You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
www.annuurpapers.co.tz

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1049 MUHARRAM 1434, IJUMAA DES. 14 - 20, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Ubaguzi katika elimu

wazidi kubainishwa

’Zubeda’ wa Divisheni 1 alinyimwa nafasi F5

Ustadh Monsignor Pengo anapotosha ukweli

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kushoto) akiwa na Ustadh Shaaban Mapeyo (kulia).

Sheikh Ponda Issa bado

yupo rumande Segerea

Sheikh wa Bakwata atoa ushahidi

Aliyeuziwa kiwanja naye ajieleza Uk. 12

TATU alikosa nafasi shule

kwa sababu jina lake

lingine Zubeda ambalo

kabisa ni la Kiislamu.

Kwa kuwa Bint Shaaban,

Binti wa Kitanzania

inayodaiwa kutokuwa na

udini, alinyimwa nafasi ya

KOMANDO! Komando!

Komando! Kibwagizo hiki

ni cha kuwahadaa watu

na kuihadaa hadhira,

ili iweze kuamini kuwa

watu hao ni waumini wa

dhati wa Raisi Mstaafu

wa Zanzibar wa CCM

mwaka 1990- 2000,

Salmin Amour.

Huyu Salmin alipendelea

mwenyewe jina la Komando,

kutokana na hulka yake ya

kukosa uvumilivu dhidi ya

wapinzani hasa, CUF.

Kuthibitisha imani hiyo

ni pale alipowapeleka jela

bila ya hatia, Viongozi 20

wa Chama cha Wananchi,

CUF.

Vibaraka wahafidhina

wanachohitaji ni CCM

Zanzibar kutawaliwa na

“Komando”.

Ili hatimaye asisalimike

yeyote kutokana na makucha

Anachotaka

Borafya katu

hakiwezekani

Uk. 3

kusoma kidato cha 5 pamoja

na kuwa na DIVISHENI

ONE!!!

N a h u o n i w a k a t i

wa Mwalimu Nyerere

anayetukuzwa leo kwamba

eti aliondoa udini!

(Soma Uk. 8)

CCM wasaliti wa Zanzibar

wajificha kwa Komandoo

Sikiliza anachosema Bi Fatma Karume

Wahafidhina wasirejeshe chuki, mikwaju

RAIS mstaafu wa SMZ

Amani Abeid Karume

ya chuma wanayostahiki.

H a o n d i o w a l e

waliokasirishwa mno na

hotuba ya Amani Abeid

Karume na waliamua

kuirarua na kuichanachana

Picha kubwa ya Karume

iliyokuwapo Michenzani,

Zanzibar.

(Soma Uk. 7)
2

AN-NUUR

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM.

www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top

Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Miaka 51 ya kutumia uhuru vibaya

JUMAPILI ya wiki

iliyopita, Tanzania bara

walisherehekea miaka 51

tangu upatikane uhuru

kutoka kwa mkoloni

Muingereza.

Sherehe zilifanyika pale

Uwanja wa Uhuru, na

kuhudhuriwa na Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania na Amir Jeshi

Mkuu Jakaya Mrisho

Kikwete.

Aidha alikuwepo Rais

wa Zanzibar, Dk. Ali

Mohammed Shein na

viongozi wengine wa ngazi

mbalimbali za kiserikali,

vyama vya kisiasa na

taasisi za kijamii.

Sherehe kwa kiasi

kikubwa zilichagizwa na

burudani za ukakamavu,

hususan magwaride ya

vikosi vya Majeshi ya

Ulinzi na Usalama.

Hata hivyo tunadhani

k w a m b a w a k a t i

tunasherehekea hiyo miaka

51 ya uhuru, kwa kiasi

kikubwa uhuru wenyewe

umetumika vibaya kwa

walio wengi.

T u n a s e m a h i v y o

kutokana na kuwepo

k w a o m b w e k u b w a

kati ya viongozi na

wanaoongozwa, matajiri

n a m a s k i n i , w e n y e

elimu na wasio bahatika

kuipata, wanaodhulumu

na wanaodhulumiwa.

Miaka 51 baada ya

uhuru tunashuhudia

Watanzania ambao wengi

ni maskini, makabwela,

wavuja jasho na walala

hoi, wakitakiwa kutoa kitu

chochote wanapohitaji

kupata huduma za msingi

katika taasisi nyingi za

huduma za kiserikali.

Wa k a t i h u o h u o ,

tunashuhudia wanaofuja

kikweli kweli matunda ya

uhuru, wakipewa huduma

hizo kwa haraka na kwa

wakati, tena kwa adabu

na kwa unyenyekevu

mkubwa, na wakati huo

huo hakuna anayethubutu

kudai chochote kwa watu

wa kaliba hii japo wao ndio

wenye ukwasi.

Wakati mtoto wa mlala

hoi akihaha kusaka ajira

baada ya kumaliza elimu

zao kwa taabu kutokana na

umasikini wa wazazi wao,

watoto wa wafuja uhuru

hupeana vyeo na nafasi

katika asasi za kiserikali

na kwenye mashirika

makubwa, bila shaka si

kwa sababu ya ujuzi au

elimu zaidi, bali ni kwa

sababu tu ya kutumia nafasi

za wazee wao, ambao ndio

vinara wa kufuja uhuru

wenyewe.

Watoto wa makabwela

wanaambiwa, mtaji wa

masikini ni nguvu zake.

Wanahamasishwa kujiunga

vicoba, saccos, vibindo

nk. kwa kuwa nafasi

wanazotaka zina wenye

uhuru wao.

Tunaona hata katika

huduma za afya, kwenye

v y o m b o v y a s h e r i a

mahakamani, vyombo vya

dola kama polisi, huko

wananchi wanalia kuwa

hakuna haki. Umekuwa ni

mtindo wa mwenye nguvu

mpishe. Mwenye cheo

na mwenye pesa ndiye

mwenye ‘haki’ na mwenye

‘sheria’.

Kwa utaratibu huu,

imekuwa miaka 51 ya

uchungu na makali ya

maisha ndani ya uhuru.

Kuna haja ya suala hili

kutizamwa kwa uzito wake.

Ifikie mahali, Watanzania

waishi maishi ya heshma

kuanzia uwezo wa kupata

mahitaji muhimu ya

kimaisha na pia kupata

haki zao za kibinadamu na

za kiuwananchi.

Vi o n g o z i w a a c h e

kujitizama tu, watizame

nchi na wananchi. Ifikie

mahali kila anayemaliza

muda wake wa uongozi,

a j i v u n i e m a z u r i

aliyowafanyia wananchi,

na wananchi watamani

lau angeendelea afanye

mengi.

Tahariri/Matangazo

AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

KAMATI YA KUENDELEZA UISLAMU TANZANIA

TAMASHA LA KANDA YA KASKAZINI,

MASHARIKI NA VISIWANI KIRINJIKO - SAME

21 – 26 DESEMBA, 2012

Waislamu wote wa Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga,

Morogoro, Dar – es – Salaam, Pwani na Visiwa vya Unguja na

Pemba wanaalikwa kuhudhuria Tamasha la Ujenzi wa Chuo

cha Ualimu na Ufundi Kirinjiko litakalofanyika 21 – 26 Desemba,

2012.

Shime Waislamu tujitahidi kuhudhuria kwa wingi. Wasio na

wasaa wa kuhudhuria wachangie fedha na vifaa vya ujenzi.

Tukumbuke, tukifanya hivyo tutakuwa tumefanya biashara na

Allah (s.w) kwa mafanikio ya hapa duniani na malipo ya Pepo

– Qur’an (61:10-13)

Wabillah Tawfiiq

AMIR

MKUZO ISLAMIC HIGH SCHOOL

P.O. Box 346, Songea Tel: +255 - 716791113, +255683155902 Email:

mkuzoipc@rocketmail.com

NAFASI ZA KIDATO CHA I - 2013

Waislamu wote mnatangaziwa nafasi za kidato cha

kwanza katika shule ya sekondari ya Kiislamu Mkuzo

iliyopo Songea mkoani Ruvuma.

Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 28/12/2012 na

usaili utafanyika tarehe 29/12/2012 katika vituo vya

mtihani vilivyoorodheshwa kwenye fomu ya maombi.

Wahi kuchukua fomu mapema, nafasi zimebakia

chache.

NB: KWA WALE WALIOCHAGULIWA WAFUATE

MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA SHULE (JOINING

INSTRUCTION) KATIKA VITUO WALIVYOFANYIA

USAILI.

Kwa maelezo zaidi piga simu: 0716 791113,

0683155902.

MKUU WA SHULE
3

Habari

AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

Anachotaka Borafya katu hakiwezekani

Na Mwandishi Wetu

A N A C H O T A K A

Mwenyekiti wa CCM wa

Mkoa wa Mjini, Borafya

Silima, katu hakiwezekani,

wamesema wachambuzi

wa siasa za Zanzibar.

Wa c h a m b u z i h a o

w a m e s e m a k u w a ,

unaposema kuwa unataka

muungano wa serikali mbili,

huwezi tena kuja na hoja ya

kutaka Rais wa Zanzibar

kuwa na mamlaka sawa na

yule wa muungano.

Maoni na uchambuzi huo

umekuja kufuatia maoni

aliyotoa Mwenyekiti huyo

wa CCM, Mjini Unguja

akisema kuwa anataka

Serikali Mbili, ya Muungano

na ya Zanzibar, lakini kila

Serikali iwe na mamlaka

yake kamili.

Mheshimiwa Borafya

alitoa maoni hayo katika

Uwanja wa Alabama,

Shehia ya Miembeni katika

mfululizo wa zoezi la

kupokea maoni ya wananchi

juu ya katiba mpya.

Kwa mujibu wa taarifa

zilizonukuliwa na baadhi ya

vyombo vya habari, katika

maoni yake mheshimiwa

Borafya amesema pia

a n a t a k a w a e n d e l e e

kuwepo Marais wawili,

wa Muungano na wa

Zanzibar.

Hata hivyo akasisitiza

kuwa, Marais wote wawili

wawe na hadhi sawa na

wawe na mamlaka kamili.

Huku akimalizia kwa

kusema kuwa anahimiza

umoja na mshikamano.

Ni kwa maoni yake

hayo wachambuzi wa

mambo wanasema kuwa

unaposema uwe na serikali

mbili, ya muungano na ya

Zanzibar, ni wazi kuwa

Rais wa Zanzibar atakuwa

chini ya Rais wa Muungano

na serikali ya Zanzibar

lazima iwe chini ya ile ya

muungano.

“Ile serikali, ile nchi,

iliyoungana na Zanzibar,

ndiyo inayoweza kuwa na

hadhi sawa na Zanzibar,

kisha juu yake iwepo hiyo

ya muungano, lakini kwa

maoni haya ya serikali mbili,

inakuwa ni kiini macho au

kujidanganya kutaka Rais

wa Zanzibar awe sawa na

wa muungano.”

Amesema mchambuzi

mmoja ambaye amehoji,

“ipo wapi hiyo nchi

inayoungana na Zanzibar na

hiyo serikali inayoungana

na ya Zanzibar ili izaliwe

ya muungano?”

K a t i k a k u f a f a n u a

a k a s e m a k u w a

kinachoonekana hapa ni

kuwa wale walioungana

na Zanzibar wamekuwa

wajanja zaidi ambapo

wamejivisha joho la

muungano na hivyo Rais

wao kuwa ndiye wa

muungano na kuwa juu ya

Zanzibar.

Mchambuzi huyo ambaye

hata hivyo hakutaka kutaja

jina lake akasema kuwa

ili Zanzibar iweze kuwa

na mamlaka na kuwa Rais

mwenye hadhi, hoja ya

kuwa na ama serikali tatu

au muungano wa mkataba

haiwezi kuepukika.

“Ni lazima itambulike

kwanza nchi inayoungana

na Zanzibar ikiwa na serikali

yake kama inavyotambulika

ya Zanzibar, ndio uweze

kuzungumzia kuwa na

serikali mbili na marais

wawili wenye hadhi,

mamlaka na haki sawa ndani

ya muungano, kinyume cha

hivyo ni kiini macho na

kujidanganya.” Alisisitiza

akimalizia maoni yake.

N i k u t o k a n a n a

uchambuzi huo baadhi ya

wananchi waliomsikiliza

kada huyo wa CCM akitoa

maoni yake wanasema

kuwa alichofanya mwana

CCM huyo ni kuunga

mkono msimamo wa wale

wasiotaka muungano wa

serikali mbili, lakini bila ya

kutamka.

“La kufurahisha ni kuwa

pamoja na kukwepa neno

Muungano wa Mkataba,

lakini sasa viongozi

wahafidhina wa CCM nao

wanaungana na Wazanzibari

kutaka mamlaka kamili.

Sisi tunawaambia wasiwe

na wasiwasi, tuko pamoja

katika kutetea haki za nchi

yetu tukufu ya Zanzibar.

Pamoja Daima.” Amesema

m t o a m a o n i m m o j a

akichambua kile alichosema

Borafya.

MWENYEKITI wa CCM wa Mkoa wa Mjini, Borafya Silima.

Mkutano Baraza Kuu kufanyika Kisarawe

Kuzindua Chuo cha Maimam nchini

Na Bakari Mwakangwale

BARAZA Kuu la Jumuiya

na Taasisi za Kiislamu (T),

lipo mbioni kujenga Chuo

Cha Maimam kitakacho

kuwa kikitoa mafunzo

ya uongozi kwa Maimam

nchini.

C h u o h i c h o

kitakachojulikana kwa jina

la Muhaga Imams Collage,

k i t a j e n g w a W i l a y a n i

Kisarawe, katika Mkoa wa

Pwani, kikilenga kuwaandaa

viongozi wa Waislamu

kuanzia ngazi ya mtaa.

U s t a d h i A b u b a k a r i

Abdulswamadu, amebainisha

hayo akiongea na gazeti

hili, katikati ya wiki hii,

akizungumzia mkutano

Mkuu wa Baraza Kuu la

Jumiya na Taasisi za Kiislamu

(T) utakaofanyika Muhaga,

Kisarawe, kuanzia Desemba

14-21, mwaka huu.

Abdulswamad, aliye

Mkurugenzi wa Uchumi

Mipango na Fedha wa

Baraza Kuu, alisema lengo

la kuanzisha Chuo hicho

ni kuandaa viongozi wa

Waislamu wakianzia kwa

Maimam, kwa kuwa wao ndio

viongozi wa daraja la chini na

muhimu kwani ndio viungo

kati ya waumini na viongozi

wa ngazi za juuu.

Alisema, mikakati hiyo ni

kutokana na kile alichodai,

kama kufeli kwa mipango

na mikakati ya Waislamu

kwa muda mrefu hivyo na

kubaini kwamba huenda ni

kwa kukosa viongozi wenye

kujua malengo kuanzia ngazi

ya chini.

Alisema, Maimamu ni

viongozi muhimu kwa jamii

ya Kiislamu kwani wao ndio

muda mwingi wanakuwa na

Waislamu kwa kukutana nao

mara tano kwa kutwa nzima,

katika Misikiti.

Alisema, Baraza Kuu

limeona endapo Maimam

watakuwa na taaluma ya

uongozi na uratibu wa

mipango na namna gani ya

kuwatumia Waislamu kwa

kuwapa mipango maaluma

ya kimaendeleo bila shaka

jamii ya Waislamu itapiga

hatua kwa haraka.

“Lengo la kuanzisha Chuo

Cha Maimam, ni kuwaanda

kuwa viongozi bora wajue

n a m n a y a k u o n g o z a ,

(utawala) wasiishie kuwa tu

na uhodari wa kusoma Qur

an vizuri wanaposwalisha.”

Alisema Abdulswamadu.

Akizungumzia mkutano

huo, alisema mkutano

utafanyika Desemba 21,

mwaka huu, katika kijiji cha

Muhaga, Kisarawe, ambao

utatanguliwa na Mkutano

Mkuu wa Kutayba Saccos,

Desemba 20.

Alisema, kufuatia mipango

na utaratibu huo, Waislamu

kutoka Jijini na Mikoani

wataanza kuelekea huko

(Kisarawe) kuanzia Desemba

14, Ijumaa ya wiki hii (leo),

kwa ajili ya kupiga kambi na

kujiandaa na mikutano hiyo.

Wakiwa huko sambamba

na kufanyia usafi viwanja

hivyo lakini kwa kipindi

chote hicho cha wiki moja

k a b l a y a k u a n z a k w a

mikutano hiyo, Waislamu

kwa ujumla watapata semina

elekezi kutoka kwa viongozi

(Masheikh) wao kutoka

katika Jumuiya na Taasisi

mbalimbali za Kiislamu

nchini.

