18.02.2015 Views

Kilimo bora cha zao - Ministry Of Agriculture, Food and Cooperatives

Kilimo bora cha zao - Ministry Of Agriculture, Food and Cooperatives

Kilimo bora cha zao - Ministry Of Agriculture, Food and Cooperatives

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA

Kilimo BORA cha

zao la Soya

IDARA YA MAENDELEO YA MAZAO

Sehemu ya Uendelezaji wa Mazao

kijitabu hitimisho.indd 1

5/17/06 11:36:00 PM

kijitabu hitimisho.indd 2

5/17/06 11:36:01 PM

KILIMO BORA CHA

ZAO LA SOYA

Kimeandikwa na :-

Bw. Beatus A. Malema

Bibi Judith M. Kitivo

Wizara ya Kilimo, Chakula na

Ushirika,

Sehemu ya Uendelezaji Mazao (CPS)

Dar es Salaam

Wizara ya Kilimo, Chakula na

Ushirika,

Sehemu ya Uendelezaji Mazao (CPS)

Dar es Salaam

Dkt. Catherine S. Madata Wizara ya Kilimo, Chakula na

Ushirika,

Kituo cha Utafiti Kanda ya

Nyanda za Juu Kusini,

Uyole- Mbeya

Dkt. Fidelis A. Myaka

Wizara ya Kilimo, Chakula na

Ushirika,

Kituo cha Utafiti Kanda ya

Mashariki,

Ilonga- Kilosa

i

kijitabu hitimisho.indd 3

5/17/06 11:36:02 PM

Kilimo Bora cha Zao la Soya,

Kimetayarishwa na kutolewa na:

Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

S.L.P. 9192, Dar - es- salaam, Tanzania.

Toleo ya Kwanza 2006

Kwa ushauri zaidi wasiliana na:

Idara ya Maendeleo ya Mazao,

Sehemu ya Uendelezaji Mazao,

S. L. P. 9192, Dar es Salaam, Tanzania

Simu: 022 2864899

Fax: 022 2864899

Barua pepe: cps@kilimo.go.tz

Tovuti: www.agriculture.go.tz

Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo,

Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,

S.L.P. 400, Mbeya, Tanzania.

Simu: 025 2510062/2510363

Fax: 025 2510065

Barua pepe: uyole@ud.co.tz

Mkurugenzi wa Utafiti,

Kanda ya Mashariki,

Sanduku la Pekee, Kilosa, Tanzania.

