C:\Users\GITOGO\Documents\8 AI6 - Excel Exams
C:\Users\GITOGO\Documents\8 AI6 - Excel Exams
C:\Users\GITOGO\Documents\8 AI6 - Excel Exams
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
EXCEL EXAM

A6

KENYA EXAMS ONLINE

DARASA LA NANE 2011

KISWAHILI

MUDA: SAA 1 DAKIKA

40

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo

zaidi kati ya yale uliyopewa.

Katika karia __1__, paliishi Mzee Kazi. Kondeni __2__ alikuwa amebuni wazo __3__ kuanzisha bustani iliyotoa

mazao na matunda mengi. Kati ya matunda hayo yalikuwa machungwa aliyoyatumia kutengeneza __4__.

Madhumuni ya sharubati yalikuwa ni matumizi yake binafsi na wanawe. Fauka ya hayo, alijitengea __5__ kwenye

bonde __6__ sana. Aliyapa maudhi __7__ kwa adinasi yeyote. Pasina shaka __8__ uadilifu.

1.A. chetu B. wetu C. yetu D. letu

2.A. lake B. chake C. mwake D. vyake

3.A. nzuri B. zuri C. mzuri D. wazuri

4.A. mkandaa B. pure C. mashendea D. sharubati

5.A. baiti B. kidurusi C. chumbani D. masika

6.A. refu B. ndefu C. mrefu D. kurefu

7.A. kipaumbele B. mawaidha C. kisogo D. jeki

8.A. alitamani B. alithamiria C. alidhamania D. alithamani

Serikali yetu __9__ kwa kutozingatia mchezo uitwao pool ambao unazidi kuwa __10__ katika sehemu mbalimbali

nchini. Ni muhimu kuzingatia umuhimu wa __11__ kwani wachezaji wanaweza __12__ katika __13__ ya kimataifa.

Mchezo huu ukichukuliwa kuwa kamari, juhudi za kuendeleza zitaambulia __14__ na mchezo __15__.

9. A. imesifiwa B. imekashifiwa C. imeimarishwa D. imetukizwa

10.A. maarufu B. marufuku C. changamoto D. duni

11.A. kuudunisha B. kuuzorotesha C. kuupuuza D. kuuimarisha

12.A. kushindwa B. kudhoofika C. kushindikana D. kutamba

13.A. sifa B. safu C. siafu D. faifu

14.A. pono B. ukingo C. nunge D. ushindi

15.A. utaimarika B. utakufa C. utapendwa D. utafaulu

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo

sahihi

16. Safari iling’oa nanga wakati jua lilikuwa

likivaa joho lake.

A. Safari ilianza wakati wa machweo.

B. Safari ilikamilika wakati wa adhuhuri.

C. Safari ilianza wakati wa macheo.

D. Safari ilikamilika wakati wa magharibi.

17. Chagua orodha iliyo na vivumishi pekee.

A. Kitisti, asteaste, uadilifu, ihsani

B. Cheka, bingiri bingiri, imani, kashifu

C. Kwa ajili, madhumuni, kichinichini,

adhuhuri

D. Sugu, kokote, mahiri, yapi

18. Bainisha kundi ambalo lina visawe

A. Fulusi, darhimu, ghawazi, njenje

B. Amali, amani, amana, dhamana

1

Available at www.kenyaexams.com

C. Gange, uganga, uchaga, changa

D. Bashasha, bahasha, mabasha, mipasho

19. Chagua sentensi iliyo katika mahali maalumu

na ni dhahiri.

A. Joka limejitoma humu shimoni

B. Huko ndiko walikonaswa.

C. Wachezaji wote wamefika hapa ugani.

D. Aliingia humo.

20. Umoja wa sentensi “Weledi wowote hawawezi

kuiudhimisha mimea hiyo.”

A. Mweledi yoyote hawezi kuidhinisha

mmea huu.

B. Mweledi yeyote hawezi kuidhinisha mmea

huo.

C. Mweledi yeyote hawezi kuidhinishwa na

mmea huo.

D. Mweledi yeyote hawezi kuidhinika na mmea

huo.
21. Chagua kinyume cha sentensi.

Mimi ndimi niliyeibandika.

A. Wewe ndiwe uliyeibandika.

B. Mimi ndiye niliyeibandua.

C. Yeye ndiye aliyeibandua.

D. Sisi ndisi tuliyeibandua.

22. Chagua usemi wa taarifa ulio sawa wa

“Nitakusubiri hapa kesho.” Maksuudi

akasema.

A. Maksuudi akasema kwamba atamsubiri

hapa siku ya kesho.

