11.07.2015 Views

KUSHEREHEKEA UTAKATIFU

KUSHEREHEKEA UTAKATIFU

KUSHEREHEKEA UTAKATIFU

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 1Maandiko: Yohana 12:20-32Utangulizi:Kumwinua Kristo JuuOmbi la Wagiriki – walitaka kumwona Yesu.Hawa walikuwa ni watu wa mataifa, mamajusi, wanasayansi waliokuwa wanatafuta ukweli.Waliwajia wanafunzi wa Yesu; Filipo na Andrea. Hawa wawili walikuwa na moyo wa kuwaelekezawatu kwa Yesu (Yohana 1:41, 45)Yesu alipolisikia ombo lao aliwajibu kwa njia isiyo ya kawaida. Halikuwa jibu wazi (Yohana 12:23-33)Jibu lilikuwa: Wagiriki na ulimwengu wote watamwona Yeye atakapoinuliwa msalabani (Yohana12:32).1. Kuinuliwa kwake msalabani ni jambo ambalo likuwa limetabiriwa awali.a. Agano la kale – Pasaka katika kitabu cha Kutoka-­‐ Damu ya kondoo na kuipaka kwenye vizingiti na miimo ya milango (Kutoka 12:7);ishara ya msalaba.-­‐ Waliotii amri hii waliokolewa kutoka kwenye kifo. (Kutoka 12:13)b. Mle jangwana wakati Musa aliinua nyoka wa shaba (Hesabu 21:4-9), ishara yakusulibiwa (Yohana 3:14).-­‐ Walioumwa na nyoka waliokolewa hawakufa kwa sababu walitii amri na kumtazamanyoka wa shaba aliye juu.-­‐ Yesu alimwambia Nikodemo, “kama vile Musa alimwinua Yule nyoka kule jangwani,vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu, Ili kila mtu amwaminiye awa nauzima wa milele”. (Yohana 3:14-15).c. Utabiri huu ulitimizwa mlima Kalvari miaka elfu mbili iliyopita wakati alisulubiwamsalabani.d. Tangu Kalvari, mafunzo ya msalaba ambamo Yesu alikufa yamekuwa nayataendelea kuwa muhimu katika imani ya Mkristo.2. Umuhimu na maana kweli ya msalaba sio hautoani na msalaba wa mbao aliosulibiwa.a) Msalaba wa mbao ulitengenezwa ili kuwa ishara ya mateso na dhihaka, haya yalikuwa nimaneno yake mwimbaji wa injili George Bennard katika wimbo, “The Old Rugged Cross.”b) Hatujui hizo mbao zilitumika kufanya nini. Ikiwa tungezipata, ingekuwa vyema kuzihifadhi.3. Msalaba kweli wa Yesu ni Yesu binafsi.a) Yeye ndiye ufunuo wa Mungu, mwokozi wa ulimwengu.b) Ni kazi ya Kristo ya wokovu.c) Ni kujitoa Kwake binafsi.d) Ni hukumu ya kifo, sio kwa ajili ya dhambi zake, kama wale wezi wawili aliokuwaamesulibiwa nao, ila ni kwa ajili ya dhambi zetu.e) Ni Kristo, ambaye alibeba aibu yetu msalabani mle jangwani mwa kifo.f) Ni Kristo, alivumilia kutenganishwa na Mungu kwa mda wa masaa matatu akiwa msalabanikwa ajili ya dhambi zetu. Kutenganishwa huku kulivunja ushirika wa uzima aliokuwa naona Mungu wa tungu milele.g) Ni kifo chake.h) Ni hali ya Kristo ya kutembea peke yake katika bonde la mauti msalabani bila tulizo kutokakwa Mungu.i) Ni dharau Kwake – aliyatoa maisha Yake kama mche mwororo (Isaya 53; Wafilipi 2:5-8)j) Ni hali yake ya kujitoa nafsi.k) Ni hali ya kutoa nafsi Yake kafaral) Ni hali ya uhudumu wa mateso.10


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 1m) Ni Wokovu na utakaso Wake ulio ndani ya damu yake.4. Kunao msalaba mwingine ambamo Kristo ameinuliwa. Huu ni msalaba wa WanafunziWake.a) Wewe kama mfuasi wake, unafaa kujikana nafsi yako, kubeba msalaba wako na kumfuata.b) Wewe ndiye msalaba huo – Ni maisha yako. Ni Wito wa Mungu maishani mwako. Yesualiinuliwa kupitia kwa wito huu.c) Yesu alipotuita na kutuamrisha kumfuata, tuliubeba msalaba wetu (maisha) na kumfuatakatika kusulubiwa kama mche mwororo, tulifia kwenye dhambi zetu na utu wetu wa kaleulisulubiwa Naye. Warumi 6:1-14d) Yesu alikufa msalabani Wake peke Yake. Simoni wa Kirene alimsaidia kwa kubeba mfanowa msalaba wala hakuwa ameubeba msalaba kweli ambao Yesu alibeba. (Mathayo 27:32)1. Alusubiwa peke Yake msalabani Mwake.2. Aliteswa peke Yake3. Aliachwa peke yake msalabani wakati Mungu wake alipomuasi.e) Ndivyo ilivyo nasi.1. Tumesulubiwa Naye (Wagalatia 2:20)2. Tunateswa Naye (Wafilipi 3:10)3. Tunakufa Naye (Warumi 6:3)4. Tumezikwa Naye. Tunafufuka Naye (Warumi 6:4)f) Tunapomfuata Yesu kwenye safari hii kuu ya Wokovu, kusulubiwa kwetu kwa binafsihakutokei, bali utu upya, mtu mpya anatokea akikwa ameunganishwa na Wokov (Warumi6:6).Tamati:1. Maisha mapya tunayoishi sio maisha yetu, ni Kristo anayeishi ndani yetu kupitia kwetu(Wagalatia 2:20)2. Mtu mpya katika Kristo anao uwezo wa kumwinua Kristo.3. Tunapobeba msalaba tunashiriki katika mateso Yake na kuyafanya mambo yaliyotajwa hapa.4. Wakati uzani wa msalaba unaobeba ni mzito na unahisi uchovu na kuanguka kwa ajili ya uzani,Yesu ndiye ‘Simoni’ wako ambaye atakusaidia. (Mathayo 11:28 – 30; Wafilipi 4:13)Nakala imetayarishwa na Dkt. Enoch H.LitsweleMstaafu Naibu wa Mkurugenzi Mkuu Eneo la Afrika11


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 1Maandiko: Tito 2:11-15Mstari wa Maandiko: Tito 2:14Madhumuni Ya Kifo Cha Kristo1. Alijitoa kwa hiari Yakea. Alijitoa nafsi katika uzima wa milele na Akafa kwa ajili ya ulimwengu. (Ufunuo wa Yohana13:8b)b. Alijitoa binafsi na kwa hiari aliacha utukufu wake wakati ulipotimia… akazaliwa namwanamke” (Wagalatia 4:4, Wafilipi 2:5-8)c. Alijitoa binafsi kukamatwa katika bustani mwa Gethsemane. Angekuwa ni jeshi la malaikaili ajilinde lakini hakufanya hivyo. (Mathayo 26:47-56)d. Alikuwa na mamlaka ya kupeana na kuchukua uhai wake. (Yohana 10:14-18)2. Alijitoa ili atuokeo kutoka kwa dhambia. Kuokoa imaanisha kurejesha kitu ama mtu katika hali ya awali iliyokuwa imepotea.b. Kwa sababu ya udhaifu wetu tuliupoteza ushirika wetu na Mungu, lakini wokovu wa Kristohuturejeshea ushirika.c. Damu ya Kristo, maisha Yake ndizo pekee zilikuwepo na zilizofaa kutuokoa. (1 Petro 1:18-21)3. Alijitolea ili kututakasa.a. Wokovu wetu hautuondolei udhaifu pekee, lakini pia hutuondolea udhaifu toka mioyonimwetu.Onyesho: Wana wa Israeli walitolewa Misri lakini Misri pia ilihitaji kuondolewa ndani yao.(Hesabu 11:4-6)b. Kusafishwa – utakaso hufanya kwa damu ya dhamana ya Yesu kristo (1 Yohana 1:9)c. Utakaso huu hutufanya wake tunapofanana na Naye (kufanana na Kristo)d. Usafi – utakaso – kuokolewa- wokovu ni neema ya Mungu inayotufunza kusema LA kwamambo yasiyo ya uungu na NDIYO kwa mambo ya uungu. (Tito 2:11-13)4. Alijitoa Ili Kutufanya tutake kufanya memaa. Kazi zetu njema za mwanga unaongara na maisha matakatifu na kuishi kulingana na injili(Mathayo 5:16)b. Kazi nzuri za kueneza Habari Njema za wokovuc. Tunafurahishwa na kutamani Paulo (Warumi 1:15)d. Tunatamani kwasababu upendo wa Kristo hututia motisha (2 Wakorintho 5:14)Nakala imetayarishwa na Dkt. Enoch H. LitsweleMstaafu Naibu wa Mkurugenzi Mkuu Eneo la Afrika13


Maandiko: Yohana 15:4-5Utangulizi:Watu Wa Kawaida Katika Huduma Ya KipekeeSisi ni watu tuliotumwa, tumetumwa ulimwenguni, ili kukuza ufalme wa Mungu kwa kulinda nakuendeleza utakatifu wa Ukristo kama ilivyo pangiliwa katika Maandiko” (Kitabu cha Mwongozo2009-2013 cha Kanisa la Mnazareti). Tumetumwa ulimwenguni ili kuwa wawakilishi wa Ufalme nakuwa katika umbo la ubinadamu na washiriki katika misheni ya Mungu katika kila sehemu yamaisha; tumetumwa ili kuyaguza maisha ya wanadamu, tamaduni na jamaa tofauti kwa Injili yaYesu Kristo.1. Kufanya kazi kwetu hutegemea sisi kukaa ndani ya Kristo.a. Yesu alisema, “Kaeni ndani Yangu, Nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyowezakuzaa matunda ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani Yangu hamwezikuzaa matunda.” (Yohana 15:4-5)b. Lazima tumtii…lazima tukae katika uwepo Wake kwavile tukikaa ndani Yake atatuongoza.Atatupa hekima, nguvu na neema. Atatuwezesha kufanya kazi Yake.c. Njia ya kukaa ndani yake ni kuwa waaminifu kwa neno Lake. “Mkizishika amri zangumtakaa katika pendo langu, kama Mimi nilivyozishika amri za Baba Yangu na kukaa katikapendo Lake”. (Yohana 15:10)2. Kufanya kazi kwetu hutegemea hisia zetu kwa kazi za Roho Mtakatifua. “Atakapokuja huyo Roho wa Kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanenakwa ajili Yake Mwenyewe, bali atanena yali yote atakayosikia, naye atawaonyesha mamboyajayo.” (Yohana 16:13)b. Utiifu wa amri za Mungu ni muhimu. Tunapofanya hivyo tunakaa ndani Yake.c. Lazima tufanye agano kutii kwa uaminifu na kushirikisha Neno la Mungu katika sehemuzote za maisha. “Roho wa kweli … ataongoza….” Tunafaa kumhisi wakati wote.Mwisho:Je, utatoa agano la kukaa ndani Yake?Nakala imetayarishwa na Dkt. Filimao ChamboMkurungenzi Mkuu, Eneo la Afrika.15


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 2Maandiko: Mwanzo 17:1-2Utangulizi:Mwaliko Kutoka Kwa Mungu!Mungu alimtokea Abramu ili kuthibitisha ahadi Yake kwa Abramu na Sarai (Mwanzo 12:15). Hiihaikuwa mara ya kwanza Mungu kumtokea Abramu. Katika sura za awali, Mungu alimtokeaAbramu na kumfanyia agano. Mungu aliahidi Abramu na Sarai mwana wa kiume na kupitia kwaoAtabariki ulimwengu. Hata hivyo, kadri miaka ilivyopita, ilionekana ni kana kwamba Munguhangetimza ahadi. Abramu na Sarai walizeeka ilhali hawakuwa na mtoto kama walivyoahidiwa naMungu. Baada ya miaka ya machungu na hasira, Mungu alimtokea Abramu tena ili kufanya upyaagano lao lakini ili agano hili litimizwe Abramu atafaa kuendelea kuwa mwaminifu katika njia zaBwana.Mungu anamwalika Abramu kutembea katika njia za haki. Neno “kutokuwa na dasari” linazo maananyingi. Limaanisha kuwa mwenye haki katika mwenendo, kuwa mwadilifu, unayefaa, mkamilifu,uliye juu, uwe mfano, usiye kosolewa na kadhalika. Mungu anawaita watu Wake ili wawe wenyehaki katika mwenendo wao na kuwa mfano wa kuishi vyema kwa watu tunaoishi nao. Watu waMungu wanafaa kuishi maisha yasiyo na dosari. Yesu alisema katika Yohana 13:34 mwenendowetu unafaa kuwaelekeza watu wengine kwa Kristo, ili wote wajue sisi ni wanafunzi Wake.Swali ni, je maneno haya yanayo maana gani kwa kanisa leo?1. Mimi ni Mungu Mwenyezi (El- Shaddai)a. Mungu anamwakikishia Abramu kuwa Yeye ni El-Shaddai (Mungu Mwenyezi). Maanake nikuwa, Yeye Ni Mungu, Mwenye Nguvu zote, Anayetuisha, Anayetupa, Anayeridhisha. Yeye niMungu Mtoshelezi. Mungu anayepeana kwa wingi na Mwenye nguvu na mwaminifu kutimizaahadi Anazotoa na hutimiza mipango na madhumuni Yake.b. Mungu aliwahakikishia Abramu kuwa atawapa mwana. Mda na umri sio kizuizi kwa Mungu. Yoteyanawezekana kwa Mungu. Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu”/ “Hamna nenolitokalo kwa Mungu litakaloshindwa” (Luka 1:37)c. Mungu alimtaka Abramu atambue kuwa alikuwa katika uwepo wa Mungu mmoja mwenyenguvu, muumba na mpaji wa uzima. Ilikuwa muhimu kwa Abramu kutambua aliyekuwaakizungumza naye.2. Kualikwa katika matembezi: Kutembea mbele Za Mungu!Mwaliko wa Mungu ni kwa watu Wake (dini, kanisa la mtaa, watu binafsi, na kadhalika, iliwatembee mbele za Mungu sila dhambi. Neno kutembea hapa pia litamaanisha kumtii Mungu,kufa, kuwa mtu wazi, kuja kutembea na kutiririka Naye. Sisitizo ni Mungu kuwaita watu Wakewatembee Naye, kumtii Yeye, kufa kwa dhambi binafsi na kutiririka Naye katika Haki. Nimwaliko wa kukaa daima katika uwepo Wake naye Mungu kukaa ndani ya watu Wake.Kama vile Abramu na Sarai kanisa leo limo katika ulimwengu wenye mazoea ya tamadunizisizoheshimu Mungu. Kanisa halifai kufuata mienendo ya za ulimwengu lakini lazimalibadilishwe na kufanya upya na Roho wa Mungu (Warumi 12:1-2) ili kuonyesha mfano kwaulimwengu wa maisha ya Mungu.3. Mwaliko kwa haki: Enenda mbele za Mungu na uwe Mwelekevu!Mwaliko kwa haki ni mwaliko wa kutii uungu (tazama Warumi 12:1-2). Watu wa Munguwamealikwa ili kuwa waaminifu katika uwepo wake (Zaburi 89:15). Ni vyema kukaa katikauwepo wake kwa sababu kwa njia Yake na ndani Yake ndipo tunapokea nguvu za kuishi kwahaki. Wanaotembea katika njia za waovu huanguka na kushindwa kuongoza kwa njia za haki16