Simu: 023 2623201

Fax: 023 2623284

Barua pepe: ilonga@africaonline.co.tz

Michoro na Usanifu

Comic Media Group, S. L. P. 3204 Morogoro, Tanzania

ii

kijitabu hitimisho.indd 4

5/17/06 11:36:02 PM

YALIYOMO

Kilimo Bora cha Soya

UTANGULIZI

i

iv

SURA YA KWANZA: HISTORIA, UMUHIMU NA AINA ZA SOYA

Historia ya zao la Soya nchini Tanzania 1

Umuhimu wa zao la Soya 2

Aina za Soya 3

SURA YA PILI: MAZINGIRA, MVUA NA RUTUBA YA UDONGO

Mazingira na mikoa inayofaa kilimo cha soya 5

Mahitaji ya Mvua 7

Rutuba ya Udongo na Mahitaji ya Mbolea 7

SURA YA TATU: UTAYARISHAJI NA UTUNZAJI WA SHAMBA LA SOYA

Kutayarisha shamba 9

Mbegu 9

Wakati wa kupanda 11

Nafasi ya kupanda 12

Palizi 14

SURA YA TANO: WADUDU, MAGONJWA NA WANYAMA

WAHARIBIFU

Wadudu 17

Magonjwa 17

Wanyama waharibifu 18

SURA YA SITA: KUVUNA, KUPURA NA KUHIFADHI SOYA

Kuvuna 19

Kupura 19

Kuhifadhi 22

SURA YA SABA: MAVUNO NA MAPATO YATOKANAYO NA SOYA

Mavuno 22

Mapato 23

KIAMBATANISHO : Wastani wa gharama na faida za

uzalishaji wa soya ukilinganisha na mazao mengine 24

MAREJEO 26

iii

kijitabu hitimisho.indd 5

5/17/06 11:36:03 PM

UTANGULIZI

Zao la soya lina protini nyingi yenye ubora wa hali ya juu kuliko

iliyoko katika aina nyingine ya mazao ya mimea. Kiasi cha protini

katika soya inazidi hata kiasi cha protini katika nyama, mayai

na maziwa. Sifa nyingine za zao la soya ni pamoja na kuwa na

mafuta yasiyo kuwa na lehemu (cholesterol), uwezo wa mmea wa

soya kuongeza mbolea aina ya nitrojeni kwenye udongo, gharama

ndogo za uzalishaji ukilinganisha na mazao mengine, uwingi wa

protini unaoweza kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto na

kinga kwa magonjwa ya kansa, shinikizo la damu na kuwaongezea

nguvu wagonjwa wa UKIMWI na magonjwa mengine. Aidha,

uwezo wa soya kustawi katika maeneo yanayostawisha mahindi

na maharage unamaanisha kwamba zao hilo linaweza kulimwa

sehemu nyingi nchini Tanzania. Sifa hizo zimefanya zao la soya

kuwa muhimu katika chakula cha binadamu na mifugo na katika

kutengeneza bidhaa mbalimbali za vyakula na madawa.

Pamoja na manufaa hayo ya zao la soya, zao hilo halifahamiki

kama ilivyo mazao mengine mfano maharage na mahindi. Wakulima

wengi hawazijui kanuni za kilimo bora cha soya. Hii inatokana

na kutojua umuhimu wa zao hilo na hivyo kutotilia maanani

katika kulilima na kulitumia kuboresha afya na kipato hasa katika

ngazi ya kaya.

Lengo kuu la kijitabu hiki ni kuwafahamisha wakulima, maafisa

ugani na wadau wengine faida zinazotokana na uzalishaji na

matumizi ya soya. Pia kijitabu hiki kina lengo la kuhamasisha

wakulima na kuendeleza uzalishaji na matumizi ya zao hilo

lililoingizwa nchini kwa mara ya kwanza mwaka wa 1907. Ni

matarajio ya Wizara ya kuwa wakulima na wadau wengine

watafaidika kwa kutumia kijitabu hiki kwa ajili ya kuendeleza na

kuongeza uzalishaji, tija na matumizi ya soya hapa nchini.

iv

kijitabu hitimisho.indd 6

5/17/06 11:36:04 PM

SURA YA KWANZA

HISTORIA, UMUHIMU NA AINA ZA SOYA

Historia ya zao la Soya nchini Tanzania

Soya (Glycine max) ni zao la jamii ya mikunde. Zao hilo asili yake

ni nchi ya China ambako lilianza kulimwa takribani miaka 4800

iliyopita. Zao la soya liliingizwa nchini Tanzania mwaka wa 1907

katika maeneo ya Amani mkoani Tanga. Kati ya miaka ya 1930

na 1960, kilimo cha soya kilipanuka na kuenea hadi maeneo ya

Nachingwea mkoa wa Mtwara, Kilosa mkoa wa Morogoro na

Peramiho mkoa wa Ruvuma. Kuenea kwa zao hilo katika maeneo

hayo kulitokana na msukumo wa mashirika ya Overseas Food

Co-operation – (OFC), State Trading Cooperation (STC), General

Agricultural Production for Export – (GAPEX) na

National Milling

Corporation – (NMC). Mashirika hayo yalisafirisha soya kwenda

katika nchi za Japan na Singapore.

Kwa kuwa uzalishaji wa zao hilo katika mikoa hiyo ulilenga soko

la nje, wananchi hawakufundishwa matumizi yake na kwa sababu

hiyo baada ya mashirika hayo kuacha biashara ya zao hilo kilimo

cha soya kilififia hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni

mwa miaka ya 1990 ambapo uzalishaji ulianza tena baada ya jamii

kuhamasika katika matumizi ya soya hasa katika kutengeneza

vyakula vya watoto.

1

kijitabu hitimisho.indd 7

5/17/06 11:36:04 PM

Umuhimu wa zao la Soya

Soya ni zao lenye virutubisho vingi vya aina ya protini ikilinganishwa

na virutubisho vya aina hiyo katika mazao mengine ya mimea na

hata katika baadhi ya vyakula vinavyotokana na wanyama kama

nyama na mayai na maziwa. Sifa hizo za soya zinafanya zao hilo,

kuwa na umuhimu wa kipekee katika kutengeneza vyakula vya

binadamu na mifugo na matumizi katika viwanda vya madawa

na matumizi mengineyo.

