12.12.2012 Views

13. NABII YONA

13. NABII YONA

13. NABII YONA

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

13. NABII YONA

''Ndipo watu wa Ninawi wakamwamini Mungu''

Shabaha

Kuonyesha jinsi rehema ya Mungu ambavyo hata watu wa mataifa walipewa. Nabii Yona

alitabiri katika Israeli baada ya kufa kwa Elisha.Katika siku zake Mungu aliwatia Israeli katika

mikono ya maadui zao wa kaskazini, lakini Yona alifahamu kuwa mpaka watu watubu na

waache njia zao za uovu na wamgeukie Mungu, maana Mungu asinge wavumilia

milele.Angewaadhibu kwa kuyaleta mataifa makubwa na yenye nguvu kuwaipiga na

kuwateka na kuwafukuza katika nchi yao(Soma Kumbu kumbu la Torati 28:15,25). Na Yona

mwenyewe pia alipata somo la kujifunza kuhusu rehema ya Mungu.

Yona 1-3

YONA ANAMWASI MUNGU: Yona1:1-3

Neno la Mungu lilimjia Yona likiwa na agizo la ajabu: “Ondoka, uende Ninawi, mji ule

mkubwa, ukapige kelele juu yake, kwa maana uovu wao umepnda juu mbele zangu”

(mstari 2).

Mungu angewapatia watu wa Ninawi siku 40 za kutubu la wasipotubu angewaangamiza

(mstari 3-4). Ninawi ulikuwa ni mji mkuu wa Ashuru, lilikuwa ni taifa ambalo lilikuwa hodari

kwa vita na wakatili sana na Israeli waliwaogopa sana kuliko mataifa mengine.

Yona aliwapenda sana watu wa taifa lake na aliutumia muda wake kuwafundisha jinsi ya

kumwabudu Mungu wao, ili Mungu aweze kuwabaliki. Hakuweza kuelewa nini Mungu alipatie

taifa ambalo ni adui mkubwa na katili kwa Israeli nafasi ya kuokoka kutoka katika adhabu

ambayo kwa hakika walistahili.

Alihofia kuwa watatubu na Mungu angewatumia kuiadhibu Israeli.

Kwa hiyo Yona aliamua kujichukulia maumuzi mikononi mwake.Akaona njia ya peke ili

wasipone, ni yeye kwenda mbali kabisa na Ninawi, wasingeweza kusikia ujumbe wa Mungu

unaowaita ili watubu na kwa hiyo wangeangamizwa. Alijua vizuri sana ubaya wa kutokumtii

Mungu, lakini alikuwa tayari amekubali afe yeye ili aokoe maisha ya watu wake.

Alikwenda moja kwa moja mpaka bandari Yopa na huko alipata pumziko la maumivu ya

moyoni mwake, meli iliyokuwa ikienda Tarshishi, nchi kavu ambayo ilikuwa mbali sana kwa

upande wa magharibi. Alilipa nauli yake na akapanda meli.

MUNGU ANATUMA WIMBI KUBWA: Yona 1:4-7

Ndipo meli ikawekwa tayari uelekeo wake na safari ikaanza.Kwa muda mfupi ilionekana

kana kwamba Yona ameepuka jukumu la kuwahubiri watu wa Ninawi. Hata hivyo, Mungu, ni

mkweli katika neno lake na anayaona yote yanayotendeka. Hapana hata moja ambalo

limefichika machoni pake asilione. Neno analolisema Mungu ni lazima lifanyike hakuna mtu

awezaye kubadilisha mpango wake (Isaya 55:10-11).

Haukupita muda mrefu Mungu alituma wimbi kubwa baharini.Wimbi la tufani kubwa

lililotishia kuivunja meli. Mabaharia wakajawa na hofu wakaanza kuililia miugu yao ili iwaokoe.

(Hii miungu ilikuwa ni sanamu tu na kamwe isingeweza kuwasaidia). Waipunguza shehena

kwa kuitupa mizigo yao baharini ili kupunguza uzito wake.

Yona alikuwa upande chini wa meli, alikuwa amelala. Nahodha wa meli alimkuta huko

akamwamsha. Akamwambia, “Una nini ewe ulalaye usingiziamka; ukamwombe Mungu

wako, labda Mungu huyo atatukumbuka tusipotee” (mstari 6).

Na kila mmoja ndani ya ile meli aliamini kuwa wimbi lile la tufani ya kutisha ni adhabu

ambayo imetoka kwa Mungu. Kwa walipiga kura wajue ni nani aliyesababisha hilo ili

alaumiwe yeye, “nayo kura ikamwangukia Yona” (mstari 7).

Wote wakaanza kumwuliza: “Kazi yako ni kazi gani? nawe umetoka wapi? nchi yako

ni nchi ipi? nawe u mtu wa kabila gani?” (mstari 8).