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 2kwa sababu wamejaa uovu, kwa hivyo wenye haki huonywa wasikae katika kikao cha waovu.(Zaburi 1:1). Somo hili laweza kutamatishwa kwamba:-a) Usitembee wala kufuata mawaidha ya wasio haki. Usiige njia mbovu za jamii (tazamaZaburi 1:1; Warumi 12:1).b) Epuka uovu, tenda yaliyo mema kwa kumtii Mungu na neno Lake. “Uwe mkamilifu kwaBwana Mungu wako”. Kumbu kumbu la Torati 18:13.c) Furahia na kuomba katika Ukweli (Neno la Mungu) mchana na usiku (Zaburi 1:2). Neno laMungu ni nguvu za Mungu za wakovu wa kila mmoja anayeamini. (Warumi 1:16). Ndipomtaijua kweli nayo kweli (Injili) itawaweka huru” (Yohana 8:32). (Tazama Warumi 6:22)d) Kujiweka kikamilifu kwa Mungu na kutaka kumjua zaidi na kuyafuata mapenzi Yake katikasehemu zote za maisha Yetu. Kujitolea kikamilifu kwa Mungu! Bwana yuko mbali na wasiohaki lakini Yeye huyasikia maombi” (Mithali 15:29).Tamati:Mungu anawaita wafuasi wake wafanye kazi za utakatifu. Analiita kanisa lake lienende mbele Zakekwa uaminifu na uelekevu katika sehemu zote za maisha yao. Heri walio kamili katika njia zao,waendao katika sheria ya BWANA”. (Zaburi 119:1). Heri yule aendaye kwa uelekevu, atendaye kwaukamilifu, asemaye kweli kwa moyo wake” (Zaburi 15:1-2)Mungu anatualikia tuenende kwa njia za haki, uadilifu na tuwe juu zaidi. Yeye ni mwenye nguvu naanao uwezo wa kutupa maisha mapya. Tukija kwake kwa imani ili atutakase, Yeye ni mwaminifu naanao uwezo wa kufanya hivyo.Nakala imetayarishwa na Dkt. Filimao ChamboMkurugenzi Mkuu, Eneo la Afrika17


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 2Maandiko: Yohana 15:5-8Utangulizi:Mzabibu wa Kweli Na Matawi Ya KweliMungu anataka watu Wake wazae matunda kwa sababu anataka mazao. Kuzaa matundahutegemea kusudi la Mungu juu yetu.Israeli inaonekana kama mti wa mzabibu ulioliwa na moto (Ezekieli 19:12), wakati angekuwamzabibu ulioteuliwa, unaotoa zabibu.Ni katika hali ndipo Yesu alisema, “Mimi ndimi mzabibu wa kweli” (Yohana 15:1)1. Katika umoja na Kristo, hakika mazao mazuri yatapatikana (Yohana 15:5)a. “ Mimi ndimi Mzabibu” – mto mkuu wa uzimab. “Kaa ndani yangu” – hali ya umoja, ushirika, maombi na kukua.c. “Bila Mimi” - kuhitimu, ushirikiano wa kuishi na Kristo ni muhimu mno; pasipo ushirikianohuu, hamna cho chote.2. Matokeo ya kutengamana na Kristo ni kunyauka na Uharibifu (Yohana 15:6)a. Mtu asiyetii kama vile, mtu ambaye kwa mapenzi yake hujitenga kutoka kwa mzabibu wakweli, amelaaniwa.b. “Kunyauka” – majuto yake hayaji baadaye, kwa sababu katika hukumu ya mwisho, lakinihatimaye kunao kutengana.c. “Tutupwa motoni ili kuangamia” – Katika ulimwengu huu, ambao umetawaliwa na tabia nasheria zake, jambo mbaya linalotokea ni wakati mwanadamu anajitenganisha na Kristo.(Tazama Yohana 13:30; Mathayo 27:5).3. Ushirikiano na Kristo Ndiyo Sababu ya kiridhisha mahitaji yako. (Yohana 15:7)a. “Ukiwa ndani Yangu na maneno yangu ndani Yako…..” ni vigumu kuomba kwa njianzuri bila ya kujua na kuamini mafundisho ya Kristo.b. “Omba utakacho nawe utapata” – mapenzi yetu kwa pamoja na uwepo wake wote.Wakati wote kutafuta kufanana Naye, kuwa wenye hisia nzito kwa kazi Yake nakatika kutembea katika njia Yake. “Mapenzi Yako yafanyike” (Mathayo 6:10; Mathayo26:39). Kuutamani ufalme Wake.Tamati:Mungu anatafuta tunda. Anayo sababu ya kutarajia tunda kutoka kwa watu Wake. Ikiwatunajihusisha na kazi ya huduma ya Mungu, hivyo tutazaa matunda. Wakristo ambao maisha yaoyamo ndani ya Kristo, yametiwa nguvu kwa ujazo wa Roho Mtakatifu, watazaa matunda.Nakala hii imetayarishwa na Kasisi Collin ElliottMkurugenzi Mkuu Kanda ya Afrika Kusini18


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 3Maandiko: Yohana 7:37–39Utangulizi:Mtiririko Wa UtakatifuKusudi la Kristo sio kutuuisha kiu pekee, ila pia anataka kutujaza na Roho wake ili tuwe chemichemi kwa waume na wake walio karibu nasi wenye kiu.1. Aina ya maji yanayomiminika toka kwetu – MitoMaji ambayo hayajasimama, yasiyomachafu, sio kama maji ya ulimwengu ambayo,a. Yenye mahangaikob. Hayatulizi kiu ya moyoc. Uhatarisha na kuuad. Hayapeani wala kudumisha uzima2. Kipimo cha maji yanayotiririka kutoka kwetua. Ni mengi kwa kila mtub. Yanatosha kwa kila wakati – kwa kila msimu, hayana barafu, hayakauki na kiangazihakiwezi kuyakausha.3. Chanzo cha maji haya – Roho Mtakatifu aliye katika Moyo wa Mkristo.a. Hili ni timizo la Roho ambaye Mungu aliahidi (Yoeli 2:28 -29)b. Nabii Isaya alitabiri (Isaya 55:1-13)c. Ujazo umo kwa Wakristo wote ambao wamekuja kwa Yesu. (Waefeso 3:14-21)Tamati:Wakristo waliojazwa kwa Roho wanatiririka kwa Roho wa Mungu. Wanatambua na wanao kazinyingi katika huduma ya Mungu na kuwafanya wanafunzi wanaofanana na Kristo ulimwenguni kote.Nakala imetayarishwa na Kasisi Collin ElliotMkurugenzi Mkuu Kanda ya Afrika Kusini19


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 3Maandiko: Warumi 1:8-17Utangulizi:Wadeni wa InjiliPaulo alikua na upendo mkuu kwa tamaduni na dini ya Wayahudi. Kwa Kuwaandikia Wafilipianasema:“Mtu ye yote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi: Nalitahiriwa siku yanane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari yakuishika torati, ni Farisayo, kwa habari ya juhudi mwenye kuliudhi Kanisa kwa habari ipatikanyo kwasheria siku wan a hatia.” (Wafilipi 3:4-6)Tamaa hii ilimpa motisha ya kupokea elimu ya Kiyahudi ya juu chini wasomi bora zaidi wa Kiyahudikama vile Gamalieli (Matendo ya Mitume 22:3). Baada ya kuhitimu, lengo lake lilikuwa kuilindatamaduni na dini ya Kiyahudi. Aliwatolea wanafunzi wa Yesu matamshi yenye vitisho (Matendo yaMitume 9:1) alilitesa Kanisa. Wakati mmoja akiwa njiani akielekea Damaski, Mungu alimtokea nakuyabadilisha maisha yake na kumwondolea tama ya kuua.Alipewa tamaa mpya – tamaa ya kuhubiri Injili ya Yesu Kristo. Aliutamani kuhubiri injili ya YesuKristo. Alitamani upendo wa Kristo ambao ulimvuta katika kimtumikia Bwana na Watu wa mataifaambao walichukiwa na Wayahudi. (II Wakorintho 5:14). Ameandika katika Wafilipi 3:7-9:“Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, nayahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.Zaidi ya hayo, nayahesambu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wakumjua Kristo Yesu Bwana wangu, ambaye kwa ajili Yake nimepata hasara ya mamboyote, nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo name nionekane mbele Zake nisiwena haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani katikaKristo, haki ile itokayo kwa Mungu kwa njia ya imani”Charles Wesley alizisema hisia za Paulo alipomwona Yesu na ile ndoto ya kiungu:“Niwonapo Mti bora, Kristo aliponifia, Kwangu pato ni hasara, Kiburi nakichukia”Tamaa yake haikuwa kwenda Roma pekee ila alitaka kuzuru ulimwenguni kote na kukiri injili.Tamaa kuu ilimfanya ahisi kuwa ni jukumu lake, na asione haya. Haya yalikuwa ni maonoaliyopokea kutoka mbinguni ambayo hangepinga (Matendo ya Mitume 26:19)1. Kazi yake ilikuwa ni kihubiri Injili – alikuwa mdenia. Hii ni lugha ya wataalam wa hesabu – mdeni ni mtu ambaye amepokea faida kutoka kwamtu mwingine. Sote tu wadeni kwa sababu tumepokea upendo wa Mungu.b. Anayetukopesha ni Mungu na wala sio watu wa mataifa ama wagiriki, na kadhalika.c. Huduma yetu kwa Mungu ni huduma kwa watu Wake wote – wenye busara na wasio nabusara. Mafumbo ya kondoo na mbuzi – (Mathayo 25:34-46).d. Deni ni msukumo mkuu wa upendo (II Wakorintho 5:14)e. Unapofuzu chuoni, msikumo wa maisha unafaa kuwa ndiyo chanzo cha msukumo wamapenzi.f. Upendo wa Mungu na mpango wote wa Wokovu ni kipawa bure cha upendo. Hanamatarajio kuwa sisi tutamlipa – hatuwezi tukamlipa. Pendo lake limetujengea tamaa yakimtolea SHUKRANI katika mioyo Yetu kwa njia ya huduma za upendo kwetu.2. Alitamani kuhubiri – Alikuwa tayari:a. Kuhubiri injili20


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 3b. Kujaribu kulipa deni ya pendo.Ni lipi nitakalo fanya ili kuonyesha Mungu shukrani zangu.Sina za kutosha; Namtolea maisha yangu.c. Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimelinda. Sasa nimewekewa tajiya haki ambayo Bwana mwamuzi wa haki, atanitunuki siku ile, wala si mimi tu, bali pai woteambao wamengoja kwa shauku kuja Kwake. 2 Timotheo 4:7-8)d. Ili uwe tayari haufai kufuzu katika chuo lakini pia fuzu katika chuo cha Yesu.(Baada ya kuwafunza wanafunzi, Yesu aliwaambia wasubiri hadi watakapovishwamavazi ya nguvu zitokazo juu Mbinguni. (Luka 24:49).Siku ya pentekoste walivishwa na kufunikwa na Roho Mtakatifu, aliyewajaza (Matendoya Mitume 2:2)e. Watu utakaohudumia hawajui alama ulizopata shuleni lakini walimu wako wanazifahamu.f. Watu utakaohudumia hawajui ikiwa u tayari lakini watajua ikiwa u tayari utakapoondokashuleni.g. Watafahamu watakapokuona ukitenda na kuangaza nuru yako mbele zao ama wakati nuruyako haitawaka mbele zao.h. Mafunzo yako yamejumlisha mambo manne yafuatayo:-1. Kutosheka2. Uwezo3. Tabia4. Yaliyomoi. Utakapokuwa unaondoka chuoni, utafanyiwa mtihani na kupewa alama – pengine utafauluama utashindwa hili litategemea utendaji wako. JInsi unavyopenda ama kushindwaitategemea alama zako (Mathayo 5:16)j. Je, u tayai kuimba: “Tayari kuondoka ……..?3. Hakuona haya kwa sababu ya injilia. Hakuona haya kwasababu Mungu alimwondolea haya.b. Alifurahia yale ambayo Mungu angemfanyia na yale ambayo angemtumia kufanya kwa njiaya injili.c. Alifurahi kwasababu Mungu angeuleta wokovu kwa waliomwamini.d. Nguvu za injili zatenda ndani yetu na kupitia kwetu.e. Nguvu ambazo Paulo anazungumzia ni nguvu zinazofanya kazi ndani yetu.“Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo autuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu, naam, atukuzwe katikaKanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele! Amina. (Waefeso3:20)Tamati:Tamaa, hamu, ari, penzi mambo haya yote yatakufanya uendelee na yatakufanya shahidi mkuuanayewaleta watu kwa Kristo. Bila ya mambo haya, utakufa moyo, utashindwa na hautafanya chochote.Ari itakusaidia kuendelea kuvumilia mateso na mwisho wa huduma yako utaweza kusema,“Nimevipiga vita vilivyo nzuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda”. (2Timotheo 4:7)Nakala imetayarishwa na Dkt. Enoch H. LitsweleAliwakilisha katika sherehe ya kufuzu ya chuo cha NTC21


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 3Mtindo wa Maisha ya Utakatifu – Wito WetuMaandiko: Isaya 35:8Utangulizi:Muuzaji magari mashuhuri kwa jina Nissan alikuwa na nembo iliyosema, “Maisha ni safari, ifurahie.Kila safari uanzapo lazima iwe na mwisho.Kila mmoja wetu yumo safarini ya maisha. Lazima tuwe na tumepanga mwisho.Isaya anazungumzia njia ambayo wokovu wa Bwana wanasafiri ijulikanayo kama barabara kuu yaUtakatifu. Mafundisho ya Wesley husema “barabara ya kawaida” na “barabara kuu” hauwezikuzichukua kama barabara mbili tofauti, lakini kama barabara moja. Barabara kuu huwa imeinuliwana huelekea kwa njia ya Utakatifu, wanaotembea katika barabara hii ni watu waadilifu, wanyonge,vipovu na walemavu ambao Mungu anaongoza na kuokoa. Barabara ni laini na nyofu kiasi kwambahata msafiri aliyemjinga zaidi kabisa hawezi akafanya kosa.1. Utakatifu ni kitendo cha Mungua. Sio kazi zetu, sio kazi zetu nzuri, lakini ni kitendo cha Mungu.b. Mambo ya Walawi 20:8 “Nanyi zishikeni sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi BWANAniwatakasaye ninyi”.2. Utakatifu sio suala la hiaria. Ni amrib. Mambo ya Walawi 20:26 inasema, “Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwamimi BWANA ni mtakatifu, ili kwamba mwe wangu.”3. Utakatifu huvutiaa. Kama vile mwanga huvutia wadudu, vivyo ndivyo utakatifu wa maisha ya Mkristo huwavutawengine kwa ufalme wa Mungu.b. Yohana 12:32 husema, “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu”.4. Utakatifu ni tiketi ya kuenda kwa Mungua. Bila utakatifu maishani mwetu, hakuna atakayemwona Mungu (Waebrania 12:14)b. Utakatifu unahitajika katiak ushirika na Munguc. Daudi aliuliza katika Zaburi 51, “BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni naniatakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu. Alikuwa akiuliza, “Bwana naniataishi katika ushirika nawe?’Jibu analopewa lapatikana katika mistari minne ifuatayo, mtuaendaye kwa ukamilifu.”Maonyesho: Kunayo hadithi ya mchungaji aliyekuwa akijenga vito za wima za kuushikiliamzabibu. Alipokuwa akiendelea na ujenzi wake, akamwona kijana mdogo akimtazama.Yule kijana hakusema lo lote, naye mchungaji akaendelea na kazi yake kwa matumainikwamba yule kijana ataondoka, lakini yule kijana hakuondoka. Mwishowe mchungajiakamwuliza, “ mwanangu naona unaendelea kupata ujuzi wa kazi za ukulima?” Akamjibuakamwambia, la, nangoja ili nisikue jinsi mchungaji anaposema anapojigonga kidole.”Tamati:Kunayo njia pana na nyembamba kulingana na Mathayo 7:13-14. Hatima yako ni ipi katika safari yamaisha unayosafiri.Nakala imetayarishwa naye Kasisi Kenneth PhiriRaisi wa Kundi la vijana eneo la Afrika22