Mafuta yatokanayo na soya hayana

lehemu (cholesterol) na hivyo kuwa na sifa ya kuboresha afya ya

walaji. Zifuatazo ni faida za kutumia soya:-

i. Soya ina virutubisho vingi na vilivyokamilika vya aina ya

protini ambayo ni muhimu katika kuboresha lishe na afya kwa

binadamu na mifugo;

ii. Soya ni chanzo rahisi na chenye gharama nafuu cha protini

ambacho hata mtu wa kipato cha chini anaweza kumudu kwa

kuwa zao hilo linaweza kulimwa maeneo mengi hapa nchini;

iii. Kwa kuwa soya ina kiasi kikubwa cha protini ikilinganishwa

na nyama na mayai na maziwa, inasaidia kupunguza kasi ya

mashambulizi ya vijidudu vya maradhi mbalimbali ikiwa ni

pamoja na magonjwa ya kansa, moyo, na kuwaongezea nguvu

wagonjwa hasa wa UKIMWI;

iv. Soya ni zao muhimu kwa watu wa kipato cha chini katika

kuondoa utapiamlo hususani kwa watoto kwa kuwa hawawezi

kumudu gharama za vyanzo vingine vya protini kama nyama

na mayai;

v. Kutokana na uwingi wa protini, matumizi ya soya kwa watoto

yanasaidia viungo kukua kwa haraka;

vi. Soya hurutubisha udongo kwa kutumia njia ya nitrogen

fixation. Kwa hiyo ni zao linalofaa kutumika katika kilimo cha

mzunguko (crop rotation) na katika kurutubisha ardhi ;

2

kijitabu hitimisho.indd 8

5/17/06 11:36:05 PM

vii. Soya huongeza kipato na ni zao linaloweza kuchangia katika

kuondoa umaskini kwa mkulima kutokana na gharama ndogo

za uzalishaji. Aidha, ni zao linaloweza kuondoa umaskini

kwa watengenezaji wa vyakula vya binadamu na mifugo,

wafanyabiashara na wafugaji na kutoa ajira kwa rika zote

yaani vijana na wazee, vijijini na mijini; na

viii. Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa mafuta ya soya

yanaweza kutumika kwa kuendeshea mitambo yaani bio-fuel

na bio-diesel.

Aina za Soya

Kuna aina mbalimbali za soya; aina zilizozoeleka Tanzania ni

pamoja na Bossier, Uyole soya 1, Ezumu Tumu, Delma Hermon,

Duiker na Kaleya. Kila aina inahitaji mazingira na hali ya hewa inakoweza

kustawi, kukomaa kwa muda maalum na kutoa mavuno

mazuri. Hata hivyo Bossier ni aina ambayo hustawi katika maeneo

mengi nchini. Kwa wastani, aina mbalimbali za soya huchukua

wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa kutegemea na

aina, mahali ilikopandwa na utunzaji katika shamba.

3

kijitabu hitimisho.indd 9

5/17/06 11:36:06 PM

4

kijitabu hitimisho.indd 10

5/17/06 11:36:06 PM

SURA YA PILI

MAZINGIRA, MVUA NA RUTUBA YA UDONGO

Mazingira na mikoa inayofaa kilimo cha soya

Soya inaweza kulimwa katika sehemu zote zenye sifa na zinazofaa

kwa kilimo cha maharage na mahindi. Sifa hizo ni pamoja na

mvua ya kutosha, udongo usiotuamisha maji na udongo tifutifu

usio na mchanga mwingi. Kutokana na kuwepo kwa maeneo

mengi nchini yenye sifa hizo, ni dalili kuwa zao la soya linaweza

kustawi katika maeneo hayo ambayo yapo karibu nchi nzima.

Jambo muhimu linalotakiwa ni kufahamu na kupanda aina za

soya zinazofaa katika eneo husika kulingana na maelekezo ya

wataalamu. Kwa sasa mikoa inayoongoza kwa kilimo cha soya

ni Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa na Morogoro. Mikoa mingine

yenye uwezo na sifa za kuzalisha soya ni Tanga, Mtwara, Lindi,

Kagera, Mara, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na Manyara (Mchoro

Na. 1).

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na Wizara ya Kilimo na

Chakula mwaka wa 2005, zaidi ya tani milioni mbili za soya

zinaweza kuzalishwa kwa mwaka endapo maeneo yote ya nchi

yanayofaa kwa kilimo cha soya yakitumika ipasavyo. Uzalishaji wa

sasa unakadiriwa kuwa tani elfu tano (5,000). Kiwango hiki cha

uzalishaji ni cha chini sana ukilinganisha na kiwango kinachoweza

kufikiwa. Aidha, kiasi hiki kidogo na uwezo unaoweza kufikiwa ni

changamoto katika kuongeza uzalishaji na matumizi ya zao hilo.