Ni hapo sasa Yona alipoamka kabisa. Mawimbi hayakumhofisha Yona, maana

aliwaambia, “Nami namcha BWANA, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi

kavu” ( mstari 9). Alikiri kuwa alikuwa amejaribu kuutoroka uso wa BWANA na watu wale

wakaogopa mno walipotambua nguvu za Mungu ambaye Yona alimwabudu. Ni lazima jambo

fulani litendeke, maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka na tufani ikiongezeka zaidi.Basi

wakamwuliza, “Basi tukutende nini, ili bahari itutulilie?” ( mstari 11). Naye akawajibu,

“Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itawatulilia; kwa maana ninajua ya kuwa ni

kwa ajili yangu tufani hii imewapata” (mstari 12).

Na ingawa watu walikuwa na nia na hofu ya kutaka kuokoa maisha yao, wazo hili la

kumtupa kwa makusudi Yona baharini liliwaogopesha sana. Walijaribu kuipeleka meli

kuelekea nchi kavu, lakini walishindwa. Watu wakamlilia BWANA. Ikaonekana kuwa ni lazima

wafanye kama Yona alivyokuwa amewaambia, uku wakimwomba ili Mungu asiwahsabie

dhambi hiyo, maana walimwamini Yona, kuwa ni Mungu aliyeleta mawimbi hayo kw sbabu

yake.

Basi wakamkata Yona, wakamtupa baharini nayo bahari ikatulia. Yoha alikuwa ameongea

kweli-Mungu wake ni kwelindiye aliyeumba bahari na nchi kavu. Wakamtolea dhmbihu ili

kuonyesha shukrani na wakeweka nadhiri ya kumtumikia BWANA. Kwa hiyo wale watu

wakapona kwa kuwa walimpeleka katika mauti.

Hata hivyo, Yona hakufa, Kwa upendo na rehema za ajabu, alikuwa ameshamwadaa

samaki mkubwa kummeza .Yona akawa katika tumbo la la samaki yule mkubwa muda siku

tatu mchanana usiku.

YONA ANALITII NENO LA MUNGU: Yona 2 na 3

Wakati Yona kw mwujiza alikuwa ndani tumbo la samaki mkubwa,alimkumbuka

Mungu,na akakumbu upumbavu wake wa kujaribu kukimbia ili asifanye kazi ya

Mungu.Aliomba na Mungu akamsamehe, akaahidi kuwa atafanya kama Mungu

alivyomwagiza.Kwa hiyo Yoona akajinyenyekeza na akatumbu kwa kutokutii agizo la Mungu.

“BWANA akasema na yule samaki, naye kmtapika Yona pwani” (Yona 2:10).

Ndipo neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, akiagizwa aondoke akarihubiri neno la

Mungu kule Ninawi. Ulikuwa ni mji mkubwa sana, yapata kama km 80 mzunguko wake. Ikawa

Yona alipoingia katika mji alianza kupaza sauti yake ili kila mmoja asikie, “Baada ya siku

arobaini Ninawi utaangamizwa” (mstari 3:4)

Watu wa Ninawi wakaogopa sana hiyo hukumu ambayo Yona alikuwa anaitangaza nao

“wakamwamini Mungu”

Na ikawa Mfalme aliposikia habari hii akaondoka katika kiti cha enzi akavua mavazi yake

ya kifalme akavaa magunia na akakaa katika majivu, hii ikiwa ni ishara ya huzuni na

kutubu.Na watu wote kuanzia aliyekuwa mdogo mpaka aliyekuwa mkuu, wakafanya hivyo

hivyo.Mfalme akatangaza kuwa kila mtu asile chakula na “wakamlilie Mungu kwa nguvu”

na wageuke, wakaache njia zao mbaya.Mfalme wa Ninawi akasema, “Ni nani ajuaye

kwamba Mungu hatageuka na kughairi, a kuiacha hasira yake kali, ili tusiangamizwe?”

(mstari 9)

Mungu alipoona jinsi walivyotubu na kugeuka kuziacha njia zao mbaya, kwa kweli Mungu

aliwaonyesha rehema na hakuwaangamiza.

FUNDISHO KWETU

Habari hiiinazungumzia sana kuhusu kutubu.Mungu aliwataka watu wa Ninawi watubu

kwa ajili ya njia zao mbaya au Mungu awaangamize.

'Kutubu' ni kuomba msamaha kwa ajili ya dhambi zetu tulizozifanya wakati uliopita na

kubadilisha njia zetu na tabia zetu pia.Yona alimwasi Mungu lakini alitubu akanyeyekea na

akaokolewa badala ya kufa akiwa katika maji. Wakati watu wa Ninawi walipomsikia Yona

akihubiri walitubu-mawazo ya mioyo yao ilibadilika na wakawomba Mungu awasamehe.Kila

mmoja wetu ni lazima atafakari njia yake kila siku.Kama wazazi wetu au walimu wetu

atatuambia mahali ambapo hatukuwafurahisha ni lazima tunyenyekee na kubadili njia

zetu.Maneno ya mtume Petro aliyoyatamka siku ile ya pentekoste ni ya mhimu kwetu na kwa

kila mmoja wetu.Petro alisema, “Tubuni, na kila mmpja abatizwe kwa jina lake Kristo,

mpate ondoleo la dhambi zenu” (Matendo ya Mitume 2:38)