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 4Maandiko: Isaya 6:1-7Utangulizi:Utakatifu Na Maadili Ya KuishiKatika kifungu hiki tunaona utakatifu ukibadilisha uovu na kuwa wema.1. Utakatifu wa Mungua. Utakatifu ni hali ya Mungu ambayo humtofautisha kutoka na maumbile Yake. Yeye ndiyepekee mtakatifu.b. Utakatifu wa Mungu kwa jumla ni Yule Mungu Aliye. Yeye na Yeye pekee ndiye mtakatifu.Hamna Aliye mtakatifu kama Bwana” (1 Samweli 2:2)c. Yeye ndiye Muumba, yeye ndiye muumba wa kila kitu na hakna mtu yeyote ama kitu chochote kilichoumbwa kinachotoshana Naye.d. Utakatifu haulinganishwi na maadili bora. Yeye sio mtakatifu tu kwasababu yeye nimwenye maadili bora.e. Yeye ni mtakatifu kwasababu Yeye pekee ni Mungu na Yeye ni Mungu kwasababu Yeyepekee ni Mtakatifu.f. Yeye hana utakatifu – Yeye binafsi ni Utakatifu – Utakatifu sio jambo lililo kando Yakekwasababu Yeye binafsi ni utakatifu.g. Pasipo Mungu hamna utakatifu na pasipo Mungu hamna Utakatifu.h. Maana tofauti na maelezo tofauti ya neno “utakatifu”Kiswahili – Utakatifu= Ukamilifu/mteule/Utakaso/UtukufuZulu – Ubungcwele = uwepo na utakasoTsonga – vukwetsimi= kungaaNhluweleko=kutenganishwaPedi – Bokgetwa= kutenganishwaTswana – moyo o Boitshepo = Roho wa kuaminikaSotho – Bohalaleli = kungaaAfrikaans – Heilig= Safi/Iliofaa/2. Utakatifu wa Wakristoa. Utakatifu wa Wakristo huwezekana hupatikana kwa njia ya ufunuo wa Mungu pekee –Isaiah alimwona Mfalme (Isaya 6:5)b. Utakatifu wa Wakristo ni utakaso (kusafishwa na kutenganishwa) wa Wakristo na RohoMtakatifu kupitia kwa Yesu Kristo.c. “Utakaso /kungaa/uaminifu” huanza kwa mabadilisho baada ya kubadilishwa tunapoasi nadhambi zetu na kutengeneshwa na Mungu (Yohana 1:12)d. “Utakaso/kungaa/uaminifu” huendelea kukua baada ya mabadilisho, tunapotembea kwauaminifu wa mwanga wa maisha, hadi tutakapotenganishwa na dhambi ambayo nikujifikiria/mtu mzee/hali ya uovu/kuzaliwa kwenye dhambi na kutenganishwa nakuondolewa katika uwepo wa Mungu.Onyesho – kubadilisha mbwa huifanya kuwa mbwa mpya (Wagalatia 2:20)e. Baada ya tukio la pili la utakaso kamili, utakaso/kungaa/uaminifu wetu huendelea kukuakutoka kwenye utukufu hadi utukufu na kutoka kwenye neema hadi neema kila sikuAnapotuongoza.f. Utakaso kamili hautufanyi kuwa Mungu, Kristo, ama Roho Mtakatifu lakini hiyo hutufanyakuwa kama Yesu Kristo – kufanana na Kristo.g. Jinsi tunavyoendelea kukua katika utukufu, kwa furaha tunaimba pambio hii:Kila siku na Yesu pamoja na Yesu ni tambu zaidi kuliko janaKila siku na Yesu, Nampenda zaidi na zaidiYesu huokoa na kutuweka, Yeye ndiye tunayesubiri23


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 4Kila siku na Yesu pamoja na Yesu ni tamu zaidi kuliko janah. Huyu ndiye ‘mtakatifu wa Israeli’ Isaya aliona katika ndoto iliyobadilisha maisha Yake.(Isaya 6)3. Kuishi kwa Utakatifu Na Uadilifu ni Kwa Wale Waliotakaswa Kwasababua. Wanafahamu kupitia kwa Maandiko Matakatifu, mema wanayofaa kutenda na maovuwasiofaa kutenda. (Mika 6:8)b. Maadili yao hayajaandikwa kwenye Biblia pekee, lakini pia imo akilini mwao na mioyoyao. (Yeremia 31:31-34)c. Fahamu zao zimeoshwa kwa damu ya Yesu kristo na zintofautisha wema na uovu.d. Tabia na maadili ya maisha ya Isaya hayakupendeza, ingawa alikuwa ndani ya huduma,ilifikia wakati ambapo fahamu zake zilioshwa (Isaya 6:5-6)“Fahamu nzuri ni ile iliyosafishwa na Roho wa kweli, na hutoa uamuzi kulingana nadesturi za neno takatifu la Mungu (H Orton Wiley).e. Utakaso Wake ulionekana alivyokuwa akiomba na kulia kwenye altari:“ Ole wangu mimi! Nimeangamia! Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nayomacho yangu yamemwona Mfalme, BWANA mwenye nguvu.”f. Kwa kaa la moto wa Roho Mtaktifu, Mungu aliyaguza maisha ya Isaya na kumsamehedhambi zake.g. Kaa la moto lilimbadilisha na kuishi kama Mkristo anayewaka katika moto wa utakatifukama chuma kilicho kwenye moto.Tamati:Je, unawasikia maserafi wakiimba.“Mtakatifu, Mtakatifu Mtakatifu ni BWANA, Mwenye Nguvu.Dunia yote imejaa utukufu wake”.Je, wanapoimba, kunao mambo ya kiroho ambayo Mungu anafumbua katika maisha yako? Ikiwaanafanya hivyo, nitakuhimiza wewe uje katika altari ya maombi, na kuomba kama vile Isayaalivyofanya. Mungu anasubiri kutimiza hitaji lako pale.Nakala imetayarishwa na Dkt. Enoch H. LitsweleKatika kongamano la Utakatifu kwenye ukumbi wa NTC19 Mei 199924


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 4Maandiko: 1 Petro 1:13-2:3Utangulizi:Tunapaswa kuwa Watakatifu kwa vile imeandikwaIli kuhalalisha jambo lo lote ni vyema liandikwe.1. Amri ya kuwa mtakatifu imeandikwa na Mungua. Ni amri kuwa:-­‐ bora kwa vile Mungu ni bora.-­‐ Wasafi katika moyo-­‐ Kutenganishwa na dhambi na kutenganishwa na Mungu-­‐ Kufanana na Kristo.b. Sheria inaunganisha, ni halali na yenye ukweli.c. Utakatifu ni tabia ya Mungu. Yeye ni mtakatifu na kwasababu hii Yeye yu tofauti na vyotealivyoumba.d. Utakatifu umeandikwa ndani Yake milele. Yeye pekee ndiye mtakatifu wa Israeli.e. Imeandikwa katika kazi zake za maumbile (Mwanzo 1:31, Zaburi 19:1-2) “Jinsi WeweUlivyo Mkuu!”f. Imeandikwa katika Biblia Takatifu (Mambo ya walawi 11:44, 19:2, 20:7)g. Maandiko yote yanatuamuru tuwe watakatifu (2Timotheo 3:15)h. Vita vyote vya Kikristo vimeandikwa ili kutuambia tuwe watakatifu.2. Zaidi ya yote, Habari zilizoandikwa Ni nzuri na zenye msaada lakini sio nzuri kutosha.a. Ufahamu kuhusu Mungu Mtakatifu haibadilishi mtu.b. Habari njema tunayopokea kutoka kwa maumbile matakatifu ya Mungu hayatubadilishi.c. Sheria ya Musa iliyoandikwa haikuwabadilisha Waisraeli; ilikuwa ni shule ya kuwaelekezakwa Kristo. (Wagalatia 3:24)d. Vitabu nzuri na vitabu vyenye mafundisho ya Ukristo, zitatusaidia kufahamika, kujifunza nakujua, lakini haviwezi kutubadilisha.3. Agano Mpya (Maandishi Mapya) Tuliyoahidiwa Na Mungu.a. Yapatikana katika Yeremaya 31:33-34b. Utakatifu sio wa midomo na akili zetu pekee lakini pia inafaa kuwa katika mioyo yetu(Mathayo 5:8)c. Utakatifu hubadilisha kitabu chetu cha maisha ya kale kichafu, kama inavyoelezwa katikaWagalatia 5:22-23d. Ulimwengu unataka kuona mabadiliko matakatifu maishani mwetu na wala sio kusikia jinsitunavyoufahamu utakatifu.e. Damu ya Yesu huondoa alama za dhambi. (1 Petro 1:18-19)f. Mwandishi wa wimbo huu alisema kweli alipoandika:“sioshwi dhambi zangu, bila damu yake YesuHapendezewi Mungu, bila damu yake YesuHakuna kabisa, dawa ya makosa, Ya kututakasa, ila damu yake Yesu.g. Inasemakana kuwa Yesu hajawai kuandika kitabu, lakini ukweli ni kwamba ameandikamamilioni ya vitabu kuhusu kuishi maisha matakatifu.h. Mwanga wa utakatifu lazima ungae vyema ili watu waone na kusoma matendo yetu mazuri(Mathayo 5:16)i. Waume na wake watakatifu ndivyo vitabu vilivyo bora zaidi vya utakatifu (2 Wakorintho 3:1-3)j. Biblia ndicho kitabu chenye mauzo bora zaidi, lakini Mkristo anayefanana na Kristo ndiyemuuzaji bora zaidi.25


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 4Tamati:Utakatifu wa Ukristo ni mfano wa Mungu ndani yetu.-­‐ ni kitambulisho chetu.-­‐ Ndiyo kinga yetu takatifu.-­‐ Ndiyo cheti cha usafiri kwa wenyeji wa mbinguni.-­‐ Ndiyo cheti kinachotupa fursa ya kuwepo katika uwepo wa Mungu wetu Mtakatifu.(Waebrania 12:14)Mwandishi wa wimbo huu alikuwa amesubiri kwa hamu kitambulisho alipoandika“Kwa mfano wako, kwa mfano wakoEwe Mkombozi, niwe wako,Unitilie muhuri yakoNigeukie kwa mfano wako.”Nakala imetayarishwa na Dkt. Enoch H. LitsweleMstaafu Naibu wa Mkurugenzi Mkuu Eneo la Afrika26


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 4Kungaza Kwa Uso wa Yesu Juu YetuMaandiko: Zaburi 67, Hesabu 6:22-27, Ufunuo wa Yohana 1:161. Kungaza kwa uso Wake ni kama vile jua lingaapo kwa viumbe vyote; wema na wabaya.2. Hili ni ombi la watu wazuri:-­‐ Kibali cha Mungu kiwe juu yetu-­‐ Mungu atambasamu juu yetu.3. Uso wake uangaze juu yetu ni baraka la kikuhani kwa wenye haki (Hesabu 6:24-26)a. Baraka (shangwe na furaha)b. Kuwa na nguvu (Yuda 24)c. Neema za kutusitiri kila dakika ya maisha (2Wakorintho 12:9)4. Kungaza kwa uso Wake juu ya wenye dhambi huwasha taa ndani yao inayoonyesha uovuwao. (Yohana 3:19-21; Warumi 2:14-16)5. Adamu na Hawa walitenda dhambi, nao uso wa Mungu unaongaa uliwafanya wahisi kuwawenye hatia (Mwanzo 3:8-10; Yohana 3:19-21)a. Musa alihukumiwa kwenye kichaka kilichowaka moto wakati Mungu aliyafunua maishayake ya uovu. (Mwanzo 3:6).b. Isaya alihukumiwa alipouona uso wa Mungu hekaluni (Isaya 6:5)c. Daudi alihukimiwa kwa ajili ya uovu wakati uso wa Mungu ulingaa juu yake kupitia kwaNabii Nathan (Zaburi 51)d. Paulo alihukumiwa alipoona nuru ya toka mbinguni (Matendo ya mitume 9:3-5)6. Uovu wa mtu muovu humfanya asiuone uso wa Mungu kama vile wenye hatia hufichanyuso zao kortini. (Isaya 59:2)7. Yesu alipokua msalabani, dhambi zetu ziliuficha uso wa Mungu toka Kwake. (Mathayo27:46) Huu ndiyo wakati pekee ambao Mungu alimwacha Yesu.8. Uso wa Mungu huanza kuangaza juu ya mtu muovu anapotubu (Mambo ya Nyakati 7:14 –15)a. Mwenye dhambi akitubu uso wa mbinguni hungaza kwa furaha ya makaribisho (2 Mamboya Nyakati 7;14-15)b. Mfungwa anapoachiliwa huru kutoka gerezani huwa hafichi uso wake.9. Kungaza kwa uso wa Mungu hufaa katika maisha ya mtu aliyejitolea na kutakaswakikamilifu. Maisha yaliyotakaswa kikamilifu.a. Kioo safi na wazi kinachoonyesha mwanga wote; mwanga wa jua.b. Mwezi unaonyesha nuru ya jua usiku. Mwezi hauna mwanga; mwezi hutoa mwangakwenye jua na kutuangazia. Lazima tuwe mwezi uliomkamilifu wala sio mwezi ¼; ½; ama3/410. Yesu anapotuangazia nuru ya uso wake ndipo tunapokea utakatifua. Nuru ya uso wake huona ndani ya moyo kama picha ya X-ray (Zaburi 139:23-24)b. Moyo wa Isaya ulitafutwa na nuru ya Mungu alipoingia Hekaluni kusali (Isaya 6:1-7)c. Yesu anasema, wakati ukiwa unatoa sadaka na uso mwanga wa uso Wake ukuonyehsekitu, tunafaa kukomesha maombi na kisha kuenda kutatua shida ile ambayoametuonyesha. (Mathayo 5:23-24)d. Nuru yake hutusafisha na kutuweka wakatifu tunapotembea katika ushirika Naye (Mwanzo17:1, 1 Yohana 1:7).e. Nuru inapoangaza juu yetu, tunaurejesha huo mwanga katika ulimwengu wa giza na uovu.27


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 411. Kuangaza kwa uso wa Mungu Juu Yetu Hutuwezesha Kuona Mungu Ndani Yetu (Mathayo5:16).a. Uso wa Mungu uliangaza juu ya Musa (Kutoka 34:29-34)b. Uso wa Mungu uliangaza juu ya Stefano (Matendo ya Mitume 6:15, 7:54-56).c. Naomba uso wa Mungu uangaze juu yetu leo.d. Naomba uso wa Mungu uangaze juu wa Wanazareti 511 000 na zaidi katika eneo la Afrika.12. Uso wa Mungu unapoangaza juu yetu, nasi kama nyota za uwingu, tuangaze nuru ya usowake katika giza za kiroho katika eneo letu.Nakala imetayarishwa na Dkt. Enoch H. LitsweleMstaafu Naibu wa Mkurugenzi Mkuu Eneo la Afrika28