B. Maksuudi alisema kwamba angemsubiri

hapa siku ya kesho.

C. Maksuudi alisema kana kwamba

atamsubiri hapo siku iliyofuatia.

D. Maksuudi alisema kwamba angemsubiri

hapo siku iliyofuata.

23. Jaribosi ni kwa sikio, kigwe ni kwa

A. shingo B. mkono

C. mguu D. kiuno

24. Chagua kivumishi na kielezi mtawalia kutoka

sentensi.

Mdarisi huyo aliwasili shuleni mafungulia

nyama.

A. aliwasili, shuleni

B. huyo, mafungulianyama

C. shuleni, mafungulianyama

D. huyo, aliwasili

25. Bainisha sentensi iliyo sahihi kisarufi.

A. Angekuwako shuleni angaliwaalika wageni.

B. Asingekuwa shuleni angewaalika wageni.

C. Angalikuwako shuleni angaliwaalika

wageni.

D. Asingalikuwako shuleni asingewaalika

wageni.

26. Chagua sentensi ambayo ni muungano sahihi

wa hizi.

Mwehu alijitoma darasani.

Mwehu aliwaogofya wanagenzi.

A. Mwehu alijitoma darasani kwa mintaarafu

ya kuwaogofya wanagenzi.

B. Mwehu alijitoma darasani lau aliwaogofya

wanagenzi

C. Mwehu alijitoma darasani na kuwaogofya

wanagenzi.

D. Mwehu alijitoma darasani na kuwaogofya

wanagenzi.

27. Methali, “Kozi halei kuku wa wana” ina

maadili gani?

A. Hutuonya dhidi ya kuwa na marafiki.

B. Hutuonya kuwa waangalifu na vitu vyetu.

C. Hutuonya kuwa tusitumie uwezo wetu

ovyovyo

D. Hutuonya tusiwadharau wale wanaokula

chakula duni.

28. ‘Kupata pashua la moyo’ ni

A. Kutokuwa na hamu ya kutenda jambo.

B. Kuwa na wasiwasi kabla ya kuamua kutenda

jambo.

C. Msukumo wa kufanya jambo

D. Kutokuwa na hamu ya kuendelea kufanya

jambo.

29. Barua inayopokewa kupitia tarakilishi ni

A. wavuti B. pataninga

C. mdahalisi D. mtandao

30. Kitendawili “Kabla sijala nyama, mwanangu

huila kwanza.” Jibu lake ni

A. Kuku B. Kisu

C. Kinu D. Jua

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31- 40

Mambo yalipochupa mipaka na kukithiri, Adili hakuweza kustahimili tena ila alimwasa na kumwambia

Jeta ya kuwa vitendo vyake alivyovitenda vilikuwa alijojo na vinamchukiza: itakuwa bora akiviacha na akawaepuka

nemsi zake Jeta alikuja juujuu na kupandwa na ghaidhi si haba, ati kwa kuwa Adili anamtuhumu anafanya

vitendo vibaya. Chambilecho wahenga, moyo wa kupenda hauna kinyongo. Adili alisunyaa na kunyerereka.

Mambo yaliendelea na kutia maji maziwani. Sasa Adili hakuweza kustahimili tena ila alimweleza mkewe vizuri.

Jeta aliangua kilio cha kutaka kureja mastakimuni kwa wavyele wake. Adili alisema ya kuwa hapana haja ya

hayo, lakini ingekuwa bora pindi wangekaa baiti mbalimbali mpaka hasira zao ziishe. Adili alihamia kiambo

kingine akamwachia nyo Jeta.

Baada ya kupita haya, manzili yao na mahaba yao yakawa segemnege. Zilipita siku ayami pasina ya

kuonana ana kwa ana’ ingawa Jeta akipeleka waraka kwao na yeye huletewa kuelezewa kila kitu, lakini hajawaarifu

yakuwa ana ugomvi na mumewe. Baada ya mwia ayami wa kupatikana ugomvi na sintofahamu, Jeta hakujali ila aliletewa

barua za simanzi na misaada iliyohitajika.

Makazi ya upweke na kuwa mbali na adinasi aliyemuenzi yalimchosha adili, na aliondoka pasina kusema

wapi anakwenda na lini atarudi. Kabla ya kuondoka alikuja kumwaga Jeta na kumsabihia chochote atakacho na

kumpa ruhusa ya kwenda atakapo. Adili aling’oa habta na kwenda zake. Jeta alisalia akicheza kidege jinsi

2
alivyotaka; mambo yalifurutu alipokuwa mumewe hayupo. Nyumba yake ilikuwa mithani ya mkahawa kila atakaye alikuwa

na fursa ya mja na kufanya atakavyo. Hazikupita siku nyingi Jeta alichoka na maisha ya namna hiyo, na akataka kwenda

kwao. Safari ilitengenezwa na Jeta akaondoka na kwenda kiamboni kwao.

