ٱهلل َِّ‏ أَندَاداً‏ يحُِب ُّونَهُمْ‏ كَحُبِّ‏ ٱهلل َِّ‏ وَٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏

أَشَد ُّ حُبّاً﴾‏

Wamina alnnasi man yattakhidhu min dooni Allahi andadan yuhibboonahum

kahubbi Allahi waalladheena amanoo ashaddu hubban lillahi (Surat Al Baqar 2:165)

Tafsir: Na miongoni mwa watu wale wanaowachukua Miungu myengine zaidi ya Allah

kama wapinzani hua ni wenye kuwapenda kama wanavyompenda Allah, lakini wale

walioamini basi hua ni wenye kumpenda sana Allah (kuliko kitu chochote).

Ambapo tunapozungumzia Mahabat na Mawaddah yaani Mapenzi kwa Upande wa

Viumbe basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala amesema katika Qur’an kua:

‏﴿وَمِنْ‏ آَتِهِ‏ أَنْ‏ خَلَقَ‏ لَكُم مِّنْ‏ أَنفُسِ‏ كُمْ‏ أَزْوَاجاً‏ لِّتَسْكُنُو ۤ اْ‏ إِلَيْهَا وَجَعَلَ‏ بَيْنَكُم

م َّوَد َّةً‏ وَرَحمَْةً‏ إِن َّ فىِ‏ ذٰلِكََ‏ لآَتٍ‏ لِّقَوْمٍ‏ يَتَفَك َّرُونَ‏ ﴾


635

Wamin ayatihi an khalaqa lakum min anfusikum azwajan litaskunoo ilayha

wajaAAala baynakum mawaddatan warahmatan inna fee dhalika laayatin

liqawmin yatafakkaroona (Surat Rum 30:21)

Tafsir: Na katika dalili zake ni kukumbieni nyinyi kutokana na Nafsi zenu miongoni

mwenu pea (Wake na Waume) ili mpate utulivu kutokana nao, na akajaalia baaina

yenu Mapenzi na Huruma, kwa hakika katika haya mna Vithitisho kwa watu wenye

kutafakkari.

Kwani hisia za hali hii ya Mahabat na Mawaddat baina ya Mwanamme na Mwanamke

hua ni yenye kutokana na Maumbile kamilifu ya Mwili wa Ibn Adam ambayo hua ni

yenye sifa ya kuzalisha kemikali nyingi miongoni mwao ikiwemo za Dopamine na

Oxytocin ambazo zinazosimamia hisia za Mapenzi, Matamanio, Mshikamano,

Kusaidiana, Kuhurumiana, n.k baina ya Mke na Mume, Baba na Mama, Kaka na Dada,

Ndugu na Familia, n.k kulingana na uhusiano wa hali ya hisia hizo zinazosababishwa

kuzalishwa kutokana na nguvu na uwezo wa Moyo na pia Ubongo wa Ibn Adam.

Kwani tunapozungumzia Oxytocin basi hua tunazungumzia kemikali ambazo kimaarufu

hua zinajulikana kama kemikali za ‘Mapenzi na Uaminifu’ na huzalishwa ndani ya miili

yetu baada ya kupatikana hisia zinazotokana na ufanyaji kazi wa viungo vya hisia za

Mwili za Kuona, Kusikia Sauti, Kuhisi Harufu au Kugusana na hivyo hutupelekea kua

na hali ya kujisikia kua na Raha, Upendo, Utulivu, Usalama, Amani pale tunapokua

karibu na wale tunaowapenda na hivyo kutuzidishia hisia za kutotaka kukosana au

kuachana na watu hao na kuwapenda, kuwajali, kuwafanyia ukarimu na kuwaonea

huruma.

Kemikali za Oxytocin pia hua ndizo zinazosimamia jukumu la kuvitayarisha viungo vya

mwili wa Mwanamme na Mwanamke kwa ajili ya kua tayari katika hali ya kuingiliana

kimwili, kwa ajili ya kuendeleza vizazi na pia kwa ajili ya kuupa utulivu na kuupumzisha

mwili kwa kuupa hisia za Raha inayotokana na kitendo cha kuingiliana kimwili, ambayo

hutegemeana na wingi wa uzalishwaji wa Oxytocin kwani kila zinavyozidi kuzalishwa

kwa wingi zaidi katika wakati wa tendo hilo basi ndio inavyozidi kupatikana hisia za

Raha ambayo haina mfano wake katika tendo hilo kama anavyoelezea Hujjat ul Islami

Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali pale aliposema kua: ‘Raha ya mda mfupi inayopatikana

katika kuingiliana kimwili basi hua ni Raha ambayo kamwe haiwezi kufananishwa

na Raha nyengine, na kama ingekua ni yenye kudumu basi ingekua ni moja kati ya

dalili ya moja kati ya Raha za Milele tulizoahidiwa Peponi’

Hujjat ul Islami Mujaddid Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali anatufafanulia zaidi pale aliposema: ‘Hikma ya Allah Subhanah wa

Ta’ala na Rehma zake zinaonekana pale unapoangalia katika kuweka Matamanio ya aina


636

mbili katika Maisha yetu. Matamanio ya kwanza hua ni ya muonekano wa kimaisha wa nje

pale mtu anapokua anaendeleza kizazi chake kupitia kwa watoto wake. Na muonekano wa

pili ni wa muonekano wa kimaisha ya ndani unaohusiana na maisha ya baadae kesho

Akhera. Kwani raha ya kuingiliana kimwili hua si yenye kudumu katika ulimwengu huu na

ni lazima iwe ni ya mda mfupi, na yenye kikomo kwa kumalizika mara tu baada ya kuihisi

raha hio kiasi ya kua humpelekea Ibn Adam kua na hamu ya kutaka raha hio iwe ni yenye

kudumu, na hivyo hii humfanya Ibn Adam kua ni mwenye kudumu katika kufanya Mema

kiibada ambayo yatampelekea kupata Raha kama hizo milele.’

Na ukweli ni kua tunapozungumzia hisia za Mapenzi na kupenda, basi hua ni miongoni

mwa neema ya Hisia za Kimaumbile na ndio maana Allah Subhanah wa Ta'ala akasema

katika Surat Al Imran kua:

‏﴿زُيِّنَ‏ لِلن َّاسِ‏ حُب ُّ ٱلش َّهَوَاتِ‏ مِنَ‏ ٱلنِّسَاءِ‏ وَٱلْبَنِينَ‏ وَٱلْقَنَاطِيرِ‏ ٱلْمُقَنْطَرَةِ‏ مِنَ‏

ٱلذ َّهَبِ‏ وَٱلْفِض َّةِ‏ وَٱلخَْيْلِ‏ ٱلْمُسَو َّمَةِ‏ وَٱلأَنْعَامِ‏ وَٱلحَْرْثِ‏ ذٰلِكَ‏ مَتَاعُ‏ ٱلحَْيَاةِ‏ ٱلد ُّنْيَا وَٱهلل َُّ‏

عِنْدَ‏ هُ‏ حُسْ‏ نُ‏ ٱلْمَآبِ‏ ﴾

Zuyyina lilnnasi hubbu alshshahawati mina alnnisa-i waalbaneena waalqanateeri

almuqantarati mina aldhdhahabi waalfidhdhati waalkhayli almusawwamati waalanAAami

waalharthi dhalika mataAAu alhayati alddunya waAllahu AAindahu

husnu almaabi (Surat Al Imran 3:14)

Tafsir: Vimependezeshwa kwa ajili ya Watu kupenda vyenye kutamanisha

vinavyotokana na Wanawake na Watoto na Wingi wa Marundo ya Dhahabu na Fedha

na Farasi (Vipando) Wazuri na Ngombe na Ardhi yenye Rutba, Hakika Haya ni

Mapambo ya Maisha ya Dunia na Kwa Allah ndiko kwenye Marudio Bora.

Ambapo kutokana na kujua hali ya uhalisia wa hisia hizo basi Bi Khadija Bint

Khuwaylid, mbali ya kua amevutiwa na anapenda Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

awe ndie Mume wake, lakini akasita na kuanza kujiuliza kwanza, hivi jee Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam atakua na hisia kama zake juu yake? Hivi jee atakubaliana na

mapendekezo yangu ya kutaka kuolewa nae kutokana na tofauti ya umri baina yao, kwani

Khadija Bint Khuwaylid alikua na umri wa miaka 40, wakati Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alikua na umri wa miaka 25 katika kipindi hiki.

Yaani hiki hua ni kitendawili kisichoteguka, na ndio maana akasema Imam Abu Hasan

Al Shadhili katika kumuomba kwake Allah Subhanah wa Ta’ala kua: ‘Ya Allah!


637

Zifanye Amali zangu mbaya kua ni amali za watu uwapendao, na wala usizifanye

Amali zangu Njema kua ni za watu usiowapenda’ na hivyo kumaanisha kua: ‘Bora

niwe na Amali sizo huku nikiwa ni mtu nnaependwa nawe kuliko kua mtu mwenye

amali ndizo lakini hapo hapo nikawa ni mtu nisie pendwa nawe, ya Allah’

Hivyo Khadija bint Khuwaylid akarudi nyumbani kwake na kubakia akitafakari athari ya

hisia zake za kimaumbile kwa Kijana Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam, na

kujiuliza masuali yasiyokua na majibu kuhusiana na hisia zake, na mara akatembelewa

na rafiki yake aitwae Nufaysa Bint Munabih ambapo Khadija Bint Khuwaylid akaanza

kumuelezea kuhusiana na hisia zake juu ya Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam na

sifa zake.

Ambapo mara baada ya Khadija Bint Khuwaylid kubainisha hisia zake kwa Nufaysa basi

Nufaysa alipotoka akaelekea moja kwa moja kwa Abu Talib na kuanza kuzungumza na

Rasul Aallah Salallahu Alayhi wa Salam kuhusiana na habari za safari na kisha

akumuuliza kwa kusema: ‘Hivi kwanini mpaka leo hii hujaoa ewe Muhammad?’

ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Sijawa na uwezo wa Kuoa

bado.’

Nufaysa akapendekeza kwa kusema: ‘Hivi jee kama atatokea Mwanamke ambae anao

uwezo utakubali kuoana nae?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akauliza:

‘Kama nani kwa mfano? ’ Nuwayla akasema: ‘Kama Khadija Bint Khuwaylid’, hapo

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Bila ya shaka nitakubaliana nae

kama akikubali.’

NDOA YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’ALAYHI WA SALAM

NA KHADIJA BINT KHUWAYLID RADHI ALLAHU ANHA.

Baada ya Nufaysa kuzungumza na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kuthibitisha

kua upo uwezekano wa kua pamoja kwa kisharia katika ndoa baina ya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na Khadijah Bint Khuwaylid basi Nufaysa akatoka na

kukimbilia kwa Khadija Bint Khuwaylid kwa ajili ya kumpa habari njema ambazo ni

zenye kumfurahisha zaidi Khadija Bint Khuwaylid kuliko hata zile za mwanzo alizokua

nazo za kupata faida kubwa kwenye biashara yake katika kipindi hicho, na kua

anaemsimamia Biashara zake atakua ni mwenye Darja ya Utume.

Ambapo kwa upande wa Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam baada ya kupata habari

ya kua Khadija yuko tayari kuolewa nae, basi nae akamfuata Abu Talib na Hamza na

kuwapa habari njema hizo, habari hizi zilikua ni nzuri sana pia kwa upande wa Abu Talib


638

na Hamza kwa sababu katika Mji wa Makkah hakukua na Mwanamke Mzuri, Mkarimu,

Mwenye tabia Nzuri, Tajiri na mwenye kujiheshimu na kuheshimika kama Kahdija Bint

Khuwaylid, kwani katika Mji wa Makkah na maeneo ya Jirani kila mtu alikua anataka

kumuoa yeye lakini Khadija Bint Khuwaylid mwenyewe alikua ni mwenye kuwakataa

wengi sana, kiasi ya kua kila mtu alikua anaogopa kwenda kuposa kutokana na kujua kua

atakataliwa, na bila ya shaka hakuna hata Mwanamme mmoja ambae angeikataa nafasi

kama hii aliyoipata Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kutoka kwa Khadijah Bint

Khuwaylid.

Hivyo Abu Talib na Hamza wakatoka na kuenda moja kwa amoja kwa Amr Ibn Asad

ambae alikua ndie Ami yake Khadijah Bint Khuwaylid Ibn Asad, ambae nae

akawakilisha posa hio na kuithibitisha kwa mwenyewe mhusika mkuu ambae ni Khadija

Bint Khuwaylid, alieipokea na kuikubali kwa Mapenzi, furaha na ridhaa kubwa ndani ya

Moyo wake kwa kujaaliwa kile kilichobora kuliko vyote kutoka kwa Mola wake,

ambacho ni kupata majibu ya kukubalika kwa mapenzi yake ya dhati yasiyokua na mfano

wake kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Baada ya makubaliano hayo basi ikapangwa siku ya harusi na Khadija Bint Khuwaylid

mwenyewe na sehemu itakayofanyika akaichagua kua ni ndani ya Nyumba yake, kwani

hii ilikua ni harusi kubwa na ya kifahari baina ya mwanamke bora wa Quraysh mwenye

darja ya Amirat Al Quraysh na Mwanamme bora kuwahi kuumbwa ambae ni Muhammad

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae pia ni Mtoto wa ndugu yake Chifu Mkuu

wa Mji wa Makkah yaani Abu Talib, hivyo kila mtu ndani ya mji wa Makkah alikua

anategemewa kualikwa na kufurahika ndani yake.

Na bila ya shaka watu walifurahika na kuburudika kwa kila kitu kizuri na kisafi na kisha

baada ya sherehe basi Abu Talib ambae ndie Mkuu wa Mji wa Makkah akasimama na

kusema: ‘Alhamd lillah, shukurani zote anastahiki Allah kwani yeye ndie

alietuumba kutokana na kizazi cha Ibrahim, kupitia kwa Ismail, kutoka kwa vizazi

vya Maada na kwa Mudar.

Ambapo kama mnavyovyojua, mtoto wa ndugu yangu Muhammad Ibn Abdullah,

ni jamaa yenu, na hakuna Kijana kutoka katika Ukoo wa Quraysh ambae anaweza

kufanana nae kwa ubora wa sifa zake, kuanzia wa sifa za Kimaumbile, Kitabia,

Kiakili, Kiheshima na Kidarja, na bila ya shaka yeye ni mtu asiekua na Mali nyingi,

lakini Mali ni nini? Mali ni kitu kilichofichikana chenye hali ya mpito, kisichokua

ni cha kudumu na ni chenye hali ya kupewa na kupokonywa kwa kila mtu.’

Hakika mimi Abu Talib nnaapa kwa jina la Allah kua Darja ya Muhammad

inapanda na itazidi kukua hivyo sasa hivi anaomba mkono wa binti yenu Khadijah

kwa kuoana nae na atalipa Ngamia 20 wa kiume kua ni Mahari.’


639

Baada ya Abu Talib kumaliza kuzungumza basi Akanyanyuka Waraqah Ibn Nawfal na

kusema: ‘Alhamd lillah, kwani Allah ndie alietuumba kama ulivyoelezea Abu Talib,

na bila ya shaka ametupa heshima kubwa zaidi kuliko ya ulivyoelezea Abu Talib,

hivyo nasi tunapenda kuendeleza na kudumisha heshima hio kwa kuunganisha

familia yetu na yenu. Hivyo Enyi watu wa Quraysh! Nataka kua muwe mashahidi

kua mimi namuozesha Bint wa Khuwaylid kwa Muhamamd Ibn Abdalla kwa

Mahari yaliyotolewa.’

Na kisha baada ya Waraqah Ibn Nawfal kumaliza khutba hio basi akasimama Amr Ibn

Asad na kusema: ‘Enyi watu wa Quraysh, Hakika mimi Amr Ibn Asad

nimewaunganisha Muhammad Ibn Abd Abdullah na Bint Khuwaylid kwa

kuwaozesha.’

Kisha baada ya hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamchukua na kumpeleka

Khadija Bint Khuwaylid kwa Ami yake ambako nako kukachinjwa Ngamia wawili na

kisha ikafanywa karamu watu wakafurahika. Na baada ya hapo Rasul Allah Sallahu

Alayhi wa Salam akahamia kwa Khadijah Bint Khuwaylid pamoja na Ummu Ayman,

kwani Rasul Al Salallahu Aalayhi wa Salam kamwe hakumsahau Baraka - Mama yake

Mlezi.

Ambapo Baraka naelezea haya kwa kusema: ‘Kwa Hakika mimi tangu

nilipokabidhiwa na Amina Bint Wahb kua kama Mwanangu basi Mimi sikuachana

nae na wala yeye Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam hakuachana na mimi,’ Kwani

Barakah anaendelea kutuambia kua: ‘Siku Moja wakati tukiwa kwa Bi Khadija, basi

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliniita Ya Ummah! (Ewe Mama)’

Kisha nilipoenda aliponiita basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: Ewe

Mama! Hakika mimi nimeshaoa na wewe Hujaolewa Bado, Hivi jee unaonaje kama

akija Mtu na kutaka kukuoa?’

Baraka akamwangalia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa Mapenzi ya Mama

kwa Mtoto wake kisha akasema kumwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam:

‘Hakika mimi kamwe sitoachana na wewe, hivi jee umeshawahi kuona wapi kua

Mama akaachana na Mtoto wake?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akatabasam kisha akamsogelea Barakah

akamshika Uso wake na kisha akalibusu Paji la Uso la Barakah huku akiwa amejawa na

furaha na kisha akamgeukia Bi Khadijah na kumwambia: ‘Khadija Huyu ni Baraka,

Huyu ni Mama yangu Mlezi baada ya Mama yangu Mzazi, hivyo yeye pia ni mmoja

kati ya Watu wa Familia yangu.’


640

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaendelea kua msimamizi wa Biashara ya

Khadijah Bibt Khuwaylid na kuziendeleza bila ya kua ni mwenye kufanya israf wala

kujionesha kutokana na kua Mkewe ni Tajiri mkubwa sana, kwani Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam aliendelea kuishi maisha ya kawaida na ya unyenyekevu kama ilivyokua

hapo kabla, ambapo kabla ya wakati huu basi Khadija Bint Khuwaylid alizawadiwa

Mtumwa ambae ni mtoto wa kiume aitwae Zayd Ibn Harith ambae alikamatwa alipokua

safarini na mama yake, na kisha akauzwa sokoni na kununuliwa na Hakim Ibn Hizam

Ibn Khuwaylid kwa Dirham 400.

Hivyo baada ya harusi Khadija Bint Khuwaylid akamzawadia Rasul Allah Salallahu

Aalyhi wa Salam Zayd Ibn Harith ili awe mtumwa wake ambae kwa wakati huo alikua

na umri wa miaka 14 na hivyo Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam akamwachia huru

na kumfanya kua mtoto wake wa kulea na pia msaidizi wake katika shughuli zake mbali

mbali badala ya kua Mtumwa wake.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Khadija Bint Khuwaylid, Ummu

Ayman na Zayd Ibn Harith wakawa ni wenye kuishi pamoja ndani ya nyumba ya Bi

Khadija Bint Khuwaylid, nyumba ambayo ilikua imejaa furaha, mapenzi, huruma,

heshima, utulivu na ukarimu ndani yake.

Tunapoangalia kuhusiana na mapenzi ndani ya Nyumba ya Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam basi tunaona pale siku moja baada ya Rasul Allah Salallahbu Alayhi wa Salam

wakati akiwa ndani ya nyumba yake basi alisikia Mlango unagongwa huku yeye

mwenyewe akiwa amevaa Suruali tu, huku akiwa kifua wazi, na alipouliza ni nani

anaegona Mlango na kujibiwa kua ni Zayd Ibn Harith basi Rasul Allah Salallahu Aalyhi

wa Salam alinyanyuka kwa furaha na akenda kufungua Mlango huo na kisha

akamkumbatia Zayd Ibn Harith kwa nguvu na kumbusu Paji lake la uso na kumkumbatia

zaidi, yaani Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam alisahau hata kuvaa joho lake juu na

kufunika kifua chake kutokana na furaha na mapenzi yake kwa watu wake.

Ambapo tunapoangalia ukarimu wake Khadija Bint Khuwaylid basi ni pale siku moja

alipotembelewa na Halima Bint Dhuayb aliemnyonyesha Rasul Allah Salallahu Aalahyi

wa Salam alipokua mdogo, na Khadija Bint Khuwaylid akamzawadia Halima Kondoo

40 kutokana na kua ndie Mama aliemnyonyesha na kumlea vizuri Mume wake.

Kwani bila ya shaka Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam na Khadija Bint Khuwaylid

walikua ni watu ambao wenye kupendana sana kiasi ya kua mapenzi haya yalikua wazi

hata baada ya kufariki wa Khadija Bint Khuwaylid basi alisema Aisha Radhi Allahu Anha

kua: ‘Hakika mimi sikua ni mwenye kumuonea wivu mke yeyote wa Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kama nilivyokua nikimuonea wivu Khadija bint

Khuwaylid.’


641

Ndoa hii ya Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam na Khadija Bint Khuwaylid ilitoa pia

matunda mema ya watoto 6 ambao ni Qasim, Zaynab, Ruqqayah, Umm Kulthum, Fatma

na Abd Allah, ambapo Qasim Ibn Muhammad ambae ndie mtoto wa mwanzo aliezaliwa

ndani ya miaka mitatu ya mwanzo ya ndoa hii yaani wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alipokua na umri wa miaka 28 na Bi Khadijah Bint Khuwaylid alikiwa na umri

wa miaka 43, ambapo Qasim aliishi kwa mda wa miaka mitatu tu na kisha akafariki.

MUHAMMAD AL AMIN SALALLAHU ALAYHI WA SALAM NA

UJENZI WA AL KAABAH.

Miaka 10 baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kumuoa Khadija Bint

Khuwaylid basi katika Mji wa Makkah ilitokea mvua kubwa sana ambayo ilisababisha

mafuriko ambayo yalisababisha mdhara makubwa sana ikiwemo Jengo la Al Kaabah,

kiasi ya kus jengo hilo likawa ni lazima lifanyiwe matengenezo, kwani vyenginevyo

litasababisha madhara makubwa zaidi kutokaa na kuwaangukia watu.

Na ili litengenezwe upya basi ilikua inabidi livunjwe lote kwanza kisha linyanyuliwe kwa

kujengwa upya, na ingawa hali ilikua kama hivyo lakini hata hivyo hakuna hata mtu

mmoja aliethubutu kulivunja jengo hilo, kutokana na khofu ya kua huenda mwenye Jengo

lake yaani Allah Subhanah wa Ta’ala atapitisha adhabu yake kwa yeyote yule

atakaelivunja jengo hilo na hivyo kwa kusababisha kutokea kama yaliyotokea miaka 35

hapo kabla katika mwaka wa Tembo dhidi ya Jeshi la watu wa Tembo.

Katika mwaka huo baada ya Mvua kumalizika basi kwa bahati mbaya kuna mwanamke

aliwasha Moto ambao cheche zake zilirukia kwenye Kitambaa cha Al Kaabah na Al

Kaabah ikawaka moto, na kama haitoshi basi baada ya tukio hilo usiku mmoja wakatokea

wezi na kuiba Dhahabu zote zilizokua ni mapambo ndani ya Jengo la Al Kaabah, hivyo

watu wa Kabila la Quraysh wakaamua kua umefika wakati wa kulivunja na kulijenga

Upya jengo hilo, lakini suali likabakia, ni kua: ‘Jee ni nani miongoni mwao atakaeweza

kuanzisha kuchukua hatua hio ya kulivunja Jengo hilo tukufu la miaka na miaka?’

Tunapozungumzia Watu wa Kabila la Quraysh basi tunaona kua ni watu ambao kwa

miaka na miaka, walikua na mfumo wa kupeana majukumu tofauti ya kuhudumia jamii

yao ya Mji wa Makkah, na kabila la Banu Makhzum lilikua lina jukumu la kusimamia na

kulinda usalama wa mji wa Makkah, kuandaa viongozi watakao ongoza mapambano

vinapotokea vita na pia kusimamia na kulinda misafara ya wafanya biashara wa Makkah

wanapoenda kufanya biashara katika maeneo mengine kama vile Sham, Yemen n.k. hili

ndio lililokua Kabila la Khalid Ibn Al Walid Al Mughirah Ibn Abdullah Ibn Umar Ibn

Makhzum Ibn Yaqza Ibn Murra Radhi Allahu Anhu.


642

Baba yake Khalid Ibn Walid ambae ni Al Walid Ibn Mughira alikua ni tajiri mkubwa

sana na pia ndie aliekua msimamizi mkuu wa kusimamia usalama wote wa watu wa mji

wa Makkah, ambapo hali hii ya kimazingira na kimajukumu katika jamii ya watu wa

Qurays ilimpelekea Khalid Ibn Walid kua hana haja ya kufanya kazi nyengine isipokua

kufanya mazoezi ya kupigana. Mazingira ya kimaisha ya kabila hili yalimfanya Khalid

kua kijana asiekua na mpinzani katika zama zake, kwani baba yake alimfundisha

kupigana kwa kutumia mwili wake na kwa kutumia silaha aina zote za kivita za wakati

huo, na pia kupigana katika mazingira yeyote yale iwe chini au juu na kwa kutumia

vipando vya wanyama wa aina zote.

Mama yake Khalid Ibn Walid alikua akiitwa Lubabah As Saghira Bint Harith Ibn Hazan

Al Hilalieh, ambae alikua ni dada yake Maymuna Bint Harith Ibn Hazan Al Hilalieh

ambae aliekua ni Mke wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na pia dada wa

Lubaba Al Ghubra Bint Harith Ibn Hazan Al Hilalieh aliekua mke wa Al Abbas Ibn Abd

Al Muttalib ambae ni Ami yake Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ambae

pia ndie aliekua baba yake Sahaba maarufu aitwae Abd Allah Ibn Abbas (Bahr ul I’lm).

Hivyo baada ya watu wa Quraysh kuamua kutaka kulivunja Jengeo la Al Kaabah basi

alikua ni kiongozi Mkuu wa Usalam wa Mji wa Makkah ambae ni Al Walid Ibn Mughira

ambae yeye ndie aliejitolea kua jukumu hilo atalianza kulibeba yeye kwa mikono yake,

huku watu wote wakiwa na khofu kubwa na kusema kua wanasubiri kitakachomtokea Al

Walid Ibn Mughira, kama akidhurika basi hakuna atakediriki kulivunja Jengo hilo, lakini

kama akiwa hajadhurika basi nao watasaidia katika kulivunja lote Jengo hilo na kulijenga

upya.

Hivyo Al Walid Ibn Mughira akachukua Nyundo yake kisha akaenda hadi kwenye Al

Kaabah na kusema: ‘Ya Allah hakika mimi sio kama siiamini Dini yako, isipokua

inabidi tufanye hivyi tunavyofanya ili kuliboresha hili jengo lako tukufu.’ Na baada

ya hapo akvunja upande mmoja wa Al Kaabah, na kisha akondoka, hukua akiwaacha

watu wakisubiri kitakachomtokea baada yake. Lakini baada ya tukio hilo hakuna

lililotokea hivyo sikua ya pili asubuhi basi Al Walid Ibn Mughira akaendelea na kazi ya

kulivunja jengo hilo, huku watu wengine nao wakaanza kumsaidia hadi likamalizika na

kuanguka lote na kukutana na msingi wa awali wa jengo hilo.

Na walipoendelea kuchimba zaidi, basi wakatutana na mawe ya rangi ya Kijani ambayo

yameshikamana pamoja, na walipoendelea kuchimba basi ghafla ukatokea Mtetemeko

wa Ardhi, hivyo watu hao wa Quraysh wakaingiwa na khofu kubwa sana, na kuanza

kutaka kuimbia, lakini walipoacvha kuchimba basi Ardhi ikatulia, hivyo wakajua kua hio

ni dalili kua hawatakiwi kuendelea kuchimba zaidi. Kwa hivyo wakawacha haliiwe kama

ilivyo.


643

Baada ya kulivunja jengo hilo basi wakuu wa kabila Quraysh wakakaa na kufikiria

watumie kitu gani kwa ajili ya kulijenga upya jengo hilo, na mara wakapata habari kua

kuna Jahazi inayotoka ambayo Misri imefunga gati katika bahari Nyekundu karibu na

Mji wa Makkah, hivyo wakatuma ujumbe ukaangalie shehena ya Jahazi hio kwani

huenda labda wakapata vifaa vitakavyowafaa kwa ujenzi wa Jengo lao hilo. Na hivyo

ujumbe huo ukarudisha Majibu yasemayo kua Jahazi hio imebeba vifaa vya ujenzi

ikiwemo Vigae, Vyuma, Mbao, n.k

Hivi ni vitu ambavyo walikua wakivihitaji sana katika ujenzi wao huo, hivyo wakaamua

kua bora wafanya mazungumzo na wafanya biashara wa bidhaa hizo kua hawatowatoza

ushuru watakapokuja kwenye Mji wao kama watakubali kuwauzia vifaa hivyo kwa

urahisi kwa ajili ya ujenzi wao huo, na hivyo watu hao wakakubaliana na wazo hilo, na

kwa kua ndani ya Jahazi hilo pia fundi Muwashi mzuri sana aitwae Bakum ambae alikua

ni Mturuki hivyo wakazungumza nae na akakubaliana nao kuwajengea Jengo hilo.

Hivyo jengo hilo likajengwa huku ikiwa kila Ukoo ukiwa unasimamia upande wake

kulingana na makubaliano waliyoafikiana hapo kabla, na lilipofikia kwenye usawa wa

sehemu ya kuliweka Jiwe Jeusi, basi katokea mvutano mkubwa sana, kwani kutokana na

utukufu wake basi hawakuweza kufikia makubaliano juu ya nani ndie anaestahiki

kuliweka jiwe hilo katika sehemu yake. Na tayari kila mmoja alikua yuko tayari kupigana

kama akipewa mwenzake jukumu hilo na kukoseshwa yeye kuliweka jiwe hilo.

Kiasi ya kua kazi ya kujenga Al Kaabah ikasita kwa siku 4 tangu kuanzia siku ya

Alkhamis hadi siku ya Jumatatu kwa ajili tu ya kutopatikana makubaliano juu ya nani

anaestahiki kuliweka Hajar Al Aswad katika sehemu yake. Hivyo viongozi wa Kabila la

Quraysh wakapanga kua wakutane katika eneo la Masjid Haram ili watafute utatuzi wa

tatizo hilo. Na baada ya kukutana kwao katika siku hio ya Jumatatu na kuvutana kwa

takriban saa moja basi mmoja wao miongoni mwao aliekua akiitwa Hudhayfah Ibn

Mughira akasema: ‘Enyi watu wa Quraysh, hakika mimi naona kua hakuna mwisho

wa kujadiliana juu ya jambo hili isipokua kumteua mtu wa mwanzo atakaeingia

kuja humu Ndani kwa kupitia mlango ule pale wa Bani Shayba basi awe ndie

mtatuzi wa Jambo hili.’

Hivyo Viongozi hao wa Kabila la Quraysh wakakubaliana na mtizamo huo wa

Hudhayfah na kusema kua huo ndio utatuzi pekee utakaotatua mzozo huo, hivyo wakakaa

kimya huku wakiwa ni wenye kuutolea macho Mlango wa Banu Shayba kwa umakini

mkubwa sana, na haukuchukua mda mrefu mara wakaona kua kuna mtu anaingia kupitia

kwenye Mlango huo wa Banu Shayba na anakuja katika sehemu waliyokaa, na watu hao

wakatizamana na kisha wakaendelea kumtizama Mtu huyo kama hawaamini macho yao

huku wakitaka wapate kumjua ni nani?


644

Na bila ya shaka Mtu huyo hakua mtu mwengine isipokua alikua ni Al Amin na hapo

hapo watu hao wakashangilia kwa sauti kubwa zilizojaa furaha na ridhaa huku wakisema:

‘Ni Muhammahd Al Amin, bila ya shaka tutakubaliana na kuridhia kutokana na

hukumu yake.’

Kiasi ya kua Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam alishangazwa na furaha hio

waliyokua nayo Viongozi hao baada ya kutaja jina lake na hakuweza kuJua juu ya

linaloendelea hadi pale alipofika mbele yao kisha nao wakamuelezea tatizo lao. Ambapo

Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akatafakari kisha akasema: ‘Nipeni Kitambaa’

ambapo Al Walid Ibn Mughira akatoa Kilemba chake na kumpa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam.

Na pia kuna wasemao kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alivua Kilemba chake

na kukitandaza ardhini na kisha akalichukua Hajar Al Aswad na kuliweka katikati ya

kilemba hicho huku akiwaacha watu wakiwa wamejawa na mshangao, kwa kujiuliza ni

kitu gani kinachotakiwa kufanywa na Al Amin na kisha Rasul Allah Salallahu Aalayhi

wa Salam akasema: ‘Nataka kila Mtu kutoka kwenye kila Ukoo awe ni mwenye

kushika ncha ya kilemba hiki’

Na baada ya watu hao kushika kitambaa hicho basi Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa

Salam akawaambia kua walisogeze Jiwe hilo karibu na sehemu yake, na liliposogezwa

basi Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akalichukua kutoka kwenye kitambaa hicho

na kulipachika kwenye sehemu yake, na baada ya hapo ujenzi wa Al Kaabah ukaendelea

na kumalizika kwa salama na amani kwani kila mmoja katia ya waliohudhuria katika

tukio hilo walikua wameridhia na maamuzi hayo ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam.

RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM NA ALI IBN ABI

TALIB

Wakati Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam alipotimia umri wa miaka 36, basi Mji

wa Makkah ukakumbwa tena na ukame mkubwa na hivyo watu wake wakawa wana njaa,

na kila mtu akawa anahitaji Msaada kutoka kwa Mwenzake, hivyo katika kipindi hiki

ingawa Abu Talib ambae ni Ami yake mkubwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alikua ni Chifu wa Mji wa Makkah, lakini kama tulivyosema hapo awali kua alikua ni

Masikini, kwani Uchifu wake haukua ni wenye Kutokana na Mali bali Ulikua ni wenye

Kutokana na Utukufu wa Kabila lake na Ukoo wake.

Ambapo Miongoni mwa Watu wa Karibu wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

katika Maami zake yaani Mababa zake wadogo na wakubwa basi alikua ni Al Abbas


645

Radhi Allahu Anhu ambae ni baba yake Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, na

huyu alikua ni rafiki yake wa karibu sana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa

sababu ingawa Al Abbas alikua ni Baba mdogo lakini alikua amepishana na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kwa miaka mitano tu.

Hivyo walikua Mtu na Baba yake mdogo na pia mtu na rafiki yake wa karibu sana kwa

sababu ya kua walicheza pamoja, hivyo katika mwaka huo wa Ukame na Njaa basi Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamwambia Al Abbas Ibn Abd Al Mutallib kua: ‘Ya

Al Abbas, hivi Jee unajua kua Kaka yako, Abu Talib ana familia kubwa sana? Na

kama unavyoona kua hali imekua ngumu kwa Ukame, hivyo wacha mimi nawe

tuende kwa Abu Talib tukamsaidie Majukumu yake, wewe utamsaidia Kulea

Mtoto Mmoja na Mimi nitachukua Mtoto mmoja kulea.’

Hivyo hapa tunaona kua ingawa Abu Talib Ibn Abd Al Mutallib alikua na watoto 7 lakini

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakusema kua Mimi nitachukua watoto Watatu

nilee na wewe utachukua Watatu kisha tukishindwa tutaomba msaada, La!..bali alisema

kua Wewe utachukua Mtoto Mmoja na Mimi nitachukua Mtoto Mmoja, na hii ni

kutokana na kujua hali ya Uwezo wake yeye Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na

uwezo wa Ami yake.

Na ndio maana Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kuhusiana nae Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua:

‏﴿ل َّقَدْ‏ كَانَ‏ لَكُمْ‏ فىِ‏ رَسُولِ‏ ٱهلل َِّ‏ أُسْوَةٌ‏ حَسَنَةٌ‏ لِّمَن كَانَ‏ يَرْجُو ٱهلل ََّ‏ وَٱلْيَوْمَ‏ ٱلآخِ‏ رَ‏

وَذَكَرَٱ هلل ََّكَثِير اً﴾‏

Laqad kana lakum fee rasooli Allahi oswatun hasanatun liman kana yarjoo Allaha

waalyawma al-akhira wadhakara Allaha katheeran (Surat Al Ahzab 33:21)

Tafsir: Kwa hakika mmepata kutoka kwa Rasul Allah mfano bora sana, kwa yule

mwenye matumaini juu ya Allah na siku ya Akhera na akamkumbuka Allah kwa

wingi.

Hivyo baada ya Makubaliano hayo basi Rasul Allah Salalahu Alayhi wa Salam na Ami

yake yaani Abbas Ibn Abd Al Mutallib Radhi Allahu Anhu wakatoka hadi kwa Abu Talib

Ibn Abd Al Mutallib na wakampa ushauri wao huo wa kutaka kumsaidia Ulezi. Hivyo

Abu Talib akakubaliana na shauri hilo la kusaidiwa Ulezi na Rasul Allah Sallahu Alayhi


646

wa Salam akapewa mtoto mmoja wa Kiume ambae ndie Ali Ibn Abu Talib Radhi Allahu

Anhu na akawa analelewa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Hivyo Nyumba ya Bi Khadija Bint Khuwaylid ikawa ameongezeka mtu mmoja ambae

ni Ali Ibn Abu Talib ambae katika kipindi hiki alikua na umri wa miaka mitano. Na Al

Abbas Radhi Allahu Anhu akapewa mtoto mwengine wa kiume amlee ambae ni Jafar Ibn

Abu Talib Radhi Allahu Anhu.

Ambapo siku moja katika nyumba hio ya Bi Khadija Bint Khuwaylid alikuja Mgeni

kutoka katika Mji wa Madinah ambae alikua anaitwa Ubayd Ibn Zayd na akamuona

Barakah na akampenda, hivyo Ubayd akazungumza na Bi Khadija na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam ambapo Bi Khadija akamwambia Baraka: ‘Barakah, hakika

wewe tayari umeshatumia Ujana wako wote kwa Ajili ya Muhammad (Salallahu

Alayhi wa Salam), hivyo nae anataka akulipe baadhi ya Majukumu yako juu yake.

Hivyo tunakuomba mimi na Muhammad (Salallahu Alayhi wa Salam) kua bora

Uolewe, hivyo usitukatalie maombi yetu juu yako’

Baraka akashangaa huku akitafakkari, kisha akauliza: ‘Hivi ni Nani atakaenitaka mimi

kunioa?’

Bi Khadija akasema: ‘Kuna mtu amekuja anaitwa Ubayd Ibn Zayd kutoka katika

Kabila la Al Khazraj la Madinah amekuja kuomba kuunga Udugu nasi, anataka

mkono wako, hivyo kwa ajili yetu, usikatae tafadhali’

Hivyo bila ya shaka Barakah akakubaliana na kuridhia Jambo hilo kwa ajili ya

Kumfurahisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Bi Khadija Bint Khuwaylid.

Hivyo Baraka akaolewa na Ubayd Ibn Zayd na kisha akahama katika Mji wa Makkah

akahamia katika Mji wa Madinah lakini hata hivyo hakukaa kwa mda mrefu kwani nae

kwa upande wake hali ilikua kama ilivyokua ya aliekua Sayyida wake yaani Bi Amina

Bint Wahb mama yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae alifiliwa na

mumewe muda mfupi baada ya kuolewa.

Hivyo na Barakah nae alikua na majaaliwa hayo hayo, kwani Allah Subhanah wa Ta'ala

alimuandikia kua aondoke katika Mji wa Makkah kwa mfupi kisha arudi tena kwa Mtoto

wake kipenzi kwani alipofika katika Mji wa Madinah baada ya kuolewa hakukaa mda

mrefu kwani Mumewe akafariki huku akimwacha Barakah akiwa Mja Mzito ambapo

baadae alijifungua mtoto wa Kiume aitwae Ayman.

Na Wanazuoni wametofautiana kuhusiana na sehemu aliyozaliwa Ayman, kwani kuna

wasemao kua alizaliwa katika Mji wa Madinah na kuna wanaosema kua Barakah alirudi

katika Mji wa Makkah akiwa mja mzito na akamzaa Ayman katika Mji wa Makkah.


647

Ambapo baada ya kujifungua mtoto huyo basi Jina la Barakah likafutika kwani kila mtu

akawa anamwita kwa jina la Mtoto wake yaani Ummu Ayman yaani Mama Ayman,

isipokua kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, kwani kwake yeye Barakah hakua

Barakah wala hakua Ummu Ayman bali alikua ni Ummu - Mama!

Hivyo baada ya kufariki Mumewe katika Mji wa Madinah basi Ummu Ayman akarudi

katika Mji wa Makka na hakua na sehemu yeyote ya kufikia na kuishi isipokua kwenye

Nyumba ya Mtoto wake Kipenzi yaani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Ingawa katika kipindi hiki Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua hajapata

Utume bado, lakini alikua anajua kua watu wa Makkah walikua wanaishi katika hali ya

Kijahiliyah katika Imani zao, vitendo vyao na hata katika maneno yao, kwani ujinga

ilikua ndio maisha yao.

Hivyo akawa anajaribu kutafakkar hali hiyo imekua kuaje? Na itaendelea hadi lini? Na

katika kipindi hiki alikua usiku anapolala hua anaona ndoto za ukweli halisia, na

zinazotokea kweli, ndoto zenye kumuingiza kwenye nuru ya muangaza wenye kung’ara,

na mchana husikia sauti na kuona nuru fulani isiyojulikana asili yake, sauti zenye

kumuusia mema na kumuonesha kua maisha wanayoishi watu wake ni maisha ya

upotovu, hivyo akawa anahisi anahitaji mda wa kukaa peke yake na kutafakari.

Hivyo akaanza kujitenga nao watu wa Makkah kwa kutafuta mda wa kukaa mbali kidogo

na aina hiyo ya maisha, kwa muda wa mwezi mmoja kila mwaka, na katika kipindi hicho

ambacho hua ni mwezi mzima wa Ramadhan na katika baadhi ya siku za miezi myengine

ndani ya miaka mitatu basi alikua akitumia mda wake mwingi peke yake, kukaa kwenye

pango liliopo katika Jabal al Hirra ambalo liko katika umbali wa Kilomita 3 kutoka

kwenye Jengo la Al Kaabah kwa ajili ya kutafakari.

Na ndio maana akasema Imam Amir Abd Kays kua: ‘Hakika mimi nimewasikia

Masahaba 10 wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam wakisema kua: ‘Nuru ya

Uislam hupatikana katika Kutafakkar’’ Imam Hasan Al Basr kua: ‘Saa moja ya

Kutafakkar ni bora kuliko Mwaka mzima wa Qiyam Al Layl’

Na anasema Aisha Radhi Allahu Anha kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi alikua

akienda kwenye Jabal Al Hira kwa ajili ya Kumuabudu Allah Subhanah wa Ta’ala

peke yake’ (Sahih Bukhari) ambapo tunapoiangalia hadithi hii basi tunaona kua sio

kwamba Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam alikua akisali sala tano, la, kwa sababu

katika kipindi hiki bado hakua ni Mtume na wala Sala hazikuamrishwa bado, hivyo alikua

akikaa na kutafakkari kama vile ambavyo alivyokua akitafakari Nabii Ibrahim:


648

‏﴿وَكَذٰ‏ لِكَ‏ نُرِي ۤ إِبْرَاهِيمَ‏ مَلَكُوتَ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَلِيَكُونَ‏ مِنَ‏ ٱلْمُوقِنِينَ‏ ﴾

Wakadhalika nuree ibraheema malakoota alssamawati waal-Ardhi waliyakoona

mina almooqineena (Surat Al AnAam 6:75)

Tafsir: Na Kadhalika tukamuonesha Ibrahim Ufalme wa Mbingu na Ardhi ili awe

miongoni mwa wenye Imani na Yaqini.

Ama kuhusiana na maneno yasemayo ‘Wakadhalika nuree ibraheema malakoota

alssamawati waal-Ardhi waliyakoona mina almooqineena’ yaani ‘Na Kadhalika

tukamuonesha Ibrahim Ufalme wa Mbinguni na Ardhini ili awe miongoni mwa wenye

Imani na Yaqini.’

Basi anasema Mujaddid ad Din, Sultan al Mutakallimin Imam Fakhr ad Din al Razi kua:

‘Juu ya neno Nuriy basi amesema Imam Abu Al Ma’ali Al Juwayni Al Haramayn

kua: I’lm ya Allah Subhanah wa Taála ni kubwa isiyokua na mpaka. Na bila ya

shaka I’lm yake juu ya kila kitu haina mwisho. Kwani kila sehemu za viumbe wake

hua zinaweza kuchukua maumbo yasiyokua na mwisho.

Hivyo I’lm ya Ufalme wake haina mwisho, na bila ya shaka kuipata I’lm hio kwa

yeyote yule miongoni mwa Viumbe wake hua haiwezekani, hivyo hubidi kupatikana

kidogo kidogo hatua kwa hatua. Na Vile vile tunaona kua hapa Allah Subhana wa

Taála hakutumia neno ‘Araynahu’ ambalo hua linamaanisha ‘Tulimuonesha’ yaani

katika hali ya kitendo kilichopita lakini ni chenye kumaanisha kuoneshwa kitu

chote kwa ghafla moja hapo kwa hapo, bali ametumia neno ‘Nuriy’ ambalo

linajumuisha hali iliyopo na hali inayokuja ambako ni kwenye kumaanisha kuwepo

kwa kitendo ambacho kinachoendelea na hivyo chenye kuambatana na muendelezo

unaoongezeka kidogo kidogo hatua kwa hatua’

Mujaddid ad Din, Sultan al Mutakallimin Imam Fakhr ad Din al Razi anamalizia

kutuelezea kuhusiana na neno Malakut lililotumika hapa kwa kusema kua: ‘Roho za Ibn

Adam hua haiwezi kukosa kuiona Nuru ya Allah Subhanah wa Taála, isipokua kuwa

sababu ya kuwepo kwa vizuizi. Na Jee ni vizuizi gani hivyo? Hivi ni vizuizi vya yale

mambo ambayo mtu hujishughulisha nayo ambayo hua hayahusiani na Muumba

na kumpelekea mtu kua mbali na Allah Subhanah wa Taála. Na bila ya shaka vizuizi

vikubwa hua ni Masanamu.

Kwani wakati Ibrahim alipoondoa kizuizi chake kwa kujitolea kwa ajili ya Allah

Subhanah wa Taála na akakataa kuwepo kwa chengine chochote kile zaidi yake

Allah Subhanah wa Taála basi alifanikiwa kupata ubainisho wa kuwepo kwa


649

Muumba. Aina hii ya Ubainisho wa kuwepo kwa Muumba hua hauonekani kwa

mtizamo wa jicho la kawaida, bali hua ni wenye kuonekana kwa mtizamo wa jicho

la ndani ya Moyo, na hili ndio jambo lililomuwezesha Nabii Ibrahim kujenga hoja

zake ambazo aliziwakilisha kwa watu wake kama inayoelezewa na aya

tunazoziangalia.

Ama kuhusiana na neno Yaqin basi ni hali ya kujihakikishia kwa Moyo ambayo

hupatikana pale wakati inapokua hakuna shaka yeyote ndani ya Moyo kutokana na

vithibitisho vinavyoonekana na Moyo husika.

Ambapo katika kipindi hiki Khadija Bint Khuwaylid alikua nae anaenda kumtembelea

Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam kwani alikua ni mwenye kumuunga mkono

mume wake katika kila kitu kiasi ya kua kuna baadhi ya siku nae alikua anakesha nae

pamoja huko huko kwenye pango hilo kwa ajili ya kutafakkar pamoja nae Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam mbali ya kua alikua ni mwanamke mwenye umri mkubwa wa

miaka 55 lakini alikua akipanda Mlima huo wa Hira kwa ajili ya kua pamoja na mtu

ampendae na kumuamini kikamilifu na kumjali sana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam

Na hivyo haishangazi kuona kua akasema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

‘Mwanamke bora wa Dunia katika wakati wake alikua ni Maryam Bint Imran, na

Mwanamke Bora wa Dunia ni Khadija katika wakati wake(Sahih Bukhari)

Na pia Allah Subhanah wa Ta’ala aliliona hili na kumpandisha Darja ya juu zaidi Khadija

Bint Khuwaylid pale alimwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

‘Mbashirie Khadija kua atakua na Kasri lililojengwa kutokana na Qasab (Lulu

kubwa na Nzuri sana za Peponi yenye Pango ndani yake) na hamtokua na sauti

wala zogo lolote ndani yake’’(Sahih Bukhari)

MAISHA YA UTUME WA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI

WA SALAM NA UPINZANI KUTOKA KWA WATU WAKE.

Jumatatu moja ya mwezi 27 wa Ramadhani, ambayo ni sawa na mwezi Julai wa mwaka

610, wakati Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akiwa na miaka 40, ilikua

kama ilivyo kawaida yake katika kutafakari kwake ndani ya pango hilo, lakini Jumatatu

hiyo ilikua tofauti na Jumatatu nyengine kwani alijihisi kua katika pango hilo hayuko

peke yake, lakini kila akitazama haoni mtu wala hasikii sauti yeyote kwani kulikua tulii

na kimya. Mara ghafla akasikia sauti inaamrisha:


650

‘Iqraa!’ (Soma!)

﴾ ‏﴿ٱقْرَأْ‏

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alishtuka akageuka kutafuta sauti imetoka

wapi na nani anaepewa amri hiyo. Lakini hakuona mtu wala kitu chochote kinachotoa

sauti hiyo wala yule anaepewa amri hiyo, hapo akajua kua yeyote yule anaetoa amri hiyo,

alikua anamuamrisha yeye amri hiyo, na kwa kua yeye alikua si miongoni mwa

waliosoma basi akajibu: ‘Ma ana bi Qari’i’ (Mimi si miongoni mwa wasomaji).

Sauti hiyo ikaamrisha tena kwa ukali: ‘Iqraa!’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu tena huku akiwa na khofu ‘Ma

ana bi Qari’i’.

Sauti hiyo ikaamrisha tena kwa ukali zaid: ‘Iqraa!’.

Kwa kua Nabii Muhammad Salallahu A’alayhi wa Salam, alikua hajui kusoma, na vile

vile alikua hakioni kitu anachoambiwa akisome, basi akajua kua kwa vyovyote vile

itakavyokua amri hiyo anayopewa yeye inamtaka asome kwa kurudia kile anachokisema

mwenye sauti hiyo. Hivyo sauti hiyo ilipoendelea kusema, ilisema kwa upole na huruma

zaid, hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam nae akafuatisha kama vile

namna inavyosema sauti hiyo kwa kusoma:

‏﴿ٱقْرَأْ‏ بِٱسْمِ‏ رَبِّكَ‏ ٱل َّذِى خَلَقَ‏ ﴾

Iqraa bi-ismi rabbika alladhii khalaqa. (Soma kwa jina la Mola wako alieumba).

‏﴿خَلَقَ‏ ٱلإِنسَانَ‏ مِنْ‏ عَلَقٍ‏ ﴾

Khalaqa al insana min A’alaqin. (Aliemuumba mtu kutokana na pande la damu).

ٱ ق ْرَأْوَرَب ُّ كَ‏ ٱ لأَكْرَمُ‏ ﴿

Iqraa warabbuka al akramu. (Soma. Na Mola wako ni mwingi wa Ukarimu).

‏﴿ٱل َّذِى عَل َّمَ‏ بِٱلْقَلَمِ‏ ﴾

Alladhii A’allama bialqalami. (Aliesomesha kwa kutumia Kalamu).

‏﴿عَل َّمَ‏ ٱلإِنسَانَ‏ مَا لمَْ‏ يَعْلَمْ‏ ﴾

A’allama al-insana ma lam yaA’lam. (Aliemfundisha mtu kile asichokijua).(Surat Al

A’laq 96: 1-5).


651

Naam, huo ndio uliokua mwanzo wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam,

kupokea ujumbe (Wahy) wake wa mwanzo kutoka kwa Allah Subhanahu wa Ta’ala

kupitia kwa njia ya Malaika wake Jibril A’layhi Salatu wa Salam. Na ujumbe huo ulikua

ni aya tano za mwanzo za sura ya 96 iliyomo katika Qur’an, nayo ni Surat Al A’laq, na

neno la mwanzo la ujumbe huo ambao ni ujumbe uliomo ndani ya Qur’an, lilikua ni neno

lenye maana ya kutafuta I’lm, ‘Iqraa!’(Soma!).

Katika kuifafanua Surat Al A’laq 95: 4-5 basi Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Al

Ghazal anasema kua hapa haizungumziwi peni au kalamu tunayoitumia leo mimi na

wewe, bali hapa panazungumziwa: ‘Kila kitu kilichoonekana kua kipo kutokana na

I’lm ya maumbile ambayo imepandikizwa au kupigiwa muhuri ndani ya Nafsi za

Ibn Adam…Kalamu hii hua ni ya hali ya kujulikana kwa Kiroho, kwani hali ya

kujulikana kuwepo kwake hua ni kwa kupitia njia ya kiroho ambayo ndio

hututhibitishia uhalisia wa undani wake…Kwani Kalamu ya kijiti au ya unyoya

unaotumiwa kuandikia hua si miongoni mwa vinavyohisabiwa kua na uhalisia wa

Kalamu hii.’

Labda baadhi wanaweza kujiuliza kwa nini ikawa ni Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam na kwanini hakupewa Utume hadi alipofikia umri wa miaka 40?

Jawabu la swali hili linapatikana katika aya zisemazo:

‏﴿وَإِذَا جَآءَتْهُمْ‏ آيَةٌ‏ قَالُواْ‏ لَن ن ُّؤْمِنَ‏ حَتى َّ ٰ ٰ نُؤْتَى مِثْلَ‏ مَآ أُوتِىَ‏ رُسُلُ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱهلل َُّ‏ أَعْلَمُ‏

حَيْثُ‏ يجَْعَلُ‏ رِسَالَتَهُ‏ سَيُصِيبُ‏ ٱل َّذِينَ‏ أَجْرَمُواْ‏ صَغَارٌ‏ عِندَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَعَذَابٌ‏ شَدِيدٌ‏ ا بمَِ‏

كَانُواْ‏ يمَْكُرُونَ‏ ﴾

Wa-idha jaat-hum ayatun qaloo lan nu/mina hatta nu/ta mithla ma ootiya rusulu

Allahi Allahu aAAlamu haythu yajAAalu risalatahu sayuseebu alladheena ajramoo

sagharun AAinda Allahi waAAadhabun shadeedun bima kanoo yamkuroona (Surat

Al An Aaam 6:124)

Tafsir: Na wakati zinapowajia Aya zetu hua ni wenye kusema: ‘Hatutoamini hadi

tutakapopewa mithili ya kile ambacho amepewa Mtume wa Allah, Allah ni mwenye

kujua wapi bora kujaalia Ujumbe wake. Yatawasibu wale ambao ni wenye kuasi,

maadhirisho kutoka kwa Allah na adhabu kali sana kutokana na yale waliyokua

wakiyapanga.’


652

Ambapo Aya inatuonesha kua Allah Subhanah wa Ta’ala ni mwenye kujua wapi aweke

ujumbe wake, na nani ampe kipi, vipi na katika wakati gani, hivyo hata mimi na wewe

tunafikwa na mitihani basi hatakiwi kuuliza kwanini mimi? Au kwanini fulani akawa

zaidi yangu, n.k

Na jibu la pili linapatikana katika aya 15 ya Surat Al Ahqaf ambayo inatufundisha hikma

na busara inayopatikana pale mtu kufikia umri wa miaka 40 kama inavyosema Qur’an:

‏﴿وَوَ‏ ص َّيْ‏ نَا ٱلإِ‏ نسَ‏ انَ‏ بِوَالِدَ‏ يْهِ‏ إِحْ‏ سَ‏ اً‏ حمََلَتْهُ‏ أُم ُّهُ‏ كُرْهاً‏ وَوَضَعَتْهُ‏ كُرْهاً‏ وَحمَْلُهُ‏ وَا فَِص لُهُ‏

ثَلاَثُونَ‏ شَهْراً‏ حَتى َّ ٰ إِذَا بَلَغَ‏ أَشُد َّهُ‏ وَبَلَغَ‏ أَرْبَعِينَ‏ سَنَةً‏ قَالَ‏ رَبِّ‏ أَوْزِعْنيِ‏ ۤ أَْن أَشكُ‏ ‏َر

نِعْمَ‏ تَكَ‏ ٱل َّتيِۤ‏ أَنْعَمْ‏ تَ‏ َّ عَلَى ٰ وَعَلَى وَالِدَ‏ ى َّ وَأَنْ‏ أَعْمَ‏ لَ‏ صَالحِ‏ اً‏ تَرْضَاهُ‏ وَأَصْ‏ لِحْ‏ لىِ‏ فىِ‏

ذُرِّي َّتيِ‏ ۤ إِنىّ‏ ِ تُبْتُ‏ إِلَيْكَ‏ وَ‏ ﴾

‏َين إِنىّ‏ مِنَ‏ ِ ٱلْمُسْلِمِ‏

Wawassayna al-insana biwalidayhi ihsanan hamalat-hu ommuhu kurhan

wawadaAAat-hu kurhan wahamluhu wafisaluhu thalathoona shahran hatta itha

balagha ashuddahu wabalagha arbaAAeena sanatan qala rabbi awziAAnee an

ashkura niAAmataka allatee anAAamta AAalayya waAAala walidayya waan

aAAmala salihan tardhahu waaslih lee fee dhurriyyatee innee tubtu ilayka wa-innee

mina almuslimeena (Surat Al Ahqaf 46:15)

Tafsir: Na tunamuusia Bani Adam kuwajibika na kua na huruma kwa wazazi wake.

Kwani Mama yake alimbeba kwa ugumu na akamzaa kwa ugumu, na akamlea na

kumyonyesha kwa miezi 30. hadi pale anapofikia kukua na kukamilia kinguvu na

anapokua ni mwenye kufikia miaka 40, husema: ‘Ya Rabb! Nijaalie nguvu na uwezo

ili niwe mwenye shukurani kwa Neema zako ulizonijaalia juu yangu na wazee wangu,

na ili niweze kufanya mambo mema, yatakayo kuridhisha, na kijaalie kizazi changu

kiwe chema, kwa Hakika nimekugeukia kutubia kwako na hakika mimi ni miongoni

mwa Muslimina (Waliojisalimisha kwako)’

Hivyo kipindi cha umri wa miaka 40 ni kipindi muhimu kwa kila mtu aliejaaliwa

kukifikia kimaisha, kwani katika kipindi hiki kila mtu hua tayari ameshatumia robo tatu

ya uhai wake, na hivyo hua ameshakamilika kinguvu na kukomaa kiakili na kiufahamu

na hivyo hua na busara na uwezo mzuri sana wa kutafakkar majukumu yake mbali mbali

katika maisha ya duniani na akhera, kwani vile vile kuna Manabii na Mitume wengi

ambao waliopewa Utume wakati walipoingia umri wa miaka 40 akiwemo Nabii Nuh

Alayhi Salaam, Nabii Musa A’layhi Salaam, Nabii Harun Alayhi Salaam n.k


653

Kwa upande wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, ingawa wakati huo

alikua ameshakamilia umri wa miaka 40, lakini tukio hili lilimtokezea katika pango la

Jabal al Hira lilimtia khofu kubwa sana Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam,

hivyo haraka sana akaamua kuondoka katika pango hilo la Jabal Al Hira lakini kabla ya

kufika popote alionana na umbo kubwa la Malaika Jibril A’layhi Salam, ambae

alimwambia: ‘Ewe Muhammad, wewe ni Rasul Allah na mimi ni Jibril’, kisha

Malaika Jibril akatoweka.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, akaona hii ishakua balaa kwani

haiwezekani kusikia aliyoyasikia pangoni na kuona aliyoyaona njiani wakati akikimbilia

nyumbani hivyo akaongeza kasi mwendo wake na alipofika nyumbani akaingia

chumbani na kukimbilia kitandani moja kwa moja, huku akiwa katika hali ya kutetemeka

akamwambia mfariji wake mkubwa Sayyida Khadija Al Kubra: ‘Zamiluni! Zamiluni!’

‘Nifunike! Nifunike!’ ‘Dathiruni! Dathiruni!’ ‘Nikumbatie kwa kunigubika!

Nikumbatie kwa kunigubika!’.

Khadijah Bint Khuwalid Al Kubra akamfunika, akamkumbatia na kumgubika, kisha

baada ya kurudi hali yake ya kawaida basi Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

akamhadithia yaliyomkuta na kumwambia kua ana khofu kua ufahamu wake unamsaliti,

lakini Khadijah Bint Khuwalid Al Kubra akamwambia: ‘La! Huu ni ubashirio mwema.

Wa Allahi! Allah hatokudhalilisha, kwani wewe ni mwenye kuwapatanisha ndugu

waliogombana, unawasaidia waliokua dhaifu, unawasaidia wasiokua na uwezo na

masikini, unawahudumia na kuwajali wageni wako na unastahmili mitihani

migumu katika kutafuta haki’, kisha akakaa nae na kumliwaza Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam hadi alipolala.

Baadae Khadijah Bint Khuwalid Al Kubra na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam wakaelekea kwa binamu yake Khadijah Bint Khuwalid Al Kubra aitwae Warraqah

Ibn Nawfal Ibn Asad Ibn Abd ul Uzza Ibn Qusay, ambae alikua ni mzee mwenye I’lm ya

vitabu vya Ahlu al Kitab, na kumhadithia yaliyotokea. Warraqah Ibn Nawfal

akaakasema: ‘Huyo ni Namus ambae Allah alimtuma kwa Musa. Nnatamani

ningelikua kijana hadi pale utakapofikia mda ambao watu watu wako

watakufukuza’, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akauliza:

‏’أَوَ‏ مخُْرِجِ‏ ي َّ هُمْ‏ ؟‘‏

‘Watanifukuza?’.

Warraqah akajibu: ‘Hakuna mtu yeyote yule aliewahi kuja na ujumbe kama wako

kwa watu wake bila ya kufanyiwa yasiyokua siyo na kufanyiwa uadui mkubwa, Na


654

kama ikiwa nitaishi hadi kufikia wakati huo basi bila ya shaka nitakuunga mkono

kwa kila hali’. Lakini hata hivyo Warraqah hakuishi kwa muda mrefu kuyashuhudia

aliyoyabashiria kwani baada ya kupita muda mfupi akafariki.

Khadijah Bint Khuwalid Al Kubra alikua ni mtu wa mwanzo kabisa kua Muislam baada

ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na pia ndie mke pekee aliezaa nae

watoto wake sita, Khadijah Bint Khuwalid Al Kubra alifanya jitihada kubwa sana katika

kumuunga mkono na kumliwaza Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam katika

wakati wote wa mitihani alipokua pamoja nae wakati wa uhai wake, kama alivyosema

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kuhusiana nae katika Hadith yake:

‘Allah Subhanah wa Ta’ala, hakuwahi kunipa mimi mtu yeyote aliekua bora kama

yeye. Alikua pamoja nami pale watu walipokaa mbali nami, Aliniamini pale watu

walipokua na shaka nami, Alitumia utajiri wake pamoja nami pale watu

waliponitenga, na Allah amenipa watoto kupitia kwake yeye.’(Sahih Muslim)

Baada ya tukio la kushushwa kwa aya tano za mwanzo za Surat Al A’laq, kilipita kipindi

kirefu cha ukimya, kipindi hiki kilijulikana kama kipindi cha Falrat Al-Wahy (kukatika

kwa Wahy). Imam Az Zuhri anaielezea hali ya kipindi hiki kwa kusema: ‘Kushushiwa

Wahy Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kulisimama kwa muda, hiki

kilikua ni kipindi kirefu kilichojaa huzuni na kisichokua na utulivu akilini (mwa

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam) kiasi ya kua akaanza kuenda mara

kadhaa katika Jabal al Hira ili akajitupe. Lakini kila akifika juu pembezoni ya

Mlima huo, Malaika Jibril alimtokea na kumuambia kua yeye ni Rasul Allah.

Jambo hili liliimliwaza Rasul Allah na kumrudishia utulivu wa akili yake’.(Imam

Ibn Jarir)

Imam Az Zuhri anasema baada ya habari hiyo, kua kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah kua:

‘Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua akikielezea kipindi cha falrat

al-wahy (kukatika kwa wahy) kwa kusema: ‘Siku moja nilikua nikipita njiani, mara

ghafla nikasikia sauti kutoka juu Mbinguni. Nikanyayua kichwa changu na

kuangalia juu nikamuona Malaika yule yule ambae alienitembelea katika pango la

Al Hira, akiwa amekaa kwenye kiti baina ya mbingu na ardhi. Jambo hili liliushtua

moyo wangu na nikakimbilia nyumbani nilipofika nyumba nikasema ‘Zamiluni!

Zamiluni!’ ‘Nifunike! Nifunike!’. Hivyo watu wa nyumbani kwangu wakanifunika

guo. Katika wakati huo Allah akanishushia: Ya Ayyuhal Muddaththiru (Ewe

uliejifunika gubi gubi)...Kuanzia hapo Wahy ukawa unateremka kwa nguvu na kwa

kuendelea.’’ (Bukhari, Muslim, Musnad Imam Ahmad, Imam Ibn Jarir)

Hiyo ilikua ni Surat Al Mudaththir isemayo:-


655

ٱ ‏َٰي ُّهَا د َّ لُْم ثِّرُ‏ ۞ قُمْ‏ فَأَنذِرْ‏ ‏۞وَرَب َّكَ‏ فَكَبرِّْ۞وَثِيَابَكَ‏ فَ‏ طَهِّرْ‏ ‏۞وَٱلر ُّجْزَ‏ فَٱهْجُرْ‏ ‏۞وَلاَ‏

تمَْنُن تَسْتَكْثِرُ۞وَلِرَبِّكَ‏ فَٱصْبرِْ﴾‏

﴿

Ya ayyuha almuddaththiru; Qum faandhir; Warabbaka fakabbir; Wathiyabaka

fatahhir; Waalrrujza faohjur; Wala tamnun tastakthiru; Walirabbika faisbir

(Surat Al Mudaththir 74:1-7)

Tafsir: Ewe uliejizungushia (mashuka); Amka na utoe onyo, na umkuzishe Mola

wako, Na Usafishe kivazi chako, Na ukae mbali na Ar-Rujz! (Masanamu) Na usitoe

kitu kwa ajili ya kupata kingi zaidi (usifikirie kufanya wema kwa kumtii Allah kua

unamsaidia Allah), Na kua ni mwenye Subra kwa ajili ya Mola wako (kwa kutekeleza

yale atakayokuamrisha).

Baada ya kushuka aya hizo za mwanzo mwanzo za Surat Al Muddaththir, kila kitu

katika maisha ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kikabadilika kwani

maamrisho hayo hayakumfanya yeye kua ni Nabii Salallahu A’layhi wa Salam tu bali pia

yalimuwekea wazi kua yeye pia ni Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam.

Siku chache baadae zikafuatia aya za mwanzo mwanzo za Surat Al Muzammil ambayo

ilikua ikimtayarisha kwa kumtaarifu kua jukumu lake litakua ni zito na kubwa sana kama

anavyosema Allah Subhanahu wa Ta’ala katika Qur’an:

ا ي ٱ َُّه لْمُز َّمِّل قُمِ‏ ٱلْل َّيْلَ‏ إِلا َّ قَلِيلاً‏ ۞ ن نِّ‏ أ َ صْفَهُ‏ ٱ وِ‏ ن قُصْ‏ مِنْهُ‏ قَلِيلاً‏ ۞ أَوْ‏ زِدْ‏

۞ هِى

َ

عَلَيْهِ‏ وَرَتِّلِ‏ ٱلْقُرْآنَ‏ تَرْتِيلاً‏ إِ َّ سَنُلْقِى عَلَيْكَ‏ قَوْلاً‏ ثَقِيلاً‏ ۞ إِن َّ ‏َشِ‏ ئَةَ‏ ٱلل َّيْلِ‏

أَشَد ُّ وَطْأً‏ وَأَقْوَمُ‏ قِيلاً‏ إِن َّ لَكَ‏ فىِ‏ ٱلن َّهَارِ‏ سَبْحَاً‏ طَوِيلاً‏ وَٱذْكُرِ‏ ٱسْمَ‏ ۞ ۞ رَبِّكَ‏

وَتَبَت َّلْ‏ إِلَيْهِ‏ تَبْتِيلاً‏ ر َّب ُّ ٱلْمَشْرِقِ‏ وَٱلْمَغْرِبِ‏ لاَ‏ إِلَٰهَ‏ إِلا َّ هُوَ‏ ۞ فَٱتخ َِّذْهُ‏ وَكِيلاً﴾‏

۞

ُ

َٰ ﴿

Ya ayuha almuzzammilu; Qumi allayla illa qaleelan; Nisfahu awi onqus minhu

qaleelan; Aw zid AAalayhi warattili alqur-ana tarteelan; Inna sanulqee AAalayka

qawlan thaqeelan; Inna nashi-ata allayli hiya ashaddu wat-an waaqwamu qeelan;

Inna laka fee alnnahari sabhan taweelan; Waodhkuri isma rabbika watabattal


656

ilayhi tabteelan; Rabbu almashriqi waalmaghribi la ilaha illa huwa faittakhidhhu

wakeelan (Surat Al Muzamil 73:1-9)

Tafsir: Ewe uliejifunika; Simama (Usali) usiku wote isipokua kidogo tu; Nusu yake au

karibia nusu yake, kidogo; Au kidogo zaidi. Na Rattil (usome kwa sauti) Qur’an kwa

Tartil (kwa kutiririka nayo kunakopendeza); Kwani kwa hakika tutakushushia wewe

Kaulan Thaqilan (Kauli nzito, yenye kuzingatia shariah na Hukmu); Kwa hakika

Nashia’h (kuamka)usiku ni kugumu na bora (kwa kuidhibiti Nafsi), hufaa zaidi kwa

(kufahamu) maneno (ya Allah); Hakika kwako wewe, mchana ni mkubwa (kwa

kutekeleza mambo yako ya kawaida); Na likumbuke Jina la Mola wako na Tabattil

(jitolee) kwake yeye kwa Tabtiilan (kwa kujitolea kikamilifu); Mola wa Mashariki na

Magharibi La ilaha illa Huwa, (Hakuna Mungu mwengine isipokua yeye) hivyo

mfanye kua Wakilan (Wakili wako wa kumtegemea).

Kuanzia hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akawa tayari

ameshaondokwa na wasi wasi, khofu na woga na tayari ameshayajua majukumu yake

kutoka kwa Mola wake na kufahamu uzito wake, uzito ambao haupo katika utekelezaji

wa majukumu hayo tu, bali pia katika upokeaji wa ujumbe wa majukumu hayo, kwani

wakati wa kupokea ujumbe wa majukumu hayo alikua akitokwa na jasho katika paji lake

la uso hata kama hali ya hewa ilikua ni ya baridi kali, uso wake hua ni wenye Tarrabad

(kwanza hubadilika rangi na kua kama mtu asiekua na damu halafu unakua ni mwekundu

wenye kuvilia damu), na vile vile uzito wa mwili wake huongezeka zaidi ya mara mbili

yake kiasi ya kua anapokua juu ya Ngamia basi Ngamia wake hua ni mwenye

ku Fataḍhrib bi jirāniha (Kunyoosha shingo yake, kuonesha kua mzigo alioubeba ni

mzito sana na umeshamchosha hivyo anahitaji kupumzika kwa kulala ardhini).

Katika kuielezea hali hiyo, Zayd Ibn Thabit Radhi Allahu Anahu ambae alikua amekaa

kitako na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam katika moja kati ya nyakati

ambazo Wahy ulikua ukishuka, na katika kukaa huko paja lake likawa liko chini ya paja

la Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, anasema Zayd Ibn Thabit Radhi Allahu

Anahu kua: ‘Allah Subhanahu wa Ta’ala alimshushia Wahy Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam wakati paja lake lilikua juu ya paja langu hivyo likaanza

kunifanya niuhisi uzito wake mkubwa sana kiasi ya kua nilikhofia kua huenda paja

langu litavurugika.’

Huo ni mmoja kati ya uzito wa majukumu yaliyokua yakishushwa Malaika Jibril A’layhi

Salaam kwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, Qur’an kupitia kwa njia ya

katika umbo la mtu asieonekana na watu wengine isipokua yeye au kwa njia ya sauti

ambayo kwa wale waliokaribu yake husikia kama mlio wa nyuki asieonekana karibu na

uso wake, lakini katika hali aliyokua nayo yeye mwenyewe Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam basi hua anasikia kama mlio wa kengele, na hivyo hujaribu haraka


657

haraka kuyahifadhi maneno yanayosikika katika ujumbe huo ili yasije yakamponyoka na

akayasahau.

Hivyo Allah Subhanahu wa Ta’ala akamwambia:

‏﴿لاَ‏ تحَُرِّكْ‏ بِهِ‏ لِسَانَكَ‏ لِتَعْجَلَ‏ بِهِ‏ ۞ إِن َّ عَلَيْنَا جمَْعَهُ‏ وَقُرْءَانَهُ‏ ۞ فَ‏ إِ‏ ذَ‏ ا قَ‏ رَأْنَ هُ‏ فَٱت َّبِعْ‏

قُرْآنَهُ‏ ۞ ثمُ َّ إِن َّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ﴾‏

La tuharrik bihi lisanaka litaAAjala bihi; Inna AAalayna jamAAahu waqur-anahu;

Fa-idha qara/nahu faittabiAA qur-anahu; Thumma inna AAalayna bayanahu

(Surat Al Qiyamah 75:16-19)

Tafsir: Usiuharakishe ulimi wako (kuhusiana na Qur’an) katika kuiharakisha kwake;

Kwani ni juu yetu kuikusanya na kukupa uwezo wa kuisoma; Na tunapokusomea

(kupitia kwa Jibril), wewe kifuatishie kisomo chake; Kisha ni juu yetu sisi kuibainisha

juu yako.

Anasema Abd Allah Ibn ʿAbbas Radhi Allahu Anhu, kuhusiana na aya hizo kua : ‘Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua akihisi uzito anaposhushiwa aya za

Qur’an na alikua akijaribu kuharakisha kufuatishia pamoja na maneno

anayoyasikia. Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala, akamwambia ‘Usiuharakishe ulimi

wako, kwa kuiharakisha, kwani ni juu yetu kuikusanya na kuifanya isomwe’, yaani

Allah Subhanahu wa Ta’ala ataihifadhi ndani ya kifua chake ili aweze kuisoma,

‘Hivyo tutakapokusomea, basi wewe fuatisha kisomo chake’, yaani kisikilize na

ufuatishe kwa makini. ‘Kisha ni juu yetu sisi kuibainisha’, yaani ni juu yetu sisi

kuhakikisha kua wewe unaisoma. Kuanzia hapo Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam, ikawa kila anapokuja Jibril hua anamsikiliza kwanza hadi

anapomaliza na kuondoka, na baada ya hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam huanza kusoma kama alivyosoma Jibril.’

Wakati Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu A’nhu alipokuwa anaishi ndani ya Nyumba ya

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi siku moja usiku aliwaona Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam na mkewe Khadija Ummul Mu’minina Radhi Allahu A’nhu

wakiwa wanarukuu na kusjudu, akashangaa na kuwauliza kufanya hivyo ndio maana

yake nini? Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akamjibu kua kufanya hivyo

ni kumuabudu Allah Subhanah wa Taala, hivyo kama anataka anaweza kujiunga nao, Ali

akasema kesho atamuuliza baba yake kama ma yeye anaweza kufanya hivyo ama la.


658

Lakini usiku kucha akawa akifikiria jambo hilo, na asubuhi yake akamfuata Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na kumwambia ‘Wakati Allah aliponiumba

mimi hakumuuliza baba yangu, hivyo kwa nini nimuulize baba yangu katika

kumtumikia Allah?’. Hivyo akaingia katika Uislam na kuwa ni mtoto wa mwanzo na

pia mwanamme wa mwanzo kuingia katika Uislam.

Anasema Yahya Ibn Afiif Radhi Allahu Anhu kua: ‘Katika kipindi cha Ujahiliyyah

mimi nilimtembelea Abbas Ibn Abd Ul Muttalib, na lilipoanza kuchomoza Jua,

nikamuona Mtu ametoka kwenye Nyumba yake sio mbali kutoka tulipokuwepo

akalielekea Al Kaabah na akaanza kusali, na haikuchukua mda mrefu mara

akatokea Mtoto wa Kiume ambae alisimama Kulia kwake na kisha akatokea

Mwanamke nae akasimama Nyuma yake. Na alipokua akiinama basi na wao

wakawa wanainama, alipokua akisujudu basi nao walisujudu, alipokua

wakasimama nao wakasimama’

Hivyo mimi nikaona ajabu na kusema: ‘Hili ni jambo la Ewe Al Abbas’ Hivyo Al

Abbas akasema: ‘Hivi jee unamjua ni nani huyo?’ nami nikajibu: ‘La Simjui’ Al

Abbas akasema: ‘Huyo ni Muhammad Ibn Abdullah mtoto wa kaka yangu, na jee

unamjua huyo Mtoto ni nani?’ Nami nikasema : ‘La’ Al Abbas akasema: ‘Huyo ni

Ali Ibn Abi Talib, na Jee unamjua huyo mwanamke ni nani?’ nami nikasema :

‘La’Al Abbas akasema: ‘Huyo ni Khadija Bint Khuwaylid ambae ndie mke wa

Mtoto wa kaka yangu’ (Imam At Tirmidhii, Musnad Imam Ahmad)

Ambapo Al Abbas Ibn Abd Ul Muttalib alikua na mkewe aitwae Lubaba Al Kubra ambae

ndie Mama yake Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na alikua

akijulikana pia kama Umm Fadhl ambae alikua ni rafiki yake Khadija Bint Khuwaylid

na hivyo akawa ni mwanamke wa pili kusilimu baada ya Khadijah Bint Khuwaylid kwani

nae alisilimu katika siku hio hio aliyosilimu Khadija Bint Khuwaylid na hii ni kutokana

na urafiki wa karibu sana baina ya Khadija Al Kubra na Lubaba Al Kubra..

Mama yake Lubaba Al Kubra alikua akiitwa Khawla na pia kama Hind Bint Awf Ibn

Zuyahr Ibn Harith na mama yake ni Aisha Bint Muhazzam. Ambapo tunapomzungumzia

Hind Bint Awf basi hua tunamzungumzia mwanamke ambae anaejulikana kama ‘Mama

Mkwe Bora kuliko wote Ardhini’ na hii ni kwa sababu watoto wake wawili waliolewa

na Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam ambao ni Maymuna Bint Harith na Zaynab

Bint Khuzaymah na watoto wake wengine waliolewa na Masahaba mbali mbali.

Kwani Hind Bint Awf aliolewa zaidi ya mara 4, ambapo ndoa yake ya kwanza ilikua ni

kwa Jazi Al Zubaydi ambae alikua ni miongoni mwa Waislam wa mwanzo na

akachaguliwa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua ni Muweka Mahesabu wa

Jamii ya Kiislam.


659

Halafu Hind Bint Awf akaachwa na akaolewa na Harith Ibn Hazan ambapo ndoa hii

ikatoka watoto wanne ambapo wa kwanza ni Lubaba Al Kubra ambae ndie mwanamke

wa pili kusilimu na ndie aliekua mke wa Al Abbas Ibn Abd Ul Muttalib ambae ndie Ami

yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, na wa pili ni Maymuna Bint Harith ambae

aliolewa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, wa tatu ni Saayib Ibn Harith na wa

nne ni Qatn Ibn Harith.

Halafu Harith Ibn Hazan akafariki na Hind Bint Awf akaolewa na Khuzaymah Ibn Harith

Al Hilali ndo ambayo ilitoa mtoto wa kike mmoja tu aitwae Zaynab Bint Khuzaymah

ambae aliolewa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Halafu Hind Bint Awf akaachwa na akaolewa na Umays Ibn Maad Ibn Tamim ndoa

ambayo ilitoa watoto watatu ambao ni Asma Bint Uways ambae aliolewa na Rabia Ibn

Riyab, na kisha akaolewa na Jafar Ibn Abi Talib Ibn Abd ul Muttalib, na kisha akaolewa

na Abu Baqr As Siddiq na kisha akaolewa na Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhum.

Mtoto wake wa pili ni Salma Bint Uways ambae aliolewa na Hamza Ibn Abd Al Muttalib

aliekua Ami yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, na kisha akaolewa na Shaddad

Ibn Usama.

Na mtoto wake wa tatu katika ndoa hii alikua ni Awn Ibn Umays.

Halafu Hind Bint Awf akaachwa na akaolewa na Al Harith Ibn Hazan ambae alikua na

mke mwengine aitwae Fakhta Bint Amr ambae mtoto wake wa kike ni Al Lubaba Al

Saghir ambae ndie Mama yake Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu.

Hivyo Lubaba Al Kubra Bint Harith Ibn Hazan Al Hilal alikua ni mtu mwenye asili ya

Yemen kama alivyokua mama yake ambae ni Hind Bint Awf kwani kabila lao halikua ni

la Quraysh bali lilikuani lenye asili ya Yemen, ila lilikua ni kabila linaloheshimika,

ambapo ndoa baina Lubaba Al Kubra na Abbas Ibn Abi Talib ilitoa watoto 7 ambao ni Al

Fadhl, Abdullah, Ubaydullah, Quthum, Mabad, Abdur-Rahman na Umm Habib.

Hivyo alisema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Madada Waumini ni Asma

na Salma na Watoto ni Lubaba na Maymuna mabinti wa Harith’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua na Rafiki yake wa karibu sana ambae

alikua akiitwa Abd Allah Ibn Abi Quhafa Ibn Uthman Ibn Amir Ibn Qaab Ibn Taymi Ibn

Murra ambapo anasema Al Hafidh Imam Ibn Asakir kua amesema Isa Ibn Yazi kua:

‘Amesema Abu Bakr As Siddiq kua: ‘Mimi nilikua nimekaa kwenye uwanja wa Al

Kaabah na pembeni yangu alikua amekaa Zayd Ibn Amr Ibn Nufayl, na mara

akapita Ummayah Ibn Abi Salt na akasema: ‘Hali zenu Enyi watafutaji Mema’


660

Nami nikasema: ‘Nzuri’ Ummayah akasema: ‘Jee mmekiona (mnachokitafuta?)’

Nami nikasema: ‘La’ nae akasema: ‘Kila Dini katika siku ya Malipo itaangamia

isipkua ile ambayo Allah ameshaikadiria, ama kuhusiana na Mtume huyo

anaesubiriwa basi jee atakua ni miongoni mwetu au ni miongoni mwenu?’

Abu Bakr anasema: ‘Mimi sikuwahi kusikia kuhusiana na Mtume anesubiriwa hapo

kabla hivyo nikatoka hadi kwa Waraqh Ibn Nawfa ambae alikua anapenda

kuangalia Mbinguni, na alikua ni mwenye kushangaza sana. Nikamuelezea

kuusiana na niliyoyasikia, nae akasema: ‘Naam ndie Ewe Mtoto wa Kaka yangu,

hakika sisi ni watu wa Ilm ya Kitabu, lakini Mtume anaesubiriwa atakua ni

miongoni mwa walio bora katika Waarabu kulingana na Kiukoo’

Nami nikasema : ‘Ami Jee Mtue huyo atakua nasema nini?’ nae akasema: ‘Atakua

naasema kile alichoambiwa seme, isipokua hatokua ni mwenye kuwadhulumu watu

na wala hatoduhlumiwa na wala hatowatafutia watu kudhulumuiwa’ Hivyo Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipotumwa basi mimi nikamkubali na

kumthibitisha’’

Hivyo Abu Bakr As Siddiq akawa ni Muislam wa pili Mtu Mzima mwanamme baada ya

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, ambapo katika kipindi cha mwanzoni Waislam

walikua wanasilimu kisiri siri hadi pale Allah Subhanh wa Ta’ala aliposhusha aya

isemayo:

‏﴿وَأَنذِرْ‏ عَشِ‏ يرَتَكَ‏ الأَْقْرَبِينَ﴾‏

Waandhir AAasheerataka al-aqrabeena (Surat Ash Shu’ara 26:214),

Tafsir: ‘Na wausie ndugu zako wa karibu’

Ambapo watu wa karibu wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika kipindi hiki

walikua ni wale ambao wako karibu nae kiukoo na kikabila yaani watu wa Al-Sha`b yaani

Banu `Adnan na Banu Qahtan, Al Qabeelah yaani Banu Rabi`ah na Banu Mudar, Al-

`Imarah yaani Banu Quraysh na Banu Kinanah, Al Batn yaani Banu `Abd Munaf, Banu

`Abd Makhzun, Al Fakhz yaani Banu Hashim, Banu Umayyah, na Al Faseelah Banu

`Abbas, Banu `Abd Al Muttalib, n,k.

Ambapo amesema Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wakati iliposhushwa

ayah hii (Surat Ash Shu’ara 26:214), basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akawakusanya Watu wake Nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha Jioni,

ambapo nao wakala na kunywa vizuri lakini hata hivyo chakula hicho na vinywaji

vilikua kama havijaguswa, na kasha akawaambia: ‘Enyi watu wa Abd Ul Muttalib


661

hakika mimi nimetumwa maalum kwa ajili yenu na kwa watu wengine, kama

mlivyosikia kwenye aya hii (Surat Ash Shu’ara 26:214), hivyo Jee mtakubaliana

nami ili muwe pamoja name Peponi?’

Na hakuna hata mtu mmoja aliesimama kwa ajili ya kukubaliana nae, hivyo mimi

nikasimama ingawa nilikua ndie mdogo kuliko wote, nae Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akawa ananiiambia: ‘Kaa chini’ hadi mara ya tatu akanishika

mkono’ (Musnad Imam Ahmad)

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Ababs Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam aliwaita watu wa Quraysh na wakaja wenyewe na baadhi

waliwatuma watu kusikiliza kuna nini, na miongoni mwao aliekuja alikuwemo Abu

Lahab, hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kwa kuwaambia:

‘Hivi jee mtasemaje kama nikikuambieni kua Nyuma ya Mlima kuna jeshi

linalokuja kukuvamieni? Mtaniamini ama la?’ Watu hao wakasema: ‘Naam

tutakuamini, kwa sababu sisi hatujawahi kusikia neno la uongo kutoka kwako’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Sasa wacheni nikuambieni kua

hakika Mimi ni Mtume wa Allah nilie mbele yenu nimetumwa kukuepusheni

kutokana Adhabu kali sana’ na hapo Abu Lahab akasema: ‘Uangamizo uwe juu

yako yaani umetuita sisi kwa ajili ya kutuambia Jambo hilo? ’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akashusha Surat Masad isemayo:

‏﴿بِ‏ سْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞تَب َّتْ‏ يَدَآ أَبىِ‏ لهََبٍ‏ وَتَب َّ آ ‏۞َم أَ‏ غْ‏ نىَٰ‏ عَنْهَُما ا لُهُوََم

كَسَبَ‏ ‏۞سَيَصْ‏ ٰ لَى َ راً‏ ذَاتَ‏ لهََبٍ‏ ‏۞وَٱمْ‏ رَأَتُهُ‏ حمَ َّالَةَ‏ ٱلحَْطَبِ‏ ۞ فىِ‏ جِ‏ يدِهَا حَبْلٌ‏ مِّن

م َّسَدٍ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Tabbat yada abee lahabin watabba; Ma aghna

AAanhu maluhu wama kasaba; Sayasla naran thata lahabin; Waimraatuhu

hammalata alhatabi; Fee jeediha hablun min masadin (Surat Masad 111:1-6)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehema Mwingi wa Huruma; Imeangamia

Mikono miwili ya Abu Lahab, na yeye mwenyewe; hawatomfaa kitu Watoto wake wala

Mali yake, Ataungua katika Moto Mkali sana, na Mke wake anaebeba Kuni; Shingoni

mwake kuna Kamba ya Kitanzi ya Masad.


662

Neno Lahab linatokana na neno Lahiba ambalo hua ni lenye kumaanisha Kua na Rangi

ya Wekundu wa Moto, Kuunguza kwa Moto, Kua na Hasira hadi Uso ukawa mwekundu,

na pia humaanisha Harufu ya Moto.

Hivyo ingawa Abu Lahab mwanzoni aliitwa Abu Lahab kwa sababu ya maumbile ya

muonekano wa Rangi ya ngozi yake ambayo ilikua ni nyeupe yenye wekundu wa damu

unaomaanisha kua ni mtu mwenye mwili wenye Afya na hivyo kua ni mzuri na wa

kuvutia kimaumbile, kutokana na kuonekana kua na damu nyingi Mwilini.

Lakini baada ya kushuka Surat Masad basi sifa yake nzuri hio ya muonekano wa kuvutia

wa Lahiba uliompatia jina la Abu Lahabi ukabadilika na kua ni muonekano wa Laana

Juu yake na hivyo kua Abu Lahabi kumaanisha Mtu mwenye Hasira kubwa sana alieingia

Motoni kwa Ujinga wake, Kibri na Hasira zake na hivyo kua ni Baba wa Moto.

Kwani kutokana na kua Nyumba ya Khadijah Bint Khuwaylid ilikua ni nyumba ambayo

ipo jirani na Nyuma ya Abu Lahabi, Hakam Ibn Al As. Uqbah Ibn Muait na Adi Ibn

Hamra ambao walikua ni miongoni mwa maadui wakubwa wa Uislam na kwa kua

walikua wakiishi jirani na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, basi walikua

wakimfanyia inda na maudhi makubwa sana kiasi ya kua walikua baadhi ya wakati

wakiona chakula kinapikwa ndani ya Nyumba ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

basi hukirushia uchafu chakula hicho, na baadhi ya wakati wakimuona Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam anasali basi humrushia Matumbo ya Mbuzi.

Ambapo kwa upande wa Arwa Bint Harb maarufu kama Ummu Jamil ambae ndie mke

wake Abu Lahab na pia ndie dada yake Abu Sufyan basi nae alikua akiamka usiku na

kisha hukusanya kuni zenye miba na kuziweka chini ya mlango wa nyumba ya Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam ili watu watakaotoka ndani yake wakanyage kisha

wapate maumivu makali sana.

Hivyo siku moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua amekaa na Abu Bakr As

Siddiq, hivyo Abu Bakr As Siddiq akamuona Arwa anakuja katika upande wao, na hivyo

aaksema kumwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Ya Rasul Allah Arwa

anakuja hakika mimi nnakhofu kua atakuona’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hakika Arwa hatoweza

kuniona mimi.’Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasoma aya isemayo:

‏﴿وَإِذَا قَرَأْتَ‏ ٱلْقُرآنَ‏ جَعَلْنَا بَيْنَكَ‏ وَبَينَْ‏ ٱل َّذِينَ‏ لاَ‏ يُؤْمِنُونَ‏ بِٱلآخِ‏ رَةِ‏ حِ‏ جَاابً‏ م َّسْتُوراً‏ ﴾


663

Wa-idha qara/ta alqur-ana jaAAalna baynaka wabayna alladheena la yu/minoona

bial-akhirati hijaban mastooran (Surat Al Israh 17:45)

Tafsir: Na unaposoma Qur’an (Ewe Muhammad) tunajaalia baina yako na baina ya

wale wasioamini juu ya Akhera pazia lisiloonekana lenye kustiri.

Hivyo Arwa Bint Harb akaja mpaka mbele ya Abu Bakr As Siddiq na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na kisha bila ya kua ni mwenye kumuona Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam basi akasema: ‘Ewe Abu Bakr! Hakika mimi

nimetaarifiwa kua Rafiki yako ametunga Mashairi ya kunilaani’ hivyo Abu Bakr

akasema: ‘La Naapa kwa Mungu wa Al Kaabah kua hajakulaani’ na hapo Arwa

akageuka na kusema: ‘Hakika Watu wa Quraysh wanajua kua mimi ni Binti wa

Kiongozi wao’

Hivyo baada ya tukio hili la kulaaniwa kwa Abu Lahabi na Ummu Jamil kutokana na

maneno na vitimbi vyao kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Allah Subhanah

wa Ta’ala kutokana na kua ni mwenye kujua kitakachofuatia baada yake kwa Waislam

basi akasema:

‏﴿وَٱخْفِضْ‏ جَنَاحَكَ‏ لِمَنِ‏ ٱت َّبَعَكَ‏ مِنَ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ۞فَإِنْ‏ عَصَوْكَ‏ فَقُلْ‏ إِنىّ‏ ِ بَرِي ۤ ءٌ‏ ممِّ َّا

تَعْمَلُونَ۞‏ وَتَوك َّلْ‏ عَلَى ٱلْعَزِيزِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ‏ ﴾

Waikhfidh janahaka limani ittabaAAaka mina almu/mineena; Fa-in AAasawka

faqul innee baree-on mimma taAAmaloona; Watawakkal AAala alAAazeezi

alrraheemi (Surat Ash Shu’ara 26:215-217)

Tafsir: Na washushie Bawa lako wale watakaokufuata miongoni mwa Waumini, na

kama wakiuasi basei sema: ‘Mimi sina makosa juu ya mnayoyafanya’ na kua na

utegemezi juu ya Mwenye mwingi wa uwezo na mwingi wa Rehma.

Ambapo aya imetumia maneno Waikhfidh janahaka yaani Washushie Bawa Lako

ambapo neno Janaha hua linamaanisha Kuinamia, Kuelemea, Kua karibu katika wakati

wa Usiku. Kwani neno Janaha ndio lililotoa neno Ajnihatun ambalo hua linamaanisha

Mbawa za Ndege, Mikono, Kwapa, Pande mbili za Kulia na kushoto za washambuliaji

iwe katika vita au katika Mpira, Wasaidizi na pia humaanisha Walinzi.

Hivyo maneno Waikhfidh janahaka hua yanamaanisha Kua Mkarimu nao, Kua na

Huruma nao, Kua na Unyenyekevu nao, Kua ni mwenye Kujali juu yao na kua na Upole

juu yao.


664

Mfano hai kimaana wa Aya ni mmithilisho wa namna Ndege anavyokua anayashushia

na kuyahifadhi Makinda yake ndani ya Mbawa zake na kuwaonesha Mapenzi Rehma na

Huruma Makinda wake hao na kuwahifadhi dhidi ya maadui zao wanaoweza kuyadhuru

Makinda hayo, na pia kuwahifadhi na mazingira ya hali ya hewa, kwa kua hawana nguvu

wala uwezo wa kuruka kutokana na udogo wao na kua, hawana manyoya mengi,n,k Kiasi

ya kua Ndege huyo yeye hua tayari kujitolea Muhanga kwa kuathirika na athari za nje

za kimaumbile kwa kupigwa na Jua, kunyeshewa na Mvua, kuangukiwa na Theluji, n,k

lakini kamwe hawachi kuyafunika makinda yake hayo kwa Mbawa zake ili yasidhurike

na Madhara hayo.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anamwambia Rasul Allh Salallahu Alayhi wa Salam

kuwaonea huruma wale watakaomuamini kwani bila ya shaka watakutwa na mitihani

baada ya kuachana na Imani yao ya zamani, na kwa wale watakaompinga basi

asiwalazimishe kwani yeye atakua hana makosa juu ya yale watakayoyafanya baada ya

kuwabainishia ukweli ulivyo.

Ama kuhusiana na Tawwakul basi anasema Jarrah Allah Imam Al Zamakhshari kua:

‘Tawakkul hua ni pale Mtu anapokabidhi mambo yake yote kwa yule ambae ni

mwenye uwezo wa kuyasimamia mambo hayo, iwe kwa njia ya kudhuru au

kunufaisha.’

Na pia Tawwakul hua ni :‘Pale mtu anapokua hashangazwi na matokeo ya jambo

wala hajaribu kujitetea kutokana na matokeo hayo kwa njia ambayo imekatazwa

na Allah Subhanah wa Ta’ala’

Kwani amesema Abd Al Wahid Al Dimashq kua: ‘Safari Moja nilimuona Abu Dardaa

Radhi Allahu Aanhu akitoa Darsa kwa watu ambao nao wakawa wanamuulliza

masuali, wakati hali hio inaendelea basi miongoni mwa watu wa familia yake

walikua wanazungumza mazungumzo ya kawaida katika upande wa pili wa

Msikiti’ hivyo nami nikasema kumwambia Abu Dardaa Radhi Allahu Aanhu: ‘Inakuaje

hadi ikawa kuna watu ambao wana ya kupata elimu kutoka kwake lakini watu

wako wa karibu hawajali na wanajishughulisha na mapambo ya kidunia?’

Abu Dardaa Radhi Allahu Aanhu akasema: ‘Hii ni kwa sababu Wacha Mungu

wanaoachana na Dunia ni Mitume, na hakuna watu wagumu dhidi yao kuliko wale

walio karibu yao zaidi’

Siku moja Abu Lahab alikutana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hivyo

akamuuliza: ‘Ewe Muhamamd hivi kama mimi nikikubaliana na Dini yako

nitanufaika na nini?’Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Utanufaika na

kile ambacho watanufaika nacho Waumini wengine’

Abu Lahab akauliza: ‘Hivi Jee hakuna upendeleo na utofauti kwa ajili yangu?’ Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kwani unataka nini zaidi?’Abu Lahab


665

akasema: ‘Natamani kua dini hii yako iangamie katika kile ambacho kitatupelekea

mimi na wengineo kua sawasawa katika kila kitu.’

Kabla ya Kupewa Utume, basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimuozesha

Mtoto wake wa kike aitwae Ruqqaya ambae alikua ni Mashaa Allah ni Mzuri sana,

Utbah Ibn Abu Lahab, na pia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimuozesha Mtoto

wake wa kike aitwae Umm Kulthoum kwa Utayibah Ibn Abu Lahab, hivyo baada ya

kushushwa Surat Masad basi Abu Lahab akawaambia watoto wake hao wa kiume kua:

‘Hakika mimi najizuia kuonana navyo hadi pale mtakapowaacha mabinti wa

Muhammad’

Na hivyo Utaibah alikua ni mwenye uadui mkubwa sana na Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam na Waislam kwa ujumla, kiasi ya kua siku moja Utaibah alikutana na Rasul

Allah Salallahu Aalayhi wa Salam: ‘Siwezi kukubaliana na An-najmi idha hawa na

Alladhi dana fatadalla’ na kisha akamtemea mate Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa

Salam.

Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akamwambia Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

‘Ya Allah, Mdhibitishe Utaibah kupitia kwa kwenye nguvu ya Mbwa miongoni

mwa Mbwa wako’

Ambapo Abu Labah aliposikia kuhusiana na apizo hilo basi akamwambia Utaibah:

‘Hakika mimi nna khofu juu ya Apizo hili La Muhammad Juu yako kua huenda

litakudhuru.’

Hivyo baada ya apizo hilo basi Utaibah Ibn Abu Lahab akafunga safari na Baba yake

kuelekea Syria, ambapo walipofika katika eneo la kupiga Kambi ambalo waliambiwa kua

hua kuna Simba wa Jangwani anaevamia wakati wa usiku, hivyo akapiga kambi na kisha

Abu Lahab akawaambia walinzi wa Msafara huo kua: ‘Hakikisheni kua Utaibah

anakua chini ya Ulinzi mkubwa sana kwani nnakhofia sana apizo la Muhammad

juu yake’

Hivyo siku hio Utaibah akawa chini ya ulinzi mkubwa sana wa kuzungukwa na watu na

Wanyama, lakini hata hivyo haukumsaidia kitu Ulinzi huo kwani Simba alipotokea Usiku

basi aliwaacha watu wote na Wanyama wote na kuenda moja kwa moja hadi kwa Utaibah

na kumrarua rarua hadi kumsababishia Kifo chake, ambapo kwa upande wa Utbah basi

yeye alisimu baada ya Kutekwa kwa Mji wa Makkah.

Ingawa kazi aliyopewa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ya kutangazia na

kuieneza Dini ya Kiislam ya Allah Subhanahu wa Ta’ala ilikua ni ngumu na nzito sana.

Kwani alipata matatizo, vikwazo na mitihani mingi sana hususan kutoka katika baadhi

ya viongozi wa kabila lake la Quraysh na baadae watu wa maeneo mengine pia, lakini

hakuvunjika moyo kutokana na iman aliyokua nayo, subra, ustahmilivu na ukarimu wake

aliendelea kuueneza ujumbe wa Uislam, na Allah Subhanahu wa Ta’ala alimsaidia na


666

kumuongoza, kama alivyobainishia Allah Subhanah wa Ta’ala kwenye Qur’an pale

alipomwambia Mtume wake Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam katika mwaka wa

nne wa Utume wake kua:

‏﴿فَٱصْ‏ دَعْ‏ بمَِا تُؤْ‏ مَرُ‏ وَأَعْرِضْ‏ عَنِ‏ ٱلْمُشْ‏ رِكِينَ‏ ‏۞إِ َّ كَفَيْنَاكَ‏ ٱلْمُسْتَهْزِ‏ ئِينَ۞ٱل َّذِينَ‏

يجَْعَلُونَ‏ مَعَ‏ ٱهلل َِّ‏ إِلٰهاً‏ آخَرَ‏ فَسَوْفَ‏ يَعْلَمُونَ۞وَلَقَدْ‏ نَعْلَمُ‏ أَن َّكَ‏ يَضِ‏ يقُ‏ صَدْ‏ رُكَ‏ بمَِا

يَقُولُونَ۞فَسَبِّحْ‏ بحَِمْدِ‏ رَبِّكَ‏ وَكُنْ‏ مِّنَ‏ ٱلس َّاجِ‏ دِينَ۞وَٱعْبُدْ‏ رَب َّكَ‏ حَ‏ تى َّ ٰ ‏َْتِيَكَ‏

ٱلْيَقِينُ‏ ﴾

FaisdaAA bima tu/maru waaAArid AAani almushrikeena; Inna kafaynaka

almustahzi-eena; Alladheena yajAAaloona maAAa Allahi ilahan akhara fasawfa

yaAAlamoona; Walaqad naAAlamu annaka yadeequ sadruka bima yaqooloona

Fasabbih bihamdi rabbika wakun mina alssajideena; WaoAAbud rabbaka hatta

ya/tiyaka alyaqeenu (Surat Al Hijr 15:94-99)

Tafsir: Hivyo Toa Dawa waziwazi Kama ulivyoamrishwa na wape mgongo

Washirikina; Kwani kwa Hakika tutakutosheleza sisi dhidi ya wanaokufanyia Vioja;

Wale ambao ni wenye kuwafanya pamoja na Allah Miungu myengine, watakuja kujua,

Kwani kwa hakika sisi tunajua kua Kifua chako kimekaza kutokana na

wanayoyasema; Hivyo Mtukuze Mola wako na kua miongoni mwa wanaosujudu; Na

muabudu Mola wako hadi utakapopata Yaqini.

Na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawausia watu hadharani kama anavyosema

Numan Ibn Bishr Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alipanda juu ya jukwaa na akaanza kutoa Khutba ambayo ilikua inasema:

‘Nakuonyeni Juu ya Moto! Nakuonyeni Juu ya Moto! Nakuonyeni Juu ya Moto!

Nakuonyeni Juu ya Moto!’ na aliendelea kuyasema maneno haya huku sauti yake

ikipanda juu na kupanda juu hadi kufikia hali ya kua watu waliokua Sokoni

walikua na uwezo wa kumsikia Muhamamd kutoka Msikitini’(Musnad Imam

Ahmad)

Anasema Imam Said Ibn Jubayr kua: ‘Miongoni mwa waliokua wakiongoza

kumfanyia Vioja Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam walikua ni Walid Ibn

Mughira, As Ibn Wail, Aswad Ibn Abd Yaghush, Aswad Ibn Abd Ul Muttalib na

Harith Ibn Qays ambao wote walifariki kabla ya vita vya Badr’


667

Ambapo anasema Imam Muhammad Ibn Ishaq kua: ‘Siku moja watu hawa walikua

wanatufu kwenye Al Kaabah, huku Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam akiwa

amesimama pembeni, na mara akashuka Malaika Jibril, na alipopita mbele yao

Aswad Ibn Abd Ul Muttalib basi Malaika Jibril akarembea Jani la kijani kwenye

Uso wake, na hapo hapo Macho ya Aswad yakapofuka, kisha akapita Aswad Ibn

Yaghush ambapo Malaika Jibril akamnyooshea Kidole na hapo hapo Tumbo lake

likaanza kuvimba na akafariki siku chache baadae kutokana na Kujaa kwa Tumbo

lake.’

‘Ambapo kwa upande wa Walid Ibn Mughira basi nae alipotokea Malaika Jibril

akamnyooshea kidole kwenye Jeraha lake ambalo alikua nalo hapo kabla kwenye

kisigino chake, na Jeraha hilo likatanuka nae akafariki kutokana nalo. Na

alipotokea As Ibn Wail basi Malaika Jibril akamuoneshea kwenye shimo la mgongo

wa Nyayo yake, nae akafariki kutokana na kuchomwa na mwiba kwenye mguu

wake huo wakati alipokua safarini kuelekea kwenye mji wa Tai’f, na Harith Ibn

Qays alipopita mbele yao basi Malaika Jibril akamuoneshea kwenye kichwa chake

nacho kikajaa Usaha ambao ndio uliomuua.’(Imam Muhammad Ibn Jarir At Tabari)

Ambapo anasema Rabia Ibn Abbad kua: ‘Hakika mimi nilipokua Mtoto mdogo

nilipokua nimefuatana na baba yangu katika Maonesho ya Dhul Majaz basi

nilimuona Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akiwaita watu kwa kusema: ‘Enyi

watu, Semeni Hakuna Mungu isipokua Allah na hivyo mtapata Uongovu’ huku

kukiwa na Mtu mmoja ambae alikua akimfuata nyuma yake na kuwaambia watu

kua: ‘Huyu Mtu ni Muongo, amepotoka yeye kutokana na kuachana na Imani ya

Mababu zake’ hivyo nami nikauliza: ‘Huyu wa nyuma ndio nani?’ na watu

wakasema: ‘Ni Ami yake aitwae Abu Lahab.’’(Musnad Imam Ahmad)

Anasema pia Tariq Ibn Abdullah Al Muharibi Kua : ‘Nilimuona kwenye Maonesho ya

Dhul Majaz kua Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam akiwa ni mwenye kusema:

‘Enyi watu semeni La Ilaha Illah, na mtakua ni wenye kufuzu.’ Na nyuma yake

kukiwa na mtu ambae alikua akimpopoa mawe hadi nyayo zake zinatoka damu, na

mtu huyo alikua akisema: ‘Msimsikilize, wani huyu ni Muongo’ nami nikawauliza

watu huyo ndie nani? Ambapo nao wakasema: ‘Ni Ami yake, Abu Lahab’(Imam

Tirmidhii)

Na katika mwaka huu wa 5 wa Utume wake Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam basi

alifikwa na msiba wa Mtoto wake wa kiume aliekua na umri wa miaka miwili ambae ni

Abdullah au maarufu pia kwa jina la Tahir Ibn Muhamamd na pia kama Tayyib Ibn

Muhammad, hivyo baada ya Abu Lahab kupata habari ya kifo hicho basi akakimbilia

kwa Viongozi wa Quraysh na kuwapa habari hio huku akiwa ni mwenye kufurahia na

kusema kua Muhammad hana tena kizazi.


668

Ambapo anasema Ikrimah kua: ‘Mara baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kuanza kuwaita watu katika Dini ya Uislam, basi watu wa Quraysh walikua

wakisema: ‘Muhammad amekatwa kutokana na watu wake kama vile Mti

ulivyokatwa kutokana na Mzizi wake, na hivyo kua ni wenye kuweza kuanguka

katika wakati wowote ule’: ’

Na Imam Muhammad Ibn Ishaq basi yeye anasema kua: ‘Kila wakati ilipokua Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipokua akitajwa mbele ya As Ibn Wail As Sehmi

ambae ni miongoni mwa Chifu wa Makkah basi alikua akisema: ‘Mwacheni, kwani

yeye hana Mtoto wa kiume wa kuendeleza kizazi, hivyo atakapofariki basi itakua

hakuna wa kumkumbuka’’

MAISHA YA DAR AL ARQAM NA HIJRA YA ABISINIYAH

Mnamo mwaka 615 yaani mwaka wa 5 wa Utume wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kutoka Makkah kuelekea katika Mji wa Madinah basi Waislam walikua

wakifanya Ibada zao katika Mji wa Makkah kwa Kisiri siri bila ya kujionesha na kutotaka

kuonekana. Kwa sababu ilikua ukionekana basi Makafiri huenda wakakuua. Hivyo katika

kipindi hicho basi Waislam walikua hawajioneshi.

Kama anavyosema Suhayb Ibn Sinan Ibn Malik Radhi Allahu Anhu ambae alikua ni

Sahaba mwenye kujulikana pia kama Suhayb Al Rumi kwa sababu alikua ni Sahaba

Mzungu mwenye nywele za Dhahabu, ambapo miaka 20 kabla ya Allah Subhanah wa

Ta'ala kumshuhia Utume Mtume wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam, basi mji

wa Basra ulikua na Gavana aitwae Sinan Ibn Malik ambae alikua na watoto kadhaa

ambapo mmoja miongoni mwao alikua ni wa Kiume aitwae Suhayb.

Mtoto Suhayb alikua na utofauti na Watoto wengine wote wa Gavana Sinan Ibn Malik

kwani ingawa Suhayb alikua na Umri wa miaka mitano lakini na baba yake ni mwenye

asili ya Kiarabu lakini yeye alikua ni mwenye weupe wa Kizungu na nywele zake pia

zilikua za rangi ya Dhahabu. Siku Moja familia ya Gavana Sinan Ibn Malik ilitoka nje ya

Mji wa Basra kwa ajili ya Mapumziko.

Ambapo kwa bahati mbaya au nzuri Mapumziko hayo yaligeuka na kua Jinamizi pale

kambi yao ilipovamiwa na kisha watu wote waliomo kwenye Kambi hio kukamatwa na

kupelekwa hadi Uturuki na kisha kuanza kuuzwa mmoja mmoja kama samaki. Ambapo

ndani yake alikuwemo pia Mtoto Suhayb, ambae nae hali yake ilibadilika ghafla baada


669

ya tukio hilo kujikuta akiwa ni Mtumwa wakati hapo kabla alikua ni Mtoto wa Gavana

anaeishi kama mtoto wa Mfalme.

Hivyo Suhayb Ibn Sinan alikua alitumia Utoto wake wote na ujana wake akiwa kama

Mtumwa kutoka Nyumba moja kuelekea Nyumba nyengine kutokana na Kuuzwa na

Kununuliwa mara kadha baina ya Nyumba za Matajiri wa Nchini Uturuki. Ambapo

katika kipindi hiki nchi ya Uturuki ilikua kikijulikana kama Konstantinopal na ilikua

ikitawaliwa na Utawala wa Roman Empire.

Ambapo kutokana na kua ni mwenye kuishi sana kama Mtumwa ndani ya Nyumba za

Wazungu, na kutokana na kuishi katika hali hio basi Suhayb Ibn Sinan akasahau hadi

Lugha yake ya Asili na hivyo akawa anazungumza Lugha ya Roman Empire na pia

kutokana na muonekano wake wa Kizungu basi Suhayb Ibn Sinan akawa moja kwa moja

ni Muzungu hivyo akawa anajulikana kama Suhayb Al Rumi.

Lakini hata hivyo Suhayb Ibn Sinan hakusasahau asili yake na yaliomtokea alipokua

mtoto mdogo hivyo siku moja aliamua kutafuta Njia ya Kutoroka kutoka kwa Wamiliki

wake na wakati alipokua na Msafara wa Watu wake katika ardhi ya Sham katika maeneo

ya Jerusalem na alipopata nafasi hio basi akatoroka na kufunga Safari ya Miezi miwili

kutoka katika Ardhi ya Sham na kukimbilia katika Ardhi ya Mji wa Makkah, kwani

alisikia kua ukifika katika Mji wa Makkah basi hata kama ukiwa Mtumwa ulietoroka basi

ndani yake ardhi hio unakua Mtu huria.

Hivyo Suhayb Ibn Sinan akakimbilia katika Mji wa Makkah kwa bahati nzuri Suhayb Al

Rumi alipofika katika Mji wa Makkah akakutana na Mfanyabiashara mmoja aitwae

Abdullah Ibn Juddan.

Na ingawa Suhayb Al Rumi alikua ni Mzungu mwenye Nywele Dhahabu na asiejua

Kiarabu vizuri kwani anazungumza Kirumi tu, lakini hapo hapo ni mwenye kujua mengi

sana kuhusiana na Biashara ya Warumi basi aliefahamiana vizuri sana na Abdullah Ibn

Juddan na hivyo wakashirikiana katika Biashara na haukuchukua mda mrefu katika

kuishi kwake Suhayb Al Rumi katika Mji wa Makkah isipokua Allah Subhanah wa

Ta'ala alimtilia Baraka katika Biashara zake hizo pamoja na Abdullah Ibn Judan na

hatimae. Suhayb Al Rumi akawa ni mwenye kujitegemea katika Biashara na akawa Tajiri

Mkubwa sana miongoni mwa Matajiri wa Mji wa Makkah.

Kwani Suhayb Al Rumi alikua na Misafara yake Mwenyewe ya Biashara kutoka Makkah

kuelekea Yemen na kutoka katika Mji wa Makkah kuelekea Syria. Ambapo safari moja

baada ya Msafara wake wa Biashara kurudi tu katika Mji wa Makka kutoka Sham basi

Suhayb Al Rumi akapata habari kua Muhammad Ibn Abdullah Salallahu Alayhi wa


670

Salam anatangazia watu kwa Siri kuhusiana na Dini mpya iitwayo Uislam, hivyo

akaulizia anapopatikana Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam na akaambiwa kua:

‘Anapatikana kwenye Nyumba ya Al Arqam Ibn Abi Al Arqam, lakini unatakiwa

uwe na tahadhari ili watu wa Quraysh wasikuone, kwani wakikuona na kujua kua

uko pamoja na Muhammad basi watakusababishia Madhara makubwa sana,

hususan kwa mtu kama wewe ambae ni mgeni aisekua na watu wa kumtetea na

kumlinda, kwani huna Ukoo wala Kabila katika Mji wa Makkah.’

Lakini hata hivyo onyo hili na tahadhari hio aliyopewa Suhayb Al Rumi halikumshtua

wala kumtia wasiwasi, bali aliondoka Moja kwa Moja hadi kwenye Nyumba ya Al

Arqam ambayo ilikua ikijulikana kama Dar Al Arqam.

Na anasema Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi nilikutana na Suhayb Ibn

Sinan katika mlango wa Al Arqam wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akiwa ndani yake, nami nikamuuliza: ‘Jee unataka nini?’ nae akaniuliza: ‘Na wewe

unataka nini?’ hivyo mimi nikajibu: ‘Nataka kuenda kwa Muhammad na

kumsikiliza anachokisema’ ambapo nae akasema: ‘Na mimi hivyo hivyo pia’ Hivyo

sote kwa pamoja tukaingia ndani ya Nyumba hio na Muhammad akatuelezea

kuhusiana na Uislam. Na tukakaa siku nzima hadi kilipoingia kiza ndio tukatoka

huku tukijficha.’

Hivyo ukweli ni kua hali ilifikia kiasi ya kua hadi Mtoto alikua akimficha Baba yake kua

yeye ni Muislam na Baba alikua akimficha Mtoto wake kua yeye ni Muislam. Mfano wa

hali hii tunaiona pale tunapoangalia katika mfano wa Nyumba ya mwanzo ambayo

Waislam walikua wakikutana kisiri na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa ajili

ya kufundishwa Dini ya Kiislam. Hii ilikua ni katika Nyumba ya Sahaba Mtoto aliekua

na Umri wa miaka 14 ambae alikua ni mwenye Nyumba alioirithi kwa Baba yake Abi

Arqam

Hivyo Mtoto huyu alikua akiitwa Arqam Ibn Abi Arqam Radhi Allahu Anhu, na Nyumba

yake ikawa inaitwa Dar Al Arqam. Hivyo katika Nyumba hii ya Arqam Radhi Allahu

Anhu Waislam walikua wakikutana kwa siri kila siku usiku. Ambapo Miongoni mwao

wanaokutana ndani ya Nyumba hio na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alikuwemo pia Sahaba Mtoto aitwae Imran Ibn Husein Radhi Allahu Anhu

Hivyo Usiku Mmoja wakati Masahaba wamo ndani ya Dar Al Arqam, mara mlango

ukagongwa Waislam wakatizamana na kuulizana ni nani agongae wakati wao

wameshatimia? Na hakuna anaejua siri ya Mkutano wao huo? Hivyo mmoja miongoni

mwa Masahaba akaenda Mlangoni na kuuliza kabla ya kufungua Mlango huo: ‘Jee ni

nani anaegonga Mlango?’


671

Sauti iliyojibu kutoka nje ikajibu: ‘Ni Mimi Husein Abu Imran’ Yaani alie Mlangoni

ni Mzee Husein ambae ni Baba yake Imran ambae yumo ndani ya Nyumba. Hivyo Sahaba

huyo akamuuliza Mzee Husein : ‘Una Shida gani?', na Mzee Husein akasema ‘Naomba

niruhusuni nataka kuingia Ndani’

Subhanah Allah! Hapo Hapo Masahaba kusikia Maombia hayo, basi Wakamficha kijana

Imran Chini ya Mapaja yao kwa kumkalia, kwani walikua wanajua kua Baba amekuja

Kumuua Mtoto wake. Kisha Baada ya kumkalia Imran Wakamfungulia Mlango Baba

Mtu yaani Mzee Husein. Na kisha akafunguliwa Mlango Mzee Husein ambae nae

alipoingia hakuuliza mtoto wake wala nini bali ailiuza : ‘Nilikua nnashida nae Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam, yuko wapi?’

Na alipoonyeshwa unajua alipofika mbele ya Rasul Allah Salallahu Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alifanyanya nini? Naam..Alimwambia Rasul Allah Salallahu Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua anataka kuingia katika Uislam, hivyo baada ya Imran

kusikia Sauti ya Baba yake ikitamka Shahada mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, basi Imran alitoka haraka chini miguu ya Masahaba na kumkimbilia Baba yake,

na kisha akamkumbatia kwa nguvu huku macho yake yakiwa yamejawa na Machozi ya

Mapenzi Imani ya Dini yake na Machozi ya mapenzi ya Baba yake yakimtiririka Kijana

Imran Ibn Husein Radhi Allahu Anhu

Kwani kijana Imran Radhi Allahu Anhu hakufikiria kua na Baba yake alikua na Imani

kama yake, na kuingia katika Uislam kama alivyoingia yeye hapo Kabla, ambapo tukio

hili la Imran Kulia kwa Mapenzi na Imani lilisababisha kila Muislam aliekuwemo ndani

Dar Al Arqam kua ni mwenye kulia na kutokwa na Machozi kwa Iman,Mapenzi,Furaha

na Umoja wa Waliokuwemo Ndani yake. Huo ni Mmoja kati ya Mifano ya hali ilivyokua

kabla ya Al Hijra.

Waislam walikua wanapendana kihisia kwa upande wa Kiimani na upande wa Kimapenzi

na kua na Umoja ndani ya Nyumba moja waliyokutana Ndani yake Majirani wenye Imani

ya Dini Moja ya Kiislam Kutoka ndani ya Mji mmoja. Hivi Jee hivi ndivyo tulivyo sisi

leo hii? Kua Waislam wa Nyumba Moja, wa Mji mmoja wa Nchi Moja tunapendana kwa

Umoja wa Kiimani na kihisia?

Hivyo hapa kila mmoja wetu anatakiwa ajue kua kama tutakua hatupendani na hatuna

Umoja na kila mmoja anafanya Ibada yake kivyake, na anaona fakhari na kujionesha

kwa kawatangulia wenzake, Wazee wake majirani zake tofauti na walivyokua Masahaba,

kwa kuchukulia mfano mmoja tu ambao ni wa Muandamo wa Mwezi basi hii

inamaanisha kua Ndani yetu Miongoni mwetu kuna Wanafiq ambao wana pia Unafiq wa

ndani ya Nafsi. Ambapo hata Wanafiq walioanzia Madinah baada ya kupatikana Uhuru

wa kuabudu basi walijifakharisha Kiibada.


672

Nyumba hii ya Dar Al Arqam ilikua ni nyumba yenye historia ya upekee katika Uislam

kwani ndani yake walisilimu Waislam wengi sana, ambapo Arqam mwenyewe aliusia

kizazi chake kua Nyumba hio isiuzwe, na ipo hadi hii leo na inajulikana kama Dar

Khayzuran na bado ina madrasa ndani yake.

Miongoni mwa Waislam waliopata mitihani ya Quraysh alikuwemo pia Ummu Ayman

na Zayd Ibn Harith walikua pia ni watu wa Mwanzo kupata mitihani ya Makuraysh dhidi

ya Uislam kutokana na kuamini Dini ya Kiislam na pia kutokana na kua ni wenye asili

ya Utumwa.

Safari Moja wakati Waislam walipokua wakikutana Usiku katika Nyumba ya Al Arqam

kufundishana Dini ya Kiislam, basi Makafiri walipogundua hilo wakaamua kuifunga njia

inayoelekea kwenye Nyumba hio na kuweka ulinzi ili Waislam wasikutane kwenye

Nyumba hio.

Lakini Hata hivyo kutokana na Bidii na ari na Imani waliyokua nayo basi Waislam

walitafuta kila njia mpaka wakawa wanaweza kukutana bila kujulikana. Hivyo siku hio

wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akiwa yupo kwenye Nyumba ya Al

Arqam basi Bi Khadijah akawa anataka kumpa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

Ujumbe muhimu sana ambae ulikua unatakiwa umfikie wakati huo huo na kipindi hicho

Simu ilikua hakuna.

Hivyo wakati Bi Khadija anatafakkari afanye nini basi Ummu Ayman akamwambia Bi

Khadija kua yeye yuko tayari kuhatarisha maisha yake hata akamatwe lakini ujumbe huo

ataufikisha kwa Mtoto wake yaani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Bi Khadija

akajaribu kumnasihi lakini Ummu Ayman akasema hamna tatizo atafikisha Ujumbe,

hivyo akapewa ujumbe huo na kutoka nao usiku akajificha jificha mpaka akafika kwenye

Nyumba ya Al Arqam

Na alipofika akagonga Mlango na kufunguliwa basi akampa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam ujumbe wake kutoka kwa Bi Khadija ambapo Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akatabasam kutokana na Ujasiri wa Umm Ayman na kusema:

‘Hakika Umebarikiwa Ya Ummi, kwani wewe ni Miongoni mwa watu ambao

wameshapata Nafasi zao katika Pepo ya Allah Subhana wa Ta'ala.’

Kisha baada ya Umm Ayman kuondoka basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akamalizia kwa kuwaambia Masahaba zake kua:: ‘Kama ikiwa kuna mtu miongoni

mwenu anataka kumuoa mwanamke wa Peponi basi na amuoe Ummu Ayman’

Kwani Ingawa Pepo ndio Pepo na ni kitu chenye Raha za Upekee za Milele zisizo na

Kifani chake, Ambapo Hujjat ul Islami Imam Abu Hamid Muhamamd Ibn Muhammad


673

Al Ghazali anasema kua Allah Subhanah wa Ta'ala ametujaalia Ibn Adam kutuonjesha

Mfano wa Ladha ya Raha ya Peponi ambayo kwa sekunde Kadhaa hapa Duniani.

Ambayo ni ile Ladha ya Raha inayopatikana katika Tendo la Kuingiliana Kimwili kwa

Mume na Mke na Utulivu wa Akili na Mwili unaopatikana baada yake Tendo hilo. Hivyo

Mfano huo wa Raha hio ya sekunde chache ya hapa Duniani ndio Unakaribiana na Raha

ya Milele inayopatikana Peponi.

Lakini hata hivyo hakuna hata Sahaba mmoja aliefumbua Mdomo wake na kumwambia

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua anataka kumuoa Umm Ayman. Na bila ya

shaka, hii inatokana na Maumbile na Maazingira ya asili ya Umm Ayman.

Kwani Kwanza Ummu Ayaman alikua tayari Mtu Mzima, fikiria kua Alikuja katika Mji

wa Makkah Kabla ya hata kufungwa ndoa ya Baba na Mama wa Rasul Allah Sallahu

Alayhi wa Salam na alipokuja alikua Mwari, akanunuliwa na Abdulla Ibn Abd Muttalib,

Abd Mutallib Akamuoa Mama yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, akazaliwa

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kisha akakaa nae Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam mpaka Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipotimia umri wa miaka 25

alipomuoa Bi Khadija Radhi Allahu Anha. Na akawa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam mpaka alipopata Utume yaani katika Mwaka 610 wakati Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akiwa na miaka 40.

Hivyo basi katika wakati huu ambao Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anawaambia

Masahaba zake wamuoe Ummy Ayman basi Ummu Ayman alikua tayari ana Umri wa

Miaka 50 na kitu. Sababu ya pili ni kua Asili ya Kua Ummu Ayman alikua Mwafrika

Mweusi, na Sababu ya tatu ni kua Ummu Ayman alikua ni mwenye asili ya kua ni

Mtumwa.

Kwani hayo yote tunapoyaangalia kwa wakati wa kipindi hicho ambacho ilikua kuna

Ubaguzi mkubwa wa Kikabila baina ya Kabila la Quraysh na Makabila mengine katika

Mji wa Makka kwa Kabila la Quraysh lilikua liko Juu kidarja. Na Ndio Maana Allah

Subhanah wa Ta'ala kwa Hikma zake akamjaalia Umm Ayman kua ingawa alikua si wa

Kabila la Quraysh na alikua Mtumwa alimjaalia kua na Darja kubwa ya kua Mama Mlezi

wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kua ni mwenye kumuita Umm Ayman Kwa jina la Ummi - Mama.

Kwa sababu tu ya kua ni Mfano bora wa kuvunja Mila na Desturi na Tabia za Watu hao

kuwadharau Wasiokua wa Kabila la Quraysh na kutowadharau Watumwa. Yaani Mfano

hai hapa wa kuwarekebisha watu basi unaanza moja kwa moja kwa Mtume wake.


674

Hivyo sifa hii ya kua ni Mama Mlezi wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

inatakiwa iwe inampasisha moja kwa moja Umm Ayman kua mwanamke Bora na

anaestahiki kuolewa na Masahaba bila kuangalia rangi yake au asili.

Vile vile kuna sifa ya pili bora aliyokua nayo Umm Ayman ambayo tayari Masahaba

wameshaekewa wazi na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam juu yake mbele yao kua

ni Mwanamke atakaeingia Peponi. Hii pia ni sababu ambayo inafuta kasoro zote za Awali

yaani Umri Mkubwa, Rangi na asili ya Utumwa.

Lakini hata hivyo kama tunavyoona kua Masahaba walikaa kimyaa na kisha baada ya

dakika kadhaa za Ukimya unaoweka wazi kua hakuna hata mmoja kati ya Masahaba

anaetaka kumuoa Umm Ayman Mwanamke alieingia Peponi hapa hapa Duniani basi

Zayd Ibn Harith akanyanyuka na kumwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kua:

‘Ya Rasul Allah! Hakika mimi nitamuoa Umm Ayman kwani kutokana na sifa zake

basi amewashinda hata Wanawake Vijana na wenye uzuri wa kuvutia’

Hivyo Zayd Ibn Harith Radhi Allahu Anhu akamuoa Ummu Ayamn, ambapo ndoa yao

hio ilibarikiwa na Allah Subhanah wa Ta'ala ambae aliwajaalia Zayd Ibn Harith na Umm

Ayman kupata mtoto wa kume aliepewa jina la Usamah.

Ambapo mtoto huyu alikua akipendwa Sana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na alikua akicheza nae na kumfanyia kila kitu kama vile anavuowafanyia Watoto wake.

Kwani mtoto huyo aliekulia katika mazingira bora chini ya Uangalizi wa M-bora wa

Viumbe, na hivyo alikua na sifa ya kua na ubora wa takriban kila kitu, mpaka katika

mbinu za Mapigano ya Vita pia.

Na ingawa hakumfikia Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu ambae mpaka leo hii rekodi

yake haijavunjwa katika fani hio ya Mapigano lakini, Hata hivyo Usamah Ibn Zayd Ibn

Harith Radhi Allahu Anhu alikua mpiganaji Mahiri kiasi ya kua aliongoza Jeshi la

Mapigano yake ya mwanzo dhidi ya Makafiri wakati akiwa na umri wa miaka 17 tu.

Usamah Ibn Harith alikua akijulikana kua kama Jenerali Kijana ambae ni Mtoto wa watu

wanaopendwa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam yaani Zayd Ibn Harith Radhi

Allahu Anhu na Umm Ayman Radhi Allahu Anha.

Na mambo yalipozidi kua magumu katika mwaka huu wa 5 wa Uislam basi Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akawaambia Masahaba zake kua wahamie Uhabeshi, kwani

ndani ya Ardhi hio kuna ‘An Najash’ yaani ‘Mfalme’ ambae anajulikana kwa jina la An

Najash Ashama Ibn Abjar ambae ni Muadilifu na hakuna anaepata madhara kutokana nae


675

kama wanavyoelezewa miongnoni mwa Ahl Al Kitab wenye sifa ya Uadilifu kama

tulivyoona hapo awali tulipozungumzia kisa cha Nabii Isa.

Kama tulivyosema kua Masahaba 10 Wanaume na Masahaba wa 4 Wanawake

wakahamia kisiri siri, ambao ni Sad Ibn Abi Waqqas, Jahsh Ibn Riyab, Abd Allah Ibn

Jahsh, Jafar Ibn Ab Talib, Uthman Ibin Affan na mkewe Ruqayyah Bint Rasul llah

Salallahu Alayhi wa Salam, Abu Hudhayfah Ibn Utbah na Mkewe Sahla Bint Suhayl

Zubayr Ibn Awwam, Musab Ibn Umair, Abd Rahman Ibn Awf, Abu Salama Abd Allah

Ibn Al Asad na mkewe Ummu Salamah Hind Bint Abi Umayyah, Uthman Ibn Mazun,

Amr Ibn Rabiah na Laylat Bint Asmah Radhi Allahu Anhum.

Masahaba hawa walisafiri kwa kutumia Jahazi kutoka katika mji wa Shuaiba na kufikia

katika mji wa Adulis, na ingawa leo hii hua liko katika ardhi ya maeneo ya Eritrea lakini

katika wakati huo eneo hilo lote lilikua linajulikana kama Abissiniyah yaani Ethiopia. Na

kisha baada ya hapo ukafuatia msafara wa Masahaba 83 ambao ni Wanaume na

Masahaba 18 ambao ni Wanawake wakahamia pia.

DAMU YA KWANZA YA MASHAHIDI WA KIISLAM.

Miongoni mwa watu walioathirika vibaya sana kutokana na adhabu na madhila ya

Makafiri ndani ya kipindi cha miaka mitano ya mwanzo ya Uislam basi ilikuwemo

familia ya Yasir Ibn Amar Ibn Malik Ibn Ansi ambae alikua ni mtu mwenye asili ya

Yemen aliehamia katika Mji wa Makkah baada ya kua ni mwenye kumtafuta Kaka yake

aliepotea na hivyo kufikia kwa Abu Hudhayfah Ibn Al Mughira Banu Makhzum, ambapo

baada ya mda Abu Hudhayfa akamuozesha Yasir Ibn Amar kwa Mtumwa wake aitwae

Summayah Bint Khabbat, ambae alikua ni Mwanamke mwenye asili ya Kiafrika hii ni

ndoa iliyotoa watoto watatu ambao ni Abd Allah Ibn Yasir, Harith Ibn Yasir na Ammar

Ibn Yasir ambae ni maarufu kama Abu Yaqzan aliezaliwa katika mwaka wa Tembo

ambao ni sawa na mwaka aliozaliwa Rasul Allah Salallahu alayhi wa Salam.

Na Abu Hudhayfah Ibn Al Mughira Banu Makhzum alipofariki basi watu wa Banu

Makhzum wakawa wanaoongoza katika kuwanyanyasa Waislam na kuwasababishia

Madhara, makubwa sana na walianza na familia ya mzee Yasir Ibn Amar kwa

kuwachukua na kuwapelekea katika sehemu ambayo ilikua na Majabali katika kipindi

cha mchana wa Jua kali sana, na kisha kuwabakisha na nguo nyepesi na kuwalaza juu ya

mawe hayo ya moto, huku wakiwaadhibu na kuwataka waikane Dini yao mpya.

Siku moja wakati Makafiri walipokua wanawatesa wanafamilia wa Yasir Ibn Amar basi

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akapita na akawaona namna wanavyoteswa huku

wakiwa wanalia hivyo akawaonea huruma sana, na kuwaambia: ‘Kuweni na Subra Enyi


676

familia ya Yasir, kuweni na Subra kwani Allah atakulipeni Pepo, hivyo kuweni na

Subra’

Hivyo Yasir Ibn Amar akamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Ya Rasul

Allah! Hivi jee yataisha lini madhila haya?’ hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala

akawaombe Dua kwa kusema: ‘Ewe Mola wangu, Usizuie Rehma na huruma juu ya

familia ya Yasir.’

Ambapo baada ya Dua hio basi Summayah Bint Khabbat Radhi Allahu Anha akapanda

Darja ya kua ni shahidi wa kwanza na kua Mwanamke ambae ni mwafrika na kua ni mtu

wa kwanza kufa shahidi kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala baada ya kuchomwa

Mkuki wa Tumbo na kupasuliwa pasuliwa tumbo lake kwa mkuki huo na Abu Jahal

ambae nie aliekua Chifu wa Banu Makhzum ambae alikua akisema kua: ‘Hakika

Umeingia kwenye hii Dini ya Muhammad kwa sababu ya uzuri wake wa

kimaumbile ewe Summayah eh?’

Lakini hata hivyo masuali hayo ya dhihaka na kuteswa kwake hayakumvunja Mopyo

Sumayyah Bint Khabbat Radhi Allahu Anha bali yalimzidishia Imani yake, na hivyo kua

ni miongoni mwa waliothibitisha kua wako tayari kujitolea muhanga kwa ajili ya Allah

Subhanah wa Ta’ala ambae ametuambia katika Qur’an kua:

‏﴿أَمْ‏ حَسِ‏ بْتُمْ‏ أَن تَدْخُلُواْ‏ ٱلجَْن َّةَ‏ وَلَم َّا ‏َْتِكُم م َّثَلُ‏ ٱل َّذِينَ‏ خَلَوْاْ‏ مِن قَبْلِكُم م َّس َّتْ‏ هُمُ‏

ٱلْبَأْسَآءُ‏ وَٱلض َّر َّآءُ‏ وَزُلْزِلُواْ‏ حَتى َّٰ‏ يَقُولَ‏ ٱلر َّسُولُ‏ وَٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ مَعَهُ‏ مَتىَٰ‏ نَصْ‏ رُ‏ ٱهلل َِّ‏ أَلا

إِن َّ نَصْرَ‏ ٱهلل َِّ‏ قَرِيبٌ‏ ﴾

ۤ

Am hasibtum an tadkhuloo aljannata walamma ya/tikum mathalu allatheena

khalaw min qablikum massat-humu alba/sao waaldhdharrao wazulziloo hatta

yaqoola alrrasoolu waalladheena amanoo maAAahu mata nasru Allahi ala inna

nasra Allahi qareebun (Surah Al-Baqarah 2:214)

Tafsir: Ama mnajihesabu kua mmtaingia Peponi na wala hamtopewa mithili ya

(Mitihani) wale ambao waliotangulia kabla yenu? Kwani wao walifikwa na Umasikini

na Madhara na mitikisiko hadi akasema Mtume na pamoja Waliomaini pamoja nae

kua: ‘Hivi Jee ikowapi Nusra yaAllah?’ Bila ya Shaka Nusra ya Allah iko Karibu.

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amesema kua: ‘Na kisha atakuja Mtu

miongoni mwa watu wa Duniani ambae alikua anaisha maisha ya Tabu sana


677

Duniani lakini ni miongoni mwa Watu wa Peponi, na ataingizwa mara moja Peponi

na ataambiwa Ewe Ibn Adam Hivi Jee uliwahi kua na Matatizo yeyote? Au

Mashaka uliwahi kua nayo?’ nae atasema: ‘Wallahi La! Ewe Mola wanguhakika

mimi sikuwahi kua na matatizo wala mashaka yeyote’(Sahih Muslim)

Hivyo hio ndio hali watakayokua nayo watu wa Peponi akiwemo Summaya Bint Khabbat

Radhi Allahu Anha ambae ni shahidi wa kwanza na pia atakayokua nayo mumewe

aliefuatia baada ya kufariki kwake na hivyo kua ni shahidi wa Pili katika Uislam ambae

ni Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu akafarikia Dunia na kupanda darja kwa kuupata

Ushahidi mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala kutokana na mateso hayo na hivyo Yasir

Ibn Amar Radhi Allahu Anhu kua ndio Mtu wa pili na ndie Mwanamme wa mwanzo

kuupata ushahid katika Uislam ambapo malipo yao ni kama zinavyosema aya:

‏﴿إِن َّ ٱهلل ََّ‏ ٱشْتَرَىٰ‏ مِ‏ نَ‏ ٱلْمُ‏ ؤْ‏ مِ‏ نِينَ‏ أَنفُسَ‏ هُ‏ مْ‏ وَأَمْ‏ وَالهَُمْ‏ أبَِن َّ لهَُمُ‏ ٱلجَّ‏ ن َّةَ‏ يُقَاتِلُونَ‏ فىِ‏ سَبِيلِ‏

ٱهلل َِّ‏ فَيَقْتُلُونَ‏ وَيُقْتَلُونَ‏ وَعْداً‏ عَلَيْهِ‏ حَقّاً‏ فىِ‏ ٱلت َّوْرَاةِ‏ وَٱلإِنجِْيلِ‏ وَٱلْقُرْآنِ‏ وَمَنْ‏ أَوْ‏ فىَٰ‏

بِعَهْدِهِ‏ مِنَ‏ ٱهلل َِّ‏ فَٱسْتَبْشِ‏ رُواْ‏ بِبَيْعِكُمُ‏ ٱل َّذِى ابَيَعْتُمْ‏ بِهِ‏ وَذٰ‏ لِ‏ كَ‏ هُ‏ وَ‏ ٱلْفَوْزُ‏ ٱلْعَظِيمُ‏ ﴾

Inna Allaha ishtara mina almu/mineena anfusahum waamwalahum bi-anna

lahumu aljannata yuqatiloona fee sabeeli Allahi fayaqtuloona wayuqtaloona

waAAdan AAalayhi haqqan fee alttawrati waal-injeeli waalqur-ani waman awfa

biAAahdihi mina Allahi faistabshiroo bibayAAikumu allathee bayaAAtum bihi

wadhalika huwa alfawzu alAAadheemu(Surat At Tawba 9:111)

Tafsir: Na kwa hakika Allah amenunua kutoka kwa Waumini Maisha yao na Mali zao,

kwa Bei ambayo kwao wao itakua ni Pepo. Kwani wanaigana kwa ajili ya Allah,

Wanaua na Kuuliwa. Na ahadi ya Allah ni ya Kweli katika Tawrat, katika Injil na

katika Qur’an, na jee ni yupi yule ambae ni mkweli kwa ahadi zake zaidi ya Allah?

Hivyo furahieni bei ambayo mmeshapatana nae, kwani huko ndiko Kufuzu kukubwa

zaidi.

Ambapo kwa upande wa Yasir Ibn Amar basi yeye alikua akilazimishwa kuvaa bangili

kubwa la chuma lenye kufuli mguuni mwake na kusimamishwa Juani hadi bangili hio

ikapata moto na kuanza kumuunguza mguu wake huo. Ambapo siku moja Amar Ibn

Yasir Radhi Allahu Anhu alipomuona Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam basi

akasema: ‘Ya Rasul Allah hakika sisi tayari tumeshateswa na kila aina ya mateso’


678

Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akasema: ‘Ewe Mola wangu Usimjaalie mtu

yeyote kutoka kwenye Familia ya Yasir kua ni mwenye kuingia Motoni.’

Na siku nyengine pia Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akasema: ‘Ewe Moto Kua

baridi na Salama kwa Ibrahim na pia kua hivyo kwa Amar’ na kisha akamwambia

Amar Ibn Yasi Radhi Allahu Anhu kwa kusema: ‘Ewe Amar! Hakika wewe hutokufa

kutokana na mateso haya bali utaishi kwa mda mrefu, na kifo chako kitatokana na

mikono ya watu wengi’

Hivyo mateso haya juu ya Amar Radhi Allahu Anhu yaliendelea hadi siku moja wakati

Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam alipomuona Amar Radhi Allahu Anhu akiwa

analia hivyo nae akatokwa na machozi na kisha akamwambia kwa kumuuliza: ‘Hivi jee

Makafiri wamekukamata na kukutumbukiza kwenye Maji tena? Hivyo mara

nyangine wakikukamanta na kusema kua useme wanayotaka useme na

wakaendelea kukutesa basi sema watakayokuambia ili wakuachie huru.’

Baada ya siku moja basi Amar Radhi Allahu Anhu akakamatwa tena na kuteswa sana na

akaambiwa kua: ‘Hakika sisi hatutokoma kukutesa hadi utakapomlaani Muhammad

na kusema kua unamuabudu Lata na Uzza na unawapenda zaidi kuliko Dini yake

Muhammad’ Hivyo ingawa Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu aligoma kwanza

kutamka maneno hayo lakini alipoendela kuteswa basi nae akayatamka maneno hayo, na

hivyo akaachiwa huru.