5

kijitabu hitimisho.indd 11

5/17/06 11:36:06 PM

Mchoro 1: Ramani ya Tanzania inayoonyesha Mikoa

inayozalisha na yenye uwezo na sifa za

kuzalisha soya

Kagera

Mara

Kigoma

Mwanza

Shinyanga

Tabora

Singida

Arusha

Kilimanjaro

Tanga

Rukwa

Mbeya

Dodoma

Iringa

Pwani

Dar es

salaam

Morogoro

Lindi

Ruvuma

Mtwara

Mikoa inayozalisha soya kwa wingi

Mikoa yenye uwezo na sifa za kuzalisha soya

Mikoa yenye uwezo wa kuzalisha soya katika

maeneo maalum

Maziwa na bahari ya Hindi

6

kijitabu hitimisho.indd 12

5/17/06 11:36:12 PM

Mahitaji ya Mvua

Soya huhitaji wastani wa mililita 350 hadi 1,500 za mvua kwa

mwaka na inayonyesha kwa mtawanyiko mzuri hususan katika

kipindi chote cha ukuaji wa zao hilo. Soya pia inafaa katika kilimo

cha umwagiliaji kwani katika maeneo hayo kunakuwa na uhakika

wa unyevu muda wote. Jambo la kuzingatia ni kutowepo kwa

mvua wakati soya inapokauka.

Rutuba ya Udongo na Mahitaji ya Mbolea

Kama ilivyo kwa mazao mengi, soya pia huhitaji udongo wenye

rutuba na usiotuamisha maji. Hivyo endapo soya italimwa katika

sehemu yenye rutuba hafifu, itahitaji mbolea kama mazao

mengine ijapokuwa huvumilia udongo wenye rutuba hafifu. Kwa

hiyo uamuzi wa kutumia au kutotumia mbolea na kiwango cha

kutumia utategemea rutuba iliyopo kwenye udongo katika eneo

husika. Hata hivyo, soya huhitaji wastani wa kilo 80 hadi 100 za

mbolea aina ya DAP na TSP kwa hekta moja na kilo 60 hadi 80 kwa

mbolea aina ya CAN kwa hekta moja. Mtaalamu aliyepo karibu na

mkulima anaweza kushauri hali ya rutuba ya udongo katika eneo

husika. Jambo la kuzingatia wakati wa kupanda ni kuhakikisha

kuwa mbolea haigusani na mbegu kwa sababu mbolea itaunguza

mbegu na hazitaota. Samadi iliyoiva pamoja na mbolea nyingine

za asili pia zinafaa kutumika katika kilimo cha soya.

7

kijitabu hitimisho.indd 13

5/17/06 11:36:14 PM

8

kijitabu hitimisho.indd 14

5/17/06 11:36:14 PM

SURA YA TATU

UTAYARISHAJI NA UTUNZAJI WA

SHAMBA LA SOYA

Kutayarisha shamba

Shamba la soya linahitaji maandalizi mazuri kama ilivyo kwa

mazao mengine. Utayarishaji huo wa shamba ni pamoja na

kuondoa magugu yote kwa kuwa soya haivumilii magugu

hasa ikiwa katika hatua za mwanzo za ukuaji (seedling stage).

Shamba la soya linaweza kulimwa kwa sesa au matuta.

Kilimo cha sesa (Mchoro Na. 2a) chaweza kulimwa kwa

kutumia jembe la mkono au la kukokotwa na wanyama kazi

kama maksai na punda au kwa kutumia trekta. Kilimo cha

matuta kukinga mteremko kinafaa na kinapendekezwa kwa

maeneo yenye mwinuko (Mchoro Na. 2b). Vilevile kilimo

cha matuta kinafaa sehemu tambarale lakini zenye mvua

nyingi ili kupunguza madhara ya maji yanayotuama baada

ya mvua kubwa kunyesha.

Mbegu

Ni muhimu kuandaa mbegu bora na safi mapema kabla ya msimu

wa mvua kuanza. Kwa wastani kilo 20 hadi 30 za mbegu za soya

zinatosha kwa hekta moja kutegemeana na aina ya mbegu. Kwa

kuwa aina nyingi za soya hazistawi kila mahali, ni muhimu kwa

mkulima kuhakikisha kuwa anatumia mbegu inayofaa katika

9

kijitabu hitimisho.indd 15

5/17/06 11:36:14 PM

Mchoro Na. 2a: Shamba la soya - Sesa.