31. Kwa mujibu wa aya ya kwanza, Adili

hakuweza kustahimili tena mambo ya Jeta

kwa sababu

A. yalikiuka miigo

B. yalipindukia hasara

C. yalipita maelezo

D. yalikiuka mipaka

32. Jeta alipandwa na ghaidhi si haba. Hivi ni

kusema alikuwa na

A. hamaki na hasira kwa sababu ya kubezwa

na mumewe

B. hasira kwa sababu ya kupuuzwa kwa ajili ya

vitendo vyake

C. hamaki kwa sababu vitendo vyake viliigwa

na mumewe

D. hasira kwa sababu ya kukanywa dhidi ya

vitendo vyake

33. Jeta alikasirika kwa sababu

A. alidai mumewe alikuwa akimsingizia uovu

B. ni kweli kuwa yeye alikuwa mwadilifu

lakini mumewe akamsingizia uovu

C. Adili aliwataka nemsi zake kuja nyumbani

kwao

D. Yeye alikuwa mama aliyekasirika mara

kwa mara

34. “Mambo yaliendelea na kutia maji maziwani”

hii ina maana kuwa

A. Adili aliendelea kumkashifu akimsingizia

uovu

B. Jeta aliendelea kukataa kuchota maji

ziwani

C. Jeta aliendelea na tabia yake mbaya bila

kujali maonyo

D. Adili na mkewe Jeta waliendelea kupigana

nyumbani

35. Kulingana na kifungu hiki, Adili alihamaki

akamwachia nyumba Jeta kwa mintaarafu ya

nini?

A. Adili aliona ilikuwa heri kuondoka mpaka

hasira zake zipungue kabisa

B. Adili alikuwa amemchukia sana Jeta kwa

sababu ya tabia yake

C. Adili alikuwa amechokeshwa sana na

maisha ya Jeta

D. Adili alikuwa akitaka Jeta awe na upuuzi

3

36. Kwa mujibu wa kifungu hiki, neno ‘kukithiri’

lina maana gani?

A. kudhihirisha

B. kuzidi

C. kupungua

D. kuonekana waziwazi

37. Kulingana na kifungu hiki ulichosoma, neno

linalotumiwa badala ya kuudhi ni gani?

A. kukereketa

B. kutuhumu

C. kuchupa mipika

D. kuchukiza

38. Jeta alituhumiwa na mumewe Adili kwa

sababu ya tabia yake. Hivi ni kusema Jeta

A. aliadhibiwa na mumewe

B. alinasihiwa na mumewe

C. alishukiwa na mumewe

D. alishutumiwa na mumewe

39. Baada ya kupita haya, manzili yao na mahaba

yao yakawa segemnege. Hivi ni kusema

baadaye

A. mambo yao na mapenzi yao yalikuwa

ndivyo sivyo

B. mambo yao na mapenzi yao yalikuwa

shwari

C. mambo yao na mapenzi yao yalirudia hali

ya kawaida

D. mambo yao na mapenzi yao yalitengenea

40. Kwa mujibu wa kifungu hiki, baada ya mume

kuondoka nyumbani mwake kwa muda mrefu,

A. hatimaye tabia ya mkewe Adili ilibadilika

na mumewe akarejea kiamboni kwao

B. hatimaye tabia ya mkewe ilimfanya ajute

mpaka akahiari kuondoka na kwenda kwa

wavyele wake.

C. hatimaye marafiki zake Jeta walimsaidia

mpaka nyumba ikawa kama mkahawa

D. hatimaye wazazi wa Jeta walikuja

kumchukuwa wakamrejesha kwao
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 41 mpaka 50

Mwaka uliopita shule yetu ilichaguliwa kuwa kituo cha kukutania kimichezo. Tulikuwa na michezo aina

ainati shuleni kwetu. Maandalizi yalikuwa kabambe bin kabambe. Mdarisi wa michezo ya riadha alikuwa na gange ya tija

na tijaranya kusimamia maandalizi hayo. Sisi wanagenzi tulikuwa katika mstari wa mbele kabisa kuhakikisha kila kitu

kiliendelea sawa kwa ajili ya kuwa nilikuwa kiranja mkuu.

Siku moja ya Jumatatu wakati wa macheo, mdarisi Bw. Jagina aligonga kengele akatuita twende uwanjani.

