نﯾﺟوزﻟا نﯾﺑ قوﻘﺣﻟا Haki Za Mume Na Mke - Alhidaaya.com
نﯾﺟوزﻟا نﯾﺑ قوﻘﺣﻟا Haki Za Mume Na Mke - Alhidaaya.com
نﯾﺟوزﻟا نﯾﺑ قوﻘﺣﻟا Haki Za Mume Na Mke - Alhidaaya.com
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
www.alhidaaya.com

نيجوزلا نيب قوقحلا

Haki Za Mume Na

Mke

(Nasaha Za Shaykh Kwa Wanandoa)

ـھ 1432-11-02

Muftiy al-´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah

Aal ash-Shaykh

Mfasiri:

Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

www.alhidaaya.com

يحرلا نمحرلا ﷲ مسب

Himidi zote zi Zake Allaah. Tunamhimidi na kumtaka msaada na

tunamuomba msamaha na tunatubia Kwake. Na tunajikinga Kwake na shari

za nafsi zetu na matendo yetu maovu.

Hakika yule Aliyemuongoza Allaah hakuna wa kumpoteza. Na Aliyempoteza

hakuna wa kumuongoza.

Nashuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah

wa pekee Asiyekuwa na mshirika. Na ninashuhudia ya kwamba Muhammad

ni mja Wake na Mtume Wake swalah za salaam zimuendee na ahli zake na

Maswahaba wake mpaka siku ya mwisho. Amma ba´ad:

Enyi watu! Mcheni Allaah ukweli wa kumcha. Enyi waja wa Allaah! Hakika

familia ndio msingi wa jamii; makazi ambayo Allaah Ameyafanya kwa mume

kuwa ndio makazi yake na kukaa humo. Katika ndoa kuna utulivu wa nafsi,

na kupumua, na mafanikio ya kutokufanya mapenzi na kuwa na usafi wa

moyo. Na ndoa ni uhusiano uliyo imara, na mkataba madhubuti, [kama

Asemavyo Allaah]:

اظيلغ ً ِ َ اقاثيم ً َ ِّ مكنم ُ ِ نذخأو َ ْ َ َ َ

“Na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti.” (04:21)

Na ni ahadi ya wanandoa, kutendeana mema, na ni kuyawekea nguvu maisha

ya kindoa. Na Katubainishia Allaah katika Kitabu Chake na Mtume Wake (

ملسو هيلع ﷲ ىلص ) ahkaam za ndoa wazi kabisa. Zipi haki za mwanaume na yapi

ya wajibu juu yake; na ni zipi haki za mwanamke na ni yapi ya wajibu juu

yake.
www.alhidaaya.com

Wakati wanandoa [mume na mke]watachunga haki hizi na yaliyo yawajibu

kwa kila mmoja, yanakuwa maisha yao - maisha mazuri.

Enyi wanandoa! Ikiwa kweli mnataka maisha mazuri yaliyo thabiti,

yaliyojengeka katika misingi ya mahaba na mapenzi; mwatakiwa nyote

wawili kumchungia [kumtekelezea] kila mmoja haki ya mwenzake kwa

usawa katika maisha haya.

Ewe dada mwenye thamani! Hakika mume wako ana haki juu yako na ya

wajibu; ni lazima kumtekelezea [kwa kufanya hivyo] ni utiifu kwa Allaah, na

ni ukurubisho unajikurubisha kwao kwa Allaah. Katika haki kubwa za mume

wako juu yako, ni kumtii katika mema. Hakika kumtii katika mema ni jambo

la wajibu kwako. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):

“Wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure.” (04:34)

ًلايبس

ِ َ نھيلع َّ ِ ْ َ َ اوغبت ْ ُ ْ َ َلاف َ مكنعطأ ْ ُ َ ْ َ َ نإف ْ ِ َ

Utiifu huwa katika mema tu. Hakuna utiifu kwa yeyote katika kumuasi

Allaah. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):

“Na kaeni nao kwa wema.” (04:19)

فورعملاب ِ ُ ْ َ ْ

ِ نھورشاعو َّ ُ ُ ِ َ َ

Ewe mwanamke wa Kiislamu! Hakika mume wako ana haki juu yako ya

kumtii katika mema. Na Mtume ( ملسو هيلع ﷲ يلص ) anasema:
www.alhidaaya.com

"Akimwita mume mke wake kitandani, [asije] na mume wake akamkasirikia,

Malaika wanamlaani mpaka asubuhi."