Mchoro Na. 2b: Shamba la soya - Matuta ya kukinga mteremko.

10

kijitabu hitimisho.indd 16

5/17/06 11:36:23 PM

eneo analotaka kulima soya hususani mahitaji ya mvua. Kwa

sababu hiyo ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri toka kwa

mtaalam aliyekaribu naye kabla ya kuamua kulima soya. Aidha,

mkulima anashauriwa kununua na kutumia mbegu kutoka katika

sehemu ambazo chanzo cha mbegu hizo kinaeleweka. Mfano

wa sehemu hizo ni pamoja na maduka ya pembejeo, wakala

wa mbegu, mashamba ya mbegu na vituo vya utafiti. Hii ni kwa

sababu mbegu ya soya hupoteza nguvu ya uotaji katika msimu

mmoja hasa katika sehemu za joto. Kwa hiyo mkulima anatakiwa

kuhakikisha kuwa anapanda mbegu itakayoota. Kama mkulima

hana uhakika na chanzo cha mbegu au ana wasiwasi wa kuota

kwa mbegu alizonazo anaweza kufanya majaribo ya uotaji

(germination test) kabla ya kupanda. Njia rahisi ni kuzilowesha

mbegu kwa maji na kisha kuziweka kwenye kitambaa mahali

penye joto la kutosha. Mbegu ziloweshwe na maji kila siku mpaka

zitakapoota. Hesabu mbegu zilizoota na iwapo mbegu zilizoota

ni chini ya 75 kati ya mbegu 100 yaani asilimia 75, mkulima

anashauriwa kutopanda mbegu hizo.

Wakati wa kupanda

Upandaji wa soya unategemea na aina na mahali husika. Kwa

aina za soya zinazokomaa mapema, soya ikipandwa mwanzoni

mwa msimu wa mvua katika maeneo yanayopata mvua kwa

kipindi kirefu itakomaa wakati mvua bado zinaendelea kunyesha

na hivyo kufanya uvunaji na ukaushaji kuwa mgumu na kuhitaji

nguvu kazi na muda wa ziada la sivyo mbegu zitaoza au kuanza

kuota na kupoteza ubora wake. Kwa hiyo ni budi kujua mwenendo

wa mvua mahali husika ili kupanda kwa wakati na aina ya soya

kulingana na mahali hapo. Jambo la muhimu ni kuhakikisha

kuwa soya inakomaa wakati hakuna mvua ili kurahisisha uvunaji

11

kijitabu hitimisho.indd 17

5/17/06 11:36:23 PM

na soya kutooza. Jedwali Namba 1 linaonyesha mahali, aina na

muda wa kupanda soya.

Jedwali Namba 1: Muda unaoshauriwa kupanda soya

Na. Mahali Mbegu Muda

1

Sumbawanga, Nkasi, Songea,

Mbeya, Njombe, Dabaga na sehemu

zenye mvua nyingi/ndefu

Uyole soya

1

Novemba/

Desemba

2

Sumbawanga, Songea, Mbeya,

Njombe na sehemu zenye mvua

nyingi/ndefu

Bossier

Januari

3

Ileje, Mbarali, Chunya, Mtwara na

sehemu zenye mvua kidogo na

fupi

Bossier

Novemba/

Desemba

4

Morogoro na Tanga Bossier Februari na

Machi

Nafasi ya kupanda

Mkulima anashuriwa kupanda soya kwa nafasi zinazo pendekezwa

na wataalamu. Nafasi hizo ni sentimeta 10 kwa sentimita 45

(Mchoro Na. 3) kwa soya fupi kama bossier na kwenye sehemu

zenye rutuba hafifu. Aidha, tumia sentimeta 10 kwa sentimita 60

kwa soya ndefu kama Uyole Soya 1 na kwenye sehemu zenye

rutuba nyingi. Panda mbegu moja kila shimo na zifukiwe kwa

kina cha sentimeta mbili hadi sentimita tano ili zisiharibiwe au

kuliwa na wanyama kama panya. Mkulima ahakikishe kuwa soya

inapandwa kwenye udongo wenye unyevu wa kutosha; haitakiwi

kabisa kupanda soya kwenye udongo mkavu au kuloweka soya

kabla ya kupanda.