Baada ya kuachiwa huru basi Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu akaenda moja kwa

moja hadi kwa Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam na alipofika mbele yake, Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuuliza: ‘Naona kutokana na muonekano wa uso

wako kua umeachiwa huru’ Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Wa Allahi,

sijaachiwa huru.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akauliza: ‘Kwanini?’ Amar Ibn Yasir Radhi

Allahu Anhu akasema: ‘Kwa sababu nimelazimishwa kua nikane, wamenilazimisha

niseme kua Dini ya Lata na Uza ni bora zaidi ya Dini yako.’ Huku Amar Ibn Yasir

Radhi Allahu Anhu akiwa ni mwenye kujawa na huzuni kubwa sana na kuchanganyikiwa

kwani mbali ya kua ameokoka kutokana na Adhabu na mateso ya Makafiri lakini alikua

akijihisi kua kama kwamba ameangikiwa na Mlima mzima wa Uhud kwa sababu ya

kufikiria uzito wa Adhabu ya Mola wake na hali yake.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuuliza Amar Ibn Yasir Radhi Allahu

Anhu kwa kusema: ‘Hivi jee ulikuaje Moyo wako wakati uliposema maneno hayo’

Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Najiona kua Moyo wangu umetulia na

wenye uimara zaidi juu ya Imani yangu’


679

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamwambia Amar Ibn Yasir Radhi Allahu Anhu

kua: ‘Huna makosa juu yako ewe Amar, kwani hata kama wakikukamata tena na

kukutesa tena na wakataka urudie maneno hayo basi, rudia maneno hayo ili

wakuachie huru.’

Na hivyo baada ya maneno hayo ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi Allah

Subhanah wa Ta’ala akashusha Aya ifuatayo:

‏﴿مَن كَ‏ فَرَ‏ بِٱهلل َِّ‏ مِن بَعْدِ‏ إيمَانِهِ‏ إِلا َّ مَنْ‏ أُكْرِهَ‏ وَقَلْبُهُ‏ مُطْمَئِن ٌّ بِٱلإِيمَانِ‏ وَلَٰكِن م َّن

شَرَحَ‏ ابِلْكُفْرِ‏ صَدْراً‏ فَعَلَيْهِمْ‏ غَضَبٌ‏ مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَلهَُمْ‏ عَذَابٌ‏ عَظِيمٌ‏ ﴾

Man kafara biAllahi min baAAdi eemanihi illa man okriha waqalbuhu mutmainnun

bial-eemani walakin man sharaha bialkufri sadran faAAalayhim ghadhabun

mina Allahi walahum AAadhabun AAadheemun (Surat An Nahl 16:106)

Tafsir: Yeyote yule atakaekufuru baada ya kuikubali Imani yake Allah Subhanah wa

Ta’ala, isipokua yule ambae alielazimishwa huku Moyo wake ukiwa una utulivu wa

Kiimani, lakini kwa yule alieufungulia Moyo wake kwa Kufuru basi juu yao ni Adhabu

kutoka kwa Allah na watapata adhabu kali sana.

Na hivyo ikawa imeruhusika kwa Waumini ambao wameikubali Imani ya Dini ya

Kiislam ndani ya Moyo wao, kua watakapofikwa na mitihani ya kulazimishwa kuiasi

Imani yao hio la sivyo watadhuriwa au kuuliwa basi na waseme wanayotakiwa kukubali

kwa ndimi zao ilia wasidhuriwe.

Na kisha baada ya hapo basi Allah Subhanah wa Ta’ala akawashushia Waislam Surat Al

Buruj kwa ajili ya kuwatia Moyo zaidi kiimani ambayo inasema baada ya:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞وَٱلس َّمَآءِ‏ ذَاتِ‏ ٱلْبُرُوجِ‏ ‏۞وَٱلْيَوْمِ‏ ٱلْمَوْعُ‏ ودِ۞وَشَاهِدٍ‏

وَمَشْهُودٍ۞قُتِلَ‏ أَصْ‏ حَ‏ ابُ‏ ٱلأُخْ‏ دُ‏ ودِ۞ٱلن َّارِ‏ ذَاتِ‏ ٱلْوَقُودِ۞إِذْ‏ هُمْ‏ عَلَيْهَا قُعُودٌ۞وَهُ‏ ‏ْم

ٰ عَلَى مَا يَفْعَلُونَ‏ بِٱلْمُؤْمِنِينَ‏ شُهُودٌ۞وَمَا نَقَمُواْ‏ مِنْهُمْ‏ إِلا َّ أَن يُؤْمِنُواْ‏ بِٱهلل َِّ‏ ٱلْعَزِيِز

ٱلحَْمِيدِ۞‏ ٱل َّذِى لَهُ‏ مُلْكُ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَٱهلل َُّ‏ عَلَى ِ كُل شَيْءٍ‏ شَهِيدٌ۞‏ إِ‏ َّن

ّ


680

ٱل َّذِينَ‏ فَتَنُواْ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ وَٱلْمُؤْمِنَاتِ‏ ثمُ َّ لمَْ‏ يَتُوبُواْ‏ فَلَهُمْ‏ عَذَابُ‏ جَهَن َّمَ‏ وَلهَُمْ‏ عَذَا ‏ُب

ٱلحَْرِيقِ‏ ‏۞إِن َّ ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ وَعَمِلُواْ‏ ٱلص َّ الحَِاتِ‏ لهَُمْ‏ جَن َّاتٌ‏ تجَْرِى مِن تحَْتِهَا ٱلأَنْهَاُر

ذٰلِكَ‏ ٱلْفَوْزُ‏ ٱلْكَبِ‏ يرُ﴾‏

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Waalssama-i dhati alburooji; Waalyawmi

almawAAoodi; Washahidin wamashhoodin; Qutila as-habu alukhdoodi;

Alnnari thati alwaqoodi; Idh hum AAalayha quAAoodun; Wahum AAala ma

yafAAaloona bialmu/mineena shuhoodun; Wama naqamoo minhum illa an

yu/minoo biAllahi alAAazeezi alhameedi; Alladhee lahu mulku alssamawati waalardhi

waAllahu AAala kulli shay-in shaheedun; Inna alladheena fatanoo

almu/mineena waalmu/minati thumma lam yatooboo falahum AAadhabu

jahannama walahum AAadhabu alhareeqi; Inna alladheena amanoo waAAamiloo

alssalihati lahum jannatun tajree min tahtiha al-anharu dhalika alfawzu alkabeeru

(Surat Al Buruj 85:1-11)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma; Naapa kwa Mbingu

na Mapambo ya mkusanyiko wa Nyota zilizomo kwenye mwendo, Na siku

iliyoahidiwa; Na Mashahidi na Walioshudiwa; Walikatiliwa watu wa Shimoni;Na

Moto uliojazwa Kuni. Huku wao (Mashahidi) wakiwa wamekaa pembeni yake. Na

huku wakishuhudia wanayoyafanya dhidi ya Waumini. Hawakua na chochote dhidi

yao isipokua ni kua wenye kuamini Allah mwenye Utukufu na mwenye kustahiki sifa

zote; Ambae kwake kuna umiliki wa Mamlaka ya Mbinguni na Ardhini, na Allah ni

mwenye kuhudia kila kitu. Kwa hakika wale waliowafitinisha (kwa kuwapa Mtihani)

Waumini wa Kiume na Waumini wa Kike (kwa kuwachoma moto kwenye shimo hilo),

Kisha wakawa hawakutubu, basi ni juu yao Adhabu ya Jahannama, na ni adhabu ya

moto mkali sana. Hakika kwa wale walioamini na wakafanya Mema basi juu yao wao

ni Malipo ya Pepo yenye mabustani yenye ipitayo ndani yake. Na huko ni Kufuzu

kukubwa sana.

Na ingawa Imam Abu Muḥammad Al Ḥusayn Ibn Masʻud Ibn Muḥammad Al Farra Al

Baghawi anasema kua ‘Tukio la Watu wa As-hab ul Ukhdud lilitokea katika kipindi

cha Mfalme Nebuchardnezzer alipowatia kwenye shimo la Moto Mayahudi’

Na Imam Muḥammad Ibn Is-haq basi yeye anasema kua ‘Tukio la Watu wa As-hab ul

Ukhdud lilitokea katikaArdhi ya Yemen’

Lakini kwa upande wa Suhayb Ibn Sinan Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua: ‘

Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Hapo zamani kulikua na na


681

Mfalme ambae alikua na Mchawi wake, hivyo Mchawi huyo alipofikia umri wa

uzeeni basi, basi akamwambia Mfalme kua: ‘Hakika mimi nimeshakua Mzee, na

uhai wangu unakaribia mwisho wake, hivyo nitumie Mtoto mwenye kipaji ili

nimfundishe fani yangu’

Hivyo Mfalme huyo akamtafuta Mtoto husika mwenye Kipaji na akampeleka kwa

Mchawi wake ili apate kufundishwa fani hio, ambapo katikati ya masafa baina ya

njia kutoka kwa Mfalme kuelekea kwa Mchawi wake kulikua kuna Mcha Mungu

ambae alikua akiishi, na huyu Mtoto katika kuenda na kurudi kwake alikua akipita

kwa huyu Mcha Mungu, kwa sababu alikua akivutiwa sana na Maneno ya Mcha

Mungu huyo, na hivyo ilikua kila siku alikua akiadhibiwa na Mchawi wakati

anapofika kwake kwa sababu ya kuchelewa kwake baada ya kupitia kwa Mcha

Mungu huyo na pia hupigwa anaporudi nyumbani wakati anapochelewa kurudi.

Hivyo Mtoto huyo akamlalamikia Mcha Mungu huyo na kumwambia ambae nae

akamwambia kua akifika kwa Mchawi basi amwambie amechelewa kwa sababu

alizuiliwa na watu wake, na akichelewa Nyumbani basi awaambie kua amechelewa

kwa sababu ya Mchawi, ambapo hali hii iliendelea hadi pale siku moja wakati Mtoto

huyo alipokutana na mnyama mkubwa njiani, na hivyo akasema: ‘Hakika leo

nitajua ni njia ipi ndio njia ambayo ni sahih zaidi kuelekea kwa Allah baina ya Njia

ya Mchawi na Mcha Mungu.’

Akaokota jiwe na kisha akasema: ‘Ya Allah kama njia ya Mcha Mungu ndio Sahih

kwako wewe kuliko ya Mchawi basi Muue mnyama huyu kutokana na jiwe hili ili

watu waweze kupita katika njia hii’ Na kisha akalirusha Jiwe hilo kwa Mnyama

huyo na likamuua Mnyama huyo. Baadae akamwambia Mcha Mungu kuhusiana

na tukio hilo, ambae nae akamwambia: ‘Ewe Mtoto wangu hakika wewe umenizidi

mimi sasa hivi na hiyvo utaanza kupatwa na mitihani, lakini utakapopatwa na

Mitiani hiyo basi mimi usinitaje.’

Hivyo Mtoto huyo akwa anawatibu Vipofu, wenye ukoma na wenye Maradhi

tofauti, ambapo miongoni mwa alikuwepo Mtumishi wa Mfalme ambae alikua ni

Kipofu na alikuja na zawadi nyingi ili atibiwe huku akisema: ‘Nitibu na hizi zawadi

zote zitakua zako’ Hivyo Mtoto akasema: ‘Sio mie nnaetibu bali ni Allah Mtukufu

hivyo kama ukimuamini basi nitakuombea kwake na atakuponesha.’

Hivyo Mtu huyo akamuamini Allah na Mtoto akamuombea Dua na akapona. Kisha

Mtumishi huyo akaenda kwa Mfalme na kumuuliza ni nani aliemponyesha.

Mtumishi huyo akasema: ‘Ni Mungu wangu’ hivyo Mfalme akauliza:

‘Unamaanisha kua ni Mimi?’ Mtumishi huyo akasema: ‘La sio wewe’ Mfalme

akauliza: ‘Jee una Mungu zaidi yangu?’ Mtumishi akajibu: ‘Naam ni Mungu


682

wangu na Mungu wako.’ Hivyo Mfalme huyo akamuadhibu Mtumishi huyo hadi

akalitaja jina la Mtoto aliemponesha.

Na hivyo Mtoto huyo akafikishwa mbele ya Mfalme na akamuuliza: ‘Ewe Mtoto

inaonekana umeendela sana katika fani ya Uchawi, kiasi ya kua sasa hivi unaweza

kutibu Vipofu, wenye Ukoma na maradhi mengineyo.’

Mtoto akajibu: ‘Sio mie nnaetibu, bali nia Allah Subhanah wa Ta’ala ndie anaetibu.’

Mfalme akauliza: ‘Umanaanisha mimi?’ Mtoto akasema: ‘La’ Mfalme akasema:

‘Jee una Mungu mwengine zaidi yangu?’ Mtoto akasema: ‘Mungu wangu na wako

wewe ni Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Hivyo Mfalme akamuadhibu Mtoto huyu hadi akamtaja Mcha Mungu na

kuwapeleka anapoishi, na alipoletwa mbele ya Mfalme basi Mfalme akasema:

‘Kubali kua mimi ndie Mungu wako.’ Lakini Mcha Mungu akakataa.

Hivyo akachukuliwa Mcha Mungu huyo na kaunzwa kukawa na Msumeno katika

pande mbili tofauti, na kisha Mtumishi alietibiwa Upofu akaambiwa amkubali

Mfalme kua ndie Mungu wake lakini nae akakataa, nae akakatwa kwa Msumeno

katika pande mbili pia.

Na kisha Mtoto akatakiwa kumkana Allah Subhanah wa Ta’ala lakini nae akakataa,

hivyo Mfalme akaamua kumpa nafasi ya mwisho, akawakabidhi Askari wake

Mtoto huyo na kuwaambia kua wakamtupe kwenye Pembe ya Jabali kubwa la

Ardhi hio kama ataendela kukataa kukubali mfalme kua ndie Mungu wake. Hivyo

walipopanda Kwenye Jabali hilo basi Mtoto akaomba Dua kwa kusema: ‘Ya Allah

hakika wewe ni mwenye kunitosheleza mimi Juu ya hali yangu dhidi yao vyovyote

vile itakavyokua’

Hivyo Jabali likatetemeka na kuwangusha Askari hao nao wakafariki wote, hivyo

Mtoto huy akashua chini na kurudi kwa Mfalme, na Mfalme alipouliza imekuaje

wako wapi Askari wake basi Mtoto akasema kua: ‘Hakika Allah amenitosheleza

Dhidi yao.’. Mfalme akaamrisha kua Mtoto huyo akamatwe halafu apelekwe

Baharini na kama atamkataa Mfalme kua ni Mungu basi, atoswe Baharini. Na

walipofikia kwenye Maji mengi ya Bahari basi Mtoto huyo akasema: ‘Ya Allah

hakika wewe ni mwenye kunitosheleza mimi Juu ya hali yangu dhidi yao

itakavyokua’ na hapo hapo Jahazi ikazama na watu wote isipokua Mtoto huyo.

Ambae nae akarudi kwa Mfalme.

Mfalme akamuuliza kuhusiana na Askari wake, Mtoto huyo nae akasema: ‘Hakika

Allah amenitosheleza mimi Dhidi yao, na hutoweza kuniua mimi hadi pale


683

utakapofanya kama nitakavyosema’ Mfalme akauliza: ‘Nifanye Kitu gani?’ Mtoto

akasema: ‘Wakusanye watu wote kwenye eneo la Uwazi, na kisha utanifunga

kwenye Msalaba, na kuchukua Mshale kutoka kwenye upinde wangu. Na kisha

utanitunga shabaha huku ukisema: ‘Kwa Jina Allah ambae ndie Mungu wa Mtoto

huyo’ hivyo ukisema hivyo kisha uanipiga Upinde huo basi utafanikiwa kua ni

mwenye kuniua’

Hivyo Mfalme akafanya kama alivyoelekezwa na Mtoto huyo na kisha akachukua

Upinde, huo na kusema: ‘Kwa Jina la Allah ambae ndie Mungu wa Mtoto huyu.’

Na kisha akauachia Mshale huo ambao ulipiga Mtoto huyo kwenye Ndewe ya Sikio.

Mtoto huyo akauchuua mkono wake na kuigusa ndewe ya Siko lake na hapo hapo

akafariki Dunia.’

Na hapo hapo watu wakasema kwa sauti kubwa: ‘Hakika sisi tunamkubali Mungu

wa Mtoto huyu.’ Hivyo Mfalme akaambiwa: ‘Hivyi jee hivi sio yale ambayo wewe

ulikua ukiogopa kua yasitokee? Hivyo bila ya shaka umetumbukia kwenye Mtego

na watu wako wameingia kwenye Imani ya Allah.’

Hivyo Mfalme huyo akaamrisha kua lichimbwe Shimo katika kila Mtaa wa Mji huo

na kisha Uwashwe Moto ndani yake, na kisha akasema: ‘Waamrisheni watu

wachague, yeyote yule atakaeikana Dini Mpya basi atakua ameokoka na

watakaobakia basi wataingia kwenye mashimo ya Moto.’ Hivyo Waumini

wakajisalimisha bila ya kusita na kutumbukizwa ndani ya mashimo ya Moto, hadi

akabakia Mama na Mtoto wake mchanga aliekua akimnyonyesha ambae alisita

lakini Mtoto huyo akamwambia Mama yake: ‘Ewe Mama yangu kua na msimamo

thabiti kwani uko kwenye njia ya Haki.’’ Hivyo Mama na mtoto wake wakaingia ndani

yake Moto huo.

Amaa baada ya kuzungumzia hali hio kwa njia ya kuwakumbushia Waislam kuhusiana

na fitna iliyowakuta Waumini wa As-hab ul Ukhdud na kuwaonesha Waislam kua

wanatakiwa wawe na subra na ustahmilivu mkubwa kwani wenzao yaliwakuta machungu

zaidi ya wanayowakuta wao Waislam wa Makkah basi tunaona kua Allah Subhanah wa

Ta’ala anawaambia Waumini hao wapya kua, mbali ya kua watu hao waliwapa Mtihani

Waumini wa kuwachoma moto lakini hata hivyo basi kama wangetubu, baada ya tukio

hilo basi yeye alikua tayari kuwasamehe.

Ambapo anasema Hasan Al Basr kua: ‘Angalia Ukarimu wa Allah Subhanah wa

Ta’ala. Yaani watu hawa wamewachoma Moto watu wake, lakini yeye yuko tayari

kuwasamehe.’

Ambapo kwa upande wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr AD Din Al Razi basi yeye

amesema kua: ‘Kisa hiki cha Waumini hawa waliowachomwa moto hadi wakafariki


684

kinaonesha kua Waumini wanapofikwa na Mitihani basi wanatakiwa wawe na

misimamo mikali kua bora wake kuliko kuishi na kua Makafiri, lakini hata hivyo

maamuzi yako wazi, kwani inaruhusika pia kukubalia kukufuru kwa maneno kama

walivyokua alifanya Sahaba, pale alipoulizwa na Mussalima Al Kadhab kama

anamuamini yeye, ambapo nae akasema naam. Na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam alipojua kuhusiana na jambo hilo basi akasema: ‘Ama kwa yule alieachiwa

kutokana na kuchukua msimamo mwepesi basi hamna dhambi juu yake.’’

Ambapo kwa upande mwengine basi ni kama tulivyoona kwenye kisa cha Amar Ibn

Yasir na sababu ya kushuswa kwa aya tuliyoiangalia ya Surat An Nahl 16:106.

Hivyo watu waliowachoma As-hab Al Ukhdud kosa lao kubwa pia ni kua hawakua ni

wenye kutubu baada ya kufanya madhambi yao hayo ya kuwachoma Waumini, na bila

ya shaka adhabu yake na mkamato wake Allah Subhana hwa Ta’ala ni mkali sana lakini

hapo hapo pia yeye ni mwingi wa Huruma na Usamehevu wake ni Mkubwa sana kama

zinavyoendela kutuambia aya za Surat ul Buruj:

‏﴿إِن َّ بَطْشَ‏ رَبِّكَ‏ لَشَدِيدٌ۞إِن َّهُ‏ هُوَ‏ يُبْدِئُ‏ وَيُعِيدُ۞وَهُوَ‏ ٱلْغَفُورُ‏ ٱلْوَدُودُ۞ذُو ٱلْعَرْشِ‏

ٱلْمَجِ‏ يدُ‏ ﴾

Inna batsha rabbika lashadeedun; Innahu huwa yubdi-o wayuAAeedu; Wahuwa

alghafooru alwadoodu; Thoo alAAarshi almajeedi(Surat Al Buruj 85:12-15)

Tafsir: Hakika Mkamato wa Mola wako ni wenye nguvu na mkubwa sana; na kwa

hakika yeye ndie Muanzishaji na ndie Muendelezeshaji. Na ni yeye Mwenye Kusamehe

na mwenye kua na Mapenzi Makubwa sana yenye kudumu kwa Milele; Mmiliki wa

Arshi Tukufu.

Hivyo Surat Al Buruj ni Sura ambayo ni yenye kuwatia ari na Imani Waumini kwa ujumla

kuhusiana na umuhimu wa kua na ithibati katika Imani ndani ya Nyoyo zao, ambapo kwa

wakati huo iliposhuka basi iliwatia hamasa kubwa sana Waislam wa Dar Al Arqam, kiasi

ya kua siku moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua amekaa na Waislam

huku Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu akiwa mbele yake, huku wakiwa wamejawa

na hamu kubwa sana ya Kutangazia kuhusiana na Imani yao hiyo hadharani, hivyo

wakamuomba ruhusa Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam kufanya hivyo.

Miongoni mwa Walioteswa pia alikuwemo mwanamke aitwae Al Nahdiya Radhi Allahu

Anha ambae alidhibiw ana Mkafiri hadi akapoteza macho yake kutokana na Imani yake,

na pia kuna mwanamke mwengine aitwae Zimmira Radhi Allahu Anha amabae yeye


685

alikau ni Mtumwa pia. Kwa upande wa Wanaume kuna kina Bilal, Musab Ibn Umayr,

Talha Ibn Ubayd Allah Radhi Allah Anhum,n.k

Lakini hata hivyo Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam akawa na tahadhari bado na

hivyo akawaambia Masahaba zake kua: ‘Hakika sisi bado tuko kidogo, hatujafikia

wingi wa kubeba jukumu hili bado’ lakini hata hivyo Waislam wakatilia mkazo kua

wako tayari vyovyote itakavyokua, hivyo Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam

akatoka nao na wakaelekea kwenye Al Kaabah na walipofika wakakutana na Makafiri.

Na walipofika mbele yao basi Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu akanadia Allahu

Akbar! Na kuanza kuwalaani Lata na Uza, ambapo tukio hili likaanzisha matatizo

makubwa sana kwai zilitokea fujo na watu wakavamiana baina ya Waislamu na Makafiri

ambapo Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu alipigwa na hakuweza kuachiwa hadi

pale watu wa Kabila lake walipoamua kuingilia kati na baada ya kumalzika mashambulzi

hya basi Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu alikua ameanguka chini na kuzimia

akabebwa na kukepelekwa nyumbani kwake huku akiwa katika hali hio ya kuzimia

hakuzindukana hadi jioni yake siku hio.

Ambapo baada ya kuzindukana tu basi akauliza: ‘Vipi kuhusiana na Rasul Allah

Salallahu A’alayhi wa Salam? Mzima hawakumdhuru?’ Abu Bakr As Siddiq Radhi

Allahu Anhu akaletewa chakula na kuambiwa kua hajala siku nzima hivyo bora ale

kwanza, lakini hata hivyo akili yake ilikua si katika hali ya nafsi yake bali katika hali ya

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kuuliza tena: ‘Vipi kuhusiana na Rasul

Allah Salallahu A’alayhi wa Salam? Yuko wapi?’

Kisha Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu akamwambia Mama yake ambae alikua

hajasilimu bado na alikau akiitwa Salma Ummu al Khayr kwa kusema: ‘Nakuomba ewe

mama yangu nenda kamuulize Umm Jamil Bint Hattab na kisha nilete habari za

Muhammad kwangu mie’ Ummu Jamil Bint Hattab alikua ni miongni mwa

Waislam waliosilimu mwanzoni kisiri siri.

Hivyo Umm Khayr akatoka hadi kwa Umm Jamil Bint Hattab na kumwambia: ‘Abu

Bakr anakuulizia kuhusiana na hali ya Muhamamd Ibn Abdulla’ hivyo Umm Jamil

Bint Hattab kwa kua laikua anaogopa kua isije kua huo ni mtego basi akasema: ‘Sijui

kitu kuhusiana ane ila, wacha twende kwa Mtoto wako nikamuone anataka nini’

Kwa Umm Khayr na Umm Jamil wakatoka hadi Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu

na hapo hapo Umm Jamil Bint Hattab alipomuona Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu

Anhu na hali ya uso wake ulivyokua umechubuka sana basi akashindwa kujizuia na

akasema: ‘Namuomba Allah akulipize kisasi dhidi ya watu waliokufanyia hivi’ na

kisha akamwambia Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu kua Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam yuko salama.


686

Lakini hata hivyo maneno haya hayakumridhisha Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu

hivyo akamuomba Umm Jamil Bint Hattab na Mama yake wamcsaidie kumpeleka katika

Dar Al Arqam ili akaonane na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam uso kwa uso ili

ahakikishe kwa macho yake, hivyo Umm Khayr na Umm Jamil wakatoka huku wakiwa

wamegemewa nae na walipofika mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi

maerafiki hawa wawili wakakumbatiana kama vile watu waliokua wamepoteana kwa

mda mrefu na kisha Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu ndio akaridhika na kusema:

‘Mama yangu na Baba yangu watolewe Kafara kwa ajili yako Ya Rasul Allah, kwani

mimi nilihuzunika sana pale Utba Ibn Rabia aliponiburura na kuusugua uso wangu

kwenye ardhi na kuufanya kua usijulikane kua ni wangu, lakini vyenginevo mimi

niko mzima’ na kisha Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu akamtambulisha Mama

yake kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kusema: ‘Ya Rasul Allah huyu ni

Salma ni mama yangu, na nakuomba umuombee kwa ajili yake ili Allah Amuokoe

na Adhabu ya Moto.’ Na hivyo Salma Umm Khayr akaingia katika Dini ya Kiislam.

Ama kwa upande mwengine basi baada ya kuonesha Uadui wao dhidi ya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam basi viongozi wa Quraysh wakiwemo Abu Sufyan, Abu Jahl

na Al Akhnas Ibn-Shurayq, walikua kila siku kinapoingia usiku wa kiza basi mmoja

mmoja wakienda kwa Nyumbani kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na

kumsikiliza alivyokua akisoma Qur’an, hicyo Allah Subhanah wa Ta’ala akawajaalia kua

ni wenye kukutana walipokua wakitoka kusikiliza Qur’an, na kisha kukubaliana na

hawatoenda tena kusikiliza Qur’an lakini badala yake wakawa ni wenye kukutana tena

katika eneo hilo ilo kila siku katika usiku wake, hadi ilipotokea tukio hilo mara tatu

mfululizo basi wakakubaliana kua hawatoenda kumsikiliza Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam wakati akisoma Qur’an.

Na hii ni kwa sababu ya mpangilio wake Qur’an kwani ingawa ilishushwa aya moja moja

baada ya nyengine kwa kipindi cha miaka 23, lakini aya hizi zilizokua katika mpangilio

wa Tawqifi (Mpangilio alioupanga Allah Subhanah wa Ta’ala), hivyo Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam alikua akiambiwa aya fulani inakaa katika sehemu fulani

baina ya aya fulani na aya fulani hadi kukamilika kwa Sura 114, ambapo kati yake Sura

86 zimeshuka Makkah na zinajulikana kama Makki Surat na 28 zimeshuka Madinah

ambazo zinajulikana kama Madani Surat.

Na baada ya miaka 23, katika jioni ya siku ya Arafah mwezi 9 Dhul Hija ya mwaka wa

9 Al Hijr, siku ya Ijumaa ilishuka aya ya mwisho ya Qur’an isemayo:


687

‏﴿وَٱخْشَوْنِ‏ ٱلْيَوْمَ‏ أَكْمَلْتُ‏ لَكُمْ‏ دِينَكُمْ‏ وَأَتمَْمْتُ‏ عَلَيْكُمْ‏ نِعْمَتىِ‏ وَرَضِيتُ‏ لَكُمُ‏

﴾ ٱلأِسْلاَمَ‏ دِيناً‏

Alyawma akmaltu lakum deenakum waatmamtu AAalaykum niAAmatee

waradeetu lakumu al-islama deenan (Surat Al Imran 3:5)

Tafsir: Leo hii nimeikamilisha kwa ajili yenu Dini yenu, Nimekamilisha Neema yangu

juu yenu, na nimekuchagulieni Uislam kua ndio Dini yenu.

Katika kuweka wazi umuhimu wa ujumbe aliokua akipewa Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam, ambao aliamrishwa kuwatangazia watu wengine ujumbe huo, basi

tunaona kua Allah Subhanahu wa Ta’ala anamsifu Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam kwa kumfananisha na Nuru na Muangaza pale alipowaambia Ahlu al Kitab

kwa kusema katika Qur’an:

﴿َ أَهْلَ‏ ٱلْكِتَابِ‏ قَدْ‏ جَآءَكُمْ‏ رَسُولُنَا يُبَينِّ‏ ُ لَكُمْ‏ كَثِيراً‏ ممِّ َّا كُنْتُمْ‏ تخُْفُونَ‏ مِنَ‏

ٱلْكِتَابِ‏ وَيَعْفُواْ‏ عَن كَثِيرٍ‏ قَ‏ دْ‏ جَآءَكُمْ‏ مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏ نُورٌ‏ وَكِتَابٌ‏ م ُّبِينٌ‏ ۞ يَهْدِى بِهِ‏ ٱهلل َُّ‏

مَنِ‏ ٱت َّبَعَ‏ رِضْوَانَهُ‏ سُبُلَ‏ ٱلس َّلاَمِ‏ وَيخُْرِجُهُمْ‏ مِّنَ‏ ٱلظ ُّلُمَاتِ‏ إِلىَ‏ ٱلن ُّورِ‏ إبِِذْنِهِ‏ وَيَهْدِيهِ‏ ‏ْم

إِلىَٰ‏ صِرَاطٍ‏ م ُّسْتَقِيمٍ‏ ﴾

Ya ahla alkitabi qad jaakum rasooluna yubayyinu lakum katheeran mimma

kuntum tukhfoona mina alkitabi wayaAAfoo AAan katheerin qad jaakum mina

Allahi noorun wakitabun mubeenun; Yahdee bihi Allahu mani ittabaAAa

ridhwanahu subula alssalami wayukhrijuhum mina aldhdhulumati ila alnnoori biidhnihi

wayahdeehim ila siratin mustaqeemin (Surat Al Maidah 5:15-16)

Tafsir: Enyi Ahl Al Kitab! Sasa hivi amekujieni Mtume wetu kukuwekeeni wazi yale

mengi ambayo mlikua mkiyaficha katika vitabu na mengi yaliyopita. Hakika

imekujieni kutoka kwa Allah Nuru na Kitabu kilichowazi. Ambacho ndani yake Allah

anawaongoza wote wale wanaotafuta ridhaa yake kuelekea katika njia ya salama, na

akawatoa kutoka katika kiza cha Dhulma kwa ruhusa yake na kuwaingiza katika

Muangaza na kuwaongoza katika njia iliyonyoooka.


688

Na vile vile Allah Subhanahu wa Ta’ala anamwambia na kumsifu Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam kwa kumfananisha na Taa na Muangaza pale alipomwambia

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na pia wale Walioamini kwa kusema

katika Qur’an:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱلن َّبىِ‏ ُّ إِ َّ أَرْسَلْنَاكَ‏ شَاهِداً‏ وَمُبَشِّ‏ راً‏ وَنَذِيراً‏ ۞ وَدَاعِياً‏ إِ‏ لىَ‏ ٱهلل َِّ‏ إبِِذْنِهِ‏ وَسِ‏ رَاجاً‏

﴾ م ُّنِيراً‏

Ya ayyuha alnnabiyyu inna arsalnaka shahidan wamubashshiran wanadheeran;

WadaAAiyan ila Allahi bi-idhnihi wasirajan muneeran. (Surat Al Ahzab :33:45-46)

Tafsir: Ewe Nabii (Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam)! Hakika sisi

tumekutuma wewe kama shahidi, na vile vile mbebaji wa habari njema, na mwenye

kuonya. Na kua ni yule anaewaita watu kumuelekea Allah kwa idhini yake, na Taa

inayoeneza Nuru.

Ingawa Allah Subhanahu wa Ta’ala amempa sifa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam kua ni Nuru, Taa na Muangaza kwa Ummah kutoka kwake lakini pia ameweka

wazi kua Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ni mtu vile vile kama walivyo

watu wengine pale aliposema katika Qur’an.

‏﴿قُلْ‏ إِنم ََّآ أََْ‏ بَشَرٌ‏ مِّثْلُكُمْ‏ ٰ يُوحَى إِلىَ َّ أَنم ََّآ إِلَٰهُكُمْ‏ إِلَٰهٌ‏ وَاحِ‏ دٌ‏ ۤ فَٱسْتَقِيمُواْ‏ إِلَيِْه

وَٱسْتَغْفِرُوهُ‏ وَوَيْلٌ‏ لِّلْمُشْ‏ رِكِينَ‏ ﴾

Qul innama ana basharun mithlukum yooha ilayya annama ilahukum ilahun

wahidun faistaqeemoo ilayhi waistaghfiroohu wawaylun lilmushrikeena (Surat

Fusilat 41:6)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad): ‘Mimi ni Mtu kama nyinyi, Nimeteremshiwa Wahy

kua Mungu wenu ni Mungu mmoja, hivyo fuateni njia iliyonyooka kuelekea kwake na

mumtii na kumuomba masamaha. Na Ole wao kwa wale wenye kumshirikisha’ .

Ama kuhusiana na na muonekano wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam basi

anasema Rabi'ah Ibn Abi 'Abd al-Rahmaan: ‘Nimemsikia Anas Ibn Malik akimuelezea

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kwa kusema: ‘Alikua si mrefu wala


689

si mfupi, ngozi yake ilikua nyeupe inayokaribiana na wekundu kwa mbali, kwani

ilikua si nyeupe sana wala si ya kiza, na nywele zake hazikukunjana sana wala

hazikunyooka sana, aliposhushiwa Wahy alikua na umri wa miaka 40, alikaa

Makkah kwa miaka 10 baada ya kuanza kushushwa Wahy, na kisha akakaa

Madinah kwa miaka 10. Alipofariki ilikua hamna zaidi ya mvi 20 kwenye nywele

zake na ndevu zake.’ (Bukhari).

Imam Ahmad Ibn Hanbal anasema kua amesema `Ata' Ibn Yasar kua alikutana na `Abd

Allah Ibn`Amr Ibn Al`As, ambae alimwambia: ‘Hebu nielezee kuhusiana na Rasul

Allah katika Taurat’, nae akasema: ‘Naam, Wa Allahi, ameelezewa katika Taurat

akiwa na sifa ambazo alizoelezewa katika Qur’an, yaani : ‘Ewe Mtume, Hakika

sisi tumekutuma wewe kama shahidi, na mwenye habari njema, na muokozi wa

wasiokua na I’lm. Wewe ni Mjumbe wangu na Mtume wangu na nimekuita Al

Mutawakkil (mwenye kutegemewa). Wewe si mkali sana wala si mwenye kupiga

kelele masokoni. Huwalipi wabaya kwa wakufanyiao ubaya, na badala yake ni

msamehevu. Allah hatoichukua roho yako hadi utakapo warekebisha wale

waliopotea waweze kusema La ilaha illa Allah, maneno ambayo hufunua macho ya

vipofu, masikio ya viziwi na nyoyo zilizozibwa’’

KUSILIMU KWA UMAR IBN AL KHATTAB RADHI ALLAHU ANHU

Mnamo Mwaka wa 5 wa Uislam ndani ya Mwezi wa Ramadhani Allah Subhanah wa

Ta’ala alimshushia Mtume wake Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam Surat An Najm

ambayo ni Sura ya mwanzo ya Quran kushushwa ndani yake katika aya ya Mwisho kuna

Sijda.

Ambapo anasema Imam Ahmad Ibn Hanbal kua: ‘Amesema Muttalib Ibn Abi Wadaa

kua Wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipoisoma Surat An Najm mbele

ya Hadhara basi alipofika mwisho wake Akasjudu na mhadhara wote ukasjudu.

Lakini mimi sikusjudu, hivyo sasa kila nikiisoma Sura hii hua nahakikisha kua

siwachi kitendo hicho cha Kusjudu.’

Kwani anasema Imam Muhammad Ibn Saad kua: ‘Kabla ya Kushuka Sura hii basi

kuna Kikundi cha Waislam kilihamia Uhabeshi. Hivyo Ramadhani ya Mwaka wa 5

ilipowadia na kutokea tukio hili la Kusjudu hadhara nzima ya watu wa Quraysh

pamoja na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Basi Waislam wa Uhabeshi

wakasikia juu tukio hili, na hivyo wakaona kua Mji mzima wa Makkah

Umeshasilimu, kutokana na kusjudu kwao huko, na hivyo baadhi ya Waislam

wakaamua kurudi katika Mji wa Makkah, lakini walipofika walikuta kua hali ya

Kunyanyaswa Waislam bado iko pale pale. Hivyo baada ya kurudi kwao na kukuta


690

kua Mji wa Makkah haukaliki basi wakarudi tena Uhabeshi na safari hii

wakuondoka kuelekea Uhabeshi na watu wengi zaid’

Ambapo Neno Najm hua linatokana na neno Najama ambalo hua linamaanisha

Kuchomoza, Kutokea, Kuanza, Muendeleo wa kuendela kwa Kitu. Ambapo neno Najm

hua linamaanisha Majani yanayotambaa na pia humaanisha Nyota. Hivyo anasema Allah

Subhanah wa Ta'ala katika Surat An Najm:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞وَٱلن َّجْ‏ مِ‏ إِذَا هَ‏ وَىٰ‏ ‏۞مَا ضَل َّ صَاحِ‏ بُكُمْ‏ وَمَ‏ ا غَوَىٰ‏ ‏۞وَمَا

يَنطِقُ‏ عَنِ‏ ٱلهَْوَىٰ‏ ‏۞إِنْ‏ هُوَ‏ إِلا َّ وَحْ‏ يٌ‏ يُوحَ‏ ى ٰ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Waalnnajmi idha hawa;

Ma dhalla sahibukum wama ghawa; Wama yantiqu AAani alhawa; In huwa illa

wahyun yooha(Surat An Najm 53:1-4)

Tafsir: Kwa Jina La Allah Mwingi wa Rehma na Mwingi wa Huruma; Naapa Kwa

Najm pale inapozama; Hajapotoka Rafiki yenu (Muhammad Salallahu Alayhi wa

Salam) Wala Hajakosea; Na Wala Hasemi Kutokana na Matamanio (Ya Nafsi) yake;

Hakika hayo (maneno ayasemayo) si chochote Isipokua ni Wahyi anaoshushiwa.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakkalimin Imam Al Mushaqqiqin

Imam Al Ghazali Al Thani Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Umar Ibn Husayn Al

Razi Al Shafii kuhusiana na Kiapo hiki cha Aya hii kua: ‘Allah Suhana wa Ta’ala

anaapa kwa Nyota kwa sababu baadhi ya Mapagani walikua wanaabudu Nyota

zenye Kung’ara sana Angani. Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala anabainisha Kasoro

ya Nyota hizo kua ni zenye kutoweka baada mda, na hivyo haziwezi kua ni Miungu,

bali ni kitu kilichoumbwa.’

Ambapo Wanazuoni wametofautiana kuhusiana na Nyota hii iliyoapiwa hapa, kwani

kuna wasemao kua ni Surrayah (Sirius) ambayo ni Nyota inayoonekana Alfajiri na kisha

huzama kabla ya Kuchomoza Jua. Ambapo huu ni mtizamo wa Bahr Ul Ilm Abd Allah

Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na pia Imam Sufyan Ath Thawry. Na pia kuna waosema

kua Ni Nyota ya Zuhra (Venus) ambao ni Mtizamo wa Imam Abd Rahman Al Suddi.

Kwani kwa upande mwengine basi unapotafakkar maana ya Aya hii kwa juu bila kuingia

ndani basi tunaona pia inatuonesha Umuhimu wa Kutafakkar pale unapoangalia Miujiza

ya Allah Subhanah wa T'aala katika kuumba kwake.


691

Kisha Allah Subhanah wa Ta'ala anawaambia Watu wa Makkah kwa Huyu Mtu

anaezungumziwa Ndani ya Aya hii yaani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, ni mtu

ambae ni Sahibu yao, yaani Rafiki yao anaeishi nao pamoja katika Mji na Mtaa Mmoja,

hivyo anajulikama ndani nje kua si Mtu wa kubabaisha, bali ni Mtu anaeaminika, na

hivyo hayuko Dhala wala Ghawa.

Ambapo neno Dhala hua Linamaanisha Mtu aliepotoka kutokana na kutoona Njia Sahihi,

na neno Ghawa hua linamaanisha Mtu aliepotoka Mbali ya kua ameiona Njia Sahih yaani

Aliifuata kisha akaachana nayo.

Hivyo hapa Allah Subhanah wa Ta'ala anabainisha kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam yuko katika Nji Iliyonyooka Sawia ya Kumuelekea Mola wake ambayo inastahiki

kufuatwa na kila Mmoja wetu.

Kisha Allah Subhanah wa Ta'ala anawabainishia wazi Makafiri wa Makkah kua Rafiki

yao huyo yaani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hazungumzi yale anayoyasema

kutokana na Matamanio yake Labda kwa kua anataka Madaraka, au Mali au Cheo n.k.

Na kwa kua ni Alieshusha Qur'an ni Allah Subhanah wa Ta'ala na ni mwenye kujua juu

ya kila kitu basi Allah Subhanah wa Ta'ala anajua kua kama hajafafanua baada ya aya

hio basi watu watakua na masuali mengi, yaani kama Rasul Allah Salalahu Alayhi wa

Salam hazungumzi kwa Matamanio yake, basi maneno yake ayasemayo yanatokana na

nini?

Naam yaani Mbali ya Aya za Qur'an lakini kila kitu akisemacho Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam hua si kitu chochote kile isipokua ni Wahyi alioshushiwa na Allah

Subhanah wa Ta'ala kupitia kwa Malaika Jibril na kupitia kwa njia ya kushushiwa Moja

kwa moja kwenye Ufaham wake.

Ambapo kutokana na uthibitisho wa maneno hayo basi tunaona kua hata anayoyaomba

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa Mola wake hua yanakua ambapo amesema

Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu alayhi wa Salam

alisema kua: ‘Ya Allah Uongeze Nguvu Uislam kwa kupitia mmoja kati ya watu

wawili unaowapenda zaidi, Abu Jahl au Umar Ibn Al Khattab’ Abd Allah Ibn Umar

Radhi Allahu Anhu anaendelea kusema kua: ‘Aliekua akipendwa zaidi ni Umar’(Imam

At Tirmidhii)’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliomba dua hii kwa sababu watu wawili hawa

walikua ndio wanaadhibu sana Waislamna wenye chuki kubwa sana dhidi ya Uislam,

kiasi ya kua Umar Ibn Al Khattab siku moja ya mwaka mmoja baada ya kushushwa Surat

An Najm basi Umar Ibn Al Khattab alikua tayari ameshachoka na namna Uislam

unavyovunja umoja wa watu wa Makkah na kusababisha uasi kwa Viungozi wa Mji wa


692

Makkah, hivyo akaamua kua amalize tatizo hili, kwa kuukata mzizi wa fitina yote hii

inayoendelea, ambao ni Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam.

Umar Ibn Al Khattab alikua ni kijana mwenye misimamo na wenye kujiamini kwa kila

kitu miongoni mwa Vijana wa Quraysh kama vila alivyokua kijana mwenzake alifanana

nae kwa kila kitu kuanzia sura hadi maumbile ya miili yao ambae ni Khalid Ibn Walid

lakini Umar Ibn Al Khattab alikua ni mwenye kumzidi Khalid Ibn Walid kwa urefu wa

Inchi moja. Ambapo vijana hawa mbali ya kua ni waliofanana sura lakini pia ni ndugu

na wenye kufanana kwa nguvu na Ubabe wao ambao unaonekana wazi pale mwaka

mmoja walipokutana katika fainali ya kumtafuta Bingwa wa kupigana katika Mji wa

Makkah.

Ambapo katika fainali ya mwaka mmoja ya vijana wasiozidi umri wa miaka 20 waliingia

na kukutana vijana wawili ambao mmoja kati yao alikua ni Khalid Ibn Walid na

mwengine alikua ni Umar Ibn Al Khattab, ambapo Umar Ibn Al Khattab alikua na uwezo

wa kutumia mikono yote miwili wa kulia na kushoto kwa nguvu zilizo sawa, tofauti na

Khalid Ibn Walid ambae alikua hana sifa hiyo

Kutokana na kufahamu uwezo zaid aliokua nao Umar Ibn Al Khattab, basi Khalid Ibn

Walid ilimbidi atumie mbinu na ujuzi wa kiakili zaid ili kumshinda mpinzani wake huyo.

Na hapo haikuchukua muda kwani Khalid Ibn Walid alimkamata mpinzani wake na kisha

ghafla akamuangusha chini. Kwa mbali ikasikika sauti ya kuvunjika kwa mfupa. Khalid

Ibn Walid alimuangalia kwa huruma Umar Ibn Al Khattab ambae alikua amelala chini

huku akilia kwa maumivu. Matokeo ya mapigano haya yalibadilisha mtizamo mzima wa

historia ya maisha ya Masahaba wawili hawa wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam na hivyo kuzidisha upinzani baina yao, Masahaba hawa walikua na udugu wa

karibu sana. Kwani mama yake Sayyidna Umar Ibn Al Khattab ambae alikua anaitwa

Hantam Bint Hisham Al Mughira alikua ni binamu yake mkubwa Khalid Ibn Walid Al

Mughira.

Ambapo Khalid Ibn Walid alikua na marafiki wengi wa karibu na ambao majina yao

ukiyaangalia katika historia ya Kiislam utaona kua yote yalikua yanatajika kwa sifa za

kua na uwezo wa kuongoza katika mapigano ya aina zote, miongoni mwao alikuwemo

Umar Ibn Al Khattab, Ikrimah Ibn Abi Hisham na Amr Ibn Al Aas. Kati ya marafiki

hawa wanne, basi hakuna yule ambae ilikua inamuuma sana kuhusiana na matukio

yanayotokea katika Mji wa Makkah tangu kushuka kwa Uislam kama Umar Ibn Al

Khattab.

Hivyo siku moja Umar Ibn Al Khattab akachukua Upanga wake na kutoka nyumbani

kwake huku akiwa ni mwenye kuamua kumtafuta Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

popote pale alipo ili amuue na hakua ni mwenye kuelekea katika maeneo ya Dar Ul


693

Arqam kwa sababu alikua hajui kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam yuko sehemu

gani, na maana baada ya kusilimu kwake aliuliza Waislam: ‘Jee Muhamamd

anapatikana wapi?’

Hivyo katika kumtafuta kwake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam njiani akakutana

na Nuaym Ibn Abd Allah Radhi Allah Anhu ambae nae alikua ni miongoni mwa Waislam

waliosilimu kisiri siri na alipomuona Umar Ibn Al Khattab yuko katika hali aliyokua nayo

basi akamuuliza: ‘Ya Umar unaenda wapi ukiwa katika kama hio?’ ambapo Umar

Ibn Al Khattab akasema: ‘Naenda kumtafuta Muhammad, ili nimuue kwani

amewachana na Dini yetu, amevunja umoja wa watu wetu na kuidhalilisha Miungu

yetu, hivyo nataka nimalizane nae ili hili tatizo liishe’

Nuaym Ibn Abd Allah Radhi Allah Anhu akasema: ‘Ama kweli Hasira zako

zimekupofua Macho kwani umekua huoni. Hivyo kwanini usiishughulikie familia

yako kwanza kabla ya kutaka kumalizana na Muhammad?’

Suali hili lilimshtua Umar Ibn Al Khattab, na kujiuliza kwani kuna nini kwenye familia

yangu? Hivyo hapo ahpo akamuuliza Nuaym Ibn Abd Allah Radhi Allah Anhu: ‘Kwani

kuna nini kwenye familia yangu?’ ambapo Nuaym Ibn Abd Allah Radhi Allah Anhu

akasema: ‘Mume wa Dada yako na Ibn Ami yako Said Ibn Zayd na Dada yako

Fatma, kwani wameingia kwenye Dini ya Muhammad na wamekubaliana nayo

hivyo kawashughulikie wao kwanza.’

Ambapo baada ya kupata habari hio basi safari ya kumtafuta Rasul Allah

Salallahu Aalyhi wa Salam ilikufa hapo hapo, na badala yae umar Ibn Al Khattab

akageuza muelekeo na kuelekea katika nyumba ya dada yake huku akiwa amejawa

na hasira zaidi, na haukuchukua mda Umar Ibn Al Khattab akawasili kwa dada

yake na kusikia katika wakati huo sauti ya Khabbab Radhi Allah Anhu

akiwasomea Said Ibn Zayd na Fatma Bint Al Khattab Radhi Allahu Anhum aya za

mwanzoni za Surat Ta-Ha.

Hivyo Umar akanyatia na kusikiliza lakini hasikii vizuri, hivyo akaharikisha

kutaka kuingia ndani ya Nyumba hio kugonga mlango hukua akitaka afunguliwa

na waliokuwemo ndani ya Nyumba ya Fatma Binti Al Khattab Radhi Allahu Anhu

waliposikia sauti ya Umar Ibn Al Kahattab basi wakataharuki na Khabbab Radhi

Allahu Anhu akakimbilia haraka sana kujificha kwenye chumba cha pembeni,

huku akimuwacha Fatma akiwa ameshikilia maandiko ya Surat Ta-Ha na

kuyaficha chini ya Mapaja yake.

Hivyo Said Ibn Zayd Radhi Allahu Anhu akaenda Mlangoni, na alipoufungua

Umar Ibn Al Khattab akauingia moja kwa moja hadi ndani na kuanza kuuliza kwa


694

ukali na hasira: ‘Kuna ujinga gani ambao nimekua nikiusikia humu ndani

mkinong’onezana?’

Ambapo Fatma na Said Ibn Zayd Radhi Allahu Anhum wakasema: ‘Hatuja

nong’onezana kitu, kwani wewe umesikia nini?’

Umar Ibn Al Khattab akasema: ‘Naam, nimegundua kua nyinyi nyote mmeingia

kwenye Kundi la Muhamamd.’ Na kisha baada ya Maneno hayo akamvamia Said

Ibn Zady Radhi Allahu Anhu na kuanza kupgana nae, katika purukushani hizo

Fatma Bint Al Khattab Radhi Allahu Anha ambae mwanzo alikua amekaa kitako

akanyanyuka na kukimbilia kuingilia kati kwa ajili ya kumtetea na kumuokoa

Mumewe, lakini alipokaribia purukushani hizo basi Umar Ibn Al Khattab

akampiga kibao kimoja na hapo hapo Fatma Bint Al Khattab Radhi Allahu Anha

akaanguka chini huku akitokwa na damu baada ya kujeruhiwa na kibao hicho.

Hapo hapo Said Ibn Zaid Radhi Allahu Anhu akamuangalia Fatma Bint Al Khattab

Radhi Allahu Anha aliyekuwepo chini akitokwa na Damu kisha wote wawili kwa

pamoja wakasema: ‘Naam tumejiunga na Dini ya Muhammad, na

tunamuamini Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume wake, hivyo wewe fanya

utakalofanya’

Umar Ibn Al Khattab hakuamini masikio yake kutokana na kusikia umoja wa kauli

hio, na kushangazwa na ujasiri wa Dada yake, hivyo akajiuliza kwani huu ujumbe

wa Muhamamd una maajabu gani hasa mpaka Fatma Bint Al Khattab Radhi

Allahu Anha anakua na msimamo kiasi hicho kutokana nao, hivyo akamuacha

Said Ibn Zayd Radhi Allahu Anhu na kumuangalia Dada yake ambae aliekua

anasimama huku akiwa anajipangusa Damu ambayo kuonekana kwake na macho

ya Umar Ibn Al Khattab kulimfanya Umar aingiwe na huruma na kujisikia aibu

kutokana na kumjeruhi Dada yake ambae nae alikua ni mwenye kua na ari na

msimamo juu ya Imani yake hio mpya, hivyo Umar Ibn Al Khattab akasema kwa

sauti tofauti na aliyoingia nayo hapo mwanzo, kwani hii ilikua ni sauti ya huruma

na upole: ‘Tafadhalini nionesheni nami njiue huu ujumbe wa Muhammad

unasemaje’

Fatma Bint Al Khattab Radhi Allahu Anha akasema : ‘La, kwani mimi nna khofu

juu ya kile utakachokifanya ukiuona’ Umar Ibn Al Khattab akasema: ‘Usiwe

na Khofu kwani sitouchana’hivyo Fatma Bint Al Khattab Radhi Allahu Anha

akasema: ‘Ewe Kaka yangu hakika wewe huko tohara kutoka na ushirikina

wako, kwani ni wale walio tohara tu ndio wanaoruhusika kugusa maandiko

ya ujumbe huu’


695

Hivyo Umar Ibn Al Khattab akatoka na akaenda kukoga na kisha alipokua msafi

akarudi kisha Fatma Bint Al Khattab Radhi Allahu Anha akampa maandiko hayo,

na mara baada ya kupewa basi akasoma maneno hayo ambayo yanasema:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞طه۞مَآ أَنَزَلْنَا عَلَيْكَ‏ ٱلْقُرْآنَ‏ لِتَشْقَى ٰ ۞ إِ‏ لا َّ تَذْكِرَةً‏ لِّمَن

يخَْشَى ٰ ۞ تَنزِيلاً‏ ممِّ َّنْ‏ خَلَق ٱلأَرْضَ‏ وَٱلس َّمَاوَاتِ‏ ٱلْعُلَى۞‏ ٱلر َّحمَْٰنُ‏ عَ‏ لَى ٱلْعَرْشِ‏

ٱسْتَوَى ٰ ۞ لَهُ‏ مَا فىِ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَمَا فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ وَمَا بَيْنَهُمَا وَمَا تحَْتَ‏ ٱلث َّرَىٰ‏ ۞

وَإِن تجَْهَرْ‏ بِٱلْقَوْلِ‏ فَإِن َّهُ‏ يَعْلَمُ‏ ٱلسِّ‏ ر َّ وَأَخْفَى۞‏ ٱهلل َُّ‏ لا ۤ إِلَٰهَ‏ إِلا َّ هُوَ‏ لَهُ‏ ٱلأَسمَْآءُ‏

ٱلحُْسْنىَٰ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Ta-Ha; Ma anzalna AAalayka alqur-ana

litashqa; Illa tadhkiratan liman yakhsha; Tanzeelan mimman khalaqa al-ardha

waalssamawati alAAula; Alrrahmanu AAala alAAarshi istawa; Lahu ma fee

alssamawati wama fee al-Ardhi wama baynahuma wama tahta alththara; Wa-in

tajhar bialqawli fa-innahu yaAAlamu alssirra waakhfa; Allahu la ilaha illa huwa

lahu al-asmao alhusna.(Surat Ta-Ha 20:1-8)

Tafsir: Kwa Jina La Allah Mwingi wa Rehma na Mwingi wa Huruma; Ta-Ha, Kwa

Hakika hatukuiteremsha hii Qur’an kwa ajili ya kukuingiza katika Khofu, Ila huu ni

ukumbusho kwa wenye kua na khofu. Imeteremshwa kutoka kwa Muumba wa Ardhi

na Mbingu alietukuka. Mwingi wa Rehma kwenye ya Arshi amesimama. Ni vyake

vilivyomo Mbinguni na Ardhini na baina yake na vilivyomo chini ya udongo wake. Na

hata kama wewe (Muhammad) utanyanyua sauti yako basi kwa hakika yeye, anajua

yaliyo ya siri na yale ambayo yamefichikana zaid. Hakuna Mungu isipokua yeye. Na

kwake yeye ndio kwenye umiliki wa Majina Bora.

Na baada ya kusoma aya hizi basi Umar Ibn Al Khattab akasema: ‘Sijawahi

kuona maneno ya heshima na Utukufu kama haya.’ Ambapo baada ya kusikia

maneno hayo ya Umar basi Khabbab akatoka kutoka kwenye sehemu aliyojifichia

na kusema: ‘Ya Umar! Nna matumaini kua Allah atakuneemesha wewe

kutokana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa sababu mimi

nilimsikia jana usiku Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akisema kua:

‘Ya Allah uimarishe Uislamkwa Abu Al Hakam au kwa Umar Ibn Al Khattab,

hivyo Umar Muogope Mola wako’’


696

Umar Ibn Al Khattab akamuomba Khabbab amuelekeze katika sehemu ambayo

anapatikana Rasul Allah Salallah Alayhi wa Salam ambapo nae akamfahamisha

ilipo Dar Al Arqam, hivyo Umar Ibn A Khattab akatoka na upanga wake kwenye

Nyumba ya Fatma bint Al Khattab Radhi Allahu Anha na moja kwa moja kuelekea

kwenye Dar Al Arqam na kugonga mlango wa Nyumba hio.

Ambapo mmoja kati ya Waislam alipoenda kutaka kufungua Mlango basi

alichungulia kwenye ufa wa Mlango huo na akamuona Umar Ibn Al Khattab akiwa

amesimama nje na upanga wake, hivyo akarudi haraka sana hadi kwa Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na kumwambia kua anaegonga Mlango ni Umar Ibn

Al Khattab huku akiwa na Upanga wake.

Ambapo Hamza Ibn Abu Talib Radhi Allahu Anhu akaingilia kati na kusema:

‘Mwache aingie ndani, kwani kama amekuja kwa nia safi basi hamna tatizo

lakini kama ikiwa amekuja kwa mbaya basi tutamuua kwa kutumia huo huo

upanga wake Mwenyewe’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akawaambia Masahaba zake kwa kusema kua: ‘Mfungulieni Mlango aingie’

hivyo Mlango ukafunguliwa na Umar Ibn Al Khattab akaingia ndani ya Nyumba

hio.

Wakati Umar Ibn Al Khattab anaingia ndani basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam akanyanyuka na kumfuata huku akilifunga joho lake vizuri na kisha

akampokea Umar Ibn Al Khattab kwa kusema: ‘Umekuja kufanya nini ewe Ibn

Al Khattab? Wallahi mimi nnaona kua kama kuna mkosi unataka kukufika

kabla ya kumaliza uliyoyafuata’

Ambapo Umar Ibn Al Khattab nae akasema kwa unyenyekevu: ‘Wa Allahi, Ya

Rasul Allah hakika mimi nimekuja kwa ajili ya Kuthibitisha Imani yangu

kwa Allah na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kile kilichoteremshwa

kutoka kwa Allah.’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akatamka ‘Takbir!!’ hivyo

Waislam wote waliomo ndani ya Dar Al Arqam wakajawa na furaha kwani Uislam

ulikua umepata Nguvu zaidi kutokana na kusilimu kwa Umar Ibn Al Khattab

Radhi Allahu Anhu ambae baadae alitangazia imani yake hio hadharani, na

kusema kua anaetaka kupigana nae kwa sababu ya Imani yake mpya basi na

amfuate.

KIFO CHA ABU TALIB NA KHADIJA BINT KHUWAYLID RADHI

ALLAHU ANHA


697

Amesema Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mara moja Ka’ab

Ibn Ashraf ambae ni Chifu wa Mayahudi wa Mji wa Madinah alikuja katika Mji

wa Makkah na Machifu wa Quraysh wakamwambia: ‘Muangalie Kijana huyu,

ambae ni Abtar (amekatwa kutokana na kendelea kizazi chake), anajifikiria kua

yuko juu zaidi yetu wakati sisi ni wasimamizi wa Ibada ya Hija tunasimamia Al

Kaabah na Kuwapa maji ya kunywa Mahujaji’’(Imam Al Bazaar)

Na akasema tena Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mtoto

Mkubwa wa Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam ni Qasim, kisha anafuatia

Zaynab, kisha Abd Allah, kisha wanafuatia mabinti watatu ambao ni Umm

Kulthoum, Fatma na Ruqqaya, wa mwanzo wao ambae ni Qasim alifariki na kisha

akafariki Abd Allah. Ambapo baada ya tukio hilo basi As Wail akasema: ‘Kizazi

chake kimekatika sasa hivi yuko Abtar’’

Hivyo tangu mwanzoni mwa kipindi cha kuanza kutangazia kuhusiana na Utume wake

na kueneza Ujumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala hadharani kwa watu wake basi Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akikabiliana na upinzani mkubwa sana wa

vitendo na maneno huku wafuasi wake wakiwa ni wenye kunyanyaswa na kudhulumiwa

hadharani, hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia Mtume wake Surat Al Kawthar

ambayo inasema:

ّ ٱلْكَوْثَرَ۞فَصَل لِرَبِّ‏ كََوٱ نحَْرْ‏ ‏۞إِن َّ شَانِئَكَ‏

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞إِ َّ أَعْطَيْنَاكَ‏ ِ

هُوَ‏ ٱلأَبْتَرُ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Inna aAAtaynaka alkawthara; Fasalli

lirabbika wainhar; Inna shani-aka huwa al-abtaru (Surat Al Kawthar 108:1-4)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma; Hakika sisi

tumekupa wewe (Muhammad Sallahu Alayhi wa Salam)Al Kawthar; Hivyo mgeukie

Mola wako kwa Kusali na Uchinje (kwa ajili yake pekee); Kwani kwa Hakika

anaekuchukia (Wewe Muhammad Sallahu Alayhi wa Salam) basi yeye atakatiwa

(kutokana na kila kitu cha Kheri cha Duniani na Akhera).

Hii Sura inatiwa Surat Al Kawthar, ambalo ni neno Kathara ambalo hua linamaanisha

Kuzidi idadi ya wingi wa kitu, Kuongezeka, Kua na wingi wa Mali au wa vitu

anavyovitaka na kuvitamani Mtu.


698

Hivyo kwa upande mmoja Allah Subhanah wa Ta’ala anamwambia Mtume wake Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Ingawa watu wako wanasema kua wewe

umekatiwa muendelezo wako na hivyo wanakuona kua huna kitu, lakini Mimi

nnakupa wewe Kila Kitu ambacho unachokitaka na kukitamani wewe hapa

Duniani na Akhera. Unachotakiwa kufanya wewe ni kuniabudu mimi na kufanya

kila kitu kwa ajili yangu, na kisha hao wanaokuchukia basi bila ya shaka ndio

nitakaowakatia kutokana na kupata kila kitu chema hapa Duniani na Akhera.’

Ambapo kwa upande mwengine basi wanasema Abd Allah Ibn Abbas, Abd Allah Ibn

Umar na Aisha Radhi Allahu Anhum kua: ‘Al Kawthar ni Mto wa Peponi ambao katika

mwambao wake umepambwa kwa Madini ya thamani na Maji yake ni Meupe

kuliko Maziwa, Utamu wake ni zaid ya Asali na Harufu yake ni zaid ya harufu ya

Miski’(Imam Tirmidhi)

Ambapo anasema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Niliingia Peponi na

nikakutana na Mto ambao Mwambao wake una Mahema ambayo yametengenezwa

kwa Mapambo ya Lulu, nami nikaingiza Mkono wangu ndani ya Maji yake

yanayotiririka na kuona kua yananukia zaidi ya harufu ya Miski nami nikamuuliza

Jibril.: ‘Jibril, Ndio nini huu?’ ambapo nae akasema: ‘Huo ndio Kawthar ambao

Allah Subhanah wa Ta’ala amejaalia kukupa wewe.’’

Na kwa upande mwengine basi kuna wasemao kua : ‘Kawthar hua inamaanisha Mto

ambao Ummah wa Kiislam utaenda Kunywa Maji yake Peponi’ na kuna wasemao

kua: ‘Kawthar humaanisha Mambo mengi mazuri ikiwemo Utume, Shaira, Qur’an,

Ilm, Wanazuoni wa Kiislam na pia Wafuasi wa Dini ya Kiislam na Amali njema

zao’

Mnamo mwaka wa 9 wa Uislam basi Ami yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

yaani Mzee Abu Talib ambae alikua na takriban Umri wa miaka 86 akaanza kuumwa na

hivyo Makafiri walipoiona hali hii basi wakaamua kumkabili Abu Talib ili amsalimishe

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ndani ya Mikono yao, na kumwambia : ‘Ewe

Abu Talib, hakika wewe ni kiongozi wetu, na sisi sasa hivi tumekua na wasiwasi juu

ya kile kinachondelea baina yetu na Mtoto wa Abdullah. Hivyo bora mwite kisha

nawe uwe hakimu baina yetu kwa aidha atengane nasi au sisi tutengane nae bila ya

kutumia nguvu, na bila ya kutuingilia katika Imani yetu’

Hivyo Abu Talib akaagizia kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aitwe mbele yake

na alipofika basi akasema: ‘Ewe Mtoto wa Kaka yangu, hawa ni viongozi wa Quraysh

wamekuja hapa wa ajili ya majadiliano kuhusiana nawe, hivyo watakuambia kile

wanachokitaka na watapokea kile unachokitaka.’


699

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Ewe Ami yangu, hakika mimi

nnataka neno moja tu ambalo walipokee na kulikubali, kwa kutokana na neno hilo

moja basi watakua na mamlaka ya Ardhi za Waarabu na za wasiokua Waarabu.’

Abu Talib akashangaa na kusema: ‘Neno Moja tu?’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam Neno Moja Tu.’

Ambapo jibu hili lilimuacha kila mtu akiwa ni mwenye kushangaa pia na kujiuliza ni

neno gani hilo lenye uwezo wa kuwapa Viongozi hawa wa Quraysh mamlaka juu ya kila

sehemu ya ardhi, hivyo Abu Jahal akasogea karibu ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam na kusema: ‘Sawa, tuambie ewe Muhammad hilo neno Moja, kisha nasi

tutaongezea maneno 100 zaid yake’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Semeni La Ilaha Illa Allah, na kisha

rembeeni Msanamu yenu yote mnayo yaabudu’

Viongozi hao wa Quraysh wakasema: ‘Muhammad, unatushangaza, hivi wewe

unataka tuwarembee miungu yetu yote kwa ajili ya Mungu wako Mmoja tu?’ kisha

wakakaa na kunong’onezana na kusema: ‘Wa Allahi Huyu Mtu hatotupa kile

tukitakacho, hivyo twendeni zetuni tukafuate Imani ya Dini yetu hadi pale Mungu

atakapoamua baina yetu.’ Allah Subhanah wa Ta’ala analizungumzia tukio hili pale

aliposema:

كَذ َّابٌ۞أَجَعَل

ۤ ‏﴿وَعَجِبُواْ‏ أَن جَآءَهُم م ٌّنذِرٌ‏ مِّنْهُمْ‏ وَقَالَ‏ ٱلْكَافِرُونَ‏ هَٰذَا سَاحِرٌ‏ َ

ٱلآلهَِةَ‏ إِلَٰهاً‏ وَاحِ‏ داً‏ إِن َّ هَٰذَا لَشَيْءٌ‏ عُجَابٌ‏ ‏۞وَٱنطَلَقَ‏ ٱلْمَلَأُ‏ مِنْهُمْ‏ أَنِ‏ ٱمْشُواْ‏ وَاْ‏ ‏ْصبرُِواْ‏

ٰ عَلَى آلهَِتِكُمْ‏ إِن َّ هَٰذَا لَشَيْءٌ‏ يُرَادُ۞مَا سمَِعْنَا هبَِٰذَا فىِ‏ ٱلْمِل َّةِ‏ ٱلآخِ‏ رَةِ‏ إِ‏ ‏ْن هَٰذَا إِلا َّ

ٱخْتِلاَقٌ۞أَأُنزِلَ‏ عَلَيْهِ‏ ٱلذِّكْرُ‏ مِن بَيْنِنَا بْل هُمْ‏ فىِ‏ شَكٍّ‏ مِّن ذِكْرِى بَل ل َّم َّا يَذُوقُ‏ واْ‏

عَذَابِ‏ ﴾

WaAAajiboo an jaahum mundhirun minhum waqala alkafiroona hadha sahirun

kadhdhabun; AjaAAala al-alihata ilahan wahidan inna hadha lashay-on AAujabun

; Waintalaqa almalao minhum ani imshoo waisbiroo AAala alihatikum inna hadha

lashay-on yuradu; Ma samiAAna bihadha fee almillati al-akhirati in hadha illa

ikhtilaqun; Aonzila AAalayhi aldhdhikru min baynina bal hum fee shakkin

min dhikree bal lamma yadhooqoo AAadhabi (Surat Sad 38:4-8)


700

Tafsir: Na wao wanaona Ajabu kua amekuja kwao Muonyaji kutoka miongoni mwao

na wakasema Makafiri: ‘Huyu ni Mchawi na ni Muongo’ Amejaalia Miungu yetu yote

kua Mungu Moja hakika hili ni jambo la ajabu sana. Na viongozi miongoni mwao

wakasema: ‘Nendeni Mkabakie na Miungu yenu, kwani kwa hiki hili ni jambo

lililoandaliwa dhidi yenu; Hatujawahi kusikia sisi kuhusiana na jambo hili kutoka kwa

watu wetu wa mwishoni. Hauwi huu ila ni Uzushi. Hivi Jee (inawezekana kua)Uonyaji

ashushiwe yeye peke yake miongoni mwetu?’(Allah Subhanah wa Ta’ala anasema)La,

bali wao (Makafiri) ni wenye kua na shaka na Uonyaji wangu (Qur’an) na bado

hawajaonja Adhabu yangu.

Hivyo kwa mtizamo wao basi Viongozi wa Qurayshi walikua wakimuita Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua ni Mchawi na Muongo, kwa sababu mbali ya kusema

anayoyasema ambayo kwao wao hayaingii akilini lakini watu walikua wakimsikiliza na

kumfuata, hivyo kwao wao ilikua hakuna njia nyengine anayoitumia Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam katika kuwapata watu wengi zaidi isipokua ni kwa kutumia

Uchawi.

Ambapo kwa upande mwengine basi Allah Subhanah wa Ta’ala analizungumzia tukio

hili kwa kusema:

‏﴿بَلْ‏ مَت َّعْتُ‏ هَٰؤُلاَءِ‏ وَآآبَءَهُمْ‏ حَتى َّ ٰ جَآءَهُمُ‏ ٱلحَْق ُّ وَرَسُولٌ‏ م ُّبِينٌ۞وَ‏ لَم َّا جَآءَهُمُ‏

ٱلْقُرْآنُ‏ ٰ سِ‏ حْرٌ‏ وَإِ َّ بِهِ‏ كَافِرُونَ۞وَقَالُواْ‏ لَوْلاَ‏ نُزِّلَ‏ هَٰذَا عَلَى رَجُ‏ ‏ٍل

ٱلحَْق ُّ قَالُواْ‏ هَٰذَا

مِّنَ‏ ٱلْقَرْيَتَينِْ‏ عَظِيمٍ۞أَهُمْ‏ يَقْسِ‏ مُونَ‏ رَحمَْةَ‏ رَبِّكَ‏ نحَْنُ‏ قَسَمْنَا بَيْنَهُمْ‏ م َّعِيشَتَهُمْ‏ ‏ِفى

ٱلحَْيَاةِ‏ ٱلد ُّنْيَا وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ‏ فَوْقَ‏ بَعْضٍ‏ دَرَجَاتٍ‏ لِّيَت َّخِ‏ ذَ‏ بَعْضُهُم بَعْضاً‏ سُخْرًِّ‏

وَرَحمَْ‏ ةُ‏ رَبِّكَ‏ خَيْرٌ‏ ممِّ َّا يجَْمَعُونَ‏ ﴾

Bal mattaAAtu haola-i waabaahum hatta jaahumu alhaqqu warasoolun mubeenun;

Walamma jaahumu alhaqqu qaloo hadha sihrun wa-inna bihi kafiroona; Waqaloo

lawla nuzzila hadha alqur-anu AAala rajulin mina alqaryatayni AAadheemun;

Ahum yaqsimoona rahmata rabbika nahnu qasamna baynahum maAAeeshatahum

fee alhayati alddunya warafaAAna baAAdhahum fawqa baAAdinn darajatin

liyattakhidha baAAdhuhum baAAdhan sukhriyyan warahmatu rabbika khayrun

mimma yajmaAAoona (Surat Az Zukhruf 43:29-32)


701

Tafsir: Bali nimewapa (Makafiri) wao na Mababa zao mapambo ya kufurahia

(Uongozi na usimamizi wa Mji Mtukufu wa Makkah na jengo Tukufu la Al Kaabah)

hadi pale ulipowajia wao Ukweli (Ujumbe wa Qur’an) na Mtume (Muhammad

Salallahu Alayhi wa Salam), Na Ukweli (Ujumbe wa Qur’an) ulipowafikia basi

wakasema: ‘Huu ni Uchawi na Tunaukufuru’ Wakawa wanasema: ‘Kwanini (Kama

ni kweli basi Hii Qur’an); Na wakasema: ‘Kwanini hakushushwa hii Qur’an kwa

Watu watukufu wa Miji yetu hii mimi (Makkah na Taif)’ Hivi Jee ni wao ndio wenye

kugawa Rehma za Mola wako? Bali ni sisi ndio tunaogawa baina yao katika riziki ya

maisha yao ya Dunia na tunawapandisha juu baadhi yao miongoni mwao darja, ili

wawaajiri baadhi yao katika kazi zao, na Rehma za Mola wako ni bora zaidi ya (Mali)

wanayojikusanyia.’

Ambapo baada tu ya Viongozi hao wa Quraysh kuanza kujadiliana kwa kunong’onezana

basi Abu Talib akasema: ‘Ewe Mtoto wa Ngugu yangu, hakika mimi sioni kua wewe

umekosea kutokana na matakwa yako.’ Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alipoyasikia haya basi akafurahia sana na kumwambia Abu Talib: ‘Ewe Ami Ynagu

sema La Ilaha Illa Allah’

Lakini Abu Talib akasema: ‘Ewe Mtoto wa Ndugu yangu, hakika mimi nnapa kwa

Allah kua kama siogopi mimi kua kubadilika kwangu kutawapelekea kua watu

hawa ni wenye kusema kua kumetokana na Uzee na kupungukiwa na kumbukumbu

na wao kua ni wenye kudumu katika kukukumbusha wewe na watoto wa mababu

zako baada ya kuodoka kwangu hapa Duniani, basi mimi ningesema maneno

unayotaka niyaseme na kukufuata, lakini watu wa Quraysh watadhani kua mimi

nimeyasema kutokana na kuogopa kifo, hivyo siwezi kuyasema maneno hayo.’

Ambapo hata hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliendelea kumuuisia Ami

yake huyo kua ashuhudie mara kadhaa lakini Abu Talib alisema kua: ‘Mimi ni Mfuasi

wa Imani ya Abd Ul Muttalib’na kisha Allah Subhanah wa Ta’ala:

‏﴿إِن َّكَ‏ لاَ‏ تَهْ‏ دِى مَنْ‏ أَحْبَبْتَ‏ وَلَٰكِن َّ ٱهلل ََّ‏ يَهْدِى مَن يَشَآءُ‏ وَهُوَ‏ أَعْلَمُ‏ بِ‏ ٱلْمُهْتَدِينَ‏ ﴾

Innaka la tahdee man ahbabta walakinna Allaha yahdee man yashao wahuwa

aAAlamu bialmuhtadeena (Surat Al Qasas 28:56)

Tafsir: Ni kwa hakika wewe hutoweza kumuongoza kila mtu unaempenda zaidi, lakini

Allah humuongoza amtakae na ni mwenye kuwajuwa wale walioongoka.

Hatimae Abu Talib akafariki Dunia huku akiwa na umri wa miaka 87, ambapo wakati

Abu Alib alipokua anafariki basi Al Abbas alikua amekaa pembeni yake na hivyo


702

akamuona Abu Talib wakati anakata roho kua midomo yake kama inasema kitu na hivyo

akamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam huku akitabasama kua: ‘Ewe Ibn

Ami nimemsikia Abu Talib akitamka kile ambacho ulichomtaka aseme.’ Kwani

katika ipindi hiki pia hata Al Abbas alikua hajasilimu bado.

Hivyo Rasul Allah Saallahu Alayhi wa Salam akasema kumuombea Ami yake huyo kua:

‘Allah, akuingize kwenye Rehma zake na akulipe kila la kheri’ na hivyo Allah

Subhanah wa Ta’ala akashusha aya isemayo:

‏﴿مَا كَانَ‏ لِلن َّبىِِّ‏ وَٱل َّذِينَ‏ آمَنُو ۤ اْ‏ أَن يَسْتَغْفِرُواْ‏ لِلْمُشْرِكِينَ‏ وَلَوْ‏ كَانُو ۤ اْ‏ أُوْلىِ‏ قُ‏ رْبىَٰ‏ مِن

بَعْدِ‏ مَا تَبَين ََّ‏ لهَُمْ‏ أَن َّهُمْ‏ أَصْحَابُ‏ ٱلجَْحِ‏ يمِ‏ ﴾

Ma kana lilnnabiyyi waalladheena amanoo an yastaghfiroo lilmushrikeena walaw

kanoo olee qurba min baAAdi ma tabayyana lahum annahum as-habu aljaheemi

(Surat At Tawbah 9:113)

Tafsir: Na si juu ya Nabii na wale Walioamini kua ni wawaombee Dua za kusamehewa

Washirikina, hata kama wakiwa ni watu wa karibu yao baada ya kubainishiwa kua

wao ni wtau wa Motoni.

Kifo hiki cha Abu Talib kilimhuzinisha sana Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam

kwani Abu Talib alikua ni Ngao yake dhidi ya Makafiri wa Makkah ambayo sasa hivi

ilikua imeanguka na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawa peke yake.

Na baada ya kufariki Abu Talib basi haikuchukua mda mrefu ulipoingia mwezi wa

Ramadhan basi Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam akafikwa na msiba mwengine

kwani akafariki na Khadija Ibn Khuwaylid Radhi Allah Anha akiwa na umri wa miaka

65.

Ambapo ingawa Khadija Bint Khuwaylid Radhi Allahu Anha alikua ni Tajiri katika

wakati wa Uhai wake lakini alipofariki alikua hana hata dinari moja, na hii ni kwa sababu

Mali yake yote alikua ni mwenye kuitumia kwa ajili ya kuusaidia Uislam na kuwasaidia

Waislam waliokua na hali mbaya ya kiuchumi na mateso yaliyotokana na vikwazo vya

Makafiri dhidi ya Waislam.

Msiba huu nao pia ulikua mzito sana kwake Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam na

hii kwa sababu ama tunavyojua kua Bi Khadijah Bint Khuwaylid Radhi Allahu Anha

alikua ni nguzo muhimu katika maisha yake na ndie mtu aliekua akimpa utulivu

anaporudi nyumbani kwake kwani ndie Mama watoto wake na ndie furaha ya Moyo


703

wake, kwani Bi Khadija Bint Khuwaylid Radhi Allah Anha alikua ni mwanamke ambae

ni mwenye sifa ya kumpenda, kumjali, kuhurumia na kumliwaza Mume wake katika kila

hali kutokana na mapenzi yake juu yake.

Bi Khadija Bint Khuwaylid Radhi Allahu Anha alikua ndie mwanamke mwenye Darja

ya Amirat Ul Quraysh kwani hata Malaika Jibril alithibitisha haya pale siku moja

alipokua pamoja na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kisha akawa anakuja

Amirat Al Quraysh akiwa na sahani ya chakula kwa ajili ya Mume wake yaani Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Ya Rasul Allah, huyo anaekuja kutoka mbali

ni Khadija, akiwa amechukua chombo cha kubebea chakula, atakapofika mbele

yako basi mpe salam zake kutoka kwa Mola wake na kwangu mie mwambie kua

Amejengewa Kasri Peponi litokanalo na Lulu kwa ajili yake ambalo ndani yake

hyamtokua na kasi wala matatizo.’

Hivyo mwaka huu kutokana na misiba hii iliyotoeka ndani yake basi ulikua unajulikana

kama Mwaka wa Huzuni. Na huzuni ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ilizidi

zaidi pale Makafiri walipozidisha Adha na kero zao juu ya Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam, kwani walikua wanajua kua hakuna wa kumlinda na kumtetea hivyo umefika

wakati wao wa kufanya wayatakayo, kiasi ya kua siku moja wakati Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alipokua akirudi Nyumbani kwake basi mmoja katika ya Majirani zake

alichukua Taka zake na kumwagia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuanzia

kichwani mwake.

Lakini hata hivyo kutokana na subra zake basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

hakumfanya kitu chochote mwanamke huyo bali alijipangusa takataka hizo kutoka

mwilini mwake na kurudi Nyumbani kwake, na alipofika Nyumbani kwake alisababisha

kilio kutoka kwa bint yake Fatma ambae alishindwa kujizuia kutokana na uchungu wa

maovu anayofanyiwa baba yake, na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akamnyamazisha Fatma na kisha akamwambia: ‘Ewe Binti yangu usilie kwani kwa

Hakika Allah atamhifadhi Baba yako’

Hali ilipozidi kua mbaya ya Manyanyaso basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akaamua kua bora atoke akatafute Wafuasi zaid katika maeneo ya Nje ya Mji wa Makkah

yaani Taif ambao uko umbali wa kilomita 75 kutoka katika Mji wa Makkah, kwani

kwenye kabila la watu wa Bani Thaqif ambao ni tofauti na watru wa Quraysh, na kama

wakimkubali basi itakua vizuri kwani atahama yeye na Wafuasi wake kuelekea kwenye

Mji wa Taif.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akafunga safari kuelekea katika Mji wa

Taif hukua akiwa amefuatana na msaidizi wake ambae ni Zaid Ibn Harith Radhi Allahu

Anhu, na alipofika katika Mji wa Taif basi hali iikua tofauti na namna alivyotegemea,

kwani watu wa Mji huo waliukataa Ujumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala alioshushiwa


704

kwa ajili ya kuwausia watu wake na Ibn Adam wote kwa ujumla, na kisha wakaanza

kumtukana na kuwaamrisha Watoto wao wawafukuze kwa kuwapiga mawe Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam pamoja na Zaid Ibn Harith Radhi Allahu Anhu.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Zaid Ibn Harith Radhi Allahu Anhu

wakakimbia kutoka katika Mji wa Taif huku wakiwa wamejeruhiwa na kuchuruzikwa na

Damu na kutafuta hifadhi katika moja kati ya Mashamba ya mpakani mwa Mji huo, kisha

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaomba Dua kwa kusema:

اللهم إليك أشكو ضعف قوتي ، وقلة حيلتي ، وهواني على الناس ، أرحم

الراحمين ، أنت أرحم الراحمين ، إلى من تكلني ، إلى عدو يتجهمني ، أو إلى

قريب ملكته أمري ، إن لم تكن غضبان علي فلا أابلي ، غير أن عافيتك

أوسع لي ، أعوذ بنور وجهك الذي أشرقت له الظلمات ، وصلح عليه أمر

الدنيا والآخرة ، أن تنز ل بي غضبك ، أو تحل علي سخطك ، لك العتبى حتى

ترضى ، ولا حول ولا قوة إلا بك

‘Kwako wewe Ya Allah, Nakusikitikia juu ya Udhaifu wangu, kukosa msaada

kuungwa mkono kwangu na manyanyaso ninayoyapata, Ewe Mwingi wa Rehma

ewe Mwingi wa Huurma Wewe ndie Mola wa Wanyonge, wewe ndie Mola wangu,

Jee unaniacha kwa nani? Kwa watu wa Mbali wanaonifanyia Uadui? Au kwa

Maadui uliowapa Uwezo zaidi yangu? Hivyo kama kuhuridhika nami, basi mimi

sijali nitakabaliana na nini lakini nitakua ni mwenye kufarahia zaid Rehma zako,

Hakika mimi natafuta hifadhi kutokana na Nuru ya Muonekano wako, ambay ni

yenye kuondosha kila sehemu yenye kiza katika Maisha haya na ya baadae baada

ya kuyarekebisha dhidi ya kupatwa na adhabu zake au kua chini ya ghadhabu zako.

Hakika mimi najisalimisha kwako kikamilifu hadi nitakapopata ridhaa yako,

kwani hakuna chenye kuwezekana bila ya uwezo wako.’

Ambapo mara baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuomba Dua hii basi

akashuka Malaika Jibril na kumuambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua

kama anataka basi basi Allah Subhnaha wa Ta’ala anaweza Kumtuma Malaika kisha

akaiangushia Milima Miwili iliyozunguka Mji wa Ta’if na kuwaangamiza watu hao

ndani yake, lakini hata hivyo kutokana na Ubora wa Maumbile na Tabia zake na wingi


705

wa Rehma zake na Upole wake basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema:

‘La, haina haja kwani mimi nnategemea kua ndani yao watu hawa watatoka watu

ambao watakua ni wenye Kumuabudu Allah Subhanah wa Ta’ala na

kutomshirikisha na chochote.’

Hivyo wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akiwa amekaa na kupumzika

kwenye jiwe moja la shamba hilo, basi mara akatokea Kijana ambae alikua na shada la

Zabibu na kumpa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Zaid Ibn Harith Radhi

Allahu Anhu. Kijana huyo alipofika mbele yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

basi akajitambulisha kua anaitwa Addas na kua ametumwa amletee Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam Zabibu hizo kutoka kwa wamiliki wawili wa Shamba hilo ambao

waliowaona namna Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Zaid Ibn Harith Radhi

Allahu Anhu walivyokua wamekaa huua wakiwa taabani na kuamua kuwakirimu Zabibu

hizo.

Baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Zaid Ibn Harith Radhi Allahu Anhu

kupewa Zabibu hizo na kushukuru basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaanza

kula kwa kusema: ‘Biismi Allah’. Ambapo tukio hili lilimshangaza sana Addas kwani

hakuwahi kusikia mtu yeyote akisema maneno hayo hapo kabla. Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akaona mshangao wake huo na akamuuliza Addas: ‘Wewe ni Mtu wa

wapi?’ ambapo Addas akasema: ‘Ni Mtu wa Nineveh’.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akatabasam kisha akasema: ‘Mji wa Yunus

Muadilifu Ibn Mata.’ Ambapo jibu hili lilimshangaza zaidi Addas, kua inakuaje mtu

huyu alie mbele yake anajua kuhusiana na Mji wake ambao ni Mji wa Nabii Yunus, na

hivyo akamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Hivi Jee umejuaje

kuhusiana na habari hio?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Yunus ni Kaka yangu. Kwani yeye

alikua ni Mtume na Mimi pia ni Mtume.’ Hivyo hapo hapo Addas akamshika kichwa

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kisha akambusu kwenye paji lake la Uso, na

kisha akaingia katika Dini ya Uislam.

SHAQQ AL QAMAR - MUUJIZA WA KUPASUKA KWA MWEZI

Mnamo mwaka wa 7 wa Utume miongoni mwa Viongozi wa watu wa kabila la Quraysh

akiwemo Walid Ibn Al Mughira, Abu Jahl, Aas Ibn Hisham. Aswad Ibn Abd Yaghush,

Aas Ibn Wail, Aswad Ibn Mutallib na wengineo walimfuata Rasul Allah Salallahu

A’alyhi wa Salam na kumwambia: ‘Kama wewe Muhammad ni Mtume kweli wa

Allah basi tuoneshe Muujiza wa Kuupasua Mwezi, kiasi ya kua sehemu yake moja


706

itatokea kwenye upande wa Mlima wa Abu Qubais na nyengine itatokea kwenye

upande wa Abu QuayQan’

Na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawauliza Makafiri hao kua: ‘Jee kama

nikifanya hivyo, Mtaingia katika Uislamu?’ ambapo nao wakasema: ‘Naam’. Hivyo

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuomba Allah Subhanah wa Ta’ala amjaalie

uwezo wa kufanya Miujiza hio kama wanavyotaka Makafiri hao katika usiku wa mwezi

mpevu yaani tarehe 14 ya Muandamo wa Mwezi ambao hua ndio mwezi mkamilifu na I

wenye kuonekana wote. Na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamuamrisha Malaika

Jibril kua ashuke kumwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua amekubaliwa

Dua yake hio, na itatekelezwa kama alivyotaka iwe.

Hivyo ilipowadia siku hio basi baada ya Salat al Isha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam akatoka na Waislam pamoja na Maquraysh hao na kuenda katika maeneo ya

Minna huku kukiwa na mwezi Kamilifu na kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akaupasua

Mwezi huo na akaupeleka upande mmoja wa mwezi huo kwenye upande wa Mlima wa

Abu Qubais sambamba na upande mwengine wa mwezi huo kwenye mlima Quayqan, na

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawanadia Waislam kwa kuwaambia:

‘Ewe Abu Salama Ibn Abd Salam, Ewe Arqam Ibn Abi Al Arqam! Shuhudieni’ na

kisha akawa geukia Makafiri hao na kuwanadia: ‘Enyi Watu wa Quraysh Shuhudieni!’

lakini hata hivyo Maquraysh hao wakasema: ‘Hakika huu ni Uchawi wa Mtoto wa Abu

Kabsha’ na kusema: ‘Hakika Muhamamd leo hii ameturoga, lakini hawezi kumroga

kila mtu hivyo wacha tuwaulize Wafasiri watakaokuja kama nao waliona ama la.’

Na siku ya pili yake watu wa Quraysh walipowauliza watu wengine waliokua ni wasafiri

waliotoka nje ya mji wa Makkah basi nao wakasema: ‘Hakika sisi tumeuona Mwezi

ulipopasuka, tumeuona mwezi ukiwa umepasuka.’ Lakini hata hivyo Makafiri hao

hawakukubaliana na Miujiza hio hivyo wakawa ni wenye kuendelea kusema kua :

‘Mjukuu wa Abd ul Muttalib ameziroga mpaka Mbingu kwa uchawi wake.’

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wakati tukiwa

tumekaa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika maeneo ya Minna basi

Mwezi ukapasuka na upande mmoja ukaenda nyuma ya Mlima mmoja na upande

mwengine ukaenda upande mwengine na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akasema: ‘Shuhudieni.’’(Imam Bukhari)

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akayakanusha maneno hayo ya Makafiri na

kuyathibitisha ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pale aliposema katika Surat Al

Qamar kua:


707

‏﴿بِ‏ سْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞ٱقْتَرَبَتِ‏ ٱلس َّاعَةُ‏ وَٱنشَق َّ ٱلْقَمَرُ۞وَ‏ إِن يَرَوْاْ‏ آيَةً‏ يُعْرِضُواْ‏

وَيَقُولُواْ‏ سِ‏ حْرٌ‏ م ُّسْتَمِر ٌّ۞وَكَ‏ ذ َّ بُواْ‏ وَٱت َّبَعُو ۤ اْ‏ أَهْ‏ وَآءَهُ‏ مْ‏ وَكُ‏ ل ُّ أَمْ‏ رٍ‏ م ُّسْ‏ تَقِر ٌّ ‏۞َولَقَدْ‏ جَآءَهُم

مِّنَ‏ ٱلأَنبَآءِ‏ مَا فِيهِ‏ مُزْدَجَرٌ۞حِ‏ كْمَةٌ‏ ابَلِغَةٌ‏ فَمَا تُغْنِى ٱلن ُّذُرُ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Iqtarabati alssaAAatu wainshaqqa alqamaru;

Wa-in yaraw ayatan yuAAridhoo wayaqooloo sihrun mustamirrun;

Wakadhdhaboo waittabaAAoo ahwaahum wakullu amrin mustaqirrun; Walaqad

jaahum mina al-anba-i ma feehi muzdajarun; Hikmatun balighatun fama tughnee

alnnudhuru (Surat Al Qamar 54:1-5)

Tafsir: Kwa Jina la Allah mwingi wa Rehma na mwingi wa huruma; Imekaribia Saa

na Mwezi umepasuka; Lakini wanapoiona Dalili basi hua ni wenye kugeuka na

kusema: ‘Ni tukio lisilodumu la Uchawi wenye Kupita’; Wamekadhibisha na kufuata

Matamanio yao; Na kila jambo hua lina mwisho wake; Kwani kwa hakika imewajia

Habari, ambayo ndani yake mna Uonyo; Na Hikma kubwa sana, lakini hata hivyo

hauwafai uonyo huo.

Na kwa upande mwengine basi tunaona kua tukio hili limehadithiwa pia na Masahaba

kadhaa waliolishuhudia kiasi ya kua Hadith zake ni Mutawattir yaani wingi wake

mkubwa sana kiasi haiwezekani kwa Masahaba hao kua ni wenye kukubaliana kusema

uwongo juu ya jambo hilo, na bila ya shaka tukio hili ni lenye kuwezekana kutokana na

Maumbile ya mwezi kua ni yenye kutokana na Mawe kama ya Volcano na hivyo

kuwezekana kutokea Mripuko na Mwezi ukagawika na kwa makadirio yake Allah

Subhanah wa Ta’ala basi mwezi huo ukaungana tena upya.

Lakini kwa wasioamini hii hua haiwezi kuwasaidia kitu kwani amesema Allah Subhanah

wa Ta’ala kua:

‏﴿قُلِ‏ ٱنظُرُواْ‏ مَاذَا فىِ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَمَا تُغْنىِ‏ ٱلآَتُ‏ وَٱلن ُّذُرُ‏ عَن قَوْمٍ‏ لا َّ

يُؤْمِنُونَ‏ ﴾

Quli ondhuroo madha fee alssamawati waal-ardhi wama tughnee al-ayatu

waalnnudhuru AAan qawmin la yu/minoona (Surat Yunus 10:101)


708

Tafsir: Waambie (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam): ‘Angalieni yote

yaliyomo Mbinguni na Ardhini’ Lakini si dalili hizo wala si Waonyaji wanaowafaa

wale Wasioamini.

SIFA ZA UPEKEE WA KIMAUMBILE WA NABII MUHAMMAD

SALALLAHU ALAYHI WA SALAM:

‏﴿م َّا كَانَ‏ محَُم َّدٌ‏ أَآبَ‏ أَحَدٍ‏ مِّن رِّجَالِكُمْ‏ وَلَٰكِن ر َّسُولَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَخَاتمََ‏ ٱلن َّبِيِّينَ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏

ّ شَيْءٍ‏ عَلِيماً‏ ﴾

بِكُل ِ

Ma kana muhammadun aba ahadin min rijalikum walakin rasoola Allahi

wakhatama alnnabiyyeena wakana Allahu bikulli shay-in AAaleeman(Surat Al

Ahzab 33:40)

Tafsir: Na hakua Muhammad ni Baba wa Mtu yeyote Miongoni mwenu, lakini ni

Mtume wa Allah, na Nabii wa Mwisho na Allah ni mwenye kujua juu ya kila kitu.

Anasema Umar Ibn Al Khattab kua: ‘Katika kipindi cha Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kulikua na Mtu ambae alikua akiitwa Abd Allah ambae jina lake la Utani

lilikua ni Khimar (Punda), na alikua anapenda kumchekesha Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kwa mambo yake. Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akampa

adhabu ya kupigwa bakora kwa sababu alikua amelewa. Siku moja akaletwa tena

mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo akapewa tena adhabu ya

bakora, mara mmoja miongoni mwa watu akasema: ‘Ya Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam mlaani! Kwani ni mara ngapi tayari analetwa kwa kosa hilo hilo.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema ‘La Msimlaani kwani Wallahi mimi

najua kua huyu ni mwenye kumpenda Allah na Mtume wake’’ (Sahih Bukhari)

Imam Bukhari anasema kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakutoka nje

kwa siku tatu, na hivyo Abu Bakr akawa ni mwenye kuongoza Sala. Wakati

Waislam wanasali basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akafunua pazia lake.

Hivyo wakati pazia liliponyanyuka basi Uso wake Mzuri wenye kung’ara

ukaonekana, basi haijawahi kuonekana muonekano unaovutia kwa uzuri kabla

yake’ (Sahih Bukhari)


709

Hadith hii pia ipo katika kitabu cha Imam Muslim ambae yeye anasema kua Masahaba

walisema: ‘Kutokana na kuzidiwa kwa Furaha ya kuuona uzuri wake, basi tukawa

ni wenye kuchanganyikiwa ndani ya Sala zetu ’(Sahih Muslim)

Mtume Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam alisema kua : ‘Mlima wa Uhud ni

Mlima katika Milima ya Peponi Unatupenda nasi Tunaupenda’(Sahih Bukhari).

Na akasema tena Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Mlima wa Uhud

Unatupenda nasi tunaupenda, Ya Allah Hakika Ibrahim ameufanya Mji wa Makkah

kua ni Mtukufu, hivyo nami nakifanya Kitukufu kila kilicho baina ya Mlima wa Uhud

(Yaani Mji wa Madinah )’(Imam At Tirmidhii)

Na baada ya vita vya Uhud Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Sayyidna

Abubakar, Sayyidna Umar na Sayyidna Uthman w Radhi Allahu Anhum alikua

wamepanda juu ya Mlima wa Uhud, ambapo nao Ukatikisika. Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akatabasam kisha akaupiga mguu wake chini huku akisema: ‘Tulia

Ewe Uhud kwani juu yako hakuna yeyote yule isipokua Rasul Allah, na Mashahidi

wawili’ hapo Mlima wa Uhud ukatulia.(Sahih Bukhari, Imam Tirmidhi)

Tunapoziangalia hadith hizi mbili basi tunaona kua Mlima wa Uhud ni Mlima wa

Volcano ambao haujawahi kuripoka tangu uliporipuka. Hivyo Mlima huu ulitikisika si

kwa ripuka la, bali ni kwa sababu ulikua umefurahia kua juu yake amepanda Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam, na hivyo ulikua unataka kuonesha kua unajua darja ya yule

aliepanda juu yake ambae ni Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Kwa upande mwengine basi tunaona kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisema

kua Mlima wa Uhud unawapenda kwa sababu Mlima huo ndio Uliomhifadhi yeye pale

walipovamiwa na Jeshi la makafiri lililokua likiongozwa na Khalid Ibn Walid kabla ya

Kusilimu katika vita vya Uhud, na vile vile mazingira ya Mlima wa Uhud ambao ni

wenye urefu wa kilomita moja kwenda juu, na ni wenye rangi Nyekundu kutokana na

udongo wake kua ni wenye asili ya Volkano wenye mchanganyiko wa madini ya quartz,

sanidine na plagioclase. Mlima wa Uhud upo kaskazini ya Mji wa Madinah kilomita 5

kutoka katika Masjid An Nabawi yanaufanya mlima huu kua ni ngao na hivyo kuua kama

vile unaukumbatia Mji wa Madinah na hivyo kua kama ngao kwa Watu wake kutokana

na Mashambulizi ya maadui zao.

Na hii pia ni kulingana na uthibitisho wa ile hadith ya Jabir Ibn Abd Allah Radhi Allahu

Anhu ambae alisema: ‘Hakika mimi nilimuona Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam katika Usiku wa mwezi Mpevu akiwa amevaa Joho Jekundu, Kisha

nikaangalia juu na nikaona mwezi Mpevu, na nikaona kua Rasul Allah Salallahu


710

Alayhi wa Salam alikua ni mzuri zaidi mbele ya macho yangu kuliko hata Uzuri wa

Mwezi mpevu’ (Shamail Tirmidhii)

Na pia Anas bin Malik Radhi Allahu Anhu amesema kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alikua si mrefu wala si mfupi, na muonekano wake haukua mweupe sana

kama wa alietiwa limau na wala hakua mwenye rangi ya kiza, wala rangi ya

kahawia ya kiza (alikua anang’ara)’(Shamail Tirmidhii)

Kwani tunapozungumzia Uzuri wa Mwezi Mpevu au Mwezi Mweupe Unaong'ara basi

hua tunazungumzia hali wanayoiona Ibn Adam wenye kujua Uzuri wa Maumbile ya Kitu

kutokana na uwezo wa Muumba usiokua na Kifani juu ya hicho alichokiumba.

Kiasi ya Kua mwenye kujua huyo hua ni mwenye kupigwa na bumbuwazi na uzuri huo

anapouona Uzuri wa kitu husika. Wengi hatuna kawaida ya kuuona na kuangalia Mwezi

kwa utulivu na hivyo hua hatuoni uzuri wake, kwani uzuri wa mwezi tena katika kiza cha

usiku basi hua ni Uzuri wa kustaajabisha, kuvutia, kutuliza Moyo wa mwenye kuuangalia

na kuutizama, lakini sisi hatuoni uzuri huo kwa sababu hatuangalii na pia kwa sababu

tumeathirika na mazingira ya taa za umeme kila sehemu.

Ndio maana wenye lugha yao hua wanasifia uzuri kwa kumithilisha kwa kusema: ‘Zayy

Al Qamar’ yaani: ‘Uzuri wa Mwezi’ Waarabu hua pia ni wenye kutumia sifa ya Uzuri

wa mwezi kiasi ya kua mtu anafikia kumsifu Mwanamke mzuri anaempenda kwa

kumwita Ya Amar! yaani Ya Qamar!

Na bila ya shaka Mwanamke wa Kiarabu ukimsifia kwa kua na sifa ya uzuri wa Mwezi

basi hua anajiona kua yuko kama Hur Al Ayn hivyo Uzuri wa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam hua ni wenye kupita Uzuri wa mwezi.

Imam Ibn Kathir anasema kua : 'Hasan bin Thabit Radhi Allahu Anhu amesema kua:

‘Rasul Allah Salallahu Alyhi wa Salam ni Sayari ambayo hata mwezi wa mwezi 14

hua ni wenye kuchukua Nuru yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam’ (Tarikh

Ibn Kathir)

Tunapomuangalia Imam At Tirmidhii basi tunaona kua kuna Hadith ya Qaylah Bint

Mabramah Radhi Allahu Anha ambae anasema kua: ‘Nilimuona Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akiwa amekaa Msikitini katika mkao wa Qarfasa (Kukaa kitako

huku akiwa amekumbatia miguu yake) na kutokana na Utukufu wa Muonekano

wake basi nikaanza kuetetemeka. Na hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alisema bila ya kuniangalia ‘Masikini, Ewe Mwanamke Kua na Utulivu. Na mara

tu baada ya kusikia maneno hayo ya Rasul Allahu Alayhi wa Salam, basi Khofu hio

ikaniondoka’.(Sharmail At Tirmidhi)


711

Ama tunapozungumzia kuhusiana na Sifa ya Kutisha, kwake Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam basi hua kuna aina mbili, kwanza kuna uzuri wa Kutisha kulingana na

mtizamo wa wale wanaompenda na pia hua ni kulingana na mtizamo wa maadui zake,

kwani kuna kutisha kwa uzuri wa kupita kiasi unaoenda sambamba na kutisha kwa kua

na Darja ya juu kupita kiasi miongoni mwa Viumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala, na

hii hua ni kwa wale wenye kumpenda.

Ama kwa wale waliokua maadui zake basi ilikua pia kuna hali ya kutisha ya mtu

kuingiwa na khofu baada ya kumuangalia kwake ambayo huambatana na khofu ya

kutoweza kufanya chochote hata uwe na uwezo gani mbele yake.

Hivyo kwanza na tuangalie kutisha kunakotokana na Uzuri na pia Utukufu wa Darja yake

Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam. Ambapo tunaona kua anasema Sahaba Abd Allah

Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu alipokua mdogo siku moja usiku aliamka akamuona Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kaamka anataka kusali, hivyo haraka sana akakurupuka

na akaenda kumchukulia Maji ili atie Udhu. Na kisha nae akaambiwa na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam atie udhu.

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasimama kwa ajili ya kusali. Lakini

kabla ya kusali basi akamwambia Abd Allah Ibn Abbas, njoo hapa,kaa pembeni yangu

Usali. Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Saalam akasali hadi akamaliza. Na

alipomaliza basi alimuona Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu akiwa hajasali

pembeni yake. Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuuliza: Ya Abda Allah,

kwani mimi nilipokuambia usali pamoja nami hukusali?

Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu alijibu: ‘Ya Rasul Allah! Hakika wewe Ni

Mwenye Darja Kubwa sana kwangu kiasi ya kua haiwezekani mimi na wewe kua

ni wenye kusali pamoja mbele ya Allah Subhanah wa Ta'ala’.

Hapa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akanyanyua mikono juu na kumuomba

Allah Subhanah wa Ta'ala kwa kusema: Ya Allah Mjaalie kua ni Mwenye Hikma.

Kutisha kwa aina nyengine ni kule kunakoelezewa na Asbab Nuzul ya aya inayofuatia

ambako hua ni kutisha kwa Utukufu wa heshima.

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ لاَ‏ تَرْفَعُو ۤ اْ‏ أَصْوَاتَكُمْ‏ فَوْقَ‏ صَوْتِ‏ ٱلن َّبىِ‏ ِّ وَلاَ‏ تجَْهَرُواْ‏ لَهُ‏ بِٱلْقَوْلِ‏

كَجَهْرِ‏ بَعْضِكُمْ‏ لِبَعْضٍ‏ أَن تحَْبَطَ‏ أَعْمَالُكُمْ‏ وَأَنتُمْ‏ لاَ‏ تَشْعُرُونَ‏ ﴾


712

Ya ayyuha alladheena amanoo la tarfaAAoo aswatakum fawqa sawti

alnnabiyyi wala tajharoo lahu bialqawli kajahri baAAdhikum libaAAdhin an tahbata

aAAmalukum waantum la tashAAuroona (Surat Al Hujurat 49:2)

Tafsir: Enyi Mlioamini Msinyanyue Sauti zenu juu ya sauti ya Nabii (Muhammad

Sallahu Alayhi wa Salam) na wala msizungumze nae kama mnavyozungumza

miongoni mwenu, ili amali zenu zisije zikawa ni za bure wakati nyinyi mkiwa hamjui.

Anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari

Al Qurtubi kuhusiana na ayah hii kua : ‘Amesema Imam Ibn Abi Mulaykah kua kuna

watu wawili wema ambao ni Abu Bakr na`Umar ilikua bado kidogo tu waangamie,

kutokana na kupaza kwao sauti mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam,

baada ya kuwasili kwa ujumbe wa Banu Tamim, ambapo mmoja kati yao alitaka

kua Aqra Ibn Rabia awe kiongozi wao, wakati mwengine alipendekeza kua kiongozi

awe mtu mwengine.’

Hivyo Abu Bakr akamwambia Umar: ‘Inaonekana kua wewe hutaki lolote isipokua

kupingana nami’ na Umar akamwambia Abu Bakr : ‘La sikua na haja hio mie!’

Hivyo wakapandishiana sauti, hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akaishusha aya hii

ya Surat Al Hujurat 49:2,’

Na kwa Abd Allah Ibn Zubayr Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua: ‘Mara tu

baada ya kushushwa ayah hii basi ilikua kila mara wakati Umar alipokua

akizungumza na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akizunguumza kwa

sauti ya chini sana kiasi ya kua ilimbidi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akimuomba Umar kurudia rudia maneno aliyokua akiyasema’ (Imam Ibn Jarir).

Na kuhusiana na ayah hii basi tunaona kua Wanazuoni wanasema kua: ‘Hairuhusiki

kupaza Sauti hata ukiwa pembeni ya Kaburi la Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, kwa sababu kupaza sauti kwa mtu karibu na kaburi lake basi hua ni sawa

na kupaza sauti wakati alipokua hai,’ na hii ni kulingana na mtizamo wa Imam Abu

Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi, Imam Ibn

Kathir n.k

Kwa upande mwengine basi anasema Imam Bukhari kua: ‘Siku Moja Umar Ibn Al

Khattab aliwasikia watu wawili wakipaza sauti zao, hivyo akawafuata na

kuwauliza: ‘Jee nyinyi mnajua mko katika sehemu gani? Na jee mnatoka katika

Mji gani?’. Wale watu wakasema kua wanatoka katika Mji wa Taif, ambapo Umar

Ibn Al Khattab akawaambia: ‘Kama nyinyi mngekua ni watu wa Madinah basi

nigekupeni adhabu ya kupigwa bakora.’’


713

Miongoni mwa Khofu ambazo walizopata maadui zake waliokua wanataka kumuua basi

pia ilikua ile Khofu ya kufa ganzi ya Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu ambae

anasema kua kabla ya kusilimu kwake basi katika Vita vya Khandaq, alimuona Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akiwa anawasalisha Waislam Sala ya Al Asr, kama

inavyoelezewa na aya:

‏﴿وَإِذَا كُنتَ‏ فِيهِمْ‏ فَأَقَمْتَ‏ لهَُمُ‏ ٱلص َّلاَةَ‏ فَلْتَقُمْ‏ طَآئِفَةٌ‏ مِّنْهُمْ‏ م َّ عَكَ‏ وَلْيَأْخُذُو ۤ اْ‏

أَسْلِحَتَهُمْ‏ فَإِذَا سَجَدُواْ‏ فَلْيَكُونُواْ‏ مِن وَرَآئِكُمْ‏ وَلْتَأْتِ‏ طَآئِفَةٌ‏ أُخْرَىٰ‏ لمَْ‏ يُصَل ُّواْ‏

فَلْيُصَل ُّواْ‏ مَعَكَ‏ وَلْيَأْخُذُواْ‏ حِ‏ ذْرَهُمْ‏ وَأَسْلِحَتَهُمْ‏ وَد َّ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ لَوْ‏ تَغْفُلُونَ‏ عَ‏ ‏ْن

أَسْلِحَتِكُمْ‏ وَأَمْتِعَتِكُمْ‏ فَيَمِيلُونَ‏ عَلَيْكُمْ‏ م َّيْلَةً‏ وَاحِ‏ دَةً‏ وَلاَ‏ جُنَاحَ‏ عَلَيْكُمْ‏ إِن كَانَ‏

بِكُمْ‏ أَذًى مِّ‏ ن م َّطَرٍ‏ أَوْ‏ كُ‏ نتُمْ‏ م َّرْضَى ۤ أَن تَضَعُو ۤ اْ‏ أَسْ‏ لِحَ‏ تَكُ‏ مْ‏ وَخُ‏ ذُ‏ واْ‏ حِ‏ ذْ‏ رَكُمْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏

أََعد َّ لِلْ‏ كَا فِ‏ رِي نَ‏ عَذَاابً‏ م ُّهِيناً‏ ﴾

Wa-idha kunta feehim faaqamta lahumu alssalata faltaqum ta-ifatun minhum

maAAaka walya/khudhoo aslihatahum fa-idha sajadoo falyakoonoo min waraikum

walta/ti ta-ifatun okhra lam yusalloo falyusalloo maAAaka walya/khudhoo

hidhrahum waaslihatahum wadda alladheena kafaroo law taghfuloona AAan

aslihatikum waamtiAAatikum fayameeloona AAalaykum maylatan wahidatan

wala junaha AAalaykum in kana bikum adhan min matarin aw kuntum mardha an

tadaAAoo aslihatakum wakhudhoo hidhrakum inna Allaha aAAadda lilkafireena

AAadhaban muheenan (Surat An Nisa’ 4:102)

Tafsir: Wakati wewe (Muhamamd Salallahu Alayhi wa Salam) unapokua pamoja nao

na kuwaongoza katika Sala, wacha kundi moja miongoni mwao lisimame pamoja

nawe wakiwa na silaha zao, na wanapomaliza Sijda zao basi na wachuue nafasi ya

Nyuma na kisha wale waliokua hawakusali wacha wasali huku nyie mkiwa na jukumu

la silaha zenu, nkwani wanatamani waliokufuru kua laiiti mghafilike na silaha zenu

na mizigo yenu kukushambulieni kwa pigo moja, lakini hakuna dhambi juu yenu

kama mkiweka pembeni silaha zenu kutokana na usumbufu wa Mvua au wa sababu

ya maradhi lakini chukueni tahadhari juu yenu, kwani kwa hakika Allah

ametayarisha Adhabu kali kwa ajili ya Makafiri.


714

Ambapo kama zinavyosema aya basi Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu alikua ana

uhakika kua anaweza akaingia katika Upande huo aliokuwepo Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam na akafanya mashambulizi ya Kumuua, na kisha akatoka katika kambi

hio ya Waislam bila ya madhara yeyote, Lakini hata hivyo anasema Khalid Ibn Walid

Radhi Allahu Anhu kua: ‘Kila nikijaribu kutaka kuelekea katika eneo hilo

alilokuwepo Muhammad Salallah Alayhi wa Salam, basi kulikua kuna nguvu fulani

nzito isiyoonekana ambayo ilikua inanizuia mimi kutekeleza azma yangu hio.’

Tukio hili ndilo lilimpelekea Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu kuuona Ukweli kua

haiwezekani kua na uadui na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, kwani atakushinda

tu kutokana na anavyotisha kwani kuna nguvu za kimaumbile zisizonekana ambazo si za

kawaida ambazo hua zinamsaidia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Hapa kwanza Inabidi tujue Uwezo wa Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu ambae kama

tunavyojua kua ndie Mtu pekee katika historia ya Uislam alieuhatarisha Uislam wakati

alipokua kafiri na hii ni katika vita vya Uhud, na hii ni kutokana na Mbinu zake katika

mapigano, Nguvu zake, Ujasiri wake wa kutoogopa kitu chochote na pia ukubwa wa

Subra zake, na pia ndie mtu pekee alieuongoza Uislam na Kuueneza katika Ardhi ya

Uarabuni baada ya Kusilimu kwake.

Tunapoangalia kwa upande wa waliofuatia baada ya Masahaba ambao ni Tabiina basi

tunakutana na Imam Malik ambae tunaona kuhusiana nae kua amesema Musab Ibn

Abdullah kua: ‘Kila wakati ambapo ilikua Nabii Muhammad Sallahu Salayhi wa

Salam, akitajwa mbele ya Imam Malik Radhi Allahu Anhu basi Imam Malik

muonekano wa uso wake hua ni wenye kubadilika na hata mkao wake hua ni wenye

kuwatia khofu wale aliokaa nao karibu yake. Siku Moja akaulizwa kwa nini anakua

katika hali hiyo? Nae akajibu: ‘Kama mngekua mnaona yale nnayoyaona mimi

kwenye Ufaham wangu basi nanyi mngekua na hali kama yangu.’’ (Ash Shifa)

Vile vile Allah Subhanah wa Ta’ala amempa Rasul Allah Sallahu Salayhi wa Salam Sifa

za upekee ambazo ni:

Kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam Ndio Mfano Bora Ulimwenguni kama

zinavyosema aya:

‏﴿ل َّقَدْ‏ كَانَ‏ لَكُمْ‏ فىِ‏ رَسُولِ‏ ٱهلل َِّ‏ أُسْوَةٌ‏ حَسَنَةٌ‏ لِّمَن كَانَ‏ يَرْجُو ٱهلل ََّ‏ وَٱلْيَوْمَ‏ ٱلآخِ‏ رَ‏

وَذَكَرَٱ هلل ََّكَثِير اً﴾‏


715

Laqad kana lakum fee rasooli Allahi oswatun hasanatun liman kana yarjoo Allaha

waalyawma al-akhira wadhakara Allaha katheeran (Surat Al Ahzab 33:21)

Tafsir: Kwa Hakika mnao kwa Rasul Allah mfano Bora kabisa kwa yule mwenye

kutarajia kurudia kwa Allah na Siku ya Mwisho na mkumbukeni Allah kwa Wingi

sana.

Kua yeye Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam ni Mtume wa watu wote kama

zinavyoonesha aya:

‏﴿قُلْ‏ ‏َٰي ُّهَا ٱلن َّاسُ‏ ِ إِنىّ‏ رَسُولُ‏ ٱهلل َِّ‏ إِلَيْكُمْ‏ جمَِيعاً‏ ٱل َّذِى لَهُ‏ مُلْكُ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏

وَٱلأَرْضِ‏ لا إِلَٰهَ‏ ۤ إِلا َّ هُوَ‏ يحُْيِى وَيمُِيتُ‏ فَآمِنُواْ‏ بِٱهلل َِّ‏ وَرَسُولِهِ‏ ٱلن َّبىِِّ‏ ٱلأُمِّىِّ‏ ٱل َّذِى يُؤْمِ‏ ‏ُن

بِٱهلل َِّ‏ وَكَلِمَاتِهِ‏ وَٱت َّبِعُوهُ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تَهْتَدُونَ‏ ﴾

Qul ya ayyuha alnnasu innee rasoolu Allahi ilaykum jameeAAan alladhee lahu

mulku alssamawati waal-ardhi la ilaha illa huwa yuhyee wayumeetu faaminoo

biAllahi warasoolihi alnnabiyyi al-ommiyyi alladhee yu/minu biAllahi wakalimatihi

waittabiAAoohu laAAallakum tahtadoona(Surat Al Araf 7:158)

Tafsir: Sema (Ewe Muhamamd): ‘Enyi watu hakika mimi ni Mtume wa Allah juu yenu

nyote, (Allah) ambae ndie mmiliki wa kila kilichomo Mbinguni na Ardhini, na hakuna

Mola isipokua yeye ambae ni mwenye kusababisha uhai na ni mwenye kusababisha

kifo, hivyo Muaminini Allah na Mtume wake (Muhammad Salallahu Alayhi wa

Salam) na Nabii wake asiejua kuandika wala kusoma ambae ni mwenye kumuamini

Allah na Kauli yake, hivyo nifuateni mpate kuongoka.’

Ambapo amesema Jabir Ibn Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakika mimi nimepewa mambo matano ambayo

hakuna Mtume aliepewa hapo kabla. Kwanza: Nimesaidiwa kua na hali ya

kuogopewa kwa masafa ya umbali wa safari ya Mwezi mmoja. Pili: Ardhi yote

imetangaziwa kua ni Tohara kwa jili yangu, hivyo popote pale mtu atakapokuwepo

anaweza Kusali wakati mda unapomfikia; Tatu: Ngawira ya Vita imehalalishwa

juu yangu, kwani ilikua ni haramu kwa mtu yeyote yule kabla yangu; Nne:

Nimejaaliwa kua na Uombezi Katika Siku ya Malipo na Tano: Kabla yangu Mitume

walitumwa kwa watu wao tu lakini mimi nimetumwa kwa Watu wote’’."(Sahih

Muslim)


716

Ambapo miongoni mwa mambo haya aliyoyaainisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kwenye Hadith hii basi pia yameainishwa kwenye Aya zifuatazo:

Kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amepewa Haki ya kua Shahidi na Kua

Mombezi katika Siku ya Malipo:

‏﴿وَكَذٰ‏ لِكَ‏ جَعَلْنَاكُمْ‏ أُم َّةً‏ وَسَطاً‏ لِّتَكُونُواْ‏ شُهَدَآءَ‏ عَلَى ٱلن َّاسِ‏ وَيَكُونَ‏ ٱلر َّسُولُ‏ عَلَيْكُ‏ مْ‏

شَهِيداً‏ وَمَا جَعَلْنَا ٱلْقِبْلَةَ‏ ٱل َّتىِ‏ كُنتَ‏ عَلَيْهَآ إِلا َّ

لِنَعْلَمَ‏ مَن يَت َّبِعُ‏ ٱلر َّسُولَ‏ ممِ َّن يَنقَلِ‏ ‏ُب

ٰ عَلَى عَقِبَيْهِ‏ وَإِن كَانَتْ‏ لَكَبِيرَةً‏ إِلا َّ عَلَى ٱل َّذِينَ‏ هَدَى ٱهلل َُّ‏ وَمَا كَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ لِيُضِي ‏َع

إِيمَانَكُمْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ بِٱلن َّاسِ‏ لَرَءُوفٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Wakadhalika jaAAalnakum ommatan wasatan litakoonoo shuhadaa AAala alnnasi

wayakoona alrrasoolu AAalaykum shaheedan wama jaAAalna alqiblata allatee

kunta AAalayha illa linaAAlama man yattabiAAu alrrasoola mimman yanqalibu

AAala AAaqibayhi wa-in kanat lakabeeratan illa AAala alladheena hada Allahu

wama kana Allahu liyudheeAAa eemanakum inna Allaha bialnnasi laraoofun

raheemun (Surat Al Baqarah, 2:143).

Tafsir: Na Kadhalika tumekujaalieni kua ni umma wa Kati na Kati ili mpate kua

Mashahidi Juu ya Watu na ili awe Shahidi Mtume juu yenu, na tumekijaalia Kibla

ambacho Mlikua Mkikieleka, kwa ajili ya kuwajaribu wale watakaomfuata Mtume

kutokana na watakaomgeuka, kwa hakika hili lilikua ni jambo kubwa isipokua kwa

wale ambao walioongozwa na Allah. Na Allah kamwe hawezi kuifanya ipotee Imani

yenu (Katika Ibada mlizofanya hapo kabla), kwa hakika Allah juu ya Watu ni

Mkarimu na ni mwingi wa Rehma.

Kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amepandishwa Darja ya kuifikia Maqam

Al Mahmudan ambayo ni sehemu ya Darja isiyowezekana kufikiwa na kiumbe yeyote

isipokua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam:

‏﴿وَمِنَ‏ ٱلْل َّيْلِ‏ فَتَهَج َّدْ‏ بِهِ‏ ‏َفِلَةً‏ ل َّكَ‏ عَسَى ٰ أَن يَبْعَثَكَ‏ رَب ُّكَ‏ مَقَ‏ اماً‏ مح َّْمُوداً‏ ﴾


717

Wamina allayli fatahajjad bihi nafilatan laka AAasa an yabAAathaka rabbuka

maqaman mahmoodan(Surat al-Isra, 17:79).

Tafsir: Na katika sehemu ya Usiku Sali Tahajjud ndani yake kama Sunna kwa ajili

yako huenda akakupandisha Mol wako katika Maqaman Mahmudan.

Kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amepewa Darja na Kuahidiwa

kuaminiwa na Mitume wengine Wote:

‏﴿وَإِذْ‏ أَخَذَ‏ ٱهلل َُّ‏ مِيثَاقَ‏ ٱلن َّبِيِّينَْ‏ لَمَآ آتَيْتُكُمْ‏ مِّنْ‏ كِتَابٍ‏ وَحِ‏ كْمَةٍ‏ ثمُ َّ جَ‏ آءَكُمْ‏ رَسُولٌ‏

م ُّصَدِّقٌ‏ لِّمَ‏ ا مَعَكُمْ‏ لَتُؤْ‏ مِ‏ نُن َّ بِهِ‏ وَلَتَ‏ نْصُرُن َّهُ‏ قَالَ‏ أَأَقْرَرْتمُْ‏ وَأَخَ‏ ذْ‏ تمُْ‏ عَلَى ٰ ذٰ‏ لِكُ‏ مْ‏ إِصْرِى

قَالُو ۤ اْ‏ أَقْرَرَْ‏ قَالَ‏ فَٱشْهَدُواْ‏ وَأََْ‏ مَعَكُمْ‏ مِّنَ‏ ٱلش َّاهِدِينَ‏ ﴾

Wa-idh akhadha Allahu meethaqa alnnabiyyeena lama ataytukum min kitabin

wahikmatin thumma jaakum rasoolun musaddiqun lima maAAakum latu/minunna

bihi walatansurunnahu qala aaqrartum waakhadhtum AAala dhalikum isree qaloo

aqrarna qala faishhadoo waana maAAakum mina alshshahideena(Surat Al Imran

3:81).

Tafsir: Na kumbuka tulipochukua Ahadi kutoka kwa Manabii tukiwaambia:

‘Chukueni kile tunachokupeni kutoka katika Kitabu na Hikma, na kisha atakuja

baada yenu Mtume atakaesadikisha mlichokuja nacho. Hivyo ni lazima juu yenu

Kumuamini na Kumsaidia; Allah akasema: Hivi Jee mnakubali na Makubaliano

yangu? Nao (Mitume) wakasema: ‘Tumekubali’ nae (Allah Subhanah wa Ta’ala)

Akasema: ‘Basi Shuhudieni, na Mimi nipo pamoja nanyi kua ni miongoni mwa mwa

Wanaoshuhudia’’

Kua Sifa zake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam zinajulikana na Watu wa Ahl

ul Kitab kama zinavyosema aya:


718

ُ

‏﴿وَلَم َّا جَآءَهُمْ‏ كِتَابٌ‏ مِّنْ‏ عِندِ‏ ٱهلل َِّ‏ مُصَدِّقٌ‏ لِّمَا مَعَهُمْ‏ وَكَانُواْ‏ مِن قَبْل

يَسْتَفْتِحُونَ‏ عَلَى ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ فَلَم َّا جَآءَهُمْ‏ م َّا عَرَفُواْ‏ كَفَرُواْ‏ بِهِ‏ فَلَعْنَةُ‏ ٱهلل َِّ‏ عَلَى

ٱلْكَافِرِينَ‏ ﴾

Walamma jaahum kitabun min AAindi Allahi musaddiqun lima maAAahum

wakanoo min qablu yastaftihoona AAala alladheena kafaroo falamma jaahum ma

AAarafoo kafaroo bihi falaAAnatu Allahi AAala alkafireena (Surat Al Baqarah,

2:89).

Tafsir: Na (Mayahudi na Wakristo) kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allah chenye

kuthibitisha juu ya vile walivyokua navyo wao, ingawa hapo kabla walikua wakiomba

ushindi juu ya wale waliokua wakikufuru, na kisha kilipowajia kile wanachokijua

wakakufuru juu yake hivyo laana ya Allah iwe juu ya Makafiri.

Na pale ziliposema aya kuhusiana na kujulikana kwake Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam na watu wa Ahl ul kitab kua:

‏﴿ٱل َّذِينَ‏ آتَيْنَاهُمُ‏ ٱلْكِتَابَ‏ يَعْرِفُونَهُ‏ كَمَا يَعْرِفُونَ‏ أَبْنَاءَهُمْ‏ وَإِن َّ فَ‏ رِيقاً‏ مِّنْهُمْ‏

لَيَكْتُمُونَ‏ ٱلحَْق َّ وَهُمْ‏ يَعْلَمُونَ‏ ﴾

Alladheena ataynahumu alkitaba yaAArifoonahu kama yaAArifoona abnaahum

wa-inna fareeqan minhum layaktumoona alhaqqa wahum yaAAlamoona (Surat al-

Baqarah, 2:146).

Tafsir: Wale ambao tumewapa Kitabu wanamjua (Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam) kama wanavyowajua Watoto wao na kwa hakika baadhi miongoni mwao

wanauficha ukweli wakati wanaujua ukweli.

Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Naapa kwa yule ambae

mkono wake uko kwenye Roho yangu, hakuna Mkristo wala Yahudi wa Ummah

huu atakaesikia kuhusiana nami na kisha akafa bila ya kuamini juu ya ujumbe

wangu, isipokua atakua ni Mtu wa Motoni’(Sahih Muslim)

Kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakutumwa kwa Ibn Adam tu bali pia

hata kwa Majini kama zinavyosema Aya:


719

‏﴿وَإِذْ‏ صَرَفْنَآ إِلَيْكَ‏ نَفَراً‏ مِّنَ‏ ٱلجِْنِّ‏ يَسْتَمِعُونَ‏ ٱلْقُرْآنَ‏ فَلَم َّا حَضَرُوهُ‏ قَالُو ۤ اْ‏ أَنصِتُ‏ واْ‏

فَلَم َّا قُضِىَ‏ وَل َّوْاْ‏ إِلىَٰ‏ قَوْمِهِم م ُّنذِرِينَ‏ ﴾

Wa-idh sarafna ilayka nafaran mina aljinni yastamiAAoona alqur-ana falamma

hadharoohu qaloo ansitoo falamma qudiya wallaw ila qawmihim mundhireena

(Surat al-Akhaf 46:29)

Tafsir: Na kumbuka (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) tulipokutumia

wewe kwa Kikundi cha Majini kusikiliza Qur’an, na kisha walipohudhuria wakasema:

‘Kaeni Kimya’ na ilipomalizika wakarudi kwa Jamii yao huku wakiwa Wausiaji.

Kua wake zake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ni Mama wa Waumini kama

zinavyosema Aya:

﴿ ٱلن َّبىِ‏ ُّ

أَوْ‏ لىَٰ‏ بِٱلْمُ‏ ؤْ‏ مِ‏ نِينَ‏ مِ‏ نْ‏ أَنْفُسِ‏ هِ‏ ‏ْم

وَأَزْوَاجُهُ‏ أُم َّهَاتُهُ‏ ‏ْم﴾‏

Alnnabiyyu awla bialmu/mineena min anfusihim waazwajuhu ommahatuhum

(Surat Al Ahzab 33:6).

Tafsir: ‘Nabii yuko karibu na Waumini kuliko wao na Nafsi zao, na wake zake ni

mama zao (kwa waumini, kuwaheshimu na kutowaoa)’

Kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amesamehewa Dhambi zake zote

zilizotangulia hapo kabla yake na zilizofuatia baada yake:

‏﴿لِّيَغْفِرَ‏ لَكَ‏ ٱهلل َُّ‏ مَا تَقَد َّمَ‏ مِن ذَنبِكَ‏ وَمَا أتََخ َّرَ‏ وَيُتِم َّ نِعْمَتَ‏ هُ‏ عَلَيْكَ‏ وَيَهْدِيَكَ‏

صِرَاطاً‏ م ُّسْتَقِيماً‏ ﴾

Liyaghfira laka Allahu ma taqaddama min dhanbika wama taakhkhara

wayutimma niAAmatahu AAalayka wayahdiyaka siratan mustaqeeman (Surat Fath

48:2)


720

Tafsir: Amekusamehe (Wewe Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam) Allah katika

yaliyopita Katika Dhambi zako na yatakayokuja, na amekamilisha Neema yake juu

yako na amekuongoza katika njia iliyonyooka.

Kua ameahidiwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua Dini yake aliyokuja

nayo itakua juu na kuhifadhiwa:

‏﴿هُوَ‏ ٱل َّذِي ۤ أَرْسَلَ‏ رَسُولَهُ‏ بِٱلهُْدَىٰ‏ وَدِينِ‏ ٱلحَْقِّ‏ لِيُظْهِرَهُ‏ عَلَى ٱلدِّينِ‏ كُلِّهِ‏ وَلَوْ‏ كَرِهَ‏

ٱلْمُشْرِكُونَ‏ ﴾

Huwa alladhee arsala rasoolahu bialhuda wadeeni alhaqqi liyudhhirahu AAala

alddeeni kullihi walaw kariha almushrikoona (Surat al-Tawbah, 9:33)

Tafsir: Ni yeye ndie ambae aliemtuma Mtume wake na Uongofu na Dini ya Haki

ambayo inajidhidhirisha juu ya Dini zote, japo kua inawakirihisha Makafiri.

Kua Malaika walikua ni wenye kumsaidia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kila mara inapohitajika:

‏﴿قَدْ‏ كَانَ‏ لَكُمْ‏ آيَةٌ‏ فىِ‏ فِئَتَينِْ‏ ٱلْتَقَتَا فِئَةٌ‏ تُقَاتِلُ‏ فىِ‏ سَبِيلِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَأُخْرَىٰ‏ كَ‏ افِرَةٌ‏

يَرَوْنَهُمْ‏ مِّثْلَيْهِمْ‏ رَأْىَ‏ ٱلْعَينِْ‏ وَٱهلل َُّ‏ يُؤَيِّدُ‏ بِنَصْرِهِ‏ مَن يَشَآءُ‏ إِ‏ ن َّ فىِ‏ ذٰلِكَ‏ لَعِبْرَةً‏ لِأُوْلىِ‏

ٱلأَبْصَارِ‏ ﴾

Qad kana lakum ayatun fee fi-atayni iltaqata fi-atun tuqatilu fee sabeeli Allahi

waokhra kafiratun yarawnahum mithlayhim ra/ya alAAayni waAllahu yu-ayyidu

binasrihi man yashao inna fee dhalika laAAibratan li-olee al-absari(Surat Al Imran,

3:13).

Tafsir: Kwa hakika tayari (Katika vita vya Badr) imeshakujieni Dalili katika pande

mbili za Majeshi zilizokutana , ambapo Moja walikua wanapigana kwa ajili ya Allah

na pande nyegine kwa Ukafiri Wao (Waumini) Wameona Makafiri kwa macho yao

mara mbili zaid yao (Wingi wao) na Allah huwasaidia kwa ushindi wake yule amtakae.

Hakika katika haya kuna dalili kuna Somo kwa wale wenye kuona.


721

Kua Kumtii Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hua ni Kumtii Allah Subhanah

wa Ta’ala kama zinavyosema Aya:

‏﴿م َّنْ‏ يُطِعِ‏ ٱلر َّسُولَ‏ فَقَدْ‏ أَطَاعَ‏ ٱهلل ََّ‏ وَمَن تَوَلى َّ ٰ فَمَآ أَرْسَلْنَاكَ‏ عَلَيْهِمْ‏ حَفِيظاً‏ ﴾

Man yutiAAi alrrasoola faqad ataAAa Allaha waman tawalla fama

arsalnaka AAalayhim hafeedhan (Surat al-Nisa, 4:80).

Tafsir: Yule atakaemtii Rasul (Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi hua ni sawa na

mwenye)Kumtii Allah Subhanah wa Ta’ala na Mwenye kumpa mgongo basi

hatukukutuma wewe (Muhamamd Salallahu Alayhi wa Salam) kua ni Msimamizi wao.

Kua Ummah wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ndio Ummah bora Kuliko

Ummah zote kama zinavyosema Aya:

‏﴿كُنْتُمْ‏ خَيْرَ‏ أُم َّةٍ‏ أُخْرِجَتْ‏ لِلن َّاسِ‏ أتَْمُرُونَ‏ بِٱلْمَعْرُوفِ‏ وَتَنْهَوْنَ‏ عَنِ‏ ٱلْمُنْكَرِ‏

ت ‏َو ُؤْمِنُو نَ‏ بِٱ آ هلل َِّوَلَوْ‏ أ َ مَنَ‏ هْلُ‏ ٱلْكِتَابِ‏ لَكَانَ‏ خَيرْ‏ اً‏ له َُّمْ‏ مِّنْهُمُ‏ ٱلْمُؤْمِنُونَ‏ وَأَكْثَرُهُ‏ مُ‏

ٱلْفَاسِ‏ قُونَ‏ ﴾

Kuntum khayra ommatin okhrijat lilnnasi ta/muroona bialmaAAroofi

watanhawna AAani almunkari watu/minoona biAllahi walaw amana ahlu alkitabi

lakana khayran lahum minhumu almu/minoona waaktharuhumu alfasiqoona

(Surat Al Imran 3:110).

Tafsir: Hakika Nyinyi ndio Umma Bora uliotokana na Watu, kwani mnaamrishana

Mema na kukatazana Mabaya na Mnamuamini Allah na lau kama wangeamini watu

wa Ahli Kitabu ingekua bora kwao, kwani miongoni mwao kuna baadhi wenye Imani.

Kua Uhai wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam umeapiwa Ndani ya Qur’an

kama zinavyoonesha Aya:

‏﴿لَعَمْرُكَ‏ إِن َّهُمْ‏ لَفِى سَكْرَهتِِمْ‏ يَعْمَهُونَ‏ ﴾


722

LaAAamruka innahum lafee sakratihim yaAAmahoona (Surat Al-Hijr, 15:72)

Tafsir: Kwa Hakika Naapa kwa Uhai wako, kua Katika kuchanganyikiwa kwao

wamekua ni wenye kutojua wanaeleeka wapi.

Kua Mji wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam umeapiwa Ndani ya Qur’an

kama zinavyoonesha Aya:

﴿ بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰ‏ نِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞لاَ‏ أُقْسِ‏ مُ‏ هبَِٰذَا ٱلْبَلَدِ۞وَأَنتَ‏ حِ‏ ل ٌّ هبَِ‏ ٰذَا ٱلْبَلَدِ‏ ﴾

Biismi Allahi AlrRahmani AlrRahim; La oqsimu bihadha albaladi; Waanta hillun

bihadha albaladi (Surat al-Balad, 90:1-3)

Tafsir: Kwa Jina La Allah Mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma, Hakika mimi

Nnaapa kwa Mji huu; Nawe uko huru katika Mji huu.

Kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Ummah wake umejaaliwa Usiku wa

Laylat ul Qadr kama zinavyoonesha Aya:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞إِ َّ أَنزَلْنَاهُ‏ فىِ‏ لَيْلَةِ‏ ٱلْقَدْرِ۞وَمَ‏ آ أَدْرَاكَ‏ مَا لَيْلَةُ‏

ٱلْقَدْرِ۞لَيْلَةُ‏ ٱلْقَدْرِ‏ خَيْرٌ‏ مِّنْ‏ أَلْفِ‏ شَهْرٍ۞تَنَز َّلُ‏ ٱلْمَلاَئِكَةُ‏ وَٱلر ُّوحُ‏ فِيهَا إبِِذْنِ‏ رَهبِِّم

ّ ل أَمْ‏ رٍ۞سَلاَمٌ‏ هِىَ‏ حَتى َّ ٰ مَطْلَعِ‏ ٱلْفَجْرِ‏ ﴾

مِّ‏ ن كُ‏ ِ

Biismi Allahi AlrRahmani AlrRahim Inna anzalnahu fee laylati alqadri; Wama

adraka ma laylatu alqadri; Laylatu alqadri khayrun min alfi shahrin; Tanazzalu

almala-ikatu waalrroohu feeha bi-idhni rabbihim min kulli amrin; Salamun hiya

hatta matlaAAi alfajri (Surat Al Qadr 97:1-6)

Tafsir: Kwa Jina La Allah Mwingi wa Rehema mwingi wa Huruma, Hakika

tumeishusha (Qur’an) ndani ya usiku wa Al Qadr; Na jee ni nini kitakachokujuulisha

ni nini huo Usikua wa Al Qadr?; Usiku wa Al Qadr ni bora kuliko Miezi Alfu Moja;

Ndani yake anashuka Malaika na Ruhi kwa Idhini ya Mola wake juu ya kila kitu;

Usalama hutawala ndani yake hadi inapoingia Alfajir.


723

Ambapo mbali ya kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam amejaaliwa Miujiza ya

Usiku wa Laylat ul Qadr unaowakilisha kushushiwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kitabu kitukufu cha Qur’an lakini pia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alijaaliwa Laylat ul Miraj ambao ni Usiku unaowakilisha kupandishwa kwake Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kutoka ardhini kuelekea Mbinguni kwa Allah Subhanah

wa Ta’ala.

SAFARI YA ISRA NA MIRAJ.

Mnamo Mwaka wa 9 wa Uislam Allah Subhanah wa Ta’ala alimpandisha Mtume wake

Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam Mbinguni katika Usiku unaojulikana kua kama

Usiku wa Miraj ambamo ndani yake mlitokea tukio ambalo Allah Subhanah wa Ta’ala

analithibitisha na kulielezea katika Sura mbili tofauti ambapo moja wapo ni ile

inayojulikana kama Surat Al Isra au pia kama Surat Bani Israil ambamo ndani yake

limeelezewa tukio la safari ya Isra ambayo ilifanyika katika Mazingira ya Ulimwengu

Unaoonekana na Ibn Adam yaani Alam Al Mulk wa Al Shahadah kwa kusema:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰ‏ نِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞‏ سُبْحَانَ‏ ٱل َّذِى أَسْرَىٰ‏ بِعَبْدِهِ‏ لَيْلاً‏ مِّنَ‏ ٱلْمَ‏ سْجِ‏ دِ‏

ٱلحَْرَامِ‏ إِلىَٰ‏ ٱلْمَسْجِ‏ دِ‏ ٱلأَقْصَى ٱل َّذِى ابَرَكْنَا حَوْلَهُ‏ لِنُرِيَهُ‏ مِنْ‏ آَتِنَآ إِن َّهُ‏ هُوَ‏ ٱلس َّمِ‏ يعُ‏

ٱلبَصِيرُ‏ ﴾

Bismi Allahi Alrrahmani Alrrahim; Subhana alladhee asra biAAabdihi laylan mina

almasjidi alharami ila almasjidi al-aqsa alladhee barakna hawlahu linuriyahu min

ayatina innahu huwa alssameeAAu albaseeru (Surat Al Isra 17:1)

Tafsir: Utukufu ni wake yule ambae amemsafirisha Usiku Mja wake katika Usiku

kutoka katika Masjid Al Haram kueleka katika Masjid Al Aqsa ambao ameyabariki

maeneo yake kwa ajili ya kumuonesha Dalili zetu, kwani kwa hakika yeye ni mwingi

wa kusikia na ni mwenye kuona juu ya kila kitu.

Neno Asra linatokana na neno Sara ambalo hua linamaanisha Kusafiri katika wakati wa

Usiku, hivyo neno Asra hua linamaanisha Yule ambae aliemfanya Mtu asafiri Usiku.

Ambapo kwa upande wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari basi yeye

anahoji kwa kusema : ‘Hivi kwa nini Allah Subhanah wa Taa’ala akatumia neno

Laylan ambalo ni lenye kumaanisha Usiku wakati tayari aya imetumia neno Asra

ambalo linamaanisha kutembea Usiku? Hivyo jibu la suali hili ni kua kusisitiza


724

kuhusiana na hii Safari ambayo kawaida hua ni ya Miezi kadhaa lakini hii ilitokea

ndani ya sehemu ya Usiku mmoja tu’

Ambapo kuhusiana na Masjid Al Haram umeitwa hivyo kwa sababu ndani ya eneo lake

mna mambo ambayo yameharamishwa lakini nje yake na sehemu nyengine basi

yamehalalishwa kufanyika kwa mfano, Hairuhusiki ndani yake Kuingia asiekua

Muislam, Kung’olewa majani, Kukata miti, na Kuwinda Wanyama ndani ya eneo la

Masjid Haram hua hakuruhusiki.

