19.06.2013 Views

C:\Users\Home\Documents\My Webs - Excel Exams

C:\Users\Home\Documents\My Webs - Excel Exams

C:\Users\Home\Documents\My Webs - Excel Exams

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

KATA YA MANISPAA YA NAKURU MASHARIKI

MTIHANI WA MAJARIBIO

DARASA LA SABA MUHULA WA KWANZA 2009

KISWAHILI

MUDA: SAA MOJA DAKIKA 40

Jaza nafasi kwa jibu lifaalo

Milka alivikunjua tena vile __1__ vya majibu na __2__ kuvisoma __3__ mara __4__. Alikuwa haamini

kabisa __5__ majibu __6__ yalikuwa kweli! Cheti __7__ kilionyesha __8__ ya uchunguzi __9__, yaani alikuwa

na virusi __10__ ukimwi na majibu __11__ matokeo ya uchunguzi __12__ Bitrisa yalionyesha __13__ yakiwa

maana __14__ na virusi __15__ ukimwi.

1. A. waraka B. cheti C. vyeti D. vitu

2. A. kwanza B. kuanza C. kuanzi D. kuwaza

3. A. na B. wa C. kwa D. vya

4. A. ingine B. mengine C. mingine D. nyingine

5. A. kule B. kweli C. kama D. vile

6. A. ile B. yale C. zile D. ule

7. A. yake B. wake C. chake D. kwake

8. A. jibu B. mfano C. tukio D. majibu

9. A. chanya B. hasi C. jumlisha D. kutoa

10. A. za B. wa C. na D. vya

11. A. kwa B. ya C. za D. vya

12. A. ya B. za C. na D. wa

13. A. kuzindisha B. hasi C. chanya D. kutoa

14. A. hakua B. hakukua C. hakuwa D. hakui

15. A. wa B. za C. via D. vya

Katika swali la 16-30, jibu kila swali kulingana na

maagizo

16. Kiyoyo ni kwa bata kama vile________ni kwa

nguruwe.

A. kichengo B. kivinimbi

C. kiwengwe D. kiluwiluwi

17. 5/

7 inaitwa____________.

A. tusui tano B. subui tano

C. tano kwa saba D. saba kwa hamsa

18. Adhuhuri ni wakati ambapo___________.

A. watu hula chajio B. watu hula staftahi

C. watu huamka D. watu hula kishuka

19. Neno ndimi liko katika ngeli ya________.

A. A-WA B. I-ZI C. U-ZI D. U-I

20. Kuna misitu mingi katika________yetu.

A. inchini B. nchi

C. ncha D. inchi

21. Tunasema thurea ya nyota na_____la nyuki.

A. kipeto B. jozi

C. safu D. bumba

22. Kila mwanafunzi______anunue______la

rangi ya manjano.

A. sharti, shati B. zana, sana

C. washa, warsha D. sabuni, zabuni

23. Unipe, usinipe kwangu ni________. Yaani

ni sawa tu.

A. moja B. wamoja

C. mamoja D. pamoja

24. Siku za_____nyasi na majani huwa kijani

kibichi.

A. kiangazi B. masika

C. kipupwe D. vuli

25. Seremala alikereza mbao kwa________.

A. msumeno B. patasi

C. randa D. bisibisi

26. Andika idadi ya tarakimu ifuatayo

Millioni mbili, mia mbili tisini na sita elfu,

mia tisa na sita.

A. 2029,966 B. 2,269,609

C. 2,296,966 D. 2,296,906

27. Tegua kitendawili kifuatacho: “Kafa huku

ananing’inia,”

A. uyoga

B. nyanya

C. biringanya

D. mwiko

1 Typeset and Printed by: Excel Printers Nakuru

28. Kanusha sentensi ifuatayo - “Mngepanda miti

mngepata mvua,”

A. hamngepanda miti mngepata mvua

B. msingepanda miti msingepata mvua

C. mngepanda miti msingepata mvua

D. hamngepanda miti msipata mvua

29. Mwana kandanda alirukaruka kama______.

A. chura B. mtumwa

C. komba D. samaki

30. Neno jingine sawa na ugonjwa ni______.

A. chelea B. udhi

C. uwele D. mkwasi

Soma taarifa kisha ujibu maswali 31-40

Mahafali ni mkusanyiko mkubwa wa watu kwa ajili ya sherehe ya kuhitimu katika masomo yoyote.

Wakati huo, waliomaliza masomo hupewa vyeti vya aina mbalimbali katika masomo yao. Ni juzi tu tarehe

ishirini na nane mwezi wa kumi na moja ambapo mimi na jamaa yangu tulihudhuria mahafali ya mwana wetu

Jittu Kamaliza. Bwana mdogo huyu alikuwa akisomea katika chuo cha Amani ndogo au kwa kimombo, Peace

Junior. Chuo hiki hupatikana katika mtaa wa Magiwa jijini Nairobi.

Vijana waliohitimu walitunukiwa vyeti mbalimbali vya kuhitimu kwa pamoja na vyeti hivyo walipewa

zawadi za aina nyingi kutokan na sifa au mafanikio yao ya hapa na pale chuoni.

Jittu Kamaliza alipokea zawadi za aina nyingi mno. Kwa mfano alikuwa kati ya wasomi bora wa mwaka.

Kisha alipokea zawadi kwa kuwa mwanafunzi mwenye nidhamu ya hali ya juu.

Baada ya mahafali ya Jittu Kamaliza, tulishuhudia mafahali ya Lilian Binti Wagallah. Huyo alikuwa

mwanafunzi katika chuo kikuu cha Nairobi. Alihitimu katika taaluma ya iktisadi. Iktisadi ni elimu inayohusika na

uchumi na biashara.