12

kijitabu hitimisho.indd 18

5/17/06 11:36:25 PM

Sm 45

Sm 10

Mchoro Na. 3: Nafasi za kupanda soya katika sesa

Sm 45

Sm 10

Mchoro Na. 4: Nafasi za kupanda soya katika matuta

13

kijitabu hitimisho.indd 19

5/17/06 11:36:29 PM

Palizi

Soya ni zao ambalo huzongwa na magugu hususani ikiwa

katika hatua za mwanzo za ukuaji. Kwa hiyo mkulima

anashauriwa kuwahi palizi katika kipindi cha wiki mbili

baada ya soya kuota. Palizi ya mara ya pili inategemeana na

kiwango cha magugu shambani. Endapo magugu yatakuwa

yamefunikwa na majani ya soya palizi ya pili inaweza

isihitajike kama inavyoonekana kwenye Picha Namba 1

ambapo soya iliyopandwa kwa nafasi zinazotakiwa imekua

na kufunika magugu yote na hivyo palizi ya pili kutohitajika.

Picha Namba 2 inaonyesha soya iliyopandwa kwa nafasi

pana na isiyotakiwa ambayo haijakua kufikia kiwango cha

kufunika magugu na hivyo kulazimisha palizi ya pili kufanyika.

Magugu katika shamba la soya yanaweza kudhibitiwa pia

kwa katumia dawa ya kuzuia magugu kama GALEX; hata

hivyo inafaa kufuata maelekezo ya kutumia ya dawa husika.

14

kijitabu hitimisho.indd 20

5/17/06 11:36:30 PM

Picha Namba 1: Soya iliyopandwa kwa nafasi zinazotakiwa imefunika

magugu.

Picha Namba 2: Soya iliyopandwa kwa nafasi pana zisizotakiwa haijafunika

magugu.

15

kijitabu hitimisho.indd 21

5/17/06 11:36:54 PM

16

kijitabu hitimisho.indd 22

5/17/06 11:36:54 PM

SURA YA TANO

WADUDU, MAGONJWA NA WANYAMA WAHARIBIFU

Wadudu

Kwa sasa, nchini Tanzania soya haishambuliwi sana na wadudu

kama ilivyo sehemu nyingine ambako zao hilo hulimwa kwa wingi.

Hata hivyo endapo wadudu watatokea mkulima anashauriwa

kutumia dawa za wadudu kama Thiodan 35% EC na Sumithion

50% EC kwenye kipimo cha mililita 40 za dawa na lita 20 za maji

au kipimo kinacho pendekezwa katika dawa husika. Upuliziaji wa

dawa ufanywe kulingana na kiasi cha mashambulizi ya wadudu

kwenye mazao.

Tofauti na mazao kama mahindi na maharage, hakuna wadudu

waharibifu wa soya ghalani. Hivyo zao hilo linaweza kutunzwa

kwa muda mrefu ghalani bila kuwa na athari za wadudu. Kwa

mkulima na wafanyabiashara, kutokuwepo wadudu waharibifu

ghalani kunapunguza gharama za utunzaji hadi bei nzuri

itakapofikiwa.

Magonjwa

Kama ilivyo kwa wadudu, magonjwa ya soya ni machache. Hata

hivyo magonjwa ambayo hutokea kwa nadra ni yale yanayotokana

na vimelea vya ukungu na bakteria. Magonjwa hayo huenezwa

kwa mbegu, masalia ya mimea shambani na wadudu mafuta.

17

kijitabu hitimisho.indd 23

5/17/06 11:36:54 PM

Hivyo ni bora kwa mkulima kuzingatia kanuni za kilimo bora

au kupata ushauri wa kitaalamu ili kuepukana na magonjwa

hayo. Njia mojawapo ya kuzuia kuenea kwa magonjwa katika

zao la soya ni kupanda mbegu safi na zilizopendekezwa mahali

husika. Aidha, panda kwa mzunguko (crop rotation) kwa kutumia

mazao yasiyoshambuliwa na magonjwa ya soya kama alizeti na

mahindi.

Wanyama waharibifu

Kwa kawaida soya hupendwa sana na panya wa shambani na

ghalani. Wanyama wengine ni pamoja na sungura, paa, swala,

n.k. Mkulima anashauriwa kutumia mbinu na njia mbalimbali

zikiwemo za asili, kukabiliana na wanyama hao bila kuharibu

mazingira.