Alisema, lengo la kuupeleka

Kisarawe, Mkutano Mkuu wa

Baraza Kuu, ni kuwaonyesha

Waislamu ardhi zao zilizo

chini ya Baraza hilo, na

kuweka mipaka baada ya

kufanyika kwa usafi, ili

wawe tayari kuilinda na

kuisimamia.
4

(i) WANAUME

Na JINA MKOA

1 IDDI R. NANA SINGIDA

2 HAMIS J. CHURY SINGIDA

3 OMARY MUSA KANIKI TANGA

4 OMAR S. WAWA SINGIDA

5 YASIN J. RAMADHAN SINGIDA

6 ISMAIL S. MALUNGA SINGIDA

7 YUNUS A. HASSAN SINGIDA

8 RAMADHAN I. MWIRU SINGIDA

9 WAZIRI SEKA TANGA

10 AHMAD K. MENGI KIGOMA

11 ISMAIL H. KULANDEA SINGIDA

12 ABDILLAH SULEIMAN SINGIDA

13 ISHAKA A. NYAMGUNDA DAR ES

14 ALI MOHAMED AMEIR UNGUJA

15 KHALFANI U. YUSUFU KIGOMA

16 JUMA K. SALAZA KIGOMA

17 JUMA JUMANNE SINGIDA

18 MOHAME A. HASSAN PWANI

19 MAHMOUD A. CHANDE RUVUMA

20 HAMZA MAJIDI SHABANI DODOMA

21 MWAZINI BAKARI MAHAMUDA UNGUJA

22 MAHAMUD J. MOHAMADI SINGIDA

23 ABDULLAH SALEH HASSAN UNGUJA

24 MUSTAFA J. ALI MTWARA

25 ABDALLAH HAMIDU MATA DAR ES

26 ABDUMAJID S. MOHAMED KAGERA

27 BASHIRI M. ATHUMAN SINGIDA

28 ALLY H. KIDUMWU SINGIDA

29 ABAS-ABDULRAHMAN SWALEHE ARUSHA

30 ABDILLAH M. LALI SINGIDA

31 KHALID KASSIMU DULLE MANYARA

32 HAMIS HALIFA PIRI DODOMA

33 MAKAME M. AHMAD PWANI

34 HAJI S. ALLY SINGIDA

35 ABDILLAHI HAMIS ARUSHA

36 SHABANI ALLY ISSANI MANYARA

37 BASHIRU OMARI HAMIS DODOMA

38 MOHAMED M. YASIN KIGOMA

39 ALLY M. SAID SINGIDA

40 AL-JABIR H. MSUKUYA SINGIDA

41 KUMSONI J. KUMMALA MTWARA

41 RAMADHANI TENA OMARI

43 SHABAN JUMA FAKI UNGUJA

44 KASSIMU RAJABU

45 MOHAMED R. MWIRU SINGIDA

(ii) WANAWAKE

Na JINA MKOA

1 KURUTHUM OMARY SINGIDA

2 KANJELU MUHAMMED RAJABU SINGIDA

3 AMINA HUSSEIN SINGIDA

4 MAIMUNA R. OMARY TABORA

5 CHIKU S. KANGARA SINGIDA

6 LINDA HUSSEIN MUSSA

7 JAMILA SUDI SINGIDA

8 HUSNA O. MUKHANDY SINGIDA

9 AMINA RAJABU SINGIDA

10 FADHILA M. MAJENGO SINGIDA

11 HIDAYA OMARY SINGIDA

12 ZAMDA I. MTUHI MTWARA

13 REHEMA J. JUMA MANYARA

14 NASRA MUNDA SINGIDA

15 ZENA M. RUGAYA KIGOMA

16 MARIAM H. SWALEHE SINGIDA

17 SHEJUNA MBWANA HUSSEIN

18 MARIAM FADHILI MNDEME ARUSHA

19 AISHA MUSSA MAULID ARUSHA

20 MWANAIMA H. CHAYOA ARUSHA

21 ZAITUNI JUMA RAJABU SINGIDA

22 TATU K. NYONI RUVUMA

23 NICE J. LUTWE KIGOMA

24 KHADIJA I. SENGE SINGIDA

25 PILI A. JUMANNE SINGIDA

26 KHADIJA VUAI HASSAN UNGUJA

27 DIA HASSAN LINDI

28 ASIA OMARY JUMA ARUSHA

29 FAUDHIA J. ALI DAR ES

30 ASHURA M. HAMIS KIGOMA

31 PILI H. LISU SINGIDA

32 ZUHURA ABDULRAHMANI KANGILE

33 TIMA OMARY HAMIS TANGA

34 ASHURA A. ANTHONY MOROGORO

35 TWAINA HAMIS SINGIDA

36 AISHA O. BENDERA TANGA

37 MWANAIDI S. MBIAJI SINGIDA

38 SHEILA MMARI

39 MWANAIDDY IDDY RAMADHANI ARUSHA

40 NZAINABU MWASHONGO

41 NASRA J. SALUM SINGIDA

42 ZAINABU ABUBAKAR SINGIDA

43 RUSMA A. AMASI SINGIDA

44 FARIDA JUMA SINGIDA

45 HABIBA H. IGAE SINGIDA

46 ZAKIA H. ATHUMAN SINGIDA

Tangazo

AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

Bismillaahir Rahmaanir Rahiim

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

MATOKEO YA USAILI WA WAOMBAJI WA MAFUNZO YA UALIMU KATIKA VYUO VYA UALIMU VYA IPC

Wafuatao wamafaulu usaili na wamechaguliwa kujiunga na Mafunzo ya muda mfupi ya Ualimu yatakayoanza mwishoni mwa Januari ,2013

katika vyuo vya Ualimu vya Kiislamu Kirinjiko na Ubungo.

Barua za maelekezo ya kujiunga na chuo (joining instructions) yanapatikana vyuoni na katika vituo walikofanyia usaili mikoani.

A: CHUO CHA UALIMU CHA KIISLAMU KIRINJIKO

47 AMINA M. MASUDI SINGIDA

48 AMINA S. KWIMBA SINGIDA

49 KHADIJA UBWA ALI UNGUJA

50 AMINA JUMA MGALA

51 MARYAM ABDALLAH MUHAMMAD DAR ES

52 ZAINAB JAMAL

53 SAIDA A. NDUI SINGIDA

54 AISHA S. HUSSEIN SINGIDA

55 SUKAINA ALLY KHALIFA DAR ES

56 RAHMA HAJI MOHAMED UNGUJA

57 SALMA YAHYA MKILINDI

58 MARIAM KADHI TANGA

59 SUMMAYA M. SULEIMAN DAR ES

60 AZIZA M. MTONDOHIMA DAR ES

61 BIMKUBWA K. AMOUL DAR ES

62 MWANTUMU BAKARY TANGA

63 KHADIJA HUSSEIN MAURIDI

64 RAMLA HASSAN AYUBU ARUSHA

65 MWAJUMA A. IBRAHIM TANGA

66 LULU JUMANNE SINGIDA

67 HADIJA MBARUKU TANGA

68 SICHANA SIMAI MOHAMED UNGUJA

69 ASHA SALEHE MKILINDI

70 ZAMZAM RAMADHANI GOMBO

71 AMINA M. MANGU SINGIDA

72 AISHA K. MITAGO MOROGORO

73 MWAJUMA HAMISI ABEID DODOMA

74 PATIMA ALI MRIDU

75 TAUSI O. RASHID MWANZA

76 JOHARIA HAMIS SINGIDA

77 ZULPHA SHABANI RAMADHANI SINGIDA

78 HAWA K. MOHAMED KIGOMA

79 SWIVAMU R. DUDE SINGIDA

80 ZANURA S. HAMIS SINGIDA

81 AMINAH. O. SALUM KUWAKA DAR ES

82 MWAJUMA A. MKWAHA MTWARA

83 ASIA SAIDI LUBUVA DODOMA

84 FATUMA BARAZA MANYARA

85 SUMAIYA MSANGI

86 SWALHA N. KASAGOLA SHINYANGA

87 TATU R. LUAMBANO RUVUMA

88 NURIAT H. ABRAHAMAN SINGIDA

89 ASHA RAMADHANI DUMA DODOMA

90 MAIMUNA SALIMU RAJABU

91 SOFIA IDDI KIMUNGU RUKWA

92 SOFIA A. NYONYI SINGIDA

93 ASHURA J. ALLY SINGIDA

94 FATMA MUSSA KIMARO

95 ZAINAB MUSTAFA HASSAN DODOMA

96 MAIMUNA A. ATHUMANI ARUSHA

97 HIDAYA HAMISI SALIMU

98 ZAINABU JUMANNE OMAR SINGIDA

99 ASIA JUMA JULA MANYARA

100 MARIAM B. HAMIS ARUSHA

101 FATUMA YAHAYA RUKWA

102 TABU Y. BAKARI SINGIDA

103 SHANIFA R. SAID SINGIDA

104 REHEMA ABBAS MOROGORO

105 NAHIDA HUSSEIN HAMZA

106 FARIDA J. KISUDA SINGIDA

107 WIDADU MOHAMED RAMADHANI ARUSHA

108 SHUFAA MUSSA IDDY ARUSHA

109 HAWA MUSSA MOHAMMED ARUSHA

110 RAMLA ISMAILI

111 ASHA BAGHAMOYO MANYARA

112 MARYAM L. JUMA

113 MWAJUMA BAKARI MANYARA

114 HAFSWA SULAYMAN PWANI

115 HALMA K. RASHID DAR ES

116 ZIADA S. RUSAMBO RUKWA

117 FATUMA S. RUVAKO TABORA

118 BINZUA HAJI MUSSA

119 KHAIRATH A. SULEIMAN ARUSHA

120 SAUDA YUSUFU JUMA DODOMA

121 RAHMA JUMANNE MANGI MANYARA

122 MWAJUMA SALIMU MADEGHE

123 SALAMA S. KAMBI TANGA

124 HAWA ABDALLAH SINGIDA

125 ZUBEDA R. HEMED TANGA

126 MWANAKHAMIS H. MOHAMED PWANI

127 MWANAHARUSI SWALEHE TANGA

128 RUKIA MOHAMEDI SINGIDA

129 PILI H. BUHULU SINGIDA

130 AMINA RAMADHANI MATEMANGA MOROGORO

131 HADIJA S. KEJO

132 FAUZIA ISSA MANYARA

133 ZEINABU KARIMU JUMA ARUSHA

134 AISHA ABDUL MSANGI

135 MARIAMU M. MTANDU MOROGORO

136 RUKIA B. KAYINGA MBEYA

137 ZAINABU ABDUL HAMIS ARUSHA

138 FATMA MUSSA

139 SAADA A. ZAHOR DAR ES

140 FATUMA HASSAN PWANI

141 ZUHURA HAJI OTHMANI SINGIDA

142 HAWA H. MTEPA DAR ES

143 MARYAM A. MUSSA DAR ES

144 HAWA J. HASSAN DAR ES

145 ASIA H. PANGANI MBEYA

146 SHADIA T. TWAIBU KAGERA

147 AMINANI SUEDI DAUDI

148 MWANAHAMIS K. MOHAMED TANGA

149 SAUMU M. KIVURANDE TANGA

150 MWAJUMA SEBA KIGOMA

151 FADHILA ATHUMANI SINGIDA

B: CHUO CHA UALIMU CHA

KIISLAMU UBUNGO

M A J I N A YA WA L I O C H A G U L I WA

KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU YA

MUDA MFUPI -2013

(i) WANAUME

Na JINA

1 ISSA RASHID MASANJA

2 MWINDADI BAUSI MZEE

3 ILYASA JUMA SAIDI

4 HAJI SAID MWINSHEHE

5 HUSENI ALLY

6 SAID MOHAMMED MIKONGO

7 IDD ATHUMANI KAMBI

8 ALLIY ABDALLAH ALIY KHAMIS

9 MOHAMMED HUSSEIN JUMA

10 JAMAL SHEIKH YAHYA

11 ISSA YUSUPH KITENGE

12 SALUM MOHAMED KINJULI

13 ABUBAKARI ALLY NGINDIKA

14 KISMA ABDILLAH ZABURA

15 KIPUKA HASSANI ISMAIL

(ii) WANAWAKE

Na JINA

1 HIDAYA ALLY KIBAVU

2 HUSNA MUHAMMAD MBELA

3 AISHA MUSSA SAIDI

4 SALMA ABDALLAH KAISI

5 HAWA HAMIDU MSANGI

6 ARAFA ALLY

7 FATMA ABDALLAH MASOUD

8 NURU HAMISI NYUMBA

9 SHARIFA JUMA IBRAHIM

10 HAMIDA ABUBAKAR

11 SOFIA YUSUF KIHAMBWE

12 ZAINAB SULEIMAN MAGWATI

13 TATU HAMZA MAALIM

14 STARA MIGILA

15 FATIMA SALUM KIMATILO

16 HAWA MZEE MANGAMBA

17 AISHA KIBWANA KASUKA

18 REHEMA HASSANI HEMEDI

19 SALMA MOHAMED ALLY

20 TIMA KHAMIS MURI

MUHIMU

Nafasi kwa chuo cha Ubungo bado

zipo

Usaili wa mara ya pili kwa chuo cha

Ubungo tu utafanyika chuoni siku ya

Jumamosi ya tarehe 05/01/2013 saa

2:00 asubuhi. Fomu za kujiunga na

kozi zinaendelea kutolewa Chuoni kwa

gharama ya Tsh 5,000/=

Tafadhali wahi nafasi hii adhimu.

Kwa maelezo zaidi fika chuoni au

wasiliana na Mkuu wa Chuo kwa namba

ya simu 0712557099 au 0688131397.

Wabillaah Tawfiiq

MKURUGENZI
5

LUSAKA

RAIS wa Zambia, Michael

Satta, ametahadharisha

juu ya harakati mpya za

kundi linalotaka kujitenga

la Barotseland Magharibi

mwa nchi hiyo.

Barotseland, ni jina la

eneo lililoko nchini Zambia,

ambalo hivi sasa linaitwa

mkoa wa Magharibi.

Wakati wa uhuru wa

Zambia kwa mujibu wa

makubaliano yaliyofikiwa

kati ya mkoloni Muingereza

na Keneth Kaunda, kiongozi

wa mapambano ya uhuru wa

nchi hiyo yaliyotiwa saini

Oktoba 24 1964, eneo hilo

lilitambuliwa kuwa ardhi ya

Zambia.

Hata hivyo kwa mtazamo

wa watu wa kabila la Lozi,

ambao ndio wakazi wengi

wa eneo hilo la Barotseland,

serikali ya Lusaka kamwe

haikuyaheshimu makubaliano

hayo.

K w a m u j i b u w a

makubaliano hayo, wakazi

wa eneo hilo walipewa hiyari

ya kuwa mamlaka ya ndani na

kujitegemea katika masuala

ya kiuchumi na kisiasa.

Baada ya kupita karibu

nusu karne tangu kutiwa

saini makubaliano hayo,

wananchi wa kabila la Lozi

walikandamizwa na polisi

katika vurugu kwenye

maandamano yaliyoitishwa

na harakati ya kukomboa

eneo hilo kwenye mji wa

Mongu, makao makuu ya

mkoa wa Magharibi.

Tukio hilo kwa mara

nyingine liliamsha azma ya

kutaka kujitenga Barotseland,

ambayo ilijitokeza mwaka

1999 nchini humo. Mwaka

mmoja baadaye. pia maelfu

ya wakazi wa mji wa Mongu

walifanya uasi ambapo baadhi

yao waliuawa.

Licha ya hayo, viongozi

wa harakati ya ukombozi wa

Barotseland, wamesisitiza

kwamba wataendeleza

harakati zao za kudai uhuru

wa eneo hilo kutoka kwa

serikali kuu kwa njia za

amani.

Wachambuzi wa mambo

wanaamini kuwa, makundi

m a t a t u m a k u m b w a

yanayopigania ukombozi

wa eneo la Barotseland,

yanapaswa kuunda chama na

kuanza harakati za kisiasa.

Mwaka 2011 wakati

wa kampeni za uchaguzi,

Rais Michael Satta aliahidi

kuwa iwapo angeshinda

angetekeleza matakwa ya

kabila la Lozi.

Lakini kiongozi huyo

hakutekeleza ahadi hiyo na

maandamano ya wakazi wa

Habari za Kimataifa/Tangazo

AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

Zambia yakumbwa na harakati za kundi linalotaka kujitenga

eneo hilo linalotaka kujitenga

yakaendelea.

Wakati huo huo, makabila

ya Nkoya na Mbunda, ambayo

yanaishi na kabila la Lozi

kwenye eneo la Barotseland,

yanapinga fikra ya kutaka

kujitenga eneo hilo.

Viongozi wa makabila

hayo mwezi Juni mwaka

2012 walisisitiza kwamba,

makabila hayo kamwe

h a y a t o h e s a b i w a k u w a

sehemu ya sehemu ya eneo

na yanapinga kugawanywa

ardhi ya Zambia.