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 4Walio Na Moyo SafiMaandiko: Mathayo 5:8“Wana heri walio na moyo saf, maana hao watamwona Mungu” (Mathayo 5:8)Utangulizi:Majadiliano muhimu ya maadili katika tamaduni zetu. Ili uwe mwadilifu ni vyema kutenda katika njiaza uadilifu. Hili ni jambo wazi. Kwa mtazamo wangu kunao mengi katika uadilifu kuliko tabia, natusipokuwa waangalifu hili ni jambo pengine litasaulika katika tamaduni zeut.Kunao uwezekano wa udhibiti wa tabia za watu binafsi kwa njia ya sheria, lakini ukweli ni kwambahatuwezi kuzidhibiti tabia za mtu kwa njia hiyo. Ukimzuia mtu kufanya yale mambo ambayo unaona,huwa hujambadilisha tabia zake za ndani. Tabia hutokana na hali ya ubinadamu. Pengine utasemani hali ya moyo.Hivi basi, Yesu aliposema, “wana heri walio na moyo safi”. Alikuwa akisisitiza kuwa kile ambachotunahitaji ni kuwa wenye haki ndani.1. Wito wa kusafisha moyoa. Katika mafundisho mlimani, Yesu anashughulikia kanuni ambazo zinaguza kila sehemu yamaisha yetu. Sentensi rahisi, “Wana heri walio na moyo safi, maana hao watamwonaMungu”, hii inakuwa barabara yenye uzito itakayotuelekeza katika ahadi ya kukutana naMungu. Ni wito wa kusafisha moyo. Yesu anasema hali ya moyo wetu mbele zake Munguni muhimu. Hakika, ni kana kwamba lililo muhimu kwetu kama Wakristo ni kuwa na moyosafi kwake Mungu.1) Kunao uwekano wa kuwadangaya watu kwa kujifanya visivyo. Tunaonekanakutembea naye Mungu lakini kumbe sivyo. Hatuwezi kumdanganya Mungu. KatikaSamweli 1 16:7, “Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usizitazame sura yakewala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. BWANA hatazami kiatika vile vitumwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakiniBWANA hutazama moyoni”. Ni wazi kwamba Mungu hatazami kwa nje ila Yeyehutazama kwa ndani – jinsi ulivyo, hali ya mioyo yetu. Tunasoma katika Mithali 21:2,Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali BWANA huupima moyo”.b. Je, Yesu alimaanisha nini aliponena juu ya walio na moyo safi? Je, maana ya safi ni nini?Je, maanake ni bora? Kutokuwa na dhambi?1) Maana ya moyo katika Andiko ni akili, mapenzi na hisia. Inamaanisha mapenzi yakweli. Mwandishi wa Mithali alitoa ulishauri, “Zaidi ya yote, linda moyo wako, kulikoyote ulindayo. Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. (Mithali 4:23). KatikaMathayo 15:19, Yesu alisema, “Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazomabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio.” Moyohujumlisha akili na mwili. Mwamuzi wa tabia ni moyo.2) Yesu anaponena juu ya walio safi wa moyo, Anazungumzia moyo ulio na nia njema.Mioyo yetu inafaa kutawaliwa na akili moja na sadaka isiogawanyika.a) Yesu alisema, “Hakuna mtu ye yote awezaye kuwatumikia mabwana wawili,kwa kuwa ama atamchukia huyu na kumpenda yule mwingine, auatashikamana sana na huyu na kimdharau huyu mwingine. Ninyi hamwezikumtumikia Mungu na mali. (Mathayo 6:24)b) Yakobo katika kitabu chake anatukumbusha, “ … Urafiki na dunia ni uadui naMungu?,” pia hapa kunao suluhu: “… Itakaseni mikono yenu, ninyi wenyedhambi na kuisafisha mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili” (Yakobo 4:4;8)c. Tunapojichunguza katika mwanga huu, je tunaona nini? Wakati mwingine hatuanguki mbalina kiwango tulichowekewa. Nia zetu hazijachanganyikana. Wakati mwingine ni nia zaubinafsi. Wakati mwingine badala ya kujitolea kikamilifu kwake Mungu, unapata tunajaliyale ambayo ni faida kwetu. .29


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 4d. Wito wa Kristo ni wazi. Hatufai kuchanganya katika kujitolea katika kumtumikia.Je,umejitolea moyo wako kikamilifu kwa Mungu pekee?2. Hatua ya usafi wa moyoa. Je, tunawezaje kuifanya mioyo yetu iwe safi? Ikiwa nia zetu zimechanganyika, je, vipitunavyoweza kumrudia Mungu kwa moyo mmoja?1) Ili kuwa safi wa moyo, lazima tutambue haja yetu na pia kuishughulikia. Ni vyemakutembea katika maendeleo tuliyoona ya mafundisho ya kwanza manne. Kama “waliomaskini wa roho” tunautambua uovu wetu. Kama “wanaoomboleza”, tunatubudhambi kwa majonzi. Mioyo yetu imevunjika mbele zake Mungu. “Heri walio wapole”na watulivu mbele za Mungu. Upole ni kitambulisho cha watu walioguzwa na Mungu.Hatua ifuatao ni kumtaka Mungu na kuona kiu ya haki” kwa sababu tumeshuhudia kwasababu tumeona wanaoridhika ni wenye haki pekee. Huu ndiyo msingi tunaotakakujenga ikiwa tunataka kufanywa safi wa moyo.2) Hakika huu ni mfumo wa utakaso. Hii ndiyo maana ya maneno ya Yesu ya kubebamsalaba kila siku. Ni kumtafuta Mungu kwa moyo wangu wote, ni kumjia Mungu kamaDaudi na kuomba, “Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabitindani yangu na uufute uovu wangu wote.” (Zaburi 51:10). Ni kumtamani Mungukuliko cho chote.3. Matokeo Ya Usafi wa Moyoa. Sababu ambao ni muhimu kuwa msafi wa moyo ni kuwa watakao mwona Mungu.1) Mungu hutuhifadhia ushirika naye kwa wale ambao mioyo yao ni kwake tu, ilahaijachanganyika.2) Usafi wa moyo ni kiongozi cha maisha yetu kinachotuweka katika mstari mmoja naMungu.3) Wakati tumelainishwa Naye, tutafurahia fursa ya kuona Utukufu Wake – maono yaukuu Wake.4) Anataka kutufunulia zaidi nguvu Zake. Anataka tumjue zaidi, ili tuelewe njia zake. Hii niahadi yake kwetu – ni matokeo ya kufanywa safi wa moyo.Utangulizi:Walio safi wa moyo ni wachache katika jamii leo. Hata pia ni wachache makanisani mwetu. Lakinininaamini Mungu anatuita turejee kwake, kujitolea kwake ambao hakujachanganyika na mambomengine lakini sehemu ambamo kunao ujazo wa Roho Wake. Lakini katika ufalme, njia ya juu nikuelekea chini. Lazima tupige magoti katika toba kabla hatujaangalia juu ili kuona utukufu Wake. EeBWANA, safisha mioyo yetu ili tumwone Yesu!Kasisi Cosmos MutowaMkurugenzi Mkuu wa Kitengo Cha Huduma Ya Huruma30


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 5Maandiko: Zaburi 15Utangulizi:Kuishi Katika Uwepo Wa Mungu MtakatifuMambo ya Walawi 19:2, “…… Iweni watakatifu kwa sababu Mimi ni Mtakatifu”. Hekaluni mlikuwa nachumba cha ndani kilichojulikana kama Mtakatifu wa Watakatifu, ambapo palikuwa ni mahala pauwepo wa Mungu kati ya watu Wake. Mahala hapa palikuwa ni patakatifu mno kwasababu uwepowa Mungu ulikuwa mahali pale. Uwepo wa Mungu ni mojawapo wa takatifu. Ni kuhani mkuu pekeyake ndiye aliyeingia ndani ya sehemu ya pili ya hema, tena hii alikuwa mara moja tu kwa mwaka,lakini si bila kuchukua damu ambayo angetoa kwa ajili yake mwenyewe na kwa ya watu walio tendadhambi bila kukusudia. (Waebrania 9:7) Ikiwa kuhani mkuu angeingia katika chumba Takatifu ikiwayeye ni mwenye dhambi, matokeo yake yalikuwa ni kifo cha ghafla, (Kutoka 28:35-36). Kulinganana tamaduni za kiyahudi, pande moja ya kamba ilifungiliwa kwenye mguu wa kuhani mkuu nasehemu nyingine ilibaki upande wa nje. Wakati akiwa humo ndani kisha kengele zilizofungiliwakwenye jozi lake ziache kupiga, basi dhana ya kwanza itakuwa ni kana kwamba amekufa, ndipowalio nje wataanza kuvuta kamba pole pole ili waone ikiwa amekufa. Kuhani mkuu hakufaa kuwana dhambi ilia pate kuhudumu katika uwepo wa Mungu,ni jambo muhimu sana kwetu ikiwahatutakuwa wenye dhambi, lakini tuwe watakatifu, lakini kuingia katika uwepo Wake.1. Zaburi 51, huonyesha mambo saba yanayotuwezesha kukaa katika uwepo wa MunguMtakatifu.a. Aendaye pasipo mawaa (mstari 2)b. Atendaye yaliyo haki (mstari 2)c. Anenaye ukweli (mstari 2)d. Pendo kwa jirani (mstari 3)1) Hana wivu2) Hatendi uovu3) Haongei maneno ya mabaya kwa watu wengine.e. Mlinzi ya maagano (anatimiza ahadi) (mstari 4)f. Hachukui vitu vya watu wengine (mtu akikuomba pesa hakulipishi na pesa za uzao) mstari 5g. Hachukui hongo (mstari 5)2. Je, kwa nini baadhi ya mambo haya ni muhimu kwa Mungu?a. Mambo haya ukiyatazama kwa juu hayana umuhimu wo wote.b. Lakini yasipochukuliwa moyoni, kunao uwezekano wa kuleta madhara katika wokovu wetu.c. Kwa hivyo ni muhimu wakati wote kulinda mioyo yetu dhidi ya aina ye yote ya uovu (Mithali4:23)d. Tunafaa kuutafuta uso wa Mungu wakati wote (Mambo ya Nyakati 16:11; zaburi 105:4).Tamati:Mungu ni Mtakatifu, angependa watu Wake wawe watakatifu na waishi katika uwepo Wake kilasiku. Chukua mda wa kuchunguza maisha yako asubuhi ya leo. Je, inaandamana na mapenzi yaMungu? Ikiwa unahitaji maombi, nakualika uje kwenye altari ukutane na BWANA. Yeye yuko tayarina Anaweza kukupa moyo mpya na roho wa kweli.Nakala imetayarishwa na Kasisi Paulo MtamboKurugenzi Mkuu, Kanda Ya Afrika ya Kati31


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 5Maandiko: 1 Yohana 1:5-10Utangulizi:Utakatifu UnaovujaUhusiano wetu na Mungu ni kuishi kwa utakatifu mda baada ya muda. Sio lazima kuhubiri nakuzungumza kuhusu utakatifu kila wakati. Hata hivyo, utakatifu unafaa kutiririka toka ndani mwetukupitia kwa maisha yao! Maana ya kuvuja: kumwagika ama kutiririka pole pole. Jinsi tunavyoishihumtiririsha Kristo na utakatifu ulimwenguni. Kristo anasema katika Mathayo 5:13-14, Ninyi nichumvi ya ulimwengu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu”. Kama chumvi ya ulimwengu, kila wakati tunafaakuwa na ladha ya utakatifu. Kama vile mji ulio mlimani hauwezi kifichwa, vivyo hivyo ndivyotunapotembea na Mungu hatufai kujificha mbali inafaa kuwa ni nuru kwa ulimwengu. Kwa urahisimaisha yetu yanafaa kuonyesha kile ambacho tunakiri.1. Wewe Ni Nuru Ya Ulimwengua. 1 Yohana 1:5-6 inatueleza, “Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka Kwake na kuwatangazianyinyi, kwamba Mungu ni nuru na ndani Yake hamna giza lo lote. Kama tukisema kwambatwashirikiana naye huku tukienda gizani, wasema uongo, wala hautendi lililo kweli.”1) Tunapokiri kuwa tumeokoka ilhali tunaendelea kuishi katika giza kwa kuendelea namaisha yetu ya uovu ya kale, basi tunadanganya.2) Maisha yetu hayaambatani na yale mambo tunayosema yalitutendekea.b. Mstari 7, “Lakini tukienenda nuruni, kama Yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi nadamu yake Yesu, Mwana Wake yatusafisha dhambi yote.”1) Tumetakaswa kikamilifu2) Roho Mtakatifu huosha na kutakasa mioyo yetu toka kwenye dhambi, na hutuongezanguvu za kuishi maisha ya ushindi juu ya dhambi.2. Toba na utakaso toka kwa dhambi ndizo huja kwanza.a. Kazi ya utakatifu ya kuosha moyo haifanyiki ikiwa hatujatubu dhambi zetu. “Kamatukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu wa haki, atatusamehe dhambi zetu nakutusafisha toka kwenye udhalimu wote (1 Yohana 1:9). Lazima tukiri na kuungamedhambi zetu na kuomba Roho Mtakatifu aoshe mioyo Yetu.b. Kabla ya kuzaliwa tena, mawazo yetu yote yamo juu yetu na tunao mazoea ya kutendadhambi na kumchukiza Mungu. Lakini, tunapotakaswa, Kristo huingia maishani mwetu nakuyadhibiti maisha yetu. Maneno haya yalinenwa na mtume Paulo katika Wagalatia 2:20,Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi bali Kristo ndiye aishiyendani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana Wa Mungu,aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.3. Utakatifu hutirika toka katika moyo safia. Toka kwa moyo ulio safi, na uliojazwa na Roho Mtakatifu, utakatifu unafaa kutiririka, kamavile mwili unavyotoa jasho baada ya zoezi ama ukiwa katika shindano.b. Tunapoishi maisha matakatifu, yataonekana kwasababu yatajishomosha katika sehemuzetu zote za maisha.c. Yesu akikaa mioyoni mwetu, Yeye hutudhibiti jinsi tulivyo na yote tutendayo. Hapa kunaobaadhi ya mambo ambayo atadhibiti anapotuongoza:1) Yeye hudhibiti macho yetu – kile tunachoona2) Yeye hudhibiti masikio yetu – kile tunachosikia3) Yeye hudhibiti midomo yetu – yale tunayosema4) Yeye hudhibiti vinywa vyetu – kile tunachokula5) Yeye hudhibiti mikono yetu – kile tunachofanya ama tusichofanya!6) Yeye hudhibiti miguu yetu – tuendako na tusikoenda!4. Maisha matakatifu huifadhi tunda la Rohoa. Katika Wagalatia 5:22-23 Paulo anazungumza kuhusu tunda la Roho Mtakatifu ambalo niupendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi.b. Mambo haya yote yamo katika maisha yaliyojazwa na Roho. Kwa njia ya kawaida, Utakatifuhutiririka kwasababu hivyo ndivyo tulivyo.32


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 5Tamati:Je, maisha yako yanatiririsha utakatifu? Ikiwa ni la, ni kitu gani kinachotiririka toka kwako kwendaulimwenguni? Je, uko tayari kumruhusu Kristo moyoni na maishani mwako ili akupe ushindi leo?Altari imo wazi ili uje na kumwomba Mungu aoshe na kutakasa moyo wao na kukujaza nguvu zaRoho Mtakatifu hili tuishi maisha ya utakatifu, tuwe chumvi na nuru ya ulimwengu.Nakala imetayarishwa na Kasisi Paulo MtamboKurugenzi Mkuu, Kanda Ya Afrika ya Kati33