18

kijitabu hitimisho.indd 24

5/17/06 11:36:55 PM

Kuvuna

SURA YA SITA

KUVUNA, KUPURA NA KUHIFADHI SOYA

Soya huchukua wastani wa miezi mitatu hadi saba kukomaa

kutegemea na aina, mahali ilikopandwa na utunzaji wa shamba.

Kwa mfano soya aina ya Bossier huchukua miezi mitatu hadi

minne kukomaa na aina ya Uyole Soya 1 miezi minne hadi mitano.

Dalili za soya kukomaa ni wakati majani yanapokuwa na rangi ya

njano. Anza kuvuna baada ya majani kuanza kupukutika.

Soya ikikauka, maganda yake hupasuka na mbegu hupukutikia

chini. Kwa hiyo mkulima anashauriwa kuwahi kuvuna soya

mara inapokomaa na kuanza kukauka. Ili kuzuia upotevu wa

zao shambani, inashauriwa kuvuna majira ya asubuhi au majira

ambayo sio ya jua kali endapo soya imekauka na kuanza kupasuka

wakati wa kuvuna.

Kupura

Soya haitakiwi kupigwa kwa nguvu kwa sababu mbegu zake

hupasuka kirahisi (Mchoro Na 5). . Mara baada ya kupura, ondoa

takataka na uchafu mwingine kwenye soya kwa kupepeta

(Mchoro Na. 6) na kupembua. Kausha soya kufikia wastani wa

asilimia 10 ya kiasi cha maji (moisture content) kisha ihifadhi

ghalani kwa matumizi au kusubiri soko.

19

kijitabu hitimisho.indd 25

5/17/06 11:36:55 PM

Mchoro Na. 5: Kupura soya

18

kijitabu hitimisho.indd 26

5/17/06 11:37:10 PM

Mchoro Na. 6: Mama anapepeta soya kabla ya kuhifadhi

19

kijitabu hitimisho.indd 27

5/17/06 11:37:31 PM

Kuhifadhi

Hifadhi soya baada ya kuhakikisha kuwa imekauka vizuri. Ni

muhimu kuhifadhi soya mahali pakavu ili soya isipate uvundo na

kuharibu soya ya mbegu na ya chakula. Soya inaweza kuhifadhiwa

kwenye vihenge au kwenye magunia kama mazao mengine,

tofauti ni kutohitajika dawa ya kuhifadhia.

20

kijitabu hitimisho.indd 28

5/17/06 11:37:31 PM

SURA YA SABA

MAVUNO NA MAPATO YATOKANAYO NA ZAO LA SOYA

Mavuno

Soya ina uwezo wa kutoa kilo 1,500 hadi 2,500 kwa hekta kutegemea

na aina,

hali ya hewa, rutuba ya udongo, matumizi ya mbolea na

utunzaji kuanzia wakati wa kuchagua mbegu, kulima, kupanda

na kuvuna. Kiasi hicho cha mavuno ni sawa na kilo 600 hadi 1,000

kwa ekari moja.

Mapato

Kutokana na mavuno ya soya, mkulima anaweza kupata mapato

mengi ukilinganisha na mazao kama mahindi na maharage

kwa eneo lililosawa na eneo la soya. Ukweli huu unabainishwa

na tathmini iliyofanyika mwaka wa 2005 na Wizara ya Kilimo

na Chakula, juu ya hali kilimo cha soya nchini. Tathmini hiyo

ilionyesha kuwa wastani wa gharama za kuzalisha kilo moja ya

soya kwa mikoa ya Nyanda za Juu za Kusini hususan Songea Vijijini

ni shilingi 130 (Kiambatanisho Na 1), kwa hiyo kama mkulima

atauza soya kwa wastani wa shilingi mia mbili (200) kwa kilo

moja bila gharama ya kusafirisha mbali na kijijini kwake anaweza

kupata faida ya kati ya shilingi 105,000 hadi 175,000 kwa hekta

moja au kati ya shilingi 42,000 na 70,000 kwa ekari moja. Hata

hivyo mapato yanaweza kuongezeka endapo mkulima atatunza

na kuuza soya wakati bei imepanda kwa kuwa soya inaweza

kutunzwa muda mrefu bila kuharibiwa na wadudu. Nidhahiri

kuwa zao la soya linaweza kumuongezea mkulima kipato na

kumuondolea umaskini.