MAELEZO YA NYONGEZA

YONA ANAJIFUNZA REHEMA YA MUNGU: Yona 4

Yona hakupenda kabisa.Basi jambo lile lile alilokuwa akilifikiria ndilo lililotokea.Alikasirika

sana.Akamwomba Mungu akasema “Kwa maana nalijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye

neema, umejaa huruma”. Yona alifikiria kuwa Mungu angeonyesha huruma hiyo kwa Israeli

tu, lakini huruma hiyo wasipewe maadui wao.Akamwomba Mungu auchukue uhai wake ili

yeye afe.Mungu, hata hivyo alimhifadhi Yona ili apate kujifunza kwamba Mungu, “hapendi

mtu yeyote apotee, bali wote wafikirie toba” (2 Petro 3:9).

Mungu atawaangamiza watu wale wanaokataa kulisikia neno lake tu -kwamba ni

Wayahudi au Watu wa mataifa.

Mtume Petro naye aliweza kujifunza somo hili miaka mingi baadaye. Alijifunza kwamba

“katika kila taifa mtu amchaye Mungu, na kutenda haki hukubaliwa na yeye” (Matendo

ya Mitume 10:35). Ni furaha kubwa iliyoje tuliyonayo kuwa na Mungu aliye na tabia hii, kwa

maana sisi ni watu wa mataifa ambao Mungu ametuonyesha kweli yake na ametupatia

tumaini la wokovu

ISHARA YA NABII YONA: Mathayo12:38-41

Bwana Yesu Kristo alitumia habari hii inayomhusu Yona kama ishara kwa Wayahudi wale

waliokuwapo siku za Yesu. Waandishi na Mafarisayo walikuwa na mashaka ya yeye kuwa

masiya, “mpakwa mafuta” wa Mungu.Kwa hiyo alitumia ishara hii kutaja yatakayompata

baadaye kuhusu kifo chake na kufufuka kwake.

Ni kwa ajili ya kufufuka kwake katika wafu kulikosababisha atu wengi waamwamini Yesu.

“Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la

nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku

katika moyo wa nchi” (mstari 40)

Mungu akamtoa Yona katika tumbo la samaki baada ya siku tatu, ambapo alipokuwa

tumboni yeye alikuwa ni sawa kabisa na aliyekufa. Kisha akaenda Ninawi moja kwa moja,

ambapo aliwahubiri watu ujumbe wa Mungu, uliowataka watu watubu.

Yesu alikuwa kaburini siku tatu mchana na usiku na baadaye alifufuka kutoka katika wafu

(Luka 24:5-7 Matendo ya Mitume 2:31)

Na baada yapo, aliwafundisha wanafunzi wake kwa muda siku arobaini, kabla hajapaa

kwenda mbinguni (Matendo ya Mitume 1:3, 9)

Bwana Yesu Kristo ni wa kwanza kufufuka katika wafu na kupewa uzima wa milele, lakini

Mungu ameweka neema hii ya tumaini moja la uzima wa milele kwa watu wote watakao

mwamini Mungu na kumtii (1Wakorintho 15:20-23)

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Ninawi ilikuwa wapi?

2. Ni ujumbe gani ambao Mungu alimpatia Yona awambie watu wa Ninawi?

3. Yona aliamua kufanya nini?

4. Yona alikuwa akifanya nini wakati wimbi lilipozidi?

5. Ni jinsi gani mabaharia walivyojua kuwa Yona ndiye wakulaumiwa kwa ajili ya mawimbi

yale?

6. Je! Yona alimwabudu nani?

7. Yona aliwaambia mabaharia wamfanyaje?

8. Mabaharia walifanya nini kabla ya kumtupa Yona baharini?

9. Palitokea nini baada ya mabaharia kumtupa Yona baharini?

10. Yona hakufa katika maji Ilitokea nini kwake?

11. Yona alikwenda wapi baada ya kufika nchi kavu?

12. Watu wa Ninawi walifanya nini baada ya kusikia ujumbe wa Yona?

Majibu ya Kina

13. Yona alijaribu kutoroka asifanye kazi aliyoagizwa na Mungu?

(a) Ni kwa nini alijaribu kutoroka uso wa Mungu?

(b) Yona alifanya nini?

14. Eleza palitokea nini wakati Mungu alipotuma mawimbi ya tufani kubwa na jinsi Yona

alivyofika nchi kavu salama?

15. Eleza kilichotokea wakati Yona alipofika Ninawi?

Majibu ya Nyongeza

16. (a) Nini maana ya kutubu?

(b) Ni kwa watu gani ambao Mungu anawaonyesha rehema?

(c) Je! hili linatusaidiaje sisi?

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!