Hata hivyo, Baraza la Taifa

la Barotseland katika kikao

cha dharura cha Julai mwaka

huu, lilijitangazia uhuru

wa upande mmoja. Taarifa

ya kikao hicho ilitumwa

kwa taasisi za kieneo za

SADC, Umoja wa Afrika,

Commonwealth na Umoja wa

Mataifa ili jamii ya kimataifa

iunge mkono na kutambua

kujitenga eneo hilo.

Hivi sasa harakati mpya

za kundi hilo zimemtia

wasiwasi Rais Michael Satta,

hasa baada ya wanaharakati

wapya 630 kujiunga na kundi

hilo. Licha ya hayo, Satta

amewataka maafisa wa jeshi

wakabiliane kwa amani na

wafuasi wa kundi hilo.

Nchi nyingi za kusini mwa

Jangwa la Sahara kama vile

Zambia, Angola na Nigeria

zinakabiliwa na makundi

yanayotaka kujitenga na

zinafanya jitihada za kutatua

migogoro hiyo kwa amani na

kuzuia kugawanyika ardhi za

nchi hizo.

The Hague kusikiliza mashtaka ya Wapalestina dhidi ya Israel

BAADA ya Baraza Kuu

la Umoja wa Mataifa

kupandisha hadhi ya

Palestina katika Umoja

wa Mataifa, na kuwa nchi

mtazamaji asiyekuwa

mwanachama rasmi, sasa

mahakama ya The Hague

huko Uholanzi imetangaza

kuwa itaanza kushughulikia

mashtaka yaliyowasilishwa

na Wapalestina dhidi ya

utawala wa Israel.

Ofisi ya Mwendesha

M a s h t a k a M k u u w a

mahakama ya The Hague

imetangaza kuwa, hivi

karibuni itachunguza suala

la kupandishwa hadhi ya

Palestina katika Umoja wa

Mataifa na kushughulikia

mashtaka ya Wapalestina

kuhusu jinai zilizofanywa na

askari wa Israel katika vita

vya siku 22 dhidi ya watu

wa Gaza.

Mwaka 2009 Wapalestina

waliwasilisha mashtaka

rasmi katika Mahakama ya

Jinai ya Kimataifa ya The

Hague, wakiitaka ichunguze

jinai zilizofanywa na jeshi la

Israel katika vita vya siku 22

huko Gaza.

Hata hivyo mashtaka hayo

yalikataliwa na mahakama ya

The Hague kwa kuwa wakati

huo, Palestina ilikuwa bado

haijatambuliwa rasmi kuwa

nchi mtazamaji katika Umoja

wa Mataifa.

K w a m s i n g i h u o ,

kuanzia sasa Mahakama

hiyo itakuwa na uwezo wa

kisheria wa kuchunguza na

kushughulikia mashtaka

yote yanayowasilishwa na

Wapalestina.

Kwa mujibu wa sheria

za kimataifa, nchi ndizo

zinazoweza kuwasilisha

mashtaka katika Mahakaya

ya Kimataifa ya The Hague.

Kabla ya uamuzi wa tarehe

29 Novemba wa Baraza Kuu

la Umoja wa Mataifa ambao

uliitambua Palestina kuwa ni

nchi mtazamaji, hapakuwepo

uwezekano wa kusikilizwa

mashtaka ya Wapalestina

dhidi ya Israel.

Hata hivyo utawala

wa Israel na washirika

wake wakubwa hususan

Marekani, walifanya jitihada

kubwa kukwamisha suala

la kutambuliwa Palestina

kuwa ni nchi, japo isiyo

mwanachama katika Umoja

wa Mataifa.

Kufuatia utambuzi huo,

Rais wa Mamlaka ya Ndani ya

Palestina, Mahmoud Abbas,

alitangaza mara tu baada ya

kurejea Ramallah akitokea

New York, kwamba Quds

Tukufu ndio mji mkuu wa

milele wa nchi ya Palestina.

Alisema sasa Wapalestina

wamepata nchi na wanaweza

kuwasilisha matakwa yao

halali katika jamii ya

kimataifa. Karibu asilimia

75 ya jamii ya kimataifa

imewapigia kura ya ndio

watu wa Palestina.

Rais Abass amesema kuwa

mafanikio hayo, yatabadilisha

mlingano wa nguvu za kisiasa

katika Mashariki ya Kati

Ustadh Abdul Basit akumbukwa

CAIRO

Shughuli ya kumkumbuka

hafidh na msomaji mashuhuri

wa Qur’ani, Ustadh Abdul

Basit Abdul Samad, imefanyika

Ijumaa iliyopita nchini Misri

na kuhudhuriwa na wasomi na

wapenzi wa Qur’ani Tukufu.

Wanafunzi na wapenzi wa

Hafidh huyo mashuhuri wa

Qur’ani, wanachama wa Jumuiya

ya Masomaji Qur’ani ya Misri na

Masheikh wakubwa kama Sheikh

Mahmoud Tablawi, Mahmoud

Siddiq Minshawi, Muhammad al

Halbawi, wawakilishi wa Kituo

cha Kiislamu cha al Azhar na

Wizara ya Wakfu ya Misri na

Mabalozi wa nchi za Kiarabu

na Kiislamu nchini humo, pia

walishiriki katika shughuli hiyo

ya kumbumbuka msomaji huyo

mashuhuri katika ulimwengu wa

Kiislamu.

U s t a d h A b d u l B a s i t

Muhammad Abdul Samad aliaga

dunia Desemba 30 mwaka 1988

huko Cairo Misri.

Alianza kujifunza Qur’ani

Tukufu akiwa bado mtoto mdogo

na alipewa tuzo ya kuhifadhi na

kusoma Qur’ani akiwa na umri

wa miaka 12. Kipindi fulani

Ustadh Abdul Basit alitumia

muda wake mwingi kusafiri

katika nchi za Kiislamu na

kuwahamasisha watu kusoma

kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Ustadh Abdul Basit ameacha

kanda nyingi za Sauti zake

akisoma Qur ’ani Tukufu,

ambazo bado zinawavutia

wasomaji wengi wa Qur’ani.

Alianza kujifunza Qur’ani

Tukufu akiwa bado mtoto mdogo

na alipewa tuzo ya kuhifadhi na

kusoma Qur’ani akiwa na umri

wa miaka 12.

Ustadh Abdul Basit wakati wa

uhai wake, alitumia muda wake

mwingi kusafiri katika nchi za

Kiislamu na kuwahamasisha

watu kusoma kitabu cha

Mwenyezi Mungu.

Abdul Basit alizaliwa

mwaka 1927 na kufariki mwaka

1988. Ni msomaji Qur’an pekee

aliyewahi kushinda mara tatu

katika mashindano ya kusoma

Qur’an duniani katika miaka

ya 1970s.

Aidha ni miongoni mwa

wasomaji walioweza kuuza kazi

nyingi zilizorekodiwa akisoma

Qur’ani na alikuwa Rais wa

chama cha wasomaji wa Qur’an

Misri.

DAEE YOUTH ART GROUP

Inakutangazia Semina ya Ndoa na

Talaka kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah

itakayofanyika.

Siku: Jumamosi na Jumapili, kwa wiki

12.

Kozi itaanza Tarehe 15-12-2012 Saa 2

Asubuhi- 8 Mchana.

Mahali: Answar Islamic Model School-

Kinondoni Studio

Vyeti vitatolewa kwa watakao maliza

m a f u n z o m p a k a m w i s h o , M a d a

zitakazofundishwa ni pamoja na, Taratibu

ya kutafuta mchumba, sifa zake, Ndoa na

Nguzo Zake, haki za Mke kwa Mume na

Mume kwa Mke, Eda Talaka na athari zake,

Mirathi kwa mjane, Ndoa ya Mke Zaidi ya

Moja na taratibu zake, Malezi ya Watoto,

Jimai na Migogoro ndani ya Ndoa N.k.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu 0715-24

7262/ 0715- 114373.

Nyote mnakaribishwa Wake kwa Waume
6

MWEZI wa Oktoba, 2012

yalitokea matukio makubwa

mawili ya kusikitisha jijini Dar

es Salaam eneo la Mbagala.

Tukio la kwanza ni la kijana

wa Kikristu kokojolea Quran

tukufu lilofuatiwa na tukio

la pili la uchomaji wa kanisa

katika eneo hilo. Tukio la

ukojoleaji Quran liliwaumiza

sana Waislam na tukio la

uchomaji kanisa liliwaumiza

sana Wakristu pia liliwaudhi

sana Waislamu. Liliwaudhi

sana Waislamu kwa maana si

katika mafundisho ya Uislamu

kufanya vitendo kama hivyo.

Wakristu wa KKKT kupitia

kwa viongozi wao walitoa

tamko kudhihirisha hisia zao.

Katika tamko lao walielezea

madhumuni yao makuu matatu

ya kutembelea eneo la Mbagala.

Madhumuni haya kwa ufupi

ni haya yafuatayo: Kuwapa

pole na kusimama pamoja na

waumini wenzao wa Mbagla

walioathirika na uchomaji

kanisa. Kuonesha majonzi kwa

vitendo vya uvunifu wa amani na

kuporomoka kwa mshikamano

wa Watanzania. Kushiriki pamoja

kupokea matumaini ya Tanzania

mpya itakayozaliwa, itakayojali

upendo, uvumilivu, ustahmilivu,

umoja, mshikamano, uhuru wa

kuabudu na dola isiyo na dini.

Dhumuni la tatu waliliandika

kwa wino uliokolezwa kuonesha

kuwa ndilo muhimu sana

kulinganisha na madhumuni

mengine mawili. Wanaeleza

kuwa kilichotokea Mbagala ni

matokeo ya mbegu iliyopandwa

katika bustani njema na sasa

inaanza kuzaa matunda, na

kwamba hizi ni dalili zilizoanza

kitambo na hazikushughulikiwa

na waliomrithi baba wa taifa.

Wanasema kuwa dalili hizo ni:

Uchochezi wa wazi kuwa taifa

hili linaendeshwa na unaoitwa

mfumokristu. Ubishi juu ya idadi

ya waumini wa dini mbalimbali.

Matumizi mabaya ya baadhi ya

vyombo vya habari. Ukimya wa

vyombo vya dola juu ya vitendo

vya uvunjifu wa sharia. Na

Madai yasiyo ya kawaida kwa

serikali inayodaiwa kutokuwa

na dini.

Wanayataja madai hayo

kuwa ni: Kulazimisha uvaaji wa

alama za dini katika taasisi za

umma. Madai ya kutaka balozi

za nchi fulani kufungwa hapa

nchini. Madai na mashinikizo

ya uanzishwaji wa mahakama

za kidini. Mashinikizo ya

kidini yanayoingilia mifumo ya

kitaalam na kisheria. Mashinikizo

ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi

wa watendaji wa serikali na

katika ofisi za umma. Kuhoji

juu ya ushirikiano wa serikali na

mashirika ya dini katika utoaji

wa huduma za afya na elimu.

Nianze na nukta ya kwanza

ya kuwa taifa linaendeshwa

na mfumokristu. Nini maana

ya mfumo? Sambamba na

mfumokristu tumekuwa pia

tukisikia MfumoDume. Hebu

tuangalie mfumodume nini?

Makala/Tangazo

AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

Maaskofu wanapiga porojo kupotosha ukweli

Na Ibni Mustafa

Lengo kuendeleza dhulma ya mfumokristo

Maana yake ni kwamba

mfumo wa utawala wa nchi

unawapendelea zaidi wanaume

kuliko wanawake. Sasa chukua

maana hii itumbukize katika

neno mfumokristu, maana yake

ni kwamba utawala wa nchi

unawapendelea zaidi wakristu

na ukristu kuliko Waislamu na

Uislamu. Kitendo cha wanaume

kuwa ndio wengi katika nafasi

za maamuzi na ajira kuliko

wanawake ndio mfumodume

wenyewe. Vilevile wanaodai

kuwa kuna mfumokristu

w a n a m a a n i s h a k w a m b a

mfumo wa utawala wa nchi

unawapendelea zaidi Wakristu

na Ukristu kuliko Waislamu.

Upendeleo kwa ukristu ni kama

vile: Nchi kutambua kuwa

siku za ibada za Wakristu za

Jumamosi na Jumapili ndizo

siku za mapumziko kwa wote

wakati Ijumaa ambayo ndio

siku ya ibada kwa Waislamu

haitambuliwi. Kutambulika

kwa tarehe ya kuanza kwa

mwaka wa Kikristu kuwa ni

siku kuu kitaifa, wakati siku ya

kuanza kwa mwaka wa Kiislamu

haitambuliwi, kwa taasisi za

umma kama mashule kupumzika

katika mwezi wa 12 katika

mwaka ambao ni mwezi mtukufu

kwa Wakristu wakati mwezi

mtukufu wa Waislamu ambao ni

Ramadhani hautambuliki. Haya

ni machache yanayoonesha nchi

kuongozwa na mfumokristu.

Mfumokristu pia unaonekana

katika idadi ya Wakristu katika

nafasi za maamuzi, taasisi za

umma zikiwemo elimu ya juu

ambayo haizidi asilimia 25. Huu

ndio mfumokristu.

Wanaopinga kuwa hakuna

mfumokristu watakwambia

mbona Rais na makamo wake

ni Waislamu. Hawa ama

wanapotosha makusudi ama

hawaelewi. Hawaangalii ni

asilimia ngapi ya Waislamu ni

Mawaziri, Wabunge, Wakuu

wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,

Wakurugenzi wa mashirika

ya umma na wafanyakazi wa

umma kwa ujumla. Wanao

dai mfumodume kwa mfano

hawamaanishi kuwa hakuna

wananwke kabisa katika nafasi

za umma la hasha, wanajua

kuwa wapo lakini idadi yao ni

ndogo kulinganisha na idadi yao

katika taifa. Wale wanaokana

kuwepo mfumokristu kwa

kumuangalia Rais na mkamu

wake wanashindwa kuelewa

kuwa hata Rais anamezwa na

mfumo wa utawala ambao

unaegemea ukristu, Rais kama

yeye hana uwezo wa kubadilisha

mfumo kwa mfano aseme

kuanzia leo siku ya Ijumaa ni

siku ya mapumziko kitaifa ili

kwa vile yeye ni Muislamu apate

nafasi ya kwenda kwenye ibada,

hana uwezo wa kubadilisha

wimbo wa Taifa ambao umo

ndani ya Biblia ya Wakristu nk.

Wanaodai mfumodume hawana

nia ya kuwafarakanisha au kuleta

uadui baina ya wanaume na

ASKOFU Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Malasusa.

wanawake bali wanchodai ni haki

itendeke kwa wote bila ubaguzi

wa kijinsia, vilevile wanaodai

mfumokristu hawana nia wala

lengo la kuwagombanisha

Waislamu na Wakristu bali

wanachotaka ni haki itendeke

bila ubaguzi wa kidini, na hii ni

kwa ajili ya mustaqabali mwema

na ustawi wa nchi. Inaeleweka

bayana kuwa mfumokristu

kama ulivyo mfumodume ni

mambo yaliyosababishwa na

historia. Tanzania ilitawaliwa

na wakoloni Wakristu kuanzia

kwa Wareno, Wajerumani

na Waingereza, mfumo wao

wa utawala uliongozwa na

Ukristu na asili ya sheria zao

ni Ukristu. Tulipodai uhuru

na hatimae kujitawala tulitaka

mambo ya upendeleo wa kidini

usiwepo, lakini bahati mbaya

tuliishia kwenye maneno wakati

matendo ni muendelzo uleule wa

ukoloni.

Kwa maoni yangu, yale

mambo yanayoupendelea

Ukristu kama vile siku za ibada

za Jumamosi na Jumapili,

sikukuu ya mwaka mpya wa

Kikristu sina matatizo navyo,

hapa ningedai kuwa siku ya

Ijumaa kuanzia saa 6 mpaka

8 mchana ambayo ni masaa

matatu yatambuliwe kuwa ni

muda wa ibada kwa Waislamu

na hivyo kipindi hicho shughuli

rasmi za serikali zisimamshwe

ili Waislamu wafanye ibada

halafu waendelee na kazi baada

ya ibada. Pia tarehe 1 ya mwaka

mpya wa Kiislamu itambuliwe

kuwa ni siku ya mapumziko.

Kwa mfumo unaowapendelea

Wakristu uwekwe utaratibu

wa kuhakikisha upendeleo

h a u e n d e l e i k a m a v i l e

ambavyo ubaguzi wa kijinsia

unavyoshughulikiwa vilevile

ubaguzi wa kidini katika

ajira na utumishi wa umma

ushughulikiwe. Ubaguzi ni

ubaguzi tu uwe wa kijinsia au

kidini. Tena wa kidini ni mbaya

sana kwa sababu matokeo yake

ni kuliparaganyisha taifa. Suala

la dini limefanywa nyeti kiasi

anayelizungumzia kwa ajili ya

kurekebeshwa anaitwa kuwa

ndie mdini.