Katika kumtii mume wako kuna thawabu kubwa mbele ya Allaah. Anasema

Mtume ( ملسو هيلع ﷲ يلص ):

"Akiswali mwanamke [swalah zake] tano, na akafunga mwezi wake,

akahifadhi tupu yake na akamtii mume wake ataingia Peponi katika mlango

wowote aupendao [katika milango minane ya Peponi]."

Hii ni fadhila kubwa na neema kubwa kwa Allaah kwako, ewe dada wa

Kiislamu kwa kumtii mume wako katika mema.

Na katika haki zake za wajibu juu yako, ni kumtekelezea haja zake atapotaka

hilo. Hakika katika ndoa kuna kuzihifadhi tupu kwa halali, kuilinda na

aliyomuharamishia Allaah kwake.Anasema Mtume ( ملسو هيلع ﷲ يلص ):

"Atapomwita mume mke wake juu ya kitanda na akakataa, akamghadhibikia,

hivyo Malaika humlaani mpaka asubuhi."

Na kwa hili kaelekezwa mume kwa mkewe, na wakajaaliwa hilo kuwa ni

swadaqah kwa wote wawili - mume na mke. Anasema Mtume ( ملسو هيلع ﷲ يلص

"Na kumuingilia mkeo ni swadaqah.” Wakasema (Maswahabah) na je, katika

kupata raha binafsi mmoja wetu analipwa??! Mtume ( ملسو هيلع ﷲ ىلص )

akasema: “Je, mnaonaje lau mtu huyo angeingiza [tupu yake] katika haramu,

je, ingelikuwa ni shari juu yake [ya madhambi, maradhi, adhabu]?, wakasema:

ndio. Akasema Mtume ( ملسو هيلع ﷲ ىلص ): “Hivyo ndivyo atakapoweka [tupu

yake] katika halali atalipwa.” [Muslim]

Na katika haki za mume wako juu yako, ni kuwa na adabu na kumheshimu,

hii ni amaanah umeaminiwa kwayo.
www.alhidaaya.com

Mwanamke mwema, mwenye mtazamo mzuri kumuangalia mume wake;

mwenye kujihifadhi ili kudumisha sifa ya kitanda chake, hivyo ni bora.

ُﷲ ّ ظفح َ ِ َ امب َ ِ بيغلل ِ ْ َ ْ ِّ تاظفاح ٌ َ ِ َ تاتناق ٌ َ ِ َ تاحلاصلاف ُ َ ِ َّ َ

“Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanaojilinda hata katika siri

kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajilinde.” (04:34)

Na katika Hadiyth, anasema ( ملسو هيلع ﷲ يلص ):

"Bora ya raha kwa mwanaume ni kupata mke mwema, [ambaye] akimtazama

anafurahi, na akimuamrisha [kitu] anamtii, na [mume] akiwa mbali naye

hujihifadhi mwenyewe [mwanamke] na mali [ya mumewe]."

Ewe dada ´Aziyzah! Hakika kumridhisha kwako mume wako na

kumheshimu, ni jambo jema, na ni kitu kizuri, na ni jambo la wajibu juu yako

Kishari´ah; Usidanganyike na hayo mafilamu machafu, ambayo yanakuweka

mbali na heshima yako na fadhila zako na yaliyojaa maovu. Allaah

Atusamehe sote kwa hayo.