Ama kwa upande wa Masjid Al Aqsa basi umeitwa hivyo kwa sababu upo katika ardhi

ya Jersualem ambayo ni Ardhi Takatifu ambayo ipo mbali kimasafa kutoka katika Masjid

Al Haram.

Ambapo aya imetumia pia neno Abd ambalo hua linamaanisha Mja na hivyo kumaanisha

kua Safari hio ilifanyika kwa Kimwili na Kiroho ambapo ndio pia neno lililotumika

kwenye tukio la pili ndani ya Usiku huu ni lile la safari ya kuanzia kwenye Masjid Al

Aqsa kuelekea Mbinguni ambalo linajulikana kama tukio la safari ya Miraj.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipowasili katika Ardhi ya Bayt Al

Maqdis ambapo alikutana na Mitume wote waliotangulia hapo kabla na kisha

akawasalisha ndani ya Msikiti huo wa Al Aqsa na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kua ni mwenye kudhihirisha kua Dini ya Kiislam ndio Dini ya asili, ya

Mwanzo na ya Mwisho na ya Ulimwengu mzima, tangu mwanzo wa kuumbwa

kwake hadi mwisho wake Ulimwengu huu.

Ambapo anasema Allamah Badr Ad Din Al Ayni Al Hanafi kua: ‘Tunapoangalia suali

la kwanini Nabii Ibrahim akawa ni Nabii Pekee alietajwa kwenye Sala (katika

Attahiyat) basi jibu lake ni kua: ‘Katika Usiku wa Miraj, Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alikutana na Mitume wote, na akawasalimia, lakini hakuna Mtume

ambae alirudisha Salam kwa Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam huku

akimjumuishia Umma wake wote isipokua Nabii Ibrahim, na hivyo basi ndio maana

Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam akauamrisha Ummah wake Kumsalia Nabii

Ibrahim kutokana na ukarimu wake huo kwa Ummah wake. ’’

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akapelekwa katika Hatim Sharif

akapokewa na Hur Layn ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliwasalimia

na kisha nao wakamrudishia Salam hio, kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akashushiwa Ngazi ambayo ni hakuna kiumbe aliewahi kuona kitu kizuri kama hicho,

ambacho kina vidaraja vilivyopishana vya Dhahabu na Fedha, na kua ni yenye kushuka

moja kwa moja kutoka Peponi huku ikiwa imezungushiwa mapambo ya Lulu na Malaika

kushoto na kulia.


725

Ambapo anasema Imam Muhammad Ibn Is-haq kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam amesema kua: ‘Ngazi iliyoshushwa kwangu mie ilikua ni nyororo kuliko kitu

chochote kile nilichowahi kukiona, kwani ndio kitu anachokiangalia Mtu pale

anapotolewa roho.’’

Ambapo tunapoangalia mapambo haya ya Dhahabu na Fedha basi tunaona kua haya ni

Madini ambayo yana sifa za upekee katika usafirishaji wa nguvu za Umeme, ambapo

Fedha ndio Madini yenye kutegemewa kwa kua na asilimia 105% ya kasi ya usafirishaji

wa nguvu ya Umeme, na upekee wa urudishaji wa Nuru wa hali ya juu kabisa, na hii hua

ni kutokana na kutoshikamana kwa elektroni zake ambao unazifanya ziwe huru na

kurahisisha zaidi usafirishaji wa Nguvu za Umeme.

Ambapo kwa upande wa Dhahabu basi ni Madini yanayoongoza kwa Umakini wa

Kutopoteza nguvu za Umeme, na ndio maana hua inatumika katika viunganisho vya

mifumo ya vifaa mbali mbali vya Umeme na chenye kuchukua sehemu ya tatu katika

usafirishaji wa umeme baada ya Shaba kwa kua na uwezo wa kusafirisha kwa kasi ya

asilimia 70%.

Hivyo mchanganyiko huu wa Madini haya katika kupitisha na kusafirisha kwake nguvu

ya Umeme au pia nguvu ya Nuru yameufanya mfumo wa Ngazi hio ya Miraj kua na

upekee wa kasi ya Usafirishaji wake, yaani hali yake inakua kama vile ukiigusa tu basi

Umefika.

Ambapo neno Miraj hua linamaanisha Ngazi au Kipandio cha Kuelekea Juu ambapo

tukio la safari hii nalo limeelezewa kwenye aya za Surat An Najm ambazo zinasema kua:

ٰ ‏﴿فَأَوْحَى إِلىَٰ‏ عَبْدِهِ‏ مَآ ٰ أَوْحَى۞‏ مَا كَذَبَ‏ ٱلْفُؤَادُ‏ مَا رَأَىٰ‏ ۞ أَفَتُمَ‏ ارُونَ‏ هُ‏ ٰ عَلَى مَا

وَلَقَدْ‏ رَآهُ‏ نَزْلَةً‏ أُخْرَىٰ‏ ۞ عِن دَ‏ سِ‏ دْ‏ رَةِ‏ ٱ ن ت لُْم َ‏ هَ‏ ٰ ى ۞ عِندَهَا جَن َّةُ‏ ٱلْمَأْوَىٰ‏ ۞ إِْذ

يَغْشَىٰ‏ ٱلسِّ‏ دْرَةَ‏ مَا ٰ يَغْشَى۞‏ مَا زَاغَ‏ ٱلْبَصَرُ‏ وَمَا ٰ طَغَى۞‏ لَقَدْ‏ رَأَىٰ‏ مِنْ‏ آَ‏ تِ‏ رَبِّهِ‏

ٱلْكُبْرَىٰ‏ ﴾

يَرَىٰ‏ ۞

Faawha ila AAabdihi ma awha; Ma kadhaba alfu-adu ma raa; Afatumaroonahu

AAala ma yara; Walaqad raahu nazlatan okhra; AAinda sidrati

almuntaha; AAindaha jannatu alma/wa; Idh yaghsha alssidrata ma yaghsha; Ma

zagha albasaru wama tagha; Laqad raa min ayati rabbihi alkubra (Surat An Najm

53:10-18)


726

Tafsir: Hivyo akamshushia Mja wake kile alichomshushia, Hakikadhibishi Kifua

chake kutokana na aliyoyaona. Hivi Jee mtabishana nae (Muhammad Salallahu

Alayhi wa Salam) Juu ya kile alichokiona? (Katika Safari ya Miraj); Na bila ya shaka

alimuona tena katika mteremko wa Pili; Karibu na Sidrat Ul Muntaha (Mti ambao

ndio Mpaka wa eneo ambalo haiwezekani kwa kiumbe yeyote kusogea Mbele yake);

Karibu yake ambapo kuna Makaazi ya Pepo (Katika Upande wa Kulia wa Arshi

Tukufu); Wakati pale kilichoufunika Mti wa Sidrat Al Muntaha kilipoufunika;

Haukugeuka Mtizamo (wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam) wala haukuvuka

mpaka; Kwani kwa Hakika ameona (Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam) Katika

Dalili zetu Kubwa sana.

Ambapo tunapoziangalia aya hizi basi tunaona kua zinazungumzia namna ya hali

ilivyokua wakati Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam alipokua katika kumuona

kwake Malaika Jibril na katika Safari ya Miraj ambayo ilifanyika katika Mazingira ya

kuingia ndani ya Ulimwengu Usiionekana na Viumbe Ibn Adam bali Unaonekana na

Viumbe Malaika yaani Al Alam Ghayb wa Al Malakut ambapo anasema Masruq Abu

Aisha kua: ‘Hakika mimi nilikua nimekaa na Aisha ambae alikua ameegemea na

akasema: ‘Ewe Abu Aisha, kuna mambo matatu ambayo kama mtu

atayazungumzia basi atakua ni mwenye kumzulia Allah Subhanah wa Ta’ala’ hivyo

nami nikauliza : ‘Ni Yepi Hayo?’’

Nae akasema: ‘Yeyote yule atakaesema kua Muhammad (Salallahu Alayhi wa

Salam) amemuona Allah Subhanah wa Ta’ala basi amesema uongo kuhusiana na

Allah Subhanah wa Ta’ala’ hivyo nami nikakakaa vizuri kisha nikauliza: ‘Ewe Ummu

Ul Muuminin, niruhusu niseme, usiwe na haraka, hivi Jee Allah Subhanah wa Ta’ala

hakusema kua:

‏﴿وَلَقَدْ‏ رَآهُ‏ بِٱلأُفُقِ‏ ٱلْمُبِينِ‏ ﴾

Walaqad raahu bialofuqi almubeeni (Surat At Takwir 81:23)

Tafsir: Kwa Hakika alimuona katika Upeo wa Macho ulio wazi

Na pia hakusema kua:

‏﴿وَلَقَدْ‏ رَآهُ‏ نَزْلَةً‏ أُخْ‏ رَىٰ‏ ﴾

Walaqad raahu nazlatan okhra; (Surat An Najm 53:13)

Tafsir: Na bila ya shaka alimuona tena katika mshuko wa Pili;?


727

Hivyo Aisha Radhi Allahu Anha akasema: ‘Hakika mimi ndie mtu wa mwanzo katika

Ummah huu kumuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, kuhusiana na hayo

ambapo nae akasema: ‘Huyo alikua ni Jibril, nami sikumuona katika maumbile

yake aliyoumbiwa isipokua mara mbili, na nilimuona akishuka kutoka Mbiguni,

huku akiwa amefunika Upepo wote wa Macho baina ya Mbingu na Ardhi.’’

Na kisha Aisha Radhi Allahu Anha akasema: ‘Hivi jee wewe hujawahi kusikia maneno

ya Allah yasemayo?’

‏﴿لا َّ تُدْرِكُهُ‏ ٱلأَبْصَارُ‏ وَهُوَ‏ يُدْرِكُ‏ ٱلأَبْصَارَ‏ وَهُوَ‏ ٱلل َّطِيفُ‏ ٱلخَْبِيرُ‏ ﴾

La tudrikuhu al-absaru wahuwa yudriku al-absara wahuwa allateefu alkhabeeru

(Surat Al Anaam 6:103)

Tafsir: Haiwezekani kumfikia Mtizamo wa Macho, lakini yeye ni mwenye kuona kila

kitu, kwani yeye ni Mpole na mwenye habari juu ya kila kitu.

Na pale aliposema:

‏﴿وَمَا كَانَ‏ لِبَشَرٍ‏ أَن يُكَلِّمَهُ‏ ٱهلل َُّ‏ إِلا َّ وَحْياً‏ أَوْ‏ مِن وَرَآءِ‏ حِ‏ جَابٍ‏ أَوْ‏ يُرْسِ‏ لَ‏ رَسُولاً‏

فَيُوحِ‏ ىَ‏ إبِِذْنِهِ‏ مَا يَشَآءُ‏ إِن َّهُ‏ عَلِي ٌّ حَكِيمٌ‏ ﴾

Wama kana libasharin an yukallimahu Allahu illa wahyan aw min wara-i hijabin

aw yursila rasoolan fayoohiya bi-idhnihi ma yashao innahu AAaliyyun hakeemun

(Surat Shura 42:51)

Tafsir: Na kamwe haiwezekani kwa Allah kuzungumza na Mtu yeyote isipokua kwa

njia ya Wahyi, au kwa Pazia, au kwa Kumtumia Mjumbe kufikisha Ujumbe kwa Idhini

yake juu ya kile akitakacho, kwani kwa hakika yeye ni mwenye Utukufu na ni mwingi

wa Hikma.

Na pia kua:

‏﴿يَۤ‏ أَي ُّهَا ٱلر َّسُولُ‏ بَلِّغْ‏ مَآ أُنزِلَ‏ إِلَيْكَ‏ مِن ر َّبِّكَ‏ وَإِن لم َّْ‏ تَفْعَلْ‏ فَمَا بَل َّغْتَ‏ رِسَالَ‏ تَهُ‏

وَٱهلل َُّ‏ يَعْصِمُكَ‏ مِنَ‏ ٱلن َّاسِ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لاَ‏ يَهْدِى ٱلْقَوْمَ‏ ٱلْكَافِرِينَ‏ ﴾


728

Ya ayyuha alrrasoolu balligh ma onzila ilayka min rabbika wa-in lam tafAAal fama

ballaghta risalatahu waAllahu yaAAsimuka mina alnnasi inna Allaha la yahdee

alqawma alkafireena (Surat Al Maidah 5:67)

Tafsir: Ewe Mtume fikisha kama ulivyoshushiwa kutoka kwa Mola wako, kwani kama

hukufanya hivyo basi utakua hukufikisha Ujumbe wake, na Allah atakulinda

kutokana na Watu, Kwa hakika Allah hawaongoi watu wenye kukufuru.

Na kisha Aisha Radhi Allahu Anha akasema: ‘Hivyo yeyote yule atakaemsingizia

Mtume Salallahu Alayhi wa Salam alikua anajua kitakachotokea kesho, basi

amesema uongo kuhusiana na Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani Allah Subhanah

wa Ta’ala amesema kua:

‏﴿قُل لا َّ يَعْلَمُ‏ مَن فىِ‏ ٱلس َّمَاواتِ‏ وٱلأَرْضِ‏ ٱلْغَيْبَ‏ إِلا َّ ٱهلل َُّ‏ وَمَا يَشْعُرُونَ‏ أَ َّنَ‏

يُبْعَثُونَ‏ ﴾

Qul la yaAAlamu man fee alssamawati waal-ardhi alghayba illa Allahu wama

yashAAuroona ayyana yubAAathoona (Surat An Naml 27:65)

Tafsir: ‘Sema, Hakuna anaejua yaliyomo Mbinguni na Ardhini yaliyofichikana

ispokua Allah na hakuna anaeona na kujua lini watafufuliwa.

Ambapo amesema Abu Dhar Al Ghifari Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi nilimuuliza

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hivi Jee Ulimuona Mola wako?’ nae

akajibu: ‘Yeye ni Nuru, Hivyo Jee nitamuonaje?’’(Sahih Muslim)

Na kwa upande wa Al Hafidh Imam Abu Hatim Abd Rahman Muhammad Ibn Idris Al

Razi Ibn Hibban Al Basti basi yeye anasema kua: ‘Muhammad Ibn Kaab Radhi Allahu

Anhu amesema kua, wao walimuuliza Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam:

‘Hivi Jee ulimuona Mola wako?’ ambapo nae akasema: ‘Naam nilimuona mara

mbili kwa Mtizamo wa Moyo wangu.’ Na kisha akasoma aya isemayo:

‏﴿مَا كَذَبَ‏ ٱلْفُؤَادُ‏ مَا رَأَىٰ‏ ﴾

Ma kadhaba alfu-adu ma raa; (Surat An Najm 53:11)

Tafsir:Hakikadhibishi Kifua chake kutokana na aliyoyaona.


729

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala alimchukua Mtume wake Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam katika safari ya Isra na Miraj na kumsafirisha ndani ya sehemu ya

Usiku mmoja kutoka katika Masjid Al Haram kuelekea Masjid Al Aqsa na kisha

kumpandisha Juu Mbinguni kwa ajili ya kumuonesha Miujiza Mikubwa sana yaani

Ayati Al Kubra.

Ambapo anasema Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abdallah Al Tustari Al Shafii

kuhusiana na Ayati Al Kubra kua: ‘Hizi ni miongoni mwa Dalili zake zinazodhihirika

kutokana na Dalili zake, na ingawa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliziona,

lakini hakuteteresha mtizamo wake kutokana na anachokishuhudia, na hakutoka

katika eneo la mwenye kuabudiwa, bali kile alichokiona kilikua ni chenye

kumzidishia Mapenzi (Mahabba) yake, Kutamani (Shawq) kwake na Uwezo

(Quwwa) wake.

Kwani Allah Subhanah wa Ta’ala alimpa Uwezo ambao ulimuwezesha kustahmili

muonekano wa Nuru yake, na hivyo hii kua ni sehemu ya Kumpandisha Darja na

kumpendelea Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam zaidi ya Mitume wengine, hivi

Jee hukuona wewe namna Nabii Musa alipozimia kutokana na Muonekano wa

Allah, lakini kwa Muhamamd Salallahu Alayhi wa Salam alistahmili wakati Nuru

hio ilipopita ndani ya Ufaham wake katika kuonana na Mola wake kupitia katika

Mtizamo wa Moyo wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na hapo hapo

kutokana na hali ya Uwezo wake na hivyo akapandishiwa hali ya Darja yake.’

Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abdallah Al Tustari Al Shafii anaendelea kusema kua:

‘Imenifikia mimi kua Allah Subhanah wa Ta’ala alimwambia Nabii Daud kua:

‘Hakikisha kua hughafiliki na mie kwani ikitokea hivyo basi utakosa kila kitu.

Kwani kwa hakika mimi nimemuumba Muhammad kwa ajili yangu, na

nimemuumba Adam kwa Ajili yake, na nimewaumba Viumbe wangu wanaoniamini

kwa ajili ya kuniabudu, na nimeumba kila kitu chengine kwa ajili ya manufaa ya

Ibn Adam, hivyo kama Ibn Adam akitumia mda wake kutokana na kile

nilichomuumbia kwa ajili ya Manufaa yake, basi nitamfunikia pazia juu ya kila kitu

ambacho nimekiumba kwa ajili yangu.’’

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Sultan Mutakalimin Imam Al Mushakikkin

Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisafiri

katika safari mbili, ambapo ya kwanza ni kutoka katika Masjid Al Haram

kuelekea katika Masjid Al Aqsa, na ya pili ni ya kipindi cha Safari ya kuelekea

Juu Mbinguni kwenye Ufalme wa Allah. Ambao huu ni mtizamo ambao

unabainisha yale yaliyotokea dhahiri’

Na tunapozungumzia kuhusiana na yale yaliyotokea kwa upande wa Kiroho

basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisafiri pia katika safari mbili

ambapo kwanza ni hali ya kusafiri kutoa kwenye Ulimwengu Unaoonekana (Al

Alam Al Shahadah) na kuingia kwenye Ulimwengu Usioonekana (Al Alam Al


730

Ghayb) ambapo Ulimwengu miwili hii imepakana ndani ya Masafa ya Baina ya

Mipinde Miwili, kama zilivyosema Aya.

‏﴿فَكَ‏ انَ‏ قَابَ‏ قَوْسَ‏ ينْ‏ ِ أَوْ‏ أَدْ‏ نىَٰ‏ ﴾

Fakana qaba qawsayni aw adna (Surat An Najm 53:9)

Tafsir: Na ilikua ni masafa ya Mipinde Miwili au karibu zaidi.

Hivyo Maneno Fakana qaba qawsayni aw adna hua ni yenye kumaanisha hali ya

Uteketezo wa Nafsi yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo Nafsi

hio kuingia katika hali ya kua na ukaribu sana kwa Mola wake.

Kwani darja ya chini kabisa ya Ulimwengu usioonekana hua ni ile ya Roho ya Ibn

Adam, na Roho ya Ibn Adam hua ni yenye kupanda juu kuanzia kwenye Mbingu

ya chini, na kisha kupanda zaidi kuelekea kwenye darja ukamilifu na furaha na

kisha huingia kwenye hali ya kiroho ya Mbingu ya pili, na kisha hufikia darja ya

wakaazi wa ngazi ya chini ya Arshi, na kisha hufikia Darja ya Malaika ambayo

ndio iliyozungumziwa kwenye aya isemayo:

‏﴿وَتَرَى ٱلْمَلاَئِكَةَ‏ حَآفِّينَ‏ مِنْ‏ حَوْلِ‏ ٱلْعَرْشِ‏ يُسَبِّحُونَ‏ بحَِمْدِ‏ رَهبِِّمْ‏ وَقُضِىَ‏ بَيْنَ‏ هُمْ‏

بِٱلحَْقِّ‏ وَقِيلَ‏ ٱلحَْمْدُ‏ هللِ َِّ‏ رَبِّ‏ ٱلْعَالَمِينَ‏ ﴾

Watara almala-ikata haffeena min hawli alAAarshi yusabbihoona bihamdi

rabbihim waqudhiya baynahum bialhaqqi waqeela alhamdu lillahi rabbi

alAAalameena (Surat Az Zumar 39:75)

Tafsir: Na Utawaona Malaika wakiwa wanazunguka Arshi katika pande zote,

wakimtukuza na kusifu sifa za Mola wao, na (Viumbe wote) watahukumiwa kwa haki

na kisha itasemwa: ‘Sifa zote na Shukrani zote anastahiki Mola wa Ulimwengu’

Na kisha Roho ya Ibn Adam inafika inapanda juu na kufikia darja ya Malaika

waliozungumziwa kwenye aya ifuatayo:

‏﴿وَٱلْمَلَكُ‏ عَلَى ٰ أَرْجَآئِهَآ وَيحَْمِلُ‏ عَرْشَ‏ رَبِّكَ‏ فَوْقَهُمْ‏ يَوْمَئِذٍ‏ ثمََانِيَةٌ‏ ﴾

Waalmalaku AAala arja-iha wayahmilu AAarsha rabbika fawqahum yawma-idhin

thamaniyatun. (Surat Al Haqqah 69: 17).

Tafsir: Na Malaika watakua pembeni mwake na wataibeba Arshi juu yao watakua

Wanane.


731

Ambapo idadi ya nambari nane ina Siri yake ambayo haiwezi kufunguliwa hapa,

Na Roho ya Ibn Adam kisha inafika inapanda juu na kufikia darja ya Roho Tukufu

ambazo hazimo ndani ya Miili, ambazo vyakula vyao Roho hizo hua ni Dhikr Allah,

Vinywaji vyao hu ni Kumpenda Allah Subhanah wa Ta’ala, Starehe yao ni

Kumtumikia Allah Subhanah wa Ta’ala, na ukaribu wao ni Kumsifu Allah

Subhanah wa Ta’ala, hawa ndio wale Malaika waliotajwa kwenye aya zifuatazo:

‏﴿وَلَهُ‏ مَن فىِ‏ ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَمَنْ‏ عِنْدَهُ‏ لاَ‏ يَسْتَكْ‏ برُِونَ‏ عَنْ‏ عِبَادَ‏ تِهِ‏ وَلاَ‏

يَسْتَحْ‏ سِ‏ رُونَ۞‏ يُسَبِّحُونَ‏ ٱلْل َّيْلَ‏ وَٱلن َّهَارَ‏ لاَ‏ يَفْتُرُونَ‏ ﴾

Walahu man fee alssamawati waal-ardhi waman AAindahu la yastakbiroona AAan

AAibadatihi wala yastahsiroona; Yusabbihoona allayla waalnnahara la

yafturoona(Surat Al Anbiyah 21:19-20)

Tafsir: Kwake yeye ndiko kwenye umiliki wa kila kilichoo Mbinguni na Ardhini. Na

wale waliokaribu nae hawana Kiburi cha kutomuabudia yeye si wenye kuchoka katika

Ibada zao; Wanamtukuza Usiku na Mchana bila ya kupumzika.

Ambapo hii hua ni darja ambayo Ufahamu wa Ibn Adam kamwe hauwezi kufahamu hali

yake, na kupanda kwake Roho inapofika katika Darja hii hua ni kwenye kuendelea hadi

pale inapomfikia Muumba, ambae ni Nuru juu ya Nuru, Sababu ya kila Sababu, Mwanzo

wa kila kitu, Chanzo cha Rehma, Asili ya kila Jema kama inavyobainishwa na Aya

isemayo:

ّ كُل ذِى عِلْمٍ‏ عَلِيمٌ‏ ﴾

‏﴿وَفَوْقَ‏ ِ

Wafawqa kulli dhiAAilmin AAaleemun(Surat Yusuf 12:76)

Tafsir: Na Kwa kila alie juu kwa Ilm, basi kuna ajuae zaid.

Wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipopandishwa Juu Mbinguni basi

alisoma aya ya mwisho ya Surat Al Baqara isemayo:

‏﴿لاَ‏ يُكَلِّفُ‏ ٱهلل َُّ‏ نَفْساً‏ إِلا َّ وُسْعَهَا لهََا مَا كَسَبَتْ‏ وَعَلَيْهَا مَا ٱكْتَسَبَتْ‏ رَب َّنَا لاَ‏

تُؤَاخِ‏ ذَْ‏ إِن ن َّسِ‏ ينَآ أَوْ‏ أَخْطَأَْ‏ رَب َّنَا وَلاَ‏ تحَْمِلْ‏ عَلَيْنَآ إِصْراً‏ كَمَا حمََلْتَهُ‏ عَلَى ٱل َّذِي ‏َن


732

مِن قَبْلِنَا رَب َّنَا وَلاَ‏ تحَُمِّلْنَا مَا لاَ‏ طَاقَةَ‏ لَنَا بِهِ‏ وَٱعْفُ‏ عَن َّا وَٱغْفِرْ‏ لَنَا وَٱرْحمَْنَآ أَن ‏َت

مَوْلاََ‏ فَٱنْصُرَْ‏ عَلَى ٱلْقَوْمِ‏ ٱلْكَافِرِينَ‏ ﴾

La yukallifu Allahu nafsan illa wusAAaha laha ma kasabat waAAalayha ma

iktasabat rabbana la tu-akhidhna in naseena aw akhta/na rabbana wala tahmil

AAalayna isran kama hamaltahu AAala alladheena min qablina rabbana wala

tuhammilna ma la taqata lana bihi waoAAfu AAanna waighfir lana wairhamna

anta mawlana faonsurna AAala alqawmi alkafireena.(Surat Al Baqara 2:286)

Tafsir: Haikalifishi Allah Nafsi (ya mtu yeyote)isipokua juu ya kile inachokiweza,

inalipwa (Nafsi ya Mtu) kutokana na (mema) iliyoyachuma na itaadhibiwa kutokana

na (dhambi) ilizozichuma. ‘Ewe Mola wetu Usituadhibu kutokana na tulichokisahau

au tulichokikosea. Ewe Mola wetu usitubebeshe mizigo kama ulivyowabebesha

waliotangulia kabla yetu. Ewe Mola wetu Usitubebeshe mizigo zaidi ya uwezo wetu,

Tusamehe na utuingize kweye Msamaha wako na utuingize kwenye Rehma zako kwani

wewe ndie Msimamizi wetu na tunusuru dhidi ya watu wenye kukufuru’

Na katika kutilia mkazo umuhimu wa Dua iliyomo ndani ya aya hii basi Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam amesema kuhusiana na aya hii pamoja na ile kabla ya aya hii

yaani aya ya 285 ya Surat Al Baqara kua: ‘Hakika mimi nimepewa aya mbili ambazo

zilikuwemo kwenye hazina iliyomo chini ya Arshi, ambazo hakuwahi kupewa

Mtume yeyote yule hapo kabla.’

Na wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipokua akishuka kutoka Mbinguni

basi alisoma Surat al Fatiha ambayo nayo ni yenye aya 7:-

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞ٱلحَْمْدُ‏ هللِ َِّ‏ رَبِّ‏ ٱلْعَالَمِينَ۞ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞مَٰلِكِ‏ يَوْمِ‏

ٱلدِّينِ۞إِ َّ كَ‏ نَعْبُدُ‏ وإِ َّ كَ‏ نَسْتَعِينُ۞ٱهْدَِ‏ ٱلصِّرَاطَ‏ ٱلْمُسْتَقِيمَ۞‏

أَنْعَمْ‏ تَ‏ عَلَيْ‏ هِمْ‏ غَيرِْ‏ ٱلْمَغْضُوبِ‏ عَلَيْهِم وَلاَ‏ ٱلض َّآلِّينَ‏ ﴾

‏ِصرَاطَ‏ ٱل َّذِينَ‏

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Alhamdu lillahi rabbi alAAalameena;

Alrrahmani alrraheemi; Maliki yawmi alddeeni; Iyyaka naAAbudu wa-iyyaka

nastaAAeenu; Ihdina alssirata almustaqeema; Sirata alladheena anAAamta

AAalayhim ghayri almaghdoobi AAalayhim wala aldhdhalleena (Surat Al Fatiha

1:1-7)


733

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwingi wa Huruma; Shukrani zote

anastahiki Mola wa Ulimwengu wote na kila kilichomo ndani ndani yake; Mfalme wa

Siku ya Malipo, Ni wewe tu ndie tunaekuabudu na ni wewe tu tunaekuomba msaada;

Tuongoze kwenye njia iliyonyoooka; Njia ya wale ambao umewaneemesha, na wala

sio njia ya wale uliowaghadhibikia na wala sio ya wale waliopotea.

Hivyo katika tukio hili la Miraj katika kushuka kwake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam basi athari ya Nuru ya Rehma yake aya hizi za Surat Al Fatiha zilikua

zikimmiminikia na kumdhihirikia kutoka kwenye Ulimwengu wa Ghayb wa kiroho na

kuingia kwenye Ulimwengu wa Dhahir wa kimwili, hivyo kila mtu anaesoma Surat Al

Fatiha katika Sala basi hua ni mwenye kumiminikiwa na athari ya Nuru ya Rehma yake

kutoka kwenye Ulimwengu wa Ghayb kuingia kwenye Ulimwengu wa Dhahir kama

alivyomiminikiwa na kudhihirikiwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipokua

akirudi katika safari ya Miraj, na hivyo kua ni kiunganisho baina ya aina mbili hizo za

Ulimwengu na ndio maana akasema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Sala

ndio Miraj ya Waumini.’

Ambapo kwa upande wa Imam Abu Bakr Ibn Abd Allah Ibn Muhammad Najm Al

Din Raz anasema kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua ni mwenye

Miujiza ya kusafiri kwa njia ya haraka na kuvuka mipaka ya kimaumbile na

kuingia kwenye hali ya mazingira ambayo waliishi Mitume waliotangulia hapo

kabla yake, huku kila mmoja wao Mitume hao akiwa ni mwenye kubakia

kwenye hali ya darja yake husika.

Kwa mfano: Nabii Adam ambae alikua kwenye darja yake ya hali ya kua

Aliechaguliwa, Nabii Nuh ambae alikua kwenye Darja yake ya Ukaribisho,

Nabii Ibrahim ambae alikua katika Darja yake ya Urafiki wa Karibu, Nabii

Musa ambae alikua kwenye Darja yake ya kua ni Mwenye Kuzungumza na

Allah, Nabii Isa Ibn Maryam ambae alikua kwenye Darja yake ya Kauli ya

Allah na Utambulisho, Nabii Daud akiwa kwenye Darja ya Ukhalifa na Nabii

Sulaiman akiwa kwenye Darja ya Ufalme.

Lakini kwa upande Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kutokana na Rehma

za Mola wake na Msaada wake basi yeye alifanikiwa kuzipita Darja zote hote

hizo za Kiroho na kuingia kwenye hali ambayo hakuna Kiumbe aliewahi

kuruhusiwa kuifikia na hivyo kua ni mwenye kupewa heshima kubwa sana

ambayo hajawahi kupewa kiumbe yeyote yule hapo kabla.’ (Mirsad Al 'Ibad)

Hivyo kuhusiana na safari ya Isra na Miraj basi anasema Fakhta Ummu Hani Bint Abu

Talib kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alichukuliwa katika safari yake

ya Usiku akitokea kwangu mie ambapo alisali Sala zake za Usiku na kila Mtu

akaelekea Kitandani kulala, na katika siku ya pili yake, tukasali Nyuma yake,

na kisha baada ya Kusali akasema: ‘Ummu Hani, nimesali pamoja nanyi Sala


734

ya Isha kama mlivyoniona, na kisha nikaelekea Bayt Ul Maqdis nikasali ndani

yake na sasa hivi nimesali nanyi Alfajir kama mnavyoniona’(Imam Muhammad Ibn

Jarir At Tabari)

Katika kuelezea tukio lililotokea kabla ya Safari ya Miraj basi wanasema Masahaba

akiwemo Anas Ibn Malik Umar Ibn al-Khattab, Ali ibn Abi Talib, Abdallah Ibn Mas`ud,

Abd Allah Ibn `Abbas, Malik Ibn Sa`sa`, Abu Dharr Al Ghifari, Abu Hurayrah, Abu

Sa`id, Shaddad Ibn Aws, Ubay Ibn. Ka`b, Jabir, Hudhayfah Ibn Al Yaman, Buraydah,

Abu Ayyub Al Ansari, Samurah Ibn Jundab, Umm Hani’, `A’isha, Asma Radhi Allahu

Anhum katika Hadith zenye Maneno tofauti kua:

‘Usiku mmoja Malaika watatu walikuja kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam wakati akiwa amelala Msikitini, ambapo mmoja miongoni mwa Malaika

hao watatu akamuuliza Malaika mwengine kwa kusema: ‘Ndie yupi kati ya

hawa?’ na Malaika wa katikati miongoni mwao akasema: ‘Mchukueni aliebora

kuliko wote’ Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawaona Malaika

hao tena katika Usiku wa Miraj huku akiwa katika hali Kulala lakini Moyo

wake ukiwa Macho, na hawakuzungumza nae, lakini walimchukua hadi kwenye

kisima cha Zamzam’

Alipofikishwa kwenye Kisima cha Zamzam basi akalazwa chini na kisha akashuka

Malaika Jibril ambae alimpasua Kifua chake ambapo : ‘Alisema Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua : ‘Wakati niko kwenye Hatim nikiwa nimelala, akatokea

Mtu akanipasua kuanzia kwenye mfupa wa kifua hadi kitovuni akautoa Moyo

wangu na kisha ikatolewa sahani iliyojaa Imani na Moyo wangu ukakoshwa

kutokana nayo na kujazwa na kujazwa Hikma, kisha akaletwa Mnyama ambae

alikua ni mweupe na Mkubwa kuliko Punda na ni Mdogo kuliko Farasi’’

Ambapo huyu Mnyama alikua ni Buraq ambae alikua tayari ameshatayarishwa kwa

safari yake ya kumbeba Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa ajili ya Safari hio

ya Isra na Miraj.

MAUMBILE YA BURAQ NA MIUJIZA YA SAFARI YA ISRA NA

MIRAJ.

Neno Buraq linatokana na neno Barq ambalo ni lenye kutokana na neno Baraqa ambalo

hua linamaanisha Kushangaza, Kuchanganya, Kupigwa na Mshangao Mkubwa sana,

hivyo neno Barq hua linamaanisha Nuru au Mwangaza wa Radi pale inapopiga.

Ambapo amesema Imam Uthman Ibn Hasan Al Juwayri kua: ‘Safari ya Miraj

imesababishwa na Ardhi kua ni yenye kujiona dhidi ya Mbingu pale iliposema


735

kuziambia Mbingu kua: ‘Hakika Mimi ni mbora zaidi yako kwa sababu Allah

Subhanah wa Ta’ala, amenipamba mimi kwa Milima, Mimea, Bahari Mito na

Maziwa’’Ambapo Mbingu zikasema kua: ‘La Mimi ni bora kwa sababu Allah

Subhanah wa Ta’ala amenipamba kwa Jua, Mwezi, Sayari na Nyota’

Ardhi ikasema: ‘La, kwani mimi nna Baytu Allahi Al Haram Nyumba ambayo

Mitume na Manabii na Mawalii na Waumini hua wanafanya Tawwaf.’ Ambapo

Mbingu zikasema: ‘La Mimi nna Bayt Al Maamur Nyumba ambayo Malaika

wanafanya Tawwaf, nna na Pepo ambazo ndani yake Wanaishi Mitume, Manabii,

Mawalii na Waumini.’

Ardhi ikasema: ‘Kwa hakika Bwana wa Mitume, Alama ya Mitume, Kiumbe

anaependwa zaidi na Allah Subhanah wa Ta’ala, na Mbora wa Viumbe, Mkamilifu

wa Viumbe yuko Juu yangu na Mafunzo yake yanasomeshwa juu yangu.’ Kutokana

na hoja hii basi Mbingu zikaona kua zimeshindwa kihoja, hivyo nazo zikamuomba Allah

Subhanah wa Ta’ala kwa kusema: ‘Ya Allah, hakika wewe ni mwenye Kujibu

unaopoombwa, nami nimeshindwa dhidi ya hoja za Ardhi juu yangu hivyo

nakuomba kua Mpandishe juu kwangu Muhammad ili nami nipate heshima na

utukufu kama uliopata Ardhi kutokana nae.’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akayakubali maombi ya Mbingu na kisha akamwambia

Malaika Jibril: ‘Nenda Peponi kisha kamchukue Buraq, kisha kamchukue

Muhammad’ hivyo Malaika Jibril akaenda Peponi na akakuta kuna Buraq 40,000 ambao

wote wakiwa na Jina la Muhammad kwenye Paji la Uso wao, na miongoni mwao

akamuona Buraq mmoja akiwa anang’ara kichwani mwake lakini akiwa na hali ya

kutokwa na Machozi.

Hivyo Malaika Jibril akamsogelea Buraq Huyo na kumuuliza: ‘Ewe Buraq, Kwanini

umekua mnyonge na mwenye kulia?’

Buraq huyo akasema: ‘Ewe Jibril, hakika mimi nimeanza kulisikia Jina la

Muhammad kwa mda wa miaka 40,000 iliyopia, nami nimempenda mwenye Jina

hili na namtamani kumuona kwa mda mrefu sana’ hivyo Malaika Jibril akasema:

‘Hakika mimi nitakupelekea kwa yule umpendae.’ Hivyo Malaika Jibril akamchukua

Buraq huyo na kushuka nae Ardhini kwa Nabii Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam.

(Nuur Dhalam)

Buraq ni Mnyama wa Peponi mwenye miguu minne, si Mnyama Jike wala si Mnyama

Dume, Si Punda wala si Farasi na anapokimbia hua ni mwenye kutua hatua zake za miguu

yake ya mbele kwenye masafa ya upeo wa Jicho huku miguu yake ya nyuma ikiwa juu

ardhini, na ameitwa Buraq kwa sababu ya nguvu, uwezo na kasi yake ni zaidi ya kasi ya


736

Nuru ya Mwangaza wa Radi pale inapopiga na rangi yake ni Nyeupe ya Nuru ya

Muangaza.

Hivyo tunapomuangalia Buraq na sifa zake basi tunaona kua kama lilivyo jina lake na

kasi yake kua ni isiyoweza kufikirika kwani safari ya kutoka katika Mji wa Makkah hadi

Jerusalem ni yenye masafa ya kilomita 1500 ambayo kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam akiwa juu ya Buraq ilikua ni kufumba na kufumbua kama inavyopiga radi

kwani unaona kwanza na kisha ndio unasikia, na ukisikia basi ndio imeshafika.

Yaani hapa tunazungumzia kasi ya mahesabu ya ndani ya sehemu ya sekunde kwa masafa

hayo kwani hii hua ni Kasi ya Muangaza wa Jua ambayo hua ni Kilomita 300,000 kwa

sekunde, yaani kufumba na kufumbua, kama kilivyoletwa na Asif Ibn Barkhiya kiti cha

Malkia Bilqis mbele ya Nabii Sulayman.

Ambapo kwa upande wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi anatuambia

kua:‘Nikaambiwa nipande Buraq, na kisha Jibril akaanza safari na mie hadi

tukafika Bayt Ul Maqdis’ huku Malaika Jibril akiwa ni mwenye kukamata sehemu za

kuwekea Miguu na Malaika Mikail akiwa ni mwenye kukamata hatamu ya Buraq huyo.

Hivyo ili kufahamu hili tunalozungumzia la kuhusiana na Buraq na juu yake Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam, basi inabidi tuingie kwenye somo la Fizikia ambapo ndani

yake mna Kanuni ya mfumo wa Uteketezaji ambao hua unaelezea kile kinachotokea pale

baada ya kupatikana mkusanyiko wa Nguvu kubwa sana inayotokana na mgongano baina

ya kitu chenye kuchukua nafasi na kitu kisichochukua nafasi katika sehemu husika na

hivyo matokeo yake kusababisha kutoweka kwa umbo la kitu hicho chenye kuchukua

nafasi na kisha baada yake hutokea Nguvu kubwa sana ya Mionzi ya Nuru ambayo nguvu

yake hua ni zaidi ya nguvu ya Mionzi ya X-ray.

Ambapo hapa tunarudi tena kwa Mujaddid Ad Din Sultan Mutakalimin Imam Al

Mushakikkin Imam Fakhr Ad Din Al Razi pale aliposema kua: ‘Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alisafiri pia katika safari mbili ambapo kwanza ni

hali ya kusafiri kutoa kwenye Ulimwengu Unaoonekana (Al Alam Al Shahadah)

na kuingia kwenye Ulimwengu Usioonekana (Al Alam Al Ghayb) ambapo

Ulimwengu miwili hii imepakana ndani ya Masafa ya Baina ya Mipinde Miwili,

kama zilivyosema Aya.

‏﴿فَكَ‏ انَ‏ قَابَ‏ قَوْسَ‏ ينْ‏ ِ أَوْ‏ أَدْ‏ نىَٰ‏ ﴾

Fakana qaba qawsayni aw adna(Surat An Najm 53:9)

Tafsir: Na ilikua ni masafa ya Mipinde Miwili au karibu zaidi.


737

Hivyo Maneno Fakana qaba qawsayni aw adna hua ni yenye kumaanisha

Uteketezo wa Nafsi yake na hivyo Nafsi hio kuingia katika hali ya kua na

ukaribu sana kwa Mola wake.

Hivyo tunapozungumzia Uteketezo aliouzugumzia Mujaddid Ad Din Sultan

Mutakalimin Imam Al Mushakikkin Imam Fakhr Ad Din Al Razi wa Nafsi ya Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi tunaona kua kulingana na Kanuni ya Mfumo wa

mahusiano ya Uteketezo wa kitu basi hupelekea kutoweka kwa kitu husika baada ya

kutokea mgongano mkubwa baina ya kituhusika chenye kuchukua Nafasi na kitu

kisichochukua Nafasi, kwa maana hio basi kulitokea mtoweko wa Maumbile ya

muonekano wa mwili wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam wenye kuchukua Nafasi

ya sehemu kutokana na Uteketezo huo, kutoka katika sehemu aliyokuwepo na kuibuka

katika sehemu nyengine kuliosababishwa na mgongano wa Maumbile yake Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na Maumbile ya Malaika Jibril ambayo ni ya kutokuchukua

nafasi katika sehemu kutokana na Makadirio ya Allah Subhanah wa Ta’ala na hapo hapo

pia ikatokea Nguvu kubwa zaidi ya Nuru ambayo ilifungamana na Nuru iliyowakilishwa

na Mnyama Buraq na kutokea yaliyotokea katika kukamilisha safari hio.

Ambapo tunapoangalia kwa upande mwengine wa utaratibu wa Elimu ya Fizikia basi hua

tunaona kua Kitu chochote kile chenye kuchukua nafasi kinapoingizwa katika hali fulani

basi kitu hicho chenyewe hua kinageuka na kua ni aina ya Nguvu ambayo inaweza

kutumika kutoa kitu chengine chenye nguvu kubwa zaidi ambacho hakikuwepo kabla

yake.

Yaani hii hua ni kulingana na ile kanuni isemayo E=mc2, ambapo E hua ni Nguvu ya

Mvutano ya ndani ya Kitu husika ambayo hua ni sawa na M ambayo hua ni Uzito wa

Kitu husika na C2 ambayo hua ni Kasi ya Muangaza wa Jua ambayo hua ni Kilomita

300,000 kwa sekunde moja mara mbili yake. Ambapo hii ndio kanuni ya Nguvu

inayotumika katika kuendeshea mashine mbali mbali kuanzia kwenye Vyombo vya

usafiri kama Gari, Ndege, Meli, Pikipiki n.k

Kwani kwenye mashine za vyombo hivi zinazotumia Mafuta iwe Petroli au Diesel basi

matone ya mafuta hayo hua yanamwagwa kwenye chumba maalum ndani ya mashine

husika na kisha kukandamizwa pamoja na hewa ndani ya sehemu hio ya mashine na hapo

hapo Mafuta hayo hutoweka na badala yake ndani sehemu hio huzalishwa Nguvu kubwa

sana ambayo huifanya Mashine kua ni yenye kuzunguka na kufanya kazi, n.k ambapo

kanuni ya mfumo huu pia hutumika kwenye Taa za Umeme, Vinu vya kusagia Nafaka.n.k

Hivyo kitu chochote kile chenye kuchukua nafasi kitakachosafiri kwa kasi ya Mwangaza

basi Maumbile ya Umbo lake hugeuka na kua ni Nguvu inayotokana ndani yake, ambapo

hapo hapo Nguvu hio inapohitajika kurudishwa katika hali ya awali ya kitu hicho basi


738

hua pia kuna uwezekano wa kurudishwa kwake katika hali yake ya asili, ingawa hata

hivyo kutakua na upungufu wa baadhi ya sehemu za Umbo lake la maumbile kitu hicho.

Ambapo ingawa kwa hali ya maumbile ya Mtu wa kawaida hua haiwezekani kusafiri kwa

kasi hio ya Mwangaza wa Jua na hii ni kwa sababu kila Kitu kinavyoongeza kasi yake

basi hua pia ni chenye kuongezeka Uzito wake kutokana na nguvu iliyomo ndani yake,

na kutokana na hali hio basi kwa upande wa maumbile ya Ibn Adam, basi yeye hua ni

mwenye hali kupoteza uwezo wa kujidhibiti yeye mwenyewe na kila kitu kilichomo

ndani ya mwili wake kutokana na nguvu inayozalishwa ndani ya mwili wake kutokana

na kasi ya mwendo huo.

Na kisha baada ya hapo Ibn Adam husika hatokua na uwezo wa kuona sawasawa kwani

ataanza kujiona kua kama mtu mwenye kusafiri kwa kasi kubwa kwa kupitia kwenye

bomba jembamba lisilokua na mwisho kwao na kila kitu atakiona kua kimejikusanya

katika sehemu ndogo iliyopo mbele yake na kisha macho yake yataanza kutofahamu nini

yanaona na taratibu huanza kuona kiza kitupu, na ufahamu wake utapoteza muelekeo na

huenda kitakachofuatia hapo ikawa ni kifo chake.

Lakini bila ya shaka tunapozungumzia Maumbile ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam basi tunaona alikua katika hali ya Maumbile ya Nuru ya Mitume kabla ya

Kuumbwa kwake, na baada ya Kuumbwa kwake, na baada ya kuzaliwa kwake na kua

hata kabla ya safari yake hio basi alikua ni mwenye kupasuliwa na kujazwa Nuru ya Iman

na Hikma ndani ya kifua chake, na bila ya shaka maumbile ya Nuru yalivyo hua ni yenye

kusambaa kwa kasi kubwa sana na kuwepo katika kila sehemu pale inapoachiwa

muangaza wake Nuru hio, kama ilivyo Nuru ya muangaza wa Jua linapoangaza Duniani,

hua ni yenye kutoka Juu Mbinguni kwa masafa ya kilomita Milioni 150 na moja kwa

moja kufika Ardhini katika wakati huo huo.

Kwani amesema Jabir Ibn Abdallah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi nilisema

kumwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam : ‘Ya Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam Baba yangu na Mama yangu watolewe Kafara kwa ajili yako, hebu

niambie ni kitu gani kilichoumbwa kabla ya Allah Kuumba kila kila kitu?’’ ‘Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Ewe Jabir, kitu cha Mwanzo

alichokiumba Allah ilikua ni Nuru ya Mtume wako, kutokana na Nuru yake, na

kisha Nuru hio ikabakia ikiangaza baina ya Uwezo wake kwa namna alivyotaka

Mwenyewe, na katika wakati huo ilikua hakuna Kitabu wala Kalamu wala Pepo

wala Moto wala Malaika wala Mbingu wala Ardhi.

Na hivyo Allah alipotaka kuumba Viumbe wake basi akaigawa Nuru hio katika

sehemu nne na kutokana na sehemu ya kwanza akatoa Kalamu, katika sehemu ya

pili akatoa Kitabu, katika sehemu ya tatu akatoa Arshi na katika sehemu ya nne

akatoa Kila kitu’’(Mawahib al Laduniyya Imam Al Qastallani)


739

Na pia yeye mwenyewe Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akiomba dua kua

aendelee kua Nuru katika kila sehemu ya Kiungo chake kwa kusema:

اللّهُم َّ اجْعَلْ‏ فيِ‏ قَلْبي نُوراً‏ ، وَفي لِسَانيِ‏ نُوراً،‏ وَفيِ‏ سمَْعِي نُوراً,‏ وَفيِ‏ بَصَرِيِ‏ نُوراً,‏

وَمِ‏ نْ‏ فَوْقِي نُوراً‏ , وَ‏ مِنْ‏ تحَْتيِ‏ نُوراً,‏ وَ‏ عَنْ‏ يمَِينيِ‏ نُوراَ,‏ وعَنْ‏ شمِ‏ ‏َاليِ‏ نُوراً,‏

وَمْن

أَماَمِي نُوراً,‏ وَمِنْ‏ خَلْفيِ‏ نُوراَ,‏ واجْعَلْ‏ فيِ‏ نَفْسِ‏ ي نُوراً,‏ وأَعْظِمْ‏ ليِ‏ نُوراً,‏ وَعظِّمْ‏ ‏ِلي

نُوراً,‏ وَاجْ‏ عَلْ‏ ليِ‏ نُوراً,‏ واجْ‏ عَلنيِ‏ نُوراً,‏ ألل َّهُم َّ أَعْطِنيِ‏ نُوراً,‏ واجْ‏ عَلْ‏ فيِ‏ ‏َعصَبيِ‏ نُوراً,‏

وَفيِ‏ لحَْمِي نُوراً,‏ وَفيِ‏ دَمِي نُوراً‏ وَفيِ‏ شَعْرِي نُوراً,‏ وفيِ‏ بَشَرِي نُوراً‏ ‏(أَلل َّهُم َّ اجِ‏ عَلْ‏ ‏ِلي

نُوراً‏ فيِ‏ قّبرِْي وَ‏ نُوراَ‏ فيِ‏ عِظاَمِي)‏ ‏(وَزِدْنيِ‏ نُوراً‏ , وَ‏ زِدْ‏ نيِ‏ نُو راَ‏ , وَزِدْنيِ‏ نُوراً)‏ ‏(وَهَ‏ ‏ْب

ليِ‏ نُوراً‏ عَلَى نُوراً‏ (

Allāhummaj'al fī qalbī nūran, wa fī lisānī nūran, wa fī sam`ī nūran, wa fī baṣarī

nūran, wa min fawqī nūran, wa min taḥtī nūran, wa `an yamīnī nūran, wa `an

shimālī nūran, wa min 'amāmī nūran, wa min khalfī nūran, waj`al fī nafsī nūran,

wa 'a`dhim lī nūran, wa `dhim lī nūran, waj`allī nūran, waj`alnī nūran, Allāhumma

'a`tinī nūran, waj'al fī `aṣabī nūran, wa fī laḥmī nūran, wa fī damī nūran, wa fī

sha`rī nūran, wa fī basharī nūran. [Allāhummaj`allī nūran fī qabrī wa nūran fī

`idhāmī.] [Wa zidnī nūran, wa zidnī nūran, wa zidnī nūran.] [Wa hab lī nūran `alā

nūr.]

Tafsir: Ya Allah, Nijaalie Nuru kwenye Moyo wangu, Na kwenye Ulimi wangu Nuru;

Na kwenye Masikio yangu Nuru; Na kwenye Macho yangu Nuru; Na juu yangu Nuru;

Na chini Yangu Nuru; Na kulia kwangu Nuru; Na Kushoto kwangu Nuru; Na mbele

yangu Nuru; Na Nyuma yangu Nuru; Na ndani ya Nafsi yangu Nuru; Itukuze Nuru

yangu; Na Ikuzishe Nuru yangu; Nijaalie niwe Nuru; Na Nijaalie niwe Nuru; Ya

Allah Nipe Nuru; Nijaalie Nuru ndani ya Hisia zangu; Ndani ya Mwili wangu Nuru;

Ndani ya Damu yangu Nuru; Kwenye Nywele zangu Nuru; Kwenye Umbo langu

Nuru; Ya Allah Nijaalie Nuru Kaburini mwangu; na Nijaalie mimi Nuru kwenye

Mifupa yangu; Na Niongezee Nuru; Na Niongezee Nuru, Na Niongezee Nuru;Na

unipe Nuru Juu ya Nuru (Imam Bukhari, Fath-Al Bari)

Kwa hivyo Maumbile yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam sio maumbile kama

ya kawaida ya viumbe wengine, kwani ndani kila kiungo cha mwili wake mna Nuru na


740

hivyo katika safari yake ya kuenda na kurudi kwa mwendo wa zaidi ya kasi ya Nuru ya

Muangaza wa Jua, basi hakukutokea mabadiliko yeyote kwenye Mwili wake Mtukufu

kutokana na Matakwa yake mwenyewe Muumba Allah Subhanah wa Ta’ala kutokana

na Utukufu wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam wa Kimaumbile mbali ya kua

alikua ni mwenye kusafiri kwa kasi ya zaidi ya Mwangaza katika Safari yake kwa

Kimwili, Kiroho na Kinafsi.

Hivyo anasema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam : ‘Wakati nikiwa safarini

alitokea Mtu katika upande wangu wa kulia na kuniita kwa kusema: ‘Muhamamd

mimi nataka kuzungumza nawe’ lakini nami sikumjibu, kisha kwa mbele zaidi mtu

mwengine akaniita kwa upande wa kushoto na kusema: ‘Muhamamd mimi nataka

kuzungumza nawe’ nami sikumjibu na ilipofikia mbele zaidi nikamuona

Mwanamke alievaa vizuri na kujipamba na kila aina ya mapambo ambae alisema:

‘Muhamamd, nataka kuzungumza nawe.’’

Ambapo ni baadae Malaika Jibril akasema kua: ‘Mtu wa kwanza alikua ni Myahudi

na wa pili alikua ni Mkristo ambao wote walikua wanataka kumuondolea umakini

kwenye safari yake ama kuhusiana na Mwanamke basi alikua ni Dunia. Hivyo

kama Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam angemsikiliza basi Ummah wake

ungeipendelea zaidi Dunia kuliko Akhera.’

Katika safari yake hio ya Isra Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisimama katika

sehemu kadhaa ambapo kwanza ilikua ni katika Mji wa Madina na kisha akasimama

kwenye Mlima Sinai katika sehemu ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala alimkabidhi

Nabii Musa Tawrat, na kisha akasimama kwenye eneo la Bethlehem katika sehemu

aliyozaliwa Nabii Isa.

Na kisha pia wakasimama kwenye Kaburi la Nabii Musa ambapo alimuona Nabii Musa

akiwa ndani kabuirni mwake amesimama akiwa anasali kama alivyosema katika hadith

kua: ‘Nilipita kwa Musa katika safari ya Isra pembeni ya kilima chekundu alipokua

amesimama akisali ndani ya Kaburi lake’(Sahih Muslim)

Walipofika Bayt Al Maqdis basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anasema kua:

‘Nami nikamfunga Buraq kwenye sehemu ambayo alikua akifungwa na Mitume

wengine, na kisha nikaingia ndani ya Msikiti huo na nikasalisha Mitume wengine

wote waliotangulia kabla yangu akiwemo Adam na waliokuja baada yake.

Ambao walikua ni Mitume 124000 waliokua wakimsubiri ndani yake, hivyo Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam anasema kua: ‘Mitume wakatambulishwa kwangu mie na

Musa alikua ni mwembamba mwenye kufanana na watu wa kabila la Shanuah, na

nikamuona Isa Ibn Maryam alikua akifanana sana na miongoni mwa niliowaona

kua ni na Urwah Ibn Masud, na nikamuona Ibrahim na mtu wa karibu aliefanana


741

nae miongoni mwa niliowaona ni Sahaba yenu (yaani yeye mwenyewe Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam), na nikamuona Jibril na wa karibu aliefanana nae

miongoni mwa niliowaonani Dihya’(Imam At Tirmidhi)

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anaendelea kusema kua: Wakati nikitoka basi

Jibril aliniletea Mabakuli mawili ambapo moja limetiwa Kilevi na jengine limetiwa

Maziwa, nami nikachukua lenye kutiwa Maziwa, hivyo Jibril akasema: ‘Maamuzi

yako yanaendana na Maumbile ya Fitra.’’

‘Na kisha tukapanda juu na Jibril hadi tulipofika katika Mbingu ya kwanza ya

karibu na Dunia’, hivyo Jibril akaomba kuruhusiwa kuingia ndani yake nae

akaulizwa: ‘Ni nani?’ nae akajibu: ‘Jibril’ akaulizwa tena: ‘Umefuatana na nani?’

nae akajibu: ‘Muhammad’ nae akaulizwa: ‘Hivi Jee amealikwa?’ Nae akajibu:

‘Naam’ hivyo akaambiwa: ‘Mkabiribishe, kwani mbora zaidi aliealikwa amewasili’

Hivyo Mbingu hio ikafunguliwa, na wakati nilipokua naingia nikakutana na Adam,

na Jibril akaniambia: ‘Huyu ndio Baba yako, hivyo Msalimie’ Nami Nikamsalimia

nae akanirudishia salamu hio na kusema: ‘Karibu Ewe Mtoto Mcha Mungu na

Mtume Mcha Mungu’

Na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuona akiwa na watu wengi sana

katika upande wake wa kulia na pia watu wengi sana katika upande wake wa kushoto,

akiangalia katika upande wake wa Kulia hua ni mwenye kutabasamu, na akiangalia

katika upande wake wa kushoto hua ni mwenye kulia. Hivyo Malaika Jibril akaelezea

kua: ‘Walio upande wake wa Kulia ni Kushoto ni Roho za kizazi chake na waliokua

katika upande wa Kulia ni watu wa Peponi na waliokua upande wa kushoto ni wa

Motoni’

‘Na kisha tukapanda juu na Jibril hadi tulipofika katika Mbingu ya pili’ hivyo Jibril

akaomba kuruhusiwa kuingia ndani yake nae akaulizwa: ‘Ni nani?’ nae akajibu:

‘Jibril’ akaulizwa tena: ‘Umefuatana na nani?’ nae akajibu: ‘Muhammad’ nae

akaulizwa: ‘Hivi Jee amealikwa?’ Nae akajibu: ‘Naam’ hivyo akaambiwa:

‘Mkabiribishe, kwani mbora zaidi aliealikwa amewasili’

Hivyo Mbingu hio ikafunguliwa, na wakati nilipokua naingia nikakutana na Isa na

Yahya, na Jibril akaniambia: ‘Hawa ndio Isa na Yahya, hivyo wasalimie’ Nami

Nikawasalimia nao wakanirudishia salamu hio na kusema: ‘Karibu Ewe Ndugu

Mcha Mungu na Mtume Mcha Mungu’

‘Na kisha tukapanda juu na Jibril hadi tulipofika katika Mbingu ya tatu’ hivyo

Jibril akaomba kuruhusiwa kuingia ndani yake nae akaulizwa: ‘Ni nani?’ nae

akajibu: ‘Jibril’ akaulizwa tena: ‘Umefuatana na nani?’ nae akajibu: ‘Muhammad’


742

nae akaulizwa: ‘Hivi Jee amealikwa?’ Nae akajibu: ‘Naam’ hivyo akaambiwa:

‘Mkabiribishe, kwani mbora zaidi aliealikwa amewasili’

Hivyo Mbingu hio ikafunguliwa, na wakati nilipokua naingia nikakutana na Yusuf,

na Jibril akaniambia: ‘Huyu ndio Yusuf, hivyo Msalimie’ Nami Nikamsalimia nae

akanirudishia salamu hio na kusema: ‘Karibu Ewe Ndugu Mcha Mungu na Mtume

Mcha Mungu’

‘Na kisha tukapanda juu na Jibril hadi tulipofika katika Mbingu ya nne’ hivyo

Jibril akaomba kuruhusiwa kuingia ndani yake nae akaulizwa: ‘Ni nani?’ nae

akajibu: ‘Jibril’ akaulizwa tena: ‘Umefuatana na nani?’ nae akajibu: ‘Muhammad’

nae akaulizwa: ‘Hivi Jee amealikwa?’ Nae akajibu: ‘Naam’ hivyo akaambiwa:

‘Mkaribishe, kwani mbora zaidi aliealikwa amewasili’

Hivyo Mbingu hio ikafunguliwa, na wakati nilipokua naingia nikakutana na Idris,

na Jibril akaniambia: ‘Huyu ndio Idris, hivyo Msalimie’ Nami Nikamsalimia nae

akanirudishia salamu hio na kusema: ‘Karibu Ewe Ndugu Mcha Mungu na Mtume

Mcha Mungu’

‘Na kisha tukapanda juu na Jibril hadi tulipofika katika Mbingu ya tano’ hivyo

Jibril akaomba kuruhusiwa kuingia ndani yake nae akaulizwa: ‘Ni nani?’ nae

akajibu: ‘Jibril’ akaulizwa tena: ‘Umefuatana na nani?’ nae akajibu: ‘Muhammad’

nae akaulizwa: ‘Hivi Jee amealikwa?’ Nae akajibu: ‘Naam’ hivyo akaambiwa:

‘Mkabiribishe, kwani mbora zaidi aliealikwa amewasili’

Hivyo Mbingu hio ikafunguliwa, na wakati nilipokua naingia nikakutana Harun,

na Jibril akaniambia: ‘Huyu ndio Harun, hivyo Msalimie’ Nami Nikamsalimia nae

akanirudishia salamu hio na kusema: ‘Karibu Ndugu Mcha Mungu na Mtume

Mcha Mungu’

‘Na kisha tukapanda juu na Jibril hadi tulipofika katika Mbingu ya sita hivyo Jibril

akaomba kuruhusiwa kuingia ndani yake nae akaulizwa: ‘Ni nani?’ nae akajibu:

‘Jibril’ akaulizwa tena: ‘Umefuatana na nani?’ nae akajibu: ‘Muhammad’ nae

akaulizwa: ‘Hivi Jee amealikwa?’ Nae akajibu: ‘Naam’ hivyo akaambiwa:

‘Mkabiribishe, kwani mbora zaidi aliealikwa amewasili’

Hivyo Mbingu hio ikafunguliwa, na wakati nilipokua naingia nikakutana na Musa

ambae alikua ni mwenye rangi ya kiza na mwili mkubwa na mwenye nyingi nyingi,

na Jibril akaniambia: ‘Huyu ndio Musa, hivyo Msalimie’ Nami Nikamsalimia nae

akanirudishia salamu hio na kusema: ‘Karibu Ewe Ndugu Mcha Mungu na Mtume

Mcha Mungu’


743

Wakati nilipokua natoka mara akaanza kulia: ‘Nami nikauliza Jee ni nini

kinachokufanya Ulie?’ nae akasema: ‘Mimi nalia kwa sababu Kijana Mdogo

alietumwa baada yangu atakua na wafuasi wengie zaidi yangu ambao wataingia

Peponi kwa wingi zaidi ya wafuasi wangu’

‘Na kisha tukapanda juu na Jibril hadi tulipofika katika Mbingu ya saba hivyo

Jibril akaomba kuruhusiwa kuingia ndani yake nae akaulizwa: ‘Ni nani?’ nae

akajibu: ‘Jibril’ akaulizwa tena: ‘Umefuatana na nani?’ nae akajibu: ‘Muhammad’

nae akaulizwa: ‘Hivi Jee amealikwa?’ Nae akajibu: ‘Naam’ hivyo akaambiwa:

‘Mkabiribishe, kwani mbora zaidi aliealikwa amewasili’

Hivyo Mbingu hio ikafunguliwa, na wakati nilipokua naingia nikakutana na

Ibrahim, na Jibril akaniambia: ‘Huyu ndio Baba yako Ibrahim, hivyo Msalimie’

Nami Nikamsalimia nae akanirudishia salamu hio na kusema: ‘Karibu Ewe Mtoto

Mcha Mungu na Mtume Mcha Mungu’

Na kisha nikachukuliwa hadi katika Bayt Al Maamur na kupewa Kikombe cha

Ulevi, Kikombe cha Maziwa, na Kikombe cha Asali nami nikachukua Maziwa na

Malaika Jibril akasema: ‘Umechagua Jambo la kimaumbile hivyo wewe na Ummah

wako watalifuata’

Katika safari yake hii Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alioneshwa Miujiza mingi

sana ambapo kwenye Bayt Maamur ambacho ndio Kibla cha Malaika kilichopo juu ya

eneo la Al Kaabah Mbinguni, na baadae akaoneshwa Pepo na Moto na yanayotokea ndani

yake sehemu hizo kwa wanaoadhiabiwa kwa makosa ya dhambi zao na kwa wanaolipwa

kutokana na amali njema zao na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua ni

mwenye kuona yale ambayo hakuna jicho lililowahi kuona wala hakuna ufahamu

uliowahi kufikiria.

Na kisha akapandishwa Juu zaidi hadi akafika katika Sidrat al Muntaha, na akaona kua

Matunda yake ni makubwa kama ya Hijr na Majani yake makubwa kama masikio ya

Tembo nae Jibril akamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Huu ndio

Sidrat Al Muntaha’ nami nikaona Mito minne inatokana nao, na hivyo nikauliza: ‘Hii

ndio nini ewe Jibril?’

Jibril akasema: ‘Mito itokanayo ndani yake ni ni Mito ya Peponi na itokayo nje yake

ni Mto Nile na Mto Furat (Euphrate)’

Na kisha baada ya hapo Malaika Jibril akamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kua amalizie safari yake peke yake kwani hakuna kiumbe mwengine ambae

aliewahi kuvuka katika eneo la Sidrat Al Muntaha, ambapo mbele yake kuna Arshi

Tukufu ya Allah Subhanah wa Ta’ala. Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam


744

akaendelea mbele zaidi peke yake kumalizia safari yake hio hadi kufikia katika masafa

ya Qaba Qawsayni aw Adna mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala.

Ambapo kilichotokea hapa hakijulikana kwani hakijaelezewa wala kuhadithiwa isipokua

kuhusiana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua ni mwenye kuambiwa kua:

‘Nimekabidhi jukumu la kusali sala 50 kwa Ummah wako katika kila sikua na

katika kila mchana.’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anaelezea kwa kusema: Kisha

nikafardhishiwa Sala 50 nami nikarudi na kukutana na Musa ambae aliuliza: ‘Jee

umeamrishwa nini?’ nami nikajibu: ‘Nimekabidhiwa Sala 50’ nae akasema: ‘Watu

wako hawatoweza kusali Sala 50 ndani ya siku moja. Wa Allahi mimi niliwajaribu

watu kabla yako na niliadhibika sana na watu wa Bani Israil, hivyo rudi kwa Mola

wako, kawaombee watu wako’

Nami nikarudi na Allah akanipunguzia Sala 10, na nikarudi kwa Musa nae

akasema tena aliyoyasema hapo kabla, hivyo nikarudi kwa Allah na nikapunguziwa

10 tena, na nikarudi kwa Musa nae akasema tena aliyoyasema hapo kabla, hivyo

nikarudi kwa Allah na nikapunguziwa 10 tena, na nikarudi kwa Musa nae akasema

tena aliyoyasema hapo kabla, hivyo nikarudi kwa Allah na nikapunguziwa 10 tena,

na nikarudi kwa Musa nae akasema tena aliyoyasema hapo kabla, hivyo nikarudi

kwa Allah na nikapunguziwa 5.

Na nikarudi kwa Musa nae akasema Watu wako hawatoweza kusali Sala 5 ndani

ya siku moja. Wa Allahi mimi niliewajaribu watu kabla yako na niliadhibika sana

na watu wa Bani Israil, hivyo rudi kwa Mola wako, kawaombee watu wako. Nami

nikasema: ‘Hakika mimi nimeshamuomba Mola wangu mpaka naona aibu, hivyo

bora niridhike na kujisalimisha’

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Imam Bukhari kua: ‘Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam aliambiwa na Allah Subhanah wa Ta’ala kua: ‘Ewe

Muhamamd. Maneno yangu hayabadiliki kwani hivyo ndivyo nilivyoandika

kwenye Umm Ul Kitab, kila jema litalipwa mara 10 zaidi yake, hivyo haya ni mema

50 katika Umm Ul Kitab na ni matano kwa ajili yako’’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaendelea kusema kua: ‘Nilipovuka Mbinguni

nikasikia sauti ikinadia: ‘Nimetimza Ahadi yangu na nimewapunguzia Waja

wangu’’

Na kisha baada ya hapo kuna matukio mbali mbali aliyoyaona Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam katika safari yake hio kabla ya kurudi kwake kutoka Mbinguni kwa

kushukia tena katika sehemu aliyopandia yaani Bayt Ul Maqdis, kisha akapanda tena


745

Buraq na akaanza Safari ya kurudi katika Mji wa Makkah, ambapo njiani akakutana na

msafara wa Quraysh ambao ulikua umepotelewa na Ngamia wao, nae alikua akiwajua

viongozi wa Msafara huo na akawasalimia nao wakasema: ‘Hii ni sauti ya Muhammad’

Ambapo asubuhi yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipotoka nje akakutana

na Abu jahl ambaea lipomsalimia basi akamuuliza: ‘Kuna mpya Gani leo?’ Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam aaelezea yaliyomtokea ndani ya usiku huo, ambapo Abu

Jahal akasema: ‘Hivi Jee kama nitawakusanya watu utarudia kusema mbele yao

kama uliyoniambia mimi?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam’

Hivyo Abu Jahl akawakusanya watu na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akawaelezea yaliyotokea lakini watu wa Mji wa Makkah hawakukubaliania nae, hivyo

mmoja kati ya watuwaliowahi kuenda Bayt Al Maqdis akamwambia Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam aelezee namna Ulivyo Msikiti wa Bayt Ul Maqdis, hivyo

Allah Subhanh wa Ta’ala akauleta Msikiti wa Bayt Ul Maqdis mbele ya macho ya Mtume

wake Salallahu Alayhi wa Salam na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akauelezea

kama ulivyo, na hivyo Mtu huyo akathibitisha kua kweli ni sahih hivyo ndivyo ulivyo

lakini hata hivyo watu hao hawakwueza kukubali ukweli wa kua alienda sehemu hio na

kupanda Mbinguni pia, na hii ni kwa sababu ya Umbali wa kimasafa wa Safari hio,

haiwezekani kufanyika hata kwa mwezi moja wacha mbali ndani ya masaa machache ya

usiku mmoja.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawaambia watu hao kua, wakati aliokua

anarudi alikutana na Ngamia aina fulani aliekua amepotea kutoka kwenye Msafara wake,

akawaonesha watu wenye msafara huo alipokimbilia Ngamia huyo, na ulipowasili

Msafara huo basi wenye Msafara huo walikubalia kua Ngamia wao huyo alipotea Usiku

mmoja na wakasikia sauti ya Mtu ikiwelekeza alipo Ngamia huyo.

Lakini kwa upande wa Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu alipopewa habari hio basi

akasema: ‘Wa Allahi kama hivyo ndivyo anavyosema basi ni kweli, kwa nini kuwe

na shaka juu yake? Hivi jee hasemi yeye kua amepata habari kutoka Juu Mbinguni

katika wakati wowote iwe Usiku au Mchana, hivyi jee ni lipi jambo la Miujiza zaidi

kati ya haya?’

Na kisha Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu akaenda kwa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam na akamwambia amuelezee maeneo aliyoyaona na alipoyaelezea basi

Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Nashuhudia kua wewe ni Rasul

Allah’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anathibitisha ayasemayo Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kuhusiana nayo kua:


746

‏﴿فَلاَ‏ أُقْسِ‏ مُ‏ بمَِا تُبْصِ‏ رُونَ‏ ۞ وَمَا لاَ‏ تُبْصِرُونَ‏ ۞ إِن َّهُ‏ لَقَوْ‏ لُ‏ رَسُولٍ‏ كَ‏ رِيمٍ‏ ۞ وَمَا هُوَ‏

بِقَوْ‏ لِشَا ا عِرٍقَلِي ت لاً َّم ُؤْمِنُو نَ‏ ۞ وَلاَ‏ بِقَوْلِ‏ كَاهِنٍ‏ قَلِيلاً‏ م َّا تَذَك َّرُونَ‏ ‏۞تَن ‏ِزي لٌ‏ مِّن

ر َّبِّ‏ ٱلْعَالَمِينَ۞وَلَوْ‏ تَقَو َّلَ‏ عَلَيْنَا بَعْضَ‏ ٱلأَقَاوِيلِ‏ ‏۞لأَخَذَْ‏ مِنْهُ‏ بِٱلْيَمِينِ۞ثمُ َّ لَقَطَعْنَا

مِنْهُ‏ ٱلْوَتِينَ۞فَمَا مِنكُمْ‏ مِّنْ‏ أَحَدٍ‏ عَنْهُ‏ حَاجِ‏ زِينَ‏ ﴾

Fala oqsimu bima tubsiroona; Wama la tubsiroona; Innahu laqawlu rasoolin

kareemin ; Wama huwa biqawli shaAAirin qaleelan ma tu/minoona ; Wala biqawli

kahinin qaleelan ma tadhakkaroona ; Tanzeelun min rabbi alAAalameena; Walaw

taqawwala AAalayna baAAda al-aqaweeli; Laakhadhna minhu bialyameeni;

Thumma laqataAAna minhu alwateena; Fama minkum min ahadin

AAanhu hajizeena (Surat Al Haaqah 69:38-47)

Tafsir: Hivyo Naapa kwa kila mnachokiona; Na kwa kila msichokiona; Hakika haya

ni maeno ya Mtume mwenye kuheshimika; Na wala si maneno ya Mshairi lakini

mnayaamini kidogo tu; Wala si kauli ya Mtabiri, ambapo mnakumbuka kidogo yake

tu; Haya ni yaliyoteremka kutoka kwa Mola wa Ulimwengu; Na kama angekua

amezua kuhusiana nasi; Basi tungemkamata kwa mkono wa kulia (kwa nguvu na

uwezo mkubwa); Na kisha tungemkata mshipa wake wa uhai; Na hakuna hata mmoja

miongoni mwenu ambae angeweza kutuzuia.

Tunaona katika aya hizi kua Allah Subhanh wa Ta’ala anatuambia kua: ‘Hakika katika

kila alilosema Muhammad Salallah Alayhi wa Salam halikua ni lenye kutokana na

Uzushi au matamanio ya nafsi yake au labda kwa Ilm ya utabiri, bali ni yenye

kutoka kwa Mola wake kwani kwa kua yeye ni Mtume ambae ni mwenye jukumu

la kufikisha Ujumbe anaopewa na Mola wake, basi haruhusikia kuzua au kusema

Uongo kuhusiana na na kitu chochote, kwani akifanya hivyo basi bila ya shaka

angeadhibiwa hapahapa Ulimwenguni, kwa adhabu kali sana, na hakuna hata

kiumbe mmoja ambae angekua ni mwenye uwezo wa kumuepusha na adhabu hio

au kumuombea kua asifikwe na adhabu hio.’

Safari ya Isra na Miraj ina umuhimu mkubwa sana na hikma kubwa sana ndani yake, si

kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Ta’ala peke yake bali kwa Waislam wote kwa

ujumla, kwani tukio hili la Isra na Miraji hua linawakilisha safari ya Kiroho ndani ya

Nafsi zetu katika kuutafuta Ukaribu wa Allah Subhanah wa Ta’ala na kuingia katika hali


747

ya Qaba Qawsayni aw Adna na Mola wetu, kama vile walivyofanya Masahaba wengi

akiwemo Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu.

MUSAB IBN UMARY BALOZI WA KWANZA WA UISLAM NA

MAKUBALIANO YA AQABAH.

Miongoni mwa Vijana waliokua wakipendeza na kuvutia kwa uzuri wa kimaumbile na

kimavazi katika Mji wa Makkah alikuwa ni kijana Musab Ibn Umayr, ambae alizaliwa

miaka 24 baada ya kuzaliwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, tunapomzungumzia

Musab Ibn Umayr basi tunamzingumzia kijana ambae alikua ni mwenye kupendwa sana

na wazee wake ambao nao ni Umayr Ibn Hashim na Khunaas Bint Malik waliokua ni

matajiri sana, kiasi walikua wakimnunulia Mtoto wao huyo wampendae aitwae Musab

Ibn Umayr kila kitu akitakacho kwa ajili yake.

Hivyo Musab Ibn Umayr alikua ni kijana mtanashati ambae alikua akivaa nguo na viatu

vya kipekeee katika mji wa Makkah, yaani ilikua kila dizain mpya ya viatu au nguo kabla

ya kuingia katika Mji wa Makkah basi kwanza alikua anaonekana nayo Musab Ibn

Umayr, na hivyo basi kila mwanamke kijana wa Mji wa Makkah alikua akivutiwa sana

na kijana Musab Ibn Umayr na kutaka kuolewa nae.

Mbali ya Uzuri wake na kupendeza kwake lakini pia kijana Musab Ibn Umayr alikua ni

kijana mwenye ufaham mzuri sana kuwapita wengi miongoni mwa vijana wenzake na

pia baadhi ya watu wazima katika jamii yake kiasi ya kua alikua ni mwenye kujumuishwa

kwenye Mikutano ya Viongozi wa Mji wa Makkah.

Wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anapokea Utume wake basi kijana Musab

Ibn Umayr alikua na umri wa miaka 15, na hivyo alipotimia umri wa miaka 19 katika

mwaka wa 4 wa Uislam, basi Musab Ibn Umayr akasikia kuhusiana na kile

kinachoendelea katika Nyumba ya Dar Al Arqam, na hivyo bila ya kupoteza mda basi

akakimbilia kisirisiri katika nyumba hio na akasilimu kisirisiri, ambapo hata hivyo siri

hio haikudumu kwa mda mrefu kwani siku moja Uthman Ibn Talha alimuona Musab Ibn

Umayr wakati akiingia ndani ya nyumba ya Dar Al Arqam, habasi zikatapakaa kwenye

Mji wa Makkah na Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu akafungiwa kifungo cha Ndani

na Mama yake na kupokonyonywa kila kitu kilichokua kinampendezesha alichonunuliwa

na wazee wake.

Lakini hata hivyo kifungo hiki hakikumvunja Moyo kijana Musab Ibn Umayr, kwani

alibakia kuendelea kudumu katika imani mpya ya Dini yake, na ilipotokea nafasi ya

Msafara wa kwanza wa Hijra ulioelekea Abyssinia basi Musab Ibn Umayr Radhi Allahu

Anhu akatoroka na kuukimbia mji wa Makkah pamoja na Msafar huo kwa ajili ya


748

kuendelea kuimarisha Imani yake ya Dini ya Kiislam kwa uhuru na Usalama, ambako

alikaa huko hadi mambo yalipopungua uzito wake katika Mji Wa Makkah na kisha

akarudi tena katika Ardhi ya Makkah huku akiwa ni mwenye Imani kubwa zaidi kuliko

hata hapo kabla yake.

Lakini akiwa katika hali inayosikitisha katika maisha yake, kwani alikua ni mtu mwenye

kukosa raha zote na mapambo yote aliyokua akiyapata hapo kabla yake kutoka kwa

wazee wake. Ambapo hata hivyo Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu alikua ni mwenye

kuvitolea kafara vitu vyote hivyo kwa ajili ya Akhera yake na akaamua kumkaribisha

mama yake kwenye Imani ya dini yake, lakini hata hivyo mama yake huyo akasema

kumwambia Musab Ibn Umayr kua:

‘Nenda zako, hakika mimi sina hamu tena ya mimi kua ni Mama yako’ Musab Ibn

Umayr Radhi Allahu Anhu akamkaribia Mama yake na kumwambia: ‘Ewe Mama yangu

nakuusia kwa Moyo wangu wote na kutokana na kua ni mwenye kukujali, hivyo

jisalimishe kwa Mola wako, kwa kusema kua Hakuna Mola anaestahiki kuabudiwa

kwa haki isipokua Allah na Muhammad ni Mja na Mtume wake.’ Lakini hata hivyo

Mama yake huyo akasema: ‘Naapa kwa Nyota zenye kutembea kwa kasi Usiku kua

sitoingia kwenye Dini yako hata kama nikionekana kua mimi sina akili.’

Hivyo Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu akaachana na Mama yake kipenzi na

kuendelea kujitolea kwa ajili ya Mola wake. Ambapo jitihada zake hizo na ufahamu wake

ulimpeleka Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kumchagua kua Balozi wake wa

kwanza kwa ajili ya kumuwakilisha yeye Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Dini

ya Allah Subhanah wa Ta’ala katika ardhi iliyo nje ya Mji wa Makkah, pale ulipowadia

mda wa kuchukua hatua hio kwa kuutambulisha Uislam katika Ardhi ya Mji wa Madinah

.

Baada ya makubaliano ya Al Aqaba yaliyofanyika katika eneo Al Aqaba ambalo ni la

kimlima kidogo kiliopo pembezoni ya mji wa Makkah, katika sherehe hizi walikuja watu

12 kutoka Madinah ambao walikua ni Abu Umamah S’ad Ibn Zurarah, Awf Ibn Al Harith

na kaka yake Mu’adh Ibn Harith, Rafi’ Ibn Malik, Thakwan Ibn Abdil Qays, Ubaadah

Ibn As Samit, Yazid Ibn Tha’labah, Al Abbas Ibn Ubadah, Uqbah Ibn Aamir, Qutbah

Ibn Aamir Radhi Allahu Anhum, waliotoka katika ukoo wa Al Khazraj, Uwaym Ibn

Sa’idah, na Abu ul Haytham Malik Ibn At Tayyihan Radhi Allahu Anhum waliotoka

katika ukoo wa Al Aws na kukutana na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

na wakakukubaliana makubaliano ya ushirikiano baina yao na Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam, na katika kiapo hicho walikubaliana kua: Watampwekesha

na kumtii Allah Subhanahu wa Ta’ala na amri zake zote, hawatoiba, hawatozini,

hawatofanya maovu, n.k


749

Watu hao waliridhika kua kama watafanikiwa katika kuishi maisha ya utiifu kwa Allah

Subhanahu wa Ta’ala basi malipo yao yatakua ni Pepo, vyenginevyo malipo yao yatakua

kwa Allah Subhanah wa Ta’ala, ikiwemo kuwaadhibu na pia akitaka kuwasamahe

atawasamehe. Baada ya makubaliano hayo Nabii Salallahu A’layhi wa Salam akawapa

Sahaba Musab Ibn Umayr aende nao Madinah ili akawasomeshe Qur’an na mambo

mengine yahusuyo dini ya Kiislam.

Bila ya shaka Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakukosea pale alipomchagua

Kijan Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu kwa ajili ya Kubeba bendera ya Uislam na

kuuwakilisha katika ardhi ya Mji wa Madinah kwani Musab Ibn Umayr Radhi Allahu

Anhu alikua ni Kijana ambae mwenye sifa stahiki na zinazotosheleza kubeba uzito wa

Jukumu hilo la kipekee.

Hivyo Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu akafunga safari na kuelekea katika Mji wa

Madinah mnamo mwaka 621 huku akiwa ni Mgeni wa Saad Ibn Zurarah Radhi Allahu

Anhu, ambapo kwa pamoja walikua ni wenye kupita nyumba hadi nyumba kuwaelezea

watu kuhusiana na dini ya Uislam na Alhamd Lillah wengi miongoni mwa watu wa

Madinah wakaukubali ujumbe wa Dini ya Kiislam.

Katika harakati zao Musab Ibn Umayr na Saad Ibn Zurarah Radhi Allahu Anhum

wakafanikia kuwakusnaya Waislam wapya kadhaa na kuaza kuwapa Mafunzo ya Imni

yao mpya, ambpo mara akatokea Usayd Ibn Khuday ambae alikua ni miongoni mwa

Machifu wa Mji wa Madinah na alipofika mbele yao huku akiwa na mkuki wake basi

alikua ni mwenye kujawa na hasira kutokana na kusikia kuhusiana na jitihada za Musab

Ibn Umayr na Saad Ibn Zurarah Radhi Allahu Anhum na hivyo akasema: ‘Hivi kwanini

nyinyi mmekuja kwenye Mji wetu na kuanzisha uchochezi kwa waliokua dhaifu

miongoni mwetu? Kwanini hamuachani nasi kama mnataka kuendelea kuishi?’

Ambapo Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu akatabasam na kisha akasema: ‘Jee

unaweza kukaa kitako wanza na kisha ukanisikiliza? Na hivyo kama utakua ni

mwenye kuridhika na ujumbe wetu basi utakubaliana nao na kama ukiwa

hukuridhika basi sisi hatutoendelea kusema tunayoyasema ambayo

hayakuridhishini na tutaondoka.’ Hivyo Usayd Ibn Khuday akachomeka Mkuki wake

ardhini na kisha akasema: ‘Naam, bila ya shaka hio itakua ni sahih kabisa’ na kisha

akakaa kitako chini.

Kisha Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu akaanza kusoma Qur’an na kufafanua aya

na Hadith za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo haukuchukua mda isipokua

Usayd Ibn Khuday akasema: ‘Kwa hakika ujumbe wa maneno yake ni mzuri sana,

hivi jee ili mtu kuingia kwenye Dini hii anatakiwa afanye nini?’ Musab Ibn Umayr

Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Jitoharishe kwa kukoga na kua na nguo safi kisha


750

shuhudia kua hauna Mola anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokua Allah na

Muhamamd ni Mtume wake na uwe ni mwenye kusali’

Kisha baada ya hapo Usayd Ibn Khudayr akaondoka na baada ya mda akarudi akiwa

amebadilika na akatoa shahada kisha akasali Rakaa mbili na akasema: ‘Baada yangu

basi kuna mtu ambae akikubalia kukufuateni basi kila mtu kwenye Kabila lake

atakua ni mwenye kumfuata yeye na hivyo wacha nikupelekeni katika mahali alipo

kwani yeye ni Sad Ibn Muadh.’ Na bila ya shaka baada ya Musab Ibn Umayr Radhi

Allahu Anhu kuzungumza na Sad Ibn Muadh basi moja kwa moja nae akaingia kwenye

Uislam na kisha baada ya hapo makundi kwa makundi ya watu wa Madinah wakaingia

katika Dini ya Uislam.

Hivyo Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu alikua ni mwenye kuiwakilisha Dini ya

Kiislam ipasavyo na ni mwenye kuyajua majukumu yake ambayo ndio yaliyopelekea

kuzaliwa kwa Taifa Jipya la Kiislam katika Ardhi ya Mji wa Madinah . Na kuandaa

matayarisho ya Maisha mapya ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, na miezi

baadae basi Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu akarudi katika Mji wa Makkah huku

akiwa na Waislam 70 na kukutana kwa mara ya pili na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam katika maeneo ya Aqabah.

Ambapo anasema Jabir Ibn Abdallah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Watu 70 miongoni

mwetu tulisafiri kukutana nae katika mwezi wa Dhl Hijjah, tuliahidiana kua

tukutane nae Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika maeneo ya Al Aqabah,

hivyo tukawasili mmoja mmoja, wawili wawili hadi tukatimia, kisha tukasema: ‘Ya

Rasul Allah unataka tukubaliane juu ya nini?’’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Mnatakiwa Mkubali kua mtakua ni

wenye kunitii katika kila jambo, kutumia Mali zenu katika wakati wa raha na shida,

kuamrishana mema na kukatazana Mabaya kusimama kwa ajili ya Allah

Subhbanah wa Ta’ala bila ya kujali kulalamikiwa na kunilinda mimi na kunisaidia

nitakapokuja kwenu kutokana na kila kitu ambacho mnawalinda watu wenu, wake

zenu na watoto wenu na badala yake malipo yenu yatakua ni Pepo’

Jabir Ibn Abdallah Radhi Allahu Anhu anaendelea kusema kua: ‘Wakati sisi tukiwa

tumesimama tunamsikiliza na Asaad Ibn Zurarah ambae alikua ni kijana moja

miongoni mwetu akanyanyua mkono kisha akasema: ‘Taratibu Enyi watu wa

Yathrib! Sisi hatukutoka na kusafiri kuja hapa kwake bila ya kujua kua yeye ni

Rasul Allah, na kukubaliana nae kwa sasa hivi ni mvutano kwa wengi miongoni

mwa Waarabu, yaani hapa tunazungumzia Kupigana na mtu wa Karibu yako, kwa

kutumia upanga wako hivyo inabidi mfahama hivyo na Malipo yako yatakua Allah

Subhanah wa Ta’ala. Au mnakhofia Maisha yenu, hivyo bora kubalini wazi wazi na

kitakua ni kisingizo chenu mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala’


751

Hivyo watu wakasema: ‘Ewe Asaad shusha chini mkono wako, kwani kwa hakika

sisi hatutoachana na Makubalino haya na wala hatutoondoka’ kisha mmoja baada

ya mmoja tukakubaliana na makubaliano hayo’

Ambapo kwa upande wa Kaab Ibn Malik Radhi Allahu Anhu basi yeye anasema kua:

‘Katika usiku huo tulilala kwenye kambi yetu, na ilipoingia robo tatu ya Usiku basi

tukaondoka mmoja kwa ajili y amakutano yetu na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam katika maeneo ya Aqabah, tulikua Wanaume 73 na Wanawake wawili ambao

ni Nasiba Bint Kaab na Asma Bint Am Ibn Adi’

‘Tukamsubiri Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na mara akatokea huku akiwa

amefuatana na Abbas Ibn Abd Ul Muttalib ambae alikua bado kwa wakati huo

akiwa na dini ya Quraysh, lakini mbali ya hivyo basi alikuja kumuwakilisha Mtoto

wa kaka yake na kuthibitisha Ukweli wake na uaminifu wake, na alipokaa chini

Rasal Allah Salallahu Alayhi wa Salam (baada ya kusema) basi yeye alikua ndio mtu

wa mwanzo kusema’

Abbas Ibn Abd Ul Muttalib akasema: ‘Enyi watu wa Yayhrib, fahamuni kua Darja

ya Muhammad miongoni mwetu ni kama mnavyoijua. Na hakika sisi tumemlinda

kutokana na madhara ya Watu wetu, ambao ni wenye mtizamo kama tuliokua nao,

na anaheshimika kwa watu wake na katika ardhi yake na sasa hivi anasisitiza

kuungana nanyi na kuhamia kwenu nyie, hivyo kama mnadhani kua mtaweza

kutimiza ahadi yenu ya kumlinda na kumhifadhi kutokana na watakaotaka

kumpinga na kumdhuru, basi hilo litakua ni jukumu lenu, lakini kama mnafikiria

kua hamtoweza kufanya hivyo na hivyo mtakua ni wenye kumsaliti basi bora

achaneni nae, kwani hapa ni kwake na yuko salama’

Kaab Ibn Malik Radhi Allahu Anhu anasema kua: ‘Sisi tukasema: ‘Tumekusikia

uliyoyasema Ya Rasul Allah, na hivyo amua mwenyewe kwa ajili yako na kwa ajili

ya Mola wako’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasoma baadhi ya aya za Qur’an, aktuusia

kuhusiana na Allah Subhanah wa Ta’ala na kisha akatualika katika Uislam na kisha

akasema: ‘Mimi nimekubaliana na makubaliano ya kua Nyinyi mtanihifadhi mimi

kutokana na kile mnachowahifadhi dhidi yao watu wenu, wake zenu na watoto

wenu.’’

Kisha Al Barra Ibn Marir Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Naam Tunaapa kwa yule

ambae aliekutuma wewe kwa haki, kua tutakulinda na kukuhifadhi kutoka na kile

ambacho tunawalinda na kuwahifadhi dhidi yake watu wetu, tumekubaliana nawe


752

Ya Rasul Allah, Wallahi sisi ni watoto wa Vita kwani tumerithi hayo kutokana na

Mababa zetu na Mababu zetu.’

Ambapo Abu Haytham Ibn Al Tahin Radhi Allahu Anhu akasema : ‘Ya Rasul Allah

hakika sisi tuna mikataba na Mayahudi, na hivyo tutaibatilisha Mikataba hio, Jee

inawezekana kua kama tukifanya hivyo basi Allah Subhanah wa Ta’ala atakupa

Ushindi na kisha utarudi wewe kwa watu na utauacha sisi?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam atabasamu na kisha akasema ‘La Damu ni Damu

na Maangamizo ni Maangamizo, Mimi ni mmoja miongoni mwenu na Nyinyi ni

Miongoni mwangu, nitapigana na yule mtakaepigana nae na nitatafuta usuluhishi

na yule mtakaesuluhishana nae’

Kisha baada ya hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawachagua Viongozi 12

ambao 9 walikua ni wenye kutoka katika Kabila la Khazraj na 3 kutoka katika Kabila la

Aws. Na kisha akawaambia kwa kusema: ‘Nyinyi ndio wasimamizi wa watu wenu

kama vile ilivyokua wale wasimizi wa Ibn Maryam na mimi ni Msimamizi wa watu

wangu.’

DARJA ZA MASAHABA WA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI

WA SALAM.

Anasema Imam Ibn Hajar Al Asqalani, kua Wanazuoni wanasema kua Sahaba ni: Mtu

alieamini na akamuona Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam japo kwa

mara moja, na mtu huyo akafa wakati akiwa ni Muislam. (Ibn Hajar, Al Isaba)

Masahaba wamegawika katika darja tofauti kutokana na nyakati za kusilimu kwao, hivyo

wale waliosilimu mwanzo hua na darja ya juu kuliko wale waliosilimu baadae. Darja hizi

zilionekana wazi katika maisha ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kwa

namna ya vile alivyokua akiishi na Masahaba zake, kwani siku moja Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam, alimkataza Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu pale

alipokua akigombana na Abd Rahman Ibn Awf Radhi Allahu A’nhu na Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam akamwambia Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu:

‘Msiwakere Masahaba zangu, kwani nnaapa kwa yule ambae Nafsi yangu imo

mikononi mwake! Hata kama mkitumia thamani ya Dhahabu yenye ukubwa wa

Mlima wa Uhud, basi hamtoweka kufikisha thamani ya vitendo vyao’.


753

Hii inatokana na ukweli kua Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu alikua ni miongoni

mwa Masahaba waliochelewa kusilimu kwani yeye aliingia katika Uislam katika kipindi

cha baina ya Mkataba wa Hudaibiyyah na kutekwa kwa mji wa Makkah lakini Abd

Rahman Ibn Awf Radhi Allahu A’nhu alikua ni miongoni mwa watu wa mwanzo kuingia

katika Uislam na pia ni miongoni mwa watu kumi waliobashiriwa Pepo.

Vile vile tunaona mfano mwengine juu ya hili pale ilipotokea siku walipogombana Umar

Ibn Al Khattab na Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu A’nhu, Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam akaingilia kati na kumwambia Umar Ibn Al Khattab: ‘Kwa nini

humuachi Sahaba yangu, kwa ajli yangu? Abu Bakr aliniamini katika wakati

ambao nyinyi nyote mlinikataa’, hapo Abu Bakr akainama na kusema: ‘Ya Rasul Allah

lilikua ni kosa langu’.

Hivyo tunapozungumzia Masahaba, tunatakiwa tujue kua kutokana na mitizamo ya

Wanazuoni basi Masahaba hua wamegawika katika makundi kumi na mbili yafuatayo:-

1. Makhalifah wanne ambao ni Abu Bakr As Siddiq, Umar ibn Al Khattab, Uthman Ibn

Affan na Ali Ibn Abi Talib, na wale waliobashiriwa Pepo wakati wakiwa bado hai, ambao

ni Zubair Ibn Al-Awwam, Abu Ubaidah Ibn Al-Jarrah, Abdur-Rahman Ibn Awf, Talha

Ibn Ubaidullah, Sa‘d Ibn Abi Waqqas na Said Ibn Zad, Radhi za Allah ziwafikie.

2. Wale waliowahi kuamini kabla ya kuamini Umar Ibn Al Khattab, ambao walikua

wakienda katika nyumba ya Arqam kisiri siri kusikiliza ujumbe wa Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam.

3. Muhajjirina waliohamia Uhabeshi (Ethiopia) kwa ajili ya Allah: katika Hijra ya

mwanzo.

4. Ansar au wale walionusuru na kuwepo wakati wa sherehe za kwanza za kula

kiapo cha kumuamini na kuwa pamoja na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam katika Al-Aqaba: Sherehe za Al Aqaba ni sherehe zilizofayika katika eneo Al

Aqaba ambalo ni la kimlima kidogo kiliopo pembezoni ya mji wa Makkah, katika sherehe

hizi walikuja watu 12 kutoka Yathrib (Madina) ambao walikua ni Abu Umamah As’ad

Ibn Zurarah, Awf Ibn Al Harith na kaka yake Mu’adh Ibn Harith, Rafi’ Ibn Malik,

Thakwan Ibn Abdil Qays, Ubaadah Ibn As Samit, Yazid Ibn Tha’labah, Al Abbas Ibn

Ubadah, Uqbah Ibn Aamir, Qutbah Ibn Aamir, waliotoka katika ukoo wa Al Khazraj,

Uwaym Ibn Sa’idah, na Abul Haytham Malik Ibn At Tayyihan waliotoka katika ukoo wa

Al Aws na kukutana na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na

wakakukubaliana makubaliano ya ushirikiano baina yao na Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam, na katika kiapo hicho walikubaliana kua: Watampwekesha na kumtii

Allah Subhanahu wa Ta’ala na amri zake zote, hawatoiba, hawatozini, hawatofanya


754

maovu, n.k na waliridhika kua kama watafanikiwa katika kuishi maisha ya utiifu kwa

Allah Subhanahu wa Ta’ala basi malipo yao yatakua ni Pepo, vyenginevyo malipo yao

yatakua kwa Allah Subhanah wa Ta’ala, ikiwemo kuwaadhibu na pia akitaka

kuwasamahe atawasamehe. Baada ya makubaliano hayo Nabii Salallahu A’layhi wa

Salam akawapa Sahaba Musab Ibn Umayr aende nao Madina ili akawasomeshe Qur’an

na mambo mengine yahusuyo dini ya Kiislam.

5. Ansar au wale walionusuru na kula kiapo cha kuwa pamoja na Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam baada ya Al-Aqaba: Hii ilikua ni katika mwaka uliofuatia

baada ya kiapo cha kwanza cha Al Aqaba, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

alikubaliana kukutana nao tena sehemu ile ile lakini safari hii watu walikua wengi zaid

kwani wanaume walikua wako 73 na wanawake wawili ambao walikua ni Umm Ammara

Nusaibat bint Ka'ab, na Umm Manee’ Asma’ bint Amr. Na hivyo wakakaubaliana

kukutana katika siku za Tashrik (Yaum Tashrik – siku za kuanzia mwezi 11, 12 hadi 13

za mwezi wa Dhul Hija), na katika kiapo hiki wakakubaliana pia kumsikiliza na kumtii

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam katika kila kitu, kujitolea kutumia kila

alichokua nacho mtu kwa ajili ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam iwe

katika wakati wa raha ama katika wakati wa shida, kumlinda Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam kutokana na kila kile anachojilinda mtu na Nafsi yake, na mke wake,

na watoto wake na familia yake, na kukatazana mabaya na kuamrishana mema kwa ajili

ya Allah, na wakifanikiwa kuyatekeleza hayo basi Pepo iko mikononi mwao.

6. Muhajjirina (Waliohama Makkah kuelekea Madinah ) wa mwanzo kuungana

na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kabla ya kuwasili katika mji wa

Madinah , alipokua Qubah ambapo alikua amepumzika kidogo akitokea Makkah katika

wakati wa Hijrah ya kwanza (Kuhama kutoka katika mji wa Makkah kwenda katika mji

wa Madinah ).

7. Ahl ul Badr : Masahaba waliopigana vita vya Badr.

8. Wale waliohamia Madinah baina ya kipindi cha vita vya Badr na mkataba wa

Hudaybiyah.

9. Masahaba waliokula kiapo kushirikiana na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam chini ya mti wakati wa mkataba wa Hudaybiyah.

10. Masahaba waliosilimu na kuhamia Madinah baada ya mkataba wa Hudaybiyah.

11. Masahaba waliosilimu baada ya kutekwa kwa mji wa Makkah.


755

12. Watoto waliomuona Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam wakati wa

uhai wake, aidha wakati wa kutekwa Makkah au katika wakati wa Hija ya mwisho ya

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, au waliomuona katika sehemu tofauti na

nyakati tofauti.

KUZALIWA KWA BAHR UL ILM ABDA ALLAH IBN ABBAS RADHI

ALLAHU ANHU.

A’bd Allah ni mtoto alietokana na baba aitwae Al ‘Abbas Ibn Al Muttalib Radhi Allahu

A’nhu, ambae ni Ami ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, na Mama aitwae

Al Lubaba Al Ghubra Bint Harith Ibn Hazan Al Hilalieh ambae alikua ni dada wa Al

Lubabab As Saghira Bint Harith Ibn Hazan Al Hilalieh ambae alikua ni mama yake

Khalid Ibn Walid na alikua ni dada yake Maymunah Bint Harith Ibn Hazan Al Hilalieh

ambae aliekua ni Mke wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam.

Abd Allah Ibn ‘Abbas Radhi Allahu A’nhu alizaliwa miaka mitatu kabla ya Hijra, wakati

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam anafariki Abd Allah Ibn ‘Abbas Radhi

Allahu A’nhu alikua na umri wa miaka kumi na tatu. Ingawa alikua ni kijana mdogo

lakini alikua na I’lm kubwa sana na hii inatokana na kua, baada ya kuzaliwa tu, mama

yake alimchukua Abd Allah Ibn ‘Abbas Radhi Allahu A’nhu na kumpeleka moja kwa

moja kwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ambae alimuwekea sehemu ya

mate yake yenye baraka kabla hata ya kuanza kunyonya.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua na ukaribu sana na binamu yake

huyu ambae alikua akiishi nyumbani kwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam,

na mara kwa mara alikua akikaa nae humuombea dua ‘Ya Rabb, mfanye awe na

ufahamu mkubwa wa I’lm ya Dini na umpe uwezo wa Tafsir’.

Anasema Abd Allah Ibn ‘Abbas Radhi Allahu A’nhu ‘Mara moja Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam alikua anataka kutia udhu, nikakimbilia kumpelekea

maji ya kutia udhu, alifurahia jambo hilo, na alipokua anataka kusali, akaniambia

nisimame pembeni yake, hata hivyo nilisimama nyuma yake, na baada ya kumaliza

kusali akaniuliza kitu gani kilichokufanya usisimame pembeni yangu, Ya Abd

Allah?’ nami nikajibu ‘Una cheo kikubwa sana katika macho yangu, kiasi ya

kwamba mimi siwezi kusimama pembeni na wewe’, hapo Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam akatabasamu na kunyanyua mikono juu na kusema ‘Ya Allah!

Mzidishie hikma’.

Bila ya shaka dua ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam hukubaliwa, Abd

Allah Ibn ‘Abbas Radhi Allahu A’nhu alipata I’lm wakati wa uhai wa Nabii Muhammad


756

Salallahu A’layhi wa Salam na baada ya kufariki kwake alikua Bahr ul I’lm (Bahari ya

I’lm ya Ummah wa Kiislamu) na alikua ni mwenye busara sana. Kila Abd Allah Ibn

‘Abbas Radhi Allahu A’nhu alipokua akikua kiumri na kiumbo alikua akikua kia I’lm,

kiufaham na kibusara pia, anasema Masruq Ibn al Ajda: ‘Kila nimuonapo Abd Allah

Ibn ‘Abbas Radhi Allahu A’nhu, hua nnasema: ni kijana anaependeza sana, na

anapozungumza hua nnasema: Ni kijana mwenye I’lm kubwa kupita watu wote’

Abd Allah Ibn ‘Abbas Radhi Allahu A’nhu alikua na kumbukumbu nzuri sana,

anapoelezea kitu huelezea kwa uwazi na kwa hoja zinazofahamika mara moja.

Sad Ibn Abi Waqqas Radhi Allahu A’nhu anamuelezea Abd Allah Ibn ‘Abbas Radhi

Allahu A’nhu kwa kusema ‘Sijawahi kuona mtu mwenye kufahamu haraka, na

mwenye I’lm kubwa na busara kuliko Abd Allah Ibn ‘Abbas, nimemuona Umar

akimwita katika kujadili matatizo magumu mbele ya Masahaba wakongwe

waliopigana vita vya Badr. Miongoni mwa Ansar na Muhajirin, Ibn ‘Abbas

anaweza akatoa hoja na Umar hatoweza kuipinga hoja yake.’ Abd Allah Ibn ‘Abbas

Radhi Allahu A’nhu alikua mrefu, mweupe mwenye sura ya kupendeza na uso

unaong’ara na alikua akipaka hina nywele zake na ndevu zake.

Na kisha baada ya hapo Waislam mmoja baada ya mmoja wakawa kidogo kidogo

wanafanya Hijra na kuhamia katika Mji wa Madinah kabla ya Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kuamrishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala kuhamia katika mji wa

Madinah baada ya Makafiri kuamua kupanga Njama za kutaka kumuua Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam.

HIJRA YA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM

Katika kulala kwake Usiku, siku mmoja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alilala

na kuota kua ameamrishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala ahame kutoka katika Mji wa

Makkah kisha ahamie katika mji wenye Mitende mingi sana, na alipouona Mji huo basi

kwanza akadhania kua ni Mji wa Al Yamamah kutokana na mazingira yake lakini Allah

Subhanah wa Ta’ala akamwambia kua Mji huo ni Madina, lakini mda wa kuhama ulikua

haujawasili bado kwani ndoto hio ilikua kabla ya Safari ya Isra na Miraj.

Hivyo mda huo ulipowadia basi akataarifiwa na hivyo katika mchana wa siku moja ya

Jumatano ya mwezi Rabbi al Awwal ambao ni sawa na September ya mwaka 622 basi

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akatoka na kuelekea katika nyumba ya Abu Bakr

Saddiq Radhi Allahu Anhu ambapo Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu aliposikia

kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliposikia ugeni huo basi alishangaa sana

kwani ilikua ni mchana wa siku ya joto kali sana hivyo akasema: ‘Wallahi Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam hakuwahi kuja Nyumbani wangu katika wakati kama


757

huu, hivyo itakua lazima kuna jambo muhimu sana.’ Na kisha akamkaribisha ndani

na kusema: ‘Ya Rasul Allah! Kuna jambo gani?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala

ameniruhusu nihame katika Mji Wa Makkah nielekee katia Mji wa Madinah ’

Abu Bakr Saddiq Radhi Allahu Anhu akauliza: ‘Jee na mimi nimepata heshima hio ya

kuenda pamoja nawe?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam’

ambapo Abu Bakr Saddiq Radhi Allahu Anhu akafurahia sana kupata fursa hio kiasi ya

kua furaha yae ilimpekea kulia kwa hisia, za mapenzi yake kwa rafiki yake kipenzi ambae

ni Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Kisha baada ya hapo, Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akakubaliana na Abu Baqr

As Siddiq Radhi Allahu Anhu kua wazungumze na Abdullah Ibn Urayqit ambae ni Kafiri

anaeaminika katika utimizaji wa ahadi kua awasaidie kuwaongoza njia kuelekea katika

mji wa Madinah kwa malipo ya Ngamia wawili, na wakakubaliana kua wakutane kwenye

Mlima wa Thawr.

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akarudi Nyumbani kwake na alipofika

mara akatokea Malaika Jibril na kumwambia kua: ‘Leo Usiku usilale katika Kitanda

chako ambacho umezoea kila siku kulala’ na kisha akamfahamisha nini cha kufanya,

hivyo ulipoingia wakati wa kulala usiku basi Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam

akamwambia Ali ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kua: ‘Leo lala kitandani kwangu,

chukua hili guo langu la kijani ujifunike na wala usiwe na khofu kwani hakuna

madhara yatakayokufika.’

Na kisha akamkabidhi Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu na Ummu Ayman Radhi

Allahu Anha amana zote alizokabidhiwa na watu wa Makkah kwa ajili ya kuwakabidhi

wenye katika siku zitakazofuata wakati yeye akiwa hayupo. Na ulipoingia wakati wa

Usiku wa Manane wa siku hio ya kuamkia Alkhamis basi Makafiri wakajiandaa kwa ajili

ya kumsubiri Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam atakapotoka alfajir wamuue, kwani

kwa mila za Kiarabu hua haikubaliki kumuua Mtu wakati akiwa ndani ya nyumba yake.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipoamua kutoka basi akatoka na

kuwakuta Makafiri hao wakiwa wamelala nje ya nyumba yake wakiwa na Silaha zao,

hivyo akachukua Mchanga na kisha akausomea aya za Surat Yasin zisemazo:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞يس ۤ ‏۞وَٱلْقُرْآنِ‏ ٱلحَْكِيمِ۞إِن َّ كَ‏ لَمِنَ‏ ٱلْمُ‏ رْسَلِينَ۞عَلَىٰ‏

صِرَاطٍ‏ م ُّسْتَقِيمٍ۞تَنزِيلَ‏ ٱلْعَزِيزِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞لِتُنذِرَ‏ قَوْماً‏ م َّآ أُنذِرَ‏ آآبَ‏ ‏ُؤهُمْ‏ فَهُ‏ ‏ْم


758

غَافِلُونَ۞لَقَدْ‏ حَق َّ ٱلْقَوْلُ‏ ٰ عَلَى أَكْثَرِهِمْ‏ فَهُمْ‏ لاَ‏ يُؤْمِنُونَ۞إِ َّ ‏َج عَلْنَا فيِۤ‏ ن ا أَْع قِهِْم

أَغْلاَلاً‏ فَهِىَ‏ إِلىَ‏ ٱلأَذْقَانِ‏ فَهُم م ُّقْمَحُونَ۞وَجَعَلْنَا مِن بَينِْ‏ أَيْدِيهِمْ‏ سَ‏ ‏ّداً‏ ومِ‏ ‏ْن

خَلْفِهِمْ‏ سَدّاً‏ فَأغْشَيْنَاهُمْ‏ فَهُمْ‏ لاَ‏ يُبْصِرُونَ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Ya-seen; Waalqur-ani alhakeemi; Innaka

lamina almursaleena; AAala siratin mustaqeemin; Tanzeela alAAazeezi

alrraheemi; Litundhira qawman ma ondhira abaohum fahum ghafiloona; Laqad

haqqa alqawlu AAala aktharihim fahum la yu/minoona; Inna jaAAalna fee

aAAnaqihim aghlalan fahiya ila al-athqani fahum muqmahoona; WajaAAalna min

bayni aydeehim saddan wamin khalfihim saddan faaghshaynahum fahum la

yubsiroona (Surat Yasin 36:1-9)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma, Yasiin, Naapa kwa

Qur’an iliyojaa hikma; Hakika wewe (Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) ni

Miongoni mwa Mitume; Ulie katika njia iliyonyooka; Hii (Qur’an) ni uteremsho

kutoka kwa Mtukufu mwenye Rehma; Ili upate kuwaonya Watu, ambao wazee wao

hawakuonywa hivyo wakawa ni wenye kughafilika; Kwa hakika kauli ya haki

imedhibitika juu yao lakini wengi wao si wenye kuamini; Kwa hakika tumeweka

Shingoni mwao vifungio vya vyuma hadi Videvuni mwao, hivyo Vichwa vyao

vimeelekea Juu; Na tumeweka pazia baina yao mbele yao, na baina yao nyuma yao na

tumewafunika hivyo hawawezi kuona kitu.

Na kisha akawarushia rushia mchanga huo kichwani na vifuani mwao, na kuwaacha

wakiwa wanaendelea kulala. Baada ya mda Makafiri hao wakaamshwa na wenzao na

wakaulizwa: ‘Mbona mmelala hapa mkiwa katika hali kama hii imekuaje?’ nao

wakajibu: ‘Tunamsubiri Muhammad’ hivyo wakaambiwa: ‘Mnaemsubiri hayupo

kwani amekumwagieni mchanga mwilini mwenu na kukuacheni kama mlivyo na

kisha akaenda zake, jiangalie namna mlivyo’

Makafiri hao wakajiangalia na kujikuta wamejaa michanga, na hapo hapo kwa haraka

sana wakanyanyuka na kukimbilia ndani ya Nyumba ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, na moja kwa moja hadi chumbani kwake, na walipofika Kitandani mwake

wakamkuta mtu ambae alikua amelala na kujifunika, wakakimbilia kumfunua guo hilo

mtu aliejifunika, na kwa mshangao wao badala ya kumuona Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam basi wakamuona Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu akiwa amelala kitandani

hapo badala yake.


759

Hivyo kwa hasira wakamkamata Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu na kumuuliza,:

‘Yuko wapi Muhammad?’ nae akajibu: ‘Hakika mimi si mwenye kujua kua

ameenda wapi.’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala analielezea hili katika Qur’an pale aliposema:

‏﴿وَإِذْ‏ يمَْكُرُ‏ بِكَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ لِيُثْبِتُوكَ‏ أَوْ‏ يَقْتُلُوكَ‏ أَوْ‏ يخُْرِجُوكَ‏ وَيمَْكُرُونَ‏ وَيمَْ‏ كُرُ‏ ٱهلل َُّ‏

وَٱهلل َُّ‏ خَيْرُ‏ ٱلْمَاكِرِينَ‏ ﴾

Wa-idh yamkuru bika alladheena kafaroo liyuthbitooka aw yaqtulooka aw

yukhrijooka wayamkuroona wayamkuru Allahu waAllahu khayru almakireena

(Surat Al Anfal 8:30)

Tafsir: Na kumbuka pale walipokupangia njama wale waliokufuru wakufunge ili

wakuue au wakufukuze (Kutoka kwako), na wakapanga njama na akapanga Allah

lakini Allah ni mbora wa kupanga.

Baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuwamwagia mchanga Watu hao na

kuondoka basi alielekea moja kwa moja hadi kwa Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu

Anhu na kisha wakachukua mahitajio yao, na wakaondoka huku Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akitumia mlango wa Nyuma na kisha wakaelekea kwenye Mlima wa

Thawr ambao upo katika umbali wa masafa ya kilomita 3 kutoka katika mji wa Makkah.

Ambapo safari yao hio ilimalizika ndani ya saa moja, na walipofika Mlimani hapo

wakakuta Pango ambalo lilikua tupu, huku ikiwa bado kiza kiza basi Abu Bakr Radhi

Allahu Anhu akaingia ndani ya Pango hilo na kisha akaanza kusafisha safisha ndani yake

ili angalau wapate kujihifadhi na kujificha ndani yake. Baada ya sehemu hio kua tayari

basi akamwita Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae nae akaingia ndani yake

na Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu akaziba uwazi wa pango hilo kwa kutumia

nguo yake na sehemu iliyobakia basi akaziba kwa kutumia unyayo wake.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuegemea rafiki yake kutokana na

uchovu wake na hapo hapo Allah Subhanah wa Ta’ala akamletea usngizi mzito sana kwa

ajili ya mapumziko yake. Ambapo ghafla Abu Baqr Radhi Allahu Anhu akahisi maumivu

makali sana katika Mguu wake ambao ndio uliokua umeegemewa na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo akashindwa kuuangalia mguu wake kutokana na kua

na khofu kua kufanya kwake hivyo kutamwamsha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam na kumkatisha usingizi wake mbali ya kua aligundua kua maumivu hayo

yametokana na sumu ya nyoka aliekua akiondoka baada ya kumtafuta mguu wake.


760

Abu Baqr Radhi Allahu Anhu aliendelea kustahmili maumivu hayo hadi taratibu machozi

yakaanza kumtoka na kumdondokea Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam usoni

mwake, jambo ambalo lilipelekea kumwamsha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na kumuuliza: ‘Vipi mbona unalia kuna kuna nini?’ ambapo Abu Baqr Radhi Allahu

Anhu akasema: ‘Ya Rasul Allah kuna Mdudu kanitafuna mguu wangu, lakini hamna

tatizo kwani bora Baba yangu na Mama yangu watolewe kafara kwa ajili yako.’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akalipaka Mate jeraha hilo na hapo hapo

maumivu aliyokua akiyahisi Abu Baqr Radhi Allahu Anhu yakatoweka na ukapona mguu

wake.

Wakati yote haya yanaendelea ya kuamka kwake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na kisha kua ni mwenye kutibu Jeraha la Abu Bakr Radhi Allahu Anhu basi Allah

Subhanah wa Ta’ala kwa makadirio yake akatokea Mdudu Buibui na kuanza kutandaza

uzi wake kwenye Mlango wa pango hilo, na kisha kwa juu yake akatokea Njiwa akataga

na hapo hapo akawa ni mwenye kulalia Mayai yake.

Na kwa upande mwengine basi watu wa Makkah wakawa wamehamanika kwani

waliekua wakimtaka amewaponyoka, hivyo wakakimbilia kwenye Nyumba ya Abu Baqr

Radhi Allahu Anhu, kwani labda huenda wamtafutae ikawa amejificha kwake, lakini

walipofika nyumbani kwake basi wakakuta pia kua hata Abu Baqr Radhi Allahu Anhu

mwenyewe hayuko kwenye nyumba yake, hivyo wakajawa na hasira zaid kwani hata

Abu Baqr Radhi Allahu Anhu nae haionekani hata dalili yake.

Makafiri hao wakatangazia zawadi ya Ngamia 100, kwa yeyote yuleatakaemkamata au

kumuua Muhamamd Salallahu Alayhi wa Salam na kuuleta mbele yao Mwili wake, hili

lilikua ni dau kubwa sana kwa kila mtu wa Mji wa Makkah kwani hata kama ukiwa

masikini basi hua ni mwenye kuagana nao umasikini kama ukipata Ngamia hao, hivyo

kila mtu akafanya jitihada kwa ajili ya kumtafuta Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam,

na kuna baadhi wakakodi watu wenye uwezo wa kusoma nyao ardhini ili kujua muelekeo

na mda wa safari ya mwenye alama ya nyayo hizo.

Na hivyo Wataalamu hao wakafuatilia Nyao za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na Abu Bakr Radhi Allahu Anhu hadi kwenye Pango liliopo kwenye Mlima Thawr,

ambapo ndipo zilipomalizikia lakini sasa kila wakiangalia ndani ya pango hio basi

walikua wakiona yale wasiyoyategemea, kwani mtandao wa uzi wa Buibui ulikua

umetanda kwenye mlango mzima wa Pango hilo, na hakuna hata dalili ya kua labda

ulipanguswa na kutengenezwa tea, kwani uzi huo ulikua mkamilifu na buibui mwenyewe

yuko juu yake, kisha na pembeni yake kwa juu zaidi kuna Njiwa ambae alikua amelalia

Mayai yake.

Mazingira ya muonekano huu yaliwafanya watu hao kutoamini kua kile wanachokitafuta

kua kinawezekana kikawa kimo ndani yake, lakini sasa haiwezekani kwa kitu chochote


761

kuingia ndani yake pango hilo bila ya kuharibu mazingira wanayoaona mbele ya macho

yao ambapo wakati Makafiri hao wanashangaa kuona kua nyao hizo zimeishia hapo

halafu zikayayuka bila kuacha athari yeyote na kushangazwa na mazingira ya mlango wa

pango hilo basi kwa upande wa Abu Baqr Radhi Allahu Anhu alikua amejawa na khofu

kwani alikua ni mwenye kumuona kila mtu anaechungulia ndani ya pango hilo, na kuhisi

kua mda wa uhai wake umeifikia ukingoni kwani mda wowote wanaweza wakaangukia

ndani ya mikono ya maadui zao.

Lakini cha kushangaza ni kua hakuna hata mtu mmoja alieonesha kua amemuona Abu

Baqr Radhi Allahu Anhu, hivyo kwa tahadhari basi Abu Baqr Radhi Allahu Anhu

akasema kumwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Ya Rasul Allah

hakika mimi sitohisi vibaya wala sitojisikia huzuni kama watu hawa wataniona na

kuniua mimi, kwa sababu mimi ni mtu mmoja peke yake, lakini kwako wewe

wakikuua basi itakua wamesababisha maangamizi kwa Ummah wako.’.

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamwambia Abu Baqr Radhi Allahu

Anhu kua: ‘Usiwe na khofu wa huzuni ewe Abu Baqr kwani kwa hakika Allah

Subhanah wa Ta’ala yuko pamoja nasi.’ Abu Baqr Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Ya

Rasul Allah hakika watu hawa kama mmoja wao atainama na kuchungulia kidogo

tu basi atatuona’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamwambia Abu Baqr Radhi

Allahu Anhu kua: ‘Ewe Abu Baqr hivi unafikiria ni nini kitakachotokea kwetu

wakati sisi ni wawili na watu aliepo pamoja nasi ni Allah Subhanah wa Ta’ala? Hivi

unadhani kua itawezekana kukamatwa kwetu?’

Wakati wanajadiliana haya basi wakasikia sauti ya Ummayah Ibn Khalaf akiwaambia

Makafiri waliokua wakishangaa juu ya pango hilo kwa kusema: ‘Hivi jee mnafikiria

kua hawa watakua wameingia ndani ya Pango hili, hivi jee nyinyi hamuoni mtandao

wa Buibui huo? Wa Allahi mimi nnaona kua huyu Buibui amejenga hapa hata

kabla ya Muhammad mwenyewe hajazaliwa’

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuombea dua Abu Baqr Radhi Allahu

Anhu ili apate utulivu ndani ya nafsi yake aondokewe na khofu na wasiwasi wake,

ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala analielezea hili kwa kusema:

‏﴿إِلا َّ تَنصُرُوهُ‏ فَقَدْ‏ نَصَرَهُ‏ ٱهلل َُّ‏ إِذْ‏ أَخْرَجَهُ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ اثَنىِ‏ َ ٱثْنَينِْ‏ إِذْ‏ همَُا فىِ‏ ٱلْغَارِ‏

إِذْ‏ يَقُولُ‏ لِصَاحِ‏ بِهِ‏ لاَ‏ تحَْزَنْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ مَعَنَا فَأَنزَلَ‏ ٱهلل َُّ‏ سَكِينَتَهُ‏ عَلَيْهِ‏ وَأَي َّدَهُ‏ بجُِنُودٍ‏ لم َّْ‏


762

وَجَعَلَ‏ كَلِمَةَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ ٱلس ُّفْلَى ٰ وَكَلِمَةُ‏ ٱهلل َِّ‏ هِىَ‏ ٱلْعُلْيَا وَٱهلل َُّ‏ عَزِيزٌ‏ تَرَوْهَا

حَكِيمٌ‏ ﴾

Illa tansuroohu faqad nasarahu Allahu idh akhrajahu alladheena kafaroo thaniya

ithnayni idh huma fee alghari idh yaqoolu lisahibihi la tahzan inna Allaha

maAAana faanzala Allahu sakeenatahu AAalayhi waayyadahu bijunoodin lam

tarawha wajaAAala kalimata alladheena kafaroo alssufla wakalimatu Allahi hiya

alAAulya waAllahu AAazeezun hakeemun (Surat At Tawba 9:40)

Tafsir: Kama hamtomnusuru (Mtume wenu Salallahu Aalyhi wa Salam basi sio

tatizo)kwani Allah atamnusuru, (kama alivyomnusuru) wakati Makafiri

walipomfukuza na wa pili kati ya wawili baina yao walipokua kwenye pango alisema

kumwambia rafiki yake: ‘Usiwe na Khofu kwani Allah yuko pamoja nasi’ kisha Allah

akatuma utulivu juu yake na kumzidishia nguvu jambo ambalo hamkuliona, na

tukajaalia kauli za wale ambao waliokufuru kua zimedhalilika, na maneno ya Allah

kua yako juu na yametukuka, kwani kwa hakika Allah ni mwenye utukufu na ni

mwenye hikma.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu

Anhu walikaa na kupata utulivu ndani ya Pango hilo na kupumzika vya kutosha, kwani

walikaa kwa siku tatu kuanzia alfajir ya Alkhamis hadi Jumapili, kwa sababu walikua

wanajua kua Makafiri wataendelea kuwatafuta kwa siku mbili tatu kabla ya kukata tamaa

kwao.

Ambapo katika kipindi hiki basi Abdullah Ibn Abu Bakr Radhi Allahu Anhu alikua akikaa

katika mji wa Makkah na kusikiliza kinachoendelea katika jamii yake kasha usiku huenda

kwenye Pango la Mlima Thawr na kuwaelezea Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu kinachoendelea katika akili na ufahamu wa

watu wa Makkah kuhusiana nao, na kisha Alfajir hurudi katika Mji wa Makkah.

Na kwa upande mwengine basi Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu alikua na

Mtumwa wake aitwae Amir Ibn Fuhayra Radhi Allahu Anhu ambae yeye alikua akifuga

Mbuzi na kazi yake ilikua ni asubuhi kuwapelekea Maziwa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam na Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu na pia kufuta alama za nyayo za

Abdallah Ibn Abu Baqr Radhi Allahu Anhu.

Hivyo baada ya siku tatu basi Makafiri wa Makkah wakakata tamaa ya kuwapata Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu na hivyo

Abdullah Ibn Abu Bakr Radhi Allahu Anhu akawasilisha habari hio, ili Abdullah Ibn Abu

Bakr Radhi Allahu Anhu ili wajitayarishe kwa ajili ya kuchukua hatua ya pili ya mipango


763

yao ya safari ambayo ni kutoka kwenye Pango hilo na kuendelea na safari yao kueleka

katika Mji wa Madinah .

Na ulipoingia Alfajiri ya kuamkia siku ya Jumatatu basi wakatoka nje ya Pango hilo na

wakakutana na Abdullah Ibn Urayqit huku akiwa na Ngamia wake wawili ambao ndio

Malipoa yake waliyokubaliana nae Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Abu Baqr

As Siddiq Radhi Allahu Anhu hapo awali, huku pembeni yake akiwepo Asma Bint Abu

Baqr Radhi Allahu Anha ambae alikua amewatayarishia chakula cha safari yao hio.

Asma Bint Abu Baqr Radhi Allahu Anha alikua ametayarsisha Nyama ya Mbuzi na Maji

kwa ajili ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu

Anhu ambapo kutokana na haraka basi akasahau kuifunga mikoba hio ya ngozi yenye

Maji na Nyama, na hivyo ikambidi achane mkanda wa kanzu yake kwa ajili hio ili maji

hayo na Nyama zisimwagike na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipojua

kuhusiana na tukio hilo basi akampa Asma Bint Abu Baqr Radhi Allahu Anha jina la

Dhat an-Nitaqayn yaani mwenye Mikanda Miwili kwa ajili yake kesho Peponi.

Kisha baada ya hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Abu Baqr As Siddiq

Radhi Allahu Anhu wakapanda Ngamia wao hao wawili, huku Amir Ibn Furayha Radhi

Allahu Anhu kwa amepanda pia nyuma ya Ngamia wa na Abu Baqr As Siddiq Radhi

Allahu Anhu na safari yao ikaanza, lakini kabla ya kufika mbali basi Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akageuka nyuma na kuuangalia Mji wake anaoupenda, Mji

aliokaa Miaka yote, Mji ulioanzishwa na Nabii Ibrahim na Nabii Ismail, hivyo kua ni Mji

ambao hataki kuachana nao, kutokana na utukufu wake, lakini alikua hana budi kwani

kama akibakia basi Maisha yake yatakua hatarini.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Wa Allahi Hakika wewe ni

Mji bora kuwahi kuumbwa na Allah Subhanah wa Taala, wewe ndie Mji

unaependwa zaidi na Allah Subhanah wa Ta’ala, na pia hakuna Mji nnaoupenda na

unaonivutia mie kama Mji wewe, hivyo wa hakika kama si kufukuzwa kwangu basi

mimi nisingekuhama na nisigetaka kuhamia katika Mji mwengine wowote zaidi

yako.’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

huyo kua:

‏﴿إِن َّ ٱل َّذِى فَرَضَ‏ عَلَيْكَ‏ ٱلْقُرْآنَ‏ لَرَآد ُّكَ‏ إِلىَٰ‏ مَعَادٍ‏ قُل ر َّبيّ‏ ِ ۤ أَعْلَمُ‏ مَن جَآءَ‏ بِ‏ ٱلهُْدَىٰ‏

وَمَنْ‏ هُوَ‏ فىِ‏ ضَلاَلٍ‏ م ُّبِينٍ‏ ﴾


764

Inna alladhee faradha AAalayka alqur-ana laradduka ila maAAadin qul rabbee

aAAlamu man jaa bialhuda waman huwa fee dhalalin mubeenin (Surat Al Qasas

28:85)

Tafsir: Hakika ya yule ambae amekufaridhishia juu yako Qur’an, atakurudisha katika

sehemu ya kurudia (katika Mji wa Makkah), sema: ‘Mola Wangu ni mwenye Kujua ni

nani aliekuja na uongofu nani alie katika upotofu mkubwa sana’

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu

Anhu, Amir Ibn Furayha Radhi Allahu Anhu na Abdullah Ibn Urayqit wakaendelea na

safari yao ya kueleka Madinah lakini iliwabidi kubadilisha njia na kutumia njia ya

mzunguko ili wasije wakafuatwa na Makafiri, hivyo kwanza walielekea upande wa

Kusini Magharibi katika maeneo ya ardhi ya Mji wa Tihama na kisha wakageuza na

kuelekea juu katika upande wa Kaskazini wakikaribia kuambaa ambaa na mwambao wa

Bahari Nyekundu.

Ambapo katika kipindi hiki cha safari yao basi mara Ngamia wa Abu Baqr As Siddiq

Radhi Allahu Anhu anamkazanisha akae mbele ya Ngamia wa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam na mara anamrudi Nyuma ya Ngamia wa Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuuliza Abu Baqr As Siddiq

Radhi Allahu Anhu : ‘Ya Abu Baqr mbona hivyo mara unaenda mbele mara unarudi

nyuma yangu kuna nini?’

Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Ya Rasul Allah, hakika mimi

nikikaa nyuma yako basi siridhiki hua nahisi bora niwe mbele yako ili nipate

kukulinda kwa ajili ya usalama wako, na nikakaa nyuma yako basi hua siridhiki na

hua nahisi bora nikae mbele yako kwa ajili ya kukulinda usalama wako kwa upande

wa mbele yako.’

Safari ilikua ndefu a ya uchovu kwani siku hio walisafiri siku nzima wakiwa juu ya

Ngamia hadi siku ya pili yake asubuhi wakaamua kupumzika kwenye mmoja katika mti

iliyokua na kivuli, Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akashuka na kulala, huku Abu

Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu akiwa ni mwenye kusimamia usalama, katika

kuangalia kwake basi kwa mbali akaona kuna mfugaji wa Kondoo, hivyo akamfuata na

kisha akarudi huku akiwa na maziwa na kumpa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

ambae alikua ameshaamka, na alipopewa akanywa.

Na kisha baada ya hapo wakaondoka na kuelekea tena kwa Mfugaji huyo ili wapate

maziwa mengine zaid lakini, mfugaji akasema: ‘Sina maziwa zaidi ya yale niliyokupeni

kwani maziwa ya Mbuzi wangu yamekauka’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam akaomba kumuangalia Mbuzi huyo na kisha akazishika chuchu za Mbuzi huyo na

hapo hapo chuchu hizo zikawa ni zenye kujaa Maziwa. Tukio hili lilimstaajabisha sana


765

Mfugaji huyo a akauliza: ‘Hebu niambie wewe nani mbona mimi sijawahi kukutana

na mtu mwenye maajabu kama wewe.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamwambia Mchungaji huyo kua:

‘Nitakuambia kama utakubalia kua hili nitakalokuambia litabakia kua ni siri yako’

Mfugaji huyo akasema: ‘Naam..sitomwambia Mtu yeyote’ Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akasema: ‘Mimi ni Muhammad Rasul Allah’

Mfugaji huyo akasema: ‘Hivyo wewe ndio yule mtu ambae watu wa Quraysh

wanasema kua umepotoka?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam

hivyo ndivyo wasemavyo’ Mfugaji huyo akasema: ‘Hakika mimi nnashuhudia kua

wewe ni Rasul Allah na kile ulichokuja nacho ni cha haki, kwani ni Mtume tu ndio

mwenye uwezo wa kufanya unayoyafanya wewe, hivyo nami nitakufuata na kukutii,

hivyo jee nami nnaweza kujumuika nanyi?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akasema: ‘La bado kwanza, hivyo subiri kwanza hadi pale utakaposikia kua

nimefanikiwa ndio unaweza kujumuika nasi.’

Msafara huo wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ukaendelea na safari yake hadi

pale ulipofika katika maeneo ya Qudayd ambapo waliichagua sehemu hii pia kua ni ya

kumpumzikia kutokana na umbali wa masafa waliyotembea kutoka katika kituo cha

kwanza cha mapumziko, na walipofika katika maeneo hayo walikuta kuna hema la bwana

mmoja aliekua akijulikana kama Abu Mabad, ambae hata hivyo mwenye alikua hayupo

na badala yake alikuwepo Mke wake aliekua akiitwa Umm Mabad na hivyo wakamuuliza

baada ya kusalimiana nae kua: ‘Jee unaweza kutusaidia aina yeyote ya chakula

ulichonacho?’ ambapo nae akajibu kua hana chakula chochote cha ziada.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipoangalia pembeni akaona kuna Mbuzi

ambae alikua amekonda na kudhoofika, hivyo akasema: ‘Jee Mbuzi huyu hana Maziwa

yeyote?’ Hivyo Umm Mabad akasema: ‘Huyu mbuzi hana hata damu jee atakua na

maziwa kweli?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kama utaniruhusu

nimkame basi nitamkama.’

Hivyo Umm Mabad akaona huyu hawa wageni wanataka kuleta ubishi, hivyo

kuwakomesha ubishi wao basi bora awaruhusu wamkame Mbuzi huyo ili wajiridhishe

kua kweli hana Maziwa, hivyo akasema: ‘Sawa Nakuruhusu Mkame’ ambapo Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamsogelea Mbuzi huyo na kisha akamshika chuchu

zake na kusema: ‘Biismi Allahi Al Rahmani Al Rahim’ na kisha akaomba dua na

kuomba aletewe chombo cha kuhifadhia maziwa.

Na alipoletewa akaanza kumkama Mbuzi huyo, na taratibu Mbuzi huyo akaanza kutoa

Maziwa ambayo kadri anavyokamwa basi ndivyo yalivyokua yakiongezeka wingi wake

maziwa hayo, chombo kilicholetwa kikajaa, Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam


766

akanywa maziwa yeye na watu wake, na mengine yakabakia na Mbuzi akawa anaendelea

kutoa Maziwa, na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaomba kua Mbuzi

huyo asichinjwe.

Na kisha msafara wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ukaendelea na safari yake,

na huku nyuma Abu Mabad aliporudi kwake akashangaa alipokuta Maziwa mengi

Nyumbani kwake, hivyo akauliza yametokea wapi maziwa hayo, basi Umm Mabad

akajibu: ‘Kuna Mtu wa Maajabu yenye Baraka alipita leo hapa kwetu, akaomba

chakula nilipomwambia hakuna basi akaomba kumkama Mbuzi wetu aliedhoofu,

mwanzo nilisita kumruhusu lakini baadae nikamruhusu, na alipomkama basi alitoa

maziwa mengi sana yaliyotosheleza watu wake na mengine yaliyobakia ndio haya

kwa ajili yetu. Na amesema kua Mbuzi huyu asichinjwe.’

Hivyo Abu Mabad akaomba aelezewe muonekano wa Mtu huyo, ambapo baada ya

Umma Mabad kumuelezea basi Abu Mabad akasema kua: ‘Wa Allahi huyu Mtu

unaemuelezea ndie mtu ambae ni Rasul Allah alieibuka katika Mji wa Makkah

miongoni mwa watu wa Quraysh, na kwa hakika kama mimi ningekuwepo hapa

wakati alipokuja basi mimi ningemkubali na kumtii na kisha ningefuatana nae.’

Ambapo anasema Umm Mabad Radhi Allahu Anha kua: ‘Mbuzi alieamrisha Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua asichinjwe aliishi hadi mnamo mwama 18 wa

Al Hijra katika wakati wa Utawala wa Amir ul Muumini Umar Ibn Al Khattab

ambapo hata pale ilipokua kuna ukame na Wanyama hawatoi Maziwa kutokana na

kukosa chakula basi Mbuzi huyo alikua akitoa maziwa asubuhi na jioni.’

Ingawa Makafiri wa Makkah walikua wamekata tamaa kuhusiana na kumkamata Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam lakini hata hivyo tamaa hio ilirudi tena upya baada ya

kupata habari kua na msafara wa Watu wanne umeonekana katika maeneo ya karibu na

Mwambao wa Bahari Nyekundu, hivyo mmoja kati ya watu wenye umahiri wa kufuata

nyayo za Watu aliekua akiitwa Suraka Ibn Malik basi akaamua kuufuatilia msafara huo

wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, kwa kutumia Farasi wake kwani Msafara wa

Ngamia hua hauna mwendo tofauti na safari ya Mpanda Farasi.

Na hivyo katika jitihada zake basi haukuchukua mda isipokua aligundua alama za nyayo

hizo na akaanza kuzifuata, na baada ya siku kadhaa akanza kuuona kwa macho yake

msafara huo na kufurahia kwa kuukimbilia, ambapo watu wote waliokuwemo kwenye

msafara huo basi waliingiwa na khofu isipokua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

ambae yeye aliwatuliza watu wake hao kwa kuwaambia kua wasiwe na khofu ya aina

yeyote.

Hivyo baada ya kuhakikishiwa usalama wao basi wakamuangalia Suraka ambae alikua

anawakaribia, lakini ghafla wakamuona kua ingawa alikua anapita mle mle walikopita


767

wao kwenye Nyayo za Ngamia wao lakini miguu ya Farasi wake Suraka ikazama hadi

magotini, na hivyo akashindwa kuwasogelea karibu, baada ya mda Farasi huyo

akakwamuka na kupiga hatu ambili tatu lakini hata hivyo farasi huyo akazama tena

kwenye mchanga na kisha mbele yake ardhini ukatoka kama Moshi Mubwa sana,

ambapo tukio hili lilimshtua sana Suraka na hivyo akanadia wa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kwa kusema: ‘Ewe Muhammad niombee ili nipate kuokoka na kisha

sitokufuata tena na wala sitowaambia watu wanaokutrafuta kuhusiana nawe’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuombea dua Suraka na akajihisi kua

yuko salama kwani Farasi wake akakwamuka na kisha yeye akamkaribia Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na kumwambia kua anataka kutoka kwake Barua ya

uthibitisho wa usalama wake, kwani anajua kua Dini ya Kiislam itaibuka na kua juu

kiutawala, hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuamrisha Abu Baqr Radhi

Allahu Anhu amuandikie Barua hio, ambapo baada ya kukabidhiwa basi Suraka akasema:

‘Ya Rasul Allah niamrishe mimi kitu chochote kile unachotaka nikitekeleze nami

nitatekeleza’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaamwambia: ‘Hakika mimi

nataka uwazuie watu wengine kutokana na kunifuata nyayo zangu katika safari

yangu hii ya kuelekea Madinah ’

Hivyo Suraka akarudi katika Mji wa Makkah na kuwaambia watu wa Quraysh kua kwa

hakika baari walizsipata kuhusiana na msafara wa watu wanne ulioonekana katika

maeneo ya mwambao wa Bahari Nyekundu hazikua ni habari za kweli, kwani walikua ni

watu wengine na hakua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na msafara wake. Na

kisha mnamo mwaka wa 8 Al Hijra Suraka akahamia katika Mji wa Madinah na kuingia

katika Dini ya Uislam.

Ambapo baada ya tukio hili basi mmoja kati ya Wafugaji aliuona Msafara huo na

akaamua kua aende akapeleke habari katika Mji wa Makkah, na alipofika basi ilikua kila

akitaka kuenda kuwaambia watu wa Kabila la Qurash kuhusiana na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam ilikua mara tu anapofika mbele yao alikua ni mwenye kusahau

kuhusiana na dhumuni la safari yake hio.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na msafara wake wakaendelea na safari yao na

njiani wakakutana na Zubayr Ibn Awaam Radhi Allahu Anhu ambae alikua akitokea

Madinah kuelekea Makkah na Biashara zake na alipowaona akasalimaiana nao na kasha

akawapa zawadi ya nguo za kutoka Syria zinazoitwa Mashlah na kasha akawaambia kua

Waislam wa Madinah wanasema kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

anachelewa kufika, wakati wao wana hamu nae sana kumpokea. Hivyo Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akaongeza kasi katika Msafara wake huo ili wasipate

kuwachosha watu wa Madinah wanaowasubiri kwa hamu.


768

Lakini hata hivyo kabla hawajafika katika Mji wa Madinah basi njiani wakakutana na

kundi la watu wapatao 80 ambao walikua wako kwenye maeneo ya Amim. Watu hawa

walikua ni watu ambao walipata habari kua watu wa Makkah wametayarisha zawadi ya

Ngamia 100 kwa atakampeleka Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika Mji wa

Makkah aidha akiwa hai au amekufa, hivyo msafara wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam ulipofika mbele yao na kuwasimamisha basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam akamuuliza kiongozi wa watu hao ni nani?

Akatoka mbele na kusema kua yeye anaitwa Burayda Ibn Husayb ambapo Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Ewe Abu Baqr hakika hali yetu imekua Baridi

na ya kupendeza’ (Kwani neno Burayda kwa kiarabu ni lenye kutoikana na neno Baridi)

kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuuliza Burayda: ‘Na Ukoo wenu

unaitwaje?’ Burayda akajibu: ‘Aslam’ ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akasema: ‘Ewe Abu Baqr hakika sisi tayari tumeshaupata Usalama’(Kwani neno

Aslam linatokana na neno Salam)

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akauliza: ‘Jee ukoo wa Aslam unatokana

na kabila gani?’ Burayda akasema: ‘Kutokana na Banu Sahm’ hivyo Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Ewe Abu Baqr, hakika Upinde wako

Umechomoza’ (kwani kwa Lugha ya Kiarabu neno Sahm hua linamanisha Upinde)

ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alifanya hivi kwa sababu alikua ni mtu

ambae hapendi kunasibisha Majina na au vitu na mambo mabaya mabaya bali alikua ni

mtu mwenye kupenda kila kitu na kila jambo kunasibisha na Vitu vizuri.