Nukta ya pili ya viongozi wa

KKKT inahusu ubishi wa idadi

ya waumini wa dini mbalimbali.

Ni kwa vipi hili linaweza

kuwa chanzo cha kuhatarisha

amani? Hawakutufafanulia.

Viongozi hawa wanaelewa wazi

kuwa kujua idadi ya waumini

halijawahi kuwa tatizo popote

kama kila raia anapata haki yake

stahiki, hili liliongelewa sana

wakati wa sensa, kwa kuvuta tu

kumbukumbu, nilifuatilia sensa

mbalimbali duniani nchi nyingi

kama sio zote zinafanya sensa

kwa idadi ya kila kundi liwe la

kidini au kabila, mfano majirani

zetu wa Kenya na Uganda katika

sensa zao wanafanya sio tu

kujua idadi ya waumini wa dini

mbalimbali bali hata madhehebu.

Mtu yeyote akitaka kujua KKKT

ni wangapi Kenya na Uganda

anapata taarifa hizi kwenye ofisi

za takwimu. Hatujasikia vita vya

kidini katika nchi hizo eti kwa

vile watu wa dini fulani ni wengi

kuliko wengine.

KKKT wanataja kuwa kuna

madai yasiyo kawaida ambayo

eti ni pamoja na kulazimisha

uvaaji wa alama za dini katika

taasisi za umma. Hawakufafanua

ni kina nani wanalazimisha na

ni alama zipi zinalazimishwa.

Sijawahi kusikia mtu yeyote

amelazimishwa kuvaa alama

yoyote ya kidini uwe msalaba

au labda hijabu. Jaalia kuwa

labda hapa walimaanisha hijabu

kwa akina mama na akina dada

Waislamu. Kwa Waislamu hijabu

ni suala la ibada.

Katika kipindi cha Baba

wa Taifa kwa kiwango fulani

kilikuwa ni kipindi cha utata kwa

Waislamu. Ilikuwa ni vigumu

kwa Muislamu kutekeleza vema

Uislamu wake bila kupoteza

haki zake za kiraia. Kwa mfano

ilikuwa haiwezekani mtoto wa

kike wa Kiislamu kupata haki

yake ya elimu bila kwenda

kinyume na maamrisho na

maadili ya dini yake ya kuvaa

hijabu. Kwa Muislamu ilikuwa

ni ama kunyoa au kusuka, yaani

avunje amri ya hijabu apate haki

ya elimu au akose haki yake ya

ibada ya hijabu apate kusoma.

Binafsi ninawafahamu akina

dada walioikosa elimu kwa

sababu wazazi wao hawakuwa

tayari kuona mabinti zao

wakitembea nusu uchi kwa

vimini ambavyo ndio ilikuwa

sare ya shule.

Kitendo cha serikali ya

awamu ya pili chini ya Mzee Ali

Hassan Mwinyi kuruhusu hijabu

mashuleni, ilikuwa kitendh cha

kishujaa kwake na cha kihistoria

na ukombozi kwa wanawake wa

Tanzania. Hata hivyo pamoja

na umuhimu wa hijabu kwa

Waislamu bado kwa Watanzania

ni suala la khiyari hakuna

anayelazimishwa kuivaa. Ni

wale tu ambao wanajua umuhimu

wake na wenye mapenzi na dini

yao wanaotekeleza ibada hii

adhimu. Pamoja na kuchukizwa

na uvaaji wa hijabu kwa akina

mama na akina dada Waislamu

bado tunawasihi wenzetu

hawa wa KKKT na wenzao

watuvumilie, watustahamilie

kama walivyoeleza katika

dhumuni lao la 3. Sitarajii kwa

serikali yoyote kuturudisha tena

gizani baada ya kupambazukiwa

wala Waislamu wa nchi hii

hawako tayari kurudishwa huko.

Hata katika katiba mpya nina

hakika kipengele cha uhuru wa

kuabudu kitaendelea kuwepo.

Kipengele hiki kinatoa hakikisho

la uhuru wa ibada ikiwemo

uvaaji wa hijabu bila kuwekewa

vikwazo.

Nimalizie kwa kutoa wito

kwa Watanzania kujifunza

k u v u m i l i a n a k w a y a l e

tunayotafutiana na kushirikiana

kwa yale yanayotushirikisha.

Waislamu hata tungetamani vipi

dunia yote wawe ni Waislamu

haiwezekani labda atake

Mwenyezi Mungu. Vilivile hata

Wakristu wangetamani vipi hata

kama kila mmoja wao angeacha

shughuli zote ili afanye shughuli

moja tu ya kuwabatiza watu

haiwezekani kuifanya dunia

kuwa ni Wakristu.

Tukifuata mafundisho na

maadili ya dini zetu yanayotutaka

kutendeana haki, ninaamini

tutaishi vizuri.

(Kamaludin@yahoo.com)
7

T U K I WA t u m e f u a t a n a

tukifuatilia umbea (maongezi

ya kawaida) kwenye simu,

njia pekee ya mawasiliano

iliyokuwapo, sambamba na

hofu ya msongamano wa

magari katika Jiji la Dar

es Salaam, rafiki yangu

mwanamke, aliniarifu juu ya

msiba wa kifo cha rafiki wa

baba yake.

Kwa kuzivuta hisia, nilitamka,

“sikudhania kwamba ulikuwa wa

karibu na marehemu”. Ukimya

na majibu yake yasiyoridhisha

“siyo uhakika lakini unajua mara

ya mwisho nilipokutana naye

alisema hayo hayo ya kushangaza

kuhusiana na baba yangu”,

huenda bila hata ya kusema,

rafiki yangu anamuhusudu sana

baba yake; naweza kuamini

sasa kwamba mawazo ni ya

pande mbili, yenye kujigawa

na hufanana. Yeye si tafauti na

wanawake wengine wote ambao

wamekuwa wakiwapenda na

kuwahusudu au hata kuwabusu

baba zao. Tungependa kusikia

mazuri kuhusu baba zetu.

Hadi anastaafu, baba

wa rafiki yangu, alikuwa ni

mfanyabiashara, sina shaka

kwamba alikuwa na mazowea

ya kuchukua gazeti na kupitia

makala iliyoandikwa na mtu wa

aina yangu, mwenye mtizamo

tafauti kuhusu baba yake na

akautangaza hadharani; au

kusikiliza hotuba ya mjumbe

wa upinzani mwenye azma ya

kudhoofisha heshima yeyote ile ya

kisiasa, hata ile ambayo alikuwa

nayo baba yake; au mbaya zaidi

akamsikiliza mjumbe wa chama

chake anayerusha makombora ili

Makala

AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

Ni wakati wa CCM wahafidhina kupevuka

Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhabib Amani Abeid Karume

kutafuta umaarufu wa kisiasa.

Lakini, kama mtoto wa

mwanasiasa mashuhuri hapa

Tanzania , ninao uzoefu wa

yote hayo, au zaidi ya haya,

siandiki hivi kutafuta huruma

ya yeyote, kwani ninafahamu

tosha kwamba ukosowaji wa

wazi ni sehemu ya maish ya

mwanasiasa, na kwa kawaida

nadhani, lazima uhamasishwe,

ndiyo sababu nikaandika hisia

zangu. Kwa udhati ninaowakosea

na kuwakera, ipo na kuangukia,

na hivyo ndivyo nilivyoishi.

Ipo kanuni muhimu isemayo,

kuwa mtoto, hasa wa kike wa

mwanasiasa ni kuchagua kuwa

na ngozi (gamba) gumu, yaani

si rahisi kukasirika. Pasi na

ngozi ngumu, nachelea kusema,

watoto wa kike wa wanasiasa,

wote wangeliathirika kutokana

na mitetemeko ya kisaikolojia.

Kwa miaka mingi mgodi

umegeuka kuwa kichaka cha

ndovu (tembo) kizee.

Kiasi ya wiki moja hivi,

CCM (Chama cha Mapinduzi)

kilihitimisha Mkutano wake

Mkuu wa 8, kwa shangwe

kubwa. Khadija Kopa, gwiji

wa taarab, akawaburudisha

takriban wajumbe 2400,

wake zao na wafuasi wao,

wote wakiwa wamevaa sare

za kijani na manjano, za

CCM, ndani ya ukumbi, mjini

Dodoma . Vibendera tele vya

CCM vikipepea, wakicheza

kwa furaha iliyopelekea

kuchagua viongozi wao wapya

kwa umakini. Viongozi hao

ni pamoja na Mwenyekiti wa

CCM Taifa na wajumbe 20 wa

NEC. Mkutano Mkuu wa 8 wa

CCM pia ulihitimisha Miaka 10

ya Uongozi wa Amani Abeid

Karume aliyoitumikia kama

Makamu Mwenyekiti wa CCM,

upande wa Zanzibar .

Kwa wale wasiomjua, mbali

ya kuwa ni Raisi Mstaafu wa

Zanzibar , pia ningelipenda

kuwajulisha kwamba Amani

Abeid Karume, ni mashuhuri

sana kwangu kwa kuwa yeye ni

baba yangu mzazi.

Jioni ya Novemba 14, 2012,

niliwasha TV kwa azma mahsusi

ya kumuangalia Amani Abeid

Karume akiagana na CCM,

kama Makamo Mwenyekiti

wa Zanzibar . Kusema ukweli,

nilitamani kumsikia yeye

akimshukuru mama yangu

mzazi aliyekuwa naye imara

kwa miaka 44. Nilimsikiliza

Abdulrahman Kinana akitoa

maazimio ya CCM; nikamuona

Khadija Kopa pamoja na mama

yangu wakicheza; nikamsikia

Pius Msekwa akitoa hotuba yake

ya kuaga, na hatimaye Amani

Karume akipanda jukwaani ili

naye atoe hotuba yake.

Hotuba ya Karume ya Kuaga

imekuwa gumzo na yenye

kujadiliwa sana kati ya zote

kutokea Mkutano Mkuu wa 8 wa

CCM; siyo azma yangu kuijadili

na kuifafanua hotuba hiyo, kwani

ninayo fursa ya dhati kabisa ya

kuelewa alichokusudia, wala

haikuwa dhamira yangu kuitetea

hotuba yake hiyo, kwamba

kulikuwapo mamia ya mistari

iliyoandikwa na kisha maelfu

ya maneno yaliyosemwa kuunga

mkono hotuba yake. Niko hapa

kujadili, kile ninachoamini kuwa

chanzo na mzizi wa fitna za

kuirudi na kuipinga hotuba

hiyo kwa baadhi ya Wana-CCM

Zanzibar.

Nilivyomsikiliza yeye

nikamuelewa, kama ilivyo

kawaida, hakuweza kuficha

furaha yake anayochukulia kuwa

ni mwisho mwema wa mafanikio

makubwa ya tangu alipoitumikia

CCM, zaidi ya miaka 10, huku

pia ukiwa muda wake muafaka

wa kuwasilisha mawazo ya

umma na pia kwa kuzingatia

mtazamo wa chama chake.

Hapakuwa na hitilafu yoyote

kutokana na kile alichokielezea,

alijadili Historia ya CCM,

Serikali ya Umoja wa Kitaifa

ya Zanzibar, na Mchakato wa

Marekebisho ya Katiba; Jukumu

la Uongozi na Uongozi Bora;

na pia furaha yake kuona damu

changa au sura mpya zikiibuka

ndani ya Uongozi wa CCM.

Kwa ufupi, juu ya Historia ya

CCM, Karume alilikumbusha

Taifa kwamba CCM ni Muungano

wa Vyama Viwili- Afro Shirazi

Party kutoka Zanzibar, na TANU

kwa upande wa Tanganyika-

ambavyo viliamua kuungana

na kwa azma ya kuufikia

ufanisi, akatanabahisha warithi

wasije kusahau azma ya

Waasisi, hususan Waasisi wa

ASP walioweka misingi imara,

inayokwenda sambamba na

utekelezaji wa dhati wa Azimio

la Umoja wa Mataifa la Haki za

Binaadamu; ili kuondosha hali

zote za ubaguzi, ukandamizaji,

na kadhalika.

Kuhusiana na Serikali ya

Umoja wa Kitaifa, Karume

alionelea kwamba hili lilikuwa

ni chaguo la Wazanzibari

wenyewe kwa asilimia 64,

ya wingi wa Kura ya Maoni,

lililopelekea Mabadiliko ya

Katiba ya Zanzibar , na hivyo

CCM lazima waheshimu chaguo

hilo .

Kwa upande wa Mchakato

wa Marekebisho ya Katiba

unaoendelea sasa, Karume

aliwataka wahusika wa Chama

chake, pamoja na Viongozi,

kuwacha watu watoe mawazo

yao kwa uhuru, na hasa juu ya

namna ya Muungano kati ya

Tanganyika na Zanzibar ; uhuru

huo unaweza kutekelezeka pale

ambapo mamlaka hazitowateza

nguvu.

Hatimaye, Karume aliinasihi

C C M k w a m b a i n a h i t a j i

kushinda nyoyo na akili za

watu, iwapo inataka kubakia

yenye kukubalika, na hiyo

inategemea utawala wa sheria

na kwa heshima ya kujali, wala

siyo kwa mabavu na vitisho.

Kwa ukweli na kwa mkato

kabisa, sitaomba radhi kwa

kutamka hadharani kwamba

Amani Karume ni mtu aliyeko

moyoni kwangu, hasa ya

kwamba pamoja na yote, aliweza

k u k u m b u k a k u m s h u k u r u

mama yangu. Baada ya kwisha

kukubainishia uhusiano wangu

na Amani Karume, na kwa

nafasi yake maalumu ndani ya

moyo wangu, nimeshaondosha

dhima, lililobaki nasema “kuwa

mwangalifu na utahadhari”.

Hata hivyo, nilishitushwa

kupita kiasi, kutokana na ile fitna

ya sumu mbaya, pale baadhi

ya wafuasi wa Chama chake

walivyoichukulia hotuba yake.

Kwa wafuatiliaji wa habari

wanajua kwamba baadhi ya

Wana-CCM walikasirishwa mno

na hotuba hiyo na waliamua

kuirarua (kuichanachana) Picha

kubwa ya Karume iliyokuwapo

Michenzani, Zanzibar .

Kwanini makundi ndani ya

CCM Zanzibar yakaguswa mno

na maneno ambayo hayakuwa na

lolote zaidi ya kueleza kwamba

mamlaka ya Chama kuongoza

inatokana na ridhaa ya watu,

na ni watu hao ambao hapana

budi kuwaheshimu, na kuachiwa

wawasilishe mawazo yao kwa

uwazi? Nahofia kwamba hii ni

athari mbaya ya kutofahamu

historia ya CCM na ya Nchi

yetu.

Kwa upande wa Zanzibar,

Mzazi au Mtangulizi wa CCM,

yaani Afro Shirazi Party, kilikuja

madarakani baada ya Mapinduzi,

na hadi Marekebisho ya Katiba

ya mwaka 1992, haki ya CCM

kuiongoza Tanzania , ikilindwa

na Katiba. CCM haikuwa na hati

ya kuongoza kutoka kwa Mungu,

lakini kwa Taifa lisiloendeshwa

kidini, kama ilivyo Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania, haki

ya Katiba ilikaribia kwamba

ni hati kutoka kwa Mungu,

ambayo CCM ilipata. Kabla ya

Marekebisho hayo ya Katiba,

Sheria No 3 (1) ya Katiba ya

Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania , ikisomeka kama

ifuatavyo:

“Jamhuri ya Muungano ni

Taifa la Kidemokrasia na la

Kijamaa la Chama kimoja”.

Hakuna bahati nasibu hapa,

ni “Chama Kimoja cha Siasa”

kilichokusudiwa na Katiba.

Uoni wangu ni kwamba,

baadhi ya Wana-CCM Zanzibar,

kwa bahati mbaya wanashindwa

kupambanua baina ya ukweli

halisi na mitizamo yao.

Utengamano huo unahamasishwa

zaidi na harakati ya hivi karibuni

ya kikundi cha takriban watu 50

hivi, akinamama na wasichana,

wakiwa wamevalia sare za

CCM, ambao kawaida hujiweka

safu za usoni za mikutano; hawa

ni kama kwamba huchochewa

ghafla na mtu, nao wakaibuka

kwa kuimba kwa kibwagizo

cha Komando! Komando!

Komando! Kibwagizo hiki ni

cha kuwahadaa watu na kuihadaa

hadhira, ili iweze kuamini kuwa

watu hao ni waumini wa dhati

wa Raisi Mstaafu wa Zanzibar

wa CCM mwaka 1990- 2000,

Salmin Amour, aliyependelea

mwenyewe jina la Komando,

kutokana na hulka yake ya kukosa

uvumilivu dhidi ya wapinzani

hasa, CUF, na kuthibitisha imani

hiyo pale alipowapeleka jela bila

ya hatia, Viongozi 20 wa Chama

cha Wananchi, CUF.