Mpangilio wa wa Mafunzo ya ya Kusheherekea Utakatifu Mafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho Mtakatifu Wiki ya 5Maandiko: Waefeso 4:12-15Utangulizi:Roho Mtakatifu AnaunganishaMaono ya Roho Mtakatifu akimiminwa kwa kanisa wakati wa Pentekosti, yale matukioyaliyoandikwa na Petro katika Matendo ya Mitume 2:16-18, yalikuwa ni maono ya Yoeli (Yoeli 2:28-32). Katika utabiri huu, tunaona Roho Mtakatifu akimiminwa juu ya watu wengi badala ya mtummoja mmoja, hapa na pale. Roho Mtakatifu hakufaa kuwamiminwa juu ya watu binafsi ila ni kwawatu wote kwa jumla. Pia alifaa kuumba jamii ya Wakristo Kanisani. Jamii hii wa Wakristo ilikuwakatika umoja. (Matendo ya mitume 2:44-47)1. Umoja kamili huja kwa njia ya Roho Mtakatifua. Kwa kupokea imani katika Kristo. (Waefeso 4:13)b. Kwa kumpenda Kristo (Waefeso 4:13)c. Utiifu kamili katika Kristo (Waefeso 4:15)2. Umoja kamili huja kwa njia ya upendoa. Katika Kristo (Waefeso 4:15; Wagalatia 4:15)b. Katika mwili wa Kanisa (Waefeso 4:16; Wagalatia 6:10; 5:14)3. Umoja kamili huja kwa Njia ya kuasi majivuno (Wagalatia 6:14)a. Kujidhibiti nafsi (Wagalatia 5:22)b. Uvumilivu wa mda mrefu (Wagalatia 6:2)4. Umoja kamili mwishowe huibuka washindia. Huwashinda watub. Huushinda ulimwenguc. Humshinda shetaniTamati:Ni wazi kwamba uunganishaji wa Roho kanisani huadhirika wakati kunao mambo mabayayanayotendeka; uasherati, uchafu, ufisadi, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi…” (Wagalatia 5:20-21). Mambo haya huzua mgawanyiko na kusababisha tamaa za mwili ambazohupigana na Roho. (Wagalatia 5:18, 5:22-26). Kuwa na upendo mioyoni mwetu (Warumi 5:5;Wagalatia 5:22; Wakolosai 3:14, Roho Mtakatifu hufunga kila kitu pamoja…. Katika umojaunaofaa….” (Wakolosai 3:14) Ili, tuone kuwa Roho Mtakatifu analeta kila kitu katika amani nzurikanisani ambacho hutiririka katika upendo kwa kila mmoja.Nakala Imetayarishwa na Kasisi Collin ElliottMkurugenzi Mkuu Eneo la Kanda Ya Afrika Kusini34


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 6Maandiko: Warumi 6:19-22Ukweli Kuhusu UtakatasoUtangulizi:“Ikiwa Yesu sio Bwana wa wote, Yeye sio Bwana.” – R S Nicholson1. Utakaso ni zawadi ambayo Mungu amemchagulia kila Mkristo: (1 Wathesalonike 4:3)Kwa maana hayo ndiyo mapenzi ya Mungu ninyi mwe watakatifu, ili kwamba mjiepushe nauasherati.a) Yaliyo bora zaidi kwa Mkristo (Waefeso 1:4)Kwa maana alituchagua katika Yeye kabla ya kuumbwa ulimwenguni ili tuwe watakatifu nabila lawama mbele Zake.b) Changamoto ya Mungu kwa Wakristo (Waebrania 12:14)Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao,hakuna mtu atakayemwona Bwana.c) Mapenzi ya Mungu kwa Mkristo (Waebania 10:14-15)Kwa sababu ya dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wotewanaotakaswa. Pia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili.d) Kusudi la Mungu kwa Mkristo (1 Wathesalonike 3:13)Tunamwomba Mungu awaimarishe mioyo yenu katika utakatifu ili msiwe na lawama, mbeleza Mungu wetu aliye Baba yetu wakati wa kuja Kwake Bwana pamoja na watakatifu wote.2. Utakaso ni Utakatifu wa MUngu Unaotolewa Kwa ajili ya Wakristo Waliokoka(1 Wathesalonike 4:7)Kwa maana Mungu hakutuitia uchafu, bali utakatifu.a. Inajumlisha kuasi tabia za uovu (Luka 14:33)“Vivyo hivyo, ye yote miongoni mwenu ambaye hawezi kuacha vyote alivyo navyo, hawezikuwa mwanafunzi Wangu.”b. Inajumlisha tabia na kiasi (1 Petro 1:15-16)“Bali kama Yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendowenu wote, Kwa maana imeandikwa: Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi ni mtakatifu.”c. Inawaita watu kujitolea katika huduma (Luka 1:74b – 75)“ …… tupate kutumika pasipo hofu 75 katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote.”d. Huangamiza imani iliyogawanyika (Warumi 5:12 – 19)“Sisi huweka wakfu, lakini Mungu hutakasa.” – F.B. Meyer3. Ukatakaso hupatikana kwa Imani (1 Wathesalonike 5:23-24)“Mungu mwenyewe, Mungu wa Amani, awatakase ninyi kabisa, roho zenu, nafsi zenu na miiliyenu, nanyi mhifadhiwe kikamilifu bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo. Yeyealiyewaita ni mwaminifu naye atafanya haya”a. Ni uzoefu wa dharura (Matendo ya Mitume 4:31)“Walipokwisha kuomba, mahali pale walipokuwa wamekutanika, pakatikiswa, nao wotewakajazwa na Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.”b. Hupatikana kwa njia ya utiifu wa imani (Yohana 14:11)“Nisadiki Mimi Kwamba niko ndani ya Baba na Baba yuko ndani Yangu, la sivyo, niaminikwa sababu ya zile kazi nizitendazo.”c. Inadhihirishwa kwa uwepo wa Roho Mtakatifu (Warumi 15:16)“ili kuwa mhudumu wa Kristo Yesu kwa watu wa Mataifa nikiwa na huduma ya kikuhani yakutangaza Injili ya Mungu, ili watu wa Mataifa wapate kuwa dhabihu inayokubaliwa naMungu, iliyotakaswa na Roho Mtakatifu”35 Somo limetayarishwa na Dkt. Stan TolerMsimamizi Mkuu Katika UtawalaKanisa la Mnazareti, Bara La Afrika


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Mafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho Mtakatifu Wiki ya 6Maandiko: Ayubu 1 – 6Utangulizi:Uadilifu UsiopingwaBaadhi ya maneno ya kibiblia tunayotumia katika mafundisho na mahubiri ni kama vile toba,wokovu, kuoshwa, upatanisho, haki, upendo, utakaso, na utakatifu. Katika kitabu cha Ayubu, mengiya haya meneno hayamo lakini kunalo neno moja ambalo lenye maana si haba na kuu ambalo ni –UADILIFU. Huu ndio uliokuwa urithi wa dhamana mno wa Ayubu.1. Hali ya uadilifu wakea. Uadilifu wa Ayubu ulikuwa wa kiungu, mtakatifu na Ukristo.b. Mwandishi wa kitabu anasema, Ayubu alikuwa (Ayubu 1:1; 8):-­‐ Asiyekuwa na hatia-­‐ Alikuwa mkamilifu-­‐ Alimcha Mungu-­‐ Mtu aliyeapuka ubayac. Maneno mazuri yanayonukuliwa kutoka kwa waraka wa kihushuda uliandikwa na Mungukwa shetani kuhusu uadilifu wa Ayubu (Ayubu 1:8)d. Maelezo ya neno uadilifu katika kamusi ya “Webster” ni kama ifuatavyo-­‐ hali isiyo na kilinganisha-­‐ enye maarifa.-­‐ Msimamo dhabiti katika sheria.-­‐ Hali ya kutotingisika-­‐ Kamilifue. Hivi ndivyo Mungu anavyotaka sisi tuwe, na Anao uwezo wa kutufanya tusiwe na hatia,wakamilifu, watu wa kumcha Mungu, na wanaoepuka uovu.f. Huu ndiyo urembo wa utakatifu, kama tunavyouona katika maisha ya Ayubu.2. Majaribio Makuu Ya Uadilifu Wakea. Uadilifu wake ulijaribiwa, lakini hakuanguka. Ondoa, kuasib. Utajiri na umaarufu wake hazimkufanya akose uadilifu wake. (Ayubu 1:2-3, 9 – 11)c. Kumbuka maneno ya Yesu, “…. Itakuwa vigumu sana kwa mwenye mali kuingia kwenyeufalme wa Mungu!” (Marko 10:23)d. Hata baada ya kupoteza kila kitu, hakuasi njia yake ya uadilifu (Ayubu 1:20-22)e. Ushuhuda wa pili wa Mungu kuhusu Ayubu kwa shetani ulitolewa baada ya majaribio(Ayubu 2:3)f. Hata baada ya mwili na mifupa yake kupata maradhi mabaya, aliendelea kushika uadilifuwake (Ayubu 2:4-8)g. Hata baada ya mke wake kumuasi, aliendelea kushikamana na uadilifu wake (Ayubu 2:9-10, Ayubu 19:17)h. Marafiki zake walimlaumu na kumvunja moyo, naye aliendelea kuwa mwaminifu kwakeMungu.i. Hata wakati ilionekana Mungu amemuasi, Ayubu hakuasi imani yake. (Ayubu 23:8-12)j. Uadilifu wake ulimsaidia kuyashinda majaribu ya uasherati. (Ayubu 31)3. Nguvu za uadilifua. Nguvu za uadilifu wake zilikuwema katika mpango wa wokovu ulioko katika Agano la kale.b. Dhabihu ya utakaso na sadaka ya kuteketezwa ilikuwa ni jambo la kawaida lilofanywa nawatu ili kujisafisha hao na jamii zao mbele za Mungu na wanadamu.c. Ayubu alifanya zoezi kama ishara ya meza ya Bwana tunayotumia leo.d. Leo tunatoa dhabihu ama sadaka za kuteketezwa kama kumbusho la dhabihu iliyotolewaKalvary. Hapa ndiko watokako watakatifu wetu, walio haki na waadilifu.e. Mambo yalipokuwa magumu kwa Ayubu, wa njia ya ushirika huu, aliweza kusema,“Ninajua kwamba mkombozi wangu yu hai………” (19:25-27)36


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 6f. Nguvu za uadilifu wetu na maisha matakatifu hutoka katika uhusiano wetu wa karibu naMungu na ushirika wa mkombozi wetu kama tunavyosoma katika maandishi ya Johannine(1 Yohana 1:5-7)Tamati:Mungu anawataka waume na wake wenye maadili makuu. Kwa kupitia kwa njia ya Wokovu naneema ya wokovu, anaweza kutupa tabia hii takatifu. Roho Mtakatifu, mfariji atatusaidia kudumishana wala sio kuasi maadili yetu tunapojaribiwa.Somo limetayarishwa na Dkt. Enoch H. LitsweleMstaafu Naibu wa Mkurugenzi Mkuu Eneo la Afrika37


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 6Kuwa Mkamilifu Kama Baba Yako Wa Mbinguni Alivyo MkamilifuMaandiko: Mathayo 5:14-48Utangulizi:Wito wa Mkristo mkamilifu linaendelea kujadiliwa kati ya Wakristo toka nyanja mbali mbali. Ukristomkamilifu waweza kupatikana, lakini si kwa urahisi. Kunao baadhi ya mambo katika maisha yaMkristo ambayo yanahitaji kutekelezwa katika shughuli za kufuatilia wito huu. Yesu Kristoanatuonyesha mambo nane ambayo wanadamu wanangangana nayo katika barabara ya ukamilifu.1. Je, mwanadamu anaweza kuwa mkamilifu kama Mungu?a. Tunaweza kuupata ukamilifu, na pia tunahitajika kufanya mambo yafuatayo:1. Usiwachukie wenzako pasipo sababu.2. Leta uwiaono katika uhusiano uliovunjika.3. Epuka mawazo ya uovu.4. Dumisha usafi wa ndoa.5. Matamshi yako yawe ni ya kweli.6. Epuka watu waovu7. Penda adui zetu na wale wanaotuchukia8. Kuwaombea wanaotutesa2. Barabara ya ukamilifu sio rahisi.Tamati:Yesu Kristo anatuonyesha njia ya Ukriso mkamilifu hata ikiwa inatofautiana na tamaduni zetu.Kukabiliana na changa moto hizi nane na kuendelea kukua katika safari yetu ya kiroho na katikauhusiano wetu na Yesu Kristo ili tupate ushindi ndiyo njia ya kutufanya tufanane na Kristo.Somo limetayarishwa na Kasisi ChansiChandaMkurugenzi mkuu Africa Middle Field38


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 7Maandiko: Kutoka 3:5-6Kutafakari Utakatifu Wa MunguUtangulizi:“Mungu akamwambia, “Usikaribie zaidi. Vua viatu vyako, kwa maana mahali unaposimama niardhi takatifu.” Kisha akamwambia, “Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu,Mungu wa Isaki na Mungu wa Yakobo.” Katika jambo hili, Mose akafunika uso wake,kwasababu aliogopa kumtazama Mungu.”Maana ya kutafakari utukufu wa Mungu ni kuasi mambo ya mtu binafisi na ubinafsi, kwa ajili yawokovu wa watu wengine.1. Tunafaa kuujali Utukufu (2 Wakorintho 7:1)“Wapenzi, kwa kuwa tunazo ahadi hizi, basi na tujitakase nafsi zetu kutokana na kila kitukitiacho mwili na roho unajisi, tukitimiza utakatifu kwa kumcha Mungu.”a. Utakatifu hueleza Mungu (1 Petro 1:16)“kwa maana imeandikwa: Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi ni mtakatifu”b. Utakatifu ni kujitolea kwake Mungu kwa moyo mmoja“Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao,hakuna mtu atakayemwona Bwana.”“Utakatifu sio jambo la kuchagua. Ni jambo muhimu katika maisha yetu ya kiroho kama vilechakula kilivyo kwa miili yetu.” – R S Taylor2. Jibu letu ni lipi katika Utakatifu wa Mungu (Warumi 1:20)“kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani ,uwezo Wake wa milele na asili Yake ya Uungu, umeonekana waziwazi ukitambuliwa kutokanana yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.a. Kukosa tamaa ya Mungu. (Mathayo 6:24)“Hakuna mtu ye yote awezaye kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa ama atamchukiahuyu na kumpenda yule mwingine, au atashikamana sana na huyu na kumdharau huyumwingine. Ninyi hamwezi kumtumikia Mungu na mali.b. Kutenganishwa na Ulimwengu (Mathayo 5:48)“Kwa hiyo iweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu”c. Kutamani kufanana na Kristo (Mathayo 22:37-38)“Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yakoyote na kwa akili zako zote. Hii ndio amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.”3. Ni vipi tunavyofaa kutafakari Utukufu wa Mungu (1 Wakorintho 1:30)“Mungu ndiye chanzo cha uzima wenu katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayokwa Mungu na haki na utakaso na ukombozi”a. Chuki kisichokuwa na kipimo (1 Yohana 3:6)“Kila mtu akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila mtu atendaye dhambi hakumwona Yeyewala hakumtambua.b. Upendo mkuu kwa watu wote (1Yohana 3:1a)“Oneni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe watoto waMungu……”c. Kujitolea kafara kwa ajili ya wema wa wengine (Yohana 3:16)“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ilikila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”Tamati:“Utakaso kamili sio mwisho, lakini mara kwa mara ndiyo mwanzo wa maisha ya hudumauliyoyatenda.” – R. S. Taylor39 Somo limetayarishwa na Dkt. Stan TolerMsimamizi Mkuu Katika UtawalaKanisa La Mnzareti, Bara la Afrika