Hivyo kutokana na uzuri wake huo wa kunasibisha kila kitu na kitu kizuri basi Burayda

akavutiwa na maumbile hayo ya kitabia na akamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kwa kusema: ‘Jee na wewe ni nani?’ ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam akajibu kwa kusema: ‘Mimi ni Muhammad Ibn Abdullah Ibn Abdul Mutallib

na pia ni Rasul Allah, hivyo nakukaribisha katika dini ya Kiislam’

Maumbile, Tabia na kauli za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam zilimvutia sana

Burayda kiasi ya kua hapo hapo bila ya kusita akakubalia kuingia kwenye Dini ya

Kiislam yeye pamoja na watu wake wote aliokua nao, na kisha wakamkaribisha Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam na msafara wake kwa ajili ya kupumzika katika eneo

lao kabla ya kumalizia safari yake kuelekea Madinah .

Na ilipowadia asubuhi yake basi Buraydah akamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam : ‘Ya Rasul Allah Sio Vizuri kuingia kwenye Mji wa Madinah bila ya kua

na Bendera’

Na kisha Buraydah akavua kilemba chake na akatengeneza Bendera kwa ajili ya Msafara

wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambapo kutokana na tukio hili Rasul Allah


769

Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Miongoni mwa Masahaba zangu basi mmoja

wao atakufa katika Nchi, ambapo atafufuliwa katika siku ya Malipo huku akiwa ni

Nuru ya Nchi hio na kiongozi wa Nchi hio’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaendelea na safari yake kuelekea katika

mji wa Madinah . Ambapo nao Watu wa Madinah walikua wametoka nje ya Mji wa

Madinah kwa hamu yao kubwa sana kiasi ya kua wameshindwa kujizuia kukaa ndani ya

Mji wao na kuamua kumsubiri Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika maeneo ya

Harra mara tu baada ya kumaliza kusali sala ya Alfajiri.

Na ilipoingia wakati wa mchana huku jua likiwa kali basi mara Myahudi mmoja aliekua

juu ya nyumba yake akanadia baada ya kuona kutoka katika maeneo ya Amim basi

akanadia: ‘Enyi Waarabu, Mtu wenu mliekua mkimsubiri yule kule anakuja!’

ambapo habari ya sauti hii ilivyosambaa kwa kasi basi ilikua kama vile hali ya moto

ulioingia wenye shamba lenye nyasi kavu, kwani Mji mzima wa Madinah ulikua kama

uliokua umelala halafu ghafla ukaamka kwa zogo linalotokana na shangwe na vigelegele

na nuru ya furaha, na hivyo kila sehemu ya Mji huo ikawa ni yenye kusheherekea juu ya

tangazo hilo, na kukimbilia kutoka nje ya Mji wa Madinah na kuelekea kwenye upande

wa maeneo ya Amim.

Ambapo walimuona Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na msafara wake akiwa

amesimama chini ya kivuli cha Mtende kutokana na Jua kali la siku hio, hivyo

wakamkaribia na kumkaribisha kwa furaha, ambapo miongoni mwao pia kulikua na watu

wa Mji wa Quba ambao walimuomba Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua

kwanza aende katika kijiji chao kabla ya kuingia na kuhamia rasmin katika mji wa

Madinah na hivyo baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuzungumza na watu

wa Madinah na watu hao wa Quba basi akaamua kuelekea katika maeneo ya upande wa

kulia wa Mji wa Madinah katika maeneo ya kijiji cha Quba ambacho kilikua kiko katika

umbali wa masafa ya kilomita 3 ambayo ni sawa na safari kama ya saa moja kutoka

Madinah .

MUHAMMAD SALALLAHU ALAYHI WA SALAM, ALI IBN ABI TALIB NA

SUHAYB AL AL RUMI RADHI ALLAHU ANHUM NDANI YA ARDHI YA

QUBA

Msafara ulipofika katika Mji wa Quba basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akafikia kwenye Nyumba ya Kulthum Ibn Hidam ambae ndie aliekua Mkuu wa kabila la

Banu Amr Ibn Awf na alikua ni mtu mzima sana, na kisha akaelekea kwenye Nyumba

ya Sad Ibn Haytham katika Nyumba iliyokua ikijulikana kama Dar ul Uzab, kwani hii

ilikua ni nyumba inayokaa Masahaba wajane watupu. Rasul Allah Salallahu Alayhi wa


770

Salam alikaa katika Kijiji cha Quba kwa kama wa wiki mbili kwa ajili ya matayarisho

kadhaa.

Ikiwemo kumsubiri Ali Ibn Talib Radhi Allahu anhu ambae yeye aliondoka katika Mji

wa Makkah siku tatu baada ya kuondoka Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, na hi

hivyo alipofika katika mji wa Quba basi alikua taabani, kwani alitembea kwa masafa yote

na hivyo Miguu yake ilikua imevimba na kufanya malengelenge, aambapo Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alipomuona basi alimkubatia na kumonea huruma sana huku

akitokwa na machozi kutokana na hali yake na kisha akamuombea Dua na kumgusa

kwenye miguu yake hio na hapo hapo miguu yake ikapona.

Na pia katika wakati huo huo wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akiwa bado

yupo katika Mji wa Qubah akawasili pia Suhayb Ibn Sinan Al Rumi Radhi Allahu Anhu

ambae alikua ni miongoni mwa Masahaba waliokua hawajahama kutokana na kumuunga

Mkono Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae nae alikua awemo ndani ya

Msafara wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu

Anhu, lakini Allah Subhanah wa Ta'ala akaamua kumjaribu zaidi Suhayb Al Rumi, kwani

katika siku hio alipotaka kuondoka nao basi yeye akakamatwa na kuwekwa chini ya

Ulinzi kwa masaa 24 kwa siku kadhaa.

Lakini mtihani huu haukua mkubwa sana kwa Suhayb Al Rumi kwani kutokana na

Ufaham wake, basi siku moja wakati akiwa chini ya ulinzi akaanza maradhi ya kuharisha,

ikawa kila wakati anaenda chooni, tumbo limembana na akienda anaharisha.

Katika siku hio walinzi hao wake walimfuata Chooni zaidi ya mara 10 mpaka wakachoka,

ikafika hali wakasema: ‘Mwache akaharishe kwani hio ni Adhabu yake kutoka kwa

Al Lata na Al Uzza kajitafutia mwenyewe’

Hali hii ya kuharisha iliendelea mpaka usiku, na hivyo usiku huo Walinzi hao wakawa

hawana khofu ya kua huenda Suhayb Al Rumi Radhi Allahu Anhu atakimbia, kwani hata

Kukimbia hawezi kwa kuharisha, hivyo wakasinzia na kulala, na hii ndio fursa dhahabiya

yaani fursa ya Dhahabu aliyokua akiisubiri Suhayb Al Rumi Radhi Allahu Anhu, na hivyo

waliposinzia walinzi wake basi alipotoka kuenda Chooni hakurudi tena ndani, bali

alitokomea moja kwa moja na Farasi wake kuelekea katika Mji wa Madinah .

Lakini hata hivyo walinzi wake wakawahi kuamka na kugundua kua amekimbia na Farasi

wake hayupo, hivyo nao wakapanda Farasi wao na kukimbilia Upande wa Madinah . Na

hakuchukua Mda isipokua Walinzi hao wakamuona na kumkaribia Suhayb Al Rumi

Radhi Allahu Anhu, ambae nao akaongeza kasi lakini hata hivyo, akaona bora asimame

ilia akabialiane nao walinzi hao kwa silaha.


771

Hivyo Suhayb Al Rumi Radhi Allahu Anhu akasimama kisha akatoa Upinde na kuanza

kuwatunga Shabaha watu wao wanaomkimbilia, na walipomkaribia basi akasema: ‘Enyi

watu wa Quraysh hakika nyinyi mnanijua mimi kwa Umahiri wangu wa Kutunga

Shabaha kwa kutumia Upinde! Mnajua kua hakuna mbora zaid yangu, na

nikiachia basi sikosei, hivyo naapa mimi kua atakaenikaribia, basi naanza ane kwa

upinde na kisha namalizana na mwengine kwa upinde mwengine na kwa upanga

pia.’

Ambapo Makuraysh hao nao wakasema: ‘Wallahi na sisi pia hatuwezi kukuachia

wewe ukiwa hai na pia ukiwa na baadhi ya mali zako zilizobakia Makkah, kwani

ulikuja katika Mji wa Makkah ukiwa masikini dhaifu na huna kitu lakini sasa hivi

umeshachuma ulichokichuma, haiwezekani tukuachie...hivyo leo ama ni siku yako

ama ni siku yetu’

Hivyo Suhayb Ibn Sinan Al Rumi Radhi Allahu Anhu akawaambia watu hao: ‘Sawa,

hivyo jee kama nikiamua kukuwachieni mali zangu zote zilizobakia katika Mji wa

Makkah, mtaachaana na Mimi?’ hivyo Makafiri hao wakakubaliana na makubaliao

hayo na kusema: ‘Naam.’

Hivyo Suhayb Al Rumi Radhi Allahu Anhu akawaelekeza alipozificha Mali zake kwenye

nyumba yake katika Mji wa Makkah, na hivyo Makafiri hao wakamwachia hivyo Suhayb

Al Rumi Radhi Allahu Anhu akaendelea na safari yake huku akiwa na hamu na ari kubwa

zaidi ya kukutana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika Mji wa Quba ambapo

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipomuona Suhayb Al Rumi Radhi Allahu Anhu

basi alifurahia sana kuwasili kwake na kisha akaMwambia Suhayb Al Rumi Radhi Allahu

Anhu kua: ‘Hakika mabadilishano ya Biashara yako yamekua na faida kubwa sana

ya Abu Yahya, biashara yako imekua na faida kubwa sana, Hakika Biashara yako

imekua na faida kubwa sana ya Abu Yahya.’

Ambapo maneno haya yalimshangaza na kumfurahisha sana Suhayb Al Rumi Radhi

Allahu Anhu na hivyo akasema: ‘Ya Rasul Allah! Wallahi, hakika mimi sijamuambia

Mtu yeyote, na hakuna mtu yeyote aliekuja kabla yangu mbele yako na kukutaarifu

juu ya hili labda kutokana na kuona yaliyotokea, hivyo inaonekana ni Jibril tu

pekee ndie atakaekua aliekuletea habari hizi’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Naam, kwani Allah

Subhanah wa Ta’ala amenishushia kupitia kwake aya isemayo:

‏﴿وَمِنَ‏ ٱلن َّاسِ‏ مَن يَشْرِى نَفْسَهُ‏ ٱبْتِغَآءَ‏ مَرْضَاتِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَٱهلل َُّ‏ رَؤُوفٌ‏ بِ‏ ٱلْعِبَادِ‏ ﴾


772

Wamina alnnasi man yashree nafsahu ibtighaa mardhati Allahi waAllahu raoofun

bialAAibadi (Surah al-Baqarah, 2:207)

Tafsir: Na miongoni mwa Watu kuna yule ambae amejitolea kuiuza Nafsi yake kwa

ajili ya kufanya vitendo vitakavyomridhisha Allah, na Allah ni Mwingi wa Upole kwa

Waja wake.

Aya zinatuonesha tunaona namna walivyokua Masahaba mbele ya Mola wao na mbele

ya Mtume wao Salallahu Alayhi wa Salam. Kiasi ya kua kutoka na Imani yao na kujitolea

kwao basi Allah Subhanah wa Ta'ala anawataja waziwazi katika Kitabu chake kitukufu

cha Qur'an kua kama Mfano kwetu mimi na wewe.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta'ala katika aya hii anamsifia Sahaba huyu aliekua

Mzungu mwenye Nywele za Dhahabu Suhayb Al Rumi. Kutokana na namna

alivyojitolea kwa Ajili ya Mola wake, na hivyo Allah Subhanah wa Ta'ala kututhibitishia

wazi kua:

Yeye Allah Subhanah wa Ta'ala haangalii kama wewe ni Muarabu, Mzungu, Mswahili,

Mchina au Mhindi, bali anachokiangalia na Kukithamini ni Imani yako Juu yake Ndani

ya Moyo wako.

Kwani Ngozi ya Rangi yako ni Tofauti ya kukutambulisha tu asili yako ni Mtu wa wapi,

ambayo haina maana kwani chenye maana ni Kua Unaelekea Wapi Maishani Mwako!

Ambapo kama kwamba aya hio haitoshelezi, yaani labda kuna watu hawajafahamu bado,

basi Allah Subhanah wa Ta'ala akaendelea Kupigilia Msumari kuhusiana na Ubora wa

Imani ya Suhayb Al Rumi kwa Kila alieamini kua awe ni mwenye kufuata Mfano wake

pale aliposema katika Aya unayofuatia baada ya hio kua:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ ٱدْخُلُواْ‏ فىِ‏ ٱلسِّ‏ لْمِ‏ كَآف َّةً‏ وَلاَ‏ تَت َّبِعُواْ‏ خُطُوَاتِ‏ ٱلش َّ يْطَانِ‏ إِن َّهُ‏ لَكُمْ‏

عَدُو ٌّ م ُّبِينٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo odkhuloo fee alssilmi kaffatan wala tattabiAAoo

khutuwati alshshaytani innahu lakum AAaduwwun mubeenun (Surat Al Baqara

2:208)

Tafsir: Enyi wale ambao ni Mlioamini, ingieni katika Uislam kikamilifu kwa Moyo

wote na wala msifuate hatua za Shaytan kwani kwa hakika yeye kwenu nyie ni adui

Mkubwa sana wa asili na wa mda mrefu.


773

Ambapo katika wakati huu pia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alibakia katika

kijiji cha Quba kwa ajili ya kujenga Msikiti wa Mwanzo katika historia ya Kiislam ambao

ulikua unajulikana kama Masjid Quba.

MASJID TAQWA - MSIKITI WA MWANZO KUJENGWA NA RASUL ALLAH

SALALLAHU ALAYHI WA SALAM.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliofika katika Mji wa Quba basi alisimamia

kujenga Msikiti wa mwanzo mara baada ya kupewa Utume wake, Ambapo ujenzi wa

Msikiti huu ulikua ukihudumiwa maji yake kutokana na kisima cha Abu Al Ansari Radhi

Allahu Anhu, ambacho ndicho kilichopata heshima ya kua ndio kima ambacho Ngamia

wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisimama na kunyweshwa maji yake baada

ya mda mrefu wa safari ya Jangwani.

Msikiti huu wa Quba ulijengwa katika Ardhi ya Kulthum Ibn Hidam Radhi Allahu Anhu

ambayo alikua akiitumia kwa ajili ya kuanika na kukaushia Tende zake, baada ya yeye

mwenyewe Kulthum Ibn Hidam Radhi Allahu Anhu kuitoa ardhi hio kwa ajili ya kutafuta

ridhaa za Allah Subhanah wa Ta’ala juu yake. Na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam hakusimamia tu ujenzi huo bali pia alishiriki kikamilifu katika kuujenga kwake,

kiasi ya kua hata Masahaba walikua wakimuonea huruma kwa namna alivyokua akibeba

Mawe makubwa makubwa kwa ajili ya kusimamisha ukuta wa Msikiti huo.

Kutokana na jitihada zake hizo basi mmoja kati ya Masahaba alimwambia Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Ya Rasul Allah Baba yangu na Mama yangu atolewe

kafara kwa ajili yako, nipe mie hilo jiwe wewe pumzika’ Rasul Allah Salallah Alayhi

wa Salam akasema: ‘La. Haiwezekani hivyo wewe nenda chukua jiwe jengine.’ Na

hivyo baada ya Msikiti huo kumalizika ukawa unaitwa Masjid Taqwa kutokana na

maneno ya zile aya zisemayo juu yake kua:

‏﴿وَٱل َّذِينَ‏ ٱتخ ََّذُواْ‏ مَسْجِ‏ داً‏ ضِرَاراً‏ وَكُفْراً‏ وَتَفْرِيقاً‏ بَينَْ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ وَإِرْصَاداً‏ لِّمَنْ‏

حَارَبَ‏ ٱهلل ََّ‏ وَرَسُولَهُ‏ مِن قَبْلُ‏ وَلَيَحْلِفُن َّ إِنْ‏ أَرَدَْ‏ إِلا َّ ٱلحُْسْنىَٰ‏ وَٱهلل َُّ‏ يَشْهَدُ‏ إِن َّهُ‏ ‏ْم

لَكَاذِبُونَ۞لاَ‏ تَقُمْ‏ فِيهِ‏ أَبَداً‏ ل َّمَسْجِ‏ دٌ‏ أُسِّ‏ سَ‏ عَلَى ٱلت َّقْوَىٰ‏ مِنْ‏ أَو َّلِ‏ يَوْمٍ‏ أَحَ‏ ُّق أَن

تَقُومَ‏ فِيهِ‏ فِيهِ‏ رِجَالٌ‏ يحُِب ُّونَ‏ أَن يَتَطَه َّرُواْ‏ وَٱهلل َُّ‏ يحُِب ُّ ٱلْمُط َّهِّرِينَ۞‏

أَفَمَنْ‏ أَس َّسَ‏ بُنْيَانَهُ‏

عَلَى ٰ تَقْوَىٰ‏ مِنَ‏ اهلل َِّ‏ وَرِضْوَانٍ‏ خَيْرٌ‏ أَم م َّنْ‏ أَس َّسَ‏ بُنْيَانَهُ‏ عَلَى ٰ شَفَا جُرُفٍ‏ هَارٍ‏


774

فَٱنْهَارَ‏ بِهِ‏ فىِ‏ ‏َرِ‏ جَهَن َّمَ‏ وَٱهلل َُّ‏ لاَ‏ يَهْدِى ٱلْقَوْمَ‏ ٱلظ َّالِمِينَ۞‏ لاَ‏ يَزَالُ‏ بُنْيَانُهُمُ‏ ٱل َّذِى

بَنَوْاْ‏ رِيبَةً‏ فىِ‏ قُلُوهبِِمْ‏ إِلا َّ أَن تَقَط َّعَ‏ قُلُوبُهُمْ‏ وَٱهلل َُّ‏ عَلِيمٌ‏ حَكِيمٌ‏ ﴾

Waalladheena ittakhadhoo masjidan diraran wakufran watafreeqan bayna

almu/mineena wa-irsadan liman haraba Allaha warasoolahu min qablu

walayahlifunna in aradna illa alhusna waAllahu yashhadu innahum lakadhiboona;

La taqum feehi abadan lamasjidun ossisa AAala alttaqwa min awwali yawmin

ahaqqu an taqooma feehi feehi rijalun yuhibboona an yatatahharoo waAllahu

yuhibbu almuttahhireena; Afaman assasa bunyanahu AAala taqwa mina Allahi

waridhwanin khayrun am man assasa bunyanahu AAala shafa jurufin harin

fainhara bihi fee nari jahannama waAllahu la yahdee alqawma aldhdhalimeena; La

yazalu bunyanuhumu alladhee banaw reebatan fee quloobihim illa an taqattaAAa

quloobuhum waAllahu AAaleemun hakeemun (Surat At Twaba 9:107-110)

Tafsir: Ama kwa wale ambao ni wenye kuweka Msikiti kwa ajili ya kusababisha

Madhara na kukufuru, na kuvunja umoja baina ya Waumini na kua kama kituo cha

wale wenye kupigana dhidi ya Allah na Mtume wake kabla yake basi wataapa kua nia

yao si chochote isipokua wema, lakini Allah Ni mwenye kushuhudia kua wao ni

waongo; Hivyo usiingie ndani yake (Msikiti huo) Ama kwa hakika Msikiti ulioasisiwa

kutokana na Taqwa, basi ni bora kwako kusimama ndani yake, kwani ndani yake mna

watu wanaopenda kujitoharisha. Na Aallah ni mwenye kupenda wanaojitoharisha.

Hivi jee yule alieasisi Jengo (La Msikiti) kutokana na Taqwa kwa Allah na kutaka

fadhila zake, ni bora zaidi au yule ambae alieasisi Jengo kwenye Mmchongoko wa

mmomonyoko wa ardhi wa ukingoni mwa Mto unaosubiri kuanguka? Ili liangamie

pamoja nae kwenye Moto wa Jahannam? Na Allah hawaongozi watu waovu.

Halitobakia Jengo lao walilolijenga isipokua ni chanzo cha shaka na unafiq ndani ya

Nyoyo zao, hadi pale zitakapokatwa katwa Nyoyo zao na Allah ni mwenye kujua juu

ya kila kitu na ni mwingi wa Hikma.

Ambapo hizi ni aya zinazozungumzia Miskiti miwili tofauti kutokana na utofauti wa

kuasisiwa kwake ambayo ni Masjid Dhirar na Masjid Taqwa yaani Masjid Quba.

Ambapo Masjid Dhirar jina lake limetokana na nene Dhara ambalo hua linamaanisha

Dhara au Dhuru, ulijengwa miaka minane baada ya kujengwa Masjid Quba na hii ilikua

ni kabla ya Vita vya Tabuq mnamo mwaka wa 8 Al Hijra, wakati Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alipokua akijitayarisha kwa ajili ya Vita hivyo, na kisha akatoka na jeshi

lake kuelekea Tabuk.

Lakini alipofika katika eneo la Dhu Awan alipokea ujumbe kutoka kwa baadhi ya watu

waliomwambia kua: ‘Ya Rasul Allah Hakika sisi tumejenga Msikiti katika eneo letu


775

kwa ajili ya Wazee, wagonjwa na inapokua kuna hali mbaya ya hewa hivyo tulikua

tunakuomba uje kuufungua kwa kusali ndani yake.’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hakika sasa hivi

nnashughulikia kuhusina na vita vya Tabuk lakini In-shaa Allah nitakuja kusali

pamoja nanyi nikirudi’

Ambapo Allah Subhana wa Ta’ala akamshushia aya hizi Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam zenye kumaanisha kua Masjid Dhirar alioalikwa akaufungue kua ni Miskiti

ambao umejengewa na Wanafiq wenye nia ya kuugawanya Uislam na kusababisha

madhara yatakayopelekea kuvunjika kwa umoja wa Kiislam, hivyo Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam hatakiwi kuingia ndani yake, na kwa maana hio basi Msikiti huo

hautakiwi kuwepo, na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamwita Malik Ibn

Dukhshum wa Banu Salim na Asim Ibn Adi wa Banu Ajlan akawaambia wakusanye watu

kisha: ‘Kisha nendeni kwenye huu Msikiti ambao watu wake si waadilifu na kisha

utieni Moto’

Ambapo anasema Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Msikiti wowote

ule ambao utakua umejengwa kwa ajili ya watu kujionesha na kushindana na

Msikiti mwengine au kwa sababu nyengine yeyote ile isiyokua ya kumridhisha Allah

Subhanah wa Ta’ala, au kwa pesa za Haramu basi hua ni wenye na sifa kama

Msikiti huu wa Dhirar’ ambapo Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi basi yeye anasema kua: ‘Ni kutokana na sababu hio

basi ndio maana Wanazuoni wakakataza Kusaliwa kwa Jamaa mbili kwenye

Msikiti mmoja, kwani hii hua inavunja Umoja wa Kiislam’

Ambapo wanazuoni wanasema kua asili ya Msikiti huu wa Dhirar ilikua ni kutokana na

Mkristo mmoja wa Madinah aliekua akiitwa kwa jina la Abu Amir Rahib ambae alisimu

kinafiki kwa ajili ya kuuteketeza Uislam ndani kwa ndani, na katika vita vya Badr baada

ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kushinda Vita basi alihama kutoka katika Mji

wa Madinah na kuhamia katika mji wa Makkah na alisema: ‘Wakati mimi nitakua nao

watu wa kupingana nawe Muhamamd basi mimi nitapingana na wewe tu’

Amir Al Rahib alipanga njama nyingi sana dhidi ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam na pia dhidi ya Waislam, kwani alishirikiana na Makafiri na kuwaambia kua bora

waungane pamoja katika kupigana na Waislam katika vita vya Khandaq, kuliko kupigana

kivikundi vikundi dhidi ya Waislam, na waliposhindwa Makafiri kwenye vita vya

Khandaq basi Amir Al Rahib akakimbilia katika Ardhi ya Syria na kushirikiana na

Warumi katika mipango ya vita dhidi ya Waislam vitakavyotokea katika ardhi ya Tabuk.

Na hivyo akawaamrisha watu wake wa Banu Ghanam katika Mji wa Madinah kua

wakajenge Msitiki ambao utakua ni sehemu ya kukutana kwao yeye baada ya kurudi tena


776

katika Mji wa Madinah katika jitihada zake za kuupiga vita Uislam, huku wakiandaa

jeshi katika Mji wa Tabuk kwa ajili ya kuuvamia Mji wa Madinah na hivyo Rasul Allah

Salallahu Alahyhi wa Salam akapata habari hio ya maandalizi hayo akaamua bora

akavamie kabla hajavamiwa, na huku Wanafiq wakataka kumchelewesha kwa kuufungua

Msikiti huo, na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akamtaarifu kua huo ni Msikiti

ulioasisiwa kwa ajili ya kuanzisha Madhara ndani ya Uislam kama zinavyosema aya.

Na bila ya shaka kutokana na kua Msikiti huo uliasisiwa kwa ajili ya Madhara, ambayo

hayakufikiwa malengo yake kama walivotaka wanafiq basi Allah Subhanah wa Ta’ala

anamtahadharisha Mtume wake Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Jengo walilolijenga

litakua ni lenye kubakia kua chanzo cha Athari ya Unafiq na shaka ndani ya Nyoyo

zao hadi pale Nyoyo hizo zitakapokatwa vipande vipande’

Na kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akausifu Miskiti wa Quba ambao ni Msikiti

ulioasisiwa kutokana na Taqwa kwani watu wake waliouasisi walikua ni wenye kupenda

Usafi wa Nyoyo zao na Miili yao, na hivyo akamuamrisha Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kua anatakiwa awe ni mwenye kuenda na kusali ndani yake, na hivyo kutokana

na amrisho hilo basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawauliza watu wa Qubah:

‘Hivi nyinyi hua mnafanya nini, hadi Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kuhusiana

nanyi kua ndani yake Msikitini wenu kuna watu wanaopenda Kujitoharisha?’

ambapo nao wakajibu kua: ‘Sisi daima tumekua ni watu ambao tunaopenda

kujitoharisha kwa kutumia mji pale tunapoenda Chooni’

Na kutokana na kuambiwa kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anatakiwa kua ni

mwenye kuenda kusali ndani ya Msikiti wa Qubah hivyo hata baada ya kuhamia katika

mji wa Madinah basi ingawa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akiishi katika

Mji wa Madinah katika eneo ambalo nyumba ya jirani yake ni Msikiti wake, na mbali ya

kua Mji wa Madinah uko mbali kwa kilomita 3 kutoka katika eneo la Qubah lakini haikua

vigumu kwake yeye Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kutekeleza amrisho hilo la

Mola wake kwani alikua katika kila siku ya Jumamosi akifunga safari kwa miguu au kwa

Ngamia na kuelekea katika Mji wa Quba kwajili ya kusali ndani yake kwenye Msikiti

huu wa Taqwa au Masjid Qubah.

Kama anavyoseama Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alikua kila siku ya Jumamosi anaenda kwenye Msikiti

wa Qubah iwe kwa miguu au kwa kipando’

Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Yeyote yule

atakaejitoharisha nyumbani kwake na kisha akaja katika Masjid Qubah na akasali

Rakaa 2 ndani yake basi atakua ni mwenye kuzawadiwa malipo yako kua ni sawa

na mtualiefanya Umra.’(Imam Ibn Majah)


777

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayi wa Salam alikaa kwa mda wa wiki mbili katika Mji

wa Quba na mara baada ya kumalizika kujenga Msikiti wa Quba basi akapumzika na

kisha, baada ya hapo akaamua kaelekea katika kituo cha mwisho cha safari yake ambacho

ni katika Mji wa Madinah katika siku ya Ijumaa, ambapo kabla ya tukio hili basi

aliwaalika watu wa Banu Najjar ambao ni wa bibi yake wa upande wa Mama yake

waliokua wakiishi katika Mji wa Madinah kua waje kwenye Mji wa Quba ili akiondoka

katika siku ya Ijumaa basi aondoke nao pamoja kurudi katika Mji wa Madinah na hivyo

Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam aliwasili katika Mji wa Madinah akiwa na Mamia

ya wafuasi waliokua nyuma yake huku pia akiwa na mamia ya wafuasi waliokua

wakimsubiri kwa hamu katika Mji wa Madinah.

KUWASILI KWA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA SALAM

KATIKA MJI WA MADINAH AN NABI.

Neno Yathrib linatokana na neno Tharaba ambalo hua linamanisha Kulaumu, Kukosoa,

Kutoa kasoro juu ya Kitu.

Na kuna wanaosema kua Mji huu uliasisiwa na watu waliotokana na kizazi cha Nabii

Nuh ambao kiongozi wao alikua anaitwa Yathrib, hivyo watu hao walihama kutoka

katika makazi yao katika Mji wa Babylon baada ya kukumbwa na mafuriko na hivyo

katika kutafuta kwao eneo salama basi wakafika katika ardhi hio ambayo ilikua ni nzuri

kimazingira kwani ina Mitende na Maji ya kutosha.

Ambapo asili ya watu wa Mji wa Yathrib ni mchanganyiko na hii ni kwa sababu ya hali

ya mazingira yake, kwani kuna watu wenye asili ya Iraq, ambao ndio waliotokana na

Yathrib mwenyewe, kuna Mayahudi ambao nao pia walitoka katika ardhi ya Iraq na

Jerusalem kutokana na kukimbia Madhila waliyokua nayo katika jamii zao na pia kuna

Wakristo waliokua ni wenye asili ya Yemen ambao nao walikimbilia katika Mji wa

Yathrib kwa ajili ya kutafuta usalama wao.

Hivyo Jina la Yathrib lilibadilishwa na Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam pale baadae

alipohamia katika Mji huo na hivyo akauita Taibah yaani Mji Uliomsafi au Taba yaani

Mji Mzuri, na baadae ukaitwa Madinat An Nabi yaani Mji wa Nabii Sallahu Alayhi wa

Salam ambapo uzuri wa Mji huu basi ulionekana wazi kutokana na ari na furaha ya watu

wake wakati walipokua wakimshindikiza Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam kutoka

katika maeneo ya Quba kuelekea katika Mji huo wa Yathrib walikua ni wenye kujawa na

Imani juu ya Dini yao Mpya na kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala na kumpenda

Mtume wake Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam ana hivyo kua ni wenye kua na darja

ya Ansaru Al Muslimin.


778

Katika safari yao ya kutoka Qubah kuelekea Yathrib katika siku hio ya Ijumaa, basi

ulipingia wakati wa Sala ya Ijumaa wakafika katika maeneo ya Ranuna, hivyo Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akashuka kutoka kwenye Ngamia wake na

akajitayarisha kwa ajili ya Sala ya Ijumaa katika eneo hilo la ardhi ambalo lilikua

linamilikiwa na watu wa Banu Salim Ibn Awf, na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akasalisha sala ya kwanza katika ardhi ya eneo hilo ambayo ilikua ni sala ya Ijumaa

ambayo ndani yake baada ya kumshukuru na kumtukuza Allah Subhanah wa Ta’ala basi

akasoma Khutba Ifuatayo:

‘Enyi watu! Jitayarisheni kwa ajili ya Akhera yenu, wakati bado mkiwa na Afya

zenu, kwani mnajua kua kila mmoja wenu ataulizwa katika siku ya Malipo hata juu

ya Kondoo aliowaacha bila ya kuwasimamia wakati alipokua akiwachunga, kwani

Allah Subhaah wa Ta’ala atakuambieni moja kwa moja kwa kusema:

Hivi Jee hakuja Mtume Wangu na kukujuulisheni juu ya hili? Na jee sikukupeni

nyinyi neema nyingi sana kutoka kwangu? Jee mmejitayarishia nini kwa ajili yenu

kutokana nazo?’ hivyo mtu ataangalia upande wa kulia na kushoto na wala asione

kitu, na atakapoangalia mbele yake hatoona kitu isipokua Moto wa Jahannam.

Hivyo mtu yeyote yule atakaeweza kujiokoa nao Moto huo hata kwa nusu ya Kokwa

ya Tende, basi na aitoe, na kama hakupata Kokwa ya Tende basi na ajiokoe kwa

Kutumia Kalima Tayyiba (Kauli Njema). Kwani kutokana nayo basi Jambo jema

moja hua linamalipo ya mara 700, Nakutakieni Rehma, Salama na Amani iwe Juu

yenu.

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akakaa kitako kidogo kisha akasimama na

kuendelea na sehmu ya pili ya Khutba yake kwa kusema: ‘Namtukuza Allah,

Namtukuza Allah na namuomba msaada wake, Tunamuomba Allah atuhifadhi

kutokana na matamanio ya Nafsi zetu na makosa yetu, kwani amuongozae Allah

basi hua ni mwenye kuongoka lakini aliepotoshwa nae basi kamwe hatopata

muongozaji wa kumrudisha kwenye njia iliyonyooka’

Nnashuhudia kua hakuna Mola anaestahiki kuabudiwa kwa Haki isipokua Allah,

ambae yuko peke yake na asiekua na Mshirika. Hakika ya Kauli bora ni maneno

ya Allah Subhanah wa Ta’ala. Kwani mtu ambae amepambwa ndani ya Moyo wake

kwa Qur’an na Allah Subhanah wa Ta’ala, Mtu ambae Allah Subhanah wa Ta’ala

amemuingiza kwenye Uislam ingawa hapo kabla alikua ni mtu asieamini, Mtu

ambae ni mwenye kuipendelea zaidi Qur’an kuliko maneno mengine basi Mtu huyu

hua ni mwenye Kuokoka.

Bila ya Shaka, Kitabu cha Allah Subhanah wa Ta’ala ni kitabu bora na chenye

maneno yaliyo fasaha, hivyo Pendeni kile anachokipenda Allah Subhanah wa


779

Taa’ala, msiyachoke maneno ya Allah Subhanah wa Ta’ala na msichoke kumtukuza

na kumkumbuka kwa sifa zake, na wala msiyafanye maneno ya Allah kua ni yenye

kuhuzunisheni nyoyoni mwenu, kwani Maneno yake yanawatofautisha waliobora

miongoni mwenu katika kila kitu.

Maneno ya Allah Subhanah wa Ta’ala yanabainisha kuhusiana na Amali njema, na

Mitume ambao ni watu bora, na hadithi bora, Maneno ya Allah Subhanah wa Ta’ala

yanabainisha kile kilicho halali na kilicho haramu. Hivyo Muabuduni Allah na wala

msimshirikishe na kitu chochote, na muogopeni ipasavyo.

Fanyeni Mema na yathibitisheni kwa Ndimi zenu. Pendaneni kutokana na Maneno

ya Allah Subhanah wa Ta’ala. Jueni kua Allah Subhanah wa Ta’ala anawaadhibu

vibaya sana wale ambao wanaovunja Ahadi zao. As Salaam Alaykum.

Na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasalisha Sala ya Ijumaa na kisha

akeingia katika Mji wa Madina, ambapo katika Khutba yake hii basi tunaona kua alikua

anawakumbusha watu wa Madina kua wameahidi kua watamlinda na kumhifadhi, hivyo

anawataka watimize ahadi yao, na wasije wakavunja ahadi yao na kuwawekea wazi kua

Allah Subhanah wa Ta’ala anawachukia wenye kuvunja Ahadi, na atawaadhibu kwa

adhabu kali sana wavunjao Ahadi.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipowasili katika mji wa Madina, basi akakuta

kua Mji huo hauna sehemu ya kukusanyikia na kusali pamoja kama vile ilivyokua katika

Mji wa Quba, na Ngamia wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipopiga Magoti

kwenye kiwanja cha Mayatima wawili wa Banu Najjar waitwao Sahl na Suhayl ambao

walikua chini ya uangalizi wa Muadh Ibn Afra Radhi Allahu Anhu, basi Rasul Allah

Salallahu A’layhi wa Salam akasema kua anataka kuinunua Ardhi hio kama watamuuzia.

Lakini Muadh Ibn Afra Radhi Allahu Anhu akasema kua atatoa sadaka malipo ya kiwanja

hicho kwa ajili ya Uislam, na Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akakataa juu ya

shauri hilo hivyo wakaitwa wahusika wenyewe na walipofika Mayatima hao wawili Sahl

na Suhayl basi wakasema kua: ‘Ya Rasul Allah, hakika sisi tunataka malipo yake

yalipwe na Allah Subhanah wa Ta’ala, hivyo tutakupa bure Ardhi yetu hii kwa ajili

ya Allah Subhanah wa Ta’ala’ lakini hata hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

hakukubaliana na shauri hilo kwa sababu wao ni Mayatima, na hivyo akainunua ardhi

hio kwa pesa 10 za dhahabu ambazo zililipwa na Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu

hapo hapo baada ya makubaliano hayo.

Na kisha haukuchukua muda isipokua ukajengwa Msikiti wa Madina ambao unajulikana

kama Masjid An Nabawi kwa kasi ya haraka sana. Masjid huu ulikua ni wa pembe 4 na

Kibla chake kimeelekea upande wa Jerusalem, na ulikua una milango mitatu na Mihrab

ambayo ilikua ni ya Vigogo vya Mitende, na pia kulikua na Kigogo cha Mtende ambacho


780

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akikiegemea katika wakati wa kutoa

Khutba.

Pembeni yake Msikiti huo kulikua na Vyumba viwili ambavyo ni vya Umm Ul Muuminin

Sawdah Radhi Allahu Anha na chengine cha Umm ul Muuminin Aisha Radhi Allahu Anha

na hii ni kwa sababu katika wakati huu Rasul Allah Sallahu Alayhi wa Salam alikua na

wake wawili hao tu, ambapo baadae Nyumba yake iliongezwa vyumba vengine.

Ambapo baadae Masahaba wakaamua kujenga Mimbar yenye vigazi vitatu ndani ya

Msikiti huo ambayo ilikua ni ya vigogo vya Mtende, hivyo mara ya kwanza Rasul Allah

Sallahu Alayhi wa Salam alipopanda kwenye Mimbar hio, basi Masahab walisikia sauti

kama Ngamia anaetaka kuzaa, na hivyo Masahaba wakaangalia huku na kule na kisha

wakaangaliana, kwa sababu hakukua na Ngamia karibu yao, lakini sauti hio iliendelea

kusikika kutoka mbele yao pembeni ya Mimbar mpya ya Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam ambayo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua amepanda juu yake.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akashuka kutoka kwenye Mimbar hio na

kuelekea kwenye kigogo cha Mtende ambacho alikua akikiegemea kabla ya kujengwa

Mimbar hio mpya, na kisha akakikaribia akakikumbatia na kukipapasa Kigogo hicho, na

mara sauti iliyokua ikisikika ikasita kusikika. Masahaba wakaanza kutokwa na machozi

kutokana na kufahamu kua Kigogo hicho ndio kilichokua kikilia kwa ajili ya kukosa

mguso wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kuwaambia Masahaba zake kua:

‘Hakika kama mimi sikukikumbatia na kukiliwaza Kigogo hiki basi kingeendelea

kulia hadi siku ya Kiama kutokana na kutengenishwa kwake na Rasul Allah.’

Ambapo baadae Kigogo hicho kikachimbiwa shimo na kuzikwa chini ya Mimbar hio

kutokana na amrisho lake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Ambapo alisema Imam Hasan Al Basr kuwaambia Wanafunzi wake kutokana na tukio

hili la kulia kwa kigogo hicho cha Mtende kutokana na kutenganishwa na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kama ikiwa Hata Kigogo kinaonesha hisia za

Mapenzi na Mwamko kwa ajili ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, basi

nyinyi mnastahiki kuonesha Mapenzi na Mwamko wa kihisia zaidi juu yake Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam’

Ambapo kuna kauli nyengine isemayo kua: ‘Wakati Kigogo hicho kilipokua kinalia

basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akakipapasa na kusema: ‘Nitakupeleka

Peponi ambapo ulipokua hapo kabla kama unataka, ambako nako utaota tena

mizizi na kunawiri na kuzaa, na kama utataka basi nitakupanda Peponi ili

waliokaribu miongoni mwa waja wa Allah wale Matunda yako.’’


781

Kigogo hiki kikasema: ‘Bora nipande Peponi ili waliokaribu miongoni mwa waja wa

Allah wale matunda yangu, na Peponi ni sehemu ambayo hakuna hali ya kuoza,

wacha nipate kuishi milele ndani yake.’ Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akasema kuwaambia Masahaba zake: ‘Kimependelea Maisha ya Akhera zaidi ya

Duniani’

Ambapo anasema Imam Muhamamd Ibn Is-haq kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam aliunganisha Udugu wa Kiislam baina ya marafiki zake wa Muhajjirin na

Ansari, na hivyo wakawa ni Ndugu wawili wawili, na kisha akachukua mkono wa

Ali Ibn Abi Talib na kusema: ‘Huyu ni Ndugu yangu’ hivi ndivyo alivyokua Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam, Bwana wa Mitume wote, Kiongozi wa wenye

Kumuogopa Allah Subhanah wa Ta’ala, Mtume wa Mola wa Viumbe wote asiekua

na mfano wake. Ambapo Hamza Ibn Abd Ul Muttalib na Zayd Ibn Harith nao

wakawa Ndugu pia. ’

Miongoni mwa Sifa za Maansari ni kama vile alivyosema Allah Subhanah wa Ta’ala

katika Qur’an kuhusiana nao kua:

‏﴿وَٱل َّذِينَ‏ تَبَو َّءُوا ٱلد َّارَ‏ وَٱلإِيمَانَ‏ مِن قَبْلِهِمْ‏ يحُِب ُّونَ‏ مَنْ‏ هَاجَرَ‏ إِلَيْهِمْ‏ وَلاَ‏ يجَِدُونَ‏ فىِ‏

صُدُورِهِمْ‏ حَاجَةً‏ ممِّ َّآ أُوتُواْ‏ وَيُؤْثِرُونَ‏ عَلَى ٰ أَنفُسِ‏ هِمْ‏ وَلَوْ‏ كَانَ‏ هبِِْم خَصَاصَةٌ‏ وَمَن

يُوقَ‏ شُح َّ نَفْسِ‏ هِ‏ فَأُوْلَٰئِكَ‏ هُمُ‏ ٱلْمُفْلِحُونَ‏ ﴾

Waalladheena tabawwaoo alddara waal-eemana min qablihim yuhibboona man

hajara ilayhim wala yajidoona fee sudoorihim hajatan mimma ootoo wayu/thiroona

AAala anfusihim walaw kana bihim khasasatun waman yooqa shuhha nafsihi faolaika

humu almuflihoona(Surat Al Hashar 59:9)

Tafsir:Na wale ambao kabla yao walikua na makazi(katika Mji wa Madina) na

wakawa na Imani waliwapenda wale waliohamia kwao na hawakua na wivu juu yao

kwenye vifua vyao kutokana na vile walivyopewa (Muhajjirina) na wakawapendelea

wao zaidi ya Nafsi zao, japo ingawa walikua wanahitajia pia, na yeyote yule

atakaeokolewa kutokana na kua ni mwenye kuidhibiti ya nafsi yake, basi hao ndio

watakaofuzu.

Ambapo anasema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi nilitoka na Walid Ibn

Walid na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawauliza Maansari : ‘Jee hali

yao itakuaje kama wakipewa Bahrayn?’ ambapo Maansari wakasema:

‘Hatutoridhika hadi ndugu zetu wa Muhajjirina watakapopewa kitu kama hicho

pia.’ Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kama ni La basi kueni


782

na Subra hadi pale mtakaponiona akhera kwani baada yangu mtakabiliana na

upendeleo juu yenu’’

Miongoni mwa mifano ya Udugu huo baina ya Muhajirina na Ansari alianzisha Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi pia ni baina ya Abd Rahman Ibn Awf Radhi Allahu

Anhu na Sad Ibn Rabia Radhi Allahu Anhu. Ambapo mara baada ya kuunganishwa udugu

wao huo, basi Saad Ibn Rabiah Radhi Allahu Anhu akasema kumwambia Abd Rahman

Ibn Awf kua: ‘Ewe Ndugu yangu hakika mimi ni tajiri sana katika Mji wa Madina,

nna mashamba mawili na nnao wake wawili, hivyo angalia Mashamba yangu kisha

uchague unalotaka, na pia waangalie wake zangu basi atakaekuvutia miongoni

mwao mimi nitamuacha ili umuoe awe wako wewe’ ambapo hata hivyo Abd

Rahman Ibn Awf akajibu: ‘Allah akungezee barka katika Mali yako na familia

yako, ila mimi nilikua nataka unioneshe wapi lilipo soko la Madina.’

Hivyo haishangazi kuona namna walivyokua Maansari kwa ukarimu wao kwa

Muhajjirina kiasi ya kua Allah Subhanah wa Ta’ala anawaelezea zaidi kwa kusema:

‏﴿وَأَل َّفَ‏ بَينَْ‏ قُلُوهبِِمْ‏ لَوْ‏ أَنفَقْتَ‏ مَا فىِ‏ ٱلأَرْضِ‏ جمَِيعاً‏ م َّآ أَل َّفْ‏ تَ‏ بَينَْ‏ قُلُوهبِِمْ‏ وَلَٰكِ‏ َّن

ٱهلل ََّ‏ أَل َّفَ‏ بَيْنَهُمْ‏ إِن َّهُ‏ عَزِيزٌ‏ حَكِيمٌ‏ ﴾

Waallafa bayna quloobihim law anfaqta ma fee al-ardhi jameeAAan ma allafta

bayna quloobihim walakinna Allaha allafa baynahum innahu AAazeezun

hakeemun(Surat Al Anfal 8:63)

Tafsir: Na yeye (Allah Subhanah wa Ta’ala) ameunganisha baina Nyoyo zao hivyo

Hata kama mtatumia kila kilichomo ardhini basi msingeweza kuziunganisha Nyoyo

zao, lakini Allah amezinganisha baina yao. Kwani kwa hakika yeye ni mwenye uwezo

juu ya kila kitu na ni mwingi wa Hikma.

Kwani kutokana na Hikma za Allah Subhanah wa Ta’ala basi aliziunganisha Nyoyo za

Waumini na hivyo kuwajaalia kua ni wenye kua na umoja na kupata ushindi baada ya

ushindi dhidi ya maadui zao, kwa kuanzia kuwaunganisha watu wa Mji wa Madina baina

ya Makabila ya Banu Aws na Al Khazraj ambao kabla ya Uislam walikua ni maadui

wakubwa sana, na kisha kuwauganisha Ansari na Muhajjirina kwa Ansari kujitolea na

kuwasaidia kila Muhajirrin.

Ambapo amesema Ansa Ibn Malik Radhi Allahu Anhu Kua: ‘Muhajirrina walisema:

‘Ya Rasul Allah hakika sisi hatujawahi kuona watu ambao wamepata malipo

makubwa kutokana na mengi tuliyoyapoteza, na hatukuwahi kuona maliwazo

makubwa kutokana na kile kidogo walichokua nacho. Kwani wametuokoa sisi


783

kutokana na kuomba, wamegawana nasi na kila neema waliyojaaliwa hadi imefikia

wakati wa kua sisi kua na khofu kua watavuna malipo yetu yote.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘La hilo halitotokea wakati pale

mtakapokua mnawashukuru na pia kuwaombea Dua kwa Allah kwa ajili yao.’

Anasema Abd Rahman Ibn Zayd Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam aliwaambia Maansari kua: ‘Ndugu zenu wamewacha Mali na Watoto wao

na kuja kwenu’ hivyo Maansari wakasema: ‘Hakika sisi tutagawana nao Mali zetu

nusu kwa nusu’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Jee tufanye lipi

zaidi?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Watu hawa (Muhajjirina)

hawakua wakifanya kazi, hivi jee mtagawana nao mazao yenu’ Maansari

wakasema: ‘Naam’’

Hii ndio hali wanayotakiwa wawe nao Waislam katika udugu wao ili kudumisha umoja

wao. hivyo tunatakiwa tujifunze kwa Waliotangulia kabla yetu, ambapo anasema Imam

Abu Yazid Al Bustami kua: ‘Hakika mimi sikuwahi kuzidiwa na yeyote kama vile

nilivyozidiwa na Kijana mmoja kutoka katika Mji wa Balk, ambae nilikutana na

alipokua akielekea katika Ibada ya Hija, na aliponiona basi alinifuata na kusema:

‘Ya Abu Yazid, hivi jee ni kipimo gani cha Kuidhibiti Nafsi na Kuachana na

Matamanio ya Dunia kwa upande wako?’

Nami nikajibu: ‘Hakika sisi kama tukipata riziki yetu basi tunakula na kama

tukikosa basi hua tunakua na Subra.’ Ambapo nae akasema: ‘Hiyo hua ni

kuidhibiti Nafsi na kuachana na Matamanio ya Mbwa wa Balkh’ hivyo mimi

nikamuuliza: ‘Sasa jee ni kipimo gani cha Kuidhibiti Nafsi na Kuachana na

Matamanio ya Dunia kwa upande wako?’

Ambapo nae akasema: ‘Tunapokua hatuna hua tunashukuru, na tunapopata hua

tunawapa wenye shida zaidi yetu’’

Ambapo Dhunun al Misri aliulizwa: ‘Jee ni nini hali ya Mwenye kuachana na Dunia

kwa Moyo mkunjufu’ ambapo ane akajibu: ‘Huonekana katika hali tatu, anapokua

anacho hua ni mwenye kutoa, anapokua hana hua si mwenye kuomba na

kuwapendelea wengine pale anapopewa yeye.’

Na ansema Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhamamd Ibn Muhammad Al Ghazali

kua: ‘Amesema Abu Hasan Al Antaki kua: ‘Kulikua kuna watu 20 katika mji wa

Ray ambao walikua wana njaa na wana vipande vya mkate ambavyo vilikua

haviwatoshelezi wao wote hata wakila. Hivyo wakachukua Mikate hio na kisha

wakaikatakata katika vipande vipande, wakaviweka juu ya meza na kisha wakakaa


784

na kuzima taa huku vipande hivyo vya mikate vikiwa mbele ya Mezani. Kisha baada

ya mda wakawasha taa na kuona kua vipande vya mikate vike vile vile, kwa sababu

kila mmoja miongoni mwao hakula kipande hata kimoja kutokana na kuona bora

ale kipande hicho ale mwenzake.’’

MAKUBALIANO BAINA RASUL ALLAH SALALLAHU ALAYHI WA

SALAM NA WATU WA MADINAH

1. Haya ni Makubaliano kutoka kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kuhusiana na Uhusiano baina ya Waumini wa Quraysh na wa Madina na wale

wanaowafuata na kujumuika nao katika Ummah wa Kiislam.

2. Muhajirrin wa Quraysh wataendelea Kulipia fidya Malipo ya Umwagaji Damu

kulingana na Mila zao.

3. Inapotokea vita basi kila pande itasimamia Mateka wake kwa Ukarimu na

kusimamia haki za Ibn Adam kama ilivyo miongoni mwa Waumini.

4. Watu wa Bani Awf wataendelea na Malipo ya kulipia fidya ya Umwagaji Damu

kuligana na Mila zao.

5. Kama ikitokea Vita dhidi ya Mtu yeyote basi pande zote zizisokua Waislam

wataendelea kuwasimamia Mateka wao kwa huruma na haki kama

inavyosimamiwa na Waislam na wala si kulingana na zama za Kijahiliyah.

6. Watu wa Banu Sidah, Banu Harith, Banu Jusham na Banu Najjar wataongozwa

kulingana na kanuni zilizotajwa hapo juu.

7. Watu wa Banu Amr, Banu Awf, Banu Nabit na Banu Aws watasimamiwa

kulingana na kanuni hizo pia.

8. Waislam hawatosita kuendelea kuwasimamia Mateka wao na watawalipia fidya

kwa ajili yao, ambalo litakua ni jukumu la Umma wa Kiislam na wala halitokua

jukumu la familia ya Waislam hao.

9. Muumini kamwe hatomfanya Mtu alieachiwa huru na Muumini mwengine kua

ni mtu wake bila ya kuwepo kwa ridhaa ya Muumini husika.

10. Waumini wanaomuogopa Allah daima watakua ni wenye kupingana na Uasi na

Dhulma na vitendo vinavyounga mkono Dhulma au Uadui au Upotovu

miongoni mwa Waumini.

11. Kama ikitokea kua kuna Mtu atafanya maovu basi Waumini wote watapingana

nae Mtu huyo hata kama mtu huyo akiwa ni Mtoto wa Mmoja kati ya Waumini

hao

12. Muumini hatomuua Muumini mwenzake kwa ajili ya Kafiri hata kama Kafiri

huyo ataka ni ndugu yake Muumini huyo.


785

13. Muumini kamwe hatomsaidia asiekua Muumini dhidi ya Muumini.

14. Hifadhi itakapotolewa kwa jina la Allah Subhnaha wa Ta’ala itakua ndio

inayotambulika, hivyo Wasiokua na Nguvu miongoni mwa Waumini

watahifadhiwa kwa jina la Allah Subhanah wa Ta’ala na juu ya hili

litasimamiwa kwa Waumini wote.

15. Waumini wote ni Marafiki miongoni mwao bila ya kujumuishwa wasiokua

Waumini.

16. Mayahudi wanaowafuatana na Waumini watasaidiwa na kusimamiwa haki zao.

17. Hakuna Yahudi atakaedhulumiwa kwa sababu ya Uyahudi wake.

18. Maadui wa Mayahudi watakaowafuata Waislam ili wasaidiwe dhidi ya

Mayahudi basi hawatosaidiwa.

19. Uslama baina ya Waumini hauwezi kuvunjwa, yaani Waumini wote wawe

kwenye Usalama au wote wawe kwenye vita, haiwezekani kua Nusu wawe

kwenye Vita na Nusu wawe kwenye Usalama.

20. Haiwezekani kutafutwe njia ya kupatikana kwa Usalama ndani ya Mji wa

Madina pale inapokua Waislam wanapigana kwa ajili ya Allah.

21. Wakati Waumini watakapoenda Vitani basi watakaopanda kipando itawabidi

kushirikiana katika kupanda kipando hicho kwa zamu.

22. Waumini lazima wawe ni wenye kulipiza Kisasi damu ya Waislam wenzao

wanapokua wanapigana kwa ajili ya Allah, yaani mapigano kwa ajili ya Allah

Subhanah wa Ta’ala hua yanawahusisha Waislam wote na kuwaathiri Waislam

wote.

23. Waumini ni wabora katika kuonesha misimamo yao kutokana na kumuogopa

Mola wao jambo ambalo hupelekea kupata uongofu kutoka kwa Allah

Subhanah wa Ta’ala na hivyo Kila Muislam anatakiwa awe na ari katika

kuonesha msimamo huo.

24. Hakuna Kafiri atakaeruhusiwa kuhodhi mali ya Quraysh aliechini ya

Usimamizi wake, kwani Mali zote za Maadui lazima zisalimishwe kwa Kiongozi

wa Kiislam.

25. Hakuna Kafiri atakaeruhsiwa kuingilia kati kwa kumpendelea Quraysh kwa

sababu watu wa Quraysh wa Makkah ni maadui.

26. Kama Kafiri akimuua Muumini bila ya sababu inayokubalika, basi Kafiri huyo

atauliwa badala yake, isipokua pale walioliwa Mtu wao watakaporidhika na

kusamehe. Na hivyo Waumini wote wanatakiwa kua ni wenye kupingana na

uovu huo, na hakuna Muumini anaeruhusiwa kumhifadhi aliefanya uovu huo.


786

27. Mtakapotofautiana juu ya Jambo lolote kuhusiana na Makubaliano haya basi

jambo hilo lilirudishwa kwa Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume wake

Salallahu Alayhi wa Salam.

28. Mayahudi watachangishwa mchango pale watakapokua wanapigana pamoja na

Waislam dhidi ya Maadui zao.

29. Mayahudi wa Bani Awf, Bani Al-Najjar, Bani Al Harith, Bani Saeeda, Bani

Jusham, Bani Al Aws, Thaalba, Jaffna, (ambao ni wa ukoo wa Bani Thaalba)

ana Bani Al Shutayba watahesabiwa kua ni Ummah mmoja na Wasialm,

ingawa Mayahudi wana Imani yao na Uhuru wao, lakini hawatotofautishwa

isipokua kwa wale watakaofanya dhulma na uovu kwani kutokana na kufanya

kwao hivyo hua ni wenye kujidhulumu nafsi zao na watu wa familia zao.

30. Ukweli hua ni wenye kutoa hifadhi dhidi ya Uongo, yaani Wakweli na

waaminifu watalindwa dhidi ya Uongo, na hivyo Mtu muaminifu na mkweli

kwa Ummah basi hua ni mwenye kujilinda kutokana na kua na usaliti.

31. Watu walio huru wa Thaalba watapewa Darja sawia kama watu wa Thaalba

wenyewe, hii ni kutokana na uadilifu wao katika mambo yao ya kimaisha na

watapewa haki yao kamilifu wanapokua katika mapigano.

32. Watakaoshirikiana na Mayahudi basi watafanyiwa kama wanavyofanyiwa

Mayahudi.

33. Hakuna hata mmoja alie katika makubalino haya atakeenda Vitani bila ya

Ruhusa ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, na hivyo yeyote

atakaedhulumiwa basi atasimamiwa haki yake.

34. Mayauhudi watasimamia matumizi ya Majeshi yao katika vita na Waislam pia

watasimamia matumizi ya Majeshi yao.

35. Yeyote yule atakaemshambulia yule aliekuwemo kwenye Makubaliano haya

basi waliokuwemo kwenye Makubaliano haya watamsaidia alieshambuliwa.

36. Wote waliokuwemo kwenye Makubaliano haya lazima wawe ni wenye

kushauriana na kutaarifiana juu ya mambo muhimu.

37. Hakuna mtu atakaehukumiwa kutokana na makosa ya mwenzake.

38. Mtu yeyote yule atakaedhulumiwa basi anastahiki kusaidiwa.

39. Mayahudi wanatakiwa walipie matumizi ya vita wa ajili ya Waislam pale

itakapokua wao hawatopigana Vita hivyo.

40. Mji wa Madina utakua ni Mji wa Usalama kwa kila aliekubaliana na

makubaliano haya.

41. Mgeni yeyote atakaehifadhiwa na aliekubaliana na makubaliano haya

atahesabika kua kama mgeni wa mtu huyo pale itakapokua hakufanya makosa


787

wala hakudhulumu, kwani kila atakaedhulumu au kufanya kosa basi

atahukumiwa.

42. Mwanamke atahifadhiwa kutokana na ridhaa ya walii au familia yake.

43. Kama ikitokea kua kutakua na ugomvi au matatizo basi moja kwa moja

yatatauliwe kupitia kwa Allah Subhanah wa Ta’ala na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam, na kwamba Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

atakubaliana na kila kilichomondani ya makubaliano haya kwa ajili ya

manufaa yaliyomo ndani yake.

44. Watu wa Quraysh hawatopewa hifadhi yeyote katika mji wa Madina.

45. Waliokubaliana na makubaliano haya wanakubaliana wataungana pamoja

katika kushirikiana kusaidia pale inapotokea kuvamiwa kwa mjiwa Madina.

46. Waliokubaliana na makubaliano haya wanatakiwa wasiamamie usalama ndani

ya mji wa Madina, na ikitakiwa iwe hivyo kwa Waislam basi ni wajibu wao

kutekeleza jukumu hilo isipokua pale itakapokua Waislam wanapigania kwa

ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala.

47. Kila mmoja kati ya waliokubaliana na makubaliano haya atakua na haki stahiki

kulingana upande aliokuwepo wa makubaliano, hivyo kila mtu ataathirika au

atanufaika kutokana na upande aliokuwepo.

48. Mayahudi wa Banu Aws na watu wao watakua na haki sawa kama ilivyokua

kwa watu wengine waliokubaliana na makubaliano haya. Ukweli na uaminifu

ni hifadhi dhidi ya Udanganyifu.

49. Kila afanyae jema au kinyume chake basi atakua ni mwenye kufanya hivyo kwa

ajili ya Nafsi yake.

50. Allah Subhnaha wa Ta’ala amekubaliana na makubaliano haya.

51. Makubaliano haya hayatomhusu atakaefanya dhulma.

52. Pale inapotokea mmoja kati ya waliokubaliana na makubaliano haya kua

ataenda vitani au atabakia nyumbani basi atakua salama isipokua kama

atafanya dhulma.

53. Allah ni mwenye kuwahifadhi wenye kufanya mema na wenye kumtii na

kumuogopa yeye na Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam ni Mtume wake na

ni mwenye kuhakikisha juu ya hilo.

KUWASILI KWA UMMU AYMAN KATIKA MJI WA MADINAH AN NABI.


788

Tunaporudi kwa upande wa Umm Ayman pia nae aliachiwa Majukumu ya kuyatekeleza

kwa ajili ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, hivyo baada ya kuyatekeleza

Majukumu hayo basi Ummu Ayman nae akafunga Safari na kufanya Hijra kutoka katika

Mji wa Makkah kuelekea Madinah kwa miguu ikiwa ni safari yake ya pili baada ya ile

aliyoifanya wakati akiwa Na Mama yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam yaani

Amina Bint Wahb pamoja na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam wakati akiwa

mdogo sana.

Ambapo mara hio ya kwanza alikua kijana na pia Walikua ni wenye kupanda Ngamia

na hivyo kua ndani ya Kibanda kinachowekwa juu ya Mgongo wa Ngamia na safari hio

ilichukua Siku 10.

Kwani Safari hii ya pili ya Barakah au Ummu Ayman kutoka Makka kuenda Madinah

ilikua ngumu zaid, kwani alikua peke yake, halafu alikua akitembea kwa miguu kwa

wasiojua basi tunazungumzka safari kama ya kutoka Dar kuelekea Tanga kwa miguu

tena kwa Mwanamke Mtu Mzima anaekaribia miaka umri wa miaka 60 tena Jangwani

hakuna miti wala Majumba bali kuna marundo na Marundo ya Mchanga, anauzamisha

mguu mchangani kisha anautoa ili kupiga hatua nyengine usiku na mchana.

Na ingawa ilikua safari ndefu na nzito lakini kwake yeye iliku rahisi kwani Umm Ayman

alikua katika hali ya Mama anaesafiri kumkimbilia Mtoto wake kipenzi ambae

hajamuona kwa siku nyingi sana yaani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Hivyo Ummu Ayman alikua ni Mwenye kufanya Hijra ya kusafiri Jangwani kwa miguu

katika umbali wa kilomita 450 kwa Ajili ya Allah Subhanah wa Ta'ala, na pia kwa ajili

ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Ambapo ndani ya tukio hili basi mna mafuzo pia ya Umuhimu wa Nia katika kila Jambo

analolifanya Ibn Adam, kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

‘Ama hakika ya Amali hua inategemeana na Nia, na Kwa Hakika Kila mtu atalipwa

Kulingana na Nia yake, Hivyo yeyote Yule aliefanya Hijra kwa Ajili ya Kidunia au

kwa ajili ya Mwanamke Basi Hijra yake hua ni kwa Ajili ya alichokifanyia

Hijra’(Sahih Bukhari)

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliisema maneno ya Hadith hii kutokana

na kuainisha Umuhimu wa Nia katika Kila Jambo.

Na tunapoangalia hadith basi tunaona kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

anazungumzia Hijra kisha ndani yake akainisha aina za Nia na Madhumuni ya Hijra.

Kwani katika Wakati huo, na hadi katika wakati wa leo pia Kuna watu hua ni wenye

Kufanya Hijra kwa ajili ya Dini yao, na kuna wanaofanya Hijra kwa ajili ya Dunia yao.


789

Na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kuhusiana na Wanawake kwa sababu

kuna Watu walifanya Hijra ya kutoka Makkah kuelekea katika Mji wa Madinah si kwa

sababu ya Dini yao wala si kwa sababu ya Mola wao na Mtume wake basi kwa sababu

tu ya Kusikia kua katika Mji wa Madinah kuna Wanawake wazuri zaid kuliko Wanawake

wa Makkah.

Kwani anasema Imam Maaruf Al Kharki kua: ‘Kila kinapotokea Kitendo

kinachofanywa na Ibn Adam basi hua ni chenye kutokana na Nia Ndani yake, Hivyo

Kama Nia ni Sahih basi na Kitendo hua Sahih. Na kama Nia si Sahih basi na

Kitendo hua pia si Sahih’

Ambapo Nia Sahih juu ya Kitendo Sahih hua katika hali 3 zifuatazo;

1-Kama ikiwa Nia juu ya Kitendo Husika hua ni yenye kutokana na Kumuogopa

Allah Subhanah wa Ta'ala - Basi kitendo hicho hua ni sawa na kufanya biashara

kwa Mja huyo mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala.

2-Kama ikiwa Nia Juu ya Kitendo Hua ni yenye kutokana na Kuikimbilia Pepo ya

Allah Subhanah wa Ta'ala – Basi kitendo hicho hua ni sawa na kufanya Biashara

kwa mja huyo mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala.

3-Kama ikiwa Nia juu ya Kitendo hicho hua ni yenye kutokana na Kuona aibu kwa

Mja Mbele ya Mola wake, na hivyo hua ni kutekeleza Wajibu wake na kuonesha

Shukrani kwa Mja huyo mbele ya Mola wake – Basi kitendo hicho hua ni sawa na

Ibada ya Mtu mwenye kujikomboa na kutaka kujitafutia uhuru uliotokana na uzito

wa Majukumu yake mbele ya Mola wake.

Naam, Inasikitisha kuona kua wengi wetu pia leo hii hua tunafanya Ibada zetu nyingi

huku tukiwa na nia ya hali ya 3 yaani kwa sababu tu ya kujipunguzia Uzito wa

Majukumu.

Yaani kwa Mfano: Watu Wanafanya Ibada fulani kwa Sababu tu ya Kumrishwa Na

Muumba kufanya Ibada hio, bila kutilia maanani kua kufanya kwao Ibada husika mbali

ya kua ni Jukumu lao lakini hua ni kwa ajili ya Manufaa yao wao wenyewe.

Na hivyo hatufanyi Vitendo kwa ajili ya Nia ya Aina ya kwanza yaani kwa Ikhlasi au

kwa ajili ya Nia ya Aina ya pili yaani kujitolea kufanya Biashara na Allah Subhanah wa

Ta’ala kwa ajili ya kuwekeza katika Akhera yetu.

Kwani mbaya zaid ni kua kutokana na kuwepo kwa Mitandao ya Kijamii, na kuendekeza

Matamanio ya Kidunia basi wengi wetu pia hukosa Nia Sahih na hivyo Waislam hufikia


790

hatua ya, Kutumia Dini yao kwa ajili ya kujitafutia maisha, Kudhalilishana, Kuanikiana

Aibu wazi wazi n.k

Kwa ajili tu ya kutafuta Wafuatiliaji wengi na watizamaji wengi kwenye Video za

Youtube zao na Instagram zao, kwani watu wanajua kua kila wakipata wafuasi wengi

zaid basi hua wanalipwa zaidi na Mitandao ya Jamii kutokana na kua Kila Ukiangaliwa

zaid na Kufuatiliwa basi unapata nafasi zaid ya kua unapata kuingiza pesa za Malipo ya

kutangazia Matangazo ya biashara mbali mbali Mtandaoni kulingana na idadi ya

Waangalizi wanakufuatilia au kukuangalia, hivyo hio hua sio Nia Sahih ya Kufanya

Mambo yako Mbele ya Mola wako

Hivyo ingawa Safari ya Ummu Ayman ilikua Ngumu na ya Taabu sana kutokana na Jua

kali na Upepo mkali unaopeperusha Mchanga wa Jangwani Usoni mwake, lakini hata

hivyo hakuvunjika Moyo kwani alikua ni Mwenye Nia Sahih na hivyo Allah Subhanah

wa Ta'ala alikua pamoja nae.

Na baada ya masiku kadhaa basi Ummu Ayman akawasili katika wa Madinah huku

akiwa taabani, kwani Miguu yake imemvimba na uso wake ulikua utadhani alievaa Mask,

ila si Mask ya Barakoa kama msimavyo Waswahili. Kwani Muonekano wa uso wake

yeye Ummu Ayman ulikua wote Umejaa Vumbi Jembamba na michanga kutokana na

Upepo mkali wa Jangwani.

Kwani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipomuona Ummu Ayman basi Machozi

yalimlenga lenga na akawa ni mwenye kusema: ‘Ya Umm Ayman! Ya Ummi! Kwa

Hakika Allah Subhanah wa Ta'ala ameweka Nafasi kwa ajili yako Peponi’

Kisha baada ya hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaupangusa Uso wa Ummu

Ayman na kisha akamnawisha Uso wake kwa mikono yake Mitukufu na si hivyo tu.

Lakini pia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaikanda kanda Miguu na Mabega

ya Mama yake huyo Mlezi kwa Mikono yake mwenyewe Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam. Naam hivyo ndivyo alivyokua Mbora wa Viumbe kwa Mama yake Mlezi, na

kama huyu alikua ni Mama yake mlezi tu, Alimfanyia hivyo Jee hali ingekuaje kama

angekua ni Mama yake Mzazi?

Kwani Baada ya hapo basi Ummu Ayman akawa ni mwenye kuishi maisha yake kama

kawaida katika kumsaidia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kila awezalo na

hukua ni mtu wa kukaa kaa tu kwani alikua akisikia Jeshi la Waislam linatoka na kuenda

Vitani basi Ummu Ayman mbali ya kua ni mwenye Umri Mkubwa, na mbali ya kua

ameshatabiriwa Pepo mara mbili lakini hata hivyo alikua akifuatana na Jeshi la Kiislam

chini ya Uongozi wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo kua ni mwenye


791

kuhudumia Wanajeshi kwa kuwapa Maji na pia kuwahudumia Wapiganaji wa Kiiislam

waliojeruhiwa vitani.

Ambapo tunapozungumzia Vita kwa ajili ya Allah Subhnah wa Ta’ala basi hua

tunazungumzia Mapigano yaliyoamrishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume

wake Salallahu Alayhi wa Salam au na viongozi wa Kiislam kwa ajili ya kugombania

haki za Waislam na kuwatoa Waislam katika Dhulma kwa kutumia njia zinazokubalika

kisharia bila ya kufanya Israfu, kama hali ilivyokua katika maamrisho ya Vita mbali

mbali alivyosimamia kupigana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika wakati wa

uhai wake ambapo vita vya kwanza vilikua ni vita vya Badr.

RASUL ALLAH SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM NA MSAFARA WA

BIASHARA WA ABU SUFYAN

Ambapo tunapoangalia historia ya maisha ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi

tunaona kua alikua ni mtu mwenye Subra na Ustahamilivu kama ilivyo Dini ya Kiislam

yenyewe ambayo ni yenye kutokana na Ujumbe wa Allah Subhanah wa Ta’ala kupitia

kwa Mtume wake Salallahu Alayhi wa Salam, ambapo Allah Subhnah wa Ta’ala

anasema katika Qur’an kuhusiana na Ustahamilivu na Subra ya Mtume wake kua:

‏﴿وَٱصْبرِْ‏ وَمَا صَبْرُكَ‏ إِلا َّ بِٱهلل َِّ‏ وَلاَ‏ تحَْزَنْ‏ عَلَيْهِمْ‏ وَلاَ‏ تَكُ‏ فىِ‏ ضَيْقٍ‏ ممِّ َّا يمَْكُرُو نَ‏ ﴾

Waisbir wama sabruka illa biAllahi wala tahzan AAalayhim wala taku fee dhayqin

mimma yamkuroona (Surat An Nahl 16:127)

Tafsir: Na kua na Subra kwani Subra yako ni kutokana msaada wa Allah na wala

usiwe na Huzuni juu yao na wala usitaabike na mbinu zao za uovu.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakua ni mtu mwenye kupenda vita na

mapigano kama wanavyodhania wengi wasiojua kutokana na kuamini kua Dini ya

Kiislam ilienezwa kwa Upanga. Kwani Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua ni

mtu mwenye huruma, upole, mwenye kupenda salama na amani si katika maisha yake tu

bali kwa kila kiumbe Ulimwenguni kwa ujumla hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam hakuwahi kushika Upanga dhidi ya Maadui zake hadi pale ilipombidi, yaani

alipoamrishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala kua afanye hivyo kwa ajili ya kugombania

haki zake na haki za Waislam kwa ujumla.

Na hivyo Amrisho hilo la kupigana kwa ajili ya kusimamia haki za Waumini kua pia ni

mtihani wa Majaribio ya Kiimani juu ya Waumini wa Dini ya Kiislam kua jee kweli


792

wameamini, wanaweza kutii amri kikamilifu? na wanaweza kusimamia na kupigania

haki zao ipasavyo? Kama zinavyosema aya:

‏﴿وَلَنَبْلُوَن َّكُمْ‏ حَتى َّ ٰ نَعْلَمَ‏ ٱلْمُجَاهِدِينَ‏ مِنكُمْ‏ وَٱلص َّابِرِينَ‏ وَنَبْلُوَ‏ أَخْبَارَكُمْ‏ ﴾

Walanabluwannakum hatta naAAlama almujahideena minkum waalssabireena

wanabluwa akhbarakum (Surat Muhammad 47:31)

Tafsir: Na kwa hakika tutakujaribuni hata tutakapojua Wanaojitolea miongoni

mwenu na wenye Subra, na tutaujaribu ukweli wa habari zenu.

Aya inatuonesha kua Allah Subhanah wa Ta’ala anathibitisha kua atawajaribu Waislam

hadi Waumini watakapowajua ni nani miongoni mwetu Wanaojitolea kwa ajili yake na

wanaokua na subra kwa ajili yake, na hii haimaanishi kua yeye hajui juu ya hayo la, bali

amesema hapa maneno haya kuweka wazi kua atawadhihirisha wazi Waislam wenye

imani dhaifu hivyo wasiokua na sifa stahiki kuhusiana na imani zao, ndani ya nyoyo zao

na pia mbele ya Waislam wengine.

Na kuhusiana na aya hii basi Imam Fudayl Ibn Iyad alikua akilia pale anapoisoma aya hii

huku akisema: ‘Ya Allah Usitujaribu kwani ukitujaribu basi Utatudhihirisha wazi

na kutuadhirisha.’

Hivyo baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuhamia katika Mji wa Madina,

na Waislam kupata nusura na hifadhi basi miaka miwili baadae Allah Subhanah wa

Ta’ala akashusha aya ya kwanza yeye amrisho la kupigana vita vya Jihad kama

alivyosema Imam Qatadah Al Sadusi ambayo hii ni ile aya inasema:

‏﴿أُذِنَ‏ لِل َّذِينَ‏ يُقَاتَلُونَ‏ أبَِن َّهُمْ‏ ظُلِمُواْ‏ وَإِن َّ ٱهلل ََّ‏ ٰ عَلَى نَصْرِهِمْ‏ لَقَدِيرٌ۞ٱل َّذِينَ‏ أُخْ‏ رِجُواْ‏

مِن دَِرِهِم بِغَيرِْ‏ حَقٍّ‏ إِلا َّ أَن يَقُولُواْ‏ رَب ُّنَا ٱهلل َُّ‏ وَلَوْلاَ‏ دَفْعُ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱلن َّاسَ‏ بَعْضَ‏ ‏ُهمْ‏ بِبَعْ‏ ‏ٍض

له َُّدِّمَتْ‏ صَوَامِعُ‏ وَبِيَعٌ‏ وَصَلَوَاتٌ‏ وَمَسَاجِ‏ دُ‏ يُذْكَرُ‏ فِيهَا ٱسمُ‏ ٱهلل َِّ‏ كَثِيراً‏ وَلَيَنصُرَن َّ ٱهلل َُّ‏

مَن يَنصُرُهُ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لَقَوِي ٌّ عَزِيزٌ‏ ﴾


793

Odhina lilladheena yuqataloona bi-annahum dhulimoo wa-inna Allaha AAala

nasrihim laqadeerun; Alladheena okhrijoo min diyarihim bighayri haqqin illa an

yaqooloo rabbuna Allahu walawla dafAAu Allahi alnnasa baAAdhahum

bibaAAdhin lahuddimat sawamiAAu wabiyaAAun wasalawatun wamasajidu

yudhkaru feeha ismu Allahi katheeran walayansuranna Allahu man yansuruhu

inna Allaha laqawiyyun AAazeezun (Surat Al Hajj 22:39-40)

Tafsir: Wametangaziwa (Waislam kupigana dhidi ya Makafiri) wale ambao

wanapigana nao kwa sababu ya kudhulumiwa na kwa hakika Allah ni mwenye uwezo

wa kuwanusuru (kwa kuwapa uwezo). Wale (Waumini) ambao wamefukuzwa kutoka

katika Majumba yao bila ya haki kwa sababu tu ya kua wamesema: ‘Mola wetu ni

Allah’ Na kama ingekua Allah hawajaribu watu baadhi yao miongoni mwa baadhi yao

basi bila ya shaka Nyumba za Makasisi, Makanisa, Masinagogi na Miskiti inayotajwa

jina la Allah kwa wingi ndani yake basi ingevunjwa. Kwa hakika Allah atawanusuru

wale watakaomnusuru kwa hakika Allah ni mwenye uwezo juu ya kila kitu na mwenye

utukufu.

Hivyo hizi ni miongoni mwa aya za mwanzo kabisa kushushwa kuzungumzia kuhusiana

na kutangaziwa kwa mapigano ya vita vya Jihadi na kama tunavyoona kua ndani yake

hayakutajwa mapigano ya kushambulia bali yametajwa mapigano ya Kujihami kwa ajili

ya wale waliodhulumiwa, na hivyo hivyo Waislam wanaamrishwa kulipiza kisasi juu ya

yale waliyofanyiwa na kudhulumiwa katika kipindi cha miaka 10 ya Uislam ndani ya Mji

wa Makkah, hivyo walikua wanaambiwa kua umewadia wakati wa kuchukua haki zenu.

Anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ib Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wakati Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alipohama kutoka katika Mji wa Makka, basi Abu Bakr

Radhi Allahu Anhu alisema kua: ‘Wamemfukuza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, Inna lillahi wa ina Ilayhi RajiA’un - Hakika sisi ni wa Allah na hakika kwake

yeye ndio marejeo yetu, basi msiba mkubwa kwani wataangamia’’ na hivyo Allah

Subhnaha wa Ta’ala aliposhusha aya hii ya Kuwatangazia wale wanaopigana nao

kwa sababu ya kudhulumiwa basi Abu Bakr Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Nilijua

kua itatokea hali ya kuja kua na Vita’

Hivyo katika tangazo hilo basi tunaona kua Allah Subhnaha wa Ta’ala alikua akiwajaribu

Waislam kuangalia Imani zao juu yake na Mtume wake na Waumini wengine kama

zinavyosema aya:


794

‏﴿أَمْ‏ حَسِ‏ بْتُمْ‏ أَن تُتْرَكُواْ‏ وَلَم َّا يَعْلَمِ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِينَ‏ جَاهَدُواْ‏ مِنكُمْ‏ وَلمَْ‏ يَت َّخِ‏ ذُواْ‏ مِن دُ‏ ونِ‏

ٱهلل َِّ‏ وَلاَ‏ رَسُولِهِ‏ وَلاَ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ وَلِيجَةً‏ وَٱهلل َُّ‏ خَبِيرٌ‏ بمَِا تَعْمَلُونَ‏ ﴾

Am hasibtum an tutrakoo walamma yaAAlami Allahu alladheena jahadoo minkum

walam yattakhithoo min dooni Allahi wala rasoolihi wala almu/mineena waleejatan

waAllahu khabeerun bima taAAmaloona(Surat At Tawbah 9:16)

Tafsir: Hivi Jee Mnafikiria kua Mtaachiwa tu wakati Allah hajakujaribuni

miongoni mwenu kati ya wale watakaojitahidi kupigana miongoni mwenu bila ya

kua na mnaowategemea wengine isipokua Allah na Mtume wake na Waumini na

Allah ni mwenye Habari juu ya kila mnachokifanya.

Kama pia pale aliposema tena kua:

‏﴿أَمْ‏ حَسِ‏ بْتُمْ‏ أَنْ‏ تَدْخُلُواْ‏ ٱلجَْن َّةَ‏ وَلَم َّا يَعْلَمِ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِينَ‏ جَاهَدُواْ‏ مِنْكُمْ‏ وَيَعْلَمَ‏

ٱلص َّابِرِينَ‏ ﴾

Am hasibtum an tadkhuloo aljannata walamma yaAAlami Allahu alladheena

jahadoo minkum wayaAAlama alssabireena (Surat Al Imran 3:142)

Tafsir: Hivi mnajihesabu kua Mtaingia Peponi wakati Allah hajajua bado ni wepi

watakaojitahidi kupigana miongoni mwenu na wale wenye kua na Subra?

Hivyo anasema Bahr Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Allah

Subhanah wa Ta’ala ametangazia Jihadi katika wakati muwafaka, kwani hiki

kilikua ni kipindi ambacho Makafiri wa Makka walikua wako wengi kiidadi, hivyo

kama Allah Subhanah wa Ta’ala angewataka wapigane nao wakati wakiwa na wingi

si wa asilimia 10 tu ya watu wao, basi ingekua vigumu kwao wao.

Kwani ingawa walikua ni 80 tu lakini Ansari walikubaliana na makubaliano ya

Aqabah ya kumuunga mkono Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pale

walipomuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam : ‘Hivi Jee hatutakiwi

kuwavamia Makafiri hapa katika maeneo ya Minna?’’ ambapo Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘La Hakika mimi sikuamrishwa hivyo’

Lakini Waislam walipofukuzwa kwenye Mji wa Makkah, wengine wakaenda

Abyssina na wengine Madina na kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akawapa makazi


795

katika Mji wa Madina na hivyo kua tayari ni wenye kuanzisha Mamlaka yao

kwenye ardhi yao, basi ndio Allah Subhanah wa Ta’ala akatangazia Jihadi kwa

kushusha aya yenye tangazo hili la Odhina lilladheena yuqataloona biannahum

dhulimoo wa-inna Allaha AAala nasrihim laqadeerun - Wametangaziwa

(Waislam kupigana dhidi ya Makafiri) wale ambao wanapigana nao kwa sababu ya

kudhulumiwa na kwa hakika Allah ni mwenye uwezo wa kuwanusuru’(Surat Al Hajj

22:39)’

Ama kuhusiana na maneno ya aya inayofuatia baada ya hio ya Surat Al Hajj 22:39 yaani

aya ya 40 yasemayo:

‏﴿وَلَوْلاَ‏ دَفْعُ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱلن َّاسَ‏ بَعْضَهُمْ‏ بِبَعْضٍ‏ له َُّدِّمَتْ‏ صَوَامِعُ‏ وَبِيَعٌ‏ وَصَلَوَاتٌ‏ وَمَ‏ سَاجِ‏ دُ‏

يُذْكَرُ‏ فِيهَا ٱسمُ‏ ٱهلل َِّ‏ كَثِيراً‏ وَلَيَنصُرَن َّ ٱهلل َُّ‏ مَن يَنصُرُهُ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لَقَوِي ٌّ عَزِيزٌ‏ ﴾

Walawla dafAAu Allahi alnnasa baAAdhahum bibaAAdhin lahuddimat

sawamiAAu wabiyaAAun wasalawatun wamasajidu yudhkaru feeha ismu Allahi

katheeran walayansuranna Allahu man yansuruhu inna Allaha laqawiyyun

AAazeezun (Surat Al Hajj 22:40)

Tafsir: Na kama ingekua Allah hawajaribu watu baadhi yao miongoni mwa baadhi

yao basi bila ya shaka Nyumba za Makasisi, Makanisa, Masinagogi na Miskiti

inayotajwa jina la Allah kwa wingi ndani yake basi ingevunjwa. Kwa hakika Allah

atawanusuru wale watakaomnusuru kwa hakika Allah ni mwenye uwezo juu ya kila

kitu na mwenye utukufu.

Basi yanamaanisha kua: ‘Lau Kama Allah Subhanah wa Ta’ala hakuhalalisha

Mapigano juu ya Mitume na Waumini, basi Makafiri wangewakandamiza

Waumini na kusababisha kutelekezwa kwa Majumba ya Ibada yanayompwekesha

Allah Subhanah wa Ta’ala, lakini Allah Subhnaha wa Ta’ala ameyanusuru kwa

kuhalalisha mapigano ili mwishowe watu wawe huyu kumuabudia ndani yake Mola

wao’

Ambapo kwa upande wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye

anasema kuhusiana na kutajwa kwa Majumba haya ya watu wa Ahl al Kitab ya Nyumba

za Makasisi, Makanisa na Masinagogi ndani ya aya hii ni kua: ‘Kwa sababu Allah

Subhnaha wa Ta’ala aliyakubali Majumba hayo katika Nyakati za Mitume wao,

lakini si katika Nyakati za alipowaleta Mitume wengine baada yake na watu hao

wakawakufuru Mitume hao waliofuata. Yaani Aya hii inasema kua Kama Allah


796

Subhaah wa Ta’ala hakua ni mwenye kuyalinda Majengo hayo katika Nyakati zake

basi yangekua tayari yameshavunjwa’

Hivyo baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuambiwa na Allah Subhanah

wa Ta’ala kua Waislam wametangaziwa kupigania haki zao walizodhulumiwa, basi

kwanza akaamua kuzidhibiti njia kuu za misafara ya kibiashara ya Mji wa Makkah

zinazopitia katika Mji wa Madina, na hivyo akatia saini mikataba ya kukubaliana amani

na usalama baina ya watu wa Waislam na Mayahudi na watu wa maeneo mengine ya

jirani ya Madina.

Na kisha akaanza kuwatuma Masahaba zake kuivamia misafara ya Makafiri wa Makkah

na kuiteka nyara Mali zao kwa ajili ya kulipiza kisasi walivyofanyiwa Waislam na

Makafiri wa Makkah kwa kuwataifishia mali zao, hivyo walifanya matukio ya uvamizi

ambayo yalitokea mara kadhaa lakini hayakua na athari kubwa hadi pale mnamo mwezi

wa Ramadhani wa mwaka wa 2 Al Hijra wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alipopata habari kua kuna Msafara wa Abu Sufyan utokao katika ardhi ya Sham kuelekea

katika Mji wa Makkah thamani ya Dinari za Dhahabu 50,000 ambao uko chini ya walinzi

40.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaona kua huu ndio Msafara unaotakiwa

zaidi kutaifishwa kwa sababu Abu Sufyan alikua ni miongoni mwa viongozi wa

wataifishaji wa Mali za Waislam katika mji wa Makkah, hivyo Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akawakusanya Masahaba zake kwa ajili ya kukutana na Msafara huo

katika maeneo ya Badr akiwa na nia ya Kuuteka na kutaifisha kila kitu kwenye Msafara

huo, lakini Allah Subhanah wa Ta’ala alikua amepanga mipango myengine ambayo

ambayo ni ya kuwapima Imani Waumini wake kama zinavyosema aya:

‏﴿وَإِذْ‏ يَ‏ عِدُكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ إِحْدَى ٱلط َّائِفَتِينِْ‏ أَن َّهَا لَكُمْ‏ وَتَوَد ُّونَ‏ أَن َّ غَيْرَ‏ ذَاتِ‏ ٱلش َّوْكَةِ‏

تَكُونُ‏ لَكُمْ‏ وَيُرِيدُ‏ ٱهلل َُّ‏ أَن يحُِق َّ الحَق َّ بِكَلِمَاتِهِ‏ وَيَقْطَعَ‏ دَابِرَ‏ ٱلْكَافِرِينَ‏ ﴾

Wa-idh yaAAidukumu Allahu ihda altta-ifatayni annaha lakum watawaddoona

anna ghayra dhati alshshawkati takoonu lakum wayureedu Allahu an yuhiqqa

alhaqqa bikalimatihi wayaqtaAAa dabira alkafireena (Surat Al Anfal 8:7)

Tafsir: Na kumbuka wakati Allah alipokuahidini nyie moja kati ya makundi mawili

(ya maadui zako aidha Msafara wao au Jeshi lao) ambapo nyinyi mlikua mnatamani

kua lisiokua na Jeshi ndio iwe lenu, Lakini Allah alikua anataka kuisimamisha haki

kwa maneno yake na kukata mizizi ya Ukafiri.


797

Ambapo anasema Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua: ‘Yaani hapa

Allah Subhanah wa Ta’ala anawaambia Waislam kua: ‘Mnatafuta mafanikio ya

haraka na ya juu juu, na mnataka kujiepusha na kile kitakacho kusababishieni

madhara kwa miili yenu au Afya zenu, lakini Allah alilenga malengo bora zaidi

ambayo ni yenye kupelekea kuisimamisha hii Dini, Ushindi juu ya ukweli, Kupanda

darja juu zaidi na kupata mafanikio ya Kidunia na Kiakhera, Ingawa Malengo

mawili hayo (Yenu na yake) yana tofauti kubwa sana baina yao, lakini hata hivyo

yeye Allah Subhanah wa Ta’ala anakuchagulieni kukabiliana na Jehi lao kubwa na

kuwaangamizia Nguvu zao kutokana na udhaifu wenu na kukujaalieni kuwazidi

wingi wa idadi yao kutokana na udogo wa idadi yeu, kuwaadhirisha wao na

kukupandisheni darja nyie na anakupeni kile ambacho hakiwezi kulinganishwa na

kile kilichobebwa na Msafara wao.’’

Tunapoiangalia aya hii tunaona kua Allah Subahan wa Ta’ala anazungumzia tukio bora

alilowachagulia Waislam kua liwatokee kua kama kipimo cha Imani yao katika siku ya

Yawm Al Furqan.

YAWM AL FURQAN – SIKU YA VITA VYA BADR.

Neno Faraqa kwa lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kubagua, Kutenganisha,

Kutofautisha, Kugawanya, Kukata katikati. Neno Faraqa ndio lililotoa neno Furqan

ambalo hua linamaanisha Uthibitisho wa tofauti baina ya mambo au vitu tofauti,

Tofautisho la Jema na Ovu.

Neno Furqan ndio lililotoa Jina la Qur’an Al Furqan yaani Kitabu kinachotofautisha

baina ya Jema na Ovu, na pia ndio lilotoa jina la siku inayojulikana kama Yawm Al

Furqan yaani Siku ya Uthibitisho wa tofauti baina ya Jema na Ovu, Nuru na Kiza, Haki

na Batil.

Ambapo tunapozungumzia Yawm Al Furqan basi hua hatuzunguzmii siku yeyote ile

isipokua ni ile siku iliyotokea tukio ambalo lilibadilisha muelekeo na mtizamo mzima wa

Historia ya Ulimwenguni, ambayo ni hii inayojulikana kua kama Siku ya Badr kama

ilivyoelezewa na Allah Subhanah wa Ta’ala katika aya ifuatayo:


798

‏﴿وَٱعْلَمُو ۤ ا أَنم ََّا غَنِمْتُمْ‏ مِّن شَيْءٍ‏ فَأَن َّ هللِ َِّ‏ خمُُسَهُ‏ وَلِلر َّسُولِ‏ وَلِذِى ٱلْ‏ قُرْبىَٰ‏ وَٱلْيَتَامَىٰ‏

وَٱلْمَسَاكِينِ‏ وَٱبْنِ‏ ٱلس َّبِيلِ‏ إِن كُنتُمْ‏ آمَنْتُمْ‏ بِٱهلل َِّ‏ وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَى ٰ عَبْدَِ‏ يَوْمَ‏ ٱلْفُرْقَا ‏ِن

ّ كُل شَيْءٍ‏ قَدِيرٌ‏ ﴾

يَوْمَ‏ ٱلْتَقَى ٱلجَْمْعَانِ‏ وَٱهلل َُّ‏ ٰ عَلَى ِ

WaiAAlamoo annama ghanimtum min shay-in faanna lillahi khumusahu

walilrrasooli walidhee alqurba waalyatama waalmasakeeni waibni alssabeeli in

kuntum amantum biAllahi wama anzalna AAala AAabdina yawma alfurqani

yawma iltaqa aljamAAani waAllahu AAala kulli shay-in qadeerun (Surat Al Anfal

8:41)

Tafsir: Na fahamuni kua katika Ngawira chochote kile mtakachokipata, basi sehemu

moja kati ya tano ni kwa ajili ya Allah na Mtume wake na Waliokaribu nae na

Mayatima na Masikini, na Wasafiri, kama kweli nyinyi mnamuamini Allah na kile

tulichomshushia Mja wetu. Katika Yawm Al Furqan – Siku ya Uthibitisho wa tofauti

baina ya Jema na Ovu, Nuru na Kiza, Haki na Batil – Siku ambayo zilikutana nguvu

mbili na Allah ni mwenye Makadirio juu ya kila kitu.

Hivyo kwa upande mwengine basi Abu Sufyan alikua ni mwenye kujua kua njia ya

kawaida anayotaka kupitia kua haina usalama baada ya mashambulizi madogo madogo

yaliyokua yakitokea hapo kabla dhidi ya misafara ya watu wa Makkah, na hivyo akawa

na wasi wasi, na alipofuatilia zaidi akagundua kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam na jeshi lake ameandaa mashambulizi kwenye maeneo ya Badr, hivyo kwanza

akatuma Mjumbe apeleke habari hizo za matayarisho ya uvamizi wa Msafara wake katika

Mji wa Makkah na kisha akaamua kubadilisha njia kwa ajili ya kuunusuru Msafara wake

huo.

Mjumbe huyo wa Abu Sufyan aitwae Damdam Ibn Amr alipofika katika Mji wa Makkah,

akamkata pua na masikio Ngamia wake kisha akachana nguo zake mgongoni na kifuani

kuashiria kua kuna vita kisha akatangazia kwa kusema: ‘Enyi Watu wa Kabila la

Quraysh, hakika mali zenu ziko pamoja na Abu Sufyan, na msafara wake unataka

kuvamiwa na Muhammad na Masahaba zake, siwezi kusema nini kitatokea

isipokua ni kuomba msaada wenu.’

Makafiri wa Makkah baada ya kupata ujumbe huo basi haraka sana wakakusanya jeshi

la watu 1300 lenye wapanda Farasi 100 na wapanda ngamia zaidi ya 100 na kisha

likaondoka na kuelekea katika Maeneo ya Badr. Ambapo kwa upande wake Abu Sufyan

akaelekea upande wa Mwambao wa Bahari Nyekundu kwa ajili ya kuliepuka eneo la


799

Badr na alipohakikisha kua yuko salama basi akatua ujumbe tena kwa watu Makkah

kuwaambia kua basi haina haja ya kupigana na Muhammad kwani Msafara na Mali zake

ziko salama, na ingawa miongoi mwa wanajeshi wa watu wa Makkah waliamua kurudi

katika Mji wa Makkah

Lakini kwa Upande wa Abu Jahal basi akatilia mkazo kua lazima wakakutane na

Waislam katika maeneo ya Badr kwa kusema: ‘Wallahi, haiwezekani kurudi hadi

tutakapofika kwenye visima vya Badr, tukachinje Ngamia, kisha Wanamuziki wa

kike wacheze kwa ajili yetu, na kutokana na tukio hili basi Waarabu watasema

kwenye historia namna tulivyosheherekea tukio hili.’ Hivyo Jeshi hilo likaendelea na

Msafara wao kuelekea kwenye maeneo ya Badr.

Baada ya mda Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akapata habari ya kubadilisha kwa

njia ya Msafara wa Abu Sufyan, na hapo hapo akapata habari ya kukaribia karibu yao

kwa jeshi kubwa la Makafiri wa Makka, hivyo akashauriana na Masahaba zake kuhusiana

na kinachotaka kutokea ambapo wao Waislam walikua hawajajitayarisha kwa ajili ya

Vita lakini kwa hali inavyokwenda basi itabidi wapigane Vita dhidi ya maaduai zao hao

ambao wingi wao ni zaidi ya 1000 huku wao wakiwa ni watu 313 tu. Hivyo Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akaomba Ushauri kwa kuwauliza Waislam; ‘Jee tufanye

nini?’

Hivyo wakati Waislam wamekaa kimya na kufikiria cha kufanya, basi akasimama

Miqdad Ibn Aswad Al Kindi Radhi Allahu Anhu kisha akasema: ‘Ya Rasul Allah

(Salallahu Alayhi wa Salam) Tekeleza mipango ambayo Allah Subhanah wa Ta’ala

ameiweka, kwani kwa hakika sisi hatutosema kama walivyosema Mayahudi

kumwambia Nabii wao Musa kua:

‏﴿فَٱذْهَبْ‏ أَنتَ‏ وَرَب ُّكَ‏ فَقَاتِلا ۤ إِ َّ هَاهُنَا قَاعِدُونَ‏ ﴾

Fa-idhhab anta warabbuka faqatila inna hahuna qaAAidoona; (Surat Al Maidah

5:24)

Tafsir: Hivyo nenda wewe na Mola wako mkapigane nao, sisi tunakaa hapa

(kukusubirini)’

Badala yake sisi tunasema: ‘Nenda wewe na Mola wako mkapigane na sisi tuko

pamoja nanyi na tutapigana. Wa Allahi! Nnaapa kwa yule ambae amekutuma wewe

kwa Haki, kua hata kama ukituongoza kwenye Birkul Ghimad (Maeneo ya

Ethiopia) basi sisi tutapigana pamoja nawe dhidi ya wale watakaopingana na haki

na hata kama ikiwa kuna makundi na makundi ya Makabila baina ya Madina na

Birkul Ghimad basi tutapigana mpaka tufike huko, na bila ya shaka tutapigana kwa


800

upande wa Kulia kwako, Kushoto kwako, Mbele yako na Nyuma yako mpaka Allah

Subhanah wa Ta’ala atupe Ushindi.’

Hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akafurahi na kutabasam kisha akawageukia

watu wa Madina na kuwauliza: ‘Jee mnasemaje? Tufanye nini?’

Ambapo kwa upande wa watu wa Madina akasimama Saad Ibn Muadh Radhi Allahu

Anhu na kasema: ‘Ya Rasul Allah (Salallahu Alayhi wa Salam) Hakika sisi

tumekuamini wewe, Tumekuamini wewe, na tumekubali kua ukisemacho ni cha

kweli. Hivyo tumeahidi kua ni wenye kukusikiliza na kukutii. Hivyo Ya Rasul Allah

(Salallahu Alayhi wa Salam) fanya unavyotaka kufanya kwani hata ukituambia

tuvuke Bahari Nyekudu basi Tutavuka.’’

Hivyo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam pamoja na Masahaba zake

wakaamua kupiga kambi na kujitayarisha kwa ajili ya vita katika maeneo hayo ya Badr,

na hapo Hubab Ibn Al Mundhir ambae alikua anasifika kwa uzoefu wa mbinu za vita

wakati huo, akamuuliza Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, ‘Ya Rasul

Allah, jee sehemu hii tuliokuwepo sasa hivi, Allah amekushushia aya kua tukae

hapa, ili tusikimbie vitani na kuikimbia sehemu hii, au ni kwa sababu ya mtazamo

wa mbinu za kivita?’

Hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu kua ni kwa sababu ya

mtazamo wake wa mbinu za kivita, hapo Hubab akasema, ‘Ya Rasul Allah, hii si

sehemu nzuri ya kukaa, bali chukua watu wako hadi karibu na visima vya maji

vilivyo karibu na Maadui. Twende tukapige kambi hapo, na kuvizuia visima viwe

nyuma yetu, tujaze maji vyombo vyetu, na kisha tupigane na maadui zetu, sisi

tutakunywa maji lakini wao watakua hawana maji ya kunywa’, hapo Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akafikiria na kuona kua hii ni mbinu bora hivyo

akaamua kufanya kama alivyosema Hubab.

Walipokaribia na bonde la Badr, Sa’d Ibn Mu’adh ambae aliekuwa Chifu wa kabila la

Banu Aws akamfuata Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na kumwambia,

‘Ya Rasul Allah, turuhusu tukujengee sehemu nyuma yetu, ambapo wewe utakaa,

na kumuweka Ngamia wako pia. Nasi tutavaana na maadui zetu. Ikiwa Allah

atatupa nguvu na kushinda basi hilo ndio tunalolitaka, lakini ikiwa litatokea jengine

zaidi ya hilo, basi wewe itakubidi upande Ngamia wako na urudi kuungana na wale

waliobakia. Kwani, Ya Rasul Allah, mapenzi yetu juu yako si makubwa kama ya

wale waliobakia juu yako, kwani kama wangelijua kua utakutana na vita basi

wasingekubali kubakia. Allah akulinde wewe kupita kwao, watakupa ushauri mzuri

na watapigana pamoja nawe’.


801

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akakubaliana na ushauri huo na

kumuombea dua Sa’d Ibn Muadh. Hivyo Waislam wakapiga kambi katika eneo hilo la

mbele ya visima vya Badr, katika siku ya Ijumaa ya mwezi 17 wa Ramadhan na hali

ilikua kama zinavyosema aya:

‏﴿إِذْ‏ يُغَشِّ‏ يكُمُ‏ ٱلن ُّعَاسَ‏ أَمَنَةً‏ مِّنْهُ‏ وَيُنَزِّلُ‏ عَلَيْكُم مِّنَ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ مَآءً‏ لِّيُطَهِّرَكُمْ‏ بِهِ‏ وَيُذْهِبَ‏

عَنكُمْ‏ رِجْزَ‏ ٱلش َّيْطَانِ‏ وَلِيَرْبِطَ‏ عَلَى ٰ قُلُوبِكُمْ‏ وَيُثَبِّتَ‏ بِهِ‏ ٱلأَقْدَامَ‏ ﴾

Idh yughashsheekumu alnnuAAasa amanatan minhu wayunazzilu AAalaykum

mina alssama-i maan liyutahhirakum bihi wayuthhiba AAankum rijza alshshaytani

waliyarbita AAala quloobikum wayuthabbita bihi al-aqdama (Surat Al Anfal 8: 11)

Tafsir: Kumbuka wakati alipokufunikeni kwa usingizi kua kama ulinzi kutoka kwake,

na akajaalia Maji kumwagika kutoka Mbinguni kwa ajili ya kukusafisheni na

kukuondeleeni athari za uchafu wa Shaytan na kukutieni nguvu nyoyo zenu na

kuithibitishia uimara miguu yenu.

Anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Kutokana na kua Ibn

Adam hua hawezi kulala anapokua katika hali ya Khofu basi ndio maana hapa

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Wakati alipokusababishieni kuweza kusinzia,

kwani kama wangelala moja kwa moja basi Maadui wangewavamia’’

Ambapo anasema Imam Muhamammad Ibn Is-haq amesema Ali Ibn Abu Talib Radhi

Allahu Anhu kua: ‘Hakika sisi hatukua na Mpanda Farasi isipokua Miqdad Al

Aswad nami sikuona yeyote miongoni mwetu aliekua macho isipokua Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam ambae alikua amekaa chini ya Mti huku akiomba Dua

na kulia hadi Alfajiri’

Ambapo Asubuhi yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akitabasamu na

kumwambia Abu Bakr Radhi Allahu Anhu kua: ‘Kua na hali nzuri ewe Abu Bakr.

Kwani amewasili Jibril kwenye Vilele vya milima’ na kisha akasoma aya isemayo:

‏﴿سَيُهْزَمُ‏ ٱلجَْمْعُ‏ وَيُوَل ُّونَ‏ ٱلد ُّبُرَ‏ ﴾

Sayuhzamu aljamAAu wayuwalloona alddubura (Surat Al Qamar 54:45)

Tafsir: Watashindwa na kuimbizwa kwa wingi wao na watageukia Nyuma yao.


802

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu

kua: ‘Wakati Waislam walipowasili kwenye Badr basi walikuta Makafiri wa

Makkah wakiwa wameshafika katika eneo hilo na kuhodhi visima vya Maji. Hili

liliwavunja nguvu Waislam kwani Makafiri walikua wametulia na kufurahia hali

ya mazingira mazuri ya kimbinu za Vita, kwa sababu wao walikua wako kwenye

eneo la juu na Waislam walikua wako bondeni, huku wakiwa ni wenye kuteleza

miguu yao kutokana na ardhi yenye mchanga iliyopo chini ya miguu yao. Vile vile

wakati wa usiku kulikua kuna wenye Janaba, na hivyo ikawabidi wasali kwa

kutayammam bila ya kutumia maji’

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akajaalia kunyesha kwa mvua, na Waislam

wakajitoharisha, wakalishia Wanyama wao na kujaza maji kwenye vyombo vyao vya

maji, na pia wakachimba mashimo kwa ajili ya kuhifadhia Maji, na Mvua hio pia

ikasababisha Mchanga uliokua laini kwenye miguu yao kua ni wenye kushikamana na

kua mgumu na hivyo kua ni wenye kuirahisishia uwezo wa uthibiti wa Miguu yao katika

harakati zao.

Ambapo Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu anasema kua: ‘Wakati Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alipowaangalia watu wa Quraysh na wingi wao na

kuwalinganisha na wingi wa Wafuasi wake waliozidiwa basi akageukia Kibla na

akaanza kuomba dua kwa kusema: ‘Ya Allah! Hakika wewe umeniahidi, hivyo

nitimizie ahadi yangu, kwani watu wangu hawa wakiamgamia basi hakutokua na

wenye kukubadu badala yake.’ Rasul Allah Salallah Alayhi wa Salam aliendelea

kuomba hivyo hadi pale lilipomuanguka Joho lake kutoka begani mwake, na Abu

Bakr akalirudisha Joho hilo begani mwake. Na kisha Abu Bakr akaondoka kutoka

nyuma mgongoni mwa Rasul Allah Salallah Alayhi wa Salam na kusema: ‘Basi

Inatosha ya Rasul Allah, hakika wazazi wangu watolewe kafara kwa ajili yako,

Hakika Allah atatimiza ahadi yake juu yako’’

Na hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akaishusha aya hii isemayo:

‏﴿إِذْ‏ تَسْتَغِيثُونَ‏ رَب َّكُمْ‏ فَٱسْتَجَابَ‏ لَكُمْ‏ أَنىّ‏ ِ ممُِد ُّكُمْ‏ أبَِلْفٍ‏ مِّنَ‏ ٱلْمَلا ۤ ئِ‏ كَ‏ ةِ‏ مُرْدِفِينَ۞وَمَا

جَعَلَهُ‏ ٱهلل َُّ‏ إِلا َّ بُشْرَىٰ‏ وَلِتَطْمَئِن َّ بِهِ‏ قُلُوبُكُمْ‏ وَمَا ٱلن َّصْرُ‏ إِلا َّ مِنْ‏ عِندِ‏ ٱهلل َِّ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ عَزِ‏ يزٌ‏

حَكِيمٌ‏ ﴾


803

Idh tastagheedhoona rabbakum faistajaba lakum annee mumiddukum bi-alfin

mina almala-ikati murdifeena; Wama jaAAalahu Allahu illa bushra walitatmainna

bihi quloobukum wama alnnasru illa min AAindi Allahi inna Allaha

AAazeezun hakeemun; (Surat Al Anfal 8:9-10)

Tafsir: Na Kumbuka wakati mlipoomba msaada kwa Mola wenu nae akajibu kwa

kusema: ‘Nitakusaidia mimi kwa Maelfu kutoka katika Malaika wangu wenye

kufuatana mmoja nyuma ya mwengine’ Allah amelijaalia hili kua kama bashirio jema

ili Nyoyo zenu zipate utulivu kutokana nalo, kwani hakuna ushindi isipokua kutoka

kwa Allah.

Anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Aya imetumia hali ya

Uombaji wa Dua wa wingi kuonesha kua pale wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alipokua anamuomba Allah Subhanah wa Ta’ala basi Waislam wengine

pia walikua wakiomba hivyo.’

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Malaika Jibril na

Mikail wote wawili walishuka wakiongoza Malaika 500 wakiwa mbele ya Jeshi la

Waislam’

Hivyo ingawa Waislam walikua ni robo tatu ya Makafiri lakini Majeshi yote mawili haya

ya Waislam na Makafiri yalipokutana, basi vita vilianza kama ilivyo kawaida ya Vita vya

asili vya Kiarabu ambapo hua ni kwenye kuwepo kwa ufunguzi mapigano ya wapiganaji

mahiri kutoka pande zote mbili kwa ajili ya kupigana wao kwanza mbele ya Majeshi

mawili hayo.

Ambapo kwa upande wa Makafiri uliwakilishwa na Utbah Ibn Rabia, na Walid Ibn Utbah

Ibn Rabia na Shaybah, wakati Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipotaka kuteua

Wapiganaji wake basi kila mmoja miongoni mwa Waislam alijitolea kwa ajili ya kua ni

muanzilishi wa Mapigano hayo kutokana na ari waliyokua nayo Waislam, lakini hata

hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akateuwa wapiganaji kutoka kwenye

familia yake kwa kumteua Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu, Hamza Ibn Abu Talib

Radhi Allahu Anhu na Ubaydah Radhi Allahu Anhu.

Ambapo mapigano hayo ya ufunguzi yalipoanza basi Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu

Anhu akashinda, Hamza Ibn Abu Talim Radhi Allahu Anhu nae pia akashinda na

Ubaydah Radhi Allahu Anhu nae akashinda lakini alijeruhiwa vibaya sana, na baadae

akafariki kutokana na majeraha hayo.

Baada ya mapigano hayo basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akachota mchanga

wa sehemu aliyokuwepo kwenye ardhi ya Badr na kisha akaurembea katika upande wa

Makafiri huku akisema: ‘Uchanganyikiwe muonekano wa Nyuso zao’ na hapo hapo

kikatokea kimbuga chenye upepo mkubwa na Mavumbi yaliyokua yakipeperukia katika


804

upande wa Makafiri na mapigano yakaanza huku yakitokea maajabu makubwa sana

kwani Waislam walikua wapo katika upande wa Kusini Magharibi wa bonde la Badr

ambapo Makafiri walikua wap katika upande wa Kaskazini Mashariki wa Bonde hilo,

huku Waislam wakiwa wako nyuma ya Mlima Asfal kwenye seheu inayojulikana kama

Jabal Malaikah.

Na hii ni kwa sababu kimbunga hicho kilianzia kutoka kwenye Mlima huo na kuelekea

katika Upnde wa Makafiri, na ingawa ilikua ni siku iliyonyehsa mvua kabla yake na

hivyo kutowekezakana kuwepo kwa vumbi lakni hali ilikua tofauti katika siku hio, kwani

Makafiri walichanganyikiwa baada ya kuona mchanga kutoka kusiko julikana unaingia

kwenye macho yao na hapo hapo kupata mashambulizi kutoka kwa viumbe wasiowaona

wala kuwajua.

Hivyo Makafiri wakageuka na kukimbia baada ya hali kubadilika hivyo ingawa Waislam

walikua kidogo lakini wakawa ni wenye kushinda na Makafiri waliokua wengi wakawa

ni wenye kushindwa na kutokana na kuzidiwana kukimbia. Ambapo Allah Subhanah wa

Ta’ala analielezea tukio hili kwa kusema kua:

يُبْلِى

‏﴿فَلَمْ‏ تَقْتُلُوهُمْ‏ وَلَٰكِن َّ ٱهلل ََّ‏ قَتَلَهُمْ‏ وَمَا رَمَيْتَ‏ إِذْ‏ رَمَيْتَ‏ وَلَٰكِن َّ ٱهلل ََّ‏ ٰ رَمَى وَلِ‏ َ

ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ مِنْهُ‏ بَلا ءً‏ ۤ حَسَناً‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ سمَِيعٌ‏ عَلِيمٌ‏ ﴾

Falam taqtuloohum walakinna Allaha qatalahum wama ramayta idh ramayta

walakinna Allaha rama waliyubliya almu/mineena minhu balaan hasanan inna

Allaha sameeAAun AAaleemun (Quran, 8: 17)

Tafsir: Na hamkuwaua wao lakini Allah ndie aliewaua, nawe (Muhammad Salallahu

Alayhi wa Salam) hukurembea pale uliporemembea bali ni Allah ndie alierembea kwa

ajili kuwajaribu Waumini kwa majaribio Mema, na kwa hakika Allah ni Mwingi wa

Kusikia na ni mwenye kujua.

Hivyo katika vita hivi vya Badr, Waislamu waliwaua Makafir wa Makkah 70 na

kuwateka mateka wengine 70, ambapo Waislamu waliokufa Mashahidi walikua ni 14 tu

Na hivyo Malaika Jibril akamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa kusema:

‘Ya Rasul Allah hivi wewe unawachukulia vipi wale ambao waliopigana kwenye

vita vya Badr?’ ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Hakika sisi

tunawahesabu kua ni wabora miongoni mwa Waislam’ na hivyo Malaika Jibril

akajibu : ‘Na Sisi pia tunawahesabu Malaiak waliopigana kwenye Vita vya Badr’


805

Naam na hii ni kwa sababu Waislam waliopigana Vita Vya Badr walipigana vita Vya

Furqan ambavyo ndivyo vilivyosimamisha Msingi Imara wa Dini ya Kiislam. Kama

alivyosema Allah Subhanah wa Ta’ala pale aliposema katika Qur’an kua:

‏﴿وَيُسَبِّحُ‏ ٱلر َّعْدُ‏ بحَِمْدِهِ‏ وَٱلْمَلاَئِكَةُ‏ مِنْ‏ خِ‏ يفَتِهِ‏ وَيُرْسِ‏ لُ‏ ٱلص َّ وَاعِقَ‏ فَيُصِيبُ‏ هبَِا مَن

يَشَآءُ‏ وَهُمْ‏ يجَُادِلُونَ‏ فىِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَهُوَ‏ شَدِيدُ‏ ٱلْمِحَالِ‏ ﴾

Qad kana lakum ayatun fee fi-atayni iltaqata fi-atun tuqatilu fee sabeeli Allahi

waokhra kafiratun yarawnahum mithlayhim ra/ya alAAayni waAllahu yu-ayyidu

binasrihi man yashao inna fee dhalika laAAibratan li-olee al-absari (Surat Al Imran

3:13)

Tafsir: Kwa hakika tayari (Katika vita vya Badr) imeshakujieni Dalili katika pande

mbili za Majeshi zilizokutana, ambapo upande mmoja walikua wanapigana kwa ajili

ya Allah na upande mwengine kwa ajili ya Ukafiri Wao (Waumini) Wameona

Makafiri kwa macho yao mara mbili zaid yao (Wingi wao) na Allah humsaidia kwa

ushindi wake yule amtakae. Hakika katika haya kuna dalili kuna Somo kwa wale

wenye kuona.

Kisha Allah Subhanah Subhanah wa Ta’ala anawaambia Waislam kua:

‏﴿وَلَقَدْ‏ نَصَرَكُ‏ مُ‏ ٱهلل َُّ‏ بِبَدْ‏ رٍ‏ وَأَنْتُمْ‏ أَذِل َّةٌ‏ فَٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تَشْ‏ كُ‏ رُونَ‏ ‏۞إِ‏ ذْ‏ تَقُولُ‏ لِلْمُؤْمِنِينَ‏

أَلَنْ‏ يَكْ‏ فِيَكُمْ‏ أَنْ‏ يمُِد َّكُ‏ مْ‏ رَب ُّكُمْ‏ بِثَلاَثَةِ‏ آلاَفٍ‏ مِّنَ‏ ۤ ٱلْمَلا ئِكَةِ‏ ۤ مُنزَلِينَ۞بَلَى إِن تَصْبرُِواْ‏

وَتَت َّقُواْ‏ وََْتُوكُمْ‏ مِّنْ‏ فَوْرِهِمْ‏ هَٰذَا يمُْدِدْكُمْ‏ رَب ُّكُمْ‏ بخَِمْسَةِ‏ ۤ آلا فٍ‏ مِّنَ‏ ۤ ٱلْمَلا ئِكَةِ‏

مُسَوِّمِينَ۞وَمَا جَعَلَهُ‏ ٱهلل َُّ‏ إِلا َّ بُشْرَىٰ‏ لَكُ‏ ‏ْم

وَلِتَطْمَئِن َّ قُلُوبُكُمْ‏ بِِه وَ‏ مَا ٱلن َّصْ‏ رُ‏ إِلا َّ مِ‏ ‏ْن

عِندِ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱلْعَزِيزِ‏ ٱلحَْكِيمِ‏ ﴾

Walaqad nasarakumu Allahu bibadrin waantum adhillatun faittaqoo Allaha

laAAallakum tashkuroona; Idh taqoolu lilmu/mineena alan yakfiyakum an

yumiddakum rabbukum bithalathati alafin mina almala-ikati munzaleena; Bala in

tasbiroo watattaqoo waya/tookum min fawrihim hadha yumdidkum rabbukum

bikhamsati alafin mina almala-ikati musawwimeena; Wama jaAAalahu Allahu illa


806

bushra lakum walitatma-inna quloobukum bihi wama alnnasru illa min AAindi

Allahi alAAazeezi alhakeemi (Surat Al Imran 3:123-126)

Tafsir: Na Allah amekunusuruni nyinyi na kukupeni Ushindi kwenye Badr wakati

mlipokua hamna nguvu, hivyo Mcheni Allah ili mpate kua ni wenye shukrani.

Kumbuka (Ewe Muhammad) wakati ulipowaambia Waumini: ‘Hivi jee haitoshelezi

kwenu nyinyi kua Mola wenu atakusaidieni kwa Malaika 3000 atakaokushushieni?

Naam, kama Mkiwa na Subra na Ucha Mungu na maadui wakija kukuvamieni basi

Mola wenu atakusaidieni nyie kwa Malaika 5000 wenye Alama za kuwatofautisha. Na

hakujaalia Allah isipokua ni ujumbe wenye habari nzuri kwa ajili yenu na

kukuhakikishieni utulivu ndani ya Nyoyo zenu. Na hakuna Ushindi isipokua kutoka

kwa Allah Mwenye wingi wa uwezo na mwenye wingi wa Hikma’

Ambapo amesema Mujaddid Ad Din Imam Ibn Hajar Al Asqalani kua: ‘Rabii Ibn Anas

amesema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala aliwasaidia Waislam katika Vita vya Badr

kwa Malaiak 1000, na kisha akawaongezea Msaadwa Malaika 3000 na kisha

akawaongezea Msaada wa Malaika 5000’

Baada ya kumalizika Vita na kukusanywa mateka waliotekwa na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kuwaona mateka hao, basi akawa hajui awafanye nini, hivyo ikabidi

akae na Masahaba zake ili washauriane na kuamua wawafanye nini, hapo Abu Bakr as

Siddiq Radhi Allahu Anhu akashauri mateka walipishwe fidya halafu waachiwe, na Umar

Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akashauri wauliwe, hapo Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam akaona bora kufanya kama alivyosema Abu Bakr Radhi Allahu Anhu

na kwa baadhi ya wanaojua kusoma miongoni mwao mateka hao basi wakapewa

Waislam wasiokua kusoma wawasomeshe, wapate kujua kusoma na kuandika.

Ambapo miongoni mwa waliokamatwa pia alikuwemo Al Abbas Ibn Abd Ul Muttalib

Radhi Allahu Anhu ambae anaelezewa na Jabir Ibn Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua:

‘Baada ya vita vya Badr basi miongoni mwa Mateka wa Vita waliletwa, na miongoni

mwao alikuwemo Al Abbas, ambae alikua hana shati hivyo Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akamtafutia Shati kwa ajili yake, na likapatikana shati la Abdullah

Ibn Ubbay lililokua ni saizi yake, hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akampa Al Abbas avae na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamfidia

Abdulla kwa kumpa Shati lake yeye.’

Ambapo baadae Al Abbas akajilipia fidya kwa ajili ya kujikomboa na kuachiwa baada

yake na akasilimu baada ya mkataba wa Huddaybiyah ambapo Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akampa jina la Muhajirun wa Mwisho, na hivyo kua ni mwenye

kuingizwa kua miongoni mwa wenye kurithi Ngawira ya Vita na kurudishiwa kazi yake

ya Usimamiaji wa Kisima cha Maji ya Zamzam.


807

Miongoni mwa waliokamatwa pia alikuwemo Abu Aziz Ibn Umayr ambae ni kaka

yake Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu, ambapo anasema Abu Azizi Ibn Umayr

kua: ‘Hakika mimi nilikua pamoja na kikundi cha Ansar, ambao ilikua kila

wakila chakula walikua wakinigaia Tende na Mkate ili nile kutokana na

maamrisho ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua wasituvunjie haki

zetu’

‘Mara kaka yangu Musab Ibn Umayr akapita karibu yangu na akaniona na hivyo

akamwambia mmoja kati ya Maansari hao wanaonisimamia kama mateka kua

‘Huyu mfunge kamba yake madhubuti sana, kwani Mama yake ni Mtu tajiri sana

na huenda akalipa pesa nzuri sana kwa ajili ya kumkomboa’’

Abu Aziz Ibn Umayr hauamini masikio yake pale aliposikia maneno hayo kutoka kwa

ndugu yake baba mmoja mama mmoja ambae ni Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu

na hivyo Abu Aziz Ibn Umayr akamuuliza Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu kwa

kusema: ‘Ewe Kaka yangu maelezo hayo unayoyatoa yaninihusu mimi?’ ambapo

Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu akamjibu kaka yake huyo kwa kumkana huku

akimnyooshea kidole yule Ansari aliempa maelekezo hayo kua: ‘Huyu Ndio Ndugu

yangu, sio wewe’’ na hivyo kuthibitisha kua Katika mapigano baina ya Imani na Kufr

basi Udugu wa Iman ni mkubwa zaidi kuliko udugu wa Kidamu

Ambapo tunapoangalia kuhuiana na watu wa Ahl Al Kitab basi tunaona kua wao walikua

hawaruhusiwi kuchukua Ngawira baada ya Vita, na kwa watu wengine basi hali ilikua

kila mpiganaji anachukua kile anachokipata katika mapigano husika, au ngawira hizo hua

zinachukuliwa na kiongozi wa Jeshi lililoshinda, na hii hupelekea kwa abadhi ya

wapiganaji kuia ngawira hizo au kuzificha kwa ajili ya manufaa yao wenyewe, lakini

kwa upande wa Waislam baada ya tukio hili la vita vya mwanzo ambavyo ni vya Badr

basi wakawa hawajuia pia wafanye nini kuhusiana na ngawira hizo, hivyo wakamuuliza

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam juu yake, ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala

akashusha aya isemayo:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞يَسْأَلُونَكَ‏ عَنِ‏ ٱلأَنْفَالِ‏ قُلِ‏ ٱلأَنفَالُ‏ هللِ َِّ‏ وَ‏ ٱلر َّسُولِ‏

فَٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَأَصْلِحُواْ‏ ذَاتَ‏ بَيْنِكُمْ‏ وَأَطِيعُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَرَسُولَ‏ هُ‏ إِ‏ ن كُنتُم م ُّؤْمِنِينَ‏ ﴾

Biismi Allahi Alrrahmani Alrrahim; Yas-aloonaka AAani al-anfali quli al-anfalu

lillahi waalrrasooli faittaqoo Allaha waaslihoo dhata baynikum waateeAAoo Allaha

warasoolahu in kuntum mu/mineena (Surat Al Anfal 8:1)


808

Tafsir: Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma; Na wanakuuliza

kuhusiana na Ngawira hivyo waambie kua (Maamuzi yake) Ngawira ni kwa ajili ya

Allah na Mtume wake, hivyo Mcheni Allah na suluhisheni yaliyopo baina yenu na

Mtiini Allah na Mtume wake kama nyinyi ni Waumini.

Hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala alipotangazia katika ayah hii ya Surat Al Anfal kua

Ngawira itasimamiwa na Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume wake Salallahu Alayhi

wa Salam basi ilikua inamaanisha kila kinachopatikana kinatakiwa kifikishwe mbele ya

Rasul Allah Salallah Alayhi wa Salam na kisha yeye ndie atakaeamua nini cha kufanya

kutokana nacho kwa kugawa kwa namna inavyostahiki.

Ambapo neno Anfal hua linatokana na neno Nafala ambalo hua linaaminisha Kumpa

Mtu zawadi, Kutoa au kufanya jambo zuri zaidi ya ilivyoamrishwa, Kutoa zawadi bila

ya kuamrishwa yaani kwa hiari, Kutunuku au Kuzawadia, Kutoa au kumpa Mtu au Watu

Ngawira au iliyopatikana vitani

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Kulikua kuna

watu watatu kutoka miongoni mwa Muhajjiruna na watu watano miongoni mwa

Maansari ambao ingawa hawakua ni wenye kupigana kwenye vita vya Badr lakini

walipewa Ngawira, ambao ni:

Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu, kwa saabu ya kua alikua akimsimamia Mke

wake aliekua akiumwa ambae ni Ruqqayah Bint Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam.’

Talha na Sad Ibn Zayd Radhi Allahu Anhum ambaowao walitumwa na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam katika ardhi ya Sham kwa ajili ya kufanya Upelelezi.

Abu Lubabah Ibn Marwan Radhi Allahu Anhu ambae aliachwa katika Mji wa

Madina Na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua ndie Msimamizi Mkuu wa

Mji.

Asim Radhi Allahu Anhu ambae yeye aliachwa asimamie Ulinzi wa maeneo ya Nje

ya mipaka ya Madina.

Harth Ib Hatib Radhi Allahu Anhu ambae yeye alitoka na jeshi la Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam lakini njiani kaambiwa arudi aende akasimamie kitu

Fulani katika mji wa Madina.


809

Harth Ibn Sumh Radhi Allahu Anhu ambae yeye alikua akiumwa njian

alipofikakatika maeneno ya Rawha hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akamwambia bora arudi Madina akapumzike.

Khuwat Ibn Jubayra Radhi Allahu Ahu.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipowapa Masahaba hawa wanane

sehemu ya Ngawira basi kuna baadhi ya Masahaba wakalalamika, na hivyo Allah

Subhanah wa Ta’ala akaishusha ayah hii ya kwanza ya Al Anfal.

Ambapo anasema Imam Abu Yalah kua: ‘Amesema Ans Ibn Malik Radhi Allahu Anhu

kua: ‘Siku moja tulikua tumekaa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na mara

akaw ani mwenye kutabasam sana, hivyo Umar akamuuliza : ‘Hakika Wazazi

wangu watolewe Kafara kwa ajili yako ya Rasul Allah, hivi jee ni kitu gani

kilichokufurahisha?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Kuna waja

wangu wawili walifikishwa mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala ambapo mmoja kati

yao alisema: ‘Ewe Mola wangu mfanye kua awe ni mwenye kunilipa Fidiya mimi

kutokana na makosa aliyonifanyia’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kumwambia yule anaeshtakiwa kua:

‘Mlipe Fidya yake kutokana na yale maovu uliyokuya ukimfanyia’ Hivyo yule

anaeshitakiwa akasema: ‘Ya Allah hakika mimi sina hata Jema moja langu

lililobakia’

Hivyo yule anaeshtaki akasema: ‘Ewe Mola wangu basi mpe sehemu ya Madhambi

yangu’

Hapa macho ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam yakajawa na Machozi kisha

akasema: ‘Hio itakua ni siku mbaya kabisa, siku ambayo watu watakua wanatafuta

watu wa kuwamwagia Mzigo wao wa Madhambi.’

Na kisha baada ya hapo basi Allah Subhanah wa Ta’ala akasema kumwambia yule

mtu anaeshtaki kua: ‘Angalia Juu kwenye Bustani za Peponi’ na Mtu huyo

akaangalia juu kisha akasema: ‘Ewe Mola wangu hakika mimi mashamba ambayo

yamejaa fedha, na Makasri yaliyopambwa Dhahabu na Lulu, hivi jee yamewekwa

kwa ajili ya Mtume gani? Kwa Siddiqina Gani? Kwa Shuhadaa gani?’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala atasema: ‘Hayo yamewekwa kwa ajili ya yeyote

yule atakaelipia kwa Malipo yake,’ ambapo Mtu huyo atasema: ‘Hivi Jee Malipo

yake ni kiasi gani na nani mwenye uwezo nayo?’ Allah Subhanah wa Ta’ala


810

atamwambia Mtu huyo kua: ‘Hata wewe unao uwezo nayo’ hivyo mtu huyo

atauliza: ‘Malipo gani?’

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Msamehe Ndugu yako huyu’ na hapo Mtu

huyo akasema: ‘Ya Allah hakika mimi nimeshamsamehe Ndugu yangu huyu’. Hapo

Allah Subhanah wa Ta’ala akasema: ‘Mshike mkono wake Ndugu yako Uingie nae

Peponi’ kisha Rasul Allah Salallah Alayhi wa Salam akasoma aya ifuatayo:

‏﴿فَٱت َّقُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَأَصْلِحُواْ‏ ذَاتَ‏ بَيْنِكُمْ‏ وَأَطِيعُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ وَرَسُولَهُ‏ إِن كُنتُم م ُّؤْ‏ مِ‏ نِينَ‏ ﴾

Faittaqoo Allaha waaslihoo dhata baynikum waateeAAoo Allaha warasoolahu in

kuntum mu/mineena (Surat Al Anfal 8:1)

Tafsir: Hivyo Mcheni Allah na suluhisheni yaliyopo baina yenu na Mtiini Allah na

Mtume wake kama nyinyi ni Waumini.’’’

Ambapo kwa upande mwengine basi anasema Sad Ibn Abi Waqqas Radhi Allahu Anhu

kua: ‘Ndugu yangu Umayr alikua ni miongoni mwa waliouliwa katika vita vya Badr,

kisha nami nikamuua Said Ibn Al Aas aliemuua Ndugu yangu huyo na kisha

nikachukua Upanga wake, na kisha nikaenda kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam ambae akaniambia kua niuweke Upanga huo pamoja na vitu vyengine

vilivyopatikana kama ngawira, nami nikafanya hivyo lakini sasa Allah Subhanah

wa Ta’ala ni mwenye kujua kuhusiana na yaliyokua yakiendelea akilini mwangu,

hivyo nilipokua nikirudi kuuweka Upanga huo basi Allah Subhanah wa Ta’ala

akaishusha aya hii, na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaniambia kua:

‘Unaweza kua nao Ule Upanga’’ (Imam At Tirmidhi)

Na kwa upande mwengine basi kuhusiana na Ngawira basi Allah Subhanah wa Ta’Ala

alifafanua tena baadae katika Sura hii pale aliposema:

‏﴿وَٱعْلَمُو ۤ ا أَنم ََّا غَنِمْتُمْ‏ مِّن شَيْءٍ‏ فَأَن َّ هللِ َِّ‏ خمُُسَهُ‏ وَلِلر َّسُولِ‏ وَلِذِى ٱلْ‏ قُرْبىَٰ‏ وَٱلْيَتَامَىٰ‏

وَٱلْمَسَاكِينِ‏ وَٱبْنِ‏ ٱلس َّبِيلِ‏ إِن كُنتُمْ‏ آمَنْتُمْ‏ بِٱهلل َِّ‏ وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَى ٰ عَبْدَِ‏ يَوْمَ‏ ٱلْفُرْقَا ‏ِن

ّ كُل شَيْءٍ‏ قَدِيرٌ‏ ﴾

يَوْمَ‏ ٱلْتَقَى ٱلجَْمْعَانِ‏ وَٱهلل َُّ‏ ٰ عَلَى ِ


811

WaiAAlamoo annama ghanimtum min shay-in faanna lillahi khumusahu

walilrrasooli walithee alqurba waalyatama waalmasakeeni waibni alssabeeli in

kuntum amantum biAllahi wama anzalna AAala AAabdina yawma alfurqani

yawma iltaqa aljamAAani waAllahu AAala kulli shay-in qadeerun(Surat Al Anfal

8:41)

Tafsir: Na Jueni kua chechote kile kutokana na Ngawira mtakachopata basi sehemu

moja kati ya 5 hua ni kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala na Mtume wake Salallahu

Alayhi wa Salam na kwa Watu wa Karibu yake Rasul Allah Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, na kwa Mayatima, na kwa Masikini, na Wasafiri, na kama ni wenye

kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala na kile tulichokiteremsha kwenye Qur’an kwa

Mja wetu(Muhamamd Salallahu Alayhi wa Salam) na Siku ya Malipo na siku

yaliyokutana Majeshi ya pande mbili (Badr)Na Allah ni mwenye uwezo juu ya kila

kitu.

Tunaporudi kwenye matukio ya baada ya vita vya Badr basi tunaona kua miogoni mwa

Makafiri waliouliwa katika vita hivi basi watu 17 walikua wanatokea katika ukoo wa

Khalid Ibn Walid wa Banu Makhzum, na katika waliotekwa pia alikuwemo Al Walid Ibn

Walid ambae ni alikua mdogo wake Khalid Ibn Walid.

Baada ya Khalid Ibn Walid kurudi safarini na kusikia yaliyotokea aliamua kushirikiana

na ndugu yake Hisham Ibn Al Walid na Ikrimah katika kupanga majadiliano na Waislam

ya kuwalipia fidya mateka waliokamatwa katika vita hivyo ili waachiwe huru baada ya

kulipwa fidiya hiyo. Waislam walitaka walipwe dirham 4000 ili waweze kumuachia huru

Walid Ibn Al Walid, lakini Hisham alikataa na kuanza kupatana ili ashushiwe kidogo,

hata hivyo Khalid Ibn Walid alimgombeza ndugu yake huyo kwa kuona kua anataka

kuitia aibu familia yao, hivyo wakakubaliana kulipa fidia hiyo hiyo bila ya mapatano.

Baada ya kumlipia Walid Ibn Al Walid fidya, ndugu hao wote watatu waliondoka

Madinah kwa pamoja na kuanza safari ya kurudi Makkah, ulipoingia usiku, wakaamua

kupiga kambi katika eneo linaloitwa Zul Halifa, na ilipofika usiku wa manane Walid Ibn

Al Walid akatoroka na kurudi tena Madinah ambapo alipofika huko alikwenda moja kwa

moja kwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na kusilimu, na huko

akathibitisha Uislamu wake kwa kua karibu sana na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam.

KHALID IBN WALID NA VITA VYA UHUD, KHANDAK NA MUTAA.


812

Mnamo mwaka 625, miaka mitatu baada ya Hijra Waislamu walipigana vita vya pili na

Makafiri, vita ambavyo vilijulikana kama vita vya Uhud. Viliitwa vita vya Uhud kwa

sababu vilipiganwa chini ya mlima wa Uhud uliopo katika umbali wa kilomita tatu

kaskazini mwa mji wa Madinah .

Vita vya Uhud viliandaliwa mashambulizi yake na watu wa Makakh wakiongozwa na

Abu Sufyan kwa ajili ya Kulipiza kisasi juu ya yale yaliyotokea katika Vita Vya Badr na

hivyo Makafiri hao kua na malengo ya Kuumua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na Kuuangamiza Uislam, hususan kutona na kua Waislam walikua bado ni kidogo kiidadi

kwani Waislam walikua na jeshi la watu 700 ukilinganisha na Makafiri ambao walikua

na jeshi la watu 3000.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam aliwapanga baadhi ya wanajeshi wake

chini ya mlima wa Uhud, na kuwaambia vyovyote itakavyokua wasiondoke chini ya

mlima huo, ili kuwalinda Waislam wasije wakapata mashambulizi ya kushtukiza kutoka

nyuma ya mlima huo. Katika vita hivi Khalid Ibn Walid alikuwa akiongoza kikundi cha

wapiganaji wa farasi waliokua katika upande wa Makafiri.

Mapigano yalipoanza na kuendelea ikawa kuna muonekano wa Waislam kushinda, na

Makafiri kushindwa, hata hivyo Khalid Ibn Walid ambae alikua amejitenga na kuangalia

mapigano alijaribu kuwavuta Waislam waliokuwepo chini ya mlima waondoke ili

akiongoze kikundi chake kuwavamia kwa nyuma Waislam lakini ikawa kazi bure, kwani

nao walijibu mapigo kwa kuwarushia mishare ya upinde.

Katikati ya mapigano Makafiri hao walizidiwa nguvu na kuanza kukimbia ovyo, hivyo

Waislam walioambiwa wasiondoke katika sehemu zao, ikabidi waingie tamaa na kuanza

kuwafuata na kufukuzia ngawira za wale Makafiri waliokua wakikimbia. Jambo ambalo

lilisababisha madhara makubwa sana baadae, kwani Khalid Ibn Walid aliekua amekaa na

subra kubwa, aliipata nafasi aliyokuwa akiisubiri kwa muda mrefu na hivyo akaitumia

kwa kukiongoza kikundi chake na kuwapa Waislamu shambulizi la kushtukiza, kwa

kuwatokezea kwa nyuma yao, kuona hivyo wale Makafiri waliokua wakikimbia

wakaamua kugeuka na kuwavamia Waislam, hivyo ikawa Waislamu wamewekwa kati

kati baina ya Makafiri na kuchanganyikiwa kutokana na kuzidiwa nguvu na Makafiri hao

baada ya Hamza Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kupigwa Mkuki na Wahshi na kufariki

Dunia.

Katika Vita hivi Rasul Allah Salallau Alyhi wa Salam alimchagua Musab Ib Umayr Radhi

Allahu Anhu kua ndie Mshika bendera ya Waislam na hivyo kua ni mwenye kuchukua

jukumu la kuwatia ari waislam katika kuongoza mapigano hayo, na hali ilipobadilika ya

mapigano basi Makafiri ikawa wanakimbilia katika sehemu aliyokuwepo Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam ili wamuue, ambapo Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu


813

akagundua juu ya jambo hili na hivyo akazidisha kuinyanyua juu bendera ya Uislam kwa

mkono mmoja huku akitamka ‘Takbir’ na kushambulia maadui zake kwa mkono wake

wa kulia, ambapo mara ghafla mpanda Farasi wa makafiri akamkaribia Muadh Ibn

Umayr Radhi Allahu Anhu na kumpiga upanga na kumkata mkono wake wa kulia,

ambapo kilichofuatia baada ya hapo ilikua ni kusikika sauti ya Musab Ibn Umayr Radhi

Allahu Anhu ikisema:

‏﴿وَمَا محَُم َّدٌ‏ إِلا َّ رَسُولٌ‏ قَدْ‏ خَلَتْ‏ مِنْ‏ قَبْلِهِ‏ ٱلر ُّسُلُ‏ أَفإِنْ‏ م َّاتَ‏ أَوْ‏ قُتِلَ‏ ٱنْقَلَبْتُمْ‏

عَلَى ٰ أَعْقَابِكُمْ‏ ﴾

Wama Muhammadun illa rasoolun qad khalat min qablihi alrrusulu afa-in mata

aw qutila inqalabtum AAala aAAqabikum (Surat Al Imran 3:144)

Tafsir: Na hakua Muhamamd isipokua ni Rasul, na wamekuja kabla yake Mitume

hivyo jee hata kama ikiwa atakufa au atauliwa, mtageuka kutokana na muelekeo wa

visigino vyenu?

Baada ya kusema maneno hayo basi Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu akapigwa tena

upanga kwenye mkono wake wa kushoto hukua akiendelea kutamka maneno haya

ayatamkayo, kisha akapigwa na Mkuki ambao ulimpeleka moja kwa moja kuanguka

chini na hvivyo Bendera ya Uislam kua ni yenye kuanguka chini pamoja nae, na

haukuchukua mda akafariki Dunia.

Ambapo maneno yake hayo aliyokua akiyasema Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu

baada ya kushambuliwa kwake katika vita hivi, basi Allah Subhanah wa Ta’ala

akayashusha kua in sehemu ya aya ya Qur’an ambayo inasema:

‏﴿وَمَا محَُم َّدٌ‏ إِلا َّ رَسُولٌ‏ قَدْ‏ خَلَتْ‏ مِنْ‏ قَبْلِهِ‏ ٱلر ُّسُلُ‏ أَفإِنْ‏ م َّاتَ‏ أَوْ‏ قُ‏ تِلَ‏ ٱنْقَلَبْتُمْ‏

عَلَى ٰ أَعْقَابِكُمْ‏ وَمَن يَنْقَلِبْ‏ عَلَى ٰ عَقِبَيْهِ‏ فَلَنْ‏ يَضُر َّ ٱهلل ََّ‏ شَيْئاً‏ وَسَيَجْزِى ٱهلل َُّ‏

ٱلش َّاكِرِينَ‏ ﴾


814

Wama muhammadun illa rasoolun qad khalat min qablihi alrrusulu afa-in mata aw

qutila inqalabtum AAala aAAqabikum waman yanqalib AAala AAaqibayhi falan

yadurra Allaha shay-an wasayajzee Allahu alshshakireena (Surat Al Imran 3:144)

Tafsir: Na hakua Muhamamd isipokua ni Rasul, na wamekuja kabla yake Mitume

hivyo jee hata kama ikiwa atakufa au atauliwa, mtageuka kutokana na muelekeo wa

visigino vyenu? Na atakaegeuka kutokana na muelekeo wa visigino vyake basi

hatomdhuru Allah Subhanah wa Ta’ala hata kidogo na Allah Subhanah wa Ta’ala

atawalipa wale wenye kuonesha shukurani.

Mapigano yakaendelea na hali ilipokua ngumu zaidi kwa upande wa Waislamu basi

baadhi walikimbilia juu ya mlima wa Uhud, wengine walikimbilia kujificha ili kuokoa

maisha yao na wengine walikimbilia kusiko julikana na kurudi siku mbili baada yake.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alijeruhiwa na kutoka na nyingi kichwani

na kung’oka meno mawili, hivyo mtoto wake, Fatma na Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu

Anhum wakamshughulikia kumpa huduma ya kwanza kwa kumfunga kitambaa kuzuia

damu na mara baadae Abu Bakr As Siddiq na Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhum

wakaungana nao.

Baada ya mapigano hayo Waislam wakakusanyika kwa ajili ya kuokota Maiti wao

waliopata Ushahidi ambao walikua ni watu 70 kwa ajili ya kuzikwa na ingawa miongoni

mwao alikuwemo pia Hamza Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu ambae ni Ami yake Rasul

Allah Salallahu Aalyhi wa Salam lakini hata hivyo, Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam hakusikitikia sana kwani ilikua ni pale alipoiona maiti ya Musab Ibn Umayr Raddi

Allahu Anhu basi ndio machozi yakamtiririka.

