26.05.2014 Views

HOTUBA YA WAZIRI WA UCHUKUZI MHE.OMARI NUNDU (MB ...

HOTUBA YA WAZIRI WA UCHUKUZI MHE.OMARI NUNDU (MB ...

HOTUBA YA WAZIRI WA UCHUKUZI MHE.OMARI NUNDU (MB ...

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

HOTUBA YA WAZIRI WA UCHUKUZI MHE.OMARI NUNDU (MB.)

WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA FUNGAMANO LA

BANDARI ZA AFRIKA NA ULAYA, UTAKAOFANYIKA ARUSHA

TANZANIA DESEMBA 6, 2010

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA

Bwana Raphael Mollel

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari,

Katibu Mkuu wa IAPH Bw. Susumu Naruse,

Wadau wa Sekta ya Usafiri Majini,

Wageni waalikwa,

Mabibi na Mabwana.

Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wadau wa Bandari

kutoka hapa nchini na sehemu mbalimbali duniani kushiriki katika Kongamano

kuhusu Kuboresha Huduma za Bandari kwa Lengo la Kuchochea Ukuaji wa

Uchumi wa Bara la Afrika. Nimetaarifiwa kuwa kongamano hili muhimu

linawakutanisha pamoja wahusika wakuu wa sekta ya usafirishaji, hususan ule

wa majini kwa lengo la kubadilishana mawazo na uzoefu wa shughuli za bandari

kwa lengo la kuziboresha na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi Afrika. Mada

kuu mliyochagua ni nzuri na imekuja wakati muafaka. Yaani kutafuta kwa njia

ya mjadala mikakati ya kuziwezesha na kuzifanya bandari za Tanzania, Afrika

na ulimwenguni kwa ujumla kufanya kazi zake ipasavyo kwa kasi, tija na

ufanisi mkubwa.

Kongamano hili ni muhimu kwa kuwa linatoa fursa kwa wadau wa Bandari

kujadiliana kwa pamoja namna ya kuboresha huduma za Bandari na usimamizi

wa Bandari katika eneo la Mashariki na Kusini mwa Afrika ili kuongeza ufanisi

wao.

Aidha, Kongamano hili ni fursa ya kuanzisha na kuendeleza mahusiano kati ya

Mamlaka za Bandari au vyama, mashirika ya kikanda na kimataifa, Serikali au

Taasisi nyingine, kwa ajili ya ushirikiano na utafiti wa masuala ya shughuli za

bahari .

Umuhimu wa Bandari:

Ndugu Mwenyekiti,

1

Umuhimu wa Bandari duniani, hususani katika bara la Afrika, hauhitaji

ufafanuzi wala msisitizo. Bandari ni chachu ya maendeleo na ukuaji wa uchumi

wa taifa lolote lile, hata lisilo na bandari. Kwa sababu hiyo kila nchi yenye

bandari na hasa nchi za Kiafrika kwa sasa inajitahidi kuwekeza katika kuboresha

miundombinu ya bandari na mfumo mzima wa usafirishaji vifikie viwango vya

kimataifa.

Changamoto za Sekta ya Bandari

Kwanini ninatilia msisitizo kwa Afrika, kwasababu kwa muda mrefu Bara la

Afrika limekuwa likikabiliwa na changamoto nyingi hususani ukuaji wa

shughuli za kiuchumi ambazo zimeongeza mahitaji ya huduma za bandari.

Lakini kwa Afrika bandari hazijaweza kumudu au kukidhi mahitaji haya. Hali

hiyo ipo pia katika usafirishaji wa nchi kavu kama barabara na reli ambayo

vinapaswa viwe na uwezo unaowiana na ule wa bandari, na pia usafiri wa anga.

Kwa ufupi ni tatizo la usafiri wa aina yeyote. Kwa Tanzania tatizo hili

limepatiwa ufumbuzi kwa kuwa sasa nchi inayo Sera ya Taifa ya Usafirishaji

ambayo inatoa muongozo wa namna ya kujenga miundombinu na utoaji huduma

za uchukuzi zilizo salama, za uhakika na endelevu kwa sekta zote za usafishaji.

Kilichobaki sasa ni Tanzania kuhakikisha kuwa na mikakati madhubuti ambayo

inazingatia uwiano na muingiliano wa miundombinu, na pia miundombinu yote

inategemeana na kusaidiana katika kujijengea uwezo wa ufanisi.