Na katika haki za mume juu yako, usimruhusu yeyote kuingia nyumbani bila

idhini [ruhusa] yake. Utaejua kuwa hatomridhia kuingia usimruhusu. Kwa

kuwa Mtume ( ملسو هيلع ﷲ ىلص ) anasema:

"Si halali kwa mwanamke kumruhusu yeyote kuingia nyumbani kwa mume

wake ila kwa idhini [ruhusa] yake."

Na katika haki za mume juu yako, kuchunga nyumba yake na mali yake.

Katika Hadiyth [anasema Mtume]:
www.alhidaaya.com

"Mwanamke ni mchungaji katika nyumba ya mume wake na ataulizwa [na

Allaah] kwa alichokichunga."

Na kakataza Mtume ( ملسو هيلع ﷲ ىلص ) kutoa katika mali ya mume wako ila

kwa idhini yake [mume].

Na katika haki za mume juu yako, usimkalifishe kukuhudumia [kukupatia

matumizi] kile asichokiweza na ni kizito kwake na hakiwezi. Hakika Allaah

Anasema:

ُﷲ َّ ُهاتآ َ امم َّ ِ قفنيلف ْ ِ ُ ْ َ هقزر ُ ُ ْ

ِ هيلع ِ ْ َ َ ردق َ ِ ُ نمو َ َ هتعس ِ ِ َ َ نم ِّ ةعس ٍ َ َ وذ ُ قفنيل ْ ِ ُ ِ

“Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na mwenye dhiki atoe katika

alichompa Allaah. Allaah Hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa.”

(65:07)

Na katika haki za mume juu mke, ni kuwapa malezi watoto na kuwaongoza;

nyote wawili mume na mke ni wenye kushiriki katika jambo hili muhimu

sana. Kuwapa malezi vijana na kuwaandaa wawe vizuri, na kuwaamrisha

mema na kuwatahadharisha na shari. Na kule baba kuwa kwake kiigizo bora

kwa watoto wakiume, katika kheri na wema. Na mama ana jukumu lakuwa

kiigizo bora kwa mabanati wake, kwa kujisitiri vizuri na usafi wa moyo, na

dhamira ya maadili ya thamani.

Na katika haki za mume juu yako, ni wewe kubaki nyumbani na kutotoka ila

tu kwa dharurah. Ama kutoka kwako nyumbani bila ya dharurah kunaifanya

nyumba kuzorota na kukosekana mwenye kuilinda na kuihifadhi.

Na katika haki za mume juu yako ni wewe kutomuudhi kwa maneno mabaya.

Mwambie [muongeleshe] maneno mazuri yenye baraka. Kuuachia ulimi

hovyo, haimpasi mwanaume wala mwanamke. Na imepokelewa kutoka kwa

Mtume ( ملسو هيلع ﷲ ىلص ) kuwa amesema:

"Akimuudhi mwanamke mume wake duniani, anasema mke wake katika

Huur al-'Iyin "Allaah Akuangamize usimuudhi, kwani huyo ni mtu wetu -

imekaribia kuachana nawe na kuja kwetu."
www.alhidaaya.com

Na katika haki za mume wajibu juu yako, usijikurubishe kwa Allaah

kwaswalah za naafilah [sunnah] na swawm [za sunnah] ila kwa idhini

[ruhusa] ya mume wako.

Hakika haki yake [mume] ni yenye kutangulia. Na kwa hili anasema Mtume (

ملسو هيلع ﷲ ىلص ):

"Si halali kwa mwanamke kufunga, na mume wake yuko ila kwa idhini yake."

Katika haki za mume juu yako, aliyobainisha Mtume ( ملسو هيلع ﷲ ىلص )

kuwatahadharisha wanandoa [mume na mke] kutoa siri ya uhusiano wa

kindoa [yafanyikayo ndani], akasema kuwa mwenye kufanya hivyo ni katika

watu waovu sana. Kwa kuwa hii ni dalili ya ukosevu wa haya na adabu.