Ambapo kila walipokua wakijaribu kumfunika Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu

kwa Sanda yake, basi haikuwezekana kumfunika mwili wake wote kwani wakimfunika

kichwani basi miguu inabakia wazi na kila wakimfunika kichwa basi miguu inabakia

wazi, hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Mfunikeni kwa Sanda

kichwani mwake na miguu yake mfunikeni kwa majani ya idhkir’

Huku akimkumbuka Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu namna alivyokua ni kijana

mtanashaji, mwenye kupendeza kwa kila kitu na kwa kila hali na nama alivyojitolea na

kuachana na yote hayo kwa ajili ya Mola wake na kufikia mwisho wake huku akiwa hata

sanda yake haimtoshi kutokana na Malaika kugombaniana na Waislam namna ya

kumvisha Sanda yake, na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema:


815

‏﴿مِّنَ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ رِجَالٌ‏ صَدَقُواْ‏ مَا عَاهَدُواْ‏ ٱهلل ََّ‏ عَلَيْهِ‏ فَمِنْهُمْ‏ م َّن قَضَى ٰ نحَْبَهُ‏ وَمِنْ‏ هُمْ‏

م َّن يَنتَظِرُ‏ وَمَا بَد َّلُواْ‏ تَبْدِيلاً‏ ﴾

Mina almu/mineena rijalun sadaqoo ma AAahadoo Allaha AAalayhi faminhum

man qada nahbahu waminhum man yantadhiru wama baddaloo tabdeelan (Surat

Al Ahzab 33:23)

Tafsir: Miongoni mwa Waumini kuna watu waliosadikisha juu ya kile walichomuahidi

Allah miongoni mwao wametekeleza majukumu yao na baadhi yao bado wanasubiri

lakini hawajabadilika hata kidogo.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Ewe Musab Ibn Umayr hakika

Rasul Allah anashuhudia kua wewe ni Shahidi mbele ya Allah Subhanah wa Ta’ala

na katika siku ya Malipo’ na kisha akawageukia Waislam na kuwaambia: ‘Enyi

Waislam watembeleeni Mashahidi, Wasalimieni kwani nnapa kwa yule ambae ni

mwenye kuimiliki Roho yangu ndai ya mikono yake kua Muislam yeyote

atakaewatumia salam mashahidi hadi katika siku ya Malipo basi nao

watamrudishia salama hio.’

As-salaamu alaykum, ma'shar ash-shudhadaa. As-salaamu alaykum wa rahmatullah wa

barakatuhu.

Ingawa hivi vilikua ni vita vya mwanzo vikubwa kwa Khalid Ibn Walid kupigana lakini

alifanikiwa kuwapa ushindi mkubwa Makafiri wa Makkah kutokana na uwezo wake wa

kua na subra, kutokukubali kushindwa, na vile vile kutokana na mbinu zake za hali ya

juu. Khalid Ibn Walid alikua ni mtu wa mwanzo katika historia ya Uislam kuuhatarisha

usalama wa Waislam a Uislam kutokana na vita hivi.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anawadhihirishia Waislam kuhusiana na kile

kilichotokea katika vita hivi vya Uhud kwa kusema:


816

‏﴿وَلَقَدْ‏ صَدَقَكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ وَعْدَهُ‏ إِذْ‏ تحَُس ُّونَهُمْ‏ إبِِذْنِهِ‏ حَتى َّ ٰ إِذَا فَشِ‏ لْتُمْ‏ وَتَنَازَعْتُمْ‏ فىِ‏ ٱلأَمْرِ‏

وَعَصَيْتُمْ‏ مِّنْ‏ بَعْدِ‏ مَآ أَرَاكُمْ‏ م َّا تحُِب ُّونَ‏ مِنْكُمْ‏ م َّنْ‏ يُرِيدُ‏ الد ُّنْيَا وَمِنْكُمْ‏ َّمنْ‏ يُرِيدُ‏ ٱلآخِ‏ رََة

ثمُ َّ صَرَفَكُمْ‏ عَنْهُمْ‏ لِيَبْتَلِيَكُمْ‏ وَلَقَدْ‏ عَفَا عَنْكُمْ‏ وَٱهلل َُّ‏ ذُو فَضْلٍ‏ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ ﴾

Walaqad sadaqakumu Allahu waAAdahu idh tahussoonahum bi-ithnihi hatta itha

fashiltum watanazaAAtum fee al-amri waAAasaytum min baAAdi ma arakum ma

tuhibboona minkum man yureedu alddunya waminkum man yureedu al-akhirata

thumma sarafakum AAanhum liyabtaliyakum walaqad AAafa AAankum

waAllahu dhoo fadlin AAala almu/mineena.(Surat Al Imran 3:152)

Tafsir: Na kwa hakika ametimiza Allah ahadi yake pale mlipokuwa mkiwaua

(Maadui zenu) kwa idhini yake; hadi pale mlipopoteza matumaini na ushujaa wenu

baada ya kuvutana kuhusiana na mlioamrishwa na mkaasi baada ya yeye (Allah

Subhah wa Ta’ala) kukuonesheni Ngawira mnayoipenda. Ambapo miongoni mwenu

kuna wenye kutamani Dunia hii na kuna wanaoitamani Akhera, kisha akakufanyeni

nyinyi kua ni wenye kuwakimbia maadui zenu ili apate kukujaribuni, lakini kwa

hakika amekusameheni kwani Allah ni mwenye kupenda kulipa fadhila kwa Waumini.

Ambapo aya inatuwekea wazi kua yote yaliyotekea ni kutokana na Waislam kughafilika

na kutotii amri ya Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam kwa hivyo huo ulikua ni mtihani

mwengine dhidi yao, baada ya kushindwa kujidhibiti dhidi ya tamaa na kukosa

unyenyekevu mbele ya Mola wao na kua niwenye kushindwa katika mtihani wa

kujaribiwa kwao, na kisha Allah Subhnaha wa Ta’ala akaendelea kudhidhirisha kwa

kuwaambia Waislam kua wasifananishe haya yaliyotokea kwenye Vita vya vya Badr na

hivi vya Uhud na yasiwe ni yenye kuwapelekea Waislam kujiuliza imekuaje? Kama

zinavyosema Aya:

‏﴿أَوَ‏ لَم َّا أَصَابَتْكُمْ‏ م ُّصِيبَةٌ‏ قَدْ‏ أَصَبْتُمْ‏ مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ‏ أَنى َّٰ‏ هَٰذَا قُلْ‏ هُوَ‏ مِ‏ نْ‏ عِنْدِ‏

أَنْفُسِ‏ كُمْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ ٰ عَلَى كُ‏ ‏ِل شَ‏ يْ‏ ءٍ‏ قَدِيرٌ۞‏ وَمَآ أَصَابَكُمْ‏ يَوْمَ‏ ٱلْتَقَى ٱلجَْمْعَانِ‏ فَبِإِذْ‏ ‏ِن

ٱهلل َِّ‏ وَلِيَعْلَمَ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ ﴾

ّ


817

Awa lamma asabatkum museebatun qad asabtum mithlayha qultum anna hadha

qul huwa min AAindi anfusikum inna Allaha AAala kulli shay-in qadeerun; Wama

asabakum yawma iltaqa aljamAAani fabi-idhni Allahi waliyaAAlama

almu/mineena (Surat Al- Imran 3:165-166)

Tafsir: (Inakuaje) Wakati mnapofikwa na Msiba mbali ya kua mmewashinda mithili

yenu mara mbili (maadui zenu) basi mnakua mnasema: ‘Imekuaje?’ Waambaie(Ewe

Muhammad): ‘Ni kutokana na Nafsi zenu kwani kwa hakika Allah ni mwenye uwezo

juu ya kila kitu.’ Ama kile kilichokufikieni katika siku yaliyokutana majeshi mawili

(katika Uhud) basi ni kutokana na matakwa ya Allah ili apate kuwajua Waumini.

Na kisha Allah Subhnaha wa Ta’ala akamalizia kwa kusema:

‏﴿إِنْ‏ يمَْسَسْكُمْ‏ قَرْحٌ‏ فَقَدْ‏ مَس َّ ٱلْقَوْمَ‏ قَرْحٌ‏ مِّثْلُهُ‏ وَتِلْكَ‏ ٱلأَ َّمُ‏ نُدَاوِلهَُا بَ‏ ينْ‏ َ ٱلن َّاسِ‏

وَلِيَعْلَمَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ وَيَت َّخِ‏ ذَ‏ مِنْكُمْ‏ شُهَدَآءَ‏ وَٱهلل َُّ‏ لاَ‏ يحُِب ُّ ٱلظ َّالِمِينَ‏ ﴾

In yamsaskum qarhun faqad massa alqawma qarhun mithluhu watilka al-ayyamu

nudawiluha bayna alnnasi waliyaAAlama Allahu alladheena amanoo

wayattakhidha minkum shuhadaa waAllahu la yuhibbu aldhdhalimeena (Surat Al

Imran 3:140)

Tafsir: kama ikiwa karaha imekuguseni (Kwa Majeruhi na Vifo) basi kueni na

uhakika kua karaha imewagusa na wengine pia. Kama inavyokua katika masiku

(mazuri na mabaya) hua tunawapa baina ya watu kwa zamu ili Allah apate kuwajaribu

wale walioamini na apate kuchukua Mashahidi miongoni mwenu na Allah si mwenye

kuwapenda Madhalimu.

Ambapo baada ya vita vya Uhud basi Khalid Ibn Walid na Abu Sufyan walikimbilia na

Farasi wao katika eneo alilokuwepo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kisha Abu

Sufyan akanadia kwa kusema: ‘Jee Yuko wapi Muhammad? Yuko wapi Abu Baqr?

Yuko wapi Umar?’

Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akajibu: ‘Sisi hapa!’ Abu Sufyan akasema:

‘Siku kwa Siku kwani Siku hua zinabadilika, na vita hua ni kama ndoo inayoingia

na kutoka kisimani.’ Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akajibu: ‘Hakika sisi

hatuko sawia kwnai Maiti wetu wako Peponi wakati wenu wako Jahannam’ Abu

Sufyan akasema: ‘Kama ni kweli hivyo msemavyo basi kwa hakika sisi ndio

tulioshindwa.’


818

Miaka miwili baadae vikatokea vita vya tatu baina ya Waislam na Makafir wa Makkah,

vita ambavyo vilijulikana kama vita vya Khandaq, baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kupewa Ushauri na Salman Al Farisi Radhi Allahu Anhu kua wachimbe

kuchimba handaki ili kuulinda wa mji wa Madinah usivamiwe na Makafiri ambao

walikau wamekuja na jeshi kubwa sana, Miongoni mwa Viongozi wa Jeshi la Makafiri

alikuwemo pia Khalid Ibn Walid alikuwemo katika jeshi la Makafiri na ingawa kulikua

na majaribio ya hapa na pale ya kuzidiana akili, lakini vita hivi havikupiganwa kwani

baada ya muda mrefu, Makafiri walishindwa kuliruka Khandaq lililochimbwa na

Waislam.

Ingawa Khalid Ibn Walid alijitahidi kwa mbinu zake zote kama kiongozi wa Jeshi la

Makafiri kutafuta sehemu ya kuanzisha Mashambulio hadi akaipata, kwani alikua ni

miongoni mwa waliomkamia sana Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam hivyo

akafanikiwa kulijua hema la Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na kisha

kuwapanga wapiganaji wake wa kurusha upinde lakini hata hivyo Waislam waliwahi

kuwaona na hivyo wakamtaarifu Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam nae

akawahi kuhama katika hema hilo kabla ya mashambulizi hayo.

Na hatimae mwishoni usiku mmoja kulitokea kimbunga cha jangwani ambacho

hakijawahi kutokea, na hivyo kambi ya Makafiri, ikavunjika baada ya mahema yao

kung’oka na kupeperuka, kamba za Ngamia na Farasi wao kukatika na baadhi ya

wanyama hao kukimbia, vyakula vyao pia viliharibika kwa kujaa mchanga wa jangwani

na hivyo bada ya muda kidogo wakaamua kurudi Makkah bila ya kupigana.

Harith Ibn Hisham, anasema katika Tabqat Ibn Sad kua: ‘Khalid Ibn Walid alisema

kua kabla ya kusilimu, ilikua kila akiingia vitani kupigana na Waislam alikua

anapata nafasi ya kumpiga upanga Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam,

lakini kila inavyotokea nafasi hiyo basi kutokana na ukubwa na utukufu wa Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, hutokea kama miale fulani ya mwangaza

inayong’ara na kuingia katika moyo wa Khalid Ibn Walid’, ambayo baadae iliotesha

mapenzi ya dini ya Uislam ndani ya moyo yake.

Kisa hiki kilitokea wakati Waislam walipokua wakitoka Madina kuelekea Makkah

kufanya Umra, walipofika katika maeneo ya Usfan ambapo ni karibu na mji wa Makkah,

walipiga kambi na hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akawa anasalisha

sala ya adh Dhuhr na wakati huo Khalid Ibn Walid akaona kua ameshapata nafasi

anayoihitaji kwa ajili ya kumuua Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam pamoja

na Waislam wengine, hivyo akakaa na majeshi yake mbele baina ya Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam na Kibla lakini hata hivyo kulikua kuna nguvu fulani ambayo

alikua akiihisi inamzuia bila ya kuiona nguvu hiyo inatokea wapi. Siku hiyo hiyo wakati

wa Sala ya Al Asr, Khalid Ibn Walid anasema akapata nafasi nyengine tena lakini


819

kilitokea kile kile kilichomzuia wakati wa Ad Dhuhr. Na hapo akajua hakuna kitu

kitakachoweza kumzuia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam katika kueneza

Dini ya Uislam.

Imam Ibn Kathir anazungumzia tukio hili pale alipozungumzia Sala ya khofu katika

Taafsir ya Surat An Nisaa kwa kusema kua:

Amesema Imam Ahmad kua amesema Abu `Ayyash Az-Zuraqi, ‘Tulikua pamoja na

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam katika maeneo ya U’sfan, na mara

wakatokea Makafir waliokua chini ya uongozi wa Khalid Ibn Walid, na

wakasimama baina yetu na Qibla, Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam

akatusalisha Salat Dhuhr na hapo Makafiri wakasema: ‘Walikua wameshughulika

na kitu fulani, tulikua na nafasi ya kuwavamia’ lakini baadae wakasema: ‘Itafuata

Sala baadae ambayo inathamani zaid kwao wao kuliko watoto wao na Nafsi zao’’.

Mara Jibril A’layhi Salaam akashuka baina ya Salat Dhuhr na Al Asr na aya isemayo:

‏﴿وَإِذَا كُنتَ‏ فِيهِمْ‏ فَأَقَمْتَ‏ لهَُمُ‏ ٱلص َّلاَةَ‏ فَلْتَقُمْ‏ طَآئِفَةٌ‏ مِّنْهُمْ‏ م َّعَكَ‏ وَلْيَأْ‏ ‏ُخذُو ۤ اْ‏

أَسْلِحَتَهُمْ‏ فَإِذَا سَجَدُواْ‏ فَلْيَكُونُواْ‏ مِن وَرَآئِكُمْ‏ وَلْتَأْتِ‏ طَآئِفَةٌ‏ أُخْرَىٰ‏ لمَْ‏ يُصَل ُّواْ‏

فَلْيُصَل ُّواْ‏ مَعَكَ‏ وَلْيَأْخُذُواْ‏ حِ‏ ذْ‏ رَهُمْ‏ وَأَسْلِحَتَهُ‏ مْ‏ وَد َّ ٱل َّذِينَ‏ كَ‏ فَرُواْ‏ لَْو تَغْفُلُونَ‏ عَ‏ ‏ْن

أَسْلِحَتِكُمْ‏ وَأَمْتِعَتِكُمْ‏ فَيَمِيلُونَ‏ عَلَيْكُمْ‏ م َّيْلَةً‏ وَاحِ‏ دَةً‏ وَلاَ‏ جُنَاحَ‏ عَلَيْكُمْ‏ إِن كَانَ‏

بِكُمْ‏ أَذًى مِّ‏ ن م َّطَرٍ‏ أَوْ‏ كُ‏ نتُمْ‏ ۤ م َّرْضَى أَن ۤ تَضَعُو اْ‏ أَسْ‏ لِحَ‏ تَكُ‏ مْ‏ وَخُ‏ ذُ‏ واْ‏ ‏ِحذْرَكُمْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏

أَعَد َّ لِلْكَافِرِينَ‏ عَذَاابً‏ م ُّهِيناً‏

Wa-idha kunta feehim faaqamta lahumu alssalata faltaqum ta-ifatun minhum

maAAaka walya/khudhoo aslihatahum fa-idha sajadoo falyakoonoo min waraikum

walta/ti ta-ifatun okhra lam yusalloo falyusalloo maAAaka walya/khudhoo

hidhrahum waaslihatahum wadda alladhina kafaroo law taghfuloona AAan

aslihatikum waamtiAAatikum fayameeloona AAalaykum maylatan wahidatan

wala junaha AAalaykum in kana bikum adhan min matarin aw kuntum mardha an

tadaAAoo aslihatakum wakhudhoo hidhrakum inna Allaha aAAadda lilkafireena

AAadhaban muheenan. (Surat An Nisaa 4:102)


820

Tafsir: Na unapokua (Ewe Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam) pamoja nao na

ukawongoza katika Sala, basi liruhusu kundi moja lisali pamoja nawe huku wakiwa

na Silaha zao; na watakapomaliza sijda zao basi wacha wabadilishe nafasi zao na

kukaa nyuma ili kuruhusu wale waliokua hawajasali kuja mbele, na waruhusu wasali

pamoja nawe wakiwa na tahadhari huku wakibeba silaha zao. Kwani wale wasioamini

wanatamani kua nyinyi msahau silaha zenu na mizigo yenu ili wakuvamieni kwa mara

moja. Lakini hakuna dhambi juu yenu ikiwa mtaweka pembeni silaha zenu kutokana

na usumbufu wa mvua au kwa sababu ya maradhi, lakini chukueni tahadhari kwa

Nafsi zenu. Kwa hakika Allah ametayarisha adhabu ifedheheshayo sana kwa

Makafiri.

Hivyo katika pindi hiki ambacho Khalid Ibn Walid alikua akihisi hisia za nguvu za ajabu

ambazo alikua hazioni na wala hajui zilikua zikitokea wapi zilikua ni miongoni mwa

miujiza ya kushuka kwa Malaika Jibril A’layhi Salaam na aya hiyo.

Muda si mrefu kupita baada ya vita vya Khandaq, Khalid Ibn Walid alipokea barua

kutoka Madinah kwa ndugu yake ambae ni Al Walid Ibn Walid, Al Walid alikua

akimpenda sana kaka yake huyo mkubwa na alikua kila mara anamuandikia barua

kumjuulia hali na pia kujua maendeleo ya muelekeo wake katika maisha, lakini katika

barua ya safari hii, Al Walid alimuuliza kaka yake masuala tofauti kabisa. Kwani ndugu

yake alikua anataka kujua, kaka yake atakaa hadi lini katika hali aliyokua nayo ya

kuendelea kutokua Muislam kwa kusema katika barua hiyo:

‘Mara kwa mara Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam anakuulizia,

kutaka kujua uko wapi na unafanya nini? Nami humjibu Insha Allah, Allah

atakuleta kwetu karibuni, na hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

hua anasema ‘Mtu mwenye akili na ujuzi kama Khalid hawezi kukaa kwa mda

mrefu bila ya kujiunga nasi, ikiwa atatumia akili na ujuzi wake huo kwa ajili ya

Uislam, atanufaika zaid, hivyo ni lazima tumpe kipaumbele’

Usiku moja kabla ya kuamua kusilimu, Khalid Ibn Walid alilala na akaota yupo katika

sehemu ndogo iliyokiza na nyembamba inayombana na kumpa dhiki, na kwa mbali

akawa anaona mwangaza, hivyo akawa anajivuta kidogo kidogo kuelekea katika

mwangaza huo, na kila akisogea mbele zaid basi hua anapata unafuu na upana wa sehemu

hiyo huongezeka hadi alipofikia katika mwangaza huo na kujiona yuko katika sehemu

nzuri inayovutia na iliyonawiri na kujisikia raha na huru katika Nafsi yake kuliko pale

alipokua kua mwanzo.

Ingawa Khalid Ibn Walid alikua si mtu mwenye imani kubwa ya dini ya kuabudu

masanamu lakini Allah Subhanahu wa Ta’ala alimuonesha njia iliyonyooka na baada ya


821

mkataba wa Hudaybiyyah, Khalid Ibn Walid akaamua na kuona kua bora aifuate dini ya

Uislam ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam.

MAKUBALIANO YA SULHU AL HUDAYBIYYAH

Mnamo mwaka wa 6 Al Hijra ambao ni sawa na mwaka 628 C.E katika mwezi wa Dhul

Qaidah huu ni mwezi ambao n mmoja kati ya miezi mitukufu ambayo ndani yake

imekatazwa kupigana, hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alilala na kisha

akaota ndoto ambayo ndani yake aliona yeye na wafuasi wake wakiwa wanaingia katika

Mji wa Makkah na kufanya Tawwaf. Hivyo akaona kua hii ni Dalili njema na hivyo bora

kwake yeye kutekeleza azimio hilo.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajaribu kuwaambia baadhi ya watu wa

Makablia ya Madina kua wasafiri nae katika msafara huo lakini hata hivyo wakakataa na

kutoa visingizio, hivyo nae akawakusanya watu wake miongoni mwa Muhajjirina na

Maansari na wengine aliowapata baada ya kukubaliana nae na kuanza safari yao hio bila

ya kuchukua silaha yeyote.

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anawazngumzia wale waliokataa kuungana nae

katika safari yake hio ambao ni watu wa Juhaynah, Banu Bakr, Muzaynah kwa kusema:

‏﴿سَيَقُولُ‏ لَكَ‏ ٱلْمُخَل َّفُونَ‏ مِنَ‏ ٱلأَعْرَابِ‏ شَغَلَتْنَآ أَمْوَالُنَا وَأَهْلُوَ‏ فَٱسْتَغْفِرْ‏ لَنَا

يَقُولُونَ‏ أبَِلْسِ‏ نَتِهِمْ‏ م َّا لَيْسَ‏ فىِ‏ قُلُوهبِِمْ‏ قُلْ‏ فَمَن يمَْلِكُ‏ لَكُمْ‏ مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏ ‏َشيْئاً‏ إِنْ‏ أَرَا ‏َد

بِكُمْ‏ ضَرّاً‏ أَوْ‏ أَرَادَ‏ بِكُمْ‏ نَفْعاً‏ بَلْ‏ كَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ بمَِا تَعْمَلُونَ‏ خَبِيراً‏ ﴾

Sayaqoolu laka almukhallafoona mina al-aAArabi shaghalatna amwaluna

waahloona faistaghfir lana yaqooloona bi-alsinatihim ma laysa fee quloobihim qul

faman yamliku lakum mina Allahi shay-an in arada bikum dharran aw arada

bikum nafAAan bal kana Allahu bima taAAmaloona khabeeran (Surat Al Fat-h

48:11)

Tafsir: Watasema kukuambia wale miongoni mwa Mabedui waliobakia kua: ‘Mali

zetu na familia zetu zimetuzuia, hivyo tuombee Msamaha juu yatu’ wanasema kwa

Ndimi zao kile ambacho hakimo ndani ya Nyoyo zao, hivyo waambie: ‘Hivi jee ni nani

atakaekua na uwezo wa kuingilia kati juu yenu dhidi ya Allah, kama akiamua

kukudhuruni na kukunufaisheni?’ La bali Allah ni mwenye kujua juu ya kila

mnachokifanya.


822

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam Waislam 1400 wakavaa Ihram katika Mji

wa Madina na kufuga safari kuelekea katika Mji wa Makkah huku wakiwa na Ngamia

70 na Kondoo kadhaa waliowatia alama inayoonesha kua ni kwa ajili ya kuchinja,

ambapo ilikua ni kawaida kwa watu wa Quraysh kua ni wenye kuruhusu Mahujaji

kuingia katika Mji wa Makkah kufanya Umra lakini bila ya kubeba Silaha.

Lakini kutokana na wingi wa Mahujaji hao wa Kiislam pamoja na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kutoka katika mji wa Madina basi watu wa Quraysh, wakaingiwa na

khofu na kuamua kutowaruhusu kuingia katika mji wa Makkah, baada ya kumtuma

Khalid Ibn Walid na jeshi la watu 200, kwa ajili ya kuwazuia Waislam hao wasiingie

katika Mji wa Makkah kwa kuwasubiri katika maeneo ya Kurah Al Ghamim.

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipopata habari hio ya kukutana na

makabaliano ya jeshi la Khalid Ibn Walid basi akaamua kushauriana na Masahaba zake

kua kama wapigane na Jeshi la Khalid Ibn Walid ama la? Lakini Abu Baqr Radhi Allah

Anhu akashauri kwa kusema kua: ‘Hakika sisi tulitia nia kufanya Ibada ya Umra na

hatukutia nia ya kupigana kwa hivyo, wacha tuenedelee na safari haina haja ya

kupigana hadi pale tutakapokatzwa kuinga ndani ya Mji wa Makkah.’

Na hivyo Waislam wakakubaliana kubadilisha njia ya msafara wao huo ili kuepuka

mapigano ya aina yeyote baina yao hivyo badala ya kutumia njia ya kawaida ya kupitia

katika maeneo ya Taniim basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaamua kukupitia

njia isiyotumika sana ambayo ni njia ya kupitia katika maeneno ya Hudaybiyyah na hivyo

kutaka kua ni mwenye kuingia katika Mji wa Makkah katika upande wa Magharibi wa

Mji huo.

Hivyo Khalid Ibn Walid alipopata habari hio basi akaamua kurudi katika mji wa Makkah

na Jeshi lake, huku Watu wa Quraysh wakaamua kutuma ujumbe wao kwa Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kwa ajili ya kupanga majadiliano ya makubaliano baina yao,

kabla ya kuingia kwenye Mji wa Makkah, kwenye maeneo ya Hudaybiyyah kwa

kumtuma Urwa Ibn Masud ambae alikua ni mtaalamu mkubwa sana wa Majadiliano ya

kimataifa miongoni mwa Waarabu.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na watu wake walipofika kwenye maeneo hayo

ya Hudaybiyyah akakuta kua visima vya maji vya maeneo hayo vina maji kidogo sana

kiasi ya kua hayatoshelezi kuwanyweseha maji wao na Wanyama wao, hivyo akachukua

upinde wake na kisha akawaambia Masahaba zake wauchomeke kwenye moja kati ya

visima hivyo.

Hivyo Khirash Ibn Ummayah Radhi Allahu Anhu akauchukua Upande huo na kushuka

nao ndani ya moja kati ya Visima hivyo huku Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam


823

akiwa ni mwenye kusoma dua na Khirash Ibn Ummayah Radhi Allahu Anhu akiwa ni

mwenye kuuchomeka Upinde huo kisimani humo na hapo hapo maji yakaanza

kumiminika kwa kufoka kutoka kwenye ukuta wa Kisima hicho ambayo yalijaza kila

kisima na hivyo Waislam wakawa na Maji ya kutosha kabisa kwa ajili yao na Wanyama

wao.

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Watu wa Quraysh wana

bahati mbaya sana, kwani Vita vimewaangamiza wakati kama wangeniachia mimi

bila ya kuniiingilia katika kuwausia watu na watu wakaingia kwenye Uislam basi

wangekua ni wenye kunufaika, kwani kama watu wangenipinga na kunikataa basi

nao wangeweza kupigana nami kutokana na hali yao kinguvu katika kila jambo,

wanafikiria nini hawa watu wa Quraysh? Wa Allahi mimi nitapingana nao kwa ajili

ya Allah hadi nitakapopata Ushindi au nitakapofariki kwa ajili yake’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaamua kumtuma Umar Ibn Al Khattab

Radhi Allahu Anhu kwa ajili ya kuzungumza na watu wa Quraysh, lakini hata hivyo

Umar Ibn Al Khattab akawa na khofu kwani alikua hana mtu wa kumlinda kutokana na

nasaba ya kiukoo, hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamteua Uthman Ibn

Affan Radhi Allahu Anhu ambae alikua na nasaba yeye nguvu kikabila miongoni mwa

watu wa Makkah.

Hivyo Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu akaelekea katika mji wa Makkah na akawa

ni mwenye kufikisha ujumbe wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Waislam

kwa ujumla kua wamekuja kwa ajili ya kufanya Ibada ya Umra. Hivyo watu hao wa

Quraysh wakamruhusu Uthmna Ibn Affan Radhi Allahu Anhu kua yeye afanye ibada hio

kama anataka hata hivyo akakataa na kusema kua hawezi kufanya Ibada hio kabla ya

kufanya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Ambapo jibu hilo la Uthman Ibn Affan

Radhi Allahu Anhu liliwakasirisha sana watu wa Quraysh na wakaamua kumkamata

Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu na kumfunga na hivyo kutokua na njia ya

kurudisha majibu kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam juu ya kile kilichotokea

katika mji wa Makkah.

Tukio hili la kukamatwa na kuzuiwa kwa Uthman Ibn Affan liliwatia wasiwasi Waislam

na hasira kwani walikua hawajui kimemfika kitu gani Uthman Ibn Affan Radhi Allahu

Anhu na hivyo Waislam wakawa wako tayari kupigana kwa ajili kumuokoa Uthman Ibn

Affan Radhi Allahu Anhu kama yuko hai, au kulipiza kisasi kama itakua ameuliwa mbali

ya kua tukio hili lilitokea ndani ya mwezi Mtukufu wa Dhul Qaidah ulioharamishwa

kupigana ndani yake.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akanyoosha mkono wake wa kulia na

kuuweka juu ya mkono wake wa kushoto hukua akisema: ‘Haya ni makubaliano ya


824

Uthman’ na baada ya hapo Masahaba wakaweka mikono yao juu ya Mkono wa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kukubaliana juu ya makubaliano hayo ambayo

Masahaba wote walikubaliana nayo isipokua mmoja tu miongoni mwao ambae alikua ni

Jadd Ibn Qays aliekua ni Mnafiq aliejificha nyuma ya Ngamia katika wakati wa

makubaliano hayo.

Ambapo Allah Subhnah wa Ta’ala anayazungumzia Makubaliano haya ambayo yalikua

yanajulikana pia kua kama Makubaliano ya Walioridhwa na Allah Subhnah wa Ta’ala

Bay’iA Ridhwan kwa kusema:

‏﴿ل َّقَدْ‏ رَضِىَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَنِ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ إِذْ‏ يُبَايِعُونَكَ‏ تحَْتَ‏ ٱلش َّجَرَةِ‏ فَعَلِمَ‏ مَا فىِ‏ قُلُو هبِِمْ‏

فَأنزَلَ‏ ٱلس َّكِينَةَ‏ عَلَيْهِمْ‏ وَأَاثَبَهُمْ‏ فَتْحاً‏ قَرِيباً‏ ﴾

Laqad radhiya Allahu AAani almu/mineena idh yubayiAAoonaka tahta

alshshajarati faAAalima ma fee quloobihim faanzala alsakeenata AAalayhim

waathabahum fat-han qareeban(Surat Al Fat-h 48:18)

Tafsir: Hakika ameridhia Allah juu ya Waumini walipokubaliana nawe (Muhammad

Salallahu Alayhi wa Salam) chini ya Mti, kwani yeye ni mwenye kujua kile kilichomo

ndani ya Nyoyo zao na amewashushia Utulivu juu yao na kuwazawadia wao kwa

ushindi unaokuja karibuni.

Ambapo alisema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Wale waliokubaliana

kwa kutoa Mikono yao katika siku ya Hudayybiyah basi hawatoingia Motoni hata

mmoja’(Imam At Tirmidhi)

Baada ya tukio hilo basi watu wa Quraysh wakatuma Mjumbe kwa Waislam kwa ajili ya

mazungumzo na wakamchagua Urwa Ibn Masud Al Thaqafi ambae alipofika mbele ya

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi akamlaumu kwanza Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kwa kusababisha maangamizo kwa watu wake wa Quraysh, na kusema

kua hakuwa ni mwenye kuona watu anaowaamini miongoni mwa Masahaba, kwani

anaona kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kazungukwa na watu ambao ni woga

na watamkimbia katika wakati wowote watakapotishwa.

Masahaba waliposikia maneno haya basi walijawa na hasira lakini wakajizuia, hadi pale

Urwa aliponyoosha mkono wake na kutaka kuzigusa Ndevu za Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam, ambapo ghafla moja alishutukia mkono wake huko ukipigwa na mpini

wa upanga wa Mughiran Ibn Shubah Radhi Allahu Anhu ambae alikua akionya kwa sauti

yenye hasira isemayo: ‘Kaa mbali na Ndevu za Rasul Allah Salallah Alayhi wa Salam’


825

Hivyo Urwa Ibn Masud baada ya kuzungumza na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

ambae alisema kua wao hawataki chochote isipokua kufanya Ibada ya Umra na kuondoka

bila ya mapigano, lakini kama watu wa Quraysh wanataka kupigana na Waislam basi

yeye yuko yuko tayari pia kwa ajili ya mapigano hivyo Urwa Ibn Masud akaondoka huku

akiwa na hali ya kua ni mwenye kuvutiwa sana na heshima, mapenzi na utiifu wa

Waislam kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kuwaambia watu wa Quraysh

kua: ‘Hakika mimi nimetembelea Kumbi za Wafalme wa Uajemi, Warumi na

Wahabeshi lakini kamwe sikuwahi kuona mfano wa heshima na namna

anavyochukuliwa kiongozi na watu wake kama wafuasi wa Muhammad

wanavyomchukulia Muhammad, wamekuja kwa ajili ya kufanya Ibada hivyo

waacheni tu waingie’ lakini hata hivyo watu hao wa Quraysh waligoma katakata.

Baada ya Urwa Ibn Masud kufikisha ujumbe huo kwa watu wa Quraysh wakamchagua

Hulays ambae alikua ni kiongozi wa Kabila la watu waliokua nje ya Mji wa Makkah

lakini walikua wakishirikiana na watu wa Quraysh katika mambo mbali mbali na Hulays

alipokaribia katika eneo la Hudaybiyah na kuona Wanyama waliotiwa alama maalum

inayoonesha kua ni kwa ajili ya kuchinjwa, basi akarudi katika Mji wa Makkah basi

akawaambia Watu wa Quraysh kua: ‘Haina haja ya kujadiliana au kupigana na mtu

ambae amekuja kwa ajilia ya kufanya Ibada ya Umra’

Lakini hata hivyo watu wa Quraysha wakamwita Hulays kua ni mwoga, ambapo nae

akawaambia watu wa Quraysh kua: ‘Kama mkiamua kupigana nao basi mimi

sitoingiza Jeshi la watu wangu kwa ajili ya kupigana nao pamoja nanyi’ Hivyo watu

wa Kabila la Quraysh wakamuomba msamaha Hulays.

Kisha baadae watu wa Quraysh wakamwachia Uthman Ibn Affan Radi Allahu Anhu huku

wakiwa ni wenye kumtuma pamoja nae Suhayl Ibn Amr Al Thaqafi ambae alikua mahiri

zaid ya Amr Ibn Al Aas na Urwa Ibn Masud katika kujadiliana, hivyo walimchamgua

makusudi kwa ajili ya kujadiliana makubaliano hayo pamoja na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam ambapo baada ya mda wa majadaliano yake na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam basi wakaubaliana katika makubaliano yanayojulikana kama

makubaliano ya Sulh Al Hudaybiyah ambayo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

aliyasema huku akimuamrisha Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu aandike yale

ayasemayo ambayo ni:

‘Bismi Allahi AlrRahmani AlrRahim’

Ambapo Suhayl Ibn Amr Al Thaqafi akapingana na kauli hio kwa kusema: ‘Hakika

mimi simjui huyu Al Rahman ndio Nani, hivyo Bismi Allahi tu inatosha’


826

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaendelea kusema: ‘Kutoka kwa

Muhamamd Rasul Allah’ ambapo Suhayl nae akatabasam kisha akasema: ‘Kama wewe

ni Rasul Allah basi bila ya shaka itakua sisi tumekukosea wewe, hivyo andika jina

Muhammad peke yake.’ Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamwambia

Ali Ibn Ali Talib Radhi Allahu Anhu ayafute maneno yasemayo Rasul Allah, lakini hata

hivyo Ali Ibn Abi Talib akagoma, na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akafuta

maneno hayo yeye mwenyewe kisha akaendelea kusema:

Bismi Allahi’

‘Haya ni makubaliano ya Sulhu baina ya Muhammad Ibn Abdullah na Suhayl Ibn

Amr ambae ni Mjumbe kutoka katika Mji wa Makkah.

1-Kutakua na kuweka silaha chini na kutosababishiana madhara baina ya pande

mbili na hakutokua na vita kwa mda wa miaka 10 inayofuata’

2-Mtu yeyote yule au Kabila lolote lile litakalotaka kujiunga na Muhammad au

kuingia katika makubaliano nae basi atakua huru kufanya hivyo, na vile vile mtu

yeyote au kabila lolote litakalotaka kujiunga na watu wa Quraysh au kushirikiana

nao basi wako huru pia kufanya hivyo.

3-Kama ikitokea kua Mtu yeyote yule wa Makkah ataebda katika Mji wa Madina

basi Waislam watamrudisha mtu huyo katika Mji wa Makkah, lakini kama

Muislam kutoka katika Mji wa Madina ataenda katika Mji wa Makkah basi

hatorudishwa.

4-Kama kijana yeyote yule ambae Baba yake yuko hai, akatoka na kuenda kwa

Muhammad bila ya idhini ya Baba yake au Msimamizi wake, basi Kijana huyo

atarudishwa kwa Baba yake au Msimamizi wake, lakini kijana yeyote atakaenda

kwa watu wa Quraysh wa Makkah basi hatorudishwa.

5-Katika mwaka huu Waislam watarudi katika mji wa Madina bila y akuingia

kwenye mji wa Makkah, lakini katika mwaka utakofuatia basi Muhamamd na

wafuasi wake wataingia katika Mji wa Makkah na kutumia sikua 3 kwa ajili ya

kufanya Ibada ya Umra.

Naam hayo ndio makubaliano ya Sulhu Al Hudaybiyah ambayo ingawa kwa upande

mmoja yanaoneana kua kama ni yenye kupendelea kusimamia maslahi ya upande wa

watu wa Quraysh zaidi kuliko maslahi ya Waislam na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kua ni mwenye kuonesha Subra na Ustahmilivu katika kukubaliana na namna

ilivyotakiwa iwe na Suhayl Ibn Amr kiasi ya kua Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu


827

Anhu alikua ni miongoni mwa wasiovutiwa na kutoridhika na Makubaliano hayo hivyo

akamfuata Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kumwambia: ‘Ya Rasul Allah!

Hivi jee wewe si Rasul Allah wa Haki?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu : ‘Naam, bila ya shaka mimi ni Rasul

Allah wa Haki’ Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Hivi jee sisi hatuko

katika njia Sahih na Makafiri wako kwenye njia ya Batil?’ Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akajibu : ‘Naam.’

Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Sasa kama ni hivyo Jee ni kwanini

sisi inatubidi tukubaliane na makubaliano ambayo yanapingana na Imani yetu?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu : ‘Hakika mimi ni Rasul Allah, na

hivyo siwezi kuenda kinyume na maamrisho yake kwani yeye ndie nnaemtegemea

na ndie anaenisaidia’

Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Hivi jee hukuambia sisi kua tunakuja

kwa ajili ya kufanya Ibada ya Umra?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu :

‘Naam, ndio lakini hivi jee mimi nilisema kua tutaifanya Ibada hio ndani ya mwaka

huu?’

Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Bila ya shaka hukusema hivyo’ hivo

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu : ‘Basi bila ya shaka mtakuja tena na

kufanya Ibada ya Umra’ ambapo jibu hili pia halikumfurahisha Umar Ibn Al Khattab

Radhi Allahu Anhu na hivyo akaelekea kwa Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu na

kumwambia kuhusiana na mahojiano yake na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

ambapo Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu akajibu: ‘Hakika yeye ni Rasul Allah,

hivyo hawezi kumuasi Mola wake’ ambapo miaka baadae Umar Ibn Al Khattab Radhi

Allahu Anhu akaona manufaa yaliyomo ndani ya Makubaliano hayo kwa Waislam, na

hivyo akafunga, akatoa sadaka na kuachia Watumwa huru kwa ajili ya kujuta na kuomba

msahama kwa Allah Subhaah wa Ta’ala kutokana na mmajadiliano yake haya dhidi ya

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Lakini kwa upande mwengine makubaliano haya yalikua ni yenye manufaa makubwa

zaidi kwa Waislam kuliko vile walivyokua wakifikiria Waislam wenyewe.

Kwani kwanza Makubaliano haya yalikua yanabainisha wazi kukubalika kwa

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kua ndio Kiongozi wa watu wa Madina na

Taifa jipya la Kiislam kwa Ujumla mbele ya watu wa Quraysh ambao walikua

hawataki kumkubali Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kutokana na chuki zao

juu yake.


828

Pili Makubaliano haya pia yalikua ni yenye kuhakikisha na kusimamia usalama wa

Waislam kutokana na madhara ya watu wa Quraysh.

Tatu Makubaliano haya yalikua yanawapa fursa Waislam kuungana na Makabila

mengineyo bila ya kua na uadui baina yao na watu wa Quraysh.

Nne Makubaliano haya yalikua yanawaahidi Waislam miaka 10 ya usalama na

kutosababishiana madhara kutoka kwa maadui zao wakubwa yaani watu wa

Quraysh na hivyo kufungua njia mpya ya kueneza ujumbe wa Kiislam katika

maeneo mbali mbali ya Uarabuni bila ya kubughudhiwa na kupata upinzani kutoka

kwa watu wa Quraysh.

Ambapo baada ya Suhayl Ibn Amr Ath Thaqafi kupitia upya makubaliano hayo na kisha

kutia saini, basi na kwa upande wa Waislam nao wakatia saini kwa kuanza na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam, Abu Bakr Radhi Allahu Anhu, `Umar Radhi Allahu Anhu, `Abd

Al Rahman Ibn `Awf Radhi Allahu Anhu,`Abdullah Ibn Suhayl Radhi Allahu Anhu, Sa`d Ibn

Abi Waqqas Radhi Allahu Anhu na muandishi mwenyewe Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu

Anhu.

Na baada ya kuwekwa saini hizo basi hapo hapo akatokea kijana Muislam ambae alikua

amefungwa minyororo na kuonekana kua kama ametoroka hivyo alikua akiomba msaada

kwa Waislam afunguliwe, na Suhayl Ibn Amr alipomuangalia kijana huyo basi akamuona

kua ni mtoto wake mwenyewe aitwae Abu Jandal Radhi Allahu Anhu, ambae alikua

amemfungia nyumbani kwake hivyo hapo hapo Suhayl Ibn Amr akasema: ‘Katika huu

Mkataba kuna kipengele nambari 4, na kulingana nacho basi kinasema kua

mumrudishe huyu mtoto kwangu mie’

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kwa kumliwaza Abu Jandal

Radhi Allahu Anhu kua : ‘Nasikitika kua ndio kwanza tumemaliza kukubaliana

makubaliano baina yetu na watu wa Quraysh, na hivyo ni wajibu wetu

kuyaheshimu makubaliano haya, hivyo kua na Subra kwa kukubaliana na

Majaaliwa ya Allah Subhana wa Ta’ala, atakujaaalia njia ya kutokea kwa wepesi’

Hivyo Abu Jandal akakabidhiwa kwa Baba yake, na baadae akatoroka tena kutoka katika

Mji wa Makkah na kukimbilia mafichoni katika maeneo ya mwambao wa Bahari

Nyekundu, ambako walikimbilia wengi miongoni mwa Waislam, na wakawa

wanaivamia Misafara ya watu wa Quraysh ipitayo katika meneo hayo, hivyo baadae watu

wa Quraysh wakaomba kua kipengele hicho kifutwe ili Waislam hao wasiihatarishe

misafara ya Quraysh na hivyo bora wakaishi katika mji wa Madina. Na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akamuandikia barua kiongozi wa Waislam hao katika

maeneno hayo aitwae Abu Basir Radhi Allahu Anhu.


829

Ambae nae pia alikua ni miongoni mwa waliokimbilia katika Mji wa Madina baada ya

kutoroka katika Mji wa Makkah, na alipofika katika Mji wa Madina basi wakatokea

Makafiri wawili ambao wakaomba kua arudishwe kwao kama ilivyokua katika

makubaliano ya Mkataba wa Hudaybiyyah, hivyo Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa

Salam akamkabidhi Abu Basir Radhi Allahu Anhu kwa Makafiri hao, na walipoondoka

basi njiani Abu Basir Radhi Allahu Anhu akapigana nao Makafiri hao na akamuua mmoja

wao na mwengine akakimbia.

Hivyo Abu Basir Radhi Allahu Anhu akarudi tena katika Mji wa Madina kwa Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na kumwambia: ‘Ya Rasul Allah bila ya shaka umetekeleza

kipengele cha Makubalaino ya mkataba wa Hudaybiyyah kwa upande wako na

kunirudisha mimi kwa watu wa Makkah, lakini kwa upande wangu mie basi Allah

Subhanah wa Ta’ala amenipatia uhuru wangu.’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Ole wake mama yake Abu

Musar, hata kama angekua na mtu mwengine pamoja nae’, haya yalikua ni maneno

yanayomaanihsa kua hata kama Abu Basir Radhi Allahu Anhu angekua na mtu mwegine

wa pili alietoroka pamoja nae basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam asingevunja

makubaliano ya Mkataba huo, kwani angewarudisha tu kwa watu wa Makkah.

Hivyo Abu Basir Radhi Allahu Anhu akafaham maana ya maneno hayo na hapo hapo

akaona bora aondoke kutoka kwenye Mji wa Madina na kukimbilia kwenye mwambao

wa Bahari nyekundu ambako alikaa na kuwaongoza Waislam wengine vijana wenzake

hadi pale alipopata barua ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua wanaruhusika

kurudi katika Mji wa Madina ambayo aliifurahia mbali ya kua alikua taabani anaumwa

na kukaribia kifo chake, na akafariki Dunia, hivyo Abu Jandal Radhi Allahu Anhu na

Masahaba wengine 70 wakahama katika maeneo hayo na kuelekea katika Mji wa Madina

na kuungana na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae alipopata habari ya kifo

cha Abu Basir Radhi Allahu Anhu basi akamsalia na kumuombea dua.

Baada ya Makubaliano haya ya Hudaybiyyah basi Waislam walikua wamevunjika Moyo

kutokana na makubaliano hayo na yaliyotokea kwa Abu Jandal Radhi Allahu Anhu na

kutoruhusiwa kufanya Ibada ya Umrah kwa mwaka huo kiasi ya kua baada ya Rasul

Allah Salallahu A’layhi wa Salam kusaini Mkataba wa Hudaybiyyah, alisema kuwaambia

Masahaba zake ‘Nyanyukeni, mchinje wanyama wenu na kisha mnyoe nywele zenu’,

lakini hakuna hata Sahaba mmoja alienyanyua mguu wake kufanya vile alivyoamrisha

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, kutokana na kuvunjika moyo kwa yale

yaliyotokea katika makubaliano ya mkataba huo.

Hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akanyanyuka na kuenda kwa

Ummu Salama Radhi Allahu Anha na kumwambia yaliyotokea na hapo Ummu


830

Salama Radhi Allahu Anha akamwambia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam ‘Ya Rasul Allah, unataka maneno yako yafanyiwe kazi? Basi nenda nje na

usizungumze na mtu yeyote hadi pale utakapomaliza kuchinja mnyama wako na

kunyoa nywele zako’, hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akatoka

nje akachinja mnyama wake na kuanza kunyoa nywele zake, na baada ya

Masahaba kumuona Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam anafanya hivyo

basi na wao wakanyanyuka na kufanya kama vile alivyokua akifanya. (Imam

Bukhari)

Hivyo baada ya makubaliano hayo ya Hudaybiyyah basi Waislam walikaa katika eneo

hilo la Hudaybiyyah kwa mda wa siku 10 na kisha wakaanza safari yao kurudi katika Mji

wa Madina na walipofika kwenye maeneo ya Usfan wakaishiwa na vyakula vyao, hivyo

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaamrisha kua Vyakula vyao Waislam vyote

vikusanywe pamoja na kisha vilipokusanywa basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam akaviombea Dua vyakula hivyo kidogo vilivyobakia na kisha akaamrisha kua

Waislam wale vyakula hivyo na walipokua kila mtu akala hadi akashiba na chakula

chengine kikabakia na kutosheleza kwa ajili ya kumalizia safari yao.

Kisha wakalala katika eneo hilo na asubuhi yake msafara ukaendelea na safari yake, na

ni katika wakati huu ndio Allah Subhnah wa Ta’ala akashusha aya za Surat Al Fat-h

zisemazo:

‏﴿بِ‏ سْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ‏ ۞ إِ َّ فَتَحْنَا لَكَ‏ فَتْحاً‏ م ُّبِيناً۞‏ لِّ‏ يَغْفِرَ‏ لَكَ‏ ٱهلل َُّ‏ مَا

تَقَد َّمَ‏ مِن ذَنبِكَ‏ وَمَا أتََخ َّرَ‏ وَيُتِم َّ نِعْمَتَهُ‏ عَلَيْكَ‏ وَيَهْدِيَكَ‏ صِرَاطاً‏ م ُّ سْتَقِيماً‏ ۞

وَيَنصُرَكَ‏ ٱهلل َُّ‏ نَصْراً‏ عَزِيزاً‏ ﴾

Bismi Allahi Alrrahmani Alrrahim; Inna fatahna laka fat-han mubeenan;

Liyaghfira laka Allahu ma taqaddama min dhanbika wama taakhkhara

wayutimma niAAmatahu AAalayka wayahdiyaka siratan mustaqeeman;

Wayansuraka Allahu nasran AAazeezan (Surat Al Fat-h 48:1-4)

Tafsir: Kwa Jina la Allah Mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma: Hakika tumekupa

wewe (Muhamamd Salallahu Alayhi wa Salam) Ushindi uliowazi. Atakusamehe juu

yako Allah yaliyotangulia katika Madhambi yako na Yatakayokuja Na

amemkukamilishia Neema zake juu yako na kukuongoza wewe kwenye njia

iliyonyooka; Na atakunusuru Allah kwa nusura iliyotukufu.


831

Ambapo baada ya kushushwa kwa aya hii basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akasema: ‘Kuna aya nimeshushiwa ambayo ni yenye thamani kubwa kwangu kuliko

Dunia na kila kitu kilichomo ndani yake’ na kisha akaisoma aya hii ya kwanza ya

Surat Al Fat-h.

Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu akauliza: ‘Hivi jee ni ushindi gani?’ ambapo

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam: ‘Naam, Wa Allahi Ni ushindi mkubwa sana’

hivyo hapa ndio Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu ndio akaridhika Nafsi yake.

Na mmoja kati ya Masahaba akasema: ‘Nakuombea Ya Rasul Allah kuwe na manufaa

nawe, kwani Allah amezungumzia kuhusiana nawe, lakini jee amesemaje kuhusiana

nasi?’ hivyo Allah Subhanah wa Ta’ala akashusha aya zisemayo:

‏﴿هُوَ‏ ٱل َّذِي ۤ أَنزَلَ‏ ٱلس َّكِينَةَ‏ فىِ‏ قُلُوبِ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ لِيَزْدَادُو ۤ اْ‏ إِيمَ‏ اً‏ م َّعَ‏ إِيمَاِِمْ‏ وَ‏ هللِ َِّ‏ جُنُودُ‏

ٱلس َّمَاوَاتِ‏ وَٱلأَرْضِ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلِيماً‏ حَكِيماً‏ ۞ لِّيُدْخِ‏ لَ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ وَٱلْمُ‏ ؤْمِنَاتِ‏

جَن َّاتٍ‏ تجَْرِى مِن تحَْتِهَا ٱلأَنْهَارُ‏ خَالِدِينَ‏ فِيهَا وَيُكَفِّرَ‏ عَنْهُمْ‏ سَيِّئَاهتِِمْ‏ وَكَانَ‏ ذٰ‏ لِكَ‏

عِندَ‏ ٱهلل َِّ‏ فَوْزاً‏ عَظِيماً‏ ﴾

Huwa alladhee anzala alssakeenata fee quloobi almu/mineena liyazdadoo eemanan

maAAa eemanihim walillahi junoodu alssamawati waal-ardhi wakana Allahu

AAaleeman hakeeman; Liyudkhila almu/mineena waalmu/minati jannatin tajree

min tahtiha al-anharu khalideena feeha wayukaffira AAanhum sayyi-atihim

wakana dhalika AAinda Allahi fawzan AAadheeman(Surat Al Fat-h 48:5-6)

Tafsir:Yeye (Allah Subhanah wa Ta’ala) ndie ambae ni mwenye kushusha utulivu

ndani ya Nyoyo za Waumini kuwazidishia Imani kutokana na Imani waliyokua nayo,

na kwake yeye Allah ndiko kwenye Majeshi ya Mbiguni na Ardhini na kwa hakika

Allah ni mwenye kujua juu ya kila kitu na ni mwingi wa Hikma. Atawaingiza Waumini

wa Kiume na Waumini wa Kike Peponi ambako chini yake kuna Mito watakamoishi

ndani yake milele na kuwasamehe juu yao Dhambi zao na kwa hilo mbele ya Allah

kuna malipo Makubwa.

Ambao Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu alikua akipenda kusema kuwaambia

Masahaba wenzake kua: ‘Nyinyi Mlikua mkifikiria kua Fat-han Mubina ni Ushindi

wa ufunguzi wa Mji wa Makkah, ambao ndio bila ya shaka ulikua ni ushindi lakini

sisi tulikua tukihesabu Sulhu Hudaybiyyah kua ndio Ushindi’


832

Tunapoangalia kwa upande mwengine basi tunaona kua Makubaliano ya Hudaybiyyah

basi tunaona kua ni Ushindi Mkubwa sana kwa sababu ilikua baada ya Makubalaino haya

ndio wakasilimua wengi miongoni mwa watu wakubwa wa Mji wa Makkah akiwemo Al

Abbas Ibn Abdul Muttalib Radhi Allahu Anhu, Abu Sufyan Radhi Allahu Anhu, Amr Ibn

Al Aas Radhi Allahu Anhu,Ikrimah Ibn Abi Jahal Radhi Allahu Anhu, Utba Ibn Abi

Lahab Radhi Allahu Anhu, Safwan Ibn Umayyah Radhi Allahu Anhu, Kaab Ibn Zuhayr

Radhi Allahu Anhu, Suhayl Ibn Amr Radhi Allahu Anhu, Hakim Ibn Hizam Radhi Allahu

Anhu, Wahshi Radhi Allahu Anhu, Uthman Ibn Talha Radhi Allahu Anhu. Hind Bint

Rabia Radhi Allahu Anha, Sayfu Allah Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu n.k

KUSILIMU KWA KHALID IBN WALID.

Anasema kabla ya kusilimu kwake kua: ‘Wakati Allah Subhanahu wa Ta’ala

aliponitakia mema kwangu mie, alinivisha mapenzi ya dini ya Kiislam ndani ya

moyo wangu. Akilini ikanijia nami nikasema: ‘Nimeshuhudia mapigano yote dhidi

ya Muhammad, na katika kila mapigano niliyoyashuhudia, nilijishuhudia

kuondoka kwenye mapigano hayo huku nikiamini kua nipo katika upande sio wa

mapigano na hakika Muhammad atakua ni miongoni mwa wenye ushindi’.

Hivyo akaamua kuwafuata marafiki zake ambao waliokua bado hawajasilimu akiwemo

Ikrimah Ibn Abi Hisham na kuwaambia: ‘Ni jambo lililo dhahir kua kutokana Bani

Adam mwenye ufahamu mzuri kujua kua Muhammad si mtunga mashairi wala si

mchawi, kama wanavyosema Maquraish, kweli ujumbe wake unatoka kwa Allah,

hivyo ni lazima kwa kila mtu mwenye akili timamu kumfuata’.

Ikrimah Ibn Abi Hisham alishangazwa na kauli hiyo na kumuuliza Khalid Ibn Walid ‘Ina

maana unaachana na imani yetu?’

Khalid Ibn Walid akajibu ‘Naam, nimeshaanza kumuamini Mungu wa kweli’

Ikrimah Ibn Abi Hisham akasema ‘Inashangaza kuona kua katika Maquraish wote

waliopo, kua wewe uwe ndie wa kusema hivyo’

Khalid Ibn Walid akauliza ‘Kwa nini?’

Ikrimah Ibn Abi Hisham akajibu: ‘Kwa sababu kuna jamaa zako wengi wapendwa

waliouliwa vitani na Waislam, kuliko jamaa wa Quraysh yeyote yule miongoni

mwetu, mimi kwa hakika sitozungumza nawe wala sitoikubali dini ya Muhammad

hadi pale utakapoyakana mawazo yako hayo, huoni kua Maquraysh wanaitaka

damu ya Muhammad?’

Khalid Ibn Walid akajibu, ‘Wanaitaka damu hiyo kwa sababu inayotokana na ujinga

wao wa kutofahamu’.


833

Abu Sufyan ambae alikua ndie kiongozi wa Quraysh wakati huo aliposikia kua Khalid

Ibn Walid anataka kusilimu, akawaita wote Ikrimah Ibn Abi Hisham na Khalid Ibn

Walid, kisha akamuuliza Khalid Ibn Walid, ‘Jee ni kweli yale ninayoyasikia?’

Khalid Ibn Walid akamuuliza ‘Na umesikia nini?’

Abu Sufyan akajibu ‘Nimesikia kua unataka kujiunga na Muhammad’

Khalid Ibn Walid akajibu ‘Na kwa nini nisijiunge nae wakati yeye Muhammad ni

ndugu yetu na ametoka katika ukoo wetu?’

Abu Sufyan akakasirika na kutaka kumtishia Khalid Ibn Walid, lakini Ikrimah Ibn Abi

Hisham akaingilia kati na kusema ‘Pole pole, Ya Abu Sufyan, kwani hasira zako

zitanifanya na mimi nimfuate Muhammad, Khalid yuko huru kufuata dini

anayoitaka.’

Ikrimah Ibn Abi Hisham ambae ni binamu wa Khalid Ibn Walid na pia rafiki yake kipenzi

alisimama na kumtetea ndugu yake, ingawa walikua wana utofauti wa iman, hivyo Khalid

Ibn Walid akaondoka na kumuacha rafiki yake huyo na kuanza safari ya Madinah ,

kuingia katika Uislam na pia kua pamoja na ndugu yake, Al Walid na vile vile kua pamoja

na binamu yake, rafiki na mpinzani wake pia ambae ni Umar Ibn Al Khattab Radhi

Allahu Anhu, lakini safari hii mpinzani wake huyo alikua yuko juu zaid na katika sehemu

bora zaid kwani Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu alikua ni Muislam wa arubaini

kusilimu, wakati Khalid Ibn Walid alisilimu baada ya mamia ya Makafir kusilimu.

Tarehe 31-5-629, Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu akiwa na umri wa miaka 43

aliwasili katika mji Madinah akiwa pamoja na Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu Anhu na

Uthman Ibn Talha Radhi Allahu Anhu.ambao alikutana nao njiani wote wakielekea

Madinah wakiwa na nia ya kuingia katika Uislamu. Walipofika Madina kwa Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, Khalid Ibn Walid akawa wa kwanza kati yao

kuingia katika nyumba ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na kusilimu

akifuatiwa na Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu A’nhu na Uthman Ibn Talha Radhi Allahu

A’nhu.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alipowaona tu na kusikia kua wamekuja

kusilimu akawaambia Masahaba zake ‘Makkah imekurushieni vipande vya Moyo

wake’, hii ni kuonesha thamani aliyokua nayo Khalid Ibn Walid pamoja na wenzake

wawili hao. Baada ya kuingia ndani Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

akamwambia Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu huku akitabasamu ‘Nilikua na

uhakika kua kutokana na ufahamu wako, ujuzi wako na uwezo wako wa kuona

mbali, kua iko siku utakuja kujiunga pamoja nami’. Baada ya kutoa shahada, Khalid

Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu alimwambia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam ‘Ya Rasul Allah, niombee msamaha kwa Allah kwani mimi nimewauwa

Waislamu wengi sana kabla ya kua Muislam’.


834

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akamjibu kwa kumwambia ‘Unapoingia

katika Uislam basi dhambi zako zote ulizozifanya wakati wa Ujahiliyah hua

zimefutika’, ingawa kauli hiyo inatoka kwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam na hivyo usahihi wake huweza kumsadikisha mtu yeyote yule lakini hata hivyo

Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu hakuamini kua dhambi zake kubwa alizozifanya

zilikua zimefutika, hivyo akamshikilia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na

kumuomba mara tatu kua amuombee msamaha kwa Allah Subhanah wa Ta’ala,

mwishoni Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akamuombea, na hapo ndipo

moyo wa Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu ukapata utulivu.

Anasema Amr Ibn Al Aas Radhi Allahu A’nhu : ‘Rasul Allah Salallahu A’layhi wa

Salam hakuwa akiwachukulia Masahaba zake kama vile alivyokua akituchukulia

mimi na Khalid Ibn Walid baada ya kusilim kwetu.’(Mustadrak al Hakim, Al-Musnad

ya Abu Ya’la na Majma’ al-Zawaa’id ya Imam Al-Haythami)

Baada ya Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu kusilim na kuhamia katika mji wa

Madinah , akawa ni mwenye kumtembelea Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam mara kwa mara jambo ambalo lilimuongezea sifa nyengine badala ya ile

anayosifika nayo kimaumbile kama tutakavyoona hapo baadae, sifa aliyojiongezea hapa

ni ile ya kupokea baadhi ya Hadith na hivyo kujiongezea I’lm ya dini, na miongoni mwa

Hadith zake zinazofundisha kuhusiana na dini ya Kiislam ni pamoja na ile isemayo:-

Anasema Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu kua, ‘Siku moja alikuja Bedui kwa

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na kumwambia:

‘Ya Rasul Allah! Nimekuja kukuuliza maswali kidogo kuhusiana na mambo ya

maisha ya kidunia na kiakhera’’,

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu kwa kumwambia Bedui huyo,

‘Uliza unachotaka’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili niwe miongoni mwa wenye I’lm sana?’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Muogope Allah Subhanahu

wa Ta’ala na utakua ni miongoni mwa wenye I’lm sana’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili niwe miongoni mwa watu matajiri Duniani?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Kinai, na utakua ni miongoni

mwa watu matajiri sana Duniani’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili niwe muadilifu?’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Watakie wenzako kile

unachokitaka wewe, na utakua muadilifu kuliko wote’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili miongoni mwa walio bora?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Wafanyie wema wenzako na

utakua miongoni mwa walio bora’.


835

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili nipendelewe na Allah?’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Mtukuze sana Allah na utakua

ni mwenye kupendelewa na Allah’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili nikamilishe Dini yangu?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukiwa na tabia nzuri utakua

umekamilisha dini yako’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili niwe miongoni mwa wafanyo mema?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Mpende sana Allah kama vile

unaemuona, na kama humuoni basi yeye anakuona, kutokana na kufanya jambo

hilo basi utakua ni miongoni mwa wenye kufanya mema’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili niwe mtiifu kwa Allah?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukitii amri za Allah utakua

Mtiifu’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili niwe msafi asiekua na Dhambi?’ .

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Jikoshe na kila lililochafu na

utakua msafi usiekua na Dhambi’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili nifufuliwe na nuru katika siku ya Malipo?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Usiwadhulumu viumbe

wengine na wala usijidhulumu Nafsi yako, na utafufuliwa na nuru katika siku ya

Malipo’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili nipate Rehma za Allah siku ya Malipo?’ .

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukiwa na Rehma juu ya

viumbe wenzako, basi na Allah atakurehemu katika siku ya Malipo’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili dhambi zangu ziwe kidogo?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukifanya Istighfar kadri

uwezavyo basi Dhambi zako zitakua ni kidogo sana’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili niwe miongoni mwa mwenye heshima sana?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukiwa hutomlalamikia

kiumbe yeyote yule basi utakua ni mwenye heshima sana’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili niwe ni mwenye nguvu?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukimtegemea Allah utakua ni

miongoni mwa wenye nguvu kabisa’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili niongeze rizki yangu?’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukiwa na moyo msafi, basi

Allah atakuongezea rizki yako’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili nipendwe na Allah na Mtume wake?’ .

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukikipenda kile

anachokipenda Allah na Mtume wake, utakua ni miongoni mwa wanaopendwa

nao’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili niepuke adhabu za siku ya Malipo?’.


836

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukiwa si mwenye hasira dhidi

ya viumbe wenzako, utaokoka na adhabu za Allah iku ya Malipo’. Bedui akauliza:

‘Nifanye nini ili dua zangu zikubaliwe?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukiwacha mambo maovu, basi

dua zako zitakubaliwa’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili Allah asiniadhirishe siku ya Malipo?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukiulinda usafi na utukufu

wako, basi Allah hatokuadhirisha katika siku ya Malipo’.

Bedui akauliza: ‘Nifanye nini ili Allah anihifadhi siku ya Malipo?’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukiyahifadhi makosa ya

viumbe wenzako, basi na Allah atakuhifadhi siku ya malipo’.

Bedui akauliza: ‘Ni nini kitakachoniokoa na madhambi?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Machozi, Unyenyekevu na

Maradhi’.

Bedui akauliza: ‘Ni jambo gani bora zaid mbele ya Allah?’

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Ukarimu, Haya na Subra’.

Bedui akauliza: ‘Ni jambo gani baya zaid mbele ya Allah?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Hasira na Ubakhili’.

Bedui akauliza: ‘Ni kitu gani kinachopunguza adhabu za Allah hapa Duniani na

kesho Akhera?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Sadaka iliyojificha na

ukarimu kwa jamaa zako’.

Bedui akauliza: ‘Ni kitu gani kitakachozima moto wa Jahannam siku ya Malipo?’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu: ‘Subra wakati wa Fitna na

Mitihani’.(Musnad Imam Ahmad Ibn Hanbal)

SAYFU ALLAH KHALID IBN WALID RADHI ALLAHU ANHU NA VITA

VYA MUTAH

Kwa muda wa miezi mitatu baada ya Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu kusilimu mji

wa Madinah ulikua uko shwari na hakuna matatizo ya vita, lakini mara Nabii Salallahu

A’layhi wa Salam akamtuma mjumbe wake na barua kwa Ghasan ambae alikua ni Chifu

wa Busra ili kumkaribisha kuingia katika uislam, lakini kabla hajafika huko alipofika

katika sehemu inayoitwa Mutah, mjumbe huyo alikamatwa na kuuliwa na chifu

mwengine wa Ghasan aliekua akiitwa Shurahbil Ibn Amr. Jambo hili la kumuua mjumbe

lilikua ni kosa kubwa sana kwani mjumbe siku zote hua hauawi, hivyo mji wa Madinah

ulipandwa na hasira kubwa sana.


837

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akaamua kuwaadhibu wauaji hao wa

Ghasan na hivyo kutayarisha jeshi lake ili liende likapigane na kabila la watu hao, na

akamchagua Zaid Ibn Harith Radhi Allahu A’nhu kua kiongozi wa jeshi hilo, kisha

akasema ikiwa Zaid Radhi Allahu A’nhu atauwa katika vita hivyo basi uongozi ashike

Jafar Ibn Abi Talib Radhi Allahu A’nhu, na akiuliwa pia basi aongoze Abd Allah Ibn

Rawah Radhi Allahu A’nhu na kumalizia kwa kusema ‘Ikiwa watauawa wote watatu

basi nyinyi wenyewe mtachagua kiongozi wa kukuongozeni’.

Vita vya Mutah vilikua ndio vita vya mwanzo kwa Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu

tangu aingie katika Uislam, na pia ilikua ndio vita vya mwanzo kuenda kupigana yeye

kama mpiganaji aliekua hana cheo chochote, askari wa chini kabisa, walipofika Mutah,

wakapigana vita hivyo na kwa bahati mbaya kati ya viongozi wote waliochaguliwa na

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam wakauawa, hivyo ikabidi Waislam

wajipange upya na kuchagua kiongozi mpya ili kuwaongoza katika vita hivyo.

Vita hivyo vilikua vikali sana kwani Waislamu walikua na jeshi la watu 3000 na Makafir

walikua na jeshi la watu 200000, vilevile Waislamu walikua wameshavunjika moyo

kutokana na kuuliwa kwa viongozi wao wakubwa wote watatu, na hapo Thabit Ibn

Akram akamwambia Khalid Ibn Walid ‘Tafadhali, kua kiongozi wetu utuongoze

kwani tuko katika hali mbaya na miongoni mwetu ni wewe peke yako mwenye

uwezo wa kutuongoza nasi tuko tayari kukufuata kama kiongozi wetu’, hata hivyo

Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu alikataa kwa sababu Thabit Ibn Akram Radhi

Allahu A’nhu alikua ni miongoni mwa waislam wa mwanzo na pia alikua ni miongoni

mwa Masahaba waliopigana katika vita vya Badr. Vile vile Khalid Ibn Walid alikua

akihisi kua Waislam watakua na Imani kubwa zaid na Thabit Ibn Akram Radhi Allahu

A’nhu kuliko watakavyokua na Iman juu yake kwa sababu yeye alikua ndio kwanza

amesilimu.

Hata vivyo kwa kulazimishwa sana ikambidi akubali wadhifa huo na kulipanga upya

jeshi la waislam, Ingawa waislamu walikua kidogo na waliokwisha vunjika moyo kama

tulivyoona lakini kutokana na utaalamu na ujuzi wa Khalid Ibn Walid Radhi Allahu

A’nhu, aliwaaacha nusu ya Waislam wajifiche nyuma yao halafu akawaambia wamfuate

baada ya kuwaonesha ishara, yeye akaelekea katika uwanja wa vita na nusu ya watu

wake, alipofika, vita vikaanza kupiganwa na haikuchukua muda Khalid Ibn Walid Radhi

Allahu A’nhu akawaashiria wale Waislamu waliojificha kuja kusaidia, na hapo likaoneka

vumbi kubwa linalosababishwa na askari wengi waliopanda farasi wakitokea nyuma ya

majeshi ya waislamu, kama kwamba kuna jeshi jengine kubwa la Waislamu ambalo

linakuja kuwaongezea nguvu.

Hapo wanajeshi wa Ghasan wakaanza kuingiwa na khofu na kuchanganyikiwa kwa

nguvu na ari za Waislamu na vile vile kuona kua ndio bado wanazidi kuongozeka zaid,


838

hivyo wakapungukiwa na ari na kuanza kujihami maisha yao, katika vita hivi Khalid Ibn

Walid Radhi Allahu A’nhu alipigana na panga tisa kuvunjikia katika mikono yake,

anasema Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu ‘Katika vita vya Mut’ah, mapanga tisa

yalivunjika, katika mkono wangu na hakuna lililobakia katika mkono wangu

isipokua hili panga langu la Yemen’.

Anasema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua ‘Nabii Salallahu A’layhi wa Salam

aliwatangazia watu kuhusiana na vifo vya Mashahidi Zayd Ibn Harith, Jafar Ibn

Abi Talib na Abdullah Ibn Rawah kabla ya kuwafikia habari ya vifo vyao, alisema

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ‘Zaid alibeba bendera (aliongoza

jeshi) na akafa Shahidi, baadae akaibeba Jafar nae akafa Shahid, na kisha akaibeba

Ibn Rawah naye pia akafa Shahid’, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

akamalizia kwa kusema huku macho yake yakiwa yamejawa na machozi ‘Baada ya

hapo, bendera ikabebwa na Upanga (Khalid Ib Walid) miongoni mwa Mapanga ya

Allah na Allah akawafanya Waislam wawe ni wenye washindi’ (Imam Bukhari).

Waislamu waliporudi katika vita hivi, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

akasema ‘Khalid ni Saifu Allah (Upanga wa Allah)’ kauli ambayo ilikua ni dua ambayo

ilimpelekea Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu kujulikana kwa jina hilo la Saifu Allah,

na vile vile dua ambayo ilimpa ushindi zaid Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu dhidi

ya maadui zake katika kila mapigano atakayopigana hadi mwisho mwa maisha yake.

FAT-H MAKKIYAH - UFUNGUZI WA MJI WA MAKKAH.

Baada ya vita vya Mu’tah, basi hali ilikua shwari katika Mji wa Madina, lakini mara watu

wa Mj wa Makkah wakavunja makubalino ya Mkataba wa Hudaybiyah, kwani ndani

yake ilikua mna makubaliano ya kutoshambuliana baina ya watu wa Mji wa Madina na

watu wa Mji wa Makkah wala na washirika wao, ambapo katika wakati huu watu wa

Makkah walikua wakishirikiana na watu wa Banu Bakr, na watu wa Madina walikua

wakishirikiana a watu wa Banu Khuza.

Ila sasa tatizo ni kua watu Banu Bakr na watu wa Banu Khuza walikua ni maadui wa

mda mrefu, hivyo mara baada ya kumalizika Vita vya Mutah ukatokea ugomvi kwenye

Mji wa Makkah na watu wa Banu Bakr wakawavamia watu wa Banu Khuza walipokua

wanatufu na hata walipokimbilia kutafuta hifadhi kwenye Al Kaabah, hivyo kiongozi

wa Banu Khuza akiwa na watu wake 40 wakaenda Madina na kuomba msaada juu ya

yaliyotokea, hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawataka Watu wa

Quraysh walipe fidia kwa watu wa Banu Khuza waliouliwa, au wavunje

makubaliano ya Ushirikiano na watu wa Banu Bakr au Uvunjwe Mkataba wa

Hudaybiyah.


839

Na kwa kua masharti mawili ya mwanzo ni magumu kwa upande wa watu wa

Quraysh kwa sababu ni yenye kuwavunjia heshima yao, basi Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akapata habari kua watu wa Makkah wamechagua

sharti la tatu, na akona kua kutokana na mtizamo huo basi itakua umewadia mda

wa kuuteka Mji wa Makkah na kuuingiza kwenye Uislam.

Hili pia ni jambo ambalo watu wa Makkah walikua hawalitaki, kwani walikua

wanajua kua Idadi ya Waislam imekua kubwa sana na haiwezekani tena kupigana

nao bila ya kushindwa, hivyo watu wa Makkah wakaamua kua bora watume

mjumbe katika Mji wa Madina kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ili

wajadiliane zaidi kuhusiana na kusimamia kutovunjika kwa makubaliano ya

Hudaybiyah.

Hivyo watu wa Makkah wakaamua kumtuma Abu Sufyan akajadiliane na Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam ili kuuokoa mkataba wa Hudaybiyah, hivyo Abu

Sufyan akaelekea katika Mji wa Madina kwa ajili ya kujaribu kuzungumza na

mtoto wake Ramla Bint Abu Sufyan Radhi Allahu Anha ambae ni mke wa Rasul

Salallahu alayhi wa Salam, lakini hata hivyo hakufanikiwa kumshawishi kwani

Ralma Radhi Allahu Anha alikataa katakata hata kukaa kwenye kitanda chake

ambacho analala pia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakumruhusu ingawa

Abu Sufyan alikua ni baba yake.

Hivyo Abu Sufyan akamfuata, Abu Bakr Radhi Allahu Anhu na kumuomba

amsaidie kuzungumza na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, lakini Abu Bakr

Radhi Allahu Anhu akakataa, hivyo Abu Sufyan akamfuata Umar Ibn Al Khattab

Radhi Allahu Anhu, kisha akamfuata Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anha na pia

akamfuata Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu lakini wote walikataa kumsaidia

juu ya jambo hilo, hivyo Abu Sufyan akarudi katika Mji wa Makkah huku akiwa

ni mtu alievunjika moyo sana kutokana na kutofanikiwa kwa safari yake hio.

Ambapo kwa upande mwengine basi Allah Subhanah wa Ta’ala akamshushia

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aya zifuatazo zenye kumfahamisha namna

ya anavyotakiwa kufanya katika Mji wa Makkah ambazo zinasema:

‏﴿وَقَاتِلُواْ‏ فىِ‏ سَبِيلِ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱل َّذِينَ‏ يُقَاتِلُونَكُمْ‏ وَلاَ‏ تَعْتَدُو ۤ اْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ لاَ‏ يحُِ‏ ُّب

ٱلْمُعْتَدِينَ۞وَٱقْتُلُوهُمْ‏ حَيْثُ‏ ثَقِفْتُمُوهُم وَأَخْ‏ رِجُوهُمْ‏ مِّنْ‏ حَيْثُ‏ أَخْ‏ رَجُوكُمْ‏ وَٱلْفِتْنَةُ‏


840

أَشَد ُّ مِنَ‏ ٱلْقَتْلِ‏ وَلاَ‏ تُقَاتِلُوهُمْ‏ عِنْدَ‏ ٱلْمَسْجِ‏ دِ‏ ٱلحَْرَامِ‏ حَتى َّ ٰ يُقَاتِلُوكُمْ‏ فِيهِ‏ فَإِن ا ت قَ‏ َلُوكُْم

فَٱقْتُلُوهُمْ‏ كَذٰ‏ لِكَ‏ جَزَآءُ‏ ٱلْكَافِرِينَ۞فَإِنِ‏ ٱنتَهَوْاْ‏ فَإِن َّ ٱهلل ََّ‏ غَفُورٌ‏ ر َِّحيمٌ۞وَقَاتِلُوهُمْ‏ حَتى َّٰ‏

لاَ‏ تَكُونَ‏ فِتْنَةٌ‏ وَيَكُونَ‏ ٱلدِّينُ‏ هلل َِّ‏ فَإِنِ‏ ٱنْتَهَواْ‏ فَلاَ‏ عُدْوَانَ‏ إِلا َّ عَلَى ٱلظ َّالِمِينَ‏ ﴾

Waqatiloo fee sabeeli Allahi alladheena yuqatiloonakum wala taAAtadoo inna

Allaha la yuhibbu almuAAtadeena; Waoqtuloohum haythu thaqiftumoohum

waakhrijoohum min haythu akhrajookum waalfitnatu ashaddu mina alqatli wala

tuqatiloohum AAinda almasjidi alharami hatta yuqatilookum feehi fa-in

qatalookum faoqtuloohum kadhalika jazao alkafireena; Fa-ini intahaw fa-inna

Allaha ghafoorun raheemun; Waqatiloohum hatta la takoona fitnatun wayakoona

alddeenu lillahi fa-ini intahaw fala AAudwana illa AAala aldhdhalimeena (Surat Al

Baqara 2:190-193)

Tafsir: Na piganeni kwa ajili ya Allah dhidi ya wale ambao wanaopigana nanyi na

wala msivuke mipaka, kwani kwa hakika Allah hawapendi wenye kuvuka mipaka. Na

waueni popote pale mtakapowakuta na wafukuzeni kutoka katika sehemu

waliyokufukuzeni na Fitna ni mbaya zaidi ya kuua. Na msipigane nao ndani ya Masjid

Al Haram isipokua pale watakapokupigeni nyinyi ndani yake, na kama

wakaikushambulieni basi waueni, kwani hayo ndio malipo ya Makafiri; Lakini kama

wakikoma basi Allah ni mwingi wa Usamehevu na ni mwingi wa Huruma. Na

piganeni nao mpaka iwe hakuna fitna tena, na dini ni ya Allah pekee lakini kama

wakisita basi msivuke mipaka isipokua dhidi ya watakaofanya dhulma.

Imam Taher Ibn 'Ashur anasema kua: ‘Amesema Abd Allah Ibn 'Abbas na 'Umar Ibn

'Abdul 'Aziz na Mujahid kua aya hii ya Surat Al Baqar 2:190 imejiweka wazi na

haihitaji ufafanuzi na haijabatilishwa’. Kisha akaendelea na kusema: ‘Ujumbe wake

halisi ni kupigana na wale watakaopigana nanyi, wale ambao wamejitayarisha

kupigana nanyi, yaani msiwavamie na kuwapiga Wazee, Wanawake na Watoto.’

Ambapo hapa inabidi tufafanue aya hizi kwani kuna watu ambao hua wamefaham sivyo

na hivyo hua ni wenye kutuma aya hizi kwa ajili ya kutangazia na kuhalalisha mapigano

ya Jihadi bila ya kuangalia kusudio na malengo ya Jihadi kisharia.

Wakati kusudio la uhalali wa kupigana Jihad au kupigana vita kwa ajili ya Allah

Subhanahu wa Ta’ala hujumisha mambo yafuatayo:

1- Kwa ajili ya kujilinda na kurudisha mashambulizi ya maadui.


841

2- Kuondoa dhulma ya kidini na kusimamisha uhuru wa kuabudu ili watu wapate uhuru

wa kuabudu na na nafasi ya kufanya Ibada zao kwa uhuru bila ya madhara.

Na masharti ya mapigano hayo huhusisha mambo yafuatayo:

1- Kusudio lake kuu lisiwe ni lenye kutokana na mapendekezo ya kibinafsi au kutafuta

faida kwa mtu fulani katika mapigano hayo.

2- Mapigano yawe ni lazima dhidi ya wale wapiganaji husika na wala sio wananchi

wasiokua na hatia ambao hawapo katika maeneo ya uwanja wa vita au wale ambao

hawahusiki kwa kutokua na silaha ama si miongoni mwa wapiganaji wa maadui.

3- Kuua wanawake na watoto hakuruhusiki kabisa. Katika Sahih Muslim kuna Hadith ya

Abd Allah Ibn Umar isemayo kua Nabii Muhammad Salallahu A’layi wa Salam aliwaona

watoto na wanawake wameuliwa katika vita na hapo akalaani kuwaua wanawake na

watoto na katika Hadith nyengine inasema kua ‘Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam ameharamisha kuua wanawake na watoto’. Anasema Imam An Nawawi

kuhusiana na Hadith hizi kua: ‘Kuna Ijma’a ya Wanazuoni kuhusiana na Hadith hizi

kua hukmu yake inatumika katika vita pale itakapokua wanawake na watoto

hawapigani na Waislam. Lakini ikiwa wanapigana basi Wanazuoni wengi

wanasema inaruhusika kuwaua’ (Sharh Sahih Muslim 12/48).

4- Kuyalinda maisha ya mateka wa vita kutovunjiwa haki zao za kibinaadamu.

5- Kuyalinda mazingira ambako kunajumuisha, makatazo ya kuua wanyama, kukata miti,

kuteketeza mazao mashambani, kuharibu mali, kuvunja majumba, kutia sumu na

kuchafua vyanzo vya maji iwe mto,visima, n.k

6- Kuulinda uhuru wa kuabudu kwa waumini wengine iwe majumbani mwao,

makanisani, mahekalu,n.k.

7- Kuvamia maadui kwa kuwashtukizia kumeharamishwa kabisa. Kwani amesema Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua: ‘Mu’umini hawaui wenzake. Imani

huondoka kwa kuua’. Imam Ibn Athir anasema kuhusiana na Hadithi hii kua ‘Mauaji

yaliyokusudiwa hapa ni kwa kuwashtukizia wengine bila ya kuwapa onyo, wakati

wakiwa hawajajitayarisha’ (Al-Nihaya fi Gharib al-Hadith wa al-Athar 3/775)

8- Ruhusa ya kuingia katika nchi hua inahesabika kama makubaliano ya kiusalama ya

ukimya kua hairuhusiki kufanya ufisadi katika nchi ya maadui. Imam al-Khurqī anasema

katika Mukhtasr wake: ‘Yeyote yule anaeingia katika nchi ya maadui zake

haruhusiwi kuwalaghai mali zao’, katika kuielezea kauli hii Imam Ibn Qudama

anasema katika Al Mughni, ‘Hairuhusiki kuwasaliti wao [Wasiokua Waislamu katika

nchi isiyokua si ya Waislam], kwa sababu kuna makubaliano ya kimya ya mtu


842

kuingia katika mji kwa usalama kutokana na sharti la kua mtu huyo anaeomba

ruhusa ya kuingia katika mji wa kigeni hatowadhuru au hatowasaliti watu wa mji

huo. Hivyo mtu yeyote yule atakaeingia katika mji wetu kwa usalama na kisha

akatusaliti hua anavunja makubaliano hayo. Hivyo hili hua ni katazo kwa sababu

kufanya hivyo hua kunasababisha hadaa ambayo imaharamishwa katika dini yetu.’

(Al-Mughn̄ i 9/237).

9- Adui ni lazima awe ni miongoni mwa wale ambao Muislam ameruhusika kupigana

nao, kwani ikiwa adui ni yule ambae kuna makubalianao ya kusitisha makubaliano na

Waislam, basi hua hairuhusiki kumvamia adui wakati wa usiku kwa sababu kufanya

hivyo hua ni kuvunja makubaliano ya usalama baina yao katika mambo yanayohusu

uhai, mali na heshima.

10- Hairuhusiki kuwatumia watu kama ngao ili kujilinda isipokua katika wakati wa vita

na katika hali maalum, ambavyo ni kama ilivyoelezewa na Wanazuoni. (Bahr Ra`iq 80\5,

Hashiyat ibn 'Abn Abdin 223\3, Rawdat al Talibin 239\10, Mughni al Muhtaj223\4,

Mughn̄ i ibn Qudama 449\8, 386/10).

Hivyo mnamo tarehe 10 ya mwezi wa Ramadhan ya mwaka wa 8 Al Hijra ambayo

ni sawa na mwaka 630, basi Rasul Allah Salallah Alayhi wa Salam alikusanya

Jeshi la watu 10,000 la Waislam na kueleka katika Mji wa Makkah, ambapo

walipofika katika maeneo ya Marr Az Zahran basi jeshi hilo likapiga kambi katika

eneo hilo, ambapo katika usiku huo Waislam wakamkamata Abu Sufyan ambae

alikua akifanya Upelelezi kutaka kujua kinachoendelea katika kambi hio.

Abu Sufyan alipopelekwa mbele ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi

nae akasilimu. Na siku ya pili yake asubuhi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam akaligawa Jeshi lake katika sehemu 4 kwa ajili ya kuuvamia Mji wa

Makkah na akawachagua viongozi wanne wakuu wa jeshi hilo ambao ni yeye

mwenyewe Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kisha Khalid Ibn Walid Radhi

Allahu Anhu, kisha Abu Ubaydah Ibn Jarrah Radhi Allahu Anhu na kisha Saad Ibn

Ubaidah Radhi Allahu Anhu.

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawaagiza Viongozi wake hao kwa

kusema: ‘Hairuhusiki kutumia silaha ya aina yeyote kumshambulia mtu

yeyote isipokua yule atakaeanzisha mashambulizi, Jaribuni kwa kila hali

kuepuka umwagaji damu, na jizuieni kuwadhuru Wazee, Wanawake na

Watoto’

Hili lilikua ni tukio la pili muhimu lililofuatia kutokea baada ya kusilimu Khalid Ibn

Walid Radhi Allahu A’nhu ambalo ni wakati wa kuuteka mji wa Makkah, kwani Nabii


843

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, alimkabidhi Khalid Ibn Walid kuongoza kundi

la wapiganaji wanaotoka katika makabila ya Banu Salim, Banu Khazima, Banu Ghaffar

na Jaheena, na kumwambia ikiwa watatokea watu ambao wataanzisha mapigano basi

anayo ruhusa ya kuutumia upanga wake na ikiwa hakuna upinzani basi haina haja ya

kuutumia upanga huo.

Walipoingia katika viunga vya Mji wa Makkah, vijana wapya waliokua wamechukua

nafasi ya Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu katika wapiganaji wa Makafiri wa

Makkah, baada ya yeye kusilimu na kuhama Makkah, waliokua wakiongozwa na Ikrimah

Ibn Abu Jahal, Safwan Ibn Ummayah na Sahal Ibn Amr, walijaribu kuwazuia Waislamu

kwa silaha zao wasiingie katika mji wa Makkah katika maeneno ya Khandamah na hapo

baada ya kuona silaha zimetolewa dhidi yao, Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu

akaamrisha vijana hao washughulikiwe na hivyo wakawaua baadhi miongoni mwao na

baadhi Ikrimah Ibn Abu Jahal wakakimbia.

Baadae Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam aliposikia Habari hii, alikasirika

kwanini Waislamu wakawapiga vijana hao, lakini hata hivyo baada ya kuambiwa kua

Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu alitoa amri hiyo, basi Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam akasema: ‘Allah hutekeleza yale yalio bora’, akimaanisha kua hayo

yalikua yameshaandikwa na Allah Subhanahu wa Ta’ala yatokee.

Baada ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kuingia katika mji wa Makkah

na kuingia ndani ya Al Kaabah kuyaangusha masaamu yaliyomo ndani yake, alikua ni

Khlaid Ibn Walid ambae ndie aliekaa nje ya mlango wa Al Kaabah kusimamia asiingie

mtu mwengine yeyote. Na baada ya kuuweka chini ya mamlaka yao, Mji wa Makkah.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akasema:

﴿ٰ َ ي ُّهَا ٱلن َّاسُ‏ إِ َّ خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ‏ ٰ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ‏ شُعُوابً‏ وَقَبَآئِلَ‏ لِتَ‏ ۤ عَارَفُو اْ‏ إِ‏ َّن

أَكْ‏ رَمَكُمْ‏ عِ‏ ندَ‏ ٱهلل َِّ‏ أَتْقَاكُمْ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ عَلِيمٌ‏ خَبِيرٌ‏ ﴾

Ya ayyuha alnnasu inna khalaqnakum min thakarin waontha wajaAAalnakum

shuAAooban waqaba-ila litaAAarafoo inna akramakum AAinda Allahi atqakum

inna Allaha AAaleemun khabeerun (Surat Al Hujrat 49:13)

Tafsir: Enyi Watu hakika sisi tumekuumbeni nyinyi kutokana na Mume na Mke, na

tukakujaalieni nyinyi kua katika Mataifa na Koo ili pate kujuana, Hakika Mwenye

Utukufu zaid mbele ya Allah ni yule Mwenye Taqwa zaidi, kwa Hakika Allah ni

mwingi wa Kujua juu ya kila kitu na ni mwenye kua na habari juu ya kila kitu.


844

Baada ya hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamuamrisha Bilal Ibn Rabah

Radhi Allahu Anhu asome Adhana na kisha akauchukua Ufunguo wa Al Jengo la Al

Kaabah na kuukabidhi kwa Uthman Ibn Talha Radhi Allahu Anhu kua yeye na kizazi

chake kua ndio wasimamizi wa Al Kaabah.

Na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamtuma Khalid Ibn Walid Radhi

Allahu A’nhu kuenda kuteketeza makazi ya Al Uzza, lakini hata hivyo Khalid Ibn Walid

Radhi Allahu A’nhu aliporudi alisema kua hakukuta kitu chochote katika sehemu hiyo

aliyotumwa, na hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akamwambia Khalid

Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu nenda tena kaangalie vizuri, hivyo alipokwenda tena mara

ya pili katika sehemu hiyo Khalid Ibn Walid Radhi Allahu A’nhu akayakuta makazi hayo

na pia akamkuta mwanamke mweusi aliekua hana nguo, hivyo akayateketeza makazi

hayo na pia akamteketeza kwa upanga wake mwanamke huyo. Aliporudi safari hii Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akamwambia huyo ndie aliekua Al Uzza.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akatoa Khutba katika maeneo ya Safa na

kisha akawauliza watu wa Makkah: ‘Hivi Jee mnajua nnataka kukupeni Adhabu Gani?’

Watu hao wa Makkah wakasema: ‘Hakika wewe ni Ndugu mwenye Utukufu kwetu

na ni Mtoto wa Ndugu yetu Mtukufu’ hivyo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam akasema: ‘Hamna kulaumiwa leo hii juu yenu hivyo nendeni kwani mko

huru.’

Ambapo kauli hii ya Huruma na Unyenyekevu iliwafurahisha sana watu wa Makkah na

hivyo wote wakaingia kwenye Uislam akiwemo Hind Bint Utbah, Ikrimah Ibn Abu Jahal

na Suhail Ibn Amr Radhi Allahu Anhum. Ambapo baada ya tukio hili basi Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akakaa katika Mji wa Makkah kwa siku 20 kumalizia

mipangilio ya mipaka ya eneo Takatifu la Al Kaabah.

WAKE WA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM.

Mchoro unaofuatia unaonesha namna ilivyokua familia ya Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam kutoka kwa babu yake ambae ni Abd ul Mutalib, kwa baadhi ya Ami

zake, wake zake, watoto wake na wajukuu zake.


845


846

Kama tunavyoona katika mchoro huo wa familia ya Rasul Allahu salallahu A’layhi wa

Salam kua kuna idadi kubwa ya wake wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

idadi ambayo imepindukia idadi iliyoruhikaa kisharia, hivyo kwa wasiofahamu huenda

wakajiuliza ni kwa sababu gani yeye akawa na idadi kubwa ya wake wakati Uislam

unasema kua mwanamme anaruhusika kuoa mwisho wake wanne?

Jibu la swali hili linaelezeka katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni kua hapo zamani

ilikua ni jambo la kawaida si kwa jamii ya Kiarabu tu kwa mwanamme kua na wake

wengi bali pia kwa jamii mbalimbali. Hivyo aya ya kushurutisha mwisho wake wanne

iliposhuka, ilikuja ili kurekebisha kwa kupunguza idadi ya wake anaotakiwa kua nao

mwanamme na vile vile kuwahifadhi Wajane na Mayatima tena kwa sharti la kuwafanyia

uadilifu wa kisharia wanawake.

Kwani aya hiyo ya Surat An Nisaa’ inasema:

‏﴿وَإِنْ‏ خِ‏ فْتُمْ‏ أَلا َّ تُقْسِ‏ طُواْ‏ فىِ‏ ٱلْيَتَامَى ٰ فَٱنكِحُواْ‏ مَا طَابَ‏ لَكُمْ‏ مِّنَ‏ ٱلنِّسَآءِ‏ مَثْنىَٰ‏

وَثُلاَثَ‏ وَرُابَعَ‏ فَإِنْ‏ خِ‏ فْتُمْ‏ أَلا َّ تَعْدِلُواْ‏ فَوَاحِ‏ دَةً‏ أَوْ‏ مَا مَلَكَتْ‏ أَيمَْانُكُ‏ مْ‏ ذٰ‏ لِكَ‏ أَدْ‏ نىَٰ‏

أَلا َّ تَعُولُواْ‏ ﴾

Wa-in khiftum alla tuqsituu fii alyatama fainkihuu ma taba lakum mina alnnisa-i

mathna wathulatha warubaAAa fa-in khiftum alla taAAdiloo fawahidatan aw ma

malakat aymanukum dhalika adna alla taAAooloo. (Surat An Nisaa’ 4:3).

Tafsir: Na ikiwa mnakhofu kua hamtoweza kuwafanyia haki mayatima wa kike, basi

Oeni wanawake wengine mnaowataka, wawili, au watatu, au wanne; lakini ikiwa

mnakhofu kua hamtoweza kuwafanyia uadilifu basi oeni mmoja tu, au wale

mnaowamiliki mikononi mwenu (Mliowateka vitani na Watumwa). Kufanya hivyo ni

kukaribia kujilinda na kutokua waadilifu.

Aya hii ilishuka siku ya mwezi tatu Shawwal, baada ya vita vya pili vilivyopiganwa baina

ya Waislam na Makafir wa Makkah, vita hivi vilikua ni vita vya Uhud ambapo Waislamu

walishindwa na miongoni mwao watu Masahaba 70 wakafa mashahidi, hivyo ghafla

ikawa takriban familia 70 katika mji wa Madinah hazina wa kuwasimamia, hili lilikua

ni tatizo kubwa sana kwa jamii ya Taifa changa la Kiislam, hivyo ufumbuzi wa tatizo hili

ukapatikana baada ya kushuka kwa aya hii, ilioruhusu kuwahudumia na kuwahifadhi

Wajane na Mayatima.


847

Anasema Imam Muhammad Tahir Ibn Ashur kuhusiana na aya hii kua “Aya hii ni yenye

kutoa onyo kwa Wanaume kua wasitumie uhusiano wao wa udugu wa Damu, kama

kisingizio cha kutowalipa mahari yao kamilifu Mayatima kama vile ambavyo

hawakuutumia uhusiano wao wa udugu huo wa damu kwa kutowaoa Mayatima

hao, na bali waliwaoa kwa sababu ya mali yao au kwa sababu ya kuvutiwa nao”

Imam Muhammad Tahir Ibn Ashur anaendelea kwa kusema kua : ‘Na neno Dhalika

liliomo katika aya hio (Dhalika Adna alla Taáuluu – Na kufanya hivyo ni kwa ajili

ya kukaribia kujilinda na kutokua waadilifu) ni Ismi al Ishara – Kiashirio

kinamaanisha aidha moja kati ya mambo mawili yafuatayo:

1- Sharti – Yaani na ikiwa mnakhofu kua hamtoweza kuwafanyia haki

mayatima wa kike

2- Hukmu – Yaani basi oeni mmoja tu, au wale mnaowamiliki mikononi

mwenu (Mliowateka vitani na Watumwa)

Hivyo kama ikiwa Dhalika - Ismi al Ishara hio ikiwa inamaanisha jambo la pili basi

hii inamaanisha kua Mwanamme anatakiwa apunguze idadi ya Wanawake

anaotaka kuwaoa hadi afikie katika hali ya kua hatokua na khofu ya kutokua

Muadilifu. Na hii ni kwa sababu kua na wake wengi humpelekea Mwanamme

kutofanya Uadilifu, hata kama akijitahid kwa uwezo wake wote kufanya Uadilifu

na hii ni kutokana na maumbile ya Nafsi ya Ibn Adam hua ni yenye matamanio na

kufanya makosa.’(Al Tahrir wa Al Tanwir)

Hivyo kuoa wake zaidi ya mmoja katika Uislam hakukupendekezwa, bali kumeruhusiwa,

chini ya muongozo maalum ambao ni kutooa kwa kuendekeza matamanio ya mwanamme

tu bali kwa kufanya uadilifu na kuwaonea huruma Wanawake, Wajane na Mayatima,

kama ilivyosema tena Qur’an:

وَلَن تَسْتَطِيعُو ۤ اْ‏ أَن تَعْدِلُواْ‏ بَينَْ‏ ٱلنّسَآءِ‏ وَلَوْ‏ حَرَصْتُمْ‏ فَلاَ‏ تمَِيلُواْ‏ كُ‏ ل َّ ٱلْمَ‏ يْ‏ ‏ِل

فَتَذَرُوهَا كَٱلْمُعَل َّقَةِ‏ وَإِن تُصْلِحُواْ‏ وَتَت َّقُواْ‏ فَإِن َّ ٱهلل ََّ‏ كَانَ‏ غَفُوراً‏ ر َّحِ‏ يماً‏ ﴾

Walan tastateeAAoo an taAAdiloo bayna alnnisa-i walaw harastum fala tameeloo

kulla almayli fatadharooha kaalmuAAallaqati wa-in tuslihoo watattaqoo fa-inna

Allaha kana ghafooran raheeman (Surat An-Nisaa’ 4:129)

Tafsir: Na hamtoweza kufanya uadilifu baina ya wanawake hata kama ikiwa hivyo

ndivyo mnavyotaka, hivyo msiegemee sana upande mmoja na hivyo kupelekea

ِ

﴿


848

mwengine kudharaulika. Mkifanya uadilifu na yote ya haki na mkamuogopa Allah

kwa kujitenga na kila ovu, basi Allah ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa Rehma.

Anasema Imam Al-Fakhr Ad Din Al Razi kuhusiana na aya hii kua: ‘Aya hii inamaanisha

kua kamwe hamtoweza kuweka usawa, au kua na hisia sawa juu yao wote, kwani

jambo hili haliko chini ya uwezo wenu, na kwa sababu hiyo basi hamtakiwi

kulifanya’.(Mafatih Al-Ghayb)

Hii inamaanisha kua sio kama imeharamishiwa kuzidisha hisia upande mmoja, kwani

hilo ni jambo ambalo halidhibiti, lakini haikuruhusiwa kuonesha kua hisia hizo zimezidi

upande mmoja iwe aidha kwa vitendo au kwa maneno.

Anasema Imam Muhammad Idris Al Shafii kua Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam alikua akiwafanyia uadilifu sawia wake zake, na kisha husema: ‘Ya Allah hivi

ndivyo niwezavyo kujidhibiti na wewe ni mwenye kujua kuhusiana na yale

nisiyoweza kuyadhibiti’.

Amesema Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam katika hadith iliyopokelewa na

Abu Hurayra kua: ‘Atakaekua na wake wawili na kisha akampendelea mke mmoja

(kwa kutofanya uadilifu baina yao) basi atafufuliwa siku ya kiama akiwa amepooza

upande mmoja wa mwili wake’. (Imam Abu Daud)

Hivyo baada ya kushuka aya inayoshurutisha mwisho kua na wake wanne, baadhi ya

Masahaba waliokua na wake zaidi ya wanne iliwabidi kuwaacha wake zao na kubakisha

wanne tu, na hata wale ambao waliosilimu baadae pia iliwabidi kuwaacha wake wengine

na kubakia na wanne tu, idadi ambayo Uislamu umeruhusu.

Kwa mfano Al Harth Ibn Qays alisema kua kabla ya kusilimu alikua na wake wanane na

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akamwambia kua katika wake zake hao

aliokua nao itambidi achague wanne tu na wanne waliobakia aachane nao. Imam Al

Tirmidhi anasema kua Ghaylan Ibn Salmah al Thaqafi Radhi Allahu Anhu alikua na

wake kumi katika siku za Ujahiliya lakini baada ya kusilimu ikambidi achague wake

wanne miongoni mwao na sita waliobakia aachane nao, Sahaba mwengine ni Nawfal Ibn

Mu’awiyah Radhi Allahu Anhu ambae alikua na wake watano na alipoamua kusilimu

ikambidi nae pia amuache mmoja kati yao ili abakie na wanne tu.

Sehemu ya pili ya jibu la swali hilo, hua inafafanulika vizuri zaidi pale tunapoiangalia

historia inayofuatia, ambayo ni ya maisha ya ndoa ya Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam.

Ingawa historia inasema kua Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alioa wake

13 lakini wakati aya Surat An Nisaa’ 4:3 inayoruhusu kuoa mwisho wake wanne


849

inashuka, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kwa wakati huo alikua na wake

tisa ambao walikua ni wafuatao:-

1. Umm al Mu’uminin Sawdah Bint Zumah.

2. Umm al Mu’uminin Aisha Bint Abu Bakr As Siddiq.

3. Umm al Mu’uminin Hafsah Bint Umar Ibn Al Khattab.

4. Umm al Mu’uminin Hind Bint Umayyah (Ummu Salamah).

5. Umm al Mu’uminin Zaynab Bint Jahsh.

6. Umm al Mu’uminin Juwayriyyah Bint Harith.

7. Umm al Mu’uminin Safiyyah Bint Huyay.

8. Umm al Mu’uminin Ramla Bint Abu Sufyan (Ummu Habiba).

9. Umm al Mu’uminin Maymunah Bint Harith Ibn Hazan Al Hilalieh.

Lakini hata hivyo aya hiyo haikumhusu kabisa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam kwani Allah Subhanahu wa Ta’ala alimshushia Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam, aya maalum kwa ajili yake inayomshurutisha kutowaacha wake

aliokua nao, wala kutoongeza mke mwengine zaid ya wale aliokua nao, kama

inavyosema Qur’an:

‏﴿لا َّ يحَِل ُّ لَكَ‏ ٱلنِّسَآءُ‏ مِن بَعْدُ‏ وَلاَ‏ أَن تَبَد َّلَ‏ هبِِن َّ مِنْ‏ أَزْوَاجٍ‏ وَلَوْ‏ أَعْجَبَكَ‏

حُسْنُهُن َّ إِلا َّ مَا مَلَكَتْ‏ يمَِينُكَ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٰ عَلَى ِ كُل شَيْءٍ‏ ر َّقِيباً‏

ّ

La yahillu laka alnnisao min baAAdu wala an tabaddala bihinna min azwajin

walaw aAAjabaka husnuhunna illa ma malakat yameenuka wakana Allahu AAala

kulli shay-in raqeeban. (Surat Al Ahzab 33:52).

Tafsir: ‘Si halali kwako, [Muhammad], kuoa wake baada ya hao, wala kuwabadilisha

kwa ajili ya wake wengine hata kama ikiwa uzuri wao unakuvutia, isipokua wale

unawamiliki (Waliotekwa vitani ama watumwa) na Allah ni muangalizi wa Kila kitu.’

Imam Al Baidawi anasema katika Tafsir yake kua, ‘Aya hii ilikua inamuelezea Nabii

Muhammad Sallahu A’layhi wa Salam kua haruhusiwi kuoa wake wengine hata

kama ikiwa mmoja kati ya wake zake hao amefariki dunia wala haruhusiwi

kuwabadilisha kwa kumpa talaka mmoja na kuoa mwengine’.

Anasema Abd Allah Ibn Abbas kuhusiana na habari hiyo kua hata wakati Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alipoamua kuuwacha wazi mlango kwa

kuwaambia wake zake kua wanayohaki ya kuamua kama kubakia na yeye na na kupata

Radhi za Allah ama kuamua kuachwa na kuwa huru na kuanza maisha mapya na bora


850

kuliko aliyokua nayo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam wakati huo ambao

ulikua ni mgumu sana, lakini wake zake hao walikataa na kusema kua watastahamili

ugumu wa maisha waliyokua nayo na kubakia na kuishi na Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam.

Na baada ya hapo Allah Subhanahu wa Ta’ala aliwapa cheo wake wa Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam pale aliposema katika Qur’an kua:

‏﴿ٱلن َّبىِ‏ ُّ أَوْ‏ لىَٰ‏ بِٱلْمُ‏ ؤْ‏ مِنِينَ‏ مِ‏ نْ‏ أَنْفُ‏ سِ‏ هِ‏ مْ‏

وَأَزْوَاجُهُ‏ أُم َّهَاتُهُ‏ ‏ْم﴾‏

Alnnabiyyu awla bialmu/mineena min anfusihim waazwajuhu ommahatuhum ..

(Surat Al Ahzab 33:6).

Tafsir: ‘Nabii yuko karibu na waumini kuliko wao na Nafsi zao, na wake zake ni mama

zao (kwa waumini, kuwaheshimu na kutowaoa)’

Tunapoangalia historia kwa kina basi tunaona kua Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam, alipomuoa Sayyida Khadija Radhi Allahu Anha, alikaa nae takriban kwa

miaka 23 bila kuongeza mke mwengine hadi pale alipofariki Sayyida Khadija, ambapo

wakati huo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua na umri wa miaka 50,

Baada ya kufariki Sayyida Khadija Radhi Allahu Anha,, Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam alikaa miaka miwili bila ya kua na mke yeyote, na alikua akikaa peke

yake pamoja na watoto wake.

Hivyo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, hakuwahi kuoa mke zaid ya

mmoja hadi pale alipohamia Madinah baada ya kuanzisha Taifa jipya la Kiislamu, kipindi

ambacho kilianza wakati akiwa na umri wa miaka 53 hadi 60, jambo hili linatuonesha

kua kuoa kwake huko wake wengi kunatokana na njia za kujenga na kuimarisha udugu

na ujamaa wa makabila tofauti katika Taifa lililokua changa la Kiislam na vile vile kwa

nia ya kuwalinda na kuwahurumia Wajane na Mayatima. Aya iliyomkataza Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kutoongeza au kutowawacha wake zake

alishushiwa wakati akiwa na umri wa miaka 60, na akiwa na wake zake hao 9, Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alitii amri hiyo hadi alipofariki akiwa na umri

wa miaka 63.

Wake zake wengine aliowahi kuwaoa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

kabla ya kushuka aya iliyomkataza kuoa au kuacha wake zake ni pamoja na Umm al

Mu’uminin Khadija Bint Khuwaylid Radhi Allahu Anha, ambae alifariki dunia miaka

mitatu kabla ya Hijra.


851

Tukiangalia kwa upande mwengine basi tunaona kua ilikua pia ni vigumu kwa Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kuwaacha wake zake hao kwa sababu ya

utukufu waliokua nao wake hao ambao mbali ya kua ni wake wa Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam lakini pia katika ukubwa na utukufu wa asili waliotoka wake

zake hao, kama inavyooneshwa hapa chini:

Umm Ul

Muuminin.

Khadija Bint

Khuwaylid.

Sawdah Bint

Zammah.

Aisha Bint

Abu Bakr

Hafsa Bin

Umar

Hind Umm

Salama

Zaynab Bint

Khuzaymah

Juwayriyah

Bint Harith

Zaynab Bint

Jahsh

Rayhana Bint

Zayd

Maria Bint

Sham

Ramla Umm

Habiba

Safiyah Bint

Huayih

Maymuna

Bint Harith

Ukoo

Wake.

Aliolewa

Akiwa.

Umri Wake

Alipoolewa.

Mwaka Alioolewa.

Banu Asad Mjane Wa Miaka 40 Miaka 25 Baada ya

Talaka

Mwaka wa Tembo

Banu Amir Mjane wa Miaka 50 Miaka 10 Baada ya

Kufiwa

Utume.

Banu Taymi Mwari Miaka 14 Mwaka wa 2 Al Hijra

Banu Adi Mjane wa Miaka 20 Mwaka wa 4 Al Hijra.

Kufiwa

Banu Amir Mjane wa Miaka 50 Mwaka wa 4 Al Hijra.

Kufiwa

Banu Amir Mjane wa Miaka 30 Mwaka wa 5 Al Hijra.

Kufiwa

Banu Mjane wa Miaka 20 Mwaka wa 5 Al Hijra.

Mustalaq Kutekwa

Banu Asad Mjane wa Miaka 38 Mwaka wa 5 Al Hijra.

Talaka

Banu Nadir Mjane wa Miaka 18 Mwaka wa 6 Al Hijra.

Kutekwa

Al Surriyah Miaka 18 Mwaka wa 7 Al Hijra

Qitbiyyah

Banu Shams Mjane wa Miaka 36 Mwaka wa 7 Al Hijra

Talaka

Banu Nazir Mjane wa Miaka 17 Mwaka wa 7 Al Hijra.

Kutekwa

Banu Amir Mjane wa Miaka 27 Mwaka wa 7 A Hijra.

Talaka


852

UMM AL MU’MININ SAWDAH BINT ZUMAH

Ingelikuaje kama Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam angempa talaka Umm

Al Mu’uminin Sawdah Bint Zumah Ibn Qays Ibn `Abdush-Shams Ibn `Abdi Widdi Ibn

Nasr Ibn Maalik Ibn Hasl Ibn `Amir Ibn Lu'ay, ambae alikua ni mke wake wa kwanza

kumuoa baada ya kufariki Sayyida Khadija Bint Khuwaylid Radhi Allahu Anha, kwani

Umm al Mu’uminin Sawdah Bint Zumah Radhi Allahu Anha alikua ni miongoni mwa

Waislam wa mwanzo kusilimu na pia miongoni mwa Waislamu wa mwazo kufanya Hijra

kwa kuhamia Uhabeshi (Ethiopia) pamoja na mumewe, aitwae Sakran Ibn Amar Radhi

Allahu Anhu ambae alisilimu kutokana na ushawishi wa Sawdah Radhi Allahu Anha

ambae alisilimu mwanzo kuliko Sakran Radhi Allahu Anhu.

Hivyo wakati walipokua wakirudi Makkah kutoka Uhabeshi ambapo Sawda Radhi

Allahu Anha alilala akaota kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akimkaribia na

kisha alipofika karibu yake basi akapiga goti pembeni yake, ambapo alipomwambia

Mume wake Ndoto hio, basi Sakran akasema kua: ‘Hii Ndoto inamaanisha kua mimi

nitafariki karibuni na kisha wewe utaolewa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam’ na haukuchukua mda isipokua akran Ibn Amar Radhi Allahu Anhu akafariki

Na baada ya kurudi katika Mji wa Makkah huku Sawdah Radhi Anha mwenye umri wa

wa miaka mitano zaidi ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na huku akiwa

Mjane mwenye watoto watano na baba yake akiwa ni kipofu, basi Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam aliamua kumuoa Sawdah Radhi Allahu Anha baada ya

kufiwa na mumewe kwa sababu kama asingemuoa basi ingembidi Sawdah Radhi Allahu

Anha abakie katika Mji wa Makkah kama mjane, jambo ambalo lingempelekea kua

katika mtihani mkubwa, kwani wakati huo mji wa Makkah ulikua bado ni wa Kikafir

hivyo familia yake ingemtenga na pia watu wa mji wa Makkah wangemlazimisha kurudi

katika ukafiri kwa kumuadhibu na pia kulikua na uwezekano wa kumuua kutokana na

kua Muislam.

Mbali ya hivyo lakini pia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alimuoa Sawdah

mnamo mwaka wa 10 wa Utume wake katika mwezi wa Ramadhan kwa ajili ya

kumsimamia na kuwahudumia watoto wake na bila ya shaka Sawdah Radhi Allahu Anha

alikua ni mwenye kutekeleza wajibu wake mbele ya Mume wake ipasavyo, kwani alikua

ni mwenye kumpenda na kumliwaza yeye na watoto wake na pia alikua ni mfano wa

kuigwa hata kwa Aisha Radhi Allahu Anha ambae anasema kuhusiana nae kua: ‘Sijawahi

kuona Mwanamke ambae ni mwenye kunitia ari zaidi kuliko Sawdah Radhi Allahu

Anha, kiasi ya kua hata mimi ningependa kua kama yeye.’


853

Sauda Bint Zummah Radhi Allahu Anha alikua ni mwanamke mwenye kufuata

kikamilifu maamrisho ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kwani katika

Hiija yake ya mwisho Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam basi aliwaambia

wake zake kua: ‘Twendeni Hija mara hii kisha mtabaki nyumbani’ ambapo Sawdah

Bint Zumah Radhi Allahu Anha akasema: ‘Hakika mimi sitoenda tena Hija baada ya

Hija hii.’

UMM AL MU’MININ AISHA BINT ABU BAKR AS SIDDIQ

Ingelikuaje kama Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam angempa talaka Umm

al Mu’uminin Aisha Bint Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu ambae alikua ni mtoto

wa Sahaba yake kipenzi cha moyo wake, Sahaba Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu

Anhu.ambae alijitolea kila kitu kwa hali na mali kwa ajili ya Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam na pia kwa ajili ya Waislamu na kueneza ujumbe wa dini ya Kiislam.

Ambapo aliulizwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na Amr Ibn Al Aas Radhi

Allahu Anhu pale aliposema: ‘Hivi Jee ni nani ambae unampenda zaidi kuliko wote?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu: ‘Aisha’ na kisha Amr Ibn Al Aas Radhi

Allahu Anhu akauliza tena: ‘Na Katika Wanaume?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam Akajibu: ‘Baba yake.’

Ambapo anasema Aisha Radhi Allahu Anha kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

aliniambia mie kua: ‘Nimekuona Aisha ndani ya Ndoto yangu, wakati Malaika Jibril

aliponiletea ukiwa kwenye Nguo ya Hariri ya rangi kijani na kuniambia: ‘Huyu

ndio Mke wako hapa Duniani na kesho Akhera’’’

Kwa kua alikua na umri mdogo basi Aisha Radhi Allahu Anha aliposwa kwanza na kisha

akaolewa miaka mitatu baada ya Vita vya Badr, ambapo anasema mwenye Aisha Radhi

Allahu Anha kutokana na Udogo wake kua: ‘Siku Moja Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alikuja Nyumbani wakati mimi nikiwa nachezea visanamu ambapo nae

aliponiona akasema: ‘Ya Aisha, Jee ndio Mchezo gani huo unaocheza?’ nami

nikasema: ‘Farasi wa Sulayman’ ambapo Rasul Allahu Salallahu Alayhi wa Salam

akacheka’

Anasema Aisha Radhi Allahu Anha kua : ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

aliniambia mimi kua: ‘Hakika wewe kwangu mie nakupenda zaidi ya Tende

inapochanganywa na Siagi’ ambapo nami nikamwambia: ‘Ya Rasul Allah hakika

wewe kwangu mimi nakupenda kuliko Asali inapochanganywa na Siagi’’


854

Ambapo ilikua ni kawaida ya Masahaba kumtumia zawadi Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam wakati inapokua ni zamu ya kulala kwa Aisha Radhi Allahu Anha kwani

walikua wanajua kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akimpenda sana

Aisha Radhi Allahu Anha, hivyo siku moja Wake zake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam walikusanyika kwenye nyumba ya Ummu Salama Radhi Allahu Anha, na

wakamwambia Ummu Salama Radhi Allahu Anha amwambie Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua awaambie Masahaba kua wanapotaka kumtumia zawadi basi sio

lazima wasubiri inapokua zamu ya Aisha Radhi Allahu Anha bali wamtumie na katika

siku nyengine za kawaida pia.

Hivyo Ummu Salamah Radhi Allahu Anha akamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam mara ya kwanza lakini Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakumjibu,

hivyo akamwambia tena mara ya pili na ikawa hakujibiwa, na hivyo akamwambia mara

ya tatu ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kumwambia Ummu

Salama Radhi Allahu Anha kua: ‘Usiniumize kuhusiana na Aisha, kwani haijawahi

kutokea kua Wahyi kushuka katika nyumba yeyote isipokua ya Aisha’ ambapo

Ummu Salama Radhi Allahu Anha akasema: ‘Naomba msamaha kwa Allah kutokana

na kukumiza hali yako’

Miongoni mwa sifa za upekee za mahusiano baina ya Aisha Radhi Allahu Anha, ni pale

Siku moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimwambia Aisha Radhi Allahu

Anha: ‘Ya Aisha hakika mimi hua nnajua pale unapokua umenikasirikia na pale

unapokua hukunikasirikia’ Aisha Radhi Allahu Anha akauliza: ‘Unajuaje ya Rasul

Allah?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajibu: ‘Unapokua unafuraha nami

basi hua unasema: ‘La, naapa kwa Mola wa Muhammad’ lakini unapokua una

hasira basi hua unasema: ‘La Naapa kwa Mola wa Ibrahim’’ hivyo Aisha Radhi

Allahu Anha akasema: ‘Naam. Ya Rasul Allah, Hua hua silitaji Jina lako.’

Ambapo anasema Imam An Nasafi kua: ‘Siku moja Aisha Radhi Allahu Anha alikua

na hasira kwa sababu hakukua na chakula ndani ya Nyumba yao, na hivyo Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakupenda namna Aisha Radhi Allahu Anha

alivyokua akizungumza nae, kwa hivyo akaingiwa na hasira na kutoka ndani ya

Nyumba yake na kuelekea Msikitini. Ambapo Aisha Radhi Allahu Anha alijaribu

kumkimbilia kumuomba msamaha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam lakini

hakuwahi kukutana ane na akaanguka chini na kuweka shavu lake ardhini na

kuanza kuomba Msamaha kwa Allah Subhanah wa Ta’ala.’

Ambapo hapo hapo akashuka Malaika Jibril na kumuwahi Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kabla hajaingiza mguu wake Msikitini na kumwambia Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala anataka urudi kwa

Aisha na kisha umsamehe’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akarudi

kwa Aisha Radhi Allahu Anha na kisha akamsamehe makosa yake, na kisha baada


855

ya hapo Malaika Jibril akashuka hukua kiwa na Kibakuli cha Vyakula vitamu na

kumwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua : ‘Allah Subhanah wa

Ta’ala anasema kua Upatanisho ulikua ni kutoka kwetu na chakula cha upatanisho

pia ni kutoka kwetu.’

Miongoni mwa sifa za kimaumbile za Aisha Radhi Allahu Anha basi ni kama

anavyomuelezea Hisham Ibn Urwa Radhi Allahu Anhu ambae amesema: ‘Hakika mimi

sijawahi kuona mtu yeyote yule ambae nimwenye Ilm kubwa ya Aaya za Qur’an,

Ibada za Wajib, Ibada za Sunnah, Ushairi, Ukoo na Makabila, Hikma na Utabibu

kama Aisha’

Naam bila ya shaka hili halishangazi kwani tunapomuangalia Aisha Radhi Allahu Anha

basi tunaona kua kutokana na ufahamu wake basi amekua ni miongoni mwa watu wanne

muhimu sana wanaotegemewa katika Ilm ya Fiqh na Hadith kwani Hadith zake ni Sahih

na ni zaidi ya 2000 ambapo anashindana na Abu Hurayrah, Abd Allah Ibn Umar na Anas

Ibn Malik Radhi Allahu Anhum kwa upokeaji wa wingi wa Hadithi na alikua si mwenye

kusita kuuliza jambo lolote kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam pale inapokua

hajafaham.

Aisha Radhi Allahu Anha alifariki katika siku ya Jumanne ya mwezi 17 Ramadhani ya

mwaka 57 Al Hijr huku akiwa na umri wa miaka 66.

UMM AL MU’MININ HAFSAH BINT UMAR IBN AL KHATTAB.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam asingeliweza kumpa talaka Umm al

Mu’uminin Hafsah Bint Umar Ibn Al Khattab ambae ni mtoto wa Sahaba Umar Ibn Al

Khattab, Imam Bukhari anasema kua siku moja Ansar mmoja aliingia katika nyumba ya

Umar Ibn Al Khattab na kusema ‘Ya Umar! kuna jambo baya sana limetokea’, Umar

akauliza ‘Jee kabila la Ghasan limetuvamia?’(Katika wakati huo kabila la Ghasan

lilikua linajitayarisha kuwavamia Waislam), Yule Ansari akajibu ‘La! Lakini limetokea

jambo baya zaidi ya hilo, kwani Rasul Allah amewataliki wake zake’, hapo Umar

akasema ‘Ama sasa hivi Hafsah ameangamia na kupotea’. Siku ya pili yake asubuhi

na mapema akaenda kwa bint yake Hafsa na akamkuta analia sana, na akamuuliza

‘Jee, Rasul Allah amekutaliki?’ nae akajibu ‘Sijui kwani, amejifungia chumbani

kwake’, hivyo Umar akaomba ruhusa ya kuingia chumbani kwa Rasul Allah, na

aliporuhusiwa, akamsalimia Rasul Allah na akamuuliza kuhusu undani wa

kuwataliki wake zake, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akajibu kua

hakuwataliki na hapo Umar akaridhika na jibu hilo’.


856

Hadithi hii inaonesha kua kwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kuwataliki

wake zake ni jambo kubwa sana kwa Waislamu kuliko hata kuvamiwa na Maadui zao.

Katika kipindi hicho Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alijitenga nao wake

zake hao kwa muda unaokaribia mwezi mmoja, kutokana na wake zake hao kutaka

kuongezewa kiwango katika matumizi yao ya maisha kwa sababu hali ya maisha yao

ilikua ni ngumu, hivyo Ummah wa Kiislamu ulifikiria kua Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam amewaacha wake zake, jambo ambalo lilileta tafrani miongoni mwao.

Kuna Hadith nyengine pia ambayo inasema kua kuliwahi kutokea mgogoro baina ya

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na Hafsa Bint Umar Ibn Al Khattab na

baada ya kufikiria kua wameachana, Umar Ibn Al Khattab akalalamika na kusema ‘Allah

hatomjali tena Umar na bint yake’, Hadith hizi na nyenginezo zinaoneyesha ukubwa

wa athari wa kutokea jambo kama hilo katika Ummah wa Kiislam.

Ambapo mwanzoni Hafsa Radhi Allahu Anha aliolewa na Khunis Ibn Hudhafa Ibn Qay

ambae alifanya Hijra mara mbili ambazo ni kelekea katika ardhi ya Uhabeshi na pia

Yathrib, na pia alipigana vita vya Badr na vita vya Uhud na akafariki kutokana na

majeraha aliyoyapata katika Vita vya Uhud, wakati Hafsa Radhi Allahu Anha akiwa na

umri wa miaka 18.

Hivyo Umar Ibn Al Khattab akawa na huzuni kubwa sana kutokana na tukio hili la binti

yake kua Mjane katika umri mdogo, basi akamfuata Abu Bakr Radhi Allahu Anhu na

kumtaka kua amuoe Hafsa lakini hata hivyo Abu Bakr Radhi Allahu Anhu akakataa kwa

sababu alimskikia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anataka kumuoa yeye Hafsa,

lakini hata hivyo Abu Bakr Radhi Allahu Anhu hakumwambia Umar Ibn Al Khattab

Radhi Allahu Anhu juu ya hilo, kwa sababu alikua anataka kua Umar Ibn Al Khattab

Radhi Allahu Anhu apate habari hio kutoka kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Na Umar Radhi Allahu Anhu alipoenda kwa Uthman Ibn Affan Radhi Allah Anhu

kumuomba amuoe bint yake basi na Uthman Radhi Allah Anhu nae akakataa kwani

alisema kua yeye ndio kwanza amefiwa na mke wake ampendae Ruqqayah Bint Rasul

Salallahu Alayhi wa Salam hivyo hawezi kuoa kwa wakati huo.

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipopata habari hio basi akatabasam na

kisha akasema: ‘Hafsa atapata Mume aliebora zaidi ya Uthman na Uthman ataoa

mwanamke bora kuliko Hafsa.’ Na Umar Radhi Allahu Anhu alifurahia sana habari hio

na hivyo akakubali kumuozesha Hafsa Bint Umar Radhi Allahu Anha kwa Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na ndoa yao ikafungwa katika mwaka wa 3 Al Hijra.

Na kisha Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu nae akaozeshwa binti wa pili wa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam aitwae Ummu Kulthoum Bint Rasul Radhi Allahu

Anha.


857

Kwa upande wa Hafsa Bint Umar Radhi Allahu Anha basi alikua na ukaribu sana na

Aisha Radhi Allahu Anha ambapo Hafsa Bint Umar Radhi Allahu Anha nae pia alikua ni

mwenye Ilm kubwa sana kutokana na kuihifadhi Qur’an ndani ya Moyo wake, ambapo

anasema Aisha Radhi Allahu Anha kuhusiana nae kua: ‘Hafsa alikua ni mtu mwenye

Msimamo katika Vitendo vyake na Kauli zake kama alivyokua Baba yake, Hakika

Hafsa alikua ni Mtoto wa Umar Ibn Al Khattab’

Hafsa Bint Umar Radhi Allahu Anha alifariki mnamo mwaka 47 Al Hijra hukua akiwa

na umri wa miaka 63.

UMM AL MU’MININ ZAYNAB BINT KUZAYMAH.

Umm al Mu’uminin Zaynab bint Khuzaymah Radhi Allahu Anha ambae pia anajulikana

kwa jina la Ummu ul Masakin kutokana na alikaa na Nabii Muhammad Salallahu Alayhi

wa Salaam kwa miezi minane halafu akafariki dunia baada ya kuumwa kwa mda mfupi

na hivyo kua ni Mke wa pili wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kufariki kabla

ya kufariki Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, na kua ni mke wa Kwanza Kusaliwa

Sala ya Jenenza na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Umm al Mu’uminin Zaynab bint Khuzaymah Radhi Allahu Anha alikua ni Mke wa Abd

Allah Ibn Jahsh Radhi Allahu Anhu ambae alikua ni Ibn Ami yake Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kwani Mama yake Abd Allah Ibn Jahsh Radhi Allahu Anhu alikua ni

Umamah Bint Abd Ul Muttalib, ambapo Abd Allah Ibn Jahsh Radhi Allahu Anhu alifariki

pia katika vita vya Uhud na hivyo kumuacha Zaynab Bint Khuzaimah Radhi Allahu Anha

akiwa mjane katika wakati huo ambao akiwa na umri wa miaka 30.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaepeleka posa yake kwa wazee wake

Zaynab Bint Khuzaymah Radhi Allahu Anha kwa ajili ya Kumsitiri, kwani amesema

Safwan Ibn Sulaim Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu A’alayhi

wa Salam kua: ‘Yeyote yule anaewahudumia Wajane na Masikini basi hua ni sawa

na Mwenyekupigana Jihad kwa ajili ya Allah Subhanah wa Ta’ala, hua sawa na

aliesimama kusali kwa miaka yote na aliefunga kwa miaka yote’’(Imam Tirmdhii)

Mama yake Zaynab bint Khuzaymah Radhi Allahu Anha alikua akiitwa Khawla na pia

kama Hind Bint Awf Ibn Zuyahr Ibn Harith ambae ndie anaejulikana kama ‘Mama

Mkwe Bora kuliko wote Ardhini’ na hii ni kwa sababu watoto wake wawili waliolewa

na Rasul Allah Salallahu Aalayhi wa Salam ambao ni Maymuna Bint Harith na Zaynab

Bint Khuzaymah na watoto wake wengine waliolewa na Masahaba mbali mbali.


858

Kwani Hind Bint Awf aliolewa zaidi ya mara 4, ambapo ndoa yake ya kwanza ilikua ni

kwa Jazi Al Zubaydi ambae alikua ni miongoni mwa Waislam wa mwanzo na

akachaguliwa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua ni Muweka Mahesabu wa

Jamii ya Kiislam.

Halafu Hind Bint Awf akaachwa na akaolewa na Harith Ibn Hazan ambapo ndoa hii

ikatoka watoto wanne ambapo wa kwanza ni Lubaba Al Kubra ambae ndie mwanamke

wa pili kusilimu na ndie aliekua mke wa Al Abbas Ibn Abd Ul Muttalib ambae ndie Ami

yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, na wa pili ni Maymuna Bint Harith ambae

aliolewa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, wa tatu ni Saayib Ibn Harith na wa

nne ni Qatn Ibn Harith.

Halafu Harith Ibn Hazan akafariki na Hind Bint Awf akaolewa na Khuzaymah Ibn Harith

Al Hilali ndo ambayo ilitoa mtoto wa kike mmoja tu aitwae Zaynab Bint Khuzaymah

ambae aliolewa na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Halafu Hind Bint Awf akaachwa na akaolewa na Umays Ibn Maad Ibn Tamim ndoa

ambayo ilitoa watoto watatu ambao ni Asma Bint Uways ambae aliolewa na Rabia Ibn

Riyab, na kisha akaolewa na Jafar Ibn Abi Talib Ibn Abd ul Muttalib, na kisha akaolewa

na Abu Baqr As Siddiq na kisha akaolewa na Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhum.

Mtoto wake wa pili ni Salma Bint Uways ambae aliolewa na Hamza Ibn Abd Al Muttalib

aliekua Ami yake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, na kisha akaolewa na Shaddad

Ibn Usama.

Na mtoto wake wa tatu katika ndoa hii alikua ni Awn Ibn Umays.

Halafu Hind Bint Awf akaachwa na akaolewa na Al Harith Ibn Hazan ambae alikua na

mke mwengine aitwae Fakhta Bint Amr ambae mtoto wake wa kike ni Al Lubaba Al

Saghir ambae ndie Mama yake Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu.

Hivyo Lubaba Al Kubra Bint Harith Ibn Hazan Al Hilal alikua ni mtu mwenye asili ya

Yemen kama alivyokua mama yake ambae ni Hind Bint Awf kwani kabila lao halikua ni

la Quraysh bali lilikuani lenye asili ya Yemen, ila lilikua ni kabila linaloheshimika,

ambapo ndoa baina Lubaba Al Kubra na Abbas Ibn Abi Talib iliyotoa watoto 7 ambao

ni Al Fadhl, Abdullah, Ubaydullah, Quthum, Mabad, Abdur-Rahman na Umm Habib.

Miongoni mwa sifa za Zaynab bint Khuzaymah Radhi Allahu Anha ni kama

zinavyoelezewa na Aisha Radhi Allahu Anhu pale aliposema: ‘Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alituambia sisi wake zake kua: ‘Miongoni mwenu atakakutana na

mie mwanzoni Akhera ni yule mwenye Mikono mirefu’’(Imam Bukhari) na bila ya


859

shaka miongoni mwa Wake zake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi aliekua na

mikono miruf kwa kutoa Sadaka ni Zaynab Bint Khuzayama Radhi Allahu Anha ambae

kutokana na kutoa kwake na kusaidia watu kwa ukarimu wake mkubwa basi alipewa jina

la Ummu al Masakin.

Ambapo safari moja kuna Masikini alipita kwenye nyumba yake Zaynab Bint Khuzayma

Radhi Allahu Anha akiwa hana chakula hivyo Zaynab Bint Khuzayma Radhi Allahu Anha

akampa chakula cake pekee kilichobakia nyumbani kwake yaani chakula cha usiku chote

na hivyo kwa usiku wa siku hio Zaynab Bint Khuzayma Radhi Allahu Anha akalala na

njaa, baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kujua juu ya tukio hilo basi ndio

akasema maneno ambayo ndio ya ile hadithi isemayo: ‘Kama ukiwa unamuamini Allah

Subhanah wa Ta’ala kama inavyostahiki basi atakuruzuku riziki yako, kama vile

ambavyo anavyowaruzuku Ndege ambapo asubuhi hua wanatoka kwenye vijumba

vyao wakiwa na njaa lakini hua ni wenye kurudi Usiku huku wakiwa wameshiba.’

UMM AL MU’MININ RAYHANA BINT ZAYD

Umm al Mu’uminin Rayhana bint Zaid ambae alikua ni mwenye asili ya Kiyahudi kutoka

katika kabila la Banu Nadir ambapo baaada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kulishinda Jeshi la Banu Qurayza katika Vita vya Khaybar kutokana na kuwazingira kwa

siku 25 na kutaka wajisalimishe, lakini wakatakataa na hivyo Wanaume wote wa Banu

Qurayza wakauliwa wakabakishwa Wanawake na Watoto ambao walifanywa kua

Watumwa wa Waislam.

Rayhan Bint Zayd alikua ni miongoni mwa Wanawake wazuri sana waliokua wajane

katika tukio hilo, na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akataka kumuoa lakini

Rayhana kwanza akakataa kutokana na kua na mapenzi makubwa sana kwa Mume wake

aliefariki, lakini baada ya mda akasilimu na kisha akolewa na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kama anavyosema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Sad Al Basr

Al Hashim kua:

‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimteka Rayhana Bint Zayd Ibn Amr Ibn

Khunafa, ambae alikua na Mumewe ambae alikua akimpenda sana, hivyo nae

akasema kua: ‘Sitompenda Yeyote baada yake (Mume wake)’ na alikua ni

Mwanamke Mzuri sana, Rayhana amesema kua: ‘Na wakati Watu wa kabila la

Qurayza walipotekwa, basi Wanawake waliletwa mbele ya Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam. Na mimi nilikua ni mmoja wao mingoni mwao, ambapo

niliamrishwa kuja mbele yake kisha nikategenashwa na wengine, na hivyo nikawa

ni sehemu ya Ngawira ambazo ni kwa ajili yake.


860

Nilipotengenishwa na wengine basi Allah alikua amenichagua na kisha wakanituma

kwenye Nyumba ya Umm al Mundhir Salma Bint Qays kwa ajili ya kukaa kwa siku

kadhaa, hadi pale Mateka walioasi walipoadhibiwa na Wanawake wakagawanywa.

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaja mbele yangu huku mimi nikiwa

nimejawa na aibu, na kisha akakaa mbele yangu na kusema: ‘Kama Ukimchagua

Allah na Rasul Allah, basi Rasul Allah nae atakuchagua wewe kwa ajili yake’ Hivyo

Nami nikajibu: ‘Kwa hakika mimi nimemchagua Allah na Rasul Allah.’

Nilisilimu basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaniwachia huru, na kisha

akanioa, na akanipa Waqqiya 12 na nahssha moja amabcho ni kiasi alichoawalipa

wake zake wengine kwa ajili ya Mahari yao. Akanichukua mimi kama mke wake

na kunipeleka kwa Ummu ul Mundhir na akanichukua na nikawa navaa Hijab.’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimpenda sana na kumfurahia na alimpa

kila alichokitaka. Na ndio maana akamwambia kua: ‘Kama ungemuomba Rasul

Allah kuhusiana na Banu Qurayza basi angewaachia huru’ na Rayhana alikua

akisema: ‘Kamwe hakua peke yake kabla ya kuwagawanya Mateka’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimuoa katika mwezi wa Muharram mwaka

wa 6 baada ya Hijra na alikaa nae hadi pale alipofariki baada ya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kurudi Hija.’

UMM AL MU’MININ HIND UMMU SALAMAH.

Kuhusiana na Umm al Mu’uminin Hind (Ummu Salamah), alikua pia ni mjane wa Abd

Allah ibn ‘Abd al Asad, ambae alikua akijulikana kama Abu Salamah ambae alikua ni

mtoto wa shangazi yake Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, aliekua akiitwa

Barah bint Abd Al Muttalib na pia alikua ni kaka yake wa kulelewa. Nao pia walihamia

Uhabeshi, Abu Salama na baada ya kurudi Abu Salamah akawa ni miongoni mwa

waliofariki katika vita vya Uhud, na kuwacha mjane, Hind ambae pia alikua ni mtu

mzima na alikua na watoto mayatima wanne. Hivyo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam akaamua kumuoa ili amhifadhi na kumsaidia ulezi wa mayatima hao.

Umm al Mu’uminin Hind au Umm ul Mu’uminin Ummu Salamah Radhi Allahu Anha

hakukubali moja kwa moja kuolewa na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

kwa kusema kua alikua ni mtu mzima sana, mwenye watoto na kimaumbile ni mtu

mwenye wivu sana, hivyo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam hakujali sana

kuhusiana na umri wa Ummu Salamah kwani kwa sababu ya utu uzima wake alikua

akihitaji kuhifadhiwa na kuhudumiwa na hivyo akamwambia, ‘Ama kwa watoto wako

nitawashughulikia, na kuhusiana na wivu wako nitamuomba Allah auondoe’


861

Miongoni mwa sifa tukufu za Umm Salama Radhi Allahu Anha ni kua mbali ya kua

alikua ni mwanamke mzee miongoni mwa wake wa Rasul Allahu Alayhi wa Salam lakini

alikua ni mwanamke mwenye ari kubwa sana ya kutafuta Ilm na hivyo alikua ni makini

sana katika kufuatilia Hadithi za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na pia likua ni

Mwanamke ambae sauti nzuri sana na ya kuvutia katika usomaji wake wa Qur’an.

Siku moja Abu Hurayrah Radhi Allahu Anhu alisema: ‘Mtu yeyote yule ambae aliekua

na janaba katika usiku wa mwezi wa Ramadhani basi ni wajibu wake kujitoharisha

kabla ya Alfajir au funga yake itabatilika’ ambapo habari hii ilipomfika Umm

Salama Radhi Allahu Anha basi akasema: ‘La, hii sio sahih kwani Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alipokua katika hali kama hii basi alikua ni mwenye

kuendelea kufunga’

Hivyo Uthibitisho huu wa Umm Salama Radhi Allahu Anha umekua ndio hukmu juu ya

jambo hili kwa kila mwenye kuamka na Janaba katika mwezi wa Ramadhani basi Janaba

hua halibatilishia funga yake. Miongoni mwa Hadith alizonukuu Ummu Salama Radhi

Allahi Anha ni 378.

Na kutokana na Busara zake Ummu Salama Radhi Allahu Anha basi Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam alikua akisikiliza ushauri wake na moja kati ya mfano wa

hilo ni pale baada ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kusaini Mkataba wa

Hudaybiyyah, aliposema kuwaambia Masahaba zake ‘Nyanyukeni, mchinje wanyama

wenu na kisha mnyoe nywele zenu’, hata hivyo hakuna hata Sahaba mmoja alienyanyua

mguu wake kufanya vile alivyoamrisha Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam,

kutokana na kuvunjika moyo kwa yale yaliyotokea katika makubaliano ya mkataba huo.

Hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akanyanyuka na kuenda kwa Ummu

Salama Radhi Allahu Anha na kumwambia yaliyotokea na hapo Ummu Salama Radhi

Allahu Anha akamwambia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ‘Ya Rasul

Allah, unataka maneno yako yafanyiwe kazi? Basi nenda nje na usizungumze na

mtu yeyote hadi pale utakapomaliza kuchinja mnyama wako na kunyoa nywele

zako’, hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akatoka nje akachinja

mnyama wake na kuanza kunyoa nywele zake, na baada ya Masahaba kumuona Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam anafanya hivyo basi na wao wakanyanyuka na

kufanya kama vile alivyokua akifanya. (Imam Bukhari)


862

UMM AL MU’MININ MAYMUNA BINT HARITH IBN HAZAN AL

HILALIEH

Ama kuhusiana na Maymuna Bint Al Harith Ibn Hazan Ibn Bujair, Ibn Al Hazm Ibn

Rubwaiba Ibn Abdullah Ibn Hilal Ibn Amir Ibn Sa'sa'a Al-Hilaliyya ambae pia

anajulikana kwa jina Barra basi ni mtoto wa Hind Bint Awf ambae tayari

tumeshamzungumzia tulipomzungumzia mke wake Al Abbas Ibn Abd Ul Muttalib

Radhi Allahu Anhu ambae pia ndie Mama ya Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu.

Ambapo Maymuna alikua ni Mwanamke Mtukufu na ni mwenye hamu ya kuolewa na

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, kutokana na kumpenda kwake sana Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na kutokana na kushindwa kujizuia kwake basi akamfuata

dada yake ambae ni Umm Fadhl ambae ndie mama yake Abd Allah Ibn Abbas Radhi

Allahu Anhu, na alipomuelezea kuhusiana na mapenzi yake hayo na hamu yake ya

kuolewa kwake na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi Umm Fadhl

akazungumza na Mumewe ambae ni Al Abbas Radhi Allahu Anhu ambae ndie Ami yake

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Hivyo Al Abbas Radhi Allahu Anhu akafikisha ujumbe wake huo wa Maymuna Bint

Harith Radhi Allahu Anha kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae nae

akaupokea na kuyakubali maombi hayo ya kumuoa Maymuna Bint Harith. Habari za

kukubaliwa kwa maombi yake hayo zilipomfika mwenyewe Maymuna Bint Hartith basi

alikua amekaa Juu ya Ngamia wake, na hivyo hapo hapo akashuka na kusema kua:

‘Ngamia na kilichokuwepo juu ya Ngamia hapo awali vyote ni vya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam.’