Mapungufu mengi bado yapo, ambayo ni pamoja na bandari zetu kuwa na

uwezo mdogo wa kuhudumia shehena za aina yote; miundombinu ya bandari

ambayo imechakaa na imepitwa na wakati; mtandao mdogo wa reli ambao ni wa

zamani na usiokidhi matakwa; mtando mdogo wa barabara na ambao sio imara;

na vyombo vya uchukuzi ambavyo havikidhi matakwa ya usafirishaji salama na

wa bei nafuu. Mapungufu haya na changamoto nyingine nyingi zinazoikabili

sekta ya bandari, zinafanya bandari za hapa nchini na Afrika kwa ujumla

zisitumike ipasavyo na hivyo kudumaza maendeleo ya uchumi. Kazi kubwa

tuliyonayo sasa ni kuyafanyia kazi mapungufu hayo na kuyapunguza sana katika

kipindi kifupi na hatimaye kuyatokomeza kabisa yale ambayo hayana sababu

kuwepo.

Mabadiliko ya Uendeshaji wa Bandari

Ili kukabiliana na changamoto hizo, mifumo ya uendeshaji wa bandari

ulimwenguni umefanyiwa mabadiliko makubwa ukiwemo mfumo wa kuiwachia

sekta binafsi kutowa huduma katika bandari Mfumo huu wa kushirikisha sekta

2

inafsi ndiyo jibu la matatizo yaliyokuwepo awali kwa nchi nyingi

zinazoendelea. Ili kuweza kunufaika na mfumo huu, inahitajika yawepo

mazingira ya kuvutia sekta binafsi.

Mojawapo ya mikakati iliyotumika kukabili changamoto hizi ni Serikali

kuondokana na kubadili mfumo wa uendeshaji wa mashirika ya kibiashara

ikiwemo bandari. Tumetoka kwenye bandari zilizoendeshwa na Serikali (state

owned and operated ports), kwenda kwenye mfumo wa uendeshaji kwa Taasisi

za Serikali (state owned but operated by semi autonomous Government

institutions), na sasa tuna bandari zinazoendeshwa na Sekta binafsi (private

operated ports).

Tanzania hatukuachwa nyuma katika mabadiliko haya. Mfumo wa uendeshaji

wa Bandari nchini umebadilika kutoka ule wa Mamlaka ya Bandari nchini

kuhodhi shughuli zote za umiliki wa Bandari na uendeshaji wa shughuli za

kuwezesha shehena zinazopita bandarini na kwenda kwenye mfumo wa kumiliki

bandari tu na kukaribisha Sekta binafsi katika uendeshaji wa shughuli za

bandari.

Bandari za Tanzania kwa sasa zinasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa

Bandari (Tanzania Ports Authority - TPA) ambayo ndiyo mmiliki wa bandari

zote nchini, yaani zile za mwambao na zilizoko kwenye maziwa makuu.

Changamoto kwa Serikali na TPA sasa hivi ni kujenga bandari mpya na

kuboresha na kuendeleza miundombinu ya bandari zilizopo ikiwa ni pamoja na

kusimamia waendeshaji wa shughuli za kupakua na kupakia shehena, shughuli

ambazo zinatakiwa kufanywa kupitia mfumo wa ushirikishwaji wa sekta

binafsi..

Ndugu Mwenyekiti,

Ushirikishwaji wa mitaji toka sekta binafsi hapa nchini sasa umewekewa sheria

kamili inayoweka bayana jinsi gani sekta ya umma itashirikiana na ile ya binafsi

katika maendeleo na miradi ya kibiashara.

Kinachofanyika hivi sasa katika bandari ni kuboresha miundombinu yake

pamoja na kubuni mifumo mipya ya kushughulikia shehena; usalama na ulinzi

ili kuweza kuvutia wawekezaji binafsi; kuwezesha shughuli za biashara kuwa

zenye ufanisi na tija ya hali ya juu, na endelevu.