Bila shaka, watambuzi

tambueni ujumbe ni huo,

vibaraka wanausambaza wazi

wazi pasi na kificho. Vibaraka

wahafidhina wanachohitaji ni

CCM Zanzibar kutawaliwa na

“Komando” katika himaya zake,

hatimaye asisalimike “adui”

yeyote kutokana na makucha

ya chuma wanayostahiki. Wapo

wanaojidanganya vipembeni,

chini ya vivuli vya Wahafidhina

wa Chama, bado wakiamini

kuwa na haki pekee ya kuendelea

kutawala, ati waliikomboa

Zanzibar kutokana na Usultani,

na ati mabadiliko ya katiba

yamewawacha solemba kama

siyo kupotea kabisa, tena

katika ulimwengu huu wa siasa

makini za ushindani ambapo

hata Watanzania wanahitaji

kuchagua chama kipi kitawale

na kinachowafaa kuwaongoza,

wala si vinginevyo.

Vyema sawa! wote ambao

wamediriki kutoa hisia zao na

ambao waliitumikia Zanzibar

kutoka katika makucha ya

Usultani, sasa wameshafariki au

vinginevyo ni watu wazima sana

; hao hawakuongoza Mapinduzi

ili hatimaye waanze ulimbukeni

waje kufia ndani ya Boma la

Sultani lisilokuwa na kitu!

La kuzingatia ni kwamba,

kila baada ya miaka mitano

tunahitaji vyama vyote vya siasa

kuwatoa wagombea wao bora

na kuwapanga mstari mbele

yetu kama kwamba ni shindano

Inaendelea Uk. 11
8

Na Khalid S Mtwangi

SALALAH! Hiyo ilikuwa

dharuba kali!! Namshukuru

sana Mhariri wa gazeti la

Raia Mwema kunijulisha

kuwa kimetokea kimbunga

hicho kabla hakikupata

nafasi ya kunisomba mpaka

labda baharini!

Wa s o m a j i w e n z a g u

w a t a i k u m b u k a m a k a l a

niliyoandika na kuchapishwa

na AN NUUR toleo lake la

tarehe 23 November, 2012.

Hoja zangu zilikuwa zimelenga

k u m u u n g a m k o n o B w

Evarist Chahali kwa maoni na

mawazo yake ya kimapinduzi

yaliyochapishwa mara tatu kwa

mfululizo. Namshukuru sana

Mhariri wa RaiaMwema kwa

hatua ya kijasiri aliyochukua

kunitumia baadhi ya maoni ya

wasomaji wenzangu ambayo

yalitumwa kwake kupitia email.

Amenifurahisha sana kwa

kitendo hicho pia nawapongeza

wale waliotoa maoni yao,

naamini kwa moyo mkunjufu

k a b i s a . N a m i n a j a r i b u

kuyajibu hayo waliyouliza ama

kunikosoa na ninafanya hivyo

kwa moyo mkunjufu kabisa

hasa kwa vile baadhi yao bila

shaka, kama walivyoeleza

wenyewe kwa majina ya

bandia, wananifahamu sana

na bila shaka tumekuwa na

uhusianao mzuri kwa muda

wote tuliofahamiana. Bahati

mbaya wameficha majina yao.

Mimi nipo wazi kabisa kwa

majadiliano, waelewe hivyo.

Hebu nianze na yale makali

sana kutoka kwa anayejiita

USTADH PENGO; namuomba

aniruhusu nami nimwite

U S TA D H M U K O M B E

MONSIGNOR PENGO. Huyu

Mukombe kweli ananifahamu

vizuri pamoja na familia yangu,

ila tu kamsahau mwanangu wa

kiume aitwaye SHABANI

MTOKA MTWANGI. Huyu

ni Telecom Engineer akiwa

na Masters. Sasa ningependa

kumjibu kuhusu ama kuandika

au kutokuandika nambari

kwenye kartasi za mitihani.

Ningemuomba afanye

utafiti wa ndani kuhusu hili.

Hata hivyo wacha nimueleze

yaliyompata huyu Tatu sasa

mwenye Ph D. (Shahada ya

Uzamivu). Kama atakumbuka

vizuri, kwanza hawa vijana

wote walisota nyumbani

kwa takriban mwaka mzima

Makala

AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

Mbagala Tena: Bado ni Uislam na Ukristo

ikiwa wamekosa shule ya

kuwapokea. Dhamira ilikuwa

wapate nafasi katika shule za

serekali. Hilo likawa gumu

sana kwa sababu ambazo

wakati ule sikuzielewa, baadae

nilielewa kuwa ni majina yao

ama langu ndiyo yalisababisha

vikwazo.

Tatu alikuwa kafaulu

mtihani wa kidato cha nne

(form IV) akiwa na Division

One nzuri kabisa akiwa na

dhamira ya kuendelea Form V

mchepuo wa sayansi. Hakika

alikuwa keshapata shule ya

kumwezesha hayo kule Kenya.

Waliofuata, yaani Mtoka na

Asha walikuwa wakitafuta

nafasi katika form III na II.

Nilipata msaada wa kigogo

(hakika huyu hakuwa kigogo

bali, kutokana na nafasi

yake serekalini, alikuwa ni

GOGO na ndivyo iliwezekana

kumpatia Tatu nafasi ya Form

V katika shule moja hapa

Dar es Salaam. Niliambiwa

a s i n g e w e z a k u f u a t i l i a

mchepuo wa sayansi kwa

sababu katika mtihani wake

wa Form IV ulichanganya

“Physics with Chemistry”

ilihali kwa kawaida masomo

haya mawili hutahiniwa mbali

mbali. Niliuliza inakuwaje

wanafunzi kutoka Kenya

wanapokewa katika vitivyo

vya uhandisi na udaktari Chuo

Kikuu cha Dar es Salaam?

Niliambiwa kwa kifupi tu

na kwa ukali kuwa nikubali

alichopata huyu binti au iwe

basi akae nyumbani. Kama

wanavyosema Waswahili,

Ustadh Monsignor Mukombe

Pengo wewe hukuwepo lakini

malaika wako alikuwepo.

Ningependa kumshukiuru

sana hili GOGO serekali kwa

msaada alioutoa kwa sababu

moja kubwa kwamba kumbe

kukosa shule kwa binti huyu

ilikuwa ni njama ambayo

alijitoa wakati mmoja wa hawa

wakubwa Wizara ya Elimu

aliropoka baada ya kupata

maagizo kutoka juu. Kumbe

jambo hilo lilimuudhi sana na

katika kuropoka ilijidhihirisha

kuwa Tatu alikosa nafasi shule

kwa sababu jina lake lingine

Zubeda ambalo kabisa ni la

Kiislamu. Kwa kuwa Bint

Shaaban, Binti wa Kitanzinia

inayodaiwa kutokuwa na udini,

alinyimwa nafasi ya kusoma

kidato cha 5 pamoja na kuwa

na DIVISHENI ONE!!!

Ningependa pia kuwajulisha

wasomaji wenzangu kuwa hilo

GOGO lililonisaidia kwanza

nilikutana naye shule katika

miaka ya hamsini ingawa

yeye akiwa mkubwa kwa umri

alikuwa madarasa ya mbele; pia

nilipomuomba msaada tulikuwa

tukikutana katika pilika pilika

za kujenga nchi. Naongeza

kuwajulisha wasomaji na hasa

huyu Mokombe Monsignor

Utadh Pengo kuwa hili Gogo

ni Mkatoliki muumini wa

dhati kabisa. Alinisaidia kwa

kuangalia urafiki wetu na

wenzake wakamshushukiwa

kwa hasira! Na huo ni

wakati wa Mwalimu Nyerere

anayetukuzwa leo kwamba eti

aliondoa udini!

Bila kuwachosha wasomaji,

itatosha kueleza kuwa hao

watoto wangu wengine nao

ilikuwa mbinde kupata nafasi

shule ya Forodhani ambayo

wakati ule ilikuwa imetaifishwa

na imekuwa mali ya umma.

Namshukuru sana rafiki yangu

mmoja aliyenisaidia sana

kufanikisha Hassan akaweza

kuendelea na shule nzuri hapa

Dar es Salaam mjini mpaka

akafanikiwa kufuzu D DS

(sio MD) kama alivyoandika

Ustadh Mukombe Monsignor

Pengo. Napenda kuwajulisha

wasomaji wenzangu kuwa

rafiki yangu huyu ni muumini

thabit wa Kanisa Katoliki

na mpaka kesho tutakuwa

tunamshukuru rafiki yetu

mpendwa.

Sijasahau historia ya

Tanganyika kuhusu elimu

hata kidogo. Nakumbuka

kweli kuwa palitungwa sera

ya upendeleo kuwasaidia

Wananchi waliokuwa nyuma

kielimu na ambayo ilijumuisha

Waislamu pia. Nadhani ni

yeye huyu Ustadh Monsignor

Pengo ambaye ama kasahau

yaliyotokea au kapuuza tu

ukweli. Kwanza nakumbuka

s e r a h i y o h a i k u f u a t w a

k w a v i t e n d o n a h i l i

nilihakikishiwa na mwalimu

mmoja ambaye alikuwa ni

Mkaguzi Mwandamizi wa

Shule na ambaye nilisoma

naye sekondari. Huyu sasa

ni marehemu. Halafu ni

mkumbushe kuhusu mitihani

ya darasa la saba katika miaka

ya sabini. Kwa mbinu za ujanja

sana haikuwa inajulikana kama

wale walioendelea Kidatu cha

Kwanza walikuwa wamepasi

(kufaulu) mitihani yao ama

hapana kwa vile kilikuja

Kiswahili cha ama kachaguliwa

au hakuchaguliwa basi. Hapa

niruhusu ni mnukuu Professor

William Ochieng’ wa Chuo

Kikuu cha Maseno, Kenya.

Aliandika hivi :-

“The Muslims in our

midst have a point when they

complain that the Western

Colonial powers in East Africa

(mainly British) did very little

to promote the welfare of the

Islamic communities in our

region……. While most Kenyan

Christian communities and

societies are today led by very

highly educated leaders Islam

and Islamic societies lack such

leaders. AND IF THE MAIN

RESPONSIBILITY OF THE

NATIONAL LEADERSHIP IS

THE DISTRIBUTION OF THE

NATIONAL CAKE, THEN

IT FOLLOWS THAT THOSE

LIKE MUSLIMS WITHOUT

STRONG REPRESENTATION

AT THE TOP CANNOT HOPE

TO GET A FAIR SHARE OF

THE CAKE. (msisitizo ni

mwandishi huyu)

(The SUNDAY NATION,

May 30, 1993)

Nadhani hakuna haja

ya kutafsiri kipande hiki

wasomaji wenzangu wengi

watakielewa.

Baada ya hayo nchi nzima

ilizuka na shangwe pale shule

binafsi zikiwemo za makanisa

zilipotaifishwa. Lakini yale

yaliyofuata baadae kwa ujanja

mkubwa yalifuta kabisa sifa

ile iliyotolewa mwanzoni.

Lililotokea ni kwamba shule

nyingi sana za makanisa (za

misheni) ziligeuzwa kuwa

seminari; hivyo zilipokea

waumini wa makanisa hayo

tu. Baada ya kubaini ujanja

huo Waislamu nao walitaka

kuigeuza shule yao moja ya

Kinondoni kuwa seminari.

Ni jambo la kusikitisha sana

kwamba hakuwa mwingine

bali Malimu Julius Nyerere

ambaye alitia guu na kukataza

jambo hilo kutokea. Wakati huo

tayari kulikuwa na seminari za

misheni zaidi ya kumi na tatu

mbazo zilikuwa zikipokea

wanafunzi wa masomo ya

kawaida na wala siyo ya upadri

au uchungaji.

Lakini hata ukija katika

hizo za serikali, waliopewa

nafasi za uongozi walikuwa

‘mapadiri’ na wafuasi wao na

ndio hao waliokuwa wanaamua

nani kachaguliwa. Watoto

wa Kikristo waliochaguliwa

wakawa asilimia 90 wakati

wale wa Kiislamu, haikuwahi

idadi yao kuzidi aslimia 15

japo walikuwa ndio wengi

kwa zaidi ya asilimia 70 katika

shule za msingi.

Hebu nimnukuu Waziri

Mkuu mstaafu Muheshimiwa

Frederick Sumaye:-

“The Prime Minister,

Frederick Sumaye, has

cautioned Tanzanians not to

harp on their religious beliefs

when undertaking development

a c t i v i t i e s , p a r t i c u l a r l y

education. Speaking at the

event (sic)at fund raising event

at the Karimjee Hall in Dar

es Salaam over the weekend,

Premier Sumaye said whereas

seminaries are thought to

be preparing students for

priesthood, in actual fact few

of them became (sic) priests

and the rest took up (sic)

responsible positions in the

society.

“Evidence has shown that

most of the students from

seminary schools are the ones

who held (sic) some similar

government positions, whereas

few of them have become priests

and bishops in Tanzania.” Said

Sumaye, adding that there is

need to support such schools.

H e t h e re f o re u rg e d

Tanzanians to avoid religious

ideologies because at the end

of the day, those in responsible

positions render services to

all people regardless of their

religious leanings.”…………..

(The African 19/07/2004)

Alisema hayo katika

harambee ya kukusanya pesa

iliyoandaliwa na Kanisa

Katoliki naye akiwa mgeni

rasmi.

Naye Kipepeo anapaa

kwa kujiamini kabisa kuwa

n i m a k o s a k u w a l a u m u

wamishionari kwa ukosefu

wa elimu miongoni mwa

Waislamu. Nakubaliana naye.

Wanachosema Waislamu ni

kupinga ile dhana potofu

kuwa Waislamu hawatafuti

ile elimu ya mzingira, ati

wao wanashughulika kufika

Madrasa tu. Ukweli ni kwamba

katika kutafuta elimu vijana

wengi wa Kiislamu walidiriki

kuingia zile shule za White

Fathers, Benedictine Fathers

na kadhalika. Badala ya

kuwapa elimu vijana hawa,

wale maFather walichukua

muda wao mwingi kuwapoteza

vijana wale na kuwabatiza.

Ni ajabu kuwa hasa Kanisa

Katoliki kamwe hawastahimili

kuwaona watu wengine

wanafuata dini zao, hasa ikiwa

dini hiyo ni Uislamu. Jambo

hilo linawakera sana. Bwana

Kipepeo atakumbuka kuwa

nilitoa mfano wa Mzazi wangu

mikasa kama hiyo ilimpata

pale Central School, Ujiji

katika miaka ya ishirini. Mpaka

leo hii vijana wa Kiislam

wanaosoma shule za Kikristo

wanalazimishwa kuhudhuria

misa kanisani.

Waislamu wanafundishwa

na dini yao kuwa ni kosa

kumlazimisha mtu kufuata

dini yeyote ile. Uhispania

ilitawaliwa na Waislamu

takriban karne saba na

wakati wote huo Wakristo

waliruhusiwa kufuata dini yao

ya Katoliki. Lakini mara nchi

hiyo ilipotekwa na Wakristo

kukatokea “INQUISITION”,

jambo ambalo mpaka leo hata

Wakristo wanaona lilikuwa

ni jambo la aibu. Nako India,

takriban nchi nzima ilikuwa

chini ya wafalme Waislamu

mpaka Waingereza walipoingia

kuitawala nchi hiyo. Mpaka leo

Wahindi wengi wamebakia

na dini zao za KIHINDU

a m a B U D D H A . H a p a

nyumbani Sultani wa Zanzibar

aliwakaribisha mishionari kwa

moyo safi kabisa; lakini leo

hii makanisa wanaupiga vita

sana Uislamu. Inanikumbusha

yule mwandishi mmoja wa

magazeti aliyeapa kuwa kamwe

hataruhusu Tanzania kujiunga

na OIC; yaani atatumia kalamu

yake kupiga vita jambo hilo.

Hana sababu ya msingi zaidi

ya chuki.

M w i s h o n i n g e p e n d a

kutoa sikitiko langu. Katika

makala zake Bwana Evarist

Chahali alionyesha kuelewa

na kutetea kidogo ile hali duni

Inaendelea Uk. 9
9

KATIKA toleo la gazeti moja

litokalo hapa nchini kwetu

kila siku ya Alhamisi, wiki

iliyopita 22/ 11/2012, ukurasa

wa 18 kulikuwa na makala

iliyoandikwa na kaka yangu

mpenzi isemayo Si lazima

Seif kuwa Makamo wa Rais.

Katika makala hiyo mwandishi

a l i a n d i k a m e n g i l a k i n i

alionekana wazi kutamani

na kuegemea zaidi katika

‘episode’ ya siasa za chuki,

ubaguzi na uhasama.