Alituambia tutengeneze uwanja wa kufanyia michezo ya riadha. Tulichora mistari yenye safu sita kuzunguka uwanja. Alituambia

hiyo ni sehemu ya wakimbiaji wa masafa au vitalifa mbalimbali. Tulijua kwamba wakimbiaji

wa masafa mafupi, kiasi cha mita mia moja, wangetimuka usawa wa goli moja hadi jingine. Wakimbiaji wa mita

mia mbili wangezunguka nusu ya mzunguko wa uwanja mzima.

Walikuwapo wakimbiaji ambao wangezunguka uwanja mzima mara moja, mara mbili na mara kadhaa

kulingana na masafa ya mbio zao. Mbio nyingine zilikuwa ni za kupokezana vijiti. Mbio hizo husisimua sana.

Wapo wanariadha waliokimbia kwa kuchupachupa mithili ya kangaruu au Abunuwasi. Watoto wadogo walipaswa

kukimbia kwa kusukuma magurudumu huku wengine wakiwa na mayai kwenye vijiko. Wengine walicheza mchezo

wa kubururana kwa kamba. Hayo yote tulielezwa na mdarisi Bw. Jagina. Katikati ya uwanja paliandaliwa michezo anuwai

kama vile; kutupa tufe, kurusha mkuki, kutupa kitumbua na ulengaji shebaha. Papo hapo palikuwa na sehemu iliyotengwa

kwa michezo ya kuruka chini na kuruka juu. Fauka ya hayo, kulikuwa na kuruka kwa upondo.

Tuliandaa mzunguko wa uwanja, mahali pa kukimbia kwa kuruka viunzi. mchezo huu ni wa ajabu zaidi.

Ilipofika siku ya Jumamosi, shule yetu ilijaa na kufurika furifuri umati wa mahuluki kiasi cha kwamba mwenzako akikupotea,

usingeweza kukutana naye tena, labda kwa bahati nasibu tu. Mimi nilikuwa mkimbiaji mahiri kiasi cha kusimama na

kushindana na swara. Basi, kabla ya kwenda kwenye mbio zangu, nilipata nafasi ya kuangalia na kutazamatazama michezo

ya kandanda, raga, mpira wa pete, magongo, jugwe, voliboli na netiboli. Hatimaye, nilijiunga na wapasua hewa wenzi

wangu kama kina Maksudi, Hekima na wengineo.

41. Shuleni kulikuwa na michezo aina ainati. Hivi

ni kusema michezo ilikuwa

A. haba

B. anuwai

C. aina ya kuchokesha

D. migumu mno

42. Shule yetu ilichaguliwa kuwa kituo chao

kukutania kimichezo. Hivi ni kusema shule

yetu

A. ndiyo iliyokuwa kituo cha maandalizi

B. ndiyo iliyowaalika wenyeji wa michezo

hiyo

C. ndiyo iliyokuwa mwenyeji

D. ndiyo ingekutana na wachezaji wote wa

michezo

43. Wanagenzi walishirikiana na mdarisi wa

michezo

A. kuandaa timu yetu ya michezo

B. kuwapokea wachezaji mbalimbali

C. kuwa katika msitari wa mbele

D. kuandaa yaliyohitajika kukimarisha

michezo

44. Kwa mujibu wa taarifa hii, mchezo wa

kubururana kwa kamba ni

A. jugwe B. magongo

C. raga D. tufe

45. Mbio za masafa marefu ni kama vile

A. kuruka viunzi

Available at www.kenyaexams.com

4

B. mbio za kupokezana vijiti

C. mbio za mita mia moja

D. mbio za nyikani

46. Mchezo mwingine wa watoto wadogo ni

A. kurusha mkuki

B. kuruka kwa upande

C. kukimbia mbio za kuchupachupa

D. kucheza raga

47. Kutupa vitumbua ni mchezo unaoshirikisha

A. wazee pekee yake

B. wazee na vijana

C. wavulana na wazee

D. wasichana na wazee

48. Mwalimu wa michezo katika shule yetu

alikuwa

A. Hekima B. Maksuudi

C. Hakutajwa jina D. Jagina

49. Msimulizi wa taarifa hii alikuwa ni

A. mwanariadha wa masafa marefu

B. mwanariadha wa mbio za kuruka viunzi

C. mwanariadha wa masafa mafupi

D. kiranja mkuu lakini sio mwanariadha

50. Kwa mujibu wa taarifa hii, ni mchezo upi

mmoja ambao hauwezi kuchezwa na

wasichana

A. mwereka B. hakuna

C. ndondi D. kuruka viunzi