Malengo yote ya maendeleo, na changamoto zinazotokana na mipango hii ni ya

umuhimu kwa bandari za Tanzania kwa sababu nchi hii ina majirani wasio na

3

andari. Nchi hizi zinatutegemea kwa usafiri wa kufikisha bidhaa zao katika

masoko ya kimataifa au zile wanazoagiza. Mapungufu yoyote yale ya kiutendaji

yatagusa na pia kudumaza kasi ya uchumi wa Tanzania na pia ule wa majirani

zake. Ni matarajio yangu kwamba Kongamano hili litatupa uzoefu wa

ushirikishwaji wa sekta binafsi katika kutoa huduma bora zenye ufanisi na kwa

gharama nafuu katika bandari zetu na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi

wa Tanzania na Kanda hii ya Afrika. Ni kwa kuzingatia hili, Serikali ya Jamhuri

ya Muungano ya Tanzania inaipa umuhimu mkubwa sekta ya bandari na

imeifanya kuwa moja ya vipaumbele vyake.

Mipango ya kuendeleza Bandari

Ndugu Mwenyekiti,

Wakati tukiweka mipango mizuri ya kutatua tatizo la miundombinu ikumbukwe

kuwa utekelezaji wa miradi hii unahitaji fedha kutoka kwa Washiriki wa

Maendeleo na pia kutoka sekta binafsi wa ndani na nje ya nchi kwa ajili ya

kuwekeza kwenye miundombinu ya uchukuzi. Napenda kuchukua fursa hii kwa

niaba ya serikali kuwakaribisha Washiriki wa Maendeleo na wenzetu wa Sekta

binafsi kushirikiana nasi kwa kuwekeza katika maeneo mbalimbali yanayohitaji

kuendelezwa. Baadhi ya maeneo ni kupanua na kuboresha miundombinu ya

bandari, reli na barabara. Fursa zipo, milango ipo wazi, miongozo ya kisera ipo

na taratibu za kisheria nazo pia zipo. Karibuni sana.

Umuhimu wa Teknohama

Ndugu Mwenyekiti,

Teknolojia ya usafirishaji duniani inakua kwa kasi ya ajabu ambao unahitaji

kwenda sambamba na huduma bora za mawasiliano. Ni dhahiri kuwa mageuzi

makubwa yamefanywa kwenye eneo hili la teknohama kwenye bandari ambazo

zina ufanisi mkubwa. Hali haipo hivyo katika bandari zilizopo kwenye nchi

zinazoendelea hasa za Afrika. Kwa upande wa Tanzania, Mamlaka ya

Usimamizi wa bandari imeonesha mwelekeo mzuri kwani imeanza na

inakamilisha mradi mkubwa kwa kuboresha mawasiliano haya. Katika mkakati

huu, TPA kwa udhamini wa Benki ya Dunia inaanda mfumo ambao

utaunganisha na kutumika na wadau wake wote. Ushauri wangu kwa nchi

zinazoendelea ni kwamba kama wenzetu wanatembea, basi sisi tukimbie

kuelekea matumizi sahihi ya teknohama. Tuboreshe teknolojia hii kwenye

bandari zetu ili zichangie katika ufanisi wa bandari zetu.

4

Uharamia

Ndugu Mwenyekiti,

Hivi sasa dunia inapambana na tatizo kubwa lililoikumba sekta ya usafiri majini

na biashara ya kimataifa kwa ujumla ambalo ni janga la uharamia. Katika Bara

la Afrika, janga hili limeenea kutoka Ghuba ya Aden hadi Afrika ya Mashariki.

Hivi karibuni tumeshuhudia uharamia ukitokea kwenye Ziwa Tanganyika.

Kutokana na ukubwa wa suala hili ambalo linatishia uchumi wa dunia na maisha

ya watu na mali hatuna budi kulipa umuhimu wa pekee katika kongamano hili

kwa kuwa kimsingi ni suala linalohitaji nguvu ya pamoja.

Naomba kutumia fursa hii pekee, kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania kuzishukuru nchi na Taasisi zote za Kimataifa ambazo

zimejitolea kwa hali na mali kupambana na uharamia. Mapambano dhidi ya

uharamia yanahitaji rasilimali kubwa, utaalamu na vifaa vyenye teknolojia ya

hali ya juu kuweza kupambana nao, ambapo sisi peke yetu tusingeweza kumudu

mapambano hayo. Taasisi hizi zimekuwa mstari wa mbele kuziwezesha nchi

zetu za Afrika Mashariki kupambana na uharamia kwa kutuimarisha kupitia

elimu, kutupa vifaa na teknolojia ya namna ya kupambana na uharamia huu.