Mwalimu Wagallah William ambaye amekuwa mfunzi zaidi ya miaka thelathini alifika jijini Nairobi akiwa

na mkewe Mama Poya, kushuhudia mafahali ya mwana wao Lillian. Baada ya mafahali hayo ya Lillian, tulipata

nafasi ya kuzuru viunga vya Nairobi hadi Kangundo, ardhi ya wakamba penye mvua kwa wingi sana. Pamoja na

Wagallah na wengine katika ziara hiyo walikuwa ni Sammy Ndiwa na Mama Bobi. Sote tulikuwa katika gari

langu tukiwatembeza watoto wetu waliohitimu elimu katika vyuo vyao kwenye mahafali yaliyofana jinsi hiyo. Je

wewe umeshajua ni lini utakapokuwa na mahafali yako? Je, utatualika tuihudhurie?

31. Watu hasa wanafunzi, hufanyiwa mahafali hivi

A. baada ya kuhitimu masomo

B. wanaposoma

C. wakianza masomo

D. kabla ya kuhitimu masomo

32. Katika mahafali waliohitimu hupewa_____.

A. shada

B. shadaa

C. shahada

D. shadidi

33. Hivi karibuni mwandishi alihudhuria mahafali

ya nani aliye aila yake?

A. Amani ndogo

B. Bwana mdogo

C. Lillian Wagallah

D. Jittu Kamaliza

34. Pamoja na vyeti vya kuhitimu, vijana hupewa

A. sifa

B. zawadi

C. nidhamu

D. mafanikio

35. Zawadi ya nidhamu bora hupewa mtu mwenye

A. adhabu njema

B. dhahabu njema

C. elimu njema

D. adabu njema

36. Aliyehitimu katika elimu ya iktisadi ni____.

A. Wagallah

B. Magiwa

C. Lillian

D. Jittu

37. Baada ya mahafali, jamaa walizuru______.

A. Nairobi B. Magiwa

C. Kangundo D. Gari

38. Kuzuru ni sawa na_________.

A. kuona B. kufika

C. kutazama D. kutembelea

39. Mtoto huhitimu___________.

A. anapofuzu B. anapozuru

C. anapofeli D. anapozulu

40. Taarifa hii ni juu ya_________.

A. Hasara za kusoma

B. Elimu ni mali

C. Mvua ya Kangundo

D. Mahafali

2

Soma habari ifuatayo, kisha uchague majibu sahihi zaidi ya maswali 41-50

Mavazi aidha humpamba mwanadamu au humuaibisha. Mavazi humpamba anapotaka kupambika na

humuaibisha anapotaka kujiaibisha.

Sababu kuu ya watu kuvaa mavazi ni kujisitiri ingawa zipo sababu mbalimbali kama vile kujikinga na

baridi, kuhifadhi utamaduni wake, kutambuliwa kwa cheo chake mbali na kule kutaka kuvutia watu.

Jambo la kustaajabisha ni kuona kwamba ile sababu kuu ya kujisitiri, siku hizi huwa haina uzito wowote

kwa mwanadamu hasa vijana. Nguo fupi na za kukaba mwili zimekuwa ni mtindo wala si aibu kwa wengi. Nguo

nyembamba zenye kuonyesha yasiyofaa kuonekana ndizo zinazotia fora. Ulimwengu umebadilika haraka kiasi

kwamba watoto hawa hutoka mbele ya wazazi wao bila ya kukatazwa na wazazi wao wala kaka au dada zao.

Wahenga hawakukosea waliposema yale waliyoyasema juu ya kukatazama makosa.

Wamasai ni kabila linalosifika ulimwenguni kote kwa kuweza mpaka leo kuhifadhi na kudumisha utamaduni

wao hasa katika mavazi. Ni kabila liloamini kwa dhati kwamba mwacha asili....................

41. Sababu alizozitaja mwandishi zinazomfanya

mwanadamu kuvaa mavazi ni_______.

A. mbili

B. tatu

C. nne

D. tano

42. Neno gani halina maana sawa na neno vijana?

A. Adinasi

B. Barobaro

C. Uledi

D. Shababi

43. Mwandishi awalaumu vijana kwa______.

A. kupenda kuhifadhi utamaduni

B. kuvuja pesa nyingi juu ya vazi

C. kutotilia maanani umuhimu wa kujisitiri

D. kusahau utamaduni wao

44. Nguo aina ngapi zilimuudhi mwandishi?

A. Mbili

B. Kabuti

C. Nne

D. Tano

45. Wamaasai pia wangeweza kutumia methali

“usiache mbachao..........”

A. kumpatia nduguyo

B. utajuta mwishowe

C. kufuata kila lijalo

D. kwa msala upitao

3

46. Kutia fora inamaanisha

A. kutia adabu

B. kutia wasiwasi

C. kutakiwa zaidi

D. kuhofiwa

47. Methali gani haingeweza kutumiwa juu ya

kukataza makosa?

A. Usipoziba ufa utajenga ukuta

B. Mtaka cha mvunguni sharti ainame

C. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na

ulimwengu

D. Ukicha mwana kulia mwisho utalia wewe

48. Ni nani kati ya hawa huvaa nguo ili ajitambulishe

cheo chake?

A. Mwalimu

B. Daktari

C. Hakimu

D. mkulima

49. Wamaasai____________.

A. wamelaumiwa kwa kusahau utamaduni wao

B. wamesifiwa kwa kujinaki na utamaduni wao

C. hawapendelei kuonekana na nguo zao

D. wamleta mabadiliko katika utamaduni wao

50. Maliza methali: Mwacha asili_______.

A. na asili humwacha

B. atadharauliwa

C. hana mwisho mwema

D. ni mtumwa

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!