21

kijitabu hitimisho.indd 29

5/17/06 11:37:32 PM

KIAMBATANISHO NA 1: Wastani wa gharama za uzalishaji wa soya,

mahindi, maharage na alizeti kwa ekari moja

Huduma Gharama kwa kila zao

Mahindi Maharage Alizeti Soya

Kusafi sha shamba

8,000 8,000 8,000 8,000

Kulima 15,000 15,000 15,000 15,000

Kupanda 5,000 10,000 5,000 10,000

Palizi ya kwanza 10,000 10,000 8,000 8,000

Kuweka mbolea 5,000 - - -

Kuweka dawa ya wadudu shambani 3,000 3,000

Palizi ya pili 5,000 5,000 - -

Kuvuna 5,000 5,000 5,000 5,000

Kusafi risha 25,000 5,000 10,000 5,000

Kupiga 5,000 3,000 3,000 3,000

Kupepeta 3,000 2,000 2,000 2,000

Kuweka kwenye magunia 2,000 1,000 1,000 1,000

21

kijitabu hitimisho.indd 30

5/17/06 11:37:33 PM

Huduma Gharama kwa kila zao

Mahindi Maharage Alizeti Soya

Kiasi cha mbegu 15 40 18 30

Gharama ya mbegu 1,500 10,000 3,000 12,000

Kiasi cha dawa (Kg) 2 1 - -

Gharama ya dawa (Tsh) 12,000 5,000 - -

Magumia ya kamba 8,000 3,000 3,500 3,000

Usafi rishaji kwenda DSM 6,000 6,000 6,000 6,000

Jumla ya gharama 118,500 91,000 69,500 78,000

Mavuna (Kg/Eka) 800 500 400 600

Gharama kwa kilo (Tshs) (Break even price) 148 182 174 130

Bei ya mazao msimu wa mavuno (Tshs / Kg) 120 200 150 200

Faida kwa kilo moja (28) 18 (24) 70

Faida kwa ekari moja (22,500) 9,000 (9,500) 42,000

22

kijitabu hitimisho.indd 31

5/17/06 11:37:34 PM

MAREJEO

1. File NAL/S./17/124. (2005). Soybean in Southern regions

of Tanzania. Dr. Mponda, O. K. K. ARI Naliendele. Personal

communication

2. Laswai, H. S., Kulwa, K. B. M., Ballegu, W. R. W., Silayo, V. C.

K., Ishengoma, C. G.; Makindara, J. A.; Mpagalile, J. J. and

Rweyemamu, C. L. (2005).

Soya kwa lishe bora. Virutubisho

na matayarisho yake kwa mapishi mbalimbali. SUA NORAD

Focal Programme.

3. Mhagama, G. (2005). Soya: The golden seed in Tanzania.

Sunnhemp seed bank. Mruma Centre, Peramiho Songea.

Personal communication.

4. Madata, C. (Januari, 2005). Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania. ilimo bora cha soya nyanda za juu kusini na Vyakula

vya soya na mapishi yake: Soya kwa afya yako. Toleo la Tatu.

5. Myaka, F. A. (1990). Soybean- “the golden bean”. Its past, present

and future in Tanzania. In Research and Training Newsletter

Vol. V, No. 1, March, 1990. Ministry of Agriculture, Livestock

Development and Co-operatives

6. Myaka, F. A. and Mwemezi E. T. (1990). Soyabean village

production and utilization: first year of prospects. In Research

and Training Newsletter Vol. V, No. 4, December, 1990. Ministry of

Agriculture, Livestock Development and Co-operatives

7. Ngeze, P. B. (1993). Jifunze kustawisha maharage ya soya.

Kagera Writer and Publishers Co-operative Society Ltd. Bukoba

Tanzania.

23

kijitabu hitimisho.indd 32

5/17/06 11:37:35 PM

8. URT (November, 2005). Soybean Study in Tanzania. Ministry of

Agriculture and Food Security.

24

kijitabu hitimisho.indd 33

5/17/06 11:37:35 PM

kijitabu hitimisho.indd 34

5/17/06 11:37:37 PM

kijitabu hitimisho.indd 35

5/17/06 11:37:38 PM

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA

Kilimo BORA cha

zao la Soya

IDARA YA MAENDELEO YA MAZAO

Sehemu ya Uendelezaji wa Mazao

kijitabu hitimisho.indd 36

5/17/06 11:38:37 PM

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA

Kilimo BORA cha

zao la Soya

IDARA YA MAENDELEO YA MAZAO

Sehemu ya Uendelezaji wa Mazao

kijitabu hitimisho.indd 37

5/17/06 11:39:12 PM

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!