(Haki Za Mke Juu Ya Mume)

Ndugu mume karimu, hakika mke wako ana ya wajibu pia juu yako na haki

zake. Lazima umtimizie - kama jinsi yeye kwako ana haki zake na ya wajibu,

na wewe hali kadhalika una haki na ya wajibu juu yake. Lazima umtimizie.

Haki yake kubwa juu yako, ni wewe kumpa mahari kwa ukamilifu; sawa

akiwa ni mwenye uwezo au si mwenye uwezo. Kwa kuwa Allaah Anasema:

ائيرم ً

ِ َّ ائينھ ً ِ َ هولكف ُ ُ ُ َ اسفن ً ْ َ هنم ُ ْ ِّ ءيش ٍ ْ َ نع َ مكل ْ ُ َ نبط َ ْ ِ نإف ِ َ ةلحن ً َ ْ ِ نھتاقدص َّ ِ ِ َ ُ َ ءاسنلا َ َّ اوتآو ْ ُ َ

“Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa nikipawa. Lakini

wakikutunukieni kitu katika mahari - kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke

kwa raha.” (04:04)

Ni wajibu kumpa haki yake kamili. Katika haki zake juu yako, ni kumpa

matumizi [kumuhudumia] chakula, mavazi na makazi. Anasema Allaah

(Ta´ala):
www.alhidaaya.com

فورعملاب ِ ُ ْ َ ْ

ِ نھتوسكو َّ ُ ُ َ ْ ِ َ نھقزر َّ ُ ُ ْ

ِ هل ُ َ دولوملا ِ ُ ْ َ ْ ىلعو َ َ َ

“Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa

ma’aruwf (mujibu wa ada).” (02:233)

Akasema tena:

نھيلع َّ ِ ْ َ َ اوقيضتل ُ ِّ َ ُ ِ نھوراضت َّ ُ ُّ َ ُ لاو َ َ مكدجو ْ ُ ِ ْ ُ نم ِّ متنكس ُ َ َ ثيح ُ ْ َ نم ْ ِ نھونكسأ َّ ُ ُ ِ ْ َ

“Wawekeni humo humo mnamokaa nyinyi kwa kadiri yapato lenu, wala

msiwaletee madhara kwa kuwadhiki.”(65:06)

Matumizi ni wajibu kwa mume kumpa mke wake, kwa mujibu wa mkataba

wa ndoa baina yao. Na Mtume ( ملسو هيلع ﷲ ىلص )anasema kumwambia Saad

bin Abi Waqqas kuhusiana na hili:

"Hakika hutotoa matumizi kwa kutaka Uso wa Allaah isipokuwa utapewa

ujira kwalo, hata ikiwa ni kitu kidogo utachokiweka kwenye kinywa cha

mkeo."

Na katika haki zake juu yako, ni kukaa nae kwa wema kwa adabu za

Kishari´ah. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):

“Na kaeni nao kwa wema.” (04:19)

Anasema tena:

فورعملاب ِ ُ ْ َ ْ

ِ نھورشاعو َّ ُ ُ ِ َ َ

فورعملاب ِ ُ ْ َ ْ

ِ نھيلع َّ ِ ْ َ َ يذلا ِ َّ لثم ُ ْ

ِ نھلو َّ ُ َ َ
www.alhidaaya.com

“Na hao wanawake wana kama ile (haki) iliyo juu yao kwa ma’aruwf (mujibu

wa shari’ah).” (02:228)

Na anasema Mtume ( ملسو هيلع ﷲ ىلص ):

"Mbora [wa wanaume ni] aliye mbora kwa familia yake, na mimi ni mbora

kwa familia yangu."

Na katika haki zake juu yako, ni kumlinda [asipatwe na] adhabu ya Allaah

kwa kumuamrisha mema na kumtahadharisha na shari [maovu].