Mwandishi ameonekana

kutamani yale yaliyopita enzi

zile za utawala wa siasa za chuki

na ubaguzi zirejee visiwani bila

ya kueleza hassa faida na mazuri

yaliyopatikana enzi za siasa hizo

chafu za kupigana bila sababu na

kufikia hadi kuamuriwa kulala

saa moja jioni kwa kisingizio

cha uvunjifu wa amani enzi zile

za utawala wa Komandoo. Kwa

hapa tulipofika sasa, sidhani

kwamba kuna Mzanzibari

(halisi) mwenye akili timamu

anaependa turudi kule tulikotoka

ambapo mwana CUF hakwenda

harusini wala kumzika mwana

CCM na mwana CCM hakwenda

kununua bidhaa dukani kwa

mwana CUF. Kipindi ambacho

hata wanafamilia walifikia

kutengana eti kwa kisingizio

cha utofauti wa kisiasa bila ya

kujali mustakbali na khatma ya

Zanzibar na watu wake.

Mwandishi huyo alimtaja

Maalim Seif kuwa ni mtu

ambae anataka kuona Zanzibar

haitawaliki. Naona tumeanza

kusahau historia. Hivi kama

Maalim Seif anataka kuona

Zanzibar haitawaliki angesimama

na kuwa mstari wa mbele yeye na

chama chake cha CUF kutafuta

maridhiano (muafaka) kila

pale palipotokea sintofahamu

Zanzibar hasa kila baada ya

matokeo ya chaguzi mbali mbali

ambazo wananchi na wapiga

kura hawakuwa na imani nazo

kutokana na kugubikwa na kila

aina ya uchakachuaji..!!?

Hivi tumesahau kwamba

amani na utulivu uliopo Zanzibar

sasa ni zao la hali ya maridhiano

na mshikamano wa Wazanzibari

ambao uliasisiwa na Katibu

Mkuu wa CUF na Makamo wa

Kwanza wa Rais Maalim Seif

Sharif Hamad pamoja nae Rais

Mstaafu wa Zanzibar Alhabib

Amani Abeid Karume chini ya

kamati ya maridhiano..!!? Si

Maalim Seif huyu aliyekuwa

wa kwanza kuyakubali na

kuyapokea kwa moyo mkunjufu

matokeo ya uchaguzi mkuu wa

mwaka 2010 pale Bwawani na

kumuweka Ikulu Rais Dkt Shein

huku wafuasi na wanachama wa

CUF kuonekana kutoridhishwa

na matokeo hayo kwa kipindi

kile..?

Unajuwa nini kiliwafanya

wafuasi wa CUF kukusanyika

karibu na sehemu ilopangwa

kutangaza matokea ya uchaguzi

kusindikiza tume ya uchaguzi

kutangaza matokeo ya uchaguzi

Makala

AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

Kwa haya ya Ummar Mukhtar…Zenji hayana nafasi tena..!

Na Soud Marhoun Al-

Slemy, Zanzibar

Rais Mstaafu wa Zanzibar

Alhabib Amani Abeid

Karume

huo kwa kuhofia “up side

down” ya matokeo hayo ya

uchaguzi..!!?

Tukumbuke ya kwamba

mkusanyiko kama ule uliotokea

pale Bwawani, watu wenye kudai

haki kwa kuhisi kudhulumiwa

inapelekea madhara makubwa

(negative effects) kwa serikali

au mamlaka husika pale subra

inapofikia kikomo kwa wale

wanaochoshwa kuomba haki

ambayo siyo ya kuombwa na

kuamuwa kupambana ili kupata

haki.

Tukumbuke ya kwamba

Rais wa Misri Hosni Mubarak

aliondoka madarakani bila

khiyari baada ya Wamisri

kukusanyika pale Tahrir Square

na maeneo mengine ya Cairo

baada ya kuona “enough is

enough” kwa yaliyowakuta.

Maalim Seif aliliona hilo na

akaamuwa kujitoa muhanga

na kuwakabili wafuasi wake

na kuwaomba wapowe moto,

ingawa hawakumuelewa vyema

kwa kipindi kile pale Bwawani.

Je! si busara na hekima zake

Maalim Seif zilizozima jazba

za wafuasi wale wa CUF

pale Bwawani siku ile..!!?

Je! mkusanyiko ule kama

haukuzimwa usingeliligharimu

taifa na amani yake..!? Vipi leo

useme Maalim Seif hataki kuona

Zanzibar inatawalika..!!?

Ni kweli kwamba Maalim

Seif ameteuliwa (appointed) na

Rais Dkt Shein kuwa makamo

wa kwanza wa rais Zanzibar.

Lakini uteuzi huo haukuja

kwa bahati mbaya wala kwa

matakwa na mapenzi binafsi ya

mheshimiwa rais, bali uteuzi

huo umekuja kutokana na katiba

ya Zanzibar iliyotungwa na

wawakilishi wa Wazanzibari

wote baada ya kuitishwa kwa

kura ya maoni iliyokusanya

maoni ya Wazanzibari waliotaka

muundo huo wa serikali baada

ya kuchoshwa na siasa chafu

za ubaguzi, kutoaminiana na

kupigana ambazo hazikuzaa

matunda yoyote kwao. Ingawa

kuna baadhi yetu tunaona hayo

ndio maisha. Hivyo Chama Cha

Wananchi CUF kilipendekeza

kwa rais Dkt Shein baada ya

kuridhishwa na sifa zake jina

la Maalim Seif Sharif kwenda

kukiwakilisha chama katika

Katibu Mkuu wa CUF na

Makamo wa Kwanza wa Rais

Maalim Seif Sharif Hamad

serikali ya Umoja wa Kitaifa

(GNU) kutokana na kupata

nafasi ya pili katika uchaguzi

mkuu wa 2010.

I n g a w a M a a l i m S e i f

ameteuliwa na rais Dkt Shein

haimaanishi ya kwamba abaki

kimya bila ya kusema au kufanya

chochote hata kama kuna

dhulma au ukiukwaji mkubwa

wa haki za kiraia ilimradi tu eti

yumo serikalini. Sasa huyo ni

kiongozi au gogo la mkarafuu

linalosubiri kupasuliwa kwa

shoka liingizwe kwenye moto

kupika chakula cha wengine bila

ya yeye kuonja..!!?

Maalim Seif ni kiongozi,

msaidizi na mshauri wa karibu

sana wa rais kwa mujibu wa

katiba ya Zanzibar. Maalim Seif

amekula kiapo kwa jina la Mungu

wake kutetea Zanzibar na watu

wake mbele ya rais. Iweje leo

aone haki haitendeki aendelee

kubaki kimya huku wananchi

ambao anawajibu wa kuwatetea

wakiwa wanalalamika..??

Ukiona ubaya uondowe kwa

mikono yako, huwezi kuondoa

ukemee au kama huwezi pia

basi uchukie. Maalim Seif

hakuwa na uwezo wa moja kwa

moja kutumia mikono yake

kuondosha ubaya ulojitokeza,

lakini alionekana kuuchukia

kwa asilimia mia moja na ndio

mana akakemea kwa sauti

kubwa iliyosikika kila ncha ya

ulimwengu huu ambapo miale

ya jua inapiga.

Kila mmoja ni mchunga na

ataulizwa kwa alichokichunga.

Kwa hili Maalim Seif Mungu

amemungoa Hamdullah!! Lakini

pia tusisahau ya kuwa uongozi

ni dhamana na utaulizwa kwa

dhamana hiyo.

Maalim Seif na chama chake

cha CUF ni chimbuko la GNU, na

umoja wa kitaifa ni sera ya CUF

tokea 1992, iweje leo unamtaka

Maalim Seif akiondoshe

chama chake katika GNU eti

kwa sababu hakuridhishwa

na yaliyofanyika Zanzibar na

ameikosoa serikali..!!? Zile zama

za divide and rule zimepitwa na

wakati na wala sidhani kwamba

zitarejea ndani ya Zanzibar

kwa sasa ambapo agenda kuu

ya Wazanzibari walio wengi

ni kudai Zanzibar huru yenye

mamlaka kamili na kutambulika

kwa heshima zote kitaifa na

kimataifa.

Tuchunge sana na kalamu

zetu, ukitumia vizuri kalamu

yako utajenga na utanufaika kwa

kalamu hiyo, kushindwa kufanya

hivyo ni kubomoa na likitokea

lolote baya na la kuchukiza na

wewe pia utaingia katika matata

kwa namna moja au nyengine,

kwa njia ya moja kwa moja au

isiwe moja kwa moja, akiumia

jirani yako umeumia wewe.

Elewa ya kwamba Zanzibar

sio mali ya CCM, CUF, taasisi

za kidini, sio ya kwangu

binafsi wala ya kwako, bali

ni mali ya Wazanzibari wote

na kila anaependa amani na

maendeleo ya Zanzibar bila ya

kujali dini, kabila, rangi wala

tofauti za kisiasa. Na katika

ulimwengu wa leo wenye

kuongozwa na kutawaliwa

kwa misingi ya kidemokrasia,

uwazi (transparency) umetawala

zaidi na kila mtu anakuwa huru

kusema alichonacho na kutoa

mawazo kuhusu juu ya kile

anachokiamini yeye akilini

mwake, na kwa upande wa

maamuzi, walio wengi (mass)

ndio wanaofuatwa. Hivyo basi

si vyema kuanza kufanya roho

mbaya, kijicho na husda juu ya

amani ya Zanzibar na mwelekeo

wa Wazanzibari walioshikana

pamoja juu ya utoaji maoni

kuhusu katiba mpya ambao

umeonekana dhahir shahir bila

ya woga, bila ya kumun’gunya

maneno wala kupepesa macho

wanadai mamlaka kamili ya

nchi yao na haki zao kiujumla

ambazo wamezikosa kwa miaka

mingi sasa. Hili limekuwa

mwiba na linawanyima usingizi

na kusosa hata hamu ya kula

baadhi ya watu wasioitakia

mema Zanzibar ambao lengo

lao ni kuifuta Zanzibar katika

uso wa dunia kwa kuizamisha

kusikojulikana. Kwa nini iwe

nongwa na kioja cha mwaka

wakati kila Mtanzania ana uhuru

wa kutoa maoni kwa mujibu wa

katiba iliyopo..!!?

Sikubaliani kabisa na

mtazamo finyu wa kuwagawa

Wazanzibari, kuibana Zanzibar

kwa maslahi binafsi, tena ya

watu wachache wasio hata

uzalendo wa Zanzibar.

Mungu ibariki Zanzibar na

watu wake!!

Mbagala tena: Bado ni Uislam na Ukristo

Inatoka Uk. 8

waliyonayo idadi kubwa ya

Waislamu nchini humu. Naona

kuwa hakueleweka kabisa

kama haya wanayoyasema

kina Ustadh Mosingnor

Mukombe Pengo na wenzake.

Nami niliandika makala ile

kujaribu kuziba mapengo

niliyoyaona katika makala za

Bw Chahali. Nilipokuwa shule

ya sekondari (takriban miaka

sitini iliyopita) kulikuwa na

somo la “comprehension”

ambalo lilikuwepo kuwasaidia

wanafunzi mbinu za kuweza

kuelewa kwa urahisi yale

wanayoyasoma. Sijui kama

somo hili liliendelea kuwepo

kwa muda gani. Sasa hivi kweli

hawa kina Ustadh (Monsognor,

Mukombe) Pengo, Bw Kali,

Bw Kipepeo, Bw (Mtume)

Moses na (Malaika) Gabriel

walishindwa kumuelewa Bw

Chahali. Tukiwa karibu zaidi

tujiulize walishindwa kuelewa

yale niliyoandika mimi?

Sidhani ilikuwa hivyo.

Nilibahatika kusoma nakala

ya jarida NEWSWEEK la tarehe

January 23, 2012. Ukurasa wa

kumi na tatu kulikuwa na

mchoro (cartoon) ulioonyesha

moyo wa BinAdam na ubongo

pia wa BinAdam wakipigana

mieleka. Katika jitihada ya

kufumbua fumbo hilo kulikuwa

na maelezo yafuatayo:-

“……..the brain operates

fundamentally in two modes.

O n e i s a u t o m a t i c a n d

emotional – in essence – a gut

reaction………….Green has

found that most of the time

when we are deciding what is

the right thing to do, what is

happening in the brain is the

emotional response, not the

reasoned one…….”

Haya ni maandishi ya Joshua

Green “a leading researcher

on morality and the brain.

Green, 37, is a professor at

Havard and a leader in moral

psychology”. Inawezekana

haya ndiyo yaliyowasibu

hawa ndugu zangu walioshika

kalamu “kunishambulia” kiasi

hicho.

Kwa hali ilivyo humu

Tanzania na nikikumbuka

u t a b i r i w a n d u g u y e t u

Omwami Salva Rweyemamu

nigependekeza kwa nguvu zote,

kwa unyenyekevu kabisa kuwa

ndugu zetu waKristo wapige

konde nyoyo zao. Katika

nyanja nyingi muhimu sana za

nchi hii wao ndio wameshika

mpini na Waislamu wameshika

kwenye makali. Ingawa kuna

viongozi kama Askofu Mkuu

Mokiwa wa Anglican Church

hakubaliani na hilo ukweli

ni kwamba mfumo mzima

katika nyanja nyingi nchini

n i “ M F U M O K R I S TO ” .

Kanisa Katoliki wanakubali

na kujigamba katika kuongoza

nchi.

H i v y o h a w a n d u g u

waKristo wanaweza kuwa

“ M A G N A N I M O U S ”

(samahani nimeshindwa

kupata neno kama hilo la

Kiswahili) na wakalegeza

kamba kidogo ili Waislam nao

wakaweza kujitikisa kidogo?

Hivi hakuna aipendaye

Tanzania akatuepusha na janga

alilotabiri ndugu yetu Salva

Rweyemamu?
10

SIKU moja aliyekuwa Rais

wa Kwanza wa Jamhuri wa

Muungano wa Tanzania,

ambae pia huitwa baba

wa Taifa, hayati Mwalimu

Julius Nyerere, alikuwa

akitembelea kisiwa cha

Pemba, kikazi. Katika safari

yake hiyo ya mzunguko

wa kikazi ilisadifu kupitia

b a r a b a r a y a m k o a n i

kwendea Chake Chake.

Karibu na kichunjuu, hivi

kuna krosi moja kubwa

sana iliyokuwa na muundo

wa herufi ‘S’.

Wakati wakipita pale na

msafara wa magari na jinsi

njia ilivyokuwa mbovu,

na makarama ya krosi ile

ilivyochongeka, Mwalimu

hakuamini kama anapelekwa

Chake chake. Akauliza;

“Tunakwenda, tunarudi?”

Akaambiwa tunakwenda,

il’hali gari ikiwa limeelekeza

uso kule linakotoka na

likiendelea na mwendo ule

ule katika msafara. Mwalimu

akasubiri ajionee kioja,

akatulia.

Miaka zaidi ya 30 tangu

Mwalimu aulize suali hili,

na sasa ni karibu miaka 13

tangu Mwalimu afariki,

hakuna mmoja wetu aliepata

kufikiria falsafa ya maneno

haya, yaliyochukuliwa

kama mzaha wa Mwalimu

tu wakati ule na hadi sasa.

Kusema ukweli maneno haya

hayakustahili kutiwa kapuni

na kama kuna aliyefanya

hivyo amekosea. Ndio maana

mimi nilie yaweka akiba

leo nayavongonyowa na

kuwatunukia. As’aa huenda

mukazinduka.

Zanzibar, nchi kinyonga,

mara nchi, mara si nchi,

vyovyote tukavyoiita, itaitika.

Hadi sasa Visiwa hivi vinapata

umri wa miaka isiyopungua

48 tangu kuachwa na mkoloni

mweupe na kujitawala.

Miaka hii si kidogo hasa

kwa kuyatathmini maendeleo

yetu na ya nchi kwa ujumla.

Naamini huu ni wakati

muafaka wa kujiuliza, ikiwa

SMZ ndie mtawala mkuu wa

visiwa hivi tangu miaka hio,

na anaehubiri maendeleo

kila uchao, tuiulize Serikali

yetu ya SMZ suali lile

lile, ‘TUNAKWENDA,

TUNARUDI?’

Nchi hii ilikuwa ina

maendeleo makubwa na

ilikuwa na akiba isiyomithilika

katika mahakibizo ya fedha

duniani mpaka zama za miaka

ya mwisho ya 1970. Serikali

zetu za SMZ zilizopita

zilikuwa zimetawaliwa

kimabavu kweli kweli

lakini mengi tuliyaona sasa

hatuyaoni. Ndani ya miaka

Makala

AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

SMZ na kasumba za maendeleo - ‘tunakwenda, tunarudi?’

nane ya Mzee Abeid Karume,

tulipata majumba makubwa

nchi nzima. Tukajengewa

sipitali na vituo vya afya.