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 7Maandiko: Mathayo 22:35-40Utangulizi:Amri Ya Kweli Ya PendoMengi kuhusu utukufu ni mapana na marefu. Kwa njia ya ubinafsi, ni kiwango cha usafishaji ambaohuonekana katika njia mbali mbali. Katika mafundisho ya Agano mpya ya Yesu katika vifungu hivi,kunao mpangilio wa njia tofauti tofauti za kumpenda Mungu na jirani zetu. Tunaishi katikaulimwengu ambapo maana ya neno “pendo” inatumika mahala po pote. Kwa Mkristo, maana ya“pendo” haifanani na maana ya neno pendo mtaani.1. Upendo ni njia moja ya kuonyesha utakatifu.2. Upendo ni tabia ya Mungua. Upendo wa mwanadamu hutoka kwa Mungub. Lazima tuonyesha upendo wa Mungu.3. Utakatifu ni kiwango cha uhusianoa. Upendo ndio ujumbe mkuu wa Musa na manabiib. Mungu alifunza upendo kwa Mungu na Jirani.c. Manabii waliwatolea watu changa moto ya kumpenda Mungu na jirani zao.d. Kumpenda Mungu pekee sio kamilie. Kumpenda mwanadamu pekee sio4. Upendo huangalia mbegu ya wema katika mwenye dhambi.5. Upendo hauwatendei wenza yale ambayo mtu binafsi hakati ketendewa6. Upendo ni mkuu kuliko matendo yetu yanayoonekanaa. Upendo ni mkuu kuliko imanib. Upendo ni mkuu kuliko matumaini7. Upendo huonyesha mabadilikoa. hurumab. kuteseka kwa mda mrefu.c. Kufurahia katika ukwelid. Uvumilivu kwa vitu vyotee. Kutumainia vitu vyotef. Kuamini vitu vyoteg. Kustahimili vitu vyoteTamati:Upendo ni jambo moja muhimu zaidi katika uhusiano wetu. Tumeitwa ili kupenda, lakini sio kwa njiaya kiulimwengu, lakini kwa njia inayofaa ya utakatifu.Somo limetayarishwa na Kasisi ChansiChandaMkurugenzi mkuu Africa Middle Field40


MpangilioMpangiliowawaMafunzoMafunzo yayaKusheherekeaKusheherekeaUtakatifuUtakatifu Mafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuWiki ya 7Maandiko: Waebrania 3:7-19Utangulizi:Pumzika – Mpaka UfuataoNatoa shukrani vile vile nimejaa furaha kwa ajili ya yote ambayo An Wake Mtakatifu. Watu wengiwalikuja kwenye altari na kupata ushindi na uponyaji katika uwepowa Bwana. Hakika Munguanatenda jambo mpya Kanisani mwetu na furaha yangu kuu ni kuona mahali tunakoelekea. Munguanayo mengi anayotaka kututendea. Anaweza kuyatenda mengi na kuliko yale tunayodhania.Ninalowazia leo ni , je, tunayaishi maisha yetu vipi tunapoondoka kwenye altari na kuondokakanisani mwetu. Je, sisi huelekea wapi?1. Ahadi ya mapumzikoa. Wana wa Israeli walikuwa na tatizo hili hili.1) Waliishi kama watumwa, walikabiliana na dhuluma nyingi na mateso katika nchi ya Misri.2) Mungu aliwaondoa mikononi mwa Farao na kuwaelekeza katika nchi walioahidiwa.3) Walionyesha imani kuu na utiifu kwa Mungu walipoamini maneno ya Musa na kumfuataalipowaondoa Misri.4) Hata hivyo, waliuona ukweli wa “uhuru” wao baada ya kuondoka Misri waligunduakwamba Farao alikuwa akiwafuata, nia yake Farao ilikuwa kuwarejesha Misri katikautumwa na ufungwa.5) Uhuru wao haukuwa mwisho ulio na furaha katika hadithi yao ya dhuluma humo Mistri;Ilikuwa ndiyo mwanzo wa kukutana naye Yahweh. Nia kuu haikuwa kupata uhuru tokakwa utumwa, lakini pia ilikuwa ni kuingia katika nchi iliiyoahidiwa, Kanaani. Mungualiwaahidi watu wake pumziko hili.b. Hivi ndivyo ilivyo hata kwetu siku ya leo1) Wokovu wetu na kumpokea Yesu kama Mwokozi Bwana na Mwokozi wetu, ni mwamzowa safari. Tuliasi nchi ya uovu na utumwa, lakini sio mwisho wa hadithi; Munguametuwekea mengi katika safari hii ya imani.2) Kama vile waisraeli, Anataka tuingie kwenye pumziko. Katika kifungu hiki maana yaKanaani sio kufa na kuenda mbinguni, lakini inamaanisha tunaweza kuingia katikapumziko la Mungu sasa hivi.2. Vikwazo vya pumzikoa. Kutoamini (Waebrania 3:19)Katika Hesabu 13:33 Mungu alisema enendeni mkaichukue ardhi, wakamjibu kwambahawawezi kwasababu hao ni kama panzi. Badala ya kumfikiria Mungu wao Mkuu, walionapingamizi iliyokuwa mbele yao na matokeo yalikuwa kuzunguka jangwani miaka 40 nahamna hata mmoja kati yao aliingia katika nchi ya ahadi isipokuwa Yoshua na Kalebu nakizazi kipya.b. Mioyo yao migumu naya uasi (3:8)c. Hawakutii (3:18)3. Matokeo ya Maisha yasiyo ya mapumziko ya Ukristo.a. Kuangaika, kutafuta lakini hamna kupata ridhisho la mioyob. Kutoridhika ambayo matokeo yake ni kujifunga kwenye minyororo.c. Ibada ya miungu, vumbi ya kusahau (inayowasababisha watu kusahau dakika chachezilizopita)d. Kuachana na Mungu4. Pumziko NzuriJe, ni pumziko lipi ambalo Mungu anatupa?a. Ni ahadi ya takatifu kwa Wakristo wote.b. Ni pumziko kutoka kwa kujaribu kujipatia wokovu na utakaso. Ni pumziko kutoka kwa haliya kujaribu na kushindwa kila wakati. Kazi ambayo Kristo alifanya msalabani ilikuwakamilifu. Sio kwa ajili ya bidii yet utu. Huu ndio ujumbe mkuu katika kitabu cha Waebrania:Kristo ni mkuu kuliko kuhani waliotajwa katika Agano la Kale na hata dhabihu kwasababu41


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 7Aliinga katika ufalme wa Mungu na kuota dhabihu wakati huo na kwajili ya msamaha wadhambi zote.c. Ni kuwa huru toka kwa mawazo mabaya. Mara nyingi tunasumbuliwa na mabayatunayofanyia watu na matendo hayo hutuibia amani yetu. Wakati mmoja mtu mmojaalilalamika kuwa hangeweza kupata usingizi, kisha mwenzake akamwuliza, “je uliua nani?”Ni kweli kuwa hisia za uovu zaweza kusababisha msukumo na matatizo mengi maishanimwetu. Hata hivyo, Mungu ametupa suluhu kwa jambo kama hili katika Yesu Kristo.Waebrania 10:22 inatueleza…… “sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imanitimilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Kristo na kuwa safi kutokana na dhamirinayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi”d. Kunao uhuru wa kufurahia uwepo wa Mungu. Kwa wana wa Israeli, Kanaani ni mahalaambapo Mungu aliishi na mahali ambapo wangeabudu Mungu kwa uhuru. Mahali ambapowangefurahia uwepo wa Mungu. Kwasababu ni mahali ambapo pamejengwa, lakini niukweli kwamba kwa ujasiri tunaingia katika uwepo wa Mungu, lakini sio kwa ajili yautendaji wetu, lakini kwasababu ya dhabihu ya Kristo. Furaha tunaopokea kanisani ni yetu.Tunaweza kufurahia uwepo wa Mungu Mkuu zaidi kila wakati maishani mwetu.e. Ni uhuru kuongezeka. Kuishi katika baraka za Mungu. Kushuhudia Mungu akitimiza ahadiZake. Hili ndilo lilokuwepo kwa ajili ya Waisraeli. Hatukuumbwa kukaa mahali ambapotumesimama bila kusonga na maisha ya kushindwa. Tumeumbwa ili kuishi katika ushindi.f. Kunao amani katika Mungu. Warumi 5:1, “Kwa hiyo, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwahaki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.”Tamati:Huu ni wito wa kuingia katika pumziko la Mungu. Waebrania 5:1 inatueleza, “leo, kama mkiisikiasauti yake msifanye mioyo yenu migumu, kama mlivyofanya katika uasi, wakati ule wa kujaribiwajangwani. Waebrania 4:inatueleza kwamba, fursa ya kuingia kwenye pumziko lake bado imo wazi.Yesu anasema, “Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, naminitawapumzisha” (Mathayo 11:28). Je, utakuja na kuingia katika pumziko la Mungu leo?Somo limetayarishwa na Kasisi Samantha ChamboKiongozi wa Kundi la MNI Eneo la Afrika42


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea Utakatifu Wiki ya 7Kuabudu: Zaburi 29:1-2Kuabudu Mungu Katika Uzuri wa Kuabudu1. Maana ya kuabudua. Ni kuheshimu kwa mtakatifu Mkuu.b. Ni sifa, utukufu na shukrani kwa Mungu.c. Ni huduma inayofanywa kwa Mungu.d. Kitendo cha kuabudu huanza punde tunapookoka na huendelea hadi milele.1) Ibada haianzi tuingiapo kanisani pekee wala haiishi tunapoomba sala za mwisho(Warumi 12:1-2)2) Zaburi na nyimbo ambazo huimbwa kanisani leo katika ibada yetu, lakini nyimbo zaHallelujah zapatikana katika kitabu cha Ufunuo, nyimbo ambazo tutaimba mbingunimilele na milele.2. Anayepokea Ibadaa. Kati kati ya ibada ya Mkristo, Mungu binafsi yumo.b. Katika ibada tunampa utukufu na sifa.c. Katika ibada, tunajisahau na kujishughulisha Naye.d. Tunastahili kuwa waangalifu wakati wa ibada ili yote tutendayo iwe ni kwa sifa na utukufuwa Jina Lake na wala sio kwetu binafsi.e. Ibada yetu isiwe ni njia ya kujifurahisha binafsi, mfano ni kama Mafarisayo katika Mathayo6:1-5, ama Farisayo katika Luka 18:9-12, lakini kama mfano wa mtoza ushuru katika Luka18:13-143. Uzuri wa Ibadaa. Tumeamriwa katika ibada ya Bwana katika uzuri wa utakatifu (Zaburi 29:2; 96:9)-­‐ Abuduni Mungu katika uzuri wa utakatifu wake.-­‐ Njooni Kwake kama mmevishwab. Utakatifu wake ni kama mavazi ya kuhani katika hekalu za duniani.1) Tamaduni ya kuvaa nguo zetu bora zaidi katika ibada ni nzuri na inafaa kuhimizwa,lakini sheria hii ni kuu kuliko hivi.2) Sare zetu za ibada ni nguo ya wokovu tunayopewa na Mungu binafsi (Isaya 61:10;Ufunuo 7:9-14)3) Sare ni mfano ulioumbwa tena na Mungu. Ni hali ya kufanana na Kristo.c. Wakati Nabii Isaya alikuja kuabudu Bwana hekaluni mavazi yake yalikuwa machafu nanyekundu, lakini alipomlilia katika toba ya dhambi zake, dhambi zake zilioshwa (Isaya1:18, 6:7)d. Mtume Paulo anasema tunafaa kuvua, watu wazee, utu wa kale na kuvaa watu wapya,utu upya (Waefeso 4:20-24; Wakolosai 3:12 – 14)Somo limetayarishwa na Dkt. Enoch H. LitsweleMstaafu Naibu wa Mkurugenzi Mkuu Eneo la Afrika43


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea UtakatifuMafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuMaandiko: Warumi 6: 1-14UtanguliziKuoshwa ili Usiendelee Kutenda DhambiNi vyema kukumbushwa mara kwa mara ni kwanini Yesu alikufa kwa ajili yetu. Tunaporuhusu kifona ufufuko wa Yesu kufanyika jambo la ‘kale na la kawaida’, kunao hatari ya kutochukulia jambo hilikwa uzito. Lazima tuwe waangalifu tusianguke katika mtego wa kufikiria kuwa kwasababu Munguhusamehe kwa haraka tunapotubu, hivi basi tunakuwa haijalishi ni kitu gani tunachofanya maishanimwetu ya kila siku bora tu, tumesamehewa na Mungu kila sika kabla ya kuenda kulala. Yesu alikujakutuweka huru toka kwenya ‘dhambi’ wala so kuweka ‘dhambi’ huru.1. Dhambi husababisha kifoa. Mshahara haujabadilika.1) Mungu aliwaambia Adamu na Hawa kuwa watakufa ikiwa hawatatii maagizo yake.2) Tangu wakati ambao hawakumtii Mungu, walitenganishwa na Mungu.3) Hata leo, dhambi bado hututenganisha na Mungu.b. Sheria za Mungu hazijabadilika1) Kutotii ni dhambi – kutii tamaa za uovu ni kutomtii Mungu.2) Uovu ni dhambi – kushiriki katika matendo ya uovu huonyesha kuasi Mungu na hakiYake.c. Lazima jambo moja life1) tukiendelea kutenda dhambi, mwishowe ni kifo.2) Ikiwa lazima tuishi, basi lazima dhambi ife.2. Kifo cha Kristo hutuweka huru toka kwenye dhambia. Walio katika Kristo sio watumwa wa dhambi.1) Nguvu za Roho Mtakatifu ni kuu kuliko nguvu za dhambi.2) Ufufuko wa Kristo ulivunja nguvu za dhambi juu wale wanaoweka imani yao katikaKristo.b. Kamwe hatutasema kuwa “majaribio yalikuwa mazito mno, hata siwezi kujisaidia’.3. Maisha Mapya ya Kristo hutupa uzima.a. Uzima kweli ni kushirikiana na Mungu1. Tuliumbwa kwa ajili ya kuwa na uhusiano na Mungu.2. Kusudi letu ni kuabudu na kutukuza Mungu katika kila njia maishani mwetu.b. Sisi ni vyombo vya haki ya Mungu1) Maisha yetu ya kila siku yanafaa kuwa shuhuda za neema.2) Uhai wetu wote – mawazo, matendo, maneno – zinafaa kuonyesha utukufu wa Mungu.Tamati:Msamaha huondoa rekodi ya dhambi zetu ili tuanze upya bila dhambi. Kifo na ufufuko wa YesuKristo huosha dhambi zetu ili tuwe huru kuishi maisha matakatifu na safi mbele zake Mungu katikanguvu za Roho Mtakatifu. Sisi tunaojitambulisha na Kristo hatufai kuhusishwa na uovu/dhambi.Badala yake, tunafaa kuwa vyombo vya Mungu vinavyowaelekeza wengine katika huruma yaMungu na katika barabara ya haki. Tunafaa kuwa watumishi wa wokovu kwa ulimwengu wa uovuunaokufa ushuhuda ulio hai wa nguvu na neema za Mungu.44