ةراجحلاوسانلا ُ َ َ ِ ْ َ ُ َّ اھدوقو َ ُ ُ َ اران ً َ مكي ْ ُ ِلھأو ْ َ َ مكسفنأ ْ ُ َ ُ َ اوق ُ اونمآ ُ َ نيذلا َ ِ َّ اھيأ َ ُّ َ ايَ

“Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahli zenu na Moto ambao kuni zake

ni watu na mawe.” (66:06)

Anasema tena:

ىوقتلل َ ْ َّ ِ ةبقاعلاو ُ َ ِ َ ْ َ كقزرن َ ُ ُ ْ َ نحن ُ ْ َّ اقزر ً ْ

ِ كلأسن َ ُ َ ْ َ لا َ اھيلع َ ْ َ َ ربطصاو ْ ِ

َ ْ َ ةلاصلاب ِ َ َّ ِ كلھأ َ َ ْ َ رمأو ْ ُ ْ َ

“Na waamrishe watu wako kusali, na uendelee mwenyewe kwa hayo. Sisi

hatukuombi wewe riziki, bali Sisi ndio tunakuruzuku. Na mwisho mwema ni

kwa mcha Mungu.” (20:132)

Katika haki zake juu yako, ni wewe kuwa na wivu kwake, wivu ambao ni

wakweli [mzuri] - kwa kumtakia kheri, na kumuonya na kila shari uijuayo;

bila ya kuwa na wasiwasi [katika wivu wako] na mashaka, na matarajio ya

makosa; bali iwe ni wivu ulioubeba kwa ajili ya kumtakia kheri na kumlinda

asipatwe na shari. Usiwe ni wivu wa wasiwasi na mashaka na kuangalia tu

udhaifu [wake]. Ni watu wangapi wamekuwa na aina ya maradhi kama haya,

na kuona wengine si kama yeye. Ni wajibu kumcha Allaah.
www.alhidaaya.com

Kama inavyotakikana kwa mwanamke pia kuwa na wivu kwa mume wake.

Lakini anapaswa kuwa na wivu uliojengeka katika mambo ya wazi; si kwa

uchunguzi wa fujo na vurugu na kuchunguza namba za simu - ukaguzi

nakadhalika, jambo ambalo linaweza kusababisha shari na balaa baina yao.

Na katika haki za mwanamke juu ya mume wake, ni kumfunza mambo ya

dini yake asiyoyajua na yatamsaidia kufanya mema.

Na katika haki zake juu yako, ni [wewe] mwanaume kuwa mwadilifu baina

ya wake [zako] ukioa wake wengi [ukewenza]. Anasema Mtume ( هيلع ﷲ ىلص

ملسو ):

"Yule mwenye wake wawili, akamkandamiza mmoja zaidi kuliko mwengine,

atakuja siku ya Qiyaamah na bega lake likiwa limepinda."

Na katika haki zake juu yako, usimkandamize na kumnyima haki zake kwa

kumdhulumu na kumfanyia uadui, kwani hakika dhuluma ni gizo siku ya

Qiyaamah. Usitumii udhaifu wake na ukosevu wake wa mabavu, ukamuonea

[mkandamiza] bila ya hatia yoyote, ukamtusi na kumtuhumu kwa mambo

ambayo kajitenga nayo mbali.

Katika haki zake juu yako, ni kumhifadhia mali yake na usimtumie na

ukaitumia mali yake; ukawa unamtisha kwa talaka akiomba haki yake na

ukawa unaitumia. Yote haya ni katika uonevu. Hakika wajibu wako ni wewe

kumhudumia sawa na uwezo wako, umejiingiza katika [maisha ya] ndoa

pambana na ndoa hii.

