46:1-51:64 UJUMBE KWA MATAIFA YA KIGENI
46:1-51:64 UJUMBE KWA MATAIFA YA KIGENI
46:1-51:64 UJUMBE KWA MATAIFA YA KIGENI
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Kwa kuwa hapo awali Wamoabi hawakuchukuliwa kifungoni, wanafananishwa na divai iliyoweza kukaa katika

chombo chake tangu mwanzo bila kukorogwa. Lakini wakati huo, kwa kuwa watachukuliwa kifungoni Babeli,

wanafananishwa na divai inayomiminwa kutoka chombo chake (11-12). Watu watapotewa na matumaini yao katika

mungu wao wa kitaifa aliyeonekana kuwa hana uwezo wa kuwaokoa (13). Askari mashujaa wa Moabu watauawa

katika mauaji ya kutisha sana, na maombolezo makubwa yatakuwepo juu ya taifa lililopondwa na kuangamia (14-17).

Watu wa sehemu zote za Moabu watashtuka wakisikia habari za kuangamia kwa majeshi yao. Taifa lililojivuna

kwa kiburi chake litaaibishwa (18-20), na taifa lenye nguvu sana litapondwa, hukumu ya Mungu inapoenea kutoka mji

mmoja wa Moabu hadi mwingine (21-25).

Watu wale wa Moabu ambao awali waliwadharau na kuwadhihaki Waisraeli na Wayuda, wakati huo wenyewe

wataaibishwa na kudhihakiwa. Watakunywa ghadhabu ya Mungu mpaka watakapolewa na kutapika (26-27). Wamoabi

waliokuwa na kiburi na kuwadharau watu wengine, wakati huo watalazimishwa kukimbia katika aibu na kutafuta

maficho katika mapango na mashimo milimani (28-30). Lakini sasa Yeremia anawaonea huruma anapoona mamlaka

yao yaliyoenea sana yamevunjwa, mavuno yao mashambani na mizabibu vimeharibiwa, na nchi yao yote imechafuliwa

(31-36). Watu hujinyoa nywele na ndevu zao wakijikata kata na kuvaa nguo za magunia kama alama ya maombolezo,

lakini wamechelewa. Taifa la Moabu limekwisha. Limefanana na chombo kilichovunjika na kutupwa jalalani (37-39).

Katika maelezo ya mwisho ya maangamizi, nabii anatoa mfano wa Wababeli wanaoshuka juu ya Moabu kama vile

tai anavyoshuka juu ya mateka yake. Hakuna atakayeweza kutoroka (40-43). Mahali po pote wanapojaribu kukimbilia

hakuna usalama kwa watu wanaoadhibiwa na Mungu (44). Miji ya maana katika Moabu itateketezwa kwa moto na

wenyeji wake watachukuliwa kifungoni (45-46; taz.Hes 21:28-29). Lakini Mungu kwa neema yake, hata katika Moabu

atawahifadhi watu wachache watakaosalia (47).

Ujumbe kuhusu Amoni (49:1-6)

Kama vile taifa la udugu wake Moabu, Amoni lilikuwa jamaa wa mbali wa taifa la Yuda. (Moabu na Amoni

walikuwa wana wa Lutu, na Wayuda walitokana na baba mkubwa wa Lutu, Ibrahimu; taz.Mwa 12:5; 19:36-38.)

Waamoni na Wamoabi waliishi katika sehemu za nyanda za nchi ya mashariki ya Yordani. Maana yake ni kwamba,

walikuwa majirani kabisa wa Yuda na Israeli upande wa mashariki.

Karne moja hivi kabla ya wakati wa Yeremia, Waashuri walikuwa wameteka ufalme wa kaskazini wa Israeli na

kuwapeleka watu wake kifungoni (2Fal 15:29; 17:6). Inavyoonekana, Waamoni, wakati ule walichukua nafasi ya

kujitwalia eneo la kabila la Gadi, yaani kabila la Israeli lililoishi mpakani. Lakini Waamoni walisahau kwamba

Waisraeli bado waliendelea kuwa watu wa Mungu. Yeremia anawaambia Waamoni kwamba nchi yao itatekwa na mji

wake mkuu, Raba, utabomolewa. Wakati huo Waisraeli watatwaa upya nchi yao wenyewe (49:1-2. Malkamu (au

Moleki) alikuwa mungu wa kitaifa wa Amoni).

Waamoni walijivunia utajiri waliojipatia, na hivyo walifikiri wako salama wala hawawezi kushambuliwa. Yeremia

anawaambia kwamba utajiri wa mali hauwezi kuwaokoa maadui wanaposhambulia. Watapelekwa kifungoni (3-5),

ingawa baada ya muda watu wachache watakaosalia watarudi tena (6).

Ujumbe kuhusu Edomu (49:7-22)

Waedomu, ambao ni wazao wa Esau, walijivuna kwamba wao walikuwa werevu kuliko mataifa ya jirani zao.

Walitumaini kwamba nchi yao ilikuwa salama wala haikuweza kutekwa, kwa sababu milima mirefu ya mipakani

mwake ilitoa nafasi nzuri sanaya kujitetea. Nabii anawaambia kwamba, si hekima wala silaha na nguvu ya kujitetea

vitaweza kuwaokoa na maafa na maangamizi ambayo Mungu aliwapangia (7-8).

Mkulima wa mizabibu huchuma zabibu zilizoiva na kuziacha zisizoiva bado; mwizi avunjaye nyumba huiba vitu

vile tu anavyovitaka na kuviacha vingine katika nyumba, lakini uharibifu wa maadui juu ya Edomu utakuwa kamili.

Hata watu wale watakaojificha katika mapango ya milimani hawataepukana na maafa hayo (9-10). Lakini Mungu

atawaangalia wale watakaokuwa yatima au wajane kutokana na vita vile (11).

Iwapo watu wasiostahili sana ghadhabu ya Mungu wanapaswa kuvumilia adhabu yake, sembuse watu waovu kama

Waedomu. Wataadhibiwa vikali zaidi. Mungu anawahakikishia kwamba miji yao iliyoendelea na kujivuna juu yake,

itaachwa magofu na kuwa mahali pa kutisha (12-13).

Waedomu walijidanganya walipofikiri kwamba, kwa sababu ya ngome zao za kujitetea walizoziweka sehemu

nyingi milimani hawakuweza kushindwa na maadui. Yeremia anawaonya kwamba, haidhum wamekwea milima mirefu

mpaka juu au walijenga ngome imara sana, hakuna kitu kitakachowaokoa na hukumu ijayo (14-16).

Kuangamizwa kwao kutakuwa moja kwa moja. Kama vile Sodoma na Gomora, Edomu itaachwa ukiwa (17-18).

Kama vile simba atokavyo msituni na kushambulia kundi la kondoo, ndivyo maadui watakavyokuja na kuangamiza

Edomu. Hakuna atakayeweza kujitetea dhidi ya jeshi ambalo Mungu atalichagua ili litekeleze hukumu yake (19-20).

Askari wa Edomu hawatakuwa na nguvu dhidi ya washambulizi. Kilio cha Waedomu kitasikika mbali sana kupita