N d a n i y a m i a k a y a

Karume, Jumbe hadi karibu

ya Ali Hassan Mwinyi, wazee

wakipewa pesa za matumizi

zikiitwa ‘ulufea’ (Welfare

benefits) na zikiwasaidia

sana. Wakati wa tawala za

SMZ za siku hizo, sipitali

zilikuwa zimejaa madawa,

usafi na hudumua za kulla

aina. Skuli zetu zilijengwa

hatua kwa hatua, hakuna

alielipia mchango wa skuli,

hakuna alienunua daftari,

kalamu wala penseli. Hakuna

mwanafunzi aliekosa huduma

za afya za kichocho, vipimo

kila muda fulani.

Ilifika wakati kwa jinsi

Serikali ilivyoikiwajali

wanafunzi, Waziri wetu

wa Elimu wa mwanzo

hapa Zanzibar, aliwahi

kupendekeza kuwa vichwa

v y a N g ’ o m b e v y o t e

vinavyochinjwa nchi nzima

v i p e l e k w e m a s h u l e n i

wanafunzi wapikiwe supu,

ili wapate wanywe wakati

wa mapumziko (recess).

Bahati mbaya mpango huu

ulivunjwa na Sheikh Karume,

pale alipomwambia Waziri

wa Elimu kuwa asijefanya

hivyo mpaka ahakikishe kila

mwanafunzi ameshapata

kijiko na kibakuli cha

kunywea supu. Mapango huu

ukafa hapo, lakini ulikuwa na

nia njema.

Enzi za SMZ ya wakati

huo, kulikuwa na huduma za

dakhalia (boarding). Ukipasi

ukipelekwa huko kupatiwa

mafunzo ya kuwa mtu

utakaejitegemea. Tukipewa

kula asubuhi mchana na jioni.

Japo tukiita bondo, lakini

tukipewa tena bure na kwa

wakati bila kuchangishwa

g h a r a m a . Wa n a f u n z i

wakiletewa meli bure kupanda

au wakifanyiwa tiketi kabisa

wakifika huchukuwa na

kusafiri tu kwenda Unguja

na Pemba. Tuache huko.

Hospitali, kula kunywa

na huduma masaa ishirini na

nne. Mgonjwa akipembejewa

na madaktari wa kikwetu na

wa kigeni. Serikali haikuwa

na meli zilizoenda kwa kasi

wala madege, lakini watu

wakisafiria meli za Serikali

za uhakika na unafuu wa

bei. Huo ndio wakati ambao

tunaweza kusema kuwa

nchi yetu ilikuwa changa,

na ilikuwa na matongo ya

ukoloni, haikuwa na uoni

wa mbali wala uwezo wa

kutuletea maendeleo.

Tupige dira ya SMZ leo.

Serikali yahubiri na kutangaza

kila siku kuwa nchi hii imepiga

hatua kubwa kimaendeleo

ukilinganisha na Zamani.

Sikatai. Maendeleo wakati

mwengine hupimwa kwa

miwani ya macho, ambayo

kigari kidogo huwa TATA,

au FUSO. Maendeleo siku

hizi hupimwa kwa kutazama

ndege zipitazo juu ya anga

letu, tivii pana majumbani, au

kila mtu ana simu ya kiganjani.

Maendeleo yetu hupimwa

kwa viongozi kuwa katika

magari makubwa ambayo

wakiwa ndani ya magari

hayo hawasikii ule uvundo

unaonuka pale Darajani kituo

cha dala dala.

Maendeleo hupimwa

wakiwa katika magari

ambayo pia yakipita njia

m b o v u h a w a h i s i w a l a

hawapati vumbi mle ndani.

Na pia licha ya kuwa nchi

ina joto la tanuri ya mbata

siku hizi kwa uchafuzi wa

mazingira, viongozi wetu

wa SMZ hawalihisi joto hili

na vuke kali, katika magari

na majumba yao yaliyo ‘full

kipupwe, full kiyoyozi, full

kujiachia’. Raha zote hizi

zilizowazunguka viongozi

wetu unawategemea kuwa

siku moja watasema kuwa

nchi hii inarudi nyuma badala

ya kwenda mbele? Ungekuwa

wewe ungetia ulimi wako

puani ukasema ukweli huu

wakati yote hayo huyaoni kwa

maraha yaliyokuzunguka?

Hebu linganisha hayo

machache niliyoyasema

yalifanywa, enzi za Karume,

Jumbe na kidogo Mwinyi

na uone. Sasa tudurusu kwa

pamoja. Nitawauliza maswali

munijibu mpaka nimalize,

sawa? Bismillah! Ule ‘ulefea’

ALHAJ Ali Hassan Mwinyi.

bado upo? Skuli zetu zina

vifaa, madafatri na kalamu

bure? Dkahalia zipo? Elimu

bado ni bure? Ndio ni bure

maana haina maana yoyote,

lakini inalipiwa. Samahani

hili nimejijibu mwenyewe.

Haya tuendelee.

Kule spitali dawa ziko?

Ndio lakini kwa pesa. Kile

chakula vipi bado wanapatiwa

wagonjwa? Ahh! Bajeti

ya Wizara ya afya ndogo,

kimefutwa Chakula. Lakini

Waziri wa Afya ana prado la

milioni 70, na mafuta yake ya

laki moja kwa wiki pengine.

Hawasemi kuwa mawaziri

waendeshe gari ndogo kama

Starlet, na Vizt kujenga taifa.

Heri wafe wagonjwa wao

waendeshe magari mazuri.

Ndio sisi bwana, wakoloni

weusi. Nani anajali kama

wagonjwa wanakufa kwa

kutukanwa tu kule Spitali,

kwa kukosa dawa tu na

hata kula sasa? Hawa ndio

viongozi wetu bwana, ni zaidi

ya majoka ya mdimu.

M a d a k t a r i j e e

wanashuhulikia wagonjwa?

Hapana, wanawatukana wala

hakuna anejali serikalini

kwani wao hawatibiwi hapa

hata wakiumwa na tambazi

(uvimbe) huenda nje ya nchi.

Kwa nini? Tumeendelea hivyo.

Tuendelee, au mshachoka?

Mmeona wapi Serikali

kujenga tena majumba ya

watu na makazi? Hapana.

Ule usafiri wa meli dhamana

za Serikali ungalipo? Hapana

zilizopo ni za matajiri na

hata tukizama SMZ husema,

haina la kufanya. Tumezama,

tunazama, na tutaendelea

kuzama. Ndio maendeleo!

Ya kale hayako tena, kweli.

Lakini pia ya sasa hayapo na

wala tusiyatarajie. Nchi hii

kama ingekuwa gari, mmoja

kati ya madereva hawa saba

tuliojaaliwa na Chimwaga

kutuongoza, lazima bila

shaka alizitowa gia zote na

kuibakishia gia ya kurudi

nyuma tu (reverse gear). Na

ndio hivi tunapelekwa msobe

msobe. SMZ wakisimama

majukwaani, huhubiri chuki,

na uhasama na uongo mwingi

kisha wakikutana katika

vyombo vya habari husema

wameleta maendeleo. Hivi ni

kweli jamani. Sikupata nafasi

ya kuchambuwa sana lakini

mpaka hapa tu jiulize ndugu

yangu, ‘TUNAKWENDA,

TUNARUDI?’

Tangazo

Kwa niaba ya Masjid Qiblatain:-

Sheikh Bawaziri na Sheikh Awadhi

wanawaalika Waislamu kuhudhuria

katika hafla ya kuhitimisha kitabu

‘BULUGHUL MARAMI’.

Mahali: Masjidi Qiblatain,

Kariakoo.

Siku: Ijumaa (Leo) Desemba,

14/201.

Muda: Baada ya Swala ya

Magharib.

Mgeni rasmi: Dkt. Babasila, Katibu

Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa

Kiislamu wa Bara la Afrika.

Wabillah Tawfiq
11

WAKATI wa Ukhalifa wa

Seyyidna Umar bin al-Khattab,

Masahaba walikubaliana

kuanza kalenda ya Kiislamu

pale Mtume wa Mwenyezi

Mungu alipofanya Hijra

kutoka Makka kuelekea

Madina, na kuasisi Dola ya

kwanza ya Kiislamu. Sasa

tunapouanza mwezi huu

Mtukufu wa Muharram,

mwaka mpya wa Kiislamu

wa 1434, basi tujikumbushe

kidogo kuhusu tukio hili la

kihistoria la Hijra na tufute

dhana potofu zinazoambatana

nalo.

M a r a n y i n g i H i j r a h

inapojadiliwa, tumekuwa

tukiishia zaidi kwenye maelezo

yanayoonyesha jinsi Mtume wa

Mwenyezi Mungu alivyojificha

pangoni au nani alilala kwenye

kitanda chake. Hali hii imekuwa

ikituondoa kwenye mjadala

wa maana, wenye kina kuhusu

masuala ya Hijra. Sisi tunaishia

kujadili matukio tu ya Hijra.

Lakini hata hivyo, matukio

ya Hijra tunayoyadili lazima

yatukumbushe kwamba Mtume

wa Mwenyezi Mungu, ingawa

alikuwa akitegemea ‘Wahyi’

kama chanzo cha ujumbe wa

Kiislamu; alikuwa akifanya

harakati za kusimamisha Uislamu

AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

Tukio la Hijra, mazingatio yaliyosahaulika!

Said Rajab

kama binadamu na kupitia mbinu

na mikakati ya kibinadamu.

Hijrah ya kuelekea Madina

haikufanyika kwa sababu

Waislamu kule Makka walitaka

kuepuka manyanyaso, au kwa

sababu walitaka kutafuta eneo

salama zaidi la kujinusuru, au

kukimbia mateso ya Maqurayshi.

Isipokuwa, Hijrah lilikuwa ni

tukio kubwa ambalo limebadili

mkondo mzima wa historia

kuelekea upande mwingine.

Hii inaweza kuonekana iwapo

tutaiangalia Sira katika mtazamo

wake sahihi.

Sira ya Mtume wa Mwenyezi

Mungu ni sehemu muhimu

sana ya Sunna, na ndiyo tafsiri

ya vitendo ya Qur’an Tukufu,

ambayo ni ufunuo wa Mwenyezi

Mungu kwa wanadamu. Ukisoma

Sira kwa umakini, utaona kuna

mbinu maalumu ya kuendesha

harakati, na kama lengo letu

ni kutafuta radhi za Mwenyezi

Mungu, basi ni jukumu letu

kuzingatia mbinu hii, hatua kwa

hatua katika kila awamu:

S e m a : “ I k i w a n i n y i

m n a m p e n d a M w e n y e z i

Mungu, basi nifuateni, (hapo)

Mwenyezi Mungu atakupendeni

na atakughufirieni madhambi

yenu. Na Mwenyezi Mungu ni

mwenye maghufira na mwenye

rehema” Qur (3:31).

“Na anachokupeni Mtume basi

pokeeni, na anachokukatazeni

jiepusheni nacho” Qur (59:7)

Kwa mujibu wa Sira, Hijrah

inahitimisha kipindi cha mpito

katika harakati kinachojulikana

kama “Kutafuta Nusra”,

kuelekea kwenye kipindi kingine

ambacho Uislamu unatekelezwa

kwa vitendo katika kiwango

cha Dola. Nusra ni kuhamisha

mamlaka kutoka kwa mtu

mmoja, kupitia kuungwa mkono

au kiapo cha utii, kutoka kwa

watu wenye nguvu katika jamii.

Kwa hiyo, Hijrah ni matokeo ya

moja kwa moja ya kutafuta na

hatimaye kupata Nusra.

Wakati Mus’ab bin Umair

(ra) alipotumwa Madina kueneza

ujumbe wa Uislamu, ilimchukua

mwaka mmoja wa kazi ngumu

katika mji huo, kabla ya viongozi

wake kusafiri mpaka Makka, na

kusalimisha mamlaka zao kwa

Mtume wa Mwenyezi Mungu

kwa kumpa Ba’yah (kiapo cha

utii). Ba’yah hii iliitwa Bayat-ul

Harb (kiapo cha vita).

Ingawa hakukuwa na vita

kipindi kile, iliitwa ‘Bayat- ul

Harb’ kwa sababu ilionyesha

nia ya Waislamu kupigana,

iwapo watalazimika, ili kulinda

harakati na Dola changa ya

Kiislamu wakati ule. Mtume

wa Mwenyezi Mungu alitumia

miaka minne ya Da’wah kwa

makabila mengi ya Najd (eneo

kubwa kati ya Makka na Madina)

kabla ya kupata Nusra.

Ni vizuri kutambua kwamba

mpaka kipindi hiki katika

Sira, licha ya shinikizo lote

ambalo Mtume wa Mwenyezi

Mungu aliliweka kwa jamii

ya Kikafiri ya Makka, mateso

ambayo Maquraysh walimpa

Mtume wa Mwenyezi Mungu

na Waislamu wa awali yalikuwa

ni cha mtoto, ikilinganishwa na

mateso ambayo yalikuja baada

ya Mtume kupata Nusra kutoka

kwa viongozi wa Madina.

Kuanzia hapo na kuendelea,

Makafiri walikuwa wakipanga

kumuua Mtume wa Mwenyezi

Mungu. Hakika ni ukweli

kwamba Shetani na wafuasi wake

wanaogopa sana utekelezaji wa

Sheria za Mwenyezi Mungu

katika ardhi.

Kwa kuzingatia nukta hizi

muhimu, kila tunapoijadili

Hijrah, ambayo watu wengi

wameishusha mpaka kufikia

kuwa kama safari ya kiroho

tu iliyofanywa na Mtume, pia

tujadili umuhimu wa Kiitikadi

wa tukio hili, kwa kuangalia

Uislamu kwa ujumla wake na

uendeshaji wa harakati.

Ni muhimu sana kwa Waislamu

kutambua kwamba tukio hili la

Hijrah si tu linaadhimisha kuanza

kwa kalenda yetu, lakini muhimu

zaidi linakumbusha kuasisiwa

kwa kiini (nucleus) cha dola

ya kwanza kabisa ya Kiislamu.

Mamia ya miaka iliyofuatia,

Ni wakati wa CCM wahafidhina kupevuka

Inatoka Uk. 7

la urembo lililopambika ili

kuwashindanisha, na hiyo ni

sifa au alama ya demokrasia

ulimwenguni kote, na kisha

tuchague aliyependeza zaidi ili

tumvishe taji.

Wacha mshindi atambe katika

Ikulu ya Zanzibar ama ya Dar es

Salaam , tunachohitaji aje ajipange

tena mbele yetu baada ya miaka

mitano, tutakapomuepuka yeye

na tukamvisha taji mwengine

pamoja na zawadi yake ya

fedha. Akibahatika kushinda na

akalivaa taji kwa mara ya pili,

kama ilivyo ada, tutamfikisha

ukingoni mwa awamu yake ya

pili ofisini pamoja na fungu lake

nono la pensheni na tumkabidhi

mkononi kisha tuendelee na

shindano la kumpata mrembo

mwengine. Jee Wahafidhina wa

CCM wataelewa na kubaini hali

ya kutofaa kwao na woga juu ya

mazingira magumu ya urembo

ama uzuri wa kisiasa, hasa

usoni kwa wapigakura ambao

hapana shaka wameshaona hawa

hawapendezi?

Mazito zaidi ya hayo, ni

kwa upande wa Zanzibar ,

mshindi wa taji na anayemfuatia,

wanalazimika kugawana ile

hawala ya fedha, zawadi yao.

Wazanzibari wanachotarajia sasa

ni kuona mshindi anashikamana

na kufanyakazi bega kwa

bega na mshindani wake wa

karibu. Hili bila shaka linahitaji

kuona mahasimu wawili

wakiheshimiana wakati wa

kampeni na baada ya chaguzi,

na kisha kutanguliza maslahi ya

Zanzibar . Hii ni adabu iliyofaa,

naweza kusema, iliyothibitishwa

na Kura ya Maoni ya Serikali

ya Umoja wa Kitaifa kwa

asilimia 64 ya Wapigakura,

ambao walichoshwa na siasa za

chuki, za kibaguzi zilizotumika,

ikibidi kote kote CUF na CCM,

kuidhoofisha Zanzibar , na

pia kuchoshwa na vilio vya

mchezo mchafu kila baada ya

Uchaguzi.

Kwa bahati mbaya, wapo

baadhi ya Wana-CCM wa

Zanzibar, wanaosumbuliwa na

ugonjwa wa kusahau kabisa juu

ya Maridhiano na Mabadiliko ya

Katiba, yaliyopelekea kuundwa

kwa Serikali ya Umoja wa

K i t a i f a ; w a p o w e n g i n e

wasioridhika na mfumo huu,

wamekuwa wakiweka vizuizi

na kunong’ona chini kwa chini,

kutokana na kukosa ustahamilivu

na pia ukosefu wa kubaini athari

za mifarakano, ndiyo maana

wanamvurumishia lawama

Amani Abeid Karume, ati yeye

ndiye aliyeasisi mizizi ya hili;

wapo waliokubali na kuridhia

matakwa ya Wazanzibari;

ingawa kwa Wahafidhina, hao ni

wasaliti, kwa chochote ambacho

ni kinyume na matakwa yao wao

(wahafidhina).