Wakati mke atapotekeleza [timiza] wajibu alionao juu ya mume wake, na

wakati mume atapotekeleza [timiza] wajibu alionao juu ya mke wake; hivyo

maisha na hali huwa nzuri. Na wakati nyumba itaachwa, wakati kila mmoja

atapoacha kutekeleza haki ya mwenzake; wakati mke atapoacha kumtimizia

mume haki zake, au mume akaacha kumtimizia mwanamke haki zake; hivyo

hutokea shari na uharibifu.
www.alhidaaya.com

Ama kila mmoja akichunga haki alionayo juu ya mwenzake, hakika hii ndio

sababu ya furaha na kuwa na maisha mazuri na familia huishi katika

muelekeo na usalama.

Enyi watu! Mcheni Allaah (Ta´ala) ukweli wa kumcha. Shari´ah ya Uislamu

imekuja kutekeleza uadilifu kwa njia zote. Na katika hayo ni uadilifu baina ya

wanandoa, kwa kila mwanandoa mmoja kumtimizia mwengine. Mwanamke

atimize yaliyo ya wajibu juu yake kwa mume wake; na mume atimizeyaliyo

ya wajibu juu yake kwa mke wake.

Hivyo ndivyo yalivyo maisha ya ndoa yaliyofanywa na Uislamu kwa

wanandoa ili waishi maisha ya furaha; maisha ya furaha na ridhaa.

Tumcheni Allaah katika nafsi zetu [kwa kila mmoja kumtimizia mwenzake

haki yake].

Ewe mume ´Aziyz! Hakika kutania [kucheza] na mke [wako], wacheza naye

na huku wamuelekeza katika mema ni katika sababu zinazoimarisha misingi

ya maisha ya ndoa. Na hakika utoaji onyo mara kwa mara pasina sababu za

kueleweka, ni katika sababu ya kufarakana.

Tahadhari muwe na kukithirisha maonyo ya mara kwa mara bila sababu.

Tahadhari na kufuatilia vijikosa vidogo vidogo ambavyo havina uziro

wowote. Kuwa mwenye kupuuza vijikosa ilimraditu havina kasoro katika

heshima na cheochako, ni juu yako kuwa na subira kwa baadhi ya makosa;

hakuna yeyote aliyesalimika kutokana na makosa. Anasema Mtume ( ﷲ ىلص

ملسو هيلع ):

"Mwanaume asimchukie muumini mwanamke [mkewe], akichukizwa na

moja ya tabia yake atapendezwa na nyingine."

Anasema tena [Mtume]:

"Ninawahusieni kuwatendea wanawake wema."

Subira kwa kila mmoja kumvumilia mwenzake ni jambo linalotakikana.

Mwanamke awe na subira kwa mume wake, na kwa baadhi ya makosa

kunako tabia yake na mwenendo wake ilimradi haijafikia katika kumvulia

cheo na heshima. Na mume awe na subira juu ya baadhi ya makosa ya mke
www.alhidaaya.com

wake, ilimradi haijafika kumvulia cheo na heshima. Iwe wote wanasaidizana

kutengeneza na kumezea [kasoro] za kila mmoja kwa mwenzake.

Na Mtume ( ملسو هيلع ﷲ ىلص ) kamtahadharisha mwanamke wa Kiislamu kwa

kukufuru kwake wema na kumlalamikia sana mume. Akasema kuwa ameona

moto na wakazi wake wengi ni wanawake; kwa tuoacha kwao kulalama na

kukufuru kwao wema.

Lau utamtendea mmoja wao wema maisha yote, akaona kutoka kwako kitu

[kasoro], atasema "Sijawahi kuona kheri [wema] wowote kutoka kwako katu."

Ndugu wapenzi! Matatizo ya kindoa yanakuwa wakati mwingine kwa sababu

zisizokuwa na maana. Wakati wakutafakari na kuzingatia vizuri mtu anakuja

kuona kuwa sababu [zilizoleta matatizo] ni za kijinga zisizo na maana yoyote.