Ndoa yao hii ilifungwa mnamo mwezi wa Shawwal wa mwaka wa 7 Al Hijra mara tu

baada ya Makubaliano ya Huddaybiyah, ambapo Waislam waliruhusiwa kuingia katika

Mji wa Makkah kwa ajili ya kufanya Umra, ambapo baada yake Allah Subhanah wa

Ta’ala akashusha aya ifuatayo:

‏﴿َٰٰي ُّهَا ٱلن َّبىِ ُّ إِ َّ أَحْلَلْنَا لَكَ‏ أَزْوَاجَكَ‏ ٱللا َّتيِ‏ ۤ آتَيْتَ‏ أُجُورَهُن َّ وََما مَلَكَتْ‏ يمَِينُ‏ ‏َك

ممِ َّآ أَفَآءَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلَيْكَ‏ وَبَنَاتِ‏ عَمِّكَ‏ وَبَنَاتِ‏ عَم َّاتِكَ‏ وَبَنَاتِ‏ خَالِكَ‏ وَبَنَاتِ‏

خَالاَتِكَ‏ ٱللا َّتِى هَاجَرْنَ‏ مَعَكَ‏ وَٱمْرَأَةً‏ م ُّؤْمِنَةً‏ إِن وَهَبَتْ‏ نَفْسَهَا لِلن َّبىِ‏ ِّ إِنْ‏ أَرَاَد

ٱلن َّبىِ ُّ أَن يَسْتَنكِحَهَا خَالِصَةً‏ ل َّكَ‏ مِن دُونِ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ قَدْ‏ عَلِمْنَا مَا فَرَضْنَا عَلَيْهِمْ‏


863

فيِ‏ ۤ أَزْوَاجِ‏ هِمْ‏ وَمَا مَلَكَتْ‏ أَيمَْانُهُمْ‏ لِكَيْلاَ‏ يَكُونَ‏ عَلَيْكَ‏ حَرَجٌ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ غَفُوراً‏

ر َّحِ‏ يماً‏ ﴾

Ya ayyuha alnnabiyyu inna ahlalna laka azwajaka allatee atayta ojoorahunna

wama malakat yameenuka mimma afaa Allahu AAalayka wabanati AAammika

wabanati AAammatika wabanati khalika wabanati khalatika allatee hajarna

maAAaka waimraatan mu/minatan in wahabat nafsaha lilnnabiyyi in arada

alnnabiyyu an yastankihaha khalisatan laka min dooni almu/mineena qad

AAalimna ma faradhna AAalayhim fee azwajihim wama malakat aymanuhum

likayla yakoona AAalayka harajun wakana Allahu ghafooran raheeman(Surat Al

Ahzab 33:50)

Tafsir: Ewe Nabii (Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam)! Kwa Hakika

tumekuhalalishia wake zako, ambao umewalipia mahari yao, na ambao mkono wako

wa kulia unawamiliki (wanawake waliotekwa vitani na watumwa) ambao Allah

amekupa, na binti wa Ami zako, bint wa Ammah (shangazi) zako, binti wa Khal

(wajomba) zako, binti wa Khalah (mama wadogo) ambao walihama (kutoka Makkah)

pamoja nawe, na mwanawake alieamini ikiwa atajipeleka (kutaka kuolewa) kwa

Mtume, na Mtume akataka kumuoa; Haki ambayo ni yako tu (kwa Nabii Muhammad

peke yake), lakini si kwa waumini wengine. Hakika tunajua ni kipi tulichowaamrisha

kuhusiana na wake zao na wale wanaomilikiwa na mikono yao ya kulia - Ili kusiwe na

uzito kwako wewe. Na Allah ni mwingi wa Kusamehe na mwingi wa Rehma.

Ingawa alikua akiitwa Barra lakini Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimbadilisha

jina na kumuita Maymuna ambalo ni lenye kumaanisha Mtu alieneemeshwa, na hii ni

kwa sababu Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua anapenda majina Mazuri na

pia alimuoa katikamwaka wa 7 Al Hijra ambao ulikua ni mwaka wa Utulivu ndani yake.

Ambapo anasema Aisha Radhi Allahu Anha kua: ‘Miongoni mwetu basi alikua na

Taqwa zaidi alikua ni Maymuna Bint Harith, na alikua ni mweye kupenda

kuunganisha Udugu, na kutokana na sifa hii basi ndio maana Rasul Allah Salallhu

Alayhi wa Salam akasema: ‘Myamuna na Umm Fadhl na Salam na Asmaa ni

Madada waumini’’

Miongoni mwa Hadith zinazojumuisha watu wa watatu wa Familia ya Rasul Salallahu

Alayhi wa Salam na hapo hapo watu watatu wa Maymuna Bit Harith Radhi Allah Anha

ni ile inayoelezea kuhusiana na Bidaa Hasan yaani Bidaa nzuri ambayo ingawa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakuyafanya, lakini hata hivyo hakuwakataza watu


864

kutoyafanya, na watu waliojumuishwa kwenye hadithi hii ni Maymuna Bint Harith Radhi

Allahu Anha, Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu ambae mama yake ni Umm Fadhl

Radhi Allahu Anha na Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu ambae mama yake ni Lubaba

Al Saghira Radhi Allahu Anha ambapo wote Mama hao wawili ni madada zake Maimuna

Bint Harith Radhi Allahu Anha.

Imam Malik anasema kutoka kwa Ibn Shihab kutoka kwa Abu Umama Ibn Sahl Ibn

Hunayf kua ‘Amesema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu: ‘Amesema Khalid

Ibn Walid kua alimtembelea Maymunah pamoja na Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam, nae Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akapewa

nyama ya mjusi mkubwa wa jangwani wa kuchoma, Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam akanyoosha mkono wake kuchukua, ambapo baadhi ya

wanawake waliokuweo katika nyumba ya Maymunah wakamwambia Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam juu ya kile anachotaka kukila, na hapo

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akarejesha mkono wake. Khalid Ibn

Walid anasema: Mimi nikasema ‘Ya Rasul Allah, jee ni Haram?’ Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam akasema ‘La! Ila hakuna katika ardhi ya watu wangu

na sijisikii kuipenda nyama hiyo’ Khalid Ibn Walid anasema ‘Mimi nikaendelea

kuitafuna na kuila huku Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

akiniangalia’ ’.

Anasema Imam Muhamamd Ibn Saad kua: ‘Amesema Maymuna kua siku moja Rasul

Allah Sallahu Alyhi wa Salam alitoka chumbani mwangu nami nikamfungia mlango,

na baadae akarudi na kugonga mlango lakini mimi nikagoma kumfungulia mlango

na kumwambia kua : ‘Unaenda kwa wke zako wengine katika usiku wangu?’ nae

Rasul Allah Salallahu Alahyi wa Salam aakajibu kwa kusema: ‘La sikufanya hivyo

bali Mkojo ulikua hautaki kutoka’

Maymuna Bint Harith alikua pia ni mwalimu wa Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu

Anhu ambae alikua ni shangazi yake pia ambapo mamo mwaka 51 Al HIjra alipofariki

Maymuna basi Ibn Ataa kua: ‘Wakati Maymuna alipofariki, mimi nilienda Mazikoni

na Abd Allah Ibn Abbas ambae alikua akiwaambia watu: ‘Msimtikise, kuweni na

upole nae kwanini Mama yangu’’

Ambapo anasema Imam Abu Sulayman Hamd ibn Muhammad Al Khattabi Al Busti kua:

‘Maymuna Radhi Allahu Anha ana Hadith 7, ambapo mbili katika yake zimo katka

Sahih Muslim na Sahih Bukhari, moja imenukuliwa katika Bukhari peke yake na

5 zimenukuliwa kwenye Sahih Muslim hivyo hadith zake kwa ujumla ni 13’


865

UMM AL MU’MININ ZAYNAB BINT JAHSH.

Mke wake wa tano alikua ni Umm al Mu’uminin Zaynab Bint Jahsh. Ilikua ni dasturi ya

waarabu kuwachukulia watoto wa kulea kuwapa jina la baba mlezi na hivyo kua kama

watoto wao wa kuwazaa hususan katika mambo ya harusi na mirathi, hivyo mke

alieachika wa mtoto wa kulea hawezi kuolewa na baba yake mlezi. Baada ya kuingia

Uislam, Allah Subhanahu wa Ta’ala alitaka kuondoa desturi hii na kutaka kuwepo kwa

tofauti baina ya mtoto wa kulea na mtoto wa kuzaa, mtu anaweza kulea mtoto lakini

mtoto huyo haruhusiwi kuchukua asili ya baba yake mlezi, ni lazima achukue asili na jina

la baba yake mzazi.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua na mtoto wa kulea aliekua akiitwa

Zayd Ibn Harith, ambae kama tulivyoona hapo kabla kua alikua mtumwa, aliezawadiwa

Bi Khadija Bint Khuwaylid Radhi Allahu Anha, kisha nae akampa Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam kama msaidizi wake hivvyo Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salaam akawa anamlea na akawa anaitwa Zayd Ibn Muhammad, na baada ya

muda ukashuka wahy ambao ulikua unashurutisha watoto wa kulea kuchukua na kutumia

majina ya baba mzazi kwa ajili ya kusimamia haki na ili kulinda asili ya watoto hao,

hivyo Zayd Ibn Muhammad akabadilishwa jina na kurudishwa katika asili yake na akawa

anaitwa Zayd Ibn Harith.

Na akasema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Yeyote yule ambae anadai

kua Fulani ni baba yake wakati akiwa ni mwenye kujua kua si Baba yake basi Mtu

huyo anaharamishiwa Pepo’ (Sahih Muslim)

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akamuozesha mtoto wake huyo wa kulea

kwa binamu yake ambae ni Zaynab Bint Jahsh ambae alikua akitoka katika miongoni

mwa familia tukufu ya Quraysh, kutokana na utofauti wao wa kidarja na kimaisha, ndoa

hiyo baina ya Zayd Ibn Harith na Zaynab Bint Jahsh haikudumu mda mrefu na hivyo

wakaachana.

Allah Subhanahu wa Ta’ala akamjaalia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

kumuoa Zaynab Bint Jahsh na kushusha aya katika Qur’an kuhusiana na jambo hili pale

aliposema:

‏﴿وَمَا كَانَ‏ لِمُؤْمِنٍ‏ وَلاَ‏ مُؤْمِنَةٍ‏ إِذَا قَضَى ٱهلل َُّ‏ وَرَسُولُهُ‏ أَمْراً‏ أَن يَكُونَ‏ لهَُمُ‏ ٱلخِْيَرَةُ‏ مِ‏ ‏ْن

أَمْرِهِمْ‏ وَمَن يَعْصِ‏ ٱهلل ََّ‏ وَرَسُولَهُ‏ فَقَدْ‏ ضَل َّ ضَلاَلاً‏ م ُّبِيناً‏ ﴾


866

Wama kana limu/minin wala mu/minatin idha qadha Allahu warasooluhu amran

an yakoona lahumu alkhiyaratu min amrihim waman yaAAsi Allaha warasoolahu

faqad dhalla dhalalan mubeenan (Surat Al Ahzab 33:36).

Tafsir: Si juu ya Waumini wa Kiume wala Waumini wa Kike pale Allah na Mtume

wake wanapoamrisha kitu, kwao wao kua na hiari yeyote juu ya maamuzi yao, na

anaemuasi Allah na Mtume wake, hua amepotea na kuingia katika dhulma kubwa.

Na kisha aya inayofuatia katika Sura hiyo inaendelea kwa kusema kua:

‏﴿وَإِذْ‏ تَقُولُ‏ ۤ لِل َّذِي أَنعَمَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلَيْهِ‏ وَأَنْعَمْتَ‏ عَلَيْهِ‏ أَمْسِ‏ كْ‏ عَلَيْكَ‏ زَوْجَكَ‏ وَٱت َّقِ‏ ٱهلل ََّ‏

وَتخُْفِى فىِ‏ نِفْسِ‏ كَ‏ مَا ٱهلل َُّ‏ مُبْدِيهِ‏ وَتخَْشَى ٱلن َّاسَ‏ وَٱهلل َُّ‏ أَحَق ُّ أَن تخَْشَاهُ‏ فَلَ َّما قَضَ‏ ٰ ى

‏ْم

زَيْدٌ‏ مِّنْهَا وَطَراً‏ زَو َّجْنَاكَهَا لِكَىْ‏ لاَ‏ يَكُونَ‏ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ حَرَجٌ‏ فيِ‏ ۤ أَزْوَاجِ‏ أَدْعِيَآئِهِ‏

إِذَا قَضَوْاْ‏ مِنْهُن َّ وَطَراً‏ وَكَانَ‏ أَمْرُ‏ ٱهلل َِّ‏ مَفْعُولاً‏ ﴾

Wa-idh taqoolu lilladhi anAAama Allahu AAalayhi waanAAamta AAalayhi amsik

AAalayka zawjaka waittaqi Allaha watukhfee fee Nafsika ma Allahu mubdeehi

watakhsha alnnasa waAllahu ahaqqu an takhshahu falamma qadha zaydun minha

wataran zawwajnakaha likay la yakoona AAala almu/mineena harajun fee azwaji

adAAiya-ihim itha qadaw minhunna wataran wakana amru Allahi mafAAoolan

(Surat Al Ahzab 33:37)

Tafsir: Na kumbuka pale ulipomwambia yeye (Zayd Ibn Harith) ambae juu yake Allah

amemuongoa (kwa kumuingiza katika Uislam), nawe (Muhammad pia) umemsaidia

(kwa kumkomboa utumwani), ‘Kaa nae Mke wako na muogope Mola wako’, lakini

kama ungelificha ndani ya Nafsi yako (kile alichokuwekea wazi Allah kua atakupa

Zaynab umuoe) kile Allah alichoweka wazi, ungeliwaogopa watu ambapo Allah ana

haki zaid ya kuogopewa, hivyo baada ya Zayd kutimiza hamu yake (kwa kumuacha),

Sisi tumekupa wewe umuoe, ili (baadae) iwe kuwe hakuna ugumu kwa Waumini

kuhusiana na (kuwaoa) wake wa watoto wa kuwalea wakati watoto hao wakiwa

hawana haja nao tena (Wameaacha). Na amri ya Allah ni lazima itekelezwe.

Dhumuni na kusudio la ndoa hii lilikua ni kukata mzizi mkuu wa desturi ya Jamii za

Kiarabu za kutoruhusu kuwaoa wake waliotalikiwa na watoto wao wa kulea. Na hapo

hapo kudhihirisha uthibitisho wa kufungishwa kwa Ndoa hio baina ya Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na Zaynab Bint Harith Radhi Allah Anha kutoka Mbinguni,


867

na hivyo Zayna Bint Harith Radhi Allahu Anha akawa ni mwenye kujisifu mbele ya Wake

wenzake wa Rasul Allah Salallah Alayhi wa Salam kwa kusema: ‘Hakika ni familia

zenu ndio zilizowafungishieni ndoa zenu lakini Ndoa yangu mimi imefungishwa na

Allah Subhanah wa Ta’ala kutoka kwenye Arshi yake.’ Na pia alisema: ‘Hakika

mimi nimekua na Walii bora kwani nyinyi ni familia zenu ndio zilizowafungishieni

ndoa zenu lakini Ndoa yangu mimi imefungishwa na Allah Subhanah wa Ta’ala

kutoka juu kwenye Mbingu ya 7.’

Ambapo kutokana na kuhisi utukufu wake na utofauti wake kidarja na wake wengine wa

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam basi Zaynab Bint Harith Radhi Allahu Anha

alikua ni mwenye kupenda sana kusali kuliko kitu chochote kile, kiasi ya kua hali ilifikia

kama anavyosema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Siku moja Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam aliingia Msikitini akakuta kuna kamba inaning’inia

baina ya nguzo mbili, hivyo akauliza: ‘Hii kamba ya nini?’ nae akajibiwa kwa

kuambiwa kua: ‘Ni kwa ajili ya Zaynab Bint Harith ambayo hua anaitumia

kujishikizia wakati anapokua amechoka kutokana na kusali sana na kwa mda

mrefu’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Ifungueni, kwani

Mtu anatakiwa asali wakati akiwa anajisikia yuko vizuri na mwenye umakini,

lakini anapokosa umakini au anapokua amechoka basi hua anatakiwa apumzike’’

Hivyo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam hakuweza kumtaliki mke wake

huyu kwa sababu ndoa yake hii ilikua imeshaandikwa na kuozeshwa na Allah Subhanahu

wa Ta’ala na pia mke huyo alikua anatoka katika ukoo mtukufu.

UMM AL MU’MININ RAMLA BINT ABU SUFYAN – UMMU HABIBA.

Mke wa sita wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua ni Umm Al

Muuminun Ramlah Bint Abu Sufyan au Umm Al Muuminun Ummu Habibah, alikua ni

mtoto wa Abu Sufyan ambae alikua ni mmoja kati ya mtu mkubwa na mwenye cheo

kikubwa katika kabila la Quraysh, Ummu Habibah aliingia katika Uislam na kupingana

na wazee wake na pia akahamia Uhabeshi yeye pamoja na mumewe aliekua akiitwa

Ubaidullah Ibn Jahsh ambapo baada ya kufika Uhabeshi, Ubaidullah aliingia katika

Ukristo na kumshawishi sana Ummu Habiba kuingia katika dini hiyo, lakini hata hivyo

Ummu Habibah akakataa, ingawa alikua Ummu Habibah ameachana na mume wake

huyo huku akiwa na mtoto wake mchanga aitwae Habibah, lakini Ummu Habibah alikua

na msimamo madhubuti ‘Mashaallah’ hakutetereka wala kuwa na wasi wasi wowote

bali alibakia na Imani yake ya Uislam na kuzidi kuikumbatia.


868

Subhana Allah! Ummu al Muuminina Ramlah Bint Abu Sufyan, Umm Habiba alibakia

na ile Imaan iliyomtoa katika giza la Ujahiliyyah na kumuingiza katika mwangaza, Imani

ambayo ilimfanya kua miongoni mwa Muhajirina wa mwanzo waliohama kwa ajili ya

kuinusuru na kuendeleza dini yao ya Kiislam, Imaan ambayo ndio ilimtoa katika mji wa

Makkah na kumpeleka katika ardhi ngeni ya Uhabesh na huko akabakia peke yake na

kumpoteza mume wake. Iman ambayo ilimtenganisha na iliyomvua cheo, hadhi ya

ukubwa unaotokana na jina la familia yake, ilimnyima utajiri na mali iliokuwepo katika

familia yake, familia ya kiongozi mkuu wa mji wa Makkah ambae ni Abu Sufyan.

Siku moja Ummu Habiba alilala kisha akaota kua ndani ya ndoto yake kuna mtu

anamwita: ‘Ya Umm Ul Muuminin!’ ambapo akaitafsiri ndoto hii maana yake kua

atakua ni mke wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam. Hazikupita siku nyingi

mara siku moja wakati yuko nyumbani kwake katika ardhi ya Habeshi akasikia Mlango

wake ukiwa unagongwa na alipoufungua mlango huo akakutana na Mfanyakazi wa Kike

wa An Najash ambae alileta Ujumbe kwa ajili yake kutoka kwa Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam kupitia kwa An Najash usemao kua Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam anataka amuoe Umm Habiba ili awe mke wake.

Ummu Habiba hakuamini masikio yake hivyo akamumba Mfanyakazi huyo wa An

Najash aurudie ujumbe huo mara 3 na kisha akasema: ‘Alhamd Lillah, Hakika Allah

amekupa Habari njema sana ewe Ummu Habibah.’ Na hapo hapo akavua mapambo

yote aliyokua nayo kwa furaha zake na kumpa Mtumwa huyo wa Mfalme Najash. Na

baada ya hapo Waislam waliokua kwenye ardhi ya Habeshi wakakusanyika kwenye

Kasri la An Najash kushuhudia ndoa hio ambayo ilifungishwa na An Najash mwenyewe

na Walii wa Ummu Habiba Radhi Allahu Anha akawa ni Khalid Ibn Said Radhi Allahu

Anhu ambae nae alikua ni mwenye kutoka katika Ukoo wa Banu Ummayah anaotoka

Umm Habiba pia.

Kisha ikafanywa Karamu kubwa na hii ilikua ni siku ya furaha kubwa sana ambapo

Ummu Habiba Radhi Allahu Anha mwenyewe anaielezea kwa kusema: ‘Wakati

nilipopokea Mahari yangu, basi nikachukua Mithakal 50 za dhahabu na kumtumia

yule mfanyakazi ambae alieniletea habari njema hizo kwa mara ya kwanza na

kumwambia : ‘Nakupa tena kile nilichokupa kwa sababu kwa wakati ule nilikua

sina pesa’ ambapo baadae Mfanyakazi huyo akanirudishia zile dhahabu nilizompa

mwanzo na kisha akanipa kisanduku ambacho kilikua kina Kidani nilichompa

hapo kabla, huku akisema: ‘An Najash ameniambia kua nisichukue kitu chochote

kutoka kwako, na badala yake amewaamrisha Wanawake wa Nyumbani kwake

kukuzawadia wewe Mafuta mazuri ya manukato ’’

‘Katika siku iliyofuata basi Yule mfanyakazi akaniletea mafuta ya manukato ya

kila aina na kisha akasema: ‘Nakuomba unisaidie kitu kimoja, kwani mimi sasa hivi

nimeingia kwenye Dini ya Kiislam na namfuata Rasul Allah Salallahu Alayhi wa


869

Salam, hivyo nifikishie Salam zangu kwake na mwambie kua Mimi namuamini

Allah na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, nakuomba usisahau tafadhali.’’

Mnamo mwaka wa 7 Al Hijra basi Waislam waliokua wakishi katika Ardhi ya Uhabeshi

wakarudi katika Mji wa Madina ambapo miongoni mwao alikuwemo pia Umm Habiba

ambae anaelezea hali ilivyokua kwa kusema: ‘Wakati Rasul Allah Salalalhu Alayhi wa

Salam nilipokutana nae, basi nikamwambia kuhusiana na mipango yote ya harusi

namna ilivyokua imetayarishwa, na kuhusiana na uhusiano wangu na yule

Mfanyakazi wa kike, na kumwambia kua amekua Muislam na anamtumia salam

zake kwake, ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawa amejawa na

furaha kutokana na habari hizo na akasema: ‘Wa Alayha as Salaam wa Rahmat

Allahi wa Barakatuh’’

Umm Habiba Radhi Allahu Anha alikua ni mwanamke aliejitolea kwa ajili ya kutii

maamrisho ya Allah Subhaanh wa Ta’ala na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kiasi ya kua mara tu baada ya Makafiri wa Makkah, walipovunja makubaliano ya

Hudaybiyah basi wakaamua kutafuta suluhisho jipya kuhusiana na makubaliano hayo.

Hivyo wakamtuma Abu Sufyan kwa ajili ya kuenda Madina kwa ajili ya Kuzungumza

na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Hivyo Abu Sufyan alipofika akaenda kwanza kwa Bint yake ambae ni Umm Habiba

Radhi Allahu Anha ambae alikua na hamu nae sana kwa sababu hajamuona kwa mda wa

takriban miaka 6 na alipofika Chumbani kwake na kusalimiana nae basi akataka kukaa

Kitako kwenye kitanda kilichomo ndani yake, lakini Umm Habiba akamkataza kua

hatakiwi hata kukaa kwenye kitanda hicho.

Hivyo Abu Sufyan akauliza: ‘Kwanini? Jee mimi ni mzuri zaidi kukaa kwenye

kitanda hicho au?’ ambapo Umm Habiba akasema kumwambia Baba yake: ‘Itakuaje

Adui Mkubwa wa Uislam awe ni mwenye kukaa kwenye Kitanda cha Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam?’

Ingawa hali ilikua ni hivyo lakini mwaka mmoja baadae Umm Habiba Radhi Allahu Anha

alifurahi sana pale aliposikia kua Baba yake huyo na kaka yake yaani Abu Sufyan na

Muawwiya wamesilimu na kua Waislam, na hivyo akasujudu kwa ajili ya Kumshukuru

Allah Subhanah wa Ta’ala. Ummu Habiba Radhi Allahu Anha aliofarikai mnamo mwaka

44 Al Hijra akiwa na umri wa miaka 70

Hivyo ndoa hii baina ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na Ramlah Radhi

Allahu Anha ikawa ndio sababu kubwa iliyomfanya Abu Sufyan aingie katika Uislam

mwaka mmoja tu baadae. Tafakar ingelikuaje kama Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam angelimuacha Ummu al Muuminun Ramlah Bint Abu Sufyan.


870

UMM AL MU’MININ JUWAYRIYAH BINT HARITH.

Mke wa saba wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua ni Ummu Al

Muuminun Juwayriyyah Bint Al Harith ambae alikua ni mtoto Chifu mkuu wa kabila la

Bani Mustalaq. Kabila la Bani Mustalaq lilikua likiishi vituo vitano (vituo vya

kupumzikia wasafiri wa jangwani) kutoka katika mji wa Al Madinah . Watu wa kabila

hili walishirikiana na waarabu wa makabila mengine na kupanga shambulizi la

kushtukiza la kushambulia mji wa Madinah .

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akapata habari yao na hivyo akamtuma

mpelelezi aliekua akijulikana kwa jina la Barid ili kuenda kupeleleza habari hizo, baada

ya Barid kurudi na kuthibitiisha habari hizo, alirudi pia na habari zenye manufaa kwa

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, kua watu wa Bani Mustalaq pia

wametuma mpelelezi kuja kuwapeleleza Waislamu, wakati huo huo mpelelezi wao

akakamatwa na kuwafanya watu wa Bani Mustalaq kua hawana habari nini kinaendelea.

Hivyo kutokana na mipango hayo Waislamu wakawapa watu wa Bani Mustalaq pamoja

na wale walioshirikiana nao shambulizi la kushtukia na kuwashinda watu hao, na

kuwateka watu wengi na mali zao pia. Miongoni mwa waliotekwa alikuwemo pia mtoto

mkubwa wa kike wa Chifu wa kabila la Bani Mustalaq aliekua akiitwa Juwayriyyah

ambae alikataa kua mateka na kusema kua atajilipia fidya ili aachiwe huru.

Baada ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kujua hadhi na ukubwa wa bint

huyo kwa watu wake, akamuambia kua itakua haina haja ya kulipa fidya kama ikiwa

atakubali kuunganisha ukoo wake na kua pamoja na Waislam kwa kuolewa na Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, na Juwayriyyah akakubaliana na wazo hilo.

Hivyo wale wote waliokamatwa mateka kutokana na vita hivyo wakaachiwa huru baada

ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kumuoa Juwayriyyah.

Sayyida Aisha aliwahi kusema kua ‘Simjui mwanamke yeyote aliekua na bahati kwa

ukoo wake kama Juwayriyyah’. Watu wote wa ukoo wa Bani Mustalaq walisilimu

kutokana na ndoa hiyo baina ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na

Juwayriyyah, hivyo ingelikua tafrani pia kama Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam angeliamua kumuacha Ummu Al Muuminun Juwayriyyah.


871

UMM AL MU’MININ SAFIYYHA BINT HUYAY IBN AKHTTAB.

Ummu al Muuminun Safiyyah Bint Huyay Ibn Akhtab, alikua ni mke wa nane wa Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, nae alikua ni bint wa kiongozi wa kabila la

Bunu Nadir ambe alikua pia ni kiongozi wa Kiyahudi lililokua likiishi katika mji wa

Yathrib. Watu wa kabila la Banu Nadir waliandikiana mkataba na Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam kutopigana na Waislam, lakini baba yake Safiyah ambae

alikua ni Kiongozi wa Banu Nadir akapanga njama ya Kumuua Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kwa kutaka kumtupia Jiwe juu ya kichwa wakati akiwa amekaa

akizungumza pamoja na Viongozi wengine wa Kiyahudi.

Hivyo Huyay akakamatwa na kufukuzwa katika Mji wa Madina, ambapo tukio hili

lilitokea mwaka wa 4 Al Hijra. Na akakimbilia katika maeneo ya Khaybar pamoja na

familia yake, ambapo miaka mitatu baadae Mayahudi hao wakavunja tena mkataba huo,

hivyo Waislamu wakawavamia na kuiteka ngome yao ya Khaybar.

Kuna Sahaba aliposikia kua ndani ya ngome hiyo alikuwemo pia Saffiyah, na alikua pia

ametekwa, hivyo akamfuata Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na

kumwambia kutokana na hadhi yake kwa watu wake, basi itakua si vizuri nae kuendelea

kukamatwa na kuwekwa pamoja na mateka wenzake kutokana na cheo chake na darja

yake. Ambapo akatumwa Bilal Ibn Rabah Radhi Allahu Anhu akamtoe katika sehemu

aliyowekwa na hivyo Bilal Ibn Rabah Radhi Allahu Anhu akamchukua Saffiyah na

Binamu yake na kuwapitisha mbele ya maiti za Wanaume wa Kiyahudi wa Khaybar

waliouliwa ambapo miongoni mwao alikuwemo pia Mumewe Saffiyah.

Wakati anapita kwenye eneo hilo basi Saffiyah alikua ni Binti mwenye Subra na

Ustahailivu jambo ambalo lilikua tofauti kwa upande wa Binamu yake ambae alikua

akilia kwa machungu, hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipoona tukio hili

basi akamwambia Bilal Ibn Rabah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Ewe Bilal hivi Allah

ameichomoa huruma ndani ya Moyo wako, kiasi ya kua umewapitisha Wanawake

wawili hawa mbele ya Waume zao waliouliwa?’

Ambapo anasema Safiyyah Radhi Allahu Anha kua: ‘Hakika Mimi nilikua ni m-bora

na kipenzi cha Baba yangu na pia kipenzi cha Mjomba wangu Yasir, kwani ilikua

kamwe haitokezei kwao wao kuniona mimi nikiwa pamoja na mmoja kati ya watoto

wao bila ya kunibeba mimi kabla ya wengine. Wakati alipokuja Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam katika Mji wa Madina, basi Baba yangu na Mjomba

wangu walienda kumsalimia, walitoka asubuhi mapema sana na hawakurudi

Nyumbani hadi jioni, huku wakiwa taabani wamechoka na pia wamevunjika

Moyo.’


872

‘Nilipowaona wanakuja basi nikawatabasamlia kama ilivyo kawaida, lakini hakuna

hata mmoja wao alieliona tabasam langu kutokana na hali yao, mara nikamsikia

Yasir akimuuliza Baba yangu: ‘Jee una uhakika Ndio Yeye?’ Baba yangu akasema:

‘Naam ndie yeye’ Yasir akauliza: ‘Jee unaweza ukathibitisha kua ndie yeye?’ Baba

yangu akajibu : ‘Naam, ndie yeye kwani mimi namjua vizuri’, Yasir akauliza: ‘Jee

unahisi nini juu yake?’ Baba akasema: ‘Uadui mkubwa nae, Uadui hadi mwisho wa

maisha yangu.’

Hali hii ilimstaajabisha sana Safiyyah kuona kua Baba yake na Mjomba wake ambao ni

miongoni mwa Viongozi wa Mayahudi wa Madina wanataka kumpiga vita Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam, Mtume ambae amebashiriwa kutokea kwake kwenye vitabu

vyao, hivyo Saffiya akajua kua Baba yake na Mjomba wake wanataka kumpiga vita Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwa sababu si Myahudi, bali ni Muarabu, na wao

walikua wanataka Mtume huyo awe Myahudi, ambapo tukio hili lilimvutia sana kihisia

Safiyyah kwa kumpenda Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika kipindi akiwa

bado ni Myahudi.

Hivyo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akaamua kumuachia huru, lakini

Safiyyah akasilimu na hapo akaambiwa anaweza kuchagua kuondoka na kurudi katika

mji wake ama aolewe na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na kisha abakie

katika mji wa Madinah . Hivyo Saffiyah akaona kua bora kuolewa na Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam na kisha abakie Madinah na kusema: ‘Ya Rasul Allah,

hakika mimi nilipokua Myahudi nilikua naomba kua niolewe nawe, hivyo jee hali

yangu itakuaje baada ya kusilimu kwangu?’

Anasema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam alikaa kwa siku tatu katia sehemu ya baina ya Khaybar na Madina, na katika

sehemu hio ndio akamuoa Saffiyah Bint Huyay, nami nikawaalika Waislam katika

karamu ambayo hakikua na Nyama wala Mkate, kwani Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam aliamrisha kutandikwe ngozi za kukalia wakati wa kula ardhini

na kisha ikawekwa Tende na Jibini na Siagi juu yake, na hio ndio iliyokua Karamu

ya Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam katika siku hio’

‘Waislam wakaulizana kama Saffiyah Bint Huyay atakua ni Mke wake Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam au atakua ni Mtumwa, na kisha wakaambiana kua:

‘Kama Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam atapita nae huku akiwa amemfunika

ili asionekane na Watu basi atakua ni Mke wake na kama atakua amepita nae akiwa

hakumfunika basi atakua ni Mtumwa wake’ Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alipokua tayari kwa safari basi akatayarisha Ngamia wake na

kumpandisha Safiyyah Nyuma yake huku akiwa amemfunika asionekane na

watu.’(Imam Bukhari)


873

Jeshi na msafara wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ulipowasilia katika Mji wa

Madina basi watu walizingira nyuma ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kutaka

kumuona Mke mpya wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambapo miongoni mwao

walikuwemo pia wake wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, akiwemo Aisha Radhi

Allahu Anha ambae alikua amejificha miongoni mwa Wanawake hao, na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alipomuona basi akamkamata kanzu yake na kisha

akamuuliza: ‘Jee umeona nini ewe Shuqaira?’ Shuqaira ni mwanamke mwenye nywele

za Dhahabu.

Aisha Radhi Allahu Anha akasema huku akiwa amejawa na Wivu kua: ‘Ni Mwanamke

tu wa Kiyahudi’ ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Usiseme

Hivyo, Kwani ameingia na kuikumbatia Dini ya Kiislam.’ Ndoa hii baina ya Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na Safiyyah ilisababisha usalama na kuvunja

uadui wa wakati huo baina ya Waislam na Mayahudi wa Madinah .

UMM AL MU’MININ MARIA BINT SHAM.

Kuhusiana na Umm ul Mu’uminin Maria Bint Sham alikua ni Mtumwa aliekua

akimilikiwa na Gavana wa Misri aliekua akiitwa Muqawqis ambae alikua ni Mkristo,

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alimpelekea mwaliko wa kuingia katika

Uislam Gavana huyo kupitia kwa Hatib Ibn Abi Baltaa Radhi Allahu Anhu, na baada ya

kupata mualiko huo Muqawqis alimchukua Maria na Dada yake aitwa Sherine na zawadi

nyengine ikiwemo mifuko 1000 ya Dhahabu na Kanzu 20 na kumpelekea Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kama zawadi ya kualikwa katika jambo jema.

Wakati Maria akiwa njiani kuelekea Madinah alijifunza mambo mengi kuhusiana na

mmiliki wake mpya ambae ni Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam pamoja na

dini yake mpya ya Kiislamu, hivyo akaamua kusilimu kabla ya kukutana na Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam.

Maria Bint Sham Radhi Allahu Anha alikua akitoka kusini mwa ardhi ya Misri katika

kijiji kinachoitwa Hifn Ahzaaka katika upande wa Mashariki ya Mto Nile, Baba yake

alikua ni Mtu wa Misri na Mama yake alikua ni mtu mwenye asili ya Rumi. Maria Bint

Sham na Sherine walipofika katika Mji wa Madina basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam alikua ndio kwanza amerudi kutoka kwenye kufunga mkataba wa Hudaybiyyah,

hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamchukua Maria na kisha Sherine

akamkabidhi kwa Hasan Ibn Thabit Radhi Allahu Anhu.

Ambapo anasema Aisha Radhi Allahu Anah kua: ‘Mimi sikua na wivu wa wake

wengine wa Rasul Allah miongoni mwetu kama nilivyokua na wivu kwa Maria kwa

sababu alikua Mzuri na ni mwenye Nywele nzuri zilizo jipinda’


874

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kutokana na mapenzi yake kwa Maria Bint Sham

Radhi Allahu Anha basi alimtafutia sehemu ya kuishi ambayo ni yenye mazingira ya

Misri katika ardhi ya Madina na hivyo akamchagulia eneo linalojulikana kama Aliaa

ambalo lina Miti na majani mengi mazingira ambayo yalikua ni kama mazingira ya

pembeni ya Mto Nile.

Ambapo kimaumbile na kimazingira basi tunaona kua kuna mfanano baina ya Maria na

Hajr ambae aliekua ni Mke wa Nabii Ibrahim ambae ndie mama yake Nabi Ismil, ambapo

wote wanawake wawili hawa ni wenye asili ya Misri, na haishangazi kuona kua Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipopata motto wake wa kiume kupitia kwa Maria

mwaka mmoja baadae basi akaamua kumuita Ibrahim, na huyu alikua ni Mtoto ambae

Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam akimpenda sana, kwani alipozaliwa tu alimchukua

na kumuonesha kwa Masahaba zake wote.

Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam alikaa na kumlea Ibrahim huku akiwa anakua

katika maumbile ya kawaida na ni mwenye kumfurahisha Rasul Allah Salallau Alayhi

wa Salam kutokana na afya yake na uzuri wake. Lakini ghafla mnamo mwaka wa pili wa

uhai wake, Ibrahim akaanza kuumwa na kisha akafariki dunia katika siku ya mwezi 10

Rabbi Al Awwal mwaka 10 Al Hijra.

Tukio hili lilimhuzunisha sana Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam na kasema: ‘Macho

yamejawa na machozi, na Moyo umejawa na Huzuni huku mimi nikiwa sina la

kusema isipokua lile litakalo mfurahisha Allah Subhanah wa Ta’ala, kua Ewe

Ibrahm hakika sisi tuna huzuni juu yako lakini hatuwezi kupingana na matakwa

yake Allah Subhanah wa Ta’ala’ kisha Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam

akamgekia Maria na kumwambia: ‘Hakika anae mlezi wake Peponi, hivyo miaka

iliyobakia ya kulelewa kwake atelelewa Peponi’

Katika siku ya Maziko yake Ibrahim Ibn Muhammad Rasul Allah Salallau Alayhi wa

Salam basi Jua na Mwezi vikapatwa ikawa kiza, na watu wakadhani kua hii ni kutokana

na kifo cha Ibrahim, lakini Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam akasema: ‘Jua na

Mwezi ni Dalili mbili kutoka kwa Allah, na hazihusiana na kufariki kwa mtu hivyo

mtakapoona vimepatwa basi kimbilieni katika Kumkumbuka Mola wenu katika

Sala.’

Abu Dhar Radhi Allahu Anhu anasema kuhusiana na Rasul Allah Salallau Alayhi wa

Salam na Maria Bint Sham na Ibrahim na Ardhi ya Misri kua: ‘Amesema Rasul Allah

Salallau Alayhi wa Salam kua: ‘Karibuni mtaiteka ardhi ya Misri na inajulikana

kua kam Ardhi ya Qirat, hivyo mtakapoiteka basi kuweni na huruma na watu wake

kwani ndani yake kuna jukumu la udugu wa kuoana nao na mnapowaona watu

wawli wanagombana baina yao hata kwa eneo la tofali basi msiiingilie’’


875

Ambapo anasema Abu Dhar Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi niliwaona Abd Rahman

Ibn Shurahbil Ibn Hasan na ndugu yake Rabia wanagombana juu ya eneo la Tofali,

hivyo nikaondoka’(Sahih Muslim)

Wanazuoni wamekhitilafiana kuhusiana na Maria bint Sham wengine wanasema kua

alikua ni Suria wake na wengine wanasema kua, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam hakumfanya Maria bint Sham kua Suria wake na badala yake alimuoa kisharia na

hivyo kuinyanyua darja yake baada ya kumuoa. Hivyo kabla ya kuendelea mbele zaid

katika kusoma kitabu hiki basi itakua ni vizuri kuweka wazi kwa kufafanua zaid

kuhusiana na neno Suria.

SURIYYAH NA MILK AL YAMIN KATIKA UISLAM

Neno la kiarabu Sariyyah ambalo kwa kiswahili tunaliita Suria linatokana na mzizi wa

neno Sin-Ra-Ra, lenye maana ya Siri, Furahia, Moyo, Asili, Chaguo, Harusi na Faragha.

Hivyo kwa matumizi na maana iliyokusudiwa hapa hua linamaanisha kua ni mwanamke

mtumwa au mwanamke alietekwa katika vita na hivyo mtumwa au mateka huyo wa kike

humilikiwa na mwanamme pasipo kuolewa na ambapo ameruhusiwa mwanamme huyo

kuwa na uhusiano nae wa faragha, wa kimapenzi na kuingiliana nae bila ya mwanamke

huyo kua na haki ya kisharia kwa mwanamme huyo. Hali hii ya kua na Suria ilikua ni

mila na desturi ambazo zilikuwepo na zilikua zinatumika tangu enzi za zamani katika

jamii mbali mbali duniani kabla ya kuja Uislam. Suria walikua ni miongoni mwa

watumwa wanawake au miongoni mwa mateka wanawake waliokamatwa vitani.

Hivyo baada ya kuanza Uislam baadhi ya mila na desturi zilikua zinaendelea kua kama

zilivyokua hadi pale iliposhuka amri ya kukataza mila na desturi hizo, miongoni mwa

mila na desturi hizo kama tulivyoona hapo awali ni pamoja na kua na wake zaidi ya

wanne, kua na Suria, kua na watumwa n.k ambapo ruhusa ya mambo yanayotokana na

mila na desturi hizo iliondolewa kidogo kidogo hatua kwa hatua.

Moja katika sifa ya Dini ya Kislam ni kua na ustahmilivu, hivyo inapotokea kukataza

kitu fulani basi kitu hicho huanzwa kukatazwa hatua baada ya hatua au kwa masharti,

hadi kufikia katika hali ya kukataza kabisa, mfano mmoja wa makatazo yaliyokatazwa

kwa njia kama hizo ni kuharamishwa kwa ulevi na vile vile kua na Suria, ingawa kua na

Suria hakujatazwa moja kwa moja lakini Qur’an na Sunnah zilipunguza uungaji mkono

wa jambo hilo pale ziliposhuka aya zilizokua zikisisitizia kua kuwaachia huru hua ni bora

zaid.


876

Tukiangalia kwa mfano aya ya 3 ya Surat an Nisaa tuliyokwisha itizama ambayo ilikua

inakataza mwisho kua na wake wanne, tunaona kua iliposhuka kukataza Waislam kua na

zaidi ya wake wanne haikukataza kua na Suria bali ilikua ikikhiyarisha kwa wale

watakaokosa kua na uadilifu basi waoe mke mmoja au wabakie na ‘Milk al Yamin’

(Kilichomo ndani ya umiliki wa kisharia wa mkono wa kulia) yaani wale wanaomilikiwa

baada ya kutekwa vitani au baada ya kua ni miongoni mwa wanaomilikiwa katika hali ya

utumwa katika wakati huo, aya hiyo imetumia hali ya maneno ya Malakat Aymanukum

kwa kusema:

‏﴿وَإِنْ‏ خِ‏ فْتُمْ‏ أَلا َّ تُقْسِ‏ طُواْ‏ فىِ‏

ٱلْيَتَامَى ٰ فَٱنكِحُواْ‏ مَا طَابَ‏ لَكُمْ‏ مِّنَ‏ ٱلنِّسَآءِ‏ مَثْنىَٰ‏

وَثُلاَثَ‏ وَرُابَعَ‏ فَإِنْ‏ خِ‏ فْتُمْ‏ أَلا َّ تَعْدِلُواْ‏ فَوَاحِ‏ دَةً‏ أَوْ‏ مَا مَلَكَتْ‏ أَيمَْانُكُمْ‏ ذٰلِكَ‏ أَدْنىَٰ‏

أَلا َّ تَعُولُواْ‏ ﴾

Wa-in khiftum alla tuqsitoo fee alyatama fainkihoo ma taba lakum mina alnnisa-i

mathna wathulatha warubaAAa fa-in khiftum alla taAAdiloo fawahidatan aw ma

malakat aymanukum dhalika adna alla taAAooloo. (Surat An-Nisaa’ 4:3).

Tafsir: Na ikiwa mnakhofu kua hamtoweza kuwafanyia haki mayatima, basi Oeni

wanawake wengine mnaowataka, wawili, au watatu, au wanne; lakini ikiwa mnakhofu

kua hamtoweza kuwafanyia uadilifu basi oeni mmoja tu, au wale mnaowamiliki

mikononi mwenu (Mliowateka vitani na Watumwa). Kufanya hivyo ni kukaribia

kujilinda na kutokua waadilifu.

Neno hili ‘Malakat aymanukum’ lenye kumaanisha ‘Kilichokuwemo ndani ya umiliki

wa mikono ya kulia’, limetumika mara kadhaa katika Qur’an katika hali na sehemu

tofauti kama vile:-

‏﴿مَا مَلَكْتَ‏ أَيمَْنُكُمْ﴾‏

Ma malakat aymanukum - Kile kinachomilikiwa na mikono yenu ya kulia. (Surat An

Nisaa 4:24-25; Surat An Nisaa 4:36; Surat An Noor 24:33)

‏﴿وَمَا مَلَكَتْ‏ يمَِينُكَ‏ ﴾

Wa Ma malakat yaminuka – Na kile kinachomilikiwa na mkono wenu wa kulia.(Surat

Al Ahzab 33:50; Surat Al Ahzab 33:52)

‏﴿ٱل َّذِينَ‏ مَلَكَ‏ تْ‏ أَيمَْانُكُ‏ ‏ْم ﴾


877

Aladhina malakat aymanukum - Wale ambao wanamilikiwa na mikono yenu ya

kulia.(Surat An Noor 24:58)

‏﴿مَا مَلَكَتْ‏ أَيمَْنُهُمْ﴾‏

Ma malakat aymanuhum – Kile kinachomilikiwa na mikono yao ya kulia. (Surat An

Nahl 16:71; Surat Al Mu’minun 23:6)

‏﴿مَا

مَلَكَ‏ تْ‏ أَيمَْ‏ نُهُ‏ ن َّ ﴾

Ma malakat aymanuhunna – Kile kinachomilikiwa na mikono yao ya kulia

(Wanawake). (Surat An Noor 24:31; Surat Al Ahzab 33:55)

Tunapoangalia mfano wa aya ya 50 ya Surat Al Ahzab, tunaona kua Allah Subhanahu wa

Ta’ala alimhalalishia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kuoa wake

awatakao, na pia kua na Suria, (Aya hii ilishuka kabla ya kushuka ile aya

iliyomshuruitisha Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kutoongeza mke wala

kuacha mke) pale aliposema katika Qur’an kua:

‏﴿َٰٰي ُّهَا ٱلن َّبىِ ُّ إِ َّ أَحْلَلْنَا لَكَ‏ أَزْوَاجَكَ‏ ٱللا َّتيِ‏ ۤ آتَيْتَ‏ أُجُورَهُن َّ وَمَا مَلَكَتْ‏ يمَِينُكَ‏

ممِ َّآ أَفَآءَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلَيْكَ‏ وَبَنَاتِ‏ عَمِّكَ‏ وَبَنَاتِ‏ عَم َّاتِكَ‏ وَبَنَاتِ‏ خَالِكَ‏ وَبَنَاتِ‏

خَالاَتِكَ‏ ٱللا َّتِى هَاجَرْنَ‏ مَعَكَ‏ وَٱمْرَأَةً‏ م ُّؤْمِنَةً‏ إِن وَهَبَتْ‏ نَفْسَهَا لِلن َّبىِِّ‏ إِنْ‏ أََر اَد

ٱلن َّبىِ ُّ أَن يَسْتَنكِحَهَا خَالِصَةً‏ ل َّكَ‏ مِن دُونِ‏ ٱلْمُؤْمِنِينَ‏ قَدْ‏ عَلِمْنَا مَا فَرَضْنَا عَلَيْهِمْ‏

فيِ‏ ۤ أَزْوَاجِ‏ هِمْ‏ وَمَا مَلَكَتْ‏ أَيمَْانُهُمْ‏ لِكَيْلاَ‏ يَكُونَ‏ عَلَيْكَ‏ حَرَجٌ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ غَفُوراً‏

ر َّحِ‏ يماً‏ ﴾

Ya ayyuha alnnabiyyu inna ahlalna laka azwajaka allatee atayta ojoorahunna

wama malakat yameenuka mimma afaa Allahu AAalayka wabanati AAammika

wabanati AAammatika wabanati khalika wabanati khalatika allatee hajarna

maAAaka waimraatan mu/minatan in wahabat nafsaha lilnnabiyyi in arada

alnnabiyyu an yastankihaha khalisatan laka min dooni almu/mineena qad

AAalimna ma faradhna AAalayhim fee azwajihim wama malakat aymanuhum

likayla yakoona AAalayka harajun wakana Allahu ghafooran raheeman(Surat Al

Ahzab 33:50)


878

Tafsir: Ewe Nabii (Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam)! Kwa Hakika

tumekuhalalishia wake zako, ambao umewalipia mahari yao, na ambao mkono wako

wa kulia unawamiliki (wanawake waliotekwa vitani na watumwa) ambao Allah

amekupa, na binti wa Ami zako, bint wa Ammah (shangazi) zako, binti wa Khal

(wajomba) zako, binti wa Khalah (mama wadogo) ambao walihama (kutoka Makkah)

pamoja nawe, na mwanawake alieamini ikiwa atajipeleka (kutaka kuolewa) kwa

Mtume, na Mtume akataka kumuoa; Haki ambayo ni yako tu (kwa Nabii Muhammad

peke yake), lakini si kwa waumini wengine. Hakika tunajua ni kipi tulichowaamrisha

kuhusiana na wake zao na wale wanaomilikiwa na mikono yao ya kulia - Ili kusiwe na

uzito kwako wewe. Na Allah ni mwingi wa Kusamehe na mwingi wa Rehma.

Sehemu ya kwanza aya hii imewekwa wazi kua inamhusu Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam peke yake kwa kumwambia kua amehalalishiwa kuwaoa wanawake

wengine walioainishwa katika aya hiyo na pia kua na Masuria. Sehemu ya pili ya aya hii

ni kwa ajili ya Waumini waliobakia, kwani wao hawakuruhusiwa kuoa wanawake kama

wale ambao alioruhusiwa kuwaoa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam,

ingawa na wao pia waliruhusiwa kua na Suria, aya inaendelea kwa kusema kua hakika

Allah anajua ni kipi amewaamrisha Waislamu waliobakia kuhusiana na wanawake

wanaotakiwa kuwaoa, kwani aya ya 23-24 ya Surat An Nisaa tayari zimeshaainisha

wanawake ambao wameharamishwa kwa Waumini kuwaowa na baada ya kuainishiwa

aina za wanawake hao, aya hizo zikawaruhusu pia Waislamu kua na Suria kwa kutumia

maneno ‘illa ma malakat aymanukum’ yaani ‘Isipokua wale ambao mkono wenu wa

kulia unawamiliki’, kwa ufafanuzi zaid tuangalie zinavyosema aya hizo za Surat An

Nisaa:

‏﴿حُرِّمَتْ‏ عَلَيْكُمْ‏ أُم َّهَاتُكُمْ‏ وَبَنَاتُكُمْ‏ وَأَخَوَاتُكُمْ‏ وَعَم َّاتُكُمْ‏ وَخَالاَتُكُمْ‏ وَبَنَاتُ‏ ٱلأَخِ‏

وَبَنَاتُ‏ ٱلأُخْتِ‏ وَأُم َّهَاتُكُمُ‏ اللا َّتِى أَرْضَعْنَكُمْ‏ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ‏ ٱلر َّضَاعَةِ‏ ‏َوأُم َّهَ‏ ا ‏ُت

نِسَآئِكُمْ‏ وَرَابَئِبُكُمُ‏ ٱللا َّتِى فىِ‏ حُجُورِكُمْ‏ مِّن نِّسَآئِكُمُ‏ ٱللا َّتِى دَخَلْتُمْ‏ هبِِن َّ فَإِن لم َّْ‏

‏ِمنْ‏ أَصْ‏ لاَبِكُ‏ مْ‏ وَأَن

تَكُونُواْ‏ دَخَلْتُمْ‏ هبِِن َّ فَلاَ‏ جُنَاحَ‏ عَلَيْكُمْ‏ وَحَلاَئِلُ‏ أَبْنَائِكُمُ‏ ٱل َّذِينَ‏

تجَْمَعُواْ‏ بَينَْ‏ ٱلاخْتَينِْ‏ إَلا َّ مَا قَدْ‏ سَلَفَ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ كَانَ‏ غَفُوراً‏ ر َّحِ‏ يماً‏

Hurrimat AAalaykum ommahatukum wabanatukum waakhawatukum

waAAammatukum wakhalatukum wabanatu al-akhi wabanatu al-okhti

waommahatukumu allatee ardaAAnakum waakhawatukum mina alrradaAAati


879

waommahatu nisa-ikum waraba-ibukumu allatee fee hujoorikum min nisa-ikumu

allatee dakhaltum bihinna fa-in lam takoonoo dakhaltum bihinna fala junaha

AAalaykum wahala-ilu abna-ikumu alladhina min aslabikum waan tajmaAAoo

bayna al-okhtayni illa ma qad salafa inna Allaha kana ghafooran raheeman (Surat

An Nisaa 4:23)

Tafsir: Mmeharamishiwa (Kuwaoa) mama zenu, dada zenu, dada wa baba zenu, dada

wa mama zenu, watoto wa ndugu zenu wa kiume, watoto wa ndugu zenu wa kike,

mama zenu waliokunyonyesheni, dada zenu mlionyonya nao, mama wa wake zenu,

watoto zenu wa kike wa kambo walio chini ya usimamizi wenu, waliozaliwa na wake

ambao mmeshawaingilia, lakini hamna tatizo ikiwa hamjawaingilia wake hao

(kuwaoa mabint zao), wake wa watoto wenu wa kiume waliotoka katika tupu zenu na

ndugu wawili wa kike kwa wakati mmoja, isipokua kwa yale yaliyokwisha pita;

Hakina, Allah ni mwingi wa kusamehe na ni mwingi wa Rehma.

Aya ya 24 ya sura hiyo ikamalizia kwa kuweka wazi aina ya wanawake wasioruhusika

kuolewa na wanaoruhusika kuolewa kwa kusema:

‏﴿وَٱلْمُحْصَنَاتُ‏ مِنَ‏ ٱلنِّسَآءِ‏ إِلا َّ مَا مَلَكْتَ‏ أَيمَْانُكُمْ‏ كِتَابَ‏ ٱهلل َِّ‏ عَلَيْكُمْ‏ وَأُحِ‏ ل َّ لَكُمْ‏

م َّا وَرَاءَ‏ ذٰلِكُمْ‏ أَن تَبْتَغُواْ‏ أبَِمْوَالِكُمْ‏ مح ُّْصِنِينَ‏ غَيْرَ‏ مُسافِحِ‏ ينَ‏ فَمَا ٱسْتَمْتَعْتُمْ‏ بِِه

‏ِد

مِنْهُن َّ فَآتُوهُن َّ أُجُورَهُن َّ فَرِيضَةً‏ وَلاَ‏ جُنَاحَ‏ عَلَيْكُمْ‏ فِيمَا تَرَاضَيْتُمْ‏ بِهِ‏ مِن بَعْ‏

َ

ٱلْفَرِيضَةِ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ كَانَ‏ عَلِيماً‏ حَكِيماً‏

Waalmuhsanatu mina alnnisa-i illa ma malakat aymanukum kitaba Allahi

AAalaykum waohilla lakum ma waraa dhalikum an tabtaghoo bi-amwalikum

muhsineena ghayra musafiheena fama istamtaAAtum bihi minhunna faatoohunna

ojoorahunna fareedhatan wala junaha AAalaykum feema taradaytum bihi min

baAAdi alfareedhati inna Allaha kana AAaleeman hakeeman (Surat An Nisaa 4:24)

Tafsir: Na (mmeharamishiwa) wanawake waliokwishaolewa, isipokua wale (illa ma

malakat aymanukum) ambao mkono wenu wa kulia unawamiliki. Hivyo Allah

amekupambieni, wote waliobakia kua ni halali juu yenu, pale mnapowataka kwa kutoa

Mahari kutoka katika mali zenu mkitaka usafi, bila ya kuingiliana ambako si kwa

kisheria, hivyo kwa wale ambao mshawaingilia basi wapeni mahari yao kama

ilivyoamrishwa, lakini baada ya kuamrishwa mahari mkikubaliana kupeana (zaid),

basi hamna dhambi. Kwa Hakika Allah ni mwenye kujua na ni Mwingi wa Busara.


880

Aya imetumia Neno Musafihiina linalotokana na neno Safaha ambalo hua linamaanisha

Kumwaga, Kutiririka au Kumimina. Hivyo neno Musafihun ambalo hua linamaanisha

Mtu anaemmwagia mwenzake au anaemwagiwa yaani anaefanya Usharati au Uzinifu.

MFUMO WA UTUMWA NA MATEKA WA VITA KATIKA UISLAM.

Tunapozungumzia asili ya Utumwa katika Uislam, basi inabidi lazima kuwekeana wazi

kua mfumo wa Maisha ya Dini ya Kiislam si mfumo ambao ndio ulioanzisha mfumo wa

kua na Watumwa Duniani, na pia si mfumo unaounga mkono Utumwa Duniani. Kwani

asili ya mfumo wa Utumwa inatokana na asili ya kutokea mapigano au vita baina ya

vizazi vya Ibn Adam, hivyo basi tunaweza kusema kua asili ya Utumwa inaenda

sambamba na asili ya vita, na Utumwa hutokana na matokeo ya vita, kwani mara tu baada

ya takriban kila vita kumalizika basi hua hutokea miongoni mwa mambo mawili

yafuatayo:

1- Kuwepo kwa watu watakaofariki, aidha iwe kwa upande wa walioshindwa, au

upande ulioshindwa au kwa pande zote mbili zilizopigana.

2- Kuwepo kwa watu watakaotekwa iwe kwa upande ulioshinda, ulioshindwa au

pande zote mbili. Na hivyo hali ya watu hao hutegemea na uhasama baina ya

pande mbili husika, kwani aidha wanaweza wakabadilishana mateka hao,

wakawaachia huru Mateka hao au wakabaki nao kama maadui zao na hivyo

kuwafanyisha kazi za Kitumwa dhidi yao.

Kwa upande wa Dini ya Kiislamu basi tunaona Uislam unakubaliana na mfumo wa

kukamata mateka katika wakati wa vita, kwani hali hiyo hua haiepukiki, kwa sababu hata

kama ikiwa Waislamu hawakukamata mateka, au watakamana lakini hawakuruhusiika

kuwafanya Watumwa mateka hao, basi Waislamu huenda nao wakakamatwa mateka na

kufanywa kua Watumwa.

Ingawa mara tu baada ya Waislamu kuwakamata mateka maadui zao, basi huchukuliwa

na kupelekwa kwa Amir mkuu wa Waislam ambae ndie hua na jukumu la kuwagawa

Mateka hao ambapo kama ikionekana kua kuna Wanawake miongoni mwa mateka hao,

basi kwa kila mpiganaji alieshiriki mapigano hayo, humilikishwa Mateka wake ambae

kisharia hua tayari ni Milk Al Yamin wake kulingana na idadi ya mateka hao, na hivyo

kila mtu aliepewa Milk al Yamin wake basi kisharia hua na haki ya kumuingilia

mwanamke kama anavyoweza kumuingilia mke wake, lakini vile vile kabla ya

kuingiliana nae huko basi kwanza hua kuna masharti yake kama vile ilivyokua kuna

masharti ya ndoa. Miongoni mwa masharti hayo ni:-


881

Kama vile ilivyokua hairuhusiki kwa Mwanamke kuolewa na waume wawili basi

vile vile Hairuhusiki kwa mwanamke mmoja kua na wamiliki wawili.

Hairuhusiki kumuingilia mwanamke alietekwa hadi pale ijulikane kama

mwanamke huyo alikua na mumewe hapo kabla katika ardhi ya Makafiri ama la,

na kama alikua ni mwenye kuolewa na hivyo amekamatwa peke yake bila ya mume

wake, basi inabidi kwanza ndoa hiyo ibatilishwe, kwa kumhamishia mwanamke

huyo katika ardhi ya Kiislam kiasi ya kua hakutokua na uwezekano wa kukutana

tena baina ya mwanamke huyo na Mumewe aliemuoa hapo kabla. Kumhamishia

mwanamke huyo katika ardhi ya Kiislam na Mumewe kubakia katika ardhi

isiyokua ya Kiislam, basi hubatilisha moja kwa moja ndoa hiyo.

Hairuhusiki kumuingilia Mwanamke alietekwa wakati mume wake akiwa pia ni

miongoni mwa waliotekwa.

Kama ilivyokua mwanamke alieachwa humbidi kusubiri kumalizika kipindi cha

‘Iddah’ basi vile vile kwa mwanamke alietekwa hua ni lazima nae asubiriwe amalize

kipindi kama hicho ambacho hua kinaitwa ’Istibraa’. Hivyo hairuhusiki

kumuingilia Mwanamke alietekwa hadi pale atakapomaliza Istibraa.

Kama ilivyokua kwa Mwanamke alieoloewa hua ni mwenye kumtegemea mume

wake kiusimamizi katika majukumu, basi vile vile Hairuhusiki kwa Mateka

kutomshughulikia kimajukumu, kwani ni jukumu la mmiliki kumshughulikia

Mateka wake kama anavyo mshughulikia mke wake.

Kama ilivyokua ndoa inamharamishia Mume kuwaoa ndugu wa damu wa Mke basi

vile vile Hairuhusiki kwa mmiliki kumuingilia au kumuoa ndugu wa damu wa

Mateka wake. n.k.

Lakini pia kwa upande mwengine ili kuondoa udhalilishwaji na uvunjwaji haki za

wanaokamatwa mateka basi Uislam unapendekeza kwani umeweka wazi kua inabidi

mateka hao waachiwe huru kwa makubaliano maalum baina ya pande mbili zilizopigana

iwe kwa kulipa fidya au bila kulipa fidya.

Qur’an na Sunnah zimetilia mkazo kua ni jambo jema kuwafanyia wema na kuwaachia

mateka na watumwa kama alivyosema Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

kua: ‘Mtu atakaekua na mateka wa kike, akamsomesha, na kumlea na

kumshughulikia kwa heshima na kisha akamuachia huru na kumuoa basi mtu huyo

hua na malipo mara mbili’(Sahih Bukhari).


882

Na katika Hadith nyengine amesema Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua

‘Yeyote yule atakaemuacha huru Mtumwa Muislam, basi Allah ataviachia huru

viungo vyote vya mwili wake visiguswe na moto wa Jahannam kama vile yeye

alivyomuachia mtumwa huru huyo’(Muslim)

Moja katika A’mal njema ni kuwaoa mateka waliosilimu au watumwa walioachiwa huru

kwa sababu ya kuilinda heshima yao, kwani hua vigumu kwa mateka au mtumwa

kuolewa baada ya kuachwa huru, na vile vile hua rahisi kwa Waislamu wasiokua na

uwezo, kuwaoa mateka au watumwa hao, kama inavyotueleza Qur’an:

‏﴿وَمَن لم َّْ‏ يَسْتَطِعْ‏ مِنكُمْ‏ طَوْلاً‏ أَن يَنكِحَ‏ ٱلْمُحْصَنَاتِ‏ ٱلْمُؤْمِنَاتِ‏ فَمِنْ‏ م َّا مَلَكَتْ‏

أَيمَْانُكُم مِّن فَتَيَاتِكُمُ‏ ٱلْمُؤْمِنَاتِ‏ وَٱهلل َُّ‏ أَعْلَمُ‏ إبِِيمَانِكُمْ‏ بَعْضُكُمْ‏ مِّن بَْع ‏ٍض

فَٱنكِحُوهُن َّ إبِِذْنِ‏ أَهْلِهِن َّ وَآتُوهُن َّ أُجُورَهُن َّ بِٱلْمَعْرُوفِ‏ محُْصَنَاتٍ‏ غَيْرَ‏ مُسَافِحَاتٍ‏

وَلاَ‏ مُت َّخِ‏ ذَاتِ‏ أَخْدَانٍ‏ فَإِذَآ أُحْصِن َّ فَإِنْ‏ أَتَينَْ‏ بِفَاحِ‏ شَةٍ‏ فَعَلَيِْهن َّ نِصْفُ‏ مَا عَلَى

ٱلْمُحْصَنَاتِ‏ مِنَ‏ ٱلْعَذَابِ‏ ذٰلِكَ‏ لِمَنْ‏ خَشِ‏ ىَ‏ ٱلْعَنَتَ‏ مِنْكُمْ‏ وَأَن تَصْبرُِواْ‏ خَيْرٌ‏ ل َّكُمْ‏

وَٱهلل َُّ‏ غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Waman lam yastatiAA minkum tawlan an yankiha almuhsanati almu/minati famin

ma malakat aymanukum min fatayatikumu almu/minati waAllahu aAAlamu bieemanikum

baAAdhukum min baAAdhin fainkihoohunna bi-idhni ahlihinna

waatoohunna ojoorahunna bialmaAAroofi muhsanatin ghayra masafihatin wala

muttakhidhati akhdanin fa-idha ohsinna fa-in atayna bifahishatin faAAalayhinna

nisfu ma AAala almuhsanati mina alAAadhabi dhalika liman khashiya alAAanata

minkum waan tasbiroo khayrun lakum waAllahu ghafoorun raheemun (Surat An

Nisaa 4:25)

Tafsir: Na ikiwa hamna uwezo wa kuoa wanawake walioamini waliokua huru, basi

mnaweza kuwaoa wanawake walioamini miongoni mwa waliotekwa na watumwa, na

Allah anajua kila kitu kuhusiana na Imani zenu baina yenu. Waoeni kwa ruhusa za

watu wao (wanaowamiliki, au waangangalizi wao) na mmwape mahari yao kutokana

na kile kinachotosheleza, wao (watumwa na mateka) wawe wasafi, na wasiwe wenye

kufanya zina, wala wasichukue wanaume na baada ya kuolewa, ikiwa watafanya zinaa

basi adhabu yao ni nusu ya wale wanawake waliokua (hawajaolewa) huru, Hii ni kwa


883

yule anaeogopa kudhuriwa kwa dini yake au kwa mwili wake. Lakini bora kwenu nyie

ikiwa mtakua na subra, Allah ni mwingi wa Kusamehe na mwingi wa rehma.

Miongoni mwa aya zilizosisitizia kuwakomboa, kuwaoa watumwa wa kike au

kuwaozesha watumwa wa kike kwa watumwa wa kiume ni pamoja na aya za 32 na 33 za

Surat An Noor zisemazo:

‏﴿وَأَنْكِحُواْ‏ ٰ ٱلأََمَى مِنْكُمْ‏ وَٱلص َّالحِِينَ‏ مِنْ‏ عِبَادِكُمْ‏ وَإِمائِكُمْ‏ إِن يَكُونُواْ‏ فُقَرَآءَ‏

يُغْنِهِمُ‏ ٱهلل َُّ‏ مِن فَضْلِهِ‏ وَٱهلل َُّ‏ وَاسِ‏ عٌ‏ عَلِيمٌ‏ ﴾

Waankihoo al-ayama minkum waalssaliheena min AAibadikum wa-ima-ikum in

yakoonoo fuqaraa yughnihimu Allahu min fadhlihi waAllahu wasiAAun

AAaleemun. (Surat An Noor 24:32)

Tafsir: Na ozesheni miongoni mwa Al Ayyama, au wafanyao a’mali njema miongoni

mwa watumwa wenu wa kiume na wa kike: Ikiwa wako katika hali ya umasikini Allah

atawapa fadhila zake, kwani kwa hakika Allah ni mwingi wa kila kitu na ni mwenye

kujua kila kitu.

Neno ‘Al Ayyama’ ambalo ni wingi wa Ayyim linamaanisha mjane awe mwanamme au

mwanammke awe aliewahi kuoa au kuolewa kabla au hajawahi kuoa au kuolewa kabla.

Kisha ikafuatia aya isemayo:

‏﴿وَلْيَسْتَعْفِفِ‏ ٱل َّذِينَ‏ لاَ‏ يجَِدُونَ‏ نِكَاحاً‏ حَتى َّ ٰ يُغْنِيَهُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ مِن فَضْلِهِ‏ وَٱل َّذِينَ‏

يَبْتَغُونَ‏ الْكِتَابَ‏ ممِ َّا مَلَكَتْ‏ أَيمَْانُكُمْ‏ فَكَاتِبُوهُمْ‏ إِنْ‏ عَلِمُتُمْ‏ فِيهِمْ‏ خَيرْ‏ اً‏ وَآتُوهُمْ‏ مِّن

م َّالِ‏ ٱهلل َِّ‏ ۤ ٱل َّذِي آاتَكُمْ‏ وَلاَ‏ تُكْرِهُواْ‏ فَتَيَاتِكُمْ‏ عَلَى ٱلْبِغَآءِ‏ إِنْ‏ أَرَدْنَ‏ تحََص ُّناً‏ لِّتَبْتَغُواْ‏

عَرَضَ‏ ٱلحَْيَاةِ‏ ٱلد ُّنْيَا وَمَن يُكْرِههُن َّ فِإِن َّ ٱهلل ََّ‏ مِن بَعْدِ‏ إِكْرَاهِهِن َّ غَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يٌم ﴾

WalyastaAAfifi alladhina la yajidoona nikahan hatta yughniyahumu Allahu min

fadhlihi waalladhina yabtaghoona alkitaba mimma malakat aymanukum

fakatiboohum in AAalimtum feehim khayran waatoohum min mali Allahi alladhi

atakum wala tukrihoo fatayatikum AAala albigha-i in aradna tahassunan


884

litabtaghoo AAarada alhayati alddunya waman yukrihhunna fa-inna Allaha min

baAAdi ikrahihinna ghafoorun raheemun (Surat An Noor 24:33)

Tafsir: Na waachieni wale waliokua hawana uwezo wa kipesa wa kuoa wakae

wajihifadhi (wasifanye maasi), hadi pale Allah atakapowapa uwezo kwa fadhila zake.

Na miongoni mwa mnaowamiliki wakitaka kuandikiwa mkataba wa uhuru wao,

waandikieni hivyo, ikiwa mnawajua kua ni waaminifu. Na wapeni baadhi ya mali zenu

zinazotokana na utajiri wa Allah aliokupeni juu yenu. Na msiwalazimishe kufanya

ukahaba, ikiwa wanataka usafi, ili mpate kunufaika kidunia. Lakini ikiwa mmoja

wenu atawalizimisha (ukahaba), basi baada ya kulazimishwa huko, Allah ni mwenye

kusamehe na ni mwingi wa rehma (Atawasamehe wanawake hao kutokana na

kulazimishwa kwao kufanya dhambi hiyo).

Tukiangalia katika aya hizo tutaona kua Allah Subhanahu wa Ta’ala anatoa ruhsa ya

kuwaoa Milk al yamiin au waliokua wakimilikiwa kwa njia ya utumwa na mateka wa

vita, hii ni moja ya kati ya njia za kuwaachia huru, na njia nyengine ni kufungiana nao

mkataba usemao kua mtumwa au mateka anaweza kufanya kazi halafu akakatwa

mshahara wake hadi kumaliziana kiwango watakachokubaliana na mmiliki wake, na

baada ya kutimia kiwango hicho mtumwa huyo anaweza kua huru kutokana na

makubaliano ya mkataba huo, vile vile aya hizo zinakataza kuwavunjia haki watumwa

au mateka hao.

Miongoni mwa njia alizotumia Allah Subhanahu wa Ta’ala kuondoa utumwa kidogo

kidogo hatua kwa hatua ni pamoja na kafara za viapo, kama inavyoonesha Qur’an:

‏﴿لاَ‏ يُؤَاخِ‏ ذُكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ بِٱلل َّغْوِ‏ فيِ‏ ۤ أَيمَْانِكُمْ‏ وَلَٰكِن يُؤَاخِ‏ ذُكُم بمَِا عَق َّدتم ُُّ‏ ٱلأَيمَْانَ‏ فَكَف َّارَتُهُ‏

إِطْعَامُ‏ عَشَرَةِ‏ مَسَاكِينَ‏ مِ‏ نْ‏ أَوْ‏ سَ‏ طِ‏ مَا تُطْعِمُونَ‏ أَهْ‏ لِيكُمْ‏ أَوْ‏ كِسْ‏ وَتُهُ‏ مْ‏ أَوْ‏ تحَْرِيُر رَقَبٍَة

فَمَن لم َّْ‏ يجَِدْ‏ فَصِيَامُ‏ ثَلاَثَةِ‏ أَ َّمٍ‏ ذٰلِكَ‏ كَف َّارَةُ‏ أَيمَْانِكُمْ‏ إِذَا حَلَفْتُمْ‏ ۤ وَٱحْفَظُواْ‏ ا أَيمَْ‏ نَ‏ كُْم

كَذٰ‏ لِكَ‏ يُبَينِّ‏ ُ ٱهلل َُّ‏ لَكُمْ‏ آَتِهِ‏ لَعَل َّكُمْ‏ تَشْ‏ كُرُو ‏َن

La yu-akhidhukumu Allahu biallaghwi fee aymanikum walakin yu-akhidhukum

bima AAaqqadtumu al-aymana fakaffaratuhu itAAamu AAasharati masakeena

min awsati ma tutAAimoona ahleekum aw kiswatuhum aw tahreeru raqabatin

faman lam yajid fasiyamu thalathati ayyamin dhalika kaffaratu aymanikum itha

halaftum waihfadhoo aymanakum kadhalika yubayyinu Allahu lakum ayatihi

laAAallakum tashkuroona (Surat Al Maidah 5:89)

Tafsir: Allah hatokuadhibuni kwa viapo vyenu msivyovikusudia, lakini atakuadhibuni


885

kwa yale mliyoyakusudia kuyaapia, na kafara yake ni kuwalisha maskini kumi,

kutokana na kipomo cha kile mnachoilisha familia zenu, au kuwavisha, au kuachia

huru watumwa, lakini asiekua na uwezo wa hayo basi na afunge kwa siku tatu; hii ni

kafara kwa viapo vyenu pale mnapo apa; hivyo lindeni viapo vyenu (msiape ovyo ovyo),

hivyo Allah anaweka wazi ili muwe na shukran.

Miongoni mwa mifano miengine ni katika aya inayozungumzia kafara ya Talaka ya

Zihar, n.k.

‏﴿وَٱل َّذِينَ‏ يُظَاهِرُونَ‏ مِن نِّسَآئِهِمْ‏ ثمُ َّ يَعُودُونَ‏ لِمَا قَالُواْ‏ فَتَحْرِيرُ‏ رَقَبَةٍ‏ مِّن قَبْلِ‏ أَن

يَتَمَآس َّا ذٰلِكُمْ‏ تُوعَظُونَ‏ بِهِ‏ وَٱهلل َُّ‏ بمَِا تَعْمَلُونَ‏ خَبِيرٌ‏ ﴾

Waalladhina yudhahiroona min nisa-ihim thumma yaAAoodoona lima qaloo

fatahreeru raqabatin min qabli an yatamassa dhalikum tooAAadhoona bihi

waAllahu bima taAAmaloona khabeerun (Surat Al Mujadala 58:3)

Tafsir: Na kwa wale wanaojiharamishia wake zao kwa kuwafananisha migongo yao

na migongo ya mama zao, basi huweza kuyarudisha yale waliyoyasema, wamuachie

huru mtumwa kabla ya kugusana tena (kurudiana) juu ya hayo mnapewa onyo (ili

msirudie mambo hayo) na Allah anajua kila mnachokifanya.

Kwa upande wa Hadith ziko nyingi na moja miongoni mwao ni ile ya Abd Allah Ibn

Umar Radhi Allahu Anhu, ambae alimwita mtumwa wake na akamuona ana alama ya

kupigwa mgongoni mwake, Abd Allah Ibn Umar Radhi Allahu Anhu akamuuliza

‘Nimekusababishia maumivu?’ yule mtumwa akajibu ‘La’ hapo Abd Allah Ibn Umar

Radhi Allahu Anhu akasema ‘Hapana, kuanzia sasa hivi uko huru’. Halafu akaokota

kijiwe ardhini na kusema, ‘Sina nililolipata, hata kulingana na uzito wa hiki, kwani

nimemsikia Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akisema kua: Yeyote

yule anaempiga mtumwa wake bila ya kosa linalofahamika, au akampiga kibao tu

basi kafara yake ni kumuachia huru mtumwa huyo.’ (Sahih Muslim)

Kwa kutilia mkazo umuhimu wa kuwaachia huru na kuwalipia fidya zao watumwa na

mateka waliokua hawana uwezo wa kujilipia ili kua huru, basi Qur’an katika kuainisha

watu wanaohitaji kufaidika na pesa za Zakkah, imesema kua miongoni mwao ni

watumwa, iwe kwa kuwalipia kwa wamiliki wao wawe huru ama kuwapa wao wenyewe

wakajikomboa, kama inavyosema Surat At Tawba:

‏﴿إِنم ََّا ٱلص َّدَقَاتُ‏ لِلْفُقَرَآءِ‏ وَٱلْمَسَاكِينِ‏ وَٱلْعَامِلِينَ‏ عَلَيْهَا وَٱلْمُؤَل َّفَةِ‏ قُلُوبُهُمْ‏ وَِفى

ٱلرِّقَابِ‏ وَٱلْغَارِمِينَ‏ وَفىِ‏ سَبِيلِ‏ ٱهلل َِّ‏ وَٱبْنِ‏ ٱلس َّبِيلِ‏ فَرِيضَةً‏ مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَٱهلل َُّ‏ ‏َعلِيٌم


886

حَكِيمٌ‏ ﴾

Innama alssadaqatu lilfuqara-i waalmasakeeni waalAAamileena AAalayha

waalmu-allafati quloobuhum wafee alrriqabi waalgharimeena wafee sabeeli Allahi

waibni alssabeeli fareedatan mina Allahi waAllahu AAaleemun hakeemun (Surat At

Tawba 9:60)

Tafsir: Hakika ya Sadaka (Zakkah) ni kwa ajili aya Mafukara, Masikini, na

walioajiriwa kukusanya Zakkah; na kuzivutia nyoyo za wale waliokua wamevutiwa na

Uislam; na kuwaachia huru Watumwa; na wale wanye madeni; na kwa ajili ya njia ya

Allah, na kwa msafiri (aliefikwa na matatizo na kukwama na akawa hana pesa za

kuendelea na safari yake); huo ni wajibu uliowekwa na Allah. Kwa hakika Allah ni

mjuzi wa kila kitu na ni mwingi wa Busara.

Baada ya kuangalia maana ya Suria na Milk al Yamini basi tunatakiwa tufahamu kua hali

inayoruhusu watu kua na Suria na Milk al Yamini kwa kisharia haipo tena katika wakati

huu tuliokua nao, na hii ni kutokana na mambo mengi sana miongoni mwao ni pamoja

na uhimizwaji wa kuondolewa kwa utumwa, kutokuwepo kwa uadilifu miongoni mwa

Waislam na hivyo kutoweka kwa hali ya kuhalisha mapigano ya vita vya Jihad kwa ajili

ya Allah Subhanah wa Ta’ala, n.k

Kwani Sharia’h ya Kiislam inasema kua kukakamata mateka na kua na watumwa

hairuhusiwi pale inapokua hakuna kiongozi Muadilifu anaeongoza Ummah wa Kiislam

yaani Khalifah Muadilifu, na kunaruhusika pale inapotokea vita vya Jihad

vilivyoruhusika kisharia, hata hivyo bado kuna kipingamizi cha kuwaachia huru bila ya

kuwalipisha fidya wale waliotekwa ili kuonesha ukarimu.

Ingawa katika ulimwengu wa leo hakuna hali ya kuhalalisha utumwa kutokana na

mtizamo wa Sharia’h wa dini ya Kiislam na pia Sharia’h za kilimwengu, lakini hata

hivyo utumwa bado upo na miongoni mwa utumwa huo ni pamoja na watu kufungwa

jela bila ya kua na makosa, au kua na hatia, kwa mfano wakati Marekani na washirika

wake, walipoamua kueneza mamlaka yao ili kuweza kuchota mafuta na gesi kwa urahisi

katika maeneo ya Mashariki ya kati na hivyo kuvamia nchi kama Afghanistan, Iraq,

Yemen, Libya n.k walikamata watu mbali mbali waliokuwemo na wasiokuwemo kwa

kisingizio cha ugaidi na kuwaweka ndani jela za nchi mbali mbali, na si katika nchi hizo

tu bali watumwa au mateka wa aina hii wamo katika takriban magereza ya kila nchi

duniani.

Vile vile kuna utumwa mwengine ambao bado unaendelea katika baadhi ya sehemu

duniani kutokana na umasikini, ambapo watu masikini huhadaiwa kupatiwa kazi kutoka


887

katika nchi moja hadi nchi nyengine, lakini matokeo yake mambo hua si kama

walivyotegemea hivyo hufanyishwa kazi ambazo hazina tofauti na utumwa kutokana na

kunyanyaswa au pia kulipwa chini ya kiwango kinachoridhisha kisharia, hivyo watu hao

hubakia katika kazi hizo kwa sababu hawana tena uwezo wa kurudi walikotoka, na pia

hata wakirudi wengine walikopa pesa za matayarisho ya safari hizo wakiwa na malengo

ya kua watalipa baada ya kupata mshahara unaotokana na kazi hizo, hivyo inabidi

hawawezi kurudi bila ya kua na uwezo wa kurudisha walichokopa.

Huu pia hua ni utumwa, unaoendelea katika nchi mbali mbali duniani, hususan katika

nchi za Uarabuni, na ukweli ni kua Uislamu unapinga sana mambo kama haya, na ndio

maana ukawainisha watu kama hawa kua ni miongoni mwa wanaofaa kupewa pesa za

Zakkah ili waweze kujikomboa kutokana na matatizo yao, katika kusisitizia kuwaonea

huruma watu kama hawa na watu walio chini ya mamalaka yetu, anasema Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua:

‘Wafanyakazi wenu ni ndugu zenu, Allah amewaweka chini ya usimamizi wenu.

Kama angelitaka basi angelikuwekeni nyinyi chini ya usimamizi wao, hivyo yeyote

yule ambae ana ndugu yake chini ya usimamizi wake, basi amlishe kile anachokula

yeye na amvishe kile anachovaa yeye, msiwape kazi zilizokuwepo nje ya uwezo wao,

ikiwa kazi ni ngumu kwao basi wasaidieni’.

Vile vile anasema Abu Mas'ud Al Ansari : ‘Nilikua nikimpiga mfanyakazi wangu,

mara nikasikia sauti ikisema kutoka nyuma kwangu: ‘Ya Abu Masoud, kumbuka

kua Allah ana mamlaka makubwa zaid ya hayo uliyokua nayo wewe kwake yeye

(huyo anaempiga)’, nilipogeuka nikamuona Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam.

Nikasema: ‘Nimemuachia huru kwa ajili ya Allah’. Na hapo Rasul Allah Salallahu

A’layhi wa Salam akasema: ‘Kama usingelifanya hivyo basi mlango wa Jahannam

ungelifunguka kwa ajili yako, au moto wa Jahannam ungelikuunguza.’’ (Sahih

Muslim, Kitab Al Iman)

Alisema Nabii Muhammad Sallahu A’layhi wa Salam alisema katika khutba yake ya

kuagia kua: ‘Na watumwa wenu hakikisheni kua mnawalisha kile ambacho mnakula

nyinyi na mnawavisha kile ambacho mnavaa nyinyi, na wanapofanya makosa

ambapo mtashindwa kuwasamehe basi wauzeni, kwani wao ni waja wa Allah na

hawastahiki kuadhibiwa’.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua akihimiza uadilifu baina ya watu

katika familia, katika jamii n.k, kwani Uislam haukutofautisha baina ya alie juu

kimamlaka na alie chini, mwenye nguvu na alie dhaifu, masikini na tajiri, mwanamme

na mwanamke n.k, na uadilifu huu ndio uliowavutia watu wengi miongoni mwa wasiokua

Waislamu kuingia katika mfumo wa maisha ya dini ya Kiislamu.


888

AAL, AHL, ZAWJ NA QAWWAM KATIKA UISLAM.

Maneno ya kiarabu A’hl na Al kwa kilugha yana maana moja ambayo hua ni kuoa,

kuzoea, kukaribisha, familia, jamii ya watu wenye kuishi ndani ya nyumba moja au

sehemu moja walio chini ya msimamizi mmoja ambae hua ni Mume au Baba, vile vile

maana ya neno hili pia hutumika kuelezea uhusiano wa kutegemeana baina ya mume na

mke ambapo ndani ya uhusiano huo huingia pia watoto, ndugu na jamaa wanaohudumiwa

na msimamizi wa familia husika.

Ambapo neno Zawj kwa kilugha humaanisha ‘Pea moja ya kitu’ na vie vile humaanisha

ndoa, na pia hua na maana ya Mume pale mzungumzaji anapokua ni Mke na humaanisha

Mke pale mzungumzaji anapokua ni Mume. Kiislam tunapozungumzia kuhusiana na

suala la Zawj yaani familia ya Mume na Mke, basi hua hamna suali la ni nani bora

miongoni mwao, kwa sababu Qur’an inawaona wote wawili kua ni “Zawj” (Wawili

wanaokamilishana bila ya mmoja kuonekana bora na kujaribu kua juu ya mwenzake),

anasema Ibn Manzur katika Lisan Al Arab kua : ‘Mfano mzuri wa maana ya neno

Zawaj hua ni ‘Zawja Na’il’ (Pea ya viatu), kwani mtu hua hajiulizi ni kipi kiatu bora,

cha kulia au cha kushoto?’

Tukiangalia jamii za watu wa zamani kabla ya kuja kwa Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam basi tuaona kua ilikua hakuna hali ya kuthaminiwa kwa A’hl, Aila wala

Zawj ambao hua wanajumuisha familia katika jamii, hususan pale inapokua wanafamilia

hao wanapokua ni wanawake. Kiasi ya kua hali ilifikia watu kuona aibu kubwa sana pale

wanapojaaliwa kupata mtoto wa kike na hivyo kua ni jambo la kawaida kwa mzee

kumzika mzima mzima mtoto wake wa kike asiekua na hatia yeyote. Allah Subhanahu

wa Ta’ala anatuthibitishia haya katika Qurán kwa kuhoji na kukataza pale aliposema:

‏﴿وَإِذَا ٱلْمَوْءُودَةُ‏ سُئِلَتْ‏ -

أبَِىِّ‏ ذَنبٍ‏ قُتِلَتْ‏ ﴾

Waidha almawuudat suilat, Bi ayyi dhanbi Qutilat (Surat At Takwir 81:8-9)

Tafsir: Na Mtoto wa kike aliezikwa akiwa hai atakapoenda kuulizwa, Alifanya dhambi

gani iliyompelekea yeye kukatiliwa Nafsi yake.

Hivyo ndivyo hali ilivyokua katika zama Jahiliyah, lakini mitizamo hiyo katika jamii

ilianza kubadilika, baada ya kuja Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam baada

ya kushuka aya tuliyoiangalia na aya nyenginezo ambazo zinazosisitizia kua Wanaume

na Wanawake si mtu na mmiliki wake bali ni wenye kusaidiana kimajukumu baina yao,

kama tunavyoona vile isemavyo aya inayofuatia:


889

‏﴿وَٱلْمُؤْمِنُونَ‏ وَٱلْمُؤْمِنَاتِ‏ بَعْضُهُمْ‏ أَوْلِيَآءُ‏ بَعْضٍ‏ ‏َْمُرُونَ‏ بِٱلْمَعْرُوفِ‏ وَيَنْهَوْنَ‏ عَنِ‏

ٱلْمُنْكَرِ‏ وَيُقِيمُونَ‏ ٱلص َّلواَةَ‏ وَيُؤْتُونَ‏ ٱلز َّكَواةَ‏ وَيُطِيعُونَ‏ ٱهلل ََّ‏ وَرَسُولَهُ‏ أُوْلَٰئِكَ‏ سَيَرْحمَُهُ‏ ‏ُم

ٱهلل َُّ‏ إِن َّ ٱهلل ََّ‏ عَزِيزٌ‏ حَكِيمٌ‏ ﴾

Waalmu/minoona waalmu/minatu baAAduhum awliyao baAAdin ya/muroona

bialmaAAroofi wayanhawna AAani almunkari wayuqeemoona alssalata

wayu/toona alzzakata wayuteeAAoona Allaha warasoolahu ola-ika

sayarhamuhumu Allahu inna Allaha AAazeezun hakeemun (Surat At Tawba 9:71)

Tafsir: Na Waumini, Wanaume na Wanawake wao kwa wao ni wasaidizi wenye

kusaidiana, huamrishana mema na kukatazana maovu, wanasali, na kutoa Zakkah na

kumtii Allah na Mtume wake (Sala Allahu A’layhi wa Salam). Allah atawaingiza

katika Rehma zake. Hakika Allah ni mwenye uwezo na mwenye Hikma.

Hii inaonesha kua Waumini wa kiume na wa kike wako sawa sawa kiutukufu lakini

wanatofautiana katika baadhi ya mambo ya kimajukumu kama inavyoweka wazi aya

inayofuatia kwa kusema:

‏﴿وَلهَُن َّ مِثْلُ‏ ٱل َّذِى عَلَيْهِن َّ بِٱلْمَعْرُوفِ‏ وَلِلرِّجَالِ‏ عَلَيْهِن َّ دَرَجَةٌ‏ وَٱهلل َُّ‏ عَزِيزٌ‏ حَكُيٌم ﴾

Walahunna mithlu alladhee AAalayhinna bialmaAAroofi walilrrijali AAalayhinna

darajatun waAllahu AAazeezun hakeemun (Surat Al Baqara 2:228)

Tafsir: Na wao (Wake) wana haki (juu ya Waume zao) kama vile (zilivyo haki za

Waume) juu yao kwa namna inavyofaa. Lakini Wanaume wana darja juu yao. Na

hakika Allah ni mwenye Uwezo na mwingi wa Hikma.

Darja hiyo ya Wanaume dhidi ya wanawake katika familia hua si ya kiutukufu bali hua

ni ya kimajukumu ya kuwashughulikia katika kuwahudumia wanawake na familia nzima

kwa ujumla, hali hii inafafanulika zaidi pale tunapoangalia katika aya inayofuatia ambayo

inasema kua:


890

‏﴿ٱلرِّجَالُ‏ قَو َّامُونَ‏ عَلَى ٱلنِّسَآءِ‏ بمَِا فَ‏ َّضلَ‏ ٱهلل َُّ‏ بَعْضَهُمْ‏ عَلَى ٰ بَعْضٍ‏ وَبمَِآ أَنْفَقُواْ‏ مِ‏ ‏ْن

أَمْ‏ وَالهِِمْ﴾‏

Alrrijalu qawwamoona AAala alnnisa-i bima fadhdhala Allahu baAAdhahum

AAala baAAdhin wabima anfaqoo min amwalihim (Surat An Nisaa 4:34)

Tafsir: Wanaume ni Qawwamoona (wasimamizi) juu ya Wanawake kwa sababu Allah

amewafadhili baadhi yao (Wanaume) juu ya baadhi yao (Wanawake) kutokana na kile

wanachokichuma na kukitumia juu yao.

Maana ya neno Qawwam kwa kilugha hua linamaanisha kusimamia au kuhudumia kitu

kwa muda mrefu, hivyo tunapozungumzia kifamilia basi neno hili hua linajumuisha

jukumu la kusimamia kimwili, kimahitaji, kiheshima na kimajukumu kwa upande wa

kidunia na kiakhera.

Hivyo maana ya neno Qawwam hua kamwe haimaanishi kama vile wanavyofikiria watu

wengi kua maana yake ni kudhibiti, kuweka chini yake au chini ya mamlaka yake, kwani

kufikiria hivyo basi hua ni kama walivyokua wakifanya jamii za watu wa Kijahiliyyah.

Katika kuieleze maana ya aya hii, basi anasema Imam Fakhr al Din Al Razi kuhusiana

na aya hii ya Surat An Nisaa 4:34 kua: ‘Alrrijalu qawwamoona AAala alnnisa-i

(Wanaume ni wasimamizi wa Wanawake) ina uhusiano na aya nyengine kabla yake

isemayo:

‏﴿وَلاَ‏ تَتَمَن َّوْاْ‏ مَا فَض َّلَ‏ ٱهلل َُّ‏ بِهِ‏ بَعْضَكُمْ‏ عَلَى ٰ بَعْضٍ‏ ﴾

Wala tatamannaw ma fadhala Allahu bihi baAAdhakum AAala baAAdhin’(Surat

An Nisaa 4:32)

Tafsir: Na wala msitamani kile ambacho Allah amewafadhili baadhi yenu kuliko

wengine.

Imam Fakhr Ad Din Al Razi anaendelea kwa kusema: Aya ambayo tulisema kua

ilishushwa kwa sababu baadhi ya Wanawake walitoa kauli kuhusiana na Allah

kuwapendelea katika Urithi Wanaume. Hivyo Allah ameweka wazi katika ayah hii

kua amewafadhili tu Wanaume juu ya Wanwake kwa sababu Wanaume ni

Wasimamizi wa Wanawake. Kwani ingawa wote Mke na Mume wanafaidika na

matunda na haki zinazotokana na kua pamoja, basi Allah amemuamrisha


891

Mwanamme kumlipa Mwanamke sehemu ya ndoa yao, na kumhudumia katika

mahitaji ya kila siku, hivyo ongezeko la upande mmoja hukabiliana na ongezeko la

upande wa pili – na hivyo hua kama vile hamna pendeleo baina yao. Jambo hili

linaweka wazi mpangilio wa namna zilivyopangika aya.’

Hivyo darja ya Qawwam aliyokua nayo mwanamme kwa familia yake hua ni kuilinda,

kuisimania na kuwahudumia A’al, Ahl, Zawj au familia yake katika hali ya kiuadilifu, na

hapa msimamizi husika hua anatakiwa kuitumia fadhila hiyo aliyopewa na Allah

Subhanah wa Ta’ala, kwa kua na umakini, huruma, busara na subra katika kutekeleza

majukumu hayo, kwani vyenginevyo itakua ni kuenda kinyume na matakwa ya mfadhili

na mtoaji wa majukumu hayo na hivyo mwanamme husika hupoteza haki ya kua na Darja

hiyo ya Qawwam.

Ndio maana Allah Subhanahu wa Ta’ala akawaambia wale walioamini katika Qur’an

kwa kusema:

‏﴿أَي ُّهَا ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ ۤ قُواْ‏ أَنفُسَكُمْ‏ وَأَهْلِيكُمْ‏ ‏َراً‏ وَقُودُهَا ٱلن َّاسُ‏ وَٱلحِْجَارَةُ‏ عَلَْيهَا

مَلاَئِكَةٌ‏ غِلاَظٌ‏ شِ‏ دَادٌ‏ لا َّ يَعْصُونَ‏ ٱهلل ََّ‏ مَآ أَمَرَهُمْ‏ وَيَفْعَلُونَ‏ مَا يُؤْمَرُونَ‏ ﴾

Ya ayyuha alladheena amanoo qoo anfusakum waahleekum naran waqooduha

alnnasu waalhijaratu AAalayha mala-ikatun ghiladhun shidadun la yaAAsoona

Allaha ma amarahum wayafAAaloona ma yu/maroona(Surat At Tahrim 66:6)

Tafsir: Enyi mlioamini, ziokoeni Nafsi zenu na Ahlikum (familia zenu) kutokana na

Moto ambao kuni zake ni watu na mawe, ambao unasimamiwa na Malaika wakali na

wenye nguvu, ambao kamwe hawaasi amri wanazozipokea kutoka kwa Allah, bali

hufanya kile wanachoamrishwa.

Hivyo basi hadhi ya Darja hiyo aliyopewa Msimamizi wa familia na ugumu wa jukumu

hilo unaoneka wazi pale tuunapoona una jukumu la Qawwam ni pamoja na kuwaokoa

ahli zake kutokana na moto kwani vyenginevyo atakuja kukimbizana nao katika siku ya

siku kama unavyoelezewa katika aya zinayofuatia:

﴿ يَوْ‏ مَ‏ يَفِر ُّ ٱلْمَ‏ رْءُ‏ مِ‏ نْ‏ أَخِ‏ يهِ‏ -

وَأَبِيهِ‏ وَأُمِّ‏ هِ‏

- وَ‏ صَ حِبَتِهُوَبَنِي هِ‏ ﴾

Yawma yafirru almaro min akheehi; Waommihi waabeehi; Wasahibatihi

wabaneehi (Surat Abasa 80:34-36)


892

Tafsir: Siku ambayo mtu atamkimbia ndugu yake; Na Mama yake na Baba yake; na

Mke wake na Watoto wake.

Aya hii inaweka wazi kua Mtu au Qawwam atakaikimbia familia yake, Mama yake, Baba

yake mke wake na Watoto wake yaani Ahl zake, Aila wake na Zawj wake ambao ni

jukumu lake, pale watakapomtaka awajibu ni kwa sababu gani hakuwa muadilifu juu yao

katika kuwatekelezea majukumu yao ipasavyo.

Amesema Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kua:

Khayrukum, khayrukum li ahlihi, wa ana khayrukum li ahlihi.

خَيْرُكُمْ‏ خَيْرُكُمْ‏ لأَِهْلِهِ،‏ وَأََ‏ خَيْرُكُمْ‏ لأَِهْلِي

‘Mbora miongoni mwenu ni yule alie mbora kwa familia yake, na mimi ni mbora

miongoni mwenu kwa familia yangu’. (Imam Ibn Majah)

Hivyo Kiislam ni wajibu kwa Mwanamme ambae ni Baba, Kaka au Mume kua mbora

kwa kuwasimamia, kuwahudumia na kuwatekelezea majukumu yao yote wale walio

chini yake katika familia. Kwani wakati Mwanamme yupo katika kazi ya kuwatafutia

rizki na mahitaji yao mengine ya lazima, basi Mwanamke ambae hua ni Mama, Dada au

Mke yeye jukumu lake hua ni kuwasimamia, kuwatunza, kuwalea na kuwaanda watoto

na familia katika muelekeo wa maisha yao ya baadae. Kutokana na hali hii basi ndio

maana Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alipoulizwa baina ya wazee wawili

Baba na Mama ni yupi wa kumheshimu na kumpenda na kumshughulikia zaidi alijibu:

‘Mama, kisha Mama, kisha Mama kisha Baba’.

Uislam haukumpa hadhi Mama pekee, bali umeupa hadhi upande wote wa mzee wa Kike

ambao kwa Kiislam hujumuisha Mama, Shangazi wa Upande wa Mama, Shangazi wa

Upande wa Baba, Bibi, Mke wa Baba n.k, kama tunavyoona katika Hadith ya Abd Allah

Ibn ‘Umar isemayo: ‘Kuna mtu alikuja kwa Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam

na kusema: ‘Hakika mimi nimefanya dhambi kubwa, Jee kuna jambo ambalo

nnaweza kulifanya kufidia dhambi hiyo?’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam

akamuuliza: ‘Jee unae Mama?’ Yule mtu akajibu: ‘La!’, Rasul Allah Salallahu

A’layhi wa Salam akamuuliza tena : ‘Unae Shangazi wa Upande wa Mama?’ Yule

mtu akajibu: ‘Naam’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akamwambia yule

mtu: ‘Basi mfanyie wema na umhumdumie sana.’’

Hadhi hii haipo kwa wanawake watu wazima tu bali pia kwa watoto wa kike na ndugu

zetu wa kike kwani amesema Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam: ‘Hakuna yeyote

katika Ummah wangu ambae mwenye watoto watatu wa kike au ndugu watatu wa


893

kike, na kisha akawasimamia na kuwahudumia hadi wakawa wakubwa, isipokua

atakua pamoja nami Peponi kama hivi – Huku akionesha vidole vyake viwili cha

shahada na cha kati vikiwa pamoja’ (Al Awsat na Majmaá Al Zawaid)

Anasema pia Abu Hurayrah kua amesema Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kua

: ‘Yeyote yule mwenye watoto watatu wa kike, akawahudumia, akawafurahisha

huku akiwa na subira, basi Allah Subhanahu wa Ta’ala atamuingiza Peponi mtu

huyo kutokana na kuwa na huruma juu yao’ mtu mmoja akauliza: ‘Vipi kama

ikiwa mtu huyo ana watoto wawili wa kike?’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam

akasema: ‘Hata kama akiwa na wawili’, mtu mwengine akauliza: ‘Ya Rasul Allah,

Vipi akiwa na mmoja tu?’, Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Hata

kama akiwa na mmoja tu.’’

Anasema Abd Allah Ibn `Abbas kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu A’layhi wa

Salam kua : ‘Yeyote yule mwenye kupata mtoto wa kike, na akawa hakumzika au

kumfedhehesha na akawa hakumpendelea mtoto wake wa kiume dhidi ya mtoto

wake wa kike, basi Allah Subhanahu wa Ta’ala atamuingiza Peponi kwa ajili yake.’’

Tukiangalia hali ilivyokua kabla ya kuja kwa Nabii Muhammad Sallahu A’layhi wa

Salam, kutokana na Hadith ya Jafar Ibn Abu Talib ambae ni Ibn Ami wa Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam katika kumuainishia Ashama Ibn Abjar ambae

ni maarufu kama Mfalme Najash baada ya kuwauliza Waislam mara tu walipowasili

nchini Uhabeshi au Ethiopia kwa kujibu swali lifuatalo alilowauliza, ‘Jee ni ipi iliyokua

dini yenu ya kwanza kabla ya dini yenu hii mpya? Jee ni hii dini yenu mpya ni dini

gani? Na kwanini mkahamia katika nchi yangu?’

Jafar Ibn Abu Talib aliuelzea Uislam kwa kusema: ‘Ewe Mfalme, sisi tulikua ni watu

wajinga, tuliokua tukiishi kama wanyama wa mwituni, mwenye nguvu miongoni

mwetu aliishi kwa kuwatumia wasiokua na nguvu. Tulikua hatuna sheria yeyote,

na tulikua hatuna mamlaka isipokua wenye nguvu dhidi ya wasiokua na nguvu.

Tulikua tukiabudu masanamu yaliyotengenezwa kutokana na udongo au miti, na

hatukujua heshima wala maana ya utu. Halafu Mungu akatushushia Rehma zake,

akatutumia Mtume kutoka miongoni mwetu, ambae anafahamika kutokana na

ukweli na uaminifu wake, tabia zake ni mfano wa kuingwa miongoni mwetu, na ni

mwenye kutoka katika ukoo bora miongoni mwa waarabu. Akatuita katika

kumuabudu Mungu mmoja, na akatukataza kuyaabudia masanamu, akatuamrisha

kusema ukweli, kuwalinda wasiokua na nguvu, masikini, wanyonge, wajane na

mayatima. Ametuamrisha kuwaheshimu wanawake na tusiwasingizie mambo ya

uongo. Wengi miongoni mwa watu wetu bado ni wenye kua na miungu mingi na

wanachukia maamuzi yetu ya kujiunga na Imani mpya ambayo inayoitwa Uislam.


894

Hivyo wameanza kututeketeza, na ni katika kukimbia mauaji yao ndio tukafuata

usalama katika Ufalme wako.’

Ingawa Jafar Ibn Abi Talib alikua ni Ibn Ami wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam lakini pia alikua ni miongoni mwa Masahaba watano waliotoka katika ukoo

wa Banu Hashim waliofanana sana kisura na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam wakiwemo pia Hasan Ibn Ali Ibn Abi Talib (mjukuu wa Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam), Abu Sufyan Ibn Al Harith, As Sayb Ibn Ubayd (Babu wa

babu yake Imam Al Shafi’i) na Qutham Ibn Al Abbas.

Bila ya kuyatumia maneno aliyoyasema Jabir Ibn Abi Talib kua kama ushahidi wa

ukombozi wa watu wa aina tofauti basi tunaona wazi kua Nabii Salallahu A’layhi wa

Salam alikua ni mfano wa kuigwa na ni Nuru iliyokuja kumurika mambo mengi

yaliyokua hayafai lakini yalikua yakifanywa katika jamii, na hivyo kumurika na

kuonesha heshima na haki za wanyonge, watumwa, masikini, wanawake, mayatima na

kadhalika katika jamii.

Anasema Abu Huraira, kua: ‘Alikuja mtu kwa Rasul Allah Salallahu A’layhi wa

Salam na kumlalamikia, kuhusiana na ugumu wa Moyo wake, ambapo Rasul Allah

Salallahu A’layhi wa Salam akamwambia: ‘Kama unataka kua na Moyo mlaini basi

walishe Masikini na wafariji Mayatima’

Vile vile akasema Sahl Ibn Sa’d kua, ‘Nabii Salallahu A’layhi wa Salam alisema ‘Mimi

na anaelea Mayatima tuko kama hivi Peponi’ na akagusanisha kidole chake cha

Shahada na kidole chake cha kati kwa pamoja.’

Tukiangalia katika Hadith nyengine basi tunaona jinsi Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam anavyotufundisha namna unavyotakiwa kua uhusiano katika familia

kama vile anavyosema, Sayyida Aisha kua: ‘Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam

amesema: ‘Kwa hakika miongoni mwa Waumini waliokua na Imani bora kabisa,

basi ni wale wenye tabia nzuri za kupendeza na wale wenye kuzifanyia wema zaidi

familia zao.’’ Vile vile tunayaona haya katika ile Hadith maarufu ya Jabir Ibn Abd Allah

ambae alikua ni miongoni mwa Masahaba vijana waliooa wakiwa na umri wa miaka 18

kua:

Safari moja alikua katika msafara pamoja na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi

wa Salam, na walipokaribia mji wa Madinah , yeye akaanza kuongeza mwendo juu

ya kipando chake. Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akamuuliza

imekuaje mbona anaharakia kurudi nyumbani? Jabir akajibu: ‘Mimi nimeoa hivi

karibuni’, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akamuuliza : ‘Umeoa

mjane au mwari?’ Jabir akajibu: ‘Mjane’.


895

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Ah sasa kwa nini hukuoa

mwanamke kijana, ambae ungeweza kucheza nae, na yeye akacheza pamoja nawe,

akakuchekesha na wewe ukamchekesha?’

Jabir akasema: ‘Ya Rasul Allah! Baba yangu alikufa Shahid katika vita vya Uhud,

hivyo akawacha nyuma yake watoto wadogo wa kike, hivyo sikuona haja ya kuoa

mwanamke mdogo kama wao, niliona bora nioe mwanamke mkubwa ambae

atakaeweza kuwasimamia wadogo zangu’, Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam akasema: ‘Naam, Umefanya uamuzi wa Busara kabisa’

Jabir anaendelea kusema: ‘Hivyo tulipo karibia kuingia mjini, Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam akaniambia, punguza mwendo, na usubiri usiku ndio

uingie, ili kwa yule ambae hajachana nywele zake azichane, na yule aliekua

hakunyoa sehemu zake za siri apate kunyoa’. Kisha akaniambia: ‘Utakapomuingilia

basi kua na busara na upole’. (Sahih Bukhari na Sahih Muslim)

Hadith hii inatuonesha ukweli na uwazi kua Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam katika familia kuhusiana na kuishi kwa kupendana, kuhurumiana, kuridhiana,

kufurahishana, kusaidiana n.k baina ya mwanamme na mwanamke, watu wazima na

watoto, familia na jamii nzima kwa ujumla.

Anasema Al-Aswad kua siku moja: ‘Nilimuuliza Aisha, `Jee Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam alikua akikaa nyumbani hufanya nini?’ Aisha akajibu,

‘Alikua akisaidia familia yake na akisikia Adhana basi hutoka nje kuenda kusali.’

(Imam Bukhari).

Hivyo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, alikua akikaa na wake zake na pia

kuwasaidia kazi mbali mbali, ijapokua miongoni mwa wake zake wote aliowaoa, hakuna

aliekua mke aliekua mdogo kiumri, mwari na bikra isipokua Ummu ul Mu’minina A’isha

bint Abu Bakr pekee na wengine waliobakia walikua ni wajane, waliofiwa na waume zao

vitani na pia walikua ni watu wazima na wakubwa pia kiumri lakini alikua akikaa nao na

kuwasadia bila kupendelea.

Wanazuoni wa Hadith wanasema kua kuna Hadith zilizopokewa na wake wa Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ziko takriban 3000, kati ya hizo Hadith 2210

zinatoka kwa Aisha Umm ul Mu’minina, 378 zinatoka kwa Ummu Salama Umm ul

Mu’minin na wake wengine waliobakia wamepokea Hadith baina ya 11 hadi 65, na hii

inategemea na mda aliokaa mke huyo kwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

kabla ya kufariki kwake na vile vile inategemea na mda wa kuolewa kwa mke huyo na

kukaa na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kabla ya kufariki kwake.


896

Mbali ya kua na wake wengi katika maisha yake, lakini tukiyazingatia maisha ya Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kabla ya kuoa kwake, baada ya kuoa kwake na

namna alivyokua akiishi na wake zake tutaona kua ni ya mfano wa kuigwa katika kuishi

kwa uadilifu, heshima, upendo, ukarimu na huruma kwa wake zetu na familia zetu.

Anasema Sayyida Aisha kua: ‘Siku moja alikuja Bedui kwa Rasul Allah na akasema:

‘Unawabusu watoto wako, wakati sisi hatufanyi hivyo.’ Rasul Allahi Salallahu

A’layhi wa Salam akasema: ‘Sina la kukufanyieni pale itakapotokea kua Allah

Subhanahu wa Ta’ala atakapoziondoa Rehma katika nyoyo zenu’’(Imam Bukhari)

Maisha yake na wake zake yanatufundisha kua wanawake ni watu walio huru kisharia,

hawawezi kuolewa bila ya ridhaa yao, wanayo haki ya kukaa na majina yao baada ya

kuolewa, wanayo haki ya kudhibiti mali zao, wanayo haki ya kurithi mali, wanayo haki

ya kubatilisha ndoa zao pale inapotokea unyanyaswaji au kuvunjiwa haki zao, wanayo

haki ya kuishi katika jamii kama vile wanavyoishi watu wengine, wanayo haki ya

kufanya Ibada zote zinazofanywa na wanaume n.k.

Kama anavyosema Allah Subhanahu wa Ta’ala katika Qur’an:

‏﴿مَنْ‏ عَمِلَ‏ صَالحِ‏ اً‏ مِّن ذَكَرٍ‏ أَوْ‏ ٰ أُنْثَى وَهُوَ‏ مُؤْمِنٌ‏ فَلَنُحْيِيَن َّهُ‏ حَيَاةً‏ طَيِّبَةً‏ وَلَنَجْزِيَ‏ ن َّ هُ‏ ‏ْم

أَجْرَهُم أبَِحْسَنِ‏ مَا كَانُواْ‏ يَعْمَلُونَ‏ ﴾

Man AAamila salihan min dhakarin aw untha wahuwa mu/minun

falanuhyiyannahu hayatan tayyibatan walanajziyannahum ajrahum bi-ahsani ma

kanoo yaAAmaloona. (Surat An Nahl 16:97)

Tafsir: Yeyote yule atakaefanya jema awe mwanamme au mwanamke na akawa ni

Mu’umini wa kweli, basi kwa hakika tutampa maisha mapya yaliyo masafi na mazuri,

na tutamlipa kutokana na ubora wa vitendo vyake.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua pia akikaa na kushauriana nao

wake zake na kusikiliza ushauri wao na moja kati ya mfano wa hilo ni pale baada ya

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kusaini Mkataba wa Hudaybiyyah,

aliposema kuwaambia Masahaba zake ‘Nyanyukeni, mchinje wanyama wenu na kisha

mnyoe nywele zenu’, hata hivyo hakuna hata Sahaba mmoja alienyanyua mguu wake

kufanya vile alivyoamrisha Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, kutokana na

kuvunjika moyo kwa yale yaliyotokea katika makubaliano ya mkataba huo.


897

Hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akanyanyuka na kuenda kwa Ummu

Salama na kumwambia yaliyotokea na hapo Ummu Salama akamwambia Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ‘Ya Rasul Allah, unataka maneno yako

yafanyiwe kazi? Basi nenda nje na usizungumze na mtu yeyote hadi pale

utakapomaliza kuchinja mnyama wako na kunyoa nywele zako’, hapo Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akatoka nje akachinja mnyama wake na kuanza

kunyoa nywele zake, na baada ya Masahaba kumuona Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam anafanya hivyo basi na wao wakanyanyuka na kufanya kama vile

alivyofanya. (Imam Bukhari)

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua pia akikaa na kutaniana na wake

zake, kama inavyothibitisha Hadith ya Nu’man Ibn Bishr isemayo kua siku moja ‘Abu

Bakr alikuja na kugonga mlango na kuomba ruhusa kuingia ndani kwa Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, akamsikia A’isha akimpandishia sauti

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, hivyo baada ya kuruhusiwa kuingia

ndani, Abu Bakr akaingia ndani na kumkamata A’isha na kumwambia, ‘Ewe mtoto

wa Umm Ruman kwa nini unanyanyua sauti zaid ya Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam?’.

Hapo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akaingilia kati na kumzuia

Abu Bakr asimpige mtoto wake mbele yake, Abu Bakr alipoondoka Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akamliwaza A’isha na kumwambia

‘Unaona nilivyokuokoa kutoka kwake?’, baada ya muda Abu Bakr akarudi na

kupiga hodi, alipokaribishwa, akawaona Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam na A’isha wanacheka na kutaniana. ‘Abu Bakr akasema, niruhusuni niwe

sehemu ya amani yenu kama mlivyoniruhusu kua sehemu ya mgogoro

wenu.’’(Imam Ahmad)

Katika Hadith nyengine ya Imam Al Tirmidhi isemayo kua, ‘Siku moja kutokana na

wivu aliokua nao A’isha kwa Safiyyah, A’isha alimwambia Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam, jee umeona jinsi Saffiyah alivyokua mfupi?, hapo Nabii

Muhammad Salallahu Alayhi wa Salaam akajibu ‘Hakika umesema kitu ambacho,

kama kingelichanganywa na bahari basi bahari yote ingelichafuka’’, hapa tunaona

namna Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alivyokua akiishi na wake zake

wote kwa uadilifu.

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alisema: Muogopeni Allah kuhusiana

na Mwanamke, kwani kwa hakika mmewaoa kutokana na Amanah ya Allah na

kuihalalisha miili yao juu yenu kwa kutumia maneno ya Allah, Mna haki juu yao

na wao wana haki juu yenu, kuhusiana na mavazi na vyakula vyao.


898

Mwanazuoni wa Hadith na mtafiti wa mambo ya Kiislam katika karne yetu aitwae

Muhammad Akram Nadwi anasema katika kufanya uchunguzi wake juu ya hadhi na darja

wa Wanawake katika Uislamu katika Qur’an na vitabu mbali mbali vya Hadith kua:

‘Mwanammke anapokua Mtoto, basi humfungulia mlango wa Pepo baba yake,

anapokua Mke, hukamilisha nusu ya Dini ya Mume wake na anapokua Mama basi

Pepo hua chini ya Miguu yake.’, Muhammad Akram Nadwi anaendelea kwa kusema:

‘Kama kila mtu angelikua anaijua thamani hasa ya mwanamke katika dini ya

Kiislam, basi hata wanaume wangeliona kua bora wangelikua Wanawake’.

Vile vile Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, alikua ni mwenye

kuwashirikisha wanawake katika mambo mbali mbali wenye utaalamu nayo katika

kunyanyua mapato yao na kujenga uchumi wa jamii ya Kiislam, kwani vile vile

wanawake wanayo haki ya kuendelea kufanya kazi za kiuchumi kwa ajili ya maisha yao,

kwa mfano Umm ul Mu’minina Zaynab bint Jahsh al Asadiya alikua ni mtaalamu

mkubwa wa kazi za mikono ikiwemo, kufuma vitambaa na kushona nguo na mapambo

mbali mbali, na vile vile mke wa Abd Allah Ibn Masoud ambae aliekua mahiri katika

utengenezaji wa mafuta mazuri na walikua wakiendeleza fani zao na bila kuvunjiwa haki

zao katika uendelezaji wa shughuli zao mbali mbali ikiwemo pia kupigana katika vita

vya Jihad kwa waliokua na uwezo huo.

Miongoni mwa wanawake waliokua katika harakati za kupigana Jihad wakati wa Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ni pamoja na : Umm Salim Ibn Malhan, Umm

Haram bint Malhan, Umm Al-Harith Al-Ansariyah, Ar-Rubayy’ bint Mu‘widh, Umm

Sanan al-Aslamiyyah, Umm Salit, Layla Al-Ghiffariyah, Ku‘aybah Bint Sa‘id Al-

Aslamiyah, Himnah, Umm Ziyad Al-Ashja‘yah bint Jahsh, Rufaidat bint Ka’ab al

Aslamiyyat; Aminat Bint Qays al Ghifariyyat; Umm ‘Atiyyah al Anasariyyat; Nusaibat

Bint Ka’ab al Maziniyyat; Umm 'Atiyyah al Ansariyat al Khadfidhat, Zainab Al Awd

ambae alikua ni mtaalamu wa macho na Rufaydah Bint Saad Al-Ansariyah n.k

Ambapo Rufaydah Bint Saad Al Ansariyah alietoka katika ukooo wa Bani Aslam kabila

la Al Khazraj alikua ni Daktari mkuu wa Jeshi la Kiislam takriban katika kila vita

alivyopigana Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, kiasi ya kua ilikua ni jambo

la kawaida katika uwanja wa vita kusikia kauli zisemazo ‘Mpelekeni katika Hema la

Rufaydah’, pale Mujahidina wanapojeruhiwa katika vita, kwani Hema la Rufaydah

lilikua ndio hospitali ya kila majeruhi miongoni mwa majeshi ya Kiislam, hospitali

ambayo ilikua ikihama na kuhamia katika kila sehemu wanayopigana vita Waislam.

Miongoni mwa wasaidizi wa Rufayda Al Ansarriya ni pamoja na Aminah, Umm Ayman,

Safiyat, Umm Sulaim na Hind.

Vile vile kuna Umm Ammara ambae pia anajulikana kama Nusaibat bint Ka'ab bin Amru

bin 'Awf bin Mabdhool bin 'Amru bin Ghanam bin Mazin bin al Najjar al Ansariyat,

ambae aliolewa na Zayd Ibn Asim na hivyo kupata watoto wawili Abd Allah na Habiib.


899

Ummu Ammara alikua anaiongoza familia yake yote kwa pamoja katika kuwahudumia

Waislam vitani kwa matibabu na majumbani. Umm Ammara alikua na familia yake

alikua ni miongoni mwa waliopigana na kusaidia katika vita vya Uhud kiasi ya kua hali

ya vita ilipobadilika na kua mbaya kwa upande wa Waislam aliamua kukamata upanga

na kumhami Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam. Umm Ammara pia

alihudhuria katika vita vya Yamammah.

Vile vile kuna Layla bint Abdullah bin Abd Shams bin Khalaf bin Shadad al-Qurashiyah

al-Adawiyah, ambae maarufu kama Shifaa Al Adawiyah au Umm Sulaiman, aliitwa Ash

Shifaa kwa sababu ya kua ni mwenye I’lm kubwa ya mambo mbali mbali ikiwemo

kuandika, kusoma na vile vile uwezo mkubwa wa kutibu kwa kutumia Ruqya, alipewa

ruhusa na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kutibu kwa kutumia Ruqya na

pia akawa mwalimu wa wanawake wengine akiwemo pia Hafsah Umm ul Muuminina.

Hali hii ni tofauti na wanavyofikiria wengi wasiomjua Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam, wasioujua Uislam na kuupinga na vile vile wasioijua historia ya watu

wa Magharibi, kwani wao huona kua Uislam unawabana kiakili, kifikra na pia

kuwavunjia wanawake haki zao, wakati ukweli ni kua Uislamu umewakomboa

Wanawake na kuwapa haki zao kwa miaka 1000 kabla ya hata watu wa Magharibi

kuanza kufikiria kuhusu haki za Wanawake, na ndio maana Hairunisaa Gul ambae ni

mke wa aliekua Rais wa Uturuki kuhusiana na Hijab yake akasema kua: ‘Hijabu yangu

ni kwa ajili ya kufunika kichwa changu, si kwa ajili ya kufunika akili zangu.’

Kwani hadi kufikia katika karne ya 17 wanawake wa Magharibi walikua kama

anavyoelezea Muingereza aliekua mpiganiaji wa haki za wanawake wa nchi za

Magharibi, aitwae Mary Wollstonecraft (1759-1797) kua: ‘Wanawake wa wakati

wangu wanafungwa kama vile ndege kwenye vijumba vyao, hawana la kufanya ila

kujipamba kwa kutumia unyoya na kuruka ruka kutoka katika tawi moja kuelekea

jengine’(A Vindication of the Rights of Woman), na kisha Mary Wollstonecraft

akawalaumu wanaume wa nchi za Magharibi kwa kuwatumia wanawake nyumbani na

kuwadhoofisha miili yao na kuzifinya akili zao kwa kutowapa kipaumbele.

Anasema Edward Turner ‘Wanawake wa Magharbi walikua hawana haki yeyote

isipokua haki ya waume zao. Hadi mwanzoni mwa karne ya 19, hali ya mwanamke

alieolewa katika nchi za Magharibi ilikua haimruhusu kufanya kazi ofisini, kupiga

kura katika uchaguzi, kuwemo katika mambo ya Sharia’h, kumiliki mali na

mwanamke anapoolewa basi mali yake yote ilikua inakua chini ya usimamizi wa

mumewe na inapotokea mke na mume kuachana basi mwanamke hua hana haki ya

kukaa na watoto.’(Edward Raymond Turner, ‘The Women's Suffrage Movement in

England’)


900

Tukirudi kwa mambo yalivyokua katika upande wa watu wa Arabuni kabla ya kuja

Uislam na namna yalivyobadilika ghafla na wanawake kujisikia kua wako huru baada ya

kuja Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam mfano mzuri ni pale tunapoangalia

Hadith ya Ubayd Ibn Umayr isemayo kua: ‘Aisha alilalamika kua Rasul Allah alikua

akikaa sana katika nyumba ya Zaynab bint Jahsh na kunywa Asali katika nyumba

yake, hivyo akasema: ‘Mimi na Hafsah tukakubaliana kua kila mmoja wetu

amuulize Mbona ninasikia harufu ya Maghafir katika mwili wako? Umekula

Maghafir?’’

Maghafir ni aina ya tunda kama ndimu tamu ambalo hutoa utufyuri au mvuke wenye

harufu, hivyo Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam alipoulizwa akasema

‏«لاَ‏ ، بَلْ‏ شَرِبْتُ‏ عَسَلاً‏ عِنْدَ‏ زَيْنَبَ‏ بِنْتِ‏ جَحْشٍ‏ وَلَنْ‏ أَعُودَ‏ لَه»‏

La! Bal sharibtu aA’salan ainda Zaynab bint Jahshi walan aAuuda lahu

‘La, sikula bali nilikunywa Asali kwa Zaynab bint Jahsh, lakini sitokula tena. ’

Kisa hiki ndio ikawa sababu ya kushuka aya ifuatayo:

﴿ َٰ ي ُّهَا ٱلن َّبىِ‏ ُّ لمَِ‏

تحَُرِّمُ‏ مَآ أَحَل َّ ٱهلل َُّ‏ لَكَ‏ تَبْتَغِى مَرْضَاةَ‏ أَزْوَاجِ‏ كَ‏ وَٱهلل َُّ‏ غَفُوٌر

ر َّحِ‏ يمٌ﴾‏

Ya ayyuha alnnabiyyu lima tuharrimu ma ahalla Allahu laka tabtaghee mardhata

azwajika waAllahu ghafoorun raheemun (Surat At Tahrim 66:1)

Tafsir: Ewe Nabii! Kwa nini unaharamisha kile ambacho Allah amekihalalisha juu

yako, Jee unatafuta kuwaridhisha wake zako? Hakika Allah ni mwingi wa Usamehevu

na ni mwingi wa Rehma.

Ingawa Hadith hii ya Ubayd In Umayr imemalizikia hapo lakini Allah Subhanahu wa

Ta’ala alimuwekea wazi Mtume wake Salallahu A’layhi wa Salam yale yaliyotokea na

hivyo Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam akawakasirikia wake zake, kama

anavyohadithia Abd Allah Ibn Abbas katika Hadith nyengine kwa kusema:


901

‘Nilikua na hamu kubwa ya kumuuliza Umar, kuhusiana na wake wawili ambao

walishirikiana dhidi ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam na hivyo

wakashushiwa aya aisemayo:

‏﴿إِن تَتُوآبَ‏ إِلىَ‏ ٱهلل َِّ‏ فَقَدْ‏ صَغَتْ‏ قُلُوبُكُمَا وَإِن تَظَاهَرَا عَلَيْهِ‏ فَإِن َّ اهلل ََّ‏ هُوَ‏ مَوْلاَهُ‏

وَجِ‏ برِْيلُ‏ وَصَالِحُ‏ الْمُؤْمِنِينَ‏ وَالْمَلاَئِكَةُ‏ بَعْدَ‏ ذٰلِكَ‏ ظَهِيرٌ‏ ﴾

In tatooba ila Allahi faqad saghat quloobukuma wa-in tadhahara AAalayhi fa-inna

Allaha huwa mawlahu wajibreelu wasalihu almu/mineena waalmala-ikatu baAAda

dhalika dhaheerun (Surat At Tahrim 66:4)

Tafsir : Ikiwa nyie wawili (Wake wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

ambao ni Aisha na Hafsah) mtatubu kwa Allah. Kwani kwa hakika nyoyo zenu

zimeegemea sana (katika kumpinga Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam

katika kile anachokipenda), lakini kama mkisaidiana dhidi yake, basi kwa hakika

Allah ni Msaidizi wake, na Jibril, na wachamungu miongoni mwa walioamini, na pia

Malaika ni wasaidizi wake.

Hadi pale Umar alipoenda Hija nami nikaenda pamoja nae, tulipokua njiani

alishuka kutoka katika kipando chake na akaenda kujisaidia, aliporudi

nikammiminia maji akanawa mikono yake na kutia udhu nami nikamuuliza, nae

akasema ‘Unashangaza Ya Ibn Abbas!’. (Az Zuhri ambae alikuwepo pia wakati huo

anasema kua: Wa Allahi Umar hakulipenda suali hilo lakini hakuficha kitu). Umar

Akajibu: ‘Walikua ni A’isha na Hafsah’, kisha Umar akaendelea: ‘Sisi Maquraysh

tulikua tunawamiliki Wanawake, hivyo tulikua hatuwaruhusu kuingilia mambo

yetu. Lakini tulipokuja Madinah tukakuta watu wamedhibitiwa na wanawake

wao, na wanawake wetu wakaanza kujifunza kutoka kwa wanawake wao.

Nyumba yangu ilikua iko karibu na nyumba za Banu Umayyah ibn Zayd, katika

Al Awali. Siku moja nilimkaripia mke wangu, nae akanijibu. Nikamwambia,

‘Inashangaza umefikia kiasi hiki sasa?!’, ‘Nae akaniambia, unakasirika kujibiwa

wakati wake wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, wanafanya hivyo

hivyo? Na mmoja kati yao atajitenga nae leo kwa siku nzima hadi usiku.’

Hivyo nikatoka na kuenda hadi kwa Hafsa na kumwambia ‘Jee unajibishana na

Rasul Allahi Salallahu A’layhi wa Salam?’ akasema ‘Naam’, nikamuuliza jee kuna

mmoja wenu ambae leo hii atajitenga nae?, nae akajibu ‘Naam’. Nami nikasema :

‘Yeyote yule miongoni mwenu atakaefanya hivyo basi atakua ameangamia, na ni

mwenye kupotea, Jee yuko yeyote yule miongoni mwenu mwenye uhakika kua


902

Allah atakua radhi nae kutokana na kumkasirisha Mtume wake Salallahu A’layhi

wa Salam? Kwani kama ni vyenginevyo basi atakua ameangamia, Usijibishane na

Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, usimshurutishe kitu chochote, bora

unaweza kunishurutishe mimi chochote kile unachokitaka, na usihadaike na

kumuiga jirani yako (yaani Aisha) kwani yeye ni mzuri zaidi kuliko wewe, na Rasul

Allah Salallahu A’layhi wa Salam anapenda zaidi kuliko wewe.’

Kisha Umar akaendelea kwa kusema ‘Kulikua na jirani yangu mmoja miongoni

mwa Ansari ambae nilikua nimepanga nae kua, ikiwa yeye atakua hayupo nami

nitakua na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, basi nitamwambia kile

alichokua hajakisikia, na mimi nikiwa sipo lakini yeye yupo basi ataniambia kile

nilichokua sijakisikia. Kwa wakati huo viongozi wa miji miengine walikua

washasalimu amri kwa Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, isipokua mfalme

wa Ghasan, ambae tulikua na wasi wasi kua huenda ikawa anajitayarisha

kutuvamia, na mara ghafla usiku mmoja yule jirani yangu akaja kuniambia:

‘Msiba! kuna jambo baya limetokea!’ nami nikamuuliza: Nini kimetokea? Mfalme

wa Ghasan kavamia?’ naye akanijibu : ‘La! Msiba mkubwa zaid ya huo, kwani

Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kaachana na wake zake wote’.

Nami nikasema ‘Hafsa ameshaangamia na kupotea, yale niliyoyafikiria yatatokea

ndio yaliyotokea’. Baada ya kusali Alfajir nikaenda kwa Hafsa na kumkuta analia na

nikamuuliza ‘Jee Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kakuacheni?’ nae akanijibu

‘Sijui ila amejitenga katika chumba cha juu’ nikaenda katika sehemu hiyo na kumkuta

mtumwa, nikamwambia nnataka kuonana na Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam,

akaingia ndani na kisha akarudi na kuniambia: ‘Nimemuambia kua unataka kuonana

nae lakini amenyamaza kimya’, nikaondoka na kuenda katika Minbar na kukuta watu

wakiwa wanalia, nikashindwa kustahmili nikarudi tena kwa yule mtumwa na

kumwambia aniombee ruhusa nionane nae Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam,

akaingia ndani na kurudi na kunijibu kama alivyonijibu mwanzo, nikaonodoka tena na

kurudi tena nikakataliwa na nilipokua nataka kuondoka nikaruhusiwa kuingia,

nilipoingia nikatoa salam na kumkuta Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam, kalala

juu ya mkeka, na mwili wake una alama ya mkeka.

Nikamuuliza ‘Ya Rasul Allah kweli umeachana na wake zako?’, akaniangalia na

kunijibu ‘La!’ Nami nikasema ‘Allahu Akbar! Ya Rasul Allah! Angalia sasa hivi

tulivyokua! Sisi Maquraysh tulikua ni wenye kuwatawala wanawake, lakini

tulipokuja Madinah tukakuta watu ambao wanatawaliwa na wanawake, na

wanawake wetu wakaanza kuwaiga wanawake hao, niligombana na mke wangu nae

akanijibu, hivyo nikakasirika na kumwambia umefikia kiasi hiki sasa hivi?’ Nae

akasema ‘Unanishangaa mie wakati wake wa Rasul Allah wanamfanyia hivyo

hivyo? Na mmoja miongoni mwao atatengana nae mchana na usiku wa leo!’ Nami

nikasema, ‘Yeyote atakaefanya hivyo basi atakua ni mwenye kuangamia, Jee yuko


903

miongoni mwao mwenye uhakika kua Allah ataridhika nae kutokana na

kumkasirisha Mtume wake?’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akatabasamu,

nami nikasema ‘Ya Rasul Allah nilienda kwa Hafsa na kumwambia Usihadaike na

kumuiga jirani yako (Aisha) kwani yeye ni mzuri zaid yako na anapendwa zaidi na

Rasu Allah kuliko wewe.’ Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akatabasamu tena.

Nikamwambia Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam: ‘Jee nijisikie huru kukuambia

jambo lolote?’ nae akasema ‘Naam’, hivyo nikakaa kitako chini na kuangaza chumbani

na kumwambia: ‘Uombee Ummah wako Ya Rasul Allah kwa Allah ili aujaalie uwe

Ummah ulionawiri, kwani amewajaalia Warumi na Waajemi kua ni watu

wanaoishi maisha mazuri, lakini hawamuamini Allah Subhanahu wa Ta’ala.’ Rasul

Allah Salallahu A’layhi wa Salam akakaa kitako na kusema: ‘Unatilia shaka Ya Ibn ul

Khattab! Hao ni watu ambao raha zao zimeharakishwa kwa ajili yao hapa Duniani.’

Hivyo nami nikasema : ‘Niombee maghfira kwa Allah, Ya Rasul Allah’. Rasul Allah

Salallahu A’layhi wa Salam aliapa kutowakaribia wake zake kwa mwezi mmoja kwani

alikua amewakasirikia sana, hadi pale Allah alipomkaripia. (Musnad Imam Ahmad, Imam

Bukhari na Imam Muslim)

Hivyo ingawa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, alikua akiwakasirikia na

kuwakaripia lakini hakuwahi kuwapiga ahl zake, bali alikua ni mpole, mwenye huruma,

mstahmilivu na muadilifu kwao kwa kila mtu na kila kitu. Allah Subhanahu wa Ta’ala

anatuthibitisha haya katika Qur’an pale aliposema:

‏﴿لَقَدْ‏ جَآءَكُمْ‏ رَسُولٌ‏ مِّنْ‏ أَنفُسِ‏ كُمْ‏ عَزِيزٌ‏ عَلَيْهِ‏ مَا عَنِت ُّمْ‏ حَرِيصٌ‏ عَلَيْكُمْ‏ بِٱلْمُؤْمِنِ‏

رَءُوفٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

‏َين

Laqad jaakum rasoolun min anfusikum AAazeezun AAalayhi ma AAanittum

hareesun AAalaykum bialmu/mineena raoofun raheemun. (Surat At Tawba 9:128)

Tafsir: Kwa hakika, amekujieni Mtume (Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam)

kutoka miongoni mwenu, Inamuuma sana kua nyinyi mdhurike au mpate matatizo,

ana wasiwasi juu yenu (ili mpate kuongoka, na mtubu kwa Mola wenu, ili mpate

kuingia Peponi na muokoke na moto) kwa waumini Yeye (Nabii Muhammad Salallahu

A’layhi wa Salam) Ni mwingi wa Huruma na mwingi wa Rehma.

Na huu ndio msingi wa Dini ya Kiislam kama inavyojionesha wazi, kwani katika kipindi

cha uhai wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam mambo mbali mbali

yahusuyo jamii ya Kiislam, matatizo na utatuzi wake yaliainishwa na kuwekwa wazi


904

hatua kwa hatua kwa manufaa ya Ummah wa Kiislam kupitia katika njia ya hukmu na

Sharia’h za Kiislam zilizokua zinaendelea kutolewa na kuteremshwa kutokana na

mazingira na maisha ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam.

Katika kipindi hiki ilikua kila Waislam wanapotokewa na tatizo basi humfuata Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam ili kuulizia utatuzi wa tatizo hilo na Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam alikua akitoa hukmu, na aidha hukmu hiyo

ilikua imepitia katika aya ya Qur’an aliyoteremshiwa, au kwa Hadith na baadhi ya wakati

hukmu zilikua zinapatikana kutokana na vitendo vyake mwenyewe Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam na pia kutokana na kukubali ama kukemea vitendo vya

Masahaba zake.

Vyovyote vile alivyoamua na kuhukumu Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam,

basi alikua hasemi tu kwa matamanio yake, bali hua ni Wahy kutoka kwa Mola wake,

iwe kwa njia ya Hadith ul Quds ama kwa njia ya Qur’an. Kwani Allah Subhanahu wa

Ta’ala amesema katika Qur’an:

‏﴿وَمَا يَنطِقُ‏ عَنِ‏ - يُوحَ‏ ٰ ى ﴾

ٱلهَْوَىٰ‏

وَحْى

ٌ

إِنْ‏ هُوَ‏ إِلا َّ

Wama yantiqu A’ani alhawa; In huwa illa wahyun yooha (Surat An Najm 53: 3-4).

Tafsir: Na hazungumzi kutokana na matamanio yake, kwa hakika haikua ila ni Wahy

tuliomshushia.

Hukmu na Sharia’h zilizokua zinatoka kwa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam, zilikua zinategemea njia mbili ambazo ni Qur’an na Sunnah. Na inapotokea kua

kumetolewa hukmu ambayo haikutokana na Qur’an na ikawa ina kasoro basi Malaika

Jibril A’layhi Salatu wa Salam ambae alikua kama mwalimu wa Nabii Muhammad

Salallahu A’layhi wa Salam hushuka na aya ya Qur’an na kurekebisha hukmu au jambo

hilo kama tulivyoona katika Hadith inayoelezea sababu ya kushuka aya ya Surat A

Tahrim 66:1.

﴿ َٰ ي ُّهَا ٱلن َّبىِ‏ ُّ لمَِ‏ تحَُرِّمُ‏

مَآ أَحَل َّ ٱهلل َُّ‏ لَكَ‏ تَبْتَغِى مَرْضَاةَ‏ أَزْوَاجِ‏ كَ‏ وَٱهلل َُّ‏ غَفُوٌر

ر َّحِ‏ يمٌ﴾‏

Ya ayyuha alnnabiyyu lima tuharrimu ma ahalla Allahu laka tabtaghee mardata

azwajika waAllahu ghafoorun raheemun (Surat At Tahrim 66:1)


905

Tafsir: Ewe Nabii! Kwa nini unaharamisha kile ambacho Allah amekihalalisha juu

yako, Jee unatafuta kuwafurahisha wake zako? Hakika Allah ni mwingi wa

Usamehevu na ni mwingi wa Rehma.

Hivyo kuna baadhi ya aya za Qur’an zilizoteremshwa kutokana na matukio maalum, au

kwa ajili ya kujibu masuala maalum, na vile vile kuna baadhi ya aya zilizoteremshwa bila

ya kutokea matokeo au maswali maalum ambayo yaliyopelekea kushuka kwa aya hizo.

Tukiiangalia Qur’an kwa ujumla basi tunaona kua kuna aya ambazo zilishuka katika mji

wa Makkah, ambazo zinahusisha theluthi mbili ya aya zote za Qur’an ambazo hizi

hujulikana kama aya za Makkah (Makki). Kwa ujumla zinajumuisha asilimia ndogo ya

hukmu (Ahkami), kwani zinazungumzia zaid kuhusiana na kuelezea na kufundisha

misingi ya Kiislam na kuwaita watu katika dini ya Kiislam, kama vile kuhusiana na

Kumuamini Allah Subhanahu wa Ta’ala na Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa

Salam, kuamini siku ya Malipo, Kuamrisha kusimamisha Sala, kufahamisha Maadili na

Akhlaq za Kiislam kama kusema ukweli, kua na uaminifu, kukataza mambo maovu,

mauaji, kuzikwa watoto wa kike walio hai, kupunja katika mizani n.k

Na vile vile kuna aya ambazo zilishuka katika mji wa Madinah ambazo hizi

zinajumuisha robo tatu ya aya zote Qur’an na zinajulikana kama aya za Madinah

(Madani). Aya hizi zinazungumzia Mu’amalat (Mambo ya kubadilishana katika biashara

kuuza, kununua, kukodishana, riba n.k). Vile vile katika aya hizi pia ziko zile

zinazozungumzia kuhusiana na Hudud (zinazohusiana na Adhabu za makosa ya Zina,

Wizi, Riba n.k ), Jinayat (zinazohusiana na adhabu za makosa ya Jinai kuhusiana na

adhabu ya mauaji ya mtu alieua kwa kukusudia, adhabu za Majambazi, n.k), Bayyinat

(zinazohusiana na namna ya kupata ushahidi katika kesi mbali mbali). Hukmu zilizobakia

zinazozungumzia kuhusiana na Ibada za Sala, Zakkah, Hijjah na Jihadi pia

ziliteremshwa katika kipindi hiki cha Madinah .

Tofauti na namna vilivyoteremshwa vitabu vyengine vyote vilivyotajwa katika Qur’an,

yaani Taurat, Zabur na Injil, ambavyo viliteremshwa kila kimoja kwa wakati mmoja,

kwani kama tulivyoona kua Qur’an ilishushwa hatua kwa hatua, na sababu ya kushuka

kwake hivyo inawekwa wazi na Allah Subhanahu wa Ta’ala pale aliposema katika Surat

al Furqan kua:

‏﴿كَذٰ‏ لِكَ‏ لِنُثَبِّتَ‏ بِهِ‏ فُؤَادَكَ‏ وَرَت َّلْنَاهُ‏ تَرْتِيلاً‏ ﴾

Kadhalika linuthabbita bihi fu-adaka warattalnahu tarteelan (Surat Al Furqan

25:32)


906

Tafsir: Kadhalika ili kukipa ithibati (kukipa nguvu) kifua chako juu yake (ya Qur’an),

na tukakushushia kwa mpangilio.

Na pia katika Surat al Israa iliposema:

‏﴿وَقُرْآً‏ فَرَقْنَاهُ‏ لِتَقْرَأَهُ‏ عَلَى ٱلن َّاسِ‏ ٰ عَلَى مُكْثٍ‏ وَنَز َّلْنَاهُ‏ تَنْزِيلاً‏ ﴾

Waqur-anan faraqnahu litaqraahu AAala alnnasi AAala mukthin wanazzalnahu

tanzeelan (Surat Al Israa 17:106)

Tafsir: Na Qur’an tuliyoigawa (katika sehemu sehemu), ili upate kuwasomea watu

hatua kwa hatua, Na kwa uteremsho uliopangika kwa vituo.