Katika Mkutano wa hivi

karibuni wa CCM uliofanyika

Zanzibar, Wahafidhina wa CCM

walitumia lugha chafu, matusi,

uchochezi, na maneno yasiyofaa

kuchochea na kukumbusha

mambo yaliyopita ambayo

yakitumiwa na Wanamapinduzi

dhidi ya Wana-CCM waliodaiwa

kuwa na msimamo wa wastani;

kwa udhati kabisa Mapinduzi ni

matokeo ya kuondosha ubaguzi,

ingawa yanatumiwa sasa na

baadhi ya Wahafidhina kufungua

na kurejesha majeraha ya zamani

yaliyokwishapoa, ili kujitafutia

umaarufu wa kisiasa.

Kama Mzanzibari mwenye

asili ya pande mbili, Muarabu na

Muafrika, ambapo Babu yangu

Muarabu aliuwawa gerezani

mara tu baada ya Mapinduzi,

bila ya sababu, zaidi ya imani

yake ya kisiasa, ambapo pia

Babu yangu mwenye asili ya

Afrika naye aliuliwa miaka 8

baada ya Mapinduzi, si kwa

lolote bali, kwa hali ile ile kama

mtangulia wake, imani yake ya

kisiasa, sijaridhika wala sifurahii

hata kidogo.

Huu ni mchezo wa biashara

ya kujinufaisha, unaoweza

kupelekea umwagaji damu. Sasa

ni wakati wa Wahafidhina ndani

ya CCM Zanzibar kupevuka,

na wakabaini kwamba hiki siyo

kiwanja cha watoto wa skuli,

wababe kuwapora wenzao

pesa yao ya chakula cha

mchana.

M i a k a 4 8 b a a d a y a

M a p i n d u z i , Z a n z i b a r

imebadilika sana. Wengi wa

Wazanzibari ni wa umri wa

chini ya miaka 40. Hawakuishi

katika Mapinduzi wala

ubaguzi wa rangi wa kisiasa,

unaotajwa kusababisha

Mapinduzi ndani ya Zanzibar

. Siasa zetu haziwezi kubaki

za kale, ingawa historia

inaweza kutumika kutuarifu,

wapi tulikuwa vile, na wapi

tunahitaji kwenda, na hivyo

kuepuka siasa chafu.

Kama CCM Zanzibar,

inaburuzwa na wahafidhina,

hivyo basi CUF inateka

ushindi wa kisiasa wa Zanzibar

. Iwapo CCM inahitaji

kutetea taji lake la urembo

mwaka 2015, lazima ijijenge,

ijirekebishe, yenyewe, na

ijiunde upya, ipambane na

iweze kuteka ushindi, kwa

sababu ni kura za Wazanzibari

wenye msimamo wa wastani,

zitakazoamua Raisi wa

baadaye wa Zanzibar .

( M A K A L A H I I

IMETAFSIRIWA KUTOKA

GAZETI LA THE GUARDIAN

LA JUMAPILI TAREHE 25

NOVEMBA, 2012, AMBAYO

ILIANDIKWA NA BI FATMA

AMANI)

kiini hiki kilisambaa katika

nchi jirani, kikiwakomboa

watu wanaokandamizwa

kwa kuwaleletea neema ya

Mwenyezi Mungu inayoitwa

Uislamu.

Kwa hiyo, tunapotaka

kuzungumzia umuhimu wa

Hijrah, basi tutambue kwamba

tukio hili linaadhimisha pia

kipindi ambacho Uislamu

kama Itikadi, umebadilika

kutoka kuwa wazo na kuwa

vitendo.

W a t u w a M a d i n a

walimkubali Muhammad

(saw) kama Mtume tu. Lakini,

hata hivyo baada ya kuhamisha

mamlaka yao (Nusra) kwa

Mtume wa Mwenyezi Mungu

wakati alipowasili Madina,

walimpokea kama mtawala

na Mtume.

Kabla Muhammad (saw)

hajafanya Hijrah, alikuwa

Mtume aliyefunuliwa sheria

mpya kutoka kwa Mwenyezi

Mungu. Baada ya Hijrah,

akawa ndiye mtekelezaji

wa sheria hizo. Uislamu

ukahama kutoka uanishaji

na ufafanuzi wa matatizo na

masuala, ukaelekea kwenye

kupambana na matatizo na

masuala hayo, ikiwa ni pamoja

na kutoa ufumbuzi wake.

Hiki ndiyo kipindi ambacho

Mtume wa Mwenyezi Mungu

aliweza kutekeleza kanuni na

mifumo ya Kiislamu katika

maisha halisi.

Hijrah, kama sehemu ya

Sira, ni tukio linalohitaji

kusomwa kwa kina sana, ili

kufahamu maana za ndani na

hekima zake.

Haina maana kwamba

maelezo madogo madogo

ya Hijrah, kama jinsi Mtume

w a M w e n y e z i M u n g u

alivyomfanya Seyyidna

Ali bin Abu Talib(ra) alale

kwenye kitanda chake, au jinsi

yeye mwenyewe alivyojificha

pangoni si muhimu. Hayo ni

matukio muhimu pia kwa

sababu yanatukumbusha

kwamba mbinu na mikakati

iliyotumiwa na Mtume

w a M w e n y e z i M u n g u

kufikia lengo, ilikuwa ni

ya kibinadamu na siyo

ya binadamu wa ajabu

(superhuman). Hazikuwa

mbinu zilizohitaji miujiza

kuzitekeleza.

Hatuwezi kudai kwamba,

kwa kuwa Muhammad

(saw) alikuwa Mtume,

na sisi siyo Mitume, basi

hatuwezi kufuata nyayo zake

kikamilifu, hasa linapokuja

s u a l a l a j i n s i M t u m e

alivyoendesha harakati za

kusimamisha Uislamu. Kama

Waislamu, lazima tukumbuke

kwamba mbinu na mikakati

iliyotumiwa na Mtume katika

harakati za kusimamisha

dini ya Mwenyezi Mungu

ipo kwa ajili yetu kufuata,

na kutofuata ni kumuasi

Mwenyezi Mungu.
AN-NUUR

12 MUHARRAM 1434, IJUMAA DESEMBA 14 - 20, 2012

IMEELEZWA kuwa viongozi

wa Jumuia ya UAMSHO

visiwani Zanzibar, ambao

bado wanashikiliwa rumande,

sasa wameanza kupatiwa

huduma muhimu kama

mahabusu wengine gerezani

Kiinua Mguu Juu Unguja.

Kabla ya hapo, viongozi hao

walidai kufanyiwa vitendo vya

kidhalilishaji huko gerezani

ikiwa ni pamoja na kukataliwa

kupewa chakula cha ndugu zao,

kusoma Qur’an, kubadili nguo

wala kukutana na wahabusu

wengine.

Wa k i l i a n a y e w a t e t e a

viongozi hao wa Kiislamu, Bw.

Salum Taufiq, amenukuliwa

akisema kuwa wateja wake

tayari wameruhusiwa kula

chakula kutoka nyumbani,

kusoma Qur’ani, kubadilisha

nguo na kutoka kwenye vyumba

vyao na kuchanganyika na

mahabusu wengine.

Awali, baada ya kushikiliwa

mahabusu bila dhamana,

viongozi hao walifungua kesi

ya kupinga kubaguliwa na

kutopewa huduma bora tangu

Usikose nakala yako ya

AN-NUUR kila

Ijumaa

Uamsho Zanzibar waanza kupatiwa huduma muhim

Na Mwandishi Wetu

walipofunguliwa mashtaka

Oktoba 21 mwaka huu.

B a a d h i y a m a s h i t a k a

yanayowakabili viongozi hao

wa UAMSHO ni kuhatarisha

usalama wa taifa na kusababisha

uharibifu wa mali.

Viongozi hao ni maarufu

kwa kupigania mabadiliko

katika muundo wa muungano

wa Tanganyika na Zanzibar

na walifanya mikutano mingi

kuhamasisha wananchi kukataa

mfumo wa hivi sasa wa

muungano wa serikali mbili.

Jumuia ya UAMSHO kabla

ya kukamatwa viongozi wake,

imekuwa mstari wa mbele

kutetea maslahi ya Mamlaka

ya Zanzibar, na kutaka uwepo

utaratibu wa kupigwa kura

ya maoni kabla ya kuendelea

mchakato wa kukusanya maoni

juu ya kuandikwa katiba mpya

visiwani humo.

Aidha Taasisi hiyo imekuwa

na jitihada za kutaka kuwepo

muungano wenye maslahi

kwa pande zote za nchi, kwa

maana ya Tanzania Bara na

Zanzibar na pendekezo kubwa

likiwa ni kuwepo muungano wa

mkataba.

SHEIKH Farid Hadd akiwa katika karandinga la Polisi Zanzibar.

Sheikh Ponda Issa bado yupo rumande Segerea

Na Shaban Rajab wakili wa washitakiwa Juma mambo ni ya kiutendaji zaidi. Aidha alisema walikaa kwamba, sahihi ya mlalamikaji

Nassoro.

Wakili Nassoro, aidha alihoji pamoja na Balozi wa Misri haikuwekwa siku ya mkataba.

SHEIKH Ponda Issa jana Aliongeza kuwa hajui kwamba Bakwata inahusika na na kujadiliana, ambapo Balozi Hivyo walisema kuna hofu ya

alirejeshwa tena rumande kiwanja hicho huko nyuma watu gani.

huyo aliwataka kuwajengea kughushiwa mkataba huo.

b a a d a y a k e s i y a k e madhumuni yake yalikuwa ni Sheikh Makusanya alijibu jengo la ghorofa chuoni Hata hivyo upande wa wa

kusikilizwa.

nini na namna kilivyopatikana kuwa Baraza hilo linawahusu Markazi kwa ajili ya mabweni Jamhuri ulisema kuwa kutizama

Ponda anaendelea kukaa pia hajui.

Waislamu wote wa Tanzania. na madarasa ya wanachuo

rumande baada ya kukataliwa Hata hivyo Wakili Nassoro Jibu hilo lilitoa mwanya

uhalali wa sahihi zilizomo

na kuwafanyia ukarabati wa

dhamana.

alipomtaka kurejea kipengele wa kuhoji iwapo Waislamu Markaz Chang’ombe.

katika mkataba huo sio kazi

Jana kesi hiyo iliposikilizwa, cha muhtasari wa kikao cha walishirikishwa vipi katika Baadae ndipo Bakwata ya mlalamikaji na kwamba,

s h a h i d i w a u p a n d e w a Baraza la Maulamaa kilichojadili mpango huo wa kubadilishana wakakabidhiwa kiwanja kwa mkataba uliowasilishwa ni

mlalamikaji katika kesi suala la kubadilishana umiliki umiliki wa ardhi na Agritanza mkataba na Agritanza.

halali kimatiki kwa kuwa

inayomkabili Sheikh Ponda wa ardhi kati ya ekari nne za na kwamba sasa ujenzi wa N y a r a k a z a m k a t a b a unakidhi uwepo wa pande mbili

Issa Ponda, ambaye ni Bakwata na ekari 40 za kampuni chuo kikuu utafanyika huko ziliwasilishwa mahakamani zilizokubaliana.

Sheikh na Kadhi wa Bakwata ya Agritanza zilizopo Kisarawe Kisarawe? Sheikh Makusanya kama kielelezo cha ushahidi Kesi hiyo iliahirishwa hadi

mkoa wa Shinyanga, Ismail Pwani, alikuta kipengele hicho alijibu kuwa hajui.

na 3.

hapo itakapotajwa ambapo

Habib Makusanya, ameieleza kikieleza kuwa Bakwata ilikuwa Shahidi mwingine aliyetoa Bw. Mohammed alisema hata

mahakama ya Hakimu Mkazi na mpango wa Kujenga Chuo utetezi wake mahakamani hapo

Sheikh Ponda na wenzake

hivyo baada ya makabidhiano na

Kisutu, Jijini Dar es Salaam Kikuu cha Kiislamu hapo alikuwa ni mmoja wa wamiliki

w a t a n o , w a l i r e j e s h w a

kuanza kuandaa vifaa vya ujenzi

kuwa, hajui ni namna gani Markazi Chang’ombe.

wa kampuni ya Agritanza Bw.

rumande.

eneo hilo limemegwa kiasi cha Hata hivyo kabla ya kukubali Suleiman Nassoro Mohammed,

wa ukuta kuzunguka kiwanja kesi hiyo imeahirishwa

kubakia kiwanja cha ekari nne kipengele hicho, shahidi huyo ambaye ni mfanyabishara wa chao, ndipo alipokuja Sheikh hadi Desemba 18 itakapotajwa

ambacho kimepewa kampuni ya alishikilia kuwa Bakwata mtaa wa India jijini Dar es Ponda na kumtaka kuacha kazi ambapo itasikilizwa tena

Agritanza Ltd.

ilikuwa na mpango huo katika Salaam.

hiyo.

Desemba 31 mwaka huu.

Aidha Sheikh Makusanya eneo la chuo cha Kiislamu Yeye alisema mbele ya Alisema baadae wakaja watu Katika kesi nyingine,

ameeleza mahakamani kuwa Al haramain cha jijini Dar es mahakama kuwa wanamiliki takriban ya 500 na kukaa eneo watuhumiwa saba waliokuwa

pamoja na kwamba yeye ni Salaam.

kiwanja cha ekari 40 huko hilo la kiwanja kwa takriban

mjumbe wa Baraza la Ulamaa Hata hivyo alipoulizwa na Kisarawe Pwani.

wakikabiliwa na kesi ya

siku saba.

la Bakwata, Sheikh Mkuu wakili huyo kuwa Aritanza K w a m b a w a l i p o s i k i a

kuchomwa Kanisa la KKKT

Hata hivyo Bw. Mohammed

na Kadhi mkoa Mkoa wa ilipatikana vipi hadi kupewa Bwakata wanahitaji eneo la

Mbagala Zakheem, wameachwa

Shinyanga, hakufahamu kuwa eneo hilo la Chang’ombe, kujenga Chuo Kikuu, walionana

alisema shitaka lao ni la huru baada ya upande wa

eneo hilo na lile kilichopo alikataa kusema lolote. Sheikh na kuwaeleza kuwa wana eneo kuvamiwa kiwanja tu lakini upelelezi kukosa ushahidi wa

Chuo cha Kiislamu Markaz M a k u s a n y a p i a h a k u w a la kutosha huko Kisarawe na hawana shitaka jingine. kuwatia hatiani.

Chang’ombe, kinachoendeshwa tayari kujibu swali lililohoji kwamba iwapo watapatiwa Baadae mawakili wa upande H a t a h i v y o P o l i s i

na Wamisri, lilipangwa na thamani ya mita mraba moja ekari nne chang’ombe, wao wa washitakiwa Bw. Juma wamewakamata watuhumiwa

Bakwata kujengwa Chuo Kikuu ya ardhi ya kiwanja hicho cha watatoa eneo lao hilo.

Nassoro na Bw. Yahya Njama, wengine watano, ambapo

cha Kiislamu nchini.

Chang’ombe.

Alisema Bwakata walituma walipotizama mkataba huo,

“Inasemekana eneo lilikuwa Alipoulizwa kwamba kwa wajumbe wao kuangalia

wameunganishwa na makosa

walieleza kuwa mkataba huo

na ekari 27 hivi, lakini nani nini Bakwata walibadilisha eneo hilo huko Kisarawe na

hayo hayo ya kupora mali za

una kasoro katika uwekaji

aliyefanya eneo hilo kuwa uamuzi wa kujenga Chuo wakaridhika nalo.

Kanisa la KKKT Mbagala

dogo hadi lisitoshe kujengwa Kikuu hapo Chang’ombe kama Kuafuatia kuridhika huko,

wa sahihi, ambapo sahihi Zakheem kwa kutumia nguvu.

chuo sijui, haya ni mambo ilivyokusudia, na kama Wamisri waliahidiwa kuwa Masheikh ya mawakili wa kampuni Kesi hiyo nayo iliahirishwa

ya kiutendaji,” alijibu Sheikh wanaoendesha Chuo cha Markaz B a k w a t a w a t a j a d i l i a n a ya uwakili ya MJ Diamond, hadi Desemba 18, 2012

Makusanya kufuatia maswali Chang’ombe nao walihusishwa na kitafuatia kikao cha ambao ndio waliotengeneza itakapokuja kwa ajili ya

aliyokuwa akiulizwa na katika mabadiliko hayo, Sheikh Wadhamini kabla ya kufikia mkataba huo hazionekanai na usikilizwaji wa awali.

Makusanya alisema hayo makabidhiano.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.