Ni juu ya wazazi wa ndugu wa mume au mke kutatua matatizo haya ndani ya

nyumba, na yasiendelee mambo kama haya hadi yakatoka nje ya nyumba.

Mume amalize tatizo lake na mke wake au na famili yake. Na juu ya familia

yake mwanamke kumkanya wakiona yeye ndo yuko makosani. Na familia ya

mwanamume hali kadhalika wamkanye watapoona kuwa yeye [mume] ndo

yuko makosani.

Familia zote mbili zikisaidizana pamoja na mume na mke kutatua tatizo hili,

hupatikana ufumbuzi mzuri. Ama ikiwa hawatokuwa makini na kujichunga,

huwaka fitna. Mwanaume [baba mkwe] akawa na kasumba kwa binti yake

bila kujali makosa yake; au mwanamume akawa na kasumba ya kushikilia rai

yake bila kujali makosa yake. Hakika huo ni msiba mkubwa.

Na Mtume wetu ( ملسو هيلع ﷲ ىلص ) kamtahadharisha mwanamke wa Kiislamu

kuomba talaka pasina sababu ya msingi. Akasema:

"Mwanamke akimuomba mume wake talaka pasina sababu muhimu, ni

haramu juu yake harufu ya Pepo."

Hivyo ni wajibu kwao mauqif yao iwe ya heshima, mauqif ya kutatua tatizo,

na kumaliza mgogoro huu, na kuzingatia tatizo hili - liangaliwe vizuri.

Iangaliwe sababu na itatuliwe, na qadhiya hii ishughulikiwe ndani ya
www.alhidaaya.com

nyumba. Isende ikatoka nje, khabari ikawafikia watu nje wasiyokuwa na

thamani kwao, na wasiyowapendea kheri - wakaja kuiharibu nyumba na

kuingamiza katika msingi wake. Hukumsikia Allaah Akisema:

ريخ ٌ ْ َ حلصلاو ُ ْ ُّ َ احلص ً ْ ُ امھنيب َ ُ َ ْ َ احلصي َ ِ ْ ُ نأ َ امھيلع َ ِ ْ َ َ حانج َ ْ َ ُ َلاف َ اضارعإ ً َ ْ ِ وأ ْ َ ازوشن ً ُ ُ اھلعب َ ِ ْ َ نم ِ تفاخ ْ َ َ ةأرما ٌ َ َ ْ نإو ِ ِ َ

“Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya

kwao wakisikizana kwa suluhu.Na suluhu ni bora.” (04:128)

Kutafuta suluhu baina ya wanandoa ni kheri, suluhu inayohitaji kuhifadhi

haki ya kila mmoja, suluhu ya kutaka kutatua tatizo na kumaliza ugomvi,

suluhu kurudi katika hali ya kawaida, na maisha ya ndoa kuendelea utulivu

wake, suluhu inayolengo kupata Uso wa Allah na Nyumba ya Aakhirah.

Tumche Allaah katika nafsi zetu.

Na hakika wengi hawatafakari katika sababu ya talaka zilizoko kati ya

wanandoa; unaweza kuona imejengeka katika misingi ya kukosekana kwa

utulivu, na sababu ya talaka hii na mwenye kuiomba si kitu muhimu kwa

kweli bali ni upumbavu wa baadhi ya wanaume au haraka za baadhi ya

familia ya mwanamke; mambo ambayo badala yake yangeliweza kutatuliwa

katika ngazi ya familia bila ya kutoka nje ya nyumba. Namuomba Allaah kwa

sote Atupe Tawfiyq na Sadaad, na msaada wa mwongozo wa kila kheri.

Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Swalah za salaam zimuendee Mtume wetu Muhammad ( ملسو هيلع ﷲ ىلص ) na

ahli zake na Maswahaba wake na watakaomfuata kwa wema mpaka siku ya

Qiyaamah.

Chanzo: http://www.mufti.af.org.sa/node/1757

Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=KiMB0LP_OWE