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea UtakatifuMafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuMaandiko: Mathayo 6:1-44Utangulizi:Kuoshwa Ili Kuyashinda MajaribuJe, ni dhambi kujaribiwa? La siyo! Kitendo chetu baada ya kujaribiwa ndicho huamua ikiwatumetenda dhambi au la. Kuyashinda majaribu ni zoezi la kiroho – kila wakati tunapoyashindamajaribu, tunapata nguvu zaidi katika misuli yetu ya kiroho. Je, hii maanisha kuwa tutakuwa nanguvu zaidi hatutajaribiwa hata kamwe? La, sivyo. Hii ni hatari ambayo tunafaaa kuichukuamaanani – majaribu yanaweza kutujia kwa njia ya ujanja na ikiwa tutakuwa wajeuri na kujichukuliakuwa majaribu hayawezi kutufikia, pengine tutaanguka na kabla ya kujua yaliyotupata tutakuwatumeumia.1. Yesu aliyashinda majaribu kwa utiifu na ufahamu wa maandikoa. Yesu alijabiriwa ili kuyaridhisha mahitaji ya kawaida ya wanaadamu kwa njia isiyo ya kweli.1) Shetani alijaribu kumshawishi Yesu kuwa kuridhisha haja isiyohalali haikuwa jambokweli.2) Yesu alimjibu na kumwambia kuwa utiifu ulikuwa muhimu zaidi kuliko haki.b. Yesu alijaribiwa ili kubadilisha maandiko na kumlazimisha Mungu kumtii Yesu.1) Shetani aliuchukua mstari wa Biblia na kuubadilisha ili ionekane kuwa Yesu angetungasheria ambazo Mungu lazima angetii.2) Yesu aliupinga mtego kwa kuyataja meneno mengine yaliyokuwa katika Biblia.c. Yesu alijabiriwa ili tuone njia nyingine ya mapenzi ya Mungu maishani mwake.1) Shetani alitoa njia tofauti yakuonyesha matokeo yale yale bila kuota malpo ye yote.2) Yesu pia tena alijibu kwa njia na maandiko na utiifu kwa mapenzi ya Mungu kama kitukilichokuwa bora zaidi kufanya.2. Je, sisi pia tunaweza kuyaepuka majaribu kwa utiifu na ufahamu wa Andikoa. Mahitaji yasio faa sio sababu ya kutenda dhambi.1) Mungu hakatai haja yetu ya chakula, mavazi, nyumba na kadhalika.2) Anataka tumpe mahitaji hayo kwake ili atuonyeshe njia iliyo bora.b. Hatuwezi kubadilisha Andiko ili kulazimisha kutotii neno la Mungu1) Wasemaji werevu huwa hawasemi ukweli wakati wote, hasa ikiwa wanasema kilewanachotaka kusema tu.2) Lazima tulisome Andiko ili tujaribu ikiwa maneno haya yanatoka kwa Mungu.c. Sio lazima tujaribu kulitimiza neno la Mungu kwa njia zetu.1) Hatuwezi kuchagua njia iliyo rahisi na kisha tuifikie hatima tuliyowekewa an Mungu.2) Kutotimiza mapenzi ya Mungu kikamilifu ni kupoteza kila kitu.3. Maandiko na Roho Mtakatifu hutupa kila kitu tunachohitaji kujuaa. Lazima tusome ili tusidanganywe.b. Lazima tumtegemee Roho Mtakatifu ili atusaidie kuyashinda majaribu.Tamati:Mungu anatarajia tujifunze kutokana maisha yetu na kumgeukia ili atuongoze wakati hatunauhakika wa barabara tunayofaa kufuata. Yesu hatupi mfano wa kufuata pekee, lakin pia humtumaRoho Mtakatifu atuongoze nguvu za kumshinda mwovu. Hamna jaribio lilonzito hatuwezi kulishinda.Tujitolee kulisoma Neno na kulificha mioyoni mwetu ili tusitende dhambi. Tugeuze mioyo na akilizetu kwa Roho Mtakatifu ili atuongoze katika njia inayompendeza Mungu.45


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea UtakatifuMafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuMaandiko: Yohana 8:1-11Utangulizi:Kuoshwa ili Kuacha Maisha ya DhambiWakati mwingine watoto wa Mungu hushughulikia zaidi kutafuta dhambi maishani mwa Wakristowenzao badala ya jinsi walivyo katika uwajibikaji wa sheria za Mungu. Pengine tunadhani kuwaMungu atatusikiza ikiwa tutajishugulisha zaidi na masuala ya watu wengine, tunadhania kuwaMungu hataona sehemu ya maisha yetu ambayo hatuishi kama inavostahili. Tatizo la hali ni kuwahata ‘dhambi ndogo’ kiasi gani haikubaliki kwake Mungu.1. Je, ni hatari gani za dhambi ambazo Mungu anatutahadharisha kuzihusu?a. Kutenda kitendo ambacho neno la Mungu lakataza1) Kuvunja sheria, kama alivyoshutuma mwanamke kwa kosa la uasherati.2) Kumjaribu Mungu, kama vile viongozi walivyojaribu kufanya kwa kufanya ujanjaYesu.b. Kutotenda kama inavyohitajika kulingana na sheria za Mungu.1) Kutoa haki - Ikiwa nia ya viongozi ilikuwa ni kumtafutia haki, huyo jamaaangeshulishwa katika mashtaka.2) Kuonyesha huruma- Ikiwa wangekuwa wanaudhamini moyo wa mwanamke,kumfedhehesha na kumgonga mawe hazingemfanya afanye toba.2. Je, Yesu anatoa mfano upi?a. Inatukumbusha kwamba Mungu atatumia kiwango chetu cha haki ili kututolea hukumu.1) Lazima tukumbuke kuwa ni neema ya Mungu pekee, ambayo imetuondolea dhambi.2) Lazima tuchunguze mioyo yetu na kuishi ili tusiwe tukiangalia vijito vilivyo kwenyemacho ya wenzetu ilhali kunalo kijito ndani ya jicho let.b. Kadiri tunavyoishi, mapenzi ya Mungu maishani mwetu sio kuhukumu ila ni toba.1) Yesu hakatai kushughulikia dhambi zetu wala kuikubali hali yetu ya uovu.2) Tunapokiri uovu wetu, Yesu hutuhurumia na kutusamehe.3. Je, Yesu anatoa maagizo yapi?a. Enenda na uasi maisha yako ya dhambi.1) Kwanza, Anasamehe na wala hakashifu.2) Kisha anatueleza wazi kuwa msamaha sio liseni kutenda dhambi.b. Kile ambacho Yesu anahamrisha, Yeye huwezesha.1) Kwa sababu Yesu anatuambia tuyaanche maisha ya uovu, tunajua kuwa hililinawezekana.2) Yesu kwa njia ya Roho Mtakatifu, anatuwezesha kuishi maisha matakatifu yasiyo nadhambi.Tamati:Je, kunao dhambi ambayo haujatubu maishani mwako? Je, unatatizwa na siri ya dhambi fulani jinsiunavyoendelea kuitenda? Je, umekuwa ukiwahukumu wengine ukitaka waadhibiwe badala yakutubu? Je, tabia zako kwa watu wengine zinaonyesha kuwa Mungu ni mwenye hasira ambaye niayake ni kuwahukumu watu, ama Mungu mwenye upendo, Ambaye yumo tayari kuhurumia nakusamehe? Hatutaki kujifanya kuwa dhambi haimo. Lakini tunataka kuishi Injili inayohurumia naambayo huonyesha kuwa dhambi sio bwana. Yesu anatuagiza tuasi maisha ya dhambi nakutembea naye katika Utakatifu. Roho wake mtakatifu anawezesha maisha haya anapoosha mioyoyetu kwa imani.46


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea UtakatifuMafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuMaandiko: 2 Samweli 11:2-5; Mathayo 5:27-30Utangulizi:Kuoshwa Ili Kuyadhibiti Mawazo YetuJe, unaweza kusoma Biblia na kisha kuendelea kudhania kuwa dhambi haimjalishi Mungu. Penginetutajishawishi hivi ikiwa tutaendelea kutimiza huduma yetu kwa Mungu, tunachofanya katika maishayetu binafsi haijalishi, lakini pia tunajidanganya. Mungu anataka tuwe tumejitolea Kwake 100% hatakatika mambo yaliyo duni zaidi maishani mwetu, yakiwemo mawazo yetu, starehe zetu, na hatandoto zetu. Hamna kiti kidogo ambacho hakiwezi kumridhisha.1. Hatutendi dhambi kwa makosa.a. Majaribio yataweza kujiwalisha kwa njia inayopendeza.1) Majaribio huwa katika mambo tunayopendelea.2) Huonyesha njia za kutimiza mahitaji yetu.3) Majaribio yatavutia lakini hayatulazimishi kutenda dhambi.b. Majaribio huwa dhambi kwetu tunapoijongelea.1) Wakati badala ya kuchungulia, tunaangalia – mfano ni kisa cha Daudi na Bethsheba.2) Tunapotenda – tunapoishi katika majaribio na kuanzi kufikiria njia za kufanya kileunachopewa.3) Tunapokataa kugeuka na kuchagua kukaa katika majaribio ama hali zinazotatanisha –kama Daudi angegeuka, pengine hangetenda dhambi.2. Sisi kuwa wasafi sio kwa bahatia. Wakristo lazima wachague njia inayofaa kila wafanyapo uchaguzi wo wote.1) Tunafaa kuchagua kuwa na kiasi kila tunapojaribiwa kwa njia ya mahitaji ya utu wetuwa kibinadamu na katika njia za uovu.2) Tunapojipata katika hali zinazotatanisha, lazima tuchague kuondoka.3) Lazima tuchague utakatifu badala ya uovub. Mungu hatarajii tuwe watakatifu kwa njia ya nguvu zetu.1) Yeye hutupa nguvu za Roho Mtakatifu ili zituondolee tamaa za dhambi.2) Tunapokataa kukaa katika dhana za majaribio, tumechagua njia ya utakatifu.3) Mungu hatulazimishi kukubali na kutii Roho Mtaktifu – sisi wenyewe tunao uhuru wakuchagua.3. Mawazo yetu ndiyo njia ya dhambi ama utakatifua. Tunapoyaruhusu mawazo yetu yaishi katika majaribio, tumechagua njia ya uovu.b. Tunapokataa kukaa katika mawazo ya majaribio, tumechagua njia ya utakatifu.c. Tunapomkataa shetani na majaribio yake, atatoroka na kuondoka kwetu, nasi tutakuawenye nguvu zaidi.Tamati:Njia pekee ya kupata misuli ya kiroho yenye nguvu ni wakati tunapofanya mazoezi. Tunafanyamazoezi kwa kukataa majaribu na kukataa dhambi. Mazoezi mengine ni katika kufuata njia zautakatifu. Njia moja bora zaidi za utakatifu ni kuruhusu Roho Mtakatifu aoshe mioyo yetu nakuyaelekeza mawazo yetu. Amri ya Mungu kwetu. Anatuwezesha kutenda. Ametuamuru kuishimaisha masafi ya matakatifu. Roho Mtakatifu huyafanya maisha haya kuwa masafi iwezekanavyo.47


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea UtakatifuMafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuKuoshwa ili Kubaki WaaminifuMaandiko: Danieli 6Tunapogundua kuwa utakatifu ulikuwemo hata katika Agano la kale, kabla ya uwepo wa RohoMtakatifu lazima pia tutambue kuwa utakatifu ni jambo liliopo kwa watu wote wanaomfuata Mungu.Rangi ya ngozi ya Danieli na dini zilikuwa ni tofauti na zile za nchi ya utumwa. Lakini Danieli alikuwana kitu kimoja kizuri maishani mwake ambacho kilifanya matatizo yake yasionekane kuwa magumukwake – alikuwa na uhusiano wa kipekee na Mungu wa ulimwengu. Uaminifu wa Danieli kwaMungu ulionyesha tabia yake ya uadilifu na aliinuliwa na kuteuliwa kuwa kiongozi mkuu katikaufalme hata kama kulikuwa na mambo mengi yaliyokuwa dhidi yake.1. Watu wa Mungu wanafaa kuwa na tabia za uadilifu.a. Danieli alijitofautisha binafsi hata aliteuliwa katika cheo kikuu cha uongozi serikalini ya nchiya ugeni.1) Mfalme alifahamu kuwa Danieli hangeaminika ili kuhakikisha kwamba mfalamehangepata hasara ye yote.2) Hata adui zake walifahamu kuwa njia ya pekee kutoa mashtaka dhidi yake ilikuwa nikupitia kwa uaminifu wake kwa Mungu.b. Je, tabia ya watu wa Mungu ni ipi leo?1) Je, utaaminika katika kutekeleza zoezi lo lote leo – hata kwa ajili ya adui zako pasipokususia ama ufisadi?2) Je, wewe ni mwaminifu kiasi kwamba adui zako wanajui hawawezi kukutoleamashtaka dhidi yako pasipo kugusa uhusiano wao na Mungu?2. Watu wa Mungu wanapaswa kukaa waaminfu kwake hata ikiwa wamo kati ya vita.a. Ibada inafaa kuwa suala muhumu maishani mwetu, pasipo kujali mambo mengineyanayotuzingira.1) Danieli aliendelea kuomba na kuabudu Mungu hata wakati sheria ilionyesha kuwatendo hili lingemgharimu maisha yake.2) Ingawa sheria ilikuwa imepitishwa baada ya muda wa siku 30, Danieli hakuhairishaibada yake, na kujiambia kuwa Mungu ataelewa jinsi mambo yalivyo.b. Je, ibada inayo sehemu gani maishani mwetu?1) Je, ni sehemu gani ya mda wako unayotumia na Mungu kila siku katika kusoma Bibliana kuomba?2) Je, unaruhusu nini maishani mwako ambacho kitakuzuia kushiriki na Wakristo wenginekatika ibada. (Jumapili ama kati kati mwa juma)Tamati:Imani ya Danieli wakati wa majaribio ilikuwa ni mfano mkuu kwetu. Lakini hali yetu ni afadhali kulikoyake. Sio kwamba tunaye Yesu pekee kama mfano, tunao uwepo wa Roho Mtakatifu wa kila sikuambao ni chanzo cha nguvu zetu. Tunaweza kuyafanya mambo makuu hata kuliko Danieli – imaniyetu ni mwamba imara wakati wa matatizo. Roho Mtakatifu anapotuosha, Yeye huondoa ubinafsi namajivuno ili tusimame imara na waaminifu katika Mungu bila kujali matokeo ye yote. Tumeoshwa ilitukae waaminifu bila kujali hali ama maadui.48