Nawashukuru sana na naomba waendelee kutusaidia.

Maelekezo yangu kwa Kongamano

Ndugu Mwenyekiti,

Kongamano hili limejaa Wajumbe wenye utajiri na manguli wa Masuala ya

Usafiri Majini, ni mategemeo yangu kuwa tutapata ushauri mwingi kutoka

kwenu na mkutano huu utatowa suluhisho la matatizo mengi yanayotukabili.

Ushauri wenu utatusaidia kuboresha sekta hii katika Tanzania na Bara zima la

Afrika.

Kazi iliyo mbele yenu katika siku tatu hizi ni kubwa hivyo nisingependa

kuchukua muda wenu mwingi kwa hotuba ndefu badala ya kuwaachia mfanye

kazi iliyowaleta. Napenda kuwashukuru TPA kwa niaba ya Serikali kwa

kuandaa mkutano huu muhimu. Vilevile shukrani zangu nyingi ni kwenu ninyi

washiriki pamoja na serikali zenu na mashirika yenu yaliyowawezesha

kughudhuria kongamano hili.

Nawasihi mwendeleze ushirikiano huu miongoni mwenu. Kwa upande wangu

nina maelekezo yafuatayo kwa Kongamano hili:

5

(i) Mjadili kwa kina changamoto za utandawazi kwenye sekta ya

uchukuzi kwa njia ya maji na huduma za bandari.

(ii) Mtupatie mikakati sahihi ya kuendeleza miundombinu ya bandari.

Hapa mtaazimia namna bora ya kupanga, kusimamia na kupata

fedha za kuendeleza miundombinu ya bandari.

(iii) Mje na mkakati wa kuhakikisha kwamba sekta ya bandari

inaendeshwa na watu waliobobea kielimu kwenye sekta.

(iv) Mtupatie mkakati wa kumaliza tatizo la uharamia.

(v) Mje na mkakati wa kuhakikisha kwamba bandari zetu ni salama na

zina mazingira mazuri.

Tuko tayari kuyapokea maazimio ya mkutano huu kama mtakavyoona inafaa

kuzishirikisha Serikali mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ya Tanzania, Jumuiya za

kikanda za uchumi pamoja na Taasisi mbalimbali za kimataifa kwa lengo la

kuboresha biashara na uchumi wa nchi zetu. Nawahakikishia kuwa Serikali ya

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itapokea dawa mtakayotupa na kwa

kuangalia namna bora ya kuitumia.

Kutembelea Vivutio vya Utalii

Ndugu Mwenyekiti,

Pamoja na kazi kubwa mliyonayo waswahili tunasema kazi na dawa. Nchi yetu

imeberikiwa kuwa na maliasili nyingi za asili na kwamba mkoa huu wa Arusha

ambapo Kongamano hili linafanyika ni eneo moja wapo linaloongoza kwa

vivutio hivyo na kwa kweli Arusha ni kitovu cha utalii.Nawasisitizia kutumia

fursa ya kuwepo kwenu hapa kwenda kufaidi mandhari nzuri ya nchi yetu na

hazina yetu. Tembeleeni Ngorongoro Crater ambayo iko karibu na hapa kiasi

cha wa mwendo wa saa mbili. Waliokwisha kutembelea Tanzania wanasema

kama hujafika Ngorongoro, basi hujafika Tanzania. Karibuni sana.

Ndugu Mwenyekiti,

Napenda pia kuwahakikishia washiriki wa mkutano huu kwamba Watanzania ni

watu wenye upendo na wapenda amani, hivyo jisikieni mpo huru katika kipindi

chote mtakapokuwa hapa nchini. Jisikieni mpo nyumbani mkiwa mbali na

nyumbani.

Ndugu Mwenyekiti,

6

Kwa haya machache, naomba sasa kutangaza rasmi kuwa mkutano wa

fungamano wa sekta ya bandari ulimwenguni kwa nchi za Afrika na Ulaya

umefunguliwa. Nawatakieni mkutano wenye mafanikio,

Asanteni kwa kunisikiliza.

Mungu Ibariki Tanzania,

Mungu Ibariki Afrika.

7

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!