sheria au roho.vp (Read Only) - Martin Bucer Seminar
sheria au roho.vp (Read Only) - Martin Bucer Seminar
sheria au roho.vp (Read Only) - Martin Bucer Seminar
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
WAGALATIA 3:8-14 : JE, SHERIA INAJIPINGA

YENYEWE?

Wagalatia 3:8-14: “Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani

kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri

Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote

watabarikiwa. Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu

aliyekuwa mwenye imani. Kwa maana wale wote walio wa matendo ya

sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu

asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.

Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu

katika sheria; kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani. Na torati

haikuja kwa imani, bali, Ayatendaye hayo ataishi katika hayo. Kristo

alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili

yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;

ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Kristo Yesu,

tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.”

Kwa mujibu wa Ragnar Bring 53 , sura ya tatu ya Wagalatia, hususani

mstari wa 12, unadhihirisha uwiano mkubwa na Warumi 10:4-5. Kwa

sababu hii, basi tuchunguze Warumi 10:4-5.

Katika Warumi 10:4-8, Paulo anasema, “Kwa maana Kristo ni mwisho

wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki. Kwa maana Musa aliandika

juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa

hiyo. Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni

mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumletea

Kristo chini), au, ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani ni

kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.) Lakini yanenaje? Lile neno li

karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile

neno tulihubirilo.”

Kwa nini Waisraeli katika kumkataa Kristo, hawakujali haki na Sheria

(Rum.10:2-3)? Walimkataa Kristo, aliye mwisho wa sheria. Neno la

Kigriki ‘telos’ lina maana nyingi, na linapaswa kutafsiriwa kama ‘mwisho’

au ‘kusudi’. Tafsiri hutegemea imani ya mtafsiri juu ya Sheria ya Musa.

Kwa maoni yangu, tafsiri, “Kristo ni utimilifu (au lengo) la sheria” inaakisi

vema maelezo ya Paulo juu ya Sheria katika Warumi (kwa mfano, 3:20,

31; au 7:7, 12-16, 22-24; 8:3-4, 13:8-10). 54 Sheria yote inatafuta lengo

lake, maana yake, ukamilifu wake na utimilifu wake katika Kristo.

32