Hikma kubwa iliyomo ndani ya kuteremshwa kwake Qur’an hatua kwa hatua ni

kumfunza mambo mapya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kila baada ya

mda, na kidogo kidogo kumuongoza katika njia sahih ili kumpa msimamo thabit, na hivyo

hua rahisi kwake yeye na kwa wafuasi wake kuweza kuihifadhi, huku wakiifanyia kazi

kwa vitendo, vile vile kwa kua Allah Subhanahu wa Ta’ala anawajua viumbe wake basi

alikua akijua kua itakua ni vigumu kwa ghafla moja kubadilisha kila njia na mifumo ya

maisha waliyokua wakiishi viumbe vyake, na hivyo katika mteremsho huo Qur’an ikawa

kidogo kidogo inafungamana na mfumo mpya wa maisha ya Kiislam unaongoza na

kubagua baya na zuri kwa manufaa yao.

Kulingana na mtizamo wa Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazal

basi tunaona kua kimpangilio Qurán ina aya ambazo zina Marijani na pia ina aya zenye

Lulu. Aya zenye Marijani ni zile aya ambazo maalum zinazungumzia kuhusiana na Allah

Subhanah wa Ta’ala, Majina yake, Sifa zake na Kazi zake. Hizi zinawakilisha

utambulisho wake Allah Subhanahu wa Ta’ala kwa ufahamu wa waja wake. Aya hizi

ziko 763 ambapo aya 7 miongoni mwao zinajumuisha aya zote za Surat al Fatiha.

Aya zenye Lulu ni zile aya ambazo zinazoielezea njia iliyonyooka na kuamrisha,

kuhamasisha na kumtia ari mtu kuifuata njia hiyo. Hizi zinawakilisha utambulisho wa

namna ya kuifanyia kazi kivitendo njia hiyo iliyonyooka. Aya hizi ziko 741, ambapo aya

46 miongoni mwao zinapatikana katika Surat Al Baqara zikiwemo aya 5 za mwanzo za

Sura hiyo.

Kutokana na mpangilio na utaratibu wa uteremsho huo basi tunaweza kuona kua

Maamrisho, Makatazo, Hukmu na Sharia’h za Kiislam hazikuteremshwa zote kwa

pamoja bali ziliteremshwa kidogo kidogo kupitia aya moja moja za Qur’an ambazo


907

baadhi yao zilikua zikijifafanua wenyewe na nyengine zilikua zikifafanulika kupitia kwa

aya nyengine na pia zikiungwa mkono na kufafanuliwa katika njia ya Hadith na Sunnah

za Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam.

Hivyo basi bila ya shaka ni jambo lililowazi kua ni vigumu kufafanua au kutoa Hukmu

na Sharia’h Sahih kutoka katika vyanzo hivyo vya Qur’an na Sunnah, kwa yule ambae

mtu hana utaalam unaotakiwa ambao utamfanya ajue ni Hukmu na Sharia’h zipi

zilizokuja kabla na ni zipi zilizokuja baadae, kutokana na kutojua aya ipi inaifafanua aya

ipi, Hadith ipi inaunga mkono aya ipi, Hadith ipi inafafanua aya ipi n.k.

WANAWAKE WALIO JIPENDEKEZESHA KINDOA NA

WALIOCHIKA WA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA

SALAM.

Naam kama tulivyoona kuhusiana na namna ilivyokua ndoa ya Maymuna Bint Harith

Radhi Allahu Anha basi tunaona pia kua kuna Wanawake wengi sana Wacha Mungu

ambao walijipendekeza pia kwa Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam ili wapate

kuolewa nae, kama inavyothibitisha hadithi isemayo : ‘Anasema Thabit Al Bunani

Radhi Allahu Anhu kua: ‘Hakika mimi nilikua niko pamoja na Anas, ambae alikua

na Bint yake. Hivyo Anas akasema: ‘Kuna Mwanamke alikuja kwa Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na akajipendekezesha kwake ili aolewe nae kwa kusema:

‘Ya Rasul Allah, Hivi Jee unaweza kunitaka mimi?’ ambapo Bint yake Anas

akasema: ‘Inakuaje mpaka inafikia hali hii kua watu hawana haya?’

Ambapo Anas akasema: ‘Hakika huyu Mwanamke ni bora zaidi kuliko wewe kwani

yeye alitaka kua aolewe na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na

akajipendekezesha kwake kwa ajili ya Ndoa.’’’(Imam Bukhari)

Imam Al Bukhari ana hadith nyengine pia ambayo inayosema kuhusiana na jambo hili

kua: ‘Aisha Radhi Allahu Anha alisema kua: ‘Hakika mimi nilikua ni mwanamke

mwenye Wivu sana dhidi ya Wanawake wanaojipendekeza wenyewe kwa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam, hadi pale Allah Subhanah wa Ta’ala aliposhusha

aya ifuatayo’’


908

‏﴿تُرْجِ‏ ى مَن تَشَآءُ‏ مِنْهُن َّ وَتُؤْوِي ۤ إِلَيْكَ‏ مَن تَشَآءُ‏ وَمَنِ‏ ٱبْتَغَيْتَ‏ ممِ َّنْ‏ عَزَ‏ لْتَ‏ فَلاَ‏

جُنَاحَ‏ عَلَيْكَ‏ ذٰلِكَ‏ أَدْنىَٰ‏ أَن تَقَر َّ أَعْيُنُهُن َّ وَلاَ‏ يحَْزَن َّ وَيَرْضَينَْ‏ بمَِآ آتَيْتَهُن َّ كُل ُّهُ‏ َّن

وَٱهلل َُّ‏ يَعْلَمُ‏ مَا فىِ‏ قلُوبِكُمْ‏ وَكَانَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلِيماً‏ حَلِيماً‏ ﴾

Turjee man tashao minhunna watu/wee ilayka man tashao wamani ibtaghayta

mimman AAazalta fala junaha AAalayka dhalika adna an taqarra aAAyunuhunna

wala yahzanna wayardhayna bima ataytahunna kulluhunna waAllahu yaAAlamu

ma fee quloobikum wakana Allahu AAaleeman haleeman(Surat Al Ahzab 33:51)

Tafsir: Nawe (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) unaweza kumrudisha

umtakae miongoni mwao (wake zako) na unaweza kumpokea umtakae. Na yeyote yule

unaemtamani miongoni mwa wale uliowaweka kando (kwa kumuacha kwa muda),

basi hamna kosa kwako (Kumrudia) hivyo ni bora, ili wawe ni wenye kuliwazika na

wasiwe ni wenye kuhuzunika na hivyo wote kua ni wenye kuridhika kutokana na kile

utakachowapa. Allah anajua kile kilichomo ndani ya Nyoyo zenu na yeye ni mwenye

kujua juu ya kila kitu na ni mwenye ustahmilivu.

Aisha Radhi Allahu Anha anaendelea kusema kua: ‘Baada ya kushuka aya hii basi

nikamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Inaonekana kua Mola

wako anaharakisha kufuatilia matamanio yako’’

Hivyo Wanawake ambao waliojipendekeza kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

ili waolewe nae wako wengi kiidadi kama vile ilivyokua pia kua kuna Wanawake wengi

ambao aliwahi kuwaposa lakini hakuwahi kuwaoa na pia aliowaposa kuwaoa na kisha

akawaaacha bila ya kuwaoa kwa sababu mbali mbali zinazokubalika kisharia, ambapo

miongoni mwao Wanawake hao basi ni pamoja na:

Amra bint Yazid Al Ghifariyya ambae alipotakiwa kuolewa na Rasul Allah Salallahu

A’layhi wa Salam basi akasema: A`udhu billah mink, hakika mimi naomba ulinzi kutoka

kwa Allah dhidi yako, na hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakumuoa.

Asma’ bint Ka`b ambae alikua mzuri sana lakini alipoolewa alizidiwa akili na wivu wa

wake wengine wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo katika usiku wake

wa ndoa akamwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua A`udhu billah mink,

hakika mimi naomba ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yako, na hivyo Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akaachana nae na hakuolewa tena Mwanamke huyu hadi kufariki

kwake.


909

Azza Bint Abi Sufyan Ibn Harb ambae ni Dada yake Ummu Habiba, ambapo Azza

mwenyewe na baba ambae ni Abu Sufyan Radhi Allahu Anhu walitaka kua Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam amuoe Azza lakini Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akasema kua hairuhusiki kwa Muislam kuwaoa Wanawake ndugu wawili kwa wakati

mmoja.

Duba`a Bint `Amir Ibn Qurt ambae aliposwa lakini hakuolewa na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam

Ummu Hani Fakhta Bint Abu Talib ambae alikua ni Bint Ami yake Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam ambae alichumbiwa na Hubayra Ibn Makhzum na Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam pia lakini Abu Talib akamuozesha kwa Hubayra na

alipoingia katika Uislam na kuachika basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akataka kumuoa lakini Umm Hani akasema: ‘Hakika mimi nilikupenda wewe tangu

wakati wa Ujahiliyah hivyo nitasema nini katika wakati wa Uislam, lakini sasa

mimi nina watoto wadogo na nnakhofu kua Watakua wanakukera wewe’ hivyo

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Wanawake bora ni wenye kupanda

Ngamia miongoni mwa Wanawake wa Quraysh, kwani wao ni wenye kuwapenda

sana watoto wao na ni wenye kujitolea kwa ajili yao na ni wenye uadilifu mkubwa

juu ya haki za Waume zao’(Imam Muslim)

Fatma Bint Al Dahhak Ibn Sufyan Al Kilabiyya ambae aliamua kuchagua Dunia yake

na akawa na hali ya Umasikini Mkubwa sana pale Allah Subhanah wa Ta’ala

alipomwamrisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuwapa hiari wake zake

wachague Dunia yao au Akhera yao ama ilivyosema aya:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱلن َّبىِ‏ ُّ قُلِ‏ لأَزْوَاجِ‏ كَ‏ إِن كُنتنُ َّ تُرِدْنَ‏ ٱلحَْيَاةَ‏ ٱلد ُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَينَْ‏ أ ُ مَتِّعْكُ َّن

وَأُسَرِّحْكُن َّ سَرَاحاً‏ جمَِيلاً‏ ‏۞وَإِن كُنتنُ َّ تُرِدْنَ‏ ٱهلل ََّ‏ وَرَسُولَهُ‏ وَٱلد َّارَ‏ ٱلآخِ‏ رَةَ‏ فَإِن َّ ٱهلل ََّ‏

أََعد َّ لِلْ‏ مُحْسِ‏ نَاتِ‏ مِنكُن َّ أَجْراً‏ عَظِيماً‏ ﴾

Ya ayyuha alnnabiyyu qul li-azwajika in kuntunna turidna alhayata alddunya

wazeenataha fataAAalayna omattiAAkunna waosarrihkunna sarahan jameelan;

Wa-in kuntunna turidna Allaha warasoolahu waalddara al-akhirata fa-inna Allaha

aAAadda lilmuhsinati minkunna ajran AAadheeman (Surat Al Ahzab 33:28-29)

Tafsir: Ewe Nabii waambie wake zako kua: ‘Kama mnataka Maisha ya Dunia na

mapambo yake basi njooni nitakupeni na nitaachana nanyi kwa njia nzuri’. Lakini

kama mnamtaka Allah na Mtume wake na maisha ya Akhera basi basi Allah

amewatayarishia wenye kufanya Mema miongoni mwenu Malipo bora sana.


910

Ambapo kuhusiana na sababu ya kushushwa aya hii pia basi anasema Jabir Ibn `Abdullah

kua: ‘Alikuja Abu Bakr kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kuomba

ruhusua kuinga ndani, lakini akakuta watu wamekaa kitako na hakuruhusiwa

kuingia Ndani, kisha akaja Umar na akaomba ruhusa kuingia Ndani lakini nae

hakuruhusiwa kuingia. Halafu wote Abu Bakr na Umar wakaruhusiwa kuingia

ndani na kumkuta Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akiwa amekaa kimyaa

akiwa na wake zake waliokua wamemzuguka.’

Hivyo Umar akasema ndani ya Nafsi yake kua: ‘Wacha mimi niseme kile ambacho

kitamfurahisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam’ hivyo akasema: ‘Ya Rasul

Allah natamani kama ungemuona Bint Zayd pale aliposema kuniambia kua

anataka nimuongezee pesa za Matumizi, kwani nilimpatia maumivu ya kwenye

shingo badala yake (yaani alimpiga kibao cha shingo)’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akacheka na kisha akasema: ‘Naam..kama

mnavyoona hata hawa walionizunguka mimi pia wanataka muongezo wa pesa za

Matumizi’. Ambapo baada ya kusikia maneno hayo basi Abu Bakr na Umar Radhi

Allahu Anhum kila mmoja akasimama na kumpiga Binti yake Kibao cha shingo yaani

Abu Bakr Radhi Allahu Anhu akampiga Aisha Radhi Allahu Anha na Umar Ibn Al

Khattab Radhi Allahu Anha akampiga Hafsa Radhi Allahu Anha.

Huku Abu Bakr na Umar Radhi Allahu Anhum wakisema: ‘Hivi Nyinyi mnamuomba

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kile ambacho asichokua na uwezo nacho?’

ambapo hapo hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaingilia kati kuwaombea

wake zake na wake zake hao Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam wakasema kua:

‘Wa Allahi kuanzia sasa hivi hatutomuomba tena kile kitu ambacho hana.’ Halafu

baaa ya hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akajitenga nao wake zake kwa

mwezi mzima na kisha Allah Subhanah wa Ta’ala akazishusha aya hizi Surat Al Ahzab

33:28-29

Hivyo baada ya hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawaambia wake zake

kuhusiana na aya hizi kwa kuanza na Aisha Radhi Allahu Anha kwa kusema kua:

‘Nilikua nataka kupendekeza kitu kwako, lakini sitaki uwe ni mwenye kua na

papapara katika kunijibu na bora ushauriane na wazee wako kwanza.’ Ambapo

Aisha Radhi Allahu Anha akauliza: ‘Kuhusiana na nini?’ Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam akamsomea aya hizi:

‏﴿َٰي ُّهَا ٱلن َّبىِ‏ ُّ قُلِ‏ لأَزْوَاجِ‏ كَ‏ إِن كُنتنُ َّ تُرِدْنَ‏ ٱلحَْيَاةَ‏ ٱلد ُّنْيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَينَْ‏ أ ُ مَتِّعْكُ َّن

وَأُسَرِّحْ‏ كُن َّ سَرَاحاً‏ جمَِيلاً۞وَإِن كُنتنُ َّ تُرِدْنَ‏ ٱهلل ََّ‏ وَرَسُولَهُ‏ وَٱلد َّارَ‏ ٱلآخِ‏ رَةَ‏ فَإِن َّ ٱهلل ََّ‏


911

أَعَد َّ لِلْمُحْسِ‏ نَاتِ‏ مِنكُن َّ أَجْراً‏ عَظِيماً‏ ﴾

Ya ayyuha alnnabiyyu qul li-azwajika in kuntunna turidna alhayata alddunya

wazeenataha fataAAalayna omattiAAkunna waosarrihkunna sarahan jameelan;

Wa-in kuntunna turidna Allaha warasoolahu waalddara al-akhirata fa-inna Allaha

aAAadda lilmuhsinati minkunna ajran AAadheeman (Surat Al Ahzab 33:28-29)

Tafsir: Ewe Nabii waambie wake zako kua: ‘Kama mnataka Maisha ya Dunia na

mapambo yake basi njooni nitakupeni na nitaachana nanyi kwa njia nzuri’. Lakini

kama mnamtaka Allah na Mtume wake na maisha ya Akhera basi basi Allah

amewatayarishia wenye kufanya Mema miongoni mwenu Malipo bora sana.

Ambapo Aisha Radhi Allahu Anha akasema: ‘Ya Rasul Allah hivi jee mimi nahitajiwa

kushauriana na wazee wangu kuhusiana nawe? hakika mimi namchagua Allah na

Mtume wake, lakini usiwaambie wake zako wengine kuhusiana na Maamuzi yangu

haya.’ Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Allah hakunituma mimi kua

mtu mwenye kuzidisha ugumu, bali amenituma kwa ajili ya kufundisha na

kurahisisha mambo, hakuna atakaeniuliza kuhusiana na maamuzi yako lakini mimi

nitabainisha maamuzi yako.’

Ambapo kwa upande mwengine basi hii aya inajulikana kua kama ni Aya ya Takhyir

yaani aya ya Khiyari, ambapo Kifiqh basi hua ni yenye kutumika kubainisha Hukmu

inayohusiana na talaka.

Pale Mume anapomwambia Mkewe kua: ‘Una khiyari aidha ya kubaki nami ama

kuondoka’

Hivyo kama Mwanamke akiamua kuondoka basi hukmu yake inakua ni kaachika

kwa Talaka Moja kati ya Talaka tatu kwa mpigo yaani Talaqa Bayin na kama

akiamua Kubakia basi hua hajaachika. Na hivyo Mume hua hawezi kua nae Mke

huyo hadi atakapomrudia tena upya kwa mahari mapya na makubaliano mapya,

ambapo hii hua inamaanisha kua Mke anaweza kukataa kurudiwa jambo ambalo

hua ni la hali tofauti na Talaq al Rajii ambayo hua inamapa Mume haki ya

Kumrudia Mke bila ya makubaliano mapya.

Na pia pale Mwanamke anapopewa haki hii basi hua hakuna upande wowote

utakaoweza kubadilisha maamuzi pale inapokua Mwanamke ameamua Kuondoka,

lakini kama Mwanamke akikaa kimya basi hua inamaanisha kua kauli ya Mume

haina nguvu ya kisharia na hivyo masharti yake hua yanabatilika.

Habiba Bint Sahl Ibn Tha`laba Al Najjariyya: Ambae hakuoana nae.


912

Jumra Bint Al Harith Ibn `Awf Al Muzani: Ambapo kulikua na Posa lakini hakukua

na Ndoa baada ya Baba Jumra kusema uongo kua Binti yake anaumwa ambapo baada ya

kusema kwake huko basi Binti huyo akapata maradhi ya Ukoma.

Khawla Bint Al Hudhayl Ibn Hubayra Al Tha`labiyya: Ambae aliolewa baada ya

kujipendekezesha kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na kukubaliwa wakati

Mwanamke huyu alipokua katika Ardhi ya Sham kabla ya kuonana na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na hivyo baada ya Ndoa hio na alipofunga Safari kutoka

Sham kuelekea Madina basi akafariki njiani.

Safiyya Bint Bashama Ibn Nadla Al`Anbariyya. Ambae alikua ni mateka wa Vita na

alipewa hiari ya kuolewa na Rasul Allah Salallahu A’alayhi wa Salam au kuachiwa huru

na kurudishwa kwa Mumewe na akachaga kuridhishwa kwa Mumewe.

Shanba’ Bint `Amr Al Ghifariyya: Aliolewa akaachika baada ya kusema kua: ‘Kama

Ibrahim alikua ni Mtoto wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi

asingefariki’

Umamah Bint Hamza Ibn Abd Ul Muttalib: Ambae alijipendekezesha kwa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam, lakini Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akakataa

kwa sababu ya kua Hamza Ibn Abd ul Muttalib Radhi Allahu Anhu alikua pia ni kaka

yake walienyonya ziwa moja.

Khuwayla Bint Hakim Ibn Umayya Al Sulamiyya: Ambae alijipendekezesha kwa

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, lakini Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam,

akamkataa na hivyo badala yake akaolewa na Uthman Ibn Madhun Radhi Allahu Anhu.

MAVAZI YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM.

Tunapoangalia mavazi ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi kuna mavazi ya

aina tofauti ambazo aliyokua akipenda kuyavaa kama ilivyokuja kwenye vitabu Hadith

tofuati za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambapo miongoni mwao kuna

zisemazo kua alikua ni mwenye kuvaa mavazi yafuatayo:

Kwani amesema Amr Ibn Hurayth Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mimi nilimuona Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akiwa juu ya Minbar huku akiwa amevaa Kilemba

cheusi ambacho ncha zake mbili zilikua zinanig’inia mabegani mwake’

Na amesema Jabir Ibn Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam aliingia kwenye Mji wa Makkah huku akiwa amevaa Kilemba

Cheusi’(Sahih Muslim)


913

Hivyo basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akivaa Kilemba cha kawaida

kama vile wanavyovyaa watu wa Yemen au Sudan ambacho hua kinajulikana kama As

Sahaab ambacho baadhi ya wakati alikua akikiwachia pembe zake ziwe ni zenye

kuning’inia kwenye mabega yake na baadhi ya wakati alikua hakiwachii na baadhi ya

wakati alikua akiupitisha upande mmoja wa kilemba hicho chini ya kidevu chake na chini

yake kilemba hicho alikua akivaa Kofia laini za kawaida zinazojulikana kama

Qalansuwah na baadhi ya wakati alikua akivaa Kilemba bila ya kofia.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua akivaa pia Qamis yaani Kanzu za Msikitni

za Mikoni mirefu na hili lilikua ndio vazi analolipenda zaidi, na pia alikua akivaa kanzu

za mikono mifupi na alikua akivaa Jubba au Joho mfano wake ambayo kama wanavyovaa

Wanazuoni wa Al Azhar Misri.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua anapokua safarini basi hua ni mwenye

kuvaa Joho ambalo ni lenye Mikono iliyobana mwishoni, na pia alikua akivaa Izzar yaani

Seruni au Kikoi kutoka Oman na kisha juu yake alikua akijifunika Ridhaa yaani

Kitambaa kama kivaachwo wakati wa Ihram.

Na pia alikua akivaa Hulla yaani Nguo mbili za juu na chini zinazofanana rangi ambazo

mara nyingi ilikua ni kutokana na kitambaa cha Mavazi ya Yemen chenye rangi

Nyekundu na mistari myeusi.

Alikua akivaa Bantaloon yaani Suruali na Khuffaayn viatu vya ngozi laini na Taasumah

yaani kama kanda mbili za Ngozi.

Imam Ibn Sa’ad anasema kutoka kwa (Sahaba) Niyar al Aslami Radhi Allahu Anhu kua

wakati Umar alipotoka kuenda kusali Sala ya mvua, alitoka akiwa amevaa burd (joho) la

Nabii Salallahu A’layhi wa Salam.

Na Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu anasema pia kua: ‘Mimi nilimuona Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akitia udhu huku akiwa amevaa Kilemba cha Qitr’(Imam

Abu Daud) ambapo Qitr hua ni iana ya Kilemba chenye kitambaa kigumu chenye rangi

Nyekundu.

Na Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Mfalme wa Rumi alimtumia Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam zawadi ya Koti la Manyoya lenye mikono mirefu ambalo

ambalo lilifumwa pembeni yake kwa upindo wa Hariri na akalivaa’(Imam Ahmad)

Ama kuhusiana na Taylasaan yaani Kilemba cha kuweka tu juu ya kichwa

kinachoangukia mabegani au kinachowekwa mabegani tu, basi amesema Anas Ibn Malik

Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam amesema kua Dajjal


914

ataibuka huku akiwa amefuatana na Mayahudi 70000 wa Asbahaan watakaokua

wamevaa Taylasaan’(Sahih Muslim) hivyo ni makruh kuvaa Taylasaan.

Na amesema Abu Rimthah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Nilimuona Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam akitoa Khutba huku akiwa amevaa Nguo mbili za rangi ya

Kijani.’(Sunan An Nasai) ambapo nguo hizi za rangi ya Kijani hua ni kama ilivyokua

nguo zake nyekundu yaani hua ni zenye mistari ya hapa na pale.

HIJA YA KUAGA YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA

SALAM.

Anasema Jabir Ibn Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alikua alifanya Hija mara mbili kabla ya Hijra.’

Na Sufyan Ath Thawry anasema kua: ‘Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

Alifanya Hija mara kadhaa kabla ya Hijra’

Ambapo mnamo mwaka wa 9 wa Utume wake basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam alishushiwa na Allah Subhanah wa Ta’ala aya inayoamrisha Ibada ya Hija kwa

Waumini wote ambayo ni yenye kusema:

‏﴿فِيهِ‏ آَتٌ‏ بَيِّ‏ نَاتٌ‏ مَقَامُ‏ إِبْرَاهِيمَ‏ وَمَنْ‏ دَخَلَهُ‏ كَانَ‏ آمِنًا وَ‏ هللِ َِّ‏ عَلَى الن َّاسِ‏ حِ‏ ج ُّ الْبَيْتِ‏

مَنِ‏ اسْتَطَاعَ‏ إِلَيْهِ‏ سَبِيلاً‏ وَمَنْ‏ كَفَرَ‏ فَإِن َّ اهلل ََّ‏ غَنيِ ٌّ عَنِ‏ الْعَالَمِينَ‏ ﴾

Feehi ayatun bayyinatun maqamu ibraheema waman dakhalahu kana aminan

walillahi AAala alnnasi hijju albayti mani istataAAa ilayhi sabeelan waman kafara

fa-inna Allaha ghaniyyun AAani alAAalameena (Surat Al Imran 3:97)

Tafsir: Ndani yake mna dalili ambazo zilizowazi katika Maqam Ibrahim, na yeyote

atakeingia ndani yake basi atakua Salama, na Allah anataka kutoka kwa watu kua

wahiji kwenye Nyumba yake kwa mwenye Uwezo, lakini kwa asieweza basi kwa hakika

Allah ni tajiri wa kuhitaji kutoka kwa Walimwengu.

Ambapo anasema Mujaddid Ad Din Imama Fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam amesema: ‘Allah ameiwajibisha Hija juu yenu hivyo ni

wajibu wenu kuenda katika Hija’ hapo kuna mtu akasimama na akauliza: ‘Ya

Rasul Allah, Jee ni wajibu wa kila mwaka?’ ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam akakaa kimya hadi pale mtu huyo alipouliza suali hilo mara 3 kisha


915

akasema: ‘Kama ningesema naam basi ingekua ni Wajib juu yenu na nyinyi

msingeweza kutekeleza hilo.’

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamalizia kwa kusema: ‘Niwacheni hadi

pale nitakapokuwacheni, kwani Umah wa watu waliotangulia uliagamizwa kwa

sababu ya kuzidi kuuliza masuali na kuhoji kwao Mitume wao. Hivyo

ninapoamrisha jambo basi lifanyeni kwa kadri mtakavyoweza kulingana na uwezo

wenu na ninapokataza jambo basi liepukeni’

Kwa maana hio basi kama Muislam anao uwezo na kisha akwa hajaenda Hija basi

ataulizwa juu yake, na jukumu lake hilo kamwe haiwezekanni kutekelezewa na mtu

mwengine badala yake. Ambapo ingawa kuna hadith isemayo kua: ‘Amesema Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Yeyote yule mwenye uwezo wa kutembelea

Nyumba ya Allah na kisha akawa hajaenda Hija basi akifariki hua ni mwenye

kufarikia katika hali ya Uyahudi au Ukristo’’ basi kulingana na Mtizamo wa

Wanazuoni miongoi mwao akiwemo Imam Ibn Kathir, Imam Ashanqiti n.k basi wao

wanasema kua hii ni Hadith Dhaif.

Na kulingana na hukmu ya kisharia kuhusiana na Hija basi kuna mitizamo ifuatayo:

1-Wengi mingoni mwa wanazuni wanasema kua Ibada ya Hija inaweza

ikacheleweshwa kutokana na hali ya Mazingira aliyokua nayo mtu isipokua

kufanywa kwa kutocheleweshwa ni bora zaidi.

2-Kama ikiwa Mtu alifanya Ibada ya Hija wakati akiwa Mtoto mdogo ambae

hajafikia Balegh basi akifikia umri wa Baleghe hua na Wajib wa kufanya Tena

Ibada hio.

3-Kama Ibada ya Hija ikimuwajibikia yule mtu ambae ana matatizo ya ulemavu au

ya kudumu basi inaruhusika kufanyiwa Ibada hio kwa ajili yake.

Hivyo kama tulivyoona kua katika mwaka huu wa 9 ilipoamrishiwa Ibada ya Hija basi

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua na ugeni wa Najran na hivyo hakuweza

kuhudhuria na kuongoza Ibada hio na badala yake Ibada hio ikaongozwa na Abu Baqr

Radhi Allahu Anhu na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akamteua Ali Ibn

Abi Talib Radhi Allahu Anhu kutangazia ujumbe wa maamrisho ya kukataza mambo

ambayo yalikua siyo, ambayo yalikua yakifanywa na Makafiri katika wakati wa Ibada

zao za Hija, ambapo kuna wengine walikua wakizuguka Al Kaabah huku wakiwa Uchi,

wengine walikua wakizunguka huku wakiwa wamebeba Wanyama wao n.k


916

Ambapo ndani yake tangazo hilo mlikua pia na amrisho la kuvunjwa kwa makubaliano

baina ya Waislam na Makafiri kua huo ndio mwaka wao wa mwisho kwa Makafiri

kufanya Ibada ya Hija na haitakiwi kwa Muislam anaetaka kuingia kufanya Ibada ya Hija

kua azuiliwe au atishiwe kwa adhabu au kwa uhai wake katika kipindi cha Hija na

makubaliano mengineyo waliyokubaliana kama zinavyosema aya:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞بَرَاءَةٌ‏ مِّنَ‏ اهلل َِّ‏ وَرَسُولِهِ‏ إِلىَ‏ ال َّذِينَ‏ عَاهَدتم ُّ مِّنَ‏

الْمُشْرِكِينَ۞فَسِ‏ ي ‏ُحوا فيِ‏ الأَْرْضِ‏ أَرْبَعَةَ‏ أَشْ‏ هُ‏ رٍ‏ وَاعْلَمُ‏ وا أَن َّكُ‏ مْ‏ غَيْ‏ رُ‏ مُعْجِ‏ زِي اهلل َِّ‏

ۙ وَأَ‏ َّن

اهلل ََّ‏ مخُْزِي الْكَافِرِينَ۞وَأَذَانٌ‏ مِّنَ‏ اهلل َِّ‏ وَرَسُولِهِ‏ إِلىَ‏ الن َّاسِ‏ يَوْمَ‏ الحَْجِّ‏ الأَْ‏ ‏ْكبرَِ‏ أَن َّ اهلل ََّ‏

بَرِيءٌ‏ مِّنَ‏ الْمُشْرِكِينَ‏ ۙ وَرَسُولُ‏ هُ‏ ﴾

Baraatun mina Allahi warasoolihi ila alladheena AAahadtum mina almushrikeena;

Faseehoo fee al-ardhi arbaAAata ashhurin waiAAlamoo annakum ghayru

muAAjizee Allahi waanna Allaha mukhzee alkafireena; Waadhanun mina Allahi

warasoolihi ila alnnasi yawma alhajji al-akbari anna Allaha baree-on mina

almushrikeena warasooluhu fa-in tubtum fahuwa khayrun lakum wa-in

tawallaytum faiAAlamoo annakum ghayru muAAjizee Allahi wabashshiri

alladheena kafaroo biAAadhabin aleemin (Surat At Tawba 9:1-3)

Tafsir: Uhuru dhidi ya Majukumu yote unatangaziwa na Allah na Mtume wake

kutokana na mliyokubaliana na Washirikina, Hivyo tembeeni huku mkiwa huria (enyi

Washrikina) kwa miezi minne ardhini lakini mnatakiwa mjue kua kamwe hamtoweza

kukimbia (Adhabu za Allah) na Allah atawaadhirisha Makafiri; Na tangazo kutoka

Allah na Mtume wake kwa Watu katia siku kubwa kua Allah yuko huru kutokana na

Washirikina na pia (Yuko huru) Mtume wake. Hivyo kama nyinyi Washirikina

mkitubu basi ni bora kwenu lakini kama mkigeuka basi jueni kua hamuwezi

kuikimbia Adhabu ya Allah na wabashirie (Ewe Muhammad) wale ambao

waliokufuru juu ya Adhabu kali sana.

Ambapo aya imetaja miezi minne kua ni kipindi maalum cha mda waliopewa Makafiri

wale ambao waliingia kwenye makubaliano na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na hapo hapo kuwapa mda wale ambao walikua hawajaingia kwenye makubaliano hayo.

Na anasema Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshshari kua: ‘Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam alimtuma Ali Ibn Abi Talib kuvunja makubaliano yake

hayo kwa sababu ni kawaida ya Waarabu wanapokubaliana juu ya jambo basi


917

litakapohitajika kuvunjwa basi atakaevunja hua ni yule mhusika mkuu au mtu wa

kutoka Ndani Nyumbani mwake’

Ambapo amesema Abu Huraira Radhi Allahu Anhu kua: ‘Katika Hija hio wakati Abu

Bakr alipokua akiongoza Hija, basi alinituma mimi kwenye siku ya Nahar ya mwezi

10 Dhulhija kua niende katika eneo la Mina kisha nitangazie kua: ‘Kuanzia mwaka

huu hakuna Kafiri atakaefanya Hija na hakuna atakaefanya Tawwaf akiwa uchi’’

Ambapo Humaid Ibn Abd Rahman Radhi Allahu Anhu anasema kua: ‘Kisha Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akamtuma Ali Ib Abi Talib Radhi Allahu Anhu baada ya

Abu Bakr kuondoka na kumuamrisha kua asome Surat At Tawbah kwa sauti

Kubwa hadharani.’ Na Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu anaendela kusema kua:

‘Hivyo Ali akasoma pamoja nasi Surath At Tawbah wa sauti mbele ya watu katika

eneo la Mina katika sikua ya Kuchinja na kisha akatangazia kwa kusema kua:

‘Hakuna Kafiri atakaeruhusiwa kufanya Ibada ya Hija baada ya mwaka huu, na

hakuna atakaefanya Tawwaf akiwa Uchi’’(Imam Bukhari)

Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam alikua alipotimia umri wa miaka 63 basi alishuka

Malaika Jibril na kumwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua katika mwaka

huo watasoma Qur’n mara mbili, kwani ilikua ni kawaida ya Malaika Jibril kushuka

katika kila mwezi wa Ramadhan na kumsomesha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

Qur’an yote hadi ilipofikia katika Ramdhani hio, ambapo mnamo mwaka wa 10 wa Al

Hijra, na Rasul Allah Salallau Alayhi wa Salam akafahamu kua mda wake wa kuishi

Ulimweguni umemalizika, na kisha Malaika Jibril alishuka na Surat Nasr ambayo

inasema:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞إِذَا جَآءَ‏ نَصْرُ‏ ٱهلل َِّ‏ وَٱلْفَتْحُ۞وَرَأَيْ‏ تَ‏ ٱلن َّاسَ‏ يَدْخُلُونَ‏

فىِ‏ دِينِ‏ ٱهلل َِّ‏ أَفْ‏ وَاجاً۞فَسَبِّحْ‏ بحَِمْدِ‏ رَبِّكَ‏ وَٱسْتَغْفِرْهُ‏ إِن َّهُ‏ كَانَ‏ تَو َّاابَ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Idha jaa nasru Allahi waalfat-hu; Waraayta

alnnasa yadkhuloona fee deeni Allahi afwajan; Fasabbih bihamdi rabbika

waistaghfirhu innahu kana tawwaban (Surat An Nasr 110:1-3)

Tafsir: Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehma na Mwingi wa Huruma; Itakapokuja

Nusra ya Allah na Ushindi; Na utawaona watu wanaingia kwenye Dini ya Allah

Makundi kwa makundi; Basi litukuze na ulisifu jina la Mola wako na umuombe

msamaha kwani kwa hakika yeye ni mwenye kupokea maombi ya Msamaha.


918

Khalifah Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu A’nhu alikua akimchukua Abd Allah Ibn

‘Abbas Radhi Allahu A’nhu wakati huo alikua mdogo kiumri katika Ijma’a, na alikua

akimwita ‘Kijana mdogo aliepevuka’, Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu A’nhu alikua

akipenda kutumia Ijma’a katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbali mbali, kwani

alikua akipenda kuwepo ufahamu zaid wa matatizo na hivyo kua na uwezo mkubwa na

unaofaa zaid katika kutatua matatizo mbali mbali.

Hivyo katika mara ya kwanza baadhi Masahaba wazee wakiwemo waliopigana vita vya

Badr walikasirika kwani walikua wakimuona mdogo na asiejua kitu na hivyo

kumlalamikia Umar Ibn Al Khattab kwa kumwambia, ‘Umar inakuaje unamchukua

mtoto mdogo aje kutoa Fatwa nasi?’ Umar akawaambia mbele ya Abd Allah Ibn

‘Abbas Radhi Allahu A’nhu ‘Hebu niambieni kama ikiwa kweli mnajua, Jee Surat

An Nasr iliposhuka ilibashiria kitu gani?’ Masahaba wakajibu, ilikua inaashiria

ushindi mkubwa kwa Uislam. Umar akamgeukia Abd Allah Ibn ‘Abbas Radhi Allahu

A’nhu na kumuuliza ‘Jee unasemaje kuhusiana na majibu hayo?’, Abd Allah Ibn

‘Abbas Radhi Allahu A’nhu akajibu ‘Surat An Nasr ilikua inatabari kifo cha Nabii

Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam’. Hapo Masahaba wakashangaa na kukubali

uwezo wa I’lm aliokua nao Abd Allah Ibn ‘Abbas Radhi Allahu A’nhu pamoja na udogo

wa umri wake.

Ambapo anasema Mujjadid Ad Din Imam fakhr Ad Din Al Razi kua: ‘Kuna uhusiano

wa baina ya Sura 3 ambazo zimefuatana sambamba ambazo ni ni Surat Al Kafirun

(109) ambayo ni yenye kubainisha kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ni

mwenye Kumuamini na Kumuabudu Allah Subhanah wa Ta’ala pekee na

kuwakanusha Miungu wengine, ambapo kutokana nayo Sura hio basi hua kuna

suali ambalo linasema: Hivi jee kutakua na Malipo gani kutokana na Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua ni mwenye kumuamini Allah Subhanah wa Ta’ala?

Na Jibu lake linapatikana kwenye hii Surat Nasr (110) ambayo inajibu kua Malipo

yake ni Kupatikana kwa Nusura na Ushindi katika Ulimwengu huu wa Dunia na

wa Akhera, na kisha Sura inayofuatia baada ya hii yaani Surat Masad(111) ni yenye

kuthibitisha Malipo waliyotayarishiwa wale ambao ni wenye kupingana na Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam.’

Na kwa Upande mwengine basi tunaona kua Allah Subhanah wa Ta’ala anamwambia

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam awe ni mwenye kufanya Istighfar, na hivyo kuna

baadhi wanaweza wakajuliza, hivi inakuaje Allah Subhanah wa Ta’ala anamwambia

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam afanye Istighfar wakati tayari katika Surat Fat-h

ameshamwambia kua amemsamehe Madhambi yake yaliyotangulia na yajayo?

Ambapo Jibu la suali hili ni kua: ‘Istighfar za Mitume wote hua ni sehemu ya Ibada

kwao wao yaani ni sehemu ya kufanya mema ambayo hua hali tofauti na Istighfar


919

zetu sisi mimi na wewe ambazo hua ni zenye kumaanisha kuomba Msahama kwa

makosa yetu mbele ya Mola wetu, na vile vile Istighfar za Mitume hua pia ni kwa

ajili ya Watu waliomo katika Ummah wao yaani hua ni wenye kuwaombea watu

wawasamehe madhambi yao’

Mnamo mwaka wa 10 Al Hijra basi Rasul Allah Salallahu Alayh wa Salam akatangazia

rasmi nia yake ya kuenda katika Ibada ya Hija ya mwaka huo, tangazo ambalo lilisambaa

kwa kasi kubwa sana kuliko moto unavyosambaa kwenye msitu uliokauka kwa ukame,

na hivyo watu wengi sana nao wakajianda kwa ajili ya kuenda katika Ibada ya Hija ya

Mwaka huo kiasi ya kua idadi ya Mahujaji mwaka huo walikua ni zaidi ya watu 100,000

ambapo anasema Jabir Ib Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Watu walikua wengi kiasi

ya kua ilikua nnaona watu hadi kwenye upeo wa Macho yangu.’

Ambapo anasema Jabir Ibn Abd Allah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alikaa katika Mji wa Madina kwa mda wa miaka 9 ambayo ndani

yake hakua ni mwenye kuhudhuria kwenye Ibada ya Hija.

Hivyo ndani ya mwaka huu wa 10 watu wengi sana walikuja katika Mji Wa Madina

kwa ajili ya kua na matumaini ya kujifunza kufanya Ibada kama afanyavyo yeye.

Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alianza safari yake kuelekea Makkah

pale ilipokua zimebakia siku 5 kabla ya kumalizika Mwezi wa Dhul Qadah, nasi

tukafunga safari pamoja nae’(Imam Ahmad, Imam Muslim)

Na anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Watu wa

Ujahiliyah walikua wakifikiria kua kufanya Umra katika wakati wa mwezi wa Dhul

Hija ni moja katia ya Dhambi kubwa sana juu ya Ardhi, na pia walikua wakifikiria

kua Mwezi wa Safar ni mwezi Mtukufu na walikua wakisema kua: ‘Wakati Jeraha

la mgongoni mwa Ngamia linapopona (baada ya kurudi katika Ibada ya Hija) na

alama ya Jeraha hilo inapotoweka, na mwezi wa Safar unapopita basi Umra hua

inaruhusiwa kwa yule anaetaka’

Hivyo Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam na Masahaba zake aliwasili katika

Mji wa Makka katika siku ya mwezi 4 ya Dhul Hijjah, wakavaa Ihram kwa ajili ya

Hija, na kisha Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akawaamrisha Masahaba

zake watie nia zao kwa ajili ya Umra tu, na hivyo Masahaba wakashangaa na

wakamuuliza Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam kwa kusema: ‘Ya Rasul Allah!

Hivi jee ni aina gani ya Ihram ya kumalizia iliyoruhusiwa?’’ na Rasul Allah

Salallahu A’layhi wa Salam akasema: ‘Malizeni Ihram kikamilifu kwani

mmeruhusiwa kufanya kila kitu’(Imam Bukhari)


920

Baada ya kuondoka katika Mji wa Madina msafara wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam ukawasili kata meneo ya Dhul Hulayfah ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi Wa

Salam akawafundisha Waislam namna ya kufanya Ibada ya HIja, na kisha akavaa Ihram

na kuelekea katika Mji wa Makkah ambapo aliwasili nje ya mipaka yake katika maeneo

ya Dhi Tuwa baada ya wiki moja na wakapiga tena kambi katika meneo hayo hadi siku

ya pili yake ndio wakaingia katika Mji wa Makkah na kuelekea moja kwa moja kwenye

Masjid Al Haram kupita katika upande wa Mlango wa Bab Al Salam.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na msafara wake wa Mahujaj hao ukafanya

Tawwaf na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akalibusu Hajar Al Aswad na

kisha akasali na kuomba dua na kunywa Maji ya Zamzam. Na kisha akaelekea kwenye

milima ya Safa na Marwah akafanya Sa’i ba kisha akaelekea kwenye maeneo ya Al

Hujjun. Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawaamrisha Masahaba zake

ambao walikua wamewasili bila ya kua na wanyama wa kuchinja kua wavae Ihram kwa

ajili ya Umra kisha wafanya Tawwaf na Saai na hii ni kwa sababu Waislam walikua na

malengo ya kufanya Hijjat Qiran ambayo ni yenye kujumiisha Umra na Haji kwa pamoja.

Hivvyo mnamo mwezi 8 Dhulhijja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akawasili

kwenye maeneo ya Minna na kusali Sala ya Adhuhuri na kushinda na kulala katika eneo

hilo hadi katika siku ya pili yake baada ya Sala ya Alfajir ya mwezi 9 akaondoka na

kuelekea kwenye maeneo ya Arafah akapiga kambi kwenye eneo la Namirah lilopo

upande wa Mashariki wa Mlima wa Arafah ambapo alipumzika kidogo na kisha

akaeleekea katika maeneo ya Uranah na kutoa Khutba yake ya Mwisho.

Na kisha akaelekea katika maeneo ya Muzdalifah katika wakati wa Magharibi ambapo

alisali Sala ya Magharibi na Isha na kupumzika hadi Alfajiri ya siku ya pili yake akarudi

tea katika maeneo ya Minna na kuelekea kwenye maeneo ya Jammarah na kufanya Ibada

ya kurusha mawe na kisha akachinja na kisha akarudi katika Mji wa Makkah na kufanya

tena Ibada ya Tawwaf na kusali sala ya Adhuhuri ndani ya Masjid Al Haram, kisha

akanywa maji ya Zamzam na kurudi katika meneo ya Minna ambapo alikaa kwa siku 3

za Ayyami Tashriq kuanzia mwezi 10,12 na mwezi 13 Dhul Hijjah na kisha akaanza

safari ya kurudi katika Mji wa Madina.

KHUTBA YA KUAGA YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI

WA SALAM.

Mnamo siku ya Ijumaa ya mwezi 9 Dhul Hijjah ya mwaka huo wa 10 Al Hijr alipokua

katika Ibada ya Hija katika maeneo ya Arafah basi Rasul Allah Salallahu A’layhi wa


921

Salam baada ya Kumshukuru Allah Subhanah wa Ta’ala na kumtukuza alitoa Khutba

ifuatayo:

‘Enyi watu, nakuombeni mnisikilize kwa umakini, kwani kwa hakika mimi ni

mwenye kujua kua baada ya mwaka huu basi sitoweza kua tena miongoni mwenu.

Hivyo nisikilizeni vizuri kuhusiana na kile nitakachokisema ili mpate kufikisha

haya nitakayoyasema kwa wale wasiokuwepo leo hii hapa tulipo.

Enyi watu ama kuhusiana na Mwezi huu, na siku hii na Mji huu na Utukufu wake,

na kuhusiana na Uhai na Mali za kila Muislam kua ni Amanah Tukufu. Hivyo

rudisheni Amanah za watu mlizopewa kwa waliokukabidhini Amana hizo. Ili

Msidhuru na wala Msipate kudhuriwa. Kumbukeni kua Mtakutana na Mola wenu

ambae nae atayahesabu Matendo yenu.

Allah Subhanah wa Ta’ala amekuharamishieni kula Riba, hivyo Kila chenye Riba

inabidi iondolewe Riba yake, Mitaji yenu ni mitaji yenu hivyo ihifadhini na

hamtodhurika wala hamtodhuru kutokana nayo Allah Subhanah wa Ta’ala ametoa

Hukmu kua: ‘Riba zate anazodaiwa Abbas Ibn Abd Al Mutallib zifutwe.’

Hivyo kila haki ambayo ilitokana na mauaji ya Ujahiliya basi imefutwa na haki ya

mwanzo ambayo nnaifuta ni ya mauaji ya Rabiah Ibn Al Harithah’

Enyi watu, hakika ya wale wasioamini hua ni wenye kuiingilia kuhusiana na

Kalenda ili kuhalalisha kile ambacho Allah Subhnaha wa Ta’ala amekiharamisha,

na kuharamisha kile ambacho amekihalalisha, ambapo Mbele ya Allah Subhanah

wa Ta’ala kuna miezi 12 na ndani yake mna miezi minne ambayo ni Mitukufu na

miongoni mwao ni yenye kuendana sambamba na mmoja kati yao ni wenye kuwepo

baina ya Jumada na Shaaban.

Hivyo kuweni na umakini dhidi ya Shaytan wa ajili ya usalama wa Dini yenu, kwani

amepoteza matumaini kutokana na kutoweza kukupotosheni katika mambo

makubwa hivyo kuweni na umakini nae katika mambo madogo madogo.

Enyi watu ni kweli kua mna haki juu ya Wanawake zenu, lakini na wao pia wana

haki juu yenu. Kumbukeni kua mmewachukua wao kua ni wake zenu kutokana na

Kuaminiwa na Allah Subhanah wa Ta’ala na kutokana na Ruhusa yake. Hivyo

kama wakikutiini basi juu yao watakua wanastahiki kulishwa na kuvishwa

kutokana nanyi kwa upole na ukarimu. Hivyo kaeni nao vizuri Wanawake wenu

kuweni na huruma nao kwani wao ni wenza wenu na ni wasaidizi wenu. Na ni haki

yenu kua wasiwe na urafiki na yeyote yule ambae hamkubaliani nae na pia wasiwe

ni wenye kufanya machafu.


922

Enyi Watu, nisikilizeni kwa umakini sana, muabudini Allah Subhanah wa Ta’ala,

salini Sala zenu 5, Fungeni Ramadhani, Toweni Zakkah na Fanyeni Ibada ya Hija

kama mtakua na uwezo.

Fahamuni kua Watu wote ni wenyekutokana na Adam na Hawa, hivyo Muarabu

hana utukufu mbele ya asiekua Muarabu na wala asiekua Muarabu hana utukufu

mbele ya Muarabu, pia Mweupe hana utukufu mbele ya Mweusi na wala Mweusi

hana utukufu mbele ya Mweupe isipokua kwa Ucha Mungu wake na wema wake.

Jifunzeni kuaKila Muislam ni ndugu wa Kila aliekua Muislam na Uislam ni Udugu,

hivyo hakitokua halalia kitu chochote cha Muislam kwa Muislam mwengine

isipokua pale kitu hicho kitakapotolewa na kugaiwa kwa uhuru na hiari.

Hivyo msifanye dhulma na wala msijidhulumu. Kumbukeni kua kuna siku ambayo

mtakutana na Mola wenu na mtaulizwa juu ya amali zenu. Hivyo tahadharini msije

mkapotoka kutoka katika njia iliyonyooka baada ya kuondoka kwangu.

Enyi watu hakika hakuna Nabii wala Mtume atakaekuja baada yangu, na hakuna

Imani mpya itakayotokea baada yangu, hivyo tafakarini ninachokuambieni Enyi

watu ili mpate kufaham ninayokuambieni, kwani nnawacha vitu viwili baada yangu

ambavyo ni Quran na Sunah hivyo mkivifuata hivi basi hamtopotoka. Na kila

aliesikia kutoka kwangu basi ni wajibu wake kufikisha maneno yangu kwa wengine

na wengine kwa wengine na naomba kua wa mwisho wawe ni wenye kunifaham

zaidi kuliko wanaonisikiliza leo hapa mbele yangu.

Hivyo Msije mkaasi baada yangu kama walivyofanya Makafiri, na mkaanza

kukatana vichwa wenyewe kwa wenyewe.

Ya Allah kua shahidi wangu kua nimefikisha ujumbe wako kwa waja wako.

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasoma aya aliyoshushiwa katika wakati

huo huo ambayo ni ile isemayo:

‏﴿ٱلْيَوْمَ‏ يَئِسَ‏ ٱل َّذِينَ‏ كَفَرُواْ‏ مِن دِينِكُمْ‏ فَلاَ‏ تخَْشَوْهُمْ‏ وَٱخْشَوْنِ‏ ٱلْيَوْ‏ مَ‏ أَكْ‏ مَ‏ لْتُ‏ لَكُ‏ مْ‏

دِينَكُمْ‏ وَأَتمَْمْتُ‏ عَلَيْكُمْ‏ نِعْمَتىِ‏ وَرَضِيتُ‏ لَكُمُ‏ ٱلأِسْلاَمَ‏ دِيناً‏ ﴾


923

Alyawma ya-isa alladheena kafaroo min deenikum fala takhshawhum waikhshawni

Alyawma akmaltu lakum deenakum waatmamtu AAalaykum niAAmatee

waradheetu lakumu al-islama deenan (Surat Al Maidah 5:3)

Tafsir: Leo hii Makafiri wamevunjika Moyo dhidi ya Dini yenu, hivyo msiwe na khofu

nao bali kuweni na khofu nami (Allah Subhanah wa Ta’ala). Siku hii nimeikamilisha

Dini kwa ajili yenu na nimekukamilishieni Neema yangu juu yenu na nimeridhia juu

yenu kua Uislam ni Dini yenu.

Ambapo khutba hii ilikua ikirudiwa na neno kwa neno na Rabiah Radhi Aallahu Anhu

ambae alikua ni mwenye sauti kali sana baada ya kuombwa na Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua afanye hivyo ili wasikie watu wengi zaidi, kisha Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akauliza: ‘Enyi watu, hivi jee nimefikisha Ujumbe kwenu

nyie ama la?’ na hapo watu wakaitikia kwa sauti kubwa sana kama radi isemayo:

‘Allahuma Naam’ hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akanyoosha juu kidole

chake cha shahada ma kusema: ‘Ya Allah, hakika wewe ni shahidi kua nimefikisha

ujumbe wako kwa waja wako.’

Miezi miwili baada ya kumalizika Ibada yake ya Hija basi Rasul Allah Salallahu A’layhi

wa Salam alifariki Dunia tukio ambalo liliwachaganya na kuwahuzunisha Viumbe wengi

sana Ulimwenguni.

KIFO CHA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM.

Neno Baka kwa Kilugha hua linamaanisha Kulia Machozi, Kutokwa na Machozi,

Kulalamika huku Machozi yakiwa yanatoka.

Katika wakati tunaoishi leo hii basi tuko katika kipindi ambacho kimejaa matukio ya

Kusikitisha na hivyo kua ni yenye kupelekea kuwatoa watu Machozi kutokana na

Uchungu wa Ubaya wake kwa wanaofanyiwa Ubaya na pia kutokwa na machozi kwa

wale wanaoyaona Matukio hayo wakiwa mbali kwa Macho yao, na kuingiwa Uchungu

na huruma ndani ya Nyoyo zao kutokana na Madhara yanayowafika Waislam wengi sana

Ulimwenguni kutokana na kuachana na Wasia wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

katika khutba yake ya mwisho hususan tukiangalia maneno yasemayo: ‘Hivyo Msije

mkaasi baada yangu kama walivyofanya Makafiri, na mkaanza kukatana vichwa

wenyewe kwa wenyewe.’

Na tunapozungumzia kuhusiana na Baka yaani Kulia Machozi basi si mimi na wewe tu

tuliojaaliwa uwezo wa kulia bali hata Mbingu na Ardhi pia nazo katika wakati huu


924

zinalia, kama anavyosema Allah Subhanah wa Ta'ala Katika Qur'an alipowazungumzia

watu wa Fir'awn kua;

‏﴿فَمَا بَكَتْ‏ عَلَيْهِمُ‏ ٱلس َّمَآءُ‏ وَٱلأَرْضُ‏ وَمَا كَانُواْ‏ مُنظَرِينَ‏ ﴾

Fama Bakat aA’layhim Alssamau wa Al Ardhu wama kanuu mundhirina (Surat Ad

Dukhan 44:29)

Tafsir: Na Hawakuliliwa (Na) Mbingu na Ardhi na Wala hawakucheleweshewa Mda

Kwani amaesema Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wakati Muumini

anapofariki basi ile sehemu ambayo alikua akiisujudia katika wakati wa kusali

kwake hua inalia kwa ajili yake, na pia ile sehemu ya Mbingu ambayo Amali njema

zake hua zinapitia kwenda juu hua pia inalia kwa ajili yake. ’

Hivyo kwa Mtu yeyote yule asiemuamini Allah Subhanah wa Ta'ala na Asiesali basi

anapofariki hali yake hua kama ya Kina Fir'awn kwani hua Haliliwi na Mbingu wala na

Ardhi kwa ajili yake.

Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Hakuna Muumini

isipokua hua kuna Milango Miwili Mbinguni kwa ajili yake kuna Mlango ambao

Riziki yake hua inashuka kupitia kwake na kuna Mlango Ambao Mema yake na

Maneno yake hua Yanapanda kupitia kwake Na anapokufa basi Humtamani na

hivyo Hulia kwa ajili yake ‘(Imam At Tirmidhii)

Na akasema Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Ardhi hua ni

yenye Kumlilia Muumini wa Allah Subhanah wa Ta'ala kwa siku 40 baada ya

kufariki kwake’(Mustadrak Al Hakim)

Na akasema tena Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Ukimona Muislam

anakaribia kufariki basi muelezee kuhusiana na Mambo Mema ili akutane na Mola

wake huku kiwa anamfikiria kwa Mema Juu yake, na ukimuona Mtu Mzima ana

Afya basi Mtie khofu juu ya Mola wake’

Naam..Waislam wa leo tuna Unafiq na Imani Dhaifu kwa sababu Hatuna Khofu juu ya

Mola wetu!

Kwani nasi pia Alhamd lillah inaonekana kua tuna Afya na wenye nguvu kimwili, na

hivyo kulingana na hadith basi sisi ni bora kuliko Waumini waliokua Dhaifu kiafya.


925

Na ingawa ni wenye Uimara wa Nguvu za Mwili na Afya lakini tuna Udhaifu wa Imani,

hivyo na tujinufaishe na wasia wa Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu

kuhusiana na Kumuogopa Allah Subhanah wa Ta'ala kwa kukumbushana kuhusiana na

Kifo Ambapo anasema Imam Abd Allah Ibn Muhammad Ibn Ad Duniyah kua:

Wakati Amir ul Muuminin Umar Ibn Abd Al Aziz anataka kukata roho, basi

aliwaambia wale waliokaribu yake wasogee Karibu

Kisha waliposogea basi akawa anasema; ‘Kwa hakika nyinyi mliniamrisha mimi

lakini nami sikutekeleza maamrisho yenu Mlinikataza nami nikawa Muasi’

akayasema kwa kuyarudia maneno hayo mara 3.

Kisha akasema: ‘Lakini La Ilaha illa Allah!’

Watu waliokuwepo hapo wakatizamana, kisha wakasema: ‘Ewe Amir ul Muuminin

Unaonekana kama Umezidiwa’

Amir ul Muuminin Umar Ibn Abd Al Azizi akasema: ‘Hakika Mimi nnaona hali ya

sehemu ambayo haina Ibn Adam wala Majini’ Na kisha akakata roho.’

Hivyo tunapozungumzia Mauti basi hua tunazungumzia kitu ambacho hakuna anaejua

siri yake isipokua Mwenyewe Rabbi Al Alamiin ambae ndie Muumba wa Kila kitu na

ambae ni Allah Subhanah wa Ta'ala.

Na ndio Maana Allah Subhanah wa Ta'ala akahoji kuhusiana na wale wasiomuamini kwa

kusema katika Qur'an:

‏﴿تَنزِيلٌ‏ مِّن ر َّبِّ‏ ٱلْعَالَمِينَ۞أَفَبِهَٰذَ‏ ا ٱلحَْدِيثِ‏ أَنتُمْ‏ م ُّدْ‏ هِ‏ نُونَ‏ ‏۞وَتجَْعَلُونَ‏ رِزْقَكُ‏ مْ‏ أَن َّكُمْ‏

تُكَذِّبُونَ۞فَلَوْلاَ‏ إِذَا بَلَغَتِ‏ ٱلحُْلْقُومَ۞وَأَنتُمْ‏ حِ‏ ينَئِذٍ‏ تَنظُرُونَ۞َونحَْنُ‏ أَقْرَبُ‏ إِلَيْهِ‏ مِنكُ‏ ‏ْم

وَلَٰكِن لا َّ تُبْصِرُونَ‏ ﴾

Tanzeelun min rabbi alAAalameena; Afabihadha alhadeethi antum mudhinoona;

WatajAAaloona rizqakum annakum tukadhdhiboona, Falawla idha balaghati

alhulqooma; Waantum heena-idhin tandhuroona; Wanahnu aqrabu ilayhi minkum

walakin la tubsiroona; (Surat Al Waqiah 56:80-85)


926

Tafsir: (Hii Qur'an) Ni Teremsho kutoka kwa Mola wa Ulimwengu wote na Kila

kilichomo ndani yake. Hivi Jee (Mnaiona Qur'an) kua hizi ni Hadith tu ambazo Nyinyi

Mnazikadhibisha? Na kwa Kukujaalieni Nyinyi Riziki zenu, Basi ndio

Mnamkadhibisha? Kwanini Basi Humiuingilii kati Wakati (Roho ya Mtu wenu

anapotaka kufa) Inapofika Kooni? Wakati Nyinyi Mkiwa hapo hapo huku

Mnangalia? Na Nasi tuko Karibu Nae kuliko Mlivyokua nae nyinyi, Lakini Nyinyi

Hamui wenye kuona.

Kwani aya inatuonesha kua kwa Muumini kukifikiria Kifo basi hua Kunamtosheleza kua

ni Sababu ya Kua na Taqwa. Kwani Haram Ibn Hayan alisema : ‘Inakuaje hali ya Mtu

anautumia Mda wake wa Mchana huku akiwa hana uhakika kama atafika Usiku

wake siku hio ama la, na kama ataenda Peponi au Motoni. Hivyo Unapoenda Kulala

Usiku basi Tegemea kukutana na Kifo, na Unapoamka Basi Sali na Umuombe Allah

akurekebishie na auweke sawa Moyo na Nia yako katika Amali zako.’

Neno Faniya kwa lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kuteketea, Kukoma kuwepo,

Kuharibika na hakifai tena, Kufariki, Kuaga Dunia, Kuyayuka, Kuoza. Na pia hua

linamanisha Kitu ambacho hua Hakiwezi kudumu Milele yaani Kitu ambacho hata kikae

vipi lakini mwisho wake kitaharibika na kutoweka.

Ambapo Neno Faniya ndio lililotoa Neno Fanin ambalo Humaanisha hali ya Umoja wa

Kitu ya Kutoweka kwake.

Kwani amesema Allah Subhanah wa Ta'ala kua:

‏﴿كُل ُّ مَنْ‏ عَلَيْهَا فَانٍ۞وَيَبْقَى ٰ وَجْهُ‏ رَبِّكَ‏ ذُو ٱلجَْلاَلِ‏ وَٱلإِكْرَامِ‏ ﴾

Kullu man AAalayha fanin; Wayabqa wajhu rabbika thoo aljalali waalikrami

(Surat Ar Rahman 55:26-27)

Tafsir: Kila Kitu Kilichopo Juu yake (Ulimwenguni) kitatoweka Na Utabakia Milele

Uso wa Mola wako Mkamilifu wa Ufalme na Utukufu.

Ambapo maana ya Neno Wajhu Ambalo nimelitafsiri kama Uso wake basi limetokana

na neno Wajaha ambalo hua linamaanisha Kueleka, Kupiga kibao cha uso, Kutunga,

Kuelekeza, Kutuma, Kuelekea.

Neno Wajaha ndio lililotoa neno Wajhun ambalo hua linamaanisha Uso, Muelekeo,

Qibla, Moyo, Nafsi, Roho, Muonekano, Mwili na pia humaanisha Lengo au Dhumuni


927

Hivyo Aya imesema kua: Kila kilichopo Juu yake Ulimwenguni hakitodumu

Kitatoweka au kitaangamia, au kitakufa na kitakachobakia Milele ni Wajhu

Rabbika yaani Uso au Muonekano wake Muumba.

Na hapa pamezungumziwa Muonekano kwa sababu ya kutubainishia sisi Ibn Adam ili

tufaham zaidi kwani hua tunajuana kutokana na Muonekano wetu, na hivyo basi Aya

unamaanisha kua ni Ufalme Kamilifu wa Allah Subhanah wa Ta'ala ndio utakaobakia

Milele

Kwani tunaona kua aya yetu zimemalizia na Neno Ikrami ambalo ni lenye kutokana na

neno Karama au Karuma ambalo hua linamaanisha Kua na Ukarimu, Kua Na Huruma

Katika kutoa, Kutokua na Ubakhili, Kua ni Mfano wa Kuigwa Katika Kutoa Msaada na

kusaidia kwa kutoa vitu vyenye Manufaa kwa wingi bila ya Kujali kupungukiwa katika

utoaji huo.

Ambapo bila ya shaka mara Nyingi hua Tunaambiana Ramadhani Karim au Ijumaa

Karim na kwa baadhi yetu bila ya Kujua maana yake. Hivyo Maana ya Ramadhani au

Ijumaa Karim hua inamaanisha Ramadhani au Ijumaa yenye Huruma na Ukarimu wa

Rehma za Allah kimanufaa.

Na pia kutokana na kua Al Karim ni Kati ya Majina Matukufu ya Allah Subhanah wa

Ta'ala basi hua pia unaposema Ramadhan Karim au Ijumaa Karim hua unamaanisha

Ramadhani au Ijumaa iliyotokana na Mwenye sifa ya Utukufu wa Mwing wa Ukarimu

yaani Allah Subhanah wa Ta'ala.

Na ndio Maana mtu unapoambiwa Ramadhan Karim au Ijumaa Karim basi unakua

unajibu Allahu Akram yaani unarhibitisha kua hii Ijumaa au hii Ramadhani imepatikana

kutokana na Allah Subhnaha wa Ta'ala ambae ni Mbora zaid wa Ukarimu kwa

kutuneemesha kila Neema tunayoihitaji katika Maisha yetu hpa Duniani kutokana na

Ukarimu wake.

Na hivyo Ukisema Ijumaa Karim basi tayari umeshainesha Shukran kwa Mola wako kwa

kukujaalia Ukarimu wa Siku ya Ijumaa au Ramadhani. Na ukijibu Allahu Akram basi

tayari hua ushafanya Dhikr Allah!

Subhanah Allah! Hio ndio sifa ya Ukarimu wa Dini ya Uislam ambayo ni Dini ya Mwingi

wa Ukarimu alietukirimu kila kitu kwa Ukarimu wake

Lakini sasa hayo mpaka uyajue, ambapo ukweli ni kua hali iko kama alivyosema Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua kila kitu chema hua ni Sadaqa


928

Na tunapoiangalia aya yetu basi tunaona kua imemalizia na neno Ikrami, Ambapo nalo

tumesema kua limetokana na neno Karama na hivyo basi hapa maneno Dhu Al Jalali wa

Al Ikrami hili hua yanamaanisha kua: Kutokana na Ukamilifu wake wa Ufalme Mtukufu

na Ukarimu wake basi Allah Subhanah wa Ta'ala hastahiki kushirikishwa na kitu

chochote kile kwani yeye ndie pekee mwenye Uwezo wa Kukirimu Viumbe wake wote

kwa Milele kwa Makadirio yake na kwa kadri atakavyo bila ya Kuathirika kwa

kupungukiwa na chochote katika Kukirimu kwake

Kwani Maneno haya yanatuwekea Wazi kua Kila Kitu na kila Kiumbe Ulimwenguni si

kua tu ni chenye kumilikiwa na Allah Subhanah wa Ta'ala, lakini pia yanaamaanisha kua

Kila kitu kilichopo Ulimwenguni Kinamhitaji yeye Allah Subhanah wa Ta'ala na pia kua

ni chenye kuhitaji Ukarimu wake, kwani vyengine basi hakuna kitakachoweza kuwepo.

Yaani kutokana na kua kila kitu kinamilikiwa na kinamhitaji yeye Mmiliki ambae ndie

Muumba wa Kila kitu yaani Allah Subhanah wa Ta'ala.

Basi Bila ya Shaka Kila kitu Alichokiumba na Kukitoa kikaja Ulimwenguni, basi

Kitarudi kwake yeye mwenyewe Muumba kulingana na Ukarimu wa Makadirio yake juu

ya kitu hicho kiishi kwa mda gani hapa Ulimwenguni.

Na bila ya Shaka kwa kua vitu hivyo kavikirimu na kuvionjesha Uhai hapa Ulimwenguni

basi pia atavikirimu kwa kuvirudisha kwake kwa kuvionjesha na Kifo. Kwani Allah

Subhanah wa Ta'ala anaelezea haya katika Qur'an pale aliposema:

‏﴿قُتِلَ‏ ٱلإِنسَانُ‏ مَآ أَكْفَرَهُ۞مِ‏ نْ‏ أَىِّ‏ شَ‏ يءٍ‏ خَ‏ لَقَهُ۞مِن ن ُّطْفَةٍ‏ خَلَقَهُ‏ فَقَ‏ د َّ رَهُ‏ ‏۞ثمُ َّ

ٱلس َّبِيلَ‏ يَس َّرَهُ۞ثمُ َّ أَمَاتَهُ‏ فَأَقْبَرَهُ۞ثمُ َّ إِذَا شَآءَ‏ أَنشَرَهُ۞كَلا َّ لَم َّا يَقْضِ‏ مَآ أَمَرَهُ‏ ﴾

Qutila al-insanu ma akfarahu; Min ayyi shay-in khalaqahu; Min nutfatin

khalaqahu faqaddarahu; Thumma alssabeela yassarahu; Thumma amatahu

faaqbarahu ; Thumma idha shaa ansharahu; Kalla lamma yaqdi ma amarahu

(Surat Abasa 80:17-23)

Tafsir: Ameangamia Mtu, (Jee ni)Nini Kilichomfanya Akufuru? Hiji Jee(Anajua)

Amemuumba Kutoka na Nini? Ni Kutokana na Tone Amemuumba na Akamkadiria

katika Umbo alilokua nalo, Na Kisha akamuonesha Njia (Sahih ya kumelekea Mola

wake) rahisu kwa ajili yake Na Kisha Akamsababishia Kifo na Kumtia ndani ya Kaburi

Na Kisha pale atakapotaka (Allah Subhanah wa Ta'ala) Atamfufua (Kiumbe wake)


929

Kwani Amir Ul Muuminin Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kumwambia Mtoto wake

Hasan Ibn Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhu kuhusiana na Uhai wake hapa Duniani

na kuhusiana na Kifo chake kua: ‘Ewe Hasan, Ewe Mtoto Wangu, Kifuatilie Kifo

Vizuri sana mpaka ukijue, ili uwe ni mwenye kukikumbuka bila ya kukisahau. Ili

kinapokujia basi kisikushangaze wala kisikughafilishe’

Kwani anasema Imam Wahb Ibn Munabih kua: ‘Kila siku asubuhi Malaika

wanatangazia kutoka Mbingu ya Nne kuwambia watu kwa kusema: Enyi Mlio

kwenye umri wa miaka 40, hakika mmepea na kuvunwa kwenu kunakaribia

Enyi Mlio kwenye Umri wa miaka 50, mmeshatangulia, Jee ni nini kilichokuzuieni

Enyi Mlio kwenye Umri wa miaka 60 Hamna kisingizio, kwani kila kiumbe

alieubwa anajua kwanini akaumbwa, hivyo mda wenu umeshawadia Jitayarisheni’

Kwani Allah Subhanah wa Ta'ala amesema katika Qur'an kua atawahoji watu kwa

kusema:

‏﴿وَهُ‏ مْ‏ يَصْطَرِخُونَ‏ فِيهَا رَب َّنَآ أَخْرِجْنَا نَعْمَلْ‏ صَالحِ‏ اً‏ غَيْرَ‏ ٱل َّذِى كُن َّا نَعْمَلُ‏ أَوَلمَْ‏

نُعَمِّرْكُمْ‏ م َّا يَتَذَك َّرُ‏ فِيهِ‏ مَن تَذَك َّرَ‏ وَجَآءَكُمُ‏ ٱلن َّذِيرُ‏ فَذُوقُواْ‏ فَمَا لِلظ َّالِمِينَ‏ مِن

ن َّصِيرٍ‏ ﴾

Wahum yastarikhoona feeha rabbana akhrijna naAAmal salihan ghayra alladhee

kunna naAAmalu awa lam nuAAammirkum ma yatadhakkaru feehi man ta

dhakkara wajaakumu alnnadheeru fadhooqoo fama lildhdhalimeena min

naseerin(Surat Fatir 35:37)

Tafsir: Huku wakiwa ni wenye kulia ndani yake kwa kusema: ‘Ewe Mola wetu tutoe

ndani yake, tutfanya Mema na hatutofanya tuliyokua tukiyafanya ’(Allah Subhanah

wa Ta’ala atawajbu)kwa kuwaambia: ‘Hivi Jee Hatukukupeni Nyinyi Umri Mrefu

Ili atakaeweza Kukumbuka Ndani yake Aweze kukuumbuka anachotakiwa

kukumbuka Wakati alikujieni Muonyaji. Hivyo onjeni kwani kwa Madhaimu basi

hakuna wa kuwasaidia.

Kwani kuhusiana na Umri mrefu uliotajwa hapa kwenye aya basi Wanazuoni

wametofautiana juu yake kwani Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu na

Hasan Al Basr basi wao wanasema kua Umri unaozungumziwa hapa ni wa kuanzia miaka


930

40. Ambapo kwa wengine kama kina Imam Qatadah Al Sadusi basi yeye anasema kua ni

miaka 18 tu.

Na bila ya shaka Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi yeye amesema katika

Hadith kua: ‘Allah hataki kisingizio kwa mtu ambae amempa mda mpaka kufikia

umri wa miaka 60’

Hivyo Ibn Adam kupewa Umri mrefu na Mola wako bila ya kua ni mwenye kufanya

mema basi kutampelekea mru huyo kua ni mwenye Kujuta kesho Akhera. Kwani

asiejisalimisha hadi kufikia Umri huo basi bila ya shaka atakua hana kisingizio kwani

atakua ni Muasi wa kukusudia mbali ya kua alipata Ukumbusho.

Kwani amesema Mujtahid Imam Imam Malik Ibn Anas ambae ndie Muanzilishi wa

Madhhab ya Maliki kua: ‘Hakika mimi nimeona Watu katika Mji wangu ambao

walikua wakitafuta Mali na Ilm na kujichanganya na watu kabla ya kufikia Umri

wa miaka 40. Na walipofikia Umri wa miaka 40 basi waliachana na Dunia na

wakajiandaa kujitafutia yale yatakayo wanufaisha na Akhera yao hadi kufa kwao’

Ambapo kuhusiana na maneno Wajaakum Al Nadhiru - Na Wakati alikujieni Muonyaji

Basi kuna wasemao kua ni Mitume

Ambapo kwa upande wa Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, Imam

Sufyan Ath Thawri, Imam Husayn Ibn Al Fadhl nk basi wao wamesema kua: ‘Muonyaji

aliekusudiwa hapa hua ni Mvi unapokua Mtu mzima, na pia hua Ni Maradhi pale

baada ya kua na Afya na Kifo cha Mwenzio pale wewe unapokua wewe upo hai.’

Naam..hivyo kila mtu ahesabu umri wake na Muonyaji wake kisha ayaangalie Malengo

yake! Kwani anasema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: Siku moja nilikua

natembea na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam katika Mashamba ya Mitende

Kisha tukasimama na Kupumzika, ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alisimama karibu na Jani la Mtende.

Mara wakapita Mayahudi ambao wakaambiana wenyewe kwa wenyewe kwa kusema

kua: Muulize kuhusiana na Roho kisha mwenzake akasema: 'Una Shaka kuhusiana na

kumuuliza kuhusiana nayo?

Mwengine akasema: Usimpe Ruhusa kukujibu juu ya kile kitu ambacho

hutokipenda kupata Jawabu lake


931

Hivyo Mayahudi hao wakamuuliza Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuhusiana na

Roho, lakini nae akakaa kimya hakuwajibu, na hapo ikanijia wazi kuhisi kua Anataka

kushushiwa Wahy, hivyo nami nikasimama karibu yake wakati inashushwa aya isemayo

‏﴿وَيَسْأَلُونَكَ‏ عَنِ‏ ٱلر ُّوحِ‏ قُلِ‏ ٱلر ُّوحُ‏ مِنْ‏ أَمْرِ‏ رَبىِّ‏ وَمَآ أُوتِيتُم مِّنَ‏ ٱلْعِلْمِ‏ إِلا َّ قَلِيلاً‏ ﴾

Wayas-aloonaka AAani alrroohi quli alrroohu min amri rabbee wama ooteetum

mina alAAilmi illa qaleelan (Surat Al Isra 17:85)

Tafsir: Na Wanakuuliza (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) Kuhusiana

na Roho,Waambie Kua Roho Ni kitu ambacho Ilm Yake iko Chini ya Mola Wangu,

Na Mmepewa Ilm juu yake Ila Kidoogo tu.

Kwani anasema pia Bahr Ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kuhusiana na

aya hii kua: Aya hii ilishuka kwa sababu Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

aliulizwa na Mayahudi kuhusiana na Roho, Maumbile yake, Iko vipi na itakuaje

iadhibiwe wakati Inakaa Ndani ya Mwili wa Kiumbe

Ambapo tunapoifuatilia aya hii basi Kulingana na Hadith ya Kwanza ya Abd Allah Ibn

Masud Radhi Allahu Anhu basi tunaona kua Hii aya ilishushwa katika Mji wa Madinah

ambako ndio kwenye Mashamba Makubwa ya Mitende na pia ndio kwenye Makazi ya

Mayahudi kwa kipindi cha Wakati huo.

Lakini pia kwa Upande mwengine basi tunapoifutailia kwa kina basi tunaona pia kuna

Mtizamo usemao kua: ‘Aya hii Ilishuka pale Mayahudi walipowapa Mbinu

Maquraysh wa Makkah ili wamkwamishe Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kwa Hoja na Masuali, hivyo wakawaambia Maquraysh kua Wamuulize kuhusiana

na Roho na Wakamuuliza’

Na pia inawezekana kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aliulizwa Suali hili

alipokua katika Mji wa Makkah na pia akaulizwa tena alipokua katika Mji wa Madinah

.

Na hii pia ni kwa Sababu Miongoni mwa Masahaba na Wanazuoni hua Wanalitafsiri

Neno Ruhi liliomo kwenye Aya hii kua Linahusiana na Jina la Malaika Jibril, ambalo ni

Ruhi Al Qudus.

Kama tulivyoona pale tulipokizungumzia kisa cha Nabii Isa Ibn Maryam pale Maryam

bint Imran aliposhukiwa na Malaika Jibril kuambiwa kua atapata Mtoto, lakini

tunaporudi kwa Masahaba tulioanza nao kwenye hadithi yaani Masahaba Abd Allah


932

Wawili ambao ni Masahaba Wanazuoni Wawili yaani Abd Allah Ibn Masud Radhi

Allahu Anhu na Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu, ambapo ingawa Abd Allah Ibn

Masud Radhi Allahu Anhu alikua mkubwa kiumri kuliko Abd Allah Ibn Abbas Radhi

Allahu Anhu.

Lakini Mtizamo wao na Ilm yao basi zinatuwekea wazi kua Hili jibu la Suali hili halikua

likihusiana na Malaika Jibril bali lilikua kama walivyosema wao kua linahusiana na Roho

ya Viumbe wakiwemo Ibn Adam.

Ambapo Suali na Jawabu lake bado linabakia pale pale, kua iwe ni Malaika Jibril au iwe

ni kuhusiana na Roho zetu basi Bila ya shaka hakuna anaejua kuhusiana navyo vitu viwili

hivyo ila Qalilan.

Kwani alisema Hujjat Ul Islami Mujaddid Ad Din Az Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii

Al Thani Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhqmmad Al Ghazali kua: Hakika ya Mimi kila ninavyozidi Kusoma na Kuzidi

Kujua basi Ndivyo Ninavyozidi kujiona kua Kumbe Mimi ndio Sijui kitu Chochote.

Na ndio maana unapokutana na Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye

alisema kuhusiana na Imam Al Ghazali kua: ‘Hujjat Ul Islam alikua na Ilm kubwa

Sana kama vile ambavyo Allah Subhanah wa Ta'ala aliikusanya Ilm Tofauti katika

sehemu Moja na kisha akamuonesha Imam Al Ghazali sehemu alipoiweka Ilm hio’

Na bila ya shaka hii hua linaonekana wazi pale unajua kua Miongoni mwa Watu

wanaofanyiwa Uchunguzi sana Ulimwenguni kuhusiana na Ilm zao na maneno yao basi

baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi wa pili ni Hujjat ul Islami Imam

Al Ghazali. Na hata hivyo mbali ya kua ni mwenye Kufanyiwa Utafiti sana na kukubalika

sana kwa Upekee wa Ukubwa wa Ilm yake lakini yeye mwenyewe alikua anasema kua

hajui kitu na Kila akisoma basi anazidi kujiona kua Yeye Hajui Kitu.

Na hivyo kwangu mimi huu ni Mmoja kati ya Mifano ambayo inabainisha maana ya

maneno:

‏﴿وَمَآ أُوتِيتُم مِّنَ‏ ٱلْعِلْمِ‏ إِلا َّ قَلِيلاً‏ ﴾

Wama Utitum mina al Aa’alman illa Qaliilan(Surat Al Isra 17:85)

Tafsir: Na Mmepewa Ilm juu yake Ila Kidoogo tu


933

Kwani tunapozungumzia Kuhusiana na Ilm ya Roho kama Roho, basi bila ya shaka, hiki

ni kitu ambacho kiko kama alivyosema Mwenyewe Allah Subhanah wa Ta'ala kua: Ibn

Adam Hatuwezi kujua juu yake isipokua kidoogo tu.

Hapa inabidi Mtu utafakari kuhusiana na hii idadi ya Maarifa juu ya kitu husika ambayo

mbali ya kua na ukubwa Mkubwa sana lakini sisi tumejaaliwa kua ni wenye kujua

Kidoogo tu. Kwa Sababu hakuna kitu Kikubwa na chenye Thamani cha Kiumbe mbele

ya Allah Subhanah wa Ta'ala kama Roho yake kiumbe Ibn Adam.

Na ndio maana Aya zikasema kua Ukiua Roho Moja ni kama Umeua Ulimwengu Mzima,

na Ukiokoa Roho Moja ni kama Umeokoa Ulimwengu Mzima. Hivyo hii inaonesha

Ukubwa na Uzito na Thamani wa hiki Kitu kinachojulikana kama Roho ambacho Mbali

ya Thamani yake na Ukubwa wake Basi hatujui chochote bali kidogo tu.

Kwani miaka na miaka Wanasayansi wamekua wakifanya Uchunguzi wa kila kitu

kuhusiana na Mwili wa Ibn Adam, na wamefanikiwa hadi kugundua DNA ambacho ni

Kitu kinachomnasibisha Ibn Adam na Asili yake kwa vizazi na vizazi, kisha Ndani yake

wakakutana na kitu Kidooogo zaid kinachoitwa Atom.

Ambapo tunapozungumzia na Atom basi tunazungumzia asili ya Mfumo wa kila kitu

Ulimwenguni, Hata Mfumo wa Jua, Nyota na Sayari zinazoelea Ulimwenguni na

kukukua na kutanuka kila miaka inavyoongezeka basi zimeanzia na kitu kinachoitwa

Atom.

Hivyo Wamegundua kuhusiana na Atom, lakini hawajagundua kuhusiana na Roho,

kwani tunapozungumzia Ilm ya Juu ya Roho basi Ilm ambayo ni imo ndani ya Mamlaka

ya Muumba yaani Allah Subhanah wa Ta'ala na hivyo tunazungumzia Kitu ambacho ni

Kizingiti cha Upeo wa Ilm ya Viumbe.

Hivyo kulingana na maneno haya ya Aya hii basi Ibn Adam wasome watakavyosoma,

wajue watakavyojua lakini hawatojua kuhusiana na Roho, isipokua Qaliilan.

Yaani hio Qaliilan ni Kua Roho ipo, na Kila Ibn Adam anayo yake, na Inakuwepo hata

Kabla ya Kuzaliwa kwake Ibn Adam husika, na anakua nayo anapokua ndani ya Mfuko

wa Uzazi wa Tumbo la Mama yake, baada ya Kuzaliwa kwake, katika kuishi kwake,

katika kufa kwake na pia baada ya Kufa kwake.n.k

Yaani hii Ibn Adam hua tunajua kutokana na kile Kidoogo tu tulichopewa na Allah

Subhanah wa Ta'ala juu yake kupitia katika Hadith na aya za Qur'an.


934

Ambapo Uthibitisho wa wazi juu ya hili ni katika kutojua ni nini Roho na hivyo

kutojulikana kutoka kwake ndani ya Mwili wa Ibn Adam yaani hakuna ajuae Vipi, Wapi

wala Saa ngapi, kwani majibu ya Masuali haya ndio Ilm Kubwa zaid.

Ingawa hivyo ndivyo ilivyo hali ya uhalisia kwetu sisi Ibn Adam lakini kwa upande

mwengine basi anasema Imam Ahmad Ibn Hanbal kua: ‘Amesema Muadh Ibn Jabal

Radhi Allahu Anhu kua: Siku Moja Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alitukawilisha Kusali mpaka ikawa tunakaribia kuliona Jua linataka kuchomoza.

Hapo akatokezea Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akiwa ni mwenye Haraka

sana na kisha Ikaakimiwa sala na kisha Akasalisha Sala ya Al Fajir kwa kuifupisha

Kisha baada ya Kusali akatuambia tubakie katika Safu zetu kama tulivyokua

tumekaa

Kisha akatugeukia na kutuambia: 'Wacheni nikuambieni kile ambacho kilinizuia

mimi leo hii Alfajir

Niliamka Usiku nikatia Udhu na kisha nikasali Qiyam Al Layl kwa kadri

nilivyojaaliwa

Na kisha nikalala, Usingizi Mzito sana, na ghafla nikajihisi nipo mbele ya Mola

wangu

Allah Subhanah wa Ta'ala, nikiwa katika hali bora kabisa

Allah Subhanah wa Ta'ala akaniambia: ‘Ewe Muhammad!’

Nami nikajibu: ‘Niko Mbele yako ya Rabb’

Allah Subhanah wa Ta'ala akasema: ‘Hivi Jee Malaika walioko kwenye Mbingu ya

Juu Wanabishaniana nini?’

Nami nikasema: ‘Sijui ya Rabb!’

Allah Subhanah wa Ta'ala akaniuliza mimi Suali hilo mara tatu nami nikamjibu

kua Sijui kisha Allah Subhanah wa Ta'ala akanigusa baina ya Kifua changu, hadi

nikahisi Ubaridi wa Mguso wake kwenye Kifua changu, na hapo kila kitu kikawa

kipo wazi kwangu mie.

Kisha Allah Subhanah wa Ta'ala akaniuliza tena: ‘Ewe Muhammad Malaika walio

Kwenye Mbingu ya Juu wanabishaniania nini?’

Nami nikajibu: ‘Wanabishana kuhusiana na Kufutiwa Dhambi na Darja zake’


935

Allah Subhanah wa Ta'ala akaniuliza tena: ‘Jee ni Kipi kinachofuta Dhambi?’

Nami nikajibu: Ni kuiendesha miguu kuelekea Msikitini Kusali na kubakia ndani

yake baada ya Sala, na Kutia Udhu ipasavyo hata kama ikiwa kuna Uzito katika

Jambo hilo

Kisha Allah Subhanah wa Ta'ala akaniuliza: Kisha na Jengine?(Yaani kuhusiana

na Darja)

Nami nikajibu: Kuwalisha Masikini, Kutumia Qawlan Layyina na Kusali wakati

watu wamelala

Allah Subhanah wa Ta'ala akaniambia: ‘Omba Ewe Muhammad’

Nami nikaomba: ‘Ya Allah nakuomba niwe ni mwenye kufanya mema, niachane na

mambo maovu, niwapende Masikini, nawe unisamehe na kuniiingiza kwenye rehma

zako na kama ukitaka kuwapa mtihani watu basi usinijaalie mimi kufa huku nikiwa

na mitihani, na nnaomba mapenzi yako na mapenzi ya wale unaowapenda na niwe

ni mwenye kupenda kufanya mema yanayokaribisha karibu nawe na karibu ya

mapenzi yako.’

Muadh Ibn Jabal Radhi Allahu Anhu anamalizia kwa kusema kua: Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akatuambia kua: Huu ni Ukweli hivyo jifunzeni

kutokana nao (Musnad Imam Ahmad)

Kwani hii ni Hadith ambayo inajulikana kua kama Hadith Al Manam, na pia inajulikana

kama Hadith Ikhtisam al Mala Al A'ala.

Na bila ya shaka hadith hii inataka ufafanuzi, na tutaifafanua ila sio leo, kwani leo

nimeitumia Hadith hii kwa lengo la kubainisha Mtizamo wa Wanazuoni ambao unasema

kua:

Ingawa aya yetu imesema kua kuhusiana na Roho basi Ibn Adam hawakupewa Ilm

juu yake isipokua Qaliilan, lakini hadith hii inarubainishia kua Hali ilikua ni tofauti

kwa upande wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, kwani yeye alibainishiwa

Kila kitu pale alipoguswa na kusema sema Ndani ya Hadhithi hii kua ‘Baada ya

hapo basi kila kitu kikawa kiko wazi kwangu mie’

Na hivyo baada ya tukio hilo basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, basi hata

kuhusiana na Roho na Kifo Alikua akijua pia, hivyo ili tufahamiane vizuri zaid

nnazungumzia kuhusiana na nini basi hapa sasa inabidi tuangalie hali ilivyokua katika


936

siku za mwishoni kabla ya kufariki Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambazo

zilikua ni siku zisizozidi wiki mbili.

Ambapo anasema Abu Said Al Khudhri Radhi Allahu Anhu kua: ‘Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam alisema kua: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala amemjaalia bahati Mja

wake ya kuchagua baina ya kile anachokipenda katika alivyomruzuku hapa Dunani

na kla anachoktaa katika Dunia hii, lakini Mja wake huyo ameamua kuichagua

Akhera yake’’

Abu Said Al Khudri Radhi Allahu Anhu anaendelea kusema kua: ‘Baada ya Abu Bakr

As Siddiq Radhi Allahu Anhu kusikia kuhusiana na maneno haya, basi akaanza

Kulia na kusema: Ya Rasul Allah Hakika Sisi tumewatoa Kafara Mama zetu na

Baba zetu’

Hivyo sisi tukajiuliza kwanini Abu Bakr akasema Maneno hayo? Kwani watu

walikua wakisema: ‘Mwangalie yule Mzee Abu Bakr! Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam’ Amezungumzia kuhusiana na Mja wa Allah amabae amejaaliwa

kuchagua baina ya Neema za Dunia na za Akhera na akachagua Neema za Akhera.

Halafu yeye anajibu kua Mama zetu na Baba zetu tumewatoa Kafara kwa Ajili yako

ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam!

Kwani Abu Said Al Khudri Radhi Allahu Anhu anaendelea kutuambia kua:

‘Baadae sisi ndio tukajua maana aliyoikusudia Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu

Anhu, kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ndie Mja ambae amejaaliwa

Bahati ya kuchagua (kuhusiana na Kubakia Duniani kuendelea na Neema za Allah

Subhanah wa Ta'ala na kila atakachokitaka au Arudi kwa Mola wake) Na baada ya

hapo ndio tukakubaliana kua Abu Bakr Radhi Allahu Anhu kua ndie mwenye Ilm

kubwa zaid kuliko sote miongoni mwetu.(Mishkat al Masabih)

Naam..siku 5 Kabla ya kufariki kwake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi

aliingia Msikitini na kusema: ‘Kama kuna yeyote yule ambae ni iwahi kumpiga

mjeledi kwenye mgongo wake, basi nami natoa Mgongo wangu aje kunipiga leo hii,

na kama kuna yeyote yule niliemvujia heshima basi nami leo nampa heshima yangu

aivunje’

Kisha baada ya hapo akawausia Waislam kufanya mema na kuachana na Mabaya na

kupendana na kutochukiana kisha baada ya kumaliza basi kuna Mtu Alisimama Msikitini

na kusema: ‘Ya Rasul Allah hakika mimi nnakudai Dirham 3’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Ewe Fadhl Mlipe pesa zake

anazonidai’


937

Kisha akasema: ‘Enyi Waislam hakika mimi nakuusieni, kua idadi ya Waumini

itaongezeka sana lakini idadi ya watakaoinusuru Dini itapungua kiasi ya kua wingi

wao itafikia kua kama vile wingi wa matumizi ya chumvi kwenye chakula. Hivyo

yeyote yule atakaekua na Madaraka, basi asiwaaadhuru na kuwadhulumu walio

chini yake. Bali anatakiwa awe ni miongoni mwa wenye kuonesha shukran na

kuthamini alivyotaminiwa na Mola wake kwa kutoziangalia na kuzisamehe kasoro

za wale walio chini yake.’

Katika siku ambayo kesho yake anafariki basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alitoa Sadaqa vitu vyake vyote, Pesa zake ambazo zilikua ni Dirham 7 tu, Upanga wake,

n.k, na katika siku ya mwisho ya Uhai wake Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam,

basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alimwita Binti yake Fatma Bint Rasul

Salallahu Alayhi wa Salam na kisha akamnong'oneza kitu, na hapo Fatma bint Rasul

Allahu Salallahu Alayhi wa Salam akaanza kulia.

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alipomuona kua analia basi akamvuta na

akamnong'oneza neno jengine na hapo Fatma bint Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa

Salam akaanza kucheka kwa Furaha Baada yake.

Ambapo alipoulizwa Fatma bint Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam kwanini akalia

na kisha akacheka basi alisema:

Mara ya Kwanza aliniambia kua hatopona na atakufa kutokana na Maradhi yake,

na kisha akaniambia kua Mimi nitakua ndie Mtu wa mwanzo kujumuika nae

Peponi (baada ya kufariki kwake)(Sahih Bukhari)

Naam..hivyo alipoulizwa Fatma bint Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam alipoulizwa

na Umm ul Muuminin Aisha Radhi Allahu Anha kwanini aliponong'onezwa na Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam kwanza akalia na kisha akacheka basi alisema: ‘Mara

ya Kwanza aliniambia kua hatopona na atakufa kutokana na Maradhi yake, na

kisha akaniambia kua Mimi nitakua ndie Mtu wa mwanzo kujumuika nae Peponi

(baada ya kufariki kwake) (Sahih Bukhari)

Kwani Kauli hio ya Ubashirio wa Kifo cha Fatma Bint Rasul kutoka kwa mwenyewe

Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam kua yeye atakua ni mtu wa Mwanzo kukutana

na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam miongoni mwa wengine wote waliokaribu nae

haikua ni Kauli ilianguka!

Na hii ni kwa Sababu Baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kufariki basi

ilipita miezi miwili tu na kisha na Fatma Bint Rasul Salallahu Alayhi wa Salam nae

akafariki, Hivyo hii pia ilikua inaonesha kua Rasul Allah Salalahu Alayhi wa Salam

alikua anajua kuhusiana na kifo cha Binti yake baada ya kufariki kwake.


938

Na Katika Siku ambayo anafariki basi Alimuona Fatma kua Yuko Mnyonge Sana juu

yake hivyo akamwambia: Ewe Binti Yangu, Usiwe Mnyonge Sana kwani kwa Hakika

Mimi Sitoumwa zaidi tena baada ya kumalizika Siku hii ya Leo!

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambapo moja kati ya siku hizo basi alisema:

‘Enyi Watu nimesikia kua Mnataka Kuchanganyikiwa kwa sababu tu ya kua Mimi

nnataka Kufariki, hivyo fahamuni kua Hakuna Mtume ambae aliishi Milele pamoja

na Watu wake, hivyo Itakuaje kwangu mimi kuwezekana hivyo? Fahamuni kua

Mimi karibuni nitakutana na Mola wangu, na bila ya shaka, Nyiny pia Mtakutana

nae.

Hivyo Enyi Maansari Wasaidieni Muhajjirina na Enyi Muhajirina Wasaidieni

Maansari, kwani nao wamekupokeeni, wakakupeni ardhi yao, wakakukaribisheni

majumbani mwao, Ingawa walikua katika Mda mgumu wa Kiuchumi hivyo

Wasaidieni na kama ikiwa mmoja wenu atawatawala basi na awaonee huruma’

Enyi Watu kila kitu hua ni chenye kutokea kulingana na Makadirio na Mipango ya

Allah Subhanah wa Ta'ala. Hivyo msijaribu kupingana na makadirio ya Allah

Subhanah wa Ta’ala, kwani ni nyinyi ndio mtakao kua walioshindwa dhidi yake.

Msijaribu kumhadaa Allah Subhanah wa Ta’ala kwani ni nnyinyi ndio mtakaokua

mkijihadaa Nafsi zenu. Hakika mimi ni mwingi wa Rehma na Huruma juu yenu,

na bila ya shaka tutakutana tena In-shaa Allah, na sehemu tutakayokutana ni

pembeni ya Chemchem ya Al Kawthar.

Hivyo kama mnataka kukutana na mimi basi kila mmoja wenu ahifadhi mikono

yake na ulimi wake kutokana na mambo yasiyomhusu. Enyi watu fahamuni kua,

kufanya dhambi hua ni sababu yakukubadilishieni Neema na Rehma zenu juu

yenu, hivyo kama ikiwa wengi katika jamii ya Watu wenu ni wenye kufanya Mema

basi hata Mamlaka yatakayokua juu yenu yatakua ni ya Kiuadilifu. Na kama wengi

katika jamii yenu watakua ni Waasi na wenye kufanya Dhambi katika jamii yenu

basi hata Mamlaka yatakayokua juu yenu yatakua ni ya Dhulma na ni yenye

kukukandamizeni (Musnad Imam Ahmad)

Kisha baada ya Maneno hayo basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akaingia ndani

katika Chumba cha Bi Aisha Radhi Allahu Anha na kuenda kulala

Naam, Man Jada Wajadda yaani Mwenye Kutafuta hupata, Hivyo nasi tufanye jitihada

katika kujistiri na Nafsi zetu na kisha na Allah Subhanah wa Ta'ala nae ndio atatustiri

kutokana na Nafsi zetu na atatusamehe kutokana na kasoro zilizosababishwa na Nafsi

zetu, lakini baada ya kujitahidi kwetu.


939

Kwani katika siku ya Mwisho wa Uhai wake basi Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alifanikiwa kusali Sala ya Alfajir ndani mwake kwani alishindwa kutoka na hivyo

hakufanikiwa kusali sala ya Adhuhuri akatangulia kwa Mola wake

Ambapo anasema Anas Ibn Malik Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wakati Waislam

wanajitayarisha Kusali Sala ya Alfajir ya Siku ya Jumatatu ambayo ilikua

inaongozwa na Abu Bakr, basi Waislam walishangaa walipomuona Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akinyanyua Pazia la Chumba cha Aisha, huku

akawatizama Waislam namna walivyojipanga Safu kwa ajili ya Sala na kisha

akatabasamu, Abu Bakr alipomuona Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, basi

akarudi Nyuma kutoka katika Sehemu ya Uimamu na Kujiunga na Safu ya

Maamuma, kwani alidhania kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anakuja

kusali pamoja nao

Hivyo Waislam walifurahi sana kua Watasalishwa Na Rasul Allah Salalahu Alayhi

wa Salam katika Sala yao Lakini Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam, Akaashiria

kwa mkono kua Abu Bakr aendelee kusalisha, na kisha yeye akarudi Ndani

Chumbani na Kufunga Pazia hilo’

Kisha Asubuhi yake akaomba waitwe wajukuu zake Hasan na Husein akawabusu na

Kuisia kua waangaliwe na kusimamiwa ipasavyo, kisha akawaita Wake zake wote na

Akawausia kua wawe ni wenye kumkumbuka Allah Subhanah wa Ta'ala na kisha

akasema: ‘Hakika bado nnahisi Maumivu kutokana na Chakula nilichokila katika

maeneo ya Khaybar, na nnahisi kua Kifo kimewadia’

Akawausia Watu wawe wanasali, na kisha akawamrisha wawaonee huruma Watumwa

wao, kwa kusisitizia juu ya jambo hilo mara kadhaa, kisha akasugua Meno yake na

akanawa Uso wake Mtukufu kisha akasema: ‘Hakuna Mola anaestahiki Kuabudiwa

kwa Haki isipokua Allah Subhanah wa Ta'ala..Ama kwa Hakika Kifo kina maumivu

makali sana’

Kisha akaangalia Juu na akasema: ‘Pamoja na wale ambao umewaingiza katika

Rehma zako, miongoni mwa Mitume na Waliosadiki, Mashahidi na wenye kufanya

Mema, Ya Allah Nakuomba Unisamehe na uniingize katika rehma zako na uniweke

pamoja na Waliokua na Darja ya Juu

Ya Allah Nijaalie niwe ni Miongoni mwa waliokua Karibu nawe Miongoni mwa

waliokua katika Darja ya juu. Hakika ya sisi Marejeo yetu ni kwa Allah Subhanah

wa Ta'ala na kwake yeye ndiko tunakokutegemea kwa ajilo ya msaada na Maisha

ya Milele’


940

Baada ya hapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akafariki huku akiwa

amemuegemea Umm ul Muuminina Aisha Radhi Allahu Anha, Dunia huku akiwa na

Umri wa miaka 63.

Ambapo habari ya kifo ikamfikia Abu Bakr Radhi Allahu Anhu aliondoka na kueleka

Msikitini alipofika akaingia ndnai bila ya kuzungumza na mtu yeyote hadi alipofika

kwenye chumba cha Aisha Radhi Allahu Anha na kumuangalia Rasul Allah Salallahu

Allahu Alayhi wa Salam ambae alikua amefunikwa shuka la Yemen, hivyo akamfunua

uso wake na kisha akamgusa na kumbusu na kisha akaanza kulia hukua akisema:

‘Hakika mimi nimemtoa Kafara Mama yangu na Baba yangu kwa ajili yako, hivyo

sitokusababishia kufariki mara mbili, kwani tayari umeshaonja mauti ambayo

Allah Subhanah wa Ta’ala ameiandikia kila Nafsi kua itayaonja.’

Na kisha Abu Bakr Radhi Allahu Anhu akatoka na kuelekea kwa Umar Radhi Allahu

Anhu ambae alimwambia: ‘Umar kaa kitako chini’ hivyo Umar Radhi Allahu Anhu

akagoma na watu wakaanza kuondoka, Umar Radhi Allahu Anhu akamsogelea Abu Bakr

Radhi Allahu Anhu ambae alisimama na kuanza kusema: ‘Ama kwa sasa hivi, kila

aliekua akimubudu Muhamamd Salallahu Aalyhi wa Salam, basi Muhammad

amefariki, lakini kwa yeyote yule aliekua akimuabudu Allah Subhanah wa Ta’ala

basi Allah Subhanah wa Ta’ala ni mwenye uhai wa Milele na kamwe hawezi kufa,

kwani Allah Subhanah wa Ta’ala amesema:

‏﴿وَمَا محَُم َّدٌ‏ إِلا َّ رَسُولٌ‏ قَدْ‏ خَلَتْ‏ مِنْ‏ قَبْلِهِ‏ ٱل ُّر سُ‏ لُ‏ أَفإِنْ‏ م َّاتَ‏ أَوْ‏ قُتِلَ‏ ٱنْقَلَبْتُمْ‏ عَلَىٰ‏

أَعْقَابِكُمْ‏ وَمَن يَنْ‏ قَلِبْ‏ عَلَى ٰ عَقِبَيْهِ‏ فَلَنْ‏ يَضُر َّ ٱهلل ََّ‏ شَيْئاً‏ وَسَيَ‏ جْزِى ٱهلل َُّ‏ ٱلش َّاكِرِينَ‏ ﴾

Wama muhammadun illa rasoolun qad khalat min qablihi alrrusulu afa-in mata aw

qutila inqalabtum AAala aAAqabikum waman yanqalib AAala AAaqibayhi falan

yadurra Allaha shay-an wasayajzee Allahu alshshakireena (Surat Al Imran 3:144)

Tafsir: Na hakua Muhammad isipokua ni Rasul, na wamekuja kabla yake Mitume

hivyo jee hata kama ikiwa atakufa au atauliwa, mtageuka kutokana na muelekeo wa

visigino vyenu? Na atakaegeuka kutokana na muelekeo wa visigino vyake basi

hatomdhuru Allah Subhanah wa Ta’ala hata kidogo na Allah Subhanah wa Ta’ala

atawalipa wale wenye kuonesha shukurani.

Ambapo anasema Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua: ‘Wa Allahi ilikua

kama vile watu hawakuwahi kusikia aya ya Qur’an kama hii hadi pale Abu Bakr

alipoisoma na kuifanya kua kama ni ukumbusho, na hivyo kila mtu akawa ni

mwenye kuisoma aya hii hadi ikawa hakuna hata mmoja ambae si mwenye

kuisoma’


941

Na anasema Said Ibn Al Musayyib kua : ‘Umar alisema, Wa Allahi mara tu

nilipomsikia Abu Bakr akiisoma aya hii basi nilianguka chini ardhini, kwani nilihisi

kua kama miguu yangu haiwezi tena kunibeba, ni pale tu nilipoisikia ndi nikajua

kua Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam amefariki kweli’(Sahih Bukhari)

Mbali ya kua hiki ni Kifo kilicho wasikitisha wengi lakini pia kilimsikitisha zaid

UmmuAyman kwani hali yake yeye ilikua ni Mama aliepoteza Mtoto wake Kipenzi na

pia kama mtu aliepoteza Dira ya Muelekeo wake ambao alikua ana matumaini kua

ataondoka yeye na kuiwacha hapa Duniani baada yake.

Ummu Ayman alipoulizwa mbona unalia sana kiasi hicho basi akajibu: ‘Hakika mimi

nilikua najua kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam iko siku atakufa, hivyo

sasa hivi nalia kwa sababu ndio nimegundua kua Hautoshuka tena Ujumbe wa

Allah Subhanah wa Ta'ala juu yetu.’

Baada ya kufariki kwa Rasul Allah Salallahu Aalyhi wa Salam kulitokea mgogoro

mkubwa sana na mvutano na mazungumzo makubwa hata kabla ya kuuzika mwili huo,

baina ya Ansari na Muhajjirun, na mwisho wakakubaliana kua Abu Bakr Radhi Allahu

Anhu awe ndie Khalifa.

Waislam walitumia siku nzima ya majadiliano na amakubaliano tangua siku hio ya

Jumatatu hadi ilipoingia Alfajir ya siku ya Jumanne ambapo mwili Mtukufu wa Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam ukakoshwa na Al Abbas Ibn Abd ul Mutalib na Al

Fadhl Ibn Abbas, Ali Ibn Abi Talib, Usama Ibn Zayd na Quthan Ibn Abbas Radhi Allahu

Anhum.

Na kisha wakamvisha Sanda na baada ya hapo Waislam wakabakia kuulizana anatakiwa

azikwe wapi? Ambapo Abu Bakr Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Mimi nimemsikia Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam akisema kua: ‘Mitume hua wanazikwa katika

sehemu waliyofia’’ hivyo Abu Talha Radhi Allahu Anhu akaondoa Kitanda kilichopo

chumbani humo na kisha chini yake likachimbwa kaburi lake Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam.

Kisha baada ya hapo watu wakaingia ndani mwake na kumsalia Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kwa zamu, ambapo watu kwanza walikua ni watu wa Kabila lake, kisha

wakafuatia Muhajirina na kisha wakafuatia Maansari na kisha Wanawake wakamsalia na

kisha Watoto na kisha akazikwa, na hivyo ndivyo ambavyo Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam alivyolakiana na kifo chake.


942

MAUTI, BARZAKH NA KABURI KATIKA AYA NA HADITH

Neno Laqiyah kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kumlaki Mtu; Kupokea Mtu au

Kitu; Kumkaribisha Mtu; Kumuegemea Mtu; Kukutana uso kwa uso na Mtu au na Kitu;

Kukiona Kitu; Kukijua Kitu; Kuelekea kwenye Muelekeo Ambao Kuna Mtu au Kitu;

Kupitiwa na hali ya Kitu au Kuhisi Hali Ya Kitu.

Naam..amesema Allah Subhanah wa Ta'ala katika aya iliyotumia neno Laqiyah kua:

‏﴿قُلْ‏ إِن َّ ٱلْمَوْتَ‏ ٱل َّذِى تَفِر ُّونَ‏ مِنْهُ‏ فَإِن َّهُ‏ مُلاَقِيكُمْ‏ ثمُ َّ تُرَد ُّونَ‏ إِلىَٰ‏ عَ‏ المِ‏ ٱلْغَيْبِ‏

وَٱلش َّهَادَةِ‏ فَيُنَبِّئُكُم بمَِا كُنتُمْ‏ تَعْمَلُونَ‏ ﴾

Qul inna almawta alladhee tafirroona minhu fa-innahu mulaqeekum thumma

turaddoona ila AAalimi alghaybi waalshshahadati fayunabbi-okum bima kuntum

taAAmaloona(Surat Al Jumuah 62:8)

Tafsir: Sema (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam kua) Hakika Ya Mauti,

Ambayo Mnayakimbia Kutokana Nayo basi Kwa Hakika Yatakulakini

(Yatakupokeeni) Kisha Mtarudishwa kwa yule Mwenye Kujua Juu ya

Yasiyojulikana na Kutoonekana na Yanayojulikana na Kuonekana kisha

Mtawekewa wazi Juu ya Yale Mliyokua Mkiyafanya.

Katika Aya hii tunaona kua Allah Subhanah wa Ta'ala anatuwekea Wazi kua Mauti ni

Kitu ambacho kila Mmoja wetu Atakumbana nacho. Hivyo hiki ni kitu ambacho

hakikimbiliki. Kwani hali yetu kuhusiana na Mauti hua inakua Kama hali ya Mtu ambae

alikua Ugenini na hivyo yuko Safarini Kurudi Nyumbani. Hivyo Bila ya Shaka Hukutana

na Wanaomsubiri kwa ajili ya Kumpokea pale atakaporudi Nyumbani baada ya kuondoka

kwa muda mrefu. Hivyo sisi Hua ni Wageni, Akhera hua Nyumbani na Mauti hua ni

yenye Kutupokea kutoka katika Safari yetu ya Ugenini na Kutukaribisha Nyumbani.

Kwa Upande Mwengine Mauti hua Kama Jini yule ambae akakushtua kutokana na

kuamua kukufanyishia, hivyo nawe ukaanza kumkimbia kwa Khofu na kuhisi kua yuko

Nyuma yako, lakini Ghafla Unashtukia Ametua Mbele yako na kwa kasi yako basi

huwezi kusimama ghafla na hivyo ukawa ni mwenye Kuvaana nae kutokana na

Kukumbana na wewe.

Naam..hio ndio maana ya Mulaqiikum hivyo aya inaendelea kutuambia kua: Thuma

Turadduuna Ila Aalimi - Kisha Mtarudishwa kwa yule mwenye Kujua


943

Na hivyo Kutuwekea wazi kua kutokana na kua Akhera ndio Nyumbani na Mauti ndio

yatakayotupokea kutukaribisha Nyumbani ambako ingawa tumeondoka kwa kitambo

lakini Mwenye Umiliki wa Makaazi yetu hayo ya Nyumbani huko tulikotoka, kua ni

Mwenye kujua juu ya kila kitu tulichokifanya katika wakati huo tulipokua Safarini.

Kwani yeye ni mwenye sifa ya kua ni AAalimi alghaybi waalshshahadati - Mwenye Ilm

ya yaliyofichikana na yaliyowazi, ya Ulimwengu unaoonekana wa hapa Safarini Duniani

Tulipo na Ulimwengu wa Nyumbani Kabla ya Kuondoka kwetu na kurudi kwetu na

kitakachofuata baada ya Kurudi kwetu Akhera

Na Kisha atabainishia Kila kitu chetu tulichokifanya hapa Ulimwenguni kimoja baada ya

kimoja. Na akasema Hasan Al Basr kwa kuusia kuhusiana na Kifo kua: ‘Ibn Adam

anapofariki Dunia basi Ibn Adam hua wanaulizana kwa kusema kua: Hivi huyu

Mtu aliefariki amewacha nini?

Lakini kwa Upande wa Malaika hua ni wenye Kuulizana kwa kusema: Hivi Huyu

Mtu aliefariki ametanguliza nini?

Na Luqman Al Hakim alimuusia Mtoto wake kuhusiana na Kifo kua: ‘Ewe Mtoto

Wangu Hakika Juu ya Kile Utakachokutana nacho bila ya Kukitarajia’ - Bora

Ujitayarishe Nacho kwani ili tufahamiane kwanini Wenye Kujua wakausia hivyo, basi

na Tuangalie maana ya Maneno ya Aya tunayoiangalia ambayo inasema kua: Hakika ya

Hayo Mauti tunayoyakimbia kutokana nayo basi tutakumbana nayo kwani yatatupokea

kwa kuwepo huko tunakokukimbilia kutokana na Ujinga wa kudhania kwetu kua

tunakoyakimbia kua ndio yalikokuwepo.

Basi tumwangalie Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Al Ghazali ambae

anatuelezea namna tutakavyokumbana nayo Mauti pale aliposema katika Ihya Ulim Ad

Din kuhusiana na Kifo na Maumivu yake kua:

Fahamuni kua Maumivu Makali ya Kifo Hua ni yenye Kujulikana na Kuhisikana

Kikamilifu na Yule tu aliekionja Kifo hicho: Hivyo Mtu yeyote yule ambae hajakionja

basi hua ni mwenye kukifikiria kutokana na hisia za Maumivu aliyowahi kuyapata,

na kukisia Ukali wake kulingana na Maumivu ya Hali ya Juu Kabisa.

Ambapo Mwili unapodhurika kwa Moto Au kwa Jeraha, basi Hisia hizo za

Maumivu husafiri kuelekea Kwenye Roho kulingana na kiwango cha Madhara

katika Kiungo husika, Na katika Kutembea kwake hisia hizo za Maumivu hua ni

Zenye kupingua kasi yake zinaposafirishwa ndani ya Mwili kupitia kwa njia ya

Ngozi, Damu n.k hadi kuifikia sehemu kuua ya Maumivu ambayo ni Roho.

Hivyo Fikiria wewe Kua Hisia hizi unazohisi hua ni zenye kuanzia kwenye Kiongo

chengine kuelekea kwenye kiungo kikuu yani Roho sasa tunapozungumzia

Maumivu ya Kutolewa Roho basi Hua tunazungumzia Maumivu yanayohisiwa


944

Moja kwa moja kutoka kwenye Kiungo kikuu cha Hisia za Maumivu ambacho ni

Roho ambacho ndio Hua chanzo cha Maumivu ya Kuvamiwa kwake Roho yako.

Kwani kwa Mtizamo mwengine basi Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad

Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali anatuambia kua: ‘Mtu anapochomwa na

Mwiba basi Maumivu yake hua ni yenye Kusambaa katika eneo lililodhurika, yaani

Kama ni Kidole basi ni sehemu ya Kidole iliyojichoma ndio Hupata maumivu zaid.

Na maumivu ya Moto hua makubwa kwa sababu ya namna unavyosambaa Moto

katika Kuunguza kwake ambapo Maumivu ya anaechomwa na Upanga hua ni

katika Sehemu ilichomwa na Upanga Husika na Kudhurika, na ndio maana

maumivu ya Upanga hua Madogo kuliko ya Moto, lakini tunapozungumzia

Maumivu ya Kutolewa Roho basi hua ni makali sana kwa sababu hua ni yenye

kuivamia Roho yenyewe ya Mtu Husika.

Na hivyo Mtu Husika anaekufa hua ni mwenye kuhisi kua anachomolewa kila kila

mshipa wa Damu wa kila sehemu ya Mwili wake, kila mshipa wa fahamu kila

mshipa wa hisia na kila sehemu ya Mwili wake. Kila mfupa wa Mwili wake na Kila

Msuli wa Mwili wake. Tangu kuanzia kwenye Mzizi wa Nywele zake hadi chini

kwenye Nyayo za Miguu yake.

Hivyo usiulize hisia za Maumivu anayohusu Mtu aliekuwepo kwenye Sakarat Al

Mawt, na ndio maana ukaambiwa kua Maumivu ya Kifo hua ni Makali sana Kuliko

Kukatwa kwa Mapanga, au kukatwa kwa Msumeno au Mkasi.

Hivyo Mtu aliekatwa na Upanga hua ni Mwenye kuweza kulia na kupiga kelele na

hivyo kupunguza Maumivu kwa kutumia Nguvu zake na Ulimi na Mdomo wake.

Lakini Mtu anaekufa hua na Maumivu katika Kila kiungo chake na hivyo hukosa

hata Nguvu na uwezo wa Kujipinguzia Maumivu yake Kwani Kifo huvamia Viungo

vyake vyote mpaka Akili na Ufaham wake.

Hua anataka kupiga Kelele kujipunguzia Maumivu ya Mwili wake au kuomba

Msaada kwa waliokaribu yake, lakini hawezi kwani hana nguvu hata kipande ndani

ya Misuli yake kutokana na Maumivu yake.

Hivyo ndivyo Roho Inavyovutwa na Kutolewa, na hivyo huanza kufa kiungo chako

kimoja baada ya kimoja na kukiwacha kikiwa Kibariidi huku Macho yako

yakiangalia unayoyaona kwa mtizamo wa Mwisho’

Hivyo amesema Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali kua: ‘Kifo huvamia Viungo vyote mpaka Akili na Ufaham

wote Mtu hutaka kupiga Kelele kujipunguzia Maumivu ya Mwili wake au kuomba

Msaada kwa waliokaribu yake, lakini hawezi kwani hana nguvu hata kipande ndani


945

ya Misuli yake kutokana na Maumivu yake hivyo ndivyo Roho Inavyovutwa na

Kutolewa, na hivyo huanza kufa kiungo chako kimoja baada ya kimoja na

kukiwacha kikiwa Kibariiidi Huku Macho yako yakiwa Yanaangalia yale

unayoyaona kwa mtizamo wa Mwisho’

Kwani amesema Umm Salamah Radhi Allahu Anha kua: Amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: Wakati Roho Inapotolewa basi Macho hua ni yenye

Kuifuata

Na akasema Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu kua: Amesema Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua: Hivi Jee hamuoni nyie kua Mtu anapokufa hua ni mwenye

kuutolea Macho Upeo wa Jicho? Hii hutokea kwa sababu Mtu hua ni mwenye

Kuifuata Roho yake wakati inapotolewa(Sahih Muslim)

Hivyo kutokana na Hadith hizi na pia na Mtizamo wa Hujjat Ul Islami Imam Al Ghazali

ambao unasema kua Macho hua ni yenye Kuangalia kwa mtizamo wa Mwisho yale

Yanayoyaona basi tunaona kua Kama ikiwa Mtizamo wa Macho unafuata Roho

inapotoka hii inamaanisha kua:

Mtu unapokua katika Sakarat Al Mawt basi mbali ya kuhisi Maumivi hayo Makali

Lakini pia Macho yako hua yanaona Roho yako inavyotoka Na Hivyo basi Hua si

Unaona Roho inavyoyolewa mpaka kutoka kwake na Unahisi Maumivu hayo

Makali sana, lakini pia hua unawaona pia Malaika Wanaokutoa Roho Hivyo kama

Ukiwa Mtu mwema basi Unawaona namna wanavyokupokea Malaika wema

waliokutayarishia Makazi yako Katika kurudi kwako Nyumbani baada ya kua

Safarini hapa Duniani.

Na kama Ukiwa Mtu Muovu basi Unawaona namna wanavyokupokea Malaika wa

Motoni waliokutayarishia Makazi yako Katika kurudi kwako Nyumbani baada ya

kua Safarini hapa Duniani,

Na pia amesema Imam Salamh Ibn Dinar kua: ‘Ka hakika Kila atakaekua Mtiifu kwa

Allah Subhanah wa Ta’ala basi atapokewa na Mola wake kama mtu aliekua Safarini

kisha akarudi Nyumbani kwake ana kupokewa na Familia yake.

Na kama Mtu Muasi kwa Mola wake basi tapokewa kwa Mola wake kama vile

Mtumwa aliekimbia kwa Bwana wake na kisha akakamatwa na kurudishwa kwa

Bwana wake’

Yaani hii hua kama zinavyosema aya:


946

‏﴿وَهُوَ‏ ٱلْقَاهِرُ‏ فَوْقَ‏ عِبَادِهِ‏ وَيُرْسِ‏ لُ‏ عَلَيْكُم حَفَظَةً‏ حَتى َّ ٰ إِذَا جَآءَ‏ أَحَدَكُمُ‏ ٱلْمَوْتُ‏

تَوَف َّتْهُ‏ رُسُلُنَا وَهُمْ‏ لاَ‏ يُفَرِّطُونَ‏ ۞ ثمُ َّ رُد ُّو ۤ اْ‏ إِلىَٰ‏ ٱهلل َِّ‏ مَوْلاَهُمُ‏ ٱلحَْقِّ‏ أَلاَ‏ لَهُ‏ ٱلحُْكْ‏ مُ‏ وَهُ‏ وَ‏

أَسْ‏ رَعُ‏ ٱلحَْاسِ‏ بِينَ‏ ﴾

Wahuwa alqahiru fawqa AAibadihi wayursilu AAalaykum hafadhatan hatta idha

jaa ahadakumu almawtu tawaffat-hu rusuluna wahum la yufarritoona; Thumma

ruddoo ila Allahi mawlahumu alhaqqi ala lahu alhukmu wahuwa asraAAu

alhasibeena (Surat Al Anaam 6:61-62)

Tafsir: Na yeye ni Mwenye Uwezo wa Kinguvu juu ya waja wake, na anawatuma

Wasimamizi wake juu yenu, hadi pale kifo kinapomfikia mmoja wenu, Wajumbe wetu

huchukua Roho yake, na si wenye kudharau majukumu yao. Kisha wanarudi kwa

Allah Mola wao, Muadilifu, kwa hakika yeye ni mwenye kuhukumu na ni mwepesi

katika kuhesabu.

Kwani amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Malaika hua wanakuja

kwa Mtu anaefariki, na kama Mtu huyo ni Mwema basi hua wanasema: ‘Toka Nje

Ewe Roho Nzuri uliekuwepo kwenye Mwili wa Ya Mja Mwema, Toka Nje Ewe

Mwenye Thamani Ili Upate Habari Njema na Rehma na Manukato kutoka kwa

Mola wako asiekua na Hasira nawe.’

Na kisha Roho hio hutolewa na kupelekwa Mbinguni, huku Maneno hayo hurudiwa

rudiwa hadi Mbinguni ya kwanza na kufunguliwa Mbingu na kuulizwa: ‘Huyu ndio

Nani?’

Ambapo Malaika hua ni wenye kujibu kwa kusema kua: ‘Huyu ni Fulani Ibn

Fulani’.

Ambapo hapo pia Malaika Huiambia Roho hio kwa kusema: Karibu Ewe Roho

Njema uliekua kwenye Mwili wa Mja mwema karibu ewe mwenye Thamani! Upate

Bashirio Jema la Rehma na Manukato kutoka kwa Mola wako asiekua na Hasira

nawe.

Kwani kama ikiwa Mtu huyo si Mwema basi Malaika hao hua ni wenye kusema:

‘Toka Nje Ewe Roho Ovu iliyokua ndani ya Mwili wa Mtu aliekua akimuasi Mola

wake toka huku ukiwa Umelaaniwa na hivyo Kubashiriwa Habari za Maji Yamoto

yachemkayo, na Usaha na kila lililobaya’


947

Hali hii huendelea hadi Roho hio kutewa kwake na kuchukuliwa na kupandishwa

juu Mbinguni lakini Malaika wakifika Mbinguni basi Milango ya Mbingu

haitofunguka kwani Wataambiwa: ‘Hakaribishwi ndani yake Roho Mbovu iliyokua

ndani ya Mwili wa Mtu Muovu, Rudi Ardhini Ulikotoka na Laana zako kwani

Milango ya Mbingu Haiwezi kufunga kwa ajili yako’ Hivyo Malaika hurudi na

Roho hio Ardhini hadi ndani ya Kaburi lake(Imam Ibn Majah)

Kwani hadithi inatuwekea wazi kua Kila mtu anapotolewa Roho hua hapo hapo anaona

kwa Macho yake kabla hayajakata Mawasiliano na Ufahamu wake kua yeye ni Mtu wa

wapi.

Hivyo kama ni ya Mja Mwema basi Roho hio ikipandishwa Mbinguni husofiwa na hua

ni iliyoridhiwa na Mola wake na Malaika wake na hivyo huwekwa Peponi. Na ndio

maana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kua: Kwa Mja mwema basi

Kaburi ni Bustani katika Mabustani Ya Peponi.

Na kama ni ya Mtu Muasi basi tangu inatolewa hadi Kupelekwa Mbinguni hua

inalaaniwa tu kutokana na kua Roho hio imekosa Ridhaa ya Mola wake kwa Uasi wake.

Na hivyo inapofika Mbinguni basi hukataliwa kuingia ndani yake na kuamriwa

kurudishwa Ardhini kaburini kwa ajili ya Adhabu ya Kaburi.

Na ndio maana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Akasema kua: Kwa Mja Muovu basi

Kaburi hua ni Shimo kati ya Mashimo ya Motoni.

Neno Rahuba kwa Kilugha hua linamaanisha Kukaribisha, Kua Kua Mkarimu,

Kutosheleza, Kua na Nafasi Kubwa, Kua na Upana wa Nafasi, Kua Mkubwa.

Kwani Allah Subhanah wa Ta'ala ametumia neno Rahuba pale aliposema katika Qur'an

kuelezea yaliyotokea kwenye Vita vya Hunain ambalo ni tukio liliozungumziwa katika

aya ya 25 ya Surat At Tawba na pia akalitumia tena katika Sura hio hio katika aya ya 118

pale alipozungumzia kuhusiana na Vita vya Tabuq, ambapo katika aya ya 25 basi

amesema:

‏﴿لَقَدْ‏ نَصَرَكُمُ‏ ٱهلل َُّ‏ فىِ‏ مَوَاطِنَ‏ كَثِيرَةٍ‏ وَيَوْمَ‏ حُنَينٍْ‏ إِذْ‏ أَعْجَبَتْكُمْ‏ كَثْرَتُكُمْ‏ فَلَ‏ مْ‏ تُغْنِ‏

عَنكُمْ‏ شَيْئاً‏ وَضَاقَتْ‏ عَلَيْكُمُ‏ ٱلأَرْضُ‏ بمَِا رَحُبَتْ‏ ثمُ َّ وَل َّيْتُم م ُّدْبِرِينَ‏ ﴾

Laqad nasarakumu Allahu fee mawatina katheeratin wayawma hunaynin idh

aAAjabatkum kathratukum falam tughni AAankum shay-an wadhaqat

AAalaykumu al-ardu bima rahubat thumma wallaytum mudbireena(Surat At

Tawba 9:25)


948

Tafsir: Kwa Hakika Allah amekunusuruni (Na kukupeni Ushindi) Katika Viwanja

Vingi vya Vita vya Katika Siku ya Vita vya Hunayn Wakati Mlipofurahia Wingi wenu

ambako Hakukusaidieni kitu chochote wakati Imetandazwa kwa ajili yenu Ardhi Kwa

Mapana halafu Mkageuka na Kukimbia

Kwani mara nyingi watu wakikaribishana kwa Kuambiana Ahlan wa Sahlan Wa

Marhaban yaani Jihisi Huru kama Uko Nyumbani kwenu, Karibu.

Naam..Neno Marhaba limetokana pia na neno Rahiba ambalo tumesema kua pia hua

linamaanisha Kukaribisha, hivyo basi neno Marhaban linamaanisha Karibu!

Ambapo tunapoiangalia Qur'an basi tunaona kua pia imetumia neno Marhaban pale

ilipowaelezea wale watu wetu tuliowazungumzia Jana. Yaani wale watu ambao ni

Waovu, na hivyo wanapotolewa Roho hua wanalaaniwa tangu mwanzo mpaka mwisho,

kuanzia Ardhini mpaka Mbinguni.

Ambapo Roho zao zikishafikishwa Mbinguni basi hawatokaribirshwa ndani yake na

badala yake watarudishwa Ardhini kwenye Makaburi yao ambayo hua ni Mashimo

miongoni mwa mashimo ya Motoni…Allah Atupe Mwisho mwema na pia atuepushe na

Adhabu ya moto.

Kwani Allah Subhanah wa Ta'ala anasema Katika Qur'an katika aya zilizotumia neno

Marhaban lakini Katika Hali ya Kukanusha Ukaribisho yaani La Marhaban pale

ziliposema:

‏﴿جَهَن َّمَ‏ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ‏ ٱلْمِهَادُ۞هَٰذَا فَلْيَذُوقُوهُ‏ حمَِيمٌ‏ وَغَس َّاقٌ۞وَ‏ آخَرُ‏ مِن شَكْلِهِ‏

أَزْوَاجٌ۞هَٰذَا فَوْجٌ‏ م ُّقْتَحِ‏ مٌ‏ م َّعَكُمْ‏ لاَ‏ مَرْحَباً‏ هبِِمْ‏ إِن َّهُمْ‏ صَالُو ٱلن َّارِ۞قَالُواْ‏ بَلْ‏ أَنتُمْ‏ لاَ‏

مَرْحَباً‏ بِكُمْ‏ أَنتُمْ‏ قَد َّمْتُمُوهُ‏ لَنَا فَبِئْسَ‏ ٱلْقَرَارُ‏ ﴾

Jahannama yaslawnaha fabi/sa almihadu; Hadha falyadhooqoohu hameemun

waghassaqun; Waakharu min shaklihi azwajun; Hadha fawjun muqtahimun

maAAakum la marhaban bihim innahum saloo alnnari; Qaloo bal antum la

marhaban bikum antum qaddamtumoohu lana fabi/sa alqararu (Surat Sad 38:56-

60)

Tafsir: Jahanama Wataungua ndani yake, na ni Mafikio Mabaya sana Ndio Hii

Wache Waionje Maji Yanayochemka na Usaha Na Adhabu Nyengine kama hizo kwa

pamoja (Wataambiwa) Hiki ni Kikundi Kitakachoingia pamoja Nanyi (Motoni)

Hakuna Marhaba (Kukaribishwa Peponi,Mbinguni) Kwao wao Kwani kwa Hakika


949

Wataungua kwenye Moto Wataambiwa (Wanaofuata Upotovu) La Na Nyie pia hakuna

Marhaban (Kukaribishwa Peponi)Kwenu Nyie(Nao watasema kuwaambia

waliowapotosha kua) Ni Nyinyi ndio MliotupotoshaHii ni sehemu Mbaya sana kufikia.

Ya Allah! Hali inatisha tena Sana! Kwani aya zinawaelezea wale watu ambao watakaokua

ni wenye Kufuata Upande sio, yaani Upande wa Upotovu kutokana na Upande wa Njia

sahih ya Allah Subhanah wa Ta'ala na hivyo kua ni wenye kumuasi Mola wao, na

kutolewa Roho zao huku wakulaaniwa na hivyo kua ni miongoni mwa Watakaoambiwa

kua "La Marhaban - Hakuna Kukaribishwa"

Leo Mtaingia Motoni tu Pamoja na Kundi lenu na Viongozi wenu Mliokua

mkiwafuataAmbapo hapo hapo Mtu akifa hua anakufa bila ya kufuatana na wenzake

aliokua anawafuata au kufuatana nao, hivyo kila mmoja anaondoka Duniani na kurudi

kwa Mola wake kivyake, Lakini katika wakati wa kukutana akishakufa basi atakutana

nao wenzake hao wenye Lebo ya ‘La Marhaban’ na kisha wataanza kulaumiana wenye

kwa wenyewe. Allah atustiri..Aamin

Ambapo kwa upande Mwengine basi pia kuna Hadith ya Al Bara Radhi Allahu Anhu

ambae yeye anasema kua: ‘Hakika sisi tulitoka na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam kwa ajili ya Maziko ya Mmoja kati ya Maansari tulipofika Makaburini

Tukazika na kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akakaa kitako nasi

tukakaa kimyaa bila ya kumzunguka kama vile kuna Ndege ambao wanaruka juu

ya vichwa vyetu kwa ukimya wetu. Huku Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Akiwa na ujiti ambao alikua akichora chora ardhini, kisha akanyanyua kichwa na

kusema na kusema: 'Ombeni hifadhi kutoka kwa Allah Subhanah wa Ta’ala

kutokana na Adhabu ya Kaburi’

Na baada ya kusema hivyo mara 2-3 basi akasema: ‘Mja Mwema anapoondoka hapa

Duniani na Kuingia Akhera, basi hua ni mwenye kushukiwa na Malaika Kutoka

Mbinguni ambao hua ni wenye Nyuso Nyeupee kama Jua, na hukaa pamoja nae na

kujaa hadi kwenye upeo wa Macho.

Hua ni wenye kuja na Sanda kutoka Peponi ambayo inanukia Marashi ya Peponi,

kisha anashuka Malakat ul Mawt na kukaa pembeni ya Kichwa Chake na kusema:

'Ewe Roho Njema Njoo Katika Usamahevu wa Allah Subhanah wa Ta'ala na Radhi

zake.

Kisha Roho hio hutoka taratibu kama Tone la Maji kutoka kwenye Kibuyu cha

Ngozi cha Maji, Na Malakat ul Mawt akishaikamata Roho hio basi Malaika hao

walioshuka Kutoka Peponi hua hawamuachii Roho hio, humpokonya haraka, na

kuitia kwenye Sanda iliyojaa Marashi ya Peponi, na hapo huenea Harufu nzuri sana

ya Miski juu Ardhini. Na kisha Hupaa na hua hawapishani na Malaika yeyoye

isipokua hua ni wenye Kuulizwa: ‘Roho ya Nani Hii Nzuri?’.


950

Malaika hao hua ni wenye Kujibu: 'Ni ya Fulani Ibn Fulani'.

Huku wakitumia Majina Mazuri Mazuri ambayo alikua akijulikana hapa Ardhini.

Hali hii huendelea hadi katika Mbingu ya kwanza na kuomba wafunguliwe waingie,

na hapo Roho hio Hukaribishwa na kushindikizwa katika Mbingu ya juu zaid na

waliokua Karibu na Allah Subhanah wa Ta'ala hadi kufikia katika Mbingu ya 7

Kisha Allah Subhanah wa Ta'ala husema: ‘Andikeni katika Kitabu cha Mja wangu

Illiyun katika Mbingu ya 7 Kisha Mrudisheni Ardhini.’

Ambapo Allah Subhanah wa Ta’ala anakielezea kitabu cha Illiyun pale aliposema katika

ya azifuatazo:

﴿ كَلا َّ إِن َّ كِتَابَ‏ ٱلأَبْرَارِ‏ لَفِى عِلِّيِّينَ‏ ۞ وَمَآ أَدَْرا ا كََم عِلِّي ُّو نَ‏ ۞ كِتَا بٌم َّرْقُو مٌ‏ ۞

يَشْ‏ هَدُ‏ هُ‏ ٱلْمُقَر َّبُونَ‏ ﴾

Kalla inna kitaba al-abrari lafee AAilliyyeena; Wama adraka ma AAilliyyoona;

Kitabun marqoomun; Yashhaduhu almuqarraboona(Surat Al Mutaffifin 83:18-21)

Tafsir: Hakika ya Kitabu cha Hesabu za Waja wema zitawekwa kwenye Illiyinna. Jee

ni nini kitakachokujuulisha hio Illiyin? Ni Kitabu Kilichoandikwa, Ambacho

kinawashuhudia wale walio karibu na Allah Subhanah wa Ta’ala.

Kisha Allah Subhanah wa Tala anabainisha kwanini akataka Roho hizo zirudishwe

Ardhini kwa kusema : ‘Kwani kutokana nayo Ardhi ndio nimemuumba, hivyo ndani

yake Watarudia na kutokana nayo nitawafufua Upya.’ Kama alivyosema tena katika

aya kua:

‏﴿ٱل َّذِى جَعَلَ‏ لَكُمُ‏ ٱلأَرْضَ‏ مَهْداً‏ وَسَلَكَ‏ لَكُمْ‏ فِيهَا سُبُلاً‏ وَأَنزَلَ‏ مِنَ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ ‏َم آءً‏

فَأَخْرَجْنَا بِهِ‏ أَزْوَاجاً‏ مِّن ن َّبَاتٍ‏ شَتى َّ ٰ ۞ كُلُواْ‏ وَٱرْعَوْا أَنْعَامَكُمْ‏ إِن َّ فىِ‏ ذٰلِكَ‏ ‏َلآ ‏ٍت

لأُِ‏ وْ‏ لىِ‏ ٱ ل ن ُّ هَ‏ ٰ ى ۞ مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ‏ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ‏ وَمِنْهَا نخُْرِجُ‏ ‏ُك ‏ْم اتَ‏ رَةً‏ أُخْ‏ رَ‏ ‏ٰى

َ

Alladhee jaAAala lakumu al-ardha mahdan wasalaka lakum feeha subulan

waanzala mina alssama-i maan faakhrajna bihi azwajan min nabatin shatta; Kuloo

wairAAaw anAAamakum inna fee dhalika laayatin li-olee alnnuha; Minha

khalaqnakum wa fiha nu`idukum wa minha nukhrijukum taratan ukhra (Surat Ta-

Ha 20:53-55).


951

Tafsir: Ni yeye ndie aliejaalia Ardhi kua ni Tandiko kwa ajili yenu, na akatoa kutokana

nayo njia tofauti (mpate kutembea juu yake), kwa ajili yenu, na akashusha Maji

kutoka Mbinguni. Na kutokana nayo tukatoa mimea ya aina tofauti; Kuleni na lisheni

wanyama wenu hakika katuika haya kuna dalili kwa wenye kufahamu; Kwani

kutokana nao (udongo) tumekuumbeni, na tutakurudisheni ndani yake, na kutokana

nao tutakutoeni upya.

Hivyo Roho hio hurududishwa ndani ya Mwili wa Mtu huyo aliekufa ndai ya udongo

baada ya kuzikwa kwake yaani kua ndani ya Kaburi na kisha hushuka Malaika Wawili

na kumkalisha na Kumuuliza Mtu huyo: 'Jee ni Nani Mola wako?' Nae atajibu : ‘Ni

Allah Subhanah wa Ta'ala’

Malaika watamuuliza Mtu huyo: ‘Jee Ni ipi Dini yako? Nae atajibu : Dini yangu ni

Uislam.’

Malaika watamuuliza Mtu huyo : ‘Jee ni Nani alietumwa Miongoni mwenu?’ Nae

atajibu: ‘Muhammad Rasul Allah Salallahu Alayhu wa Salam’’

Malaika watamuuliza Mtu huyo : ‘Jee wewe ulifanya nini?’ Nae atajibu: ‘Nilisoma

kitabu cha Allah Subhanah wa Ta'ala Na nilikuamini’

Kisha Sauti itasema Kutoka Mbinguni: ‘Hakika Mja wangu amesema Ukweli hivyo

Mtayarishieni Kitanda cha Peponi na Mvisheni Nguo za Peponi na Mfungulieni

Mlango wa Peponi’

Kisha baada ya hapo Kaburi lake huanza kunukia na kutanuka kwa ukubwa wa upeo wa

Macho, kisha anatokea Mtu aliependeza akiwa na Nguo na Manukato ya za Peponi na

kumwambia

Pokea habari njema za Peponi ambazo zitakufurahisha leo hii, nae atasema: ‘Wewe ni

Nani? Mbona uso wako ni Muonekano wenye kubashiria Habari Njema?’

Mtu huyo atasema: ‘Mimi ni Amali zako njema’, nae Mja huyo atasema: ‘Ya Allah

Harakisha Siku ya Malipo nipate kua na Jamaa zangu na Mali zangu’

Ambapo baada ya Kutolewa Roho basi Malaika watasifiana kuhusiana na Mtu huyo

kutokana na Majina Mazuri yake.

Kwa mfano, Mwenye Kusali, Mkarimu, mwenye Kutoa Sadaqah na Zakkah, Mwenye

Kufunga, Kusoma Qur'an, Kufanya Dhikr, Kupenda Kusaidia Watu, Mpole, Mcha

Mungu, Mwenye Kukataza Mabaya na Kuamrisha Mema,n.k

Na kisha Mtu huyo atapongezwa na Malaika na ataoneshwa Sehemu yake Peponi

akishaingizwa kaburini.


952

Kisha Al Baraa Radhi Allahu Anhu anaendelea kutuambia kua Rasul Allah Salallahu

aAlayhi wa Salam akasema:

‘Lakini Mtu Muovu anapofariki na kutaka kuondoka hapa Duniani basi na kuingia

Akhera basi hushukiwa na Malaika ambao Wamevaa Maguo Meusi, huku wakiwa

na Gunia Jeusi na kukaa kwa kumzunguka Mtu huyo.Wingi wake Malaika hao hua

ni wa kujaza Upeo wa Macho kwa kila upande’

Halafu anashuka Malakut Al Mawt na Kukaa pembeni ya Kichwa cha Mtu huyo,

na kusema: ‘Ewe Roho Ovu! Toka nje kwenye Laana na Adhabu ya Allah Subhanah

wa Ta'ala, Kisha Roho yake Mtu huyo hutoka nje nya Mwili wake Mtu Huyo na

kuchana chana Mishipa yake na Neva zake za Hisia kama vile Reki inavyopita

kwenye Sufi iliyoroa’

Hapa tunaoan kua namna Rasul Allah Salallahu Alayhi w Salam alivyofananua Tukio

hili, la mtu ambae kua ni Muovu basi ni hali mbaya sana Kwani kwanza anashukiwa na

Malaika waliovaa Nguo Nyeusi. Na hii inatuonesha Kwanini Majaji Mahkamani wakawa

hawavai Nguo Nyeupe, kwani Nguo Nyeusi hua zinatia Khofu zaid, tofauti na kama

Wangekua wanavaa nguo Nyeupe hua inatuliza.

Halafu Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anaelezea namna Roho inavyotoka kwa

kusema kama Reki linavyopita kwenuye Sufi iliyoroa maji.

Hapa inabidi tuchukulie Mfano wa Pamba ili tupate kufaham Zaidi Ambapo Pamba ikiwa

Kavu basi hua haishikamani hivyo hua rahisi na ina wepesi kuchambulika Lakini ikiroa

hua inashikamana na kua ngumu na hivyo hua ili kuichambua basi inabidi utumie Nguvu

nyingi zaid.

Na ndio maana Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kua: Inachana chana

mishipa yote na neva za hisia sasa fikira Maumivu yake, kwani tukio hililinaonesha kua

kama hujaandikiwa kufa tu basi lazima Uzimie na kupoteza Faham.