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea UtakatifuMafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuMaandiko: Mathayo 26: 14-16, 27:1-10Utangulizi:Kuoshwa Ili Usiwe Na TamaaKwa kiwango fulani, sisi sote huja kwake Yesu Kristo kwa nia ya ubinafsi – hatutaki kuendajehanamu, tunataka msamaha, tunataka kuondolewa mashtaka na kadhalika. Hizi tamaa zafaakuondolewa na mahala pake kuchukuliwa na kutaka kuabudu na kumtumikia Mungu kwasababu yaJinsi alivyo. Hata hivyo, baadhi ya watu wanataka uhusiano na Yesu, ili waweze kufaidi kutokanana uhusiano huu. Wahubiri wanaoahidi “utajiri”, afya nzuri, na mafanikio kwa kawaida shirika laohukua kwa haraka. Ilikuwa vivyo hivyo siku za Yesu – wengi walifuata kwa vile walifurahia miujizana mafundisho yake, lakini hawakutaka uhusiano na Yesu ambao utawabadilisha. Watu wengi hatana wanafunzi wake 12 walitarajia Yesu awarejeshee utukufu wa ufalme wa Daudi katika Israeli.Ilivyobainika kuwa hii haikuwa nia ya Yesu, wengi walichanganyikiwa na kumuasi Yesu. YudaIskarioti alikuwa mmoja wao.1. Uwe mwangalifu na nia ya ulafia. Hatufai kumfuata Yesu kwa tamaa ya faida yetu binafsi.1. Faida hugeuka na kuwa ‘miungu’ yetu badala ya Yesu.2. Tusiabudu miungu mingine.b. Hatufai kumfuata Yesu kwa tamaa ya kupata mamlaka ama kutambuliwa1. Yesu sio kifaa ama silaha ya kutumia wakati tunahataji kuwashinda watu wengine.2. Yesu hakufa ili tuweze kuhuisha ulafi zetu za kutambuliwa.c. Tunapojaribu kugeuza mapenzi ya Mungu ili yawe kama tutakavyo, basi tutaudhika mno.2. Ulafi husababisha usalitia. Tunaporuhusu ulafi maishani mwetu, uaminifu wetu kwa Yesu Kristo unaondolewa.1. Itakuwa rahisi kwetu kutetea tamaa zetu.2. Kupea kipao mbele kwa mtu ama jambo fulani ni usaliti kwa dhabihu ya Yesuinayorejesha uhusiano wetu na Mungu.b. Wakati uhusiano wetu na Mungu umeyeyuka, kujitolea kwetu kwake kunakuwa ni dhaifu.1) Tunajidanganya kwa kuamini kuwa tunaweza kutumikia Mungu na pesa (tazamaMathayo 6:24)2) Tunaanza kujihalalisha mbele zake Mungu, kwa kujaribu kumshawishi kuwa tunastahilikupata vitu fulani wa fulani na hivyo mahitaji na matendo yetu ni mema na yanakubalika.3. Roho Mtakatifu hutusafisha tamaa zetu za ubinafsi.a. Roho Mtakatifu anatusafisha ubinafsi wetu, kwahivyo njia pekee ambayo mbegu hiiinaweza kukua ni ikiwa mbegu hii ya tamaa itatia mizizi na kukua.b. Roho Mtakatifu atangoa kutoka kwa utu wetu tamaa na ubinafsi zitakapojaribu kumea.Tamati:Wale ambao Kristo ameweka huru, ni huru kamili. Sisi tuko huru kutokana na tamaa na ubinafsi.Roho Mtakatifu husafisha mioyo yetu, ili kila wakati tuwe na motisha ya kuhakikisha kuwa tamaa namatendo yetu yanaambatana na utukufu wa Mungu na wema wa Ufalme Wake.49


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea UtakatifuMafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuMaandiko: Mwanzo 42, 45:3-7Utangulizi:Kuoshwa Ili Usamehe Na UsahauWatu wa Afrika wamepitia matatizo mengi mikononi mwa watu mbali mbali miaka ya kale –waliowadhulumu pengine ilikuwa ni majirani toka kabila zingine, pengine toka nchi ama taifa jirani.Vivyo hivyo, Wana wa Israeli, wateule wa Mungu, walidhulumiwa miaka mingi. Leo tunasomahadithi ya Yusufu, mtu mmoja ambaye aliteswa sana na nduguze, kisha wakamwuza katikautumwa. Mambo mabaya ambayo hayawezi kuwamehewa huwafanyikia watu wa Mungu. Je watuwa Mungu wanafaa kuishi aje katika hali kama hizi?1) Tusiyakubali matukio ya kale ama ya sasa kutuweka mbali na Mungua. Hata kama mtumwa katika nchi ya ugeni, Yusufu alidumisha uhusiano wake na Mungu.1) Ingawa hali yake ilikuwa chungu mno, Yusufu aliamini Mungu atamlinda.2) Yusufu alipokea hekima toka kwa Mungu ambayo ilimpa fursa ya kuteuliwa katika cheokikuu ili kumtumikia Mungu.b. Je, wewe ni mtumwa wa matukio ya kale ama sasa maishani mwako?1) Je, wewe hujipata unayafikiria makosa ambayo ulitenda kale ama mambo ambayo watuwamekusema ama kukufanyia?2) Je, umejawa na hasira ama tamaa ya kulipisha kisasi kiwango kwamba umejizuiakupokea uwepo wa Mungu maishani mwako?2) Msamaha ni utu wa kiungu, kwahivyo uhusiano wetu Naye unaonekana katika uhusianowetu na watu wengine.a. Lazima tuwashawishi watu wengine watubu ili wapokee msamaha.1) Yusufu aliwajaribu nduguze, alitaka kujua ikiwa walikuwa wametubu na kubadilishanjia zao.2) Hata ikiwa tumetendewa ubaya, dhambi kuu ni dhidi Yake Mungu.b. Palipo ama pasipo toba, lazima tusamehe.1. Kukataa kusamehe hutuumiza kuliko watu wengine.2. Msamaha hutuweka huru kutoka kwa ufungwa wa makosa ya kale.3. Roho Mtakatifu anapotusafisha mioyo, tunakuwa huru kusamehea. Tuutazamie msaada wa Kristo wa kuishi vyema.1) Tunatambua kiwango cha dhambi zetu na msamaha tuliopokea.2) Tunakiri kuwa Mungu ni mwaminifu, Yeye hutoa haki kwa wakati Wake.b. Roho Mtakatifu huwezesha lile ambalo linaonekana haliwezekani.1) Kile ambacho hutewezi kusamehe kwa uwezo wetu, Anatuwezesha kusamehe.2) Wale ambao hatuwezi kupenda kwa nguvu zetu, Yeye huwapenda kwa njia yetu.Tamati:Jambo moja linalotofautisha watu wa Mungu na ulimwengu inafaa kuwa ni kiwango cha msamaha.Upendo, neema na nguvu za Roho Mtakatifu zimo ili zitusaidie katika msamaha, ikiwa tu tutakubali.Isiwe hata mara moja kuwa itasemekana kuwa watu wa Mungu hawataki kusamehe, lakini tunafaakuwa shahidi walio hai kwa ajili ya msamaha wa Mungu katika Kristo Yesu kwa kuwasamehewaliotukosea. Hatuwezi kwa nguvu zetu, lakini tunafaa kuishi kama walioshwa na Roho Mtakatifu ilikusamehe makosa tuliosamehewa.50


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea UtakatifuMafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuMaandiko: Marko 10:17-31Utangulizi:Njaa Na Kiu Ya Uzima Wa MileleBaadhi ya maswali muhimu katika Biblia ni: “Nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?” (Marko10:17): “Tutendeje, ndugu zetu nipate kuokoka? (Matendo Mitume 2:37): “Bwana zangu, yanipasanifanye nini nipate kuokoka? (Matendo ya Mitume 16:30).Maswali haya yanatuonyesha ni nani aliye na njaa na kiu cha wokovu. Biblia inasema: “Heri wenyenjaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa” (Mathayo 5:6). Hapa tunamwona mtu tajiri na swalikuu akitafuta jibu.1. Njaa yake Kuu na Kiu ya Uzima wa Milelea. Pengine anaweza kufikiria kwamba alikuwa na njaa ya elimu.b. Alijaribu kutafuta kushibishwa kupitia dini; alifuata sheria (Marko 10:20).c. Alijaribu kuhuisha kiu yake kwa kupata cheo kikuu – Kiongozi (Luka 18:18). Penginealikuwa alikuwa mkurugenzi mkuu sinagogi, mwalimu na/au mshirika wa Baraza (Yohana3:1-2).d. Alijaribu utajiri (Marko 10:22)e. Kama mwalimu mkuu wa mhubiri aliyejaribu kuhuisha kiu kwa mali ya ulimwengu, baadayealigundua kuwa kila kitu ni ubatili ni mtupu (Mhubiri 1:2)(Maelezo)2. Kukutana kwake na Yesu kwa hali Kuu, Uzima wa milelea. Mwishowe alielewa kuwa hitaji lake kuu lilikuwa uzima wa milele, haja ambayo hata pesahaziwezi zikanunua.b. Alifahamu kuwa Yesu pekee ndiye awezaye kumwokoa (Yohana 14:6)c. Aliona kiu na njaa hata akasahau cheo chake na kunyenyekea mbele zake Yesu. (Marko10:17, 2 Mambo ya Nyakati 7:14)d. Aliona kiu na njaa hata akamkimbilia Yesu (Yohana 10:17)e. Alimjia Yesu na kumwuliza swali nzuri mno.- Aliambiwa atimize sheria kwasababu hili lilikuwa ni tatizo ngumu mno.- Alikuwa amevunja sheria ya kwanza – utajiri wake ulikuwa miungu yake.- Alivunja sheria ya pili – hakuwapenda majirani zake maskini. (Mathayo 19:19)f. Yesu alimpenda (Marko 10:21)g. Alihitaji kitu kimoja tu – uzima wa milele – na wala vitu vyote alivyokuwa navyo.3. Kukataa kwake kwa hali ya juu kwa Kumkubali Yesu, Uzima wa Milelea. Alikataa kuasi vitu ambavyo vilimfanya aisi njaa na kuona kiu.b. Alikataa utajiri wa mbinguni na badala yake kupokea utajiri wa dunia.c. Alikataa mwaliko wa kumfuata Yesu.d. Aliinamisha uso wake, kwa huzuni akaondoka mahali Yesu alipokuwa.e. Alimjia Yesu kwasababu ya tatizo moja lakini alipokuwa akiondoka matatizo yakeyaliongezeka.f. Alitembelea utajiri wa mbinguni lakini akataa kuingi ndani.g. Alipomjia Yesu, alikuwa akielekea mbinguni, lakini alipoondoka alikuwa akielekea kwenyeangamizo la milele.Tamati:Kijana alipoondoka, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “je, ni vigumu je kwa tajiri kuingia katikaufalme wa Mungu” (Luka 10:23). Sasa anakutazama, anaona hitaji lako na kusikia maswali mengikutoka moyoni mwako. Anapokutazama, Anakupenda kama alivyompenda yule kijana maskinimiaka 2000 iliyopita. Umesimama mlangoni mwa mbinguni lakini na unahitaji kuingia mlangoni52


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea UtakatifuMafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuWatu wa Mungu Wageuka na Kuasi Njia Zao MbayaMaandiko: 2 Mambo Ya Nyakati 7:14Utangulizi:Kichwa cha ujumbe huu hakiambatani na tamaduni zetu za utakatifu – watu wa Mungu wageuka nakuasi njia zao mbovu.Kulingana na mawazo yetu, watu wasio na uungu na wasioamini Mungu ndio hugeuka na kuasidhambi na uovu. Hata hivyo, masomo yetu ya maandiko yanatuonyesha wazi kuwa Watu waMungu hawamo juu ya dhambi, na ikiwa watatenda dhambi wanafaa kunyenyekea na kutubudhambi zao.1. Watu wa Mungu sio Watu Waovua. Wameokolewa toka kwa uovu wao.b. Wamesamehewa na kuagizwa watende dhambi tena (Yohana 8:11)c. Hawaendelei kutenda dhambi kwasababu wamekufa katika dhambi (Warumi 8:11)d. Wamewekwa huru kutoka kwa sheria ya dhambi na kifo (Warumi 8)e. Kupitia kwa neema ya Mungu, wanaweza kukataa uovu.(Tito 2:11-122. Watu wa Mungu wanaweza kuchagua kutenda dhambi.a. Adamu na Hawa walikuwa watu wa Mungu walioumbwa katika mfano wa Mungu.Hawakuwa na alama zo zote za dhambi lakini walianguka toka kwenye neema.Walianguka toka hali bora ya Uadamu.b. Dhambi ya watu wa Mungu, wanaojiita kwa jina Lake, humwumiza Mungu zaidi kulikodhambi ya mpagani. Haya ni kweli katika Agano la Kale, Agano mpya na katika kanisa letuleo.c. Uovu wa watu wa Mungu huzuia baraka zitokazo kwa mbinguni.3. Watu wa Mungu husamehewa wanapotubu na kuasi dhambia. Sauli na Daudi walikuwa watu wa Mungu na wote walitenda dhambi. Dhambi ya Sauliilikuwa kutotii nay a Daudi ilikuwa mauaji na uasherati. Sauli alikataa kutubu lakini Daudialitubu.b. Isaya alikuwa nabii wa Mungu lakini alikuwa alitenda uovu. Alipohukumiwa kwa ajili yadhambi zake, alinyenyekea na kutubu. (Isaya 6).c. Petro na Yuda Iskarioti walikuwa watu wa Mungu na wote walitenda dhambi. Wotewalishurutishwa kwa ajili ya dhambi zao. Yuda alikataa kutubu na kujinyonga (Mathayo 27:3-5). Petro alinyenyekea na kuomba msamaha (Luka 22:60-62).d. Hatufai kutenda dhambi, lakini tukitenda dhambi, tunaye Kristo, anayeosha dhambi zetu.e. 1 Yohana 1:9 ni kwa watoto wa Mungu na wala sio wapagani.Somo limetayarishwa na Dkt. Enoch H.LitsweleMstaafu Naibu wa Mkurugenzi Mkuu Eneo la Afrika54


Mpangilio wa Mafunzo ya Kusheherekea UtakatifuMafundisho ya ziada: Kuoshwa Na Roho MtakatifuMaandiko: 2 Wafalme 5:1-19Dhambi, Tatizo la KiubinadamuMara nyingi tunawaona watu wenye maradhi mbali mbali, baadhi ni nyingi kuliko zingine. Naamanialikuwa na maradhi yaliyohitaji msaada. Ingawa alionekana kama mtu mwenye mafanikio maishanimachano mwa wanadamu na mfalme alimpenda, Alikuwa na tatizo.1. Dhambi ni mbayaa. Ukoma ni maradhi mabaya yasipotibiwa, hivyo ndivyo dhambi ilivyo; inaweza kuangamizamaisha ya mtu.b. Moyo utendao dhambi hufa (Ezekieli 18:20)2. Dhambi ni ambukizia. Wenye ukoma kama Naamani walitengwa na pia walivaa kengele shingoni mwao iliwanapokaribia wawapatie onyo kuwa wanakuja ili waondokewe. Kama jinsi ukoma ulivyo,dhambi pia inao msukumo mkuu.b. Watu tunaokaa nao mda mrefu wanao ushawishi kwetu. “Bshirika na watu wabaya huaributabia njema (1 Wakorintho 15:33)3. Dhambi ina tibaa. Kasisi huchunguza ngozi ya mtu mwenye ukoma ama mtu ye yote mgonjwa na kutoamatokeo ya uchunguzi wake ikiwa ni mgonjwa ama la. Kwa hivyo leo, kwasababu Kristoametuosha kutoka kwenye dhambi, kila Mkristo, “mteule wa Mungu, kuhani mkuu, taifatakafitu (1 Peter 1:9), anafaa kuona dhambi maishani mwao punde tu wanapoitambua.b. Naamani alizijua habari za nabii kupitia kwa mjakazi wake aliyetoka Samaria. Alipotiimaagizo ya Elisha ya kuoga, ndipo alipona.c. Katika Warumi 7:24-25, Paulo anasema, “Ole wangu, mimi maskini! Ninani atakayeniokoana mwili huu wa mauti? Ashukuruwe Mungu kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu!d. Tumeoshwa kwa damu ya Yesu. “Lakini tukienda nuruni, kama Yeye alivyo nuru,twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Yesu, Mwana wake yatusafisha dhambi yote.(1 Yohana 1:7)Tamati:Duniani watu wengi wanatenda mema na kupendwa na binadamu, lakini mioyoni mwao kunadhambi ijuliakanayo kama dhambi. Dhambi ni mbaya, huambukizwa na hata inaua, lakini inawezakuoshwa kwa Damu ya Yesu Kristo, mwana kondoo wa Mungu.“Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! (Yohana 1:29)Je, umeoshwa kwa damu ya kondoo? Unaweza kuoshwa sasa na kuwekwa huru kuishi maisha yaushindi katika Kristo.Kasisi Kenneth PhiriRaisi wa Kundi la vijana, Eneo la Afrika55

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!