Lakini kwa kua hii ni adhabu ya Allah Subhanah wa Ta'ala, basi unahisi maumivu hayo

na unaona bora uzimie lakini huzimii na maumivu yanazidi.

Naam..Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anaendelea kutuambia kua: ‘Roho hio

ikitoka tu na Malakatul Mawt kuikamata basi Malaika waliovaa nguo nyeusi hawaiwachi

kwenye Mikono ya Malakat ul Mawt bali wanampokonya Hapo hapo na kuitia kwenye

Gunia Jeusi walilokuja nalo, Na hivyo Gunia hilo hutoa Harufu Mbaya sana

isiyostahmilika ya Mtu aliekufa juu ya Ardhi.

Na kisha wanapaa Nayo Mbinguni na katika kila hatua yao wanayopita hukutana na

Malaika ambao


953

Huwauliza: ‘Roho ya Nani hio yenye Uovu kama huo?'

Malaika hao nao husema: ‘Ni ya Fulani Ibn Fulani’, kwa kumuita kwa Majina Mabaya

kabisa aliyokua akiitwa Ulimwenguni, hadi watakapofika Mbinguni, Malaika hao

wataomba kua Milango ya Mbingu ifunguliwe lakini haifunguliwi.

Subhana Allah!

Naam...Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anasema kua Malaika watakapoulizwa,

Ni nani huyo mwenye Roho Ovu inayonuka kama hivyo na Malaika wenzao basi Malaika

hao watamtaja Mtu huyo kwa Majina mabaya aliyokua akiitwa kutokana na amali zake

alipokua hai hapa Ulimwenguni.

Yaani kama Mtu Huyo ni Dhalim, Basi watamwita Dhalim.

Kama ni Tapeli watamwita kua ni Tapeli.

Kama ni Mwizi basi watamwita kua ni Mwizi.

Kama ni Mzinifu basi Watamwita kua ni Mzinifu.

Kama ni Mnafiq basi watamwita kua ni Mnafiq.

Kama ni Mwenye kudharau Sala basi watamwita kua ni mwenye kudharau Sala.

Kama Mfitinishaji basi watamwita kua ni Mfitinishaji.

Kama Muongo watakuita Muongo n.k.

Kwani hayo Masafa ya kutoka Ardhini mpaka Mbinguni na Malaika hao Mpaka Upeo

wa Macho Wanailaani Roho hio Ovu. Na Wanapishana na Malaika wangapi hadi

Mbinguni? Yaani hizo Laana za Malaika hao tu basi zinatosha Kumuangamiza Mtu

Muovu. Hapo bado Roho hio haijahesabiwa Makosa ya Uovu wake. Hii hua ni

Maangamizo juu ya Maangamizo.

Ambapo sehemu hii tu basi inatuonesha Umuhimu wa Kujipamba kwa Sifa Nzuri, Kuishi

vizuri na Watu, kwa Kufanya Mema, Kua na Tabia Nzuri,na Kuitana kwa Majina Mazuri

kama ilivyoamrishwa na Allah na Mtume wake Salallahu Alayhi wa Salam

Na kuzikimbia Sifa Mbaya na Yaliyokatazwa na Allah na Mtume wake Salallahu Alayhi

wa Salam

Kisha anasema Al Baraa Radhi Allahu Anhu kua Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi

wa Salam kua: Malaika hao walioichukua Roho ya Mja huyo Muovu wanapofika

kwenye Milango ya Mbingu na Kugonga, basi Milango hio hua haifunguliwi


954

Kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasoma aya ifuatayo:

‏﴿إِن َّ ٱل َّذِينَ‏ كَذ َّبُواْ‏ آبَِتِنَا وَٱسْتَكْبَرُواْ‏ عَنْهَا لاَ‏ تُفَت َّحُ‏ لهَُمْ‏ أَبْوَابُ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ وَلاَ‏

يَدْخُلُونَ‏ ٱلجَْن َّةَ‏ حَتى َّ ٰ يَلِجَ‏ ٱلجَْمَلُ‏ فىِ‏ سَمِّ‏ ٱلخِْيَاطِ‏ وَكَذٰ‏ لِكَ‏ نجَْزِى ٱلْمُجْرِمِينَ‏ ﴾

Inna allatheena kadhdhaboo bi-ayatina waistakbaroo AAanha la tufattahu lahum

abwabu alssama-i wala yadkhuloona aljannata hatta yalija aljamalu fee sammi

alkhiyati wakadhalika najzee almujrimeena(Surat Al Araf 7:40)

Tafsiri: Ama kwa Hakika wale ambao wamekadhibisha Aya zetu na Wakawa wana

Kibri juu yake Haitofunguliwa kwa ajili yao Milango Ya Mbingu Na Wala

Hawatoingia Peponi Hadi Pale Atakapoingia Ngamia na Kupenya kwenye tundu ya

Sindano Na Hivyo Ndivyo Titakavyowalipa Wahalifu walioasi.

Aya zinasema kua Watu waovu hawatofunguliwa Milango ya Mbingu na hivyo

hawatopata Rehma za Mola wao hadi pale Itakapowezeakana kwa Ngamia Kupenya

kwenye tundu ya Sindano. Jambo Ambalo Kamwe Haliwezekani...au linawezekana?

Ambapo kwa Upande mwengine Basi wale wanaosafiri Baharini hua ni wenye Kuzijua

zile Kamba nene ambazo hutumika kufungia Nanga ya Meli, au Kuizuia Meli isiondoke

Bandarini na kwa wasiojua basi yaani tunazungumzia Kamba ambayo unene wake hua

kama wa inchi mbili mpaka tatu.

Hivyo Wenye Lugha yao basi hua wanaziita Kamba zenye Unene huo kua ni Jumal yaani

Kamba Nene iliyopatikana kutokana na kuzongwa pamoja kwa Kujumuishwa kamba

mbili mpaka tatu.

Kwa hivyo kama tukichukulia mfano wa kua Ngamia hawezi Kupenya kwenye Tundu

ya Sindano kwa sababu hilo si Jambo la kawaida, basi Wanazuoni wamesema kua

unaweza ukatafsiri neno Jamal kua ni Jumal kutokana na kua Kamba au Uzi hua una

maumbile ya Kuingia Kwenye tundu ya Sindano au Shazia.

Lakini jee hata hii kamba ya kuzulia Meli Bandarini itaweza kupenya kwenye Tunu ya

Sindano? Kwani Jambo hilo ni Jambo lisilowezekana kamwe kutokea.

Kisha baada ya kusema Maneno ya aya hii ya Surat Al Aaraf 7:40 basi Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akaendelea kusema kua: Kisha Allah Subhanah wa Ta'ala


955

atasema : Muandikieni Mja wangu ndani ya Kitabu cha Sijjin chini Kabisa ya

Ardhi

Na kisha Mrudisheni Ardhini kwani kwa hakika Nimewaumba Kutokana nayo, na

Ndani yake nitawarudisha na Kutokana nayo nitawafufua tena Kisha Roho ya Mtu

huyo itavurumishwa Ardhini kisha Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasoma

aya ifuatayo:

‏﴿حُنَفَآءَ‏ هلل َِّ‏ غَيْرَ‏ مُشْرِكِينَ‏ بِهِ‏ وَمَن يُشْرِكْ‏ بِٱهلل َِّ‏ فَكَأَنم ََّا خَر َّ مِنَ‏ ٱلس َّمَآءِ‏ فَتَ‏ خْطَفُهُ‏

ٱلط َّيْرُ‏ أَوْ‏ تَهْوِى بِهِ‏ ٱلرِّيحُ‏ فىِ‏ مَكَانٍ‏ سَحِ‏ يقٍ‏ ﴾

Hunafaa lillahi ghayra mushrikeena bihi waman yushrik biAllahi fakaannama

kharra mina alssama-i fatakhtafuhu alttayru aw tahwee bihi alrreehu fee makanin

saheeqin(Surat Al Hajj 22:31)

Tafsir: Na Wenye Kumshirikisha Allah Basi hua Kama alieanguka Kutoka Mbinguni

Kisha Akanyakuliwa na Ndege (kama anavyonyakua Eagle) Au Akapeperushwa na

Upepo katika sehemu ya Mbali Kabisa (Na hivyo kutojulikana ameangukia wapi, na

ana hali gani kama mzima au amekufa)

Kwani aya hii tumeshaitafsiri tulipozungumzia aina za upepo ndani ya Qur'an katika

juzuu ya kwanza ya Kitabu hiki ambapo tulisema kua Qur'an inapozungumzia Upepo

Katika Hali ya Umoja yaani Rihan basi hua ni Upepo wa Adhabu.

Na inapozungumzia Upepo Katika Hali ya wingi yaani Riyah basi hua ni Upepo wa

Rehma, ambapo hapa tunaona kua Aya imezungumzia Hali ya Umoja ya Upepo...yaani

Upepo wa Rihu

Ambapo ili kuujua Upepo huu basi Tukumbuke yaliyowakuta watu wa Nabii Hud, ambao

tulisema kua Walipigwa na Upepo wa hali ya Umoja wa Rihan wa Adhabu ambao

Ukikupiga Tumboni basi unatokea Upande wa Piki na Kuunguza kila kitu ndani ya tumbo

lako na kuacha Mifupa mitupu Unakua Kama Bua

Hivyo hii ndio hali ambayo Roho ya Mtu Muasi kwa Mola wake Itakutana nayo katika

kushushwa kwake Ardhini, yaani itapata kama ya Adhabu ya Watu wa Nabii Hud au

itakutana na hali ya kua Kama Mtu anaeanguka Kutoka Juu Angani kisha akanyakuliwa

na Kucha za Eagle (Tai) na kisha kunyofolewa nyofolewa na Mdomo wa Tai


956

Naam..hivyo Al Baraa Radhi Allahu Anhu anaendelea kutuambia kua Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam aliendelea kusema baada ya Roho ya mtu Muovu kukataliwa

kufunguliwa Milango ya Pepo na Kuamrishwa kurudishwa Chini Ardhini kua:

Roho hio Inarudishwa ndani ya Mwili wake Mtu muovu huyo, na kisha anatokewa na

Malaika Wawili ambao wanamkalisha kitako kisha wanaanza kumhoji kwa kusema: ‘Jee

ni Nani wewe Mola wako? Na atasema Sijui Ataulizwa Jee ni Ipi Dini yako?’

Nae atasema: ‘Sijui’

Kisha Itasikika Sauti Kutoka Mbinguni ambayo itanadia kwa kusema: ‘Mtayarishieni

kwa ajili yake Kitanda cha Motoni, Na kisha Mvalisheni Mavazi ya Motoni, na

Mfungulieni Mlango wa Motoni’ Kisha baada ya hapo Unamjia Mvuke Wa Moto wa

Jahannam na Kaburi lake linaanza Kubana na kubana hadi Mifupa ya Mbavu zake

zinaanza Kuvaana.

Kisha anakuja mbele yake Mtu Mwenye Sura Mbaya Sana, na Nguo Mbovu Mbaya Sana

hukua akiwa amejawa na Harufu Mbaya isiokua na mfano wake, ambae atasema ‘Pokea

Bashirio la Habari Mbaya Kabisa, Kua hii ndio Siku Ambayo mliahidiwa kua

Itafika’

Hivyo Maiti huyo atauliza kwa kusema: ‘Wewe Ndio Ndani, Mbona Uso wako ni Uso

ambao Umebeba Mambo Mabaya Maovu sana?’

Mtu huyo Mwenye Sura Mbaya aliemtokea Maiti huyo Muovu anaeulizwa nae atajibu:

‘Mimi Ndio Uovu wa Amali zako!’

Maiti hio itasema: ‘Ya Rabb! Usiiharakishe Siku ya Malipo! Usiijalie Kuja Siku ya

Malipo’ (Musnad Imam Ahmad).

Ambapo Hadithi hii iliyopokewa na Al Baraa Radhi Allahu Anhu inatuonesha kua Wale

watu watakao kua ni wenye kutii Maamrisho ya Allah Subhanah wa Ta'ala na hivyo kua

ni Waja wema basi ingawa Watakua na hali ya Maumivu katika Wakati wa kutolewa

Roho, lakini hapo hapo Watakua wanatolewa kwa Huruma huku waliombewa dua na

Mamilioni ya Malaika.

Kiasi ya Kitakachofuatia baada ya Kutolewa Roho yake basi itakua ni hali ya kua katika

Mazingira ya Raha na Utulivu kwani itakua ni yenye kuingizwa kwenye Mazingira ya

Peponi, kiasi ya kua Roho ya Mtu huyo atajuta kwanini hakua ni mwenye kufanya Mema

zaid hapo kabla alipokua Duniani.


957

Na Akirudishwa Kaburini ambalo ingawa litatanuka na kua na Mapana ya Mbingu na

Ardhi, lakini hatotosheka na hivyo kuomba kwa Mola wake kua Siku ya Malipo

iharakishwe, kwani anahamu aone Malipo yake na Pepo yake.

Kwani kwa upande mwengine basi tunaona kua sehemu ya pili ya Hadithi hii

inawazungumzia wale Wenye Kukadhibisha Dini na Siku ya Malipo. Na matokeo yake

katika siku ya kitolewa Roho watu hao basi watakua ni wenye kuonja Uchungu wa

Kutolewa Roho mara 100 zaidi ya Watu Wema.

Kwani Watu waovu hawa Watatolewa Roho bila ya huruma, huku Wakilaaaniwa na

Mamilioni ya Malaika, na Huyo Mtoaji mwenye nae anatoa kwa Hasira. Hapa tuchukulie

Mfano Mdogo ambao si chochote si lolote.

Ambao ni Mfano wa Mtu anaeumwa na Jino kisha akaenda kung'olewa Jino kwa

Kupigwa Sindano ya Ganzi kwanza na Daktari Mzuri anaependeza na kisha Unapewa

Kilo ya Dhahabu kwa Jino hilo..na kisha anaambiwa kuna Mlima wa Dhahabu katika

siku ya Malipo kwa ajili yake

Naam huu ni Mfano wa kutolewa Roho na kuingizwa Kaburini kwa Mja mwema..Atakua

anaomba kua Siku ya Malipo Ifike haraka ili apate na Huo Mlima wa Dhahabu kutoka

kwa Mola wake

Halafu Mtu Mwengine kuenda kung'olewa na Mtu anaetisha sana tena hana sindano ya

Ganzi na anakung'oa kwa Nyundo na Patasi, na kisha baada ya hapo kuna Watakao

kushindikiza kwa Mijeledi hadi Rumande baada ya kutoa Jino

Huku akijua kua Adhabu zinazomsubiri Rumande basi si chochote si lolote ukilinganisha

na Adhabu ya Jela ya Kutumbukizwa kwenye Shimo la Moto wa Milele unaomsubiri

katika siku ya Malipo

Hivyo mtu huyo atakua anaomba kua Hio Siku ya Kuhukumiwa kwa ajili ya Kuenda Jela

ya Shimo La Moto kua isifike, kwani bora kupata hio Mijeledi na Mvuke wa Moto kuliko

Moto wenyewe

Naam.. Hio ndio hali ya Mtu Muovu anaemuasi Mola wake na kukadhibisha kuwepo kwa

siku ya Malipo ambapo amesema Umm Ul Muuminina Aisha Radhi Allahu Anha kua:

‘Alikuja Mwanamke Mmoja wa Kiyahudi Mlangoni kwangu akaniomba Chakula

huku akisema: ‘Nisaidie Chakula, Allah atakuhifadhi na Mtihani wa Dajjal na

Mtihani wa Adhabu ya Kaburi’


958

Aisha Radhi Allahu Anha anaendelea kusema kua: Hivyo Nami nikaendelea kumfanya

awe ni Mwenye kuzungumza hadi akatokea Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kisha

nikasema: ‘Ya Rasul Allah, Hivi Huyu Mwanamke anazungumzia kuhusiana na

nini? Hivi anavyosema kua Allah Akuhifadhi na Mtihani wa Dajjal na Mtihani wa

Adhabu ya Kaburi?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akanyanyua Mikono yake juu na kisha akaomba

Dua ya kupata Hifadhi ya Fitna ya Dajjal na Fitna ya Adhabu ya Kaburi, kisha akasema:

‘Ama kuhusiana na Fitna ya Dajjal basi hakuna Mtume isipokua alikua ni mwenye

kuwausia watu wake kutokana nae Lakini mimi nitakuambieni kitu ambacho

hakuna Mtume aliewaambia watu wake: Ambacho ni kua Dajjal ni mwenye Jicho

Moja, na Allah si mwenye Jicho Moja, Dajjal ana maandishi kwenye Paji lake la

Uso yasemayo Kaffir ambayo kila Muumini atayasoma’

Ama kuhusiana na Mtihani wa Adhabu…basi Maiti hio itaulizwa: ‘Jee ni kipi kile

ambacho ulikua ukisema kuhusiana na Uislam? Jee ni mtu gani alikua ni Miongoni

mwenu? Nae atasema Muhammad ni Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam ambae

ndie alieleta vithibitisho dhahir kuhusiana na Allah Subhanah wa Ta'ala na sisi

tukamuamini.’

Kisha baada ya hapo Litafunguliwa Shimo ambalo ndani yake ataona Moto ambao

sehemu yake moja inaiunguza sehemu nyengine na kisha ataambiwa: ‘Angalia kile

Ambacho Allah amekuepusha Nacho!’

Na kisha atafunguliwa Shimo Jengine ambapo ndani yake ataiona Pepo na Mapambo

yake yote na kisha ataambiwa, Haya ndio Makazo yake Ataambiwa tena: ‘Hakika wewe

ulikua na Imani Thabiti na utafufuliwa na Imani Thabiti Inshaa Allah,’

Na kama atakuwa ni Mja Muovu basi atakalishwa kitako kwenye Kaburi huku akiwa na

khofu na wasi wasi, na kisha ataulizwa. ‘Jee ulikua ukisema nini?’

Nae atasema: ‘Mimi nilikua nikisikia watu wakisema kadhaa w kadhaa hivyo na

mimi nikasema hivyo hivyo’

Hivyo shimo litafunguliwa ambalo ndani yake ataona Pepo na Mapambo take na kisha

ataambiwa: ‘Angalia kile ambacho Allah Subhanah wa Ta'ala amekukosesha!’

Kisha atafunguliwa Shimo Jengine na ataoneshwa Moto ambao sehemu yake moja

inaiunguza sehemu Nyengine na ataambiwa: ‘Haya ndio Makazi yako ambayo ulikua

ukiyatilia shaka na utaufuliwa, Huku ukiwa na shaka Juu yake na kisha

ataadhibiwa’


959

Naam, hivyo ndivyo hali inavyokua Ndani ya Qaburi na ndio maana Amr Ibn Al Aas

Radhi Allahu Anhu akasema kua: ‘Baada ya kunizika basi Msioondoke, tumieni mda

kiasi kama wa kuchinja Ngamia na Kumtawanya Nyama yake, ili niwe na utulivu

kutokana na kuwepo kwenu, hadi pale nitakapoona nitawajibu vipi Wajumbe wa

Mola wangu.’

Hivyo hii ni kuhusiana na hali Kaburi ambalo hua ni neno lenye kutokana na neno

Qabara ambalo kwa Kilugha bua linamaamisha Kuzika Maiti, Neno Qabara ndio

lililotoa neno Aqabara ambalo hua linamaanisha Kusababisha Mtu Kuzikwa, Kua na

Siku Mbaya iliyojaa Huzuni

Na pia neno Qabara ndio lililotoa neno Qabur ambalo hua linamaanisha Kaburi, au hali

ya Roho wakati inapotoka baada ya Kufariki mtu hadi katika siku ya Kufufuliwa.

Ambapo hali ya Qabur hua pia inajulikana kama Barzakh Kwani neno Qabur hua pia

linamaanisha neno Barzakh kwa sababu neno Barzakh hua linamaanisha Kizuizi, Kitu

kinachotengenisha baina ya vitu viwili.

Na hivyo Barzakh hua ni Hali Baina ya Kuishi kwa Roho baina ya hali za Maisha Mawili

tofauti. Ambapo hali ya kwanza hua ni ya Maisha ya Mpito ya Kidunia na hali ya pili ni

ya Maisha ya Milele ya Kiakhera.

Hivyo tunapozungumzia kuhusiana na Qabur au Barzakh basi hua tunazungumzia hali

ya 4 kati ya 5 za Maisha ya Viumbe Ibn Adam ambazo ni:

Ambapo hali ya kwanza hua ni ile ya kua Ndani ya Kiza cha Mapazia ya kuwemo

ndani ya Sehemu za Siri za Wazee wetu kwa miaka na miaka kutoka kizazi mpaka

kizazi.

Hali ya pili hua ni hali ya Kutoka kwenye Sehemu za Siri za Baba na Kuanza Kuishi

Ndani ya Kiza ndani ya Fuko la Uzazi la Mama, Fuko la Uzazi la Mama ambalo Ibn

Adam hua katika Hali ya Ndani ya Kiza cha Matabaka Matatu, Ambayo ni Ndani

ya Fuko la Uzazi, liliomo ndani ya Sehemu ya Kizazi kilichomo ndani ya Tumbo la

Mama.

Hali ya 3 hua ni Pale unapotoka katika katika Tumbo la Mama baada ya kuzaliwa

na kuanza Maisha ya Kuishi Duniani Mpaka Kufariki kwa Mtu Husika Na Hali ya

4 hua ni Maisha ya Barzakh au ya Qabur ambayo huanzia mara baada ya Kufariki

na kuendelea hado siku ya Kufufuliwa.

Na Hali ya 5 hua ndio hali inayoanza baada ya kufufliwa katika Siku ya Malipo

Kwani hali zote hizo hua ni za Mpito isipokua hali ya Mwisho ambayo ni hali ya


960

baada ya kufufuliwa kwa ajili ya kuhesabiwa Amali zetu Ambayo hii hua ni hali ya

Milele.

Ambapo katika hali zote hizi basi hali ya kwanza hua ni Hali ya Maumbile ya baada ya

Kiapo na Ahadi ya Kubeba Amanah mbele ya Muumba hadi ndani ya sehemu za Siri za

Baba. Hali ya pili ni hali ya Ndani ya Kizazi cha Mama kwa ajili ya Matayarisho ya

kutimiza Ahadi na Kiapo tulichokila kama tulivyoona hapo kabla. Hali ya tatu ni hali ya

Duniani ya Utekelezaji wa Amana na Utimizaji wa Ahadi na Mitihani ndani yake. Kwani

Hali hizi tatu za Mwanzo hua ni kama hali za Kua katika Ndoto.

Na ndio maana akasema Hujjati Ul Islam Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad

Al Ghazali kua: ‘Watu wote hua ni wenye kulala na kuota Hapa Ulimwenguni hadi

watakapoingia Makaburini ndio hua ni wenye kuamka na Kuuona Uhalisia

Isipokua wale wenye Taqwa ndio hua si wenye Kua Usingizini’

Ambapo hii inawekwa wazi na Surat At Takathur pale iliposema:

‏﴿بِسْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞أَلهَْاكُ‏ مُ‏ ٱلت َّك َّاثُرُ‏ ‏۞حَتى َّ ٰ زُرْتمُُ‏ ٱلْمَقَ‏ ابِرَ۞كَلا َّ سَوْفَ‏

تَعْلَمُونَ۞ثمُ َّ كَ‏ لا َّ سَ‏ وْ‏ فَ‏ تَعْلَمُ‏ ونَ‏ ‏۞كَلا َّ لَوْ‏ تَعْلَمُونَ‏ عِلْمَ‏ ٱلْيَقِينِ۞لَتَرَوُ‏ َّن

ٱلجَْحِ‏ يمَ۞ثمُ َّ لَتَرَوُن َّهَا عَينَْ‏ ٱلْيَقِينِ۞ثمُ َّ لَتُسْأَلُن َّ يَوْمَئِذٍ‏ عَنِ‏ ٱلن َّ عِيمِ‏ ﴾

Bismi Allahi alrrahmani alrraheemi; Alhakumu alttakathuru; Hatta zurtumu

almaqabira; Kalla sawfa taAAlamoona; Thumma kalla sawfa taAAlamoona; Kalla

law taAAlamoona AAilma alyaqeeni; Latarawunna aljaheema; Thumma

latarawunnaha AAayna alyaqeeni; Thumma latus-alunna yawma-dthin AAani

alnnaAAeemi(Surat At Takathur 102:1-8)

Tafsir: Kwa jina la Allah Mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma, Ushindani wa

kukusanya Mapambo ya Kidunia unakutoeni kwenye Malengo ya kiakhera, hadi pale

mtakapotembelea na kuingia Makaburini, Lakini baada yake Mtakuja kujua, Kisha

baada yake mtakuja kujua, Kama mngejua kwa Ilm ya Yaqini, basi wa hakika

Mngeuona Moto Mkali, Kisha Mtaona kwa Mtizamo wa Jicho la Yaqini, Kisha katika

siku hio mtaulizwa kuhusiana na Neema mlizopewa.

Ambapo tunaona kua Sura hii inatuwekea wazi kuhusiana madhara ya kukumbatia

mapambo ya kidunia na kukusanya Mali kunakowapelekea watu kuisahau Akhera na


961

kuhusiana na kuulizwa juu ya Mali tulizochuma, ambapo amesema: ‘Abd Allah Ibn

Habib kua kutoka kwa Baba yake, kuptia kwa Mjomba wake kua: ‘Siku moja Rasul

Allah Salallahu A’layh wa Salam alitoka nje huku akiwa ameroa maji kwenye

nywele zake huku kiwa na uchangamfu kwenye Uso wake, hivyo nasi tukasema kua:

‘Tunakuona kua una muonekano wa Furaha ya Rasul Allah!’.

Rasul Allah Salallahu A’layh wa Salam akasema: ‘Naam’ kisha akakaa pamoja nasi

na kutufahamisha kuhusiana na Neema za Allah Subhanah wa Ta’ala, kisha

akamalizia kwa kusema: ‘Mali hua haina madhara kwa yule ambae ni mwenye kua

na Taqwa, lakini Afya njema hua ni bora kuliko mali kwa yule mwenye kumuogopa

Allah Subhanah wa Ta’la. Na uchangamfu hua ni Neema’(Musnad Imam Ahmad Ibn

Hanbal)

Naam, hii ni kwa sababu mtu anapokua Mcha Mungu basi hua ni mweye kutafakkar sana

kuhusiana na hali hii ya nne ya Maisha ya kuingia Kaburini baada ya Kufa na ya tano

baada ya Kufufuliwa hua ni Hali ambazo ni za Uhalisia, ambazo hua zenye kuonekana

kwa mtizamo wa Yaqini kwani kila kitu kinakua wazi kutokana na kupata Ufunuo na

hivyo kua ni mwenye kuona bila ya kuwepo kwa Pazia la macho au mara baada ya

kuingia kwenye Barzakh hadi katika Siku ya Malipo kwa ajili ya kulipwa kutokana na

tuliyoyafanya.

Ambapo tunapoangalia kuhusiana na Ilm Al Yaqin na Ayn Al Yaqin basi anasema Shaykh

Muhammad Al Naquib Ibn Ali al Attas ambae ni Mwanzuoni wa Kiislam kutoka

Malaysia kua: ‘Hikma hua ni Ilm lakini si Kila I’lm hua ni Hikma’ yaani baadhi ya

wakati hua kile ambacho hua kinachukuliwa kua ni Ilm hua si chengine bali hua ni

Ufaham wa Mtu kutokana na Kutafakkari kwake, hivyo kila mtu anavyotafakkari

zaidi basi hua ni mwenye kupata vithibitisho zaidi na hivyo hua ni mwenye kua na

Hikma zaidi. Na hivyo basi Hikma hua ni hitimisho linalotokana na Tafakkur ya

Mtu. Na hii ndio hua ile ambayo Qur’an imeizungumzia kua ni Ilm Al Yaqin, Ayn

Al Yaqin na Haq al Yaqin.

Hivyo tofauti baina ya Hikma na Ilm hua ni katika Upana wa Ufaham wa Mtu husika.

Kwa maana hio basi bila ya shaka haitowezekana Kujua uhalisia wa Barzakh had pale

tutakapokaa na kua ni wenye Kutafakkari Uhalisia halisi wa Jambo hili, ambalo haliwezi

kufahamka kiufaham wakati ukiwa hai hapa Duniani hadi pale utakapokua na Ilm na

Hikma au baada ya kuondolewa pazia la macho baada ya kuinga Kaburini kwenye hatua

ya nne ya Maisha.

Hivyo tuamshane tusizinzie na Kulala ili tuamke kabla hatujaamshwa na Mauti kwa

kuangala maana ya neno Umm ambalo hua linamaanisha Mama, Chanzo, Kanuni, Asili,

Mwanzo, Mfano au Kigezo cha asili. Kwani nalo pia linahusika katika kuifafanua hali ya


962

kile kinachotokea baada ya Mtu Kutolewa Roho yake Ambapo anasema Allah Subhanah

wa Ta'ala katika Surat Al Qaria katika aya zilizotumia neno Umm kua:

‏﴿وَأَم َّا مَنْ‏ خَ‏ ف َّتْ‏ مَوَازِينُهُ۞فَأُم ُّهُ‏ هَاوِيَةٌ۞وَمَآ أَدْرَاكَ‏ مَا هِيَهْ۞َرٌ‏ حَ‏ امِيَةٌ‏ ﴾

Waamma man khaffat mawazeenuhu; Faommuhu hawiyatun; Wama adraka ma

hiyah; Narun hamiyatun (Surat Al Qaria 101:8-11)

Tafsir: Ama Kwa Yule Ambae itakua Hafifu Mezani yake (ya Amali Njema) Basi

Mama yake (atakua) ni Hawiyah. Na Nini Kitakacho kujuulisha ni nini hio (Hawiya)?

(Ni) Moto Mkali Sana

Naam...aya zinatuonesha kua: Yeyote yule atakaekua ni mwenye kufanya maovu mengi

zaid kuliko mema na hivyo mema yake kua ni kidogo basi atakapoingia Kaburini Mama

yake atakua ni Moto wa Hawiya

Na bila ya shaka sisi sote ni wenye kujua kua Kimaumbile Jukumu la Mama hua ni

Kumlea Mtoto wake tangu Mwanzoni anapobeba Ujauzito ndani ya Tumbo lake mpaka

kumtoa mtoto huyo nje ya Tumbo lake na kumlea hadi kua mkubwa na pia kamaa kuna

majaaliwa basi hadi kufa kwake. Yaani siku zote Mtu hata awe na miaka 100 basi kama

Mama yake yuko hai basi Mtu huyo hua ni Mtoto kwa Mama yake, na Mama hua ni

Mama kwa Mtoto wake hachoki kumjalia na kumsimamia.

Sasa Aya zinatuambia kua Kama Mizani ya Mema yako itakua Nyepesi zaidi ya Maovu

yako basi na wewe Mara tu utakapotolewa Roho Utakua ni Mwenye Kulelewa na Mama

yako, ambae ni Moto wa Jahannam yaani hutotoka ndani yake!

Ambapo anasema Imam Muhammad Ibn Jariri At Tabari kua: ‘Amesema Abu Hurayra

Radhi Allahu Anhu kua: Amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua:

Wakati Muumini anapofariki, basi Malaika wa Rehma humjia na Nguo za Hariri

na kumwambia: ‘Njoo ewe Roho kwa Allah Subhanah wa Ta'ala, na hivyo Roho hio

hutoka huku ikiwa inanukia kwa harufu ya Miski nzuri kabisa

Na kisha Malaika hupokezana Roho hio huku wakiinusa hadi katika Mbingu ya

kwanza, na kuambiana ‘Hakika inanukia harufu Nzuri Sana kutoka Duniani’ Roho

hio hupandishwa Juu Mbingu baada ya Mbingu na kujumuishwa na Roho za

Waumini wengine, Ambapo Roho za Waumini hao wengine hufurahia kukutakana

na Roho hio na Kuikaribisha kwa Furaha zaid ya anavyokaribishwa Mtu aliekua

hayupo kwa mda Mrefu pale anaporudi Nyumbani.


963

Kisha Roho hizo zilizoikaribisha Roho hio Huiuliza Roho hio iliyowasili kwa

kusema: ‘Ni nini Kimetokea Kwa Fulani Ibn Fulani?’

Hapo Malaika husema: ‘Iwacheni Ipimzike (Kwanza hii Roho) Kwani Imechoka

kutokana na ya Duniani’

Kisha Roho hio husema (Kujibu kuhusiana na hio Roho ya fulani alieuliziwa na

Roho hizo za Peponi) kua ‘(Fulani Ibn Fulani) Amekufa Hivi Hajaja Huku kwenu?’

Ambapo hapa Malaika hua ni wenye kujibu Suali hio kwa kusema kua:

‘Faommuhu hawiyatun’ yaani Huku Peponi hajaja kwa sababu ameenda kwa

Mama yake Mlezi atakaemlea ambae ni Shimo la Moto Mkali sana.

Ambapo Kwa Upande wa Imam Qatadah Al Sadusi basi yeye anasema kua: ‘Maneno

Faommuhu hawiyatun yanamaanisha kua Mtu huyo atatumbukia kwenye Shimo

hilo la Motoni Kichwa kichwa’ na hivyo aya kua ni zenye kutukumbusha Umuhimu

wa Kuzidisha kufanya Mema kabla hatujaingia Kaburini!’

Kwani alisema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kaburi hua linabana na

kama kuna Mtu ambae ataweza kuepukana na m-bano wa Kaburi basi ni Saad Ibn

Muadh.’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alisema hivyo kuhusiana na Saad Ibn

Muadh Radhi Allahu Anhu kwa sababu alikua ni Chifu wa Kabila la Banu Aws la Watu

wa Madinah .

Saad Ibn Muadh Radhi Allahu Anhu alisilimu wakati akiwa na Umri wa miaka 31 baada

ya kusikia Ujumbe wa Allah Subhanah wa Ta'ala kutoka kwa Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kupitia kwa Balozi wa kwanza kumuwakilisha Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam katika Mji wa Madinah ambae ni Musab Ibn Umayr Radhi Allahu Anhu

ambae alikua anakaa katika Nyumba ya Asad Ibn Dhurara Radhi Allahu Anhu ambae

alkua ni Mtoto wa Dada yake Saad Ibn Muadh Radhi Allahu Anhu.

Hivyo Waislam walipohamia Madinah basi Kabila la Saad Ibn Muadh Radhi Allahu

Anhu lilijitolea kwa kila kitu na kuwakaribisha Waislam hao katika Majumba yao ya

Banu Ashshal bila ya kujisifu wala kujiona wala kuweka mipaka kwa ajili ya Waislam

hao waliohama kutoka Makkah kuelekea Madinah .

Ambapo katika Vita vya Badr baada ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

kukusanya Jeshi lake la watu wa Makkah basi alipomuuliza Saad Ibn Muadh Radhi Allah


964

Anhu kama Watu wa Madinah wako tayari kupigana pamoja nao katika vita hivyo

ambapo Saad Ibn Muadh Radhi Allahu Anhu akasimama na kusema:

‘Ya Rasul Allah! Hakika sisi Tunakuamini wewe kikamilifu na tunashuhudia kua

Ujumbe wako ni wa Haki. Tunaapa na kuahidi kua sisi tuko Pamoja nawe kayika

kila kitu, hivyo qmua unaloamua na sisi tutafuata na kusimama ubavuni mwako.

Tunaapa kwa Jina la Allah Subhanah wa Ta'ala kua, ukienda Kwenye Bahari

pamoja nasi na kuvuka basi nasi tutavuka pamoja nawe, hakuna hata mmoja kati

ya Watu wangu atakaebakia bila kukufuata. Hivyo kwa hakika Sisi tuko Pamoja

nawe kupigana vita dhidi ya Maadui zetu Kesho kwani Tunahamu nao

Kupigana nao na tunahamu ya kukutana na Mola wetu, na tuna matumaini kua

Allah Subhanah wa Ta'ala atatuwezesha sisi kua ni wenye Kufanya kile ambacho

kitakufanya Ujivune kutokana nasi, Hivyo ya Rasul Allah! Panga unavyopanga

hakika sisi tuko pamoja nawe’

Kwani majibu haya ya Sad Ibn Muadh Radhi Allahu Anhu yaliusababishia Uso mtukufu

wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua ni Wenye Kung'ara kwa Furaha na hivyo

akasema: ‘Sherehekeni kwani Allah Subhanah wa Ta'ala ameniahidi mimi sehemu

moja kati ya sehemu mbili za Maaduni zetu.(Msafara wao au Jeshi lao) Wallahi

nnakaribia kuona mimi kwa macho katika kila sehemu ambayo utalala mwili wa

Maiti wa maadui zetu’

Saad Ibn Muadh Radhi Allahu Anhu alifariki miaka 7 baadae katika Vita vya Khandaq

kutokana na Majeraha baada ya kushabuliwa kwa upinde kadhaa kwenye mwili wake, na

hivyo alipokua kumwa basi akawa ni mwenye kusema kua: ‘Ya Allah! Kama mapigano

ya vita hivi dhidi ya Quraysh yataendelea zaid, basi usiniwache mimi nikabaki hivi

bila ya kuendelea kupigana nao. Kwani kwa hakika kwangu mimi hakuna kitu

nnachokipenda zaidi kuliko kuigana na Watu wanaotaka kumdhuru Mtume wako

Salallahu Alayhi wa Salam, kutokana na kutomuamini kwao hadi kufikia

kumfukuza katika ardhi ya kwao. Lakini kama mapigano yamemalizika basi

yasababishie majeraha yangu kusafisha njia ya kuupata Ushahidi. Ya Allah

nakuomba usinasababishie mimi kufariki kabla ya kulipiza dhidi ya Banu

Qurayza.’

Wakati akiwa bado yuko taabani kitandani akiendelea kuuguza majeraha basi

alitembelewa na Rasul Allah Salallahu Alayhi Wa Salam ambae alikichukua kichwa cha

Saad Ibn Muadh Radhi Allahu Anhu na kukiweka kwenye mapaja yake, kisha Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akaomba dua kwa kusema: ‘Ya Allah! Saad amejitahidi


965

kwa ajili yako, Saad amemuamini Mtume wako na amefanya jitihada zote kwa ajili

yake, hivyo tafadhali ipokee Roho yake kwa mapokeo yaliyo mema.’

Maneno haya ya Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam yalikua kama ni utulivu wa

Macho ya Roho ya Saad Ibn Muadh Radhi Allahu Anhu ambayo ilikua ni yenye kutoka

ndani ya Mwili wake, huku akijaribu kufumbua macho yake kumuangalia kwa mtizamo

wa Mwisho kipenzi chake kiliopo mbele yake ambae ni Rasul Allah Salallahu Alyhi wa

Salam na kisha Saad Ibn Muadh Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Ya Rasul Allah Hakika

mimi nnashuhudia kua wewe ni Rasul Allah.’

Ambapo alisema Abu Said Al Hudri Radhi Allahu Anhu kua: Hakika mimi nilikua ni

mmoja kato ya Waliochimba Kaburi la Saad Ibn Muadh ambapo kila tukichimba

basi Ardhini ilikua ikitoka Harufu nzuri ya Miski hadi kwenye Mwana wa Ndani.

Na akasema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Arshi ya Allah Subhanah wa

Ta'ala imetikisika kutokana na Kifo cha Saad Ibn Muadh.’

Turudi tena katika kisa cha Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu kupitia katika Hii ndoto

yake, aliyoiota kua yuko kwenye sehemu inayobana na yenye kiza kikubwa sana lakini

mbele yake kuna sehemu yenye Muangaza, akajihisia kua kuna ulazima wa kujitoa

kwenye kizo hicho na akafanya jitihada hadi akafanikiwa kutoka kwenye kiza hizo na

sehemu hio inayombana, na tunazungumzia kuhusiana na Ndoto kwa sababu kila mmoja

wetu ni Mwenye kujua kuhusiana na Ndoto, ambapo hua unaweza kua Umelala kwenye

Kitanda chako cha Kingsize 8x8 lakini Ukaota uko Mwituni unafukuzwa na Joka Au

Chui, Au Unazama Baharini au Uko Shimoni na kua na hali ambayo isiyoelezeka

kutokana na Khofu na Tafrani ziliomo ndani ya Ndoto hio ambayo unaota huku ukiwa

Chumbani Mwako na Kitandani Mwako Pembeni ya Mkeo au Mume wako na ukamshtua

kutokana na Kelele au Mateke yako ndani ya Ndoto zako. Ambapo Athari zake

zinavyoitokeza basi huenda ukapiga Kelele: Nisaidie Nakufa!

Hivyo Mwenza wako alie pembeni yako akakutuliza na Kusema: ‘Ya Albi! (Ewe Moyo

wangu) Usiwe na Khofu kwani uko kwenye Jinamizi Unaota Sauti hio na Utulizo

wake ndio hua Salama yako!’

Ambapo tumeona kua amesema Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kaburi

hua linabana na kama kuna Mtu ambae ataweza kuepukana na m-bano wa Kaburi

basi ni Saad Ibn Muadh.’

Hivyo kama hali inavyokua wakati unapoona Jinamizi kwenye Kitanda cha kingsize

chako basi ndio hivyo hivyo hali Inavyokua wakati unapokua Umefariki. Yaani Wakati

unapokua Maiti, basi Uwe Kaburini, Uwe kwenye Chumba kilichosakafiwa na kigae, iwe


966

kwenye Sanduku la Dhahabu, Uwe kwenye Tumbo la Nyangumi, Au Umeunguzwa na

kua Jivu, basi Ukishafariki na Kuingia kwenye Barzakh basi wewe mbele ya Mola wako

hua Unahesabiwa kua Uko Kaburini.

Na utajikuta Kaburini na kupatwa na Adhabu kama za walio kaburini, kama vile ambavyo

unapokua unaota uko Mwituni unakimbia, au umetumbukia Shimoni mna Nyoka, wakati

Uko Kitandani, tofauti ni kua badala ya kua Unaota, basi Kaburini hua Huoti bli uko

katika hali ya uhalisia wa mazingira ya Kiroho, kwani ndio hali mpya ya Maisha yako ya

Barzakh, na unapatwa na Maumivu na kila kiumbe hua anasikia Kelele na Vilio

vitokanavyo na Maumivu yako, isipokua Majini na Ibn Adam wenzako ambao wao

hawakusikii kwani Mola wako ameyawekea pazia Masikio yao, ili waendelee na Maisha

yao!

Allah atustiri hapa Juu ya Ardhi, Na Ndani ya Ardhi na Katika Siku ya Kutoka Ndani ya

Ardhi...Allahuma Amiin!

Kwani amesema Al Muhaqiq Al Imam Shihab Ad Din Abu Al Abbas Ahmad Ibn

Muhammad Ibn Ali Ibn Hajjar Al Haytami Al Maki Al Ansari Al Shafii kua: ‘Amesema

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kua: Wakati Maiti inaingizwa Kaburini basi

Kaburi hua ni Lenye Kumuuliza Maiti huyo kwa kusema: ‘Ole wako ewe Ibn

Adam! Hivi ni Kitu Gani kilichokufanya wewe Usitafakari kuhusiana nami?’

Hivi Jee Hukujua wewe Kua mimi ni Nyumba ya Mitihani? Kua mimi ni Nyumba

ya Kiza?

Nyumba ya Upweke na Mafunza? Ni Kitu gani kilichokughafilisha Nami?’ Ulikua

Ukinipita Juu yangu kwa Kudunda na Maringo.’

Hivyo kama Maiti ya Mtu huyo ni ya Mtu mwema basi Maiti itasikia Sauti nyengine

Ikisema Kuliambia Kaburi: ‘Hivi Hukuona wewe Kua huyu Mtu alikua ni Mwenye

Kuamrisha Mema na Kukataza Mabaya?’

Hivyo Kaburi hilo litajibu: ‘Kama ni hivyo basi kwa ajili yake Mtu huyu Mimi

nitabadilika na kua Ardhi Nzuri na ya Kupendeza kwa ajili yake ili Mwili wake

Ubakie katika hali nzuro ya Kunga'ara’

Na Roho yake Ipate Kupaa na Kuelea Juu kwa Allah Subhanah wa Ta'ala (Imam

Ibn Hajar Al Haytami, Imam At Tirmidhii na Imam Abu YaAla)

Hivyo ndivyo hali inavyokua..kwa kila Roho na Mwili wa Ibn Adam na Jini hivyo kama

ni Mtu mwemwa Basi Ardhi ya Kaburi itajibadilisha na Kua Pepo kwa ajili yake. Na


967

kama ni Mtu Muovu basi hali itakua kama Inavyotakiwa tutafakkari kuhusiana na Kaburi

kua ndani yake Mnabana, Mna Kiza, Mna Upweke na Mna Adhabu na Wadudu.

Na akasema Imam Said Ibn Ubaid Ibn Umar Al Layth kua: ‘Hakuna Mtu hata mmoja

atakaekufa Isipokua ataitwa na Kaburi lake ambalo litamnadia kwa kusema:

Hakika mimi Ndio Nyumba ya Huzuni, Ndio Nyumba ya Upweke. Hivyo kama

ulikua ni Mtiifu kwa Allah Subhanah wa Ta’ala katika Uhai wako Duniani basi

Mimi leo Nitakua na Rehma na Huruma kwako. Lakini Kama Ulikua Muasi kwa

Allah Subhanah wa Ta’ala katika Uhai waki Duniani, basi Mimi Ninalipiza Kisasi

Juu yako. Ambapo kwa kila aliekua Mtiifu basi atakua na Raha na Furaha ndani

yangu. Na kwa kile aliekua Muovu basi atakua katika hali ya Maangamizo ndani

yangu.’

Hivyo kila mmoja wetu anatakiwa kujaribu kua Mtiifu kwa Mola wake na pia kuwausia

wenzake na kuwakataza anapowaona wanafanya maovu wakati bado yuko Juu Ardhini

ya kabla hajaingia Ndani ya Ardhi Kaburini. Kwani amesema Imam Said Ibn Jubayr kua:

‘Kuna Ansari Mmoja alikuja kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam huku

akiwa na Uso wenye Huzuni sana. Hivyo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

akamuuliza Ansari huyo kwanini ana huzuni?

Ansari huyo akasema: ‘Ya Rasul Allah hakika mimi nilikua nafikiria Jambo fulani’

Na alipoulizwa ni Jambo Gani, basi nae akasema: ‘Ya Rasul Allah (Salallahu Alayhi

wa Salam) Hakika sisi tuko pamoja nawe Mchana na Jioni hua tunakaa pamoja

nawe. Lakini kesho Akhera wewe Utakua ni mwenye Kukaa pamoja na Mitume

Wenzako, hivyo Sisi hatutokua na uwezo wa Kukufikia wewe Katika sehemu

utakayokuwepo.’

Naam..hili lilikua ni Suali kwa Rasul Allah Salalalhu Alayhi wa Salam ambalo

aliloulizwa na Sahaba ambae ni mwenye hamu ya kutaka kujua Ya Kaburini na Akhera

yake.

Rasul Allah Salallahu Alayh Wa Salam, akawa hana la Kujibu akakaa kimya. Hivyo hapo

hapo Allah Subhanah wa Ta'ala akamtuma Malaika Jibri amshukie Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua anasema Allah Subhanah wa Ta'ala kua:

‏﴿وَمَن يُطِعِ‏ ٱهلل ََّ‏ وَٱلر َّسُولَ‏ فَأُوْلَٰئِكَ‏ مَعَ‏ ٱل َّذِينَ‏ أَنْعَمَ‏ ٱهلل َُّ‏ عَلَيْهِم مِّنَ‏ ٱلن َّبِيِّينَ‏

وَٱلصِّدِّيقِينَ‏ وَٱلش ُّهَدَآءِ‏ وَٱلص َّالحِِينَ‏ وَحَ‏ سُنَ‏ أُولَٰئِكَ‏ رَفِيقاً‏ ﴾


968

Waman yutiAAi Allaha waalrrasoola faola-ika maAAa alladheena anAAama

Allahu AAalayhim mina alnnabiyyeena waalssiddeeqeena waalshshuhada-i

waalssaliheena wahasuna ola-ika rafeeqan(Surat An Nisaa 4:69)

Tafsir: Na Yeyote atakaemtii Allah (Subhanah wa Ta'ala) na Mtume (Salallahu Alayhi

wa Salam) basi Atakua Pamoja na wale Ambao Wameneemeshwa na Allah Juu yao

Miongoni mwa Manabii na Waliosadikisha (Kwa Kukubali kumfuata Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam) Na Mashahidi (Waliokufa Katika Vita vya Jihadi), Na

Waja Wafanyao Mema Na Hawa ni Wabora Miongoni mwa Marafiki.

Hii ni Aya inayobainisha wazi kua Roho za Viumbe Ibn Adam na Majini zitakutana

baada ya Kutoka Duniani na Kuingia Akhera baada ya Kufariki kwa Kiumbe husika

kama vile ambavyo zilivyokua zikikutana wakati watu hao walipokua hai. Yaani Roho

Hukutana na Kuwasiliana katika Mazingira Matatu ambayo ni ya:

Wakati tuko hai kama sasa hivi tunavyokaa na kuishi pamoja hapa Duniani.

Baada ya Kuingia katika Barzakh wakati zinapokua Makaburini.

Katika Siku ya Malipo na baada yake ambapo kila Mmoja atakua na yule

ampendae.

Kwani amesema Amir ul Muuminin Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhua kua: ‘Kulikua

na Waumini wawili ambao walikua ni Marafiki, hivyo mmoja kati yao akafariki,

na alipofika Kaburini na kubashiriwa Pepo basi akamkumbuka Rafiki yake na

kusema: Ya Allah Rafiki yangu Fulani alikua kila siku ananihimiza Kukutii wewe

na Mtume wako Salallahu Alayhi wa Salam. Na alikua akiniamrisha kufanya mema

na kuachana na mabaya.

Hivyo Maiti huyo atamuombea Rafiki yake huyo aliekua hai kua asipotoke na hivyo

akija kufariki basi Roho zao hukutana na kuambiana Mashaa Allah Hakika wewe

ni Rafiki Mzuri sana.

Kwani kwa upande Wasioamini basi anapokufa na kuingizwa Kaburini na kubashiriwa

kuhusiana na Moto, basi hua ni mwenye kumkumbuka Rafiki yake na kusema: ‘Ya Allah

Hakika mimi nna Rafiki yangu Fulani ambae alikua kila siku akinisihi kukuasi

wewe na Mtume wako Salallahu Alayhi wa Salam na kufanya Mambo maovu, na

hakunihimiza kuhusiana na mambo mema’


969

Hivyo Mpotoshe ili nae aadhibiwe kama nitakavyoadhibiwa mie, umkasirikie kama

unavyonikasirikia mie. Hivyo Rafiki huyo Fulani anapofariki basi hukutana na

Rafiki yake Muovu mwenzake na kusema Hakika wewe ni Rafiki Mbaya sana!.

Na ndio maana wakati Bilal Ibn Rabbah Radhi Allahu Anhu alipokua anataka kufariki

basi Mkewe alikua anataka kulia, hivyo Bilal Ibn Rabah Radhi Allahu Anhu akamwambia

Mke wake huyo kua: ‘Hakika mimi nna furaha hivyo Usilie bali furahia kuondoka

kwangu kwa sababu nitakua Pamoja na Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na

Masahaba zake waliotangulia Kabla yangu.’

Ambapo kwa upande wa Imam Said Ibn Al Musayyad basi yeye amesema kua: ‘Hakika

Mtu anapokufa basi hua ni mwenye kupokelewa na Mtoto wake aliefariki, kama

vile ambavyo anavyopokewa anapokua anarudi Nyumbani kutoka Vitani’

Na akasema Imam Abd Allah Ibn Mubarak kua: ‘Amesema Ayub Al Ansari Radhi

Allahu Anhu kua: Amali njema za watu walio hai Hua ni zenye kuwafikia habari

zake Maiti, na hivyo kama wakipata Habari nzuri basi nao hufurahika na wakipata

habari za Uasi basi huhuzunika na kuomba kua Allah amuongoze Mtu huyo.’

Kwani kasema Imam Said Ibn Jubayr kua: ‘Kwa hakika Watu waliofariki hua ni

wenye kupata habari za Watu waliokua hai. Kwani hakuna Mtu ambae Jamaa yake

amefariki na akawa hajapeleka Habari kuhusiana na Watu aliowaacha hai kwa

jamaa zake Waliofariki baada ya kukutana nao Kiroho Akhera’

Naam..na ndio Maana Abu Dardaa Radhi Allahu Anhu alikua akipenda sana kuomba Dua

isemayo: ‘Ya Allah hakika mimi naomba Ulinzi wako kutoka kwa maiti ambao

watawanyafanya Ndugu zangu waliotangulia Akhera kua ni wenye kuona aibu

kuhusiana na mimi.’

Subhana Allah! Sijui kama tunafahamiana ama la! Lakini kama hatujafahamiana basi

tuchukulie Mfano wa Mtu ambae anafiliwa na Ndugu yake wa Karibu, Kisha Mtu huyo

aliekua hai anapolala Usiku anamuota Ndugu yake huyo na kisha Kumpa maelezo kua

Nifanyie hivi na hivi na ukweli ni kua Tunapozungumzia kuhusiana na Ndoto basi

Ukimuota Maiti basi Ujue hua hasemi Uongo.

Hivyo kama kakuamrisha kitu kwenye Ndoto hio basi wajibu wako kukifanya kitu hicho

iwe kwa ajili yake au kwa ajili yako na kama amekukataza kitu basi inabidi uachane

nacho kitu hicho iwe kwa ajili yake au kwa ajili yako.

Na tuangalie mfano wa Imam Sufyan Ibn Uyaynah ambae ni mwalimu wa Mujaddid Ad

Din Imam Al Madhhab Al Shafii Imam Muhammad Idris Al Shafii siku moja alipolala


970

alimuona Mwalimu wake ambae ni Imam Sufyan Al Thawry ambae katika wakati huo

alikua ameshafariki na hivyo akamuuliza: ‘Ya Ath Thawry hivi jee ni Amali gani

ambayo imemfanya Allah Subhanah wa Ta’ala akupende?’

Imam Sufyan Ath Thawry akasema: ‘Kutokujua kitu juu ya Watu’ Imam Sufyan Ibn

Uyaynah akasema kumwambia Imam Sufyan Ath Thawry: ‘Naomba uniusie ewe Ath

Thawry!’ Imam Sufyan Ath Thawry akasema: ‘Kifanyie kazi hicho nilichokuambia’

Imam Sufyan Ibn Uyaynah akasema: ‘Allah Subhanah wa Ta’ala akuingize kwenye

Rehma zake ewe Ath Thawry, kwani huku kuna ndugu wengi wazuri na kila mmoja

mongoni mwao anaweza akamuombea mwenzake katika siku ya Malipo.’

Imam Sufyan Ath Thawry akasema: ‘Ya Ibn Uyaynah, hakika mimi sitaki kujuana

nawe tena kuanza leo. Hivi wewe umeshawahi kuona madhara yanayotokana na

mtu mwengine yeyote yule zaidi ya unaejuana nae? ’ Imam Sufyan Ibn Uyaynah

anaendelea kusema: ‘Hapo hapo mimi nikaamka kutoka usingizini huku nikiwa

nnalia kwa sauti.’

Kwani Miongoni mwa Masahaba basi walikuwepo Saab Ibn Jasama na Awf Ibn Malik

Radhi Allahu Anhum, hawa walikua ni Masahaba ambao walikua na Udugu wa Waislam

wa Madinah kuwapokea Waislam wa Makkah walipohamia Madinah na kugawana Mali

zao sawa kwa sawa.

Na hivyo wakaahidiana kua Udugu wao na Urafiki utaendelea hadi baada ya Kufariki

kwao. Ambapo Allah Subhanah wa Ta'ala akajaaliwa kua Saab Radhi Allahu Anhu kua

ni mwenye Kufariki mwanzo. Hivyo baada ya Saab Radhi Allahu Anhu kufariki basi Aws

Radhi Allahu Anhu alipolala akamuona Saab usingizini. Ambapo ndani ya Usingizi huo

ndotoni basi Saab Radhi Allahu Anhu alikua akimwambia Aws Radhi Allahu Anhu kua

Alhamd lillah Masuali aliyoulizwa Na Malaika ameyajibu kikamilifu

Awf Radhi Allahu Anhu akamuuliza Saab: ‘Mbona hapo kifuani una Doa Jeusi

ambalo ulikua huna ulipokua hai? imekuaje?’

Saab Radhi Allahu Anhu akasema: ‘Hakika mimi nilipofariki niliacha Deni, kwani

kuna Yahudi fulani ananidai Dirham 10, na Dirham zake sijawahi kumpa, zipo

sehemu fulani kampe’

Kisha Saab Radhi Allahu Anhu akaendelea kusema: ‘Halafu pia ya Aws fahamu kua

Binti yangu nae pia karibuni atanifuata huku Akhera, hivyo usihuzunike pale hili

pia litakapotokea’


971

Asubuhi ilipofika na Aws Radhi Allahu Anhu alipoamka basi akaenda Nyumbani kwa

Rafiki yake aliefariki yaani Saab Radhi Allahu Anhu, na akazikuta Dirham 10 katika

sehemu aliyofahamishwa kwenye Ndoto, hivyo akazichukua kisha akamfuata yule

Yahudi na kumuuloza kama anamjua Saab, na Yahudi akasema ndio kwani anamdai

Dirham 10. Hivyo Awf Radhi Allahu Anhu akamlipa Dirham hizo 10

Kwani amesema pia Imam Mujahid Ibn Sulayman kua: ‘Mtu aliefariki hua anapewa

Habari za Amali njema Amali njema anazofanya Mtoto wake baada ya Kufariki

kwake.’

Na kwa kua Maiti hua ni mwenye kupata habari Njema za Mema ya Mtoto wake aliehai

na pia Maovu ya Mtoto wake aliemuacha hai basi hii inatuonesha pia na inatufunza kua

haifai kabisa kua Muislam anapofariki basi Ndugu zake walio hai wakawa wanagombana

kwa sababu ya Mali alizowacha Marehemu, kwani Maiti wanapata Habari na Kuaibika

kutokana na Matendo hayo ya watu wao Walio hai.

Kwani Amir ul Muuminin Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu alikua kila akizungumzia

kuhusiana na Jahanama na akisimama pembeni ya Kaburi alikua akilia sana kiasi ya kua

hadi Ndevu zake hua ni zenye Kuroa kwa Machozi. Hivyo Masahaba wenzake

wakamuuliza: ‘Ya Amir ul Muuminin Mbona Ukizungumzia kuhusiana na Pepo hua

si Mwenye Kulia? Lakini Ukizungumzia kuhusiana na Moto na Kaburi hua ni

mwenye Kulia?’

Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu akajibu: ‘Kwa sababu amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Kaburi ndio hatua ya mwanzo ya kuingia Akhera,

hivyo yeyote yule atakaefuzu na kuokoka na Mitihani ya Kaburi, basi

kitakachofuatia baada yake huko Akhera kitakua ni chepesi sana kwake, na

asieokoka na Mitihani ya Kaburini basi bila ya shaka kitakachofuatia baaada yake

huko Akhera basi kitakua kibaya zaid na kwa Hakika mimi sijawahi kuona Kitu

chenye Matukio Mabaya kama Kaburi’’

Kwani Aya, Hadithi na Habari zinazothibitisha kuwepo kwa Uhai wa Kaburini baada ya

Mauti na Kaburi ziko nyingi sana ambazo ni zenye kutubainishia kua Jambo muhimu

zaidi kwetu sisi Waislam ni kujitayarisha na Kifo na Maisha yanayofuatia baada yake.

Kwani Kinachofariki na Kufufuliwa tena Upya hua ni Miili yenu na wala haiwi Roho

zetu.

Na hii ni kwa Sababu Roho hua zina Maumbile ya Kutokufa, bali hua na Maumbile ya

Kutolewa katika hali Moja ya Mazingira na Kuingizwa katika hali nyengine. Yaani kama

tulivyosema kua Roho zetu zilikubali kuchukua Amanah Kutoka kwa Mola wetu, na

zikala Kiapo na Kuthibitisha kua Allah Subhanah wa Ta'ala ndie Mola wetu.


972

Roho zetu ndio zilizokua hai Miaka yote hio huku zikisubiri wakati wake wa kuingia

kwenye hali ya Manii ya Mababa zetu na kisha kuingia kwenye Matumbo ya Mama zetu

kwa ajili ya Kuvaliwa na Miili yetu itakayotuwezesha kuja Kuishi katika mazingira yetu

Ulimwenguni. Hivyo Mda wa kuishi unapomalizika basi inabidi tuhame kwenye

Maumbile ya Mazingira ya Ulimwenguni na kurudi Akhera kurudisha Amanah kwa

Muumba wetu aliyotukabidhi baada ya kutuumba.

Hivyo tunapotoka Ulimwenguni basi inabidi tuyavue Mavazi ya Ulimwenguni ambayo

ni Miili yetu yenye kuonekana na yenye kua na uwezo wa Kuoza. Kwa ajili ya Kuingia

kwenye Maisha yanayofuata ambayo unapatiwa Maumbile ya Mwili Mpya ambao Ubora

wake hua unategemeana na namna Ulivyoishi hapa Ulimwenguni kabla ya Kuyavua

Mavazi ya Mwili uliokuwezesha kuishi Duniani.

Kama Uliishia kwa Kuisimamia Ipasavyo Amanah Uliyokabidhiwa na Mola wako, basi

Utaepukana na Mitihani ya Kaburini na Utafurahia Akhera yako. Na kama uliishi kwa

kutoijali na kutoisimamia Amanah yako Amanah yako uliyokabidhiwa na Mola wako

basi Utafeli Mitihani ya Kaburini na Utaijutia Akhera yako.

Kwani Roho na Mwili hua ni sawa na Balbu ya Umeme. Roho ni Umeme na Balbu ni

Mwili. Hivyo Inapoungua Balbu basi hua haimaanishi kua Umeme kwenye Waya

hakuna, kwa sababu Umeme ni Kama Roho haionekani. Hivyo Roho inakuwepo kwa

Allah Subhanah wa Ta’ala na inalipwa malipo ya amali ulizokua unazifanya kama mbaya

basi malipo mabaya na kama nzuri basi malipo mazuri, hivyo ijali Balbu yako kwa

kufanya amali njema kabla Haijaungua kwani Umeme wa Muumba Haukatiki na

unakuwepo katika mazingira stahiki na wakati stahiki.

Tunapoagalia Lugha ya Kiarabu basi tunaona kua Neno Sabaha ambalo hua ni Jina la

Mtu Mwanamke hua linamaanisha kipindi cha wakati Unaochomoza Jua yaani Asubuhi.

Ambapo kwa Upande Mwengine basi Wakati huu pia hua unajulikana kama Ghuduwan.

Neno Ghuduwan linatokana na neno Ghada ambalo kwa lugha ya Kiarabu hua

linamaanisha Kuenda, Kuendeleza, Kutoka, Kufanya Kitu katka wakati wa Asubuhi,

Wakati ulopo au wakati wowote. Neno Ghada pia limelotoa neno Ghadan ambalo hua

linamaanisha Kesho. Na pia Likatoa neno Ghadaun ambalo hua linamaanisha Chakula

cha Asubuhi.

Naam..hio ni kuhusiana na wakati wa Asubuhi yaani Sabaha au Ghuduwwan. Ambapo

kwa upande mwengine basi neno A'asha ambalo pia hua ni Jina la Mtu Mwanamke yaani

Asha, hua limetokana na neno A'asha ambalo hua linamaanisha Kipindi Cha wakati wa

Siku ambacho hua ni chenye Kuanza Mara baada ya Kuzama Jua na Kuingia Kiza

ambacho pia ndio wakati ulitoa jina la Sala ya Isha.


973

Na tunaangalia na kufahamishana kuhusiana na Nyakati hizi kwa sababu Tuko katika

kukumbushana kuhusiana na Mauti na Hali inavyokua Mara baada ya kuingia kwenye

Barzakh au Kaburini.

Ambapo anasema Allah Subhanah wa Ta'ala katika aya iliyotumia maneno tuliyaanza

nayo kuyaangalia maana zake ambayo ni Ghuduwwan yaani Asubuhi, Wakati wa

Mapambazuko ya Jua na A’ashiyyan yaani wakati wa Isha kinapoingia Kiza kuhusiana

na Watu waovu kua:

‏﴿ٱلن َّارُ‏ يُعْرَضُونَ‏ عَلَيْهَا غُدُوّاً‏ وَعَشِ‏ يّاً‏ وَيَوْمَ‏ تَقُومُ‏ ٱلس َّاعَةُ‏ أَدْخِ‏ لُو ۤ اْ‏ آلَ‏ فِرْعَوْنَ‏ أَشَ‏ َّد

ٱلْعَذَابِ‏ ﴾

Alnnaru yuAAradoona AAalayha ghuduwwan waAAashiyyan wayawma taqoomu

alssaAAatu adkhiloo ala firAAawna ashadda alAAadhabi (Surat Al Ghafir 40:46)

Tafsir: Moto ambao Wanapambanishwa Nao (Wakati wakiwa Makaburini) Asubuhi

Kunapopambazuka na Usiku Kinapoingia kiza, Na Itakapofika Saa ya Siku ya Malipo

(Wataambiwa Malaika) Waingizeni Kina Fir'awn katika Adhabu Kali

Ambapo ingawa baadhi wanaweza kusema kua hii aya ni yenye kuwazungumzia kina

Fir'awn na Watu wake na bila ya shaka hawajakosea, lakini kwa Upande mwengine basi

wanasema Mujaddid Ad Din Sultan Al Mutakallimin, Imam Al Mushakikin Imam Fakhr

Ad Din Al Razi, na pia Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari kua:

‘Aya hii ni Miongoni mwa aya zenye Kuthibitisha kuhusiana na Maisha ya Barzakh

yaani Ndani ya Kaburi hususan kuhusiana na maneno Ghuduwwan waA’ashiyan

Yaani Asubuhi na Usiku kua Katika Makaburi Hakutokua na Jahannama Bali

kutakua Na Adhabu ya Moto wa Jahannam Asubuhi na Jioni, Kwani Jahannam

yenyewe hua ni katika Siku ya Malipo ambapo itakua ni Adhabu ya Kudumu’

Hivyo Aya inatuwekea wazi kua kwa watu waovu basi baada ya kuingia Kaburini basi

hua Kuna Adhabu ya Moto ambayo hua inarudiwa Kila Masaa 12 yaani Asubuhi na Jioni.

Ambapo amesema Abd Allah Ibn Masud Radhi Allahu Anhu kua: Amesema Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam kua: ‘Waliokufa hua wanaadhibiwa Makaburini Mwao

na hata Wanyama hua wansikia sauti zao’ Na akasema tena Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua: ‘Ummah huu utapata Mtihani wa Ndani ya Makaburi. Hivyo

kma mimi sikua ni mwenye kuogopa kua nyinyi mtaingiwa na Khofu ya Kuwazika


974

watu wenu. Bas nngekuombeeni kwa Allah Subhanah wa Ta’ala mkawa na uwezo

wa kusikia ninayoyasikia mimi.’(Musnad Imam Hanbal)

Kwani alisema Amr Ibn Dinar kua: ‘Kuna Dada wa Mmoja kati ya Watu wa Madinah

alifariki nasi tukamzika lakini ndugu yake aliporudi baada ya kuzika basi

akakumbuka kua amedondosha kitu chake Kaburini hivyo akaomba msaada kwa

mmoja kati ya Marafiki zake ili aende akamsaidie Kufukua Kaburi ili akitoe kitu

chake hicho kilichomdondoka. Hivyo wakaenda na Kufukua na mara akaiona kitu

chake hicho, akakichukua lakini akamwambia Rafiki yake huyo, kua Wacha

tuendelee Kufukua ili tupate kuona hali yake Dada yangu ikoje baada ya Kumzika.

Wakafukua hadi kwenye Mwana wa ndani na mara wakakutana na Moto, hivyo

wakafunika na kufukia kwa khofu, Kisha wakarudi Nyumbani walipofika

Nyumbani Kaka mtu akaulizwa kuhusiana na Dada yake.

Nae akajibu: ‘Kwanini Mnamuulizia wakati ni Mtu ambae ameshafariki?’

Akaambiwa ‘Sema kwani tumesikia kua ulienda kufukua’.

Akasema ‘Niambieni kwani alikua akifanya nini?

Hivyo akaambiwa: ‘Alikua akichelewasha Sala zake, na pia alikua anapenda

kusikiliza maneno ya watu na kuyasambaza.’

Na anasema Mujaddid Ad Din Shaykh Ul Islam Imam Abd Rahman Al Suyuti kua:

‘Hadith zinazozungumzia Adhabu ya Kaburi ziko Nyingi sana kiasi ya kua

zimefikia hali ya Kua zimefikia hali ya kua ni zenye kuthibitisha Uhakika wa

kuwepo kwake, kwani zimenukuliwa na Masahaba wengi sana’

Na akasema Imam Al Mufasir Abu Abd Allah Muhammad Al Qurtubi kua: ‘Kuamini

kuhusiana na Adhabu ya Kaburi na Mitihani yake Ni Wajib na Kudhibitisha ni

Wajibu’

Na ingawa tumeona katika aya na hadith kua kuna Watu wataadhibiwa kwa kupata

Adhabu za Milele hadi katika siku ya Kufufuliwa.

Lakini kwa upande mwengine basi tunapoiangalia Qur'an basi tunaona kua anasema

Allah Subhanah wa TaAla kua kuna watu watasema katika Siku ya Kufufuliwa kua:

‏﴿قَالُواْ‏ يٰوَيْلَنَا مَن بَعَثَنَا مِن م َّرْقَدَِ‏ هَذَا مَا وَعَدَ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنُ‏ وَصَدَقَ‏ ٱلْمُرْسَلُونَ‏ ﴾


975

Qaloo ya waylana man baAAathana min marqadina hadha ma waAAada

alrrahmanu wasadaqa almursaloona(Surat Yasin 36:52)

Tafsir: Watasema Ole Wetu ni Nani alietufufua kutoka katika Usingizi wetu

(Wataambiwa kua) Haya Ndio aliyoyaahidi Mwingi wa Rehma na Wakasadikisha

Mitume.

Ambapo Aya hii inatuonesha kua Hawa Watakaojuta watakua ni waliofanya Maovu, na

aya inaonesha kua Walikua Wamelela Hivi Jee walipumzishwa au?

Kwani Neno Ruqud kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kulala, Kusinzia, Kua

Mregevu, Kua na hali ya Uchovu, Kua na Muonekano wa Mtu ambae ndie kwanza

ameamka hata uso hajanawa.

Neno Ruqud limetumika pia kwenye kisa cha As-hab Al Kahf pale Allah Subhanah wa

Ta'ala alipomwambia Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kuhusiana na watu wa Ashab

Al Kahf walivyokua wamelala kwa kusema:

‏﴿وَتحَْسَبُهُمْ‏ أَيْقَاظاً‏ وَهُمْ‏ رُقُودٌ‏ وَنُقَلِّبُهُمْ‏ ذَاتَ‏ ٱليَمِينِ‏ وَذَاتَ‏ ٱلشِّ‏ مَ‏ الِ‏ وَكَلْبُهُمْ‏ ابَسِ‏ طٌ‏

ذِرَاعَيْهِ‏ بِٱلوَصِيدِ‏

لَوِ‏ ٱط َّلَعْتَ‏ عَلَيْهِمْ‏ لَوَ‏ ل َّيْتَ‏ مِنْهُمْ‏ فِرَاراً‏ وَلَمُلِئْ‏ تَ‏ مِنْهُمْ‏ رُعْباً‏ ﴾

Watahsabuhum ayqadhan wahum ruqoodun wanuqallibuhum dhata alyameeni

wadhata alshshimali wakalbuhum basitun dhiraAAayhi bialwaseedi lawi

ittalaAAta AAalayhim lawallayta minhum firaran walamuli/ta minhum

ruAAban(Surat Al Kahf 18:18)

Tafsir: (Kama ungewaona) Ungewadhania kua Wako Macho, wakati wakiwa

Wamelela, nasi tulikua tukiwageuza katika upande wa kulia kwao na kushoto kwao,

huku Mbwa wao akiwa amenyoosha miguu yake kwenye mlango (wa kuingilia Pango

hilo) kama ungewaona basi bila ya shaka ungegeuka na kukimbia kutokana nao na

ungeshangazwa nao.

Yaani kama Rasul Salallahu Alayhi wa Salam, au pia kama mimi na wewe tunaosoma

Qur'an tungewaona Watu hao walivyokua Ruqudun (Wamelala Usingizi) basi

tungedhania kua Wako macho, huku Mbwa wao akiwa amelala kwenye mlango wa

Pango hilo, na bila ya shaka tungekimbia kutokana na muonekano wao unaoshangaza,

Hivyo hapa tunaoneshana wa neno Raqada kwa Sababu neno hili ndio lililotoa neno


976

Marqad, ambalo hua linamaanisha Kitanda au Sehemu ya Kulalia iwe kwa Mtu alie hai

au aliefariki.

Ambapo kuhusiana na Aya yetu hii ya Surat Yasin 36:52 basi nayo pia imetumia neno

Raqada katika hali ya Marqadina yaani Malazi au Vitanda vyetu vya kupumzikia basi

anasema Abu Hurayrah Radhi Allahu Anhu kua: ‘Amesema Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kua: ‘Baina ya Kupulizwa Baragumu kutakua na kipindi cha

Arubaini Abu Hurayra Radhi Allahu Anhu akamuuliza Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam kwa kusema kua: Ya Rasul Allah hivi Unamaanisha Arubaini

MaSiku au?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Siwezi kusema chochote zaid’

Masahaba Wakauliza: ‘Unamaanisha Arubaini miezi?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘La siwezi kusema’

Masahaba wakauliza: ‘Arubaini Miaka?’

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema: ‘Siwezi kusema chochote, lakini

baada ya hapo Allah atajaalia Maji kushuka kutoka Mbinguni na kisha Watu

watachipua kama inavyochipua Mimea, kwani ni kitu kimoja tu cha Ibn Adam

ambacho hakitooza ambacho ni kimfupa kidogo cha mwisho cha Uti wa mgongo,

ambacho ndicho kitakachochipua Ibn Adam kutokana nacho katika Siku ya

Malipo’ (Sahih Muslim)

Naam..hii ni hadith ambayo inatuelezea kuhusiana na tukio la Kupulizwa kwa Baragumu

mara 2 yaani katika siku ya Kiama. Ambapo anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas

Radhi Allahu Anhu, na Ubay Ibn Kaab Radhi Allahu Anhu kua: ‘Baragumu litapulizwa

mara mbili, ambapo litakapopulizwa mara ya kwanza basi adhabu za Kaburi

zitasitishwa na hivyo Watu watalala usingizi hadi litakapopigwa kwa mara ya pili

ndio watu wataamka na kutakua na kpindi cha miaka arubaini baina yake’

Kutokana na Hali hio basi wale waliolala watasema Ya Waylana Ma Baathana Min

Marqadina (Surat Yasin 36:52)

Ama kwa Upande wa Mujaddid Ad Din Imam Fakhr Ad Din Al Razi basi yeye anasema

kuhusiana na aya hii kua: Maneno haya yanamaanisha kua: ‘Watu hao watasema Jee

ni Nani alietuamsha kutoka katika Sehemu zetu za Kulalia na Mapumziko? Yaani

watakua ni wenye kujiuliza Jee ni Allah Subhanah wa Ta'ala ndio Ametufufua au

Tumeamshwa kutoka Usingizini? Na hivyo hii inamaanisha kua watu hawa


977

hawatokua na Uhakika kama walikua wamelala na kuamshwa au kua walikua

wamekufa kisha wakafufuliwa’

Na kuna hadith kadhaa za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salan zinazohimiza

kuwaombea Dua Maiti wetu, kuwatolea Sadaqat Al Jariah n.k. Na hii ni kwa sababu

unavyofanya hivyo basi hua inawasaidia kuwapunguzia Adhabu za Kaburi Maiti hao. Na

pia kufanya kwetu huko hua pia ni sehemu ya sisi pia kuja kufanyiwa hivyo na Vizazi

vyetu katika wakati ambao tutakua tunahihitaji msaada kutoka kwao wao ndugu zetu hao

waliohai.

Na kuhusiana na haya basi Imam Abd Allah Ibn Muhammad Ibn Abi Duniya ambae yeye

amesema Imam Ibn Abi Duniya kua: ‘Abu Ubayd Ibn Buhayr aliniambia mimi kua:

Rafiki yangu aliniambia kua: Hakika mimi nilimuona usingizi Ndugu yangu baada

ya kufariki kwake Hivyo nikamwambia, Nakuombea kua Dua zetu zikufikie, nae

akajibu Naam Allah Subhanah wa Ta'ala anatumurika na Nuru ya Dua hizo.’

Imam Abd Allah Ibn Muhammad Ibn Abi Duniya anaendelea kutuambia kua: ‘Amesema

Bashar Ibn Ghalib kua, hakika mimi nilimuona Ndugu yangu kwenye Ndoto ambae

nilikua nikimuombea Dua sana baada ya Kufariki kwake, Nilipomuona usingizini

akaniambia kua Ewe Bashir hakika ya zawadi zako hua zinatufikia zikiwa kwenye

Sahani iliyojaa Nuru yenye Vitambaa vya hariri’

Nami nikamuuliza: ‘Imekuaje?’

Nae akasema: ‘Hua tunapokea Dua kutoka kwa Waumini waliohai pale

wanapowaombea wale waliofariki, hivyo wakiwaombea basi hua zinajibiwa na

Allah Subhanah wa Ta'ala na kisha zinawekwa kwenye Sahani za Nuru na

kupelekewa yule alieombewa kwa jina lake na kuambiwa kua Maombezi yako haya

yametoka kwa fulani ibn Fulani’.

Kuna mtu alikua anampenda sana Rabia Al Adawiyyah na hivyo alkua anapenda

sana kumuombea Dua. Hivo siku moja alpoalala akamuona usingizini akiwa na

tabasam na kumwambia kua: ‘Zawadi zako hua tnaletewa zikiwa kwenye Sahani

iliyojaa Nuru na zenyewe zikiwa zimejaa Nuru.’’

Hivyo kutokana na vithibitisho hivyo basi tunaona kua Kuna baadhi ya Adhabu za

Kaburini hua zinasitishwa kutokana na Maombi ya Waumini juu ya Waumini. Na

tunapozungumzia Waumini basi hua tunamaanisha Kila Waislam wakisoma Dua au

wakisoma Quran ambayo ndani yake mna aya zenye Kuwaombea Waislam waliotangulia

basi Dua na aya hizo hua zinawanufaisha Maiti hao, kama alivyosema Allah Subhanah

wa Ta'ala kua:


978

‏﴿وَ‏ ٱل َّذِينَ‏ جَآءُوا مِن بَعْدِهِمْ‏ يَقُولُونَ‏ رَب َّنَا ٱغْفِرْ‏ لَنَا وَلإِخْوَانِنَا ٱل َّذِينَ‏ سَبَقُوَ‏ بِ‏ ٱلإِيمَانِ‏

وَلاَ‏ تجَْعَلْ‏ فىِ‏ قُلُوبِنَا غِلاًّ‏ لِّل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏ رَب َّنَآ إِن َّكَ‏ رَءُوفٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾

Waalladheena jaoo min baAAdihim yaqooloona rabbana ighfir lana waliikhwanina

alladheena sabaqoona bial-eemani wala tajAAal fee quloobina ghillan

lilladheena amanoo rabbana innaka raoofun raheemun(Surat Al Hashr 59:10)

Tafsir: Na Wale waliokuja baada yao Wakasema Ewe Mola wetu Tusamehe sisi Na

Ndugu zetu waliotutangulia kwenye Imani ya Dini ya Kiislam Na Wala Usijaalie

kwenye Nyoyo zetu kinyongo na Chuki dhidi ya Walioamini wenzetu, Kwani ewe Mola

wetu Hakika wewe ni Mwingi wa Ukarimu na Huruma

Ambapo kwa Upande mwengine basi anasema Mujaddid Ad Din Imam Shihab Ad Din

Abd Fadhl Ibn Hajar Al Asqallani kua: ‘Adhabu ya Kaburi hua ni ya Kudumu pale

mtu anapokua ni Kafiri au Mnafiq. Ama kuhusiana na Muislam mwenye

Madhambi basi hali yake hua inategemea na madhambi yake, kwani kuna makosa

yanayosamehewa, kuna makosa yasiyosamehewa, kuna makosa yanayoendelea

adhabu zake kwa mda mrefu na kuna makosa yatakayositishwa adhabu zake.’

Ambapo tumeona kuhusiana na vithibisho vya kuwepo kwa adhabu za Kaburini na pia

Kusimamishwa kwa Adhabu kutokana na msaada wa Waumini walio hai wanaoufanya

kwa ajili ya kuwasaidia waliotangulia mbele ya Mola wao ambao wao hua hawana uwezo

tena wa kuyafanya mambo mema hayo na hivyo kututia ari ya kua ni wenye kutakiwa

kukumbukana na kupendana si tu katika wakato wa uhai wetu bali pia katika wakati wa

baada ya Kufariki kwetu baina yetu.

Na tunapoangalia kwa upande wa mifano ya Hadith za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa

Salam, basi tunaona ile hadith ya Sahaba aitwae Sad Ibn Ubaidah Radhi Allahu Anhu

ambae yeye alifiliwa na Mama yake. Ambapo baada ya kumzika na mda kidogo kupita

basi siku moja Saad Radhi Allahu Anhu alimfuata Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

na kumwambia: ‘Ya Rasul Allah, hakika Ummu Saad ameshafariki, hivi jee nimtolee

Sadaqa gani?’

Ambapo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam akasema kumwambia Saad Radhi

Allahu Anhu kua: ‘Sadaqa bora ni Maji’


979

Hivyo Saad Radhi Allahu Anhu akachimba Kisima na kisha akatangazia kua: Hiki ni

kisima cha Maji cha Ummu Saad (Imam An Nasai, Imam Abu Daud, Imqm Ibn Majah

na Musnad Imam Ahmad)

Kwani Amesema Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu kua: ‘ Kila mara Rasul Allahi

Salallahu Alayhi wa Salam alipomaliza kumzika Mtu yeyote yule basi alikua

akisimama Pembeni ya Kaburi na kisha alikua akisema: Ninachokuombeni hivi

sasa Nyote kua ni wenye kumuomba Allah Subhanah wa Ta'ala kumpa Msimamo

Thabit, Maiti huyu kwani sasa hivi yuko Katika hali ya Kuhojiwa’

Ambapo haya yote yanatuonesha kua:

Maiti hua anasikia Manemo ya Mtu aliehai.

Maiti hua anaulizwa Kaburini.

Ni halali na hakuna Ubaya wowote Kumuomba Allah Subhanah wa Ta'ala

amsamehe Maiti mara tu baada ya kuzikwa na kumpa Msimamo Thabit Maiti huyo

katika wakati wa kuhojiwa na Malaika wawili Kaburini.

Inakukubalika Kufanya Jambo la Kheri kwa ajili ya Mtu alietangulia Akhera, iwe

Kumtolea Sadaqa, kwa kumchimbia Kisima, Kumjengea Msikiti, n.k Kumuombea

Dua, Kumuombea Msamaha, Kusoma Qur'an kwa nia ya kua Allah Subhanah wa

Ta'ala amfikishie malipo ya kisomo hicho yamfikie Maiti wako au Maiti wote wa

Kiislam.

Kwani kweli Amesema Allah Subhanah wa Ta'ala amesema kua:

‏﴿وَأَن ل َّيْسَ‏ لِلإِنسَانِ‏ إِلا َّ مَا سَعَى ٰ ﴾

Waan laysa lil-insani illa ma saAAa (Surat An Najm 53:39)

Tafsir: Na Hana Mtu (Malipo) isipokua juu ya kile alichokifanya.

Ambapo maana ya aya hii ni kua Hatopata Mtu malpo isipokua juu ya lile alilolifanya

Mtu huyo iwe zuri au ovu. Hivyo aya hii inamzungumzia Mtu kama Mtu na amali zake

kua hatodhulumiwa alichokifanya iwe chema au kiovu bali atalipwa ipasavyo.


980

Na maana ya Aya na Hadith za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam tulizoziangalia

basi ni kua: Muislam aliefariki anapofanyiwa mema na Mrithi wake au Muislam

mwenzake au na Waislam wenzake waliokua hai basi malipo hayo humfikia Maiti

huyo, kwani jema hilo hua hakufanya mwenyewe bali amefanyiwa kwa ajili yake.

Hii hua pia ni Sawa na Pale Maiti anapodaiwa kisha watu wakaulizwa wanaomdai

na wanaodaiwa nae ili Maiti ili walipe au walipwe.

Kwani amesema Imam Ahmad Ibn Hanbal kua: ‘Mnapoingia Makaburini someni Ayat

ul Qursy mara 3, Surat Ikhlas mara Moja halafu semeni: Ya Allah Ya Rahim hizi ni

kwa ajili ya Watu wa Makaburini’

Na akasema Hujjat Ul Islami Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn

Muhammad Al Ghazali kua: ‘Mnapoingia Makaburini Someni Surat Al Fatiha na

Surat Nas na Surat Al Falaq na Surat Al Ikhlas kisha semeni: Allahu La Ilaha Illa

Huwa, Ya Rahim hizi ni kwa ajili ya watu wa Makaburini’

Ambapo hapa inabidi tukumbuke kua hili ni jambo rahisi sana na la kujipatia Thawabu

za bure tena za kumwaga kwa sababu kwa kila harufi ya Qur'an utakayoisoma kisha

ukaitoa Sadaqa kwa Maiti waliozikwa Makaburi basi wewe unalipwa 10 bila ya

kuwapunguzia wao. Ambapo ayat Kursiy ina herufi 170 mara 10 hua ni 1700..sasa

Tafakkar makaburini hapo kuna maiti wangapi waliozikwa tangu miaka na miaka?

Naam..Hivyo, tusisahau Sadaqat Jarriyah, Kuwaombea Dua Maiti wetu, Kujidhibiti

Nafsi zetu ili tusiwe na Dhambi zenye kutudumisha kwenye Adhabu, bali tuwe ni wenye

kushikamana na Qur’an.

KUHIFADHIWA NA KURAHISISHWA KWA QUR’AN.

Mnamo Mwezi 11 Shawwal wa mwaka 11 Al Hijra Waislam wakiwa chini ya Uongozi

wa Amir ul Muumin Sayyidna Abu Bakr As Siddiq Radhi Allahu Anhu basi Jeshi la

Waislam lilikokuwa chini ya Uongozi wa Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu liliingia

vitani kupigana dhidi ya watu waliokua wakijiita kua Mitume walioibuka baada ya

kufariki Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam. Ambapo mmoja kati ya watu hawa

alikuwepo aliekua akiitwa Musalima Al Kadhaab ambae alikua na Jeshi kubwa sana.

Hivyo Khalid Ibn Walid Radhi Allahu Anhu akawaongoza Waislam walio chini yake na

kufanikiwa kuliteketeza jeshi la watu 21000 la Musalimah na pia kufanikiwa kumuua

Musalimah mwenyewe. Hivyo ingawa Waislam walishinda lakini na wao walipoteza

wanajeshi 1200 ambapo wengi ndani yao walikua 70 ambao ni wale waliohifadhi Qur'an.


981

Na ingawa Waislam walishinda lakini tukio hili la kufariki kwa wengi miongoni mwa

waliohifadhi Qur'an lilimshtua sana Umar Ibn Khattab Radhi Allahu Anhu, hivyo

akamwambia Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu kua, yeye anakhofu kua ikitokea

tena hali kama hio basi huenda Qur'an ikatoweka.

Hivyo bora Qur'an ikusanywe yote kwenye sehemu moja, yaani kwenye Mas-haf. Wazo

hili lilimshtua pia Abu Bakar Radhi Allahu Anhu kwani hakuwahi kumsikia Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akiwa na wazo hilo, hivyo nae akasita kufanya hivyo.

Kwani akifanya basi itakua tayari imeshakua ni Bidaa, kwa sababu Rasul Allah Salallahu

Alayhi wa Salam hakufanya hivyo. Lakini Allah Subhanah wa Ta'ala akamtulia wepesi

Moyo wa Abu Baqr As Siddiq Radhi Allahu Anhu nae akaona kua kuna kweli haja ya

kufanya hivyo.

Na ingawa kulikua na Khalifa ambae ni Abu Baqr Radhi Allahu Anhu na msaidizi wake

ambae ni Umar Ibn Al Khattan katika Mji wa Madinah Lakini Mji huo ulikua na Qadhi

Mkuu wa Mji wa Madinah ambae ni Sahaba mwanazuoni aitwae Zayd Ibn Thabit Radhi

Allahu Anhu.

Hivyo Abu Bakr Radhi Allahu Anhu na Umar Ibn Al Khattab Radhi Allahu Anhu

wakalifikisha shauri lao hilo kwa Qadhi Zayd Ibn Thabit Radhi Allahu Anhu ambae nae

akagoma.

Kwani nae aliona kua hawezi kufanya lile ambalo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

hakulifanya, kiasi ya kwamba alisema kua kwake yeye bora aambiwe auhamishe Mlima

wa Uhud kuliko kuambia aikusanye Qur'an katika sehemu moja.

Lakini hata hivyo Abu Baqr Radhi Allahu Anhu na Umar Ibn Al Khattab wakaweka wazi

sababu zao na kusema kua hilo ni jambo jema kufanywa kwani lina manufaa. Hivyo Zayd

Ibn Thabit Radhi Allahu Anhu akakubalina nalo jambo hilo Na hivyo Qur'an

ikakusanywa juzuu 30 katika kitabu kimoja kwa mara ya kwanza na ndio ambayo

tunayoisoma leo Waislam.

Na amesema Imam Abu Sulayman Al Khattabi kua: ‘Imam Abu Amr Ibn Al A’ala

amesema kua: ‘Lugha ya Qur’an iliyoshushiwa ilikua ni lugha ambayo Waarabu

walikua wakiizungumza katika wakati wa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam,

na hivyo h ni lugha tofauti na yetu sisi leo hii, na wale waliokua ni mabingwa wa

Lugha hio wametoweka kwa mda mrefu.’’

Kwani katika kipindi cha Khalifa Abu Bakr Radhi Allahu Anhu na kipindi cha Umar Ibn

Al Khattab Radhi Allahu Anhu basi Qur'an ilikua inasomwa katika Lafdhi 7 tofauti.


982

Hivyo siku moja katika kipindi cha Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu basi Sahaba

Hudhayfah Ibn Yaman Radhi Allahu Anhu baada ya kutoka katika Vita vya Jihad basi

alienda moja kwa moja mpaka kwa Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu na

kumwambia, kua ‘Inashangaza kua kila anakopita katika Miji aliyoenda basi

anakuta Waislam wanasoma Qur'an kwa Lafdhi zao, na hakuna hata mmoja

anaefaham lafdhi ya Mwenzake’

Kwani watu wa Basra wanasoma kivyao, Watu wa Syria wanasoma kivayo, Wayemen

kivyao.n.k Hivyo basi Hudhayfah aIbn Al Yaman Radhi Allahu Anhu kamwambia

Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu kua kutokana na hali hii basi bora Qur'an iwe

inasomwa katika Lafdhi moja tu ya Kiarabu cha Quraysh.

Hivyo Sayyidna Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu akaona kweli Hili ni Jambo Sahih,

hivyo hakuzibatilisha Lafdhi nyengine zote hizo bali alisema kua Qur'an isomwe kwa

lafdhi ya Kikureish yaani ndio iwe Lafdhi ya Umoja wa Kimataifa wa Qur'an.

Naam, hayo ni miongoni mwa matukio makubwa yaliyotokea kuhisiana na uhifadhiwaji

wa Qur'an baada ya kufariki Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam na ndio ambayo

yalifanyika ndani ya kipindi cha Makhalifa wanne wa Kiislam yaani Abu Bakar As

Siddiq, Umar Ibn Al Khattab, Uthman Ibn Affan na Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu

Anhum. Ambapo kwa kipindi chote hicho basi Qur'an ilikua inasomwa lakini haijatiwa

Harkah yaani Fat-ha, Kisra, Shadda, Dhuma na Sekn.

Na Alhamdlillah kua Masahaba waliyafanya yote haya kwa ajili yetu sisi mimi na wewe

ili Itufikie Qur'an pamoja na Vizazi vyetu na hivyo Masahaba hao kua ni wenye kufanya

yale ambayo Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam hakuwahi kuyafanya na kisharia

haya yote waliyoyafanya yalikua ni mambo ambayo waliyaanzisha wao wenyewe na

hivyo ingawa inakua ni Bidaa lakini hata hivyo ni kwa manufaa yetu sote, kwa hivyo hii

inakua ni Bidaa nzuri yenye manufaa.

Kwa sababu kama isingefanywa basi sijui mimi nawe Waislam wa leo tungekua na hali

gani na Qur'an yetu kwani imekusanywa pamoja tu na hatuiihifadhi Nyoyoni jee ingekua

ipo kama ilivyokua katika wakati wa Nabi Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam

ingekuaje? hivyo makusudi nimeanza kwa Masahaba kuhusiana na Qur'an kwa sababu

nataka tufahamiane kama inavyotakiwa tujue na pia inavyotakiwa tufaham.

Kwani anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al

Ansari Al Qurtubi kua: ‘Ama kuhusiana na Harkah (Hamza, Sukn, Shadda, Dhuma,

na Kisra) na Vidoto vyake Qur'an, Basi Wanasema Wanazuoni kua alikua ni

Khalifa Abdul Malik Ibn Marwan ambae ndie alieamrisha Viongezwe vitu hivyo.


983

Na Kazi hio ilifanywa na Hajjaj Ibn Yusuf alipokua katika Mji wa Al Wasit Nchini

Iraq, ambae ndie alieisimamia, na akamuamrisha Al Hasan na Yahya Ibn Ya'mur

kufanya Hivyo

Ambapo Muhammad Ibn Sirin alikua na Mas-haf ambayo iliongezewa hivyo na

Yahya Ibn Ya'mur.’

Ambapo tunapomzungumzia Hajjaj Ibn Yusuf ambaea alikau ni Kiongozi katili sana

katika kusimamia Maslahi ya Khalifa Abdul Malik Ibn Marwan ambao ni Utawala wa

Kiislam wa Banu Ummayah uliokua wenye Makao makuu yao Mjini Damascus nchini

Syria ambapo mnamo mwaka 86 Al Hijra Abdul Malik Ibn Marwan Alifariki Dunia na

pia ndio mwaka ambao Khaifa Umar Ibn Abdul Aziz Ibn Marwan alikua Gavana wa Mji

wa Madina na katika wakati wa mwaka huu basi Imam basi Imam Jabir Ibn Zayd wa

Ibadhi alikua na umri wa miaka 66, Imama Abu Hanifa alikua na miaka 6 na Imam Jafar

As Sadiq pia.

Wakati Imam Malik alizaliwa miaka 7 baadae, na kwa upande wa Imam Muhammad

Idris Al Shafii na Imam Ahmad Ibn Hanbal nao ndio hata mababa zao hawajazaliwa.

Hivyo Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al

Qurtubi anaendelea kutuambia kua: ‘Ama kuhusiana na idadi ya Herufi zake na

Juzuu basi amesema Salam Al Himani kua: Al Hajjaj Ibn Yusuf aliwakusanya

Wasomaji wa Qur'an, Waliohifadhi na Waandishi na Kuwahoji, kwa kusema jee

katika Qur'an mna Herufi ngapi?

Nami nilikuwemo kwenye wenye Kuulizwa hivyo tukazihesabu na kukubaliana kua

Qur'an ina herufi 340,740 Kisha Hajjaj Ibn Yusuf akaniuliza Jee ni Herufi Gani

inamalizia Sehemu ya Mwanzo ya Katikati ya Qur'an nami nikasema ni katika

Surat Al Kahf katika herufi Fe ya neno Walyatallataf :

Walyatallataf (Surat Al Kahf 18:19)

‏﴿وَلْيَتَلَط َّفْ‏ ﴾

Tafsir: Na wacha awe Makini kwa ukarimu.

Ambapo neno hili lina herufi 7, na herufi Waw,Lam,Ya na Ta ziko katika nusu ya

kwanza ya Qur’an na herufi Lam,Tta na Fa ziko kwenye nusu ya pili ya Qur’an.


984

Akaniuliza Niambie kuhusiana na Sehemu zake 3 nasi tukamwambia inaanzia

mwanzoni mwa Surat Tawba 9:10, ya pili mwanzoni mwa Surat Ash Shuara 26:100

na ya tatu ni kuanzia hapo mpaka mwisho wa Qur'an.

Salam Al Himani anaendelea kusema kua: Hakika sisi tuliifanya kazi hii kwa mda

wa miezi minne na kila siku Usiku Al Hajjaj Ibn Yusuf alikua anakuja na tunasoma

Robo yake

Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi

anatuelezea pia mitizamo myengine ambayo ni kua: ‘Ama kuhusiana na Harkah

(Hamza, Sukn, Shadda, Dhuma, na Kisra) na Vidoto vyake Qur'an basi Wanasema

Wanazuoni kua alikua ni Abdul Malik Ibn Marwan ambae ndie alieamrisha

Viongezwe vitu hivyo, Na Kazi hio ilifanywa na Hajjaj Ibn Yusuf alipokua katika

Mji wa Al Wasit Nchini Iraq, ambae ndie aliemuamrisha Al Hasan na Yahya Ibn

Ya'mur kufanya Hivyo’

Na vile vile akasema Imam Abu Muhammad Abd Al Haqq Ibn Ghalib Ibn Attiyah kua:

‘Hakika mimi nimesoma katika moja kati ya Vitabu kua alikua ni Khalifa Al

Mamun wa Utawala Al Abbas ndie aliemarisha kufanywa hivyo’

Na pia kuna wanaosema kua alikua ni Hajjaj Ibn Yusuf ndie aliefanya hivyo, Na si hivyo

tu kwani Qur'an asili yake ilikua haina hata vidoto kwa mfano kimoja chini ya herufi Ba,

Kimoja juu ya Herufi Nun, Fe, Viwili juu ya herufi Ta, n.k.

Ambapo anasema Imam Yahya Ibn Abi Kathir kua: ‘Qur'an katika kopi zake za asilia

ilikua tupu haina hata vidoto, ambapo jambo la kwanza walilolifanya ilikua ni kutia

Vidoto, juu ya Ba, Ta, That, na kusema kua hakuna tatizo lolote, bali kufanya hivyo

kunaifanya Qur'an iwe inafahamika zaidi, na kisha wakatia alama mwishoni mwa

kila aya, na ikatiwa alama mwanzoni na mwishoni mwa kila Sura.’

Kwa upande wmengine basi anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad

Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi kua amesema Ad Dani kua: ‘Kauli zote hizo

zilizoruhusu kuanzishwa kutiwa alama kwa mwanzo mwa kila aya na mwishoni,

mwa kila sura, mwisho mwa kila sura, n.k zilifanywa na Masahaba ambao

walifanya hivyo kutokana na Jitihada zilizowapelekea kufanya hivyo, Na nnadhani

kua wale waliopinga kuhusiana na hayo basi walipinga pale ilipokua imetumika

Rangi katika kutiwa alama hizo kwa mfano rangi nyekundu, manjano n.k

Ingawa Waislam wa Maeneo mengine hawakupinga na walikubaliana na jambo

hilo baada ya kulinganisha na kopi za asilia na hivyo zilizokokosewa kuondolewa

kasoro zake katika waliyokubaliana, wa Allahu Aalam.’


985

Ambapo amesema Imam Muhammd Ibn Sirin kua: ‘Hakika mimi nnao Msahafu

ambao umetiwa vidoto na Yahya Ibn Ya’mur’ na kwa upande wa Akhbar Al Fuquha

Imam Muḥammad Ibn Al Ḥasan Ibn Abd Allah Ibn Madḥij Al Faqih Muḥammad Ibn Al

Ḥasan Al Zubaydi basi anasema kua: ‘Al Mubarrad amesema kua Mtu wa mwanzo

kutia vidoto kwenye Qur’an ni Abu Al Aswad.’

Kwani tunapoangalia juhusiana na idadi ya aya za Qur'an basi pia Wanazuoni

wametofautiana kwani anasema Imam Muhammad Ibn Isa kua: Jumla ya aya katika

Msahafu wa Madinah ni 6000.

Na akasema Imam Ismail Ibn Jafar kua: ‘Msahafu wa Madinah una aya 6214.’

Ambapo kwa upande wa Imama Al Fadhl basi yeye anasema kua:

‘Msahafu wa Makkah una aya 6219.’

Ambapo kwa upande wa Imam Muhammad Al Kisai basi anasema kua: ‘Idadi ya aya

za Qur'an kwa mtizamo wa watu wa Basra ni 6204.’

Na kwa upande wa Imama Yahya Ibn Harith basi anasema kua : ‘Msahafu wa Syria una

aya 6226.’

Naam..hapa kuhusiana na hili la habari ya Aya basi nadhani nifafanue kidogo Ili

tufahamiane, na hivyo watu wasije wakafaham sivyo.

Hivyo kwa wale wasiofaham ili wasichanganyikiwe ilikuaje ukawa Misahafu hii ina

idadi ya aya tofauti basi inabidi wajue kua haya tote yametokea kwa sababu baada ya

Kufariki Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam basi Uislam ulizidi kutanuka katika

maeneo tofauti. Hivyo na Masahaba nao pia walitawanyika katika maeneo tofauti. Na

kutokana na kutawanyika kwao basi watu wa Maeneo husika wakawa wanafuata

mitizamo ya Masahaba husika.

Kwa mfano Sahaba Abd Allah Ibn Masud ambae ni Sahaba mwanazuoni alihamia Iraq,

hivyo Watu wa Iraq wakawa anafuata Mtizamo wake, na ndio maana unakuta Fiqh ya

Madhhab ya Imama Abu Hanifa imejaa mitizamo ya Abdullah Ibn Masud Radhi Allahu

Anhu.

Ambapo Abd Allah Ibn Umar, Zayd Ibn Thabit, Ubbay Ibn Qaab Radhi Allahu Anhum

walibakia Madinah na ndio maana pia Fiqh ya Madhhab ya Imam Malik imejaa Mitizamo

yao.

Na Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu alikua Makkah na Hivyo bila ya Shaka

ingawa imechukua sehemu tofauti lakini Mitizamo ya Imam Al Shafii imeegemea kwa


986

Abd Allah Ibn Abbas kwa Sababu Msingi wa Ilm ya Imam Al Shafii ni kwa Imam Al

Zuhri na Imam Sufyan Ibn Uyayna ambao wametoa kwa Abd Allah Ibn Abbas Radhi

Allahu Anhu n.k.

Hivyo utawanyikaji huo wa Masahaba Wanazuoni ndio uliopelekea kutokea kwa sababu

ya pili ya kua na kila Sehemu na Idadi yake ya Aya. Na labda tuchukulie mfano hai ili

tufaham zaid.

Katika Upande wa Madhhab ya Imam Al Shafii unaposali kwa Sala ya kutoa Sauti basi

Bismi Allahi Rahmani Rahim lazima uitamke kwa sauti. Na kila unapoanza na Mwanzo

wa Sura basi lazima Utamke Bismi Allahi kwa Sauti, ila ukianza kati kati ya Sura basi

hua si lazima kusema Bismi Allahi kwa Sauti.

Jee unajua kwanini?

Naam hii ni kwa Sababu kwa upande wa Madhhab ya Imam Al Shafii basi Biismi Allahi

hua ni aya miongoni mwa aya za Qur'an na ni sehemu ya Sura hivyo lazima uisome kwa

sauti ukisali sala ya sauti. Isipokua kama utasoma Sura ya 9 ambayo ni. Surat At Tawba.

Na anasema Imam An Nawawi kua: ‘Mtu atakapoanza mwanzo wa Sura bila kuisoma

Biismi Allahi basi hua amewacha sehemu ya Qur'an.’

Ambapo kwa Upande mwengine kuna Wanaosali sala za Sauti lakini baada ya Surat Al

Fatiha kisha kwa mfano akasoma Surat An Nas basi moja kwa moja hua wanaanza na

Qul aAuudhu Birabbi AlNass, Maliki Nnnas...mpaka mwisho.

Na hii ni kwa sababu kwao wao Biismilahi hua ni sehemu ya Ufunguzi tu wa Sura, hivyo

hii nikutokana na utofauti wa Mitizamo kulingana na Vithibitisho vya Wanazuoni kupitia

kwenye Hadith za Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam.

Na ni kwa upande wa Madhhab ya Imam Al Shafii basi Biismi Allahi ni Aya na ni sehemu

ya Sura yeyote utakaoianza kuisoma mwanzo wake isipokua Surat At Tawba.

Ambapo awali watu wa kabila la Quraysh walikua na mazoea ya kuweka kichwa cha

habari katika barua zao ambacho kilikua kinasema Biismika Liihumma ambapo na Rasul

Allah Salallahu Alayh wa Salam alikua akifanya hivyo pia, hadi pale Allah Subhanah wa

Ta’ala aliposhusha aya ya Surat Hud ambayo inamzungumzia Nabii Nuh kwa kusema:

‏﴿وَقَالَ‏ ٱرْكَبُواْ‏ فِيهَا بِسْمِ‏ ٱهلل َِّ‏ مجَْرَاهَا وَمُرْسَاهَا إِن َّ رَبىِّ‏ لَغَفُورٌ‏ ر َّحِ‏ يمٌ‏ ﴾


987

Waqala irkaboo feeha bismi Allahi majraha wamursaha inna rabbee laghafoorun

raheemun (Surat Hud 11:40-41)

Tafsir: Na yeye (Nuh) akasema: Ingieni ndani yake, Kwa Jina la Allah katika Kuelea

kwake na katika Kutia Nanga kwake, kwani kwa hakika Mola wangu ni mwingi wa

Usamehevu na ni mwingi wa Rehma.

Hivyo baada ya kushushwa aya hii basi Rasul Allahi Salallahu Alayhi wa Salam

akamrisha kutumiwa kwa maneno Biismi Allahi Al Rahmani, na iliposhushwa aya ya

Surat An Naml isemayo:

‏﴿إِن َّهُ‏ مِن سُلَيْمَانَ‏ وَإِن َّهُ‏ بِسْ‏ مِ‏ ٱهلل َِّ‏ ٱلر َّحمَْٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ‏ ﴾

Innahu min sulaymana wa-innahu bismi Allahi alrrahmani alrraheemi (Surat An

Naml 27:30)

Tafsir: Kwa hakika hii ni kutoka kwa Sulaymani na kwa hakika (Inasema) Kutoka

kwa Allah Mwingi wa Rehma mwingi wa Huruma.

Hivyo baada ya kushushwa aya hii basi Rasul Allah Salallahu A’layhi wa Salam akaamua

kutumia Biismi Allahi Al Rahmani Al Rahim baada ya kusema: ‘Ndugu yangu Sulayman

ameanza aya na jina lake hivyo mimi nitaanza na Jina la Allah’ hivyo akaanzisha

Biismi Allahi Al Rahmani Al Rahim kua ndio kichwa cha Barua zake na kianzio cha Kila

Sura isispokua Surat At Tawbah.

Na ndio maana ikawa kuna wengine mongoni mwa Wanazuoni wakawa wamesema kua

hua sio lazima kuitamka Biismi Allahi kwa Sauti kwa sababu kwao wao hua ni Ufunguo

tu wa Kila Sura lakini si sehemu ya Sura.

Kwani hio ni sababu ya kwaza na mfano hai, hivyo kabla ya kuendelea basi nataka

tufahamiane vizuri sana kua:

Ingawa Wanazuoni wametofautiana kuhusiana na Idadi ya Aya za Qur'an, lakini hii

haimaanishi Kua Qur'an imetiwa mikono, au imetofautiana baina ya Msahafu mmoja na

Mwengine la!

Sio Hivyo na wala hatutakiwi tufahamu kua ni hivyo, kwa sababu tukifahamu hivyo basi

tayari tunakua tushavunja Nguzo ya Imani. Hivyo basi ili tusiwe ni wenye kuvunja Nguzo

ya Imani na badala yake tuwe ni wenye kuipa nguvu Imani yetu kuhusiana na Qur'an basi

na tuangalie sababu ya pili ambayo ilipelekea kuparaganyika idadi ya Aya.


988

Kwani anasema Mujaddid Ad Din Shaykh Ul Islami Imam Abd Rahma Al Suyuti Al

Shafii katika kitabu cha Al Itiqan fi Ulum ul Qur'an kua: ‘Mtizamo Sahih wa Idadi za

Aya za Qur’an ni 6236, na sababu ya kuwepo kwa utofuti wa Idadi hio ni kua kuna

baadhi ya Watu walizifupisha Aya zilizokua Ndefu na kuzigawa aya hizo katika

sehemu mbili mpaka tatu’

Sijui hapa tumefahamiana ama la? Hivyo kama hatujafahamiana basi na tuangalie mfano

wa hio sababu aliyoitoa Imam Al Suyuti ambapo hapo mimi nimeelezea kwa kutumia

maneno 41, bila ya kuweka nukta isipokua nimeweka koma.

Sasa kwa kua maneno hayo ni mengi basi ili kurahisisha ufahamu wake zaid ilikua

niyagawe katika sehemu mbili...yaani maneno hayo hayo lakini badala ya kuyaandika

kama yalivyo basi ni vizuri kuyagawa mara 2 badala ya mara moja ili watu wafaham,

wahifadhi na wazingatie mara moja.

Sasa hivi ndivyo walivyofanya baadhi ya Masahaba kwani wao walizigawa aya kubwa

na ndefu katika mara mbili mpaka tatu kulingana na ukubwa wa aya bila ya kupunguza

maneno ya aya.

Kwani pia hata tukichukulia mfano wa hio idadi ya Wanayokubaliana Wanazuoni kua ni

6236, basi hii pia hua ni Idadi ya aya bila ya kuihesabu Biismi Allahi ya Kila Sura na

hivyo idadi hii hua ya wale wasioihesabu Biismi Allahi ya kila Sura kua ni sehemu ya

Sura. Na hivyo basi kama tukiihesabu pamoja na Biismi Allahi basi aya zinakua 6348.

Kwani pia kwa upande wa Imam Ibn Huzaymah basi yeye anasema kua Qur'an ina aina

ya aya zifuatazo:

Aya 1000 kuhusiana na Ahadi.

Aya 1000 kuhusiana na Mawaidha.

Aya 1000 kuhusiana na Maamrisho.

Aya 1000 kuhusiana na Makatazo

Aya 1000 kuhusiana na Visa

Aya 1000 maonyo

Aya 500 kuhusiana na Hukmu

Aya 100 kuhusiana na Dua

Aya 66 kuhusiana na Mabatilisho na Yaliyobatilishwa

Hivyo ukijumlisha idadi hio basi unapata aya 6666, ambapo idadi hii pia ndio Idadi sahih

kulingana na Mtizamo wa Jarrah Allah Imam Abu Qasim Al Zamakhshari.


989

Hivyo basi Ukweli ni kua Allah Subhanah wa Ta'ala na Mtume wake ndie mwenye kujua

zaid juu ya hili, kwani kwa Upande wa Masahaba na Wanazuoni ndio kama tulivyoona

kua kila mtu na Mtizamo wake kulingana na Usomaji wake wa Qur'an yenyewe na namna

alivyofahamu, na kutokana na Kufanya Jitihada kwake na namna alivyojaaliwa na Allah

Subhanah wa Ta'ala.

Qur'an ni ile ile haijazidi wala haijapungua ila Mitizamo ya Watu tu juu yake ndio

Inayotofautiana katika kuifaham kwake, Kuitafakkari na kuifafanua kwake

Hivyo Wanazuoni Wanakubaliana na kufungamana na Mtizamo wa Masahaba wa Mji

wa Kufa ulioko Iraq na hivyo basi hapa inamaana tunazungumzia Mtizamo wa Sahaba

Abd Allah Ibn Masud na pia Ali Ibn Abi Talib Radhi Allahu Anhum ambao ilm yao ndio

chanzo kikuu cha Fiqh ya watu wa Iraq hususan watu wa Madhhab ya Imam Abu Hanifa.

Ambapo kwa upande mwengine basi tunaona kua huo pia ndio mtizamo wa Ummu Ul

Muuminin Aisha Radhi Allahu Anha ambao unasema kua Qur'an ina aya 6236. Na hizo

ndio aya zilizomo ndani ya Qur'an leo hii.

Kwani kwa kua Mada hii ni pana na kubwa na hivyo inataka utulivu wa ufaham na

umakini wa kutafakkari basi wacha tuzame zaidi kidogo ili tupate kufaham vizuri zaid.

Ambapo anasema Bahr ul Ilm Abd Allah Ibn Abbas Radhi Allahu Anhu kua:

Mimi nilimwambia Uthman Ibn Affan, hivi kwa ufaham wako ilikuaje Surat Al

Anfal ambayo ni Muthani (Sura yenye aya zisizozidi 100) na Surat Baraa (Surat At

Tawba) ambayo ni Mii'in (Sura yenye aya zaid ya 100) ukaziweka pamoja bila ya

kuandika Biismi Allah Rahmani Rahiim baina yake? Na kisha ukaziweka pamoja

na Sura 7 ambazo ni ndefu zaidi yake?

Uthman Ibn Affan Radhi Allahu Anhu akajibu: Kwa sababu unapita mda mrefu bila ya

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kupokea aya yeyote na kisha baadhi ya Wakati

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam anashushiwa Sura yenye aya nyingi. Hivyo

anaposhushiwa aya basi Humwita mtu anaeweza kuandika na kumwambia: Iweke

Aya hii kwenye Sura inayozungumzia hili na hili ndani yake kisha atashushiwa aya

nyengine na kusema: Iweke aya hii kwenye Sura inayozungumzia hili na hili.

Sasa Surat Al Anfal ni miongoni mwa Sura za Mwanzo zilizoshushwa katika Mji wa

Madinah na Surat Baraa (At Tawba) ni miongoji mwa Sura za Mwisho kushushwa.

Na Maneno yake (Surat At Tawba) yanafanana na maneno ya Surat Al Anfal hivyo

sisi tukadhani kua ni sehemu ya Sura hio (ya Al Anfal) Na kisha Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam akafariki, na haikuwekwa wazi juu yetu kua kama ni

sehemu ya Sura hio ama la. Hivyo ni kutokana na sababu hii ndio tukaweka Biismi


990

Allahi Rahmani Rahim baina yake na tukaiweka pamoja na Sura 7 ndefu (Imam At

Tirmidhii)

Kwani tunapozungumzia Ushushwaji wa Qur'an basi hua tunazungumzia Ushushwaji wa

Aya za Qur'an kuanzia Moja na Kuendelea kwa wakati mmoja au nyakati tofauti.

Ambapo katika Nzima basi hakuna Sura iliyoshushwa nzima nzima isipokua sura 2 tu.

Ambazo ni Surat Al Fatiha na Surat Al Mulk. Na hapo hapo kuna Wanazuoni wasemao

ni Surat Al Fatiha tu peke yake.

Na bila ya shaka katika upangwaji wa aya zake basi ni kama tulivyowahi kusema mara

kadhaa yaani zaidi ya mara 4 nishasema juu ya hili kua Malaika Jibri alikua akimwambia

Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam aya hii iweke sehemu fulani kabla au baada ya

Aya fulani.

Sasa pia tunapozungumzia kuhusiana na hesabu ya idadi ya aya basi pia Masahaba

waliokua wakiandika kutoka kwa Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam kutoka kwa

Malaika Jibril walikua wakiandika na kuifunga aya kulingana na kisomo cha Rasul Allah

Salallahu Alayhi wa Salam na hii ni kulingana na hadith ya Ummu Salamah Radhi Allahu

Anha ambapo anasema Ummu Salamah kua: Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam

alikua akisoma: Bismi Allahi Al Rahmani Al Rahim Al Hamd lillahi Rabbi Al Alamiin

Al Rahmani Al Rahiim, Malik yawm Ad Din (Imam Ahmad)

Hivyo basi ukweli ni kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua hasemi kua Sura

fulani ina aya ngapi isipokua mara moja moja kama kwenye Surat Al Fatiha. Hivyo

Masahaba walikua wakijua kua hapa ndio mwisho wa aya kulingana na namna Rasul

Allah Salallahu Alayhi wa Salam alivyokua akisita anapofika kwenye kituo cha kusitia

kwenye aya na wao hujua kua hapa ndio mwisho wa aya katika kuandika kwao.

Kutokana na hali hio basi ndio maana pia Masahaba wakatofautiana kuhusiana na idadi

ya aya hapo kabla, kwani kama tulivyoona kwenye Mfano jana kua Walipoona aya ni

ndefu sana basi waliigawa mara 2 hadi 3 bila ya kupunguza maneno wala maana ya aya.

Na ndio maana pia kuna baadhi ya Masahaba wakaihesamu Bismi Allahi kua ni sehemu

ya Sura na kuna baadhi wakawa hawakuihesabu kua ni sehemu ya sura kama

tulivyofafanua jana.

Hivyo Qur'an ina aya 6236 lakini kwa wale wanaosema kua Bismi Allahi Al Rahmani Al

Rahim si sehemu ya Sura.

Ambapo kwa wale wanaosema kua ni sehemu ya Sura basi unaongeza Bismi Allahi Al

Rahmani Al Rahim 112 yaani baada ya kuitoa Bismi Allahi Al Rahmani Al Rahim ya Surat


991

Al Fatiha na Bismi Allahi Al Rahmani Al Rahim iliyomo ndani ya Surat At Tawba hivyo

inakua aya 6236+112 = 6348.

Kwani Neno Sara kwa Lugha ya Kiarabu hua linamaanisha Kupanda Mlima au Ukuta,

Kushambulia au Kukimbilia.

Neno Sara ndio lililotoa neno Suratun ambalo hua linamaanisha Heshima, Darja, Cheo,

Alama, Utukufu, Mpangilio wa Mawe au Matofali Katika Ukuta, Jengo zuri linalovutia,

Kitu kizuri kilichokamilika vizuri.

Na Neno Sara ndio lililotoa neno Suratun ambalo hua Jina la Sehemu moja kamilifu

miongoni mwa sehemu 114 kamilifu za Qur’an yaani Sura.

Hivyo Sura za Qur'an zimeitwa Sura kwa sababu:

1-Mtu anaposoma Sehemu hio ya Qur'an basi Hua ni Mwenye Kupanda Darja

kutokana na Malipo yaliyomo ndani yake kutokana na Kuisoma kwake.

2-Kila Sura Moja ya Qur'an ni kama Jengo au Umbo Kamilifu linalojitegemea na

Kupendeza na Kuvutia.

3-Kwa Sababu Hua ni alama inayowakilisha Sehemu ya Qur'an ambayo yenye

Mwanzo wake na Mwisho wake, kulingana na mada husika ndani yake.

Ambapo neno Sura limetajwa ndani ya Qur'an katika Surat Al Baqara pale iliposema:

‏﴿وَإِن كُنْتُمْ‏ فىِ‏ رَيْبٍ‏ ممِّ َّا نَز َّلْنَا عَلَى ٰ عَبْدَِ‏ فَأْتُواْ‏ بِسُورَةٍ‏ مِّن مِّ‏ ثْلِهِ‏ وَٱدْعُواْ‏ شُهَدَ‏ آءَكُم

مِّن دُونِ‏ ٱهلل َِّ‏ إِنْ‏ كُنْتُمْ‏ صَادِقِينَ‏ ﴾

Wa-in kuntum fee raybin mimma nazzalna AAala AAabdina fa/too bisooratin min

mithlihi waodAAoo shuhadaakum min dooni Allahi in kuntum sadiqeena (Surat Al

Baqara 2:23)

Tafsir: Na Kama Nyinyi (Makafiri) mkiwa mnashaka kuhusiana na Tulichomshushia

Mja wetu (Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) Basi Toeni Sura Yenye Mfano

Kama Mithili yake na waiteni Mashahidi wenu (mnaowaabudu) zaidi ya Allah kama

nyinyi kweli ni wakweli.


992

Kwani neno Sura limetajwa tena pale aliposema Allah Subhanah wa Ta'ala:

‏﴿أَمْ‏ يَقُولُونَ‏ ٱفْتَرَاهُ‏ قُلْ‏ فَأْتُواْ‏ بِسُورَةٍ‏ مِّثْلِهِ‏ وَٱدْعُواْ‏ مَنِ‏ ٱسْتَطَعْتُمْ‏ مِّن دُونِ‏ ٱهلل َِّ‏ نِإ

كُنتُمْ‏ صَادِقِينَ‏ ﴾

Am yaqooloona iftarahu qul fa/too bisooratin mithlihi waodAAoo mani

istataAAtum min dooni Allahi in kuntum sadiqeena (Surat Yunus 10:38)

Tafsiri: Wanasema kua ‘(Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) Kaighushi

(Qur’an)’ Waambie (Ewe Muhammad Salallahu Alayhi wa Salam) Basi Leteni Sura

Mithili yake Na Waiteni Muwatakao Zaidi ya Allah Kama nyinyi ni Wakweli.

Kwani Masahaba walikua wakijua kua Sura humaanisha sehemu kamilifu ya Qur'an

kutokana na kua Rasul Allah Salallahu Alayhi wa Salam alikua anaposhushiwa Sura ya

Qur'an basi husema Sasa hivi nimeshushiwa Sura ambayo inasema kadha w kadha w

kadha, na anaposhushiwa aya husema nimeshushiwa aya inasema kadha w kadha w

kadha.

Kwani anasema Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al

Ansari Al Qurtubi kua: ‘Aya Maana yake hua ni Alama, na hua ni Alama kwa sababu

hua ni tofauti kimaneno na maneno yaliyo kabla yake na maneno yaliyo baada yake

na hivyo hua inajitegemea peke yake, Aya vile vile hua inamaanisha kua ni

Uthibitisho au Dalili, na imeitwa Aya kwa sababu Aya hua ni mchanganyiko wa

herufi za Qur'an, na pia imeitwa Aya kwa sababu hua ni Dalili au Uthibitisho wa

kimaajabu ambao hakuna anaeweza kuuiga.’

Na Wanazuoni wa Lugha wametofautiana kuhusiana na asili ya Mzizi wa Neno Aya,

Kwani Imam As Sibawayh basi yeye anasema kua : 'Neno Aya limetokana na neno

Ayaya na kwa sababu Ye ni herufi ambayo ikiwa na Fat-ha kabla yake, basi hua

inageuka na kua Alif basi ndio baada ya Kuitwa Ayay ikawa ni Aya Ambapo kwa

upande wa Imam Muhammad Al Kisai basi yeye anasema kua: 'Mzizi wa neno Aya

ni Ayaya na Ye inapokua na Alif yenye Fat-ha kabla yake basi hua ni kitu kimoja na

zote hua moja na ndio maana ikawa Aya'

Na akasema Imam Al Farra kua: ‘Aya inatokana na Mzizi wa neno Ayaya ambalo hua

linajumuishwa na Alif kutokana kutopendeza kutamkwa Maradufu na hivyo

huitwa Aya’


993

Hapa nataka watu wawe makini tena kwa sababu ndani yake kuna uthibitisho pia wa lile

jambo nililolirudia juzi kulifafanua hapo kabla ambalo ni kuhusiana na idadi ya Aya za

Qur'an na kwanini Masahaba wakatofautiana juu yake.

Kwani ingawa mara nyingi Aya hua ni kikundi cha maneno lakini pia baadhi ya wakati

Aya hua pia ni neno Moja tu na ndio maana Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn

Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi akasema pia Aya hua pia ni

Mchanganyiko wa Herufi za Kiarabu za Qur'an.

Hivyo basi hata neno moja lenye Mchanganyiko wa Herufi za Kiarabu katika sehemu ya

Mwanzo wa Sura za Qur'an hua ni Aya kwa mfano:

Wa Al Fajr, Wa Al Asr, Alif-Lam-Mim Alif-Lam-Sad, Ha-Mim, Ta-Ha, Ya-Sin, Alif-Lam-

Mim-Sad n.k

Hivyo ingawa humu ndani yake mna Harfu Muqataat yaani Harufi zilizotengana kama

Alif-Lam n,k lakini nazo pia hua ni Aya pale inapokua ziko mwanzoni mwa Sura.

Ambapo kwa Upande wa Wanazuoni wa Kufah Iraq basi wao walikua wakisema kua:

Maneno Ha-Mim-Ayn-Sin-Qadf ni Aya Mbili badala ya Moja, yaani Ha-Mim ni Aya

moja na Ayn-Sin-Qaf hua ni aya ya Pili

Hivyo ingawa wengine walikua wanaona kua Ha-Mim-Ayn-Sin-Qaf (Surat Ashuara

42:1)

‏﴿بِ‏ سْمِ‏ اهلل َِّ‏ ٱلر َّحمْ‏ ٰنِ‏ ٱلر َّحِ‏ يمِ۞حم ۤ ‏۞ع ۤ س ۤ ق ۤ ﴾

Kua ni aya moja lakini wao walikua wanaona kua ni aya 2 tofauti na ndio tunavyofuata

sisi leo, kwani tulisema kua Wanazuoni wamekubaliana na Mfumo wa idadi ya Aya wa

Watu wa Kufah, Iraq.

Ambapo hali hii hua pale inapokua mwanzo mwa Sura lakini kama herufi hizi zikiwa

ndani ya Sura basi hua si Aya bali hua ni maneno ya aya, kwani hua zinajumuishwa na

herufi nyenzake ili kukamilisha aya.

Na anasema Imam Abu Amr Ad Dani : ‘Hakika mimi sijawahi kuona Neno Lolote lile

liliomo kwenye Quran ambalo hua linajitegemea peke yake kua ni Aya isipokua

neno: ‘Mud-hammatan’ liliomo katika Surat Al Rahman’


994

Pale iliposema aya ya 55:64 inayozungumzia Bustani za Peponi zenye majani

yaliyonawiri katika aya zifuatazo:

‏﴿فَبِأَىِّ‏ آلا ۤ ءِ‏ رَبِّكُمَا تُكَذِّابَنِ۞مُدْهَآم َّتَانِ۞فَبِأَىِّ‏ آلا ۤ ءِ‏ رَبِّكُمَا تُكَذِّ‏ ابَنِ‏ ﴾

Fabi-ayyi ala-i rabbikuma tukadhdhibani; Mud-hammatani; Fabi-ayyi ala-i

rabbikuma tukadhdhibani (Surat Rahman 55:63-65)

Tafsir :Jee Ni zipi kati ya Neema za Mola wenu nyinyi Mtazikadhibisha?(Majini na

Ibn Adam); Zenye Rangi Ya Kijani Iliyovia; Jee Ni zipi kati ya Neema za Mola wenu

nyinyi Mtazikadhibisha?(Majini na Ibn Adam)

Naam bila ya shaka hakuna neema hata moja kutoka kwa Mola wenu tutakayoweza

kuikadhibisha, isipokua wengi wetu wamo katika hali ambayo inaelezewa na Mujaddid

Ad Din Hujjat Ul Islami, Az Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani Imam Abu Hamid

Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al Shafii kua:

‘Kulikua Na Kijana ambae alikua anatembea Msituni, na mara Ghafla moja

akashtukia amekumbana na Simba uso kwa Uso.

Khofu ikamjaa Kijana na Hivyo akaona aokoe Maisha yake kwa Kukimbia, hivyo

kijana huyo akakimbia kwa kadiri ya uwezo wake wote, akatumia nguvu zake zote

kumkimbia Simba huyo.

Katika kukimbia kwake akaona kua kuna Kisima Mbele yake, hivyo akaamua Bora

Ajitupe ndani yake kuliko kuendelea Kukimbia kisha akaliwa na Simba badala

yake.

Kwani kisima hicho ndio Tegemeo lake peke yake la kuokoa Maisha yake, Hivyo

Kijana akajivuta kuelekea Kisimani na alipokukaribia akaruka na kabla ya kutua

akajikuta kua ni mwenye kuingia kwa kuangukia ndani yake.

Wakati anaanguka ndani yake, mikono yake ikawahi kukamata Kamba iliyokua

ikining'ingia ndani yake.

Alipoikamata kamba akapata afueni na utulivu wa Nafsi yake, kua Alhamd lillah

ameokoka kutpkana na kuliwa na Simba na hivyo boa ilivyokua ananing'inia

kisimani kutokana na kamba aliyoishikilia mkononi, Wakati kijana anamshukuru

Mola wake kutokana na hali ya kuokoka kwake, basi akasikia sauti kutoka ndani

chini kisimani.


995

Kijana akatupa Jicho chini, na Hamad! Akaona Kuna Joka Kubwa ndani chini

Kisimani, Kijana akachanganyikiwa akajiona kumbe hajaokoka, hivyo ili aokoke

basi bora kwake apande juu awe nje ya Kisima Kwani ameshayasahau ya Simba na

anayafikiria ya Joka lilimo Kisimani likimsubiri tu atue chini.

Hivyo Kijana akaangalia juu, ili ajivute kuelekea nje ya Kisima hicho, lakini mara

akaona Panya wawili mmoja mweusi na mwengine mweupe anaitafuna Kamba

yake aliyoikamata na kuitegemea kwa ajili ya kuokoa Maisha yake. Kisha

alipoangalia juu zaid akaona Simba amekaaa anamsubiri ili atoke kisimani awe ni

chakula kwa ajili ya njaa yake.

Hivyo Kijana akataharuki kutokana na kuzidiwa na vishindo vinavyo hisika ndani

ya mwili wake vinavyotokana na mapigo ya Moyo wake kwani utulivu

umemuondoka na amejawa na khofu kutokana na kua katika hali mbaya na ya

hatari ambao inayonekana kutokana na hali ya mazingira yake.

Wakati anafikiria nini afanye mara akili yake ikamwambia aangalie Upande wa

Ukutani, alipoangalia Ukutani akaona Sega lililojaa Asali ambayo inatiririka

taratibu kisimani, Kijana akapeleka Kidole kwenye sega la Asali akakutana na

alipokitoa kilikua kimejaa asali.

Moja kwa moja akakipeleka Kidole hicho Mdomoni kuonja Utamu wa Asali hio na

hapo hapo akasahau kuhusiana na sehemu aliyokuwepo kwenye kamba

anayoning'inia, akamsahau Simba aliejuu, akawasahau Panya wawili Mweupe na

Mweusi wanaoitafuna Kamba hio, na akalosahau hata Joka liliokua linamsubiri

ndani chini kisimani.

Kwani Hujjat Ul Islam Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad

Al Ghazali anaendelea kutuambia kua: ‘Hali aliyokua nayo Ibn Adam Duniani,

ambapo Simba aliekua akimfukuza basi ndio Malakat ul Mawt ambae kila siku yuko

nyuma ya kila mtu katika maisha yake. Joka aliloliona Kisimani ndio Adhabu ya

Kaburini inayomsubiri baada ya kufariki kwake kutokana na maasi yake, na Panya

Mweusi na Mweupe wanaashiria, nyakati za Usiku na Mchana na namna

zinavyokula Uzi wa Uhai wetu hapa Duniani. Na Asali ni mapambo ya Mpito ya

Kidunia yanayomhadaa kila Ibn Adam na kumfanya aisahau Akhera yake na

kuiendekeza Dunia yake’

Mujaddid Ad Din Hujjat Ul Islami, Az Zukhruf Ad Din Imam Al Shafii Al Thani Imam

Abu Hamid Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Tusi Al

Shafii anatuusia cha kufanya ili tusihadaike na Dunia kwa kutuambia kua: ‘Taqwa hua

hua inararua Matamanio na Kuyachafua Mapambo ya Dunia, kiasi ya kua dhambi


996

huonekana kua ni zenye kuchukiza, kama vile Mtu mwenye kupenda Asali

anapochukizwa nayo pale anapoona kua Asali hio imetiwa sumu ndani yake, hivyo

ndivyo Taqwa inavyoyaangamiza Matamanio.

Hivyo Taqwa huidibiti iungo vyako, na huutuliza Moyo wako na kuupa utulivu.

Taqwa huufanya Moyo utupilie mbali Kiburi, Kujiona, Kua na wivu na kuuwacha

ukiwa na khofu juu ya Mola wake. Na hivyo Moyo hua hua unajihesabia makosa

yake na kuanza kufuatilia kuhusiana na maslahi yake ya baadae kwa kutafakkari

ndani yake na kujiangalia na hivyo Moyo hua ni wenye kuthamini kila mda na

wakati uliopo mbele yake.’

Na amesema Allah Subhanah wa Ta’ala kua:

‏﴿مح َُّم َّدٌ‏ ر َّسُولُ‏ ٱهلل َِّ‏ وَٱل َّذِينَ‏ مَعَهُ‏ أَشِ‏ د َّآءُ‏ عَلَى ٱلْكُف َّارِ‏ رُحمََآءُ‏ بَيْنَهُمْ‏ تَرَاهُمْ‏ رُك َّ عاً‏

سُج َّداً‏ يَبْتَغُونَ‏ فَضْلاً‏ مِّنَ‏ ٱهلل َِّ‏ وَرِضْوَاً‏ سِ‏ يمَاهُمْ‏ فىِ‏ وُجُوهِهِمْ‏ مِّنْ‏ أَثَرِ‏ ٱلس ُّجُودِ‏

ذٰلِكَ‏ مَثَلُُهمْ‏ فىِ‏ ٱلت َّوْرَاةِ‏ وَمَثَلُهُمْ‏ فىِ‏ ٱلإِنجِيلِ‏ كَزَرْعٍ‏ أَخْرَجَ‏ شَطْأَهُ‏ فَآزَرَهُ‏ فَٱسْتَغْلَ‏ ‏َظ

فَٱسْتَوَىٰ‏ عَلَى ٰ سُوقِهِ‏ يُعْجِ‏ بُ‏ ٱلز ُّر َّاعَ‏ لِيَغِيظَ‏ هبِِمُ‏ ٱلْكُف َّارَ‏ وَعَدَ‏ ٱهلل َُّ‏ ٱل َّذِينَ‏ آمَنُواْ‏

وَعَمِلُواْ‏ ٱلص َّ الحَِاتِ‏ مِنْهُم م َّغْفِرَةً‏ وَأَجْ‏ راً‏ عَظِيماً‏ ﴾

Muhammadun rasoolu Allahi waalladheena maAAahu ashiddao AAala alkuffari

ruhamao baynahum tarahum rukkaAAan sujjadan yabtaghoona fadhlan mina

Allahi waridhwanan seemahum fee wujoohihim min athari alssujoodi dhalika

mathaluhum fee alttawrati wamathaluhum fee al-injeeli kazarAAin akhraja shatahu

faazarahu faistaghladha faistawa AAala sooqihi yuAAjibu alzzurraAAa

liyagheedha bihimu alkuffara waAAada Allahu alladheena amanoo waAAamiloo

alssalihati minhum maghfiratan waajran AAadheeman(Surat Al Fat-h 48:29)

Tafsir: Muhammad ni Rasul Allah na wale waliokua pamoja nae ni wakali dhidi ya

Makafiri na ni wenye kuhurumiana miongoni mwao, hakika mnawaona wao

wakirukuu na kusjudu wakitafuta rehma za Allah na Fadhila zake. Alama walizokua

nayo kwenye mapaji ya Nyuso zao zinatokana na athari ya kusujudu kwao, huu ndio

utambulisho wao kwenye Tawrat lakini utambulisho wao kwenye Injil hua ni kama

mbegu inayochipua na kua imara na kua nene na kusimamia kwenye shina lake na

kumfurahisha mkulima na hivyo kua ni mwenye kwa kukasirisha Makafiri kutokana


997

nayo. Allah amewaahidi wale walioamini na kufanya mema na usamehevu na malipo

yaliyo bora zaidi.

Wa Billahi Tawfiq


998

MARUDIO YA VITABU VILIVYOTUMIKA KATIKA KITABU HIKI:

AL BURHANI FII ULUM UL QUR’AN – Shaykh Islami Imam Abu Abd Allah Badr

Ad Din Muhammad Ibn Abd Allah Ibn Bahadir Al Zarkashi Al Shafii.

AL DIWAN AL IMAM AL SHAFII – Mujaddid Ad Din Imam Abu Abd Allah

Muhammad Idris Al Shafii.

AL HAWI AL KABBIR FII FIQH MADHHAB AL IMAM AL SHAFII - Imam Abu

Hasan Ali Ibn Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al Shafii

AL ITQAN FII ULUM UL QUR’AN – Mujaddid ud Din ImamAbu Fadhl Abd Rahman

Ibn Kamal Al Din Abi Baqr Ibn Muhammad Ibn Sabiq Al Din Jalal Ad Din Al Misri Al

Suyuti Al Shafii.

AL MUTAMMAD FI FIQH UL SHAFII – Imam Muhammad Al Zuhayly Ad Dimashq

Al Shafii.

AL RISALAT AL QUDSIYYAH FII QAWAID AL AQAID – Hujjat ul Islami Mujaddid

Ad Din Imam Abu Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al

Shafii.

AR RUH AL MAÁNI FI TAFSIR AL QURAN AL ADHIM WA SABAA AL

MATHANI - Imam Abu Al Thana Shihab Din Sayyid Mahmud Ibn Abd Allah Al Husayn

Al Alusi Al Baghdadi Al Hanafi.

ARAIS FI MAJALIS FI QASAS AL ANBIYAH – Imam Abu Is-haq Ahmad Ibn

Muhammad Ibn Ibrahim Al Thalabi Al Shafii.

BAYAN AL FARQ BAYN AL SADR WA AL QALB WA AL FUAD WA AL LUBB -

Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Ali Ibn Hasan Ibn Bashir Al Hakim Al Tirmidhi

Al Shafii.

FAYDHUL AL QADIR – Imam Muhammad Abdur Rauf Bin Taj Al Arifin Ibn Ali Bin

Zainal Abidin Ibn Yahya Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Ibn Ahmad

Ibn Makhluf Ibn Abd Salam Al Hadadiy Al Munawiy Al Qahiriy Al Misriy Al Shafii

FUSUS AL HIKAM – Shaykh Al Akbar Muhyi ad Din Imam Abu Bakar Ibn Arabi Al

Andalus Al Maliki.

HUJJAT UL BALIGHA - Mujaddid ud Din Qutb Ad Din Imam Ahmad Shah Waliyyu

Allah Ibn Abd Rahman Ibn Umar Ad Dahlawi.

INSAN UL UYUNI – Al Imam Al Ulamaa Imam Al Burhan Din Al Halabi.

JAMI’I LI AHKAM AL QUR’AN - TAFSIR AL QURTUBI - Imam Abu Abd Allah

Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abu Bakr Al Ansari Al Qurtubi.

KASHF AL ASRAR WA UDDAT AL ABRAR – Imam Rashid Al Din Al Maybudi.

KITAB AL ARBAIN FI USUL AD DIN - Hujjat ul Islami Mujaddid ad Din Imam Abu

Hamid Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Shafii.

KITAB JAWAHIR AL QUR’AN - Hujjat ul Islami Mujaddid ad Din Imam Abu Hamid

Muhammad Ibn Muhammad Ibn Muhammad Al Ghazali Al Shafii.

MASNAWI NURIYA - Baddiuzzamman Said Nursi Al Turkiy Al Hanafi.


999

MISHKAT UL MASABIH – Shaykh Waliuddin Abu Abdullah Al Khatib Al Tibrizi Al

Hanafi.

MUFRADAT FI GHARIB AL QURAN - Allamah Abu Qasim Ibn Husein Ibn Mufadal

Ibn Muhammad Raghib Al Isfahani.

QISAS AL ANBIYAAH- Allamah Nasiruddin Burhan Ad Din Al Rabghuzi.

RISALAT AL QUSHAYRIYAH - Imam Jamal Islam Abu Qasim Abd Al Karim Ibn

Hawazin Al Qushayri

RISALE NURI - Baddiuzzamman Said Nursi Al Turkiy Al Hanafi.

TAFHIM AL QURAN – Allamah Sayyid Abu Ala Mawdudi Al Hanafi.

TAFSIR AL KABIR – MAFATIH AL GHAYB – Sultan al Mutakallimin Mujaddid ud

Din Imam Abu Abd Allah Muhammad Ibn Umar Ibn Al Husayn Al Taymi Al Bakri Al

Tabaristan Fakhr Ad Din Al Razi Al Shafii.

TAFSIR AL KASHSHAF AN TAHQIQ AL TANZIL - Sultan Al Balagha Jarrah Allah

Imam Abu Al Qasim Mahmud Ibn Umar Ibn Ahmad Al Zamakhshari Al Hanafi Al

Mutazila.

TAFSIR AL MAWARDI AN NUQAT WA AL UYUN - Imam Abu Hasan Ali Ibn

Muhammad Ibn Habib Al Mawardi Al Shafii.

TAFSIR AL QURÁN AL ADHIM – Imam Abu Muhammad Sahl Ibn Abdallah Al

Tustari Al Shafii.

TARIKH AL RUSUL W AL MULUK– Imam Abu Jafar Muhammad Ibn Jarir at Tabari

Al Shafii.

TAFSIR AL QASIMI AL MUSSAMA MAHASIN AL TA’WIL- Imam Jamal Al Din

Muhammad Al Qasimi Al Dimashq.

TARIKH AL KHULAFA – Mujaddid ud Din Imam Abu Fadhl Abd Rahman Ibn Kamal

Al Din Abi Baqr Ibn Muhammad Ibn Sabiq Al Din Jalal Ad Din Al Misri Al Suyuti Al

Shafii.

MARUDIO YA MITANDAO ILIVYOTUMIKA KATIKA KITABU HIKI

www.aliftaa.jo

www.dar-alifta.org

www.eshaykh.com

www.islamqa.org

www.muftiwp.gov.my

www.seekersguidance.com

www.shafiifiqh.com

www.sunnahmuakada.wordpress.com

www.questionsonislam.com

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!